Bonyeza hapa
Maelezo Kwa Mukhtasari Kuhusu Tarjama Ya Maana Ya Al-Qur-aan Al-‘Adhwiym Alhidaaya.com [2]
اضغط هنا
الكلمة المختصرة بخصوص ترجمة القرآن العظيم باللغة السواحيلية لموقع [3]
Alhidaaya.com [3]
Click here
Utangulizi Wa Tarjama Ya Maana Ya Al-Qur-aan Al-‘Adhiwym
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
Himdi zote Anastahiki Allaah (سبحانه وتعالى) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba zake (رضي الله عنهم) na wote waliowafuata kwa ihsaan mpaka Siku ya Mwisho.
Qur-aan ni Maneno Matukufu ya Allaah Aliyoteremshiwa Nabiy wa mwisho Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) yenye kusadikisha yale yaliyokuja kabla yake katika Vitabu vilivyotangulia, na ni Maneno yasiyoweza kufikiwa na upotofu mbele yake wala nyuma yake kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِۖ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ ﴿٤٢﴾
“Hakitokifikia ubatili mbele yake wala nyuma yake. Ni Uteremsho kutoka kwa Mwenye Hikmah wa yote, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.”[1]
Pia Qur-aan ni Kitabu cha mwisho chenye Risala (Ujumbe) kwa viumbe wote kutoka kwa Rabb wa walimwengu, kwa lengo la kuwaongoza viumbe kwenye njia iliyonyooka; na ni Mwongozo, Rahmah na Shifaa kwa Waumini.
Pia Qur-aan ni muujiza wa pekee, na wakati huo huo ni changamoto kwa viumbe wote. Hata kama viumbe vyote vitashirikiana ili vilete mfano wa Qur-aan basi havitoweza kuleta mfano wake; katika ufasaha wake, hukumu zake, ilimu zake, mwongozo wake na yote iliyoyaelezea.[2]
Qur-aan imekusanya yale yote yenye kuhitajiwa na viumbe; yawe ya dunia au ya Aakhirah yao, zikiwemo khabari za kabla yao na khabari za baada yao, na ni muamuzi na hakimu kwa Waumini wake, na ni Kitabu Alichohitimishia Allaah Sharia Zake.
Ni katika desturi Zake Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa kila Rasuli akitumwa huwa anapelekwa kwa lugha ya watu wake ili aweze kuwafikishia ujumbe. Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوْمِهِ لِيُبَيِّنَ لَهُمْ ۖ
“Na Hatukutuma Rasuli yeyote isipokuwa kwa lugha ya kaumu yake ili awabainishie (Risala).”[3]
Ni jambo lenye kujulikana kuwa lugha ya Quraysh ambayo ni lugha ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), ilikuwa ni Kiarabu sanifu. Na kwa sababu hiyo, ujumbe uliokuja ndani ya Qur-aan ulikuja katika lugha ya Kiarabu, ambayo ndiyo lugha fasaha kuliko lugha zote.[4]
Usomaji wa Qur-aan katika lugha yake, kwa walengwa wake wengi wasiokuwa Waarabu ambao hawakuafikishwa kuisoma lugha ya Kiarabu na kuifahamu vizuri, haswa Qur-aan na taaluma zake, haukuweza kuwafikisha kufahamu misingi ya Dini yao, hivyo basi, ndio pakawa na haja na umuhimu mkubwa wa kuweko Tarjama itakayoweza kumsaidia Muislamu kuweza kufahamu anachosemeshwa na Rabb wake, ikiwa maamrisho apate kuyatekeleza, na ikiwa makatazo apate kuyaepuka.
Kadhaalika, kuna ilimu na fani nyingi ambazo zimefungamana na kushikamana na Qur-aan zenye kuweza kusaidia katika kufikia kufahamu Tafsiyr ya Aayah. Ni kama vile ilimu ya Uswuwl ya Tafsiyr pamoja na kutabahari (kubobea) katika fani zote zile ambazo hakuna njia ya kufahamika Tafsiyr wala kuwa sahihi isipokuwa kwayo, kama vile kufahamu sababu za kuteremka kwa Suwrah au Aayah (Asbaab An-Nuzuwl) pamoja na za mwanzo na za mwisho kuteremka. Pia Naasikh wa Mansuwkh (kinachofuta na kilichofutwa), ukusanyaji wake, mpangilio wa Aayah na Suwrah zake, visa vyake, mifano yake, kujibu tuhuma dhidi yake na kadhalika. Hivyo, Tafsiyr inayokubalika ni ile yenye kufuata Manhaj iliyoelezwa juu inayotegemea zaidi nukuu badala ya mawazo au rai ya Mfasiri.
Mkusanyiko wa hayo yote na mengineyo ndani ya sayansi hiyo unadhihirisha kuwa kunahitajika uangalifu mkubwa katika kukata shauri na kutoa hukumu kuhusu maana ya Maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى). Ndio ikawa njia pekee sahihi na ya salama ya kufanikisha hilo, ni kwa kushikamana na kutegemea yale yaliyopokelewa na kuthibiti kutoka kwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba (رضي الله عنهم) na wala si kutokana na rai.
La msingi na lililo muhimu katika kazi ya Tarjama ambalo ni sharti katika masharti ya anayefanya hiyo Tarjama ni kuwa awe mtu mwenye kushikamana na msingi madhubuti wa kufuata Manhaj ya Salaf[5] na wala si msingi wa kuzusha au ubunifu. Atakapokuwa ameshikamana na Manhaj sahihi ya Salaf, basi hivyo ndivyo kutampeleka na kumlazimisha kama ni sehemu ya ‘Aqiydah yake, kushikamana na zile Tarjama zenye kwenda sambamba na mafundisho ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), zenye kunukuu kauli za Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), au kauli za Swahaba (رضي الله عنهم) au kauli za Taabi’iyn[6] na Atbaa’ Taabi’iyn.[7]
Kutokana na hali hii basi, Mufassiruna wa Qur-aan wameweka Manhaj maalumu ya Tafsiyr ya kufuatwa na kushikiliwa na ambayo kwayo kwa kuipitia vizuri, ndipo tutaweza kupata Tarjama iliyo sahihi.
1. Tafsiyr Ya Qur-aan Kwa Qur-aan
Kufasiri Qur-aan kwa Qur-aan ndio njia ya kwanza inayopasa kufuatwa, kwani Qur-aan inajifasiri yenyewe kwa yenyewe. Utakuta pahala inaeleza jambo kwa kifupi na pahala pengine inalieleza jambo hilo hilo kwa ufafanuzi na kwa uchambuzi. Jambo inalolieleza kwa ujumla katika sehemu moja hulieleza kwa kuliwekea ima mipaka au kulihusisha kwa watu makhsusi katika sehemu nyingine. Hivyo, njia iliyo sahihi kabisa katika kufasiri Qur-aan, ni kufasiri Qur-aan kwa Qur-aan.[8]
Ibn Al-Qayyim (رحمه الله) amesema: “Kufasiri Qur-aan kwa Qur-aan ni njia bora kabisa inayofikisha Risala (Ujumbe) na kuifafanua. Na si ajabu kwani Allaah (سبحانه وتعالى) ni Mjuzi wa malengo na makusudio Yake. Anafafanua Aayah Zake kwa Aayah nyinginezo. Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
وَكَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ وَلِيَقُولُوا دَرَسْتَ وَلِنُبَيِّنَهُ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿١٠٥﴾
“Na hivyo ndivyo Tunavyosarifu namna kwa namna Aayaat ili (makafiri) waseme: Umedurusu (kutoka kwa Watu wa Kitabu), na ili pia Tuibainishe kwa watu wenye kujua.”[9]
Ni jambo lisilopingika kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akifahamu kikamilifu kila kilichoelezwa ndani ya Qur-aan na ndio akawa wa kwanza kufasiri Qur-aan kwa Qur-aan kama ilivyopokewa kuwa alifasiri baadhi ya Aayah kwa Aayah nyinginezo.[10]
Swahaba (رضي الله عنهم) walishuhudia na kumsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akifasiri Qur-aan kwa Qur-aan, hivyo nao kama ilivyo desturi yao, walimuiga katika hilo pia kama walivyokuwa wakimuiga katika mengineyo, na kwa kufahamu kuwa ni jukumu lao kufikisha kila walichochukua kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na kuwafikishia wataokuja baada yao. Hivyo basi Swahaba (رضي الله عنهم) waliwafunza Taabi’iyn [Waislamu ambao hawakumuwahi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika uhai wake], kila walichopokea kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) tena kwa muradi wake Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Taabi’iyn nao waliwafunza Atbaa’ Taabi’iyn (Waislamu ambao hawakuwawahi Swahaba katika uhai wao) kila walichopokea na kuchukua kutoka kwa waalimu wao ambao ni Swahaba (رضي الله عنهم). Kisha nao kwa upande wao walinukuu na kufikisha kwa waliokuja baada yao, tena kwa muradi ule ule walioupokea na kuuchukua kutoka kwa Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na katika waliyoyapokea ni aina hii ya kufasiri Qur-aan kwa Qur-aan.
Hivyo, haijuzu wala si sahihi kuiacha aina hii ya Tafsiyr na kuiendea nyingine ikiwa Aayah husika ina Aayah nyingine iliyoifasiri kama ilivyo katika mifano ifuatayo: Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّة فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٥٩﴾
“Na Kwake (Allaah) zipo funguo za ghaibu, hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Anajua yale yote yaliyomo barani na baharini. Na halianguki jani lolote ila Hulijua, wala punje katika viza vya ardhi, wala kinyevu na kikavu isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha wazi.”[11]
Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwabainishia na kuwawekea wazi kuwa funguo za ghaibu ni tano; kwa kuwasomea kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) ifuatayo:
إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ الْغَيْثَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْأَرْحَامِ ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿٣٤﴾
“Hakika Allaah Ana ujuzi wa Saa (Qiyaamah), na Anateremsha mvua na Anajua yale yaliyomo katika matumbo ya uzazi. Na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani. Hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye Khabari za dhahiri na siri.”[12]
Mfano mwengine ni pale Allaah (سبحانه وتعالى) Anaposema:
الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٨٢﴾
“Wale walioamini na hawakuchanganya imaan zao na dhulma, hao ndio watakaopata amani nao ndio waliohidika.”[13]
Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwabainishia Swahaba na kuwawekea wazi kuwa dhulma ni shirki kwa kuwasomea Aayah ifuatayo:
وَإِذْ قَالَ لُقْمَانُ لِابْنِهِ وَهُوَ يَعِظُهُ يَا بُنَيَّ لَا تُشْرِكْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ ﴿١٣﴾
“Na Luqmaan alipomwambia mwanawe huku akimuwaidhi: Ee mwanangu! Usimshirikishe Allaah, hakika shirki ni dhulma kubwa mno!”[14]
2. Kufasiri Qur-aan Kwa Sunnah[15] Za Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)
Sunnah inafasiri, inasherehesha na inabainisha Qur-aan kwa kudhihirisha yasiyokuwa dhahiri. Sunnah inaisherehesha Qur-aan kwa kuyachambua, kuyapambanua na kwa kuyaainisha yale ambayo Qur-aan imeyaelezea kwa ujumla. Sunnah inaweka mipaka kwa yale yasiyokuwa yamewekewa mipaka na Qur-aan. Sunnah inayachambua yaliyotolewa hukumu kwa pamoja, ikifafanua yaliyoachwa wazi hukumu zake. Yote hayo kwa kuwa katika Qur-aan, kuna yasiyoweza kufahamika isipokuwa kwa kupata ufafanuzi na kuwekwa wazi na Sunnah za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kama vile uchambuzi wake (صلى الله عليه وآله وسلم) katika namna za amri na makatazo, idadi za Rakaa za Swalaah, utekelezaji wa ‘Umrah na Hajj, viwango vya yale Aliyofaradhisha Allaah (سبحانه وتعالى) katika hukumu.[16]
Basi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alibainisha na kufafanua kwa kufasiri maana za Aayah za Qur-aan kwa Swahaba zake (رضي الله عنهم) kama inavyoashiria Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٤٤﴾
“Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao huenda wakapata kutafakari.”[17]
Ufafanuzi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kitu kisichoweza kuepukika, na ndio akaweka wazi kwa kusema kuwa hakupewa Qur-aan pekee, bali alipewa pamoja na Qur-aan kinachofanana nayo.[18]
Umahiri katika lugha ya Kiarabu pekee haukuwa wenye kutosheleza wala hautatosheleza katika kufahamu kusudio la Maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى) bila ya kutafuta msaada kutoka kwenye Sunnah. Kama ilivyokuwa hali kwa Swahaba (رضي الله عنهم) japokuwa walikuwa wenye ufasaha na umiliki kamili wa lugha ya Kiarabu, lakini walikuwa wakitatanishwa au wakati mwengine wakifahamu baadhi za Aayah kinyume na inavyotakiwa ifahamike, jambo lililowapelekea kurejea kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kutafuta ufafanuzi. Basi hufasiri Aayah au neno ambalo Swahaba (رضي الله عنهم) hawakuweza kuifahamu Tafsiyr yake au walipofahamu kinyume na inavyotakiwa ifahamike.
Kuna mifano mingi tu ya Aayah za Qur-aan ambapo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amezifasiri na kuzifafanua.
Mfano neno la الْكَوْثَرَ
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alilifasiri nenoالْكَوْثَرَ katika Suwrah Al-Kawthar:
إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ ﴿١﴾
“Hakika Sisi Tumekupa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Al-Kawthar[19] (Mto katika Jannah).”
kuwa ni Mto katika Jannnah, maana ambayo haikufahamika isipokuwa kwa njia ya kufafanuliwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ أَنَسٍ (رضي الله عنه) : ((إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ)) أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: ((هُوَ نَهْرٌ فِي الْجَنَّةِ))
Amesimulia Anas (رضي الله عنه) : Kuhusu kauli yake Allaah:
إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ
“Hakika Sisi Tumekupa Al-Kawthar.”
Kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Huo ni Mto katika Jannah.”[20]
Mfano mwengine ni neno زِيَادَةٌ
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alifasiri kwa kubainisha kuwa neno زِيَادَةٌ katika Aayah ya Suwrat Yuwnus,
لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ
“Kwa wale waliofanya ihsaan watapata (huko Jannah) jazaa nzuri kabisa na ziada (kumuona Allaah).”[21]
Kuwa maana ya ziada ni kumuona Allaah (سبحانه وتعالى), maana ambayo haikufahamika isipokuwa kwa njia ya ufafanuzi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ صُهَيْبٍ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِذَا دَخَلَ أَهْلُ الْجَنَّةِ الْجَنَّةَ نُودُوا: يَا أَهْلَ الْجَنَّةِ، إِنَّ لَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ مَوْعِدًا لَمْ تَرَوْهُ، فَقَالُوا: وَمَا هُوَ؟ أَلَمْ تُبَيِّضْ وُجُوهَنَا وَتُزَحْزِحْنَا عَنِ النَّارِ، وَتُدْخِلْنَا الْجَنَّةَ؟)) قَالَ: ((فَيُكْشَفُ الْحِجَابُ، فَيَنْظُرُونَ إِلَيْهِ، فَوَاللَّهِ مَا أَعْطَاهُمْ اللَّهُ شَيْئًا أَحَبَّ إِلَيْهِمْ مِنْهُ)) ثُمَّ تَلاَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَى وَزِيَادَةٌ))
Amesimulia Swuhayb (رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Watakapoingia Watu wa Jannah katika Jannah (Pepo), wataitwa: Enyi Watu wa Jannah! Hakika nyinyi mna ahadi kwa Rabb wenu bado hamjaiona. Watauliza: Ni (ahadi) ipi hiyo? Kwani Hukuzing’arisha nyuso zetu, na Hukutuokoa na moto, na Hukutuingiza Jannah?” Akasema: “Litaondoshwa pazia, na watamtazama Allaah. Basi Wa-Allaahi, Hakuwahi Allaah kuwapa jambo walolipenda zaidi kuliko hilo (kumuona Allaah).” Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasoma Aayah hii:
لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ
“Kwa wale waliofanya ihsaan watapata (huko Jannah) jazaa nzuri kabisa na ziada (kumuona Allaah).”[22]
Hii inathibitisha kuwa ufafanuzi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni wenye umuhimu mkubwa katika kufasiri Qur-aan, kwani ni ufafanuzi wa aina yake pekee na wenye thamani isiyoweza kununulika wala kukadirika. Ndio ikawa Qur-aan inaihitaji Sunnah (Hadiyth), na ndio ikawa hakuna kitabu katika vitabu vya Hadiyth isipokuwa kutakuwepo mlango wa Tafsiyr Maathuwr.[23]
3. Kufasiri Qur-aan Kwa Kauli Za Swahaba (رضي الله عنهم)
Kauli (Tafsiyr) za Swahaba (رضي الله عنهم) ni chanzo cha tatu cha kutafuta ufafanuzi pale inapokuwa haujapatikana kutoka vyanzo viwili vilivyotangulia, kama alivyosema Al-Haafidhw Ibn Kathiyr katika utangulizi wa Tafsiyr yake kuwa: “Tutakapokuwa hatukufanikiwa kupata Tafsiyr katika Qur-aan au Sunnah, tutarejea katika kauli za Swahaba (رضي الله عنهم) kwani wao waliifahamu Qur-aan vilivyo kwa ufasaha na sarufi zake, na kwa kuwa walishuhudia matukio yaliyosababisha kuteremshwa kwa Aayah au Suwrah husika. Hakuna aliyeyashuhudia isipokuwa wao, na pia kutokana na wao kuwa na ilimu sahihi na amali njema haswa haswa Wanachuoni miongoni mwao.”[24]
Swahaba (رضي الله عنهم) walijifunza Qur-aan na ilimu yake kwa kina kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).[25]
Hata hivyo, ufahamu wa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Qur-aan haukuwa wa daraja moja kwani miongoni mwao (رضي الله عنهم) wako waliojulikana kuwa ni wafasiri wa Qur-aan, kama vile Makhalifa wanne (رضي الله عنهم), Ibn Mas’uwd[26] ambaye alikuwa akijulikana miongoni mwa Swahaba kuwa ni mjuzi wao wa Qur-aan (kuisoma na kuifasiri). Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما),[27] pia Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) na wengineo ambao walikuwa na ufahamu uliokamilika kwa vile ulijengeka juu ya ilimu iliyo sahihi iliyopambika kwa amali njema. Hivyo, Tafsiyr zao zina thamani, uzito na umuhimu mkubwa mpaka ikawa Tafsiyr ya Swahaba inachukua hukumu ya Al-Marfuw[28] haswa inapojulikana kuwa Swahaba huyo hakuwahi kupokea Israaiyliyyaat[29] katika hilo.
Kilichojitokeza ni kuwa hakuna Tafsiyr iliyoandikwa katika wakati wao, kwani ilikuwa ni sehemu katika Hadiyth.
Mfano wa Tafsiyr ya neno لَامَسْتُمُ (mmewagusa) kuwa ni kujimai katika kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ
“au mmewagusa wanawake.”[30]
Ibn ‘Abbaas alilitafsiri kwa kusema kuwa: “Ni kujimai.”[31]
Mfano mwengine ni Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْتَرِى لَهْوَ الْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا ۚ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٦﴾
“Na miongoni mwa watu, yuko ambaye hununua maneno ya upuuzi ili apoteze (watu) Njia ya Allaah bila ilimu, na huzichukulia (Aayaat) mzaha. Hao watapata adhabu ya kudhalilisha.”[32]
Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) amesema kuhusu Aayah hii: “Naapa kwa Jina la Allaah! Hii inamaanisha ni muziki.”[33]
Mfano mwengine ni kuhusu Sa’yi baina ya majabali mawili ya Swafaa na Marwah kulikotajwa kwenye kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ اللَّـهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ ﴿١٥٨﴾
“Hakika Swafaa na Marwah ni katika Alama za Allaah. Kwa hiyo yeyote anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akatekeleza ‘Umrah, hakuna lawama kwake kutufu (vilima) viwili hivyo. Na atakayejitolea kufanya kheri, basi hakika Allaah Ni Mwenye Kupokea Shukurani, Mjuzi wa yote.”[34]
Baadhi ya Swahaba (رضي الله عنهم) walifahamu kinyume na vile inavyotakiwa ifahamike Aayah hiyo. Mmojawao ni baba wa Hishaam bin ‘Urwah. Alimuuliza Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) ambaye alimfahamisha kwa kutumia Sababun-Nuzuwl (Sababu ya kuteremshwa) ili aweze kufahamu usahihi wa maana ya Aayah kama ilivyothibiti katika kauli ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) katika usimulizi ufuatao:
عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّهُ قَالَ: قُلْتُ لِعَائِشَةَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَأَنَا يَوْمَئِذٍ حَدِيثُ السِّنِّ: "أَرَأَيْتِ قَوْلَ اللَّهِ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: ((إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِنْ شَعَائِرِ اللَّهِ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَنْ يَطَّوَّفَ بِهِمَا)) فَمَا أُرَى عَلَى أَحَدٍ شَيْئًا أَنْ لَا يَطَّوَّفَ بِهِمَا، فَقَالَتْ عَائِشَةُ: "كَلَّا، لَوْ كَانَتْ كَمَا تَقُولُ، كَانَتْ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَنْ لَا يَطَّوَّفَ بِهِمَا، إِنَّمَا أُنْزِلَتْ هَذِهِ الْآيَةُ فِي الْأَنْصَارِ كَانُوا يُهِلُّونَ لِمَنَاةَ، وَكَانَتْ مَنَاةُ حَذْوَ قُدَيْدٍ، وَكَانُوا يَتَحَرَّجُونَ أَنْ يَطُوفُوا بَيْنَ الصَّفَا وَالْمَرْوَةِ، فَلَمَّا جَاءَ الْإِسْلَامُ سَأَلُوا رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ ذَلِكَ، فَأَنْزَلَ اللَّهُ: ((إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِنْ شَعَائِرِ اللَّهِ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَنْ يَطَّوَّفَ بِهِمَا))
Amesimulia Hishaam bin ‘Urwah kutoka kwa baba yake alisema: Nilimwambia ‘Aaishah (رضي الله عنها) mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na mimi wakati huo ni kijana mdogo: Unaionaje Kauli ya Allaah (تبارك وتعالى),
إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ
“Hakika Swafaa na Marwah ni katika Alama za Allaah. Kwa hiyo yeyote anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akatekeleza ‘Umrah, hakuna lawama kwake kutufu (vilima) viwili hivyo. Na atakayejitolea kufanya kheri, basi hakika Allaah Ni Mwenye Kupokea Shukurani, Mjuzi wa yote.”
Sioni kama kutakuwa na kitu juu ya yeyote ikiwa hatotufu baina yake. Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) akasema: Si hivyo! Ingelikuwa kama unavyosema basi ingekuwa (hivi): Hakutokuwa na dhambi juu yake kama hatotufu baina ya (vilima) viwili hivyo. Kwa hakika Aayah hii imeteremshwa kuhusiana na Answaar ambao walikuwa wakilitukuza Manaat (wakiliabudu sanamu hilo na wakilifanyia Hijjah na wakilitufu), lakini walikuwa hawatufu (Sa’yi baina ya Swafaa na Marwah) na lilikuwa hilo sanamu la Manaat likielekea (kijiji cha) Qadiyd, hivyo walikuwa wakiona tabu kulitufu. Ulipokuja Uislamu walimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu hivyo (Sa’yi baina ya Swafaa na Marwah), ndio Allaah Akateremsha:
إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ اللَّـهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ ﴿١٥٨﴾
“Hakika Swafaa na Marwah ni katika Alama za Allaah. Kwa hiyo yeyote anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akatekeleza ‘Umrah, hakuna lawama kwake kutufu (vilima) viwili hivyo. Na atakayejitolea kufanya kheri, basi hakika Allaah Ni Mwenye Kupokea Shukurani, Mjuzi wa yote.[35]
4. Kufasiri Qur-aan Kwa Kauli Za Taabi’iyn
Kutakaposhindwa kupatikana Tafsiyr ya Aayah husika kwenye Qur-aan, au kwenye Sunnah, au kwenye kauli za Swahaba (رضي الله عنهم), ‘Ulamaa[36] hurejea kwenye kauli za Taabi’iyn, kwani kama walivyotajika baadhi ya Swahaba (رضي الله عنهم) kwa Tafsiyr, wametajika pia baadhi ya Taabi’iyn[37] kwa Tafsiyr.
Taabi’iyn walitegemea katika Tafsiyr zao, ufahamu wao wa Qur-aan kutokana na yaliyokuja ndani ya Qur-aan yenyewe, na yale waliyoyapokea kutokana na Swahaba (رضي الله عنهم), kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na yale Aliyowafungulia Allaah kupitia njia ya ijtihaad na utafiti wao katika Qur-aan na wala hawakuwa tayari kutumia rai zao.[38]
Kinachofahamika ni kuwa Tafsiyr zilizopokelewa kutokana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na pia kutokana na Swahaba (رضي الله عنهم) hazikuwa za Qur-aan yote, bali zilikuwa ni zenye kuhusiana na baadhi ya Aayah za Qur-aan au baadhi ya maneno ya Aayah ambayo yalionekana kuwa ni miongoni mwa yale yenye kuhitaji ufafanuzi kwa wale waliokuwa katika zama hizo. Kutofahamika huku, huwa kunazidi kila pale wanapobaidika watu na zama za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba (رضي الله عنهم). Hivyo wale wenye kujishughulisha na fani ya Tafsiyr miongoni mwa Taabi’iyn, wakaongeza katika Tafsiyr kadiri ya kule kuongezeka kutofahamika, kisha baada yao wakaja wale waliokamilisha Tafsiyr ya Qur-aan huku wakitegemea juu ya yale waliyoyafahamu katika lugha na lahaja za Waarabu, na juu ya yale yaliyothibiti kuwa ni sahihi kwao katika matukio yaliyotokea wakati wa kuteremka Qur-aan.
Taabi’iyn wametunukiwa daraja ya kuwa miongoni mwa watu bora kabisa[39] kwa kuwa walichukua na kuchota ilimu zao kutoka vyanzo sahihi na vilivyoasisiwa kwa misingi sahihi.
Mfano wa Tafsiyr ya neno قَانِتُونَ katika Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَقَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۖ بَل لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ ﴿١١٦﴾
“Na wakasema: Allaah Amejichukulia mwana. Utakasifu Ni Wake! Bali ni Vyake vilivyomo mbinguni na ardhini, vyote vinamtii.”[40]
Kuhusiana na neno قَانِتُونَ Mujaahid alilifasiri kwa kusema kuwa: “Ni kutii. Na kwamba utiifu wa kafiri hupatikana pale kivuli chake kinaposujudu wakati ambapo yeye mwenyewe (kafiri) ni mwenye kuchukia hilo.”[41]
Mfano mwengine ni kuhusiana na Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
قَالَ أَنَا أُحْيِي وَأُمِيتُ ﴿٢٥٨﴾
“Akasema: Mimi (pia) nahuisha na kufisha.”[42]
Kuhusiana na ibara hii: “Mimi (pia) nahuisha na kufisha.” Qataadah amesema kuwa yule mfalme aliyemuhoji Nabiy Ibraahiym (عليه السلام) alimaanisha kuwa: Watu wawili waliostahiki kuuawa, wangeletwa mbele yake, na angeliamrisha mmoja wao auawe basi angeliuawa. Na angeliamrisha kuwa mtu wa pili asamehewe, basi angesamehewa. Hivi ndivyo ninavyoleta uhai na kifo.[43]
Hivyo Tafsiyr ya Taabi’iyn ni chanzo chengine cha kutafuta ufafanuzi pale inapokuwa haujapatikana ufafanuzi kutoka kwenye vyanzo vilivyotangulia. Hata hivyo baadhi ya Wanachuoni wanaonelea kuwa Tafsiyr za Taabi’iyn na wanafunzi wao hazitoki moja kwa moja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na wala si kama Tafsiyr za Swahaba (رضي الله عنهم), yote kwa kuwa Taabi’iyn na wanafunzi wao hawajamuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na wala hawakushuhudia Wahy pale zinapoteremshwa Aayah. Na vilevile si wote wanakubalika uaminifu wao, kwa kuwa wao si kama Swahaba (رضي الله عنهم) ambao uaminifu na uadilifu wao umeshuhudiwa na kuthibitishwa na Qur-aan. Ama wao Taabi’iyn na wanafunzi wao wamesifiwa kama ni ‘karne’ na si mmoja mmoja.
Hata hivyo, maelezo mazuri na ya salama ni yale ya Shu‘bah bin Al-Hajjaaj na wengineo ambayo ameyanukuu Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: “Kauli za Taabi’iyn katika furuw’ (matawi ya Sharia) si hoja, basi vipi zitakuwa hoja katika Tafsiyr. Kwa maana kuwa haziwi hoja juu ya wengineo wasiokuwa wao miongoni mwa wale waliowakhalifu, na hii ndio sahihi. Ama pale watakapokubaliana juu ya kitu, basi bila shaka yoyote ile ni hoja. Na endapo watakhitalifiana basi haitokuwa kauli ya baadhi yao hoja juu ya wengine. Na wala juu ya watakaokuja baada yao, bali kutafuatwa na kutazamwa lugha ya Qur-aan, au Sunnah, au kauli za Swahaba (رضي الله عنهم).“[44]
Hakuna shaka yoyote ile kwamba ujuzi wa lugha ya Kiarabu na matawi yake una mchango mkubwa na ni ufunguo katika kuifahamu Qur-aan na kuweza kupata Tafsiyr yenye kukubalika. Hivyo basi, ufahamu sahihi wa Tafsiyr ya Qur-aan, makusudio yake na yote yenye kufungamana nayo, unafungamana pia na ufahamu sahihi wa lugha ya Kiarabu na matawi yake.
Ilimu ya Tarjama ilibuniwa na kupelekea kuweko Tarjama nyingi sana katika kila zama na kila pahala na kwa lugha maarufu za walimwengu, jambo lililopelekea kumwezesha mlengwa kuweza kufahamu aliyolengewa kuyafahamu. Lakini, huenda Tarjama nyingi zikawa zimefanikiwa kumwezesha mlengwa kufahamu Maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kiasi fulani na kufahamu baadhi ya makusudio ya Aayaat katika upande wa Sharia. Ama kwenye upande wa ‘Aqiydah (Itikadi), baadhi ya Tarjama, hazikufanikiwa kumwezesha Muislamu kupata ufahamu wa wazi wa mas-ala muhimu ya ‘Aqiydah Sahihi kwa kuyatanabahisha na kuyafafanua kiwaziwazi baadhi ya mas-ala hayo ya ‘Aqiydah, mas-ala ambayo yana ufahamu usio sahihi katika itikadi za madhehebu mengineyo.
Hivyo basi, katika Tarjama hii[45], tumejitahidi kubainisha na kuyafafanua kwa dalili baadhi ya mas-ala yanayohusiana na ‘Aqiydah sahihi ili yamwezeshe mwenye kuzungumza Kiswahili afahamu pale alipotakiwa kufika kiitikadi; ‘Aqiydah iliyobalighishwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na inayorandana na ‘Aqiydah ya Salaf Asw-Swaalih (Wema waliotangulia) miongoni mwa Swahaba, Taabi’iyn na Atbaa' Taabi’iyn na waliowafuata kwa wema.
Mifano ya baadhi ya mas-ala hayo ya ‘Aqiydah:
(i) Kuthibitisha Sifa za Allaah (سبحانه وتعالى) kama Aliyojithibitishia Mwenyewe (سبحانه وتعالى). Mifano: Wajihi Wake, rejea Al-Qaswasw (28:88), Al-Baqarah (2:115) na Ar-Rahmaan (55:27). Mkono au Mikono Yake, rejea Swaad (38:75), Al-Fat-h (48:10). Macho Yake, rejea Huwd (11:37), Al-Muuminuwn (23:27), Twaahaa (20:39). Kusikia na Kuona Kwake, rejea Twaahaa (20:46). Nafsi Yake, rejea Aal-‘Imraan (3:28), na Sifa nyenginezo bila ya Ta'twiyl (kuzipinga, kukanusha uwezekano), wala Tamthiyl (kumithilisha, kufafanisha, kulinganisha), wala Takyiyf (kuainisha maana na kuziulizia namna yake au kuuliza ni vipi Sifa hiyo ipo, kuchunguza ni kwa “namna gani” zimefungamana au kuambatana na Allaah), wala Tahriyf (kubadilisha maana, kupotosha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kutoa maana isiyo sahihi).
Na hakuna khofu wala shaka kuwa Sifa za Allaah (سبحانه وتعالى) zikithibitishwa kama zilivyotajwa katika Qur-aan, kwamba atashabihishwa Muumba na Viumbe Vyake! Hiyo si hoja muwafaka, kwani imaan thabiti ya Muislamu kuhusiana na Allaah (سبحانه وتعالى) ni kuwa: Hapana anayefanana Naye (Muumba) hata mmoja wala hakuna kitu chochote mfano Wake kama inavyothibitishwa na Allaah (سبحانه وتعالى) Mwenyewe.[46]
(ii) Kuthibitisha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya Al-‘Uluww. Na kwamba Allaah Yuko juu ya Mbingu Zake saba, juu ya ‘Arsh Yake, na Ametenganishwa na viumbe Vyake, na viumbe Vyake vimetenganishwa Naye. Rejea Al-Mulk (67:16). Ama Anaposema Yuko na Waja Wake basi ‘Aqiydah sahihi ni kuamini kwamba Yuko na Waja Wake kwa Ujuzi Wake tu na si kwa Dhati Yake. Rejea Al-Mujaadalah (58:7).
(iii) Istawaa: Kuamini Kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Yuko juu Ya ‘Arsh Yake kama Alivyojijulisha Mwenyewe. Na kuweko huko juu ya ‘Arsh Yake, ni kulingana na Utukufu, Uadhama, Uajalali Wake na Ukamilifu Wake. Rejea Al-A’raaf (7:54) na Twaahaa (20:5).
(iv) Kuamini kwamba Qur-aan ni Kalaamu-Allaah (Maneno ya Allaah) na kwamba hayakuumbwa. Rejea At-Tawbah (9:6).
(v) Kuamini kwamba Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Yuhai na Atateremka duniani kutoka mbinguni iwe ni alama mojawapo kubwa za Qiyaamah. Rejea An-Nisaa (4:159), Aal-‘Imraan (3:55) na rejea nyenginezo zilizotajwa humo.
(vi) Kuamini kwamba Waumini watamuona Allaah (سبحانه وتعالى) watakapokuwa Jannah (Peponi). Rejea Yuwnus (10:26) na Al-Qiyaamah (75:23).
(vii) Kuamini Kalaam (Kuongea): Kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Anaongea kama Alivyoongea na Nabiy Muwsaa (عليه السّلام). Rejea An-Nisaa (4:164), Al-A’raaf (7:143).
Kwa minajili hiyo, tukaona kuna umuhimu wa kuweko kwa Tarjama itakayokwenda sambamba na Manhaj ya Salaf haswa katika kuibalighisha na kuidhihirisha ile ‘Aqiydah iliyobalighishwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambayo iko wazi kwenye Qur-aan kwa atakaye kushikamana nayo.
Pia, tumeona ni vyema na ndio sahihi ndani ya kazi hii pia, kulithibitisha Jina la ‘Allaah’ badala ya kulifasiri kwa kuligeuza na kutumia neno ‘Mwenyezi Mungu’, kama linavyotumika katika karibu Tarjama zote za lugha ya Kiswahili, kwani Allaah ni Pekee na mungu inatumika kwa miungu wengi hata kama itaunganishwa na ‘mwenyezi.’ Ni imaan yetu kuwa kulithibitisha jina Lake ‘Allaah’ kama lilivyothibiti, ni kumuadhimisha Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) na kulipa haki Jina Lake Tukufu kwani hakuna mwenye Majina kama Yake Allaah (سبحانه وتعالى). Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا ﴿٦٥﴾
“Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake. Basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika Ibaada Yake. Je, unamjua yeyote anayefanana Naye (Allaah)?” [Maryam (19:65)][47]
Na kubwa na la muhimu zaidi ni kuwa kuna thawabu kwa kuwa ndivyo lilivyothibiti. Hivyo, tutalitumia na kulithibitisha Jina la ‘Allaah’ pote katika Tarjama hii kama lilivyothibitishwa na Qur-aan na Sunnah za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa lengo la kuwarejesha Waumini katika kutumia Majina ya Allaah kama yalivyothibiti.
Hali kadhaalika, tumethibitisha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya ‘Rabb’ kwa kuibakisha kama ilivyo katika asli yake bila kuipa maana, kwa sababu neno ‘Rabb’ linatumika Kiswahili kama ‘Rabi’ na linafahamika. Ama kulipa maana ya ‘Mola’ tumeona ni maana finyu isiyokidhi taarifu kamili ya ‘Rabb’ kwa sababu ‘Ar-Rabb’ ina maana nyingi na pana. Inaweza kumaanisha: Mfalme, Bwana, Mlezi, Mwendeshaji, Mpangaji, Mola, Msimamiaji, Mwenye Kuneemesha, Mwenye Kuruzuku n.k. Hivyo, tumeonelea litumike kwenye Tarjama hii hivyo hivyo lilivyo.
Pia, tumejaribu sana kutumia misamiati ya lugha ya Kiswahili, ambayo inalingana sawasawa katika maana na misamiati ya lugha ya Kiarabu, ili iwafikiane na makusudio ya neno la asili la Kiarabu. Na misamiati mingineyo ambayo hayafahamiki kiwepesi katika jamii, tumeyawekea ufafanuzi katika Faharasa. Na baadhi ya misamiati hiyo, inapatikana katika Kamusi za Kiswahili zifuatazo: (i) Kamusi Ya Kiswahili Sanifu (ii) Kamusi Ya Maana Na Matumizi (iii) Kamusi Ya Visawe.
Vilevile, tumeweka baadhi ya faida au tanbihi ili nazo zimpanulie ufahamu msomaji na kumuongezea ilimu ya ufahamu wa Qur-aan.
Pia katika kila Suwrah, tumetanguliza Tangulizi za Suwrah; humo tumetaja Maqaaswid As-Suwrah[48] (Makusudio ya Suwrah), maudhui za Suwrah kwa mukhtasari, fadhila za Suwrah na faida nyenginezo.
Pia tumeambatanisha katika faharasa, kurasa zenye maana ya Majina Mazuri Kabisa ya Allaah na Sifa Zake Kamilifu, ili zimfaidishe msomaji na kumuongezea ilimu.
Msomaji akipendelea kupata faida ya ziyada zifuatazo: (i) Sababu Za Kuteremshwa (Asbaabun-Nuzuwl) Suwrah au Aayah za Qur-aan (ii) Kinachofuta Na Kinachofutwa (An-Naasikh Wal-Mansuwkh) ambayo ni ujuzi wa kujua Aayah zilizofutwa hukmu zake na ambazo zikateremshwa Aayah nyenginezo badala yake (iii) Aayah Na Mafunzo (iv) Tafsiyr Al-Muyassar iliyofasiriwa kwa Kiswahili, basi atembelee Tovuti ya Alhidaaya.com [7] ambako masomo hayo yameorodheshwa kwa bayana. Njia ya kuzifikia ni ifuatavyo:
Maudhui Za Qur-aan > Tangulizi Za Suwrah
Maudhui Za Qur-aan > Tafsiyr Al-Muyassar (Kiswahili)
Maudhui Za Qur-aan > Tafseer As-Sa’di (Kiarabu)
Maudhui Za Qur-aan > Tafseer As-Sa’di (Kiingereza)
Maudhui Za Qur-aan > Asbaabun-Nuzuwl (Sababu Za Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah.
Maudhui Za Qur-aan > An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa)
Maudhui Za Qur-aan > Aayah Na Mafunzo.
Basi hizo hazitamzidishia faida pekee, bali atazidisha ilimu yake ya ufahamu wa Qur-aan kwa kina, na atapata ladha, raghba (utashi), ilhamu na mapenzi ya Qur-aan.
Tumetegemea zaidi katika kuikamilisha kazi hii Tafsiyr zifuatazo:
تفسير القرآن العظيم للإمام الحافظ ابن كثير
Tafsiyr Al-Qur-aan Al-‘Adhwiym ya Al-Haafidhw ‘Imaad Ad-Diyn Abi Al-Fidaa Ismaa’iyl bin Kathiyr. Au umaarufu wake تفسير ابن كثير Tafsiyr Ibn Kathiyr.
تيسير الكريم الرحمن في تفسير كلام المنان
Taysiyr Al-Kariym Ar-Rahmaan Fiy Tafsiyr Kalaam Al-Manaan ya Al-‘Allaamah Ash-Shaykh ‘Abdur-Rahmaan bin Naaswir As-Sa’diy. Au umaarufu wake kama تفسير السعدي Tafsiyr As-Sa’diy.
التفسير الميسر - نخبة من العلماء
At-Tafsiyr Al-Muyassar – Nukhbat Minal ‘Ulamaa
Na Tarjama ya Kiingereza:
Interpretation of The Meanings of The Noble Quran in The English Language (A Summarized Version of At-Tabari, Al-Qurtubi and Ibn Kathir with Comments from Sahih Al-Bukhari) Dr. Muhammad Taqi-ud-Diyn Al-Hilaaliy, Dr Muhammad Muhsin Khan.
Mwisho tunamshukuru Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kutuwafikisha kuweza kuikamilisha kazi hii tukufu, kazi ambayo ni jukumu kubwa mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) wala hatusemi kuwa Tarjama hii itakuwa haina kasoro, kwani hakuna mkamilifu isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى).
Tunawaomba ndugu zetu watuarifu kwa kosa lolote lile watakaloligundua au kasoro yoyote ile watakayoiona kwa kuwasiliana nasi kupitiwa webmaster@alhidaaya.com [8].
Tunamuomba Allaah (سبحانه وتعالى) Atughufurie kwa makosa yetu na Aijaalie kazi hii iwe ni kwa ajili ya kuzipata Radhi Zake Pekee na Atutakabalie.
Na Allaah Ni Mjuzi Zaidi
الحمد لله رب العالمين وصلى الله على محمد وعلى آله واصحابه وسلم
Imeandaliwa Na: Alhidaaya.com [9]
[1] Fusw-Swilat (41:42).
[2] Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَـٰذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا ﴿٨٨ [10]﴾
“Sema: Ikiwa watajumuika wanaadamu na majini ili walete mfano wa hii Qur-aan, hawatoweza kuleta mfano wake na japokuwa watasaidiana wao kwa wao.” [Al-Israa (17:88)]
[3] Ibraahiym (14:4).
[4] Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّهُمْ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُ بَشَرٌ ۗ لِّسَانُ الَّذِي يُلْحِدُونَ إِلَيْهِ أَعْجَمِيٌّ وَهَـٰذَا لِسَانٌ عَرَبِيٌّ مُّبِينٌ ﴿١٠٣﴾
“Na kwa yakini Tunajua kwamba wao wanasema: Hakika hapana isipokuwa mtu anamfundisha (Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم Qur-aan). Lugha wanayomnasibishia nayo ni ya kigeni, na hii ni lugha ya Kiarabu bayana.” [An-Nahl (16:103)]
[5] Salaf:
Maana yake kilugha ni kilichopita, kilichotangulia.
Na wanaokusudiwa kuwa ni Salafus-Swaalih ni Wema Waliotangulia. Nao ni Waumini wa karne ya kwanza ambao ni Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Muhaajirina na Answaar kama Anavyosema Allaah (عزّ وجلّ):
وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِى تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١٠٠﴾
“Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhajirina na Answaar na wale waliowafuata kwa ihsaan, Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Na Amewaandalia Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo abadi. Huko ndiko kufuzu kukubwa kabisa.” [At-Tawbah (9:100)] Rejea pia Al-Hashr (59:8-10).
Kisha wale waliokuja baada yao na wakajifunza kwao miongoni mwa Taabi’iyn na Atbaa’ At-Taabi’iyn, halafu pia waliokuja baada yao katika karne iliyo bora kabisa aliyosema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ): “Wabora wenu zaidi ni wa karne yangu, kisha wale wanaowafuatia (Taabi’iyna), kisha wale wanaowafuatia hao (Atbaa’ Taabi’iyn).” [Al-Bukhaari - Yamenukuliwa kutoka Manhaj As-Salaf Asw-Swaalih Wa Haajatul-Ummati Ilayhi, Tovuti Rasmi ya Ma’aaliy Shaykh Ad-Duktuwr Swaalih Bin Fawzaan Bin ‘Abdillaah Al-Fawzaan]
Kisha wengineo ambao wamewafuata hao wote katika Manhaj ya Salaf kwa kufuata mafundisho ya Kitabu na Sunnah, kuyalingania kwa watu, na kuyafanyia kazi mpaka Siku ya Qiyaamah. Na kwa mwenendo huu, wanakuwa ni Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah.”
[6] Taabi’iyn: Ni Waislamu waliokuja baada ya zama za Unabii na hawakuwahi kukutana na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ), bali walikutana na Swahaba wake wakasuhubiana nao. Miongoni mwa hao ni: Hasan Al-Baswriy, Qtaadah, ‘Urwah bin Az-Zubayr, Sa’iyd bin Al-Musayyib, Mujaahid bin Jabar, Sa’iyd bin Jubayr, Naafi’ (Mtumwa aliyeachwa huru na Ibn ‘Umar رَضِيَ اللهُ عَنهُمَا), na ‘Ikrimah (Mtumwa aliyeachwa huru na Ibn ‘Abbaas رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا).
[7] Atbaa' Taabi’iyn: Ni Waislamu ambao hawakuwahi kukutana na Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ), bali walikutana na Taabi’iyn na wakasuhubiana nao. Miongoni mwa hao ni: Maalik, Abu Haniyfah (ingawa baadhi ya Wanachuoni wanasema ni Taabiy' kwa sababu alikutana na Swahaba wa mwisho mwisho), Ash-Shaafi’iy, Ahmad bin Hanbal, Sufyaan Ath-Thawriy, Sufyaan bin ‘Uyaynah, Ibn ‘Abiy Laylaa, Rabiy’ah, Abu ‘Abdirrahmaan Al-Awzaa’iy, Ibn Hurmuz, Al-Hasan Ibn Swaalih, ‘Abdullaah Ibn al-Hasan, na Ibn Shubrumah.
Kisha baada ya hao wakaja Taabiy' Atbaa' Taabi'iyn, na katika hao ni Imaam wa Hadiyth ambao ni: Al-Bukhaariy, Muslim Abu Daawuwd At-Tirmidhiy An-Nasaay, Ibn Maajah.
[8] Tazama Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl At-Tafsiyr - Ibn Taymiyyah.
[9] Al-An’aam (6:105).
[10] Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ ﴿١٧ [11]﴾ فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ ﴿١٨ [12]﴾ ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ ﴿١٩﴾
“Hakika ni juu Yetu Kuikusanya na Kukuwezesha kuisoma kwake. Basi Tunapoisoma (kupitia Jibriyl), fuata kusomwa kwake. Kisha ni juu Yetu Kuibainisha (kwako).” [Al-Qiyaamah (75:17-19)]
[11] Al-An’aam (6:59).
[12] Luqmaan (31:34).
[13] Al-An‘aam (6:82).
[14] Luqmaan (31:13).
[15] Sunnah:
Ni kila kilichonasibishwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika kauli au kitendo au yale aliyoyakubali au sifa za kimaumbile au tabia au mwenendo.
[16]Hakika kila kile alichohukumu kwacho Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni katika yale aliyoyaelewa (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na Qur-aan kama alivyosema Imaam Ash-Shaafi’y. Taz. Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl At-Tafsiyr. Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
إِنَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِتَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ بِمَا أَرَاكَ اللَّـهُ ۚ وَلَا تَكُن لِّلْخَائِنِينَ خَصِيمًا ﴿١٠٥﴾
“Hakika Sisi Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu kwa haki ili uhukumu baina ya watu kwa Aliyokuonyesha Allaah. Wala usiwe mtetezi kwa makhaini.” [An Nisaa (4:105)]
Pia Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
وَمَا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ إِلَّا لِتُبَيِّنَ لَهُمُ الَّذِي اخْتَلَفُوا فِيهِ ۙ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٦٤﴾
“Na Hatukukuteremshia Kitabu (Qur-aan) isipokuwa uwabainishie yale waliyokhitilafiana, na pia ni Mwongozo na Rahmah kwa watu wanaoamini.” [An Nahl (16:64)]
[17] An-Nahl (16:44). Kadhalika Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ ﴿١٩ [13]﴾
“Kisha ni juu Yetu kuibainisha (kwako).” [Al-Qiyaamah (75:19)] inawarudi kwa uwazi kabisa wale wenye kudai kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakubainisha maana ya Majina na Sifa za Allaah, na kwa kauli yao hii, ima wanakusudia kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa hajui maana ya Majina na Sifa za Allaah, au Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alificha kile alichokifahamu. Taz. Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl At-Tafsiyr.
[18] Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
أَلَا إِنِّي أُوتِيتُ الْقُرْآنَ وَمِثْلَهُ، أَلَا يُوشِكُ رَجُلٌ يَنْثَنِي شَبْعَانًا عَلَى أَرِيكَتِهِ يَقُولُ: "عَلَيْكُمْ بِالْقُرْآنِ فَمَا وَجَدْتُمْ فِيهِ مِنْ حَلَال فَأَحِلُّوهُ وَمَا وَجَدْتُمْ فِيهِ مِنْ حَرَامٍ فَحَرِّمُوهُ... رواه أبو داود والترمذي والحاكم وصححه وأحمد بسند صحيح
“Tanabahi! Hakika nimepewa Qur-aan na inayofanana nayo (Sunnah) Tanabahi! Utafika wakati mtu aliyeshiba mno ataegemea kwenye kochi na kusema: “Shikamaneni na Qur-aan, mtakayokuta humo ya halali halalisheni, na mtakayokuta ya haramu haramisheni.” [Imepokewa na Abu Daawuwd, na At-Tirmidhiy, na Al-Haakim na ameisahihisha Ahmad kwa isnaad Swahiyh]
[19] Al-Kawthar (108:1).
[20] Al-Bukhaariy katika Kitabu cha Tafsiyr ya Qur-aan, At-Tirmidhiy katika Kitabu cha Tafsiyr ya Qur-aan.
[21] Yuwnus (10:26).
[22] Ahmad katika Musnad, Kumi waliobashiriwa Jannah, Ukamilisho wa Musnad ya Kuufiyyiyn; na At-Tirmidhiy, katika Kitabu cha Tafsiyr ya Qur-aan, na Riwaaya nyenginezo.
[23]Ni Tafsiyr yenye kutegemea yaliyo sahihi katika yaliyopokelewa kulingana na mpangilio huu: Tafsiyr ya Qur-aan kwa Qur-aan, Tafsiyr ya Qur-aan kwa Sunnah, Tafsiyr ya Qur-aan kwa kauli za Swahaba (رضي الله عنهم), Tafsiyr ya Qur-aan kwa kauli za Taabi’iyn kwa kuwa wao walichukua Tafsiyr zao kutokana na Swahaba (رضي الله عنهم). Vitabu vinavyotajika katika fani hii ya Tafsiyr ni kama:
i. Jaami’ul Bayaan Fiy Tafsiyril Qur-aan ya Ibn Jariyr Atw-Twabariy.
ii. Tafsiyrul Qur-aanil ‘Adhwiym ya Ibn Kathiyr.
iii. Fat-hul Qadiyr ya Ash-Shawkaaniy.
[24] Utangulizi wa Tafsiyr Ibn Kathiyr; vyanzo vya Tafsiyr.
[25]Amesema Abuu ‘Abdir-Rahmaan As-Sulamy: “Wametuhadithia wale waliokuwa wakitusomesha Qur-aan kama ‘Uthmaan bin ‘Affaan (رضي الله عنه) na ‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه) na wengineo kuwa wao walikuwa pale wanapojifunza kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Aayah kumi huwa hawaongezi nyingine mpaka pale watakapojifunza (na kutekeleza) yale yaliyomo ya ilimu na amali katika hizo Aayah kumi walizojifunza, basi wakasema: Tulijifunza Qur-aan na ilimu na amali kwa pamoja, na kwa sababu hiyo ndio walikuwa wakichukua muda kati kuhifadhi Suwrah.” Taz. Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl At-Tafsiyr.
[26]Aliyepokelewa akisema: “Naapa kwa Yule Ambaye hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, hakuna katika Kitabu cha Allaah Suwrah isipokuwa mimi najua ilivyoteremka, na hakuna Aayah isipokuwa najua imeteremshwa kwa ajili gani (sababu) na lau ningelimjua yeyote kuwa yeye ni mjuzi zaidi yangu kwa Kitabu cha Allaah, na ngamia anaweza kufika kwake, basi ningepanda kwenda kwake.” [Imepokelewa na Muslim, katika Kitabu cha Fadhila za Swahaba, mlango wa fadhila za ‘Abdullaah bin Mas’uwd na mama yake (رضي الله عنهما)]
[27]Ibn ‘Abbaas aliyetambulikana kama ni ‘Tur-jumanil Qur-aan’ na aliyeombewa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم):
((اللَّهُمَّ عَلِّمْهُ الْحِكْمَةَ وَتَأْوِيلَ الْكِتَابِ))
“Ee Allaah, Mfunze Hikmah na Ta-awiyl (ufasiri, utambuzi) wa Kitabu (Qur-aan).” [Imepokelewa na At-Tirmidhiyy, katika Kitabu cha Ad-Da’waat, milango ya Manaaqiyb; na Sunan Ibn Maajah, katika Kitabu cha Ibn Maajah, milango ya fadhila za Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)]
[28]Ni kila kilichotegemezwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika kauli au kitendo au kuthibitisha jambo au sifa katika tabia zake au umbo lake.
[29] Israaiyliyyaat: Ni khabari, visa, simulizi zitokazo kwa Mayahudi katika Vitabu vya Tafsiyr, Taariykh n.k.
[30]An-Nisaa (4:43).
[31]Tafsiyr Ibn Kathiyr.
[32] Luqmaan (31:6). Tanbih: Kinachoruhusiwa ni dufu na sio ala nyenginezo za muziki.
[33] Atw-Twabariy (20:127).
[34] Al-Baqarah (2:158).
[35] Al-Baqarah (2:158).
[36] Tazama Ibn Taymiyyah, Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl at-Tafsiyr.
[37] Kama vile Mujaahid, Sa’iyd bin Jubayr, ‘Ikrimah, Twaawuws, ‘Atwaa, Zayd bin Aslam, Abul ‘Aaliyah na Muhammad bin Ka’b, ‘Alqamah bin Qays, Masruwq, ‘Aamir Ash-Sha’biy na Hasan Al-Baswriy na Qataadah.
[38] Imaam At-Tirmidhiy amesema: “Ama yale yaliyopokelewa kutokana na Mujaahid na Qataadah na wengineo miongoni mwa Ahlul-‘Ilmi kwamba walifasiri Qur-aan, basi hakuna haja ya kuwadhania kuwa walifasiri Qur-aan bila ya ilimu –kwa rai zao- au kutokana na nafsi zao, na kumekwishapokewa kutokana na wao yale tuliyoyasema yenye kuthibitisha kwamba wao hawakuifasiri Qur-aan kutokana na nafsi zao bila ya ilimu kama ilivyothibiti kutokana na Al-Hassan bin Al-Mahdiy Al-Baswriyy amesema: Ametupa khabari ‘Abdur-Razzaaq kutokana na Ma’mar kutoka kwa Qataadah amesema: “Katika Qur-aan hakuna Aayah yoyote ile isipokuwa nimesikia kitu kuhusiana nayo.” [At-Tirmidhiyy katika Kitabu cha Tafsiyr ya Qur-aan, mlango wa katika yale yaliyokuja kwa yule anayefasiri Qur-aan kwa rai yake]
[39] Kutoka kwa Ibn Mas’uwd(رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
((خَيْرُ النَّاسِ قَرْنِي، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ)) صحيح البخاري ومسلم
“Watu bora kabisa ni karne yangu, kisha wanaowafuatia, kisha wanaowafuatia.” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, katika Kitabu Al-Manaaqib, mlango wa Fadhila za Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), Muslim Kitabu cha Fadhila za Swahaba, mlango wa Fadhila za Swahaba (رضي الله عنهم)]
[40] Al-Baqarah (2:116).
[41] Tafsiyr Ibn Kathiyr.
[42] Al-Baqarah (2:258).
[43] Tafsiyr Ibn Kathiyr.
[44] Tazama Ibn Taymiyyah, Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl At-Tafsiyr.
[45] Tarjama Hii Ziko Mbili: Ya Mtandaoni Na Iliyochapishwa:
(i) Tarjama Iliyoko Mtandaoni Alhidaaya.com:
Tarjama hii imetoa maelezo na fafanuzi kwa baadhi ya Aayah kwa faida ya msomaji. Maelezo hayo yanahusiana na mas-ala ya ‘Aqiydah kama Al-Istiwaa (Uwepo wa Allaah (سبحانه وتعالى) juu ya ‘Arsh). Pia kuthibitisha Sifa Zake kama Alivyojithibitishia Mwenyewe na kadhalika. Vile vile, imefafanua baadhi ya maneno ya Kiarabu au ya Kiswahili ambayo hayafahamiki kiwepesi katika jamii. Isitoshe, pametajwa ndani yake rejea za Aayah zilizo katika Suwrah tofauti ambazo zinagusia maudhui moja, ili msomaji aweze kuzipata kirahisi pale zilipo, na kulifahamu suala kwa ujumla wake. Na hatimaye, zimetajwa rejea za mtandaoni Alhidaaya.com [6] za maudhui kwenye makala na vitabu vya maudhui husika, zikiwemo rejea za Asbaabun-Nuzuwl (Sababu Za Kuteremshwa) Aayah au Suwrah., ambazo zitampa msomaji uelewa kamili na mzuri wa Aayah au Suwrah husika ili msomaji ajinufaishe zaidi na aweze kuongeza ilimu yake.
(ii) Tarjama Iliyochapishwa:
Tarjama hii iliyochapishwa kwenye karatasi haikuwekewa maelezo au fafanuzi kuhusu baadhi ya Aayaat. Sababu, ni kuzipa nafasi hati ziwe kubwa za wazi zinazosomeka kirahisi, na pia upatikane mjeledi mmoja tu wa Tarjama ili msomaji aweze kuutumia kiwepesi.
[46] Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿١١﴾
“Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.” [Ash-Shuwraa (42:11)]
[47] Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Hakuna yeyote anayeitwa Ar-Rahmaan isipokuwa Allaah (تبارك وتعالى) na Jina Lake linatukuzwa [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[48] Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym Nukhbah Min Al-‘Ulamaa – Markaz Tafsiyr Lid-Diraasaat Al-Qur-aaniyyah. Na Maqaaswid nyenginezo.
مركز تفسير للدراسات القرآنية
الْفَأتِحَة
001-Al-Faatihah
001-Al-Faatihah: Utangulizi Wa Suwrah [15]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿١﴾
1. Kwa Jina la Allaah Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), Ar-Rahiym (Mwenye Kurehemu)[1].
الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٢﴾
2. AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki) Allaah Rabb wa walimwengu.
الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿٣﴾
3. Mwingi wa Rehma, Mwenye Kurehemu.
مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ ﴿٤﴾
4. Mfalme wa Siku ya Malipo.
إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾
5. Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada.[2]
اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿٦﴾
6. Tuongoze njia iliyonyooka.[3]
صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ ﴿٧﴾
7. Njia ya wale Uliowaneemesha, si ya walioghadhibikiwa wala waliopotea.[4]
[1] Tofauti Ya Jina Na Sifa Ya Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), Ar-Rahiym (Mwenye Kurehemu).
Ar-Rahmaan: Sifa ya Jina hili ni pana zaidi na ni Sifa yenye kuenea zaidi kuliko Ar-Rahiym (Mwenye Kurehemu). Sifa hii inakusanya maana zote za Rehma, huruma n.k. Allaah Ndiye Mwenye Rehma iliyokusanya kila kitu, iliyoenea kwa viumbe Vyake vyote duniani; wanaadamu, majini, Waumini, makafiri, wanyama, mimea na kadhaalika. Hakuna yeyote au chochote katika kuwepo kwake ila Rehma Yake imemuenea. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥﴾
Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), Yuko juu ya ‘Arshi. [Twaahaa (20:50]
Na Sifa ya Majina mawili ya Ar-Rahmaan na Ar-Rahiym yanatokana na herufi tatu za asili, hivyo basi asili yake ni maana moja, isipokuwa tu kama ilivyobainishwa katika Sifa ya Rahmaan kuwa ni Rehma inayowafikia viumbe wote. Ama Rahiym ni Sifa khaswa kwa ajili ya Waumini pekee kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا ﴿٤٣﴾
Naye daima Ni Mwenye Kurehemu Waumini. [Al-Ahzaab: (33:43)]
[2] Isti’aanah (Kuomba Msaada):
Rejea makala ifuatayo kupata faida:
18-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aanah (Kuomba Msaada) Kwa Asiyekuwa Allaah [16]
Rejea pia Al-Anfaal (8:9), Al-Qaswasw (28:15) kupata maana ya Istighaathah (Kuomba Uokozi).
[3] Maana Ya Swiraatw Al-Mustaqiym (Njia Iliyonyooka):
Hadiyth Ya Kwanza:
Amesimulia An-Nawaas bin Sam’aan (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah (تعالى) Amepiga mfano Swiraatw (njia) iliyonyooka, imezungukwa pande zote na kuta mbili na kila ukuta una milango iliyo wazi na imefunikwa na mapazia. Na katika lango la Swiraatw kuna mlinganiaji akiita: “Enyi watu! Ingieni nyote katika swiraatw na msipite pembeni.” Na juu ya Swiraatw, kuna mlinganiaji mwengine anamuonya mtu yeyote anayetaka kufungua hiyo milango akiwaambia: Ole wenu! Msiufungue! Kwani mkifungua mtapita ndani! Kwani Asw-Swiraatw ni Uislaam, na kuta mbili ni mipaka Aliyoiweka Allaah. Na milango iliyofunguliwa ni yaliyoharamishwa na Allaah. Na huyo mlinganiaji juu ya lango la Swiraatw ni Kitabu cha Allaah, na mlinganiaji juu ya Swiraatw ni Maonyo ya Allaah yaliyo ndani ya kila nafsi ya Muislamu.” [Ahmad, ameisahihisha Al-Albaaniy; Swahiyh Al-Jaami’ (3887)]
Hadiyth Ya Pili:
Amesimulia Jaabir (رضي الله عنه): Tulikuwa tumekaa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akachora mstari mbele yake, kisha akachora mistari miwili kuliani, na mistari miwili kushotoni, kisha akaweka mkono wake katika njia ya katikati akasema: “Hii Njia ya Allaah.” Kisha akasoma:
وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ
Na kwamba hii ndiyo njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na Njia Yake. [Al-An’aam (6:153)]
[Ahmad, Swahiyh Ibn Maajah (11)]
Rejea pia (Aal-‘Imraan (3:103) (3:105), Al-An’aam (6:153).
[4] Nani Walioghadhibikiwa Na Waliopotea:
Amesimulia ‘Adiy bin Haatim (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Walioghadhibikiwa ni Mayahudi, na waliopotea ni Manaswara.” [At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Ghariyb na taz. Silsilah Asw-Swahiyhah (363)]
الْبَقَرَة
002-Al-Baqarah
002-Al-Baqarah: Utangulizi Wa Suwrah [18]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الم ﴿١﴾
1. Alif Laam Miym.[1]
ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٢﴾
2. Hiki[2] ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake, ni mwongozo[3] kwa wenye taqwa.[4]
الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٣﴾
3. Ambao huamini ya ghaibu[5] na husimamisha Swalaah[6] na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa.
وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَبِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ ﴿٤﴾
4. Na ambao huamini yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako na ni wenye yakini na Aakhirah.
أُولَـٰئِكَ عَلَىٰ هُدًى مِّن رَّبِّهِمْ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٥﴾
5. Hao wako juu ya mwongozo kutoka kwa Rabb wao, na hao ndio wenye kufaulu.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٦﴾
6. Hakika wale waliokufuru ni sawa kwao, ukiwaonya au usiwaonye wao hawatoamini.
خَتَمَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَعَلَىٰ سَمْعِهِمْ ۖ وَعَلَىٰ أَبْصَارِهِمْ غِشَاوَةٌ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٧﴾
7. Allaah Amepiga mhuri juu ya nyoyo zao, na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko, na watapata adhabu kuu kabisa.
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ ﴿٨﴾
8. Na miongoni mwa watu wako wasemao: Tumemuamini Allaah na Siku ya Mwisho hali ya kuwa si wenye kuamini.
يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَمَا يَخْدَعُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٩﴾
9. (Wanadhani) wanamhadaa Allaah, na wale walioamini, lakini hawahadai ila nafsi zao, wala hawahisi.
فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّـهُ مَرَضًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ ﴿١٠﴾
10. Ndani ya nyoyo zao mna maradhi (shubuhaat, unafiki)[7] na Allaah Akawazidishia maradhi, na watapata adhabu iumizayo kwa waliyokuwa wakiyakadhibisha.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ قَالُوا إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ ﴿١١﴾
11. Na wanapoambiwa: Msifanye ufisadi katika ardhi husema: Hakika sisi ni watengenezaji.
أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَـٰكِن لَّا يَشْعُرُونَ ﴿١٢﴾
12. Tanabahi! Hakika wao ndio mafisadi lakini hawahisi.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا كَمَا آمَنَ النَّاسُ قَالُوا أَنُؤْمِنُ كَمَا آمَنَ السُّفَهَاءُ ۗ أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ السُّفَهَاءُ وَلَـٰكِن لَّا يَعْلَمُونَ ﴿١٣﴾
13. Na wanapoambiwa: Aminini kama walivyoamini watu husema: Je, tuamini kama walivyoamini wapumbavu? Tanabahi! Hakika wao ndio wapumbavu lakini hawajui.
وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا إِلَىٰ شَيَاطِينِهِمْ قَالُوا إِنَّا مَعَكُمْ إِنَّمَا نَحْنُ مُسْتَهْزِئُونَ ﴿١٤﴾
14. Na wanapokutana na wale walioamini husema: Tumeamini. Na wanapokuwa peke yao pamoja na mashaytwaan wao, husema: Hakika sisi tuko pamoja nanyi, hakika sisi ni wenye kuwadhihaki tu.
اللَّـهُ يَسْتَهْزِئُ بِهِمْ وَيَمُدُّهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١٥﴾
15. Allaah Anawadhihaki[8] wao na Atawaendeleza katika hali yao ya upindukiaji mipaka wa kuasi, wakitangatanga kwa upofu.
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الضَّلَالَةَ بِالْهُدَىٰ فَمَا رَبِحَت تِّجَارَتُهُمْ وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ ﴿١٦﴾
16. Hao ndio wale waliobadilisha upotofu badala ya uongofu, basi haikupata faida biashara yao na wala hawakuwa wenye kuhidika.
مَثَلُهُمْ كَمَثَلِ الَّذِي اسْتَوْقَدَ نَارًا فَلَمَّا أَضَاءَتْ مَا حَوْلَهُ ذَهَبَ اللَّـهُ بِنُورِهِمْ وَتَرَكَهُمْ فِي ظُلُمَاتٍ لَّا يُبْصِرُونَ ﴿١٧﴾
17. Mfano wao ni kama mfano wa aliyekoka moto, ulipoyaangaza yaliyopo pembezoni mwake, Allaah Akawaondoshea nuru yao na Akawaacha katika viza, hawaoni.
صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ ﴿١٨﴾
18. Viziwi, mabubu, vipofu basi hawatorejea.
أَوْ كَصَيِّبٍ مِّنَ السَّمَاءِ فِيهِ ظُلُمَاتٌ وَرَعْدٌ وَبَرْقٌ يَجْعَلُونَ أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِم مِّنَ الصَّوَاعِقِ حَذَرَ الْمَوْتِ ۚ وَاللَّـهُ مُحِيطٌ بِالْكَافِرِينَ ﴿١٩﴾
19. Au ni kama mvua kubwa kutoka mbinguni, ndani yake mna viza na radi na umeme, wanatia vidole vyao katika masikio yao kutokana na mingurumo wakikhofu mauti, na Allaah Ni Mwenye Kuwazunguka makafiri.
يَكَادُ الْبَرْقُ يَخْطَفُ أَبْصَارَهُمْ ۖ كُلَّمَا أَضَاءَ لَهُم مَّشَوْا فِيهِ وَإِذَا أَظْلَمَ عَلَيْهِمْ قَامُوا ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَذَهَبَ بِسَمْعِهِمْ وَأَبْصَارِهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٠﴾
20. Unakaribia umeme kunyakua macho yao, kila unapowaangazia (njia) hutembea humo, na unapowafanyia kiza husimama. Na lau Allaah Angelitaka, basi Angeliwaondoshea kusikia kwao na kuona kwao. Hakika Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿٢١﴾
21. Enyi watu! Mwabuduni Rabb wenu Ambaye Amekuumbeni, na wale wa kabla yenu, mpate kuwa na taqwa.
الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٢﴾
22. Ambaye Amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa, na Akateremsha kutoka mbinguni maji, Akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye na hali ya kuwa nyinyi mnajua.
وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِ وَادْعُوا شُهَدَاءَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٣﴾
23. Na ikiwa mko katika shaka kutokana na Tuliyoyateremsha juu ya Mja Wetu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi leteni Suwrah mfano wake,[9] na waiteni mashahidi wenu pasipo na Allaah mkiwa ni wakweli.
فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا وَلَن تَفْعَلُوا فَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ ۖ أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ ﴿٢٤﴾
24. Msipofanya, na wala hamtoweza kufanya, basi ogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe, umeandaliwa kwa makafiri.
وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ كُلَّمَا رُزِقُوا مِنْهَا مِن ثَمَرَةٍ رِّزْقًا ۙ قَالُوا هَـٰذَا الَّذِي رُزِقْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَأُتُوا بِهِ مُتَشَابِهًا ۖ وَلَهُمْ فِيهَا أَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ ۖ وَهُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٥﴾
25. Na wabashirie wale walioamini na wakatenda mema, kwamba watapata Jannaat (bustani) zipitazo chini yake mito, kila watakaporuzukiwa humo katika matunda kuwa ni riziki husema: Haya ndiyo yale tuliyoruzukiwa kabla. Na wataletewa hali ya kuwa yanashabihiana, na watapata humo wake waliotakaswa, nao humo watadumu.
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَسْتَحْيِي أَن يَضْرِبَ مَثَلًا مَّا بَعُوضَةً فَمَا فَوْقَهَا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۖ وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَيَقُولُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۘ يُضِلُّ بِهِ كَثِيرًا وَيَهْدِي بِهِ كَثِيرًا ۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِ إِلَّا الْفَاسِقِينَ ﴿٢٦﴾
26. Hakika Allaah Haoni haya kupiga mfano wa mbu[10] na ulio zaidi yake (kwa udogo). Basi wale walioamini wanajua kwamba hiyo ni haki kutoka kwa Rabb wao. Ama wale waliokufuru husema: Anataka nini Allaah kwa mfano huu? Kwa (mfano) huo, Huwapoteza wengi na Huwaongoza kwao wengi na wala Hawapotezi kwao ila mafasiki.[11]
الَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٢٧﴾
27. Wale wanaovunja Ahadi ya Allaah baada ya kuifunga Kwake na wanakata Aliyoyaamrisha Allaah kuungwa,[12] na wanafanya ufisadi katika ardhi, hao ndio wenye khasara.
كَيْفَ تَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَكُنتُمْ أَمْوَاتًا فَأَحْيَاكُمْ ۖ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٨﴾
28. Vipi mnamkufuru Allaah na hali mlikuwa wafu Akakuhuisheni, kisha Atakufisheni, kisha Atakuhuisheni, kisha Kwake mtarejeshwa?[13]
هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ فَسَوَّاهُنَّ سَبْع سَمَاوَاتٍ ۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٩﴾
29. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbieni vyote vilivyomo ardhini kisha Kisha Akazikusudia mbingu (Kuziumba)[14] na Akazifanya timilifu mbingu saba, Naye kwa kila kitu Ni Mjuzi.
وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ۖ قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٣٠﴾
30. Na pindi Rabb wako Alipowaambia Malaika: Hakika Mimi Nitaweka katika ardhi khalifa.[15] Wakasema: Utaweka humo atakayefanya ufisadi humo na kumwaga damu, na hali sisi tunakusabihi kwa Himdi Zako na tunakutukuza kwa Utakatifu Wako? (Allaah) Akasema: Hakika Mimi Nayajua zaidi msiyoyajua.
وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى الْمَلَائِكَةِ فَقَالَ أَنبِئُونِي بِأَسْمَاءِ هَـٰؤُلَاءِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٣١﴾
31. Na Akamfunza Aadam majina yote (ya kila kitu), kisha Akavionyesha mbele ya Malaika Akasema: Niambieni majina ya hivi mkiwa ni wakweli.
قَالُوا سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ ﴿٣٢﴾
32. Wakasema: Utakasifu ni Wako! Hatuna ilimu isipokuwa Uliyotufunza, hakika Wewe Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
قَالَ يَا آدَمُ أَنبِئْهُم بِأَسْمَائِهِمْ ۖ فَلَمَّا أَنبَأَهُم بِأَسْمَائِهِمْ قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ إِنِّي أَعْلَمُ غَيْبَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَأَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ ﴿٣٣﴾
33. Akasema: Ee Aadam, wajulishe kwa majina yao. Basi alipowatajia majina yao, (Allaah) Akasema: Je, Sikuwaambieni kuwa hakika Mimi Najua ghaibu ya mbingu na ardhi na Najua mnayoyadhihirisha na mliyokuwa mkiyaficha?
وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ ﴿٣٤﴾
34. Na pale Tulipowaambia Malaika: Msujudieni Aadam. Wakasujudu isipokuwa Ibliys alikataa na akatakabari,[16] akawa miongoni mwa makafiri.
وَقُلْنَا يَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ وَكُلَا مِنْهَا رَغَدًا حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٣٥﴾
35. Na Tukasema: Ee Aadam, kaa wewe na mkeo (Hawaa) Jannah na kuleni humo maridhawa popote mpendapo na wala msiukaribie mti huu, mtakuwa miongoni mwa madhalimu.
فَأَزَلَّهُمَا الشَّيْطَانُ عَنْهَا فَأَخْرَجَهُمَا مِمَّا كَانَا فِيهِ ۖ وَقُلْنَا اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ ﴿٣٦﴾
36. Shaytwaan akawatelezesha wote wawili kwayo, Akawatoa kutoka katika hali waliyokuwa nayo. Tukasema: Shukeni mkiwa maadui nyinyi kwa nyinyi, na mtapata katika ardhi makazi na starehe hadi muda maalumu.
فَتَلَقَّىٰ آدَمُ مِن رَّبِّهِ كَلِمَاتٍ فَتَابَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿٣٧﴾
37. Kisha Aadam akapokea maneno kutoka kwa Rabb wake, na (Rabb wake) Akapokea tawbah yake. Hakika Yeye Ndiye Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.
قُلْنَا اهْبِطُوا مِنْهَا جَمِيعًا ۖ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَن تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٣٨﴾
38. Tukasema: Shukeni kutoka humo nyote! Utakapokufikieni kutoka Kwangu mwongozo, basi yeyote atakayefuata Mwongozo Wangu hakutokuwa na khofu juu yao wala hawatohuzunika.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٣٩﴾
39. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili) Zetu, hao ni watu wa motoni, wao humo watadumu.
يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَوْفُوا بِعَهْدِي أُوفِ بِعَهْدِكُمْ وَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ ﴿٤٠﴾
40. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni Neema Yangu Niliyokuneemesheni, na timizeni Ahadi Yangu Nikutimizieni ahadi yenu, na Mimi Pekee niogopeni.
وَآمِنُوا بِمَا أَنزَلْتُ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُمْ وَلَا تَكُونُوا أَوَّلَ كَافِرٍ بِهِ ۖ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا وَإِيَّايَ فَاتَّقُونِ ﴿٤١﴾
41. Na aminini yale Niliyoyateremsha yenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nanyi, na wala msiwe wa kwanza wenye kuyakanusha, na wala msibadilishe Aayaat Zangu kwa thamani ndogo, na muwe na taqwa kunikhofu Mimi tu.
وَلَا تَلْبِسُوا الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُوا الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٤٢﴾
42. Na wala msichanganye haki kwa baatwil na mkaficha haki na hali mnajua.
وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَارْكَعُوا مَعَ الرَّاكِعِينَ ﴿٤٣﴾
43. Na simamisheni Swalaah na toeni Zakaah na rukuuni pamoja na wanaorukuu (katika utiifu).
أَتَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنسَوْنَ أَنفُسَكُمْ وَأَنتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٤٤﴾
44. Je, mnaamrisha watu watende mema na mnajisahu nafsi zenu na hali ya kuwa nyinyi mnasoma Kitabu, je hamtii akilini?[17]
وَاسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلَّا عَلَى الْخَاشِعِينَ ﴿٤٥﴾
45. Na tafuteni msaada kupitia subira na Swalaah, na hakika hilo ni kubwa isipokuwa kwa wanyenyekevu.
الَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَاقُو رَبِّهِمْ وَأَنَّهُمْ إِلَيْهِ رَاجِعُونَ ﴿٤٦﴾
46. Ambao wana yakini kwamba hakika wao watakutana na Rabb wao na hakika wao Kwake watarejea.
يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٤٧﴾
47. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni Neema Yangu Niliyokuneemesheni na hakika Mimi Nimekufadhilisheni juu ya walimwengu wote.[18]
وَاتَّقُوا يَوْمًا لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا شَفَاعَةٌ وَلَا يُؤْخَذُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٤٨﴾
48. Na iogopeni Siku ambayo nafsi haitoifaa nafsi nyingine kwa kitu chochote kile, na wala haitokubaliwa kutoka kwake uombezi wowote, na wala hakitochukuliwa kutoka kwake kikomboleo, na wala hawatonusuriwa.
وَإِذْ نَجَّيْنَاكُم مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ يُذَبِّحُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ ۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَاءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ ﴿٤٩﴾
49. Na pindi Tulipokuokoeni kutoka kwa watu wa Firawni walipokusibuni adhabu mbaya, wakiwachinja watoto wenu wa kiume na wakiacha hai wanawake wenu, na katika hayo kwenu, ulikuwa ni mtihani mkuu kabisa kutoka kwa Rabb wenu.
وَإِذْ فَرَقْنَا بِكُمُ الْبَحْرَ فَأَنجَيْنَاكُمْ وَأَغْرَقْنَا آلَ فِرْعَوْنَ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ ﴿٥٠﴾
50. Na pindi Tulipoitenganisha bahari kwa ajili yenu, Tukakuokoeni na Tukawagharikisha watu wa Firawni na huku nyinyi mnatazama.
وَإِذْ وَاعَدْنَا مُوسَىٰ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً ثُمَّ اتَّخَذْتُمُ الْعِجْلَ مِن بَعْدِهِ وَأَنتُمْ ظَالِمُونَ ﴿٥١﴾
51. Na pindi Tulipomuahidi Muwsaa siku arubaini kisha mkamwabudu ndama baada yake na mkawa madhalimu.
ثُمَّ عَفَوْنَا عَنكُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٥٢﴾
52. Kisha Tukawasameheni baada ya hapo ili mpate kushukuru.
وَإِذْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَالْفُرْقَانَ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿٥٣﴾
53. Na pindi Tulipompa Muwsaa Kitabu na pambanuo[19] (la haki na baatwil) ili mpate kuongoka.
وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِنَّكُمْ ظَلَمْتُمْ أَنفُسَكُم بِاتِّخَاذِكُمُ الْعِجْلَ فَتُوبُوا إِلَىٰ بَارِئِكُمْ فَاقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ عِندَ بَارِئِكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۚ إِنَّهُ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿٥٤﴾
54. Na pindi Muwsaa alipowaambia kaumu yake: Enyi kaumu yangu! Hakika nyinyi mmedhulumu nafsi zenu kwa kuabudu kwenu ndama, basi tubuni kwa Muumbaji wenu, na ziueni nafsi zenu, hivyo ni bora kwenu mbele ya Muumbaji wenu. Akapokea tawbah yenu, hakika Yeye Ndiye Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.
وَإِذْ قُلْتُمْ يَا مُوسَىٰ لَن نُّؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ نَرَى اللَّـهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْكُمُ الصَّاعِقَةُ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ ﴿٥٥﴾
55. Na pindi mliposema: Ee Muwsaa! Hatutokuamini mpaka tumuone Allaah wazi wazi, ikakuchukueni radi na umeme angamizi nanyi mnatazama.
ثُمَّ بَعَثْنَاكُم مِّن بَعْدِ مَوْتِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٥٦﴾
56. Kisha Tukakufufueni baada ya kufa kwenu ili mpate kushukuru.
وَظَلَّلْنَا عَلَيْكُمُ الْغَمَامَ وَأَنزَلْنَا عَلَيْكُمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ ۖ كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ ۖ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٥٧﴾
57. Na Tukakufunikeni kwa mawingu na Tukakuteremshieni al-manna na as-salwaa[20]. (Tukakwambieni): Kuleni katika vizuri Tulivyokuruzukuni. Hawakutudhulumu Sisi lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.
وَإِذْ قُلْنَا ادْخُلُوا هَـٰذِهِ الْقَرْيَةَ فَكُلُوا مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ رَغَدًا وَادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا وَقُولُوا حِطَّةٌ نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطَايَاكُمْ ۚ وَسَنَزِيدُ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٨﴾
58. Na pindi Tuliposema: Ingieni mji huu (Quds) na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, na ingieni katika mlango wake huku mmeinama kunyenyekea na semeni Hittwah[21] (Tuondolee uzito wa madhambi),Tutakughufurieni makosa yenu na Tutawazidishia (thawabu) wafanyao ihsaan.
فَبَدَّلَ الَّذِينَ ظَلَمُوا قَوْلًا غَيْرَ الَّذِي قِيلَ لَهُمْ فَأَنزَلْنَا عَلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿٥٩﴾
59. Basi wale waliodhulumu walibadilisha kauli kinyume na ile waliyoambiwa, Tukateremsha juu ya waliodhulumu adhabu ya kufadhaika kutoka mbinguni kwa yale waliyokuwa wakifanya ya ufasiki.
وَإِذِ اسْتَسْقَىٰ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ فَقُلْنَا اضْرِب بِّعَصَاكَ الْحَجَرَ ۖ فَانفَجَرَتْ مِنْهُ اثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا ۖ قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ ۖ كُلُوا وَاشْرَبُوا مِن رِّزْقِ اللَّـهِ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿٦٠﴾
60. Na pindi Muwsaa alipoomba maji kwa ajili ya kaumu yake. Tukasema: Piga kwa fimbo yako jiwe. Zikachimbuka na kububujika kutoka kwalo chemchemu kumi na mbili. Kila kabila likajua mahala pake pa kunywea. Kuleni na kunyweni kutokana na Riziki ya Allaah, wala msieneze uovu katika ardhi hali ya kuwa ni wenye kufanya ufisadi.
وَإِذْ قُلْتُمْ يَا مُوسَىٰ لَن نَّصْبِرَ عَلَىٰ طَعَامٍ وَاحِدٍ فَادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُخْرِجْ لَنَا مِمَّا تُنبِتُ الْأَرْضُ مِن بَقْلِهَا وَقِثَّائِهَا وَفُومِهَا وَعَدَسِهَا وَبَصَلِهَا ۖ قَالَ أَتَسْتَبْدِلُونَ الَّذِي هُوَ أَدْنَىٰ بِالَّذِي هُوَ خَيْرٌ ۚ اهْبِطُوا مِصْرًا فَإِنَّ لَكُم مَّا سَأَلْتُمْ ۗ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ وَالْمَسْكَنَةُ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ ۗ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۗ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿٦١﴾
61. Na pindi mliposema: Ee Muwsaa! Hatuwezi kusubiri kwa chakula cha aina moja tu, basi tuombee kwa Rabb wako Atutolee katika inavyoviotesha ardhi; kati ya mboga zake, matango yake, thomu (au ngano) yake, adesi zake na vitunguu vyake. (Muwsaa) akasema: Je mnataka kubadilisha yaliyo duni kwa yaliyo bora? Shukeni mjini, hakika huko mtapata mnayoyauliza. Na ikapigwa juu yao dhila na umaskini na wakastahiki ghadhabu kutoka kwa Allaah! Hayo ni kwa kuwa wao walikuwa wakikanusha Aayaat (na Ishara, Dalili) za Allaah na wakiwaua Manabii bila ya haki. Hayo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakitaadi.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالنَّصَارَىٰ وَالصَّابِئِينَ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٦٢﴾
62. Hakika wale walioamini, na wale ambao (kabla ya Uislamu) ni Mayahudi, na Manaswara na Wasabai[22]; yeyote atakayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na akatenda mema, basi watapata ujira wao kutoka kwa Rabb wao, na hakutokuwa na khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.
وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاذْكُرُوا مَا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿٦٣﴾
63. Na pindi Tulipochukua ahadi yenu na Tukaunyanyua juu yenu mlima (Tukasema): Shikilieni Tuliyokupeni kwa nguvu na kumbukeni yaliyomo humo mpate kuwa na taqwa.
ثُمَّ تَوَلَّيْتُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ ۖ فَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَكُنتُم مِّنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٦٤﴾
64. Kisha mkakengeuka baada ya hayo, na lau si Fadhila za Allaah juu yenu na Rehma Yake mngekuwa miongoni mwa wenye kukhasirika.
وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ الَّذِينَ اعْتَدَوْا مِنكُمْ فِي السَّبْتِ فَقُلْنَا لَهُمْ كُونُوا قِرَدَةً خَاسِئِينَ ﴿٦٥﴾
65. Na kwa yakini mlikwishawajua wale miongoni mwenu waliotaadi mipaka ya As-Sabt[23] Tukawaambia: Kuweni manyani waliobezwa.
فَجَعَلْنَاهَا نَكَالًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهَا وَمَا خَلْفَهَا وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٦٦﴾
66. Tukaifanya kuwa ni adhabu ya tahadharisho na fundisho kwa waliokuweko zama zao na wataokuja baada yao, na ni mawaidha kwa wenye taqwa.
وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تَذْبَحُوا بَقَرَةً ۖ قَالُوا أَتَتَّخِذُنَا هُزُوًا ۖ قَالَ أَعُوذُ بِاللَّـهِ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ ﴿٦٧﴾
67. Na pindi Muwsaa alipowaambia kaumu wake: Hakika Allaah Anakuamuruni mchinje ng’ombe.[24] Wakasema: Unatufanyia mzaha? Akasema: Najikinga kwa Allaah kuwa miongoni mwa wajinga.
قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ ۚ قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَّا فَارِضٌ وَلَا بِكْرٌ عَوَانٌ بَيْنَ ذَٰلِكَ ۖ فَافْعَلُوا مَا تُؤْمَرُونَ ﴿٦٨﴾
68. Wakasema: Tuombee kwa Rabb wako Atubainishie ni ng’ombe wa aina gani huyo? (Muwsaa) akasema: Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ng’ombe mwenyewe si mpevu wala si mchanga, bali ni wa katikati baina ya hao, basi fanyeni mnavyoamrishwa.
قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا لَوْنُهَا ۚ قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ صَفْرَاءُ فَاقِعٌ لَّوْنُهَا تَسُرُّ النَّاظِرِينَ ﴿٦٩﴾
69. Wakasema: Tuombee kwa Rabb wako Atubainishie rangi yake. (Muwsaa) akasema: Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ni ng’ombe wa rangi ya njano iliyoiva mno, rangi yake huwapendeza wanaotazama.
قَالُوا ادْعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَ إِنَّ الْبَقَرَ تَشَابَهَ عَلَيْنَا وَإِنَّا إِن شَاءَ اللَّـهُ لَمُهْتَدُونَ ﴿٧٠﴾
70. Wakasema: Tuombee kwa Rabb wako Atubainishie ni ng’ombe wa aina gani huyo? Kwa hakika ng’ombe wametutatiza na hakika sisi In-Shaa-Allaah tutakuwa wenye kuhidika.
قَالَ إِنَّهُ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌ لَّا ذَلُولٌ تُثِيرُ الْأَرْضَ وَلَا تَسْقِي الْحَرْثَ مُسَلَّمَةٌ لَّا شِيَةَ فِيهَا ۚ قَالُوا الْآنَ جِئْتَ بِالْحَقِّ ۚ فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُوا يَفْعَلُونَ ﴿٧١﴾
71. (Muwsaa) akasema: Hakika Yeye (Allaah) Anasema kwamba ni ng’ombe ambaye hakutiishwa wa kulima ardhi wala kwa kumwagilia maji shamba, ni mkamilifu hana dosari. Wakasema: Sasa umekuja na haki. Basi wakamchinja na hawakuwa wenye kukaribia kufanya hivyo.
وَإِذْ قَتَلْتُمْ نَفْسًا فَادَّارَأْتُمْ فِيهَا ۖ وَاللَّـهُ مُخْرِجٌ مَّا كُنتُمْ تَكْتُمُونَ ﴿٧٢﴾
72. Na pindi mlipoiua nafsi, kisha mkakhitilafiana kwayo, na Allaah Ni Mwenye Kutoa hayo mliyokuwa mkiyaficha.
فَقُلْنَا اضْرِبُوهُ بِبَعْضِهَا ۚ كَذَٰلِكَ يُحْيِي اللَّـهُ الْمَوْتَىٰ وَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٧٣﴾
73. Tukasema: Mpigeni (huyo maiti) kwa kipande chake (huyo ng’ombe). Hivyo ndivyo Allaah Anavyohuisha wafu na Anakuonyesheni Aayaat (Miujiza na Dalili) Zake huenda mkatia akilini.
ثُمَّ قَسَتْ قُلُوبُكُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ فَهِيَ كَالْحِجَارَةِ أَوْ أَشَدُّ قَسْوَةً ۚ وَإِنَّ مِنَ الْحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنْهُ الْأَنْهَارُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخْرُجُ مِنْهُ الْمَاءُ ۚ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَهْبِطُ مِنْ خَشْيَةِ اللَّـهِ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٧٤﴾
74. Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, zikawa kama mawe au ngumu zaidi. Na kwa hakika katika mawe kuna yanayobubujika humo mito. Na hakika katika hayo kuna yanayopasuka yakatoka humo maji. Na hakika katika hayo kuna mengine yanayoporomoka kutokana na khofu ya Allaah. Na Allaah Si Mwenye Kughafilika kuhusu myatendayo.
أَفَتَطْمَعُونَ أَن يُؤْمِنُوا لَكُمْ وَقَدْ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَسْمَعُونَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ يُحَرِّفُونَهُ مِن بَعْدِ مَا عَقَلُوهُ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٥﴾
75. Je, mnatumai kwamba watakuaminini na hali lilikuwa kundi miongoni mwao linasikia Maneno ya Allaah kisha linayageuza baada ya kuyaelewa na hali wanajua?
وَإِذَا لَقُوا الَّذِينَ آمَنُوا قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَا بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ قَالُوا أَتُحَدِّثُونَهُم بِمَا فَتَحَ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ لِيُحَاجُّوكُم بِهِ عِندَ رَبِّكُمْ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٧٦﴾
76. Na wanapokutana na wale walioamini husema: Tumeamini. Na wanapokuwa peke yao, wao kwa wao, husema: Hivi mnawasimulia yale Aliyokufungulieni Allaah ili wapate kukuhojini kwayo mbele ya Rabb wenu? Hamtii akilini?
أَوَلَا يَعْلَمُونَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴿٧٧﴾
77. Je, hawajui kwamba Allaah Anajua wanayoyaficha na wanayoyatangaza?
وَمِنْهُمْ أُمِّيُّونَ لَا يَعْلَمُونَ الْكِتَابَ إِلَّا أَمَانِيَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ ﴿٧٨﴾
78. Na miongoni mwao wako wasiojua kusoma wala kuandika, hawakijui Kitabu ila matamanio ya kuwaza tu, nao hawana ila kudhania tu.
فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَـٰذَا مِنْ عِندِ اللَّـهِ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا يَكْسِبُونَ ﴿٧٩﴾
79. Basi ole kwa wale wenye kuandika kitabu kwa mikono yao kisha wakasema: Hiki ni kutoka kwa Allaah ili wabadilishe kwa thamani ndogo. Basi ole wao kwa yale yaliyoandikwa na mikono yao, na ole wao kwa yale wanayoyachuma![25]
وَقَالُوا لَن تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَّعْدُودَةً ۚ قُلْ أَتَّخَذْتُمْ عِندَ اللَّـهِ عَهْدًا فَلَن يُخْلِفَ اللَّـهُ عَهْدَهُ ۖ أَمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٨٠﴾
80. Na walisema: Hautotugusa moto ila siku chache tu. Sema: Je, mmechukua ahadi kwa Allaah? Basi Allaah Hakhalifu Ahadi Yake, au mnasema kuhusu Allaah msiyoyajua?
بَلَىٰ مَن كَسَبَ سَيِّئَةً وَأَحَاطَتْ بِهِ خَطِيئَتُهُ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٨١﴾
81. Naam! Yeyote aliyechuma uovu na yakamzunguka makosa yake, basi hao ni watu wa motoni, wao humo watadumu.
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٨٢﴾
82. Na wale walioamini na wakatenda mema, hao ni watu wa Jannah, wao humo watadumu.
وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ لَا تَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّـهَ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَقُولُوا لِلنَّاسِ حُسْنًا وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ ثُمَّ تَوَلَّيْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنكُمْ وَأَنتُم مُّعْرِضُونَ ﴿٨٣﴾
83. Na pindi Tulipochukua fungamano la wana wa Israaiyl (Tukawaambia): Msiabudu isipokuwa Allaah, na muwafanyie ihsaan wazazi wawili, na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini, na semeni na watu kwa uzuri na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, kisha mkakengeuka ila wachache miongoni mwenu na huku nyinyi mnapuuza.
وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ لَا تَسْفِكُونَ دِمَاءَكُمْ وَلَا تُخْرِجُونَ أَنفُسَكُم مِّن دِيَارِكُمْ ثُمَّ أَقْرَرْتُمْ وَأَنتُمْ تَشْهَدُونَ ﴿٨٤﴾
84. Na pindi Tulipochukua fungamano lenu (Tukawaambia): Msimwage damu zenu, wala msijitoe majumbani mwenu, kisha mkakubali nanyi mnashuhudia.
ثُمَّ أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ تَقْتُلُونَ أَنفُسَكُمْ وَتُخْرِجُونَ فَرِيقًا مِّنكُم مِّن دِيَارِهِمْ تَظَاهَرُونَ عَلَيْهِم بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَإِن يَأْتُوكُمْ أُسَارَىٰ تُفَادُوهُمْ وَهُوَ مُحَرَّمٌ عَلَيْكُمْ إِخْرَاجُهُمْ ۚ أَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ الْكِتَابِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍ ۚ فَمَا جَزَاءُ مَن يَفْعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمْ إِلَّا خِزْيٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرَدُّونَ إِلَىٰ أَشَدِّ الْعَذَابِ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٨٥﴾
85. Kisha nyinyi ndio hao mnauana na mnawatoa kundi miongoni mwenu kutoka majumbani mwao, mnasaidiana dhidi yao kwa dhambi na uadui, na wanapokujieni mateka mnawakomboa na hali hilo la kuwatoa limeharamishwa kwenu. Je, mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakanusha baadhi yake? Basi hapana jazaa ya anayefanya hayo miongoni mwenu isipokuwa hizaya katika dunia, na Siku ya Qiyaamah watapelekwa kwenye adhabu kali zaidi. Na Allaah Si Mwenye Kughafilika kuhusu myatendayo.
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا بِالْآخِرَةِ ۖ فَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٨٦﴾
86. Hao ndio wale waliobadilisha uhai wa dunia badala ya Aakhirah, basi hawatapunguziwa adhabu wala hawatonusuriwa.
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَقَفَّيْنَا مِن بَعْدِهِ بِالرُّسُلِ ۖ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ أَفَكُلَّمَا جَاءَكُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُكُمُ اسْتَكْبَرْتُمْ فَفَرِيقًا كَذَّبْتُمْ وَفَرِيقًا تَقْتُلُونَ ﴿٨٧﴾
87. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu na Tukafuatisha Rusuli baada yake. Na Tukampa ‘Iysaa mwana wa Maryam hoja bayana na Tukamtia nguvu kwa Ruwh[26] Al-Qudus (Jibriyl (عليه السلام. Je, basi kila alipokujieni Rasuli kwa yale ambayo nafsi zenu haziyapendi, mlitakabari, kundi mkalikadhibisha na jingine mnaliua.
وَقَالُوا قُلُوبُنَا غُلْفٌ ۚ بَل لَّعَنَهُمُ اللَّـهُ بِكُفْرِهِمْ فَقَلِيلًا مَّا يُؤْمِنُونَ ﴿٨٨﴾
88. Na wakasema: Nyoyo zetu zimefunikwa. Bali Allaah Amewalaani kwa kufuru zao, kwa hivyo ni kidogo tu wanayoyaamini.
وَلَمَّا جَاءَهُمْ كِتَابٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ وَكَانُوا مِن قَبْلُ يَسْتَفْتِحُونَ عَلَى الَّذِينَ كَفَرُوا فَلَمَّا جَاءَهُم مَّا عَرَفُوا كَفَرُوا بِهِ ۚ فَلَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٨٩﴾
89. Na kilipowajia Kitabu kutoka kwa Allaah kisadikishacho yale yaliyo pamoja nao - japokuwa kabla ya hapo walikuwa wakiomba ushindi dhidi ya wale waliokufuru – lakini (kisha) yalipowajia yale waliyokuwa wakiyatambua waliyakanusha, basi Laana ya Allaah iwe juu ya makafiri.[27]
بِئْسَمَا اشْتَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ أَن يَكْفُرُوا بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ بَغْيًا أَن يُنَزِّلَ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ فَبَاءُوا بِغَضَبٍ عَلَىٰ غَضَبٍ ۚ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٩٠﴾
90. Ubaya ulioje walichojibadilishia nafsi zao, kwamba wakufuru yale Aliyoyateremsha Allaah kwa baghi[28] (chuki na uhasidi) kwa kuwa Allaah Kateremsha katika Fadhila Zake juu ya Amtakae katika Waja Wake. Basi wakarudi kustahiki ghadhabu juu ya ghadhabu. Na makafiri watapata adhabu ya kudhalilisha.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُوا بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا نُؤْمِنُ بِمَا أُنزِلَ عَلَيْنَا وَيَكْفُرُونَ بِمَا وَرَاءَهُ وَهُوَ الْحَقُّ مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَهُمْ ۗ قُلْ فَلِمَ تَقْتُلُونَ أَنبِيَاءَ اللَّـهِ مِن قَبْلُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٩١﴾
91. Na wanapoambiwa: Aminini yale Aliyoyateremsha Allaah, husema: Tunaamini yale yaliyoteremshwa kwetu na wanayakanusha yale yaliyokuja baada yake, na hali ya kuwa hayo ni haki yenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nao. Sema: Kwa nini basi mnawaua Manabii wa Allaah hapo zamani kama kweli mlikuwa waumini?
وَلَقَدْ جَاءَكُم مُّوسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ اتَّخَذْتُمُ الْعِجْلَ مِن بَعْدِهِ وَأَنتُمْ ظَالِمُونَ ﴿٩٢﴾
92. Na kwa yakini alikujieni Muwsaa kwa hoja bayana kisha mkamwabudu ndama baada yake na mkawa madhalimu.
وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاسْمَعُوا ۖ قَالُوا سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَأُشْرِبُوا فِي قُلُوبِهِمُ الْعِجْلَ بِكُفْرِهِمْ ۚ قُلْ بِئْسَمَا يَأْمُرُكُم بِهِ إِيمَانُكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٩٣﴾
93. Na Tulipochukua fungamano lenu na Tukaunyanyua juu yenu mlima (Tukasema): Shikilieni Tuliyokupeni kwa nguvu na sikilizeni. Wakasema: Tumesikia na tumeasi. Wakanyweshwa katika nyoyo zao (kumwabudu) ndama kwa kufuru yao. Sema: Ubaya ulioje inakuamrisheni kwayo imaan yenu mkiwa ni waumini!
قُلْ إِن كَانَتْ لَكُمُ الدَّارُ الْآخِرَةُ عِندَ اللَّـهِ خَالِصَةً مِّن دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُا الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٩٤﴾
94. Sema: Ikiwa nyumba ya Aakhirah iliyoko kwa Allaah ni makhsusi kwenu pekee pasi na watu wengine, basi tamanini mauti mkiwa ni wakweli.
وَلَن يَتَمَنَّوْهُ أَبَدًا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ ﴿٩٥﴾
95. Na hawatoyatamani abadani kwa sababu ya iliyoyatanguliza mikono yao. Na Allaah Ni Mjuzi wa madhalimu.
وَلَتَجِدَنَّهُمْ أَحْرَصَ النَّاسِ عَلَىٰ حَيَاةٍ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا ۚ يَوَدُّ أَحَدُهُمْ لَوْ يُعَمَّرُ أَلْفَ سَنَةٍ وَمَا هُوَ بِمُزَحْزِحِهِ مِنَ الْعَذَابِ أَن يُعَمَّرَ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ ﴿٩٦﴾
96. Na kwa yakini utawakuta wao (Mayahudi) ni watu wenye pupa zaidi ya kuishi na kuliko washirikina. Kila mmoja wao anapenda lau angelipewa umri wa miaka elfu. Wala huko kuzidishiwa umri hakutamuondoshea adhabu. Na Allaah Ni Mwenye Kuona wanayoyatenda.
قُلْ مَن كَانَ عَدُوًّا لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلَىٰ قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللَّـهِ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ ﴿٩٧﴾
97. Sema: Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha Qur-aan katika moyo wako (ee Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Idhini ya Allaah inayosadikisha yaliyo kabla yake, na mwongozo na bishara kwa Waumini.[29]
مَن كَانَ عَدُوًّا لِّلَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَرُسُلِهِ وَجِبْرِيلَ وَمِيكَالَ فَإِنَّ اللَّـهَ عَدُوٌّ لِّلْكَافِرِينَ ﴿٩٨﴾
98. Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake, na Rusuli Wake, na Jibriyl, na Miykaaiyl,[30] basi hakika Allaah Ni adui wa makafiri.
وَلَقَدْ أَنزَلْنَا إِلَيْكَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۖ وَمَا يَكْفُرُ بِهَا إِلَّا الْفَاسِقُونَ ﴿٩٩﴾
99. Na kwa yakini Tumeteremsha kwako Aayaat bayana, na hawazikanushi isipokuwa mafasiki.
أَوَكُلَّمَا عَاهَدُوا عَهْدًا نَّبَذَهُ فَرِيقٌ مِّنْهُم ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠٠﴾
100. Je! Eti ndio kila wanapochukua ahadi kundi miongoni mwao huivunja? Bali wengi wao hawaamini.
وَلَمَّا جَاءَهُمْ رَسُولٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ نَبَذَ فَرِيقٌ مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ كِتَابَ اللَّـهِ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ كَأَنَّهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٠١﴾
101. Na alipowajia Rasuli kutoka kwa Allaah mwenye kusadikisha yale yaliyo pamoja nao, kundi miongoni mwa wale waliopewa Kitabu walikitupa Kitabu cha Allaah nyuma ya migongo yao kana kwamba hawajui.
وَاتَّبَعُوا مَا تَتْلُو الشَّيَاطِينُ عَلَىٰ مُلْكِ سُلَيْمَانَ ۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ وَمَا أُنزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَ ۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ ۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ ۚ وَمَا هُم بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ ۚ وَلَقَدْ عَلِمُوا لَمَنِ اشْتَرَاهُ مَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ۚ وَلَبِئْسَ مَا شَرَوْا بِهِ أَنفُسَهُمْ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿١٠٢﴾
102. Na wakafuata yale (ya uchawi) waliyoyatoa mashaytwaan (kuuzulia) ufalme wa Sulaymaan. Na Sulaymaan hakukufuru lakini mashaytwaan ndio waliokufuru, wanafundisha watu sihiri na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili katika (mji wa) Baabil; Haaruwt na Maaruwt.[31] Wala hao wawili hawamfundishi yeyote mpaka waseme: Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru. Kisha wakajifunza kutoka kwa hao wawili yenye kupelekea kufarikisha kwayo baina ya mtu na mkewe. Na wao hawawezi kamwe kumdhuru yeyote kwayo isipokuwa kwa Idhini ya Allaah, na wanajifunza yanayowadhuru na wala hayawanufaishi. Na kwa yakini walijua kwamba atakayechuma haya hatopata katika Aakhirah fungu lolote, na ni ubaya ulioje walichojiuzia nafsi zao, lau wangelikuwa wanajua.
وَلَوْ أَنَّهُمْ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَمَثُوبَةٌ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ خَيْرٌ ۖ لَّوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿١٠٣﴾
103. Na lau wangeliamini na wakawa na taqwa, basi malipo kutoka kwa Allaah yangekuwa ni kheri lau wangekuwa wanajua.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقُولُوا رَاعِنَا وَقُولُوا انظُرْنَا وَاسْمَعُوا ۗ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٠٤﴾
104. Enyi walioamini! Msiseme (kumwambia Nabiy) “raa’inaa”[32] lakini semeni “undhwurnaa” na sikilizeni. Na makafiri watapata adhabu iumizayo.
مَّا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلَا الْمُشْرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْكُم مِّنْ خَيْرٍ مِّن رَّبِّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿١٠٥﴾
105. Hawapendi wale waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu, wala washirikina kwamba iteremshwe kwenu kheri yoyote ile kutoka kwa Rabb wenu. Na Allaah Anamkhusisha kwa Rehma Yake Amtakaye. Na Allaah Ni Mwenye Fadhila kuu kabisa.
مَا نَنسَخْ مِنْ آيَةٍ أَوْ نُنسِهَا نَأْتِ بِخَيْرٍ مِّنْهَا أَوْ مِثْلِهَا ۗ أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٠٦﴾
106. Hatufuti Aayah yoyote au Tunayoisahaulisha ila Tunaleta iliyo bora kuliko hiyo au mfano wake.[33] Je, hujui kwamba Allaah Ni Mweza wa kila kitu?
أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿١٠٧﴾
107. Je, hujui kwamba Allaah Ana ufalme wa mbingu na ardhi. Nanyi hamna pasi na Allaah rafiki mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru.
أَمْ تُرِيدُونَ أَن تَسْأَلُوا رَسُولَكُمْ كَمَا سُئِلَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ ۗ وَمَن يَتَبَدَّلِ الْكُفْرَ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ ﴿١٠٨﴾
108. Au mnataka kumuuliza Rasuli wenu kama alivyoulizwa Muwsaa hapo kabla? Na yeyote atakayebadilisha imaan kwa kufru, basi kwa yakini amepotea njia iliyo sawa.
وَدَّ كَثِيرٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يَرُدُّونَكُم مِّن بَعْدِ إِيمَانِكُمْ كُفَّارًا حَسَدًا مِّنْ عِندِ أَنفُسِهِم مِّن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْحَقُّ ۖ فَاعْفُوا وَاصْفَحُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٠٩﴾
109. Wengi katika Watu wa Kitabu wametamani kama wangelikurudisheni baada ya kuamini kwenu mkawa makafiri kwa husuda iliyomo katika nafsi zao baada ya kuwabainikia kwao haki. Basi sameheni na puuzeni mpaka Allaah Alete Amri Yake. Hakika Allaah Ni Muweza wa kila kitu.[34]
وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿١١٠﴾
110. Na simamisheni Swalaah na toeni Zakaah, na lolote la kheri mnalolitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtalikuta kwa Allaah, hakika Allaah kwa yale myafanyayo Ni Mwenye Kuona.
وَقَالُوا لَن يَدْخُلَ الْجَنَّةَ إِلَّا مَن كَانَ هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ ۗ تِلْكَ أَمَانِيُّهُمْ ۗ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١١١﴾
111. Na walisema: Hatoingia Jannah isipokuwa aliyekuwa Yahudi au Naswaara. Hilo ni tamanio lao. Sema: Leteni ushahidi wenu wa wazi mkiwa ni wakweli.
بَلَىٰ مَنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَلَهُ أَجْرُهُ عِندَ رَبِّهِ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿١١٢﴾
112. Sivyo hivyo! Bali yeyote aliyeusalimisha uso wake kwa Allaah, na ilhali yeye ni mwenye kufanya ihsaan, basi atapata ujira wake kwa Rabb wake, na wala haitokuwa khofu juu yao wala hawatohuzunika.
وَقَالَتِ الْيَهُودُ لَيْسَتِ النَّصَارَىٰ عَلَىٰ شَيْءٍ وَقَالَتِ النَّصَارَىٰ لَيْسَتِ الْيَهُودُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَهُمْ يَتْلُونَ الْكِتَابَ ۗ كَذَٰلِكَ قَالَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ مِثْلَ قَوْلِهِمْ ۚ فَاللَّـهُ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿١١٣﴾
113. Na Mayahudi wakasema: Manaswara hawana lao jambo. Na Manaswara wakasema: Mayahudi hawana lao jambo, na hali wao wanasoma Kitabu (Tawraat na Injiyl). Hivyo hivyo ndivyo walivyosema wale wasiojua mfano wa kauli yao (hii). Basi Allaah Atawahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah katika yale waliyokuwa wakikhitilafiana.
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَاجِدَ اللَّـهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ وَسَعَىٰ فِي خَرَابِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ مَا كَانَ لَهُمْ أَن يَدْخُلُوهَا إِلَّا خَائِفِينَ ۚ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١١٤﴾
114. Na ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule anayezuia Misikiti ya Allaah kutajwa ndani yake Jina Lake na akajitahidi katika kuiharibu? Hao haitawafaa kuingia humo isipokuwa wakiwa ni wenye khofu. Watapata duniani hizaya na Aakhirah watapata adhabu kuu kabisa.
وَلِلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا فَثَمَّ وَجْهُ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿١١٥﴾
115. Na Mashariki na Magharibi ni ya Allaah. Basi popote mnapogeuka kuna Wajihi wa Allaah.[35] Hakika Allaah Ni Mwenye Wasaa, Mjuzi wa yote.[36]
وَقَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۖ بَل لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ ﴿١١٦﴾
116. Na wakasema: Allaah Amejichukulia mwana. Utakasifu Ni Wake! Bali ni Vyake vilivyomo mbinguni na ardhini, vyote vinamtii.[37]
بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَإِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿١١٧﴾
117. Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Anapohukumu jambo huliambia Kun![38] (Kuwa!) Basi nalo huwa.
وَقَالَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ لَوْلَا يُكَلِّمُنَا اللَّـهُ أَوْ تَأْتِينَا آيَةٌ ۗ كَذَٰلِكَ قَالَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّثْلَ قَوْلِهِمْ ۘ تَشَابَهَتْ قُلُوبُهُمْ ۗ قَدْ بَيَّنَّا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ ﴿١١٨﴾
118. Na wakasema wale (majahili) wasiojua kitu: Lau Angetusemesha Allaah au ingetujia Aayah (Ishara)! Kadhalika walisema wale waliokuwa kabla yao mfano wa kauli yao hiyo. Zimeshabihiana nyoyo zao. Kwa yakini Tumekwishabainisha Aayaat (Ishara, Dalili za wazi) kwa watu wenye yakini.
إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ بِالْحَقِّ بَشِيرًا وَنَذِيرًا ۖ وَلَا تُسْأَلُ عَنْ أَصْحَابِ الْجَحِيمِ ﴿١١٩﴾
119. Hakika Tumekutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki ukiwa mwenye kutoa bishara njema na mwonyaji wala hutoulizwa kuhusu watu wa moto uwakao vikali.
وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّـهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۗ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ مَا لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿١٢٠﴾
120. Na hawatoridhika nawe Mayahudi wala Manaswara mpaka ufuate mila zao. Sema: Hakika Mwongozo wa Allaah ndio Mwongozo (pekee). Na ukifuata hawaa zao baada ya yale ambayo yamekujia katika ilimu, basi hutopata kutoka kwa Allaah rafiki mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru.
الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَتْلُونَهُ حَقَّ تِلَاوَتِهِ أُولَـٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿١٢١﴾
121. Wale Tuliowapa Kitabu wanakisoma kwa haki ipasavyo ya kusomwa kwake. Hao ndio wanaokiamini, na atakayekikanusha basi hao ndio waliokhasirika.[39]
يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿١٢٢﴾
122. Enyi wana wa Israaiyl! Kumbukeni Neema Yangu Niliyokuneemesheni na hakika Mimi Nimekufadhilisheni juu ya walimwengu.
وَاتَّقُوا يَوْمًا لَّا تَجْزِي نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْئًا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا تَنفَعُهَا شَفَاعَةٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿١٢٣﴾
123. Na iogopeni Siku ambayo nafsi haitoifaa nafsi nyingine kwa lolote, wala haitokubaliwa kutoka kwake kikomboleo wala haitoifalia uombezi wowote, na wala wao hawatonusuriwa.
وَإِذِ ابْتَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ رَبُّهُ بِكَلِمَاتٍ فَأَتَمَّهُنَّ ۖ قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا ۖ قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِي ۖ قَالَ لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ ﴿١٢٤﴾
124. Na pindi Alipojaribiwa Ibraahiym na Rabb wake kwa amri nyingi, naye akazitimiza. Akasema: Hakika Mimi Nakufanya uwe Imaam[40] kwa watu. (Ibraahiym) akasema: Na katika kizazi changu? (Allaah) Akasema: Haiwafikii Ahadi Yangu madhalimu.
وَإِذْ جَعَلْنَا الْبَيْتَ مَثَابَةً لِّلنَّاسِ وَأَمْنًا وَاتَّخِذُوا مِن مَّقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى ۖ وَعَهِدْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْعَاكِفِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ ﴿١٢٥﴾
125. Na Tulipoifanya Nyumba (Al-Ka’bah) kuwa ni mahali pa kurejewa na watu na pa amani, na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym[41] kuwa ni pahala pa kuswalia. Na Tulichukua ahadi kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl kwamba: Itakaseni Nyumba Yangu kwa wanaotufu na wanaokaa i’tikaaf, na wanaorukuu na kusujudu.[42]
وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ اجْعَلْ هَـٰذَا بَلَدًا آمِنًا وَارْزُقْ أَهْلَهُ مِنَ الثَّمَرَاتِ مَنْ آمَنَ مِنْهُم بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ قَالَ وَمَن كَفَرَ فَأُمَتِّعُهُ قَلِيلًا ثُمَّ أَضْطَرُّهُ إِلَىٰ عَذَابِ النَّارِ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿١٢٦﴾
126. Na pindi aliposema Ibraahiym: Rabb wangu Ufanye mji huu (Makkah) kuwa wa amani na Waruzuku watu wake katika matunda, atakayemwamini Allaah miongoni mwao na Siku ya Mwisho. (Allaah) Akasema: Na atakayekufuru Nitamstarehesha kidogo kisha Nitamsukumiza katika adhabu ya moto, na ubaya ulioje mahali pa kuishia.
وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَاهِيمُ الْقَوَاعِدَ مِنَ الْبَيْتِ وَإِسْمَاعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا ۖ إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٢٧﴾
127. Na aliponyanyua Ibraahiym na Ismaa’iyl msingi wa Nyumba (Al-Ka’bah): Rabb wetu, Tutakabalie, hakika Wewe Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿١٢٨﴾
128. Rabb wetu, Tujaalie tuwe wenye kujisalimisha Kwako pamoja na kizazi chetu wawe ummah wenye kujisalimisha Kwako, na Tuonyeshe taratibu za ibaada zetu na Pokea tawbah zetu, hakika Wewe Ni Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.
رَبَّنَا وَابْعَثْ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُزَكِّيهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٢٩﴾
129. Rabb wetu, Wapelekee Rasuli miongoni mwao atakayewasomea Aayaat Zako na atakayewafunza Kitabu na Hikmah na atakayewatakasa. Hakika Wewe Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.[43]
وَمَن يَرْغَبُ عَن مِّلَّةِ إِبْرَاهِيمَ إِلَّا مَن سَفِهَ نَفْسَهُ ۚ وَلَقَدِ اصْطَفَيْنَاهُ فِي الدُّنْيَا ۖ وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١٣٠﴾
130. Na ni nani atakayejitenga na mila ya Ibraahiym isipokuwa anayeitia nafsi yake upumbavu? Na kwa yakini Tumemkhitari duniani, naye Aakhirah ni miongoni mwa Swalihina.[44]
إِذْ قَالَ لَهُ رَبُّهُ أَسْلِمْ ۖ قَالَ أَسْلَمْتُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٣١﴾
131. Rabb wake Alipomwambia: Jisalimishe na utii. Akasema (Ibraahiym): Nimejisalimisha na kutii kwa Rabb wa walimwengu.
وَوَصَّىٰ بِهَا إِبْرَاهِيمُ بَنِيهِ وَيَعْقُوبُ يَا بَنِيَّ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ لَكُمُ الدِّينَ فَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٣٢﴾
132. Na Ibraahiym akawausia hayo wanawe na Ya’quwb (akawausia wanawe pia): Enyi wanangu! Hakika Allaah Amekukhitarieni nyinyi Dini, basi chungeni sana, angalieni msife isipokuwa nyinyi ni Waislamu.
أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ حَضَرَ يَعْقُوبَ الْمَوْتُ إِذْ قَالَ لِبَنِيهِ مَا تَعْبُدُونَ مِن بَعْدِي قَالُوا نَعْبُدُ إِلَـٰهَكَ وَإِلَـٰهَ آبَائِكَ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٣﴾
133. Je, mlikuwa mashahidi wakati mauti yalipomfikia Ya’quwb pale alipowaambia wanawe: Mtaabudu nini baada yangu? Wakasema: Tutamwabudu Ilaaha wako (Allaah) na Ilaaha wa baba zako Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq; Ilaaha Mmoja, nasi ni Waislamu (Wenye kujisalimisha) Kwake.
تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ ۖ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُم مَّا كَسَبْتُمْ ۖ وَلَا تُسْأَلُونَ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٣٤﴾
134. Huo ni ummah uliokwishapita, utapata uliyoyachuma nanyi mtapata mliyoyachuma, na wala hamtoulizwa kuhusu waliyokuwa wakiyatenda.
وَقَالُوا كُونُوا هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ تَهْتَدُوا ۗ قُلْ بَلْ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۖ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٣٥﴾
135. Na wakasema: Kuweni Mayahudi au Manaswara mtaongoka. Sema: Bali (tunafuata) mila ya Ibraahiym aliyeelemea haki na wala hakuwa katika washirikina.[45]
قُولُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَا أُوتِيَ النَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٦﴾
136. Semeni: Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na Al-Asbaatw[46], na aliyopewa Muwsaa na ‘Iysaa na waliyopewa Manabii kutoka kwa Rabb wao, hatutofautishi baina ya mmoja yeyote miongoni mwao, nasi ni Waislamu (wenye kujisalimisha) Kwake.
فَإِنْ آمَنُوا بِمِثْلِ مَا آمَنتُم بِهِ فَقَدِ اهْتَدَوا ۖ وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا هُمْ فِي شِقَاقٍ ۖ فَسَيَكْفِيكَهُمُ اللَّـهُ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٣٧﴾
137. Watakapoamini kama vile mlivyoamini nyinyi, basi kwa yakini watakuwa wameongoka. Na wakikengeuka, basi hakika wao wamo katika upinzani, na Allaah Atakutosheleza nao, Naye Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
صِبْغَةَ اللَّـهِ ۖ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ صِبْغَةً ۖ وَنَحْنُ لَهُ عَابِدُونَ ﴿١٣٨﴾
138. (Swibghah [Dini] yetu ni) Swibghah[47] (Dini) ya Allaah. Na Swibghah (dini) gani yaweza kuwa bora zaidi kuliko Swibghah (Dini) ya Allaah? Na sisi ni wenye kumwabudu Yeye Pekee.
قُلْ أَتُحَاجُّونَنَا فِي اللَّـهِ وَهُوَ رَبُّنَا وَرَبُّكُمْ وَلَنَا أَعْمَالُنَا وَلَكُمْ أَعْمَالُكُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُخْلِصُونَ ﴿١٣٩﴾
139. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Je, mnahojiana nasi kuhusu Allaah na hali Yeye ni Rabb wetu na Rabb wenu? Nasi tuna amali zetu nanyi mna amali zenu, na sisi tunamtakasia Yeye tu ibaada?
أَمْ تَقُولُونَ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطَ كَانُوا هُودًا أَوْ نَصَارَىٰ ۗ قُلْ أَأَنتُمْ أَعْلَمُ أَمِ اللَّـهُ ۗ وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَتَمَ شَهَادَةً عِندَهُ مِنَ اللَّـهِ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿١٤٠﴾
140. Je, mnasema kwamba Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na Al-Asbaatw (kizazi chake) walikuwa Mayahudi au Manaswara? Sema: Je, nyinyi mnajua zaidi au Allaah? Na ni nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyeficha ushahidi alionao kutoka kwa Allaah? Na Allaah Si Mwenye Kughafilika na yale myatendayo.
تِلْكَ أُمَّةٌ قَدْ خَلَتْ ۖ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَلَكُم مَّا كَسَبْتُمْ ۖ وَلَا تُسْأَلُونَ عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٤١﴾
141. Huo ni ummah uliokwishapita, utapata uliyoyachuma nanyi mtapata mliyoyachuma, na wala hamtoulizwa waliyokuwa wakitenda.
سَيَقُولُ السُّفَهَاءُ مِنَ النَّاسِ مَا وَلَّاهُمْ عَن قِبْلَتِهِمُ الَّتِي كَانُوا عَلَيْهَا ۚ قُل لِّلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٤٢﴾
142. Watasema wapumbavu miongoni mwa watu: Nini kilichowageuza kutoka Qiblah chao ambacho walikuwa wakikielekea! Sema: Mashariki na Magharibi ni ya Allaah, Anamwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.[48]
وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ وَمَا جَعَلْنَا الْقِبْلَةَ الَّتِي كُنتَ عَلَيْهَا إِلَّا لِنَعْلَمَ مَن يَتَّبِعُ الرَّسُولَ مِمَّن يَنقَلِبُ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ ۚ وَإِن كَانَتْ لَكَبِيرَةً إِلَّا عَلَى الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۗ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِالنَّاسِ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤٣﴾
143. Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu.[49] Na Hatukukifanya Qiblah[50] ambacho ulikuwa ukikielekea (Baytul-Maqdis) isipokuwa Tupate kupambanua nani anayemfuata Rasuli kikweli, na nani atakayegeuka arudi nyuma. Na hakika ilikuwa ni jambo gumu isipokuwa kwa wale ambao Allaah Amewaongoza. Na Allaah Hakuwa Mwenye Kupoteza imaan yenu. Hakika Allaah Ni Mwenye Huruma mno kwa tu na Mwenye Kurehemu.[51]
قَدْ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي السَّمَاءِ ۖ فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَاهَا ۚ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِۚ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ ۗ وَإِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ ﴿١٤٤﴾
144. Kwa yakini Tunaona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unavyogeuza geuza uso wako mbinguni. Basi Sisi bila shaka Tutakuelekeza Qiblah unachokiridhia. Kwa hiyo, elekeza uso wako upande wa Masjid Al-Haraam (Ka’bah; Makkah). Na popote mtakapokuwepo (mkataka kuswali), basi elekezeni nyuso zenu upande wake. Na hakika wale waliopewa Kitabu bila shaka wanajua kwamba hivyo ni haki kutoka kwa Rabb wao. Na Allaah Si Mwenye Kughafilika na yale wayatendayo.[52]
وَلَئِنْ أَتَيْتَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ بِكُلِّ آيَةٍ مَّا تَبِعُوا قِبْلَتَكَ ۚ وَمَا أَنتَ بِتَابِعٍ قِبْلَتَهُمْ ۚ وَمَا بَعْضُهُم بِتَابِعٍ قِبْلَةَ بَعْضٍ ۚ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ إِنَّكَ إِذًا لَّمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٤٥﴾
145. Na hata ukiwaletea wale waliopewa Kitabu Aayah (Ishara, Dalili) za kila aina, hawatofuata Qiblah chako. Na wewe hutofuata Qiblah chao. Na wala baadhi yao hawatofuata Qiblah cha wengineo. Na kama ukiyafuata matamanio yao baada ya kukufikia ilimu, hakika hapo utakuwa miongoni mwa madhalimu.
الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمْ ۖ وَإِنَّ فَرِيقًا مِّنْهُمْ لَيَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٤٦﴾
146. Wale Tuliowapa Kitabu wanamtambua (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kama wanavyotambua watoto wao, na hakika kundi miongoni mwao wanaficha haki na hali wao wanajua.
الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ ﴿١٤٧﴾
147. (Ni) Haki kutoka kwa Rabb wako, basi kamwe usiwe miongoni mwa wenye kufanya shaka.
وَلِكُلٍّ وِجْهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَا ۖ فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ ۚ أَيْنَ مَا تَكُونُوا يَأْتِ بِكُمُ اللَّـهُ جَمِيعًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٤٨﴾
148. Na kila mmoja ana upande wa kuuelekea. Basi shindaneni mambo ya kheri. Popote mtakapokuwa Allaah Atakuleteni nyote pamoja (Qiyaamah). Hakika Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.
وَمِنْ حَيْثُ خَرَجْتَ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۖ وَإِنَّهُ لَلْحَقُّ مِن رَّبِّكَ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿١٤٩﴾
149. Na popote utokako (ili kuswali), basi elekeza uso wako upande wa Masjid Al-Haraam. Na hiyo ni haki kutoka kwa Rabb wako. Na Allaah Si Mwenye Kughafilika na yale myatendayo.
وَمِنْ حَيْثُ خَرَجْتَ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَيْكُمْ حُجَّةٌ إِلَّا الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِي وَلِأُتِمَّ نِعْمَتِي عَلَيْكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿١٥٠﴾
150. Na popote utokako (ili kuswali), elekeza uso wako upande wa Masjid Al-Haraam. Na popote mtakapokuwa, elekezeni nyuso zenu upande wake, ili watu wasiwe na hoja juu yenu isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Basi msiwaogope bali Niogopeni Mimi, na ili Nitimize Neema Yangu juu yenu na ili mpate kuhidika.
كَمَا أَرْسَلْنَا فِيكُمْ رَسُولًا مِّنكُمْ يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِنَا وَيُزَكِّيكُمْ وَيُعَلِّمُكُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُعَلِّمُكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ ﴿١٥١﴾
151. Kama Tulivyomtuma kwenu Rasuli anayetokana na nyinyi, anawasomea Aayaat Zetu na anakutakaseni na anakufunzeni Kitabu na Hikmah (Sunnah), na anakufundisheni mambo ambayo hamkuwa mkiyajua.
فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُوا لِي وَلَا تَكْفُرُونِ﴿١٥٢﴾
152. Basi nidhukuruni na Mimi Nitakukumbukeni, na nishukuruni wala msinikufuru.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلَاةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٣﴾
153. Enyi walioamini! Tafuteni msaada kwa subira na Swalaah, hakika Allaah Yu pamoja na wenye subira.
وَلَا تَقُولُوا لِمَن يُقْتَلُ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتٌ ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ وَلَـٰكِن لَّا تَشْعُرُونَ ﴿١٥٤﴾
154. Wala msiseme kuwa (Shuhadaa) waliouawa katika Njia ya Allaah ni wafu, bali wako hai lakini hamhisi.
وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٥﴾
155. Na bila shaka Tutakujaribuni kwa jambo katika khofu, njaa, upungufu wa mali, nafsi na mazao. Na wabashirie wenye subira.[53]
الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴿١٥٦﴾
156. Wale ambao unapowafika msiba husema: Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea.
أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ ﴿١٥٧﴾
157. Hao zitakuwa juu yao Barakah kutoka kwa Rabb wao na Rehma, na hao ndio wenye kuhidika.
إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ اللَّـهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ ﴿١٥٨﴾
158. Hakika Swafaa na Marwah ni katika Alama za Allaah. Kwa hiyo yeyote anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akatekeleza ‘Umrah, hakuna lawama kwake kutufu (vilima) viwili hivyo. Na atakayejitolea kufanya kheri, basi hakika Allaah Ni Mwenye Kupokea Shukurani, Mjuzi wa yote.[54]
إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِن بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَـٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّـهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ ﴿١٥٩﴾
159. Hakika wale wanaoficha yale Tuliyoyateremsha katika hoja bayana na mwongozo baada ya kuwa Tumeyabainisha kwa watu katika Kitabu, hao ndio Allaah Anawalaani na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani.
إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَبَيَّنُوا فَأُولَـٰئِكَ أَتُوبُ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنَا التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٠﴾
160. Isipokuwa wale waliotubu na wakatengeneza (waliyoharibu) na wakabainisha (haki), basi hao Napokea tawbah zao. Na Mimi Ni Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ لَعْنَةُ اللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿١٦١﴾
161. Hakika wale waliokufuru na wakafa hali ya kuwa ni makafiri, hao iko juu yao Laana ya Allaah na ya Malaika na ya watu wote.
خَالِدِينَ فِيهَا ۖ لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿١٦٢﴾
162. Watadumu humo (ndani ya moto), hawatopunguziwa adhabu na wala hawatopewa muhula wa kupumzika.
وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾
163. Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Mwingi wa Rehma, Mwenye Kurehemu.[55]
إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَالْفُلْكِ الَّتِي تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِمَا يَنفَعُ النَّاسَ وَمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ السَّمَاءِ مِن مَّاءٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَابَّةٍ وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ وَالسَّحَابِ الْمُسَخَّرِ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ﴿١٦٤﴾
164. Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya usiku na mchana, na merikebu zipitazo katika bahari kwa vile viwafaavyo watu, na maji ambayo Allaah Ameyateremsha toka mbinguni Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake, na Akaeneza humo kila aina ya mnyama, na mgeuko wa upepo wa rehma, na mawingu yanayotiishwa baina ya mbingu na ardhi, ni Aayaat (Dalili, Mazingatio) kwa watu wenye akili.
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ وَلَوْ يَرَى الَّذِينَ ظَلَمُوا إِذْ يَرَوْنَ الْعَذَابَ أَنَّ الْقُوَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا وَأَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعَذَابِ ﴿١٦٥﴾
165. Na miongoni mwa watu wako wenye kuwafanya viumbe miungu badala ya Allaah, wanawapenda kama kumpenda Allaah. Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. Na lau wale waliodhulumu wangelitambua watakapoona adhabu, kwamba nguvu zote ni za Allaah, na kwamba hakika Allaah ni Mkali wa Kuadhibu, (basi wasingelimfanyia Allaah washirika).
إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُوا مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا وَرَأَوُا الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ﴿١٦٦﴾
166. Waliofuatwa watakapowakana wale waliowafuata na hali ya kuwa wamekwishaiona adhabu, na yatawakatikia mafungamano yao.
وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّءُوا مِنَّا ۗ كَذَٰلِكَ يُرِيهِمُ اللَّـهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ ۖ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ ﴿١٦٧﴾
167. Na watasema wale waliofuata: Lau tungelipata fursa ya kurudi (duniani) tungewakana kama walivyotukana. Hivyo ndivyo Allaah Atakavyowaonyesha amali zao kuwa ni majuto yao. Na wala hawatokuwa wenye kutoka motoni.
يَا أَيُّهَا النَّاسُ كُلُوا مِمَّا فِي الْأَرْضِ حَلَالًا طَيِّبًا وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿١٦٨﴾
168. Enyi watu! Kuleni katika vilivyomo ardhini vya halali, vizuri na wala msifuate hatua za shaytwaan. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.
إِنَّمَا يَأْمُرُكُم بِالسُّوءِ وَالْفَحْشَاءِ وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿١٦٩﴾
169. Hakika hakuna isipokuwa anakuamrisheni maovu na machafu (na ubakhili) na mseme dhidi ya Allaah msiyoyajua.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا بَلْ نَتَّبِعُ مَا أَلْفَيْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۗ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ ﴿١٧٠﴾
170. Na wanapoambiwa: Fuateni Aliyoyateremsha Allaah husema: Bali tunafuata tuliyowakuta nayo baba zetu. Je, japokuwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu chochote na wala hawakuongoka?
وَمَثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا كَمَثَلِ الَّذِي يَنْعِقُ بِمَا لَا يَسْمَعُ إِلَّا دُعَاءً وَنِدَاءً ۚ صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿١٧١﴾
171. Na mfano wa wale waliokufuru ni kama mfano wa yule ambaye anapiga kelele kwa ambaye hasikii ila sauti na mwito. Viziwi, mabubu, vipofu kwa hiyo hawatii akilini.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّـهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ ﴿١٧٢﴾
172. Enyi walioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni[56] na mshukuruni Allaah mkiwa mnamwabudu Yeye Pekee.
إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ بِهِ لِغَيْرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٧٣﴾
173. Hakika Allaah Amekuharamishieni mzoga na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa asiyekuwa Allaah wakati wa kuchinjwa. Lakini aliyefikwa na dharura (akala) bila ya kutamani wala kupindukia mipaka, basi si dhambi juu yake. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.
إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ الْكِتَابِ وَيَشْتَرُونَ بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۙ أُولَـٰئِكَ مَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ إِلَّا النَّارَ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّـهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٧٤﴾
174. Hakika wale wanaoficha yale Aliyoyateremsha Allaah katika Kitabu na wakakibadilisha kwa thamani ndogo, hao hawali katika matumbo yao isipokuwa moto, na wala Allaah Hatowasemesha Siku ya Qiyaamah na wala Hatowatakasa, nao watapata adhabu iumizayo.
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الضَّلَالَةَ بِالْهُدَىٰ وَالْعَذَابَ بِالْمَغْفِرَةِ ۚ فَمَا أَصْبَرَهُمْ عَلَى النَّارِ ﴿١٧٥﴾
175. Hao ndio wale waliobadilisha upotofu badala ya hidaaya, na adhabu kwa maghfirah. Basi kuvumilia gani huko kwao ndani ya moto?
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ نَزَّلَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ ۗ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِي الْكِتَابِ لَفِي شِقَاقٍ بَعِيدٍ ﴿١٧٦﴾
176. Hayo ni kwa sababu Allaah Amekiteremsha Kitabu kwa haki. Na hakika wale waliokhitilafiana katika Kitabu wamo katika upinzani wa mbali.
لَّيْسَ الْبِرَّ أَن تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ وَآتَى الْمَالَ عَلَىٰ حُبِّهِ ذَوِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَالسَّائِلِينَ وَفِي الرِّقَابِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَالْمُوفُونَ بِعَهْدِهِمْ إِذَا عَاهَدُوا ۖ وَالصَّابِرِينَ فِي الْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ وَحِينَ الْبَأْسِ ۗ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ صَدَقُوا ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ ﴿١٧٧﴾
177. Sio wema[57] kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na Magharibi, lakini wema ni mwenye kuamini Allaah na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na akawapa mali juu ya kuipenda kwake jamaa wa karibu na mayatima na masikini na msafiri na waombao na katika kukomboa watumwa, na akasimamisha Swalaah na akatoa Zakaah, na watimizao ahadi zao wanapoahidi, na wenye subira katika dhiki za ufukara na maafa ya magonjwa na njaa na katika vita. Hao ndio waliosadikisha na hao ndio wenye taqwa.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِصَاصُ فِي الْقَتْلَى ۖ الْحُرُّ بِالْحُرِّ وَالْعَبْدُ بِالْعَبْدِ وَالْأُنثَىٰ بِالْأُنثَىٰ ۚ فَمَنْ عُفِيَ لَهُ مِنْ أَخِيهِ شَيْءٌ فَاتِّبَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ وَأَدَاءٌ إِلَيْهِ بِإِحْسَانٍ ۗ ذَٰلِكَ تَخْفِيفٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَرَحْمَةٌ ۗ فَمَنِ اعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٧٨﴾
178. Enyi walioamini! Mmeandikiwa sharia ya kisasi kwa waliouawa. Muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke, na anayesamehewa na nduguye kwa lolote basi kufuatilizwa kwake kuwe kwa wema na kumlipa kwake iwe kwa ihsaan. Hiyo ni takhafifu kutoka kwa Rabb wenu na Rehma. Na atakayevuka mipaka baada ya hapo basi atapata adhabu iumizayo.
وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٧٩﴾
179. Na mtapata katika kisasi (kuokoa) uhai enyi wenye akili ili mpate kuwa na taqwa.
كُتِبَ عَلَيْكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ إِن تَرَكَ خَيْرًا الْوَصِيَّةُ لِلْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُتَّقِينَ ﴿١٨٠﴾
180. Mmeandikiwa sharia kuwa anapofikiwa mmoja wenu na mauti kama ameacha mali, kufanya wasia kwa wazazi wawili, na jamaa wa karibu kwa namna inayoeleweka katika sharia. (Haya) ni wajibu kwa wenye taqwa.
فَمَن بَدَّلَهُ بَعْدَ مَا سَمِعَهُ فَإِنَّمَا إِثْمُهُ عَلَى الَّذِينَ يُبَدِّلُونَهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿١٨١﴾
181. Atakayeubadilisha (wasia) baada ya kuusikia, basi hakika dhambi yake ni juu ya wale watakaoubadilisha. Hakika Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
فَمَنْ خَافَ مِن مُّوصٍ جَنَفًا أَوْ إِثْمًا فَأَصْلَحَ بَيْنَهُمْ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٨٢﴾
182. Na mwenye kumkhofia muusiaji kwamba kaenda kombo bila kukusudia, au kakusudia dhambi kisha akasuluhisha baina yao, basi hana dhambi juu yake. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٨٣﴾
183. Enyi walioamini! Mmefaridhishwa Swiyaam kama ilivyofaridhishwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na taqwa.
أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۚ وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ ۖ فَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ ۚ وَأَن تَصُومُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١٨٤﴾
184. (Swiyaam ni) siku za kuhesabika. Lakini atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safarini, basi (inapaswa kulipa) idadi sawa katika masiku mengineyo. Na kwa wale wanaoiweza lakini kwa mashaka na kutaabika watoe fidia kulisha masikini. Na atakayefanya wema kwa hiari yake, basi hivyo ni bora kwake. Na mkifunga (Swiyaam) ni bora kwenu mkiwa mnajua.
شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٨٥﴾
185. Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo[58] (la haki na baatwil). Kwa hiyo atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi na afunge. Na atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi (inampasa kulipa) idadi sawa katika masiku mengineyo. Allaah Anakutakieni mepesi na wala Hakutakieni magumu ili mkamilishe idadi na ili mumtukuze Allaah kwa kuwa Amekuongozeni, na ili mpate kushukuru.
وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ ﴿١٨٦﴾
186. Na watakapokuuliza Waja Wangu kuhusu Mimi, basi (waambie) hakika Mimi Niko Karibu (kwa ujuzi). Naitikia duaa ya muombaji anaponiomba. Hivyo basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka.[59]
أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ ۗ عَلِمَ اللَّـهُ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَخْتَانُونَ أَنفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنكُمْ ۖ فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ ۚ وَلَا تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ فَلَا تَقْرَبُوهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿١٨٧﴾
187. Mmehalalishiwa usiku wa Swiyaam kujamiiana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao. Allaah Anajua kwamba nyinyi mlikuwa mkijifanyia khiyana nafsi zenu, hivyo Akapokea tawbah yenu na Akakusameheni. Basi sasa waingilieni na tafuteni Aliyokuandikieni Allaah kwenu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku). Kisha timizeni Swiyaam mpaka usiku. Na wala msiwaingilie hali ya kuwa nyinyi mko katika i’tikaaf misikitini. Hiyo ni Mipaka ya Allaah basi msiikaribie. Hivyo ndivyo Allaah Anavyobainisha Aayaat (na Hukmu) Zake kwa watu wapate kuwa na taqwa.[60]
وَلَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُم بَيْنَكُم بِالْبَاطِلِ وَتُدْلُوا بِهَا إِلَى الْحُكَّامِ لِتَأْكُلُوا فَرِيقًا مِّنْ أَمْوَالِ النَّاسِ بِالْإِثْمِ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١٨٨﴾
188. Na wala msiliane mali zenu kwa ubatwilifu na mkazipeleka (rushwa) kwa mahakimu ili mle sehemu katika mali ya watu kwa dhambi na hali mnajua.
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَهِلَّةِ ۖ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ ۗ وَلَيْسَ الْبِرُّ بِأَن تَأْتُوا الْبُيُوتَ مِن ظُهُورِهَا وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَأْتُوا الْبُيُوتَ مِنْ أَبْوَابِهَا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٨٩﴾
189. Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu miandamo ya mwezi. Sema: Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa watu na Hajj. Na si wema kuingia nyumba kwa nyuma yake, lakini wema ni kuwa na taqwa. Na ingieni majumbani kupitia milango yake. Na mcheni Allaah mpate kufaulu.[61]
وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿١٩٠﴾
190. Na piganeni katika Njia ya Allaah na wale wanaokupigeni, wala msitaadi. Hakika Allaah Hapendi wenye kutaadi.
وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ ۚ وَالْفِتْنَةُ أَشَدُّ مِنَ الْقَتْلِ ۚ وَلَا تُقَاتِلُوهُمْ عِندَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ حَتَّىٰ يُقَاتِلُوكُمْ فِيهِ ۖ فَإِن قَاتَلُوكُمْ فَاقْتُلُوهُمْ ۗ كَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْكَافِرِينَ ﴿١٩١﴾
191. Na wauweni popote muwakutapo, na watoeni popote walipokutoeni. Na fitnah ni mbaya zaidi kuliko kuua. Na wala msipigane nao kwenye Masjid Al-Haraam mpaka wakupigeni humo, watakapokupigeni basi wauweni. Namna hivi ndivyo jazaa ya makafiri.
فَإِنِ انتَهَوْا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٩٢﴾
192. Wakikoma, basi Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.
وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلَّـهِ ۖ فَإِنِ انتَهَوْا فَلَا عُدْوَانَ إِلَّا عَلَى الظَّالِمِينَ ﴿١٩٣﴾
193. Na piganeni nao mpaka kusiweko fitnah (shirki, kufru) na Dini iwe kwa ajili ya Allaah Pekee, wakikoma basi kusiweko na uadui ila kwa madhalimu.
الشَّهْرُ الْحَرَامُ بِالشَّهْرِ الْحَرَامِ وَالْحُرُمَاتُ قِصَاصٌ ۚ فَمَنِ اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ فَاعْتَدُوا عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ ﴿١٩٤﴾
194. Mwezi mtukufu kwa mwezi mtukufu na vitukufu vimewekewa kisasi. Basi anayekushambulieni nanyi mshambulieni kwa kadiri ya alivyokushambulieni. Na mcheni Allaah, na jueni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa.
وَأَنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ ۛ وَأَحْسِنُوا ۛ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٩٥﴾
195. Na toeni katika Njia ya Allaah wala msijitupe katika maangamizi kwa (kuzuia) mikono yenu (isitoe). Na fanyeni ihsaan, hakika Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.[62]
وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّـهِ ۚ فَإِنْ أُحْصِرْتُمْ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ ۖ وَلَا تَحْلِقُوا رُءُوسَكُمْ حَتَّىٰ يَبْلُغَ الْهَدْيُ مَحِلَّهُ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ بِهِ أَذًى مِّن رَّأْسِهِ فَفِدْيَةٌ مِّن صِيَامٍ أَوْ صَدَقَةٍ أَوْ نُسُكٍ ۚ فَإِذَا أَمِنتُمْ فَمَن تَمَتَّعَ بِالْعُمْرَةِ إِلَى الْحَجِّ فَمَا اسْتَيْسَرَ مِنَ الْهَدْيِ ۚ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ فِي الْحَجِّ وَسَبْعَةٍ إِذَا رَجَعْتُمْ ۗ تِلْكَ عَشَرَةٌ كَامِلَةٌ ۗ ذَٰلِكَ لِمَن لَّمْ يَكُنْ أَهْلُهُ حَاضِرِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿١٩٦﴾
196. Na timizeni Hajj na ‘Umrah kwa ajili ya Allaah. Na kama mkizuilika basi chinjeni wanyama walio wepesi kupatikana. Na wala msinyoe vichwa vyenu mpaka mnyama afikie machinjoni pake. Na atakayekuwa miongoni mwenu mgonjwa au ana vya kumuudhi kichwani mwake (ikambidi anyoe), basi atoe fidia kwa kufunga (Swiyaam) au kutoa swadaqa au kuchinja mnyama. Na mtakapopata amani, basi mwenye kufanya Tamattu’u[63] kwa kutekeleza ‘Umrah kwanza kisha Hajj, achinje mnyama aliye mwepesi. Na asiyepata afunge Swiyaam siku tatu katika Hajj na saba mtakaporejea. Hizo ni kumi kamili. Hayo ni kwa ajili ya yule ambaye watu wake hawaishi karibu na Masjid Al-Haraam. Na mcheni Allaah, na jueni kwamba Allaah Ni Mkali wa Kuakibu.[64]
الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ ۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ ۚ وَاتَّقُونِ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٧﴾
197. Hajj ni miezi maalumu.[65] Na atakayekusudia kuhiji ndani ya miezi hiyo (akahirimia), basi asifanye tendo la ndoa wala ufasiki wala mabishano katika Hajj. Na lolote la kheri mlifanyalo Allaah Analijua. Na chukueni masurufu. Na hakika bora ya masurufu ni taqwa. Na nicheni Mimi enyi wenye akili![66]
لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَبْتَغُوا فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ ۚ فَإِذَا أَفَضْتُم مِّنْ عَرَفَاتٍ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ عِندَ الْمَشْعَرِ الْحَرَامِ ۖ وَاذْكُرُوهُ كَمَا هَدَاكُمْ وَإِن كُنتُم مِّن قَبْلِهِ لَمِنَ الضَّالِّينَ ﴿١٩٨﴾
198. Hapana dhambi kwenu kutafuta fadhila toka kwa Rabb wenu. Basi mtakapomiminika kutoka ‘Arafaat mdhukuruni Allaah kwenye Mash’aril-Haraam (Muzdalifah) na mdhukuruni Yeye kama Alivyokuongozeni, kwani hakika mlikuwa kabla ya hapo ni miongoni mwa waliopotea.[67]
ثُمَّ أَفِيضُوا مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ النَّاسُ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٩٩﴾
199. Kisha miminikeni kutoka pale wamiminikapo watu na ombeni maghfirah kwa Allaah. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.[68]
فَإِذَا قَضَيْتُم مَّنَاسِكَكُمْ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَذِكْرِكُمْ آبَاءَكُمْ أَوْ أَشَدَّ ذِكْرًا ۗ فَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِنْ خَلَاقٍ ﴿٢٠٠﴾
200. Mtakapomaliza kutekeleza ibaada zenu za Hajj, basi mdhukuruni Allaah kama mnavyowadhukuru baba zenu bali mdhukuruni (Yeye) zaidi. Kwani kuna baadhi ya watu wasemao: Rabb wetu Tupe katika dunia (mazuri yake lakini wanasahau Aakhirah), naye katika Aakhirah hana sehemu yoyote.
وَمِنْهُم مَّن يَقُولُ رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴿٢٠١﴾
201. Na miongoni mwao kuna wasemao: Rabb wetu Tupe katika dunia mazuri na katika Aakhirah mazuri na Tukinge na adhabu ya moto.[69]
أُولَـٰئِكَ لَهُمْ نَصِيبٌ مِّمَّا كَسَبُوا ۚ وَاللَّـهُ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿٢٠٢﴾
202. Hao watapata pato lao kutokana na waliyoyachuma, na Allaah Ni Mwepesi wa Kuhesabu.
وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن تَعَجَّلَ فِي يَوْمَيْنِ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ لِمَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٢٠٣﴾
203. Na mdhukuruni Allaah katika siku za kuhesabika.[70] Atakayeharakisha kuondoka katika siku mbili basi hakuna dhambi juu yake, na atakayeakhirisha, basi hakuna dhambi juu yake, kwa mwenye taqwa. Na mcheni Allaah, na jueni kwamba Kwake mtakusanywa.
وَمِنَ النَّاسِ مَن يُعْجِبُكَ قَوْلُهُ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيُشْهِدُ اللَّـهَ عَلَىٰ مَا فِي قَلْبِهِ وَهُوَ أَلَدُّ الْخِصَامِ ﴿٢٠٤﴾
204. Na miongoni mwa watu yupo anayekuvutia kauli yake katika uhai wa dunia na humshuhudisha Allaah kwa yale yaliyomo katika moyo wake na hali yeye ndiye mpinzani muovu zaidi.
وَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِي الْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ ﴿٢٠٥﴾
205. Na anapoondoka hufanya bidii katika ardhi ili afisidi humo na aangamize mimea na vizazi. Na Allaah Hapendi ufisadi.
وَإِذَا قِيلَ لَهُ اتَّقِ اللَّـهَ أَخَذَتْهُ الْعِزَّةُ بِالْإِثْمِ ۚ فَحَسْبُهُ جَهَنَّمُ ۚ وَلَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿٢٠٦﴾
206. Na anapoambiwa: Mche Allaah! Hupandwa kiburi kinachompeleka kutenda madhambi. Basi Jahannam inamtosheleza, na mahali pabaya palioje pa kupumzikia.
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْرِي نَفْسَهُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ ﴿٢٠٧﴾
207. Na miongoni mwa watu yupo anayeiuza nafsi yake kutafuta Radhi za Allaah. Na Allaah Ni Mwenye Huruma mno kwa waja.[71]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿٢٠٨﴾
208. Enyi walioamini! Ingieni katika Uislamu kikamilifu, na wala msifuate hatua za shaytwaan. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.
فَإِن زَلَلْتُم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَتْكُمُ الْبَيِّنَاتُ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٠٩﴾
209. Lakini mkiteleza baada ya kukujieni hoja bayana, basi jueni kwamba hakika Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿٢١٠﴾
210. Je, wanangojea nini isipokuwa Allaah Awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika (Siku ya Qiyaamah),[72] na jambo lihukumiwe. Na kwa Allaah ndipo hurudishwa mambo.
سَلْ بَنِي إِسْرَائِيلَ كَمْ آتَيْنَاهُم مِّنْ آيَةٍ بَيِّنَةٍ ۗ وَمَن يُبَدِّلْ نِعْمَةَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُ فَإِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٢١١﴾
211. Waulize wana wa Israaiyl, ni Aayah (Ishara, Dalili) ngapi Tumewapa zilizo bayana? Na atakayebadilisha Neema ya Allaah (kwa kufru) baada ya kumjia, basi hakika Allaah Ni Mkali wa Kuakibu.[73]
زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَيَسْخَرُونَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا ۘ وَالَّذِينَ اتَّقَوْا فَوْقَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ وَاللَّـهُ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٢١٢﴾
212. Wamepambiwa wale waliokufuru uhai wa dunia na wanawakejeli wale walioamini. Na wale walio na taqwa watakuwa juu yao Siku ya Qiyaamah. Na Allaah Humruzuku Amtakaye bila ya hesabu.
كَانَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً فَبَعَثَ اللَّـهُ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ فِيمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ ۚ وَمَا اخْتَلَفَ فِيهِ إِلَّا الَّذِينَ أُوتُوهُ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۖ فَهَدَى اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا لِمَا اخْتَلَفُوا فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِهِ ۗ وَاللَّـهُ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٢١٣﴾
213. Watu walikuwa ummah mmoja, kisha Allaah Akatuma Manabii wabashiriaji na waonyaji, na Akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki ili kihukumu baina ya watu katika ambayo wamekhitilafiana kwayo. Na hawakukhitilafiana katika hayo isipokuwa wale waliopewa hicho (Kitabu) baada ya kuwajia hoja bayana kwa kufanyiana baghi[74] (chuki na husuda) baina yao. Allaah Akawaongoza wale walioamini kuendea haki katika yale waliyokhitilafiana, kwa Idhini Yake. Na Allaah Humwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.
أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُم مَّثَلُ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِكُم ۖ مَّسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُوا حَتَّىٰ يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ مَتَىٰ نَصْرُ اللَّـهِ ۗ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّـهِ قَرِيبٌ ﴿٢١٤﴾
214. Je, mnadhani kwamba mtaingia Jannah na hali bado haijakufikieni (mitihani) kama ya wale waliopita kabla yenu? Ziliwagusa dhiki za umasikini na maafa ya magonjwa na njaa, na wakatetemeshwa mpaka Rasuli na wale walioamini pamoja naye wakasema: Lini itafika Nusura ya Allaah? Tanabahi! Hakika Nusura ya Allaah iko karibu.
يَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ ۖ قُلْ مَا أَنفَقْتُم مِّنْ خَيْرٍ فَلِلْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٢١٥﴾
215. Wanakuuliza nini watoe? Sema: Mnachotoa chochote katika kheri basi ni kwa ajili ya wazazi wawili, jamaa wa karibu, mayatima, masikini, na msafiri. Na lolote mlifanyalo katika kheri basi hakika Allaah kwa hilo Ni Mjuzi.
كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢١٦﴾
216. Mmeandikiwa sharia kupigana vita nako kunachukiza mno kwenu. Lakini asaa mkachukia jambo na hali lenyewe ni la kheri kwenu. Na asaa mkapenda jambo na hali lenyewe ni la shari kwenu. Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui.
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الشَّهْرِ الْحَرَامِ قِتَالٍ فِيهِ ۖ قُلْ قِتَالٌ فِيهِ كَبِيرٌ ۖ وَصَدٌّ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَكُفْرٌ بِهِ وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَإِخْرَاجُ أَهْلِهِ مِنْهُ أَكْبَرُ عِندَ اللَّـهِ ۚ وَالْفِتْنَةُ أَكْبَرُ مِنَ الْقَتْلِ ۗ وَلَا يَزَالُونَ يُقَاتِلُونَكُمْ حَتَّىٰ يَرُدُّوكُمْ عَن دِينِكُمْ إِنِ اسْتَطَاعُوا ۚ وَمَن يَرْتَدِدْ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢١٧﴾
217. Wanakuuliza kuhusu mwezi mtukufu na (swala la) kupigana humo. Sema: Kupigana humo ni dhambi kubwa, lakini kuzuia Njia ya Allaah na kumkufuru Yeye na (kuzuia) Masjid Al-Haraam na kuwatoa watu wake humo, ni (dhambi) kubwa zaidi mbele ya Allaah. Na fitnah ni mbaya zaidi kuliko kuua. Na wala hawatoacha kukupigeni vita mpaka wakutoeni katika Dini yenu wakiweza. Na atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, akafariki hali ya kuwa ni kafiri, basi hao zimeporomoka amali zao katika dunia na Aakhirah. Na hao ni watu wa motoni, wao humo watadumu.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ يَرْجُونَ رَحْمَتَ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢١٨﴾
218. Hakika wale walioamini na wale waliohajiri na wakapigana Jihaad katika Njia ya Allaah, hao wanataraji Rehma ya Allaah, na Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١٩﴾
219. Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na (baadhi ya) manufaa kwa watu. Na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake. Na wanakuuliza nini watoe. Sema: Yaliyokuzidieni. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na Sharia) ili mpate kutafakari.[75]
فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۗ وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْيَتَامَىٰ ۖ قُلْ إِصْلَاحٌ لَّهُمْ خَيْرٌ ۖ وَإِن تُخَالِطُوهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ الْمُفْسِدَ مِنَ الْمُصْلِحِ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَأَعْنَتَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٢٠﴾
220. Katika dunia na Aakhirah. Na wanakuuliza kuhusu mayatima. Sema: Kuwatengenezea (ya kuwafaa) ni kheri zaidi. Na mkichanganya mambo yenu na yao basi hao ni ndugu zenu. Na Allaah Anamjua fisadi na mtengenezaji. Na lau Angetaka Allaah Angelikutieni katika shida. Hakika Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.[76]
وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ ۖ وَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٢١﴾
221. Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Na wala msiwaozeshe (wanawake wa Kiislamu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Hao wanaitia katika moto na Allaah Anaitia katika Jannah (Pepo) na maghfirah kwa Idhini Yake. Na Anabainisha Aayaat (na Sharia) Zake ili wapate kukumbuka.
وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ ﴿٢٢٢﴾
222. Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: Hiyo ni dhara, hivyo basi waepukeni wanawake katika hedhi. Wala msiwakaribie kujimai nao mpaka watwaharike. Watakapotwaharika basi waendeeni kupitia pale Alipokuamrisheni Allaah. Hakika Allaah Anapenda wenye kutubia na Anapenda wenye kujitwaharisha.[77]
نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُم مُّلَاقُوهُ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢٢٣﴾
223. Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi)[78] vyovyote mpendavyo. Na kadimisheni (mema) kwa ajili ya nafsi zenu. Na mcheni Allaah na jueni kwamba hakika nyinyi mtakutana Naye. Na wabashirie Waumini.[79]
وَلَا تَجْعَلُوا اللَّـهَ عُرْضَةً لِّأَيْمَانِكُمْ أَن تَبَرُّوا وَتَتَّقُوا وَتُصْلِحُوا بَيْنَ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٢٤﴾
224. Na wala msifanye (Jina la) Allaah kuwa ni nyudhuru ya viapo vyenu[80] kukuzuieni katika kutenda wema na kuwa na taqwa na kusuluhisha baina ya watu. Na Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا كَسَبَتْ قُلُوبُكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿٢٢٥﴾
225. Allaah Hatokushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi[81] lakini Atakuchukulieni kwa yaliyochuma nyoyo zenu. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mvumilivu.[82]
لِّلَّذِينَ يُؤْلُونَ مِن نِّسَائِهِمْ تَرَبُّصُ أَرْبَعَةِ أَشْهُرٍ ۖ فَإِن فَاءُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٢٦﴾
226. Kwa wale walioapa kujitenga na wake zao (kutokujamiiana) wangojee miezi minne. Wakirejea, basi hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.
وَإِنْ عَزَمُوا الطَّلَاقَ فَإِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿٢٢٧﴾
227. Na wakiazimia talaka, basi hakika Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلَاثَةَ قُرُوءٍ ۚ وَلَا يَحِلُّ لَهُنَّ أَن يَكْتُمْنَ مَا خَلَقَ اللَّـهُ فِي أَرْحَامِهِنَّ إِن كُنَّ يُؤْمِنَّ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَبُعُولَتُهُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ فِي ذَٰلِكَ إِنْ أَرَادُوا إِصْلَاحًا ۚ وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٢٨﴾
228. Na wanawake waliotalikiwa wabakie kungojea zipite hedhi (na twahara) tatu. Na wala si halali kwao kuficha Aliyoumba Allaah katika matumbo yao ikiwa wao ni wenye kumwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Na waume zao wana haki kuwarejea katika muda huo ikiwa watataka suluhu. Nao wake wana haki kama ambayo (ya waume zao) iliyo juu yao kwa mujibu wa sharia. Na wanaume wana daraja zaidi juu yao. Na Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
الطَّلَاقُ مَرَّتَانِ ۖ فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ ۗ وَلَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَأْخُذُوا مِمَّا آتَيْتُمُوهُنَّ شَيْئًا إِلَّا أَن يَخَافَا أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا فِيمَا افْتَدَتْ بِهِ ۗ تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ فَلَا تَعْتَدُوهَا ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٢٢٩﴾
229. Talaka ni mara mbili. Hivyo kuzuia kwa mujibu wa sharia au kuachia kwa ihsaan. Wala si halali kwenu kuchukua chochote katika mlivyowapa wanawake, isipokuwa wote wawili wakikhofu kuwa hawatoweza kusimamisha Mipaka ya Allaah. Mtakapokhofu kuwa wote wawili hawatoweza kusimamisha mipaka Mipaka ya Allaah, basi hakuna lawama juu yao katika ambacho (mke) amejikombolea kwacho (khul’u)[83]. Hiyo ni Mipaka ya Allaah basi msitaadi. Na atakayetaadi Mipaka ya Allaah basi hao ndio madhalimu.
فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا تَحِلُّ لَهُ مِن بَعْدُ حَتَّىٰ تَنكِحَ زَوْجًا غَيْرَهُ ۗ فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يَتَرَاجَعَا إِن ظَنَّا أَن يُقِيمَا حُدُودَ اللَّـهِ ۗ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ يُبَيِّنُهَا لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٢٣٠﴾
230. Na akimtaliki (mara ya tatu), basi hatokuwa halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwengine.[84] Akimtaliki (au akifariki) hapatokuwa dhambi juu yao wawili kurejeana wakidhani kwamba watasimamisha Mipaka ya Allaah. Na hiyo ni Mipaka ya Allaah Anaibainisha kwa watu wanaojua.
وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ سَرِّحُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ ۚ وَلَا تُمْسِكُوهُنَّ ضِرَارًا لِّتَعْتَدُوا ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ ۚ وَلَا تَتَّخِذُوا آيَاتِ اللَّـهِ هُزُوًا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَمَا أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّنَ الْكِتَابِ وَالْحِكْمَةِ يَعِظُكُم بِهِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٣١﴾
231. Na mtakapowataliki wanawake wakafikia muda wa kumaliza eda yao, basi wazuieni kwa wema au waachilieni kwa wema. Na wala msiwazuie kuwakusudia dhara mkafanya uonevu. Na atakayefanya hivyo basi kwa yakini amejidhulumu nafsi yake. Na wala msizifanyie mzaha Aayaat (na Sharia) za Allaah. Na kumbukeni Neema za Allaah juu yenu na Aliyokuteremshieni katika Kitabu na Hikmah (Sunnah) Anakuwaidhini kwacho. Na mcheni Allaah na jueni kwamba Allaah Ni Mjuzi wa kila kitu.
وَإِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا تَعْضُلُوهُنَّ أَن يَنكِحْنَ أَزْوَاجَهُنَّ إِذَا تَرَاضَوْا بَيْنَهُم بِالْمَعْرُوفِ ۗ ذَٰلِكَ يُوعَظُ بِهِ مَن كَانَ مِنكُمْ يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۗ ذَٰلِكُمْ أَزْكَىٰ لَكُمْ وَأَطْهَرُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢٣٢﴾
232. Na mtakapowataliki wanawake wakafikia muda wa kumaliza eda yao, msiwazuie kuolewa na waume zao (wa awali) ikiwa wameridhiana baina yao kwa mujibu wa ada. Hayo anawaidhiwa kwayo, yeyote miongoni mwenu, mwenye kumwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo kwenu ni wema zaidi na safi kabisa. Na Allaah Anajua nanyi hamjui.[85]
وَالْوَالِدَاتُ يُرْضِعْنَ أَوْلَادَهُنَّ حَوْلَيْنِ كَامِلَيْنِ ۖ لِمَنْ أَرَادَ أَن يُتِمَّ الرَّضَاعَةَ ۚ وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ لَا تُكَلَّفُ نَفْسٌ إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَا تُضَارَّ وَالِدَةٌ بِوَلَدِهَا وَلَا مَوْلُودٌ لَّهُ بِوَلَدِهِ ۚ وَعَلَى الْوَارِثِ مِثْلُ ذَٰلِكَ ۗ فَإِنْ أَرَادَا فِصَالًا عَن تَرَاضٍ مِّنْهُمَا وَتَشَاوُرٍ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا ۗ وَإِنْ أَرَدتُّمْ أَن تَسْتَرْضِعُوا أَوْلَادَكُمْ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِذَا سَلَّمْتُم مَّا آتَيْتُم بِالْمَعْرُوفِ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٣٣﴾
233. Na wazazi wa kike wanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili, kwa mwenye kutaka kutimiza kunyonyesha. Na ni juu ya mzazi wa kiume kuwapatia chakula chao na nguo kwa mujibu wa ada. Hailazimishwi nafsi ila kwa iliwezalo. Asidhuriwe mzazi wa kike kwa ajili ya mwanawe, na wala mzazi wa kiume kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi (wa baba) mfano wa hivyo. Watakapotaka kumwachisha kunyonya kwa maridhiano baina yao wawili na mashauriano, basi hapana dhambi juu ya wawili hao. Na mtakapotaka kutafuta wa kuwayonyesha watoto wenu, basi si dhambi kwenu ikiwa mtalipa mlichoahidi kwa mujibu wa sharia. Na mcheni Allaah na jueni kwamba hakika Allaah Ni Mwenye Kuona yale myatendayo.
وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا ۖ فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا فَعَلْنَ فِي أَنفُسِهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٣٤﴾
234. Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, hao wake wajisubirishe wenyewe (kwa kukaa eda) miezi minne na siku kumi.[86] Watakapofikia muda wao, si dhambi kwenu katika yale waliyoyafanya katika nafsi zao kwa ada ya kisharia. Na Allaah kwa yale myatendayo, Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا عَرَّضْتُم بِهِ مِنْ خِطْبَةِ النِّسَاءِ أَوْ أَكْنَنتُمْ فِي أَنفُسِكُمْ ۚ عَلِمَ اللَّـهُ أَنَّكُمْ سَتَذْكُرُونَهُنَّ وَلَـٰكِن لَّا تُوَاعِدُوهُنَّ سِرًّا إِلَّا أَن تَقُولُوا قَوْلًا مَّعْرُوفًا ۚ وَلَا تَعْزِمُوا عُقْدَةَ النِّكَاحِ حَتَّىٰ يَبْلُغَ الْكِتَابُ أَجَلَهُ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي أَنفُسِكُمْ فَاحْذَرُوهُ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿٢٣٥﴾
235. Wala si dhambi juu yenu katika ambayo mmedokezea ya kuposa wanawake hao au mliyoficha katika nafsi zenu. Allaah Anajua kwamba nyinyi mtawakumbuka lakini msifunge nao ahadi kisiri isipokuwa mseme kauli inayoeleweka kawaida. Na wala msiazimie kufunga ndoa mpaka muda ulioandikwa kisharia (katika eda) ufike mwisho wake. Na jueni kwamba Allaah Anajua yaliyomo katika nafsi zenu basi jihadharini Naye. Na jueni kwamba hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mvumilivu.
لَّا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ مَا لَمْ تَمَسُّوهُنَّ أَوْ تَفْرِضُوا لَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَمَتِّعُوهُنَّ عَلَى الْمُوسِعِ قَدَرُهُ وَعَلَى الْمُقْتِرِ قَدَرُهُ مَتَاعًا بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُحْسِنِينَ ﴿٢٣٦﴾
236. Hakuna dhambi kwenu mkiwataliki wanawake ambao hamkuwagusa au kuwabainishia mahari yao. Wapeni kiliwazo kwa mwenye wasaa kadiri ya uwezo wake, na mwenye dhiki kadiri ya uwezo wake. Maliwaza kwa mujibu wa ada, ni haki kwa wafanya ihsaan.
وَإِن طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ وَقَدْ فَرَضْتُمْ لَهُنَّ فَرِيضَةً فَنِصْفُ مَا فَرَضْتُمْ إِلَّا أَن يَعْفُونَ أَوْ يَعْفُوَ الَّذِي بِيَدِهِ عُقْدَةُ النِّكَاحِ ۚ وَأَن تَعْفُوا أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۚ وَلَا تَنسَوُا الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٣٧﴾
237. Na mkiwataliki kabla ya kuwagusa na mkawa mmeshawabainishia mahari yao, basi (wapeni) nusu ya hayo mliyobainisha, isipokuwa wakisamehe au asamehe yule ambaye fungamano la ndoa liko mikononi mwake. Na kusamehe kuko karibu zaidi na taqwa. Na wala msisahau fadhila baina yenu. Hakika Allaah Ni Mwenye Kuona myatendayo.
حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ﴿٢٣٨﴾
238. Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati (Alasiri), na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu.[87]
فَإِنْ خِفْتُمْ فَرِجَالًا أَوْ رُكْبَانًا ۖ فَإِذَا أَمِنتُمْ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَمَا عَلَّمَكُم مَّا لَمْ تَكُونُوا تَعْلَمُونَ ﴿٢٣٩﴾
239. Mkikhofu, basi (swalini) huku mnatembea au mmepanda kipando. Mtakapokuwa katika amani, mdhukuruni Allaah kama Alivyokufunzeni yale mliyokuwa hamuyajui.
وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا وَصِيَّةً لِّأَزْوَاجِهِم مَّتَاعًا إِلَى الْحَوْلِ غَيْرَ إِخْرَاجٍ ۚ فَإِنْ خَرَجْنَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِي مَا فَعَلْنَ فِي أَنفُسِهِنَّ مِن مَّعْرُوفٍ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٤٠﴾
240. Na wale waliofishwa miongoni mwenu wakaacha wake, wausie kwa ajili ya wake zao masurufu kwa mwaka mmoja bila ya kuwatoa. Watakapotoka wenyewe basi hakuna dhambi juu yenu katika yale waliyojifanyia wenyewe katika yanayokubalika na sharia.[88] Na Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
وَلِلْمُطَلَّقَاتِ مَتَاعٌ بِالْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى الْمُتَّقِينَ ﴿٢٤١﴾
241. Na wanawake waliotalikiwa wapewe kiliwazo (kitoka nyumba) kwa mujibu wa sharia, ni haki juu ya wenye taqwa.
كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ﴿٢٤٢﴾
242. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na Sharia) Zake mpate kutia akilini.
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ خَرَجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَهُمْ أُلُوفٌ حَذَرَ الْمَوْتِ فَقَالَ لَهُمُ اللَّـهُ مُوتُوا ثُمَّ أَحْيَاهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ ﴿٢٤٣﴾
243. Je, hukuwaona wale waliotoka majumbani mwao nao wakiwa ni maelfu wakikhofu mauti, Allaah Akawaambia: Kufeni kisha Akawahuisha? Hakika Allaah Ni Mwenye Fadhila kwa watu lakini watu wengi hawashukuru.
وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿٢٤٤﴾
244. Na piganeni katika Njia ya Allaah, na jueni kwamba Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
مَّن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ أَضْعَافًا كَثِيرَةً ۚ وَاللَّـهُ يَقْبِضُ وَيَبْسُطُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٤٥﴾
245. Ni nani atakayemkopesha Allaah karadha nzuri kisha (Allaah) Amzidishie mzidisho mwingi. Na Allaah Anakunja na Anakunjua, na Kwake mtarejeshwa.
أَلَمْ تَرَ إِلَى الْمَلَإِ مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ مِن بَعْدِ مُوسَىٰ إِذْ قَالُوا لِنَبِيٍّ لَّهُمُ ابْعَثْ لَنَا مَلِكًا نُّقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ قَالَ هَلْ عَسَيْتُمْ إِن كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ أَلَّا تُقَاتِلُوا ۖ قَالُوا وَمَا لَنَا أَلَّا نُقَاتِلَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَقَدْ أُخْرِجْنَا مِن دِيَارِنَا وَأَبْنَائِنَا ۖ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقِتَالُ تَوَلَّوْا إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ ﴿٢٤٦﴾
246. Je, hukuwazingatia wakuu katika wana wa Israaiyl baada ya Muwsaa walipomwambia Nabiy wao: Tutumie mfalme tupigane katika Njia ya Allaah. (Nabiy) akasema: Je, haiyumkiniki kuwa hamtopigana ikiwa mtaandikiwa kupigana vita? Wakasema: Tuna nini hata tusipigane katika Njia ya Allaah na hali tumekwishatolewa kutoka majumbani mwetu pamoja na watoto wetu? Walipoandikiwa wapigane vita, walikengeuka isipokuwa wachache miongoni mwao. Na Allaah Ni Mjuzi wa madhalimu.
وَقَالَ لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ اللَّـهَ قَدْ بَعَثَ لَكُمْ طَالُوتَ مَلِكًا ۚ قَالُوا أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ الْمُلْكُ عَلَيْنَا وَنَحْنُ أَحَقُّ بِالْمُلْكِ مِنْهُ وَلَمْ يُؤْتَ سَعَةً مِّنَ الْمَالِ ۚ قَالَ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَاهُ عَلَيْكُمْ وَزَادَهُ بَسْطَةً فِي الْعِلْمِ وَالْجِسْمِ ۖ وَاللَّـهُ يُؤْتِي مُلْكَهُ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٤٧﴾
247. Nabiy wao akawaambia: Hakika Allaah Amekutumieni Twaaluwt kuwa ni mfalme. Wakasema: Vipi yeye atakuwa na ufalme juu yetu, na hali sisi tunastahiki zaidi ufalme kuliko yeye, na wala hakupewa wasaa katika mali? (Nabiy) akasema: Hakika Allaah Amemkhitari juu yenu na Akamuongezea ukunjufu katika ilimu na kiwiliwili, na Allaah Humpa Amtakaye Ufalme Wake. Na Allaah Ni Mwenye Wasaa, Mjuzi wa yote.
وَقَالَ لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ آيَةَ مُلْكِهِ أَن يَأْتِيَكُمُ التَّابُوتُ فِيهِ سَكِينَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَبَقِيَّةٌ مِّمَّا تَرَكَ آلُ مُوسَىٰ وَآلُ هَارُونَ تَحْمِلُهُ الْمَلَائِكَةُ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٢٤٨﴾
248. Nabiy wao akawaambia: Hakika Aayah (Ishara, Dalili) ya ufalme wake ni kwamba litakujieni kasha ndani yake mna kituliza nyoyo kutoka kwa Rabb wenu na mabaki katika yale waliyoacha watu wa Muwsaa na watu wa Haaruwn, watalibeba Malaika. Hakika katika hayo mna Aayah (Ishara, Dalili, Hoja) kwenu mkiwa ni Waumini.
فَلَمَّا فَصَلَ طَالُوتُ بِالْجُنُودِ قَالَ إِنَّ اللَّـهَ مُبْتَلِيكُم بِنَهَرٍ فَمَن شَرِبَ مِنْهُ فَلَيْسَ مِنِّي وَمَن لَّمْ يَطْعَمْهُ فَإِنَّهُ مِنِّي إِلَّا مَنِ اغْتَرَفَ غُرْفَةً بِيَدِهِ ۚ فَشَرِبُوا مِنْهُ إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۚ فَلَمَّا جَاوَزَهُ هُوَ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ قَالُوا لَا طَاقَةَ لَنَا الْيَوْمَ بِجَالُوتَ وَجُنُودِهِ ۚ قَالَ الَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَاقُو اللَّـهِ كَم مِّن فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةً بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ مَعَ الصَّابِرِينَ ﴿٢٤٩﴾
249. Alipoondoka Twaaluwt na jeshi alisema: Hakika Allaah Atakujaribuni kwa mto. Hivyo basi atakayekunywa humo, hatokuwa pamoja nami, na ambaye hatoyaonja (hatoyagusa kabisa) hakika huyu yu pamoja nami, isipokuwa atakayeteka teko moja kwa mkono wake. Basi wakanywa kutoka humo isipokuwa wachache miongoni mwao. Alipouvuka yeye na wale walioamini pamoja naye, walisema: Leo hatuna nguvu kabisa kukabiliana na Jaaluwt na jeshi lake. Wakasema wale walio na yakini kwamba wao watakutana na Allaah: Makundi mangapi machache yameyashinda makundi mengi kwa Idhini ya Allaah? Na Allaah Yu pamoja na wenye subira.
وَلَمَّا بَرَزُوا لِجَالُوتَ وَجُنُودِهِ قَالُوا رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ﴿٢٥٠﴾
250. Na walipokabiliana uso kwa uso na Jaaluwt na jeshi lake walisema (wakiomba): Rabb wetu! Tumiminie subira na Ithibitishe miguu yetu isimame imara na Tusaidie tuwashinde watu makafiri.
فَهَزَمُوهُم بِإِذْنِ اللَّـهِ وَقَتَلَ دَاوُودُ جَالُوتَ وَآتَاهُ اللَّـهُ الْمُلْكَ وَالْحِكْمَةَ وَعَلَّمَهُ مِمَّا يَشَاءُ ۗ وَلَوْلَا دَفْعُ اللَّـهِ النَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّفَسَدَتِ الْأَرْضُ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ ذُو فَضْلٍ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٢٥١﴾
251. Wakawashinda kwa Idhini ya Allaah na Daawuwd akamuua Jaaluwt, na Allaah Akampa ufalme na hikmah, na Akamfunza Aliyoyataka. Na lau Allaah Asingelikinga baadhi ya watu kwa wengine, basi ingelifisidika ardhi. Lakini Allaah Ni Mwenye Fadhila juu ya walimwengu.
تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ ۚ وَإِنَّكَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٢٥٢﴾
252. Hizo ni Aayaat za Allaah Tunakusomea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki. Na hakika wewe ni miongoni mwa Rusuli.
تِلْكَ الرُّسُلُ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۘ مِّنْهُم مَّن كَلَّمَ اللَّـهُ ۖ وَرَفَعَ بَعْضَهُمْ دَرَجَاتٍ ۚ وَآتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ وَأَيَّدْنَاهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ ۗ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلَ الَّذِينَ مِن بَعْدِهِم مِّن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ وَلَـٰكِنِ اخْتَلَفُوا فَمِنْهُم مَّنْ آمَنَ وَمِنْهُم مَّن كَفَرَ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا اقْتَتَلُوا وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ ﴿٢٥٣﴾
253. Rusuli hao, Tumewafadhilisha baadhi yao juu ya wengine. Miongoni mwao kuna aliyesemeshwa na Allaah, na Akawapandisha baadhi yao vyeo. Na Tukampa ‘Iysaa mwana wa Maryam hoja bayana na Tukamtia nguvu kwa Ruwh[89] Al-Qudus (Jibriyl (عليه السلام. Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana waliokuwa baada yao, baada ya kuwajia hoja bayana. Lakini walikhitalifiana. Basi wapo miongoni mwao ambao waliamini na wengine ambao walikufuru. Na lau kuwa Allaah Angelitaka, wasingelipigana lakini Allaah Anafanya Atakavyo.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِمَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خُلَّةٌ وَلَا شَفَاعَةٌ ۗ وَالْكَافِرُونَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٢٥٤﴾
254. Enyi walioamini! Toeni katika Tulivyokuruzukuni kabla haijafika Siku ambayo hakutokuweko mapatano humo wala urafiki wala uombezi. Na makafiri ndio madhalimu.
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾
255. Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Al-Hayyu (Aliye Hai daima) Al-Qayyuwm (Msimamia kila kitu).[90] Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake Pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya Idhini Yake?[91] Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kufikia kuelewa chochote kuhusu Ujuzi Wake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy[92] Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Mwenye ‘Uluwa, Mwenye Taadhima[93],[94].
لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ ۚ فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٥٦﴾
256. Hapana kulazimisha katika Dini, kwani imekwishabainika kati ya uongofu na upotofu. Basi atakayemkanusha twaghuti[95] na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika, na Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.[96]
اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ ۗ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٥٧﴾
257. Allaah Ni Rafiki Mlinzi wa wale walioamini, Anawatoa kutoka katika viza na kuwaingiza katika nuru. Na wale waliokufuru marafiki wao wandani na walinzi ni twaghuti, huwatoa kutoka katika nuru na kuwaingiza katika viza. Hao ni watu wa motoni wao humo watadumu.
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِي حَاجَّ إِبْرَاهِيمَ فِي رَبِّهِ أَنْ آتَاهُ اللَّـهُ الْمُلْكَ إِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّيَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ قَالَ أَنَا أُحْيِي وَأُمِيتُ ۖ قَالَ إِبْرَاهِيمُ فَإِنَّ اللَّـهَ يَأْتِي بِالشَّمْسِ مِنَ الْمَشْرِقِ فَأْتِ بِهَا مِنَ الْمَغْرِبِ فَبُهِتَ الَّذِي كَفَرَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٢٥٨﴾
258. Je, hukumzingatia yule[97] ambaye alimuhoji Ibraahiym kuhusu Rabb wake kwa vile Allaah Alimpa ufalme aliposema Ibraahiym: Rabb wangu ni Yule Ambaye Anahuisha na Kufisha. Akasema: Mimi (pia) nahuisha na kufisha. Ibraahiym akasema: Hakika Allaah Analileta jua kutoka Mashariki basi wewe lilete kutoka Magharibi. Aliyekufuru akabaki kinywa wazi bila jibu, akataghayuri rangi. Na Allaah Haongoi watu madhalimu.
أَوْ كَالَّذِي مَرَّ عَلَىٰ قَرْيَةٍ وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا قَالَ أَنَّىٰ يُحْيِي هَـٰذِهِ اللَّـهُ بَعْدَ مَوْتِهَا ۖ فَأَمَاتَهُ اللَّـهُ مِائَةَ عَامٍ ثُمَّ بَعَثَهُ ۖ قَالَ كَمْ لَبِثْتَ ۖ قَالَ لَبِثْتُ يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ ۖ قَالَ بَل لَّبِثْتَ مِائَةَ عَامٍ فَانظُرْ إِلَىٰ طَعَامِكَ وَشَرَابِكَ لَمْ يَتَسَنَّهْ ۖ وَانظُرْ إِلَىٰ حِمَارِكَ وَلِنَجْعَلَكَ آيَةً لِّلنَّاسِ ۖ وَانظُرْ إِلَى الْعِظَامِ كَيْفَ نُنشِزُهَا ثُمَّ نَكْسُوهَا لَحْمًا ۚ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ قَالَ أَعْلَمُ أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٥٩﴾
259. Au kama yule[98] aliyepita katika kijiji kilichoporomoka kabisa juu ya mapaa yake na kuwa magofu akasema: Vipi Allaah Atakihuisha hiki (kijiji) baada ya kufa kwake? Allaah Akamfisha miaka mia, kisha Akamfufua. (Allaah) Akamuuliza: Umekaa muda gani? Akasema: Nimekaa siku moja au sehemu ya siku. Akasema: Bali umekaa miaka mia. Hebu kitazame chakula chako na kinywaji chako, havikuharibika. Halafu mtazame punda wako. Na ili Tukufanye wewe uwe ni Aayah (Ishara, Dalili) kwa watu (za Uwezo wa Allaah), basi itazame mifupa jinsi Tunavyoinyanyua, kisha Tunaivisha nyama. Yalipombainikia hayo alisema: Najua kwamba hakika Allaah Ni Muweza wa kila kitu.
وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ أَرِنِي كَيْفَ تُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۖ قَالَ أَوَلَمْ تُؤْمِن ۖ قَالَ بَلَىٰ وَلَـٰكِن لِّيَطْمَئِنَّ قَلْبِي ۖ قَالَ فَخُذْ أَرْبَعَةً مِّنَ الطَّيْرِ فَصُرْهُنَّ إِلَيْكَ ثُمَّ اجْعَلْ عَلَىٰ كُلِّ جَبَلٍ مِّنْهُنَّ جُزْءًا ثُمَّ ادْعُهُنَّ يَأْتِينَكَ سَعْيًا ۚ وَاعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٦٠﴾
260. Na pindi aliposema Ibraahiym: Rabb wangu! Nionyeshe vipi Unahuisha wafu? (Allaah) Akasema: Je, kwani huamini? Akasema: Sivyo hivyo! Bali Naam (naamini)! Lakini ili moyo wangu utumainike. (Allaah) Akasema: Basi chukua ndege wanne wazoeshe kwako, (uwachinje), kisha weka juu ya kila jabali sehemu ya hao (ndege), kisha waite watakujia mbio (wakiumbika upya), na jua kwamba hakika Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
مَّثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ كَمَثَلِ حَبَّةٍ أَنبَتَتْ سَبْعَ سَنَابِلَ فِي كُلِّ سُنبُلَةٍ مِّائَةُ حَبَّةٍ ۗ وَاللَّـهُ يُضَاعِفُ لِمَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦١﴾
261. Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika Njia ya Allaah ni kama mfano wa punje moja ya mbegu iliyotoa mashuke saba, katika kila shuke kuna punje mia. Na Allaah Humzidishia Amtakaye, na Allaah Ni Mwenye Wasaa, Mjuzi wa yote.[99]
الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ثُمَّ لَا يُتْبِعُونَ مَا أَنفَقُوا مَنًّا وَلَا أَذًى ۙ لَّهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٢٦٢﴾
262. Wale wanaotoa mali zao katika Njia ya Allaah kisha hawafuatishii kwa waliyoyatoa masimbulizi wala udhia watapa ujira wao kwa Rabb wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.
قَوْلٌ مَّعْرُوفٌ وَمَغْفِرَةٌ خَيْرٌ مِّن صَدَقَةٍ يَتْبَعُهَا أَذًى ۗ وَاللَّـهُ غَنِيٌّ حَلِيمٌ ﴿٢٦٣﴾
263. Kauli njema na msamaha ni bora kuliko swadaqa inayofuatiwa na udhia. Na Allaah Ni Mkwasi, Mvumilivu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ كَالَّذِي يُنفِقُ مَالَهُ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ صَفْوَانٍ عَلَيْهِ تُرَابٌ فَأَصَابَهُ وَابِلٌ فَتَرَكَهُ صَلْدًا ۖ لَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّمَّا كَسَبُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٢٦٤﴾
264. Enyi walioamini! Msibatwilishe swadaqa zenu kwa masimbulizi na udhia kama yule ambaye anatoa mali yake riyaa-a[100] (kujionyesha) kwa watu wala hamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Basi mfano wake ni kama jabali juu yake pana udongo, kisha likapigwa na mvua kubwa ikaliacha tupu. Hawana uwezo juu ya lolote katika waliyoyachuma. Na Allaah Haongoi watu makafiri.
وَمَثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ وَتَثْبِيتًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ كَمَثَلِ جَنَّةٍ بِرَبْوَةٍ أَصَابَهَا وَابِلٌ فَآتَتْ أُكُلَهَا ضِعْفَيْنِ فَإِن لَّمْ يُصِبْهَا وَابِلٌ فَطَلٌّ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٦٥﴾
265. Na mfano wa wale wanaotoa mali zao kutafuta Radhi za Allaah na kujithibitisha nafsi zao, ni kama mfano wa bustani iliyoko pahala paliponyanyuka, ikapigwa na mvua kubwa, kisha ikatoa mazao yake maradufu, na hata kama haikupigwa na mvua kubwa basi mvua ndogo huitosheleza. Na Allaah Ni Mwenye Kuona yale myatendayo.
أَيَوَدُّ أَحَدُكُمْ أَن تَكُونَ لَهُ جَنَّةٌ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَابٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ لَهُ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَأَصَابَهُ الْكِبَرُ وَلَهُ ذُرِّيَّةٌ ضُعَفَاءُ فَأَصَابَهَا إِعْصَارٌ فِيهِ نَارٌ فَاحْتَرَقَتْ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ ﴿٢٦٦﴾
266. Je! Anapenda mmoja wenu awe ana bustani ya mitende na mizabibu ipitayo chini yake mito, anayo humo kila aina ya mazao, ukamfikia uzee, naye ana kizazi dhaifu, kisha ikapigwa na kimbunga cha moto kikaiteketeza? Hivyo ndivyo Allaah Anavyobainisha Aayaat (Ishara na Mazingatio) kwenu mpate kutafakari.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ الْأَرْضِ ۖ وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ وَلَسْتُم بِآخِذِيهِ إِلَّا أَن تُغْمِضُوا فِيهِ ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴿٢٦٧﴾
267. Enyi walioamini! Toeni katika vizuri mlivyochuma na katika ambavyo Tumekutoleeni kutoka katika ardhi. Na wala msikusudie kutoa vibaya humo, mkavitoa ilhali nyinyi wenyewe msingevipokea isipokuwa kwa kuvifumbia macho. Na jueni kwamba hakika Allaah Ni Mkwasi, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa.[101]
الشَّيْطَانُ يَعِدُكُمُ الْفَقْرَ وَيَأْمُرُكُم بِالْفَحْشَاءِ ۖ وَاللَّـهُ يَعِدُكُم مَّغْفِرَةً مِّنْهُ وَفَضْلًا ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٦٨﴾
268. Shaytwaan anakutishieni ufukara na anakuamrisheni machafu, (ubakhili), na Allaah Anakuahidini Maghfirah kutoka Kwake na Fadhila. Na Allaah Ni Mwenye Wasaa, Mjuzi wa yote.
يُؤْتِي الْحِكْمَةَ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُؤْتَ الْحِكْمَةَ فَقَدْ أُوتِيَ خَيْرًا كَثِيرًا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٢٦٩﴾
269. Humpa hikmah Amtakaye. Na anayepewa hikmah basi kwa yakini huwa amepewa kheri nyingi. Lakini hawakumbuki isipokuwa wenye akili.
وَمَا أَنفَقْتُم مِّن نَّفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُم مِّن نَّذْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُهُ ۗ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿٢٧٠﴾
270. Na chochote mtoacho au mkiwekacho nadhiri, basi hakika Allaah Anakijua. Na madhalimu hawana wa kuwanusuru.
إِن تُبْدُوا الصَّدَقَاتِ فَنِعِمَّا هِيَ ۖ وَإِن تُخْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا الْفُقَرَاءَ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ وَيُكَفِّرُ عَنكُم مِّن سَيِّئَاتِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٧١﴾
271. Mkidhihirisha swadaqa basi ni vizuri hivyo, na mkizificha na kuwapa mafakiri, basi hilo ni kheri kwenu. Na Atakufutieni katika maovu yenu. Na Allaah kwa yale myatendayo Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
لَّيْسَ عَلَيْكَ هُدَاهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَلِأَنفُسِكُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُونَ إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ اللَّـهِ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٢﴾
272. Si juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwahidi, lakini Allaah Humhidi Amtakaye. Na chochote cha kheri mtoacho basi ni kwa ajili ya nafsi zenu. Na hamtoi ila kutaka Wajhi wa Allaah. Na chochote mtoacho katika kheri mtalipwa kamilifu nanyi hamtodhulumiwa.[102]
لِلْفُقَرَاءِ الَّذِينَ أُحْصِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ ضَرْبًا فِي الْأَرْضِ يَحْسَبُهُمُ الْجَاهِلُ أَغْنِيَاءَ مِنَ التَّعَفُّفِ تَعْرِفُهُم بِسِيمَاهُمْ لَا يَسْأَلُونَ النَّاسَ إِلْحَافًا ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٢٧٣﴾
273. (Swadaqa ni) kwa ajili ya mafakiri waliozuilika katika Njia ya Allaah, hawawezi kwenda huku na kule katika ardhi (kutafuta rizki). Asiyewajua huwadhania kuwa ni matajiri kutokana na staha ya kujizua kwao, unawatambua kwa alama zao, hawaombi watu kwa ung’ang’anizi. Na chochote mtoacho katika kheri, basi hakika Allaah Anakijua vyema.
الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ سِرًّا وَعَلَانِيَةً فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٢٧٤﴾
274. Wale wanaotoa mali zao usiku na mchana, kwa siri na kwa dhahiri, watapata ujira wao kwa Rabb wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.
الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا إِنَّمَا الْبَيْعُ مِثْلُ الرِّبَا ۗ وَأَحَلَّ اللَّـهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا ۚ فَمَن جَاءَهُ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَانتَهَىٰ فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَمَنْ عَادَ فَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٧٥﴾
275. Wale wanaokula riba hawatosimama (Siku ya Qiyaamah) ila kama anavyosimama aliyezugwa na shaytwaan kwa kuguswa na kupatwa. Hivyo kwa sababu wao wamesema: Hakika biashara ni kama riba. Na Allaah Amehalalisha biashara na Ameharamisha riba. Na atakayefikiwa na mawaidha kutoka kwa Rabb wake akakoma, basi yake ni yaliyokwishapita, na hukumu yake iko kwa Allaah. Na atakayerudia basi hao ni watu wa motoni, wao humo watadumu.
يَمْحَقُ اللَّـهُ الرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ ﴿٢٧٦﴾
276. Allaah Huifuta baraka (mali ya) riba na Huzibariki swadaqa. Na Allaah Hampendi kila aliye mwingi wa kukufuru apapiae madhambi.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٢٧٧﴾
277. Hakika wale walioamini na wakatenda mema na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah, (hao) watapata ujira wao kutoka kwa Rabb wao, na wala hakuna khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿٢٧٨﴾
278. Enyi walioamini! Mcheni Allaah na acheni yaliyobakia katika riba[103] ikiwa nyinyi ni Waumini.
فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ ﴿٢٧٩﴾
279. Na msipofanya, basi tangazeni vita[104] kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake. Na mkitubu, mtapata rasilimali zenu, msidhulumu na wala msidhulumiwe.
وَإِن كَانَ ذُو عُسْرَةٍ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيْسَرَةٍ ۚ وَأَن تَصَدَّقُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٨٠﴾
280. Na ikiwa (mdaiwa) ni mwenye hali ngumu, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na mkifanya deni kuwa ni swadaqa, basi ni kheri kwenu mkiwa mnajua.
وَاتَّقُوا يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى اللَّـهِ ۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٢٨١﴾
281. Na iogopeni Siku mtakayorejeshwa ndani yake kwa Allaah, kisha kila nafsi italipwa kamilifu iliyoyachuma, nao hawatodhulumiwa.[105]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَدَايَنتُم بِدَيْنٍ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى فَاكْتُبُوهُ ۚ وَلْيَكْتُب بَّيْنَكُمْ كَاتِبٌ بِالْعَدْلِ ۚ وَلَا يَأْبَ كَاتِبٌ أَن يَكْتُبَ كَمَا عَلَّمَهُ اللَّـهُ ۚ فَلْيَكْتُبْ وَلْيُمْلِلِ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ وَلَا يَبْخَسْ مِنْهُ شَيْئًا ۚ فَإِن كَانَ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ سَفِيهًا أَوْ ضَعِيفًا أَوْ لَا يَسْتَطِيعُ أَن يُمِلَّ هُوَ فَلْيُمْلِلْ وَلِيُّهُ بِالْعَدْلِ ۚ وَاسْتَشْهِدُوا شَهِيدَيْنِ مِن رِّجَالِكُمْ ۖ فَإِن لَّمْ يَكُونَا رَجُلَيْنِ فَرَجُلٌ وَامْرَأَتَانِ مِمَّن تَرْضَوْنَ مِنَ الشُّهَدَاءِ أَن تَضِلَّ إِحْدَاهُمَا فَتُذَكِّرَ إِحْدَاهُمَا الْأُخْرَىٰ ۚ وَلَا يَأْبَ الشُّهَدَاءُ إِذَا مَا دُعُوا ۚ وَلَا تَسْأَمُوا أَن تَكْتُبُوهُ صَغِيرًا أَوْ كَبِيرًا إِلَىٰ أَجَلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ أَقْسَطُ عِندَ اللَّـهِ وَأَقْوَمُ لِلشَّهَادَةِ وَأَدْنَىٰ أَلَّا تَرْتَابُوا ۖ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً حَاضِرَةً تُدِيرُونَهَا بَيْنَكُمْ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَلَّا تَكْتُبُوهَا ۗ وَأَشْهِدُوا إِذَا تَبَايَعْتُمْ ۚ وَلَا يُضَارَّ كَاتِبٌ وَلَا شَهِيدٌ ۚ وَإِن تَفْعَلُوا فَإِنَّهُ فُسُوقٌ بِكُمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ وَيُعَلِّمُكُمُ اللَّـهُ ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٨٢﴾
282. Enyi walioamini! Mtakapokopeshana deni mpaka muda maalumu uliopangwa, liandikeni. Na aandike baina yenu mwandishi kwa uadilifu. Na wala asikatae mwandishi kuandika kama Allaah Alivyomfunza. Na aandikishe kwa imla yule ambaye ana haki (mdai) na amuogope Allaah, Rabb wake, na wala asipunguze humo kitu chochote. Na ikiwa yule ambaye ana haki amepumbaa kiakili au mnyonge, au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe msimamizi wake kwa uadilifu. Na mshuhudishe mashahidi wawili wanaume miongoni mwenu. Na ikiwa hakuna wanaume wawili, basi mwanamme mmoja na wanawake wawili katika wale mnaowaridhia miongoni mwa mashahidi, ili kama mmoja wao hao wanawake wawili akikosea (akasahau), basi mmoja wao atamkumbusha mwengine. Na mashahidi wasikatae watapoitwa. Na wala msichukie kuliandika (deni) dogo au kubwa mpaka muda wake. Hivyo kwenu ndiyo uadilifu upasavyo mbele ya Allaah na ndio unyoofu zaidi kwa Ushahidi, na ni karibu zaidi ili msiwe na shaka, isipokuwa itakapokuwa biashara taslimu mnayoiendesha baina yenu, basi si dhambi kwenu msipoiandika. Lakini shuhudisheni mnapouziana. Wala asidhuriwe mwandishi wala shahidi. Na mkifanya hivyo, basi hakika huo ni ufasiki kwenu. Na mcheni Allaah, na Allaah Anakufunzeni, na Allaah ni Mjuzi wa kila kitu.
وَإِن كُنتُمْ عَلَىٰ سَفَرٍ وَلَمْ تَجِدُوا كَاتِبًا فَرِهَانٌ مَّقْبُوضَةٌ ۖ فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ ۗ وَلَا تَكْتُمُوا الشَّهَادَةَ ۚ وَمَن يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُ آثِمٌ قَلْبُهُ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ ﴿٢٨٣﴾
283. Na mkiwa safarini na hamkumpata mwandishi, (mdai) akabidhiwe rahani. Na ikiwa mmoja wenu amewekewa amana na mwengine, basi airudishe yule ambaye ameaminiwa amana ya mwenzake, na amche Allaah, Rabb wake, wala msifiche ushahidi, na mwenye kuuficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Allaah Ni Mjuzi wa mnayoyatenda.
لِّلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَإِن تُبْدُوا مَا فِي أَنفُسِكُمْ أَوْ تُخْفُوهُ يُحَاسِبْكُم بِهِ اللَّـهُ ۖ فَيَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٨٤﴾
284. Ni vya Allaah Pekee vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na mkidhihirisha yale yaliyomo ndani ya nafsi zenu au mkiyaficha, Allaah Atakuhesabuni kwayo. Humghufuria Amtakaye na Humuadhibu Amtakaye. Na Allaah Ni Mweza wa kila kitu.[106]
آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ ۚ وَقَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ ﴿٢٨٥﴾
285. Rasuli ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Rabb wake na Waumini (pia). Wote wamemwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Rusuli Wake. (Nao husema): Hatutofautishi baina ya yeyote kati ya Rusuli Wake. Na wakasema: Tumesikia na tumetii, tunakuomba maghfirah Rabb wetu, na Kwako ndio mahali pa kuishia.[107]
لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِ ۖ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۚ أَنتَ مَوْلَانَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٢٨٦﴾
286. Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. Itapata malipo ya (mema) iliyoyachuma, na itabeba (matokeo ya maovu) iliyojichumia. Rabb wetu! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Rabb wetu! Usitubebeshe mzigo kama Uliowabebesha waliokuwa kabla yetu. Rabb wetu! Usitutwike tusiyoyaweza, na Tusamehe, na Tughufurie na Turehemu, Wewe Ni Mawlaa[108] wetu, basi Tusaidie tuwashinde watu makafiri.[109]
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Herufi hizi zinajulikana kuwa ni Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah. Herufi hizo zimetokea katika mwanzoni mwa baadhi ya Suwrah. Na idadi ya Suwrah hizo ni ishirini na tisa katika Qur-aan. Wafasiri wa Qur-aan wamekhitilafiana kuhusu maana zake, wakataja maana mbili tatu ila wote wamekubaliana kuwa rai iliyo ya nguvu na sahihi kabisa ni: Maana zake hazijulikani kwa sababu ni katika ilimu ya ghaibu ambayo hakuna ajuaye isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rai hiyo imetajwa na Abu Bakr, ‘Umar, ‘Uthmaan, ‘Aliy na Ibn Mas‘uwd (رضي الله عنهم). [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[2] “Hiki Ni Kitabu” Badala Ya “Hicho Ni Kitabu”
Tarjama hii na nyenginezo za kuaminika zimefasiri: “Hiki ni Kitabu” badala ya “Hicho ni Kitabu” ilhali katika Aayah limetajwa neno ذَٰلِكَ ambalo katika uhalisia wa lugha ya Kiarabu ni: Ismul-Ishaarah lil-ba’iyd (Kiashirio Cha Mbali). Hivyo ni kwa sababu:
(i) Kitabu Hicho ذَٰلِكَ الْكِتَابُ kimekusudiwa Kitabu kilichokuweko mbinguni katika Lawh Al-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa) kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ ﴿٧٧﴾ فِي كِتَابٍ مَّكْنُونٍ ﴿٧٨﴾
Hakika hii bila shaka ni Qur-aan tukufu. Katika Kitabu kilichohifadhiwa. [Al-Waaqi’ah (56: 77-78)]
Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَإِنَّهُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ﴿٤﴾
Na hakika hii (Qur-aan) iko Kwetu katika Mama wa Kitabu, Imetukuka kwa hakika, imejaa Hikmah. [Az-Zukhruf (43:4)]
(ii) ذَٰلِكَ Ambayo ni Ismul-Ishaarah lil-ba’iyd (Kiashirio Cha Mbali) hutumika pia kwa ajili ya kuadhimisha (kukitukuza) kitu. Na kiashirio cha mbali kinginecho ni تلك kama ilivyotajwa katika mwanzo wa Aayah kadhaa kama Yuwnus (10:1), Yuwsuf (12:1), Al-Hijr (15:1), An-Naml (27:1), Al-Qaswasw (28:2), Luqmaan (31:2) na nyenginezo.
[3] Hudaa, Hidaaya Ni Aina Mbili:
(i) Hidaayatut-Tawfiyq (Hidaaya ya tawfiyq): Ni imaan ambayo mahali pake ni moyoni na ni Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee Awezaye kuiweka katika nyoyo za waja. Dalili ni Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) Alipomwambia Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye alipendelea kumuongoza ammi yake Abuu Twaalib katika Uislamu alipokuwa anakaribia kuaga dunia. Allaah Akasema:
إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿٥٦﴾
Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye, lakini Allaah Humhidi Amtakaye, Naye Anawajua zaidi wenye kuongoka. [Al-Qaswasw (28:56)]
(ii) Hidaayatul-Irshaad (Hidaaya ya kuongoza): Ni kuelekeza, kubainisha, kuongoza njia, kumwongoza mtu katika Uislamu kama vile Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomwongoza ammi yake Abuu Twaalib aingie Uislamu akamtaka atamke Shahaada (laa ilaaha illa-Allaah) lakini akakataa ikawa hakupata Hidaaya ya tawfiyq. Hali kadhaalika Hidaaya hii ya irshaad ni kama vile kumwongoza mtu kutekeleza mema, kuelekea katika njia iliyonyooka n.k. Na hii ni sawa na Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ ﴿١٠﴾
Na Tukambainishia njia mbili (ya haki na upotofu)? [Al-Balad (90:10)]
وَأَمَّا ثَمُودُ فَهَدَيْنَاهُمْ فَاسْتَحَبُّوا الْعَمَىٰ عَلَى الْهُدَىٰ
Na ama kina Thamuwd, wao Tuliwaongoza, lakini walistahabu upofu kuliko hidaaya. [Fusw-Sswilat (41:17)]
إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا﴿٣﴾
Hakika Sisi Tumemuongoza njia; ima (awe) ni mwenye kushukuru au mwingi wa kukufuru. [Al-Insaan (76:3)]
وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٢﴾
Na hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka. [Ash-Shuwraa (42:52)]
[4] Maana Ya Taqwa:
Taqwa ni mojawapo ya maneno ya kipekee katika lugha ya Kiarabu ambayo hayawezi kutafsiriwa kwa neno moja au mawili. Kwa hiyo maana yake kilugha ni kinga, kujilinda, himaya, hifadhi, kutahadhari na kukhofu.
Katika istilahi, Salaf wametaja mengi kuhusu taqwa, miongoni mwayo ni kumwabudu Allaah ipasavyo, kutekeleza yaliyoamrishwa na Allaah (سبحانه وتعالى) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), kujiepusha makatazo Yao na kubakia katika mipaka ya sharia ya Dini, kumkhofu Allaah na kukhofu Adhabu na Ghadhabu Zake, kuwa na raghba (utashi) na kutaraji Thawabu Zake, kumuadhimisha Allaah (سبحانه وتعالى) na kumpenda mapenzi ya kikweli pamoja na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم).
Taqwa haihitajii kuhakikishwa mtu kuwa mahali fulani au wakati fulani, bali taqwa ya hakika ni pale mtu anapokua yuko peke yake, akajiepusha na yaliyo haramu japokuwa hakuna mtu anayemuona. Na ndipo aliposema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa “Taqwa ipo hapa!” Akiashiria kwenye kifua chake palipo na moyo na kusema mara tatu.
Umar (رضي الله عنه) alimuuliza Ubayy bin Ka’b (رضي الله عنه): “Taqwa ni nini?” Akajibu: “Ee Amiri Wa Waumini! Je, hukuwahi kupita njia yenye miiba?” Akasema: “Naam!” Akasema: “Ulifanya nini?” Akasema: “Niliinua miguu yangu huku nikiitazama na kuinua mguu mmoja na mwingine, nikikhofia mwiba usije kunichoma.” ‘Ubay akamwambia: “Hiyo ndiyo taqwa!”
‘Aliy bin Abi Twaalib (رضي الله عنه) amesema: “Taqwa ni kumkhofu Al-Jaliyl (Allaah) na kufanyia kazi Tanziyl (Qur-aan) na kuridhika na kidogo, na kujiandaa na Siku ya rahiyl (kuondoka duniani, kufariki).”
[5] Maana Ya Ghaibu:
Ghaibu ni kila ambayo yametambulishwa kwetu na Allaah (سبحانه وتعالى) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم). Ni mambo ambayo hayaonekani kwetu wala akili haidiriki utambuzi wake au kutambua uhalisi wake. Mifano ya baadhi ya ghaibu ni kutomuona Allaah (سبحانه وتعالى) hapa duniani lakini tunamuamini. Pia kumuamini na kumpenda Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ingawa hatukumuona. Pia kuamini kwamba walikuweko Swahaba zake (رضي الله عنهم) na kuwapenda wote ingawa hatukuwaona, na kuamini yote yaliyokuja katika Siyrah ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Hali kadhalika kuamini Manabii waliotangulia, kuamini Malaika na mambo yote mengineyo ya ghaibu yakiwemo alama za Qiyaamah, adhabu za kaburi na neema zake, Hayaatul-Barzakh (kipindi baina ya mtu kufariki hadi Siku ya Qiyaamah), Al-Ba’ath (kufufuliwa), Al-Hashr (mkusanyiko wa viumbe Siku ya Qiyaamah katika ardhi ya mkusanyiko), Al-Hisaab (kuhesabiwa matendo), Asw-Swiraatw (daraja watakalovuka watu Siku ya Qiyaamah ima kuingia Peponi au motoni), Miyzaan (Mizani itakayopima amali za watu), Jannah (Pepo) na An-Naar (moto), na mambo mengineyo ya ghaibu. Na ghaibu ni sifa ambayo anaimiliki Muumini wa kweli na mwenye taqwa kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah hiyo tukufu ambayo Ameitanguliza mwanzo kabisa katika Qur-aan kwenye Suwrah hii ya pili, kutokana na umuhimu wake.
Rejea pia Al-An’aam (6:59), Luqmaan (31:34), An-Naml (27:65).
[6] Maana Ya Kusimamisha Swalaah:
Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: “Ni kuswali kwa kuzingatia nguzo na sharti zake.” Adhw-Dhwahaak amesema kuwa Ibn ‘Abbaas alisema: “Iqaamat Asw-Swalaah maana yake ni kukamilisha rukuu, sujuwd, kusoma Qur-aan, kuwa na khushuu (unyenyekevu), na kuhudhurisha moyo katika Swalaah.” Qataadah alisema: “Iqaamat Asw-Swalaah maana yake ni kuchunga wakati, wudhuu, rukuu na sujuwd za Swalaah.” Muqaatil bin Hayyaan alisema: “Iqaamat Asw-Swalaah ina maana: Kuchunga wakati, kujitwaharisha kwa ajili yake, kukamilisha rukuu, sujuwd na kusoma Qur-aan, tashahhud na kumwombea Rehma Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Hiyo ndiyo Iqaamat Asw-Swalaah.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr] Rejea An-Nisaa (4:108), Al-Muuminuwn (23:1).
[7] Nyoyo Zenye Maradhi:
Rejea Suwrah Muhammad (47:20) kwenye maana ya nyoyo zenye maradhi na rejea mbalimbali za nyoyo zenye maradhi.
Rejea pia Al-Hajj (22:46) kwenye maelezo kuhusu maana ya moyo uliopofuka.
Rejea pia Ash-Shu’araa (26:88-89) kwenye ufafanuzi na maelezo kuhusu moyo uliosalimika.
[8] Allaah (سبحانه وتعالى) Hana Sifa Mbaya Isipokuwa Anarudisha Ubaya (Muqaabalah): Rejea Aal-‘Imraan (3:54).
[9] Changamoto Ya Kuleta Mfano Wa Qur-aan Wala Hakuna Awezaye Kamwe!
Rejea Yuwnus (10:38), Al-Israa (17:88), Huwd (11:13-14), Atw-Twuur (52:33-34), Rejea pia Al-An’aam (6:93) ambako kumetajwa waongo waliodai Unabii.
[10] Mifano Ya Kipekee Ya Allaah: Rejea Al-A’raaf (7:40).
[12] Kuunga Aliyoyaamrisha Allaah: Rejea Ar-Ra’d (13:21).
[13] Mauti Ya Mara Mbili Na Uhai Wa Mara Mbili:
Mlikuwa wafu (kabla ya kuumbwa): Ni mauti ya kwanza.
Akakuhuisheni (kupulizwa roho tumboni mwa mama na kuzaliwa na kuishi uhai wa duniani): Ni uhai wa kwanza.
Kisha Atakufisheni (kukufisheni baada ya kumalizika muda wa kuishi duniani [kufariki dunia]): Ni mauti ya pili.
Kisha Atakuhuisheni (kurudishwa kuwa hai tena pindi mtakapofufuliwa kutoka makaburini Siku ya Qiyaamah): Ni uhai wa pili. (Na huku ndio kurudishwa Kwake Allaah (سبحانه وتعالى) ili kuhesabiwa na kulipwa mema na maovu).
Rejea Suwrah Ghaafir (40:11) kwenye Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) kama hii:
[14] اسْتَوَى إِلَى السَّمَاءِ" Amezikusudia (Kuziumba Mbingu):
Kwa hakika maana ya “Istawaa” ina unyeti katika kuielezea. Na katika Tarjama hii, maana ya “Istawaa” imeelezewa kwa bayana, maana zake zinazotofautiana, kwa mujibu wa maelezo ya ‘Ulamaa, katika Suwrah mbili: Katika Suwrah hii Al-Baqarah (2:29) na Al-A’raaf (7:54).
Hivyo basi, maana ya "اسْتَوَى" katika Aayah hii ya Suwrat Al-Baqarah (2:29) na Suwrat Fusswilat (41:11), kwa mujibu wa kauli za ‘Ulamaa wa Ahlu As Sunnah wal Jama’ah na Mufassiruna, wanasema ina maana ya "قَصَدَ", yaani Amekusudia. Na ikiwa "اسْتَوَى إِلَى السَّمَاءِ" inakuwa kwa maana ya: قَصَدَ إِلَى خَلْقِهَا yaani Amekusudia kuziumba. Kwa hiyo maana munaasib katika Suuwrah hizi mbili ni: “Kisha Akazikusudia mbingu (Kuziumba).”
[15] Khalifa:
Katika Aayah hiyo imekusudiwa watu wanaokuja baada ya wengine, au wanaofuatana karne kwa karne, vizazi baada ya vizazi. Ama maana nyengine ya khalifa, ni Khalifa Walioongoka wanne wa Waumini baada ya kufariki (صلى الله عليه وآله وسلم) ambao walikuwa ni Abu Bakr Asw-Swiddiyq, ‘Umar bin Al-Khattwaab, ‘Uthmaan bin ‘Affaan na ‘Aliy bin Abiy Twaalib (رضي الله عنهم).
[16] Maasi Ya Kwanza Ya Kumuasi Allaah (سبحانه وتعالى):
Ibn ‘Atwiyyah amesema: Jambo la kwanza la kumuasi Allaah, lilikuwa ni uhasidi, nalo lilidhihirika kutoka kwa Ibliys. [Al-Muharrar Al-Wajiyz (3/469)] Na sababu alizozitaja Ibliys za kukataa kwake kumsujudia Aadam ni kwamba, yeye alijiona ni mbora kuliko Aadam, hivyo akadhihirisha kibri. Rejea Al-A’raaf (7:11-12), Al-Hijr (15:28-33), Al-Israa (17:61-62), Swaad (38:71-76).
[18] Ummah Bora Kabisa Ni Ummah Wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):
Makusudio ya kufadhilishwa kwa Baniy Israaiyl juu ya walimwengu wote, ni kufadhilishwa kwao juu ya walimwengu wa zama zao, kwani inafahamika kuwa ummah ambao ni bora kuliko ummah zote ni ummah wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa dalili ya Kauli ya Allaah (تعالى):
كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿١١٠﴾
Mmekuwa ummah bora kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu, mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Watu wa Kitabu ingelikuwa ni bora kwao, miongoni mwao wako wanaoamini na wengi wao ni mafasiki. [Aal-‘Imraan (3:110)]
[19] Maana ya Al-Furqaan: Pambanuo: Rejea Al-Furqaan (25:1).
[20] Al-Manna Na As-Salwaa:
Wafasiri wamekhitilafiana juu ya makusudio ya al-manna na as-salwaa. Lakini bila shaka ni aina ya chakula kama ilivyonukuliwa kutoka Tafsiyr ya Imaam Ibn Kathiyr kwamba: Al-manna ilikuwa ikiteremka kutoka mitini na walikuwa wakila kadiri walivyotaka kula. Na Qataadah amesema: “Al-manna ambayo ni nyeupe kuliko maziwa na tamu mno kulikoni asali ilikuwa ikiwanyeshea (kutoka mbinguni) kama vile barafu inavyoanguka kuanzia alfajiri hadi jua kuchomoza. Mmoja wao aliikusanya ya kutosha kwa ajili ya siku ile tu kwani ingebakia zaidi ya hivyo ingeharibika.” Imesimuliwa na Sa’iyd bin Zayd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Al-kama-ah (uyoga) ni aina ya manna na maji yake ni shifaa (ponyo) ya macho.” [Al-Bukhaariy (4478)]
Ama as-salwaa, Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: As-salwaa ni aina ya ndege anayefanana na kware. Ama ‘Ikrimah na Qataadah (رضي الله عنهما) wamesema: As-salwaa ni ndege wa Jannah (Peponi) anayefanana au ambaye ni kiasi cha ukubwa wa shomoro. [Tafisyr Ibn Kathiyr]
[21] Hittwah: Tuondolee Uzito Wa Madhambi: Mayahudi Kubadilisha Maana Ya Neno:
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wana wa Israaiyl waliamrishwa kuingia kupitia mlangoni huku wameinama na wanyenyekee na waseme ‘Hittwah’ (Tuondolee uzito wa madhambi). Lakini waliingia kinyumenyume wakipotosha maneno wakisema: Habbat fiy sha’arah (mbegu katika unywele).” [Al-Bukhaariy]
Rejea pia Al-Baqarah (2:104).
[22] Wasabai:
Wasabai ni nani, nini imaan na ‘aqiydah (itikadi) zao. Rejea Al-Hajj (22:17).
Nukuu nyengine zimetaja: “Wasabai ni watu waliobakia katika maumbile yao na maadili ya asili (au asili ya Uislamu), hawana dini maalumu wanayoifuata.” [Tafsiyr Al-Muyassar]
“Hukmu hii inawahusu Watu wa Kitabu kwa sababu lilokuwa sahihi ni kwamba wao ni katika kundi la Manaswara.” [Tafsiyr As-Sa’diy]
[23] As-Sabt:
Maana yake asili ni mapumziko na hivyo Siku hiyo yao Mayahudi ya mapumziko (Jumamosi), waliwekewa sharia wasivue samaki. Lakini walikhalifu amri kwa kutumia njama na ujanja wakavua samaki kumuasi Allaah. Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaghadhibikia na kuwageuza manyani. Rejea An-Nisaa (4:47) na Al-A’raaf (7:163-166).
[24] Kisa Cha Al-Baqarah (Ng’ombe) Na Ndio Jina La Suwrah Hii:
Kisa chake kinaanzia Aayah hii ya (2:67) hadi Aayah (2:76). Kulikuweko na mtu aliyepooza (asiyekuwa wa kawaida) na alikuwa na mali nyingi. Hakuwa na mrithi isipokuwa jamaa yake mmoja. Mrithi huyo alimuua huyo bwana ili apate kurithi mali. Kisha akachukua mwili wake akautupa nje na nyumba ya mtu mmoja kumsingizia kuwa kamuua. Siku ya pili akadai kulipiza kisasi, pakatokea mzozano na watu walikaribia kuuana. Mwishowe wakasema “Mnaye Rasuli wa Allaah mwendeeni.” Walipomwendea Nabiy Muwsaa akawaambia:
إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تَذْبَحُوا بَقَرَةً ۖ
Hakika Allaah Anakuamuruni mchinje ng’ombe.
Wakafanya ugumu wa kutii amri hii kwa kubishana na wakazidi kufanyiwa ugumu kumtafuta ng’ombe mwenye sifa fulani. Wasingebishana basi ingewatosheleza kuchinja ng’ombe yoyote yule. Ng’ombe mwenye sifa hizo akapatikana kwa mtu mmoja pekee naye akataka alipwe dhahabu iliyojaza ngozi ya ng’ombe. Wakamlipa na wakamchinja na kisha wakachukua sehemu ya ng’ombe kumpigia huyo mtu aliyeuliwa, akazindukana na wakamuuliza nani aliyemuua? Akamuashiria mrithi wake, basi hakuruhusiwa tena kumrithi. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[26] Maana Za Ruwh Katika Qur-aan:
Rejea An-Nahl (16:2).
Na Uthibitisho Kuwa Jibriyl ( (عليه السلام Ndiye Ruwh Al-Qudus:
Amesimulia Ibn Mas‘uwd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ruwh Al-Qudus alinifahamisha kuwa hakuna roho itakayokufa mpaka imalizike rizki yake na muda wake, kwa hiyo mcheni Allaah na mtakeni rizki katika hali iliyo bora.” [As-Sunnah: (14/304), ameisahihisha Al-Albaaniy katika Mushkilat Al-Faqar (15), Swahiyh Al-Jaami’ (2085). Hadiyth kutoka Abuu Umaamah Al-Baahiliy (رضي الله عنه)]
[28] Maana Ya Baghyun/Baghaa Katika Qur-aan:
Rejea Ash-Shuwraa (42:14) kupata maana zake mbalimbali.
[30] Malaika Jibriyl Na Miykaail:
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anapoamka usiku akisoma duaa ambayo akiwataja Malaika hao wawili pamoja na Malaika Israafiyl; Hadiyth imethibiti:
Amesimulia Abuu Salamah bin ‘Abdir-Rahmaan bin ‘Awf (رضي الله عنه): Nilimuuliza ‘Aaishah (رضي الله عنها) : Je, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akifungulia Swalaah yake kwa kitu gani alipoamka usiku? Akasema: alikuwa anapoamka usiku anafungulia Swalaah yake kwa:
اللَّهُمَّ رَبَّ جَبْرَائِيلَ وَمِيكَائِيلَ وَإِسْرَافِيلَ. فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ. عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ. أَنْتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ. اهْدِنِي لِمَا اخْتُلِفَ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِكَ إِنَّكَ تَهْدِي مَنْ تَشَاءُ إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيم
Ee Allaah Rabb wa Jibraaiyl na Miykaail na Israafiyl, Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa ghaibu na dhahiri, Wewe Utahukumu baina ya waja Wako katika ambayo walikuwa wakikhitilafiana nayo. Niongoze mimi kwenye haki katika yale ambayo (watu) wamekhitilafiana kwa idhini Yako. Hakika Wewe unamuongoza Umtakae kwenye njia ilionyoka.” [Muslim (1/534)]
Rejea Az-Zukhruf (43:77) kwenye maelezo bayana kuhusu baadhi ya Malaika; Majina yao, kazi zao, na idadi zao na faida nyenginezo.
[31] Haaruwt na Maaruwt:
Haaruwt na Maaruwt ni Malaika wawili katika Malaika wa mbinguni, ambao Allaah (عزّ وجلّ) Aliwateremsha ardhini kuwa ni fitnah (jaribio na mtihani) kwa watu. Walikuwa wakiwafundisha watu sihri (uchawi) kwa amri ya Allaah (عزّ وجلّ). Lakini kila walipotaka kuwafundisha watu sihri, waliwatahadharisha kwanza wakiwaambia:
إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ ۖ
Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru.
[32] Maana Ya: رَاعِنَا Na انظُرْنَا Na Tabia Ya Mayahudi Kubadilisha Maneno:
Swahaba (رضي الله عنهم) walikuwa wakimwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Raa’inaa! Yaani: “Tega sikio lako utusikilize na utufahamu.” Lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Aliwakataza usemi huo kwa sababu usemi huo wa “raa’inaa” ulitumiwa na Mayahudi kukusudia neno ovu na ufidhuli kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Walipokuwa wakimtembelea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), walijaribu kutoa chuki zao kwa kutumia maneno ya kutatanisha katika maamkizi na maongezi yao. Walikuwa wakitumia maneno yenye maana mbili; moja yenye maana nzuri na nyengine ya tusi au ufidhuli. Na walipotamka maneno yafaayo walinong’ona maneno maovu. Walijifanya kudumisha adabu na heshima na huku wakiwa hawaachi njia yoyote ya kumtusi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Na kila walipotaka kumalizia chochote walichotaka kusema, walitumia usemi wa raa'inaa, ambao ulimaanisha “tafadhali tukubalie” au “tafadhali tutegee sikio utusikilize.”
Iliwezekana kwa usemi huo kutumiwa kwa maana tofauti kabisa katika lugha yao Mayahudi kwa mfano, kuna neno linalofanana nalo ambalo linamaanisha: “Sikiliza na uwe kiziwi!” Pia katika lugha hiyo hiyo ina maana ya ufidhuli, jahili, mjinga. Usemi huo pia ulitumiwa pindi mtu alitaka kusema: “Ukinisikiliza nitakusikiliza.” Na ilipotamkwa kwa kupindisha ulimi kidogo iligeuka kuwa “raa'inaa”, ikimaanisha “mchungaji wetu.” Ni kwa sababu ya uwezekano wa neno hilo kutumika katika maana hizi tofauti ndipo Waislamu wakaamriwa kuliepuka na badala yake watumie usemi ulionyooka na bayana kabisa usio na utata nao ni: انظُرْنَا “undhwurnaa,” yenye maana: “Tafadhali tuangalie kwa makini, au tafadhali tuangalie na tupe muhula tukufuate (unayotuambia au kutuamrisha).” Rejea pia An-Nisaa (4:46), Al-Baqarah (2:58).
[33] Hukmu Ya An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa):
Somo hili lina maelezo mapana lakini kifupi ni: An-Naasikh ni Aayah Inayofuta. Al-Mansuwkh ni Aayah inayofutwa. Na katika Sunnah pia kuna Hadiyth inayofuta na inayofutwa, mfano hukmu ya ndoa ya mut’ah kuwa kwanza iliruhusika kisha ikafutwa ikaja haramisho lake. Rejea An-Nisaa (4:23). Pia hukmu ya kuzuru makaburi ilikuja kwanza makatazo ya kuzuru kisha ikaja ruhusa ya kuzuru kwa kauli yake Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Nilikuwa nimewakataza kuzuru makaburi, sasa zuruni kwani hilo linawakumbusha nyinyi Aakhirah .” [Muslim na wengineo]
Maelezo kwa mukhtasari yanapatikana katika kiungo kifuatacho:
An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa) [23]
Rejea pia An-Nahl (16:101).
[35] ‘Aqiydah Sahihi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Ni Kuthibisha Sifa Za Allaah.
Aayah tukufu imetaja Nafsi ya Allaah (سبحانه وتعالى). Na ‘Aqiydah sahihi ni kuithibitisha hivyo hivyo bila ya kuipa maana nyenginezo; Rejea Huwd (11:47) kwenye maelezo bayana.
[37] Kumsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwa Ana Mwana:
Rejea An-Nisaa (4:171), Maryam (19:30-36), (At-Tawbah (9:30).
[38] Maana Ya Neno Kun!
Ni neno Analotumia Allaah (سبحانه وتعالى) pindi Akitaka kufanya au kuamrisha jambo basi huliambia Kun! (Kuwa!) nalo hapo hapo jambo hilo huwa. Mfano katika Miujiza Yake ya kumuumba Nabiy ‘Aadam (عليه السّلام)kwa udongo. Au katika kumfanya Maryam ashike mimba na amzae Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) bila ya baba. Au Anapotaka kutoa Amri Yake yoyote ile basi hakuna jambo ambalo Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) linamshinda bali Husema tu Kun! (Kuwa!) na hapo hapo jambo huwa!
[39] Maana Ya Kuisoma Qur-aan Ipasavyo Na Kuipa Haki Yake:
Ibn Mas‘uwd (رضي الله عنه) amesema maana yake ni: “Anahalalisha Aliyohalalisha Allaah, na Anaharamisha Aliyoyaharamisha Allaah, na anasoma kama Alivyoteremsha Allaah, na wala hapotoshi maneno sehemu zake, na wala hafanyii taawiyl lolote humo isiyokuwa taawiyl yake.” (Taawiyl: kukwepesha maana yake ya kihakika kwa kuipa maana ndogo au tofauti, ishara ambayo ni tofauti na maana ya juu, ni kukanusha maana).
Na Hudhayfah bin Al-Yamaan amehadithia kuhusu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba alipokuwa akiswali, pale anapopita Aayah ya Rehma aliomba Rehma, anapopita Aayah ya adhabu anajikinga nayo, anapopita Aayah ya kumsabihi Allaah anamsabihi (kumtukuza). [Swahiyh Ibn Maajah (1119)]
Na Al-Hasan Al-Baswriy amesema: “Wanaifanyia kazi sharia (hukmu) zake na wanaamini mutashaabih zake (mutashaabih: zilizofanana) na wanapeleka yanayowatatiza kufahamu kwa ‘Ulamaa wake.”
Pia, baadhi ya ‘Ulamaa wamesema kuwa: Ni kuisoma kwa hukmu zake za tajwiyd, kufahamu maana yake, kuyafanyia kazi maamrisho yake, kujiepusha na makatazo yake, kujifundisha na kuifundisha. Hali kadhaalika, kusabbih kila panapotajwa Tasbiyh, kumtukuza Allaah (عزّ وجلّ), kuomba rehma, kuomba maghfirah, kuomba kuingizwa Jannah (Peponi) na kuomba kinga ya moto kila panapotajwa moto.
[40] Imaam (Kiongozi). Neno La أُمَّةً Katika Qur-aan Lina Maana Kadhaa: Rejea An-Nahl (16:120) kwenye maana zake.
[41] Maqaam Ibraahiym: Ni jiwe ambalo Nabiy Ibraahiym (عَلَيْهِ السَّلاَمُ) alisimama juu yake wakati wa ujenzi wa Al-Ka’bah.
[42] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
125-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 125: وَاتَّخِذُوا مِنْ مَقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى [26]
[43] Kujengwa Al-Ka’bah Na Duaa Za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) Ukatoka Ummah Wa Mwisho Wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):
Aliyoyaomba Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) katika Aayah hii ni kama Anayosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah zifuatazo: Suwrah hii Al-Baqarah (2:151), Aal-‘Imraan (3:164), Al-Jumu’ah (6:2).
Aayaat hizi kuanzia (127-129) zinatuthibitishia kuwa Nabiy Ibraahiym na mwanawe Nabiy Ismaa’iyl (عليهما السّلام) ndio walionyanyua misingi ya Al-Ka’bah na kuijenga. Wakaomba duaa wakati wa shughuli hiyo ya ujenzi Allaah Awataqabalie kazi yao hiyo, atokee Nabiy kuwaongoza watu katika Uislamu kutoka katika kizazi cha Nabiy Ismaa’iyl (عليه السّلام). Na katika kizazi hicho ndipo alipotoka Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa ni Nabiy wa Mwisho na ujumbe wake ni ujumbe wa mwisho kabisa. Nao ndio umekusudiwa kwa ummah huu wetu wa Kiislamu na Kitabu cha mwisho Al-Qur-aan. Rejea Al-An’aam (6:92), Ibraahiym (14:35-41).
[44] Swalihina Na Tofauti Yao Na Manabii, Swiddiyqiyna, Shuhadaa Na Swahaba (رضي الله عنهم):
Rejea An-Nisaa (4:69) kwenye maelezo bayana.
[45] Dini Ya Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) Ni Dini Ya Kiislamu: Rejea Aal-‘Imraan (3:67).
[47] Maana Ya Swibghah Ya Allaah (عزّ وجلّ):
Swibghah kilugha maana yake ni rangi au kupaka rangi. Ama makusudio ya maana yake katika Aayah hii tukufu ni Dini ya Allaah. Wamesema hivyo Ibn ‘Abbaas, Qataadah na Al-Hasan (رضي الله عنهم) na kwamba imeitwa Swibghah (rangi) kwa sababu athari ya Dini inaonekana wazi kwa mwenye kushikamana na Dini kama vile athari ya rangi inavyodhihirika kwenye nguo.
Imaam As-Sa’adiy (رحمه الله) katika Tafsiyr yake amesema: Maana yake: Wamefaradhishiwa Swibghah ya Allaah, nayo ni Dini Yake, na isimamisheni kwa msimamo timilifu na njia sahihi kwa matendo yake yote ya nje na ya ndani. Na kwa ‘Aqiydah (itikadi) yake yote wakati wote, mpaka iwe kama Swibghah (rangi). Na Swibghah iwe ni moja ya sifa zenu. Kwa hivyo basi, inapokuwa ni moja ya sifa zenu, inakuwa imewajibika kwenu kutekeleza amri Zake kwa utiifu na kwa khiari, na kwa upendo. Hapo Dini huwa ni asasi na asili yao kama vile Swibghah ambayo imepaka rangi nguo kabisa kiasi kwamba ikachukua sifa hiyo (ya rangi yake). Na hii itawaletea furaha katika maisha ya dunia na Aakhirah kwa kuwa Dini inawaongoza katika khulqa (tabia) njema, amali njema, kutenda ihsaan na amali tukufu. Hivyo kwa sababu hii kama njia ya balagha ya kuthibitisha jambo hilo na kwa wale wenye akili safi ndio Akasema:
وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ صِبْغَةً ۖ
Na Swibghah (dini) gani yaweza kuwa bora zaidi kuliko Dini ya Allaah?
Inamaanisha: Hakuna Swibghah (Dini) iliyo bora kuliko Swibghah (Dini) ya Allaah.
Na ukitaka kujua mfano, amekubainishieni tofauti ya Swibghah ya Allaah na Swibghah nyinginezo, kwani jambo linabainishwa kwa kinyume chake. Basi mtazame mja anayemuamini Rabb wake kwa imaan sahihi, ambayo athari zake ni moyo ulionyenyekea na viungo vilivyotiishwa kiasi kwamba anabakia kuwa na kila sifa njema, matendo mazuri, tabia njema kamilifu, sifa tukufu, na hivyo anakuwa ameepukana na kila sifa ovu za kuchukiza na za aibu. Basi mja huyo anasifika kwa asw-swidq (ukweli) katika kauli zake, matendo yake, subira na uvumilivu wake, upole, ushujaa, na kuwa na ihsaan kwa kauli na matendo, na kumpenda Allaah na kumcha na kumkhofu, na kutaraji Kwake. Basi hii ndio hali yake ya ikhlaasw kwa Mwenye kustahiki kuabudiwa na kutenda ihsaan kwa Waja Wake.
Na haya yote kwa kinyume chake, yanatofautishwa na mja anayemkufuru Rabb wake na akamkimbia, na akawaelekea viumbe wengine badala Yake. Hivyo basi ndivyo anavyosifika kwa sifa ovu za kufr, shirk, kuongopa, khiyana, makri (kupanga njama), udanganyifu na ukosefu wa maadili mema, na kuwatendea uovu viumbe katika kauli zake, matendo yake, wala hana ikhlaasw kwa Mwenye Kustahiki Kuabudiwa, na wala hana ihsaan kwa Waja wa Allaah (سبحانه وتعالى).
Kwa hivyo hii inadhihirisha tofauti kubwa kati ya viwili hivi kwako, na inakubainishia kwamba hakuna Swibghah bora kuliko Swibghah ya Allaah. Na katika hili ni kwamba hakuna Swibghah mbaya zaidi kuliko yule aliyetiwa rangi kwa dini isiyokuwa Dini Yake Allaah (سبحانه وتعالى).
[49] Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Atakuwa Shahidi Kwa Ummah Wake Wa Kiislamu Na Ummah Wa Kiislamu Watakuwa Mashahidi Kwa Rusuli Waliotangulia Kwamba Wamebalighisha Ujumbe.
Rejea pia Al-Hajj (22:78), An-Nisaa (4:41), Al-Jaathiyah (45:28), Al-Israa (17:71), Az-Zumar (39:69).
حَدَّثَنَا يُوسُفُ بْنُ رَاشِدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، وَأَبُو أُسَامَةَ ـ وَاللَّفْظُ لِجَرِيرٍ ـ عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، وَقَالَ أَبُو أُسَامَةَ، حَدَّثَنَا أَبُو صَالِحٍ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " يُدْعَى نُوحٌ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَيَقُولُ لَبَّيْكَ وَسَعْدَيْكَ يَا رَبِّ. فَيَقُولُ هَلْ بَلَّغْتَ فَيَقُولُ نَعَمْ. فَيُقَالُ لأُمَّتِهِ هَلْ بَلَّغَكُمْ فَيَقُولُونَ مَا أَتَانَا مِنْ نَذِيرٍ. فَيَقُولُ مَنْ يَشْهَدُ لَكَ فَيَقُولُ مُحَمَّدٌ وَأُمَّتُهُ. فَتَشْهَدُونَ أَنَّهُ قَدْ بَلَّغَ ". وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا فَذَلِكَ قَوْلُهُ جَلَّ ذِكْرُهُ وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا وَالْوَسَطُ الْعَدْلُ.
Amesimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nuwh ataitwa Siku ya Qiyaamah naye ataitikia: Labbayka wa Sa‘dayka, Ee Rabb! Allaah Atasema: Je, ulibalighisha ujumbe? Nuwh atasema: Naam! Ummah wake utaulizwa: Je amewabalighishia ujumbe? Watasema: Hakutujia mwonyaji yeyote! Allaah Atasema: Ni nani atakayekushuhudia? (Nuwh) atasema: Muhammad na Ummah wake.” Nanyi mtashuhudia kuwa yeye amebalighisha ujumbe.
وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ
Na awe Rasuli shahidi juu yenu. [Al-Baqarah (2:143)]
Na ndio iliyokusudiwa Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ
Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah bora na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu na awe Rasuli shahidi juu yenu. [Al-Baqarah (2:143)]
Na Al-Wasatw ni Uadilifu. [Al-Bukhaariy]
[50] Sababu Ya Kuitwa Masjid Al-Qiblatayn (Msikiti Wa Vibla Viwili):
Waislamu kwanza walielekea Baytul-Maqdis kama ndio Qiblah chao. Kisha ilipoteremshwa Aayah (2:144) ambayo alipewa amri Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ageuze uso wake kuelekea Masjd Al-Haraam Makkah, khabari zikawafikia Swahaba wakiwa ndani ya Swalaah, ndipo nao wakageuza Qiblah chao hapo hapo ndani ya Swalaah kuelekea Al-Ka’bah iliyoko Masjid Al-Haraam. Na kuanzia hapo Msikiti huo ukapewa jina la Masjid Al-Qiblatayn (Msikiti wa Vibla Viwili) yaani, kuelekea kwao ndani ya Swalaah moja, kwanza Baytul-Maqdis (Palestina) kisha kuelekea kwao Al-Ka’bah baada ya kuteremshwa Aayah Al-Baqarah (2:144).
[51] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
143-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 143: وَمَا كَانَ اللَّهُ لِيُضِيعَ إِيمَانَكُمْ [28]
[52] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
144-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 144: قَدْ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي السَّمَاءِ [29]
[53] Fadhila Za Subira Katika Mitihani, Maafa Na Misiba:
Rejea Al-Hadiyd (57:22-23)
La Kusema Na Kuomba Duaa Pindi Mtu Anapopatwa Msiba Au Janga Lolote Lile:
Aayah namba (156):
Muislamu apatapo msiba au janga lolote lile na si lazima liwe ni kufariki kwa mtu tu, bali ni kwa aina yoyote ile ya msiba, janga na balaa. Na pia ikiwa ni maradhi, au kupata khasara katika mali, au kupata mateso, au maafa ya aina yoyote, au mitihani, fitnah, n.k. Basi hapo hapo atamke kauli hii inayoitwa Istirjaa’ (kurejesha jambo kwa Allaah) kwani kutamka hivyo, atapata fadhila kadhaa zilizotajwa katika Aayah inayofuatia nazo ni Barakah na Rehma ya Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ
Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea.
Kisha aombe duaa ifuatayo kwani pindi mtu akiiomba, basi Allaah (سبحانه وتعالى) Humpa badala yake kilicho bora zaidi kuliko hicho alichopoteza au Humbadilishia hali ikawa bora kabisa. [Muslim (918) na Abu Daawuud (3115)]
اللَّهُمَّ أْجُرْنِي فِي مُصِيبَتِي وَأَخْلِفْ لِي خَيْرًا مِنْهَا
Allaahumma Ajirniy fiy muswiybatiy wa-Akhlif-liy khayran minhaa.
Ee Allaah! Nilipe katika msiba wangu huu, na Unipe badali iliyo bora kuliko hiyo.
[54] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
158-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 158: إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ [30]
[55] Jina Adhimu (Tukufu) Kabisa La Allaah (سبحانه وتعالى) Limo Katika Aayah Hii:
Amesimulia Asmaa bint Yaziyd (رضي الله عنها): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Jina Adhimu kabisa la Allaah limo katika Aayah zifuatazo:
وَإِلَهُكُمْ إِلَهٌ وَاحِدٌ لاَ إِلَهَ إلاَّ هُوَ الرَّحْمَنُ الرَّحِيمُ
[Al-Baqarah: (163)] na za mwanzo wa ‘Aal-‘Imraan:
الم اللَّهُ لاَ إِلَهَ إلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّوم
[Aal-‘Imraan: (1-2) - Swahiyh At-Tirmidhiy (3478), Swahiyh Ibn Maajah (3123), Swahiyh Al-Jaami’ (980), Swahiyh Abiy Daawuwd (1496) na Swahiyh At-Targhiyb (1642)]
[56] Amrisho La Kula Vilivyo Vizuri Na Vya Halali Na Ni Sababu Ya Kutaqabaliwa Duaa: Rejea Al-Muuminuwn (23:51).
[58] Furqaan: Pambanuo: Rejea Al-Furqaan (25:1) kwenye maelezo bayana.
[59] Ramadhwaan, Swiyaam Na Yanayohusu Duaa:
i-Ramadhwaan Ni Mwezi Wa Duaa Na Duaa Ya Mwenye Swawm Inaitikiwa:
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله) amesema: “Faida zinapatikana kutokana na Aayah hii. Kwanza: Kwamba kuna uwezekano mkubwa katika Swiyaam (funga) kuitikiwa duaa, kwa sababu Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja Aayah hii baada ya kutaja Aayah za Swiyaam, khasa vile Anavotaja mwishoni mwa kutaja Aayaat za Swiyaam. Pili: Baadhi ya watu wa ilimu wamesema kwamba inaweza kupatikana katika humo faida nyengineyo, kwamba duaa iombwe mwisho wa Siku ya Swawm (kabla ya kufuturu). [Tafsiyr Imaan Ibn ‘Uthaymiyn]
Na Hadiyth kadhaa zimethibitisha kuitikiwa duaa ya mwenye Swawm, miongoni mwazo ni:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((ثَلاثَةٌ لا تُرَدُّ دَعْوَتُهُمْ الإِمَامُ الْعَادِلُ وَالصَّائِمُ حِينَ يُفْطِرُ وَدَعْوَةُ الْمَظْلُومِ ))
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Watatu duaa zao hazirejeshwi: Imaam (kiongozi) mtenda haki, mwenye Swawm wakati anapofungua, na duaa ya aliyedhulumiwa.” [Imesimuliwa na At-Tirmidhiy Hadiyth nambari (2525), na Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh katika Swahihy At-Tirmidhiy Hadiyth nambari (2050)]
ii-Kuomba Duaa Kwa Allaah (عزّ وجلّ) Pekee Bila Ya Kumshirikisha:
Swahaba walikuwa wanamuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) maswali mbalimbali. Allaah (سبحانه وتعالى) Ameyataja katika Qur-aan na Akatoa majibu kwa kutanguliza kumwambia Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) aseme kuwajibu Swahaba “Sema!”. Mifano michache:
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ ...
Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema… [Al-Baqarah (2:219)]
يَسْأَلُكَ النَّاسُ عَنِ السَّاعَةِ ۖ قُلْ ...
Watu wanakuuliza kuhusu Saa (Qiyaamah). Sema… [Al-Ahzaab (33:63)]
وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ ...
Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema… [Al-Baqarah (2:222)]
Na maswali yote mengineyo katika Qur-aan, jibu la Allaah (سبحانه وتعالى) limeanzia hivyo hivyo: “Sema….” isipokuwa swali hili ambalo Allaah (عزّ وجلّ) Analijibu Mwenyewe moja kwa moja Anaposema:
فَإِنِّي قَرِيبٌ
Basi hakika Mimi ni Niko karibu.
Hivyo ni kwa sababu Allaah (سبحانه وتعالى) Anadhihirisha kwamba Yuko karibu kabisa na hakuhitaji mtu kuomba duaa kupitia kwa mtu yeyote ili isije kuwa ni kumshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) katika kuabudiwa Kwake, kwa sababu duaa ni ibaada kama alivyosema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth aliyosimulia Nu’umaan bin Bashiyr (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika kauli yake Allaah (سبحانه وتعالى)
وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ
Na Rabb wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni. Amesema: “Duaa ni ibaada.” Kisha akasoma Aayah hiyo tukufu. [Ghaafir (40:60)] [Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, na Ahmad – Hadiyth Hasan Swahiyh]
Basi watanabahi na wazingatie na wamche Allaah wanaomshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) katika duaa zao kupitia viumbe kama wafanyavyo wenye kutufu makaburi kuwaomba wafu, jambo ambalo linaingia katika shirki kubwa ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Haisamehi pindi mtu akifariki bila ya kutubia.
Rejea Ghaafir (40:60).
[63] Tamattu’: Aina Mojawapo Ya Hajj Kati Ya Aina Tatu:
Tamattu’: Mwenye kuhiji ananuia ‘Umrah katika miezi ya Hajj, kisha anajivua Ihraam baada ya kumaliza ‘Umrah yake, kisha anasubiri hadi siku ya Tarwiyyah; tarehe nane Dhul-Hijjah aingie tena katika Ihraam atekeleze yote yanayompasa ya Hajj. Aina hii ya Hajj ni lazima mwenye kuhiji achinje mnyama. Aina nyenginezo ni Ifraad na Qiraan na kila moja ina sifa na hukmu zake tofauti na hiyo ya Tamattu’.
[64] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
196-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 196: وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّـهِ [34]
[65] Miezi Ya Hajj:
Ibn ‘Umar (رضي الله عنه) amesema: “Miezi ya Hajj ni Shawwaal, Dhul-Qa’dah na siku kumi za mwanzo za Dhul-Hijjah. [Fat-hul-Baariy (3/491)]
[66] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
197-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 197: وَتَزَوَّدُوا فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَىٰ [35]
[69] Duaa Aliyokuwa Akiomba Sana Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ambayo Imejumuisha Kheri Za Dunia Na Aakhirah:
Amesimulia Anas (رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiomba sana duaa:
رَبَّنَا آتِنَا فِي اَلدُّنْيَا حَسَنَةً, وَفِي اَلْآخِرَةِ حَسَنَةً, وَقِنَا عَذَابَ اَلنَّارِ
Rabb wetu Tupe katika dunia mazuri na katika Aakhirah mazuri na Tukinge na adhabu ya moto. [Al-Bukhaariy na Muslim]
[70] Kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) Katika Siku Za Kuhesabika:
Ni siku za tashriyq (11, 12, 13 Dhul-Hijjah) kama alivyosema Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما). Na imetajwa kumdhukuru Allaah katika masiku maalumu katika Suwrah Al-Hajj (22:28).
[72] Kuteremka Allaah Na Malaika Siku Ya Qiyaamah:
Rejea Al-An’aam (6:158), Al-Furqaan (25:25), Al-Haaqah (69:13-18).
[74] Maana Ya Baghyun/Baghaa Katika Qur-aan:
Rejea Ash-Shuwraa (42:14) kupata maana zake mbalimbali.
[75] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
Hatua Za Uharamisho Wa Pombe Na Kikomo Chake.
Rejea An-Nisaa (4:43), na pia Al-Maaidah (5:90-91) ambako kuna maelezo bayana ya Hatua Za Uharamisho Wa Pombe Na Kikomo Chake.
[78] Haramisho La Kumuingilia Mwanamke Kupitia Dubur (Uchi Wa Nyuma):
Hadiyth kadhaa zimethibiti za haramisho lake, baadhi yake ni hizi zifuatazo:
“Allaah Hatomtazama mwanamume mwenye kumuingilia mkewe kwa nyuma.” [An-Nasaaiy na Ibn Hibbaan kwa Isnaad nzuri]
"Amelaaniwa mwenye kumuingilia mwanamke kwa nyuma." [Ahmad, Abuu Daawuwd na Ibn 'Adiy]
"Mwenye kumuingilia mwenye hedhi, au mwanamke kwa nyuma, au kumwendea mchawi na kumuamini kwa anayosema, basi amekufuru aliyoteremshiwa Muhammad." [Abu Daawuud, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah, na Isnaad yake ni Sahihi]
[80] Kutimiza Au Kuvunja Viapo: Rejea An-Nahl (16:92).
[81] Imekatazwa Kuapa Ovyo Ovyo:
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba Aayah hii ya Al-Baqarah (2:225):
لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ
Allaah Hatokushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi.
Ni kutokana na kauli ya mtu (kusema kwake mara kwa mara): “Hapana wa-Allaahi, ndio wa-Allaahi.” [Al-Bukhaariy Kitaab At-Tafsiyr]
Rejea Al-Maaidah (5:89) na Al-Qalam (68:10). Pia An-Nahl (16:92) kwenye maelezo bayana kuhusu kutimiza au kuvunja viapo.
[82] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
225-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 225: لَّا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ [43]
[84] Uharamu Wa Kuhalalisha Ndoa Baaba Ya Talaka Tatu:
Ni haramu kabisa kufunga nikaah ya uongo kwa ajili ya kuhalalisha ndoa baada ya talaka tatu. Amelaaniwa afanyaye hivyo. Amesimulia Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amemlaani anayefanya tahliyl (mhalalishaji ndoa) na mhalalishiwa, na wale wanaokula riba na wanaotoa riba.” [At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah na Ahmad]
[86] Hikma Ya Kufaridhiwa Eda Miezi Minne Na Siku Kumi:
Sa’iyd bin Muswayyib, Abuu ‘Aaliyah na wengineo wamesema kuwa: Hikma ya kuifanya eda ya mjane kuwa miezi minne na siku kumi ni kuwa yawezekana kuwepo mimba. Mwanamke anaposubiri kwa kipindi hicho itathibitika kama ana mimba au la. Na dalili ni Hadiyth ifuatayo: Kutoka kwa Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdillaah bin Mas-‘uwd (رضي الله عنه) kwamba: Ametusimulia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa: “Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho yake.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
[88]An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa): Hukmu Ya Kufutwa Eda Mwaka Mzima:
Hukumu ya eda hii ya mwaka mzima imefutwa na badala yake ni hukmu ya miezi minne na siku kumi. Rejea Aayah (2:234).
