Al-Lajnah Ad-Daaimah: Kusoma Al-Faatihah Katika ‘Aqdi Za Ndoa Na Katika Misiba Ni Bid’ah
Kusoma Al-Faatihah Katika ‘Aqdi Za Ndoa Na Katika Misiba Ni Bid’ah
Al-Lajnah Ad-Daaimah
Haikuthibiti kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala kutoka kwa Maswahaba wake kwamba walikuwa wakisoma Al-Faatihah katika ‘Aqdi za Ndoa au katika misiba au katika mikataba ya biashara.
Na ingelikuwa hivyo (kusoma Al-Faatihah) ni khayr, basi wangelitutangulia (kufanya hivyo).
[Al-Lajnah Ad-Daaimah (19/46)]