Imaam Ibn Taymiyyah: Miongoni Mwa Ufisadi Ni Kumshirikisha Allaah Na Kutokumfuata Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Miongoni Mwa Ufisadi Katika Ardhi Ni Kumshirikisha Allaah Na Kutokumfuata Nabiy (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)
Imaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah)
Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
“Kwa ujumla shirki na kumwomba du’aa asiyekuwa Allaah na kumwabudu ghairi Yake, au mwenye kutiiwa anayefuatwa asiyekuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni ufisadi mkubwa kabisa katika ardhi.
Hakuna kutengenea watu wake isipokuwa mpaka iwe Allaah Ndiye Mwabudiwa Pekee na kuombwa du’aa Yeye na si mwenginewe, na utiifu na ittibaa’ (kufuata kama ilivyopokelewa mwongozo wa) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
[Majmuw’ Al-Fataawa, 25/15)]