[90] Jina Tukufu Kabisa La Allaah (Al-Hayyu Al-Qayyuwm):
Aayah hii ina Jina Tukufu kabisa la Allaah katika Kauli Yake (تعالى):
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ
Na dalili ni Hadiyth ya Abuu Umaamah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ”Jina Tukufu kabisa la Allaah Ambalo likiombewa kwalo Anaitikia limo katika Suwrah tatu: Al-Baqarah, Aal-‘Imraan, na Twaaha’. [At-Tirmdhiy, Silsilah Asw-Swahiyhah (746)] Na mapokezi mengineyo yaliyothibitisha kuhusu Ismul-A’dhwam (Jina Tukufu kabisa).
[91] Hakuna Atakayemiliki Ash-Shafaa’ah (Uombezi) Isipokuwa Kwa Idhini Ya Allaah:
Rejea Twaahaa (20:109), An-Najm (53:26). Rejea pia Al-Israa (17:79) ambako kumetajwa kuwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Nabii Pekee atakayeruhusiwa ash-shafaa’ah atakapokuwa katika Maqaaman Mahmuwdan (Cheo Cha Kuhimidiwa).
[92] Kursiyy Ya Allaah (سبحانه وتعالى):
Kuhusu Kauli ya Allaah (تعالى):
وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ
Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi.
Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: “Iwapo mbingu saba na ardhi saba zingekunjuliwa na kulazwa sambamba, basi zingefikia kipimo cha (udogo wa) pete katika jangwa, kulinganisha na ‘Arsh.” [Ibn Abiy Haatim (3/981)]
[93] Al-‘Aliyyu Al-‘Adhwiym: Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Na Sifa Zake.
[94] Aayatul-Kursiyy Ni Aayah Tukufu Kabisa Katika Qur-aan
Aayah hii inayojulikana kwa Aayatul-Kursiyy, ni Aayah adhimu kabisa katika Qur-aan kwa dalili ya Hadiyth ya Muslim (810) kutoka kwa ‘Abdullaahi bin Rabaah Al-Answaariy kutoka kwa Ubayy bin Ka’b ambaye amehadithia: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Yaa Abal-Mundhir! Hivi unajua ni Aayah gani ndani ya Kitabu cha Allaah ambayo ni adhimu kabisa?” Nikasema: Allaah na Rasuli Wake Ni Wajuzi zaidi. Akasema: “Yaa Abal-Mundhir! Hivi unajua ni Aayah gani ndani ya Kitabu cha Allaah ambayo ni adhimu kabisa?” Akasema: Nikasema:
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ
Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Al-Hayyu (Aliye Hai daima) Al-Qayyuwm (Msimamia kila kitu). (mpaka mwisho wa Aayah).
Akasema Ubayy: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akanipiga kifuani kisha akasema: “Wa-Allaahi upongezwe kwa ilimu yako yaa Abal-Mundir.” [Muslim] Na katika mapokezi ya Ahmad imeendelea: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, Aayah hii ina ulimi na midomo miwili ambayo inamtukuza Mfalme (Allaah) katika mguu wa ‘Arsh.” [Swahiyh Targhiyb (1471)]
[95] Twaghuti:
Maana ya طَاغُوْتُ kilugha: Asili ya neno hilo linatokana na طغيان yenye kumaanisha uvukaji mipaka.
Na katika istilaahi, طُغْيَانُ ni kuasi, uvukaji mipaka, kwenda kinyume na Sharia ya Allaah (عزّ وجلّ), kuabudu asiyekuwa Muumba (Allaah), kwa sababu asili ya kuumbwa ni kumwabudu Allaah (عزّ وجلّ) Pekee. Na kumwabudu ipasavyo ni kama vile inavyotaka sharia. Kinyume chake ni uvukaji mipaka ya sharia na hivyo atakua mtu ameasi na amevuka mipaka.
‘Ulamaa wamefafanua twaghuti kuwa ni kila kinachoabudiwa pasi na Allaah. Kadhaalika twaghuti ni kila anayelingania watu katika upotofu, au kuwaongoza watu katika kufru, shirki, au kumuasi Allaah (سبحانه وتعالى). Mifano ya twaghuti ni ibliys, shaytwaan, mizimu, mchawi, mganga, na kahini (mtabiri). Hali kadhaalika, twaghuti ni anayedai kuwa anajua ilimu ya ghaibu. Hayo yote ni uvukaji mipaka wa kutoka kwenye haki kuelekea ubatwilifu.
Aayah inayofuatia imetaja pia twaghuti. Na rejea An-Nisaa (4:51), (4:60), (4:76), Al-Maaidah (5:60), An-Nahl (16:36), Az-Zumar (39:17).
[97] Nimruwdh Mfalme Dhalimu Aliyejifanya Ni Mwabudiwa Aliyebishana Na Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) Akafishwa Kwa Mbu Kuingia Sikioni Na Puani Mwake:
Jina lake ni Nimruwdh bin Kina’aan, bin Rayb, bin Nimruwdh bin Kuwsh bin Nuwh (عليه السّلام).
Alikuwa mfalme kafiri, dhalimu, mwenye kiburi, aliyejifanya jabari, aliyeitawala dunia kutoka katika ufalme wake Baabiyl huko Iraq katika zama za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام). Nimruwdh alikuwa dhalimu wa kwanza katika ardhi aliyedai kuwa yeye ndiye apasaye kuabudiwa, ndipo Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) alipobishana naye kuhusu kudai kwake hivyo, akampa changamoto hiyo iliyotajwa katika Aayah ya kumtaka alifanye jua lichomoze Magharibi badala ya kuchomza Mashariki, akashindwa na akahizika!
Kifo cha Nimruwdh kimesimuliwa katika Hadiyth za Israaiyliyyaat na hakuna kosa kusimulia ili tupate kupata mafunzo yake. Na katika kisa hiki tunapata funzo kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Alimfisha mfalme aliyejidai kuwa yeye ndiye anayepasa kuabudiwa, kwa kidudu dhalili na kidogo mno! [Hadiyth ya ‘Amr bin Al-Aasw (رضي الله عنه) ameipokea Al-Bukhaariy]
Imaam Atw-Twabariy ameitoa katika Jaami’u Al-Bayaan (14/204) kutoka kwa Zayd bin Aslam kwamba: “Nimruwdh hakika alikuwa dhalimu wa kwanza duniani. Allaah (سبحانه وتعالى) Akampelekea mbu, wakaingia masikioni na puani mwake. Alibaki kujipiga kichwa chake kwa nyundo kwa miaka mia nne! Watu waliokuwa na huruma zaidi walikuwa ni wale waliounganisha mikono wakawa wanampiga kichwani (kutuliza mbu). Alijifanya jabari na alikuwa dhalimu kwa muda wa miaka mia nne, basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akamuadhibu miaka mia nne sawa na muda wa utawala wake. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akamfisha.”
[98] Mja Aliyefishwa Miaka Mia Ni ‘Uzayr?
Wafasiri wa Qur-aan wamekhitilafiana kama mja huyo aliyepita katika kijiji kilichoporomoka akafishwa miaka mia ni ‘Uzayr au la. Na kauli iliyo mashuhuri ni kwamba aliyekusudiwa hapo ni ‘Uzayr. [Imepokewa na Ibn Jariyr na Ibn Abiy Haatim kutoka kwa Ibn ‘Abbaas, Al-Hasan, Qataadah, As-Suddiy, na Sulaymaan Bin Buraydah [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Mayahudi wamesema kuwa yeye ni Nabiy miongoni mwa Manabii wa Bani Israa’iyl lakini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuthibitisha hilo. Rejea At-Tawbah (9:30).
[99] Fadhila Za Kutoa Mali Kwa Ajili Ya Allaah:
Fadhila za kutoa mali kwa ajili ya Allaah, na maonyo yanayohusiana na utoaji wa swadaqa yametajwa katika Suwrah hii ya Al-Baqarah kuanzia Aayah hii namba (261) hadi namba (267). Kisha Aayah (270) hadi (274).
Kisha rejea Al-Hadiyd (57:11) kwenye viungo vingi vilivyo na faida tele kuhusu fadhila za kutoa mali kwa ajili ya Allaah zikiwemo rejea mbalimbali za Aayah za Qur-aan na Hadiyth.
[100] Riyaa-a (Kujionyesha Kwa Watu) Ni Shirki Inayobatwilisha Amali:
Hii ni riyaa-a ya kutoa mali katika njia ya Allaah. Rejea An-Nisaa (4:142). Rejea pia Az-Zumar (39:65) kwenye maelezo kuhusu aina za shirki.
[103] Adhabu Za Anayejihusisha Na Riba:
Hadiyth kadhaa za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) zimethibiti kutahadharisha riba na adhabu zake, miongoni mwazo ni:
“Dirhamu ya riba anayokula mtu na huku anajua, ni mbaya zaidi kuliko kuzini mara thelathini na sita.” [Ahmad]
“Riba ina milango sabini na tatu (73). Iliyo nyepesi na sahali ni mtu kumuoa mamake.” [Al-Haakim]
“Jiepusheni na mambo saba yenye kuangamiza… kula riba.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
[104] Anayejihusisha Na Riba Atangaze Vita Baina Yake Na Allaah Na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم)
Ilipoteremka Aayah namba (2:275), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: “Yeyote asiyejizuia kufanya “mukhaabarah” (kukodisha shamba kwa malipo ya kugawana sehemu ya mazao), basi apokee tangazo la vita kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[105] Aayah Ya Mwisho Kuteremshwa:
‘Ulamaa wengi wamekubaliana kwamba hii ni Aayah ya mwisho kuteremshwa. Na miongoni mwa Salaf waliokiri ni Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما), na Sa’iyd bin Jubayr (رحمه الله) kwa Riwayaah mbalimbali, kwamba baada ya kuteremshwa Aayah hii, yalipita masiku kadhaa kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akafariki. [An-Nasaaiy – Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Na Imaam As-Sa’dy (رحمه الله) amesema: “Hii ni Aayah ya mwisho iliyoteremshwa katika Qur-aan, na ikafanywa ni hatima ya hukmu hizi za maamrisho na makatazo kwa sababu humo mna ahadi za kutenda mema na kheri, na onyo kali la kutenda maovu. Na kwamba anayejua kwamba yeye atarejeshwa kwa Allaah, basi Allaah Atamlipa kwa dogo na kubwa (aliyoyatenda), na yaliyodhahiri na ya siri, na kwamba Allaah Hatomdhulumu uzito wa chembe ya hardali (au atomu). Hivyo basi itamwajibikia awe na raghbah (utashi, matumaini) na khofu. Na bila kuyajua hayo moyoni, kutakuwa hakuna sababu ya kuongozwa kuyatekeleza.”
[106] An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa):
Aayah hii imefutwa hukmu yake. Na badala yake ikateremshwa Aayah ya mwisho ya Suwrah hii:
لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ
Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. [Al-Baqarah: (286)]
[108] Mawlaa: Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake.
[109] Fadhila Za Aayah Mbili Za Mwisho Suwrah Al-Baqarah:
(i) Kutokuhesabiwa katika kusahau na kukosea.
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ummah wangu umenyanyuliwa makosa na kusahau na wanayoshurutishwa.” [Ibn Maajah, Ibn Hibbaan, Ad-Daaraqutwniy, At-Twabaraaniy na Al-Haakim, Irwaa Al-Ghaliyl (1027)]
(ii) Atakayezisoma usiku zitamtosheleza:
Abuu Mas‘uwd Al-Answaariyy ‘Uqbah bin ‘Amr bin Tha’alabah (رضي الله عنه) amesimulia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayesoma usiku Aayah mbili za mwisho wa Suwratul-Baqarah zitamtosheleza.” Yaani: zinamtosheleza kumkinga na kila baya na kila lenye kumdhuru. [Al-Bukhaariy na Muslim]
(iii) Hakuna Nabiy aliyepewa Aayah hizi isipokuwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):
Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesimulia: Jibriyl (عليه السّلام) alipokuwa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisikia sauti kutoka juu. Jibriyl (عليه السّلام) akatazama juu akasema: “Huu mlango wa mbinguni umefunguliwa na haujapatapo kamwe kufunguliwa isipokuwa leo! Malaika akateremka humo akasema: Huyu Malaika ameteremka ardhini, hajapatapo kuteremka kamwe isipokuwa leo! Akasalimia kisha akasema: Pokea bishara ya Nuru mbili ulizopewa ambazo hakuna Nabiy aliyepewa kabla yako: Ufunguo wa Kitabu (Al-Faatihah), na Aayah (mbili) za mwisho wa Suwratul-Baqarah. Hutosoma herufi humo ila utapewa barakah zake zilizomo.” [Muslim]
(iv) Aayah mbili hizi ni Aayah pekee ambazo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Amepewa Wahy mbinguni wakati alipofika mbingu ya saba katika tukio la Al-Israa Wal-Mi’raaj.
Hadiyth ya Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipopelekwa safari ya usiku mbinguni (Al-Israa Wal-Mi’raaj), aliishia Sidratul-Muntahaa (Mkunazi wa mpaka wa mwisho kabisa) katika mbingu ya sita ambapo huishia kila kitu (hakuna ajuaye ilimu ya baada ya hapo isipokuwa Allaah) ambapo pia kunaishia kila kinachopanda kutoka ardhini (amali za watu n.k) na kushikiliwa hapo, na kinapoishia kila kitu kinachoteremka kutoka juu yake na kushikiliwa hapo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ ﴿١٦﴾
Ulipoufunika mkunazi huo unachokifunika. [An-Najm: (16)]
(Msimulizi) akasema: (kilichofunika mkunazi) ni vipepeo vya dhahabu. Akasema: Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akapewa (mambo) matatu: Akapewa Swalaah tano za kila siku, na akapewa hitimisho la Suwrah Al-Baqarah, na kughufuriwa katika ummah wake ambaye hamshirikishi Allaah na chochote. [Muslim]
آل عِمْران
003-Aal-‘Imraan
003-Aal-'Imraan: Utangulizi Wa Suwrah [51]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الم ﴿١﴾
1. Alif Laam Miym.[1]
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ﴿٢﴾
2. Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Al-Hayyu (Aliye Hai daima) Al-Qayyuwm (Msimamia kila kitu).[2]
نَزَّلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَأَنزَلَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ﴿٣﴾
3. Amekuteremshia Kitabu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki kinachosadikisha yaliyo kabla yake na Akateremsha Tawraat na Injiyl.
مِن قَبْلُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَأَنزَلَ الْفُرْقَانَ ۗ إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٤﴾
4. Kabla (ya kuteremshwa Qur-aan), iwe ni mwongozo kwa watu na Akateremsha pambanuo (la haki na baatwil). Hakika wale waliokufuru Aayaat (na Ishara, Hoja, Dalili) za Allaah watapata adhabu kali. Na Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kulipiza.
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَخْفَىٰ عَلَيْهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ ﴿٥﴾
5. Hakika Allaah Hakifichiki Kwake chochote katika ardhi wala katika mbingu.
هُوَ الَّذِي يُصَوِّرُكُمْ فِي الْأَرْحَامِ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦﴾
6. Yeye Ndiye Anayekusawirini umbo katika matumbo ya uzazi vile Atakavyo.[3] Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ ۖ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ ۗ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّـهُ ۗ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٧﴾
7. Yeye Ndiye Aliyekuteremshia Kitabu. Humo mna Aayaat zenye maana wazi, hizo ndio msingi wa Kitabu, na nyinginezo zisizokuwa wazi maana zake. Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotovu hufuata zile zisizokuwa wazi maana zake kutafuta fitnah (upotofu)[4] na kutafuta maana zake zilizofichika, na hakuna ajuae maana zake isipokuwa Allaah. Na wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Tumeziamini, zote ni kutoka kwa Rabb wetu. Na hawakumbuki ila wenye akili.[5]
رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ ﴿٨﴾
8. (Husema): Rabb wetu! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kuwa Umetuhidi na Tutunukie kutoka Kwako Rehma. Hakika Wewe Ni Mwingi wa Kutunuku na Kuneemesha.
رَبَّنَا إِنَّكَ جَامِعُ النَّاسِ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُخْلِفُ الْمِيعَادَ ﴿٩﴾
9. Rabb wetu! Hakika Wewe Ni Mkusanyaji watu Siku isiyo na shaka ndani yake. Hakika Allaah Havunji miadi.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَن تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمْ وَقُودُ النَّارِ ﴿١٠﴾
10. Hakika wale waliokufuru hazitowafaa kitu mali zao wala watoto wao mbele ya Allaah, na hao ndio kuni za moto.
كَدَأْبِ آلِ فِرْعَوْنَ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا فَأَخَذَهُمُ اللَّـهُ بِذُنُوبِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿١١﴾
11. Kama mwenendo wa watu wa Firawni na wale waliokuwa kabla yao. Walikadhibisha Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu na Allaah Akawaadhibu kwa madhambi yao, na Allaah Ni Mkali wa Kuakibu.[6]
قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا سَتُغْلَبُونَ وَتُحْشَرُونَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ ۚ وَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿١٢﴾
12. Waambie waliokufuru: Mtashindwa na mtakusanywa katika Jahannam, na ni pabaya mno mahala hapo pa kupumzika.
قَدْ كَانَ لَكُمْ آيَةٌ فِي فِئَتَيْنِ الْتَقَتَا ۖ فِئَةٌ تُقَاتِلُ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَأُخْرَىٰ كَافِرَةٌ يَرَوْنَهُم مِّثْلَيْهِمْ رَأْيَ الْعَيْنِ ۚ وَاللَّـهُ يُؤَيِّدُ بِنَصْرِهِ مَن يَشَاءُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّأُولِي الْأَبْصَارِ ﴿١٣﴾
13. Kwa hakika ilikuwa ni Aayah (Dalili, Funzo na Zingatio) kwenu katika makundi mawili yalipokutana (Vita vya Badr). Kundi linapigana katika Njia ya Allaah na jingine la makafiri. Wanawaona (Waislamu) mara mbili yao kwa mtazamo wa macho. Na Allaah Humsaidia kwa Nusura Yake Amtakaye. Hakika katika hayo bila shaka kuna mazingatio kwa wenye utambuzi.
زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْبَنِينَ وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ الْمُسَوَّمَةِ وَالْأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ ۗ ذَٰلِكَ مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الْمَآبِ ﴿١٤﴾
14. Watu wamepambiwa huba ya matamanio ya kupenda wanawake na watoto, mirundi ya mali iliyolimbikizwa ya dhahabu na fedha, farasi wenye chapa ya aina bora, wanyama wa mifugo na mashamba. Hayo ni starehe za uhai wa dunia, na marejeo mazuri yako Kwake Allaah.
قُلْ أَؤُنَبِّئُكُم بِخَيْرٍ مِّن ذَٰلِكُمْ ۚ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَأَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ وَرِضْوَانٌ مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴿١٥﴾
15. Sema: Je, nikujulisheni yaliyo bora kuliko hayo? Kwa wale waliokuwa na taqwa, watapata kwa Rabb wao Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo, pamoja na wake waliotakasika na Radhi kutoka kwa Allaah. Na Allaah Ni Mwenye Kuwaona vyema waja.
الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا إِنَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ﴿١٦﴾
16. Wale wasemao: Rabb wetu! Hakika sisi tumeamini, basi Tughufurie madhambi yetu na Tukinge na adhabu ya moto.
الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ﴿١٧﴾
17. Wenye kuvuta subira, wasemao kweli, watiifu, watoaji mali katika Njia ya Allaah na waombao maghfirah kabla ya Alfajiri.[7]
شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾
18. Allaah Ameshuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, na (pia) Malaika na wenye ilimu wameshuhudia hilo. Na Yeye mbali ya hilo, Anasifika kwa uadilifu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ ۗ وَمَا اخْتَلَفَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِآيَاتِ اللَّـهِ فَإِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿١٩﴾
19. Hakika Dini mbele ya Allaah ni Uislamu.[8] Na hawakukhitilafiana wale waliopewa Kitabu ila baada ya kuwajia ilimu kutokana na baghi[9] (chuki na hasadi) iliyotamalaki baina yao. Na atakayekanusha Aayaat (na Ishara, Dalili) za Allaah basi hakika Allaah Ni Mwepesi wa Kuhesabu.
فَإِنْ حَاجُّوكَ فَقُلْ أَسْلَمْتُ وَجْهِيَ لِلَّـهِ وَمَنِ اتَّبَعَنِ ۗ وَقُل لِّلَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْأُمِّيِّينَ أَأَسْلَمْتُمْ ۚ فَإِنْ أَسْلَمُوا فَقَدِ اهْتَدَوا ۖ وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴿٢٠﴾
20. Na wakikuhoji, basi sema: Nimejisalimisha kwa Allaah mimi pamoja na walionifuata. Na waambie waliopewa Kitabu na wasiojua kusoma na kuandika: Je, mmesilimu? Wakisilimu basi wamehidika, na wakikengeuka basi hakika juu yako ni kubalighisha tu. Na Allaah Ni Mwenye Kuwaona waja.[10]
إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَيَقْتُلُونَ الَّذِينَ يَأْمُرُونَ بِالْقِسْطِ مِنَ النَّاسِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٢١﴾
21. Hakika wanaokanusha Aayaat (na Ishara, Dalili) za Allaah na wakaua Manabii bila ya haki, na wakaua wale wanaoamrisha haki miongoni mwa watu, basi wabashirie adhabu iumizayo.
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٢٢﴾
22. Hao ndio ambao amali zao zimeporomoka katika dunia na Aakhirah na hawatopata watu wa kuwasaidia.
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُدْعَوْنَ إِلَىٰ كِتَابِ اللَّـهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ وَهُم مُّعْرِضُونَ ﴿٢٣﴾
23. Je, hukuzingatia wale waliopewa sehemu katika Kitabu wanaitwa katika Kitabu cha Allaah ili kiwahukumu baina yao, kisha kundi miongoni mwao linageuka na huku wanapuuza.
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَن تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ۖ وَغَرَّهُمْ فِي دِينِهِم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٢٤﴾
24. Hivyo ni kwa sababu wamesema: Hautotugusa moto isipokuwa siku chache za kuhesabika. Na yakawadanganya katika dini yao yale waliyokuwa wakiyatunga (ya uongo).
فَكَيْفَ إِذَا جَمَعْنَاهُمْ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ وَوُفِّيَتْ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٢٥﴾
25. Basi itakuwa vipi Tutakapowakusanya katika Siku ambayo haina shaka ndani yake, na kila nafsi italipwa kikamilifu yale iliyochuma, nao hawatodhulumiwa.
قُلِ اللَّـهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَن تَشَاءُ وَتَنزِعُ الْمُلْكَ مِمَّن تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَاءُ ۖ بِيَدِكَ الْخَيْرُ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٦﴾
26. Sema: Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote, Unampa ufalme Umtakaye, na Unamuondoshea ufalme Umtakaye, na Unamtukuza Umtakaye, na Unamdhalilisha Umtakaye, kheri imo Mkononi Mwako. Hakika Wewe Ni Muweza wa kila kitu.
تُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَتُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ ۖ وَتُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَتُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ ۖ وَتَرْزُقُ مَن تَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٢٧﴾
27. Unauingiza usiku katika mchana na Unauingiza mchana katika usiku, na Unatoa kilicho hai kutokana na kilicho mfu na Unatoa kilicho mfu kutokana na kilicho hai[11], na Unamruzuku Umtakaye bila ya hesabu.
لَّا يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللَّـهِ فِي شَيْءٍ إِلَّا أَن تَتَّقُوا مِنْهُمْ تُقَاةً ۗ وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ ۗ وَإِلَى اللَّـهِ الْمَصِيرُ ﴿٢٨﴾
28. Waumini wasiwafanye makafiri kuwa marafiki wandani na walinzi badala ya Waumini. Na atakayefanya hivyo, basi hatokua na chochote mbele ya Allaah, isipokuwa ikiwa kwa ajili ya kujilinda hatari kutoka kwao. Na Allaah Anakutahadharisheni na Nafsi Yake.[12] Na kwa Allaah ni mahali pa kuishia.
قُلْ إِن تُخْفُوا مَا فِي صُدُورِكُمْ أَوْ تُبْدُوهُ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ وَيَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٩﴾
29. Sema: Mkificha yale yaliyomo katika vifua vyenu au mkiyafichua, Allaah Anayajua. Na Anajua yale yaliyomo katika mbingu na yale yaliyomo katika ardhi. Na Allaah Ni Muweza wa kila kitu.
يَوْمَ تَجِدُ كُلُّ نَفْسٍ مَّا عَمِلَتْ مِنْ خَيْرٍ مُّحْضَرًا وَمَا عَمِلَتْ مِن سُوءٍ تَوَدُّ لَوْ أَنَّ بَيْنَهَا وَبَيْنَهُ أَمَدًا بَعِيدًا ۗ وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ ۗ وَاللَّـهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ ﴿٣٠﴾
30. Siku itayokuta kila nafsi yale iliyoyatenda katika kheri yamehudhurishwa, na yale iliyoyatenda katika maovu, itatamani nafsi lau kama ingelikuwa baina yake na baina ya (maovu) hayo masafa ya mbali. Na Allaah Anakutahadharisheni na Nafsi Yake Na Allaah Ni Mwenye Huruma mno kwa waja.
قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾
31. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Allaah Atakupendeni na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.[13]
قُلْ أَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ ﴿٣٢﴾
32. Sema: Mtiini Allaah na Rasuli, lakini mkikengeuka basi hakika Allaah Hapendi makafiri.
إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ آدَمَ وَنُوحًا وَآلَ إِبْرَاهِيمَ وَآلَ عِمْرَانَ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٣٣﴾
33. Hakika Allaah Amemkhitari Aadam na Nuwh na kizazi cha Ibraahiym na kizazi cha ‘Imraan juu ya walimwengu.
ذُرِّيَّةً بَعْضُهَا مِن بَعْضٍ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٣٤﴾
34. Kizazi cha wao kwa wao, na Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
إِذْ قَالَتِ امْرَأَتُ عِمْرَانَ رَبِّ إِنِّي نَذَرْتُ لَكَ مَا فِي بَطْنِي مُحَرَّرًا فَتَقَبَّلْ مِنِّي ۖ إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٣٥﴾
35. Pale aliposema mke wa ‘Imraan: Rabb wangu! Hakika mimi nimeweka nadhiri Kwako kilichomo katika tumbo langu kuwa ni wakfu kukutumikia, basi Nitakabalie. Hakika Wewe Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote[14].
فَلَمَّا وَضَعَتْهَا قَالَتْ رَبِّ إِنِّي وَضَعْتُهَا أُنثَىٰ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا وَضَعَتْ وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالْأُنثَىٰ ۖ وَإِنِّي سَمَّيْتُهَا مَرْيَمَ وَإِنِّي أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ ﴿٣٦﴾
36. Basi alipomzaa akasema: Rabb wangu! Hakika mimi nimezaa mwanamke, na Allaah Anajua zaidi alichokizaa. Na mwanamme si kama mwanamke. Nami nimemwita Maryam, nami namkinga Kwako na dhuria wake kutokana na shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa.
فَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٍ وَأَنبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنًا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّا ۖ كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيْهَا زَكَرِيَّا الْمِحْرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزْقًا ۖ قَالَ يَا مَرْيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَـٰذَا ۖ قَالَتْ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ ۖ إِنَّ اللَّـهَ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٣٧﴾
37. Basi Rabb wake Akampokea kwa kabuli njema, na Akamkuza mkuzo mwema, na Akamfanya Zakariyyaa kuwa mlezi wake. Kila Zakariyyaa alipoingia kwake katika chumba cha kuswalia alikuta kwake vyakula. Akasema: Ee Maryam! Umepata wapi hivi? Akasema: Hivi ni kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah Anamruzuku Amtakaye bila ya hesabu.[15]
هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُ ۖ قَالَ رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً ۖ إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ ﴿٣٨﴾
38. Hapo hapo Zakariyyaa akamwomba Rabb wake, akasema: Rabb wangu! Nitunukie kutoka Kwako kizazi chema, hakika Wewe Ni Mwenye Kusikia duaa yangu.
فَنَادَتْهُ الْمَلَائِكَةُ وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي فِي الْمِحْرَابِ أَنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحْيَىٰ مُصَدِّقًا بِكَلِمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَسَيِّدًا وَحَصُورًا وَنَبِيًّا مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٣٩﴾
39. Malaika wakamwita (Zakariyyaa) naye akiwa amesimama anaswali katika chumba chake cha ibaada wakamwambia: Hakika Allaah Anakubashiria Yahyaa atakayesadikisha Neno (la Kun!) kutoka kwa Allaah. Atakuwa mtu wa kuheshimika, mtawa anayejitenga mbali na matamanio, na Nabiy miongoni mwa Swalihina.[16]
قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَقَدْ بَلَغَنِيَ الْكِبَرُ وَامْرَأَتِي عَاقِرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكَ اللَّـهُ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ ﴿٤٠﴾
40. (Zakariyyaa) akasema: Nitapataje ghulamu (mwana) na hali uzee umeshanifikia na mke wangu ni tasa?! Akasema: Hivyo ndivyo Allaah Anafanya Atakavyo.
قَالَ رَبِّ اجْعَل لِّي آيَةً ۖ قَالَ آيَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ النَّاسَ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ إِلَّا رَمْزًا ۗ وَاذْكُر رَّبَّكَ كَثِيرًا وَسَبِّحْ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ ﴿٤١﴾
41. (Zakariyyaa) akasema: Rabb wangu! Niwekee Aayah (Ishara). Akasema: Aayah (Ishara) yako ni kwamba hutoweza kuwasemesha watu siku tatu ila kwa kuashiria tu. Na mdhukuru Rabb wako kwa wingi na msabihi jioni na asubuhi.
وَإِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَاكِ وَطَهَّرَكِ وَاصْطَفَاكِ عَلَىٰ نِسَاءِ الْعَالَمِينَ ﴿٤٢﴾
42. Na pale Malaika (Jibriyl) aliposema:[17] Ee Maryam! Hakika Allaah Amekuteua na Amekutakasa na Amekukhitari juu ya wanawake wa walimwengu.[18]
يَا مَرْيَمُ اقْنُتِي لِرَبِّكِ وَاسْجُدِي وَارْكَعِي مَعَ الرَّاكِعِينَ ﴿٤٣﴾
43. Ee Maryam! Kuwa mtiifu kwa Rabb wako, na sujudu, na rukuu pamoja na wanaorukuu.
ذَٰلِكَ مِنْ أَنبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهِ إِلَيْكَ ۚ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يُلْقُونَ أَقْلَامَهُمْ أَيُّهُمْ يَكْفُلُ مَرْيَمَ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يَخْتَصِمُونَ ﴿٤٤﴾
44. Hizo ni khabari za ghaibu Tunakufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na hukuwa pamoja nao walipotupa kalamu zao[19], ili nani kati yao amlee Maryam. Na hukuwa pamoja nao waliposhindana.
إِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٍ مِّنْهُ اسْمُهُ الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ وَجِيهًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ ﴿٤٥﴾
45. Na pale Malaika waliposema: Ee Maryam! Hakika Allaah Anakubashiria Neno (la Kun!) kutoka Kwake (umzae mtoto), jina lake ni Al-Masiyhu ‘Iysaa mwana wa Maryam, mwenye taadhima katika dunia na Aakhirah, na ni miongoni mwa waliokurubishwa (kwa Allaah).
وَيُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا وَمِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٤٦﴾
46. Na Atawasemesha watu utotoni mwake na katika utu uzima wake, na ni miongoni mwa Swalihina.
قَالَتْ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي وَلَدٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكِ اللَّـهُ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ إِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٤٧﴾
47. (Maryam) Akasema: Itakuwaje nipate mtoto na hali hakunigusa mtu? (Malaika) Akasema: Hivyo ndivyo Allaah Huumba Akitakacho. Anapohukumu jambo basi huliambia: Kun! (Kuwa!) Basi nalo huwa.
وَيُعَلِّمُهُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ﴿٤٨﴾
48. Na Atamfunza Kitabu na Hikmah na Tawraat na Injiyl.
وَرَسُولًا إِلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنِّي قَدْ جِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ أَنِّي أَخْلُقُ لَكُم مِّنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ فَأَنفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۖ وَأُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ وَأُحْيِي الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۖ وَأُنَبِّئُكُم بِمَا تَأْكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِي بُيُوتِكُمْ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٤٩﴾
49. Na ni Rasuli kwa wana wa Israaiyl (atakayewaambia): Hakika mimi nimekujieni na Aayah (Dalili, Muujiza) kutoka kwa Rabb wenu, kwamba mimi nakuundieni kutokana na udongo, mfano wa umbo la ndege, kisha napuliza humo na anakuwa ndege kwa Idhini ya Allaah. Na naponyesha vipofu na wenye ubarasi, na nahuisha wafu kwa Idhini ya Allaah. Isitoshe, nakujulisheni pia mtakavyokula na mtakavyoweka akiba majumbani mwenu. Hakika katika hayo bila shaka kuna Aayah (Ishara, Dalili) kwenu mkiwa Waumini.[20]
وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَلِأُحِلَّ لَكُم بَعْضَ الَّذِي حُرِّمَ عَلَيْكُمْ ۚ وَجِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿٥٠﴾
50. Na mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat, na ili nikuhalalishieni baadhi ya yale yaliyoharamishwa kwenu. Na nimekujieni na Aayah (Ishara, Dalili, Hoja) kutoka kwa Rabb wenu. Basi mcheni Allaah na nitiini.
إِنَّ اللَّـهَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۗ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ﴿٥١﴾
51. Hakika Allaah ni Rabb wangu na Rabb wenu basi mwabuduni. Hii ndio njia iliyonyooka.
فَلَمَّا أَحَسَّ عِيسَىٰ مِنْهُمُ الْكُفْرَ قَالَ مَنْ أَنصَارِي إِلَى اللَّـهِ ۖ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللَّـهِ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَاشْهَدْ بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٥٢﴾
52. Basi ‘Iysaa alipohisi ukafiri kutoka kwao alisema: Nani watakaokuwa wasaidizi wangu kwa ajili ya Allaah? Wakasema wafuasi watiifu: Sisi ni wasaidizi wa Allaah. Tumemwamini Allaah, na shuhudia kwamba sisi ni Waislamu (wenye kujisalimisha Kwake).
رَبَّنَا آمَنَّا بِمَا أَنزَلْتَ وَاتَّبَعْنَا الرَّسُولَ فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ ﴿٥٣﴾
53. Rabb wetu! Tumeamini Uliyoyateremsha na tumemfuata Rasuli, basi Tuandike pamoja na wanaoshuhudia (haki).
وَمَكَرُوا وَمَكَرَ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ ﴿٥٤﴾
54. Wakapanga makri (njama) na Allaah Akapanga makri. Na Allaah Ni Mbora wa wenye kupanga makri.[21]
إِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَىٰ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ وَمُطَهِّرُكَ مِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا وَجَاعِلُ الَّذِينَ اتَّبَعُوكَ فَوْقَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۖ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأَحْكُمُ بَيْنَكُمْ فِيمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿٥٥﴾
55. Pale Allaah Aliposema: Ee ‘Iysaa! Hakika Mimi Nitakuchukua na Nitakupandisha Kwangu na Nitakutakasa na wale waliokufuru na Nitawafanya wale waliokufuata (kujisalimisha kwa Allaah) kuwa juu ya wale waliokufuru mpaka Siku ya Qiyaamah, kisha Kwangu ndio marejeo yenu na Nitahukumu baina yenu katika yale mliyokuwa mkikhitilafiana.[22]
فَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَأُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٥٦﴾
56. Ama wale waliokufuru, Nitawaadhibu adhabu kali katika dunia na Aakhirah, na hawatopata wa kuwasaidia.
وَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُوَفِّيهِمْ أُجُورَهُمْ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ ﴿٥٧﴾
57. Na ama wale waliomini na wakatenda mema, basi hao Atawalipa ujira wao kikamilifu. Na Allaah Hapendi madhalimu.
ذَٰلِكَ نَتْلُوهُ عَلَيْكَ مِنَ الْآيَاتِ وَالذِّكْرِ الْحَكِيمِ ﴿٥٨﴾
58. Hizi Tunazokusomea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ni katika Aayaat na ukumbusho wenye hikmah.
إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ اللَّـهِ كَمَثَلِ آدَمَ ۖ خَلَقَهُ مِن تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٥٩﴾
59. Hakika mfano wa ‘Iysaa kwa Allaah ni kama mfano wa Aadam. Amemuumba kutokana na udongo kisha Akamwambia: Kun! Basi akawa.[23]
الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُن مِّنَ الْمُمْتَرِينَ ﴿٦٠﴾
60. Ni Haki kutoka kwa Rabb wako, basi usiwe miongoni mwa wanaotia shaka.
فَمَنْ حَاجَّكَ فِيهِ مِن بَعْدِ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ فَقُلْ تَعَالَوْا نَدْعُ أَبْنَاءَنَا وَأَبْنَاءَكُمْ وَنِسَاءَنَا وَنِسَاءَكُمْ وَأَنفُسَنَا وَأَنفُسَكُمْ ثُمَّ نَبْتَهِلْ فَنَجْعَل لَّعْنَتَ اللَّـهِ عَلَى الْكَاذِبِينَ ﴿٦١﴾
61. Basi yeyote atakayekuhoji kwayo baada ya kukujia ilimu, sema: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na sisi wenyewe na nyinyi wenyewe, kisha tuombe kwa unyenyekevu Laana ya Allaah iwe juu ya waongo (mubaahalah).[24]
إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْقَصَصُ الْحَقُّ ۚ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦٢﴾
62. Kwa hakika haya ni masimulizi ya haki. Na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah. Na hakika Allaah Yeye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِالْمُفْسِدِينَ ﴿٦٣﴾
63. Wakikengeuka, basi hakika Allaah ni Mjuzi wa mafisadi.
قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٦٤﴾
64. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, kwamba tusiabudu isipokuwa Allaah Pekee, na wala tusimshirikishe na chochote, na wala wasichukue baadhi yetu wengine kuwa miola badala ya Allaah. Wakikengeuka, basi semeni: Shuhudieni kwamba sisi ni Waislamu.
يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تُحَاجُّونَ فِي إِبْرَاهِيمَ وَمَا أُنزِلَتِ التَّوْرَاةُ وَالْإِنجِيلُ إِلَّا مِن بَعْدِهِ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٥﴾
65. Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnahojiana kuhusu Ibraahiym na hali haikuteremshwa Tawraat na Injiyl isipokuwa baada yake? Je, hamtii akilini?
هَا أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ حَاجَجْتُمْ فِيمَا لَكُم بِهِ عِلْمٌ فَلِمَ تُحَاجُّونَ فِيمَا لَيْسَ لَكُم بِهِ عِلْمٌ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٦٦﴾
66. Ha! Nyinyi ndio hawa mliohojiana katika yale ambayo mnayo ilimu nayo, basi kwa nini mnahojiana katika yale msiyokuwa na ilimu nayo? Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui.
مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَـٰكِن كَانَ حَنِيفًا مُّسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٦٧﴾
67. Ibraahiym hakuwa Yahudi wala Naswara, lakini alikuwa mwenye kujiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki, Muislamu na hakuwa miongoni mwa washirikina.[25]
إِنَّ أَوْلَى النَّاسِ بِإِبْرَاهِيمَ لَلَّذِينَ اتَّبَعُوهُ وَهَـٰذَا النَّبِيُّ وَالَّذِينَ آمَنُوا ۗ وَاللَّـهُ وَلِيُّ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٦٨﴾
68. Hakika watu walio karibu zaidi kwa Ibraahiym ni wale waliomfuata na huyu Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na wale walioamini. Na Allaah Ni Rafiki Mlinzi wa Waumini.
وَدَّت طَّائِفَةٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يُضِلُّونَكُمْ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٦٩﴾
69. Linatamani kundi katika Watu wa Kitabu kama wangelikupotezeni, lakini hawapotezi ila nafsi zao na wao hawahisi.
يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَأَنتُمْ تَشْهَدُونَ ﴿٧٠﴾
70. Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnakanusha Aayaat (na Ishara, Miujiza, Dalili) za Allaah na hali nyinyi mnashuhudia?
يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَلْبِسُونَ الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٧١﴾
71. Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnachanganya haki na baatwil na mnaficha haki na hali nyinyi mnajua?
وَقَالَت طَّائِفَةٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ آمِنُوا بِالَّذِي أُنزِلَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَجْهَ النَّهَارِ وَاكْفُرُوا آخِرَهُ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٧٢﴾
72. Na kundi miongoni mwa Watu wa Kitabu likasema (kuambiana): Aminini yale ambayo yameteremshwa kwa wale walioamini mwanzo wa mchana na kanusheni mwisho wake, wapate kurejea (waache dini yao).
وَلَا تُؤْمِنُوا إِلَّا لِمَن تَبِعَ دِينَكُمْ قُلْ إِنَّ الْهُدَىٰ هُدَى اللَّـهِ أَن يُؤْتَىٰ أَحَدٌ مِّثْلَ مَا أُوتِيتُمْ أَوْ يُحَاجُّوكُمْ عِندَ رَبِّكُمْ ۗ قُلْ إِنَّ الْفَضْلَ بِيَدِ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٧٣﴾
73. Na wala msimwamini isipokuwa yule anayefuata dini yenu. Sema: Hakika mwongozo wa kweli ni Mwongozo wa Allaah, (mnakhofu) kwamba atapewa mmoja (ilimu) mfano wa yale mliyopewa au wakuhojini mbele ya Rabb wenu. Sema: Hakika fadhila zi Mkononi mwa Allaah, Humpa Amtakaye. Na Allaah Ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.
يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٧٤﴾
74. Humchagua kwa Rehma Yake Amtakaye, na Allaah Ni Mwenye Fadhila kuu kabisa.
وَمِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مَنْ إِن تَأْمَنْهُ بِقِنطَارٍ يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ وَمِنْهُم مَّنْ إِن تَأْمَنْهُ بِدِينَارٍ لَّا يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ إِلَّا مَا دُمْتَ عَلَيْهِ قَائِمًا ۗ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَيْسَ عَلَيْنَا فِي الْأُمِّيِّينَ سَبِيلٌ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٥﴾
75. Na katika Watu wa Kitabu yuko ambaye ukimpa amana ya mrundi wa mali atakurejeshea, na katika wao yuko ambaye ukimpa amana ya dinari moja tu hatoirudisha kwako isipokuwa utakapodumisha kumsimamia (kumdai). Hilo ni kwa sababu wao wamesema: Hakuna juu yetu lawama kwa wasiojua kusoma na kuandika na wanamsingizia uongo Allaah, na hali wao wanajua.
بَلَىٰ مَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ وَاتَّقَىٰ فَإِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ ﴿٧٦﴾
76. Sivyo hivyo! Bali atakayetimiza ahadi yake akawa na taqwa, basi hakika Allaah Anapenda wenye taqwa.
إِنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللَّـهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَنًا قَلِيلًا أُولَـٰئِكَ لَا خَلَاقَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّـهُ وَلَا يَنظُرُ إِلَيْهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٧﴾
77. Hakika wale wanaobadilisha Ahadi ya Allaah na viapo vyao kwa thamani ndogo, hao hawana sehemu yoyote katika Aakhirah na wala Allaah Hatowasemesha na wala Hatowatazama Siku Ya Qiyaamah na wala Hatowatakasa na watapata adhabu iumizayo.[26]
وَإِنَّ مِنْهُمْ لَفَرِيقًا يَلْوُونَ أَلْسِنَتَهُم بِالْكِتَابِ لِتَحْسَبُوهُ مِنَ الْكِتَابِ وَمَا هُوَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَقُولُونَ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَمَا هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٨﴾
78. Na hakika miongoni mwao kuna kundi wanaopotosha Kitabu kwa ndimi zao (wanaposoma) ili mdhanie kuwa hayo yanayotoka katika Kitabu, na hali hayo si yenye kutoka katika Kitabu, na wanasema: Hayo ni kutoka kwa Allaah, ilhali hayo si kutoka kwa Allaah, na wanamsingizia uongo Allaah na wao wanajua.
مَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُؤْتِيَهُ اللَّـهُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُوا عِبَادًا لِّي مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِن كُونُوا رَبَّانِيِّينَ بِمَا كُنتُمْ تُعَلِّمُونَ الْكِتَابَ وَبِمَا كُنتُمْ تَدْرُسُونَ ﴿٧٩﴾
79. Ni mustahili kwa mtu kwamba Allaah Amempa Kitabu na Al-Hukma[27] na Unabii kisha aje awaambie watu: Kuweni wenye kuniabudu mimi badala ya Allaah, bali (atawaambia): Kuweni Rabbaaniyyuwn[28] (Marabi) kwa yale mliyokuwa mkiyafundisha ya Kitabu na kwa yale mliyokuwa mkiyadurusu.
وَلَا يَأْمُرَكُمْ أَن تَتَّخِذُوا الْمَلَائِكَةَ وَالنَّبِيِّينَ أَرْبَابًا ۗ أَيَأْمُرُكُم بِالْكُفْرِ بَعْدَ إِذْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿٨٠﴾
80. Na wala hakuamuruni kuwachukua Malaika na Manabii kuwafanya miola. Je, anakuamrisheni ukafiri baada ya nyinyi kuwa mmejisalimisha kwa Allaah?
وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ النَّبِيِّينَ لَمَا آتَيْتُكُم مِّن كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنصُرُنَّهُ ۚ قَالَ أَأَقْرَرْتُمْ وَأَخَذْتُمْ عَلَىٰ ذَٰلِكُمْ إِصْرِي ۖ قَالُوا أَقْرَرْنَا ۚ قَالَ فَاشْهَدُوا وَأَنَا مَعَكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨١﴾
81. Na pale Allaah Alipochukua fungamano kwa Manabii (akawaambia): Ninayokupeni katika Kitabu na Hikmah, kisha akakujieni Rasuli (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nanyi, basi ni lazima kumwamini na kumnusuru. (Kisha Allaah) Akasema: Je, mmekubali na mtashika fungamano Langu juu ya hayo? Wakasema: Tumekubali. (Allaah) Akasema: Basi shuhudieni na Mimi Niko pamoja nanyi katika wenye kushuhudia.[29]
فَمَن تَوَلَّىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿٨٢﴾
82. Atakayekengeuka baada ya hayo, basi hao ni mafasiki.
أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّـهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ ﴿٨٣﴾
83. Je, wanataka dini isiyokuwa ya Allaah, na hali amejisalimisha Kwake kila aliye katika mbingu na katika ardhi akipenda asipende na Kwake watarejeshwa?
قُلْ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ عَلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَالنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿٨٤﴾
84. Sema: Tumemwamini Allaah, na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym, na Ismaa’iyl na Is-haaq, na Ya’quwb na Al-Asbaatw[30] (kizazi chake), na yale aliyopewa Muwsaa na ‘Iysaa na Manabii kutoka kwa Rabb wao, hatutofautishi baina ya yeyote miongoni mwao, nasi ni Waislamu Wenye kujisalimisha) Kwake.
وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾
85. Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake, naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.[31]
كَيْفَ يَهْدِي اللَّـهُ قَوْمًا كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ وَشَهِدُوا أَنَّ الرَّسُولَ حَقٌّ وَجَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٦﴾
86. Vipi Allaah Atawaongoza watu waliokufuru baada ya kuamini kwao na wakashuhudia kwamba Rasuli ni haki na zikawajia hoja bayana? Na Allaah Hawahidi watu madhalimu.[32]
أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُمْ أَنَّ عَلَيْهِمْ لَعْنَةَ اللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿٨٧﴾
87. Hao jazaa yao ni kwamba juu yao ipo Laana ya Allaah na ya Malaika na ya watu wote.
خَالِدِينَ فِيهَا لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿٨٨﴾
88. Wadumu humo, hawatopunguziwa adhabu wala hawatopewa muda wa kuakhirishwa adhabu.
إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٨٩﴾
89. Isipokuwa wale waliotubu baada ya hayo na wakatengeneza, kwani hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَّن تُقْبَلَ تَوْبَتُهُمْ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الضَّالُّونَ ﴿٩٠﴾
90. Hakika wale waliokufuru baada ya kuamini kwao kisha wakazidi kukufuru, haitokubaliwa tawbah yao, na hao ndio waliopotoka.[33]
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِم مِّلْءُ الْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ افْتَدَىٰ بِهِ ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٩١﴾
91. Hakika wale waliokufuru na wakafa nao wakiwa makafiri, basi kamwe haitakubaliwa kutoka kwa mmoja wao, dhahabu ya ujazo wa dunia nzima lau wakitaka kujifidia nayo. Hao watapata adhabu iumizayo na hawatopata watu wa kuwasaidia.
لَن تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٩٢﴾
92. Hamtoweza kuufikia wema uliokunjuka mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda. Na kitu chochote mnachotoa basi hakika Allaah kwacho Ni Mjuzi.
كُلُّ الطَّعَامِ كَانَ حِلًّا لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ إِلَّا مَا حَرَّمَ إِسْرَائِيلُ عَلَىٰ نَفْسِهِ مِن قَبْلِ أَن تُنَزَّلَ التَّوْرَاةُ ۗ قُلْ فَأْتُوا بِالتَّوْرَاةِ فَاتْلُوهَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٩٣﴾
93. Kila chakula kilikuwa halali kwa wana wa Israaiyl, isipokuwa kile alichojiharamishia Israaiyl[34] (Ya’quwb (عليه السّلام mwenyewe kabla ya kuteremshwa Tawraat. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Basi leteni Tawraat kisha muisome mkiwa wakweli.
فَمَنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٩٤﴾
94. Na yeyote atakayemtungia Allaah uongo baada ya hayo, basi hao ndio madhalimu.
قُلْ صَدَقَ اللَّـهُ ۗ فَاتَّبِعُوا مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٩٥﴾
95. Sema: Allaah Amesema kweli. Basi fuateni mila ya Ibraahiym aliyejiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki na hakuwa miongoni mwa washirikina.[35]
إِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِّلْعَالَمِينَ ﴿٩٦﴾
96. Hakika nyumba (Al-Ka’bah) ya awali iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ibaada) ni ile ambayo iko Bakkah (Makkah),[36] yenye barakah na mwongozo kwa walimwengu.
فِيهِ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ مَّقَامُ إِبْرَاهِيمَ ۖ وَمَن دَخَلَهُ كَانَ آمِنًا ۗ وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٩٧﴾
97. Ndani yake kuna Aayaat (Ishara na Dalili) zilizo wazi mahali aliposimama Ibraahiym (kujenga). Na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Allaah imewajibika watu watekeleze Hajj katika nyumba (Al-Ka’bah) hiyo kwa mwenye uwezo. Na atakayekufuru, basi hakika Allaah Ni Mkwasi kwa walimwengu.
قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَاللَّـهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا تَعْمَلُونَ ﴿٩٨﴾
98. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnakanusha Aayaat (na Ishara, Miujiza, Dalili) za Allaah ilhali Allaah Ni Shahidi juu ya myatendayo?
قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ مَنْ آمَنَ تَبْغُونَهَا عِوَجًا وَأَنتُمْ شُهَدَاءُ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٩٩﴾
99. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnamzuilia aliyeamini Njia ya Allaah, mnaitafutia ionekane kombo na hali nyinyi ni mashahidi (juu ya haki)? Na Allaah Si Mwenye Kughafilika na hayo myatendayo.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تُطِيعُوا فَرِيقًا مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ يَرُدُّوكُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ كَافِرِينَ ﴿١٠٠﴾
100. Enyi walioamini! Mkilitii kundi la waliopewa Kitabu watakurudisheni baada ya nyinyi kuamini muwe makafiri.
وَكَيْفَ تَكْفُرُونَ وَأَنتُمْ تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ آيَاتُ اللَّـهِ وَفِيكُمْ رَسُولُهُ ۗ وَمَن يَعْتَصِم بِاللَّـهِ فَقَدْ هُدِيَ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٠١﴾
101. Na vipi mkufuru na hali mnasomewa Aayaat za Allaah na Rasuli Wake yuko kati yenu? Na atakayeshikamana na Allaah basi kwa yakini ameongozwa kuelekea njia iliyonyooka.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٠٢﴾
102. Enyi walioamini! Mcheni Allaah kama ipasavyo kumcha na chungeni sana, angalieni msife isipokuwa nyinyi ni Waislamu.
وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ النَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿١٠٣﴾
103. Na shikamaneni kwa Kamba ya Allaah nyote pamoja, wala msifarikiane.[37] Na kumbukeni Neema ya Allaah juu yenu, pale mlipokuwa maadui (kati yenu), kisha Akaunganisha nyoyo zenu, mkawa ndugu kwa Neema Yake, na mlikuwa ukingoni mwa shimo la moto Akakuokoeni humo. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na Ishara) Zake mpate kuhidika.
وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفلِحُونَ ﴿١٠٤﴾
104. Na watokeze kutoka kwenu ummah wa watu unaolingania kheri, na unaoamrisha mema na unaokataza munkari. Na hao ndio waliofaulu.
وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١٠٥﴾
105. Na wala msiwe kama wale waliofarikiana na wakakhitilafiana[38] baada ya kuwajia hoja bayana. Na hao watapata adhabu kuu kabisa.
يَوْمَ تَبْيَضُّ وُجُوهٌ وَتَسْوَدُّ وُجُوهٌ ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ اسْوَدَّتْ وُجُوهُهُمْ أَكَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿١٠٦﴾
106. Siku nyuso zitakuwa nyeupe na nyuso (nyingine) zitakuwa nyeusi. Basi wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeusi[39] (wataambiwa): Je, mlikufuru baada ya kuamini kwenu?! Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyakanusha.
وَأَمَّا الَّذِينَ ابْيَضَّتْ وُجُوهُهُمْ فَفِي رَحْمَةِ اللَّـهِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿١٠٧﴾
107. Na wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeupe, basi watakuwa katika Rehma ya Allaah. Wao humo watadumu.
تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ ۗ وَمَا اللَّـهُ يُرِيدُ ظُلْمًا لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٠٨﴾
108. Hizi ni Aayaat za Allaah Tunakusomea kwa haki (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na Allaah Hataki dhulma kwa walimwengu.
وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿١٠٩﴾
109. Na ni vya Allaah vilivyomo katika mbingu na katika ardhi. Na kwa Allaah Pekee mambo (yote) yatarejeshwa.
كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿١١٠﴾
110. Mmekuwa ummah bora[40] kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu, mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Watu wa Kitabu, basi ingelikuwa ni bora kwao. Wako miongoni mwao wanaoamini lakini wengi wao ni mafasiki.
لَن يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى ۖ وَإِن يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنصَرُونَ ﴿١١١﴾
111. Hawatokudhuruni isipokuwa udhia tu, na wakikupigeni vita watakupeni migongo (wakimbie), kisha hawatonusuriwa.
ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا إِلَّا بِحَبْلٍ مِّنَ اللَّـهِ وَحَبْلٍ مِّنَ النَّاسِ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الْمَسْكَنَةُ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿١١٢﴾
112. Wamepigwa na udhalili popote wanapopatikana ila tu pale wanapolindwa na Ahadi ya Allaah na ahadi ya watu, na (pamoja na hayo) wamestahiki ghadhabu kutoka kwa Allaah, na wakapigwa na umasikini. Sababu ya hayo ni kuwa wao walikuwa wakikanusha Aayaat (na Ishara, Dalili) za Allaah na wakiua Manabii pasi na haki. Hayo (pia) ni kwa sababu ya kuasi kwao, na walikuwa wanataadi (kuvuka mipaka).
لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ ﴿١١٣﴾
113. Hawako sawa sawa. Miongoni mwa Watu wa Kitabu wako watu wenye kusimama (kwa utiifu), wanasoma Aayaat za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu (katika Swalaah).[41]
يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَأُولَـٰئِكَ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١١٤﴾
114. Wanamwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na wanaamrisha mema na wanakataza munkari[42] na wanakimbilia katika mambo ya kheri, na hao ni miongoni mwa Swalihina.
وَمَا يَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَلَن يُكْفَرُوهُ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالْمُتَّقِينَ ﴿١١٥﴾
115. Na kheri yoyote waifanyayo basi hawatokanushiwa (thawabu zake). Na Allaah Anawajua vyema wenye taqwa.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَن تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۖ وَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۚ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿١١٦﴾
116. Hakika wale waliokufuru hazitowafaa kitu mali zao wala watoto wao mbele ya Allaah. Hao ni watu wa motoni. Wao humo watadumu.
مَثَلُ مَا يُنفِقُونَ فِي هَـٰذِهِ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَثَلِ رِيحٍ فِيهَا صِرٌّ أَصَابَتْ حَرْثَ قَوْمٍ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ فَأَهْلَكَتْهُ ۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ اللَّـهُ وَلَـٰكِنْ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿١١٧﴾
117. Mfano wa vile wanavyovitoa katika uhai (wao) huu wa duniani ni kama mfano wa upepo ndani yake mna baridi ya barafu, ukasibu shamba lilolimwa la watu waliojidhulumu nafsi zao ukaliangamiza. Na Allaah Hakuwadhulumu lakini wamejidhulumu nafsi zao.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِّن دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالًا وَدُّوا مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ ۚ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١١٨﴾
118. Enyi walioamini! Msifanye rafiki mwandani na msiri (wenu) wasiokuwa nyinyi. Hawatoacha kukuharibieni. Wanatamani kama mngetaabika. Imekwishajitokeza bughudha kutoka midomoni mwao. Na yale yanayoficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Aayaat (Ishara, Dalili, Alama) [zao] mkiwa mtatia akilini.
هَا أَنتُمْ أُولَاءِ تُحِبُّونَهُمْ وَلَا يُحِبُّونَكُمْ وَتُؤْمِنُونَ بِالْكِتَابِ كُلِّهِ وَإِذَا لَقُوكُمْ قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا عَضُّوا عَلَيْكُمُ الْأَنَامِلَ مِنَ الْغَيْظِ ۚ قُلْ مُوتُوا بِغَيْظِكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿١١٩﴾
119. Ha! Nyinyi ndio wale mnaowapenda na wala wao hawakupendeni, na mnaamini Kitabu chote, na wanapokukuteni husema: Tumeamini, na wanapokuwa peke yao wanakutafunieni ncha za vidole kutokana na chuki. Sema: Kufeni kwa chuki zenu! Hakika Allaah Anayajua vyema yaliyomo vifuani.
إِن تَمْسَسْكُمْ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ وَإِن تُصِبْكُمْ سَيِّئَةٌ يَفْرَحُوا بِهَا ۖ وَإِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا لَا يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ ﴿١٢٠﴾
120. Ikikupateni kheri (nusura, ushindi) inawachukiza, na likikusibuni baya hulifurahia. Na kama mtasubiri na mkashikamana na taqwa, basi hila zao hazitakudhuruni kitu. Hakika Allaah Ni Mwenye Kuyazunguka wayatendayo.
وَإِذْ غَدَوْتَ مِنْ أَهْلِكَ تُبَوِّئُ الْمُؤْمِنِينَ مَقَاعِدَ لِلْقِتَالِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿١٢١﴾
121. Na pale ulipotoka asubuhi mapema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ukaacha ahli zako ili uwapangie Waumini vituo vya kupigana (Vita vya Uhud).[43] Na Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
إِذْ هَمَّت طَّائِفَتَانِ مِنكُمْ أَن تَفْشَلَا وَاللَّـهُ وَلِيُّهُمَا ۗ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٢٢﴾
122. Pale makundi mawili miongoni mwenu walipofanya wasiwasi kwamba watashindwa nailhali Allaah Ndiye Rafiki Mlinzi wao. Basi kwa Allaah Pekee Waumini watawakali.[44]
وَلَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّـهُ بِبَدْرٍ وَأَنتُمْ أَذِلَّةٌ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٢٣﴾
123. Kwa yakini Allaah Alikunusuruni katika Badr[45] na hali nyinyi ni wanyonge. Basi mcheni Allaah mpate kushukuru.
إِذْ تَقُولُ لِلْمُؤْمِنِينَ أَلَن يَكْفِيَكُمْ أَن يُمِدَّكُمْ رَبُّكُم بِثَلَاثَةِ آلَافٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُنزَلِينَ ﴿١٢٤﴾
124. Pindi ulipowaambia Waumini: Je, haikutosheni ikiwa Rabb wenu Atakuongezeeni nguvu kwa Malaika elfu tatu walioteremshwa?
بَلَىٰ ۚ إِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا وَيَأْتُوكُم مِّن فَوْرِهِمْ هَـٰذَا يُمْدِدْكُمْ رَبُّكُم بِخَمْسَةِ آلَافٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُسَوِّمِينَ ﴿١٢٥﴾
125. Bali, naam! Mkisubiri na mkashikamana na taqwa na hata wakikujieni kwa ghafla hivi (kukumalizeni), basi (mkitekeleza mawili hayo), Rabb wenu Atakuongezeeni nguvu kwa Malaika elfu tano waliojitia wenyewe na farasi wao alama maalum.
وَمَا جَعَلَهُ اللَّـهُ إِلَّا بُشْرَىٰ لَكُمْ وَلِتَطْمَئِنَّ قُلُوبُكُم بِهِ ۗ وَمَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ ﴿١٢٦﴾
126. Na Allaah Hakujaalia hayo isipokuwa ni bishara kwenu, na ili zitue nyoyo zenu kwayo. Na hakuna ushindi isipokuwa kutoka kwa Allaah Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
لِيَقْطَعَ طَرَفًا مِّنَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَوْ يَكْبِتَهُمْ فَيَنقَلِبُوا خَائِبِينَ ﴿١٢٧﴾
127. Ili Akate sehemu ya waliokufuru au Awafedheheshe, warudi nyuma wakiwa wamekata tamaa.
لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾
128. Jambo hili halikuhusu wewe, ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu.[46]
وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ يَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢٩﴾
129. Ni vya Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na katika ardhi. Anamghufuria Amtakaye na Anamuadhibu Amtakaye. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا الرِّبَا أَضْعَافًا مُّضَاعَفَةً ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٣٠﴾
130. Enyi walioamini! Msile riba mkizidisha maradufu juu ya maradufu. Na mcheni Allaah mpate kufaulu.[47]
وَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ ﴿١٣١﴾
131. Na uogopeni moto ambao umeandaliwa kwa makafiri.
وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٣٢﴾
132. Na mtiini Allaah na Rasuli mpate kurehemewa.
وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ﴿١٣٣﴾
133. Na kimbilieni maghfirah kutoka kwa Rabb wenu, na Jannah upana wake ni wa mbingu na ardhi imeandaliwa kwa wenye taqwa.
الَّذِينَ يُنفِقُونَ فِي السَّرَّاءِ وَالضَّرَّاءِ وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣٤﴾
134. Ambao wanatoa (kwa ajili ya Allaah) katika hali ya wasaa na katika hali ya shida, na wanazuia ghadhabu, na wenye kusamehe watu. Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.
وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٣٥﴾
135. Na ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao (kwa maasi), humdhukuru Allaah wakaomba maghfirah kwa madhambi yao. Na nani anayeghufuria madhambi isipokuwa Allaah. Na hawaendelei katika waliyoyafanya na hali wanajua.[48]
أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُم مَّغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَجَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿١٣٦﴾
136. Hao jazaa yao ni maghfirah kutoka kwa Rabb wao na Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo. Ni uzuri ulioje ujira wa watendaji (wema).
قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُمْ سُنَنٌ فَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكذِّبِينَ ﴿١٣٧﴾
137. Kwa hakika zimekwishapita kabla yenu nyendo nyingi (kama hali yenu), basi tembeeni katika ardhi kisha mtazame vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha.[49]
هَـٰذَا بَيَانٌ لِّلنَّاسِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ ﴿١٣٨﴾
138. Hii (Qur-aan) ni ubainisho kwa watu na mwongozo na mawaidha kwa wenye taqwa.
وَلَا تَهِنُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَنتُمُ الْأَعْلَوْنَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٣٩﴾
139. Na wala msilegee na wala msihuzunike ilhali nyinyi mko juu mkiwa ni Waumini.
إِن يَمْسَسْكُمْ قَرْحٌ فَقَدْ مَسَّ الْقَوْمَ قَرْحٌ مِّثْلُهُ ۚ وَتِلْكَ الْأَيَّامُ نُدَاوِلُهَا بَيْنَ النَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَيَتَّخِذَ مِنكُمْ شُهَدَاءَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ ﴿١٤٠﴾
140. Yakikupateni majeraha basi yamekwishawapata watu majeraha kama hayo. Na hizo ni siku Tunazizungusha zamu (za mabadiliko ya hali) baina ya watu, na ili Allaah Adhihirishe walioamini na Afanye miongoni mwenu Shuhadaa[50] (waliofariki katika vita vya Jihaad). Na Allaah Hapendi madhalimu.
وَلِيُمَحِّصَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَيَمْحَقَ الْكَافِرِينَ ﴿١٤١﴾
141. Na ili Allaah Awajaribu (au Awatakase) walioamini na Awafutilie mbali makafiri.
أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّـهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنكُمْ وَيَعْلَمَ الصَّابِرِينَ ﴿١٤٢﴾
142. Je, Mnadhani kwamba mtaingia Jannah na hali Allaah bado Hajawadhihirisha wale waliofanya Jihaad miongoni mwenu na Akadhihirisha wenye subira?
وَلَقَدْ كُنتُمْ تَمَنَّوْنَ الْمَوْتَ مِن قَبْلِ أَن تَلْقَوْهُ فَقَدْ رَأَيْتُمُوهُ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ ﴿١٤٣﴾
143. Na kwa yakini mlikuwa mnatamani mauti kabla hamjakutana nayo, basi mmekwishayaona na huku mnayatazama.
وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ ۚ أَفَإِن مَّاتَ أَوْ قُتِلَ انقَلَبْتُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُمْ ۚ وَمَن يَنقَلِبْ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ فَلَن يَضُرَّ اللَّـهَ شَيْئًا ۗ وَسَيَجْزِي اللَّـهُ الشَّاكِرِينَ ﴿١٤٤﴾
144. Na Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuwa isipokuwa ni Rasuli tu. Wamekwishapita kabla yake Rusuli. Je, akifa au akiuawa ndio mtageuka nyuma mrudi mlikotoka (ukafirini)? Na atakayegeuka nyuma akarudi alikotoka basi hatomdhuru Allaah kwa chochote. Na Allaah Atawalipa wenye kushukuru.
وَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَن تَمُوتَ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ كِتَابًا مُّؤَجَّلًا ۗ وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ الْآخِرَةِ نُؤْتِهِ مِنْهَا ۚ وَسَنَجْزِي الشَّاكِرِينَ ﴿١٤٥﴾
145. Na haiwezekani nafsi yeyote kufa isipokuwa kwa Idhini ya Allaah, kwani imeandikiwa muda wake maalumu. Na yeyote anayetaka malipo ya dunia basi Tutampa sehemu tu ya hayo (Tuliyomkadiria). Na yeyote anayetaka thawabu za Aakhirah basi Tutampa sehemu ya hayo (bila mipaka) na Tutawalipa wenye kushukuru.
وَكَأَيِّن مِّن نَّبِيٍّ قَاتَلَ مَعَهُ رِبِّيُّونَ كَثِيرٌ فَمَا وَهَنُوا لِمَا أَصَابَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَمَا ضَعُفُوا وَمَا اسْتَكَانُوا ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الصَّابِرِينَ ﴿١٤٦﴾
146. Na Manabii wangapi walipigana vita wakiwa pamoja nao Waumini wengi waliojaa imaan ya kikweli, basi hawakulegea kwa yaliyowasibu katika Njia ya Allaah, wala hawakudhoofika na wala hawakunyong’onyea. Na Allaah Anapenda wenye subira.
وَمَا كَانَ قَوْلَهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَإِسْرَافَنَا فِي أَمْرِنَا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿١٤٧﴾
147. Na haikuwa kauli yao isipokuwa walisema: Rabb wetu! Tughufurie madhambi yetu na upindukaji wetu mipaka katika mambo yetu, na Ithibitishe miguu yetu na Tunusuru dhidi ya watu makafiri.
فَآتَاهُمُ اللَّـهُ ثَوَابَ الدُّنْيَا وَحُسْنَ ثَوَابِ الْآخِرَةِ ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٤٨﴾
148. Basi Allaah Akawalipa malipo ya dunia na thawabu nzuri za Aakhirah. Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تُطِيعُوا الَّذِينَ كَفَرُوا يَرُدُّوكُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُمْ فَتَنقَلِبُوا خَاسِرِينَ ﴿١٤٩﴾
149. Enyi walioamini! Mkiwatii wale waliokufuru watakurudisheni nyuma mlikotoka kisha mtageuka mkiwa wenye kukhasirika.
بَلِ اللَّـهُ مَوْلَاكُمْ ۖ وَهُوَ خَيْرُ النَّاصِرِينَ ﴿١٥٠﴾
150. Bali Allaah Ndio Rafiki Mlinzi wenu. Naye Ndiye Mbora kabisa kuliko wote wenye kusaidia.
سَنُلْقِي فِي قُلُوبِ الَّذِينَ كَفَرُوا الرُّعْبَ بِمَا أَشْرَكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا ۖ وَمَأْوَاهُمُ النَّارُ ۚ وَبِئْسَ مَثْوَى الظَّالِمِينَ ﴿١٥١﴾
151. Tutatia hofu na woga katika nyoyo za waliokufuru kwa sababu ya kumshirikisha Allaah na (masanamu) ambayo Hakuyateremshia hoja wala dalili (kwamba yanastahiki kuabudiwa). Na makazi yao ni moto, na ubaya ulioje maskani ya madhalimu.
وَلَقَدْ صَدَقَكُمُ اللَّـهُ وَعْدَهُ إِذْ تَحُسُّونَهُم بِإِذْنِهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا فَشِلْتُمْ وَتَنَازَعْتُمْ فِي الْأَمْرِ وَعَصَيْتُم مِّن بَعْدِ مَا أَرَاكُم مَّا تُحِبُّونَ ۚ مِنكُم مَّن يُرِيدُ الدُّنْيَا وَمِنكُم مَّن يُرِيدُ الْآخِرَةَ ۚ ثُمَّ صَرَفَكُمْ عَنْهُمْ لِيَبْتَلِيَكُمْ ۖ وَلَقَدْ عَفَا عَنكُمْ ۗ وَاللَّـهُ ذُو فَضْلٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٥٢﴾
152. Na kwa yakini Allaah Amekwisha kusadikishieni Ahadi Yake mlipowaua vikali kwa Idhini Yake, mpaka mliposhindwa na mkazozana katika amri (aliyokupeni Rasuli) na mkaasi baada ya Yeye kukuonyesheni yale mnayoyapenda. Miongoni mwenu wako wenye kutaka dunia, na miongoni mwenu wako wenye kutaka Aakhirah. Kisha Akakugeuzeni nyuma mbali nao (hao maadui) ili Akujaribuni. Na kwa yakini Amekwisha kusameheni. Na Allaah Ni Mwenye Fadhila kwa Waumini.
إِذْ تُصْعِدُونَ وَلَا تَلْوُونَ عَلَىٰ أَحَدٍ وَالرَّسُولُ يَدْعُوكُمْ فِي أُخْرَاكُمْ فَأَثَابَكُمْ غَمًّا بِغَمٍّ لِّكَيْلَا تَحْزَنُوا عَلَىٰ مَا فَاتَكُمْ وَلَا مَا أَصَابَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿١٥٣﴾
153. Pale mlipotimka kukimbia mbali wala hamgeuki nyuma kumtazama yeyote, na Rasuli anakuiteni nyuma yenu, kisha Allaah Akakulipizeni dhiki juu ya dhiki ili (kukufundisheni) msihuzunike kwa yaliyokupiteni na wala kwa yaliyokusibuni. Na Allaah Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri kwa yale myatendayo.
ثُمَّ أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّن بَعْدِ الْغَمِّ أَمَنَةً نُّعَاسًا يَغْشَىٰ طَائِفَةً مِّنكُمْ ۖ وَطَائِفَةٌ قَدْ أَهَمَّتْهُمْ أَنفُسُهُمْ يَظُنُّونَ بِاللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ ظَنَّ الْجَاهِلِيَّةِ ۖ يَقُولُونَ هَل لَّنَا مِنَ الْأَمْرِ مِن شَيْءٍ ۗ قُلْ إِنَّ الْأَمْرَ كُلَّهُ لِلَّـهِ ۗ يُخْفُونَ فِي أَنفُسِهِم مَّا لَا يُبْدُونَ لَكَ ۖ يَقُولُونَ لَوْ كَانَ لَنَا مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ مَّا قُتِلْنَا هَاهُنَا ۗ قُل لَّوْ كُنتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ الَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقَتْلُ إِلَىٰ مَضَاجِعِهِمْ ۖ وَلِيَبْتَلِيَ اللَّـهُ مَا فِي صُدُورِكُمْ وَلِيُمَحِّصَ مَا فِي قُلُوبِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿١٥٤﴾
154. Kisha Akakuteremshieni amani baada ya dhiki; usingizi unaofunika kundi miongoni mwenu na kundi likawashughulisha nafsi zao wakamdhania Allaah pasi na haki dhana ya kijahili, wanasema: Je, tuna amri yoyote sisi katika jambo hili? Sema: Hakika amri yote ni ya Allaah. Wanaficha katika nafsi zao yale wasiyokubainishia. Wanasema: Lau tungelikuwa tuna amri yoyote katika jambo basi tusingeliuliwa hapa. Sema: Lau mngelikuwa majumbani mwenu, bila shaka wangejitokeza wale walioandikiwa kuuawa kwenye mahali pa kuangukia wafe. Ili Allaah Ayajaribu yale yaliyomo katika vifua vyenu na Atakase yale yaliyomo katika nyoyo zenu. Na Allaah Anayajua vyema yaliyomo vifuani.[51]
إِنَّ الَّذِينَ تَوَلَّوْا مِنكُمْ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ إِنَّمَا اسْتَزَلَّهُمُ الشَّيْطَانُ بِبَعْضِ مَا كَسَبُوا ۖ وَلَقَدْ عَفَا اللَّـهُ عَنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿١٥٥﴾
155. Hakika wale waliokengeuka miongoni mwenu siku yalipokutana makundi mawili (kwa mapambano), hakika hapana ila shaytwaan aliwatelezesha kutokana na baadhi ya waliyoyachuma. Na kwa yakini Allaah Aliwasamehe. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mvumilivu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ كَفَرُوا وَقَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ إِذَا ضَرَبُوا فِي الْأَرْضِ أَوْ كَانُوا غُزًّى لَّوْ كَانُوا عِندَنَا مَا مَاتُوا وَمَا قُتِلُوا لِيَجْعَلَ اللَّـهُ ذَٰلِكَ حَسْرَةً فِي قُلُوبِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿١٥٦﴾
156. Enyi walioamini! Msiwe kama wale waliokufuru na wakasema kuhusu ndugu zao waliposafiri katika ardhi au walipokuwa vitani: Lau wangelikuwa kwetu wasingelikufa na wala wasingeliuawa, ili Allaah Afanye hayo (yaliyoeleweka vibaya) kuwa majuto katika nyoyo zao. Na Allaah Anahuisha na Anafisha. Na Allaah Anayaona vyema myatendayo.
وَلَئِن قُتِلْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَوْ مُتُّمْ لَمَغْفِرَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَحْمَةٌ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ ﴿١٥٧﴾
157. Na kama mtauliwa katika Njia ya Allaah au mtakufa, basi bila shaka Maghfirah kutoka kwa Allaah na Rehma ni bora kuliko yale wanayoyakusanya.
وَلَئِن مُّتُّمْ أَوْ قُتِلْتُمْ لَإِلَى اللَّـهِ تُحْشَرُونَ ﴿١٥٨﴾
158. Na kama mtakufa au mtauliwa, bila shaka kwa Allaah mtakusanywa.
فَبِمَا رَحْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ لِنتَ لَهُمْ ۖ وَلَوْ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ الْقَلْبِ لَانفَضُّوا مِنْ حَوْلِكَ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚإِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَوكِّلِينَ ﴿١٥٩﴾
159. Basi ni kwa sababu ya Rehma kutoka kwa Allaah ndio umekuwa mpole kwao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).[52] Na lau ungelikuwa mjeuri mwenye moyo mgumu, wangelitawanyika mbali nawe. Basi wasamehe na waombee maghfirah na washauri katika mambo. Na unapoazimia, basi tawakali kwa Allaah. Hakika Allaah Anapenda wanaotawakali.
إِن يَنصُرْكُمُ اللَّـهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ ۖ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا الَّذِي يَنصُرُكُم مِّن بَعْدِهِ ۗ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٦٠﴾
160. Akikunusuruni Allaah, basi hakuna wa kukushindeni. Na Akikutelekezeni, basi nani atakunusuruni baada Yake? Na kwa Allaah Pekee watawakali Waumini.
وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ ۚ وَمَن يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦١﴾
161. Na haikuwa (ni tabia) kwa Nabiy yeyote kukhini (ngawira). Na yeyote atakayekhini atakuja na kile alichokikhini Siku ya Qiyaamah. Kisha kila nafsi italipwa kamilifu yale iliyoyachuma, nao hawatodhulumiwa.[53]
أَفَمَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَ اللَّـهِ كَمَن بَاءَ بِسَخَطٍ مِّنَ اللَّـهِ وَمَأْوَاهُ جَهَنَّمُ ۚ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿١٦٢﴾
162. Je, aliyefuata Radhi za Allaah ni kama aliyestahiki ghadhabu kutoka kwa Allaah?! Na makazi yake ni Jahannam, na ubaya ulioje mahali pa kuishia!
هُمْ دَرَجَاتٌ عِندَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ ﴿١٦٣﴾
163. Wao wana vyeo mbali mbali mbele ya Allaah. Na Allaah Anayaona vyema yale wayatendayo.
لَقَدْ مَنَّ اللَّـهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿١٦٤﴾
164. Kwa yakini Allaah Amewafanyia fadhila Waumini pale Alipomtuma kwao Rasuli miongoni mwao wenyewe, anawasomea Aayaat Zake na anawatakasa na anawafunza Kitabu na Hikmah (Sunnah)[54], japokuwa walikuwa kabla katika upotofu bayana.
أَوَلَمَّا أَصَابَتْكُم مُّصِيبَةٌ قَدْ أَصَبْتُم مِّثْلَيْهَا قُلْتُمْ أَنَّىٰ هَـٰذَا ۖ قُلْ هُوَ مِنْ عِندِ أَنفُسِكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٦٥﴾
165. Ulipokusibuni msiba ingawa nyinyi mliwasibu (maadui) mara mbili yake mlisema: Umetoka wapi huu? Sema: Huo ni kutoka kwenu wenyewe. Hakika Allaah Ni Muweza juu ya kila kitu.[55]
وَمَا أَصَابَكُمْ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ فَبِإِذْنِ اللَّـهِ وَلِيَعْلَمَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٦٦﴾
166. Na yale yaliyokusibuni siku yalipokutana makundi mawili (katika Uhud), basi ni kwa Idhini ya Allaah na ili Adhihirishe Waumini.
وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ نَافَقُوا ۚ وَقِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا قَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَوِ ادْفَعُوا ۖ قَالُوا لَوْ نَعْلَمُ قِتَالًا لَّاتَّبَعْنَاكُمْ ۗ هُمْ لِلْكُفْرِ يَوْمَئِذٍ أَقْرَبُ مِنْهُمْ لِلْإِيمَانِ ۚ يَقُولُونَ بِأَفْوَاهِهِم مَّا لَيْسَ فِي قُلُوبِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يَكْتُمُونَ ﴿١٦٧﴾
167. Na ili Adhihirishe wale waliofanya unafiki na wakaambiwa: Njooni mpigane katika Njia ya Allaah au (angalau) lindeni. Wakasema: Lau tungelijua kuwa kuna kupigana bila shaka tungelikufuateni. Wao siku hiyo walikuwa karibu zaidi na ukafiri kuliko imaan. Wanasema kwa midomo yao yasiyokuwemo ndani ya nyoyo zao. Na Allaah Anajua zaidi wanayoyaficha.
الَّذِينَ قَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ وَقَعَدُوا لَوْ أَطَاعُونَا مَا قُتِلُوا ۗ قُلْ فَادْرَءُوا عَنْ أَنفُسِكُمُ الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٦٨﴾
168. Wale waliowaambia ndugu zao nao wakakaa (wasiende vitani): Lau wangelitutii basi wasingeliuawa. Sema: Basi ziondoleeni nafsi zenu mauti mkiwa ni wakweli.
وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ ﴿١٦٩﴾
169. Na wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika Njia ya Allaah[56] kuwa ni wafu, bali wahai, wako kwa Rabb wao wanaruzukiwa.[57]
فَرِحِينَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُوا بِهِم مِّنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿١٧٠﴾
170. Wanafurahia kwa Aliyowapa Allaah kwa Fadhila Zake na wanawashangilia ambao bado hawajaungana nao, walio nyuma yao, kwamba: Hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.
يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٧١﴾
171. Wanashangilia Neema kutoka kwa Allaah na Fadhila na kwamba Allaah Hapotezi ujira wa Waumini.
الَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ مِن بَعْدِ مَا أَصَابَهُمُ الْقَرْحُ ۚ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا مِنْهُمْ وَاتَّقَوْا أَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿١٧٢﴾
172. Wale waliomwitikia Allaah na Rasuli baada ya kuwasibu majeraha. Kwa wale waliofanya ihsaan miongoni mwao na wakawa na taqwa watapa ujira mkuu kabisa.[58]
الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّـهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ ﴿١٧٣﴾
173. Wale walioambiwa na watu: Hakika watu wamejumuika dhidi yenu, basi waogopeni. Lakini hilo liliwazidishia imaan wakasema: Hasbuna-Allaah! (Allaah Anatutosheleza) Mzuri Alioje Mtegemewa.[59]
فَانقَلَبُوا بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ لَّمْ يَمْسَسْهُمْ سُوءٌ وَاتَّبَعُوا رِضْوَانَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ ذُو فَضْلٍ عَظِيمٍ ﴿١٧٤﴾
174. Basi wakarudi na Neema kutoka kwa Allaah na Fadhila, halijawagusa ovu lolote na wakafuatilia Radhi za Allaah. Na Allaah Ni Mwenye Fadhila kuu kabisa.
إِنَّمَا ذَٰلِكُمُ الشَّيْطَانُ يُخَوِّفُ أَوْلِيَاءَهُ فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٧٥﴾
175. Hakika huyo ni shaytwaan anawakhofisha marafiki wake wandani. Basi msiwakhofu, na nikhofuni Mimi mkiwa ni Waumini.
وَلَا يَحْزُنكَ الَّذِينَ يُسَارِعُونَ فِي الْكُفْرِ ۚ إِنَّهُمْ لَن يَضُرُّوا اللَّـهَ شَيْئًا ۗ يُرِيدُ اللَّـهُ أَلَّا يَجْعَلَ لَهُمْ حَظًّا فِي الْآخِرَةِ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١٧٦﴾
176. Wala wasikuhuzunishe kabisa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wale wanaokimbilia katika ukafiri. Hakika wao hawamdhuru Allaah kitu chochote. Allaah Anakusudia Asiwawekee fungu lolote Aakhirah, na watapata adhabu kuu kabisa.
إِنَّ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الْكُفْرَ بِالْإِيمَانِ لَن يَضُرُّوا اللَّـهَ شَيْئًا وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٧٧﴾
177. Hakika wale waliobadilisha ukafiri badala ya imaan, hawatomdhuru Allaah kitu chochote, nao watapata adhabu iumizayo.
وَلَا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّمَا نُمْلِي لَهُمْ خَيْرٌ لِّأَنفُسِهِمْ ۚ إِنَّمَا نُمْلِي لَهُمْ لِيَزْدَادُوا إِثْمًا ۚ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿١٧٨﴾
178. Na wala wasidhanie kabisa wale waliokufuru kwamba muhula Tunaowapa (wa kustarehe) ni kheri kwao. Hakika Tunawapa muhula ili wazidi (kuchuma) dhambi. Nao watapata adhabu ya kudhalilisha.
مَّا كَانَ اللَّـهُ لِيَذَرَ الْمُؤْمِنِينَ عَلَىٰ مَا أَنتُمْ عَلَيْهِ حَتَّىٰ يَمِيزَ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ ۗ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُطْلِعَكُمْ عَلَى الْغَيْبِ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَجْتَبِي مِن رُّسُلِهِ مَن يَشَاءُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ ۚ وَإِن تُؤْمِنُوا وَتَتَّقُوا فَلَكُمْ أَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿١٧٩﴾
179. Haiwi kwa Allaah kuwaacha Waumini katika hali mliyo nayo mpaka Apambanue mbaya na mwema. Na haiwi kwa Allaah Akujulisheni ya ghaibu, lakini Allaah Humteua katika Rusuli Wake Amtakaye. Basi mwaminini Allaah na Rusuli Wake. Na mkiamini (imaan ya kweli) na mkawa na taqwa basi mtapata ujira mkuu kabisa.
وَلَا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَبْخَلُونَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ هُوَ خَيْرًا لَّهُم ۖ بَلْ هُوَ شَرٌّ لَّهُمْ ۖ سَيُطَوَّقُونَ مَا بَخِلُوا بِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ وَلِلَّـهِ مِيرَاثُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿١٨٠﴾
180. Wala wasidhani kabisa wale wanaofanya ubakhili kwa yale Aliyowapa Allaah katika Fadhila Zake kwamba hayo ni kheri kwao, bali ni shari kwao. Watafungwa kongwa yale waliyoyafanyia ubakhili Siku ya Qiyaamah. [60] Na Ni Wake Allaah Pekee urithi wa mbingu na ardhi. Na Allaah kwa yale myatendayo Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
لَّقَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَاءُ ۘ سَنَكْتُبُ مَا قَالُوا وَقَتْلَهُمُ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَنَقُولُ ذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ ﴿١٨١﴾
181. Kwa yakini Allaah Ameisikia kauli ya wale (Mayahudi) waliosema: Hakika Allaah ni fakiri na sisi ni matajiri.[61] Tutayaandika waliyoyasema na kuua kwao Manabii pasi na haki na Tutasema: Onjeni adhabu ya kuunguza!
ذَٰلِكَ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيكُمْ وَأَنَّ اللَّـهَ لَيْسَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ ﴿١٨٢﴾
182. Hivyo ni kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yenu na kwamba Allaah Si dhalimu kabisa kwa waja.
الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ عَهِدَ إِلَيْنَا أَلَّا نُؤْمِنَ لِرَسُولٍ حَتَّىٰ يَأْتِيَنَا بِقُرْبَانٍ تَأْكُلُهُ النَّارُ ۗ قُلْ قَدْ جَاءَكُمْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِي بِالْبَيِّنَاتِ وَبِالَّذِي قُلْتُمْ فَلِمَ قَتَلْتُمُوهُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٨٣﴾
183. (Hao ndio) Wale waliosema: Hakika Allaah Ametuahidi kwamba tusimwamini Rasuli yeyote mpaka atuletee dhabihu itakayoangamizwa na moto. Sema: Kwa yakini walikujieni Rusuli kabla yangu kwa hoja bayana, na hata kwa haya ambayo mmesema, basi kwa nini mliwaua mkiwa ni wakweli?
فَإِن كَذَّبُوكَ فَقَدْ كُذِّبَ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ جَاءُوا بِالْبَيِّنَاتِ وَالزُّبُرِ وَالْكِتَابِ الْمُنِيرِ ﴿١٨٤﴾
184. Basi wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), kwa yakini wamekadhibishwa Rusuli kabla yako. Walikuja na hoja bayana na Vitabu vya Hukumu, na Kitabu chenye Nuru.
كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۖ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ ۗ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ ﴿١٨٥﴾
185. Kila nafsi itaonja mauti. Na hakika mtalipwa kikamilifu ujira wenu Siku ya Qiyaamah. Basi atakayewekwa mbali na moto na akaingizwa Jannah, huyo kwa yakini amefuzu. Na uhai wa dunia si lolote ila ni starehe ya udanganyifu.
لَتُبْلَوُنَّ فِي أَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ وَلَتَسْمَعُنَّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا أَذًى كَثِيرًا ۚ وَإِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ ذَٰلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ ﴿١٨٦﴾
186. Bila shaka mtajaribiwa katika mali zenu na nafsi zenu, na bila shaka mtasikia kutoka kwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu na kutoka kwa wale walioshirikisha udhia mwingi. Lakini mkisubiri na mkawa na taqwa basi hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.[62]
وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ فَنَبَذُوهُ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ وَاشْتَرَوْا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَبِئْسَ مَا يَشْتَرُونَ ﴿١٨٧﴾
187. Na pale Alipochukua Allaah fungamano la wale waliopewa Kitabu (Allaah Akawaambia): Bila shaka mtakibainisha kwa watu na wala hamtokificha. Lakini walikitupa nyuma ya migongo yao na wakakibadilisha kwa thamani ndogo. Basi ubaya ulioje kwa yale wanayoyanunua!
لَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَفْرَحُونَ بِمَا أَتَوا وَّيُحِبُّونَ أَن يُحْمَدُوا بِمَا لَمْ يَفْعَلُوا فَلَا تَحْسَبَنَّهُم بِمَفَازَةٍ مِّنَ الْعَذَابِ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٨٨﴾
188. Usiwadhanie kabisa wale wanaofurahia (mabaya) waliyoyafanya na wanapenda wasifiwe kwa (mazuri) wasiyoyatenda. Usiwadhanie kabisa kuwa watasalimika na adhabu. Nao watapata adhabu iumizayo.[63]
وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٨٩﴾
189. Ni Wake Allaah ufalme wa mbingu na ardhi. Na Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.
إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾
190. Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana, bila shaka ni Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa wenye akili.[64]
الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَـٰذَا بَاطِلًا سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴿١٩١﴾
191. Ambao wanamdhukuru Allaah wakiwa wima, au wamekaa au wamejinyoosha, na wanatafakari katika kuumbwa mbingu na ardhi (wakisema): Rabb wetu, Hukuumba haya bure, Utakasifu Ni Wako! Basi Tukinge na adhabu ya moto.
رَبَّنَا إِنَّكَ مَن تُدْخِلِ النَّارَ فَقَدْ أَخْزَيْتَهُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿١٩٢﴾
192. Rabb wetu! Hakika Umuingizaye motoni, kwa yakini Umemhizi. Na madhalimu hawana wasaidizi wa kuwanusuru.
رَّبَّنَا إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِيًا يُنَادِي لِلْإِيمَانِ أَنْ آمِنُوا بِرَبِّكُمْ فَآمَنَّا ۚ رَبَّنَا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّئَاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ الْأَبْرَارِ ﴿١٩٣﴾
193. Rabb wetu! Hakika sisi tumemsikia mwitaji anaita kwenye imaan kwamba: Mwaminini Rabb wenu. Basi tukaamini. Rabb wetu! Tghufurie madhambi yetu na Tufutie mabaya yetu na Tufishe pamoja na Waumini wema.
رَبَّنَا وَآتِنَا مَا وَعَدتَّنَا عَلَىٰ رُسُلِكَ وَلَا تُخْزِنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ إِنَّكَ لَا تُخْلِفُ الْمِيعَادَ ﴿١٩٤﴾
194. Rabb wetu! Tupe pia Uliyotuahidi kupitia Rusuli Wako, wala Usituhizi Siku ya Qiyaamah. Hakika Wewe Huendi kinyume na ahadi.
فَاسْتَجَابَ لَهُمْ رَبُّهُمْ أَنِّي لَا أُضِيعُ عَمَلَ عَامِلٍ مِّنكُم مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ ۖ بَعْضُكُم مِّن بَعْضٍ ۖ فَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَأُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأُوذُوا فِي سَبِيلِي وَقَاتَلُوا وَقُتِلُوا لَأُكَفِّرَنَّ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَأُدْخِلَنَّهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ثَوَابًا مِّنْ عِندِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الثَّوَابِ ﴿١٩٥﴾
195. Rabb wao Akiwajibu: Hakika Mimi Sipotezi amali za mtendaji yeyote yule miongoni mwenu akiwa mwanamume au mwanamke, nyinyi kwa nyinyi. Basi wale waliohajiri na wakatolewa majumbani mwao na wakaudhiwa katika Njia Yangu, wakapigana na wakauliwa, bila shaka Nitawafutia makosa yao, na kwa yakini Nitawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito. Hayo ni malipo kutoka kwa Allaah. Na kwa Allaah kuna thawabu nzuri kabisa.
لَا يَغُرَّنَّكَ تَقَلُّبُ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي الْبِلَادِ ﴿١٩٦﴾
196. Kusikubabaishe kabisa kuzunguka makafiri kwa vishindo huku na kule katika ardhi.
مَتَاعٌ قَلِيلٌ ثُمَّ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۚ وَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿١٩٧﴾
197. Ni starehe ndogo, kisha makazi yao ni Jahannam. Na ni mahala pabaya mno pa kupumzikia.
لَـٰكِنِ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا نُزُلًا مِّنْ عِندِ اللَّـهِ ۗ وَمَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ لِّلْأَبْرَارِ ﴿١٩٨﴾
198. Lakini wale waliomcha Rabb wao watapata Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo. Ni mapokezi kutoka kwa Allaah. Na vilioko kwa Allaah ni bora zaidi kwa ajili ya wema watiifu.
وَإِنَّ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَمَن يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُمْ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِمْ خَاشِعِينَ لِلَّـهِ لَا يَشْتَرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿١٩٩﴾
199. Na miongoni mwa Watu wa Kitabu wamo ambao kwa hakika wanamwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwenu, na yaliyoteremshwa kwao, wananyenyekea kwa Allaah, na hawabadilishi Aayaat za Allaah kwa thamani ndogo. Hao watapata ujira wao kwa Rabb wao. Hakika Allaah Ni Mwepesi Mno wa Kuhesabu.[65]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٢٠٠﴾
200. Enyi walioamini! Subirini na zidini kuvuta subira, na bakieni imara na mcheni Allaah ili mpate kufaulu.[66]
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Al-Hayyu Al-Qayyuwm: Jina Tukufu Kabisa La Allaah (سبحانه وتعالى):
Rejea Tanbihi Al-Baqarah (2:255).
[3] Binaadam Ameumbwa Katika Sura Na Umbo Bora Kabisa:
Rejea Al-Muuminuwn (23:14), Rejea Al-Infitwaar (82:7-8), At-Tiyn (95:4).
[4] Nyoyo Zenye Upotovu, Shaka, Na Kadhaalika:
Rejea Al-Hajj (22:46) kwenye faida na rejea nyenginezo.
[5] Aayaat Muhkamaat Na Mutashaabihaat:
Aayaat Muhkamaat: Ni Aayaat ambazo maana zake zinafahamika kiwepesi, hazina mushkila wala utata, na dalili zake ziko wazi. Ama Aayaat Mutashaabihaat, hizi ni Aayah ambazo ni ngumu kufahamika, na zinawatatanisha baadhi ya watu wasio na ilimu ya kutosha. Hivyo warudie kwa ‘Ulamaa kuelewa maana zake.
Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliisoma Aayah hii:
هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ
“Yeye Ndiye Aliyekuteremshia Kitabu. Humo mna Aayaat zenye maana wazi, hizo ndio msingi wa Kitabu, na nyinginezo zisizokuwa wazi maana zake…”
mpaka mwisho wa Aayah. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Ee ‘Aaishah! Pindi utakapowaona wale ambao wanafuata zile Aayaat ambazo haziko wazi zaidi, basi fahamu kuwa hao ndio wale ambao Allaah Amewataja katika hii Aayah, basi tahadharini nao.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
[6] Tofauti Ya Ikabu Na Adhabu: Rejea Al-Hashr (59:4).
[7] Kuomba Maghfirah Kabla Ya Alfajiri: Rejea Adh-Dhaariyaat (51:18).
[8] Dini Ya Kiislamu Ni Dini Pekee Anayoiridhia Allaah (سبحانه وتعالى):
Dini ya Kiislamu ni Dini ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Amewachagulia Waja Wake, na Akawatumiliza kwayo Rusuli Wake, na ambayo Hakubali isipokuwa Dini hii ya Uislamu. Nayo ni kunyenyekea kwa Allaah (عزّ وجلّ) kwa utiifu na kujisalimisha Kwake kwa kumwabudu Yeye Pekee na kuwafuata Rusuli wote katika yale waliyotumiliziwa kwayo katika zama zote, mpaka wakakhitimishiwa kwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye baada ya kutumilizwa kwake, Allaah (عزّ وجلّ) Hakubali dini yoyote ile isipokuwa Uislamu. Na hata pia kwa Rusuli wote waliomtangulia Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kabla, wote hao waliulingania Uislamu (Tawhiyd) ingawa sharia tu ndizo zilizotofautiana kati ya Rasuli na Rasuli kwa mujibu wa hali na mazingira, na wote walikuwa ni Waislamu.
Khitilafu ya Watu wa Kitabu; Mayahudi na Manaswara iliyowafanya watengane wawe mapote na makundi, haikutokea ila baada ya kuthibiti hoja juu yao kwa kupelekwa Rusuli wao na kuteremshwa Vitabu. Hiyo ilitokana na uadui na uhasidi kwa kutafuta mafao ya dunia. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Hivyo basi ni kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) pia katika Aayah namba (85):
وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾
“Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu haitokubaliwa kwake, naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”
[10] Onyo Kwa Mayahudi Na Manaswaara Kwa Kutokumuamini Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, hatosikia yeyote yule kuhusu mimi katika ummah huu; Yahudi wala Naswara, kisha akafariki bila ya kuamini yale ambayo nimetumwa nayo, isipokuwa atakuwa miongoni mwa watu wa motoni.” [Al-Bukhaariy]
Na pia amesimulia Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنهما): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Na alikuwa (kila) Nabiy akitumwa kwa watu wake pekee, lakini mimi nimetumwa kwa watu wote.” [Al-Bukhaariy]
[11] Allaah (سبحانه وتعالى) Anatoa Kilicho Hai Kutokana Na Kilicho Mfu, Na Anatoa Kilicho Mfu Kutokana Na Kilicho Hai:
Rejea Al-An’aam (6:95), Ar-Ruwm (30:19).
[12] ‘Aqiydah Sahihi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Ni Kuthibisha Sifa Za Allaah.
Aayah tukufu imetaja Nafsi ya Allaah (سبحانه وتعالى). Na ‘Aqiydah sahihi ni kuithibitisha hivyo hivyo bila ya kuipa maana nyenginezo. Rejea Huwd (11:47) kwenye maelezo bayana.
[13] Kumpenda Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Kufuata Sunnah Zake Na Kujiepusha Na Yasiyo Sunnah:
Aayah hii tukufu inathibitisha kuwa mapenzi ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hayawezi kutimia isipokuwa kwa kufuata Sunnah zake. Ni hoja ya wazi pia kwa wanaodai kuwa wanampenda Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) lakini wakawa hawafuati matendo yake (Sunnah zake) na kinyume chake wanafanya bid’ah katika Dini kama kusoma mawlid, khitmah, talqiyn (kumsomea maiti), mikusanyiko ya kuomba duaa, kusheherekea maadhimisho na kumbukumbu za miaka, kusherehekea siku wanazosherehekea wasiokuwa Waislamu, na yote mengineyo yasiyokuwemo katika sharia. Na kufuata Sunnah zake ni kutenda yale ambayo ameyasema, ameyatenda au amayeridhia kutendwa; kuanzia khulqa (tabia) zake na jinsi alivyotaamuli na wake zake na Swahaba zake na watumishi wake. Jinsi alivyolingania (da’awah) watu wake, na hata jinsi alivyotendeana na maadui zake. Vile vile jinsi alivyotekeleza ibaada zake za Swalaah za mchana na za usiku. Alivyokuwa akiomba duaa, na jinsi alivyokuwa akileta Adhkaar zake (za kumdhukuru Allaah). Pia alivyokuwa akifunga (Swawm) Jumatatu, Alkhamiys na Masiku Meupe. Hali kadhaalika aliyokuwa akiyatenda na kuyatamka katika siku moja kuanzia kuamka kwake hadi usiku ikijumuisha aina ya chakula chake na jinsi alivyokuwa akila, na alivyokuwa akiamka usiku, na matendo yote mengineyo katika uhai wake. Akasisitiza mno kushikamana na Sunnah zake katika Hadiyth zifuatazo:
Amesimulia Abu Najiyh Al-‘Irbaadhw bin Saariyah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitupa mawaidha mazito (yenye maana kubwa), nyoyo zikaogopa na macho yakabubujikwa machozi. Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah! Yanaonekana kama kwamba mawaidha ya kutuaga, basi tuusie. Akasema: “Nakuusieni kuwa na taqwa kwa Allaah, na usikivu, na utiifu japokuwa mtaongozwa na mtumwa. Hakika atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona ikhtilafu nyingi. Kwa hiyo, shikamaneni na Sunnah zangu na mwenendo wa Makhalifa Waongofu, yashikilieni kwa magego (mambo yao). Na tahadharini na mambo yenye kuzushwa, kwani kila uzushi ni bid’ah, na kila bid-ah ni upotofu, na kila upotofu ni motoni.” [Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]
Na katika kila khutbah alitanguliza kusema: “Ammaa Ba’adu. Hakika maneno bora kabisa ni Kitabu cha Allaah (Qur-aan), na mwongozo bora kabisa ni mwongozo wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), na uovu zaidi wa mambo ni yale yenye kuzushwa (bila dalili ya kisharia), na kila bid'ah ni upotofu. [Muslim]
[14] Kuzaliwa Kwa Maryam Mama Wa Nabiy ‘Iysaa, Kutajwa Nabiy Zakariyyaa, Kuzaliwa Yahyaa Na kuzaliwa ‘Iysaa (عليهم السّلام):
Kuanzia Aayah (35-45) ni maelezo kuhusu Bi Hannah ambaye alikuwa ni mke wa ‘Imraan na kuzaliwa kwa Maryam. Imeanzia hapa Bi Hannah alipoweka nadhiri ya mimba aliyoibeba baada ya kufariki mumewe ‘Imraan. Akamzaa mtoto na kumpa jina la Maryam likimaanisha “Mtumishi wa Allaah.” Dada yake Hannah kwa maana ni khaalat (mama mdogo au mkubwa) wa Maryam, alikuwa ni mke wa Nabiy Zakariyyaa (عليه السّلام). Naye Zakariyyaa (عليه السّلام) ndiye aliyemlea Maryam baada ya kufariki baba yake ‘Imraan. Kwa hiyo Zakariyyaa (عليه السّلام) ni mume wa khaalat yake Maryam. Aayah zinaendelea kutaja muujiza wa Maryam vile alivyokuwa anaruzukiwa vyakula na Allaah (سبحانه وتعالى). Aayah zinataja pia muujiza wa kuzaliwa Nabiy Yahyaa (عليه السّلام) ilhali baba yake na mama yake walikuwa ni vizee vikongwe. Pia Aayah zimetaja muujiza wa kuzaliwa kwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام).
[15] Aina Ya Vyakula Alivyoruzukiwa Maryam:
Zakariyyaa (عليه السّلام) alimkuta akiwa na matunda ya majira ya joto katika majira ya baridi, na matunda ya majira ya baridi katika majira ya joto. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[16] Neno Kun! (Kuwa!) Rejea Al-Baqarah (2:117).
[17] Malaika Kutajwa Kwa Wingi Ilhali Ni Jibriyl (عليه السّلام):
Katika Sarufi ya Lugha ya Kiarabu, wingi unaweza kurejelea umoja. Na katika Aayah hii bila shaka amekusudiwa Jibriyl (عليه السّلام) ambaye daima ndiye mwenye kuteremsha Wahyi wa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Rusuli na Waja Wake, kama vile Jibriyl alivyomjia Maryam kumbashiria mwana katika Suwrah hii ya Aal-‘Imraan (3:45), na Suwrat Maryam (19:17-21). Mfano pia Allaah (سبحانه وتعالى) Anapotaja kwa wingi “Sisi” ilhali Anakusudia Yeye Pekee Mwenyewe kama katika Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ ﴿٩﴾
“Hakika Sisi Tumeteremsha Adh-Dhikra (Qur-aan) na hakika Sisi bila shaka Ndio Wenye Kuihifadhi.” [Al-Hjr (15:9)]
[18] Maryam Ni Miongoni Mwa Wanawake Bora Kabisa:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anamtakasa na kumsifia Maryam katika Aayah hizi. Rejea pia At-Tahriym (66:12) ambako amesifiwa tena Maryam bint ‘Imraan
Na katika Hadiyth ametajwa kuwa ni miongoni mwa wanawake bora kabisa:
عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: (( كَمَلَ مِنَ الرِّجَالِ كَثِيرٌ، وَلَمْ يَكْمُلْ مِنَ النِّسَاءِ إِلاَّ مَرْيَمُ بِنْتُ عِمْرَانَ، وَآسِيَةُ امْرَأَةُ فِرْعَوْنَ، وَفَضْلُ عَائِشَةَ عَلَى النِّسَاءِ كَفَضْلِ الثَّرِيدِ عَلَى سَائِرِ الطَّعَامِ ))
Amesimulia Abuu Muwsaa Al-Ash’ariyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wanaume wengi wamefikia daraja ya ukamilifu lakini hakuna mwanamke aliyefikia daraja hiyo isipokuwa Aasiyah mke wa Firawni, na Maryam bint 'Imraan. Na ubora wa 'Aaishah (رضي الله عنها) kwa wanawake wengine ni kama mfano wa ubora wa thariyd kwa vyakula vingine.” [Al-Bukhaariy na wengineo]
Rejea pia Suwrah Maryam (19:16). Rejea kisa chake kwa urefu na kuhusu kumzaa kwake Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) katika Suwrah Maryam (19:16-36).
Rejea pia At-Tahriym (66:11) ambamo wametajwa pia Khadiyjah Bint Khuwaylid mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Faatwimah bint yake Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa wao pia ni katika wanawake bora kabisa ulimwenguni.
[19] Kalamu Zilitupwa Katika Mto Kupiga Kura:
Kura ilipigwa baina ya Nabiy Zakariyyaa (عليه السّلام) na Marabi wa Bayt Al-Maqdis kwa sababu kila mmoja alipendelea kumlea Maryam. Basi wakapiga kura kwa kutupa kalamu zao mtoni na kwamba yeyote kati yao ambaye kalamu yake haitaibuka katika maji, ndiye atayestahiki kumlea Maryam. Basi walipotupa kalamu zao mtoni, maji yalizamisha kalamu zote isipokuwa kalamu ya Nabiy Zakariyyaa (عليه السّلام) ilibakia pale pale ikielea.
[20] Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Alifanya Miujiza Kwa Idhini Ya Allaah Wala Sio Kwa Uwezo Wake Tu:
Katika Aayah hii, na ya Suwrah Al-Maaidah (5:110), ni hoja na dalili ya wazi kabisa kwamba Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) ni mja wa Allaah na kwamba hakuwa na Uwezo wa kipekee katika kuleta miujiza iliyotajwa katika Aayah hizo mbili. Hivyo ni kwa sababu, alikuwa kila anapoleta miujiza hiyo iliyotajwa, alimalizia kwa kusema: “Kwa Idhini ya Allaah.” Basi hii ni hoja bayana na raddi kwa Manaswara wanaodai kuwa Nabiy Iysaa ni mungu kwa miujiza hii ilhali yote imetokana na Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى).
[21] Allaah (سبحانه وتعالى) Hana Sifa Mbaya Isipokuwa Anarudisha Ubaya (Muqaabalah):
Sifa ya makri (njama) huthibitishwa kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa njia ya muqaabalah, kwa maana: ukipanga mabaya, Naye Ataamiliana nawe kwa ubaya, na ubaya utakurudia wewe mwenyewe. Na ukipanga mazuri, Naye Ataamiliana nawe kwa uzuri, Atakusaidia na Atakulipa mema. Na Sifa hii kama zilivyo zingine, huthibitishwa kwa Allaah kwa maana inayoendana na kulaikiana na Allaah (عزّ وجلّ). Kwa hiyo, Allaah Anamfanyia makri (njama) yule anayestahiki, na pia yule ambaye anawafanyia makri (njama) waja Wake Waumini.
Hali kadhaalika, kumfanyia istihzai Allaah (عزّ وجلّ) au Waja Wake, au kuwadhihaki, au aina yoyote ya shutuma kama kudai kwamba Mkono wa Allaah umefumbwa kama katika Aayah ya Al-Maaidah (5:64) na mengineyo. Haya yote na mengineyo mabaya, Allaah Huwarudishia wahusika wake kwa adhabu za kidunia, au kwa namna ambayo Yeye Allaah Anaona kuwa inanasibiana na makosa yao.
[22] Uthibitisho Kuwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Yu Hai Mbinguni Na Atateremka Duniani Kama Alama Kubwa Za Qiyaamah:
Allaah (سبحانه وتعالى) Alimnyanyua Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) kuelekea mbinguni akiwa hai, na wala hakuuliwa kabla ya hapo. Na atakuja kuteremka duniani zama za mwisho, atamuua Masiyh Ad-Dajjaal, atawaua nguruwe wote, atavunja misalaba yote, ataondosha kodi, hatokubali isipokuwa Uislamu, na atahukumu kwa sharia ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Dalili ipo katika Suwrat An-Nisaa (4:157-159).
Aayah hii tukufu ni dalili ya wazi kwa wanaodai kwamba neno la مُتَوَفِّيكَ lina maana “kukufisha kikamilifu.” Neno hilo hilo Amelitaja Allaah (سبحانه وتعالى) katika Al-An’aam (6:60) na Az-Zumar (39:42):
وَهُوَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُم بِاللَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُم بِالنَّهَارِ ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَىٰ أَجَلٌ مُّسَمًّى ۖ
“Naye Ndiye Anayekufisheni usiku (mnapolala) na Anajua yale yote mnayoyafanya mchana, kisha Anakufufueni humo ili utimizwe muda maalumu uliokadiriwa.” [Al-An'aam (6:60)]
اللَّـهُ يَتَوَفَّى الْأَنفُسَ حِينَ مَوْتِهَا وَالَّتِي لَمْ تَمُتْ فِي مَنَامِهَا ۖ فَيُمْسِكُ الَّتِي قَضَىٰ عَلَيْهَا الْمَوْتَ وَيُرْسِلُ الْأُخْرَىٰ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ
“Allaah Huzichukua roho wakati wa kufa kwake, na zile zisizokufa katika usingizi wake, kisha Huzizuia ambazo Amezikidhia mauti, na Huzirudisha nyingine mpaka muda maalumu uliokadiriwa.” [Az-Zumar (39:42)]
Hapo tunafahamu kwamba, mtu anapolala anachukuliwa au anafishwa usingizini na kurudishwa katika uhai kwa kuwa roho yake inachukuliwa na ndio inayojulikana kuwa ni Al-Mawt As-Sughraa (mauti madogo). Kwa dalili pia kutoka katika mafunzo ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika nyiradi za kulala; mojawapo ni kusema pindi mtu anapoingia kulala:
بِاسْـمِكَ اللّهُـمَّ أَموتُ وَأَحْـيا
”Kwa Jina Lako Ee Allaah ninakufa na ninakuwa hai”.
Na anapoamka aseme:
الحَمْـدُ لِلّهِ الّذي أَحْـيانا بَعْـدَ ما أَماتَـنا وَإليه النُّـشور
”Himdi Anastahiki Allaah Ambaye Ametupa uhai baada ya kutufisha, na Ni Kwake tu kufufuliwa”.
Rejea pia Az-Zumar (39:42).
[23] Kuumbwa Kwa Nabiy Aadam (عليه السّلام) Na Kuzaliwa Nabiy Iysaa (عليه السّلام):
Kuumbwa kwa Nabiy Aadam (عليه السّلام) ni muujiza mkubwa zaidi kulikoni kuzaliwa kwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) kwa sababu Nabiy Aadam (عليه السّلام) hakuzaliwa na baba wala mama bali ameumbwa kwa udongo tu! Ama Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) amezaliwa na mama bila ya baba. Basi hii ni dalili, ushahidi na hoja ya wazi kabisa na raddi kwa Manaswara wanaodai kuwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) ni mungu kwa sababu ya kuzaliwa kwake kimuujiza.
[24] Mubaahalah:
Kilugha ni kuomba kwa unyenyekevu na juhudi. Na katika istilahi ni kuomba Laana ya Allaah imfikie mmoja kati ya watu wanaokhitilafiana katika jambo.
Wajumbe wa kikanisa wa Najraan, walitumwa waende Madiynah kwa lengo la kubishana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) ni mwana wa Allaah. Walipofika, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akawataka mubaahalah, kwamba wakusanyike pande mbili; wao na familia zao, na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na familia yake kisha waapize Laana ya Allaah iwaangukie waongo na wakanushaji. Lakini hakuna hata mmoja wao aliyejitokeza katika mubaahalah huo, kwa sababu walijua vilivyo kuwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni mkweli na Risala aliyotumwa nayo na Allaah ni Risala ya haki. Hivyo basi wakaogopa laana ya Allaah kuwafikia. Hapo basi uongo wao ukadhihirika.
[25] Dini Ya Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) Ni Dini Ya Kiislamu:
Amesimulia Ibn ’Umar (رضي الله عنهما) kwamba: Zayd bin ‘Amr bin Nufayl, alitoka kuelekea Sham, akiulizia kuhusu dini ili aifuate. Akakutana na mwanazuoni wa ki-Yahudi, akamuuliza kuhusu dini na akasema: Mimi huenda nikaingia dini yenu, basi nielezee. Akasema: Huwezi kuwa katika dini yetu mpaka uchukue fungu lako katika Ghadhabu za Allaah. Akasema Zayd: Mimi hakuna ninachokikimbia ila Ghadhabu za Allaah, wala sivumilii Ghadhabu za Allaah kwa kitu chochote, na vipi nitaweza! Je, utanielekeza (dini) nyingine? Akasema (mwanachuoni wa ki-Yahudi): Sijui ila dini iliyotakasika, akasema Zayd: Ni (dini) ipi hiyo iliyotakasika? Akasema: Dini ya Ibraahiym, hakuwa Myahudi wala Mnaswara, wala haabudu ila Allaah. Akatoka Zayd akakutana na mwanazuoni wa ki-Naswara, akamuuliza kama vile (alivyomuuliza Myahudi), akasema: Huwezi kuwa katika dini yetu mpaka uchukue fungu lako katika Laana za Allaah. Akasema: Mimi hakuna ninachokimbia ila nakimbia Laana za Allaah, wala sivumilii Laana za Allaah wala Ghadhabu Zake kwa chochote, na vipi nitaweza! Je, utanielekeza (dini) nyingine? Akasema: sijui ila (Dini) iliyotakasika. Akasema: Ni ipi hiyo (dini) iliyotakasika? Akasema: Dini ya Ibraahiym, hakuwa Myahudi wala Mnaswara wala haabudu ila Allaah. Basi Zayd alipoona maneno yao kuhusu Ibraahiym (عليه السّلام) aliondoka sehemu hiyo, na alipokuwa nje aliinua mikono yake akasema: “Ee Allaah, mimi nashuhudia niko katika Dini ya Ibraahiym.” [Al-Bukhaariy (3827)]
Rejea Al-Baqarah (2:135).
[28] Maana Ya Rabbaaniyyuwna (Marabi) Na Sifa Zake:
Rabbaaniy maana yake ya asili ni mlezi. Na baadhi ya Wafasiri wa Qur-aan wamesema kuwa wanalea watu kwa sifa zao njema na wanawatengenezea mambo yao.
Na wengi kati ya Salaf wametaja maana kadhaa zifuatazo:
Ni ‘Ulamaa na wenye kumwabudu Allaah (سبحانه وتعالى). Ni wenye ikhlaasw (kumtakasia Allaah Dini). Ni Maimaam (Viongozi) Fuqahaa (wenye ilimu ya hali ya juu kabisa) na wanafanyia kazi ilimu zao. Ni Maimaam (Viongozi) Swalihina wenye taqwa ya hali ya juu. Ni wenye busara na hikmah. Ni wenye zuhd (kuipa mgongo dunia). Ni wanyenyekevu kwa Allaah (سبحانه وتعالى) na kwa watu. Ni wapole mno. Ni wenye kuwafundisha watu mambo mepesi kwanza kabla yaliyo magumu.
Na baadhi ya Sifa zao, Rabbaaniyyuwn wameelezwa katika Qur-aan kuwa ni wenye kuamrisha mema na kukataza maovu [Al-Maaidah (5:63)] Pia, wana uthibati katika Jihaad na subra katika mitihani na dhiki [Aal-‘Imraan (3:146)] pamoja na sifa njema nyenginezo. Basi kwa sababu ya sifa hizo ndipo Allaah (سبحانه وتعالى) Anawaambia Rusuli Wake wawaamrishe watu wawe Rabbaaniyyuwn kuwafundisha watu ilimu waliyonayo na kukanusha kuwa Rusuli Wake Allaah (سبحانه وتعالى) wametaka waabudiwe na watu au eti wamewaamrisha watu wawaabudu.
[29] Dalili Kuwa Al-Khidhwr Hayuko Hai:
Aayah hii ni miongoni mwa dalili za kufariki kwa Khidhwr (عليه السّلام) na kuwa yeye amekwishakufa na si kama wanavyodai Masufi kuwa Khidhwr yupo hai. Na lau kama angelikuwa yupo hai, basi angesimama kumnusuru Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kauli na matendo.
[30] Al-Asbaatw: Rejea Al-Baqarah (2:136).
[31] Dini Ya Kiislamu Ni Dini Pekee Anayoiridhia Allaah (سبحانه وتعالى) : Rejea Suwrah hii Aal-’Imraan (3:19-20).
[34] Israaiyl Ni Nabiy Ya’quwb (عليه السّلام) :
Israaiyl ni Nabiy Ya’quwb (عليه السّلام), na watoto wake na vizazi vyao wametajwa kuwa ni Bani Israaiyl kama katika Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ مِن ذُرِّيَّةِ آدَمَ وَمِمَّنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ وَمِن ذُرِّيَّةِ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْرَائِيلَ وَمِمَّنْ هَدَيْنَا وَاجْتَبَيْنَا
“Hao ndio ambao Allaah Amewaneemesha miongoni mwa Manabii katika uzao wa Aadam, na wale Tuliowapandisha (katika jahazi) pamoja na Nuwh na katika uzao wa Ibraahiym na (uzao wa) Israaiyl (Ya’quwb) na wale Tuliowaongoa na Tukawateua.” [Maryam (19:58)]
[35] Fadhila Na Sifa Za Ibraahiym (عليه السّلام): Rejea An-Nahl (16:120).
[36] Nyumba Ya Kwanza Kwa Ajili Ya Ibaadah (Al-Ka’bah): Rejea Al-An’aam (6:92)
[37] Maana Ya Kushikamana Na Kamba Ya Allaah Bila Kufarikiana.
Kushikamana na Kamba ya Allaah bila ya kufarikiana imekusudiwa kubakia katika Swiraatw Al-Mustaqiym (njia iliyonyooka). Rejea Tanbihi ya Al-Faatihah (1:6) (6:153).
Na pia Kauli ya Allaah (عزّ وجلّ) :
وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٥٣﴾
“Na kwamba hii ndio Njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na Njia Yake. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kuwa na taqwa.” [Al-An’aam (6:153)]
Pia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ametahadharisha mno kuhusu kuthibitika katika Swiraatw Al-Mustaqiym ambayo inamaanisha kutokutoka nje ya mafunzo ya Qur-aan na Sunnah. Miongoni mwa maonyo yake ni Hadiyth ifuatayo:
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Anawaridhia mambo matatu na Anachukia kwenu mambo matatu: Anawaridhia mumwabudu Yeye, wala msimshirikishe kwa chochote, na mshikamane nyote na Kamba ya Allaah wala msifarikiane. Na anachukia kwenu uvumi, kuuliza sana na kupoteza mali.” [Muslim, na katika riwayaah: “Na muwanasihi wenye kuwatawalia mambo yenu.” Swahiyh Adab Al-Mufrad (343)]
[38] Makundi Sabini Na Tatu Yataingia Motoni Isipokuwa Kundi Moja Tu!
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wamegawanyika Mayahudi katika mapote sabini na moja, na wakagawanyika Manaswara katika mapote sabini na mbili, na ummah wangu utagawanyika mapote sabini na tatu. Yote hayo yataingia motoni ila moja tu.” Swahaba waliuliza: Ni lipi hilo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Ni lile nililokuwemo mimi na Swahaba zangu.” [Ahmad, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ad-Daarimiy]
Rejea pia Al-Faatihah (1:6), Suwrah hii Aal-‘Imraan (3:31), (3:103), Al-An’aam (6:153), (6:159), Ar-Ruwm (30:32), Ash-Shuwraa (42:14), Al-Bayyinah (98:4).
[39] Nyuso Za Waumini Na Nyuso Za Makafiri Zitakavyokuwa Siku Ya Qiyaamah:
Aayah hii namba (106) na inayofuatia (107) zinataja hali za nyuso za Waumini na makafiri zitakavyokuwa Siku ya Qiyaamah. Rejea ‘Abasa (80:38) kwenye faida na rejea za maudhui hii.
[40] Ummah Wa Kiislamu Ni Ummah Bora Kabisa:
Hadiyth kadhaa zimetaja fadhila za ummah huu wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Miongoni mwa fadhila hizo ni:
Mu’aawiyah bin Haydah Al-Qash-riyy (رضي الله عنه) amehadithia kutoka kwa baba yake kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nyinyi mnakamilisha ummah sabini. Nyinyi ndio bora wao na ndio watukufu zaidi mbele ya Allaah (عزّ وجلّ).” [Ahmad, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Al-Haakim, na wengineo kwa riwaayah tofauti kidogo taz. Swahiyh Al-Jaami’ (2301), Swahiyh At-Tirmidhiy (3001)]
Na pia, Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Sisi (Waislamu) ni wa mwisho (kuja) na (tutakuwa) wa mwisho Siku ya Qiyaamah na wa mwanzo kuingia Jannah…” [Al-Bukhaariy na Muslim]
[42] Amri Ya Kuamrisha Mema Na Kukataza Maovu:
Kuamrisha mema na kukataza maovu ni sifa ya ummah huu wa Kiislamu, nayo imesisitizwa katika Aayah kadhaa za Qur-aan, na pia katika Sunnah imesisitizwa mno. Miongoni mwazo ni Hadiyth zifuatazo:
Hudhayfah bin Al-Yamaani (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake! Mtaamrisha mema na mtakataza maovu au sivyo Allaah Atakuleteeni adhabu kutoka Kwake, kisha mtamuomba wala Hatokuitikieni.” [Ahmad na At-Tirmidhy - Swahiyh At-Tirmdhiy (2169), Swahiyh Al-Jaami’ (7070)]
Pia: Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: “Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Atakayeona munkari (uovu) basi aubadilishe kwa mkono wake, na asipoweza basi kwa ulimi wake, na asipoweza basi kwa moyo wake (achukizwe) na huo ni udhaifu wa imaan.” [Muslim]
Kuamrishana mema na kukatazana maovu ni moja ya sifa za ummah huu wetu wa Kiislamu. Rejea Suwrah hii Aal-‘Imraan (3:110).
Rejea pia Adh-Dhaariyaat (51:55) kwenye faida nyenginezo na rejea zake.
[43] Ghazwat-Uhud: Vita Vitukufu Vya Uhud:
Vita vitukufu vya Uhud vimetajwa katika Aayah zifuatazo za Suwrah hii Aal-‘Imraan:
(121-128), (139-146), (148), (150), (152-153), (157-158), (166), (168-171). Na Allaah Mjuzi zaidi.
Vita vya Uhud ni katika vita vikubwa vya Jihaad. Vilifanyika mwaka mmoja baada ya Vita vya Badr. Waislamu walipigana na makafiri wa Kiquraysh siku ya Jumamosi mnamo mwezi wa Shawwaal mwaka wa tatu baada ya Hijrah.
Vimeitwa Uhud kwa sababu vilitokea katika maeneo ya mlima wa Uhud.
Washirikina hawakuwa na raha baada ya kushindwa Vita vya Badr, wakawa na raghba na ghamu kubwa ya kulipiza kisasi kwa yale yaliyowasibu katika Vita vya Badr, kwa kuuliwa wengi wao wakiwemo vigogo vyao. Hivyo basi Maquraysh walikuwa na unyonge, huzuni na ghadhabu kubwa. Basi wakawa wakikutana katika vikao vyao wakipanga namna ya kulipa kisasi dhidi ya Waislamu waweze kuondosha huzuni na ghadhabu zao.
Waliokuwa na nashati na hamasa zaidi katika kutayarisha vita hivi upande wa washirikina, ni ‘Ikrimah bin Abiy Jahl, Safwaan bin Umayyah, Abu Sufyaan bin Harb na ‘Abdullaah bin Abi Rabiy’ah.
Walikusanya mali nyingi na wakatayarisha jeshi kubwa lililokusanya watu wa makabila maarufu ya Bani Kinaanah na Tihaamah na mabedui wa Ahaabish na makabila mbali mbali ya Kiarabu, waliowajaza chuki nyoyoni mwao.
Al-’Abbaas (رضي الله عنه) ammi yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), baada ya kuona jeshi likiondoka, alimtumia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ujumbe wa kumjulisha nyendo za washirikina na idadi yao. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akashauriana na Swahaba wake kama wapambane na Maquraysh au wabakie Madiynah, basi rai ya wengi ilikuwa ni kutoka kupambana na Maquraysh, na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akakubali rai hiyo.
Idadi ya jeshi la Waislamu ilikuwa ni elfu moja. Imepokewa kwamba wanafiki walijitenga na jeshi la Waislamu kabla ya vita, na idadi yao ilikuwa mia tatu, kwa hivyo walibakia Waislamu mia saba tu waliobaki kukabiliana na Vita vya Uhud. Na katika Suwrah hii wanafiki wamefichuliwa siri zao za dhahiri na siri za kutokutaka kushiriki katika Vita vya Uhud.
Waislamu walipofika kwenye uwanja wa vita, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aligawanya jeshi katika vikosi vitatu. Cha kwanza kilikuwa ni kikosi cha Muhajirina, na bendera yake ilibebwa na Musw-ab bin ‘Umayr (رضي الله عنه). Kikosi cha pili kilikuwa ni kikosi cha Al-Aws na kiliongozwa na Usayd bin Hudhwayr (رضي الله عنه). Na kikosi cha tatu kilikuwa ni kikosi cha Khazraj kikiongozwa na Al-Hubbaab bin Mundhir (رضي الله عنه). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawapanga Waislamu hamsini wa kupiga mishale juu ya mlima. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawataka wabakie hapo wasiondoke. Mapigano yalipoanza, ushindi ulikuwa kwanza wa Waislamu, na jeshi la washirikina likaanza kurudi nyuma. Lakini wapiga mishale katika jeshi la Waislamu wakafikiri kwamba vita vimeisha. Wakateremka kutoka mlimani juu ya kwamba waliamrishwa awali wasiondoke, wakikimbilia kuteka ngawira za makafiri waliokuwa wanakimbilia mbali. Wakamuasi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa hili. Wakabakia hapo mlimani waliobakia katika Waumini wa kweli.
Khaalid bin Waliyd ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi wa Quraysh, akachukua fursa ya kuwateremkia Waislamu. Akauzunguka mlima ili awazunguke Waislamu kwa nyuma, na kwa vile alikuwa na sifa ya ushujaa wa kupigana, alishambulia kwa ujasiri, na hapo basi wimbi la vita likageuka, Waislamu wengi wakauliwa na ushindi ukawa kwa makafiri.
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alijeruhiwa katika vita hivi, uso wake ulijaa damu. Swahaba Twalhah Bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه) alijiweka karibu na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiulinda uso wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) dhidi ya mishale. Twalhah (رضي الله عنه) alipigwa mara mbili kichwani na akapata majeraha mengi mwilini mwake. Aliitwa “Shahidi aliye hai.” Rejea Al-Ahzaab (33:23). Na Abu Bakr (رضي الله عنه) aliita siku hiyo ya Uhud kuwa ni siku ya Twalhah (رضي الله عنه) kwa sababu ya kumhami kwake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) bila ya kujali kujeruhiwa.
Swahaba sabiini waliuawa kama Shahidi, akiwemo Hamzah bin ‘Abdil-Muttwalib (رضي الله عنه) ambaye ni ammi yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
Amesimulia Al-Baraa Bin ‘Aazib (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimchagua ‘Abdullaah bin Jubayr (رضي الله عنه) kuwa jemadari wa kikosi cha miguu (warusha mishale) ambao walikuwa hamsini siku ya Vita vya Uhud. Akawaagizia: “Bakieni mahali penu, na msiondoke hata mkiona ndege wakitunyakua, mpaka niwatumie (mjumbe). Na mkiona tumewashinda kaumu na kuwafanya kukimbia, hata hivyo msiondoke mpaka niwatumie (mjumbe).” Kisha tukawashinda. Wa-Allaahi niliwaona wanawake wakikimbia na huku wamenyanyua nguo zao, hivyo vikuku vya miguu kuonekana na miundi yao. Wakasema Swahaba wa ‘Abdullaah bin Jubayr (رضي الله عنه): “Ngawira! Enyi watu, ngawira! Swahaba zenu wameshinda, mnasubiri nini?” ‘Abdullaah bin Jubayr akasema: “Je, mmesahau aliyowaambia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)?” Wakasema: “Wa-Allaahi, tutakwenda kwa watu (yaani maadui) tukusanye sehemu yetu ya ngawira!” Walipokwenda kwao, walilazimishwa kugeuka na huku wameshindwa. Wakati huo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa nyuma yao akiwaita. Wanaume kumi na mbili (12) tu ndio walobakia pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na wakauliwa sabiini miongoni mwetu. [Al-Bukhaariy – Kitaab Al-Jihaad]
Hayo ni matokeo ya kumuasi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Anataja Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah: (152-153).
Baadhi Ya Ghazwah (Vita Vitukufu Vya Jihaad) Vilivyotajwa Katika Qur-aan:
Ghazwat-Uhud: Suwrah hii ya Aal-‘Imraan (3).
Ghazwat-Badr: Suwrah hii ya Aal-‘Imraan (3) na Al-Anfaal (8).
Ghazwat-Khandaq au Al-Ahzaab (33).
Ghazwat-Tabuwk: At-Tawbah: (9).
Ghazwat-Hudaybiyah: Al-Fat-h (48).
Ghazwat-Khaybar: Al-Fat-h (48)
Ghazwat-Hunayn: At-Tawbah (9).
Na vita vinginevyo, ambavyo vimetajwa katika Suwrah nyenginezo. kama vita dhidi ya Bani Nadhwiyr ambavyo vimetajwa katika Suwrah Al-Hashr (59). Na pia Fat-h Makkah (Ufunguzi wa Makkah) ambavyo vimetajwa katika Suwrah An-Naswr (110). Na kuna Hadiyth kadhaa pia zilizotaja kuhusu vita vitukufu vyote hivyo.
[45] Maana Ya Badr:
‘Ulamaa wametofautiana kuhusu maana ya ‘Badr’. Baadhi yao wamesema ni jina la mtu, na wengine wamesema ni jina la kisima. Sehemu hiyo iko baina ya Makkah na Madiynah, na umbali kati yake na Madiynah ni kilometa mia na khamsini. Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi. Rejea pia Al-Anfaal (8:7) kuna maelezo bayana kuhusu Vita hivi vitukufu.
[47] Haramisho La Riba Na Matahadharisho: Rejea Al-Baqarah: (2:275–279).
[48] Kuomba Maghfirah Na Kutubia Baada Ya Kutenda Maasi:
Rejea An-Nisaa (4:110) na At-Tahriym (66:8).
[49] Waumini Kuliwazwa Katika Vita Vya Jihaad Kwamba Watembee Katika Ardhi Wakaone Hatima Ya Waliokadhibisha Na Nusra Kuwa Ya Waumini, Na Hii Ndio Desturi Ya Allaah (سبحانه وتعالى):
Aayah hii na zinazofuatia zinaendelea kutaja kuhusu Vita Vitukufu vya Uhud pale Waumini walipokuwa katika shida, dhiki na mtihani wa kujeruhiwa vitani na baadhi yao kuuliwa. Hivyo Allaah (عزّ وجلّ) Anawaliwaza Waja Wake Waumini na kuwaambia watembee katika sehemu ambapo kuna athari za Adhabu za Allaah (سبحانه وتعالى) kwa makafiri wa nyumati za nyuma. Na kwamba vizazi na nyumati nyingi zilizopita kabla yao, walitahiniwa na kujaribiwa. Walijaribiwa kwa kupigana na makafiri, wakaendelea kumahanika na kuhangaika mpaka Allaah (عزّ وجلّ) Akawaletea Nusra yake na mwisho mwema, na ushindi ukawa wa Waja Wake wema. Na kwamba makafiri waliangamizwa pamoja na majumba yao, wakala khasara na wakahizika! Basi hiyo ndiyo Desturi ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya kuwaadhibu makafiri na badala yake kuwajaalia Nusra na ushindi Waumini. Hivyo basi, Waumini katika Vita vya Uhud wanapaswa wayajue hayo, wapate nguvu, wathibiti katika imaan yao, na watambue kwamba hali yao ni kama hali za wenzao wa nyuma, lakini mwisho mwema ni wao; ima wapate ushindi au walipwe malipo mema Aakhirah.
Rejea Faatwir (35:43-44), Al-An’aam (6:11), Yuwsuf (12:109), Al-Kahf (18:55), Al-Hajj (22:46) na Ghaafir (40:21) (40:82), (40:85).
[50] Shuhadaa Rejea Aayah (3:169).
[52] Fadhila Na Upole Wa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):
Fadhila na sifa zake imetajwa mara tele katika Qur-aan na Sunnah. Rejea At-Tawbah (9:128).
[54] Waumini Wamefadhilishwa Kutumiwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):
Rejea Al-Baqarah (2:151), Al-Jumu’ah (6:2) kwenye Kauli ya Allaah kama hiyo. Na duaa ya Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) alipoomba:
رَبَّنَا وَابْعَثْ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُزَكِّيهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٢٩﴾
“Rabb wetu, Wapelekee Rasuli miongoni mwao atakayewasomea Aayaat Zako na atakayewafunza Kitabu na Hikmah na atakayewatakasa. Hakika Wewe Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.” [Al-Baqarah (2:129)]
[56] Shuhadaa: Waliofariki Katika Vita Vitukufu Vya Jihaad Wako Hai Peponi. Rejea An-Nisaa (4:69).
Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Pale walipopatwa na msiba ndugu zenu wa Uhud, Allaah Alijaalia roho zao kuwa katika maumbile ya ndege wa kijani ambao wanakunywa katika mito ya Jannah. na wanakula katika matunda ya Jannah, na hurukia na hustarehe kwenye kandili ya dhahabu chini ya kivuli cha ‘Arshi ya Allaah. Kisha roho hizo zilipopatwa na utamu wa kunywa na kula katika neema za humo ndani ya Jannah, na uzuri wa makazi, na marejeo yao wakasema: Laiti wangelifahamu ndugu zetu yale Allaah Aliyotufanyia sisi ili wasipuuze jambo la Jihaad na wala wasirejee na kuogopa vita. Basi hapo Allaah Akasema: “Mimi Ninayafikisha hayo kutoka kwenu!” Ndipo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:
وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ ﴿١٦٩﴾
“Na wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika Njia ya Allaah kuwa ni wafu, bali wahai, wako kwa Rabb wao wanaruzukiwa…” [Aal-‘Imraan (3:169) mpaka Aayah (171) - Imaam Ahmad]
[59]Aliyoyasema Nabiy ‘Ibraahiym (عليه السّلام) Alipoingizwa Katika Moto Na Makafiri:
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Kauli ya mwisho ya Ibraahiym wakati alipoingizwa katika moto (na makafiri) ilikuwa ni:
حَسْبِيَ اللَّهُ ونِعْمَ الوَكِيلُ
Hasbiya-Allaahu wa Ni’mal-Wakiyl
(Allaah Ananitosheleza na Mzuri Alioje Mtegemewa) [Al-Bukhaariy]
Al-Wakiyl: Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake.
[60] Tahadharisho Na Adhabu Ya Kutokutoa Zakaah:
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Yeyote yule ambaye Allaah Amemruzuku mali kisha asiitolee Zakaah yake, basi (Siku ya Qiyaamah) mali yake itakuwa kama nyoka dume kipara aliye na madoto mawili juu ya macho yake. Atamvingirita shingoni na kumuuma mashavu yake huku akisema: Mimi mali yako! Mimi hazina yako!” [Al-Bukhaariy]
[61] Mayahudi Kumfanyia Allaah (سبحانه وتعالى) Utovu Wa Adabu Mkubwa, Ufidhuli Na Dhulma Ya Kuvuka Mipaka:
‘Ulamaa wametaja kwamba Aayah hii iliteremkwa kuhusu kundi la Mayahudi waliotaja hayo. Wakataja kuwa katika hao, ni Fanhaasw Bin ‘Aazuwraa ambaye ni miongoni mwa wanachuoni wakuu wa ki-Yahudi waliokuwa Madiynah. Na kwamba waliposikia Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
مَّن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّـهَ قَرْضًا
“Ni nani atakayemkopesha Allaah karadha nzuri kisha (Allaah).” [Al-Baqarah (2:245)]
Na:
وَأَقْرَضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا
“Na wakamkopesha Allaah karadha mzuri.” [Al-Hadiyd (57:18)]
Akasema kwa kiburi chake kikubwa mno kauli hiyo. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Na Sa’iyd bin Jubayr Amesimulia kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba ilipoteremka:
مَّن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ أَضْعَافًا كَثِيرَةً ۚ
“Ni nani atakayemkopesha Allaah karadha nzuri kisha (Allaah) Amzidishie mzidisho mwingi.” [Al-Baqarah (2:245)]
Yahudi akasema: “Ee Muhammad! Je, kwani Rabb wako Amekuwa faqiri hata anaomba karadha kutoka kwa Waje Wake?” Hapo ikateremka kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
لَّقَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَاءُ ۘ سَنَكْتُبُ مَا قَالُوا وَقَتْلَهُمُ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَنَقُولُ ذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ ﴿١٨١﴾
“Kwa yakini Allaah Ameisikia kauli ya wale (Mayahudi) waliosema: Hakika Allaah ni fakiri na sisi ni matajiri. Tutayaandika waliyoyasema na kuua kwao Manabii pasi na haki na Tutasema: Onjeni adhabu ya kuunguza!” [Aal-‘Imraan (3:181), Tafsiyr ibn Kathiyr]
[64] Ni Sunnah Kusoma Aayah Za Mwisho Za Suwrah Aal-‘Imraan (190-200) Anapoamka Mtu Usiku Kuswali (Tahajjud):
Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما) alimuuliza Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) : Tueleze jambo la ajabu zaidi uliloliona kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Anasema: (Mama wa Waumini ‘Aaishah) akanyamaza (kukumbuka moja kati ya mambo hayo) kisha akasema: Ulipokuwa usiku mmoja kati ya nyusiku, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: “Ee ‘Aaishah! Niruhusu nifanye ibaada usiku huu kwa ajili ya Rabb wangu.” Nikamwambia: Wa-Allaahi, mimi napenda kuwa nawe karibu, na ninapenda linalokufurahisha. Akaenda kujitwaharisha, kisha akasimama na kuanza kuswali. (Akalia), na hakuacha kuendelea kulia mpaka akailowesha nguo yake. Alikuwa amekaa, na akaendelea kulia mpaka akazitotesha ndevu zake. Kisha akalia, na akaendelea kulia mpaka akailowesha sakafu. Halafu Bilaal akaja kumjulisha kuwadia wakati wa Swalaah. Alipomwona analia alimwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Kwa nini unalia nailhali wewe umeshasamehewa madhambi yako yaliyopita na yajayo?! Akamwambia: “Kwa nini nisiwe mja mwingi wa kushukuru! Hakika zimeniteremkia usiku huu Aayah hizi. Basi ole wake atakayezisoma na asiyataamuli yaliyomo humo.” Akasoma:
إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾
“Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana, bila shaka ni Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa wenye akili…” (mpaka mwisho wa Suwrah). [Imesimuliwa na Ibn Hibaan katika Swahiyh yake. Al-Albaaniy kasema: Isnaad yake ni nzuri. Kuna Riwaaya nyengine kama hiyo katika Al-Bukhaariy na Muslim]
[66] Baadhi Ya Maana Ya Ribaatw (رِبَاطٌ) Na Fadhila Zake:
Kwanza: Kubakia, kusimama imara katika kuchunga na kulinda mipaka katika Jihaad fiy SabiliLLaah.
Pili: Kubakia katika ibaada baina ya Swalaah Na Swalaah ya pili.
Fadhila za Ribaatw:
Amesimulia Sahl bin Sa’ad (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ar-Ribaatw (kusimama imara katika kulinda mipaka kwenye vita vya Jihaad) ya siku moja kwa ajili ya Allaah, ni bora kuliko dunia na vilivyomo. Na sehemu ndogo katika Jannah (Peponi), kiasi cha ukubwa wa fimbo ya mmoja wenu, ni bora kuliko dunia na yaliyomo ndani yake. Na safari ya asubuhi au ya jioni anayosafiri mja katika Njia ya Allaah, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Pia: Amesimulia Salmaan (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ribaatw (kusimama imara katika kulinda mipaka kwenye vita vya Jihaad) ya siku moja na usiku wake, ni bora (katika malipo) kuliko Swiyaam ya mwezi mzima na Qiyaam (kisimamo cha kuswali usiku) chake. Na mtu akifariki (akiwa katika ribaatw), amali zake zitaendelea kuandikwa, na riziki yake ataendelea kuipata, na atasalimika na fitnah (za kaburi).” [Muslim]
النِّسَاء
004-An-Nisaa
004-An-Nisaa: Utangulizi Wa Suwrah [67]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا ﴿١﴾
1. Enyi watu! Mcheni Rabb wenu Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja (Aadam) na Akaumba kutoka humo mke wake (Hawwaa) na Akaeneza kutoka hao wawili wanaume na wanawake wengi. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mnaombana (haki zenu kwa kuunga) undugu.[1] Hakika Allaah daima Ni Mwenye Kuwachungeni.
وَآتُوا الْيَتَامَىٰ أَمْوَالَهُمْ ۖ وَلَا تَتَبَدَّلُوا الْخَبِيثَ بِالطَّيِّبِ ۖ وَلَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَهُمْ إِلَىٰ أَمْوَالِكُمْ ۚ إِنَّهُ كَانَ حُوبًا كَبِيرًا ﴿٢﴾
2. Na wapeni mayatima mali zao, wala msibadilishe kibaya (chenu) kwa kizuri (chao). Na wala msile mali zao pamoja na mali zenu. Hakika hilo limekuwa ni dhambi kubwa.
وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُوا فِي الْيَتَامَىٰ فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَلَّا تَعُولُوا ﴿٣﴾
3. Na mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu kwa mayatima, basi oeni waliokupendezeni katika wanawake (wengine); wawili au watatu au wanne. Lakini mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi mmoja tu au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki.[2] Hivyo ni karibu zaidi kwamba hamtoelemea kudhulumu.[3]
وَآتُوا النِّسَاءَ صَدُقَاتِهِنَّ نِحْلَةً ۚ فَإِن طِبْنَ لَكُمْ عَن شَيْءٍ مِّنْهُ نَفْسًا فَكُلُوهُ هَنِيئًا مَّرِيئًا ﴿٤﴾
4. Na wapeni wanawake mahari zao kwa maridhawa. Lakini wakitoa chochote wenyewe katika mahari yao kwa khiari zao, basi kuleni kwa kufurahia na kunufaika.
وَلَا تُؤْتُوا السُّفَهَاءَ أَمْوَالَكُمُ الَّتِي جَعَلَ اللَّـهُ لَكُمْ قِيَامًا وَارْزُقُوهُمْ فِيهَا وَاكْسُوهُمْ وَقُولُوا لَهُمْ قَوْلًا مَّعْرُوفًا ﴿٥﴾
5. Wala msiwape wasiokomaa kiakili mali yenu ambayo Allaah Ameijaalia kuwa ni kisaidizi chenu cha maisha, na walisheni humo na wavisheni na waambieni maneno ya haki na kwa huruma.
وَابْتَلُوا الْيَتَامَىٰ حَتَّىٰ إِذَا بَلَغُوا النِّكَاحَ فَإِنْ آنَسْتُم مِّنْهُمْ رُشْدًا فَادْفَعُوا إِلَيْهِمْ أَمْوَالَهُمْ ۖ وَلَا تَأْكُلُوهَا إِسْرَافًا وَبِدَارًا أَن يَكْبَرُوا ۚ وَمَن كَانَ غَنِيًّا فَلْيَسْتَعْفِفْ ۖ وَمَن كَانَ فَقِيرًا فَلْيَأْكُلْ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِذَا دَفَعْتُمْ إِلَيْهِمْ أَمْوَالَهُمْ فَأَشْهِدُوا عَلَيْهِمْ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ حَسِيبًا ﴿٦﴾
6. Na wajaribuni mayatima (akili zao) mpaka wakifikia umri wa kuoa. Na mkihisi kupevuka kwao, basi wapeni mali zao. Wala msiile kwa israfu na pupa kwa (kuhofia) kuwa watakuja kuwa watu wazima. Na aliyekuwa tajiri, ajizuilie (kuchukua ujira), na aliyekuwa fakiri basi ale kwa kadiri ya kukubalika kisharia. Mtapowapa mali zao washuhudizeni. Na Allaah Anatosheleza kuwa Mwenye Kuhisabu.[4]
لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِّمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ مِمَّا قَلَّ مِنْهُ أَوْ كَثُرَ ۚ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا ﴿٧﴾
7. Wanaume wana fungu katika yale waliyoacha wazazi na jamaa wa karibu. Na wanawake wana fungu katika yale waliyoacha wazazi na jamaa wa karibu, ikiwa ni kidogo au kingi. Ni fungu la kisharia lilofaridhishwa.
وَإِذَا حَضَرَ الْقِسْمَةَ أُولُو الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينُ فَارْزُقُوهُم مِّنْهُ وَقُولُوا لَهُمْ قَوْلًا مَّعْرُوفًا ﴿٨﴾
8. Na wakati wa kugawa, wakihudhuria jamaa wa karibu na mayatima na masikini, basi wapeni kitu katika hayo na wasemezeni kauli njema ya haki na kwa huruma.
وَلْيَخْشَ الَّذِينَ لَوْ تَرَكُوا مِنْ خَلْفِهِمْ ذُرِّيَّةً ضِعَافًا خَافُوا عَلَيْهِمْ فَلْيَتَّقُوا اللَّـهَ وَلْيَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا ﴿٩﴾
9. Na waogope (wasimamizi kukhini) wale ambao lau nao wangeliacha nyuma yao dhuriya dhaifu, wangeliwakhofia. Basi wamche Allaah na waseme kauli iliyo sawa ya haki.
إِنَّ الَّذِينَ يَأْكُلُونَ أَمْوَالَ الْيَتَامَىٰ ظُلْمًا إِنَّمَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ نَارًا ۖ وَسَيَصْلَوْنَ سَعِيرًا ﴿١٠﴾
10. Hakika wale wanaokula mali ya mayatima kwa dhulma hapana shaka kwamba wanakula katika matumbo yao moto, na watauingia moto uliowashwa vikali mno.
يُوصِيكُمُ اللَّـهُ فِي أَوْلَادِكُمْ ۖ لِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ ۚ فَإِن كُنَّ نِسَاءً فَوْقَ اثْنَتَيْنِ فَلَهُنَّ ثُلُثَا مَا تَرَكَ ۖ وَإِن كَانَتْ وَاحِدَةً فَلَهَا النِّصْفُ ۚ وَلِأَبَوَيْهِ لِكُلِّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا السُّدُسُ مِمَّا تَرَكَ إِن كَانَ لَهُ وَلَدٌ ۚ فَإِن لَّمْ يَكُن لَّهُ وَلَدٌ وَوَرِثَهُ أَبَوَاهُ فَلِأُمِّهِ الثُّلُثُ ۚ فَإِن كَانَ لَهُ إِخْوَةٌ فَلِأُمِّهِ السُّدُسُ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِي بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۗ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ لَا تَدْرُونَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ لَكُمْ نَفْعًا ۚ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١١﴾
11. Allaah Anakuamrisheni kuhusu watoto wenu. Mwanamume atastahiki mfano wa fungu la wanawake wawili. Na ikiwa wanawake ni zaidi ya wawili basi watastahiki theluthi mbili za alichoacha (maiti). Lakini akiwa mtoto wa kike ni mmoja pekee basi atastahiki nusu, na wazazi wake wawili kila mmoja wao atastahiki sudusi katika alichoacha ikiwa anaye mtoto. Na ikiwa hakuwa na mtoto na wazazi wake wawili ndio warithi wake, basi mama yake atastahiki theluthi moja. Na ikiwa anao ndugu, basi mama yake atastahiki sudusi, baada ya kutoa wasia aliousia (maiti) au kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu, hamjui ni yupi miongoni mwao aliye karibu zaidi kwenu kwa manufaa. Ni sharia kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.[5]
وَلَكُمْ نِصْفُ مَا تَرَكَ أَزْوَاجُكُمْ إِن لَّمْ يَكُن لَّهُنَّ وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَ لَهُنَّ وَلَدٌ فَلَكُمُ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكْنَ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِينَ بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۚ وَلَهُنَّ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكْتُمْ إِن لَّمْ يَكُن لَّكُمْ وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَ لَكُمْ وَلَدٌ فَلَهُنَّ الثُّمُنُ مِمَّا تَرَكْتُم ۚ مِّن بَعْدِ وَصِيَّةٍ تُوصُونَ بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۗ وَإِن كَانَ رَجُلٌ يُورَثُ كَلَالَةً أَوِ امْرَأَةٌ وَلَهُ أَخٌ أَوْ أُخْتٌ فَلِكُلِّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا السُّدُسُ ۚ فَإِن كَانُوا أَكْثَرَ مِن ذَٰلِكَ فَهُمْ شُرَكَاءُ فِي الثُّلُثِ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصَىٰ بِهَا أَوْ دَيْنٍ غَيْرَ مُضَارٍّ ۚ وَصِيَّةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَلِيمٌ ﴿١٢﴾
12. Nanyi mtastahiki nusu katika walichoacha wake zenu ikiwa hawakuwa na mtoto. Na ikiwa wana mtoto, basi mtastahiki robo katika walichoacha, baada ya kutoa wasia waliyousia au kulipa deni. Nao wake zenu watastahiki robo katika mlichoacha ikiwa hamna mtoto. Na ikiwa mna mtoto, basi watastahiki thumni katika mlichoacha, baada ya kutoa wasia mliousia au kulipa deni. Na ikiwa mwanamume au mwanamke anayerithiwa hana mtoto wala wazazi, lakini anaye kaka au dada, basi kila mmoja kati yao atastahiki sudusi. Na wakiwa ni wengi ya hivyo, basi watashirikiana katika theluthi, baada ya kutoa wasia uliousiwa na kulipwa deni pasipo kuleta dhara. Huu ni wasia kutoka kwa Allaah, na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mvumilivu.
تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ ۚ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٣﴾
13. Hiyo ni Mipaka ya Allaah. Na yeyote atakayemtii Allaah na Rasuli Wake Atamuingiza Jannaat zipitazo chini yake mito, watadumu humo, na huko ndiko kufuzu kukubwa mno.
وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُ يُدْخِلْهُ نَارًا خَالِدًا فِيهَا وَلَهُ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿١٤﴾
14. Na yeyote atakayemuasi Allaah na Rasuli Wake na akataadi Mipaka Yake Atamuingiza motoni, atadumu humo na atapata adhabu ya kudhalilisha.
وَاللَّاتِي يَأْتِينَ الْفَاحِشَةَ مِن نِّسَائِكُمْ فَاسْتَشْهِدُوا عَلَيْهِنَّ أَرْبَعَةً مِّنكُمْ ۖ فَإِن شَهِدُوا فَأَمْسِكُوهُنَّ فِي الْبُيُوتِ حَتَّىٰ يَتَوَفَّاهُنَّ الْمَوْتُ أَوْ يَجْعَلَ اللَّـهُ لَهُنَّ سَبِيلًا ﴿١٥﴾
15. Na wale wanaofanya uchafu miongoni mwa wanawake wenu, basi washuhudisheni mashahidi wanne kati yenu. Na wakishuhudia basi wazuieni majumbani mpaka mauti yawafishe au Allaah Awajaalie njia (nyingine).
وَاللَّذَانِ يَأْتِيَانِهَا مِنكُمْ فَآذُوهُمَا ۖ فَإِن تَابَا وَأَصْلَحَا فَأَعْرِضُوا عَنْهُمَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ تَوَّابًا رَّحِيمًا ﴿١٦﴾
16. Na wale wawili wanaofanya huo (uchafu) waadhibuni. Wakitubu na wakajirekebisha basi waacheni. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.
إِنَّمَا التَّوْبَةُ عَلَى اللَّـهِ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السُّوءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٍ فَأُولَـٰئِكَ يَتُوبُ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١٧﴾
17. Hakika tawbah inayokubaliwa na Allaah ni ya wale wanaofanya uovu kwa ujahili kisha wakatubia haraka, basi hao Allaah Anapokea tawbah yao. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
وَلَيْسَتِ التَّوْبَةُ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ حَتَّىٰ إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ إِنِّي تُبْتُ الْآنَ وَلَا الَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمْ كُفَّارٌ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٨﴾
18. Lakini tawbah si kwa wale wanaofanya maovu mpaka mauti yanapomjia mmoja wao ndipo aseme: Hakika mimi sasa nimetubu. Na wala wale wanaokufa na hali wao ni makafiri. Hao Tumewaandalia adhabu iumizayo.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَحِلُّ لَكُمْ أَن تَرِثُوا النِّسَاءَ كَرْهًا ۖ وَلَا تَعْضُلُوهُنَّ لِتَذْهَبُوا بِبَعْضِ مَا آتَيْتُمُوهُنَّ إِلَّا أَن يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ ۚ وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ فَإِن كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَيَجْعَلَ اللَّـهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا ﴿١٩﴾
19. Enyi walioamini! Si halali kwenu kurithi wanawake kwa kuwalazimisha. Na wala msiwazuie kwa inda ili mpokonye baadhi ya vile mlivyowapa isipokuwa wakiwa wamefanya uchafu bayana. Na kaeni nao kwa wema. Na mkiwachukia, basi asaa mkachukia jambo na Allaah Akalijaalia kuwa lenye kheri nyingi ndani yake.[6]
وَإِنْ أَرَدتُّمُ اسْتِبْدَالَ زَوْجٍ مَّكَانَ زَوْجٍ وَآتَيْتُمْ إِحْدَاهُنَّ قِنطَارًا فَلَا تَأْخُذُوا مِنْهُ شَيْئًا ۚ أَتَأْخُذُونَهُ بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿٢٠﴾
20. Na mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, na mmempa mmoja wao mirundi ya mali, basi msichukue humo chochote. Je, mnaichukua kwa dhulma na dhambi iliyo bayana?
وَكَيْفَ تَأْخُذُونَهُ وَقَدْ أَفْضَىٰ بَعْضُكُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ وَأَخَذْنَ مِنكُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا ﴿٢١﴾
21. Na mtaichukuaje na hali nyinyi kwa nyinyi mmeingiliana (kimwili na kustarehe), na wao wanawake wamechukua toka kwenu fungamano thabiti?
وَلَا تَنكِحُوا مَا نَكَحَ آبَاؤُكُم مِّنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۚ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَمَقْتًا وَسَاءَ سَبِيلًا ﴿٢٢﴾
22. Na wala msiwaoe wanawake waliowaoa baba zenu isipokuwa yaliyokwisha pita. Hakika hayo yalikuwa ni uchafu na chukizo na njia ovu.[7]
حُرِّمَتْ عَلَيْكُمْ أُمَّهَاتُكُمْ وَبَنَاتُكُمْ وَأَخَوَاتُكُمْ وَعَمَّاتُكُمْ وَخَالَاتُكُمْ وَبَنَاتُ الْأَخِ وَبَنَاتُ الْأُخْتِ وَأُمَّهَاتُكُمُ اللَّاتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُم مِّنَ الرَّضَاعَةِ وَأُمَّهَاتُ نِسَائِكُمْ وَرَبَائِبُكُمُ اللَّاتِي فِي حُجُورِكُم مِّن نِّسَائِكُمُ اللَّاتِي دَخَلْتُم بِهِنَّ فَإِن لَّمْ تَكُونُوا دَخَلْتُم بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ وَحَلَائِلُ أَبْنَائِكُمُ الَّذِينَ مِنْ أَصْلَابِكُمْ وَأَن تَجْمَعُوا بَيْنَ الْأُخْتَيْنِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٢٣﴾
23. Mmeharamishiwa (kuwaoa) mama zenu, na mabinti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na makhalati zenu (mama wakubwa na wadogo), na mabinti wa kaka, na mabinti wa dada, na mama zenu ambao wamekunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu waliozaliwa na wake zenu ambao mmewaingilia. Lakini ikiwa hamkuwaingilia basi hakuna dhambi (kuwaoa). Na (mmeharamishwa) wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu, na kuwaoa dada wawili kwa wakati mmoja, isipokuwa yaliyokwisha pita. Hakika Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.
وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۖ كِتَابَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ ۚ وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَاءَ ذَٰلِكُمْ أَن تَبْتَغُوا بِأَمْوَالِكُم مُّحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ ۚ فَمَا اسْتَمْتَعْتُم بِهِ مِنْهُنَّ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا تَرَاضَيْتُم بِهِ مِن بَعْدِ الْفَرِيضَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿٢٤﴾
24. Na (Mmeharamishiwa pia) wanawake walio katika ndoa isipokuwa iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ni sharia ya Allaah kwenu. Na mmehalalishiwa wengineo wasiokuwa hao, mtafute (kuwaoa) kwa mali zenu mkijistahi pasi na kuzini. Basi mliostarehe nao[8], wapeni mahari yao kwa kuwa ni waajib. Na wala si dhambi kwenu katika mliyoridhiana baada ya kukamilika ya waajib. Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.[9]
وَمَن لَّمْ يَسْتَطِعْ مِنكُمْ طَوْلًا أَن يَنكِحَ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ فَمِن مَّا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُم مِّن فَتَيَاتِكُمُ الْمُؤْمِنَاتِ ۚ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِكُم ۚ بَعْضُكُم مِّن بَعْضٍ ۚ فَانكِحُوهُنَّ بِإِذْنِ أَهْلِهِنَّ وَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ مُحْصَنَاتٍ غَيْرَ مُسَافِحَاتٍ وَلَا مُتَّخِذَاتِ أَخْدَانٍ ۚ فَإِذَا أُحْصِنَّ فَإِنْ أَتَيْنَ بِفَاحِشَةٍ فَعَلَيْهِنَّ نِصْفُ مَا عَلَى الْمُحْصَنَاتِ مِنَ الْعَذَابِ ۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِيَ الْعَنَتَ مِنكُمْ ۚ وَأَن تَصْبِرُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٥﴾
25. Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea wanawake Waumini walio huru, basi (aoe) katika wale iliyomiliki mikono yenu ya kulia miongoni mwa wajakazi wenu Waumini. Na Allaah Anajua zaidi imaan yenu. Nyinyi (Waumini) mmetokana wenyewe kwa wenyewe. Basi waoeni kwa idhini ya watu wao na wapeni mahari yao kwa ada inayokubalika, wawe wanawake wanaojistiri na machafu si makahaba na wala si wenye kuchukua hawara. Na watakapohifadhiwa katika ndoa, kisha wakafanya uchafu basi adhabu yao itakuwa ni nusu ya adhabu ya waliyowekewa wanawake walio huru (wasioolewa). Hayo ni kwa yule anayeogopa dhambi ya zinaa miongoni mwenu. Na mkisubiri itakuwa ni kheri kwenu. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُبَيِّنَ لَكُمْ وَيَهْدِيَكُمْ سُنَنَ الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ وَيَتُوبَ عَلَيْكُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿٢٦﴾
26. Allaah Anataka kukubainishieni na kukuongozeni nyendo za wale walio kabla yenu, na Apokee tawbah kwenu. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
وَاللَّـهُ يُرِيدُ أَن يَتُوبَ عَلَيْكُمْ وَيُرِيدُ الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الشَّهَوَاتِ أَن تَمِيلُوا مَيْلًا عَظِيمًا ﴿٢٧﴾
27. Na Allaah Anataka kupokea tawbah kwenu, na wale wanaofuata matamanio wanataka mkengeuke, mkengeuko mkubwa mno.
يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمْ ۚ وَخُلِقَ الْإِنسَانُ ضَعِيفًا ﴿٢٨﴾
28. Allaah Anataka kukukhafifishieni (tabu zenu), kwani binaadam ameumbwa dhaifu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُم بَيْنَكُم بِالْبَاطِلِ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً عَن تَرَاضٍ مِّنكُمْ ۚ وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا ﴿٢٩﴾
29. Enyi walioamini! Msiliane mali zenu kwa ubatwilifu, isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana baina yenu. Wala msijiue. Hakika Allaah Ni Mwenye Kuwarehemuni.
وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ عُدْوَانًا وَظُلْمًا فَسَوْفَ نُصْلِيهِ نَارًا ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿٣٠﴾
30. Na atakayefanya hivyo kwa uadui na dhulma, basi Tutamuingiza motoni. Na hilo kwa Allaah ni jepesi mno.
إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا ﴿٣١﴾
31. Mkijiepusha na madhambi makubwa mnayokatazwa Tutakufutieni madhambi yenu madogo na Tutakuingizeni katika mahali patukufu.[10]
وَلَا تَتَمَنَّوْا مَا فَضَّلَ اللَّـهُ بِهِ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ لِّلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبُوا ۖ وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِّمَّا اكْتَسَبْنَ ۚ وَاسْأَلُوا اللَّـهَ مِن فَضْلِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٣٢﴾
32. Wala msitamani ambayo Allaah Amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wanayo sehemu katika waliyoyachuma, na wanawake wana sehemu katika waliyoyachuma. Na muombeni Allaah katika Fadhila Zake. Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa kila kitu.
وَلِكُلٍّ جَعَلْنَا مَوَالِيَ مِمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ ۚ وَالَّذِينَ عَقَدَتْ أَيْمَانُكُمْ فَآتُوهُمْ نَصِيبَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدًا ﴿٣٣﴾
33. Na kila mmoja Tumemuwekea warithi katika yale waliyoyaacha wazazi wawili na jamaa wa karibu. Na wale mliofungamana nao viapo (vya undugu) basi wapeni fungu lao. Hakika Allaah daima Ni Shahidi juu ya kila kitu.
الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّـهُ ۚ وَاللَّاتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ ۖ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلَا تَبْغُوا عَلَيْهِنَّ سَبِيلًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا ﴿٣٤﴾
34. Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine, na pia kwa ambayo wanatoa katika mali zao. Basi wanawake wema ni wale watiifu, wenye kujihifadhi katika hali ya kutokuweko waume zao kwa kuwa Allaah Ameamrisha wajihifadhi. Na wale ambao mnakhofu uasi wao wa ndoa, basi wanasihini na wahameni katika malazi na wapigeni[11] (kipigo kisichodhuru). Wakikutiini, basi msitafute njia dhidi yao (ya kuwaudhi). Hakika Allaah daima Ni Mwenye ‘Uluwa Uliotukuka, Mkubwa Kabisa.[12]
وَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَابْعَثُوا حَكَمًا مِّنْ أَهْلِهِ وَحَكَمًا مِّنْ أَهْلِهَا إِن يُرِيدَا إِصْلَاحًا يُوَفِّقِ اللَّـهُ بَيْنَهُمَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرًا ﴿٣٥﴾
35. Na mkikhofu mafarikiano baina yao wawili, basi pelekeni mwamuzi kutoka watu wa mume na mwamuzi kutoka watu wa mke. Wakitaka sulhu, basi Allaah Atawawafikisha baina yao. Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Khabari za dhahiri na siri.
وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَالْجَارِ الْجُنُبِ وَالصَّاحِبِ بِالْجَنبِ وَابْنِ السَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ مُخْتَالًا فَخُورًا ﴿٣٦﴾
36. Na mwabuduni Allaah wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni ihsaan wazazi wawili, na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini, na jirani mwenye ujamaa na jirani asiye na ujamaa, na rafiki wa karibu, na msafiri aliyeishiwa masurufu, na wale iliyowamiliki mikono yenu ya kulia. Hakika Allaah Hapendi mwenye majivuno na mwenye kujifakharisha.
الَّذِينَ يَبْخَلُونَ وَيَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبُخْلِ وَيَكْتُمُونَ مَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۗ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿٣٧﴾
37. (Pia Hawapendi) Wale wanaofanya ubakhili na wanawaamrisha watu ubakhili na wanaficha Aliyowapa Allaah katika Fadhila Zake. Na Tumewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.
وَالَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ رِئَاءَ النَّاسِ وَلَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ ۗ وَمَن يَكُنِ الشَّيْطَانُ لَهُ قَرِينًا فَسَاءَ قَرِينًا ﴿٣٨﴾
38. Na (Tumewaandalia pia adhabu hiyo) wale wanaotoa mali zao riyaa-a[13] (kujionyesha) kwa watu wala hawamwamini Allaah wala Siku ya Mwisho. Na yule ambaye shaytwaan amekuwa ni rafiki yake mwandani, basi mbaya alioje rafiki mwandani (huyo)!
وَمَاذَا عَلَيْهِمْ لَوْ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقَهُمُ اللَّـهُ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِهِمْ عَلِيمًا ﴿٣٩﴾
39. Na ingeliwadhuru nini wao lau wangelimwamini Allaah na Siku ya Mwisho na wakatoa katika yale Aliyowaruzuku Allaah? Na Allaah Ni Mwenye Kuwajua vyema.
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةً يُضَاعِفْهَا وَيُؤْتِ مِن لَّدُنْهُ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٤٠﴾
40. Hakika Allaah Hadhulumu hata uzito au chembe (kama atomu). Na ikiwa ni amali njema Huizidisha na Hutoa kutoka Kwake ujira mkuu kabisa.
فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ شَهِيدًا ﴿٤١﴾
41. Basi itakuwaje Tutakapoleta kutoka kila ummah shahidi, na Tukakuleta (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa shahidi juu ya hawa?[14]
يَوْمَئِذٍ يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَعَصَوُا الرَّسُولَ لَوْ تُسَوَّىٰ بِهِمُ الْأَرْضُ وَلَا يَكْتُمُونَ اللَّـهَ حَدِيثًا ﴿٤٢﴾
42. Siku hiyo wale waliokufuru na wakamuasi Rasuli watatamani lau ardhi ingesawazishwa juu yao. Na wala hawatoweza kumficha Allaah kauli hata moja.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَفُوًّا غَفُورًا ﴿٤٣﴾
43. Enyi walioamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa[15] mpaka mjue mnayoyasema, wala mkiwa mna janaba isipokuwa mmo safarini mpaka muoge josho. Na mkiwa wagonjwa au safarini au mmoja wenu ametoka msalani au mmewagusa wanawake kisha hamkupata maji, basi ikusudieni ardhi safi ya mchanga (mtayammam)[16]; mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Allaah daima Ni Mwingi wa Kusamehe, Mwingi wa Kughufuria.[17]
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يَشْتَرُونَ الضَّلَالَةَ وَيُرِيدُونَ أَن تَضِلُّوا السَّبِيلَ ﴿٤٤﴾
44. Je, huoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanakhiari upotofu na wanataka mpotee njia?
وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِأَعْدَائِكُمْ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَلِيًّا وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ نَصِيرًا ﴿٤٥﴾
45. Na Allaah Anawajua zaidi maadui zenu, na Allaah Anatosha kuwa Rafiki Mlinzi na Allaah Anatosha kuwa Mwenye Kunusuru.
مِّنَ الَّذِينَ هَادُوا يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ وَيَقُولُونَ سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَاسْمَعْ غَيْرَ مُسْمَعٍ وَرَاعِنَا لَيًّا بِأَلْسِنَتِهِمْ وَطَعْنًا فِي الدِّينِ ۚ وَلَوْ أَنَّهُمْ قَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا وَاسْمَعْ وَانظُرْنَا لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَقْوَمَ وَلَـٰكِن لَّعَنَهُمُ اللَّـهُ بِكُفْرِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُونَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٤٦﴾
46. Katika Mayahudi wako wanaobadilisha maneno kuyatoa mahali pake, na husema (kumwambia Rasuli): Tumesikia (maneno yako) na tumeasi, na sikia bila ya kusikilizwa. Na (humwambia pia): Raa’inaa[18] kwa kuzipotoa ndimi zao na kutukana Dini. Na lau wangesema: Tumesikia na tumetii, na sikia na undhwurnaa, basi ingelikuwa kheri kwao na sawa zaidi. Lakini Allaah Amewalaani kwa kufru yao, basi hawaamini isipokuwa wachache tu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ آمِنُوا بِمَا نَزَّلْنَا مُصَدِّقًا لِّمَا مَعَكُم مِّن قَبْلِ أَن نَّطْمِسَ وُجُوهًا فَنَرُدَّهَا عَلَىٰ أَدْبَارِهَا أَوْ نَلْعَنَهُمْ كَمَا لَعَنَّا أَصْحَابَ السَّبْتِ ۚ وَكَانَ أَمْرُ اللَّـهِ مَفْعُولًا ﴿٤٧﴾
47. Enyi mliopewa Kitabu! Aminini yale Tuliyoyateremsha (kwa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) yanayosadikisha yale mliyonayo, kabla hatujabadilisha nyuso Tukazirudisha kisogoni, au Tukawalaani kama Tulivyowalaani watu wa As-Sabt.[19] Na Amri ya Allaah itafanyika tu.
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا ﴿٤٨﴾
48. Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa, lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha[20] Allaah basi kwa yakini amezua dhambi kuu kabisa.
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يُزَكُّونَ أَنفُسَهُم ۚ بَلِ اللَّـهُ يُزَكِّي مَن يَشَاءُ وَلَا يُظْلَمُونَ فَتِيلًا ﴿٤٩﴾
49. Je, hukuwaona wale wanaojitakasa nafsi zao? Bali Allaah Humtakasa Amtakaye, na wala hawatodhulumiwa hata kadiri ya uzi katika kokwa ya tende.
انظُرْ كَيْفَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۖ وَكَفَىٰ بِهِ إِثْمًا مُّبِينًا ﴿٥٠﴾
50. Tazama vipi wanavyomtungia uongo Allaah, na yatosha haya kuwa dhambi za dhahiri.
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُؤْمِنُونَ بِالْجِبْتِ وَالطَّاغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا هَـٰؤُلَاءِ أَهْدَىٰ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا سَبِيلًا ﴿٥١﴾
51. Je, huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanaamini Al-Jibt (itikadi potofu) na twaghuti[21] na wanasema juu ya wale waliokufuru kuwa: Hawa wameongoka zaidi katika njia kuliko wale walioamini.[22]
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ ۖ وَمَن يَلْعَنِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ نَصِيرًا ﴿٥٢﴾
52. Hao ndio wale Allaah Aliowalaani. Na ambaye Allaah Amemlaani, kamwe hutamkuta kuwa na (mtu) wa kumsaidia.
أَمْ لَهُمْ نَصِيبٌ مِّنَ الْمُلْكِ فَإِذًا لَّا يُؤْتُونَ النَّاسَ نَقِيرًا ﴿٥٣﴾
53. Au wanayo sehemu ya ufalme (wa Allaah?). Basi hapo wasingeliwapa watu kadiri ya kitone cha kokwa ya tende.
أَمْ يَحْسُدُونَ النَّاسَ عَلَىٰ مَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۖ فَقَدْ آتَيْنَا آلَ إِبْرَاهِيمَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَآتَيْنَاهُم مُّلْكًا عَظِيمًا ﴿٥٤﴾
54. Au wanawahusudu watu (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم na Waumini) kwa yale Aliyowapa Allaah katika Fadhila Zake? Basi kwa yakini Tuliwapa kizazi cha Ibraahiym Kitabu na Hikmah na Tukawapa ufalme mkubwa mno.
فَمِنْهُم مَّنْ آمَنَ بِهِ وَمِنْهُم مَّن صَدَّ عَنْهُ ۚ وَكَفَىٰ بِجَهَنَّمَ سَعِيرًا ﴿٥٥﴾
55. Basi miongoni mwao wako waliomuamini (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na miongoni mwao wako waliomkengeuka. Na Jahannam inatosheleza kuwa ni moto uliowashwa vikali mno.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا سَوْفَ نُصْلِيهِمْ نَارًا كُلَّمَا نَضِجَتْ جُلُودُهُم بَدَّلْنَاهُمْ جُلُودًا غَيْرَهَا لِيَذُوقُوا الْعَذَابَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿٥٦﴾
56. Hakika wale waliokanusha Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) Zetu Tutawaingiza motoni. Kila ngozi zao zitakapobanikika zikaungua Tutawabadilishia ngozi nyingine ili waionje adhabu. Hakika Allaah daima Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَنُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ لَّهُمْ فِيهَا أَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ ۖ وَنُدْخِلُهُمْ ظِلًّا ظَلِيلًا ﴿٥٧﴾
57. Na wale walioamini na wakatenda mema Tutawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito, watadumu humo abadi. Watapata humo wake waliotakasika na Tutawaingiza katika vivuli vizuri vya raha tele.
إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ النَّاسِ أَن تَحْكُمُوا بِالْعَدْلِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ سَمِيعًا بَصِيرًا ﴿٥٨﴾
58. Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe. Na mtakapohukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Ni uzuri ulioje wa Anayokuwaidhini kwayo Allaah! Hakika Allaah daima Ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.[23]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا ﴿٥٩﴾
59. Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli mkiwa mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri zaidi.[24]
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَن يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿٦٠﴾
60. Je, huoni wale wanaodai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako, wanataka wahukumiane kwa twaghuti (ubatwilifu) na hali wameamrishwa wakanushe hayo. Na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali.[25]
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودًا ﴿٦١﴾
61. Na wanapoambiwa: Njooni kwenye yale Aliyoyateremsha Allaah na kwa Rasuli, utawaona wanafiki wanakugeukilia mbali kwa mkengeuko.
فَكَيْفَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ثُمَّ جَاءُوكَ يَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا إِحْسَانًا وَتَوْفِيقًا ﴿٦٢﴾
62. Basi itakuwaje utakapowafika msiba kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yao? Kisha wakakujia wakiapa: Wa-Allaahi hatukutaka ila mazuri na mapatano.
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَعْلَمُ اللَّـهُ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَعِظْهُمْ وَقُل لَّهُمْ فِي أَنفُسِهِمْ قَوْلًا بَلِيغًا ﴿٦٣﴾
63. Hao ndio ambao Allaah Anayajua yaliyomo ndani ya nyoyo zao. Basi waachilie mbali na wape mawaidha (ya kuwaonya) na waambie kwa siri maneno mazito ya kuwatua na kuwagonga.
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا لِيُطَاعَ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذ ظَّلَمُوا أَنفُسَهُمْ جَاءُوكَ فَاسْتَغْفَرُوا اللَّـهَ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمُ الرَّسُولُ لَوَجَدُوا اللَّـهَ تَوَّابًا رَّحِيمًا﴿٦٤﴾
64. Na Hatukutuma Rasuli yeyote ila atiiwe kwa Idhini ya Allaah. Na lau wao pale walipojidhulumu nafsi zao wangelikujia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wakamwomba Allaah maghfirah na Rasuli akawaombea maghfirah, basi wangelimkuta Allaah Ni Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.
فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾
65. Basi mambo si kama wanavyodai. Naapa kwa Rabb wako, hawatakuwa Waumini wa kweli mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao ukakasi katika yale uliyohukumu, na waikubali hukmu yako kwa moyo safi na maridhio.[26]
وَلَوْ أَنَّا كَتَبْنَا عَلَيْهِمْ أَنِ اقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ أَوِ اخْرُجُوا مِن دِيَارِكُم مَّا فَعَلُوهُ إِلَّا قَلِيلٌ مِّنْهُمْ ۖ وَلَوْ أَنَّهُمْ فَعَلُوا مَا يُوعَظُونَ بِهِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَشَدَّ تَثْبِيتًا ﴿٦٦﴾
66. Na lau Tungeliwaandikia amri: Jiueni nafsi zenu na tokeni katika majumba yenu, wasingelifanya hayo ila wachache miongoni mwao. Na lau wangelifanya yale waliyowaidhiwa kwayo ingelikuwa kheri kwao na uthibitisho wa nguvu zaidi (wa imaan zao).
وَإِذًا لَّآتَيْنَاهُم مِّن لَّدُنَّا أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٦٧﴾
67. Na hapo Tungeliwapa kutoka Kwetu ujira mkubwa mno.
وَلَهَدَيْنَاهُمْ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا ﴿٦٨﴾
68. Na Tungewaongoza njia iliyonyooka.
وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا ﴿٦٩﴾
69. Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah Aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na Swiddiqiyna na Shuhadaa na Swalihina, na uzuri ulioje kuwa pamoja na hao![27]
ذَٰلِكَ الْفَضْلُ مِنَ اللَّـهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ عَلِيمًا ﴿٧٠﴾
70. Hiyo ni fadhila kutoka kwa Allaah. Na inatosheleza Allaah kuwa Ni Mjuzi wa yote.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا خُذُوا حِذْرَكُمْ فَانفِرُوا ثُبَاتٍ أَوِ انفِرُوا جَمِيعًا ﴿٧١﴾
71. Enyi walioamini! Chukueni tahadhari yenu! Na tokeni kwa vikosi vikosi au tokeni kwa pamoja.
وَإِنَّ مِنكُمْ لَمَن لَّيُبَطِّئَنَّ فَإِنْ أَصَابَتْكُم مُّصِيبَةٌ قَالَ قَدْ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيَّ إِذْ لَمْ أَكُن مَّعَهُمْ شَهِيدًا ﴿٧٢﴾
72. Na katika nyinyi yuko anayejikokota abakie nyuma (asiende vitani). Na unapokusibuni msiba husema: Kwa yakini Allaah Kanipenda nilivyokuwa sikwenda nao vitani.
وَلَئِنْ أَصَابَكُمْ فَضْلٌ مِّنَ اللَّـهِ لَيَقُولَنَّ كَأَن لَّمْ تَكُن بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُ مَوَدَّةٌ يَا لَيْتَنِي كُنتُ مَعَهُمْ فَأَفُوزَ فَوْزًا عَظِيمًا ﴿٧٣﴾
73. Na ikikufikieni fadhila kutoka kwa Allaah husema (kwa majuto) kama kwamba hakukuwa baina yenu na yeye mapenzi: Laiti ningelikuwa pamoja nao nikapata kufuzu mafanikio makubwa mno.
فَلْيُقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ الَّذِينَ يَشْرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا بِالْآخِرَةِ ۚ وَمَن يُقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيُقْتَلْ أَوْ يَغْلِبْ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٧٤﴾
74. Basi wapigane katika Njia ya Allaah wale wanaouza uhai (wao) wa dunia kwa Aakhirah. Na atakayepigana katika Njia ya Allaah akauliwa au akashinda basi Tutampa ujira mkubwa mno.
وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـٰذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا ﴿٧٥﴾
75. Na mna nini hata msipigane katika Njia ya Allaah, nailhali walio wanyonge kati ya wanaume na wanawake na watoto ambao (kwa vile hawana wa kuwasaidia isipokuwa kuelekea kwa Rabb wao) husema: Rabb wetu! Tutoe kutoka katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na Tujaalie kutoka Kwako rafiki mlinzi na Tujaalie kutoka Kwako mwenye kunusuru.
الَّذِينَ آمَنُوا يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ الطَّاغُوتِ فَقَاتِلُوا أَوْلِيَاءَ الشَّيْطَانِ ۖ إِنَّ كَيْدَ الشَّيْطَانِ كَانَ ضَعِيفًا ﴿٧٦﴾
76. Wale walioamini hupigana katika Njia ya Allaah. Na wale waliokufuru hupigana katika njia ya twaghuti (kumtii shaytwaan). Basi wapigeni marafiki wandani na walinzi wa shaytwaan. Hakika hila za shaytwaan daima ni dhaifu.
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ قِيلَ لَهُمْ كُفُّوا أَيْدِيَكُمْ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقِتَالُ إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَخْشَوْنَ النَّاسَ كَخَشْيَةِ اللَّـهِ أَوْ أَشَدَّ خَشْيَةً ۚ وَقَالُوا رَبَّنَا لِمَ كَتَبْتَ عَلَيْنَا الْقِتَالَ لَوْلَا أَخَّرْتَنَا إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ ۗ قُلْ مَتَاعُ الدُّنْيَا قَلِيلٌ وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ لِّمَنِ اتَّقَىٰ وَلَا تُظْلَمُونَ فَتِيلًا ﴿٧٧﴾
77. Je, huoni wale walioambiwa: Zuieni mikono yenu (msipigane) na simamisheni Swalaah na toeni Zakaah. Basi walipoandikiwa amri kupigana, mara kundi miongoni mwao linawaogopa watu kama kumwogopa Allaah au woga zaidi. Na husema: Rabb wetu! Kwa nini Umetuamrisha kupigana? Lau Ungelituakhirishia hadi muda kidogo hivi! Sema: Starehe za dunia ni chache, na Aakhirah ni bora zaidi kwa mwenye taqwa, wala hamtodhulumiwa kadiri ya uzi wa kokwa ya tende.[28]
أَيْنَمَا تَكُونُوا يُدْرِككُّمُ الْمَوْتُ وَلَوْ كُنتُمْ فِي بُرُوجٍ مُّشَيَّدَةٍ ۗ وَإِن تُصِبْهُمْ حَسَنَةٌ يَقُولُوا هَـٰذِهِ مِنْ عِندِ اللَّـهِ ۖ وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ يَقُولُوا هَـٰذِهِ مِنْ عِندِكَ ۚ قُلْ كُلٌّ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ ۖ فَمَالِ هَـٰؤُلَاءِ الْقَوْمِ لَا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ حَدِيثًا ﴿٧٨﴾
78. Popote mtakapokuwa yatakufikieni mauti, japo mkiwa katika minara (au ngome) imara na madhubuti. Na likiwafikia jambo zuri husema: Hili linatoka kwa Allaah. Na likiwasibu ovu husema: Hili linatoka kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Sema: Yote ni yanatoka kwa Allaah. Basi wana nini hawa watu hawakaribii kufahamu maneno?
مَّا أَصَابَكَ مِنْ حَسَنَةٍ فَمِنَ اللَّـهِ ۖ وَمَا أَصَابَكَ مِن سَيِّئَةٍ فَمِن نَّفْسِكَ ۚ وَأَرْسَلْنَاكَ لِلنَّاسِ رَسُولًا ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا ﴿٧٩﴾
79. Zuri lililokufikia linatoka kwa Allaah. Na ubaya uliokusibu (ee mwanaadam) ni kutokana na nafsi yako. Na Tumekutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa watu uwe Rasuli na inatosheleza Allaah kuwa Ni Mwenye Kushuhudia yote.
مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ ۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ﴿٨٠﴾
80. Atakayemtii Rasuli basi kwa yakini amemtii Allaah.[29] Na atakayekengeuka basi Hatukukutuma kuwa mlinzi juu yao.
وَيَقُولُونَ طَاعَةٌ فَإِذَا بَرَزُوا مِنْ عِندِكَ بَيَّتَ طَائِفَةٌ مِّنْهُمْ غَيْرَ الَّذِي تَقُولُ ۖ وَاللَّـهُ يَكْتُبُ مَا يُبَيِّتُونَ ۖ فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿٨١﴾
81. Na wanasema (wanafiki): Tunatii. Lakini wanapotoka kutoka kwako, kundi miongoni mwao hukesha kushauriana na kupanga kinyume na unayoyasema. Na Allaah Anayaandika yale wanayoyapanga usiku. Basi waachilie mbali na tawakali kwa Allaah. Na inatosheleza Allaah kuwa Ni Mtegemewa.[30]
أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ ۚ وَلَوْ كَانَ مِنْ عِندِ غَيْرِ اللَّـهِ لَوَجَدُوا فِيهِ اخْتِلَافًا كَثِيرًا ﴿٨٢﴾
82. Je, hawaizingatii Qur-aan? Na lau ingelikuwa imetoka kwa asiyekuwa Allaah, bila shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi.[31]
وَإِذَا جَاءَهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الْأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُوا بِهِ ۖ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَىٰ أُولِي الْأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ ۗ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٨٣﴾
83. Na linapowafikia jambo lolote kuhusu amani au khofu hulitangaza. Na lau wangelirudisha kwa Rasuli na kwa wenye madaraka kati yao, basi watakaolitafiti miongoni mwao wangelipatia jibu jambo hilo (kama linafaa kutangazwa au kufichwa). Na lau si Fadhila ya Allaah juu yenu na Rehma Yake kwa yakini mngelimfuata shaytwaan ila wachache tu.[32]
فَقَاتِلْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ لَا تُكَلَّفُ إِلَّا نَفْسَكَ ۚ وَحَرِّضِ الْمُؤْمِنِينَ ۖ عَسَى اللَّـهُ أَن يَكُفَّ بَأْسَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ وَاللَّـهُ أَشَدُّ بَأْسًا وَأَشَدُّ تَنكِيلًا ﴿٨٤﴾
84. Basi pigana (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika Njia ya Allaah, hukalifishwi ila nafsi yako. Na wahimize Waumini (wakuunge). Allaah kwa hakika Atazuia mashambulizi ya nguvu ya waliokufuru. Na Allaah Ni Mkali zaidi wa Kushambulia na Mkali zaidi wa Kuadhibu adhabu ya tahadharisho na fundisho.
مَّن يَشْفَعْ شَفَاعَةً حَسَنَةً يَكُن لَّهُ نَصِيبٌ مِّنْهَا ۖ وَمَن يَشْفَعْ شَفَاعَةً سَيِّئَةً يَكُن لَّهُ كِفْلٌ مِّنْهَا ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُّقِيتًا ﴿٨٥﴾
85. Atakayesaidia kufanikisha jambo la kheri atapata fungu lake katika hayo. Na atakayesaidia kuunganisha jambo la shari atapata sehemu yake katika hayo. Na Allaah daima Ni Mwenye Kudhibiti na Mwangalizi wa kila kitu.
وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَسِيبًا ﴿٨٦﴾
86. Na mtapoamkiwa kwa maamkiziyoyote, basi itikieni kwa yaliyo mazuri zaidi kuliko hayo au yarudisheni hayo hayo.[33] Hakika Allaah daima Ni Mwenye Kuhesabu kila kitu.
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۗ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ حَدِيثًا ﴿٨٧﴾
87. Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Bila ya shaka Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah, haina shaka ndani yake. Na nani mkweli zaidi katika maneno kuliko Allaah?
فَمَا لَكُمْ فِي الْمُنَافِقِينَ فِئَتَيْنِ وَاللَّـهُ أَرْكَسَهُم بِمَا كَسَبُوا ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَهْدُوا مَنْ أَضَلَّ اللَّـهُ ۖ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا ﴿٨٨﴾
88. Basi mna nini hata mmekuwa makundi mawili kuhusu wanafiki, na hali Allaah Amewageuza (warudie ukafiri) kwa sababu ya waliyoyachuma? Je, mnataka kumhidi ambaye Allaah Amempotoa? Na aliyepotozwa na Allaah basi hutompatia kamwe njia (ya kumhidi).[34]
وَدُّوا لَوْ تَكْفُرُونَ كَمَا كَفَرُوا فَتَكُونُونَ سَوَاءً ۖ فَلَا تَتَّخِذُوا مِنْهُمْ أَوْلِيَاءَ حَتَّىٰ يُهَاجِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَخُذُوهُمْ وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ ۖ وَلَا تَتَّخِذُوا مِنْهُمْ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿٨٩﴾
89. Wanatamani kama mtakufuru kama walivyokufuru wao, ili muwe sawa sawa. Basi msiwafanye miongoni mwao marafiki wandani na walinzi mpaka wahajiri katika Njia ya Allaah. Wakikengeuka basi wakamateni na waueni popote muwapatapo. Wala msimfanye yeyote kati yao kuwa rafiki yenu wala msaidizi.
إِلَّا الَّذِينَ يَصِلُونَ إِلَىٰ قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَاقٌ أَوْ جَاءُوكُمْ حَصِرَتْ صُدُورُهُمْ أَن يُقَاتِلُوكُمْ أَوْ يُقَاتِلُوا قَوْمَهُمْ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَسَلَّطَهُمْ عَلَيْكُمْ فَلَقَاتَلُوكُمْ ۚ فَإِنِ اعْتَزَلُوكُمْ فَلَمْ يُقَاتِلُوكُمْ وَأَلْقَوْا إِلَيْكُمُ السَّلَمَ فَمَا جَعَلَ اللَّـهُ لَكُمْ عَلَيْهِمْ سَبِيلًا ﴿٩٠﴾
90. Isipokuwa wale waliokimbilia kupata hifadhi kwa watu ambao kuna mkataba kati yenu na wao, au wale waliokujieni vifua vyao vimedhikika kupigana nanyi au kupigana na watu wao (hao msiwapige). Na lau Allaah Angelitaka, Angeliwasalitisha juu yenu, wakapigana nanyi. Watakapojitenga nanyi na wasipigane nanyi, na wakakuwekeeni amani, basi Allaah Hakukufanyieni njia dhidi yao.
سَتَجِدُونَ آخَرِينَ يُرِيدُونَ أَن يَأْمَنُوكُمْ وَيَأْمَنُوا قَوْمَهُمْ كُلَّ مَا رُدُّوا إِلَى الْفِتْنَةِ أُرْكِسُوا فِيهَا ۚ فَإِن لَّمْ يَعْتَزِلُوكُمْ وَيُلْقُوا إِلَيْكُمُ السَّلَمَ وَيَكُفُّوا أَيْدِيَهُمْ فَخُذُوهُمْ وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ ۚ وَأُولَـٰئِكُمْ جَعَلْنَا لَكُمْ عَلَيْهِمْ سُلْطَانًا مُّبِينًا ﴿٩١﴾
91. Mtawakuta wengine wanataka kupata amani kwenu na kupata amani kwa watu wao, kila wanaporudishwa katika fitnah huangushwa humo. Wasipojitenga nanyi au wasiweze kukuleteeni amani au kuizuia mikono yao (kukupigeni), basi wakamateni na waueni popote muwapatapo. Na hao Tumekufanyieni hoja bayana dhidi yao.
وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ أَن يَقْتُلَ مُؤْمِنًا إِلَّا خَطَأً ۚ وَمَن قَتَلَ مُؤْمِنًا خَطَأً فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ وَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰ أَهْلِهِ إِلَّا أَن يَصَّدَّقُوا ۚ فَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ عَدُوٍّ لَّكُمْ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ ۖ وَإِن كَانَ مِن قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَاقٌ فَدِيَةٌ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰ أَهْلِهِ وَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُّؤْمِنَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ تَوْبَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿٩٢﴾
92. Na haiwi kwa Muumini amuue Muumini ila kwa kukosea tu. Na atakayemuua Muumini kwa kukosea, basi aachilie huru mtumwa Muumini na atoe diya kwa kuifikisha kwa ahli zake, isipokuwa kama wenyewe watasamehe. Na akiwa ni jamaa wa maadui zenu naye ni Muumini, basi (aliyeua) aachilie huru mtumwa Muumini. Na akiwa ni miongoni mwa watu ambao kuna mkataba baina yenu na baina yao, basi wapewe diya watu wake na aachiliwe huru mtumwa Muumini. Asiyepata, afunge (Swiyaam) miezi miwili mfululizo kuwa ni tawbah kwa Allaah.[35] Na Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا ﴿٩٣﴾
93. Na atakayemuua Muumini kwa kusudi, basi jazaa yake ni Jahannam, atadumu humo, na Allaah Atamghadhibikia, Atamlaani na Atamuandalia adhabu kubwa mno.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا ضَرَبْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَتَبَيَّنُوا وَلَا تَقُولُوا لِمَنْ أَلْقَىٰ إِلَيْكُمُ السَّلَامَ لَسْتَ مُؤْمِنًا تَبْتَغُونَ عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ مَغَانِمُ كَثِيرَةٌ ۚ كَذَٰلِكَ كُنتُم مِّن قَبْلُ فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَتَبَيَّنُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿٩٤﴾
94. Enyi walioamini! Mnapotoka kwenda kwenye Jihaad basi hakikini kila jambo, na wala msimwambie anayekuamkieni kwa As-salaam: Wewe si Muumini kwa sababu ya kutamani mafao yapitayo ya uhai wa dunia na hali kwa Allaah kuna ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyokuwa kabla na Allaah Akakufanyieni ihsaan, basi fanyeni uhakiki. Hakika Allaah kwa yale myatendayo Ni Mjuzi daima wa Khabari za dhahiri na siri.[36]
لَّا يَسْتَوِي الْقَاعِدُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ غَيْرُ أُولِي الضَّرَرِ وَالْمُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۚ فَضَّلَ اللَّـهُ الْمُجَاهِدِينَ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ عَلَى الْقَاعِدِينَ دَرَجَةً ۚ وَكُلًّا وَعَدَ اللَّـهُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَفَضَّلَ اللَّـهُ الْمُجَاهِدِينَ عَلَى الْقَاعِدِينَ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٩٥﴾
95. Hawawi sawa kati ya Waumini wanaokaa (nyumbani), isipokuwa wale wenye udhuru, na kati ya wenye kupigana Jihaad katika Njia ya Allaah kwa mali zao na nafsi zao. Allaah Amewafadhilisha kwa cheo wenye kupigana Jihaad kwa mali zao na nafsi zao kuliko waliokaa nyuma. Na wote Allaah Amewaahidi Al-Husnaa (Jannah). Na Allaah Amewafadhilisha wenye kupigana Jihaad kwa ujira mkubwa mno kuliko wanaokaa (nyuma).[37]
دَرَجَاتٍ مِّنْهُ وَمَغْفِرَةً وَرَحْمَةً ۚ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٩٦﴾
96. Ni daraja za vyeo (vya juu) kutoka Kwake na maghfirah na rehma. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚ قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿٩٧﴾
97. Hakika wale ambao Malaika wanawafisha, hali ya kuwa wamejidhulumu nafsi zao, (Malaika) watawaambia: Mlikuwa katika hali gani? Watasema: Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi. (Malaika) Watasema: Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa ya wasaa mkahajiri? Basi hao makazi yao yatakuwa ni Jahannam, na uovu ulioje mahali pa kuishia![38]
إِلَّا الْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلًا ﴿٩٨﴾
98. Isipokuwa wale waliokandamizwa kati ya wanaume na wanawake na watoto ambao hawakuweza kupata hila yoyote wala hawawezi kuongoza njia.
فَأُولَـٰئِكَ عَسَى اللَّـهُ أَن يَعْفُوَ عَنْهُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَفُوًّا غَفُورًا ﴿٩٩﴾
99. Basi hao bila shaka Allaah Atawasamehe. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kusamehe, Mwingi wa Kughufuria.
وَمَن يُهَاجِرْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ يَجِدْ فِي الْأَرْضِ مُرَاغَمًا كَثِيرًا وَسَعَةً ۚ وَمَن يَخْرُجْ مِن بَيْتِهِ مُهَاجِرًا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ يُدْرِكْهُ الْمَوْتُ فَقَدْ وَقَعَ أَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٠٠﴾
100. Na anayehajiri katika Njia ya Allaah atapata katika ardhi mahali pengi pa kukimbilia kujihifadhi na wasaa (wa kila kitu). Na atakayetoka nyumbani kwake akiwa ni mwenye kuhajiri kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake, kisha mauti yakamfikia, basi ujira wake umehakikika kwa Allaah. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[39]
وَإِذَا ضَرَبْتُمْ فِي الْأَرْضِ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَقْصُرُوا مِنَ الصَّلَاةِ إِنْ خِفْتُمْ أَن يَفْتِنَكُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ إِنَّ الْكَافِرِينَ كَانُوا لَكُمْ عَدُوًّا مُّبِينًا ﴿١٠١﴾
101. Na mtakaposafiri katika ardhi basi si dhambi kwenu kufupisha Swalaah mkikhofu kwamba waliokufuru watakushambulieni. Hakika makafiri wamekuwa kwenu ni maadui dhahiri.
وَإِذَا كُنتَ فِيهِمْ فَأَقَمْتَ لَهُمُ الصَّلَاةَ فَلْتَقُمْ طَائِفَةٌ مِّنْهُم مَّعَكَ وَلْيَأْخُذُوا أَسْلِحَتَهُمْ فَإِذَا سَجَدُوا فَلْيَكُونُوا مِن وَرَائِكُمْ وَلْتَأْتِ طَائِفَةٌ أُخْرَىٰ لَمْ يُصَلُّوا فَلْيُصَلُّوا مَعَكَ وَلْيَأْخُذُوا حِذْرَهُمْ وَأَسْلِحَتَهُمْ ۗ وَدَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ تَغْفُلُونَ عَنْ أَسْلِحَتِكُمْ وَأَمْتِعَتِكُمْ فَيَمِيلُونَ عَلَيْكُم مَّيْلَةً وَاحِدَةً ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ إِن كَانَ بِكُمْ أَذًى مِّن مَّطَرٍ أَوْ كُنتُم مَّرْضَىٰ أَن تَضَعُوا أَسْلِحَتَكُمْ ۖ وَخُذُوا حِذْرَكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ أَعَدَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿١٠٢﴾
102. Na utapokuwa upo kati yao, ukawaswalisha, basi lisimame kundi miongoni mwao pamoja nawe, na wachukue silaha zao. Watakaposujudu, wawe nyuma yenu (kuwalinda). Na lije kundi jingine ambalo halikuswali, liswali pamoja nawe, nao washike hadhari na silaha zao. Wale waliokufuru wanatamani kama mtaghafilika na silaha zenu na vifaa vyenu wakuvamieni mvamio mmoja. Na wala si dhambi kwenu ikiwa mna maudhiko kutokana na mvua au mkiwa wagonjwa kuweka (chini) silaha zenu. Na mshike hadhari zenu. Hakika Allaah Amewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.[40]
فَإِذَا قَضَيْتُمُ الصَّلَاةَ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمْ ۚ فَإِذَا اطْمَأْنَنتُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ ۚ إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا ﴿١٠٣﴾
103. Mtakapomaliza Swalaah, mdhukuruni Allaah mkiwa wima, mmeketi, au mmejinyoosha. Na mtakapopata utulivu, basi simamisheni Swalaah (kama desturi), hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekewa nyakati maalumu.[41]
وَلَا تَهِنُوا فِي ابْتِغَاءِ الْقَوْمِ ۖ إِن تَكُونُوا تَأْلَمُونَ فَإِنَّهُمْ يَأْلَمُونَ كَمَا تَأْلَمُونَ ۖ وَتَرْجُونَ مِنَ اللَّـهِ مَا لَا يَرْجُونَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١٠٤﴾
104. Wala msilegee katika kuwaandama watu (maadui). Mkiwa mnaumia basi nao pia wanaumia kama mnavyoumia. Lakini nyinyi mnataraji kutoka kwa Allaah wasiyoyataraji wao. Na Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
إِنَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِتَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ بِمَا أَرَاكَ اللَّـهُ ۚ وَلَا تَكُن لِّلْخَائِنِينَ خَصِيمًا ﴿١٠٥﴾
105. Hakika Sisi Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu kwa haki ili uhukumu baina ya watu kwa Aliyokuonyesha Allaah. Wala usiwe mtetezi kwa makhaini.
وَاسْتَغْفِرِ اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٠٦﴾
106. Na muombe Allaah maghfirah. Hakika Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَلَا تُجَادِلْ عَنِ الَّذِينَ يَخْتَانُونَ أَنفُسَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ خَوَّانًا أَثِيمًا ﴿١٠٧﴾
107. Wala usiwatetee wale wanaokhini nafsi zao. Hakika Allaah Hampendi aliye mwingi wa kukhini na kutenda dhambi.
يَسْتَخْفُونَ مِنَ النَّاسِ وَلَا يَسْتَخْفُونَ مِنَ اللَّـهِ وَهُوَ مَعَهُمْ إِذْ يُبَيِّتُونَ مَا لَا يَرْضَىٰ مِنَ الْقَوْلِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطًا ﴿١٠٨﴾
108. Wanajificha watu wasiwaone (wakitenda machafu) na wala hawajifichi kwa Allaah (wakamwonea haya), Naye Yu pamoja nao (kwa Ujuzi Wake) pale wanapokesha kupanga makri kwa maneno Asiyoyaridhia. Na Allaah daima Ni Mwenye Kuyazunguka yale wayatendayo.
هَا أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ جَادَلْتُمْ عَنْهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فَمَن يُجَادِلُ اللَّـهَ عَنْهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَم مَّن يَكُونُ عَلَيْهِمْ وَكِيلًا ﴿١٠٩﴾
109. Ha! Nyinyi ndio hawa mliowatetea katika uhai huu wa duniani. Basi nani atakayewatetea kwa Allaah Siku ya Qiyaamah? Au nani atakayekuwa mwakilishi wao wa kumtegemea?
وَمَن يَعْمَلْ سُوءًا أَوْ يَظْلِمْ نَفْسَهُ ثُمَّ يَسْتَغْفِرِ اللَّـهَ يَجِدِ اللَّـهَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١١٠﴾
110. Na atakayetenda ovu au akajidhulumu nafsi yake, kisha akamwomba Allaah maghfirah, basi atamkuta Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[42]
وَمَن يَكْسِبْ إِثْمًا فَإِنَّمَا يَكْسِبُهُ عَلَىٰ نَفْسِهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١١١﴾
111. Na atakayechuma dhambi, basi hakika anaichumia madhara nafsi yake. Na Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
وَمَن يَكْسِبْ خَطِيئَةً أَوْ إِثْمًا ثُمَّ يَرْمِ بِهِ بَرِيئًا فَقَدِ احْتَمَلَ بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿١١٢﴾
112. Na atakayechuma kosa au dhambi kisha akamtupia asiye na hatia, basi kwa yakini amejitweka (dhulma ya) usingiziaji na dhambi bayana.
وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكَ وَرَحْمَتُهُ لَهَمَّت طَّائِفَةٌ مِّنْهُمْ أَن يُضِلُّوكَ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ ۖ وَمَا يَضُرُّونَكَ مِن شَيْءٍ ۚ وَأَنزَلَ اللَّـهُ عَلَيْكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَعَلَّمَكَ مَا لَمْ تَكُن تَعْلَمُ ۚ وَكَانَ فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكَ عَظِيمًا ﴿١١٣﴾
113. Na lau kuwa si Fadhila ya Allaah na Rehma Yake juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), bila shaka kundi miongoni mwao lingefanya hima kudhamiria kukupoteza. Na hawazipotezi ila nafsi zao, na hawakudhuru kwa chochote. Na Allaah Amekuteremshia Kitabu na Hikmah na Akakufunza yale ambayo hukuwa unayajua. Na Fadhila za Allaah juu yako daima ni adhimu (na kubwa mno).[43]
لَّا خَيْرَ فِي كَثِيرٍ مِّن نَّجْوَاهُمْ إِلَّا مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلَاحٍ بَيْنَ النَّاسِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١١٤﴾
114. Hakuna kheri katika minong’ono yao mingi isipokuwa anayeamrisha kutoa swadaqa, au mema, au kusuluhisha baina ya watu. Na atakayefanya hivyo kutaka Radhi za Allaah, basi Tutampa ujira mkubwa kabisa.
وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿١١٥﴾
115. Na atakayempinga Rasuli baada ya kuwa imeshambainikia hidaaya na akaifuata njia isiyokuwa ya Waumini, Tutamgeuza alikogeukia na Tutamuingiza Jahannam. Na uovu ulioje mahali pa kuishia!
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿١١٦﴾
116. Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa, lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha[44] Allaah basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali.
إِن يَدْعُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا إِنَاثًا وَإِن يَدْعُونَ إِلَّا شَيْطَانًا مَّرِيدًا ﴿١١٧﴾
117. Hawaombi badala Yake isipokuwa miungu ya kike na hawaombi isipokuwa shaytwaan muasi.
لَّعَنَهُ اللَّـهُ ۘ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنْ عِبَادِكَ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا ﴿١١٨﴾
118. Allaah Amemlaani. Na (shaytwaan) akasema: Kwa hakika nitashika katika waja Wako sehemu maalumu!
وَلَأُضِلَّنَّهُمْ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الْأَنْعَامِ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَتَّخِذِ الشَّيْطَانَ وَلِيًّا مِّن دُونِ اللَّـهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًا مُّبِينًا ﴿١١٩﴾
119. Na hakika nitawapoteza, na nitawashawishi matamanio ya kulaghai, na nitawaamrisha. Basi watakata masikio ya wanyama (wawatukuze), na nitawaamrisha watabadili Uumbaji wa Allaah. Na atakayemfanya shaytwaan kuwa rafiki mlinzi badala ya Allaah basi kwa yakini amekhasirika khasara bayana.[45]
يَعِدُهُمْ وَيُمَنِّيهِمْ ۖ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلَّا غُرُورًا ﴿١٢٠﴾
120. Anawaahidi na anawashawishi matamanio ya uongo. Na shaytwaan hawaahidi isipokuwa ulaghai tu.
أُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ وَلَا يَجِدُونَ عَنْهَا مَحِيصًا ﴿١٢١﴾
121. Hao makaazi yao ni Jahannam, wala hawatopata makimbilio ya kutoka humo.
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَنُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ وَعْدَ اللَّـهِ حَقًّا ۚ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ قِيلًا ﴿١٢٢﴾
122. Na wale walioamini na wakatenda mema Tutawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo abadi. Ahadi ya Allaah ni haki. Na nani aliye mkweli zaidi kwa kauli kuliko Allaah?
لَّيْسَ بِأَمَانِيِّكُمْ وَلَا أَمَانِيِّ أَهْلِ الْكِتَابِ ۗ مَن يَعْمَلْ سُوءًا يُجْزَ بِهِ وَلَا يَجِدْ لَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٢٣﴾
123. Si kwa matamanio yenu wala kwa matamanio ya Watu wa Kitabu. Atakayefanya uovu atalipwa kwalo, na wala hatopata rafiki mlinzi wala mwenye kumnusuru isipokuwa Allaah.[46]
وَمَن يَعْمَلْ مِنَ الصَّالِحَاتِ مِن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلَا يُظْلَمُونَ نَقِيرًا ﴿١٢٤﴾
124. Na atakayefanya mema akiwa mwanamume au mwanamke, hali ya kuwa ni Muumini, basi hao wataingia Jannah na wala hawatodhulumiwa kadiri ya kitone cha kokwa ya tende.
وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَاتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۗ وَاتَّخَذَ اللَّـهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا ﴿١٢٥﴾
125. Na nani aliye bora zaidi kwa Dini kuliko yule aliyejisalimisha kwa Allaah naye anatekeleza maamrisho kwa uzuri unaotakikana, na akafuata mila ya Ibraahiym aliyejiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki? Na Allaah Amemfanya Ibraahiym kuwa ni kipenzi.
وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ مُّحِيطًا ﴿١٢٦﴾
126 Ni vya Allaah vilivyomo katika mbingu na katika ardhi. Na Allaah daima Ni Mwenye Kuvizunguka kila kitu.
وَيَسْتَفْتُونَكَ فِي النِّسَاءِ ۖ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ وَمَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ فِي يَتَامَى النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا تُؤْتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرْغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الْوِلْدَانِ وَأَن تَقُومُوا لِلْيَتَامَىٰ بِالْقِسْطِ ۚ وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِهِ عَلِيمًا ﴿١٢٧﴾
127. Na wanakuuliza wewe hukmu ya kisharia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu wanawake. Sema: Allaah Anakubainishieni hukmu ya kisharia kuhusu wao na (hukmu ya) yale mnayosomewa katika Kitabu kuhusu mayatima wanawake ambao hamuwapi (mahari) waliyoandikiwa nanyi mna raghba ya kuwaoa, na kuhusu wanaokandamizwa miongoni mwa watoto, na wajibu ulio juu yenu wa kuwasimamia mayatima kwa uadilifu. Na lolote mlifanyalo katika la kheri basi hakika Allaah daima kwa hilo Ni Mjuzi.[47]
وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ الْأَنفُسُ الشُّحَّ ۚ وَإِن تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٢٨﴾
128. Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa, basi si vibaya kwao wawili wakisikilizana baina yao kwa suluhu. Na suluhu ni bora zaidi. Na nafsi zimeumbiwa tabia ya uchoyo na ubahili. Na mkifanya ihsaan (kwa wanawake) na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah kwa yale myatendayo Ni Mjuzi daima wa Khabari za dhahiri na siri.[48]
وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ ۖ فَلَا تَمِيلُوا كُلَّ الْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَالْمُعَلَّقَةِ ۚ وَإِن تُصْلِحُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٢٩﴾
129. Na wala hamtoweza kuadilisha baina ya wake japokuwa mkipania. Basi msimili muelemeo wote (kwa mke mmoja) mkamuacha (mwengine) kama aliyeachwa njia panda. Na mkiyaweka mambo vizuri na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَإِن يَتَفَرَّقَا يُغْنِ اللَّـهُ كُلًّا مِّن سَعَتِهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ وَاسِعًا حَكِيمًا ﴿١٣٠﴾
130. Na wakifarikiana basi Allaah Atamtosheleza kila mmoja kwa Wasaa Wake. Na Allaah daima Ni Mwenye Wasaa, Mwenye Hikmah wa yote.
وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَلَقَدْ وَصَّيْنَا الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَإِيَّاكُمْ أَنِ اتَّقُوا اللَّـهَ ۚ وَإِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ غَنِيًّا حَمِيدًا ﴿١٣١﴾
131. Ni vya Allaah vyote vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Na kwa yakini Tumewausia wale waliopewa Kitabu kabla yenu na nyinyi kwamba: Mcheni Allaah. Na mkikufuru basi hakika ni vya Allaah Pekee vyote vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Na Allaah daima Ni Mkwasi, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa.
وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿١٣٢﴾
132. Na ni vya Allaah vyote vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Na inatosheleza Allaah kuwa Ni Mtegemewa.[49]
إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ أَيُّهَا النَّاسُ وَيَأْتِ بِآخَرِينَ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ قَدِيرًا ﴿١٣٣﴾
133. Akitaka, Atakuondoeni mbali enyi watu, na Ataleta wengine. Na Allaah kwa hayo daima Ni Muweza.
مَّن كَانَ يُرِيدُ ثَوَابَ الدُّنْيَا فَعِندَ اللَّـهِ ثَوَابُ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ سَمِيعًا بَصِيرًا ﴿١٣٤﴾
134. Anayetaka thawabu za dunia, basi kwa Allaah kuna thawabu za dunia na Aakhirah. Na Allaah daima Ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاءَ لِلَّـهِ وَلَوْ عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ ۚ إِن يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقِيرًا فَاللَّـهُ أَوْلَىٰ بِهِمَا ۖ فَلَا تَتَّبِعُوا الْهَوَىٰ أَن تَعْدِلُوا ۚ وَإِن تَلْوُوا أَوْ تُعْرِضُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٣٥﴾
135. Enyi walioamini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu kwa nguvu zote (na) wenye kutoa ushahidi kwa ajili ya Allaah tu japokuwa ni dhidi ya nafsi zenu, au wazazi wawili, au jamaa wa karibu. Akiwa tajiri au maskini, Allaah Anawastahikia zaidi. Basi msifuate hawaa mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkikanusha basi hakika Allaah kwa yale myatendayo Ni Mjuzi daima wa Khabari za dhahiri na siri.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا آمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَالْكِتَابِ الَّذِي نَزَّلَ عَلَىٰ رَسُولِهِ وَالْكِتَابِ الَّذِي أَنزَلَ مِن قَبْلُ ۚ وَمَن يَكْفُرْ بِاللَّـهِ وَمَلَائِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿١٣٦﴾
136. Enyi walioamini! Mwaminini Allaah na Rasuli Wake na Kitabu Alichokiteremsha kwa Rasuli Wake na Kitabu Alichokiteremsha kabla. Na atakayemkufuru Allaah na Malaika Wake, na Vitabu Vyake na Rusuli Wake na Siku ya Mwisho, basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا ثُمَّ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَّمْ يَكُنِ اللَّـهُ لِيَغْفِرَ لَهُمْ وَلَا لِيَهْدِيَهُمْ سَبِيلًا ﴿١٣٧﴾
137. Hakika wale walioamini kisha wakakufuru, kisha wakaamini kisha wakakufuru, kisha wakazidi kufru, Allaah Hatowaghufiria na wala Hatowaongoza njia.
بَشِّرِ الْمُنَافِقِينَ بِأَنَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٣٨﴾
138. Wabashirie wanafiki kwamba watapata adhabu iumizayo.
الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۚ أَيَبْتَغُونَ عِندَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا ﴿١٣٩﴾
139. Wale wanaofanya makafiri kuwa ni marafiki wandani na walinzi badala ya Waumini. Je, wanatafuta utukufu kutoka kwao? Basi hakika utukufu wote ni wa Allaah Pekee.
وَقَدْ نَزَّلَ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ أَنْ إِذَا سَمِعْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ يُكْفَرُ بِهَا وَيُسْتَهْزَأُ بِهَا فَلَا تَقْعُدُوا مَعَهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ إِنَّكُمْ إِذًا مِّثْلُهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ جَامِعُ الْمُنَافِقِينَ وَالْكَافِرِينَ فِي جَهَنَّمَ جَمِيعًا ﴿١٤٠﴾
140. Na kwa yakini Amekwishakuteremshieni katika Kitabu kwamba mnaposikia Aayaat za Allaah zinakanushwa na zinafanyiwa istihzai,[50] basi msikae pamoja nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Au sivyo mtakuwa kama wao. Hakika Allaah Atawakusanya wanafiki na makafiri wote pamoja katika Jahannam.
الَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمْ فَإِن كَانَ لَكُمْ فَتْحٌ مِّنَ اللَّـهِ قَالُوا أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ وَإِن كَانَ لِلْكَافِرِينَ نَصِيبٌ قَالُوا أَلَمْ نَسْتَحْوِذْ عَلَيْكُمْ وَنَمْنَعْكُم مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ ۚ فَاللَّـهُ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ وَلَن يَجْعَلَ اللَّـهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا ﴿١٤١﴾
141. Wale wanaofuatilia khabari zenu wakisubiri nini kitawasibu; inapokuwa ni ushindi kwenu kutoka kwa Allaah husema: Je, hatukuwa pamoja nanyi? Na inapokuwa sehemu ya ushindi kwa makafiri husema: Je, hatukuwa wenye uwezo wa kukudhibitini nasi tukakuzuilieni na Waumini? Basi Allaah Atawahukumu baina yenu Siku ya Qiyaamah. Na Allaah Hatojaalia kwa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.
إِنَّ الْمُنَافِقِينَ يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَهُوَ خَادِعُهُمْ وَإِذَا قَامُوا إِلَى الصَّلَاةِ قَامُوا كُسَالَىٰ يُرَاءُونَ النَّاسَ وَلَا يَذْكُرُونَ اللَّـهَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿١٤٢﴾
142. Hakika wanafiki (wanadhani) wanamhadaa Allaah, na hali Yeye (Allaah) Ndiye Mwenye kuwahadaa. Na wanaposimama kuswali husimama kwa uvivu, wakijionyesha[51] kwa watu na wala hawamdhukuru Allaah isipokuwa kidogo tu.
مُّذَبْذَبِينَ بَيْنَ ذَٰلِكَ لَا إِلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ وَلَا إِلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ ۚ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَن تَجِدَ لَهُ سَبِيلًا ﴿١٤٣﴾
143. Madhabidhabina baina ya hayo (imaan na kufru), hawako kwa hawa wala hawako kwa wale. Na ambaye Allaah Amempotoa huwezi kumpatia njia (ya kumhidi).
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَجْعَلُوا لِلَّـهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَانًا مُّبِينًا ﴿١٤٤﴾
144. Enyi walioamini! Msiwafanye makafiri kuwa marafiki wandani na walinzi badala ya Waumini. Je, mnataka Allaah Awe na hoja bayana dhidi yenu?
إِنَّ الْمُنَافِقِينَ فِي الدَّرْكِ الْأَسْفَلِ مِنَ النَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمْ نَصِيرًا ﴿١٤٥﴾
145. Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa katika moto, na wala hutompata kwa ajili yao mwenye kunusuru.
إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا وَأَصْلَحُوا وَاعْتَصَمُوا بِاللَّـهِ وَأَخْلَصُوا دِينَهُمْ لِلَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَسَوْفَ يُؤْتِ اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١٤٦﴾
146. Isipokuwa wale waliotubu, na wakarekebisha mwenendo wao, na wakashikamana na Allaah, na wakakhalisisha Dini yao kwa ajili ya Allaah, basi hao watakuwa pamoja na Waumini. Na Allaah Atawapa Waumini ujira mkubwa kabisa.
مَّا يَفْعَلُ اللَّـهُ بِعَذَابِكُمْ إِن شَكَرْتُمْ وَآمَنتُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ شَاكِرًا عَلِيمًا ﴿١٤٧﴾
147. Allaah Hatokuadhibuni ikiwa mtashukuru na mtaamini. Na Allaah daima Ni Mwenye Kupokea Shukurani, Mjuzi wa yote.
لَّا يُحِبُّ اللَّـهُ الْجَهْرَ بِالسُّوءِ مِنَ الْقَوْلِ إِلَّا مَن ظُلِمَ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ سَمِيعًا عَلِيمًا ﴿١٤٨﴾
148. Allaah Hapendi uovu utajwe hadharani isipokuwa kwa yule aliyedhulumiwa. Na Allaah daima Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
إِن تُبْدُوا خَيْرًا أَوْ تُخْفُوهُ أَوْ تَعْفُوا عَن سُوءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَفُوًّا قَدِيرًا ﴿١٤٩﴾
149. Mkidhihirisha kheri au mkiificha au mkisamehe uovu, basi hakika Allaah daima Ni Mwingi wa Kusamehe, Muweza wa yote.
إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيُرِيدُونَ أَن يُفَرِّقُوا بَيْنَ اللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيَقُولُونَ نُؤْمِنُ بِبَعْضٍ وَنَكْفُرُ بِبَعْضٍ وَيُرِيدُونَ أَن يَتَّخِذُوا بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا ﴿١٥٠﴾
150. Hakika wale wanaomkufuru Allaah na Rusuli Wake, na wanataka kufarikisha baina ya Allaah na Rusuli Wake, na wanasema: Tunaamini baadhi na tunawakanusha baadhi, na wanataka kuchukua njia iliyo baina ya hayo.
أُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ حَقًّا ۚ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿١٥١﴾
151. Hao ndio makafiri wa kweli. Na Tumewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.
وَالَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَلَمْ يُفَرِّقُوا بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ أُولَـٰئِكَ سَوْفَ يُؤْتِيهِمْ أُجُورَهُمْ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٥٢﴾
152. Na wale waliomwamini Allaah na Rusuli Wake na hawakumfarikisha yeyote baina yao, hao Atawapa ujira wao. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
يَسْأَلُكَ أَهْلُ الْكِتَابِ أَن تُنَزِّلَ عَلَيْهِمْ كِتَابًا مِّنَ السَّمَاءِ ۚ فَقَدْ سَأَلُوا مُوسَىٰ أَكْبَرَ مِن ذَٰلِكَ فَقَالُوا أَرِنَا اللَّـهَ جَهْرَةً فَأَخَذَتْهُمُ الصَّاعِقَةُ بِظُلْمِهِمْ ۚ ثُمَّ اتَّخَذُوا الْعِجْلَ مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَاتُ فَعَفَوْنَا عَن ذَٰلِكَ ۚ وَآتَيْنَا مُوسَىٰ سُلْطَانًا مُّبِينًا ﴿١٥٣﴾
153. Wanakuuliza Watu wa Kitabu uwateremshie kitabu kutoka mbinguni. Kwa yakini walimuuliza Muwsaa makubwa kuliko hayo. Walisema: Tuonyeshe Allaah waziwazi. Basi iliwachukua radi na umeme angamizi kwa dhulma yao. Kisha wakamchukua ndama kumwabudu baada ya kwisha kuwajia hoja bayana. Tukawasamehe hayo, na Tukampa Muwsaa mamlaka bayana.
وَرَفَعْنَا فَوْقَهُمُ الطُّورَ بِمِيثَاقِهِمْ وَقُلْنَا لَهُمُ ادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا وَقُلْنَا لَهُمْ لَا تَعْدُوا فِي السَّبْتِ وَأَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا﴿١٥٤﴾
154. Na kwa (kuvunja) fungamano lao, Tuliunyanyua juu yao mlima, na Tukawaambia: Ingieni mlangoni hali mkiwa mmeinama kwa kunyenyekea, na Tukawaambia: Msitaadi mipaka ya As-Sabt[52] (Jumamosi). Na Tukachukua kutoka kwao fungamano madhubuti.
فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ وَكُفْرِهِم بِآيَاتِ اللَّـهِ وَقَتْلِهِمُ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَقَوْلِهِمْ قُلُوبُنَا غُلْفٌ ۚ بَلْ طَبَعَ اللَّـهُ عَلَيْهَا بِكُفْرِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُونَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿١٥٥﴾
155. Basi (Tuliwalaani) kwa kuvunja kwao fungamano lao, na kukanusha kwao Aayaat (na Ishara, Miujiza, Dalili, Hoja) za Allaah, na kuua kwao Manabii bila ya haki, na kusema kwao: Nyoyo zetu zimefumbwa; bali Allaah Amezipiga chapa juu yake kwa sababu ya kufuru zao, basi hawatoamini ila kidogo.
وَبِكُفْرِهِمْ وَقَوْلِهِمْ عَلَىٰ مَرْيَمَ بُهْتَانًا عَظِيمًا ﴿١٥٦﴾
156. Na kwa kufuru yao (kumpinga Iysaa), na kumzushia kwao Maryam uongo mkubwa mno!
وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا الْمَسِيحَ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ رَسُولَ اللَّـهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَـٰكِن شُبِّهَ لَهُمْ ۚ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ ۚ مَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ إِلَّا اتِّبَاعَ الظَّنِّ ۚ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينًا ﴿١٥٧﴾
157. Na kusema kwao (kwa kujifaharisha): Hakika sisi tumemuua Al-Masiyh ‘Iysaa mwana wa Maryam, Rasuli wa Allaah. Na hawakumuua wala hawakumsulubu lakini walishabihishiwa tu. Na hakika wale waliokhitilafiana katika hayo, kwa hakika wamo katika shaka nayo. Hawana ujuzi nalo kabisa isipokuwa kufuata dhana tu. Na kwa yakini hawakumuua.[53]
بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿١٥٨﴾
158. Bali Allaah Alimnyanyua Kwake. Na Allaah daima Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا ﴿١٥٩﴾
159. Na hakuna yeyote katika Watu wa Kitabu ila atamwamini kabla ya kufa kwake. Na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao.[54]
فَبِظُلْمٍ مِّنَ الَّذِينَ هَادُوا حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ طَيِّبَاتٍ أُحِلَّتْ لَهُمْ وَبِصَدِّهِمْ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ كَثِيرًا ﴿١٦٠﴾
160. Basi kwa dhulma ya Mayahudi, Tuliwaharamishia vizuri walivyohalalishiwa, na kwa sababu ya kuwazuilia kwao wengi Njia ya Allaah.
وَأَخْذِهِمُ الرِّبَا وَقَدْ نُهُوا عَنْهُ وَأَكْلِهِمْ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ ۚ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ مِنْهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٦١﴾
161. Na kuchukua kwao riba na hali wamekatazwa kuichukua, na kula kwao mali za watu kwa ubatwilifu. Na Tumewaandalia makafiri katika wao adhabu iumizayo.
لَّـٰكِنِ الرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ مِنْهُمْ وَالْمُؤْمِنُونَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ ۚ وَالْمُقِيمِينَ الصَّلَاةَ ۚ وَالْمُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالْمُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ أُولَـٰئِكَ سَنُؤْتِيهِمْ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١٦٢﴾
162. Lakini wenye msingi madhubuti katika ilimu miongoni mwao na Waumini (kati yao), wanaamini yale uliyoteremshiwa (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako. Na pia wasimamishao Swalaah, na watoao Zakaah na wanaomwamini Allaah na Siku ya Mwisho, hao (wote) Tutawapa ujira mkubwa kabisa.
إِنَّا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ كَمَا أَوْحَيْنَا إِلَىٰ نُوحٍ وَالنَّبِيِّينَ مِن بَعْدِهِ ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَارُونَ وَسُلَيْمَانَ ۚ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا ﴿١٦٣﴾
163. Hakika Tumekufunulia Wahy (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم) kama Tulivyomfunulia Wahy Nuwh na Manabii baada yake. Na Tumemfunulia Wahy Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na Al-Asbaatw,[55] (kizazi chake) na ‘Iysaa na Ayyuwb na Yuwnus na Haaruwn, na Sulaymaan. Na Tumempa Daawuwd Zabuwr.
وَرُسُلًا قَدْ قَصَصْنَاهُمْ عَلَيْكَ مِن قَبْلُ وَرُسُلًا لَّمْ نَقْصُصْهُمْ عَلَيْكَ ۚ وَكَلَّمَ اللَّـهُ مُوسَىٰ تَكْلِيمًا ﴿١٦٤﴾
164. Na Rusuli Tuliokwishakusimulia kabla, na Rusuli (wengine) Hatukukusimulia.[56] Na bila shaka Allaah Alimsemesha Muwsaa maneno moja kwa moja.[57]
رُّسُلًا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى اللَّـهِ حُجَّةٌ بَعْدَ الرُّسُلِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا ﴿١٦٥﴾
165. Rusuli ni wabashiriaji na waonyaji ili pasikuweko kutoka kwa watu hoja yoyote juu ya Allaah baada ya (kuletwa) Rusuli. Na Allaah daima Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
لَّـٰكِنِ اللَّـهُ يَشْهَدُ بِمَا أَنزَلَ إِلَيْكَ ۖ أَنزَلَهُ بِعِلْمِهِ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ يَشْهَدُونَ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا ﴿١٦٦﴾
166. Lakini Allaah Anayashuhudia Aliyoyateremsha kwako. Ameyateremsha kwa Ilimu Yake, na Malaika pia wanashuhudia. Na Anatosheleza Allaah kuwa Mwenye Kushuhudia yote.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ قَدْ ضَلُّوا ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿١٦٧﴾
167. Hakika wale waliokufuru na wakazuia Njia ya Allaah, kwa yakini wamekwishapotea upotofu wa mbali.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَظَلَمُوا لَمْ يَكُنِ اللَّـهُ لِيَغْفِرَ لَهُمْ وَلَا لِيَهْدِيَهُمْ طَرِيقًا ﴿١٦٨﴾
168. Hakika wale waliokufuru na wakadhulumu, haitokuwa kwa Allaah kuwaghufuria wala kuwaongoza njia.
إِلَّا طَرِيقَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿١٦٩﴾
169. Isipokuwa njia ya Jahannam wadumu humo milele. Na hayo kwa Allaah ni mepesi.
يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُمُ الرَّسُولُ بِالْحَقِّ مِن رَّبِّكُمْ فَآمِنُوا خَيْرًا لَّكُمْ ۚ وَإِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١٧٠﴾
170. Enyi watu! Kwa yakini amekujieni Rasuli kwa haki kutoka kwa Rabb wenu. Basi aminini, ni bora kwenu. Na mkikufuru, basi hakika ni vya Allaah Pekee vilivyomo mbinguni na ardhini. Na Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ وَلَا تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ إِلَّا الْحَقَّ ۚ إِنَّمَا الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ رَسُولُ اللَّـهِ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَىٰ مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِّنْهُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ ۖ وَلَا تَقُولُوا ثَلَاثَةٌ ۚ انتَهُوا خَيْرًا لَّكُمْ ۚ إِنَّمَا اللَّـهُ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖسُبْحَانَهُ أَن يَكُونَ لَهُ وَلَدٌ ۘ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿١٧١﴾
171. Enyi Watu wa Kitabu! Msipindukie mipaka katika dini yenu, wala msimzungumzie Allaah isipokuwa ukweli. Hakika Al-Masiyh ‘Iysaa mwana wa Maryam ni Rasuli wa Allaah na ni Neno Lake (la Kun!) Alompelekea Maryam na Ruwh (roho Aliyoumba kwa amrisho) kutoka Kwake. Basi mwaminini Allaah na Rusuli Wake. Wala msiseme: ‘watatu’. Komeni! Ni kheri kwenu. Hakika Allaah ni Mwabudiwa wa haki Mmoja Pekee, Ametakasika na kuwa na mwana![58] Ni Vyake vyote vilivyomo mbinguni na vyote vilivyomo ardhini. Na Anatosheleza Allaah kuwa Ni Mtegemewa wa yote.
لَّن يَسْتَنكِفَ الْمَسِيحُ أَن يَكُونَ عَبْدًا لِّلَّـهِ وَلَا الْمَلَائِكَةُ الْمُقَرَّبُونَ ۚ وَمَن يَسْتَنكِفْ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيَسْتَكْبِرْ فَسَيَحْشُرُهُمْ إِلَيْهِ جَمِيعًا ﴿١٧٢﴾
172. Al-Masiyh kamwe hatojiona bora aje akatae kuwa ni mja kwa Allaah, wala Malaika waliokurubishwa. Na atakayejiona bora akakataa Kumwabudu (Allaah) na akatakabari, basi Atawakusanya wote Kwake.
فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُوَفِّيهِمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدُهُم مِّن فَضْلِهِ ۖ وَأَمَّا الَّذِينَ اسْتَنكَفُوا وَاسْتَكْبَرُوا فَيُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَلَا يَجِدُونَ لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٧٣﴾
173. Ama wale walioamini na wakatenda mema, (Allaah) Atawalipa kwa ukamilifu ujira wao, na Atawazidishia katika Fadhila Zake. Ama waliojiona bora wakagoma na wakatakabari, basi hao Atawaadhibu adhabu iumizayo, na wala hawatopata asiyekuwa Allaah rafiki mlinzi wala mwenye kunusuru.
يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُم بُرْهَانٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ نُورًا مُّبِينًا ﴿١٧٤﴾
174. Enyi watu! Kwa yakini imekujieni burhani[59] (hoja, dalili, muujiza) kutoka kwa Rabb wenu na Tumekuteremshieni Nuru bayana.
فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَاعْتَصَمُوا بِهِ فَسَيُدْخِلُهُمْ فِي رَحْمَةٍ مِّنْهُ وَفَضْلٍ وَيَهْدِيهِمْ إِلَيْهِ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا ﴿١٧٥﴾
175. Ama wale waliomwamini Allaah, na wakashikamana Naye, hao Atawaingiza katika rehma itokayo Kwake na fadhila, na Atawaongoza njia iliyonyooka kuelekea Kwake.
يَسْتَفْتُونَكَ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِي الْكَلَالَةِ ۚ إِنِ امْرُؤٌ هَلَكَ لَيْسَ لَهُ وَلَدٌ وَلَهُ أُخْتٌ فَلَهَا نِصْفُ مَا تَرَكَ ۚ وَهُوَ يَرِثُهَا إِن لَّمْ يَكُن لَّهَا وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَتَا اثْنَتَيْنِ فَلَهُمَا الثُّلُثَانِ مِمَّا تَرَكَ ۚ وَإِن كَانُوا إِخْوَةً رِّجَالًا وَنِسَاءً فَلِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ ۗ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ أَن تَضِلُّوا ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٧٦﴾
176. Wanakuuliza hukmu ya kisharia. Sema: Allaah Anakubainishieni kuhusu Al-Kalaalah (asiye na wazazi wala watoto). Ikiwa mtu amefariki hana mtoto lakini ana dada, basi atastahiki nusu ya yale aliyoyaacha. Na yeye (huyo mtu) atamrithi huyo dada kama hana mtoto. Na ikiwa madada ni wawili, basi watastahiki thuluthi mbili ya yale aliyoyaacha (maiti). Na wakiwa ni ndugu wanaume na wanawake, basi mwanamme atastahiki sehemu iliyo sawa na sehemu ya wanawake wawili. Allaah Anakubainishieni ili msipotee, na Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.[60]
[1] Amrisho La Kuunga Undugu Na Matahadharisho Ya Kukata Undugu:
Rejea Ar-Ra’d (13:21), Muhammad (47:22-23).
[2] Iliowamiliki Mikono Yao Ya Kulia:
Inayomiliki mikono ya kuume ni wale watumwa wa kike waliotekwa na Waislamu katika vita vya Jihaad kisha ikaruhusika kuwaingilia kujamii nao. Uislamu ulipokuja, ulikuja ili kusawazisha baina ya watu na kuwafanya wawe waadilifu. Na Uislamu ukahimiza kuwafanyia wema watumwa na kuwaacha huru. Na Uislamu ukafanya kafara ya matendo mengi kuwa ni kuacha huru watumwa, na ikawa kukomboa watumwa ni fadhila na thawabu nyingi mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) ili Waislamu wapendezewe kuacha huru na kuwakomboa watumwa. Uislamu ulikuja kuhifadhi heshima ya wanawake na sio kuwatiisha kwa wanaume, kama baadhi ya wanafiki wanaofasiri Maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى) kutokana na matamanio na upotofu wao. Rejea pia An-Nisaa (5:25), Al-Muuminuwn (23:6), Al-Ma’aarij (70:30), Al-Ahzaab (33:50) (33:55).
[8] Uharamisho Wa Ndoa Ya Mut-’ah:
Mut’ah: Maana yake kilugha ni kustarehe. Ama kisharia ni ndoa inayofungwa kwa muda maalumu na kiasi cha pesa maalumu kinachojulikana.
Imeitwa jina hilo kwa sababu mwanamume anapata faida na kustarehe kwa muda uliowekwa.
Aina hii ya ndoa ilikuwepo katika zama za Jaahiliyyah. Kuna wakati Uislamu ulikataza na wakati uliruhusu kwa masharti maalumu, lakini mwishowe ndoa hii iliharamishwa haramisho la wazi kabisa katika Hijjatul-Wada’ (Hijjah ya mwisho ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Hadiyth ifuatayo:
Sabrah bin Ma’abad Al-Juhniy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba baba yake aliandamana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika (ukombozi wa) Fat-h Makkah, akasema: “Enyi watu! Nilikuruhusuni ndoa ya mut-’ah hapo mwanzo. Leo Allaah Ameiharamisha mpaka Siku ya Qiyaamah! Basi ikiwa kuna yeyote ambaye ana mke wa ndoa ya mut-’ah amwache, na wala asichukue chochote katika alichompa.” [Muslim na wengineo]
[10] Al-Kabaair (Madhambi Makubwa):
Ni madhambi yaliyotajiwa ndani yake laana, au haddi (adhabu) hapa duniani, au yameahidiwa juu yake Ghadhabu za Allaah au moto. Na pia madhambi saba yanayoangamiza yaliyotajwa katika Hadiyth ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) :
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Jiepusheni na mambo saba yanayoangamiza!” Wakauliza: Ni yepi hayo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Ni kumshirikisha Allaah, sihri (uchawi), kuua nafsi Aliyoiharamisha Allaah isipokuwa kwa haki, kula riba, kula mali ya yatima, kukimbia wakati wa kupambana na adui, na kuwatuhumu uzinifu wanawake Waumini waliohifadhika walioghafilika.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
[11] Jinsi Ya Kuwatia Adabu Wanawake Wenye Kuasi Katika Ndoa
Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ
“Na wahameni katika malazi na wapigeni (kipigo kisichodhuru).”
Imekusudiwa kutokulala nao na kutokujimai nao, kwa ujumla ni kuwagomea. Ama kuhusu: “na wapigeni”, hii imekusudiwa kipigo kidogo kisichokuwa cha kuwadhuru, wala haipasi kupigwa usoni.
[12] Al-‘Aliyy (الْعَلِيُّ) Al-Kabiyr(الْكَبِيْرُ) : Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake.
[13] Riyaa-a (Kujionyesha Kwa Watu) Ni Shirki Inayobatwilisha Amali: Rejea Az-Zumar (39:65).
[14] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Alilia Kusikia Qiraa Cha Aayah Hii:
Amesimulia ‘Abdullaah bin Mas‘uwd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniambia: “Nisomee!” Nikamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Nikusomee na hali (Qur-aan) imeteremshwa kwako? Akasema: “Naam! Lakini mimi napenda kusikia wengine wakiisoma.” Nikasoma Suwratun-Nisaa mpaka nilipofikia Aayah:
فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ شَهِيدًا ﴿٤١﴾
“Basi itakuwaje Tutakapoleta kutoka kila ummah shahidi, na Tukakuleta (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa shahidi juu ya hawa?”
Akasema: “Hasbuka! (Inatosha, simama hapo).” Nikaona machozi yamejaa machoni mwake. [Al-Bukhaariy]
Kila Ummah Utahudhurishwa Na Shahidi Wake:
Rejea Al-Baqarah (2:143), Al-Israa (17:71), Al-Hajj (22:78), An-Nahl (16:89), Az-Zumar (39:69), Al-Jaathiyah (45:28).
[15] Hatua Za Uharamisho Wa Pombe Na Kikomo Chake:
Rejea Al-Baqarah (2:219), na pia Al-Maaidah (5:90-91) ambako kuna maelezo bayana ya Hatua Za Uharamisho Wa Pombe Na Kikomo Chake.
[16] Tayammum: Rejea Al-Maaidah (5:6).
[18] Maana Ya: رَاعِنَا (Raa’inaa) Na انْظُرْنَا (Undhwurnaa):
Miongoni mwa ada za Mayahudi ni kuyapotosha Maneno ya Allaah (عزّ وجلّ) kwa kuyatoa kwenye makusudio yake, na pia wanayatafsiri kinyume na maana yake halisi. Na watu wa bid’ah wamejifananisha nao katika kupindisha na kupotosha maana ya Majina ya Allaah na Sifa Zake. Rejea Tanbihi ya Suwrat Al-Baqarah (2:104) ambako kuna maelezo bayana kuhusu maana mbili hizo.
[19] As-Sabt: Rejea Al-Baqarah (2:65), Al-A’raaf (7:163-166).
[20] Shirki Ni Dhambi Pekee Ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Hamghufurii Mtu Akifariki
Rejea pia Suwrah hii An-Nisaa (4:116).
Muislamu anapotenda dhambi, anapaswa kukimbilia haraka kuomba maghfirah na kutubia kwa Allaah (سبحانه وتعالى). Kwa sababu shirki ni dhambi pekee ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Hamghufurii mtu pindi akifariki bila ya kutubia. Hivyo basi, hatima yake ni kuingizwa motoni! Makemeo mazito yametajwa katika Qur-aan na Sunnah. Kati ya Hadiyth zinazozungumzia hilo ni:
Amesimulia Ibn Mas‘uwd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayefariki akiwa katika hali ya kumshirikisha Allaah kwa chochote, basi ataingia motoni.” [Al-Bukhaariy 1238, Muslim 92]
Shirki pia inawahusu makafiri wanaomshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) nao pia wametahadharishwa na kunasihiwa watubie kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwrah Al-Maaidah (5:72-74).
[21] Tofauti Ya Al-Jibt (الجِبْتُ) Na At-Twaaghuwt الطَّاغُوْتُ):
Al-Jibt inajumuisha sihri (uchawi), mchawi, kahini na kila aina ya shari na kila ambalo halina kheri.
Ama twaghuti, ni uvukaji mipaka wa kumtoa Allaah (سبحانه وتعالى) kutoka nje ya Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah (Kumpwekesha katika Uola Wake), na Tawhiyd Al-Uluwhiyyah (Kumpwekesha katika kumwabudu), au katika Sharia au Hukmu Yake. Kwa hiyo kila anayemkosea Allaah (عزّ وجلّ) katika hayo, basi yeye ni twaghuti. Ndio maana ‘Ulamaa wamesema kuwa twaghuti ni wengi mno, lakini viongozi wao ni watano: (i) Ibliys laana ya Allaah iwe juu yake, naye ni wa kwanza wao. (ii) Kiumbe yeyote anayeabudiwa akiwa ameridhia hivyo. (iii) Anayelingania watu aabudiwe yeye. (iv) Anayedai kuwa anajua ilimu ya ghaibu. (v) Anayehukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah. [Fat-h Al-Majiyd Sharh Kitaab At-Tawhiyd]
Rejea pia Al-Baqarah (2:256).
[23] Aayah Pekee Katika Suwrah Hii Kuteremshwa Makkah Na Wasimamizi Wa Funguo Za Al-Ka’abah:
Aayah hii ni ya pekee katika Suwrah hii ya An-Nisaa (4:58) ambayo imeteremka Makkah. Imeteremshwa Siku ya Fat-h Makkah (Ukombozi). Ibn Jurayj amehadithia kwamba imeteremshwa kuhusu ‘Uthmaan bin Twalhah pale Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipochukua ufunguo wa Ka’bah kutoka kwake akaingia Ka’bah. Alipotoka nje ya Ka’bah, alitoka huku akiwa anasoma:
إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَىٰ أَهْلِهَا
“Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe.”
Hapo akamwita ‘Uthmaan bin Twalhah na akampa funguo. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Funguo hizo zimeendelea kubakia katika ukoo huo, kizazi baada ya kizazi mpaka zama zetu hizi. Na mpaka Siku ya Qiyaamah ukoo huo umefadhilishwa kuwa ndio wenye amana ya kukamata funguo za Al-Ka’bah.
Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
[24] Amri Na Masisitizo Ya Kuwatii Watawala Na Viongozi:
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ameamrisha na kusisitiza katika Hadiyth kadhaa suala la kutii watawala na viongozi. Miongoni mwazo ni: “Muislamu anapaswa kusikia na kutii kwa anayoyapenda na anayoyachukia, madhali hakuamrishwa kuasi. Na pindi akiamrishwa katika maasi, basi hakuna kusikia wala kutii.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na amesema pia: “Sikieni na tiini (watawala na viongozi wenu) hata kama ni mtumwa wa Uhabeshi (Ethiopea) ambaye kichwa chake ni kama zabibu.” [Al-Bukhaariy]
Amri ya kuwatii kwa wema watawala na viongozi wa mambo ya Waislamu, ni jambo ambalo limenukuliwa na Ijmaa’ juu yake, bali ndiyo ‘Aqiydah sahihi ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah. Lakini kwa masikitiko makubwa jambo hili wamelipuuza wengi katika Waislamu na wale wasiofahamu mafunzo ya Dini yao. Na matokeo ya kwenda kinyume na jambo hilo na ‘Aqiydah hiyo, ni kuleta munkari mkubwa katika Ummah na ufisadi mpana. Kuna wanaofanya maandamano kupinga viongozi, kuna wanaojilipua kwa mabomu na kuua watu, kuna wanaoua watu kwa njia mbali mbali na kadhalika kumwaga damu za wanaadamu bure! Matokeo yake ni kuwa maadui wa Uislamu wametumia njia hiyo ili kuuchafua Uislamu na kuudidimiza.
Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
[27] Tofauti Ya Manabii, Swiddiqiyn, Shuhadaa Na Swalihina.
Manabii (الأَنْبِيَاءُ):
Manabii na Rusuli ni wengi mno. Baadhi yao wametajwa kwenye Qur-aan na Sunnah na wengineo hawakutajwa. Na baadhi yao visa vyao vimesimuliwa katika Qur-aan na baadhi yao havikusimuliwa. Rejea Ghaafir (40:78) na An-Nisaa (4:164).
Wa kwanza wao ni Nabiy Aadam (عليه السّلام) na wa mwisho wao ni Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).
Tofauti Kati Ya Nabiy Na Rasuli:
‘Ulamaa wamezungumza mengi kuhusu tofauti baina ya Nabiy na Rasuli. Kimukhtasari ni kwamba Nabiy ni yule ambaye Ametumwa na Allaah (عزّ وجلّ) bila ya kuteremshiwa sharia au hukmu mpya. Ama Rasuli, ni yule ambaye ameteremshiwa sharia mpya na kuamriwa kufikisha Risala kwa watu wake. Hivyo, Nabiy hutumia sharia ya Rasuli aliyemtangulia.
Kwa msingi huu, kila Rasuli ni Nabiy, lakini si kila Nabiy ana sifa ya Rasuli. Na Rasuli ana daraja kubwa kuliko Nabiy kwa sababu Rasuli hubalighisha Risala (Ujumbe) kwa watu wake, huwaonya na huwabashiria. Na jukumu hili bila shaka linahitajia kuwa na subira ya hali ya juu kwa sababu watu wao waliwapinga vikali, wakawakadhibisha, wakawashutumu, wakawasingizia sifa mbaya, na wakawafanyia istihzai, dhihaka, kejeli na hata kuwapangia makri kutaka kuwaua. Kati ya hao ni Rusuli watano waliotajwa katika Suwrat Al-Ahzaab (33:7) ambao walitoa fungamano gumu kwa Allaah (سبحانه وتعالى). Wanajulikana kuwa ni Ulul-‘Azmi; wenye azimio la nguvu. Rejea Al-Ahqaaf (46:35).
Imaam Ibn Baaz (رحمه الله) amesema: “Linalojulikana sana miongoni mwa ‘Ulamaa ni kwamba, Nabiy ni ambaye ameteremshiwa sharia, lakini hakuamrishwa kubalighisha Risala (Ujumbe) kwa watu. Huamrishwa afanye kadhaa na kadhaa, aswali namna kadhaa, afunge Swawm namna kadhaa, lakini haamrishwi kubalighisha Ujumbe kwa watu. Hivyo huyu ni Nabiy. Ama akiamrishwa kubalighisha (Ujumbe) kwa kuwabashiria na kuwaonya watu, huyo anakuwa ni Nabiy na Rasuli kama vile Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), Muwsaa, ‘Iysaa, Nuwh, Huwd, Swaalih (عليهم السلام) na wengineo”. [Mawqi' Ar-Rasmiy li-Samaahat Ash-Shaykh Ibn Baaz]
Swiddiyquwn(الصِّدِّيْقُوْنَ) :
Asw-Swiddiyq ni Muumini ambaye ni mkweli wa dhati, kwa kauli na matendo, katika Manabii na wafuasi wao, na akathibiti imara katika ukweli kwa imaan, na akaamini kila kinachomfikia kutoka kwa Rabb wake au Rasuli wake. Rejea (57:19).
Na Allaah (سبحانه وتعالى) Amewataja katika Qur-aan Manabii kwa sifa hii ya Asw-Swiddiyq Katika Yuwsuf (12:46), Maryam (19:41), (19:56) na kwengineko. Kwa hiyo Swiddiyquwn ni wengi. Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Ametajwa na Allaah (سبحانه وتعالى) kwa sifa hiyo katika Kauli Yake:
وَالَّذِي جَاءَ بِالصِّدْقِ وَصَدَّقَ بِهِ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ﴿٣٣﴾
“Na yule aliyekuja na ukweli na akausadikisha, hao ndio wenye taqwa.” [Az-Zumar: (39:33)]
Wafasiri wa Qur-aan wengi wamesema makusudio ya: “Aliyekuja na ukweli” ni Jibriyl (عليه السلام)alipoteremsha Wahyi (Qur-aan). Na “aliyeusadikisha” ni Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). [Tafsiyr Ibn Kathiyr na Wafasiri wengineo]
Abu Bakr (رضي الله عنه) pia amepewa sifa ya Asw-Swiddiyq kwa sababu ya kumwamini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) baada ya safari ya muujiza ya Al-Israa Wal-Mi’raaj (kutoka Makkah hadi mbingu ya saba na kurudi Makkah kwa usiku mmoja). Yeye alimwamini Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na akamsadikisha yote aliyoyasema hapo hapo mbele ya watu, wakati ma-Quraysh wa Makkah walimkadhibisha na kudai kwamba ni uongo. Na bint yake Mama wa Waumin ‘Aaishah (رضي الله عنها), pia amepewa sifa hii kuwa ni Bint Asw-Swiddiyqah (binti wa Abu Bakr (رضي الله عنهما).
