Ameishi Na Mumewe Miaka 30 Lakini Anamtesa Na Kumnyanyasa Na Hamtimizii Matumizi

SWALI:

ASSALAM ALEHKUM.

NASHUKURU SANA KWA KUTUFAHAMISHA MAMBO AMBAYO TULIKUA ATUFAHAM YA DINI YETU YA KIISLAM.

 NAOMBA KULIZA : MWANAMKE ALIE SLIM AKAFUNG ANDOA YA KISLAM WAKAJALIWA KUPATA MALI NA MUMEWE .MUMEA AME BADILIKA ANAMNYANYASA, ANA MTUSI MBELA YA WATOTO NA WAFANYAKAZI AKIPIKA ANA MWAMBIA CHAKULA UMEPONDA NA MIGUU AMEDIRIKI KUMTUKANA MBELE YA HADHARA LAKINI MWANA MKE AKUJIBU ILA PRESHA ILIPANDA . NA WAMEISHI KWA MUDA WA MIAKA 30.

VILEVILE MAMA HUYO MATUMIZI YA MUHIMU MUMEWE HAMPATII ANATEGEMEA WATOTO. MAMA HUYO PAMOJA NA MATESO YOTE BADO YUPO NYUMBANI KWAKE .MWANAMKE AMEVUMILIA VYAKUTOSHA ANASHINDWA AFANYE NINI KWANI KILA JAMBO ANALO FANYA KWA MUME WAKE HALIWI ZURI YANI MWANAUME HARIDHIKI NA TUNAAMBIWA PEPO YA MWANAMKE IPO MIGUUNI MWA MUMEWE .JE MAMA HUYOU AFANYAJE ILI AWEZE KUIPATA PEPO KWANI HUJIULIZA NA “KUSEMA SIJUI KAMA NITAIPATA PEPO KWANI MUMEWANGU HAISHI LAWAMA NA MASIMANGO NA HARIDHIKI NA NINACHO FANYA”

NI ANAO MBA USHAURI MIMI NDUGU YENU KATIKA IMAN


 

JIBU:

Sifa zote njema zamstahikia Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Rehma na amani zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukran kwa swali lako.

 

Kinachotakiwa na kutarajiwa ni kuhakikisha kuwa unatekeleza majukumu yako na hayo ndio utayokuja ulizwa na Mola wako; na Pepo si ya mtu bali ni ya Mola na Mola humuingiza Amtakaye na Aliyemridhia.. 

 

Mke hutakiwa kumtii mumewe kulingana na amri za Uislamu. Ikiwa mume atakuwa anamuamrisha yasiyokubalika katika Dini hana haki ya kutii, ama upande wa mwenzako -mumeo- wewe kubwa lako ni kumnasihi na kumuaidhii na kama hakusikiliza basi ushatekeleza wajibu wako wa kuhakikisha kuwa unajilinda nafsi yako na ahli zako na moto wa Jahannam.

Subira uliyonayo ndio subira yenye kutakiwa; na kila akifanyacho yeye kwako subiri na mwachie Mola wako na tegemea malipo yako kutoka kwake Mola ikiwemo hiyo pepo.  Ni neema na fadhila kwako kuwa   umeacha dini ya upotofu na kuingia Dini ya haki. Na kuolewa kwako pamoja na kumtii mume wako, ukavumilia  maudhi yake utakuwa miongoni mwa watu wa Peponi Inshaa-Allaah

Na ujira wa mwenye kusubiri ni kama huu unaosemwa katika Qur-aan:

“Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu.” Az-Zumar: 10

 

Lakini ukishindwa kuvumilia na maudhi yakizidi kutoka kwa mumeo, pamoja na kukufedhehesha mbele za watu, kukudharau n.k. na pia kuwa hakupatii haki yako ya kukupatia matumizi, basi tunakushauri  kwanza kukaa naye umwelezee waziwazi na kumpa nasaha kwanza ajirekeibshe tabia yake kwako na akutimizie matumizi.  Na ikiwa hatakubali kupokea nasaha, basi itisha kikao baina ya watu wake na wako ili ipatikane sulhu kama Anavyosema Allaah:

“Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Allaah Atawawezesha. Hakika Allaah ni Mjuzi Mwenye khabari.” [An-Nisaa: 35.]

 

Ukishindwa kufanya hivyo basi peleka kesi yako kwa Qadhi ambaye atakuamulia la kheri kufanya. Na ikiwa hukupata Qadhi  basi nenda kwa   Shaykh muadilifu ambaye atawasikiliza nyote wawili na kutoa uamuzi kulingana na sheria ya Kiislamu.

Bonyeza pia viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Mume Ananionea, Hanipendi Ananiadhiri Mbele Za Watu, Anajuta Kunioa Nami Naumia Sana Na Mateso Haya Nifanyeje?

 

Mume Inampasa Amhudumie Mke Katika Eda? Mume Anayo Haki Ya Kudai Mahari Ikiwa Mke Anataka Kuachika?

 

Mume Haniheshimu Anawadharau Wazazi Wangu Anawatukana Watoto Wangu

 

Sina Raha Na Maisha Ya Ndoa Mume Hana Hamu Na Mimi Wala Hanishughulikii

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share