Imaam Ibn 'Uthyamiyn: Kutangamana Walio Dhaifu Masikini Na Mayatima Kunaulainisha Moyo
Kutangamana Na Walio Dhaifu, Masikini Na Mayatima,
Kunaulainisha Moyo Na Kuupa Rahmah
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah) amesema:
“Tambua kwamba kutangamana na walio dhaifu na mayatima na (Watoto) wadogo, kunaufanya moyo kuwa na rahmah, na kuwa laini na huruma na kulemea kwa Allaah ('Azza wa Jalla). Lakini hadiriki hayo isipokuwa yule anayejaribu (kufanya) hivyo.”
[Sharh Riyaadhw Asw-Swaalihiyn (3/89)]