Maryam mama wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السلام) pia amepewa sifa hii kama Alivyomtaja Allaah (سبحانه وتعالى) katika Kauli Yake:
مَّا الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ وَأُمُّهُ صِدِّيقَةٌ ۖ
“Al-Masiyh mwana wa Maryam si chochote ila ni Rasuli tu, wamekwishapita kabla yake Rusuli (wengine). Na mama yake ni Muumini mkweli wa dhati.” [Al-Maaidah (5:75)]
Katika Hadiyth sifa ya Swiddiyqah imetajwa kuwa ni msema kweli:
Amesimulia ‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika ukweli unaongoza katika wema, na hakika wema unaongoza katika Jannah, na mtu ataendelea kusema ukweli mpaka aandikiwe mbele ya Allaah kuwa ni Swiddiyqaa (mkweli wa dhati). Na hakika uongo unaongoza katika uovu, na hakika uovu unapelekea motoni, na mtu ataendelea kusema uongo mpaka aandikiwe mbele ya Allaah kuwa ni muongo.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Shuhadaa(شُهَدَاءُ) :
Ni Waumini waliouwawa katika Vita Vitukufu vya Jihaad. Hawa sifa yao ni kwamba juu ya kuwa wamefariki duniani, lakini wako hai wanaendelea kuruzukiwa Jannah. Rejea Aal-‘Imraan (3:169-171).
Swalihina(صَالِحُوْنَ) :
Ni waja wema, Waumini walionyooka katika Dini ya Allaah (سبحانه وتعالى) wakatimiza haki ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kufuata Amri Zake. Pia ni wale wenye ikhlaasw (kutakasa amali zao), na ni wenye taqwa, na watiifu. Nao ni katika Manabii, Rusuli, Shuhadaa (waliofariki au kuuwawa katika vita vitukufu vya Jihaad), Swahaba, na waja wema wengineo wenye sifa hizo. Na pindi inapotajwa Swalihina kwa ujumla basi wote hao ni wenye sifa hizo. Ama inapotajwa Swalihina pamoja na Manabii, Swiddiyqiyna, Shuhadaa na wengineo kama katika Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَـٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ ۚ وَحَسُنَ أُولَـٰئِكَ رَفِيقًا ﴿٦٩﴾
“Na atakayemtii Allaah na Rasuli, basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah Aliowaneemesha miongoni mwa Manabii na Swiddiyqiyna na Shuhadaa na Swalihina, na uzuri ulioje kuwa pamoja na hao.” [An-Nisaa (4:69)]
basi hapo hubainisha kuwa kila mmoja katika hao anatofautiana na mwingine katika daraja na fadhila nyenginezo kama vile ilivyotajwa katika Hadiyth kwamba Shuhadaa (waliofariki katika vita vitukufu) wako hai Peponi. Au kuhusu Manabii kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ameiharamishia ardhi kuila miili yao. Hali kadhalika Swahaba nao wana daraja na fadhila tofauti tofauti.
Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
[29] Kumtii Rasuli Ni Kumtii Allaah Na Kumuasi Ni Kumuasi Allaah:
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayenitii basi atakuwa amemtii Allaah, na atakayeniasi basi atakuwa amemuasi Allaah, na atakayemtii Amiri wangu (kiongozi niliyemteua), basi atakuwa amenitii mimi na atakayemuasi atakuwa ameniasi mimi.” [Al-Bukhaariy, Muslim, An-Nasaaiy, Ibn Maajah]
Na pia: Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amesimulia: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ummah wangu wote wataingia Jannah isipokuwa atakayekataa.” Akaulizwa: Ni yupi atakayekataa ee Rasuli wa Allaah? Akajibu: “Atakayenitii mimi ataingia Jannah, na atakayeniasi basi amekataa.” [Al-Bukhaariy]
[30] Al-Wakiyl (الوَكِيْلُ): Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake.
[31] Radd Kwa Kundi La Al-Mufawwidhwah Wanaodai Kuwa Sifa Za Allaah (سبحانه وتعالى) Hazifahamiki:
Aayah hii ni miongoni mwa dalili na radd juu ya kundi la Al-Mufawwidhwah. Wafuasi wa kundi hili wanazikubali Sifa za Allaah, lakini wakati huo huo wanadai kuwa hazifahamiki. Wanasema kuwa Majina ya Allaah na Sifa Zake, maana Zake hazifahamiki, na kwa hivyo Allaah Kawaletea Waja Wake mafundisho ambayo hayaeleweki maana yake. Hii ni itikadi baatwil mno. Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah (رحمه الله) amesema alipolizungumzia pote hili la Mufawwidhwah kuwa ni katika mapote ya bid’ah. Kisha wakainasibisha kauli hii kuwa ni kauli ya Salaf! Huko ni kuwazulia wema waliotangulia (رحمهم الله). Imaam Ahmad anawaona Mufawwidhwah kuwa ni wabaya zaidi kuliko Jahmiyyah.
[32] Maonyo Ya Kutangaza Khabari Bila Kuhakikisha:
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Inamtosha mtu kuwa ni muongo kwa kusema kila anachokisikia.” [Amehadithia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) na Muslim kaipokea]
Na pia: Amesimulia Al-Mughiyrah bin Shu’bah (رضي الله عنه): Nimemsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Hakika Allaah Anachukia kwenu “qiylaa wa qaala” (utesi, udaku n.k), kupoteza mali na kuuliza maswali mengi.” [Al-Bukhaariy na wengineo] “Qiylaa wa qaal” kwa maana: “imesemwa na amesema”, ni ibara inayokusudiwa uvumi, utesi, udaku, umbeya, usengenyaji n.k. Rejea pia Al-Hujuraat (49:6).
Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
[33] Jinsi Ya Kuyaitikia Maamkizi Ya Kiislamu Na Baadhi Ya Fadhila Zake:
'Imraan bin Al-Huswayn (رضي الله عنهما) amehadithia: Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuamkia: "Assalaamu 'alaykum." (Nabiy) akamrudishia salaam). Kisha yule mtu akakaa kitako. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Kumi.” (Kwa maana amepata thawabu kumi). Kisha akaja mtu mwengine, akasema: "Assalaamu 'alaykum wa RahmatuLLaah." Naye akamrudishia, kisha yule mtu akakaa kitako, na Nabiy akasema: “Ishirini.” Kisha akaja mtu mwengine akasema: "Assalaamu 'alaykum wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh.” Naye akamrudishia, kisha akasema: “Thelathini.” [Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na amesema Hadiyth Hasan]
Na maamkizi ya Kiislamu ni funguo za Jannah: Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hamtoingia Jannah hadi muamini, na wala hamuwezi kuamini hadi mpendane. Je, nikujulisheni jambo ambalo mtakapolifanya mtapendana? Toleaneni Salaam baina yenu.” [Muslim]
Pia katika khutbah yake ya mwanzo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipohajiri Madiynah alisema: “Enyi watu! Enezeni salaam, na lisheni chakula, na swalini watu wakiwa wamelala (Qiyaam), mtaingia Jannah kwa amani.” [At-Tirmidhiy – Hadiyth Hasan]
[35] Haramisho La Kuua Bila Haki Na Adhabu Zake:
Allaah (سبحانه وتعالى) Ameharamisha mauaji bila ya haki, na Anatoa adhabu kali kabisa kwa kosa hili! Aayah hii na inayofuatia (4:92-93) ni miongoni mwa dalili za haramisho hilo. Hali kadhaalika dalili zimo katika Sunnah. Miongoni mwazo ni Hadiyth hii:
Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Amru (رضي الله عنه) Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kutokomea dunia ni kwepesi zaidi kuliko kuua Muislamu.” [Swahiyh An-Nasaaiy (3998)]
Pia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wangeshirikiana watu wa mbinguni na ardhini kumwaga damu ya Muumini, Allaah Angewaingiza (wote) motoni.” [Amehadithia Al-Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه), na Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh katika Swahiyh At-Targhiyb]
Amesema pia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Muumini hatoacha kuwa katika Dini yake madamu hajagusa damu ya haramu (hajamwaga damu).” [Al-Bukhaariy]
[41] Maamrisho Ya Kusimamisha Swalaah Kwa Nyakati Zake Na Makemeo Ya Kuipuuza:
Maamrisho ya kusimamisha Swalaah kwa nyakati zake yamesisitizwa katika Qur-aan na Sunnah. Na miongoni mwa Hadiyth za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) zinazogusia hilo ni: “Kitu cha kwanza atakachohesabiwa nacho mja Siku ya Qiyaamah katika amali zake ni Swalaah, ikitengenea atakuwa amefuzu na amefanikiwa, na ikiharibika atakuwa ameshapita patupu na amekhasirika…” [At-Tirmidhiy, na amesema Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]
Pia Buraydah bin Al-Haswiyb (رضي الله عنه) amehadithia: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Mafungamano baina yetu na baina yao (wasio Waislamu) ni Swalaah, atakayeiacha atakuwa amekufuru.” [Ahmad, Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]
Imaam ibn Baaz (رحمه الله) amesema: “Yeyote atakayeweka makusudi kengele ya saa imuamshe baada ya kutoka jua akakosa Swalaah ya Alfajiri, basi mtu huyo amepuuza kuswali kwa wakati wake, na kufanya hivyo ni kufru kubwa kama walivyokubaliana ‘Ulamaa wengi, kwa sababu amekusudia kuswali baada ya jua kutoka. Ni sawa na mtu ambaye anachelewesha kuswali Alfajiri akaiswali karibu na Adhuhuri. [Fataawa Ibn Baaz, Kitaab As-Swalaah (10/374)]
Rejea pia Maana Ya Kusimamisha Swalaah katika Al-Baqarah (2:3). Rejea pia Al-Muuminuwn (23:1).
[42] Kuswali Rakaa Mbili Baada Ya Kutenda Dhambi Kwa Ajili Ya Maghfirah:
Amesimulia ‘Aliy bin Abiy Twaalib (رضي الله عنه): Kila niliposikia jambo kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), Allaah Huninufaisha kwa Apendayo kuninufaisha. Abuu Bakr amenihadithia, na Abuu Bakr amesadikisha, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna Muislamu yeyote atakayetenda dhambi, kisha akatawadha akaswali rakaa mbili, kisha aombe maghfirah, basi hakuna isipokuwa Allaah Atamghufuria.” Kisha akasoma Aayah mbili hizi:
وَمَن يَعْمَلْ سُوءًا أَوْ يَظْلِمْ نَفْسَهُ ثُمَّ يَسْتَغْفِرِ اللَّـهَ يَجِدِ اللَّـهَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١١٠﴾
“Na atakayetenda ovu au akajidhulumu nafsi yake, kisha akamwomba Allaah maghfirah, basi atamkuta Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.” [An-Nisaa (4:110)]
Na:
وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٣٥﴾
“Na ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao (kwa maasi), humdhukuru Allaah wakaomba maghfirah kwa madhambi yao. Na nani anayeghufuria madhambi isipokuwa Allaah. Na hawaendelei katika waliyoyafanya na hali wanajua.” [Aal-‘Imraan (3:135)]
[Imepokelewa na Ahmad katika Musnad yake, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, na Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (406) na Swahiyh At-Targhiyb (680)]
Rejea Huwd (11:3) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali, At-Tahriym (66:8), Nuwh (71:10), Adh-Dhaariyaat (51:18).
[43] Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida tele:
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Fadhila Zake Mbalimbali [89]
Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Miujiza Yake [90]
[44] Shirk Ni Dhambi Pekee Ambayo Allaah Hamghufurii Mtu. Rejea Suwrah hii (4:48).
[45] Laana Ya Allaah Kwa Mwenye Kujibadilisha Maumbile:
‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه) alisema: “Allaah Anawalaani wanaopiga chale na wanaotaka kupigwa chale, na wanaochonga nyusi, na wanaochonga meno wakaacha mwanya kwa sababu ya uzuri, wanaobadilisha maumbile Aliyoyaumba Allaah.” Mwanamke mmoja akamlaumu juu ya jambo hilo (la kulaani). Akasema (‘Abdullaah): “Kwa nini nisimlaani aliyelaaniwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na ilhali iko ndani ya Kitabu cha Allaah? Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
وَمَا آتَاكُمْ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانْتَهُوا
“Na lolote analokupeni Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) basi lichukueni, na analokukatazeni, basi liepukeni.” [Al-Hashr (59:7)] [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na katika riwaayah nyingine imetajwa: “Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amemlaani mwenye kuunga na mwenye kuungwa (nywele)…”
Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
[49] Al-Wakiyl (الوَكِيْلُ): Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake.
[50] Kufanya Istihzai Ni Miongoni Mwa Yanayomtoa Mtu Nje Ya Uislamu:
Miongoni mwa yanayomtoa mtu nje ya Uislamu ni kufanyia istihzai Maneno ya Allaah! Ni kama ilivyotajwa katika Nawaaqidhw Al-Islaam: “Mwenye kufanyia istihzai (shere, dhihaka, masikhara) kwa chochote katika Dini ya Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), au akafanya utani katika Thawabu au katika Adhabu za Allaah, basi amekufuru.” [Muhammad bin ‘Abdil-Wahhaab, Nawaaqidhw Al-Islaam]
Ni tahadharisho na onyo kubwa kwa Waislamu, kwani wengi katika mabaraza yao wanapoongea, hupenda kufanya istihzai kwa mambo ya Dini wakidhania kuwa ni jambo la kawaida ilhali hatari yake ni kubwa mno! Rejea At-Tawbah (9:64-66) ambapo Allaah (سبحانه وتعالى) Amehukumu kuwa kufanya istihzai katika Dini ni kufru!
Kuna wanaofanya istihzai na dhihaka kwa Aayah au maneno ya Qur-aan au Majina ya Suwrah za Qur-aan! Au kuhusu Manabii na Rusuli waliopita pamoja na kaumu zao. Wengine hufanya istihzai na dhihaka katika sharia za Dini kama vile kuwacheka Waumini kuhusu Isbaal (kanzu kutokuvuka mafundo ya miguu), au istihzai kuhusu ndevu n.k. Hayo yote na mengineyo yoyote ya istihzai na dhihaka katika Dini ni kukufuru!
[51] Riyaa-a (Kujionyesha Kwa Watu): Riyaa-a Inabatwilisha Amali:
Riyaa-a katika kuswali ni aina mojawapo ya riyaa-a. Rejea Al-Maa’uwn (107:4-6). Rejea pia Az-Zumar (39:65) kwenye maelezo kuhusu aina za shirki.
[52] As-Sabt: Rejea Al-Baqarah (2:65), An-Nisaa (4:47), Al-A’raaf (7:165) na An-Nahl (16:124).
[53] Dalili Nyengineyo Kwamba Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Hakufishwa Bali Yu Hai Mbinguni:
Aayah hii na zinazofuatia (155-157), ni dalili nyengineyo inayothibitisha kwamba Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) hakufishwa, bali amenyanyuliwa na Allaah mbinguni. Maelezo zaidi Rejea Aal-‘Imraan (3:55).
[54] Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Yu Hai Mbinguni Na Atateremka Duniani Kama Ni Alama Kubwa Za Qiyaamah:
Ni hoja na dalili bayana kwa wanaokanusha kuteremka kwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) katika zama za mwisho kukaribia Qiyaamah. Rejea pia Az-Zukhruf (43:61). Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) atateremka kutoka mbinguni kuja duniani kama ni miongoni mwa alama kubwa za Qiyaamah, na atatekeleza mambo ambayo yametajwa katika Hadiyth ifuatayo ambayo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَيُوشِكَنَّ أَنْ يَنْزِلَ فِيكُمْ ابْنُ مَرْيَمَ حَكَمًا مُقْسِطًا
“Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake! Hivi karibuni atateremka kwenu mwana wa Maryam ('Iysaa) akiwa ni kiongozi muadilifu. [Al-Bukhaariy, Muslim]
Hali kadhaalika, kuna Hadiyth nyinginezo za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) zenye kuthibitisha hilo kama hizi zifuatazo:
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake! Hivi karibuni atateremka kwenu mwana wa Maryam ('Iysaa) akiwa ni kiongozi muadilifu, na atavunja misalaba na kuua nguruwe, na ataondosha jizyah (ushuru kutoka kwa wasio Waislamu ambao wamo katika himaya ya serikali ya Waislamu). Kisha kutakuwa na mali nyingi hadi itafikia kuwa hakuna mtu wa kupokea swadaqa. Wakati huu sijda moja itakuwa ni bora kwao kuliko maisha haya na yote yaliyomo (katika dunia).” Kisha Abuu Huraryah akasema: Someni mkipenda:
وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا ﴿١٥٩﴾
“Na hakuna yeyote katika Watu wa Kitabu ila atamwamini kabla ya kufa kwake. Na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao.” (4:159) [Al-Bukhaariy]
Na pia: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mtakuwaje atakapoteremka Al-Masiyh, mwana wa Maryam (‘Iysaa) akiwa Imaam wenu miongoni mwenu wenyewe?” [Al-Bukhaariy]
Na pia amesema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Manabii ni bin-‘ammi; mama zao tofauti, lakini Dini yao moja. Mimi ndiye mwenye haki zaidi kwa ‘Iysaa mwana wa Maryam kuliko yeyote mwengine, kwani hapajakuwa na Nabiy baina yake na mimi. Atateremka, na mtakapomuona mtamtambua. Ni mtu aliyeumbika vizuri, rangi (ya ngozi) yake iko baina ya nyekundu na nyeupe. Atateremka akiwa amevaa nguo mbili ndefu, rangi ya njano isiyokoza. Kichwa chake kitakuwa kina michirizi ya matone ya maji, japokuwa umande haukugusa. Atavunja misalaba, ataua nguruwe, ataondosha jizyah na atawaita watu katika Uislamu. Wakati huu, Allaah Ataangamiza dini zote isipokuwa Uislamu, na Allaah Atamuangamiza Masiyh-Dajjaal. Usalama utajaa ardhini, hadi kwamba simba watachanganyika na ngamia, chui na ng'ombe, fisi na kondoo, na watoto watacheza na nyoka na hawatowadhuru. ‘Iysaa atabakia muda wa miaka arubaini kisha atafariki, na Waislamu watamswalia Swalaah ya janaazah.” [Abuu Daawuwd, Ahmad na Al-Albaaniy ameisahihisha katika Swahiyh Al-Jaami’ (2182)]
Rejea pia Aal-‘Imraan (3:55).
[55] Al-Asbaatw: Rejea Al-Baqarah (2:136).
[56] Baadhi Ya Rusuli Vimesimuliwa Visa Vyao Na Baadhi Yao Havikusimuliwa:
Rejea Ghaafir (40:78). Al-‘An’aam (6:83), pia An-Nisaa (4:69) kupata maelezo kuhusu tofauti ya Manabii na Rusuli.
[57] Allaah (سبحانه وتعالى) Alimsemesha Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) Kwa Uhakika Wake Na Hii Ndio ‘Aqiydah Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Kuhusiana Na Sifa Zake Allaah (سبحانه وتعالى).
Allaah (سبحانه وتعالى) Alimsemesha Muwsaa (عليه السلام) Maneno kwa uhakika wake na si kwa majazi kama wanavyosema watu wa bid’ah, bali ni maneno yaliyojengeka kwa herufi na sauti. Na Sifa ya Maneno ni Sifa iliyothibiti kwa Allaah kwa uhakika wake bila kuifanyia Ta'twiyl (kuzipinga, kukanusha uwezekano), wala Tamthiyl (kumithilisha, kufafanisha, kulinganisha), wala Takyiyf (kuainisha maana na kuziulizia namna yake au kuuliza ni vipi Sifa hiyo ipo, kuchunguza ni kwa “namna gani” zimefungamana au kuambatana na Allaah), wala Tahriyf (kubadilisha maana, kupotosha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kutoa maana isiyo sahihi).
Na hii ndiyo kauli ya sawa ambayo wamepita kwayo Salaf na Imaam wa haki katika Uislamu katika Sifa zote zilizokuja ndani ya Qur-aan, rejea pia Al-A’raaf (7:143). Na katika Sunnah, Hadiyth zifuatazo:
Amesimulia ‘Adiy Bin Haatim (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna yeyote miongoni mwenu isipokuwa Allaah Atazungumza naye Siku ya Qiyaamah, kutakuwa hakuna mkalimani kati yake na Allaah. Kisha ataangalia na wala hatoona kitu alichokitanguliza, kisha ataangalia mbele yake ataona moto unampokea. Kwa hiyo, awezaye kuiokoa nafsi yake na moto kwa kutoa (swadaqa) kipande cha tende moja, na afanye hivyo.” [Al-Bukhaariy]
Na pia Hadiyth ndefu ya Ash-Shafaa’ah (uombezi) Siku ya Qiyaamah, ambayo amesimulia Anas (رضي الله عنه): …Watakwenda kwa Ibraahiym. Naye atawaambia: Siwezi kufanya mnaloomba! Nendeni kwa Muwsaa mja ambaye Allaah Alizungumza naye na Akampa Tawraat. [Al-Bukhaariy]
[58] Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Na Mama Yake Si Washirika Wa Allaah:
Allaah (سبحانه وتعالى) Amewakataza Watu Wa Kitabu (Mayahudi Na Manaswara) wasimfanye ‘Iysaa na Mama yake kuwa ni washirika wa Allaah, bali hao ni waja wawili katika waja wema wa Allaah, na si washirika Wake kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) Akimzungumzia Maryam na kumzaa kwake Nabiy ‘Iysaa (عليه السلام) katika Suwrat Maryam (19:16-36). Na pia katika Suwrah Al-Maaidah (5:17), (72-76), (116-118), Rejea pia At-Tawbah (9:30-31).
Pia ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit (رضي الله عنه) amehadithia: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kushuhudia kuwa laa ilaaha illa Allaah (hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah), Pekee, Hana mshirika, na kwamba Muhammad ni mja wake na Rasuli Wake, na kwamba ‘Iysaa ni mja wa Allaah na Rasuli Wake, na Neno Lake (la Kun!) Aliloliweka kwa Maryam na roho ni kutoka Kwake (Ameiumba), na Jannah (Pepo) ni haki, na moto ni haki, Allaah Atamuingiza Jannah kwa ‘amali zozote alizonazo.” [Al-Bukhaariy] Na katika riwaayah nyingine: “Ataingizwa Jannah katika milango minane ataingia katika wowote aupendao.” [Muslim]
[59] Burhani: Muujiza, Ushahidi, Ishara, Dalili, Hoja za waziwazi kabisa zenye kuthibitisha kwa yakini na bila ya shaka na bila ya kupingika.
[60] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
176-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 176: يَسْتَفْتُونَكَ قُلِ اللَّـهُ يُفْتِيكُمْ فِي الْكَلَالَةِ [95]
الْمَائِدَة
005-Al-Maaidah
005-Al-Maaidah: Utangulizi Wa Suwrah [97]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَوْفُوا بِالْعُقُودِ ۚ أُحِلَّتْ لَكُم بَهِيمَةُ الْأَنْعَامِ إِلَّا مَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ غَيْرَ مُحِلِّي الصَّيْدِ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۗ إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ مَا يُرِيدُ ﴿١﴾
1. Enyi walioamini! Timizeni mikataba. Mmehalalishiwa wanyama wa mifugo wanaopelekwa malishoni, isipokuwa mnaosomewa (humu kuwa si halali). Ila tu msijiruhusu mkawinda mkiwa katika ihraam,[1] ni marufuku. Hakika Allaah Anahukumu Atakayo.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحِلُّوا شَعَائِرَ اللَّـهِ وَلَا الشَّهْرَ الْحَرَامَ وَلَا الْهَدْيَ وَلَا الْقَلَائِدَ وَلَا آمِّينَ الْبَيْتَ الْحَرَامَ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّن رَّبِّهِمْ وَرِضْوَانًا ۚ وَإِذَا حَلَلْتُمْ فَاصْطَادُوا ۚ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ أَن صَدُّوكُمْ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ أَن تَعْتَدُوا ۘ وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٢﴾
2. Enyi walioamini! Msikhalifu utukufu wa Ishara za Allaah, wala Miezi Mitukufu wala wanyama wanaopelekwa Haram kuchinjwa, wala vigwe (vyao), wala (kukhalifu) amani kwa) wanaoiendea Nyumba Tukufu (Makkah) wanatafuta Fadhila kutoka kwa Rabb wao na Radhi. Na mkishatoka kwenye ihraam basi windeni (mkitaka). Na wala isikuchocheeni chuki mliyonayo kwa watu kwa vile walikuzuieni na Al-Masjid-Al-Haraam ikakupelekeni kufanya uonevu. Na shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. Na Mcheni Allaah, hakika Allaah Ni Mkali wa Kuakibu.[2]
حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ وَالْمُنْخَنِقَةُ وَالْمَوْقُوذَةُ وَالْمُتَرَدِّيَةُ وَالنَّطِيحَةُ وَمَا أَكَلَ السَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيْتُمْ وَمَا ذُبِحَ عَلَى النُّصُبِ وَأَن تَسْتَقْسِمُوا بِالْأَزْلَامِ ۚ ذَٰلِكُمْ فِسْقٌ ۗ الْيَوْمَ يَئِسَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن دِينِكُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِ ۚ الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ فَمَنِ اضْطُرَّ فِي مَخْمَصَةٍ غَيْرَ مُتَجَانِفٍ لِّإِثْمٍ ۙ فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣﴾
3. Mmeharamishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na kilichotajiwa asiyekuwa Allaah katika kuchinjwa kwake, na (pia) mnyama aliyekufa kwa kukosa hewa au aliyepigwa akafa, au aliyeporomoka toka juu, au aliyepigwa pembe, na aliyeliwa na mnyama mwitu, isipokuwa mliyewahi kumchinja kihalali (kabla ya kufa), na waliochinjwa kwa ajili ya ibaada ya waabudiwa, na kupiga ramli kwa mishale. Hayo kwenu ni ufasiki. Leo wamekata tamaa wale waliokufuru na Dini yenu, basi msiwaogope, bali Niogopeni Mimi. Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni Neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislamu uwe Dini yenu. Basi atakayelazimika katika njaa kali bila kulalia kwenye dhambi (akala vilivyoharamishwa), basi hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[3]
يَسْأَلُونَكَ مَاذَا أُحِلَّ لَهُمْ ۖ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۙ وَمَا عَلَّمْتُم مِّنَ الْجَوَارِحِ مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ اللَّـهُ ۖ فَكُلُوا مِمَّا أَمْسَكْنَ عَلَيْكُمْ وَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿٤﴾
4. Wanakuuliza wamehalalishiwa nini? Sema: Mmehalalishiwa vilivyo vizuri na mlivyowindiwa na wanyama na ndege wakali mliowafundisha kiweledi, na mnawafunza katika ambayo Allaah Amekufunzeni. Basi kuleni walichokukamatieni, na mkitajie Jina la Allaah. Na mcheni Allaah, hakika Allaah Ni Mwepesi wa Kuhesabu.
الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَّهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٥﴾
5. Leo mmehalalishiwa vilivyo vizuri. Na nyama iliyochinjwa na waliopewa Kitabu ni halali kwenu, na nyama mliyochinja nyinyi ni halali kwao. Na (mmehalalishiwa pia) wanawake waungwana wema katika Waumini na wanawake waungwana wema katika wale waliopewa Kitabu kabla yenu, mtakapowapa mahari yao bila kuwa maasherati wala kuchukua hawara. Na yeyote atakayekanusha imani basi kwa yakini imeporomoka amali yake naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ ۚ وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ ۚ مَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُم مِّنْ حَرَجٍ وَلَـٰكِن يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٦﴾
6. Enyi walioamini! Mnaposimama kwa ajili ya Swalaah, osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi, na panguseni (kwa kupaka maji) vichwa vyenu na (osheni) miguu yenu hadi vifundoni. Na mkiwa na janaba basi jitwaharisheni. Na mkiwa wagonjwa au mko safarini au mmoja wenu ametoka msalani, au mmewagusa wanawake, kisha hamkupata maji, basi ikusudieni ardhi safi ya mchanga (mtayammam), panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu. Allaah Hataki kukufanyieni magumu, lakini Anataka kukutwaharisheni na Akutimizieni Neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru.[4]
وَاذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَمِيثَاقَهُ الَّذِي وَاثَقَكُم بِهِ إِذْ قُلْتُمْ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ﴿٧﴾
7. Na kumbukeni Neema ya Allaah juu yenu na fungamano Lake ambalo Amekufungamanisheni nalo mliposema: Tumesikia na Tumetii. Na mcheni Allaah, hakika Allaah Ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ لِلَّـهِ شُهَدَاءَ بِالْقِسْطِ ۖ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَىٰ أَلَّا تَعْدِلُوا ۚ اعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿٨﴾
8. Enyi walioamini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Allaah na wenye kutoa ushahidi kwa uadilifu. Na wala chuki mliyonayo kwa watu isikuchocheeni ikakupelekeeni kutokufanya uadilifu. Fanyeni uadilifu, huko ndiko kuliko karibu zaidi na taqwa. Na mcheni Allaah, hakika Allaah Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri kwa yale myatendayo.
وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ۙ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿٩﴾
9. Allaah Amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema kwamba watapata maghfirah na ujira mkubwa mno.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿١٠﴾
10. Na waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) Zetu, hao ni watu wa moto uwakao vikali mno.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ هَمَّ قَوْمٌ أَن يَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ فَكَفَّ أَيْدِيَهُمْ عَنكُمْ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١١﴾
11. Enyi walioamini! Kumbukeni Neema ya Allaah juu yenu, pale walipopania watu kukunyosheeni mikono yao (kukushambulieni), kisha Allaah Akazuia mikono yao isikufikieni. Na mcheni Allaah, na kwa Allaah Pekee watawakali Waumini.
وَلَقَدْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَبَعَثْنَا مِنْهُمُ اثْنَيْ عَشَرَ نَقِيبًا ۖ وَقَالَ اللَّـهُ إِنِّي مَعَكُمْ ۖ لَئِنْ أَقَمْتُمُ الصَّلَاةَ وَآتَيْتُمُ الزَّكَاةَ وَآمَنتُم بِرُسُلِي وَعَزَّرْتُمُوهُمْ وَأَقْرَضْتُمُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا لَّأُكَفِّرَنَّ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَلَأُدْخِلَنَّكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۚ فَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ مِنكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ﴿١٢﴾
12. Na kwa yakini Allaah Alichukua fungamano la nguvu la wana wa Israaiyl, na Tukawapelekea miongoni mwao wakuu kumi na mbili. Na Allaah Akasema: Hakika Mimi Niko pamoja nanyi. Mkisimamisha Swalaah, na mkatoa Zakaah, na mkawaamini Rusuli Wangu, na mkawaunga mkono na kuwasaidia, na mkamkopesha Allaah karadha mzuri, bila shaka Nitakufutieni maovu yenu, na Nitakuingizeni Jannaat zipitazo chini yake mito. Na yeyote atakayekufuru baada ya hapo miongoni mwenu, basi kwa yakini amepotea njia iliyo sawa.
فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ لَعَنَّاهُمْ وَجَعَلْنَا قُلُوبَهُمْ قَاسِيَةً ۖ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ ۙ وَنَسُوا حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا بِهِ ۚ وَلَا تَزَالُ تَطَّلِعُ عَلَىٰ خَائِنَةٍ مِّنْهُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاصْفَحْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣﴾
13. Kwa sababu ya kuvunja kwao fungamano lao, Tuliwalaani na Tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanageuza maneno (ya Allaah) kutoka mahali pake, na wakasahau sehemu ya yale waliyokumbushwa. Na utaendelea kujionea khiyana kutoka kwao isipokuwa wachache tu miongoni mwao. Basi wasamehe na achilia mbali. Hakika Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.
وَمِنَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَىٰ أَخَذْنَا مِيثَاقَهُمْ فَنَسُوا حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا بِهِ فَأَغْرَيْنَا بَيْنَهُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۚ وَسَوْفَ يُنَبِّئُهُمُ اللَّـهُ بِمَا كَانُوا يَصْنَعُونَ ﴿١٤﴾
14. Na kwa wale waliosema: Hakika sisi ni Naswara, Tulichukua fungamano lao, nao wakasahau sehemu ya yale waliyokumbushwa. Basi Tukapandikiza baina yao uadui na bughudha mpaka Siku ya Qiyaamah. Na Allaah Atawajulisha waliyokuwa wakiyatenda.
يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا مِّمَّا كُنتُمْ تُخْفُونَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ ۚ قَدْ جَاءَكُم مِّنَ اللَّـهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾
15. Enyi Watu wa Kitabu! Hakika amekwishakujieni Rasuli Wetu anayekubainishieni mengi katika yale mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu, na ananyamazia mengi (yasiyo na lazima kuyafichua). Kwa yakini imekufikieni kutoka kwa Allaah Nuru na Kitabu kinachobainisha.
يَهْدِي بِهِ اللَّـهُ مَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَهُ سُبُلَ السَّلَامِ وَيُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِهِ وَيَهْدِيهِمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٦﴾
16. Allaah Anamwongoza kwacho yeyote atakayefuata Radhi Zake kumfikisha njia za salama, na Anawatoa (walio mfano wa huyo) katika viza kuingia katika nuru kwa Tawfiyq Yake, na Anawaongoza kuelekea njia iliyonyooka.
لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۚ قُلْ فَمَن يَمْلِكُ مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا إِنْ أَرَادَ أَن يُهْلِكَ الْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُ وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ۗ وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۚ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٧﴾
17. Kwa yakini, wamekufuru wale waliosema: Allaah Ndiye Al-Masiyh mwana wa Maryam. Sema: Nani awezaye kuzuia lolote litokalo kwa Allaah Akitaka kumwangamiza Al-Masiyh mwana wa Maryam na mama yake na walioko ardhini wote? Na ufalme ni wa Allaah wa mbingu na ardhi na vyote vilivyo baina yake, Anaumba Atakacho. Na Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.[5]
وَقَالَتِ الْيَهُودُ وَالنَّصَارَىٰ نَحْنُ أَبْنَاءُ اللَّـهِ وَأَحِبَّاؤُهُ ۚ قُلْ فَلِمَ يُعَذِّبُكُم بِذُنُوبِكُم ۖ بَلْ أَنتُم بَشَرٌ مِّمَّنْ خَلَقَ ۚ يَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۚ وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ ﴿١٨﴾
18. Na Mayahudi na Manaswara wamesema: Sisi ni wana wa Allaah na vipenzi Vyake. Sema: Kwa nini basi Anakuadhibuni kwa dhambi zenu? Bali nyinyi ni watu kama wengine Aliowaumba. Anamghufuria Amtakaye na Anamuadhibu Amtakaye. Na ufalme ni wa Allaah wa mbingu na ardhi na vyote vilivyo baina yake, na Kwake Pekee ndio mahali pa kuishia.
يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ عَلَىٰ فَتْرَةٍ مِّنَ الرُّسُلِ أَن تَقُولُوا مَا جَاءَنَا مِن بَشِيرٍ وَلَا نَذِيرٍ ۖ فَقَدْ جَاءَكُم بَشِيرٌ وَنَذِيرٌ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٩﴾
19. Enyi Watu wa Kitabu! Kwa yakini amekwishakujieni Rasuli Wetu anayekubainishieni (mambo) katika wakati wa kusita ujio wa Rusuli wa kulingania. Msije kusema: Hakutujia mbashiriaji yeyote wala mwonyaji. Kwa yakini amekujieni mbashiriaji na mwonyaji. Na Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.
وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ جَعَلَ فِيكُمْ أَنبِيَاءَ وَجَعَلَكُم مُّلُوكًا وَآتَاكُم مَّا لَمْ يُؤْتِ أَحَدًا مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿٢٠﴾
20. Na pindi Muwsaa alipowaambia kaumu yake: Enyi kaumu yangu! Kumbukeni Neema ya Allaah juu yenu Alipojaalia miongoni mwenu Manabii, na Akakufanyeni wenye kujitawala wenyewe (baada ya kumgharikisha Firawni) na Akakupeni yale Asiyowahi kumpa yeyote miongoni mwa walimwengu.
يَا قَوْمِ ادْخُلُوا الْأَرْضَ الْمُقَدَّسَةَ الَّتِي كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ وَلَا تَرْتَدُّوا عَلَىٰ أَدْبَارِكُمْ فَتَنقَلِبُوا خَاسِرِينَ ﴿٢١﴾
21. Enyi kaumu yangu! Ingieni ardhi iliyotakaswa ambayo Amekuandikieni Allaah, na wala msirudi kugeuka nyuma mkakimbia (kupigana), hapo mtageuka kuwa wenye kukhasirika.
قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِنَّ فِيهَا قَوْمًا جَبَّارِينَ وَإِنَّا لَن نَّدْخُلَهَا حَتَّىٰ يَخْرُجُوا مِنْهَا فَإِن يَخْرُجُوا مِنْهَا فَإِنَّا دَاخِلُونَ ﴿٢٢﴾
22. Wakasema: Ee Muwsaa! Hakika humo kuna watu majabari, nasi hatutoingia humo mpaka watoke humo. Watakapotoka humo, basi hakika sisi tutaingia.
قَالَ رَجُلَانِ مِنَ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِمَا ادْخُلُوا عَلَيْهِمُ الْبَابَ فَإِذَا دَخَلْتُمُوهُ فَإِنَّكُمْ غَالِبُونَ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَتَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٢٣﴾
23. Watu wawili[6] katika wenye kumcha Allaah ambao Allaah Amewaneemesha wakasema: Waingilieni katika mlango. Mkiwaingilia, basi hakika nyinyi mtashinda. Na kwa Allaah tawakalini ikiwa nyinyi ni Waumini.
قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِنَّا لَن نَّدْخُلَهَا أَبَدًا مَّا دَامُوا فِيهَا ۖ فَاذْهَبْ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَاتِلَا إِنَّا هَاهُنَا قَاعِدُونَ ﴿٢٤﴾
24. Wakasema: Ee Muwsaa! Hakika sisi hatutoingia humo abadani madamu watabakia humo. Basi nenda wewe na Rabb wako mkapigane, hakika sisi tunakaa hapa hapa.
قَالَ رَبِّ إِنِّي لَا أَمْلِكُ إِلَّا نَفْسِي وَأَخِي ۖ فَافْرُقْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ ﴿٢٥﴾
25. (Muwsaa) akasema: Rabb wangu! Hakika mimi similiki ila nafsi yangu na ndugu yangu. Basi Tutenganishe sisi na watu mafasiki (kwa Hukmu Yako).
قَالَ فَإِنَّهَا مُحَرَّمَةٌ عَلَيْهِمْ ۛ أَرْبَعِينَ سَنَةً ۛ يَتِيهُونَ فِي الْأَرْضِ ۚ فَلَا تَأْسَ عَلَى الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ ﴿٢٦﴾
26. (Allaah) Akasema: Kwa hiyo basi (ardhi tukufu) hiyo imeharamishwa kwao miaka arubaini. Watatangatanga ardhini. Basi usisikitike juu ya watu mafasiki.
وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ ابْنَيْ آدَمَ بِالْحَقِّ إِذْ قَرَّبَا قُرْبَانًا فَتُقُبِّلَ مِنْ أَحَدِهِمَا وَلَمْ يُتَقَبَّلْ مِنَ الْآخَرِ قَالَ لَأَقْتُلَنَّكَ ۖ قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ اللَّـهُ مِنَ الْمُتَّقِينَ ﴿٢٧﴾
27. Na wasomee khabari ya wana wawili wa Aadam kwa haki walipotoa dhabihu ya kafara, ikakubaliwa ya mmoja wao lakini ya mwengine haikukubaliwa. (Asiyekubaliwa) akasema: Nitakuua tu! (Aliyekubaliwa) akasema: Hakika Allaah Anatakabalia wenye taqwa.
لَئِن بَسَطتَ إِلَيَّ يَدَكَ لِتَقْتُلَنِي مَا أَنَا بِبَاسِطٍ يَدِيَ إِلَيْكَ لِأَقْتُلَكَ ۖ إِنِّي أَخَافُ اللَّـهَ رَبَّ الْعَالَمِينَ ﴿٢٨﴾
28. Ukininyoshea mkono wako ili uniue, mimi sitokunyoshea mkono wangu kukuua. Hakika mimi namkhofu Allaah Rabb wa walimwengu.
إِنِّي أُرِيدُ أَن تَبُوءَ بِإِثْمِي وَإِثْمِكَ فَتَكُونَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الظَّالِمِينَ ﴿٢٩﴾
29. Hakika mimi nataka urudi na ubebe dhambi zangu na dhambi zako, hapo utakuwa miongoni mwa watu wa motoni. Na hiyo ndiyo jazaa ya madhalimu.
فَطَوَّعَتْ لَهُ نَفْسُهُ قَتْلَ أَخِيهِ فَقَتَلَهُ فَأَصْبَحَ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٣٠﴾
30. Basi nafsi yake ikamwezesha kwa wepesi kumuua ndugu yake, akamuua na akawa miongoni mwa waliokhasirika.
فَبَعَثَ اللَّـهُ غُرَابًا يَبْحَثُ فِي الْأَرْضِ لِيُرِيَهُ كَيْفَ يُوَارِي سَوْءَةَ أَخِيهِ ۚ قَالَ يَا وَيْلَتَىٰ أَعَجَزْتُ أَنْ أَكُونَ مِثْلَ هَـٰذَا الْغُرَابِ فَأُوَارِيَ سَوْءَةَ أَخِي ۖ فَأَصْبَحَ مِنَ النَّادِمِينَ ﴿٣١﴾
31. Kisha Allaah Akamleta kunguru akifukua katika ardhi ili amwonyeshe vipi asitiri maiti ya ndugu yake. (Muuaji) akasema: Ole wangu! Hivi nimeshindwa kuwa mimi kama huyu kunguru nikamsitiri ndugu yangu? Akawa miongoni mwa wajutao.
مِنْ أَجْلِ ذَٰلِكَ كَتَبْنَا عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنَّهُ مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا ۚ وَلَقَدْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُنَا بِالْبَيِّنَاتِ ثُمَّ إِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم بَعْدَ ذَٰلِكَ فِي الْأَرْضِ لَمُسْرِفُونَ ﴿٣٢﴾
32. Kwa ajili ya hilo, Tukawaandikia sharia wana wa Israaiyl kwamba: Atakayeiua nafsi bila ya nafsi (kuua), au kufanya ufisadi katika ardhi, basi ni kama ameua watu wote. Na atakayeiokoa na mauti, basi ni kama amewaokoa watu wote. Na bila shaka walifikiwa na Rusuli Wetu kwa hoja bayana, kisha wengi miongoni mwao baada ya hayo wamekuwa wapindukao mipaka ya kuasi.
إِنَّمَا جَزَاءُ الَّذِينَ يُحَارِبُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا أَن يُقَتَّلُوا أَوْ يُصَلَّبُوا أَوْ تُقَطَّعَ أَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُم مِّنْ خِلَافٍ أَوْ يُنفَوْا مِنَ الْأَرْضِ ۚ ذَٰلِكَ لَهُمْ خِزْيٌ فِي الدُّنْيَا ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٣٣﴾
33. Hakika jazaa ya wale wanaompiga vita Allaah na Rasuli Wake na wakapania kufanya ufisadi katika ardhi, wauawe au wasulubiwe au ikatwe mikono yao na miguu yao kwa kutofautisha[7] au watolewe katika nchi. Hiyo ndiyo hizaya yao duniani. Na Aakhirah watapata adhabu kubwa mno.[8]
إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن قَبْلِ أَن تَقْدِرُوا عَلَيْهِمْ ۖ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٤﴾
34. Isipokuwa wale waliotubia kabla ya kuwashinda nguvu. Basi jueni kwamba hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُوا فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٣٥﴾
35. Enyi walioamini! Mcheni Allaah na tafuteni njia ya kumkurubia, na fanyeni Jihaad katika Njia Yake ili mpate kufaulu.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ أَنَّ لَهُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا وَمِثْلَهُ مَعَهُ لِيَفْتَدُوا بِهِ مِنْ عَذَابِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَا تُقُبِّلَ مِنْهُمْ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٣٦﴾
36. Hakika wale waliokufuru, kama watakuwa na yale yote yaliyomo ardhini na mengineyo mfano kama hayo, ili watoe fidia kwayo kuepukana na adhabu ya Siku ya Qiyaamah, hayatokubaliwa kutoka kwao, na watapata adhabu iumizayo.
يُرِيدُونَ أَن يَخْرُجُوا مِنَ النَّارِ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنْهَا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّقِيمٌ ﴿٣٧﴾
37. Watataka kutoka katika moto, lakini wao hawatatoka kamwe humo, na watapata adhabu ya kudumu.
وَالسَّارِقُ وَالسَّارِقَةُ فَاقْطَعُوا أَيْدِيَهُمَا جَزَاءً بِمَا كَسَبَا نَكَالًا مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٣٨﴾
38. Mwizi mwanamume na mwizi mwanamke ikateni (kitanga cha) mikono yao, ni malipo kwa yale waliyoyachuma, na adhabu ya tahadharisho na fundisho kwa watu kutoka kwa Allaah. Na Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.[9]
فَمَن تَابَ مِن بَعْدِ ظُلْمِهِ وَأَصْلَحَ فَإِنَّ اللَّـهَ يَتُوبُ عَلَيْهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٩﴾
39. Lakini atakayetubia baada ya dhulma yake na akarekebisha matendo yake na kuwa mwema, basi hakika Allaah Atapokea tawbah yake. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ وَيَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٤٠﴾
40. Je, hujui ya kwamba Allaah Anao ufalme wa mbingu na ardhi? Humwadhibu Amtakae na Humghufiria Amtakae. Na Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.
يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ لَا يَحْزُنكَ الَّذِينَ يُسَارِعُونَ فِي الْكُفْرِ مِنَ الَّذِينَ قَالُوا آمَنَّا بِأَفْوَاهِهِمْ وَلَمْ تُؤْمِن قُلُوبُهُمْ ۛ وَمِنَ الَّذِينَ هَادُوا ۛ سَمَّاعُونَ لِلْكَذِبِ سَمَّاعُونَ لِقَوْمٍ آخَرِينَ لَمْ يَأْتُوكَ ۖ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ مِن بَعْدِ مَوَاضِعِهِ ۖ يَقُولُونَ إِنْ أُوتِيتُمْ هَـٰذَا فَخُذُوهُ وَإِن لَّمْ تُؤْتَوْهُ فَاحْذَرُوا ۚ وَمَن يُرِدِ اللَّـهُ فِتْنَتَهُ فَلَن تَمْلِكَ لَهُ مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۚ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَمْ يُرِدِ اللَّـهُ أَن يُطَهِّرَ قُلُوبَهُمْ ۚ لَهُمْ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٤١﴾
41. Ee Rasuli! Wasikuhuzunishe wale wanaokimbilia kukufuru, miongoni mwa wasemao kwa midomo yao: Tumeamini na hali nyoyo zao hazikuamini. Na miongoni mwa Mayahudi wako wanaosikiliza kwa makini kwa ajili ya uongo, wanaosikiliza kwa makini kwa ajili ya watu wengine wasiokufikia. Wanageuza maneno kutoka mahali pake wanasema: Mkipewa haya yachukueni, na msipopewa hayo basi jihadharini! Na yule ambaye Allaah Anataka kumtia mtihanini, hutokuwa na uwezo wowote (kusaidia) kwa ajili yake mbele ya Allaah. Hao ndio ambao Allaah Hakutaka kuzitakasa nyoyo zao. Watapata hizaya duniani na Aakhirah watapata adhabu kubwa mno.[10]
سَمَّاعُونَ لِلْكَذِبِ أَكَّالُونَ لِلسُّحْتِ ۚ فَإِن جَاءُوكَ فَاحْكُم بَيْنَهُمْ أَوْ أَعْرِضْ عَنْهُمْ ۖ وَإِن تُعْرِضْ عَنْهُمْ فَلَن يَضُرُّوكَ شَيْئًا ۖ وَإِنْ حَكَمْتَ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ﴿٤٢﴾
42. (Hao ni) wenye kusikiliza kwa makini uongo, walaji haramu kwa pupa. Basi wakikujia wahukumu baina yao au wapuuze. Na ukiwapuuza, hawatoweza kukudhuru chochote. Na kama ukihukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika Allaah Anapenda waadilifu.[11]
وَكَيْفَ يُحَكِّمُونَكَ وَعِندَهُمُ التَّوْرَاةُ فِيهَا حُكْمُ اللَّـهِ ثُمَّ يَتَوَلَّوْنَ مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ ۚ وَمَا أُولَـٰئِكَ بِالْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٣﴾
43. Na vipi watakufanya wewe kuwa hakimu wao na hali wana Tawraat yenye Hukumu ya Allaah ndani yake, kisha baada ya hayo wanakengeuka? Na hao si wenye kuamini.
إِنَّا أَنزَلْنَا التَّوْرَاةَ فِيهَا هُدًى وَنُورٌ ۚ يَحْكُمُ بِهَا النَّبِيُّونَ الَّذِينَ أَسْلَمُوا لِلَّذِينَ هَادُوا وَالرَّبَّانِيُّونَ وَالْأَحْبَارُ بِمَا اسْتُحْفِظُوا مِن كِتَابِ اللَّـهِ وَكَانُوا عَلَيْهِ شُهَدَاءَ ۚ فَلَا تَخْشَوُا النَّاسَ وَاخْشَوْنِ وَلَا تَشْتَرُوا بِآيَاتِي ثَمَنًا قَلِيلًا ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ ﴿٤٤﴾
44. Hakika Sisi Tumeteremsha Tawraat yenye mwongozo na nuru ambayo Manabii waliojisalimisha kikamilifu (kwa Allaah), pamoja na Ar-Rabbaaniyyuwn[12] (Marabi) na Al-Ahbaar[13] (Mafuqahaa weledi) wanawahukumia kwayo Mayahudi. Kwa sababu wao wamebebeshwa jukumu la kutakwa kukilinda na kukihifadhi Kitabu cha Allaah, na wakawa mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali Niogopeni Mimi, na wala msibadilishe Aayaat (Hukmu, Sharia) Zangu kwa thamani ndogo. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.
وَكَتَبْنَا عَلَيْهِمْ فِيهَا أَنَّ النَّفْسَ بِالنَّفْسِ وَالْعَيْنَ بِالْعَيْنِ وَالْأَنفَ بِالْأَنفِ وَالْأُذُنَ بِالْأُذُنِ وَالسِّنَّ بِالسِّنِّ وَالْجُرُوحَ قِصَاصٌ ۚ فَمَن تَصَدَّقَ بِهِ فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَّهُ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٤٥﴾
45. Na Tumewaandikia sharia humo kwamba nafsi kwa nafsi, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, jino kwa jino, na majaraha ni kisasi. Lakini atakayesamehe kwa kutolea sadaka, basi itakuwa ni kafara kwake. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu.
وَقَفَّيْنَا عَلَىٰ آثَارِهِم بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ ۖ وَآتَيْنَاهُ الْإِنجِيلَ فِيهِ هُدًى وَنُورٌ وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ التَّوْرَاةِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٤٦﴾
46. Na Tukamfuatishia katika njia yao (Manabii hao), ‘Iysaa mwana wa Maryam akisadikisha yale yaliyoko kabla yake katika Tawraat. Na Tukampa Injiyl yenye mwongozo na nuru ndani yake, inasadikisha yale yaliyokuwa kabla yake katika Tawraat, na Tumeifanya mwongozo na mawaidha kwa wenye taqwa.
وَلْيَحْكُمْ أَهْلُ الْإِنجِيلِ بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فِيهِ ۚ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿٤٧﴾
47. Na watu wa Injiyl wahukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah ndani yake. Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio mafasiki.
وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ الْكِتَابِ وَمُهَيْمِنًا عَلَيْهِ ۖ فَاحْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ عَمَّا جَاءَكَ مِنَ الْحَقِّ ۚ لِكُلٍّ جَعَلْنَا مِنكُمْ شِرْعَةً وَمِنْهَاجًا ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَعَلَكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَـٰكِن لِّيَبْلُوَكُمْ فِي مَا آتَاكُمْ ۖ فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ ۚ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿٤٨﴾
48. Na Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu kwa haki kinachosadikisha Vitabu vilivyokuwa kabla yake. Kinayadhibiti, kinayalinda na kuyashuhudia yaliyomo humo.[14] Basi hukumu baina yao kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, na wala usifuate hawaa zao ukaacha haki iliyokujia. Kila ummah katika nyinyi Tumeupangia sharia na manhaj. Na kama Allaah Angetaka, basi Angelikufanyeni ummah mmoja, lakini (Hakufanya) ili Akujaribuni katika yale Aliyokupeni. Basi shindaneni mambo ya kheri. Kwa Allaah Pekee ndio marejeo yenu nyote, kisha Atakujulisheni yale mliyokuwa mkikhitilafiana.
وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ إِلَيْكَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَاعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ لَفَاسِقُونَ ﴿٤٩﴾
49. Na wahukumu baina yao kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, na wala usifuate hawaa zao, na tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya yale Aliyokuteremshia Allaah. Na wakikengeuka, basi jua kuwa hakika Allaah Anataka kuwaadhibu kwa baadhi ya madhambi yao. Na hakika wengi katika watu ni mafasiki.
أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ ﴿٥٠﴾
50. Je, wanataka hukumu za kijahiliya? Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu kwa watu wenye yakini?
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٥١﴾
51. Enyi walioamini! Msifanye Mayahudi na Manaswara marafiki wandani na walinzi. Wao kwa wao ni marafiki wandani. Na yeyote atakayewafanya marafiki wao wandani, basi hakika yeye ni miongoni mwao. Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu.
فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَىٰ أَن تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ ۚ فَعَسَى اللَّـهُ أَن يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِّنْ عِندِهِ فَيُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا أَسَرُّوا فِي أَنفُسِهِمْ نَادِمِينَ ﴿٥٢﴾
52. Utawaona wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi[15] (ya unafiki) wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu usitusibu mgeuko. Basi asaa Allaah Akaleta ushindi au jambo (jengine) litokalo Kwake, wakawa wenye kujuta kwa waliyoyaficha katika nafsi zao.
وَيَقُولُ الَّذِينَ آمَنُوا أَهَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ ۙ إِنَّهُمْ لَمَعَكُمْ ۚ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَأَصْبَحُوا خَاسِرِينَ ﴿٥٣﴾
53. Na hapo walioamini watasema (wanafiki wakifichuka): Je, hawa ndio wale ambao waliapa kwa Allaah kwa viapo vyao thabiti vya nguvu, kwamba wao wapo pamoja nanyi? Zimeporomoka amali zao, na wamekuwa wenye kukhasirika.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٥٤﴾
54. Enyi walioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu akaacha Dini yake, basi Allaah Ataleta watu (badala yao) Atakaowapenda nao watampenda, wanyenyekevu kwa Waumini, washupavu juu ya makafiri, wanafanya Jihaad katika Njia ya Allaah na wala hawakhofu lawama za mwenye kulaumu. Hiyo ni Fadhila ya Allaah, Humpa Amtakaye. Na Allaah Ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.
إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ ﴿٥٥﴾
55. Hakika Rafiki wenu Mlinzi ni Allaah na Rasuli Wake na wale walioamini, ambao wanasimamisha Swalaah na wanatoa Zakaah hali ya kuwa wananyenyekea.
وَمَن يَتَوَلَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا فَإِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْغَالِبُونَ ﴿٥٦﴾
56. Na atakayemfanya Allaah kuwa ni Rafiki Mlinzi na Rasuli Wake na wale walioamini, basi hakika kundi la Allaah ndio washindi.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَكُمْ هُزُوًا وَلَعِبًا مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَالْكُفَّارَ أَوْلِيَاءَ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٥٧﴾
57. Enyi walioamini! Msiwafanye wale walioifanyia Dini yenu mzaha na mchezo miongoni mwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu na makafiri kuwa marafiki wandani na walinzi. Na mcheni Allaah, kama nyinyi ni Waumini kweli.
وَإِذَا نَادَيْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ اتَّخَذُوهَا هُزُوًا وَلَعِبًا ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ ﴿٥٨﴾
58. Na mnapoinadia Swalaah, wao huifanyia mzaha na mchezo. Hivyo ni kwa kuwa wao ni watu hawana akili.
قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ هَلْ تَنقِمُونَ مِنَّا إِلَّا أَنْ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلُ وَأَنَّ أَكْثَرَكُمْ فَاسِقُونَ ﴿٥٩﴾
59. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Je, mnatuchukia tu kwa vile tumemwamini Allaah na yale yaliyoteremshwa kwetu na yale yaliyoteremshwa kabla, na kwamba wengi wenu ni mafasiki?
قُلْ هَلْ أُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ مِّن ذَٰلِكَ مَثُوبَةً عِندَ اللَّـهِ ۚ مَن لَّعَنَهُ اللَّـهُ وَغَضِبَ عَلَيْهِ وَجَعَلَ مِنْهُمُ الْقِرَدَةَ وَالْخَنَازِيرَ وَعَبَدَ الطَّاغُوتَ ۚ أُولَـٰئِكَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضَلُّ عَن سَوَاءِ السَّبِيلِ ﴿٦٠﴾
60. Sema: Je, nikujulisheni la shari zaidi kuliko hayo kwa malipo (mabaya) mbele ya Allaah? Yule ambaye Allaah Amemlaani na Akamghadhibikia na Akawafanya miongoni mwao manyani na nguruwe na wakaabudu twaghuti, hao wana mahali pabaya mno (Aakhirah) na wapotofu zaidi na njia iliyo sawa (duniani).
وَإِذَا جَاءُوكُمْ قَالُوا آمَنَّا وَقَد دَّخَلُوا بِالْكُفْرِ وَهُمْ قَدْ خَرَجُوا بِهِ ۚ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا كَانُوا يَكْتُمُونَ ﴿٦١﴾
61. Na wanapokujieni husema: Tumeamini. Na hali wameingia na ukafiri wao na wakatoka nao. Na Allaah Anajua zaidi yale waliyokuwa wakiyaficha.
وَتَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يُسَارِعُونَ فِي الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٦٢﴾
62. Na utawaona wengi miongoni mwao wanakimbilia katika dhambi na uadui na kula kwao haramu. Bila shaka ni mabaya mno waliyokuwa wanatenda.
لَوْلَا يَنْهَاهُمُ الرَّبَّانِيُّونَ وَالْأَحْبَارُ عَن قَوْلِهِمُ الْإِثْمَ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَصْنَعُونَ ﴿٦٣﴾
63. Basi mbona Ar-Rabbaaniyyuwn (Marabi) na Al-Ahbaar[16] hawawakatazi maneno yao ya dhambi na ulaji wao wa haramu? Bila shaka ni mabaya mno waliyokuwa wanayafanya.
وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّـهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا ۘ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم مَّا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ طُغْيَانًا وَكُفْرًا ۚ وَأَلْقَيْنَا بَيْنَهُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۚ كُلَّمَا أَوْقَدُوا نَارًا لِّلْحَرْبِ أَطْفَأَهَا اللَّـهُ ۚ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا ۚ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ ﴿٦٤﴾
64. Na Mayahudi wakasema: Mkono wa Allaah umefumbwa. Mikono yao ndio iliyofumbwa na wamelaaniwa kwa yale waliyoyasema! Bali Mikono Yake (Allaah)[17] imefumbuliwa Hutoa Atakavyo. Kwa yakini yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako, yatawazidisha wengi miongoni mwao upindukaji mipaka ya kuasi na kufuru. Na Tumewatilia baina yao uadui na bughudha mpaka Siku ya Qiyaamah. Kila wanapouwasha moto wa vita (dhidi yako), Allaah Huuzima. Na wanapania kwa bidii kufanya ufisadi katika ardhi. Na Allaah Hapendi mafisadi.
وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْكِتَابِ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَكَفَّرْنَا عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَأَدْخَلْنَاهُمْ جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿٦٥﴾
65. Na lau kama Watu wa Kitabu wangeamini na wakawa na taqwa, bila shaka Tungeliwafutia maovu yao, na bila shaka Tungeliwaingiza katika Jannaat (Pepo) za neema.
وَلَوْ أَنَّهُمْ أَقَامُوا التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِم مِّن رَّبِّهِمْ لَأَكَلُوا مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِم ۚ مِّنْهُمْ أُمَّةٌ مُّقْتَصِدَةٌ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ سَاءَ مَا يَعْمَلُونَ ﴿٦٦﴾
66. Na lau kama wangeliishika vyema Tawraat na Injiyl na yale yaliyoteremshwa kwao kutoka kwa Rabb wao, bila shaka wangelikula (rizki) kutoka juu yao na kutoka chini ya miguu yao. Miongoni mwao liko kundi la watu walioko katika njia ya sawa na wengi wao wanayoyafanya ni mabaya mno.
يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٦٧﴾
67. Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukubalighisha Risala Yake. Na Allaah Atakuhifadhi na watu. Hakika Allaah Haongoi watu makafiri.[18]
قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَسْتُمْ عَلَىٰ شَيْءٍ حَتَّىٰ تُقِيمُوا التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ ۗ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم مَّا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ طُغْيَانًا وَكُفْرًا ۖ فَلَا تَأْسَ عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿٦٨﴾
68. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Hamtaambulia chochote mpaka muishike ipasavyo Tawraat na Injiyl na yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa Rabb wenu. Kwa yakini yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako, yatawazidisha wengi miongoni mwao upindukaji mipaka ya kuasi na kufuru. Basi usisikitike juu ya watu makafiri.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالصَّابِئُونَ وَالنَّصَارَىٰ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٦٩﴾
69. Hakika wale walioamini na Mayahudi na Wasabai[19] na Manaswara; atakayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho na akatenda mema, basi hawatokuwa na khofu na wala hawatohuzunika.
لَقَدْ أَخَذْنَا مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَأَرْسَلْنَا إِلَيْهِمْ رُسُلًا ۖ كُلَّمَا جَاءَهُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُهُمْ فَرِيقًا كَذَّبُوا وَفَرِيقًا يَقْتُلُونَ ﴿٧٠﴾
70. Kwa yakini Tulichukua agano la wana wa Israaiyl na Tukawapelekea Rusuli. Basi kila alipowajia Rasuli kwa yale yasiyopenda nafsi zao, kundi waliwakadhibisha na kundi wakawaua.
وَحَسِبُوا أَلَّا تَكُونَ فِتْنَةٌ فَعَمُوا وَصَمُّوا ثُمَّ تَابَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ ثُمَّ عَمُوا وَصَمُّوا كَثِيرٌ مِّنْهُمْ ۚ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ ﴿٧١﴾
71. Na walidhani kwamba yatapita hayo bila adhabu, basi wakawa vipofu na wakawa viziwi, kisha Allaah Akapokea tawbah yao. Tena wengi wao wakawa vipofu na wakawa viziwi. Na Allaah Ni Mwenye Kuona yale wayatendayo.
لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ﴿٧٢﴾
72. Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: Allaah ni Al-Masiyh mwana wa Maryam. Na ilhali Al-Masiyh alisema (kukadhibisha madai yao): Enyi wana wa Israaiyl! Mwabuduni Allaah, Rabb wangu na Rabb wenu. Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni.[20] Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru.
لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ وَإِن لَّمْ يَنتَهُوا عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٣﴾
73. Kwa yakini wamekufuru wale waliosema Allaah ni wa tatu wa watatu. Ilhali hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Ilaah Mmoja Pekee. Na wasipoacha yale wanayoyasema, bila ya shaka itawagusa adhabu iumizayo wale waliokufuru miongoni mwao.
أَفَلَا يَتُوبُونَ إِلَى اللَّـهِ وَيَسْتَغْفِرُونَهُ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٧٤﴾
74. Je, hawatubii kwa Allaah na wakamwomba maghfirah? Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
مَّا الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ وَأُمُّهُ صِدِّيقَةٌ ۖ كَانَا يَأْكُلَانِ الطَّعَامَ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ الْآيَاتِ ثُمَّ انظُرْ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٧٥﴾
75. Al-Masiyh mwana wa Maryam si chochote ila ni Rasuli tu, wamekwishapita kabla yake Rusuli (wengine). Na mama yake ni Muumini mkweli wa dhati. Wote wawili walikuwa wanakula chakula. Tazama jinsi Tunavyowabainishia Aayaat (Ishara, Hoja, Dalili) kisha tazama vipi wanavyoghilibiwa.
قُلْ أَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا ۚ وَاللَّـهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٧٦﴾
76. Sema: Vipi mnaabudu visivyokuwa na uwezo wa kukudhuruni wala kukunufaisheni badala ya Allaah! Na Allaah Ndiye Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ غَيْرَ الْحَقِّ وَلَا تَتَّبِعُوا أَهْوَاءَ قَوْمٍ قَدْ ضَلُّوا مِن قَبْلُ وَأَضَلُّوا كَثِيرًا وَضَلُّوا عَن سَوَاءِ السَّبِيلِ ﴿٧٧﴾
77. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Msipindukie mipaka katika dini yenu bila ya haki, na wala msifuate hawaa za watu waliokwishapotea kabla na wakapotosha wengi na wakapotea njia iliyo sawa.
لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿٧٨﴾
78. Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israaiyl kwa lisani ya Daawuwd na ‘Iysaa mwana wa Maryam. Hivyo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakitaadi.
كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٧٩﴾
79. Walikuwa hawakatazani munkari yoyote waliyofanya. Uovu ulioje waliyokuwa wakiyafanya!
تَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يَتَوَلَّوْنَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ لَبِئْسَ مَا قَدَّمَتْ لَهُمْ أَنفُسُهُمْ أَن سَخِطَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ وَفِي الْعَذَابِ هُمْ خَالِدُونَ ﴿٨٠﴾
80. Utawaona wengi miongoni mwao wanawafanya marafiki wandani na walinzi wale waliokufuru. Ubaya ulioje yale yaliyowatangulizia nafsi zao, hata Allaah Amewaghadhibikia na katika adhabu wao watadumu.
وَلَوْ كَانُوا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالنَّبِيِّ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مَا اتَّخَذُوهُمْ أَوْلِيَاءَ وَلَـٰكِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿٨١﴾
81. Na lau wangelikuwa wanamwamini Allaah na Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kwake, wasingeliwafanya hao marafiki wandani na walinzi, lakini wengi miongoni mwao ni mafasiki.
لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا ۖ وَلَتَجِدَنَّ أَقْرَبَهُم مَّوَدَّةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّ مِنْهُمْ قِسِّيسِينَ وَرُهْبَانًا وَأَنَّهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ﴿٨٢﴾
82. Bila shaka utawakuta walio na uadui mkali zaidi kuliko watu wote, kwa walioamini, ni Mayahudi na wale walioshirikisha. Na bila shaka utawakuta walio karibu zaidi kimapenzi kwa Waumini ni wale wanaosema: Sisi ni Manaswara. Hivyo ni kwa kuwa miongoni mwao kuna Qissiysiyna[21] (Makasisi) na Ruhbaan[22] (Wamonaki) na kwamba wao hawatakabari.[23]
وَإِذَا سَمِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَى الرَّسُولِ تَرَىٰ أَعْيُنَهُمْ تَفِيضُ مِنَ الدَّمْعِ مِمَّا عَرَفُوا مِنَ الْحَقِّ ۖ يَقُولُونَ رَبَّنَا آمَنَّا فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨٣﴾
83. Na wanaposikia yale yaliyoteremshwa kwa Rasuli utaona macho yao yanachuruzika machozi kutokana na yale waliyoyatambua ya haki. Wanasema: Rabb wetu tumeamini, basi Tuandike pamoja na wenye kushuhudia.
وَمَا لَنَا لَا نُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَمَا جَاءَنَا مِنَ الْحَقِّ وَنَطْمَعُ أَن يُدْخِلَنَا رَبُّنَا مَعَ الْقَوْمِ الصَّالِحِينَ ﴿٨٤﴾
84. Na kwa nini Tusimwamini Allaah na haki iliyotufikia na hali tunatumai Rabb wetu Atuingize (Jannah) pamoja na watu Swalihina?
فَأَثَابَهُمُ اللَّـهُ بِمَا قَالُوا جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٥﴾
85. Basi Allaah Akawalipa tuzo ya Jannaat zipitazo chini yake mito kwa yale waliyoyasema, wadumu humo. Na hiyo ndio jazaa ya wafanyao ihsaan.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿٨٦﴾
86. Na wale waliokufuru na wakazikadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) Zetu hao ni watu wa moto uwakao vikali mno.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحَرِّمُوا طَيِّبَاتِ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٨٧﴾
87. Enyi walioamini! Msiharamishe vilivyo vizuri Alivyokuhalalishieni Allaah, na wala msipindukie mipaka. Hakika Allaah Hapendi wapindukao mipaka.
وَكُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ حَلَالًا طَيِّبًا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي أَنتُم بِهِ مُؤْمِنُونَ ﴿٨٨﴾
88. Na kuleni katika vile Alivyowaruzukuni Allaah vya halali na vizuri. Na mcheni Allaah Ambaye nyinyi mnamwamini.
لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٨٩﴾
89. Allaah Hatokuchukulieni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini Atakuchukulieni kwa (kuvunja) viapo mlivyoapa kwa niya mlioifunga thabiti. Basi kafara yake ni kulisha maskini kumi chakula cha wastani mnachowalisha ahli zenu, au kuwavisha nguo, au kuacha huru mtumwa. Lakini asiyeweza kupata (katika hayo), basi (afunge) Swiyaam siku tatu. Hiyo ndio kafara ya viapo vyenu mnapoapa. Na hifadhini yamini zenu.[24] Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na Hukmu, Sharia) Zake ili mpate kushukuru.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٩٠﴾
90. Enyi walioamini! Hakika pombe na kamari na masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli, ni najisi na chukizo kutokana na kazi ya shaytwaan. Basi jiepusheni navyo mpate kufaulu.[25]
إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ ﴿٩١﴾
91. Hakika shaytwaan anataka kukutilieni baina yenu uadui na bughudha, katika pombe na kamari na akuzuieni kumdhukuru Allaah na Swalaah, basi je mtakoma?
وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَاحْذَرُوا ۚ فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ ﴿٩٢﴾
92. Na mtiini Allaah na mtiini Rasuli na tahadharini! Mkikengeuka, basi jueni kwamba juu ya Rasuli Wetu ni kubalighisha ujumbe tu ulio bayana.
لَيْسَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جُنَاحٌ فِيمَا طَعِمُوا إِذَا مَا اتَّقَوا وَّآمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ثُمَّ اتَّقَوا وَّآمَنُوا ثُمَّ اتَّقَوا وَّأَحْسَنُوا ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿٩٣﴾
93. Hakuna lawama juu ya wale walioamini na wakatenda mema katika vile walivyokula (kabla ya kuharimishwa) ikiwa watakuwa na taqwa na wakaamini na wakatenda mema, kisha wakawa na taqwa na wakaamini, kisha wakawa na taqwa na wakafanya ihsaan. Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.[26]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَيَبْلُوَنَّكُمُ اللَّـهُ بِشَيْءٍ مِّنَ الصَّيْدِ تَنَالُهُ أَيْدِيكُمْ وَرِمَاحُكُمْ لِيَعْلَمَ اللَّـهُ مَن يَخَافُهُ بِالْغَيْبِ ۚ فَمَنِ اعْتَدَىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَلَهُ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٩٤﴾
94. Enyi walioamini! Bila shaka Allaah Atakujaribuni mtihani mdogo kwa baadhi ya wanyama wa kuwinda inayowafikia mikono yenu na mikuki yenu, ili Allaah Ampambanue mwenye kumkhofu bila kumwona. Na atakayetaadi baada ya hayo, basi atapata adhabu iumizayo.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْتُلُوا الصَّيْدَ وَأَنتُمْ حُرُمٌ ۚ وَمَن قَتَلَهُ مِنكُم مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاءٌ مِّثْلُ مَا قَتَلَ مِنَ النَّعَمِ يَحْكُمُ بِهِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ هَدْيًا بَالِغَ الْكَعْبَةِ أَوْ كَفَّارَةٌ طَعَامُ مَسَاكِينَ أَوْ عَدْلُ ذَٰلِكَ صِيَامًا لِّيَذُوقَ وَبَالَ أَمْرِهِ ۗ عَفَا اللَّـهُ عَمَّا سَلَفَ ۚ وَمَنْ عَادَ فَيَنتَقِمُ اللَّـهُ مِنْهُ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٩٥﴾
95. Enyi walioamini! Msiue mawindo na hali mko katika ihraam.[27] Na atakayemuua (mnyama) miongoni mwenu kwa kusudi, basi malipo yake itakuwa ni kilicho sawa na alichokiua katika wanyama wa mifugo. Watamkadiria anayelingana naye wajuzi wawili waadilifu miongoni mwenu. Mnyama huyo afikishwe Ka’bah, au atoe kafara ya kulisha maskini, au badala ya hayo, (afunge) Swiyaam ili aonje matokeo maovu ya jambo lake. Allaah Ameshasamehe yaliyopita, na yeyote atakayerudia tena, basi Allaah Atamlipiza (kumuadhibu). Na Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kulipiza.
أُحِلَّ لَكُمْ صَيْدُ الْبَحْرِ وَطَعَامُهُ مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِلسَّيَّارَةِ ۖ وَحُرِّمَ عَلَيْكُمْ صَيْدُ الْبَرِّ مَا دُمْتُمْ حُرُمًا ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٩٦﴾
96. Mmehalalishiwa mawindo ya bahari, na chakula chake ni manufaa kwenu na kwa wasafiri. Na mmeharamishiwa mawindo ya nchi kavu madamu mtakuwa katika ihraam. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mtakusanywa.
جَعَلَ اللَّـهُ الْكَعْبَةَ الْبَيْتَ الْحَرَامَ قِيَامًا لِّلنَّاسِ وَالشَّهْرَ الْحَرَامَ وَالْهَدْيَ وَالْقَلَائِدَ ۚ ذَٰلِكَ لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَأَنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٩٧﴾
97. Allaah Amejaalia Ka’bah ambayo ni Nyumba Tukufu kuwa kiini cha manufaa na matengeneo kwa watu, na pia Miezi Mitukufu na wanyama wa kafara na vigwe. Hivyo ili mpate kujua kuwa Allaah Anajua yale yaliyomo mbinguni na ardhini na kwamba Allaah Ni Mjuzi kwa kila kitu.
اعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ وَأَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٩٨﴾
98. Jueni kuwa Allaah Ni Mkali wa Kuakibu[28] na kwamba Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
مَّا عَلَى الرَّسُولِ إِلَّا الْبَلَاغُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا تَكْتُمُونَ ﴿٩٩﴾
99. Rasuli hana jingine zaidi ila kubalighisha tu. Na Allaah Anayajua yale mnayoyadhihirisha na yale mnayoyaficha.
قُل لَّا يَسْتَوِي الْخَبِيثُ وَالطَّيِّبُ وَلَوْ أَعْجَبَكَ كَثْرَةُ الْخَبِيثِ ۚ فَاتَّقُوا اللَّـهَ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٠٠﴾
100. Sema: Haviwi sawasawa viovu na vizuri japokuwa utakupendezea wingi wa viovu. Basi mcheni Allaah, enyi wenye akili ili mpate kufaulu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ وَإِن تَسْأَلُوا عَنْهَا حِينَ يُنَزَّلُ الْقُرْآنُ تُبْدَ لَكُمْ عَفَا اللَّـهُ عَنْهَا ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿١٠١﴾
101. Enyi walioamini! Msiulizie mambo ambayo mkifichuliwa yatakuchukizeni. Na mkiyaulizia pale inapoteremshwa Qur-aan mtafichuliwa. Allaah Ameyasamehe hayo. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mvumilivu.[29]
قَدْ سَأَلَهَا قَوْمٌ مِّن قَبْلِكُمْ ثُمَّ أَصْبَحُوا بِهَا كَافِرِينَ ﴿١٠٢﴾
102. Walikwishayauliza hayo watu wa kabla yenu, kisha kutokana nayo, wakawa makafiri.
مَا جَعَلَ اللَّـهُ مِن بَحِيرَةٍ وَلَا سَائِبَةٍ وَلَا وَصِيلَةٍ وَلَا حَامٍ ۙ وَلَـٰكِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۖ وَأَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿١٠٣﴾
103. Allaah Hakuweka sharia yoyote ya kuharamisha bahiyrah[30], wala saaibah[31] wala waswiylah[32] wala haam[33] lakini wale waliokufuru wanamtungia Allaah uongo, na wengi wao hawatumii akili.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ قَالُوا حَسْبُنَا مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۚ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ ﴿١٠٤﴾
104. Na wanapoambiwa: Njooni katika yale Aliyoyateremsha Allaah na kwa Rasuli Husema: Yanatutosheleza yale tuliyowakuta nayo baba zetu. Je, japokuwa walikuwa baba zao hawajui chochote na wala hawakuhidika?
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ ۚ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٠٥﴾
105. Enyi walioamini! Jiangalieni nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotoka ikiwa mmehidika. Kwa Allaah Pekee ndio marejeo yenu nyote, kisha Atakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda.[34]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا شَهَادَةُ بَيْنِكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ حِينَ الْوَصِيَّةِ اثْنَانِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ أَوْ آخَرَانِ مِنْ غَيْرِكُمْ إِنْ أَنتُمْ ضَرَبْتُمْ فِي الْأَرْضِ فَأَصَابَتْكُم مُّصِيبَةُ الْمَوْتِ ۚ تَحْبِسُونَهُمَا مِن بَعْدِ الصَّلَاةِ فَيُقْسِمَانِ بِاللَّـهِ إِنِ ارْتَبْتُمْ لَا نَشْتَرِي بِهِ ثَمَنًا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۙ وَلَا نَكْتُمُ شَهَادَةَ اللَّـهِ إِنَّا إِذًا لَّمِنَ الْآثِمِينَ ﴿١٠٦﴾
106. Enyi walioamini! Ushahidi uliofaradhishwa kati yenu ni wa watu wawili waadilifu wakati wa kuandika (au kutamka) usia, anapohisi mmoja wenu dalili za kukurubia kufa, au wawili wengineo wasiokuwa nyinyi pale mnapokuwa safarini ukakufikeni msiba wa mauti. Muwazuie baada ya Swalaah, na waape kwa Allaah mkitilia shaka, (waseme): Hatutovibadilisha (viapo vyetu) kwa thamani yoyote ile japo akiwa ni jamaa yetu wa karibu. Na wala hatutoficha ushuhuda wa Allaah, kwani hakika hapo tutakuwa miongoni mwa wenye kutenda dhambi.
فَإِنْ عُثِرَ عَلَىٰ أَنَّهُمَا اسْتَحَقَّا إِثْمًا فَآخَرَانِ يَقُومَانِ مَقَامَهُمَا مِنَ الَّذِينَ اسْتَحَقَّ عَلَيْهِمُ الْأَوْلَيَانِ فَيُقْسِمَانِ بِاللَّـهِ لَشَهَادَتُنَا أَحَقُّ مِن شَهَادَتِهِمَا وَمَا اعْتَدَيْنَا إِنَّا إِذًا لَّمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٠٧﴾
107. Ikigundulikana kwamba hao wawili wana hatia ya kukhini, basi wawili wengine wanaostahiki kudai haki kisharia, na walio karibu zaidi (na mrithiwa) wasimame mahala pao, kisha waape kwa Allaah: Bila shaka ushahidi wetu ni wa kweli zaidi kuliko ushahidi wa wawili wao, nasi hatukufanya taksiri, kwani bila shaka hapo sisi tutakuwa miongoni mwa madhalimu.
ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يَأْتُوا بِالشَّهَادَةِ عَلَىٰ وَجْهِهَا أَوْ يَخَافُوا أَن تُرَدَّ أَيْمَانٌ بَعْدَ أَيْمَانِهِمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَاسْمَعُوا ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ ﴿١٠٨﴾
108. Hivyo inaelekea zaidi ya kwamba watatoa ushahidi kama ipasavyo au watakhofu visije vikaletwa viapo (vingine) baada ya viapo vyao. Na mcheni Allaah na sikizeni! Na Allaah Haongoi watu mafasiki.[35]
يَوْمَ يَجْمَعُ اللَّـهُ الرُّسُلَ فَيَقُولُ مَاذَا أُجِبْتُمْ ۖ قَالُوا لَا عِلْمَ لَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿١٠٩﴾
109. Siku Allaah Atakayowakusanya Rusuli na Kuwaambia: Mlijibiwa nini? Watasema: Hatujui lolote, hakika Wewe Ndiye Mjuzi wa Ghaibu.
إِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ اذْكُرْ نِعْمَتِي عَلَيْكَ وَعَلَىٰ وَالِدَتِكَ إِذْ أَيَّدتُّكَ بِرُوحِ الْقُدُسِ تُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا ۖ وَإِذْ عَلَّمْتُكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ۖ وَإِذْ تَخْلُقُ مِنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ بِإِذْنِي فَتَنفُخُ فِيهَا فَتَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِي ۖ وَتُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ بِإِذْنِي ۖ وَإِذْ تُخْرِجُ الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِي ۖ وَإِذْ كَفَفْتُ بَنِي إِسْرَائِيلَ عَنكَ إِذْ جِئْتَهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿١١٠﴾
110. (Siku) Allaah Ataposema: Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Kumbuka Neema Yangu juu yako na juu ya mama yako, pale Nilipokutia nguvu kupitia kwa Ruwhil-Qudus (Jibriyl (عليه السلام, unasemesha watu katika utoto na utu uzimani, na Nilipokufunza kuandika na hikmah (ilimu na ufahamu wa kina), na Tawraat na Injiyl, na ulipounda kutokana na udongo kama umbo la ndege kwa Idhini Yangu, ukapulizia likawa ndege kwa Idhini Yangu, na ulipomponyesha aliyezaliwa na upofu na mwenye barasi kwa Idhini Yangu, na ulipowafufua wafu kwa Idhini Yangu, na Nilipowazuia wana wa Israaiyl dhidi yako ulipowajia kwa hoja bayana, wakasema wale waliokufuru miongoni mwao: Haya si chochote ila ni sihiri bayana.
وَإِذْ أَوْحَيْتُ إِلَى الْحَوَارِيِّينَ أَنْ آمِنُوا بِي وَبِرَسُولِي قَالُوا آمَنَّا وَاشْهَدْ بِأَنَّنَا مُسْلِمُونَ ﴿١١١﴾
111. Na Nilipowatia ilhamu wafuasi watiifu kwamba: Niaminini Mimi na Rasuli Wangu. Wakasema: Tumeamini na shuhudia kwamba sisi ni Waislamu.
إِذْ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ هَلْ يَسْتَطِيعُ رَبُّكَ أَن يُنَزِّلَ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ ۖ قَالَ اتَّقُوا اللَّـهَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١١٢﴾
112. Pindi waliposema wafuasi watiifu: Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Je, Anaweza Rabb wako Kututeremshia meza ya chakula kutoka mbinguni? Akasema: Mcheni Allaah, kama nyinyi ni Waumini.
قَالُوا نُرِيدُ أَن نَّأْكُلَ مِنْهَا وَتَطْمَئِنَّ قُلُوبُنَا وَنَعْلَمَ أَن قَدْ صَدَقْتَنَا وَنَكُونَ عَلَيْهَا مِنَ الشَّاهِدِينَ ﴿١١٣﴾
113. Wakasema: Tunataka kula kwenye meza hiyo ili nyoyo zetu zitulie, na tujue kwamba umetuambia kweli, na tuwe katika wenye kulishuhudia hilo.
قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ اللَّـهُمَّ رَبَّنَا أَنزِلْ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ تَكُونُ لَنَا عِيدًا لِّأَوَّلِنَا وَآخِرِنَا وَآيَةً مِّنكَ ۖ وَارْزُقْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿١١٤﴾
114. Akasema ‘Iysaa mwana wa Maryam: Ee Allaah, Rabb wetu! Tuteremshie meza ya chakula kutoka mbinguni ili iwe kwetu ni sikukuu kwa wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na iwe Aayah (Ishara, Hoja, Dalili) itokayo Kwako, basi Turuzuku, kwani Wewe Ni Mbora wa wenye kuruzuku.
قَالَ اللَّـهُ إِنِّي مُنَزِّلُهَا عَلَيْكُمْ ۖ فَمَن يَكْفُرْ بَعْدُ مِنكُمْ فَإِنِّي أُعَذِّبُهُ عَذَابًا لَّا أُعَذِّبُهُ أَحَدًا مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿١١٥﴾
115. Akasema Allaah: Hakika Mimi Nitaiteremsha kwenu. Lakini atakayekufuru miongoni mwenu baada ya hapo, basi hakika Nitamuadhibu adhabu ambayo Sitomuadhibu mmoja yeyote katika walimwengu.
وَإِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ أَأَنتَ قُلْتَ لِلنَّاسِ اتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَـٰهَيْنِ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالَ سُبْحَانَكَ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أَقُولَ مَا لَيْسَ لِي بِحَقٍّ ۚ إِن كُنتُ قُلْتُهُ فَقَدْ عَلِمْتَهُ ۚ تَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِي وَلَا أَعْلَمُ مَا فِي نَفْسِكَ ۚ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿١١٦﴾
116. Na pindi Allaah Atakaposema: Ee ‘Iysaa mwana wa Maryam! Je, wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni waabudiwa wawili badala ya Allaah? (‘Iysaa) atasema: Subhaanak! (Utakasifu ni Wako). Hainipasi mimi kusema yasiyo kuwa haki kwangu. Ikiwa nimesema hayo basi kwa yakini Ungeliyajua. (Kwani) Unayajua yale yote yaliyomo katika nafsi yangu, na wala mimi sijui yale yaliyomo katika Nafsi Yako, hakika Wewe Ni Mjuzi wa Ghaibu.
مَا قُلْتُ لَهُمْ إِلَّا مَا أَمَرْتَنِي بِهِ أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۚ وَكُنتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَّا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنتَ أَنتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿١١٧﴾
117. Sijawaambia (lolote) ila yale tu Uliyoniamrisha kwamba: Mwabuduni Allaah Rabb wangu na Rabb wenu. Na nilikuwa juu yao shahidi wakati nilipokuwa nao. Uliponikamilishia muda Ukanichukua juu, Ulikuwa Wewe Ndiye Mwangalizi juu yao. Na Wewe Ni Mwenye Kushuhudia kila kitu.
إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١١٨﴾
118. Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni Waja Wako, na Ukiwaghufuria basi hakika Wewe Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.[36]
قَالَ اللَّـهُ هَـٰذَا يَوْمُ يَنفَعُ الصَّادِقِينَ صِدْقُهُمْ ۚ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١١٩﴾
119. Allaah Atasema: Hii ndiyo Siku ambayo Asw-Swaadiqiyna utawafaa ukweli wao, watapata Jannaat zipitazo chini yake mito wadumu humo milele. Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Huko ni kufuzu kukubwa mno.
لِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا فِيهِنَّ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٢٠﴾
120. Ni wa Allaah ufalme wa mbingu na ardhi na yote yaliyomo humo. Naye juu ya kila kitu Ni Muweza.
[1] Ihraam: Rejea Aayah namba (95) Suwrah hii.
[2] Tofauti Ya Ikabu Na Adhabu: Rejea Al-Hashr (59:4).
[3] Aayah Ambayo Ingeliteremshwa Kwa Mayahudi, Wangelisherehekea Siku Iliyoteremshwa:
‘Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Myahudi mmoja alimwambia: Ee Amiri wa Waumini, lau ingeliteremka kwetu sisi Aayah hii:
الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ
“Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni Neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislamu uwe Dini yenu.” [Al-Maaidah (5:3)] Basi tungeliifanya kuwa ni siku ya kusherehekea. ‘Umar akasema: Wa-Allaahi, naijua siku gani imeteremka Aayah hii. Imeteremka Siku ya ‘Arafah, siku ya Ijumaa. [Al-Bukhaariy]
[4] Sababu Ya Kuteremshwa Hukmu Ya Tayammum (Kuikusudia Ardhi Safi Ya Mchanga Kwa Ajili Ya Wudhuu):
Mama wa ‘Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) amehadithia: “Tulikwenda katika moja ya safari tukafika Al-Baydaa au Dhaatul-Jaysh ambako kidani changu kilivunjika (na kikapotea). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawa anakitafuta, kisha pia watu wengineo wakainuka kukitafuta. Hapakuweko na maji sehemu hiyo, basi watu wakamwendea Abuu Bakr Asw-Swiddiyq na kusema: Huoni alivyofanya ‘Aaishah? Kamfanya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na watu wakae sehemu ambayo hakuna maji! Abuu Bakr akaja wakati Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa amelala akiwa amelaza kichwa chake mapajani mwangu. Akaniambia: Umemzuia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na watu sehemu ambako hakuna maji na wala hawana (akiba ya) maji. Basi akanigombesha na akasema Aliyomjaalia (Allaah) kusema kuhusu mimi, na akanipiga ubavuni kwa mkono wake. Hakuna kilichonizuia kusogea (kutokana na maumivu) isipokuwa kwa vile Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa amelala mapajani mwangu. Hapo Allaah Akateremsha Aayah ya tayammum (kutia Wudhuu kwa mchanga), basi wakatayammam. ‘Usayd bin Al-Hudhwayr akasema: Ee ahli wa Abuu Bakr! Hii si baraka ya kwanza kwenu. Kisha akaendeshwa ngamia ambaye nilikuwa nimempanda na tukakipata kidani kilichokuwa (kimejificha) chini yake.” [Al-Bukhaariy]
Rejea pia An-Nisaa Aayah (4:43) ambayo pia ni sababu ya kuteremshwa hukmu ya Tayammum.
Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
[5] Al-Masiyh (Nabiy ‘Iysaa) Sio Allaah Bali Ni Mwana Wa Maryam Na Ni Rasuli Wa Allaah:
Rejeja An-Nisaa (4:171) na Rejea Suwrat Maryam (19:16-36) ambako kumetajwa kisa cha Maryam; Mama wa Nabiy ‘Iysaa, na yeye mwenyewe Nabiy ‘Iysaa amekanusha alipokuwa angali mtoto mchanga baada ya kuzaliwa tu kuwa yeye siye anayepaswa kuabudiwa, na kwamba yeye ni mja na Rasuli wa Allaah, na kwamba anayepaswa kuabudiwa ni Allaah. Hali kadhaalika Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) amekanusha hayo katika Suwrah hii (5:116-118). Amekanusha pia katika Suwrat Az-Zukhruf (43:64). Rejea pia Aal-‘Imraan (3:51).
[6] Watu Wawili Waliomcha Allaah:
Watu wawili hao waliomcha Allaah ni Yuwsha’ Bin Nuwn Na Kaalib Bin Yuwfaan [Tafsiyr Ibn Kathiyr] Rejea Al-Kahf (18:60)
[7] Vipi Kukatwa Mikono Na Miguu Kwa Kutofautisha:
Kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
أَوْ تُقَطَّعَ أَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُم مِّنْ خِلَافٍ
“Au ikatwe mikono yao na miguu yao kwa kutofautisha.”
Ni kukatwa mikono ya kulia kwa miguu ya kushoto au miguu ya kushoto kwa mikono ya kulia.
[9] Radd Kwa Kundi La Qur-aaniyyuwn Wanaoamini Qur-aan Pekee Na Kupinga Sunnah:
Aayah hii tukufu ambayo imetaja hukmu ya mwizi kukatwa mkono, ni Aayah mojawapo ambayo haiwezi kufahamika na wala kupata hukmu yake kamili ya suala la mwizi kukatwa mkono. Ni lazima mtu arudie katika Sunnah kupata ufafanuzi wa suala zima la hukmu hii kama vile kiwango gani cha chini alichoiba hata astahiki kukatwa mkono. Na je mkono gani, na kuanzia wapi? Na ‘Aliy (رضي الله عنه) alikuwa akikata mkono kuanzia kifundoni. Na Qataadah amesema kuhusiana na mwanamke aliyeiba naye akakatwa mkono wake wa kushoto: “Usiwe ni mwenye kukata chochote chengine.” [Imaam Al-Bukhaariy katika Kitaab cha Huduwd (Mipaka)]
Hadiyth kadhaa zimethibiti kutoa hukmu ya suala hili. Ni kama hii ifuatayo inayotaja kiwango cha alichoiba mwizi:
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Unakatwa mkono wa mwizi aliyeiba robo dinaar ya dhahabu.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth hii ni hoja bayana kwa kundi la Qur-aaniyuwn wanaoikubali Qur-aan pekee na kukanusha Hadiyth za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba hawawezi kuifahamu Qur-aan kwa waziwazi na kupata hukmu za baadhi ya mas-ala ila kupitia Hadiyth. Na ajabu mno kwa kundi hilo kukanusha Hadiyth za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ilhali Qur-aan haikufafanua mas-ala mengi ya ibaada za Muislamu ambazo bila ya Hadiyth za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) haiwezekani kufahamu jinsi ya kuzitekeleza. Na katika ibaada hizo ni nguzo za Kiislamu kama Swalaah kuanzia Twahara yake, idadi ya Rakaa zake kwa nyakati zote tano; Alfajiri, Adhuhuri, Alasiri, Magharibi na ‘Ishaa ambazo hazikutajwa katika Qur-aan, na utekelezaji mzima wa Swalaah ambayo ina nguzo zake, yanayowajibika, yaliyo Sunnah na kadhaalika. Hali kadhaalika Manaasik (taratibu) za Hajj; hukmu zake na utekelezaji wake hayakufafanuliwa katika Qur-aan. Pia hukmu za Swawm ya Mwezi wa Ramadhwaan na wakati wa kuanzia kufunga hadi kufuturu. Kiwango cha utoaji wa Zakaah nacho hakikutajwa katika Qur-aan. Na mengi mengineyo ambayo yote hayakufafanuliwa katika Qur-aan bali Sunnah ndio imekuja kufafanua. Basi vipi waamini Qur-aan na wasifuate Anayoamrisha Allaah (سبحانه وتعالى) kumtii na kumfuata Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ilhali Anaamrisha hilo?! Na pia Allaah (سبحانه وتعالى) Mwenyewe Amemtaka Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) afafanue na awafahamishe Waumini yaliyomo ndani ya Qur-aan. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٤٤﴾
“Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao huenda wakapata kutafakari.” [An-Nahl (16:44)]
Na pia Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ إِلَّا لِتُبَيِّنَ لَهُمُ الَّذِي اخْتَلَفُوا فِيهِ ۙ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿٦٤﴾
“Na Hatukukuteremshia Kitabu (Qur-aan) isipokuwa uwabainishie yale waliyokhitilafiana, na pia ni mwongozo na rehma kwa watu wanaoamini.” [An-Nahl (16:64)]
Na Aayah hii pia ni zingatio kwa makafiri wanaoitafutia upogo Qur-aan kuwa inatoa hukmu kali kama hii ya wizi na nyenginezo kama adhabu ya zinaa, bila ya kufahamu kwa kina hukmu zake ambazo ufafanuzi wake unapatikana katika Sunnah (Hadiyth) ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).
[12] Ar-Rabbaaniyyuwn (Marabi): Ni Wanavyuoni Waswalihina wa Kiyahudi wenye kufanya ibaada mno na kuitumia ilimu yao. Rejea Aal-‘Imraan (3:79) kupata maelezo ziyada kuhusu maana hii na sifa zake.
[13] Al-Ahbaar: Mafuqahaa wa dini ya Kiyahudi ambao ni weledi mno.
[14] Qur-aan Inashuhudia Na Inadhibiti Vitabu Vilivyotangulia.
Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja katika Aayah kadhaa kwamba Vitabu Vyake vya nyuma Alivyoviteremsha toka mbinguni kwa Mayahudi na Manaswara vimebadilishwa maneno yake kwa sababu ya kuficha haki au kufuata manufaa ya kidunia. Akateremsha Qur-aan kuwa ni Kitabu cha mwisho kwa Rasuli wa mwisho kabisa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) , na kwamba Qur-aan hii haina shaka kabisa, na wala hakuna awezaye kuibadilisha au kuleta mfano wake. Rejea Al-Baqarah (2:79) (2:174), Aal-‘Imraan (3:78), (3:187).
[15] Nyoyo Zenye Maradhi:
Rejea Suwrah Muhammad (47:20) kwenye maelezo na rejea mbalimbali kuhusu nyoyo zenye maradhi.
Rejea pia Al-Hajj (22:46) kwenye maelezo kuhusu maana ya moyo uliopofuka.
Rejea pia Ash-Shu’araa (26:88-89) kwenye ufafanuzi na maelezo kuhusu moyo uliosalimika.
[16] Ar-Rabbaaniyyuwn (Marabi), Al-Ahbaar: Rejea Suwrah hii Al-Maaidah (5:44).
[17] Aqiydah Sahihi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Ni Kuthibisha Sifa Za Allaah Kama Mikono Yake:
Rejea Al-Fat-h (48:10).
[18] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ametimiza Risala (Ujumbe) Ipasavyo:
Hakika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliifikisha na kuitangaza Dini ya Allaah (سبحانه وتعالى) na akaieneza daawah yake mpaka ikawafikia majini na watu. Na akawafundisha yote Aliyoyaweka Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa ni sharia. Akausimamia uwajibu huu kwa nguvu zote, na Allaah (سبحانه وتعالى) Hakumfisha mpaka Alipoinyoosha kupitia yeye dini iliyopindishwa na Akayafungua kupitia yeye macho yenye upofu, na kuzifungua nyoyo zilizokuwa zimefunikwa na ujinga.
Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
067-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Maaidah Aayah 067: وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ [102]
[20] Kumshirikisha Allaah Ni Dhambi Pekee Asiyoighufuria Allaah (سبحانه وتعالى) Isipokuwa Mtu Atubie Kabla Ya Kufariki Kwake:
Rejea An-Nisaa (4:48), (4:116).
Na ‘Iysaa Hapasi Kuabudiwa Kwani Yeye Ni Mja Wa Allaah Na Rasuli Wake:
Rejea (4:171), At-Tawbah (9:30). Na pia Aayah (5:17) ya Suwrah hii Al-Maaidah.
[21] Qissiysiyna: (Makasisi) Wanavyuoni Wakuu wa Kinaswara wenye kufanya ibaada mno.
[22] Ruhbaan: Monaki wa Kinaswara wenye taqwa na wanaomkhofu mno Allaah (سبحانه وتعالى).
[24] Kafara Ya Kuapa Ifuatwe Kwa Mpangilio Wa Aayah Na Haifai Kuapa Ovyo Ovyo:
Aayah hii Tukufu imebainisha kwamba kafara ya yamini iliyofungika ni waajib kwa kuchaguzwa mhusika kwa mujibu wa utaratibu ufuatao:
1-Kulisha.
2-Kuvisha nguo.
3-Kuacha huru mtumwa.
4-Swiyaam (kufunga) siku tatu pindi mtu akishindwa hayo matatu ya kwanza. Na haijuzu kufanya kafara hii ya Swawm ila baada ya kushindwa kuyafanya mambo matatu hayo ya kwanza. Hili ndilo lililokubaliwa kwa ‘Ijmaa ya ‘Ulamaa wote. [Swahiyh Fiqh As-Sunnah Mlango Wa Viapo Na Nadhiri]
Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Anaamrisha kuhifadhi viapo Anaposema:
وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ
“Na hifadhini yamini zenu.”
Kwa maana haifai mtu kuapa ovyo ovyo. Na hikma ya watu kuamuriwa kuapa kwa ufinyu iwezekanavyo, ni kuwa mtu anayeapa kwa Allaah kwa kila kichache na kingi, basi ulimi wake utakuja kuzoea hilo, na kiapo hakitakuwa na uzito wala thamani kwenye moyo wake, na hatokuwa na muamana wa kuthubutu kuapa kiapo cha uongo. Na hapo lengo asili la kiapo litapoteza mwelekeo. [Swahiyh Fiqh As-Sunnah Mlango Wa Viapo Na Nadhiri]
Rejea Al-Baqarah (2:225), Al-Qalam (68:10).
Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
[25] Hatua Za Uharamisho Wa Pombe Na Kikomo Chake:
Rejea Al-Baqarah (2:219), An-Nisaa (4:43).
Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
Hatua ya kwanza. Ni swali alilouliza Swahaba, na jibu lake lipo katika Suwratul-Baqarah (2:219):
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ
“Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na (baadhi ya) manufaa kwa watu. Na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake.” [Al-Baqarah (2:219)]
Hatua ya pili. Ilikuwa ni kukatazwa pombe katika nyakati za Swalaah kwa sababu Swahaba walikosea kusoma Qur-aan katika Swalaah kutokana na kulewa. Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha Aayah katika Suwrat An-Nisaa (4:43):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ
“Enyi walioamini! Msikaribie Swalaah na hali mmelewa mpaka mjue mnayoyasema.” [An-Nisaa (4:43)]
Hatua ya tatu. Ni pale zilipofutwa hukmu hizo na ikabakia pombe kuwa ni haramu nyakati zote kwa Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٩٠﴾
“Enyi walioamini! Hakika pombe na kamari na masanamu na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli, ni najisi na chukizo kutokana na kazi ya shaytwaan. Basi jiepusheni navyo mpate kufaulu.”
إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ ﴿٩١﴾
“Hakika shaytwaan anataka kukutilieni baina yenu uadui na bughudha katika pombe na kamari na akuzuieni kumdhukuru Allaah na Swalaah, basi je mtakoma?” [Al-Maaidah (5:90-91)]
Baada ya kuteremshwa Aayah hizo za Suwrat Al-Maaidah (5:90-91), hapo hapo Swahaba wakaacha moja kwa moja kulewa, na ikawa ndio kikomo cha kunywa pombe.
[27] Ihraam:
Ni mambo ambayo Allaah Amemkataza aliyehirimia kuyafanya, na Akamharamishia madhali yuko kwenye ihraam. Na ihraam (kuhirimia) ni kutia niya ya Hajj au ‘Umrah toka kwenye Miyqaat inayotambulika kisharia. Ni nguzo kati ya nguzo za Hajj na ‘Umrah kwa mujibu wa Jumhuri ya ‘Ulamaa, na ni sharti ya kuswihi Hajj au ‘Umrah. [Swahiyh Fiqh As-Sunnah]
[28] Tofauti Ya Ikabu Na Adhabu: Rejea Al-Hashr (59:4).
[30] Bahira: Ngamia aliyezaa matumbo matano.
[31] Saaibah: Ngamia aliyeachiliwa kwa nadhiri.
[32] Waswiylah: Kondoo aliyezaa matumbo saba.
[33] Haam: Fahali lililozalisha matumbo kumi.
[34] Kuzuia Dhulma Ili Kuepukana Na Adhabu Za Allaah (سبحانه وتعالى):
Abuu Bakr Asw-Swiddiyq (رضي الله عنه) amesema: Enyi watu! Hakika nyinyi mnaisoma Aayah hii:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ ۚ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٠٥﴾
“Enyi walioamini! Jiangalieni nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotoka ikiwa mmehidika. Kwa Allaah Pekee ndio marejeo yenu nyote, kisha Atakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda. ” [Al-Maaidah (5 :105)]
Hakika mimi nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Watu pindi watakapomuona mfanya dhulma na wakawa hawakumzuwia na hiyo dhulma, basi wafahamu kuwa Allaah Hukaribia kuwaadhibu wote kwa adhabu itokayo Kwake.” [At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Hadiyth Swahiyh]
[36] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Akijali Mno Ummah Wake Na Akiwakhofia Adhabu:
Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Amru bin Al-‘Aasw (رضي الله عنه) : Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisoma Kauli ya Allaah (عزّ وجلّ) kuhusu Nabiy Ibraahiym:
رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ ۖ فَمَن تَبِعَنِي فَإِنَّهُ مِنِّي ۖ
“Rabb wangu! Hakika hao (masanamu) wamepoteza watu wengi. Basi atakayenifuata, huyo yuko nami.” [Ibraahiym: 36]
Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasoma alivyosema ‘Iysaa (عليه السّلام) :
إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١١٨﴾
“Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni Waja Wako, na Ukiwaghufuria basi hakika Wewe Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.” [Al-Maaidah: 118]
Akanyanyua mikono yake akisema: “Ee Allaah! Ummah wangu! Ummah Wangu! Akalia, kisha Allaah (عزّ وجلّ) Akasema: “Ee Jibriyl! Nenda kwa Muhammad, na Rabb wako Anajua zaidi, kisha muulize kitu kigani kinachomliza? Basi Jibriyl akamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuuliza (sababu ya kulia kwake), na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamjulisha, na Allaah Anajua zaidi, Hapo Allaah Akasema: “Ee Jibriyl! Nenda kwa Muhammad na mwambie: Hakika Sisi Tutauridhia ummah wako wala Hatutaudhika nawe.” [Muslim]
Imaam An-Nawawiy (رحمه الله) amesema katika Sharh Muslim: “Hadiyth hii imejumuisha aina za faida zikiwemo: Bainisho kamilifu la huruma zake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa ummah wake, kujali kwake kutunza maslahi yao, na kutilia hima mambo yao. Na hii ni bishara adhimu kwa ummah huu kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ameuzidishia (ummah) sharaf (taadhima) kutokana na yale ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Amemuahidi Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Kauli Yake: “Tutauridhia ummah wako wala Hatutaudhika nawe.” Na hii ni Hadiyth itoayo matarajio makubwa kabisa kwa ummah huu.
Inaruhusika Kuirudia Aayah Moja Katika Swalaah Ya Sunnah:
Amesimulia Abuu Dharri (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliisoma Aayah hii akairudia rudia mpaka asubuhi. [Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (1010), Ahmad (20831) na Al-Haakim. Katika Sanad yake kuna ulaini]
الأنْعَام
006-Al-An’aam
006-Al-An'aam: Utangulizi Wa Suwrah [110]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَجَعَلَ الظُّلُمَاتِ وَالنُّورَ ۖ ثُمَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ ﴿١﴾
1. AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na Akajaalia viza na nuru, kisha wale ambao wamekufuru wanawasawazisha wengine na Rabb wao.
هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن طِينٍ ثُمَّ قَضَىٰ أَجَلًا ۖ وَأَجَلٌ مُّسَمًّى عِندَهُ ۖ ثُمَّ أَنتُمْ تَمْتَرُونَ ﴿٢﴾
2. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na udongo kisha Akahukumu muda maalumu, na uko Kwake muda maalumu uliokadariwa, kisha nyinyi mnatilia shaka!
وَهُوَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَفِي الْأَرْضِ ۖ يَعْلَمُ سِرَّكُمْ وَجَهْرَكُمْ وَيَعْلَمُ مَا تَكْسِبُونَ ﴿٣﴾
3. Na Yeye Ndiye Allaah mbinguni na ardhini, Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu, na Anajua yale mnayoyachuma.[1]
وَمَا تَأْتِيهِم مِّنْ آيَةٍ مِّنْ آيَاتِ رَبِّهِمْ إِلَّا كَانُوا عَنْهَا مُعْرِضِينَ ﴿٤﴾
4. Na haiwafikii Aayah (Ishara, Muujiza, Hoja bayana) yoyote ile katika Aayaat (Ishara, Miujiza, Hoja bayana) za Rabb wao isipokuwa huwa ni wenye kuipuuza.
فَقَدْ كَذَّبُوا بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ ۖ فَسَوْفَ يَأْتِيهِمْ أَنبَاءُ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٥﴾
5. Kwa yakini wameikadhibisha haki ilipowajia, basi zitawafikia khabari muhimu za yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.
أَلَمْ يَرَوْا كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّن قَرْنٍ مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ مَا لَمْ نُمَكِّن لَّكُمْ وَأَرْسَلْنَا السَّمَاءَ عَلَيْهِم مِّدْرَارًا وَجَعَلْنَا الْأَنْهَارَ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمْ فَأَهْلَكْنَاهُم بِذُنُوبِهِمْ وَأَنشَأْنَا مِن بَعْدِهِمْ قَرْنًا آخَرِينَ ﴿٦﴾
6. Je, hawaoni ni karne ngapi za vizazi Tumeziangamiza kabla yao? Tuliwamakinisha katika ardhi kwa namna ambayo Hatujapata kuwamakinisha nyinyi, na Tukawapelekea mvua tele iendeleayo, na Tukajaalia mito ipitayo chini yao. Hatimaye Tukawaangamiza kwa dhambi zao na Tukaanzisha baada yao karne nyingine ya vizazi.
وَلَوْ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ كِتَابًا فِي قِرْطَاسٍ فَلَمَسُوهُ بِأَيْدِيهِمْ لَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿٧﴾
7. Na lau Tungelikuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) maneno yaliyoandikwa katika karatasi, kisha wakaigusa kwa mikono yao, bila shaka wale waliokufuru wangelisema: Hii si chochote isipokuwa ni sihiri (uchawi) bayana.
وَقَالُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ مَلَكٌ ۖ وَلَوْ أَنزَلْنَا مَلَكًا لَّقُضِيَ الْأَمْرُ ثُمَّ لَا يُنظَرُونَ ﴿٨﴾
8. Na wakasema: Mbona hakuteremshiwa Malaika? Na lau Tungeliteremsha Malaika, basi amri ingepitishwa kisha wasingelipewa muhula.
وَلَوْ جَعَلْنَاهُ مَلَكًا لَّجَعَلْنَاهُ رَجُلًا وَلَلَبَسْنَا عَلَيْهِم مَّا يَلْبِسُونَ ﴿٩﴾
9. Na lau Tungelimfanya Malaika, bila shaka Tungelimfanya binaadam mwanamume, na Tungeliwatatanishia yale wanayojitatanisha.
وَلَقَدِ اسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَحَاقَ بِالَّذِينَ سَخِرُوا مِنْهُم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿١٠﴾
10. Na kwa yakini walifanyiwa istihzai Rusuli kabla yako, lakini wale waliowafanyia dhihaka, yaliwazunguka yale yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.
قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ ثُمَّ انظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ ﴿١١﴾
11. Sema: Nendeni katika ardhi, kisha mtazame vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha.[2]
قُل لِّمَن مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ قُل لِّلَّـهِ ۚ كَتَبَ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۚ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٢﴾
12. Sema: Ni vya nani vilivyomo mbinguni na ardhini? Sema: Ni vya Allaah. Amejiwajibishia Nafsi Yake[3] Rehmah. Bila shaka Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah, hapana shaka yoyote ndani yake. Wale ambao wamekhasiri nafsi zao basi wao hawaamini.
وَلَهُ مَا سَكَنَ فِي اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٣﴾
13. Na ni Vyake vyote vinavyotulia katika usiku na mchana. Naye Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَتَّخِذُ وَلِيًّا فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَهُوَ يُطْعِمُ وَلَا يُطْعَمُ ۗ قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ أَوَّلَ مَنْ أَسْلَمَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٤﴾
14. Sema: Je, nimfanye rafiki mlinzi asiyekuwa Allaah Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Naye Ndiye Anayelisha na wala Halishwi? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu. Na wala usijekuwa kabisa miongoni mwa washirikina.
قُلْ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٥﴾
15. Sema: Hakika mimi nakhofu, ikiwa nitamuasi Rabb wangu, adhabu ya Siku iliyo kuu kabisa.
مَّن يُصْرَفْ عَنْهُ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمَهُ ۚ وَذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْمُبِينُ ﴿١٦﴾
16. Atakayeepushwa nayo (adhabu) Siku hiyo, basi kwa yakini (Allaah) Amemrehemu. Na huko ndiko kufuzu kulio wazi.
وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يَمْسَسْكَ بِخَيْرٍ فَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٧﴾
17. Na Allaah Akikugusisha kwa dhara, basi hakuna yeyote wa kuiondoa isipokuwa Yeye, na Akikugusisha kheri, basi Yeye juu ya kila kitu Ni Muweza.
وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿١٨﴾
18. Naye Ndiye Aliyedhibiti vyote chini ya Mamlaka Yake Aliye juu ya Waja Wake. Naye Ndiye Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
قُلْ أَيُّ شَيْءٍ أَكْبَرُ شَهَادَةً ۖ قُلِ اللَّـهُ ۖ شَهِيدٌ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۚ وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ ۚ أَئِنَّكُمْ لَتَشْهَدُونَ أَنَّ مَعَ اللَّـهِ آلِهَةً أُخْرَىٰ ۚ قُل لَّا أَشْهَدُ ۚ قُلْ إِنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ وَإِنَّنِي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ ﴿١٩﴾
19. Sema: Kitu gani ushahidi wake ndio mkubwa zaidi? Sema: Allaah. Yeye Ni Shahidi baina yangu na baina yenu. Na nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayemfikia. Je, hivi kweli nyinyi mnashuhudia kwamba wako waabudiwa wengine pamoja na Allaah? Sema: Mimi sishuhudii (hayo). Sema: Hakika Yeye Ni Mwabudiwa wa haki Mmoja (Pekee), na hakika mimi sihusiki na mnavyomshirikisha navyo.
الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمُ ۘ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٢٠﴾
20. Wale Tuliowapa Kitabu wanamjua (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) au wanaijua Tawhiyd) kama wanavyowajua watoto wao. Wale ambao wamekhasiri nafsi zao basi wao hawaamini.
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۗ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ ﴿٢١﴾
21. Na nani mdhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia Allaah uongo au anayekadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili bayana) Zake? Hakika madhalimu hawatofaulu.
وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا أَيْنَ شُرَكَاؤُكُمُ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٢٢﴾
22. Na Siku Tutakayowakusanya wote pamoja, kisha Tutawaambia wale walioshirikisha: Wako wapi washirika wenu ambao mlikuwa mnadai (kuwa waungu wawaombeeni)?
ثُمَّ لَمْ تَكُن فِتْنَتُهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا وَاللَّـهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا مُشْرِكِينَ ﴿٢٣﴾
23. Kisha haitokuwa hoja yao ya kujitetea isipokuwa kusema: Wa-Allaahi Rabb wetu! Hatukuwa washirikina.
انظُرْ كَيْفَ كَذَبُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ ۚ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٢٤﴾
24. Tazama vipi walivyojiongopea wenyewe na yamewapotea yale waliyokuwa wakiyatunga (ya uongo).
وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ ۖ وَجَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا ۚ وَإِن يَرَوْا كُلَّ آيَةٍ لَّا يُؤْمِنُوا بِهَا ۚ حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوكَ يُجَادِلُونَكَ يَقُولُ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿٢٥﴾
25. Na wako miongoni mwao wanaotega sikio kukusikiliza. Nasi Tumeweka vifuniko kwenye nyoyo zao wasipate kuyafahamu na katika masikio yao uziwi.[4] Na wanapoona Aayah (Ishara, Ushahidi, Dalili) yoyote (ya kuthibitisha ukweli wako) hawaiamini. Hata wanapokujia kukubishia husema wale waliokufuru: Hizi si chochote ila ni hekaya za watu wa kale.
وَهُمْ يَنْهَوْنَ عَنْهُ وَيَنْأَوْنَ عَنْهُ ۖ وَإِن يُهْلِكُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٢٦﴾
26. Wao wanazuia asifuatwe, na wenyewe wanajiweka mbali naye. Lakini hawaangamizi isipokuwa nafsi zao wala hawahisi.
وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ وُقِفُوا عَلَى النَّارِ فَقَالُوا يَا لَيْتَنَا نُرَدُّ وَلَا نُكَذِّبَ بِآيَاتِ رَبِّنَا وَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢٧﴾
27. Na lau ungeliona watakaposimamishwa kwenye moto kisha wakasema: Laiti tungelirudishwa (duniani) na wala hatutakadhibisha Aayaat (na Ishara) za Rabb wetu, na tutakuwa miongoni mwa waumini!
بَلْ بَدَا لَهُم مَّا كَانُوا يُخْفُونَ مِن قَبْلُ ۖ وَلَوْ رُدُّوا لَعَادُوا لِمَا نُهُوا عَنْهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿٢٨﴾
28. Bali yamewadhihirikia yale waliyokuwa wakiyaficha kabla. Na lau wangelirudishwa, kwa yakini wangeyarudia yale waliyokatazwa, na hakika wao ni waongo!
وَقَالُوا إِنْ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ ﴿٢٩﴾
29. Na walisema: Haya si chochote isipokuwa ni uhai wetu wa dunia tu, na wala sisi hatutofufuliwa.[5]
وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ وُقِفُوا عَلَىٰ رَبِّهِمْ ۚ قَالَ أَلَيْسَ هَـٰذَا بِالْحَقِّ ۚ قَالُوا بَلَىٰ وَرَبِّنَا ۚ قَالَ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿٣٠﴾
30. Na lau ungeliona watakaposimamishwa mbele ya Rabb wao. Atasema: Je, haya si ya kweli? Watasema: Ndio (kweli kabisa), tunaapa kwa Rabb wetu! Atasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkikufuru.
قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِلِقَاءِ اللَّـهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءَتْهُمُ السَّاعَةُ بَغْتَةً قَالُوا يَا حَسْرَتَنَا عَلَىٰ مَا فَرَّطْنَا فِيهَا وَهُمْ يَحْمِلُونَ أَوْزَارَهُمْ عَلَىٰ ظُهُورِهِمْ ۚ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ ﴿٣١﴾
31. Kwa yakini wamekhasirika wale waliokadhibisha kukutana na Allaah. Hata itakapowajia Saa (mauti) kwa ghafla watasema: Ee majuto yetu kwa yale tuliyokusuru humo! Na ilhali wao wanabeba mizigo yao (ya dhambi) migongoni mwao. Tanabahi! Uovu ulioje wanayobeba!
وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَعِبٌ وَلَهْوٌ ۖ وَلَلدَّارُ الْآخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٣٢﴾
32. Na uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni mchezo na pumbao. Na bila shaka nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi kwa wenye taqwa. Je, basi hamtii akilini?
قَدْ نَعْلَمُ إِنَّهُ لَيَحْزُنُكَ الَّذِي يَقُولُونَ ۖ فَإِنَّهُمْ لَا يُكَذِّبُونَكَ وَلَـٰكِنَّ الظَّالِمِينَ بِآيَاتِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ ﴿٣٣﴾
33. Kwa yakini Tunajua (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba yanakuhuzunisha yale wanayoyasema. Basi hakika wao hawakukadhibishi wewe (kwa vile wanakujua ni mkweli) lakini wanachokanusha madhalimu ni Aayaat (na Ishara) za Allaah.
وَلَقَدْ كُذِّبَتْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ فَصَبَرُوا عَلَىٰ مَا كُذِّبُوا وَأُوذُوا حَتَّىٰ أَتَاهُمْ نَصْرُنَا ۚ وَلَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِ اللَّـهِ ۚ وَلَقَدْ جَاءَكَ مِن نَّبَإِ الْمُرْسَلِينَ ﴿٣٤﴾
34. Na kwa yakini walikadhibishwa Rusuli kabla yako, na wao walivuta subira kwa kukadhibishwa huko, na waliudhiwa na kusumbuliwa mpaka ilipowafikia Nusura Yetu. Na hakuna yeyote awezaye kubadilisha Maneno ya Allaah. Zimekwishakujia khabari za Rusuli (waliopita kukuliwaza).
وَإِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكَ إِعْرَاضُهُمْ فَإِنِ اسْتَطَعْتَ أَن تَبْتَغِيَ نَفَقًا فِي الْأَرْضِ أَوْ سُلَّمًا فِي السَّمَاءِ فَتَأْتِيَهُم بِآيَةٍ ۚ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَمَعَهُمْ عَلَى الْهُدَىٰ ۚ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْجَاهِلِينَ ﴿٣٥﴾
35. Na kama kukengeuka kwao kumekuwa ni mashaka mno kwako, basi ukiweza kutafuta njia ya chini kwa chini katika ardhi au ngazi kwendea mbinguni ili uwaletee Aayah (Ishara, Dalili) yoyote (basi fanya). Na kama Allaah Angetaka Angeliwakusanya katika hidaaya. Basi chunga usiwe miongoni mwa majahili.
إِنَّمَا يَسْتَجِيبُ الَّذِينَ يَسْمَعُونَ ۘ وَالْمَوْتَىٰ يَبْعَثُهُمُ اللَّـهُ ثُمَّ إِلَيْهِ يُرْجَعُونَ ﴿٣٦﴾
36. Hakika wanaitikia wale wanaosikia (kwa nyoyo za imaan). Ama wafu (wa nyoyo) Allaah Atawafufua, kisha Kwake watarejeshwa.
وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِّن رَّبِّهِ ۚ قُلْ إِنَّ اللَّـهَ قَادِرٌ عَلَىٰ أَن يُنَزِّلَ آيَةً وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٧﴾
37. Na walisema: Kwa nini hakuteremshiwa Aayah (Muujiza) kutoka kwa Rabb wake? Sema: Hakika Allaah Ni Muweza wa Kuteremsha Aayah (Muujiza) lakini wengi wao hawajui.
وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا طَائِرٍ يَطِيرُ بِجَنَاحَيْهِ إِلَّا أُمَمٌ أَمْثَالُكُم ۚ مَّا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِن شَيْءٍ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِمْ يُحْشَرُونَ ﴿٣٨﴾
38. Na hakuna kiumbe chochote kinachotembea katika ardhi wala ndege anayeruka kwa mbawa zake mbili, isipokuwa ni nyumati mfano wenu. Hatujaacha wala kusahau chochote katika Kitabu[6]. Kisha watakusanywa kwa Rabb wao.
وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا صُمٌّ وَبُكْمٌ فِي الظُّلُمَاتِ ۗ مَن يَشَإِ اللَّـهُ يُضْلِلْـهُ وَمَن يَشَأْ يَجْعَلْهُ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٣٩﴾
39. Na wale waliokadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili) Zetu ni viziwi na mabubu waliozama ndani ya viza. Allaah Humpotoa Amtakaye na Humweka Amtakaye juu ya njia iliyonyooka.
قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّـهِ أَوْ أَتَتْكُمُ السَّاعَةُ أَغَيْرَ اللَّـهِ تَدْعُونَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤٠﴾
40. Sema: Je, mnaonaje ikikufikieni adhabu ya Allaah au ikakufikieni Saa (Qiyaamah), je, mtamwomba ghairi ya Allaah? (Jibuni) mkiwa ni wakweli!
بَلْ إِيَّاهُ تَدْعُونَ فَيَكْشِفُ مَا تَدْعُونَ إِلَيْهِ إِن شَاءَ وَتَنسَوْنَ مَا تُشْرِكُونَ ﴿٤١﴾
41. Bali Yeye Pekee Ndiye mtayemwomba, kisha Akitaka Ataondoa yale (ya dhiki) mliyomwomba na mtasahau mnayoyashirikisha (pamoja Naye).
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَأَخَذْنَاهُم بِالْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَتَضَرَّعُونَ ﴿٤٢﴾
42. Na kwa yakini Tulipeleka (Rusuli) kwa nyumati nyingi kabla yako, Tukawatia katika dhiki za ufukara na madhara ya magonjwa na misiba ili wapate kunyenyekea.
فَلَوْلَا إِذْ جَاءَهُم بَأْسُنَا تَضَرَّعُوا وَلَـٰكِن قَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٤٣﴾
43. Basi kwa nini ilipowafikia adhabu Yetu wasinyenyekee? Lakini nyoyo zao zimekuwa ngumu na shaytwaan akawapambia yale waliyokuwa wakiyatenda.
فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ أَبْوَابَ كُلِّ شَيْءٍ حَتَّىٰ إِذَا فَرِحُوا بِمَا أُوتُوا أَخَذْنَاهُم بَغْتَةً فَإِذَا هُم مُّبْلِسُونَ ﴿٤٤﴾
44. Waliposahau yale waliyokumbushwa, Tuliwafungulia milango ya (neema za) kila kitu, mpaka walipofurahia kwa yale waliyopewa, Tukawachukua ghafla (kuwaadhibu), basi tahamaki wakawa wenye kukata tamaa.
فَقُطِعَ دَابِرُ الْقَوْمِ الَّذِينَ ظَلَمُوا ۚ وَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٤٥﴾
45. Basi ikakatwa mizizi ya watu waliodhulumu, na AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah) Rabb wa walimwengu.
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَخَذَ اللَّـهُ سَمْعَكُمْ وَأَبْصَارَكُمْ وَخَتَمَ عَلَىٰ قُلُوبِكُم مَّنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ يَأْتِيكُم بِهِ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ ثُمَّ هُمْ يَصْدِفُونَ ﴿٤٦﴾
46. Sema: Mnaonaje ikiwa Allaah Atakuondoleeni kusikia kwenu (mkawa viziwi) na kuona kwenu (mkawa vipofu) na Akapiga mhuri juu ya nyoyo zenu (mkawa hamufahamu), je, ni mwabudiwa wa haki yupi ghairi ya Allaah Atakuleteeni hayo? Tazama jinsi Tunavyosarifu Aayaat (Hoja, Dalili) namna kwa namna kisha wao wanakengeuka.
قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّـهِ بَغْتَةً أَوْ جَهْرَةً هَلْ يُهْلَكُ إِلَّا الْقَوْمُ الظَّالِمُونَ ﴿٤٧﴾
47. Sema: Mnaonaje ikikufikieni Adhabu ya Allaah ghafla au kwa kuiona inavyokujieni? Je, wataangamizwa isipokuwa watu madhalimu?
وَمَا نُرْسِلُ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ ۖ فَمَنْ آمَنَ وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٤٨﴾
48. Na Hatupeleki Rusuli isipokuwa kuwa wabashiriaji na waonyaji tu. Na yeyote atakayeamini na akatengeneza (imaan yake na vitendo vyake), basi haitokuwa khofu juu yao na wala wao hawatohuzunika.
وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا يَمَسُّهُمُ الْعَذَابُ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿٤٩﴾
49. Na wale waliokadhibisha Aayaat (na Miujiza, Ishara) Zetu, itawagusa adhabu kwa sababu ya ufasiki waliokuwa wanaufanya.
قُل لَّا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّـهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ لَكُمْ إِنِّي مَلَكٌ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ ۚ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ ۚ أَفَلَا تَتَفَكَّرُونَ ﴿٥٠﴾
50. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Sikuambieni kuwa mimi nina hazina ya Allaah, na wala kwamba najua ya ghaibu, na wala sikuambieni kuwa mimi ni Malaika. Sifuati ila yale niliyofunuliwa Wahy. Sema: Je, analingana sawasawa kipofu na mwenye kuona? Basi hamtafakari?
وَأَنذِرْ بِهِ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحْشَرُوا إِلَىٰ رَبِّهِمْ ۙ لَيْسَ لَهُم مِّن دُونِهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿٥١﴾
51. Na waonye kwayo (Qur-aan) wale wanaokhofu ya kwamba watakusanywa kwa Rabb wao, na hali ya kuwa hawana rafiki mlinzi wala mwombezi isipokuwa Yeye ili wapate kumcha Allaah (zaidi).
وَلَا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ مَا عَلَيْكَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَمَا مِنْ حِسَابِكَ عَلَيْهِم مِّن شَيْءٍ فَتَطْرُدَهُمْ فَتَكُونَ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٢﴾
52. Na wala usiwafukuze wale wanaomwomba Rabb wao asubuhi na jioni wanataka Wajihi Wake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, na wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, hata uwafukuze ukaja kuwa miongoni mwa madhalimu.[7]
وَكَذَٰلِكَ فَتَنَّا بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لِّيَقُولُوا أَهَـٰؤُلَاءِ مَنَّ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّن بَيْنِنَا ۗ أَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَعْلَمَ بِالشَّاكِرِينَ ﴿٥٣﴾
53. Na hivyo ndivyo Tulivyowafanyia mtihani baadhi yao kwa baadhi ili waseme: Je, hawa ndio wale Aliowafadhilisha Allaah baina yetu? Je, kwani Allaah Hajui wanaoshukuru?
وَإِذَا جَاءَكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِنَا فَقُلْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ ۖ كَتَبَ رَبُّكُمْ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۖ أَنَّهُ مَنْ عَمِلَ مِنكُمْ سُوءًا بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابَ مِن بَعْدِهِ وَأَصْلَحَ فَأَنَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٥٤﴾
54. Na wanapokujia wale wanaoamini Aayaat (na Ishara) Zetu basi sema: Salaamun ‘alaykum! (Amani iwe juu yenu). Rabb wenu Amejiwajibishia Nafsi Yake[8] Rehma; kwamba yeyote miongoni mwenu atakayetenda ovu kwa ujahili, kisha akatubia baada yake na akarekebisha (matendo yake), basi hakika Yeye Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ وَلِتَسْتَبِينَ سَبِيلُ الْمُجْرِمِينَ ﴿٥٥﴾
55. Na hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat (na Ishara) na ili idhihirike njia ya wahalifu.
قُلْ إِنِّي نُهِيتُ أَنْ أَعْبُدَ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ ۚ قُل لَّا أَتَّبِعُ أَهْوَاءَكُمْ ۙ قَدْ ضَلَلْتُ إِذًا وَمَا أَنَا مِنَ الْمُهْتَدِينَ ﴿٥٦﴾
56. Sema: Hakika mimi nimekatazwa kuabudu wale mnaowaomba badala ya Allaah. Sema: Sifuati hawaa zenu (kwani nikifuata,) kwa yakini nitakuwa nimepotoka, na hapo nami sitokuwa miongoni mwa waliohidika.
قُلْ إِنِّي عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَكَذَّبْتُم بِهِ ۚ مَا عِندِي مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ ۚ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ ۖ يَقُصُّ الْحَقَّ ۖ وَهُوَ خَيْرُ الْفَاصِلِينَ ﴿٥٧﴾
57. Sema: Hakika mimi niko juu ya hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu nanyi mumeikadhibisha. Sina yale mnayoyahimiza. Hakuna hukumu isipokuwa ya Allaah Pekee. Anasimulia ya haki, Naye Ni Mbora wa Kuhukumu kuliko wote wenye kuhukumu.
قُل لَّوْ أَنَّ عِندِي مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ لَقُضِيَ الْأَمْرُ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِالظَّالِمِينَ ﴿٥٨﴾
58. Sema: Lau ningelikuwa ninayo yale mnayoyaharakiza, basi bila shaka lingehukumiwa jambo baina yangu na baina yenu. Na Allaah Anawajua zaidi madhalimu.
وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٥٩﴾
59. Na Kwake (Allaah) zipo funguo za ghaibu, hakuna azijuaye ila Yeye tu.[9] Na Anajua yale yote yaliyomo barani na baharini. Na halianguki jani lolote ila Hulijua, wala punje katika viza vya ardhi, wala kinyevu na kikavu isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha wazi.[10]
وَهُوَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُم بِاللَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُم بِالنَّهَارِ ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَىٰ أَجَلٌ مُّسَمًّى ۖ ثُمَّ إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ ثُمَّ يُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٦٠﴾
60. Naye Ndiye Anayekufisheni usiku (mnapolala)[11] na Anajua yale yote mnayoyafanya mchana, kisha Anakufufueni humo ili utimizwe muda maalumu uliokadariwa. Kisha Kwake Pekee ni marejeo yenu, kisha Atakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda.
وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۖ وَيُرْسِلُ عَلَيْكُمْ حَفَظَةً حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ تَوَفَّتْهُ رُسُلُنَا وَهُمْ لَا يُفَرِّطُونَ ﴿٦١﴾
61. Naye Ndiye Aliyedhibiti vyote chini ya Mamlaka Yake, Aliye juu ya Waja Wake. Na Anakutumieni Malaika wachungaji wadhibiti, hata yanapomfikia mmoja wenu mauti, Wajumbe Wetu humfisha, nao hawafanyi taksiri.
ثُمَّ رُدُّوا إِلَى اللَّـهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ ۚ أَلَا لَهُ الْحُكْمُ وَهُوَ أَسْرَعُ الْحَاسِبِينَ ﴿٦٢﴾
62. Kisha watarudishwa (wote waliofishwa) kwa Allaah Rabb wao wa haki. Tanabahi! Hukumu ni Yake Pekee! Naye Ni Mwepesi zaidi wa Kuhisabu kuliko wote wanaohisabu.
قُلْ مَن يُنَجِّيكُم مِّن ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ تَدْعُونَهُ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً لَّئِنْ أَنجَانَا مِنْ هَـٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ ﴿٦٣﴾
63. Sema: Nani Anakuokoeni katika viza vya bara na bahari mnapomuomba kwa kunyenyekea na kwa siri (mkisema): Akituokoa kutokana na (janga) hili, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wenye kushukuru.
قُلِ اللَّـهُ يُنَجِّيكُم مِّنْهَا وَمِن كُلِّ كَرْبٍ ثُمَّ أَنتُمْ تُشْرِكُونَ ﴿٦٤﴾
64. Sema: Allaah Anakuokoeni kutokana na hayo na katika kila janga kisha nyinyi mnamshirikisha.
قُلْ هُوَ الْقَادِرُ عَلَىٰ أَن يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عَذَابًا مِّن فَوْقِكُمْ أَوْ مِن تَحْتِ أَرْجُلِكُمْ أَوْ يَلْبِسَكُمْ شِيَعًا وَيُذِيقَ بَعْضَكُم بَأْسَ بَعْضٍ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ لَعَلَّهُمْ يَفْقَهُونَ ﴿٦٥﴾
65. Sema: Yeye ni Muweza wa kukuleteeni adhabu kutoka juu yenu, au kutoka chini ya miguu yenu, au Akutatanisheni mfarikiane kuwa makundi na Akuonjesheni baadhi yenu (vurugu la) nguvu za wengineo. Tazama jinsi Tunavyosarifu Aayaat (Ishara, Hoja, Dalili) namna kwa namna wapate kufahamu.
وَكَذَّبَ بِهِ قَوْمُكَ وَهُوَ الْحَقُّ ۚ قُل لَّسْتُ عَلَيْكُم بِوَكِيلٍ ﴿٦٦﴾
66. Na watu wako wameikadhibisha (Qur-aan) nayo ni haki. Sema: Mimi si mdhamini wenu.
لِّكُلِّ نَبَإٍ مُّسْتَقَرٌّ ۚ وَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٦٧﴾
67. Kila khabari ina wakati maalumu, na mtakuja kujua.
وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٦٨﴾
68. Na unapowaona wale wanaoshughulika kuzisakama Aayaat Zetu, jitenge nao mpaka watumbukie kwenye mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka, usikae pamoja na watu madhalimu.
وَمَا عَلَى الَّذِينَ يَتَّقُونَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَلَـٰكِن ذِكْرَىٰ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿٦٩﴾
69. Wenye taqwa, hawana jukumu la hisabu yao (kwa Allaah), lakini jukumu ni kuwakumbusha ili wapate kujirudi.
وَذَرِ الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَهُمْ لَعِبًا وَلَهْوًا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۚ وَذَكِّرْ بِهِ أَن تُبْسَلَ نَفْسٌ بِمَا كَسَبَتْ لَيْسَ لَهَا مِن دُونِ اللَّـهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ وَإِن تَعْدِلْ كُلَّ عَدْلٍ لَّا يُؤْخَذْ مِنْهَا ۗ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ أُبْسِلُوا بِمَا كَسَبُوا ۖ لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ ﴿٧٠﴾
70. Na waachilie mbali wale walioifanya Dini yao mchezo na pumbao, na ukawaghuri uhai wa dunia. Basi wakumbushe kwayo (Qur-aan) isije kila nafsi ikaangamizwa kwa yale iliyoyachuma. Haina pasi na Allaah rafiki mlinzi wala mwombezi. Na hata ikitoa fidia ya kila aina haitopokelewa. Hao ndio wale walioangamizwa kwa sababu ya yale waliyoyachuma. Watapata kinywaji cha maji ya kutokota na adhabu iumizayo kwa sababu ya ukafiri wao.
قُلْ أَنَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُنَا وَلَا يَضُرُّنَا وَنُرَدُّ عَلَىٰ أَعْقَابِنَا بَعْدَ إِذْ هَدَانَا اللَّـهُ كَالَّذِي اسْتَهْوَتْهُ الشَّيَاطِينُ فِي الْأَرْضِ حَيْرَانَ لَهُ أَصْحَابٌ يَدْعُونَهُ إِلَى الْهُدَى ائْتِنَا ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّـهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۖ وَأُمِرْنَا لِنُسْلِمَ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٧١﴾
71. Sema: Je, badala ya Allaah tuviombe visivyoweza kutunufaisha wala kutudhuru tuje kurudishwa nyuma tulikotoka baada ya Allaah kutuhidi? Tuwe kama yule ambaye ameshawishiwa na mashaytwaan akikanganyika katika ardhi, anao marafiki wanamwita katika mwongozo: Njoo kwetu! Sema: Hakika Hidaya ya Allaah ndio Hidaya na tumeamrishwa tujisalimishe kwa Rabb wa walimwengu.
وَأَنْ أَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَاتَّقُوهُ ۚ وَهُوَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٧٢﴾
72. Na kuwa simamisheni Swalaah na mcheni Yeye, Naye Ndiye Ambaye Kwake mtakusanywa.
وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۖ وَيَوْمَ يَقُولُ كُن فَيَكُونُ ۚ قَوْلُهُ الْحَقُّ ۚ وَلَهُ الْمُلْكُ يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ ۚ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿٧٣﴾
73. Naye Ndiye Ambaye Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Na Siku Atakaposema: Kun! Basi (jambo) huwa! Kauli Yake ni haki. Ni Wake Yeye tu ufalme Siku litakapopulizwa baragumu. Mjuzi wa ghaibu na dhahiri. Naye Ni Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ آزَرَ أَتَتَّخِذُ أَصْنَامًا آلِهَةً ۖ إِنِّي أَرَاكَ وَقَوْمَكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٧٤﴾
74. Na pindi Ibraahiym alipomwambia baba yake Aazar: Je, unafanya masanamu kuwa ni waabudiwa? Hakika mimi nakuona wewe pamoja na watu wako katika upotofu bayana.
وَكَذَٰلِكَ نُرِي إِبْرَاهِيمَ مَلَكُوتَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلِيَكُونَ مِنَ الْمُوقِنِينَ ﴿٧٥﴾
75. Na hivyo ndivyo Tunavyomwonyesha Ibraahiym ufalme mkubwa wa mbingu na ardhi na ili awe miongoni mwa wenye yakini.
فَلَمَّا جَنَّ عَلَيْهِ اللَّيْلُ رَأَىٰ كَوْكَبًا ۖ قَالَ هَـٰذَا رَبِّي ۖ فَلَمَّا أَفَلَ قَالَ لَا أُحِبُّ الْآفِلِينَ ﴿٧٦﴾
76. Na ulipomwingilia usiku akaona nyota. Akasema: Huyu ni Rabb wangu. Ilipotoweka akasema: Hakika mimi sipendi wanaotoweka.
فَلَمَّا رَأَى الْقَمَرَ بَازِغًا قَالَ هَـٰذَا رَبِّي ۖ فَلَمَّا أَفَلَ قَالَ لَئِن لَّمْ يَهْدِنِي رَبِّي لَأَكُونَنَّ مِنَ الْقَوْمِ الضَّالِّينَ ﴿٧٧﴾
77. Kisha alipoona mwezi umechomoza akasema: Huyu ni Rabb wangu. Ulipotoweka akasema: Asiponiongoza Rabb wangu bila shaka nitakuwa miongoni mwa watu waliopotea.
فَلَمَّا رَأَى الشَّمْسَ بَازِغَةً قَالَ هَـٰذَا رَبِّي هَـٰذَا أَكْبَرُ ۖ فَلَمَّا أَفَلَتْ قَالَ يَا قَوْمِ إِنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ ﴿٧٨﴾
78. Kisha alipoliona jua limechomoza akasema: Huyu ni Rabb wangu, huyu ni mkubwa zaidi. Lilipotoweka akasema: Enyi watu wangu! Hakika mimi simo katika yale mnayoyashirikisha (na Allaah).
إِنِّي وَجَّهْتُ وَجْهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ حَنِيفًا ۖ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٧٩﴾
79. Hakika mimi nimeelekeza uso wangu kwa Ambaye Ameanzisha mbingu na ardhi, nikijitenga na itikadi potofu na kuelemea haki, nami si katika washirikina.
وَحَاجَّهُ قَوْمُهُ ۚ قَالَ أَتُحَاجُّونِّي فِي اللَّـهِ وَقَدْ هَدَانِ ۚ وَلَا أَخَافُ مَا تُشْرِكُونَ بِهِ إِلَّا أَن يَشَاءَ رَبِّي شَيْئًا ۗ وَسِعَ رَبِّي كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا ۗ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ ﴿٨٠﴾
80. Na watu wake wakamhoji. Akasema: Je, mnahojiana nami kuhusu Allaah na hali Amenihidi? Na wala sikhofu hayo mnayomshirikisha Naye (kwani sitodhurika) isipokuwa Rabb wangu Akitaka jambo. Rabb wangu Amezunguka kila kitu (kwa Ujuzi). Je, basi hamkumbuki?
وَكَيْفَ أَخَافُ مَا أَشْرَكْتُمْ وَلَا تَخَافُونَ أَنَّكُمْ أَشْرَكْتُم بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَانًا ۚ فَأَيُّ الْفَرِيقَيْنِ أَحَقُّ بِالْأَمْنِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٨١﴾
81. Na vipi nikhofu yale mnayoyashirikisha, nanyi hamkhofu kwamba mnamshirikisha Allaah na ambayo Hakuyateremshia kwenu hoja. Je, basi kundi gani kati ya mawili linastahiki zaidi kuwa katika amani kama nyinyi mnajua?
الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٨٢﴾
82. Wale walioamini na hawakuchanganya imaan zao na dhulma,[12] hao ndio watakaopata amani nao ndio waliohidika.
وَتِلْكَ حُجَّتُنَا آتَيْنَاهَا إِبْرَاهِيمَ عَلَىٰ قَوْمِهِ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاءُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿٨٣﴾
83. Na hiyo ndio hoja Yetu Tuliyompa Ibraahiym juu ya watu wake. Tunampandisha cheo Tumtakaye. Hakika Rabb wako Ni Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.[13]
وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ كُلًّا هَدَيْنَا ۚ وَنُوحًا هَدَيْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِ دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَارُونَ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٤﴾
84. Na Tukamtunukia Is-haaq na Ya’quwb. Wote Tukawahidi. Na Nuwh Tulimhidi kabla. Na katika dhuria wake (Tuliwahidi pia) Daawuwd, na Sulaymaan, na Ayyuwb, na Yuwsuf, na Muwsaa, na Haaruwn. Na hivyo ndivyo Tulipavyo wafanyao ihsaan.
وَزَكَرِيَّا وَيَحْيَىٰ وَعِيسَىٰ وَإِلْيَاسَ ۖ كُلٌّ مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٨٥﴾
85. Na Zakariyyaa, na Yahyaa, na ‘Iysaa, na Ilyaas. Wote ni miongoni mwa Swalihina.
وَإِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطًا ۚ وَكُلًّا فَضَّلْنَا عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٨٦﴾
86. Na Ismaa’iyl, na Al-Yasa’a na Yuwnus, na Luutw. Na wote Tuliwafadhilisha juu ya walimwengu.
وَمِنْ آبَائِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ وَإِخْوَانِهِمْ ۖ وَاجْتَبَيْنَاهُمْ وَهَدَيْنَاهُمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٨٧﴾
87. Na katika baba zao, na dhuriya wao, na ndugu zao. Na Tukawateua na Tukawaongoza kuelekea njia iliyonyooka.
ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚ وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٨﴾
88. Hiyo ndiyo Hidaya ya Allaah, Humwongoza kwayo Amtakaye kati ya Waja Wake. Na kama wangemshirikisha basi yangeporomoka yale waliyokuwa wakiyatenda.[14]
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ۚ فَإِن يَكْفُرْ بِهَا هَـٰؤُلَاءِ فَقَدْ وَكَّلْنَا بِهَا قَوْمًا لَّيْسُوا بِهَا بِكَافِرِينَ ﴿٨٩﴾
89. Hao ndio Tuliowapa Kitabu na Hikmah na Unabii. Wakiyakanusha hawa (makafiri), basi kwa yakini Tumekwishayawakilisha kwa watu wasioyakanusha.
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ هَدَى اللَّـهُ ۖ فَبِهُدَاهُمُ اقْتَدِهْ ۗ قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا ۖ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْعَالَمِينَ ﴿٩٠﴾
90. Hao ndio ambao Allaah Amewahidi. Basi fuata kama kigezo uongofu wao. Sema: Sikuombeni ujira kwa hayo. Hayakuwa haya ila ni ukumbusho kwa walimwengu.
وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ إِذْ قَالُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ عَلَىٰ بَشَرٍ مِّن شَيْءٍ ۗ قُلْ مَنْ أَنزَلَ الْكِتَابَ الَّذِي جَاءَ بِهِ مُوسَىٰ نُورًا وَهُدًى لِّلنَّاسِ ۖ تَجْعَلُونَهُ قَرَاطِيسَ تُبْدُونَهَا وَتُخْفُونَ كَثِيرًا ۖ وَعُلِّمْتُم مَّا لَمْ تَعْلَمُوا أَنتُمْ وَلَا آبَاؤُكُمْ ۖ قُلِ اللَّـهُ ۖ ثُمَّ ذَرْهُمْ فِي خَوْضِهِمْ يَلْعَبُونَ ﴿٩١﴾
91. Na hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria, pale waliposema: Allaah Hakuteremsha chochote kwa mtu. Sema: Nani aliyeteremsha Kitabu ambacho amekuja nacho Muwsaa, (chenye) nuru na mwongozo kwa watu? Mnakifanya kurasa kurasa mkizifichua na mkificha mengi. Na mkafunzwa yale mliyokuwa hamuyajui nyinyi na baba zenu. Sema: Allaah (Ameiteremsha), kisha waachilie mbali katika shughuliko la porojo lao wakicheza.
وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ مُّصَدِّقُ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَلِتُنذِرَ أُمَّ الْقُرَىٰ وَمَنْ حَوْلَهَا ۚ وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۖ وَهُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ ﴿٩٢﴾
92. Na hiki ni Kitabu (Qur-aan) Tumekiteremsha chenye baraka kinachosadikisha yale yaliyokitangulia, na ili uonye (kwacho) Ummul-Quraa[15] (Mama wa miji [Makkah]), na wale ambao wameuzunguka. Na wale wanaoamini Aakhirah wanakiamini. Nao wanahifadhi Swalaah zao.
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ قَالَ أُوحِيَ إِلَيَّ وَلَمْ يُوحَ إِلَيْهِ شَيْءٌ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثْلَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ ۗ وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الظَّالِمُونَ فِي غَمَرَاتِ الْمَوْتِ وَالْمَلَائِكَةُ بَاسِطُو أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوا أَنفُسَكُمُ ۖ الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ وَكُنتُمْ عَنْ آيَاتِهِ تَسْتَكْبِرُونَ ﴿٩٣﴾
93. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemtungia uongo Allaah au akasema: Nimefunuliwa Wahy na hali hakufunuliwa Wahy wowote. Na yule asemaye: Nitateremsha mfano wa yale Aliyoyateremsha Allaah.[16] Na lau ungeliona madhalimu pale wakiwa katika mateso makali ya mauti (ungeona jambo la kutisha mno), na Malaika wamenyosha mikono yao (wakiwaambia): Toeni nafsi zenu! Leo mnalipwa adhabu ya kudhalilisha kwa yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Allaah pasi na haki, na mlikuwa mkitakabari msizifuate Aayaat Zake.
وَلَقَدْ جِئْتُمُونَا فُرَادَىٰ كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَتَرَكْتُم مَّا خَوَّلْنَاكُمْ وَرَاءَ ظُهُورِكُمْ ۖ وَمَا نَرَىٰ مَعَكُمْ شُفَعَاءَكُمُ الَّذِينَ زَعَمْتُمْ أَنَّهُمْ فِيكُمْ شُرَكَاءُ ۚ لَقَد تَّقَطَّعَ بَيْنَكُمْ وَضَلَّ عَنكُم مَّا كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٩٤﴾
94. Na kwa yakini mmetujia mmoja mmoja kama Tulivyokuumbeni mara ya kwanza[17], na mmeyaacha nyuma yenu yote Tuliyokuruzukuni. Na Hatuwaoni pamoja nanyi waombezi wenu ambao mlidai kwamba wao ni washirika wenu. Kwa yakini yamekatika (mahusiano) baina yenu na yamekupoteeni mliyokuwa mkidai.
إِنَّ اللَّـهَ فَالِقُ الْحَبِّ وَالنَّوَىٰ ۖ يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَمُخْرِجُ الْمَيِّتِ مِنَ الْحَيِّ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٩٥﴾
95. Hakika Allaah Ni Mpasuaji wa mbegu na kokwa (zikawa miche). Anatoa kilicho hai kutokana na kilicho mfu, na Mtoaji wa kilicho mfu kutokana na kilicho hai.[18] Huyo Ndiye Allaah kwenu. Basi vipi mnaghilibiwa?
فَالِقُ الْإِصْبَاحِ وَجَعَلَ اللَّيْلَ سَكَنًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ حُسْبَانًا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ﴿٩٦﴾
96. Mpasuaji wa mapambazuko ya asubuhi, na Akajaalia usiku kuwa ni mapumziko, na jua na mwezi kwenda kwa hisabu. Hiyo ndio Takdiri ya Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.[19]
وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ النُّجُومَ لِتَهْتَدُوا بِهَا فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٩٧﴾
97. Na Yeye Ndiye Aliyekufanyieni nyota ili zikusaidieni kujua mwendako katika viza vya bara na bahari.[20] Kwa yakini Tumezifasili waziwazi Aayaat (Ishara na vielelezo) kwa watu wanaojua.
وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ فَمُسْتَقَرٌّ وَمُسْتَوْدَعٌ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَفْقَهُونَ ﴿٩٨﴾
98. Na Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja, basi (pako) mahali pa kustakiri na pa kuhifadhiwa.[21] Kwa yakini Tumezifasili waziwazi Aayaat (Ishara, Hoja, Dalili) kwa watu wanaofahamu.
وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ نَبَاتَ كُلِّ شَيْءٍ فَأَخْرَجْنَا مِنْهُ خَضِرًا نُّخْرِجُ مِنْهُ حَبًّا مُّتَرَاكِبًا وَمِنَ النَّخْلِ مِن طَلْعِهَا قِنْوَانٌ دَانِيَةٌ وَجَنَّاتٍ مِّنْ أَعْنَابٍ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُشْتَبِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ ۗ انظُرُوا إِلَىٰ ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَيَنْعِهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكُمْ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٩٩﴾
99. Na Yeye Ndiye Ambaye Ameteremsha kutoka mbinguni maji, Tukatoa kwayo mimea ya kila kitu, na Tukatoa kutoka humo mimea ya kijani, Tunatoa kutoka humo punje zinazopandana. Na katika mitende, yanatoka katika makole yake mashada yenye kuning’inia chini kwa chini, na mabustani ya mizabibu na zaytuni, na makomamanga, yanayofanana na yasiyofanana. Tazameni matunda yake yanapozaa na kuiva kwake. Hakika katika hayo mna Aayaat (Ishara, Mazingatio) kwenu kwa watu wanaoamini.
وَجَعَلُوا لِلَّـهِ شُرَكَاءَ الْجِنَّ وَخَلَقَهُمْ ۖ وَخَرَقُوا لَهُ بَنِينَ وَبَنَاتٍ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٠٠﴾
100. Na wakamfanyia Allaah majini kuwa ni washirika Wake ilhali Amewaumba. Na wakampachikia uongo bila ya ujuzi wowote kuwa Ana wana wa kiume na wa kike.[22] Utakasifu ni Wake na Ametukuka kwa ‘Uluwa kutokana na ambayo wanavumisha.
بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ وَلَدٌ وَلَمْ تَكُن لَّهُ صَاحِبَةٌ ۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٠١﴾
101. Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Inamkinikaje kuwa Yeye Ana mwana ilhali Hana mke! Naye Ameumba kila kitu, Naye Ni Mjuzi wa kila kitu.
ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ ﴿١٠٢﴾
102. Huyo kwenu Ndiye Allaah, Rabb wenu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye Muumbaji wa kila kitu, basi mwabuduni Yeye Pekee. Naye Ni Mtegemewa wa kila kitu.
لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٠٣﴾
103. Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote,[23] Naye Ni Mwenye Kudabiri mambo kwa Ulatifu, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
قَدْ جَاءَكُم بَصَائِرُ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَنْ أَبْصَرَ فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ عَمِيَ فَعَلَيْهَا ۚ وَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِحَفِيظٍ ﴿١٠٤﴾
104. Kwa yakini zimekujieni hoja, ishara na dalili wazi kutoka kwa Rabb wenu. Atakayeona na kuzitambua, basi ni kwa faida yake mwenyewe, na atakayepofuka asizione basi hasara itamrudia mwenyewe, (sema) nami si msimamizi.
وَكَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ وَلِيَقُولُوا دَرَسْتَ وَلِنُبَيِّنَهُ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿١٠٥﴾
105. Na hivyo ndivyo Tunavyosarifu namna kwa namna Aayaat ili (makafiri) waseme: Umedurusu (kutoka kwa Watu wa Kitabu), na ili pia Tuibainishe kwa watu wenye kujua.
اتَّبِعْ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٠٦﴾
106. Fuata (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uliyofunuliwa Wahy toka kwa Rabb wako. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, na jitenge na washirikina.
وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا أَشْرَكُوا ۗ وَمَا جَعَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ۖ وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ ﴿١٠٧﴾
107. Na lau Allaah Angetaka wasingelifanya shirki. Na Hatukukufanya wewe msimamizi wa mambo yao na wala wewe si mdhamini wao.
وَلَا تَسُبُّوا الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ فَيَسُبُّوا اللَّـهَ عَدْوًا بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ كَذَٰلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِم مَّرْجِعُهُمْ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٠٨﴾
108. Na wala msiwatukane wale wanaowaomba asiyekuwa Allaah, wasije nao kumtukana Allaah kwa uadui bila ya ujuzi.[24] Hivyo ndivyo Tumewapambia kila ummah amali zao, kisha kwa Rabb wao Pekee yatakuwa marejeo yao, Atawajulisha yale waliyokuwa wakiyatenda.
وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ لَئِن جَاءَتْهُمْ آيَةٌ لَّيُؤْمِنُنَّ بِهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا الْآيَاتُ عِندَ اللَّـهِ ۖ وَمَا يُشْعِرُكُمْ أَنَّهَا إِذَا جَاءَتْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠٩﴾
109. Na wakaapa kwa Allaah, viapo vyao thabiti vya nguvu, kwamba ikiwafikia Aayah (Muujiza) bila shaka wataiamini. Sema: Hakika Aayaat (Miujiza, Ishara) ziko kwa Allaah. Na kitu gani kitakutambulisheni kwamba zitakapokuja hawatoamini?
وَنُقَلِّبُ أَفْئِدَتَهُمْ وَأَبْصَارَهُمْ كَمَا لَمْ يُؤْمِنُوا بِهِ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَنَذَرُهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١١٠﴾
110. Na Tunazigeuza nyoyo zao na macho yao kama wasivyoiamini mara ya kwanza. Na Tunawaacha katika upindukaji mipaka ya kuasi kwao, wanatangatanga kwa upofu.
وَلَوْ أَنَّنَا نَزَّلْنَا إِلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ الْمَوْتَىٰ وَحَشَرْنَا عَلَيْهِمْ كُلَّ شَيْءٍ قُبُلًا مَّا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ يَجْهَلُونَ ﴿١١١﴾
111. Na lau kama Sisi Tungeliwateremshia Malaika, na wao wakasemeshwa na wafu, na Tukawakusanyia kila kitu mbele yao, basi bado wasingeliamini ila Allaah Atake, lakini wengi wamo katika ujahili.
وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا شَيَاطِينَ الْإِنسِ وَالْجِنِّ يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا ۚ وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ ﴿١١٢﴾
112. Na hivyo ndivyo Tulivyojaalia kwa kila Nabiy maadui mashaytwaan wa kibinaadam na kijini, wanadokezana wenyewe kwa wenyewe maneno ya kupambapamba na ya ghururi. Na lau Angetaka Rabb wako wasingeliyafanya hayo. Basi waachilie mbali na wanayoyatunga (ya uongo).
وَلِتَصْغَىٰ إِلَيْهِ أَفْئِدَةُ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَلِيَرْضَوْهُ وَلِيَقْتَرِفُوا مَا هُم مُّقْتَرِفُونَ ﴿١١٣﴾
113. Na ili zielemee katika (udanganyifu) nyoyo za wale wasioamini Aakhirah, na ili waridhike nayo, na ili wachume (madhambi) wanayoyachuma.
أَفَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْتَغِي حَكَمًا وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ إِلَيْكُمُ الْكِتَابَ مُفَصَّلًا ۚ وَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْلَمُونَ أَنَّهُ مُنَزَّلٌ مِّن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ ﴿١١٤﴾
114. (Sema): Je, nitafute hakimu ghairi ya Allaah na hali Yeye Ndiye Aliyekuteremshieni Kitabu kilichofasiliwa waziwazi? Na wale Tuliowapa Kitabu (kabla) wanajua kwamba kimeteremshwa kutoka kwa Rabb wako kwa haki. Basi usijekuwa miongoni mwa wanaotia shaka.
وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقًا وَعَدْلًا ۚ لَّا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١١٥﴾
115. Na limetimia Neno la Rabb wako kiukweli na kiadilifu. Hakuna awezaye kuyabadilisha Maneno Yake. Naye Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ ﴿١١٦﴾
116. Na kama ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, watakupoteza Njia ya Allaah. Hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawakuwa ila wenye kubuni uongo.
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ مَن يَضِلُّ عَن سَبِيلِهِ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿١١٧﴾
117. Hakika Rabb wako Anajua zaidi mwenye kupotea Njia Yake. Naye Anajua zaidi wenye kuhidika.
فَكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ إِن كُنتُم بِآيَاتِهِ مُؤْمِنِينَ ﴿١١٨﴾
118. Basi kuleni katika ambavyo limetajwa Jina la Allaah (wakati wa kuchinjwa) mkiwa nyinyi ni wenye kuziamini Aayaat (na Hukmu) Zake.
وَمَا لَكُمْ أَلَّا تَأْكُلُوا مِمَّا ذُكِرَ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا لَّيُضِلُّونَ بِأَهْوَائِهِم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِالْمُعْتَدِينَ ﴿١١٩﴾
119. Na mna nini hata msile katika ambavyo limetajwa Jina la Allaah na ilhali Ameshafasilisha waziwazi kwenu yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura navyo. Na hakika wengi wanapotoa (wengine) kwa hawaa zao bila ya ilimu. Hakika Rabb wako Yeye Anajua zaidi wenye kutaadi.
وَذَرُوا ظَاهِرَ الْإِثْمِ وَبَاطِنَهُ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَكْسِبُونَ الْإِثْمَ سَيُجْزَوْنَ بِمَا كَانُوا يَقْتَرِفُونَ ﴿١٢٠﴾
120. Na acheni dhambi za dhahiri na zilizofichika. Hakika wale wanaochuma dhambi watalipwa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.
وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُ لَفِسْقٌ ۗ وَإِنَّ الشَّيَاطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰ أَوْلِيَائِهِمْ لِيُجَادِلُوكُمْ ۖ وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ ﴿١٢١﴾
121. Na wala msile katika ambavyo halikutajwa Jina la Allaah (wakati wa kuchinjwa), kwani huo ni ukiukaji wa utiifu kwa Allaah. Na hakika mashaytwaan wanawashawishi marafiki wao wandani wabishane nanyi. Na kama mtawatii basi hakika mtakuwa washirikina.[25]
أَوَمَن كَانَ مَيْتًا فَأَحْيَيْنَاهُ وَجَعَلْنَا لَهُ نُورًا يَمْشِي بِهِ فِي النَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُ فِي الظُّلُمَاتِ لَيْسَ بِخَارِجٍ مِّنْهَا ۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْكَافِرِينَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٢٢﴾
122. Je, aliyekuwa maiti kisha Tukamhuisha na Tukamjaalia nuru anatembea nayo kati ya watu, ni sawa na yule ambaye yumo katika viza hawezi kutoka humo?[26] Hivyo ndivyo walivyopambiwa makafiri yale waliyokuwa wakiyatenda.
وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا فِي كُلِّ قَرْيَةٍ أَكَابِرَ مُجْرِمِيهَا لِيَمْكُرُوا فِيهَا ۖ وَمَا يَمْكُرُونَ إِلَّا بِأَنفُسِهِمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿١٢٣﴾
123. Na hivyo ndivyo Tulivyojaalia katika kila mji wahalifu wake wakuu ili wafanyie makri (njama) humo. Na hawafanyii makri ila nafsi zao, na wala hawahisi.
وَإِذَا جَاءَتْهُمْ آيَةٌ قَالُوا لَن نُّؤْمِنَ حَتَّىٰ نُؤْتَىٰ مِثْلَ مَا أُوتِيَ رُسُلُ اللَّـهِ ۘ اللَّـهُ أَعْلَمُ حَيْثُ يَجْعَلُ رِسَالَتَهُ ۗ سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِندَ اللَّـهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ ﴿١٢٤﴾
124. Na inapowajia Aayah (Muujiza, Ushahidi bayana) husema: Hatutoamini mpaka tupewe mfano wa yale waliopewa Rusuli wa Allaah. Allaah Anajua zaidi wapi Aweke Ujumbe Wake. Utawasibu wale waliohalifu udhalilifu mbele ya Allaah na adhabu kali kwa sababu ya makri (njama) walizokuwa wakifanya.
فَمَن يُرِدِ اللَّـهُ أَن يَهْدِيَهُ يَشْرَحْ صَدْرَهُ لِلْإِسْلَامِ ۖ وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُ يَجْعَلْ صَدْرَهُ ضَيِّقًا حَرَجًا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِي السَّمَاءِ ۚ كَذَٰلِكَ يَجْعَلُ اللَّـهُ الرِّجْسَ عَلَى الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٢٥﴾
125. Basi yule ambaye Allaah Anataka kumhidi, Humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na yule ambaye Anataka kumpotoa, Hufanya kifua chake kiwe na dhiki chenye kubana kama kwamba anapanda kwa tabu mbinguni. Hivyo ndivyo Allaah Anavyojaalia adhabu (au Anavyowasalitishia shaytwaan) kwa wale wasioamini.
وَهَـٰذَا صِرَاطُ رَبِّكَ مُسْتَقِيمًا ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ ﴿١٢٦﴾
126. Na hii ni Njia ya Rabb wako iliyonyooka. Kwa yakini Tumefasili waziwazi Aayaat kwa watu wanaokumbuka.
لَهُمْ دَارُ السَّلَامِ عِندَ رَبِّهِمْ ۖ وَهُوَ وَلِيُّهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٢٧﴾
127. Watapata Daarus-Salaam (nyumba ya amani Jannah) kwa Rabb wao. Naye Ndiye Rafiki wao Mlinzi kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyatenda.
وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ قَدِ اسْتَكْثَرْتُم مِّنَ الْإِنسِ ۖ وَقَالَ أَوْلِيَاؤُهُم مِّنَ الْإِنسِ رَبَّنَا اسْتَمْتَعَ بَعْضُنَا بِبَعْضٍ وَبَلَغْنَا أَجَلَنَا الَّذِي أَجَّلْتَ لَنَا ۚ قَالَ النَّارُ مَثْوَاكُمْ خَالِدِينَ فِيهَا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿١٢٨﴾
128. Na Siku Atakapowakusanya wote (Allaah Atasema): Enyi hadhara ya majini! Kwa yakini mmewapoteza wanaadamu wengi sana. Na watasema marafiki wao wandani katika wanaadamu: Rabb wetu! Tulinufaishana sisi kwa sisi, na (leo) tumefikia muda wetu ambao Umetupangia. (Allaah) Atasema: Moto ndio makazi yenu, mtadumu humo, isipokuwa Atakavyo Allaah. Hakika Rabb wako Ni Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.
وَكَذَٰلِكَ نُوَلِّي بَعْضَ الظَّالِمِينَ بَعْضًا بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿١٢٩﴾
129. Na hivyo ndivyo Tunavyowafanya madhalimu kuwa marafiki wandani wao kwa wao kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.
يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِي وَيُنذِرُونَكُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا ۚ قَالُوا شَهِدْنَا عَلَىٰ أَنفُسِنَا ۖ وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَشَهِدُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَنَّهُمْ كَانُوا كَافِرِينَ ﴿١٣٠﴾
130. Enyi hadhara ya majini na wanaadamu! Je hawajakufikieni Rusuli miongoni mwenu wanakusimulieni Aayaat Zangu na wanakuonyeni kukutana na Siku yenu hii? Watasema: Tumeshuhudia dhidi ya nafsi zetu. Na uliwaghuri uhai wa dunia, na wameshuhudia dhidi ya nafsi zao kwamba hakika wao walikuwa ni makafiri.
ذَٰلِكَ أَن لَّمْ يَكُن رَّبُّكَ مُهْلِكَ الْقُرَىٰ بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا غَافِلُونَ ﴿١٣١﴾
131. Hivyo ni kwa kuwa Rabb wako Hakuwa Mwenye Kuangamiza mji kwa dhulma hali wenyewe hawajazindushwa.
وَلِكُلٍّ دَرَجَاتٌ مِّمَّا عَمِلُوا ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ ﴿١٣٢﴾
132. Na wote wana daraja mbalimbali kwa yale waliyoyatenda. Na Rabb wako Si Mwenye Kughafilika na yale wanayoyatenda.
وَرَبُّكَ الْغَنِيُّ ذُو الرَّحْمَةِ ۚ إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَسْتَخْلِفْ مِن بَعْدِكُم مَّا يَشَاءُ كَمَا أَنشَأَكُم مِّن ذُرِّيَّةِ قَوْمٍ آخَرِينَ ﴿١٣٣﴾
133. Na Rabb wako Ni Mkwasi Mwenye Rehma. Akitaka Atakuondosheni na Aweke wengine Awatakao badala yenu kama Alivyokuzalisheni nyinyi kutokana na vizazi vya watu wengine.
إِنَّ مَا تُوعَدُونَ لَآتٍ ۖ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ ﴿١٣٤﴾
134. Hakika mnayoahidiwa bila shaka yatakuja tu! Nanyi si wenye kuweza kushinda (kukwepa adhabu).
قُلْ يَا قَوْمِ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن تَكُونُ لَهُ عَاقِبَةُ الدَّارِ ۗ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ ﴿١٣٥﴾
135. Sema: Enyi kaumu yangu! Tendeni kwa namna yenu, nami pia natenda yangu. Mtakuja kujua nani atakayekuwa na hatima njema ya makazi Aakhirah. Hakika madhalimu hawatofaulu.
وَجَعَلُوا لِلَّـهِ مِمَّا ذَرَأَ مِنَ الْحَرْثِ وَالْأَنْعَامِ نَصِيبًا فَقَالُوا هَـٰذَا لِلَّـهِ بِزَعْمِهِمْ وَهَـٰذَا لِشُرَكَائِنَا ۖ فَمَا كَانَ لِشُرَكَائِهِمْ فَلَا يَصِلُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَمَا كَانَ لِلَّـهِ فَهُوَ يَصِلُ إِلَىٰ شُرَكَائِهِمْ ۗ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ ﴿١٣٦﴾
136. Na wamemfanyia Allaah fungu katika mimea na wanyama Aliyoumba. Wakasema: Hili ni la Allaah kwa madai yao, na hili ni kwa ajili ya washirika wetu. Basi yaliyokuwa kwa ajili ya washirika wao hayamfikii Allaah. Na yaliyokuwa kwa ajili ya Allaah hufika kwa washirika wao. Uovu ulioje wanayoyahukumu!
وَكَذَٰلِكَ زَيَّنَ لِكَثِيرٍ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ قَتْلَ أَوْلَادِهِمْ شُرَكَاؤُهُمْ لِيُرْدُوهُمْ وَلِيَلْبِسُوا عَلَيْهِمْ دِينَهُمْ ۖ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ ﴿١٣٧﴾
137. Na hivyo ndivyo washirika (mashaytwaan) wao walivyowapambia washirikina wengi kuua watoto wao ili wawateketeze na wawakorogee dini yao. Na lau Allaah Angetaka, wasingeliyafanya hayo. Basi waachilie mbali na wanayoyatunga (ya uongo).
وَقَالُوا هَـٰذِهِ أَنْعَامٌ وَحَرْثٌ حِجْرٌ لَّا يَطْعَمُهَا إِلَّا مَن نَّشَاءُ بِزَعْمِهِمْ وَأَنْعَامٌ حُرِّمَتْ ظُهُورُهَا وَأَنْعَامٌ لَّا يَذْكُرُونَ اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهَا افْتِرَاءً عَلَيْهِ ۚ سَيَجْزِيهِم بِمَا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿١٣٨﴾
138. Na wakasema kwa madai yao: Wanyama hawa (ngamia) na mazao ni marufuku, hawatowala ila wale tuwatakao, na wanyama (hawa) imeharamishwa migongo yao (kuwapanda). Na wanyama (wengine) hawalitaji Jina la Allaah juu yao (wanapowachinja), wanamtungia uongo (Allaah). Atawalipa kwa yale waliyokuwa wakiyatunga.
وَقَالُوا مَا فِي بُطُونِ هَـٰذِهِ الْأَنْعَامِ خَالِصَةٌ لِّذُكُورِنَا وَمُحَرَّمٌ عَلَىٰ أَزْوَاجِنَا ۖ وَإِن يَكُن مَّيْتَةً فَهُمْ فِيهِ شُرَكَاءُ ۚ سَيَجْزِيهِمْ وَصْفَهُمْ ۚ إِنَّهُ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ﴿١٣٩﴾
139. Na wakasema: Waliomo matumboni mwa wanyama hawa ni makhsusi kwa wanaume wetu na marufuku kwa wake zetu. Lakini wakiwa ni nyamafu (wanapozaliwa), basi wanashirikiana katika hao (na wanawake kula). Hakika Atawalipa uvumishi wao. Hakika Yeye Ni Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.
قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ قَتَلُوا أَوْلَادَهُمْ سَفَهًا بِغَيْرِ عِلْمٍ وَحَرَّمُوا مَا رَزَقَهُمُ اللَّـهُ افْتِرَاءً عَلَى اللَّـهِ ۚ قَدْ ضَلُّوا وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ ﴿١٤٠﴾
140. Kwa yakini wamekhasirika wale waliowaua watoto wao kwa upumbavu bila ya ujuzi na wakaharamisha vile Alivyowaruzuku Allaah kwa kumtungia uongo Allaah. Kwa yakini wamepotea na wala hawakuwa wenye kuhidika.
وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَ جَنَّاتٍ مَّعْرُوشَاتٍ وَغَيْرَ مَعْرُوشَاتٍ وَالنَّخْلَ وَالزَّرْعَ مُخْتَلِفًا أُكُلُهُ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُتَشَابِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ ۚ كُلُوا مِن ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَآتُوا حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ ۖ وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿١٤١﴾
141. Naye (Allaah) Ndiye Aliyezalisha mabustani yanayotambaa na yasiyotambaa. Na mitende na mimea yenye kutofautiana ladha yake, na zaytuni na makomamanga yanayoshabihiana na yasiyoshabihiana. Kuleni katika matunda yake yanapotoa mazao na toeni haki yake (Zakaah) siku ya kuvunwa kwake na wala msifanye israfu. Hakika Yeye Hapendi wafanyao israfu.
وَمِنَ الْأَنْعَامِ حَمُولَةً وَفَرْشًا ۚ كُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿١٤٢﴾
142. Na katika wanyama wa mifugo (Amekuumbieni) wabebao mzigo na wadogodogo. Kuleni katika Alivyokuruzukuni Allaah na wala msifuate hatua za shaytwaan, hakika yeye ni adui bayana kwenu.
ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ ۖ مِّنَ الضَّأْنِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْمَعْزِ اثْنَيْنِ ۗ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الْأُنثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الْأُنثَيَيْنِ ۖ نَبِّئُونِي بِعِلْمٍ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٤٣﴾
143. Jozi nane: (za dume na jike) katika kondoo wawili na katika mbuzi wawili. Sema: Je, Ameharamisha wote madume wawili au majike mawili, au waliomo ndani ya fuko la uzazi mwa majike yote mawili? Nijulisheni kwa ilimu ikiwa nyinyi mnasema kweli.
وَمِنَ الْإِبِلِ اثْنَيْنِ وَمِنَ الْبَقَرِ اثْنَيْنِ ۗ قُلْ آلذَّكَرَيْنِ حَرَّمَ أَمِ الْأُنثَيَيْنِ أَمَّا اشْتَمَلَتْ عَلَيْهِ أَرْحَامُ الْأُنثَيَيْنِ ۖ أَمْ كُنتُمْ شُهَدَاءَ إِذْ وَصَّاكُمُ اللَّـهُ بِهَـٰذَا ۚ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا لِّيُضِلَّ النَّاسَ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿١٤٤﴾
144. Na katika ngamia wawili na katika ng’ombe wawili. Sema: Je, Ameharamisha madume wawili au majike mawili, au waliomo ndani ya fuko la uzazi mwa majike wawili? Au nyinyi mlishuhudia Allaah Alipokuusieni haya? Basi nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia Allaah uongo ili apoteze watu bila ilimu. Hakika Allaah Hawaongozi watu madhalimu.
قُل لَّا أَجِدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلَّا أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ أَوْ فِسْقًا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ ۚ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ رَبَّكَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٤٥﴾
145. Sema: Sipati katika yale niliyofunuliwa Wahyi kwangu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu au damu inayomwagika au nyama ya nguruwe, kwani hivyo ni vichafu, au kilichochinjwa kinyume na utiifu kwa Allaah kwa kutajiwa asiyekuwa Allaah. Lakini atakayefikwa na dharura bila ya kutamani wala kuvuka mipaka, basi hakika Rabb wako Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَعَلَى الَّذِينَ هَادُوا حَرَّمْنَا كُلَّ ذِي ظُفُرٍ ۖ وَمِنَ الْبَقَرِ وَالْغَنَمِ حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ شُحُومَهُمَا إِلَّا مَا حَمَلَتْ ظُهُورُهُمَا أَوِ الْحَوَايَا أَوْ مَا اخْتَلَطَ بِعَظْمٍ ۚ ذَٰلِكَ جَزَيْنَاهُم بِبَغْيِهِمْ ۖ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ ﴿١٤٦﴾
146. Na kwa wale walio Mayahudi Tuliharamisha kila (mnyama) mwenye kucha. Na katika ng’ombe na mbuzi Tuliwaharamishia shahamu zao isipokuwa iliyobeba migongo yao au utumbo wao au iliyochanganyika na mifupa. Hivyo ndivyo Tulivyowalipa kwa baghi[27] (dhulma) yao. Na bila shaka Sisi Ni Wakweli.
فَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل رَّبُّكُمْ ذُو رَحْمَةٍ وَاسِعَةٍ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُهُ عَنِ الْقَوْمِ الْمُجْرِمِينَ ﴿١٤٧﴾
147. Wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) basi sema: Rabb wenu Ni Mwenye Rehma iliyoenea. Na wala haizuiliwi Adhabu Yake kwa watu wahalifu.
سَيَقُولُ الَّذِينَ أَشْرَكُوا لَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا أَشْرَكْنَا وَلَا آبَاؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن شَيْءٍ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ حَتَّىٰ ذَاقُوا بَأْسَنَا ۗ قُلْ هَلْ عِندَكُم مِّنْ عِلْمٍ فَتُخْرِجُوهُ لَنَا ۖ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَخْرُصُونَ ﴿١٤٨﴾
148. Watasema wale walioshirikisha: Lau Allaah Angetaka, tusingelifanya shirki, wala baba zetu pia na wala tusingeliharamisha chochote. Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale wa kabla yao mpaka walipoonja Adhabu Yetu. Sema: Je, mna ilimu yoyote mtutolee? Hamfuati isipokuwa dhana tu, nanyi si lolote ila mnabuni uongo.
قُلْ فَلِلَّـهِ الْحُجَّةُ الْبَالِغَةُ ۖ فَلَوْ شَاءَ لَهَدَاكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿١٤٩﴾
149. Sema: Basi Ni Allaah Pekee Mwenye hoja timilifu. Na Angelitaka Angelikuhidini nyote.
قُلْ هَلُمَّ شُهَدَاءَكُمُ الَّذِينَ يَشْهَدُونَ أَنَّ اللَّـهَ حَرَّمَ هَـٰذَا ۖ فَإِن شَهِدُوا فَلَا تَشْهَدْ مَعَهُمْ ۚ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ وَهُم بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ ﴿١٥٠﴾
150. Sema: Leteni mashahidi wenu wanaoshuhudia kwamba Allaah Ameharamisha (wanyama) hawa. Wakishuhudia, basi usishuhudie pamoja nao. Na wala usifuate hawaa za wale wanaokadhibisha Aayaat Zetu, na wale wasioamini Aakhirah, nao wanawasawazisha wengine na Rabb wao.
قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۖ وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُم مِّنْ إِمْلَاقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ ۖ وَلَا تَقْرَبُوا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ ۖ وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١٥١﴾
151. Sema: Njooni nikusomeeni yale Aliyoyaharamisha Rabb wenu kwenu. Kwamba msimshirikishe na chochote, na muwafanyie ihsaan wazazi wawili, na wala msiwaue watoto wenu kutokana na umasikini. Sisi Tunakuruzukuni pamoja nao. Na wala msikaribie machafu yaliyo dhahiri na yaliyofichika. Na wala msiue nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha (kuiua) isipokuwa kwa haki (ya sharia). Hivyo ndivyo Alivyokuusieni kwayo mpate kutia akilini.
وَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّىٰ يَبْلُغَ أَشُدَّهُ ۖ وَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ ۖ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۖ وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُوا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۖ وَبِعَهْدِ اللَّـهِ أَوْفُوا ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ ﴿١٥٢﴾
152. Na wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia njema ya manufaa mpaka afikie umri wa kupevuka. Na timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu. Hatukalifishi nafsi isipokuwa kadiri ya uwezo wake. Na mnaposema basi fanyeni uadilifu japokuwa ni jamaa wa karibu. Na timizeni Ahadi ya Allaah. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kukumbuka.
وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٥٣﴾
153. Na kwamba hii ndiyo njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na Njia Yake.[28] Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kuwa na taqwa.
ثُمَّ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ تَمَامًا عَلَى الَّذِي أَحْسَنَ وَتَفْصِيلًا لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً لَّعَلَّهُم بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ يُؤْمِنُونَ ﴿١٥٤﴾
154. Tena Tulimpa Muwsaa Kitabu kutimiza (neema) juu ya yule aliyefanya vitendo vyema, na kiwe chenye kuchambua wazi kila kitu, na kiwe mwongozo na rehma ili wapate kuamini kukutana na Rabb wao.
وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ فَاتَّبِعُوهُ وَاتَّقُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٥٥﴾
155. Na hiki ni Kitabu (Qur-aan) Tumekiteremsha kilichobarikiwa, basi kifuateni na muwe na taqwa mpate kurehemewa.
أَن تَقُولُوا إِنَّمَا أُنزِلَ الْكِتَابُ عَلَىٰ طَائِفَتَيْنِ مِن قَبْلِنَا وَإِن كُنَّا عَن دِرَاسَتِهِمْ لَغَافِلِينَ ﴿١٥٦﴾
156. Msije kusema: Hakika Kitabu kimeteremshwa juu ya makundi mawili kabla yetu, lakini tulikuwa hatuna habari yoyote kuhusu waliyokuwa wakiyasoma.
أَوْ تَقُولُوا لَوْ أَنَّا أُنزِلَ عَلَيْنَا الْكِتَابُ لَكُنَّا أَهْدَىٰ مِنْهُمْ ۚ فَقَدْ جَاءَكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ ۚ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَذَّبَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَصَدَفَ عَنْهَا ۗ سَنَجْزِي الَّذِينَ يَصْدِفُونَ عَنْ آيَاتِنَا سُوءَ الْعَذَابِ بِمَا كَانُوا يَصْدِفُونَ ﴿١٥٧﴾
157. Au mkaseme: Lau tungeliteremshiwa Kitabu basi bila shaka tungelikuwa tumehidika zaidi kuliko wao. Kwa yakini imekwishakufikieni hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu na mwongozo na rehma. Hivyo basi nani ni dhalimu zaidi kuliko yule aliyekadhibisha Aayaat za Allaah na akajitenga nazo? Tutawalipa wale wanaojitenga na Aayaat Zetu adhabu ovu kwa sababu ya kujitenga kwao.
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ أَوْ يَأْتِيَ بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ ۗ يَوْمَ يَأْتِي بَعْضُ آيَاتِ رَبِّكَ لَا يَنفَعُ نَفْسًا إِيمَانُهَا لَمْ تَكُنْ آمَنَتْ مِن قَبْلُ أَوْ كَسَبَتْ فِي إِيمَانِهَا خَيْرًا ۗ قُلِ انتَظِرُوا إِنَّا مُنتَظِرُونَ ﴿١٥٨﴾
158. Je, wanangojea nini isipokuwa Malaika wawafikie (kuwatoa roho), au Awafikie Rabb wako (kuwahukumu)[29], au ziwajie baadhi ya Aayaat (Ishara, Alama za Qiyaamah)[30] za Rabb wako? Siku zitakapokuja baadhi ya Aayaat za Rabb wako haitoifaa nafsi imaan yake, ikiwa haikuamini kabla au haikuchuma katika imaan yake kheri yoyote. Sema: Ngojeeni hakika nasi tunangojea.
إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَّسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ ۚ إِنَّمَا أَمْرُهُمْ إِلَى اللَّـهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿١٥٩﴾
159. Hakika wale waliofarakisha dini yao na wakawa makundi makundi,[31] wewe huhusiki nao kwa lolote. Hakika kesi yao iko kwa Allaah, kisha Atawajulisha yale waliyokuwa wakiyatenda.
مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا ۖ وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦٠﴾
160. Atakayekuja na amali njema basi atapata (thawabu) kumi mfano wake. Na Atakayekuja na ovu basi hatolipwa ila mfano wake,[32] nao hawatodhulumiwa.
قُلْ إِنَّنِي هَدَانِي رَبِّي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ دِينًا قِيَمًا مِّلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۚ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٦١﴾
161. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi Ameniongoza Rabb wangu kuelekea njia iliyonyooka, Dini iliyosimama thabiti, mila ya Ibraahiym aliyejitenga na itikadi potofu na kuelemea haki na hakuwa miongoni mwa washirikina.
قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٢﴾
162. Sema: Hakika Swalaah yangu, na ibaada yangu ya kuchinja, na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah Pekee Rabb wa walimwengu.[33]
لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ ﴿١٦٣﴾
163. Hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza (katika ummah huu).
قُلْ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْغِي رَبًّا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَيْءٍ ۚ وَلَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ إِلَّا عَلَيْهَا ۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرْجِعُكُمْ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿١٦٤﴾
164. Sema Je, nitake ghairi ya Allaah kuwa ni Rabb ilhali Yeye Ndiye Rabb wa kila kitu? Na nafsi yoyote haichumi (kheri au shari) ila itabeba yenyewe. Na wala habebi mbebaji, mzigo (wa dhambi) wa mwengine. Kisha kwa Rabb wenu ndio marejeo yenu, Atakujulisheni yale mliyokuwa mkikhitilafiana.
وَهُوَ الَّذِي جَعَلَكُمْ خَلَائِفَ الْأَرْضِ وَرَفَعَ بَعْضَكُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِّيَبْلُوَكُمْ فِي مَا آتَاكُمْ ۗ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ الْعِقَابِ وَإِنَّهُ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٦٥﴾
165. Naye (Allaah) Ndiye Aliyekufanyeni warithi waandamizi wa duniani na Akanyanyua baadhi yenu juu ya wengine kwa daraja mbali mbali ili Akujaribuni katika yale Aliyokupeni. Hakika Rabb wako Ni Mwepesi wa Kuakibu, na hakika Yeye bila shaka Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
[1] Yeye Ndiye Allaah Mwabudiwa Wa Mbinguni Na Ardhini:
Wafasiri wa Qur-aan wamekhitilafiana katika kauli nne kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَهُوَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَفِي الْأَرْضِ ۖ يَعْلَمُ سِرَّكُمْ وَجَهْرَكُمْ وَيَعْلَمُ مَا تَكْسِبُونَ ﴿٣﴾
“Na Yeye Ndiye Allaah mbinguni na ardhini, Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu, na Anajua yale mnayoyachuma.” [Al-An'aam (6:3)]
Kauli Ya Kwanza:
Maana yake ni: Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) ni Ilaah (Apasaye kuabudiwa kwa haki), Anayeabudiwa mbinguni na ardhini, kwa sababu Yeye Pekee Ndiye Mwabudiwa wa haki katika ardhi na mbingu, kwa ushahidi wa Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَـٰهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَـٰهٌ ۚ
“Na Yeye Ndiye Mwabudiwa wa haki mbinguni na ardhini pia (Ndiye Huyo Huyo) Ilaah.” [Az-Zukhruf (43:84)]
[Al-Qurtwubiy, Ibn Kathiyr, Ash-Shanqiytwiy, Ibn Al-Anbaariy na wengineo. Rejea Al-Jaami’u li-Ahkaamil-Qur-aan (6/390), Tafsiyr Al-Qur-aan Al-‘Adhwiym (3/240) na Adhwaau Al-Bayaan (7/4)]
Kauli Ya Pili:
Maana yake ni: Yeye Allaah Anajua siri zenu mbinguni na ardhini, na ushahidi ni Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
قُلْ أَنزَلَهُ الَّذِي يَعْلَمُ السِّرَّ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ
“Sema (ee Muhammad صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ): “Ameiteremsha Ambaye Anajua siri katika mbingu na ardhi.” [Al-Furqaan (25:6)]
Kwa kuzingatia kwamba Kauli Yake:
“mbinguni na ardhini” [Al-An’aam (6:3)] inahusiana na: “Anajua siri zenu.”
Imaam Ad-Daaniyy amesema: Na imesemwa kuwa maana yake ni: Yeye Ndiye Mwabudiwa mbinguni na ardhini. Na Al-Ashmuwniyy kaunga mkono ufafanuzi huo.
Na amesema An-Nahhaas kuwa kauli hiyo ni bora katika yaliyoelezwa juu ya Aayah hiyo.
[Al-Muktafaa Fiy Al-Waqf Wal-Ibtidaa Fiy KitaabiLLaah ‘Azza Wa Jalla (273), Manaaru Al-Hudaa Fiy Bayaan Al-Waqf Wal-Ibtidaa (265). Adhwaau Al-Bayaan Fiy Iydhwaah Al-Qur-aan bil-Qur-aan (4/7)]
Kauli Ya Tatu:
Ni kwamba Yeye Allaah, Ambaye Yuko mbinguni na katika ardhi, Anajua siri zenu na ya dhahiri yenu katika ardhi. Naye Yuko juu ya ‘Arsh Yake Akiwa juu ya Viumbe Vyake wote, Akiwa Anajua siri za watu wa ardhini na ya dhahiri yao, hakuna kinachofichika Kwake katika hayo. Na ushahidi ni Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ﴿١٦﴾
“Je, mnadhani mko katika amani na (Allaah) Aliyeko mbinguni kwamba Hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika?”
أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ﴿١٧﴾
“Au mnadhani mko katika amani na (Allaah) Aliyeko mbinguni kwamba Hatokutumieni tufani ya mawe? Basi mtajua vipi Maonyo Yangu!” [Al-Mulk (67:16-17)]
Na Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥﴾
“Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), Yuko juu (Istawaa) ya ‘Arsh.” [Twaahaa (20:5)]
Kauli Ya Nne:
Ina maana kutangulizwa na kuakhirishwa, yaani: Yeye Allaah Anajua siri zenu na ya dhahiri yenu mbinguni na ardhini. Na hii ni kauli ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما).
Kauli iliyo na nguvu kabisa katika kauli hizo nne ni:
Kauli ya kwanza ambayo ni kauli ya wengi katika Wafasiri wa Qur-aan, pamoja na kwamba kuna uwezekano wa kauli nyingine katika hizo, kwa sababu kila kauli ina ushahidi wake katika Qur-aan.
Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (رحمه الله) amesema: “Imaam wakubwa kama Imaam Ahmad na wengineo wameifasiri kwamba: “Kuwa Yeye Ni Mwabudiwa mbinguni na ardhini.” [Al-Furqaan Bayna Awliyaair-Rahmaan Wa-Awliyaa Ash-Shaytwaan (244)]
Ibn Kathiyr (رحمه الله) amesema “Kauli iliyo sahihi kabisa ni kwamba: “Allaah Anaombwa mbinguni na ardhini, yaani Anaabudiwa, Anapwekeshwa, Anakiriwa kwa Uabudiwa na Anaitwa Allaah. Naye Anaombwa na wote kwa utashi na khofu isipokuwa wakanushaji katika majini na wanaadamu.” [Tafsiyr Al-Qur-aan Al-‘Adhwiym, (3/240)]
[2] Makafiri Wanatakiwa Watembee Maeneo Mbalimbali Wakatambue Hatima Za Waliokanusha Kabla Yao:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anawatanabahisha makafiri, washirikina na wakanushaji wowote wale wa Tawhiyd Yake na Kuwakanusha Rusuli Wake kwa kuwataka waende nchi na maeneo mbalimbali ili wakajionee na watambue adhabu zilizowakumba wenzao wa kabla yao. Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja hivyo katika Suwrah na Aayah mbalimbali. Kati ya Suwrah hizo ni pamoja na Aal-‘Imraan (3:137), Faatwir (35:43-44), Yuwsuf (12:109), An-Naml (37:69), Al-‘Ankabuwt (29:20), Ar-Ruwm (30:9) (30:42), Al-Hajj (22:46), Ghaafir (40:82) na Muhammad (47:10).
[3] Kuthibitisha Sifa Za Allaah (سبحانه وتعالى): Rejea Al-Fat-h (48:10), Huwd (11:37).
[4] Nyoyo Za Makafiri Zimefunikwa Na Masikio Yao Yana Uziwi:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anafahamisha kuwa miongoni mwa washirikina ni wale wanaoisikiliza Qur-aan kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) lakini hawanufaiki na kusikiliza huku. Na kwa sababu hiyo, Allaah (سبحانه وتعالى) Anajaalia vifuniko juu ya nyoyo zao ili wasije wakaifahamu, na Anaweka uziwi masikioni mwao ili wasiisikie kwa sababu ya ukaidi wao na ukanushaji wao, na hata wangeona dalili gani na hoja zilizowazi vipi, wasingeliamini.
Na si kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Anawajaalia vifuniko nyoyoni mwao na uziwi masikioni bila ya sababu tu kama kwamba ni dhulma, Hasha! Allaah (سبحانه وتعالى) Hadhulumu chembe ya uzito wa atomu! Bali Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Ujuzi Wake Ameshajua kuwa watu hawa kamwe hawataamini kama vile Alivyojua kuwa Abu Lahab ambaye ni ammi yake Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) hatoamini, Akateremsha Wahy wa Suwrat Al-Masad (111) wakati Abu Lahab yungali hai, kwani Allaah (سبحانه وتعالى) Angelijua kuwa atakuja kuamini angali yuhai, basi Asingeteremsha Suwrah ya Qur-aan inayomtaja jina Lake, ukanushaji wake, ukafiri wake na adhabu yake. Na hivyo ndivyo hali ya washirikina na makafiri hawa, kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ameshajua kuwa hawataamini kamwe ndipo Anapojaalia vifuniko nyoyoni mwao na uziwi masikioni mwao.
Na maneno haya Ayasemayo Allaah katika Aayah hii, yalisemwa na wenyewe makafiri na washirikina wa Makkah:
وَقَالُوا قُلُوبُنَا فِي أَكِنَّةٍ مِّمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ وَفِي آذَانِنَا وَقْرٌ وَمِن بَيْنِنَا وَبَيْنِكَ حِجَابٌ فَاعْمَلْ إِنَّنَا عَامِلُونَ﴿٥﴾
“Na wakasema: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa yale unayotuitia, na masikioni mwetu mna uziwi, na baina yetu na baina yako kuna kizuizi, basi tenda nasi tunatenda.” [Fusw-Swilat (41:5)]
Na Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja kuweka vifuniko nyoyoni ili zisifahamu kitu kama Anavyosema:
فَإِنَّهَا لَا تَعْمَى الْأَبْصَارُ وَلَـٰكِن تَعْمَى الْقُلُوبُ الَّتِي فِي الصُّدُورِ ﴿٤٦﴾
“Kwani hakika hayapofuki macho, lakini zinazopofuka ni nyoyo zilizomo vifuani.” Rejea Al-Hajj (22:46) ambako kuna maelezo bayana kuhusu maana ya kupofuliwa nyoyo badala ya macho.
Kwa muktadha huu, mtu ambaye haamini Aakhirah, basi kamwe hatauona ujumbe wa Qur-aan kuwa una thamani kwake, wala hatokuwa na hisia ya imaan ya kuiamini Qur-aan, bali atahangaikia maisha na manufaa ya dunia na starehe za dunia anazoweza kuzihisi na kuzifurahikia. Ama Qur-aan, hiyo haitamfikia moyoni mwake kamwe!
Na hii inarejelea Qadar ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba Anafanya hivyo kwa kuwa mtu ana uhuru wa kufuata njia mbili; ya hidaya na ya upotofu. Naye ni Mjuzi wa anayehidika na anayepotoka. Kwa ajili hiyo, wale wanaomkanusha Yeye na Ujumbe Wake na wakamshirikisha, Anawaachia wafanye watakavyo bila ya kuwaadhibu, lakini huko Aakhirah watakapofika ndipo watakapojuta na wakatamani kurudi duniani waamini.
[5] Makafiri Hawakuamini Kwamba Watafufuliwa: Rejea Al-Israa (17:49).
[6] Kitabu:
Lawh Al-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa) Au Qur-aan [Tafsiyr Imaam As-Sa’diy] Rejea Al-Buruwj (85:22).
[8] Kuthibitisha Sifa Za Allaah (سبحانه وتعالى): Rejea Aayah (12) ya Suwrah hii.
[9] Maana Ya Ghaibu: Rejea Al-Baqarah (2:3), Luqmaan (31:34) na An-Naml (27:65).
[10] Hakuna Kinachofichika Kwa Allaah (سبحانه وتعالى); Kiwe Cha Dhahiri Wala Cha Siri, Kikubwa Wala Kidogo Vipi:
Rejea Ghaafir (40:19).
[11] Usingizi Ni Mauti Madogo. Rejea Az-Zumar (39:42).
[13] Manabii Na Rusuli Kumi Na Nane Wametajwa Kuanzia Aayah Hii Na Zinazofuatia:
Kuanzia Aayah hii Al-An’aam (6:83) hadi (6:86) wametajwa Manabii kumi na nane, akijumuika na Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) ambaye ameelezewa katika Aayah zilizotangulia. Wengineo waliotajwa katika Suwrah nyenginezo ni: Aadam, Idriys, Huwd, Swaalih, Shu’ayb (عليهم السّلام) na Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).
Suwrah nyenginezo zilotaja Manabii kwa wingi ni: Al-Anbiyaa (21), Maryam (19), Asw-Swaffaat (37), Swaad (38).
Rejea pia An-Nisaa (4:69) kupata maelezo kuhusu Manabii na tofauti ya Manabii na Rusuli.
Na Manabii na Rusuli, si wote waliosimuliwa katika Qur-aan kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Kauli Zake kwenye Suwrah An-Nisaa (4:164) na Ghaafir (40:78).
[14] Shirki Inabatilisha Amali: Rejea Az-Zumar (39:65) kwenye maelezo ya aina za shirki.
[15] Ummul-Quraa (Makkah): Sababu Za Kuitwa Ummul-Quraa (Mama Wa Miji), Umuhimu Na Fadhila Zake:
Mji wa Makkah unaitwa Ummul-Quraa (Mama wa miji) kwa sababu kadhaa. Miongoni mwazo ni:
(i) Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلِتُنذِرَ أُمَّ الْقُرَىٰ وَمَنْ حَوْلَهَا
“Na ili uonye (kwacho) Ummul-Quraa (Mama wa miji [Makkah]), na wale ambao wameuzunguka.”
Baadhi ya ‘Ulamaa wamesema: Mji wa Makkah umeitwa “Ummul Quraa” (Mama wa miji) kwa kuwa ndio asili ya miji yote ya ardhi, na kutokea hapo, ardhi ndipo ilipotandazwa. Na kwa sababu hiyo, mji wa Makkah uko katikati ya dunia.
Na ndio maana Makkah ukawa ni mji mkongwe kabisa uliojulikana kwa watu.
(ii) Mji wa Makkah una historia ya Nabiy Ismaa’iyl na baba yake Nabiy Ibraahiym (عليهما السلام). Pia Mama yake Nabiy Ismaa’iyl (Haajar) ambaye alisai baina ya Swafaa na Marwaa kusaka maji na kububujika kwa maji ya Zamzam. Pia Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) kujenga Al-Ka’bah, kisha akasimama kuomba duaa katika Maqaam Ibraahiym (Jiwe ambalo alisimama juu yake wakati wa ujenzi wa Al-Ka’bah) ambapo Waislamu wote wanaswali Rakaa mbili baada ya kutufu Al-Ka’bah. Rejea Al-Baqarah (2:125-129), Ibraahiym (14:35-42).
(iii) Nyumba ya kwanza ambayo imeasisiwa kwa ajili ya watu kufanya ibaada kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwrat Aal-‘Imraan (3:96).
(iv) Nabiy wa Mwisho kabisa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye ametokana na kizazi cha Nabiy Ismaa’iyl (عليه السّلام), kuzaliwa humo na akaishi humo na ndipo alipoteremshiwa Wahy wa Qur-aan humo akaishi humo hadi kuhajiri Madiynah.
(v) Masjid Al-Haraam iliyoko Makkah ni Msikiti wa kwanza kuanzishwa duniani kama ilivyothibiti katika Hadiyth: Abuu Dharr (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Masjid gani ilijengwa ardhini mwanzo? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Masjid Al-Haraam (Makkah).” Nikasema: Kisha upi? Akasema: “Masjid Al-Aqswaa (Palestina).” Nikasema: Kuna muda gani baina ya kuwepo Masjid mbili hizo? Akasema: “Miaka arubaini na popote itakapokudiriki Swalaah basi swali hapo pia ardhi ni mahala pa kuswali.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
(vi) Ni kivutio na kipenzi cha Waumini wa ulimwengu wote kwa sababu, baada ya Nabiy Ibraahim (عليه السّلام) [na mwanawe Nabiy Ismaa’iyl (عليه السّلام)] kujenga Al-Ka’bah, aliomba duaa kwamba nyoyo za watu zipendelee kuelekea huko. Rejea Ibraahiym (14:38).
(vii) Qibla cha Waislamu wote duniani kimo humo, kwa maana, Waislamu wote ulimwenguni wanaekelekea huko katika Swalaah zao, kitendo ambacho bila ya kuelekea Qiblah, Swalaah hitimii.
(viii) Swalaah inayoswaliwa humo ina thawabu maradufu: Amesimulia Jaabir (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Swalaah katika Msikiti wangu ni bora kuliko Swalaah elfu kwengineko isipokuwa Al-Masjid Al-Haraam. Na Swalaah katika Al-Masjid Al-Haraam ni bora kuliko Swalaah elfu mia (laki moja) kwengineko.” [Ahmad, Ibn Maajah na imesahihishwa na Imaam Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Maajah (1163), Swahiyh Al-Jaami’ (3838)]
(ix) Makkah ni mji Mtukufu kabisa na mambo kadhaa yameharamishwa ndani yake na ndio maana Makkah ikaitwa Haram Makkah. Hadiyth ifuatayo imetaja baadhi ya maharamisho: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Ameuharamisha Mji huu Siku Allaah Alipoumba mbingu na ardhi. Basi Mji huu ni hifadhi isiyoguswa kwa Haramisho la Allaah hadi Siku ya Qiyaamah, na hakuruhusiwa yeyote kabla yangu kupigana ndani yake, na haikuruhusiwa kwangu isipokuwa saa moja ya mchana. Basi ni hifadhi isiyoguswa kwa Haramisho la Allaah mpaka Siku ya Qiyaamah. Mwiba wake haukatwi, wala wanyama wake wa kuwindwa hawatimuliwi, wala haokoti chenye kupotezwa humo isipokuwa mwenye kukitangazia, na wala manyasi yake hayakatwi.” Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Isipokuwa “idh-khir” (aina ya mmea wenye harufu nzuri, [mchaichai]), kwani huo ni kwa mhunzi (kuwashia moto) na kwa (kuezekea paa za) nyumba zao. Akasema: “Isipokuwa idh-khir.” [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (1834) na Muslim (1353)]
(x) Umrah na Hajj inatekelezwa huko Makkah na Hajj ni nguzo mojawapo katika nguzo tano za Uislamu.
Na mengineyo yametajwa kuhusu utukufu wa Makkah na Allaah Mjuzi zaidi.
[16] Waongo Waliodai Unabii Baada Ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):
Amesema ‘Ikrimah na Qataadah (رضي الله عنهما): “Aayah hii imeteremshwa kumhusu Musaylamah Al-Kadh-dhaab Laana ya Allaah imfikie!” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Na Imaam As-Sa’adiy (رحمه الله) amesema: “Waliojumuishwa katika Aayah hii ni wale wote wanaodai Unabii kama Musaylamah Al-Kadh-dhaab, Al-Aswad Al-‘Ansiyy, Mukhtaar na wengineo.” [Tafsiyr As-Sa’diy]. Wametajwa wawili hao katika Hadiyth ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).
Amesimulia Naafi’ Bin Jubayr (رضي الله عنه): Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Musaylamah Al-Kadh-dhaab (yaani mrongo), alikuja na watu wake wengi Madiynah) katika zama za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawa anasema: “Lau Muhammad atanifanya mimi kuwa mrithi baada yake, basi nitamfuata.” Na watu wengi katika kaumu yake wakamfuata. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwendea akiwa na Thaabit bin Qays bin Sham-maas, na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa ameshika mkononi mwake kitagaa cha mtende (kipande cha jani la mtende). Akasimama mbele ya Musaylamah na watu wake, akasema: “Lau utaniomba kipande hiki (kitagaa), sitokupatia. Na wala huwezi kuikwepa Amri ya Allaah Aliyokuhukumia. Na ukiukanusha Uislamu, basi Allaah Atakuangamiza. Na wewe kwa hakika nakuona ni mtu mwenye sifa zile zile nilizoonyeshwa kwenye njozi.” Abu Hurayrah (رضي الله عنه) aliniambia kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nilipokuwa nimelala, niliona katika njozi vikuku viwili vya dhahabu mkononi mwangu, na hilo likanitia hamu mno. Kisha nikafunuliwa Wahy katika njozi hiyo nivipulize, nikavipuliza navyo vikaruka. Nikatafsiri njozi ya vikuku hivyo kuwa ni ishara ya waongo wawili watakaokuja baada yangu. Mmoja wao ni Al-‘Ansiyy, na mwengine ni Musaylamah Al-Kadh-dhaab kutoka Al-Yamaamah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
[17] Viumbe Watafufuliwa Wakiwa Kama Walivyozaliwa: Rejea Al-Kahf (18:48), Al-Anbiyaa (21:104).
[18] Allaah (سبحانه وتعالى) Mpasuaji Mbegu Na Anatoa Kilicho Hai Kutokana Na Kilicho Mfu, Na Mtoaji Wa Kilicho Mfu Kutokana Na Kilicho Hai.
Allaah (سبحانه وتعالى) Anaeleza kuwa Yeye huzifanya mbegu za nafaka na za matunda kupasuka na kuchipua ardhini, na kutoa aina mbalimbali ya nafaka, matunda, mboga na kadhaalika zikiwa katika rangi mbalimbali, umbo wa kila aina na ladha tofauti katika mazao hayo. Rejea Ar-Ra’d (13:3-4). Na kwamba Analeta mmea ulio hai kutoka mbegu ya nafaka na mbegu ya matunda, (mbegu) ambazo zisizokuwa na uhai na hii ni ishara na dalili mojawapo ya kuwa Yeye Ni Muumbaji wa kila kitu [Az-Zumar (39:62)] Na kama Anavyosema:
وَآيَةٌ لَّهُمُ الْأَرْضُ الْمَيْتَةُ أَحْيَيْنَاهَا وَأَخْرَجْنَا مِنْهَا حَبًّا فَمِنْهُ يَأْكُلُونَ ﴿٣٣﴾
“Na Aayah (Ishara, Dalili) kwao ni ardhi iliyokufa, Tukaihuisha, na Tukatoa humo nafaka, wakapata kuzila.” [Yaasiyn (36:33)]
Hali kadhalika Kauli Yake hii Allaah (سبحانه وتعالى):
يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَمُخْرِجُ الْمَيِّتِ مِنَ الْحَيِّ
“Anatoa kilicho hai kutokana na kilicho mfu, na Mtoaji wa kilicho mfu kutokana na kilicho hai.” [Al-An’aam (6:95)]
Ni mfano wa Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Kujaalia yai kutoka kwa kuku, kuzaliwa kuku kutokana na yai. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Rejea Aal-‘Imraan (3:26-27), Yuwnus (10:31), Ar-Ruwm (30:19), (30:50), na Yaasiyn (36:38) kwenye faida tele na maelezo bayana kuhusu Qudura, Takdiri ya Allaah (سبحانه وتعالى).
[19] Takdiri (Qudura, Ukadariaji) Ya Allaah (سبحانه وتعالى): Rejea Aal-‘Imraan (3:190), (3:26-27) Yaasiyn (36:38), Al-Falaq (113:1).
[20] Nyota Zimeumbwa Kwa Ajili Ya Mambo Matatu:
Rejea pia An-Nahl (16:16), Asw-Swaaffaat (37:10), Al-Mulk (67:5).
عَن قتادةَ قَالَ: خلقَ اللَّهُ تَعَالَى هَذِه النجومَ لثلاثٍ جَعَلَهَا زِينَةً لِلسَّمَاءِ وَرُجُومًا لِلشَّيَاطِينِ وَعَلَامَاتٍ يُهْتَدَى بهَا فَمن تأوَّلَ فِيهَا بِغَيْرِ ذَلِكَ أَخَطَأَ وَأَضَاعَ نَصِيبَهُ وَتَكَلَّفَ مَالا يَعْلَمُ.
Amesimulia Qataadah (رضي الله عنه) : “Allaah Ameumba hizi nyota kwa malengo matatu: (i) mapambo ya mbingu (ii) vimondo vya (kuwafukuza na kuwapiga) shaytwaan, (iii) alama za kuongoza njia (wasafiri wa majangwani na baharini). Basi atakayefasiri vingine amekosea na atakuta patupu Aakhirah (atakosa thawabu) kwani atakuwa amebeba asio na ilimu nayo kwa kuchupa mipaka ya ujuzi Wake.” [Al-Bukhaariy]
Nyota zimeumbwa kwa ajili ya mambo matatu hayo tu! Basi Hadiyth hii inawakanusha wanajimu (watabiri wa nyota) jambo ambalo ni la kumshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) nayo ni shirki kubwa ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Haisamehe.
[21] Mustaqarr (Mahali pa kustakiri) ni tumboni mwa mama au duniani. Mustawda’ (Mahali pa kuhifadhiwa) ima migongoni mwa baba au kaburini.
[22] Washirikina Wamempachikia Uongo Allaah Kuwa Ana Wana Wa Kike Na Wa Kiume: Rejea Asw-Swaffaat (37:149).
[23] Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Hakumuona Allaah (سبحانه وتعالى):
Masruwq (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Nilimwambia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Ee Mama! Je Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake? Akasema: Hayo uliyoyasema yamefanya nywele zangu zisimame kunisisimka mwili! Tambua kwamba mtu akikutajia mambo matatu yafuatayo basi yeye ni muongo! Atakayesema kwamba Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) amemuona Rabb wake, kisha akasoma:
لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ ﴿١٠٣﴾
“Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote, Naye Ni Mwenye Kudabiri mambo kwa Ulatifu, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.” [Al-An'aam (6:103)]
Na akasoma pia:
وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ اللَّـهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا فَيُوحِيَ بِإِذْنِهِ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ عَلِيٌّ حَكِيمٌ﴿٥١﴾
“Na wala haikuwa kwa mtu yeyote kwamba Allaah Amsemeze isipokuwa kwa Wahy au kutoka nyuma ya kizuizi, au Hutuma Mjumbe, kisha Anamfunulia Wahy Ayatakayo kwa Idhini Yake. Hakika Yeye Ni Mwenye ‘Uluwa, Mwenye Hikmah wa yote.” [Ash-Shuwraa (42:51)]
Kisha akaendelea kusema: Na atakayesema kwamba Nabiy anajua yatakayotokea kesho basi ni muongo. Kisha Akasoma:
وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ
“Na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani.” [Luqmaan (31:34)]
Kisha akasema: Na atakayesema kuwa Nabiy ameficha aliyofunuliwa Wahyi (na maamrisho) basi ni muongo! Kisha akasoma:
يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ
“Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukubalighisha ujumbe Wake.” [Al-Maaidah (5:67)]
Kisha akasema: Lakini Nabiy alimuona Jibriyl katika umbile lake khalisi mara mbili. [Al-Bukhaariy]
Kwa upande mwengine Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Allaah, na akasema kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake mara mbili. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Al-Haafidhw, Ibn Hajar amesema: “Maelezo ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) yamekuja katika hali ya kutodhibitiwa (hayaelezi kama Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake kwa macho yake au vipi) wakati kauli za Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) na wenziwe zimedhibitiwa kwa kusema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumuona Allaah “Kwa macho yake.” Tunaweza kuunganisha kauli hizo mbili kwa kusema Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) alikataa muono “Kwa macho yake” na kauli ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kuwa ni kamuona kiroho.” [Fat-hul-Baariy (8/608)]
Na Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwa riwaaya nyingine alisema kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake wakati akiwa katika usingizi, na hii ni njozi ya kweli. Na kauli ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) inakataa, na kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumuona Rabb wake wakati yeye akiwa macho, lakini kauli hiyo haikatazi kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake akiwa usingizini. Alichokana hapa ni kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumuona Allaah kwa macho yake meupe, akiwa macho.
Wale ambao wanao msimamo kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake kwa macho yake meupe wanaleta Hadiyth dhaifu. Hakuna Hadiyth Swahiyh ambayo inaeleza ya kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake kwa macho yake akiwa macho. Wenye msimamo huo wanaleta Hadiyth ya At-Tirmidhiy ambayo Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) anasema kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake. ‘Ikrimah alimuuliza: “Vipi Aayah ambayo inasema:
لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ
“Macho hayamzunguki, bali Yeye Anayazunguka macho yote.” [Al-An’aam (6:103)]
Alijibu, kuwa ni wakati tu Allaah amezungukwa na Nuru, lakini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Rabb wake mara mbili. “Hadiyth hii ni dhaifu.”
Kwa hali hiyo, hakuna mgongano wa kauli, na Allaah Anajua zaidi [Sharh ya Uswuwl Al-I’itiqaad cha Al-Laalika’iy, (93/512), As-Sunnah (1/181) na Swifaat Al-Maqdisiy ukurasa (109-111]
Hapa kunathibitishwa kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumuona Rabb wake wakati alipopelekwa Al-Israa Wal Mi’raaj, na dalili nyengine ni Hadiyth ifuatayo:
Amesimulia Abu Dharr (رضي الله عنه): Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): Je ulimuona Rabb wako? Akasema: “(Yeye ni) Nuru; vipi niweze kumuona?” [Muslim]
Na hii ndio ‘Aqiydah ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah kuwa Allaah Haonekani duniani, kinyume na ‘Aqiydah ya Masufi wanaoamini kuwa Allaah Anaonekana duniani kwa kuegemeza tukio hilo la Al-Israa Wal Mi’raaj.
Kadhaalika, Aayah hiyo vilevile haikanushi kuonekana Allaah Qiyaamah, bali Qiyaamah Allaah Ataonekana katika kisimamo cha Qiyaamah katika Jannah (Peponi) kwa dalili nyingi kutoka katika Qur-aan na Sunnah, kinyume na ‘Aqiydah ya makundi potofu yanayoamini kuwa Allaah Hatoonekana Aakhirah.
[24] Haramisho La Kuwatukana Watu Ili Tusi Lisimrudie Asiyestahiki Kutukanwa:
Tahadharisho kama hili la kutokuwatukana waabudiwa wa washirikina ili tusi lisimrudie Allaah (سبحانه وتعالى), limeharamishwa pia vile mtu kumtukana mzazi wa mwenziwe, ili tusi lisimrudie mzazi wake:
عَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: {مِنْ اَلْكَبَائِرِ شَتْمُ اَلرَّجُلِ وَالِدَيْهِ. قِيلَ: وَهَلْ يَسُبُّ اَلرَّجُلُ وَالِدَيْهِ؟ قَالَ: نَعَمْ. يَسُبُّ أَبَا اَلرَّجُلِ، فَيَسُبُّ أَبَاهُ، وَيَسُبُّ أُمَّهُ، فَيَسُبُّ أُمَّهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Miongoni mwa madhambi makubwa ni mtu kutukana wazazi wake.” Swahaba wakasema: Mtu anaweza kutukana wazazi wake? Akasema: “Ndiyo, atamtukana baba wa mtu naye anamtukana baba yake, na atamtukana mama wa mtu naye atamtukana mama yake.” [Bukhaariy, Muslim]
Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) amesema: Allaah (سبحانه وتعالى) Anawakataza Waumini kufanya jambo ambalo mwanzo waliruhusiwa na hata kuamrishwa kulifanya; nalo ni kudharau na kutukana masanamu ya washirikina ambao wamewafanya ni waabudiwa wao badala ya Allaah. Kuruhusika kwake ilikuwa ni kwa sababu kuwatukana waabudiwa wao ni kuwadhalilisha na ilikuwa ni njia ya kujikurubisha kwa Allaah. Lakini kwa sababu kufanya hivyo kungeweza kupelekea washirikina kumtukana Rabb wa ulimwengu, Ambaye Anatakasika na kila kosa na matukano au ovu lolote, Allaah Anakataza kuwatukana waabudiwa wa washirikina, kwa sababu watahamasika kulinda dini yao na watataka kujikurubisha kwa waabudiwa wao. Hivyo ni kwa kuwa Allaah Amewapambia kila umma matendo yake, wanafikiri kwamba njia zao ni nzuri, basi ikiwa Waislamu watatukana waabudiwa wao, wao washirikina watawalinda kwa njia zote, hata kama ni matusi kwa Allaah Rabb wa walimwengu.
Lakini watu wote watarejea kwa Allaah Siku ya Qiyaamah kisha watahudhurishwa wao na vitendo vyao mbele Yake, na Awajulishe yale waliyokuwa wakiyafanya, mema na mabaya.
Aayah hii ni dalili kwamba njia za kutumika kufikisha jambo, zinapaswa kuzingatiwa kwa malengo, na kwamba njia ambazo zinaweza kusababisha kitu kuwa haramu hata kama njia hizo zinaruhusiwa- basi zinapaswa kuzingatiwa kuwa ni haramu pia, ikiwa zitaongoza kwenye maovu. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[26] Mfano Wa Kafiri Aliyekuwa Maiti (Katika Viza) Na Muumini Aliyekuwa Hai (Katika Nuru):
Aliyekuwa maiti kabla ya hidaaya ya Allaah, yaani alikuwa mwanzo katika viza vya kufru, ujahili na uasi, kisha Allaah Akamhuisha katika nuru ya imaan, ilimu na utiifu, akatembea na nuru kati ya watu, akawa ni mtu ambaye ana utambuzi wa mambo yake, akiiongoza njia yake na akajua lililo jema na akajitahidi kulitekeleza mwenyewe na pia akalitekeleza katika uhusiano wake na wengineo. Hali kadhalika akatambua uovu na akauchukia na akijitahidi kuuepuka mwenyewe na kuwaepushia wenziwe. Je, huyu yuko sawa na aliye katika viza vya ujahili, upindukiaji mipaka, kufru na maasi, hawezi kutoka humo, kwa sababu amechanganyikiwa; hajui apitie njia gani, hivyo amefunikwa na wasiwasi, shaka, dhiki na huzuni.
Hapa Allaah Anabainisha watu wenye busara kwamba, wao tayari wanajua na kuelewa kwamba hawa wawili hawawezi kulingana sawa, kama vile hauwezi usiku na mchana kuwa sawa au mwanga na giza au walio hai na wafu... [Tafsiyr As-Sa’diy]
Rejea pia Faatwir (35:19) kwenye maelezo na faida ziyada kuhusu mifano ya Allaah baina ya kafiri na Muumin. Rejea pia Huwd (11:24).
[27] Maana Ya Baghyun/Baghaa Katika Qur-aan:
Rejea Ash-Shuwraa (42:14) kupata maana zake mbalimbali.
[28] Maana Ya Kutokufarikiana:
Rejea Al-Faatihah (1:6), Aal-‘Imraan (3:103), (3:105), Ar-Ruwm (30:32), Ash-Shuwraa (42:14), Al-Bayyinah (98:4).
[29] Kuteremka Allaah Na Malaika Siku Ya Qiyaamah:
Rejea Al-Fuqaan (25:25), Al-Haaqah (69:13-18), Al-Baqarah (2:210).
[30] Alama Kubwa Za Qiyaamah: Makafiri Hawakuamini Kuwa Qiyaamah Kitatokea:
Washirikina wa Makkah walikuwa haweshi kuuliza lini Qiyaamah kitatokea. Rejea Al-A’raaf (7:187), Al-Ahzaab (33:63), An-Naazi’aat (79:42). Al-Mulk (67:25), Ash-Shuwraa (42:18), Ghaafir (40:59).
Aayah hii tukufu imetaja kuwa kutatokea Alama kuu kabla ya kufika Qiyaamah ambazo wale wasioamini kabla ya kutokea alama hizo, watakapotaka kuamini, basi imaan zao hazitawafaa lolote kwa kuwa hawatakubaliwa kuamini kwao.
‘Ulamaa wametaja alama hizo kubwa ingawa wamekhitilafiana katika mpangilio wake na kuzitaja kwake nazo ni:
(i) Kuja kwa Mahdi: Mja kutoka katika ahli wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) (ii) Kutokeza kwa Masiyh Ad-Dajjaal (iii) Kuteremka kwa Nabiy ‘Iysaa na (عليه السّلام) na kumuua Masiyh Ad-Dajjaal na kuondosha misalaba, kuua nguruwe na kuondosha dini zote nyenginezo isipokuwa Uislamu (iv) Kuchomoza kwa Yaajuwj na Maajuwj (v) Kubomolewa Ka’bah na kutoka moshi (vi) Kuondoshwa Qur-aan nyoyoni mwa Waumini na Miswahafu (vii) Jua kuchomoza Magharibi (viii) Kutokeza mnyama mwitu mkubwa atakayewasemesha watu (ix) Mididimizo mitatu ya ardhi: Mdidimizo wa Mashariki, Magharibi na katika Jaziyrah ya Arabia (x) Moto utakaotoka kutoka Yemen utawapeleka watu kufika katika Ardhi ya Mkusanyiko.
Na Hadiyth ifuatayo imeorodhesha alama kumi:
Amesimulia Hudhayfah Bin Asiyd (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa chumbani nasi tulikuwa chini yake, akachungulia na kutuuliza: “Mnajadiliana nini?” Tukasema: (Tunajadili kuhusu) Saa (Qiyaamah). Hapo akasema: Saa (Qiyaamah) hakitatokea mpaka zionekane alama (au ishara) kumi: (i) Kudidimia kwa Mashariki (ii) Kudidimia kwa Magharibi. (iii) Kudidimia Bara la Arabu (iv) Moshi. (v) (Masiyh) Ad-Dajjaal. (vi) Mnyama mkubwa wa ardhi (atakayewasemesha watu) (vii) Ya-ajuwj na Ma-ajuwj (viii) Kuchomoza jua upande wa Magharibi (ix) Moto utakaotokea upande wa chini ya ‘Aden utakaowasukuma watu (kufikia Ardhi ya Mkusanyiko).” Shu'bah amesema na amenihadithia ‘Abdul-‘Aziyz bin Rufa’y kutoka kwa Abiy Atw-Twufayl kutoka kwa Abiy Sariyhah Hadiyth kama hiyo ila Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuitaja (alama ya kumi) lakini alisema kuwa katika kumi, mojawapo ni kuteremka Nabiy ‘Iysaa bin Maryam (عليه السّلام) na katika riwaaya nyengine ni: Upepo mkali utakaowaendesha watu na kutupwa baharini. [Muslim]
Rejea Al-Kahf (18:94) kulikotajwa kuhusu Yaajuwj na Maajuwj.
[31] Kugawanyika Watu Makundi Makundi:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anawakemea wale wanaoigawa Dini yao, yaani, kuigawanya na kufarikiana ndani yake, na kila mmoja anajiwekea sehemu ya majina ambayo haimnufaishi mtu katika dini yake chochote, kama vile Uyahudi, Unaswara na Umajusi. Au (Majina hayo) hayamtimizii mtu imaan yake kwayo, kwa kuchukua kitu katika sharia na kukifanya kuwa ndio dini yake, na kuacha kitu mfano wake, au kinachostahiki zaidi yake. Hivyo ni kama ilivyo kwa watu wa makundi ya bid’ah na upotofu na wanao farakanisha ummah. Na Aayah tukufu ikaashiria kuwa Dini inaamrisha umoja na muungano, na inakataza mifarakano na khitilafu katika watu wa dini, na katika masuala yake yote ya msingi na matawi. Akamuamuru kuwatenga wale walioigawa dini yao. [Imaam As-Sa’diy katika Tafisyr yake]
Rejea pia Aayah (153) Suwrah hii ya Al-An’aam.
[32] Rahmah Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kwa Waumini Kuongezewa Thawabu Mara Kumi Kwa Amali Njema Moja Na Kuandikiwa Dhambi Moja Tu Kwa Tendo Ovu:
Ukitia niya kutenda amali moja lakini ukawa hukujaaliwa kuitenda utaandikiwa moja. Utakapoweza kuitenda utalipwa mara kumi yake.
Ukitia niya kutenda uovu haitoandikwa kwanza kwa kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Anampa mja muhula ajirudi ili asitende uovu au dhambi. Na atakapotenda basi ataandikiwa dhambi moja.
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah Ameandika mema na mabaya, kisha Akayabainisha, basi atakayetia niya kutenda jema kisha asilifanye, ataandikiwa jema moja kamili. Atakapofanya hima na akalitenda, ataandikiwa mema kumi hadi kuzidi mia saba na ziada nyingi. Na atakayetia niya kufanya kitendo kibaya kisha asikifanye, ataandikiwa jema moja kamili. Atakapokifanya, ataandikiwa dhambi moja.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
[33] Dua Mojawapo Ya Kufungulia Swalaah:
Aayah (6:162-163) ni mojawapo ya Dua ya kufungulia Swalaah kama ilivyothibiti katika Sunnah kusema:
وَجَّهـتُ وَجْهِـيَ لِلَّذي فَطَرَ السَّمـواتِ وَالأَرْضَ حَنـيفَاً وَمـا أَنا مِنَ المشْرِكين، إِنَّ صَلاتـي، وَنُسُكي، وَمَحْـيايَ، وَمَماتـي للهِ رَبِّ العالَمين، لا شَريـكَ لَهُ وَبِذلكَ أُمِرْتُ وَأَنا مِنَ المسْلِـمين.
Nimeuelekeza uso wangu kwa yule Ambaye Ameanzisha mbingu na ardhi hali ya kuelemea katika haki, na sikuwa mimi ni katika washirikina, hakika Swalaah yangu na kuchinja kwangu na uhai wangu, na kufa kwangu ni kwa Allaah Rabb walimwengu, Hana mshirika, na kwa hilo nimeamrishwa nami ni katika Waislamu.
Na katika riwaaya nyenginezo inaishia kwa:
وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ
nami ni Muislamu wa kwanza.
(Kisha dua inaendelea)
Pia Aayah hii ni dalili mojawapo ya haramisho la kuchinja kwa kukusudia asiyekuwa Allaah.
الأَعْرَاف
007-Al-A’raaf
007-Al-A'raaf: Utangulizi Wa Suwrah [114]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
المص ﴿١﴾
1. Alif Laam Miym Swaad.[1]
كِتَابٌ أُنزِلَ إِلَيْكَ فَلَا يَكُن فِي صَدْرِكَ حَرَجٌ مِّنْهُ لِتُنذِرَ بِهِ وَذِكْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ ﴿٢﴾
2. Kitabu (hiki) kimeteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) basi isiwe katika kifua chako dhiki kwa ajili yake, ili uwaonye kwacho na ni ukumbusho kwa Waumini.
اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٣﴾
3. Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Rabb wenu na wala msifuate badala Yake marafiki walinzi. Ni machache mnayoyakumbuka.
وَكَم مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا فَجَاءَهَا بَأْسُنَا بَيَاتًا أَوْ هُمْ قَائِلُونَ ﴿٤﴾
4. Ni miji mingi sana Tumeiangamiza ikaifikia Adhabu Yetu usiku au walipokuwa katika usingizi wa mchana (qayluwlah).
فَمَا كَانَ دَعْوَاهُمْ إِذْ جَاءَهُم بَأْسُنَا إِلَّا أَن قَالُوا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿٥﴾
5. Basi hakikuwa kilio chao ilipowajia Adhabu Yetu isipokuwa walisema: Hakika sisi tulikuwa madhalimu.
فَلَنَسْأَلَنَّ الَّذِينَ أُرْسِلَ إِلَيْهِمْ وَلَنَسْأَلَنَّ الْمُرْسَلِينَ ﴿٦﴾
6. Hivo bila shaka Tutawauliza wale waliopelekewa Rusuli, na bila shaka Tutawauliza hao Rusuli.
فَلَنَقُصَّنَّ عَلَيْهِم بِعِلْمٍ ۖ وَمَا كُنَّا غَائِبِينَ ﴿٧﴾
7. Kisha Tutawasimulia kwa ilimu (amali zao), na Hatukuwa Wenye Kukosekana.
وَالْوَزْنُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ ۚ فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٨﴾
8. Upimaji wa haki utathibiti Siku hiyo. Basi ambao mizani zao zitakuwa nzito, hao ndio watakaofaulu.[2]
وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُم بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَظْلِمُونَ ﴿٩﴾
9. Na ambao mizani zao zitakuwa khafifu, basi hao ni wale waliojikhasiri wenyewe kwa sababu ya kutozitendea haki Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) Zetu.
وَلَقَدْ مَكَّنَّاكُمْ فِي الْأَرْضِ وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَايِشَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ ﴿١٠﴾
10. Kwa yakini Tumekumakinisheni katika ardhi na Tukawawekeeni humo mahitaji ya maisha. Kidogo sana kushukuru kwenu.
وَلَقَدْ خَلَقْنَاكُمْ ثُمَّ صَوَّرْنَاكُمْ ثُمَّ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ لَمْ يَكُن مِّنَ السَّاجِدِينَ ﴿١١﴾
11. Na kwa yakini Tumekuumbeni kisha Tukakutieni sura, kisha Tukawaambia Malaika: Msujudieni Aadam. Wakasujudu isipokuwa Ibliys hakuwa miongoni mwa waliosujudu.
قَالَ مَا مَنَعَكَ أَلَّا تَسْجُدَ إِذْ أَمَرْتُكَ ۖ قَالَ أَنَا خَيْرٌ مِّنْهُ خَلَقْتَنِي مِن نَّارٍ وَخَلَقْتَهُ مِن طِينٍ ﴿١٢﴾
12. (Allaah) Akasema: Nini kilichokuzuia usisujudu Nilipokuamrisha? (Ibliys) akasema: Mimi ni mbora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye Umemuumba kwa udongo.
قَالَ فَاهْبِطْ مِنْهَا فَمَا يَكُونُ لَكَ أَن تَتَكَبَّرَ فِيهَا فَاخْرُجْ إِنَّكَ مِنَ الصَّاغِرِينَ ﴿١٣﴾
13. (Allaah) Akasema: Basi shuka kutoka humo, kwani haikupasa kwako utakabari humo. Hivyo toka! Hakika wewe ni miongoni mwa walio duni na dhalili.
قَالَ أَنظِرْنِي إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٤﴾
14. (Ibliys) akasema: Nipe muhula hadi Siku watakapofufuliwa
قَالَ إِنَّكَ مِنَ الْمُنظَرِينَ ﴿١٥﴾
15. (Allaah) Akasema: Hakika wewe ni miongoni mwa waliopewa muhula.
قَالَ فَبِمَا أَغْوَيْتَنِي لَأَقْعُدَنَّ لَهُمْ صِرَاطَكَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿١٦﴾
16. (Ibliys) akasema: Basi kwa kuwa Umenihukumia kupotoka, nitawakalia chonjo (Waja Wako) katika Njia Yako iliyonyooka.
ثُمَّ لَآتِيَنَّهُم مِّن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ وَعَنْ أَيْمَانِهِمْ وَعَن شَمَائِلِهِمْ ۖ وَلَا تَجِدُ أَكْثَرَهُمْ شَاكِرِينَ ﴿١٧﴾
17. Kisha nitawaandama mbele yao na nyuma na kuliani kwao na kushotoni kwao, na wala Hutopata wengi wao wenye kushukuru.
قَالَ اخْرُجْ مِنْهَا مَذْءُومًا مَّدْحُورًا ۖ لَّمَن تَبِعَكَ مِنْهُمْ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿١٨﴾
18. (Allaah) Akasema: Toka humo ukiwa umekosa heshima na umefukuzwa! Atakayekufuata miongoni mwao, bila shaka Nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote.
وَيَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ فَكُلَا مِنْ حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿١٩﴾
19. Na ee Aadam! Ishi wewe na mkeo Jannah na mle humo popote mpendapo, na wala msikaribie mti huu, msijekuwa miongoni mwa madhalimu.
فَوَسْوَسَ لَهُمَا الشَّيْطَانُ لِيُبْدِيَ لَهُمَا مَا وُورِيَ عَنْهُمَا مِن سَوْآتِهِمَا وَقَالَ مَا نَهَاكُمَا رَبُّكُمَا عَنْ هَـٰذِهِ الشَّجَرَةِ إِلَّا أَن تَكُونَا مَلَكَيْنِ أَوْ تَكُونَا مِنَ الْخَالِدِينَ ﴿٢٠﴾
20. Basi shaytwaan (naye ni Ibliys) akawatia wasiwasi ili awafichulie sehemu zao za siri zilizositiriwa. Na akasema: Rabb wenu Hakukukatazeni huu mti isipokuwa msijekuwa Malaika wawili au kuwa miongoni mwa wenye kudumu milele.
وَقَاسَمَهُمَا إِنِّي لَكُمَا لَمِنَ النَّاصِحِينَ ﴿٢١﴾
21. Naye akawaapia: Hakika mimi ni katika wenye kukunasihini kidhati.
فَدَلَّاهُمَا بِغُرُورٍ ۚ فَلَمَّا ذَاقَا الشَّجَرَةَ بَدَتْ لَهُمَا سَوْآتُهُمَا وَطَفِقَا يَخْصِفَانِ عَلَيْهِمَا مِن وَرَقِ الْجَنَّةِ ۖ وَنَادَاهُمَا رَبُّهُمَا أَلَمْ أَنْهَكُمَا عَن تِلْكُمَا الشَّجَرَةِ وَأَقُل لَّكُمَا إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمَا عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿٢٢﴾
22. Basi akawachota (wote wawili) kwa kuwalaghai. Walipoonja mti ule tupu zao zilifichuka, hapo wakaanza kuzibandika majani ya Jannah. Na Rabb wao Akawaita: Je, kwani Mimi Sikukukatazeni mti huo na kukuambieni kwamba shaytwaan ni adui bayana kwenu?
قَالَا رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٢٣﴾
23. Wakasema: Rabb wetu! Tumedhulumu nafsi zetu, na Usipotughufuria na Ukaturehemu, bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliokhasirika.
قَالَ اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ ﴿٢٤﴾
24. (Allaah) Akasema: Shukeni! Nyinyi kwa nyinyi ni maadui. Na ardhi itakuwa ndio mastakimu yenu na starehe kwenu mpaka muda mahsusi.
قَالَ فِيهَا تَحْيَوْنَ وَفِيهَا تَمُوتُونَ وَمِنْهَا تُخْرَجُونَ ﴿٢٥﴾
25. Akasema: Humo mtaishi, na humo mtakufa, na kutoka humo mtatolewa (kufufuliwa).
يَا بَنِي آدَمَ قَدْ أَنزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًا يُوَارِي سَوْآتِكُمْ وَرِيشًا ۖ وَلِبَاسُ التَّقْوَىٰ ذَٰلِكَ خَيْرٌ ۚ ذَٰلِكَ مِنْ آيَاتِ اللَّـهِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ ﴿٢٦﴾
26. Enyi wana wa Aadam! Kwa yakini Tumekuteremshieni libasi (nguo) inayositiri tupu zenu na libasi ya mapambo. Na libasi ya taqwa ndiyo bora zaidi. Hizo ni katika Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) za Allaah ili wapate kukumbuka.
يَا بَنِي آدَمَ لَا يَفْتِنَنَّكُمُ الشَّيْطَانُ كَمَا أَخْرَجَ أَبَوَيْكُم مِّنَ الْجَنَّةِ يَنزِعُ عَنْهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوْآتِهِمَا ۗ إِنَّهُ يَرَاكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُ مِنْ حَيْثُ لَا تَرَوْنَهُمْ ۗ إِنَّا جَعَلْنَا الشَّيَاطِينَ أَوْلِيَاءَ لِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٢٧﴾
27. Enyi wana wa Aadam! Asikufitinisheni kabisa shaytwaan kama alivyowatoa wazazi wenu katika Jannah huku akiwavua nguo zao ili awaonyeshe sehemu zao za siri. Hakika yeye (Ibliys) na kabila yake (ya mashaytwaan) wanakuoneni, na nyinyi hamuwaoni. Hakika Sisi Tumewafanya mashaytwaan kuwa ni marafiki wandani kwa wale wasioamini.
وَإِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً قَالُوا وَجَدْنَا عَلَيْهَا آبَاءَنَا وَاللَّـهُ أَمَرَنَا بِهَا ۗ قُلْ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَأْمُرُ بِالْفَحْشَاءِ ۖ أَتَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢٨﴾
28. Na wanapofanya jambo chafu husema: Tumewakuta katika hali hii baba zetu, na Allaah Ametuamrisha hayo. Sema: Hakika Allaah Haamrishi machafu. Je mnamzulia Allaah msiyoyajua?
قُلْ أَمَرَ رَبِّي بِالْقِسْطِ ۖ وَأَقِيمُوا وُجُوهَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ ۚ كَمَا بَدَأَكُمْ تَعُودُونَ ﴿٢٩﴾
29. Sema: Rabb wangu Ameniamrisha uadilifu. Na elekezeni nyuso zenu (Kwake Pekee Allaah) katika kila sehemu (au nyakati) mnaposujudu na mwombeni Yeye kwa kumtakasia Yeye Dini. Kama Alivyokuanzisheni mtarudi (tena Kwake).
فَرِيقًا هَدَىٰ وَفَرِيقًا حَقَّ عَلَيْهِمُ الضَّلَالَةُ ۗ إِنَّهُمُ اتَّخَذُوا الشَّيَاطِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٣٠﴾
30. Kundi Amelihidi, na kundi (jingine) limethibitikiwa upotofu. Hakika wao wamewafanya mashaytwaan kuwa marafiki walinzi badala ya Allaah na wanadhani kwamba wao wamehidika.
يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿٣١﴾
31. Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu (ya mavazi ya sitara na twahara) katika kila mahala pa ibaada.[3] Na kuleni na kunyweni na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu.[4]
قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللَّـهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ مِنَ الرِّزْقِ ۚ قُلْ هِيَ لِلَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا خَالِصَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٣٢﴾
32. Sema: Nani aliyeharamisha Mapambo ya Allaah ambayo Amewatolea Waja Wake na vilivyo vizuri katika riziki? Sema: Hivyo ni kwa ajili ya wale walioamini katika uhai wa dunia, (na) makhsusi (kwa Waumini) Siku ya Qiyaamah. Hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat (na Hukmu, Sharia) kwa watu wanaojua.
قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٣٣﴾
33. Sema: Hakika Rabb wangu Ameharamisha machafu ya wazi na ya siri, na dhambi, na baghi[5] (ukandamizaji) bila ya haki, na kumshirikisha Allaah kwa ambayo Hakuyateremshia mamlaka, na kusema juu ya Allaah yale ambayo hamyajui.[6]
وَلِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ ۖ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ ﴿٣٤﴾
34. Na kila ummah una muda uliokadiriwa. Basi utakapofika muda wao huo, hawataakhirisha wala hawatatangulia saa.
يَا بَنِي آدَمَ إِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِي ۙ فَمَنِ اتَّقَىٰ وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿٣٥﴾
35. Enyi wana wa Aadam! Watakapokufikieni Rusuli miongoni mwenu wakakubainishieni Aayaat (na Ishara, Dalili, Hukmu) Zangu, basi atakayekuwa na taqwa na akajiweka sawa, haitokuwa khofu juu yao na hawatohuzunika.
وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٣٦﴾
36. Na wale waliokadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili) Zetu na wakazifanyia kiburi, hao ni watu wa motoni, wao humo watadumu.
فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۚ أُولَـٰئِكَ يَنَالُهُمْ نَصِيبُهُم مِّنَ الْكِتَابِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءَتْهُمْ رُسُلُنَا يَتَوَفَّوْنَهُمْ قَالُوا أَيْنَ مَا كُنتُمْ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالُوا ضَلُّوا عَنَّا وَشَهِدُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَنَّهُمْ كَانُوا كَافِرِينَ ﴿٣٧﴾
37. Basi nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemtungia Allaah uongo au aliyekadhibisha Aayaat Zake. Hao itawafikia sehemu yao waliyoandikiwa mpaka watakapowajia Wajumbe Wetu kuwafisha watawaambia: Wako wapi wale mliokuwa mkiwaomba pasi na Allaah? Watasema: Wametupotea! Na watajishuhudia nafsi zao wenyewe kwamba walikuwa makafiri.
قَالَ ادْخُلُوا فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ فِي النَّارِ ۖ كُلَّمَا دَخَلَتْ أُمَّةٌ لَّعَنَتْ أُخْتَهَا ۖ حَتَّىٰ إِذَا ادَّارَكُوا فِيهَا جَمِيعًا قَالَتْ أُخْرَاهُمْ لِأُولَاهُمْ رَبَّنَا هَـٰؤُلَاءِ أَضَلُّونَا فَآتِهِمْ عَذَابًا ضِعْفًا مِّنَ النَّارِ ۖ قَالَ لِكُلٍّ ضِعْفٌ وَلَـٰكِن لَّا تَعْلَمُونَ ﴿٣٨﴾
38. (Allaah) Atasema: Ingieni motoni pamoja na nyumati zilizokwishapita kabla yenu za majini na wanaadamu. Kila utakapoingia ummah utalaani nduguye. Mpaka watakapokusanyika mrundo humo wote pamoja[7] wa mwisho wao (waliofuata wakuu) watawasema wa mwanzo wao (wakuu wao): Rabb wetu! Hawa wametupoteza, basi Wape adhabu maradufu ya moto. (Allaah) Atasema: Kila mmoja atapata (adhabu ya) maradufu lakini hamjui.
وَقَالَتْ أُولَاهُمْ لِأُخْرَاهُمْ فَمَا كَانَ لَكُمْ عَلَيْنَا مِن فَضْلٍ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْسِبُونَ ﴿٣٩﴾
39. Na wa mwanzo wao watawaambia wa mwisho wao: Basi hamkuwa na ubora kuliko sisi. Hivyo onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyachuma.
إِنَّ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا لَا تُفَتَّحُ لَهُمْ أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَلَا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ حَتَّىٰ يَلِجَ الْجَمَلُ فِي سَمِّ الْخِيَاطِ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُجْرِمِينَ ﴿٤٠﴾
40. Hakika wale waliokadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili) Zetu na wakazifanyia kiburi, hawatofunguliwa kamwe milango ya mbingu na wala hawatoingia Jannah mpaka ngamia aingie katika tundu ya sindano. Na hivyo ndivyo Tunavyowalipa wahalifu.[8]
لَهُم مِّن جَهَنَّمَ مِهَادٌ وَمِن فَوْقِهِمْ غَوَاشٍ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ ﴿٤١﴾
41. Jahannam itakuwa ni kitanda chao na juu yao miguo ya kuwafunika, na hivyo ndivyo Tunavyowalipa madhalimu.
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٤٢﴾
42. Na wale walioamini na wakatenda mema - Nasi Hatuikalifishi nafsi ila kadiri ya uwezo wake - hao ni watu wa Jannah, wao humo watadumu.
وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ ۖ وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي هَدَانَا لِهَـٰذَا وَمَا كُنَّا لِنَهْتَدِيَ لَوْلَا أَنْ هَدَانَا اللَّـهُ ۖ لَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ ۖ وَنُودُوا أَن تِلْكُمُ الْجَنَّةُ أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٤٣﴾
43. Na Tutaondosha mizizi ya mafundo ya kinyongo yaliyomo vifuani mwao,[9] itapita chini yao mito. Na watasema: AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Ambaye Ametuongoza kwa haya, na tusingelikuwa wenye kuhidika kama Allaah Asingetuongoza. Kwa yakini wamekuja Rusuli wa Rabb wetu na haki. Na wataitwa (kuambiwa): Hii ndiyo Jannah mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mnayatenda.
وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ أَصْحَابَ النَّارِ أَن قَدْ وَجَدْنَا مَا وَعَدَنَا رَبُّنَا حَقًّا فَهَلْ وَجَدتُّم مَّا وَعَدَ رَبُّكُمْ حَقًّا ۖ قَالُوا نَعَمْ ۚ فَأَذَّنَ مُؤَذِّنٌ بَيْنَهُمْ أَن لَّعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ ﴿٤٤﴾
44. Na watu wa Jannah watawaita watu wa motoni kuwaambia: Kwa yakini tumeyakuta Aliyotuahidi Rabb wetu kuwa ni kweli. Je, basi nyinyi mmeyakuta Aliyokuahidini Rabb wenu kuwa ni kweli? Watasema: Naam! Basi mtangazaji atatangaza baina yao kwamba: Laana ya Allaah iwe juu ya madhalimu!
الَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا وَهُم بِالْآخِرَةِ كَافِرُونَ ﴿٤٥﴾
45. Ambao wanazuia Njia ya Allaah na wanaitafutia upogo, na wao wanaikanusha Aakhirah.
وَبَيْنَهُمَا حِجَابٌ ۚ وَعَلَى الْأَعْرَافِ رِجَالٌ يَعْرِفُونَ كُلًّا بِسِيمَاهُمْ ۚ وَنَادَوْا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَن سَلَامٌ عَلَيْكُمْ ۚ لَمْ يَدْخُلُوهَا وَهُمْ يَطْمَعُونَ ﴿٤٦﴾
46. Na baina yao kitakuwepo kizuizi. Na juu ya Al-A’raaf[10] (ukuta wa mwinuko) patakuweko watu watakaowatambua wote (wabaya na wema) kwa alama zao. Na watawaita watu wa Jannah: Salaamun ‘Alaykum! Hawakuingia humo lakini bado wanatumaini.
وَإِذَا صُرِفَتْ أَبْصَارُهُمْ تِلْقَاءَ أَصْحَابِ النَّارِ قَالُوا رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٤٧﴾
47. Na yatakapogeuzwa macho yao kuelekea watu wa motoni watasema: Rabb wetu! Usitujaalie kuwa pamoja na watu madhalimu.
وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْأَعْرَافِ رِجَالًا يَعْرِفُونَهُم بِسِيمَاهُمْ قَالُوا مَا أَغْنَىٰ عَنكُمْ جَمْعُكُمْ وَمَا كُنتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ ﴿٤٨﴾
48. Na watu wa Al-A’raaf watawaita watu (wa motoni) wanaowatambua kwa alama zao, watasema: Hakukufaeni kujumuika kwenu (duniani) na vile mlivyokuwa mkitakabari.
أَهَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمْتُمْ لَا يَنَالُهُمُ اللَّـهُ بِرَحْمَةٍ ۚ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمْ وَلَا أَنتُمْ تَحْزَنُونَ ﴿٤٩﴾
49. Je, hawa si wale ambao mliapa kwamba Allaah Hatowapa rehma yoyote ile? (Leo wanaambiwa) Ingieni Jannah! Hakuna khofu juu yenu na wala nyinyi hamtohuzunika.
وَنَادَىٰ أَصْحَابُ النَّارِ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَنْ أَفِيضُوا عَلَيْنَا مِنَ الْمَاءِ أَوْ مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ ۚ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ حَرَّمَهُمَا عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٥٠﴾
50. Na watu wa motoni watawaita watu wa Jannah: Tumiminieni maji au katika ambavyo Amekuruzukuni Allaah. Watasema: Hakika Allaah Ameviharamisha kwa makafiri.
الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَهُمْ لَهْوًا وَلَعِبًا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۚ فَالْيَوْمَ نَنسَاهُمْ كَمَا نَسُوا لِقَاءَ يَوْمِهِمْ هَـٰذَا وَمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ ﴿٥١﴾
51. Ambao wameifanya dini yao pumbao na mchezo, na ukawaghuri uhai wa dunia. Basi leo Tunawasahau kama walivyosahau kukutana na Siku yao hii, na kuwa kwao wakizikanusha kwa jeuri Aayaat (na Ishara, Dalili) Zetu.
وَلَقَدْ جِئْنَاهُم بِكِتَابٍ فَصَّلْنَاهُ عَلَىٰ عِلْمٍ هُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٥٢﴾
52. Kwa yakini Tumewaletea Kitabu Tulichokifasili waziwazi kwa ujuzi; ni mwongozo na rehma kwa watu wanaoamini.
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا تَأْوِيلَهُ ۚ يَوْمَ يَأْتِي تَأْوِيلُهُ يَقُولُ الَّذِينَ نَسُوهُ مِن قَبْلُ قَدْ جَاءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ فَهَل لَّنَا مِن شُفَعَاءَ فَيَشْفَعُوا لَنَا أَوْ نُرَدُّ فَنَعْمَلَ غَيْرَ الَّذِي كُنَّا نَعْمَلُ ۚ قَدْ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٥٣﴾
53. Je, wanangojea nini isipokuwa matokeo yake? Siku (ya Qiyaamah) yatakapofika matokeo yake watasema wale walioisahau kabla: Kwa yakini walikuja Rusuli wa Rabb wetu kwa haki. Je, tuna waombezi wowote watuombee, au turudishwe (duniani) ili tufanye ghairi ya yale tuliyokuwa tunafanya? Kwa yakini wamekhasiri nafsi zao na yamewapotea yale waliyokuwa wakiyatunga (ya uongo).
إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ ۗ أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٥٤﴾
54. Hakika Rabb wenu ni Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Akawa juu[11] ya ‘Arsh, Anafunika usiku kwa mchana, unaufuatia upesi upesi, na (Ameumba) jua na mwezi na nyota, (vyote) vimetiishwa kwa Amri Yake. Tanabahi! Uumbaji ni Wake Pekee na kupitisha amri. Amebarikika Allaah Rabb wa walimwengu.[12]
ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٥٥﴾
55. Muombeni Rabb wenu kwa unyenyekevu na kwa siri, hakika Yeye Hapendi wenye kupindukia mipaka.[13]
وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا وَادْعُوهُ خَوْفًا وَطَمَعًا ۚ إِنَّ رَحْمَتَ اللَّـهِ قَرِيبٌ مِّنَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٦﴾
56. Na wala msifanye ufisadi katika ardhi baada ya (Allaah) kuitengeneza sawa, na muombeni kwa khofu na matumaini. Hakika Rehma ya Allaah iko karibu na wafanyao ihsaan.
وَهُوَ الَّذِي يُرْسِلُ الرِّيَاحَ بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا أَقَلَّتْ سَحَابًا ثِقَالًا سُقْنَاهُ لِبَلَدٍ مَّيِّتٍ فَأَنزَلْنَا بِهِ الْمَاءَ فَأَخْرَجْنَا بِهِ مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ ۚ كَذَٰلِكَ نُخْرِجُ الْمَوْتَىٰ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ ﴿٥٧﴾
57. Naye Ndiye Anayetuma upepo wa kheri kuwa bishara kabla ya Rehma Yake. Hadi unapobeba mawingu mazito Tunayasukuma kwenye nchi iliyokufa. Kisha Tunateremsha kwayo maji na kisha Tunatoa kwayo kila (aina ya) mazao. Hivyo ndivyo Tunavyotoa wafu, ili mpate kukumbuka (au kuwaidhika).
