Kukidhi Swalah Ya Safari Na Namna Ya Kunuia

  SWALI:

Swali langu ni  ktk swalah za kuunganisha ukiwa safarini.

Adhuhur na Alasir(takdimah au taahirah),Magharibi na Ishah (takdimah au taahirah).Kwa bahati mbaya ukipitiwa kama vile kwa kulala,muda ukapita wa kusali takdimah na taahirah pia,na imebidi usali kadhwa,HAPA NDIPO PENYE SWALI LANGU. Unanuia kadhwa ya takdimar au taahirah(rakaa mbili mbili) AU unanuia kadhwa ya Adhuhur au Alasir (sala moja moja bila kuunganisha)?



 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa muulizaji swali kuhusu suala la kuchanganya Swalah. Suala lako linaingia katika nyudhuru za kuakhirisha Swalah kwani kulala ni mojawapo ya sababu inayokubaliwa. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

Kalamu imenyanyuliwa kwa watatu: Aliyelala mpaka aamke, mtoto mpaka abaleghe na mwendawazimu mpaka awe na akili timamu” (Ahmad, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaaiy, Ibn Maajah, na al-Haakim, akasema ni sahihi).

 

Ni wajibu kulipa Swalah kwa kuzikidhi kwa nyudhuru zinazokubalika kisheria. Hivyo, inatakiwa pindi unapoamka kutoka katika usingizi uswali Swalah ya Adhuhuri kisha Alasiri kama bado unaswali Swalah ya safari utaswali rakaa mbili mbili na kama ni mkaazi itakuwa rakaa nne nne. Hizi hazitakuwa takdima wala taahira bali ni Qadhwaa.

 

Na nia pahala pake ni moyoni na hufai kutamka wala kukariri kama kisomo. Unapopitisha maamuzi kuwa unaelekea kuswali Swalah Fulani, basi hiyo ndio nia yako na hutakiwa kujikalifisha kwa kujifundisha maneno ya kiarabu ya kuhifadhi kwa ajili ya nia na pia kuirudia rudia hiyo nia hadi uhisi imekita au imekutana na Takbiyra kama wengine wanavyofanya.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share