Mashairi: Mgeni Si Yule Aliyekwenda Shaam Na Yemen

 

Mgeni Si Yule Aliyekwenda Shaam Na Yemen

 

Zaynul-‘Aabidiyn ‘Aliy Bin Al-Husayn bin ‘Aliy Bin Abi Twaalib (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

  

 

لَيْسَ الغَريبُ غَريبَ الشَّامِ واليَمَنِ                      إِنَّ الغَريبَ غَريبُ اللَّحدِ والكَفَنِ

Mgeni si yule aliyekwenda Sham au Yemen,

bali mgeni hasa ni yule wa mwanandani wa kaburi na sanda.

 

 

إِنَّ الغَريِبَ لَهُ حَقٌّ لِغُرْبَتـِهِ                              على الْمُقيمينَ في الأَوطــانِ والسَّكَنِ

Bila shaka mgeni kwa ugeni wake, ana haki ya kukirimiwa

na wenyeji wake katika nchi na makazi.

 

سَفَري بَعيدٌ وَزادي لَنْ يُبَلِّغَنـي                           وَقُوَّتي ضَعُفَتْ والمـوتُ يَطلُبُنـي

Safari yangu ni ndefu na masurufu yangu hayatonifikisha popote,

na nguvu zangu zimedhoofu huku mauti yakiniandama.

 

وَلي بَقايــا ذُنوبٍ لَسْتُ أَعْلَمُها                         الله يَعْلَمُهــا في السِّرِ والعَلَنِ

Nina mabaki ya madhambi na mimi siyajui,

Allaah Anayajua nikiyafanya kwa siri au hadharani.

 

مـَا أَحْلَمَ اللهَ عَني حَيْثُ أَمْهَلَني                         وقَدْ تَمـادَيْتُ في ذَنْبي ويَسْتُرُنِي

Ni upole ulioje Anaonifanyia Allaah pale Anapoendelea kunipa muda,

wakati mimi nimezamia kwenye madhambi Naye Ananisitiri.

 

تَمُرُّ سـاعـاتُ أَيّـَامي بِلا نَدَمٍ                          ولا بُكاءٍ وَلاخَـوْفٍ ولا حـَزَنِ

Masaa ya umri wangu yanapita bila mimi kujuta,

wala kulia, wala kuogopa na wala hata kuhuzunika.

 

أَنَـا الَّذِي أُغْلِقُ الأَبْوابَ مُجْتَهِداً                        عَلى المعاصِي وَعَيْنُ اللهِ تَنْظُرُنـي

 Mimi ndiye ninayejifungia kwa hima milango

ya maasi na ilhali Jicho la Allaah linanitizama

 

يَـا زَلَّةً كُتِبَتْ في غَفْلَةٍ ذَهَبَتْ                           يَـا حَسْرَةً بَقِيَتْ في القَلبِ تُحْرِقُني

.Ee dhambi lililoandikwa, limekwenda bila kuhisi,

ee majuto yaliyosalia moyoni yakiniunguza

 

دَعْني أَنُوحُ عَلى نَفْسي وَأَنْدِبُـهـا                     وَأَقْطَعُ الدَّهْرَ بِالتَّذْكِيـرِ وَالحَزَنِ

Niache niililie na niiombolezee nafsi yangu,

na niumalize umri wangu wote kwa kukumbusha na kuhuzunika.

 

كَأَنَّني بَينَ تلك الأَهلِ مُنطَرِحــَاً                         عَلى الفِراشِ وَأَيْديهِمْ تُقَلِّبُنــي

Kama kwamba mimi nimejibwaga kitandani

katikati ya watu hao, huku mikono yao ikinigeuzageuza.

 

وَقد أَتَوْا بِطَبيبٍ كَـيْ يُعالِجَنـي                         وَلَمْ أَرَ الطِّبَّ هـذا اليـومَ يَنْفَعُني

Na nikaletewa tabibu ili aniponyeshe,

wala sikuona tabibu wa kunifaa siku hii

 

واشَتد نَزْعِي وَصَار المَوتُ يَجْذِبُـها                      مِن كُلِّ عِرْقٍ بِلا رِفقٍ ولا هَوَنِ

Kung’olewa roho kumekuwa kugumu na kuzito, na mauti yamekuwa yakiivuta, toka kwenye kila mshipa bila huruma wala upole.

