Shaykh Fawzaan: Sha'baan: Hukmu Swiyaam Mwezi Wa Sha’baan
Hukmu Swiyaam Mwezi Wa Sha’baan
Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Je kuna lolote lilotajwa kuhusu Swiyaam ya Sha’baan? Nini Hukmu ya kuihusisha tarehe 15 mwezi wa Sha’baan kila mwaka kwa Swiyaam?
JIBU:
Na’aam. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifunga Swawm katika Sha’baan na akifunga zaidi humo. Hivyo Sunnah ni kufunga katika Sha’baaan na kukithirisha kufunga.
[Mawqi' Ar-Rasmiy li-Ma'aaliy Shaykh Swaalih bin Fawzaan]
