Imaam Ibn Taymiyyah: Kutamka Niyyah Katika ‘Ibaadah Ni Upungufuu Wa Akili Na Dini
Kutamka Niyyah Katika ‘Ibaadah Ni Upungufu Katika Akili Na Dini
Imaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu-Allaah)
Amesema Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu-Allaah):
Kutamka niyyah ni upungufu katika akili na Dini.
Ama katika Dini kwa sababu ni bid’ah, na katika akili ni kwa sababu ni sawa na ambaye anataka kula chakula husema: “Nanuia kuweka mkono wangu katika chombo hiki kwa kutaka nichote humo tonge la chakula niweke mdomoni mwangu kisha nimeze ili nishibe.”
Basi huu ni ujinga na upumbavu.
[Al-Fataawaa Al-Kubraa (2/213)]