 

واستَخْرَجَ الرُّوحَ مِني في تَغَرْغُرِها                    وصـَارَ رِيقي مَريراً حِينَ غَرْغَرَني

Mauti yakaitoa roho yangu kwa mkoromo wake kooni, na mate yakawa machungu yaliposakama kooni.

 

وَغَمَّضُوني وَراحَ الكُلُّ وانْصَرَفوا                       بَعْدَ الإِياسِ وَجَدُّوا في شِرَا الكَفَنِ

Wakanifunga macho kisha wote wakaondoka, baada ya kukata tamaa na wakafanya hima ya kununua sanda.

 

وَقـامَ مَنْ كانَ حِبَّ لنّاسِ في عَجَلٍ                   نَحْوَ المُغَسِّلِ يَأْتينـي يُغَسِّلُنــي

Na yule aliyekuwa akinipenda zaidi akasimama haraka,

kwenda kuniletea mwoshaji wa kuniosha.

 

وَقــالَ يـا قَوْمِ نَبْغِي غاسِلاً حَذِقاً                   حُراً أَرِيباً لَبِيبـاً عَارِفـاً فَطِنِ

Akasema: Enyi watu wangu! Tunataka mwoshaji mmakinifu, hodari, mwerevu, mjuzi na stadi.

 

فَجــاءَني رَجُلٌ مِنْهُمْ فَجَرَّدَني                       مِنَ الثِّيــابِ وَأَعْرَاني وأَفْرَدَني

Hapo akaja mtu kati yao, akanivua nguo

na kuniacha uchi bila chochote.

 

وَأَوْدَعوني عَلى الأَلْواحِ مُنْطَرِحـاً                    وَصـَارَ فَوْقي خَرِيرُ الماءِ يَنْظِفُني

Kisha wakanipeleka wakanibwaga juu ya vibao,

 na pakawa juu yangu sauti ya maji yanayonisafisha.

 

وَأَسْكَبَ الماءَ مِنْ فَوقي وَغَسَّلَني                    غُسْلاً ثَلاثاً وَنَادَى القَوْمَ بِالكَفَنِ

Akanimiminia maji juu yangu, akiniosha

mara tatu tatu na kuwanadia watu walete sanda.

 

وَأَلْبَسُوني ثِيابـاً لا كِمامَ لهـا                     وَصارَ زَادي حَنُوطِي حيـنَ حَنَّطَني

Wakanivalisha nguo isiyo na mikono,

 na masurufu yangu yakawa ni dawa ya kuzuia nisinuke anayonipaka mwoshaji.

 

وأَخْرَجوني مِنَ الدُّنيـا فَوا أَسَفاً                  عَلى رَحِيـلٍ بِلا زادٍ يُبَلِّغُنـي

Kisha wakaniondosha duniani, ee majuto ya kusafiri

bila kuwa na masurufu ya kunifikisha niendako.

 

وَحَمَّلوني على الأْكتـافِ أَربَعَةٌ                      مِنَ الرِّجـالِ وَخَلْفِي مَنْ يُشَيِّعُني

Wakanibeba watu wanne mabegani,

na nyuma yangu wakafuata wanaokwenda kunizika.

 

وَقَدَّموني إِلى المحرابِ وانصَرَفوا                   خَلْفَ الإِمـَامِ فَصَلَّى ثـمّ وَدَّعَني

Wakanifikisha kwenye mihrabu,

kisha wakasimama nyuma ya Imamu, akaniswalia kisha akaniaga.

 

صَلَّوْا عَلَيَّ صَلاةً لا رُكوعَ لهـا                      ولا سُجـودَ لَعَلَّ اللـهَ يَرْحَمُني

Wakaniswalia Swalah isiyo na rukuu

wala sijda, ili pengine Allaah Akanirehemu.

 

وَأَنْزَلوني إلـى قَبري على مَهَلٍ                    وَقَدَّمُوا واحِداً مِنهـم يُلَحِّدُنـي

Wakaniteremsha taratibu kaburini mwangu,

na wakamtanguliza mmoja wao anilaze kwenye mwanandani.

