Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Tuige Unyenyekevu Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

 

Tuige Unyenyekevu Wa Nabiy (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallaam)
 

 Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 
 
 
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
 
 
"Na katika unyenyekevu wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), alikuwa nyumbani kwake akiwahudumia ahli zake. Alikuwa akikamua mbuzi maziwa, akikarabati ndala (zilizokatika), akiwahudumia (wake zake) katika kazi za nyumbani.
 
Aliulizwa mama wa Waumini 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): 'Alikuwa akifanya nini Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nyumbani kwake?
Akajibu:
"Alikuwa katika majukumu ya ahli zake, yaani akiwahudumia."
 
Imaam Ibn 'Uthaymiyn akaendelea kueleza:
Hivyo, mfano mtu anakuwa nyumbani kwake, basi ni katika Sunnah mtu akajitengenezea chai, na akapika ikiwa anajua, na akafua vyenye kuhitajika kufuliwa; yote haya ni katika Sunnah.
Ikiwa utayafanya hayo, basi utapata thawabu za (kutekeleza) Sunnah, kwa kumuiga Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), na ni katika unyenyekevu kwa Allaah ('Azza wa Jalla), kwani haya yanaleta mapenzi baina yako na ahli wako/zako.
Wanapohisi ahli zako (mke wako au wake zako) kuwa unawasaidia katika kazi za nyumbani, watakupenda, na itazidi thamani yako kwao, na itakuwa (kutapatikana) katika haya maslahi makubwa."
 
 
[Sharh Riyaadhw Asw-swaalihiyn, mj. 2, uk. 264]
 
Share