وَالْبَلَدُ الطَّيِّبُ يَخْرُجُ نَبَاتُهُ بِإِذْنِ رَبِّهِ ۖ وَالَّذِي خَبُثَ لَا يَخْرُجُ إِلَّا نَكِدًا ۚ كَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَشْكُرُونَ ﴿٥٨﴾
58. Na nchi nzuri mimea yake hutoka kwa Idhini ya Rabb wake. Na ile ambayo ni mbaya haitoki ila kwa uadimu.[14] Hivyo ndivyo Tunavyosarifu namna kwa namna Aayaat (na Ishara, Dalili) kwa watu wanaoshukuru.
لَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَقَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٥٩﴾
59. Kwa yakini Tulimpeleka Nuwh kwa kaumu yake[15] akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku iliyo kuu kabisa.
قَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِهِ إِنَّا لَنَرَاكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٦٠﴾
60. Wakasema wakuu katika kaumu yake: Hakika sisi tunakuona umo katika upotofu bayana.
قَالَ يَا قَوْمِ لَيْسَ بِي ضَلَالَةٌ وَلَـٰكِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦١﴾
61. (Nuwh) akasema: Enyi kaumu yangu! Mimi siko katika upotofu lakini mimi ni Rasuli kutoka kwa Rabb wa walimwengu.
أُبَلِّغُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَأَنصَحُ لَكُمْ وَأَعْلَمُ مِنَ اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٦٢﴾
62. Nakubalighishieni Risala za Rabb wangu na nakunasihini, na ninajua kutoka kwa Allaah msiyoyajua.
أَوَعَجِبْتُمْ أَن جَاءَكُمْ ذِكْرٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنكُمْ لِيُنذِرَكُمْ وَلِتَتَّقُوا وَلَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٦٣﴾
63. Je, mmestaajabu kwamba umekujieni ukumbusho kutoka kwa Rabb wenu kupitia kwa mtu miongoni mwenu ili akuonyeni na ili muwe na taqwa na mpate kurehemewa?
فَكَذَّبُوهُ فَأَنجَيْنَاهُ وَالَّذِينَ مَعَهُ فِي الْفُلْكِ وَأَغْرَقْنَا الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا عَمِينَ ﴿٦٤﴾
64. Basi walimkadhibisha na Tukamuokoa pamoja na wale waliokuwa naye katika jahazi, na Tukawagharikisha wale waliokadhibisha Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) Zetu. Hakika wao walikuwa watu vipofu.
وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۚ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٦٥﴾
65. Na kwa ‘Aad[16] (Tuliwapelekea) kaka yao Huwd. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Je, basi hamtokuwa na taqwa?
قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ إِنَّا لَنَرَاكَ فِي سَفَاهَةٍ وَإِنَّا لَنَظُنُّكَ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٦٦﴾
66. Wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake: Hakika sisi tunakuona umo katika upumbavu, na sisi tuna yakini wewe ni miongoni mwa waongo.
قَالَ يَا قَوْمِ لَيْسَ بِي سَفَاهَةٌ وَلَـٰكِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦٧﴾
67. (Huwd) akasema: Enyi kaumu yangu! Mimi sina upumbavu lakini mimi ni Rasuli kutoka kwa Rabb wa walimwengu.
أُبَلِّغُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَأَنَا لَكُمْ نَاصِحٌ أَمِينٌ ﴿٦٨﴾
68. Nakubalighishieni Risala za Rabb wangu, nami kwenu ni mtoaji nasiha mwaminifu.
أَوَعَجِبْتُمْ أَن جَاءَكُمْ ذِكْرٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنكُمْ لِيُنذِرَكُمْ ۚ وَاذْكُرُوا إِذْ جَعَلَكُمْ خُلَفَاءَ مِن بَعْدِ قَوْمِ نُوحٍ وَزَادَكُمْ فِي الْخَلْقِ بَسْطَةً ۖ فَاذْكُرُوا آلَاءَ اللَّـهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٦٩﴾
69. Je, mmestaajabu kwamba umekujieni ukumbusho kutoka kwa Rabb wenu kupitia kwa mtu miongoni mwenu ili akuonyeni? Na kumbukeni Alipokufanyeni warithi baada ya kaumu ya Nuwh, na Akakuzidisheni kwa maumbo (ya mwili) na nguvu. Basi kumbukeni Neema Nyingi za Allaah mpate kufaulu.
قَالُوا أَجِئْتَنَا لِنَعْبُدَ اللَّـهَ وَحْدَهُ وَنَذَرَ مَا كَانَ يَعْبُدُ آبَاؤُنَا ۖ فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٧٠﴾
70. Wakasema: Je, umetujia ili tumwabudu Allaah Pekee na tuache yale waliyokuwa wakiabudu baba zetu? Basi tuletee hayo unayotutishia ukiwa ni miongoni mwa wakweli.
قَالَ قَدْ وَقَعَ عَلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ رِجْسٌ وَغَضَبٌ ۖ أَتُجَادِلُونَنِي فِي أَسْمَاءٍ سَمَّيْتُمُوهَا أَنتُمْ وَآبَاؤُكُم مَّا نَزَّلَ اللَّـهُ بِهَا مِن سُلْطَانٍ ۚ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ ﴿٧١﴾
71. (Huwd) akasema: Kwa yakini imekwishakuangukieni adhabu na ghadhabu kutoka kwa Rabb wenu. Je, mnabishana nami kuhusu majina (ya masanamu) mliyoyaita nyinyi na baba zenu bila ya Allaah kuyateremshia kwayo mamlaka? Basi ngojeeni, hakika mimi niko pamoja nanyi katika wanaongojea.
فَأَنجَيْنَاهُ وَالَّذِينَ مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَقَطَعْنَا دَابِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۖ وَمَا كَانُوا مُؤْمِنِينَ ﴿٧٢﴾
72. Basi Tukamuokoa (Huwd) na wale waliokuwa pamoja naye kwa Rehma kutoka Kwetu na Tukakata mizizi ya wale waliokadhibisha Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) Zetu na hawakuwa wenye kuamini.
وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ قَدْ جَاءَتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ هَـٰذِهِ نَاقَةُ اللَّـهِ لَكُمْ آيَةً ۖ فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللَّـهِ ۖ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٣﴾
73. Na kwa Thamuwd[17] (Tuliwapelekea) kaka yao Swaalih. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Kwa yakini imekujieni hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu. Huyu ngamia jike wa Allaah ni Aayah (Ishara, Dalili, Hoja) kwenu. Basi muacheni ale katika Ardhi ya Allaah, na wala msimguse kwa uovu isije ikakuchukueni adhabu iumizayo.
وَاذْكُرُوا إِذْ جَعَلَكُمْ خُلَفَاءَ مِن بَعْدِ عَادٍ وَبَوَّأَكُمْ فِي الْأَرْضِ تَتَّخِذُونَ مِن سُهُولِهَا قُصُورًا وَتَنْحِتُونَ الْجِبَالَ بُيُوتًا ۖ فَاذْكُرُوا آلَاءَ اللَّـهِ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿٧٤﴾
74. Na kumbukeni Alipokufanyeni warithi baada ya ‘Aad, Akakufanyieni makazi katika ardhi mnajenga katika nyanda zake tambarare majumba ya fakhari na mnachonga majumba katika majabali. Basi kumbukeni Neema Nyingi za Allaah na wala msifanye vitendo vya hujuma katika ardhi mkifisidi.
قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا مِن قَوْمِهِ لِلَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا لِمَنْ آمَنَ مِنْهُمْ أَتَعْلَمُونَ أَنَّ صَالِحًا مُّرْسَلٌ مِّن رَّبِّهِ ۚ قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلَ بِهِ مُؤْمِنُونَ ﴿٧٥﴾
75. Wakasema wakuu waliotakabari katika kaumu yake kuwaambia wale waliokandamizwa ambao wameamini miongoni mwao: Kwa uhakika gani mnajua kwamba Swaalih ametumwa kutoka kwa Rabb wake? Wakasema: Hakika sisi tunayaamini aliyotumwa nayo.
قَالَ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا بِالَّذِي آمَنتُم بِهِ كَافِرُونَ ﴿٧٦﴾
76. Wakasema wale waliotakabari: Basi sisi tunayakanusha hayo mliyoyaamini.
فَعَقَرُوا النَّاقَةَ وَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ وَقَالُوا يَا صَالِحُ ائْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٧٧﴾
77. Wakamuua yule ngamia jike na wakaasi Amri ya Rabb wao, na wakasema: Ee Swaalih, tuletee hayo unayotutishia ukiwa ni miongoni mwa Rusuli.
فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٧٨﴾
78. Basi likawachukua tetemeko la ardhi wakawa majumbani mwao wameanguka kifudifudi (wamekufa).
فَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا قَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَةَ رَبِّي وَنَصَحْتُ لَكُمْ وَلَـٰكِن لَّا تُحِبُّونَ النَّاصِحِينَ ﴿٧٩﴾
79. (Swaalih) akajitenga nao na akasema: Enyi kaumu yangu! Kwa yakini nilishakubalighishieni Risala ya Rabb wangu na nilikunasihini, lakini nyinyi hamuwapendi wenye kunasihi.
وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنْ أَحَدٍ مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿٨٠﴾
80. Na (Tulimtuma) Luutw[18], alipowaambia kaumu yake: Je, mnafanya uchafu (wa liwati) ambao hajakutangulieni nao yeyote katika walimwengu?
إِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ شَهْوَةً مِّن دُونِ النِّسَاءِ ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ ﴿٨١﴾
81. Hakika nyinyi mnawaingilia wanaume kwa matamanio badala ya wanawake? Bali nyinyi ni watu wapindukiaji mipaka.
وَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَن قَالُوا أَخْرِجُوهُم مِّن قَرْيَتِكُمْ ۖ إِنَّهُمْ أُنَاسٌ يَتَطَهَّرُونَ ﴿٨٢﴾
82. Na halikuwa jibu la kaumu yake isipokuwa walisema: Wafukuzeni kutoka mji wenu, kwani wao eti ni watu wanaojitakasa.
فَأَنجَيْنَاهُ وَأَهْلَهُ إِلَّا امْرَأَتَهُ كَانَتْ مِنَ الْغَابِرِينَ ﴿٨٣﴾
83. Basi Tukamuokoa (Luutw) na ahli yake isipokuwa mkewe alikuwa miongoni mwa waliobaki nyuma.
وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُجْرِمِينَ ﴿٨٤﴾
84. Na Tukawanyeshea mvua, (ya mawe). Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya wahalifu.
وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ قَدْ جَاءَتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ فَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٨٥﴾
85. Na kwa (watu wa) Madyan[19] (Tuliwapelekea) kaka yao Shu’ayb. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Kwa yakini imekujieni hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu. Basi timizeni kipimo na mizani wala msipunje watu vitu vyao wala msifanye ufisadi ardhini baada ya (Allaah) kuitengeneza vyema. Hivyo ni bora kwenu ikiwa mmeamini.
وَلَا تَقْعُدُوا بِكُلِّ صِرَاطٍ تُوعِدُونَ وَتَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ مَنْ آمَنَ بِهِ وَتَبْغُونَهَا عِوَجًا ۚ وَاذْكُرُوا إِذْ كُنتُمْ قَلِيلًا فَكَثَّرَكُمْ ۖ وَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ ﴿٨٦﴾
86. Na wala msikae katika kila njia kutisha watu na kuwazuilia Njia ya Allaah wale wenye kumuamini, na huku mnaitafutia upogo. Na kumbukeni mlipokuwa wachache Akakukithirisheni. Na tazameni vipi ilikuwa hatima ya mafisadi.
وَإِن كَانَ طَائِفَةٌ مِّنكُمْ آمَنُوا بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ وَطَائِفَةٌ لَّمْ يُؤْمِنُوا فَاصْبِرُوا حَتَّىٰ يَحْكُمَ اللَّـهُ بَيْنَنَا ۚ وَهُوَ خَيْرُ الْحَاكِمِينَ ﴿٨٧﴾
87. Na kama liko kundi miongoni mwenu limeamini yale niliyotumwa nayo na kundi halikuamini, basi subirini mpaka Allaah Ahukumu baina yetu. Naye Ndiye Mbora wa Kuhukumu kuliko wote.
قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا مِن قَوْمِهِ لَنُخْرِجَنَّكَ يَا شُعَيْبُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَكَ مِن قَرْيَتِنَا أَوْ لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَا ۚ قَالَ أَوَلَوْ كُنَّا كَارِهِينَ ﴿٨٨﴾
88. Wakasema wakuu waliotakabari katika kaumu yake: Lazima tutakutoa ewe Shua’yb na wale walioamini pamoja nawe kutoka mji wetu, au mrejee katika mila yetu. (Shu’ayb) akasema: Hata kwa kulazimishwa bila kuiridhia?
قَدِ افْتَرَيْنَا عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا إِنْ عُدْنَا فِي مِلَّتِكُم بَعْدَ إِذْ نَجَّانَا اللَّـهُ مِنْهَا ۚ وَمَا يَكُونُ لَنَا أَن نَّعُودَ فِيهَا إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّنَا ۚ وَسِعَ رَبُّنَا كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا ۚ عَلَى اللَّـهِ تَوَكَّلْنَا ۚ رَبَّنَا افْتَحْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمِنَا بِالْحَقِّ وَأَنتَ خَيْرُ الْفَاتِحِينَ ﴿٨٩﴾
89. Kwa yakini itakuwa tumemtungia Allaah uongo ikiwa tutarudi katika mila yenu baada ya Allaah kutuokoa nayo. Na haiwi kwetu kurejea humo isipokuwa Akitaka Allaah Rabb wetu. Rabb wetu Amekienea kila kitu kwa ujuzi. Kwa Allaah tunatawakali. Rabb wetu! Hukumu baina yetu na baina ya kaumu yetu kwa haki, Nawe Ndiye Mbora wa kuhukumu kuliko wote.
وَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ لَئِنِ اتَّبَعْتُمْ شُعَيْبًا إِنَّكُمْ إِذًا لَّخَاسِرُونَ ﴿٩٠﴾
90. Na wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake: Mkimfuata Shu’ayb hakika hapo mtakuwa bila shaka wenye kukhasirika.
فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٩١﴾
91. Basi likawachukua tetemeko la ardhi wakawa majumbani mwao wameanguka kifudifudi (wamekufa).
الَّذِينَ كَذَّبُوا شُعَيْبًا كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۚ الَّذِينَ كَذَّبُوا شُعَيْبًا كَانُوا هُمُ الْخَاسِرِينَ ﴿٩٢﴾
92. Wale waliomkadhibisha Shu’ayb (wakawa) kama kwamba hawakuishi wakineemeka humo. Waliomkadhibisha Shu’ayb wakawa ndio wenye kukhasirika.
فَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا قَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَنَصَحْتُ لَكُمْ ۖ فَكَيْفَ آسَىٰ عَلَىٰ قَوْمٍ كَافِرِينَ ﴿٩٣﴾
93. Basi (Shu’ayb) akajitenga nao na akasema: Enyi kaumu yangu! Kwa yakini nimekubalighishieni Risala za Rabb wangu na nimekunasihini, basi vipi niwe na majonzi juu ya watu makafiri?
وَمَا أَرْسَلْنَا فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّبِيٍّ إِلَّا أَخَذْنَا أَهْلَهَا بِالْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَضَّرَّعُونَ ﴿٩٤﴾
94. Na Hatukutuma katika mji Nabiy yeyote (akakanushwa) isipokuwa Tunawashika watu wake kwa dhiki za ufukara, na maafa ya magonjwa na njaa, huenda wapate kunyenyekea (kwa Allaah).
ثُمَّ بَدَّلْنَا مَكَانَ السَّيِّئَةِ الْحَسَنَةَ حَتَّىٰ عَفَوا وَّقَالُوا قَدْ مَسَّ آبَاءَنَا الضَّرَّاءُ وَالسَّرَّاءُ فَأَخَذْنَاهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٩٥﴾
95. Kisha Tukabadilisha mahali pa hali mbaya kwa hali nzuri hata wakaongezeka na kutengenekewa na maisha. Hapo wakasema: Hata baba zetu pia yaliwagusa madhara na raha. Basi Tukawachukuwa ghafla nao huku hawahisi.
وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَىٰ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِم بَرَكَاتٍ مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَـٰكِن كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُم بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿٩٦﴾
96. Na lau kama watu wa miji wangeliamimi na wakashikamana na taqwa, Tungeliwafungulia baraka tele kutoka mbinguni na ardhini, lakini walikadhibisha, Nasi Tukawachukua kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.
أَفَأَمِنَ أَهْلُ الْقُرَىٰ أَن يَأْتِيَهُم بَأْسُنَا بَيَاتًا وَهُمْ نَائِمُونَ ﴿٩٧﴾
97. Je, watu wa miji wameaminisha ya kuwa haitowafikia Adhabu Yetu wakati wa usiku hali wao wamelala?
أَوَأَمِنَ أَهْلُ الْقُرَىٰ أَن يَأْتِيَهُم بَأْسُنَا ضُحًى وَهُمْ يَلْعَبُونَ ﴿٩٨﴾
98. Au watu wa miji wameaminisha ya kuwa haitowafikia Adhabu Yetu wakati wa kabla ya mchana hali wao wanacheza?
أَفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّـهِ ۚ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٩٩﴾
99. Je, wameaminisha Mipango ya (adhabu za) Allaah? Basi hawaaminishi Mipango ya Allaah isipokuwa watu wenye kukhasirika.
أَوَلَمْ يَهْدِ لِلَّذِينَ يَرِثُونَ الْأَرْضَ مِن بَعْدِ أَهْلِهَا أَن لَّوْ نَشَاءُ أَصَبْنَاهُم بِذُنُوبِهِمْ ۚ وَنَطْبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ ﴿١٠٠﴾
100. Je, haikuwabainikia wale wanaorithi ardhi baada ya watu wake (walioangamizwa) kwamba lau Tungelitaka Tungeliwasibu kwa dhambi zao! Na Tutapiga chapa juu ya nyoyo zao wasisikie tena?
تِلْكَ الْقُرَىٰ نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنبَائِهَا ۚ وَلَقَدْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا بِمَا كَذَّبُوا مِن قَبْلُ ۚ كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِ الْكَافِرِينَ ﴿١٠١﴾
101. Hiyo ni miji Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) baadhi ya khabari zake. Na kwa yakini waliwajia Rusuli wao kwa hoja bayana, lakini hawakuwa wenye kuamini yale waliyoyakadhibisha kabla. Hivyo ndivyo Allaah Anavyopiga chapa juu ya nyoyo za makafiri.
وَمَا وَجَدْنَا لِأَكْثَرِهِم مِّنْ عَهْدٍ ۖ وَإِن وَجَدْنَا أَكْثَرَهُمْ لَفَاسِقِينَ ﴿١٠٢﴾
102. Na Hatukuwakuta wengi wao kuwa ni wakweli wa ahadi. Bali kwa yakini Tumewakuta wengi wao ni mafasiki.
ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِم مُّوسَىٰ بِآيَاتِنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَظَلَمُوا بِهَا ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ ﴿١٠٣﴾
103. Kisha Tukamtuma baada yao Muwsaa na Aayaat (Ishara, Dalili, Miujiza) Yetu kwa Firawni[20] na wakuu wake nao wakaipinga na kukataa. Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya mafisadi.
وَقَالَ مُوسَىٰ يَا فِرْعَوْنُ إِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٠٤﴾
104. Na Muwsaa akasema: Ee Firawni! Hakika mimi ni Rasuli kutoka kwa Rabb wa walimwengu.
حَقِيقٌ عَلَىٰ أَن لَّا أَقُولَ عَلَى اللَّـهِ إِلَّا الْحَقَّ ۚ قَدْ جِئْتُكُم بِبَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ فَأَرْسِلْ مَعِيَ بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿١٠٥﴾
105. Napaswa nisiseme juu ya Allaah isipokuwa ya haki. Kwa yakini nimekujieni kwa hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu, basi waachie wana wa Israaiyl wawe pamoja nami.
قَالَ إِن كُنتَ جِئْتَ بِآيَةٍ فَأْتِ بِهَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿١٠٦﴾
106. (Firawni) akasema: Ikiwa umekuja na Aayah (Ishara, Ushahidi, Hoja) yoyote basi ilete, ukiwa ni miongoni mwa wakweli.
فَأَلْقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعْبَانٌ مُّبِينٌ ﴿١٠٧﴾
107. Basi (Muwsaa) akaitupa fimbo yake, na mara tahamaki imegeuka joka la kweli.
وَنَزَعَ يَدَهُ فَإِذَا هِيَ بَيْضَاءُ لِلنَّاظِرِينَ ﴿١٠٨﴾
108. Na akatoa mkono wake, mara tahamaki umekuwa mweupe (unang’ara) kwa watazamao.
قَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ عَلِيمٌ ﴿١٠٩﴾
109. Wakasema wakuu katika kaumu ya Firawni: Bila shaka huyu ni mchawi mjuzi.
يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُمْ ۖ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ ﴿١١٠﴾
110. Anataka kukutoeni kutoka ardhini mwenu, basi mnaamrisha nini?
قَالُوا أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَأَرْسِلْ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ ﴿١١١﴾
111. Wakasema: Muahirishe kidogo na kaka yake na tuma katika miji wenye kukusanya.
يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَاحِرٍ عَلِيمٍ ﴿١١٢﴾
112. Wakuletee kila mchawi mjuzi.
وَجَاءَ السَّحَرَةُ فِرْعَوْنَ قَالُوا إِنَّ لَنَا لَأَجْرًا إِن كُنَّا نَحْنُ الْغَالِبِينَ ﴿١١٣﴾
113. Wakaja wachawi kwa Firawni, wakasema: Je, tutapata ujira ikiwa sisi tutashinda?
قَالَ نَعَمْ وَإِنَّكُمْ لَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ ﴿١١٤﴾
114. (Firawni) akasema: Naam! Bila shaka nanyi mtakuwa miongoni mwa waliokurubishwa (kwangu).
قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِمَّا أَن تُلْقِيَ وَإِمَّا أَن نَّكُونَ نَحْنُ الْمُلْقِينَ ﴿١١٥﴾
115. (Wachawi) wakasema: Ee Muwsaa, ima utupe wewe au tuanze sisi kutupa?
قَالَ أَلْقُوا ۖ فَلَمَّا أَلْقَوْا سَحَرُوا أَعْيُنَ النَّاسِ وَاسْتَرْهَبُوهُمْ وَجَاءُوا بِسِحْرٍ عَظِيمٍ ﴿١١٦﴾
116. (Muwsaa) akasema: Tupeni! Basi walipotupa, waliyasihiri macho ya watu na wakawatia woga, na wakaja na sihiri kubwa mno.
وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنْ أَلْقِ عَصَاكَ ۖ فَإِذَا هِيَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ ﴿١١٧﴾
117. Na Tukamtia ilhamu Muwsaa ya kwamba: Tupa fimbo yako! Mara tahamaki ikameza vyote walivyovibuni.
فَوَقَعَ الْحَقُّ وَبَطَلَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١١٨﴾
118. Ukweli ukathibiti na yakabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.
فَغُلِبُوا هُنَالِكَ وَانقَلَبُوا صَاغِرِينَ ﴿١١٩﴾
119. Wakashindwa hapo, na wakageuka kuwa wenye kudhalilika.
وَأُلْقِيَ السَّحَرَةُ سَاجِدِينَ ﴿١٢٠﴾
120. Na wachawi wakajiangusha wakisujudu.
قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٢١﴾
121. Wakasema: Tumemwamini Rabb wa walimwengu.
رَبِّ مُوسَىٰ وَهَارُونَ ﴿١٢٢﴾
122. Rabb wa Muwsaa na Haaruwn.
قَالَ فِرْعَوْنُ آمَنتُم بِهِ قَبْلَ أَنْ آذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَمَكْرٌ مَّكَرْتُمُوهُ فِي الْمَدِينَةِ لِتُخْرِجُوا مِنْهَا أَهْلَهَا ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿١٢٣﴾
123. Firawni akasema: Je, mumemwamini kabla sijakupeni ruhusa? Hakika hii bila shaka ni makri mliyoipanga (na Muwsaa) katika mji ili muwatoe watu wake humo. Basi mtanitambua!
لَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَافٍ ثُمَّ لَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿١٢٤﴾
124. Nitaikatakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutofautisha[21] kisha nitakusulubuni vibaya nyote.
قَالُوا إِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ ﴿١٢٥﴾
125. (Wachawi) wakasema: Hakika sisi kwa Rabb wetu tutarudi.
وَمَا تَنقِمُ مِنَّا إِلَّا أَنْ آمَنَّا بِآيَاتِ رَبِّنَا لَمَّا جَاءَتْنَا ۚ رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَتَوَفَّنَا مُسْلِمِينَ ﴿١٢٦﴾
126. Na huchukizwi nasi isipokuwa tu kwa kuwa tumeamini Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) za Rabb wetu zilipotujia. Ee Rabb wetu! Tumiminie subira na Tufishe tukiwa Waislamu.
وَقَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوْمَهُ لِيُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَيَذَرَكَ وَآلِهَتَكَ ۚ قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبْنَاءَهُمْ وَنَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ وَإِنَّا فَوْقَهُمْ قَاهِرُونَ ﴿١٢٧﴾
127. Na wakasema wakuu katika kaumu ya Firawni: Je, unamwacha Muwsaa na kaumu yake wafisidi katika ardhi, na akuache wewe na waabudiwa wako? (Firawni) akasema: Tutawaua watoto wao wa kiume na tutaacha hai wanawake wao, na hakika sisi ni wenye kushinda nguvu juu yao.
قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ اسْتَعِينُوا بِاللَّـهِ وَاصْبِرُوا ۖ إِنَّ الْأَرْضَ لِلَّـهِ يُورِثُهَا مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ ﴿١٢٨﴾
128. Muwsaa akawaambia kaumu yake: Ombeni msaada kwa Allaah na vuteni subira. Hakika ardhi ni ya Allaah, Humrithisha Amtakaye katika Waja Wake. Na mwisho (mzuri) ni kwa wenye taqwa.
قَالُوا أُوذِينَا مِن قَبْلِ أَن تَأْتِيَنَا وَمِن بَعْدِ مَا جِئْتَنَا ۚ قَالَ عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُهْلِكَ عَدُوَّكُمْ وَيَسْتَخْلِفَكُمْ فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ ﴿١٢٩﴾
129. Wakasema: Tumeudhiwa kabla ya kutujia na baada ya kutujia. (Muwsaa) akasema: Asaa Rabb wenu Akamuangamiza adui yenu na Akufanyeni watawala katika nchi, Atazame mtakavyotenda.
وَلَقَدْ أَخَذْنَا آلَ فِرْعَوْنَ بِالسِّنِينَ وَنَقْصٍ مِّنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ ﴿١٣٠﴾
130. Na kwa yakini Tuliwatia majaribuni watu wa Firawni kwa ukame na upungufu wa mazao ili wapate kukumbuka.[22]
فَإِذَا جَاءَتْهُمُ الْحَسَنَةُ قَالُوا لَنَا هَـٰذِهِ ۖ وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ يَطَّيَّرُوا بِمُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُ ۗ أَلَا إِنَّمَا طَائِرُهُمْ عِندَ اللَّـهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٣١﴾
131. Na likiwajia zuri husema: Hili letu. Na likiwasibu ovu basi hunasibisha nuksi kwa Muwsaa na walio pamoja naye. Tanabahi! Hakika nuksi yao iko kwa Allaah lakini wengi wao hawajui.
وَقَالُوا مَهْمَا تَأْتِنَا بِهِ مِنْ آيَةٍ لِّتَسْحَرَنَا بِهَا فَمَا نَحْنُ لَكَ بِمُؤْمِنِينَ ﴿١٣٢﴾
132. Na wakasema: Hata ukituletea Aayah (Ishara, Dalili, Hoja) yoyote ile ili utusihiri nayo, basi sisi hatutokuamini.
فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الطُّوفَانَ وَالْجَرَادَ وَالْقُمَّلَ وَالضَّفَادِعَ وَالدَّمَ آيَاتٍ مُّفَصَّلَاتٍ فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا مُّجْرِمِينَ ﴿١٣٣﴾
133. Tukawapelekea tufani na nzige na chawa na vyura na damu kama Aayaat (Ishara, Hoja, Dalili) za wazi bainifu, lakini walitakabari wakawa watu wahalifu.[23]
وَلَمَّا وَقَعَ عَلَيْهِمُ الرِّجْزُ قَالُوا يَا مُوسَى ادْعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَ ۖ لَئِن كَشَفْتَ عَنَّا الرِّجْزَ لَنُؤْمِنَنَّ لَكَ وَلَنُرْسِلَنَّ مَعَكَ بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿١٣٤﴾
134. Na kila ilipowaangukia adhabu walisema: Ee Muwsaa! Tuombee kwa Rabb wako kwa yale Aliyokuahidi. Ukituondolea adhabu, bila shaka tutakuamini na bila shaka tutawaachia wana Israaiyl (waondoke) pamoja nawe.
فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُمُ الرِّجْزَ إِلَىٰ أَجَلٍ هُم بَالِغُوهُ إِذَا هُمْ يَنكُثُونَ ﴿١٣٥﴾
135. Tulipowaondolea adhabu mpaka muda maalumu wao waufikie, tahamaki wao wanavunja ahadi.
فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ بِأَنَّهُمْ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا عَنْهَا غَافِلِينَ ﴿١٣٦﴾
136. Basi Tukawalipiza, Tukawagharikisha baharini kwa kuwa wao walikadhibisha Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) Zetu na walikuwa ni wenye kughafilika nazo.
وَأَوْرَثْنَا الْقَوْمَ الَّذِينَ كَانُوا يُسْتَضْعَفُونَ مَشَارِقَ الْأَرْضِ وَمَغَارِبَهَا الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا ۖ وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ الْحُسْنَىٰ عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ بِمَا صَبَرُوا ۖ وَدَمَّرْنَا مَا كَانَ يَصْنَعُ فِرْعَوْنُ وَقَوْمُهُ وَمَا كَانُوا يَعْرِشُونَ ﴿١٣٧﴾
137. Na Tukawarithisha watu waliokuwa wakikandamizwa Mashariki ya ardhi na Magharibi yake ambayo Tumeibariki. Na likatimia Neno Zuri la Rabb wako kwa wana wa Israaiyl kwa kule kuvuta subira kwao. Na Tukayadamirisha yale aliyokuwa Firawni na kaumu yake wakiyaamirisha na yale waliyokuwa wakiyajenga.
وَجَاوَزْنَا بِبَنِي إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَأَتَوْا عَلَىٰ قَوْمٍ يَعْكُفُونَ عَلَىٰ أَصْنَامٍ لَّهُمْ ۚ قَالُوا يَا مُوسَى اجْعَل لَّنَا إِلَـٰهًا كَمَا لَهُمْ آلِهَةٌ ۚ قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ تَجْهَلُونَ ﴿١٣٨﴾
138. Na Tukawavusha wana wa Israaiyl bahari. Wakawafikia watu waliokuwa wanasabilia kwa utiifu masanamu yao. Wakasema: Ee Muwsaa! Tufanyie nasi mwabudiwa kama walivyokuwa hao wana waabudiwa. (Muwsaa) akasema: Hakika nyinyi ni watu mfanyao ujinga.
إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ مُتَبَّرٌ مَّا هُمْ فِيهِ وَبَاطِلٌ مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٣٩﴾
139. Hakika hawa yatateketezwa waliyo nayo, na ni batili waliyokuwa wakiyatenda.
قَالَ أَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْغِيكُمْ إِلَـٰهًا وَهُوَ فَضَّلَكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿١٤٠﴾
140. (Muwsaa) akasema: Je, nikutafutieni mwabudiwa ghairi ya Allaah, na hali Yeye Amekufadhilisheni juu ya walimwengu?
وَإِذْ أَنجَيْنَاكُم مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ ۖ يُقَتِّلُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ ۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَاءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ ﴿١٤١﴾
141. Na Tulipokuokoeni kutoka kwa watu wa Firawni walipokusibuni adhabu mbaya, wakiwaua watoto wenu wa kiume na wakiacha hai wanawake wenu, na katika hayo ulikuwa ni mtihani mkuu kwenu kutoka kwa Rabb wenu.
وَوَاعَدْنَا مُوسَىٰ ثَلَاثِينَ لَيْلَةً وَأَتْمَمْنَاهَا بِعَشْرٍ فَتَمَّ مِيقَاتُ رَبِّهِ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً ۚ وَقَالَ مُوسَىٰ لِأَخِيهِ هَارُونَ اخْلُفْنِي فِي قَوْمِي وَأَصْلِحْ وَلَا تَتَّبِعْ سَبِيلَ الْمُفْسِدِينَ ﴿١٤٢﴾
142. Na Tukamuahidi Muwsaa masiku thelathini na Tukayatimiza kwa kumi, na ukatimia muda wa miadi wa Rabb wake siku arubaini. Muwsaa akamwambia kaka yake Haaruwn: Kuwa kaimu wangu kwa watu wangu na tengeneza, na wala usifuate njia ya mafisadi.
وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ قَالَ رَبِّ أَرِنِي أَنظُرْ إِلَيْكَ ۚ قَالَ لَن تَرَانِي وَلَـٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي ۚ فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقًا ۚ فَلَمَّا أَفَاقَ قَالَ سُبْحَانَكَ تُبْتُ إِلَيْكَ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٤٣﴾
143. Na alipokuja Muwsaa katika pahala kwa muda maalumu ya Miadi Yetu, na Rabb wake Akamsemesha[24], akasema Rabb wangu! Nionyeshe ili nikutazame. (Allaah) Akasema: Hutoniona! Lakini tazama mlima. Ukitulia mahali pake, basi utaniona. Basi Rabb wake Alipojidhihirisha katika mlima, Aliufanya uvurugike kuwa vumbi, na Muwsaa akaanguka hali ya kuzimia. Alipozindukana akasema: Subhaanak! (Utakasifu ni Wako!) Nimetubu Kwako, nami ni wa kwanza wa wanaoamini.
قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنِّي اصْطَفَيْتُكَ عَلَى النَّاسِ بِرِسَالَاتِي وَبِكَلَامِي فَخُذْ مَا آتَيْتُكَ وَكُن مِّنَ الشَّاكِرِينَ ﴿١٤٤﴾
144. (Allaah) Akasema: Ee Muwsaa hakika Mimi Nimekukhitari juu ya watu kwa Risala Zangu na Maneno Yangu. Basi pokea Niliyokupa na kuwa miongoni mwa wanaoshukuru.
وَكَتَبْنَا لَهُ فِي الْأَلْوَاحِ مِن كُلِّ شَيْءٍ مَّوْعِظَةً وَتَفْصِيلًا لِّكُلِّ شَيْءٍ فَخُذْهَا بِقُوَّةٍ وَأْمُرْ قَوْمَكَ يَأْخُذُوا بِأَحْسَنِهَا ۚ سَأُرِيكُمْ دَارَ الْفَاسِقِينَ ﴿١٤٥﴾
145. Na Tukamwandikia kwenye vibao kila kitu; mawaidha na tafsili ya waziwazi ya kila kitu. (Tukamwambia): Basi yashikilie kwa nguvu na uwaamrishe watu wako wayashike mazuri yake. Nitakuonyesheni miji ya mafasiki.
سَأَصْرِفُ عَنْ آيَاتِيَ الَّذِينَ يَتَكَبَّرُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَإِن يَرَوْا كُلَّ آيَةٍ لَّا يُؤْمِنُوا بِهَا وَإِن يَرَوْا سَبِيلَ الرُّشْدِ لَا يَتَّخِذُوهُ سَبِيلًا وَإِن يَرَوْا سَبِيلَ الْغَيِّ يَتَّخِذُوهُ سَبِيلًا ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا عَنْهَا غَافِلِينَ ﴿١٤٦﴾
146. Nitawaepusha na Aayaat (na Ishara, Dalili, Hukmu, Hoja) Zangu wale waliotakabari katika ardhi bila ya haki. Na wanapoona kila Aayah (Ishara, Dalili) hawaiamini. Na wanapoona njia ya uongofu hawaishiki kuwa ndio njia. Na wanapoona njia ya upotofu wanaishika kuwa ndio njia. Hivyo ni kwa kuwa wao walikadhibisha Aayaat Zetu na walikuwa wenye kughafilika nazo.
وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَلِقَاءِ الْآخِرَةِ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ ۚ هَلْ يُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٤٧﴾
147. Na wale waliokadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) Zetu na makutano ya Aakhirah, zimeporomoka amali zao. Je, kwani watalipwa isipokuwa yale waliyokuwa wakiyatenda?
وَاتَّخَذَ قَوْمُ مُوسَىٰ مِن بَعْدِهِ مِنْ حُلِيِّهِمْ عِجْلًا جَسَدًا لَّهُ خُوَارٌ ۚ أَلَمْ يَرَوْا أَنَّهُ لَا يُكَلِّمُهُمْ وَلَا يَهْدِيهِمْ سَبِيلًا ۘ اتَّخَذُوهُ وَكَانُوا ظَالِمِينَ ﴿١٤٨﴾
148. Na watu wa Muwsaa baada ya kuondoka kwake, walijifanyia ndama; kiwiliwili chenye sauti ya ng’ombe kwa kutumia mapambo yao. Je, hawakuona kwamba huyo (ndama) hawasemeshi wala hawaongozi njia? Walimfanya (mwabudiwa) na wakawa madhalimu.[25]
وَلَمَّا سُقِطَ فِي أَيْدِيهِمْ وَرَأَوْا أَنَّهُمْ قَدْ ضَلُّوا قَالُوا لَئِن لَّمْ يَرْحَمْنَا رَبُّنَا وَيَغْفِرْ لَنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿١٤٩﴾
149. Na walipopatwa na majuto na wakaona kwamba kwa yakini wamepotoka walisema: Asipoturehemu Rabb wetu na Akatughufuria, bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliokhasirika.
وَلَمَّا رَجَعَ مُوسَىٰ إِلَىٰ قَوْمِهِ غَضْبَانَ أَسِفًا قَالَ بِئْسَمَا خَلَفْتُمُونِي مِن بَعْدِي ۖ أَعَجِلْتُمْ أَمْرَ رَبِّكُمْ ۖ وَأَلْقَى الْأَلْوَاحَ وَأَخَذَ بِرَأْسِ أَخِيهِ يَجُرُّهُ إِلَيْهِ ۚ قَالَ ابْنَ أُمَّ إِنَّ الْقَوْمَ اسْتَضْعَفُونِي وَكَادُوا يَقْتُلُونَنِي فَلَا تُشْمِتْ بِيَ الْأَعْدَاءَ وَلَا تَجْعَلْنِي مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿١٥٠﴾
150. Na Muwsaa aliporejea kwa kaumu yake hali ya kuwa ameghadhibika na kusikitika, alisema: Ubaya ulioje mmeniwakilisha baada yangu. Je, mmeharakiza Amri ya Rabb wenu? Akatupa vile vibao na akakamata kichwa cha kaka yake akimvuta kwake. (Haaruwn) akasema: Ee mwana wa mama yangu! Hakika watu (hawa) walinizidi nguvu na walikaribia kuniua, basi usinifanye kifurahisho cha maadui, na wala usiniweke pamoja na watu madhalimu.
قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِأَخِي وَأَدْخِلْنَا فِي رَحْمَتِكَ ۖ وَأَنتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ ﴿١٥١﴾
151. (Muwsaa) akasema: Rabb wangu! Nighufurie mimi na kaka yangu, na Utuingize katika Rehma Yako. Nawe Ndiye Mbora zaidi wa Kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu.
إِنَّ الَّذِينَ اتَّخَذُوا الْعِجْلَ سَيَنَالُهُمْ غَضَبٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَذِلَّةٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُفْتَرِينَ ﴿١٥٢﴾
152. Hakika wale waliomchukua ndama (kumwabudu) itawafika ghadhabu kutoka kwa Rabb wao na udhalilifu katika uhai wa dunia. Na hivyo ndivyo Tunavyowalipa watungaji (uongo).
وَالَّذِينَ عَمِلُوا السَّيِّئَاتِ ثُمَّ تَابُوا مِن بَعْدِهَا وَآمَنُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٥٣﴾
153. Na wale waliotenda maovu kisha wakatubu baada yake na wakaamini, hakika Rabb wako baada ya hayo bila shaka Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَلَمَّا سَكَتَ عَن مُّوسَى الْغَضَبُ أَخَذَ الْأَلْوَاحَ ۖ وَفِي نُسْخَتِهَا هُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلَّذِينَ هُمْ لِرَبِّهِمْ يَرْهَبُونَ ﴿١٥٤﴾
154. Na ghadhabu zilipomtulia Muwsaa, alivichukua vile vibao. Na katika maandiko yake mna mwongozo na rehma kwa ambao wao wanamkhofu Rabb wao.
وَاخْتَارَ مُوسَىٰ قَوْمَهُ سَبْعِينَ رَجُلًا لِّمِيقَاتِنَا ۖ فَلَمَّا أَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ قَالَ رَبِّ لَوْ شِئْتَ أَهْلَكْتَهُم مِّن قَبْلُ وَإِيَّايَ ۖ أَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ السُّفَهَاءُ مِنَّا ۖ إِنْ هِيَ إِلَّا فِتْنَتُكَ تُضِلُّ بِهَا مَن تَشَاءُ وَتَهْدِي مَن تَشَاءُ ۖ أَنتَ وَلِيُّنَا فَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا ۖ وَأَنتَ خَيْرُ الْغَافِرِينَ ﴿١٥٥﴾
155. Na Muwsaa akachagua watu sabini wa kaumu yake kwa ajili ya miadi Yetu kukutana kwa wakati na mahali. Kisha lilipowachukua tetemeko la ardhi, (Muwsaa) alisema: “Rabb wangu! Ungelitaka Ungeliwahiliki wao na mimi kabla (ya kutoka). Je, Unatuhiliki kwa yale waliyoyafanya wapumbavu miongoni mwetu? Haya si chochote isipokuwa ni Majaribio Yako. Unampotoa kwayo Umtakaye, na Unamhidi (kwayo) Umtakaye. Wewe Ndiye Mlinzi wetu, basi Tughufurie na Turehemu, Nawe Ni Mbora kuliko wote wenye kughufuria.”
وَاكْتُبْ لَنَا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ إِنَّا هُدْنَا إِلَيْكَ ۚ قَالَ عَذَابِي أُصِيبُ بِهِ مَنْ أَشَاءُ ۖ وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ فَسَأَكْتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالَّذِينَ هُم بِآيَاتِنَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٥٦﴾
156. Na Tuandikie katika dunia hii mazuri na katika Aakhirah. Hakika sisi tumerudi kutubu Kwako. (Allaah) Akasema: Adhabu Yangu Nitamsibu nayo Nimtakaye. Na Rehma Yangu imeenea kila kitu.[26] Basi Nitawaandikia wale wenye taqwa na wanaotoa Zakaah na ambao wao wanaziamini Aayaat, (na Ishara, Hoja, Dalili) Zetu.
الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ يَأْمُرُهُم بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ ۚ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٥٧﴾
157. Wale wanaomfuata Rasuli; Nabiy asiyejua kusoma wala kuandika ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Tawraat na Injiyl, anawaamrisha mema na anawakataza munkari, na anawahalalishia vilivyo vizuri na anawaharamishia vilivyo vibaya na anawaondoshea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao. Basi wale waliomwamini na wakamtukuza, na wakamnusuru na wakafuata Nuru (Qur-aan) ambayo imeteremshwa pamoja naye, hao ndio wenye kufaulu.[27]
قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ الَّذِي يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَكَلِمَاتِهِ وَاتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿١٥٨﴾
158. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Enyi watu! Hakika mimi ni Rasuli wa Allaah kwenu nyinyi nyote.[28] (Allaah) Ambaye ni Wake ufalme wa mbingu na ardhi. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Anahuisha na Anafisha. Basi mwaminini Allaah na Rasuli Wake; Nabiy asiyejua kusoma wala kuandika ambaye anamwamini Allaah na Maneno Yake, na mfuateni ili mpate kuhidika.
وَمِن قَوْمِ مُوسَىٰ أُمَّةٌ يَهْدُونَ بِالْحَقِّ وَبِهِ يَعْدِلُونَ ﴿١٥٩﴾
159. Na katika kaumu ya Muwsaa (walikuweko) ummah wanaongoza kwa haki, na kwayo wanahukumu kiadilifu.
وَقَطَّعْنَاهُمُ اثْنَتَيْ عَشْرَةَ أَسْبَاطًا أُمَمًا ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ إِذِ اسْتَسْقَاهُ قَوْمُهُ أَنِ اضْرِب بِّعَصَاكَ الْحَجَرَ ۖ فَانبَجَسَتْ مِنْهُ اثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْنًا ۖ قَدْ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ ۚ وَظَلَّلْنَا عَلَيْهِمُ الْغَمَامَ وَأَنزَلْنَا عَلَيْهِمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ ۖ كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ ۚ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿١٦٠﴾
160. Na Tukawagawanya makabila kumi na mbili;[29] mataifa mbalimbali (ya Bani Israaiyl). Na Tukamfunulia Wahy Muwsaa walipomuomba maji kaumu yake, kwamba: Piga jiwe kwa fimbo yako. Zikachimbuka toka humo chemchemu kumi na mbili. Kila kabila likajua mahali pake pa kunywea maji. Na Tukawawekea kivuli kwa mawingu na Tukawateremshia al-manna na as-salwaa.[30] (Tukawaambia): Kuleni katika vizuri Tulivyokuruzukuni. Hawakutudhulumu Sisi lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao.
وَإِذْ قِيلَ لَهُمُ اسْكُنُوا هَـٰذِهِ الْقَرْيَةَ وَكُلُوا مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ وَقُولُوا حِطَّةٌ وَادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطِيئَاتِكُمْ ۚ سَنَزِيدُ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٦١﴾
161. Na pale walipoambiwa: Kaeni katika mji huu (Quds), na kuleni humo popote mpendapo, na semeni: Hittwah[31] (Tuondolee uzito wa madhambi) na ingieni katika mlango wake huku mmeinama kwa unyenyekevu. Tutakughufurieni makosa yenu, Tutawazidishia (neema na thawabu) wafanyao ihsaan.
فَبَدَّلَ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ قَوْلًا غَيْرَ الَّذِي قِيلَ لَهُمْ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَظْلِمُونَ ﴿١٦٢﴾
162. Lakini waliodhulumu miongoni mwao walibadilisha kauli tofauti na ile waliyoambiwa, Tukawapelekea adhabu ya kufadhaika kutoka mbinguni kwa sababu ya wao kujidhulumu.
وَاسْأَلْهُمْ عَنِ الْقَرْيَةِ الَّتِي كَانَتْ حَاضِرَةَ الْبَحْرِ إِذْ يَعْدُونَ فِي السَّبْتِ إِذْ تَأْتِيهِمْ حِيتَانُهُمْ يَوْمَ سَبْتِهِمْ شُرَّعًا وَيَوْمَ لَا يَسْبِتُونَ ۙ لَا تَأْتِيهِمْ ۚ كَذَٰلِكَ نَبْلُوهُم بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿١٦٣﴾
163. Na waulize kuhusu mji ambao ulikuwa kando ya bahari, waliporuka mipaka ya As-Sabt[32] walipowajia samaki wao waziwazi siku yao ya As-Sabt lakini siku zisizokuwa za As-Sabt hawakuwajia. Hivyo ndivyo Tulivyowajaribu kutokana na kukhalifu kwao amri.[33]
وَإِذْ قَالَتْ أُمَّةٌ مِّنْهُمْ لِمَ تَعِظُونَ قَوْمًا ۙ اللَّـهُ مُهْلِكُهُمْ أَوْ مُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ قَالُوا مَعْذِرَةً إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿١٦٤﴾
164. Na pale kundi miongoni mwao waliposema: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao Allaah Atawahilikisha tu au Atawaadhibu adhabu kali? Wakasema: Tupate kuwa na udhuru mbele ya Rabb wenu, na huenda wakawa watu wa taqwa.
فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ أَنجَيْنَا الَّذِينَ يَنْهَوْنَ عَنِ السُّوءِ وَأَخَذْنَا الَّذِينَ ظَلَمُوا بِعَذَابٍ بَئِيسٍ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿١٦٥﴾
165. Waliposahau yale waliyokumbushwa nayo, Tuliwaokoa wale wanaokataza uovu, na Tukawachukua wale waliodhulumu kwa adhabu mbaya kabisa kwa sababu ya kukhalifu kwao amri.
فَلَمَّا عَتَوْا عَن مَّا نُهُوا عَنْهُ قُلْنَا لَهُمْ كُونُوا قِرَدَةً خَاسِئِينَ ﴿١٦٦﴾
166. Basi walipozidi kuasi kwenye hilo walilokatazwa, Tulisema: Kuweni manyani waliotezwa!
وَإِذْ تَأَذَّنَ رَبُّكَ لَيَبْعَثَنَّ عَلَيْهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَن يَسُومُهُمْ سُوءَ الْعَذَابِ ۗ إِنَّ رَبَّكَ لَسَرِيعُ الْعِقَابِ ۖ وَإِنَّهُ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٦٧﴾
167. Na pindi Alipotangaza Rabb wako kwamba bila shaka Atawatumia (Mayahudi) watu waliowazidi nguvu, ambao watawaonjesha adhabu mbaya mpaka Siku ya Qiyaamah. Hakika Rabb wako Ni Mwepesi wa Kuakibu, na hakika Yeye bila shaka Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَقَطَّعْنَاهُمْ فِي الْأَرْضِ أُمَمًا ۖ مِّنْهُمُ الصَّالِحُونَ وَمِنْهُمْ دُونَ ذَٰلِكَ ۖ وَبَلَوْنَاهُم بِالْحَسَنَاتِ وَالسَّيِّئَاتِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿١٦٨﴾
168. Na Tuliwafarakisha katika ardhi makundi makundi. Miongoni mwao wako wema na miongoni mwao wako kinyume chake. Na Tukawajaribu kwa ya faraja na ya dhiki ili wapate kurejea (katika utiifu).
فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ وَرِثُوا الْكِتَابَ يَأْخُذُونَ عَرَضَ هَـٰذَا الْأَدْنَىٰ وَيَقُولُونَ سَيُغْفَرُ لَنَا وَإِن يَأْتِهِمْ عَرَضٌ مِّثْلُهُ يَأْخُذُوهُ ۚ أَلَمْ يُؤْخَذْ عَلَيْهِم مِّيثَاقُ الْكِتَابِ أَن لَّا يَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ إِلَّا الْحَقَّ وَدَرَسُوا مَا فِيهِ ۗ وَالدَّارُ الْآخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿١٦٩﴾
169. Na wakafuatia baada yao kizazi kiovu waliorithi Kitabu. Wanachukua manufaa duni ya hii dunia na wanasema: Tutaghufuriwa. Na yakiwajia tena manufaa kama hayo hayo wanayachukua. Je, halikuchukuliwa kwao fungamano la Kitabu kwamba wasiseme juu ya Allaah isipokuwa haki tu na hali wao wameshayadurusu yaliyomo humo? Na nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi kwa wale wenye taqwa. Je, basi hamtii akilini?
وَالَّذِينَ يُمَسِّكُونَ بِالْكِتَابِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ الْمُصْلِحِينَ ﴿١٧٠﴾
170. Na wale wanaoshikilia imara Kitabu na wakasimamisha Swalaah, hakika Sisi Hatupotezi ujira wa watendao mema.
وَإِذْ نَتَقْنَا الْجَبَلَ فَوْقَهُمْ كَأَنَّهُ ظُلَّةٌ وَظَنُّوا أَنَّهُ وَاقِعٌ بِهِمْ خُذُوا مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاذْكُرُوا مَا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٧١﴾
171. Na pindi Tulipong’oa na kuinua mlima juu yao kama kwamba ni kanopi na wakadhani kwamba utawaangukia. (Tukawaambia): Chukueni Tuliyokupeni kwa nguvu, na kumbukeni yale yaliyomo humo ili mpate kuwa na taqwa.
وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَا ۛ أَن تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَـٰذَا غَافِلِينَ ﴿١٧٢﴾
172. Na pindi Rabb wako Alipowaleta wana wa Aadam kutoka migongoni mwao kizazi chao, Akawashuhudisha juu ya nafsi zao, Je, Mimi siye Rabb wenu? Wakasema: Sivyo hivyo bali naam tumeshuhudia! (Allaah Akawaambia): Msije kusema Siku ya Qiyaamah: hakika sisi tulikuwa tumeghafilika nayo haya.[34]
أَوْ تَقُولُوا إِنَّمَا أَشْرَكَ آبَاؤُنَا مِن قَبْلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةً مِّن بَعْدِهِمْ ۖ أَفَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ الْمُبْطِلُونَ ﴿١٧٣﴾
173. Au mkasema: Hakika baba zetu ndio waliofanya shirki kabla, nasi tulikuwa kizazi baada yao. Basi Utatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wabatilifu?
وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ وَلَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿١٧٤﴾
174. Na hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat na ili wapate kurejea (katika utiifu).
وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ الَّذِي آتَيْنَاهُ آيَاتِنَا فَانسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ الشَّيْطَانُ فَكَانَ مِنَ الْغَاوِينَ ﴿١٧٥﴾
175. Na wasomee (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) khabari za yule Tuliyempa (ilimu) ya Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) Zetu, akajivua nazo na shaytwaan akamfuata, na akawa miongoni mwa waliopotoka.[35]
وَلَوْ شِئْنَا لَرَفَعْنَاهُ بِهَا وَلَـٰكِنَّهُ أَخْلَدَ إِلَى الْأَرْضِ وَاتَّبَعَ هَوَاهُ ۚ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ الْكَلْبِ إِن تَحْمِلْ عَلَيْهِ يَلْهَثْ أَوْ تَتْرُكْهُ يَلْهَث ۚ ذَّٰلِكَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۚ فَاقْصُصِ الْقَصَصَ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ ﴿١٧٦﴾
176. Na lau Tungelitaka Tungelimnyanyua kwazo (hizo Aayaat), lakini aligandamana na dunia na akafuata hawaa zake. Basi mfano wake ni kama mfano wa mbwa, ukimhujumu ananing’iniza ulimi nje na kuhema, na ukimwacha pia ananing’iniza ulimi nje na kuhema. Hivyo ndiyo mfano wa watu waliokadhibisha Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) Zetu. Basi simulia visa huenda wakatafakari.
سَاءَ مَثَلًا الْقَوْمُ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَأَنفُسَهُمْ كَانُوا يَظْلِمُونَ ﴿١٧٧﴾
177. Uovu ulioje mfano wa watu waliokadhibisha Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) Zetu na wakawa wanajidhulumu nafsi zao!
مَن يَهْدِ اللَّـهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِي ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿١٧٨﴾
178. Atakaowaongoza Allaah, basi ndio watakaohidika, na Atakaowaachia kupotoka, basi hao ndio wenye kukhasirika.
وَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرًا مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ لَهُمْ قُلُوبٌ لَّا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَّا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لَّا يَسْمَعُونَ بِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ ﴿١٧٩﴾
179. Kwa yakini Tumeumba Jahannam kwa ajili ya wengi katika majini na wanaadamu.[36] Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo.[37] Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama, bali wao ni wapotovu zaidi. Hao ndio walioghafilika.
وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٨٠﴾
180. Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa[38], basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopotoa na kuharibu[39] Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda.
وَمِمَّنْ خَلَقْنَا أُمَّةٌ يَهْدُونَ بِالْحَقِّ وَبِهِ يَعْدِلُونَ ﴿١٨١﴾
181. Na katika Tuliowaumba, wako ummah wanaoongoza kwa haki na kwayo wanahukumu kiadilifu.[40]
وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا سَنَسْتَدْرِجُهُم مِّنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٨٢﴾
182. Na wale waliokadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) Zetu Tutawavuta polepole (kuwaadhibu) kwa namna wasiyoijua.
وَأُمْلِي لَهُمْ ۚ إِنَّ كَيْدِي مَتِينٌ ﴿١٨٣﴾
183. Nami Ninawapa muhula. Hakika Mpango Wangu (wa adhabu) ni wenye nguvu.
أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا ۗ مَا بِصَاحِبِهِم مِّن جِنَّةٍ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿١٨٤﴾
184. Je, hawatafakari? Swahibu yao (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) hana wazimu! Hakuwa yeye ila ni mwonyaji bayana.
أَوَلَمْ يَنظُرُوا فِي مَلَكُوتِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا خَلَقَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ وَأَنْ عَسَىٰ أَن يَكُونَ قَدِ اقْتَرَبَ أَجَلُهُمْ ۖ فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ ﴿١٨٥﴾
185. Je, hawatazami ufalme mkuu wa mbingu na ardhi na vitu Alivyoviumba Allaah, na asaa ukawa muda wao uliopangwa umeshakaribia? Basi ujumbe gani baada yake (hii Qur-aan) wataamini?
مَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَلَا هَادِيَ لَهُ ۚ وَيَذَرُهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿١٨٦﴾
186. Ambao Allaah Amewapotoa, basi hakuna wa kuwahidi. Na Atawaacha katika upindukaji mipaka ya kuasi kwao, wakitangatanga kwa upofu.
يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ رَبِّي ۖ لَا يُجَلِّيهَا لِوَقْتِهَا إِلَّا هُوَ ۚ ثَقُلَتْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ لَا تَأْتِيكُمْ إِلَّا بَغْتَةً ۗ يَسْأَلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِيٌّ عَنْهَا ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ اللَّـهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٨٧﴾
187. Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Saa (Qiyaamah), lini kutokea kwake?[41] Sema: Hakika ujuzi wake uko kwa Rabb wangu. Hakuna wa kuidhihirisha wakati wake isipokuwa Yeye. Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haitokufikieni isipokuwa kwa ghafla. Wanakuuliza kama kwamba wewe unaijua vyema. Sema: Hakika ujuzi wake uko kwa Allaah (Pekee), lakini watu wengi hawajui.
قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي نَفْعًا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۚ وَلَوْ كُنتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ ۚ إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿١٨٨﴾
188. Sema: Siimilikii nafsi yangu manufaa yoyote wala dhara yoyote isipokuwa Apendavyo Allaah. Na lau ningekuwa najua ya ghaibu, bila shaka ningelijikithirishia ya kheri, na wala lisingelinigusa ovu. Mimi si chochote isipokuwa ni mwonyaji na mbashiriaji kwa watu wanaoamini.
هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَجَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا لِيَسْكُنَ إِلَيْهَا ۖ فَلَمَّا تَغَشَّاهَا حَمَلَتْ حَمْلًا خَفِيفًا فَمَرَّتْ بِهِ ۖ فَلَمَّا أَثْقَلَت دَّعَوَا اللَّـهَ رَبَّهُمَا لَئِنْ آتَيْتَنَا صَالِحًا لَّنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ ﴿١٨٩﴾
189. Yeye (Allaah) Ndiye Aliyekuumbeni kutokana na nafsi moja na Akafanya kutokana nayo mke wake ili apate utulivu. Basi anapomuingilia hubeba mimba khafifu anayotembea nayo. Kisha inapokuwa nzito humwomba Allaah Rabb wao: Ukitupa (mwana) mwema asiyekuwa na kasoro, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.
فَلَمَّا آتَاهُمَا صَالِحًا جَعَلَا لَهُ شُرَكَاءَ فِيمَا آتَاهُمَا ۚ فَتَعَالَى اللَّـهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿١٩٠﴾
190. Lakini Anapowapa (mwana) mwema asiyekuwa na kasoro, wanamfanyia (Allaah) washirika katika kile Alichowapa. Basi Ametukuka Allaah kwa Uluwa kutokana na yale yote wanayofanya shirki.
أَيُشْرِكُونَ مَا لَا يَخْلُقُ شَيْئًا وَهُمْ يُخْلَقُونَ ﴿١٩١﴾
191. Je, wanawashirikisha (na Allaah) wale ambao hawaumbi kitu na hali wao wameumbwa?
وَلَا يَسْتَطِيعُونَ لَهُمْ نَصْرًا وَلَا أَنفُسَهُمْ يَنصُرُونَ ﴿١٩٢﴾
192. Na wala hawawezi kuwanusuru wala hawawezi kujinusuru nafsi zao.
وَإِن تَدْعُوهُمْ إِلَى الْهُدَىٰ لَا يَتَّبِعُوكُمْ ۚ سَوَاءٌ عَلَيْكُمْ أَدَعَوْتُمُوهُمْ أَمْ أَنتُمْ صَامِتُونَ ﴿١٩٣﴾
193. Na mkiwaita kwenye uongofu hawatokufuateni. Ni sawasawa kwenu, mkiwaita au mkiwanyamazia.
إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ عِبَادٌ أَمْثَالُكُمْ ۖ فَادْعُوهُمْ فَلْيَسْتَجِيبُوا لَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٩٤﴾
194. Hakika wale mnaowaomba badala ya Allaah ni waja kama nyinyi. Hebu waiteni wakuitikieni ikiwa nyinyi ni wakweli.
أَلَهُمْ أَرْجُلٌ يَمْشُونَ بِهَا ۖ أَمْ لَهُمْ أَيْدٍ يَبْطِشُونَ بِهَا ۖ أَمْ لَهُمْ أَعْيُنٌ يُبْصِرُونَ بِهَا ۖ أَمْ لَهُمْ آذَانٌ يَسْمَعُونَ بِهَا ۗ قُلِ ادْعُوا شُرَكَاءَكُمْ ثُمَّ كِيدُونِ فَلَا تُنظِرُونِ ﴿١٩٥﴾
195. Je, kwani wana miguu wanayotembelea nayo? Au wana mikono wanayokamatia kwayo? Au wana macho wanayoonea kwayo? Au wana masikio wanayosikilizia kwayo? Sema: Waiteni washirika wenu, kisha nifanyieni njama, wala msinipe muhula.
إِنَّ وَلِيِّيَ اللَّـهُ الَّذِي نَزَّلَ الْكِتَابَ ۖ وَهُوَ يَتَوَلَّى الصَّالِحِينَ ﴿١٩٦﴾
196. Hakika Mlinzi wangu Ni Allaah Ambaye Ameteremsha Kitabu, Naye Ndiye Anayewalinda na kuwasaidia Swalihina.
وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَكُمْ وَلَا أَنفُسَهُمْ يَنصُرُونَ ﴿١٩٧﴾
197. Na wale mnaowaomba (na kuwaabudu) badala ya Allaah hawawezi kuwanusuru wala hawawezi kujinusuru nafsi zao.
وَإِن تَدْعُوهُمْ إِلَى الْهُدَىٰ لَا يَسْمَعُوا ۖ وَتَرَاهُمْ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ وَهُمْ لَا يُبْصِرُونَ ﴿١٩٨﴾
198. Na ukiwaita katika uongofu hawasikii, na utawaona wanakutazama na hali wao hawaoni.
خُذِ الْعَفْوَ وَأْمُرْ بِالْعُرْفِ وَأَعْرِضْ عَنِ الْجَاهِلِينَ ﴿١٩٩﴾
199. Shikamana na usamehevu, na amrisha mema na jiepushe na majahili.
وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۚ إِنَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢٠٠﴾
200. Na pindi utakapokuchochea uchochezi kutokana na shaytwaan, basi omba kinga kwa Allaah. Hakika Yeye Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
إِنَّ الَّذِينَ اتَّقَوْا إِذَا مَسَّهُمْ طَائِفٌ مِّنَ الشَّيْطَانِ تَذَكَّرُوا فَإِذَا هُم مُّبْصِرُونَ ﴿٢٠١﴾
201. Hakika wale wenye taqwa zinapowagusa pepesi za shaytwaan hukumbuka, basi mara wao huwa wenye kuona kwa utambuzi.
وَإِخْوَانُهُمْ يَمُدُّونَهُمْ فِي الْغَيِّ ثُمَّ لَا يُقْصِرُونَ ﴿٢٠٢﴾
202. Na ndugu zao wanawavutia katika upotofu, kisha hawakasiri.
وَإِذَا لَمْ تَأْتِهِم بِآيَةٍ قَالُوا لَوْلَا اجْتَبَيْتَهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا أَتَّبِعُ مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ مِن رَّبِّي ۚ هَـٰذَا بَصَائِرُ مِن رَّبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٢٠٣﴾
203. Na usipowaletea Aayah (Muujiza, Ishara) husema: Kwa nini hukuibuni? Sema: Hakika nafuata yale tu niliyofunuliwa Wahy kutoka kwa Rabb wangu. Hii (Qur-aan) ni hoja, ishara na dalili wazi kutoka kwa Rabb wenu, na ni mwongozo na rehma kwa watu wanaoamini.
وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٢٠٤﴾
204. Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na bakieni kimya (mzingatie) ili mpate kurehemewa.[42]
وَاذْكُر رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعًا وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ ﴿٢٠٥﴾
205. Na mdhukuru Rabb wako katika nafsi yako kwa unyenyekevu na kwa khofu na kwa ulimi bila sauti kubwa asubuhi na jioni, wala usiwe miongoni mwa walioghafilika.
إِنَّ الَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيُسَبِّحُونَهُ وَلَهُ يَسْجُدُونَ ۩﴿٢٠٦﴾
206. Hakika wale (Malaika) walioko kwa Rabb wako hawatakabari wakaacha kumwabudu na wanamsabihi[43], na Yeye tu wanamsujudia.[44] [45]
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Mizani Nzito Na Mizani Nyepesi Za Matendo Ya Wanaadam Siku Ya Qiyaamah:
Rejea Al-Qaari’ah (101:6) kwenye faida.
[3] Amri Ya Kuvaa Mavazi Mazuri, Masafi, Na Ya Twahara Sehemu Za Ibaada:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anaamrisha Waja Wake Waumini kuvaa nguo nzuri, safi, za twahara, na pia kusafisha kinywa na usafi wa mwili kiujumla wanaposwali au wanapokuwa katika sehemu zozote zile za Ibaada kama katika Manaasik ya ‘Umrah na Hajj, katika kutufu Al-Ka’bah na kwengineko. Na nguo bora kabisa ni ya rangi nyeupe (kwa wanaume) kama alivyohadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Vaeni nguo nyeupe kwani ndio nguo zenu bora kabisa, na kafinini kwazo maiti wenu...” [Ahmad]
Jambo hili ni muhimu mno kwa Muislamu. Anapokwenda kuswali, akavaa nguo nzuri safi, hali ya kuwa mwili wake pia ni msafi na kinywa chake, na hata kujitia manukato mazuri kabisa, kwa sababu hivi hii inamaanisha anamheshimu Allaah (سبحانه وتعالى) na kumwadhimisha, kwa kuwa anakwenda kusimama mbele Yake. Muislamu kuingia Msikitini akiwa na harufu mbaya au kwenye mikusanyiko yoyote ya kiibada, bila shaka atasababisha khushuu (utulivu) kuondoka kwa atakayesimama naye pembeni katika safu moja, na hata Malaika nao wataudhika, kwani kinachowaudhi wanaadamu pia huwaudhi Malaika. Kwa hilo atakuwa ametenda kosa kubwa sana. Ndio maana Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwakataza Swahaba wasiukaribie kabisa Msikiti kwa aliekula kitunguu.
Kuna baadhi ya Misikiti, unaposujudu unakutana na harufu kali ya soksi. Ni jambo la kusikitisha sana wanaosababisha hali hiyo!
Na hata wanawake wanapaswa nao wavae nguo nzuri na safi wanaposwali majumbani mwao, na hata wanaruhusika kujitia manukato madamu wako na maharimu wao tu. Lakini wanapokwenda Misikitini, basi watahadhari kuwa nguo zao zisiwe ni zenye mapambo na marangi mengi zikamshughulisha katika Swalaah yake akapoteza khushuu (utulivu), au zikawavutia wanaume ikaja kuwa ni maasi makubwa kutokana na kauli ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambayo inawaharamisha kujitia manukato wanapotoka nje: “Mwanamke yeyote atakayejitia manukato akapita mbele ya watu wakapata harufu yake, basi atakuwa amezini.” [Ahmad na wengineo]
Ni sikitiko kubwa kuwa wanawake wengi wa Kiislamu hawachungi jambo hili, bali huwa wanakwenda Misikitini wakiwa wamejipamba mno kwa nguo za rangi na za mapambo, na wengineo hata nguo zenyewe sio za kumsitiri mwili wake mzima. Basi hii haijuzu kabisa kwao!
Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
[4] Katazo La Kufanya Israfu:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anakataza kufanya israfu; nayo ni israfu katika kula, kunywa, na hata katika mavazi, na upotezaji wa neema nyenginezo.
Katika kula, kuna nasaha ya kutokula kwa wingi mno mpaka mtu ashindwe kutekeleza ibaada zake. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwanaadam hajijazii chombo vibaya kama anavyojaza tumbo lake. Inamtosheleza mwanaadam ale kidogo tu kiasi cha kumtia nguvu uti wa mgongo wake. Lakini akitaka kula zaidi, basi thuluthi ya chakula, na thuluthi ya maji na thuluthi aache kwa ajili ya hewa.” [Amehadithia Al-Miqdaam bin Ma’diykarib (رضي الله عنه) na imepokelewa na Ahmad, At-Tirmidhiy]
Rejea Al-Israa (17:26) kupata faida kuhusu tofauti ya israfu na ubadhirifu.
[6] Haramisho La Maasi:
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Ana hisia ya ghera, na Ghera ya Allaah (inachomoza) pale mtu anapofanya (maasi) Aliyoyaharamisha Allaah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na pia amesema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakuna mwenye ghera zaidi ya Allaah wakati anapozini Mja Wake au ummah Wake uzini.” [Al-Bukhaariy]
Haramisho la ukandamizaji, rejea An-Nahl (16:90).
Haramisho la kumshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى), rejea An-Nisaa (4:48), (4:116), Al-Maaidah (5:72-74).
[7] Moto Wa Jahnnam Utajazwa Kwa Wanaadam Na Majini:
Rejea Qaaf (50:30) kwenye maelezo na rejea zake.
[8] Mifano Ya Kipekee Ya Allaah: Mustahili Kwa Waliokufuru Kuingia Janna (Peponi) Kama Vile Mustahili Ngamia Kuingia Katika Tundu Ya Sindano:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema kuwa Anawapigia watu mifano mbali mbali katika Qur-aan. Rejea: Al-Israa (17:89), Al-Kahf (18:54), Al-‘Ankabuwt (29:43), Ar-Ruwm (30:58), Muhammad (47:3), Al-Hashr (59:21). Na Mifano Yake ni mifano ya kipekee, yenye hikmah, yenye mafundisho na mazingatio kwa wenye kutafakari. Rejea Al-Baqarah (2:261), (2:264-265), Aal-‘Imraan (3:117), Suwrah hii Al-A’raaf (7:176), Yuwnus (10:24), Huwd (11:24), Ar-Ra’d (13:17), Ibraahiym (14:18), (14:24-26), An-Nahl (16:75-76), Al-Kahf (18:32), (18:45), Al-Hajj (22:73), An-Nuwr (24:35), Ar-Ruwm (30:28), Al-‘Ankabuwt (29:41), Az-Zumar (39:29), Al-Hadiyd (57:20), Al-Jumu’ah (62:5), At-Tahriym (66:10-11) na kwengineko katika Qur-aan. Na katika Sunnah hali kadhaalika, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amepiga mifano mingi. Mmoja wapo ni kuhusu Swalaah tano jinsi zinavyomsafisha mtu na madhambi:
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mnaonaje kungekuwa na mto mlangoni mwa mmoja wenu na akaoga mara tano kwa siku, je, atabakiwa na tone la uchafu (mwilini mwake)?” Wakasema: “Hatabakiwa na tone la uchafu.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ”Basi hivyo ni mfano wa Swalaah tano ambazo Allaah Anafuta madhambi kwazo.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Maelezo Ya Faida Ya Aayah:
Imaam Bin Baaz (رحمه الله) amesema alipoulizwa kuhusu Aayah hii:
إِنَّ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا لَا تُفَتَّحُ لَهُمْ أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَلَا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ حَتَّىٰ يَلِجَ الْجَمَلُ فِي سَمِّ الْخِيَاطِ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُجْرِمِينَ ﴿٤٠﴾
"Hakika wale waliokadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili) Zetu na wakazifanyia kiburi, hawatofunguliwa kamwe milango ya mbingu na wala hawatoingia Jannah mpaka ngamia aingie katika tundu ya sindano. Na hivyo ndivyo Tunavyowalipa wahalifu.” [Al-A’raaf (7:40)]
“Ni dhahiri kuwa mwenye kukadhibisha Aayaat za Allaah akatakabari kufuata haki, hivyo ndivyo itakavyokuwa hali yake, haitopanda roho yake mbinguni, bali itarudishwa ardhini katika mwili wake atahiniwe na aadhibishwe kaburini mwake. Kisha atahamishwa motoni, tunamuomba Allaah Al-‘Aafiyah (usalama wa dunia na Dini). Kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) kuhusu Firawni:
النَّارُ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا غُدُوًّا وَعَشِيًّا ۖ وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ أَدْخِلُوا آلَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ الْعَذَابِ﴿٤٦﴾
“Wanadhihirishiwa moto asubuhi na jioni, na Siku itakayosimama Saa (itasemwa): Waingizeni watu wa Firawni katika adhabu kali kabisa.” [Ghaafir (40:46)]
Hivyo ndivyo hali ya kila atakayetakabari na haki na asifuate mwongozo, haitofunguliwa milango ya mbingu wala hazirudishwi roho zao mbinguni wala kwa Allaah (سبحانه وتعالى), bali itarudi roho yake katika mwili wake muovu na ataadhibiwa kaburini mwake pamoja na adhabu ya moto Siku ya Qiyaamah. Tunamuomba Allaah Al-‘Aafiyah. Na pia hawatoingia Jannah kamwe. Ndipo Allaah (سبحانه وتعالى) Anabainisha kuwa hatoingia kamwe Jannah mpaka iwezekane ngamia aingie katika tundu ya sindano. Na inajulikana wazi kuwa ngamia hawezi kuingia kamwe katika tundu ya sindano! Na lililokusudiwa hapa ni kuwa ni mustahili kafiri aingie Jannah kama vile ilivyokuwa mustahili ngamia aingie katika tundu ya sindano kutokana na kufru zao na upotofu wao. Ni mustahili kuingia Jannah, bali wao wataingia motoni milele. Tunamuomba Allaah Al-‘Aafiyah.” [Fataawa Ibn Baaz]
Rejea Fusw-Swilat (41:30) kwenye Hadiyth iliyothibitisha hayo.
[9] Qantwarah: Ni Daraja Baina Ya Jannah Na Moto Ambalo Waumini Watalipana Kisasi Na Kuondoshewa Mafundo Na Vinyongo Baina Yao:
Amesimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Baada ya Waumini kuokolewa na moto, watazuiliwa wangojee katika Qantwarah (daraja) baina ya Jannah na moto. Kisha watahojiwa kuhusu dhulma zote walizotendeana duniani. Watakapotakaswa (madhambi yao kuhukumiwa) watapewa ruhusa kuingia Jannah. Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake, kila mtu atatambua makazi yake Jannah kuliko anavyotambua makazi yake ya duniani.” [Al-Bukhaariy]
Shukurani Za Watu Kuingia Jannah Na Majuto Kuingia Motoni:
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kila mmoja katika watu wa Jannah ataona sehemu ya kikao chake cha motoni na atasema: Ingekuwa Allaah Hakunihidi! Basi itakuwa ndio shukurani yake. Na kila mtu wa motoni ataona sehemu yake ya kikao chake Jannah atasema: Ingekuwa Allaah Kanihidi! Basi huwa ndio majuto yake.” [An-Nasaaiy]
Rejea Al-Hijr (15:47).
[10] Al-A’raaf:
Al-A’raaf ni jina la Suwrah hii. Na Ibn ‘Abbaas, Ibn Mas’uwd, Ibn Jariyr na Salaf wengineo wamesema: Al-A’raaf ni sehemu watakayosimama watu ambao amali zao njema na mbaya zimelingana sawasawa. Amali zao ovu zimewazuia kuingia Jannah, na amali zao njema zimewastahiki waepukane na moto. Kwa hiyo watasimamishwa hapo katika mnyanyuko wa Al-A’raaf mpaka Allaah Awahukumu. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[11] Istawaa اسْتَوَى
Yuko juu kwa namna inayolingana na Uadhama na Ujalali Wake Yeye Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى).
Kwa hakika maana ya “Istawaa” ina unyeti katika kuielezea. Na katika Tarjama hii, maana ya “Istawaa” imeelezewa kwa bayana, maana zake zinazotofautiana, kwa mujibu wa maelezo ya ‘Ulamaa, katika Suwrah mbili: Katika Suwrah ya Al-Baqarah (2:29) kuna maelezo yake yanayohusiana na Suwrat Fusswilat (41:11). Na katika Suwrah hii Al-A’raaf (7:54) maelezo yake ni kama ifuatavyo:.
Kitenzi hiki "اسْتَوَى" kikifuatiwa na Harful Jarri "عَلَى" kimekuja katika Suwrah hii ya Al-A’raaf (7:54) na Yuwnus (10:3), Ar-Ra’ad (13:2), Twaahaa (20:5), Al-Furqaan (25:59), As-Sajdah (32:4), na Al-Hadiyd (57:4). Na kwa mujibu wa kauli za Mufassiruna na ‘Ulamaa wengi wa Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah ni kuwa maana ya "اسْتَوَى" ni: "عَلَا" و "ارْتَفَعَ", yaani Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى). Au Amepanda juu, au Amenyanyuka juu, na hususan baada ya kufuatiliwa na Harf Al Jarri "عَلَى" yenye kudulisha ujuu. Na maana hizi zote zinalaikiana na Uadhama Wake Allaah (سبحانه وتعالى) kwa namna Anayoijua Yeye Mwenyewe Aliyetakasika. Kwa hiyo tafsiri yake ni: Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى). Na hii ni ‘Aqiydah ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah kuthibitisha Sifa hii ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya Istawaa. Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amethibitisha pia katika Hadiyth:
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Pindi Allaah Alipoviumba viumbe, Aliandika katika kitabu, ambacho kipo Kwake juu ya 'Arsh Yake: Hakika Rehma Yangu inashinda ghadhabu Yangu."
Na katika riwaayah nyingine: "Imeshinda ghadhabu Yangu."
Na katika riwaayah nyengine: "Imepita ghadhabu Yangu." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhy]
Rejea pia Twaahaa (20:5) kwenye maelezo kuhusu msimamo wa Salaf katika Tafsiyr ya Aayah yenye kitenzi hiki.
Na pia Aayah kadhaa zimethibitisha Allaah (سبحانه وتعالى) Kuweko Juu. Rejea Al-Mulk (67:16-17) ambako kuna maelezo bayana na rejea mbalilmbali.
Na kitenzi hiki kimekuja pia kwenye Suwrah nyinginezo kwa wakati uliopo يَسْتَوِي kikiwa na maana ya ulinganishi kati ya vitu viwili vilivyo kinyume. Kama je kipofu anaweza kuwa sawa na anayeona? Au giza na nuru? Au kibaya na kizuri? Au walio hai na wafu? Na kadhalika. Ni kama kwenye Suwrat An-Nisaa (4:95), Al-Maaidah (5:100), Al-An’aam (6:50) na nyinginezo.
Pia kwingineko kwa wakati uliopita kwa maana ya kutua na kutulia kama kwenye Suwrat Huwd (11:44). Pia kwa maana ya kupanda juu ya chombo au kitu na kumakinika juu yake kama kwenye Suwrat Al-Muuminuwna (23:28), na kwa maana ya kuimarika vyema kiafya na kiakili kama kwenye Suwrat Al-Qaswas (28:14).
[12] Masiku Yaliyoumbwa Dunia Na Viliyomo Ndani Yake:
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah (عزَّ وجلَّ) Ameumba mchana siku ya Jumamosi, Akaumba milima Jumapili, Akaumba miti Jumatatu, Akaumba yanayochukiza Jumanne, Akaumba nuru Jumatano, kisha Akaeneza humo viumbe vinavyotembea Alkhamiys. Kisha Akamuumba Aadam (عليه السّلام) Ijumaa baada ya Alasiri. Alikuwa ni wa mwisho kuumbwa katika saa ya mwisho katika saa za Ijumaa, baina ya Alasiri na usiku.” [Ahmad]
[13] Miongoni Mwa Adabu Za Kuomba Duaa:
Aayah hii ya Al-A’raaf (7:55) na inayofuatia (7:56) zimetajwa baadhi ya adabu za kuomba duaa nazo ni: Kuomba kwa unyenyekevu, kwa siri, kwa sauti ndogo, kwa khofu na matumaini.
Amesimulia Abuu Muwsaa Al-Ash-‘ariyy (رضي الله عنه) : Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na tukawa kila tukipanda bonde, tunatamka tahliyl (Laa Ilaaha Ila-Allaah), tunakabbir (Allaahu Akbar), zikapanda sauti zetu, akasema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Enyi watu, jizuieni nafsi zenu, kwani hamumwombi kiziwi wala asiyekuwepo, hakika Yeye Yupo nanyi (kwa Ujuzi Wake), hakika Yeye Ni Mwenye Kusikia yote, Yupo Karibu, Limetakasika Jina Lake na Ametukuka ...” [Al-Bukhaariy]
Rejea pia Al-Baqarah (2:186).
[14] Mfano Wa Uongofu Na Ilimu Kulingana Na Ardhi Yenye Rutuba:
Amesimulia Abuu Muwsaa Al-Ash-‘ariyy (رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mfano wa uongofu na ilimu ambayo Allaah Amenituma kufikisha ni kama mvua kubwa inayoanguka juu ya ardhi, baadhi yake (hufikia) katika ardhi yenye rutuba ikanyonya maji ya mvua na ikaleta mimea na majani kwa wingi. Na baadhi yake (ardhi) ikawa nzito na ikazuia maji ya mvua (kupenya katika ardhi), na Allaah Akawanemeesha watu kutokana nayo, na wakaitumia kwa kunywa, kunyweshea wanyama wao, na kwa ajili ya umwagiliaji na kilimo kwenye ardhi hiyo. Na baadhi yake ikawa si yenye rutuba ambayo haikuweza kukamata maji wala kutoa mimea (hivyo ardhi hiyo haikutoa faida yoyote). (Ardhi) ya mwanzo ni mfano wa mtu anayetambua Dini ya Allaah na akapata faida (kutokana na ilimu) ambayo Allaah Ameishusha kupitia kwangu (Manabii na ‘Ulamaa), na akaisomesha kwa wengine. (Ardhi) ya mwisho ni mfano wa yule mtu asiyejali na hafuati Uongofu wa Allaah Alioushusha kupitia kwangu (ni mfano wa hiyo ardhi isiyo na rutuba).” [Al-Bukhaariy]
[15] Kaumu Ya Nabiy Nuwh (عليه السّلام):
Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye uchambuzi wa kaumu za nyumati za awali, maasi yao na adhabu zao.
[16] Kina ‘Aad:
Ni kaumu ya Nabiy Huwd (عليه السّلام). Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye uchambuzi wa kaumu za nyumati za awali, maasi yao na adhabu zao.
[17] Kaumu Ya Thamuwd:
Ni kaumu ya Nabiy Swaalih (عليه السّلام). Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye uchambuzi wa kaumu za nyumati za awali, maasi yao na adhabu zao.
[18] Kaumu Ya Nabiy Luutw (عليه السّلام):
Kaumu ya Nabiy Luutw (عليه السّلام) ni watu waliokuwa wakitenda machafu ya kuwaingilia wanaume wenzao kupitia duburi zao. Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye uchambuzi wa kaumu za nyumati za awali, maasi yao na adhabu zao.
[19] Madyan:
Ni mji wa kaumu ya Nabiy Shu’ayb (عليه السّلام). Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye uchambuzi wa kaumu za nyumati za awali, maasi yao na adhabu zao.
[20] Firawni, Haamaan Na Jeshi Lake:
Firawni alikuwa akiwatesa wana wa Israaiyl na akitenda maasi na kufru nyenginezo. Allaah (سبحانه وتعالى) Akamtumia Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) kwa dalili bayana za miujiza, lakini alimkanusha na akataka kumuua Nabiy Muwsaa (عليه السّلام), na akazidisha ujeuri wake na kutakabari kwake, na akapindukia mipaka hadi kujiona yeye ndiye anayepasa kuabudiwa. Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye uchambuzi wa kaumu za nyumati za awali, maasi yao na adhabu zao.
[21] Kukatwa Mikono Na Miguu Kwa Kutofautisha: Rejea Al-Maaidah (5:33).
[22] Miujiza Tisa Ya Allaah Ya Kwa Watu Wa Firawni:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja kuwa Aliwapelekea watu wa Firawni miujiza tisa, ambayo ilikuwa ni baadhi ya adhabu zao. Idadi hiyo imetajwa katika Suwrah ya Al-Israa (17:101) na An-Naml (27:12).
Miujiza yenyewe ambayo yote imejumuika kutajwa katika Suwrah hii ni ifuatayo:
Ukame na upungufu wa mazao: Aayah hii namba (130). Fimbo ya Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) kugeuka nyoka: Aayah namba (107). Mkono wake kugeuka mweupe na kung’ara: Aayah namba (108). Tufani, nzige, chawa, vyura, damu: Aayah (133). Jumla ni miujiza tisa.
Rejea Aayah (133) ya Suwrah hii kwa maelezo ya baadhi ya miujiza hiyo:
[23] Maelezo Ya Baadhi Ya Miujiza Kwa Watu Wa Muwsaa:
“Tukawapelekea wao mafuriko yenye kumaliza yaliyozamisha makulima na matunda; tukapeleka nzige wakazila nafaka zao, matunda yao, milango yao, sakafu zao na nguo zao; na tukapeleka chawa wanaoharibu matunda na kumaliza wanyama na mimea; tukapeleka vyura wakajaa kwenye vyombo vyao na vyakula vyao na malazi yao; na pia tukapeleka damu, ikawa mito yao na visima vyao vimegeuka damu, wasipate maji safi ya kunywa. Hii ni miujiza kati ya miujiza (tisa) ya Allaah (سبحانه وتعالى), hakuna aiwezae isipokuwa Yeye. baadhi yake imetengwa na mingine. Pamoja na haya yote, watu wa Firawni walijiona watukufu, wakafanya kiburi kwa kukataa kumuamini Allaah, wakawa ni watu wanatenda mambo Anayoyakataza Allaah ya maasia na uhalifu kwa, ujeuri na uasi.” [Tafsiyr Al-Muyassar]
[24] Kuthibitisha Sifa Ya Allaah Ya Kalaam (Kuongea): Rejea an-Nisaa (5:164).
[25] Saamiriyy Ndiye Aliyewafanyia Ndama Watu Wamwabudu Badala Ya Allaah: Rejea Twaahaa: (20:85).
[26] Rehma Za Allaah (سبحانه وتعالى) Ni Mia: Moja Ameeneza Duniani Na Rehma Tisini Na Tisa Ziko Aakhirah:
Amesimulia Salmaan (رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah (عزَّ وجلَّ) Ana rehma mia. Katika hizo, rehma moja wanarehemiana viumbe baina yao, hata mnyama mwitu anakihurumia kizazi chake. Rehma tisini na tisa Ameziweka kwa ajili ya Siku ya Qiyaamah.” [Ahmad]
Rejea Al-Faatihah (1:1).
[27] Sifa Za Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Zimo Katika Tawraat Na Injiyl:
Maana ya Aayah: Rehma hii Nitawaandikia wale wanaomuogopa Allaah na kujiepusha na mambo ya kumuasi, na wanaomfuata Rasuli aliye Nabii, ambaye hasomi wala haandiki, naye ni Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), ambaye wanazipata sifa zake na mambo yake yaandikwa huko kwao katika Tawraat na Injiyl. Anawaamrisha kumpwekesha Allaah na kumtii na kila lijulikanalo kuwa ni jema, na anawakataza ushirikina na maasia na kila lijulikanalo kuwa ni baya, na anawahalalishia vizuri vya vyakula na vinywaji na kuoana, na anawaharamishia vichafu vya hivyo, kama nyama ya nguruwe na vile ambavyo walikuwa wakijihalalishia miongoni mwa vyakula na vinywaji, ambavyo Aliviharamisha Allaah, na anawaondolea wao mambo magumu waliokalifishwa nayo kama kukata mahali pa najisi nguoni, kuzichoma moto ngawira, ulazimu wa kisasi juu ya aliyeua kwa kukusudia au kwa kukosea. Basi wale ambao walimuamini Nabii asiyejua kuandika wala kusoma kilichoandikwa, Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na wakaukubali Unabii wake, wakamheshimu, wakamtukuza na wakamuhami na wakaifuata Qur-aan aliyoteremshiwa, wakaufuata mwendo wake kivitendo, hao ni wenye kufaulu kwa kupata yale ambayo Allaah Aliwaahidi waja wake Waumini. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[28] Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Ametumwa Kwa Walimwengu Wote:
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
وَكَانَ النَّبِيُّ يُبْعَثُ إِلَى قَوْمِهِ خَاصَّةً، وَبُعِثْتُ إِلَى النَّاسِ عَامَّةً
Na alikuwa Nabiy akitumwa kwa watu wake pekee, lakini mimi nimetumwa kwa watu wote.” [Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه) -Al-Bukhaariy (5011)]
[29] Asbaatw: Rejea Al-Baqarah (2:136).
[30] Al-Manna Na As-Salwaa: Rejea Al-Baqarah (2:57).
[31] Hittwah: Tuondolee Uzito Wa Madhambi: Ada Ya Mayahudi Kubadilisha Maana Za Maneno Rejea Al-Baqarah (2.58).
[32] As-Sabt: Rejea Al-Baqarah (2:65), An-Nisaa (4:47).
[33] Maasi Ya Mayahudi Kwa Mukhtasari Na Namna Walivyokuwa Jeuri Kwa Manabii Wao:
Mayahudi walikatazwa na Allaah (سبحانه وتعالى) kuvua samaki siku ya As-Sabt (mapumziko, Jumamosi), lakini wao kwa ujeuri wao wakavua samaki siku hiyo kwa kufanya hila za kuwatega samaki. Pia Allaah (سبحانه وتعالى) Akawakumbusha wajukuu zao kuhusu siku hiyo ya As-Sabt ambayo babu zao Mayahudi waliasi ndani yake, kiasi kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Aliwageuza kuwa nyani na nguruwe. Na mwenye kusoma visa vya Mayahudi dhidi ya Manabii wao na miongoni mwa swaalihina katika wao, atakuta kuwa waliwaudhi mno Manabii wao na wakawapinga na kwenda kinyume nao. Na pia wakafanyia inadi na ujeuri Maamrisho ya Allaah (سبحانه وتعالى) na wakawa na ujeuri uliopindukia. Miongoni mwa mifano ya hayo ni: Kisa cha ng’ombe katika Suwrah Al-Baqarah. Pia kumwabudu ndama kama ilivyotajwa katika Suwrah Al-Baqarah (2:51) na Suwrah hii Al-A’raaf (7:148). Pia kutaka kwao kumuona Allaah (سبحانه وتعالى) wazi wazi. Tena hayo wameyafanya baada tu ya kuvukishwa bahari kwa salama na kuokolewa kutokana na adui wao Firawni aliyezamishwa baharini. Pia uasi wao wa kuwaua baadhi ya Manabii bila ya haki. Na mifano mingine mingi kuhusu uasi na ujeuri wa Mayahudi.
[34] Ahadi Ya Alastu:
Ahadi ya “Alastu” ni ile ambayo viumbe vyote kabla ya kuzaliwa kwao lakini ni baada ya roho zao kuumbwa. Basi viumbe katika hali hiyo, waliaahidi kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kutokumshirikisha na kumtii Amri Zake. Hapo viumbe walikuwa katika hali ya Fitwrah (asili ya maumbile). Rejea Ar-Ruwm (30:30).
[35] Aliyepewa Ilimu Akajivua Nayo Kisha Akapotoka:
Wamekhitilafiana Salaf kuhusu mtu huyo:
‘Abdullaah Bin Mas’uwd na wengineo: Ni mtu kutoka Bani Israaiyl akiitwa Ba’lam bin Abar.
Ibn ‘Abbaas: Ni Swayfiy Bin Ar-Raahib.
Qataadah na Ka’ab: Ni mtu kutoka watu wa Al-Balqaa na alikuwa anajua Jina Tukufu la Allaah na alikuwa akiishi katika Bayt Al-Maqdis pamoja na Al-Ahbaar (Mafuqahaa wa Kiyahudi).
Na kauli nyenginezo [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Imaam As-Sa’diy amesema:
وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ الَّذِي آتَيْنَاهُ آيَاتِنَا
“Na wasomee (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) khabari za yule Tuliyempa (ilimu) ya Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) Zetu.”
Tulimfundisha Kitabu cha Allaah, akawa ‘Aalim (Ahbaar – Fuqahaa wa Kiyahudi) mkubwa.
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
فَانسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ الشَّيْطَانُ
“Akajivua nazo na shaytwaan akamfuata.”
Yaani akajivua na sifa zinazotarajiwa kwa mwenye ilimu hii, kwani mwenye ilimu hii, anapaswa kuwa mwenye sifa tukufu za maadili mema na matendo mema, na huinuliwa hadi daraja za juu na huwa na hadhi tukufu. Lakini huyu alikiacha Kitabu cha Allaah nyuma ya mgongo wake na kukana maadili ambayo kitabu hicho kiliamuru. Akaivua (ilimu) kama mtu anavyovua mavazi. Shaytwaan akamshinda nguvu, akapotoka na akatoka kutoka katika ngome iliyokuwa ya nguvu na akamshawishi kutenda dhambi. Hivyo basi akawa mtu wa chini kabisa. Akawa katika walipotoka baada ya kuwa mwongofu na mwenye kuongoza watu.” [Tafsiyr As-Sa’diy]
Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
[36] Moto Wa Jahnnam Utajazwa Kwa Wanaadam Na Majini:
Rejea Qaaf (50:30) kwenye maelezo na rejea zake.
[37] Nyoyo Zilopofoka Hazifahamu Wala Hazikubali Haqq:
Rejea Al-Hajj (22:46) kwenye faida na rejea mbalimbali kuhusu nyoyo zilizopofoka.
[38] Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Faharasa ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake.
[39] Kumpwekesha Allaah Katika Majina Yake Na Kuthibitisha Sifa Za Allaah (سبحانه وتعالى) Na Ndio ‘Aqiydah Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Kuhusiana Na Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Na Sifa Zake:
‘Aqiydah ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah kuhusiana na Majina Mazuri kabisa ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Sifa Zake ni Tawqiyfiyyah (Yanathibitishwa Aliyoyathibitisha Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى) katika Qur-aan na Sunnah) bila kuzifanyia Ta'atwiyl (kuzipinga, kukanusha uwezekano), wala Tamthiyl (kumithilisha, kufananisha, kulinganisha), wala Takyiyf (kuainisha maana na kuziulizia namna yake au kuuliza ni vipi Sifa hiyo ipo, kuchunguza ni kwa “namna gani” zimefungamana au kuambatana na Allaah), wala Tahriyf (kubadilisha maana, kupotosha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kutoa maana isiyo sahihi).
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " إِنَّ لِلَّهِ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ اسْمَا مِائَةً إِلاَّ وَاحِدًا مَنْ أَحْصَاهَا دَخَلَ الْجَنَّةَ ".
Amesimulia Abuu Hurayrah(رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Ana Majina tisini na tisa, atakayeyahifadhi ataingia Jannah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Maana ya أَحْصَاهَا ni: Kufahamu maana Zake, kuyahifadhi, kuyafanyia kazi, na kuyatumia katika kuomba duaa.
[40] Watakaothibitika Katika Haki Mpaka Siku Ya Qiyaamah:
Amesimulia Mu’aawiyah bin Abiy Sufyaan (رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kutakuweko kundi katika ummah wangu litaendelea kuwa juu ya haki likiwa na nguvu, hawezi kuwadhuru yeyote aliyekwenda nao kinyume au aliyesaliti mpaka Siku ya Qiyaamah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
[41] Ada Ya Makafiri Kuuliza Qiyaamah Kitatokea Lini Na Kuhimiza Adhabu:
Rejea An-Naazi’aat (79:42), Al-Ahzaab (33:63), Al-Mulk (67:25).
Na wakihimiza adhabu, Rejea: Al-Hajj (22:47), Al-Anfaal (8:32-33). Swaad (38:16), na Ash-Shuwraa (42:18).
[42] Amri Ya Kusikiliza Qur-aan Kwa Makini Na Kubakia Kimya Inaposomwa:
Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) amesema: Hii ni amri kwa kila anayesikiliza Kitabu cha Allaah (سبحانه وتعالى) kikisomwa, ameamrishwa kuisikiliza na kunyamaza. Tofauti kati ya neno إستماع (Is-timaa’) na إنصات (Inswaat) ni kwamba neno إنصات dhahiri yake ni kuacha kuongea au kujishughulisha na jambo linaloenda kinyume na kusikiliza. Ama neno la إستماع ni kusikiliza kwa mazingatio ya moyo, na akawa anayazingatia anayoyasikiliza. Basi Hakika atakayejilazimisha na mambo haya mawili wakati kinasomwa Kitabu cha Allaah, mtu huyo atapata kheri nyingi na ilimu tele, na atapata imaan endelevu, na atapata hidaaya ya ziada, na pia atakuwa mwenye nuru za ilimu ya Dini na utambuzi katika Dini yake, na kwa sababu hiyo ndio Allaah (سبحانه وتعالى) Amepanga kuwa mtu atapata Rehma Yake kupitia mambo hayo mawili.
Likajulisha jambo hilo kwamba atakayesomewa Kitabu cha Allaah kisha hakusikiliza wala kunyamaza, atakuwa amenyimwa neema kubwa ya kupata Rehma za Allaah, na amepitwa na kheri nyingi. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[43] Kila Kitu Kinamsabbih Allaah (عزّ وجلّ):
Rejea Al-Hashr (57:1) kwenye rejea zinazotaja viumbe na vitu Alivyoviumba Allaah kuwa vinamsabbih Yeye Allaah (عزّ وجلّ).
[44] Kila Kitu Kinamsujudia Allaah (عزّ وجلّ):
Rejea Ar-Rahmaan (55:6) kwenye rejea zinazotaja viumbe na vitu Alivyoviumba Allaah kuwa vinamsujudia Yeye Allaah (عزّ وجلّ).
[45] Sajdatut-Tilaawah: Sijdah Za Kisomo.
Alama za kusujudu zimebainishwa katika Qur-aan katika Aayah za Suwrah mbalimbali, na Suwrah hii ya Al-A’raaf ni alama ya kwanza ya kusujudu katika Mswahafu kuanzia mpangilio wa Suwrah unaoanzia Al-Faatihah. Muislamu anaposoma au kusikiliza Qur-aan, anapofikia katika alama hizo, anatakiwa afanye yafuatayo: Atamke “Allaahu Akbar”, kisha asujudu Sijdah moja kuelekea Qiblah, na aseme kama isemwavyo katika Swalaah:
سُبْـحانَ رَبِّـيَ الأَعْلـى
Subhaana Rabbiyal A’alaa
Ametakasika Rabb wangu Aliye juu
Kisha ainuke bila ya kutamka Takbiyrah wala kutamka Salaam.
Maudhui ya Sajdatut-Tilaawah ina maelezo mengineyo marefu na Hadiyth kadhaa zimethibiti. Miongoni mwazo ni:
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)amesema: “Mwanaadam anaposoma Aayah ya Sijdah akasujudu, shaytwaan hujitenga kando akilia huku akisema: Ee maangamivu yangu! Ameamriwa kusujudu akasujudu, naye ataipata Jannah (Pepo), nami niliamriwa kusujudu nikakataa, nami nitaupata moto.” [Muslim (81), Ibn Maajah (1052) na Ahmad (9336)]
Amesimulia Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akitusomea Suwrah yenye Aayah ya Sijdah, kisha yeye husujudu nasi tunaporomoka kusujudu pamoja naye mpaka mmoja wetu anakosa sehemu ya kuweka paji lake. [Al-Bukhaariy (1075) na Muslim (575)]
الأَنْفَال
008-Al-Anfaal
008-Al-Anfaal: Utangulizi Wa Suwrah [118]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ ۖ قُلِ الْأَنفَالُ لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ ۖ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١﴾
1. Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Anfaal (mali inayopatikana katika vita). Sema: Mali inayopatikana katika vita ni ya Allaah na Rasuli. Basi mcheni Allaah na suluhisheni yaliyo baina yenu. Na mtiini Allaah na Rasuli Wake mkiwa ni Waumini.[1]
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ﴿٢﴾
2. Hakika Waumini ni wale ambao Anapotajwa Allaah, nyoyo zao zinajaa khofu na wanaposomewa Aayaat Zake huwazidishia imaan, na kwa Rabb wao wanatawakali.
الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ﴿٣﴾
3. Ambao wanasimamisha Swalaah na katika yale Tuliyowaruzuku hutoa.
أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا ۚ لَّهُمْ دَرَجَاتٌ عِندَ رَبِّهِمْ وَمَغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ﴿٤﴾
4. Hao ndio Waumini wa kweli! Wana daraja (za Jannah) kwa Rabb wao na maghfira na riziki karimu.
كَمَا أَخْرَجَكَ رَبُّكَ مِن بَيْتِكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّ فَرِيقًا مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ لَكَارِهُونَ﴿٥﴾
5. Kama Alivyokutoa Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kutoka nyumbani kwako kwa haki (kwa ajili ya Vita vya Badr[2]) na hakika kundi miongoni mwa Waumini linachukia.
يُجَادِلُونَكَ فِي الْحَقِّ بَعْدَ مَا تَبَيَّنَ كَأَنَّمَا يُسَاقُونَ إِلَى الْمَوْتِ وَهُمْ يَنظُرُونَ﴿٦﴾
6. Wanajadiliana nawe katika haki baada ya kubainika, kama kwamba wanasukumwa kwenda katika mauti nao huku wanatazama.
وَإِذْ يَعِدُكُمُ اللَّـهُ إِحْدَى الطَّائِفَتَيْنِ أَنَّهَا لَكُمْ وَتَوَدُّونَ أَنَّ غَيْرَ ذَاتِ الشَّوْكَةِ تَكُونُ لَكُمْ وَيُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُحِقَّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَيَقْطَعَ دَابِرَ الْكَافِرِينَ﴿٧﴾
7. Na pale Allaah Alipokuahidini moja kati ya makundi mawili (la msafara au la jeshi) kwamba ni lenu, nanyi mkatamani kwamba lisilo na silaha liwe lenu, na Allaah Anataka Athibitishe haki kwa Maneno Yake, na Akate mizizi ya makafiri.
لِيُحِقَّ الْحَقَّ وَيُبْطِلَ الْبَاطِلَ وَلَوْ كَرِهَ الْمُجْرِمُونَ﴿٨﴾
8. Ili Athibitishe haki na Abatilishe ubatilifu japokuwa wahalifu wamekirihika.
إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ أَنِّي مُمِدُّكُم بِأَلْفٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُرْدِفِينَ﴿٩﴾
9. Na pale mlipomuomba uokovu[3] Rabb wenu Naye Akakuitikieni kuwa: Hakika Mimi Nitakusaidieni kwa Malaika elfu wafuatanao mfululizo.[4]
وَمَا جَعَلَهُ اللَّـهُ إِلَّا بُشْرَىٰ وَلِتَطْمَئِنَّ بِهِ قُلُوبُكُمْ ۚ وَمَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿١٠﴾
10. Na Allaah Hakujaalia haya isipokuwa ni bishara na ili zitumainike nyoyo zenu kwayo. Na hakuna nusura isipokuwa kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
إِذْ يُغَشِّيكُمُ النُّعَاسَ أَمَنَةً مِّنْهُ وَيُنَزِّلُ عَلَيْكُم مِّنَ السَّمَاءِ مَاءً لِّيُطَهِّرَكُم بِهِ وَيُذْهِبَ عَنكُمْ رِجْزَ الشَّيْطَانِ وَلِيَرْبِطَ عَلَىٰ قُلُوبِكُمْ وَيُثَبِّتَ بِهِ الْأَقْدَامَ﴿١١﴾
11. Pindi Alipokufunikeni kwa usingizi kuwa ni amani kutoka Kwake, na Akakuteremshieni maji kutoka mbinguni, ili Akutwaharisheni kwayo, na Akuondosheeni wasiwasi na rai ovu za shaytwaan, na ili Atie nguvu nyoyo zenu, na Aisimamishe kwayo imara miguu.
إِذْ يُوحِي رَبُّكَ إِلَى الْمَلَائِكَةِ أَنِّي مَعَكُمْ فَثَبِّتُوا الَّذِينَ آمَنُوا ۚ سَأُلْقِي فِي قُلُوبِ الَّذِينَ كَفَرُوا الرُّعْبَ فَاضْرِبُوا فَوْقَ الْأَعْنَاقِ وَاضْرِبُوا مِنْهُمْ كُلَّ بَنَانٍ﴿١٢﴾
12. Pindi Rabb wako Alipowatia ilhamu Malaika (kuwaambia): Hakika Mimi Niko pamoja nanyi, basi wathibitisheni wale walioamini. Nitatia kizaazaa katika nyoyo za waliokufuru. Basi wapigeni juu ya shingo na wapigeni kila kiungo (au ncha za vidole).
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ شَاقُّوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ وَمَن يُشَاقِقِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴿١٣﴾
13. Hivyo kwa kuwa wao wamempinga Allaah na Rasuli Wake. Na yeyote ampingae Allaah na Rasuli Wake basi hakika Allaah Ni Mkali wa Kuakibu.[5]
ذَٰلِكُمْ فَذُوقُوهُ وَأَنَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابَ النَّارِ﴿١٤﴾
14. Hayo yaliyokupateni, basi yaonjeni (nyie makafiri). Na jueni (enyi Waumini) kwamba makafiri wana adhabu ya moto.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا زَحْفًا فَلَا تُوَلُّوهُمُ الْأَدْبَارَ﴿١٥﴾
15. Enyi walioamini! Mtapokutana na wale waliokufuru vitani, basi msiwageuzie migongo (kukimbia).[6]
وَمَن يُوَلِّهِمْ يَوْمَئِذٍ دُبُرَهُ إِلَّا مُتَحَرِّفًا لِّقِتَالٍ أَوْ مُتَحَيِّزًا إِلَىٰ فِئَةٍ فَقَدْ بَاءَ بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَمَأْوَاهُ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿١٦﴾
16. Na yeyote atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo - isipokuwa akigeuka kama mbinu ya kupigana au kujiunga na kikosi kingine - basi amestahiki Ghadhabu ya Allaah, na makazi yake ni Jahannam, na ni pabaya palioje mahali pa kuishia.[7]
فَلَمْ تَقْتُلُوهُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ قَتَلَهُمْ ۚ وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ رَمَىٰ ۚ وَلِيُبْلِيَ الْمُؤْمِنِينَ مِنْهُ بَلَاءً حَسَنًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿١٧﴾
17. Hamkuwaua nyinyi, lakini Allaah Ndiye Aliyewaua. Na wala hukurusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم mchanga) pale uliporusha lakini Allaah Ndiye Aliyerusha, na ili Awajaribu Waumini jaribio zuri kutoka Kwake. Hakika Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.[8]
ذَٰلِكُمْ وَأَنَّ اللَّـهَ مُوهِنُ كَيْدِ الْكَافِرِينَ﴿١٨﴾
18. Ndio hivyo! Na hakika Allaah Ni Mwenye Kudhoofisha mbinu za makafiri.
إِن تَسْتَفْتِحُوا فَقَدْ جَاءَكُمُ الْفَتْحُ ۖ وَإِن تَنتَهُوا فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَإِن تَعُودُوا نَعُدْ وَلَن تُغْنِيَ عَنكُمْ فِئَتُكُمْ شَيْئًا وَلَوْ كَثُرَتْ وَأَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٩﴾
19. Mkitafuta hukmu (enyi makafiri), basi imeshakujieni hukmu. Na mkikoma (uhalifu) basi hivyo ni kheri kwenu. Na mkirudia (kuhujumu) Nasi Tutarudia, na wala kundi lenu halitokufaeni kitu chochote japo likikithiri. Na Hakika Allaah Yu Pamoja na Waumini.[9]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَا تَوَلَّوْا عَنْهُ وَأَنتُمْ تَسْمَعُونَ﴿٢٠﴾
20. Enyi walioamini! Mtiini Allaah na Rasuli Wake, na wala msijiepushe nazo (amri za Rasuli) na hali nyinyi mnasikia.
وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ قَالُوا سَمِعْنَا وَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ﴿٢١﴾
21. Na wala msiwe kama wale waliosema: Tumesikia na hali wao hawasikii.
إِنَّ شَرَّ الدَّوَابِّ عِندَ اللَّـهِ الصُّمُّ الْبُكْمُ الَّذِينَ لَا يَعْقِلُونَ﴿٢٢﴾
22. Hakika viumbe viovu kabisa mbele ya Allaah ni viziwi, mabubu ambao hawatumii akili.
وَلَوْ عَلِمَ اللَّـهُ فِيهِمْ خَيْرًا لَّأَسْمَعَهُمْ ۖ وَلَوْ أَسْمَعَهُمْ لَتَوَلَّوا وَّهُم مُّعْرِضُونَ﴿٢٣﴾
23. Na kama Allaah Angelijua kuwa wana kheri yoyote ile, basi Angeliwasikilizisha. Na kama Angeliwasikilizisha, wangeligeuka nao huku wakipuuza.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّـهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ ۖ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ﴿٢٤﴾
24. Enyi walioamini! Muitikieni Allaah na Rasuli Anapokuiteni kwenye yale yenye kukupeni uhai mwema (wa dunia na Aakhirah). na jueni kwamba Allaah Anaingilia kati baina ya mtu na moyo wake, na kwamba Kwake mtakusanywa.
وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَّا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنكُمْ خَاصَّةً ۖ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴿٢٥﴾
25. Na ogopeni mitihani ambayo haitowasibu pekee wale waliodhulumu miongoni mwenu. Na jueni kwamba Allaah Ni Mkali wa Kuakibu.
وَاذْكُرُوا إِذْ أَنتُمْ قَلِيلٌ مُّسْتَضْعَفُونَ فِي الْأَرْضِ تَخَافُونَ أَن يَتَخَطَّفَكُمُ النَّاسُ فَآوَاكُمْ وَأَيَّدَكُم بِنَصْرِهِ وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴿٢٦﴾
26. Na kumbukeni pale mlipokuwa wachache, mkikandamizwa ardhini, mnakhofu watu wasikunyakueni. (Allaah) Akakupeni makazi na Akakutieni nguvu kwa Nusra Yake, na Akakuruzukuni katika vizuri mpate kushukuru.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَخُونُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُوا أَمَانَاتِكُمْ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿٢٧﴾
27. Enyi walioamini! Msimfanyie khiyana Allaah na Rasuli na wala msikhini amana zenu na hali nyinyi mnajua.
وَاعْلَمُوا أَنَّمَا أَمْوَالُكُمْ وَأَوْلَادُكُمْ فِتْنَةٌ وَأَنَّ اللَّـهَ عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ﴿٢٨﴾
28. Na jueni kwamba mali zenu na watoto wenu ni jaribio, na kwamba kwa Allaah uko ujira mkubwa mno.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَتَّقُوا اللَّـهَ يَجْعَل لَّكُمْ فُرْقَانًا وَيُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ﴿٢٩﴾
29. Enyi walioamini! Mkimcha Allaah Atakupeni upambanuzi na Atakufutieni maovu yenu, na Atakughufurieni. Na Allaah Ni Mwenye Fadhila kubwa mno.
وَإِذْ يَمْكُرُ بِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِيُثْبِتُوكَ أَوْ يَقْتُلُوكَ أَوْ يُخْرِجُوكَ ۚ وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ﴿٣٠﴾
30. Na pindi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) walipokupangia makri wale waliokufuru ili wakufunge, au wakuue, au wakutoe (Makkah). Na wanapanga makri, na Allaah Anapanga makri[10] (kupindua njama zao), na Allaah Ni Mbora wa kupanga makri kuliko wote.
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا قَالُوا قَدْ سَمِعْنَا لَوْ نَشَاءُ لَقُلْنَا مِثْلَ هَـٰذَا ۙ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ﴿٣١﴾
31. Na wanaposomewa Aayaat Zetu, husema: Tumekwishasikia. Lau tungelitaka tungelisema kama haya. Haya si chochote isipokuwa ni hekaya za watu wa kale.
وَإِذْ قَالُوا اللَّـهُمَّ إِن كَانَ هَـٰذَا هُوَ الْحَقَّ مِنْ عِندِكَ فَأَمْطِرْ عَلَيْنَا حِجَارَةً مِّنَ السَّمَاءِ أَوِ ائْتِنَا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣٢﴾
32. Na pindi waliposema: Ee Allaah! Kama haya ni haki kutoka Kwako, basi Tunyeshee mvua ya mawe kutoka mbinguni au Tuletee adhabu iumizayo.[11]
وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُعَذِّبَهُمْ وَأَنتَ فِيهِمْ ۚ وَمَا كَانَ اللَّـهُ مُعَذِّبَهُمْ وَهُمْ يَسْتَغْفِرُونَ﴿٣٣﴾
33. Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu na hali wewe (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uko nao. Na Allaah Hakuwa wa kuwaadhibu hali wao wanaomba maghfirah.[12]
وَمَا لَهُمْ أَلَّا يُعَذِّبَهُمُ اللَّـهُ وَهُمْ يَصُدُّونَ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَمَا كَانُوا أَوْلِيَاءَهُ ۚ إِنْ أَوْلِيَاؤُهُ إِلَّا الْمُتَّقُونَ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٣٤﴾
34. Na wana nini hata Allaah Asiwaadhibu na hali wao wanazuia (watu) na Al-Masjidil-Haraam, na hawakuwa walinzi wake (Msikiti huo). Hawakuwa Rafiki Wake walinzi isipokuwa wenye taqwa, lakini wengi wao hawajui.
وَمَا كَانَ صَلَاتُهُمْ عِندَ الْبَيْتِ إِلَّا مُكَاءً وَتَصْدِيَةً ۚ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ﴿٣٥﴾
35. Na haikuwa Swalaah zao (makafiri) kwenye Nyumba (Al-Ka’bah) isipokuwa ni miruzi na kupiga makofi. Basi onjeni adhabu kwa sababu ya kufru yenu.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ ۗ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ﴿٣٦﴾
36. Hakika wale waliokufuru wanatoa mali zao ili wazuie Njia ya Allaah. Basi watazitoa, kisha zitakuwa ni majuto juu yao, kisha watashindwa. Na wale waliokufuru watakusanywa kwenye Jahannam.
لِيَمِيزَ اللَّـهُ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ وَيَجْعَلَ الْخَبِيثَ بَعْضَهُ عَلَىٰ بَعْضٍ فَيَرْكُمَهُ جَمِيعًا فَيَجْعَلَهُ فِي جَهَنَّمَ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿٣٧﴾
37. Ili Allaah Apambanue waovu na wema, kisha Awaweke waovu juu ya waovu wengine, halafu Awarundike pamoja Awatie katika Jahannam. Hao ndio waliokhasirika.
قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا إِن يَنتَهُوا يُغْفَرْ لَهُم مَّا قَدْ سَلَفَ وَإِن يَعُودُوا فَقَدْ مَضَتْ سُنَّتُ الْأَوَّلِينَ﴿٣٨﴾
38. Waambie waliokufuru kwamba wakikoma wataghufuriwa yaliyopita, lakini wakirudia, basi imekwishapita desturi[13] (ya Allaah) ya watu wa awali.
وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّـهِ ۚ فَإِنِ انتَهَوْا فَإِنَّ اللَّـهَ بِمَا يَعْمَلُونَ بَصِيرٌ﴿٣٩﴾
39. Na piganeni nao mpaka kusiweko fitnah, na Dini yote iwe kwa ajili ya Allaah. Na wakikoma, basi hakika Allaah kwa wanayoyatenda Ni Mwenye Kuona.
وَإِن تَوَلَّوْا فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَوْلَاكُمْ ۚ نِعْمَ الْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ النَّصِيرُ﴿٤٠﴾
40. Na wakikengeuka, basi jueni kwamba Allaah ni Mawlaa[14] wenu; Mawlaa Mzuri Alioje, na Mnusuruji Mzuri Alioje!
وَاعْلَمُوا أَنَّمَا غَنِمْتُم مِّن شَيْءٍ فَأَنَّ لِلَّـهِ خُمُسَهُ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ إِن كُنتُمْ آمَنتُم بِاللَّـهِ وَمَا أَنزَلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا يَوْمَ الْفُرْقَانِ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٤١﴾
41. Na jueni ya kwamba ghanima[15] yoyote mnayoipata (vitani), basi humusi yake ni ya Allaah na Rasuli, na jamaa wa karibu, na mayatima, na maskini, na wasafiri (walioharibikiwa), ikiwa nyinyi mumemwamini Allaah na yale Tuliyoyateremsha kwa mja Wetu siku ya upambanuzi; siku yalipokutana makundi mawili (vita vya Badr) na Allaah juu ya kila kitu Ni Mweza.
إِذْ أَنتُم بِالْعُدْوَةِ الدُّنْيَا وَهُم بِالْعُدْوَةِ الْقُصْوَىٰ وَالرَّكْبُ أَسْفَلَ مِنكُمْ ۚ وَلَوْ تَوَاعَدتُّمْ لَاخْتَلَفْتُمْ فِي الْمِيعَادِ ۙ وَلَـٰكِن لِّيَقْضِيَ اللَّـهُ أَمْرًا كَانَ مَفْعُولًا لِّيَهْلِكَ مَنْ هَلَكَ عَن بَيِّنَةٍ وَيَحْيَىٰ مَنْ حَيَّ عَن بَيِّنَةٍ ۗ وَإِنَّ اللَّـهَ لَسَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿٤٢﴾
42. Pale nyinyi mlipokuwa kando ya bonde la karibu, na wao (Makafiri) walipokuwa kando ya bonde la mbali, na msafara (wa mali zao) ulikuwa uko chini yenu. Na lau mngeliahidiana basi mngelikhitalifiana katika miadi hiyo, lakini ili Allaah Akidhie jambo lililokuwa lazima litendwe ili ahiliki (kwa ukafiri) yule wa kuhiliki kwa hoja bayana na ahuike (kwa imaan) mwenye kuhuika kwa hoja bayana. Na kwamba Allaah bila shaka Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
إِذْ يُرِيكَهُمُ اللَّـهُ فِي مَنَامِكَ قَلِيلًا ۖ وَلَوْ أَرَاكَهُمْ كَثِيرًا لَّفَشِلْتُمْ وَلَتَنَازَعْتُمْ فِي الْأَمْرِ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ سَلَّمَ ۗ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ﴿٤٣﴾
43. Pale Allaah Alipokuonyesha usingizini mwako kwamba wao ni wachache. Na lau Angelikuonyesha kuwa wao ni wengi, basi mngelivunjikwa moyo, na mngelizozana katika jambo hilo (la kupigana), lakini Allaah Amesalimisha (hayo). Hakika Yeye Ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.
وَإِذْ يُرِيكُمُوهُمْ إِذِ الْتَقَيْتُمْ فِي أَعْيُنِكُمْ قَلِيلًا وَيُقَلِّلُكُمْ فِي أَعْيُنِهِمْ لِيَقْضِيَ اللَّـهُ أَمْرًا كَانَ مَفْعُولًا ۗ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ﴿٤٤﴾
44. Na pindi (Allaah) Alipokuonyesheni machoni mwenu, pale mlipokutana, kuwa wao ni wachache na Akakufanyeni nyinyi kuwa wachache machoni mwao ili Allaah Akidhie jambo lililokuwa lazima litendwe. Na kwa Allaah Pekee hurejeshwa mambo yote.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا لَقِيتُمْ فِئَةً فَاثْبُتُوا وَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ﴿٤٥﴾
45. Enyi walioamini! Mtapokutana na kikosi (cha makafiri), basi simameni imara, na mdhukuruni Allaah kwa wingi ili mpate kufaulu.
وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَا تَنَازَعُوا فَتَفْشَلُوا وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ ۖ وَاصْبِرُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الصَّابِرِينَ﴿٤٦﴾
46. Na mtiini Allaah na Rasuli Wake, na wala msizozane, mtavunjikwa moyo, na nguvu zenu zitatoweka, na subirini. Hakika Allaah Yu Pamoja na wanaosubiri.
وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ خَرَجُوا مِن دِيَارِهِم بَطَرًا وَرِئَاءَ النَّاسِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ﴿٤٧﴾
47. Na wala msiwe kama wale waliotoka majumbani mwao kwa majivuno na riyaa-a[16] (kujionyesha) kwa watu, na wanazuia Njia ya Allaah. Na Allaah Ni Mwenye Kuyazunguka yote wanayoyatenda.
وَإِذْ زَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ وَقَالَ لَا غَالِبَ لَكُمُ الْيَوْمَ مِنَ النَّاسِ وَإِنِّي جَارٌ لَّكُمْ ۖ فَلَمَّا تَرَاءَتِ الْفِئَتَانِ نَكَصَ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ وَقَالَ إِنِّي بَرِيءٌ مِّنكُمْ إِنِّي أَرَىٰ مَا لَا تَرَوْنَ إِنِّي أَخَافُ اللَّـهَ ۚ وَاللَّـهُ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴿٤٨﴾
48. Na pindi shaytwaan alipowapambia amali zao na akasema: Hakuna watu wa kukushindeni leo, na mimi ni mlinzi wenu. Vilipoonana vikosi viwili, (shaytwaan) alirejea nyuma akigeuka[17] na kusema: Hakika mimi nimejitoa dhima nanyi (sihusiki), hakika mimi naona msiyoyaona, hakika mimi namkhofu Allaah. Na Allaah Ni Mkali wa Kuakibu.
إِذْ يَقُولُ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ غَرَّ هَـٰؤُلَاءِ دِينُهُمْ ۗ وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ فَإِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٤٩﴾
49. Na waliposema wanafiki na wale walio na maradhi katika nyoyo zao[18]: Dini yao (hawa Waislamu) imewaghuri. Na anayetawakali kwa Allaah (atashinda tu kwani), hakika Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ يَتَوَفَّى الَّذِينَ كَفَرُوا ۙ الْمَلَائِكَةُ يَضْرِبُونَ وُجُوهَهُمْ وَأَدْبَارَهُمْ وَذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ﴿٥٠﴾
50. Na lau ungeliona pale Malaika wanapowafisha wale waliokufuru, wanawapiga nyuso zao na migongo yao na (wanawaambia): Onjeni adhabu iunguzayo!
ذَٰلِكَ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيكُمْ وَأَنَّ اللَّـهَ لَيْسَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ ﴿٥١﴾
51. Hayo ni kwa yale (maovu) yaliyotangulizwa na mikono yenu, na hakika Allaah Si Mwenye Kudhulumu waja.
كَدَأْبِ آلِ فِرْعَوْنَ ۙ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ فَأَخَذَهُمُ اللَّـهُ بِذُنُوبِهِمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ قَوِيٌّ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴿٥٢﴾
52. Ni kama mwenendo wa watu wa Firawni na wale wa kabla yao. Walizikufuru Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) za Allaah. Basi Allaah Akawachukua kwa sababu ya madhambi yao. Hakika Allaah Ni Mwenye nguvu zote, Mkali wa Kuakibu.
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ لَمْ يَكُ مُغَيِّرًا نِّعْمَةً أَنْعَمَهَا عَلَىٰ قَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ ۙ وَأَنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿٥٣﴾
53. Hayo ni kwa kuwa Allaah Hakuwa Mwenye Kubadilisha neema yoyote Aliyoineemesha kwa watu mpaka wao wabadilishe yaliyomo ndani ya nafsi zao. Na hakika Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
كَدَأْبِ آلِ فِرْعَوْنَ ۙ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَذَّبُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ فَأَهْلَكْنَاهُم بِذُنُوبِهِمْ وَأَغْرَقْنَا آلَ فِرْعَوْنَ ۚ وَكُلٌّ كَانُوا ظَالِمِينَ﴿٥٤﴾
54. Ni kama mwenendo wa watu wa Firawni na wale wa kabla yao. Walikadhibisha Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) za Rabb wao, Tukawaangamiza kwa sababu ya madhambi yao, na Tukawagharikisha watu wa Firawni, na wote walikuwa madhalimu.
إِنَّ شَرَّ الدَّوَابِّ عِندَ اللَّـهِ الَّذِينَ كَفَرُوا فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ﴿٥٥﴾
55. Hakika viumbe viovu kabisa mbele ya Allaah ni wale waliokufuru nao hawaamini.
الَّذِينَ عَاهَدتَّ مِنْهُمْ ثُمَّ يَنقُضُونَ عَهْدَهُمْ فِي كُلِّ مَرَّةٍ وَهُمْ لَا يَتَّقُونَ﴿٥٦﴾
56. Ambao umepeana nao ahadi, kisha wanavunja ahadi yao kila mara, na wala hawamwogopi na kumstahi Allaah.
فَإِمَّا تَثْقَفَنَّهُمْ فِي الْحَرْبِ فَشَرِّدْ بِهِم مَّنْ خَلْفَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ﴿٥٧﴾
57. Basi mkiwashinda vitani (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), waadhibu vikali ili wakimbie mbali walio nyuma yao wapate kuwaidhika.
وَإِمَّا تَخَافَنَّ مِن قَوْمٍ خِيَانَةً فَانبِذْ إِلَيْهِمْ عَلَىٰ سَوَاءٍ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْخَائِنِينَ﴿٥٨﴾
58. Na kama ukikhofu khiyana kwa watu basi watupilie (ahadi yao) ili iwe sawasawa (kusiweko tena kuahidiana). Hakika Allaah Hapendi makhaini.
وَلَا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا سَبَقُوا ۚ إِنَّهُمْ لَا يُعْجِزُونَ﴿٥٩﴾
59. Na wala wasidhanie kabisa wale waliokufuru kwamba wao wamesabiki mbele (kuokoka). Hakika wao hawataweza kushinda (kukwepa Adhabu ya Allaah).
وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ وَمِن رِّبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّـهِ وَعَدُوَّكُمْ وَآخَرِينَ مِن دُونِهِمْ لَا تَعْلَمُونَهُمُ اللَّـهُ يَعْلَمُهُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ﴿٦٠﴾
60. Na waandalieni nguvu[19] (za kiakili na kila aina za silaha) na farasi waliofungwa tayari kwa vita muwaogopeshe kwao maadui wa Allaah na maadui zenu, na wengineo wasiokuwa wao, hamuwajui, (lakini) Allaah Anawajua. Na chochote mkitoacho katika Njia ya Allaah mtalipwa kikamilifu, nanyi hamtodhulumiwa.
وَإِن جَنَحُوا لِلسَّلْمِ فَاجْنَحْ لَهَا وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿٦١﴾
61. Na kama (maadui) wakielemea kwenye amani basi nawe ielemee na tawakali kwa Allaah. Hakika Yeye Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
وَإِن يُرِيدُوا أَن يَخْدَعُوكَ فَإِنَّ حَسْبَكَ اللَّـهُ ۚ هُوَ الَّذِي أَيَّدَكَ بِنَصْرِهِ وَبِالْمُؤْمِنِينَ﴿٦٢﴾
62. Na wakitaka kukuhadaa, basi hakika Allaah Anakutosheleza. Yeye Ndiye Ambaye Amekusaidia kwa Nusra Yake, na kwa Waumini.
وَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ ۚ لَوْ أَنفَقْتَ مَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا مَّا أَلَّفْتَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ أَلَّفَ بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٦٣﴾
63. Na Akaunganisha nyoyo zao. Lau ungelitoa vyote vilivyomo ardhini, basi usingeliweza kuunganisha nyoyo zao, lakini Allaah Amewaunganisha. Hakika Yeye Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ حَسْبُكَ اللَّـهُ وَمَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ﴿٦٤﴾
64. Ee Nabiy! Allaah Anakutosheleza wewe pamoja na Waumini waliokufuata.
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ حَرِّضِ الْمُؤْمِنِينَ عَلَى الْقِتَالِ ۚ إِن يَكُن مِّنكُمْ عِشْرُونَ صَابِرُونَ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ ۚ وَإِن يَكُن مِّنكُم مِّائَةٌ يَغْلِبُوا أَلْفًا مِّنَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ﴿٦٥﴾
65. Ee Nabiy! Shajiisha Waumini kupigana vita. Wakiweko miongoni mwenu (Waumini) wahimilivu ishirini basi watawashinda (makafiri) mia mbili. Na wakiweko miongoni mwenu mia, watawashinda elfu katika wale waliokufuru, kwa kuwa wao ni watu wasiofahamu.
الْآنَ خَفَّفَ اللَّـهُ عَنكُمْ وَعَلِمَ أَنَّ فِيكُمْ ضَعْفًا ۚ فَإِن يَكُن مِّنكُم مِّائَةٌ صَابِرَةٌ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ ۚ وَإِن يَكُن مِّنكُمْ أَلْفٌ يَغْلِبُوا أَلْفَيْنِ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ مَعَ الصَّابِرِينَ﴿٦٦﴾
66. Sasa Allaah Amekukhafifishieni na Amejua kwamba kuna udhaifu kwenu. Hivyo basi wakiweko miongoni mwenu (Waumini) wahimilivu mia, watawashinda (makafiri) mia mbili. Na wakiweko miongoni mwenu (Waumini) elfu, wawatashinda (makafiri) elfu mbili kwa Idhini ya Allaah. Na Allaah Yu pamoja na wenye subira.[20]
مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَكُونَ لَهُ أَسْرَىٰ حَتَّىٰ يُثْخِنَ فِي الْأَرْضِ ۚ تُرِيدُونَ عَرَضَ الدُّنْيَا وَاللَّـهُ يُرِيدُ الْآخِرَةَ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٦٧﴾
67. Haikumpasa Nabiy yeyote awe ana mateka mpaka apigane vikali mno kuwaua na kuwajeruhi (maadui wa Allaah) nchini. Mnataka vitu vya dunia, na hali Allaah Anataka (mpate vya) Aakhirah. Na Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.[21]
لَّوْلَا كِتَابٌ مِّنَ اللَّـهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَا أَخَذْتُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿٦٨﴾
68. Lau kama si hukumu iliyotangulia kutoka kwa Allaah, bila shaka ingekupateni adhabu kuu mno kwa vile mlivyochukua.[22]
فَكُلُوا مِمَّا غَنِمْتُمْ حَلَالًا طَيِّبًا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٦٩﴾
69. Basi kuleni katika ghanima mlizozipata, ni halali na ni vizuri, na mcheni Allaah. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّمَن فِي أَيْدِيكُم مِّنَ الْأَسْرَىٰ إِن يَعْلَمِ اللَّـهُ فِي قُلُوبِكُمْ خَيْرًا يُؤْتِكُمْ خَيْرًا مِّمَّا أُخِذَ مِنكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٧٠﴾
70. Ee Nabiy! Waambie wale waliomo mikononi mwenu katika mateka: Kama Allaah Akijua kheri yoyote katika nyoyo zenu, Atakupeni ya bora kuliko vilivyochukuliwa kwenu, na Atakughufurieni. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَإِن يُرِيدُوا خِيَانَتَكَ فَقَدْ خَانُوا اللَّـهَ مِن قَبْلُ فَأَمْكَنَ مِنْهُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٧١﴾
71. Na wakitaka kukufanyia khiyana, basi wao wamekwishamfanyia khiyana Allaah kabla yake, Naye Akakuwezesha kuwashinda. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَالَّذِينَ آوَوا وَّنَصَرُوا أُولَـٰئِكَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يُهَاجِرُوا مَا لَكُم مِّن وَلَايَتِهِم مِّن شَيْءٍ حَتَّىٰ يُهَاجِرُوا ۚ وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ إِلَّا عَلَىٰ قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَاقٌ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ﴿٧٢﴾
72. Hakika wale walioamini na wakahajiri (Muhaajirina) na wakafanya Jihaad kwa mali zao na nafsi zao katika Njia ya Allaah, na wale waliowapa makazi (Answaar) na wakanusuru (Dini ya Allaah), hao ni marafiki wandani na walinzi, wao kwa wao. Na wale walioamini lakini hawakuhajiri, hamna nyinyi wajibu wowote wa kuwalinda mpaka wahajiri. Na wakikuombeni msaada katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia isipokuwa juu ya watu mliofungamana nao mapatano baina yenu na wao. Na Allaah Ni Mwenye Kuona myatendayo.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ إِلَّا تَفْعَلُوهُ تَكُن فِتْنَةٌ فِي الْأَرْضِ وَفَسَادٌ كَبِيرٌ﴿٧٣﴾
73. Na wale waliokufuru ni marafiki wandani na walinzi, wao kwa wao. (Nanyi Waislamu) Msipofanya hivi itakuweko fitnah katika ardhi na ufisadi mkubwa.
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَالَّذِينَ آوَوا وَّنَصَرُوا أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا ۚ لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ﴿٧٤﴾
74. Na wale walioamini na wakahajiri na wakafanya Jihaad katika Njia ya Allaah, na wale waliotoa makazi na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata maghfirah na riziki karimu.
وَالَّذِينَ آمَنُوا مِن بَعْدُ وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا مَعَكُمْ فَأُولَـٰئِكَ مِنكُمْ ۚ وَأُولُو الْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَىٰ بِبَعْضٍ فِي كِتَابِ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴿٧٥﴾
75. Na wale walioamini baada (ya hijra) na wakahajiri na wakafanya Jihaad pamoja nanyi, basi hao ni miongoni mwenu. Na ndugu wa uhusiano wa damu wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe (kwa kurithiana), katika Sharia ya Allaah. Hakika Allaah Ni Mjuzi wa kila kitu.[23]
[2] Ghazwat-Badr (Vita Vitukufu Vya Badr):
Vita vitukufu vya Badr vimetajwa katika Aayah zifuatazo za Suwrah hii Al-Anfaal:
(5-10), (12), (15-19), (37-40), (42-47), (64-70). Na Allaah Mjuzi zaidi.
Hali kadhaalika vita vya Badr vimetajwa katika Suwrah Aal-‘Imraan.
Badr ni jina la mji ulioko kilomita mia na khamsini mbali na Madiynah. Mahali hapo kulikuwa na bonde tu na kisima kilichokuwa milki ya mtu aitwaye “Badr.” Na hii ni kauli mojawapo ya ‘Ulamaa; Rejea Aal-‘Imraan (3:123).
Vita vikubwa vya Badr vilitokea Ramadhwaan ya kumi na saba, asubuhi ya siku ya Ijumaa, mwaka wa pili baada ya Hijrah.
Kulikuwa na msafara wa biashara wa makafiri ukiongozwa na Abu Sufyaan ambaye alikuwa bin ammi wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Bint yake Abu Sufyaan aliyeitwa Habiybah, alikuwa mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Hapo Abu Sufyaan alikuwa bado ni kafiri kisha akaja kusilimu katika mwaka wa Fat-h Makkah (Ushindi wa Makkah).
Msafara huo uliotoka Sham ulikuwa unarudi Makkah ukiwa na watu wasiozidi arubaini, na msafara ulibeba mali nyingi mno ya watu wa Makkah. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliona ni fursa ya kulipiza kisasi kwa makafiri waliowalazimisha Wasilamu kuziacha mali zao Makkah walipohajiri kwenda Madiynah. Waislamu hawakujua kama msafara huo utakuja kugeuka kuwa vita vya kupambanua haki na batili. Makafiri wa Quraysh waliandaa jeshi kubwa la watu wakiongozwa na Abu Jahal bin Hishaam na vigogo vya Quraysh wa Makkah. Waliandaa pia nguvu za farasi na ngamia wengi. Waislamu walipopata khabari ya jeshi kubwa lilowakabili waliingiwa khofu kubwa kwa sababu walikuwa wachache na hawana silaha za kutosha, na baadhi yao wakatoa nyudhuru. Basi Waislamu ikawa ima wakabiliane na jeshi kubwa la Quraysh au waukabili msafara wapate kuteka mali. Lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Alitaka na Aliqadiria wakabiliane na jeshi la Quraysh ili kudhihirike pambanuo la haki na batili kwa Qudra Yake Allaah (سبحانه وتعالى).
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasimama kuomba; Rejea Suwrah hii Al-Anfaal (8:9). Na Allaah (سبحانه وتعالى) Akatoa Ahadi Yake na Akateremsha Miujiza Yake kama kuteremsha maelfu ya Malaika wawatie nguvu Waislamu kupigana vita na makafiri wa Quraysh.
Pia Allaah (سبحانه وتعالى) Alifanya Kuwaua makafiri pale Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipowarushia mchanga: Rejea Suwrah hii Al-Anfaal (8:17).
Pia Allaah (سبحانه وتعالى) Akawateremshia Waislamu utulivu wakapata usingizi mzito hadi wakaota na Akawateremshia mvua ya kujitwaharisha, na Akathibitisha miguu yao ardhini; Rejea Suwrah hii Al-Anfaal (8:11). Na miujiza mengineyo ambayo Aayah tukufu zinaendelea kutaja. Basi katika vita hivi Makafiri wakubwa wa Quraysh waliuliwa wakiwemo vigogo vyao wakubwa Abu Jahal, na ‘Utbah bin Rabiy’ah. Na kwa Rehma ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Uwezo Wake Akajaalia ushindi kwa Waislamu juu ya kuwa wao walikuwa ni wachache.
Hakika ilikuwa Vita vya Miujiza vinavyosisimua pindi mtu akipata ilimu ya Tafsiyr yake pamoja na Hadiyth husika.
[3] Maana Ya Istighaathah Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Aliomba Duaa Siku Ya Vita Vya Badr Anusuriwe:
Istighaathah maana yake ni kuomba uokozi kwa ambaye ataweza kuokoa kutokana na hali ya shida, dhiki na kukaribia kudhurika au kuangamia. Na istighaathah kwa Allaah (سبحانه وتعالى) inajumuisha kujidhalilisha Kwake na kuitakidi kwamba hakuna mwengine atakayeweza kuokoa isipokuwa Yeye.
[5] Tofauti Ya Ikabu Na Adhabu: Rejea Al-Hashr (59:4).
[6] Kukimbia Vita Vya Jihaad Ni Miongoni Mwa Dhambi Saba Zinazoangamiza:
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) : Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Jiepusheni na mambo saba yanayoangamiza!” Wakauliza: Ni yepi hayo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Ni kumshirikisha Allaah, sihri (uchawi), kuua nafsi Aliyoiharamisha Allaah isipokuwa kwa haki, kula riba, kula mali ya yatima, kukimbia wakati wa kupambana na adui, na kuwatuhumu uzinifu wanawake Waumini waliohifadhika walioghafilika”. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
[7] Aayah hii imeteremshwa siku ya Vita vya Badr. [Sunan Abiy Daawuwd, Kitaab Al-Jihaad, Hadiyth ya Abuu Sa’iyd, na ameisahihisha Al-Albaaniy]
[10] Allaah Hana Sifa Mbaya Ila Analipiza Uovu. Rejea Aal-‘Imraan (3:54).
[11] Ada Ya Makafiri Kuhimiza Adhabu: Rejea Al-Hajj (22:47), Swaad (38:16), Ash-Shuwraa (42:18).
[12] Uwepo Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ulikuwa Ni Neema Kwa Makafiri Kutokuadhibiwa. Na Fadhila Za Istighfaar (Kuomba Maghfirah)
Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) amesema: “Kutokana na kauli yao hiyo ya Aayah (32) ya kuomba adhabu) ni dhahiri kuwa wao ni wajinga wapumbavu, madhalimu. Lau kama Allaah Angewaharakishia adhabu basi wasingebakia kuishi. Lakini Allaah Amewakinga na adhabu kwa sababu ya uwepo wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) miongoni mwao. Basi uwepo wa Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) ni amani kwao kutokana na adhabu.” [Tafsiyr As-Sa’diy]
Fadhila Za Istighfaar (Kuomba Maghfirah):
Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema kuwa Hakuwaadhibu makafiri kwa sababu ya kuomba kwao maghfirah. Hivyo inadhihirisha kwamba kuomba maghfirah inasababisha kutokuadhibiwa na Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Huwd (11:3) kwenye faida kadhaa na fadhila za kuomba Istighfaar.
Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
[13] Desturi Ya Allaah (سبحانه وتعالى):
Ni kuadhibu na kuangamiza makafiri na wanafiki wa nyumati za nyuma zilizokadhibisha Rusuli Wake na Ishara Zake. Na kwamba ushindi unakuwa daima kwa Rusuli Wake. Na desturi hii hutoiona kamwe kubadilika. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja hayo mara kadhaa katika visa vya nyumati za nyuma. Rejea Aal-‘Imraan (3:137).
[14] Mawlaa "مَوْلَى": Rejea Faharasa Ya Majina Ya Allaah (سبحانه وتعالى).
[15] Ghanima: Ngawira Inayopatikana Baada Ya Kupigana Vita:
Ghanima (ambalo ni neno la Kiarabu ("غنيمة" ni mali inayopatikana kwa kutekwa baada ya ushindi katika vita kama mifugo, watu, mazao, zana na kadhalika kama ilivyotajwa katika Suwrah hii na Al-Fat-h (48:19-20). Ama mali inayopatikana bila ya kupigana vita, hii inaitwa katika Qur-aan Al-Fay-u "الفَيْءُ" ambayo imetajwa katika Al-Hashr (59:6-7).
[16] Riyaa-a (Kujionyesha Kwa Watu): Ni Shirki Inayobatilisha Amali:
Hii ni riyaa-a ya kwenda katika Jihaad. Na juu ya hivyo kusudio la wanafiki lilikuwa ni kuzuia watu njia ya Allaah. Rejea Az-Zumar (39:65) kwenye maelezo kuhusu aina za shirki
[17] Shaytwaan Huwapotosha Watu Kisha Huwakanusha Na Kuwagueka:
Rejea pia Suwrah Ibraahiym (14:22), Al-Israa (17:64) kwenye maelezo bayana.
[18] Nyoyo Zenye Maradhi:
Rejea Suwrah Muhammad (47:20) kwenye maelezo na rejea mbalimbali kuhusu nyoyo zenye maradhi.
Rejea pia Al-Hajj (22:46) kwenye maelezo kuhusu maana ya moyo uliopofuka.
Rejea pia Ash-Shu’araa (26:88-89) kwenye ufafanuzi na maelezo kuhusu moyo uliosalimika.
[19] Maana Ya قُوَّةٍ:
Imekusudiwa pia kujifunza kutupa mishale kama ilivyotajwa katika Hadiyth: Amesimulia ‘Uqbah bin ‘Aamir (رضي الله عنه) : Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa juu ya minbar akisema:
وَأَعِدُّوا لَهُمْ مَا اسْتَطَعْتُمْ مِنْ قُوَّةٍ
“Na waandalieni nguvu zozote mziwezazo …” Tanabahi! Hakika Al-Quwwah ni Ar-Ramyu (kutupa mshale, kulenga kwa kutumia silaha), hakika Al-Quwwah ni Ar-Ramyu, hakika Al-Quwwah ni Ar-Ramyu.” [Muslim]
Pia kujifunza ushujaa, mipango ya kuandaa jeshi mbali na hayo yaliyotajwa ya kujiandaa kwa silaha za kila aina zikiwemo ndege za vita, mizinga, bunduki, gari za ardhini na boti za baharini, ngome, mahandaki, mashine za ulinzi na mengineyo yote ya vita ili Waislamu waweze kuwashinda maadui zao.
التَّوْبَة
009-At-Tawbah
009-At-Tawbah: Utangulizi Wa Suwrah [130]
Alhidaaya.com [6]
بَرَاءَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ إِلَى الَّذِينَ عَاهَدتُّم مِّنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١﴾
1. (Hii ni) Kujitoa katika dhima (kunatangazwa) kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake kwa wale mlioahidiana nao katika washirikina.[1]
فَسِيحُوا فِي الْأَرْضِ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِي اللَّـهِ ۙ وَأَنَّ اللَّـهَ مُخْزِي الْكَافِرِينَ﴿٢﴾
2. Basi vinjarini ardhini miezi minne, na jueni kwamba nyinyi hamuwezi kumshinda Allaah (kumkwepa), na kwamba Allaah Ni Mwenye Kuwahizi makafiri.
وَأَذَانٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ إِلَى النَّاسِ يَوْمَ الْحَجِّ الْأَكْبَرِ أَنَّ اللَّـهَ بَرِيءٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ ۙ وَرَسُولُهُ ۚ فَإِن تُبْتُمْ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِي اللَّـهِ ۗ وَبَشِّرِ الَّذِينَ كَفَرُوا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣﴾
3. Na ni tangazo kutoka kwa Allaah na Rasuli Wake kwa watu siku ya Hajj kubwa, kwamba Allaah na Rasuli Wake hawana dhima yoyote kwa washirikina. Basi mkitubu, itakuwa kheri kwenu, na kama mtakengeuka, basi jueni kwamba nyinyi hamuwezi kumshinda Allaah (kumkwepa). Na wabashirie wale waliokufuru watapata adhabu iumizayo.
إِلَّا الَّذِينَ عَاهَدتُّم مِّنَ الْمُشْرِكِينَ ثُمَّ لَمْ يَنقُصُوكُمْ شَيْئًا وَلَمْ يُظَاهِرُوا عَلَيْكُمْ أَحَدًا فَأَتِمُّوا إِلَيْهِمْ عَهْدَهُمْ إِلَىٰ مُدَّتِهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ﴿٤﴾
4. Isipokuwa wale mlioahidiana nao katika washirikina, kisha hawakukupunguzieni chochote na wala hawakumsaidia yeyote dhidi yenu, basi watimizieni ahadi yao mpaka muda wao (umalizike). Hakika Allaah Anapenda wenye taqwa.
فَإِذَا انسَلَخَ الْأَشْهُرُ الْحُرُمُ فَاقْتُلُوا الْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ وَخُذُوهُمْ وَاحْصُرُوهُمْ وَاقْعُدُوا لَهُمْ كُلَّ مَرْصَدٍ ۚ فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٥﴾
5. Itapomalizika Miezi Mitukufu, basi waueni washirikina popote muwakutapo, na wachukueni (mateka) na wahusuruni, na wakalieni katika kila kivuko cha njia zao. Lakini wakitubu, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah, basi waachieni huru njia zao. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ اسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَامَ اللَّـهِ ثُمَّ أَبْلِغْهُ مَأْمَنَهُ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْلَمُونَ﴿٦﴾
6. Na ikiwa mmoja wa washirikina amekuomba umlinde, basi mlinde mpaka asikie Maneno ya Allaah (Qur-aan)[2] kisha mfikishe mahali pake pa amani. Hivyo kwa kuwa wao ni watu wasiojua.
كَيْفَ يَكُونُ لِلْمُشْرِكِينَ عَهْدٌ عِندَ اللَّـهِ وَعِندَ رَسُولِهِ إِلَّا الَّذِينَ عَاهَدتُّمْ عِندَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ ۖ فَمَا اسْتَقَامُوا لَكُمْ فَاسْتَقِيمُوا لَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ﴿٧﴾
7. Vipi iweko ahadi na washirikina mbele ya Allaah na mbele ya Rasuli Wake, isipokuwa wale mlioahidiana mbele ya Masjid Al-Haraam? Basi wakikunyookeeni (kwa uzuri), nanyi wanyookeeni. Hakika Allaah Anapenda wenye taqwa.
كَيْفَ وَإِن يَظْهَرُوا عَلَيْكُمْ لَا يَرْقُبُوا فِيكُمْ إِلًّا وَلَا ذِمَّةً ۚ يُرْضُونَكُم بِأَفْوَاهِهِمْ وَتَأْبَىٰ قُلُوبُهُمْ وَأَكْثَرُهُمْ فَاسِقُونَ﴿٨﴾
8. Vipi (mtashikamana na mkataba)? Hali wao wakikushindeni hawachungi kwenu udugu wa damu wala ahadi ya himaya? Wanakuridhisheni kwa midomo yao, na hali nyoyo zao zinakataa (makubaliano), na wengi wao ni mafasiki.
اشْتَرَوْا بِآيَاتِ اللَّـهِ ثَمَنًا قَلِيلًا فَصَدُّوا عَن سَبِيلِهِ ۚ إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩﴾
9. Wamebadili Aayaat za Allaah kwa thamani ndogo, na wakazuilia Njia Yake. Hakika ni maovu waliyokuwa wakitenda.
لَا يَرْقُبُونَ فِي مُؤْمِنٍ إِلًّا وَلَا ذِمَّةً ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُعْتَدُونَ﴿١٠﴾
10. Hawachungi kwa Muumini udugu wa damu wala ahadi ya himaya. Na hao ndio wenye kutaadi.
فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ ۗ وَنُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ﴿١١﴾
11. Wakitubu, na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa Zakaah, basi ni ndugu zenu katika Dini. Na Tunafasili waziwazi Aayaat (Ishara, Dalili, Hukmu) kwa watu wanaojua.
وَإِن نَّكَثُوا أَيْمَانَهُم مِّن بَعْدِ عَهْدِهِمْ وَطَعَنُوا فِي دِينِكُمْ فَقَاتِلُوا أَئِمَّةَ الْكُفْرِ ۙ إِنَّهُمْ لَا أَيْمَانَ لَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَنتَهُونَ﴿١٢﴾
12. Na wakivunja viapo vyao baada ya ahadi yao, na wakatukana Dini yenu, basi wapigeni vita viongozi wa ukafiri. Hakika viapo vyao havina maana. (Piganeni nao) ili wapate kukoma.
أَلَا تُقَاتِلُونَ قَوْمًا نَّكَثُوا أَيْمَانَهُمْ وَهَمُّوا بِإِخْرَاجِ الرَّسُولِ وَهُم بَدَءُوكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۚ أَتَخْشَوْنَهُمْ ۚ فَاللَّـهُ أَحَقُّ أَن تَخْشَوْهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١٣﴾
13. Je, hamtopigana na watu waliovunja viapo vyao, na wakafanya hima kumtoa Rasuli, nao ndio waliokuanzeni mara ya kwanza? Je, mnawaogopa? Basi Allaah Anastahiki zaidi mumwogope ikiwa nyinyi ni Waumini (wa kweli).
قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللَّـهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ﴿١٤﴾
14. Piganeni nao, Allaah Atawaadhibu kwa mikono yenu, na Atawahizi na Atakunusuruni dhidi yao, na Atapozesha vifua vya kundi la Waumini.
وَيُذْهِبْ غَيْظَ قُلُوبِهِمْ ۗ وَيَتُوبُ اللَّـهُ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿١٥﴾
15. Na Ataondosha ghaidhi za nyoyo zao (Waumini). Na Allaah Anapokea tawbah kwa Amtakaye, na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تُتْرَكُوا وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّـهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنكُمْ وَلَمْ يَتَّخِذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَا رَسُولِهِ وَلَا الْمُؤْمِنِينَ وَلِيجَةً ۚ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴿١٦﴾
16. Je, mmedhani kuwa mtaachwa tu nailhali Allaah bado Hajawadhihirisha wale waliofanya Jihaad miongoni mwenu, na hawakufanya yeyote kuwa rafiki mwandani isipokuwa Allaah na Rasuli Wake na Waumini (wenzao)? Na Allaah Ndiye Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri kwa yale myatendayo.
مَا كَانَ لِلْمُشْرِكِينَ أَن يَعْمُرُوا مَسَاجِدَ اللَّـهِ شَاهِدِينَ عَلَىٰ أَنفُسِهِم بِالْكُفْرِ ۚ أُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ وَفِي النَّارِ هُمْ خَالِدُونَ﴿١٧﴾
17. Haiwi kwa washirikina kuamirisha Misikiti ya Allaah hali wanajishuhudia nafsi zao kwa ukafiri. Hao zimeporomoka amali zao, na katika moto wao watadumu.
إِنَّمَا يَعْمُرُ مَسَاجِدَ اللَّـهِ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَلَمْ يَخْشَ إِلَّا اللَّـهَ ۖ فَعَسَىٰ أُولَـٰئِكَ أَن يَكُونُوا مِنَ الْمُهْتَدِينَ﴿١٨﴾
18. Hakika wanaoamirisha Misikiti ya Allaah ni wale wanaomwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na wakasimamisha Swalaah na wakatoa Zakaah na hawamkhofu (yeyote) isipokuwa Allaah. Basi asaa hao wakawa miongoni mwa waliohidika.
أَجَعَلْتُمْ سِقَايَةَ الْحَاجِّ وَعِمَارَةَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ كَمَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَجَاهَدَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ لَا يَسْتَوُونَ عِندَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿١٩﴾
19. Je, mmefanya kunywesha maji Hujaji na kuamirisha Masjid Al-Haraam kama sawasawa na (amali za) anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na akafanya Jihaad katika Njia ya Allaah? (Hapana!) Hawawi sawa mbele ya Allaah. Na Allaah Hawahidi watu madhalimu.[3]
الَّذِينَ آمَنُوا وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ أَعْظَمُ دَرَجَةً عِندَ اللَّـهِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَائِزُونَ﴿٢٠﴾
20. Wale walioamini na wakahajiri na wakafanya Jihaad katika Njia ya Allaah kwa mali zao na nafsi zao, wana daraja kubwa zaidi kwa Allaah. Na hao ndio waliofuzu.
يُبَشِّرُهُمْ رَبُّهُم بِرَحْمَةٍ مِّنْهُ وَرِضْوَانٍ وَجَنَّاتٍ لَّهُمْ فِيهَا نَعِيمٌ مُّقِيمٌ﴿٢١﴾
21. Rabb wao Anawabashiria Rehma kutoka Kwake na Radhi na Jannaat (Pepo), watapata humo neema zenye kudumu.
خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ﴿٢٢﴾
22. Wadumu humo abadi. Hakika kwa Allaah kuna ujira mkubwa mno.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا آبَاءَكُمْ وَإِخْوَانَكُمْ أَوْلِيَاءَ إِنِ اسْتَحَبُّوا الْكُفْرَ عَلَى الْإِيمَانِ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿٢٣﴾
23. Enyi walioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu marafiki wandani ikiwa wanapendelea ukafiri badala ya imaan. Na atakayewafanya marafiki wandani miongoni mwenu, basi hao ndio madhalimu.
قُلْ إِن كَانَ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ وَإِخْوَانُكُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَالٌ اقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَارَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَاكِنُ تَرْضَوْنَهَا أَحَبَّ إِلَيْكُم مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَجِهَادٍ فِي سَبِيلِهِ فَتَرَبَّصُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴿٢٤﴾
24. Sema: Ikiwa baba zenu, na watoto wenu, na ndugu zenu, na wake (au waume) zenu, na jamaa zenu, na mali mliyoichuma, na biashara mnayoikhofia kuharibika kwake, na majumba mnayoridhika nayo, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Allaah na Rasuli Wake na kufanya Jihaad katika Njia Yake, basi ngojeeni mpaka Allaah Alete Amri Yake (ya adhabu). Na Allaah Hawahidi watu mafasiki.
لَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّـهُ فِي مَوَاطِنَ كَثِيرَةٍ ۙ وَيَوْمَ حُنَيْنٍ ۙ إِذْ أَعْجَبَتْكُمْ كَثْرَتُكُمْ فَلَمْ تُغْنِ عَنكُمْ شَيْئًا وَضَاقَتْ عَلَيْكُمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ ثُمَّ وَلَّيْتُم مُّدْبِرِينَ﴿٢٥﴾
25. Kwa yakini Allaah Amekunusuruni katika maeneo mengi (ya vita) na Siku ya (Vita vya) Hunayn[4] (pia) ulipokughururini wingi wenu (kwa kujigamba), lakini haukukufaeni chochote, na ardhi ikawa dhiki juu yenu juu ya upana wake, kisha mkageuka na kurudi nyuma kukimbia.
ثُمَّ أَنزَلَ اللَّـهُ سَكِينَتَهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ وَعَلَى الْمُؤْمِنِينَ وَأَنزَلَ جُنُودًا لَّمْ تَرَوْهَا وَعَذَّبَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الْكَافِرِينَ﴿٢٦﴾
26. Kisha Allaah Akateremsha utulivu Wake kwa Rasuli Wake na kwa Waumini, na Akateremsha majeshi (ya Malaika) msiyoyaona, na Akawaadhibu wale waliokufuru. Na hivyo ndio jazaa ya makafiri.
ثُمَّ يَتُوبُ اللَّـهُ مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٢٧﴾
27. Kisha Allaah Anapokea tawbah baada ya hapo kwa Amtakaye. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَـٰذَا ۚ وَإِنْ خِفْتُمْ عَيْلَةً فَسَوْفَ يُغْنِيكُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ إِن شَاءَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٢٨﴾
28. Enyi walioamini! Hakika washirikiana ni najisi (wachafu wa ‘aqiydah na vitendo), basi wasikaribie Masjid Al-Haraam baada ya mwaka wao huu. Na mkikhofu umasikini basi Allaah Atakutajirisheni kutokana na Fadhila Zake Akitaka. Hakika Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
قَاتِلُوا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَلَا يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَلَا يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حَتَّىٰ يُعْطُوا الْجِزْيَةَ عَن يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ ﴿٢٩﴾
29. Piganeni na wale wasiomwamini Allaah na wala Siku ya Mwisho, na wala hawaharamishi Aliyoyaharamisha Allaah na Rasuli Wake, na wala hawafuati Dini ya haki miongoni mwa wale waliopewa Kitabu, (piganeni nao) mpaka watoe jizyah (kodi) kwa khiyari, wakiwa wanyonge wadhalilifu.
وَقَالَتِ الْيَهُودُ عُزَيْرٌ ابْنُ اللَّـهِ وَقَالَتِ النَّصَارَى الْمَسِيحُ ابْنُ اللَّـهِ ۖ ذَٰلِكَ قَوْلُهُم بِأَفْوَاهِهِمْ ۖ يُضَاهِئُونَ قَوْلَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَبْلُ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّـهُ ۚ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ﴿٣٠﴾
30. Na Mayahudi wanasema: ‘Uzayr[5] ni mwana wa Allaah. Na Manaswara wanasema: Al-Masiyh (‘Iysaa) ni mwana wa Allaah. Hiyo ni kauli yao kwa midomo yao. Wanaiga kauli ya wale waliokufuru kabla. Allaah Awaangamize! Basi namna gani wanaghilibiwa wasione haki?
اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٣١﴾
31. Wamewafanya Ahbaar[6] (Mafuqahaa weledi) wao na Ruhbaan (Monaki)[7] wao kuwa ni miola badala ya Allaah, na (pia) Al-Masiyh mwana wa Maryam na hali hawakuamrishwa isipokuwa kumwabudu Ilaah Mmoja Pekee.[8] Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye tu. Utakasifu ni Wake kutokana na yale yote wanayomshirikisha nayo.
يُرِيدُونَ أَن يُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّـهُ إِلَّا أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ﴿٣٢﴾
32. Wanataka kuzima Nuru ya Allaah kwa vinywa vyao lakini Allaah Anakataa isipokuwa Atimize Nuru Yake, japo watakirihika makafiri.
هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿٣٣﴾
33. Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina.[9]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ كَثِيرًا مِّنَ الْأَحْبَارِ وَالرُّهْبَانِ لَيَأْكُلُونَ أَمْوَالَ النَّاسِ بِالْبَاطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۗ وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣٤﴾
34. Enyi walioamini! Hakika wengi katika Ahbaar (Mafuqahaa weledi wa Kiyahudi) na Ruhbaan (Monaki wa Kinaswara) wanakula mali za watu kwa batili, na wanazuia Njia ya Allaah. Na wale wanaorundika dhahabu na fedha na wala hawazitoi katika Njia ya Allaah, basi wabashirie adhabu iumizayo.[10]
يَوْمَ يُحْمَىٰ عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنُوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ ۖ هَـٰذَا مَا كَنَزْتُمْ لِأَنفُسِكُمْ فَذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَكْنِزُونَ﴿٣٥﴾
35. Siku zitakapopashwa katika moto wa Jahannam, na kwazo vikachomwa moto vipaji vyao, na mbavu zao, na migongo yao (wakiambiwa): Haya ndiyo mliyoyarundika kwa ajili ya nafsi zenu. Basi onjeni yale mliyokuwa mkiyarundika.
إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِندَ اللَّـهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِي كِتَابِ اللَّـهِ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ ۚ فَلَا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ ۚ وَقَاتِلُوا الْمُشْرِكِينَ كَافَّةً كَمَا يُقَاتِلُونَكُمْ كَافَّةً ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ﴿٣٦﴾
36. Hakika idadi ya miezi mbele ya Allaah ni kumi na mbili katika hukmu ya makadirio ya Allaah, (tangu) siku Aliyoumba mbingu na ardhi. Kati ya hiyo iko Minne Mitukufu.[11] Hiyo ndiyo Dini iliyo nyoofu. Basi msijidhulumu humo nafsi zenu. Na piganeni vita na washirikina wote kama wao wanavyokupigeni vita nyote. Na jueni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa.
إِنَّمَا النَّسِيءُ زِيَادَةٌ فِي الْكُفْرِ ۖ يُضَلُّ بِهِ الَّذِينَ كَفَرُوا يُحِلُّونَهُ عَامًا وَيُحَرِّمُونَهُ عَامًا لِّيُوَاطِئُوا عِدَّةَ مَا حَرَّمَ اللَّـهُ فَيُحِلُّوا مَا حَرَّمَ اللَّـهُ ۚ زُيِّنَ لَهُمْ سُوءُ أَعْمَالِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ﴿٣٧﴾
37. Hakika kuakhirisha (au kuizuia Miezi Mitukufu) ni kuzidi katika kufuru. Hupotezwa kwayo wale waliokufuru, wanauhalalisha mwaka na wanauharamisha mwaka (mwingine) ili kuusawazisha na idadi ya (miezi) Aliyoitukuza Allaah. Basi huhalalisha Alivyoviharamisha Allaah. Wamepambiwa uovu wa amali zao. Na Allaah Hawahidi watu makafiri.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ ۚ أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ ۚ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ﴿٣٨﴾
38. Enyi walioamini! Mna nini mnapoambiwa tokeni (mwende Jihaad)[12] katika Njia ya Allaah, mnajitia uzito katika ardhi. Je, mmeridhika na uhai wa dunia badala ya Aakhirah? Basi starehe za uhai wa dunia kulinganisha na Aakhirah ni chache.
إِلَّا تَنفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَيَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئًا ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٣٩﴾
39. Msipotoka kwenda Atakuadhibuni adhabu iumizayo, na Atabadilisha watu wasiokuwa nyinyi, na wala hamtomdhuru chochote. Na Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.
إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدْ نَصَرَهُ اللَّـهُ إِذْ أَخْرَجَهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ثَانِيَ اثْنَيْنِ إِذْ هُمَا فِي الْغَارِ إِذْ يَقُولُ لِصَاحِبِهِ لَا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّـهَ مَعَنَا ۖ فَأَنزَلَ اللَّـهُ سَكِينَتَهُ عَلَيْهِ وَأَيَّدَهُ بِجُنُودٍ لَّمْ تَرَوْهَا وَجَعَلَ كَلِمَةَ الَّذِينَ كَفَرُوا السُّفْلَىٰ ۗ وَكَلِمَةُ اللَّـهِ هِيَ الْعُلْيَا ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٤٠﴾
40. Msipomnusuru (Rasuli), basi Allaah Amekwishamnusuru, pale walipomtoa (Makkah) wale waliokufuru akiwa mmoja katika wawili, walipokuwa katika pango, alipomwambia swahibu[13] yake: Usihuzunike, hakika Allaah Yu Pamoja nasi. Basi Allaah Akamteremshia Utulivu Wake, na Akamsaidia kwa majeshi ambayo hamkuyaona, na Akajaalia neno la waliokufuru kuwa chini. Na Neno la Allaah ndilo lililo juu. Na Allaah Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
انفِرُوا خِفَافًا وَثِقَالًا وَجَاهِدُوا بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿٤١﴾
41. Tokeni mwende (ni sawa) mkiwa na hali ya wepesi na mkiwa na hali ya uzito na fanyeni Jihaad kwa mali zenu na nafsi zenu katika Njia ya Allaah. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua.
لَوْ كَانَ عَرَضًا قَرِيبًا وَسَفَرًا قَاصِدًا لَّاتَّبَعُوكَ وَلَـٰكِن بَعُدَتْ عَلَيْهِمُ الشُّقَّةُ ۚ وَسَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَوِ اسْتَطَعْنَا لَخَرَجْنَا مَعَكُمْ يُهْلِكُونَ أَنفُسَهُمْ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ﴿٤٢﴾
42. Kama ingelikuwa pato la karibu na safari nyepesi ya karibu, basi (wanafiki) wangelikufuata, lakini imekuwa ni ya masafa ya mbali kwao na ina mashaka. Na watakuapia kwa Jina la Allaah: Lau tungeliweza, bila shaka tungelitoka pamoja nanyi. Wanaangamiza nafsi zao na Allaah Anajua kwamba wao bila shaka ni waongo.
عَفَا اللَّـهُ عَنكَ لِمَ أَذِنتَ لَهُمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكَ الَّذِينَ صَدَقُوا وَتَعْلَمَ الْكَاذِبِينَ﴿٤٣﴾
43. Allaah Akusamehe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), kwa nini umewapa ruhusa? (Usingelifanya hivyo) mpaka wakubainikie wale waliosadikisha na uwajue waliokadhibisha.
لَا يَسْتَأْذِنُكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ أَن يُجَاهِدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالْمُتَّقِينَ﴿٤٤﴾
44. Hawakuombi ruhusa wale waliomwamini Allaah na Siku ya Mwisho wasifanye Jihaad kwa mali zao na nafsi zao. Na Allaah Anawajua vyema wenye taqwa.
إِنَّمَا يَسْتَأْذِنُكَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَارْتَابَتْ قُلُوبُهُمْ فَهُمْ فِي رَيْبِهِمْ يَتَرَدَّدُونَ﴿٤٥﴾
45. Hakika wanaokuomba ruhusa ni wale ambao hawamwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na nyoyo zao zina shaka, basi wao katika shaka zao wanasitasita.
وَلَوْ أَرَادُوا الْخُرُوجَ لَأَعَدُّوا لَهُ عُدَّةً وَلَـٰكِن كَرِهَ اللَّـهُ انبِعَاثَهُمْ فَثَبَّطَهُمْ وَقِيلَ اقْعُدُوا مَعَ الْقَاعِدِينَ﴿٤٦﴾
46. Na ingelikuwa wametaka kutoka, wangeliandaa maandalizi yake, lakini Allaah Amekirihika kutoka kwao, basi Akawazuia na ikasemwa: Kaeni pamoja na wanaokaa.
لَوْ خَرَجُوا فِيكُم مَّا زَادُوكُمْ إِلَّا خَبَالًا وَلَأَوْضَعُوا خِلَالَكُمْ يَبْغُونَكُمُ الْفِتْنَةَ وَفِيكُمْ سَمَّاعُونَ لَهُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ﴿٤٧﴾
47. Lau wangelitoka nanyi, wasingelikuzidishieni isipokuwa machafuko (vurugu, rabsha) na wangeliharakia huku na huku baina yenu kukutieni fitnah, na miongoni mwenu wako wanaowasikiliza kwa makini. Na Allaah Anawajua vyema madhalimu.
لَقَدِ ابْتَغَوُا الْفِتْنَةَ مِن قَبْلُ وَقَلَّبُوا لَكَ الْأُمُورَ حَتَّىٰ جَاءَ الْحَقُّ وَظَهَرَ أَمْرُ اللَّـهِ وَهُمْ كَارِهُونَ﴿٤٨﴾
48. Walikwishataka kabla kukuleteeni fitnah, na wakakupindulia mambo mpaka ikaja haki na ikadhihirika Amri ya Allaah, nao wamekirihika.
وَمِنْهُم مَّن يَقُولُ ائْذَن لِّي وَلَا تَفْتِنِّي ۚ أَلَا فِي الْفِتْنَةِ سَقَطُوا ۗ وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمُحِيطَةٌ بِالْكَافِرِينَ﴿٤٩﴾
49. Na miongoni mwao yuko anayesema: Niruhusu (nibaki) na wala usiniingize kwenye fitnah. Tanabahi! Wamekwishaanguka katika fitnah. Na hakika Jahannam imewazingira makafiri.
إِن تُصِبْكَ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ ۖ وَإِن تُصِبْكَ مُصِيبَةٌ يَقُولُوا قَدْ أَخَذْنَا أَمْرَنَا مِن قَبْلُ وَيَتَوَلَّوا وَّهُمْ فَرِحُونَ﴿٥٠﴾
50. Linapokusibu zuri lolote lile linawachukiza. Na unapokusibu msiba wowote ule, wanasema: Tumechukua tahadhari jambo letu tokea mwanzo, na wanageuka kwenda zao na huku wanafurahia.
قُل لَّن يُصِيبَنَا إِلَّا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَنَا هُوَ مَوْلَانَا ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ﴿٥١﴾
51. Sema: Halitusibu (lolote) isipokuwa lile Alilotukidhia Allaah. Yeye ni Mawlaa[14] wetu. Basi kwa Allaah watawakali Waumini.
قُلْ هَلْ تَرَبَّصُونَ بِنَا إِلَّا إِحْدَى الْحُسْنَيَيْنِ ۖ وَنَحْنُ نَتَرَبَّصُ بِكُمْ أَن يُصِيبَكُمُ اللَّـهُ بِعَذَابٍ مِّنْ عِندِهِ أَوْ بِأَيْدِينَا ۖ فَتَرَبَّصُوا إِنَّا مَعَكُم مُّتَرَبِّصُونَ﴿٥٢﴾
52. Sema: Je, mnalo la kungojea kututazamia isipokuwa mojawapo ya mazuri mawili? Na sisi tunangojea kukutazamieni kwamba Allaah Atakusibuni kwa adhabu kutoka Kwake au kutokana na mikono yetu. Basi ngojeeni, nasi tuko pamoja nanyi tunangojea.
قُلْ أَنفِقُوا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا لَّن يُتَقَبَّلَ مِنكُمْ ۖ إِنَّكُمْ كُنتُمْ قَوْمًا فَاسِقِينَ﴿٥٣﴾
53. Sema: Toeni (mali) kwa khiari au kutokupenda haitokubaliwa kwenu. Hakika nyinyi mmekuwa ni watu mafasiki.
وَمَا مَنَعَهُمْ أَن تُقْبَلَ مِنْهُمْ نَفَقَاتُهُمْ إِلَّا أَنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّـهِ وَبِرَسُولِهِ وَلَا يَأْتُونَ الصَّلَاةَ إِلَّا وَهُمْ كُسَالَىٰ وَلَا يُنفِقُونَ إِلَّا وَهُمْ كَارِهُونَ﴿٥٤﴾
54. Na haikuwazuilia ikubaliwe michango yao isipokuwa kwa kuwa wao walimkufuru Allaah na Rasuli Wake, na wala hawafiki katika Swalaah isipokuwa wao huwa katika hali ya uvivu, na wala hawatoi isipokuwa wakiwa wamekirihika.
فَلَا تُعْجِبْكَ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُمْ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُعَذِّبَهُم بِهَا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَتَزْهَقَ أَنفُسُهُمْ وَهُمْ كَافِرُونَ﴿٥٥﴾
55. Basi zisikubabaishe mali zao wala watoto wao. Hakika Allaah Anataka kuwaadhibu kwayo katika uhai wa dunia, na zitokelee mbali nafsi zao na huku wao wakiwa makafiri.
وَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ إِنَّهُمْ لَمِنكُمْ وَمَا هُم مِّنكُمْ وَلَـٰكِنَّهُمْ قَوْمٌ يَفْرَقُونَ﴿٥٦﴾
56. Na wanaapa kwa Jina la Allaah kwamba wao ni miongoni mwenu. Na wala wao si katika nyinyi, lakini wao (wanafiki) ni watu wanaoogopa mno.
لَوْ يَجِدُونَ مَلْجَأً أَوْ مَغَارَاتٍ أَوْ مُدَّخَلًا لَّوَلَّوْا إِلَيْهِ وَهُمْ يَجْمَحُونَ﴿٥٧﴾
57. Lau wangelipata mahali pa kukimbilia, au mapango, au mahali finyu pa kuingia (na kujificha), basi wangelielekea huko wakikimbia mbio kali.
وَمِنْهُم مَّن يَلْمِزُكَ فِي الصَّدَقَاتِ فَإِنْ أُعْطُوا مِنْهَا رَضُوا وَإِن لَّمْ يُعْطَوْا مِنْهَا إِذَا هُمْ يَسْخَطُونَ﴿٥٨﴾
58. Na miongoni mwao wako wanaokukosoa katika (ugawaji wa) swadaqa. Wakipewa fungu wanaridhika, na wasipopewa fungu tahamaki wao wanaghadhibika.[15]
وَلَوْ أَنَّهُمْ رَضُوا مَا آتَاهُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّـهُ سَيُؤْتِينَا اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ وَرَسُولُهُ إِنَّا إِلَى اللَّـهِ رَاغِبُونَ﴿٥٩﴾
59. Na lau wangeliridhiya yale Aliyowapa Allaah na Rasuli Wake, na wakasema: Anatutosheleza Allaah, karibuni Allaah Atatupa katika Fadhila Zake na Rasuli Wake (pia), hakika sisi kwa Allaah tuna raghba.
إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۖ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٦٠﴾
60. Hakika Zakaah ni kwa ajili ya mafakiri, na masikini, na wanaozitumikia, na wanaotiwa nguvu nyoyo zao (katika Uislamu) na kuwakomboa mateka, na wenye deni, na katika Njia ya Allaah, na msafiri (aliyeharibikiwa). Ni faradhi itokayo kwa Allaah. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.[16]
وَمِنْهُمُ الَّذِينَ يُؤْذُونَ النَّبِيَّ وَيَقُولُونَ هُوَ أُذُنٌ ۚ قُلْ أُذُنُ خَيْرٍ لَّكُمْ يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَيُؤْمِنُ لِلْمُؤْمِنِينَ وَرَحْمَةٌ لِّلَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ ۚ وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ رَسُولَ اللَّـهِ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٦١﴾
61. Na miongoni mwao wako wale wanaomuudhi Nabiy, na wanasema: Yeye ni mtegaji sikio tu.[17] Sema: Sikio la kheri kwenu. Anamwamini Allaah na anawasadiki Waumini, na ni rehma kwa wale walioamini miongoni mwenu. Na wale wanaomuudhi Rasuli wa Allaah watapata adhabu iumizayo.
يَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَكُمْ لِيُرْضُوكُمْ وَاللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَحَقُّ أَن يُرْضُوهُ إِن كَانُوا مُؤْمِنِينَ﴿٦٢﴾
62. Wanakuapieni kwa Jina la Allaah ili wakuridhisheni, hali ya kuwa Allaah na Rasuli Wake ndio wanaostahiki zaidi kuridhishwa lau kama wao ni Waumini.
أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّهُ مَن يُحَادِدِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَأَنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدًا فِيهَا ۚ ذَٰلِكَ الْخِزْيُ الْعَظِيمُ﴿٦٣﴾
63. Je, hawajui kwamba yeyote mwenye kumpinga Allaah na Rasuli Wake basi hakika atapata Jahannam adumu humo. Hiyo ni hizaaya kubwa mno.
يَحْذَرُ الْمُنَافِقُونَ أَن تُنَزَّلَ عَلَيْهِمْ سُورَةٌ تُنَبِّئُهُم بِمَا فِي قُلُوبِهِمْ ۚ قُلِ اسْتَهْزِئُوا إِنَّ اللَّـهَ مُخْرِجٌ مَّا تَحْذَرُونَ﴿٦٤﴾
64. Wanafiki wanatahadhari isije kuteremshwa Suwrah itakayowajulisha yaliyomo nyoyoni mwao. Sema: Fanyeni istihzai, hakika Allaah Atayatoa yale mnayotahadhari nayo.
وَلَئِن سَأَلْتَهُمْ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلْعَبُ ۚ قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ﴿٦٥﴾
65. Na ukiwauliza, bila shaka watasema: Hakika tulikuwa tunaporoja na tunacheza. Sema: Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayaat Zake na Rasuli Wake?
لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ ۚ إِن نَّعْفُ عَن طَائِفَةٍ مِّنكُمْ نُعَذِّبْ طَائِفَةً بِأَنَّهُمْ كَانُوا مُجْرِمِينَ﴿٦٦﴾
66. Msitoe udhuru. Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.[18] Tukilisamehe kundi miongoni mwenu, Tutaliadhibu kundi (jingine), kwa kuwa wao walikuwa wahalifu.
الْمُنَافِقُونَ وَالْمُنَافِقَاتُ بَعْضُهُم مِّن بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمُنكَرِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمَعْرُوفِ وَيَقْبِضُونَ أَيْدِيَهُمْ ۚ نَسُوا اللَّـهَ فَنَسِيَهُمْ ۗ إِنَّ الْمُنَافِقِينَ هُمُ الْفَاسِقُونَ﴿٦٧﴾
67. Wanafiki wanaume na wanafiki wanawake wote ni washirika wamoja, wanaamrisha munkari na wanakataza mema na hufumba mikono yao. Wamemsahau Allaah, basi Naye Amewasahau. Hakika wanafiki wao ndio mafasiki.
وَعَدَ اللَّـهُ الْمُنَافِقِينَ وَالْمُنَافِقَاتِ وَالْكُفَّارَ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ هِيَ حَسْبُهُمْ ۚ وَلَعَنَهُمُ اللَّـهُ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّقِيمٌ﴿٦٨﴾
68. Allaah Amewaahidi wanafiki wanaume na wanafiki wanawake na makafiri moto wa Jahannam, wadumu humo, inawatosheleza hiyo (adhabu)! Na Allaah Amewalaani, na watapata adhabu ya kudumu.
كَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ كَانُوا أَشَدَّ مِنكُمْ قُوَّةً وَأَكْثَرَ أَمْوَالًا وَأَوْلَادًا فَاسْتَمْتَعُوا بِخَلَاقِهِمْ فَاسْتَمْتَعْتُم بِخَلَاقِكُمْ كَمَا اسْتَمْتَعَ الَّذِينَ مِن قَبْلِكُم بِخَلَاقِهِمْ وَخُضْتُمْ كَالَّذِي خَاضُوا ۚ أُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿٦٩﴾
69. Ni kama wale wa kabla yenu, walikuwa wana nguvu zaidi kuliko nyinyi, na wana mali na watoto wengi zaidi. Basi walistarehe kwa fungu lao nanyi mnastarehe kwa fungu lenu, kama walivyostarehe kwa fungu lao wale wa kabla yenu, na mkatumbukia katika ubatilifu na ukanushaji kama walivyotumbukia. Hao zimeporomoka amali zao duniani na Aakhirah. Na hao ndio waliokhasirika.
أَلَمْ يَأْتِهِمْ نَبَأُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ وَقَوْمِ إِبْرَاهِيمَ وَأَصْحَابِ مَدْيَنَ وَالْمُؤْتَفِكَاتِ ۚ أَتَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ ۖ فَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴿٧٠﴾
70. Je, haikuwafikia khabari ya wale wa kabla yao; kaumu ya Nuwh, na ‘Aad na Thamuwd, na kaumu ya Ibraahiym, na watu ya Madyan, na miji iliyopinduliwa juu chini? Rusuli wao waliwafikia kwa hoja bayana. Na Allaah Hakuwa Mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao wenyewe.
وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ اللَّـهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٧١﴾
71. Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki wandani.[19] Wanaamrisha mema na wanakataza munkari[20] na wanasimamisha Swalaah na wanatoa Zakaah na wanamtii Allaah na Rasuli Wake. Hao Allaah Atawarehemu. Hakika Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
وَعَدَ اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ۚ وَرِضْوَانٌ مِّنَ اللَّـهِ أَكْبَرُ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٧٢﴾
72. Allaah Amewaahidi Waumini wanaume na Waumini wanawake Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo, na makazi mazuri katika Jannaat za kudumu milele. Na Radhi kutoka kwa Allaah ndio kubwa zaidi. Huko ndiko kufuzu kukubwa kabisa.
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ جَاهِدِ الْكُفَّارَ وَالْمُنَافِقِينَ وَاغْلُظْ عَلَيْهِمْ ۚ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿٧٣﴾
73. Ee Nabiy! Fanya Jihaad dhidi ya makafiri na wanafiki na kuwa mkali kwao. Na makazi yao ni Jahannam, na ubaya ulioje mahali pa kuishia!
يَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ مَا قَالُوا وَلَقَدْ قَالُوا كَلِمَةَ الْكُفْرِ وَكَفَرُوا بَعْدَ إِسْلَامِهِمْ وَهَمُّوا بِمَا لَمْ يَنَالُوا ۚ وَمَا نَقَمُوا إِلَّا أَنْ أَغْنَاهُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ مِن فَضْلِهِ ۚ فَإِن يَتُوبُوا يَكُ خَيْرًا لَّهُمْ ۖ وَإِن يَتَوَلَّوْا يُعَذِّبْهُمُ اللَّـهُ عَذَابًا أَلِيمًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَمَا لَهُمْ فِي الْأَرْضِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ﴿٧٤﴾
74. Wanaapa kwa Jina la Allaah kuwa hawakusema ilhali wamekwishasema neno la kufuru, na wakakufuru baada ya kusilimu kwao. Na wakaazimia yale ambayo hawakuweza kuyafikia. Na hawakuchukia isipokuwa kwa kuwa Allaah na Rasuli Wake Amewatajirisha kwa Fadhila Zake. Basi wakitubia, itakuwa ni kheri kwao. Na wakikengeuka, Allaah Atawaadhibu adhabu iumizayo duniani na Aakhirah. Na hawatopata katika ardhi rafiki mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru.
وَمِنْهُم مَّنْ عَاهَدَ اللَّـهَ لَئِنْ آتَانَا مِن فَضْلِهِ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ الصَّالِحِينَ﴿٧٥﴾
75. Na miongoni mwao wako waliomuahidi Allaah (kuwa): Akitupa katika Fadhila Zake, bila shaka tutatoa swadaqa, na bila shaka tutakuwa miongoni mwa wema.[21]
فَلَمَّا آتَاهُم مِّن فَضْلِهِ بَخِلُوا بِهِ وَتَوَلَّوا وَّهُم مُّعْرِضُونَ﴿٧٦﴾
76. Alipowapa katika Fadhila Zake, walizifanyia ubakhili, na wakakengeuka huku wakipuuza.
فَأَعْقَبَهُمْ نِفَاقًا فِي قُلُوبِهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ يَلْقَوْنَهُ بِمَا أَخْلَفُوا اللَّـهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ﴿٧٧﴾
77. Basi Akawapatilizia unafiki katika nyoyo zao mpaka Siku watakayokutana Naye kwa sababu ya kumkhalifu kwao Allaah yale waliyomuahidi, na kwa sababu ya kukadhibisha kwao.
أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُمْ وَأَنَّ اللَّـهَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ﴿٧٨﴾
78. Je, hawajui kwamba Allaah Anajua siri zao na minong’ono yao, na kwamba Allaah ni Mjuzi wa Ghaibu?
الَّذِينَ يَلْمِزُونَ الْمُطَّوِّعِينَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ فِي الصَّدَقَاتِ وَالَّذِينَ لَا يَجِدُونَ إِلَّا جُهْدَهُمْ فَيَسْخَرُونَ مِنْهُمْ ۙ سَخِرَ اللَّـهُ مِنْهُمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٧٩﴾
79. Wale (wanafiki) wanaowafanyia tashtiti Waumini wenye kujitolea kwa khiari katika kutoa swadaqa na wale wasiopata (cha kutoa) isipokuwa kadri ya juhudi zao, basi wanawafanyia dhihaka, Allaah Analipiza dhihaka zao na watapata adhabu iumizayo.[22]
اسْتَغْفِرْ لَهُمْ أَوْ لَا تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ إِن تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ سَبْعِينَ مَرَّةً فَلَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَهُمْ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴿٨٠﴾
80. Waombee maghfirah (ee, Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), au usiwaombee maghfirah, hata ukiwaombea maghfirah mara sabini, Allaah Hatowaghufuria. Hivyo kwa kuwa wao wamemkufuru Allaah na Rasuli Wake. Na Allaah Hawahidi watu mafasiki.
فَرِحَ الْمُخَلَّفُونَ بِمَقْعَدِهِمْ خِلَافَ رَسُولِ اللَّـهِ وَكَرِهُوا أَن يُجَاهِدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَقَالُوا لَا تَنفِرُوا فِي الْحَرِّ ۗ قُلْ نَارُ جَهَنَّمَ أَشَدُّ حَرًّا ۚ لَّوْ كَانُوا يَفْقَهُونَ﴿٨١﴾
81. Waliobaki nyuma walifurahi kwa kule kukaa kwao (wasiende vitani) baada ya Rasuli wa Allaah (kutoka), na walikirihika kufanya Jihaad kwa mali zao na nafsi zao katika Njia ya Allaah na wakasema: Msitoke kwenda katika joto. Sema: Moto wa Jahannam ni mkali zaidi lau wangelifahamu.
فَلْيَضْحَكُوا قَلِيلًا وَلْيَبْكُوا كَثِيرًا جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٨٢﴾
82. Basi na wacheke kidogo (duniani), na watalia sana (Aakhirah) ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.
فَإِن رَّجَعَكَ اللَّـهُ إِلَىٰ طَائِفَةٍ مِّنْهُمْ فَاسْتَأْذَنُو كَ لِلْخُرُوجِ فَقُل لَّن تَخْرُجُوا مَعِيَ أَبَدًا وَلَن تُقَاتِلُوا مَعِيَ عَدُوًّا ۖ إِنَّكُمْ رَضِيتُم بِالْقُعُودِ أَوَّلَ مَرَّةٍ فَاقْعُدُوا مَعَ الْخَالِفِينَ﴿٨٣﴾
83. Basi Allaah Akikurejesha kwenye kundi moja miongoni mwao na wakakutaka idhini ya kutoka, sema: Hamtotoka pamoja nami abadani, na wala hamtopigana na maadui pamoja nami. Nyinyi mliridhika kubakia nyuma mara ya kwanza, basi kaeni pamoja na hao wanaobakia nyuma.
وَلَا تُصَلِّ عَلَىٰ أَحَدٍ مِّنْهُم مَّاتَ أَبَدًا وَلَا تَقُمْ عَلَىٰ قَبْرِهِ ۖ إِنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَمَاتُوا وَهُمْ فَاسِقُونَ﴿٨٤﴾
84. Na wala usimswalie yeyote abadani miongoni mwao akifa, na wala usisimame kaburini kwake. Hakika wao wamemkufuru Allaah na Rasuli Wake, na wakafa hali wao ni mafasiki.[23]
وَلَا تُعْجِبْكَ أَمْوَالُهُمْ وَأَوْلَادُهُمْ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُعَذِّبَهُم بِهَا فِي الدُّنْيَا وَتَزْهَقَ أَنفُسُهُمْ وَهُمْ كَافِرُونَ﴿٨٥﴾
85. Na wala zisikubabaishe mali zao na watoto wao. Hakika Allaah Anataka Awaadhibu kwayo duniani, na zitokelee mbali nafsi zao na huku wao wakiwa ni makafiri.
وَإِذَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ أَنْ آمِنُوا بِاللَّـهِ وَجَاهِدُوا مَعَ رَسُولِهِ اسْتَأْذَنَكَ أُولُو الطَّوْلِ مِنْهُمْ وَقَالُوا ذَرْنَا نَكُن مَّعَ الْقَاعِدِينَ﴿٨٦﴾
86. Na inapoteremshwa Suwrah kwamba muaminini Allaah, na fanyeni Jihaad pamoja na Rasuli Wake, wanakuomba idhini wale (wanafiki) wenye utajiri miongoni mwao, na husema: Tuache tubakie pamoja na wanaokaa nyuma.
رَضُوا بِأَن يَكُونُوا مَعَ الْخَوَالِفِ وَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَفْقَهُونَ﴿٨٧﴾
87. Wameridhika kuwa pamoja na waliobakia nyuma, na zikapigwa chapa nyoyo zao, basi wao hawafahamu.
لَـٰكِنِ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ جَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۚ وَأُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْخَيْرَاتُ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿٨٨﴾
88. Lakini Rasuli na walioamini pamoja naye, wamefanya Jihaad kwa mali zao na nafsi zao. Na hao watapata kheri nyingi. Na hao ndio wenye kufaulu.
أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٨٩﴾
89. Allaah Amewaandalia Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo. Huko ndiko kufuzu kukubwa kabisa.
وَجَاءَ الْمُعَذِّرُونَ مِنَ الْأَعْرَابِ لِيُؤْذَنَ لَهُمْ وَقَعَدَ الَّذِينَ كَذَبُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ سَيُصِيبُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٩٠﴾
90. Na wakaja wenye kutoa udhuru katika Mabedui ili waruhusiwe (wasiende vitani), na wakabakia (majumbani) wale waliomwambia uwongo Allaah na Rasuli Wake. Itawasibu waliokufuru katika wao adhabu iumizayo.
لَّيْسَ عَلَى الضُّعَفَاءِ وَلَا عَلَى الْمَرْضَىٰ وَلَا عَلَى الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ مَا يُنفِقُونَ حَرَجٌ إِذَا نَصَحُوا لِلَّـهِ وَرَسُولِهِ ۚ مَا عَلَى الْمُحْسِنِينَ مِن سَبِيلٍ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٩١﴾
91. Hapana lawama juu ya wale walio dhaifu na wala juu ya walio wagonjwa, na wala juu ya wale wasiopata cha kuchangia (katika Jihaad), madamu wanamsafia niya Allaah na Rasuli Wake. Hapana njia ya kuwalaumu wafanyao ihsaan. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَلَا عَلَى الَّذِينَ إِذَا مَا أَتَوْكَ لِتَحْمِلَهُمْ قُلْتَ لَا أَجِدُ مَا أَحْمِلُكُمْ عَلَيْهِ تَوَلَّوا وَّأَعْيُنُهُمْ تَفِيضُ مِنَ الدَّمْعِ حَزَنًا أَلَّا يَجِدُوا مَا يُنفِقُونَ﴿٩٢﴾
92. Na wala (hakuna lawama) juu ya wale ambao wanapokujia ili uwapatie kipando, ukasema: Sijapata cha kukupandisheni, wanaondoka na huku macho yao yanamiminika machozi kwa huzuni ya kukosa cha kuchangia.
إِنَّمَا السَّبِيلُ عَلَى الَّذِينَ يَسْتَأْذِنُونَكَ وَهُمْ أَغْنِيَاءُ ۚ رَضُوا بِأَن يَكُونُوا مَعَ الْخَوَالِفِ وَطَبَعَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٩٣﴾
93. Hakika (ipo) sababu ya kulaumu kwa wale wanaokuomba idhini na hali wao ni matajiri. Wameridhia kuwa pamoja na waliobakia nyuma, na Allaah Akapiga chapa juu ya nyoyo zao, basi wao hawajui.
يَعْتَذِرُونَ إِلَيْكُمْ إِذَا رَجَعْتُمْ إِلَيْهِمْ ۚ قُل لَّا تَعْتَذِرُوا لَن نُّؤْمِنَ لَكُمْ قَدْ نَبَّأَنَا اللَّـهُ مِنْ أَخْبَارِكُمْ ۚ وَسَيَرَى اللَّـهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٩٤﴾
94. Watakutoleeni udhuru mtakaporejea kwao. Sema: Msitoe udhuru, hatutokuaminini! Allaah Amekwishatujulisha khabari zenu. Na hivi karibuni Allaah na Rasuli Wake wataona amali zenu. Kisha mtarudishwa kwa Mjuzi wa ghaibu na dhahiri, Atakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda.
سَيَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ لَكُمْ إِذَا انقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ لِتُعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ فَأَعْرِضُوا عَنْهُمْ ۖ إِنَّهُمْ رِجْسٌ ۖ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٩٥﴾
95. Watakuapieni kwa Allaah, mtakaporudi kwao ili muwaachilie mbali. Basi waachilieni mbali. Hakika wao ni najsi (wachafu wa aqiydah na niya), na makazi yao ni Jahannam. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.[24]
يَحْلِفُونَ لَكُمْ لِتَرْضَوْا عَنْهُمْ ۖ فَإِن تَرْضَوْا عَنْهُمْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يَرْضَىٰ عَنِ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ﴿٩٦﴾
96. Watakuapieni ili muwaridhie. Mkiwaridhia, basi hakika Allaah Haridhii watu mafasiki.
الْأَعْرَابُ أَشَدُّ كُفْرًا وَنِفَاقًا وَأَجْدَرُ أَلَّا يَعْلَمُوا حُدُودَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٩٧﴾
97. Mabedui wamezidi zaidi kufuru na unafiki, na wameelekea zaidi kwamba wasijue mipaka ya (sharia) Alizoteremsha Allaah juu ya Rasuli Wake. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
وَمِنَ الْأَعْرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغْرَمًا وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ الدَّوَائِرَ ۚ عَلَيْهِمْ دَائِرَةُ السَّوْءِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿٩٨﴾
98. Na katika Mabedui, wako wanaochukulia yale wanayoyatoa kuwa ni gharama tupu, na wanakungojeleeni migeuko ya misiba. Misiba mibaya itawafika wao! Na Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
وَمِنَ الْأَعْرَابِ مَن يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ قُرُبَاتٍ عِندَ اللَّـهِ وَصَلَوَاتِ الرَّسُولِ ۚ أَلَا إِنَّهَا قُرْبَةٌ لَّهُمْ ۚ سَيُدْخِلُهُمُ اللَّـهُ فِي رَحْمَتِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٩٩﴾
99. Na katika Mabedui, wako wanaomwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na wanachukulia yale wanayoyatoa kuwa ni njia ya makurubisho mbele ya Allaah, na kupata duaa za Rasuli. Tanabahi! Hakika hiyo ni njia ya kikurubisho kwao. Allaah Atawaingiza katika Rehma Yake. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١٠٠﴾
100. Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhaajiruwn na Answaar na wale waliowafuata kwa ihsaan[25], Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Na Amewaandalia Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo abadi. Huko ndiko kufuzu kukubwa kabisa.
وَمِمَّنْ حَوْلَكُم مِّنَ الْأَعْرَابِ مُنَافِقُونَ ۖ وَمِنْ أَهْلِ الْمَدِينَةِ ۖ مَرَدُوا عَلَى النِّفَاقِ لَا تَعْلَمُهُمْ ۖ نَحْنُ نَعْلَمُهُمْ ۚ سَنُعَذِّبُهُم مَّرَّتَيْنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَىٰ عَذَابٍ عَظِيمٍ﴿١٠١﴾
101. Na katika Mabedui wanaokuzungukeni wako wanafiki. Na katika watu wa Madiynah (pia) wapo waliobobea katika unafiki. Huwajui (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Sisi Tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili kisha watarudishwa katika adhabu kubwa mno.
وَآخَرُونَ اعْتَرَفُوا بِذُنُوبِهِمْ خَلَطُوا عَمَلًا صَالِحًا وَآخَرَ سَيِّئًا عَسَى اللَّـهُ أَن يَتُوبَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٠٢﴾
102. Na wengineo wamekiri madhambi yao, wamechanganya amali njema na nyinginezo ovu, asaa Allaah Atapokea tawbah zao. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّ صَلَاتَكَ سَكَنٌ لَّهُمْ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿١٠٣﴾
103. Chukua (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika mali zao swadaqa, uwatwaharishe na uwatakase kwazo, na waombee duaa (na maghfirah). Hakika duaa yako ni utulivu kwao. Allaah Ndiye Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
أَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ هُوَ يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَأْخُذُ الصَّدَقَاتِ وَأَنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ﴿١٠٤﴾
104. Je, hawajui kwamba Allaah Ndiye Anayekubali tawbah ya Waja Wake, na Anapokea swadaqa, na kwamba Allaah Ndiye Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.
وَقُلِ اعْمَلُوا فَسَيَرَى اللَّـهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ ۖ وَسَتُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿١٠٥﴾
105. Na sema: Fanyeni (mtakavyo). Allaah Ataona amali zenu na Rasuli Wake na Waumini (pia wataona). Na mtarudishwa kwa Mjuzi wa Ghaibu na dhahiri, kisha Atakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda.
وَآخَرُونَ مُرْجَوْنَ لِأَمْرِ اللَّـهِ إِمَّا يُعَذِّبُهُمْ وَإِمَّا يَتُوبُ عَلَيْهِمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿١٠٦﴾
106. Na wengineo wamengojeshewa Amri ya Allaah. Ama Atawaadhibu au Atawapokelea tawbah zao. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مَسْجِدًا ضِرَارًا وَكُفْرًا وَتَفْرِيقًا بَيْنَ الْمُؤْمِنِينَ وَإِرْصَادًا لِّمَنْ حَارَبَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ مِن قَبْلُ ۚ وَلَيَحْلِفُنَّ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا الْحُسْنَىٰ ۖ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ﴿١٠٧﴾
107. Na wale waliojenga Msikiti kwa ajili ya kuleta madhara,[26] na kufuru, na kufarikisha baina ya Waumini, na kuwa ngome kwa waliompiga vita Allaah na Rasuli Wake hapo kabla. Na bila shaka wanaapa: Hatukukusudia ila jambo zuri. Na Allaah Anashuhudia kwamba hakika wao ni waongo.
لَا تَقُمْ فِيهِ أَبَدًا ۚ لَّمَسْجِدٌ أُسِّسَ عَلَى التَّقْوَىٰ مِنْ أَوَّلِ يَوْمٍ أَحَقُّ أَن تَقُومَ فِيهِ ۚ فِيهِ رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَن يَتَطَهَّرُوا ۚ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُطَّهِّرِينَ﴿١٠٨﴾
108. Usisimame humo abadani! Bila shaka Msikiti ulioasisiwa juu ya taqwa[27] tokea siku ya kwanza unastahiki zaidi usimame humo. Humo mna watu wanaopenda kujitwaharisha. Na Allaah Anapenda wanaojitwaharisha.
أَفَمَنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىٰ تَقْوَىٰ مِنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانٍ خَيْرٌ أَم مَّنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىٰ شَفَا جُرُفٍ هَارٍ فَانْهَارَ بِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿١٠٩﴾
109. Je, yule aliyeasisi jengo lake juu ya taqwa ya Allaah na Radhi (Zake), ni bora au yule aliyeasisi jengo lake juu ya ukingo wa bonde lenye ufa na lenye kuburugunyika na likaporomoka pamoja naye katika moto wa Jahannam? Na Allaah Hawahidi watu madhalimu.
لَا يَزَالُ بُنْيَانُهُمُ الَّذِي بَنَوْا رِيبَةً فِي قُلُوبِهِمْ إِلَّا أَن تَقَطَّعَ قُلُوبُهُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿١١٠﴾
110. Halitoacha jengo lao hilo walilolijenga kuwa ni sababu ya kuwatia shaka katika nyoyo zao mpaka nyoyo zao zikatike katike. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
إِنَّ اللَّـهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ ۚ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ ۖ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ ۚ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّـهِ ۚ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١١١﴾
111. Hakika Allaah Amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwamba watapata Jannah. Wanapigana katika Njia ya Allaah, wanaua na wanauawa. Hii ni ahadi ya haki Aliyojiwekea katika Tawraat na Injiyl na Qur-aan. Na nani atimizae zaidi ahadi yake kuliko Allaah? Basi furahieni kwa biashara yenu mliyofungamana Naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa kabisa.
التَّائِبُونَ الْعَابِدُونَ الْحَامِدُونَ السَّائِحُونَ الرَّاكِعُونَ السَّاجِدُونَ الْآمِرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَالنَّاهُونَ عَنِ الْمُنكَرِ وَالْحَافِظُونَ لِحُدُودِ اللَّـهِ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ﴿١١٢﴾
112. (Waumini hao ni) wanaotubia, wanaodumisha ibaada (kwa ikhlaasw na utiifu), wanaomhimidi (Allaah), wenye kusafiri kwa ajili ya ibaada (au wenye kufunga Swawm[28], wanaorukuu, wanaosujudu, wanaoamrisha mema na wanaokataza munkari, na wanaohifadhi Mipaka ya Allaah. Na wabashirie Waumini.
مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ﴿١١٣﴾
113. Haimpasi Nabiy na wale walioamini kuwaombea maghfirah washirikina japokuwa ni jamaa zao wa karibu baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa motoni.[29]
وَمَا كَانَ اسْتِغْفَارُ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوْعِدَةٍ وَعَدَهَا إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ عَدُوٌّ لِّلَّـهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ ۚ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَأَوَّاهٌ حَلِيمٌ ﴿١١٤﴾
114. Na haikuwa Ibraahiym kumuombea maghfirah baba yake isipokuwa kwa sababu ya ahadi aliyoahidiana naye. Lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui wa Allaah, alijiepusha naye. Hakika Ibraahiym ni mwenye huruma mno na mvumilivu.
وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُضِلَّ قَوْمًا بَعْدَ إِذْ هَدَاهُمْ حَتَّىٰ يُبَيِّنَ لَهُم مَّا يَتَّقُونَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴿١١٥﴾
115. Na haiwi kwa Allaah Awapotoze watu baada ya kuwa Amewahidi mpaka Awabainishie ya kujikinga nayo. Hakika Allaah kwa kila kitu Ni Mjuzi.
إِنَّ اللَّـهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۚ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ﴿١١٦﴾
116. Hakika Ni Wake Allaah ufalme wa mbingu na ardhi. Anahuisha na Anafisha. Nanyi hamna pasi na Allaah rafiki mlinzi wala mwenye kunusuru.
لَّقَد تَّابَ اللَّـهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ الْعُسْرَةِ مِن بَعْدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٍ مِّنْهُمْ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّهُ بِهِمْ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١١٧﴾
117. Kwa yakini Allaah Amepokea tawbah ya Nabiy na Muhaajiruwn na Answaar ambao wamemfuata (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) katika saa ya dhiki baada ya nyoyo za kundi miongoni mwao kukurubia kuelemea mbali na haki, kisha Akapokea tawbah yao. Hakika Yeye kwao Ni Mwenye huruma mno, Mwenye Kurehemu.[30]
وَعَلَى الثَّلَاثَةِ الَّذِينَ خُلِّفُوا حَتَّىٰ إِذَا ضَاقَتْ عَلَيْهِمُ الْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ وَضَاقَتْ عَلَيْهِمْ أَنفُسُهُمْ وَظَنُّوا أَن لَّا مَلْجَأَ مِنَ اللَّـهِ إِلَّا إِلَيْهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ لِيَتُوبُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ﴿١١٨﴾
118. Na (akapokea tawbah) ya wale watatu[31] waliobaki nyuma (wakajuta mno) mpaka ardhi ikadhikika kwao juu ya kuwa ni pana na zikadhikika nafsi zao, na wakatambua kwamba hakuna pa kumkimbia Allaah isipokuwa kuelekea Kwake, kisha (Allaah) Akapokea tawbah yao, ili watubie. Hakika Allaah Yeye Ndiye Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ﴿١١٩﴾
119. Enyi walioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli.
مَا كَانَ لِأَهْلِ الْمَدِينَةِ وَمَنْ حَوْلَهُم مِّنَ الْأَعْرَابِ أَن يَتَخَلَّفُوا عَن رَّسُولِ اللَّـهِ وَلَا يَرْغَبُوا بِأَنفُسِهِمْ عَن نَّفْسِهِ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ لَا يُصِيبُهُمْ ظَمَأٌ وَلَا نَصَبٌ وَلَا مَخْمَصَةٌ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَطَئُونَ مَوْطِئًا يَغِيظُ الْكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنْ عَدُوٍّ نَّيْلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُم بِهِ عَمَلٌ صَالِحٌ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ﴿١٢٠﴾
120. Haikuwapasa watu wa Madiynah na Mabedui walio pembezoni mwao kwamba wabakie nyuma wasitoke na Rasuli wa Allaah, wala kujipendelea nafsi zao kuliko nafsi yake. Hilo ni kwa kuwa hakiwasibu wao kiu wala machofu, wala njaa kali katika Njia ya Allaah, na wala hawakanyagi ardhi yoyote inayowaghadhibisha makafiri (wao kuikanyaga), na wala hawawasibu maadui msiba wowote ila wanaandikiwa kwayo amali njema. Hakika Allaah Hapotezi ujira wa wafanyao ihsaan.
وَلَا يُنفِقُونَ نَفَقَةً صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً وَلَا يَقْطَعُونَ وَادِيًا إِلَّا كُتِبَ لَهُمْ لِيَجْزِيَهُمُ اللَّـهُ أَحْسَنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٢١﴾
121. Na wala hawatoi mchango wowote mdogo au mkubwa na wala hawavuki bonde lolote isipokuwa huandikiwa (ujira), ili Allaah Awalipe mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wanayatenda.
وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا كَافَّةً ۚ فَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَائِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ﴿١٢٢﴾
122. Na haiwapasi Waumini watoke wote pamoja (kupigana Jihaad). Basi kwa nini lisitoke katika kila kundi miongoni mwao, kundi (moja tu) wajifunze vyema Dini na ili waonye watu wao watakaporejea kwao ili wapate kujihadharisha.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قَاتِلُوا الَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ الْكُفَّارِ وَلْيَجِدُوا فِيكُمْ غِلْظَةً ۚ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ﴿١٢٣﴾
123. Enyi walioamini! Piganeni Jihaad na wale makafiri walio karibu nanyi na waukute kwenu ukali. Na jueni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa.
وَإِذَا مَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ فَمِنْهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمْ زَادَتْهُ هَـٰذِهِ إِيمَانًا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَزَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَهُمْ يَسْتَبْشِرُونَ﴿١٢٤﴾
124. Na inapoteremshwa Suwrah, basi miongoni mwao wako wanaosema: Nani kati yenu imemzidishia (Suwrah) hii imaan? Ama wale walioamini huwazidishia imaan nao wanafurahia.[32]
وَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَتْهُمْ رِجْسًا إِلَىٰ رِجْسِهِمْ وَمَاتُوا وَهُمْ كَافِرُونَ﴿١٢٥﴾
125. Na ama wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi, huwazidishia rijs (unafiki, shaka n.k.) juu ya rijs yao, na wakafa hali wao ni makafiri.
أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٍ مَّرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُونَ﴿١٢٦﴾
126. Je, hawaoni kwamba wao wanatahiniwa kila mwaka mara moja au mara mbili, kisha hawatubii na wala wao hawakumbuki?
وَإِذَا مَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ نَّظَرَ بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ هَلْ يَرَاكُم مِّنْ أَحَدٍ ثُمَّ انصَرَفُوا ۚ صَرَفَ اللَّـهُ قُلُوبَهُم بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ﴿١٢٧﴾
127. Na inapoteremshwa Suwrah wanatazamana wenyewe kwa wenyewe (wakisema:) Je, kuna mmoja yeyote anayekuoneni? Kisha wanageuka kuondokea mbali. Allaah Amezigeuza nyoyo zao kwa kuwa wao ni watu wasiofahamu.
لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١٢٨﴾
128. Kwa yakini amekujieni Rasuli anayetokana na nyinyi wenyewe, yanamtia mashaka (na huzuni) yanayokutaabisheni, anakujalini, kwa Waumini ni mwenye huruma mno, mwenye rehma.[33]
فَإِن تَوَلَّوْا فَقُلْ حَسْبِيَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ ۖ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ﴿١٢٩﴾
129. Na wakikengeuka, basi sema: Amenitosheleza Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Kwake nimetawakali. Naye Ni Rabb wa ‘Arsh Adhimu.[34]
[1] Suwrah Pekee Isiyoanza kwa بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم (Kwa Jina la Allaah Mwingi wa Reahma Mwenye Kurehemu):
Kauli Za ‘Ulamaa:
(i) Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله):
Suwrah At-Tawbah haikuanzwa na Basmalah kwa sababu hivyo ndivyo ilivyokuja, na kwamba lau Basmalah ingekuwa ina nafasi ndani yake, ingelihifadhiwa na ingekuwepo kwani Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ ﴿٩﴾
“Hakika Sisi Tumeteremsha Adh-Dhikra (Qur-aan) na hakika Sisi bila shaka Ndio Wenye Kuihifadhi.” [Al-Hijr (15:9)]
[Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb Shariytw (103) - Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله)]
(iii) Shaykh Swaalih Bin Fawzaan (حفظه الله):
Kwanza: Suwrat Al-Anfaal inaendelezwa na Suwrat At-Tawbah, kwa hivyo haikuja mwanzoni mwake kwa
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم
Pili: Suwrat At-Tawbah haikuanzwa na
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم
kwa sababu ni Suwrah iliyotajwa ndani yake Jihaad na makafiri, na pia kuna maonyo, makemeo na vitisho vikali kwa wanafiki, na kufichua fedheha, kashfa na khiyana zao. Kwa hayo, haikupasa kuanziwa kwa
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم
kwani humu mna Rehma ambayo haiwafikiani na hayo yaliyotajwa kuhusu wanafiki na makafiri na sifa zao. Kwa hivyo haikuanziwa kwa
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم
[Shaykh Swaalih Bin Fawzaan Al-Fawzaan]
(iii) Imaam Ibn Baaz (رحمه الله):
Sababu ya kutokuweko
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم
katika Suwrat At-Tawbah ni kwamba ‘Uthmaan (رضي الله عنه) aliulizwa kuhusu hili akasema: Suwrat Al-Anfaal na Suwrat Al-Baraa (At-Tawbah) zinakaribiana kimaana, kwa hivyo haikuteremshwa baina yake
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم
Hivyo ‘Uthmaan na Swahaba (رضي الله عنهم) walidhania kwamba ni Suwrah moja kwa kuwa zimewekwa pamoja na hakuna Aayah baina yake ya
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم
na pia hakuna dalili inayoonyesha kuwa ni Suwrah mbili. Swahaba walikuwa makini, na wakazifanya ziwe karibu pamoja kwa sababu hawakuhifadhi Uteremsho wa
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيْمِ
baina ya Suwrah hizi mbili. Na rai hii ndio iliyo mashuhuri kama ilivyopokelewa na ‘Ulamaa kutoka kwa ‘Uthmaan pale alipokusanya Mswahafu katika ukhalifa wake. [Nuwr ‘Alad-Darb - Al-Mawqi' Ar-Rasmiy li-Samaahat Ash-Shaykh Al-Imaam Ibn Baaz]
[2] Qur-aan Ni Maneno Ya Allaah Hayakuumbwa:
Qur-aan ni Maneno ya Allaah (عزّ وجلّ) kwa herufi zake na maana zake. Allaah (عزّ وجلّ) Ameizungumzia kwa namna Aliyoitaka. Hivyo, nasi tunamueleza Allaah kwa Sifa Yake ya Kuzungumza. Na Al-Kalaam (Maneno) ni kutoka kwenye Sifa za Allaah Ambazo ni Swifaat Fi’liyyah (Sifa za vitendo). Na hatuulizi kayfiyyah (namna) yake, au hatuleti Takyiyf (kuainisha maana na kuziulizia namna yake, au kuuliza ni vipi Sifa hiyo ipo, au kuchunguza ni kwa “namna gani” zimefungamana au kuambatana na Allaah).
‘Ulamaa wameelezea mengi kuhusu kauli hiyo ya Allaah (عزّ وجلّ). Miongoni mwao ni Imaam Al-Qurtwubiy (رحمه الله) ambaye amesema kuhusiana na Aayah hii: “Allaah (سبحانه وتعالى) Akadalilisha kwamba Maneno Yake yanasikilizwa pindi msomaji wa Qur-aan anapoyasoma. Na jambo hili linawafikiana na Waislamu kuwa msomaji Qur-aan akisoma Suwratul-Faatihah au Suwrah yoyote, wanasema tumeyasikia Maneno ya Allaah.”
Pia, Imaam ‘Abdur-Rahmaan Naaswir As-Sa’diy (رحمه الله) amesema: “Katika Aayah hii, kuna hoja ya wazi kuhusiana na mafundisho ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa'ah wanaosema kuwa Qur-aan ni Maneno ya Allaah Ambayo hayakuumbwa, kwa sababu Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Anayeizungumza, na Akaihusisha Kwake Mwenyewe kuongezea sifa ya kielelezo chake. Na hii inabatilisha madhehebu ya Mu-‘utazilah na wengineo wanaosema kwamba Qur-aan imeumbwa. Ni dalili ngapi zipo zinazothibitisha ubatilifu wa msemo huu? (Bila shaka ni nyingi), lakini hapa si mahala pa kuzitaja au kuzielezea. [Tafsiyr As-Sa’adiy]
Rejea pia Suwrat An-Nisaa (4:164), Aayah ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema kuwa Alimsemesha Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) kwa Maneno ya uhakika, na kuna maelezo katika tanbihi ya Aayah hiyo.
[4] Ghazwat Hunayn:
Hunayn ni bonde baina ya Twaaif na Makkah.
Vita vya Hunayn vilitokea mwezi wa Shawwaal mwaka wa 8 Hijriyyah.
Baada ya Fat-h Makkah, Uislamu ulisambaa na yakabakia makabila machache ambayo watu wake hawakuingia Uislamu. Miongoni mwa makabila hayo ni kabila la Thaqiyb na Hawaazin ambao waliendelea na ushirikina. Wakachukia wito wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na wakampinga. Basi wakapanga vita kupigana na Waislamu. Na ikawa mara ya mwanzo Waislamu kupigana vita kwa idadi kubwa zaidi kuliko idadi ya makafiri. Hakupata Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kutoka na jeshi kubwa kuliko la siku hiyo, alitoka na watu elfu kumi na mbili, hata Waislamu wakawa wanasema: “Hatutoshindwa leo kwa tuko wengi.” Ndio Anataja haya Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah hii tukufu kuwa Waislamu walijigamba kwa kuwa walijiamini na wakadhani kuwa hawatashindwa. Walijisahau hali yao ilivyokuwa katika Vita vya Badr ambavyo Allaah Aliwapa ushindi juu ya uchache wao. Wakawa hawakujitayarisha kuingia vitani kwa silaha kwa kuamini wingi wao.
Wakatekwa na makafiri kwa mishale hapo basi wakaanza kumahanika. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakukata tamaa na Rehma ya Allaah akawa anawatuliza Waislamu kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Atawapa ushindi. Wakapata nguvu kwa kutiwa nguvu na maneno ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Allaah Akawateremshia Utulivu Wake. Wakapigana na makabila hayo ya Thaqiyf na Hawaazin mpaka wakashinda. Makafiri hao wakakimbia na wakaacha ngawira tele za farasi, mbuzi na mateka ya wanawake.
Miongoni mwa Hadiyth zinzoaelezea tukio la Vita hivi vitukufu ni zifuatazo:
حَدَّثَنَا قُتَيْبَةُ، حَدَّثَنَا سَهْلُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ أَبِي إِسْحَاقَ،. قَالَ رَجُلٌ لِلْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ ـ رضى الله عنهما ـ أَفَرَرْتُمْ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَوْمَ حُنَيْنٍ قَالَ لَكِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لَمْ يَفِرَّ، إِنَّ هَوَازِنَ كَانُوا قَوْمًا رُمَاةً، وَإِنَّا لَمَّا لَقِينَاهُمْ حَمَلْنَا عَلَيْهِمْ فَانْهَزَمُوا، فَأَقْبَلَ الْمُسْلِمُونَ عَلَى الْغَنَائِمِ وَاسْتَقْبَلُونَا بِالسِّهَامِ، فَأَمَّا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَلَمْ يَفِرَّ، فَلَقَدْ رَأَيْتُهُ وَإِنَّهُ لَعَلَى بَغْلَتِهِ الْبَيْضَاءِ وَإِنَّ أَبَا سُفْيَانَ آخِذٌ بِلِجَامِهَا، وَالنَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ " أَنَا النَّبِيُّ لاَ كَذِبْ أَنَا ابْنُ عَبْدِ الْمُطَّلِبْ ".
Amesimulia Abuu Is-haaq kuwa mtu mmoja alimuuliza Al-Baraa Bin ‘Aazib (رضي الله عنهما): Je, mlikimbia mkamuacha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) siku ya Hunayn? Al-Baraa akajibu: Lakini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakukimbia. Hakika Hawaazin walikuwa ni watu hodari sana kurusha mishale. Tulipopambana nao, tuliwashambulia, nao wakakimbia. Pindi Waislamu walipoanza kukusanya ngawira, wakapambana nasi kwa mishale, lakini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakukimbia, kwani nilimuona juu ya nyumbu wake mweupe, ilhali Abuu Sufyaan ameshika hatamu, huku Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Mimi ni Nabiy wa kweli, mimi ni mtoto wa ‘Abdul-Mutw-twalib.” [Al-Bukhaariy Kitaabu Cha Jihaad (56)]
عن أبي الفضل العباس بن عبد المطلب رضي الله عنه قال : شَهِدْتُ مَعَ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَومَ حُنَيْن ، فَلَزِمْتُ أنا وأبو سُفْيَانَ بن الحارثِ بن عبد المطلب رَسُول الله صلى الله عليه وسلم ، فَلَمْ نُفَارِقْهُ ، وَرسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، عَلَى بَغْلَةٍ لَهُ بَيْضَاءَ ، فَلَمَّا التَقَى المُسْلِمُونَ وَالمُشْرِكُونَ ، وَلَّى المُسْلِمُونَ مُدْبِريِنَ ، فَطَفِقَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يَرْكُضُ بَغْلَتَهُ قِبلَ الكُفَّارِ ، وأنا آخِذٌ بِلِجَامِ بَغْلَةِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، أكُفُّهَا إرَادَةَ أنْ لاَ تُسْرِعَ ، وأبُو سُفْيَانَ آخِذٌ بِرِكَابِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فقالَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( أيْ عَبَّاسُ ، نَادِ أصْحَابَ السَّمُرَةِ )) . قالَ العَبَّاسُ - وَكَانَ رَجُلاً صَيِّتاً - فَقُلْتُ بِأَعْلَى صَوْتِي : أيْنَ أصْحَابُ السَّمُرَةِ ، فَوَاللهِ لَكَأنَّ عَطْفَتَهُمْ حِينَ سَمِعُوا صَوْتِي عَطْفَةُ البَقَرِ عَلَى أَوْلاَدِهَا ، فقالوا : يَا لَبَّيْكَ يَا لَبَّيْكَ ، فَاقْتَتَلُوا هُمْ وَالكُفَّارُ ، وَالدَّعْوَةُ في الأنْصَارِ يَقُولُونَ : يَا مَعْشَرَ الأَنْصَارِ ، يَا مَعْشَرَ الأنْصَارِ ، ثُمَّ قَصُرَتِ الدَّعْوَةُ عَلَى بَنِي الحَارِثِ بْنِ الخَزْرَجِ ، فَنَظَرَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، وَهُوَ عَلَى بَغْلَتِهِ كَالمُتَطَاوِلِ عَلَيْهَا إلَى قِتَالِهِمْ ، فَقَالَ : (( هَذَا حِينَ حَمِيَ الوَطِيسُ )) ، ثُمَّ أَخَذَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، حَصَيَاتٍ فَرَمَى بِهِنَّ وُجُوهَ الكُفَّارِ ، ثُمَّ قَالَ : (( انْهَزَمُوا وَرَبِّ مُحَمَّدٍ )) ، فَذَهَبْتُ أنْظُرُ فَإذَا القِتَالُ عَلَى هَيْئَتِهِ فِيما أرَى ، فَواللهِ مَا هُوَ إلاَّ أنْ رَمَاهُمْ بِحَصَيَاتِهِ ، فَمَا زِلْتُ أرَى حَدَّهُمْ كَلِيلاً وَأَمْرَهُمْ مُدْبِراً . رواه مسلم .
Amesema Abul-Faadhwl Al-'Abbaas bin 'Abdil-Muttwalib (رضي الله عنه): Nilishuhudia pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Vita vya Hunayn. Mimi na Abu Sufyaan bin Al-Haarith bin 'Abdil-Muttwalib tulijilazimisha kuwa karibu na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wala hatukuachana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliyekuwa amempanda nyumbu mweupe. Walipokutana Waislamu na mushirikina katika Vita hivyo, Waislamu waligeuza migongo yao na kuanza kukimbia. Hata hivyo, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aalimtia chonjo nyumbu wake kuwakabili makafiri, nami nilikuwa nimeshika hatamu ya nyumbu wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ili kumzuia asiende kwa kasi mno. Na Abu Sufyaan alikuwa amezishikilia *zikuku* (za kupandia) za mnyama huyo wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ee 'Abbaas! Waite Swahaba wa Samurah (wale waliokuwepo katika Bay’atur-Ridhwaan (Ahadi ya utiifu ya Radhi).” Anasema 'Abbaas (رضي الله عنهما): Mimi nilikuwa na sauti kubwa. Nikawaita kwa sauti yangu ya juu kabisa: Wako wapi Swahaba wa Samurah? Naapa kwa Allaah! Walipoisikia sauti walikimbia haraka haraka kuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kama ng'ombe kuwakimbilia ndama wake. wakasema: Tuko hapa, tuko hapa! Hapo hapo wakaanza kupigana na makafiri. Kwa wakati huo viongozi wa Answaar wakaanza kuita: Enyi kongamano la Answaar! Kisha wakaita Bani Al-Haarith ibn Al-Khazraj. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alinyanyua kichwa chake kuangalia vita vinavyoendelea akiwa juu ya nyumbu wake. Akasema: "Hii ni pindi vita vinapopamba moto na kufikia kilele." Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alichukua changarawe na kuvirusha kwenye nyuso za makafiri, kisha akasema: "Kwa Rabb wa Muhammad, wameshindwa!" Baada ya muda nilikwenda kutizama hali ya vita ambavyo vilikuwa kama awali, lakini naapa kwa Allaah pindi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliporusha zile changarawe nikaona ile harara na nguvu za makafiri zimepungua, hivyo kuanza kukimbia." [Muslim]
Na ugawaji wa ngawira uliwatia mtihani Answaar wa Madiynah kama zinavyoelezea Hadiyth zifuatazo:
حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا أَزْهَرُ، عَنِ ابْنِ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا هِشَامُ بْنُ زَيْدِ بْنِ أَنَسٍ، عَنْ أَنَسٍ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ لَمَّا كَانَ يَوْمَ حُنَيْنٍ الْتَقَى هَوَازِنُ وَمَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم عَشَرَةُ آلاَفٍ وَالطُّلَقَاءُ فَأَدْبَرُوا قَالَ " يَا مَعْشَرَ الأَنْصَارِ ". قَالُوا لَبَّيْكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ وَسَعْدَيْكَ، لَبَّيْكَ نَحْنُ بَيْنَ يَدَيْكَ، فَنَزَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ " أَنَا عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ ". فَانْهَزَمَ الْمُشْرِكُونَ، فَأَعْطَى الطُّلَقَاءَ وَالْمُهَاجِرِينَ وَلَمْ يُعْطِ الأَنْصَارَ شَيْئًا فَقَالُوا، فَدَعَاهُمْ فَأَدْخَلَهُمْ فِي قُبَّةٍ فَقَالَ " أَمَا تَرْضَوْنَ أَنْ يَذْهَبَ النَّاسُ بِالشَّاةِ وَالْبَعِيرِ، وَتَذْهَبُونَ بِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم "، فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم "لَوْ سَلَكَ النَّاسُ وَادِيًا وَسَلَكَتِ الأَنْصَارُ شِعْبًا لاَخْتَرْتُ شِعْبَ الأَنْصَارِ "
Amesimulia Anas Bin Maalik (رضي الله عنه): Katika siku ya (vita vya) Hunayn, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwakabili kabila la Hawaazin ilhali kulikuwa na watu elfu kumi na Atw-Twulaqaa (waliosilimu katika Siku ya Fat-h [ukombozi] wa Makkah) pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). (Waislamu) walipokimbia, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaambia, “Enyi kundi la Answaar!” Wakajibu: "Labbayka, Ee Rasuli wa Allaah wa Sa’dayka! Tuko chini ya amri yako.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akateremka chini (kutoka juu ya nyumbu wake) na kusema: "Mimi ni Mja wa Allaah na Rasuli Wake.” Washirikina wakashindwa vita. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawagawia ghanima (mateka) ya vita Atw-Twulaqaa na Muhaajiruwn na hakuwapa chochote Answaar. Answaar wakasema (maneno ya kutoridhika) basi akawaita na kuwakaribisha chini ya hema la ngozi na kuwaambia: "Je, hamtoridhia kuwa wao wamechukua kondoo na ngamia na nyinyi mtaondoka pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)?” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaongeza: “Kama watu wangepita njia ya bondeni na Answaar wakapita njia ya milimani, basi ningepita njia ya milimani ya Answaar." [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Maghaazi]
عن عبد الله ابن مسعودٍ رضي الله عنه قَالَ: لَمَّا كَانَ يَومُ حُنَينٍ آثَرَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم نَاسًا في القسْمَةِ، فَأعْطَى الأقْرَعَ بْنَ حَابسٍ مائَةً مِنَ الإِبِلِ، وَأَعْطَى عُيَيْنَة بْنَ حصن مِثْلَ ذلِكَ، وَأَعطَى نَاسًا مِنْ أشْرافِ العَرَبِ وآثَرَهُمْ يَوْمَئِذٍ في القسْمَةِ. فَقَالَ رَجُلٌ: واللهِ إنَّ هذِهِ قِسْمَةٌ مَا عُدِلَ فِيهَا، وَمَا أُريدَ فيهَا وَجْهُ اللهِ، فَقُلْتُ: وَاللهِ لأُخْبِرَنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم، فَأَتَيْتُهُ فَأخْبَرتُهُ بمَا قَالَ، فَتَغَيَّرَ وَجْهُهُ حَتَّى كَانَ كالصِّرْفِ. ثُمَّ قَالَ: ((فَمَنْ يَعْدِلُ إِذَا لم يَعْدِلِ اللهُ وَرسولُهُ؟)) ثُمَّ قَالَ: ((يَرْحَمُ اللهُ مُوسَى قَدْ أُوذِيَ بأكْثَرَ مِنْ هَذَا فَصَبر)). فَقُلْتُ: لا جَرَمَ لا أرْفَعُ إِلَيْه بَعدَهَا حَدِيثًا. مُتَّفَقٌ عَلَيه
‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه) amesema: “Siku ya vita vya Hunayn, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwafadhilisha baadhi ya watu katika mgao. Akampa Al-Aqra’ bin Haabis ngamia mia moja, akampa Uyaynah bin Hiswn mfano wake, na akawapa watu watukufu wa Kiarabu na akawafadhilisha katika mgao siku hiyo. Mtu mmoja akasema: Wa-Allaahi huu ni mgao usio na uadilifu! Wala haujakusudiwa Radhi ya Allaah! Nikasema: Wa-Allaahi nitamueleza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Nikaenda na kumueleza aliyoyasema mtu huyo. Uso wake Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ukabadilika hata ukawa mwekundu. Kisha akasema: “Ni nani atakaefanya uadilifu ikiwa Allaah na Rasuli wake Hawakufanya uadilifu?” Halafu akasema: “Allaah Amrehemu Muwsaa, hakika aliudhiwa zaidi ya hivi na akasubiri!” Nikasema: Kwa hakika sitomueleza tena (mazungumzo kama haya ya kumuudhi). [Al-Bukhaariy na Muslim]
[5] ‘Uzayr Hakuwa Nabiy Wala Haiwezekani Allaah (سبحانه وتعالى) Ajifanyie Mwana:
‘Uzayr alikuwa ni mja mwema miongoni mwa Wana wa Israaiyl. Na haijathibitika kuwa yeye ni Nabii, lakini Mayahudi wanasema kuwa ‘Uzayr ni Nabii miongoni mwa Manabii wa Bani Israaiyl. [Ibn Kathiyr, Al-Bidaaya Wan-Nihaayah (2/389)]
Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Sijui kama Tubba’ (Mfalme wa Yemen alikuwa mshirikina kisha akasilimu) alilaaniwa au laa! Na sijui kama ‘Uzayr ni Nabii au laa.” [Sunan Abiy Daawuwd, ameisahihisha Imaam Al-Albaaniy]
Rejea Al-Baqarah (2:259) kuhusu ‘Uzayr.
Kuhusu Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) rejea Aayah inayofuatia (9:31) na tanbihi yake.
Na pia:
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ ـ رضى الله عنه ـ أَنَّ أُنَاسًا فِي زَمَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ، هَلْ نَرَى رَبَّنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " نَعَمْ، هَلْ تُضَارُّونَ فِي رُؤْيَةِ الشَّمْسِ بِالظَّهِيرَةِ، ضَوْءٌ لَيْسَ فِيهَا سَحَابٌ ". قَالُوا لاَ. قَالَ " وَهَلْ تُضَارُّونَ فِي رُؤْيَةِ الْقَمَرِ لَيْلَةَ الْبَدْرِ، ضَوْءٌ لَيْسَ فِيهَا سَحَابٌ ". قَالُوا لاَ. قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " مَا تُضَارُّونَ فِي رُؤْيَةِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، إِلاَّ كَمَا تُضَارُّونَ فِي رُؤْيَةِ أَحَدِهِمَا، إِذَا كَانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ أَذَّنَ مُؤَذِّنٌ تَتْبَعُ كُلُّ أُمَّةٍ مَا كَانَتْ تَعْبُدُ. فَلاَ يَبْقَى مَنْ كَانَ يَعْبُدُ غَيْرَ اللَّهِ مِنَ الأَصْنَامِ وَالأَنْصَابِ إِلاَّ يَتَسَاقَطُونَ فِي النَّارِ، حَتَّى إِذَا لَمْ يَبْقَ إِلاَّ مَنْ كَانَ يَعْبُدُ اللَّهَ، بَرٌّ أَوْ فَاجِرٌ وَغُبَّرَاتُ أَهْلِ الْكِتَابِ، فَيُدْعَى الْيَهُودُ فَيُقَالُ لَهُمْ مَنْ كُنْتُمْ تَعْبُدُونَ قَالُوا كُنَّا نَعْبُدُ عُزَيْرَ ابْنَ اللَّهِ. فَيُقَالُ لَهُمْ كَذَبْتُمْ، مَا اتَّخَذَ اللَّهُ مِنْ صَاحِبَةٍ وَلاَ وَلَدٍ، فَمَاذَا تَبْغُونَ فَقَالُوا عَطِشْنَا رَبَّنَا فَاسْقِنَا. فَيُشَارُ أَلاَ تَرِدُونَ، فَيُحْشَرُونَ إِلَى النَّارِ كَأَنَّهَا سَرَابٌ، يَحْطِمُ بَعْضُهَا بَعْضًا فَيَتَسَاقَطُونَ فِي النَّارِ، ثُمَّ يُدْعَى النَّصَارَى، فَيُقَالُ لَهُمْ مَنْ كُنْتُمْ تَعْبُدُونَ قَالُوا كُنَّا نَعْبُدُ الْمَسِيحَ ابْنَ اللَّهِ. فَيُقَالُ لَهُمْ كَذَبْتُمْ، مَا اتَّخَذَ اللَّهُ مِنْ صَاحِبَةٍ وَلاَ وَلَدٍ. فَيُقَالُ لَهُمْ مَاذَا تَبْغُونَ فَكَذَلِكَ مِثْلَ الأَوَّلِ، حَتَّى إِذَا لَمْ يَبْقَ إِلاَّ مَنْ كَانَ يَعْبُدُ اللَّهَ مِنْ بَرٍّ أَوْ فَاجِرٍ، أَتَاهُمْ رَبُّ الْعَالَمِينَ فِي أَدْنَى صُورَةٍ مِنَ الَّتِي رَأَوْهُ فِيهَا، فَيُقَالُ مَاذَا تَنْتَظِرُونَ تَتْبَعُ كُلُّ أُمَّةٍ مَا كَانَتْ تَعْبُدُ. قَالُوا فَارَقْنَا النَّاسَ فِي الدُّنْيَا عَلَى أَفْقَرِ مَا كُنَّا إِلَيْهِمْ، وَلَمْ نُصَاحِبْهُمْ، وَنَحْنُ نَنْتَظِرُ رَبَّنَا الَّذِي كُنَّا نَعْبُدُ. فَيَقُولُ أَنَا رَبُّكُمْ، فَيَقُولُونَ لاَ نُشْرِكُ بِاللَّهِ شَيْئًا. مَرَّتَيْنِ أَوْ ثَلاَثًا ".
Amesimulia Abu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Hakika watu katika zama za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) walisema: Ee Rasuli wa Allaah! Je, tutamuona Rabb wetu Siku ya Qiyaamah? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Naam! Je, kwani mna shida yoyote ya kuliona jua adhuhuri yenye mwangaza na hakuna mawingu (mbinguni)?” Wakajibu: Hapana. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Je, mna tatizo lolote la kuuona mwezi usiku unapokuwa umekamilika ukiwa umeng’ara na hakuna mawingu mbinguni?” Wakajibu: Hapana. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “(Hivyo hivyo) hamtakuwa na shida kumuona Allaah (عزَّ وجلَّ) Siku ya Qiyaamah kama ambavyo kwamba hamna tatizo kuviona hivyo viwili (jua na mwezi). Siku ya Qiyaamah, atanadi mwenye kunadi: Kila ummah ufuate kile ambacho walikuwa wakiabudu. Hawatobakia wale wote waliokuwa wakiabudu asiyekuwa Allaah, miongoni mwa masanamu na miungu mingine isipokuwa wataanguka motoni mpaka hakutabakia isipokuwa waliokuwa wakimuabudu Allaah tu katika wema au waovu, na waliobakia katika katika kundi la waliopewa Kitabu. Kisha Mayahudi wataitwa na wataulizwa: Mlikuwa mkimuabudu nani? Watasema: Tulikuwa tukimuabudu ‘Uzayr mwana wa Allaah. Wataambiwa: Nyinyi ni waongo, kwani Allaah Hakumfanya yeyote kuwa mke au mwana. Je, mnataka nini sasa? Watasema: Ee Rabb wetu! Tuna kiu, hivyo Tunyweshe kinywaji. Wataelekezwa na wataambiwa: Je, mtakunywa? Hapo watakusanywa motoni, moto ambao utaonekana kama sarabi ambayo pande zake tofauti zitajivunjavunja. Kisha wataanguka motoni. Baada ya hapo wataitwa Manaswara wataulizwa: Je, mlikuwa mkimuabudu nani? Watasema: Tulikuwa tukimuabudu Masiyh mwana wa Allaah. Wataambiwa: Mumesema uwongo, kwani Allaah Hakumfanya yeyote kuwa mkewe au mwana. Kisha wataambiwa: Je, mnataka nini? Watasema kama walivyosema wale waliotangulia (yaani Mayahudi). Hatimaye, watabakia (katika mkusanyiko) wale tu waliokuwa wakimuabudu Allaah Pekee, katika wema na waovu. Kisha (Allaah) Rabb wa walimwengu Atakuja kwao katika sura iliyo karibu waliyofikiria akilini mwao kumhusu Yeye. Kutasemwa: Je, mnasubiri nini? Kila ummah umefuata walichokuwa wakiabudu. Watajibu: Tuliwaacha watu duniani tulipokuwa na haja kubwa nao, nasi hatukuwafanya wao kuwa rafiki zetu. Sasa tunamsubiri Rabb wetu tuliyekuwa tukimuabudu. Allaah Atasema: Mimi Ndiye Rabb wenu. Watasema mara mbili au tatu: Sisi hatumshirikishi yeyote na Allaah.” [Al-Bukhaariy, Kitaab At-Tafsiyr]
[6] Ahbaar: Ni Mafuqahaa weledi wa Kiyahudi:
[7] Ruhbaan: Ni Monaki wa Kinaswara: Rejea Al-Maaidah (5:82).
[8] Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Amekanusha Kuabudiwa:
Rejea An-Nisaa (4:171), Al-Maaidah (5:17), (5:72-76), (5:116-118), na Maryam (19:30-36). Ni Aayah ambazo Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) mwenyewe amekanusha kuwa yeye hapasi kuabudiwa, bali yeye ni mja na Rasuli wa Allaah, na kwamba anayepasa kuabudiwa ni Allaah Pekee.
[9] Dini Ya Kiislamu Ndio Dini Itakayoshinda Dini Nyenginezo:
Rejea Al-Fat-h (48:28) na Asw-Swaff (6:9) kwenye maelezo bayana.
[11] Miezi Minne Mitukufu:
عن أبي بَكْرَةَ رضي الله عنه عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أنه قَالَ: ((إن الزَّمَانَ قَدْ اسْتَدَارَ كَهَيْئَتِهِ يَوْمَ خَلَقَ اللَّهُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضَ السَّنَةُ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ثَلاثٌ مُتَوَالِيَاتٌ ذُو الْقَعْدَةِ وَذُو الْحِجَّةِ وَالْمُحَرَّمُ وَرَجَبُ مُضَرَ الَّذِي بَيْنَ جُمَادَى وَشَعْبَانَ))
Amesimulia Abu Bakr (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika mgawano wa zama umerudi katika hali yake ya asili siku Allaah Alipoumba mbingu na ardhi. Mwaka una miezi kumi na mbili; minne miongoni mwa hiyo ni Mitukufu, mitatu inafuatana pamoja, nayo ni Dhul-Qa'dah, Dhul-Hijjah na Al-Muharram, na mwengine ni Rajab wa (kabila la) Mudhwarr ambao uko baina ya Jumaadaa na Sha'baan.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Imeharamishwa kufanya aina yoyote ile ya maasi ndani ya miezi mitukufu ikiwemo amri ya kutokupigana vita. Rejea pia Al-Baqarah (2:217).
Na imeamrishwa pia kutenda mema kwa wingi ndani ya Miezi hii kwa kuwa malipo yake yanakuwa maradufu. Na kutenda maasi pia jazaa yake ni maradufu. Imaam Atw-Twabariy (رحمه الله) amesema: “Katika miezi yote kumi na mbili, Allaah (سبحانه وتعالى) Ameichagua hii minne, na Ameifanya kuwa ni mitukufu, na Amesisitiza itakaswe, na kwamba dhambi zitakazofanyika humo malipo yake ni maradufu, na hali kadhalika thawabu za amali njema zinakuwa maradufu na zaidi. [Atw-Twabariy (14:238)].
Na Qataadah amesema kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
فَلَا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ ۚ
“Basi msijidhulumu humo nafsi zenu humo.”
"Dhulma itakayotendeka katika Miezi Mitukufu ni mbaya na kubwa (au hatari) kuliko dhulma itakayotendeka katika miezi mingine. Hakika dhulma daima ni dhambi, lakini Allaah Hufanya baadhi ya vitu kuwa ni vizito kuliko vingine vile Apendavyo Mwenyewe. Akachagua baadhi ya Viumbe Vyake na baadhi ya vitu kuwa bora zaidi kuliko vingine. Amechagua Wajumbe kutoka Malaika na kutoka wanaadamu. Vile vile Amechagua baadhi ya kauli Zake kuwa ni bora kuliko nyingine, Misikiti kuwa bora kuliko sehemu nyingine za ardhi, Ramadhwaan na Miezi Mitukufu kuwa bora kuliko miezi mingine, siku ya Ijumaa kuwa ni bora kuliko siku nyingine, na usiku wa Laylatul-Qadr kuwa ni bora kuliko masiku mengine. Kwa hiyo basi, vitakase vile Alivyovitakasa Allaah, kwani kufanya hivyo ni vitendo vya watu wenye akili na wenye kufahamu." [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[12] Ghazwat-Tabuwk:
Tambua kwamba, sehemu kubwa ya Suwrah hii imeteremshwa wakati wa Vita vya Tabuwk [Imaam As-Sa’diy]. Na Vita vitukufu vya Tabuwk vimetajwa katika Aayah zifuatazo za Suwrah hii At-Tawbah: (38-39), (46), (48), (64-66), (74), (107-110), (117-118).
[13] Ghaar (Pango) Thawr Na Swahibu Yake Ni Abu Bakr (رضي الله عنه):
Swahibu yake katika pango hilo ni Abu Bakr (رضي الله عنه) pale walipohajiri kutoka Makkah kuelekea Madiynah huku makafiri wa ki-Quraysh wakiwa wanawasaka ili wawaue, ndipo wakajificha katika pango hilo kwa siku tatu. Na humo Allaah (سبحانه وتعالى) Aliwahifadhi kwa Uwezo na Miujiza Yake. Pango hilo lilikuwa linaitwa Jabal Thawr ambalo ni refu na njia yake ni hatari mno, lakini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahibu yake Abu Bakr (رضي الله عنه) walifanikiwa kulipanda na kulifikia pango hilo lililoko juu ya jabali hilo. Ndipo likajulikana baadaye kwa jina la Ghaar Thawr (Pango la Thawr), wakajificha humo.
عَنْ أَنَسٍ، عَنْ أَبِي بَكْرٍ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ كُنْتُ مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي الْغَارِ فَرَفَعْتُ رَأْسِي، فَإِذَا أَنَا بِأَقْدَامِ الْقَوْمِ، فَقُلْتُ يَا نَبِيَّ اللَّهِ، لَوْ أَنَّ بَعْضَهُمْ طَأْطَأَ بَصَرَهُ رَآنَا. قَالَ " اسْكُتْ يَا أَبَا بَكْرٍ، اثْنَانِ اللَّهُ ثَالِثُهُمَا
Amesimulia Anas (رضي الله عنه) kwamba amemsikia Abu Bakr (رضي الله عنه) akisema: Nilikuwa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pangoni, nikanyanyua kichwa changu (kutazama), nikaiona miguu ya watu (ikitusogelea). Nikasema: Ee Nabiy wa Allaah! Mmoja wao akitazama chini (kidogo tu) atatuona! Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaniambia: "Nyamaza ee Abu Bakr, (sisi) wawili, wa tatu wetu ni Allaah." [Al-Bukhaariy]
Na katika Riwaaya nyingine: "Unaonaje juu ya wawili, Allaah wa tatu wao?"
[14] Mawlaa "مَوْلَى": Ni Rafiki Mwandani Wa Karibu Na Mlinzi, Msaidizi, Bwana.
Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Sifa Zake.
[15] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
058-Asbaabun-Nuzuwl: At-Tawbah Aayah 058: وَمِنْهُم مَّن يَلْمِزُكَ فِي الصَّدَقَاتِ [133]
[16] Aina Ya Watu Wanane Wanaostahiki Zakaah Ya Mali:
(i) Mafakiri (ii) Masikini (iii) Wanaozitumikia kazi za ugawaji wa Zakaah (iv) Wanaotiwa nguvu nyoyo zao katika Uislamu (v) Kuwakomboa mateka (vi) Wenye Deni (vii) Katika Njia ya Allaah (viii) Msafiri Aliyeharibikiwa.
Na Tafsiyr ni kama ifuatavyo:
Zakaah za lazima (faradhi) zinapewa: (i) Wahitaji wasiomiliki kitu. (ii) Masikini wasiomiliki kiwango kinachowatosha kwa mahitaji yao. (iii) Wenye kuzishughulikia kwa kuzikusanya. (iv) Wale ambao mwazizoeza nyoyo zao miongoni mwa wale mnaotarajia wasilimu au ipate nguvu imaan yao au wawe na manufaa kwa Waislamu au mzuie kwazo madhara ya mtu yoyote yasiwafikie Waislamu. (v) Pia zinatolewa katika kuacha huru watumwa na wale wenye mikataba ya uhuru. (vi) Na zinatolewa kupewa wenye kuingia kwenye madeni kwa sababu ya kuleta maelewano baina ya watu na wenye kulemewa na madeni waliyokopa kwa lengo lisiliokuwa la uharibifu au utumiaji wa kupita kiasi kisha wakashindwa kulipa. (vii) Na zinapewa wapiganaji katika Njia ya Allaah. (viii) Na zinapewa msafiri aliyeishiwa na matumizi.
Ugawaji huu ni lazima Aliyoifaradhia Allaah na Akaikadiria. Na Allaah ni Mjuzi mno wa mambo yanayowafaa waja Wake, ni Mwingi wa Hikma katika Uendeshaji wa Mambo Yake na Sharia Zake. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[17] Maana Waliyokusudia Wanafiki Ya Mtegaji Sikio:
Wanafiki wamekusudia kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) anaposikia lolote hulikubali, na kwamba hapambanuwi baina ya kweli na uongo, wala kati ya baya na zuri. Na akiambiwa jambo lolote anaamini tu, na wakimwendea kumwapia anaamini, na wakimwendea kutoa nyudhuru na kuomba msamaha anawakubalia tu.
[18] Kufanya Istihzai Katika Mambo Ya Dini Ni Kukufuru:
Kuanzia Aayah namba (64-66), ni haramisho la kufanya istihzai, bali Aayah hii ‘Ulamaa wamesema kuwa ni dalili kuwa anayefanya istihzai katika mambo ya Dini, basi huyo amekufuru! Rejea An-Nisaa (4:140).
[19] Al-Walaa Wal-Baraa (Kupenda Na Kuandamana, Kuchukia Na Kutengana Kwa Ajili Ya Allaah):
Rejea Al-Mujaadalah (58:22) kwenye faida ya maudhui hii.
[20] Mahimizo Ya Kuamrishana Mema Na Kukatazana Munkari (Maovu):
Rejea pia Adh-Dhaariyaat (51:55) kwenye faida nyenginezo na rejea zake.
[21] Kisa Kinachonasibishwa Na Tha’labah Bin Haatwib (رضي الله عنه) Si Cha Kweli:
Baadhi ya makhatibu hutafsiri Aayah kuanza hii (75) hadi namba (77) kwamba zinamhusu Swahaba Mtukufu Tha’labah Bin Haatwib (رضي الله عنه). Lakini ‘Ulamaa wamepinga hili kwa maelezo kadhaa miongoni mwa ‘Ulamaa hao na kauli zao ni:
(i)-Imaam Al-Qurtwuby amesema katika Jaami’ al-Ahkaam:
“Tha’labah alipigana vita vya Badr, na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alishuhudia kuwa ni Muislamu wa kweli, kwa hivyo kisa hiki anachonasibishwa nacho si cha kweli.”
(ii)-Al-Haafidh Al-‘Iraaqiy amesema katika tahakiki ya Hadiyth za kitabu cha Al-Ihyaa ‘Uluwm ad-Diyn cha Ghazaaliy:
“Hadiyth hii imetolewa na Atw-Twabaraaniy na Isnaad yake ni dhaifu.”
(iii)-Ibn Hajar amesema katika Al-Iswaabah Fiy Tamyiyz Asw-Swahaabah:
“Kisa hiki sidhani kama ni sahihi kwa sababu Tha’labah huyu amepigana vita vya Badr, na Hadiyth Swahiyh ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) inasema: “Waliopigana vita vya Badr hawaingii motoni, na kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaambia; “Fanyeni mtakacho, mumekwisha ghufuriwa madhambi yenu.”
Kwa hiyo iweje Tha’labah awe mnafiki?”
Hali kadhaalika Fataawaa za ‘Ulamaa Wa Al-Lajnah al-Lajnah ad-Daaimah Lil-Buhuwth al-‘Ilmiyyah wal Iftaa’ (49/26) na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn [Sharh Uswuwl fiy Tafsiyr - Ibn ‘Uthaymiyn]
[25] Waliotangulia Awali (Salaf):
Hao ndio Salaf Swaalih, nao ndio waliokuweko katika karne tatu za mwanzo; Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Taabi’iyn ni wanafunzi wao, pamoja na Atbaa’ Taabi’iyn (waliowafuata Taabi’iyn) ambao Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amewashuhudia kwa kheri aliposema:
خَيْرُ النَّاسِ قَرْنِي، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ
“Watu bora kabisa ni karne yangu, kisha wanaowafuatia, kisha wanaowafuatia.” [Al-Bukhaari]
Kisha wengineo waliowafuata hao kwa ihsaan katika Manhaj yao ya mafundisho ya Kitabu na Sunnah, na kuifanyia daawah (kuilingania), na kuifanyia kazi. Na wakawa kwa hayo ni Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah. Rejea Al-Hashr (59:10).
