Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Dhulma Ina Malipo Ima Duniani Ama Aakhirah

 

Dhulma Ina Malipo Ima Duniani Ama Aakhirah

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com 

 

Amesema Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah):

"Usidhani dhulma yoyote inayokuwa duniani itaenda bure daima. Haki ya kiumbe lazima ichukuliwe siku ya Qiyaamah (aliyedhulumiwa atapewa haki yake). Basi tambua kuwa wewe utasimamishwa pamoja nao (waliokudhulumu) mbele ya Allaah Mwenye Utukufu, Mwenye Ujalali, ili Awahukumu kwa uadilifu.
Basi fanya subira, na ungojee faraja."

 

 

[Sharhu Riyaadhw Asw-Swaalihiyn, mj. 2, uk. 38]

Share