Kahama Nyumba Kwa Sababu Hataki Kuishi Na Mke Mwenza
SWALI:
Kuna ndugu yangu aliachwa na mumewe talaka moja na kabla ya kuondosha vitu vyake yaani (vitanda, makabati n.k), mumewe akamleta mke mwenzie alale chumba kile cha yule ndugu yangu kwa muda kiasi, baada ya hapo akaja kumrejea yule ndugu yangu.
Sasa ndugu yangu hataki kurejea kwa mumewe mpaka mumewe amtafutie sehemu nyingine, na hivi sasa ni kama mwaka mmoja umepita tokea waishi mbali mbali na mumewe na yule mume keshajenga nyumba ila mama wa mume amemwambia mwanaye iwapo watahamia huko kwenye hiyo nyumba, yeye haendi (yaani huyo mama wa mume)
Sasa msaada wenu wa haraka ili kuinusuru ndoa hii, kwa kuwa huu ndugu yangu sasa hivi anaona ni bora apewe talaka.
Ahsanteni
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani ndugu yetu kwa swali lako
Ni muhimu wanandoa kuelewana, na ni makosa kwa mume kumuingizia mkewe mke mwengine kabla hajaondoa vitu vyake baada ya kuachana. Kama vile ni makosa kwa mume kumtoa mkewe kwenye nyumba baada ya talaka kwani huo ni muda uliowekwa na Muumba na Mjuzi wa maumbile yetu ili wanandoa hao waweze kurudiana kama mume na mke. Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Anatuagiza kuwa mke katika kipindi hicho hafai kutoka wala kutolewa ila tu ikiwa mke amefanya jambo la ufasiki ulio wazi,
“Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitoke wenyewe, ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu, msiikiuke. Na mwenye kuikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi amejidhulumu nafsi yake. Hujui; labda Mwenyezi Mungu Ataleta jambo jengine baada ya haya.” (65: 1). Hakika ni kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) katika wakati wa eda ameziita nyumba hata zikiwa ni za mwanamume kuwa ni nyumba za mke.
Kuna maneno hapa ambayo yanachanganya na huenda mpaka yawekwe wazi ndio tupate ufumbuzi wa haraka. Ibara hiyo ni “..baada ya hapo akaja akamrejea yule ndugu yangu” na “hivi sasa ni
- Mume alimrudia mkewe katika kipindi cha eda (hedhi au twahara tatu)?
- Ikiwa ni hivyo, huo mwaka uliosema wa kuishi mbali mbali umetokea wapi?
- Ikiwa alimrudia baada ya eda je, mke aliridhika kuolewa? Je, kulifungwa Nikaah mpya na mke kupatiwa mahari?
Ikiwa eda yake lilipita inabidi mume amuoe kwa ndoa mpya na kabla ya ndoa mke ana haki kuweka masharti yake. Masharti hayo
Ikiwa mama wa mume ameweka sharti
Tunamuomba Allaah Aliyetukuka amfanyie sahali dada yako na wengine wenye matatizo mbalimbali.
Na Allaah Anajua zaidi