[26] Masjid Dhwiraar (Msikiti wa madhara):
Aayah hizi At-Tawbah (9:107-110), zinazungumzia msikiti wa madhara. Ni msikiti waliojenga wanafiki kwa sababu hawakutaka kuswali jamaa pamoja na Waislamu katika Masjid Qubaa ambao ulikuwa karibu na sehemu hiyo. Walioujenga msikiti huo wa madhara ni wanafiki kumi na mbili. Wakadai kuwa wameujenga kwa niya ya kusaidia walio dhaifu na wagonjwa kutokana na nyusiku za mvua na za baridi, na kwamba hawakukusudia isipokuwa wema. Wakamuomba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aswali humo ili awatilie barakah. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anajiandaa wakati huo kuelekea katika vita vya Jihaad vya Tabuwk, hivyo akawaitikia kuwa pindi watakaporudi atakuja kuswali. Lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Aliteremsha Aayah hizo tukufu kufichua ubaya wao, na Akamkataza Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kuswali humo.
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله) amesema: “Masjid Dhwiraar (msikiti wa madhara) ulijengwa kwa niya ya ufisadi kutokana na Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) ya Aayah hii ya At-Tawbah (9:107). Walioujenga ni wanafiki, na makusudio yao (kama ilivyotajwa katika Aayah) ni:
(i) Kuleta madhara kwa Masjid Qubaa, ndio maana ukaitwa msikiti wa madhara.
(ii) Kumkufuru Allaah, kwa kuwa ukafiri unapangwa humo na kupitishwa humo - tunaomba kinga kwa Allaah - na walioujenga pia ni wanafiki.
(iii) Kuwafarikisha Waumini, kwani badala ya kuswali katika Masjid Qubaa safu moja au safu mbili, iswaliwe nusu safu, na wengineo waswali msikiti mwengine. Na kuna sharia (hukumu) kuhusu mijumuiko ya Waumini.
(iv) Kuwa ngome kwa waliompiga vita Allaah na Rasuli Wake. Mtu mmoja aitwaye Abu ‘Aamir Al-Faasiq alikwenda Sham. Kulikuweko mawasiliano baina yake na wanafiki walioujenga msikiti huo kwa maelekezo yake, wakawa wanajumuika humo kupanga waliyoyakusudia ya njama na hadaa za kumfanyia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba zake. Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
وَلَيَحْلِفُنَّ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا الْحُسْنَىٰ ۖ
“Na “Bila shaka wanaapa: Hatujakusudia ila jambo zuri.”
Basi hii ndio kawaida ya wanafiki; viapo vya uongo! [Majmuw’u Fataawaa wa Rasaail Ibn ‘Uthaymiyn (9:226-227)]
[27] Msikiti Ulioasisiwa Juu Ya Taqwa:
Kuna kauli mbili kuhusu Msikiti huo uliokusudiwa. (i) Masjid Qubaa (ii) Masjid Nabawiy (Msikiti wa Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) Lakini ‘Ulamaa wanaona kuwa kauli hazipingani, kwani Misikiti yote hiyo miwili iliasisiwa, au ilikuwa Misikiti ya mwanzo kujengwa kwa ajili ya Waislamu.
(i) Masjid Qubaa: Ni Msikiti wa kwanza kabisa kujengwa na Waislamu walipofika Madiynah baada ya kuhajiri kutoka Makkah. Ngamia wake Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipiga magoti sehemu hiyo. Akapendelea hapo kujengwe Msikiti huo. Na hapo kulikuwa na kisima cha Swahaba Mtukufu Abu Ayyuwb Al-Answaariy. Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akabashiria fadhila za kuswali rakaa mbili katika Masjid Qubaa kuwa ni sawa na thawabu za kutekeleza ‘Umrah kutokana na kauli yake (صلى الله عليه وآله وسلم): “Mwenye kutawadha nyumbani kwake, kisha akauendea Masjid Qubaa, akaswali ndani yake Swalaah moja, basi anapata thawabu za mfano wa ‘Umrah.”. [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh. Imekharijiwa na Ibn Maajah (1412)]
(ii) Masjid Nabawiy: Ni Msikiti wa kwanza kujengwa na Waislamu walipofika Madiynah, na ndio Masjid Nabawiy (Msikiti wa Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) na ndipo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipofanya kuwa ni maskani yake pamoja na wakeze. Na aghlabu ya Swahaba pia walifanya masikani zao pembezoni mwake. Baina yake na Masjid Qubaa ni umbali wa kilo mita tano.
[28] As-Saaihuwn:
‘Ulamaa wametaja maana mbili za As-Saaihuwn:
(i) Wenye kufunga Swiyaam kama vile walivyokusudiwa wakeze Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Suwrat At-Tahriym (66:5).
(ii) Wenye kusafiri kwa ajili ya ibaada kama vile Hajj, ‘Umrah, Jihaad katika Njia ya Allaah, kutafuta ilimu, Muhaajiruwn (wahamao kwa ajili ya Dini), kudumisha kuunga undugu wa damu na jamaa wa karibu, na mengineyo yote yaliyomo ndani ya juhudi za kwenda huku na kule kwa ajili ya ibaada na kufanya khayraat (mambo ya kheri).
[29] Haramisho La Kuwaombea Makafiri Maghfirah:
Aayah hii (113) imeteremshwa kumhusu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipotaka kumuombea maghfirah ammi yake Abu Twaalib pindi alipofariki. Allaah (سبحانه وتعالى) Akamkataza kufanya hivyo. Bonyeza viungo vifuatavyo vya Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Kwa hiyo haramisho hili linahusu yeyote yule aliyekafiri hata kama ni mzazi kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah inayofuatia namba (114), kuhusu Nabiy Ibraahiiym (عليه السّلام) ambaye naye aliacha kumuombea maghfirah baba yake baada ya kutambua ni adui wa Allaah. Rejea pia Al-Mumtahinah (60:4).
Rejea pia Al-Qaswasw (28:56).
[30] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
Rehma Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwaghufuria Swahaba:
Tafsiyr:
Allaah (سبحانه وتعالى) Amemuelekeza Nabiy Wake Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kurudi Kwake na kumtii, na Aakawakubalia tawbah Muhaajiruwn waliohama nyumba zao na jamaa zao wakaenda kwenye makazi ya amani (Madiynah), na pia Aliwakubalia tawbah Anaswaar waliomuhami Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), waliotoka pamoja na yeye kupambana na maadui katika vita vya Tabuwk, katika kipindi cha joto kali na shida ya chakula na vipando. Allaah (سبحانه وتعالى) Amwakubalia tawbah yao baada ya hali kufikia kiwango kwamba nyoyo za baadhi yao zilikaribia kuiyepuka haki na kupendelea ulegevu na utulivu. Lakini Allaah (عزّ وجلّ) Aliwathibitisha na Akawapa nguvu na Akawakubalia tawbah. Hakika Yeye kwao ni Mwingi wa Upole ni Mwenye Huruma. Na miongoni mwa Huruma Yake kwao ni kwamba Aliwapa neema ya kutubia, Akaikubali tawbah yao na Akawathibitisha juu yake. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[31] Watatu Hao Ni: Ka’ab Bin Maalik, Hilaal Bin Umayyah, Muraarah Bin Ar-Rabiy’ (رضي الله عنهم):
Swahaba watatu hao wamekusudiwa kuanzia Aayah (117-119), na ndio sababu ya kuteremshwa Aayah hizi. Kisa chao amekisimulia mwenyewe Ka’ab (رضي الله عنه) , na kimeanzia pale walipotangaziwa kwenda Jihaad ya vita vya Tabuwk ambavyo vilikuwa ni vita vya hali ngumu kabisa na mashaka makubwa kutokana na jua kali, ukosefu wa vifaa, zana, na vipando, mbali na wingi wa maadui. Na hii ndio sababu Allaah (سبحانه وتعالى) Amevitaja Vita hivi katika Aayah (117) kuwa ni “Saa ya dhiki.”
Swahaba hawa watatu walikhalifu amri ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ya kutoka kwenda vitani wakabakia nyuma, lakini walikuja kujuta mno, wakaomba tawbah, lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Aliwangojelesha muda mrefu kupokea tawbah yao hadi wakafikwa na dhiki kubwa, lakini nao hawakukata tamaa na Rehma ya Allaah (سبحانه وتعالى). Hatimaye Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaghufuria.
Kisa hiki kina mafundisho kadhaa kwa Waumini: (i) Kutokuasi Amri ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) (ii) Kuvumilia kwa subira ya juu katika hali ya dhiki (ii) Kutokukata tamaa katika kumuomba Allaah (سبحانه وتعالى) maghfirah (iv) Shaytwaan anaweza kuwaghilibu hata Waumini wa kweli kama Swahaba hao watukufu ambao waliteleza katika kutii amri.
Pia kuna mafundisho mengineyo mengi yaliyotokana na vita vyenyewe. Ni kisa kirefu ambacho kimepokelewa na Imaam [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Ahmad]
Bonyeza kiungo kifuatacho katika Hadiyth namba (9) ambayo Ka’b Bin Maalik (رضي الله عنه) anaelezea mwenyewe kisa chao hicho:
[32] Qur-aan Inaposomwa, Inawazidisha Waumini Imaan. Ama Kafiri Na Wenye Maradhi Katika Nyoyo Zao, Haiwazidishii Ila Rijs (Unafiki, Shaka Kufru n.k).
Aayah hii namba (124) na inayofuatia (125), inataja kuwa Qur-aan inawazidisha imaan Waumini. Ama wenye maradhi ya moyo, inawazidishia rijs (unafiki, shaka, kufru n.k). Rejea Al-Israa (17:82) kwenye maelezo kuhusu Qur-aan kwamba ni shifaa na rehma kwa Waumini. Ama kwa makafiri, haiwazidishii isipokuwa khasara.
Rejea pia Al-Hajj (22:46) kwenye maelezo kuhusu maana ya moyo uliopofuka.
Rejea pia Fusw-Swilat (41:44) kwenye uchambuzi kuhusu Qur-aan kuwa ni shifaa (poza na tiba), mawaidha na rehma kwa Waumini.
Rejea pia Suwrah Muhammad (47:20) kwenye maelezo na rejea mbalimbali kuhusu nyoyo zenye maradhi.
Rejea pia Ash-Shu’araa (26:88-89) kwenye ufafanuzi na maelezo kuhusu moyo uliosalimika.
[33] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kuwa Na Upole, Huruma, Na Kuwajali Mno Waumini.
Utakuta katika Siyrah ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) jinsi alivyokuwa na sifa hizo zote kwa Waumini, bali hata aliwajali Waumini asiokutana nao, yaani katika ummah wake wa zama zote. Rejea Al-Maaidah (5:118).
Hadiyth nyingi zimetaja sifa hizo zake. Kati yake ni hii ifuatayo ambayo amejali na kukhofia Waumini wakingwe na moto:
Amesimulia Jaabir (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mfano wangu na mfano wenu ni kama mtu anayewasha moto, kisha wadudu na nondo wala nguo wakawa wanaangukia humo, kisha yeye (huyo mtu) anajaribu kuwatoa humo nami huku nawazuia migongo yenu isiangukie katika moto, lakini mnateleza mikononi mwangu.” [Muslim]
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwajali hata Swahaba walio duni kabisa:
عَنْ أَبِي بَرْزَةَ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ فِي مَغْزًى لَهُ فَأَفَاءَ اللَّهُ عَلَيْهِ فَقَالَ لأَصْحَابِهِ " هَلْ تَفْقِدُونَ مِنْ أَحَدٍ " . قَالُوا نَعَمْ فُلاَنًا وَفُلاَنًا وَفُلاَنًا . ثُمَّ قَالَ " هَلْ تَفْقِدُونَ مِنْ أَحَدٍ " . قَالُوا نَعَمْ فُلاَنًا وَفُلاَنًا وَفُلاَنًا . ثُمَّ قَالَ " هَلْ تَفْقِدُونَ مِنْ أَحَدٍ " . قَالُوا لاَ . قَالَ " لَكِنِّي أَفْقِدُ جُلَيْبِيبًا فَاطْلُبُوهُ " . فَطُلِبَ فِي الْقَتْلَى فَوَجَدُوهُ إِلَى جَنْبِ سَبْعَةٍ قَدْ قَتَلَهُمْ ثُمَّ قَتَلُوهُ فَأَتَى النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَوَقَفَ عَلَيْهِ فَقَالَ " قَتَلَ سَبْعَةً ثُمَّ قَتَلُوهُ هَذَا مِنِّي وَأَنَا مِنْهُ هَذَا مِنِّي وَأَنَا مِنْهُ " . قَالَ فَوَضَعَهُ عَلَى سَاعِدَيْهِ لَيْسَ لَهُ إِلاَّ سَاعِدَا النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ فَحُفِرَ لَهُ وَوُضِعَ فِي قَبْرِهِ . وَلَمْ يَذْكُرْ غَسْلاً .
Amesimlia Abuu Barzah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuweko katika uwanja wa vita ambao Allaah Alijaalia (ushindi) na kupata ngawira za vita. Akawaambia Swahaba zake: “Je! Kuna yeyote amekosekana kati yenu?” Wakasema: Naam, fulani na fulani. Akasema tena: “Je! Kuna yeyote kati yenu aliyekosekana?” Wakasema: Naam, fulani na fulani. Kisha akasema tena: “Je! Kuna yeyote kati yenu aliyekosekana?” Wakasema: Hapana. Hapo (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Lakini nimemkosa (simuoni) Julaybiyb, hebu mtafuteni.” (Swahaba) wakamtafuta (Julaybiyb) kati ya wale waliouawa, wakamkuta kando ya (maiti) saba ambao yeye aliwaua na yeye akauliwa (na adui). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaenda pale akasimama (kando yake) na akasema: “Amewaua watu saba. Ndipo (adui zake) wakamuua. Yeye ni wangu na mimi ni wake.” Kisha akamweka mikononi mwake na hakukuwa na mwingine yeyote wa kumuinua isipokuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Kisha kaburi lilichimbwa kwa ajili yake, akawekwa kaburini na haikutajwa kuhusu kuoshwa kwake”. [Muslim]
Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) amefafanua Aayah hii kwa sifa kama hizo na nyenginezo za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kisha mwishowe akasema:
“Basi kwa hayo, ndio maana haki yake inatangulizwa kuliko haki nyingine zote za viumbe wengineo, na ni wajibu kwa ummah kumwamini, kumuadhimisha, na kumheshimu kwa utukuzo.”
Bonyeza kiungo kifuatacho kupata faida tele kuhusu Sifa na Akhlaaq za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
Sifa-Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) [141]
[34] Miongoni Mwa Adhkaar Za Asubuhi Na Jioni Ni Kusema Mara Saba:
حَسْبِيَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ ۖ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ
“Amenitosha Allaah Ambaye hakuna mwabudiwa wa haki ila Yeye tu, nimetawakkal Kwake, Naye Ndiye Rabbi wa ‘Arshi Adhimu.”
يُونُس
010-Yuwnus
010-Yuwnus: Utangulizi Wa Suwrah [143]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْحَكِيمِ﴿١﴾
1. Alif Laam Raa.[1] Hizi[2] ni Aayaat za Kitabu chenye hikmah.
أَكَانَ لِلنَّاسِ عَجَبًا أَنْ أَوْحَيْنَا إِلَىٰ رَجُلٍ مِّنْهُمْ أَنْ أَنذِرِ النَّاسَ وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا أَنَّ لَهُمْ قَدَمَ صِدْقٍ عِندَ رَبِّهِمْ ۗ قَالَ الْكَافِرُونَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ مُّبِينٌ﴿٢﴾
2. Je, imekuwa ni ajabu kwa watu kwamba Tumemfunulia Wahy mtu miongoni mwao kwamba: Waonye watu na wabashirie wale walioamini kwamba watapata cheo kitukufu mbele ya Rabb wao. Makafiri wakasema: Hakika huyu bila shaka ni mchawi bayana.
إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۖ مَا مِن شَفِيعٍ إِلَّا مِن بَعْدِ إِذْنِهِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿٣﴾
3. Hakika Rabb wenu ni Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Akawa juu[3] ya ‘Arsh. Anaendesha mambo yote. Hakuna mwombezi yeyote ila baada ya Idhini Yake. Huyu Ndiye Allaah Rabb Wenu, basi mwabuduni. Je, hamkumbuki?
إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا ۖ وَعْدَ اللَّـهِ حَقًّا ۚ إِنَّهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ بِالْقِسْطِ ۚ وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ﴿٤﴾
4. Kwake ni marejeo yenu nyote. Ni Ahadi ya Allaah ya kweli. Hakika Yeye Anaanzisha uumbaji, kisha Anaurejesha ili Awalipe kwa uadilifu wale walioamini na wakatenda mema. Na wale waliokufuru watapata kinywaji cha maji ya kuchemka mno, na adhabu iumizayo kwa sababu ya kukufuru kwao.
هُوَ الَّذِي جَعَلَ الشَّمْسَ ضِيَاءً وَالْقَمَرَ نُورًا وَقَدَّرَهُ مَنَازِلَ لِتَعْلَمُوا عَدَدَ السِّنِينَ وَالْحِسَابَ ۚ مَا خَلَقَ اللَّـهُ ذَٰلِكَ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ يُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ﴿٥﴾
5. Yeye Ndiye Aliyejaalia jua kuwa ni mwanga na mwezi kuwa ni nuru, na Akaukadiria[4] vituo ili mjue idadi ya miaka na hesabu. Allaah Hakuumba hivyo ila kwa haki. Anafasili waziwazi Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) kwa watu wanaojua.
إِنَّ فِي اخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمَا خَلَقَ اللَّـهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَّقُونَ﴿٦﴾
6. Hakika katika kukhitilafiana usiku na mchana na Alivyoviumba Allaah katika mbingu na ardhi, bila shaka kuna Aayaat (Ishara, Dalili za wazi) kwa watu walio na taqwa.
إِنَّ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا وَرَضُوا بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَاطْمَأَنُّوا بِهَا وَالَّذِينَ هُمْ عَنْ آيَاتِنَا غَافِلُونَ﴿٧﴾
7. Hakika wale wasiotaraji kukutana Nasi, na wakaridhika na uhai wa dunia na wakakinaika nayo, na wale ambao wanaghafilika na Aayaat Zetu (za kiulimwengu na kisharia).
أولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمُ النَّارُ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٨﴾
8. Hao makazi yao ni moto, kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ يَهْدِيهِمْ رَبُّهُم بِإِيمَانِهِمْ ۖتَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ﴿٩﴾
9. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Rabb wao Atawaongoza kwa sababu ya imaan zao. Itapita chini yao mito katika Jannaat zilojaa neema.
دَعْوَاهُمْ فِيهَا سُبْحَانَكَ اللَّـهُمَّ وَتَحِيَّتُهُمْ فِيهَا سَلَامٌ ۚ وَآخِرُ دَعْوَاهُمْ أَنِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿١٠﴾
10. Wito wao humo ni: Subhaanak (Utakasifu ni Wako) ee Allaah! Na maamkizi yao humo ni Salaamun! Na wito wao wa mwisho ni AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Rabb wa walimwengu.
وَلَوْ يُعَجِّلُ اللَّـهُ لِلنَّاسِ الشَّرَّ اسْتِعْجَالَهُم بِالْخَيْرِ لَقُضِيَ إِلَيْهِمْ أَجَلُهُمْ ۖ فَنَذَرُ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ﴿١١﴾
11. Na lau Allaah Angeliwaharakizia watu shari kama wanavyojihimizia kheri, bila shaka wangehukumiwa muda wao (wa kuangamizwa). Basi Tunawaacha wale wasiotarajia kukutana Nasi katika upindukaji mipaka ya kuasi kwao, wakitangatanga kwa upofu.
وَإِذَا مَسَّ الْإِنسَانَ الضُّرُّ دَعَانَا لِجَنبِهِ أَوْ قَاعِدًا أَوْ قَائِمًا فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُ ضُرَّهُ مَرَّ كَأَن لَّمْ يَدْعُنَا إِلَىٰ ضُرٍّ مَّسَّهُ ۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْمُسْرِفِينَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٢﴾
12. Na inapomgusa binaadamu dhara hutuomba anapolala ubavu, au anapokaa au anaposimama wima. Tunapomuondolea dhara, hupita kama kwamba hakutuomba dhara iliyomgusa.[5] Hivyo ndivyo walivyopambiwa wapindukao mipaka yale waliyokuwa wakiyatenda.
وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا الْقُرُونَ مِن قَبْلِكُمْ لَمَّا ظَلَمُوا ۙ وَجَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ وَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْقَوْمَ الْمُجْرِمِينَ﴿١٣﴾
13. Na kwa yakini Tuliangamiza karne nyingi kabla yenu walipodhulumu na wakawajia Rusuli wao kwa hoja bayana, na hawakuwa wa kuamini. Hivyo ndivyo Tunavyowalipa watu wahalifu.
ثُمَّ جَعَلْنَاكُمْ خَلَائِفَ فِي الْأَرْضِ مِن بَعْدِهِمْ لِنَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ﴿١٤﴾
14. Kisha Tukakufanyeni warithi waandamizi katika ardhi baada yao, ili Tutazame vipi mtatenda.
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ ۙ قَالَ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا ائْتِ بِقُرْآنٍ غَيْرِ هَـٰذَا أَوْ بَدِّلْهُ ۚ قُلْ مَا يَكُونُ لِي أَنْ أُبَدِّلَهُ مِن تِلْقَاءِ نَفْسِي ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ ۖ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ﴿١٥﴾
15. Na wanaposomewa Aayaat Zetu bayana, wale wasiotaraji kukutana Nasi husema: Lete Qur-aan isiyokuwa hii au ibadilishe. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hainipasii mimi kuibadilisha kwa khiyari ya nafsi yangu. Mimi sifuati ila tu yale niliyofunuliwa Wahy. Hakika mimi nakhofu nikimuasi Rabb wangu, adhabu ya Siku iliyo kuu kabisa.
قُل لَّوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا تَلَوْتُهُ عَلَيْكُمْ وَلَا أَدْرَاكُم بِهِ ۖ فَقَدْ لَبِثْتُ فِيكُمْ عُمُرًا مِّن قَبْلِهِ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ﴿١٦﴾
16. Sema: Kama Angetaka Allaah nisingelikusomeeni (hii Qur-aan) na wala Asingelikujulisheni nayo. Kwani nimekwishaishi nanyi umri wote kabla yake. Je, basi hamtii akilini?
فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْمُجْرِمُونَ﴿١٧﴾
17. Basi nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia Allaah uongo au akazikadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili) Zake? Hakika wahalifu hawatofaulu.
وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ ۚ قُلْ أَتُنَبِّئُونَ اللَّـهَ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿١٨﴾
18. Na wanaabudu pasi na Allaah ambavyo haviwadhuru wala haviwanufaishi na wanasema: Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah. Sema: Je, mnamjulisha Allaah yale Asiyoyajua katika mbingu na ardhini? Utakasifu ni Wake na Ametukuka kwa ‘Uluwa na yale yote wanayomshirikisha.
وَمَا كَانَ النَّاسُ إِلَّا أُمَّةً وَاحِدَةً فَاخْتَلَفُوا ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ فِيمَا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ﴿١٩﴾
19. Na watu hawakuwa ila ni ummah mmoja kisha wakakhitilafiana. Na kama si neno lililotangulia kutoka kwa Rabb wako, bila shaka ingehukumiwa baina yao katika yale wanayokhitilafiana.
وَيَقُولُونَ لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِّن رَّبِّهِ ۖ فَقُلْ إِنَّمَا الْغَيْبُ لِلَّـهِ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ﴿٢٠﴾
20. Na wanasema: Kwa nini hakuteremshiwa Aayah (Ishara, Dalili) yoyote (ya kihisia) kutoka kwa Rabb wake? Basi sema: Hakika ya ghaibu ni ya Allaah Pekee. Basi ngojeeni, hakika na mimi niko pamoja nanyi katika wanaongojea.
وَإِذَا أَذَقْنَا النَّاسَ رَحْمَةً مِّن بَعْدِ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُمْ إِذَا لَهُم مَّكْرٌ فِي آيَاتِنَا ۚ قُلِ اللَّـهُ أَسْرَعُ مَكْرًا ۚ إِنَّ رُسُلَنَا يَكْتُبُونَ مَا تَمْكُرُونَ﴿٢١﴾
21. Na Tunapowaonjesha watu rehma baada ya dhara iliyowagusa, tahamaki wanafanya hila kuzichafua Aayaat (na Ishara, Dalili) Zetu. Sema: Allaah Ni Mwepesi zaidi wa Kutibua hila. Hakika Wajumbe Wetu wanaandika hila mnazopanga.
هُوَ الَّذِي يُسَيِّرُكُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا كُنتُمْ فِي الْفُلْكِ وَجَرَيْنَ بِهِم بِرِيحٍ طَيِّبَةٍ وَفَرِحُوا بِهَا جَاءَتْهَا رِيحٌ عَاصِفٌ وَجَاءَهُمُ الْمَوْجُ مِن كُلِّ مَكَانٍ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ أُحِيطَ بِهِمْ ۙ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ لَئِنْ أَنجَيْتَنَا مِنْ هَـٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ﴿٢٢﴾
22. Yeye Ndiye Anayekuendesheni katika bara na bahari. Mpaka mnapokuwa katika majahazi na yakawa yanakwenda nao kwa upepo wa kheri, mzuri, na wao wakafurahia, mara ukawajia upepo wa dhoruba, na yakawajia mawimbi kutoka kila upande, na wakayakinisha kwamba wameshazungukwa. Hapo humwomba Allaah wakimtakasia Yeye Dini[6] (wakisema): Ukituokoa katika haya, bila shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.
فَلَمَّا أَنجَاهُمْ إِذَا هُمْ يَبْغُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۗ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّمَا بَغْيُكُمْ عَلَىٰ أَنفُسِكُم ۖ مَّتَاعَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُكُمْ فَنُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٢٣﴾
23. Lakini Anapowaokoa, tahamaki wao wanafanya tena uovu wa maasi na dhulma katika ardhi bila ya haki. Enyi watu! Hakika baghi[7] yenu (uovu wenu) utawarudia wenyewe. Ni starehe ya uhai wa dunia. Kisha Kwetu marejeo yenu, na Tutakujulisheni mliyokuwa mkiyatenda.
إِنَّمَا مَثَلُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ مِمَّا يَأْكُلُ النَّاسُ وَالْأَنْعَامُ حَتَّىٰ إِذَا أَخَذَتِ الْأَرْضُ زُخْرُفَهَا وَازَّيَّنَتْ وَظَنَّ أَهْلُهَا أَنَّهُمْ قَادِرُونَ عَلَيْهَا أَتَاهَا أَمْرُنَا لَيْلًا أَوْ نَهَارًا فَجَعَلْنَاهَا حَصِيدًا كَأَن لَّمْ تَغْنَ بِالْأَمْسِ ۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿٢٤﴾
24. Hakika mfano wa uhai wa dunia ni kama maji Tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, kisha yakachanganyika nayo mimea ya ardhi katika wanayoila watu na wanyama. Mpaka ardhi inapokamilisha uzuri wake na ikapambika, na wakayakinisha watu wake kwamba wanao uwezo juu yake (kuivuna), tahamaki Amri Yetu ikaijia usiku au mchana, Tukaifanya kama iliyofyekwa kama kwamba haikusitawi jana. Hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) kwa watu wanaotafakari.
وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَىٰ دَارِ السَّلَامِ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٢٥﴾
25. Na Allaah Anaitia katika Daar As-Salaam (Nyumba ya amani) na Anamwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.
لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ وَلَا يَرْهَقُ وُجُوهَهُمْ قَتَرٌ وَلَا ذِلَّةٌ ۚ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿٢٦﴾
26. Kwa wale waliofanya ihsaan watapata (huko Jannah) jazaa nzuri kabisa na ziada (kumuona Allaah).[8] Na vumbi halitowafunika nyuso zao wala madhila.[9] Hao ni watu wa Jannah, humo wao watadumu.
وَالَّذِينَ كَسَبُوا السَّيِّئَاتِ جَزَاءُ سَيِّئَةٍ بِمِثْلِهَا وَتَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۖ مَّا لَهُم مِّنَ اللَّـهِ مِنْ عَاصِمٍ ۖ كَأَنَّمَا أُغْشِيَتْ وُجُوهُهُمْ قِطَعًا مِّنَ اللَّيْلِ مُظْلِمًا ۚ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿٢٧﴾
27. Na wale waliochuma maovu, jazaa ya uovu ni mfano wake vile vile, na madhila yatawafunika. Hawatopata atakayewaepusha na (Adhabu ya) Allaah. (Zitakuwa) nyuso zao kama kwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wenye giza kubwa. Hao ni watu wa motoni, humo wao watadumu.
وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا مَكَانَكُمْ أَنتُمْ وَشُرَكَاؤُكُمْ ۚ فَزَيَّلْنَا بَيْنَهُمْ ۖ وَقَالَ شُرَكَاؤُهُم مَّا كُنتُمْ إِيَّانَا تَعْبُدُونَ﴿٢٨﴾
28. Na Siku Tutakayowakusanya wote, kisha Tutawaambia wale walioshirikisha: Bakieni mahali penu nyinyi na washirika wenu. Kisha Tutawatenganisha baina yao. Na washirika wao watasema: Hamkuwa mkituabudu sisi.
فَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ إِن كُنَّا عَنْ عِبَادَتِكُمْ لَغَافِلِينَ﴿٢٩﴾
29. Basi Allaah Anatosheleza kuwa Mwenye Kushuhudia yote baina yetu na baina yenu kwamba sisi tulikuwa hatuna khabari na ibaada zenu.
هُنَالِكَ تَبْلُو كُلُّ نَفْسٍ مَّا أَسْلَفَتْ ۚ وَرُدُّوا إِلَى اللَّـهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ ۖ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ﴿٣٠﴾
30. Huko (Qiyaamah) kila nafsi itatiwa mtihanini[10] kwa yote iliyoyatanguliza. Na watarudishwa kwa Allaah, Mawlaa[11] wao wa haki. Na yatawapotea yale yote waliyokuwa wakiyatunga (ya uongo).
قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَمَن يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۚ فَسَيَقُولُونَ اللَّـهُ ۚ فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ﴿٣١﴾
31. Sema: Nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini? Au nani anayemiliki kusikia na kuona? Na nani anayemtoa aliye hai kutoka mfu, na anayemtoa mfu kutoka aliye hai? Na nani anayeendesha mambo (yote)? Watasema: Ni Allaah. Basi sema: Je, basi hamuwi na taqwa?[12]
فَذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمُ الْحَقُّ ۖ فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ﴿٣٢﴾
32. Basi Huyo Ndiye Allaah, Rabb wenu wa haki. Na kuna nini baada ya haki ila upotofu? Basi vipi mnageuzwa?
كَذَٰلِكَ حَقَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى الَّذِينَ فَسَقُوا أَنَّهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ﴿٣٣﴾
33. Hivyo ndivyo Neno la Rabb wako lilivyothibiti juu ya wale waliofanya ufasiki kwamba hawatoamini.
قُلْ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ۚ قُلِ اللَّـهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ﴿٣٤﴾
34. Sema: Je, yuko kati ya washirika wenu anayeanzisha uumbaji kisha anaurudisha? Sema: Allaah Anaanzisha uumbaji kisha Anaurudisha. Basi vipi mnaghilibiwa?
قُلْ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ ۚ قُلِ اللَّـهُ يَهْدِي لِلْحَقِّ ۗ أَفَمَن يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ أَحَقُّ أَن يُتَّبَعَ أَمَّن لَّا يَهِدِّي إِلَّا أَن يُهْدَىٰ ۖ فَمَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ﴿٣٥﴾
35. Sema: Je, yuko kati ya washirika wenu anayeongoza kwenye haki? Sema: Allaah Anaongoza kwenye haki. Je, basi anayeongoza kwenye haki anastahiki zaidi kufuatwa au yule asiyeongoza isipokuwa tu yeye aongozwe? Basi mna nini? Vipi mnahukumu?
وَمَا يَتَّبِعُ أَكْثَرُهُمْ إِلَّا ظَنًّا ۚ إِنَّ الظَّنَّ لَا يُغْنِي مِنَ الْحَقِّ شَيْئًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِمَا يَفْعَلُونَ﴿٣٦﴾
36. Na wengi wao hawafuati ila dhana tu. Hakika dhana haifai kitu chochote mbele ya haki. Hakika Allaah Ni Mjuzi kwa yale yote wayatendayo.
وَمَا كَانَ هَـٰذَا الْقُرْآنُ أَن يُفْتَرَىٰ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِن تَصْدِيقَ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ الْكِتَابِ لَا رَيْبَ فِيهِ مِن رَّبِّ الْعَالَمِينَ﴿٣٧﴾
37. Na haiwezekani hii Qur-aan kuwa imetungwa bila kuwa imetoka kwa Allaah, lakini inasadikisha yale yaliyokuja kabla yake na ni tafsili ya Vitabu (vilivyoitangulia).[13] Haina shaka ndani yake, imetoka kwa Rabb wa walimwengu.
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّثْلِهِ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٣٨﴾
38. Je, wanasema (Qur-aan) ameitunga (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)? Sema: Hebu basi leteni Suwrah ya mfano wake,[14] na waiteni mnaoweza pasi na Allaah mkiwa ni wakweli.
بَلْ كَذَّبُوا بِمَا لَمْ يُحِيطُوا بِعِلْمِهِ وَلَمَّا يَأْتِهِمْ تَأْوِيلُهُ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الظَّالِمِينَ﴿٣٩﴾
39. Bali wamekadhibisha yale wasiyoyaelewa vyema ilimu yake, na wala uhakika wake halisi haujawafikia. Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale wa kabla yao. Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya madhalimu.
وَمِنْهُم مَّن يُؤْمِنُ بِهِ وَمِنْهُم مَّن لَّا يُؤْمِنُ بِهِ ۚ وَرَبُّكَ أَعْلَمُ بِالْمُفْسِدِينَ﴿٤٠﴾
40. Na miongoni mwao wako wanaoiamini, na miongoni mwao wako wasioiamini. Na Rabb wako Anawajua zaidi mafisadi.
وَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل لِّي عَمَلِي وَلَكُمْ عَمَلُكُمْ ۖ أَنتُم بَرِيئُونَ مِمَّا أَعْمَلُ وَأَنَا بَرِيءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ﴿٤١﴾
41. Na wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi sema: Mimi nina amali zangu, nanyi mna amali zenu. Nyinyi hamna dhima na yale niyatendayo, na wala mimi sina dhima na yale myatendayo.
وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُونَ إِلَيْكَ ۚ أَفَأَنتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ وَلَوْ كَانُوا لَا يَعْقِلُونَ﴿٤٢﴾
42. Na miongoni mwao wako wanaokusikiliza. Je, kwani wewe unasikilizisha viziwi japokuwa hawatii akilini?
وَمِنْهُم مَّن يَنظُرُ إِلَيْكَ ۚ أَفَأَنتَ تَهْدِي الْعُمْيَ وَلَوْ كَانُوا لَا يُبْصِرُونَ﴿٤٣﴾
43. Na miongoni mwao wako wanaokutazama. Je, kwani wewe unaongoza (wahidike) vipofu japokuwa hawaoni?
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَظْلِمُ النَّاسَ شَيْئًا وَلَـٰكِنَّ النَّاسَ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴿٤٤﴾
44. Hakika Allaah Hadhulumu watu chochote, lakini watu wenyewe ni wenye kudhulumu nafsi zao.
وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ كَأَن لَّمْ يَلْبَثُوا إِلَّا سَاعَةً مِّنَ النَّهَارِ يَتَعَارَفُونَ بَيْنَهُمْ ۚ قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِلِقَاءِ اللَّـهِ وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ﴿٤٥﴾
45. Na Siku Atakayowakusanya (wataona) kama kwamba hawakuishi isipokuwa saa moja ya mchana, watatambuana. Kwa yakini wamekhasirika wale waliokadhibisha kukutana na Allaah, na hawakuwa wenye kuhidika.
وَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ الَّذِي نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ ثُمَّ اللَّـهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ﴿٤٦﴾
46. Na kama Tutakuonyesha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) baadhi ya yale Tunayowaahidi (ya adhabu) au Tukikufisha, basi Kwetu ni marejeo yao, kisha Allaah Ni Mwenye Kushuhudia yote juu ya yale wanayoyatenda.
وَلِكُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولٌ ۖ فَإِذَا جَاءَ رَسُولُهُمْ قُضِيَ بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿٤٧﴾
47. Na kila ummah una Rasuli. Basi anapokuja Rasuli wao inahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatodhulumiwa.
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٤٨﴾
48. Na wanasema: Lini (itafika) hiyo ahadi[15] mkiwa ni wakweli?
قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي ضَرًّا وَلَا نَفْعًا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۗ لِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ ۚ إِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ فَلَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ﴿٤٩﴾
49. Sema: Siimilikii nafsi yangu dhara wala manufaa isipokuwa Aliyotaka Allaah. Kila ummah una muda maalumu. Utakapofika muda wao, basi hawatoweza kuakhirisha saa moja wala hawatoweza kutanguliza.
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُهُ بَيَاتًا أَوْ نَهَارًا مَّاذَا يَسْتَعْجِلُ مِنْهُ الْمُجْرِمُونَ﴿٥٠﴾
50. Sema: Mnaonaje ikikufikieni Adhabu Yake usiku au mchana, sehemu ipi wanaihimiza wahalifu?
أَثُمَّ إِذَا مَا وَقَعَ آمَنتُم بِهِ ۚ آلْآنَ وَقَدْ كُنتُم بِهِ تَسْتَعْجِلُونَ﴿٥١﴾
51. Kisha tena itakapotokea ndio mtaiamini? Je, sasa tena? Na ilhali mlikuwa mnaihimiza?
ثُمَّ قِيلَ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذُوقُوا عَذَابَ الْخُلْدِ هَلْ تُجْزَوْنَ إِلَّا بِمَا كُنتُمْ تَكْسِبُونَ﴿٥٢﴾
52. Kisha wataambiwa wale waliodhulumu: Onjeni adhabu ya kudumu milele. Kwani je, mtalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyachuma?
وَيَسْتَنبِئُونَكَ أَحَقٌّ هُوَ ۖ قُلْ إِي وَرَبِّي إِنَّهُ لَحَقٌّ ۖ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ﴿٥٣﴾
53. Na wanakuuliza: Je, hiyo (adhabu na Qiyaamah) ni kweli? Sema: Ndio! Naapa kwa Rabb wangu! Hakika hiyo bila shaka ni kweli! Nanyi si wenye kuweza kushinda (kuikwepa).
وَلَوْ أَنَّ لِكُلِّ نَفْسٍ ظَلَمَتْ مَا فِي الْأَرْضِ لَافْتَدَتْ بِهِ ۗ وَأَسَرُّوا النَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُا الْعَذَابَ ۖ وَقُضِيَ بَيْنَهُم بِالْقِسْطِ ۚ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿٥٤﴾
54. Na kama ingelikuwa kila nafsi iliyodhulumu, inamiliki yote yaliyomo katika ardhi, bila shaka ingeliyatolea fidia kwayo. Na wataficha (au watafichua) majuto watakapoona adhabu. Na itahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatodhulumiwa.
أَلَا إِنَّ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ أَلَا إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٥٥﴾
55. Tanabahi! Hakika ni vya Allaah vilivyomo katika mbingu na ardhi. Tanabahi! Hakika Ahadi ya Allaah ni kweli, lakini wengi wao hawajui.
هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٥٦﴾
56. Yeye Ndiye Anayehuisha na Anayefisha, na Kwake mtarejeshwa.
يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَشِفَاءٌ لِّمَا فِي الصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ﴿٥٧﴾
57. Enyi watu! Kwa yakini yamekujieni mawaidha kutoka kwa Rabb wenu, na shifaa ya yale yaliyomo vifuani, na mwongozo na rehma kwa Waumini.[16]
قُلْ بِفَضْلِ اللَّـهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ﴿٥٨﴾
58. Sema: Kwa Fadhila za Allaah na kwa Rehma Yake basi kwa hayo wafurahi. Hayo ni kheri kuliko wanayoyakusanya.[17]
قُلْ أَرَأَيْتُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ لَكُم مِّن رِّزْقٍ فَجَعَلْتُم مِّنْهُ حَرَامًا وَحَلَالًا قُلْ آللَّـهُ أَذِنَ لَكُمْ ۖ أَمْ عَلَى اللَّـهِ تَفْتَرُونَ﴿٥٩﴾
59. Sema: Mnaonaje zile riziki Alizokuteremshieni Allaah, kisha mkazifanya katika hizo ni haramu na halali. Sema: Je, Allaah Amekupeni idhini au mnamtungia (uongo) Allaah?
وَمَا ظَنُّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَشْكُرُونَ﴿٦٠﴾
60. Na nini dhana ya wale wanaomtungia Allaah uongo Siku ya Qiyaamah? Hakika Allaah bila shaka Ana Fadhila (nyingi) juu ya watu, lakini wengi wao hawashukuru.
وَمَا تَكُونُ فِي شَأْنٍ وَمَا تَتْلُو مِنْهُ مِن قُرْآنٍ وَلَا تَعْمَلُونَ مِنْ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيْكُمْ شُهُودًا إِذْ تُفِيضُونَ فِيهِ ۚ وَمَا يَعْزُبُ عَن رَّبِّكَ مِن مِّثْقَالِ ذَرَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ وَلَا أَصْغَرَ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرَ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ﴿٦١﴾
61. Na hushughuliki katika jambo lolote, wala husomi humo katika Qur-aan, wala hamtendi amali yoyote isipokuwa Tunakuwa Mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo. Na hakifichiki kwa Rabb wako hata cha uzito wa chembe (kama atomu) katika ardhi, wala mbinguni, wala kidogo kuliko hicho, wala kikubwa zaidi ya hicho, isipokuwa kimo katika Kitabu bainifu.[18]
أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٦٢﴾
62. Tanabahi! Hakika Vipenzi wa Allaah hawana khofu na wala hawatohuzunika.[19]
الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ﴿٦٣﴾
63. Ambao wameamini na wakawa wana taqwa.
لَهُمُ الْبُشْرَىٰ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۚ لَا تَبْدِيلَ لِكَلِمَاتِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٦٤﴾
64. Watapata bishara katika uhai wa dunia na katika Aakhirah. Hakuna mabadiliko katika Maneno ya Allaah. Huko ndiko kufuzu kukubwa mno.
وَلَا يَحْزُنكَ قَوْلُهُمْ ۘ إِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا ۚ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿٦٥﴾
65. Na wala maneno yao yasikuhuzunishe. Hakika taadhima zote ni za Allaah Pekee. Yeye Ndiye Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
أَلَا إِنَّ لِلَّـهِ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ ۗ وَمَا يَتَّبِعُ الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ شُرَكَاءَ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ﴿٦٦﴾
66. Tanabahi kwamba ni wa Allaah wote waliomo mbinguni na waliomo ardhini. Na hawafuati wale wanawaomba pasi na Allaah kuwa ni washirika (Wake). Hawafuati isipokuwa dhana, nao hawana isipokuwa wanabuni uongo.
هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَالنَّهَارَ مُبْصِرًا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ﴿٦٧﴾
67. Yeye Ndiye Aliyekufanyieni usiku ili mpate utulivu humo, na mchana kwa ajili ya kuonea. Hakika katika hayo zipo Aayaat (Ishara, Hoja, Dalili) kwa watu wanaosikia (wakazingatia).
قَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۖ هُوَ الْغَنِيُّ ۖ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ إِنْ عِندَكُم مِّن سُلْطَانٍ بِهَـٰذَا ۚ أَتَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ﴿٦٨﴾
68. Wanasema: Allaah Amejifanyia mwana![20] Subhaanah! (Utakasifu ni Wake) Yeye Ni Mkwasi. Ni Vyake vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Hamna nyinyi dalili kwa hayo. Je, mnasema juu ya Allaah msiyoyajua?
قُلْ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ﴿٦٩﴾
69. Sema: Hakika wale wanaomtungia uongo Allaah hawatofaulu.
مَتَاعٌ فِي الدُّنْيَا ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ ثُمَّ نُذِيقُهُمُ الْعَذَابَ الشَّدِيدَ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ﴿٧٠﴾
70. Starehe ya muda katika dunia, kisha Kwetu ndio marejeo yao, kisha Tutawaonjesha adhabu kali kwa sababu ya ukafiri wao.
وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ نُوحٍ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكُم مَّقَامِي وَتَذْكِيرِي بِآيَاتِ اللَّـهِ فَعَلَى اللَّـهِ تَوَكَّلْتُ فَأَجْمِعُوا أَمْرَكُمْ وَشُرَكَاءَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُنْ أَمْرُكُمْ عَلَيْكُمْ غُمَّةً ثُمَّ اقْضُوا إِلَيَّ وَلَا تُنظِرُونِ﴿٧١﴾
71. Na wasomee khabari ya Nuwh, alipoiambia kaumu yake: Enyi kaumu yangu! Ikiwa kukaa kwangu na kukumbusha kwangu Aayaat (Ishara, Hoja, Dalili) za Allaah kumekuwa ni mashaka juu yenu, basi kwa Allaah natawakali. Hivyo pangeni jambo lenu na washirika wenu (mnidhuru), kisha jambo lenu lisifichike kwenu, kisha nihukumuni (kwa adhabu) wala msinipe muhula.
فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَمَا سَأَلْتُكُم مِّنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴿٧٢﴾
72. Lakini mkikengeuka, basi sijakuombeni ujira wowote. Sitaki ujira isipokuwa kwa Allaah na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu.
فَكَذَّبُوهُ فَنَجَّيْنَاهُ وَمَن مَّعَهُ فِي الْفُلْكِ وَجَعَلْنَاهُمْ خَلَائِفَ وَأَغْرَقْنَا الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُنذَرِينَ﴿٧٣﴾
73. Lakini walimkadhibisha. Tukamuokoa (Nuwh) pamoja na waliokuwa naye katika jahazi, na Tukawafanya wao ndio waliobakia (warithi)[21] na Tukawagharikisha wale waliokadhibisha Aayaat (Ishara, Hoja, Dalili) Zetu. Basi tazama vipi ilikuwa khatima ya walioonywa.
ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَاءُوهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا بِمَا كَذَّبُوا بِهِ مِن قَبْلُ ۚ كَذَٰلِكَ نَطْبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِ الْمُعْتَدِينَ﴿٧٤﴾
74. Kisha Tukapeleka baada yake Rusuli kwa kaumu zao, wakawajia kwa hoja bayana, lakini hawakuwa wenye kuyaamini yale waliyoyakadhibisha zamani. Hivyo ndivyo Tunavyopiga chapa juu ya nyoyo za wenye kutaadi.
ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِم مُّوسَىٰ وَهَارُونَ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ بِآيَاتِنَا فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا مُّجْرِمِينَ﴿٧٥﴾
75. Kisha baada ya hao, Tukamtuma Muwsaa na Haaruwn kwa Firawni na wakuu wake kwa Aayaat (Miujiza, Ishara) Zetu, wakatakabari na wakawa watu wahalifu.
فَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا إِنَّ هَـٰذَا لَسِحْرٌ مُّبِينٌ﴿٧٦﴾
76. Ilipowajia haki kutoka Kwetu, walisema: Hii bila shaka ni sihiri bayana.
قَالَ مُوسَىٰ أَتَقُولُونَ لِلْحَقِّ لَمَّا جَاءَكُمْ ۖ أَسِحْرٌ هَـٰذَا وَلَا يُفْلِحُ السَّاحِرُونَ﴿٧٧﴾
77. Muwsaa akasema: Je, mnasema (ni sihiri bayana) haki ilipokujeni? Hii ni sihiri hii? Na wachawi hawafaulu.
قَالُوا أَجِئْتَنَا لِتَلْفِتَنَا عَمَّا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا وَتَكُونَ لَكُمَا الْكِبْرِيَاءُ فِي الْأَرْضِ وَمَا نَحْنُ لَكُمَا بِمُؤْمِنِينَ﴿٧٨﴾
78. Wakasema: Je, umetujia ili utugeuze tuyaache yale tuliyowakuta nayo baba zetu, na ili muwe nyinyi wawili na ukubwa na uadhama katika nchi? Na sisi hatutawaamini nyinyi.
وَقَالَ فِرْعَوْنُ ائْتُونِي بِكُلِّ سَاحِرٍ عَلِيمٍ﴿٧٩﴾
79. Na Firawni akasema: Nileteeni kila mchawi mjuzi.
فَلَمَّا جَاءَ السَّحَرَةُ قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ أَلْقُوا مَا أَنتُم مُّلْقُونَ﴿٨٠﴾
80. Walipokuja wachawi, Muwsaa akawaambia: Tupeni mnavyotaka kuvitupa.
فَلَمَّا أَلْقَوْا قَالَ مُوسَىٰ مَا جِئْتُم بِهِ السِّحْرُ ۖ إِنَّ اللَّـهَ سَيُبْطِلُهُ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُصْلِحُ عَمَلَ الْمُفْسِدِينَ﴿٨١﴾
81. Basi walipotupa, Muwsaa alisema: Mliyokuja nayo ni sihiri. Hakika Allaah Atayabatilisha. Hakika Allaah Hatengenezi amali za mafisadi.
وَيُحِقُّ اللَّـهُ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُجْرِمُونَ﴿٨٢﴾
82. Na Allaah Atathibitisha haki kwa Maneno Yake japokuwa watakirihika wahalifu.
فَمَا آمَنَ لِمُوسَىٰ إِلَّا ذُرِّيَّةٌ مِّن قَوْمِهِ عَلَىٰ خَوْفٍ مِّن فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِمْ أَن يَفْتِنَهُمْ ۚ وَإِنَّ فِرْعَوْنَ لَعَالٍ فِي الْأَرْضِ وَإِنَّهُ لَمِنَ الْمُسْرِفِينَ﴿٨٣﴾
83. Basi hawakumwamini Muwsaa isipokuwa vijana katika kaumu yake kwa sababu ya kumkhofu Firawni na wakuu wao wasiwatese. Na hakika Firawni ni jeuri katika ardhi, na hakika yeye bila shaka ni miongoni mwa wapindukao mipaka.
وَقَالَ مُوسَىٰ يَا قَوْمِ إِن كُنتُمْ آمَنتُم بِاللَّـهِ فَعَلَيْهِ تَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّسْلِمِينَ﴿٨٤﴾
84. Na Muwsaa akasema: Enyi kaumu yangu! Ikiwa mmemwamini Allaah, basi Kwake mtawakali, mkiwa ni Waislamu.
فَقَالُوا عَلَى اللَّـهِ تَوَكَّلْنَا رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ﴿٨٥﴾
85. Wakasema: Tumetawakali kwa Allaah. Ee Rabb wetu! Usitujaalie kuwa ni mtihani kwa watu madhalimu.
وَنَجِّنَا بِرَحْمَتِكَ مِنَ الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ﴿٨٦﴾
86. Na Tuokoe kwa Rehma Yako na watu makafiri.
وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ وَأَخِيهِ أَن تَبَوَّآ لِقَوْمِكُمَا بِمِصْرَ بُيُوتًا وَاجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ قِبْلَةً وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ﴿٨٧﴾
87. Na Tukamfunulia Wahy Muwsaa na kaka yake kwamba: Watengenezeeni watu wenu katika mji nyumba, na zifanyeni nyumba zenu sehemu za ibaada na simamisheni Swalaah. Na wabashirie Waumini.
وَقَالَ مُوسَىٰ رَبَّنَا إِنَّكَ آتَيْتَ فِرْعَوْنَ وَمَلَأَهُ زِينَةً وَأَمْوَالًا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا رَبَّنَا لِيُضِلُّوا عَن سَبِيلِكَ ۖ رَبَّنَا اطْمِسْ عَلَىٰ أَمْوَالِهِمْ وَاشْدُدْ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُوا حَتَّىٰ يَرَوُا الْعَذَابَ الْأَلِيمَ﴿٨٨﴾
88. Na Muwsaa akasema: Ee Rabb Wetu! Hakika Wewe Umempa Firawni na wakuu wake mapambo na mali katika uhai wa dunia. Ee Rabb wetu, ili wapoteze (watu) Njia Yako. Rabb wetu! Ziangamize mali zao na fanya nyoyo zao ziwe ngumu kwani hawatoamini mpaka waone adhabu iumizayo.
قَالَ قَدْ أُجِيبَت دَّعْوَتُكُمَا فَاسْتَقِيمَا وَلَا تَتَّبِعَانِّ سَبِيلَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ﴿٨٩﴾
89. (Allaah) Akasema: Imekwishaitikiwa duaa yenu nyinyi wawili, basi lingamaneni sawasawa na wala msifuate njia ya wale ambao hawajui.
وَجَاوَزْنَا بِبَنِي إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ وَجُنُودُهُ بَغْيًا وَعَدْوًا ۖ حَتَّىٰ إِذَا أَدْرَكَهُ الْغَرَقُ قَالَ آمَنتُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا الَّذِي آمَنَتْ بِهِ بَنُو إِسْرَائِيلَ وَأَنَا مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴿٩٠﴾
90. Tukawavukisha wana wa Israaiyl bahari. Basi Firawni akawafuata na jeshi lake kwa baghi[22] (dhulma) na uonevu mpaka ilipomfikia (Firawni) gharka akasema: Nimeamini kwamba hapana mwabudiwa wa haki, isipokuwa Yule waliyemwamini wana wa Israaiyl, na mimi ni miongoni mwa Waislamu.
آلْآنَ وَقَدْ عَصَيْتَ قَبْلُ وَكُنتَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ﴿٩١﴾
91. Sasa (ndio unaamini) na ihali umeasi kabla, na ulikuwa miongoni mwa mafisadi!?
فَالْيَوْمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ لِتَكُونَ لِمَنْ خَلْفَكَ آيَةً ۚ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ عَنْ آيَاتِنَا لَغَافِلُونَ﴿٩٢﴾
92. Basi leo Tunakuokoa kwa (kuuweka) mwili wako ili uwe Aayah (Ishara, Zingatio, Dalili) kwa watakaokuja nyuma yako. Na hakika watu wengi wameghafilika na Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu.
وَلَقَدْ بَوَّأْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ مُبَوَّأَ صِدْقٍ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ فَمَا اخْتَلَفُوا حَتَّىٰ جَاءَهُمُ الْعِلْمُ ۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ﴿٩٣﴾
93. Na kwa yakini Tuliwapa makazi wana wa Israaiyl; makazi mazuri, na Tukawaruzuku katika vizuri, na hawakukhitilafiana mpaka ilipowajia ilimu. Hakika Rabb wako Atahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah katika yale yote waliyokuwa wakikhitilafiana.
فَإِن كُنتَ فِي شَكٍّ مِّمَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ فَاسْأَلِ الَّذِينَ يَقْرَءُونَ الْكِتَابَ مِن قَبْلِكَ ۚ لَقَدْ جَاءَكَ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ﴿٩٤﴾
94. Na ukiwa una shaka (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika yale Tuliyokuteremshia, basi waulize wale wanaosoma Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekujia haki kutoka kwa Rabb wako, basi usijekuwa miongoni mwa wanaoshuku.[23]
وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ فَتَكُونَ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴿٩٥﴾
95. Wala usijekuwa miongoni mwa wale waliokadhibisha Aayaat (Ishara, Hoja, Dalili) za Allaah ukawa miongoni mwa waliokhasirika.
إِنَّ الَّذِينَ حَقَّتْ عَلَيْهِمْ كَلِمَتُ رَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ﴿٩٦﴾
96. Hakika wale ambao Neno la (ghadhabu la) Rabb wako limethibiti juu yao, hawataamini.
وَلَوْ جَاءَتْهُمْ كُلُّ آيَةٍ حَتَّىٰ يَرَوُا الْعَذَابَ الْأَلِيمَ﴿٩٧﴾
97. Japokuwa itawajia kila Aayah (Ishara, Dalili, Mawaidha) mpaka waone adhabu iumizayo.
فَلَوْلَا كَانَتْ قَرْيَةٌ آمَنَتْ فَنَفَعَهَا إِيمَانُهَا إِلَّا قَوْمَ يُونُسَ لَمَّا آمَنُوا كَشَفْنَا عَنْهُمْ عَذَابَ الْخِزْيِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَتَّعْنَاهُمْ إِلَىٰ حِينٍ﴿٩٨﴾
98. Basi kwa nini usiweko mji mmoja ukaamini na imaan yake ikawafaa - (haukutokea) isipokuwa kaumu ya Yuwnus. Walipoamini, Tuliwaondoshea adhabu ya hizaya duniani, na Tukawasterehesha mpaka muda maalumu.[24]
وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَآمَنَ مَن فِي الْأَرْضِ كُلُّهُمْ جَمِيعًا ۚ أَفَأَنتَ تُكْرِهُ النَّاسَ حَتَّىٰ يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ﴿٩٩﴾
99. Na kama Angetaka Rabb wako, basi wangeliamini wote pamoja walioko katika ardhi. Je, basi wewe (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) utashurutisha watu mpaka wawe Waumini?
وَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَن تُؤْمِنَ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَيَجْعَلُ الرِّجْسَ عَلَى الَّذِينَ لَا يَعْقِلُونَ﴿١٠٠﴾
100. Na haiwezekani nafsi yoyote ikaamini isipokuwa kwa Idhini ya Allaah. Naye Hujaalia adhabu (na upotofu) kwa wale wasiotia akilini.
قُلِ انظُرُوا مَاذَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَا تُغْنِي الْآيَاتُ وَالنُّذُرُ عَن قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ﴿١٠١﴾
101. Sema: Tazameni yaliyoko mbinguni na ardhini. Lakini Aayaat (Ishara, Dalili) zote na maonyo (ya Rusuli) hayawafai kitu watu wasioamini.
فَهَلْ يَنتَظِرُونَ إِلَّا مِثْلَ أَيَّامِ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِهِمْ ۚ قُلْ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ﴿١٠٢﴾
102. Je, wanangojea jingine (la maangamizi) isipokuwa mfano wa siku za wale waliopita kabla yao? Sema: Basi ngojeeni, hakika mimi ni pamoja nanyi miongoni mwa wanaongojea.
ثُمَّ نُنَجِّي رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا ۚ كَذَٰلِكَ حَقًّا عَلَيْنَا نُنجِ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٠٣﴾
103. Kisha Tunawaokoa Rusuli Wetu na wale walioamini. Hivyo ndivyo haki Kwetu kuwaokoa Waumini.
قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِن كُنتُمْ فِي شَكٍّ مِّن دِينِي فَلَا أَعْبُدُ الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِنْ أَعْبُدُ اللَّـهَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُمْ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٠٤﴾
104. Sema (Ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Enyi watu! Ikiwa mna shaka na Dini yangu, basi mimi siabudu ambavyo mnaviabudu badala ya Allaah, lakini namwabudu Allaah Ambaye Anakufisheni. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waumini.
وَأَنْ أَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١٠٥﴾
105. Na elekeza uso wako kwa Dini (ya Allaah), usimili kwengine na wala usijekuwa miongoni mwa washirikina.
وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ ۖ فَإِن فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذًا مِّنَ الظَّالِمِينَ﴿١٠٦﴾
106. Na wala usiombe badala ya Allaah visivyokufaa wala visivyokudhuru. Na ukifanya, basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu.
وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّـهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يُرِدْكَ بِخَيْرٍ فَلَا رَادَّ لِفَضْلِهِ ۚ يُصِيبُ بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚ وَهُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿١٠٧﴾
107. Na Allaah Akikugusisha dhara, basi hakuna wa kuiondosha isipokuwa Yeye. Na Akikutakia kheri, basi hakuna wa kurudisha Fadhila Zake. Humfikishia (Fadhila Yake) Amtakaye katika Waja Wake. Naye Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُمُ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَنِ اهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِي لِنَفْسِهِ ۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَا ۖ وَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِوَكِيلٍ﴿١٠٨﴾
108. Sema: Enyi watu! Kwa yakini imekujieni haki kutoka kwa Rabb wenu. Basi atakayehidika, hakika anahidika kwa faida ya nafsi yake. Na atakayepotoka, hakika anapotoka kwa hasara ya nafsi yake. Nami si mdhamini wenu.
وَاتَّبِعْ مَا يُوحَىٰ إِلَيْكَ وَاصْبِرْ حَتَّىٰ يَحْكُمَ اللَّـهُ ۚ وَهُوَ خَيْرُ الْحَاكِمِينَ﴿١٠٩﴾
109. Na fuata (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) yale uliyofunuliwa Wahy, na subiri mpaka Allaah Ahukumu. Naye Ni Mbora wa wanaohukumu.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Sababu Ya Kutarjumi “Hizi” Badala Ya “Hizo” Kulingana Na Neno تِلْكَ:
Rejea Al-Baqarah (2:2). Na Suwrat Yuwsuf (12:1), Ar-Ra’ad (13:1), Al-Hijr (15:1), An-Naml (27:1), na Luqmaan (31:2), Suwrah zote zimeanzia kama hivyo.
[3] Istawaa اسْتَوَى
Yuko juu kwa namna inayolingana na Uadhama na Ujalali Wake Yeye Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-A'raaf (7:54) kwenye maelezo bayana ya maana yake, yenye kutofautiana na maana ya katika Suwrah Al-Baqarah (2:29) na Suwrat Fusswilat (41:11).
[4] Takdiri (Qudura, Uwezo, Ukadiriaji) Wa Allaah (عزّ وجلّ) Katika Uumbaji Na Uendeshaji Wa Ulimwengu:
Aayah inayofuatia pia inahusiana uumbaji wa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Yaasiyn (36:38) kwenye maelezo yenye faida tele.
[5] Hali Ya Binaadam Asiyekuwa Muumini Anapopatwa Dhara:
Rejea pia Huwd (11:10-11), Al-Israa (17:83), Ar-Ruwm (30:33), Az-Zumar (39:49), Fusw-Swilat (41:49) (41:51).
Muumini hapaswi kuwa katika hali hiyo ilivyotajwa katika Aayah tukufu kwamba awe mwenye kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kumwabudu na kumnyenyekea na kumuomba duaa tele wakati anapopatwa dhara. Na pindi anapoondoshewa dhara hizo, basi humsahau Allaah (سبحانه وتعالى)! Ametufunza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth ifuatayo:
عن ابنِ عباسٍ رضي الله عنهما، قَالَ: كنت خلف النَّبيّ صلى الله عليه وسلم يومًا، فَقَالَ: يَا غُلامُ، إنِّي أعلّمُكَ كَلِمَاتٍ: احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ تُجَاهَكَ، إِذَا سَألْتَ فَاسأَلِ الله، وإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ باللهِ. وَاعْلَمْ: أنَّ الأُمَّةَ لَوْ اجْتَمَعَتْ عَلَى أنْ يَنْفَعُوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبهُ اللهُ لَكَ، وَإِن اجتَمَعُوا عَلَى أنْ يَضُرُّوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَضُرُّوكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللهُ عَلَيْكَ، رُفِعَتِ الأَقْلاَمُ وَجَفَّتِ الصُّحفُ . رواه الترمذي، وَقالَ: حديث حسن صحيح
Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Siku moja nilikuwa nyuma ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) [juu ya mnyama]. Akaniambia: “Ee kijana! Mimi nitakufundisha maneno: Mhifadhi Allaah Naye Atakuhifadhi. Mhifadhi Allaah utamkuta yupo mbele yako. Unapoomba, muombe Allaah. Unapotaka msaada, mtake Allaah. Fahamu kuwa, lau ummah (wote) utajikusanya ili wakunufaishe kwa jambo, basi hawataweza kukunufaisha ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah. Na wakijumuika ili wakudhuru kwa jambo, hawataweza kukudhuru ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah. Kalamu zimeshasimama na karatasi zimeshakauka.” [At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyh]
وفي رواية غيرِ الترمذي: احْفَظِ الله تَجِدْهُ أَمَامَكَ، تَعرَّفْ إِلَى اللهِ في الرَّخَاءِ يَعْرِفكَ في الشِّدَّةِ، وَاعْلَمْ: أنَّ مَا أَخْطَأكَ لَمْ يَكُنْ لِيُصِيبكَ، وَمَا أصَابَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُخْطِئَكَ، وَاعْلَمْ: أنَّ النَّصْرَ مَعَ الصَّبْرِ، وَأَنَّ الفَرَجَ مَعَ الكَرْبِ، وَأَنَّ مَعَ العُسْرِ يُسْرًا
Riwaayah nyingine isiyokuwa ya At-Tirmidhiy imesema:
“Mhifadhi Allaah utamkuta Yupo mbele yako. Mjue Allaah katika raha Naye Atakujua katika shida. Ujue kuwa, lililokukosa halikuwa ni lenye kukupata, na lililokusibu halikuwa ni lenye kukukosa. Ujue kuwa nusura ipo pamoja na subira, faraja ipo pamoja na dhiki, na kwenye uzito kuna wepesi.”
Basi Muumini anapaswa kumshukuru Rabb wake katika hali yoyote ile. Na hilo ni jambo la jaabu kwa Muumini wa kweli kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
وعن أبي يحيى صهيب بن سنانٍ رضي الله عنه، قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: عَجَبًا لأمْرِ المُؤمنِ إنَّ أمْرَهُ كُلَّهُ لَهُ خيرٌ ولَيسَ ذلِكَ لأَحَدٍ إلا للمُؤْمِن: إنْ أَصَابَتْهُ سَرَّاءُ شَكَرَ فَكانَ خَيرًا لَهُ، وإنْ أصَابَتْهُ ضرَاءُ صَبَرَ فَكانَ خَيْرًا لَهُ رواه مسلم
Amesimulia Abuu Yahyaa Swuhayb (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ajabu ya hali ya Muumini kuwa mambo yake yote ni kheri. Na haiwi hivyo (sifa hiyo) kwa yeyote ila kwa Muumini. Anapofikwa na furaha hushukuru na huwa kheri kwake, na anapofikwa na matatizo husubiri na huwa ni kheri kwake.” [Muslim]
[6] Shirki Za Washirikina Wa Zama Hizi Ni Kubwa Zaidi Kuliko Za Washirikina Wa Awali:
Rejea pia Al-Israa (17:67), Al-‘Ankabuwt (29:65), na Luqmaan (31:32) ambako Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja hali kama hiyo ya washirikina. Washirikina wa zamani walikuwa wakimshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) katika hali za raha. Lakini wanapokumbwa na shida kama hiyo ya bahari kuchafuka, wakapatwa na hofu kubwa ya kuangamia na kughariki, hapo walikuwa hawaombi miungu au washirika wao, bali walimuomba Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee na kuelekea Kwake.
Ama washirikina wa zama hizi, hawa shirki zao hazina tofauti katika hali zao za raha au za shida. Kuna wanaowaomba wafu katika makaburi daima dawamu, ni sawa iwe katika hali ya raha au ya dhiki. Pia utakuta hata maskini au fakiri akipatwa na mtihani akawa katika dhiki kubwa, anamwendea mganga, au mtabiri, au hata mchawi ili amwondolee hali yake hiyo wakati mganga mwenyewe hawezi kujiondoshea matatizo aliyonayo. Hivyo watu hawa, shirki zao ni za kudumu nyakati zote. Imaam Muhammad Bin ‘Abdil-Wahhaab (رحمه الله) amesema: “Washirikina wa zama zetu ni waovu zaidi katika shirki zao kuliko washirikina wa zamani kwa sababu, wa zamani walimshirikisha Allaah katika raha, lakini walitakasa (ibaada zao) wakati wa shida. Ama washirikina wa sasa, shirki zao ni za kuendelea daima wakiwa katika raha au katika shida. [Kanuni Ya Nne -Al-Qawaaid Al-Arba’]
[8] Waumini Watamuona Allaah (عزّ وجلّ) Katika Jannah (Pepo):
Kumuona Allaah (عزّ وجلّ) Peponi ni katika ‘Aqiydah ya Ahlus-Sunnah Wal Jamaa’ah ambayo baadhi ya makundi potofu hawaiamini ilhali dalili zake zimethibiti katika Qur-aan na Sunnah. Rejea Suwrah Al-Qiyaamah (75:22-23). Rejea Al-Mutwaffifiyn (83:15). Na katika Sunnah ni Hadiyth ifuatayo:
عَنْ صُهَيْبٍ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي قَوْلِه: لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَى وَزِيَادَةٌ قَالَ " إِذَا دَخَلَ أَهْلُ الْجَنَّةِ الْجَنَّةَ نَادَى مُنَادٍ إِنَّ لَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ مَوْعِدًا يُرِيدُ أَنْ يُنْجِزَكُمُوهُ قَالُوا أَلَمْ تُبَيِّضْ وُجُوهَنَا وَتُنَجِّنَا مِنَ النَّارِ وَتُدْخِلْنَا الْجَنَّةَ قَالَ فَيُكْشَفُ الْحِجَابُ . قَالَ فَوَاللَّهِ مَا أَعْطَاهُمُ اللَّهُ شَيْئًا أَحَبَّ إِلَيْهِمْ مِنَ النَّظَرِ إِلَيْهِ
Amesimulia Swuhayb (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ
“Kwa wale waliofanya ihsaan watapata (huko Jannah) jazaa nzuri kabisa na ziada (kumuona Allaah).” [Yuwnus (10:26)]
“Watakapoingia Watu wa Jannah katika Jannah, wataitwa: Enyi Watu wa Jannah! Hakika nyinyi mna ahadi (kwa Allaah) na Anataka Kuitimiza. Watauliza: (Ni ahadi ipi hiyo?) Kwani Hukuzing’arisha nyuso zetu, na Hukutuokoa na moto, na Hukutuingiza Jannah?” Akasema: “Litaondoshwa pazia. (Na watamtazama Allaah) Akasema: Basi Wa-Allaahi, Hakuwahi Allaah kuwapa jambo walilolipenda zaidi kuliko hilo (kumuona Allaah).” [At-Tirmidhiy, Na riwaayah nyenginezo kama hiyo zimepokelewa na Imaam Muslim, Ibn Maajah]
[9] Nyuso Za Waumini Zitang’ara Siku Ya Qiyaamah:
Rejea ‘Abasa (80:38) kwenye kubainisha hali za nyuso za Waumini na makafiri zitakavyokuwa Siku ya Qiyaamah.
[10] Kila Nafsi Itatiwa Mtihanini:
Kila nafsi itatahiniwa kwa kuhesabiwa amali alizotenda mtu duniani; ikiwa ni za kheri alipwe kheri, na ikiwa ni uovu alipwe maovu. Amali hizo ambazo zimerekodiwa katika Sahifa ya kila mtu, hakuna hata chembe ya atomu itakayokosekana kurekodiwa ndani yake. Rejea Az-Zalzalah (99:6-8), Fus-swilat (41:20-22), Yaasiyn (36:12) (36:65), An-Nuwr (24:24), Al-Israa (17:13-14), Al-Infitwaar (82:10-12), Qaaf (50:18), Ghaafir (40:16-17), na Al-Anbiyaa (21:47).
[11] Mawlaa "مَوْلَى": Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Na Sifa Zake.
[12] Washirikina Waliamini Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah Lakini Walikanusha Tawhiyd Al-Uluwhiyyah:
Imaam Muhammad Bin ‘Abdil-Wahhaab (رحمه الله) ametaja katika Al-Qawaaid Al-Arba’ kwamba Aayah hii na nyenginezo; Rejea Al-‘Ankabuwt (29:61) kwenye faida ziyada. Rejea pia (29:63), Luqmaan (31:25), Az-Zumar (39:38), na Az-Zukhruf (43:9) (43:87), ni dalili kuwa washirikina waliamini Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah (Kumpwekesha Allaah katika Uola Wake) kwamba Yeye ni Rabb Aliyewaumba, na Aliyeumba mbingu na ardhi, na Anayewaruzuku, na Anayewaendeshea mambo yao yote. Lakini ushirikina wao umekuja katika kutokumpwekesha Allaah (سبحانه وتعالى) katika Tawhiyd ya Uluwhiyyah (Kumpwekesha Allaah katika ibaada) walipowaabudu masanamu kwa kuwaelekezea ibaada zao.
[14] Changamoto Kwa Makafiri Walete Mfano Wa Qur-aan Lakini Kamwe Hakuna Awezaye!:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anatoa changamoto kama hii na Anatoa changamoto na vitisho kwa kiumbe yoyote yule kati ya majini na wanaadam kwamba ikiwa hawamwamini, basi walete mfano wa Qur-aan, lakini hakuna awezaye! Rejea Al-Israa (17:88), Al-Baqarah (2:23-24), Huwd (11:13-14), na At-Twuwr (52:33-34). Watu walijaribu, lakini walishindwa! Mmoja wao ni Musaylamah Al-kadh-dhaab (mrongo) aliyedai kuwa amepewa Unabii baada ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Rejea Al-An’aam (6:93) kwenye Hadiyth inayowataja waongo hao.
[15] Ada Ya Makafiri Kuuliza Lini Adhabu Itawafikia Au Lini Qiyaamah Kitatokea:
Aayah hii hadi Aayah (10:54), Allaah (سبحانه وتعالى) Anawahakikishia makafiri kwamba Atawateremshia adhabu na Atakisimamisha Qiyaamah, na hapo watataka kuamini, lakini imaan zao hazitawafaa lolote, na majuto yatakuwa ni yao kwa kutokuamini! Rejea: Al-Hajj (22:47), Al-Anbiyaa (21:38-40), An-Naml (27:71-72), Saba-a (34:29-30), Yaasiyn (36:48-54), na Al-Mulk (67:25-28).
[16] Qur-aan Ni Shifaa (Poza, Tiba), Mawaidha, Mwongozo Na Rehma:
Rejea Al-Israa (17:82) na Fusw-Swilat (41:44) kwenye uchambuzi na faida kadhaa.
[17] Fadhila Za Allaah Na Rehma Yake:
Fadhila ya Allaah ni Qur-aan ambayo ni neema kubwa kabisa. Rehma Yake ni Dini ya haki, mwongozo na imaan, kumwabudu Allaah kwa mapenzi, na kumtambua (kwa Majina na Sifa Zake). Basi hayo wayafurahie, kwa sababu hayo ni kheri (na bora) kuliko wanayoyakusanya katika mapambo, mafao na anasa za dunia. [Imaam As-Sa’diy]
[18] Hakuna Kinachofichika Kwa Allaah (سبحانه وتعالى); Kiwe Cha Dhahiri Wala Cha Siri, Kikubwa Wala Kidogo Vipi:
Rejea Al-An’aam (6:59). Na rejea pia Ghaafir (40:19) kwenye maelezo na rejea mbalimbali. Na pia Luqmaan (31:16).
[19] Awliyaa (Vipenzi) Wa Allaah (عزّ وجلّ):
Aayah tukufu imetaja sifa mbili kwa Muislamu zinazomfanya kuwa yeye ni Kipenzi cha Allaah. Sifa hizo ni imaan na taqwa. Na zote mbili zinapatikana moyoni. Rejea Al-Baqarah (2:2) kupata maana ya taqwa. Na Vipenzi wa Allaah (عزّ وجلّ) ni kuanzia Manabii Wake wote, Swahaba (رضي الله عنهم), Shuhadaa, na Swalihina wote wengineo ambao Allaah (سبحانه وتعالى) Amewaridhia. Hadiyth nyingi zimetaja Waumini wenye kupendwa na Allaah (سبحانه وتعالى). Hadiyth hizo zinataja amali zao watendazo, sifa zao na fadhila zao. Miongoni mwazo ni:
1-Wenye Kutenda Amali Zaidi Ya Alizofaridhisha Allaah (سبحانه وتعالى):
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: إِنَّ اللَّهَ قَال:َ مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ، وَمَا تَقَرَّبَ إِلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إِلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُ عَلَيْهِ، وَمَا يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إِلَيَّ بِالنَّوَافِلِ حَتَّى أُحِبَّهُ، فَإِذَا أَحْبَبْتُهُ كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ، وَيَدَهُ الَّتِي يَبْطِشُ بِهَا، وَرِجْلَهُ الَّتِي يَمْشِي بِهَا، وَإِنْ سَأَلَنِي لَأُعْطِيَنَّهُ، وَلَئِنْ اسْتَعَاذَنِي لَأُعِيذَنَّهُ البخاري
Amesimulia Abu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah (سبحانه وتعالى) Amesema: Atakayemfanyia uadui Kipenzi Changu, basi Ninatangaza vita dhidi yake. Mja Wangu hanikaribii na kitu chochote Ninachokipenda zaidi kama amali Nilizomfaridhishia. Na haachi Mja Wangu kuwa anajikurubisha Kwangu kwa amali za Sunnah mpaka Napata Kumpenda. Ninapompenda, basi Mimi Huwa masikio yake yanayosikilizia, macho yake anayoonea, mikono yake anayonyoshea, na miguu yake anayotembelea nayo. Na kama ataniomba, kwa hakika Nitampa, na kama ataniomba kinga, kwa hakika Nitamlinda.” [Al-Bukhaariy]
Pia,
2-Wenye Kushikamana Na Qur-aan Kwa Kuisoma, Kuihifadhi, Na Kufuata Maamrisho Yake:
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ لِلَّهِ أَهْلِينَ مِنْ النَّاسِ)) قَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ مَنْ هُمْ قَالَ: ((هُمْ أَهْلُ الْقُرْآنِ أَهْلُ اللَّهِ وَخَاصَّتُهُ)) أحمد و إبن ماجه
Amesimulia Anas bin Maalik (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah Anao watu wake maalum kati ya wanaadam.” Wakamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah ni nani hao? Akasema: “Hao ni watu wa Qur-aan (wenye kuifanyia kazi), hao ndio Watu wa Allaah na Wateule Wake.” [Ahmad, Ibn Maajah]
[20] Kumsingizia Allaah Kuwa Ana Mwana:
Rejea Al-Maaidah (5:17), (72-76), (116-118), Maryam (19:88), na At-Tawbah (9:30-31).
[21] Nabiy Nuwh (عليه السّلام) Na Kizazi Kilobakia, Naye Ni Rasuli Wa Kwanza Ardhini, Na Ni Baba Wa Wanaadam Baada Ya Nabiy Aadam (عليه السّلام):
Rejea Asw-Swaaffaat (37:77) kwenye maelezo bayana na rejea zake mbalimbali.
Rejea pia Rejea Huwd (11:40), Maryam (19:58), Al-Muuminuwn (23:27), Nuwh (71:1), Al-Israa (17:3).
[22] Maana Ya Baghyun/Baghaa Katika Qur-aan:
Rejea Ash-Shuwraa (42:14) kupata maana zake mbalimbali.
[23] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Hakuwa Na Shaka Kamwe Wala Hakukadhibisha Aayaat Za Allaah (سبحانه وتعالى):
Aayah Hii Na Ifuatayo Yuwnus (10:94-95), Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) hakutilia shaka lolote Aliloteremshiwa na Allaah (سبحانه وتعالى), bali yeye alikuwa ni mwenye yaqini kabisa. Hili linathibitishwa kwa Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ ۚ ﴾
“Rasuli ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Rabb wake na Waumini (pia).” [Al-Baqarah (2:285)]
Qataadah, Ibn ‘Abbaas, Sa’iyd bin Jubayr, Hasan Al-Baswiry wamesema kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakutia shaka wala hakuuliza lolote (katika Wahy). [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Kauli Yake hiyo Allaah (سبحانه وتعالى) kumwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
فَإِن كُنتَ فِي شَكٍّ
“Ukiwa una shaka…”
Ni katika njia Anazozitumia Allaah (سبحانه وتعالى) kuelekeza maswali kama hayo kwa makafiri kama vile Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
قُلْ إِن كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدٌ فَأَنَا أَوَّلُ الْعَابِدِينَ﴿٨١﴾
“Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Kama ingelikuwa Ar-Rahmaan Ana mwana (kama mnavyodai), basi mimi ningekuwa wa mwanzo katika waja (Wake).” [Az-Zukhfur (43:81)]
Ufafanuzi wa:
فَأَنَا أَوَّلُ الْعَابِدِينَ
“Basi mimi ningekuwa wa mwanzo katika waja (Wake):
Ina maana: Ningekuwa wa mwanzo wa wanaokanusha madai yenu, na wa mwanzo kuamini kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Hana mwana. Kwa sababu inajulikana wazi kuwa washirikina wa Makkah walimzulia Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa Malaika ni watoto Wake wa kike. Na Mayahudi wakamzulia kuwa ‘Uzayr ni mwana wa Allaah. Na Manaswara wakamzulia kuwa Nabiy ‘Iysaa ni mwana wa Allaah. Basi ndio maana hapa Allaah (سبحانه وتعالى) Anamwambia Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم): “Sema…..” lakini swali hilo hakika ni kuligeuza kwa Manaswara. Na kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Anathibitisha kwa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم):
لَقَدْ جَاءَكَ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ﴿٩٤﴾
“Kwa yakini imekujia haki kutoka kwa Rabb wako, basi usijekuwa miongoni mwa wanaoshuku.” [Yuwnus (10:94)]
Na Aayah hizi mbili na nyenginezo kama hizi makafiri huzichukulia hoja kutaka kuipotosha Qur-aan na kutaka kuitia upogo Risala ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ametilia shaka Wahy alioteremshiwa, na kwamba alikadhibisha Aayah Za Allaah (سبحانه وتعالى) na madai yao mengineyo. Lakini uhakika ni kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Anazielekezea kwa makafiri. ‘Ulamaa wameelezea mengi na kufafanua kwa upana Aayah kama hizi.
[24] Kaumu Ya Nabiy Yuwnus (عليه السّلام) Hawakuteremshiwa Adhabu:
Imaan haikuwafaa watu wa mji wowote walioamini walipoishuhudia adhabu isipokuwa watu wa mji wa Yuwnus mwana wa Mattaa. Kwani wao walipohakikisha kwamba adhabu ni yenye kuwashukia, walirejea kwa Allaah kwa kutubia kidhati, na ulipofunuka ukweli wa tawbah yao, Allaah Aliwaondolea adhabu ya hizaya baada ya kuwa karibu na wao, na Akawaacha ulimwenguni wakisterehe mpaka muda wao wa kuishi kukoma. [Tafsiyr Al-Muyassar]
هُود
011-Huwd
011-Huwd: Utangulizi Wa Suwrah [145]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الر ۚ كِتَابٌ أُحْكِمَتْ آيَاتُهُ ثُمَّ فُصِّلَتْ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ خَبِيرٍ﴿١﴾
1. Alif Laam Raa.[1] Kitabu ambacho Aayaat Zake zimetimizwa barabara, kisha zikafasiliwa waziwazi kutoka kwa Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ ۚ إِنَّنِي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ﴿٢﴾
2. Kwamba: Msiabudu isipokuwa Allaah. Hakika mimi (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ni mwonyaji kwenu na mbashiriaji.
وَأَنِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُمَتِّعْكُم مَّتَاعًا حَسَنًا إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى وَيُؤْتِ كُلَّ ذِي فَضْلٍ فَضْلَهُ ۖ وَإِن تَوَلَّوْا فَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ كَبِيرٍ﴿٣﴾
3. Na kwamba: Mwombeni Rabb wenu maghfirah kisha tubuni Kwake, Atakustarehesheni starehe nzuri mpaka muda maalumu uliokadiriwa, na Atampa kila mwenye fadhila (amali njema), Fadhila Zake (malipo yake).[2] Na mkikengeuka, basi hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku Kubwa.
إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٤﴾
4. Kwa Allaah ni marejeo yenu. Naye juu ya kila kitu Ni Muweza.
أَلَا إِنَّهُمْ يَثْنُونَ صُدُورَهُمْ لِيَسْتَخْفُوا مِنْهُ ۚ أَلَا حِينَ يَسْتَغْشُونَ ثِيَابَهُمْ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ۚ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ﴿٥﴾
5. Tanabahi! Hakika wao wanainamisha vifua[3] vyao ili wamfiche (Allaah). Tanabahi! Wanapojigubika nguo zao, Anajua wanayoyafanya siri na wanayoyatangaza. Hakika Yeye Ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.[4]
وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ رِزْقُهَا وَيَعْلَمُ مُسْتَقَرَّهَا وَمُسْتَوْدَعَهَا ۚ كُلٌّ فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ﴿٦﴾
6. Na hakuna kiumbe chochote kitembeacho katika ardhi isipokuwa riziki yake iko kwa Allaah, na (Allaah) Anajua mahali pake pa kustakiri na pa kuhifadhiwa kwake. Yote yamo katika Kitabu kinachobainisha.
وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَكَانَ عَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ۗ وَلَئِن قُلْتَ إِنَّكُم مَّبْعُوثُونَ مِن بَعْدِ الْمَوْتِ لَيَقُولَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ﴿٧﴾
7. Na Yeye Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita, na ‘Arshi Yake ilikuwa juu ya maji[5], (kakuumbeni) ili Akujaribuni nani kati yenu mwenye amali nzuri zaidi. Na kama ukisema: Nyinyi mtafufuliwa baada ya mauti, wale waliokufuru bila shaka watasema: Hakika haya si chochote isipokuwa ni sihiri bayana.
وَلَئِنْ أَخَّرْنَا عَنْهُمُ الْعَذَابَ إِلَىٰ أُمَّةٍ مَّعْدُودَةٍ لَّيَقُولُنَّ مَا يَحْبِسُهُ ۗ أَلَا يَوْمَ يَأْتِيهِمْ لَيْسَ مَصْرُوفًا عَنْهُمْ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٨﴾
8. Na kama Tukiwaakhirishia adhabu mpaka muda[6] uliokwishahesabiwa, bila shaka watasema: Ni nini kinachoizuia? Tanabahi! Siku itakayowafikia haitaondoshwa kwao, na yatawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.
وَلَئِنْ أَذَقْنَا الْإِنسَانَ مِنَّا رَحْمَةً ثُمَّ نَزَعْنَاهَا مِنْهُ إِنَّهُ لَيَئُوسٌ كَفُورٌ﴿٩﴾
9. Na Tunapomuonjesha binaadam Rehma kutoka Kwetu, kisha Tukamuondolea, hakika yeye huwa ni mwenye kukata tamaa sana asiye na shukurani.[7]
وَلَئِنْ أَذَقْنَاهُ نَعْمَاءَ بَعْدَ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ ذَهَبَ السَّيِّئَاتُ عَنِّي ۚ إِنَّهُ لَفَرِحٌ فَخُورٌ﴿١٠﴾
10. Na Tunapomuonjesha neema baada ya dhara iliyomgusa, bila shaka husema: Maovu yemeniondokea. Hakika yeye ni mwenye kufurahi sana kwa kujigamba na kujifaharisha.[8]
إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ﴿١١﴾
11. Isipokuwa wale waliosubiri na wakatenda mema hao watapata maghfirah na ujira mkubwa.
فَلَعَلَّكَ تَارِكٌ بَعْضَ مَا يُوحَىٰ إِلَيْكَ وَضَائِقٌ بِهِ صَدْرُكَ أَن يَقُولُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ كَنزٌ أَوْ جَاءَ مَعَهُ مَلَكٌ ۚ إِنَّمَا أَنتَ نَذِيرٌ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ﴿١٢﴾
12. Basi labda wewe utaacha baadhi ya yale uliyofunuliwa Wahy na kifua chako kitaona dhiki kwa hayo kwa sababu wanasema: Mbona hakuteremshiwa hazina au hakuja pamoja naye Malaika? Hakika wewe ni mwonyaji tu, na Allaah Ni Mtegemewa wa kila kitu.
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا بِعَشْرِ سُوَرٍ مِّثْلِهِ مُفْتَرَيَاتٍ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿١٣﴾
13. Je, wanasema ameitunga (hii Qur-aan)? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Leteni Suwrah kumi mfano wake zilizotungwa, na iteni muwawezao (wakusaidieni) pasina Allaah mkiwa ni wakweli.[9]
فَإِلَّمْ يَسْتَجِيبُوا لَكُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا أُنزِلَ بِعِلْمِ اللَّـهِ وَأَن لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ﴿١٤﴾
14. Wasipokujibuni, basi jueni kwamba hakika (hii Qur-aan) imeteremshwa kwa Ujuzi wa Allaah, na kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Basi je, nyinyi mtakubali kuwa Waislamu?
مَن كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لَا يُبْخَسُونَ﴿١٥﴾
15. Anayetaka uhai wa dunia na mapambo yake Tutawalipa kikamilifu amali zao humo, nao hawatopunjwa humo.[10]
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ إِلَّا النَّارُ ۖ وَحَبِطَ مَا صَنَعُوا فِيهَا وَبَاطِلٌ مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٦﴾
16. Hao ndio wale ambao hawatokuwa na chochote katika Aakhirah isipokuwa moto. Na yataporomoka yale waliyoyafanya humo (duniani), na yatabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.
أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّهِ وَيَتْلُوهُ شَاهِدٌ مِّنْهُ وَمِن قَبْلِهِ كِتَابُ مُوسَىٰ إِمَامًا وَرَحْمَةً ۚ أُولَـٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۚ وَمَن يَكْفُرْ بِهِ مِنَ الْأَحْزَابِ فَالنَّارُ مَوْعِدُهُ ۚ فَلَا تَكُ فِي مِرْيَةٍ مِّنْهُ ۚ إِنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ﴿١٧﴾
17. Je, basi yule aliye na hoja bayana kutoka kwa Rabb wake, na akafuatiwa na Shahidi[11] kutoka Kwake, na kabla yake (kilikuwa) Kitabu cha Muwsaa kilichokuwa kiongozi na rehma (je, huyo ni sawa na aliye kwenye giza la ukafiri?). Hao ndio wanaoiamini (Qur-aan). Na atakayeikanusha kati ya makundi, basi moto ndio mahali pa miadi yake. Basi usiwe katika shaka nacho. Hakika hiyo ni haki kutoka kwa Rabb wako, lakini watu wengi hawaamini.
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا ۚ أُولَـٰئِكَ يُعْرَضُونَ عَلَىٰ رَبِّهِمْ وَيَقُولُ الْأَشْهَادُ هَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ كَذَبُوا عَلَىٰ رَبِّهِمْ ۚ أَلَا لَعْنَةُ اللَّـهِ عَلَى الظَّالِمِينَ﴿١٨﴾
18. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia uongo Allaah? Hao watahudhurishwa mbele ya Rabb wao, na mashahidi watasema: Hawa ndio wale waliomzulia uongo Rabb wao! Tanabahi! Laana ya Allaah iko juu ya waliodhulumu.
الَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ﴿١٩﴾
19. Wale wanaozuia Njia ya Allaah na wanaitafutia upogo na wao ni wenye kuikanusha Aakhirah.
أُولَـٰئِكَ لَمْ يَكُونُوا مُعْجِزِينَ فِي الْأَرْضِ وَمَا كَانَ لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ۘ يُضَاعَفُ لَهُمُ الْعَذَابُ ۚ مَا كَانُوا يَسْتَطِيعُونَ السَّمْعَ وَمَا كَانُوا يُبْصِرُونَ﴿٢٠﴾
20. Hao hawakuwa na uwezo wa kukwepa (Adhabu ya Allaah) katika ardhi (lau Angelitaka Kuwaadhibu) na wasingepata walinzi badala ya Allaah. Hao watazidishiwa adhabu. Hawakuwa wakiweza kusikia na hawakuwa wakiona (haki).
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ﴿٢١﴾
21. Hao ndio wale waliokhasirika nafsi zao, na yakawapotea yale waliyokuwa wakiyatunga (ya uongo).
لَا جَرَمَ أَنَّهُمْ فِي الْآخِرَةِ هُمُ الْأَخْسَرُونَ﴿٢٢﴾
22. Hapana shaka kwamba wao huko Aakhirah ni wenye kukhasirika zaidi.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَأَخْبَتُوا إِلَىٰ رَبِّهِمْ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿٢٣﴾
23. Hakika wale walioamini na wakatenda mema na wakanyenyekea kwa Rabb wao, hao ni watu wa Jannah, na humo wao watadumu.
مَثَلُ الْفَرِيقَيْنِ كَالْأَعْمَىٰ وَالْأَصَمِّ وَالْبَصِيرِ وَالسَّمِيعِ ۚ هَلْ يَسْتَوِيَانِ مَثَلًا ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿٢٤﴾
24. Mfano wa makundi mawili ni kama kipofu na kiziwi na mwenye kuona na kusikia. Je, wanalingana sawa kwa kufananishwa?[12] Basi je, hamkumbuki?
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ إِنِّي لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ﴿٢٥﴾
25. Na kwa yakini Tulimtuma Nuwh kwa kaumu yake (akawaambia): Hakika mimi ni mwonyaji bayana kwenu.
أَن لَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ ۖ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ أَلِيمٍ﴿٢٦﴾
26. Ya kwamba msiabudu isipokuwa Allaah. Hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku inayoumiza.
فَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ مَا نَرَاكَ إِلَّا بَشَرًا مِّثْلَنَا وَمَا نَرَاكَ اتَّبَعَكَ إِلَّا الَّذِينَ هُمْ أَرَاذِلُنَا بَادِيَ الرَّأْيِ وَمَا نَرَىٰ لَكُمْ عَلَيْنَا مِن فَضْلٍ بَلْ نَظُنُّكُمْ كَاذِبِينَ﴿٢٧﴾
27. Wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake: Hatukuoni isipokuwa ni mtu tu kama sisi, na hatukuoni wanaokufuata isipokuwa wale ambao ni duni wetu, wasiopevuka kifikra, na hatukuoneni kuwa mna chochote bora cha kutuzidi sisi, bali tuna yakini nyinyi ni waongo.
قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَآتَانِي رَحْمَةً مِّنْ عِندِهِ فَعُمِّيَتْ عَلَيْكُمْ أَنُلْزِمُكُمُوهَا وَأَنتُمْ لَهَا كَارِهُونَ﴿٢٨﴾
28. (Nuwh) akasema: Enyi kaumu yangu! Je, mnaonaje ikiwa niko katika hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu, na Amenipa Rehma (ya Unabiy na Risala) kutoka Kwake kisha ikakufichikieni, je, tukulazimisheni kuikubali (Tawhiyd ya Allaah) na hali nyinyi mnaichukia?
وَيَا قَوْمِ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مَالًا ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ ۚ وَمَا أَنَا بِطَارِدِ الَّذِينَ آمَنُوا ۚ إِنَّهُم مُّلَاقُو رَبِّهِمْ وَلَـٰكِنِّي أَرَاكُمْ قَوْمًا تَجْهَلُونَ﴿٢٩﴾
29. Na enyi kaumu yangu! Sikuombeni mali juu ya (Risala) hii. Sina ujira isipokuwa kwa Allaah. Nami sitowafukuza wale walioamini. Hakika wao ni wenye kukutana na Rabb wao, lakini mimi nakuoneni ni watu majahili.
وَيَا قَوْمِ مَن يَنصُرُنِي مِنَ اللَّـهِ إِن طَرَدتُّهُمْ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿٣٠﴾
30. Na enyi kaumu yangu! Nani atakayeninusuru na Allaah nikiwafukuza? Je, hamkumbuki?
وَلَا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّـهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا أَقُولُ إِنِّي مَلَكٌ وَلَا أَقُولُ لِلَّذِينَ تَزْدَرِي أَعْيُنُكُمْ لَن يُؤْتِيَهُمُ اللَّـهُ خَيْرًا ۖ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا فِي أَنفُسِهِمْ ۖ إِنِّي إِذًا لَّمِنَ الظَّالِمِينَ﴿٣١﴾
31. Na wala sikuambieni kwamba mimi nina Hazina za Allaah, na wala sijui ya ghaibu, na wala sisemi mimi ni Malaika, na wala siwaambii wale ambao yanawadharau macho yenu kwamba Allaah Hatowapa kheri. Allaah Anajua zaidi yaliyomo katika nafsi zao. Hakika mimi hapo (nikifanya), bila shaka nitakuwa miongoni mwa madhalimu.
قَالُوا يَا نُوحُ قَدْ جَادَلْتَنَا فَأَكْثَرْتَ جِدَالَنَا فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ﴿٣٢﴾
32. Wakasema: Ee Nuwh, kwa yakini umelumbana nasi na umekithirisha malumbano nasi, basi tuletee hayo unayotuahidi ukiwa ni miongoni mwa wakweli.
قَالَ إِنَّمَا يَأْتِيكُم بِهِ اللَّـهُ إِن شَاءَ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ﴿٣٣﴾
33. (Nuwh) akasema: Hakika hayo Atakuleteeni Allaah Akitaka, nanyi hamtaweza kushinda (kukwepa adhabu).
وَلَا يَنفَعُكُمْ نُصْحِي إِنْ أَرَدتُّ أَنْ أَنصَحَ لَكُمْ إِن كَانَ اللَّـهُ يُرِيدُ أَن يُغْوِيَكُمْ ۚ هُوَ رَبُّكُمْ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٣٤﴾
34. Na wala haitokufaeni nasaha yangu nikitaka kukunasihini ikiwa Allaah Anataka kukuacheni mpotee. Yeye Ndiye Rabb wenu, na Kwake mtarejeshwa.
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ إِنِ افْتَرَيْتُهُ فَعَلَيَّ إِجْرَامِي وَأَنَا بَرِيءٌ مِّمَّا تُجْرِمُونَ﴿٣٥﴾
35. Bali wanasema ameitunga (Qur-aan). Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ikiwa nimeitunga, basi jarima hilo ni juu yangu, nami sina hatia ya jarima (zote) mnazofanya.
وَأُوحِيَ إِلَىٰ نُوحٍ أَنَّهُ لَن يُؤْمِنَ مِن قَوْمِكَ إِلَّا مَن قَدْ آمَنَ فَلَا تَبْتَئِسْ بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ﴿٣٦﴾
36. Na Nuwh akafunuliwa Wahy kwamba: Hatoamini katika watu wako isipokuwa wale waliokwishaamini. Basi usisononeke kwa waliyokuwa wanayafanya.
وَاصْنَعِ الْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا وَلَا تُخَاطِبْنِي فِي الَّذِينَ ظَلَمُوا ۚإِنَّهُم مُّغْرَقُونَ﴿٣٧﴾
37. Na unda jahazi mbele ya Macho Yetu[13] na kwa ufunuzi wa Wahy Wetu, na wala usinisemeze kuhusu wale waliodhulumu, hakika wao ni wenye kugharikishwa.
وَيَصْنَعُ الْفُلْكَ وَكُلَّمَا مَرَّ عَلَيْهِ مَلَأٌ مِّن قَوْمِهِ سَخِرُوا مِنْهُ ۚ قَالَ إِن تَسْخَرُوا مِنَّا فَإِنَّا نَسْخَرُ مِنكُمْ كَمَا تَسْخَرُونَ﴿٣٨﴾
38. (Nuwh) akawa anaunda jahazi. Basi kila walipompitia wakuu katika kaumu yake walimfanyia dhihaka. Akasema: Ikiwa mnatufanyia dhihaka, basi nasi tutakufanyieni dhihaka kama vile mnavyotufanyia dhihaka.
فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَيَحِلُّ عَلَيْهِ عَذَابٌ مُّقِيمٌ﴿٣٩﴾
39. Mtakuja kujua nani itakayemfikia adhabu itakayomhizi, na itakayemwangukia adhabu ya kudumu.
حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَمْرُنَا وَفَارَ التَّنُّورُ قُلْنَا احْمِلْ فِيهَا مِن كُلٍّ زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ وَأَهْلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيْهِ الْقَوْلُ وَمَنْ آمَنَ ۚ وَمَا آمَنَ مَعَهُ إِلَّا قَلِيلٌ﴿٤٠﴾
40. Mpaka ilipokuja Amri Yetu na tanuri likafoka, Tukasema: Beba humo (jahazini) wawili wawili kutoka kila aina; dume na jike na ahli zako, isipokuwa (kafiri) ambaye imemtangulia kauli ya hukmu na (beba humo) wale walioamini. Na hawakuamini pamoja naye isipokuwa wachache.[14]
وَقَالَ ارْكَبُوا فِيهَا بِسْمِ اللَّـهِ مَجْرَاهَا وَمُرْسَاهَا ۚ إِنَّ رَبِّي لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٤١﴾
41. Na (Nuwh) akasema: Pandeni humo! Kwa Jina la Allaah,[15] kwenda kwake na kutia nanga kwake. Hakika Rabb wangu bila shaka Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَهِيَ تَجْرِي بِهِمْ فِي مَوْجٍ كَالْجِبَالِ وَنَادَىٰ نُوحٌ ابْنَهُ وَكَانَ فِي مَعْزِلٍ يَا بُنَيَّ ارْكَب مَّعَنَا وَلَا تَكُن مَّعَ الْكَافِرِينَ﴿٤٢﴾
42. Basi hilo (jahazi) likawa linakwenda nao katikati ya mawimbi kama milima. Nuwh akamwita mwanawe naye alikuwa kandoni: Ee mwanangu! Panda pamoja nasi, na wala usiwe pamoja na makafiri.
قَالَ سَآوِي إِلَىٰ جَبَلٍ يَعْصِمُنِي مِنَ الْمَاءِ ۚ قَالَ لَا عَاصِمَ الْيَوْمَ مِنْ أَمْرِ اللَّـهِ إِلَّا مَن رَّحِمَ ۚ وَحَالَ بَيْنَهُمَا الْمَوْجُ فَكَانَ مِنَ الْمُغْرَقِينَ﴿٤٣﴾
43. Akasema: Nitakimbilia kwenye mlima utanilinda na maji. (Nuwh) akasema: Hapana wa kulindwa leo na Amri ya Allaah isipokuwa Aliyemrehemu. Tahamaki! Mawimbi yakaingia kati baina yao, akawa miongoni mwa waliogharikishwa.
وَقِيلَ يَا أَرْضُ ابْلَعِي مَاءَكِ وَيَا سَمَاءُ أَقْلِعِي وَغِيضَ الْمَاءُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ وَاسْتَوَتْ عَلَى الْجُودِيِّ ۖ وَقِيلَ بُعْدًا لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ﴿٤٤﴾
44. Na pakasemwa: Ee ardhi! Meza maji yako na ee mbingu, zuia (mvua), na maji yakadidimizwa, na hukmu ikatimizwa, na (jahazi) likatua juu ya (mlima wa) Judi. Na pakasemwa: Wametokomelea mbali watu madhalimu!
وَنَادَىٰ نُوحٌ رَّبَّهُ فَقَالَ رَبِّ إِنَّ ابْنِي مِنْ أَهْلِي وَإِنَّ وَعْدَكَ الْحَقُّ وَأَنتَ أَحْكَمُ الْحَاكِمِينَ﴿٤٥﴾
45. Na Nuwh akamwita Rabb wake, akasema: Rabb wangu! Hakika mwanangu ni katika ahli zangu, na hakika Ahadi Yako ni ya kweli, Nawe Ni Mwadilifu zaidi wa kuhukumu kuliko mahakimu wote.
قَالَ يَا نُوحُ إِنَّهُ لَيْسَ مِنْ أَهْلِكَ ۖ إِنَّهُ عَمَلٌ غَيْرُ صَالِحٍ ۖ فَلَا تَسْأَلْنِ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۖ إِنِّي أَعِظُكَ أَن تَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ﴿٤٦﴾
46. (Allaah) Akasema: Ee Nuwh! Hakika huyo si miongoni mwa ahli zako.[16] Hakika yeye amali zake si njema. Basi usiniombe yale usiyokuwa na ilimu nayo. Mimi Nakuwaidhi usijekuwa miongoni mwa majahili.
قَالَ رَبِّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ أَنْ أَسْأَلَكَ مَا لَيْسَ لِي بِهِ عِلْمٌ ۖ وَإِلَّا تَغْفِرْ لِي وَتَرْحَمْنِي أَكُن مِّنَ الْخَاسِرِينَ﴿٤٧﴾
47. Akasema: Ee Rabb wangu! Hakika mimi najikinga Kwako kukuomba yale nisiyo na ilimu nayo. Na Usiponighufuria na Ukanirehemu, nitakuwa miongoni mwa waliokhasirika.
قِيلَ يَا نُوحُ اهْبِطْ بِسَلَامٍ مِّنَّا وَبَرَكَاتٍ عَلَيْكَ وَعَلَىٰ أُمَمٍ مِّمَّن مَّعَكَ ۚ وَأُمَمٌ سَنُمَتِّعُهُمْ ثُمَّ يَمَسُّهُم مِّنَّا عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٤٨﴾
48. Pakasemwa: Ee Nuwh! Teremka (jahazini) kwa salama (na amani) kutoka Kwetu na baraka nyingi juu yako, na juu ya nyumati zilizo pamoja na wewe. Na nyumati Tutakazozistarehesha, kisha zitawagusa kutoka Kwetu adhabu iumizayo.
تِلْكَ مِنْ أَنبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهَا إِلَيْكَ ۖ مَا كُنتَ تَعْلَمُهَا أَنتَ وَلَا قَوْمُكَ مِن قَبْلِ هَـٰذَا ۖ فَاصْبِرْ ۖ إِنَّ الْعَاقِبَةَ لِلْمُتَّقِينَ﴿٤٩﴾
49. Hizo ni katika khabari za ghaibu Tunazokufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Hukuwa unazijua wewe wala watu wako kabla ya hii (Qur-aan). Basi vuta subira, hakika hatima (nzuri) ni kwa wenye taqwa.
وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا مُفْتَرُونَ﴿٥٠﴾
50. Na kwa kina ‘Aad (Tulimpeleka) ndugu yao Huwd. Akasema: Ee kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Nyinyi si chochote isipokuwa watungao uongo.
يَا قَوْمِ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى الَّذِي فَطَرَنِي ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ﴿٥١﴾
51. Enyi kaumu yangu! Sikuombeni ujira juu ya hii (Risala). Haukuwa ujira wangu isipokuwa kwa Yule Aliyeniumba. Je, basi hamtii akilini?
وَيَا قَوْمِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا وَيَزِدْكُمْ قُوَّةً إِلَىٰ قُوَّتِكُمْ وَلَا تَتَوَلَّوْا مُجْرِمِينَ﴿٥٢﴾
52. Na enyi kaumu yangu! Mwombeni maghfirah Rabb wenu, kisha tubieni Kwake, Atakuleteeni mbingu zenye kunyesha mvua tele ya kumiminika na Atakuzidishieni nguvu juu ya nguvu zenu, na wala msikengeuke mkawa wahalifu.
قَالُوا يَا هُودُ مَا جِئْتَنَا بِبَيِّنَةٍ وَمَا نَحْنُ بِتَارِكِي آلِهَتِنَا عَن قَوْلِكَ وَمَا نَحْنُ لَكَ بِمُؤْمِنِينَ﴿٥٣﴾
53. Wakasema: Ee Huwd! Hukutuletea hoja bayana, nasi hatutoacha kamwe waabudiwa wetu kutokana na kauli yako, nasi hatutokuwa wenye kukuamini.
إِن نَّقُولُ إِلَّا اعْتَرَاكَ بَعْضُ آلِهَتِنَا بِسُوءٍ ۗ قَالَ إِنِّي أُشْهِدُ اللَّـهَ وَاشْهَدُوا أَنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ﴿٥٤﴾
54. Hatusemi ila kuwa baadhi ya waabudiwa wetu wamekusibu kwa uovu. (Huwd) akasema: Hakika mimi namshuhudisha Allaah, na shuhudieni kwamba mimi niko mbali na waabudiwa mnaowashirikisha.
مِن دُونِهِ ۖ فَكِيدُونِي جَمِيعًا ثُمَّ لَا تُنظِرُونِ﴿٥٥﴾
55. Bila kumjumuisha Yeye (Allaah). Basi nifanyieni njama nyote kisha msinipe muhula.
إِنِّي تَوَكَّلْتُ عَلَى اللَّـهِ رَبِّي وَرَبِّكُم ۚ مَّا مِن دَابَّةٍ إِلَّا هُوَ آخِذٌ بِنَاصِيَتِهَا ۚ إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٦﴾
56. Hakika mimi nimetawakali kwa Allaah, Rabb wangu na Rabb wenu. Hakuna kiumbe chochote kitembeacho isipokuwa Yeye (Allaah) Ni Mwenye Kukamata hatamu za paji lake (Kukipeleka Atakavyo Yeye). Hakika Rabb wangu Yuko juu ya njia iliyonyooka.[17]
فَإِن تَوَلَّوْا فَقَدْ أَبْلَغْتُكُم مَّا أُرْسِلْتُ بِهِ إِلَيْكُمْ ۚ وَيَسْتَخْلِفُ رَبِّي قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّونَهُ شَيْئًا ۚ إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَفِيظٌ﴿٥٧﴾
57. Mkikengeuka, basi nimekwishakubalighishieni (Risala) niliyotumwa nayo kwenu. Na Rabb wangu Atarithisha watu wengineo wasiokuwa nyinyi, na wala hamtaweza kumdhuru chochote. Hakika Rabb wangu Ni Mwenye Kuhifadhi kila kitu.
وَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا هُودًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَنَجَّيْنَاهُم مِّنْ عَذَابٍ غَلِيظٍ﴿٥٨﴾
58. Na ilipokuja Amri Yetu, Tulimuokoa Huwd na wale walioamini pamoja naye kwa Rehma itokayo Kwetu, na Tukawaokoa kutokana na adhabu ngumu.
وَتِلْكَ عَادٌ ۖ جَحَدُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَعَصَوْا رُسُلَهُ وَاتَّبَعُوا أَمْرَ كُلِّ جَبَّارٍ عَنِيدٍ﴿٥٩﴾
59. Na hao ni kina ‘Aad. Wamezikanusha kwa ushupavu Aayaat (Ishara, Hoja, Dalili) za Rabb wao, na wakawaasi Rusuli Wake, na wakafuata amri ya kila jabari mkaidi.
وَأُتْبِعُوا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ أَلَا إِنَّ عَادًا كَفَرُوا رَبَّهُمْ ۗ أَلَا بُعْدًا لِّعَادٍ قَوْمِ هُودٍ﴿٦٠﴾
60. Na wakafuatishwa na laana katika dunia hii, na Siku ya Qiyaamah. Tanabahi! Hakika kina ‘Aad walimkufuru Rabb wao. Tanabahi! Wameangamiziliwa mbali kina ‘Aad; kaumu ya Huwd.
وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَاسْتَعْمَرَكُمْ فِيهَا فَاسْتَغْفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي قَرِيبٌ مُّجِيبٌ﴿٦١﴾
61. Na kwa Thamuwd (Tulimpeleka) ndugu yao Swaalih. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Yeye Ndiye Aliyekuanzisheni kutokana na ardhi, na Akakufanyieni makazi humo, basi mwombeni maghfirah, kisha tubieni Kwake. Hakika Rabb wangu Yuko Karibu, Mwenye Kuitikia.
قَالُوا يَا صَالِحُ قَدْ كُنتَ فِينَا مَرْجُوًّا قَبْلَ هَـٰذَا ۖ أَتَنْهَانَا أَن نَّعْبُدَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا وَإِنَّنَا لَفِي شَكٍّ مِّمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ مُرِيبٍ﴿٦٢﴾
62. Wakasema: Ee Swaalih! Kwa yakini ulikuwa kwetu mwenye kutarajiwa (kheri) kabla ya haya. Je, unatukataza kuabudu wale wanaoabudiwa na baba zetu, na hakika sisi tumo katika shaka na wasiwasi katika unayotuitia.
قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَآتَانِي مِنْهُ رَحْمَةً فَمَن يَنصُرُنِي مِنَ اللَّـهِ إِنْ عَصَيْتُهُ ۖ فَمَا تَزِيدُونَنِي غَيْرَ تَخْسِيرٍ﴿٦٣﴾
63. (Swaalih) akasema: Enyi kaumu yangu! Je, mnaonaje ikiwa niko katika hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu, Naye Amenipa Rehma (Unabii na Risala) kutoka Kwake, hivo nani atakayeninusuru nikimuasi? Basi hamnizidishii ila khasara.
وَيَا قَوْمِ هَـٰذِهِ نَاقَةُ اللَّـهِ لَكُمْ آيَةً فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللَّـهِ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ قَرِيبٌ﴿٦٤﴾
64. Enyi kaumu yangu! Huyu ni Ngamia Jike wa Allaah, ni Aayah (Ishara, Muujiza, Dalili ya wazi) kwenu, basi mwacheni ale katika Ardhi ya Allaah, na wala msimguse kwa uovu ikakupateni adhabu iliyo karibu.
فَعَقَرُوهَا فَقَالَ تَمَتَّعُوا فِي دَارِكُمْ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ ۖ ذَٰلِكَ وَعْدٌ غَيْرُ مَكْذُوبٍ﴿٦٥﴾
65. Lakini wakamuua. (Swaalih) akasema: Stareheni majumbani mwenu siku tatu. Hiyo ni ahadi isiyo ya uongo.
فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا صَالِحًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَمِنْ خِزْيِ يَوْمِئِذٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ الْقَوِيُّ الْعَزِيزُ﴿٦٦﴾
66. Basi ilipokuja Amri Yetu, Tulimuokoa Swaalih na wale walioamini pamoja naye kwa Rehma kutoka Kwetu, na (kuwaokoa) kutokana na hizaya ya Siku hiyo. Hakika Rabb wako Yeye Ndiye Mwenye nguvu, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika.
وَأَخَذَ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ﴿٦٧﴾
67. Na wale waliodhulumu uliwachukuwa ukelele angamizi, wakapambazukiwa wameanguka kifudifudi majumbani mwao (wamekufa).
كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۗ أَلَا إِنَّ ثَمُودَ كَفَرُوا رَبَّهُمْ ۗ أَلَا بُعْدًا لِّثَمُودَ﴿٦٨﴾
68. Kama kwamba hawakuishi wakineemeka humo. Tanabahi! Hakika kina Thamuwd walimkufuru Rabb wao. Tanabahi! Wameangamiziliwa mbali kina Thamuwd.
وَلَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُنَا إِبْرَاهِيمَ بِالْبُشْرَىٰ قَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ ۖ فَمَا لَبِثَ أَن جَاءَ بِعِجْلٍ حَنِيذٍ﴿٦٩﴾
69. Na kwa yakini walimjia Ibraahiym Wajumbe Wetu kwa bishara, wakasema: Salaam! (Naye) Akasema: Salaam. Basi hakukawia ila alikuja na ndama aliyebanikwa.
فَلَمَّا رَأَىٰ أَيْدِيَهُمْ لَا تَصِلُ إِلَيْهِ نَكِرَهُمْ وَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۚ قَالُوا لَا تَخَفْ إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمِ لُوطٍ﴿٧٠﴾
70. Alipoona mikono yao haisogei kumla (ndama) aliwashangaa na ikamuingia khofu kutokana nao. Wakasema: Usiogope! Hakika Sisi Tumetumwa kwa kaumu ya Luutw.
وَامْرَأَتُهُ قَائِمَةٌ فَضَحِكَتْ فَبَشَّرْنَاهَا بِإِسْحَاقَ وَمِن وَرَاءِ إِسْحَاقَ يَعْقُوبَ﴿٧١﴾
71. Na mkewe amesimama wima, akacheka. Tukambashiria Is-haaq na baada ya Is-haaq ni Ya’quwb.
قَالَتْ يَا وَيْلَتَىٰ أَأَلِدُ وَأَنَا عَجُوزٌ وَهَـٰذَا بَعْلِي شَيْخًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عَجِيبٌ﴿٧٢﴾
72. Akasema: Yatakuwaje haya jamani! Je, nitazaa na hali mimi ni mkongwe na huyu mume wangu ni kizee? Hakika hili ni jambo la ajabu!
قَالُوا أَتَعْجَبِينَ مِنْ أَمْرِ اللَّـهِ ۖ رَحْمَتُ اللَّـهِ وَبَرَكَاتُهُ عَلَيْكُمْ أَهْلَ الْبَيْتِ ۚ إِنَّهُ حَمِيدٌ مَّجِيدٌ﴿٧٣﴾
73. (Malaika) wakasema: Je, unastaajabia Amri ya Allaah? Rehma ya Allaah na Baraka Zake ziko juu yenu enyi ahli wa nyumba (ya Nabiy Ibraahiym). Hakika Yeye Ni Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa, Mwenye Utukufu kamili na Enzi.
فَلَمَّا ذَهَبَ عَنْ إِبْرَاهِيمَ الرَّوْعُ وَجَاءَتْهُ الْبُشْرَىٰ يُجَادِلُنَا فِي قَوْمِ لُوطٍ﴿٧٤﴾
74. Kisha kiwewe cha tisho la moyo kilipomuondoka Ibraahiym, na habari njema akawa ameipata (alianza) kujadiliana Nasi kuhusu kaumu ya Luutw.
إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَحَلِيمٌ أَوَّاهٌ مُّنِيبٌ﴿٧٥﴾
75. Hakika Ibraahiym bila shaka ni mvumilivu sana, mnyenyekevu mno kwa Allaah, na mwingi wa kurejea Kwake.
يَا إِبْرَاهِيمُ أَعْرِضْ عَنْ هَـٰذَا ۖ إِنَّهُ قَدْ جَاءَ أَمْرُ رَبِّكَ ۖ وَإِنَّهُمْ آتِيهِمْ عَذَابٌ غَيْرُ مَرْدُودٍ﴿٧٦﴾
76. (Malaika wakamwambia): ee Ibraahiym! Achilia mbali haya! Hakika imekwishakuja Amri ya Rabb wako, na hakika wao itawafikia adhabu isiyorudishwa.
وَلَمَّا جَاءَتْ رُسُلُنَا لُوطًا سِيءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْعًا وَقَالَ هَـٰذَا يَوْمٌ عَصِيبٌ﴿٧٧﴾
77. Na Wajumbe Wetu walipomjia Luutw, alisononeka kwa ajili yao na akawaonea dhiki, akasema: Hii ni siku ngumu!
وَجَاءَهُ قَوْمُهُ يُهْرَعُونَ إِلَيْهِ وَمِن قَبْلُ كَانُوا يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ ۚ قَالَ يَا قَوْمِ هَـٰؤُلَاءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطْهَرُ لَكُمْ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَلَا تُخْزُونِ فِي ضَيْفِي ۖ أَلَيْسَ مِنكُمْ رَجُلٌ رَّشِيدٌ﴿٧٨﴾
78. Wakamjia kaumu yake haraka, na kabla ya hapo walikuwa wakitenda maovu. (Luutw) akasema: Enyi kaumu yangu! Hawa ni mabinti zangu, wao wametwaharika kwenu (kuwaoa kihalali). Basi mcheni Allaah, na wala msinifedheheshe mbele ya wageni wangu. Je, hakuna miongoni mwenu mtu muongofu?
قَالُوا لَقَدْ عَلِمْتَ مَا لَنَا فِي بَنَاتِكَ مِنْ حَقٍّ وَإِنَّكَ لَتَعْلَمُ مَا نُرِيدُ﴿٧٩﴾
79. Wakasema: Kwa yakini umekwishajua kwamba hatuhitaji wala hatuna matamanio yoyote kwa mabinti zako na bila shaka wewe unajua tunalolitaka.
قَالَ لَوْ أَنَّ لِي بِكُمْ قُوَّةً أَوْ آوِي إِلَىٰ رُكْنٍ شَدِيدٍ﴿٨٠﴾
80. (Luutw) akasema: Lau ningelikuwa nina nguvu ya kuzuia shari yenu, au nikimbilie katika nguzo madhubuti.
قَالُوا يَا لُوطُ إِنَّا رُسُلُ رَبِّكَ لَن يَصِلُوا إِلَيْكَ ۖ فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ اللَّيْلِ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ إِلَّا امْرَأَتَكَ ۖ إِنَّهُ مُصِيبُهَا مَا أَصَابَهُمْ ۚ إِنَّ مَوْعِدَهُمُ الصُّبْحُ ۚ أَلَيْسَ الصُّبْحُ بِقَرِيبٍ﴿٨١﴾
81. (Malaika) wakasema: Ee Luutw! Hakika sisi ni Wajumbe wa Rabb wako, hawatokufikia (kwa uovu). Basi toka usiku (huu) na ahli zako sehemu iliyobakia ya usiku, na wala asitazame nyuma yeyote miongoni mwenu, isipokuwa mke wako (atabaki nyuma), kwani yeye yatamsibu yatakayowasibu wao. Hakika miadi yao ni asubuhi. Je, kwani asubuhi haiko karibu?
فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا جَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهَا حِجَارَةً مِّن سِجِّيلٍ مَّنضُودٍ﴿٨٢﴾
82. Basi ilipokuja Amri Yetu, Tuliupindua (mji wao) juu chini, na Tukauteremshia mvua ya mawe ya udongo mgumu uliookwa motoni, yenye kuandamana.
مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ ۖ وَمَا هِيَ مِنَ الظَّالِمِينَ بِبَعِيدٍ﴿٨٣﴾
83. Yametiwa alama kutoka kwa Rabb wako. Na adhabu hiyo haiko mbali na madhalimu (mfano wao).
وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ وَلَا تَنقُصُوا الْمِكْيَالَ وَالْمِيزَانَ ۚ إِنِّي أَرَاكُم بِخَيْرٍ وَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ مُّحِيطٍ﴿٨٤﴾
84. Na kwa Madyan (Tulimpeleka) ndugu yao Shu’ayb. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Na wala msipunguze kipimo na mizani. Hakika mimi nakuoneni mko katika kheri (na neema), na hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku yenye kuzingira.
وَيَا قَوْمِ أَوْفُوا الْمِكْيَالَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ ۖ وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ﴿٨٥﴾
85. Na enyi kaumu yangu! Timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu, na wala msipunje watu vitu vyao, na wala msifanye uovu katika ardhi mkawa mafisadi.
بَقِيَّتُ اللَّـهِ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ۚ وَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِحَفِيظٍ﴿٨٦﴾
86. Mabakisho ya Allaah (Aliyokuwekeeni) ni bora kwenu, mkiwa ni wenye kuamini. Nami si mlinzi wa kuwachungeni.
قَالُوا يَا شُعَيْبُ أَصَلَاتُكَ تَأْمُرُكَ أَن نَّتْرُكَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا أَوْ أَن نَّفْعَلَ فِي أَمْوَالِنَا مَا نَشَاءُ ۖ إِنَّكَ لَأَنتَ الْحَلِيمُ الرَّشِيدُ﴿٨٧﴾
87. Wakasema: Ee Shu’ayb! Hivi Swalaah zako ndizo zinakuamrisha kuwa sisi tuache yale baba zetu wanayoyaabudu, au tuache kufanya tunavyotaka katika mali zetu? Wewe kweli ni mvumilivu, uliyeongoka.
قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَرَزَقَنِي مِنْهُ رِزْقًا حَسَنًا ۚ وَمَا أُرِيدُ أَنْ أُخَالِفَكُمْ إِلَىٰ مَا أَنْهَاكُمْ عَنْهُ ۚ إِنْ أُرِيدُ إِلَّا الْإِصْلَاحَ مَا اسْتَطَعْتُ ۚ وَمَا تَوْفِيقِي إِلَّا بِاللَّـهِ ۚ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ﴿٨٨﴾
88. (Shu’ayb) akasema: Enyi kaumu yangu! Je, mnaonaje ikiwa niko katika hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu, Naye Ameniruzuku riziki nzuri toka Kwake. Nami sitaki kukukhalifuni kufanya ninayokukatazeni. Sitaki lolote ila kutengeneza niwezavyo. Na sipati Tawfiyq ila kwa Allaah. Kwake natawakali na Kwake narejea kutubu.
وَيَا قَوْمِ لَا يَجْرِمَنَّكُمْ شِقَاقِي أَن يُصِيبَكُم مِّثْلُ مَا أَصَابَ قَوْمَ نُوحٍ أَوْ قَوْمَ هُودٍ أَوْ قَوْمَ صَالِحٍ ۚ وَمَا قَوْمُ لُوطٍ مِّنكُم بِبَعِيدٍ﴿٨٩﴾
89. Enyi kaumu yangu! Kupingana nami kwa uhasama kusikuchocheeni kabisa yakakusibuni yale yaliyowasibu kaumu ya Nuwh au kaumu ya Huwd, au watu ya Swaalih. Na kaumu ya Luutw hawako mbali nanyi.
وَاسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي رَحِيمٌ وَدُودٌ﴿٩٠﴾
90. Na ombeni maghfirah kwa Rabb wenu, kisha tubieni Kwake. Hakika Rabb wangu ni Mwenye Kurehemu, Mwenye upendo khalisi.
قَالُوا يَا شُعَيْبُ مَا نَفْقَهُ كَثِيرًا مِّمَّا تَقُولُ وَإِنَّا لَنَرَاكَ فِينَا ضَعِيفًا ۖ وَلَوْلَا رَهْطُكَ لَرَجَمْنَاكَ ۖ وَمَا أَنتَ عَلَيْنَا بِعَزِيزٍ﴿٩١﴾
91. Wakasema: Ee Shu’ayb! Hatufahamu mengi unayoyasema, na hakika sisi tunakuona ni dhaifu kati yetu. Na lau kama si (kabila au) jamaa zako tungelikupiga mawe. Nawe si azizi kwetu.
قَالَ يَا قَوْمِ أَرَهْطِي أَعَزُّ عَلَيْكُم مِّنَ اللَّـهِ وَاتَّخَذْتُمُوهُ وَرَاءَكُمْ ظِهْرِيًّا ۖ إِنَّ رَبِّي بِمَا تَعْمَلُونَ مُحِيطٌ﴿٩٢﴾
92. (Shu’ayb) akasema: Enyi kaumu yangu! Je, jamaa zangu wana utukufu zaidi kwenu kuliko Allaah, na mmemuweka Yeye (Allaah) nyuma ya migongo yenu? Hakika Rabb wangu ni Mwenye Kuyazunguka yale myatendayo.
وَيَا قَوْمِ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ ۖ سَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَمَنْ هُوَ كَاذِبٌ ۖ وَارْتَقِبُوا إِنِّي مَعَكُمْ رَقِيبٌ﴿٩٣﴾
93. Na enyi kaumu yangu! Fanyeni kwa namna zenu, nami pia nafanya. Mtakuja kujua nani itamfika adhabu itakayomhizi, na ni nani aliye muongo. Na ngojeeni mchunge. Hakika mimi niko pamoja nanyi nikingojea na kuchunga.
وَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا شُعَيْبًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَأَخَذَتِ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ﴿٩٤﴾
94. Na ilipokuja Amri Yetu, Tulimuokoa Shu’ayb na wale walioamini pamoja naye kwa Rehma itokayo Kwetu. Na ukawachukuwa wale waliodhulumu ukelele angamizi wakapambazukiwa wameanguka kifudifudi majumbani mwao (wamekufa).
كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۗ أَلَا بُعْدًا لِّمَدْيَنَ كَمَا بَعِدَتْ ثَمُودُ﴿٩٥﴾
95. Kama kwamba hawakuishi wakineemeka humo. Tanabahi! Watokomee mbali (watu wa) Madyan kama walivyotokomea Thamuwd.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُّبِينٍ﴿٩٦﴾
96. Na kwa yakini Tulimpeleka Muwsaa kwa Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu na hoja bayana.
إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَاتَّبَعُوا أَمْرَ فِرْعَوْنَ ۖ وَمَا أَمْرُ فِرْعَوْنَ بِرَشِيدٍ﴿٩٧﴾
97. Kwa Firawni na wakuu wake, lakini walifuata amri ya Firawni. Na amri ya Firawni haikuwa yenye uongofu.
يَقْدُمُ قَوْمَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَأَوْرَدَهُمُ النَّارَ ۖ وَبِئْسَ الْوِرْدُ الْمَوْرُودُ﴿٩٨﴾
98. (Firawni) atawatangulia watu wake Siku ya Qiyaamah, na atawafikisha motoni. Na ubaya ulioje mahali pa maingio watakapoingizwa!
وَأُتْبِعُوا فِي هَـٰذِهِ لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ بِئْسَ الرِّفْدُ الْمَرْفُودُ﴿٩٩﴾
99. Na wamefuatishwa na laana katika (dunia) hii na Siku ya Qiyaamah (pia). Ubaya ulioje wa watakayotunukiwa (laana ya dunia na ya Aakhirah)!
ذَٰلِكَ مِنْ أَنبَاءِ الْقُرَىٰ نَقُصُّهُ عَلَيْكَ ۖ مِنْهَا قَائِمٌ وَحَصِيدٌ﴿١٠٠﴾
100. Hizo ni baadhi ya khabari za miji Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), miongoni mwake ingalipo bado, na iliyofekwa.
وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَـٰكِن ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ۖ فَمَا أَغْنَتْ عَنْهُمْ آلِهَتُهُمُ الَّتِي يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ لَّمَّا جَاءَ أَمْرُ رَبِّكَ ۖ وَمَا زَادُوهُمْ غَيْرَ تَتْبِيبٍ﴿١٠١﴾
101. Nasi Hatukuwadhulumu, lakini wamejidhulumu nafsi zao wenyewe. Basi hawakuwafaa kitu chochote waabudiwa wao waliokuwa wakiwaomba badala ya Allaah ilipokuja Amri ya Rabb wako. Na wala hawakuwazidishia isipokuwa mateketezo.
وَكَذَٰلِكَ أَخْذُ رَبِّكَ إِذَا أَخَذَ الْقُرَىٰ وَهِيَ ظَالِمَةٌ ۚ إِنَّ أَخْذَهُ أَلِيمٌ شَدِيدٌ﴿١٠٢﴾
102. Na hivyo ndivyo Mkamato wa Rabb wako unavyokuwa Anapokamata miji inapokuwa imedhulumu. Hakika Mkamato Wake unaumiza vikali.
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّمَنْ خَافَ عَذَابَ الْآخِرَةِ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّجْمُوعٌ لَّهُ النَّاسُ وَذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّشْهُودٌ﴿١٠٣﴾
103. Hakika katika hayo mna Aayah (Ishara, Mazingatio) kwa anayekhofu adhabu ya Aakhirah. Hiyo ni Siku ya kujumuishwa watu, na hiyo ni Siku ya kushuhudiwa.
وَمَا نُؤَخِّرُهُ إِلَّا لِأَجَلٍ مَّعْدُودٍ﴿١٠٤﴾
104. Na hatuiakhirishi isipokuwa kwa muda maalumu unaohesabiwa.
يَوْمَ يَأْتِ لَا تَكَلَّمُ نَفْسٌ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ فَمِنْهُمْ شَقِيٌّ وَسَعِيدٌ﴿١٠٥﴾
105. Siku itakapofika, haitosema nafsi yeyote isipokuwa kwa Idhini Yake (Allaah). Basi miongoni mwao watakuwa wenye mashaka na wenye furaha na neema.
فَأَمَّا الَّذِينَ شَقُوا فَفِي النَّارِ لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَشَهِيقٌ﴿١٠٦﴾
106. Ama wale walio mashakani, basi watakuwa motoni, lao humo ni kupumua kwa mngurumo na kuvuta pumzi kwa mkoromo.
خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ﴿١٠٧﴾
107. Watadumu humo zitakavyodumu mbingu na ardhi isipokuwa Atakavyo Rabb wako. Hakika Rabb wako Anafanya Atakavyo.
وَأَمَّا الَّذِينَ سُعِدُوا فَفِي الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ ۖ عَطَاءً غَيْرَ مَجْذُوذٍ﴿١٠٨﴾
108. Na ama wale walio furahani, basi watakuwa katika Jannah, watadumu humo zitakavyodumu mbingu na ardhi isipokuwa Atakavyo Rabb wako. Ni hiba isiyokatizwa.
فَلَا تَكُ فِي مِرْيَةٍ مِّمَّا يَعْبُدُ هَـٰؤُلَاءِ ۚ مَا يَعْبُدُونَ إِلَّا كَمَا يَعْبُدُ آبَاؤُهُم مِّن قَبْلُ ۚ وَإِنَّا لَمُوَفُّوهُمْ نَصِيبَهُمْ غَيْرَ مَنقُوصٍ﴿١٠٩﴾
109. Basi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) usiwe katika shaka kutokana na wanayoyaabudu hao (washirikina). Hawaabudu ila kama walivyoabudu baba zao kabla. Na hakika Tutawalipa kikamilifu fungu lao bila ya kupunguzwa.
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَاخْتُلِفَ فِيهِ ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ مُرِيبٍ﴿١١٠﴾
110. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu, zikatiwa ikhtilaafu ndani yake. Na kama si Neno lililotangulia kutoka kwa Rabb wako, bila shaka ingelihukumiwa baina yao. Na hakika wao wako katika shaka juu yake (hii Qur-aan) inayowatia wasiwasi.
وَإِنَّ كُلًّا لَّمَّا لَيُوَفِّيَنَّهُمْ رَبُّكَ أَعْمَالَهُمْ ۚ إِنَّهُ بِمَا يَعْمَلُونَ خَبِيرٌ﴿١١١﴾
111. Na hakika wote Rabb wako Atawalipa kikamilifu amali zao. Hakika Yeye kwa yale wayatendayo Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
فَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ وَمَن تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطْغَوْا ۚ إِنَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ﴿١١٢﴾
112. Basi thibitika imara kama ulivyoamrishwa wewe na aliyetubia pamoja nawe, na wala msiruke mipaka. Hakika Yeye Ni Mwenye Kuona myatendayo.
وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ﴿١١٣﴾
113. Na wala msielemee kwa wale waliodhulumu usije ukakuguseni moto, na hamtokuwa na walinzi badala ya Allaah, kisha hamtonusuriwa.
وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ﴿١١٤﴾
114. Na simamisha Swalaah katika ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku, hakika mema yanaondosha maovu.[18] Haya ni ukumbusho kwa wanaokumbuka.[19]
وَاصْبِرْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ﴿١١٥﴾
115. Na vuta subira kwani hakika Allaah Hapotezi ujira wa wafanyao ihsaan.
فَلَوْلَا كَانَ مِنَ الْقُرُونِ مِن قَبْلِكُمْ أُولُو بَقِيَّةٍ يَنْهَوْنَ عَنِ الْفَسَادِ فِي الْأَرْضِ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّنْ أَنجَيْنَا مِنْهُمْ ۗ وَاتَّبَعَ الَّذِينَ ظَلَمُوا مَا أُتْرِفُوا فِيهِ وَكَانُوا مُجْرِمِينَ﴿١١٦﴾
116. Basi kwa nini hawakuweko katika karne za kabla yenu, walio weledi na wasaa wanakataza ufisadi katika ardhi isipokuwa wachache kati ya Tuliowaokoa miongoni mwao? Na wale waliodhulumu wakafuata anasa walizostareheshwa nazo na wakawa wahalifu.
وَمَا كَانَ رَبُّكَ لِيُهْلِكَ الْقُرَىٰ بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا مُصْلِحُونَ﴿١١٧﴾
117. Na Rabb wako Hakuwa Mwenye Kuangamiza miji kwa dhulma na hali watu wake ni wenye kupigania mema.
وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ النَّاسَ أُمَّةً وَاحِدَةً ۖ وَلَا يَزَالُونَ مُخْتَلِفِينَ﴿١١٨﴾
118. Na kama Angetaka Rabb wako, basi Angejaalia watu wote kuwa ni ummah mmoja. Na hawatoacha kukhitilafiana.
إِلَّا مَن رَّحِمَ رَبُّكَ ۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمْ ۗ وَتَمَّتْ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ﴿١١٩﴾
119. Isipokuwa yule Aliyemrehemu Rabb wako. Na kwa hayo ndio Amewaumba. Na limetimia Neno la Rabb wako (kwamba): Bila shaka Nitajaza Jahannam kwa majini na watu wote pamoja.
وَكُلًّا نَّقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنبَاءِ الرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِ فُؤَادَكَ ۚ وَجَاءَكَ فِي هَـٰذِهِ الْحَقُّ وَمَوْعِظَةٌ وَذِكْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ﴿١٢٠﴾
120. Na yote Tunayokusimulia katika khabari muhimu za Rusuli, ni ambayo kwayo Tunathibitisha moyo wako. Na imekujia katika haya haki na mawaidha na ukumbusho kwa Waumini.
وَقُل لِّلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنَّا عَامِلُونَ﴿١٢١﴾
121. Na waambie wale wasioamini: Fanyeni kwa namna zenu, nasi pia tunafanya.
وَانتَظِرُوا إِنَّا مُنتَظِرُونَ﴿١٢٢﴾
122. Na ngojeeni, nasi pia tunangojea.
وَلِلَّـهِ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَإِلَيْهِ يُرْجَعُ الْأَمْرُ كُلُّهُ فَاعْبُدْهُ وَتَوَكَّلْ عَلَيْهِ ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ﴿١٢٣﴾
123. Na ni ya Allaah (Pekee) ghaibu ya mbingu na ardhi, na Kwake hurudishwa mambo yote, basi mwabudu Yeye na tawakali Kwake. Na Rabb wako Si Mwenye Kughafilika na yale myatendayo.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Umuhimu Na Faida Za Istighfaar (Kuomba Maghfirah) Na Kutubia Kwa Allaah (عزّ وجلّ):
Katika Suwrah hii Tukufu, Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja fadhila za Istighfaar (kuomba maghfirah) na kutubia katika Aayah kadhaa kama ifuatavyo:
(i) Kupata starehe nzuri. (ii) Kupewa Fadhila za Allaah (عزّ وجلّ), rejea Huwd (11:3). (iii) Kuteremshiwa mvua nyingi na kuzidishiwa nguvu, rejea Huwd (11:52). (iv) Kufanyiwa makazi. (v) Allaah Huwa Karibu na kuwaitikia duaa zao, rejea Huwd (11:61). (vi) Allaah Huwarehemu na Kuwa Mwenye Upendo Halisi kwao, rejea Huwd (11:90). Na katika Suwrah nyenginezo mbalimbali, zimetajwa fadhila kama hizi na nyenginezo za kuomba maghfirah na kutubia. Rejea Suwrah Nuwh (71:10-12), na pia Aal-‘Imraan (3:125-136) ambamo kumetajwa fadhila ya kuingizwa Jannah. Hali kadhaalika, fadhila ya kuwekewa Nuru katika Swiraatw Siku ya Qiyaamah ambayo itammulikia mtu atakapokuwa akiivuka hiyo njia nyembamba mno kama unywele, rejea At-Tahriym (66:8). Pia ni mmojawapo ya sifa za Waja wa Ar-Rahmaan, rejea Al-Furqaan (25:70:71). Pia Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja katika Qur-aan kuwa Anawapenda wenye kuomba maghfirah na tawbah, rejea Al-Baqarah (2:222).
Na kuomba maghfirah ni katika nyakati zozote zile, ila Allaah (سبحانه وتعالى) Amezitaja nyakati zilizo bora zaidi ambazo Anawasifu waja wema wanaoomba maghfirah katika nyakati hizo. Nyakati hizo ni za kabla ya Alfajiri, na Anawaahidi waja hao kuwaingiza Jannah. Rejea Adh-Dhaariyaat (51:15-18), Aal-‘Imraan (3:17). Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amehimizia waja kuomba maghfirah katika Hadiyth mbalimbali na akaonyesha mfano wake yeye kuwa anaomba maghfirah mara mia kwa siku moja kwa kauli yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): “Enyi watu! Tubieni kwa Allaah na muombe maghfirah, kwani mimi natubia kwa Allaah na namuomba maghfirah mara mia kwa siku.” [Muslim]
Na fadhila za kuomba maghfirah katika Hadiyth za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni nyingi mno, bali Allaah Anafurahiwa mno na wenye kuomba maghfirah hata kwa mja aliyemkosea Allaah (سبحانه وتعالى) katika kumtaja Kwake!
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Allaah Hufurahikiwa mno na tawbah ya mja Wake wakati anapotubia Kwake kuliko furaha ya mmoja wenu aliyekuwa amempanda mnyama wake kwenye jangwa (la joto kali, hakuna mtu yeyote), kisha mnyama huyo aliyebeba chakula chake na maji yake akampotea, na akakata tamaa kabisa ya kumpata tena. Akaenda kwenye mti, akalala chini ya kivuli chake huku akiwa amekata tamaa kabisa ya kumpata tena mnyama wake. Akiwa katika hali hiyo (ya kutojua nini la kufanya), mara anashtuka kumwona huyo amesimama mbele yake, akaikamata hatamu yake, na kwa ile furaha akasema: "Ee Allaah, Wewe ni mja wangu na mimi ni Rabb wako.” Alikosea (kumshukuru Rabb wake) kwa wingi wa furaha aliyokuwa nayo.” [Muslim]
Na Hadiyth Al-Qudsiy ifuatayo inaonyesha kwamba Allaah (عزّ وجلّ) Hajali Mja Wake kuwa na madhambi madamu anamuomba maghfirah na tawbah:
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Allaah (تبارك وتعالى) Amesema: Ee binaadam! Hakika ukiniomba na ukanitaraji (kwa malipo) Nitakughufuria yale yote uliyonayo na wala Sijali. Ee binaadam! Lau zingefikia dhambi zako ukubwa wa mbingu, kisha ukaniomba maghfirah, Ningekughufuria bila ya kujali (kiasi cha madhambi uliyoyafanya). Ee binaadam! Hakika ungenijia na madhambi yakaribiayo ukubwa wa ardhi, kisha ukakutana Nami na hali hukunishirikisha chochote, basi Nami Nitakujia na maghfirah yanayolinga nayo.” [At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy kaipa daraja ya Hasan]
Rejea An-Nisaa (4:110), Nuwh (71:10), Adh-Dhaariyaat (51:18), na At-Tahriym (66:8) ambako kumetajwa Tawbah ya kikweli na sharti za maghfirah na tawbah.
[3] Sababu Ya Makafiri Kuinamisha Vifua Vyao:
Makafiri walikuwa wakiinamisha vifua vyao kwa sababu wakimstahi Allaah (سبحانه وتعالى). Hadiyth ifuatayo imethibiti:
Amesimulia Muhammad Bin ‘Abaada Bin Ja’far (رضي الله عنه): ‘Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) alisoma:
أَلَا إِنَّهُمْ يَثْنُونَ صُدُورَهُمْ
“Tanabahi! Hakika wao wanainamisha vifua vyao.” [Huwd (11:5)]
Nikamuuliza: Ee Ibn ‘Abbaas! Inamaanisha nini wanainamisha vifua vyao? Akasema: Mtu alikuwa akistahi kujamiiana na mkewe (katika sehemu iliyo wazi ili wasiwe ni wenye kuiona mbingu) au mtu alipokuwa akienda kufanya haja) basi Aayah hii iliteremshwa:
أَلَا إِنَّهُمْ يَثْنُونَ صُدُورَهُمْ
“Tanabahi! Hakika wao wanainamisha vifua vyao.”
Na pia Aayah inaendelea kutaja ada za makafiri kuweka vidole masikioni mwao na kujigubika nguo wasisikie Risala wala wasiwaone Rusuli wanaowalingania. Rejea Nuwh (71:7).
[5] ‘Arshi ya Allaah Kuwa Juu Ya Maji:
Aayah hii tukufu inataja kuwa ‘Arshi ya Allaah (سبحانه وتعالى) ilikuwa juu ya maji kabla ya kuumba mbingu na ardhi. Na ‘Arshi hiyo ya Allaah (سبحانه وتعالى) na hayo maji ni vitu Alivyoviumba Allaah (عزّ وجلّ) na ambavyo Amevinasibisha Kwake Mwenyewe Allaah عزّ وجلّ)), hatuvijui uhakika wake, bali tunaamini kama Anavyosema. Rejea Twaahaa (10:5). Na baadhi ya Hadiyth zifuatazo zinathibitisha na zinatilia nguvu Kauli ya Allaah (عزّ وجلّ) ya Aayah hii tukufu kuhusu ‘Arsh Yake Allaah (عزّ وجلّ) kuwa ilikuwa juu ya maji:
Amesimulia ‘Imraan Bin Huswayn (رضي الله عنه): Nilikwenda kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumfunga ngamia wangu jike mlangoni. Watu wa Bani Tamiym walikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Enyi Bani Tamiym! Pokeeni bishara njema.” Wakasema mara mbili: “Umetupatia bishara njema, sasa tupatie kitu.” Kisha baadhi ya watu wa Yemen walikuja kwake, akasema: “Pokeeni bishara njema, enyi watu wa Yemen, kwani Bani Tamiym wamekataa.” Wakasema: “Tunaipokea ee Rasuli wa Allaah! Tumekuja kukuuliza kuhusu jambo hili (yaani mwanzo wa uumbaji).” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Kwanza kabisa, hapakuwa na chochote ila Allaah (kisha Akaumba ‘Arshi Yake). ‘Arshi Yake ilikuwa juu ya maji, na Akaandika kila kitu katika Kitabu (cha mbinguni) na Akaumba mbingu na ardhi." Akanadi mtu mmoja kwa sauti: “Ee Ibn Huswayn! Ngamia wako jike amekimbia!” Nikaondoka mbio, lakini sikuweza kumuona ngamia wangu jike kwa sababu ya mazigazi. Naapa kwa Allaah! Natamani ningekuwa nimemuachilia mbali ngamia huyo jike (na sio kuacha kikao hicho). [Al-Bukhaariy]
Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Aliandika (kwenye Al-Lawh Al-Mahfuwdh) makadirio na hatima ya viumbe wote kabla ya kuumba mbingu na ardhi kwa miaka elfu khamsini, na 'Arsh Yake ilikuwa juu ya maji." [Muslim]
Na pia, Amesimulia Abu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mkono wa Allaah Umejaa (pomoni) na (kujaa kwake) hakuathiriki kwa kutoa mfululizo usiku na mchana.” Na Akasema tena: “Je, hamuoni kwa Alivyotoa kuanzia Alipoumba mbingu na ardhi? Hata hivyo, vilivyo mkononi Mwake havijapungua.” Na akasema tena: “Arshi Yake ipo juu ya maji, na katika Mkono Wake mwengine kuna Mizani (ya uadilifu), kwayo Hunyanyua (watu wengine) na kuwateremsha (wengine).” [Al-Bukhaariy Kitaab At-Tawhiyd]
[7] Hali Ya Makafiri Na Waumini Katika Kupatwa Dhara Na Kuondoshewa Neema:
Aayah hii ya Huwd (11:9), inyofuatia (11:10), inataja hali ya makafiri ambao hawana subira wanapopatwa na dhara au mitihani, au wanapoondoshewa Rehma na Neema za Allaah (سبحانه وتعالى), wala hawana shukurani kwa Allaah (سبحانه وتعالى) katika kila hali. Ama Waumini wanapofikwa na dhara au mitihani, wao ni kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah inayofuatia ya Huwd (11:10) kwamba wao ni wenye kuvuta subira na kuendelea kuthibitia katika imaan zao wakaendelea kutenda mema. Basi Waumini hao ni kama walivyosifiwa katika Hadiyth ifuatayo:
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ajabu ya hali ya Muumini kuwa mambo yake yote ni kheri; anapofikwa na furaha hushukuru na huwa kheri kwake, na anapofikwa na matatizo husubiri na huwa ni kheri kwake, na haiwi hivyo (sifa hiyo) ila kwa Muumini.”[Muslim]
Rejea pia Yuwnus (10:12), Az-Zumar (39:49), Ar-Ruwm (30: 33).
[9] Changamoto Makafiri Walete Mfano Wa Qur-aan Lakini Kamwe Hawatoweza!
Rejea Yuwnus (10:38), Al-Israa (17:88), Al-Baqarah (2:23-24), Atw-Twuwr (52:33-34). Rejea pia Al-An’aam (6:93) ambako kumetajwa waongo waliodai Unabii.
[11] Shahidi: Ni Jibriyl Au Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na Tawraat:
Je yule aliyekuwa kwenye hoja na baswiyrah (dalili bayana, ujuzi, umaizi) kutoka kwa Rabb wake katika kile anachokiamini na anachokilingania kwa Wahy ambao Allaah (سبحانه وتعالى) Ameuteremsha ushahidi huu, ukafuatiwa na hoja nyengine kutoka Kwake yenye kuutolea ushahidi; naye ni Jibril au ni Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na ukatiliwa nguvu, na dalili ya tatu kabla ya Qur-aan, nayo ni Tawraat kitabu alichoteremshiwa Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) chenye uongozi na Rehma kwa waliokiamini, basi (je yeye) ni kama yule ambaye hima yake ilikuwa ni maisha yenye mapambo na ya kutoweka? Hao wanaiamini hii Qur-aan, wanazifuata hukmu zake kivitendo. Na mwenye kuikanusha hii Qur-aan miongoni mwa wale waliojikusanya kumpinga Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), basi jazaa yake ni moto, hapana budi atauingia. Basi [ee Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)] usiwe na shaka juu ya Qur-aan kwamba inatoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى) baada ya dalili na hoja kuitolea ushahidi. Na ujue kwamba Dini hii ndio ya haki na ya ukweli unaotoka kwa Rabb wako, lakini wengi wa watu hawaamini wala hawayatendi yale wanayoamrishwa. Huu ni mwongozo jumuishi kwa Ummah wa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). [Tafsiyr Al-Muyassar]
[13] Sifa Za Allaah (سبحانه وتعالى) Ni Tawqiyfiyyah Na Hii Ndio ‘Aqiydah Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah:
Macho ya Allaah (سبحانه وتعالى) ni Sifa inayopaswa kuthibitishwa hivyo hivyo kama Anavyoitaja Mwenyewe bila ya Ta'twiyl (kuzipinga, kukanusha uwezekano), wala Tamthiyl (kumithilisha, kufafanisha, kulinganisha), wala Takyiyf (kuainisha maana na kuziulizia namna yake au kuuliza ni vipi Sifa hiyo ipo, kuchunguza ni kwa “namna gani” zimefungamana au kuambatana na Allaah), wala Tahriyf (kubadilisha maana, kupotosha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kutoa maana isiyo sahihi).
Hivyo basi Anaposema kuwa Anayo Macho, sisi ni lazima tuamini kuwa Anayo Macho. Na Anaposema kuwa Ana Masikio, sisi ni lazima tuamini kuwa Anayo Masikio. Anaposema kuwa Anayo Mikono, sisi ni lazima tuamini kuwa Anayo Mikono, na Anaposema kuwa Anayo Nafsi, na sisi ni lazima tuamini kuwa Anayo Nafsi. Na Anaposema kuwa Anao Wajihi, sisi ni lazima tuamini kuwa Anao Wajihi. Lakini Macho Yake au Masikio Yake au Mikono Yake, Au Nafsi Yake, au Wajihi Wake, hakuna kabisa mfano Wake kwa kiumbe chochote kile kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ﴿١١﴾
“Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.” [Ash-Shuwraa (42:11)]
Rejea zifuatazo zinataja baadhi ya Sifa Zake: Nafsi Yake: Aal-‘Imraan (3:28), Al-An’aam (6:12), (6:54), Wajihi Wake: Al-Qaswasw (28:88), Al-Baqarah (2:115) na Ar-Rahmaan (55:27). Mkono au Mikono Yake: Swaad (38:75), Al-Fat-h (48:10). Macho Yake: Suwrah hii ya Huwd (11:37), Al-Muuminuwn (23:27), Twaahaa (20:39). Kusikia na Kuona Kwake: Twaahaa (20:46).
[14] Nabiy Nuwh (عليه السّلام) Na Kizazi Kilobakia, Naye Ni Rasuli Wa Kwanza Ardhini Na Ni Baba Wa Wanaadam Baada Ya Nabiy Aadam (عليه السّلام):
Ijtihaad za Mufassiruwn wamesema kuwa watu walioamini wakapanda jahazini, walikuwa ni themanini. Miongoni mwao, walikuwa watoto watatu wa Nabiy Nuwh (عليه السّلام) ambao ni Saam, Haam na Yaafith. Na pia walikuwemo wake zao. Wengine wanasema walikuwa watu sabini na mbili, na wengine wamesema ni watu kumi.
Ibn ‘Abbaas amesema walikuwa watu themanini wakiwemo wanawake wao. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Basi hao ndio walioeneza tena kizazi cha wanaadam mpaka tukapatikana sisi na Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
ذُرِّيَّةَ مَنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَبْدًا شَكُورًا ﴿٣﴾
“Enyi kizazi cha ambao Tuliwabeba pamoja na Nuwh (katika jahazi). Hakika yeye alikuwa mja mwingi wa shukurani.” [Al-Israa (17:3)]
Rejea Asw-Swaaffaat (37:77) kwenye maelezo bayana na rejea zake mbalimbali.
Rejea Yuwnus (10:73), Maryam (19:58), Al-Muuminuwn (23:27), Nuwh (71:1).
[15] Kutaja Jina La Allaah Katika Kupanda Chombo:
Muislamu anapopanda chombo chochote anatakiwa kuanza kwa بِسْمِ اللَّـهِ . Na pia kuna duaa ya kupanda kipando, rejea Az-Zukhruf (43:13-14), na pia Al-Muuminuwn (23:28-28).
[16] Nabii Ambao Ahli Zao Walikuwa Makafiri:
Baadhi ya Nabii walikuwa na ahli zao ambao hawakuamini, bali walikanusha Risala, au walikuwa katika maasi, nao ni:
Nabiy Nuwh: Mwanawe kama ilivyotajwa katika Aayah hizi (11:42-47), na mkewe. Rejea Suwrah hii Aayah (11:40), kwani waliokusudiwa katika Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيْهِ الْقَوْلُ
“Isipokuwa (kafiri) ambaye imemtangulia kauli ya hukmu.”
Ni mke wa Nuhw ambaye hakuamini. [Tafsiyr Al-Muyassar, Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Nabiy Luutw: Rejea Suwrah hii Huwd (11:81), Al-Hijr (15:60), na Al-‘Ankabuwt (29: 33).
Nabiy Ibraahiym: Baba yake Aazar. Rejea Al-An’aam (6:74), na At-Tawbah (9:114).
Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم): ‘Amm yake Abu Twaalib. Alijaribu kumlingania katika Uislamu lakini alikataa, akafariki akiwa ni kafiri. Rejea Al-Qaswasw (28:56).
Hivyo basi, uhusiano wa undugu wa Kiislamu, ni undugu ulio na nguvu, imaan na mapenzi kulikoni uhusiano wa damu wa makafiri, na ndio maana Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema: Waumini ni ndugu. Rejea Al-Hujuraat (49:10).
[17] Maana Ya: Rabbi Yuko Juu Ya Njia Iliyonyooka:
Maana ya:
إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٦﴾
“Hakika Rabb wangu Yuko juu ya njia iliyonyooka.” [Huwd (11:56)]
Ina maana: Ana uadilifu, Ana Hikmah, Ana Himdi katika Qadhwaa na Qadar (Yaliyohukumiwa na Yaliyokadiriwa), katika Sharia Zake na Amri Zake, katika Jazaa (Malipo) Yake na Thawabu Zake, na Adhabu Zake, Matendo Yake hayaondoki kwenye Njia Iliyonyooka, ambayo Inahimidiwa Na Kutukuzwa. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[18] Swalaah Inafuta Madhambi Na Mema Yanaondosha Maovu:
Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) amesimulia: Mwanamume mmoja alimbusu mwanamke (kinyume na sharia) kisha akaenda kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kumhadithia. Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:
وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ﴿١١٤﴾
“Na simamisha Swalaah katika ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku, hakika mema yanaondosha maovu. Haya ni ukumbusho kwa wanaokumbuka.” [Huwd (11:114)]
Yule mtu akamuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): Je, hii (Aayah) ni kwa ajili yangu tu? Akajibu: “Ni kwa ajili ya watakaoitendea kazi katika ummah wangu.” [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
Pia Hadiyth nyenginezo kadhaa zimetaja kuhusu Muislamu anapotenda mema Allaah (سبحانه وتعالى) Humfutia makosa au madhambi yake, baadhi yake ni zifuatazo:
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mnaonaje ingelikuwa kuna mto mbele ya nyumba ya mmoja wenu kisha akawa anaoga humo kila siku mara tano, je atabakiwa na uchafu?” Wakasema: “Habakiwi na uchafu.” Akasema: “Hivyo ni mfano wa Swalaah ambazo Allaah hufuta madhambi kwazo.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Amesimulia ‘Uthmaan bin ‘Affaan (رضي الله عنه): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Atakayetawadha kwa ajili ya Swalaah, akafanya vizuri wudhuu wake, kisha akaenda kuswali Swalaah za fardhi, akaziswali pamoja na watu au jamaa au Msikitini, basi Allaah Atamfutia madhambi yake.” [Muslim]
Abu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Swalaah tano, na Ijumaa hadi Ijumaa, na Ramadhwaan hadi Ramadhwaan, zinafuta madhambi baina yake pindi madhambi makubwa yakiepukwa.” [Muslim]
Rejea pia Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى): Al-Furqaan (25:70), Al-Maaidah (5:65), Ar-Ra’d (13:22), Fusswilat (41:24), na Al-Muuminuwn (23:96).
يُوسُفْ
012-Yuwsuf
012-Yuwsuf: Utangulizi Wa Suwrah [149]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿١﴾
1. Alif Laam Raa.[1] Hizi ni Aayaat za Kitabu kinachobainisha.
إِنَّا أَنزَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٢﴾
2. Hakika Sisi Tumekiteremsha kikisomeka kwa (lugha ya) Kiarabu ili mufahamu.
نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ بِمَا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ هَـٰذَا الْقُرْآنَ وَإِن كُنتَ مِن قَبْلِهِ لَمِنَ الْغَافِلِينَ ﴿٣﴾
3. Sisi Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) simulizi nzuri kabisa katika Tuliyokufunulia Wahy hii Qur-aan. Na japokuwa kabla yake ulikuwa miongoni mwa wasiojua.[2]
إِذْ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ إِنِّي رَأَيْتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوْكَبًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ رَأَيْتُهُمْ لِي سَاجِدِينَ ﴿٤﴾
4. Pale Yuwsuf[3] alipomwambia baba yake: Ee baba yangu kipenzi! Hakika mimi nimeona (njozini)[4] nyota kumi na moja na jua na mwezi,[5] nimeziona zikinisujudia.
قَالَ يَا بُنَيَّ لَا تَقْصُصْ رُؤْيَاكَ عَلَىٰ إِخْوَتِكَ فَيَكِيدُوا لَكَ كَيْدًا ۖ إِنَّ الشَّيْطَانَ لِلْإِنسَانِ عَدُوٌّ مُّبِينٌ﴿٥﴾
5. Akasema: Ee mwanangu! Usisimulie njozi yako kwa kaka zako watakupangia njama. Hakika shaytwaan kwa mwanaadam ni adui bayana.
وَكَذَٰلِكَ يَجْتَبِيكَ رَبُّكَ وَيُعَلِّمُكَ مِن تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ وَيُتِمُّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَعَلَىٰ آلِ يَعْقُوبَ كَمَا أَتَمَّهَا عَلَىٰ أَبَوَيْكَ مِن قَبْلُ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٦﴾
6. Na hivyo ndivyo Atakavyokuteua Rabb wako na Atakufunza tafsiri ya khabari (kuhusu ndoto na matukio) na Atakutimizia Neema Yake juu yako, na juu ya kizazi cha Ya’quwb, kama Alivyoitimiza kabla juu ya baba zako wawili; Ibraahiym na Is-haaq. Hakika Rabb wako Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
لَّقَدْ كَانَ فِي يُوسُفَ وَإِخْوَتِهِ آيَاتٌ لِّلسَّائِلِينَ﴿٧﴾
7. Kwa yakini kuna Aayaat (Mazingatio, Dalili, Mawaidha) katika (kisa cha) Yuwsuf na kaka zake kwa waulizao.
إِذْ قَالُوا لَيُوسُفُ وَأَخُوهُ أَحَبُّ إِلَىٰ أَبِينَا مِنَّا وَنَحْنُ عُصْبَةٌ إِنَّ أَبَانَا لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٨﴾
8. Pale waliposema: Bila shaka Yuwsuf na ndugu yake (shakiki Binyaamiyn)[6] ni vipenzi zaidi kwa baba yetu kuliko sisi, na hali sisi ni kundi (lenye idadi kubwa), hakika baba yetu yumo katika makosa ya bayana.
اقْتُلُوا يُوسُفَ أَوِ اطْرَحُوهُ أَرْضًا يَخْلُ لَكُمْ وَجْهُ أَبِيكُمْ وَتَكُونُوا مِن بَعْدِهِ قَوْمًا صَالِحِينَ﴿٩﴾
9. Muueni Yuwsuf, au mtupilieni mbali katika ardhi (ya mbali) ili uso wa baba yenu ukuelekeeni nyinyi na muwe baada ya hapo watu Swalihina.
قَالَ قَائِلٌ مِّنْهُمْ لَا تَقْتُلُوا يُوسُفَ وَأَلْقُوهُ فِي غَيَابَتِ الْجُبِّ يَلْتَقِطْهُ بَعْضُ السَّيَّارَةِ إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ﴿١٠﴾
10. Akasema msemaji miongoni mwao: Msimuue Yuwsuf, bali mtumbukizeni katika kisima kirefu watamwokota baadhi ya wasafiri, ikiwa nyinyi ni wenye (kuazimia) kufanya.
قَالُوا يَا أَبَانَا مَا لَكَ لَا تَأْمَنَّا عَلَىٰ يُوسُفَ وَإِنَّا لَهُ لَنَاصِحُونَ﴿١١﴾
11. Wakasema: Ee baba yetu! Una nini hata hutuamini kwa Yuwsuf, wakati sisi tunampendelea kila jema?
أَرْسِلْهُ مَعَنَا غَدًا يَرْتَعْ وَيَلْعَبْ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ﴿١٢﴾
12. Mwache atoke pamoja nasi kesho, ale atakacho na acheze, na hakika sisi tutamhifadhi.
قَالَ إِنِّي لَيَحْزُنُنِي أَن تَذْهَبُوا بِهِ وَأَخَافُ أَن يَأْكُلَهُ الذِّئْبُ وَأَنتُمْ عَنْهُ غَافِلُونَ﴿١٣﴾
13. Akasema: Hakika mimi inanihuzunisha kwamba nyinyi mwende naye, na nakhofu asije kuliwa na mbwa mwitu, nanyi muwe mmeghafilika naye.
قَالُوا لَئِنْ أَكَلَهُ الذِّئْبُ وَنَحْنُ عُصْبَةٌ إِنَّا إِذًا لَّخَاسِرُونَ﴿١٤﴾
14. Wakasema: Ikiwa mbwa mwitu atamla na hali sisi ni kikundi (cha idadi kubwa na nguvu) hakika sisi hapo bila shaka tutakuwa watu wasiofaa kwa lolote.
فَلَمَّا ذَهَبُوا بِهِ وَأَجْمَعُوا أَن يَجْعَلُوهُ فِي غَيَابَتِ الْجُبِّ ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِ لَتُنَبِّئَنَّهُم بِأَمْرِهِمْ هَـٰذَا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ﴿١٥﴾
15. Basi walipokwenda naye, na wakakubaliana wamtie katika kisima kirefu, Tulimtia ilhamu (Yuwsuf) kwamba bila shaka utakuja kuwajulisha jambo lao hili wala wao hawahisi.
وَجَاءُوا أَبَاهُمْ عِشَاءً يَبْكُونَ﴿١٦﴾
16. Wakaja kwa baba yao usiku wanalia.
قَالُوا يَا أَبَانَا إِنَّا ذَهَبْنَا نَسْتَبِقُ وَتَرَكْنَا يُوسُفَ عِندَ مَتَاعِنَا فَأَكَلَهُ الذِّئْبُ ۖ وَمَا أَنتَ بِمُؤْمِنٍ لَّنَا وَلَوْ كُنَّا صَادِقِينَ﴿١٧﴾
17. Wakasema: Ee baba yetu! Hakika sisi tulikwenda kushindana mbio na tulimwacha Yuwsuf kwenye vitu vyetu, basi mbwa mwitu akamla. Nawe hutotuamini japo ni wakweli.
وَجَاءُوا عَلَىٰ قَمِيصِهِ بِدَمٍ كَذِبٍ ۚ قَالَ بَلْ سَوَّلَتْ لَكُمْ أَنفُسُكُمْ أَمْرًا ۖ فَصَبْرٌ جَمِيلٌ ۖ وَاللَّـهُ الْمُسْتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ﴿١٨﴾
18. Wakaja na kanzu yake ikiwa na damu ya uongo. (Baba yao) akasema: Bali nafsi zenu zimekushawishini jambo. Basi subira njema, na Allaah Ni Mwenye kuombwa msaada juu ya mnayoyaeleza.
وَجَاءَتْ سَيَّارَةٌ فَأَرْسَلُوا وَارِدَهُمْ فَأَدْلَىٰ دَلْوَهُ ۖ قَالَ يَا بُشْرَىٰ هَـٰذَا غُلَامٌ ۚ وَأَسَرُّوهُ بِضَاعَةً ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِمَا يَعْمَلُونَ﴿١٩﴾
19. Ukaja msafara, wakamtuma mtekaji maji wao, naye akatumbukiza ndoo yake. Akasema: Eh, bishara nzuri hii! Huyu ni ghulamu! Na wakamficha kumfanya bidhaa. Na Allaah Ni Mjuzi kwa yale wanayoyatenda.
وَشَرَوْهُ بِثَمَنٍ بَخْسٍ دَرَاهِمَ مَعْدُودَةٍ وَكَانُوا فِيهِ مِنَ الزَّاهِدِينَ﴿٢٠﴾
20. Wakamuuza kwa thamani ndogo mno ya dirham za kuhesabika, na walikuwa hawana hamu ya kubaki naye.
وَقَالَ الَّذِي اشْتَرَاهُ مِن مِّصْرَ لِامْرَأَتِهِ أَكْرِمِي مَثْوَاهُ عَسَىٰ أَن يَنفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا ۚ وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي الْأَرْضِ وَلِنُعَلِّمَهُ مِن تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ ۚ وَاللَّـهُ غَالِبٌ عَلَىٰ أَمْرِهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٢١﴾
21. Na yule (kigogo au waziri)[7] aliyemnunua huko Misri alimwambia mke wake: Mkirimu makazi yake, asaa akatufaa au tutamchukua kama ni mwanetu. Na hivyo ndivyo Tulivyommakinisha Yuwsuf katika ardhi na ili Tumfunze tafsiri za khabari (za ndoto na matukio). Na Allaah Ni Mwenye Kushinda juu ya Jambo Lake, lakini watu wengi hawajui.
وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ﴿٢٢﴾
22. Na (Yuwsuf) alipofikia umri wa kupevuka, Tulimpa hikmah na ilimu. Na hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.
وَرَاوَدَتْهُ الَّتِي هُوَ فِي بَيْتِهَا عَن نَّفْسِهِ وَغَلَّقَتِ الْأَبْوَابَ وَقَالَتْ هَيْتَ لَكَ ۚ قَالَ مَعَاذَ اللَّـهِ ۖ إِنَّهُ رَبِّي أَحْسَنَ مَثْوَايَ ۖ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ﴿٢٣﴾
23. Na yule mwanamke ambaye yeye (Yuwsuf) alikuwa katika nyumba yake alimtongoza kinyume na nafsi yake, na akafunga milango na kumwambia: Haya njoo! (Yuwsuf) akasema: Najikinga kwa Allaah! Hakika yeye bwana wangu[8] amenifanyia makazi mazuri. Hakika madhalimu hawafaulu.
وَلَقَدْ هَمَّتْ بِهِ ۖ وَهَمَّ بِهَا لَوْلَا أَن رَّأَىٰ بُرْهَانَ رَبِّهِ ۚ كَذَٰلِكَ لِنَصْرِفَ عَنْهُ السُّوءَ وَالْفَحْشَاءَ ۚ إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُخْلَصِينَ﴿٢٤﴾
24. Na kwa yakini alimtamani (Yuwsuf) (kwa ari na azima) na (Yuwsuf) angelimtamani (kwa maumbile ya kibinaadam) lau kwamba asingeliona buruhani (ishara) kutoka kwa Rabb wake. Tumefanya hayo ili Tumwepushe na uovu na machafu. Hakika yeye ni miongoni mwa Waja Wetu waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.
وَاسْتَبَقَا الْبَابَ وَقَدَّتْ قَمِيصَهُ مِن دُبُرٍ وَأَلْفَيَا سَيِّدَهَا لَدَى الْبَابِ ۚ قَالَتْ مَا جَزَاءُ مَنْ أَرَادَ بِأَهْلِكَ سُوءًا إِلَّا أَن يُسْجَنَ أَوْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٢٥﴾
25. Wakakimbilia mlangoni wote wawili (Yuwsuf awahi kutoka nje na yeye awahi kumzuia), akairarua kanzu yake (Yuwsuf) kwa nyuma (katika patashika hiyo), na wakamkuta bwana (mume) wake mlangoni. (Mke wa ‘aziyz) akasema: Hakuna jazaa ya anayetaka kufanya uovu na ahli wako isipokuwa kufungwa jela au adhabu iumizayo.
قَالَ هِيَ رَاوَدَتْنِي عَن نَّفْسِي ۚ وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِّنْ أَهْلِهَا إِن كَانَ قَمِيصُهُ قُدَّ مِن قُبُلٍ فَصَدَقَتْ وَهُوَ مِنَ الْكَاذِبِينَ﴿٢٦﴾
26. (Yuwsuf) akasema: Yeye ndiye aliyenitongoza kinyume na nafsi yangu. Na akashuhudia shahidi miongoni mwa ahli zake mwanamke (akasema): Ikiwa kanzu yake imechanwa mbele, basi mwanamke amesema kweli, naye (Yuwsuf) ni miongoni mwa waongo.
وَإِن كَانَ قَمِيصُهُ قُدَّ مِن دُبُرٍ فَكَذَبَتْ وَهُوَ مِنَ الصَّادِقِينَ﴿٢٧﴾
27. Na ikiwa kanzu yake imechanwa nyuma, basi mwanamke amesema uongo, naye (Yuwsuf) ni miongoni mwa wakweli.
فَلَمَّا رَأَىٰ قَمِيصَهُ قُدَّ مِن دُبُرٍ قَالَ إِنَّهُ مِن كَيْدِكُنَّ ۖ إِنَّ كَيْدَكُنَّ عَظِيمٌ﴿٢٨﴾
28. Basi (mumewe) alipoona kanzu yake imechanwa nyuma, alisema: Hakika hii ni katika vitimbi vyenu wanawake. Hakika vitimbi vyenu wanawake ni vikubwa mno.
يُوسُفُ أَعْرِضْ عَنْ هَـٰذَا ۚ وَاسْتَغْفِرِي لِذَنبِكِ ۖ إِنَّكِ كُنتِ مِنَ الْخَاطِئِينَ﴿٢٩﴾
29. (Ee) Yuwsuf yaachilie mbali haya. Na (wewe) mwanamke omba maghfirah kwa ajili ya dhambi yako. Hakika wewe ulikuwa miongoni mwa wenye hatia.
وَقَالَ نِسْوَةٌ فِي الْمَدِينَةِ امْرَأَتُ الْعَزِيزِ تُرَاوِدُ فَتَاهَا عَن نَّفْسِهِ ۖ قَدْ شَغَفَهَا حُبًّا ۖ إِنَّا لَنَرَاهَا فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٣٠﴾
30. Na wanawake katika mji ule wakasema: Mke wa ‘aziyz anamtongoza kijana wake kinyume na nafsi yake. Kijana kashammaliza kwa mapenzi, haoni hasikii. Hakika sisi tunamuona yumo katika upotofu bayana.
فَلَمَّا سَمِعَتْ بِمَكْرِهِنَّ أَرْسَلَتْ إِلَيْهِنَّ وَأَعْتَدَتْ لَهُنَّ مُتَّكَأً وَآتَتْ كُلَّ وَاحِدَةٍ مِّنْهُنَّ سِكِّينًا وَقَالَتِ اخْرُجْ عَلَيْهِنَّ ۖ فَلَمَّا رَأَيْنَهُ أَكْبَرْنَهُ وَقَطَّعْنَ أَيْدِيَهُنَّ وَقُلْنَ حَاشَ لِلَّـهِ مَا هَـٰذَا بَشَرًا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا مَلَكٌ كَرِيمٌ﴿٣١﴾
31. (Mke wa ‘aziyz) aliposikia hila zao (za kumchafulia jina zaidi), aliwaalika na akawaandalia hafla (na matakia), na akampa kila mmoja wao kisu. Kisha akasema: Tokeza mbele yao. Basi walipomuona (Yuwsuf) walimpa haiba na utukuzo, wakajikatakata mikono yao, na wakasema: Haasha li-LLaah! (Ametakasika Allaah Mkamilifu wa Kuumba). Huyu si mtu! Hakuwa huyu ila ni Malaika mtukufu.
قَالَتْ فَذَٰلِكُنَّ الَّذِي لُمْتُنَّنِي فِيهِ ۖ وَلَقَدْ رَاوَدتُّهُ عَن نَّفْسِهِ فَاسْتَعْصَمَ ۖ وَلَئِن لَّمْ يَفْعَلْ مَا آمُرُهُ لَيُسْجَنَنَّ وَلَيَكُونًا مِّنَ الصَّاغِرِينَ﴿٣٢﴾
32. Akasema: Basi huyo ndiye mliyekuwa mkinilaumia. Na kwa yakini nilimtamani kinyume na nafsi yake, akajilinda. Na kama hatofanya ninalomuamrisha, basi bila shaka atafungwa jela, na bila shaka atakuwa miongoni mwa waliodhalilishwa.
قَالَ رَبِّ السِّجْنُ أَحَبُّ إِلَيَّ مِمَّا يَدْعُونَنِي إِلَيْهِ ۖ وَإِلَّا تَصْرِفْ عَنِّي كَيْدَهُنَّ أَصْبُ إِلَيْهِنَّ وَأَكُن مِّنَ الْجَاهِلِينَ﴿٣٣﴾
33. (Yuwsuf) akasema: Ee Rabb wangu! Nastahabu zaidi jela kuliko yale wanayoniitia. Na Usiponiepusha na vitimbi vyao nitaelemea kwao na nitakuwa miongoni mwa majahili.
فَاسْتَجَابَ لَهُ رَبُّهُ فَصَرَفَ عَنْهُ كَيْدَهُنَّ ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿٣٤﴾
34. Basi Rabb wake Akamuitikia na Akamuepusha na vitimbi vyao. Hakika Yeye Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
ثُمَّ بَدَا لَهُم مِّن بَعْدِ مَا رَأَوُا الْآيَاتِ لَيَسْجُنُنَّهُ حَتَّى حِينٍ﴿٣٥﴾
35. Kisha ikawadhihirikia baada ya kuona Aayaat (Dalili, Vielelezo) [vya kumtoa hatiani] kuwa wamfunge jela kwa muda fulani.
وَدَخَلَ مَعَهُ السِّجْنَ فَتَيَانِ ۖ قَالَ أَحَدُهُمَا إِنِّي أَرَانِي أَعْصِرُ خَمْرًا ۖ وَقَالَ الْآخَرُ إِنِّي أَرَانِي أَحْ مِلُ فَوْقَ رَأْسِي خُبْزًا تَأْكُلُ الطَّيْرُ مِنْهُ ۖ نَبِّئْنَا بِتَأْوِيلِهِ ۖ إِنَّا نَرَاكَ مِنَ الْمُحْسِنِينَ﴿٣٦﴾
36. Wakaingia pamoja naye jela vijana wawili. Mmoja wao akasema: Hakika mimi nimeona ndotoni kuwa nakamua (zabibu ziwe) mvinyo. Na mwengine akasema: Hakika mimi nimeona ndotoni nabeba juu ya kichwa changu (kapu la) mikate wanaila ndege humo. Tujulishe tafsiri yake, hakika sisi tunakuona ni miongoni mwa wafanyao ihsaan.
قَالَ لَا يَأْتِيكُمَا طَعَامٌ تُرْزَقَانِهِ إِلَّا نَبَّأْتُكُمَا بِتَأْوِيلِهِ قَبْلَ أَن يَأْتِيَكُمَا ۚ ذَٰلِكُمَا مِمَّا عَلَّمَنِي رَبِّي ۚ إِنِّي تَرَكْتُ مِلَّةَ قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ﴿٣٧﴾
37. (Yuwsuf) akasema: Hakitokufikieni chakula chochote mtakachopewa kula isipokuwa nitakujulisheni wasifu wake kabla hakijakufikieni. Hayo nitakayowafasiria ni katika Aliyonifunza Rabb wangu. Hakika mimi nimeacha mila ya watu wasiomwamini Allaah na wao ni wenye kuikanusha Aakhirah.
وَاتَّبَعْتُ مِلَّةَ آبَائِي إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ مَا كَانَ لَنَا أَن نُّشْرِكَ بِاللَّـهِ مِن شَيْءٍ ۚ ذَٰلِكَ مِن فَضْلِ اللَّـهِ عَلَيْنَا وَعَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ﴿٣٨﴾
38. Na nimefuata Dini ya baba zangu Ibraahiym, na Is-haaq na Ya’quwb. Haikutupasa kumshirikisha Allaah na kitu chochote. Hilo (la kutomshirikisha) ni katika Fadhila za Allaah juu yetu na juu ya watu, lakini watu wengi hawashukuru.
يَا صَاحِبَيِ السِّجْنِ أَأَرْبَابٌ مُّتَفَرِّقُونَ خَيْرٌ أَمِ اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ﴿٣٩﴾
39. Enyi masahibu wangu wawili wa jela! Je, miola wengi wanaofarakana ni bora au Allaah Mmoja Pekee, Asiyepingika?
مَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا أَسْمَاءً سَمَّيْتُمُوهَا أَنتُمْ وَآبَاؤُكُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ بِهَا مِن سُلْطَانٍ ۚ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ ۚ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٤٠﴾
40. Hamuabudu pasi Naye (Allaah) isipokuwa majina tu mmeyaita nyinyi na baba zenu, Hakuyateremshia Allaah mamlaka yoyote. Hakuna hukumu isipokuwa ya Allaah. Ameamrisha kwamba msiabudu chochote isipokuwa Yeye Pekee. Hiyo ndio Dini iliyonyooka, lakini watu wengi hawajui.
يَا صَاحِبَيِ السِّجْنِ أَمَّا أَحَدُكُمَا فَيَسْقِي رَبَّهُ خَمْرًا ۖ وَأَمَّا الْآخَرُ فَيُصْلَبُ فَتَأْكُلُ الطَّيْرُ مِن رَّأْسِهِ ۚ قُضِيَ الْأَمْرُ الَّذِي فِيهِ تَسْتَفْتِيَانِ﴿٤١﴾
41. Enyi masahibu wangu wawili wa jela! Ama mmoja wenu atamnywesha bwana wake mvinyo. Na ama mwengine atasulubiwa, na ndege watakula kichwani mwake. Limeshahukumiwa jambo ambalo mnaliulizia.
وَقَالَ لِلَّذِي ظَنَّ أَنَّهُ نَاجٍ مِّنْهُمَا اذْكُرْنِي عِندَ رَبِّكَ فَأَنسَاهُ الشَّيْطَانُ ذِكْرَ رَبِّهِ فَلَبِثَ فِي السِّجْنِ بِضْعَ سِنِينَ﴿٤٢﴾
42. (Yuwsuf) akasema kumwambia yule aliyejua kuwa ataokoka miongoni mwa wale wawili: Nikumbuke mbele ya bwana wako. Lakini shaytwaan alimsahaulisha kumkumbuka kwa bwana wake. Basi akabakia jela miaka kadhaa.
وَقَالَ الْمَلِكُ إِنِّي أَرَىٰ سَبْعَ بَقَرَاتٍ سِمَانٍ يَأْكُلُهُنَّ سَبْعٌ عِجَافٌ وَسَبْعَ سُنبُلَاتٍ خُضْرٍ وَأُخَرَ يَابِسَاتٍ ۖ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ أَفْتُونِي فِي رُؤْيَايَ إِن كُنتُمْ لِلرُّؤْيَا تَعْبُرُونَ﴿٤٣﴾
43. (Kisha) na mfalme akasema: Hakika mimi naona ndotoni ng’ombe saba wanene wanaliwa na ng’ombe saba waliokonda, na mashuke saba ya kijani na mengineyo (saba) yabisi. Enyi wakuu! Nifutuni kuhusu ndoto yangu, mkiwa ni wenye kuagua ndoto.
قَالُوا أَضْغَاثُ أَحْلَامٍ ۖ وَمَا نَحْنُ بِتَأْوِيلِ الْأَحْلَامِ بِعَالِمِينَ﴿٤٤﴾
44. Wakasema: Mkorogano wa ndoto! Nasi si wenye kujua kufasiri ndoto.
وَقَالَ الَّذِي نَجَا مِنْهُمَا وَادَّكَرَ بَعْدَ أُمَّةٍ أَنَا أُنَبِّئُكُم بِتَأْوِيلِهِ فَأَرْسِلُونِ﴿٤٥﴾
45. Akasema yule aliyeokoka kati ya wale wawili na akakumbuka baada ya muda: Mimi nitakujulisheni kuhusu tafsiri yake. Basi, nitumeni (kwa Yuwsuf nikamuulize).
يُوسُفُ أَيُّهَا الصِّدِّيقُ أَفْتِنَا فِي سَبْعِ بَقَرَاتٍ سِمَانٍ يَأْكُلُهُنَّ سَبْعٌ عِجَافٌ وَسَبْعِ سُنبُلَاتٍ خُضْرٍ وَأُخَرَ يَابِسَاتٍ لَّعَلِّي أَرْجِعُ إِلَى النَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَعْلَمُونَ﴿٤٦﴾
46. Yuwsuf! Ee mkweli wa dhati! Tufutu kuhusiana na ng’ombe saba wanene wanaliwa na ng’ombe saba waliokonda, na mashuke saba ya kijani na mengineyo (saba) yabisi, ili nirejee kwa watu ili wapate kujua.
قَالَ تَزْرَعُونَ سَبْعَ سِنِينَ دَأَبًا فَمَا حَصَدتُّمْ فَذَرُوهُ فِي سُنبُلِهِ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّا تَأْكُلُونَ﴿٤٧﴾
47. Akasema: Mtalima miaka saba mfululizo bila kusita. Mtakachokivuna kiacheni katika mashuke yake isipokuwa kichache mtakachokula.
ثُمَّ يَأْتِي مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ سَبْعٌ شِدَادٌ يَأْكُلْنَ مَا قَدَّمْتُمْ لَهُنَّ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّا تُحْصِنُونَ﴿٤٨﴾
48. Kisha itakuja baada ya hapo (miaka) saba ya shida itakayokula vile mlivyovitanguliza kuviweka kwa ajili yao isipokuwa kidogo katika vile mtakavyoweka akiba.
ثُمَّ يَأْتِي مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ عَامٌ فِيهِ يُغَاثُ النَّاسُ وَفِيهِ يَعْصِرُونَ﴿٤٩﴾
49. Kisha utakuja baada ya hapo mwaka humo watu watasaidiwa kwa kunyweshewa mvua na humo watakamua (vya kukamuliwa).
وَقَالَ الْمَلِكُ ائْتُونِي بِهِ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُ الرَّسُولُ قَالَ ارْجِعْ إِلَىٰ رَبِّكَ فَاسْأَلْهُ مَا بَالُ النِّسْوَةِ اللَّاتِي قَطَّعْنَ أَيْدِيَهُنَّ ۚ إِنَّ رَبِّي بِكَيْدِهِنَّ عَلِيمٌ﴿٥٠﴾
50. Mfalme akasema: Nileteeni (Yuwsuf). Basi (Yuwsuf) alipojiwa na mjumbe alisema: Rejea kwa bwana wako umuulize nini mkasa wa wanawake waliojikata mikono yao. Hakika Rabb wangu kwa vitimbi vyao Ni Mjuzi.
قَالَ مَا خَطْبُكُنَّ إِذْ رَاوَدتُّنَّ يُوسُفَ عَن نَّفْسِهِ ۚ قُلْنَ حَاشَ لِلَّـهِ مَا عَلِمْنَا عَلَيْهِ مِن سُوءٍ ۚ قَالَتِ امْرَأَتُ الْعَزِيزِ الْآنَ حَصْحَصَ الْحَقُّ أَنَا رَاوَدتُّهُ عَن نَّفْسِهِ وَإِنَّهُ لَمِنَ الصَّادِقِينَ﴿٥١﴾
51. (Mfalme) akasema: Mlikuwa na jambo gani kubwa mlipomtongoza Yuwsuf kinyume na nafsi yake? Wakasema: Haasha liLlaah! (Ametakasika Allaah Mkamilifu wa Kuumba). Hatukuona uovu wowote kwake. Mke wa ‘aziyz akasema: Hivi sasa umefichuka ukweli! Mimi nilimtongoza kinyume na nafsi yake. Na hakika yeye bila shaka ni miongoni mwa wakweli.
ذَٰلِكَ لِيَعْلَمَ أَنِّي لَمْ أَخُنْهُ بِالْغَيْبِ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي كَيْدَ الْخَائِنِينَ﴿٥٢﴾
52. (Yuwsuf akasema:) Nimekiri hilo ili (‘aziyz) apate kujua kwamba mimi sikumfanyia khiyana kwa siri, na kwamba Allaah Haongozi hila za makhaini.
وَمَا أُبَرِّئُ نَفْسِي ۚ إِنَّ النَّفْسَ لَأَمَّارَةٌ بِالسُّوءِ إِلَّا مَا رَحِمَ رَبِّي ۚ إِنَّ رَبِّي غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٥٣﴾
53. Nami siitoi hatiani nafsi yangu. Hakika nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu[9] isipokuwa ambayo Rabb wangu Ameirehemu. Hakika Rabb wangu Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَقَالَ الْمَلِكُ ائْتُونِي بِهِ أَسْتَخْلِصْهُ لِنَفْسِي ۖ فَلَمَّا كَلَّمَهُ قَالَ إِنَّكَ الْيَوْمَ لَدَيْنَا مَكِينٌ أَمِينٌ ﴿٥٤﴾
54. Na mfalme akasema: Nileteeni (Yuwsuf) nimteue makhsusi kwangu. Basi aliposema naye, akasema: Hakika wewe leo kwetu umetamakani kwa cheo na umekuwa muaminiwa.
قَالَ اجْعَلْنِي عَلَىٰ خَزَائِنِ الْأَرْضِ ۖ إِنِّي حَفِيظٌ عَلِيمٌ ﴿٥٥﴾
55. (Yuwsuf) akasema: Niteue niwe msimamizi wa mapato ya ardhi, hakika mimi ni mhifadhi mjuzi.
وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي الْأَرْضِ يَتَبَوَّأُ مِنْهَا حَيْثُ يَشَاءُ ۚ نُصِيبُ بِرَحْمَتِنَا مَن نَّشَاءُ ۖ وَلَا نُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٦﴾
56. Na hivyo ndivyo Tulivyommakinisha Yuwsuf katika ardhi, anakaa humo popote atakapo. Tunamfikishia Rehma Yetu Tumtakaye, na wala Hatupotezi ujira wa watendao ihsaan.
وَلَأَجْرُ الْآخِرَةِ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ ﴿٥٧﴾
57. Na bila shaka ujira wa Aakhirah ni bora zaidi kwa wale walioamini na wakawa na taqwa.
وَجَاءَ إِخْوَةُ يُوسُفَ فَدَخَلُوا عَلَيْهِ فَعَرَفَهُمْ وَهُمْ لَهُ مُنكِرُونَ ﴿٥٨﴾
58. Wakaja kaka zake Yuwsuf wakaingia kwake, yeye akawatambua, lakini wao hawakumtambua.
وَلَمَّا جَهَّزَهُم بِجَهَازِهِمْ قَالَ ائْتُونِي بِأَخٍ لَّكُم مِّنْ أَبِيكُمْ ۚ أَلَا تَرَوْنَ أَنِّي أُوفِي الْكَيْلَ وَأَنَا خَيْرُ الْمُنزِلِينَ﴿٥٩﴾
59. Na alipowatayarishia mizigo yao akasema: Nileteeni ndugu yenu kwa baba yenu. Je, hamuoni kwamba mimi natimiza kikamilifu kipimo nami ni mbora wa wenye kukirimu?
فَإِن لَّمْ تَأْتُونِي بِهِ فَلَا كَيْلَ لَكُمْ عِندِي وَلَا تَقْرَبُونِ ﴿٦٠﴾
60. Msiponijia naye, basi hamtokuwa na kipimo kwangu wala msinikurubie.
قَالُوا سَنُرَاوِدُ عَنْهُ أَبَاهُ وَإِنَّا لَفَاعِلُونَ ﴿٦١﴾
61. Wakasema: Tutamrairai baba yake aturuhusu tutoke naye na bila shaka tutafanya.
وَقَالَ لِفِتْيَانِهِ اجْعَلُوا بِضَاعَتَهُمْ فِي رِحَالِهِمْ لَعَلَّهُمْ يَعْرِفُونَهَا إِذَا انقَلَبُوا إِلَىٰ أَهْلِهِمْ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٦٢﴾
62. (Yuwsuf) akawaambia watumishi wake: Wekeni bidhaa zao katika mizigo yao, watapata kuzitambua watakaporudi kwa ahli zao, huenda wakarejea.
فَلَمَّا رَجَعُوا إِلَىٰ أَبِيهِمْ قَالُوا يَا أَبَانَا مُنِعَ مِنَّا الْكَيْلُ فَأَرْسِلْ مَعَنَا أَخَانَا نَكْتَلْ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ﴿٦٣﴾
63. Waliporejea kwa baba yao, walisema: Ee baba yetu! Tumenyimwa kipimo, basi mwachie ndugu yetu atoke pamoja nasi tupate kupimiwa, na sisi bila shaka tutamhifadhi.
قَالَ هَلْ آمَنُكُمْ عَلَيْهِ إِلَّا كَمَا أَمِنتُكُمْ عَلَىٰ أَخِيهِ مِن قَبْلُ ۖ فَاللَّـهُ خَيْرٌ حَافِظًا ۖ وَهُوَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ ﴿٦٤﴾
64. Akasema: Vipi nimwaminishe kwenu kama nilivyokuaminini kwa kaka yake kabla? Basi Allaah ni Ni Mbora wa wenye kuhifadhi. Naye Ni Mbora zaidi wa Kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu.
وَلَمَّا فَتَحُوا مَتَاعَهُمْ وَجَدُوا بِضَاعَتَهُمْ رُدَّتْ إِلَيْهِمْ ۖ قَالُوا يَا أَبَانَا مَا نَبْغِي ۖ هَـٰذِهِ بِضَاعَتُنَا رُدَّتْ إِلَيْنَا ۖ وَنَمِيرُ أَهْلَنَا وَنَحْفَظُ أَخَانَا وَنَزْدَادُ كَيْلَ بَعِيرٍ ۖ ذَٰلِكَ كَيْلٌ يَسِيرٌ ﴿٦٥﴾
65. Walipofungua mizigo yao, walikuta bidhaa zao zimerudishwa kwao. Wakasema: Ee baba yetu! Tunataka nini zaidi? Hizi bidhaa zetu tumerejeshewa, nasi tutawaletea chakula ahli zetu, na tutamhifadhi ndugu yetu, na tutapata ziada ya shehena ya ngamia. Hicho ni kipimo chepesi.
قَالَ لَنْ أُرْسِلَهُ مَعَكُمْ حَتَّىٰ تُؤْتُونِ مَوْثِقًا مِّنَ اللَّـهِ لَتَأْتُنَّنِي بِهِ إِلَّا أَن يُحَاطَ بِكُمْ ۖ فَلَمَّا آتَوْهُ مَوْثِقَهُمْ قَالَ اللَّـهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَكِيلٌ ﴿٦٦﴾
66. Akasema: Sitompeleka pamoja nanyi mpaka mnipe Ahadi ya Allaah kwamba lazima nyinyi mtamrudisha kwangu isipokuwa ikiwa mmezungukwa. Basi walipompa ahadi yao, akasema: Allaah kwa tuyasemayo Ni Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.
وَقَالَ يَا بَنِيَّ لَا تَدْخُلُوا مِن بَابٍ وَاحِدٍ وَادْخُلُوا مِنْ أَبْوَابٍ مُّتَفَرِّقَةٍ ۖ وَمَا أُغْنِي عَنكُم مِّنَ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ ۖ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّـهِ ۖ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ ۖوَعَلَيْهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُتَوَكِّلُونَ ﴿٦٧﴾
67. Na akasema: Enyi wanangu! Msiingie kupitia mlango mmoja, bali ingieni kupitia milango tofauti. Na mimi siwezi kukufaeni chochote kwa Alilolipanga Allaah. Hapana hukumu isipokuwa ya Allaah tu. Kwake natawakali. Na Kwake watawakali wanaotawakali.
وَلَمَّا دَخَلُوا مِنْ حَيْثُ أَمَرَهُمْ أَبُوهُم مَّا كَانَ يُغْنِي عَنْهُم مِّنَ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ إِلَّا حَاجَةً فِي نَفْسِ يَعْقُوبَ قَضَاهَا ۚ وَإِنَّهُ لَذُو عِلْمٍ لِّمَا عَلَّمْنَاهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٦٨﴾
68. Na walipoingia kwa namna alivyowaamrisha baba yao, haikuwafaa kitu kwa Allaah isipokuwa haja iliyokuwa katika nafsi ya Ya’quwb aliyoitimiza.[10] Na hakika yeye alikuwa mwenye ilimu Tuliyomfunza, lakini watu wengi hawajui.
وَلَمَّا دَخَلُوا عَلَىٰ يُوسُفَ آوَىٰ إِلَيْهِ أَخَاهُ ۖ قَالَ إِنِّي أَنَا أَخُوكَ فَلَا تَبْتَئِسْ بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٦٩﴾
69. Na walipoingia kwa Yuwsuf, alimuweka ndugu yake karibu naye. Akasema: Hakika mimi ni kaka yako, basi usisikitike kwa yale waliyokuwa wakiyafanya.
فَلَمَّا جَهَّزَهُم بِجَهَازِهِمْ جَعَلَ السِّقَايَةَ فِي رَحْلِ أَخِيهِ ثُمَّ أَذَّنَ مُؤَذِّنٌ أَيَّتُهَا الْعِيرُ إِنَّكُمْ لَسَارِقُونَ﴿٧٠﴾
70. Na alipowatayarishia mizigo yao alikitia kikopo cha kutekea katika mzigo wa ndugu yake, kisha mwenye kunadi akanadi: Enyi wasafiri! Hakika nyinyi ni wezi!
قَالُوا وَأَقْبَلُوا عَلَيْهِم مَّاذَا تَفْقِدُونَ ﴿٧١﴾
71. Wakasema na huku wamewakabili: Mmepoteza nini?
قَالُوا نَفْقِدُ صُوَاعَ الْمَلِكِ وَلِمَن جَاءَ بِهِ حِمْلُ بَعِيرٍ وَأَنَا بِهِ زَعِيمٌ ﴿٧٢﴾
72. Wakasema: Tumepoteza bika ya kupimia ya mfalme. Na atakayekuja nayo atapewa shehena ya ngamia, nami kwa hayo ni mdhamini.
قَالُوا تَاللَّـهِ لَقَدْ عَلِمْتُم مَّا جِئْنَا لِنُفْسِدَ فِي الْأَرْضِ وَمَا كُنَّا سَارِقِينَ ﴿٧٣﴾
73. Wakasema: Ta-Allaahi (Tunaapa kwa Allaah)![11] Nyinyi mmeshapata uhakika kuwa hatukuja kufanya ufisadi katika ardhi, na hatuna historia ya kuwa wezi.
قَالُوا فَمَا جَزَاؤُهُ إِن كُنتُمْ كَاذِبِينَ ﴿٧٤﴾
74. Wakasema: Basi nini adhabu yake, mkiwa ni waongo?
قَالُوا جَزَاؤُهُ مَن وُجِدَ فِي رَحْلِهِ فَهُوَ جَزَاؤُهُ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ ﴿٧٥﴾
75. Wakasema: Adhabu yake ni yule ambaye itapatikana (bika ya mfalme) kwenye mzigo wake, basi yeye ndiye adhabu yake.[12] Hivyo ndivyo tunavyowalipa madhalimu
فَبَدَأَ بِأَوْعِيَتِهِمْ قَبْلَ وِعَاءِ أَخِيهِ ثُمَّ اسْتَخْرَجَهَا مِن وِعَاءِ أَخِيهِ ۚ كَذَٰلِكَ كِدْنَا لِيُوسُفَ ۖ مَا كَانَ لِيَأْخُذَ أَخَاهُ فِي دِينِ الْمَلِكِ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاءُ ۗ وَفَوْقَ كُلِّ ذِي عِلْمٍ عَلِيمٌ ﴿٧٦﴾
76. Akaanza (kutafuta) katika mizigo yao kabla ya mzigo wa ndugu yake. Kisha akaitoa kutoka katika mzigo wa ndugu yake. Hivyo ndivyo Tulivyosahilisha mpango[13] wa Yuwsuf. Hakuweza kumchukua ndugu yake katika sharia ya mfalme isipokuwa Atake Allaah. Tunampandisha vyeo Tumtakaye. Na juu ya kila mwenye ilimu yuko mwenye ilimu zaidi.
قَالُوا إِن يَسْرِقْ فَقَدْ سَرَقَ أَخٌ لَّهُ مِن قَبْلُ ۚ فَأَسَرَّهَا يُوسُفُ فِي نَفْسِهِ وَلَمْ يُبْدِهَا لَهُمْ ۚ قَالَ أَنتُمْ شَرٌّ مَّكَانًا ۖ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا تَصِفُونَ ﴿٧٧﴾
77. Wakasema: Ikiwa ameiba, basi kaka yake aliiba pia zamani. Yuwsuf aliyafutika moyoni na wala hakuwadhihirishia. Akasema (moyoni): Nyinyi mna hali mbaya zaidi, na Allaah Anajua zaidi yale mnayoyavumisha.
قَالُوا يَا أَيُّهَا الْعَزِيزُ إِنَّ لَهُ أَبًا شَيْخًا كَبِيرًا فَخُذْ أَحَدَنَا مَكَانَهُ ۖ إِنَّا نَرَاكَ مِنَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٧٨﴾
78. Wakasema: Ee ‘aziyz! Hakika yeye ana baba mkongwe, basi chukua mmoja wetu mahali pake. Hakika sisi tunakuona ni miongoni mwa wafanyao ihsaan.
قَالَ مَعَاذَ اللَّـهِ أَن نَّأْخُذَ إِلَّا مَن وَجَدْنَا مَتَاعَنَا عِندَهُ إِنَّا إِذًا لَّظَالِمُونَ﴿٧٩﴾
79. Akasema: Tunajikinga kwa Allaah kumchukua isipokuwa yule tuliyekuta kifaa chetu kwake (tukifanya), hakika sisi hapo bila shaka tutakuwa madhalimu.
فَلَمَّا اسْتَيْأَسُوا مِنْهُ خَلَصُوا نَجِيًّا ۖ قَالَ كَبِيرُهُمْ أَلَمْ تَعْلَمُوا أَنَّ أَبَاكُمْ قَدْ أَخَذَ عَلَيْكُم مَّوْثِقًا مِّنَ اللَّـهِ وَمِن قَبْلُ مَا فَرَّطتُمْ فِي يُوسُفَ ۖ فَلَنْ أَبْرَحَ الْأَرْضَ حَتَّىٰ يَأْذَنَ لِي أَبِي أَوْ يَحْكُمَ اللَّـهُ لِي ۖ وَهُوَ خَيْرُ الْحَاكِمِينَ ﴿٨٠﴾
80. Basi walipokata tamaa ya kumpata, walijitenga kando kushauriana kisiri. Mkubwa wao akasema: Je, hamkumbuki kwamba baba yenu amekwishachukua kwenu ahadi kutoka kwa Allaah, na kabla ya hapo uovu mliomfanyia Yuwsuf? Basi sitoondoka ardhi hii mpaka anipe idhini baba yangu, au Allaah Anihukumie. Naye Ni Mbora wa kuhukumu kuliko wote wenye kuhukumu.
ارْجِعُوا إِلَىٰ أَبِيكُمْ فَقُولُوا يَا أَبَانَا إِنَّ ابْنَكَ سَرَقَ وَمَا شَهِدْنَا إِلَّا بِمَا عَلِمْنَا وَمَا كُنَّا لِلْغَيْبِ حَافِظِينَ ﴿٨١﴾
81. Rejeeni kwa baba yenu, na semeni: Ee baba yetu! Hakika mwanao ameiba, nasi hatukutoa ushahidi (dhidi yake) isipokuwa kwa yale tuliyoyajua, na hatukuwa wenye kujua yatakayotokea mbeleni.
وَاسْأَلِ الْقَرْيَةَ الَّتِي كُنَّا فِيهَا وَالْعِيرَ الَّتِي أَقْبَلْنَا فِيهَا ۖ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ ﴿٨٢﴾
82. Na uliza mji ambao tulikuwa humo, na msafara ambao tumekuja nao, na hakika sisi ni wakweli.
قَالَ بَلْ سَوَّلَتْ لَكُمْ أَنفُسُكُمْ أَمْرًا ۖ فَصَبْرٌ جَمِيلٌ ۖ عَسَى اللَّـهُ أَن يَأْتِيَنِي بِهِمْ جَمِيعًا ۚ إِنَّهُ هُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ ﴿٨٣﴾
83. (Ya’quwb) akasema: Bali nafsi zenu zimekushawishini jambo. Basi subira njema nitaishikilia. Asaa Allaah Aniletee wote pamoja. Hakika Yeye Ndiye Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
وَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا أَسَفَىٰ عَلَىٰ يُوسُفَ وَابْيَضَّتْ عَيْنَاهُ مِنَ الْحُزْنِ فَهُوَ كَظِيمٌ ﴿٨٤﴾
84. Akajitenga nao, na akasema: Ee majonzi yangu juu ya Yuwsuf. Na macho yake yakageuka meupe kutokana na huzuni, naye huku akiwa amezuia ghaidhi za huzuni zilizomjaa.
قَالُوا تَاللَّـهِ تَفْتَأُ تَذْكُرُ يُوسُفَ حَتَّىٰ تَكُونَ حَرَضًا أَوْ تَكُونَ مِنَ الْهَالِكِينَ ﴿٨٥﴾
85. Wakasema: Ta-Allaahi (Tunaapa kwa Allaah)! Hutoacha kumkumbuka Yuwsuf mpaka uwe mgonjwa mahututi, au uwe miongoni mwa wenye kuhilaki.
قَالَ إِنَّمَا أَشْكُو بَثِّي وَحُزْنِي إِلَى اللَّـهِ وَأَعْلَمُ مِنَ اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٨٦﴾
86. Akasema: Hakika mimi nashitakia dhiki ya majonzi yangu na huzuni zangu kwa Allaah. Na najua kutoka kwa Allaah yale msiyoyajua.
يَا بَنِيَّ اذْهَبُوا فَتَحَسَّسُوا مِن يُوسُفَ وَأَخِيهِ وَلَا تَيْأَسُوا مِن رَّوْحِ اللَّـهِ ۖ إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِن رَّوْحِ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ ﴿٨٧﴾
87. Ee wanangu! Nendeni mkawatafute Yuwsuf na ndugu yake, na wala msikate tamaa na Faraja ya Allaah. Hakika hawakati tamaa na Faraja ya Allaah isipokuwa watu makafiri.
فَلَمَّا دَخَلُوا عَلَيْهِ قَالُوا يَا أَيُّهَا الْعَزِيزُ مَسَّنَا وَأَهْلَنَا الضُّرُّ وَجِئْنَا بِبِضَاعَةٍ مُّزْجَاةٍ فَأَوْفِ لَنَا الْكَيْلَ وَتَصَدَّقْ عَلَيْنَا ۖ إِنَّ اللَّـهَ يَجْزِي الْمُتَصَدِّقِينَ ﴿٨٨﴾
88. Walipoingia kwake wakasema: Ee ‘aziyz! Dhara imetugusa sisi pamoja na ahli zetu, na tumekuja na bidhaa isiyo na thamani, basi tutimizie kipimo, na tupe swadaqa. Hakika Allaah Anawalipa watoao swadaqa.
قَالَ هَلْ عَلِمْتُم مَّا فَعَلْتُم بِيُوسُفَ وَأَخِيهِ إِذْ أَنتُمْ جَاهِلُونَ ﴿٨٩﴾
89. Akasema: Je, mmejua yale mliyomfanyia Yuwsuf na ndugu yake wakati nyinyi majahili?
قَالُوا أَإِنَّكَ لَأَنتَ يُوسُفُ ۖ قَالَ أَنَا يُوسُفُ وَهَـٰذَا أَخِي ۖ قَدْ مَنَّ اللَّـهُ عَلَيْنَا ۖ إِنَّهُ مَن يَتَّقِ وَيَصْبِرْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٩٠﴾
90. Wakasema: Je, kwani wewe ndio Yuwsuf? Akasema: Mimi ni Yuwsuf, na huyu ni ndugu yangu. Kwa yakini Allaah Ametufanyia ihsaan. Hakika mwenye kuwa na taqwa na akasubiri, basi hakika Allaah Hapotezi ujira wa watendao ihsaan.
قَالُوا تَاللَّـهِ لَقَدْ آثَرَكَ اللَّـهُ عَلَيْنَا وَإِن كُنَّا لَخَاطِئِينَ ﴿٩١﴾
91. Wakasema: Ta-Allaahi (Tunaapa kwa Allaah)! Kwa yakini Allaah Amekufadhilisha wewe kuliko sisi (kwa tabia zote njema), nasi bila shaka tulikuwa wakosa.
قَالَ لَا تَثْرِيبَ عَلَيْكُمُ الْيَوْمَ ۖ يَغْفِرُ اللَّـهُ لَكُمْ ۖ وَهُوَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ ﴿٩٢﴾
92. Akasema: Hakuna lawama juu yenu leo. Allaah Atakughufurieni. Naye Ni Mbora zaidi wa Kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu.
اذْهَبُوا بِقَمِيصِي هَـٰذَا فَأَلْقُوهُ عَلَىٰ وَجْهِ أَبِي يَأْتِ بَصِيرًا وَأْتُونِي بِأَهْلِكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٩٣﴾
93. Nendeni na kanzu yangu hii, na itupeni kwenye uso wa baba yangu, atakuwa mwenye kuona, na nijieni na ahli zenu nyote pamoja.
وَلَمَّا فَصَلَتِ الْعِيرُ قَالَ أَبُوهُمْ إِنِّي لَأَجِدُ رِيحَ يُوسُفَ ۖ لَوْلَا أَن تُفَنِّدُونِ ﴿٩٤﴾
94. Na ulipoondoka msafara, baba yao alisema: Hakika mimi nasikia harufu ya Yuwsuf, ikiwa hamkunidhania nachanganyikiwa akili.
قَالُوا تَاللَّـهِ إِنَّكَ لَفِي ضَلَالِكَ الْقَدِيمِ ﴿٩٥﴾
95. Wakasema: Ta-Allaahi (Tunaapa kwa Allaah)! Hakika wewe bado umo katika kosa lako la zamani.
فَلَمَّا أَن جَاءَ الْبَشِيرُ أَلْقَاهُ عَلَىٰ وَجْهِهِ فَارْتَدَّ بَصِيرًا ۖ قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ إِنِّي أَعْلَمُ مِنَ اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٩٦﴾
96. Basi alipokuja mtoaji bishara (ya kuwa Yuwsuf kapatikana), aliitupa (kanzu) juu ya uso wake akarudi kuona. Akasema: Je, sikukuambieni kwamba hakika mimi najua zaidi kutoka kwa Allaah yale msiyoyajua?
قَالُوا يَا أَبَانَا اسْتَغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا إِنَّا كُنَّا خَاطِئِينَ ﴿٩٧﴾
97. Wakasema: Ee baba yetu! Tuombee maghfirah madhambi yetu, hakika sisi tulikuwa wakosa.
قَالَ سَوْفَ أَسْتَغْفِرُ لَكُمْ رَبِّي ۖ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ ﴿٩٨﴾
98. Akasema: Nitakuombeeni maghfirah kwa Rabb wangu. Hakika Yeye Ndiye Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
فَلَمَّا دَخَلُوا عَلَىٰ يُوسُفَ آوَىٰ إِلَيْهِ أَبَوَيْهِ وَقَالَ ادْخُلُوا مِصْرَ إِن شَاءَ اللَّـهُ آمِنِينَ ﴿٩٩﴾
99. Na walipoingia kwa Yuwsuf akawaweka karibu naye wazazi wake. Na akasema: Ingieni Misri In Shaa Allaah mkiwa mmo katika amani.
وَرَفَعَ أَبَوَيْهِ عَلَى الْعَرْشِ وَخَرُّوا لَهُ سُجَّدًا ۖ وَقَالَ يَا أَبَتِ هَـٰذَا تَأْوِيلُ رُؤْيَايَ مِن قَبْلُ قَدْ جَعَلَهَا رَبِّي حَقًّا ۖ وَقَدْ أَحْسَنَ بِي إِذْ أَخْرَجَنِي مِنَ السِّجْنِ وَجَاءَ بِكُم مِّنَ الْبَدْوِ مِن بَعْدِ أَن نَّزَغَ الشَّيْطَانُ بَيْنِي وَبَيْنَ إِخْوَتِي ۚ إِنَّ رَبِّي لَطِيفٌ لِّمَا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ هُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ ﴿١٠٠﴾
100. Akawapandisha wazazi wake wawili juu ya kiti cha ufalme, wakaporomoka wote kumsujudia.[14] Na akasema: Ee baba yangu kipenzi! Hii ni tafsiri ya njozi yangu hapo kabla, Rabb wangu Ameijaalia kweli. Na hakika Amenifanyia ihsaan Aliponitoa kutoka jela, na Akakuleteni kutoka jangwani baada ya shaytwaan kuchochea baina yangu na baina ya kaka zangu. Hakika Rabb wangu Ni Latifu kwa Atakayo. Hakika Yeye Ndiye Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
رَبِّ قَدْ آتَيْتَنِي مِنَ الْمُلْكِ وَعَلَّمْتَنِي مِن تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ ۚ فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَنتَ وَلِيِّي فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ تَوَفَّنِي مُسْلِمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ ﴿١٠١﴾
101. Rabb wangu! Kwa yakini Umenipa utawala, na Umenifunza tafsiri ya khabari (kuhusu njozi, ndoto na matukio). Muanzilishi wa mbingu na ardhi. Wewe ni Mlinzi wangu duniani na Aakhirah. Nifishe hali ya kuwa Muislamu na Unikutanishe na Swalihina.
ذَٰلِكَ مِنْ أَنبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهِ إِلَيْكَ ۖ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ أَجْمَعُوا أَمْرَهُمْ وَهُمْ يَمْكُرُونَ ﴿١٠٢﴾
102. Hizo ni baadhi ya khabari za ghaibu Tunakufunulia Wahy kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na hukuwa pamoja nao pale walipokubaliana jambo lao, nao wakifanya njama.
وَمَا أَكْثَرُ النَّاسِ وَلَوْ حَرَصْتَ بِمُؤْمِنِينَ ﴿١٠٣﴾
103. Na wengi wa watu hawatoamini japokuwa utatilia hima.[15]
وَمَا تَسْأَلُهُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٠٤﴾
104. Na huwaombi kwa haya ujira wowote (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Hii (Qur-aan) si chochote isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu.
وَكَأَيِّن مِّنْ آيَةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يَمُرُّونَ عَلَيْهَا وَهُمْ عَنْهَا مُعْرِضُونَ ﴿١٠٥﴾
105. Ni Aayah (Ishara, Dalili) nyingi sana katika mbingu na ardhi wanazipitia na huku wao wanazipuuza.[16]
وَمَا يُؤْمِنُ أَكْثَرُهُم بِاللَّـهِ إِلَّا وَهُم مُّشْرِكُونَ ﴿١٠٦﴾
106. Na wengi kati yao hawamwamini Allaah isipokuwa wao ni wenye kufanya shirki.
أَفَأَمِنُوا أَن تَأْتِيَهُمْ غَاشِيَةٌ مِّنْ عَذَابِ اللَّـهِ أَوْ تَأْتِيَهُمُ السَّاعَةُ بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿١٠٧﴾
107. Je, wanaaminisha kuwa haitowafikia Adhabu ya Allaah ifunikizayo au itawafikia Saa kwa ghafla nao hawahisi?
قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي ۖ وَسُبْحَانَ اللَّـهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿١٠٨﴾
108. Sema: Hii ndio njia yangu nalingania kwa Allaah, juu ya baswiyrah (nuru za ilimu na utambuzi) mimi na anayenifuata. Na Utakasifu ni wa Allaah, nami si miongoni mwa washirikina.
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِي إِلَيْهِم مِّنْ أَهْلِ الْقُرَىٰ ۗ أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۗ وَلَدَارُ الْآخِرَةِ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ اتَّقَوْا ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿١٠٩﴾
109. Na Hatukutuma kabla yako (Rasuli) isipokuwa wanaume Tuliowafunulia Wahy katika watu wa miji. Je, basi hawatembei katika ardhi wakatazama vipi ilikuwa hatima ya wale wa kabla yao?[17] Na bila shaka nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi kwa wale waliokuwa na taqwa. Je, basi hawatii akilini?
حَتَّىٰ إِذَا اسْتَيْأَسَ الرُّسُلُ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ قَدْ كُذِبُوا جَاءَهُمْ نَصْرُنَا فَنُجِّيَ مَن نَّشَاءُ ۖ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُنَا عَنِ الْقَوْمِ الْمُجْرِمِينَ ﴿١١٠﴾
110. (Wakaendelea kulingania) mpaka walipokata tamaa Rusuli, na wakawa na yakini kuwa wamekadhibishwa (hakuna tena tamaa ya watu wao kuamini), hapo ikawajia Nusra Yetu na Tukawaokoa Tuwatakao. Na Adhabu Yetu hairudishwi nyuma kwa watu wakhalifu.
لَقَدْ كَانَ فِي قَصَصِهِمْ عِبْرَةٌ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ۗ مَا كَانَ حَدِيثًا يُفْتَرَىٰ وَلَـٰكِن تَصْدِيقَ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ كُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿١١١﴾
111. Kwa yakini katika visa vyao kuna mazingatio (na mafunzo) kwa wenye akili. Haikuwa (Qur-aan) hadithi zinazotungwa, lakini ni sadikisho la (Vitabu) vya kabla yake na tafsili ya waziwazi ya kila kitu, na ni mwongozo na rehma kwa watu wanaoamini.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Sababu ya kuteremshwa Aayah (1-3): Bonyeza kiungo kifuatacho:
012-Asbaabun-Nuzuwl: Yuwsuf Aayah 1-3: نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَص [150]
[3] Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام) Ni Mtukufu Zaidi Miongoni Mwa Watu Na Amepewa Nusu Ya Ujamali Wa Dunia:
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amemsifia Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام) kuwa ni mtu mtukufu zaidi miongoni mwa watu. Naye ni Nabiy pekee ambaye baba yake ni Nabiy naye ni Ya’quwb (عليه السّلام), na kisha babu yake Is-haaq (عليه السّلام) ambaye pia ni Nabiy, kisha baba wa babu yake Ibraahiym (عليه السّلام) ambaye pia ni Nabiy:
Amesimulia Abu Hurayrah (رضي الله عنه): Baadhi ya watu walimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Nani aliye mtukufu zaidi miongoni mwa watu? Akajibu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): "Mtukufu zaidi miongoni mwao ni yule mwenye taqwa zaidi.” Wakasema: Ee Nabiy wa Allaah! Hatuulizi hili. Akasema: "Basi mtukufu zaidi ni Yuwsuf, Nabiy wa Allaah, mwana wa Nabiy wa Allaah, mwana wa Nabiy wa Allaah, mwana wa Kipenzi cha Allaah (Nabiy Ibraahiym).” Wakasema: Hatuulizi hili. Akasema: “Basi mnataka kuniuliza kuhusu koo asili za Waarabu?” Wakasema: Naam. Akasema: “Wale waliokuwa bora katika zama za Ujaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Uislamu) ndio wabora katika Uislamu, kama watakuwa na ufahamu wa kina (wa Dini).” [Al-Bukhaariy]
Na pia: Amesimulia Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mtukufu (kati ya watu) ni mwana wa mtukufu, mwana wa mtukufu, mwana wa mtukufu; ni Yuwsuf bin Ya’quwb bin Is-haaq bin Ibraahiym (عليهم السّلام)” [Al-Bukhaariy]
Nabiy Yuwsuf amesifika pia kwa ujamali (uzuri) kama alivyosema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth ndefu ya Israa wal-Mi’raaj: “Nikamuona Yuwsuf (عليه السّلام) ambaye alimepwa nusu ya ujamali wa dunia.” [Muslim]
[4] Njozi Za Manabii Ni Wahyi Kutoka Kwa Allaah (سبحانه وتعالى):
Tofauti Kati Ya Ndoto Na Njozi:
Kwa mujibu wa Hadiyth ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), anayoyaona mwenye kulala usingizini ni matatu:
i- Njozi "رُؤْيَا" . Hii aghalabu huwa inatoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى). Mtu huona njozini mambo ya kupendeza na kufurahisha, au ya kumtahadharisha na shari, au ya kumwongoza. Akiona haya, imesuniwa amhimidi Allaah (سبحانه وتعالى) na awajulishe tu jamaa zake, na si watu wengineo.
ii- Ndoto "حُلْمٌ". Hii aghalabu huwa inatokana na shaytwaan, na mtu huona usingizini mambo ya kuchukiza. Akiota hivi, basi imesuniwa ajilinde kwa Allaah kutokana na shaytwaan, atafili upande wake wa kushoto mara tatu, ageuze ubavu aliokuwa ameulalia, na aswali rakaa mbili ikiwezekana. Pia asiisimulie kwa watu.
iii- Mtu kuzungumza mwenyewe usingizini "حَدِيْثُ النَّفْسِ". Hii si njozi wala ndoto, bali hutokana na hofu au matukio yaliyoko ndani ya kumbukumbu ya mtu na kwenye akili yake ya ndani. Haya yote hujiunda wakati mtu amelala, na hata wakati mwingine husikika akizungumza peke yake yasiyofahamika.
Katika Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Muda utakapokuwa mfupi, njozi ya Muumini itakuwa haiongopi tena, na mwenye njozi ya kweli zaidi kati yenu ni yule aliye msema kweli zaidi, na njozi ya Muumini ni sehemu moja kati ya sehemu 46 za Unabii. Na ndoto ni aina tatu: Njozi njema ambayo ni bishara toka kwa Allaah, na ndoto ya kuhuzunisha itokanayo na shaytwaan, na ndoto kutokana na mtu kuizungumzisha nafsi yake (mawazo yaliyotawala zaidi kwenye akili yake).” [Muslim 2263]
Na ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema kuwa njozi za Manabii ni Wahyi kutoka kwa Allaah [Tafsiyr Ibn Kathiyr] Ni kama vile ndoto ya Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) alipoota anamchinja mwanawe Ismaaiyl (عليه السّلام). Rejea Aw-Swaffaat (37:102). Na pia njozi ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) pindi walipozuiliwa na makafiri kuingia Makkah walipofika Hudaybiyah, akaona njozini kwamba wataingia Masjid Al-Haraam Makkah kutekeleza ‘Umrah na kuwa watanyoa au kupunguza nywele zao. Rejea Al-Fat-h (48:27) na ikaja kuhakiki.
[5] Nyota Kumi Na Moja, Jua Na Mwezi Katika Njozi Ya Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام):
Wafasiri wa Qur-aan wameelezea kuwa njozi ya Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام) ya kusujudiwa na nyota kumi na moja, ni ndugu zake ambao walikuwa ni kumi na moja. Na jua na mwezi ni baba yake na mama yake. Imesimuliwa na Ibn ‘Abbaas, Adhw-Dhwahhaak, Qataadah, Sufyaan Ath-Thawriy na ‘Abdur-Rahmaan bin Zayd Bin Aslam. Na kwamba njozi hii imekuja kuhakiki baada ya miaka arubaini. Wengineo wamesema imehakiki baada ya miaka themanini wakati Yuwsuf alipowapandisha wazazi wake katika kiti chake cha enzi na nduguze wakiwa mbele yake. Rejea Aayah namba (100). [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[6] Bin-yamiyn Mdogo Wa Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام):
Bin-yamiyn ni mdogo wake Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام) ambaye ni shakiki (wa baba na mama mmoja). Ama ndugu zake wengineo, hao wamechangia, na hawa wawili kwa baba tu ambaye ni Nabiy Ya’quwb (عليه السّلام).
[7] Maana Ya ‘Aziyz:
Maana ya ‘aziyz ni kigogo au waziri. Huyo ndiye mtu aliyepewa cheo cha ‘aziyz ambaye ametajwa katika Aayah (23), (25), (30), (31), (51) na (52), na ambaye ndiye aliyemlea Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام) nyumbani kwake baada ya kumnunua hapo alipotolewa kisimani. Kisha alipofikia umri wa kubaleghe, ndipo ikatokea mkasa wa mke wa ‘aziyz kumtongoza Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام). Hivyo basi, ‘aziyz ilitumika Misri kwa mtu mwenye cheo kikubwa ambaye hawezi kupingwa wala kuasiwa. Na pia kauli nyenginezo za ‘Ulamaa ni kwamba ‘aziyz ilitumika kwa mfalme wa Misri katika zama hizo. [Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb Juz (5) Uk. (2)]. Na kwa mujibu wa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما), ‘aziyz alikuwa ni afisa wa hazina ya kifalme. [Ibn Jariyr]. Na kauli hii ya ‘Ibn ‘Abbaas inakubalika zaidi kwa sababu Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام) alipewa cheo hiki cha ‘aziyz pale mfalme wa Misri alipompa madaraka ya hazina za Misri. Na nduguze waliporudi tena Misri kutoka Palestina kuja kuomba chakula, wakamwita Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام) kwa cheo hicho cha ‘aziyz kama ilivyotajwa katika Aayah: (78) (88).
[8] Rabbiy:
Katika Aayah imetajwa Rabb ambalo linatumika kwa “bwana wa nyumba au mlezi.” Na rabb imetumika tena kumaanisha “bwana wa nyumba” katika Aayah (41), (42), na (50). Basi isije kufahamika ndivyo sivyo kwamba Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام) amemfanya ‘aziyz ambaye ni mlezi wake na bwana wa nyumba yake kuwa ni Mola au Muumba wake. Haiwezekani hivyo kwa sababu: Kwanza: Ni mustahili kwa hadhi ya Nabiy kutenda dhambi ya kumshirikisha Allaah kwa kumhusisha kiumbe kuwa sawa na Allaah. Pili: Hakuna mfano hata mmoja katika Qur-aan ambao Nabiy aliwahi kumwita yeyote asiyekuwa Allaah kuwa ni Rabb wake. Nabiy Yuwsuf mwenyewe anatofautisha kati ya ‘Aqiydah (itikadi) yake na ile ya Wamisri waliokuwa katika jela pamoja naye katika Suwrah hii ya Yuwsuf Aayah (37-40) akiweka wazi kwamba Rabb wake ni Allaah wakati wao wamewafanya wanaadam wengine kuwa Mola wao.
[9] Aina Tatu Za Nafsi:
Nafsi ziko aina tatu: (i) Nafsi yenye kuamrisha sana maovu; Rejea Yuwsuf: (12:53). (ii) Nafsi ya kulaumu; Rejea Al-Qiyaamah (75:2). (iii) Nafsi iliyotua; Rejea Al-Fajr (89:27).
Nafsi ya kuamrisha sana maovu ni ile ambayo inamwamrisha mtu wake kufanya inayoyopenda katika matamanio ya haramu na kufuata batili. Ama nafsi ya kulaumu, hii ni ile ambayo inamlaumu mtu wake kuhusu mambo ya kheri (na ibaada) yaliyompita (akawa hakuyatenda), hivyo basi nafsi inayajutia. Ama nafsi iliyotua, hii ni ile ambayo imejikita na kutulia thabiti kwa Rabb wake, na katika kumtii, kufuata amri Zake na kumdhukuru, na haijatuama kwa mwingine yoyote isipokuwa Kwake tu. [Shaykh Swaalih Fawzaan Al-Fawzaan]
[10] Haja Katika Nafsi Ya Ya’quwb:
Ni huruma ndani ya nafsi yake ili wasipate jicho na husuda. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[11] Herufi Za Kuapia: Rejea An-Nahl (16:56).
[12] Hukmu Ya Mwizi Katika Dini Ya Zama Hizo: Hiyo ilikuwa ni (hukumu katika) Dini yao kwamba mwizi akithibitika kuwa ameiba, basi anakuwa anamilikiwa na mwenye mali iliyoibiwa. [Tafsiyr As-Sa’dy]
[13] Hila Au Mpango Wa Yuwsuf:
Ni mpango ambao Anauridhia Allaah (عزّ وجلّ) kutokana na hikma yake kutafuta maslahi yake. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Imaam As-Sa’diy amesema: Tulimsahilishia hila hii iliyompeleka kwenye jambo lisilokuwa la lawama. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[14] Kumsujudia Binaadam Ni Haramu Katika Sharia Yetu Ya Kiislamu:
Katika sharia ya zama hizo, Sujuwd iliruhusika kwa binaadam kwa kuwa ilimaanisha heshima. Na hapo wazazi wake Yuwsuf na nduguze, ambao jumla yao walikuwa kumi na moja, walimsujudia Yuwsuf kumdhihirishia heshima yao kwake. Wala haikumaanisha kuwa ni ibaada ya kunyenyekea au kuabudu. Ama katika sharia yetu imeharamishwa kwa sababu ya kuzuia kumshirikisha Allaah (عزّ وجلّ). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amethibitisha haya katika Hadiyth aliyosimulia ‘Abdullaah bin Abiy Awfaa (رضي الله عنه): Muaadh aliporudi kutoka Shaam, alimsujudia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Nabiy akasema: “Ee Mu’aadh! Imekuwaje kufanya hivyo?” Akasema: Nimekuja kutoka Shaam, nikawakuta wanawasujudia Maaskofu na Mapadri wao, basi nafsi yangu ikapenda nikufanyie hivyo. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Usifanye hivyo! Kwani ingekuwa ni kumuamrisha mtu amsujudie asiyekuwa Allaah, basi ningeliamrisha mke amsujudie mumewe.” [Kuna Riwaayah mbali mbali kama hiyo, na hii ni lafdhw ya Ibn Maajah (1853), na Al-Albaaniy ameisahihisha]
[15] Kufuata Watu Wengi Jambo La Haramu Au Batili Au La Uzushi:
Imaam Ibn Baaz (رحمه الله) amesema katika nasaha zilizoelekezwa kwa Waislamu wote: Na kila Muislamu ajitahadhari na kudanganywa na wengi, na kusema: “Watu wamefuata jambo kadha wa kadha na wamezoea jambo kadha wa kadha, basi mimi niko pamoja nao.” Huu ni msiba mkubwa, na wengi waliopita wameangamia kwa hayo. Lakini ee mwenye akili! Inakupasa ujitazame nafsi yako, na ujitathmini na ushikamane na haki hata watu wakiiacha. Na jitahadhari na yale Aliyokataza Allaah (سبحانه وتعالى) hata watu wakiyafanya, kwani ukweli ndio unaostahiki zaidi kufuatwa kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ ﴿١١٦﴾
“Na kama ukiwatii wengi walioko ulimwenguni, watakupoteza Njia ya Allaah. Hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawakuwa ila wenye kubuni uongo.” [Al-An’aam (6:116] Na pia Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) kwenye Aayah hii ya Suwrat Yuwsuf (12:103)]. Na baadhi ya Salaf (رحمهم الله) wamesema: “Usiikane haki kwa sababu ni wachache wanaoifuata, na wala usidanganywe na uwongo kwa sababu ya wingi wa walioangamia.” [Fataawaa Al-Lajnah Na Maimamu Wawili]
Basi na wazingatie na watahadhari watu wanaofuata mambo na vitendo vinavyoharamishwa katika Dini ili kujiepusha na haramu na adhabu za Allaah (سبحانه وتعالى). Na pia kutahadhari na kujiepusha na mambo au vitendo ambavyo havikuthibiti katika mafundisho ya Sunnah ili kujiepusha na uzushi japokuwa watu wengi wanafuata, kwani kila uzushi ni upotofu, na kila upotofu unaelekeza motoni kama ilivyothibiti katika Hadiyth ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).
[16] Ishara Na Dalili Za Allaah (عزّ وجلّ) Mbinguni Na Ardhini Zinathibitisha Tawhiyd Yake:
Rejea Fusw-Swilat (41:53), Adh-Dhaariyaat (51:20). Rejea pia Al-Qamar (54:5) kwenye maelezo na rejea mbalimbali:
[17] Zingatio Kwa Makafiri Watembee Maeneo Ya Ardhi Mbalimbali Wajionee Na Watambue Hatima Za Waliokadhibisha. Rejea Aal-‘Imraan (3:137). Al-An’aam (6:11), Faatwir (35:43-44).
الرَّعْد
013-Ar-Ra’d
013-Ar-Ra'd: Utangulizi Wa Suwrah [152]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
المر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ ۗ وَالَّذِي أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ الْحَقُّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ﴿١﴾
1. Alif Laam Miym Raa.[1] Hizi ni Aayaat za Kitabu. Na yale yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kutoka kwa Rabb wako ni haki, lakini watu wengi hawaamini.
اللَّـهُ الَّذِي رَفَعَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ۖ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ يُفَصِّلُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُم بِلِقَاءِ رَبِّكُمْ تُوقِنُونَ ﴿٢﴾
2. Allaah Ambaye Ameinua mbingu bila ya nguzo mnaziona, kisha Akawa juu[2] ya ‘Arsh. Na Akavitiisha jua na mwezi, vyote vinakwenda mzunguko hadi muda maalumu uliokadiriwa. Anadabiri mambo, Anazifasili waziwazi Aayaat (Ishara, Dalili) ili mpate kuwa na yakini ya kukutana na Rabb wenu.
وَهُوَ الَّذِي مَدَّ الْأَرْضَ وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنْهَارًا ۖ وَمِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ جَعَلَ فِيهَا زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ ۖ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٣﴾
3. Na Yeye Ndiye Aliyetandaza ardhi na Akajaalia humo milima thabiti na mito, na kila aina ya mazao Amejaalia humo jozi mbilimbili (za kiume na kike). Anafunika usiku juu ya mchana. Hakika katika hayo kuna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaotafakari.
وَفِي الْأَرْضِ قِطَعٌ مُّتَجَاوِرَاتٌ وَجَنَّاتٌ مِّنْ أَعْنَابٍ وَزَرْعٌ وَنَخِيلٌ صِنْوَانٌ وَغَيْرُ صِنْوَانٍ يُسْقَىٰ بِمَاءٍ وَاحِدٍ وَنُفَضِّلُ بَعْضَهَا عَلَىٰ بَعْضٍ فِي الْأُكُلِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿٤﴾
4. Na katika ardhi kuna vipande vyake tofauti vinavyopakana, na mabustani ya mizabibu na mazao (mengineyo), na mitende inayochipuka katika shina moja na isiyochipuka katika shina moja, vinanyweshezwa kwa maji ya aina moja, na Tunavifanya baadhi kuwa bora zaidi kuliko vingine katika ladha na lishe. Hakika katika hayo kuna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaotia akilini.[3]
وَإِن تَعْجَبْ فَعَجَبٌ قَوْلُهُمْ أَإِذَا كُنَّا تُرَابًا أَإِنَّا لَفِي خَلْقٍ جَدِيدٍ ۗ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ ۖ وَأُولَـٰئِكَ الْأَغْلَالُ فِي أَعْنَاقِهِمْ ۖ وَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٥﴾
5. Na ukistaajabu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi cha ajabu ni kauli yao: Je, tukiwa mchanga, hivi kweli sisi tutakuja kuwa katika umbo jipya?[4] Hao ndio wale waliomkufuru Rabb wao. Hao watafungwa minyororo katika shingo zao.[5] Na hao ndio watu wa motoni, wao humo watadumu.
وَيَسْتَعْجِلُونَكَ بِالسَّيِّئَةِ قَبْلَ الْحَسَنَةِ وَقَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِمُ الْمَثُلَاتُ ۗ وَإِنَّ رَبَّكَ لَذُو مَغْفِرَةٍ لِّلنَّاسِ عَلَىٰ ظُلْمِهِمْ ۖ وَإِنَّ رَبَّكَ لَشَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿٦﴾
6. Na wanakuhimiza kwa maovu kabla ya mazuri, na hali imekwishapita kabla yao mifano ya adhabu. Na hakika Rabb wako Ni Mwenye Maghfirah kwa watu juu ya dhulma zao, na hakika Rabb wako Ni Mkali wa Kuakibu.
وَيَقُولُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِّن رَّبِّهِ ۗ إِنَّمَا أَنتَ مُنذِرٌ ۖ وَلِكُلِّ قَوْمٍ هَادٍ ﴿٧﴾
7. Na wanasema wale waliokufuru: Kwa nini hakuteremshiwa Aayah (Muujiza) kutoka kwa Rabb wake? Hakika wewe ni mwonyaji tu na kila kaumu ina mwenye kuongoza.
اللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تَحْمِلُ كُلُّ أُنثَىٰ وَمَا تَغِيضُ الْأَرْحَامُ وَمَا تَزْدَادُ ۖ وَكُلُّ شَيْءٍ عِندَهُ بِمِقْدَارٍ ﴿٨﴾
8. Allaah Anajua mimba abebayo kila mwanamke na yanayokipunguza matumbo ya uzazi na yanayokizidisha (muda au umbile). Na kila kitu Kwake ni kwa kipimo.
عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْكَبِيرُ الْمُتَعَالِ ﴿٩﴾
9. Mjuzi wa ghaibu na dhahiri, Mkubwa kabisa Mwenye Uluwa.
سَوَاءٌ مِّنكُم مَّنْ أَسَرَّ الْقَوْلَ وَمَن جَهَرَ بِهِ وَمَنْ هُوَ مُسْتَخْفٍ بِاللَّيْلِ وَسَارِبٌ بِالنَّهَارِ ﴿١٠﴾
10. Ni sawa (Kwake) mmoja wenu akisema maneno yake kwa siri au kwa sauti, na anayenyemelea usiku na anayetembea mchana kwa uhuru.
لَهُ مُعَقِّبَاتٌ مِّن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ يَحْفَظُونَهُ مِنْ أَمْرِ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ ۗ وَإِذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِقَوْمٍ سُوءًا فَلَا مَرَدَّ لَهُ ۚ وَمَا لَهُم مِّن دُونِهِ مِن وَالٍ ﴿١١﴾
11. Ana Malaika wanaofuatana kwa zamu mbele yake na nyuma yake wanamhifadhi kwa Amri ya Allaah.[6] Hakika Allaah Habadilishi yale yaliyoko kwa watu mpaka wao wenyewe wabadilishe yale yaliyomo katika nafsi zao. Na Allaah Akiwakusudia watu adhabu, basi hakuna wa kuirudisha. Nao hawana mlinzi yeyote ghairi Yake.
هُوَ الَّذِي يُرِيكُمُ الْبَرْقَ خَوْفًا وَطَمَعًا وَيُنشِئُ السَّحَابَ الثِّقَالَ ﴿١٢﴾
12. Yeye Ndiye Anayekuonyesheni umeme mkaingiwa khofu (ya radi na mvua kubwa za kuharibu) na mkapata matumaini (ya manufaa na kheri zake), na Anaanzisha mawingu mazito.
وَيُسَبِّحُ الرَّعْدُ بِحَمْدِهِ وَالْمَلَائِكَةُ مِنْ خِيفَتِهِ وَيُرْسِلُ الصَّوَاعِقَ فَيُصِيبُ بِهَا مَن يَشَاءُ وَهُمْ يُجَادِلُونَ فِي اللَّـهِ وَهُوَ شَدِيدُ الْمِحَالِ ﴿١٣﴾
13. Na radi inamsabihi (Allaah) na kumhimidi na Malaika pia (wanamsabihi)[7] kwa sababu ya kumkhofu[8], na Anatuma radi na umeme angamizi, Akamsibu kwayo Amtakaye, nao huku (makafiri) wakiwa wanabishana kuhusu Allaah, Naye ni Ni Mkali na Mwenye nguvu za kuhujumu.[9]
لَهُ دَعْوَةُ الْحَقِّ ۖ وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَسْتَجِيبُونَ لَهُم بِشَيْءٍ إِلَّا كَبَاسِطِ كَفَّيْهِ إِلَى الْمَاءِ لِيَبْلُغَ فَاهُ وَمَا هُوَ بِبَالِغِهِ ۚ وَمَا دُعَاءُ الْكَافِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَالٍ ﴿١٤﴾
14. Yeye Ndiye wa haki kuombwa (na kuabudiwa).[10] Na wale wanaowaomba badala Yake, hawawaitikii kwa chochote isipokuwa kama anayenyoosha viganja vyake viwili vya mikono kwenye maji ili yafikie kinywani mwake, na wala hayafikii hata kidogo. Na duaa za makafiri hazipo ila katika upotofu.[11]
وَلِلَّـهِ يَسْجُدُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَظِلَالُهُم بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ ۩﴿١٥﴾
15. Na waliomo mbinguni na ardhini humsujudia Allaah Pekee wakipenda wasipende na vivuli vyao pia (vinamsujudia) asubuhi na jioni.[12]
قُلْ مَن رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ قُلِ اللَّـهُ ۚ قُلْ أَفَاتَّخَذْتُم مِّن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ لَا يَمْلِكُونَ لِأَنفُسِهِمْ نَفْعًا وَلَا ضَرًّا ۚ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ أَمْ هَلْ تَسْتَوِي الظُّلُمَاتُ وَالنُّورُ ۗ أَمْ جَعَلُوا لِلَّـهِ شُرَكَاءَ خَلَقُوا كَخَلْقِهِ فَتَشَابَهَ الْخَلْقُ عَلَيْهِمْ ۚ قُلِ اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿١٦﴾
16. Sema: Ni nani Rabb wa mbingu na ardhi? Sema: Ni Allaah. Sema: Je, mnawafanya wengineo badala Yake kuwa rafiki walinzi na hali hawamiliki manufaa wala dhara kwa nafsi zao? Sema: Je, kipofu analingana sawa na mwenye kuona, au je, viza vinalingana sawa na nuru? Au wamemfanyia Allaah washirika walioumba kama uumbaji Wake, kisha ukafanana uumbaji kwao (wakakanganyikiwa)?[13] Sema: Allaah Ni Muumbaji wa kila kitu, Naye Ni Mmoja Pekee, Asiyepingika.
أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَسَالَتْ أَوْدِيَةٌ بِقَدَرِهَا فَاحْتَمَلَ السَّيْلُ زَبَدًا رَّابِيًا ۚ وَمِمَّا يُوقِدُونَ عَلَيْهِ فِي النَّارِ ابْتِغَاءَ حِلْيَةٍ أَوْ مَتَاعٍ زَبَدٌ مِّثْلُهُ ۚ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ اللَّـهُ الْحَقَّ وَالْبَاطِلَ ۚ فَأَمَّا الزَّبَدُ فَيَذْهَبُ جُفَاءً ۖ وَأَمَّا مَا يَنفَعُ النَّاسَ فَيَمْكُثُ فِي الْأَرْضِ ۚ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ اللَّـهُ الْأَمْثَالَ ﴿١٧﴾
17. (Allaah) Ameteremsha kutoka mbinguni maji na mabonde yakatiririka kwa kadiri yake, kisha mbubujiko ukabeba mapovu ya takataka yanayopanda juu yake. Na katika vile wanavyoviwashia moto ili kutaka mapambo au vyombo hutokea povu vile vile. Hivyo ndivyo Anavyopiga Allaah (mfano wa) haki na batili. Basi povu la takataka linapita bure bila ya kufaa. Lakini vile vinavyowafaa watu hubakia ardhini. Hivyo ndivyo Allaah Anavyopiga mifano.[14]
لِلَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِرَبِّهِمُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَالَّذِينَ لَمْ يَسْتَجِيبُوا لَهُ لَوْ أَنَّ لَهُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا وَمِثْلَهُ مَعَهُ لَافْتَدَوْا بِهِ ۚ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ سُوءُ الْحِسَابِ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ الْمِهَادُ﴿١٨﴾
18. Wale waliomuitikia Rabb wao watapata Al-Husnaa (Jannah). Na wale wasiomuitikia hata kama wangelikuwa wana vyote viliomo ardhini na mfano wa kama hivyo pamoja, wangelivitoa kujikombolea navyo. Hao watapata hesabu mbaya, na makazi yao ni Jahannam. Ni mahali pabaya mno pa kupumzikia.
أَفَمَن يَعْلَمُ أَنَّمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ الْحَقُّ كَمَنْ هُوَ أَعْمَىٰ ۚ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿١٩﴾
19. Je, anayejua kwamba yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kutoka kwa Rabb wako ni haki, (je,) ni sawa na ambaye yeye ni kipofu? Hakika wanazingatia wenye akili tu.
الَّذِينَ يُوفُونَ بِعَهْدِ اللَّـهِ وَلَا يَنقُضُونَ الْمِيثَاقَ ﴿٢٠﴾
20. Ambao wanatimiza Ahadi ya Allaah,[15] wala hawavunji fungamano.
وَالَّذِينَ يَصِلُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ وَيَخَافُونَ سُوءَ الْحِسَابِ ﴿٢١﴾
21. Na ambao wanaunga yale Aliyoamrisha Allaah kuungwa[16] na wanamkhofu Rabb wao, na wanakhofu hesabu mbaya.
وَالَّذِينَ صَبَرُوا ابْتِغَاءَ وَجْهِ رَبِّهِمْ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً وَيَدْرَءُونَ بِالْحَسَنَةِ السَّيِّئَةَ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عُقْبَى الدَّارِ ﴿٢٢﴾
22. Na ambao wamesubiri kutaka Wajihi wa Rabb wao, na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa katika yale Tuliyowaruzuku kwa siri na dhahiri, na wanaepusha ovu kwa zuri, hao watapata hatima njema ya makazi ya Aakhirah.
جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا وَمَن صَلَحَ مِنْ آبَائِهِمْ وَأَزْوَاجِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ يَدْخُلُونَ عَلَيْهِم مِّن كُلِّ بَابٍ﴿٢٣﴾
23. Jannaat za kudumu milele wataingia pamoja na waliotengenea miongoni mwa baba zao na wake zao na dhuria zao.[17] Na Malaika wanawaingilia katika kila milango (wakiwaamkua).
سَلَامٌ عَلَيْكُم بِمَا صَبَرْتُمْ ۚ فَنِعْمَ عُقْبَى الدَّارِ ﴿٢٤﴾
24. Salaamun ‘Alaykum! (Amani iwe juu yenu) kwa subira mliyoshikamana nayo. Basi uzuri ulioje hatima njema ya makazi ya Aakhirah!
وَالَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ ۙ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ اللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوءُ الدَّارِ ﴿٢٥﴾
25. Na wale wanaovunja Ahadi ya Allaah baada ya kufungamana kwake na wanakata yale Aliyoyaamrisha Allaah kuwa yaungwe na wanafanya ufisadi katika ardhi, hao watapata laana na watapata makazi mabaya (motoni).
اللَّـهُ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ ۚ وَفَرِحُوا بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا مَتَاعٌ ﴿٢٦﴾
26. Allaah Anamkunjulia riziki Amtakaye na Humkadiria kwa kipimo (Amtakaye). Nao wamefurahia uhai wa dunia, na hali uhai wa dunia kulingana na Aakhirah si chochote ila ni starehe ya muda tu.
وَيَقُولُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِّن رَّبِّهِ ۗ قُلْ إِنَّ اللَّـهَ يُضِلُّ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي إِلَيْهِ مَنْ أَنَابَ ﴿٢٧﴾
27. Na wanasema wale waliokufuru: Mbona basi asiteremshiwe Aayah (Muujiza) kutoka kwa Rabb wake? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika Allaah Anampotoa Amtakaye na Anamuongoza kuelekea Kwake anayerudi kutubia.
الَّذِينَ آمَنُوا وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُم بِذِكْرِ اللَّـهِ ۗ أَلَا بِذِكْرِ اللَّـهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ ﴿٢٨﴾
28. Wale walioamini na zikatua nyoyo zao kwa Dhikru-Allaah. Tanabahi! Kwa kumdhukuru Allaah nyoyo hutulia![18]
الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ طُوبَىٰ لَهُمْ وَحُسْنُ مَآبٍ ﴿٢٩﴾
29. Wale walioamini na wakatenda mema watapata mazuri ya kuwafurahisha na kutuza nyoyo na marejeo mazuri (Jannah).
كَذَٰلِكَ أَرْسَلْنَاكَ فِي أُمَّةٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهَا أُمَمٌ لِّتَتْلُوَ عَلَيْهِمُ الَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَهُمْ يَكْفُرُونَ بِالرَّحْمَـٰنِ ۚ قُلْ هُوَ رَبِّي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ مَتَابِ ﴿٣٠﴾
30. Hivyo ndivyo Tumekutuma katika ummah ambao zimepita kabla yake nyumati (nyenginezo) ili uwasomee yale Tuliyokufunulia Wahy, nao wanamkufuru Ar-Rahmaan. Sema: Yeye Ndiye Rabb wangu, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Kwake natawakali na Kwake ni marejeo yangu na tubio langu.
وَلَوْ أَنَّ قُرْآنًا سُيِّرَتْ بِهِ الْجِبَالُ أَوْ قُطِّعَتْ بِهِ الْأَرْضُ أَوْ كُلِّمَ بِهِ الْمَوْتَىٰ ۗ بَل لِّلَّـهِ الْأَمْرُ جَمِيعًا ۗ أَفَلَمْ يَيْأَسِ الَّذِينَ آمَنُوا أَن لَّوْ يَشَاءُ اللَّـهُ لَهَدَى النَّاسَ جَمِيعًا ۗ وَلَا يَزَالُ الَّذِينَ كَفَرُوا تُصِيبُهُم بِمَا صَنَعُوا قَارِعَةٌ أَوْ تَحُلُّ قَرِيبًا مِّن دَارِهِمْ حَتَّىٰ يَأْتِيَ وَعْدُ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُخْلِفُ الْمِيعَادَ ﴿٣١﴾
31. Na kama ingelikuweko Qur-aan ambayo kwayo milima ingeliondoshwa au ardhi ikapasuliwa au wafu wakasemeshwa (basi ni Qur-aan hii hii), bali ni ya Allaah amri ya mambo yote. Je, hawakukata tamaa wale walioamini kwamba kama Angetaka Allaah bila shaka Angeliwahidi watu wote. Na hayatoacha kuwasibu wale waliokufuru maafa ya kuteketeza kwa sababu ya yale waliyoyatenda, au yakawateremkia karibu na nyumba zao, mpaka ifike Ahadi ya Allaah. Hakika Allaah Hakhalifu miadi.
وَلَقَدِ اسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَأَمْلَيْتُ لِلَّذِينَ كَفَرُوا ثُمَّ أَخَذْتُهُمْ ۖ فَكَيْفَ كَانَ عِقَابِ ﴿٣٢﴾
32. Na kwa yakini walifanyiwa istihzai Rusuli kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Nikawapa muhula wale waliokufuru, kisha Nikawachukua kuwaadhibu. Basi ilikuwaje Ikabu[19] Yangu!
أَفَمَنْ هُوَ قَائِمٌ عَلَىٰ كُلِّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ ۗ وَجَعَلُوا لِلَّـهِ شُرَكَاءَ قُلْ سَمُّوهُمْ ۚ أَمْ تُنَبِّئُونَهُ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِي الْأَرْضِ أَم بِظَاهِرٍ مِّنَ الْقَوْلِ ۗ بَلْ زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا مَكْرُهُمْ وَصُدُّوا عَنِ السَّبِيلِ ۗ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ ﴿٣٣﴾
33. Je, basi Anayeisimamia kila nafsi kwa yale iliyoyachuma, (ni sawa na waabudiwa wa uongo?). Hata hivyo wanamfanyia Allaah washirika. Sema: Watajeni! Au, mnampa khabari kwa yale Asiyoyajua katika ardhi, au ni kudhihirisha maneno ya uongo tu? Bali waliokufuru wamepambiwa njama zao na wamezuiliwa na njia (ya haki). Na ambaye Allaah Amempotoa, basi hana wa kumhidi.
لَّهُمْ عَذَابٌ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَشَقُّ ۖ وَمَا لَهُم مِّنَ اللَّـهِ مِن وَاقٍ ﴿٣٤﴾
34. Watapata adhabu katika uhai wa dunia, na bila shaka adhabu ya Aakhirah ni ya mashaka zaidi. Na hawatopata mbele ya Allaah wa kuwahami.
