Imaam Ibn Al-Qayyim - Kuswali Juu Ya Makaburi Ni Miongoni Mwa Shirki Kubwa
Kuswali Juu Ya Makaburi Ni Miongoni Mwa Shirki Kubwa
Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:
“Kuna njia nyingi ambazo Shaytwaan aliwahadaa nazo Washirikina na kuwaingiza kwenye kuabudu masanamu. Aliwachezea Ummah na mataifa mengi kwa kuwapeleka kule akili zao na nafsi zao zinapopapenda. Aliwavuta watu waabudu masanamu kupitia njia ya kuwatukuza maiti zao.
Hawa watu wakaishia kuwachongea masanamu (hao) watu wao wema kama ilivyotokea katika kaumu ya Nuwh (‘Alayhis-Salaam). Hii ndio ikapelekea Mtume wa Allaah صلى الله عليه وآله وسلم kuwalaani wale wanaojenga Misikiti kwenye makaburi na akakataza Swalaah juu ya makaburi.”
[Ighaathatu Al-Lahfaan, 2/222-223]