Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Hajj: Haijuzu Kumpa Mchinjaji Wa Udhwhiyah Nyama Kama Ujira Wake
Haijuzu Kumpa Mchinjaji Wa Udhw-hiyah Nyama Kama Ujira Wake
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je, inajuzu kumlipa mchinjaji nyama kama ndio ujira wake wa kuchinja?
JIBU:
Kumpa nyama mchinjai (aliyoichinja) kama ni ujira wake, haijuzu. Ama kumgaia kama zawadi hakuna ubaya.
[Majmuw’ Fataawa Wa Rasaail Al-‘Uthaymiyn (25/110)]
