SWALI:
ASSALAM ALAIKUM WARAHMATU LLAHI WABARAKATU. KWANZA NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZA DHATI KWA KAZI YENI NZURI YA KUTUONGOZA NA KUTUTOA KWENYE UJINGA MWENYEZI MUNGU ATAWALIPA INSHAALLAH. MIMI NAISHI ..... NA KAZI YA VIJANA WENGI WANAOTOKA AFRIKA KWA ASILIMIA KUBWA NI UDALALI (BROKER) YAANI WAKIJA WAFANYA BIASHARA KURANGUA BIDHAA AO GARI WENYEWE NDIO WANAWAPELEKA KUNUNUA, WAKIFIKA DUKANI AO KWENYE MA SHOO ROOM HUA WANAULIZA KWANZA KAMA WATAPATA BAASHISHI (WANAJITAHIDI KUULIZA KWA NJIA AMBAYO ULE MFANYA BIASHARA ASIJUI) KAMA WAKIKUBALIWA WANAMSHAURI KUNUNUA NA KAMA WAKITATALIWA WATATAFUTA SABABU YEYOTE YA KUMKATAZA HUYO MFANYA BIASHARA ASININUI. OMBI LANGU NI KUJUA FATWA YA HIYO KAZI NAOMBA MNGETUTAYARISHIA MADA KAMILI ILI NI PRINT NA WENYEWE WAFAIDIKE. WAHADHA ASSALAAM ALAIKUM WARAHMATU LLAHI WABARAKATUH
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu udalali wa udanganyifu unaofanywa na watu huko ..... Ni wazi kuwa Uislamu kwa ujumla wake umekataza kabisa udanganyifu na uwongo kwa kiasi ambacho Allaah Aliyetukuka Anasema: “Enyi mlioamini! Mcheni Allaah, na kuweni pamoja na wakweli” (at-Tawbah [9]: 119). Hapa Allaah Aliyetukuka Anatuhimiza tuwe na wakweli, hivyo sisi wenyewe tunahitajika kuwa wakweli kimatendo na kauli. Anasema tena Aliyetukuka: “Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na semeni maneno ya sawasawa” (al-Ahzaab [33]: 70).
Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) naye amesema: “Mwenye kutughushi (kutudanganya) si katika sisi” (Muslim). Kwa hiyo biashara yoyote ile ambayo Muislamu atakuwa anaifanya ni lazima awe mkweli. Kwa kuwa kuwapeleka wafanyi biashara katika maduka ya biashara ili wapate kununua vitu nayo ni kazi inatakiwa dalali asikilizane ujira pamoja na mfanyi biashara ili aweze kumfanyia kazi yake. Mkishaagana atakacho kupatia mfanyi biashara kama ujira wa kazi yako itakuwa hufai tena kuchukua bakhshishi kutoka kwa mwenye duka kwani wewe ushalipwa.
Hakika ni makosa kutumia hila ya kumfanya mfanyi biashara asiwe ni mwenye kununua kutoka katika duka fulani kwa sababu mwenye duka hilo amekataa kukuhonga. Na hongo ni haraam kabisa, na mwenye kufanya hilo amelaaniwa.
Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:
Mimi Ni Msimamizi Wa Kampuni Na Kila Ninapowapa Kazi Vibarua, Hunipa Posho Kama Shukurani, Ni Sawa Kupokea?
Posho Nje Ya Mshahara
Na Allaah Anajua zaidi.