مَّثَلُ الْجَنَّةِ الَّتِي وُعِدَ الْمُتَّقُونَ ۖ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ أُكُلُهَا دَائِمٌ وَظِلُّهَا ۚ تِلْكَ عُقْبَى الَّذِينَ اتَّقَوا ۖ وَّعُقْبَى الْكَافِرِينَ النَّارُ ﴿٣٥﴾
35. Mfano wa Jannah ambayo wameahidiwa wenye taqwa, inapita chini yake mito. Makulaji yake ya kudumu, na pia kivuli chake. Hiyo ndiyo hatima ya Aakhirah ya wale waliokuwa na taqwa. Na hatima ya makafiri ni moto.
وَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَفْرَحُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ ۖ وَمِنَ الْأَحْزَابِ مَن يُنكِرُ بَعْضَهُ ۚ قُلْ إِنَّمَا أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ اللَّـهَ وَلَا أُشْرِكَ بِهِ ۚ إِلَيْهِ أَدْعُو وَإِلَيْهِ مَآبِ ﴿٣٦﴾
36. Na wale Tuliowapa Kitabu (wakaamini) wanafurahia kwa yale yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na miongoni mwa makundi wako wanaoyakanusha baadhi yake. Sema: Hakika mimi nimeamrishwa nimwabudu Allaah, na nisimshirikishe. Kwake nalingania na Kwake ni marejeo yangu.
وَكَذَٰلِكَ أَنزَلْنَاهُ حُكْمًا عَرَبِيًّا ۚ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم بَعْدَ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا وَاقٍ ﴿٣٧﴾
37. Na hivyo ndivyo Tumeiteremsha (Qur-aan) kuwa ni Hukmu (Sharia) kwa Kiarabu. Na kama utafuata hawaa zao baada ya kukujia ilimu, basi hutokuwa na rafiki msaidizi yeyote wala mwenye kukuhami mbele ya Allaah.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ وَجَعَلْنَا لَهُمْ أَزْوَاجًا وَذُرِّيَّةً ۚ وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأْتِيَ بِآيَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ لِكُلِّ أَجَلٍ كِتَابٌ﴿٣٨﴾
38. Na kwa yakini Tulituma Rusuli kabla yako, na Tukawajaalia wawe na wake na dhuria. Na haiwi kwa Rasuli yeyote kuleta Aayah (Muujiza) isipokuwa kwa Idhini ya Allaah. Kila kipindi kina hukmu iliyoandikwa.
يَمْحُو اللَّـهُ مَا يَشَاءُ وَيُثْبِتُ ۖ وَعِندَهُ أُمُّ الْكِتَابِ﴿٣٩﴾
39. Allaah Anafuta yale Ayatakayo na Anathibitisha (Ayatakayo), na Kwake kiko Ummul-Kitaab.[20]
وَإِن مَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ الَّذِي نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ وَعَلَيْنَا الْحِسَابُ ﴿٤٠﴾
40. Na kama Tutakuonyesha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) baadhi ya yale Tunayowaahidi (ya adhabu), au Tukikufisha (basi usijali), lako wewe ni kubalighisha (Risala) tu, na Letu Sisi ni hesabu.
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا نَأْتِي الْأَرْضَ نَنقُصُهَا مِنْ أَطْرَافِهَا ۚ وَاللَّـهُ يَحْكُمُ لَا مُعَقِّبَ لِحُكْمِهِ ۚ وَهُوَ سَرِيعُ الْحِسَابِ﴿٤١﴾
41. Je, hawaoni kwamba Tunaifikia ardhi Tukaipunguza mipaka yake? Na Allaah Anahukumu na hakuna wa kupinga Hukmu Yake. Naye Ni Mwepesi wa kuhesabu.
وَقَدْ مَكَرَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَلِلَّـهِ الْمَكْرُ جَمِيعًا ۖ يَعْلَمُ مَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ ۗ وَسَيَعْلَمُ الْكُفَّارُ لِمَنْ عُقْبَى الدَّارِ ﴿٤٢﴾
42. Na kwa yakini walifanya makri wale wa kabla yao, basi Allaah Ana mipango yote ya kulipiza makri. Allaah Anajua yale yote yanayochumwa na kila nafsi. Na makafiri watajua ni ya nani itakuwa hatima njema ya makazi ya Aakhirah.
وَيَقُولُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَسْتَ مُرْسَلًا ۚ قُلْ كَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ وَمَنْ عِندَهُ عِلْمُ الْكِتَابِ﴿٤٣﴾
43. Na wanasema waliokufuru: Wewe si Rasuli uliyetumwa. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Anatosheleza Allaah kuwa Ni Shahidi baina yangu na baina yenu, na pia (shahidi) yule mwenye ilimu ya Kitabu.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Istawaa اسْتَوَى
Yuko juu kwa namna inayolingana na Uadhama na Ujalali Wake Yeye Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-A'raaf (7:54) kwenye maelezo bayana ya maana yake, yenye kutofautiana na maana ya katika Suwrah Al-Baqarah (2:29) na Suwrat Fusswilat (41:11).
[3] Dalili Za Allaah (سبحانه وتعالى) Kwa Watu Wanaotia Akilini:
Na kwenye ardhi kuna sehemu zinazopakana. Kati ya hizo kuna zilizo nzuri zenye kuotesha mimea inayowafaa watu, na kati ya hizo kuna kavu zenye chumvi zisizootesha chochote. Na katika ardhi nzuri kuna mashamba ya zabibu, na Amejaalia humo aina tafauti za mazao na mitende iliyokusanyika mahali pamoja na isiyokusanyika hapo, vyote hivyo viko katika mchanga mmoja na vinakunywa maji mamoja, isipokuwa vinatafautiana katika matunda, ukubwa, utamu na mengineyo; hili ni tamu na hili ni kali, hili ni chungu, na mengine ni bora kuliko mengine katika kula. Katika hilo kuna dalili kwa mwenye moyo unaoyaelewa maamrisho ya Allaah (سبحانه وتعالى) na makatazo Yake. [Tafsiyr Al-Muyassar] Na Imaam As-Sa’diy ameuliza baada ya maelezo hayo:
“Je, tofauti hizo zinatokana na mimea yenyewe na asili zake, au hayo yote ni Qudura ya Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika Mwenye Kurehemu? [Tafsiyr As-Sa’diy]
Rejea pia Yaasiyn (36:38).
[4] Washirikina Hawakuamini Kuwa Watafufuliwa:
Rejea Al-Israa (17:49) kwenye maelezo bayana na rejea mbali mbali.
[5] Makafiri Wataingizwa Motoni Na Kufungwa Minyororo Shingoni Mwao:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja kuwa makafiri watafungwa minyororo shingoni mwao. Hii ni ishara ya kifungo kama vile mtu anayefungwa gerezani. Rejea pia Yaasiyn (36:8), Saba-a (34:33), Ghaafir (40:71), na Al-Insaan (76:4). Allaah (سبحانه وتعالى) Anatumia maneno haya hapa na katika Aayah nyenginezo kimafumbo ili kuonyesha kuwa wao ni watumwa wa ujinga, ukaidi, na tamaa, na ni wafuasi vipofu wa mababu zao. Kwa vile mawazo yao yameathiriwa na chuki zao, hawawezi kuamini Aakhirah. Wanakanusha kufufuliwa na kuhesabiwa ilhali kuna kila sababu ya kuamini kwamba hayo hayaepukiki. Na wao walikuwa si chochote kabla ya kuumbwa, na Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) kuwafufua viumbe ni jambo jepesi mno Kwake. Rejea At-Taghaabun (64:7). Juu ya hivyo, Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) kuumba kiumbe ni jambo jepesi mno kuliko kuumba mbingu na ardhi. Rejea Ghaafir (40:57). Na kufufua viumbe na kuwaumba upya ni jambo jepesi mno Kwake Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Ar-Ruwm (30:27).
[6] Malaika Wanaolinda Waja Wa Allaah Usiku Na Mchana:
Imaam As-Sa’diy amesema: Wanaulinda mwili na roho yake kutokana na kila anayemtakia mabaya, na wanachunga amali zake, na wanaambatana naye daima. Na juu ya kuwa Ilimu ya Allaah inamzunguka, pamoja na hivyo, Allaah Amewatuma Malaika hawa walinzi kwa Waja Wake, kwa namna ambayo hali zao na matendo yao haiwezekani kufichika, na hakuna chochote kinachosahaulika kutokana na hayo. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Na Hadiyth ifuatayo imefafanua:
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، قَالَ حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ أَبِي الزِّنَادِ، عَنِ الأَعْرَجِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " يَتَعَاقَبُونَ فِيكُمْ مَلاَئِكَةٌ بِاللَّيْلِ وَمَلاَئِكَةٌ بِالنَّهَارِ، وَيَجْتَمِعُونَ فِي صَلاَةِ الْفَجْرِ وَصَلاَةِ الْعَصْرِ، ثُمَّ يَعْرُجُ الَّذِينَ بَاتُوا فِيكُمْ، فَيَسْأَلُهُمْ وَهْوَ أَعْلَمُ بِهِمْ كَيْفَ تَرَكْتُمْ عِبَادِي فَيَقُولُونَ تَرَكْنَاهُمْ وَهُمْ يُصَلُّونَ، وَأَتَيْنَاهُمْ وَهُمْ يُصَلُّونَ ".
Amesimulia Abu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wanakujieni kwa zamu; Malaika wa mchana na Malaika wa usiku, na wote wanajumuika wakati wa Swalaah ya Alfajiri na Swalaah ya Alasiri. Wale waliokesha nanyi usiku hupanda (mbinguni) na Allaah Huwauliza - Naye Allaah Anajua vyema hali yao- Mmewaachaje Waja Wangu? Malaika hujibu: Tumewaacha wakiwa wanaswali, na tumewafikia wakiwa wanaswali.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
[7] Kila Kitu Kinamsabbih Allaah (عزّ وجلّ):
Rejea Al-Hashr (57:1) kwenye rejea zinazotaja viumbe na vitu Alivyoviumba Allaah kuwa vinamsabbih Yeye Allaah (عزّ وجلّ).
[8] Duaa Ya Kuomba Inapotokea Radi:
‘Abdullaah bin Zubayr (رضي الله عنه) alikuwa anaposikia radi, basi huacha mazungumzo na badala yake husema:
سُبْـحانَ الّذي يُسَبِّـحُ الـرَّعْدُ بِحَمْـدِهِ، وَالملائِكـةُ مِنْ خيـفَته.
Ametakasika Yule Ambaye radi zinamsabihi kwa Himdi Zake na Malaika pia (wanamsabihi) kwa kumkhofu. [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Zubayr (رضي الله عنه), Al-Muwattwa (2/992), na Al-Albaaniy (رحمه الله) amesema: Isnaad yake ni Swahiyh Mawquwfaa]
[10] Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee Ana Haki Ya Kuabudiwa:
Ni kumwabudu Yeye (Allaah) Pekee Asiye na mshirika, na kumtakasia Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) niyya katika duaa ya ibaada na maombi mengineyo; yaani Yeye Ndiye Anayepaswa kuelekezewa duaa, khofu, matarajio, mapenzi. raghba (utashi), kuogopwa, na kurejea Kwake, kwa sababu Uluwhiyyah (kumpwekesha Allaah katika ibaada) Kwake ndio Uluwhiyyah ya haki, na Uluwhiyyah kwa asiyekuwa Yeye ni batili. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[11] Duaa Za Washirikina Na Makafiri Kwa Waabudiwa Wao Haziitikiwi, Mfano Wa Maji Kutokuwafikia Vinywani Mwao Katika Kiu Kikali:
Ni kama hali ya mtu mwenye kiu kikali mno anayenyoosha mkono wake kuyaelekea maji yaliyoko mbali ayachote yamfikie mdomoni mwake lakini hayamfikii! Na hii ndio hali ya makafiri na washirikina wanaowaomba waabudiwa wao lakini hawawaitikii kwa lolote wala hawawapatii haja zao, kwa sababu wao wenyewe ni masikini wahitaji kama walivyo waabudiwa wao wanaowaomba, hawamiliki uzito wa chembe ardhini wala mbinguni. Rejea Saba-a (34:22), Faatwir (35:13-14).
[12] Kila Kitu Kinamsujudia Allaah (عزّ وجلّ):
Rejea Ar-Rahmaan (55:6) kwenye rejea zinazotaja viumbe na vitu Alivyoviumba Allaah kuwa vinamsujudia Yeye Allaah (عزّ وجلّ).
[13] Ufafanuzi Wa Washirikina Kwamba Wamechanganyikiwa Akili Hawatambui Walivyoumba Wao Na Alivyoumba Allaah (عزّ وجلّ):
Au ni kwamba wale wasimamizi wao wanaowafanya ni washirika wa Allaah (سبحانه وتعالى) wanaumba kama Anavyoumba Allaah (سبحانه وتعالى) vikawatatiza (na kuwachanganya akili) viumbe vya washirika na viumbe vya Allaah (سبحانه وتعالى) ndipo wakaitakidi kwamba wao wanastahiki kuabudiwa? [Tafsiyr Al-Muyassar].
Je, hawa washirikina wanaabudu miungu isiyokuwa Yeye (Allaah) inayoshindana Naye katika Alichokiumba? Je, waungu wao wa uwongo wameumba viumbe vinavyofanana na Alivyoviumba Allaah, na hivyo wamechanganyikiwa (akili) baina ya aina mbili za viumbe, bila ya kujua ni kipi kimeumbwa na wengine badala ya Allaah! [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Ni swali la kuwataka wafungue akili zao. Allaah Kawaumba wao, Akawapa uhai, nguvu, afya, akili na kila kitu, nao bado ni viumbe ajizi, hawawezi lolote. Na hiyo miungu yao ambayo wao wanaitengeneza kwa mikono yao, ndio ajizi zaidi kuliko wao wenyewe. Vipi basi itaweza kuumba chochote kifanane na Alivyoviumba Allaah?
[14] Mfano Wa Haki Na Batili:
Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akapiga mfano wa ukweli na urongo kuwa ni kama maji Aliyoyateremsha kutoka juu, yakapita kwenye mabonde ya ardhi kwa kadiri ya udogo wake na ukubwa wake. Mikondo ya maji ikabeba povu likiwa juu yake lisilo na faida. Na Akapiga mfano mwingine wa madini ambayo watu huyachoma moto ili kuyayeyusha kutaka kutengeneza pambo, kama vile dhahabu na fedha, au kutaka manufaa ya kujinufaisha, kama vile shaba, ukatoka uchafu wake usio na faida kama ule uliokuwa pamoja na maji. Kwa mfano huu, Allaah (سبحانه وتعالى) Apigia mfano ukweli na urongo. Urongo ni kama povu la maji, linapotea au linatupwa kwa kuwa halina faida, na ukweli ni kama maji safi na madini yaliyotakasika, yanasalia kwenye ardhi kwa kunufaika nayo. Kama Alivyowafafanulia nyinyi mifano hii, hivyo ndivyo Anavyoipiga kwa watu upate kufunuka wazi ukweli ujitenge na urongo, na uongofu ujitenge na upotevu. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[15] Ahadi ya Alastu - Rejea Al-Ar’aaf (7:172), na Suwrah hii Ar-Ra’d (13:25).
[16] Kuunga Aliyoyaamrisha Allaah:
Ni kuunga mambo ya kiujumla, nayo ni mengi katika kila Alichoamrisha Allaah (سبحانه وتعالى) kuungwa kama vile kumuamini Yeye na Rasuli Wake, kumpenda Yeye na Rasuli Wake, kumuabudu Yeye Pekee bila ya kumshirikisha, na kumtii Yeye na Rasuli Wake. Na Pia, kuwasiliana na kuungana na baba zao na mama zao kwa ihsaan na wema kwa kauli na matendo, bila kuwaasi. Vile vile, wanawasiliana na kuwaunga jamaa na Arhaam (ndugu na jamaa wenye uhusiano wa damu) kwa kuwatendea ihsaan na wema kwa kauli na matendo, na wanaunganisha yaliyo baina yao na baina ya waume na wake zao, rafiki zao na watumwa wao kwa kutimizia haki zao kikamilifu, haki za kidini na za dunia. [Tafsiyr As-Sa’diy)]
Rejea Suwrah hii Ar-Ra’d (13:25). Ama kuhusu kukata undugu, basi kuna Laana ya Allaah, Rejea Muhammad (47:22-23).
[17] Fadhila Ya Kuhidika Pamoja Na Wazee, Wana Na Jamaa Wa Karibu:
Hii ni sawa na Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwrah Atw-Twuwr (52:21) kwamba watu wenye uhusiano kama huu wa imaan watakutanishwa kuwa pamoja katika Jannah.
[18] Nyoyo Kutua Kwa Dhikru-Allaah (Kumdhukuru Allaah):
Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja alama za Waumini Anaposema:
الَّذِينَ آمَنُوا وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُم بِذِكْرِ اللَّـهِ ۗ
“Wale walioamini na zikatua nyoyo zao kwa Dhikru-Allaah.”
Yaani: Wahka, wasiwasi, mashaka yao hutoweka, na badala yake kubadilishiswa furaha na raha.
أَلَا بِذِكْرِ اللَّـهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ ﴿٢٨﴾
“Tanabahi! Kwa kumdhukuru Allaah nyoyo hutulia.”
Yaani: Hii ni asili yao (Waumini) na ni ya kutarajiwa kwamba wao hawapati faraja kwa chochote isipokuwa kwa Dhikru-Allaah kwa sababu hakuna kinacholeta furaha kubwa ya nyoyo na hakuna kitu kinachohitajika zaidi na chenye ladha zaidi moyoni isipokuwa Kumpenda Muumba wake, na kujikurubisha Kwake na maarifa Yake (kumtambua Kwa Majina Yake Mazuri na Sifa Zake). Basi kulingana na jinsi ya maarifa ya Allaah na kumpenda Kwake, ndivyo itakavyokuwa kiwango cha kumdhukuru. Kinachomaanishwa ni kuwa Dhikru-Allaah, ni mja kumdhukuru Allaah kwa Tasbiyh (Kumtakasa), Tahliyl (Kumpwekesha), na Takbiyr (Kumtukuza) na vinginevyo.
Na ikasemwa: Maana ya Dhikru-Allaah ni Kitabu Chake Alichokiteremsha kuwa ukumbusho kwa Waumini. Na kinachomaanisha nyoyo kutulia kwa Dhikru-Allaah, ni pindi moyo unapojua na kufahamu maana za Qur-aan na hukumu zake basi moyo hutulia kwa sababu (Qur-aan) inabainisha ukweli uliowazi unaoungwa mkono na burhani (dalili za waziwazi) hivyo basi nyoyo hutulia kwani nyoyo hazitulii ila kwa yakini na ilimu. Na hayo yamo katika Kitabu cha Allaah kilichohakikishwa kwa utimilifu na ukamilifu. Ama vitabu vingine ambavyo haviambatani na nyoyo, basi nyoyo hazitapata utulivu bali zitabakia kuwa na wahka, mashaka wasiwasi kwa sababu ya kukinzana ushahidi wake na hukmu zake. Na ndio Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ ۚ وَلَوْ كَانَ مِنْ عِندِ غَيْرِ اللَّـهِ لَوَجَدُوا فِيهِ اخْتِلَافًا كَثِيرًا ﴿٨٢﴾
“Je, hawaizingatii Qur-aan? Na lau ingelikuwa imetoka kwa asiyekuwa Allaah, bila shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi.” [An-Nisaa (4:82)]
[Tafsiyr As-Sa’diy]
[19] Tofauti Ya Ikabu Na Adhabu: Rejea Al-Hashr (59:4).
[20] Ummul-Kitaab (Mama Wa Kitabu):
Katika Aayah hii, Ummul-Kitaab imekusudiwa Al-Lawh Al-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa) Rejea Al-Buruwj (85:22). Ndani yake humo, Allaah Ameandika yote yaliyotokea na yatakayotokea mpaka Siku ya Qiyaamah. Na maana nyengineyo ya Ummul-Kitaab ni mojawapo ya majina ya Suwrah Al-Faatihah.
إِبْرَاهِيم
014-Ibraahiym
014-Ibraahiym: Utangulizi Wa Suwrah [155]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الر ۚ كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ ﴿١﴾
1. Alif Laam Raa.[1] Kitabu Tumekiteremsha kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ili uwatoe watu kutoka kwenye viza kuwaingiza katika nuru[2] kwa Idhini ya Rabb wao, waelekee katika njia ya Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.
اللَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَوَيْلٌ لِّلْكَافِرِينَ مِنْ عَذَابٍ شَدِيدٍ ﴿٢﴾
2. Naye ni Allaah Ambaye ni Vyake vilivyomo katika mbingu na katika ardhi. Na ole kwa makafiri kwa adhabu kali.
الَّذِينَ يَسْتَحِبُّونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا ۚ أُولَـٰئِكَ فِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ ﴿٣﴾
3. Ambao wanasitahabu uhai wa dunia kuliko wa Aakhirah, na wanazuia Njia ya Allaah, na wanaitafutia upogo. Hao wamo katika upotofu wa mbali.
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوْمِهِ لِيُبَيِّنَ لَهُمْ ۖ فَيُضِلُّ اللَّـهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٤﴾
4. Na Hatukutuma Rasuli yeyote isipokuwa kwa lugha ya kaumu yake ili awabainishie (Risala). Basi Allaah Humpotoa Amtakaye na Humhidi Amtakaye. Naye Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا أَنْ أَخْرِجْ قَوْمَكَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَذَكِّرْهُم بِأَيَّامِ اللَّـهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ﴿٥﴾
5. Na kwa yakini Tulimpeleka Muwsaa akiwa pamoja na Aayaat (Ishara, Miujiza, Dalili) Zetu (Tukimwambia): Itoe kaumu yako kutoka kwenye viza kwenda katika nuru, na wakumbushe Siku za Allaah.[3] Hakika katika hayo kuna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa kila mwingi wa kusubiri na kushukuru.
وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ أَنجَاكُم مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَسُومُونَكُمْ سُوءَ الْعَذَابِ وَيُذَبِّحُونَ أَبْنَاءَكُمْ وَيَسْتَحْيُونَ نِسَاءَكُمْ ۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَاءٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَظِيمٌ ﴿٦﴾
6. Na pindi Muwsaa alipoiambia kaumu yake: Kumbukeni Neema ya Allaah juu yenu, Alipokuokoeni kutokana na watu wa Firawni walipokusibuni adhabu mbaya, na wakiwachinja watoto wenu wa kiume na wakiacha hai wanawake wenu. Na katika hayo ulikuwa ni mtihani mkuu kutoka kwa Rabb wenu.
وَإِذْ تَأَذَّنَ رَبُّكُمْ لَئِن شَكَرْتُمْ لَأَزِيدَنَّكُمْ ۖ وَلَئِن كَفَرْتُمْ إِنَّ عَذَابِي لَشَدِيدٌ﴿٧﴾
7. Na pindi Alipotangaza Rabb wenu: Ikiwa mtashukuru, bila shaka Nitakuzidishieni (Neema Zangu), na mkikufuru, basi hakika Adhabu Yangu ni kali.
وَقَالَ مُوسَىٰ إِن تَكْفُرُوا أَنتُمْ وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا فَإِنَّ اللَّـهَ لَغَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴿٨﴾
8. Na Muwsaa alisema: Mkikufuru nyinyi na wote walioko ardhini, basi hakika Allaah Ni Mkwasi, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.
أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَبَأُ الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ ۛ وَالَّذِينَ مِن بَعْدِهِمْ ۛ لَا يَعْلَمُهُمْ إِلَّا اللَّـهُ ۚ جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَرَدُّوا أَيْدِيَهُمْ فِي أَفْوَاهِهِمْ وَقَالُوا إِنَّا كَفَرْنَا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ وَإِنَّا لَفِي شَكٍّ مِّمَّا تَدْعُونَنَا إِلَيْهِ مُرِيبٍ ﴿٩﴾
9. Je, haijakufikieni khabari ya wale wa kabla yenu; watu wa Nuwh, na ‘Aad na Thamuwd, na wale wa baada yao? Hakuna Awajuao isipokuwa Allaah. Rusuli wao waliwajia kwa hoja bayana, nao wakarudisha mikono yao katika vinywa vyao[4] na wakasema: Hakika sisi tumeyakanusha yale mliyotumwa nayo, na hakika sisi tumo katika shaka kutokana na mnayotuitia kwayo na tunayashuku.
قَالَتْ رُسُلُهُمْ أَفِي اللَّـهِ شَكٌّ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يَدْعُوكُمْ لِيَغْفِرَ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرَكُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ قَالُوا إِنْ أَنتُمْ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا تُرِيدُونَ أَن تَصُدُّونَا عَمَّا كَانَ يَعْبُدُ آبَاؤُنَا فَأْتُونَا بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ ﴿١٠﴾
10. Wakasema Rusuli wao: Je, kuna shaka kuhusiana na Allaah, Muanzilishi wa mbingu na ardhi? Anakuiteni ili Akughufurieni madhambi yenu na Akuakhirisheni mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Wakasema: Nyinyi si chochote isipokuwa ni watu tu kama sisi, mnachotaka ni kutuzuia tu na yale waliyokuwa wakiabudu baba zetu. Basi tuleteeni uthibitisho bayana.
قَالَتْ لَهُمْ رُسُلُهُمْ إِن نَّحْنُ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَمُنُّ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ وَمَا كَانَ لَنَا أَن نَّأْتِيَكُم بِسُلْطَانٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١١﴾
11. Wakasema Rusuli wao: Sisi si chochote isipokuwa ni watu tu kama nyinyi, lakini Allaah Anamfadhilisha Amtakaye miongoni mwa Waja Wake. Na haitupasi sisi kuwaleteeni uthibitisho isipokuwa kwa Idhini ya Allaah. Na kwa Allaah watawakali Waumini.
وَمَا لَنَا أَلَّا نَتَوَكَّلَ عَلَى اللَّـهِ وَقَدْ هَدَانَا سُبُلَنَا ۚ وَلَنَصْبِرَنَّ عَلَىٰ مَا آذَيْتُمُونَا ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُتَوَكِّلُونَ ﴿١٢﴾
12. Na tuna nini (sisi) hata tusitawakali kwa Allaah na hali Amekwishatuongoza njia yetu? Na kwa yakini tutasubiri juu ya maudhi yenu kwetu. Na kwa Allaah watawakali wanaotawakali.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِرُسُلِهِمْ لَنُخْرِجَنَّكُم مِّنْ أَرْضِنَا أَوْ لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَا ۖ فَأَوْحَىٰ إِلَيْهِمْ رَبُّهُمْ لَنُهْلِكَنَّ الظَّالِمِينَ ﴿١٣﴾
13. Wakasema wale waliokufuru kuwaambia Rusuli wao: Lazima tutakutoeni katika ardhi yetu, au mtarudi kwa nguvu katika dini yetu. Basi Rabb wao Akawafunulia Wahy kwamba: Hakika Tutawahiliki madhalimu.
وَلَنُسْكِنَنَّكُمُ الْأَرْضَ مِن بَعْدِهِمْ ۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَافَ مَقَامِي وَخَافَ وَعِيدِ ﴿١٤﴾
14. Na bila shaka Tutakuwekeni maskani katika ardhi baada yao. Haya ni kwa yule anayekhofu kusimamishwa mbele Yangu na akakhofu Maonyo Yangu.
وَاسْتَفْتَحُوا وَخَابَ كُلُّ جَبَّارٍ عَنِيدٍ﴿١٥﴾
15. Na wakaomba ushindi (kwa Allaah), na akapita patupu kila (aliyejifanya) jabari, mkaidi.
مِّن وَرَائِهِ جَهَنَّمُ وَيُسْقَىٰ مِن مَّاءٍ صَدِيدٍ ﴿١٦﴾
16. Nyuma yake kuna Jahannam, na atanyweshwa maji ya usaha.
يَتَجَرَّعُهُ وَلَا يَكَادُ يُسِيغُهُ وَيَأْتِيهِ الْمَوْتُ مِن كُلِّ مَكَانٍ وَمَا هُوَ بِمَيِّتٍ ۖ وَمِن وَرَائِهِ عَذَابٌ غَلِيظٌ ﴿١٧﴾
17. Atayagugumia kwa tabu na atakurubia asiweze kuyameza yakashuka kooni, na yatamjia mauti kutoka kila upande, naye hatokufa hata kidogo. Na nyuma yake kuna adhabu nzito.[5]
مَّثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ ۖ أَعْمَالُهُمْ كَرَمَادٍ اشْتَدَّتْ بِهِ الرِّيحُ فِي يَوْمٍ عَاصِفٍ ۖ لَّا يَقْدِرُونَ مِمَّا كَسَبُوا عَلَىٰ شَيْءٍ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الضَّلَالُ الْبَعِيدُ ﴿١٨﴾
18. Mfano wa wale waliomkufuru Rabb wao, amali zao ni kama jivu linalopeperushwa kwa nguvu za upepo siku ya dhoruba. Hawatoweza kupata chochote katika yale waliyoyachuma. Huo ndio upotofu wa mbali.
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۚ إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَأْتِ بِخَلْقٍ جَدِيدٍ ﴿١٩﴾
19. Je, huoni kwamba Allaah Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Akitaka Atakuondosheleeni mbali na Alete viumbe vipya.
وَمَا ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ بِعَزِيزٍ ﴿٢٠﴾
20. Na hilo halina uzito wowote kwa Allaah.
وَبَرَزُوا لِلَّـهِ جَمِيعًا فَقَالَ الضُّعَفَاءُ لِلَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا كُنَّا لَكُمْ تَبَعًا فَهَلْ أَنتُم مُّغْنُونَ عَنَّا مِنْ عَذَابِ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ ۚ قَالُوا لَوْ هَدَانَا اللَّـهُ لَهَدَيْنَاكُمْ ۖ سَوَاءٌ عَلَيْنَا أَجَزِعْنَا أَمْ صَبَرْنَا مَا لَنَا مِن مَّحِيصٍ ﴿٢١﴾
21. Na watahudhuria wote mbele ya Allaah. Wanyonge watawaambia wale waliotakabari: Hakika sisi tulikuwa wafuasi wenu (tukikutiini), basi je, nyinyi mtaweza kutuondolea chochote katika Adhabu ya Allaah? Watasema: Kama Allaah Angetuhidi, bila shaka tungelikuongozeni. Ni sawasawa kwetu tukipapatika au tukisubiri, hatuna mahali pa kukimbilia.
وَقَالَ الشَّيْطَانُ لَمَّا قُضِيَ الْأَمْرُ إِنَّ اللَّـهَ وَعَدَكُمْ وَعْدَ الْحَقِّ وَوَعَدتُّكُمْ فَأَخْلَفْتُكُمْ ۖ وَمَا كَانَ لِيَ عَلَيْكُم مِّن سُلْطَانٍ إِلَّا أَن دَعَوْتُكُمْ فَاسْتَجَبْتُمْ لِي ۖ فَلَا تَلُومُونِي وَلُومُوا أَنفُسَكُم ۖ مَّا أَنَا بِمُصْرِخِكُمْ وَمَا أَنتُم بِمُصْرِخِيَّ ۖ إِنِّي كَفَرْتُ بِمَا أَشْرَكْتُمُونِ مِن قَبْلُ ۗ إِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٢٢﴾
22. Na shaytwaan atasema litakapokidhiwa jambo: Hakika Allaah Alikuahidini ahadi ya haki (na Ameitimiza), nami nilikuahidini kisha nikakukhalifuni. Na sikuwa na mamlaka juu yenu isipokuwa nilikuiteni mkaniitikia. Basi msinilaumu, bali laumuni nafsi zenu. Mimi siwezi kukusaidieni kukuokoeni wala nyinyi hamuwezi kunisaidia kuniokoa. Hakika mimi nilikanusha yale mliyonishirikisha zamani. Hakika madhalimu watapata adhabu iumizayo.[6]
وَأُدْخِلَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِمْ ۖ تَحِيَّتُهُمْ فِيهَا سَلَامٌ ﴿٢٣﴾
23. Na wataingizwa wale walioamini na wakatenda mema, Jannaat zipitazo chini yake mito wadumu humo kwa Idhini ya Rabb wao. Maamkizi yao humo yatakuwa ni Salaam.
أَلَمْ تَرَ كَيْفَ ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا كَلِمَةً طَيِّبَةً كَشَجَرَةٍ طَيِّبَةٍ أَصْلُهَا ثَابِتٌ وَفَرْعُهَا فِي السَّمَاءِ ﴿٢٤﴾
24. Je, huoni vipi Allaah Amepiga mfano wa neno zuri? Ni kama mti mzuri,[7] mizizi yake imethibitika imara na matawi yake yanafika mbinguni.
تُؤْتِي أُكُلَهَا كُلَّ حِينٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا ۗ وَيَضْرِبُ اللَّـهُ الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٥﴾
25. Unatoa mazao yake kila wakati kwa Idhini ya Rabb wake. Na Allaah Anapiga mifano kwa watu ili wapate kukumbuka.
وَمَثَلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٍ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ اجْتُثَّتْ مِن فَوْقِ الْأَرْضِ مَا لَهَا مِن قَرَارٍ ﴿٢٦﴾
26. Na mfano wa neno baya ni kama mti mbaya uliong’olewa juu ya ardhi hauna uimara.
يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَيُضِلُّ اللَّـهُ الظَّالِمِينَ ۚ وَيَفْعَلُ اللَّـهُ مَا يَشَاءُ﴿٢٧﴾
27. Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhira.[8] Na Allaah Huwaacha kupotoka madhalimu. Na Allaah Anafanya Atakavyo.
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ بَدَّلُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ كُفْرًا وَأَحَلُّوا قَوْمَهُمْ دَارَ الْبَوَارِ﴿٢٨﴾
28. Je, huoni wale waliobadilisha Neema ya Allaah kwa kufru, na wakawafikisha watu wao nyumba ya mateketezo?
جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا ۖ وَبِئْسَ الْقَرَارُ ﴿٢٩﴾
29. Jahannam wataiingia na kuungua, na ubaya ulioje mahala pa kutulia!
وَجَعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا لِّيُضِلُّوا عَن سَبِيلِهِ ۗ قُلْ تَمَتَّعُوا فَإِنَّ مَصِيرَكُمْ إِلَى النَّارِ ﴿٣٠﴾
30. Na wakamfanyia Allaah walinganishi ili wapoteze (watu) na Njia Yake. Sema: Stareheni! Kwani hakika mahali penu pa kurudia hatimaye ni motoni.
قُل لِّعِبَادِيَ الَّذِينَ آمَنُوا يُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُنفِقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا بَيْعٌ فِيهِ وَلَا خِلَالٌ ﴿٣١﴾
31. Waambie (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Waja Wangu ambao wameamini: Wasimamishe Swalaah na watoe katika yale Tuliyowaruzuku kwa siri na dhahiri kabla haijafika Siku ambayo hakutakuweko biashara wala urafiki wa kweli.
اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ الْفُلْكَ لِتَجْرِيَ فِي الْبَحْرِ بِأَمْرِهِ ۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ الْأَنْهَارَ﴿٣٢﴾
32. Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi, na Akateremsha maji kutoka mbinguni, Akatoa kwayo mazao kuwa ni riziki kwenu. Na Akakutiishieni majahazi ili yapite baharini kwa Amri Yake. Na Akakutiishieni mito.
وَسَخَّرَ لَكُمُ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ دَائِبَيْنِ ۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ ﴿٣٣﴾
33. Na Akakutiishieni jua na mwezi vinavyozunguka daima dawamu na Akakutiishieni usiku na mchana.
وَآتَاكُم مِّن كُلِّ مَا سَأَلْتُمُوهُ ۚ وَإِن تَعُدُّوا نِعْمَتَ اللَّـهِ لَا تُحْصُوهَا ۗ إِنَّ الْإِنسَانَ لَظَلُومٌ كَفَّارٌ ﴿٣٤﴾
34. Na Akakupeni kila mlichomuomba. Na mkihesabu Neema za Allaah hamtoweza kuziorodhesha hesabuni.[9] Hakika binaadam ni mwingi wa dhulma, mwingi wa kukufuru.
وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ اجْعَلْ هَـٰذَا الْبَلَدَ آمِنًا وَاجْنُبْنِي وَبَنِيَّ أَن نَّعْبُدَ الْأَصْنَامَ ﴿٣٥﴾
35. Na Ibraahiym aliposema: Ee Rabb wangu! Ujaalie mji huu (Makkah) uwe wa amani, na Uniepushe na wanangu kuabudu masanamu.[10]
رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ ۖ فَمَن تَبِعَنِي فَإِنَّهُ مِنِّي ۖ وَمَنْ عَصَانِي فَإِنَّكَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٦﴾
36. Rabb wangu! Hakika hao (masanamu) wamepoteza watu wengi. Basi atakayenifuata, huyo yuko nami, na atakayeniasi, basi hakika Wewe Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
رَّبَّنَا إِنِّي أَسْكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيْرِ ذِي زَرْعٍ عِندَ بَيْتِكَ الْمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُوا الصَّلَاةَ فَاجْعَلْ أَفْئِدَةً مِّنَ النَّاسِ تَهْوِي إِلَيْهِمْ وَارْزُقْهُم مِّنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَشْكُرُونَ ﴿٣٧﴾
37. Rabb wetu! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuria wangu katika bonde lisilokuwa na mmea wowote, kwenye Nyumba Yako Tukufu (Al-Ka’bah), ee Rabb wetu ili wasimamishe Swalaah. Basi Zijaalie nyoyo za watu zielekee kwao na Uwaruzuku mazao ili wapate kushukuru.
رَبَّنَا إِنَّكَ تَعْلَمُ مَا نُخْفِي وَمَا نُعْلِنُ ۗ وَمَا يَخْفَىٰ عَلَى اللَّـهِ مِن شَيْءٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ ﴿٣٨﴾
38. Rabb wetu! Hakika Wewe Unajua tunayoyaficha na tunayoyadhihirisha. Na hakifichiki kitu chochote kwa Allaah katika ardhi wala katika mbingu.
الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي وَهَبَ لِي عَلَى الْكِبَرِ إِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ ۚ إِنَّ رَبِّي لَسَمِيعُ الدُّعَاءِ ﴿٣٩﴾
39. AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Ambaye Amenitunukia juu ya umri mkubwa wangu Ismaa’iyl na Is-haaq. Hakika Rabb wangu bila shaka Ni Mwenye Kusikia duaa yangu.
رَبِّ اجْعَلْنِي مُقِيمَ الصَّلَاةِ وَمِن ذُرِّيَّتِي ۚ رَبَّنَا وَتَقَبَّلْ دُعَاءِ﴿٤٠﴾
40. Rabb wangu! Nijaalie niwe mwenye kusimamisha Swalaah pamoja na dhuria wangu. Rabb wetu! Nitakabalie duaa yangu.
رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَابُ ﴿٤١﴾
41. Rabb wetu! Nighufurie mimi na wazazi wangu wawili[11] na Waumini Siku itakayosimama hesabu.
وَلَا تَحْسَبَنَّ اللَّـهَ غَافِلًا عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ ۚ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الْأَبْصَارُ ﴿٤٢﴾
42. Na wala usidhanie kabisa kwamba Allaah Ameghafilika na yale wanayoyatenda madhalimu. Hakika Anawaakhirisha kwa ajili ya Siku ambayo macho yatakodoka.
مُهْطِعِينَ مُقْنِعِي رُءُوسِهِمْ لَا يَرْتَدُّ إِلَيْهِمْ طَرْفُهُمْ ۖ وَأَفْئِدَتُهُمْ هَوَاءٌ ﴿٤٣﴾
43. Watoke haraka haraka (makaburini), wakiwa wamenyanyua vichwa vyao juu, macho yao hayapepesi na nyoyo zao ni tupu (kwa kiwewe na huzuni).
وَأَنذِرِ النَّاسَ يَوْمَ يَأْتِيهِمُ الْعَذَابُ فَيَقُولُ الَّذِينَ ظَلَمُوا رَبَّنَا أَخِّرْنَا إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ نُّجِبْ دَعْوَتَكَ وَنَتَّبِعِ الرُّسُلَ ۗ أَوَلَمْ تَكُونُوا أَقْسَمْتُم مِّن قَبْلُ مَا لَكُم مِّن زَوَالٍ﴿٤٤﴾
44. Na waonye watu Siku itakayowafikia adhabu, na wale waliodhulumu waseme: Rabb wetu! Tuakhirishe mpaka muda mdogo ili tuitikie Wito Wako na tuwafuate Rusuli. (Wataambiwa): Je, kwani hamkuwa mmeapa kabla kwamba hamtokuwa wenye kuondoshwa (duniani?).
وَسَكَنتُمْ فِي مَسَاكِنِ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ وَتَبَيَّنَ لَكُمْ كَيْفَ فَعَلْنَا بِهِمْ وَضَرَبْنَا لَكُمُ الْأَمْثَالَ ﴿٤٥﴾
45. Na mkakaa katika maskani za wale waliodhulumu nafsi zao na ikakubainikieni vipi Tulivyowafanya, na Tukakupigieni mifano mingi?
وَقَدْ مَكَرُوا مَكْرَهُمْ وَعِندَ اللَّـهِ مَكْرُهُمْ وَإِن كَانَ مَكْرُهُمْ لِتَزُولَ مِنْهُ الْجِبَالُ﴿٤٦﴾
46. Na kwa yakini wamefanya mipango ya makri zao, na kwa Allaah kuna (rekodi ya) makri zao japokuwa makri zao haziwezi kuondosha milima.
فَلَا تَحْسَبَنَّ اللَّـهَ مُخْلِفَ وَعْدِهِ رُسُلَهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٤٧﴾
47. Basi usidhanie kabisa kwamba Allaah Ni Mwenye Kukhalifu Ahadi Yake kwa Rusuli Wake. Hakika Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kulipiza.
يَوْمَ تُبَدَّلُ الْأَرْضُ غَيْرَ الْأَرْضِ وَالسَّمَاوَاتُ ۖ وَبَرَزُوا لِلَّـهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ﴿٤٨﴾
48. Siku ardhi itakapobadilishwa kuwa ardhi nyingine[12] na mbingu pia, na (viumbe wote) watahudhuria kwa Allaah Mmoja Pekee, Asiyepingika.
وَتَرَى الْمُجْرِمِينَ يَوْمَئِذٍ مُّقَرَّنِينَ فِي الْأَصْفَادِ ﴿٤٩﴾
49. Na utawaona wahalifu Siku hiyo wamezongoreshwa katika minyororo.
سَرَابِيلُهُم مِّن قَطِرَانٍ وَتَغْشَىٰ وُجُوهَهُمُ النَّارُ﴿٥٠﴾
50. Mavazi yao ni ya lami na moto utafunika nyuso zao.
لِيَجْزِيَ اللَّـهُ كُلَّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿٥١﴾
51. Ili Allaah Alipe kila nafsi yale iliyoyachuma. Hakika Allaah Ni Mwepesi wa Kuhesabu.
هَـٰذَا بَلَاغٌ لِّلنَّاسِ وَلِيُنذَرُوا بِهِ وَلِيَعْلَمُوا أَنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ وَلِيَذَّكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ﴿٥٢﴾
52. Hii (Qur-aan) ni ubalighisho wa Risala kwa watu, na ili waonywe kwayo, na ili wapate kujua kwamba hakika Yeye Ni Muabudiwa wa haki Mmoja Pekee, na ili wakumbuke (na wawaidhike) wenye akili.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Viza Na Nuru (Mwanga):
a-Maana Ya Kiza Kilugha:
Ni kutokuweko nuru (mwanga) kama vile kiza cha usiku katika hali ya kutokuweko taa au nyota, au mwezi wa kutoa mwanga kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
أَمَّن يَهْدِيكُمْ فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ
“Au nani Anayekuongozeni katika viza vya nchi kavu na bahari?” [An-Naml (27:63)]
b) Maana Ya Kiza Kiistilahi:
Ni kufru, shirki, unafiki, bid’ah, ujahili, maasi, na kila aina ya upotofu na kadhaalika. Na maelezo yake yanafuatia.
c-Maana Ya Nuru (Mwanga) Kilugha:
Ni mwanga unaodhihirisha vitu kuonekana wazi kama mwanga wa mchana, au mwanga wa taa zinapowashwa usiku.
d-Maana Ya Nuru Kiistilahi:
Ni imaan, taqwa, utiifu, na kila aina ya hidaaya
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn amesema:
[Tafsiyr Suwrah Al-An’aam (6:1)]
Sababu ya kutajwa dhwulumaat (viza) kwa wingi, ni kama walivyosema ‘Ulamaa kwamba kwa sababu vyanzo vyake ni vingi; vinaweza kuwa ni nafsi ya mtu, au hawaa (matamanio), au shaytwaan, taghuti na kadhaalika. Na ndio maana adhwulumaat ikatajwa kwa wingi. Na hivyo inampelekea mtu katika viza vya kufru, shirki, unafiki, bid’ah, ujahili, maasi, na kila aina ya upotofu.
Ama An-Nuwr (mwanga), chanzo chake ni njia moja tu iliyonyooka, nacho ni Kitaabu cha Allaah kinachoongoza katika Swiraatw Al-Mustaqiym (Njia Iliyonyooka). Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِّنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَـٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا نَّهْدِي بِهِ مَن نَّشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٢﴾ صِرَاطِ اللَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا إِلَى اللَّـهِ تَصِيرُ الْأُمُورُ﴿٥٣﴾
“Na hivyo ndivyo Tulivyokuletea Ruwh (Qur-aan) kutokana na Amri Yetu. Hukuwa unajua nini Kitabu wala imaan, lakini Tumeifanya ni Nuru, Tunaongoa kwayo Tumtakaye miongoni mwa Waja Wetu. Na hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka. Njia ya Allaah Ambaye ni Vyake Pekee vyote vilivyomo mbinguni na vyote vilivyomo ardhini. Tanabahi! Kwa Allaah Pekee yanaishia mambo yote.” [Ash-Shuwraa (42:52-52)]
Rejea Suwrah Ibraahiym (13:1-2) kwenye maelezo bayana na faida nyenginezo. Na pia rejea Al-An’aam (6:122).
Amesema Ibnul-Qayyim Al-Jawziyyah (رحمه الله):
“Njia ya haki ni moja, kwani inarejea kwa Allaah Mfalme wa Haki, na njia za baatwili (ubatilifu) ni nyingi. Na hii ni moja katika miujiza ya Qur-aan, kutajwa viza kwa wingi, na Nuru kwa umoja. Hii ina maana kwamba neno viza linajumuisha kila aina ya giza; njia zote potofu zinazoelekea gizani, na hiyo Nuru inaashiria njia moja tu iliyonyooka.” [Badaai’u Al-Fawaaid]
Kumetajwa viza kwa wingi na Nuru kwa umoja katika Aayah kadhaa. Kwanza katika Suwrah hii ya Ibraahiym Aayah namba (1) na Aayah namba (5). Rejea pia Al-Baqarah (2:257), Al-Maaidah (5:16), Al-An’aam (6:1), Ar-Ra’d (13:16), An-Nuwr (24:40), Al-Ahzaab (33:43), Faatwir (35:20), Al-Hadiyd (57:9), Atw-Twalaaq (65:11).
Na duaa imethibiti ya kuomba mtu kutolewa kutoka katika viza na kuingizwa katika Nuru:
حَدَّثَنَا تَمِيمُ بْنُ الْمُنْتَصِرِ، أَخْبَرَنَا إِسْحَاقُ، - يَعْنِي ابْنَ يُوسُفَ - عَنْ شَرِيكٍ، عَنْ أَبِي إِسْحَاقَ، عَنْ أَبِي الأَحْوَصِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ كُنَّا لاَ نَدْرِي مَا نَقُولُ إِذَا جَلَسْنَا فِي الصَّلاَةِ وَكَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَدْ عَلِمَ فَذَكَرَ نَحْوَهُ . قَالَ شَرِيكٌ وَحَدَّثَنَا جَامِعٌ، - يَعْنِي ابْنَ شَدَّادٍ - عَنْ أَبِي وَائِلٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، بِمِثْلِهِ قَالَ وَكَانَ يُعَلِّمُنَا كَلِمَاتٍ وَلَمْ يَكُنْ يُعَلِّمُنَاهُنَّ كَمَا يُعَلِّمُنَا التَّشَهُّدَ " اللَّهُمَّ أَلِّفْ بَيْنَ قُلُوبِنَا وَأَصْلِحْ ذَاتَ بَيْنِنَا وَاهْدِنَا سُبُلَ السَّلاَمِ وَنَجِّنَا مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَجَنِّبْنَا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَبَارِكْ لَنَا فِي أَسْمَاعِنَا وَأَبْصَارِنَا وَقُلُوبِنَا وَأَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا وَتُبْ عَلَيْنَا إِنَّكَ أَنْتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ وَاجْعَلْنَا شَاكِرِينَ لِنِعْمَتِكَ مُثْنِينَ بِهَا قَابِلِيهَا وَأَتِمَّهَا عَلَيْنَا "
Amesimulia ‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akitufundisha maneno mengine lakini hakuyafundisha kama alivyokuwa akitufundisha Tashahhud:
اللَّهُمَّ أَلِّفْ بَيْنَ قُلُوبِنَا وَأَصْلِحْ ذَاتَ بَيْنِنَا وَاهْدِنَا سُبُلَ السَّلاَمِ وَنَجِّنَا مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ وَجَنِّبْنَا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَبَارِكْ لَنَا فِي أَسْمَاعِنَا وَأَبْصَارِنَا وَقُلُوبِنَا وَأَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا وَتُبْ عَلَيْنَا إِنَّكَ أَنْتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ وَاجْعَلْنَا شَاكِرِينَ لِنِعْمَتِكَ مُثْنِينَ بِهَا قَابِلِيهَا وَأَتِمَّهَا عَلَيْنَا
Ee Allaah! Unganisha baina ya nyoyo zetu, na Suluhisha yaliyo baina yetu, na Tuongoze njia za amani, na Tuokoe kutokana na viza Utuingize katika Nuru, na Tuepushe machafu ya dhahiri na ya siri, na Tubarikie katika kusikia kwetu na kuona kwetu, nyoyo zetu, na wake zetu, na vizazi vyetu, na Tupokelee tawbah zetu, hakika Wewe ni At-Tawwaabur-Rahiym (Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye Kurehemu), na Tujaalie kuwa wenye kushukuru neema Zako, wenye kuzielezea kwa uzuri, wenye kuzipokea (kwa shukrani), na Zitimize kwetu. [Abuu Daawuwd, Al-Haakim kasema: Swahiyh kwa sharti ya Muslim, na ameikubali Adh-Dhahabiy (1/265) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Adab Al-Mufrad (490)]
[3] Siku Za Allaah:
Ayyaamu "أَيَّامٌ", kwa lugha ya kiarabu ni masiku. Lakini masiku kama haya hayamaanishi siku tu, bali ni siku za kumbukumbu ambazo matukio muhimu ya kihistoria yanatokea au yalitokea. Na katika Aayah hii, masiku yaliyokusudiwa ni Neema za Allaah kama walivyosema Ibn ‘Abbaas, Mujaahid, Qataadah na wengineo: Ni Neema za Allaah za kila aina Alizowaneemesha Bani Israaiyl na kheri nyingi Alizowapa kama kuwafunika kwa mawingu na kuwateremshia Al-Manna na As-Salwaa. Rejea Al-Baqarah (2:57). Na pia kuwafanyia ihsaan na kuwaokoa kutokana na Firawni Alipotenganisha bahari wakavuka na akaghariki adui yao Firawni.
[4] Kurudisha Mikono Yao Katika Vinywa Vyao:
Wafasiri wa Qur-aan wamekhitilafiana katika maoni mbalimbali kuhusu kauli hiyo. Kuna waliosema: Wakaiuma mikono yao kwa hasira na kiburi cha kutotaka kuamini na kukanusha haki. Na hii inaonyesha hasira za makafiri, na kutoweza kwao kuvumilia baada ya kusikia ujumbe wa Rasuli wao. Na hii inathibitishwa na kauli inayoendelea katika Aayah hii tukufu ambapo makafiri hao wanasema wazi kwamba hawakubali Risala ya Rasuli wao na wanaitilia shaka. Hiyo ni aina ya kibri kama kibri cha kuweka vidole vyao masikioni na kujigubika kwa nguo zao wasione wasisikie. Rejea pia Nuwh (71:7).
[5] Makafiri Wataadhibiwa Bila Ya Kufa:
Mwenye kiburi atajaribu kumeza usaha na damu na vinginevyo vinavyotiririka mara kwa mara kutoka kwa watu wa motoni, na hataweza kumeza kwa uchafu wake, kuunguza kwake na uchungu wake. Na adhabu kali ya kila aina itamjia kwenye kila kiungo katika mwili wake. Hatakuwa ni mwenye kufa akapumzika. Na baada ya adhabu hii, atapatiwa adhabu nyingine yenye kuumiza. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Na adhabu za makafiri motoni zimetajwa katika Suwrah kadhaa zikiwemo Al-Kahf (18:29), Muhammad (47:15), Swaad (38:55-57), Asw-Swaaffaat (37:62-68), Ar-Rahmaan (55:43-44), Ad-Dukhaan (44:43-48), Al-Haaqqah (69:30-37), Al-Waaqi’ah (56:41-44), pia Al-Waaqi’ah (56:51-56) na Suwrah nyenginezo.
[6] Shaytwaan Huwapotosha Watu Kisha Huwakanusha Na Kuwageuka!:
Rejea pia Al-Anfaal (8:48) ambako Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja jinsi shaytwaan anavyokanusha upotoshaji wake baada ya mambo kuwa magumu. Rejea pia Al-Israa (17:64).
Na hivi ndivyo ilivyo, kawaida ya shaytwaan, kuwa huwapotosha wanaadam duniani kisha pindi mambo yanapokuwa magumu au adhabu inapohakiki au inapofika Siku ya Qiyaamah huwakanusha na kuwageuka.
Na Allaah (سبحانه وتعالى) Anatahadharisha waja Wake na adui huyu katika Aayah kadhaa; miongoni mwazo ni: Al-Baqarah (2:208), (268), An-Nisaa (4:119-120), Al-An’aam (6:112), Al-Israa (17:53), (64), An-Nuwr (24:21), Al-Furqaan (25:29), Faatwir (35:5-6), Yaasiyn (36:60), Az-Zukhruf (43:36-39), (62), Al-Hashr (59:16-17).
[7] Mti Mzuri:
Mti uliokusudiwa katika Aayah hii na inayoifuatia ni mtende kama ilivyothibiti katika Hadiyth:
Amesimulia Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما): Tulikuwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akauliza: “Niambieni kuhusu mti unaofanana na (au) ulio kama Muislamu, ambao majani yake hayaanguki wakati wa majira ya joto, wala wakati wa majira ya baridi, na hutoa matunda yake kila mara kwa idhini ya Rabb wake.” Ibn ‘Umar akasema: Niliufikiria kuwa ni mtende, lakini niliona vibaya kujibu nilipoona Abuu Bakr na ‘Umar hawakujibu. Akasema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Ni mtende.” Tulipoondoka, nilimwambia ‘Umar: Ee baba yangu! Wa-Allaahi nilihisi kuwa ni mtende. Akasema: Kwa nini basi hukutaja? Nikasema: Nilikuoneni kimya, nikaona vibaya kusema kitu. Akasema ‘Umar: Ungelisema, ingelikuwa bora kwangu kuliko kadhaa na kadhaa. (Yaani ningelikuwa na fakhari zaidi kuwa wewe mwanangu ndiye uliyeweza kujibu pekee). [Al-Bukhaariy]
[8] Al-Qawl Ath-Thaabit: Kauli Thabiti Duniani Na Aakhirah:
Imekusudiwa Shahaada ya Uislamu katika Maswali matatu atakayoulizwa mtu kaburini:
Amesimulia Al-Baraa bin ‘Aazib (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Muislamu akiulizwa katika kaburi, atashuhudia kwamba:
لاَ إِلَه إِلاَّ اللَّه وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُول اللَّه
Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli wa Allaah.
Basi hiyo ndiyo maana ya Kauli ya Allaah:
يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ
“Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah.” [Ibraahiym (14:27) Al-Bukhaariy na Muslim na wengineo]
Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
014-Asbaabun-Nuzuwl: Ibraahiym Aayah 27: يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ [156]
[9] Neema Za Allaah (سبحانه وتعالى) Haiwezekani Kuzihesabu Zote:
Rejea pia An-Nahl (16:5), Luqmaan (31:20), Al-Muuminuwn (23:17).
Neema za kwanza kwa Muislamu ni:
(i) Uislamu kwa kuwa Allaah Katuvua kutoka ukafiri. Hii ni neema kubwa kwani wangapi bado juu ya kuusikia Uislamu, hawajaweza kuukubali Uislamu.
(ii) Kuwa na imaan: Kuamini nguzo sita za imaan, na kuziitakidi na kutenda matendo ya Muumini.
(iii) Kutumwa kwetu Nabiy na Rasuli wa mwisho kabisa, Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye, amekuja kuwa ni mwongozo kwetu kutuongoza vipi kuishi katika dunia, na vipi kutaamuli na wanaadam wenzetu. Allaah (سبحانه وتعالى) Hakutuacha tu bila ya kutuletea Rasuli wa kutubainishia yaliyo ya haki ili tuyafuate na tutekeleze, na kutubainishia yaliyo ya batili ili tujiepushe nayo na haya yote ni kwa ajili ya kubakia katika Al-‘Aafiyah (usalama wa kila aina katika Dini yetu na maisha ya duniani na ya Aakhirah).
(iv) Kuteremshiwa Kitabu cha mwisho; Qur-aan Adhimu ambacho ni mwongozo kwetu, tunapata mawaidha, tulizo za nyoyo, shifaa (poza) kutokana na maradhi ya moyo yaliyotajwa ndani ya Qur-aan kama kutukinga na shirki, ukafiri, unafiki na kadhaalika. Pia Qur-aan ni shifaa na tiba maradhi ya mwili. Na ndani ya Qur-aan, pia kuna kanuni za kuishi katika hii dunia ili tuishi kama wanaadam kinyume na vile wanavyoishi wananyama. Na kuweza kutimiza Uislamu wetu ili kubakia katika Ridhaa ya Allaah.
(v) Sunnah zake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Mfano Sunnah za ibaada ambazo tunapata ujira kuzitekeleza kwake. Pia, Sunnah nyenginezo za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ambazo, kwazo, zinatufunza jinsi ya kuishi na wanaadam wenzetu, na tunapata maslahi ndani yake na tunabakia katika usalama na amani katika jamii. Na juu ya hivyo, kutekeleza kwake ni kujichumia thawabu za kujenga Aakhirah yetu.
(vi) Kujaaliwa uwepo wa Swahaba wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ambao tunapata mafunzo mengi mema kutokana na sifa zao.
(vii) Kuthibiti imara katika Dini na khasa katika Manhaj ya Salaf Swaalih (Wema waliotangulia).
Ama neema nyenginezo, ni kama Anavyosema Allaah (عزّ وجلّ) kwamba hawezi mtu kuziorodhesha hesabuni! Basi mwanaadam ajaribu kutafakari angalau aweze kufikia utambuzi wa neema chache mno miongoni mwa neema nyingi za Allaah (سبحانه وتعالى) ili aweze kumshukuru.
Neema zinazoonekana na ambazo hazionekani. Rejea Luqmaan (31:20). Basi na ajaribu mtu kuzitafakari katika mgawanyo ufuatao:
Umbile La Mwanaadam:
Kuanzia viungo vya mwanaadam vinavyoonekana kama mikono ya kufanyia kazi na ya kulia chakula. Miguu ya kuendea shughulini mwake na kwengineko. Viungo vya kichwa; macho ya kuonea, masikio ya kusikia, mdomo ambao humo mna meno ya kutafunia chakula na ulimi wa kuonjea chakula na kuongelea, pua ya kunusia harufu na kuvutia pumzi na kadhaalika.
Vile vile, viungo visivyoonekana kwa macho ya kawaida; viungo vilivyomo ndani ya mwili wa mwanaadam kama moyo, mishipa yote ya mwili, viungo vinavyotumika katika mfumo wa umeng'enyaji wa chakula. Ubongo wenye akili ambayo ni neema kubwa mno kuwa na akili timamu na kipaji. Almuradi ni neema adhimu jinsi Allaah (سبحانه وتعالى) Alivyouumba mwili wa mwanaadam na jinsi kila viungo hivyo vinavyofanya kazi kuendesha uhai wa mwanaadam:
فَتَبَارَكَ اللَّـهُ أَحْسَنُ الْخَالِقِينَ ﴿١٤﴾
“Basi Amebarikika Allaah Mbora wa wenye kuumba.” Rejea Al-Muuminuwn (23:12-14), na pia Ghaafir (40:64), At-Tiyn (95:4).
Rejea pia Al-Israa (17:70) kwenye faida kuhusu jinsi binaadam alivyokirimiwa na kufadhilishwa.
Neema Zisizoonekana:
Imaan, taqwa ambazo zimo moyoni mwa mwanaadam, na mengineyo yote ya ghaibu ya duniani na ya Aakhirah. Rejea Al-Baqarah (2:3). Na katika neema za ghaibu za Aakhirah, ni neema za Jannah (Peponi), na neema kubwa kabisa huko ni kumwona Allaah (عزّ وجلّ). Rejea Yuwnus (10:26), na Al-Qiyaamah (75:22-23). Neema hizo na nyenginezo, zimetajwa katika Suwrah mbali mbali, na hapa si mahali pake kuzitaja zote, wala haiwezekani kuorodhesha zote!
Neema Za Ardhini, Baharini, Angani Na Katika Falaki:
Rejea Yaasiyn (36:38) kwenye maelezo bayana ya faida tele.
Na katika Qur-aan, neema za aina hizi zimetajwa katika Suwrah na Aayah mbalimbali. Mfano Suwrah An-Nahl ambayo inajulikana pia kama Suwrah Ya Neema, humo Allaah (عزّ وجلّ) Ametaja Neema tele za ardhini, baharini, angani na falakini! Rejea An-Nahl (16:4-16).
Pia, neema kama hizo na nyenginezo zimetajwa mwanzoni mwa Suwrah An-Nabaa (78:6-16). Pia Rejea Al-Furqaan (25:45-49), Suwrah ‘Abasa (80:18-32), na kwengineko; hapa si mahali pake kuzitaja zote, wala haiwezekani kuorodhesha zote!
Basi Hizo zote zilizotajwa hapo juu na katika rejea za Suwrah hizo, ni neema chache mno kati ya Neema nyingi za Allaah (عزّ وجلّ).
Na wanaadam wachache wenye kumshukuru Allaah (سبحانه وتعالى) kama Anavyosema kumhusu Nabiy Daawuwd (عليه السّلام):
اعْمَلُوا آلَ دَاوُودَ شُكْرًا ۚ وَقَلِيلٌ مِّنْ عِبَادِيَ الشَّكُورُ ﴿١٣﴾
“Tendeni enyi familia ya Daawuwd kwa shukurani! Na wachache miongoni mwa Waja Wangu ni wenye kushukuru.” [Sabaa (34:13)]
Na tujifunze shukurani ya Nabiy Sulaymaan (عليه السّلام) kama alivyoomba:
رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَدْخِلْنِي بِرَحْمَتِكَ فِي عِبَادِكَ الصَّالِحِينَ ﴿١٩﴾
Rabb wangu! Nipe ilhamu na uwezo nishukuru Neema Yako ambayo Umenineemesha juu yangu na wazazi wangu, na nipate kutenda mema Utakayoridhia, na Niingize kwa Rehma Yako katika Waja Wako Swalihina [An-Naml (27:19)]
Kadhaalika shukurani za mja mwema aliyeomba:
رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَصْلِحْ لِي فِي ذُرِّيَّتِي ۖ إِنِّي تُبْتُ إِلَيْكَ وَإِنِّي مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴿١٥﴾
Rabb wangu! Nipe ilhamu na uwezo nishukuru Neema Yako ambayo Umenineemesha juu yangu na wazazi wangu, na nipate kutenda mema Utakayoridhia, na Nitengenezee dhuria wangu. Hakika mimi nimetubu Kwako, na hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu. [Al-Ahqaaf (46:15)]
Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida na mwongozo wa kumshukuru Allaah (عزّ وجلّ):
Rejea pia Adhw-Dhwuhaa (93:11) kwenye faida kuhusu kukiri Neema za Allaah, kushukuru, na kuomba kuhifadhiwa na kuzidishiwa Neema za Allaah (عزّ وجلّ).
[10] Ujenzi Wa Ka’bah Na Duaa Za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) :
Kuanzia Aayah hii ya (14:35) hadi (14:41), panazungumziwa kuhusu kujengwa Al-Ka’bah na duaa za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) alizoomba. Rejea pia Al-Baqarah (2:127-129).
[11] Duaa Ya Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) Kwa Wazazi Wake:
Duaa hiyo ya kuwaombea wazazi wake pia ni kabla ya kumbainikia kwamba wao ni adui wa Allaah. [Tafsiyr As-Sa’diy, Tafsiyr Al-Muyassar]
[12] Siku Ya Qiyaamah Watu Watafufuliwa Na Kukusanywa Katika Ardhi Tofauti Na Ya Dunia:
Amesimulia Sahl bin Sa’d (رضي الله عنه) : Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Watu watafufuliwa Siku ya Qiyaamah katika ardhi nyeupe yenye wekundu kama vile mkate safi (uliotengenezwa kwa unga safi kabisa).” Sahl akaongeza kusema: Ardhi hiyo haitakuwa na alama kwa mtu yeyote (kuitumia). [Al-Bukhaariy na Muslim]
الْحِجْر
015-Al-Hijr
015-Al-Hijr: Utangulizi Wa Suwrah [162]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرّحِيمِ
الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ وَقُرْآنٍ مُّبِينٍ ﴿١﴾
1. Alif Laam Raa.[1] Hizi ni Aayaat za Kitabu na Qur-aan iliyo bayana.
رُّبَمَا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ كَانُوا مُسْلِمِينَ ﴿٢﴾
2. Watatamani wale waliokufuru lau wangelikuwa Waislamu.
ذَرْهُمْ يَأْكُلُوا وَيَتَمَتَّعُوا وَيُلْهِهِمُ الْأَمَلُ ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ ﴿٣﴾
3. Waache wale na wastarehe na yawashughulishe matumaini (ya uongo), basi watakuja kujua.
وَمَا أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ إِلَّا وَلَهَا كِتَابٌ مَّعْلُومٌ ﴿٤﴾
4. Na Hatukuangamiza mji wowote isipokuwa ulikuwa na majaaliwa yaliyokadiriwa maalumu.
مَّا تَسْبِقُ مِنْ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسْتَأْخِرُونَ ﴿٥﴾
5. Ummah wowote hauwezi kutangulia muda wake (wa kuangamizwa) wala hauwezi kuakhirisha.
وَقَالُوا يَا أَيُّهَا الَّذِي نُزِّلَ عَلَيْهِ الذِّكْرُ إِنَّكَ لَمَجْنُونٌ ﴿٦﴾
6. Na wakasema: Ee ambaye umeteremshiwa Adh-Dhikru (Qur-aan)! Hakika wewe ni majnuni tu.
لَّوْ مَا تَأْتِينَا بِالْمَلَائِكَةِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٧﴾
7. Mbona basi usituletee Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli?
مَا نُنَزِّلُ الْمَلَائِكَةَ إِلَّا بِالْحَقِّ وَمَا كَانُوا إِذًا مُّنظَرِينَ ﴿٨﴾
8. Hatuteremshi Malaika isipokuwa kwa jambo la haki, na hawatokuwa hapo wenye kupewa muhula.
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ ﴿٩﴾
9. Hakika Sisi Tumeteremsha Adh-Dhikra (Qur-aan) na hakika Sisi bila shaka Ndio Wenye Kuihifadhi.[2]
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِي شِيَعِ الْأَوَّلِينَ ﴿١٠﴾
10. Na kwa yakini Tulipeleka (Rusuli) kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika makundi ya (nyumati za) awali.
وَمَا يَأْتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿١١﴾
11. Na hakuwafikia Rasuli yeyote ila walikuwa wakimfanyia istihzai.
كَذَٰلِكَ نَسْلُكُهُ فِي قُلُوبِ الْمُجْرِمِينَ ﴿١٢﴾
12. Hivyo ndivyo Tunavyoingiza hilo (istihzai, kadhibisho) katika nyoyo za wahalifu.
لَا يُؤْمِنُونَ بِهِ ۖ وَقَدْ خَلَتْ سُنَّةُ الْأَوَّلِينَ ﴿١٣﴾
13. Hawaiamini (Qur-aan), na hali imekwishapita ada ya (kuadhibiwa) watu wa awali.
وَلَوْ فَتَحْنَا عَلَيْهِم بَابًا مِّنَ السَّمَاءِ فَظَلُّوا فِيهِ يَعْرُجُونَ ﴿١٤﴾
14. Na hata kama Tungeliwafungulia mlango wa mbingu wakabakia kupanda huko.
لَقَالُوا إِنَّمَا سُكِّرَتْ أَبْصَارُنَا بَلْ نَحْنُ قَوْمٌ مَّسْحُورُونَ ﴿١٥﴾
15. Wangelisema: Hapana ila macho yetu yamelevywa, bali sisi ni watu tuliorogwa.
وَلَقَدْ جَعَلْنَا فِي السَّمَاءِ بُرُوجًا وَزَيَّنَّاهَا لِلنَّاظِرِينَ﴿١٦﴾
16. Na kwa yakini Tumejaalia katika mbingu buruji[3] na Tumeipamba kwa wenye kutazama.
وَحَفِظْنَاهَا مِن كُلِّ شَيْطَانٍ رَّجِيمٍ﴿١٧﴾
17. Na Tumeilinda na kila shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa.
إِلَّا مَنِ اسْتَرَقَ السَّمْعَ فَأَتْبَعَهُ شِهَابٌ مُّبِينٌ﴿١٨﴾
18. Isipokuwa mdukizi basi huyo humfuatia kimondo kinachoonekana bayana.
وَالْأَرْضَ مَدَدْنَاهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ شَيْءٍ مَّوْزُونٍ﴿١٩﴾
19. Na ardhi Tumeitandaza na Tukatupa humo milima iliyosimama thabiti, na Tukaotesha humo kila kitu kwa uwiano.
وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَايِشَ وَمَن لَّسْتُمْ لَهُ بِرَازِقِينَ﴿٢٠﴾
20. Na Tukakuwekeeni humo njia na mbinu za maisha, na ya hao ambao nyinyi si wenye kuwaruzuku.
وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا عِندَنَا خَزَائِنُهُ وَمَا نُنَزِّلُهُ إِلَّا بِقَدَرٍ مَّعْلُومٍ﴿٢١﴾
21. Na hakuna kitu chochote isipokuwa Tuna hazina zake, na Hatukiteremshi isipokuwa kwa kadiri maalumu.
وَأَرْسَلْنَا الرِّيَاحَ لَوَاقِحَ فَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَسْقَيْنَاكُمُوهُ وَمَا أَنتُمْ لَهُ بِخَازِنِينَ﴿٢٢﴾
22. Na Tukatuma pepo za rehma zikibeba umande, na Tukateremsha kutoka mbinguni maji kisha Tukakunywesheni kwayo, wala nyinyi si wenye kuyahifadhi.
وَإِنَّا لَنَحْنُ نُحْيِي وَنُمِيتُ وَنَحْنُ الْوَارِثُونَ﴿٢٣﴾
23. Na hakika Sisi Tunahuisha na Tunafisha, na Sisi Ndio Warithi.
وَلَقَدْ عَلِمْنَا الْمُسْتَقْدِمِينَ مِنكُمْ وَلَقَدْ عَلِمْنَا الْمُسْتَأْخِرِينَ﴿٢٤﴾
24. Na Tumekwishajua (vizazi) waliotangulia miongoni mwenu, na Tumekwishajua wenye kutaakhari.
وَإِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَحْشُرُهُمْ ۚ إِنَّهُ حَكِيمٌ عَلِيمٌ﴿٢٥﴾
25. Na hakika Rabb wako Ndiye Atakayewakusanya. Na hakika Yeye Ni Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.
وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ﴿٢٦﴾
26. Na kwa yakini Tumemuumba binaadam kutokana na udongo wa mfinyanzi mkavu, unaotoa sauti, unaotokana na tope nyeusi iliyotaghayari.
وَالْجَانَّ خَلَقْنَاهُ مِن قَبْلُ مِن نَّارِ السَّمُومِ﴿٢٧﴾
27. Na majini Tuliwaumba kabla kutokana na moto ulio mkali mno.
وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِّن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ﴿٢٨﴾
28. Na pindi Rabb wako Alipowaambia Malaika: Hakika Mimi Namuumba mtu kutokana na udongo wa mfinyanzi mkavu, unaotoa sauti, unaotokana na tope nyeusi iliyotaghayari.
فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُوا لَهُ سَاجِدِينَ﴿٢٩﴾
29. Basi Nitakapomsawazisha na Nikampuliza Roho Niliyomuumbia, muangukieni kumsujudia.
فَسَجَدَ الْمَلَائِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ﴿٣٠﴾
30. Basi wakasujudu Malaika wote pamoja.
إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ أَن يَكُونَ مَعَ السَّاجِدِينَ﴿٣١﴾
31. Isipokuwa Ibliys, alikataa kuwa pamoja na waliosujudu.
قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا لَكَ أَلَّا تَكُونَ مَعَ السَّاجِدِينَ﴿٣٢﴾
32. (Allaah) Akasema: Ee Ibliys! Una nini hata hukuwa pamoja na waliosujudu?
قَالَ لَمْ أَكُن لِّأَسْجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقْتَهُ مِن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ﴿٣٣﴾
33. (Ibliys) akasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu Uliyemuumba kutokana na udongo mkavu unaotoa sauti, unaotokana na tope nyeusi iliyotaghayari.
قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ﴿٣٤﴾
34. (Allaah) Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umetokomezwa mbali na kulaaniwa.
وَإِنَّ عَلَيْكَ اللَّعْنَةَ إِلَىٰ يَوْمِ الدِّينِ﴿٣٥﴾
35. Na hakika juu yako ipo laana mpaka Siku ya Malipo.
قَالَ رَبِّ فَأَنظِرْنِي إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ﴿٣٦﴾
36. Akasema: Rabb wangu! Nipe muhula mpaka Siku watakayofufuliwa.
قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ الْمُنظَرِينَ﴿٣٧﴾
37. (Allaah) Akasema: Basi hakika wewe ni miongoni mwa waliopewa muhula.
إِلَىٰ يَوْمِ الْوَقْتِ الْمَعْلُومِ﴿٣٨﴾
38. Mpaka siku ya wakati maalumu.
قَالَ رَبِّ بِمَا أَغْوَيْتَنِي لَأُزَيِّنَنَّ لَهُمْ فِي الْأَرْضِ وَلَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ﴿٣٩﴾
39. (Ibliys) akasema: Rabb wangu! Kwa vile Umenihukumia kupotoka, basi bila shaka nitawapambia (maasi) katika ardhi na nitawapotoa wote.
إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ الْمُخْلَصِينَ﴿٤٠﴾
40. Isipokuwa Waja Wako miongoni mwao waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.
قَالَ هَـٰذَا صِرَاطٌ عَلَيَّ مُسْتَقِيمٌ﴿٤١﴾
41. (Allaah) Akasema: Hii ni njia ya kufikia Kwangu iliyonyooka.
إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ إِلَّا مَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْغَاوِينَ﴿٤٢﴾
42. Hakika Waja Wangu huna mamlaka nao isipokuwa ambaye atakufuata miongoni mwa waliopotoka.
وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوْعِدُهُمْ أَجْمَعِينَ﴿٤٣﴾
43. Na hakika Jahannam ni miadi yao wote pamoja.
لَهَا سَبْعَةُ أَبْوَابٍ لِّكُلِّ بَابٍ مِّنْهُمْ جُزْءٌ مَّقْسُومٌ﴿٤٤﴾
44. Ina milango saba, na kwa kila mlango iko sehemu (makhsusi) iliyogawanywa kwao wao.[4]
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ﴿٤٥﴾
45. Hakika wenye taqwa watakuwa katika Jannaat na chemchemu.
ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ آمِنِينَ﴿٤٦﴾
46. (Wataambiwa): Ingieni humo kwa salama mkiwa katika amani.
وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ إِخْوَانًا عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَابِلِينَ﴿٤٧﴾
47. Na Tutaondosha mafundo ya kinyongo yaliyomo vifuani mwao,[5] wakiwa ndugu, juu ya makochi yaliyoinuliwa wakikabiliana.
لَا يَمَسُّهُمْ فِيهَا نَصَبٌ وَمَا هُم مِّنْهَا بِمُخْرَجِينَ﴿٤٨﴾
48. Hautowagusa humo uchovu nao humo hawatotolewa.
نَبِّئْ عِبَادِي أَنِّي أَنَا الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٤٩﴾
49. (Ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)! Wajulishe Waja Wangu, kwamba: Hakika Mimi Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَأَنَّ عَذَابِي هُوَ الْعَذَابُ الْأَلِيمُ﴿٥٠﴾
50. Na kwamba Adhabu Yangu, ndiyo adhabu iumizayo.
وَنَبِّئْهُمْ عَن ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ﴿٥١﴾
51. Na wajulishe kuhusu wageni wa Ibraahiym.
إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا قَالَ إِنَّا مِنكُمْ وَجِلُونَ﴿٥٢﴾
52. Pale walipoingia kwake, wakasema: Salaama! (Ibraahiym) akasema: Hakika sisi tunakuogopeni.
قَالُوا لَا تَوْجَلْ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ﴿٥٣﴾
53. (Malaika) wakasema: Usiogope! Hakika sisi tunakubashiria ghulamu mjuzi.
قَالَ أَبَشَّرْتُمُونِي عَلَىٰ أَن مَّسَّنِيَ الْكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ﴿٥٤﴾
54. (Ibraahiym) akasema: Je, mnanibashiria (mwana) na hali uzee umeshanishika, basi kwa njia gani mnanibashiria?
قَالُوا بَشَّرْنَاكَ بِالْحَقِّ فَلَا تَكُن مِّنَ الْقَانِطِينَ﴿٥٥﴾
55. Wakasema: Tunakubashiria kwa haki, basi usiwe miongoni mwa wakatao tamaa.
قَالَ وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلَّا الضَّالُّونَ﴿٥٦﴾
56. Akasema: Na nani anayekata tamaa na Rehma ya Rabb wake isipokuwa wapotofu?
قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ﴿٥٧﴾
57. Akasema: Basi nini jambo lenu muhimu enyi Wajumbe?
قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ﴿٥٨﴾
58. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wahalifu.
إِلَّا آلَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمْ أَجْمَعِينَ﴿٥٩﴾
59. Isipokuwa familia ya Luutw, hakika Sisi Tutawaokoa wote.
إِلَّا امْرَأَتَهُ قَدَّرْنَا ۙ إِنَّهَا لَمِنَ الْغَابِرِينَ﴿٦٠﴾
60. Isipokuwa mkewe. Tumehukumu kwamba yeye bila shaka ni miongoni mwa watakaobakia nyuma (kuangamizwa).
فَلَمَّا جَاءَ آلَ لُوطٍ الْمُرْسَلُونَ﴿٦١﴾
61. Basi Wajumbe walipokuja kwa familia ya Luutw.
قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ﴿٦٢﴾
62. (Luutw) akasema: Hakika nyinyi ni watu msiojulikana.
قَالُوا بَلْ جِئْنَاكَ بِمَا كَانُوا فِيهِ يَمْتَرُونَ﴿٦٣﴾
63. (Malaika) wakasema: Bali tumekujia kwa yale waliyokuwa wanatilia shaka.
وَأَتَيْنَاكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ﴿٦٤﴾
64. Na tumekujia kwa haki na hakika sisi ni wakweli.
فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ اللَّيْلِ وَاتَّبِعْ أَدْبَارَهُمْ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ وَامْضُوا حَيْثُ تُؤْمَرُونَ﴿٦٥﴾
65. Basi toka usiku (huu) na ahli wako sehemu iliyobakia ya usiku na ufuate nyuma yao, wala asigeuke nyuma yeyote miongoni mwenu, na endeleeni kwenda mnakoamrishwa.
وَقَضَيْنَا إِلَيْهِ ذَٰلِكَ الْأَمْرَ أَنَّ دَابِرَ هَـٰؤُلَاءِ مَقْطُوعٌ مُّصْبِحِينَ﴿٦٦﴾
66. Na Tukamjulisha hukumu ya jambo hilo, kwamba: Mtu wa mwisho wa hawa (watendaji uliwati) atakuwa amemalizwa wakipambaukiwa asubuhi.
وَجَاءَ أَهْلُ الْمَدِينَةِ يَسْتَبْشِرُونَ﴿٦٧﴾
67. Na wakaja watu wa mji ule wakifurahia.
قَالَ إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ ضَيْفِي فَلَا تَفْضَحُونِ﴿٦٨﴾
68. (Luutw) akasema: Hakika hawa ni wageni wangu, basi msinifedheheshe.
وَاتَّقُوا اللَّـهَ وَلَا تُخْزُونِ﴿٦٩﴾
69. Na mcheni Allaah wala msinihizi.
قَالُوا أَوَلَمْ نَنْهَكَ عَنِ الْعَالَمِينَ﴿٧٠﴾
70. Wakasema: Je, hatujakukataza kukaribisha (au kuwalinda) watu wowote?
قَالَ هَـٰؤُلَاءِ بَنَاتِي إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ﴿٧١﴾
71. Akasema: Hawa hapa mabinti zangu (wa kuwaoa kihalali) ikiwa nyinyi ni wafanyaji.
لَعَمْرُكَ إِنَّهُمْ لَفِي سَكْرَتِهِمْ يَعْمَهُونَ﴿٧٢﴾
72. Naapa kwa uhai wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)![6] Hakika wao (washirikina wa Makkah) wako katika ulevi wao wanatangatanga kwa upofu.
فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ مُشْرِقِينَ﴿٧٣﴾
73. Basi uliwachukua ukelele angamizi wakati wanapambaukiwa.
فَجَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِّن سِجِّيلٍ﴿٧٤﴾
74. Tukaupindua (mji huo) juu chini, na Tukawanyeshea mvua ya mawe ya udongo uliookwa (motoni).
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّلْمُتَوَسِّمِينَ﴿٧٥﴾
75. Hakika katika hayo mna Aayaat (Ishara, Mawaidha, Mazingatio) kwa watambuzi.
وَإِنَّهَا لَبِسَبِيلٍ مُّقِيمٍ﴿٧٦﴾
76. Na hakika hiyo (miji) iko katika barabara kuu inayopitwa.
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّلْمُؤْمِنِينَ﴿٧٧﴾
77. Hakika katika hayo ipo Aayah (Ishara, Dalili) [za wazi] kwa Waumini.
وَإِن كَانَ أَصْحَابُ الْأَيْكَةِ لَظَالِمِينَ﴿٧٨﴾
78. Na hakika watu wa Al-Aykah[7] walikuwa madhalimu.
فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ وَإِنَّهُمَا لَبِإِمَامٍ مُّبِينٍ﴿٧٩﴾
79. Tukawalipiza (kuwaadhibu) na miji yote miwili hiyo iko katika njia kuu mashuhuri.
وَلَقَدْ كَذَّبَ أَصْحَابُ الْحِجْرِ الْمُرْسَلِينَ﴿٨٠﴾
80. Na kwa yakini watu wa Al-Hijr (kina Thamuwd) waliwakadhibisha Rusuli.[8]
وَآتَيْنَاهُمْ آيَاتِنَا فَكَانُوا عَنْهَا مُعْرِضِينَ﴿٨١﴾
81. Na Tuliwapa Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu wakawa wenye kuzipuuza.
وَكَانُوا يَنْحِتُونَ مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا آمِنِينَ﴿٨٢﴾
82. Na walikuwa wanachonga majumba katika majabali wakiwa katika amani.
فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ مُصْبِحِينَ﴿٨٣﴾
83. Ukawachukua ukelele angamizi wakipambaukiwa asubuhi.
فَمَا أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٨٤﴾
84. Basi hayakuwasaidia yale waliyokuwa wakichuma.
وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ ۗ وَإِنَّ السَّاعَةَ لَآتِيَةٌ ۖ فَاصْفَحِ الصَّفْحَ الْجَمِيلَ﴿٨٥﴾
85. Na Hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake isipokuwa kwa haki. Na hakika Saa bila shaka itafika. Basi samehe msamaha mzuri.
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ الْخَلَّاقُ الْعَلِيمُ﴿٨٦﴾
86. Hakika Rabb wako Ndiye Mwingi wa Kuumba Atakavyo, Mjuzi wa yote.
وَلَقَدْ آتَيْنَاكَ سَبْعًا مِّنَ الْمَثَانِي وَالْقُرْآنَ الْعَظِيمَ﴿٨٧﴾
87. Na kwa yakini Tumekupa (Suwrah au Aayaat) Saba zinazokaririwa (kusomwa) na Qur-aan Adhimu.[9]
لَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّنْهُمْ وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِلْمُؤْمِنِينَ﴿٨٨﴾
88. Usikodoe kabisa macho yako kwa yale ya starehe Tuliyowaneemesha baadhi ya makundi (ya kikafiri) miongoni mwao, wala usiwahuzunikie. Na inamisha bawa lako kwa Waumini (kuwahurumia).
وَقُلْ إِنِّي أَنَا النَّذِيرُ الْمُبِينُ﴿٨٩﴾
89. Na sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi ni mwonyaji mwenye kubainisha.
كَمَا أَنزَلْنَا عَلَى الْمُقْتَسِمِينَ﴿٩٠﴾
90. Kama Tulivyowateremshia (adhabu) waliojigawanya.
الَّذِينَ جَعَلُوا الْقُرْآنَ عِضِينَ﴿٩١﴾
91. Ambao wameifanya Qur-aan sehemu mbali mbali.[10]
فَوَرَبِّكَ لَنَسْأَلَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ﴿٩٢﴾
92. Basi Naapa kwa Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)! Bila shaka Tutawauliza wote.
عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٣﴾
93. Kuhusu yale waliyokuwa wakitenda.
فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ﴿٩٤﴾
94. Basi tangaza wazi yale unayoamrishwa na jitenge na washirikina.
إِنَّا كَفَيْنَاكَ الْمُسْتَهْزِئِينَ﴿٩٥﴾
95. Hakika sisi Tunakutosheleza dhidi ya wafanyao istihzai.
الَّذِينَ يَجْعَلُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ ۚ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ﴿٩٦﴾
96. Ambao wanafanya pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine, basi watakuja kujua.
وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّكَ يَضِيقُ صَدْرُكَ بِمَا يَقُولُونَ﴿٩٧﴾
97. Na kwa yakini Tunajua kwamba kifua chako kinadhikika kwa yale wanayoyasema.
فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَكُن مِّنَ السَّاجِدِينَ﴿٩٨﴾
98. Basi Msabbih Rabb wako kwa Himdi Zake na uwe miongoni mwa wanaosujudu.
وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ﴿٩٩﴾
99. Na mwabudu Rabb wako mpaka ikufikie yakini (mauti).
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Qur-aan Imehifadhiwa:
Ni Ahadi ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kuihifadhi Qur-aan, na Ahadi Yake kamwe haiendi kinyume! Wala haiwezekani Qur-aan kubadilishwa au kuitia pogo au kuitowesha ipotee kabisa kwa sababu Allaah (سبحانه وتعالى) Aliiteremsha kwanza katika kifua cha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kisha Swahaba zake (رضي الله عنهم) wakaihifadhi nyoyoni mwao, kisha Waumini waliofuatia, na inaendelea kuhifadhika katika vifua vya Waislamu, na itaendelea hivyo hadi Siku ya Qiyaamah. Na hii ni muujiza, kwa sababu imedhihirika wazi kuwa Waislamu wengi ulimwenguni wamehifadhi Qur-aan katika vifua vyao. Bali hata wale ambao hawajui lugha ya kiarabu, Allaah (سبحانه وتعالى) Amewawezesha waihifadhi Qur-aan vifuani mwao. Na maadui wa Uislamu waliochoma Miswahafu wamefeli! Kwani hata wakichoma Miswahafu yote waliyonayo, Qur-aan bado itabakia vifuani vya Waislamu!
Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) amesema: Yaani wakati inateremshwa na baada ya kuteremshwa. Wakati inateremshwa, ilihifadhiwa isidukuliwe na kila shaytwaan aliyelaaniwa na kubaidishwa na Rehma ya Allaah. Kisha baada ya kuteremshwa, Allaah (عزّ وجلّ) Aliihifadhi katika moyo wa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), kisha kwenye nyoyo za ummah wake. Halafu Allaah (سبحانه وتعالى) Akayahifadhi maneno yake yasibadilishwe ndani yake, yasiongezwe, wala yasipunguzwe, na maana zake zisibadilishwe. Na kwa hifadhi kama hii, hawezi mpotoshaji kupotosha maana zake zozote zile isipokuwa Allaah (عزّ وجلّ) Atamuibulia mtu wa kubainisha haki waziwazi. Na hii ni katika Dalili Kubwa kabisa za Allaah pamoja na Neema Zake kwa Waja Wake Waumini. Ama Hifadhi nyingine, ni kwamba Allaah Anawalinda wenye kushikamana na Qur-aan kutokana na maadui zao, na Hawapi kabisa nafasi maadui hao ya kuweza kuwadhuru kama watawavamia. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[3] Buruji:
Rejea Suwrah Al-Burujw (85:1) kulikotajwa maana zake kadhaa kutokana na kauli za ‘Ulamaa.
[4] Milango Ya Jahannam:
Jahnnam ina milango saba. Kila mlango uko chini ya mwengine. Kila mlango utakuwa na fungu na sehemu la wafuasi wa Ibliys kulingana na matendo yao. [Tafsiyr Al-Muyassar na As-Sa’diy]
[5] Waumini Wataondoshewa Mafundo, Vinyongo Kabla Ya Kuingia Peponi: Rejea Al-A’raaf (7:43).
[6] Kuapia Kwa Asiyekuwa Allaah Ni Haramu Na Ni Shirk:
Allaah (سبحانه وتعالى) Ambaye ni Muumba wa kila kitu, Anaapia kwa chochote Atakacho. Ama viumbe, haijuzu kuapia kwa chochote isipokuwa kuapia kwa Allaah. Na Allaah (عزّ وجلّ) Anaapia hapa kwa uhai wa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kama ni taadhima. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Na tunaona kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Anaapia vitu mbalimbali katika Suwrah kadhaa. Anaapia kwa mbingu na ardhi, Anaapia pia kwa tini na zaytuni, jua na mwezi, usiku na mchana, alasiri n.k. Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Ana haki ya kuapia chochote Anachotaka. Ama sisi viumbe Vyake, ni haramu kuapia kwa chochote isipokuwa kwa Allaah (سبحانه وتعالى) tu. Na kuapia huku ni kutumia herufi tatu tu. Rejea An-Nahl (16:56).
Wengi kati ya Waislamu wanaapia vitu vitukufu vya Allaah (سبحانه وتعالى) wakidhania kuwa inafaa, kama kuapia Mswahafu, Al-Ka’bah, kuapia kwa kumtaja Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Basi hivi na vinginevyo vyovyote haijuzu kabisa kuapia!
Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameharamisha kuapia kwa Asiyekuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Hadiyth kadhaa zimegusia hili, na mojawapo ni ifuatayo: Amesimulia Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما) kwamba alimsikia mtu mmoja akisema: Laa, naapa kwa Al-Ka’bah. Ibn ‘Umar akamwambia: Haapiwi asiye Allaah, kwani hakika mimi nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Mwenye kuapa kwa asiye Allaah, basi hakika amefanya shirki.” [Hadiyth Hasan. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (1535) na Abu Daawuwd (3251)]
[7] Watu Wa Al-Aykah ni watu wa kichakani katika mji wa Madyan. Ni watu wa Nabiy Shu’ayb (عليه السّلام). Rejea Ash-Shu’araa (26:176) kupata maelezo bayana.
[8] Watu Wa Al-Hijr (Thamuwd):
Watu wa Al-Hijr ni kina Thamuwd ambao walitumiwa Nabiy Swaalih (عليه السّلام) kuwalingania Tawhiyd ya Allaah. Wameitwa Al-Hijr kwa sababu waliishi Al-Hijr; eneo lilioko baina ya Sham na Hijaaz. Rejea Ash-Shams (91:11-15) kwenye maelezo kuhusu kisa chao. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa anaelekea katika Vita vya Tabuwk alipita na Swahaba wake (رضي الله عنهم) katika masikani zao walizokua wakiishi. Akawatahadharisha Swahaba kwa kauli yake (صلى الله عليه وآله وسلم): “Msiingie masikani za waliodhulumu nafsi zao isipokuwa muingie huku mnalia ili isije kukusibuni yaliyowasibu wao.” Kisha akafunika kichwa chake na kuharakiza mwendo wa kasi mpaka akavuka bonde. [Al-Bukhaari, Muslim na wengineo]
[9] Suwrah Au Aayah Saba Zinazokaririwa.
Wafasiri wa Qur-aan wamekhitilafiana kuhusu Suwrah au Aayaat. Kuna waliosema ni Suwrah saba ndefu: (i) Al-Baqarah (ii) Aal-‘Imraan (iii) An-Nisaa (iv) Al-Maaidah (v) Al-An’aam (vi) Al-A’raaf (vii) Al-Anfaal, (viii) At-Tawbah ambayo haina BismiLLaah. Na rai nyengine ni Aayaat Saba za Suwrah Al-Faatihah kwa kuwa zinakaririwa katika kila Swalaah. [Tafsiyr As-Sa’diy, Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[10] Makafiri Kuifanya Qur-aan Katika Sehemu Mbalimbali:
Waliosema ni sihri (uchawi), imetungwa, mashairi, ukuhani, hekaya za awali, n.k. ili wawazuie watu kufuata uongofu. [Tafsiyr Al-Muyassar, As-Sa’diy, Imaam Ibn Kathiyr] Na Imaam Ibn Kathiyr ameongezea kunukuu Hadiyth ya Ibn ‘Abaas (رضي الله عنهما) “Hao waloifanya Qur-aan sehemu mbalimbali ni Watu wa Kitabu (Mayahudi na Manaswaara), wameamini baadhi yake na wamekanusha baadhi yake.” [Al-Bukaariy]
Na pia rejea Al-Furqaan (25:4) kwenye uchambuzi na maelezo bayana kuhusu makafiri na kuikanusha kwao Qur-aan, na kuipa sifa ovu mbali mbali, pamoja na kumpachika sifa ovu mbali mbali Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).
النَّحْل
016-An-Nahl
016-An-Nahl: Utangulizi Wa Suwrah [164]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
أَتَىٰ أَمْرُ اللَّـهِ فَلَا تَسْتَعْجِلُوهُ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿١﴾
1. Amri ya Allaah (ya Qiyaamah au adhabu) inakuja (karibu), basi msiihimize. Utakasifu ni Wake na Ametukuka kwa Uluwa kutokana na wanayomshirikisha nayo.
يُنَزِّلُ الْمَلَائِكَةَ بِالرُّوحِ مِنْ أَمْرِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ أَنْ أَنذِرُوا أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاتَّقُونِ﴿٢﴾
2. Anateremsha Malaika wakiwa na Ruwh[1] (Wahy) kwa Amri Yake juu ya Amtakaye miongoni mwa Waja Wake, wakiwaambia: Onyeni kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, basi Nicheni.
خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۚ تَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٣﴾
3. Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Ametukuka kwa Uluwa kutokana na yale wanayoshirikisha.
خَلَقَ الْإِنسَانَ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ﴿٤﴾
4. Amemuumba binaadam kutokana na tone la manii, tahamaki yeye ni mbishani fasaha wa maneno.
وَالْأَنْعَامَ خَلَقَهَا ۗ لَكُمْ فِيهَا دِفْءٌ وَمَنَافِعُ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ﴿٥﴾
5. Na wanyama wa mifugo Amewaumba. Mnapata kwao (sufi, ngozi za kutia) ujotojoto na manufaa (mengineyo), na miongoni mwao mnawala.[2]
وَلَكُمْ فِيهَا جَمَالٌ حِينَ تُرِيحُونَ وَحِينَ تَسْرَحُونَ﴿٦﴾
6. Na mnapata humo burudiko wakati mnapowarudisha jioni na mnapowapeleka machungani asubuhi.
وَتَحْمِلُ أَثْقَالَكُمْ إِلَىٰ بَلَدٍ لَّمْ تَكُونُوا بَالِغِيهِ إِلَّا بِشِقِّ الْأَنفُسِ ۚ إِنَّ رَبَّكُم ْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿٧﴾
7. Na wanabeba mizigo yenu kupeleka nchi msizoweza kuzifikia isipokuwa kwa mashaka mazito ya kuwalemeeni. Hakika Rabb wenu bila shaka Ni Mwenye Huruma mno, Mwenye Kurehemu.
وَالْخَيْلَ وَالْبِغَالَ وَالْحَمِيرَ لِتَرْكَبُوهَا وَزِينَةً ۚ وَيَخْلُقُ مَا لَا تَعْلَمُونَ﴿٨﴾
8. Na farasi na baghala na punda ili muwapande na wawe mapambo. Na Anaumba msivyovijua.
وَعَلَى اللَّـهِ قَصْدُ السَّبِيلِ وَمِنْهَا جَائِرٌ ۚ وَلَوْ شَاءَ لَهَدَاكُمْ أَجْمَعِينَ﴿٩﴾
9. Na ni Jukumu la Allaah kubainisha njia (ya haki), na ziko miongoni mwazo za kupotoka. Na kama Angetaka Angekuhidini nyote.
هُوَ الَّذِي أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً ۖ لَّكُم مِّنْهُ شَرَابٌ وَمِنْهُ شَجَرٌ فِيهِ تُسِيمُونَ﴿١٠﴾
10. Yeye Ndiye Aliyeteremsha kutoka mbinguni maji.[3] Kwayo mnapata ya kunywa, na pia ya miti ambayo mnalishia.
يُنبِتُ لَكُم بِهِ الزَّرْعَ وَالزَّيْتُونَ وَالنَّخِيلَ وَالْأَعْنَابَ وَمِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿١١﴾
11. (Kadhalika) Anakuotesheeni kwayo mimea, na mizaytuni na mitende na mizabibu, na kila (aina ya) mazao. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayah (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaotafakari.
وَسَخَّرَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ وَالنُّجُومُ مُسَخَّرَاتٌ بِأَمْرِهِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ﴿١٢﴾
12. Na Amekutiishieni usiku na mchana, na jua na mwezi. Na nyota zimetiishwa kwa Amri Yake. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaotia akilini.
وَمَا ذَرَأَ لَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُخْتَلِفًا أَلْوَانُهُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ﴿١٣﴾
13. Na (Ametiisha pia) Alivyoviumba katika ardhi vya rangi tofauti. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayah (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaokumbuka.
وَهُوَ الَّذِي سَخَّرَ الْبَحْرَ لِتَأْكُلُوا مِنْهُ لَحْمًا طَرِيًّا وَتَسْتَخْرِجُوا مِنْهُ حِلْيَةً تَلْبَسُونَهَا وَتَرَى الْفُلْكَ مَوَاخِرَ فِيهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴿١٤﴾
14. Naye Ndiye Ambaye Ametiisha bahari ili mle kutoka humo nyama laini safi, na mtoe humo mapambo mnayoyavaa, na utaona merikebu zikipasua maji humo, (Ameitiisha) ili mtafute katika Fadhila Zake, na ili mpate kushukuru.
وَأَلْقَىٰ فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمْ وَأَنْهَارًا وَسُبُلًا لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ﴿١٥﴾
15. Na Ameweka katika ardhi milima iliyosimama imara ili isiyumbeyumbe nanyi, na (Akaweka) mito na njia ili mpate kujua mwendako.
وَعَلَامَاتٍ ۚ وَبِالنَّجْمِ هُمْ يَهْتَدُونَ﴿١٦﴾
16. Na alama za kutambulisha, na kwa nyota wao wanaojiongoza (njia).[4]
أَفَمَن يَخْلُقُ كَمَن لَّا يَخْلُقُ ۗ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿١٧﴾
17. Je, (Allaah) Anayeumba ni sawa na asiyeumba? Je, basi hamkumbuki?
وَإِن تَعُدُّوا نِعْمَةَ اللَّـهِ لَا تُحْصُوهَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٨﴾
18. Na kama mkihesabu Neema za Allaah basi hamtoweza kuziorodhesha hesabuni.[5] Hakika Allaah bila shaka Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعْلِنُونَ﴿١٩﴾
19. Na Allaah Anajua mnayoyafanya siri na mnayoyadhihirisha.
وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَا يَخْلُقُونَ شَيْئًا وَهُمْ يُخْلَقُونَ﴿٢٠﴾
20. Na wale wanaowaomba badala ya Allaah hawaumbi kitu chochote, bali wao wanaumbwa.
أَمْوَاتٌ غَيْرُ أَحْيَاءٍ ۖ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ﴿٢١﴾
21. Ni wafu si wahai, na hawatambui lini watafufuliwa.
إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ فَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ قُلُوبُهُم مُّنكِرَةٌ وَهُم مُّسْتَكْبِرُونَ﴿٢٢﴾
22. Mwabudiwa wenu wa haki ni Ilaah (Allaah) Mmoja. Basi wale wasioamini Aakhirah nyoyo zao zinakanusha nao wanatakabari.
لَا جَرَمَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْتَكْبِرِينَ﴿٢٣﴾
23. Hapana shaka kwamba Allaah Anajua wanayoyafanya kwa siri na wanayoyadhihirisha. Hakika Yeye Hapendi wanaotakabari.
وَإِذَا قِيلَ لَهُم مَّاذَا أَنزَلَ رَبُّكُمْ ۙ قَالُوا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ﴿٢٤﴾
24. Na pale wanapoambiwa: Nini Ameteremsha Rabb wenu (kwa Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)? Husema: Hekaya za watu wa kale.
لِيَحْمِلُوا أَوْزَارَهُمْ كَامِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۙ وَمِنْ أَوْزَارِ الَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ﴿٢٥﴾
25. Ili wabebe mizigo (ya madhambi) yao kwa ukamilifu Siku ya Qiyaamah, pamoja na mizigo ya wale waliowapoteza bila ya kujua. Tanabahi! Uovu ulioje wanayoyabeba!
قَدْ مَكَرَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَأَتَى اللَّـهُ بُنْيَانَهُم مِّنَ الْقَوَاعِدِ فَخَرَّ عَلَيْهِمُ السَّقْفُ مِن فَوْقِهِمْ وَأَتَاهُمُ الْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ﴿٢٦﴾
26. Walikwishafanya makri wale wa kabla yao, na Allaah Akayasukua majengo yao kwenye misingi, sakafu zikawaporomokea juu yao, na ikawajia adhabu kutoka pande wasizozitambua.
ثُمَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يُخْزِيهِمْ وَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تُشَاقُّونَ فِيهِمْ ۚ قَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ إِنَّ الْخِزْيَ الْيَوْمَ وَالسُّوءَ عَلَى الْكَافِرِينَ﴿٢٧﴾
27. Kisha Siku ya Qiyaamah (Allaah) Atawahizi na Atasema: Wako wapi washirika Wangu ambao mlikuwa kwa ajili yao mnapingana kuwahasimu (Rusuli na Waumini)? Watasema waliopewa ilimu: Hakika hizaya leo na uovu ni juu ya makafiri.
الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ ۖ فَأَلْقَوُا السَّلَمَ مَا كُنَّا نَعْمَلُ مِن سُوءٍ ۚ بَلَىٰ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٢٨﴾
28. Ambao Malaika huwafisha wakiwa wamejidhulumu nafsi zao, watasalimu amri (watasema): Hatukuwa tukitenda uovu wowote. (Wataambiwa): Hapana! Hakika Allaah Anayajua vyema mliyokuwa mkitenda.
فَادْخُلُوا أَبْوَابَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۖ فَلَبِئْسَ مَثْوَى الْمُتَكَبِّرِينَ﴿٢٩﴾
29. Basi ingieni milango ya Jahannam mdumu humo. Ni uovu ulioje makazi ya wanaotakabari!
وَقِيلَ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا مَاذَا أَنزَلَ رَبُّكُمْ ۚ قَالُوا خَيْرًا ۗ لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةٌ ۚ وَلَدَارُ الْآخِرَةِ خَيْرٌ ۚ وَلَنِعْمَ دَارُ الْمُتَّقِينَ﴿٣٠﴾
30. Na wanapoambiwa wale waliokuwa na taqwa: Nini Ameteremsha Rabb wenu? Husema: Kheri. Kwa wale waliofanya ihsaan katika dunia hii watapata hasanah (mazuri). Na bila shaka nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi. Na uzuri ulioje nyumba ya wenye taqwa!
جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ لَهُمْ فِيهَا مَا يَشَاءُونَ ۚ كَذَٰلِكَ يَجْزِي اللَّـهُ الْمُتَّقِينَ﴿٣١﴾
31. Jannaat (bustani) za kudumu milele wataziingia inapita chini yake mito. Watapata humo wayatakayo. Hivyo ndivyo Allaah Anavyowalipa wenye taqwa.
الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ طَيِّبِينَ ۙ يَقُولُونَ سَلَامٌ عَلَيْكُمُ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٣٢﴾
32. Wale ambao Malaika wanawafisha katika hali njema watawaambia: Salaamun ‘Alaykum (amani iwe juu yenu), ingieni Jannah kwa sababu ya yale mliyokuwa mkitenda.
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ أَمْرُ رَبِّكَ ۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ اللَّـهُ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴿٣٣﴾
33. Je, wanangojea lolote isipokuwa wawafikie Malaika (kuwatoa roho) au ije Amri ya Rabb wako (ya adhabu). Hivyo ndivyo walivyofanya wale wa kabla yao. Na Allaah Hakuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao wenyewe.
فَأَصَابَهُمْ سَيِّئَاتُ مَا عَمِلُوا وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٣٤﴾
34. Basi yakawasibu maovu ya waliyoyatenda, na yakawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.
وَقَالَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا لَوْ شَاءَ اللَّـهُ مَا عَبَدْنَا مِن دُونِهِ مِن شَيْءٍ نَّحْنُ وَلَا آبَاؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن دُونِهِ مِن شَيْءٍ ۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ فَهَلْ عَلَى الرُّسُلِ إِلَّا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ﴿٣٥﴾
35. Na wale washirikina walisema: Kama Angelitaka Allaah tusingeliabudu chochote badala Yake, sisi wala baba zetu, wala tusingeliharamisha chochote bila Yeye Kuturuhusu. Hivyo ndivyo walivyofanya wale wa kabla yao. Basi je, kuna lolote juu ya Rusuli isipokuwa kufikisha Ujumbe kwa ubainifu?
وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ فَمِنْهُم مَّنْ هَدَى اللَّـهُ وَمِنْهُم مَّنْ حَقَّتْ عَلَيْهِ الضَّلَالَةُ ۚ فَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ﴿٣٦﴾
36. Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Rasuli (alinganie) kwamba: Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaghuti.[6] Basi miongoni mwao wako ambao Allaah Amewahidi, na miongoni mwao wako ambao umewathibitikia upotofu. Basi nendeni katika ardhi kisha mtazame vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha.[7]
إِن تَحْرِصْ عَلَىٰ هُدَاهُمْ فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَن يُضِلُّ ۖ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ﴿٣٧﴾
37. Ukiwa na hima ya kwamba wahidike (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi hakika Allaah Hamhidi Aliyemtakia kupotea. Na hawatopata wenye kuwanusuru.
وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ ۙ لَا يَبْعَثُ اللَّـهُ مَن يَمُوتُ ۚ بَلَىٰ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٣٨﴾
38. Na wakaapa kwa Allaah, viapo vyao thabiti vya nguvu, kwamba: Allaah Hatomfufua aliyekufa. Sivyo hivyo! Bali Ahadi Yake ni haki (Atafufua wote), lakini watu wengi hawajui.
لِيُبَيِّنَ لَهُمُ الَّذِي يَخْتَلِفُونَ فِيهِ وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّهُمْ كَانُوا كَاذِبِينَ﴿٣٩﴾
39. Ili Awabainishie yale wanayokhitilafiana, na ili wajue wale waliokufuru kwamba wao walikuwa waongo.
إِنَّمَا قَوْلُنَا لِشَيْءٍ إِذَا أَرَدْنَاهُ أَن نَّقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ﴿٤٠﴾
40. Hakika Kauli Yetu kwa kitu Tunapokikusudia, Tunakiambia: Kun! (Kuwa) Basi kinakuwa!
وَالَّذِينَ هَاجَرُوا فِي اللَّـهِ مِن بَعْدِ مَا ظُلِمُوا لَنُبَوِّئَنَّهُمْ فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً ۖ وَلَأَجْرُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ﴿٤١﴾
41. Na wale waliohajiri kwa ajili ya Allaah baada ya kudhulumiwa, kwa hakika Tutawapa makazi mazuri duniani. Na bila shaka ujira wa Aakhirah ni mkubwa zaidi lau wangelikuwa wanajua.
الَّذِينَ صَبَرُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ﴿٤٢﴾
42. (Hao ndio) Wale waliovuta subira na wakatawakali kwa Rabb wao.
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِي إِلَيْهِمْ ۚ فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ﴿٤٣﴾
43. Na Hatukutuma (Rasuli) kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa ni wanaume Tunawafunulia Wahy. Basi ulizeni watu wenye ukumbusho[8] ikiwa nyinyi hamjui.
بِالْبَيِّنَاتِ وَالزُّبُرِ ۗ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٤٤﴾
44. (Tumewatuma) Kwa hoja bayana na Vitabu vya Hukumu. Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao huenda wakapata kutafakari.
أَفَأَمِنَ الَّذِينَ مَكَرُوا السَّيِّئَاتِ أَن يَخْسِفَ اللَّـهُ بِهِمُ الْأَرْضَ أَوْ يَأْتِيَهُمُ الْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ﴿٤٥﴾
45. Je, wameaminisha wale waliopanga makri za uovu kwamba Allaah Hatowadidimiza katika ardhi au haitowafikia adhabu kutoka wasipotambua?
أَوْ يَأْخُذَهُمْ فِي تَقَلُّبِهِمْ فَمَا هُم بِمُعْجِزِينَ﴿٤٦﴾
46. Au (Allaah) Hatowakamata wakiwa katika harakati zao na wao wasiweze kukwepa?
أَوْ يَأْخُذَهُمْ عَلَىٰ تَخَوُّفٍ فَإِنَّ رَبَّكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿٤٧﴾
47. Au (Allaah) Hatowakamata katika hali ya khofu ya kusubiri adhabu? Hakika Rabb wako bila shaka Ni Mwenye Huruma mno, Mwenye Kurehemu.
أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَىٰ مَا خَلَقَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ يَتَفَيَّأُ ظِلَالُهُ عَنِ الْيَمِينِ وَالشَّمَائِلِ سُجَّدًا لِّلَّـهِ وَهُمْ دَاخِرُونَ﴿٤٨﴾
48. Je, hawaoni vile vitu Alivyoumba Allaah ambavyo vivuli vyake vinasogea huku na kule, kuliani na kushotoni, vikimsujudia Allaah[9], na huku wao (wenye vivuli) wananyenyekea?
وَلِلَّـهِ يَسْجُدُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مِن دَابَّةٍ وَالْمَلَائِكَةُ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ﴿٤٩﴾
49. Na ni Allaah Pekee vinamsujudia vyote vilivyomo mbinguni na ardhini katika viumbe vitembeavyo, na Malaika, nao hawatakabari.
يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ۩﴿٥٠﴾
50. Wanamkhofu Rabb wao Aliye juu yao[10], na wanafanya yale wanayoamrishwa.
وَقَالَ اللَّـهُ لَا تَتَّخِذُوا إِلَـٰهَيْنِ اثْنَيْنِ ۖ إِنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ﴿٥١﴾
51. Na Allaah Anasema: Msijichukulie waabudiwa wawili, hakika Yeye Ndiye Mwabudiwa wa haki Mmoja Pekee, basi niogopeni Mimi tu.
وَلَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَهُ الدِّينُ وَاصِبًا ۚ أَفَغَيْرَ اللَّـهِ تَتَّقُونَ﴿٥٢﴾
52. Na ni Vyake vyote vilivyomo katika mbingu na ardhi, na ni Yeye Pekee Astahikiye kuabudiwa na kutiiwa daima. Je, basi mtamcha asiyekuwa Allaah?
وَمَا بِكُم مِّن نِّعْمَةٍ فَمِنَ اللَّـهِ ۖ ثُمَّ إِذَا مَسَّكُمُ الضُّرُّ فَإِلَيْهِ تَجْأَرُونَ﴿٥٣﴾
53. Na Neema yoyote mliyo nayo, basi ni kutoka kwa Allaah. Kisha inapokuguseni dhara, mnamlilia Yeye tu kuomba msaada.
ثُمَّ إِذَا كَشَفَ الضُّرَّ عَنكُمْ إِذَا فَرِيقٌ مِّنكُم بِرَبِّهِمْ يُشْرِكُونَ﴿٥٤﴾
54. Kisha Anapokuondosheeni dhara tahamaki kundi miongoni mwenu wanamshirikisha Rabb wao.
لِيَكْفُرُوا بِمَا آتَيْنَاهُمْ ۚ فَتَمَتَّعُوا ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ﴿٥٥﴾
55. Ili waje wakanushe (Neema) Tulizowapa. Basi stareheni kidogo, mtakuja kujua.
وَيَجْعَلُونَ لِمَا لَا يَعْلَمُونَ نَصِيبًا مِّمَّا رَزَقْنَاهُمْ ۗ تَاللَّـهِ لَتُسْأَلُنَّ عَمَّا كُنتُمْ تَفْتَرُونَ﴿٥٦﴾
56. Na wanawawekea (waabudiwa wao) wasiojua (wanayofanyiwa), fungu katika ambavyo Tumewaruzuku. Ta-Allaahi![11] Bila shaka mtaulizwa juu ya yale mliyokuwa mkiyatunga (ya uongo).
وَيَجْعَلُونَ لِلَّـهِ الْبَنَاتِ سُبْحَانَهُ ۙ وَلَهُم مَّا يَشْتَهُونَ﴿٥٧﴾
57. Na wanamfanyia Allaah kuwa ana mabinti! Utakasifu ni Wake! Na wao wawe na (wana wa kiume) wanaowatamani.[12]
وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِالْأُنثَىٰ ظَلَّ وَجْهُهُ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ﴿٥٨﴾
58. Na anapoletewa khabari mmoja wao ya kuzaliwa mtoto wa kike, uso wake husawijika na kujawa majonzi na ghamu.
يَتَوَارَىٰ مِنَ الْقَوْمِ مِن سُوءِ مَا بُشِّرَ بِهِ ۚ أَيُمْسِكُهُ عَلَىٰ هُونٍ أَمْ يَدُسُّهُ فِي التُّرَابِ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ﴿٥٩﴾
59. Anajificha asikutane na watu kutokana na khabari mbaya aliyoletewa. Je, abaki naye kwa fedheha au amfukie ardhini (mzimamzima)? Tanabahi! Uovu ulioje wanayohukumu!
لِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ مَثَلُ السَّوْءِ ۖ وَلِلَّـهِ الْمَثَلُ الْأَعْلَىٰ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٦٠﴾
60. Wale wasioamini Aakhirah wana mfano mbaya (wa upungufu), lakini Allaah Ana Sifa Kamilifu Tukufu Kabisa. Naye Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
وَلَوْ يُؤَاخِذُ اللَّـهُ النَّاسَ بِظُلْمِهِم مَّا تَرَكَ عَلَيْهَا مِن دَابَّةٍ وَلَـٰكِن يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۖ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ﴿٦١﴾
61. Na kama Allaah Angeliwachukulia watu kwa dhulma zao, Asingeliacha juu ya ardhi kiumbe chochote, lakini Anawaakhirisha mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Basi utakapofika muda wao hawatoakhirisha saa na wala hawatotanguliza.
وَيَجْعَلُونَ لِلَّـهِ مَا يَكْرَهُونَ وَتَصِفُ أَلْسِنَتُهُمُ الْكَذِبَ أَنَّ لَهُمُ الْحُسْنَىٰ ۖ لَا جَرَمَ أَنَّ لَهُمُ النَّارَ وَأَنَّهُم مُّفْرَطُونَ﴿٦٢﴾
62. Na wanamfanyia Allaah yale wanayoyachukia (wao wenyewe), na ndimi zao zinaeleza uongo kwamba watapata mazuri kabisa. Hapana shaka kwamba watapata moto na watatelekezwa humo.
تَاللَّـهِ لَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَهُوَ وَلِيُّهُمُ الْيَوْمَ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٦٣﴾
63. Ta-Allaahi![13] Kwa yakini Tulipeleka (Rusuli) kwa nyumati za kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), shaytwaan akawapambia vitendo vyao. Na yeye leo ni rafiki yao mlinzi, nao watapata adhabu iumizayo.
وَمَا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ إِلَّا لِتُبَيِّنَ لَهُمُ الَّذِي اخْتَلَفُوا فِيهِ ۙ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿٦٤﴾
64. Na Hatukukuteremshia Kitabu (Qur-aan) isipokuwa uwabainishie yale waliyokhitilafiana, na pia ni mwongozo na rehma kwa watu wanaoamini.
وَاللَّـهُ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ﴿٦٥﴾
65. Na Allaah Ameteremsha kutoka mbinguni maji Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayah (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaosikia.
وَإِنَّ لَكُمْ فِي الْأَنْعَامِ لَعِبْرَةً ۖ نُّسْقِيكُم مِّمَّا فِي بُطُونِهِ مِن بَيْنِ فَرْثٍ وَدَمٍ لَّبَنًا خَالِصًا سَائِغًا لِّلشَّارِبِينَ﴿٦٦﴾
66. Na hakika kuna mazingatio kwenu katika wanyama wa mifugo. Tunakunywesheni katika yale yaliyomo matumboni mwao yaliyo baina ya kinyesi na damu; (nayo ni) maziwa safi ya ladha ya kuburudisha kwa wanywaji.
وَمِن ثَمَرَاتِ النَّخِيلِ وَالْأَعْنَابِ تَتَّخِذُونَ مِنْهُ سَكَرًا وَرِزْقًا حَسَنًا ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ﴿٦٧﴾
67. Na katika matunda ya mitende na mizabibu mnafanya kutokana nayo vinywaji vikali vya ulevi (kabla ya kuharamishwa)[14] na riziki nzuri. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayah (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa wanaotia akilini.
وَأَوْحَىٰ رَبُّكَ إِلَى النَّحْلِ أَنِ اتَّخِذِي مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا وَمِنَ الشَّجَرِ وَمِمَّا يَعْرِشُونَ﴿٦٨﴾
68. Na Rabb wako Amemtia ilhamu nyuki kwamba: Jitengenezee nyumba katika majabali, na katika miti, na katika wanavyojenga.
ثُمَّ كُلِي مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ فَاسْلُكِي سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلًا ۚ يَخْرُجُ مِن بُطُونِهَا شَرَابٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ فِيهِ شِفَاءٌ لِّلنَّاسِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿٦٩﴾
69. Kisha kula katika kila matunda, na fuata njia za Rabb wako zilizofanywa nyepesi (kuzipita). Kinatoka katika matumbo yao kinywaji cha rangi mbali mbali, ndani yake mna shifaa (ya magonjwa) kwa watu. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayah (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaotafakari.
وَاللَّـهُ خَلَقَكُمْ ثُمَّ يَتَوَفَّاكُمْ ۚ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰ أَرْذَلِ الْعُمُرِ لِكَيْ لَا يَعْلَمَ بَعْدَ عِلْمٍ شَيْئًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ قَدِيرٌ﴿٧٠﴾
70. Na Allaah Amekuumbeni, kisha Anakufisheni. Na yuko miongoni mwenu anayerudishwa katika umri mbaya na dhaifu zaidi awe hajui tena kitu chochote baada ya (kuwa na) ilimu. Hakika Allaah Ni Mjuzi wa yote, Muweza wa yote.
وَاللَّـهُ فَضَّلَ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ فِي الرِّزْقِ ۚ فَمَا الَّذِينَ فُضِّلُوا بِرَادِّي رِزْقِهِمْ عَلَىٰ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَهُمْ فِيهِ سَوَاءٌ ۚ أَفَبِنِعْمَةِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ﴿٧١﴾
71. Na Allaah Amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengineo katika riziki. Basi wale waliofadhilishwa hawagawi riziki zao kwa wale iliowamiliki mikono yao ya kulia ili wawe sawa katika hiyo (riziki). Je, basi wanakanusha Neema za Allaah?
وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنْ أَزْوَاجِكُم بَنِينَ وَحَفَدَةً وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ ۚ أَفَبِالْبَاطِلِ يُؤْمِنُونَ وَبِنِعْمَتِ اللَّـهِ هُمْ يَكْفُرُونَ﴿٧٢﴾
72. Na Allaah Amekufanyieni wake katika jinsi yenu, na Amekufanyieni kutokana na wake zenu wana na wajukuu, na Amekuruzukuni vizuri. Je, basi wanaamini ya batili na wanakufuru Neema za Allaah?
وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَهُمْ رِزْقًا مِّنَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ شَيْئًا وَلَا يَسْتَطِيعُونَ﴿٧٣﴾
73. Na wanaabudu pasi na Allaah wasiowamilikia (uwezo wa) riziki ya kitu chochote kutoka mbinguni na ardhini, na (hakika) wala hawawezi.
فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ﴿٧٤﴾
74. Basi msimpigie mifano Allaah. Hakika Allaah Anajua nanyi hamjui.
ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا عَبْدًا مَّمْلُوكًا لَّا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَمَن رَّزَقْنَاهُ مِنَّا رِزْقًا حَسَنًا فَهُوَ يُنفِقُ مِنْهُ سِرًّا وَجَهْرًا ۖ هَلْ يَسْتَوُونَ ۚ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٧٥﴾
75. Allaah Amepiga mfano wa mtumwa anayemilikiwa hana uwezo juu ya chochote, na mtu (huru) ambaye Tumemruzuku kutoka Kwetu riziki nzuri, naye akawa anaitoa kwa siri na dhahiri. Je, wanalingana sawa? AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah)! Bali wengi wao hawajui.[15]
وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا رَّجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوْلَاهُ أَيْنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأْتِ بِخَيْرٍ ۖ هَلْ يَسْتَوِي هُوَ وَمَن يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ ۙ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٧٦﴾
76. Na Allaah Amepiga mfano (mwingine) wa watu wawili; mmoja ni bubu asiye na uwezo juu ya chochote, naye ni mzigo mzito kwa anayemsimamia mambo yake, na popote anapomuelekeza haleti kheri. Je, analingana sawa yeye na yule anayeamrisha uadilifu, naye yuko juu ya njia iliyonyooka?
وَلِلَّـهِ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَا أَمْرُ السَّاعَةِ إِلَّا كَلَمْحِ الْبَصَرِ أَوْ هُوَ أَقْرَبُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٧٧﴾
77. Na ni ya Allaah ghaibu ya mbingu na ardhi. Na haikuwa amri ya Saa (Qiyaamah) isipokuwa kama upepeso wa jicho au karibu zaidi.[16] Hakika Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.
وَاللَّـهُ أَخْرَجَكُم مِّن بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ لَا تَعْلَمُونَ شَيْئًا وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ ۙ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴿٧٨﴾
78. Na Allaah Amekutoeni kutoka matumboni mwa mama zenu mkiwa hamjui lolote, na Amekujaalieni kusikia na kuona na nyoyo ili mpate kushukuru.
أَلَمْ يَرَوْا إِلَى الطَّيْرِ مُسَخَّرَاتٍ فِي جَوِّ السَّمَاءِ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا اللَّـهُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿٧٩﴾
79. Je, hawaoni ndege wanavyotiishwa katika anga la mbingu, hakuna anayewashika isipokuwa Allaah. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaoamini.
وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُم مِّن بُيُوتِكُمْ سَكَنًا وَجَعَلَ لَكُم مِّن جُلُودِ الْأَنْعَامِ بُيُوتًا تَسْتَخِفُّونَهَا يَوْمَ ظَعْنِكُمْ وَيَوْمَ إِقَامَتِكُمْ ۙ وَمِنْ أَصْوَافِهَا وَأَوْبَارِهَا وَأَشْعَارِهَا أَثَاثًا وَمَتَاعًا إِلَىٰ حِينٍ﴿٨٠﴾
80. Na Allaah Amekufanyieni majumba yenu yawe maskani. Na Amekujaalieni kutokana na ngozi za wanyama wa mifugo mahema ambayo mnayahisi mepesi siku ya kusafiri kwenu na siku ya kupiga kwenu kambi, na kutokana na sufi zao na manyoya yao, na nywele zao (Amekujaalieni) fanicha na vifaa vya kutumia mpaka muda fulani.
وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُم مِّمَّا خَلَقَ ظِلَالًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ الْجِبَالِ أَكْنَانًا وَجَعَلَ لَكُمْ سَرَابِيلَ تَقِيكُمُ الْحَرَّ وَسَرَابِيلَ تَقِيكُم بَأْسَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُتِمُّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تُسْلِمُونَ﴿٨١﴾
81. Na Allaah Amekufanyieni vivuli katika Alivyoumba, na Akakujaalieni katika majabali mapango, na Amekujaalieni mavazi yanakukingeni na joto na mavazi (ya chuma) yanakukingeni katika vita vyenu. Hivyo ndivyo Anavyotimiza Neema Yake juu yenu ili mpate kujisalimisha.
فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ الْمُبِينُ﴿٨٢﴾
82. Wakikengeuka, basi hakika ni juu yako ubalighisho wa bayana.
يَعْرِفُونَ نِعْمَتَ اللَّـهِ ثُمَّ يُنكِرُونَهَا وَأَكْثَرُهُمُ الْكَافِرُونَ﴿٨٣﴾
83. Wanazijua Neema za Allaah, kisha wanazikanusha, na wengi wao ni makafiri.
وَيَوْمَ نَبْعَثُ مِن كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا ثُمَّ لَا يُؤْذَنُ لِلَّذِينَ كَفَرُوا وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ﴿٨٤﴾
84. Na Siku Tutakapohudhurisha shahidi kwa kila ummah, kisha waliokufuru hawatoruhusiwa (kutoa nyudhuru) na wala hawatapewa nafasi ya kujitetea (kwa Allaah).
وَإِذَا رَأَى الَّذِينَ ظَلَمُوا الْعَذَابَ فَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمْ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ﴿٨٥﴾
85. Na wale waliodhulumu watakapoiona adhabu, basi hawatopunguziwa wala hawatopewa muhula.
وَإِذَا رَأَى الَّذِينَ أَشْرَكُوا شُرَكَاءَهُمْ قَالُوا رَبَّنَا هَـٰؤُلَاءِ شُرَكَاؤُنَا الَّذِينَ كُنَّا نَدْعُو مِن دُونِكَ ۖ فَأَلْقَوْا إِلَيْهِمُ الْقَوْلَ إِنَّكُمْ لَكَاذِبُونَ﴿٨٦﴾
86. Na wale waliomshirikisha (Allaah) watakapowaona washirika wao watasema: Rabb wetu! Hawa ni washirikishwa wetu ambao tulikuwa tunawaomba badala Yako. Hapo hapo watatamka kuwarudi: Hakika nyinyi ni waongo!
وَأَلْقَوْا إِلَى اللَّـهِ يَوْمَئِذٍ السَّلَمَ ۖ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ﴿٨٧﴾
87. Na watajisalimisha kwa Allaah Siku hiyo. Na yatawapotea waliyokuwa wakiyatunga (ya uongo).
الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ زِدْنَاهُمْ عَذَابًا فَوْقَ الْعَذَابِ بِمَا كَانُوا يُفْسِدُونَ﴿٨٨﴾
88. Wale waliokufuru na wakazuia Njia ya Allaah, Tutawazidishia adhabu juu ya adhabu kwa sababu ya ufisadi waliokuwa wakiufanya.
وَيَوْمَ نَبْعَثُ فِي كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا عَلَيْهِم مِّنْ أَنفُسِهِمْ ۖ وَجِئْنَا بِكَ شَهِيدًا عَلَىٰ هَـٰؤُلَاءِ ۚ وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَانًا لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ﴿٨٩﴾
89. Na Siku Tutakapohudhurisha shahidi kwa kila ummah anayetokana na wao wenyewe awatolee ushuhuda. Na Tutakuleta (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uwe shahidi juu ya hawa (ummah wako).[17] Na Tumekuteremshia Kitabu kikiwa ni kielezo bayana cha kila kitu, na ni mwongozo, na rehma, na bishara kwa Waislamu.
إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ﴿٩٠﴾
90. Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu, na ihsaan, na kuwapa (msaada) jamaa wa karibu, na Anakataza machafu, na munkari, na baghi[18] (udhalimu). Anakuwaidhini ili huenda mkapata kukumbuka.
وَأَوْفُوا بِعَهْدِ اللَّـهِ إِذَا عَاهَدتُّمْ وَلَا تَنقُضُوا الْأَيْمَانَ بَعْدَ تَوْكِيدِهَا وَقَدْ جَعَلْتُمُ اللَّـهَ عَلَيْكُمْ كَفِيلًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ﴿٩١﴾
91. Na timizeni Ahadi ya Allaah mnapoahidi, na wala msivunje viapo baada ya kuvithibitisha, na hali ya kuwa mmekwishamfanya Allaah Kuwa Mdhamini wenu. Hakika Allaah Anajua yale mnayoyafanya.
وَلَا تَكُونُوا كَالَّتِي نَقَضَتْ غَزْلَهَا مِن بَعْدِ قُوَّةٍ أَنكَاثًا تَتَّخِذُونَ أَيْمَانَكُمْ دَخَلًا بَيْنَكُمْ أَن تَكُونَ أُمَّةٌ هِيَ أَرْبَىٰ مِنْ أُمَّةٍ ۚ إِنَّمَا يَبْلُوكُمُ اللَّـهُ بِهِ ۚ وَلَيُبَيِّنَنَّ لَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ﴿٩٢﴾
92. Na wala msiwe kama yule mwanamke aliyezongoa uzi wake vipande vipande baada ya (kuusokota na) kuwa mgumu, mnafanya viapo vyenu kuwa njia ya kudaganyana baina yenu[19], kwa kuwa ati ummah mmoja una nguvu zaidi kwa idadi na utajiri kuliko ummah mwengine. Hakika hapana ila Allaah Anakujaribuni kwavyo. Na bila shaka Atakubainishieni Siku ya Qiyaamah yale mliyokuwa mkikhitilafiana nayo.
وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَعَلَكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَـٰكِن يُضِلُّ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَلَتُسْأَلُنَّ عَمَّا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٩٣﴾
93. Na kama Allaah Angelitaka Angelikufanyeni ummah mmoja, lakini Humpotoa Amtakaye na Anamhidi Amtakaye. Na bila shaka mtaulizwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
وَلَا تَتَّخِذُوا أَيْمَانَكُمْ دَخَلًا بَيْنَكُمْ فَتَزِلَّ قَدَمٌ بَعْدَ ثُبُوتِهَا وَتَذُوقُوا السُّوءَ بِمَا صَدَدتُّمْ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ وَلَكُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿٩٤﴾
94. Na wala msifanye viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganyana baina yenu ukateleza mguu baada ya kuthibitika kwake na mkaonja uovu wenu (duniani) kwa sababu ya kuzuia kwenu Njia ya Allaah. Na mtapata (Aakhirah) adhabu kuu.[20]
وَلَا تَشْتَرُوا بِعَهْدِ اللَّـهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۚ إِنَّمَا عِندَ اللَّـهِ هُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿٩٥﴾
95. Na wala msibadilishe Ahadi ya Allaah kwa thamani ndogo. Hakika yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi kwenu, mngelikuwa mnajua.
مَا عِندَكُمْ يَنفَدُ ۖ وَمَا عِندَ اللَّـهِ بَاقٍ ۗ وَلَنَجْزِيَنَّ الَّذِينَ صَبَرُوا أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٦﴾
96. Mlivyo navyo nyinyi vinatoweka, na vilivyoko kwa Allaah ni vya kubakia. Na kwa yakini Tutawalipa wale waliovuta subira ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda.
مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٧﴾
97. Mwenye kutenda mema miongoni mwa wanamume au wanawake naye ni Muumin, hakika Tutamhuisha uhai mzuri,[21] na bila shaka Tutawalipa ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda.
فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ﴿٩٨﴾
98. Unaposoma Qur-aan basi (kwanza) omba kinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa.[22]
إِنَّهُ لَيْسَ لَهُ سُلْطَانٌ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ﴿٩٩﴾
99. Hakika yeye hana mamlaka juu ya wale walioamini na kwa Rabb wao wanatawakali.
إِنَّمَا سُلْطَانُهُ عَلَى الَّذِينَ يَتَوَلَّوْنَهُ وَالَّذِينَ هُم بِهِ مُشْرِكُونَ﴿١٠٠﴾
100. Hakika mamlaka yake yako juu ya wale wanaomfanya rafiki mwandani na ambao wao wanamshirikisha (Allaah) naye.
وَإِذَا بَدَّلْنَا آيَةً مَّكَانَ آيَةٍ ۙ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مُفْتَرٍ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿١٠١﴾
101. Na Tunapobadilisha Aayah mahala pa Aayah nyingine,[23] na Allaah Anajua zaidi Anayoyateremsha, husema: Hakika wewe ni mtungaji (uongo). Bali wengi wao hawajui.
قُلْ نَزَّلَهُ رُوحُ الْقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ لِيُثَبِّتَ الَّذِينَ آمَنُوا وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ﴿١٠٢﴾
102. Sema: Ameiteremsha Ruwh[24] Al-Qudus (Jibriyl) kutoka kwa Rabb wako kwa haki ili iwathibitishe wale walioamini, na ni mwongozo na bishara kwa Waislamu.
وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّهُمْ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُ بَشَرٌ ۗ لِّسَانُ الَّذِي يُلْحِدُونَ إِلَيْهِ أَعْجَمِيٌّ وَهَـٰذَا لِسَانٌ عَرَبِيٌّ مُّبِينٌ﴿١٠٣﴾
103. Na kwa yakini Tunajua kwamba wao wanasema: Hakika hapana isipokuwa mtu anamfundisha (Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم Qur-aan). Lugha wanayomnasibishia nayo ni ya kigeni, na hii ni lugha ya Kiarabu bayana.[25]
إِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ لَا يَهْدِيهِمُ اللَّـهُ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١٠٤﴾
104. Hakika wale wasioamini Aayaat (na Ishara, Hoja, Dalili) za Allaah, Allaah Hatowahidi, na watapata adhabu iumizayo.
إِنَّمَا يَفْتَرِي الْكَذِبَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَاذِبُونَ﴿١٠٥﴾
105. Hakika wanaotunga uongo ni wale ambao hawaamini Aayaat (na Ishara, Hoja, Dalili) za Allaah. Na hao ndio waongo.
مَن كَفَرَ بِاللَّـهِ مِن بَعْدِ إِيمَانِهِ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ وَلَـٰكِن مَّن شَرَحَ بِالْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِّنَ اللَّـهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿١٠٦﴾
106. Atakayemkufuru Allaah baada ya imaan yake - isipokuwa yule aliyekirihishwa (kukanusha) na huku moyo wake umetua juu ya imaan - lakini aliyekifungulia ukafiri kifua chake, basi hao juu yao ni ghadhabu kutoka kwa Allaah na watapata adhabu kuu kabisa.
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اسْتَحَبُّوا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ﴿١٠٧﴾
107. Hivyo ni kwa sababu wao wamestahabu uhai wa dunia kuliko wa Aakhirah, na kwa kuwa Allaah Haongoi watu makafiri.
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ طَبَعَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَسَمْعِهِمْ وَأَبْصَارِهِمْ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ﴿١٠٨﴾
108. Hao ni wale ambao Allaah Amepiga chapa juu ya nyoyo zao, na masikio yao, na macho yao. Na hao ndio walioghafilika.
لَا جَرَمَ أَنَّهُمْ فِي الْآخِرَةِ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿١٠٩﴾
109. Hakuna shaka kwamba wao Aakhirah ni wenye kukhasirika.
ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ هَاجَرُوا مِن بَعْدِ مَا فُتِنُوا ثُمَّ جَاهَدُوا وَصَبَرُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١١٠﴾
110. Kisha hakika Rabb wako, kwa wale waliohajiri baada ya kutiwa matesoni, kisha wakafanya Jihaad na wakavuta subira, hakika Rabb wako baada ya hayo bila shaka Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[26]
يَوْمَ تَأْتِي كُلُّ نَفْسٍ تُجَادِلُ عَن نَّفْسِهَا وَتُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا عَمِلَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿١١١﴾
111. Siku itakapokuja kila nafsi huku ikijitetea yenyewe, na kila nafsi italipwa kikamilifu yale iliyofanya, nao hawatodhulumiwa.
وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا قَرْيَةً كَانَتْ آمِنَةً مُّطْمَئِنَّةً يَأْتِيهَا رِزْقُهَا رَغَدًا مِّن كُلِّ مَكَانٍ فَكَفَرَتْ بِأَنْعُمِ اللَّـهِ فَأَذَاقَهَا اللَّـهُ لِبَاسَ الْجُوعِ وَالْخَوْفِ بِمَا كَانُوا يَصْنَعُونَ﴿١١٢﴾
112. Na Allaah Amepiga mfano wa mji (wa Makkah) uliokuwa katika amani na utulivu, inaufikia riziki yake maridhawa kutoka kila mahali, kisha ukakufuru Neema za Allaah. Basi Allaah Akauonjesha funiko la njaa na khofu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakitenda.
وَلَقَدْ جَاءَهُمْ رَسُولٌ مِّنْهُمْ فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمُ الْعَذَابُ وَهُمْ ظَالِمُونَ﴿١١٣﴾
113. Na kwa yakini aliwajia Rasuli miongoni mwao wakamkadhibisha, basi ikawachukuwa adhabu hali ya kuwa ni madhalimu.
فَكُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ حَلَالًا طَيِّبًا وَاشْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ﴿١١٤﴾
114. Basi kuleni katika vile Alivyokuruzukuni Allaah vya halali vizuri, na shukuruni Neema za Allaah ikiwa mnamwabudu Yeye Pekee.
إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّـهِ بِهِ ۖ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١١٥﴾
115. Hakika (Allaah) Amekuharamishieni nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na kilichotajiwa katika kuchinjwa kwake ghairi ya Allaah. Lakini atakayefikwa na dharura bila ya kutamani wala kuvuka mipaka, basi hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَلَا تَقُولُوا لِمَا تَصِفُ أَلْسِنَتُكُمُ الْكَذِبَ هَـٰذَا حَلَالٌ وَهَـٰذَا حَرَامٌ لِّتَفْتَرُوا عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ﴿١١٦﴾
116. Na wala msiseme kwa ndimi zenu zinazopambia uongo: Hii halali na hii haramu ili mumtungie uongo Allaah. Hakika wale wanaomtungia uongo Allaah hawafaulu.
مَتَاعٌ قَلِيلٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١١٧﴾
117. Ni starehe ndogo (tu duniani), na watapata adhabu iumizayo.
وَعَلَى الَّذِينَ هَادُوا حَرَّمْنَا مَا قَصَصْنَا عَلَيْكَ مِن قَبْلُ ۖ وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ﴿١١٨﴾
118. Na wale Mayahudi Tuliwaharamishia yale Tuliyokusimulia kabla (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na Hatukuwadhulumu, lakini walikuwa wanajidhulumu nafsi zao wenyewe.
ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُوا السُّوءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١١٩﴾
119. Kisha hakika Rabb wako, kwa wale waliotenda uovu kwa ujahili, kisha wakatubu baada yake, na wakatengeneza walivyoharibu, hakika Rabb wako baada ya hayo bila shaka Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
إِنَّ إِبْرَاهِيمَ كَانَ أُمَّةً قَانِتًا لِّلَّـهِ حَنِيفًا وَلَمْ يَكُ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١٢٠﴾
120. Hakika Ibraahiym alikuwa mwenye akhlaaq na maadili yote mema[27], mtiifu kwa Allaah, aliyeelemea haki, na hakuwa miongoni mwa washirikina.[28]
شَاكِرًا لِّأَنْعُمِهِ ۚ اجْتَبَاهُ وَهَدَاهُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿١٢١﴾
121. Mwenye kushukuru Neema Zake, (Naye Allaah) Akamteua na Akamuongoza kuelekea njia iliyonyooka.
وَآتَيْنَاهُ فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً ۖ وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ﴿١٢٢﴾
122. Na Tukampa duniani mazuri. Na hakika yeye Aakhirah bila shaka ni miongoni mwa Swalihina.
ثُمَّ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ أَنِ اتَّبِعْ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۖ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١٢٣﴾
123. Kisha Tukakufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba fuata mila ya Ibraahim aliyeelemea haki na hakuwa miongoni mwa washirikina.
إِنَّمَا جُعِلَ السَّبْتُ عَلَى الَّذِينَ اخْتَلَفُوا فِيهِ ۚ وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَحْكُمُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ﴿١٢٤﴾
124. Hakika As-Sabt[29] imefanywa kwa wale waliokhitilafiana kwayo. Na hakika Rabb wako Atahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah katika yale waliyokuwa wanakhitilafiana kwayo.
ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ﴿١٢٥﴾
125. Lingania waje katika Njia ya Rabb wako kwa hikmah na mawaidha mazuri. Na jadiliana nao kwa njia bora yenye kunasibiana na hali. Hakika Rabb wako, Yeye Anamjua zaidi aliyepotea Njia Yake, Naye Anawajua zaidi waliohidika.
وَإِنْ عَاقَبْتُمْ فَعَاقِبُوا بِمِثْلِ مَا عُوقِبْتُم بِهِ ۖ وَلَئِن صَبَرْتُمْ لَهُوَ خَيْرٌ لِّلصَّابِرِينَ﴿١٢٦﴾
126. Na mkilipiza, basi lipizeni kulingana na vile mlivyoadhibiwa. Na mkivuta subira, basi bila shaka hivyo ni bora zaidi kwa wenye subira.[30]
وَاصْبِرْ وَمَا صَبْرُكَ إِلَّا بِاللَّـهِ ۚ وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلَا تَكُ فِي ضَيْقٍ مِّمَّا يَمْكُرُونَ﴿١٢٧﴾
127. Na vuta subira (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na haiwi subira yako isipokuwa kwa Msaada na Tawfiyq ya Allaah. Na wala usiwahuzunikie, na wala usiwe katika dhiki kutokana na njama wanazozifanya.
إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ﴿١٢٨﴾
128. Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa, na wale ambao wao ni wenye kufanya ihsaan.
[1] Maana Za Ruwh Katika Qur-aan:
Ruwh katika Qur-aan ina maana kadhaa ambazo zimo katika Suwrah na Aayah mbalimbali miongoni mwazo ni:
(i) Wahy: Yaani Qur-aan kama ilivyo katika Suwrah hii ya An-Nahl (16:2), na pia Ash-Shuwraa (42:52).
(ii) Jibriyl (عليه السّلام): Ni kama katika Suwrah hii ya An-Nahl (16:102) na pia Ash-Shu’araa (26:193), Maryam (19:17), Al-Baqarah (2:87) (2:253) na Al-Qadr (97:4).
(iii) Roho ya mwanaadam: Ni katika Suwrat Al-Israa (17:85).
[2] Miongoni Mwa Neema Za Allaah (سبحانه وتعالى):
Kuanzia Aayah hii (16:5) hadi (16), Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja baadhi ya Neema Zake. Hali kadhaalika katika Suwrah hii Neema nyenginezo za Allaah (سبحانه وتعالى) zimetajwa katika Aayah, (65-69), (72), (80-81). Na Suwrah hii inajulikana pia kama ni Suwrah ya Neema. Rejea pia Al-Muuminuwn (23:17). Rejea pia Ibraahiym (14:34) kwenye uchambuzi wa Neema za Allaah.
[3] Neema Ya Maji Na Hewa:
Miongoni mwa neema kubwa humo ni vitu viwili ambavyo mwanaadam hawezi kuishi bila ya uwepo wake. Allaah (عزّ وجلّ) Amevijaalia vitu hivi viwili vipatikane bure, kwa maana hata masikini aweze kuvipata! Navyo ni hewa tunayovutia pumzi, na maji Anayoyateremsha Allaah (سبحانه وتعالى) kutoka mbinguni kama mvua kwa ajili ya kunywa na kuotesha mimea na matumizi mengineyo yaliyo muhimu kwa binaadam. Na pia maji yanayopatikana katika tumbo la ardhi, baharini, kwenye maziwa na katika mito.
[4] Nyota Zimeumbwa Kwa Ajili Ya Mambo Matatu:
Rejea Al-An’aam (6:97), Asw-Swaaffaat (37:10), Al-Mulk (67:5).
[5] Neema Za Allaah (سبحانه وتعالى) Haiwezekani Kuzihesabu Zote:
Aayah kama hii imekariri katika Suwrah Ibraahiym (14:34). Rejea humo ambako kuna uchambuzi wa Neema za Allaah.
[6] Twaghuti: Rejea Al-Baqarah (2:256), An-Nisaa (4:51).
[7] Zingatio Na Tahadharisho Kwa Makafiri Watembee Maeneo Mbalimbali Ya Ardhi:
Zingatio na tahadharisho hili ili wapate kujionea wenyewe, na wapate kutambua hatima mbaya za waliokadhibisha kabla yao. Rejea Aal-‘Imraan (3:137).
[8] Ahl Adh-Dhikr "أَهْلُ الذِّكْرِ" (Watu wa Ukumbusho):
Ni watu waliopewa Vitabu Nyuma. Ni watu wenye ilimu ambao wameteremshiwa Vitabu na hoja bayana [Tafsiyr As-Sa’diy] (kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah inayofuatia).
[9] Kila Kitu Kinamsujudia Allaah (عزّ وجلّ):
Aayah hii namba (48) na inayofuatia (49) inataja viumbe na vitu kumsujudia Allaah. Rejea pia Ar-Rahmaan (55:6) kwenye rejea nyenginezo zinazotaja viumbe na vitu Alivyoviumba Allaah kuwa vinamsujudia Yeye Allaah (عزّ وجلّ).
[10] Uthibitisho Kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Yuko Juu Ya Viumbe Vyake Vyote:
Hao Malaika wanamuogopa Rabb wao Ambaye Yuko juu yao kwa Dhati Yake, utendeshaji nguvu Wake na ukamilifu wa Sifa Zake na wanafanya anayoamrishwa ya kumtii Allaah (سبحانه وتعالى). Katika Aayah hii, pana kuthibitisha sifa ya kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Yuko juu ya viumbe Vyake vyote, kama inavyonasibiana na Utukufu Wake na ukamilifu Wake. [Tafsiyr Al-Muyassar] Rejea pia Al-A’raaf (7:54) na Al-Mulk (67:16).
[11] (تَاللَّهِ) Ta-Allaahi, (وَاللَّهِ) Wa-Allaahi, (بِاللَّهِ) Bi-Llaahi, Ni Kuapa Kwa Jina La Allaah:
Ni Neno la kuapia kwa Jina la Allaah. Herufi tatu zinatumika kuapia kwa namna hii ambazo ni “Waaw” (الواو), “Baa” (الباء) na “Taa” (التاء). Wa-Allaahi, Bi-Llaahi, na Ta-Allaahi,. Na yote ina maana moja ya (Naapa kwa Allaah). Ta-Allaahi imekariri mara kadhaa katika Suwrah Yuwsuf (12:73), (12:5), (12:91), (12:95).
[12] Washirikina Waliwachukia Watoto Wa Kike Lakini Wakimsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwa Ana Mabinti!
Katika Aayah hii ya An-Nahl (57 hadi 59), washirikina wamemsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa Ana watoto wa kike ilhali wao wenyewe waliwachukia wakawa wanawazika wazima wazima pindi wanapozaliwa. Rejea: At-Takwiyr (81:8-9), Asw-Swaaffaat (37:149-153), Al-Israa (17:40) na Az-Zukhruf (43:15-19).
[13] Ta-Allaahi: Neno La Kuapia Kwa Jina La Allaah. Rejea Aayah (16:56).
[14] Ulevi, Pombe Vimeharamishwa: Rejea Al-Maaidah (5:90).
Aayah hiyo tukufu inamaanisha kuwa juisi ya matunda ya mitende na mizabibu ina vitu viwili: Moja ni kile ambacho ni chakula safi na chenye afya kwa mwanaadam. Na kingine ni kile kinachogeuka kuwa ulevi baada ya kuchachuka. Lakini katika Aayah hiyo, ulevi, pombe ilikuwa kabla ya kuharamishwa kwake. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akaharamsiha ulevi, pombe na Akabadilisha kwa twayyibaat (vilivyo halali vizuri) kama nabiydh ambayo ni ulowekaji wa zabibu, tende, asali, ngano na shayiri na kunywa kinywaji chake kabla ya kuchachuka. Na kuchachuka kikawaida kunatokea baada ya siku tatu kama ilivyothibiti katika Hadiyth:
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akilowekewa zabibu akawa anakunywa maji yake siku hiyo na kesho yake na siku inayofuatia hadi jioni ya siku ya tatu. Kisha aliamuru inywewe (kabla ya kumalizika siku) au imwagwe. [Muslim]
Inapochachuka haifai kuinywa kwa sababu hugeuka ulevi au pombe na hapo inakuwa haramu.
Amesimulia ‘Aaishah: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kila kinywaji kinacholevya ni haramu.” [Al-Bukhaariy]
[16] Hoja Na Dalili Ya Wazi Kuwa Kusimamisha Saa (Qiyaamah) Ni Jambo Jepesi Mno Kwa Allaah (سبحانه وتعالى). Na Kwamba Watu Watafufuliwa:
Rejea Al-An’aam (6:158), Ash-Shuwraa (42:17-18), Al-Israa (17:49), Ghaafir (40:59).
[17] Kila Ummah Utahuduhurishwa Na Shahidi Wake:
Rejea Al-Baqarah (2:143), An-Nisaa (4:41), Al-Israa (17:71), Al-Hajj (22:78), Az-Zumar (39:69), Al-Jaathiyah (45:28).
[18] Maana Ya Baghyun/Baghaa Katika Qur-aan:
Rejea Ash-Shuwraa (42:14) kupata maana zake mbalimbali.
[19] Kutimiza Ahadi Na Mfano Wa Anayetimiza Ahadi Kisha Akabatilisha Ni Kama Aliyesokota Uzi Kisha Akauzongoa.
Allaah (سبحانه وتعالى) Anapiga mfano wa mwanamke aliyekuwa Makkah ambaye alikuwa kila alipousokota uzi wake kwa juhudi, alirudi kuufumua na kuuzongoa ukarudi kama ulivyokuwa. Mfano huu ni kama Muumini anayefunga ahadi na viapo kisha akavivunja bila kujali. Na Aayah hii inahusiana na Aayah mbili zilizotangulia (90-91). Inamaanisha kuwa mtu asije kuvunja ahadi inayofungamana kati yake na Rabb wake, amtii na atekeleze yote Anayoamrisha, na afanye wema na ihsaan baina yake na watu. Kadhalika, ajiepushe na maharamisho yote, ajiepushe na shirki, ajitahidi awezavyo kutimiza viapo na nadhiri, na achunge ahadi au mkataba aliowekeana na mtu mwingine kwa mujibu wa Kitabu na Sunnah. Hivyo basi, asije mtu akabatilisha viapo na ahadi zilizo baina yake na Rabb wake, au baina yake na mtu mwengine.
Kutimiza ahadi ni sifa mojawapo inayoweza kumpatia mtu kuingizwa katika Jannatul-Firdaw kama Alivyoeleza Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwrah Al-Muuminuwn (23:1-11) na Al-Ma’aarij (7:23-35).
Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameonya kuwa kuvunja ahadi ni katika sifa ya unafiki: Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Alama za mnafiki ni tatu: Anapozungumza husema uongo, anapotoa ahadi hukhalifu (hatimizi), na anapoaminiwa hufanya khiyana.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
[20] Kuteleza Mguu Baada Ya Kuthibitika Kwake:
Wala msivifanye viapo mnavyoviapa kuwa ndio njia ya kuwahadaa, kuwadanganya au kuwatapeli wale mliowaapia, mkaja kuangamia baada ya kuwa (mlithibitika) kwenye amani. Ni kama yule ambaye nyayo zake ziliteleza baada ya kuwa zimekita. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Wala msivichukulie viapo vyenu, ahadi zenu na mafungamano yenu kwa kufuata matamanio yenu; mnapotaka mnatimiza na mnapotaka mnazivunja. Basi mkifanya hivyo (kwa kutowajibika ipasavyo na hayo), miguu yenu itateleza baada ya kuwa imethibitika katika njia iliyonyooka. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Maana Ya Kuzuia Njia Ya Allaah:
Kafiri aliyekaribia kuingia Uislamu, akaja kuona tabia mbaya za baadhi ya Waislamu kama hiyo ya viapo vya udanganyifu zikamchukiza, huyo hatouthamini tena Uislamu, kwa kuona kuwa hakuna tofauti kubwa kati ya Waislamu na makafiri katika maadili na muamala wao. Na kwa tabia hiyo na mambo mengineyo ya ovyo yanayofanywa na baadhi ya Waislamu, inakuwa ni sababu ya kuwakimbiza wasio Waislamu kuingia kwenye Uislamu. Dini ni muamala mwema.
[21] Hayaatan Twayyibah (Uhai Au Maisha Mazuri):
Uhai au maisha mazuri haimaanishi mtu kuwa na utajiri wa mali na watoto, au siha nzuri, au maisha yaliyomjalia mafao na starehe. Bali uhai mzuri ni utulivu wa moyo na nafsi ya Muumini katika yote ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Amemkadiria na Kumjaalia, naye akaridhika nayo, na akawa na imaan thabiti bila kutetereka na mambo ya kidunia yanayomsibu. Mfano ni Muumini maskini anayepatwa na mitihani na maradhi, lakini akaridhika na Majaaliwa hayo kutoka kwa Rabb wake, na akaendelea kuishi kwa utulivu katika maisha yake kwa kuridhika na kushikamana na imaan thabiti. Hakufuru wala hapunguzi imaan yake kwa sababu ya mitihani aliyojaaliwa. Kinyume chake ni watu wengi ambao wako katika maisha ya utajiri, mali, watoto, raha, siha, na nguvu za miili, lakini watu hao wana dhiki za moyo za kuyafanya maisha yao kuwa ya dhiki tupu! Basi hao ndio ambao hawana maisha au uhai mzuri.
[22] Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Dhidi Ya Shaytwaan Unapoanza Kusoma Qur-aan:
Inapaswa kusema:
أَعـوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّيْـطانِ الرَّجيـم
Najikinga kwa Allaah dhidi ya shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa.
[23] Hukmu Ya An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa):
Rejea Al-Baqarah (2:106). Na bonyeza kiungo kifuatacho:
An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa) [23]
[27] Neno La أُمَّةً Katika Qur-aan Lina Maana Kadhaa:
Maana zake mbali mbali na baadhi ya Aayah zinazothibitisha maana zake:
(i) Umati wa watu; Rejea Al-Qaswasw (28:23), Al-A’raaf (7:164). (ii) Nyumati za karne zilizopita; Rejea Yuwnus (10:47), An-Nahl (16: 36). (iii) Mtu mwongofu au kiongozi mwenye taqwa na maadili na tabia njema; Rejea Al-Baqarah (2:124), na pia Aayah hii inayomkusudia Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام). (iv) Muda au kipindi fulani au zama; Rejea Huwd (11:8], Yuwsuf (12:45). (v) Sharia, Dini, manhaj au mila inayofuatwa; Rejea Az-Zukhruf (43:22-23).
[28] Fadhila Na Sifa Za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام):
Katika Aayah (120-123) za Suwrah hii An-Nahl, Allaah (سبحانه وتعالى) Amemsifia Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) kwa sifa zifuatazo: Mwenye akhlaaq na maadili yote mema, mtiifu, Haniyfah (ameelemea katika haki), hakuwa katika washirikina, mwenye kushukuru Neema za Allaah (سبحانه وتعالى), mwongofu na miongoni mwa Swalihina.
Na katika Suwrah nyenginezo, Allaah (سبحانه وتعالى) Amemsifia pia kwa sifa nyenginezo mbalimbali na Akamjaalia kuwa na fadhila tele.
Miongoni Mwa Fadhila Za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام):
(i) Allaah (سبحانه وتعالى) Amemteua yeye Nabiy Ibraahiym na mwanawe Nabiy Ismaa’iyl (عليهما السّلام) waijenge Al-Ka’bah. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akamteua Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) awatangazie watu kwenda kutekeleza Hajj. Hivyo basi, akawa yeye (عليه السّلام) na ahli wake ni mwongozo kwa watu katika utekelezaji wa manaasik (ibaada na taratibu) za Hajj na ‘Umrah. Rejea Al-Hajj (22:26-37). Na miongoni mwa manaasik hizo, ni kuswali katika Maqaam Ibraahiym baada ya kutufu Al-Ka’bah. Rejea Al-Baqarah (2:125). Pia, kusai baina ya Swafaa na Marwah, rejea Al-Baqarah (2:158) kama ni kigezo cha mkewe Haajar alipokuwa akihangaika kumtafutia maji mwanawe Ismaa’iyl (عليه السّلام). Na huko ndiko palipotokea mbubujiko wa maji ya Zamzam ambayo watu wanakunywa kwa niya tofauti kama alivyogusia hilo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Pia kuchinja mnyama baada ya yeye kupewa mtihani au majaribio makubwa, pindi alipoona njozini kuwa anamchinja mwanawe, naye kutokana na utiifu wake, akataka kutekeleza njozi hiyo akiamini kuwa ni Amri ya Allaah (سبحانه وتعالى). Lakini kumbe ilikuwa ni mtihani na jaribio, hivyo akafaulu katika hili, na hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akambadilishia kwa kumteremshia kondoo kutoka mbinguni ili amchinje badala ya mwanawe. Rejea Asw-Swaaffaat (37:101-107). Pia kutupia vijiwe Jamaraat ambayo ni katika waajibaat za Hajji na Sunnah zake nyenginezo.
(ii) Ni kipenzi cha Allaah. Rejea An-Nisaa (4:125).
(iii) Ameitwa Baba wa Manabii: Kama ilivyokuwa hali ya Nabiy Nuwh (عليه السّلام): Al-‘Ankabuwt (29:27). Na katika Al-Hadiyd (57:26), ametajwa yeye Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) pekee kuwa amejaaliwa kuwa na Unabii na kupewa Kitabu.
Imaam Ibn Kathiyr amesema kuhusu Aayah ya Suwrah Al-‘Ankabuwt: “Hii ni fadhila na baraka kubwa sana. Sio tu kwamba Allaah Alimfanya (Nabiy Ibraahiym) kuwa ni kipenzi Chake na kumfanya Imaam wa watu, bali pia Alijaalia Unabii na Kitabu kuwa katika dhuriya zake. Baada ya zama za Ibraahiym, hapakuwa na Nabii ambaye hakutokana na kizazi chake. Manabii wote wa Wana wa Israaiyl (Ya’quwb) walikuwa katika kizazi chake, kuanzia Ya’quwb bin Is-haaq bin Ibraahiym hadi wa mwisho wao, `Iysa bin Maryam, ambaye alisimama kuwatangazia kaumu yake, bishara ya kuja kwa Nabii Mwarabu, Al-Qurashiy, Al-Haashimiy, Nabii wa mwisho wa Manabii wote, bwana wa wana wa Aadam katika dunia hii na Aakhirah, ambaye Allaah Alimteua kutoka kwa Waarabu safi wa asili kutoka kwa kizazi cha Ismaa’iyl bin Ibraahiym (عليهما السلام). Hakuna Nabii yeyote katika ukoo wa Ismaa’iyl isipokuwa yeye Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
(iv) Ameomba duaa kizazi chake kitoe Nabii wa mwisho; Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) baada ya kujenga Al-Ka’bah. Rejea (2:129).
(v) Ibraahiym (عليه السّلام) ni Imaam wa Tawhiyd:
Allaah (سبحانه وتعالى) Amemfanya kuwa ni Imaam wa watu wa kufuatwa katika Tawhiyd. Rejea Al-Baqarah (2:124). Na pia Ummah umeusiwa kufuata mila yake. Rejea Al-Baqarah (2:135), Aal-‘Imraan (3:95), An-Nisaa (4:125), Al-An’aam (6:161), na An-Nahl (16:123). Na pia, Amewausia wanawe na kizazi chake Uislamu. Rejea Al-Baqarah (2:130-132). Na pia Amefanya neno la Tawhiyd (laa ilaaha illa-Allaah) lenye kubakia katika kizazi chake. Rejea Az-Zukhruf (43:28). Ingawa Rusuli wengineo wote wamekuja pia katika kulingania Tawhiyd, ila Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) amekuwa ni makhsusi kwa Tawhiyd. Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله) amesema alipoulizwa:
Kwa nini Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) amehusishwa zaidi na Tawhiyd, ilhali Manabii wote wengineo wamelingania Tawhiyd?
Akajibu: Manabii wote wamekuja na (kulingania) Tawhiyd. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ ﴿٢٥﴾
“Na Hatukutuma kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Rasuli yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: Hakika hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, basi Niabuduni.” [Al-Anbiyaa (21:25)]
Lakini Ibraahiym ni baba wa Waarabu, na baba wa Waisrael, naye amelingania Tawhiyd khalisi, na Mayahudi na Manaswara wamedai kuwa ni wafuasi wake, na Waislamu ndio wafuasi wake. Kwa hiyo yeye (عليه السّلام) akahusishwa kuwa ni baba wa Manabii, na kwamba yeye ndiye mwenye Haniyfiyyah (sifa ya kuelemea haki na kujiweka kando na shirki). Na sisi tumeamrishwa kumfuata, kwa sababu sisi ndio tulio karibu zaidi Ibraahiym kama Anavyosema Allaah (عزّ وجلّ):
إِنَّ أَوْلَى النَّاسِ بِإِبْرَاهِيمَ لَلَّذِينَ اتَّبَعُوهُ وَهَـٰذَا النَّبِيُّ وَالَّذِينَ آمَنُوا ۗ وَاللَّـهُ وَلِيُّ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٦٨﴾
“Hakika watu walio karibu zaidi kwa Ibraahiym ni wale waliomfuata na huyu Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na wale walioamini. Na Allaah Ni Mlinzi wa Waumini.” [Aal-‘Imraan (3:68)]
Na Akasema kuwaradi Mayahudi na Manaswaara:
مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَـٰكِن كَانَ حَنِيفًا مُّسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٦٧﴾
“Ibraahiym hakuwa Yahudi wala Naswara, lakini alikuwa mwenye kujiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki, Muislamu na hakuwa miongoni mwa washirikina.” [Aal-‘Imraan (3:67)]
[Liqaa-a Al-Baab Al-Maftuwh Swali namba (7/189).
(vi) Anatajwa katika kila Swalaah, kwenye Tashahhud, kwa Swalaah inayojulikana kama Swalaatul-Ibraahiymiyyah.
Na fadhila hii tukufu ni kutokana na sababu zilizotangulia kutajwa juu na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn. Pia kutokana na sababu zifuatazo kama walivyosema ‘Ulamaa: Kwamba (عليه السّلام) Ibraahiym ni babu (kizazi kilichoanzia kwa Ismaaiyl) wa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).
Na ‘Allaamah Badr Ad-Diyn Al-Hanafiy (رحمه الله) ana maelezo mengineyo katika kubainisha sababu ya hili. Amesema: “Ikiwa mtu atauliza: Kwa nini Ibraahiym (عليه السّلام) ameteuliwa yeye pekee kutajwa katika Swalaah badala ya Manabii wengine (عليهم السّلام)?
Nitajibu: Kwa sababu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaona katika usiku wa Mi’iraaj, Manabii na Rusuli wote, na akamtolea Salaam kila Nabii, na hakuna hata mmoja wao aliyesalimia ummah wake isipokuwa Ibraahiym (عليه السّلام) . Hivyo basi, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ametuamrisha tumswalie kila mwisho wa Swalaah mpaka Siku ya Qiyaamah, kama malipo ya wema wake. Na imesemwa: Ibraahiym (عليه السّلام) alipomaliza kuijenga Al-Ka’bah, aliuombea Ummah wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: Ee Allaah! Atakayehiji Nyumba hii miongoni mwa Ummah wa Muhammad, basi Mpe amani kutoka kwangu. Pia akawaombea ahli zake na watoto wake kwa duaa hii. Hivyo basi tukaamrishwa tuwakumbuke katika Swalaah kama malipo ya wema wao.” Mwisho. Ufafanuzi wa Sunan Abi Daawuwd cha Al-‘Ayniy (4/260). Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.
(vii) Kizazi chake kimepewa ufalme mkubwa: An-Nisaa (4:54).
(viii) Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimkuta mbingu ya saba akielemea Bayt Al-Ma’muwr inayozungukwa na Malaika elfu sabiini. (Haya yapo katika Hadiyth ndefu iliyopokelewa na Imaam Muslim katika Kitaab Al-Iymaan, na wengineo).
(ix) Alijaaliwa Ar-Rushd (Uongofu) na Allaah (سبحانه وتعالى) Alimjua vyema: Al-Anbiyaa (21:51).
(x) Ni Nabii ambaye amemshabihi Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم): Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) [Al-Bukhaariy, Muslim]
(xi) Ni miongoni mwa Rusuli watano wa Ulul-‘Azmi: Al-Ahzaab (33:7).
(xii) Amewaombea Waislamu wawe wenye kuelekeza nyoyo zao kuipenda Makkah na Al-Ka’bah. Ibraahiym (14:37).
(xiii) Amewaombea duaa kizazi chake wasimamishe Swalaah, na Amewaombea Waumini maghfirah Siku ya Hesabu. Ibraahiym (14:40-41).
(xiv) Atakuwa wa kwanza kuvalishwa nguo baada ya kufufuliwa kutokana na vile washirikina katika kaumu yake walivyomuingiza motoni akiwa uchi baada ya kuvunja masanamu yao. Yapo haya kwenye Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما):
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Enyi watu, hakika mtafufuliwa na Allaah hali ya kuwa hamna viatu, mpo uchi na bila kutahiriwa (na magovi). ”Kisha akasoma:
كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُ ۚ
“Kama Tulivyoanza umbo la awali Tutalirudisha tena.” [Al-Anbiyaa (21:104)]
Tanabahini! Hakika mtu wa kwanza atakayevishwa nguo ni Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام). [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na ‘Ulamaa wameeleza pia kuwa sababu ya kutangulizwa Ibraahiym kuvishwa nguo Siku ya Qiyaamah kabla ya wengine ni kuwa hapakuweko miongoni mwa watu wa mwanzo na wa baadae, waliomkhofu zaidi Allaah kuliko yeye. Hivyo basi, nguo zitamharakia ili kumhifadhi, na moyo wake upate kutulia.
Na sababu nyingine -kama ilivyoeleza Hadiyth- ni kuwa, inawezekana kwamba yeye alikuwa ni wa kwanza kuvaa suruali wakati anaposwali ili kupata sitara ya ziada isiyo na shaka na kulinda tupu yake isigusane na sehemu yake ya kuswalia, naye akafanya kama alivyoamrishwa, na akalipwa hilo kuwa wa kwanza kusitiriwa Siku ya Qiyaamah.
Kadhalika, inawezekana kuwa wale waliomtupa motoni, walimwacha uchi na wakamvua nguo zote mbele ya watu kama anavyofanywa mtu anayetekelezewa adhabu ya kifo. Hivyo atalipwa nguo zake Siku ya Qiyaamah, na atakuwa mtu wa kwanza kuvaa mbele ya halaiki, na haya ni malipo mazuri zaidi. [Al-Qurtwubiy katika At-Tadhkirah]
(xv) Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema kwamba yeye ni kiumbe bora kabisa: Amesimulia Anas bin Maalik (رضي الله عنه): Alikuja mtu mmoja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Ee kiumbe bora kabisa!” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamjibu: “Huyo ni Ibraahiym (عليه السّلام). [Muslim]
Sifa Za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام):
(i) Hakuwa mshirikina kabisa. Ametajwa kwa sifa hii katika Suwrah kadhaa kwenye Qur-aan ikiwemo Suwrah hii An-Nahl (16:120). Pia, kisa chake katika Al-An’aam (6:74-81) cha kutokuabudu nyota wala mwezi wala jua kinathibitisha sifa hii. Kadhalika, alimuomba Allaah Amuepusha yeye na wanawe wasiwe washirikina: Ibraahiym (14:35). Isitoshe, alimnasihi baba yake pia asiwe mshirikina lakini hakumsikiliza bali alimfukuzilia mbali: Maryam (19:41-48) na Ash-Shu’araa (26:69-89).
(ii) Alikuwa ni mtimizaji ahadi: An-Najm (53:37).
(iii) Ni mwenye huruma mno na mvumilivu: At-Tawbah (9:114).
(iv) Ni mvumilivu sana, mnyenyekevu mno kwa Allaah, na mwingi wa kurejea Kwake. Huwd (11:75).
(v) Mkarimu mno: Huwd (11:69), na Adh-Dhaariyaat (51:24-26).
(vi) Mwenye utukufu: Rejea Tanbihi namba 1 ya Aayah namba (4) katika Suwrah Yuwsuf.
(vii) Mnyeyekevu, kwani aliomba duaa baada ya kujenga Al-Ka’bah: Al-Baqarah (2:128). Al-Ka’bah ni Nyumba Tukufu kabisa katika Vitukufu vya Allaah katika Mji Mtukufu kabisa. Lakini juu ya utukufu huu, alikuwa na wasiwasi juu ya kutaqabaliwa kitendo hiki, kwa maana hakuwa na kibri kuwa madamu amejenga kitu kitukufu kabisa cha Allaah, basi awe amesifika au ni mtu bora kabisa.
(viii) Ana kisa muhimu cha uthibitisho wa Tawhiyd iliyojikita moyoni mwake wakati alipoingizwa motoni na watu wake kwa sababu aliyavunja masanamu waliyokuwa wakiyaabudu: Al-Anbiyaa (21:51-70), na Asw-Swaaffaat (37:83-99).
(ix) Mwenye moyo uliosalimika: Asw-Swaaffaat (37:84).
(x) Swiddiyq (mkweli wa kidhati): Maryam (19:41).
(xi) Mwenye akhlaaq na mfano wa maadili mema: Al-Mumtahinah (60:4).
(xii) Amekhitariwa duniani, na Aakhirah ni miongoni mwa Swalihina: Al-Baqarah (2:130).
(xiii) Mwenye nguvu na busara: Swaad (38:45). Na katika busara zake, alimwambia mwanawe Ismaa’iyl abadilishe kizingiti chake badala ya kumwambia moja kwa moja “mwache mkeo.” Hii ni kutokana na malalamiko ya mke huyo kuhusu maisha yao na shida zao. Kisha akamtaka athibitishe kizingiti chake, akimaanisha aendeleze ndoa yake na mkewe mwengine (asimtaliki), mke wa pili ambaye hakulalamika shida zao za kimaisha. Maelezo ya hili yapo katika Hadiyth ndefu ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) iliyopokelewa na Al-Bukhaariy, Kitaab Ahaadiyth Al-Anbiyaa.
Pia katika busara zake ni kumtaka mfalme Namruwd aliyejifanya kuwa yeye ni Mola na mwabudiwa, alichomoze jua kutoka Magharibi badala ya Mashariki, lakini mfalme huyo akabakia kinywa wazi ameduwaa. Rejea Al-Baqarah (2:258) kwenye maelezo bayana katika faida ya Aayah hiyo.
Pia katika busara yake nyengineyo ni vile alivyovunja masanamu kisha akatundika shoka ya sanamu lilokuwa kubwa lao. Kaumu yake walipomuuliza nani aliyevunja masanamu yetu, alijibu: “Waulizeni wakiwa wanaweza kunena!” Akikusudia pia kama kweli wanastahiki kuabudiwa ikiwa hawawezi kujihami wenyewe kusingiziwa uvunjaji wa masanamu yao. Rejea Al-Anbiyaa (21:57-63), na Asw-Swaafaat (37:88-96)
(xiv) Alikhofia familia yake wasije kuabudu masanamu. Naye mwenyewe tokea utotoni alichukia ibaada ya shirki na masanamu. Na alikhiari Dini kuliko dunia, napo ni pale alipowaacha familia yake katika bonde la Makkah ambako hapakuwa na chochote, na alitaja sababu yake kuwa ili wasimamishe Swalaah: Ibraahiym (14:35-37).
Hizo ni baadhi ya fadhila na sifa za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) , na bila shaka zinapatikana nyenginezo katika Kitabu na Sunnah.
[29] As-Sabt: Rejea Al-Baqarah (2:65).
الإِسْرَاء
017-Al-Israa
017-Al-Israa: Utangulizi Wa Suwrah [170]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَىٰ بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿١﴾
1. Utakasifu ni wa Ambaye Amemsafirisha usiku Mja Wake kutoka Al-Masjid Al-Haraam mpaka Al-Masjid Al-Aqswaa ambao Tumebariki pembezoni mwake, ili Tumuonyeshe baadhi ya Aayaat (Ishara) Zetu (kubwa mno)[1] Hakika Yeye (Allaah) Ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.
وَآتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَجَعَلْنَاهُ هُدًى لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ أَلَّا تَتَّخِذُوا مِن دُونِي وَكِيلًا ﴿٢﴾
2. Na Tumempa Muwsaa Kitabu na Tukakifanya mwongozo kwa wana wa Israaiyl kwamba: Msimfanye yeyote badala Yangu kuwa ni mtegemewa.
ذُرِّيَّةَ مَنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَبْدًا شَكُورًا ﴿٣﴾
3. Enyi kizazi cha ambao Tuliwabeba pamoja na Nuwh (katika jahazi).[2] Hakika yeye alikuwa mja mwingi wa shukurani.
وَقَضَيْنَا إِلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ فِي الْكِتَابِ لَتُفْسِدُنَّ فِي الْأَرْضِ مَرَّتَيْنِ وَلَتَعْلُنَّ عُلُوًّا كَبِيرًا ﴿٤﴾
4. Na Tuliwajulisha wana wa Israaiyl katika Kitabu kwamba: Bila shaka mtafanya ufisadi katika ardhi mara mbili, na kwa hakika mtapanda kiburi cha dhulma na kutakabari kukubwa.
فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ أُولَاهُمَا بَعَثْنَا عَلَيْكُمْ عِبَادًا لَّنَا أُولِي بَأْسٍ شَدِيدٍ فَجَاسُوا خِلَالَ الدِّيَارِ ۚ وَكَانَ وَعْدًا مَّفْعُولًا ﴿٥﴾
5. Basi utakapowadia wakati wa mara ya kwanza yao (fisadi mbili) Tutakutumieni Waja Wetu wenye nguvu kali za kupigana vita, waingie kusaka nyumba kwa nyumba.[3] Na hii ni ahadi, lazima itekelezwe.
ثُمَّ رَدَدْنَا لَكُمُ الْكَرَّةَ عَلَيْهِمْ وَأَمْدَدْنَاكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَجَعَلْنَاكُمْ أَكْثَرَ نَفِيرًا ﴿٦﴾
6. Kisha Tukakurudishieni nguvu zenu dhidi yao, na Tukakuongezeeni mali na wana, na Tukakufanyeni wengi zaidi kwa idadi na nguvu.
إِنْ أَحْسَنتُمْ أَحْسَنتُمْ لِأَنفُسِكُمْ ۖ وَإِنْ أَسَأْتُمْ فَلَهَا ۚ فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ لِيَسُوءُوا وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِيرًا ﴿٧﴾
7. (Na Tukasema): Mkifanya ihsaan basi mnanjifanyia ihsaan kwa ajili ya nafsi zenu wenyewe, na mkifanya uovu, basi hasara ni juu yake. Na utakapowadia wakati wa mara ya pili, (Tutakutumieni tena maadui) ili wadhalilishe nyuso zenu, na ili waingie Msikitini (Bayt Al-Maqdis) kama walivyouingia mara ya kwanza, na ili wateketeze kila walichokiteka kwa mateketezo makubwa.
عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يَرْحَمَكُمْ ۚ وَإِنْ عُدتُّمْ عُدْنَا ۘ وَجَعَلْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَافِرِينَ حَصِيرًا ﴿٨﴾
8. Asaa Rabb wenu Akakurehemuni. Na mkirudi (kwenye ufisadi na dhulma), Nasi Tutarudi (kukuadhibuni). Na Tumeifanya Jahannam kwa makafiri kuwa ni gereza.
إِنَّ هَـٰذَا الْقُرْآنَ يَهْدِي لِلَّتِي هِيَ أَقْوَمُ وَيُبَشِّرُ الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا كَبِيرًا ﴿٩﴾
9. Hakika hii Qur-aan inaongoza katika yaliyonyooka kabisa,[4] na inawabashiria Waumini wanaotenda mema kwamba watapata ujira mkubwa.
وَأَنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ أَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٠﴾
10. Na kwamba wale wasioamini Aakhirah Tumewaandalia adhabu iumizayo.
وَيَدْعُ الْإِنسَانُ بِالشَّرِّ دُعَاءَهُ بِالْخَيْرِ ۖ وَكَانَ الْإِنسَانُ عَجُولًا ﴿١١﴾
11. Na binaadam huomba shari kama vile aombavyo kheri. Na binaadam ni mwenye pupa mno.
وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ آيَتَيْنِ ۖ فَمَحَوْنَا آيَةَ اللَّيْلِ وَجَعَلْنَا آيَةَ النَّهَارِ مُبْصِرَةً لِّتَبْتَغُوا فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ وَلِتَعْلَمُوا عَدَدَ السِّنِينَ وَالْحِسَابَ ۚ وَكُلَّ شَيْءٍ فَصَّلْنَاهُ تَفْصِيلًا ﴿١٢﴾
12. Na Tumejaalia usiku na mchana kuwa ni Aayah (Ishara, Alama) mbili. Tukafuta Aayah ya usiku na Tukajaalia Aayah ya mchana kuwa ni ya mwangaza ili mtafute Fadhila kutoka kwa Rabb wenu, na ili mjue idadi ya miaka na hesabu (nyinginezo). Na kila kitu Tumekifasili tafsili ya waziwazi kabisa.
وَكُلَّ إِنسَانٍ أَلْزَمْنَاهُ طَائِرَهُ فِي عُنُقِهِ ۖ وَنُخْرِجُ لَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ كِتَابًا يَلْقَاهُ مَنشُورًا ﴿١٣﴾
13. Na kila binaadam Tumemuambatanishia amali zake alizokadariwa (kuzitenda) shingoni mwake. Na Tutamtolea Siku ya Qiyaamah kitabu akikute kimekunjuliwa.[5]
اقْرَأْ كِتَابَكَ كَفَىٰ بِنَفْسِكَ الْيَوْمَ عَلَيْكَ حَسِيبًا ﴿١٤﴾
14. (Ataambiwa): Soma kitabu chako! Nafsi yako inakutosheleza leo kukuhesabu.[6]
مَّنِ اهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِي لِنَفْسِهِ ۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَا ۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۗ وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبْعَثَ رَسُولًا ﴿١٥﴾
15. Anayehidika, basi anahidika kwa manufaa ya nafsi yake. Na anayepotoka, basi anapotoka kwa hasara yake. Na wala mbebaji (wa dhambi) hatobeba mzigo wa mwengine. Na Hatukuwa Wenye Kuadhibu mpaka Tupeleke Rasuli.
وَإِذَا أَرَدْنَا أَن نُّهْلِكَ قَرْيَةً أَمَرْنَا مُتْرَفِيهَا فَفَسَقُوا فِيهَا فَحَقَّ عَلَيْهَا الْقَوْلُ فَدَمَّرْنَاهَا تَدْمِيرًا ﴿١٦﴾
16. Na Tunapotaka kuangamiza mji, Tunawaamrisha wastareheshwa wake wa anasa za dunia, nao wakaendelea kufanya ufasiki humo, na hapo ikastahiki juu yake kauli (ya adhabu), kisha hapo Tunaudamirisha kwa mateketezo makubwa.
وَكَمْ أَهْلَكْنَا مِنَ الْقُرُونِ مِن بَعْدِ نُوحٍ ۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ بِذُنُوبِ عِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا ﴿١٧﴾
17. Ni nyumati nyingi sana Tumeziangamiza baada ya Nuwh. Na Rabb wako Anatosheleza kabisa Kuwa Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri, Mwenye Kuona dhambi za Waja Wake.
مَّن كَانَ يُرِيدُ الْعَاجِلَةَ عَجَّلْنَا لَهُ فِيهَا مَا نَشَاءُ لِمَن نُّرِيدُ ثُمَّ جَعَلْنَا لَهُ جَهَنَّمَ يَصْلَاهَا مَذْمُومًا مَّدْحُورًا ﴿١٨﴾
18. Yeyote anayetaka (starehe za dunia) ipitayo upesi upesi Tunamharakizia humo Tuyatakayo, kwa Tumtakaye. Kisha Tutamjaalia Jahannam aingie na kuungua hali ya kuwa mwenye kushutumiwa na kufukuziliwa mbali.
وَمَنْ أَرَادَ الْآخِرَةَ وَسَعَىٰ لَهَا سَعْيَهَا وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ كَانَ سَعْيُهُم مَّشْكُورًا ﴿١٩﴾
19. Na anayetaka Aakhirah na akaifanyia juhudi inayostahiki kufanyiwa, naye ni Muumin, basi hao juhudi zao ni za kushukuriwa.[7]
كُلًّا نُّمِدُّ هَـٰؤُلَاءِ وَهَـٰؤُلَاءِ مِنْ عَطَاءِ رَبِّكَ ۚ وَمَا كَانَ عَطَاءُ رَبِّكَ مَحْظُورًا ﴿٢٠﴾
20. Wote hao Tunawakunjulia - hawa na hao - katika Hiba za Rabb wako. Na hazikuwa Hiba za Rabb wako zenye kuzuiliwa.
انظُرْ كَيْفَ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ وَلَلْآخِرَةُ أَكْبَرُ دَرَجَاتٍ وَأَكْبَرُ تَفْضِيلًا ﴿٢١﴾
21. Tazama vipi Tulivyowafadhilisha baadhi yao juu ya wengineo. Na bila shaka Aakhirah ni yenye daraja kubwa zaidi na fadhila kubwa zaidi.
لَّا تَجْعَلْ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتَقْعُدَ مَذْمُومًا مَّخْذُولًا ﴿٢٢﴾
22. Usifanye pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine, ukaja kushutumiwa na kutelekezwa mbali (motoni).[8]
وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا ﴿٢٣﴾
23. Na Rabb wako Ameamuru kwamba: Msiabudu isipokuwa Yeye Pekee na kuwafanyia ihsaan wazazi wawili.[9] Kama mmoja wao akifikia uzee naye yuko pamoja nawe, au wote wawili basi usiwaambie, Uff![10] Na wala usiwakemee, na waambie maneno ya heshima.
وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا ﴿٢٤﴾
24. Na wainamishie bawa la unyenyekevu kwa huruma, na useme: Rabb wangu! Warehemu kama walivyonilea udogoni.
رَّبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا فِي نُفُوسِكُمْ ۚ إِن تَكُونُوا صَالِحِينَ فَإِنَّهُ كَانَ لِلْأَوَّابِينَ غَفُورًا ﴿٢٥﴾
25. Rabb wenu Anajua zaidi yaliyomo katika nafsi zenu. Mkiwa ni Swalihina basi hakika Yeye daima Ni Mwingi wa Kughufuria wenye kutubia kila mara Kwake.
وَآتِ ذَا الْقُرْبَىٰ حَقَّهُ وَالْمِسْكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَلَا تُبَذِّرْ تَبْذِيرًا ﴿٢٦﴾
26. Na mpe jamaa wa karibu haki yake, na masikini, na msafiri (aliyeharibikiwa), na wala usifanye ubadhirifu[11] wa ufujaji mkubwa.
إِنَّ الْمُبَذِّرِينَ كَانُوا إِخْوَانَ الشَّيَاطِينِ ۖ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِرَبِّهِ كَفُورًا ﴿٢٧﴾
27. Hakika wabadhirifu wamekuwa ni ndugu wa mashaytwaan, na shaytwaan amekuwa ni mwingi wa kumkufuru Rabb wake.
وَإِمَّا تُعْرِضَنَّ عَنْهُمُ ابْتِغَاءَ رَحْمَةٍ مِّن رَّبِّكَ تَرْجُوهَا فَقُل لَّهُمْ قَوْلًا مَّيْسُورًا ﴿٢٨﴾
28. Na kama unajikurupusha nao na huku unatafuta Rehma ya Rabb wako unayoitaraji, basi sema nao kauli laini.
وَلَا تَجْعَلْ يَدَكَ مَغْلُولَةً إِلَىٰ عُنُقِكَ وَلَا تَبْسُطْهَا كُلَّ الْبَسْطِ فَتَقْعُدَ مَلُومًا مَّحْسُورًا ﴿٢٩﴾
29. Na wala usifanye mkono wako kama uliofungwa shingoni mwako (ubakhili), na wala usiukunjue wote kabisa (kwa israfu) ukaja kubakia mwenye kulaumiwa, mwenye kufilisika.
إِنَّ رَبَّكَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّهُ كَانَ بِعِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا ﴿٣٠﴾
30. Hakika Rabb wako Anamkunjulia riziki Amtakaye na Humkadiria kwa kipimo (Amtakaye). Hakika Yeye daima kwa Waja Wake Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na za siri, Mwenye Kuona yote.
وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُمْ خَشْيَةَ إِمْلَاقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُهُمْ وَإِيَّاكُمْ ۚ إِنَّ قَتْلَهُمْ كَانَ خِطْئًا كَبِيرًا ﴿٣١﴾
31. Na wala msiue watoto wenu kwa kukhofia ufukara. Sisi Tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua imekuwa ni hatia kubwa.
وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَىٰ ۖ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا ﴿٣٢﴾
32. Na wala msiikaribie zinaa. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya kabisa.
وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۗ وَمَن قُتِلَ مَظْلُومًا فَقَدْ جَعَلْنَا لِوَلِيِّهِ سُلْطَانًا فَلَا يُسْرِف فِّي الْقَتْلِ ۖ إِنَّهُ كَانَ مَنصُورًا ﴿٣٣﴾
33. Na wala msiue nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha (kuiua) isipokuwa kwa haki. Na atakayeuliwa kwa kudhulumiwa, basi Tumemfanya mrithi wake awe na mamlaka. Lakini asipindukie mipaka katika kuua. Hakika yeye atasaidiwa (kwa sharia).
وَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّىٰ يَبْلُغَ أَشُدَّهُ ۚ وَأَوْفُوا بِالْعَهْدِ ۖ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْئُولًا ﴿٣٤﴾
34. Na wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia ya ihsaan mpaka afikie umri wa kupevuka. Na timizeni ahadi, hakika ahadi itakuwa ni ya kuulizwa.
وَأَوْفُوا الْكَيْلَ إِذَا كِلْتُمْ وَزِنُوا بِالْقِسْطَاسِ الْمُسْتَقِيمِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا ﴿٣٥﴾
35. Na timizeni kamilifu kipimo mnapopima, na pimeni kwa kipimo cha sawasawa. Hivyo ni kheri na bora zaidi matokeo yake.
وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَـٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا ﴿٣٦﴾
36. Na wala usifuate usiyo na ilimu nayo. Hakika masikio na macho na moyo; vyote hivyo vitaulizwa.
وَلَا تَمْشِ فِي الْأَرْضِ مَرَحًا ۖ إِنَّكَ لَن تَخْرِقَ الْأَرْضَ وَلَن تَبْلُغَ الْجِبَالَ طُولًا ﴿٣٧﴾
37. Na wala usitembee katika ardhi kwa majivuno. Hakika wewe huwezi kupasua ardhi, na wala huwezi kufikia urefu wa milima.
كُلُّ ذَٰلِكَ كَانَ سَيِّئُهُ عِندَ رَبِّكَ مَكْرُوهًا ﴿٣٨﴾
38. Yote hayo, uovu wake umekuwa ni wa kukirihisha mbele ya Rabb wako.
ذَٰلِكَ مِمَّا أَوْحَىٰ إِلَيْكَ رَبُّكَ مِنَ الْحِكْمَةِ ۗ وَلَا تَجْعَلْ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتُلْقَىٰ فِي جَهَنَّمَ مَلُومًا مَّدْحُورًا ﴿٣٩﴾
39. Hayo ni miongoni mwa hikmah ambayo Amekufunulia Wahy Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na wala usifanye pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine ukaja kutupwa katika Jahannam hali ya kuwa mwenye kulaumiwa na kufukuziliwa mbali.
أَفَأَصْفَاكُمْ رَبُّكُم بِالْبَنِينَ وَاتَّخَذَ مِنَ الْمَلَائِكَةِ إِنَاثًا ۚ إِنَّكُمْ لَتَقُولُونَ قَوْلًا عَظِيمًا ﴿٤٠﴾
40. Je, Rabb wenu Amekukhitarieni watoto wa kiume na Yeye Amejichukulia Malaika watoto wa kike? Hakika nyinyi mnasema kauli nzito mno![12]
وَلَقَدْ صَرَّفْنَا فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ لِيَذَّكَّرُوا وَمَا يَزِيدُهُمْ إِلَّا نُفُورًا ﴿٤١﴾
41. Na kwa yakini Tumesarifu namna kwa namna katika hii Qur-aan ili wakumbuke, lakini haiwazidishii ila kukimbia (haki) kwa chuki.
قُل لَّوْ كَانَ مَعَهُ آلِهَةٌ كَمَا يَقُولُونَ إِذًا لَّابْتَغَوْا إِلَىٰ ذِي الْعَرْشِ سَبِيلًا ﴿٤٢﴾
42. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Kama wangelikuwa pamoja Naye waabudiwa kama wasemavyo, basi hapo wangelitafuta njia ya kumfikia Mwenye ‘Arshi.[13]
سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يَقُولُونَ عُلُوًّا كَبِيرًا ﴿٤٣﴾
43. Ametakasika Allaah na Ametukuka kutokana na wanayoyasema ya uongo na dhulma kubwa ya hali ya juu kabisa!
تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ ۚ وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِ وَلَـٰكِن لَّا تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ ۗ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا ﴿٤٤﴾
44. Zinamsabihi mbingu saba na ardhi na waliomo humo. Na hakuna kitu chochote isipokuwa kinasabihi na kumhimidi Yeye, lakini hamzifahamu tasbihi zao.[14] Hakika Yeye Ni Mvumilivu, Mwingi wa Kughufuria.
وَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ جَعَلْنَا بَيْنَكَ وَبَيْنَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ حِجَابًا مَّسْتُورًا ﴿٤٥﴾
45. Na unaposoma Qur-aan Tunajaalia baina yako na baina ya wale wasioamini Aakhirah kizuizi kinachofunika (akili wasiifahamu).
وَجَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا ۚ وَإِذَا ذَكَرْتَ رَبَّكَ فِي الْقُرْآنِ وَحْدَهُ وَلَّوْا عَلَىٰ أَدْبَارِهِمْ نُفُورًا ﴿٤٦﴾
46. Na Tumetia juu ya nyoyo zao vifuniko wasiifahamu, na katika masikio yao uziwi.[15] Na unapomtaja Rabb wako katika Qur-aan Pekee wanageuza migongo kukimbia (haki) kwa chuki.
نَّحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَسْتَمِعُونَ بِهِ إِذْ يَسْتَمِعُونَ إِلَيْكَ وَإِذْ هُمْ نَجْوَىٰ إِذْ يَقُولُ الظَّالِمُونَ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا رَجُلًا مَّسْحُورًا ﴿٤٧﴾
47. Sisi Tunajua zaidi kile wanacholenga kukisikiliza pale wanapokusikiliza kwa makini, na wakati wanaponong’ona. (Na Tunajua pia) wanaposema madhalimu: Hamfuati isipokuwa mtu aliyefanyiwa sihri.
انظُرْ كَيْفَ ضَرَبُوا لَكَ الْأَمْثَالَ فَضَلُّوا فَلَا يَسْتَطِيعُونَ سَبِيلًا ﴿٤٨﴾
48. Tazama vipi walivyokupigia mifano wakapotoka, basi hawawezi kupata njia (ya kuwahidi).
وَقَالُوا أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا وَرُفَاتًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ خَلْقًا جَدِيدًا ﴿٤٩﴾
49. Na wakasema: Je, hivi sisi tukiwa mifupa, na mapande yaliyosagika sagika, je, hivi sisi hivyo tutafufuliwa katika umbo jipya?[16]
قُلْ كُونُوا حِجَارَةً أَوْ حَدِيدًا ﴿٥٠﴾
50. Sema: Kuweni mawe au chuma.
أَوْ خَلْقًا مِّمَّا يَكْبُرُ فِي صُدُورِكُمْ ۚ فَسَيَقُولُونَ مَن يُعِيدُنَا ۖ قُلِ الَّذِي فَطَرَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۚ فَسَيُنْغِضُونَ إِلَيْكَ رُءُوسَهُمْ وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هُوَ ۖ قُلْ عَسَىٰ أَن يَكُونَ قَرِيبًا ﴿٥١﴾
51. Au umbo katika vile vinavyohisiwa vikubwa (au vigumu) katika vifua vyenu. Basi watasema: Nani atakayeturudisha (kuwa hai?). Sema: Ni Yule Aliyekuanzisheni mara ya kwanza! Basi watakutingishia vichwa vyao na kusema: Lini hayo?! Sema: Asaa yawe karibu.
يَوْمَ يَدْعُوكُمْ فَتَسْتَجِيبُونَ بِحَمْدِهِ وَتَظُنُّونَ إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٥٢﴾
52. Siku Atakayokuiteni, nanyi mtamuitika huku mkimhimidi, na mtaona kama vile hamkubakia (duniani) isipokuwa kidogo tu.
وَقُل لِّعِبَادِي يَقُولُوا الَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ۚ إِنَّ الشَّيْطَانَ يَنزَغُ بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّ الشَّيْطَانَ كَانَ لِلْإِنسَانِ عَدُوًّا مُّبِينًا ﴿٥٣﴾
53. Na waambie Waja Wangu waseme maneno yaliyo mazuri zaidi. Hakika shaytwaan anachochea baina yao. Hakika shaytwaan kwa binaadam daima ni adui bayana.[17]
رَّبُّكُمْ أَعْلَمُ بِكُمْ ۖ إِن يَشَأْ يَرْحَمْكُمْ أَوْ إِن يَشَأْ يُعَذِّبْكُمْ ۚ وَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ وَكِيلًا ﴿٥٤﴾
54. Rabb wenu Anakujueni vizuri zaidi. Akitaka Atakurehemuni au Akitaka Atakuadhibuni. Na Hatukukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa mlinzi wao.
وَرَبُّكَ أَعْلَمُ بِمَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَلَقَدْ فَضَّلْنَا بَعْضَ النَّبِيِّينَ عَلَىٰ بَعْضٍ ۖ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا ﴿٥٥﴾
55. Na Rabb wako Anawajua vilivyo waliomo katika mbingu na ardhi. Na kwa yakini Tumewafadhilisha baadhi ya Manabii juu ya wengineo. Na Tukampa Daawuwd Zabuwr.
قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِهِ فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ الضُّرِّ عَنكُمْ وَلَا تَحْوِيلًا ﴿٥٦﴾
56. Sema: Iteni wale ambao mnadai (ni waabudiwa) pasi Naye, basi hawamiliki uwezo wa kukuondosheeni dhara wala kuihamisha (kwa mwengine).
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ ۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحْذُورًا ﴿٥٧﴾
57. Hao wanaowaomba (wao wenyewe) wanatafuta kwa Rabb wao njia ya kujikurubisha, yupi miongoni mwao awe karibu zaidi, na wanataraji Rehma Yake, na wanakhofu Adhabu Yake. Hakika Adhabu ya Rabb wako ni ya kutahadhariwa daima.[18]
وَإِن مِّن قَرْيَةٍ إِلَّا نَحْنُ مُهْلِكُوهَا قَبْلَ يَوْمِ الْقِيَامَةِ أَوْ مُعَذِّبُوهَا عَذَابًا شَدِيدًا ۚ كَانَ ذَٰلِكَ فِي الْكِتَابِ مَسْطُورًا ﴿٥٨﴾
58. Na hakuna mji wowote isipokuwa Sisi Tutauangamiza kabla ya Siku ya Qiyaamah, au Tutauadhibu adhabu kali. Hayo yameandikwa katika Kitabu (Lawh Al-Mahfuwdhw)[19].
وَمَا مَنَعَنَا أَن نُّرْسِلَ بِالْآيَاتِ إِلَّا أَن كَذَّبَ بِهَا الْأَوَّلُونَ ۚ وَآتَيْنَا ثَمُودَ النَّاقَةَ مُبْصِرَةً فَظَلَمُوا بِهَا ۚ وَمَا نُرْسِلُ بِالْآيَاتِ إِلَّا تَخْوِيفًا ﴿٥٩﴾
59. Na hakuna kinachotuzuia kuleta Aayaat (Ishara, Dalili, Miujiza) isipokuwa ni kuwa watu wa awali waliikadhibisha. Na Tuliwapa kina Thamuwd ngamia jike kuwa dalili dhahiri lakini wakamdhulumu. Na Hatupeleki Aayaat (Ishara, Miujiza) isipokuwa kwa ajili ya (kuonya na) kukhofisha (ili wazingatie).[20]
وَإِذْ قُلْنَا لَكَ إِنَّ رَبَّكَ أَحَاطَ بِالنَّاسِ ۚ وَمَا جَعَلْنَا الرُّؤْيَا الَّتِي أَرَيْنَاكَ إِلَّا فِتْنَةً لِّلنَّاسِ وَالشَّجَرَةَ الْمَلْعُونَةَ فِي الْقُرْآنِ ۚ وَنُخَوِّفُهُمْ فَمَا يَزِيدُهُمْ إِلَّا طُغْيَانًا كَبِيرًا ﴿٦٠﴾
60. Na (kumbuka ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Tulipokuambia: Hakika Rabb wako Amekwishawazunguka watu. Na Hatukuijaalia ndoto ambayo Tulikuonyesha isipokuwa ni mtihani kwa watu, na mti uliolaaniwa katika Qur-aan.[21] Na Tunawatisha, basi haiwazidishii isipokuwa upindukaji mipaka mkubwa wa kuasi.
وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ قَالَ أَأَسْجُدُ لِمَنْ خَلَقْتَ طِينًا ﴿٦١﴾
61. Na pindi Tulipowaambia Malaika: Msujudieni Aadam. Wakasujudu isipokuwa Ibliys. Akasema: Je, nimsujudie Uliyemuumba kwa udongo?[22]
قَالَ أَرَأَيْتَكَ هَـٰذَا الَّذِي كَرَّمْتَ عَلَيَّ لَئِنْ أَخَّرْتَنِ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَأَحْتَنِكَنَّ ذُرِّيَّتَهُ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٦٢﴾
62. (Ibliys) akasema: Unamwona huyu ambaye Umemkirimu zaidi yangu! Basi Ukiniakhirisha mpaka Siku ya Qiyaamah, bila shaka nitaangamiza kabisa kizazi chake isipokuwa wachache.
قَالَ اذْهَبْ فَمَن تَبِعَكَ مِنْهُمْ فَإِنَّ جَهَنَّمَ جَزَاؤُكُمْ جَزَاءً مَّوْفُورًا ﴿٦٣﴾
63. (Allaah) Akasema: Nenda! Kwani atakayekufuata miongoni mwao, basi hakika Jahannam ni jazaa yenu, jazaa timilifu.
وَاسْتَفْزِزْ مَنِ اسْتَطَعْتَ مِنْهُم بِصَوْتِكَ وَأَجْلِبْ عَلَيْهِم بِخَيْلِكَ وَرَجِلِكَ وَشَارِكْهُمْ فِي الْأَمْوَالِ وَالْأَوْلَادِ وَعِدْهُمْ ۚ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلَّا غُرُورًا ﴿٦٤﴾
64. Na wachochee kilaini uwawezao miongoni mwao kwa sauti yako, na wakusanyie kikosi chako cha farasi, na askari wako waendao kwa miguu, na shirikiana nao katika mali na watoto na waahidi. Lakini shaytwaan hawapi ahadi isipokuwa ni udanganyifu.[23]
إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ ۚ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ وَكِيلًا ﴿٦٥﴾
65. Hakika Waja Wangu huna mamlaka juu yao. Na Rabb wako Anatosheleza Kuwa Mtegemewa wa yote.
رَّبُّكُمُ الَّذِي يُزْجِي لَكُمُ الْفُلْكَ فِي الْبَحْرِ لِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ ۚ إِنَّهُ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا ﴿٦٦﴾
66. Rabb wenu Ndiye Ambaye Anakuendesheeni merikebu baharini ili mtafute Fadhila Zake. Hakika Yeye Ni Mwenye Kukurehemuni.
وَإِذَا مَسَّكُمُ الضُّرُّ فِي الْبَحْرِ ضَلَّ مَن تَدْعُونَ إِلَّا إِيَّاهُ ۖ فَلَمَّا نَجَّاكُمْ إِلَى الْبَرِّ أَعْرَضْتُمْ ۚ وَكَانَ الْإِنسَانُ كَفُورًا ﴿٦٧﴾
67. Na inapokuguseni dhara baharini wale mnaowaomba hupotea isipokuwa Yeye Pekee. Anapokuokoeni katika ardhi kavu mnakengeuka. Na binaadam amekuwa ni mwingi wa kukufuru, asiyeshukuru.
أَفَأَمِنتُمْ أَن يَخْسِفَ بِكُمْ جَانِبَ الْبَرِّ أَوْ يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ثُمَّ لَا تَجِدُوا لَكُمْ وَكِيلًا ﴿٦٨﴾
68. Je, mmeaminisha kwamba (Allaah) Hatokudidimizeni upande wowote wa ardhi kavu, au Hatokuleteeni tufani ya mawe, kisha hamtopata wa kumtegemea?
أَمْ أَمِنتُمْ أَن يُعِيدَكُمْ فِيهِ تَارَةً أُخْرَىٰ فَيُرْسِلَ عَلَيْكُمْ قَاصِفًا مِّنَ الرِّيحِ فَيُغْرِقَكُم بِمَا كَفَرْتُمْ ۙ ثُمَّ لَا تَجِدُوا لَكُمْ عَلَيْنَا بِهِ تَبِيعًا ﴿٦٩﴾
69. Au je, mmeaminisha kwamba (Allaah) Hatokurudisheni huko (baharini) mara nyingine, kisha Akakutumieni kimbunga cha upepo Akakugharikisheni kwa sababu ya kufru yenu kisha hamtopata mteteaji wa kukunusuruni Nasi?
وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آدَمَ وَحَمَلْنَاهُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَىٰ كَثِيرٍ مِّمَّنْ خَلَقْنَا تَفْضِيلًا ﴿٧٠﴾
70. Na kwa yakini Tumewakirimu wana wa Aadam, na Tukawabeba katika ardhi kavu na baharini, na Tukawaruzuku katika vizuri na Tukawafadhilisha juu ya wengi miongoni mwa Tuliowaumba kwa ufadhilisho mkubwa.[24]
يَوْمَ نَدْعُو كُلَّ أُنَاسٍ بِإِمَامِهِمْ ۖ فَمَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَأُولَـٰئِكَ يَقْرَءُونَ كِتَابَهُمْ وَلَا يُظْلَمُونَ فَتِيلًا ﴿٧١﴾
71. Siku Tutakayoita watu wote pamoja na rekodi zao za matendo (au Nabii wao).[25] Basi atakayepewa kitabu chake kuliani mwake, hao watasoma kitabu chao na wala hawatodhulumiwa kadiri ya uzi katika kokwa ya tende.
وَمَن كَانَ فِي هَـٰذِهِ أَعْمَىٰ فَهُوَ فِي الْآخِرَةِ أَعْمَىٰ وَأَضَلُّ سَبِيلًا ﴿٧٢﴾
72. Na atakayekuwa kipofu katika hii (dunia) basi yeye Aakhirah atakuwa kipofu na atapotea zaidi njia.
وَإِن كَادُوا لَيَفْتِنُونَكَ عَنِ الَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ لِتَفْتَرِيَ عَلَيْنَا غَيْرَهُ ۖ وَإِذًا لَّاتَّخَذُوكَ خَلِيلًا ﴿٧٣﴾
73. Na hakika walikaribia kukukengeusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale Tuliyokufunulia Wahy ili upate kututungia mengineyo. Basi hapo ndipo wangelikufanya rafiki mwandani.
وَلَوْلَا أَن ثَبَّتْنَاكَ لَقَدْ كِدتَّ تَرْكَنُ إِلَيْهِمْ شَيْئًا قَلِيلًا ﴿٧٤﴾
74. Na lau kama Hatukukuthibitisha, kwa yakini ungelikaribia kuelemea kwao kidogo.
إِذًا لَّأَذَقْنَاكَ ضِعْفَ الْحَيَاةِ وَضِعْفَ الْمَمَاتِ ثُمَّ لَا تَجِدُ لَكَ عَلَيْنَا نَصِيرًا ﴿٧٥﴾
75. Hapo basi bila shaka Tungelikuonjesha (adhabu) maradufu ya uhai na (adhabu) maradufu ya mauti kisha usingelipata wa kukunusuru Nasi.
وَإِن كَادُوا لَيَسْتَفِزُّونَكَ مِنَ الْأَرْضِ لِيُخْرِجُوكَ مِنْهَا ۖ وَإِذًا لَّا يَلْبَثُونَ خِلَافَكَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٧٦﴾
76. Na hakika walikaribia wakusumbue mno katika ardhi ili wakutoe humo. Na hapo wao wasingelibakia baada yako isipokuwa kidogo tu.
سُنَّةَ مَن قَدْ أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ مِن رُّسُلِنَا ۖ وَلَا تَجِدُ لِسُنَّتِنَا تَحْوِيلًا ﴿٧٧﴾
77. (Hiyo ndiyo) desturi ya Tuliowatuma kabla yako miongoni mwa Rusuli Wetu. Na wala hutopata mabadiliko katika desturi Zetu.[26]
أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَىٰ غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ ۖ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا ﴿٧٨﴾
78. Simamisha Swalaah jua linapopinduka hadi kiza cha usiku na (refusha) Qur-aan ya (Swalaah ya) Alfajiri. Hakika Qur-aan ya Alfajiri ni yenye kushuhudiwa.
وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا ﴿٧٩﴾
79. Na katika usiku, amka uswali (tahajjud)[27] kwa kuisoma (Qur-aan) ikiwa ni ziada kwako. Asaa Rabb wako Akakuinua cheo cha kuhimidiwa (kusifika).[28]
وَقُل رَّبِّ أَدْخِلْنِي مُدْخَلَ صِدْقٍ وَأَخْرِجْنِي مُخْرَجَ صِدْقٍ وَاجْعَل لِّي مِن لَّدُنكَ سُلْطَانًا نَّصِيرًا ﴿٨٠﴾
80. Na sema: Ee Rabb wangu! Niingize mwingizo wa kheri na Nitoe pa kutokea pa kheri na Nijaalie kutoka Kwako (hoja au) mamlaka yenye kunusuru.[29]
وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ ۚ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا ﴿٨١﴾
81. Na sema: Haki imekuja, na ubatili umetoweka. Hakika ubatili ni wenye kutoweka daima.[30]
وَنُنَزِّلُ مِنَ الْقُرْآنِ مَا هُوَ شِفَاءٌ وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ۙ وَلَا يَزِيدُ الظَّالِمِينَ إِلَّا خَسَارًا ﴿٨٢﴾
82. Na Tunateremsha katika Qur-aan ambayo ni shifaa na rehmakwa Waumini na wala haiwazidishii madhalimu isipokuwa khasara.[31]
وَإِذَا أَنْعَمْنَا عَلَى الْإِنسَانِ أَعْرَضَ وَنَأَىٰ بِجَانِبِهِ ۖ وَإِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ كَانَ يَئُوسًا ﴿٨٣﴾
83. Na Tunapomneemesha binaadam, hukengeuka na kujitenga mbali, lakini inapomgusa shari, huwa mwenye kukata tamaa.[32]
قُلْ كُلٌّ يَعْمَلُ عَلَىٰ شَاكِلَتِهِ فَرَبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَنْ هُوَ أَهْدَىٰ سَبِيلًا ﴿٨٤﴾
84. Sema: Kila mmoja anatenda kwa namna yake. Basi Rabb wenu Anamjua zaidi yule aliyehidika zaidi katika njia (ya haki).
وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ ۖ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتِيتُم مِّنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٨٥﴾
85. Na wanakuuliza kuhusu Ruwh[33] (roho). [34] Sema: Roho ni katika Jambo la Rabb wangu. Na hamkupewa ujuzi isipokuwa kidogo tu.[35]
وَلَئِن شِئْنَا لَنَذْهَبَنَّ بِالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ ثُمَّ لَا تَجِدُ لَكَ بِهِ عَلَيْنَا وَكِيلًا ﴿٨٦﴾
86. Na kama Tungelitaka, bila shaka Tungeliondosha yale Tuliyokufunulia Wahy, kisha usingelipata kwa haya, mtegemewa wa kukunusuru Nasi.
إِلَّا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ إِنَّ فَضْلَهُ كَانَ عَلَيْكَ كَبِيرًا ﴿٨٧﴾
87. Isipokuwa Rehma kutoka kwa Rabb wako. Hakika Fadhila Zake juu yako daima ni kubwa.
قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَـٰذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا ﴿٨٨﴾
88. Sema: Ikiwa watajumuika wanaadam na majini ili walete mfano wa hii Qur-aan, hawatoweza kuleta mfano wake na japokuwa watasaidiana wao kwa wao.[36]
وَلَقَدْ صَرَّفْنَا لِلنَّاسِ فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ مِن كُلِّ مَثَلٍ فَأَبَىٰ أَكْثَرُ النَّاسِ إِلَّا كُفُورًا ﴿٨٩﴾
89. Na kwa yakini Tumesarifu namna kwa namna hii Qur-aan kwa watu, kwa kila mfano, lakini watu wengi wamekataa kabisa (haki; hawakukubali) isipokuwa kukufuru tu.
وَقَالُوا لَن نُّؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ تَفْجُرَ لَنَا مِنَ الْأَرْضِ يَنبُوعًا ﴿٩٠﴾
90. Na wakasema: Hatutakuamini (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) mpaka utububujie kutoka ardhini chemchemu.[37]
أَوْ تَكُونَ لَكَ جَنَّةٌ مِّن نَّخِيلٍ وَعِنَبٍ فَتُفَجِّرَ الْأَنْهَارَ خِلَالَهَا تَفْجِيرًا ﴿٩١﴾
91. Au uwe na bustani ya mitende na mizabibu, kisha utububujie mito kati yake mbubujiko mkubwa.
أَوْ تُسْقِطَ السَّمَاءَ كَمَا زَعَمْتَ عَلَيْنَا كِسَفًا أَوْ تَأْتِيَ بِاللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ قَبِيلًا ﴿٩٢﴾
92. Au utuangushie mbingu vipande vipande kama ulivyodai, au umlete Allaah na Malaika uso kwa uso.
أَوْ يَكُونَ لَكَ بَيْتٌ مِّن زُخْرُفٍ أَوْ تَرْقَىٰ فِي السَّمَاءِ وَلَن نُّؤْمِنَ لِرُقِيِّكَ حَتَّىٰ تُنَزِّلَ عَلَيْنَا كِتَابًا نَّقْرَؤُهُ ۗ قُلْ سُبْحَانَ رَبِّي هَلْ كُنتُ إِلَّا بَشَرًا رَّسُولًا ﴿٩٣﴾
93. Au uwe na nyumba ya dhahabu, au upande mbinguni. Na wala hatutoamini kamwe kupanda kwako mpaka ututeremshie kitabu tukisome. Sema: Utakasifu ni wa Rabb wangu! Kwani mimi nimekuwa nani isipokuwa ni binaadam (na) Rasuli!
وَمَا مَنَعَ النَّاسَ أَن يُؤْمِنُوا إِذْ جَاءَهُمُ الْهُدَىٰ إِلَّا أَن قَالُوا أَبَعَثَ اللَّـهُ بَشَرًا رَّسُولًا ﴿٩٤﴾
94. Na hakuna kilichowazuia watu wasiamini ulipowajia mwongozo isipokuwa husema: Je, Allaah Ametuma binaadam kuwa ni Rasuli?
قُل لَّوْ كَانَ فِي الْأَرْضِ مَلَائِكَةٌ يَمْشُونَ مُطْمَئِنِّينَ لَنَزَّلْنَا عَلَيْهِم مِّنَ السَّمَاءِ مَلَكًا رَّسُولًا ﴿٩٥﴾
95. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Kama ingelikuwa katika ardhi kuna Malaika wanatembea kwa utulivu na amani, basi bila shaka Tungeliwateremshia kutoka mbinguni Malaika kuwa ni Rasuli.
قُلْ كَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۚ إِنَّهُ كَانَ بِعِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا ﴿٩٦﴾
96. Sema: Anatosheleza Allaah kuwa Shahidi baina yangu na baina yenu. Hakika Yeye daima Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na za siri za Waja Wake, Mwenye Kuona yote.
وَمَن يَهْدِ اللَّـهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِ ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُمْ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِهِ ۖ وَنَحْشُرُهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ عُمْيًا وَبُكْمًا وَصُمًّا ۖ مَّأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ كُلَّمَا خَبَتْ زِدْنَاهُمْ سَعِيرًا ﴿٩٧﴾
97. Na ambaye Allaah Amemhidi, basi huyo ndiye aliyehidika. Na Anayempotoa, basi hutowapatia rafiki walinzi pasi Naye. Na Tutawakusanya Siku ya Qiyaamah juu ya nyuso zao[38] (wakiwa) vipofu, mabubu na viziwi, makazi yao ni (moto wa) Jahannam, kila ukififia Tutawazidishia moto uliowashwa vikali mno.
ذَٰلِكَ جَزَاؤُهُم بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا وَقَالُوا أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا وَرُفَاتًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ خَلْقًا جَدِيدًا ﴿٩٨﴾
98. Hiyo ndiyo jazaa yao kwa kuwa wao walizikanusha Aayaat (na Ishara, Hoja, Dalili) Zetu na wakasema: Je, hivi sisi tukiwa mifupa na mapande yaliyosagika sagika, hivi kweli sisi tutafufuliwa katika umbo jipya?[39]
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ قَادِرٌ عَلَىٰ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُمْ وَجَعَلَ لَهُمْ أَجَلًا لَّا رَيْبَ فِيهِ فَأَبَى الظَّالِمُونَ إِلَّا كُفُورًا ﴿٩٩﴾
99. Je, hawajaona kwamba Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi Ni Mweza wa Kuumba mfano wao? Na Amewawekea muda maalumu usio na shaka? Lakini madhalimu wamekataa kabisa hawana isipokuwa kukufuru tu.
قُل لَّوْ أَنتُمْ تَمْلِكُونَ خَزَائِنَ رَحْمَةِ رَبِّي إِذًا لَّأَمْسَكْتُمْ خَشْيَةَ الْإِنفَاقِ ۚ وَكَانَ الْإِنسَانُ قَتُورًا ﴿١٠٠﴾
100. Sema: Ingekuwa nyinyi mnamiliki hazina za Rehma ya Rabb wangu bila shaka hapo mngelizuia kuzitumia kwa ajili ya kukhofu (zisimalizike). Na binaadam amekuwa ni mchoyo kupindukia.
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَىٰ تِسْعَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۖ فَاسْأَلْ بَنِي إِسْرَائِيلَ إِذْ جَاءَهُمْ فَقَالَ لَهُ فِرْعَوْنُ إِنِّي لَأَظُنُّكَ يَا مُوسَىٰ مَسْحُورًا ﴿١٠١﴾
101. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Aayaat (Ishara, Dalili, Miujiza) tisa bayana.[40] Basi waulize wana wa Israaiyl alipowajia, na Firawni akamwambia: Hakika mimi nakuona ewe Muwsaa kuwa umerogwa.
قَالَ لَقَدْ عَلِمْتَ مَا أَنزَلَ هَـٰؤُلَاءِ إِلَّا رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ بَصَائِرَ وَإِنِّي لَأَظُنُّكَ يَا فِرْعَوْنُ مَثْبُورًا ﴿١٠٢﴾
102. (Muwsaa) akasema: Kwa yakini umekwishajua kwamba hakuna Aliyeteremsha haya isipokuwa Rabb wa mbingu na ardhi kuwa ni dalili za kuonekana dhahiri, na hakika mimi bila shaka nakuona ewe Firawni kuwa umekwisha angamia.
فَأَرَادَ أَن يَسْتَفِزَّهُم مِّنَ الْأَرْضِ فَأَغْرَقْنَاهُ وَمَن مَّعَهُ جَمِيعًا ﴿١٠٣﴾
103. Basi akataka awasumbue na kuwafukuza katika ardhi, Tukamgharikisha yeye na waliokuwa pamoja naye wote.
وَقُلْنَا مِن بَعْدِهِ لِبَنِي إِسْرَائِيلَ اسْكُنُوا الْأَرْضَ فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ جِئْنَا بِكُمْ لَفِيفًا ﴿١٠٤﴾
104. Na Tukawaambia baada yake wana wa Israaiyl: Kaeni katika ardhi, na itakapokuja ahadi ya Aakhirah Tutakuleteni nyote pamoja kwa makundi mchanganyiko.
وَبِالْحَقِّ أَنزَلْنَاهُ وَبِالْحَقِّ نَزَلَ ۗ وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا مُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿١٠٥﴾
105. Na kwa haki Tumeiteremsha (Qur-aan), na kwa haki imeteremka. Na Hatukukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa ni mbashiriaji na mwonyaji tu.
وَقُرْآنًا فَرَقْنَاهُ لِتَقْرَأَهُ عَلَى النَّاسِ عَلَىٰ مُكْثٍ وَنَزَّلْنَاهُ تَنزِيلًا ﴿١٠٦﴾
106. Na Qur-aan Tumeigawanya sehemu mbali mbali ili uwasomee watu kwa kituo, na Tumeiteremsha kidogo kidogo.[41]
قُلْ آمِنُوا بِهِ أَوْ لَا تُؤْمِنُوا ۚ إِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مِن قَبْلِهِ إِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ يَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ سُجَّدًا ﴿١٠٧﴾
107. Sema: Iaminini au msiamini. Hakika wale waliopewa ilimu kabla yake wanaposomewa (Qur-aan) wanaporomoka kifudifudi wanasujudu.
وَيَقُولُونَ سُبْحَانَ رَبِّنَا إِن كَانَ وَعْدُ رَبِّنَا لَمَفْعُولًا ﴿١٠٨﴾
108. Na wanasema: Utakasifu ni wa Rabb wetu, hakika Ahadi ya Rabb wetu lazima itimizwe.
وَيَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ يَبْكُونَ وَيَزِيدُهُمْ خُشُوعًا ۩﴿١٠٩﴾
109. Na wanaporomoka kifudifudi huku wanalia na inawazidishia unyenyekevu.
قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا وَابْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا ﴿١١٠﴾
110. Sema: Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan[42], vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa.[43] Na wala usisome (Qur-aan) kwa sauti ya juu katika Swalaah yako wala usiiteremshe sana, bali shika njia ya wastani baina yake. [44]
وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي لَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَلَمْ يَكُن لَّهُ وَلِيٌّ مِّنَ الذُّلِّ ۖ وَكَبِّرْهُ تَكْبِيرًا ﴿١١١﴾
111. Na sema: AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah) Ambaye Hakujifanyia mwana na wala Hakuwa na mshirika katika ufalme, na wala Hakuwa dhalili hata Awe (Anahitaji) mlinzi (na msaidizi), na mtukuze matukuzo makubwa kabisa.[45]
[1] Safari Ya Al-Israa Na Al-Mi’raaj:
Maana Ya Al-Israa kilugha: Ni safari ya usiku.
Kiistilahi: Ni safari ya baadhi ya usiku mmoja, ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) yeye mwenyewe kwa mwili wake na akili zake na roho yake kuanzia Masjid Al-Haraam (Msikiti Mtukufu - Makkah) kufika Masjid-Al-Aqswaa (Msikiti wa Mbali -Al-Quds) na kurejea kwake Makkah usiku huo huo. Alisafiri akiwa ameambatana na Malaika Mtukufu Jibriyl (عليه السّلام) kwa kipando cha mnyama wa ajabu mwenye umbo la kuvutia kabisa aliyejulikana kwa Al-Buraaq.
Maana Ya Al-Mi’raaj kilugha: Ni kupanda juu.
Kiistilahi: Ni kupanda kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) mbinguni kuanzia Masjid Al-Aqaswaa hadi kufika mbingu ya saba.
Maana ya Al-Buraaq kilugha ni: Mwale unaotoka katika mwanga.
Kiistilahi: Ni kama alivyoelezea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth:
“Nililetewa Al-Buraaq, mnyama mrefu wa umbo na mweupe, ni mkubwa kiasi zaidi ya punda lakini ni mdogo kuliko nyumbu, ambaye anapokwenda mbio hatua yake ni upeo wa macho yake. Nilimpanda mnyama huyo mpaka nikafika Al-Masjid Al-Aqswaa huko Al-Quds (Jerusalem). Hapo nilimfunga pale mahali ambapo Manabii wengine walikuwa wakifunga wanyama wao.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Matukio ya safari hii tukufu ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ya Al-Israa na Al-Mi’raaj yameelezewa kwa tafasili katika Hadiyth ndefu ya [Al-Bukhaariy] Na Hadiyth kadhaa nyenginezo za tukio tukufu la Al-Israa Wal Mi’raaj zimethibiti; mojawapo inaeleza kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali na Manabii wengine hapo katika Msikiti wa Al-Aqswaa na yeye akiwa Imaam kwa kauli Yake (صلى الله عليه وآله وسلم): “Kisha niliingia Al-Masjid Al-Aqswaa, nikaswali rakaa mbili.” [Swahiyh Muslim]
Msikiti wa Al-Aqswaa umekuwa na sifa ya kuwa ni kituo cha Manabii wote, toka enzi ya Al-Khaliyl Ibraahiym (عليه السّلام). Hivyo Manabii wote walikusanyika hapo na Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) akawa Imaam wao. Hii ni dalili juu ya cheo kikubwa alicho nacho Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye ni Nabiy wa mwisho miongoni mwa Manabii wengine (عليهم السّلام). [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Rejea pia An-Najm (53:1-18) Aayah zinazoelezea bado tukio hili na Allaah (سبحانه وتعالى) kumuunga mkono kuwa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) ni mkweli na hakukadhibisha tukio hili.
Kwa maelezo bayana rejea Alhidaaya.com makala zifuatazo:
[2] Kizazi Alichokibeba Nabiy Nuwh (عليه السّلام) Jahazini Ndicho Kizazi Kilichobakia, Akawa Yeye, Ni Baba Wa Wanaadam Baada Ya Nabiy Aadam (عليه السّلام):
Rejea Asw-Swaaffaat (37:77) kwenye maelezo bayana na rejea zake mbalimbali.
Rejea Yuwnus (10:73), Huwd (11:40), Maryam (19:58), Al-Muuminuwn (23:27), Nuwh (71:1).
[3] Waliotumwa Kuwadhalilisha Baniy Israaiyl:
Wafasiri wamekhitilafiana kuhusu nani hao waliotumwa kuwadhalilisha Baniy Israaiyl? Ambalo hawakukhitilafiana ni kuwa watu hao walikuwa ni makafiri. Ima ni watu kutoka Iraq, au Jazeera, au kwingineko. Watu hawa Allaah Aliwapa nguvu dhidi ya Baniy Israaiyl wakati walipokithiri kutenda maasia, wakaacha kutekeleza sharia zao nyingi na wakadhulumu kwenye nchi. Imaam As-Sa’diy amesema walikuwa ni makafiri. [Tafsiyr As Sa’diy]
Ibn Kathiyr amesema: Wamekhitilafiana Wafasiri wa Salaf na waliotangulia kuhusu ni nani waliopelekewa watu wa kuwaadhibu na kuwadhalilisha Ibn ‘Abaaas na Qataadah wamesema: Ni Jaaluwt Al-Jazariy na askari wake, walitumiwa mwanzo wakadhalilishwa, kisha zamu ikawa yao baada ya hapo wakapata nguvu. Lakini katika vita, Daawuwd alimuua Jaaluwt. Na ndiyo sababu Allaah Akasema: Kisha Tukakurudishieni nguvu zenu dhidi yao. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[4] Qur-aan Inaongoza Katika Njia Iliyonyooka:
Rejea Suwrah Fusw-Swilat (41:44) kwenye maelezo bayana.
[5] Amali Kuambatanishwa Shingoni:
Amali zinazoambatanishwa shingoni mwa binaadam, ni amali za kheri au shari alizokadariwa au alizojaaliwa binaadam kuzitenda kwa khiyari yake mwenyewe. Amali hizo zimeambatanishwa shingoni mwake na zitamhusu yeye pekee, kwa maana, hatahesabiwa kwa matendo ya mtu mwengine wala mwengine hatahesabiwa kwa matendo yake yeye. Rejea Az-Zalzalah (99:6-8), Al-Kahf (18:49), Qaaf (50:17-18), Al-Infitwaar (82:10-12).
Na kuhusu kukunjuliwa kitabu cha matendo, rejea At-Takwiyr (81:10), Al-Anbiyaa (21:104).
[6] Binaadam Hataweza Kukanusha Ovu Lolote Alilolitenda Duniani:
Aayah hii inahusiana na Aayah iliyotangulia. Na hapa, Allaah (سبحانه وتعالى) Anabainisha kuwa hakuna mtu atakayeweza kukanusha jambo lolote lile ovu alilolitenda, kwani ataambiwa asome mwenyewe kitabu chake! Kamwe hatoweza kukanusha jambo, kwani hata viungo vya binadaam vitashuhudia matendo yake aliyoyatenda duniani. Rejea Yaasiyn (36:65), An-Nuwr (24:24), na Fus-swilat (41:20-22).
[8] Makatazo Na Maamrisho Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kuanzia Aayah Ya (22) Hadi Ya (39):
Kuanzia Aayah hii ya (22), Allaah (سبحانه وتعالى) Anaanza katazo la kutokumshirikisha Yeye na chochote. Kisha Anaendelea kutaja maamrisho na makatazo mengineyo mbalimbali hadi Aayah ya (39) ambayo Anamalizia pia kwa kutoa amri na tahadharisho la kutokumshirikisha Yeye (سبحانه وتعالى).
[9] Kuwafanyia Ihsaan Wazazi Wawili:
Rejea Luqmaan (31:14) na Al-Ahqaaf (46:15) kwenye maelezo bayana na fadia tele:
[10] Uff (Neno La Kudhihirisha Karaha)
Ni neno la kuudhika na kuonyesha karaha ya kiwango cha chini kabisa. Na linaweza kuwa kwa kauli au kwa ishara ya kuchukizwa au kutokuridhika na jambo. Yaani, usionyeshe hata kidogo kuwa umechukizwa au umeudhika nao au hukuridhika na wazazi.
[11] Tofauti Ya Israfu Na Ubadhirifu:
Israfu inaweza kuwa na maana ya kuvuka mipaka kwa kutenda dhambi. Mfano ni katika Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwrat za Yaasiyn (36:19), Al-A’raaf (7:81), Al-Anbiyaa (21:9) na nyenginezo kadhaa.
Kuna ujumuishi na umahususi baina ya israaf (israfu) na tabdhiyr (ubadhirifu), kwani huweza kuja pamoja baadhi ya nyakati zikawa na maana moja, na iliyo jumuishi zaidi ambayo ni israaf, inaweza ikabaki yenyewe na maana yake ya asili.
Na pia inaweza kuwa kwa maana ya kuvuka kikomo cha matumizi ya pesa katika mambo yanayoruhusika kama chakula, nguo na kadhalika. Kwa lugha nyingine, ni kuitumia Neema ya Allaah (سبحانه وتعالى) zaidi ya kiwango cha mahitaji ya mtu. Mfano ni mtu kununua nguo nyingi akawa hazivai baadhi yake. Au mtu kununua chakula zaidi ya anachokihitaji, kisha akala cha kumtosha, na kinachobakia kikaharibika akakitupa. Rejea Al-‘Araaf (7:31).
Ama Tabdhiyr (ubadhirifu), hii inahusiana na mali tu bila ya upindukaji mipaka ya maasi. Kwa maana nyingine, tabdhiyr ni utumiaji wa mali katika kisichojuzu (cha haramu), ni sawa utumiaji uwe mdogo kama kutumia pesa kununulia sigara, pombe na kadhalika. Au uwe mkubwa, kama vile mtu kufunga safari za starehe zenye maasi. Pia utumiaji wa mali katika shughuli kwa ajili ya kujionyesha na kujifakharisha. Na hili ni tatizo ambalo linaendelea kutendeka katika jamii zetu za Kiislamu. Mfano utaona katika shughuli za ndoa, mali nyingi zinatumika kufanya mambo ya ziyada ya shughuli hizo, na mambo mengineyo ni ya haramu kama kuweka bendi za muziki na mambo mengineyo ya kuwaigiza makafiri. Na zaidi huwa ni kwa ajili ya kujionyesha, kujifakharisha na kushindana; kila mmoja amshinde mwengine katika shughuli yake aonekana amefanya jambo kuu kuliko mwenziwe.
Yote mawili, israfu na tabdhiyr (ubadhirifu), ni utumiaji wa Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) katika yasiyomridhisha. Lakini binaadam akumbuke na atambue kuwa atakuja kuulizwa na Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kila neema aliyonayo; ameipataje na ameitumiaje. Rejea Suwrah At-Takaathur (102). Na mali ni katika mambo manne ambayo mwanaadam lazima atasimamishwa kuulizwa Siku ya Qiyaamah. Hadiyth ifuatayo imethibitisha:
عَنْ أَبِي بَرْزَةَ الأَسْلَمِيِّ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((لاَ تَزُولُ قَدَمَا عَبْدٍ يَوْمَ الْقِيَامَةِ حَتَّى يُسْأَلَ عَنْ عُمُرِهِ فِيمَا أَفْنَاهُ، وَعَنْ عِلْمِهِ فِيمَ فَعَلَ، وَعَنْ مَالِهِ مِنْ أَيْنَ اكْتَسَبَهُ وَفِيمَ أَنْفَقَهُ وَعَنْ جِسْمِهِ فِيمَ أَبْلاَهُ)) رواه الترمذي وقال: حديث حسن صحيح
Amesimulia Abuu Barzah Al-Aslamiyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nyayo za mja hazitoondoka (Siku ya Qiyaamah) mpaka aulizwe juu ya umri wake alivyoumaliza, ilimu yake alivyoifanyia, mali yake ameichuma kutoka wapi na ameitumia kwa mambo gani, na mwili wake aliutumia kwa kazi gani.” [At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyh]
[12] Kauli Nzito Mno Kumsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwa Ana Wana Wa Kike!
Mbingu na majabali yanakaribia kupasuka kwa kauli nzito ya usingiziaji kama huu: Rejea Maryam (19:88-95).
Na usingiziaji mwengine ni kudai kwamba Malaika ni banaati (wana wa kike) wa Allaah (سبحانه وتعالى)! Rejea Asw-Swaaffaat (37:149-156), Az-Zukhruf (43:19), na An-Nahl (16:57-59).
Na kwa ujumla, usingiziaji wa kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Ana mwana umetajwa kwenye An-Nisaa (4:171), na Al-Maaidah (5:73-75).
[13] Makafiri Wangelitafuta Njia Ya Kufikia Katika ‘Arsh Ya Allaah (عزّ وجلّ)
Imaam As-Sa’diy amesema: Yaani wangechukua njia ya kumfikia Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kumwabudu, na kurudia Kwake, na kujikurubisha Kwake. Basi vipi mja faqiri ambaye anaona shida ya ufaqiri wake amwabudu mungu mwengineo pamoja na Allaah? Hii hapana isipokuwa dhulma katika dhulma kubwa na ujinga ulio mkubwa kabisa. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Yaani: Wanatafuta njia na wanajitahidi kumshinda Allaah (سبحانه وتعالى), kwa hivyo ama wapande wawe juu Yake, lakini Anayetukuka na kushinda na kudhibiti ni Rabb Mwabudiwa. Ama wanajua na wanakiri kwamba miungu yao wanayoiabudu badala ya Allaah imetiishwa na hawana uhusiano wowote na jambo hilo. Basi kwa nini waliwachukua wakiwa katika hali hii? Hii itakuwa kama Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) katika Al-Muuminuwn (23:91). [Tafsiyr As-Sa’diy]
[15] Nyoyo Za Makafiri Zimefunikwa Na Masikio Yana Uziwi:
Rejea Al-An’aam (6:25), Fusw-Swilat (41:5), Al-Kahf (18:57).
[16] Kufufuliwa Ni Katika Nguzo Sita Za Imaan Na Katika Mambo Ya Ghaibu. Makafiri Hawakuamini Kwamba Watafufuliwa:
Aayah hii na zinazofuatia hadi ya (59) na pia Aayah ya (98), zinataja kuwa makafiri hawakuwa wanaamini kabisa kwamba watafufuliwa Siku ya Qiyaamah na kwamba watarudi kuwa katika umbo jipya. Rejea Al-An’aam (6:29), Ar-Ra’d (13:5), Qaaf (50:3), Al-Muuminuwn (23:35-37), (23:82-83), Asw-Swaaffaat (37:16-17), Al-Qiyaamah (75:3-4) Na hawakuamini kwamba watakusanywa na kusimamishwa kuhesabiwa matendo yao, ilhali Allaah (سبحانه وتعالى) Amethibitisha hilo katika Qur-aan kwamba Atafufua viumbe vyote na watahesabiwa matendo yao na kulipwa wanavyostahiki kulipwa. Miongoni mwa Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى) kuhusu hayo ni katika Suwrah za Yaasiyn (36:48-54), (36:77-83), Al-Waaqi’ah (56:47-50), Al-Hajj (22:5–7), na At-Taghaabun (64:7), Al-Qiyaamah (75:36-40). Na iweje Allaah (سبحانه وتعالى) Asiweze kuwafufua ilhali Yeye ni Mweza wa kuwafufua viumbe katika umbo jipya kabisa. Rejea Al-Anbiyaa (17:104). Na hilo ni jambo jepesi kabisa kama Anavyosema katika Kauli Zake za Suwrah Luqmaan (31:28), na Ar-Ruwm (30:27). Na Anasema kuwa uumbaji Wake wa mbingu na ardhi ni mkubwa zaidi kulikoni kumuumba mwanaadam, rejea Kauli Yake katika Ghaafir (40:57). Reja pia An-Naazi’aat (79:27). Hali kadhaalika, Hadiyth kadhaa za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) zimethibitisha jambo hili la kufufuliwa Siku ya Qiyaamah na kuhesabiwa matendo. Na kuamini Aakhirah na matukio yake kama ya kufufuliwa ni mojawapo ya nguzo sita za imaan. Na haya ni katika mambo ya ghaibu ambayo kuyaamini ni katika sifa kuu za Muumini. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Amelitilia umuhimu mkubwa hadi kwamba likawa ni jambo la kwanza kutangulizwa katika Suwrah ya pili ya Qur-aan. Rejea Al-Baqarah (2:3) kwenye maelezo bayana kuhusu yepi ya ghaibu.
Rejea pia Suwrah zifuatazo zenye ukanushaji wa makafiri kuhusu kufufuliwa: Sabaa (34:3), Yuwnus (10:53), Yaasiyn (36:78).
[17] Shaytwaan Huchochea Waja Wa Allaah Na Ni Adui Bayana!:
Rejea Suwrah hii Aayah (64) na Suwrah Ibraahiym (14:22) kwenye rejea nyenginezo za kutahadharishwa na shaytwaan.
[19] Al-Lawh Al-Mahfuwdh (Ubao Uliohifadhiwa): Rejea Ar-Ra’d (13:39).
[21] Ndoto Aliyoonyeshwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Na Ni Mti Wa Az-Zaqquwm:
Ndoto aliyoonyeshwa katika safari ya muujiza ya Al-Israa Wal-Mi’raaj [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Mti huo ni Mti wa Az-Zaqquwm ambao ni mti ulioko katika Moto wa Jahannam. [Tafsiyr As-Sa’diy, na Ibn Kathiyr]. Rejea Ad-Dukhaan (44:43-46), na Asw-Swaaffaat (37:62-68).
[22] Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwaamrisha Malaika Wamsujudie Binaadam Wakasujudu Wote Isipokuwa Ibliys:
Rejea Al-Baqarah (2:34), Al-A’raaf (7:11-18), Al-Hijr (15:28-40), Swaad (38-37-85).
[23] Njia Za Shaytwaan Kuwachochea Wanaadam:
Kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَاسْتَفْزِزْ مَنِ اسْتَطَعْتَ مِنْهُم بِصَوْتِكَ
“Na wachochee kilaini uwawezao miongoni mwao kwa sauti yako.”
Mujaahid amesema: Ni upuuzi na nyimbo (muziki). [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Na Imaam As-Sa’diy amesema: Aayah hii inamhusu kila anayelingania maasi. Na maana yake ni kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Amewafanyia mtihani Waja Wake kwa adui huyu wa wazi, anayewaitia katika kumuasi Allaah (سبحانه وتعالى) kwa maneno yake na matendo yake.
Hii ni pamoja na kila uasi unaohusiana na mali zao na watoto wao, kama vile kuzuia Zakaah, kutokutimiza kafara, na haki za wajibu. Pia, kutokuwafunza adabu njema Watoto, kutokuwalea malezi mema ya kheri, na kutowaongoza njia ya kuepuka shari. Kadhalika, kuchukua mali za watu bila ya haki (kwa dhulma), au kuiweka mali mahala pasipostahiki, au kutumia chumo haramu kujinufaisha.
Bali Mufassiruna wengi wameeleza kwamba kutokupiga BismiLLaahi wakati wa kula au kunywa au kufanya jimai, yote hayo yanaingia katika kushirikiana na shaytwaan katika mali na watoto, na kwamba kama mtu hakupiga BismiLLaahi katika haya, basi shaytwaan hushirikiana naye kama ilivyoelezwa katika Hadiyth. [Imaam As-Sa’diy]
عَنْ عِيَاضِ بْنِ حِمَارٍ الْمُجَاشِعِيِّ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ ذَاتَ يَوْمٍ فِي خُطْبَتِهِ " أَلاَ إِنَّ رَبِّي أَمَرَنِي أَنْ أُعَلِّمَكُمْ مَا جَهِلْتُمْ مِمَّا عَلَّمَنِي يَوْمِي هَذَا كُلُّ مَالٍ نَحَلْتُهُ عَبْدًا حَلاَلٌ وَإِنِّي خَلَقْتُ عِبَادِي حُنَفَاءَ كُلَّهُمْ وَإِنَّهُمْ أَتَتْهُمُ الشَّيَاطِينُ فَاجْتَالَتْهُمْ عَنْ دِينِهِمْ وَحَرَّمَتْ عَلَيْهِمْ مَا أَحْلَلْتُ لَهُمْ وَأَمَرَتْهُمْ أَنْ يُشْرِكُوا بِي مَا لَمْ أُنْزِلْ بِهِ سُلْطَانًا
Hadiyth ya ‘Iyaadhw bin Himaar Al-Mujaashi’iyy (رضي الله عنه): Kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema siku ile katika khutba yake: “Jueni na tambueni kwamba hakika Rabbi wangu Ameniamuru niwafundisheni msiyoyajua katika mambo Aliyonifundisha hivi leo. (Hayo Aliyonifundisha ni): Mali yoyote Niliyomtunuku mja basi ni halali yake, na hakika Mimi Nimewaumba Waja Wangu wote wakiwa safi wenye kuelemea haki, lakini mashaytwaan wakawajia, wakawaengua mbali na dini yao, lakini pia wakawaharamishia Niliyowahalalishia, na wakawaamuru wanishirikishe Mimi kwa mambo ambayo Sikuteremsha kwayo dalili.” [Muslim]
Rejea Suwrah Ibraahiym (14:22) na rejea nyenginezo zilizotajwa humo za jinsi shaytwaan anavyokanusha wanaadam aliowapoteza na matahadharisho ya kumfuata shaytwaan.
[24] Wanaadam Kukirimiwa Na Kutukuzwa Na Allaah (سبحانه وتعالى):
Haya ni kutokana na Ukarimu Wake Allaah (سبحانه وتعالى) kwao, na Ihsaan Yake bila ya kipimo, kwani Amewatukuza wanaadam kwa sifa zote za utukufu. Akawatukuza kwa ilimu na akili, na kuwatumia Rusuli, na kuwateremshia Vitabu, na kuwajaalia miongoni mwao kuwa ni awliyaa (vipenzi) na waliotakaswa, na Akajaalia neema za dhahiri na za kufichika. [Imaam As-Sa’diy]
[25] Maana Ya إمام )Imaam(:
Imaam ina maana kadhaa. Rejea An-Nahl (16:120).
‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu maana ya بِإِمَامِهِمْ katika Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
يَوْمَ نَدْعُو كُلَّ أُنَاسٍ بِإِمَامِهِمْ ۖ
“Siku Tutakayoita watu wote pamoja na rekodi zao za matendo (au Nabii wao).”
Mujaahid na Qataadah wamesema ni Nabii wao kutokana na Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwrah Yuwnus (10:47).
Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Ni Kitabu cha amali zao walizozitenda duniani. Na wamesema hivyo pia Abu Al-‘Aaliyah, Al-Hasan na Adhw-Dhwahaak, na kwamba hii ni kauli iliyo na nguvu kabisa, na wakataja Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى) katika Yaasiyn (36:12), Al-Kahf (18:49), Al-Jaathiyah (45:28-29).
Lakini hii haipingani pia na kuja kwa Nabii wao pindi Allaah (سبحانه وتعالى) Atakapohukumu nyumati zote Siku ya Qiyaamah, kwa sababu hakuna budi aweko wa kushuhudia amali zao kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwrah Al-Baqarah (2:143), An-Nisaa (4:41), Al-Hajj (22:78), Az-Zumar (39:69-70) na Al-Jaathiyah (45:28). Lakini hapa imekusudiwa Kitabu cha amali, ndio maana Allaah (سبحانه وتعالى) Anamalizia kusema katika Aayah hii:
يَوْمَ نَدْعُو كُلَّ أُنَاسٍ بِإِمَامِهِمْ ۖ فَمَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَأُولَـٰئِكَ يَقْرَءُونَ كِتَابَهُمْ وَلَا يُظْلَمُونَ فَتِيلًا ﴿٧١﴾
“Siku Tutakayoita watu wote pamoja na rekodi zao za matendo (au Nabii wao). Basi atakayepewa kitabu chake kuliani mwake, hao watasoma kitabu chao na wala hawatodhulumiwa kadiri ya uzi katika kokwa ya tende.” [Al-Israa (17:71)]
[26] Desturi Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwaadhibu Makafiri Na Kuwajaalia Ushindi Waumini: Rejea Aal-‘Imraan (3:137), Yuwsuf (12:109).
[27] Fadhila Za Qiyaamul-Layl (Kisimamo Cha Usiku):
Fadhila za Qiyaamul-Layl (kisimamo cha usiku) kufanya ibaada zimetajwa katika Qur-aan na Sunnah sehemu nyingi. Rejea As-Sajdah (32:17), Adh-Dhaariyaat: (51:15-19), Al-Furqaan (25:63-64), Az-Zumar (39:9), Aal-‘Imraan (3:17), (3:113), Al-Muzzammil: (73:2).
[28] مَقَامًا مَّحْمُودًا : Maqaaman Mahmuwdan:: (Cheo Cha Kuhimidiwa)
“Maqaamun Mahmuwdun” ni cheo cha kuhimidiwa (kusifiwa). Ni cheo ambacho Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ataomba Uombezi Mkuu "الشَّفَاعَةُ العُظْمَى" ili mambo yafunguke baada ya watu kuchoshwa na kutaabika mno na kisimamo kirefu cha kusubiri hisabu Siku ya Qiyaamah. Kwanza, watu watamwendea Nabiy Aadam (عليه السّلام) wamtake aombe Shafaa’ah ili mambo yafunguke, naye atatoa udhuru, kisha watamwendea Nabiy Nuwh (عليه السّلام), kisha Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام), kisha Nabiy Muwsaa (عليه السّلام), na Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام), lakini wote watatoa nyudhuru. Hatimaye wataelekezwa waombe kwa Sayyid (Bwana) wa wana wa Aadam yaani Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), ili Allaah Awarehemu kutokana na khofu ya hali ya juu na dhiki ya Siku hiyo. Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) atawaombea Shafaa’ah kwa Rabb wake, na Allaah (عزّ وجلّ) Atamuitikia na Atamsimamisha mahali patakapotamaniwa na kila wa mwanzo na wa mwisho, na itakuwa ni fadhila kwake juu ya viumbe wote. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Duaa Baada Ya Adhaan Kumuombea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Maqaamun Mahmuwdun Ili Upate Shafaa-ah (Uombezi) Wake:
Amesimulia Jaabir Bin ‘Abdillaah (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayesema baada ya kusikia Adhaana:
اللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ الدَّعْوَةِ التَّامَّةِ وَالصَّلاَةِ الْقَائِمَةِ آتِ مُحَمَّدًا الْوَسِيلَةَ وَالْفَضِيلَةَ وَابْعَثْهُ مَقَامًا مَحْمُودًا الَّذِي وَعَدْتَهُ
Ee Rabb wa wito huu uliotimu, na Swalaah ya kudumu! Mpe Muhammad Wasiylah na daraja ya juu zaidi, na Mfufue Umpe Maqaam ya kuhimidiwa Uliyomwahidi.
Basi hapo atastahiki kupata Shafaa’ah (uombezi) yangu Siku ya Qiyaamah.”
[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (614), Abuu Daawuwd (529), At-Tirmidhiy (211) na An-Nasaaiy (2/27)]
[29] Kuingizwa Pa Kheri Na Kutolewa Pa Kheri:
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
رَّبِّ أَدْخِلْنِي مُدْخَلَ صِدْقٍ وَأَخْرِجْنِي مُخْرَجَ صِدْقٍ وَاجْعَل لِّي مِن لَّدُنكَ سُلْطَانًا نَّصِيرًا ﴿٨٠﴾
“Ee Rabb wangu! Niingize mwingizo wa kheri na Nitoe pa kutokea pa kheri na Nijaalie kutoka Kwako (hoja au) mamlaka yenye kunusuru.”
Yaani: Fanya kokote niingiako na kokote nitokako kuwe ni kwa ajili ya kukutii Wewe na kuzitafuta Radhi Zako. Na hii ni kwa sababu ya kujumuisha kwake kumtakasia Allaah na kuafikiana na Amri Yake (ya kuomba duaa hii).
Na:
وَاجْعَل لِّي مِن لَّدُنكَ سُلْطَانًا نَّصِيرًا ﴿٨٠﴾
“Na Nijaalie kutoka Kwako (hoja au) mamlaka yenye kunusuru.”
Yaani: Hoja ya dhahiri kabisa, na uthibitisho usio na shaka kwa yote ninayoyaendea na ninayoyaacha.
Na hii ndiyo hali ya juu kabisa Anayoiteremsha Allaah (عزّ وجلّ) kwa mja, nayo ni kuwa, hali zake zote zinakuwa ni kheri na zenye kumkurubisha kwa Rabb wake, na pia anakuwa na dalili na ushahidi wa wazi kabisa katika hali zake zote. Na hiyo inajumuisha ilimu yenye manufaa, na amali njema, kwa kuyajua yote hayo vyema kwa dalili zake na ushahidi wake. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[30] Haki Itabakia Na Ubatili Utatoweka:
Amesimulia ‘Abdullaah Bin Mas’uwd (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliingia Makkah (mwaka wa kuiteka) na yalikuwepo masanamu mia tatu na sitini kwenye Al-Ka‘bah. Akaanza kuyagonga na bakora iliyokuwa mkononi mwake, huku anasema:
جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ ۚ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا ﴿٨١﴾
“Haki imekuja, na ubatili umetoweka. Hakika ubatili ni wenye kutoweka daima.” [Al-Israa (17:81)]
Na:
جَاءَ الْحَقُّ وَمَا يُبْدِئُ الْبَاطِلُ وَمَا يُعِيدُ ﴿٤٩﴾
“Haki imekuja, na ubatilifu hausimamishi (tena chochote), na wala haurudishi (kitu).” [Saba-a (34:49)] [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
Rejea pia Saba-a (34:49).
