Mume Mlevi, Mtusi, Anaiba Vitu Vyangu Na Ananipiga Nimeamua Kumfukuza. Je, Nimekosea?
SW
As/aleikum, sheikh, mimi nina mume ambaye ni mlevi, mtusi mpigaji, mwizi wa vitu vyangu vya dhahabu, kauza vitu vyangu vyote vya dhahabu, analeta ulevi ndani ya nyumba, nikimkataza anatoa maneno mabaya kwangu na watoto. Nikuwa mja mzito ikawa ananipiga nakuniapiza maapizo mabaya, mpaka akanambia nitakufa juu ya kitanda wakati wa kujifungua. Nimejifungua kwa uperesheni.
Baada ya wiki nimetoka hosp. akaanza tena kunitukana, nimeshamwitia watu kumsema nae ajirekebishe lakini hataki. Nimeamua kumtoa katika nyumba yangu, na nimemuomba anipe talaka hataki. JEE SHEKHE NINI HUKUMU YA NDOA HII? KWA SABABU MIMI SIMTAKI TENA HATA KUMUONA KWA VITENDO VYAKE VIOVU NAOMBA USHAURI WA KISHERIA YA DINI YETU TUKUFU. ASSALAM ALEIKUM.
MWISHO WA Y
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika Salaam hazifai kufupishwa kwa kuandikwa (A.A) au (A.A.W.W.) au kama ulivyoandika kwani haijafundishwa hivyo na pia ni kujikosesha fadhila za Salaam
Shukran zetu za dhati kwa swali lako kuhusu vurugu za mumeo kwako. Hakika, matatizo ya kijamii na kwa wanandoa ni mengi hasa katika jamii yetu.
Hata hivyo, hata matatizo na misiba
Tunajitakia sisi wenyewe kivipi? Hili ni swali zuri na jawabu
Hayo kando, madhara makubwa yanaweza kukupata ikiwa unaishi na mlevi, mtu asiyejali maslahi yako kabisa. Shari'ah inakupatia wewe fursa ya kujivua katika ndoa hiyo lakini kabla ya kufanya hivyo inabidi wewe uitishe kikao ambacho utakuwepo wewe, yeye, mzazi (au wazazi) wako na wake. Katika kikao hicho unatakiwa uelezee yote hayo nao wanaweza kutoa uamuzi ambao unaofaa, ima wa mumeo kupatiwa muda mwingine wa kujirekebisha au kukuacha au kuachishwa. Ikiwa hakuna natija yoyote katika kikao hicho basi itabidi upeleke kesi yako kwa Qaadhi ikiwa yupo katika mji wako au kwa Shaykh muadilifu, yule aliyefungisha nikaah yenu au mwengine. Naye amepatiwa ruhusa kwa maonevu
Tunakuombea kila la kheri katika mambo yako yote.
Na Allaah Anajua zaidi