Maulidi Kusherehekewa Wakati Msichana Anavunja Ungo Na Kwa Biharusi

 

 

Maulidi Kusherehekewa Wakati Msichana Anavunja Ungo Na Kwa Biharusi

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Asalaam Aeikum Ndugu zangu katika Uislam

Kwanza napenda kuchukua nafasi hii, kumshukuru Mwenyezi Mungu Subhaana waala Taala, kwa kunijaalia uzima na afya njema na uwezo wa kuweza kufahamu mtandao huu wa Alhidaaya. Katika siku ya leo napenda kuuliza maswali yafautayo ambayo yamekuwa yakinitatiza kichwani mwangu.

 

Kuna tabia katika baaaadhi ya jamii hapa kufanya sherehe, pengine husoma hata maulidi kwa mabinti zao baaada ya kuvunja ungo (kubalehe) Katika sherehe hizo pamoja na mambo mengine binti hufundishwa jinsi ya kuishi na mume pindi anapoolewa. Je mafunzo haya ni sahihi katika uislamu. Na kama si sahihi ni vipi binti wa kiislamu akikuwa hufunzwa

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Hakuna katika shariY’ah ya Kiislamu sherehe yoyote inayofanywa baada ya msichana kubaleghe. Inatakiwa watoto, wasichana na wavulana waanze kufundishwa na wazazi wao kuanzia wanapofika miaka saba namna ya kufanya ‘Ibaadah kama Swaalah na kufunga. Hilo ni agizo la Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pale aliposema:

Waamrisheni watoto wenu kuswali wakiwa na miaka saba na watenganisheni katika malazi wakiwa na miaka kumi …” [Abuu Daawuwd].

 

Uislamu unatutaka sisi tuanze mapema kuwafundisha wasichana mambo mengi zaidi kwani wao wana tofauti kubwa na wenziwao wavulana kama kujisitiri, kujihifadhi kwa kuvaa hifadha wanapoanza kutoka damu ya hedhi na kujihifadhi.

 

Hakuna sherehe mbali na mafunzo kwa wasichana. Kisha kuna mafunzo ya kukaa na mume watakapoolewa kwa njia nzuri ya Kiislamu. Mambo hayo wanaweza kuyapata katika Madrasah kwani Uislamu unatuongoza katika kila jambo. Vilevile wanaweza kupata mafunzo hayo katika vitabu vya Kiislamu vinavyoeleza suala hilo. Na bila shaka wa kufundisha hayo kwa njia nzuri na muafaka zaidi ni mama mzazi au mlezi ili binti ainukie katika malezi ya Kiislamu na kuishi vizuri na mume wake Kiislamu pindi anapoolewa.  

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Kusoma Maulidi Kwenye Harusi Badala Kupiga Ngoma Inafaa?

 

Kuna Ushahidi Aliyerudi Hajj Asomewe Maulidi?

 

Yanayopasa Na Yasiyopasa Kutendeka Katika Ndoa

 

Yanayompasa Bwana Harusi Na Bibi Harusi Siku Ya kufunga Ndoa

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share