[31] Qur-aan Ni Shifaa (Poza, Tiba), Mawaidha, Mwongozo, Rehma:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anatuambia kwamba Kitabu Chake, Alichomteremshia Rasuli Wake Muhammad, (صلى الله عليه وآله وسلم), nayo ni Qur-aan ambayo:
لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ ۖ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ﴿٤٢﴾
“Hakitokifikia ubatili mbele yake wala nyuma yake. Ni Uteremsho kutoka kwa Mwenye Hikmah wa yote, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.” [Fusw-Swilat (41:42)]
Ni shifaa (poza, tiba) na rehma kwa Waumini. Yaani: Inawaondolea yale yaliyomo ndani ya nyoyo zao za shaka, unafiki, shirki, kuchanganyikiwa na kuelemea ubatilifu. Qur-aan inaponya yote hayo. Pia ni rehma ambayo kwayo mtu hupata imaan na hikma na kutafuta wema. Haya ni kwa wale tu wanaoiamini na kuikubali kuwa ni ya haqq (kweli), ni shifaa (poza na tiba) na rehma kwa watu kama hao. Ama kafiri ambaye anajidhulumu nafsi yake kwa ukafiri wake, anapoisikia Qur-aan haimzidishii isipokuwa kujitenga nayo, kuikadhibisha, na kufru (kuikanusha). Tatizo liko kwa kafiri mwenyewe, sio kwa Qur-aan, kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
قُلْ هُوَ لِلَّذِينَ آمَنُوا هُدًى وَشِفَاءٌ ۖ وَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ فِي آذَانِهِمْ وَقْرٌ وَهُوَ عَلَيْهِمْ عَمًى ۚ أُولَـٰئِكَ يُنَادَوْنَ مِن مَّكَانٍ بَعِيدٍ﴿٤٤﴾
“Sema: Hii (Qur-aan) kwa walioamini ni mwongozo na shifaa. Na wale wasioamini, wana uziwi masikioni mwao nayo ni upofu kwao. Hao wanaitwa kutoka mahali mbali.” [Fusw-Swilat (41:44)]
Rejea Suwrah hiyo ya Fusw-Swilat (41:44) na Yuwnus (10:57-58) kwenye uchambuzi kuhusu Qur-aan kuwa ni shifaa (poza na tiba), mawaidha na rehma kwa Waumini.
Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَإِذَا مَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ فَمِنْهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمْ زَادَتْهُ هَـٰذِهِ إِيمَانًا ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا فَزَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَهُمْ يَسْتَبْشِرُونَ﴿١٢٤﴾ وَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَتْهُمْ رِجْسًا إِلَىٰ رِجْسِهِمْ وَمَاتُوا وَهُمْ كَافِرُونَ﴿١٢٥﴾
“Na inapoteremshwa Suwrah, basi miongoni mwao wako wanaosema: Nani kati yenu imemzidishia (Suwrah) hii imaan? Ama wale walioamini huwazidishia imaan nao wanafurahia. Na ama wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi, huwazidishia rijs (unafiki, shaka n.k.) juu ya rijs yao, na wakafa hali wao ni makafiri.” [At-Tawbah (9:124-125)].
Na kuna Aayah nyingi zinazotaja haya. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Rejea Suwrah hiyo ya At-Tawbah (9:124-135) kwenye maelezo kuhusu Qur-aan inaposomwa, inawazidisha Waumini imaan. Ama kafiri na wenye maradhi katika nyoyo zao, haiwazidishii ila rijs (unafiki, shaka kufru n.k).
[34] Roho Ni Jambo La Allaah Pekee:
Sababu ya kuteremka Aayah hii inapatikana Alhidaaya.com 085-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Israa Aayah 085: وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ ۖ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتِيتُم مِّنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا [175]
Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu roho ilokusudiwa: Kuna waliosema ni roho za binaadam, au Jibriyl au Malaika?
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ كُنْتُ أَمْشِي مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي حَرْثٍ بِالْمَدِينَةِ وَهْوَ مُتَّكِئٌ عَلَى عَسِيبٍ، فَمَرَّ بِقَوْمٍ مِنَ الْيَهُودِ فَقَالَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ سَلُوهُ عَنِ الرُّوحِ. وَقَالَ بَعْضُهُمْ لاَ تَسْأَلُوهُ عَنِ الرُّوحِ. فَسَأَلُوهُ فَقَامَ مُتَوَكِّئًا عَلَى الْعَسِيبِ وَأَنَا خَلْفَهُ، فَظَنَنْتُ أَنَّهُ يُوحَى إِلَيْهِ فَقَالَ ((وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتِيتُمْ مِنَ الْعِلْمِ إِلاَّ قَلِيلاً)) فَقَالَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ قَدْ قُلْنَا لَكُمْ لاَ تَسْأَلُوهُ.
Amesimulia ‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه): Nilikuwa natembea na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika mashamba ya Madiynah, naye alikuwa akitembea kwa kuegemea kuti la mtende. Mara akalipita kundi la Mayahudi na wao wakaambizana wamuulize kuhusu roho. Baadhi yao wakasema: Msimuulize kuhusu roho. Lakini wakamuuliza. Akainuka kwa kutegemea kuti la mtende, nami niko nyuma yake, nikidhani kuwa anateremshiwa Wahyi. Kisha akasoma:
وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ ۖ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتِيتُم مِّنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا ﴿٨٥﴾
“Na wanakuuliza kuhusu roho. Sema: Roho ni katika amri ya Rabb wangu. Na hamkupewa ujuzi isipokuwa kidogo tu.”
Hapo baadhi ya Mayahudi wakasema (kuwaambia wenzao): “Si tulikuambieni kuwa msimuulize (hamkusikia)?”
[Al-Bukhaariy – Kitaab At-Tawhiyd]
[36] Changamoto Kwa Makafiri Walete Mfano Wa Qur-aan Lakini Hilo Ni Mustahili:
Rejea Yuwnus (10:38), Al-Baqarah (2:23-24), Atw-Twuwr (52:33-34), Huwd (11:13-14). Rejea pia Al-An’aam (6:93) ambako kumetajwa waongo waliodai Unabii.
[37] Washirikina Kudai Kutumiwa Rasuli Asiyekuwa Binaadam:
Kuanzia Aayah hii (90) hadi (93) washirikina wa Makkah wanadai kuteremshiwa mambo ya ajabu kabisa yote kumpinga Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kuwa yeye ni binaadam. Lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Anawahoji kwa dalili za nguvu kabisa katika Aayah namba (95).
Na hii ndio ada ya washirikina kutowaamini Rusuli wao kwa sababu tu ni binaadam.
Na washirikina wa kaumu za kale walidai hivyo pia. Basi wao na hawa wa Makkah madai yao kama haya kutaka kuteremshiwa asiyekuwa binaadam yalilingana. Rejea Huwd (11:27), Ibraahiym (14:10), Al-Anbiyaa (21:3), Al-Muuminuwn: (23:24), (33-34), (47). Rejea pia Al-Furqaan (25:7), Ash-Shu’araa (26:154), (186). Pia Yaasiyn (36:15), Al-Qamar (54:24) na At-Taghaabun (64:6).
[39] Makafiri Hawakuamini Kwamba Watafufuliwa: Rejea Aayah kwenye Suwrah hii ya Al-Israa (17:49).
[40] Miujiza Tisa Ya Allaah Kwa Watu Wa Firawni: Rejea Al-A’raaf (7:130).
[41] Hikma Ya Qur-aan Kuteremshwa Kwa Vituo Na Kidogo Kidogo:
Kuna hikma kadhaa za kuteremshwa
Qur-aan kwa vituo na kidogo kidogo. Miongoni mwazo ni: kuwasahilishia Swahaba hukmu za makatazo ya maasi waliyokuwa nayo katika Ujaahiliyyah:
Rejea Alhidaaya.com Makala ya: Hikmah Ya Kuteremshwa Qur-aan Kidogokidogo Wakati Mbali Mbali. [176]
Moja ya hikma ni kuwavutia watu kuingia katika Dini kwa kufuata maamrisho yake na makatazo yake polepole, na hii ni njia itumikayo na yenye matunda katika daawah. Kwani ingelikuwa ni kufuata makatazo yote na kufuata maamrisho yote kwa pamoja, basi ingelikuwa ni vigumu sana watu kufuata, na ndio maana kwa muda wa miaka kumi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa Makkah, hakukuwa na zaidi ya kuwaita watu kuingia katika Dini. Neno la “Laa ilaah illa-Allaah” ndilo lililokuwa lengo, hakukuwa na amri za fardhi yoyote wala hukmu zozote.
Mfano, makatazo ya ulevi, kwa vile ulevi ulikuwa ni moja ya maasi makuu, na hata baada ya kuja Uislamu, baadhi ya Swahaba walikuwa bado wakilewa. Hii ni kwa sababu ilikuwa ni ada na desturi zao walizozirithi katika ujaahiliyyah kama zilivyo desturi nyinginezo walizokuwa nazo kama kuwaua watoto wa kike, kuwanyima urithi wanawake n.k. Ukaja Uislamu na kuondosha dhulma zote hizo. Hivyo, jambo kama ulevi lilihitajika hikma ya kuukataza kwa polepole na ndio maana tunaona kwamba kuna Aayah tatu zinazohusiana na makatazo ya ulevi. Ilianza kwanza kwa kutaja madhara yake na manufaa yake, kisha polepole hadi kukataza kabisa. Hadiyth ifuatayo imethibitisha hayo:
حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ مُوسَى، أَخْبَرَنَا هِشَامُ بْنُ يُوسُفَ، أَنَّ ابْنَ جُرَيْجٍ، أَخْبَرَهُمْ قَالَ وَأَخْبَرَنِي يُوسُفُ بْنُ مَاهَكَ، قَالَ إِنِّي عِنْدَ عَائِشَةَ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ ـ رضى الله عنها ـ إِذْ جَاءَهَا عِرَاقِيٌّ فَقَالَ أَىُّ الْكَفَنِ خَيْرٌ قَالَتْ وَيْحَكَ وَمَا يَضُرُّكَ قَالَ يَا أُمَّ الْمُؤْمِنِينَ أَرِينِي مُصْحَفَكِ. قَالَتْ لِمَ قَالَ لَعَلِّي أُوَلِّفُ الْقُرْآنَ عَلَيْهِ فَإِنَّهُ يُقْرَأُ غَيْرَ مُؤَلَّفٍ. قَالَتْ وَمَا يَضُرُّكَ أَيَّهُ قَرَأْتَ قَبْلُ، إِنَّمَا نَزَلَ أَوَّلَ مَا نَزَلَ مِنْهُ سُورَةٌ مِنَ الْمُفَصَّلِ فِيهَا ذِكْرُ الْجَنَّةِ وَالنَّارِ حَتَّى إِذَا ثَابَ النَّاسُ إِلَى الإِسْلاَمِ نَزَلَ الْحَلاَلُ وَالْحَرَامُ، وَلَوْ نَزَلَ أَوَّلَ شَىْءٍ لاَ تَشْرَبُوا الْخَمْرَ. لَقَالُوا لاَ نَدَعُ الْخَمْرَ أَبَدًا. وَلَوْ نَزَلَ. لاَ تَزْنُوا. لَقَالُوا لاَ نَدَعُ الزِّنَا أَبَدًا.
Ametuhadithia Ibraahiym bin Muwsaa, ametujulisha Hishaam bin Yuwsuf, kwamba Ibn Jurayj amewajulisha amesema: Amesema au amenijulisha Yuwsuf bin Maahak kuwa alipokuwa pamoja na ‘Aaishah Mama wa Waumini (رضي الله عنها), mara akaja kwake mtu kutoka Iraaq, akamuuliza: Ni kafani (sanda) gani iliyo bora zaidi? Akasema (رضي الله عنها): Allaah Akurehemu! Itakusaidia nini kujua hilo (ukiwa maiti sanda yoyote utakafiniwa nayo)?! Akasema: Ee Mama wa Waumini, nionyeshe Mswahafu wako. Akasema (رضي الله عنها): Kwa nini? Akasema: Huenda nikaukusanya na kuipanga Qur-aan kulingana nayo, kwani watu wanaisoma pamoja na Suwrah zake sio kwa mpangilio wa sawasawa. Akasema (رضي الله عنها): Haijalishi ni sehemu gani unayosoma mwanzo. (Fahamu kuwa) kitu cha kwanza kuteremshwa kwayo ni Suwrah za al-Mufaswswal (fupi fupi) ambazo kumetajwa ndani yake Jannah na Moto. Na watu wanapokuwa wamekomaa na nafsi zao kutulia juu ya hilo, Aayah kuhusiana na halali na haramu ziliteremshwa. Na lau ingeteremshwa mwanzo (kwa mfano): “Msinywe pombe (mvinyo)”, watu wangesema: “Hatutaacha kunywa (pombe)”. Na lau kungeteremshwa: “Msizini”, watu wangesema: “Hatutaacha kuzini”. [Al-Bukhaariy]
[42] Washirikina Walipinga Jina La Ar-Rahmaan:
Rejea pia Al-Furqaan (25:60).
Sifa hii ya Rahmah ni ya dhati Yake Allaah ambayo haiwezi kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى). Makafiri wa Makkah hawakupenda Sifa na Jina hili la Ar-Rahmaan. Basi wakakataa kuliandika katika mkataba wa Hudaybiyah, pale Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomuamrisha mwandishi wa mkataba andike “BismiLLaah (Kwa Jina la Allaah) Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma) Ar-Rahiym (Mwenye kurehemu).” Wakasema: “Andika: Biismika-Allaahumma.” Hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:
قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ
“Sema: Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan, vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa.” [Al-Israa: 110]
[Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Na ndio maana Suwrah za Qur-aan zinaanza na BismiLLaah ambayo inataja Majina Yake Mawili ya Ar-Rahmaan na Ar-Rahiym. Pia Allaah (سبحانه وتعالى) Ametanguliza katika ufunguzi wa Suwrat Al-Faatihah Akaanza na Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma) na Ar-Rahiym (Mwenye Kurehemu).
Na Imaam As-Sa’diy amefafanua: “Sema, ee Rasuli kuwaambia washirikina wa watu wako waliokupinga kutumia kwako “Yaa Allaah”, “Yaa Rahmaan”, katika duaa zako. Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan kwani kwa Majina yoyote Yake mkimuomba huwa mnamuomba Rabb Mmoja, kwa kuwa Majina Yake yote ni Mazuri. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[43] Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah (سبحانه وتعالى): Rejea Faharasa ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake.
[45] Allaah Yu Mmoja Pekee Hana Mwana Wala Mshirika Wala Msaidizi Basi Mtukuze Matukuzo Makubwa Kabisa:
Washirikina walidai na kumsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba Ana mwana na kwamba Anao wasaidizi na walinzi kwa ajili ya usimamizi wa Ufalme Wake kana kwamba Hana uwezo wa kutekeleza usimamizi wa Ufalme Wake, kwa hiyo Anahitajia wasaidizi na walinzi. Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Anakusha hilo, kwani Ufalme wa mbingu na ardhi ni Wake wote Yeye (سبحانه وتعالى). Naye Yuko Pekee Hana mwana wala mshirika wala msaidizi. Yeye ni Mkwasi, Hahitaji chochote kwa viumbe, bali wao mafakiri ndio wenye kumhitaji, na wao ndio wenye udhalili. Hivyo, Allaah Anaamrisha kumhimidi Yeye na kumsifu na kumtukuza kwa Majina Yake Mazuri Kabisa na Sifa Zake Kamilifu. Basi mtukuze kwa matukuzo makubwa kabisa ya Ujalali na Utukufu Wake. AlhamduliLlaah, Yeye ni Allaahu Akbar (Mkuu wa Dhati kwa Sifa na Matendo).
الْكَهْف
018-Al-Kahf
018-Al-Kahf: Utangulizi Wa Suwrah [179]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي أَنزَلَ عَلَىٰ عَبْدِهِ الْكِتَابَ وَلَمْ يَجْعَل لَّهُ عِوَجًا ۜ﴿١﴾
1. AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah) Ambaye Amemteremshia Mja Wake (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu na wala Hakukifanya kiwe upogo.[1]
قَيِّمًا لِّيُنذِرَ بَأْسًا شَدِيدًا مِّن لَّدُنْهُ وَيُبَشِّرَ الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا حَسَنًا ﴿٢﴾
2. Kimenyooka sawa ili kionye adhabu shadidi kutoka Kwake (Allaah), na kiwabashirie Waumini watendao mema kwamba watapata ujira mzuri.
مَّاكِثِينَ فِيهِ أَبَدًا ﴿٣﴾
3. Wakae humo abadi.
وَيُنذِرَ الَّذِينَ قَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا ﴿٤﴾
4. Na kiwaonye wanaosema: Allaah Amejifanyia mwana.
مَّا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ وَلَا لِآبَائِهِمْ ۚ كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ ۚ إِن يَقُولُونَ إِلَّا كَذِبًا ﴿٥﴾
5. Hawana ilimu yoyote kwayo wao na hata baba zao. Neno kubwa kabisa linatoka vinywani mwao. Hawasemi isipokuwa uongo tu.
فَلَعَلَّكَ بَاخِعٌ نَّفْسَكَ عَلَىٰ آثَارِهِمْ إِن لَّمْ يُؤْمِنُوا بِهَـٰذَا الْحَدِيثِ أَسَفًا ﴿٦﴾
6. Basi huenda ukaiangamiza nafsi yako (kwa ghamu na huzuni ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa ajili yao kwa ghamu na huzuni kwa kuwa wao hawatoamini ujumbe huu (Qur-aan).
إِنَّا جَعَلْنَا مَا عَلَى الْأَرْضِ زِينَةً لَّهَا لِنَبْلُوَهُمْ أَيُّهُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ﴿٧﴾
7. Hakika Sisi Tumefanya vilivyoko juu ya ardhi kuwa ni pambo lake ili Tuwajaribu, nani miongoni mwao mwenye amali nzuri zaidi.
وَإِنَّا لَجَاعِلُونَ مَا عَلَيْهَا صَعِيدًا جُرُزًا ﴿٨﴾
8. Na hakika Sisi bila shaka Tutafanya vilivyo juu yake kuwa udongo mkavu usiomea chochote.
أَمْ حَسِبْتَ أَنَّ أَصْحَابَ الْكَهْفِ وَالرَّقِيمِ كَانُوا مِنْ آيَاتِنَا عَجَبًا ﴿٩﴾
9. Je, unadhani kwamba watu wa pangoni[2] na maandiko walikuwa ni ajabu zaidi kati ya Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu?
إِذْ أَوَى الْفِتْيَةُ إِلَى الْكَهْفِ فَقَالُوا رَبَّنَا آتِنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً وَهَيِّئْ لَنَا مِنْ أَمْرِنَا رَشَدًا ﴿١٠﴾
10. Pale vijana walipokimbilia katika pango wakasema: Rabb wetu! Tupe kutoka Kwako Rehma, na Tutengenezee katika jambo letu mwongozo wa sawa.
فَضَرَبْنَا عَلَىٰ آذَانِهِمْ فِي الْكَهْفِ سِنِينَ عَدَدًا ﴿١١﴾
11. Tukawaziba masikio yao pangoni (kuwalaza) kwa idadi ya miaka mingi.
ثُمَّ بَعَثْنَاهُمْ لِنَعْلَمَ أَيُّ الْحِزْبَيْنِ أَحْصَىٰ لِمَا لَبِثُوا أَمَدًا ﴿١٢﴾
12. Kisha Tukawainua ili Tupambanue nani kati ya makundi mawili lililohesabu madhubuti zaidi kuhusu muda wao waliobakia.
نَّحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ نَبَأَهُم بِالْحَقِّ ۚ إِنَّهُمْ فِتْيَةٌ آمَنُوا بِرَبِّهِمْ وَزِدْنَاهُمْ هُدًى ﴿١٣﴾
13. Sisi Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) khabari zao kwa haki. Hakika wao ni vijana waliomwamini Rabb wao na Tukawazidishia hidaya.
وَرَبَطْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ إِذْ قَامُوا فَقَالُوا رَبُّنَا رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَن نَّدْعُوَ مِن دُونِهِ إِلَـٰهًا ۖ لَّقَدْ قُلْنَا إِذًا شَطَطًا ﴿١٤﴾
14. Na Tukazitia nguvu nyoyo zao waliposimama wakasema: Rabb wetu, ni Rabb wa mbingu na ardhi. Hatutomuomba asiyekuwa Yeye kuwa mwabudiwa, (laa sivyo) kwa yakini hapo tutakuwa tumesema kauli ya kufuru na kuvuka mpaka.
هَـٰؤُلَاءِ قَوْمُنَا اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ آلِهَةً ۖ لَّوْلَا يَأْتُونَ عَلَيْهِم بِسُلْطَانٍ بَيِّنٍ ۖ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا ﴿١٥﴾
15. Hawa watu wetu wamejichukulia waabudiwa wengine badala Yake. Kwa nini basi hawawatolei ushahidi wa bayana? Basi nani dhalimu zaidi kuliko anayemtungia Allaah uongo?
وَإِذِ اعْتَزَلْتُمُوهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّـهَ فَأْوُوا إِلَى الْكَهْفِ يَنشُرْ لَكُمْ رَبُّكُم مِّن رَّحْمَتِهِ وَيُهَيِّئْ لَكُم مِّنْ أَمْرِكُم مِّرْفَقًا ﴿١٦﴾
16. Na mkijitenga nao na vile wanavyoviabudu badala ya Allaah, basi kimbilieni pangoni. Rabb wenu Atakukunjulieni Rehma Zake, na Atakutengenezeeni kwa wepesi ya kukufaeni katika mambo yenu.
وَتَرَى الشَّمْسَ إِذَا طَلَعَت تَّزَاوَرُ عَن كَهْفِهِمْ ذَاتَ الْيَمِينِ وَإِذَا غَرَبَت تَّقْرِضُهُمْ ذَاتَ الشِّمَالِ وَهُمْ فِي فَجْوَةٍ مِّنْهُ ۚ ذَٰلِكَ مِنْ آيَاتِ اللَّـهِ ۗ مَن يَهْدِ اللَّـهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِ ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُ وَلِيًّا مُّرْشِدًا ﴿١٧﴾
17. Na (ungelikuweko, basi ungelikuwa) unaliona jua linapochomoza linaelemea pango lao kwa upande wa kulia, na linapokuchwa linawakwepa upande wa kushoto, nao wamo katika uwazi wa humo. Hiyo ni miongoni mwa Aayaat (Ishara, Dalili) za Allaah. Ambaye Allaah Amemwongoza, basi huyo ndiye aliyehidika. Na Anayemwacha kupotoka basi hutompatia rafiki mlinzi wa kumuongoza.
وَتَحْسَبُهُمْ أَيْقَاظًا وَهُمْ رُقُودٌ ۚ وَنُقَلِّبُهُمْ ذَاتَ الْيَمِينِ وَذَاتَ الشِّمَالِ ۖ وَكَلْبُهُم بَاسِطٌ ذِرَاعَيْهِ بِالْوَصِيدِ ۚ لَوِ اطَّلَعْتَ عَلَيْهِمْ لَوَلَّيْتَ مِنْهُمْ فِرَارًا وَلَمُلِئْتَ مِنْهُمْ رُعْبًا ﴿١٨﴾
18. Na (ungeliwaona, basi) utawadhania wako wamacho na hali wao wamelala. Na Tunawageuza upande wa kulia na upande wa kushoto. Na mbwa wao amenyoosha miguu yake ya mbele kizingitini. Kama ungeliwatokea, bila shaka ungegeuka kuwakimbia, na bila shaka ungejazwa tisho kubwa kuwaogopa.
وَكَذَٰلِكَ بَعَثْنَاهُمْ لِيَتَسَاءَلُوا بَيْنَهُمْ ۚ قَالَ قَائِلٌ مِّنْهُمْ كَمْ لَبِثْتُمْ ۖ قَالُوا لَبِثْنَا يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ ۚ قَالُوا رَبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا لَبِثْتُمْ فَابْعَثُوا أَحَدَكُم بِوَرِقِكُمْ هَـٰذِهِ إِلَى الْمَدِينَةِ فَلْيَنظُرْ أَيُّهَا أَزْكَىٰ طَعَامًا فَلْيَأْتِكُم بِرِزْقٍ مِّنْهُ وَلْيَتَلَطَّفْ وَلَا يُشْعِرَنَّ بِكُمْ أَحَدًا ﴿١٩﴾
19. Na hivyo ndivyo Tulivyowaamsha (katika usingizi mrefu) ili waulizane baina yao. Msemaji miongoni mwao akasema: Muda gani mmekaa? Wakasema: Tumekaa siku moja au sehemu ya siku. Wakasema: Rabb wenu Anajua zaidi muda mliokaa. Basi tumeni mmoja wenu mjini kwa noti zenu hizi atazame chakula chake kipi kifaacho zaidi kisha akuleteeni chakula hicho. Na awe makini na busara, na wala asikutambulisheni kwa yeyote.
إِنَّهُمْ إِن يَظْهَرُوا عَلَيْكُمْ يَرْجُمُوكُمْ أَوْ يُعِيدُوكُمْ فِي مِلَّتِهِمْ وَلَن تُفْلِحُوا إِذًا أَبَدًا ﴿٢٠﴾
20. Hakika wao wakikugundueni, watakupigeni mawe au watakurudisheni katika dini yao, na hapo hamtofaulu abadani.
وَكَذَٰلِكَ أَعْثَرْنَا عَلَيْهِمْ لِيَعْلَمُوا أَنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَأَنَّ السَّاعَةَ لَا رَيْبَ فِيهَا إِذْ يَتَنَازَعُونَ بَيْنَهُمْ أَمْرَهُمْ ۖ فَقَالُوا ابْنُوا عَلَيْهِم بُنْيَانًا ۖ رَّبُّهُمْ أَعْلَمُ بِهِمْ ۚ قَالَ الَّذِينَ غَلَبُوا عَلَىٰ أَمْرِهِمْ لَنَتَّخِذَنَّ عَلَيْهِم مَّسْجِدًا ﴿٢١﴾
21. Na hivyo ndivyo Tulivyowatambulisha kwa watu ili wajue kwamba Ahadi ya Allaah ni haki. Na kwamba Saa (Qiyaamah) haina shaka yoyote. Pale walipozozana baina yao kuhusu jambo lao. Wakasema: Jengeni jengo juu yao, Rabb wao Anawajua vyema. Wakasema wale walioshinda katika shauri lao: Bila shaka tutajenga mahali pa ibaada juu yao.
سَيَقُولُونَ ثَلَاثَةٌ رَّابِعُهُمْ كَلْبُهُمْ وَيَقُولُونَ خَمْسَةٌ سَادِسُهُمْ كَلْبُهُمْ رَجْمًا بِالْغَيْبِ ۖ وَيَقُولُونَ سَبْعَةٌ وَثَامِنُهُمْ كَلْبُهُمْ ۚ قُل رَّبِّي أَعْلَمُ بِعِدَّتِهِم مَّا يَعْلَمُهُمْ إِلَّا قَلِيلٌ ۗ فَلَا تُمَارِ فِيهِمْ إِلَّا مِرَاءً ظَاهِرًا وَلَا تَسْتَفْتِ فِيهِم مِّنْهُمْ أَحَدًا ﴿٢٢﴾
22. Watasema: Watatu na wanne wao ni mbwa wao. Na (wengine) wanasema: Watano, na wa sita wao ni mbwa wao - kwa kuvurumisha bila ya kujua. Na (wengine) wanasema: Saba, na wa nane wao ni mbwa wao. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Rabb wangu Anajua zaidi idadi yao. Hakuna anayewajua isipokuwa wachache tu. Basi usibishane nao isipokuwa mabishano ya hoja kuntu (Tuliyokufunulia Wahy), na wala usimuulize yeyote kuhusu khabari zao.
وَلَا تَقُولَنَّ لِشَيْءٍ إِنِّي فَاعِلٌ ذَٰلِكَ غَدًا ﴿٢٣﴾
23. Na wala usiseme kamwe kwa jambo lolote lile: Nitalifanya hilo kesho.[3]
إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ ۚ وَاذْكُر رَّبَّكَ إِذَا نَسِيتَ وَقُلْ عَسَىٰ أَن يَهْدِيَنِ رَبِّي لِأَقْرَبَ مِنْ هَـٰذَا رَشَدًا ﴿٢٤﴾
24. Isipokuwa (useme): In Shaa Allaah. Na mdhukuru Rabb wako unaposahau.[4] Na sema: Asaa Rabb wangu Akaniongoa njia iliyo karibu zaidi ya uongofu kuliko hii.
وَلَبِثُوا فِي كَهْفِهِمْ ثَلَاثَ مِائَةٍ سِنِينَ وَازْدَادُوا تِسْعًا ﴿٢٥﴾
25. Na walikaa pangoni mwao miaka mia tatu na wakazidisha tisa.
قُلِ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا لَبِثُوا ۖ لَهُ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ أَبْصِرْ بِهِ وَأَسْمِعْ ۚ مَا لَهُم مِّن دُونِهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا يُشْرِكُ فِي حُكْمِهِ أَحَدًا ﴿٢٦﴾
26. Sema: Allaah Anajua zaidi muda waliokaa. Ni Yake Pekee ghaibu za mbingu na ardhi. Kuona kulioje Kwake na Kusikia! Hawana pasi Naye mlinzi yeyote na wala Hamshirikishi katika Hukumu Zake yeyote.
وَاتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِن كِتَابِ رَبِّكَ ۖ لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ وَلَن تَجِدَ مِن دُونِهِ مُلْتَحَدًا ﴿٢٧﴾
27. Na soma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uliyofunuliwa Wahy katika Kitabu cha Rabb wako. Hakuna yeyote atakayeweza kubadilisha Maneno Yake, na wala hutopata kamwe makimbilio isipokuwa Kwake.
وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ تُرِيدُ زِينَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُ عَن ذِكْرِنَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا ﴿٢٨﴾
28. Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Rabb wao asubuhi kabla jua kucha na jioni, wanataka Wajihi Wake. Na wala macho yako yasiwavuke kwa kutaka pambo la uhai wa dunia. Na wala usimtii Tuliyemghafilisha moyo wake na Ukumbusho Wetu akafuata hawaa zake, na jambo lake limekuwa la kuzidi kuvuka mipaka.
وَقُلِ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَن شَاءَ فَلْيُؤْمِن وَمَن شَاءَ فَلْيَكْفُرْ ۚ إِنَّا أَعْتَدْنَا لِلظَّالِمِينَ نَارًا أَحَاطَ بِهِمْ سُرَادِقُهَا ۚ وَإِن يَسْتَغِيثُوا يُغَاثُوا بِمَاءٍ كَالْمُهْلِ يَشْوِي الْوُجُوهَ ۚ بِئْسَ الشَّرَابُ وَسَاءَتْ مُرْتَفَقًا ﴿٢٩﴾
29. Na sema: Hii ni haki kutoka kwa Rabb wenu. Basi anayetaka aamini, na anayetaka akufuru. Hakika Sisi Tumewaandalia madhalimu moto ambao kuta zake zitawazunguka. Na wakiomba uokozi, watapewa maji kama masazo ya zebaki nyeusi iliyoyeyushwa yanayobabua nyuso. Ubaya ulioje kinywaji hicho, na uovu ulioje mahali pa kupumzikia!
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ مَنْ أَحْسَنَ عَمَلًا ﴿٣٠﴾
30. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, hakika Sisi Hatupotezi ujira wa anayetenda amali nzuri kabisa.
أُولَـٰئِكَ لَهُمْ جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ وَيَلْبَسُونَ ثِيَابًا خُضْرًا مِّن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَّكِئِينَ فِيهَا عَلَى الْأَرَائِكِ ۚ نِعْمَ الثَّوَابُ وَحَسُنَتْ مُرْتَفَقًا ﴿٣١﴾
31. Hao watapata Jannaat za kudumu milele zipitazo chini yao mito, watapambwa humo vikuku vya dhahabu, na watavaa nguo za kijani za hariri laini na hariri nzito nyororo, wakiegemea humo kwenye makochi ya fakhari. Uzuri ulioje wa thawabu na mahali pazuri palioje pa kupumzikia!
وَاضْرِبْ لَهُم مَّثَلًا رَّجُلَيْنِ جَعَلْنَا لِأَحَدِهِمَا جَنَّتَيْنِ مِنْ أَعْنَابٍ وَحَفَفْنَاهُمَا بِنَخْلٍ وَجَعَلْنَا بَيْنَهُمَا زَرْعًا ﴿٣٢﴾
32. Na wapigie mfano wa watu wawili. Tulimjaalia mmoja wao bustani mbili za mizabibu, na Tukazizungushia kwa mitende, na Tukaweka baina yake mimea.
كِلْتَا الْجَنَّتَيْنِ آتَتْ أُكُلَهَا وَلَمْ تَظْلِم مِّنْهُ شَيْئًا ۚ وَفَجَّرْنَا خِلَالَهُمَا نَهَرًا ﴿٣٣﴾
33. Bustani zote mbili zilitoa mazao yake, na wala hazikupunguza humo chochote. Na Tukabubujua baina yake mto.
وَكَانَ لَهُ ثَمَرٌ فَقَالَ لِصَاحِبِهِ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ أَنَا أَكْثَرُ مِنكَ مَالًا وَأَعَزُّ نَفَرًا ﴿٣٤﴾
34. Naye alikuwa ana mazao mengine (mbali ya bustani mbili). Akamwambia sahibu yake naye huku akizungumza na kujibishana naye: Mimi nina mali zaidi kuliko wewe, na nguvu zaidi za watu.
وَدَخَلَ جَنَّتَهُ وَهُوَ ظَالِمٌ لِّنَفْسِهِ قَالَ مَا أَظُنُّ أَن تَبِيدَ هَـٰذِهِ أَبَدًا ﴿٣٥﴾
35. Akaingia bustanini mwake hali ya kuwa anajidhulumu nafsi yake, akasema: Sidhani kama haya yatatoweka abadani.
وَمَا أَظُنُّ السَّاعَةَ قَائِمَةً وَلَئِن رُّدِدتُّ إِلَىٰ رَبِّي لَأَجِدَنَّ خَيْرًا مِّنْهَا مُنقَلَبًا ﴿٣٦﴾
36. Na wala sidhani kama Saa itasimama. Na hata kama nitarudishwa kwa Rabb wangu, bila shaka nitakuta marejeo bora kuliko haya.
قَالَ لَهُ صَاحِبُهُ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ أَكَفَرْتَ بِالَّذِي خَلَقَكَ مِن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ سَوَّاكَ رَجُلًا ﴿٣٧﴾
37. Sahibu yake akamwambia na huku anajadiliana naye: Je, umemkufuru Yule Aliyekuumba kutokana na mchanga, kisha kutokana na manii, kisha Akakusawazisha kuwa mtu?
لَّـٰكِنَّا هُوَ اللَّـهُ رَبِّي وَلَا أُشْرِكُ بِرَبِّي أَحَدًا ﴿٣٨﴾
38. Lakini (mimi naamini) Yeye Allaah Ndiye Rabb wangu, na wala sitomshirikisha Rabb wangu na yeyote.
وَلَوْلَا إِذْ دَخَلْتَ جَنَّتَكَ قُلْتَ مَا شَاءَ اللَّـهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّـهِ ۚ إِن تَرَنِ أَنَا أَقَلَّ مِنكَ مَالًا وَوَلَدًا ﴿٣٩﴾
39. Na lau ulipoingia bustanini mwako ungelisema: Maa Shaa Allaah! Hapana nguvu ila za Allaah. Japo kama unaniona mimi nina mali na watoto kidogo kuliko wewe.
فَعَسَىٰ رَبِّي أَن يُؤْتِيَنِ خَيْرًا مِّن جَنَّتِكَ وَيُرْسِلَ عَلَيْهَا حُسْبَانًا مِّنَ السَّمَاءِ فَتُصْبِحَ صَعِيدًا زَلَقًا ﴿٤٠﴾
40. Basi asaa Rabb wangu Akanipa yaliyo bora kuliko bustani yako, na Akaipelekea maafa kutoka mbinguni, ikapambazukiwa kuwa ardhi kame inayoteleza.
أَوْ يُصْبِحَ مَاؤُهَا غَوْرًا فَلَن تَسْتَطِيعَ لَهُ طَلَبًا ﴿٤١﴾
41. Au yakawa maji yake ya kudidimia kisha hutoweza kuyafuatilia (na kuyapata).
وَأُحِيطَ بِثَمَرِهِ فَأَصْبَحَ يُقَلِّبُ كَفَّيْهِ عَلَىٰ مَا أَنفَقَ فِيهَا وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا وَيَقُولُ يَا لَيْتَنِي لَمْ أُشْرِكْ بِرَبِّي أَحَدًا ﴿٤٢﴾
42. Basi mazao yake yakazungukwa (na maafa), akabakia anapindua pindua viganja vyake (kusikitika) juu ya yale aliyoyagharamia humo, nayo imeporomoka juu ya chanja zake na huku anasema: Laiti nisingelimshirikisha Rabb wangu na yeyote.
وَلَمْ تَكُن لَّهُ فِئَةٌ يَنصُرُونَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَمَا كَانَ مُنتَصِرًا ﴿٤٣﴾
43. Na hakuwa ana kundi lolote la kumnusuru pasina Allaah, na wala hakuweza kujisaidia.
هُنَالِكَ الْوَلَايَةُ لِلَّـهِ الْحَقِّ ۚ هُوَ خَيْرٌ ثَوَابًا وَخَيْرٌ عُقْبًا ﴿٤٤﴾
44. Huko (Aakhirah) utawala ni wa Allaah Pekee wa haki. Yeye ni Mbora zaidi wa Kulipa thawabu, na Mbora zaidi wa matokeo ya mwisho.
وَاضْرِبْ لَهُم مَّثَلَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ فَأَصْبَحَ هَشِيمًا تَذْرُوهُ الرِّيَاحُ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُّقْتَدِرًا ﴿٤٥﴾
45. Na wapigie mfano wa uhai wa dunia. Ni kama maji Tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, ikachanganyika nayo mimea ya ardhi (ikasitawi), kisha ikawa mikavu iliyovurugika, inapeperushwa na upepo. Na Allaah daima Ni Mwenye Uwezo wa juu kabisa kwa kila kitu.
الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا ﴿٤٦﴾
46. Mali na watoto ni pambo la uhai wa dunia. Na mema yanayobakia[5] ni bora mbele ya Rabb wako kwa thawabu na matumaini mema zaidi.
وَيَوْمَ نُسَيِّرُ الْجِبَالَ وَتَرَى الْأَرْضَ بَارِزَةً وَحَشَرْنَاهُمْ فَلَمْ نُغَادِرْ مِنْهُمْ أَحَدًا ﴿٤٧﴾
47. Na Siku Tutakapoiendesha milima, na utaiona ardhi tambarare tupu, na Tutawakusanya wala Hatutomwacha hata mmoja katika wao.
وَعُرِضُوا عَلَىٰ رَبِّكَ صَفًّا لَّقَدْ جِئْتُمُونَا كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۚ بَلْ زَعَمْتُمْ أَلَّن نَّجْعَلَ لَكُم مَّوْعِدًا ﴿٤٨﴾
48. Na watahudhurishwa mbele ya Rabb wako safu safu. (Allaah Atawaambia): Kwa yakini mmetujia kama Tulivyokuumbeni mara ya kwanza.[6] Bali mlidai kwamba Hatutakuwekeeni miadi (hii).
وَوُضِعَ الْكِتَابُ فَتَرَى الْمُجْرِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا فِيهِ وَيَقُولُونَ يَا وَيْلَتَنَا مَالِ هَـٰذَا الْكِتَابِ لَا يُغَادِرُ صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً إِلَّا أَحْصَاهَا ۚ وَوَجَدُوا مَا عَمِلُوا حَاضِرًا ۗ وَلَا يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا ﴿٤٩﴾
49. Na kitawekwa Kitabu, basi utaona wahalifu ni wenye khofu kwa yale yaliyomo ndani yake, watasema: Ole wetu! Kitabu hiki kina nini? Hakiachi dogo wala kubwa isipokuwa kimerekodi hesabuni![7] Na watakuta yale waliyoyatenda yamehudhuria hapo. Na Rabb wako Hamdhulumu yeyote.
وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ الْجِنِّ فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِ ۗ أَفَتَتَّخِذُونَهُ وَذُرِّيَّتَهُ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِي وَهُمْ لَكُمْ عَدُوٌّ ۚ بِئْسَ لِلظَّالِمِينَ بَدَلًا ﴿٥٠﴾
50. Na pindi Tulipowaambia Malaika: Msujudieni Aadam. Wakasujudu isipokuwa Ibliys, alikuwa miongoni mwa majini, akaasi Amri ya Rabb wake. Je, basi mnamfanya yeye na kizazi chake rafiki walinzi pasi Nami na hali wao kwenu ni maadui? Ubaya ulioje mbadala huu kwa madhalimu!
مَّا أَشْهَدتُّهُمْ خَلْقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَا خَلْقَ أَنفُسِهِمْ وَمَا كُنتُ مُتَّخِذَ الْمُضِلِّينَ عَضُدًا ﴿٥١﴾
51. (Allaah Anasema): Sikuwashuhudisha kuumbwa mbingu na ardhi, wala kuumbwa nafsi zao, na wala Sikuwafanya wapotoshaji kuwa wasaidizi.
وَيَوْمَ يَقُولُ نَادُوا شُرَكَائِيَ الَّذِينَ زَعَمْتُمْ فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا لَهُمْ وَجَعَلْنَا بَيْنَهُم مَّوْبِقًا ﴿٥٢﴾
52. Na Siku Tutakayosema: Iteni mliodai kuwa ni washirika Wangu Watawaita, lakini hawatowaitikia, na Tutaweka baina yao mahali pa maangamizi.
وَرَأَى الْمُجْرِمُونَ النَّارَ فَظَنُّوا أَنَّهُم مُّوَاقِعُوهَا وَلَمْ يَجِدُوا عَنْهَا مَصْرِفًا ﴿٥٣﴾
53. Na wahalifu watauona moto, watajua hakika kwamba wao wataangukia humo, na hawatopata njia ya kuuepuka.
وَلَقَدْ صَرَّفْنَا فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ لِلنَّاسِ مِن كُلِّ مَثَلٍ ۚ وَكَانَ الْإِنسَانُ أَكْثَرَ شَيْءٍ جَدَلًا ﴿٥٤﴾
54. Na kwa yakini Tumesarifu namna kwa namna katika hii Qur-aan kwa watu, kwa kila mifano. Lakini binaadam amezidi kuliko kila kitu kwa ubishi.
وَمَا مَنَعَ النَّاسَ أَن يُؤْمِنُوا إِذْ جَاءَهُمُ الْهُدَىٰ وَيَسْتَغْفِرُوا رَبَّهُمْ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمْ سُنَّةُ الْأَوَّلِينَ أَوْ يَأْتِيَهُمُ الْعَذَابُ قُبُلًا ﴿٥٥﴾
55. Na hakuna kilichowazuia watu kuamini ulipowajia mwongozo na wakamwomba maghfirah Rabb wao isipokuwa iwafikie desturi ya watu wa awali,[8] au iwafikie adhabu ya kuwakabili.
وَمَا نُرْسِلُ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ ۚ وَيُجَادِلُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِالْبَاطِلِ لِيُدْحِضُوا بِهِ الْحَقَّ ۖ وَاتَّخَذُوا آيَاتِي وَمَا أُنذِرُوا هُزُوًا ﴿٥٦﴾
56. Na Hatukutuma Rusuli isipokuwa wabashiriaji na waonyaji. Na wale waliokufuru wanabisha kwa batili ili watengue haki kwa batili hiyo. Na wakazichukua Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) Zangu na yale waliyoonywa nayo kuwa ni mzaha.
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ فَأَعْرَضَ عَنْهَا وَنَسِيَ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ ۚ إِنَّا جَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا ۖ وَإِن تَدْعُهُمْ إِلَى الْهُدَىٰ فَلَن يَهْتَدُوا إِذًا أَبَدًا ﴿٥٧﴾
57. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyekumbushwa Aayaat za Rabb wake, akazipuuza na akayasahu yale iliyotanguliza mikono yake? Hakika Sisi Tumeweka nyoyoni mwao vifuniko wasizifahamu (Aayaat), na katika masikio yao uziwi.[9] Na ukiwaita kwenye mwongozo hawataongoka abadani!
وَرَبُّكَ الْغَفُورُ ذُو الرَّحْمَةِ ۖ لَوْ يُؤَاخِذُهُم بِمَا كَسَبُوا لَعَجَّلَ لَهُمُ الْعَذَابَ ۚ بَل لَّهُم مَّوْعِدٌ لَّن يَجِدُوا مِن دُونِهِ مَوْئِلًا ﴿٥٨﴾
58. Na Rabb wako ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Rehma. Kama Angeliwachukulia kwa yale waliyoyachuma, Angeliwaharakizia adhabu. Bali wao wana miadi, hawatopata pasi Naye kimbilio la kuepukana nayo.
وَتِلْكَ الْقُرَىٰ أَهْلَكْنَاهُمْ لَمَّا ظَلَمُوا وَجَعَلْنَا لِمَهْلِكِهِم مَّوْعِدًا ﴿٥٩﴾
59. Na miji hiyo, Tuliwaangamiza (wakazi wake) walipodhulumu, na Tukaweka miadi kwa ajili ya maangamizo yao.
وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِفَتَاهُ لَا أَبْرَحُ حَتَّىٰ أَبْلُغَ مَجْمَعَ الْبَحْرَيْنِ أَوْ أَمْضِيَ حُقُبًا ﴿٦٠﴾
60. Na pindi Muwsaa alipomwambia kijana wake:[10] Sitoacha kuendelea (safari) mpaka nifikie zinapokutana bahari mbili, au nitaendelea muda mrefu.[11]
فَلَمَّا بَلَغَا مَجْمَعَ بَيْنِهِمَا نَسِيَا حُوتَهُمَا فَاتَّخَذَ سَبِيلَهُ فِي الْبَحْرِ سَرَبًا ﴿٦١﴾
61. Basi walipofika zinapoungana bahari mbili, walimsahau samaki wao, naye akachukua njia yake baharini akiponyoka chini kwa chini.
فَلَمَّا جَاوَزَا قَالَ لِفَتَاهُ آتِنَا غَدَاءَنَا لَقَدْ لَقِينَا مِن سَفَرِنَا هَـٰذَا نَصَبًا ﴿٦٢﴾
62. Walipokwishapita, alimwambia kijana wake: Tuletee chakula chetu cha mchana, kwa hakika tumepata machofu ya kutosha katika safari yetu hii.
قَالَ أَرَأَيْتَ إِذْ أَوَيْنَا إِلَى الصَّخْرَةِ فَإِنِّي نَسِيتُ الْحُوتَ وَمَا أَنسَانِيهُ إِلَّا الشَّيْطَانُ أَنْ أَذْكُرَهُ ۚ وَاتَّخَذَ سَبِيلَهُ فِي الْبَحْرِ عَجَبًا ﴿٦٣﴾
63. (Kijana wake) akasema: Unaona pale tulipopumzika katika mwamba. Basi mimi nilimsahau samaki, na hakunisahaulisha isipokuwa shaytwaan nisimkumbuke. Akachukua njia yake baharini kimaajabu.
قَالَ ذَٰلِكَ مَا كُنَّا نَبْغِ ۚ فَارْتَدَّا عَلَىٰ آثَارِهِمَا قَصَصًا ﴿٦٤﴾
64. (Muwsaa) akasema: Hapo ndipo tulipokuwa tunapataka. Basi wakarudi nyuma kwa kufuata athari za nyayo zao.
فَوَجَدَا عَبْدًا مِّنْ عِبَادِنَا آتَيْنَاهُ رَحْمَةً مِّنْ عِندِنَا وَعَلَّمْنَاهُ مِن لَّدُنَّا عِلْمًا ﴿٦٥﴾
65. Wakamkuta mja miongoni mwa Waja Wetu (Khidhwr), Tuliyempa Rehma kutoka Kwetu, na Tumemfunza kutoka Kwetu ilimu.
قَالَ لَهُ مُوسَىٰ هَلْ أَتَّبِعُكَ عَلَىٰ أَن تُعَلِّمَنِ مِمَّا عُلِّمْتَ رُشْدًا ﴿٦٦﴾
66. Muwsaa akamwambia: Je, nikufuate ili unifunze katika yale uliyofunzwa ya busara?
قَالَ إِنَّكَ لَن تَسْتَطِيعَ مَعِيَ صَبْرًا ﴿٦٧﴾
67. (Khidhwr) akasema: Hakika hutoweza kustahamili pamoja nami.
وَكَيْفَ تَصْبِرُ عَلَىٰ مَا لَمْ تُحِطْ بِهِ خُبْرًا ﴿٦٨﴾
68. Na vipi utastahamili kwa ambayo huyaelewi vyema utambuzi wake?
قَالَ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ صَابِرًا وَلَا أَعْصِي لَكَ أَمْرًا ﴿٦٩﴾
69. (Muwsaa) akasema: Utanikuta In Shaa Allaah mwenye subira na wala sitokuasi amri.
قَالَ فَإِنِ اتَّبَعْتَنِي فَلَا تَسْأَلْنِي عَن شَيْءٍ حَتَّىٰ أُحْدِثَ لَكَ مِنْهُ ذِكْرًا ﴿٧٠﴾
70. (Khidhwr) akasema: Basi utakaponifuata, usiniulize kuhusu lolote mpaka nianze kukutajia.
فَانطَلَقَا حَتَّىٰ إِذَا رَكِبَا فِي السَّفِينَةِ خَرَقَهَا ۖ قَالَ أَخَرَقْتَهَا لِتُغْرِقَ أَهْلَهَا لَقَدْ جِئْتَ شَيْئًا إِمْرًا ﴿٧١﴾
71. Wakatoka kuendelea kwenda, mpaka walipopanda jahazi. (Khidhwr) akaitoboa. Akasema: Umeitoboa ili ugharikishe watu wake? Kwa yakini umeleta jambo zito la munkari!
قَالَ أَلَمْ أَقُلْ إِنَّكَ لَن تَسْتَطِيعَ مَعِيَ صَبْرًا ﴿٧٢﴾
72. (Khidhwr) akasema: Je, sikusema kwamba hakika wewe hutoweza kustahamili pamoja nami?
قَالَ لَا تُؤَاخِذْنِي بِمَا نَسِيتُ وَلَا تُرْهِقْنِي مِنْ أَمْرِي عُسْرًا ﴿٧٣﴾
73. (Muwsaa) akasema: Usinichukulie kwa niliyoyasahau, na wala usinifanyie tashdidi kubwa kwa jambo langu hili.
فَانطَلَقَا حَتَّىٰ إِذَا لَقِيَا غُلَامًا فَقَتَلَهُ قَالَ أَقَتَلْتَ نَفْسًا زَكِيَّةً بِغَيْرِ نَفْسٍ لَّقَدْ جِئْتَ شَيْئًا نُّكْرًا ﴿٧٤﴾
74. Wakatoka kuendelea kwenda, mpaka wakakutana na ghulamu (kijana mwanamume) akamuua. (Muwsaa) akasema: Umeua mtu asiye na hatia na wala hakuua mtu? Kwa yakini umeleta jambo linalokirihisha mno lisilokubalika!
قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكَ إِنَّكَ لَن تَسْتَطِيعَ مَعِيَ صَبْرًا ﴿٧٥﴾
75. (Khidhwr) akasema: Je, sikukwambia kwamba hakika wewe hutoweza kustahamili pamoja nami?
قَالَ إِن سَأَلْتُكَ عَن شَيْءٍ بَعْدَهَا فَلَا تُصَاحِبْنِي ۖ قَدْ بَلَغْتَ مِن لَّدُنِّي عُذْرًا ﴿٧٦﴾
76. (Muwsaa) akasema: Nikikuuliza kuhusu chochote baada ya haya, basi usisuhubiane nami, maana umekwishapata udhuru kwangu.
فَانطَلَقَا حَتَّىٰ إِذَا أَتَيَا أَهْلَ قَرْيَةٍ اسْتَطْعَمَا أَهْلَهَا فَأَبَوْا أَن يُضَيِّفُوهُمَا فَوَجَدَا فِيهَا جِدَارًا يُرِيدُ أَن يَنقَضَّ فَأَقَامَهُ ۖ قَالَ لَوْ شِئْتَ لَاتَّخَذْتَ عَلَيْهِ أَجْرًا ﴿٧٧﴾
77. Wakatoka kuendelea kwenda, mpaka wakawafikia watu wa mji, wakawaomba watu wake chakula lakini walikataa kuwakaribisha. Wakakuta humo ukuta unataka kuanguka, na (Khidhwr) akausimamisha. (Muwsaa) akasema: Ungelitaka ungeliuchukulia ujira.
قَالَ هَـٰذَا فِرَاقُ بَيْنِي وَبَيْنِكَ ۚ سَأُنَبِّئُكَ بِتَأْوِيلِ مَا لَمْ تَسْتَطِع عَّلَيْهِ صَبْرًا ﴿٧٨﴾
78. (Khidhwr) akasema: Huku ndiko kufarikiana baina yangu na baina yako. Hivi punde nitakujulisha tafsiri ya hakika ya yale uliyoshindwa kuyavutia subira.
أَمَّا السَّفِينَةُ فَكَانَتْ لِمَسَاكِينَ يَعْمَلُونَ فِي الْبَحْرِ فَأَرَدتُّ أَنْ أَعِيبَهَا وَكَانَ وَرَاءَهُم مَّلِكٌ يَأْخُذُ كُلَّ سَفِينَةٍ غَصْبًا ﴿٧٩﴾
79. Ama jahazi (niliyoitoboa), ilikuwa ya masikini wanaofanya kazi baharini. Nikataka kuitia dosari, kwani mbele yao alikuweko mfalme anayechukua kila jahazi kwa kupora.
وَأَمَّا الْغُلَامُ فَكَانَ أَبَوَاهُ مُؤْمِنَيْنِ فَخَشِينَا أَن يُرْهِقَهُمَا طُغْيَانًا وَكُفْرًا ﴿٨٠﴾
80. Na ama ghulamu (niliyemuua), wazazi wake wawili walikuwa Waumini. Basi Tukakhofu asije kuwatia mashakani kwa upindukaji mipaka ya kuasi na kufuru.
فَأَرَدْنَا أَن يُبْدِلَهُمَا رَبُّهُمَا خَيْرًا مِّنْهُ زَكَاةً وَأَقْرَبَ رُحْمًا ﴿٨١﴾
81. Tukakusudia Rabb wao Awabadilishie aliye bora zaidi kuliko yeye kiutakasifu na aliyekuwa karibu zaidi kihuruma.
وَأَمَّا الْجِدَارُ فَكَانَ لِغُلَامَيْنِ يَتِيمَيْنِ فِي الْمَدِينَةِ وَكَانَ تَحْتَهُ كَنزٌ لَّهُمَا وَكَانَ أَبُوهُمَا صَالِحًا فَأَرَادَ رَبُّكَ أَن يَبْلُغَا أَشُدَّهُمَا وَيَسْتَخْرِجَا كَنزَهُمَا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ وَمَا فَعَلْتُهُ عَنْ أَمْرِي ۚ ذَٰلِكَ تَأْوِيلُ مَا لَمْ تَسْطِع عَّلَيْهِ صَبْرًا ﴿٨٢﴾
82. Na ama ukuta (niliounyanyua), ulikuwa ni wa ghulamu wawili mayatima katika mji ule, na kulikuweko chini yake hazina yao, na baba yao alikuwa mwema. Basi Rabb wako Alitaka wafikie umri wa kupevuka na watoe hazina yao ikiwa ni Rehma kutoka kwa Rabb wako. Na sikufanya hayo kwa amri yangu. Hiyo ni tafsiri ya hakika ya yale ambayo hukuweza kuyavutia subira.
وَيَسْأَلُونَكَ عَن ذِي الْقَرْنَيْنِ ۖ قُلْ سَأَتْلُو عَلَيْكُم مِّنْهُ ذِكْرًا ﴿٨٣﴾
83. Na wanakuuliza kuhusu Dhul-Qarnayn. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Nitakusomeeni kuhusu baadhi ya khabari zake.[12]
إِنَّا مَكَّنَّا لَهُ فِي الْأَرْضِ وَآتَيْنَاهُ مِن كُلِّ شَيْءٍ سَبَبًا ﴿٨٤﴾
84. Hakika Sisi Tulimmakinisha katika ardhi, na Tukampa njia ya kila kitu.
فَأَتْبَعَ سَبَبًا ﴿٨٥﴾
85. Basi akaifuata njia.
حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ مَغْرِبَ الشَّمْسِ وَجَدَهَا تَغْرُبُ فِي عَيْنٍ حَمِئَةٍ وَوَجَدَ عِندَهَا قَوْمًا ۗ قُلْنَا يَا ذَا الْقَرْنَيْنِ إِمَّا أَن تُعَذِّبَ وَإِمَّا أَن تَتَّخِذَ فِيهِمْ حُسْنًا ﴿٨٦﴾
86. Hata alipofika machweo ya jua, akalikuta (kama) linatua katika chemchemu ya matope meusi (au ya moto), na akakuta huko watu. Tukasema: Ee Dhul-Qarnayn! Ima uwaadhibu au wafanyie ihsaan.
قَالَ أَمَّا مَن ظَلَمَ فَسَوْفَ نُعَذِّبُهُ ثُمَّ يُرَدُّ إِلَىٰ رَبِّهِ فَيُعَذِّبُهُ عَذَابًا نُّكْرًا ﴿٨٧﴾
87. (Dhul-Qarnayn) akasema: Ama aliyedhulumu, basi Tutamuadhibu, kisha atarudishwa kwa Rabb wake, Amuadhibu adhabu kali kabisa ya kukirihisha, isiyovumilika.
وَأَمَّا مَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَلَهُ جَزَاءً الْحُسْنَىٰ ۖ وَسَنَقُولُ لَهُ مِنْ أَمْرِنَا يُسْرًا ﴿٨٨﴾
88. Na ama aliyeamini na akatenda mema, basi atapata jazaa nzuri kabisa. Na Tutamwambia yaliyo mepesi katika Amri Yetu.
ثُمَّ أَتْبَعَ سَبَبًا ﴿٨٩﴾
89. Kisha akaifuata njia.
حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ مَطْلِعَ الشَّمْسِ وَجَدَهَا تَطْلُعُ عَلَىٰ قَوْمٍ لَّمْ نَجْعَل لَّهُم مِّن دُونِهَا سِتْرًا ﴿٩٠﴾
90. Hata alipofikia panapochomoza jua, alilikuta linachomoza kwa watu Hatukuwafanyia kizuizi cha kuwakinga nalo.
كَذَٰلِكَ وَقَدْ أَحَطْنَا بِمَا لَدَيْهِ خُبْرًا ﴿٩١﴾
91. Ndio hivyo. Na Tulikwishazijua vyema khabari za vyote alivyonavyo.
ثُمَّ أَتْبَعَ سَبَبًا ﴿٩٢﴾
92. Kisha akaifuata njia.
حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ بَيْنَ السَّدَّيْنِ وَجَدَ مِن دُونِهِمَا قَوْمًا لَّا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ قَوْلًا ﴿٩٣﴾
93. Hata alipofikia baina ya milima miwili, akakuta nyuma yake watu ambao takriban hawafahamu neno lolote.
قَالُوا يَا ذَا الْقَرْنَيْنِ إِنَّ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ فَهَلْ نَجْعَلُ لَكَ خَرْجًا عَلَىٰ أَن تَجْعَلَ بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمْ سَدًّا ﴿٩٤﴾
94. Wakasema: Ee Dhul-Qarnayn! Hakika Yaajuwj na Maajuwj[13] ni mafisadi katika ardhi. Basi je, tukufanyie ujira ili uweke baina yetu na baina yao kizuizi?
قَالَ مَا مَكَّنِّي فِيهِ رَبِّي خَيْرٌ فَأَعِينُونِي بِقُوَّةٍ أَجْعَلْ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُمْ رَدْمًا ﴿٩٥﴾
95. Akasema: Alivyonimakinisha Rabb wangu ni bora zaidi (kuliko ujira). Basi nisaidieni kwa nguvu (za watu), niweke baina yenu na baina yao kizuizi imara.
آتُونِي زُبَرَ الْحَدِيدِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا سَاوَىٰ بَيْنَ الصَّدَفَيْنِ قَالَ انفُخُوا ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَعَلَهُ نَارًا قَالَ آتُونِي أُفْرِغْ عَلَيْهِ قِطْرًا ﴿٩٦﴾
96. Nileteeni vipande vya chuma. Mpaka aliposawazisha kujaza baina ya kingo mbili za majabali akasema: Chocheeni moto. Hata alipovifanya moto, akasema: Nipeni nimwagie juu yake shaba iliyoyayushwa.
فَمَا اسْطَاعُوا أَن يَظْهَرُوهُ وَمَا اسْتَطَاعُوا لَهُ نَقْبًا ﴿٩٧﴾
97. Basi (Ya-juwj na Ma-juwj) hawakuweza kukikwea na wala hawakuweza kukitoboa.
قَالَ هَـٰذَا رَحْمَةٌ مِّن رَّبِّي ۖ فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ رَبِّي جَعَلَهُ دَكَّاءَ ۖ وَكَانَ وَعْدُ رَبِّي حَقًّا ﴿٩٨﴾
98. (Dhul-Qarnayn) akasema: Hii ni Rehma kutoka kwa Rabb wangu. Basi itakapokuja Ahadi ya Rabb wangu[14], Atakijaalia kibomoke, kipondeke kiwe tambarare. Na Ahadi ya Rabb wangu daima ni ya kweli.
وَتَرَكْنَا بَعْضَهُمْ يَوْمَئِذٍ يَمُوجُ فِي بَعْضٍ ۖ وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَجَمَعْنَاهُمْ جَمْعًا ﴿٩٩﴾
99. Na siku hiyo Tutawaacha wasongamane kama mawimbi wenyewe kwa wenyewe.[15] Na litapulizwa baragumu, Tutawakusanya wote katika mkusanyo mmoja.
وَعَرَضْنَا جَهَنَّمَ يَوْمَئِذٍ لِّلْكَافِرِينَ عَرْضًا ﴿١٠٠﴾
100. Na siku hiyo Tutaiweka Jahannam kwa makafiri (waione) waziwazi.
الَّذِينَ كَانَتْ أَعْيُنُهُمْ فِي غِطَاءٍ عَن ذِكْرِي وَكَانُوا لَا يَسْتَطِيعُونَ سَمْعًا ﴿١٠١﴾
101. Ambao macho yao yalikuwa katika pazia wasiweze kunidhukuru na walikuwa hawawezi kusikia.
أَفَحَسِبَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن يَتَّخِذُوا عِبَادِي مِن دُونِي أَوْلِيَاءَ ۚ إِنَّا أَعْتَدْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَافِرِينَ نُزُلًا ﴿١٠٢﴾
102. Je, wanadhania wale waliokufuru kwamba wanaweza kuwafanya Waja Wangu kuwa rafiki walinzi badala Yangu? Hakika Sisi Tumeandaa Jahannam kwa ajili ya makafiri kuwa mahala pa kuteremkia.
قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُم بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا ﴿١٠٣﴾
103. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Je, Tukujulisheni wenye kukhasirika mno kwa amali?[16]
الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا ﴿١٠٤﴾
104. Ni wale ambao juhudi zao zimepotea bure katika uhai wa dunia, na huku wao wakidhani kwamba wanafanya matendo mazuri (ya kuwanufaisha).
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَلِقَائِهِ فَحَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَلَا نُقِيمُ لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَزْنًا ﴿١٠٥﴾
105. Hao ni wale waliozikanusha Aayaat (na Ishara, Hoja, Dalili) za Rabb wao na kukutana Naye, amali zao zikaporomoka. Hivyo Hatutowathamini wala Kuwajali hata kidogo Siku ya Qiyaamah.
ذَٰلِكَ جَزَاؤُهُمْ جَهَنَّمُ بِمَا كَفَرُوا وَاتَّخَذُوا آيَاتِي وَرُسُلِي هُزُوًا ﴿١٠٦﴾
106. Kwa hayo, malipo yao ni Jahannam kwa sababu ya ukafiri wao, na wamezifanyia mzaha Aayaat (na Ishara, Hoja, Dalili) Zangu na Rusuli Wangu.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَانَتْ لَهُمْ جَنَّاتُ الْفِرْدَوْسِ نُزُلًا ﴿١٠٧﴾
107. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, watapata Jannaat za Al-Firdaws[17] kuwa ni mahali pao pa makaribisho.
خَالِدِينَ فِيهَا لَا يَبْغُونَ عَنْهَا حِوَلًا ﴿١٠٨﴾
108. Wadumu humo, hawatotaka kuihama.
قُل لَّوْ كَانَ الْبَحْرُ مِدَادًا لِّكَلِمَاتِ رَبِّي لَنَفِدَ الْبَحْرُ قَبْلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَاتُ رَبِّي وَلَوْ جِئْنَا بِمِثْلِهِ مَدَدًا ﴿١٠٩﴾
109. Sema: Kama bahari ingelikuwa ni wino wa (kuandika) Maneno ya Rabb wangu, basi ingelimalizika bahari kabla ya kumalizika Maneno ya Rabb wangu, japokuwa Tungelileta mfano wake kujaza tena.[18]
قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا ﴿١١٠﴾
110. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi ni mtu kama nyinyi, nafunuliwa Wahy kwamba: Hakika Mwabudiwa wa haki wenu ni Ilaah Mmoja Pekee. Hivyo anayetaraji kukutana na Rabb wake, basi na atende amali njema na wala asimshirikishe yeyote katika ibaada za Rabb wake.[19]
[1] Kumhimidi Allaah Kwa Kitabu Kisichokuwa Na Upogo:
AlhamduliLLaah, ni kumtukuza na kumsifu Allaah kwa Sifa Zake ambazo ni sifa zote za ukamilifu, na kwa Neema Zake zilizo dhahiri na siri, za kidini na kidunia. Na neema kubwa zaidi kuliko zote ni kuteremsha Kwake Kitabu hiki kitukufu kwa Mja Wake na Rasuli Wake Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Na kwa ajili hiyo, Anajihimidi Mwenyewe. Himdi hii imebeba ndani yake maelekezo kwa waja kwamba nao pia wamhimidi Yeye kwa kuwatumia Rasuli na kuwateremshia Kitabu.
Kisha Akakielezea Kitabu hiki kuwa kina sifa mbili kusanyifu zinazokifanya kuwa ni Kitabu kikamilifu katika kila upande. Sifa ya kwanza ni kukanusha kuwepo upogo ndani yake, na ya pili ni kuthibitisha kuwa ni Kitabu kilichonyooka barabara. Kukanusha kuwa hakina upogo ndani yake, inamaanisha kuwa hakuna khabari za uwongo ndani yake, na wala hakuna dhulma wala chochote cha upuuzi au kisichokuwa na makusudio katika amri Zake na makatazo Yake.
Ama kuthibitisha kuwa ni Kitabu kilichonyooka barabara, hii inamaanisha kwamba, hakijulishi jambo wala amri isipokuwa ni njema, wala hakitaji lolote isipokuwa ni masuala matukufu zaidi ambayo ni masuala yanayojaza moyo ilimu, imaan na hikma, kama kujuzisha Majina ya Allaah na Sifa Zake na Matendo Yake, na visa vya ghaibu vitakavyotokea na vilivyokwishatokea. Na kwamba amri zake na makatazo yake yanatakasa na yanazitwaharisha nafsi kuzifanya zikue na ziwe njema kwa sababu zinategemea haki kamilifu, ikhlaasw, na utumwa wa kweli kwa Rabb Pekee wa ulimwengu Ambaye Hana mshirika. Na kutokana na sifa hizi zilizotajwa kuhusiana na Kitabu hiki, imekuwa ni jambo linalostahiki kwa Allaah Kujihimidi Yeye Mwenyewe kwa kukiteremsha, na kuwataka Waja Wake wamsifu kwa Sifa njema kutokana na yote yaliyomo ndani yake.
[2] Al-Kahf: Jina La Suwrah. Maana ya Al-Kahf na Ar-Raqiym:
Al-Kahf ni pango katika jabali ambalo vijana hao walikimbilia kujificha humo. Na kuhusu neno la Ar-Raqiym, kuna kauli mbalimbali za Salaf kama ifuatavyo: (i) Ibn 'Abbaas na wengineo: Bonde. (ii) Pango katika bonde na Ar-Raqiym ni jina la bonde. (iii) Ar-Raqiym inakusudiwa majengo yao. (iv) Ni bonde ambalo pango lao lilikuwepo. (v) Ni mji. (vi) Jabali ambalo pango hilo lilikuwepo. (vii) Ubamba wa jiwe wenye maandiko walioandikia kisa cha Asw-haabul-Kahf kisha wakaliweka katika maingilio ya mlango wa pango. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[3] Amrisho La Kusema In Shaa Allaah Anapotaka Mtu Kufanya Jambo Na Hikma Zake:
Katazo hilo ni kama mengineyo (katika Qur-aan) ambayo yanamwelekea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na sababu fulani, lakini pia linawahusu wanaadam. Na hikma yake ni kutokuingilia mambo ya ghaibu, kwa sababu hakuna ajuaye kama jambo litafanyika nyakati za mbele, au kesho, au halifanyiki isipokuwa Allaah. Pia kusema In Shaa Allaah inalifanya jambo liwe jepesi na lenye baraka kwa sababu mja anakusudia kutaka msaada wa Allaah. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما amesema makafiri wa Kiquraysh walimtuma Yahudi amwendee Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ili amuulize maswali matatu: (i) Kuhusu vijana wa wakati wa kale na kisa chao, kwani kisa chao ni cha kustaajabisha, nao ni Asw-haabul-Kahf (vijana wa pangoni) ambao wameelezewa katika Suwrah hii (ii) Nini kisa cha mtu aliyesafiri sana hadi akafika Mashariki na Magharibi ya dunia, yaani Dhul-Qarnayn katika Suwrah hii Al-Kahf (18:83) (iii) Kuhusu roho (nafsi) ni kitu gani hicho? Rejea Al-Israa (17:85). Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwajibu kuwa atawajulisha kesho, bila ya kusema In Shaa Allaah. Akakaa siku kumi na tano bila ya Jibriyl (عليه السّلام) kumjia kama ilivyo kawaida yake kumpa Wahyi kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى). Watu wa Makkah wakaanza kumtilia shaka na kupita wakisema: "Muhammad katuahidi kutujibu mas-ala tuliyomuuliza siku ya pili na hadi leo siku ya kumi na tano zimepita hakutujibu lolote katika hayo."
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akafikwa na huzuni kubwa kwa kuchelewa kupata Wahyi na akadhikika kwa maneno ya watu wa Makkah waliyokuwa wakisema. Kisha Jibriyl (عليه السّلام) akaja kumteremshia Suwrah ya Al-Kahf kwa kuanzia Aayah namba (6). Kwa hilo, Allaah (سبحانه وتعالى) Alimtahini Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kama alivyotahiniwa Nabiy Sulaymaan (عليه السّلام) kwa mujibu wa maelezo yaliyopo katika Hadiyth iliyosimuliwa na Abu Hurayrah (رضي الله عنه):
قَالَ اللَّيْثُ حَدَّثَنِي جَعْفَرُ بْنُ رَبِيعَةَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ هُرْمُزَ، قَالَ سَمِعْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " قَالَ سُلَيْمَانُ بْنُ دَاوُدَ ـ عَلَيْهِمَا السَّلاَمُ ـ لأَطُوفَنَّ اللَّيْلَةَ عَلَى مِائَةِ امْرَأَةٍ ـ أَوْ تِسْعٍ وَتِسْعِينَ ـ كُلُّهُنَّ يَأْتِي بِفَارِسٍ يُجَاهِدُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ، فَقَالَ لَهُ صَاحِبُهُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ. فَلَمْ يَقُلْ إِنْ شَاءَ اللَّهُ. فَلَمْ يَحْمِلْ مِنْهُنَّ إِلاَّ امْرَأَةٌ وَاحِدَةٌ، جَاءَتْ بِشِقِّ رَجُلٍ، وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ، لَوْ قَالَ إِنْ شَاءَ اللَّهُ، لَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فُرْسَانًا أَجْمَعُونَ ".
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wakati mmoja Sulaymaan bin Daawuwd (عليهما السّلام) alisema: (Wa-Allaahi) Usiku wa leo nitawapitia wake zangu wote mia au tisini na tisa, (kwa kujimai nao), na kila mmoja wao atazaa shujaa mpandaji farasi atakayepigana katika Njia ya Allaah.” Sahibu yake akamwambia: “Sema: In Shaa Allaah (Allaah Akipenda).” Lakini yeye hakusema In Shaa Allaah. Kwa hiyo, aliyebeba mimba na kuzaa alikuwa mwanamke mmoja peke yake, naye alizaa nusu mtu (kilema). Naapa kwa Yule Ambaye nafsi ya Muhammad iko Mikononi Mwake, lau angesema In Shaa Allaah, basi wangekuwa ni wenye kuipigania (Dini) katika Njia ya Allaah wote wakiwa juu ya farasi.” [Al-Bukhaariy]
Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Ametaka kumfunza Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu kurejea Kwake kwa kila jambo analotaka kufanya, kwani Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Mwenye Qudra (Uwezo) wa kila kitu, Ndiye Mwenye Kudabiri mambo yote, na Ndiye Mjuzi wa mambo ya ghaibu. Hakuna jambo linaloweza kutendeka ila kwa Matakwa Yake.
[4] Anaposahau Mtu Kusema In Shaa Allaah:
Ibn 'Abbaas aliifasiri Aayah hii kuwa mtu anaweza kusema In Shaa Allaah hata baada ya mwaka ikiwa amesahau kusema baada ya kuweka kiapo au kusema atafanya jambo fulani. Hivi atakuwa amefanya Sunnah ya kusema In Shaa Allaah hata kama baada ya kuvunja kiapo. Hii vile vile ni rai ya Ibn Jariyr. Lakini kasema, hii haina maana kwamba inafidia kuvunja kiapo cha mtu, bali mtu anapovunja kiapo lazima afanye kafara yake (malipo ya kiapo). [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[5] Al-Baaqiyaatu Asw-Swaalihaatu: Mema Yanayobakia:
Hadiyth ifuatayo imebainisha maana ya al-baaqiyaatu asw-swaalihaatu:
Amesimulia Abu Sa’iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Amali njema yenye kubakia ni:
لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ، وَسُبْحَانَ اَللَّهِ، وَاَللَّهُ أَكْبَرُ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاَللَّهِ
Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na Utakasifu ni wa Allaah, na Allaah ni Mkubwa, na Himdi Anastahiki Allaah, na hapana uwezo wala nguvu ila za Allaah.
[Imetolewa na An-Nasaaiy na akaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim]
Kauli za ‘Ulamaa kuhusu maana ya al-baaqiyaatu asw-swaalihaatu:
‘Ulamaa wametaja kama hivyo na mfano wa kama hivyo. Ama Ibn ‘Abbaas, Sa’iyd bin Jubayr, na Salaf wengineo wamesema kuwa al-baaqiyaatu asw-swaalihaatu ni: Swalaah tano.
Na Amiri wa Waumini ‘Uthmaan bin ‘Affaan (رضي الله عنه) aliulizwa kuhusu al-baaqiyaatu asw-swaalihaatu akasema hayo ni:
لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ، وسُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، واللَّهُ أَكْبَرُ، وَلاَ حَوْلَ ولاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ
[Tafsiyr Ibn Kathiyr(رحمه الله) ]
Na Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) amesema kuhusu:
الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ
“Mali na watoto ni pambo la uhai wa dunia.”
Maana yake: Hakuna katika hayo kitu kitakachobakia nyuma, na kwamba kinachobakia kwa binaadam na kitakachomnufaisha na kumfurahisha ni al-baaqiyaatu asw-swaalihaatu (mema yatakayobakia). Na haya yanajumuisha matendo yote ya utiifu ya faradhi na ya Sunnah katika haki za Allaah, na haki za Waja Wake; kama vile Swalaah, Zakaah, swadaqa, Hajj, ‘Umrah, Tasbiyh (Kumtakasa Allaah), Tahmiyd (Kumhimidi Allaah), Tahliyl (Kumpwekesha Allaah), Takbiyr (Kumtukuza Allaah), mja kusoma (Qur-aan), kutafuta ilimu yenye manufaa, kuamrisha mema na kukataza munkari, “swilatur-rahim” (kuunga undugu wa uhusiano wa damu), kuwafanyia wema na ihsaan wazazi, kutimiza haki za mke na mume, haki za watumwa, na haki za wanyama, na kila aina za ihsaan kwa viumbe. Yote haya ni al-baaqiyaatu asw-swaalihaatu (mema yatakayobakia). Basi haya yote ni
خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا
“Bora mbele ya Rabb wako kwa thawabu na matumaini mema zaidi.”
Hivyo basi thawabu zake zinabakia na zinaongezeka milele, na malipo yake, nyongeza zake na manufaa yake yana dhamana ya kupatikana wakati wa kulipwa na Allaah. Basi haya ndiyo ambayo yanapaswa washindane nayo wenye kushindana (katika mema), na wayakimbilie watendao (mema), na wajitahidi kuyapata wenye kujitahidi. Na tazama utaamuli, wakati Allaah Alivyopiga mfano wa dunia, hali yake na kutoweka kwake Ametaja kuwa vilivyomo humo ni aina mbili; aina ya mapambo yake ambayo binaadam ananufaika nayo kidogo tu, kisha yanatoweka bila ya faida yake kumrudia mtu mwenyewe. Bali huenda hata hayo yakamletea madhara, nayo ni mali na watoto. Na aina nyengine ambayo inabakia na itamfaa mtu mwenyewe daima dawamu, nayo ni al-baaqiyaatu asw- swaalihaatu. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[6] Viumbe Watafufuliwa Wakiwa Kama Walivyozaliwa:
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Watu watafufuliwa Siku ya Qiyaamah ilhali hawana viatu, wako uchi, ni mazunga (hawakutahiriwa).” Nikamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Wanaume na wanawake wote watatazamana? Akasema: “Ee ‘Aaishah! Hali itakuwa ngumu mno hata hawatoweza kushughulika na jambo hilo!”
Katika riwaayah nyingine imesema: “Hali itakuwa ngumu mno kiasi kwamba hawatoweza kutazamana.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Rejea Al-An’aam (6:94), na Al-Anbiyaa (21:104)
[7] Matendo Yote Ya Binaadam Yanarekodiwa Hata Liwe Tendo Dogo Vipi:
Rejea Al-Israa (17:13-14) (17:71), Az-Zalzalah (99:6-8), Qaaf (50:17-18), Al-Haaqqah (69:19-29), na Al-Infitwaar (82:10-12).
[8] Desturi Ya Watu Wa Awali:
Rejea Aal-‘Imraan (3:137), Faatwir (35:43-44), Yuwsuf (12:109), Al-An’aam (6:11), An-Naml (37:69).
[9] Nyoyo Za Makafiri Zimefunikwa Na Masikio Yana Uziwi:
Rejea Al-An’aam (6:25), Al-Israa (17:45-46), Fusswilat (41:5).
[10] Yuwsha’ Bin Nuwn:
Yuwsha’ bin Nuwn ametajwa katika Hadiyth kadhaa zilizo ndefu kwenye Al-Bukhaariy na Muslim kuwa alikuwa ni kijana aliyekuwa akimhudumia Nabiy Muwsaa (عليه السّلام). Naye ndiye aliyeshika Unabii baada ya kufariki kwa Nabiy Muwsa (عليه السّلام). Na yeye ndiye mmojawapo wa watu wawili walioingia Bayt Al-Maqdis. Rejea Suwrah Al-Maaidah (5:23).
[11] Kisa Cha Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) Na Al-Khidhwr:
Kuanzia Aayah hii hadi Aayah namba (82), kinazungumziwa kisa cha Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) na Khidhwr ambaye amekusudiwa katika Aayah namba (65). Na ‘Ulamaa wamekhitilafiana kama Al-Khidhwr ni Nabii au laa. Lakini wengi wao wameona kuwa Al-Khidhwr si Nabii, bali ni mja mwema wa Allaah aliyepewa ilhamu, hikmah na ilimu ya hali ya juu.
[12] Dhul-Qarnayn:
Watu wa Kitabu au washirikina (wa Makkah) walimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu kisa cha Dhul-Qarnayn (18:83-98). Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akamuamuru Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) awajibu:
قُلْ سَأَتْلُو عَلَيْكُم مِّنْهُ ذِكْرًا ﴿٨٣﴾
“Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Nitakusomeeni kuhusu baadhi ya khabari zake.”
Khabari muhimu na za ajabu (mpate kukumbuka na kuzingatia) [Tafsiyr As-Sa’diy na At-Tafsiyr Al-Muyassar]
‘Ulamaa wamekubaliana kwamba Dhul-Qarnayn hakuwa Nabii, bali alikuwa ni mja mwema na mfalme miongoni mwa wafalme wa ardhi aliyezunguka duniani akilingania kwa uadilifu kutokana na khabari zilizoelezwa katika Suwrah hii Al-Kahf. Mujaahid amesema: “Ni mfalme aliyekuwa Muumini.” Ibn Kathiyr amesema: “Allaah (سبحانه وتعالى) Amemtaja huyu Dhul-Qarnayn na Akamsifu kwa uadilifu, na kwamba alifika Mashariki na Magharibi (ya dunia).” Ibn ‘Uthaymiyn amesema: “Ni mfalme muadilifu aliyekuwa wakati wa Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) na inasemekana kuwa aliizunguka Al-Ka’bah pamoja naye, na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi. [Fataawaa Nuwr Alad-Darb (60/4)]
Kisa chake ndio hiki kama Alivyoelezea Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwrah hii ya Al-Kahf na ambayo ni Suwrah pekee iliyotajwa khabari zake.
[13] Yaajuwj Na Maajuwj Ni Katika Alama Kumi Kubwa Za Kutokea Qiyaamah:
Rejea Al-An’aam (6:158) kwenye Hadiyth na maelezo yanayotaja alama zote kubwa za Qiyaamah.
Hadiyth kadhaa nyenginezo zimethibiti kuhusu Yaajuwj na Maajuwj kwamba ni katika alama kubwa za Qiyaamah; mojawapo ni:
Amesimulia Zaynab bint Jahsh (رضي الله عنها): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliamka kutoka usingizini uso wake ukiwa umeiva kwa wekundu, huku akisema:
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ
“Laa ilaaha illa-Allaah! (Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah)
Ole wao Waarabu kwa shari iliyokaribia. Limefunguliwa leo tundu katika ukuta unaowazuilia Yaajuwj na Maajuwj mfano huu.” Sufyaan akaonyesha kwa kufanya namba tisini au mia kwa vidole vyake. Pakasemwa: Je, tutaangamizwa na miongoni mwetu kuna watu wema? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ndio, pindi maovu yatakapokithiri.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Rejea pia Al-Anbiyaa (21:96-97).
[14]Ahadi Ya Allaah: Ni Kuchomoza Kwa Yaajuwj na Maajuwj.
[15] Watakaosongamana:
Huenda imekusudiwa Yaajuwj na Maajuwj watakapojitokeza kwa watu, kwa sababu ya idadi yao kubwa mno, na kufika kwao pande zote za ardhi. Hivo basi, watasongamana kama mawimbi wenyewe kwa wenyewe.
Au huenda ni viumbe Siku ya kufufuliwa kwa vile watakusanywa kwa idadi kubwa mno hadi kwamba watasongamana kama mawimbi wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya hali ya kiwewe itakavyokuwa pamoja na tetemeko kubwa la adhi. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[16] Amali Batili Hazina Thamani:
Aayah hii na inayofuatia (105), inathibitisha kuwa amali batili hazina thamani mbele ya Allaah na wala hazipokelewi. Ni amali zozote zile ambazo hazina dalili katika Sharia ya Dini hii tukufu. Ameonya haya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth:
عن أُمِّ المُؤمِنينَ أُمِّ عَبْدِ الله عائِشَةَ رَضي اللهُ عنها قالَتْ: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ أَحْدَثَ في أَمْرِنا هذا ما لَيْسَ منهُ فَهُوَ رَد)) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ
وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ : ((مَن عَمِلَ عَمَلاً لَيْسَ عَلَيْهِ أَمْرُنَا فَهُوَ رَدٌّ ))
Amesimulia Mama wa Waumini Ummu Abdillaah ‘Aaishah (رضي الله عنها): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayezusha katika jambo letu hili (la Dini) lolote ambalo halimo humo litarudishwa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na katika riwaayah ya Muslim: ”Atakayetenda kitendo kisichokuwa chetu (katika Dini) basi kitarudishwa.”
Rejea Az-Zumar (39:65).
Na Imaam Ibn Kathiyr amesema inamaanisha: Wametenda amali batili ambazo haziendani na Sharia inayoridhiwa na Allaah. Na wanadhani kuwa wako juu ya msingi fulani kwa matendo yao na kupendwa. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[17] Jannah Ya Al-Firdaws Na Aina Za Jannah Na Makazi Ya Aakhirah:
Rejea An-Najm (53:15) kwenye faida kuhusu aina za Jannah na makazi ya Aakhirah.
[18] Bahari Ingekuwa Ni Wino Wa Kuandika Maneno Ya Allaah: Rejea Luqmaan (31:27).
مَرْيَم
019-Maryam
019-Maryam: Utangulizi Wa Suwrah [181]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
كهيعص ﴿١﴾
1. Kaaf Haa Yaa ‘Ayn Swaad.[1]
ذِكْرُ رَحْمَتِ رَبِّكَ عَبْدَهُ زَكَرِيَّا ﴿٢﴾
2. (Huu ni) ukumbusho wa Rehma ya Rabb wako kwa Mja Wake Zakariyyaa.
إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ نِدَاءً خَفِيًّا ﴿٣﴾
3. Alipomwita Rabb wake mwito wa siri.
قَالَ رَبِّ إِنِّي وَهَنَ الْعَظْمُ مِنِّي وَاشْتَعَلَ الرَّأْسُ شَيْبًا وَلَمْ أَكُن بِدُعَائِكَ رَبِّ شَقِيًّا ﴿٤﴾
4. Akasema: Rabb wangu! Hakika mimi mifupa imeninyong’onyea na kichwa kimeng’aa mvi, na wala sikuwa mwenye kunyimwa katika kukuomba Duaa, ee Rabb wangu.[2]
وَإِنِّي خِفْتُ الْمَوَالِيَ مِن وَرَائِي وَكَانَتِ امْرَأَتِي عَاقِرًا فَهَبْ لِي مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا ﴿٥﴾
5. Nami nakhofia jamaa zangu nyuma yangu, na mke wangu ni tasa. Basi Nitunukie kutoka kwako (mwana) mrithi.[3]
يَرِثُنِي وَيَرِثُ مِنْ آلِ يَعْقُوبَ ۖ وَاجْعَلْهُ رَبِّ رَضِيًّا ﴿٦﴾
6. Anirithi na arithi kizazi cha Ya’quwb, na Mjaalie Rabb wangu awe mwenye kuridhisha
يَا زَكَرِيَّا إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ اسْمُهُ يَحْيَىٰ لَمْ نَجْعَل لَّهُ مِن قَبْلُ سَمِيًّا ﴿٧﴾
7. (Akaambiwa): Ee Zakariyyaa! Hakika Sisi Tunakubashiria ghulamu jina lake Yahyaa, Hatukupata kabla kumpa jina hilo yeyote.
قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَكَانَتِ امْرَأَتِي عَاقِرًا وَقَدْ بَلَغْتُ مِنَ الْكِبَرِ عِتِيًّا ﴿٨﴾
8. (Zakariyyaa) akasema: Ee Rabb wangu! Vipi nitapata ghulamu na hali mke wangu ni tasa, na nimeshafikia uzee wa kupindukia mipaka?
قَالَ كَذَٰلِكَ قَالَ رَبُّكَ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ وَقَدْ خَلَقْتُكَ مِن قَبْلُ وَلَمْ تَكُ شَيْئًا ﴿٩﴾
9. Akasema: Ni hivyo hivyo (lakini) Rabb wako Amesema: Haya ni sahali Kwangu kwani Nilikwishakukuumba kabla na wala hukuwa chochote.
قَالَ رَبِّ اجْعَل لِّي آيَةً ۚ قَالَ آيَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ النَّاسَ ثَلَاثَ لَيَالٍ سَوِيًّا ﴿١٠﴾
10. (Zakariyyaa) akasema: Rabb wangu! Nijaalie Aayah (Ishara, Alama). Akasema: Aayah yako ni kwamba hutoweza kuwasemesha watu nyusiku tatu ilhali huna kasoro.
فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ مِنَ الْمِحْرَابِ فَأَوْحَىٰ إِلَيْهِمْ أَن سَبِّحُوا بُكْرَةً وَعَشِيًّا ﴿١١﴾
11. Basi akawatokea watu wake kutoka mihrabuni, akawaashiria: Msabihini (Allaah) asubuhi na jioni.
يَا يَحْيَىٰ خُذِ الْكِتَابَ بِقُوَّةٍ ۖ وَآتَيْنَاهُ الْحُكْمَ صَبِيًّا ﴿١٢﴾
12. Ee Yahyaa! Chukua Kitabu kwa nguvu. Na Tukampa hukma[4] angali mtoto.
وَحَنَانًا مِّن لَّدُنَّا وَزَكَاةً ۖ وَكَانَ تَقِيًّا ﴿١٣﴾
13. Na (Tukampa pia) upole na huruma kutoka Kwetu, na utakaso (pia), na akawa mwenye taqwa.
وَبَرًّا بِوَالِدَيْهِ وَلَمْ يَكُن جَبَّارًا عَصِيًّا ﴿١٤﴾
14. Na mtiifu mno kwa wazazi wake wawili, na wala hakuwa jabari wala muasi.
وَسَلَامٌ عَلَيْهِ يَوْمَ وُلِدَ وَيَوْمَ يَمُوتُ وَيَوْمَ يُبْعَثُ حَيًّا ﴿١٥﴾
15. Na amani iwe juu yake siku aliyozaliwa, na siku atakayokufa na siku atakayofufuliwa kuwa hai.
وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مَرْيَمَ إِذِ انتَبَذَتْ مِنْ أَهْلِهَا مَكَانًا شَرْقِيًّا ﴿١٦﴾
16. Na mtaje katika Kitabu Maryam[5] alipojiondosha kutoka kwa ahli zake, mahali pa Mashariki.
فَاتَّخَذَتْ مِن دُونِهِمْ حِجَابًا فَأَرْسَلْنَا إِلَيْهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرًا سَوِيًّا ﴿١٧﴾
17. Akafanya pazia kujitenga nao, Tukampelekea Ruwh[6] Wetu (Jibriyl عليه السلام) akajimithilisha kwake kama binaadam timamu.
قَالَتْ إِنِّي أَعُوذُ بِالرَّحْمَـٰنِ مِنكَ إِن كُنتَ تَقِيًّا ﴿١٨﴾
18. (Maryam) akasema: Najikinga kwa Ar-Rahmaan usinidhuru, ukiwa ni mwenye taqwa.
قَالَ إِنَّمَا أَنَا رَسُولُ رَبِّكِ لِأَهَبَ لَكِ غُلَامًا زَكِيًّا ﴿١٩﴾
19. (Jibriyl عليه السلام) akasema: Hakika mimi ni Mjumbe wa Rabb wako ili nikubashirie tunu ya ghulamu aliyetakasika.
قَالَتْ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ وَلَمْ أَكُ بَغِيًّا ﴿٢٠﴾
20. (Maryam) akasema: Itakuwaje niwe na ghulamu na hali hakunigusa mtu yeyote, na wala mimi si kahaba?
قَالَ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ ۖ وَلِنَجْعَلَهُ آيَةً لِّلنَّاسِ وَرَحْمَةً مِّنَّا ۚ وَكَانَ أَمْرًا مَّقْضِيًّا ﴿٢١﴾
21. (Jibriyl) akasema: Ni hivyo hivyo (lakini) Rabb wako Amesema: Haya ni sahali Kwangu! Na ili Tumfanye awe Aayah (Ishara, Alama, Dalili) kwa watu na Rehma kutoka Kwetu, na limekuwa jambo lililokwisha hukumiwa.
فَحَمَلَتْهُ فَانتَبَذَتْ بِهِ مَكَانًا قَصِيًّا ﴿٢٢﴾
22. Basi akaibeba mimba, na akaondoka nayo mahali pa mbali.
فَأَجَاءَهَا الْمَخَاضُ إِلَىٰ جِذْعِ النَّخْلَةِ قَالَتْ يَا لَيْتَنِي مِتُّ قَبْلَ هَـٰذَا وَكُنتُ نَسْيًا مَّنسِيًّا ﴿٢٣﴾
23. Uchungu wa uzazi ukampeleka mpaka katika shina la mtende. Akasema: Laiti ningelikufa kabla ya haya na nikawa niliyesahaulika kabisa!
فَنَادَاهَا مِن تَحْتِهَا أَلَّا تَحْزَنِي قَدْ جَعَلَ رَبُّكِ تَحْتَكِ سَرِيًّا ﴿٢٤﴾
24. (Jibriyl au ‘Iysaa) akamnadia kutoka chini yake kwamba: Usihuzunike! Rabb wako Amekwishakufanyia kijito cha maji.
وَهُزِّي إِلَيْكِ بِجِذْعِ النَّخْلَةِ تُسَاقِطْ عَلَيْكِ رُطَبًا جَنِيًّا ﴿٢٥﴾
25. Na tingisha kuelekea kwako shina la mtende, litakuangushia tende safi zilizoiva na zilizo tayari kuchumwa.
فَكُلِي وَاشْرَبِي وَقَرِّي عَيْنًا ۖ فَإِمَّا تَرَيِنَّ مِنَ الْبَشَرِ أَحَدًا فَقُولِي إِنِّي نَذَرْتُ لِلرَّحْمَـٰنِ صَوْمًا فَلَنْ أُكَلِّمَ الْيَوْمَ إِنسِيًّا ﴿٢٦﴾
26. Basi kula na kunywa na litue jicho lako. Na utakapokutana na mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri ya kunyamaza kwa Ar-Rahmaan, hivyo leo sitomsemesha mtu yeyote.
فَأَتَتْ بِهِ قَوْمَهَا تَحْمِلُهُ ۖ قَالُوا يَا مَرْيَمُ لَقَدْ جِئْتِ شَيْئًا فَرِيًّا ﴿٢٧﴾
27. Akawafikia watu wake akiwa amembeba (mtoto), wakasema: Ee Maryam! Kwa yakini umeleta jambo la ajabu, kuu na ovu mno!
يَا أُخْتَ هَارُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ امْرَأَ سَوْءٍ وَمَا كَانَتْ أُمُّكِ بَغِيًّا ﴿٢٨﴾
28. Ee dada wa Haaruwn! Hakuwa baba yako mtu muovu, na wala hakuwa mama yako kahaba.
فَأَشَارَتْ إِلَيْهِ ۖ قَالُوا كَيْفَ نُكَلِّمُ مَن كَانَ فِي الْمَهْدِ صَبِيًّا ﴿٢٩﴾
29. Akamuashiria. Wakasema: Vipi tuseme na aliye kwenye susu (kitanda) akiwa bado ni mtoto mchanga?
قَالَ إِنِّي عَبْدُ اللَّـهِ آتَانِيَ الْكِتَابَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا ﴿٣٠﴾
30. (Mtoto huyo ‘Iysaa) akasema:[7] Hakika mimi ni Mja wa Allaah, Amenipa Kitabu (Injiyl) na Amenijaalia kuwa Nabiy.[8]
وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيْنَ مَا كُنتُ وَأَوْصَانِي بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ مَا دُمْتُ حَيًّا ﴿٣١﴾
31. Na Amenijaalia kuwa mwenye kubarikiwa popote nitakapokuweko, na Ameniusia Swalaah na Zakaah madamu niko katika uhai.
وَبَرًّا بِوَالِدَتِي وَلَمْ يَجْعَلْنِي جَبَّارًا شَقِيًّا ﴿٣٢﴾
32. Na niwe mtiifu mno kwa mama yangu, na wala Hakunijaalia kuwa jabari, mwovu.
وَالسَّلَامُ عَلَيَّ يَوْمَ وُلِدتُّ وَيَوْمَ أَمُوتُ وَيَوْمَ أُبْعَثُ حَيًّا ﴿٣٣﴾
33. Na amani iwe juu yangu siku niliyozaliwa, na siku nitakayokufa, na siku nitakayofufuliwa kuwa hai.
ذَٰلِكَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ ۚ قَوْلَ الْحَقِّ الَّذِي فِيهِ يَمْتَرُونَ ﴿٣٤﴾
34. Huyo ndiye ‘Iysaa mwana wa Maryam! Kauli ya haki ambayo wanaitilia shaka.
مَا كَانَ لِلَّـهِ أَن يَتَّخِذَ مِن وَلَدٍ ۖ سُبْحَانَهُ ۚ إِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٣٥﴾
35. Haiwi kwa Allaah kamwe Ajichukulie mwana yeyote. Subhaanah! (Utakasifu ni Wake!) Anapokidhia jambo basi huliambia: Kun! (Kuwa) nalo linakuwa!
وَإِنَّ اللَّـهَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ﴿٣٦﴾
36. (Nabiy ‘Iysaa akasema): Na kwamba hakika Allaah Ni Rabb wangu, na Rabb wenu, basi mwabuduni Yeye (Pekee). Hii ndio njia iliyonyooka.
فَاخْتَلَفَ الْأَحْزَابُ مِن بَيْنِهِمْ ۖ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِن مَّشْهَدِ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٣٧﴾
37. Lakini makundi yakakhitilafiana baina yao (kuhusu Nabiy ‘Iysaa). Basi ole wao wale waliokufuru na hudhurisho la Siku iliyo kuu kabisa.[9]
أَسْمِعْ بِهِمْ وَأَبْصِرْ يَوْمَ يَأْتُونَنَا ۖ لَـٰكِنِ الظَّالِمُونَ الْيَوْمَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٣٨﴾
38. Watasikia na wataona vizuri vilioje Siku watakayotujia. Lakini madhalimu hivi sasa wako katika upotofu ulio bayana.
وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ الْحَسْرَةِ إِذْ قُضِيَ الْأَمْرُ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ وَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٣٩﴾
39. Na waonye Siku ya majuto itakapohukumiwa amri, na hali wao wamo katika mghafala, wala hawaamini.
إِنَّا نَحْنُ نَرِثُ الْأَرْضَ وَمَنْ عَلَيْهَا وَإِلَيْنَا يُرْجَعُونَ ﴿٤٠﴾
40. Hakika Sisi Tutairithi ardhi na waliokuwemo humo, na Kwetu watarejeshwa.
وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِبْرَاهِيمَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صِدِّيقًا نَّبِيًّا ﴿٤١﴾
41. Na mtaje katika Kitabu Ibraahiym. Hakika yeye alikuwa mkweli wa kidhati, Nabiy.
إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ لِمَ تَعْبُدُ مَا لَا يَسْمَعُ وَلَا يُبْصِرُ وَلَا يُغْنِي عَنكَ شَيْئًا ﴿٤٢﴾
42. Pindi alipomwambia baba yake: Ee baba yangu kipenzi! Kwa nini unaabudu vile visivyosikia na visivyoona na visivyokufaa kitu chochote?
يَا أَبَتِ إِنِّي قَدْ جَاءَنِي مِنَ الْعِلْمِ مَا لَمْ يَأْتِكَ فَاتَّبِعْنِي أَهْدِكَ صِرَاطًا سَوِيًّا ﴿٤٣﴾
43. Ee baba yangu kipenzi! Hakika mimi imekwishanijia elimu isiyokufikia wewe, basi nifuate nikuongoze njia iliyonyooka.
يَا أَبَتِ لَا تَعْبُدِ الشَّيْطَانَ ۖ إِنَّ الشَّيْطَانَ كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ عَصِيًّا ﴿٤٤﴾
44. Ee baba yangu kipenzi! Usimwabudu shaytwaan. Hakika shaytwaan daima ni mwenye kumuasi Ar-Rahmaan.
يَا أَبَتِ إِنِّي أَخَافُ أَن يَمَسَّكَ عَذَابٌ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ فَتَكُونَ لِلشَّيْطَانِ وَلِيًّا ﴿٤٥﴾
45. Ee baba yangu kipenzi! Hakika mimi nakhofu isije kukushika adhabu kutoka kwa Ar-Rahmaan, ukaja kuwa rafiki wa shaytwaan.
قَالَ أَرَاغِبٌ أَنتَ عَنْ آلِهَتِي يَا إِبْرَاهِيمُ ۖ لَئِن لَّمْ تَنتَهِ لَأَرْجُمَنَّكَ ۖ وَاهْجُرْنِي مَلِيًّا ﴿٤٦﴾
46. (Baba yake) akasema: Unachukia waabudiwa wangu ee Ibraahiym? Usipokoma, basi lazima nitakupiga mawe, na niondokelee mbali kwa muda mrefu!
قَالَ سَلَامٌ عَلَيْكَ ۖ سَأَسْتَغْفِرُ لَكَ رَبِّي ۖ إِنَّهُ كَانَ بِي حَفِيًّا ﴿٤٧﴾
47. (Ibraahiym) akasema: Salaamun ‘Alayka. (Amani iwe juu yako). Nitakuombea maghfirah kwa Rabb wangu. Hakika Yeye daima Ni Mwenye Kunihurumia sana.
وَأَعْتَزِلُكُمْ وَمَا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَأَدْعُو رَبِّي عَسَىٰ أَلَّا أَكُونَ بِدُعَاءِ رَبِّي شَقِيًّا ﴿٤٨﴾
48. Na natengana nanyi na mnavyoviomba badala ya Allaah. Na namuomba Rabb wangu, asaa nisijekuwa mwenye kunyimwa duaa yangu kwa kumwomba Rabb wangu.
فَلَمَّا اعْتَزَلَهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۖ وَكُلًّا جَعَلْنَا نَبِيًّا ﴿٤٩﴾
49. Basi alipotengana nao na wanayoyaabudu badala ya Allaah, Tulimtunukia Is-haaq, na (mjukuu) Ya’quwb. Na kila mmoja wao Tulimjaalia kuwa Nabiy.
وَوَهَبْنَا لَهُم مِّن رَّحْمَتِنَا وَجَعَلْنَا لَهُمْ لِسَانَ صِدْقٍ عَلِيًّا ﴿٥٠﴾
50. Na Tukawatunukia katika Rehma Zetu, na Tukawajaalia wenye kutajwa kwa sifa nzuri za kutukuka.
وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مُوسَىٰ ۚ إِنَّهُ كَانَ مُخْلَصًا وَكَانَ رَسُولًا نَّبِيًّا ﴿٥١﴾
51. Na mtaje katika Kitabu Muwsaa. Hakika yeye alikuwa amekhitariwa kwa ikhlaasw yake na alikuwa Rasuli na Nabiy.
وَنَادَيْنَاهُ مِن جَانِبِ الطُّورِ الْأَيْمَنِ وَقَرَّبْنَاهُ نَجِيًّا ﴿٥٢﴾
52. Na Tukamwita kutoka upande wa kulia wa mlima na Tukamkurubisha kuzungumza naye kwa siri.
وَوَهَبْنَا لَهُ مِن رَّحْمَتِنَا أَخَاهُ هَارُونَ نَبِيًّا ﴿٥٣﴾
53. Na Tukamtunukia kutokana na Rehma Zetu, kaka yake Haaruwn awe Nabiy.
وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِسْمَاعِيلَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صَادِقَ الْوَعْدِ وَكَانَ رَسُولًا نَّبِيًّا ﴿٥٤﴾
54. Na mtaje katika Kitabu Ismaa’iyl. Hakika yeye alikuwa mkweli wa ahadi na alikuwa Rasuli na Nabiy.
وَكَانَ يَأْمُرُ أَهْلَهُ بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ وَكَانَ عِندَ رَبِّهِ مَرْضِيًّا ﴿٥٥﴾
55. Na alikuwa akiwaamrisha ahli zake Swalaah na Zakaah, na alikuwa mridhiwa mbele ya Rabb wake.
وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِدْرِيسَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صِدِّيقًا نَّبِيًّا ﴿٥٦﴾
56. Na mtaje katika Kitabu Idriys. Hakika yeye alikuwa mkweli wa kidhati, Nabiy.
وَرَفَعْنَاهُ مَكَانًا عَلِيًّا﴿٥٧﴾
57. Na Tukamuinua daraja ya juu.
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ مِن ذُرِّيَّةِ آدَمَ وَمِمَّنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ وَمِن ذُرِّيَّةِ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْرَائِيلَ وَمِمَّنْ هَدَيْنَا وَاجْتَبَيْنَا ۚ إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُ الرَّحْمَـٰنِ خَرُّوا سُجَّدًا وَبُكِيًّا ۩﴿٥٨﴾
58. Hao ndio ambao Allaah Amewaneemesha miongoni mwa Manabii katika uzao wa Aadam, na wale Tuliowapandisha (katika jahazi) pamoja na Nuwh[10] na katika uzao wa Ibraahiym na (uzao wa) Israaiyl (Ya’quwb) na wale Tuliowaongoa na Tukawateua. Wanaposomewa Aayaat za Ar-Rahmaan huporomoka kifudifudi wakisujudu na kulia.
فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ ۖ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا ﴿٥٩﴾
59. Wakafuata baada yao waovu, walipoteza Swalaah na wakafuata matamanio, basi watakutana na adhabu motoni.
إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلَا يُظْلَمُونَ شَيْئًا ﴿٦٠﴾
60. Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda mema. Basi hao wataingia Jannah na wala hawatodhulumiwa chochote.
جَنَّاتِ عَدْنٍ الَّتِي وَعَدَ الرَّحْمَـٰنُ عِبَادَهُ بِالْغَيْبِ ۚ إِنَّهُ كَانَ وَعْدُهُ مَأْتِيًّا ﴿٦١﴾
61. Jannaat za kudumu milele ambazo Ar-Rahmaan Amewaahidi Waja Wake bila wao kuziona. Hakika Ahadi Yake itafika tu.
لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا إِلَّا سَلَامًا ۖ وَلَهُمْ رِزْقُهُمْ فِيهَا بُكْرَةً وَعَشِيًّا ﴿٦٢﴾
62. Hawatosikia humo upuuzi wowote ule isipokuwa salama tu. Na watapata riziki zao humo asubuhi na jioni.
تِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي نُورِثُ مِنْ عِبَادِنَا مَن كَانَ تَقِيًّا ﴿٦٣﴾
63. Hiyo ni Jannah ambayo Tutawarithisha miongoni mwa Waja Wetu waliokuwa na taqwa.
وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلَّا بِأَمْرِ رَبِّكَ ۖ لَهُ مَا بَيْنَ أَيْدِينَا وَمَا خَلْفَنَا وَمَا بَيْنَ ذَٰلِكَ ۚ وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيًّا ﴿٦٤﴾
64. Na (sisi Malaika) hatuteremki ila kwa Amri ya Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Ni Yake Yeye yaliyoko mbele yetu, na yaliyoko nyuma yetu, na yaliyoko baina ya hayo. Na Rabb wako Si Mwenye Kusahau kamwe.[11]
رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا ﴿٦٥﴾
65. Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake. Basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika Ibaada Yake. Je, unamjua yeyote anayefanana Naye (Allaah)?[12]
وَيَقُولُ الْإِنسَانُ أَإِذَا مَا مِتُّ لَسَوْفَ أُخْرَجُ حَيًّا ﴿٦٦﴾
66. Na binaadam husema: Je, nitakapokufa, hivi kweli nitatolewa nikiwa hai?
أَوَلَا يَذْكُرُ الْإِنسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِن قَبْلُ وَلَمْ يَكُ شَيْئًا ﴿٦٧﴾
67. Je, hakumbuki binaadam kwamba Tulimuumba kabla, na hali hakuwa chochote?
فَوَرَبِّكَ لَنَحْشُرَنَّهُمْ وَالشَّيَاطِينَ ثُمَّ لَنُحْضِرَنَّهُمْ حَوْلَ جَهَنَّمَ جِثِيًّا ﴿٦٨﴾
68. Basi Naapa kwa Rabb wako. Bila shaka Tutawakusanya wao pamoja na mashaytwaan, kisha Tutawahudhurisha pembezoni mwa Jahannam huku wamepiga magoti.
ثُمَّ لَنَنزِعَنَّ مِن كُلِّ شِيعَةٍ أَيُّهُمْ أَشَدُّ عَلَى الرَّحْمَـٰنِ عِتِيًّا ﴿٦٩﴾
69. Kisha bila shaka Tutawachomoa kutoka katika kila kundi wale ambao walimuasi zaidi Ar-Rahmaan.
ثُمَّ لَنَحْنُ أَعْلَمُ بِالَّذِينَ هُمْ أَوْلَىٰ بِهَا صِلِيًّا ﴿٧٠﴾
70. Kisha bila shaka Sisi Tunawajua zaidi wale wanaostahiki zaidi kuunguzwa humo.
وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتْمًا مَّقْضِيًّا ﴿٧١﴾
71. Na hakuna yeyote miongoni mwenu, isipokuwa ni mwenye kuufikia (moto).[13] Hiyo ni hukumu ya Rabb wako lazima itimizwe.
ثُمَّ نُنَجِّي الَّذِينَ اتَّقَوا وَّنَذَرُ الظَّالِمِينَ فِيهَا جِثِيًّا ﴿٧٢﴾
72. Kisha Tutawaokoa wale waliokuwa na taqwa, na Tutawaacha madhalimu humo wamepiga magoti.
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ قَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا أَيُّ الْفَرِيقَيْنِ خَيْرٌ مَّقَامًا وَأَحْسَنُ نَدِيًّا ﴿٧٣﴾
73. Na wanaposomewa Aayaat Zetu zilizo wazi, wale waliokufuru huwaambia walioamini: Kundi lipi kati ya mawili haya lenye cheo bora zaidi na majilisi mazuri zaidi?
وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّن قَرْنٍ هُمْ أَحْسَنُ أَثَاثًا وَرِئْيًا ﴿٧٤﴾
74. Ni karne nyingi sana Tumeziangamiza kabla yao. Wao walikuwa na mapambo mazuri zaidi na mwonekano maridadi zaidi.
قُلْ مَن كَانَ فِي الضَّلَالَةِ فَلْيَمْدُدْ لَهُ الرَّحْمَـٰنُ مَدًّا ۚ حَتَّىٰ إِذَا رَأَوْا مَا يُوعَدُونَ إِمَّا الْعَذَابَ وَإِمَّا السَّاعَةَ فَسَيَعْلَمُونَ مَنْ هُوَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضْعَفُ جُندًا ﴿٧٥﴾
75. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Aliyekuwa katika upotofu, basi Ar-Rahmaan Atawapanulia muda. Hata watakapoona waliyotishiwa; ima adhabu au ima Saa, basi watakuja kujua ni nani aliye mahali paovu zaidi na mwenye askari dhaifu.
وَيَزِيدُ اللَّـهُ الَّذِينَ اهْتَدَوْا هُدًى ۗ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ مَّرَدًّا ﴿٧٦﴾
76. Na Allaah Atawazidishia hidaaya wale wenye kushika uongofu. Na mema yanayobakia[14] ni bora zaidi mbele ya Rabb wako kwa thawabu na matokeo bora zaidi ya mwisho.
أَفَرَأَيْتَ الَّذِي كَفَرَ بِآيَاتِنَا وَقَالَ لَأُوتَيَنَّ مَالًا وَوَلَدًا ﴿٧٧﴾
77. Je, umemuona yule aliyezikufuru Aayaat Zetu na akasema: Bila shaka nitapewa (Aakhirah) mali na watoto?[15]
أَطَّلَعَ الْغَيْبَ أَمِ اتَّخَذَ عِندَ الرَّحْمَـٰنِ عَهْدًا ﴿٧٨﴾
78. Je, kwani ameyajua ya ghaibu au amechukua ahadi kwa Ar-Rahmaan?
كَلَّا ۚ سَنَكْتُبُ مَا يَقُولُ وَنَمُدُّ لَهُ مِنَ الْعَذَابِ مَدًّا ﴿٧٩﴾
79. Laa, hasha! Tutayaandika yale anayoyasema na Tutampanulia muda wa adhabu ya kurefuka.
وَنَرِثُهُ مَا يَقُولُ وَيَأْتِينَا فَرْدًا ﴿٨٠﴾
80. Na Tutamrithi yale anayoyasema (mali na watoto), na atatujia peke yake!
وَاتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ آلِهَةً لِّيَكُونُوا لَهُمْ عِزًّا ﴿٨١﴾
81. Na wakachukua badala ya Allaah waabudiwa ili eti iwape taadhima na nguvu.
كَلَّا ۚ سَيَكْفُرُونَ بِعِبَادَتِهِمْ وَيَكُونُونَ عَلَيْهِمْ ضِدًّا ﴿٨٢﴾
82. Laa, hasha! Watakanusha ibaada zao, na watakuwa wapinzani wao.
أَلَمْ تَرَ أَنَّا أَرْسَلْنَا الشَّيَاطِينَ عَلَى الْكَافِرِينَ تَؤُزُّهُمْ أَزًّا ﴿٨٣﴾
83. Je, huoni kwamba Sisi Tunapeleka mashaytwaan kwa makafiri ili wawachochee (uovu) kwa uchochezi?
فَلَا تَعْجَلْ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّمَا نَعُدُّ لَهُمْ عَدًّا ﴿٨٤﴾
84. Basi usiwafanyie haraka. Hakika Sisi Tunawahesabia idadi za (siku) zao.
يَوْمَ نَحْشُرُ الْمُتَّقِينَ إِلَى الرَّحْمَـٰنِ وَفْدًا ﴿٨٥﴾
85. Siku Tutakayowakusanya wenye taqwa kwenda kwa Ar-Rahmaan wakiwa (juu ya vipando) kama ni wawakilishi wa heshima.
وَنَسُوقُ الْمُجْرِمِينَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ وِرْدًا ﴿٨٦﴾
86. Na Tutawaendesha wahalifu kuelekea Jahannam wakiwa na kiu.
لَّا يَمْلِكُونَ الشَّفَاعَةَ إِلَّا مَنِ اتَّخَذَ عِندَ الرَّحْمَـٰنِ عَهْدًا ﴿٨٧﴾
87. Hawatokuwa na mamlaka ya shufaa isipokuwa yule aliyechukua ahadi kwa Ar-Rahmaan.
وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَـٰنُ وَلَدًا ﴿٨٨﴾
88. Na wamesema: Ar-Rahmaan Amejifanyia mwana.[16]
لَّقَدْ جِئْتُمْ شَيْئًا إِدًّا ﴿٨٩﴾
89. Kwa yakini mmeleta jambo kuu ovu na la kuchukiza mno!
تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ الْأَرْضُ وَتَخِرُّ الْجِبَالُ هَدًّا ﴿٩٠﴾
90. Zinakaribia mbingu kupasuka kwa (tamko) hilo, na ardhi kuraruka, na milima kuporomoka na kubomoka![17]
أَن دَعَوْا لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدًا ﴿٩١﴾
91. Kwa kule kudai kwao kuwa Ar-Rahmaan Ana mwana.
وَمَا يَنبَغِي لِلرَّحْمَـٰنِ أَن يَتَّخِذَ وَلَدًا ﴿٩٢﴾
92. Na wala haipasi kwa Ar-Rahmaan Kujifanyia mwana.
إِن كُلُّ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ إِلَّا آتِي الرَّحْمَـٰنِ عَبْدًا ﴿٩٣﴾
93. Hakuna yeyote yule aliyeko katika mbingu na ardhi isipokuwa atamjia Ar-Rahmaan akiwa ni mtumwa Kwake.
لَّقَدْ أَحْصَاهُمْ وَعَدَّهُمْ عَدًّا ﴿٩٤﴾
94. Kwa hakika Amewadhibiti barabara, na Akawahesabu hesabu ya sawasawa.
وَكُلُّهُمْ آتِيهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَرْدًا ﴿٩٥﴾
95. Na kila mmoja wao atamjia (Allaah) Siku ya Qiyaamah akiwa peke yake.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَيَجْعَلُ لَهُمُ الرَّحْمَـٰنُ وُدًّا ﴿٩٦﴾
96. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Ar-Rahmaan Atawajaalia kwao mapenzi.
فَإِنَّمَا يَسَّرْنَاهُ بِلِسَانِكَ لِتُبَشِّرَ بِهِ الْمُتَّقِينَ وَتُنذِرَ بِهِ قَوْمًا لُّدًّا ﴿٩٧﴾
97. Basi hakika Tumeiwepesisha (Qur-aan) kwa lugha yako ili uwabashirie kwayo wenye taqwa, na uwaonye kwayo watu maadui wapinzani (wa haki).
وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّن قَرْنٍ هَلْ تُحِسُّ مِنْهُم مِّنْ أَحَدٍ أَوْ تَسْمَعُ لَهُمْ رِكْزًا ﴿٩٨﴾
98. Na ni karne nyingi sana Tumeziangamiza kabla yao. Je unamhisi hata mmoja katika wao, au unasikia mchakato wowote wao?
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Kutawassal Katika Duaa Kwa Hali Na Sababu Ya Kutaka Duaa Itaqabaliwe:
Aayah hii ya (3) hadi namba (6), Nabiy Zakariyyaa (عليه السّلام) anatawassal (anajikurubisha kwa Allaah) wakati anapoomba duaa yake hii kwa kutaja hali yake ilivyo ya siha na uzee pamoja na mkewe kwamba ni tasa. Na akataja sababu ya kuhitaji haja yake, nayo ni kuomba mtoto ili amrithi. Akataja kwanza mifupa yake kuwa dhaifu na nywele zake kugeuka mvi. Kisha akataja sababu kwamba alikhofu baada ya kufariki kwake kubakia kizazi kiovu, hivyo aliomba mtoto ili awe Nabiy baada yake atakayeongoza watu katika Dini. Hivyo basi, kutaja sababu na kujieleza kwa Allaah wakati wa kuomba duaa ya mas-ala ya kidunia na kiaakhirah, ni jambo linaloruhusiwa madam tu ni jambo lenye kumridhisha Allaah (سبحانه وتعالى).
[3] Urithi Wa Unabii Ni Wa Ilimu Na Kulingania Dini:
Kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth:
وَإنَّ العُلَمَاءَ وَرَثَةُ الأنْبِيَاءِ ، وَإنَّ الأنْبِيَاءَ لَمْ يَوَرِّثُوا دِينَاراً وَلاَ دِرْهَماً وَإنَّمَا وَرَّثُوا العِلْمَ ، فَمَنْ أَخَذَهُ أَخَذَ بحَظٍّ وَافِرٍ. رواه أَبُو داود والترمذي .
Na hakika ‘Ulamaa ni warithi wa Manabii. Na hakika Manabii hawarithi dinari wala dirham, na bila shaka wao hurithiwa ilimu. [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
[4] Hukma:
Kumjua Allaah na Mipaka Yake, ilimu nyingi ya Dini yenye ufaqihi, ufahamu wa kina, busara, na utambuzi wa Sharia (hukumu) ya halali na haramu, na uwezo wa kuhukumu baina ya watu.
[5] Fadhila Za Maryam Mama Wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام):
Maryam Bint ‘Imraan ambaye ni mama yake Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) ni miongoni mwa wanawake bora kabisa wa ulimwengu. Rejea pia Aal-‘Imraan (3:42) ambamo Allaah (سبحانه وتعالى) Amemtakasa na kumsifia. Juu ya hayo, Allaah (سبحانه وتعالى) Amemfadhilisha kwa kujaalia Suwrah hii kuwa ni Suwrah pekee ya jina la mwanamke; Maryam.
Rejea pia At-Tahriym (66:12) ambako amesifiwa tena Maryam bint ‘Imraan
[7] Watoto Wachanga Watatu Walioongea:
Kuanzia Aayah hii namba (30) hadi namba (33) kisha namba (35-36) ni kauli ya Nabiy Iysaa (عليه السّلام) alipokuwa angali mchanga.
Na Hadiyth ifuatayo imethibitisha kuongea kwake angali mchanga pamoja na watoto wawili wengineo:
حَدَّثَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا جَرِيرُ بْنُ حَازِمٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سِيرِينَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " لَمْ يَتَكَلَّمْ فِي الْمَهْدِ إِلاَّ ثَلاَثَةٌ عِيسَى، وَكَانَ فِي بَنِي إِسْرَائِيلَ رَجُلٌ يُقَالُ لَهُ جُرَيْجٌ، كَانَ يُصَلِّي، فَجَاءَتْهُ أُمُّهُ فَدَعَتْهُ، فَقَالَ أُجِيبُهَا أَوْ أُصَلِّي. فَقَالَتِ اللَّهُمَّ لاَ تُمِتْهُ حَتَّى تُرِيَهُ وُجُوهَ الْمُومِسَاتِ. وَكَانَ جُرَيْجٌ فِي صَوْمَعَتِهِ، فَتَعَرَّضَتْ لَهُ امْرَأَةٌ وَكَلَّمَتْهُ فَأَبَى، فَأَتَتْ رَاعِيًا، فَأَمْكَنَتْهُ مِنْ نَفْسِهَا فَوَلَدَتْ غُلاَمًا، فَقَالَتْ مِنْ جُرَيْجٍ. فَأَتَوْهُ فَكَسَرُوا صَوْمَعَتَهُ، وَأَنْزَلُوهُ وَسَبُّوهُ، فَتَوَضَّأَ وَصَلَّى ثُمَّ أَتَى الْغُلاَمَ فَقَالَ مَنْ أَبُوكَ يَا غُلاَمُ قَالَ الرَّاعِي. قَالُوا نَبْنِي صَوْمَعَتَكَ مِنْ ذَهَبٍ. قَالَ لاَ إِلاَّ مِنْ طِينٍ. وَكَانَتِ امْرَأَةٌ تُرْضِعُ ابْنًا لَهَا مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ، فَمَرَّ بِهَا رَجُلٌ رَاكِبٌ ذُو شَارَةٍ، فَقَالَتِ اللَّهُمَّ اجْعَلِ ابْنِي مِثْلَهُ. فَتَرَكَ ثَدْيَهَا، وَأَقْبَلَ عَلَى الرَّاكِبِ فَقَالَ اللَّهُمَّ لاَ تَجْعَلْنِي مِثْلَهُ. ثُمَّ أَقْبَلَ عَلَى ثَدْيِهَا يَمَصُّهُ ـ قَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ كَأَنِّي أَنْظُرُ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم يَمَصُّ إِصْبَعَهُ ـ ثُمَّ مُرَّ بِأَمَةٍ فَقَالَتِ اللَّهُمَّ لاَ تَجْعَلِ ابْنِي مِثْلَ هَذِهِ. فَتَرَكَ ثَدْيَهَا فَقَالَ اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مِثْلَهَا. فَقَالَتْ لِمَ ذَاكَ فَقَالَ الرَّاكِبُ جَبَّارٌ مِنَ الْجَبَابِرَةِ، وَهَذِهِ الأَمَةُ يَقُولُونَ سَرَقْتِ زَنَيْتِ. وَلَمْ تَفْعَلْ ".
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hawakuzungumza mbelekoni ila watu watatu: (Mtoto wa kwanza ni) ‘Iysaa. (Mtoto wa pili ni mtoto) katika wana wa Israaiyl kulikuwa na mtu akiitwa Jurayj, mtu huyu alikuwa anaswali. Siku moja mama yake akaja akamwita lakini yule Jurayj akawa anawaza kwa kujiuliza: Je, nimjibu mama yangu au niendelee kuswali? Akaamua kuendelea kuswali na hakumjibu mama yake. Mama yake akasema: “Ee Allaah! Usimfishe mpaka umuoneshe nyuso za malaya.” Siku moja Jurayj alikuwa katika nyumba yake ya ibaada akamjia mwanamke, akamueleza anachokitaka (kufanya ya machafu). Jurayj akakataa. Yule mwanamke akaenda kwa mchungaji, na kutoa mwili wake kwake, basi (akashika mimba) na akazaa mtoto mwanamme, baada ya kufanya tendo la ndoa na yule mchungaji. Yule mwanamke akawa anadai kuwa yule mtoto amezaa na Jurayj. Watu wakamjia Jurayj na wakaivunja nyumba yake ya ibaada, na wakamtoa nje na kumtukana. Jurayj akatawadha na akaswali kisha akaenda kwa yule mtoto. Akamuuliza yule mtoto: “Je, baba yako ni nani, ee kijana?” Yule mtoto Akajibu: “Baba yangu ni mchungaji.” Watu baada ya kusikia haya wakamwambia Jurayj: “Tutakujengea nyumba yako kwa dhahabu.” Jurayj Akajibu: “Hapana, bali nijengeeni kwa udongo.” (Ama mtoto wa tatu ni) mwanamke fulani katika Bani Israaiyl ana mnyonyesha mtoto wake, mara akampitia mtu amepanda mnyama, mtu anayeashiriwa kwa hadhi na umaridadi. Yule mama akasema: “Ee Allaah! Mfanye mwanangu awe kama yule.” Yule mtoto akaliacha titi la mama yake akamuelekea yule aliyepanda akasema: “Ee Allaah! Usinijaalie kuwa kama yule!” Kisha akalielekea titi la mama yake huku anaendelea kunyonya.” Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) akaendelea: Kama vile ninamuangalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) anakinyonya kidole chake (akiashiria mtoto alivyokuwa). Kisha baada ya muda watu wakapita wakiwa na mjakazi. Mama yake yule mtoto akasema: “Ee Allaah! Usimfanye mwanangu kama huyu.” (yaani kama yule mjakazi). Yule mtoto akaliacha titi la mama yakekisha akasema: “Ee Allaah! Nijaalie kuwa kama yule.” Mama akasema: “Kwa nini unasema hivyo?” Yule mtoto akasema: “‘Yule mtu aliyekuwa amepanda ni dhalimu. Ama huyu mjakazi, wale watu wanasema kuwa ameiba, amezini ilhali hakufanya hivyo.” [Al-Bukhaariy Kitaab Cha Hadiyth Za Manabii]
[8] Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Anakiri Kuwa Yeye Ni Mja Wa Allaah Na Wala Sio Mwana Au Mshirika Wa Allaah:
Aayah hii ya Maryam (30 hadi 36), ni dalili ya wazi kuwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) ni mja wa Allaah na si mtoto Wake wala mshirika Wake. Rejea pia Az-Zukhruf (43:63-64), Al-Maaidah (5:17), na An-Nisaa (4:171).
[9] Kauli Walizokhitilafiana Mayahudi Na Naswara Kuhusu Nabiy Iysaa (عليه السّلام) :
Baada ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kubainisha hali ya ‘Iysaa mwana wa Maryam, jambo ambalo halina shaka, Allaah (سبحانه وتعالى) Anatuambia sasa kuwa makundi, yaani makundi ya upotofu kutoka kwa Mayahudi, Manaswara na wengineo katika daraja tofauti - wakakhitilafiana kuhusu Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام); ima kuvuka mipaka katika kumtukuza au kumkana na kumzushia. Basi baadhi yao wakasema: “Yeye ni Allaah.” Na baadhi yao wakasema: “Yeye ni mwana wa Allaah.” Na baadhi ya wao wakasema: “Yeye ni tatu wa watatu.” Na baadhi yao kama Mayahudi, hawakumfanya ni Rasuli bali walimtuhumu kuwa ni mwana wa kahaba. Na kauli zote hizi ni baatwil na za uongo!
Maoni yao hayo ya baatwil yametokana na uvumi, ukaidi, ushahidi wa uongo na shubha na hoja zisizokuwa na nguvu. Watu wote hawa wanastahiki onyo hili kali na ndipo Anasema (سبحانه وتعالى) Anasema:
فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِن مَّشْهَدِ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٣٧﴾
“Basi ole wao wale waliokufuru na hudhurisho la Siku iliyo kuu kabisa.”
Yaani: Hudhurisho la Qiyaamah ambalo watahudhurishwa na kushuhudia wote; kuanzia wa mwanzo hadi wa mwisho, waja wa mbinguni na ardhini. Atakuweko Muumba na viumbe Alivyoviumba. Siku ambayo itajaa zilzala (mitetemeko ya ardhi) na viwewe. Na Siku ambayo itafanyika hesabu ya matendo. Juu ya hivyo, hiyo Siku itakuja kubainisha wazi kabisa yote waliyokuwa wakiyaficha na kuyafichua na waliyokuwa wakiyanyamazia (kuficha haki). [Tafsiyr As-Sa’diy]
[10] Nabiy Nuwh (عليه السّلام) Na Kizazi Kilobakia, Naye Ni Rasuli Wa Kwanza Ardhini Na Ni Baba Wa Wanaadam Baada Ya Nabiy Aadam (عليه السّلام):
Rejea Asw-Swaaffaat (37:77) kwenye maelezo bayana na rejea zake mbalimbali.
Rejea Yuwnus (10:73), Huwd (11:40), Al-Muuminuwn (23:27), Nuwh (71:1), Al-Israa (17:3).
[12] Aayah Imekusanya Aina Tatu Za Tawhiyd:
‘Ulamaa wamesema kwamba Aayah hii imekusanya aina tatu za Tawhiyd kama ifuatavyo:
Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah (Kumpwekesha Allaah katika Uola Wake), na hii ni katika Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا
“Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake.”
Tawhiyd Al-Uluwhiyyah (Kumpwekesha Allaah katika ibaada), na hii ni katika Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ
“Basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika Ibaada Yake.”
Tawhiyd Asmaa Wasw-Swifaat (Kumpwekesha Allaah katika Majina Yake Mazuri na Sifa Zake Tukufu Kamilifu), na hii ni katika Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا
“Je, unamjua yeyote anayefanana Naye (Allaah)?”
Hakuna Anayefanana Na Allaah (سبحانه وتعالى) Kwa Majina Yake Wala Kwa Lolote:
Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا
“Je, unamjua yeyote anayefanana Naye (Allaah)?”
Naam! Hakuna anayefanana Naye kwa vyovyote wala kwa lolote, kwani Yeye Ni Mwenye Sifa za Pekee kama Anavyosema Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى) :
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿١١﴾
“Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.”
[Ash-Shuwraa (42:11)]
Na Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Hakuna yeyote anayeitwa Ar-Rahmaan isipokuwa Allaah (تبارك وتعالى) na Jina Lake linatukuzwa [Tafsiyr Ibn Kathiyr] Na hakuna pia anayeitwa Allaah isipokuwa Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee!
[13] Hakuna Budi Kuupitia Moto Wa Jahannam:
Kauli hii wanaambiwa viumbe wote; wema wao na wapotofu wao, Waumini wao na makafiri wao, kwamba hakuna hata mmoja wao isipokuwa aupitie na aufikie moto. Hukmu ambayo Allaah (عزّ وجلّ) Ameilazimisha Nafsi Yake kutimizwa, na Akawatishia kwayo Waja Wake. Hapana budi kutokea kwake na hakuna kuiepuka.
Na ‘Ulamaa wamekhitalafiana katika maana ya neno al-wuruwd "الوُرُوْدُ", ambalo liko ndani ya Aayah hii kwa wizani wa “Ismu Faa’il” (وَارِدُ). Kundi la kwanza limesema kwamba maana yake ni kuufikia huo moto, kuhudhurishwa kwa viumbe wote mbele yake hadi kila mtu afazaike, kisha baada ya hapo Allaah Awaokoe Waumini wenye taqwa.
Ama kundi la pili, wao wamesema: Maana ya al-wuruwd ni kuingia ndani ya moto huo, lakini kwa Waumini utakuwa baridi na salama na amani kwao.
Ama kundi la tatu, wao wanaona kwamba maana ya al-wuruwd ni kupita juu ya Asw-Swiraatw ambayo chini yake kuna Jahannam, na watu watapita kwa kadiri ya 'amali zao. Kuna ambao watavuka kwa kadiri ya upepesaji wa jicho, na wengine watavuka kama upepo, na wengineo kama mwendo wa farasi, na wengineo kama mwendo wa kawaida wa vipando, na wengineo watakuwa wanatembea haraka haraka, na wengine watakuwa wanavuka kwa mwendo wa kawaida wa kutembea, na wengineo watakuwa wanatambaa, na wengineo watanyakuliwa kisha watupwe motoni. Wote kulingana na uchaji wao (amali zao). [Tafsiyr As-Sa’diy]
[14] Al-Baaqiyaatu Asw-Swaalihaatu: Mema Yanayobakia: Rejea Al-Kahf (17:46).
[16] Kumsingizia Na Kumshutumu Allaah (سبحانه وتعالى) Kwamba Ana Mwana!
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: (قَالَ اللَّهُ: كَذَّبَنِي ابْنُ آدَمَ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ، وَشَتَمَنِي وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ، أَمَّا تَكْذِيبُهُ إِيَّاىَ أَنْ يَقُولَ إِنِّي لَنْ أُعِيدَهُ كَمَا بَدَأْتُهُ، وَأَمَّا شَتْمُهُ إِيَّاىَ أَنْ يَقُولَ اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا، وَأَنَا الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ أَلِدْ وَلَمْ أُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لِي كُفُؤًا أَحَدٌ))
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah Amesema: Binaadam amenikadhibisha, na wala hapaswi hilo! Na amenishutumu mja Wangu na wala hapaswi hilo! Ama kunikadhibisha kwake, amedai kuwa Sitoweza kumrudisha (kumfufua) kama alivyokuwa. Ama kunishutumu, ni kudai kuwa Nina mwana na ilhali Mimi Ni Asw-Swamad (Aliyekamilika Sifa za Utukufu Wake, Mkusudiwa wa haja zote) Ambaye Sikuzaa wala Sikuzaliwa na hakuna chochote kinachofanana na kulingana Nami.” [Al-Bukhaariy]
Rejea Al-Baqarah (2:116), An-Nisaa (4:171), Al-Maaidah (5:17), (5:75), At-Tawbah (9:30).
[17] Mbingu Kuraruka Kutokana Na Kumzulia Allaah (سبحانه وتعالى) Ana Mwana:
Imaam As-Sa’diy:
Kauli Ya Allaah (سبحانه وتعالى):
تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ الْأَرْضُ وَتَخِرُّ الْجِبَالُ هَدًّا ﴿٩٠﴾
“Zinakaribia mbingu kupasuka kwa (tamko) hilo, na ardhi kuraruka, na milima kuporomoka na kubomoka!” [Maryam (19:90)]
Hili ni chukizo na fedheha kwa maneno ya watu wakaidi, wasio na shukrani ambao walidai kuwa Ar-Rahmaan Amejichukulia mtoto wa kiume. Ni kama walivyodai Manaswara kuwa Al-Masiyh, yaani Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) ni mwana wa Allaah, na Mayahudi kuwa ‘Uzayr ni mwana wa Allaah, na washirikina kuwa Malaika ni mabinti wa Allaah! Allaah Ametakasika na madai yao hayo na Yuko mbali nayo kabisa. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Imaam Ibn Kathiyr:
Yaani: (Mbingu zinakaribia kupasuka) kutokana na Utukufu wake kwa Allaah zinaposikia kauli hii ya uovu itokayo kwa wanaadam. Sababu yake ni kuwa hizi (mbingu, ardhi n.k) ni viumbe vya Allaah na vimethibiti juu ya Tawhiyd Yake, na kwamba hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, Hana washirika, Hana rika, Hana mtoto, Hana mwenzi na Hana mwenza, bali Yeye ni Mmoja Pekee Mkusudiwa wa haja zote, Hakuzaa wala Hakuzaliwa. [Al-Ikhlaasw]
Ibn ’Abbaas (رضي الله عنهما) amesema kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) :
تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ الْأَرْضُ وَتَخِرُّ الْجِبَالُ هَدًّا ﴿٩٠﴾
“Zinakaribia mbingu kupasuka kwa (tamko) hilo, na ardhi kuraruka, na milima kuporomoka na kubomoka!”
Hakika mbingu na ardhi na milima na viumbe vyote - isipokuwa wanaadam na majini - vinaogopa mno shirki. Na kutokana na U’adhwama wa Allaah, viumbe hivi vinakaribia kutoweka Allaah Anapofanyiwa mshirika. Kama vile mshirikina hafaidiki na matendo yake mema kwa sababu ya kumshirikisha Allaah, kadhalika tunataraji kuwa Allaah Atawaghufuria madhambi wale waliompwekesha Allaah. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Na Hadiyth kadhaa zimethibiti kuhusu umuhimu na uzito wa kumpwekesha Allaah na Neno zito la Tawhiyd na fadhila za Neno hili la:
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ
Laa ilaaha illa-Allaah
Bonyeza viungo vifuatavyo vyenye faida tele:
Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd [184]
Hadiyth: Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah - أحاديثُ عَنْ فضْل لا إلَهَ إلاَّ الله [185]
Miongoni mwa Hadiyth hizo, ni hii ifuatayo:
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرَيِّ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) عَنْ رَسُولِ الله (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ ((قَالَ مُوسَى عَلَيْهِ السَّلامُ يَا رَبِّ! عَلِّمْنِي شَيْئًا أَذْكُرُكَ وَأَدْعُوكَ بِهِ. قَالَ: قُلْ يَا مُوسَى: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ. قَالَ يَا رَبِّ! كُلُّ عِبَادِكَ يَقُولُونَ هَذَا. قَالَ: يَا مُوسَى، لَوْ أَنَّ السَّمَوَاتِ السَّبْعَ وَعَامِرَهُنَّ غَيْرِي وَالأَرَضِينَ السَّبْعَ فِي كِفَّةٍ، وَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ فِي كِفَّةٍ، مَالَتْ بِهِنَّ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ)) رَوَاهُ ابْنُ حِبَّانَ وَالْحَاكِمُ وَصَحَّحَهُ.
Amesimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Muwsaa alisema: Ee Rabb wangu! Nifundishe kitu mahsusi kwangu ambacho kwacho nitakudhukuru na kukuomba duaa. (Allaah) Akasema: Ee Muwsaa! Sema:
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ
Laa ilaaha illa-Allaah.
Muwsaa akasema: Ee Rabb wangu! Waja Wako wote wanasema hivi. (Allaah) Akasema: Ee Muwsaa, lau kama mbingu saba na kila kilichokuwemo isipokuwa Mimi, na ardhi saba zikiwekwa katika kiganja cha mizani, na laa ilaaha illa-Allaah ikawekwa katika kiganja kingine cha mizani, basi laa ilaaha illa-Allaah itazishinda hizo.” [Ibn Hibaan, na Al-Haakim ameikiri kuwa ni Swahiyh]
Rejea Ash-Shuwraa (42:5), Al-Hashr (59:21).
طه
020-Twaaha
020-Twaahaa: Utangulizi Wa Suwrah [187]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم
طه ﴿١﴾
1. Twaaha.[1]
مَا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْقُرْآنَ لِتَشْقَىٰ ﴿٢﴾
2. Hatujakuteremshia Qur-aan ili upate mashaka.
إِلَّا تَذْكِرَةً لِّمَن يَخْشَىٰ ﴿٣﴾
3. Isipokuwa ni ukumbusho kwa anayekhofu.
تَنزِيلًا مِّمَّنْ خَلَقَ الْأَرْضَ وَالسَّمَاوَاتِ الْعُلَى ﴿٤﴾
4. Ni uteremsho kutoka kwa Yule Aliyeumba ardhi na mbingu zilizo juu kabisa.
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥﴾
5. Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma) Yuko juu[2] ya ‘Arsh[3].
لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَمَا تَحْتَ الثَّرَىٰ ﴿٦﴾
6. Ni Vyake Pekee vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini, na vilivyomo baina yake, na vilivyomo chini ya udongo.
وَإِن تَجْهَرْ بِالْقَوْلِ فَإِنَّهُ يَعْلَمُ السِّرَّ وَأَخْفَى ﴿٧﴾
7. Na ukinena kwa jahara, basi hakika Yeye Anajua siri na yanayofichika zaidi ya siri.
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ﴿٨﴾
8. Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Anayo Majina Mazuri kabisa.[4]
وَهَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ مُوسَىٰ ﴿٩﴾
9. Na je, imekufikia hadithi ya Muwsaa?
إِذْ رَأَىٰ نَارًا فَقَالَ لِأَهْلِهِ امْكُثُوا إِنِّي آنَسْتُ نَارًا لَّعَلِّي آتِيكُم مِّنْهَا بِقَبَسٍ أَوْ أَجِدُ عَلَى النَّارِ هُدًى ﴿١٠﴾
10. Alipouona moto, akawaambia ahli zake: Bakieni (hapa), kwa yakini nimeona moto, huenda nikakuleteeni kutoka humo kijinga cha moto, au nipate mwongozo kwenye huo moto.
فَلَمَّا أَتَاهَا نُودِيَ يَا مُوسَىٰ ﴿١١﴾
11. Basi alipoufikia, aliitwa: Ee Muwsaa!
إِنِّي أَنَا رَبُّكَ فَاخْلَعْ نَعْلَيْكَ ۖ إِنَّكَ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى ﴿١٢﴾
12. Hakika Mimi ni Rabb wako. Basi vua viatu vyako, kwani wewe hakika uko katika bonde takatifu la Twuwaa.
وَأَنَا اخْتَرْتُكَ فَاسْتَمِعْ لِمَا يُوحَىٰ ﴿١٣﴾
13. Nami Nimekuchagua. Basi sikiliza kwa makini yanayofunuliwa Wahy (kwako).
إِنَّنِي أَنَا اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدْنِي وَأَقِمِ الصَّلَاةَ لِذِكْرِي ﴿١٤﴾
14. Hakika Mimi Ni Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi. Basi niabudu, na simamisha Swalaah kwa ajili ya kunidhukuru.
إِنَّ السَّاعَةَ آتِيَةٌ أَكَادُ أُخْفِيهَا لِتُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا تَسْعَىٰ ﴿١٥﴾
15. Hakika Saa itafika tu. Nimekurubia kuificha ili kila nafsi ilipwe kwa yale iliyoyafanyia juhudi.
فَلَا يَصُدَّنَّكَ عَنْهَا مَن لَّا يُؤْمِنُ بِهَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ فَتَرْدَىٰ ﴿١٦﴾
16. Basi angalia asikukengeushe nayo yule asiyeiamini na akafuata hawaa, ukaja kuangamia.
وَمَا تِلْكَ بِيَمِينِكَ يَا مُوسَىٰ ﴿١٧﴾
17. Na nini hicho kilichoko katika mkono wako wa kulia ee Muwsaa?
قَالَ هِيَ عَصَايَ أَتَوَكَّأُ عَلَيْهَا وَأَهُشُّ بِهَا عَلَىٰ غَنَمِي وَلِيَ فِيهَا مَآرِبُ أُخْرَىٰ ﴿١٨﴾
18. (Muwsaa) akasema: Hii ni fimbo yangu, naiegemelea, na naangushia majani kwa ajili ya kondoo wangu, na pia nina maarubu mengineyo.
قَالَ أَلْقِهَا يَا مُوسَىٰ ﴿١٩﴾
19. (Allaah) Akasema: Basi iangushe ee Muwsaa.
فَأَلْقَاهَا فَإِذَا هِيَ حَيَّةٌ تَسْعَىٰ ﴿٢٠﴾
20. (Muwsaa) akaiangusha. Tahamaki hiyo ikawa ni nyoka anayetambaa mbio.
قَالَ خُذْهَا وَلَا تَخَفْ ۖ سَنُعِيدُهَا سِيرَتَهَا الْأُولَىٰ ﴿٢١﴾
21. (Allaah) Akasema: Ichukue na wala usikhofu. Tutairudisha katika hali yake ya awali.
وَاضْمُمْ يَدَكَ إِلَىٰ جَنَاحِكَ تَخْرُجْ بَيْضَاءَ مِنْ غَيْرِ سُوءٍ آيَةً أُخْرَىٰ ﴿٢٢﴾
22. Na ambatisha mkono wako katika ubavu wako, utatoka ukiwa mweupe bila ya madhara yoyote. Ni Aayah (Ishara, Dalili) nyengineo.
لِنُرِيَكَ مِنْ آيَاتِنَا الْكُبْرَى ﴿٢٣﴾
23. Ili Tukuonyeshe baadhi ya Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu kubwa kabisa.
اذْهَبْ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ ﴿٢٤﴾
24. Nenda kwa Firawni, hakika yeye amepindukia mipaka ya kuasi.
قَالَ رَبِّ اشْرَحْ لِي صَدْرِي ﴿٢٥﴾
25. (Muwsaa) akasema: Rabb wangu, Nikunjulie kifua changu.
وَيَسِّرْ لِي أَمْرِي ﴿٢٦﴾
26. Na Niwepesishie shughuli yangu.
وَاحْلُلْ عُقْدَةً مِّن لِّسَانِي ﴿٢٧﴾
27. Na Fungua fundo (la kigugumizi) katika ulimi wangu.
يَفْقَهُوا قَوْلِي ﴿٢٨﴾
28. Ili wafahamu kauli yangu.
وَاجْعَل لِّي وَزِيرًا مِّنْ أَهْلِي ﴿٢٩﴾
29. Na Nifanyie msaidizi kutoka ahli zangu.
هَارُونَ أَخِي ﴿٣٠﴾
30. Haaruwn, ndugu yangu.
اشْدُدْ بِهِ أَزْرِي ﴿٣١﴾
31. Nitie nguvu kwaye.
وَأَشْرِكْهُ فِي أَمْرِي ﴿٣٢﴾
32. Na Mshirikishe katika shughuli yangu.
كَيْ نُسَبِّحَكَ كَثِيرًا ﴿٣٣﴾
33. Ili tukusabihi kwa wingi.
وَنَذْكُرَكَ كَثِيرًا ﴿٣٤﴾
34. Na tukudhukuru kwa wingi.
إِنَّكَ كُنتَ بِنَا بَصِيرًا ﴿٣٥﴾
35. Hakika Wewe Ni Mwenye Kutuona sisi daima.
قَالَ قَدْ أُوتِيتَ سُؤْلَكَ يَا مُوسَىٰ ﴿٣٦﴾
36. (Allaah) Akasema: Umekwishapewa ombi lako ee Muwsaa.
وَلَقَدْ مَنَنَّا عَلَيْكَ مَرَّةً أُخْرَىٰ ﴿٣٧﴾
37. Na kwa yakini Tulikufanyia ihsaan mara nyingine.
إِذْ أَوْحَيْنَا إِلَىٰ أُمِّكَ مَا يُوحَىٰ ﴿٣٨﴾
38. Tulipomfunulia ilhamu mama yako yale yaliyofunuliwa.
أَنِ اقْذِفِيهِ فِي التَّابُوتِ فَاقْذِفِيهِ فِي الْيَمِّ فَلْيُلْقِهِ الْيَمُّ بِالسَّاحِلِ يَأْخُذْهُ عَدُوٌّ لِّي وَعَدُوٌّ لَّهُ ۚ وَأَلْقَيْتُ عَلَيْكَ مَحَبَّةً مِّنِّي وَلِتُصْنَعَ عَلَىٰ عَيْنِي ﴿٣٩﴾
39. Kwamba, mtie (Muwsaa) katika sanduku, kisha mtie katika mto (wa Nile). Kisha nao mto utamtupa ufukoni ili amchukue adui Yangu na adui wake (Firawni). Na Nikakutilia mahaba kutoka Kwangu, na ili ulelewe vyema Machoni Mwangu.[5]
إِذْ تَمْشِي أُخْتُكَ فَتَقُولُ هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ مَن يَكْفُلُهُ ۖ فَرَجَعْنَاكَ إِلَىٰ أُمِّكَ كَيْ تَقَرَّ عَيْنُهَا وَلَا تَحْزَنَ ۚ وَقَتَلْتَ نَفْسًا فَنَجَّيْنَاكَ مِنَ الْغَمِّ وَفَتَنَّاكَ فُتُونًا ۚ فَلَبِثْتَ سِنِينَ فِي أَهْلِ مَدْيَنَ ثُمَّ جِئْتَ عَلَىٰ قَدَرٍ يَا مُوسَىٰ ﴿٤٠﴾
40. Alipokwenda dada yako akasema: Je, nikuelekezeni kwa ambaye atamlea? Kisha Tukakurudisha kwa mama yako ili yaburudike macho yake, na wala asihuzunike. Kisha ukaua mtu Tukakuokoa na janga, na Tukakujaribu majaribio mazito. Ukaishi miaka kwa watu wa Madyan, kisha ukaja kama ilivyokadiriwa ee Muwsaa.
وَاصْطَنَعْتُكَ لِنَفْسِي ﴿٤١﴾
41. Na Nimekutayarisha na kukuchagua kwa ajili Yangu ee Muwsaa.
اذْهَبْ أَنتَ وَأَخُوكَ بِآيَاتِي وَلَا تَنِيَا فِي ذِكْرِي ﴿٤٢﴾
42. Nenda wewe na kaka yako pamoja na Aayaat (Ishara, Dalili) Zangu, na wala msinyong’onyee katika kunidhukuru.
اذْهَبَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ ﴿٤٣﴾
43. Nendeni wawili nyie kwa Firawni, hakika yeye amepindukia mipaka ya kuasi.
فَقُولَا لَهُ قَوْلًا لَّيِّنًا لَّعَلَّهُ يَتَذَكَّرُ أَوْ يَخْشَىٰ ﴿٤٤﴾
44. Mwambieni maneno laini, huenda akawaidhika au akakhofu.
قَالَا رَبَّنَا إِنَّنَا نَخَافُ أَن يَفْرُطَ عَلَيْنَا أَوْ أَن يَطْغَىٰ ﴿٤٥﴾
45. Wakasema: Rabb wetu! Hakika sisi tunakhofu asije kuharakiza ubaya juu yetu au akapinduka mipaka kuasi.
قَالَ لَا تَخَافَا ۖ إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ ﴿٤٦﴾
46. (Allaah) Akasema: Msikhofu. Hakika Mimi Niko pamoja nanyi, Nasikia na Naona.[6]
فَأْتِيَاهُ فَقُولَا إِنَّا رَسُولَا رَبِّكَ فَأَرْسِلْ مَعَنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلَا تُعَذِّبْهُمْ ۖ قَدْ جِئْنَاكَ بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكَ ۖ وَالسَّلَامُ عَلَىٰ مَنِ اتَّبَعَ الْهُدَىٰ ﴿٤٧﴾
47. Basi mwendeeni, na mwambieni: Hakika sisi ni Rusuli wa Rabb wako, basi waachie wana wa Israaiyl watoke pamoja nasi, na wala usiwatese. Kwa yakini tumekujia na Aayah (Ishara, Dalili, Muujiza) kutoka kwa Rabb wako. Na amani iwe juu ya yule atakayefuata mwongozo.[7]
إِنَّا قَدْ أُوحِيَ إِلَيْنَا أَنَّ الْعَذَابَ عَلَىٰ مَن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿٤٨﴾
48. Hakika tumefunuliwa Wahy ya kwamba adhabu itakuwa kwa yule atakayekadhibisha na akakengeuka.
قَالَ فَمَن رَّبُّكُمَا يَا مُوسَىٰ ﴿٤٩﴾
49. (Firawni) akasema: Basi ni nani Rabb wenu ee Muwsaa?
قَالَ رَبُّنَا الَّذِي أَعْطَىٰ كُلَّ شَيْءٍ خَلْقَهُ ثُمَّ هَدَىٰ ﴿٥٠﴾
50. (Muwsaa) akasema: Rabb wetu ni Yule Aliyekipa kila kitu umbo lake, kisha Akakiongoza.
قَالَ فَمَا بَالُ الْقُرُونِ الْأُولَىٰ ﴿٥١﴾
51. (Firawni) akasema: Basi nini hali ya karne za awali?
قَالَ عِلْمُهَا عِندَ رَبِّي فِي كِتَابٍ ۖ لَّا يَضِلُّ رَبِّي وَلَا يَنسَى ﴿٥٢﴾
52. (Muwsaa) akasema: Ujuzi wake uko kwa Rabb wangu katika Kitabu. Rabb wangu Hakosei na wala Hasahau.
الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ مَهْدًا وَسَلَكَ لَكُمْ فِيهَا سُبُلًا وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّن نَّبَاتٍ شَتَّىٰ ﴿٥٣﴾
53. Ambaye Amekufanyieni ardhi kuwa tandiko, na Akakupitishieni humo njia, na Akateremsha kutoka mbinguni maji. Na kwayo Tukatoa aina za mimea mbali mbali.
كُلُوا وَارْعَوْا أَنْعَامَكُمْ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّأُولِي النُّهَىٰ ﴿٥٤﴾
54. Kuleni na lisheni wanyama wenu. Hakika katika hayo bila shaka kuna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa wenye umaizi.
مِنْهَا خَلَقْنَاكُمْ وَفِيهَا نُعِيدُكُمْ وَمِنْهَا نُخْرِجُكُمْ تَارَةً أُخْرَىٰ ﴿٥٥﴾
55. Kutokana nayo (ardhi) Tumekuumbeni, na humo Tutakurudisheni, na kutoka humo Tutakutoeni mara nyingine.[8]
وَلَقَدْ أَرَيْنَاهُ آيَاتِنَا كُلَّهَا فَكَذَّبَ وَأَبَىٰ ﴿٥٦﴾
56. Na kwa yakini Tulimuonyesha (Firawni) Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu zote, lakini alikadhibisha na akakataa kabisa.
قَالَ أَجِئْتَنَا لِتُخْرِجَنَا مِنْ أَرْضِنَا بِسِحْرِكَ يَا مُوسَىٰ ﴿٥٧﴾
57. (Firawni) akasema: Je, umetujia ili ututoe katika ardhi yetu kwa sihiri yako ewe Muwsaa?
فَلَنَأْتِيَنَّكَ بِسِحْرٍ مِّثْلِهِ فَاجْعَلْ بَيْنَنَا وَبَيْنَكَ مَوْعِدًا لَّا نُخْلِفُهُ نَحْنُ وَلَا أَنتَ مَكَانًا سُوًى ﴿٥٨﴾
58. Basi bila shaka tutakuletea sihiri mfano wake. Hivyo panga baina yetu na baina yako miadi, tusiiendee kinyume sisi na wala wewe, mahali patakapokuwa sawa.
قَالَ مَوْعِدُكُمْ يَوْمُ الزِّينَةِ وَأَن يُحْشَرَ النَّاسُ ضُحًى ﴿٥٩﴾
59. Akasema: Miadi yenu ni siku ya mapambo (sikukuu), na watu wakusanywe wakati wa dhuha (jua linapopanda).
فَتَوَلَّىٰ فِرْعَوْنُ فَجَمَعَ كَيْدَهُ ثُمَّ أَتَىٰ ﴿٦٠﴾
60. Basi Firawni akageuka, akakusanya hila zake, kisha akaja.
قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ وَيْلَكُمْ لَا تَفْتَرُوا عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا فَيُسْحِتَكُم بِعَذَابٍ ۖ وَقَدْ خَابَ مَنِ افْتَرَىٰ ﴿٦١﴾
61. (Muwsaa) akawaambia: Ole wenu! Msimtungie Allaah uongo, Akakufutilieni mbali kwa adhabu. Na kwa yakini ameambulia patupu anayetunga uongo.
فَتَنَازَعُوا أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ وَأَسَرُّوا النَّجْوَىٰ ﴿٦٢﴾
62. Wakajadiliana shauri lao baina yao na wakanong’ona kwa siri.
قَالُوا إِنْ هَـٰذَانِ لَسَاحِرَانِ يُرِيدَانِ أَن يُخْرِجَاكُم مِّنْ أَرْضِكُم بِسِحْرِهِمَا وَيَذْهَبَا بِطَرِيقَتِكُمُ الْمُثْلَىٰ ﴿٦٣﴾
63. Wakasema: Hakika hawa wawili ni wachawi wanataka kukutoeni katika ardhi yenu kwa sihiri yao na waondoshe mila zenu zilizo kamilifu kabisa.
فَأَجْمِعُوا كَيْدَكُمْ ثُمَّ ائْتُوا صَفًّا ۚ وَقَدْ أَفْلَحَ الْيَوْمَ مَنِ اسْتَعْلَىٰ ﴿٦٤﴾
64. Basi jumuisheni kwa pamoja hila zenu, kisha fikeni kwa kujipanga safu. Na kwa yakini atafaulu leo atakayeshinda.
قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِمَّا أَن تُلْقِيَ وَإِمَّا أَن نَّكُونَ أَوَّلَ مَنْ أَلْقَىٰ ﴿٦٥﴾
65. Wakasema: Ee Muwsaa, ima utupe wewe au tuwe sisi wa kwanza kutupa.
قَالَ بَلْ أَلْقُوا ۖ فَإِذَا حِبَالُهُمْ وَعِصِيُّهُمْ يُخَيَّلُ إِلَيْهِ مِن سِحْرِهِمْ أَنَّهَا تَسْعَىٰ ﴿٦٦﴾
66. (Muwsaa) akasema: Bali tupeni nyinyi. Tahamaki kamba zao na fimbo zao zikaonekana kwake kutokana na sihiri yao kwamba zinakwenda mbio.
فَأَوْجَسَ فِي نَفْسِهِ خِيفَةً مُّوسَىٰ ﴿٦٧﴾
67. Basi Muwsaa akahisi khofu katika nafsi yake.
قُلْنَا لَا تَخَفْ إِنَّكَ أَنتَ الْأَعْلَىٰ ﴿٦٨﴾
68. Tukasema: Usikhofu. Hakika wewe ndiye utakayeshinda.
وَأَلْقِ مَا فِي يَمِينِكَ تَلْقَفْ مَا صَنَعُوا ۖ إِنَّمَا صَنَعُوا كَيْدُ سَاحِرٍ ۖ وَلَا يُفْلِحُ السَّاحِرُ حَيْثُ أَتَىٰ ﴿٦٩﴾
69. Na tupa kilicho katika mkono wako wa kulia, kitameza vile walivyoviunda. Hakika walivyoviunda ni hila za mchawi, na wala mchawi hafaulu popote ajapo.
فَأُلْقِيَ السَّحَرَةُ سُجَّدًا قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ هَارُونَ وَمُوسَىٰ ﴿٧٠﴾
70. Basi wachawi wakajikuta wameanguka wakisujudu. Wakasema Tumemwamini Rabb wa Haaruwn na Muwsaa.
قَالَ آمَنتُمْ لَهُ قَبْلَ أَنْ آذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّهُ لَكَبِيرُكُمُ الَّذِي عَلَّمَكُمُ السِّحْرَ ۖ فَلَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَافٍ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ فِي جُذُوعِ النَّخْلِ وَلَتَعْلَمُنَّ أَيُّنَا أَشَدُّ عَذَابًا وَأَبْقَىٰ ﴿٧١﴾
71. (Firawni) akasema: Mmemwamini kabla sijakupeni idhini? Hakika yeye ndiye mkubwa wenu ambaye amekufunzeni sihiri. Basi bila shaka nitakukatenikateni mikono yenu na miguu yenu kwa kutofautisha, kisha nitakusulubuni katika mashina ya mitende. Na bila shaka mtajua yupi kati yetu ni mkali zaidi wa kuadhibu na wa kudumisha zaidi.
قَالُوا لَن نُّؤْثِرَكَ عَلَىٰ مَا جَاءَنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالَّذِي فَطَرَنَا ۖ فَاقْضِ مَا أَنتَ قَاضٍ ۖ إِنَّمَا تَقْضِي هَـٰذِهِ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿٧٢﴾
72. (Wachawi) wakasema: Hatutokukhiyari kuliko ambayo yametujia ya dalili za waziwazi na Yule Aliyetuumba. Basi hukumu unavyotaka kuhukumu, kwani hakika wewe unahukumu (katika) uhai huu wa duniani tu.
إِنَّا آمَنَّا بِرَبِّنَا لِيَغْفِرَ لَنَا خَطَايَانَا وَمَا أَكْرَهْتَنَا عَلَيْهِ مِنَ السِّحْرِ ۗ وَاللَّـهُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ﴿٧٣﴾
73. Hakika sisi tumemwamini Rabb wetu ili Atughufurie madhambi yetu, na yale uliyotushurutisha katika mambo ya sihiri. Na Allaah Ni Mbora Zaidi na Mwenye Kudumu zaidi.
إِنَّهُ مَن يَأْتِ رَبَّهُ مُجْرِمًا فَإِنَّ لَهُ جَهَنَّمَ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ ﴿٧٤﴾
74. Hakika atakayemjia Rabb wake akiwa mhalifu, basi hakika atapata Jahannam. Hafi humo (akapumzika) na wala haishi (maisha ya raha).
وَمَن يَأْتِهِ مُؤْمِنًا قَدْ عَمِلَ الصَّالِحَاتِ فَأُولَـٰئِكَ لَهُمُ الدَّرَجَاتُ الْعُلَىٰ ﴿٧٥﴾
75. Na atakayemjia akiwa Muumini ametenda mema, basi hao watapata vyeo vya juu kabisa.
جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ مَن تَزَكَّىٰ ﴿٧٦﴾
76. Jannaat za kudumu milele zipitazo chini yake mito, watadumu humo. Na hiyo ndio jazaa ya mwenye kujitakasa.
وَلَقَدْ أَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنْ أَسْرِ بِعِبَادِي فَاضْرِبْ لَهُمْ طَرِيقًا فِي الْبَحْرِ يَبَسًا لَّا تَخَافُ دَرَكًا وَلَا تَخْشَىٰ ﴿٧٧﴾
77. Na kwa yakini Tulimfunulia Wahy Muwsaa kwamba: Safiri usiku pamoja na waja Wangu, wapigie njia kavu baharini, usikhofu kukamatwa na wala usikhofu (kuzama).
فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ بِجُنُودِهِ فَغَشِيَهُم مِّنَ الْيَمِّ مَا غَشِيَهُمْ ﴿٧٨﴾
78. Basi Firawni akawafuata pamoja na jeshi lake. Yakawafunika humo baharini yaliyowafunika.
وَأَضَلَّ فِرْعَوْنُ قَوْمَهُ وَمَا هَدَىٰ ﴿٧٩﴾
79. Na Firawni akawapoteza watu wake, na wala hakuwaongoza.
يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ قَدْ أَنجَيْنَاكُم مِّنْ عَدُوِّكُمْ وَوَاعَدْنَاكُمْ جَانِبَ الطُّورِ الْأَيْمَنَ وَنَزَّلْنَا عَلَيْكُمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ ﴿٨٠﴾
80. Enyi wana wa Israaiyl! Kwa yakini Tulikuokoeni kutokana na adui wenu, na Tukakuahidini upande wa kulia wa mlima, na Tukakuteremshieni al-manna na as-salwaa.[9]
كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَلَا تَطْغَوْا فِيهِ فَيَحِلَّ عَلَيْكُمْ غَضَبِي ۖ وَمَن يَحْلِلْ عَلَيْهِ غَضَبِي فَقَدْ هَوَىٰ ﴿٨١﴾
81. Kuleni katika vizuri Tulivyokuruzukuni, na wala msivuke mipaka katika hayo, ikakushukieni Ghadhabu Yangu. Na itakayemshukia Ghadhabu Yangu, basi kwa yakini ameangamia.
وَإِنِّي لَغَفَّارٌ لِّمَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا ثُمَّ اهْتَدَىٰ ﴿٨٢﴾
82. Na hakika Mimi bila shaka Ni Mwingi mno wa Kughufuria kwa anayetubia na akaamini na akatenda mema, tena akathibiti katika njia ya sawa.
وَمَا أَعْجَلَكَ عَن قَوْمِكَ يَا مُوسَىٰ ﴿٨٣﴾
83. Na nini kilichokuharakisha ukaacha watu wako ee Muwsaa?
قَالَ هُمْ أُولَاءِ عَلَىٰ أَثَرِي وَعَجِلْتُ إِلَيْكَ رَبِّ لِتَرْضَىٰ ﴿٨٤﴾
84. (Muwsaa) akasema: Hao wako nyuma yangu, na nimeharakiza kukujia Rabb wangu ili Uridhike.
قَالَ فَإِنَّا قَدْ فَتَنَّا قَوْمَكَ مِن بَعْدِكَ وَأَضَلَّهُمُ السَّامِرِيُّ ﴿٨٥﴾
85. (Allaah) Akasema: Basi hakika Tumewatia mtihanini watu wako baada yako, na Saamiriyyu amewapoteza.[10]
فَرَجَعَ مُوسَىٰ إِلَىٰ قَوْمِهِ غَضْبَانَ أَسِفًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ أَلَمْ يَعِدْكُمْ رَبُّكُمْ وَعْدًا حَسَنًا ۚ أَفَطَالَ عَلَيْكُمُ الْعَهْدُ أَمْ أَرَدتُّمْ أَن يَحِلَّ عَلَيْكُمْ غَضَبٌ مِّن رَّبِّكُمْ فَأَخْلَفْتُم مَّوْعِدِي ﴿٨٦﴾
86. Basi Muwsaa akarejea kwa watu wake akiwa ameghadhibika na kusikitika. Akasema: Enyi watu wangu! Je, Rabb wenu Hakukuahidini ahadi nzuri? Je, imerefuka kwenu ahadi, au mmetaka ikushukieni ghadhabu kutoka kwa Rabb wenu, na kwa hiyo mkakhalifu miadi yangu?
قَالُوا مَا أَخْلَفْنَا مَوْعِدَكَ بِمَلْكِنَا وَلَـٰكِنَّا حُمِّلْنَا أَوْزَارًا مِّن زِينَةِ الْقَوْمِ فَقَذَفْنَاهَا فَكَذَٰلِكَ أَلْقَى السَّامِرِيُّ ﴿٨٧﴾
87. Wakasema: Hatukukhalifu miadi yako kwa khiyari yetu, lakini tulibebeshwa mizigo ya mapambo ya watu, basi tukaitupa na hivyo ndivyo Saamiriyyu alivyotupa.
فَأَخْرَجَ لَهُمْ عِجْلًا جَسَدًا لَّهُ خُوَارٌ فَقَالُوا هَـٰذَا إِلَـٰهُكُمْ وَإِلَـٰهُ مُوسَىٰ فَنَسِيَ ﴿٨٨﴾
88. Akawaundia ndama kiwiliwili chenye sauti. Wakasema: Huyu ndiye mwabudiwa wenu na mwabudiwa wa Muwsaa lakini amesahau (mwabudiwa wake).
أَفَلَا يَرَوْنَ أَلَّا يَرْجِعُ إِلَيْهِمْ قَوْلًا وَلَا يَمْلِكُ لَهُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا ﴿٨٩﴾
89. Je, hawaoni kwamba (huyo ndama) hawarejeshei neno, na wala hawezi kuwadhuru wala kuwanufaisha?
وَلَقَدْ قَالَ لَهُمْ هَارُونُ مِن قَبْلُ يَا قَوْمِ إِنَّمَا فُتِنتُم بِهِ ۖ وَإِنَّ رَبَّكُمُ الرَّحْمَـٰنُ فَاتَّبِعُونِي وَأَطِيعُوا أَمْرِي ﴿٩٠﴾
90. Na Haaruwn alikwishawaambia kabla: Enyi watu! Hakika mmetiwa mtihanini naye (ndama), na hakika Rabb wenu ni Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), basi nifuateni na tiini amri yangu.
قَالُوا لَن نَّبْرَحَ عَلَيْهِ عَاكِفِينَ حَتَّىٰ يَرْجِعَ إِلَيْنَا مُوسَىٰ ﴿٩١﴾
91. Wakasema: Hatutoacha kumwabudu mpaka Muwsaa arudi kwetu.
قَالَ يَا هَارُونُ مَا مَنَعَكَ إِذْ رَأَيْتَهُمْ ضَلُّوا ﴿٩٢﴾
92. (Muwsaa aliporejea) alisema: Ee Haaruwn! Nini kimekuzuia ulipowaona wanapotoka?
أَلَّا تَتَّبِعَنِ ۖ أَفَعَصَيْتَ أَمْرِي ﴿٩٣﴾
93. Kwamba unifuate. Je, umeasi amri yangu?
قَالَ يَا ابْنَ أُمَّ لَا تَأْخُذْ بِلِحْيَتِي وَلَا بِرَأْسِي ۖ إِنِّي خَشِيتُ أَن تَقُولَ فَرَّقْتَ بَيْنَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلَمْ تَرْقُبْ قَوْلِي ﴿٩٤﴾
94. (Haaruwn) akasema: Ee mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu, wala kichwa changu. Hakika mimi niliogopa usije kusema: Umefarikisha baina ya wana wa Israaiyl na wala hukuchunga kauli yangu.
قَالَ فَمَا خَطْبُكَ يَا سَامِرِيُّ ﴿٩٥﴾
95. (Muwsaa) akasema: Una jambo gani ee Saamiriyy?
قَالَ بَصُرْتُ بِمَا لَمْ يَبْصُرُوا بِهِ فَقَبَضْتُ قَبْضَةً مِّنْ أَثَرِ الرَّسُولِ فَنَبَذْتُهَا وَكَذَٰلِكَ سَوَّلَتْ لِي نَفْسِي ﴿٩٦﴾
96. (Saamirriy) akasema: Niliona yale wasiyoyaona na nikateka teko (la udongo) katika kwato za (farasi wa) Jibriyl kisha nikautupa. Na hivyo ndivyo ilivyonishawishi nafsi yangu.
قَالَ فَاذْهَبْ فَإِنَّ لَكَ فِي الْحَيَاةِ أَن تَقُولَ لَا مِسَاسَ ۖ وَإِنَّ لَكَ مَوْعِدًا لَّن تُخْلَفَهُ ۖ وَانظُرْ إِلَىٰ إِلَـٰهِكَ الَّذِي ظَلْتَ عَلَيْهِ عَاكِفًا ۖ لَّنُحَرِّقَنَّهُ ثُمَّ لَنَنسِفَنَّهُ فِي الْيَمِّ نَسْفًا ﴿٩٧﴾
97. (Muwsaa) akasema: Nenda zako! Kwani hakika utakuwa katika uhai wako ukisema: Usiniguse![11] Na hakika una miadi hutovunjiwa. Na mtazame mwabudiwa wako ambaye umeendelea kukaa kumwabudu. Bila shaka tutamuunguza, kisha tutampeperusha baharini chembechembe.
إِنَّمَا إِلَـٰهُكُمُ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ وَسِعَ كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا ﴿٩٨﴾
98. Hakika Mwabudiwa wenu wa haki Ni Allaah Ambaye hapana ilaah ila Yeye. Amekienea kila kitu kwa Ilimu Yake.
كَذَٰلِكَ نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنبَاءِ مَا قَدْ سَبَقَ ۚ وَقَدْ آتَيْنَاكَ مِن لَّدُنَّا ذِكْرًا ﴿٩٩﴾
99. Hivyo ndivyo Tunavyokusimulia miongoni mwa khabari zilizotangulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na kwa yakini Tumekupa kutoka Kwetu Ukumbusho (Qur-aan).
مَّنْ أَعْرَضَ عَنْهُ فَإِنَّهُ يَحْمِلُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وِزْرًا ﴿١٠٠﴾
100. Atakayejitenga nayo, basi hakika yeye atabeba Siku ya Qiyaamah mzigo (wa dhambi).
خَالِدِينَ فِيهِ ۖ وَسَاءَ لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ حِمْلًا ﴿١٠١﴾
101. Wadumu ndani yake (adhabu). Na mzigo mbaya ulioje kwao kuubeba Siku ya Qiyaamah.
يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ ۚ وَنَحْشُرُ الْمُجْرِمِينَ يَوْمَئِذٍ زُرْقًا ﴿١٠٢﴾
102. Siku litakapopulizwa baragumu. Na Tutawakusanya wahalifu Siku hiyo macho yao yakiwa rangi ya buluu (kwa kiwewe).
يَتَخَافَتُونَ بَيْنَهُمْ إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا عَشْرًا ﴿١٠٣﴾
103. Wakinong'onezana baina yao: Hamkukaa (duniani) isipokuwa (siku) kumi tu.
نَّحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُونَ إِذْ يَقُولُ أَمْثَلُهُمْ طَرِيقَةً إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا يَوْمًا ﴿١٠٤﴾
104. Sisi Tunajua zaidi yale wanayoyasema. Atakaposema mbora wao katika mwendo: Hamkukaa isipokuwa siku moja tu.
وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْجِبَالِ فَقُلْ يَنسِفُهَا رَبِّي نَسْفًا ﴿١٠٥﴾
105. Na wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu milima. Sema: Rabb wangu Ataing’olea mbali ibaki chembechembe.
فَيَذَرُهَا قَاعًا صَفْصَفًا ﴿١٠٦﴾
106. Kisha Ataiacha ardhi kuwa tambarare, uwanda ulio sawasawa.
لَّا تَرَىٰ فِيهَا عِوَجًا وَلَا أَمْتًا ﴿١٠٧﴾
107. Hutoona humo mdidimio wala mwinuko.
يَوْمَئِذٍ يَتَّبِعُونَ الدَّاعِيَ لَا عِوَجَ لَهُ ۖ وَخَشَعَتِ الْأَصْوَاتُ لِلرَّحْمَـٰنِ فَلَا تَسْمَعُ إِلَّا هَمْسًا ﴿١٠٨﴾
108. Siku hiyo watamfuata mwitaji hakuna kumkengeuka. Na sauti zitafifia kwa Ar-Rahmaan, basi hutosikia isipokuwa mchakato wa nyayo.
يَوْمَئِذٍ لَّا تَنفَعُ الشَّفَاعَةُ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَـٰنُ وَرَضِيَ لَهُ قَوْلًا ﴿١٠٩﴾
109. Siku hiyo haitofaa shafaa’ah (uombezi) isipokuwa ya yule atakayepewa idhini na Ar-Rahmaan na Akamridhia kusema.[12]
يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا ﴿١١٠﴾
110. Anajua yale yaliyoko mbele yao, na yale yaliyoko nyuma yao, na wala hawawezi kufikia kuelewa chochote cha Ujuzi Wake.
وَعَنَتِ الْوُجُوهُ لِلْحَيِّ الْقَيُّومِ ۖ وَقَدْ خَابَ مَنْ حَمَلَ ظُلْمًا ﴿١١١﴾
111. Nyuso zitanyenyekea kwa Al-Hayyu (Aliye Hai daima), Al-Qayyuwm (Msimamizi wa kila kitu).[13] Na kwa yakini ameharibikiwa abebaye dhulma.
وَمَن يَعْمَلْ مِنَ الصَّالِحَاتِ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَا يَخَافُ ظُلْمًا وَلَا هَضْمًا ﴿١١٢﴾
112. Na yeyote atakayetenda mema naye ni Muumini, basi hatokhofu dhulma wala kupunjwa.
وَكَذَٰلِكَ أَنزَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا وَصَرَّفْنَا فِيهِ مِنَ الْوَعِيدِ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ أَوْ يُحْدِثُ لَهُمْ ذِكْرًا ﴿١١٣﴾
113. Na hivyo ndivyo Tumeiteremsha Qur-aan kwa Kiarabu, na Tukaisarifu waziwazi humo vitisho kadhaa, huenda wakapata kuwa na taqwa au ikawapa makumbusho.
فَتَعَالَى اللَّـهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ ۗ وَلَا تَعْجَلْ بِالْقُرْآنِ مِن قَبْلِ أَن يُقْضَىٰ إِلَيْكَ وَحْيُهُ ۖ وَقُل رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا ﴿١١٤﴾
114. Basi Ametukuka Allaah kwa ‘Uluwa, Mfalme wa haki. Na wala usiiharakize Qur-aan (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kabla haikumalizwa kufunuliwa Wahy kwako. Na sema: Rabb wangu! Nizidishie Ilimu.
وَلَقَدْ عَهِدْنَا إِلَىٰ آدَمَ مِن قَبْلُ فَنَسِيَ وَلَمْ نَجِدْ لَهُ عَزْمًا ﴿١١٥﴾
115. Na kwa yakini Tulimpa Aadam ahadi kabla, lakini akasahau, na wala Hatukuona kwake azimio.
وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ ﴿١١٦﴾
116. Na pindi Tulipowaambia Malaika: Msujudieni Aadam. Wakasujudu isipokuwa Ibliys, alikataa kabisa.
فَقُلْنَا يَا آدَمُ إِنَّ هَـٰذَا عَدُوٌّ لَّكَ وَلِزَوْجِكَ فَلَا يُخْرِجَنَّكُمَا مِنَ الْجَنَّةِ فَتَشْقَىٰ ﴿١١٧﴾
117. Tukasema: Ee Aadam! Hakika huyu (Ibliys) ni adui wako na wa mkeo, basi angalieni asikutoeni katika Jannah ukapata mashaka.
إِنَّ لَكَ أَلَّا تَجُوعَ فِيهَا وَلَا تَعْرَىٰ ﴿١١٨﴾
118. Hakika wewe humo hutopata njaa, na wala hutokuwa uchi.
وَأَنَّكَ لَا تَظْمَأُ فِيهَا وَلَا تَضْحَىٰ ﴿١١٩﴾
119. Na hakika wewe hutopata kiu humo, na wala hutopigwa na joto la jua
فَوَسْوَسَ إِلَيْهِ الشَّيْطَانُ قَالَ يَا آدَمُ هَلْ أَدُلُّكَ عَلَىٰ شَجَرَةِ الْخُلْدِ وَمُلْكٍ لَّا يَبْلَىٰ ﴿١٢٠﴾
120. Lakini shaytwaan alimtia wasiwasi, akasema: Ee Aadam! Je, nikuelekeze mti wa kudumu na ufalme usiochakaa?
فَأَكَلَا مِنْهَا فَبَدَتْ لَهُمَا سَوْآتُهُمَا وَطَفِقَا يَخْصِفَانِ عَلَيْهِمَا مِن وَرَقِ الْجَنَّةِ ۚ وَعَصَىٰ آدَمُ رَبَّهُ فَغَوَىٰ ﴿١٢١﴾
121. Basi waliula. Uchi wao ukawadhihirikia na wakaanza kujibandika majani ya Jannah. Na Aadam akamuasi Rabb wake, akapotoka.
ثُمَّ اجْتَبَاهُ رَبُّهُ فَتَابَ عَلَيْهِ وَهَدَىٰ ﴿١٢٢﴾
122. Kisha Rabb wake Akamteua, Akapokea tawbah yake na Akamwongoza.
قَالَ اهْبِطَا مِنْهَا جَمِيعًا ۖ بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَىٰ ﴿١٢٣﴾
123. (Allaah) Akasema: Teremkeni toka humo nyote, hali ya kuwa maadui nyinyi kwa nyinyi. Kisha utakapokufikieni kutoka Kwangu Mwongozo, basi atakayefuata Mwongozo Wangu, hatopotea na wala hatopata mashaka.
وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ ﴿١٢٤﴾
124. Na atakayejitenga na Ukumbusho Wangu basi hakika atapata maisha ya dhiki, na Tutamfufua Siku ya Qiyaamah akiwa kipofu.[14]
قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا ﴿١٢٥﴾
125. Atasema: Rabb wangu! Kwa nini Umenifufua kipofu, na hali nilikuwa naona?
قَالَ كَذَٰلِكَ أَتَتْكَ آيَاتُنَا فَنَسِيتَهَا ۖ وَكَذَٰلِكَ الْيَوْمَ تُنسَىٰ ﴿١٢٦﴾
126. (Allaah) Atasema: Hivyo ndivyo, zilikufikia Aayaat Zetu ukazisahau, na kadhalika leo unasahauliwa.
وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي مَنْ أَسْرَفَ وَلَمْ يُؤْمِن بِآيَاتِ رَبِّهِ ۚ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَشَدُّ وَأَبْقَىٰ ﴿١٢٧﴾
127. Na hivyo ndivyo Tunavyomlipa yule aliyevuka mipaka na hakuamini Aayaat za Rabb wake. Na bila shaka adhabu ya Aakhirah ni kali zaidi na ni ya kudumu zaidi.
أَفَلَمْ يَهْدِ لَهُمْ كَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّنَ الْقُرُونِ يَمْشُونَ فِي مَسَاكِنِهِمْ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّأُولِي النُّهَىٰ ﴿١٢٨﴾
128. Je, haijawadhihirikia tu kuwa ni kaumu ngapi Tumeziangamiza kabla yao, huku wakiwa wanatembea (kwa amani na raha) katika maskani zao? Hakika katika hayo bila shaka kuna Aayaat (Mazingatio, Mawaidha) kwa wenye kumaizi.
وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَكَانَ لِزَامًا وَأَجَلٌ مُّسَمًّى ﴿١٢٩﴾
129. Na ingekuwa si neno lililotangulia kutoka kwa Rabb wako, na muda uliokadiriwa, bila shaka ingelazimika (adhabu hapa duniani).
فَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ غُرُوبِهَا ۖ وَمِنْ آنَاءِ اللَّيْلِ فَسَبِّحْ وَأَطْرَافَ النَّهَارِ لَعَلَّكَ تَرْضَىٰ ﴿١٣٠﴾
130. Basi subiri juu ya yale wanayoyasema. Na sabihi ukimhimidi Rabb wako kabla ya kuchomoza jua, na kabla ya kuchwa kwake. Na katika nyakati za usiku pia sabbih na katikati ya mchana, huenda ukapata ya kukuridhisha.
وَلَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّنْهُمْ زَهْرَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا لِنَفْتِنَهُمْ فِيهِ ۚ وَرِزْقُ رَبِّكَ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ﴿١٣١﴾
131. Na wala usikodoe kabisa macho yako kwa yale ya starehe Tuliyowaneemesha baadhi ya makundi (ya kikafiri) miongoni mwao. Hayo ni mapambo ya uhai wa dunia tu, ili Tuwajaribu kwayo. Na riziki ya Rabb wako ni bora zaidi na ni yenye kudumu zaidi.
وَأْمُرْ أَهْلَكَ بِالصَّلَاةِ وَاصْطَبِرْ عَلَيْهَا ۖ لَا نَسْأَلُكَ رِزْقًا ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكَ ۗ وَالْعَاقِبَةُ لِلتَّقْوَىٰ ﴿١٣٢﴾
132. Na amrisha ahli zako Swalaah, na dumisha uvumilivu juu ya mazito yake. Hatukukalifishi riziki bali Sisi Ndio Tunaokuruzuku. Na hatima njema ni kwa wenye taqwa.[15]
وَقَالُوا لَوْلَا يَأْتِينَا بِآيَةٍ مِّن رَّبِّهِ ۚ أَوَلَمْ تَأْتِهِم بَيِّنَةُ مَا فِي الصُّحُفِ الْأُولَىٰ ﴿١٣٣﴾
133. Na (makafiri) wakasema: Kwa nini hatuletei Aayah (Ishara, Dalili, Muujiza) kutoka kwa Rabb wake? Je, kwani hazikuwafikia hoja bayana zilizomo katika Sahifa za awali?[16]
وَلَوْ أَنَّا أَهْلَكْنَاهُم بِعَذَابٍ مِّن قَبْلِهِ لَقَالُوا رَبَّنَا لَوْلَا أَرْسَلْتَ إِلَيْنَا رَسُولًا فَنَتَّبِعَ آيَاتِكَ مِن قَبْلِ أَن نَّذِلَّ وَنَخْزَىٰ ﴿١٣٤﴾
134. Na lau Tungeliwaangamiza kwa adhabu kabla yake, wangelisema: Rabb wetu! Kwa nini Usituletee Rasuli tukafuata Aayaat Zako kabla hatujadhalilika na hatujahizika?
قُلْ كُلٌّ مُّتَرَبِّصٌ فَتَرَبَّصُوا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ مَنْ أَصْحَابُ الصِّرَاطِ السَّوِيِّ وَمَنِ اهْتَدَىٰ ﴿١٣٥﴾
135. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Kila mmoja ni mwenye kungojea na kutazamia, basi ngojeeni na tazamieni. Karibuni mtajua ni nani mwenye njia iliyo sawa na ni nani aliyeongoka.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Istawaa اسْتَوَى
Yuko juu kwa namna inayolingana na Uadhama na Ujalali Wake Yeye Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-A'raaf (7:54) kwenye maelezo bayana ya maana yake, yenye kutofautiana na maana ya katika Suwrah Al-Baqarah (2:29) na Suwrat Fusswilat (41:11).
Na msimamo wa Salaf katika Tafsiyr ya Aayah yenye kitenzi hiki, ni kama huu uliopokelewa kuwa, Ja‘afar bin ‘Abdillaah na wengine miongoni mwao walisema: “Tulikuwa kwa Imaam Maalik bin Anas, akatokea mtu akamuuliza: Ee Abaa ‘Abdillaah! Allaah (سُبْحَانَهُ وَتَعَالَى) Anasema:
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥ [188]﴾
“Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma) Yuko juu ya ‘Arsh.” [Twaahaa (20:5)].
Je, ni vipi Istawaa? Basi Imaam Maalik hakuwahi kughadhibika kutokana na kitu chochote kile kama alivyoghadhibika kutokana na swali la mtu huyo. Kisha (Imaam Maalik) akatazama chini na huku akikwaruza kwaruza kwa kijiti kilichokuwa kwenye mkono wake mpaka akarowa jasho, halafu akanyanyua kichwa chake na kukirembea kile kijiti kisha akasema: ‘Vipi’ ni ghayr-ma’quwl (hakutambuliki), na Al-Istiwaa ghayr-maj-huwl (si jambo lisilojulikana), na kuamini hilo ni waajib (lazima), na kuuliza (au kuhoji hilo) ni bid’ah (uzushi), na nina khofu kuwa wewe ni mzushi!” Akaamrisha mtu huyo atolewe, basi akatolewa.”
[Al-Hilyah (6/325-326)]. Na pia imesimuliwa na Abu ‘Uthmaan As-Swaabuwniy katika ‘Aqiydatus Salaf Asw-haab Al-Hadiyth Uk. (17-18), kutoka kwa Ja‘afar bin ‘Abdillaah, kutoka kwa Maalik, na Ibn ‘Abdil-Barr katika At-Tamhiyd (7/151), kutoka kwa ‘Abdullaah bin Naafi’, kutoka kwa Maalik na Al-Bayhaqiyy katika Al-Asmaa wasw-Swifaat Uk. (408), kutoka kwa ‘Abdullaah bin Wahb, kutoka kwa Maalik. Ibn Hajar amesema katika Al-Fat-h (13/406-407) kuwa mlolongo wake ni mzuri, na imesahihishwa na Adh-Dhahabiy katika Al-‘Uluww Uk. (103). Imaam Muhammad Naaswirud-Diyn Al-Albaaniy amesema Hadiyth hii ni Swahiyh katika Mukhtaswar Al-‘Uluww cha Imaam Adh-Dhahabiy, na pia ameihakiki katika Uk. (131).
[3] ‘Arsh Ya Ar-Rahmaan Na Tofauti Yake Na ’Arsh Ya Wanaadam: Rejea Al-Haaqqah (69:17).
[4] Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah (سبحانه وتعالى): Rejea Faharasa ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake.
[5] Kuthibitisha Sifa Ya Allaah (سبحانه وتعالى): Rejea Huwd (11:37) na Suwrah hii Aayah (46).
[6] Kuthibitisha Sifa Za Allaah (سبحانه وتعالى) Ni ‘Aqiydah Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah:
Sifa Ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya Kuona na Kusikia ni Sifa inayopaswa kuthibitishwa kama Alivyoitaja Mwenyewe. Na hii ni ‘Aqiydah ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah. Rejea Huwd (11:37) kwenye maelezo bayana. Na katika Suwrah na Aayah nyingi, Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja kuwa Yeye Ni Mwenye Kusikia na Kuona. Rejea Ghaafir (40:20), An-Nisaa (4:58), (4:134), na Al-Mujaadalah (58:1). Na dalili mojawapo katika Sunnah ni:
عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَكُنَّا إِذَا أَشْرَفْنَا عَلَى وَادٍ هَلَّلْنَا وَكَبَّرْنَا. ارْتَفَعَتْ أَصْوَاتُنَا فَقَالَ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ: ((يَا أَيُّهَا النَّاسُ ارْبَعُوا عَلَى أَنْفُسِكُمْ فَإِنَّكُمْ لاَ تَدْعُونَ أَصَمَّ ولاَ غَائِبًا إِنَّهُ مَعَكُمْ إِنَّهُ سَمِيعٌ قَرِيبٌ تَبَارَكَ اسْمُهُ وَتَعَالَى جَدُّهُ))
Amesimulia Abu Muwsaa Al-Ash’ariyy (رضي الله عنه): Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na tukawa kila tukipanda bonde, tunafanya tahliyl (Laa Ilaaha Illa-Allaah), na tunaleta takbiyr (Allaahu Akbar). Zikapanda sauti zetu, na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Enyi watu, zihurumieni nafsi zenu, kwani hamumwombi kiziwi wala asiyekuwepo, hakika Yeye Yupo nanyi (kwa Ujuzi Wake), hakika Yeye Ni Mwenye Kusikia yote, Yupo Karibu, Limebarikika Jina Lake na Umetukuka Ujalali Wake.” [Al-Bukhaariy]
[7] Amani Ya Dunia Na Ya Aakhirah Kwa Atakayefuata Mwongozo:
Yaani: Atakayefuata Njia Iliyonyooka, na akafuata Sharia iliyo wazi, basi atapata na amani ya dunia na ya Aakhirah. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[8] Ardhi: Tumeumbwa Kutoka Humo, Na Humo Tutarudishwa, Na Kutoka Humo Tutafufuliwa:
Alipotaja manufaa makubwa ya ardhi, na kujibishana kwake vyema na mvua Anayoiteremsha Allaah (سبحانه وتعالى) juu yake, na kwamba ardhi hii kwa Idhini ya Rabb wake, inatoa mimea ya namna mbalimbali, Allaah Akasema kwamba Ametuumba kutokana nayo, na ndani yake humo Ataturudisha tutakapofariki na kuzikwa humo, na kutoka humo Atatutoa tena mara nyengine (kufufuliwa). Kadhalika, Yeye Ametuumba tukapatikana kutokana na ardhi baada ya kuwa hatupo, na hili tumelijua fika na tumelithibitisha. Hivyo basi, Ataturejesha kwa kutufufua kutoka humo baada ya sisi kufa ili Atulipe matendo yetu tuliyoyafanya juu ya mgongo wake. Na hizi ni dalili mbili za kiakili zilizo wazi juu ya kurejeshwa tena; kutoa mimea kutoka katika ardhi baada ya kufa kwake, na kuwatoa wenye kuhesabiwa (matendo) kutoka humo kama walivyokuwa mwanzo. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[9] Al-Manna Na As-Salwaa: Rejea Al-Baqarah (2:57).
[10] Saamiriyyu Aliyewapotosha Watu Kumwabudu Ndama:
Aayah hii kuanzia namba (88) hadi (97), zinataja kuhusu mtu katika kaumu ya Nabiy Muwsaa (عليه السّلام), ambaye alikuwa ni mkaribu wake, aliyeitwa Saamiriyyu. Alikuwa ni mtu mwenye akili na ujuzi maalum. Lakini alikuwa mnafiki na alikuwa mjanja mno! Alijua udhaifu wa watu. Basi pindi Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) alipokwenda katika miyqaat (mahali na muda maalumu pa miadi) ya kuzungumza na Allaah (سبحانه وتعالى); rejea Al-A’raaf (7:142-143), alitumia ujanja wake kuwapumbaza watu na kwa lengo la kuwapotosha.
Alikusanya dhahabu walizokuwa nazo watu wa Firawni. Akayayusha dhahabu na kuimimina katika chombo chenye ukina fulani kinachotumika kufinyanga na kutoa shepu au umbo fulani baada ya myayuko kupoa na kuwa mgumu. Na dhahabu ilipopoa, alipasua chombo hicho akatoka ndama wa dhahabu aliyevutia watu machoni. Akapuliza ndani ya uwazi wa ndama ukatoa sauti kama ya ndama. Alimuunda ndama huyo kwa siri, kisha akamtoa kwa ghafla mbele ya watu. Kisha akaeneza uvumi ionekane kana kwamba watu walikuwa wakifanya ibaada hiyo ya kuabudu ndama na kwamba ni ibaada ya kawaida iliyokubalika. Watu walitumbukia katika njia zake za ujanja, wakadanganyika, wakamwabudu ndama na hivyo kuingia katika shirki kubwa. Walisahau kabisa kwamba Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) aliwajulisha kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Pekee Apasaye kuabudiwa kwa haki. Rejea Aayah namba (97) kwenye maelezo kuhusu adhabu Aliyopewa na Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kitendo chake hiki kiovu kabisa.
[11] Adhabu Ya Saamiriyyu Duniani: Hatoweza Kugusa Watu Na Watu Hawataweza Kumgusa:
Saamiriyyu: Rejea Aayah namba (85), ni mtu katika kaumu ya Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) ambaye ndiye aliyewaamrisha watu wamwabudu ndama. Basi adhabu yake ikawa ni hiyo ya yeye kutokuweza kugusa au kuguswa. Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) amesema: Yaani: Utaadhibiwa maishani, na hakuna wa kukukaribia, na hakuna wa kukugusa, mpaka anayetaka kukukaribia, utamwambia: “Usiniguse, na usinikaribie!” Hiyo ni adhabu kwa ajili ya hilo, kwa vile aligusa kitu ambacho hakupaswa mtu kukigusa (kwato za (farasi wa Jibriyl) na kufanya kile ambacho hakuna mtu mwingine alifanya. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[12] Hakuna Atakayemiliki Ash-Shafaa’ah (Uombezi) Isipokuwa Kwa Idhini Ya Allaah:
Rejea Al-Baqarah (2:255), An-Najm (53:26). Rejea pia Al-Israa (17:79) ambako kumetajwa kuwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Nabii Pekee atakayeruhusiwa ash-shafaa’ah atakapokuwa katika Maqaaman Mahmuwdan (Cheo Cha Kuhimidiwa).
[13] Jina Tukufu Kabisa La Allaah (Al-Hayyu Al-Qayyuwm) Limo Katika Aayah Hii:
Rejea Al-Baqarah (2:255), Aal-‘Imraan (3:2).
[14] Kujitenga Na Ukumbusho Ni Kupata Maisha Ya Dhiki:
Aayah hii na Aayah zinazofuata (124-127), zinahusiana na hayo ya mtu anayejitenga au anayepuuza Ukumbusho wa Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba atakuwa na maisha ya dhiki: Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) amefasiri Aayah hii:
Yaani: (Kupuuza au kujitenga nacho) Kitabu ambacho kinataja kila yanayoamrishwa na kuyaacha kwa kuyapuuza. Au kufanya lilokubwa zaidi, nalo ni kukanusha na kukufuru. Basi atapata maisha ya dhiki. Yaani malipo yake, ni kuyafanya maisha yake, yawe ya dhiki na mashaka. Basi hana anachokipata isipokuwa adhabu tu. Na pia maisha ya dhiki, yamefasiriwa kuwa ni adhabu ya kaburi, kwamba kaburi litakuwa la kumdhikisha na hivo kumbana kabisa na ataadhibika humo. Hayo ni malipo ya kupuuza au kujitenga na Ukumbusho wa Rabb wake. Na hii ni mojawapo ya Aayah zinazodulisha adhabu ya kaburi. Na ya pili ni Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الظَّالِمُونَ فِي غَمَرَاتِ الْمَوْتِ وَالْمَلَائِكَةُ بَاسِطُو أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوا أَنفُسَكُمُ ۖ الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ وَكُنتُمْ عَنْ آيَاتِهِ تَسْتَكْبِرُونَ ﴿٩٣﴾
“Na lau ungeliona madhalimu pale wakiwa katika mateso makali ya mauti (ungeona jambo la kutisha mno), na Malaika wamenyosha mikono yao (wakiwaambia): Toeni nafsi zenu! Leo mnalipwa adhabu ya kudhalilisha kwa yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Allaah pasi na haki, na mlikuwa mkitakabari msizifuate Aayaat Zake.” [Al-An’aam (6:93)]
Na ya tatu ni Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَنُذِيقَنَّهُم مِّنَ الْعَذَابِ الْأَدْنَىٰ دُونَ الْعَذَابِ الْأَكْبَرِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٢١﴾
“Na bila shaka Tutawaonjesha adhabu ndogo kabla ya adhabu kubwa huenda wakarejea (kutubia).” [As-Sadjah (32:21)]
Na ya nne ni Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) kuhusu watu wa Firawni:
النَّارُ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا غُدُوًّا وَعَشِيًّا ۖ وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ أَدْخِلُوا آلَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ الْعَذَابِ﴿٤٦﴾
“Wanadhihirishiwa moto asubuhi na jioni, na Siku itakayosimama Saa (itasemwa): Waingizeni watu wa Firawni katika adhabu kali kabisa.” [Ghaafir (40:46)]
Waliosema kuwa ni adhabu ya kaburi ni Salaf. Na Wafasiri wengineo wanaona kuwa maisha ya dhiki ni ya ujumla; maisha ya duniani yanayomsibu anayepuuza au anayejitenga na Ukumbusho wa Rabb wake kama ghamu (na huzuni), dhiki, na maumivu, ambayo ni adhabu za kutangulia. Na katika maisha ya Barzakh, na katika maisha ya Aakhira kwa ujumla, ni maisha ya dhiki, na wala si vinginevyo. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[15] Kuamrisha Ahli Kuswali:
عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى اللّه عليه وسلم أنه قال: ((مُرُوا أَوْلادَكُمْ بِالصَّلاةِ وَهُمْ أَبْنَاءُ سَبْعِ سِنِينَ، وَاضْرِبُوهُمْ عَلَيْهَا وَهُمْ أَبْنَاءُ عَشْرٍ، وَفَرِّقُوا بَيْنَهُمْ فِي الْمَضَاجِعِ)) البخاري
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Amrisheni watoto wenu kuswali wakiwa na umri wa miaka saba, na wapigeni (pigo khafifu wakiwa hawataki kuswali) wakiwa na umri wa miaka kumi, na watenganisheni vitanda.”(kuwatenganisha wasichana na wavulana vyumbani) [Al-Bukhaariy]
وَعَنِ ابْنِ عُمَرَ أَنَّ أَبَاهُ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ كَانَ يُصَلِّي مِنَ اللَّيْلِ مَا شَاءَ اللَّهُ حَتَّى إِذَا كَانَ مِنْ آخِرِ اللَّيْلِ أَيْقَظَ أَهْلَهُ لِلصَّلَاةِ يَقُولُ لَهُمْ: الصَّلَاةُ ثُمَّ يَتْلُو هَذِهِ الْآيَةَ: (وَأْمُرْ أَهْلَكَ بِالصَّلَاةِ وَاصْطَبِرْ عَلَيْهَا لَا نَسْأَلُكَ رِزْقًا نَحن نرزقك وَالْعَاقبَة للتقوى)
Amesimulia Ibn ‘Umar kwamba baba yake ‘Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) alikuwa akiswali usiku kiasi Anavyomwezesha Allaah, mpaka inapofika mwisho wa usiku, huamsha ahli wake kwa ajili ya Swalaah huku akiwaambia: Swalaah! Kisha husoma Aayah hii:
وَأْمُرْ أَهْلَكَ بِالصَّلَاةِ وَاصْطَبِرْ عَلَيْهَا ۖ لَا نَسْأَلُكَ رِزْقًا ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكَ ۗ وَالْعَاقِبَةُ لِلتَّقْوَىٰ ﴿١٣٢﴾
“Na amrisha ahli zako Swalaah, na dumisha uvumilivu juu ya mazito yake. Hatukukalifishi riziki bali Sisi Ndio Tunaokuruzuku. Na hatima njema ni kwa wenye taqwa.” [Twaahaa (20:132) – Imepokelewa na Imaam Maalik na ameisahihisha Al-Albaaniy]
Rejea pia At-Tahriym (66:6) kwenye faida nyenginezo.
[16] Suhuf (Maandiko Matukufu) Na Tofauti Baina Yake Na Vitabu Vinginevyo Vya Mbinguni: Rejea Al-A’laa (87:18-19).
الأنْبِيآء
021-Al-Anbiyaa
021-Al-Anbiyaa: Utangulizi Wa Suwrah [190]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
اقْتَرَبَ لِلنَّاسِ حِسَابُهُمْ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ مُّعْرِضُونَ ﴿١﴾
1. Imewakaribia watu hesabu yao, nao wamo katika mghafala wanakengeuka (na wanapuuza).
مَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّن رَّبِّهِم مُّحْدَثٍ إِلَّا اسْتَمَعُوهُ وَهُمْ يَلْعَبُونَ ﴿٢﴾
2. Hauwafikii Ukumbusho wowote ule mpya kutoka kwa Rabb wao isipokuwa huusikiliza kwa makini na huku wao wanacheza.
لَاهِيَةً قُلُوبُهُمْ ۗ وَأَسَرُّوا النَّجْوَى الَّذِينَ ظَلَمُوا هَلْ هَـٰذَا إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ ۖ أَفَتَأْتُونَ السِّحْرَ وَأَنتُمْ تُبْصِرُونَ ﴿٣﴾
3. Huku nyoyo zao zimeghafilika. Na wale waliodhulumu hunong’onezana kwa siri: Je, ni nani huyu isipokuwa ni binaadam kama nyinyi? Je, mnaiendea sihiri hii na hali nyinyi mnaona?
قَالَ رَبِّي يَعْلَمُ الْقَوْلَ فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٤﴾
4. (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Rabb wangu Anajua yasemwayo katika mbingu na ardhi, Naye Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
بَلْ قَالُوا أَضْغَاثُ أَحْلَامٍ بَلِ افْتَرَاهُ بَلْ هُوَ شَاعِرٌ فَلْيَأْتِنَا بِآيَةٍ كَمَا أُرْسِلَ الْأَوَّلُونَ ﴿٥﴾
5. Lakini wakasema: (Qur-aan) Ni ndoto za mkorogano! Bali ameitunga! Bali yeye ni mshairi![1] Basi atuletee Aayah (Muujiza) kama walivyotumwa wa awali.
مَا آمَنَتْ قَبْلَهُم مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا ۖ أَفَهُمْ يُؤْمِنُونَ ﴿٦﴾
6. Hawakuamini kabla yao (umati wa) mji wowote Tuliouangamiza. Je, basi wao wataamini?
وَمَا أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِي إِلَيْهِمْ ۖ فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٧﴾
7. Na Hatukutuma kabla yako isipokuwa wanaume Tunawafunulia Wahy. Basi waulizeni wajuzi (wa Taurati na Injiyl) mkiwa hamjui.
وَمَا جَعَلْنَاهُمْ جَسَدًا لَّا يَأْكُلُونَ الطَّعَامَ وَمَا كَانُوا خَالِدِينَ ﴿٨﴾
8. Na Hatukuwafanya (hao Rusuli) kuwa na miili isiyokula chakula, na hawakuwa wenye kudumu.
ثُمَّ صَدَقْنَاهُمُ الْوَعْدَ فَأَنجَيْنَاهُمْ وَمَن نَّشَاءُ وَأَهْلَكْنَا الْمُسْرِفِينَ ﴿٩﴾
9. Kisha Tukawasadikishia ahadi, Tukawaokoa wao na wale Tuliowataka, na Tukaangamiza wapindukiaji mipaka.
لَقَدْ أَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ كِتَابًا فِيهِ ذِكْرُكُمْ ۖ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿١٠﴾
10. Kwa yakini Tumekuteremshieni Kitabu (Qur-aan) ambacho ndani yake mna makumbusho kwenu. Je, basi hamtii akilini?
وَكَمْ قَصَمْنَا مِن قَرْيَةٍ كَانَتْ ظَالِمَةً وَأَنشَأْنَا بَعْدَهَا قَوْمًا آخَرِينَ ﴿١١﴾
11. Ni miji mingi sana Tumeiteketeza iliyokuwa ikidhulumu, na Tukaanzisha baada yake kaumu nyinginezo.
فَلَمَّا أَحَسُّوا بَأْسَنَا إِذَا هُم مِّنْهَا يَرْكُضُونَ ﴿١٢﴾
12. Basi walipohisi Adhabu Yetu, mara wao wakajaribu kuikimbia.
لَا تَرْكُضُوا وَارْجِعُوا إِلَىٰ مَا أُتْرِفْتُمْ فِيهِ وَمَسَاكِنِكُمْ لَعَلَّكُمْ تُسْأَلُونَ ﴿١٣﴾
13. (Waliambiwa) msikimbie! Na rejeeni kwenye yale mliyoneemeshwa na kuyastarehea, na kwenye maskani zenu ili mpate kuulizwa.
قَالُوا يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿١٤﴾
14. Wakasema: Ole wetu! Hakika sisi tulikuwa madhalimu.
فَمَا زَالَت تِّلْكَ دَعْوَاهُمْ حَتَّىٰ جَعَلْنَاهُمْ حَصِيدًا خَامِدِينَ ﴿١٥﴾
15. Basi ukaendelea huo kuwa ni wito wao mpaka Tukawafanya waliofyekwa wamezimika.
وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاءَ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَاعِبِينَ ﴿١٦﴾
16. Na Hatukuumba mbingu na ardhi na yaliyo baina yake kwa mchezo.
لَوْ أَرَدْنَا أَن نَّتَّخِذَ لَهْوًا لَّاتَّخَذْنَاهُ مِن لَّدُنَّا إِن كُنَّا فَاعِلِينَ ﴿١٧﴾
17. Lau Tungelitaka kufanya pumbao, basi Tungejifanyia Sisi Wenyewe, lau kama Tungelikuwa Wafanyaji (pumbao).
بَلْ نَقْذِفُ بِالْحَقِّ عَلَى الْبَاطِلِ فَيَدْمَغُهُ فَإِذَا هُوَ زَاهِقٌ ۚ وَلَكُمُ الْوَيْلُ مِمَّا تَصِفُونَ ﴿١٨﴾
18. Bali Tunavurumisha haki dhidi ya batili ikaitengua, na mara hiyo inatoweka. Na ole wenu kutokana na mnayoyavumisha.
وَلَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَنْ عِندَهُ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ وَلَا يَسْتَحْسِرُونَ ﴿١٩﴾
19. Na ni Wake wote waliomo katika mbingu na ardhi. Na (Malaika) ambao wako Kwake hawatakabari wakaacha kumwabudu, na wala hawachoki.
يُسَبِّحُونَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لَا يَفْتُرُونَ ﴿٢٠﴾
20. Wanasabihi usiku na mchana, hawaishiwi nguvu.
أَمِ اتَّخَذُوا آلِهَةً مِّنَ الْأَرْضِ هُمْ يُنشِرُونَ ﴿٢١﴾
21. Je, wamechukua waabudiwa katika ardhi wanaofufua?
لَوْ كَانَ فِيهِمَا آلِهَةٌ إِلَّا اللَّـهُ لَفَسَدَتَا ۚ فَسُبْحَانَ اللَّـهِ رَبِّ الْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿٢٢﴾
22. Lau wangelikuweko humo (mbinguni na ardhini) waabudiwa badala ya Allaah, bila shaka zingelifisidika. Basi Subhaana Allaah! Utakasifu ni wa Allaah Rabb wa ‘Arsh kutokana na ambayo wanavumisha.[2]
لَا يُسْأَلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْأَلُونَ ﴿٢٣﴾
23. Haulizwi (Allaah) kwa yale Anayoyafanya, lakini wao wataulizwa.
أَمِ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ آلِهَةً ۖ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ ۖ هَـٰذَا ذِكْرُ مَن مَّعِيَ وَذِكْرُ مَن قَبْلِي ۗ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ الْحَقَّ ۖ فَهُم مُّعْرِضُونَ ﴿٢٤﴾
24. Je, wamejichukulia badala Yake waabudiwa? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآلهوسلم): Leteni burhani yenu. Hii (Qur-aan) ni ukumbusho wa walio pamoja nami, na ni ukumbusho wa walio kabla yangu, bali wengi wao hawajui haki, na kwa hivyo wao ni wenye kukengeuka.
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ ﴿٢٥﴾
25. Na Hatukutuma kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Rasuli yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: Hakika hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, basi Niabuduni.[3]
وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَـٰنُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۚ بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ ﴿٢٦﴾
26. Na wakasema: Ar-Rahmaan Amejifanyia mwana! Subhaanah! (Utakasifu ni Wake!) Bali (hao) ni waja waliokirimiwa.[4]
لَا يَسْبِقُونَهُ بِالْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِ يَعْمَلُونَ ﴿٢٧﴾
27. Hawamtangulii (Allaah) kwa kauli, nao kwa Amri Yake wanatenda.
يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ وَهُم مِّنْ خَشْيَتِهِ مُشْفِقُونَ ﴿٢٨﴾
28. Anajua yale yaliyoko mbele yao, na yale yaliyoko nyuma yao, na wala hawataomba shafaa’ah (uombezi wowote) isipokuwa kwa yule ambaye (Allaah) Amemridhia[5], nao kutokana na kumkhofu, ni wenye khofu na kutahadhari.
وَمَن يَقُلْ مِنْهُمْ إِنِّي إِلَـٰهٌ مِّن دُونِهِ فَذَٰلِكَ نَجْزِيهِ جَهَنَّمَ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ ﴿٢٩﴾
29. Na yeyote yule miongoni mwao atakayesema: Mimi ni mwabudiwa badala Yake, basi huyo Tutamlipa Jahannam. Hivyo ndivyo Tunavyolipa madhalimu.
أَوَلَمْ يَرَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ كَانَتَا رَتْقًا فَفَتَقْنَاهُمَا ۖ وَجَعَلْنَا مِنَ الْمَاءِ كُلَّ شَيْءٍ حَيٍّ ۖ أَفَلَا يُؤْمِنُونَ ﴿٣٠﴾
30. Je, hawakuona wale waliokufuru kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeshikamana Tukazibabandua? Na Tukajaalia kutokana na maji kila kitu kilicho hai? Je, basi hawaamini?[6]
وَجَعَلْنَا فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِهِمْ وَجَعَلْنَا فِيهَا فِجَاجًا سُبُلًا لَّعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ ﴿٣١﴾
31. Na Tukajaalia katika ardhi milima thabiti isiwayumbie yumbie, na Tukajaalia humo njia pana za kupitika ili wapate kujua waendako.
وَجَعَلْنَا السَّمَاءَ سَقْفًا مَّحْفُوظًا ۖ وَهُمْ عَنْ آيَاتِهَا مُعْرِضُونَ ﴿٣٢﴾
32. Na Tukajaalia mbingu kuwa ni paa lililohifadhiwa. Lakini wao wanazipuuzilia mbali Aayaat (Ishara, Dalili) zake.
وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ فِي فَلَكٍ يَسْبَحُونَ ﴿٣٣﴾
33. Naye Ndiye Ambaye Ameumba usiku na mchana, na jua na mwezi. Vyote vinaogelea katika falaki.[7]
وَمَا جَعَلْنَا لِبَشَرٍ مِّن قَبْلِكَ الْخُلْدَ ۖ أَفَإِن مِّتَّ فَهُمُ الْخَالِدُونَ ﴿٣٤﴾
34. Na Hatukujaalia kwa mtu yeyote kabla yako kuwa ni mwenye kudumu. Je, kwani ukifa basi wao watadumu?
كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَنَبْلُوكُم بِالشَّرِّ وَالْخَيْرِ فِتْنَةً ۖ وَإِلَيْنَا تُرْجَعُونَ ﴿٣٥﴾
35. Kila nafsi itaonja mauti. Na Tutakujaribuni kwa mitihani ya shari na kheri. Na Kwetu mtarejeshwa.
وَإِذَا رَآكَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلَّا هُزُوًا أَهَـٰذَا الَّذِي يَذْكُرُ آلِهَتَكُمْ وَهُم بِذِكْرِ الرَّحْمَـٰنِ هُمْ كَافِرُونَ ﴿٣٦﴾
36. Na wanapokuona wale waliokufuru hawakufanyi wewe isipokuwa kichekesho tu. (Wakisema): Je, si ndiye huyu anayewataja (vibaya) waabudiwa wenu? Na hali wao ni wenye kukufuru kwa kutajwa Ar-Rahmaan.[8]
خُلِقَ الْإِنسَانُ مِنْ عَجَلٍ ۚ سَأُرِيكُمْ آيَاتِي فَلَا تَسْتَعْجِلُونِ ﴿٣٧﴾
37. Binaadam ameumbwa kuwa na pupa. Nitakuonyesheni Aayaat (Adhabu, Kisasi, Hukmu) Zangu, basi msiniharakize.
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٣٨﴾
38. Na wanasema: Lini itakuwa hiyo ahadi (ya kuadhibiwa)[9] mkiwa ni wakweli?
لَوْ يَعْلَمُ الَّذِينَ كَفَرُوا حِينَ لَا يَكُفُّونَ عَن وُجُوهِهِمُ النَّارَ وَلَا عَن ظُهُورِهِمْ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٣٩﴾
39. Lau wangelijua wale waliokufuru wakati pale ambapo hawatoweza kukinga nyuso zao na moto, na wala migongo yao, na wala wao hawatonusuriwa.
بَلْ تَأْتِيهِم بَغْتَةً فَتَبْهَتُهُمْ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ رَدَّهَا وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿٤٠﴾
40. Bali utawafikia ghafla, uwashtue wapigwe na butwaa, kisha hawatoweza kuurudisha, na wala wao hawatopewa muhula.
وَلَقَدِ اسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَحَاقَ بِالَّذِينَ سَخِرُوا مِنْهُم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٤١﴾
41. Na walikwishafanyiwa istihzai Rusuli kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Kwa hiyo wale waliowafanyia dhihaka, iliwafikia (adhabu) kwa sababu ya waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.
قُلْ مَن يَكْلَؤُكُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ مِنَ الرَّحْمَـٰنِ ۗ بَلْ هُمْ عَن ذِكْرِ رَبِّهِم مُّعْرِضُونَ ﴿٤٢﴾
42. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Nani awezaye kukulindeni na kukuhifadhini usiku na mchana kutokana na (adhabu ya) Ar-Rahmaan? Bali wao ni wenye kupuuzilia mbali Ukumbusho wa Rabb wao.
أَمْ لَهُمْ آلِهَةٌ تَمْنَعُهُم مِّن دُونِنَا ۚ لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَ أَنفُسِهِمْ وَلَا هُم مِّنَّا يُصْحَبُونَ ﴿٤٣﴾
43. Je, kwani wana waabudiwa wanaoweza kuwakinga Nasi? Hawawezi kujinusuru nafsi zao na wala hawatolindwa Nasi.
بَلْ مَتَّعْنَا هَـٰؤُلَاءِ وَآبَاءَهُمْ حَتَّىٰ طَالَ عَلَيْهِمُ الْعُمُرُ ۗ أَفَلَا يَرَوْنَ أَنَّا نَأْتِي الْأَرْضَ نَنقُصُهَا مِنْ أَطْرَافِهَا ۚ أَفَهُمُ الْغَالِبُونَ ﴿٤٤﴾
44. Bali Tuliwastarehesha hawa (makafiri) na baba zao mpaka ukatawilika umri kwao. Je, hawaoni kwamba Tunaifikia ardhi hii, Tunaipunguza ncha zake?[10] Je, basi wao watashinda?
قُلْ إِنَّمَا أُنذِرُكُم بِالْوَحْيِ ۚ وَلَا يَسْمَعُ الصُّمُّ الدُّعَاءَ إِذَا مَا يُنذَرُونَ ﴿٤٥﴾
45. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi nakuonyeni kwa Wahy. Lakini viziwi hawasikii wito wanapotahadharishwa.
وَلَئِن مَّسَّتْهُمْ نَفْحَةٌ مِّنْ عَذَابِ رَبِّكَ لَيَقُولُنَّ يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿٤٦﴾
46. Na kama wataguswa na mpapaso mdogo tu wa Adhabu ya Rabb wako, kwa hakika watasema: Ole wetu! Hakika sisi tulikuwa madhalimu.
وَنَضَعُ الْمَوَازِينَ الْقِسْطَ لِيَوْمِ الْقِيَامَةِ فَلَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا ۖ وَإِن كَانَ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ أَتَيْنَا بِهَا ۗ وَكَفَىٰ بِنَا حَاسِبِينَ ﴿٤٧﴾
47. Na Tutaweka mizani za uadilifu Siku ya Qiyaamah. Basi nafsi haitodhulumiwa kitu chochote. Na japo ikiwa (amali ina) uzito wa punje ya haradali,[11] Tutaileta. Nasi Tunatosha Kuwa Wadhibiti hesabu.
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَىٰ وَهَارُونَ الْفُرْقَانَ وَضِيَاءً وَذِكْرًا لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٤٨﴾
48. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa na Haaruwn pambanuo (la haki na batili), na mwanga, na ukumbusho kwa wenye taqwa.
الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِالْغَيْبِ وَهُم مِّنَ السَّاعَةِ مُشْفِقُونَ ﴿٤٩﴾
49. Wale wanaomkhofu Rabb wao wakiwa mbali na macho ya watu, nao wanaikhofu Saa.
وَهَـٰذَا ذِكْرٌ مُّبَارَكٌ أَنزَلْنَاهُ ۚ أَفَأَنتُمْ لَهُ مُنكِرُونَ ﴿٥٠﴾
50. Na huu ni ukumbusho wenye baraka (Qur-aan), Tumeuteremsha. Je, basi nyinyi mtaukanusha?
وَلَقَدْ آتَيْنَا إِبْرَاهِيمَ رُشْدَهُ مِن قَبْلُ وَكُنَّا بِهِ عَالِمِينَ ﴿٥١﴾
51. Na kwa yakini Tulimpa Ibraahiym uongofu wake kabla, na Tulikuwa Wenye kumjua vizuri.
إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ مَا هَـٰذِهِ التَّمَاثِيلُ الَّتِي أَنتُمْ لَهَا عَاكِفُونَ ﴿٥٢﴾
52. Alipomwambia baba yake na watu wake: Nini haya masanamu ambayo nyinyi mnayakalia kuyaabudu?
قَالُوا وَجَدْنَا آبَاءَنَا لَهَا عَابِدِينَ ﴿٥٣﴾
53. Wakasema: Tumewakuta baba zetu wakiyaabudu.
قَالَ لَقَدْ كُنتُمْ أَنتُمْ وَآبَاؤُكُمْ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٥٤﴾
54. Akasema: Kwa yakini mmekuwa nyinyi na baba zenu katika upotofu bayana.
قَالُوا أَجِئْتَنَا بِالْحَقِّ أَمْ أَنتَ مِنَ اللَّاعِبِينَ ﴿٥٥﴾
55. Wakasema: Je, umetujia kwa haki, au wewe ni miongoni mwa wafanyao mchezo?
قَالَ بَل رَّبُّكُمْ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الَّذِي فَطَرَهُنَّ وَأَنَا عَلَىٰ ذَٰلِكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٥٦﴾
56. Akasema: Bali Rabb wenu ni Rabb wa mbingu na ardhi, Ambaye Amezianzisha, nami ni katika wenye kushuhudia hayo.
وَتَاللَّـهِ لَأَكِيدَنَّ أَصْنَامَكُم بَعْدَ أَن تُوَلُّوا مُدْبِرِينَ ﴿٥٧﴾
57. Na naapa kwa Allaah! Lazima nitafanyia hila masanamu yenu baada ya mkishageuka kwenda zenu.
فَجَعَلَهُمْ جُذَاذًا إِلَّا كَبِيرًا لَّهُمْ لَعَلَّهُمْ إِلَيْهِ يَرْجِعُونَ ﴿٥٨﴾
58. Basi akayavunja vipande vipande isipokuwa kubwa lao ili wapate kulirejea.
قَالُوا مَن فَعَلَ هَـٰذَا بِآلِهَتِنَا إِنَّهُ لَمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٩﴾
59. Wakasema: Nani amefanya hivi kwa waabudiwa wetu? Hakika yeye ni miongoni mwa madhalimu.
قَالُوا سَمِعْنَا فَتًى يَذْكُرُهُمْ يُقَالُ لَهُ إِبْرَاهِيمُ ﴿٦٠﴾
60. Wakasema: Tulimsikia kijana akiwataja anaitwa Ibraahiym.
قَالُوا فَأْتُوا بِهِ عَلَىٰ أَعْيُنِ النَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَشْهَدُونَ ﴿٦١﴾
61. Wakasema: Mleteni mbele ya macho ya watu ili wapate kushuhudia.
قَالُوا أَأَنتَ فَعَلْتَ هَـٰذَا بِآلِهَتِنَا يَا إِبْرَاهِيمُ ﴿٦٢﴾
62. Wakasema: Je, ni wewe uliyefanya hivi kwa waabudiwa wetu, ee Ibraahiym?
قَالَ بَلْ فَعَلَهُ كَبِيرُهُمْ هَـٰذَا فَاسْأَلُوهُمْ إِن كَانُوا يَنطِقُونَ ﴿٦٣﴾
63. Akasema: Hapana, bali amefanya hayo hili kubwa lao. Hivyo waulizeni wakiwa wanaweza kunena!
فَرَجَعُوا إِلَىٰ أَنفُسِهِمْ فَقَالُوا إِنَّكُمْ أَنتُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٦٤﴾
64. Basi wakajirudia nafsi zao, wakasema: Hakika nyinyi ndio madhalimu.
ثُمَّ نُكِسُوا عَلَىٰ رُءُوسِهِمْ لَقَدْ عَلِمْتَ مَا هَـٰؤُلَاءِ يَنطِقُونَ ﴿٦٥﴾
65. Kisha wakarudia hali yao ya mwanzo ya upotofu. (Wakasema): Umekwishajua kwamba hawa hawasemi.
قَالَ أَفَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكُمْ شَيْئًا وَلَا يَضُرُّكُمْ ﴿٦٦﴾
66. (Ibraahiym) akasema: Je, basi mnaabudu badala ya Allaah visivyokunufaisheni kitu chochote wala kukudhuruni?
أُفٍّ لَّكُمْ وَلِمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٧﴾
67. Aibu yenu nyinyi na vile mnavyoviabudu badala ya Allaah. Je, hamtii akilini?
قَالُوا حَرِّقُوهُ وَانصُرُوا آلِهَتَكُمْ إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ ﴿٦٨﴾
68. Wakasema: Mchomeni moto na mnusuru waabudiwa wenu, mkiwa ni wafanyao (kunusuru).[12]
قُلْنَا يَا نَارُ كُونِي بَرْدًا وَسَلَامًا عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ ﴿٦٩﴾
69. Tukasema: Ee moto! Kuwa baridi, na salama juu ya Ibraahiym.[13]
وَأَرَادُوا بِهِ كَيْدًا فَجَعَلْنَاهُمُ الْأَخْسَرِينَ ﴿٧٠﴾
70. Na wakamkusudia njama, lakini Tukawafanya wao ndio wenye kukhasirika.
وَنَجَّيْنَاهُ وَلُوطًا إِلَى الْأَرْضِ الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا لِلْعَالَمِينَ ﴿٧١﴾
71. Na Tukamuokoa yeye pamoja na Luutw kuelekea ardhi (ya Sham) ambayo Tumeibariki humo kwa walimwengu.[14]
وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ نَافِلَةً ۖ وَكُلًّا جَعَلْنَا صَالِحِينَ ﴿٧٢﴾
72. Na Tukamtunukia Is-haaq na (mjukuu) Ya’quwb kuwa ni ziada. Na wote Tumewajaalia kuwa Swalihina.
وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا وَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِمْ فِعْلَ الْخَيْرَاتِ وَإِقَامَ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءَ الزَّكَاةِ ۖ وَكَانُوا لَنَا عَابِدِينَ ﴿٧٣﴾
73. Na Tukawafanya Imaam wanaongoza kwa Amri Yetu, na Tukawatia ilhamu kufanya kheri, na kusimamisha Swalaah, na kutoa Zakaah. Na wakawa wenye kutuabudu.
وَلُوطًا آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا وَنَجَّيْنَاهُ مِنَ الْقَرْيَةِ الَّتِي كَانَت تَّعْمَلُ الْخَبَائِثَ ۗ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمَ سَوْءٍ فَاسِقِينَ ﴿٧٤﴾
74. Na Luutw Tulimpa hikmah na ilimu, na Tukamuokoa kutoka mji ambao ulikuwa unatenda ukhabithi. Hakika wao walikuwa watu waovu, mafasiki.
وَأَدْخَلْنَاهُ فِي رَحْمَتِنَا ۖ إِنَّهُ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٧٥﴾
75. Na Tukamuingiza katika Rehma Yetu. Hakika yeye ni miongoni mwa Swalihina.
وَنُوحًا إِذْ نَادَىٰ مِن قَبْلُ فَاسْتَجَبْنَا لَهُ فَنَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ ﴿٧٦﴾
76. Na Nuwh alipoita hapo zamani. Tukamuitikia na Tukamuokoa pamoja na ahli zake kutokana na janga kuu.[15]
وَنَصَرْنَاهُ مِنَ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمَ سَوْءٍ فَأَغْرَقْنَاهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٧٧﴾
77. Na Tukamnusuru kutokana na watu ambao walikadhibisha Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu. Hakika wao walikuwa watu waovu, basi Tuliwagharikisha wote.
وَدَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ إِذْ يَحْكُمَانِ فِي الْحَرْثِ إِذْ نَفَشَتْ فِيهِ غَنَمُ الْقَوْمِ وَكُنَّا لِحُكْمِهِمْ شَاهِدِينَ ﴿٧٨﴾
78. Na Daawuwd na Sulaymaan walipotoa hukmu juu ya konde, walipoingia humo usiku kondoo wa watu wakala mimea, Nasi Tukawa katika hukmu yao hiyo Ni Wenye Kushuhudia.
فَفَهَّمْنَاهَا سُلَيْمَانَ ۚ وَكُلًّا آتَيْنَا حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَسَخَّرْنَا مَعَ دَاوُودَ الْجِبَالَ يُسَبِّحْنَ وَالطَّيْرَ ۚ وَكُنَّا فَاعِلِينَ ﴿٧٩﴾
79. Tukamfahamisha Sulaymaan kadhia hiyo (na hukumu mwafaka). Na kila mmoja Tulimpa hikmah na ilimu. Na Tukatiisha milima iwe pamoja na Daawuwd ikisabihi[16] pamoja na ndege. Na Tukawa Ni Wenye Kufanya (haya).
وَعَلَّمْنَاهُ صَنْعَةَ لَبُوسٍ لَّكُمْ لِتُحْصِنَكُم مِّن بَأْسِكُمْ ۖ فَهَلْ أَنتُمْ شَاكِرُونَ ﴿٨٠﴾
80. Na Tukamfunza (Daawuwd) uundaji wa mavazi ya kivita ya chuma kwa ajili yenu ili yakuhifadhini kutokana na kupigana vita kwenu. Je, basi nyinyi ni wenye kushukuru?
وَلِسُلَيْمَانَ الرِّيحَ عَاصِفَةً تَجْرِي بِأَمْرِهِ إِلَى الْأَرْضِ الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا ۚ وَكُنَّا بِكُلِّ شَيْءٍ عَالِمِينَ ﴿٨١﴾
81. Na kwa Sulaymaan, (Tulimtiishia) upepo wa dhoruba unaokwenda kwa amri yake katika ardhi ambayo Tumeibariki humo. Nasi Tulikuwa Wenye Kukijua kila kitu.
وَمِنَ الشَّيَاطِينِ مَن يَغُوصُونَ لَهُ وَيَعْمَلُونَ عَمَلًا دُونَ ذَٰلِكَ ۖ وَكُنَّا لَهُمْ حَافِظِينَ ﴿٨٢﴾
82. Na (Tukamtiishia) miongoni mwa mashaytwaan wakimpigia mbizi na wakimfanyia kazi nyinginezo zisizokuwa hizo. Nasi Tulikuwa Ni Wenye Kuwalinda.
وَأَيُّوبَ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ أَنِّي مَسَّنِيَ الضُّرُّ وَأَنتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ ﴿٨٣﴾
83. Na Ayyuwb, alipomwita Rabb wake: Hakika mimi imenigusa dhara, Nawe Ndiye Mbora zaidi wa Kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu.
فَاسْتَجَبْنَا لَهُ فَكَشَفْنَا مَا بِهِ مِن ضُرٍّ ۖ وَآتَيْنَاهُ أَهْلَهُ وَمِثْلَهُم مَّعَهُمْ رَحْمَةً مِّنْ عِندِنَا وَذِكْرَىٰ لِلْعَابِدِينَ ﴿٨٤﴾
84. Tukamuitikia. Basi Tukamuondoshea dhara aliyokuwa nayo, na Tukampa ahli zake na mfano wao pamoja nao. Ni Rehma kutoka Kwetu, na ni ukumbusho kwa wanaoabudu (Allaah).
وَإِسْمَاعِيلَ وَإِدْرِيسَ وَذَا الْكِفْلِ ۖ كُلٌّ مِّنَ الصَّابِرِينَ ﴿٨٥﴾
85. Na Ismaa’iyl na Idriys na Dhul-Kifl[17], wote ni miongoni mwa wenye kusubiri.
وَأَدْخَلْنَاهُمْ فِي رَحْمَتِنَا ۖ إِنَّهُم مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٨٦﴾
86. Na Tukawaingiza katika Rehma Yetu. Hakika wao ni miongoni mwa Swalihina.
وَذَا النُّونِ إِذ ذَّهَبَ مُغَاضِبًا فَظَنَّ أَن لَّن نَّقْدِرَ عَلَيْهِ فَنَادَىٰ فِي الظُّلُمَاتِ أَن لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٧﴾
87. Na Dhan-Nuwn (Yuwnus), alipoondoka akiwa ameghadhibika, akadhani kwamba Hatutamdhikisha. Akaita vizani kwamba: Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Utakasifu ni Wako, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.[18]
فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَنَجَّيْنَاهُ مِنَ الْغَمِّ ۚ وَكَذَٰلِكَ نُنجِي الْمُؤْمِنِينَ ﴿٨٨﴾
88. Basi Tukamuitikia, na Tukamuokoa kutokana na ghamu. Na hivyo ndivyo Tuwaokowavyo Waumini.
وَزَكَرِيَّا إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ رَبِّ لَا تَذَرْنِي فَرْدًا وَأَنتَ خَيْرُ الْوَارِثِينَ ﴿٨٩﴾
89. Na Zakariyyaa, alipomwita Rabb wake: Rabb wangu! Usiniache pekee, Nawe Ndiye Mbora wa wenye kubaki.
فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَوَهَبْنَا لَهُ يَحْيَىٰ وَأَصْلَحْنَا لَهُ زَوْجَهُ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ ﴿٩٠﴾
90. Basi Tukamuitikia na Tukamtunukia Yahyaa, na Tukamtengenezea mke wake. Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri na wakituomba kwa raghba na khofu, na walikuwa wenye kutunyenyekea.[19]
وَالَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهَا مِن رُّوحِنَا وَجَعَلْنَاهَا وَابْنَهَا آيَةً لِّلْعَالَمِينَ ﴿٩١﴾
91. Na (Maryam) ambaye alilinda tupu yake, Tukampulizia (nguoni mwake) katika Ruwh Yetu, na Tukamjaaliya yeye na mwanawe kuwa ni Aayah (Muujiza, Ishara) kwa walimwengu.
إِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ ﴿٩٢﴾
92. Hakika huu ummah wenu ni ummah mmoja. Nami ni Rabb wenu, basi niabuduni.
وَتَقَطَّعُوا أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ ۖ كُلٌّ إِلَيْنَا رَاجِعُونَ ﴿٩٣﴾
93. Wakafarikiana na kuwa makundi baina yao kuhusu Dini yao. Wote ni wenye kurejea Kwetu.
فَمَن يَعْمَلْ مِنَ الصَّالِحَاتِ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَا كُفْرَانَ لِسَعْيِهِ وَإِنَّا لَهُ كَاتِبُونَ ﴿٩٤﴾
94. Basi atakayetenda mema naye ni Muumini, haitakanushwa juhudi yake. Na hakika Sisi Tunamuandikia.
وَحَرَامٌ عَلَىٰ قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا أَنَّهُمْ لَا يَرْجِعُونَ ﴿٩٥﴾
95. Na haiwezekani kwa wanamji wowote ule Tuliouangamiza, kurejea (duniani).
حَتَّىٰ إِذَا فُتِحَتْ يَأْجُوجُ وَمَأْجُوجُ وَهُم مِّن كُلِّ حَدَبٍ يَنسِلُونَ ﴿٩٦﴾
96. Mpaka watakapofunguliwa Yaajuwj na Maajuwj, nao kutoka kila mwinuko watateremka.[20]
وَاقْتَرَبَ الْوَعْدُ الْحَقُّ فَإِذَا هِيَ شَاخِصَةٌ أَبْصَارُ الَّذِينَ كَفَرُوا يَا وَيْلَنَا قَدْ كُنَّا فِي غَفْلَةٍ مِّنْ هَـٰذَا بَلْ كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿٩٧﴾
97. Na itakaribia ahadi ya haki (ya Qiyaamah). Tahamaki macho ya wale waliokufuru yanakodoka (waseme): Ole wetu! Kwa yakini tulikuwa katika mghafala na haya. Bali tulikuwa madhalimu.
إِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ حَصَبُ جَهَنَّمَ أَنتُمْ لَهَا وَارِدُونَ ﴿٩٨﴾
98. Hakika nyinyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah ni vichochezi vya moto wa Jahannam, nyinyi mtauingia.[21]
لَوْ كَانَ هَـٰؤُلَاءِ آلِهَةً مَّا وَرَدُوهَا ۖ وَكُلٌّ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٩٩﴾
99. Lau wangelikuwa hawa ni waabudiwa wanaostahiki kuabudiwa basi wasingeliuingia, lakini wote humo ni wenye kudumu.
لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَهُمْ فِيهَا لَا يَسْمَعُونَ ﴿١٠٠﴾
100. Lao kwao humo, ni kupumua kwa mngurumo, nao humo hawatosikia lolote.
إِنَّ الَّذِينَ سَبَقَتْ لَهُم مِّنَّا الْحُسْنَىٰ أُولَـٰئِكَ عَنْهَا مُبْعَدُونَ ﴿١٠١﴾
101. Hakika wale ambao imewatangulia Al-Husnaa (furaha, Rehma) kutoka Kwetu, hao watabaidishwa nao (moto).[22]
لَا يَسْمَعُونَ حَسِيسَهَا ۖ وَهُمْ فِي مَا اشْتَهَتْ أَنفُسُهُمْ خَالِدُونَ ﴿١٠٢﴾
102. Hawatosikia mvumo wake. Nao watadumu katika ambayo zimetamani nafsi zao.
لَا يَحْزُنُهُمُ الْفَزَعُ الْأَكْبَرُ وَتَتَلَقَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ هَـٰذَا يَوْمُكُمُ الَّذِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ ﴿١٠٣﴾
103. Hautowahuzunisha mfazaiko mkubwa kabisa, na Malaika watawapokea (wakiwaambia): Hii ni ile Siku yenu mliyokuwa mkiahidiwa.
يَوْمَ نَطْوِي السَّمَاءَ كَطَيِّ السِّجِلِّ لِلْكُتُبِ ۚ كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُ ۚ وَعْدًا عَلَيْنَا ۚ إِنَّا كُنَّا فَاعِلِينَ ﴿١٠٤﴾
104. Siku Tutakapozikunja mbingu kama mkunjo wa karatasi zilizoandikwa.[23] Kama Tulivyoanza umbo la awali Tutalirudisha tena.[24] Ni ahadi iliyo juu Yetu. Hakika Sisi Ni Wenye Kufanya
وَلَقَدْ كَتَبْنَا فِي الزَّبُورِ مِن بَعْدِ الذِّكْرِ أَنَّ الْأَرْضَ يَرِثُهَا عِبَادِيَ الصَّالِحُونَ ﴿١٠٥﴾
105. Na kwa yakini Tuliandika katika Vitabu Vilivyoteremshwa baada ya (kuandikwa katika) Al-Lawh Al-Mahfuwdh (Ubao Uliohifadhiwa) ya kwamba ardhi watairithi Waja Wangu wema.
إِنَّ فِي هَـٰذَا لَبَلَاغًا لِّقَوْمٍ عَابِدِينَ ﴿١٠٦﴾
106. Hakika katika hii (Qur-aan) bila shaka kuna ujumbe maridhawa kwa watu wenye kuabudu.
وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٠٧﴾
107. Na Hatujakutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa ni rehma kwa walimwengu.
قُلْ إِنَّمَا يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٠٨﴾
108. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika nimefunuliwa Wahy kwamba: Mwabudiwa wenu wa haki ni Ilaah Mmoja. Basi je, nyinyi mumesilimu?
فَإِن تَوَلَّوْا فَقُلْ آذَنتُكُمْ عَلَىٰ سَوَاءٍ ۖ وَإِنْ أَدْرِي أَقَرِيبٌ أَم بَعِيدٌ مَّا تُوعَدُونَ ﴿١٠٩﴾
109. Na kama wakikengeuka, basi sema: Nimekutangazieni sawasawa, na wala sijui ni yako karibu au baidi yale mnayoahidiwa.
إِنَّهُ يَعْلَمُ الْجَهْرَ مِنَ الْقَوْلِ وَيَعْلَمُ مَا تَكْتُمُونَ ﴿١١٠﴾
110. Hakika Yeye Anajua kauli za kutamkwa jahara, na Anajua mnayoyaficha.
وَإِنْ أَدْرِي لَعَلَّهُ فِتْنَةٌ لَّكُمْ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ ﴿١١١﴾
111. Na wala sijui kama hii huenda ikawa ni mtihani kwenu na starehe mpaka muda fulani.
قَالَ رَبِّ احْكُم بِالْحَقِّ ۗ وَرَبُّنَا الرَّحْمَـٰنُ الْمُسْتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ ﴿١١٢﴾
112. Akasema: Rabb wangu! Hukumu kwa haki. Na Rabb wetu ni Ar-Rahmaan Aombwaye msaada juu ya yale mnayovumisha.
[1] Makafiri Kumpachika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Sifa Ovu:
Rejea Al-Furqaan (25:4), na Asw-Swaaffaat (37:36).
[3] Rusuli Wote Wamekuja Kulingania Tawhiyd:
Rejea Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى): An-Nahl (16:36), Az-Zukhruf (43:45).
[4] Kumsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwa Kajifanyia Mwana:
Rejea Maryam (19:88), Al-Baqarah (2:116), An-Nisaa (4:171), At-Tawbah (9:30)
[5] Ash-Shafaa (Uombezi) Kwa Ambaye Tu Allaah (سبحانه وتعالى) Amemridhia:
Rejea An-Najm (53:26), Yuwnus (10:3), Maryam (19:87), Twaahaa (20:109), Saba-a (34:23), Az-Zumar (39:44).
[6] Mbingu Na Ardhi Zilikuwa Zimeunganishwa:
Je, hawaoni ya kwamba mbingu na ardhi ziliunganishwa! Yaani, hapo mwanzo zilikuwa kipande kimoja, zimeshikamana na zimerundikana juu ya kila kitu, kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akazitenganisha baina yao, na Akazifanya mbingu kuwa saba, na ardhi saba, Akatenganisha baina yao kwa hewa, kisha Akateremsha mvua kutoka mbinguni na kuotesha mimea kutoka ardhini. Na ndipo Anaendelea kusema:
وَجَعَلْنَا مِنَ الْمَاءِ كُلَّ شَيْءٍ حَيٍّ ۖ
“Na Tukajaalia kutokana na maji kila kitu kilicho hai.”
Sufyaan Ath-Thawriy amesimulia kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ‘Ikrimah kwamba Ibn ‘Abbaas aliulizwa: “Je usiku ulikuwa kabla ya mchana?” Akasema: Kwani hamjui kwamba
السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ كَانَتَا رَتْقًا فَفَتَقْنَاهُمَا ۖ
“Mbingu na ardhi zilikuwa zimeshikamana.”
Si kulikuwa na kiza tu baina yao? Hivyo ili mjue kwamba usiku ulikuwa kabla ya mchana.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[7] Mzunguko Maalumu Wa Sayari Angani.
[9] Ada Ya Makafiri Kuuliza Lini Adhabu Itawafikia Au Lini Qiyaamah Kitatokea:
Rejea Yuwnus (10:48).
[10] Kupunguzwa Ncha Ya Ardhi:
Yaani, kwa kufa watu wake na kutoweka kwao, kidogo kidogo, mpaka Allaah (سبحانه وتعالى) Airithi ardhi na walio juu yake, Naye Ndiye Mbora wa Warithi. Na lau wangelitambua hali hii, basi wasingelidanganyika na kuendelea na hali zao walizonazo. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[11] Hakuna Amali Inayosahaulika Kwa Allaah (سبحانه وتعالى) Iwe Njema Au Ovu:
Rejea Az-Zalzalah (99:7-8), An-Nisaa (4:40), Yuwnus (10:61), Saba-a (34:22).
[13] Moto Uliamrishwa Uwe Baridi Na Salama:
Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Lau Allaah (عزّ وجلّ) Asingelisema “Na Salama”, basi moto ungelimdhuru Ibraahiym kutokana na ubaridi wake mkali. Na Salaf wengineo wamenukuu kama hivo. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Qataadah amesema: "Siku hiyo hakikuweko kiumbe kisichojaribu kuuzima moto wa Ibraahiym (عليه السّلام) ila mjusi." Na Hadiyth imethibitisha:
حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، أَوِ ابْنُ سَلاَمٍ عَنْهُ أَخْبَرَنَا ابْنُ جُرَيْجٍ، عَنْ عَبْدِ الْحَمِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيَّبِ، عَنْ أُمِّ شَرِيكٍ ـ رضى الله عنها أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَمَرَ بِقَتْلِ الْوَزَغِ وَقَالَ " كَانَ يَنْفُخُ عَلَى إِبْرَاهِيمَ عَلَيْهِ السَّلاَمُ ".
Amesimulia Umm Shariyk (رضي الله عنها): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ameamuru mjusi auliwe akasema: Alikuwa akipuliza (moto) kwa Ibraahiym (عليه السّلام).” [Al-Bukhaariy]
[14] Ardhi Ya Shaam Iliyobarikiwa:
Miongoni mwa baraka za Sham, ni wingi wa Manabii waliokuweko humo. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Ameichagua kwa ajili ya Khaliyl Wake Ibraahiym (عليه السّلام) ahajiri huko. Na humo mna mojawapo ya Nyumba Zake tukufu tatu, nayo ni Bayt Al-Maqdis: [Tafsiyr As-Sa’diy]
[15] Janga Kuu:
Ni maudhi, mashaka, shida, kukadhibishwa kwa muda wa miaka mia tisa na khamsini akilingania watu wake katika Tawhiyd, na hawakuamini isipokuwa wachache tu.
[16] Kila Kitu Kinamsabbih Allaah (عزّ وجلّ):
Rejea Al-Hashr (57:1) kwenye rejea zinazotaja viumbe na vitu Alivyoviumba Allaah kuwa vinamsabbih Yeye Allaah (عزّ وجلّ).
[17] Dhul-Kifl Ni Nabiy Au Mja Mwema:
‘Ulamaa wamekhitilafiana katika kauli mbili kama ni Nabiy au ni mja mwema, na kauli iliyo na nguvu zaidi ni kwamba, Dhul-Kifl ni Nabiy kutokana na kutajwa kwake pamoja na Manabii (katika Suwrah hii na Suwrah Swaad 38:48). [Tafsiyr Ibn Kathiyr] Na Allaah Ni Mjuzi zaidi.
[18] Duaa Yenye Kutaqabaliwa Haja, Duaa Ya Kuomba Katika Janga Na Balaa:
عَنْ سَعْدٍ بن أبي وقاص (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ: ((دَعْوَةُ ذِي النُّونِ إِذْ دَعَا وَهُوَ فِي بَطْنِ الْحُوتِ: "لاَ إِلَهَ إلاَّ أَنْتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنْتُ مِنْ الظَّالِمِينَ" فَإِنَّهُ لَمْ يَدْعُ بِهَا رَجُلٌ مُسْلِمٌ فِي شَيْءٍ قَطُّ إِلاَّ اسْتَجَابَ اللَّهُ لَهُ))
Amesimulia Sa’d bin Abiy Waqqaasw (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Duaa ya Dhan-Nuwn (Nabiy Yuwnus) alipoomba alipokuwa katika tumbo la nyangumi:
لاَ إِلَهَ إلاَّ أَنْتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنْتُ مِنْ الظَّالِمِينَ
Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Utakasifu ni Wako, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.
Basi hakika hakuna Muislamu aombaye kwayo kitu chochote kile ila Allaah Atamuitikia.” [Swahiyh At-Tirmidhiy (3505), Swahiyh Al-Jaami’ (3383), As-Silsilah Asw-Swahiyhah (1744)]
Bonyeza pia viungo vifuatavyo kupata faida nyenginezo:
Rejea pia Asw-Swaffaat (37:143-144) kwenye maelezo mengineyo kuhusu hali ya Nabiy Yuwnus (عليه السّلام) alipokuwa tumboni mwa Samaki. Rejea pia Al-Qalam (68:48).
[19] Sifa Ya Waumini Wanapotenda Mema Huwa Baina Ya Khofu Na Matarajio:
Rejea Al-Muuminuwn (23:60-61).
[20] Yaajuwj Na Maajuwj Ni Katika Alama Kubwa Za Qiyaamah:
Rejea Al-Kahf (18:93-99).
Hili ni tahadharisho la Allaah (سبحانه وتعالى) kwa watu kwamba wasije wakang'ang'ania ukafiri na maasi, kwani wakati umekaribia wa kudhihiri Yaajuwj na Maajuwj. Haya ni makabila mawili makubwa ya wana wa Aadam. Dhul-Qarnayn alijenga kizuizi cha kuwazuia, wakati aliposhitakiwa juu ya uharibifu wao katika ardhi. Na katika nyakati za mwisho (Alama kubwa za Qiyaamah kama inavyotaja Aayah inayofuatia (97), kizuizi kitavunjwa na watajitokea kwa nguvu kwa watu kutoka kila pande za mnyanyuko, kwa namna Aliyoelezea Allaah (سبحانه وتعالى). Hii ni dalili juu ya idadi yao kubwa mno, na kasi kubwa watakayozunguka nayo duniani kote, kutokana na ima nguvu zao wenyewe au kutokana na nyenzo ambazo Allaah (سبحانه وتعالى) Atawaumbia. Ina maana kwamba watakuwa na uwezo wa kuvuka masafa makubwa, na kufanya yaliyo magumu kwao yawe ni mepesi. Na kwamba watawatawala watu na kuwakandamiza katika dunia, na kwamba hapatakuwa na mwenye uwezo wa kupigana nao. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[21] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
Makafiri Kuifahamu Ndivyo Sivyo Kauli Ya Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ حَصَبُ جَهَنَّمَ أَنتُمْ لَهَا وَارِدُونَ ﴿٩٨﴾
Hakika nyinyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah ni vichochezi vya moto wa Jahannam, nyinyi mtauingia.
Makafiri wa ki-Quraysh wa Makkah waliifahamu ndivyo sivyo Aayah hii kwamba, wanaoabudiwa wote, wakiwemo masanamu yao. Na pia wakawahusisha waja wa Allaah (سبحانه وتعالى) kama mja mwema ‘Uzayr, aliyekuwa akiabudiwa na Mayahudi, na Nabiy ‘Isyaa (عليه السّلام) aliyekuwa akiabudiwa na Manaswara, kwamba wamo katika hukmu hii, yaani, wawe vichochezi vya moto wa Jahannam pamoja na wao wanawaabudu. Washirikina walimwendea Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kumfanyia kejeli kwa hayo lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha Aayah hizo namba (98–103) kuwajibu washirikina wa Makkah.
Basi ufahamu huo ulikuwa wa batili kwa sababu Aayah hiyo ilikuwa inawaelekezea washirikina wa Makkah na masanamu yao waliyokuwa wakiyaabudu. Na ‘Ulamaa wamefafanua Aayah hii kwa maelezo bayana. Na hii ni radd pia kwa makafiri wengineo wanaotaka kuitafutia upogo Qur-aan Tukufu kwa akili zao finyu, na inadi zao.
Rejea pia Az-Zukhruf (43:57).
