Boga La Nazi
Boga La Nazi
Vipimo
Boga la kiasi - nusu yake
Tui zito la nazi 1 ½ gilasi
Sukari ½ kikombe
Hiliki ½ kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Menya boga kisha katakata vipande vya kiasi.
- Weka katika sufuri tia maji kiasi ya kuchemshia na kuwiva bila ya kubakia maji mengi.
- Changanya tui na sukari na hiliki kisha mimina juu ya boga wacha katika moto dakika chache tu bila ya kufunika.
- Epua mimina katika chombo likiwa tayari.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)