 

وَكَشَّفَ الثّوْبَ عَن وَجْهي لِيَنْظُرَني                  وَأَسْكَبَ الدَّمْعَ مِنْ عَيْنيهِ أَغْرَقَني

Akanifunua uso ili anitizame, na machozi yanayobubujika

machoni mwake yakanilowesha.

 

 

فَقامَ مُحتَرِمــاً بِالعَزمِ مُشْتَمِلاً                    وَصَفَّفَ اللَّبِنَ مِنْ فَوْقِي وفـارَقَني

 

Akasimama kwa heshima na azma kamili,

akapanga matofali juu yangu kisha akaniacha.

 

 

وقَالَ هُلُّوا عليه التُّرْبَ واغْتَنِموا                   حُسْنَ الثَّوابِ مِنَ الرَّحمنِ ذِي المِنَنِ

 

Kisha akasema: Haya mmiminieni mchanga,

na ziwahini thawabu njema toka kwa Allaah Mrehemevu na Mwenye wema.

 

في ظُلْمَةِ القبرِ لا أُمٌّ هنــاك ولا                  أَبٌ شَفـيقٌ ولا أَخٌ يُؤَنِّسُنــي

Ndani ya giza la kaburi, hakuna huko mama, wala baba wa kunionea huruma wala ndugu wa kuniliwaza.

 

فَرِيدٌ وَحِيدُ القبرِ، يــا أَسَفـاً                     عَلى الفِراقِ بِلا عَمَلٍ يُزَوِّدُنـي

Niko peke yangu kaburini,

ee majuto ya kuiacha dunia bila amali za kunisaidia.

 

 

فَلا تَغُرَّنَّكَ الدُّنْيــا وَزِينَتُها                   وانْظُرْ إلى فِعْلِهــا في الأَهْلِ والوَطَنِ

Basi kamwe dunia na mapambo yake isikudanganye,

angalia imewafanya nini watu na nchi.

 

وانْظُرْ إِلى مَنْ حَوَى الدُّنْيا بِأَجْمَعِها                هَلْ رَاحَ مِنْها بِغَيْرِ الحَنْطِ والكَفَنِ

Hebu mwangalie yule aliyejilimbikizia dunia yote,

hakuondoka na chochote isipokuwa dawa .ya kuzuia asinuke na sanda yake tu

 

خُذِ القَنـَاعَةَ مِنْ دُنْيَاك وارْضَ بِها              لَوْ لم يَكُنْ لَكَ إِلا رَاحَةُ البَدَنِ

Kinaika na ridhika na ukipatacho duniani,

na kama si hivyo, basi hutakuwa na raha.

 

 

يا زَارِعَ الخَيْرِ تحصُدْ بَعْدَهُ ثَمَراً                 يَا زَارِعَ الشَّرِّ مَوْقُوفٌ عَلَى الوَهَنِ

Ee mwenye kupandikiza kheri! Matunda utayachuma baadaye.

Ee mwenye kupandikiza shari! Utasimamishwa juu ya unyonge

 

 

 

يـَا نَفْسُ كُفِّي عَنِ العِصْيانِ واكْتَسِبِي              فِعْلاً جميلاً لَعَلَّ اللهَ يَرحَمُني

Ewe nafsi! Jizuie na maasia na chuma vitendo vyema,

 pengine Allaah Akanirehemu.

 

 

يَا نَفْسُ وَيْحَكِ تُوبي واعمَلِي حَسَناً             عَسى تُجازَيْنَ بَعْدَ الموتِ بِالحَسَنِ

.Ewe nafsi! Kwanini usitubie na ukatenda mema?

Huenda Ukalipwa mema baada ya kufa

 

ثمَّ الصلاةُ على الْمُختـارِ سَيِّدِنـا               مَا وَصَّـا البَرْقَ في شَّامٍ وفي يَمَنِ

Kisha rehma kwa Bwana wetu mteuliwa,

 kwa nuru aliyousia Shaam na Yemen.

 

والحمدُ لله مُمْسِينَـا وَمُصْبِحِنَا                  بِالخَيْرِ والعَفْوْ والإِحْســانِ وَالمِنَنِ

Tunamshukuru Allaah Anayetufikisha jioni na asubuhi,

kwa kheri, msamaha, ihsani na wema.

 

 

 

 

 

Share