Kutumia Miti Shamba Kwa Ajili Ya Uzazi Inafaa
SWALI:
nilikua na taka kuuliza kuhusu wale wenye matatizo ya kizazi ikiwa mtu kakaa siku nyingi hajapata kizazi na akajaribu kuomba mungu kwa kutumia dawa kama za hospitali au za majani au za miti ya kuchemsha ikawa pengine mungu akamjaalia ikawa ni dawa ya kuweza kumsaidia yeye na matatizo hayo jee kuna tatizo lolote kuhusu swala hilo inshaalla m/mungu atakuwezesheni zaidi kuyajibu maswali yetu kwa uwezo wake.
JIBU:
AlhamduliLLaah - Sifa njema zote Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Hakuna ubaya wowote kutumia dawa za miti shamba maadam tu hazihusiani na aina yoyote ya shirk
Kutumia dawa zozote za miti shamba hakuna shaka kwani asili ya dawa ya maradhi yote yanapatikana kutoka miti na mimea mbali mbali
Hadiyth ya kwanza:
عن أبي الدرداء رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((إن الله تعالى أنزل الداء والدواء وجعل لكل داء دواء فتداووا ولا تداووا بالحرام))
Imetoka kwa Abu Ad-Dardaa رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema: ((Allaah Ameteremsha maradhi na dawa zake. Kwa kila maradhi kuna dawa yake, basi jitibuni wala msijitibu kwa yaliyo haraamu))
[Al-Bukhaariy na Abu Daawuud]
Hadiyth ya pili:
عن عبدالله بن مسعود :قال رسول الله صلى الله عليه وآله وسلم (( ما أنزل الله داء إلا أنزل له دواء فعليكم بألبان البقر فإنها ترم من كل الشجر)) صحيح أو حسن - ألأباني
Imetoka kwa 'Abdullahi bin Mas'uud رضي الله عنه : Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema: ((Allaah Hakuteremsha maradhi ila Ameteremsha dawa zake, basi juu yenu (kunyweni) maziwa ya ng'ombe kwani yanatokana na kila aina ya miti)) [Hadiyth sahiyh au hasan- Sh Albaaniy]
Na dawa iliyo bora kabisa kutumia ni asali na habbatus-sawdaa (mbegu nyeusi)
Katika Qur'aan:
((وَأَوْحَى رَبُّكَ إِلَى النَّحْلِ أَنِ اتَّخِذِي مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا وَمِنَ الشَّجَرِ وَمِمَّا يَعْرِشُونَ))
((ثُمَّ كُلِي مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ فَاسْلُكِي سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلاً يَخْرُجُ مِن بُطُونِهَا شَرَابٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ فِيهِ شِفَاء لِلنَّاس))
((Na Mola wako Amemfunulia nyuki: Jitengenezee majumba yako katika milima, na katika miti, na katika wanayojenga watu))
((Kisha kula katika kila matunda, na upite katika njia za Mola wako zilizofanywa nyepesi kuzipita. Na kutoka matumbo
Katika Sunnah:
يقول رسول الله - صلى الله عليه وسلم)) إن في الحبة السوداء شفاء من كل داء إلا السأم)) . اخرجه البخاري
Amesema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ((katika habbatus-sawdaa kuna shifaa (matibabu) ya kila maradhi isipokuwa sumu)) [Al-Bukhaariy]
Kwa hiyo ikiwa umetumia aina yoyote ya dawa za miti shamba kisha ukashika mimba basi hakuna makosa Insha Allaah.
Na Allaah Anajua zaidi.