Baklawa Za Pistachio Na Lozi

Baklawa Za Pistachio Na Lozi

Vipimo

 

Philo (thin pastry) manda nyembamba - 1 paketi                                                  

Siagi - ¼ Kikombe cha chai

Baking powder  - 2 Vijiko vya chai

Pistachio/ lozi -   2 vikombe vya chai

Mafuta -  ½ Kikombe

 

Shira

Sukari -  2 Vikombe vya chai

Maji - 2 ½ Vikombe vya chai

ndimu -   ½ kijiko cha chai

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Tafuta treya iliyokuwa sawa na ukubwa wa hizo manda nyembamba (philo) au zikate hizo manda kwa ukubwa wa treya (mraba au mstatili)
  2. Kisha yeyusha siagi changanya na mafuta.
  3. Kisha panga manda moja pakaza mafuta juu yake kisha weka manda nyingine juu yake kisha pakaza mafuta tena weka manda nyingine juu yake, endelea kufanya hivyo mpaka ziwe kama sita au saba kisha nyunyizia pistachio na lozi halafu panga tena manda na mafuta manda na mafuta tena sita au saba kisha nyunyizia tena pistachio na  lozi.
  4. Panga namna hivyo mpaka treya ijae inapofika manda ya mwisho kata vipande vya mraba vidogodogo humo humo kwenye treya kisha nyunyizia mafuta yaliyobaki.
  5. Washa moto wa oven 350°F kwa muda wa dakika 20 au hadi rangi ibadilike kidogo (isikauke sana)
  6. Chemsha syrup yako kama shira ya majimaji lakini isiwe nzito sana ikishakuwa tayari mwisho tia ndimu acha ipoe kidogo kisha miminia juu ya treya yote halafu malizia kunyunyizia pistachio na lozi zilizobaki.
  7. Zikishakuwa tayari zipange kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

Vidokezo:

  1. Ukishatoa treya kwenye oven wacha ipoe kidogo na syrup yako pia wacha ipoe kidogo kabla hujamimina, ukitia ya motomoto zitalainika.
  2. Manda nyembamba za baklawa zinauzwa tiyari madukani kwenye pakiti.

 

 

 

 

 

Share