[22] Makafiri Kuifahamu Ndivyo Sivyo Kauli Za Allaah (سبحانه وتعالى) Na Kufanya Inadi:
Rejea Az-Zukhruf (43:57) kwenye kiungo kifuatacho cha Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Ambao Imewatangulia Al-Husnaa (Furaha, Rehma) Ya Allaah (عزّ وجلّ):
Ni utangulizi wa furaha katika ilimu ya Allaah na katika Al-Lawh Al-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa) katika usahilishaji wao hapa duniani kwa ajili ya wepesi na matendo mema. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Hao ni wema wa Allaah; Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام), ‘Uzayr, Malaika, na wengineo ambao wameabudiwa bila ya wao kuridhia. Na Aayah hii inahusiana na Aayah iliyotangulia (98) ambayo washirikina walidai kuwa, hawa nao wataingia Jahannam wawe vichochezi vya moto. Basi hawa hawataadhibiwa. Na ndio wanaingia katika Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) ya Aayah hii ya (101) na zinazofuatia (102-103).
[23] Sahifa (Kurasa) Za Matendo Maovu Aliyoyatenda Kila Mmoja Duniani:
Rejea Al-Israa (17:13), Al-Haaqqah (69:19-29), Al-Inshiqaaq (84:7-15), Az-Zalzalah (99).
حَدَّثَنَا سُوَيْدُ بْنُ نَصْرٍ، أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الْمُبَارَكِ، عَنْ لَيْثِ بْنِ سَعْدٍ، حَدَّثَنِي عَامِرُ بْنُ يَحْيَى، عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ الْمَعَافِرِيِّ، ثُمَّ الْحُبُلِيِّ قَالَ سَمِعْتُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ، يَقُولُ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " إِنَّ اللَّهَ سَيُخَلِّصُ رَجُلاً مِنْ أُمَّتِي عَلَى رُءُوسِ الْخَلاَئِقِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَيَنْشُرُ عَلَيْهِ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ سِجِلاًّ كُلُّ سِجِلٍّ مِثْلُ مَدِّ الْبَصَرِ ثُمَّ يَقُولُ أَتُنْكِرُ مِنْ هَذَا شَيْئًا أَظَلَمَكَ كَتَبَتِي الْحَافِظُونَ فَيَقُولُ لاَ يَا رَبِّ . فَيَقُولُ أَفَلَكَ عُذْرٌ فَيَقُولُ لاَ يَا رَبِّ . فَيَقُولُ بَلَى إِنَّ لَكَ عِنْدَنَا حَسَنَةً فَإِنَّهُ لاَ ظُلْمَ عَلَيْكَ الْيَوْمَ فَتَخْرُجُ بِطَاقَةٌ فِيهَا أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ فَيَقُولُ احْضُرْ وَزْنَكَ فَيَقُولُ يَا رَبِّ مَا هَذِهِ الْبِطَاقَةُ مَعَ هَذِهِ السِّجِلاَّتِ فَقَالَ إِنَّكَ لاَ تُظْلَمُ . قَالَ فَتُوضَعُ السِّجِلاَّتُ فِي كِفَّةٍ وَالْبِطَاقَةُ فِي كِفَّةٍ فَطَاشَتِ السِّجِلاَّتُ وَثَقُلَتِ الْبِطَاقَةُ فَلاَ يَثْقُلُ مَعَ اسْمِ اللَّهِ شَيْءٌ " . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ غَرِيبٌ .حَدَّثَنَا قُتَيْبَةُ، حَدَّثَنَا ابْنُ لَهِيعَةَ، عَنْ عَامِرِ بْنِ يَحْيَى، بِهَذَا الإِسْنَادِ نَحْوَهُ بِمَعْنَاهُ . وَالْبِطَاقَةُ هِيَ الْقِطْعَةُ .
Amesimulia ‘Abdullaah Bin ‘Amr Bin Al-‘Aasw (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Atampambanua mtu katika ummah wangu mbele ya viumbe vyote siku ya Qiyaamah. Atakunjuliwa Sahifa (kurasa) tisini na tisa (za matendo maovu ya duniani), kila sahifa itakuwa ndefu kadiri ya jicho linavyoweza kuona. Kisha (Allaah) Atasema: Je! Unakanusha jambo lolote katika haya? Je! Waandishi Wangu (Malaika) wamekudhulumu kitu humo? (Mtu huyo) atasema: Hapana ee Rabb! (Allaah) Atasema: Je, una udhuru wowote? Atasema: Hapana ee Rabb! (Allaah) Atasema: Bali unalo jambo jema Kwetu, kwani leo hutodhulumiwa! Kisha Atatoa kadi ndani yake imeandikwa:
أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ
Ninashuhudia kwamba laa ilaaha illa-Allaah, na ninashuhudia kwamba Muhammad ni Mja Wake na Rasuli Wake.
(Allaah) Atasema: Lete mizani yako. Atasema: Ee Rabb! Je, kadi hii ina thamani gani mbele ya sahifa hizo? (Allaah) Atasema: Hakika hutodhulumiwa. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Sahifa (zilorekodi amali) zitawekwa juu ya sahani mojawapo ya sahani mbili za mizani na kadi itawekwa katika sahani nyengineyo. Basi sahifa zitakuwa nyepesi katika mizani na kadi itakuwa nzito. Hakuna chochote kitakachokuwa kizito zaidi kuliko Jina la Allaah.” [At-Tirmidhiy, Sunan Ibn Maajah na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (1533)]
[24] Watu Watafufuliwa Katika Umbo La Awali Kama Walivyozaliwa:
Rejea Al-Kahf (18:48), Al-An’aam (6:94). Na Hadiyth ifuatayo inaelezea hali za watu watakavyofufuliwa Siku hiyo ya Qiyaamah na watu wengine watakaokanwa kwa sababu ya kuzusha mambo katika Dini.
‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Siku moja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisimama na kututolea mawaidha akasema: “Enyi watu, hakika mtafufuliwa na Allaah hali ya kuwa hamna viatu, mpo uchi na bila kutahiriwa (na magovi). (Akasoma) Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُ
“Kama Tulivyoanza umbo la awali Tutalirudisha tena.” [Al-Anbiyaa: (104)]
Tanabahini! Hakika mtu wa kwanza atakayevishwa nguo ni Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام). Tanabahini! Wataletwa watu katika Ummah wangu na watapelekwa upande wa kushoto (motoni), nami nitasema: “Ee Rabb wangu, Swahaba wangu!” Nitaambiwa: “Wewe hujui watu hawa walichokizua baada yako.” Hapo nitasema kama alivyosema mja mwema (Nabiy ‘Iysaa):
وَكُنتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَّا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنتَ أَنتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿١١٧﴾
“Na nilikuwa juu yao shahidi wakati nilipokuwa nao. Uliponikamilishia muda Ukanichukua juu, Ulikuwa Wewe Ndiye Mwangalizi juu yao. Na Wewe Ni Mwenye Kushuhudia kila kitu.”
إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١١٨﴾
“Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni Waja Wako, na Ukiwaghufuria basi hakika Wewe Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.” [Al-Maaidah (5:117-118]
Nitaambiwa: “Wao waliendelea kukengeuka na kugeuka nyuma kuondokelea mbali ulipowaacha.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
الْحَجّ
022-Al-Hajj
022-Al-Hajj:Utangulizi Wa Suwrah [196]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ ۚ إِنَّ زَلْزَلَةَ السَّاعَةِ شَيْءٌ عَظِيمٌ ﴿١﴾
1. Enyi watu! Mcheni Rabb wenu. Hakika zilizala la Saa ni jambo kuu.[1]
يَوْمَ تَرَوْنَهَا تَذْهَلُ كُلُّ مُرْضِعَةٍ عَمَّا أَرْضَعَتْ وَتَضَعُ كُلُّ ذَاتِ حَمْلٍ حَمْلَهَا وَتَرَى النَّاسَ سُكَارَىٰ وَمَا هُم بِسُكَارَىٰ وَلَـٰكِنَّ عَذَابَ اللَّـهِ شَدِيدٌ ﴿٢﴾
2. Siku mtakapoiona, kila mnyonyeshaji atamsahau anayemnyonyesha, na kila mwenye mimba ataizaa mimba yake, na utawaona watu wamelewa, kumbe hawakulewa lakini ni Adhabu ya Allaah kali!
وَمِنَ النَّاسِ مَن يُجَادِلُ فِي اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّبِعُ كُلَّ شَيْطَانٍ مَّرِيدٍ ﴿٣﴾
3. Na miongoni mwa watu kuna ambao wanaobishana kuhusu Allaah bila ya ilimu, na wanafuata kila shaytwaan asi.
كُتِبَ عَلَيْهِ أَنَّهُ مَن تَوَلَّاهُ فَأَنَّهُ يُضِلُّهُ وَيَهْدِيهِ إِلَىٰ عَذَابِ السَّعِيرِ ﴿٤﴾
4. Ameandikiwa (shaytwaan) kwamba atakayemfanya rafiki, basi yeye atampoteza na atamuongoza katika adhabu ya moto uliowashwa vikali mno!
يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّنَ الْبَعْثِ فَإِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَةٍ ثُمَّ مِن مُّضْغَةٍ مُّخَلَّقَةٍ وَغَيْرِ مُخَلَّقَةٍ لِّنُبَيِّنَ لَكُمْ ۚ وَنُقِرُّ فِي الْأَرْحَامِ مَا نَشَاءُ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ثُمَّ نُخْرِجُكُمْ طِفْلًا ثُمَّ لِتَبْلُغُوا أَشُدَّكُمْ ۖ وَمِنكُم مَّن يُتَوَفَّىٰ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰ أَرْذَلِ الْعُمُرِ لِكَيْلَا يَعْلَمَ مِن بَعْدِ عِلْمٍ شَيْئًا ۚ وَتَرَى الْأَرْضَ هَامِدَةً فَإِذَا أَنزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ وَأَنبَتَتْ مِن كُلِّ زَوْجٍ بَهِيجٍ ﴿٥﴾
5. Enyi watu! Mkiwa mko katika shaka ya kufufuliwa, basi hakika Sisi Tumekuumbeni kutokana na udongo, kisha kutokana na manii, kisha kutokana na pande la damu linaloning’inia, kisha kutokana na kinofu cha nyama kinachotiwa umbo kamili na kisichotiwa umbo kamili, ili Tukubainishieni. Na Tunakikalisha katika fuko la uzazi Tukitakacho mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Kisha Tunakutoeni mkiwa watoto wadogo, kisha ili mfikie umri wa kupevuka kwenu. Na miongoni mwenu yuko anayefishwa, na miongoni mwenu yuko anayerudishwa kwenye umri mbaya na dhaifu zaidi hata awe hajui kitu chochote kile baada ya kuwa anakijua. Na utaona ardhi kame, lakini Tunapoiteremshia maji hutikisika na kuumuka, na inaotesha mimea ya kila namna, mizuri yakupendeza.[2]
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّهُ يُحْيِي الْمَوْتَىٰ وَأَنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٦﴾
6. Hayo (Tuliyoyataja ni dalili) kuwa Allaah Ndiye wa Haki, na kwamba Yeye Anahuisha wafu, na kwamba Yeye juu ya kila kitu Ni Muweza.
وَأَنَّ السَّاعَةَ آتِيَةٌ لَّا رَيْبَ فِيهَا وَأَنَّ اللَّـهَ يَبْعَثُ مَن فِي الْقُبُورِ ﴿٧﴾
7. Na kwamba Saa itafika tu haina shaka ndani yake, na kwamba Allaah Atafufua waliomo makaburini.
وَمِنَ النَّاسِ مَن يُجَادِلُ فِي اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَلَا هُدًى وَلَا كِتَابٍ مُّنِيرٍ ﴿٨﴾
8. Na miongoni mwa watu wako wanaobishana kuhusu Allaah bila ya ilimu wala mwongozo wala Kitabu chenye Nuru.
ثَانِيَ عِطْفِهِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ لَهُ فِي الدُّنْيَا خِزْيٌ ۖ وَنُذِيقُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَذَابَ الْحَرِيقِ ﴿٩﴾
9. Mwenye kugeuza shingo yake kwa kibri ili apoteze (watu) Njia ya Allaah. Atapata duniani hizaya, na Tutamuonjesha Siku ya Qiyaamah adhabu ya kuungua.
ذَٰلِكَ بِمَا قَدَّمَتْ يَدَاكَ وَأَنَّ اللَّـهَ لَيْسَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ ﴿١٠﴾
10. (Ataambiwa): Hayo ni kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yako, na kwamba Allaah Si Mwenye Kudhulumu waja katu.
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَعْبُدُ اللَّـهَ عَلَىٰ حَرْفٍ ۖ فَإِنْ أَصَابَهُ خَيْرٌ اطْمَأَنَّ بِهِ ۖ وَإِنْ أَصَابَتْهُ فِتْنَةٌ انقَلَبَ عَلَىٰ وَجْهِهِ خَسِرَ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْخُسْرَانُ الْمُبِينُ ﴿١١﴾
11. Na miongoni mwa watu yuko anayemwabudu Allaah ukingoni. Inapompata kheri hutumainika kwayo, lakini unapompata mtihani hugeuka kurudi kule kwa mwanzo (kwenye kufru).[3] Amekhasirika duniani na Aakhirah. Hiyo ndiyo khasara bayana.
يَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُ وَمَا لَا يَنفَعُهُ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الضَّلَالُ الْبَعِيدُ ﴿١٢﴾
12. Badala ya Allaah, yeye huviomba ambavyo havimdhuru na ambavyo havimnufaishi. Huo ndio upotofu wa mbali.
يَدْعُو لَمَن ضَرُّهُ أَقْرَبُ مِن نَّفْعِهِ ۚ لَبِئْسَ الْمَوْلَىٰ وَلَبِئْسَ الْعَشِيرُ ﴿١٣﴾
13. Humwomba yule ambaye madhara yake yako karibu kuliko manufaa yake. Bila shaka ni mlinzi muovu kabisa, na bila shaka ni rafiki muovu kabisa.
إِنَّ اللَّـهَ يُدْخِلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ ﴿١٤﴾
14. Hakika Allaah Atawaingiza wale walioamini na wakatenda mema Jannaat zipitazo chini yake mito. Hakika Allaah Anafanya Atakavyo.
مَن كَانَ يَظُنُّ أَن لَّن يَنصُرَهُ اللَّـهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ فَلْيَمْدُدْ بِسَبَبٍ إِلَى السَّمَاءِ ثُمَّ لْيَقْطَعْ فَلْيَنظُرْ هَلْ يُذْهِبَنَّ كَيْدُهُ مَا يَغِيظُ ﴿١٥﴾
15. Yeyote yule anayedhani kwamba Allaah Hatomnusuru (Rasuli) duniani na Aakhirah, basi na afunge kitanzi juu, kisha akikate (ajinyoge), na atazame. Je, hila zake zaweza kuondoa yaliyomghadhibisha?
وَكَذَٰلِكَ أَنزَلْنَاهُ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ وَأَنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يُرِيدُ ﴿١٦﴾
16. Na hivyo ndivyo Tumeiteremsha (Qur-aan yenye) Aayaat bayana, na kwamba Allaah Humwongoza Amtakaye.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَادُوا وَالصَّابِئِينَ وَالنَّصَارَىٰ وَالْمَجُوسَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا إِنَّ اللَّـهَ يَفْصِلُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿١٧﴾
17. Hakika wale walioamini, na ambao ni Mayahudi, na Wasabai na Manaswara, na Majusi, na wale wanaoshirikisha[4], hakika Allaah Atahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah. Hakika Allaah Ni Shahidi juu ya kila kitu.
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يَسْجُدُ لَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ وَالنُّجُومُ وَالْجِبَالُ وَالشَّجَرُ وَالدَّوَابُّ وَكَثِيرٌ مِّنَ النَّاسِ ۖ وَكَثِيرٌ حَقَّ عَلَيْهِ الْعَذَابُ ۗ وَمَن يُهِنِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِن مُّكْرِمٍ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ ۩﴿١٨﴾
18. Je, huoni kwamba wanamsujudia Allaah walioko mbinguni na ardhini, na jua, na mwezi, na nyota, na milima, na miti, na viumbe vinavyotembea, na wengi miongoni mwa watu? Na wengi imewastahikia adhabu. Na ambaye Allaah Amemdhalilisha, basi hatopata wa kumthamini. Hakika Allaah Anafanya Atakavyo.[5]
هَـٰذَانِ خَصْمَانِ اخْتَصَمُوا فِي رَبِّهِمْ ۖ فَالَّذِينَ كَفَرُوا قُطِّعَتْ لَهُمْ ثِيَابٌ مِّن نَّارٍ يُصَبُّ مِن فَوْقِ رُءُوسِهِمُ الْحَمِيمُ ﴿١٩﴾
19. Hawa ni wapinzani wawili (walioamini na makafiri) wanabishana kuhusu Rabb wao.[6] Basi wale waliokufuru, watakatiwa nguo za moto na watamwagiwa juu ya vichwa vyao maji yachemkayo sana.
يُصْهَرُ بِهِ مَا فِي بُطُونِهِمْ وَالْجُلُودُ ﴿٢٠﴾
20. Yatayeyushwa kwayo (maji hayo) yaliyomo matumboni mwao na ngozi zao.
وَلَهُم مَّقَامِعُ مِنْ حَدِيدٍ ﴿٢١﴾
21. Na watapata marungu ya chuma.
كُلَّمَا أَرَادُوا أَن يَخْرُجُوا مِنْهَا مِنْ غَمٍّ أُعِيدُوا فِيهَا وَذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ ﴿٢٢﴾
22. Kila watakapotaka kutoka humo kwa sababu ya dhiki, watarudishwa humo, na (wataambiwa): Onjeni adhabu ya kuunguza.
إِنَّ اللَّـهَ يُدْخِلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ وَلُؤْلُؤًا ۖ وَلِبَاسُهُمْ فِيهَا حَرِيرٌ ﴿٢٣﴾
23. Hakika Allaah Atawaingiza wale walioamini na wakatenda mema Jannaat zipitazo chini yake mito, watapambwa humo kwa vikuku vya dhahabu na lulu, na mavazi yao humo ni hariri.
وَهُدُوا إِلَى الطَّيِّبِ مِنَ الْقَوْلِ وَهُدُوا إِلَىٰ صِرَاطِ الْحَمِيدِ ﴿٢٤﴾
24. Na wataongozwa kwenye kauli nzuri na wataongozwa kwenye njia ya Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ الَّذِي جَعَلْنَاهُ لِلنَّاسِ سَوَاءً الْعَاكِفُ فِيهِ وَالْبَادِ ۚ وَمَن يُرِدْ فِيهِ بِإِلْحَادٍ بِظُلْمٍ نُّذِقْهُ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٢٥﴾
25. Hakika wale waliokufuru na wanazuia Njia ya Allaah na Al-Masjid Al-Haraam ambao Tumeufanya kwa watu wote kuwa ni sawasawa; kwa wakaao humo na wageni. Na yeyote anayekusudia humo kufanya upotofu kwa dhulma Tutamuonjesha adhabu iumizayo.
وَإِذْ بَوَّأْنَا لِإِبْرَاهِيمَ مَكَانَ الْبَيْتِ أَن لَّا تُشْرِكْ بِي شَيْئًا وَطَهِّرْ بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْقَائِمِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ ﴿٢٦﴾
26. Na (taja) Tulipomwonyesha Ibraahiym mahali pa Nyumba; Al-Ka’bah, (Tukamwambia): Usinishirikishe na chochote, na twaharisha Nyumba Yangu kwa wafanyao Twawaaf, na wanaosimama kuswali na wanaorukuu na kusujudu.[7]
وَأَذِّن فِي النَّاسِ بِالْحَجِّ يَأْتُوكَ رِجَالًا وَعَلَىٰ كُلِّ ضَامِرٍ يَأْتِينَ مِن كُلِّ فَجٍّ عَمِيقٍ ﴿٢٧﴾
27. Na tangaza kwa watu Hajj, watakufikia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliyekonda, watakuja kutoka katika kila njia pana za milima zilioko mbali kabisa.
لِّيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ فِي أَيَّامٍ مَّعْلُومَاتٍ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّن بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ ۖ فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْبَائِسَ الْفَقِيرَ ﴿٢٨﴾
28. Ili washuhudie manufaa yao, na walitaje Jina la Allaah katika siku maalumu[8] kupitia yale Aliyowaruzuku kati ya wanyama wenye miguu minne wa mifugo. Basi kuleni sehemu ya nyama yake, na lisheni mwenye shida fakiri.
ثُمَّ لْيَقْضُوا تَفَثَهُمْ وَلْيُوفُوا نُذُورَهُمْ وَلْيَطَّوَّفُوا بِالْبَيْتِ الْعَتِيقِ ﴿٢٩﴾
29. Kisha wajisafishe taka zao na watimize nadhiri zao, na watufu kwenye Nyumba ya Kale (Al-Ka’bah).
ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّـهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ عِندَ رَبِّهِ ۗ وَأُحِلَّتْ لَكُمُ الْأَنْعَامُ إِلَّا مَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ ۖ فَاجْتَنِبُوا الرِّجْسَ مِنَ الْأَوْثَانِ وَاجْتَنِبُوا قَوْلَ الزُّورِ ﴿٣٠﴾
30. Ndio hivyo iwe. Na yeyote anayeadhimisha Vitukufu vya Allaah basi hivyo ni kheri kwake mbele ya Rabb wake. Na mmehalalishiwa wanyama wa mifugo isipokuwa wale mnaosomewa. Basi jiepusheni na uchafu wa (kuabudu) masanamu, na jiepusheni na kauli za uongo.
حُنَفَاءَ لِلَّـهِ غَيْرَ مُشْرِكِينَ بِهِ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَكَأَنَّمَا خَرَّ مِنَ السَّمَاءِ فَتَخْطَفُهُ الطَّيْرُ أَوْ تَهْوِي بِهِ الرِّيحُ فِي مَكَانٍ سَحِيقٍ ﴿٣١﴾
31. Huku mkiielemea haki kwa kumwabudu Allaah Pekee bila ya kumshirikisha. Na yeyote anayemshirikisha Allaah, basi ni kama kwamba ameporomoka kutoka mbinguni, wakamnyakua ndege au upepo ukamtupa mahali mbali mno.
ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّـهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ ﴿٣٢﴾
32. Hayo ndio hivyo. Na yeyote anayeadhimisha Ishara za Allaah, basi hayo ni katika taqwa ya nyoyo.
لَكُمْ فِيهَا مَنَافِعُ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ثُمَّ مَحِلُّهَا إِلَى الْبَيْتِ الْعَتِيقِ ﴿٣٣﴾
33. Katika hao (wanyama) mnapata humo manufaa mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Kisha kuhalalika kwake kuchinjwa ni kwenye Nyumba ya Kale. (Haram ya Makkah).
وَلِكُلِّ أُمَّةٍ جَعَلْنَا مَنسَكًا لِّيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّن بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ ۗ فَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ فَلَهُ أَسْلِمُوا ۗ وَبَشِّرِ الْمُخْبِتِينَ ﴿٣٤﴾
34. Na kwa kila Ummah Tumeweka taratibu za ibaada ili wataje Jina la Allaah kwa yale Aliyowaruzuku ya wanyama wa miguu minne wa mifugo. Kwa hiyo Mwabudiwa wenu wa haki Ni Ilaah Mmoja Pekee, basi jisalimisheni Kwake. Na wabashirie wanyenyekevu.
الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَالصَّابِرِينَ عَلَىٰ مَا أَصَابَهُمْ وَالْمُقِيمِي الصَّلَاةِ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٣٥﴾
35. Ambao Anapotajwa Allaah nyoyo zao zinajaa khofu, na wanaosubiri juu ya yale yaliyowasibu, na wanaosimamisha Swalaah na katika vile Tulivyowaruzuku wanatoa.
وَالْبُدْنَ جَعَلْنَاهَا لَكُم مِّن شَعَائِرِ اللَّـهِ لَكُمْ فِيهَا خَيْرٌ ۖ فَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهَا صَوَافَّ ۖ فَإِذَا وَجَبَتْ جُنُوبُهَا فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْقَانِعَ وَالْمُعْتَرَّ ۚ كَذَٰلِكَ سَخَّرْنَاهَا لَكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٣٦﴾
36. Na ngamia na ng’ombe Tumekufanyieni kuwa ni miongoni mwa Ishara za Allaah, kwa hao mnapata kheri nyingi. Basi tajeni Jina la Allaah juu yao wanapopangwa safu (kuchinjwa). Na waangukapo ubavu, basi kuleni sehemu ya nyama yao, na lisheni waliokinai na wanaolazimika kuomba. Hivyo ndivyo Tulivyowatiisha kwa ajili yenu ili mpate kushukuru.
لَن يَنَالَ اللَّـهَ لُحُومُهَا وَلَا دِمَاؤُهَا وَلَـٰكِن يَنَالُهُ التَّقْوَىٰ مِنكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ سَخَّرَهَا لَكُمْ لِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ ۗ وَبَشِّرِ الْمُحْسِنِينَ ﴿٣٧﴾
37. Hazimfikii Allaah nyama zake wala damu zake, lakini inamfikia taqwa kutoka kwenu. Hivyo ndivyo Tulivyowatiisha kwenu ili mpate kumtukuza Allaah kwa kuwa Amekuongozeni. Na wabashirie wafanyao ihsaan.
إِنَّ اللَّـهَ يُدَافِعُ عَنِ الَّذِينَ آمَنُوا ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ خَوَّانٍ كَفُورٍ ﴿٣٨﴾
38. Hakika Allaah Anawalinda wale walioamini. Hakika Allaah Hampendi kila mwenye tabia ya kukhini, mwingi wa kukufuru.
أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ ﴿٣٩﴾
39. Wameruhusiwa (kupigana) wale wanaopigwa kwa kuwa wamedhulumiwa. Na hakika Allaah bila shaka Ni Muweza wa Kuwanusuru.
الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِم بِغَيْرِ حَقٍّ إِلَّا أَن يَقُولُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ۗ وَلَوْلَا دَفْعُ اللَّـهِ النَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّهُدِّمَتْ صَوَامِعُ وَبِيَعٌ وَصَلَوَاتٌ وَمَسَاجِدُ يُذْكَرُ فِيهَا اسْمُ اللَّـهِ كَثِيرًا ۗ وَلَيَنصُرَنَّ اللَّـهُ مَن يَنصُرُهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ ﴿٤٠﴾
40. Ambao wametolewa majumbani mwao bila ya haki isipokuwa kwa kuwa tu wanasema: Rabb wetu Ni Allaah. Na lau ingelikuwa Allaah Hawakingi watu baadhi yao kwa wengine, bila shaka yangelivunjwa mahekalu na makanisa, na masinagogi na Misikiti inayotajwa humo Jina la Allaah kwa wingi. Na bila shaka Allaah Atamnusuru yeyote yule anayenusuru Dini Yake. Hakika Allaah bila shaka Ni Mwenye nguvu zote, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika.
الَّذِينَ إِن مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنكَرِ ۗ وَلِلَّـهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ ﴿٤١﴾
41. Ambao Tukiwamakinisha katika ardhi, husimamisha Swalaah na hutoa Zakaah, na huamrisha mema na hukataza munkari. Na kwa Allaah Pekee ndio hatima ya mambo yote.
وَإِن يُكَذِّبُوكَ فَقَدْ كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَعَادٌ وَثَمُودُ ﴿٤٢﴾
42. Na wakikukadhibisha, basi wamekwishakadhibisha kabla yao watu wa Nuwh na ‘Aad na Thamuwd.
وَقَوْمُ إِبْرَاهِيمَ وَقَوْمُ لُوطٍ ﴿٤٣﴾
43. Na watu wa Ibraahiym, na watu wa Luutw.
وَأَصْحَابُ مَدْيَنَ ۖ وَكُذِّبَ مُوسَىٰ فَأَمْلَيْتُ لِلْكَافِرِينَ ثُمَّ أَخَذْتُهُمْ ۖ فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ ﴿٤٤﴾
44. Na watu wa Madyan. Na Muwsaa alikadhibishwa pia basi Nikawapa muhula makafiri, kisha Nikawachukua. Basi vipi ilikuwa Adhabu Yangu!
فَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا وَهِيَ ظَالِمَةٌ فَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا وَبِئْرٍ مُّعَطَّلَةٍ وَقَصْرٍ مَّشِيدٍ ﴿٤٥﴾
45. Miji mingapi Tumeiangamiza iliyokuwa ikidhulumu, ikaanguka juu ya mapaa yake na kuwa magofu, na visima vilivyohamwa, na makasri madhubuti.
أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَتَكُونَ لَهُمْ قُلُوبٌ يَعْقِلُونَ بِهَا أَوْ آذَانٌ يَسْمَعُونَ بِهَا ۖ فَإِنَّهَا لَا تَعْمَى الْأَبْصَارُ وَلَـٰكِن تَعْمَى الْقُلُوبُ الَّتِي فِي الصُّدُورِ ﴿٤٦﴾
46. Je, basi hawatembei katika ardhi ili wapate kuwa na nyoyo za kuzingatia au masikio ya kusikilizia?[9] Kwani hakika hayapofuki macho, lakini zinazopofuka ni nyoyo zilizomo vifuani.[10]
وَيَسْتَعْجِلُونَكَ بِالْعَذَابِ وَلَن يُخْلِفَ اللَّـهُ وَعْدَهُ ۚ وَإِنَّ يَوْمًا عِندَ رَبِّكَ كَأَلْفِ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ ﴿٤٧﴾
47. Na wanakuhimiza adhabu, na hali ya kuwa Allaah Hatokhalifu Ahadi Yake. Na hakika siku moja kwa Rabb wako ni kama miaka elfu katika ile mnayoihesabu.[11]
وَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ أَمْلَيْتُ لَهَا وَهِيَ ظَالِمَةٌ ثُمَّ أَخَذْتُهَا وَإِلَيَّ الْمَصِيرُ ﴿٤٨﴾
48. Na miji mingapi Nimeipa muhula hali ya kuwa imedhulumu, kisha Nikaikamata (Kuiadhibu)? Na Kwangu Pekee ni mahali pa kuishia.
قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّمَا أَنَا لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٤٩﴾
49. Sema: Enyi watu! Hakika mimi kwenu ni mwonyaji mwenye kubainisha kila kitu.
فَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ ﴿٥٠﴾
50. Basi wale walioamini na wakatenda mema, watapata maghfirah na riziki karimu.
وَالَّذِينَ سَعَوْا فِي آيَاتِنَا مُعَاجِزِينَ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿٥١﴾
51. Na wale waliokwenda mbio katika kupinga Aayaat Zetu, hao ni watu wa moto uwakao vikali mno.
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ وَلَا نَبِيٍّ إِلَّا إِذَا تَمَنَّىٰ أَلْقَى الشَّيْطَانُ فِي أُمْنِيَّتِهِ فَيَنسَخُ اللَّـهُ مَا يُلْقِي الشَّيْطَانُ ثُمَّ يُحْكِمُ اللَّـهُ آيَاتِهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿٥٢﴾
52. Na Hatukutuma kabla yako Rasuli yeyote wala Nabiy yeyote isipokuwa anaposoma Kitabu cha Allaah au kubalighisha ujumbe, shaytwaan hutupia ya kuvuruga anayoyasoma, lakini Allaah Hufuta yale anayoyatupia shaytwaan kisha Allaah Anathibitisha Aayaat Zake. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
لِّيَجْعَلَ مَا يُلْقِي الشَّيْطَانُ فِتْنَةً لِّلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْقَاسِيَةِ قُلُوبُهُمْ ۗ وَإِنَّ الظَّالِمِينَ لَفِي شِقَاقٍ بَعِيدٍ ﴿٥٣﴾
53. Ili (Allaah) Afanye yale aliyoyatupa shaytwaan kuwa ni fitnah kwa wale wenye maradhi katika nyoyo[12] zao na wale ambao nyoyo zao ni ngumu. Na hakika madhalimu bila shaka wamo katika upinzani wa mbali.
وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ أَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَيُؤْمِنُوا بِهِ فَتُخْبِتَ لَهُ قُلُوبُهُمْ ۗ وَإِنَّ اللَّـهَ لَهَادِ الَّذِينَ آمَنُوا إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٥٤﴾
54. Na ili wajue wale waliopewa ilimu kwamba hii (Qur-aan) ni haki kutoka kwa Rabb wao wapate kuiamini, na nyoyo zao zipate kutulia kwayo. Na hakika Allaah Ndiye Anayewaongoza wale walioamini kuelekea njia iliyonyooka.
وَلَا يَزَالُ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي مِرْيَةٍ مِّنْهُ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ السَّاعَةُ بَغْتَةً أَوْ يَأْتِيَهُمْ عَذَابُ يَوْمٍ عَقِيمٍ ﴿٥٥﴾
55. Na hawatoacha wale waliokufuru kuwa katika shaka nayo (Qur-aan), mpaka iwafikie Saa ghafla, au iwafikie adhabu ya siku kame (isiyokuwa na kheri kwao).
الْمُلْكُ يَوْمَئِذٍ لِّلَّـهِ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ ۚ فَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿٥٦﴾
56. Ufalme Siku hiyo ni wa Allaah Pekee, Atahukumu baina yao. Basi wale walioamini na wakatenda mema, watakuwa katika Jannaat za Neema.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا فَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٥٧﴾
57. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) Zetu, basi hao watapata adhabu ya kudhalilisha.
وَالَّذِينَ هَاجَرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ثُمَّ قُتِلُوا أَوْ مَاتُوا لَيَرْزُقَنَّهُمُ اللَّـهُ رِزْقًا حَسَنًا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَهُوَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿٥٨﴾
58. Na wale waliohajiri katika Njia ya Allaah, kisha wakauawa, au wakafa, bila shaka Allaah Atawaruzuku riziki nzuri. Na hakika Allaah bila shaka Yeye Ndiye Mbora wa wenye kuruzuku.
لَيُدْخِلَنَّهُم مُّدْخَلًا يَرْضَوْنَهُ ۗ وَإِنَّ اللَّـهَ لَعَلِيمٌ حَلِيمٌ ﴿٥٩﴾
59. Bila shaka Atawaingiza mahala watakapoparidhia. Na hakika Allaah bila shaka ni Ni Mjuzi wa yote, Mvumilivu.
ذَٰلِكَ وَمَنْ عَاقَبَ بِمِثْلِ مَا عُوقِبَ بِهِ ثُمَّ بُغِيَ عَلَيْهِ لَيَنصُرَنَّهُ اللَّـهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٌ ﴿٦٠﴾
60. Ndivyo hivyo, na yeyote anayejilipizia mfano wa ubaya aliofanyiwa, kisha akaja kufanyiwa baghi[13] (kudhulumiwa) tena, bila shaka Allaah Atamnusuru. Hakika Allaah bila shaka Ni Mwingi wa Kusamehe, Mwingi wa Kughufuria.
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَأَنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ ﴿٦١﴾
61. Hivyo ni kwa kuwa Allaah Anaingiza usiku katika mchana, na Anaingiza mchana katika usiku, na kwamba Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ هُوَ الْبَاطِلُ وَأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ ﴿٦٢﴾
62. Hivyo ni kwa kuwa Allaah Ndiye wa Haki, na kwamba vile wanavyoomba badala Yake ndiyo batili, na kwamba Allaah Ndiye Mwenye ‘Uluwa Uliotukuka, Mkubwa Kabisa.
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَتُصْبِحُ الْأَرْضُ مُخْضَرَّةً ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَطِيفٌ خَبِيرٌ ﴿٦٣﴾
63. Je, huoni kwamba Allaah Ameteremsha kutoka mbinguni maji kisha ardhi ikawa chanikiwiti. Hakika Allaah bila shaka ni Mwenye Kudabiri mambo kwa Ulatifu, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَإِنَّ اللَّـهَ لَهُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ ﴿٦٤﴾
64. Ni Vyake pekee vyote vile vilivyomo mbinguni na vile vilivyomo ardhini. Na hakika Allaah bila shaka Yeye Ndiye Mkwasi, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ سَخَّرَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ وَالْفُلْكَ تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِأَمْرِهِ وَيُمْسِكُ السَّمَاءَ أَن تَقَعَ عَلَى الْأَرْضِ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِالنَّاسِ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿٦٥﴾
65. Je, huoni kwamba Allaah Amevitiisha kwa ajili yenu vile vilivyomo katika ardhi na merikebu zipitazo baharini kwa Amri Yake. Na Anazuia mbingu zisianguke juu ya ardhi isipokuwa kwa Idhini Yake. Hakika Allaah kwa watu ni Mwenye huruma mno, Mwenye Kurehemu.
وَهُوَ الَّذِي أَحْيَاكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ۗ إِنَّ الْإِنسَانَ لَكَفُورٌ ﴿٦٦﴾
66. Naye Ndiye Ambaye Anakuhuisheni, kisha Anakufisheni, kisha Atakuhuisheni. Hakika binaadam ni mwingi wa kukufuru.
لِّكُلِّ أُمَّةٍ جَعَلْنَا مَنسَكًا هُمْ نَاسِكُوهُ ۖ فَلَا يُنَازِعُنَّكَ فِي الْأَمْرِ ۚ وَادْعُ إِلَىٰ رَبِّكَ ۖ إِنَّكَ لَعَلَىٰ هُدًى مُّسْتَقِيمٍ ﴿٦٧﴾
67. Kila ummah Tumejaalia taratibu za ibaada wanazozifuata. Basi wasizozane nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kabisa katika jambo hili, na walinganie kwa Rabb wako. Hakika wewe bila shaka uko juu ya mwongozo ulionyooka.
وَإِن جَادَلُوكَ فَقُلِ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿٦٨﴾
68. Na wakibishana nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi sema: Allaah Anajua zaidi yale mnayoyafanya.
اللَّـهُ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿٦٩﴾
69. Allaah Atahukumu baina yenu Siku ya Qiyaamah katika yale mliyokuwa mnakhitilafiana.
أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۗ إِنَّ ذَٰلِكَ فِي كِتَابٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿٧٠﴾
70. Je, hujui kwamba Allaah Anajua yale yote yaliyomo katika mbingu na ardhi? Hakika hayo yamo katika Kitabu. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.
وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَمَا لَيْسَ لَهُم بِهِ عِلْمٌ ۗ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِن نَّصِيرٍ ﴿٧١﴾
71. Wanaabudu badala ya Allaah ambayo Hakuyateremshia mamlaka, na ambayo hawana ilimu nayo. Na madhalimu hawana yeyote mwenye kunusuru.
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ تَعْرِفُ فِي وُجُوهِ الَّذِينَ كَفَرُوا الْمُنكَرَ ۖ يَكَادُونَ يَسْطُونَ بِالَّذِينَ يَتْلُونَ عَلَيْهِمْ آيَاتِنَا ۗ قُلْ أَفَأُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ مِّن ذَٰلِكُمُ ۗ النَّارُ وَعَدَهَا اللَّـهُ الَّذِينَ كَفَرُوا ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿٧٢﴾
72. Na wanaposomewa Aayaat Zetu bayana, utatambua katika nyuso za wale waliokufuru karaha. Wanakaribia kuwashambulia wale wanaowasomea Aayaat Zetu. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Je, nikujulisheni yaliyo shari zaidi kuliko hayo kwenu? Ni moto Aliowaahidi Allaah wale waliokufuru. Na ni ubaya ulioje mahali pa kuishia!
يَا أَيُّهَا النَّاسُ ضُرِبَ مَثَلٌ فَاسْتَمِعُوا لَهُ ۚ إِنَّ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَن يَخْلُقُوا ذُبَابًا وَلَوِ اجْتَمَعُوا لَهُ ۖ وَإِن يَسْلُبْهُمُ الذُّبَابُ شَيْئًا لَّا يَسْتَنقِذُوهُ مِنْهُ ۚ ضَعُفَ الطَّالِبُ وَالْمَطْلُوبُ ﴿٧٣﴾
73. Enyi watu! Umepigwa mfano basi usikilizeni kwa makini! Hakika wale mnaowaomba badala ya Allaah hawawezi kuumba nzi japo wakijumuika kwa hilo. Na nzi akiwapokonya kitu chochote kile hawawezi kukiambua tena. Amedhoofika mwenye kutaka matilabu na mwenye kutakiwa.[14]
مَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ ﴿٧٤﴾
74. Hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria. Hakika Allaah bila shaka ni Mwenye nguvu zote, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika.
اللَّـهُ يَصْطَفِي مِنَ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا وَمِنَ النَّاسِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ ﴿٧٥﴾
75. Allaah Anakhitari Wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa watu. Hakika Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.
يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۗ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿٧٦﴾
76. Anajua yale yaliyoko mbele yao, na yale yaliyoko nyuma yao. Na kwa Allaah yanarejeshwa mambo yote.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ارْكَعُوا وَاسْجُدُوا وَاعْبُدُوا رَبَّكُمْ وَافْعَلُوا الْخَيْرَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ۩﴿٧٧﴾
77. Enyi walioamini! Rukuuni, na sujuduni na mwabuduni Rabb wenu, na fanyeni ya kheri ili mpate kufaulu.
وَجَاهِدُوا فِي اللَّـهِ حَقَّ جِهَادِهِ ۚ هُوَ اجْتَبَاكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ ۚ مِّلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ ۚ هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمِينَ مِن قَبْلُ وَفِي هَـٰذَا لِيَكُونَ الرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيْكُمْ وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ ۚ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَاعْتَصِمُوا بِاللَّـهِ هُوَ مَوْلَاكُمْ ۖ فَنِعْمَ الْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ النَّصِيرُ ﴿٧٨﴾
78. Na fanyeni Jihaad katika Njia ya Allaah kama inavyostahiki kufanyiwa Jihaad. Yeye Ndiye Amekuteueni, na Hakukufanyieni ugumu wowote ule katika Dini. Mila ya baba yenu Ibraahiym. Yeye (Allaah) Ndiye Aliyekuiteni Waislamu hapo zamani na pia katika hii (Qur-aan). Ili Rasuli (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) awe shahidi juu yenu, nanyi muwe mashahidi juu ya watu.[15] Basi simamisheni Swalaah na toeni Zakaah, na shikamaneni pamoja kwa ajili ya Allaah, Yeye Ndiye Mola Mlinzi wenu. Basi Mzuri Alioje Mola Mlinzi na Mzuri Alioje Mwenye Kunusuru.
[1] Zilizala (Tetemeko) La Ardhi:
Aayah ya (1-2): Mufassiruwn wamekhitilafiana katika kauli mbalimbali kuhusu wakati wa kutokea zilizala hii:
(i) Baada ya watu kufufuliwa kutokana na Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِذَا زُلْزِلَتِ الْأَرْضُ زِلْزَالَهَا ﴿١﴾ وَأَخْرَجَتِ الْأَرْضُ أَثْقَالَهَا ﴿٢﴾
“Itakapotetemeshwa ardhi zilzala yake (ya mwisho). Na itakapotoa ardhi mizigo yake.” [Az-Zalzalah (99:1-2)]
Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَحُمِلَتِ الْأَرْضُ وَالْجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةً وَاحِدَةً﴿١٤﴾ فَيَوْمَئِذٍ وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ﴿١٥﴾
“Na ardhi na milima ikaondolewa kisha ikapondwa mpondo mmoja. 15. Basi siku hiyo ndio litatokea tukio la kutokea.” [Al-Haaqqah (69:14-15)]
Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِذَا رُجَّتِ الْأَرْضُ رَجًّا ﴿٤﴾ وَبُسَّتِ الْجِبَالُ بَسًّا ﴿٥﴾ فَكَانَتْ هَبَاءً مُّنبَثًّا ﴿٦﴾
“Itakapotikiswa ardhi mtikiso mkubwa. Na milima itakapopondwa pondwa. Ikawa chembechembe za vumbi zinazoelea hewani zikitawanyika.” [Al-Waaqi’ah (56:4-6)]
(ii) Zama za mwisho inapokaribia Qiyaamah na ni katika alama za Qiyaamah.
(iii) Kabla ya Qiyaamah.
(iv) Duniani kabla ya Qiyaamah.
Rejea pia Az-Zalzalah (99).
[2] Uumbaji Wa Mwanaadam Tumboni Na Kupulizwa Roho Anapofikia Miezi Minne:
عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم -وَهُوَ الصَّادِقُ الْمَصْدُوقُ: ((إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يُرْسَلُ إلَيْهِ الْمَلَكُ فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ، وَيُؤْمَرُ بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ، وَأَجَلِهِ، وَعَمَلِهِ، وَشَقِيٍّ أَمْ سَعِيدٍ؛ فَوَاَللَّهِ الَّذِي لَا إلَهَ غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُهَا. وَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ فَيَدْخُلُهَا)) رواه البخاري ومسلم
Amesimulia Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdillaah bin Mas-‘uwd (رضي الله عنه): Ametusimulia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa: “Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho (yake). Na (Malaika huyo) anaamrishwa maneno manne: Kuandika rizki yake, ajali yake (umri atakaoishi duniani), amali zake, mtu muovu au mwema. Wa-Allaahi! Naapa kwa Yule Ambaye hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, hakika mmoja wenu huenda afanye amali za watu wa Jannah hadi ikawa baina yake na Jannah ni dhiraa, na kile kilichoandikwa kikathibiti, akafanya amali ya watu wa motoni akaingia motoni. Na mmoja wenu hufanya amali za watu wa motoni hadi ikawa baina yake na moto ni dhiraa, na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti, akafanya amali ya watu wa Jannah akaingia Jannah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Rejea pia Al-Muuminuwn (23:12), Ghaafir (40:67).
[3] Kuwa Baina Ya Imaan Na Kufru Pindi Mtu Anapopata Mitihani:
حَدَّثَنِي إِبْرَاهِيمُ بْنُ الْحَارِثِ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ أَبِي بُكَيْرٍ، حَدَّثَنَا إِسْرَائِيلُ، عَنْ أَبِي حَصِينٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما ـ قَالَ وَمِنَ النَّاسِ مَنْ يَعْبُدُ اللَّهَ عَلَى حَرْفٍ قَالَ كَانَ الرَّجُلُ يَقْدَمُ الْمَدِينَةَ، فَإِنْ وَلَدَتِ امْرَأَتُهُ غُلاَمًا، وَنُتِجَتْ خَيْلُهُ قَالَ هَذَا دِينٌ صَالِحٌ. وَإِنْ لَمْ تَلِدِ امْرَأَتُهُ وَلَمْ تُنْتَجْ خَيْلُهُ قَالَ هَذَا دِينُ سُوءٍ.
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kuhusiana na Aayah hii na ifuatayo:
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَعْبُدُ اللَّـهَ عَلَىٰ حَرْفٍ ۖ
“Na miongoni mwa watu yuko anayemwabudu Allaah ukingoni.” [Al-Hajj (22:11-12)]
Akasema: “Alikuwa mtu akija Madiynah, na ikiwa mkewe atazaa mtoto wa kiume na farasi wake vile vile akazaa, husema: “Dini hii (ya Kiislamu) ni nzuri.” Lakini ikiwa mkewe atakosa kuzaa na farasi wake vile vile akakosa kuzaa, basi husema: “Dini hii (ya Kiislamu) ni mbaya.” [Al-Bukhaariy]
[4] Wasabai, Majusi Na Washirikina:
Wasabai:
Maana yake kiasili ni ‘kutoka.’ Inasemekana “Fulani alitoka katika dini moja hadi nyingine.” Imaam Atw-Twabariy (رحمه الله) amesema: “Ni mtu mpya katika dini, kama mtu aliyeritadi kutoka katika Dini ya Kiislamu. Na kila anayetoka katika dini akaingia katika dini nyengine basi Waarabu wanasema Swaabia. Na nyota hung’aa zinapotoka kutoka katika miinuko yake.”
Ama kuhusu imaan na itikadi zao, Salaf wamekhitilafiana katika semi mbalimbali, miongoni mwazo ni:
‘Umar na Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) wamesema: “Hao (Wasabai) ni Watu wa Kitabu.” Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: “Haijuzu dhabihu zao wala kuingiliana nao.” Na Sufyaan amepokea kutoka kwa Layth kutoka kwa Mujaahid kwamba “Wasabai ni watu baina ya Mayahudi na Majusi, hawana dini.” Na Qataadah amesema: “Wasabai ni watu wanaoabudu Malaika.”
Majusi:
Majusi ni waabudu moto ambao wanaamini kwamba miungu ni aina mbili: Mungu wa nuru na mungu wa giza. Itikadi yao imepotoshwa hadi kwamba kaka anaweza kufunga ndoa na dada yake.
Washirikina:
Ni washirikina wa Makkah waliokuwa wanaabudu masanamu, na inajumuisha washirikina wowote wengineo katika nchi yoyote ile wasiotajwa humo.
[5] Kila Kitu Kinamsujudia Allaah (عزّ وجلّ):
Rejea Ar-Rahmaan (55:6) kwenye rejea zinazotaja viumbe na vitu Alivyoviumba Allaah kuwa vinamsujudia Yeye Allaah (عزّ وجلّ).
Na Hadiyth ifuatayo inathibitisha jua kumsujudia Allaah (سبحانه وتعالى):
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ التَّيْمِيِّ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي ذَرٍّ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم لأَبِي ذَرٍّ حِينَ غَرَبَتِ الشَّمْسُ " تَدْرِي أَيْنَ تَذْهَبُ ". قُلْتُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ. قَالَ " فَإِنَّهَا تَذْهَبُ حَتَّى تَسْجُدَ تَحْتَ الْعَرْشِ، فَتَسْتَأْذِنَ فَيُؤْذَنَ لَهَا، وَيُوشِكُ أَنْ تَسْجُدَ فَلاَ يُقْبَلَ مِنْهَا، وَتَسْتَأْذِنَ فَلاَ يُؤْذَنَ لَهَا، يُقَالُ لَهَا ارْجِعِي مِنْ حَيْثُ جِئْتِ. فَتَطْلُعُ مِنْ مَغْرِبِهَا، فَذَلِكَ قَوْلُهُ تَعَالَى وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَهَا ذَلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ
Amesimulia Abuu Dharr (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniuliza wakati wa machweo: “Je, unajua jua linapokwenda (wakati wa kuzama kwake)?” Nikamjibu: Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi. Akasema: “Hakika linakwenda mpaka linasujudu chini ya ‘Arsh, na kutaka idhini kuchomoza tena, nalo linaruhusiwa. Na inachelewa kuwa (itafika wakati ambapo) litakaribia kusujudu lakini sijda yake haitokubaliwa, na litaomba idhini lakini litakataliwa (kutimiza mizunguko yake). Litaambiwa: ‘Rudi ulipotoka’. Hivyo, litachomoza Magharibi. Na hiyo ndiyo Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَّهَا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ﴿٣٨﴾
“Na jua linatembea hadi matulio yake. Hayo ni Takdiri ya Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.” [Yaasiyn 36:38) - Hadiyth ameipokea Imaam Al-Bukhaariy]
Kuhusu Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَكَثِيرٌ حَقَّ عَلَيْهِ الْعَذَابُ ۗ
“Na wengi imewastahikia adhabu.”
Ina maana wale ambao hawataki kusujudu. [Ibn Kathiyr (6:540)]
[6] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
022-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Hajj Aayah 19: هَـٰذَانِ خَصْمَانِ اخْتَصَمُوا فِي رَبِّهِمْ [197]
[7] Aayah Zinazohusiana Na Manaasik Za Hajj:
Aayah hii hadi namba (37) zinataja kuhusu Manaasik za Hajj. Rejea pia Al-Baqarah (2:125), (2:196-203).
[8] Kumdhukuru Allaah Siku Maalumu:
Ni siku kumi bora kabisa za Allaah ambazo ni tarehe 1 hadi 10 Dhul-Hijjah kama alivyosema Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما). Ama siku za kuhesabika, rejea Al-Baqarah (2:203).
[9] Kutembea Katika Ardhi Kupata Mafunzo Na Mazingatio:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anawataka watu watembee katika ardhi wapate mafunzo na mazingatio, na wapate kutambua hatima ya waliokadhibisha. Rejea Yuwsuf (12:109), Faatwir (35:43-44), Al-An’aam (6:11), Al-Kahf (18:55), na Aal-‘Imraan (3:137).
[10] Maana Ya Kupofuka Moyo:
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
فَإِنَّهَا لَا تَعْمَى الْأَبْصَارُ وَلَـٰكِن تَعْمَى الْقُلُوبُ الَّتِي فِي الصُّدُورِ ﴿٤٦﴾
“Kwani hakika hayapofuki macho, lakini zinazopofuka ni nyoyo zilizomo vifuani.”
Maneno haya yametumiwa kwa njia ya sitiari na si kwa maana halisi kuwa moyo upofoke. Kwa kuwa moyo unachukuliwa kuwa ni kitovu cha imaan na taqwa. Rejea Al-Baqarah (2:2) kupata maana ya taqwa. Rejea pia Al-Maaidah (5:41) kuhusu moyo kutokuwa na imaan. Na nyoyoni ndimo ambamo kuna hisia za kiakili na kimaadili. Basi maneno haya yametumiwa kuashiria kwamba ukaidi wao umewazuia kuhisi na kutenda kwa busara, kwani japokuwa wana nyoyo, lakini hawafahamu Rejea Al-A’raaf (7:179). Wala nyoyo hizo haziwezi kuzingatia Qur-aan kwani kama zimefungiwa kufuli. Rejea Muhammad (47:24). Na rejea Aal-‘Imraan (3:7) kulikotajwa watu wenye upotofu katika nyoyo zao kwa kufuata fitnah na mambo yenye shaka, na matamanio na kuacha yaliyo haqq.
Na katika Qur-aan, kumetajwa maradhi ya nyoyoni ambayo ni kufru, shirki, unafiki, shaka, matamanio, ukaidi wa kukubali haqq, maasi na kila aina ya maovu. Rejea Suwrah Muhammad (47:20) kwenye uchambuzi na maelezo bayana na rejea mbalimbali za kuhusu nyoyo zenye maradhi.
Kinyume chake ni nyoyo zenye imaan, taqwa, khofu, unyenyekevu na yote yenye hisia nzuri na maadili mema. Rejea Suwrah hii Al-Hajj Aayah (54), Al-Anfaal (8:2-4). Rejea pia Ar-Ra’d (13:28) Anaposema Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa kwa Dhikru-Allaah nyoyo hutulia! Na Aayah nyingine nyingi mno ambazo zimetaja nyoyo njema zilizosalimika ambazo Siku ya Qiyaamah ndizo zitakazowafaa watu. Rejea Asw-Swaffaat (37:84). Rejea pia Ash-Shu’araa (26:88-89) kwenye ufafanuzi na maelezo kuhusu moyo uliosalimika.
[11] Ada Ya Washirikina Na Makafiri Kuhimiza Adhabu Au Qiyaamah.
Hawa wakanushaji (washirikina na makafiri) wanakuhimiza adhabu kwa sababu ya ujinga wao, na dhulma yao, na ukaidi wao, na kudhania kwao kuwa Allaah Hatoweza, na kuwakanusha kwao Rusuli Wake. Lakini Allaah Haendi kinyume na Ahadi Yake, na yale Aliyoyaahidi lazima yatokee na hakuna atakayeweza kuzuia. Ama kuhimiza kwake, sio juu yako ee Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) wala kusikushughulishe kuhimiza kwao wala kudhania kwao kwamba Tutashindwa, kwani mbele yao kuna Siku ya Qiyaamah ambayo watajumuika wa mwanzo wao na wa mwisho wao, na watalipwa kwa amali zao, na adhabu ya kudumu iumizayo itawapata tu, ndio maana Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
وَإِنَّ يَوْمًا عِندَ رَبِّكَ كَأَلْفِ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ ﴿٤٧﴾
“Siku moja kwa Rabb wako ni kama miaka elfu katika ile mnayoihesabu.” Kutokana na urefu wake na hali ngumu na shida zake. Basi ni sawasawa tu ikiwafika adhabu duniani au wakiakhirishiwa adhabu, kwani Siku hiyo ni lazima tu waidiriki. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Rejea pia Swaad (38:16), Al-Anfaal (8:32-33)
Na wakiulizia lini Qiyaamah kitatokea: Rejea Al-Mulk (67:25), Al-A’araaf (7:187), Al-Ahzaab (33:63), An-Naazi’aat (79:42), na Ash-Shuwraa (42:18).
[12] Maradhi Ya Nyoyo: Rejea Aayah namba (46) ya Suwrah hii.
[14] Mifano Ya Hikmah Anayopiga Allaah (سبحانه وتعالى): Rejea Al-A’raaf (7:40).
[15] Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Atakuwa Shahidi Kwa Ummah Wake Wa Kiislamu Na Ummah Wa Kiislamu Watakuwa Mashahidi Kwa Rusuli Waliotangulia Kwamba Wamebalighisha Ujumbe.
Rejea Al-Baqara (2:143), An-Nisaa (4:41), Al-Hajj (22:78), Az-Zumar (39:69-70) na Al-Jaathiyah (45:28).
الْمُؤمِنُون
023-Al-Muuminuwn
023-Al-Muuminuwn: Utangulizi Wa Suwrah [199]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١﴾
1. Kwa yakini wamefaulu Waumini.[1]
الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ ﴿٢﴾
2. Ambao katika Swalaah zao huwa wananyenyekea.
وَالَّذِينَ هُمْ عَنِ اللَّغْوِ مُعْرِضُونَ ﴿٣﴾
3. Na ambao wanajiepusha na mambo ya upuuzi.
وَالَّذِينَ هُمْ لِلزَّكَاةِ فَاعِلُونَ ﴿٤﴾
4. Na ambao wanatoa Zakaah.
وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ ﴿٥﴾
5. Na ambao wanazihifadhi tupu zao.
إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ ﴿٦﴾
6. Isipokuwa kwa wake zao, au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kuume basi hao hawalaumiwi.
فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ ﴿٧﴾
7. Lakini atakayetaka kinyume ya hayo, basi hao ndio wapindukao mipaka.
وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ ﴿٨﴾
8. Na ambao amana zao na ahadi zao wanazichunga.[2]
وَالَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَوَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ ﴿٩﴾
9. Na ambao wanazihifadhi Swalaah zao.
أُولَـٰئِكَ هُمُ الْوَارِثُونَ ﴿١٠﴾
10. Hao ndio warithi.
الَّذِينَ يَرِثُونَ الْفِرْدَوْسَ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿١١﴾
11. Ambao watarithi (Jannah ya) Al-Firdaws,[3] wao humo ni wenye kudumu.
وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن سُلَالَةٍ مِّن طِينٍ ﴿١٢﴾
12. Kwa yakini Tumemuumba binaadam kutokana na mchujo safi wa udongo.[4]
ثُمَّ جَعَلْنَاهُ نُطْفَةً فِي قَرَارٍ مَّكِينٍ ﴿١٣﴾
13. Kisha Tukamfanya kuwa tone la manii katika kalio makini.
ثُمَّ خَلَقْنَا النُّطْفَةَ عَلَقَةً فَخَلَقْنَا الْعَلَقَةَ مُضْغَةً فَخَلَقْنَا الْمُضْغَةَ عِظَامًا فَكَسَوْنَا الْعِظَامَ لَحْمًا ثُمَّ أَنشَأْنَاهُ خَلْقًا آخَرَ ۚ فَتَبَارَكَ اللَّـهُ أَحْسَنُ الْخَالِقِينَ ﴿١٤﴾
14. Kisha Tukaumba tone la manii kuwa pande la damu linaloning’inia, Tukaumba pande la damu hilo linaloning’inia kuwa kinofu cha nyama, Tukaumba kinofu hicho cha nyama kuwa mifupa, Tukavisha mifupa hiyo nyama, kisha Tukamuanzisha kiumbe kingine. Basi Amebarikika Allaah Mbora wa wenye kuumba.[5]
ثُمَّ إِنَّكُم بَعْدَ ذَٰلِكَ لَمَيِّتُونَ ﴿١٥﴾
15. Kisha hakika nyinyi baada ya hayo, ni wenye kufa.
ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ تُبْعَثُونَ ﴿١٦﴾
16. Kisha hakika nyinyi Siku ya Qiyaamah mtafufuliwa.
وَلَقَدْ خَلَقْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعَ طَرَائِقَ وَمَا كُنَّا عَنِ الْخَلْقِ غَافِلِينَ ﴿١٧﴾
17. Kwa yakini Tumeumba juu yenu tabaka za mbingu saba, na Hatukuwa Wenye Kughafilika kuhusu uumbaji.[6]
وَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً بِقَدَرٍ فَأَسْكَنَّاهُ فِي الْأَرْضِ ۖ وَإِنَّا عَلَىٰ ذَهَابٍ بِهِ لَقَادِرُونَ ﴿١٨﴾
18. Na Tukateremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi, na Tukayawekea maskani ardhini. Nasi kwa kuyaondosha bila shaka Ni Wenye uwezo.
فَأَنشَأْنَا لَكُم بِهِ جَنَّاتٍ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَابٍ لَّكُمْ فِيهَا فَوَاكِهُ كَثِيرَةٌ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ ﴿١٩﴾
19. Kisha Tukakuanzishieni kwa maji hayo mabustani ya mitende na mizabibu, mnapata humo matunda mengi, na katika hayo mnakula.
وَشَجَرَةً تَخْرُجُ مِن طُورِ سَيْنَاءَ تَنبُتُ بِالدُّهْنِ وَصِبْغٍ لِّلْآكِلِينَ ﴿٢٠﴾
20. Na mti (wa zaituni pia) unaotoka katika Mlima wa Sinai, unaozalisha mafuta na kuwa kitoweo cha ladha kwa walaji.
وَإِنَّ لَكُمْ فِي الْأَنْعَامِ لَعِبْرَةً ۖ نُّسْقِيكُم مِّمَّا فِي بُطُونِهَا وَلَكُمْ فِيهَا مَنَافِعُ كَثِيرَةٌ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ ﴿٢١﴾
21. Na hakika katika wanyama wa mifugo mnapata zingatio. Tunakunywisheni kile kitokacho matumboni mwao (maziwa), na mnapata humo manufaa mengi, na kati yao mnawala.
وَعَلَيْهَا وَعَلَى الْفُلْكِ تُحْمَلُونَ ﴿٢٢﴾
22. Na juu yao (hao wanyama), na juu ya merikebu mnabebwa.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَقَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٢٣﴾
23. Kwa yakini Tulimpeleka Nuwh kwa kaumu yake, akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Je, basi hamtokuwa na taqwa?
فَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ مَا هَـٰذَا إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُرِيدُ أَن يَتَفَضَّلَ عَلَيْكُمْ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَأَنزَلَ مَلَائِكَةً مَّا سَمِعْنَا بِهَـٰذَا فِي آبَائِنَا الْأَوَّلِينَ ﴿٢٤﴾
24. Wakasema wakuu waliokufuru miongoni mwa kaumu yake: Huyu si chochote ila ni binaadam kama nyinyi, anataka ajifadhilishe juu yenu. Na lau Allaah Angelitaka (kutuma Rasuli), bila shaka Angeliteremsha Malaika. Hatukusikia haya kwa baba zetu wa awali.
إِنْ هُوَ إِلَّا رَجُلٌ بِهِ جِنَّةٌ فَتَرَبَّصُوا بِهِ حَتَّىٰ حِينٍ ﴿٢٥﴾
25. Yeye si lolote ila ni mtu ana wazimu, basi mngojeeni na mwangalieni tu kwa muda.
قَالَ رَبِّ انصُرْنِي بِمَا كَذَّبُونِ ﴿٢٦﴾
26. (Nuwh) akasema: Rabb wangu! Ninusuru kwa kuwa wamenikadhibisha.
فَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِ أَنِ اصْنَعِ الْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا فَإِذَا جَاءَ أَمْرُنَا وَفَارَ التَّنُّورُ ۙ فَاسْلُكْ فِيهَا مِن كُلٍّ زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ وَأَهْلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيْهِ الْقَوْلُ مِنْهُمْ ۖ وَلَا تُخَاطِبْنِي فِي الَّذِينَ ظَلَمُوا ۖ إِنَّهُم مُّغْرَقُونَ ﴿٢٧﴾
27. Basi Tukamfunulia Wahy kwamba: Unda jahazi mbele ya Macho Yetu[7] na Wahy Wetu. Itakapokuja Amri Yetu, na tanuri likafoka, basi waingize humo kila namna dume na jike na ahli zako isipokuwa yule miongoni mwao iliyekwishamtangulia kauli, na wala usinisemeshe kuhusu hao waliodhulumu, hakika wao ni wenye kugharikishwa.[8]
فَإِذَا اسْتَوَيْتَ أَنتَ وَمَن مَّعَكَ عَلَى الْفُلْكِ فَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي نَجَّانَا مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٢٨﴾
28. Basi utakapopanda na kutulia wewe na wale walio pamoja nawe jahazini, sema: AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah) Ambaye Ametuokoa kutokana na watu madhalimu.
وَقُل رَّبِّ أَنزِلْنِي مُنزَلًا مُّبَارَكًا وَأَنتَ خَيْرُ الْمُنزِلِينَ ﴿٢٩﴾
29. Na sema: Rabb wangu! Niteremshe mteremko wa baraka, Nawe ni Mbora wa wenye kuteremsha.
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ وَإِن كُنَّا لَمُبْتَلِينَ ﴿٣٠﴾
30. Hakika katika hayo bila shaka kuna Aayaat (Ishara, Dalili, Mawaidha, Mazingatio) na hakika Tumekuwa Wenye Kuwafanyia mitihani.
ثُمَّ أَنشَأْنَا مِن بَعْدِهِمْ قَرْنًا آخَرِينَ ﴿٣١﴾
31. Kisha Tukaanzisha baada yao karne nyingine.
فَأَرْسَلْنَا فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْهُمْ أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٣٢﴾
32. Tukawapelekea Rasuli miongoni mwao (awalinganie) kwamba: Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Je, basi hamtokuwa na taqwa?
وَقَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِهِ الَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِلِقَاءِ الْآخِرَةِ وَأَتْرَفْنَاهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا مَا هَـٰذَا إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يَأْكُلُ مِمَّا تَأْكُلُونَ مِنْهُ وَيَشْرَبُ مِمَّا تَشْرَبُونَ ﴿٣٣﴾
33. Na wakasema wakuu miongoni mwa kaumu yake waliokufuru na wakakadhibisha mkutano wa Aakhirah, na Tukawaneemesha na kuwastarehesha katika uhai wa dunia: Huyu si lolote ila ni binaadam kama nyinyi, anakula vile vile mlavyo nyinyi, na anakunywa vile vile mnywavyo.[9]
وَلَئِنْ أَطَعْتُم بَشَرًا مِّثْلَكُمْ إِنَّكُمْ إِذًا لَّخَاسِرُونَ ﴿٣٤﴾
34. Na mkimtii binaadam kama nyinyi, basi hapo hakika nyinyi mtakuwa wenye kukhasirika.
أَيَعِدُكُمْ أَنَّكُمْ إِذَا مِتُّمْ وَكُنتُمْ تُرَابًا وَعِظَامًا أَنَّكُم مُّخْرَجُونَ ﴿٣٥﴾
35. Je, anakuahidini kwamba nyinyi mtakapokufa, mkawa mchanga na mifupa kuwa ati mtatolewa (kuwa hai)?[10]
هَيْهَاتَ هَيْهَاتَ لِمَا تُوعَدُونَ ﴿٣٦﴾
36. Mbali kabisa, hayawezekani kabisa! Hayo mnayoahidiwa.
إِنْ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ ﴿٣٧﴾
37. Hakuna lolote isipokuwa tu uhai wetu wa duniani, tunakufa na tunaishi, na wala sisi hatutofufuliwa.
إِنْ هُوَ إِلَّا رَجُلٌ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا وَمَا نَحْنُ لَهُ بِمُؤْمِنِينَ ﴿٣٨﴾
38. Yeye si lolote isipokuwa mtu aliyemtungia Allaah uongo, nasi hatutomwamini.
قَالَ رَبِّ انصُرْنِي بِمَا كَذَّبُونِ ﴿٣٩﴾
39. (Rasuli huyo) akasema: Rabb wangu! Ninusuru kwa sababu wamenikadhibisha.
قَالَ عَمَّا قَلِيلٍ لَّيُصْبِحُنَّ نَادِمِينَ ﴿٤٠﴾
40. (Allaah) Akasema: Muda mchache tu, bila shaka watapambazukiwa wawe wenye kujuta.
فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ بِالْحَقِّ فَجَعَلْنَاهُمْ غُثَاءً ۚ فَبُعْدًا لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٤١﴾
41. Basi ukawachukua ukelele angamizi kwa haki, Tukawafanya kama takataka za majani zinazoelea juu ya maji. Basi wametokomelea mbali watu madhalimu.
ثُمَّ أَنشَأْنَا مِن بَعْدِهِمْ قُرُونًا آخَرِينَ ﴿٤٢﴾
42. Kisha Tukaanzisha baada yao karne nyingi nyinginezo.
مَا تَسْبِقُ مِنْ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسْتَأْخِرُونَ ﴿٤٣﴾
43. Hapana ummah uwezao kutanguliza ajali yake, na wala hawawezi kuakhirisha.
ثُمَّ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا تَتْرَىٰ ۖ كُلَّ مَا جَاءَ أُمَّةً رَّسُولُهَا كَذَّبُوهُ ۚ فَأَتْبَعْنَا بَعْضَهُم بَعْضًا وَجَعَلْنَاهُمْ أَحَادِيثَ ۚ فَبُعْدًا لِّقَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ ﴿٤٤﴾
44. Kisha Tukatuma Rusuli Wetu waliofuatana mfululizo. Kila ummah alipowajia Rasuli wao, walimkadhibisha. Basi Tukawafuatanisha baadhi yao kwa wao (kwa maangamizi). Na Tukawafanya ni hadithi za kusimuliwa. Basi wametokomelea mbali watu wasioamini.
ثُمَّ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ وَأَخَاهُ هَارُونَ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُّبِينٍ ﴿٤٥﴾
45. Kisha Tukamtuma Muwsaa na kaka yake Haaruwn kwa Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu na mamlaka bayana.
إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا عَالِينَ ﴿٤٦﴾
46. Kwa Firawni, na wakuu wake, lakini walitakabari, na wakawa watu waliojiona.
فَقَالُوا أَنُؤْمِنُ لِبَشَرَيْنِ مِثْلِنَا وَقَوْمُهُمَا لَنَا عَابِدُونَ ﴿٤٧﴾
47. Wakasema: Itawezekanaje tuwaamini binaadam wawili kama sisi, na hali watu wao kwetu ni watumwa?
فَكَذَّبُوهُمَا فَكَانُوا مِنَ الْمُهْلَكِينَ ﴿٤٨﴾
48. Wakawakadhibisha. Basi wakawa miongoni mwa walioangamizwa.
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ لَعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ ﴿٤٩﴾
49. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu (Tawraat) ili waongoke.
وَجَعَلْنَا ابْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُ آيَةً وَآوَيْنَاهُمَا إِلَىٰ رَبْوَةٍ ذَاتِ قَرَارٍ وَمَعِينٍ ﴿٥٠﴾
50. Na Tukamjaalia mwana wa Maryam na mama yake kuwa ni Aayah (Ishara za Muujiza, Hoja, Dalili kubwa ya wazi), na Tukawapa kimbilio katika sehemu iliyoinuka na penye utulivu na chemchemu.
يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا ۖ إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ ﴿٥١﴾
51. Enyi Rusuli! Kuleni katika vizuri na tendeni mema, hakika Mimi kwa yale myatendayo Ni Mjuzi.[11]
وَإِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاتَّقُونِ ﴿٥٢﴾
52. Na kwamba hakika huu ummah wenu, ni ummah mmoja, Nami Ni Rabb wenu, basi Nicheni.
فَتَقَطَّعُوا أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ زُبُرًا ۖ كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ ﴿٥٣﴾
53. Wakafarikiana makundi makundi baina yao kuhusu Dini yao, kila kundi kwa waliyo nayo linafurahia.
فَذَرْهُمْ فِي غَمْرَتِهِمْ حَتَّىٰ حِينٍ ﴿٥٤﴾
54. Basi waachilie mbali katika mkanganyiko wao kwa muda.
أَيَحْسَبُونَ أَنَّمَا نُمِدُّهُم بِهِ مِن مَّالٍ وَبَنِينَ ﴿٥٥﴾
55. Je, wanadhani kwamba kwa vile Tunavyowakunjulia kwa mali na watoto.
نُسَارِعُ لَهُمْ فِي الْخَيْرَاتِ ۚ بَل لَّا يَشْعُرُونَ ﴿٥٦﴾
56. (Ndio kuwa) Tunawaharakishia katika kheri (Zetu)? Bali hawahisi.
إِنَّ الَّذِينَ هُم مِّنْ خَشْيَةِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ ﴿٥٧﴾
57. Hakika wale ambao pamoja na kumwogopa Rabbi wao, bado ni wenye kuchelea (Adhabu Yake).
وَالَّذِينَ هُم بِآيَاتِ رَبِّهِمْ يُؤْمِنُونَ ﴿٥٨﴾
58. Na wale ambao Aayaat (na Ishara za kiulimwengu) za Rabb wao wanaziamini.
وَالَّذِينَ هُم بِرَبِّهِمْ لَا يُشْرِكُونَ ﴿٥٩﴾
59. Na wale ambao Rabb wao hawamshirikishi.
وَالَّذِينَ يُؤْتُونَ مَا آتَوا وَّقُلُوبُهُمْ وَجِلَةٌ أَنَّهُمْ إِلَىٰ رَبِّهِمْ رَاجِعُونَ ﴿٦٠﴾
60. Na ambao wanatoa vile wavitoavyo na huku nyoyo zao zinakhofu kwamba hakika watarejea kwa Rabb wao.[12]
أُولَـٰئِكَ يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَهُمْ لَهَا سَابِقُونَ ﴿٦١﴾
61. Hao wanakimbilia katika mambo ya kheri, na wao ndio wenye kuyatanguliza.
وَلَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۖ وَلَدَيْنَا كِتَابٌ يَنطِقُ بِالْحَقِّ ۚ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٦٢﴾
62. Na wala Hatuikalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake. Na Kwetu kuna Kitabu kisemacho haki, nao hawatodhulumiwa.
بَلْ قُلُوبُهُمْ فِي غَمْرَةٍ مِّنْ هَـٰذَا وَلَهُمْ أَعْمَالٌ مِّن دُونِ ذَٰلِكَ هُمْ لَهَا عَامِلُونَ ﴿٦٣﴾
63. Bali nyoyo zao zimo katika mkanganyiko kutokana na haya. Na wanazo amali (ovu) pasi na hizo, wao wanazitenda.
حَتَّىٰ إِذَا أَخَذْنَا مُتْرَفِيهِم بِالْعَذَابِ إِذَا هُمْ يَجْأَرُونَ ﴿٦٤﴾
64. Mpaka Tutakapowachukua kwa adhabu wastareheshwa wao wa anasa za dunia, basi wao hapo watapiga mayowe.
لَا تَجْأَرُوا الْيَوْمَ ۖ إِنَّكُم مِّنَّا لَا تُنصَرُونَ ﴿٦٥﴾
65. Msipige mayowe leo. Hakika nyinyi Kwetu hamtonusuriwa.
قَدْ كَانَتْ آيَاتِي تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فَكُنتُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُمْ تَنكِصُونَ ﴿٦٦﴾
66. Kwa yakini zilikuwa Aayaat Zangu zikisomwa kwenu, lakini mlikuwa mnarudi nyuma juu ya visigino vyenu (kukanusha).
مُسْتَكْبِرِينَ بِهِ سَامِرًا تَهْجُرُونَ ﴿٦٧﴾
67. Mkitakabari kwayo, mkikaa usiku kuisimulia (Qur-aan) kwa kubwabwaja maovu ya batili.
أَفَلَمْ يَدَّبَّرُوا الْقَوْلَ أَمْ جَاءَهُم مَّا لَمْ يَأْتِ آبَاءَهُمُ الْأَوَّلِينَ ﴿٦٨﴾
68. Je, hawakuzingatia kauli (ya Allaah; Qur-aan) au yamewajia yasiyowafikia baba zao wa awali?
أَمْ لَمْ يَعْرِفُوا رَسُولَهُمْ فَهُمْ لَهُ مُنكِرُونَ ﴿٦٩﴾
69. Au hawajamtambua Rasuli wao (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi wao ndio wanamkanusha?
أَمْ يَقُولُونَ بِهِ جِنَّةٌ ۚ بَلْ جَاءَهُم بِالْحَقِّ وَأَكْثَرُهُمْ لِلْحَقِّ كَارِهُونَ ﴿٧٠﴾
70. Au wanasema ana wazimu? Bali amewajia kwa haki, na wengi wao hiyo haki wanaichukia.
وَلَوِ اتَّبَعَ الْحَقُّ أَهْوَاءَهُمْ لَفَسَدَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ ۚ بَلْ أَتَيْنَاهُم بِذِكْرِهِمْ فَهُمْ عَن ذِكْرِهِم مُّعْرِضُونَ ﴿٧١﴾
71. Na lau kama haki ingelifuata hawaa zao, basi zingelifisidika mbingu na ardhi na waliokuwemo humo. Bali Tumewaletea ukumbusho wao lakini wao ni wenye kupuuza ukumbusho wao.
أَمْ تَسْأَلُهُمْ خَرْجًا فَخَرَاجُ رَبِّكَ خَيْرٌ ۖ وَهُوَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿٧٢﴾
72. Au unawaomba ujira? Basi ujira wa Rabb wako ni bora zaidi. Naye Ni Mbora wa wenye kuruzuku.
وَإِنَّكَ لَتَدْعُوهُمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٧٣﴾
73. Na bila shaka wewe (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unawaita kuelekea njia iliyonyooka.
وَإِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ عَنِ الصِّرَاطِ لَنَاكِبُونَ ﴿٧٤﴾
74. Na hakika wale wasioiamini Aakhirah wanajitenga na njia hiyo.
وَلَوْ رَحِمْنَاهُمْ وَكَشَفْنَا مَا بِهِم مِّن ضُرٍّ لَّلَجُّوا فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ ﴿٧٥﴾
75. Na lau kama Tungeliwarehemu, na Tukawaondoshea dhara waliyokuwa nayo, bila shaka wangeng’ang’ania ukaidi katika upindukaji mipaka wa kuasi kwao, wakitangatanga kwa upofu.
وَلَقَدْ أَخَذْنَاهُم بِالْعَذَابِ فَمَا اسْتَكَانُوا لِرَبِّهِمْ وَمَا يَتَضَرَّعُونَ ﴿٧٦﴾
76. Kwa yakini Tuliwachukua kwa adhabu, basi hawakunyenyekea kujisalimisha kwa Rabb wao, na wala hawakuomba duaa kwa udhalili na unyenyekevu.[13]
حَتَّىٰ إِذَا فَتَحْنَا عَلَيْهِم بَابًا ذَا عَذَابٍ شَدِيدٍ إِذَا هُمْ فِيهِ مُبْلِسُونَ ﴿٧٧﴾
77. Mpaka Tutakapowafungulia mlango wenye adhabu kali, tahamaki watakuwa humo ni wenye kukata tamaa.
وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ ۚ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ ﴿٧٨﴾
78. Naye (Allaah) Ndiye Ambaye Amekuumbieni kusikia na kuona na nyoyo. Ni kudogo mno kushukuru kwenu.
وَهُوَ الَّذِي ذَرَأَكُمْ فِي الْأَرْضِ وَإِلَيْهِ تُحْشَرُونَ ﴿٧٩﴾
79. Naye Ndiye Ambaye Amekutawanyeni katika ardhi, na Kwake mtakusanywa.
وَهُوَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ وَلَهُ اخْتِلَافُ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٨٠﴾
80. Naye Ndiye Ambaye Anahuisha na Kufisha, na ni Yake mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana. Je, basi hamtii akilini?
بَلْ قَالُوا مِثْلَ مَا قَالَ الْأَوَّلُونَ ﴿٨١﴾
81. Bali wamesema kama walivyosema watu wa awali.
قَالُوا أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ ﴿٨٢﴾
82. Wamesema: Je, tutakapokufa na tukawa mchanga na mifupa, je, hivi sisi tutafufuliwa? [14]
لَقَدْ وُعِدْنَا نَحْنُ وَآبَاؤُنَا هَـٰذَا مِن قَبْلُ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿٨٣﴾
83. Kwa yakini tumeahidiwa haya sisi na baba zetu kabla. Haya si chochote isipokuwa hekaya za watu wa kale.
قُل لِّمَنِ الْأَرْضُ وَمَن فِيهَا إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٨٤﴾
84. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ni ya nani ardhi na wale waliomo humo mkiwa mnajua?
سَيَقُولُونَ لِلَّـهِ ۚ قُلْ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ﴿٨٥﴾
85. Watasema: Ni ya Allaah Pekee. Sema: Je, basi hamkumbuki?
قُلْ مَن رَّبُّ السَّمَاوَاتِ السَّبْعِ وَرَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ ﴿٨٦﴾
86. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Nani Rabb wa mbingu saba, na Rabb wa ‘Arsh ‘Adhimu?
سَيَقُولُونَ لِلَّـهِ ۚ قُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٨٧﴾
87. Watasema: Ni ya Allaah Pekee Sema: Je, basi hamtokuwa na taqwa?
قُلْ مَن بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ يُجِيرُ وَلَا يُجَارُ عَلَيْهِ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٨٨﴾
88. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Nani katika mikono Yake uko ufalme wa kila kitu, Naye Ndiye Alindae, na wala hakilindwi chochote kinyume Naye, ikiwa mnajua?
سَيَقُولُونَ لِلَّـهِ ۚ قُلْ فَأَنَّىٰ تُسْحَرُونَ ﴿٨٩﴾
89. Watasema: Ni Allaah Pekee. Sema: Basi vipi mnazugwa?
بَلْ أَتَيْنَاهُم بِالْحَقِّ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿٩٠﴾
90. Bali Tumewajia na haki, na kwa hakika wao ni wenye kukadhibisha.
مَا اتَّخَذَ اللَّـهُ مِن وَلَدٍ وَمَا كَانَ مَعَهُ مِنْ إِلَـٰهٍ ۚ إِذًا لَّذَهَبَ كُلُّ إِلَـٰهٍ بِمَا خَلَقَ وَلَعَلَا بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿٩١﴾
91. Allaah Hakujifanyia mwana yeyote, na wala hakuna pamoja Naye mwabudiwa yeyote. Ingekuwa hivyo, basi kila mwabudiwa angelichukua vile alivyoviumba, na baadhi yao wangeliwashinda wengineo. Subhaana Allaah (Utakasifu ni wa Allaah) kutokana na ambayo wanayavumisha.[15]
عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٩٢﴾
92. Mjuzi wa ghaibu na dhahiri. Basi Ametukuka kwa ‘Uluwa kutokana na yale wanayomshirikisha.
قُل رَّبِّ إِمَّا تُرِيَنِّي مَا يُوعَدُونَ ﴿٩٣﴾
93. Sema: Rabb wangu! Ukinionyesha yale wanayoahidiwa (ya kuletewa adhabu).
رَبِّ فَلَا تَجْعَلْنِي فِي الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٩٤﴾
94. Rabb wangu! Basi Usinijaalie kuwemo ndani ya watu hao madhalimu.
وَإِنَّا عَلَىٰ أَن نُّرِيَكَ مَا نَعِدُهُمْ لَقَادِرُونَ ﴿٩٥﴾
95. Na hakika Sisi Kukuonyesha yale Tunayowaahidi (ya adhabu) Tunaweza bila shaka yoyote.
ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ السَّيِّئَةَ ۚ نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَصِفُونَ ﴿٩٦﴾
96. Zuia maovu kwa (kuwarudishia) yale ambayo ni mema zaidi. Sisi Tunajua zaidi yale wanayoyavumisha.
وَقُل رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ ﴿٩٧﴾
97. Na sema: Rabb wangu! Najikinga Kwako kutokana na udokezi wa mashaytwaan.[16]
وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحْضُرُونِ ﴿٩٨﴾
98. Na najikinga Kwako Rabb wasinihudhurie.
حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ رَبِّ ارْجِعُونِ ﴿٩٩﴾
99. Mpaka yatakapomfikia mmoja wao mauti, atasema: Rabb wangu! Nirejesheni (duniani).[17]
لَعَلِّي أَعْمَلُ صَالِحًا فِيمَا تَرَكْتُ ۚ كَلَّا ۚ إِنَّهَا كَلِمَةٌ هُوَ قَائِلُهَا ۖ وَمِن وَرَائِهِم بَرْزَخٌ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٠٠﴾
100. Ili nikatende mema katika yale niliyoyaacha. (Ataambiwa) Laa hasha! Hakika hilo ni neno alisemalo yeye tu. Na mbele yao kuna Barzakh[18] mpaka Siku watakayofufuliwa.
فَإِذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ فَلَا أَنسَابَ بَيْنَهُمْ يَوْمَئِذٍ وَلَا يَتَسَاءَلُونَ ﴿١٠١﴾
101. Na litakapopulizwa baragumu, basi hakutokuwa na unasaba baina yao Siku hiyo, na wala hawatoulizana.[19]
فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٠٢﴾
102. Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, hao ndio wenye kufaulu.[20]
وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ ﴿١٠٣﴾
103. Na yule ambaye mizani zake zitakuwa khafifu, basi hao ni wale ambao wamekhasirika nafsi zao. Watadumu ndani ya Jahannam.
تَلْفَحُ وُجُوهَهُمُ النَّارُ وَهُمْ فِيهَا كَالِحُونَ ﴿١٠٤﴾
104. Moto utababua nyuso zao. Nao humo watakuwa ni wenye midomo iliyosinyaa na kuvutika mbali na meno.
أَلَمْ تَكُنْ آيَاتِي تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فَكُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ ﴿١٠٥﴾
105. (Wataambiwa): Je, hazikuwa Aayaat Zangu zinasomwa kwenu na nyinyi mkawa mnazikadhibisha?
قَالُوا رَبَّنَا غَلَبَتْ عَلَيْنَا شِقْوَتُنَا وَكُنَّا قَوْمًا ضَالِّينَ ﴿١٠٦﴾
106. Watasema: Rabb wetu! Ulitughilibu ufedhuli wetu, na tulikuwa watu waliopotea.
رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْهَا فَإِنْ عُدْنَا فَإِنَّا ظَالِمُونَ ﴿١٠٧﴾
107. Rabb wetu! Tutoe humo (motoni), na tukirudia tena, basi hakika sisi ni madhalimu.
قَالَ اخْسَئُوا فِيهَا وَلَا تُكَلِّمُونِ ﴿١٠٨﴾
108. Wataambiwa: Hizikeni humo! Na wala msinisemeshe!
إِنَّهُ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْ عِبَادِي يَقُولُونَ رَبَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّاحِمِينَ ﴿١٠٩﴾
109. Hakika lilikuwa kundi miongoni mwa Waja Wangu, wakisema: Rabb wetu! Tumeamini, basi Tughufurie na Uturehemu, Nawe Ni Mbora wa wenye kurehemu.
فَاتَّخَذْتُمُوهُمْ سِخْرِيًّا حَتَّىٰ أَنسَوْكُمْ ذِكْرِي وَكُنتُم مِّنْهُمْ تَضْحَكُونَ ﴿١١٠﴾
110. Mkawafanyia dhihaka, hadi wakakusahaulisheni kunidhukuru na mlikuwa ni wenye kuwacheka.
إِنِّي جَزَيْتُهُمُ الْيَوْمَ بِمَا صَبَرُوا أَنَّهُمْ هُمُ الْفَائِزُونَ ﴿١١١﴾
111. Hakika Mimi Nimewalipa leo (Jannah) kwa vile walivyosubiri, hakika wao ndio wenye kufuzu.
قَالَ كَمْ لَبِثْتُمْ فِي الْأَرْضِ عَدَدَ سِنِينَ ﴿١١٢﴾
112. (Allaah) Atasema: Muda gani mlikaa katika ardhi kwa idadi ya miaka?
قَالُوا لَبِثْنَا يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ فَاسْأَلِ الْعَادِّينَ ﴿١١٣﴾
113. Watasema: Tumekaa siku au sehemu tu ya siku. Basi waulize wanaohesabu.
قَالَ إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا ۖ لَّوْ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١١٤﴾
114. (Allaah) Atasema: Hamkukaa (huko duniani) isipokuwa kidogo tu, lau mngelikuwa mnajua.
أَفَحَسِبْتُمْ أَنَّمَا خَلَقْنَاكُمْ عَبَثًا وَأَنَّكُمْ إِلَيْنَا لَا تُرْجَعُونَ ﴿١١٥﴾
115. Je, mlidhania kwamba Sisi Tulikuumbeni bila kusudio mcheze tu, na kwamba nyinyi Kwetu hamtorejeshwa?
فَتَعَالَى اللَّـهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ ﴿١١٦﴾
116. Basi Ametukuka Allaah kwa ‘Uluwa, Mfalme wa haki. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Rabb wa ‘Arsh Kariym.[21]
وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ ﴿١١٧﴾
117. Na yeyote yule anayeomba duaa (au kuabudu) pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine ambapo hana ushahidi wa hilo, basi hakika hesabu yake iko kwa Rabb wake. Hakika hawafaulu makafiri.
وَقُل رَّبِّ اغْفِرْ وَارْحَمْ وَأَنتَ خَيْرُ الرَّاحِمِينَ ﴿١١٨﴾
118. Na sema: Rabb wangu! Ghufuria na Rehemu, Nawe Ni Mbora wa wenye kurehemu.
[1] Sifa Za Watakaofaulu Na Kujaaliwa Kupata Jannatul-Firdaws:
Sifa za watakaofaulu na kujaaliwa kupata Jannatul- Firdaws zimetajwa katika Suwrah hii kuanzia Aayah namba (2) hadi namba (9). Na sifa hizo zimeanza kutaja khushuw’ (unyenyekevu) katika Swalaah na kumalizikia kwa kuhifadhi Swalaah. Hali kadhaalika, sifa kama hizi taqriban, zimetajwa katika Suwrah Al-Ma’aarij (70:23-34) ila katika Suwrah hiyo Swalaah imeanza kutajwa kwa kuidumisha na imemalizwa kutajwa kwa kuihifadhi kama ilivyotajwa katika Suwrah hii ya Al-Muuminuwn. Kisha katika Suwrah Al-Ma’aarij Allaah (سبحانه وتعالى) Anaahidi Jannah baada ya hapo Aayah namba (35). Basi hii inadhihirisha umuhimu wa kudumisha na kuhifadhi Swalaah na kuiswali kwa khushuw’. Rejea pia Al-Baqarah (2:3), na An-Nisaa (4:108).
[2] Amrisho La Kutimiza Ahadi:
Rejea An-Nahl (16:90-92, 94), Al-Ma’aarij (70:32), Al-Ahzaab (33:72).
[3] Jannah Ya Al-Firdaws:
Katika Qur-aan, aina kadhaa za Jannah (Pepo) zimetajwa. Miongoni mwazo ni الفردوس (Al-Firdaws) iliyotajwa katika Aayah hii ambayo ni ya juu kabisa, ambako Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), Swahaba Watukufu na waja wema Atakaowakhitari Allaah (عزّ وجلّ) watakuweko huko kutokana na imaan, taqwa zao na matendo yao.
Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amenasihi Muumini anapoomba Jannah, aombe Jannah ya Al-Firdaws kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنَا فُلَيْحٌ، عَنْ هِلاَلِ بْنِ عَلِيٍّ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَبِرَسُولِهِ وَأَقَامَ الصَّلاَةَ وَصَامَ رَمَضَانَ، كَانَ حَقًّا عَلَى اللَّهِ أَنْ يُدْخِلَهُ الْجَنَّةَ جَاهَدَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ، أَوْ جَلَسَ فِي أَرْضِهِ الَّتِي وُلِدَ فِيهَا ". فَقَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ أَفَلاَ نُبَشِّرُ النَّاسَ. قَالَ " إِنَّ فِي الْجَنَّةِ مِائَةَ دَرَجَةٍ أَعَدَّهَا اللَّهُ لِلْمُجَاهِدِينَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ، مَا بَيْنَ الدَّرَجَتَيْنِ كَمَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ، فَإِذَا سَأَلْتُمُ اللَّهَ فَاسْأَلُوهُ الْفِرْدَوْسَ، فَإِنَّهُ أَوْسَطُ الْجَنَّةِ وَأَعْلَى الْجَنَّةِ، أُرَاهُ فَوْقَهُ عَرْشُ الرَّحْمَنِ، وَمِنْهُ تَفَجَّرُ أَنْهَارُ الْجَنَّةِ ". قَالَ مُحَمَّدُ بْنُ فُلَيْحٍ عَنْ أَبِيهِ " وَفَوْقَهُ عَرْشُ الرَّحْمَنِ ".
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Yeyote anayemuamini Allaah na Rasuli Wake, akasimamisha Swalaah na akafunga Ramadhwaan, imekuwa haki juu ya Allaah kumuingiza Jannah (Peponi) ikiwa amepigana katika Njia ya Allaah au ameketi nchini mwake alimozaliwa.” Watu wakasema: Ee Rasuli wa Allaah! Je, tuwape bishara hii watu? Akasema (صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika katika Jannah kuna daraja mia moja, ambazo Allaah Amewaandalia Mujaahidina wanaopigana katika Njia ya Allaah, na masafa baina ya daraja mbili ni baina ya mbingu na ardhi. Hivyo, mnapomuomba Allaah, muombeni (Jannah ya) Al-Firdaws, kwani ndiyo iliyo nzuri zaidi (katikati) na ya juu Peponi.” Naona alisema: “Na juu yake (Al-Firdaws) kuna ‘Arsh ya Ar-Rahmaan na kwayo kunachepuza mito ya Jannah.” Na imepokewa kwa Muhammad bin Fulayh kutoka kwa babake kwamba, “Na juu yake kuna ‘Arsh ya Ar-Rahmaan.” [Al-Bukhaariy Kitabu cha Jihaad (56), Kitabu Cha Tawhiyd (97).
Sifa za baadhi ya watakaojaaliwa kuweko katika Jannatul-Firdaws zimetajwa katika Suwrah hii Al-Muuminuwn (23:1-11). Rejea pia Al-Kahf (18:107).
Rejea pia An-Najm (53:15) kwenye faida kuhusu aina za Jannah na makazi ya Aakhirah.
[4] Uumbaji Wa Mwanaadam:
Aayah hii hadi namba (16) zinataja daraja za kuumbwa binaadam hadi kufufuliwa. Rejea Al-Hajj (22:5), Ghaafir (40:67).
[5] Binaadam Ameumbwa Katika Umbo Bora Kabisa:
Allaah (سبحانه وتعالى) na Amebarikika, Anataja katika Aayah hii kuwa Amemuumba binaadam katika umbo bora na zuri kabisa:
ثُمَّ أَنشَأْنَاهُ خَلْقًا آخَرَ ۚ فَتَبَارَكَ اللَّـهُ أَحْسَنُ الْخَالِقِينَ ﴿١٤﴾
Kisha Tukamuanzisha kiumbe kingine. Basi Amebarikika Allaah Mbora wa wenye kuumba.
Rejea Aal-‘Imraan (3:6), Al-Infitwaar (82:7-8), At-Tiyn (95:4).
[6] Baadhi Ya Neema Za Allaah (سبحانه وتعالى) Kwa Wanaadam:
Kuanzia Aayah hii hadi namba (22), Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja baadhi ya Neema Zake. Na neema kama hizi na zaidi Anazitaja katika An-Nahl kwenye Aayah mbali mbali. Rejea An-Nahl (16:5-16), (65-69), (72), (80-81). Rejea pia Ibraahiym (14:34) kwenye maelezo bayana.
[7] Kuthibitisha Sifa Za Allaah (سبحانه وتعالى): Rejea Huwd (11:37).
[8] Nuwh (عليه السّلام) Na Kizazi Kilobakia:
Aayah hii hadi namba (31), zinathibitisha kuwa Nabiy Nuwh (عليه السّلام) na kizazi kilichopanda katika safina (jahazi), ndio kizazi kilichobakia na kuendelea kuzaliana karne kwa karne. Na ndio maana Nabiy Nuwh (عليه السّلام) akawa baba wa wanaadam baada ya Nabiy Aadam (عليه السّلام) na pia yeye ni Rasuli wa kwanza ardhini.
Rejea Asw-Swaaffaat (37:77) kwenye maelezo bayana na rejea zake mbalimbali.
Rejea Yuwnus (10:73), Huwd (11:40), Maryam (19:58), Nuwh (71:1), Al-Israa (17:3).
[9] Ada Ya Washirikina Kutaka Kutumiwa Rasuli Asiye Binaadam:
Washirikina wa kaumu za kale kama kaumu ya Nuwh (عليه السّلام) hawakumwamini Rasuli wao kwa kutoa sababu mojawapo ya kuwa wanakula na kunywa. Hivo walitaka kutumiwa asiyekuwa binaadam kama Malaika. Na hii ni sawa na ada ya washirikina wa zama za Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) . Rejea Al-Furqaan (25:7) na Al-Israa (17:90-95) ambako walidai mengineyo. Na kuna rejea humo nyenginezo.
[10] Makafiri Hawakuamini Kuwa Watafufuliwa:
Rejea Al-Israa (17:49) kwenye maelezo bayana na rejea mbali mbali.
[11] Kula Vizuri Na Vya Halali Ni Sababu Mojawapo Ya Kutaqabaliwa Duaa:
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Enyi watu, hakika Allaah ni Mzuri na Hapokei ila kilicho kizuri. Na Allaah Amewaamrisha Waumini yale yale Aliyowaamrisha Rusuli (Mitume) Akasema:
يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا ۖ إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ ﴿٥١﴾
“Enyi Rusuli! Kuleni katika vizuri na tendeni mema, hakika Mimi kwa yale myatendayo Ni Mjuzi.” [Al-Muuminuwn (23:51)]
Na Anasema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ
“Enyi walioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni.” [Al-Baqarah (2:172)].
Kisha akamtaja mtu aliyekuwa safarini, nywele zimemsimama timtim na mwili umejaa vumbi, anainua mikono yake mbinguni akiomba: Ee Rabb! Ee Rabb! Na hali chakula chake ni haramu, kinywaji chake ni haramu na mavazi yake ni haramu, na amelishwa vya haramu, basi vipi ataitikiwa duaa yake?!” [Muslim]
[12] Sifa Ya Waumini Wanapotenda Mema Huwa Baina Ya Khofu Na Matarajio:
Amesimulia ‘Abdur-Rahmaan bin Sa’iyd bin Wahab Al-Hamdaaniyy kwamba ‘Aaishah (رضي الله عنها) mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Aayah hii:
وَالَّذِينَ يُؤْتُونَ مَا آتَوا وَّقُلُوبُهُمْ وَجِلَةٌ
“Na ambao wanatoa vile wavitoavyo na huku nyoyo zao zinakhofu.”
‘Aaishah akasema: Je, hao ni wale wanaokunywa pombe na wanaoiba? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hapana ee bint wa Asw-Swiddiyq! Lakini hao ni wale wanaofunga (Swiyaam), na wanaswali, na wanatoa swadaqa, na huku (pamoja na hayo yote) wanakhofu wasitaqabaliwe.” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaendelea kusema kwa kutaja Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
أُولَـٰئِكَ يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَهُمْ لَهَا سَابِقُونَ ﴿٦١﴾
“Hao wanakimbilia katika mambo ya kheri, na wao ndio wenye kuyatanguliza.”
[14] Makafiri Hawaamini Kufufuliwa:
Rejea Al-Israa (17:49) kwenye maelezo bayana na rejea mbali mbali.
[15] Haiwezekani Kuweko Waabudiwa Na Waumbaji Zaidi Ya Mmoja:
Rejea pia Al-Anbiyaa (21:22).
Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) ameifafanua akisema
Uongo unaojulikana kutokana na Maelezo haya ya Allaah, na Maelezo ya Rusuli Wake, na unajulikana pia kwa akili sahihi (ya kawaida). Kwa sababu hiyo, ndio Allaah (سبحانه وتعالى) Akatanabahisha kwa dalili za kiakili juu ya kutowezekana kuwa na waabudiwa wawili, ndio Anasema:
إِذًا
“Ingekuwa hivyo”
Anakusudia: Kama kungekuwa na mwabudiwa mwingine kinyume na Allaah kama wanavyosema (makafiri),
لَّذَهَبَ كُلُّ إِلَـٰهٍ بِمَا خَلَقَ
“Basi kila mwabudiwa angelichukua vile alivyoviumba.”
Anakusudia: Angejitenga kila mmoja wa waabudiwa wawili kwa viumbe aliowaumba, na akawa nao hao tu, na angepupia kumzuia mwenzie na kumshinda kabisa:
وَلَعَلَا بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ
“Na baadhi yao wangeliwashinda wengineo.”
Atakaeshinda ndiye atakuwa mwabudiwa. Na si hivyo ikiwa kila mmoja anamzuia mwenzie tu, hapa haiwezekani ulimwengu kuwa hivyo, na wala haikubaliki kiakili mpangilio huu wa kushangaza. Chukua mazingatio ya hilo kwa jua na mwezi, nyota zinazotembea na zisizotembea. Hivyo vyote tangu vimeumbwa vipo katika nidhamu moja na mpangilio mmoja, hivyo vyote vimedhalilishwa (vinanyenyekea na kufuata) kwa Uwezo wa Allaah, uliopangiliwa kwa hikmah ikiwa ni mambo yenye maslahi kwa viumbe wote, na wala si maslahi ya mmoja kinyume na mwingine. Na hautaona mapungufu yeyote yale, na wala hakuna tofauti japo ndogo kwenye jambo lolote lile. Sasa je, inakubalika kiakili jambo kama hili kuwa la waabudiwa wawili ambao wote ni waumbaji?!
سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿٩١﴾
“Subhaana Allaah (Utakasifu ni wa Allaah) kutokana na ambayo wanayavumisha.”
Hakika uhalisia na muonekano mzuri na mpangilio wa ulimwengu na vilivyopo, vyote vinatufahamisha kuwa Mwendeshaji wa haya ni Mwabudiwa Mmoja tu, Mkamilifu wa Majina na Sifa. Viumbe wote wanamuhitajia Yeye, katika Rubuwbiyyah Yake (Uola, umiliki, uendeshaji wa ulimwengu, uumbaji, utoaji rizki, uhuishaji na ufishaji, nk), na katika Uluwhiyyah Yake (kutekelezwa ibaada kwa ajili Yake), kama ilivyo visinge kuwepo viumbe wala kudumu isipokuwa baada ya kuviumba Allaah, ndio kama hivyo, viumbe hawatokuwa na maisha mazuri na hali nzuri isipokuwa kwa kumwabudu Yeye, na kufanya utiifu kwa ajili ya Allaah Pekee. [Tafsiyr Imaam As-Sa’diy]
[16] Kinga Dhidi Ya Udokezi Wa Mashaytwaan Na Kufazaika Usingizini:
Hii ni miongoni mwa Adhkaar Za Asubuhi Na Jioni. Rejea Hiswnul-Muslim Duaa Namba (30). Na Hadiyth yake ni hii ifuatayo:
حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ حُجْرٍ، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيلُ بْنُ عَيَّاشٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِسْحَاقَ، عَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " إِذَا فَزِعَ أَحَدُكُمْ فِي النَّوْمِ فَلْيَقُلْ أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّةِ مِنْ غَضَبِهِ وَعِقَابِهِ وَشَرِّ عِبَادِهِ وَمِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ وَأَنْ يَحْضُرُونِ . فَإِنَّهَا لَنْ تَضُرَّهُ " . قَالَ وَكَانَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عَمْرٍو يُلَقِّنُهَا مَنْ بَلَغَ مِنْ وَلَدِهِ وَمَنْ لَمْ يَبْلُغْ مِنْهُمْ كَتَبَهَا فِي صَكٍّ ثُمَّ عَلَّقَهَا فِي عُنُقِهِ . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ غَرِيبٌ
Amesimulia ‘Amr Bin Shu’ayb kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake (رضي الله عنهم) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Pindi mmoja wenu akifazaika usingizini basi aseme:
أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّاتِ مِنْ غَضَبِهِ وَعِقَابِهِ وَشَرِّ عِبَادِهِ وَمِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ وَأَنْ يَحْضُرُونِ
Najikinga na maneno ya Allaah yaliotimia kutokana na ghadhabu Zake, na adhabu Yake, na shari ya waja Wake, na kutokana na vioja vya mashaytwaan na kunijia kwao, basi hawatomdhuru. [At-Tirmidhiy na pia Abu Daawuwd, Ahmad, ameisahihisha Al-Albaaniy - Swahiyh Abi Daawuwd (3893), Swahiyh At-Tirmidhiy (3/171), Adhkaar za kuondosha wasiwasi usingizini au kusikia uoga na mfadhaiko]
Rejea Alhidaaya.com Makala Kutoka Duaa Toka Kwenye Qur-aan Tukufu Na Sharh Yake Duaa Namba (23).
[17] Binaadam Hujuta Anapotolewa Roho Akiwa Ni Kafiri Au Muasi Au Asipotenda Mema:
Aayah hii na ifuatayo inataja jinsi mtu anavyojuta pindi akiwa ni kafiri, au ni muasi au asiyetenda mema alipokuwa hai duniani. Rejea Al-Munaafiquwn (63:10-11).
[18] Barzakh:
Maana yake katika lugha ni: kizuizi. Rejea Ar-Rahmaan (55:20).
Kiistilahi, ni kipindi ambacho kinatenganisha dunia na Aakhirah. Ni kipindi baina ya kifo cha mtu hadi atakapofufuliwa siku ya Qiyaamah, nayo ni maisha ya mtu kuanzia anapofariki akazikwa kwa kuingizwa kaburini akabakia humo hadi Siku ya Qiyaamah. Na maisha hayo humo ni kulingana na aina ya mtu. Akiwa ni Muumini, basi maisha yake yatakuwa ni ya raha. Ama akiwa ni kafiri au muasi, basi maisha yake yatakuwa ni adhabu kutokana na dalili kutoka kwenye Qur-aan. Rejea Ghaafir (40:45-46).
Na Barzakh ni katika mambo ya ghaibu ambayo Muumini anapaswa kuamini kama ilivyothibiti katika Qur-aan na Sunnah. Imaam Ibn Baaz (رحمه الله) ameelezea katika Fatwa ifuatayo alipoulizwa:
“Maisha ya mwanaadamu yamegawanyika katika sehemu tatu: Maisha ya dunia ambayo ndiyo tunayoishi, maisha ya Aakhirah ambayo yanajulikana, kati ya maisha ya dunia na Aakhirah ni maisha ya barzakh, basi ni yapi maisha ya barzakh? Je, mtu huwa kwa mwili wake na roho yake?”
Akajibu: “Maisha ya barzakh ni kulingana na maisha yake hapa duniani. Muumini hustareheshwa katika barzakh huku roho yake ikiwa iko Jannah, na mwili wake utapata baadhi ya starehe. Na kafiri roho yake itaonyeshwa moto, yeye atapata sehemu ya adhabu yake, na mwili wake utapata sehemu ya adhabu yake. Haya ndio maisha ya barzakh. Muumini atakuwa yuko katika furaha na raha. Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema kuwa roho za Waumini zinazunguka Peponi popote zinapotaka. Ama makafiri, hao ni kama Alivyoeleza Allaah kuhusu watu wa Firawni: (Rejea Ghaafir (40:45-46). Hivyo basi, roho za makafiri zinaadhibiwa na miili yao itapata sehemu ya adhabu zake mpaka Allaah Awafufue wote, kisha roho za Waumini zitabaki Peponi, na roho za makafiri zitaingia motoni - tunamuomba Allaah Atusalimishe nao - zidumu humo milele; hawa watadumu milele Peponi, na hawa watadumu milele Motoni. Tunamuomba Allaah Atusalimishe.” [Al-Mawqi' Ar-Rasmiy li-Samaahat Ash-Shaykh Al-Imaam Ibn Baaz]
Na Hadiyth nyenginezo zimethibiti:
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ مَرَّ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَلَى قَبْرَيْنِ فَقَالَ: ((أَمَا إِنَّهُمَا لَيُعَذَّبَانِ وَمَا يُعَذَّبَانِ فِي كَبِيرٍ أَمَّا أَحَدُهُمَا فَكَانَ يَمْشِي بِالنَّمِيمَةِ وَأَمَّا الآخَرُ فَكَانَ لاَ يَسْتَتِرُ مِنْ بَوْلِهِ)) متفق عليه
Amesimulia Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliyapitia makaburi mawili na akasema: “Hakika hawa wawili wanaadhibiwa, na wala hawaadhibiwi kwa sababu ya jambo kubwa (la kuwashinda kulitekeleza au kujiepusha nalo).” Kisha hapo hapo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ”Hapana! Bali ni kubwa (dhambi kubwa na adhabu zake)! Ama mmoja wao, huyu alikuwa akipita kufitinisha watu, na ama mwingine, huyu alikuwa hajikingi na mkojo wake [anapokojoa].” [Al-Bukhaariy na Muslim]
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيَّ (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِذَا وُضِعَتْ الْجِنَازَةُ وَاحْتَمَلَهَا النَّاسُ – أوِ الرِّجَالُ عَلَى أَعْنَاقِهِمْ، فَإِنْ كَانَتْ صَالِحَةً قَالَتْ: قَدِّمُونِي. وَإِنْ كَانَتْ غَيْرَ صَالِحَةٍ قَالَتْ: يَا وَيْلَهَا! أَيْنَ يَذْهَبُونَ بِهَا؟ يَسْمَعُ صَوْتَهَا كُلُّ شَيْءٍ إلاَّ الإِنْسَانَ وَلَوْ سَمِعَهُ صَعِقَ)) البخاري
Amesimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Linapowekwa jeneza na likabebwa na watu - au wanaume shingoni mwao -, basi ikiwa ni la mtu mwema husema: Niwahisheni [nitangulizeni]. Lakini ikiwa si la mtu mwema husema: Ole wake! Wanalipeleka wapi? Sauti yake inasikika na kila kitu isipokuwa binaadamu. Na lau angeisikia angelizimia.” [Al-Bukhaariy].
[19] Siku Ya Qiyaamah Hakuna Ndugu Wala Jamaa Atakayetaka Kumsaidia Ndugu Ya Jamaa Yake: Rejea ‘Abasa (80:33-42).
[20] Mizani Nzito Na Mizani Nyepesi Za Matendo Ya Wanaadam Siku Ya Qiyaamah:
Rejea Al-Qaari’ah (101:6) kwenye faida.
[21] ‘Arsh Kariym:
Maana yake ni ‘Arsh yenye mwonekano mzuri na umbo la kuvutia. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Tofauti Kati Ya ‘Arsh Ya Ar-Rahmaan Na ’Arsh Ya Wanaadamu: Rejea Al-Haaqqah (69:17).
النُّور
024-An-Nuwr
024-An-Nuwr: Utangulizi Wa Suwrah [202]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
سُورَةٌ أَنزَلْنَاهَا وَفَرَضْنَاهَا وَأَنزَلْنَا فِيهَا آيَاٍ بَيِّنَاتٍ لَّعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ ﴿١﴾
1. Suwrah Tumeiteremsha, na Tukaifaradhisha (hukmu zake), na Tukateremsha humo Aayaat bayana ili mpate kukumbuka.
الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا مِائَةَ جَلْدَةٍ ۖ وَلَا تَأْخُذْكُم بِهِمَا رَأْفَةٌ فِي دِينِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ وَلْيَشْهَدْ عَذَابَهُمَا طَائِفَةٌ مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢﴾
2. Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamme mpigeni kila mmoja katika wawili hao mijeledi mia. Na wala isiwashikeni huruma kwa ajili yao katika Hukmu ya Allaah mkiwa nyinyi mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Na washuhudie adhabu yao kundi la Waumini.
الزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ ۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ ﴿٣﴾
3. Mwanamme mzinifu hafungi nikaah isipokuwa na mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina, na mwanamke mzinifu haolewi isipokuwa na mwanamme mzinifu au mshirikina. Na imeharamishwa hivyo kwa Waumini.[1]
وَالَّذِينَ يَرْمُونَ الْمُحْصَنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَأْتُوا بِأَرْبَعَةِ شُهَدَاءَ فَاجْلِدُوهُمْ ثَمَانِينَ جَلْدَةً وَلَا تَقْبَلُوا لَهُمْ شَهَادَةً أَبَدًا ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿٤﴾
4. Na wale wanaowasingizia wanawake watwaharifu[2] kisha hawaleti mashahidi wanne, basi wapigeni mijeledi themanini. Na wala msipokee ushahidi wao abadani. Na hao ndio mafasiki.
إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٥﴾
5. Isipokuwa wale waliotubu baada ya hayo na wakanyoosha sawa matendo yao, basi hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَالَّذِينَ يَرْمُونَ أَزْوَاجَهُمْ وَلَمْ يَكُن لَّهُمْ شُهَدَاءُ إِلَّا أَنفُسُهُمْ فَشَهَادَةُ أَحَدِهِمْ أَرْبَعُ شَهَادَاتٍ بِاللَّـهِ ۙ إِنَّهُ لَمِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٦﴾
6. Na wale wanaowasingizia wake zao na hawana mashahidi isipokuwa nafsi zao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa ni kushuhudia mara nne kwa kiapo cha Allaah kwamba yeye ni miongoni mwa wakweli.[3]
وَالْخَامِسَةُ أَنَّ لَعْنَتَ اللَّـهِ عَلَيْهِ إِن كَانَ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٧﴾
7. Na (kiapo) cha tano kwamba Laana ya Allaah iwe juu yake, akiwa ni miongoni mwa waongo.
وَيَدْرَأُ عَنْهَا الْعَذَابَ أَن تَشْهَدَ أَرْبَعَ شَهَادَاتٍ بِاللَّـهِ ۙ إِنَّهُ لَمِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٨﴾
8. Na itamwondokea (mke) adhabu atakapotoa ushahidi mara nne kwa kiapo cha Allaah kwamba yeye (mumewe) ni miongoni mwa waongo.
وَالْخَامِسَةَ أَنَّ غَضَبَ اللَّـهِ عَلَيْهَا إِن كَانَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٩﴾
9. Na (kiapo) cha tano kwamba Ghadhabu ya Allaah iwe juu yake akiwa (mumewe) ni miongoni mwa wakweli.
وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ وَأَنَّ اللَّـهَ تَوَّابٌ حَكِيمٌ ﴿١٠﴾
10. Na lau kama si Fadhila ya Allaah juu yenu na Rehma Yake, na kwamba Allaah Ni Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Hikmah wa yote (basi Angeliwaadhibuni bila kukawia).
إِنَّ الَّذِينَ جَاءُوا بِالْإِفْكِ عُصْبَةٌ مِّنكُمْ ۚ لَا تَحْسَبُوهُ شَرًّا لَّكُم ۖ بَلْ هُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُم مَّا اكْتَسَبَ مِنَ الْإِثْمِ ۚ وَالَّذِي تَوَلَّىٰ كِبْرَهُ مِنْهُمْ لَهُ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١١﴾
11. Hakika wale walioleta singizio la kashfa (kumzulia Mama wa Waumini ‘Aaishah رضي الله عنها), ni kundi miongoni mwenu. Msilichukulie kuwa ni shari kwenu, bali ni kheri kwenu. Kila mtu katika wao atapata yale aliyochuma katika dhambi. Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao atapata adhabu kuu.[4]
لَّوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ ظَنَّ الْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بِأَنفُسِهِمْ خَيْرًا وَقَالُوا هَـٰذَا إِفْكٌ مُّبِينٌ ﴿١٢﴾
12. Kwa nini mlipoisikia (tetesi la kashfa), Waumini wanaume na Waumini wanawake wasiwadhanie wenzao kheri, na wakasema: Hii ni kashfa ya kusingizwa iliyo dhahiri?
لَّوْلَا جَاءُوا عَلَيْهِ بِأَرْبَعَةِ شُهَدَاءَ ۚ فَإِذْ لَمْ يَأْتُوا بِالشُّهَدَاءِ فَأُولَـٰئِكَ عِندَ اللَّـهِ هُمُ الْكَاذِبُونَ ﴿١٣﴾
13. Kwa nini hawakuleta mashahidi wanne? Na kwa vile hawakuleta mashahidi, basi hao mbele ya Allaah ndio waongo.
وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ لَمَسَّكُمْ فِي مَا أَفَضْتُمْ فِيهِ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١٤﴾
14. Na lau si Fadhila ya Allaah juu yenu na Rehma Yake duniani na Aakhirah, ingekuguseni adhabu kuu kwa yale mliyojishughulisha nayo kuyaropoka.
إِذْ تَلَقَّوْنَهُ بِأَلْسِنَتِكُمْ وَتَقُولُونَ بِأَفْوَاهِكُم مَّا لَيْسَ لَكُم بِهِ عِلْمٌ وَتَحْسَبُونَهُ هَيِّنًا وَهُوَ عِندَ اللَّـهِ عَظِيمٌ ﴿١٥﴾
15. Mlipolipokea (tetesi la kashfa) kwa ndimi zenu, na mkasema kwa midomo yenu, yale ambayo hamkuwa na ilimu nayo. Na mnalidhania ni jambo jepesi, ilhali hili mbele ya Allaah ni kubwa mno.
وَلَوْلَا إِذْ سَمِعْتُمُوهُ قُلْتُم مَّا يَكُونُ لَنَا أَن نَّتَكَلَّمَ بِهَـٰذَا سُبْحَانَكَ هَـٰذَا بُهْتَانٌ عَظِيمٌ ﴿١٦﴾
16. Na kwa nini mlipolisikia (tetesi la kashfa) msiseme: Haitupasi sisi tuzungumze haya; Subhaanak! (Utakasifu ni Wako). Huu ni usingiziaji wa dhulma mkubwa mno!
يَعِظُكُمُ اللَّـهُ أَن تَعُودُوا لِمِثْلِهِ أَبَدًا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٧﴾
17. Allaah Anakuwaidhini msirudie abadani mfano wa haya, mkiwa ni Waumini wa kweli.
وَيُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿١٨﴾
18. Na Allaah Anakubainishieni Aayaat (Hukumu za Sharia, Mawaidha). Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
إِنَّ الَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ الْفَاحِشَةُ فِي الَّذِينَ آمَنُوا لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿١٩﴾
19. Hakika wale wanaopenda uenee uchafu wa kashfa kwa wale walioamini, watapata adhabu iumizayo duniani na Aakhirah. Na Allaah Anajua nanyi hamjui.
وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ وَأَنَّ اللَّـهَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٠﴾
20. Na lau si Fadhila ya Allaah juu yenu na Rehma Yake, na kwamba Allaah Ni Mwenye huruma mno, Mwenye Kurehemu (basi Angeliwaadhibuni bila kukawia).
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ وَمَن يَتَّبِعْ خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ فَإِنَّهُ يَأْمُرُ بِالْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ ۚ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ مَا زَكَىٰ مِنكُم مِّنْ أَحَدٍ أَبَدًا وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يُزَكِّي مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٢١﴾
21. Enyi walioamini! Msifuate nyayo za shaytwaan. Na yeyote atakayefuata nyayo za shaytwaan, basi hakika yeye anaamrisha machafu na munkari.[5] Na lau si Fadhila ya Allaah juu yenu na Rehma Yake, basi asingelitakasika miongoni mwenu hata mmoja abadani, lakini Allaah Anamtakasa Amtakaye. Na Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
وَلَا يَأْتَلِ أُولُو الْفَضْلِ مِنكُمْ وَالسَّعَةِ أَن يُؤْتُوا أُولِي الْقُرْبَىٰ وَالْمَسَاكِينَ وَالْمُهَاجِرِينَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ وَلْيَعْفُوا وَلْيَصْفَحُوا ۗ أَلَا تُحِبُّونَ أَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٢﴾
22. Na wala wasiape wale wenye fadhila miongoni mwenu na wenye wasaa wa mali kuwa hawatowapa (swadaqah) jamaa wa karibu, na masikini, na Muhaajiriyn katika Njia ya Allaah. Na wasamehe na waachilie mbali. Je, hampendi Allaah Akughufurieni? Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[6]
إِنَّ الَّذِينَ يَرْمُونَ الْمُحْصَنَاتِ الْغَافِلَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ لُعِنُوا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿٢٣﴾
23. Hakika wale wanaowasingizia machafu wanawake watwaharifu, walio mbali na hayo, Waumini, wamelaaniwa duniani na Aakhirah na watapata adhabu kuu.[7]
يَوْمَ تَشْهَدُ عَلَيْهِمْ أَلْسِنَتُهُمْ وَأَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٢٤﴾
24. Siku zitakaposhuhudia dhidi yao ndimi zao, na mikono yao, na miguu yao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda.[8]
يَوْمَئِذٍ يُوَفِّيهِمُ اللَّـهُ دِينَهُمُ الْحَقَّ وَيَعْلَمُونَ أَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ الْمُبِينُ ﴿٢٥﴾
25. Siku hiyo Allaah Atawalipa kikamilifu malipo yao ya haki, na watajua kwamba Allaah Ndiye wa Haki, Mwenye Kubainisha.
الْخَبِيثَاتُ لِلْخَبِيثِينَ وَالْخَبِيثُونَ لِلْخَبِيثَاتِ ۖ وَالطَّيِّبَاتُ لِلطَّيِّبِينَ وَالطَّيِّبُونَ لِلطَّيِّبَاتِ ۚ أُولَـٰئِكَ مُبَرَّءُونَ مِمَّا يَقُولُونَ ۖ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ ﴿٢٦﴾
26. Kauli ovu inaendana na watu waovu, na watu waovu wanaendana na kauli ovu. Na kauli njema inaendana na watu wema, na watu wema wanaendana na kauli njema.[9] Hao wametakaswa na tuhuma za wanayoyasema, watapata Maghfirah na riziki karimu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتًا غَيْرَ بُيُوتِكُمْ حَتَّىٰ تَسْتَأْنِسُوا وَتُسَلِّمُوا عَلَىٰ أَهْلِهَا ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ ﴿٢٧﴾
27. Enyi walioamini! Msiingie nyumba zisizokuwa nyumba zenu mpaka muombe ruhusa na muwatolee Salaam (‘alaykum) wenyewe. Hivyo ni bora kwenu ili mpate kukumbuka.
فَإِن لَّمْ تَجِدُوا فِيهَا أَحَدًا فَلَا تَدْخُلُوهَا حَتَّىٰ يُؤْذَنَ لَكُمْ ۖ وَإِن قِيلَ لَكُمُ ارْجِعُوا فَارْجِعُوا ۖ هُوَ أَزْكَىٰ لَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ ﴿٢٨﴾
28. Na msipokuta humo yeyote, basi msiingie mpaka mruhusiwe. Na mkiambiwa: Rejeeni! Basi rejeeni. Huo ni utakaso zaidi kwenu. Na Allaah Ni Mjuzi wa myatendayo.
لَّيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَدْخُلُوا بُيُوتًا غَيْرَ مَسْكُونَةٍ فِيهَا مَتَاعٌ لَّكُمْ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا تَكْتُمُونَ ﴿٢٩﴾
29. Hakuna kosa kuingia majumba yasiyokaliwa ambako humo mna manufaa yenu. Na Allaah Anajua yale yote mnayoyadhihirisha na yale yote mnayoyaficha.
قُل لِّلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا مِنْ أَبْصَارِهِمْ وَيَحْفَظُوا فُرُوجَهُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَزْكَىٰ لَهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا يَصْنَعُونَ ﴿٣٠﴾
30. Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao na wahifadhi tupu zao. Hivyo ni utakaso zaidi kwao. Hakika Allaah Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri kwa yale wayatendayo.
وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَىٰ عَوْرَاتِ النِّسَاءِ ۖ وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ ۚ وَتُوبُوا إِلَى اللَّـهِ جَمِيعًا أَيُّهَ الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٣١﴾
31. Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao na wahifadhi tupu zao, na wala wasidhihirishe mapambo yao[10] isipokuwa yale yanayodhihirika. Na waangushe khimaar (shungi) zao mpaka vifuani mwao, na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume wao, au wana wao wa kiume, au wana wa kiume wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kiume wa kaka zao, au wana wa kiume wa dada zao, au wanawake wao (wa Kiislamu), au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume[11], au wafuasi wanaume wasio na matamanio ya jimai miongoni mwa wanaume au watoto ambao hawatambui kitu kuhusu sehemu za siri za wanawake. Na wala wasipige miguu yao yakajulikana yale wanayoyaficha katika mapambo yao (vikuku na kadhaalika). Na tubuni kwa Allaah nyote, enyi Waumini mpate kufaulu.
وَأَنكِحُوا الْأَيَامَىٰ مِنكُمْ وَالصَّالِحِينَ مِنْ عِبَادِكُمْ وَإِمَائِكُمْ ۚ إِن يَكُونُوا فُقَرَاءَ يُغْنِهِمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٣٢﴾
32. Na waozesheni wajane miongoni mwenu na walio Swalihina kati ya watumwa wenu wanaume na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Allaah Atawatajirisha katika Fadhila Zake. Na Allaah Ni Mwenye Wasaa, Mjuzi wa yote.
وَلْيَسْتَعْفِفِ الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ نِكَاحًا حَتَّىٰ يُغْنِيَهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۗ وَالَّذِينَ يَبْتَغُونَ الْكِتَابَ مِمَّا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ فَكَاتِبُوهُمْ إِنْ عَلِمْتُمْ فِيهِمْ خَيْرًا ۖوَآتُوهُم مِّن مَّالِ اللَّـهِ الَّذِي آتَاكُمْ ۚ وَلَا تُكْرِهُوا فَتَيَاتِكُمْ عَلَى الْبِغَاءِ إِنْ أَرَدْنَ تَحَصُّنًا لِّتَبْتَغُوا عَرَضَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَمَن يُكْرِههُّنَّ فَإِنَّ اللَّـهَ مِن بَعْدِ إِكْرَاهِهِنَّ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٣﴾
33. Na wajizuie (yaliyoharamishwa) wale ambao hawapati uwezo wa ndoa mpaka Allaah Awatajirishe kwa Fadhila Zake. Na wale wanaotaka kuandikiwa kuachiwa huru katika wale ambao imemiliki mikono yenu ya kuume, basi waandikieni kama mkijua wema kwao. Na wapeni katika Mali ya Allaah Aliyokupeni. Na wala msiwalazimishe vijakazi wenu kufanya ukahaba kama wakitaka kujisitiri, ili mtafute mafao ya uhai wa dunia. Na yeyote yule atakayewalazimisha, basi hakika Allaah, baada ya kulazimishwa kwao huko, ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[12]
وَلَقَدْ أَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ آيَاتٍ مُّبَيِّنَاتٍ وَمَثَلًا مِّنَ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِكُمْ وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٣٤﴾
34. Na kwa yakini Tumekuteremshieni Aayaat zinazobainisha wazi, na mifano kutoka kwa wale waliopita kabla yenu, na mawaidha kwa wenye taqwa.
اللَّـهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ مَثَلُ نُورِهِ كَمِشْكَاةٍ فِيهَا مِصْبَاحٌ ۖ الْمِصْبَاحُ فِي زُجَاجَةٍ ۖ الزُّجَاجَةُ كَأَنَّهَا كَوْكَبٌ دُرِّيٌّ يُوقَدُ مِن شَجَرَةٍ مُّبَارَكَةٍ زَيْتُونَةٍ لَّا شَرْقِيَّةٍ وَلَا غَرْبِيَّةٍ يَكَادُ زَيْتُهَا يُضِيءُ وَلَوْ لَمْ تَمْسَسْهُ نَارٌ ۚ نُّورٌ عَلَىٰ نُورٍ ۗ يَهْدِي اللَّـهُ لِنُورِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَيَضْرِبُ اللَّـهُ الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٣٥﴾
35. Allaah Ni Nuru ya mbingu na ardhi. Mfano wa Nuru Yake ni kama shubaka, ndani yake mna taa yenye mwanga mkali. Taa hiyo yenye mwanga mkali iko katika (tungi la) gilasi. Gilasi hiyo ni kama kwamba nyota inayong’aa na kumeremeta, inawashwa kutokana na mti wa baraka wa zaytuni, hauko Mashariki wala Magharibi. Yanakaribia mafuta yake kung’aa japokuwa moto haujayagusa, Nuru juu ya Nuru. Allaah Anamwongoza kwa Nuru Yake Amtakaye. Na Allaah Anapiga mifano kwa watu. Na Allaah kwa kila kitu Ni Mjuzi.[13]
فِي بُيُوتٍ أَذِنَ اللَّـهُ أَن تُرْفَعَ وَيُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ يُسَبِّحُ لَهُ فِيهَا بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ ﴿٣٦﴾
36. Katika nyumba ambazo Allaah Ameidhinisha litukuzwe na litajwe humo Jina Lake, wanamsabihi humo asubuhi na jioni.
رِجَالٌ لَّا تُلْهِيهِمْ تِجَارَةٌ وَلَا بَيْعٌ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ وَإِقَامِ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ ۙ يَخَافُونَ يَوْمًا تَتَقَلَّبُ فِيهِ الْقُلُوبُ وَالْأَبْصَارُ ﴿٣٧﴾
37. Wanaume ambao haiwashughulishi tijara wala uuzaji na kumdhukuru Allaah na kusimamisha Swalaah, na kutoa Zakaah wanakhofu Siku zitakapopinduka humo nyoyo na macho.
لِيَجْزِيَهُمُ اللَّـهُ أَحْسَنَ مَا عَمِلُوا وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ ۗ وَاللَّـهُ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٣٨﴾
38. Ili Allaah Awalipe mazuri zaidi kutokana na yale waliyoyatenda, na Awazidishie katika Fadhila Zake. Na Allaah Humruzuku Amtakaye bila ya hesabu.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَعْمَالُهُمْ كَسَرَابٍ بِقِيعَةٍ يَحْسَبُهُ الظَّمْآنُ مَاءً حَتَّىٰ إِذَا جَاءَهُ لَمْ يَجِدْهُ شَيْئًا وَوَجَدَ اللَّـهَ عِندَهُ فَوَفَّاهُ حِسَابَهُ ۗ وَاللَّـهُ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿٣٩﴾
39. Na wale waliokufuru, amali zao ni kama sarabi jangwani. Mwenye kiu hudhania kuwa ni maji. Hata anapoyafikia hayakuti kitu chochote, na anamkuta Allaah mbele Yake, Naye Amlipe kikamilifu hesabu yake. Na Allaah Ni Mwepesi wa Kuhesabu.[14]
أَوْ كَظُلُمَاتٍ فِي بَحْرٍ لُّجِّيٍّ يَغْشَاهُ مَوْجٌ مِّن فَوْقِهِ مَوْجٌ مِّن فَوْقِهِ سَحَابٌ ۚ ظُلُمَاتٌ بَعْضُهَا فَوْقَ بَعْضٍ إِذَا أَخْرَجَ يَدَهُ لَمْ يَكَدْ يَرَاهَا ۗ وَمَن لَّمْ يَجْعَلِ اللَّـهُ لَهُ نُورًا فَمَا لَهُ مِن نُّورٍ ﴿٤٠﴾
40. Au ni kama viza katika bahari ya kina kirefu, imefunikwa na mawimbi juu ya mawimbi, na juu yake kuna mawingu. (Tabaka za) Viza juu yake viza. Anapoutoa mkono wake, anakaribia asiuone. Na ambaye Allaah Hakumjaalia Nuru, basi hawi na Nuru.
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يُسَبِّحُ لَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَالطَّيْرُ صَافَّاتٍ ۖ كُلٌّ قَدْ عَلِمَ صَلَاتَهُ وَتَسْبِيحَهُ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِمَا يَفْعَلُونَ ﴿٤١﴾
41. Je, huoni kwamba wanamsabihi Allaah walioko mbinguni na ardhini[15], na (pia) ndege wakiwa wamekunjua mbawa zao. Kila mmoja (Allaah) Amekwishajua Swalaah yake na tasbihi yake. Na Allaah Ni Mjuzi kwa yale wayafanyao.
وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَإِلَى اللَّـهِ الْمَصِيرُ ﴿٤٢﴾
42. Na Ni wa Allaah Pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Na kwa Allaah Pekee ndio mahali pa kuishia.
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يُزْجِي سَحَابًا ثُمَّ يُؤَلِّفُ بَيْنَهُ ثُمَّ يَجْعَلُهُ رُكَامًا فَتَرَى الْوَدْقَ يَخْرُجُ مِنْ خِلَالِهِ وَيُنَزِّلُ مِنَ السَّمَاءِ مِن جِبَالٍ فِيهَا مِن بَرَدٍ فَيُصِيبُ بِهِ مَن يَشَاءُ وَيَصْرِفُهُ عَن مَّن يَشَاءُ ۖ يَكَادُ سَنَا بَرْقِهِ يَذْهَبُ بِالْأَبْصَارِ ﴿٤٣﴾
43. Je, huoni kwamba Allaah Anasukuma mawingu, kisha Anayaambatisha baina yake, kisha Anayafanya matabaka ya mirundi? Basi utaona matone ya mvua yanatoka katikati yake. Na Anateremsha kutoka mbinguni katika milima ya mawingu mvua ya mawe, Akamsibu nayo Amtakaye, na Akamuepushia Amtakaye. Hukaribia mwako wa umeme wake kupofua macho.
يُقَلِّبُ اللَّـهُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّأُولِي الْأَبْصَارِ ﴿٤٤﴾
44. Allaah Hubadilisha usiku na mchana. Hakika katika hayo kuna zingatio kwa wenye kuona kwa umaizi.
وَاللَّـهُ خَلَقَ كُلَّ دَابَّةٍ مِّن مَّاءٍ ۖ فَمِنْهُم مَّن يَمْشِي عَلَىٰ بَطْنِهِ وَمِنْهُم مَّن يَمْشِي عَلَىٰ رِجْلَيْنِ وَمِنْهُم مَّن يَمْشِي عَلَىٰ أَرْبَعٍ ۚ يَخْلُقُ اللَّـهُ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٤٥﴾
45. Na Allaah Ameumba kila kiumbe kinachotembea kutokana na maji. Basi miongoni mwao wako wanaotembea juu ya matumbo yao, na miongoni mwao wanaotembea kwa miguu miwili, na miongoni mwao wanaotembea juu ya minne. Allaah Anaumba Atakavyo. Hakika Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.[16]
لَّقَدْ أَنزَلْنَا آيَاتٍ مُّبَيِّنَاتٍ ۚ وَاللَّـهُ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٤٦﴾
46. Kwa yakini Tumeteremsha Aayaat bainifu, na Allaah Anamwongoza Amtakaye kuelekea Njia Iliyonyooka.
وَيَقُولُونَ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالرَّسُولِ وَأَطَعْنَا ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٌ مِّنْهُم مِّن بَعْدِ ذَٰلِكَ ۚ وَمَا أُولَـٰئِكَ بِالْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٧﴾
47. Na (wanafiki) wanasema: Tumemwamini Allaah na Rasuli, na Tumetii. Kisha hugeuka kundi miongoni mwao baada ya hayo. Na wala hao si wenye kuamini.
وَإِذَا دُعُوا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُم مُّعْرِضُونَ ﴿٤٨﴾
48. Na wanapoitwa kwa Allaah na Rasuli Wake ili Awahukumu baina yao, mara hapo kundi miongoni mwao wanakengeuka.
وَإِن يَكُن لَّهُمُ الْحَقُّ يَأْتُوا إِلَيْهِ مُذْعِنِينَ ﴿٤٩﴾
49. Na inapokuwa haki ni yao, wanamjia (Rasuli) wakitii.
أَفِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ أَمِ ارْتَابُوا أَمْ يَخَافُونَ أَن يَحِيفَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ وَرَسُولُهُ ۚ بَلْ أُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٥٠﴾
50. Je, mna maradhi katika nyoyo zao[17], au wametia shaka, au wanakhofu kwamba Allaah na Rasuli Wake watawadhulumu katika kuwahukumu? Bali hao ndio madhalimu.
إِنَّمَا كَانَ قَوْلَ الْمُؤْمِنِينَ إِذَا دُعُوا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ أَن يَقُولُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٥١﴾
51. Hakika kauli ya Waumini (wa kweli) wanapoitwa kwa Allaah na Rasuli Wake ili Awahukumu baina yao ni kusema: Tumesikia na Tumetii. Na hao ndio wenye kufaulu.
وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَخْشَ اللَّـهَ وَيَتَّقْهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَائِزُونَ ﴿٥٢﴾
52. Na yeyote yule atakayemtii Allaah na Rasuli Wake, na akamkhofu Allaah na akamcha, basi hao ndio wenye kufuzu.
وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ لَئِنْ أَمَرْتَهُمْ لَيَخْرُجُنَّ ۖ قُل لَّا تُقْسِمُوا ۖ طَاعَةٌ مَّعْرُوفَةٌ ۚ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿٥٣﴾
53. Na wakaapa kwa Allaah, viapo vyao thabiti vya nguvu, kwamba: Ukiwaamrisha, bila shaka watatoka. Sema: Msiape! Utiifu unajulikana. Hakika Allaah Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri kwa yale myatendayo.
قُلْ أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْهِ مَا حُمِّلَ وَعَلَيْكُم مَّا حُمِّلْتُمْ ۖ وَإِن تُطِيعُوهُ تَهْتَدُوا ۚ وَمَا عَلَى الرَّسُولِ إِلَّا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ ﴿٥٤﴾
54. Sema: Mtiini Allaah na mtiini Rasuli. Mkigeukilia mbali, basi hakika jukumu lake ni lile alilobebeshwa tu, nanyi ni juu yenu yale mliyobebeshwa. Na mkimtii mtaongoka, na hapana juu ya Rasuli isipokuwa ubalighisho bayana.
وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿٥٥﴾
55. Allaah Amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema kwamba bila shaka Atawafanya warithi katika ardhi kama Alivyowafanya warithi wale waliokuwa kabla yao, na bila shaka Atawamakinishia Dini yao Aliyowaridhia, na bila shaka Atawabadilishia amani badala ya khofu yao, wawe wananiabudu Mimi wasinishirikishe na chochote. Na na yeyote atakayekufuru baada ya hapo, basi hao ndio mafasiki.[18]
وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٥٦﴾
56. Na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, na mtiini Rasuli ili mpate kurehemewa.
لَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مُعْجِزِينَ فِي الْأَرْضِ ۚ وَمَأْوَاهُمُ النَّارُ ۖ وَلَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿٥٧﴾
57. Usidhanie kabisa wale waliokufuru kuwa ni wenye kushinda katika ardhi, na makazi yao ni moto. Na ubaya ulioje kwa hakika wa mahali pa kuishia!
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِيَسْتَأْذِنكُمُ الَّذِينَ مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ وَالَّذِينَ لَمْ يَبْلُغُوا الْحُلُمَ مِنكُمْ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ ۚ مِّن قَبْلِ صَلَاةِ الْفَجْرِ وَحِينَ تَضَعُونَ ثِيَابَكُم مِّنَ الظَّهِيرَةِ وَمِن بَعْدِ صَلَاةِ الْعِشَاءِ ۚ ثَلَاثُ عَوْرَاتٍ لَّكُمْ ۚ لَيْسَ عَلَيْكُمْ وَلَا عَلَيْهِمْ جُنَاحٌ بَعْدَهُنَّ ۚ طَوَّافُونَ عَلَيْكُم بَعْضُكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿٥٨﴾
58. Enyi walioamini! Wakuombeni idhini wale iliyowamiliki mikono yenu ya kuume, na wale wasiofikia umri wa kubaleghe miongoni mwenu mara tatu: kabla ya Swalaah ya Alfajiri na wakati mnapovua nguo zenu adhuhuri (kulala) na baada ya Swalaah ya ‘Ishaa. Nyakati tatu za faragha kwenu. Hakuna ubaya kwenu na wala kwao baada ya nyakati hizo, kuzungukiana nyinyi kwa nyinyi. Hivyo ndivyo Allaah Anakubainishieni Aayaat na (Ishara, Hukmu za Sharia, Dalili). Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.[19]
وَإِذَا بَلَغَ الْأَطْفَالُ مِنكُمُ الْحُلُمَ فَلْيَسْتَأْذِنُوا كَمَا اسْتَأْذَنَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴿٥٩﴾
59. Na watoto miongoni mwenu watakapofikia baleghe, basi waombe idhini (wakati wote) kama walivyoomba idhini wale wa kabla yao. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat na (Ishara, Hukmu za Sharia, Dalili) Zake. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
وَالْقَوَاعِدُ مِنَ النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا يَرْجُونَ نِكَاحًا فَلَيْسَ عَلَيْهِنَّ جُنَاحٌ أَن يَضَعْنَ ثِيَابَهُنَّ غَيْرَ مُتَبَرِّجَاتٍ بِزِينَةٍ ۖ وَأَن يَسْتَعْفِفْنَ خَيْرٌ لَّهُنَّ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٦٠﴾
60. Na wanawake wazee waliokatika hedhi ambao hawataraji kuolewa, hakuna ubaya juu yao kupunguza baadhi ya nguo zao bila ya kudhihirisha mapambo yao. Na kama wakijiwekea staha kujisitiri ni kheri kwao. Na Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
لَّيْسَ عَلَى الْأَعْمَىٰ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْأَعْرَجِ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْمَرِيضِ حَرَجٌ وَلَا عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ أَن تَأْكُلُوا مِن بُيُوتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ آبَائِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أُمَّهَاتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ إِخْوَانِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَخَوَاتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَعْمَامِكُمْ أَوْ بُيُوتِ عَمَّاتِكُمْ أَوْ بُيُوتِ أَخْوَالِكُمْ أَوْ بُيُوتِ خَالَاتِكُمْ أَوْ مَا مَلَكْتُم مَّفَاتِحَهُ أَوْ صَدِيقِكُمْ ۚ لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَأْكُلُوا جَمِيعًا أَوْ أَشْتَاتًا ۚ فَإِذَا دَخَلْتُم بُيُوتًا فَسَلِّمُوا عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ تَحِيَّةً مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُبَارَكَةً طَيِّبَةً ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٦١﴾
61. Si vibaya kwa kipofu, na wala si vibaya kwa kilema, na wala si vibaya kwa mgonjwa, na wala nyinyi wenyewe kama mtakula majumbani mwenu, au majumbani mwa baba zenu, au majumbani mwa mama zenu, au majumbani mwa kaka zenu, au majumbani mwa dada zenu, au majumbani mwa ‘ammi zenu, au majumbani mwa shangazi zenu, au majumbani mwa wajomba zenu, au majumbani mwa makhalati zenu au za mliowashikia funguo zao, au rafiki yenu. Hakuna ubaya kama mkila pamoja au mbali mbali. Mtakapoingia majumbani toleaneni Salaam (‘alaykum) maamkizi kutoka kwa Allaah, yenye Baraka, mazuri. Hivyo ndivyo Anavyokubainishieni Allaah Aayaat na (Ishara, Hukmu za Sharia, Dalili) ili mpate kutia akilini.[20]
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَإِذَا كَانُوا مَعَهُ عَلَىٰ أَمْرٍ جَامِعٍ لَّمْ يَذْهَبُوا حَتَّىٰ يَسْتَأْذِنُوهُ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَأْذِنُونَكَ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۚ فَإِذَا اسْتَأْذَنُوكَ لِبَعْضِ شَأْنِهِمْ فَأْذَن لِّمَن شِئْتَ مِنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمُ اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٦٢﴾
62. Hakika Waumini wa kweli ni wale waliomwamini Allaah na Rasuli Wake. Na wanapokuwa pamoja naye (Rasuli) katika jambo la umoja hawaondoki mpaka wamuombe idhini. Hakika wale wanaokuomba idhini, hao ni wale wanaomwamini (kweli) Allaah na Rasuli Wake. Basi wanapokuomba idhini (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa ajili ya baadhi ya shughuli zao, basi mpe idhini umtakaye miongoni mwao, na waombee Maghfirah kwa Allaah. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
لَّا تَجْعَلُوا دُعَاءَ الرَّسُولِ بَيْنَكُمْ كَدُعَاءِ بَعْضِكُم بَعْضًا ۚ قَدْ يَعْلَمُ اللَّـهُ الَّذِينَ يَتَسَلَّلُونَ مِنكُمْ لِوَاذًا ۚ فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٦٣﴾
63. Msifanye wito wa Rasuli baina yenu kama wito wa nyinyi kwa nyinyi. Kwa yakini Allaah Anawajua miongoni mwenu wale wanaoondoka kwa kunyemelea. Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah au ikawasibu adhabu iumizayo.
أَلَا إِنَّ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ قَدْ يَعْلَمُ مَا أَنتُمْ عَلَيْهِ وَيَوْمَ يُرْجَعُونَ إِلَيْهِ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٦٤﴾
64. Tanabahi! Hakika ni vya Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kwa yakini (Allaah) Anajua mliyo nayo. Na Siku watakayorejeshwa Kwake, Atawajulisha yale yote waliyoyatenda. Na Allaah kwa kila kitu Ni Mjuzi.
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah/ Hukmu Ya Zinaa Na
Bonyeza kiungo kifuatacho:
[2] Kuwasingizia Machafu Wanawake Watwaharifu Ni Miongoni Mwa Mambo Saba Yanayoangamiza:
Rejea Aayah (23) ya Suwrah hii An-Nuwr.
[3] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah/Hukmu Ya Zinaa Na Kuweko Mashahidi Na
Bonyeza kiungo kifuatacho:
[4] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah/Kutakaswa Kwa Mama Wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) Kutokana Na Singizio La Kashfa Na Radd Kwa Wanaoendelea Kumzulia
Bonyeza kiungo kifuatacho ambako kuna uthibitisho wa Hadiyth inayoelezea tukio hilo kwa maelezo marefu na bayana kabisa. Na Aayah zinazofuatia An-Nuwr (24:23-26) pia zinahusiana na tukio hili.
024-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nuwr Aayah 11-22: إِنَّ الَّذِينَ جَاءُوا بِالْإِفْكِ عُصْبَةٌ مِّنكُمْ [205]
Aayah hii ya (11) hadi (22), ni Aayah zinazomtakasa Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) kutokana na singizio la kashfa juu yake. Singizio ambalo lilisababisha rabsha, huzuni na dhiki katika nyumba ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na jamii nzima katika mji wa Madiynah. Tetesi la singizio hilo lilimuumiza mno Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na ahli wake na liliwatia dhiki, huzuni na ukosaji wa utulivu. Ikawa ni kipindi kigumu mno kuvumilia mpaka zilipoteremka Aayah hizi kumtakasa ‘Aaishah Mama wa Waumini (رضي الله عنها).
Na hii ni radd kwa wanaojinasibisha na Uislamu kuendelea kumzulia mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumtusi hadharani pamoja na Swahaba wengineo wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Aayah hizi ni ushahidi, hoja, burhani na dalili za waziwazi kabisa. Aayah ambazo zimesomwa tokea hapo zilipoteremka, na zinasomwa hadi leo, na zitaendelea kusomwa hadi Siku ya Qiyaamah.
[5] Shaytwaan Anachochea Na Kuamuru Machafu Na Ni Adui Bayana:
Rejea Suwrah Ibraahiym (14:22) kwenye rejea nyenginezo za kutahadharishwa na shaytwaan. Rejea pia Al-Israa (17:64).
[6] Wenye Fadhila: Amekusudiwa Abu Bakr Asw-Swiddiyq:
Aayah hii iliteremka kwa ajili ya Abubakar Asw-Swiddiyq (رضي الله عنه), wakati alipoapa kuwa hatomsaidia Mistwah Bin Uthaathah kwa lolote lile, baada ya kuongea maneno mabaya ya kumtuhumu ‘Aaishah (رضي الله عنها). Baada ya Allaah kuteremsha Aayah za kumtakasa Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها), na nafsi zenye imaan zikatulia na kupata ahueni, na Allaah (سبحانه وتعالى) Akapokea tawbah za wote walioyazungumza hayo katika Waumini, na wakasimamishiwa hadd waliosimamishiwa, ndio Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Fadhila Zake Akamuingiza upole na huruma Abubakar (رضي الله عنه) kwa ndugu yake, ambae ni Mistwah Bin Uthaathah, kwani yeye ni mtoto wa Mama mdogo wa Abubakar (رضي الله عنه), na alikuwa maskini asiyekuwa na mali isipokuwa ile anayopewa na Abubakar (رضي الله عنه). Na alikuwa ni katika wale waliohajiri katika njia ya Allaah. Hakika aliharakisha kufanya tawbah ambayo Allaah Aliikubalia kutokana na kosa hilo.
Abubakar (رضي الله عنه) alikuwa ni maarufu kwa kutenda wema, mwenye fadhila kubwa, na mwenye kujitolea katika kuwasaidia ndugu na wasiokuwa ndugu. Baada ya kuteremka Aayah hii mpaka Kauli Yake Allaah:
أَلَا تُحِبُّونَ أَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٢﴾
“Je, hampendi Allaah Akughufurieni? Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.”
Yaani: Hakika malipo ni kwa mujibu wa matendo, kama utakavyoweza kumsamehe aliyekukosea, ndio na Sisi Tutakusamehe wewe, na kama utakavyoachilia mbali mabaya uliyofanyiwa na Sisi pia Tutaachilia mbali mabaya yako. Baada ya kuyasikia maneno hayo, Abubakar (رضي الله عنه) akasema: “Bali tunahitajia (msamaha). Naapa kwa Allaah! Hakika sisi tunapenda ee Rabb wetu Utughufurie.” Kisha akarejea kumfanyia Mistwahi yale yote aliyokuwa akimfanyia yakiwemo kumpatia matumizi, na akasema: “Naapa kwa Allaah! Sitoacha kumsaidia tena!” Haya maneno yanakuwa kama majibu ya alichokisema awali: “Naapa kwa Allaah sitomsaidia kwa lolote lile,” Kwa sababu hii, ndio maana Abubakar (رضي الله عنه) amekuwa ni mkweli msadikishaji. Allaah Amridhie yeye pamoja na bint yake. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[7] Kuwasingizia Machafu Wanawake Watwaharifu Ni Miongoni Mwa Mambo Saba Yanayoangamiza:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عن النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((اجْتَنِبُوا السَّبْعَ الْمُوبِقَاتِ)) قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَمَا هُنَّ؟ قَالَ: ((الشِّرْكُ بِاللَّهِ وَالسِّحْرُ وَقَتْلُ النَّفْسِ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلاَّ بِالْحَقِّ وَأَكْلُ الرِّبَا وَأَكْلُ مَالِ الْيَتِيمِ وَالتَّوَلِّي يَوْمَ الزَّحْفِ وَقَذْفُ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ الْغَافلاَتِ)) متفق عليه
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Jiepusheni na mambo saba yanayoangamiza!” Wakauliza: Ni yepi hayo ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Ni kumshirikisha Allaah, sihri (uchawi), kuua nafsi Aliyoiharamisha Allaah isipokuwa kwa haki, kula riba, kula mali ya yatima, kukimbia wakati wa kupambana na adui na kuwatuhumu uzinifu wanawake Waumini waliohifadhika walioghafilika.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
[8] Viungo Vya Mwili Vitashuhudia Matendo Ya Binaadamu:
Rejea Yaasiyn (36:65), Fusw-swilat: (41:20-22), Al-Israa (17:13-14).
[9] Kauli Ovu Zinaendana Na Watu Waovu Kauli Njema Zinaendana Na Watu Wema:
Yaani: Kila mtu muovu katika wanaume na wanawake, ni lazima maneno yake na matendo yake yawe sawa na uovu wake ulivyo. Ni hulka inayoendana naye, inayonasibiana naye na inayofanana naye. Na kila mtu mwema katika wanaume na wanawake, ni lazima maneno yake na matendo yake yawe sawa na wema wake ulivyo. Ni hulka inayoendana naye, inayonasibiana naye na inayofanana naye.
Maneno haya ni jumuishi yaliyofunga duara, hayatoi mpenyo wa kutoka chochote ndani yake. Na kati ya vipengele muhimu zaidi vilivyo ndani ya maneno haya ni kwamba Manabii hasa wale Ulul-‘azmi (waliofungamana na ahadi ya nguvu), wakiongozwa na bwana wao Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye ndiye mbora wa wema katika viumbe, hanasibiani nao isipokuwa kila mwanamke aliye mwema. Hivyo basi, kumzushia uongo ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwa jambo hili, ni kumtia dosari Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na ndio makusudio ya uzushi huu waliyoyakusudia wanafiki. Na vile tu bibi ‘Aaishah (رضي الله عنها) amekuwa mke wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), inajulikana moja kwa moja kuwa hawezi kuwa isipokuwa ni mwanamke mwema aliyetakasika na kuwa mbali kabisa na jambo hili baya.
Kwa nini asiwe hivyo? Kwani kuna asiyemjua?! Mkweli katika wanawake, mbora wao, mwenye ilimu zaidi kuliko wao, na mwema wao. Isitoshe, ni kipenzi cha Rasuli wa Rabb wa walimwengu ambaye haujateremshwa Wahyi kwake akiwa kitandani mwa mke kati ya wakeze, isipokuwa pale alipokuwa kitandani mwa ‘Aaishah tu, si kwa mke mwingine yeyote.
Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akaweka wazi jambo hilo, kwa namna inayomfunga kabisa mdomo mwenye lengo la kuchafua, wala kuacha nafasi yoyote kwa shaka na shubha ndipo Anasema (سبحانه وتعالى):
أُولَـٰئِكَ مُبَرَّءُونَ مِمَّا يَقُولُونَ ۖ
“Hao wametakaswa na tuhuma za wanayoyasema.”
Hao wanaoashiriwa hapa ni ‘Aaishah (رضي الله عنها) pamoja na wanawake wengine ambao wako mbali na kufanya uchafu.
لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ ﴿٢٦﴾
“Watapata Maghfirah na riziki karimu.”
Ni maghfirah yanayozamisha madhambi, na rizki watayoipata Peponi itokayo kwa Rabb Mkarimu. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[10] Hijaab Na Ahkaam Zake
[11] Iliowamiliki Mikono Yao Ya Kulia: Rejea An-Nisaa (4:3).
[13] Allaah Ni Nuru Ya Mbingu Na Ardhi:
اللَّهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ
“Allaah Ni Nuru ya mbingu na ardhi.”
Ni Nuru ya kihisia (inayoonekana) na Nuru ya kidhahania (isiyoonekana), na hilo ni kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Dhati Yake Ni ni Nuru, na Stara Yake ni Nuru.
Kupitia Nuru hiyo, ndio ‘Arsh ikapata Nuru, Kursiy ikapata Nuru, jua, mwezi, na Jannah (Pepo) pia. Vile vile, Nuru ya kidhahania inarudi kwa Allaah (سبحانه وتعالى), kwa maana kwamba, Kitabu Chake ni Nuru, Sharia Zake ni Nuru, imaan na maarifa katika nyoyo za Manabii na Waja Wake Waumini pia Nuru. Kama si Nuru ya Allaah, basi giza juu ya giza lingepandana na kubebana, kwa sababu hii ndio utakuta kila panapokosekana Nuru panakuwa na giza.
مَثَلُ نُورِهِ
“Mfano wa Nuru Yake.”
Ambayo Huwaongoza kwayo watu kuifuata, ni Nuru ya imaan na Qur-aan katika nyoyo za Waumini.
كَمِشْكَاةٍ
“Ni kama shubaka.”
Tundu liliopo ukutani (kwa ajili ya kuwekea taa).
فِيهَا مِصْبَاحٌ
“Ndani yake mna taa yenye mwanga mkali.”
Kwa sababu hilo tundu huwa linakusanya mwanga usisambae.
الْمِصْبَاحُ فِي زُجَاجَةٍ الزُّجَاجَةُ
“Taa hiyo yenye mwanga mkali iko katika (tungi la) gilasi.”
Kutokana na usafi wake na kupendeza kwake.
كَأَنَّهَا كَوْكَبٌ دُرِّيٌّ
“Gilasi hiyo ni kama kwamba nyota inayong’aa na kumeremeta.”
Inaangaza kama lulu
يُوقَدُ مِنْ شَجَرَةٍ مُبَارَكَةٍ زَيْتُونَةٍ
“Inawashwa kutokana na mti wa baraka wa zaytuni.”
Inawashwa taa hiyo, kutokana na mafuta ya zaytuni ambayo Nuru yake inaangaza sana.
لَّا شَرْقِيَّةٍ وَلَا غَرْبِيَّةٍ
“Hauko Mashariki wala Magharibi.”
Haiangazi Mashariki tu, kiasi kwamba jioni hakufikiwi na Nuru, na wala si Magharibi tu kwamba asubuhi hakufikiwi na Nuru. Na yasipo kuwepo mambo haya mawili basi inakuwa kati na kati katika ardhi, kama zaytuni za Sham, zinapatwa na jua asubuhi na jioni, zinakuwa nzuri, na mafuta yake yanakuwa masafi zaidi, ndio Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
يَكَادُ زَيْتُهَا يُضِيءُ وَلَوْ لَمْ تَمْسَسْهُ نَارٌ ۚ
“Yanakaribia mafuta yake kung’aa japokuwa moto haujayagusa.”
Kutokana na usafi wake, yakiguswa na moto yanawaka sana.
نُّورٌ عَلَىٰ نُورٍ ۗ
“Nuru juu ya Nuru.”
Nuru ya moto na nuru ya mafuta. Na picha ya mfano huu ambao Allaah (سبحانه وتعالى) Ameupiga na Akautumia kuelezea hali ya Muumini ambaye Nuru ya Allaah (سبحانه وتعالى) iko ndani ya moyo wake ni kwamba umbile asilia aliloumbiwa nalo mwanaadam ni sawasawa na mafuta safi, kwani umbile lake liko safi na limeandalika (kupokea) mafundisho ya kumuabudu Allaah (سبحانه وتعالى), na kufanya kila kilicho halali, ikifika (kwenye moyo) ilimu na imaan, basi Nuru hiyo itawaka kwenye moyo wake. Ni sawa na moto uliopo kwenye utambi wa hiyo taa, naye akiwa na moyo msafi usiokuwa na makusudio mabaya, wala ufahamu mbaya kuhusu Allaah (سبحانه وتعالى), basi ikiwa imaan itaingia ndani ya moyo huo, utanunurisha mwanga wa ajabu, kwa kuwa hauna takataka za aina yoyote. Hii inakuwa sawa na taa yenye mng’ao wa lulu. Kwa hali hii, itamkusanyikia Muumini huyu Nuru ya fitwrah (maumbile ya asili), Nuru ya imaan, Nuru ya ilimu, na Nuru ya maarifa. Kwa hiyo ni Nuru juu ya Nuru.
Na baada ya kuwa hii ni Nuru ya Allaah (سبحانه وتعالى), sio kila mmoja anafaa kuipata ndio Allaah Anasema:
يَهْدِي اللَّـهُ لِنُورِهِ مَن يَشَاءُ
“Anamwongoza kwa Nuru Yake Amtakaye.”
Ni katika wale ambao Allaah (سبحانه وتعالى) Anafahamu utakasifu wao, na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Atazidisha kuwatakasa, na kuwakuza kiimani.
وَيَضْرِبُ اللَّهُ الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ
“Na Allaah Anapiga mifano kwa watu.”
Ili wapate kufahamu na kutambua huruma ya Allaah kwao, na Ihsaan Yake kwao, na ili haki iwe wazi wapate kuiacha baatwil. Hakika mifano huwa inakaribisha maana hasa kutokana na vitu vinavyoonekana na kuhisika, ndio waja wataelewa kwa uwazi zaidi.
وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ
“Na Allaah kwa kila kitu Ni Mjuzi.”
Ilimu ya Allaah (سبحانه وتعالى) imeenea katika vitu vyote, ili mtambue kwamba Aliyepiga mifano hiyo, ni Yule Anayetambua uhakika wa mambo na uchambuzi wake, na kwamba mifano hiyo ni maslahi kwa waja, hivyo basi, la kukushughulisheni ni kulizingatia hilo, si kulipuuza, kwani Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Anajua na ninyi hamjui. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[14] Waliokufuru Amali Zao Ni Kama Sarabi Jangwani:
Mifano miwili hii Allaah (سبحانه وتعالى) Ameipigia kwenye matendo ya makafiri kwamba ni baatwil yatakwenda bure na atakuja kujuta yule aliyeyatenda, ndio Akasema: Waliomkufuru Rabb wao na kuwakadhibisha Manabii Wake, amali zao ni kama sarabi jangwani. Mwenye kiu hudhania kuwa ni maji.
Mtu mwenye kiu kikali anadanganyika tofauti na mtu mwingine kutokana na kuhitajia maji kutokana na kiu, na hii ndio kudhania kuliko baatwil, atapakusudia ili azime kiu alicho nacho, lakini akifika anajuta sana, na hapo kiu kinazidi, kwa sababu ya kukatika matarajio yake. Hayo ndio matendo ya makafiri ambayo ni sawa sawa na sarabi. Mtu mjinga asiyejua mambo anahisi kuwa ni matendo yenye manufaa. Ule muonekano wake unamdanganya kutokana na matamanio ya nafsi yake, anahisi kuwa ni matendo yenye manufaa, na yeye anayahitajia hayo, bali analazimika kuyahitaji kama anavyohitaji maji mtu mwenye kiu, mpaka siku akiyafikia matendo yake siku ya Qiyaamah atayakuta yamepotea, na hatokuta chochote kile, na hali kuwa hayajaondoka, na hayamsaidii kwa lolote, bali anamkuta Allaah (سبحانه وتعالى) mbele Yake, Naye Amlipe kikamilifu hesabu yake. Yaani: Hakitofichika Kwake kitu chochote kile kidogo, kikubwa, kingi na kichache. Na Allaah Ni Mwepesi wa Kuhesabu. Yaani: Na wala watu majaahili wasidhanie lina uzito hilo, ni lazima litokee, na Allaah (سبحانه وتعالى) Amepiga mfano wa sarabi jangwani, pasipo na miti wala mimea. Na huu ni mfano wa nyoyo zao; hakuna kheri humo wala wema, ikawa sababu ya matendo yao kuwa safi, bali ni kwa sababu ya kizuizi kilichopo ambacho ni ukafiri. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[15] Kila Kitu Kinamsabbih Allaah (عزّ وجلّ):
Rejea Al-Hashr (57:1) kwenye rejea zinazotaja viumbe na vitu Alivyoviumba Allaah kuwa vinamsabbih Yeye Allaah (عزّ وجلّ).
[16] Baadhi Ya Aina Ya Viumbe Alivyoumba Allaah (سبحانه وتعالى):
Na Allaah (سبحانه وتعالى) Amekiumba kila kitambaacho ardhini kutokana na maji, kwani maji ndio asili ya kuumbwa kwake. Na miongoni mwa vitambaavyo. Kuna anayetembea kwa matumbo yake kama vile nyoka na mfano wake, na katika hao kuna anayetembea kwa miguu miwli kama binaadam, na miongoni mwao kuna anayetembea kwa miguu minne kama wanyama na mfano wake. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Anaumba Anachotaka, na Yeye ni Muweza wa kila kitu. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[17] Nyoyo Zenye Maradhi:
Rejea Suwrah Muhammad (47:20) kwenye maelezo na rejea mbalimbali kuhusu nyoyo zenye maradhi.
Rejea pia Al-Hajj (22:46) kwenye maelezo kuhusu maana ya moyo uliopofuka.
Rejea pia Ash-Shu’araa (26:88-89) kwenye ufafanuzi na maelezo kuhusu moyo uliosalimika.
[18] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah/Ahadi Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kwa Waumini Watiifu, Wenye Kutenda Mema Wasiomshirikisha Na Chochote
Bonyeza kiungo kifuatacho:
Allaah (سبحانه وتعالى) Amewaahidi walioamini miongoni mwenu na wakafanya matendo mema kwamba, Atawarithisha ardhi ya washirikina na atawafanya ni wasimamizi wa hiyo ardhi, kama Alivyofanya kwa waliokuja kabla yao kati ya wale waliomuamini Allaah na Rusuli Wake. Na Aifanye Dini yao ambayo Ameridhika nayo na Akawachagulia, nayo ni Uislamu, ni Dini yenye ushindi na uthabiti, na Azigeuze hali zao kwa kuwaondolea kicho na kuwaletea amani, iwapo watamwabudu Allaah Peke Yake, na watasimama imara kwa kumtii, na wasimshirikishe na kitu chochote. Na Mwenye kukanusha baada ya hilo la kupewa usimamizi, amani, uthabiti na utawala kamili, na akakanusha Neema za Allaah, basi hao ndio waliotoka nje ya utiifu kwa Allaah. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[19] Baadhi Ya Adabu Za Sitara Katika Familia:
Enyi ambao mlimuamini Allaah na Rasuli Wake, na mkazifanyia kazi sheria Zake! Waamrisheni watumwa wenu, wajakazi wenu na watoto waungwana ambao umri wao haujafikia wa kubaleghe, waombe ruhusa wakitaka kuingia (vyumbani) kwenu katika nyakati za mapumziko yenu na kuvua nguo zenu; Kabla ya Swalaah ya Alfajiri, kwa kuwa huo ni wakati wa kuvua nguo za kulalia na kuvaa nguo za baada ya kuamka, na wakati wa kuvua nguo kwa mapumziko ya kipindi cha mchana wakati wa jua kali, na baada ya Swalaah ya ‘Ishaa, kwa kuwa huo ni wakati wa kulala. Nyakati tatu hizi ni za kujifunua na kujiacha wazi na kunapungua kujisitiri. Lakini katika nyakati sizokuwa hizo, si makosa wakiingia bila ya idhini, kwa kuwa wao wanahitaji kuingia kwenu, wao ni wa kuingia na kutoka mara kwa mara kwa kutumika, na kwa kuwa dasturi iliyozoeleka ni kuwa nyinyi mnatembeleana nyakati hizi kwa kutimiza haja zenu zenye maslahi kwenu. Na kama Alivyowafafanulia Allaah (سبحانه وتعالى) hukumu za kutaka ruhusa (ya kuingia majumbani), Anawafafanulia Aayaat Zake, Hukumu Zake, Hoja Zake na Sharia za Dini Yake. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Anayajua sana yanayowafaa viumbe Wake, Yeye ni Mwingi wa hekima katika Upelekeshaji Wake mambo yao. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[20] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah/ Baadhi Ya Adabu Za Kula Na Za Kuingia Katika Nyumba:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
Hawana dhambi watu wenye nyudhuru miongoni mwa vipofu, viguru na wagonjwa, kuyaacha mambo ya lazima ambayo hawawezi kuyatekeleza, kama kupigana Jihaad na mfano wake katika vitu ambavyo vinahitajia kwa kipofu aweze kuona, na kiguru awe mzima (aweze kutembea na kukimbia), na mgonjwa awe na afya nzuri. Na nyinyi, enyi Waumini, hamuna makosa kula kwenye majumba ambayo ndani yake kuna wake zenu na watoto wenu. Na hapa yanaingia majumba ya watoto, au majumba ya baba zenu, au mama zenu, au ndugu zenu wa kiume, au dada zenu, au ami zenu, au mashangazi zenu, au wajomba zenu, au mama zenu wadogo, au kwenye nyumba ambazo mliwakilishwa kuzisimamia wakati wenyewe hawapo kwa ruhusa yao, au kwenye nyumba za marafiki. Hakuna makosa yoyote kwenu kula mkiwa pamoja au mbalimbali. Na muingiapo kwenye nyumba zinazokaliwa au zisizokaliwa, amkianeni nyinyi kwa nyinyi kwa maamkizi ya Kiislamu, nayo ni:
السَّلامُ عَلَيْكُم ورَحْمَةُ اللهِ وَبَرَكاتُهُ
au
السلام علينا وعلى عباد الله الصالحين
Maamkizi haya Allaah (سبحانه وتعالى) Ameyaweka, nayo yana baraka, yanakuza kusafiana niya na kupendana, ni mazuri yanayopendeza kwa mwenye kuyasikia. Na kwa mfano wa ufafanuzi huu anawafafanulia Allaah alama za Dini Yake na Aayaat Zake, ili mzifahamu na mzitumie. [Tafsiyr Al-Muyassar]
الْفُرْقان
025-Al-Furqaan
024-Al-Furqaan: Utangulizi Wa Suwrah [210]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَىٰ عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًا ﴿١﴾
1. Amebarikika Ambaye Ameteremsha kwa Mja Wake pambanuo[1] ili awe muonyaji kwa walimwengu.
الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا ﴿٢﴾
2. Ambaye Ni Wake Pekee ufalme wa mbingu na ardhi, na Hakujichukulia mwana wala Hakuwa na mshirika katika ufalme, na Ameumba kila kitu, kisha Akakikadiria kipimo cha sawa sawa.
وَاتَّخَذُوا مِن دُونِهِ آلِهَةً لَّا يَخْلُقُونَ شَيْئًا وَهُمْ يُخْلَقُونَ وَلَا يَمْلِكُونَ لِأَنفُسِهِمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا وَلَا يَمْلِكُونَ مَوْتًا وَلَا حَيَاةً وَلَا نُشُورًا ﴿٣﴾
3. Na wakachukua badala Yake (Allaah) waabudiwa wasioumba chochote na hali wao wanaumbwa, wala hawamiliki kwa ajili ya nafsi zao dhara wala manufaa, wala hawamiliki mauti wala uhai wala ufufuo.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا إِفْكٌ افْتَرَاهُ وَأَعَانَهُ عَلَيْهِ قَوْمٌ آخَرُونَ ۖ فَقَدْ جَاءُوا ظُلْمًا وَزُورًا ﴿٤﴾
4. Wakasema wale waliokufuru: Hii (Qur-aan) si chochote isipokuwa ni uzushi alioutunga (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na wamemsaidia watu wengine. Kwa yakini wameleta dhulma na uongo.[2]
وَقَالُوا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ اكْتَتَبَهَا فَهِيَ تُمْلَىٰ عَلَيْهِ بُكْرَةً وَأَصِيلًا ﴿٥﴾
5. Na wakasema: Ni hekaya za kale ameziandikisha kisha anasomewa asubuhi na jioni.
قُلْ أَنزَلَهُ الَّذِي يَعْلَمُ السِّرَّ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ إِنَّهُ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٦﴾
6. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ameiteremsha Ambaye Anajua siri katika mbingu na ardhi. Hakika Yeye daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَقَالُوا مَالِ هَـٰذَا الرَّسُولِ يَأْكُلُ الطَّعَامَ وَيَمْشِي فِي الْأَسْوَاقِ ۙ لَوْلَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مَلَكٌ فَيَكُونَ مَعَهُ نَذِيرًا ﴿٧﴾
7. Na wakasema: Ni Rasuli gani huyu? Anakula chakula na anatembea masokoni! Kwa nini asiteremshiwe Malaika akawa muonyaji pamoja naye?[3]
أَوْ يُلْقَىٰ إِلَيْهِ كَنزٌ أَوْ تَكُونُ لَهُ جَنَّةٌ يَأْكُلُ مِنْهَا ۚ وَقَالَ الظَّالِمُونَ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا رَجُلًا مَّسْحُورًا ﴿٨﴾
8. Au aangushiwe hazina juu yake au awe na bustani awe anakula humo? Na wakasema madhalimu: Hamfuati isipokuwa mtu aliyerogwa.
انظُرْ كَيْفَ ضَرَبُوا لَكَ الْأَمْثَالَ فَضَلُّوا فَلَا يَسْتَطِيعُونَ سَبِيلًا ﴿٩﴾
9. Tazama vipi walivyokupigia mifano, basi wamepotea, hawatoweza kupata njia (ya haki).
تَبَارَكَ الَّذِي إِن شَاءَ جَعَلَ لَكَ خَيْرًا مِّن ذَٰلِكَ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَيَجْعَل لَّكَ قُصُورًا ﴿١٠﴾
10. Amebarikika Ambaye Akitaka Atakujaalia kheri kuliko hayo; ni Jannaat zipitazo katikati yake mito na Akujaalie maqasri.
بَلْ كَذَّبُوا بِالسَّاعَةِ ۖ وَأَعْتَدْنَا لِمَن كَذَّبَ بِالسَّاعَةِ سَعِيرًا ﴿١١﴾
11. Bali wameikadhibisha Saa. Na Tumeandaa kwa anayeikadhibisha Saa moto uliowashwa vikali mno.
إِذَا رَأَتْهُم مِّن مَّكَانٍ بَعِيدٍ سَمِعُوا لَهَا تَغَيُّظًا وَزَفِيرًا ﴿١٢﴾
12. (Moto huo) Utakapowaona kutoka mahali mbali, watausikia ghadhabu zake na mngurumo wake.
وَإِذَا أُلْقُوا مِنْهَا مَكَانًا ضَيِّقًا مُّقَرَّنِينَ دَعَوْا هُنَالِكَ ثُبُورًا ﴿١٣﴾
13. Na watakapotupwa humo mahali pa dhiki wakiwa wamefungashwa pamoja wataomba huko kuteketea.
لَّا تَدْعُوا الْيَوْمَ ثُبُورًا وَاحِدًا وَادْعُوا ثُبُورًا كَثِيرًا ﴿١٤﴾
14. Msiombe leo kuteketea kumoja, bali ombeni kuteketea kwingi!
قُلْ أَذَٰلِكَ خَيْرٌ أَمْ جَنَّةُ الْخُلْدِ الَّتِي وُعِدَ الْمُتَّقُونَ ۚ كَانَتْ لَهُمْ جَزَاءً وَمَصِيرًا ﴿١٥﴾
15. Sema: Je, hayo ni bora, au Jannah ya yenye kudumu ambayo wameahidiwa wenye taqwa? Itakuwa kwao ni jazaa na mahali pa kuishia.
لَّهُمْ فِيهَا مَا يَشَاءُونَ خَالِدِينَ ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ وَعْدًا مَّسْئُولًا ﴿١٦﴾
16. Watapata humo kila wanachokitaka, wadumu milele. Imekuwa ni ahadi juu ya Rabb wako ya kuombwa.
وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ فَيَقُولُ أَأَنتُمْ أَضْلَلْتُمْ عِبَادِي هَـٰؤُلَاءِ أَمْ هُمْ ضَلُّوا السَّبِيلَ ﴿١٧﴾
17. Na Siku Atakayowakusanya pamoja na yale wanayoyaabudu badala ya Allaah Aseme: Je, ni nyinyi ndio mliowapoteza Waja Wangu, au wao ndio waliopotea njia?
قَالُوا سُبْحَانَكَ مَا كَانَ يَنبَغِي لَنَا أَن نَّتَّخِذَ مِن دُونِكَ مِنْ أَوْلِيَاءَ وَلَـٰكِن مَّتَّعْتَهُمْ وَآبَاءَهُمْ حَتَّىٰ نَسُوا الذِّكْرَ وَكَانُوا قَوْمًا بُورًا ﴿١٨﴾
18. Watasema: Subhaanak! (Utakasifu ni Wako!) Haikutupasa sisi kuchukua badala Yako rafiki walinzi wowote, lakini Uliwastarehesha na baba zao mpaka wakasahau ukumbusho na wakawa watu wa kuteketea.
فَقَدْ كَذَّبُوكُم بِمَا تَقُولُونَ فَمَا تَسْتَطِيعُونَ صَرْفًا وَلَا نَصْرًا ۚ وَمَن يَظْلِم مِّنكُمْ نُذِقْهُ عَذَابًا كَبِيرًا ﴿١٩﴾
19. Basi wamekwisha kukadhibisheni kwa yale myasemayo, hivyo hamtoweza kujiondoshea wala kujinusuru. Na yeyote atakayedhulumu miongoni mwenu Tutamuonjesha adhabu kubwa.
وَمَا أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ مِنَ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا إِنَّهُمْ لَيَأْكُلُونَ الطَّعَامَ وَيَمْشُونَ فِي الْأَسْوَاقِ ۗ وَجَعَلْنَا بَعْضَكُمْ لِبَعْضٍ فِتْنَةً أَتَصْبِرُونَ ۗ وَكَانَ رَبُّكَ بَصِيرًا ﴿٢٠﴾
20. Na Hatukupeleka kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Rusuli wowote isipokuwa bila shaka wakila chakula, na wanatembea masokoni. Na Tumejaalia baadhi yenu nyinyi kwa nyinyi kuwa ni majaribio.[4] Je, mtasubiri? Na Rabb wako Ni Mwenye Kuona daima.
وَقَالَ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْنَا الْمَلَائِكَةُ أَوْ نَرَىٰ رَبَّنَا ۗ لَقَدِ اسْتَكْبَرُوا فِي أَنفُسِهِمْ وَعَتَوْا عُتُوًّا كَبِيرًا ﴿٢١﴾
21. Na walisema wale wasiotaraji kukutana Nasi: Kwa nini hatuteremshiwi Malaika, au hatumwoni Rabb wetu? Kwa yakini wametakabari katika nafsi zao na wakavuka mipaka ya ufedhuli na uasi mkubwa.[5]
يَوْمَ يَرَوْنَ الْمَلَائِكَةَ لَا بُشْرَىٰ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُجْرِمِينَ وَيَقُولُونَ حِجْرًا مَّحْجُورًا ﴿٢٢﴾
22. Siku watakayowaona Malaika hakutakuwa na bishara njema Siku hiyo kwa wakhalifu na (Malaika) watasema: Marufuku tena marufuku kabisa (nyinyi kupata mafanikio yoyote leo).[6]
وَقَدِمْنَا إِلَىٰ مَا عَمِلُوا مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَاهُ هَبَاءً مَّنثُورًا ﴿٢٣﴾
23. Na Tutayaendea yale waliyoyatenda ya ‘amali yoyote ile, Tutayafanya chembechembe za vumbi zinazoelea hewani zikitawanyika.[7]
أَصْحَابُ الْجَنَّةِ يَوْمَئِذٍ خَيْرٌ مُّسْتَقَرًّا وَأَحْسَنُ مَقِيلًا ﴿٢٤﴾
24. Watu wa Jannah Siku hiyo watakuwa katika makazi bora ya kustakiri, na mahali pazuri kabisa pa kupumzikia.
وَيَوْمَ تَشَقَّقُ السَّمَاءُ بِالْغَمَامِ وَنُزِّلَ الْمَلَائِكَةُ تَنزِيلًا ﴿٢٥﴾
25. Na Siku itakayofunguka mbingu kwa mawingu, na Malaika watateremshwa mteremsho mkubwa wa mfuatano.[8]
الْمُلْكُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ لِلرَّحْمَـٰنِ ۚ وَكَانَ يَوْمًا عَلَى الْكَافِرِينَ عَسِيرًا ﴿٢٦﴾
26. Ufalme wa haki Siku hiyo utakuwa ni wa Ar-Rahmaan. Na itakuwa ni siku ngumu kwa makafiri.
وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ يَقُولُ يَا لَيْتَنِي اتَّخَذْتُ مَعَ الرَّسُولِ سَبِيلًا ﴿٢٧﴾
27. Na siku dhalimu atakapouma mikono yake akisema: Laiti ningeshika njia pamoja na Rasuli.[9]
يَا وَيْلَتَىٰ لَيْتَنِي لَمْ أَتَّخِذْ فُلَانًا خَلِيلًا ﴿٢٨﴾
28. Ee ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki mwandani.
لَّقَدْ أَضَلَّنِي عَنِ الذِّكْرِ بَعْدَ إِذْ جَاءَنِي ۗ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِلْإِنسَانِ خَذُولًا ﴿٢٩﴾
29. Kwa yakini amenipoteza mbali na Ukumbusho baada ya kunijia. Na shaytwaan kwa binaadam daima ni msaliti.
وَقَالَ الرَّسُولُ يَا رَبِّ إِنَّ قَوْمِي اتَّخَذُوا هَـٰذَا الْقُرْآنَ مَهْجُورًا ﴿٣٠﴾
30. Na Rasuli akasema: Rabb wangu! Hakika watu wangu wameifanya hii Qur-aan yenye kuhamwa.[10]
وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا مِّنَ الْمُجْرِمِينَ ۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ هَادِيًا وَنَصِيرًا ﴿٣١﴾
31. Na hivyo ndivyo Tumemfanyia kila Nabiy adui miongoni mwa wakhalifu. Na Rabb wako Anatosheleza kuwa ni Mwenye Kuongoza na Mwenye Kunusuru.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ الْقُرْآنُ جُمْلَةً وَاحِدَةً ۚ كَذَٰلِكَ لِنُثَبِّتَ بِهِ فُؤَادَكَ ۖ وَرَتَّلْنَاهُ تَرْتِيلًا ﴿٣٢﴾
32. Na wakasema wale waliokufuru: Kwa nini hakuteremshiwa Qur-aan kwa ujumla mara moja tu? Ndio hivyo hivyo, ili Tukithibitishe kifua chako. Na Tumeifunulia Wahyi punde kwa punde kwa kuratibu. [11]
وَلَا يَأْتُونَكَ بِمَثَلٍ إِلَّا جِئْنَاكَ بِالْحَقِّ وَأَحْسَنَ تَفْسِيرًا ﴿٣٣﴾
33. Na wala hawakujii kwa mfano wowote isipokuwa Tunakuletea haki na tafsiri nzuri kabisa.
الَّذِينَ يُحْشَرُونَ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ إِلَىٰ جَهَنَّمَ أُولَـٰئِكَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضَلُّ سَبِيلًا ﴿٣٤﴾
34. Wale ambao watakusanywa juu ya nyuso zaokuelekea Jahannam[12], hao wana mahali pabaya mno, na wamepotea zaidi njia.
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَجَعَلْنَا مَعَهُ أَخَاهُ هَارُونَ وَزِيرًا ﴿٣٥﴾
35. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Maandiko (ya Tawraat) na Tukamjaalia pamoja naye kaka yake Haaruwn kuwa msaidizi.
فَقُلْنَا اذْهَبَا إِلَى الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا فَدَمَّرْنَاهُمْ تَدْمِيرًا ﴿٣٦﴾
36. Tukasema: Nendeni kwa watu ambao wamekadhibisha Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu, basi Tukawadamirisha vibaya.
وَقَوْمَ نُوحٍ لَّمَّا كَذَّبُوا الرُّسُلَ أَغْرَقْنَاهُمْ وَجَعَلْنَاهُمْ لِلنَّاسِ آيَةً ۖ وَأَعْتَدْنَا لِلظَّالِمِينَ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿٣٧﴾
37. Na watu wa Nuwh walipowakadhibisha Rusuli, Tuliwagharikisha, na Tukawafanya kuwa Aayah (Mazingatio) kwa watu. Na Tumewaandalia madhalimu adhabu iumizayo.
وَعَادًا وَثَمُودَ وَأَصْحَابَ الرَّسِّ وَقُرُونًا بَيْنَ ذَٰلِكَ كَثِيرًا ﴿٣٨﴾
38. Na kina ‘Aad na Thamuwd na watu wa Ar-Rass[13] na karne nyingi zilizokuwa baina yao.
وَكُلًّا ضَرَبْنَا لَهُ الْأَمْثَالَ ۖ وَكُلًّا تَبَّرْنَا تَتْبِيرًا ﴿٣٩﴾
39. Na kila mmoja Tuliwapigia mifano na kila mmoja Tuliwateketeza mateketezo kamilifu.
وَلَقَدْ أَتَوْا عَلَى الْقَرْيَةِ الَّتِي أُمْطِرَتْ مَطَرَ السَّوْءِ ۚ أَفَلَمْ يَكُونُوا يَرَوْنَهَا ۚ بَلْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ نُشُورًا ﴿٤٠﴾
40. Na kwa yakini walipita katika mji ambao ulinyeshewa mvua mbaya. Je, basi hawakuwa wakiuona? Bali walikuwa hawataraji kufufuliwa.
وَإِذَا رَأَوْكَ إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلَّا هُزُوًا أَهَـٰذَا الَّذِي بَعَثَ اللَّـهُ رَسُولًا ﴿٤١﴾
41. Na wanapokuona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) hawakuchukulii isipokuwa mzaha (wakisema): Je, ndiye huyu ambaye Allaah Amemtuma kuwa Rasuli?
إِن كَادَ لَيُضِلُّنَا عَنْ آلِهَتِنَا لَوْلَا أَن صَبَرْنَا عَلَيْهَا ۚ وَسَوْفَ يَعْلَمُونَ حِينَ يَرَوْنَ الْعَذَابَ مَنْ أَضَلُّ سَبِيلًا ﴿٤٢﴾
42. Kwa yakini alikaribia kutupoteza na waabudiwa wetu, ingelikuwa hatukuvumilia kuwaabudu. Lakini watakuja kujua wakati watakapoona adhabu, ni nani aliyepotea zaidi njia.
أَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهُ أَفَأَنتَ تَكُونُ عَلَيْهِ وَكِيلًا ﴿٤٣﴾
43. Je, umemuona yule aliyefanya hawaa yake kuwa ndio mwabudiwa wake? Je, basi utaweza wewe kuwa ni mdhamini wake?[14]
أَمْ تَحْسَبُ أَنَّ أَكْثَرَهُمْ يَسْمَعُونَ أَوْ يَعْقِلُونَ ۚ إِنْ هُمْ إِلَّا كَالْأَنْعَامِ ۖ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلًا ﴿٤٤﴾
44. Je, unadhania kwamba wengi wao wanasikia au wanatia akilini? Wao si chochote isipokuwa kama wanyama, bali wao wamepotea zaidi njia.
أَلَمْ تَرَ إِلَىٰ رَبِّكَ كَيْفَ مَدَّ الظِّلَّ وَلَوْ شَاءَ لَجَعَلَهُ سَاكِنًا ثُمَّ جَعَلْنَا الشَّمْسَ عَلَيْهِ دَلِيلًا ﴿٤٥﴾
45. Je, huoni vipi Rabb wako Alivyotandaza kivuli? Angelitaka Angelikifanya kitulie tu kisha Tukalifanya jua kuwa kielekezo juu yake.
ثُمَّ قَبَضْنَاهُ إِلَيْنَا قَبْضًا يَسِيرًا ﴿٤٦﴾
46. Kisha Tunakivutia Kwetu mvuto wa polepole.
وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ لِبَاسًا وَالنَّوْمَ سُبَاتًا وَجَعَلَ النَّهَارَ نُشُورًا ﴿٤٧﴾
47. Naye Ndiye Ambaye Amekujaalieni usiku kuwa ni libasi na usingizi wa mapumziko ya kama kufa, na Amefanya mchana ni wa kuinuka na kutawanyika.
وَهُوَ الَّذِي أَرْسَلَ الرِّيَاحَ بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ ۚ وَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً طَهُورًا ﴿٤٨﴾
48. Naye Ndiye Ambaye Ametuma upepo wa kheri kuwa bishara njema kabla ya Rehma Yake. Na Tunateremsha kutoka mbinguni maji yaliyo safi.
لِّنُحْيِيَ بِهِ بَلْدَةً مَّيْتًا وَنُسْقِيَهُ مِمَّا خَلَقْنَا أَنْعَامًا وَأَنَاسِيَّ كَثِيرًا ﴿٤٩﴾
49. Ili Tuhuishe kwayo nchi iliyokufa,[15] na Tuwanyweshe kwayo kati ya wale Tuliowaumba; wanyama na watu wengi.
وَلَقَدْ صَرَّفْنَاهُ بَيْنَهُمْ لِيَذَّكَّرُوا فَأَبَىٰ أَكْثَرُ النَّاسِ إِلَّا كُفُورًا ﴿٥٠﴾
50. Na kwa yakini Tumeigawa (mvua) baina yao ili wakumbuke (Neema za Allaah), lakini watu wengi wanakataa kabisa, (hawana) isipokuwa kukufuru tu.
وَلَوْ شِئْنَا لَبَعَثْنَا فِي كُلِّ قَرْيَةٍ نَّذِيرًا ﴿٥١﴾
51. Na lau Tungelitaka, bila shaka Tungelipeleka katika kila mji mwonyaji.
فَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَجَاهِدْهُم بِهِ جِهَادًا كَبِيرًا ﴿٥٢﴾
52. Basi usiwatii makafiri. Na pambana nao kwayo (Qur-aan) kwa juhudi za upeo wako wa mwisho.
وَهُوَ الَّذِي مَرَجَ الْبَحْرَيْنِ هَـٰذَا عَذْبٌ فُرَاتٌ وَهَـٰذَا مِلْحٌ أُجَاجٌ وَجَعَلَ بَيْنَهُمَا بَرْزَخًا وَحِجْرًا مَّحْجُورًا ﴿٥٣﴾
53. Naye Ndiye Aliyeunganisha bahari mbili; hii ni tamu ikatayo kiu, na hii ni ya chumvi, kali. Na Akajaalia baina yao kitenganisho na kizuizi kinachozuia kabisa.[16]
وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ مِنَ الْمَاءِ بَشَرًا فَجَعَلَهُ نَسَبًا وَصِهْرًا ۗ وَكَانَ رَبُّكَ قَدِيرًا ﴿٥٤﴾
54. Naye Ndiye Aliyeumba mtu kutokana na maji, kisha Akamjaalia kuwa na unasaba wa damu na uhusiano wa ndoa. Na Rabb wako daima Ni Mweza wa yote.
وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُهُمْ وَلَا يَضُرُّهُمْ ۗ وَكَانَ الْكَافِرُ عَلَىٰ رَبِّهِ ظَهِيرًا ﴿٥٥﴾
55. Na wanaabudu badala ya Allaah vile visivyowafaa na visivyowadhuru. Na kafiri daima ni msaidizi wa kumpinga Rabb wake.
وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا مُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿٥٦﴾
56. Na Hatukukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa ni mbashiriaji na mwonyaji.
قُلْ مَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِلَّا مَن شَاءَ أَن يَتَّخِذَ إِلَىٰ رَبِّهِ سَبِيلًا ﴿٥٧﴾
57. Sema: Sikuombeni ujira juu yake isipokuwa atakaye achukue njia kuelekea kwa Rabb wake.
وَتَوَكَّلْ عَلَى الْحَيِّ الَّذِي لَا يَمُوتُ وَسَبِّحْ بِحَمْدِهِ ۚ وَكَفَىٰ بِهِ بِذُنُوبِ عِبَادِهِ خَبِيرًا ﴿٥٨﴾
58. Na tawakali kwa Aliye Hai Ambaye Hafi, na sabihi ukimhimidi. Na Inamtosheleza kuwa Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri kuhusu dhambi za Waja Wake.
الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ الرَّحْمَـٰنُ فَاسْأَلْ بِهِ خَبِيرًا ﴿٥٩﴾
59. Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita, kisha Akawa juu[17] ya ‘Arsh. (Yeye ni) Ar-Rahmaan, basi ulizia kuhusu Yeye, kwani Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اسْجُدُوا لِلرَّحْمَـٰنِ قَالُوا وَمَا الرَّحْمَـٰنُ أَنَسْجُدُ لِمَا تَأْمُرُنَا وَزَادَهُمْ نُفُورًا ۩﴿٦٠﴾
60. Na wanapoambiwa: Msujudieni Ar-Rahmaan husema: Ni nani huyo Ar-Rahmaan? Tumsujudie unayetuamrisha, na inawazidishia kukengeuka kwa chuki.[18]
تَبَارَكَ الَّذِي جَعَلَ فِي السَّمَاءِ بُرُوجًا وَجَعَلَ فِيهَا سِرَاجًا وَقَمَرًا مُّنِيرًا ﴿٦١﴾
61. Amebarikika Ambaye Amejaalia buruji[19] katika mbingu na Amejaalia humo taa yenye mwanga mkali na mwezi wenye nuru.
وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ خِلْفَةً لِّمَنْ أَرَادَ أَن يَذَّكَّرَ أَوْ أَرَادَ شُكُورًا ﴿٦٢﴾
62. Naye Ndiye Aliyejaalia usiku na mchana ufuatane kwa atakaye kukumbuka au atakaye kushukuru.
وَعِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا ﴿٦٣﴾
63. Na Waja wa Ar-Rahmaan[20] ni wale wanaotembea katika ardhi kwa unyenyekevu na upole, na majahili wanapowasemesha, wao husema: Salaamaa (amani)!
وَالَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَامًا ﴿٦٤﴾
64. Na wale wanaokesha usiku kwa ajili ya Rabb wao wakisujudu na kusimama.[21]
وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ ۖ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا ﴿٦٥﴾
65. Na wale wanaosema: Rabb wetu! Tuepushe adhabu ya Jahannam. Hakika adhabu yake ni yenye kugandamana daima; isiyomwacha mtu.
إِنَّهَا سَاءَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا ﴿٦٦﴾
66. Hakika hiyo (Jahannam) ni mahali paovu mno pa kustakiri na mahali pa kuishi.
وَالَّذِينَ إِذَا أَنفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَٰلِكَ قَوَامًا ﴿٦٧﴾
67. Na wale ambao wanapotoa huwa hawafanyi israfu[22] na wala hawafanyi uchoyo na wanakuwa wastani baina ya hayo.
وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا ﴿٦٨﴾
68. Na wale ambao hawaombi pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine na wala hawaui nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha isipokuwa kwa haki, na wala hawazini. Na atakayefanya hivyo atakutana na adhabu.[23]
يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا ﴿٦٩﴾
69. Ataongezewa adhabu maradufu Siku ya Qiyaamah, na atadumu humo akidhalilishwa.
إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٧٠﴾
70. Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda amali njema. Basi hao Allaah Atawabadilishia maovu yao kuwa mema. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[24]
وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَإِنَّهُ يَتُوبُ إِلَى اللَّـهِ مَتَابًا ﴿٧١﴾
71. Na atakayetubu na akatenda mema, basi hakika yeye anatubia kwa Allaah tawbah ya kweli.[25]
وَالَّذِينَ لَا يَشْهَدُونَ الزُّورَ وَإِذَا مَرُّوا بِاللَّغْوِ مَرُّوا كِرَامًا ﴿٧٢﴾
72. Na wale ambao hawashuhudii uongo, na wanapopita kwenye upuuzi hupita kwa heshima.
وَالَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ لَمْ يَخِرُّوا عَلَيْهَا صُمًّا وَعُمْيَانًا ﴿٧٣﴾
73. Na wale ambao wanapokumbushwa Aayaat za Rabb wao, hawapinduki kuzifanyia uziwi na upofu.
وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا ﴿٧٤﴾
74. Na wale wanaosema: Rabb wetu! Tutunukie katika wake zetu na dhuria wetu viburudisho vya macho yetu, na Tujaalie kuwa waongozi kwa wenye taqwa.
أُولَـٰئِكَ يُجْزَوْنَ الْغُرْفَةَ بِمَا صَبَرُوا وَيُلَقَّوْنَ فِيهَا تَحِيَّةً وَسَلَامًا ﴿٧٥﴾
75. Hao ndio watakaolipwa maghorofa ya juu (Jannah) kwa kuwa walisubiri, na watapokelewa humo kwa maamkizi na amani.
خَالِدِينَ فِيهَا ۚ حَسُنَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا ﴿٧٦﴾
76. Wadumu humo. Uzuri ulioje wa mahali pa kustakiri na makazi ya kuishi daima!
قُلْ مَا يَعْبَأُ بِكُمْ رَبِّي لَوْلَا دُعَاؤُكُمْ ۖ فَقَدْ كَذَّبْتُمْ فَسَوْفَ يَكُونُ لِزَامًا ﴿٧٧﴾
77. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Rabb wangu Asingekujalini lau kama si duaa zenu. Kwa yakini mmekadhibisha, basi adhabu itakuwa ya lazima kukugandeni tu!
[1] Maana ya Al-Furqaan: Pambanuo
Maana ya Furqaan kilugha ni kupambanua baina ya vitu viwili.
Ama kiistilahi, ni kupambanua baina ya haki na batili. Hivyo basi, ni kupambanua baina ya hidaaya na upotofu, baina ya imaan na kufru, baina ya shirki na Tawhiyd, baina ya Sunnah na bid’ah n.k.
Neno hili limetajwa katika Suwrat Al-Baqarah Aayah (2:53), (2:185). Na katika Al-Anfaal (8:41), imemaanishwa kupambanua baina ya makundi mawili; ya Waislamu na makafiri katika vita vya Badr. Hali kadhaalika, Furqaan imetajwa katika Al-Anbiyaa (21:48). Na inamaanisha pia baswiyrah (nuru za ilimu, utambuzi, umaizi) ambayo inapambanua baina yake na baina ya yaliyo kinyume chake, ambayo ni viza, ujinga, ujahili n.k.
[2] Kufru Za Washirikina Kumkanusha, Kumsingizia, Kumpachika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Sifa Kadhaa Ovu, Kumfanyia Istihzai Yeye Pamoja Na Kuifanyia Istihzai Qur-aan Na Kuikanusha:
Kuanzia Aayah hii namba (4) hadi namba (8), Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja kufru za washirikina kumkanusha Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), na kumsingizia, na kumpachika sifa ovu kadhaa. Na kwa ujumla, sifa ovu walizomsingizia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni zifuatazo:
(i) Mchawi:
Rejea Yuwnus (10:2), Al-Israa (17:47), Al-Anbiyaa (21:3), Suwrah hii Al-Furqaan (25:8), Swaad (38:4), Al-Muddath-thir (74:25).
(ii) Kuhani:
Rejea Al-Anbiyaa (21:5), Atw-Twuwr (52:30).
(iii) Mshairi:
Rejea Al-Hijr (15:6), Al-Muuminuwn (23:70), Asw-Swaaffaat (37:36), Ad-Dukhaan (44:14), Al-Qalam (68:51).
(iv) Majnuni na muongo:
Rejea Saba-a (34:8), Swaad (38:4).
Allaah (سبحانه وتعالى) Anawaraddi hao kwa Kauli Zake kwenye Al-A’raaf (7:184), Atw-Twuwr (52:29), Al-Haaqqah (69:40-43), Saba-a (34:46), Yaasiyn (36:70), Al-Qalam (68:2), At-Takwiyr (81:22).
Na kufru kama hizo pia zilikuwa za washirikina na makafiri wa awali, ambao nao waliwakanusha Rusuli (Mitume) wao kwa kauli kama hizo. Allaah (سبحانه وتعالى) Anathibitisha hayo katika Kauli Zake kadhaa kama katika Suwrah Adh-Dhaariyaat (51:52).
Na katika kuisingizia Qur-aan, kuifanyia istihzai na kuikanusha, madai yao yalikuwa kama ifuatavyo:
(i) Ameibuni, ameitunga, ni hekaya za awali, ndoto za mkorogano:
Rejea Aayah hii ya Al-Furqaan (25:4), (6), Al-Anbiyaa (21:5), Atw-Twuwr (52:30).
Rejea pia Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah katika Suwrah An-Nahl (16:103)
(ii) Ni Sihri (uchawi):
Rejea Al-An’aam (6:7), Al-Anbiyaa (21:3), Saba-a (34:42), Asw-Swaaffaat (37:15), Az-Zukhruf (43:30), Al-Ahqaaf (46:7), Al-Qamar (54:2), Al-Muddath-thir (74:24).
Lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Anaraddi kauli za hao makafiri na washirikina za kuikanusha na kuisingizia Qur-aan katika Kauli Zake mbalimbali. Miongoni mwazo ni katika Suwrah hii ya Al-Furqaan Aayah namba (6) kwamba Ameiteremsha Yeye Qur-aan; Muumba wa mbingu na ardhi na Mjuzi wa siri.
Na kwengineko kwingi katika Qur-aan, Allaah (سبحانه وتعالى) Ametaja aina kama hizo za kufru zao washirikina na makafiri, wa awali na wa zama za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) za kukanusha Rusuli Wake (عليهم السّلام) na kupinga Vitabu Vyake Vitukufu Alivyoviteremsha.
[3] Washirikina Kudai Waletewe Asiyekuwa Binaadam:
Hizi ni katika kauli za wakanushaji wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambazo kwazo walitilia doa Risala yake. Walipinga kwa kuuliza kwa nini asiwe ni Malaika au mfalme, au kwa nini Malaika hakuteremshwa kumsaidia, wakasema:
مَالِ هَـٰذَا الرَّسُولِ
“Ni Rasuli gani huyu?”
Yaani: Ni nani huyu anayedai Urasuli? Wamesema hivyo kukusudia dhihaka na kumfanyia istihzai.
Wakasema pia:
يَأْكُلُ الطَّعَامَ
“Anakula chakula.”
Ilhali hii ni sifa mojawapo ya wanaadam.
Wakadai: Kwa nini asitumwe Malaika ambaye hali chakula na hahitaji mambo wanayoyahitajia wanaadam?
Wakaendelea kusema:
وَيَمْشِي فِي الْأَسْوَاقِ ۙ
“Na anatembea masokoni!”
Yaani: Kuuza na kununua.
Kwa mujibu wa madai yao, wamekusudia kuwa hayafai haya kwa Rasuli ilhali Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
وَمَا أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ مِنَ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا إِنَّهُمْ لَيَأْكُلُونَ الطَّعَامَ وَيَمْشُونَ فِي الْأَسْوَاقِ ۗ
“Na Hatukupeleka kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Rusuli wowote isipokuwa bila shaka wakila chakula, na wanatembea masokoni.” [Al-Furqaan (25:20)]
Wakaendelea kusema:
لَوْلَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مَلَكٌ
“Kwa nini asiteremshiwe Malaika.”
Yaani: Kwa nini asiteremshwe Malaika pamoja naye kumsaidia?
فَيَكُونَ مَعَهُ نَذِيرًا ﴿٧﴾
“Akawa muonyaji pamoja naye? “
Kutokana na madai yao, wamekusudia kwamba Rasuli hatoshelezi kubalighisha Risala (Ujumbe) na hakuwa na uwezo wa kutekeleza Risala. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Rejea pia Al-Israa (17:90-94) kwenye madai kama hayo ya washirikina kutaka wateremshiwe asiyekuwa binaadam.
Pia Allaah (سبحانه وتعالى) Ametaja kufru zao hizo katika Aayah nyenginezo na Akaraddi kauli zao. Rejea katika Suwrah hii Al-Furqaan (25:20), na rejea pia Al-An’aam (6:8-9) na Al-Anbiyaa (21:8). Na Akawaraddi Manaswara pia waliomfanya Nabii wao kuwa ni mwabudiwa. Rejea Al-Maaidah (5:75).
Na makafiri wa awali pia waliwakanusha Rusuli wao kwa madai kama hayo. Rejea Al-Muuminuwn (23:33-34) kujua baadhi ya kufru zao.
[4] Majaribio (Na Mitihani) Baina Ya Watu:
Rasuli anakuwa ni majaribio na mtihani kwa watu ambao ametumwa kuwafikishia Ujumbe. Ni majaribio na mtihani pia kwa watakaomkubali (wabebe makalifisho) na watakaomkataa (wafanye watakavyo wao). Na Rusuli wote Allaah Aliwapa mtihani na majaribio ya kuwalingania watu.
Na tajiri ni jaribio na mtihani kwa maskini, na maskini pia ni jaribio na mtihani kwa tajiri na kadhalika. Aina zote za watu hapa duniani ni majaribio na mtihani baina yao, kwani dunia ni nyumba ya fitnah, majaribio na mitihani. [Tafsiyr As-Sa’diy].
Kuhusu kauli ya kwanza iliyotangulia katika Aayah hii kuwa Rusuli wote walikuwa ni binaadam wanaokula na kunywa, rejea Suwrah hii Al-Furqaan Aayah namba (7).
[6] Marufuku Kwa Washirikina Na Makafiri Kupata Mafanikio:
Siku watakapowaona Malaika wakati wa kufariki kwao, na wakiwa ndani ya makaburi yao, na Siku ya Qiyaamah, kwa sura ambayo siyo ile waliyoitaka. Sio kuwapa bishara ya Jannah (Pepo), lakini kuwaambia: “Allaah Ameifanya Jannah ni mahali palipoharamishwa kwenu.” [Tafsiyr Al-Muyassar]
[7] Amali Ambazo Hazina Dalili Ni Batili Hivyo Hazipokelewi:
Rejea Al-Kahf (18:103), Az-Zumar (39:65).
[8] Malaika Na Allaah Watateremka Siku Ya Qiyaamah:
Rejea Al-Haaqqah (69:13-18), Al-Fajr (89:21-22), Al-Baqarah (2:210), Al-An’aam (6:158).
Ikumbuke ee Rasuli! Siku hiyo ambayo mbingu zitapasukapasuka, na yatatokeza kupitia mianya ya mipasuko yake mawingu meupe yaliyo membamba. Na Siku hiyo, Allaah (سبحانه وتعالى) Atawateremsha Malaika wa mbinguni wawazunguke viumbe katika sehemu walipokusanywa wote (mahshar), na kisha Aje Allaah (تبارك وتعالى), ujio unaolingana na Utukufu Wake, kuwahukumu waja. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[9] Sababu Ya Kuteremshwa Aayah/Majuto Ya Mtu Kwa Kumfuata Shaytwaan Na Watu Waovu:
Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
025-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Furqaan Aayah 27-29: وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ [211]
Aayah hii hadi namba (29), zinataja jinsi mtu anavyojuta kwa kutokumfuata Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na badala yake akamfuata shaytwaan na rafiki muovu.
Tafsiyr za Aayah hizo:
Na ikumbuke ee Rasuli! Siku ambayo mwenye kujidhulumu nafsi yake ataiuma mikono yake kwa majuto na maunguliko kwa kusema: “Laiti mimi niliandamana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na nikamfuata katika kuufanya Uislamu kuwa ni njia ya Peponi.” Na atasema kwa maunguliko: “Laiti mimi sikumfanya fulani kuwa ni rafiki mwandani wa kumfuata na kumpenda. Amenipoteza rafiki huyu na kuniepusha na Qur-aan baada ya kunijia.” Na shaytwaan aliyefukuzwa kwenye Rehma ya Allaah amekuwa daima ni mwenye kumtupa na kumwacha mkono mwanaadam.
Katika Aayah hizi, kuna onyo kwamba rafiki mbaya asifuatwe, kwani yeye huenda akawa ni sababu ya kumtia motoni yule anayefuatana naye. [Tafsiyr Al-Muyassar].
Rejea pia Asw-Swaaffaat (37:50-57) ambako rafiki aliyeepukana na rafiki muovu akaingizwa Peponi, anashukuru kutokumfuata rafiki muovu aliyekuwa motoni kwa kuwa alitaka kumpotosha.
Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amenasihi kufuatana na rafiki mwema na kuepukana na rafiki muovu akapiga mfano baina yao:
عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِنَّمَا مَثَلُ الْجَلِيسِ الصَّالِحِ وَالسَّوْءِ كَحَامِلِ الْمِسْكِ وَنَافِخِ الْكِيرِ. فَحَامِلُ الْمِسْكِ إِمَّا أَنْ يُحْذِيَكَ، وَإِمَّا أَنْ تَبْتَاعَ مِنْهُ، وَإِمَّا أَنْ تَجِدَ مِنْهُ رِيحًا طَيِّبَةً. وَنَافِخُ الْكِيرِ إِمَّا أَنْ يُحْرِقَ ثِيَابَكَ، وَإِمَّا أَنْ تَجِدَ مِنْهُ رِيحًا مُنْتِنَةً)) متفق عليه
Amesimulia Abuu Muwsaa Al-Ash-‘ariyyi (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika mfano wa mtu mwema anayekaa na watu, na mtu mwovu anayekaa na watu, ni kama mfano wa mbebaji miski na (mfua chuma) anayevuvia kipulizo. Mbebaji miski, ima atakupa, au utanunua kutoka kwake, au utapata harufu nzuri kwake. Ama anayevuvia kipulizo, ima atachoma nguo zako, au utapata harufu mbaya kutoka kwake.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
[10] Kuihama Qur-aan Ni Kuipuuza Na Kutokufuata Yaliyoamrishwa:
Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwita Rabb wake kumlalamikia na kumsikitikia kupuuzwa na watu wake katika yale aliyoyaleta. Akasema: Ee Rabb wangu! Hakika watu wangu ambao Umenituma kwao ili niwaongoze na kuwabalighishia Risala, wameihama hii Qur-aan. Yaani: Wameipuuza, wameikwepa, na wakaiacha ilhali wajibu ulio juu yao ni kuzitii hukmu zake, kuzitekeleza sharia zake na kuyafuata yote yaliyomo ndani yake. [Tafsiyr As-Sa’diy].
Kuihama pia inamaanisha kuipuuza kwa kutokuisoma, kwani baadhi ya Salaf wamefafanua maana ya watu kuihama na kupuuza Qur-aan kama ifuatavyo:
(i) Wasioisoma kabisa.
(ii) Wanaoisoma lakini hawajifunzi maana yake.
(iii) Wanaoisoma na kujifunza maana yake lakini hawafuati maamrisho yake na hawajiepushi na makatazo yake.
[11] Hikma Ya Qur-aan Kuteremshwa Kidogo Kidogo
Rejea Alhidaaya.com: Hikmah Ya Kuteremshwa Qur-aan Kidogo Kidogo Wakati Mbali Mbali [212]
[12] Makafiri Watakusanywa Juu Ya Nyuso Zao Waelekee Jahannam:
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا يُونُسُ بْنُ مُحَمَّدٍ الْبَغْدَادِيُّ، حَدَّثَنَا شَيْبَانُ، عَنْ قَتَادَةَ، حَدَّثَنَا أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ ـ رضى الله عنه أَنَّ رَجُلاً، قَالَ يَا نَبِيَّ اللَّهِ كَيْفَ يُحْشَرُ الْكَافِرُ عَلَى وَجْهِهِ قَالَ " أَلَيْسَ الَّذِي أَمْشَاهُ عَلَى الرِّجْلَيْنِ فِي الدُّنْيَا قَادِرًا عَلَى أَنَّ يُمْشِيَهُ عَلَى وَجْهِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ". قَالَ قَتَادَةُ بَلَى وَعِزَّةِ رَبِّنَا.
Amesimulia Qataadah (رضي الله عنه): Anas bin Maalik (رضي الله عنه) amesema: Mtu mmoja alisema: Ee Nabii wa Allaah! Vipi kafiri atakusanywa juu ya uso wake? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Je, kwani Yule Aliyemfanya kutembea kwa miguu yake duniani Hana uwezo wa kumfanya atembee kwa uso wake Siku ya Qiyaamah?” Qataadah amesema: “Bali Naam! Kwa Utukufu wa Rabb wetu.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Rejea pia Al-Israa (17:97).
[13] Watu Wa Ar-Rass:
Ar-Rass imesemekana kuwa ni kisima kwa mujibu wa Tafsiyr ya Ibn Kathiyr. Lakini kuhusu watu wa Ar-Rass, ‘Ulamaa wamekhitilafiana. Na hakuna dalili iliyothibiti kuelezewa ni watu gani. Hivyo basi, Rasuli aliyetumwa kwa watu hao, ni miongoni mwa Rusuli ambao Allaah (سبحانه وتعالى) Hakuwasimulia visa vyao kama Anavyosema katika Suwrah Ghaafir (40:78) na An-Nisaa (4:164). Naye Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Awajuaye zaidi. Imetajwa Watu wa Ar-Rass katika Suwrah hii na katika Qaaf (50:12).
[14] Hawaa (Matamanio) Ya Mtu Kuwa Ndio Mwabudiwa:
Uislamu ni kujisalimisha kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa utii. Ina maana: Mja asiwe na mashaka yoyote kuhusu Amri za Allaah (سبحانه وتعالى) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم). Na pia akubali kwa kuridhia Amri za Rabb Wake na amri za Rasuli Wake katika vipengele vyote vya maisha. Huu ndio msingi wa Uislamu. Yeyote atakaepinga Sharia za Allaah kwa maoni yake, basi atakuwa hakujisalimisha kwa Allaah, bali yeye ni mtumwa tu wa hawaa (matamanio) zake, na yeye ndie yule aliyekusudiwa katika Kauli hii ya Allaah (سبحانه وتعالى):
أَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهُ
“Je, umemuona yule aliyefanya hawaa yake kuwa ndio mwabudiwa wake?”
Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameonya:
عَنْ أَبِي مُحَمَّدٍ عَبْدِ اللَّهِ بِنْ عَمْرُو بِنْ العَاصِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم: ((لا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يَكُونَ هَوَاهُ تَبَعَاً لِمَا جِئْتُ بِهِ)) حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ، رَوَيْنَاهُ فِي كِتَابِ الْحُجَّةِ بِإِسْنَادٍ صَحِيحٍ.
Amesimulia Abuu Muhammad ‘Abdillaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hatoamini mmoja wenu mpaka hawaa (matamanio) zake zitakapomili kutii yale niliyokuja nayo.” [Hadiyth Hasan Swahiyh, katika Kitabu “Al-Hujjah” kwa Isnaad Swahiyh]
Rejea pia Al-Jaathiyah (45:23).
[15] Allaah (سبحانه وتعالى) Anahuisha Ardhi Iliyokufa; Ni Kama Mfano Wa Kufufuliwa Watu:
Rejea Al-An’aam (6:95), Ar-Ruwm (30:50), Yaasiyn (36:33).
[17] Istawaa اسْتَوَى
Yuko juu kwa namna inayolingana na Uadhama na Ujalali Wake Yeye Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-A'raaf (7:54) kwenye maelezo bayana ya maana yake, yenye kutofautiana na maana ya katika Suwrah Al-Baqarah (2:29) na Suwrat Fusswilat (41:11).
[18] Makafiri Walipinga Jina La Ar-Rahmaan:
Bonyeza kiungo kifuatacho ambapo kumetajwa sababu ya kuteremshwa Aayah kuhusiana na haya.
[19] Maana Ya Buruji:
‘Ulamaa wana rai kadhaa kuhusu maana ya buruji. Rejea Al-Buruwj (85:1) kwenye maelezo bayana ya maana yake.
[20] Waja Wa Ar-Rahmaan Na Sifa Zao:
Kuanzia Aayah hii (25:63) hadi (25:76), Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja Sifa njema za Waja Wake.
[21] Qiyaamul-Layl: (Kisimamo Cha Usiku) Kwa Ajili Ya Ibaada:
Rejea Al-Israa (17:79), As-Sajdah (32:17). Pia rejea Adh-Dhaariyaat (51:15-19) ambapo fadhila zake zimetajwa. Rejea pia Az-Zumar (39:9), Aal-‘Imraan (3:17), (3:113) na Al-Muzzammil: (73:2).
[22] Tofauti Kati Ya Israfu Na Ubadhirifu. Rejea Al-Israa (17:26).
[24] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
025-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Furqaan Aayah 70: إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا [215]
[25] Tawbah Ya Kikweli Na Fadhila Zake:
Rejea Huwd (11:3) kwenye faida tele za istighfaar na tawbah. Rejea pia At-Tahriym (66:8) kwenye faida kuhusu tawbah ya kikweli na masharti yake.
الشُّعَرآء
026-Ash-Shu’araa
026-Ash-Shu’araa: Utangulizi Wa Suwrah [217]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
طسم ﴿١﴾
1. Twaa Siyn Miym.[1]
تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿٢﴾
2. Hizi ni Aayaat za Kitabu kilicho bayana.
لَعَلَّكَ بَاخِعٌ نَّفْسَكَ أَلَّا يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ ﴿٣﴾
3. Huenda utaiangamiza nafsi yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) (kwa sikitiko) kwamba hawawi wenye kuamini.
إِن نَّشَأْ نُنَزِّلْ عَلَيْهِم مِّنَ السَّمَاءِ آيَةً فَظَلَّتْ أَعْنَاقُهُمْ لَهَا خَاضِعِينَ ﴿٤﴾
4. Tungetaka Tungewateremshia kutoka mbinguni Aayah (Muujiza), kisha zingebakia shingo zao zenye kuunyenyekea.
وَمَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ مُحْدَثٍ إِلَّا كَانُوا عَنْهُ مُعْرِضِينَ ﴿٥﴾
5. Na hauwafikii ukumbusho wowote ule mpya kutoka kwa Ar-Rahmaan isipokuwa walikuwa ni wenye kuupuuza.
فَقَدْ كَذَّبُوا فَسَيَأْتِيهِمْ أَنبَاءُ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٦﴾
6. Kwa yakini wamekadhibisha, basi itawafikia khabari ya yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.
أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَى الْأَرْضِ كَمْ أَنبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ ﴿٧﴾
7. Je, hawaioni ardhi? Mimea mingapi Tumeiotesha humo ya kila aina nzuri?
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٨﴾
8. Hakika katika hayo pana Aayah (Ishara),[2] lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿٩﴾
9. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu.
وَإِذْ نَادَىٰ رَبُّكَ مُوسَىٰ أَنِ ائْتِ الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿١٠﴾
10. Na Rabb wako Alipomwita Muwsaa kwamba: Nenda kwa watu madhalimu.[3]
قَوْمَ فِرْعَوْنَ ۚ أَلَا يَتَّقُونَ ﴿١١﴾
11. Watu wa Firawni. Je, hawamchi Allaah?
قَالَ رَبِّ إِنِّي أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ ﴿١٢﴾
12. (Muwsaa) akasema: Rabb wangu! Hakika mimi nakhofu wasije kunikadhibisha.
وَيَضِيقُ صَدْرِي وَلَا يَنطَلِقُ لِسَانِي فَأَرْسِلْ إِلَىٰ هَارُونَ ﴿١٣﴾
13. Na kifua changu kinadhikika, na ulimi wangu haukunjuki vizuri, basi Tuma (Jibriyl na Wahyi) kwa Haaruwn (aje kunisaidia).
وَلَهُمْ عَلَيَّ ذَنبٌ فَأَخَافُ أَن يَقْتُلُونِ ﴿١٤﴾
14. Nao wana shtaka la kosa dhidi yangu, basi nakhofu wasiniue.
قَالَ كَلَّا ۖ فَاذْهَبَا بِآيَاتِنَا ۖ إِنَّا مَعَكُم مُّسْتَمِعُونَ ﴿١٥﴾
15. (Allaah) Akasema: Hapana! Nendeni na Aayaat (Miujiza) Yetu, hakika Sisi Tuko pamoja nanyi Wenye Kusikiliza.
فَأْتِيَا فِرْعَوْنَ فَقُولَا إِنَّا رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦﴾
16. Basi mfikieni Firawni, na mseme: Hakika sisi ni Rasuli wa Rabb wa walimwengu.
أَنْ أَرْسِلْ مَعَنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿١٧﴾
17. Ya kwamba waachilie wana wa Israaiyl wende pamoja nasi.
قَالَ أَلَمْ نُرَبِّكَ فِينَا وَلِيدًا وَلَبِثْتَ فِينَا مِنْ عُمُرِكَ سِنِينَ ﴿١٨﴾
18. (Fira’wn) akasema: Je, hatukukulea kwetu ulipokuwa mtoto, na ukaishi kwetu miaka mingi ya umri wako?
وَفَعَلْتَ فَعْلَتَكَ الَّتِي فَعَلْتَ وَأَنتَ مِنَ الْكَافِرِينَ ﴿١٩﴾
19. Na ukafanya kitendo chako ambacho ulikifanya nawe ni miongoni mwa wasio na shukurani.
قَالَ فَعَلْتُهَا إِذًا وَأَنَا مِنَ الضَّالِّينَ ﴿٢٠﴾
20. (Muwsaa) akasema: Nilikifanya hapo wakati nilikuwa miongoni mwa waliokosea.
فَفَرَرْتُ مِنكُمْ لَمَّا خِفْتُكُمْ فَوَهَبَ لِي رَبِّي حُكْمًا وَجَعَلَنِي مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٢١﴾
21. Nikakukimbieni nilipokukhofuni, na Rabb wangu Akanitunukia hikmah na Akanijaalia miongoni mwa Rusuli.
وَتِلْكَ نِعْمَةٌ تَمُنُّهَا عَلَيَّ أَنْ عَبَّدتَّ بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿٢٢﴾
22. Na hiyo ni neema unayonisimbulia, na wewe umewatia utumwani wana wa Israaiyl.
قَالَ فِرْعَوْنُ وَمَا رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٢٣﴾
23. Firawni akasema: Na ni nani kwani Rabb wa walimwengu?
قَالَ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ ﴿٢٤﴾
24. (Muwsaa) akasema: Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake mkiwa ni wenye yakini.
قَالَ لِمَنْ حَوْلَهُ أَلَا تَسْتَمِعُونَ ﴿٢٥﴾
25. (Firawni) akawaambia waliomzunguka: Hivi mnasikia?
قَالَ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ ﴿٢٦﴾
26. (Muwsaa) akasema: Rabb wenu na Rabb wa baba zenu wa awali.
قَالَ إِنَّ رَسُولَكُمُ الَّذِي أُرْسِلَ إِلَيْكُمْ لَمَجْنُونٌ ﴿٢٧﴾
27. (Firawni) akasema: Hakika Rasuli wenu ambaye ametumwa kwenu bila shaka ni majnuni.
قَالَ رَبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٢٨﴾
28. (Muwsaa) akasema: Rabb wa Mashariki na Magharibi na vilivyo baina yake, mkiwa nyinyi ni wenye kutia akilini.
قَالَ لَئِنِ اتَّخَذْتَ إِلَـٰهًا غَيْرِي لَأَجْعَلَنَّكَ مِنَ الْمَسْجُونِينَ ﴿٢٩﴾
29. (Firawni) akasema: Ukichagua mwabudiwa mwengine badala yangu, nitakufanya bila shaka miongoni mwa wafungwao gerezani.
قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكَ بِشَيْءٍ مُّبِينٍ ﴿٣٠﴾
30. (Muwsaa) akasema: Je, hata kama nikikujia na kitu bayana?
قَالَ فَأْتِ بِهِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٣١﴾
31. (Firawni) akasema: Kilete ukiwa wewe ni miongoni mwa wakweli.
فَأَلْقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعْبَانٌ مُّبِينٌ ﴿٣٢﴾
32. (Muwsaa) akatupa fimbo yake, tahamaki hiyo ikawa joka kubwa bayana.
وَنَزَعَ يَدَهُ فَإِذَا هِيَ بَيْضَاءُ لِلنَّاظِرِينَ ﴿٣٣﴾
33. Na akavuta mkono wake, tahamaki huo ukawa mweupe kwa watazamao.
قَالَ لِلْمَلَإِ حَوْلَهُ إِنَّ هَـٰذَا لَسَاحِرٌ عَلِيمٌ ﴿٣٤﴾
34. (Firawni) akawaambia wakuu waliomzunguka: Hakika huyu bila shaka ni mchawi mjuzi.[4]
يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُم بِسِحْرِهِ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ ﴿٣٥﴾
35. Anataka kukutoeni kutoka ardhi yenu kwa sihiri yake, basi mnashauri nini?
قَالُوا أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَابْعَثْ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ ﴿٣٦﴾
36. Wakasema: Muakhirishe kidogo na kaka yake, na tuma katika miji wakusanyao wachawi.
يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَحَّارٍ عَلِيمٍ ﴿٣٧﴾
37. Watakujia na kila mchawi mjuzi.
فَجُمِعَ السَّحَرَةُ لِمِيقَاتِ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ ﴿٣٨﴾
38. Basi wakakusanywa wachawi katika mahali na wakati wa siku maalumu.
وَقِيلَ لِلنَّاسِ هَلْ أَنتُم مُّجْتَمِعُونَ ﴿٣٩﴾
39. Na wakaambiwa watu: Je, mmekwishakusanyika?
لَعَلَّنَا نَتَّبِعُ السَّحَرَةَ إِن كَانُوا هُمُ الْغَالِبِينَ ﴿٤٠﴾
40. Ili tuwafuate wachawi, wakiwa wao ndio watakaoshinda.
فَلَمَّا جَاءَ السَّحَرَةُ قَالُوا لِفِرْعَوْنَ أَئِنَّ لَنَا لَأَجْرًا إِن كُنَّا نَحْنُ الْغَالِبِينَ ﴿٤١﴾
41. Basi walipokuja wachawi walimwambia Firawni: Je, tutapata ujira wowote ikiwa sisi tutakuwa wenye kushinda?
قَالَ نَعَمْ وَإِنَّكُمْ إِذًا لَّمِنَ الْمُقَرَّبِينَ ﴿٤٢﴾
42. (Firawni) akasema: Naam! Na bila shaka nyinyi hapo mtakuwa miongoni mwa waliokurubishwa (kwangu).
قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ أَلْقُوا مَا أَنتُم مُّلْقُونَ ﴿٤٣﴾
43. Muwsaa akawaambia: Tupeni vile mnavyotupa.
فَأَلْقَوْا حِبَالَهُمْ وَعِصِيَّهُمْ وَقَالُوا بِعِزَّةِ فِرْعَوْنَ إِنَّا لَنَحْنُ الْغَالِبُونَ ﴿٤٤﴾
44. Wakatupa kamba zao na fimbo zao, na wakasema: Kwa utukufu wa Firawni! Hakika sisi ni wenye kushinda.
فَأَلْقَىٰ مُوسَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ ﴿٤٥﴾
45. Muwsaa akatupa fimbo yake, tahamaki inameza vyote walivyovizua.
فَأُلْقِيَ السَّحَرَةُ سَاجِدِينَ ﴿٤٦﴾
46. Basi wachawi wakajikuta wameanguka huku wakisujudu.
قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٤٧﴾
47. Wakasema: Tumemwamini Rabb wa walimwengu.
رَبِّ مُوسَىٰ وَهَارُونَ ﴿٤٨﴾
48. Rabb wa Muwsaa na Haaruwn.
قَالَ آمَنتُمْ لَهُ قَبْلَ أَنْ آذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّهُ لَكَبِيرُكُمُ الَّذِي عَلَّمَكُمُ السِّحْرَ فَلَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ۚ لَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَافٍ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٤٩﴾
49. (Firawni) akasema: Je, mmemwamini kabla sijakupeni idhini? Hakika bila shaka yeye ndiye mkubwa wenu aliyekufunzeni sihiri. Basi mtakuja kujua. Nitakukatenikateni mikono yenu na miguu yenu kinyume (kulia kwa kushoto), kisha nitakusulubuni nyote.
قَالُوا لَا ضَيْرَ ۖ إِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ ﴿٥٠﴾
50. Wakasema: Hakuna dhara yoyote! Hakika sisi tunarudi kwa Rabb wetu.
إِنَّا نَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لَنَا رَبُّنَا خَطَايَانَا أَن كُنَّا أَوَّلَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٥١﴾
51. Hakika sisi tunatumai kwamba Rabb wetu Atatughufuria madhambi yetu kwa vile tumekuwa wa kwanza wenye kuamini.
وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنْ أَسْرِ بِعِبَادِي إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ ﴿٥٢﴾
52. Na Tukamfunulia Wahy Muwsaa kwamba: Safiri usiku pamoja na Waja Wangu, hakika nyinyi ni wenye kufuatwa.
فَأَرْسَلَ فِرْعَوْنُ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ ﴿٥٣﴾
53. Basi Firawni akawatuma wakusanyao wachawi katika miji.
إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ لَشِرْذِمَةٌ قَلِيلُونَ ﴿٥٤﴾
54. (Akisema): Hakika hawa ni kikundi kidhaifu kidogo, wachache.
وَإِنَّهُمْ لَنَا لَغَائِظُونَ ﴿٥٥﴾
55. Na hakika wao wanatughadhibisha.
وَإِنَّا لَجَمِيعٌ حَاذِرُونَ ﴿٥٦﴾
56. Na hakika sisi, bila shaka ni wengi wenye kuchukua hadhari mno.
فَأَخْرَجْنَاهُم مِّن جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ ﴿٥٧﴾
57. Basi Tukawatoa katika mabustani na chemchemu.
وَكُنُوزٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ ﴿٥٨﴾
58. Na hazina za aina kwa aina na vyeo vya heshima.
كَذَٰلِكَ وَأَوْرَثْنَاهَا بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿٥٩﴾
59. Hivyo ndivyo (Tulivyofanya), na Tukayarithisha hayo wana wa Israaiyl.
فَأَتْبَعُوهُم مُّشْرِقِينَ ﴿٦٠﴾
60. Basi wakawafuata walipopambazukiwa.
فَلَمَّا تَرَاءَى الْجَمْعَانِ قَالَ أَصْحَابُ مُوسَىٰ إِنَّا لَمُدْرَكُونَ ﴿٦١﴾
61. Yalipoonana makundi mawili, wakasema watu wa Muwsaa: Hakika sisi bila shaka tutadirikiwa kukamatwa.
قَالَ كَلَّا ۖ إِنَّ مَعِيَ رَبِّي سَيَهْدِينِ ﴿٦٢﴾
62. (Muwsaa) akasema: Hapana! Hakika Rabb wangu Yu pamoja nami Ataniongoza.
فَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنِ اضْرِب بِّعَصَاكَ الْبَحْرَ ۖ فَانفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرْقٍ كَالطَّوْدِ الْعَظِيمِ ﴿٦٣﴾
63. Tukamfunulia Wahy Muwsaa kwamba: Piga kwa fimbo yako bahari. Basi ikatengana ikawa kila sehemu kama jabali kubwa mno.
وَأَزْلَفْنَا ثَمَّ الْآخَرِينَ ﴿٦٤﴾
64. Na Tukawaleta karibu hapo wengine.
وَأَنجَيْنَا مُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُ أَجْمَعِينَ ﴿٦٥﴾
65. Tukamuokoa Muwsaa na walio pamoja naye wote.
ثُمَّ أَغْرَقْنَا الْآخَرِينَ ﴿٦٦﴾
66. Kisha Tukawagharikisha wengine.
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٦٧﴾
67. Hakika katika hayo pana Aayah (Ishara), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿٦٨﴾
68. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu.
وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ إِبْرَاهِيمَ ﴿٦٩﴾
69. Na wasomee (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) khabari za Ibraahiym.
إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ مَا تَعْبُدُونَ ﴿٧٠﴾
70. Alipomwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini?
قَالُوا نَعْبُدُ أَصْنَامًا فَنَظَلُّ لَهَا عَاكِفِينَ ﴿٧١﴾
71. Wakasema: Tunaabudu masanamu, na tutaendelea kuyakalia kwa kuyaabudu.
قَالَ هَلْ يَسْمَعُونَكُمْ إِذْ تَدْعُونَ ﴿٧٢﴾
72. Akasema: Je, yanakusikieni mnapoyaomba?
أَوْ يَنفَعُونَكُمْ أَوْ يَضُرُّونَ ﴿٧٣﴾
73. Au yanakunufaisheni au yanakudhuruni?
قَالُوا بَلْ وَجَدْنَا آبَاءَنَا كَذَٰلِكَ يَفْعَلُونَ ﴿٧٤﴾
74. Wakasema: Bali tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo.
قَالَ أَفَرَأَيْتُم مَّا كُنتُمْ تَعْبُدُونَ ﴿٧٥﴾
75. Akasema: Je, mnaona hivyo mlivyokuwa mkiviabudu?
أَنتُمْ وَآبَاؤُكُمُ الْأَقْدَمُونَ ﴿٧٦﴾
76. Nyinyi na baba zenu waliotangulia?
فَإِنَّهُمْ عَدُوٌّ لِّي إِلَّا رَبَّ الْعَالَمِينَ ﴿٧٧﴾
77. Basi hakika hao ni adui zangu isipokuwa Rabb wa walimwengu.
الَّذِي خَلَقَنِي فَهُوَ يَهْدِينِ ﴿٧٨﴾
78. Ambaye Ameniumba, Naye Ananiongoza.
وَالَّذِي هُوَ يُطْعِمُنِي وَيَسْقِينِ ﴿٧٩﴾
79. Na Ambaye Ndiye Anayenilisha na Ananinywesha.
وَإِذَا مَرِضْتُ فَهُوَ يَشْفِينِ ﴿٨٠﴾
80. Na ninapokuwa mgonjwa, basi Yeye Ananiponyesha.
وَالَّذِي يُمِيتُنِي ثُمَّ يُحْيِينِ ﴿٨١﴾
81. Na Ambaye Atanifisha kisha Atanihuisha.
وَالَّذِي أَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لِي خَطِيئَتِي يَوْمَ الدِّينِ ﴿٨٢﴾
82. Na Ambaye natumai Atanighufuria makosa yangu Siku ya Malipo.
رَبِّ هَبْ لِي حُكْمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ ﴿٨٣﴾
83. Rabb wangu! Nitunukie hukma,[5] na Unikutanishe na Swalihina.
وَاجْعَل لِّي لِسَانَ صِدْقٍ فِي الْآخِرِينَ ﴿٨٤﴾
84. Na Nijaalie kusifika kwa heshima kwa vizazi watakaokuja baadaye.
وَاجْعَلْنِي مِن وَرَثَةِ جَنَّةِ النَّعِيمِ ﴿٨٥﴾
85. Na Nijaalie miongoni mwa warithi wa Jannah ya Neema.
وَاغْفِرْ لِأَبِي إِنَّهُ كَانَ مِنَ الضَّالِّينَ ﴿٨٦﴾
86. Na Mghufurie baba yangu, hakika yeye amekuwa miongoni mwa waliopotea.
وَلَا تُخْزِنِي يَوْمَ يُبْعَثُونَ ﴿٨٧﴾
87. Na wala Usinihizi Siku watakayofufuliwa.
يَوْمَ لَا يَنفَعُ مَالٌ وَلَا بَنُونَ ﴿٨٨﴾
88. Siku hayatofaa mali wala watoto.
إِلَّا مَنْ أَتَى اللَّـهَ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ ﴿٨٩﴾
89. Isipokuwa yule atakayemfikia Allaah na moyo uliosalimika.[6]
وَأُزْلِفَتِ الْجَنَّةُ لِلْمُتَّقِينَ ﴿٩٠﴾
90. Na itakurubishwa Jannah kwa wenye taqwa.
وَبُرِّزَتِ الْجَحِيمُ لِلْغَاوِينَ ﴿٩١﴾
91. Na utadhihirishwa moto uwakao vikali mno kwa wapotofu.
وَقِيلَ لَهُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ تَعْبُدُونَ ﴿٩٢﴾
92. Na wataambiwa: Wako wapi wale mliokuwa mkiwaabudu?
مِن دُونِ اللَّـهِ هَلْ يَنصُرُونَكُمْ أَوْ يَنتَصِرُونَ ﴿٩٣﴾
93. Badala ya Allaah. Je, wataweza kukunusuruni au kujinusuru wenyewe?
فَكُبْكِبُوا فِيهَا هُمْ وَالْغَاوُونَ ﴿٩٤﴾
94. Watapinduliwa gubigubi humo wao na wapotofu.
وَجُنُودُ إِبْلِيسَ أَجْمَعُونَ ﴿٩٥﴾
95. Na majeshi ya Ibliys yote.
قَالُوا وَهُمْ فِيهَا يَخْتَصِمُونَ ﴿٩٦﴾
96. Watasema na huku wao wanagombana humo.
تَاللَّـهِ إِن كُنَّا لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٩٧﴾
97. Wa-Allaahi! Hakika tulikuwa bila shaka katika upotofu bayana.
إِذْ نُسَوِّيكُم بِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٩٨﴾
98. Tulipokusawazisheni na Rabb wa walimwengu.
وَمَا أَضَلَّنَا إِلَّا الْمُجْرِمُونَ ﴿٩٩﴾
99. Na hakuna aliyetupoteza isipokuwa wahalifu.
فَمَا لَنَا مِن شَافِعِينَ ﴿١٠٠﴾
100. Basi hatuna waombezi wowote.
وَلَا صَدِيقٍ حَمِيمٍ ﴿١٠١﴾
101. Wala rafiki khalisi.
فَلَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٠٢﴾
102. Basi lau tungelikuwa tuna fursa ya kurudi (duniani) tungekuwa miongoni mwa Waumini.
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٠٣﴾
103. Hakika katika hayo pana Aayah (Ishara), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿١٠٤﴾
104. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu.
كَذَّبَتْ قَوْمُ نُوحٍ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٠٥﴾
105. Watu wa Nuwh waliwakadhibisha Rusuli.
إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ نُوحٌ أَلَا تَتَّقُونَ ﴿١٠٦﴾
106. Alipowaambia ndugu yao Nuwh: Je, hamtokuwa na taqwa?
إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ ﴿١٠٧﴾
107. Hakika mimi kwenu ni Rasuli mwaminifu.
فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١٠٨﴾
108. Basi mcheni Allaah na nitiini.
وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٠٩﴾
109. Na wala sikuombeni ujira wowote juu yake. Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Rabb wa walimwengu.
فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١١٠﴾
110. Basi mcheni Allaah na nitiini.
قَالُوا أَنُؤْمِنُ لَكَ وَاتَّبَعَكَ الْأَرْذَلُونَ ﴿١١١﴾
111. Wakasema: Je, tukuamini na hali kuwa waliokufuata ni watu duni?
قَالَ وَمَا عِلْمِي بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١١٢﴾
112. Akasema: Na najuaje waliyokuwa wanayatenda?
إِنْ حِسَابُهُمْ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّي ۖ لَوْ تَشْعُرُونَ ﴿١١٣﴾
113. Hesabu yao haiko isipokuwa kwa Rabb wangu, lau mngetambua.
وَمَا أَنَا بِطَارِدِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١١٤﴾
114. Nami sitowafukuza walioamini.
إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿١١٥﴾
115. Mimi sina kingine zaidi ya kuwa mwonyaji mbainishaji.
قَالُوا لَئِن لَّمْ تَنتَهِ يَا نُوحُ لَتَكُونَنَّ مِنَ الْمَرْجُومِينَ ﴿١١٦﴾
116. Wakasema: Usipoacha ewe Nuwh bila shaka utakuwa miongoni mwa wenye kurajimiwa.
قَالَ رَبِّ إِنَّ قَوْمِي كَذَّبُونِ ﴿١١٧﴾
117. Akasema: Rabb wangu! Hakika watu wangu wamenikadhibisha.
فَافْتَحْ بَيْنِي وَبَيْنَهُمْ فَتْحًا وَنَجِّنِي وَمَن مَّعِيَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١١٨﴾
118. Basi Hukumu baina yangu na baina yao (kwa) Hukmu (Yako), na Uniokoe mimi na wale walio pamoja nami miongoni mwa Waumini.
فَأَنجَيْنَاهُ وَمَن مَّعَهُ فِي الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ ﴿١١٩﴾
119. Tukamuokoa pamoja na wale waliokuwa naye katika jahazi iliyosheheni.
ثُمَّ أَغْرَقْنَا بَعْدُ الْبَاقِينَ ﴿١٢٠﴾
120. Kisha Tukawagharikisha baada ya hapo waliobakia.
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٢١﴾
121. Hakika katika hayo pana Aayah (Ishara), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿١٢٢﴾
122. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu.
كَذَّبَتْ عَادٌ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٢٣﴾
123. Kina ‘Aad waliwakadhibisha Rusuli.
إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ هُودٌ أَلَا تَتَّقُونَ ﴿١٢٤﴾
124. Alipowaambia ndugu yao Huwd: Je, hamtokuwa na taqwa?
إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ ﴿١٢٥﴾
125. Hakika mimi kwenu ni Rasuli mwaminifu.
فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١٢٦﴾
126. Basi mcheni Allaah na nitiini.
وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٢٧﴾
127. Na wala sikuombeni ujira wowote juu yake. Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Rabb wa walimwengu.
أَتَبْنُونَ بِكُلِّ رِيعٍ آيَةً تَعْبَثُونَ ﴿١٢٨﴾
128. Je, mnajenga katika kila sehemu maarufu za mnyanyuko majengo marefurefu kwa ajili ya burudani tu?
وَتَتَّخِذُونَ مَصَانِعَ لَعَلَّكُمْ تَخْلُدُونَ ﴿١٢٩﴾
129. Na mnafanya ngome madhubuti kama kwamba mtaishi milele?
وَإِذَا بَطَشْتُم بَطَشْتُمْ جَبَّارِينَ ﴿١٣٠﴾
130. Na mnapofanya uonevu, mnatumia nguvu kijabari.
فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١٣١﴾
131. Basi mcheni Allaah na nitiini.
وَاتَّقُوا الَّذِي أَمَدَّكُم بِمَا تَعْلَمُونَ ﴿١٣٢﴾
132. Na mcheni Ambaye Amekupeni yale mnayoyajua.
أَمَدَّكُم بِأَنْعَامٍ وَبَنِينَ ﴿١٣٣﴾
133. Amekupeni wanyama wa mifugo na watoto.
وَجَنَّاتٍ وَعُيُونٍ ﴿١٣٤﴾
134. Na mabustani na chemchemu.
إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٣٥﴾
135. Hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku iliyo kubwa kabisa.
قَالُوا سَوَاءٌ عَلَيْنَا أَوَعَظْتَ أَمْ لَمْ تَكُن مِّنَ الْوَاعِظِينَ ﴿١٣٦﴾
136. Wakasema: Ni sawa sawa kwetu, ukiwaidhi au usipokuwa miongoni mwa wanaowaidhi.
إِنْ هَـٰذَا إِلَّا خُلُقُ الْأَوَّلِينَ ﴿١٣٧﴾
137. Haya si chochote isipokuwa ni desturi ya watu wa awali.
وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ ﴿١٣٨﴾
138. Na sisi hatutoadhibiwa.
فَكَذَّبُوهُ فَأَهْلَكْنَاهُمْ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٣٩﴾
139. Wakamkadhibisha, basi Tuliwaangamiza. Hakika katika hayo pana Aayah (Ishara), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿١٤٠﴾
140. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu.
كَذَّبَتْ ثَمُودُ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٤١﴾
141. Kina Thamuwd waliwakadhibisha Rusuli.
إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ صَالِحٌ أَلَا تَتَّقُونَ ﴿١٤٢﴾
142. Alipowaambia ndugu yao Swaalih: Je, hamtokuwa na taqwa?
إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ ﴿١٤٣﴾
143. Hakika mimi kwenu ni Rasuli mwaminifu.
فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١٤٤﴾
144. Basi mcheni Allaah na nitiini.
وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٤٥﴾
145. Na wala sikuombeni ujira wowote juu yake. Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Rabb wa walimwengu.
أَتُتْرَكُونَ فِي مَا هَاهُنَا آمِنِينَ ﴿١٤٦﴾
146. Je, (mnadhani) mtaachwa mkiwa katika amani kwenye haya hapa mliyonayo?
فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ ﴿١٤٧﴾
147. Katika mabustani na chemchemu.
وَزُرُوعٍ وَنَخْلٍ طَلْعُهَا هَضِيمٌ ﴿١٤٨﴾
148. Na mimea na mitende makole yake laini, yamewiva.
وَتَنْحِتُونَ مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا فَارِهِينَ ﴿١٤٩﴾
149. Na mnachonga milimani nyumba kwa uhodari kabisa.
فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١٥٠﴾
150. Basi mcheni Allaah na nitiini.
وَلَا تُطِيعُوا أَمْرَ الْمُسْرِفِينَ ﴿١٥١﴾
151. Na wala msitii amri ya wenye kupindukia mipaka.
الَّذِينَ يُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ وَلَا يُصْلِحُونَ ﴿١٥٢﴾
152. Ambao wanafanya ufisadi katika ardhi na wala hawatengenezi.
قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مِنَ الْمُسَحَّرِينَ ﴿١٥٣﴾
153. Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa.
مَا أَنتَ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا فَأْتِ بِآيَةٍ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿١٥٤﴾
154. Wewe si chochote isipokuwa mtu kama sisi tu, basi lete Aayah (Ishara, Dalili) ukiwa wewe ni miongoni mwa wakweli.
قَالَ هَـٰذِهِ نَاقَةٌ لَّهَا شِرْبٌ وَلَكُمْ شِرْبُ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ ﴿١٥٥﴾
155. Akasema: Huyu hapa ngamia jike, ana zamu ya kunywa, nanyi mna zamu ya kunywa siku maalumu.
وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابُ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٥٦﴾
156. Na wala msimguse kwa uovu, ikaja kukuchukueni adhabu ya Siku iliyo kuu kabisa.
فَعَقَرُوهَا فَأَصْبَحُوا نَادِمِينَ ﴿١٥٧﴾
157. Basi wakamuua. Wakapambazukiwa wenye kujuta.
فَأَخَذَهُمُ الْعَذَابُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٥٨﴾
158. Ikawachukuwa adhabu. Hakika katika hayo pana Aayah (Ishara), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿١٥٩﴾
159. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu.
كَذَّبَتْ قَوْمُ لُوطٍ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٦٠﴾
160. Watu wa Luutw waliwakadhibisha Rusuli.
إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ لُوطٌ أَلَا تَتَّقُونَ ﴿١٦١﴾
161. Alipowaambia ndugu yao Luutw: Je, hamtokuwa na taqwa?
إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ ﴿١٦٢﴾
162. Hakika mimi kwenu ni Rasuli mwaminifu.
فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١٦٣﴾
163. Basi mcheni Allaah na nitiini.
وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٤﴾
164. Na wala sikuombeni ujira wowote juu yake. Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Rabb wa walimwengu.
أَتَأْتُونَ الذُّكْرَانَ مِنَ الْعَالَمِينَ ﴿١٦٥﴾
165. Je, mnawaendea wanaume miongoni mwa walimwengu?
وَتَذَرُونَ مَا خَلَقَ لَكُمْ رَبُّكُم مِّنْ أَزْوَاجِكُم ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ عَادُونَ ﴿١٦٦﴾
166. Na mnaacha kile Alichokuumbieni Rabb wenu katika wake zenu. Bali nyinyi ni watu mliopindukia mipaka.
قَالُوا لَئِن لَّمْ تَنتَهِ يَا لُوطُ لَتَكُونَنَّ مِنَ الْمُخْرَجِينَ ﴿١٦٧﴾
167. Wakasema: Usipoacha ee Luutw, bila shaka utakuwa miongoni mwa watakaofukuzwa.
قَالَ إِنِّي لِعَمَلِكُم مِّنَ الْقَالِينَ ﴿١٦٨﴾
168. Akasema: Hakika mimi ni katika wanaochukia mno kitendo chenu.
رَبِّ نَجِّنِي وَأَهْلِي مِمَّا يَعْمَلُونَ ﴿١٦٩﴾
169. Rabb wangu! Niokoe na ahli zangu kutokana na yale wanayotenda.
فَنَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ أَجْمَعِينَ ﴿١٧٠﴾
170. Basi Tukamuokoa na ahli zake wote.
إِلَّا عَجُوزًا فِي الْغَابِرِينَ ﴿١٧١﴾
171. Isipokuwa kikongwe katika waliobaki nyuma.
ثُمَّ دَمَّرْنَا الْآخَرِينَ ﴿١٧٢﴾
172. Kisha Tukadamiri wengineo.
وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا ۖ فَسَاءَ مَطَرُ الْمُنذَرِينَ ﴿١٧٣﴾
173. Na Tukawanyeshea mvua (ya adhabu). Basi uovu ulioje mvua ya walioonywa!
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٧٤﴾
174. Hakika katika hayo pana Aayah (Ishara), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿١٧٥﴾
175. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu.
كَذَّبَ أَصْحَابُ الْأَيْكَةِ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٧٦﴾
176. Watu wa Al-Aykah[7] waliwakadhibisha Rusuli.
إِذْ قَالَ لَهُمْ شُعَيْبٌ أَلَا تَتَّقُونَ ﴿١٧٧﴾
177. Alipowaambia Shu’ayb: Je, hamtokuwa na taqwa?
إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ ﴿١٧٨﴾
178. Hakika mimi kwenu ni Rasuli mwaminifu.
فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿١٧٩﴾
179. Basi mcheni Allaah na nitiini.
وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٨٠﴾
180. Na wala sikuombeni ujira wowote juu yake. Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Rabb wa walimwengu.
أَوْفُوا الْكَيْلَ وَلَا تَكُونُوا مِنَ الْمُخْسِرِينَ ﴿١٨١﴾
181. Timizeni kipimo na wala msiwe miongoni mwa wenye kupunja.
وَزِنُوا بِالْقِسْطَاسِ الْمُسْتَقِيمِ ﴿١٨٢﴾
182. Na pimeni kwa mizani iliyosawa.
وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿١٨٣﴾
183. Na wala msiwapunje watu vitu vyao, na wala msieneze uovu katika ardhi hali ya kuwa ni wenye kufanya ufisadi.
وَاتَّقُوا الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالْجِبِلَّةَ الْأَوَّلِينَ ﴿١٨٤﴾
184. Na mcheni Ambaye Amekuumbeni na viumbe vingi wa awali.
قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مِنَ الْمُسَحَّرِينَ ﴿١٨٥﴾
185. Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa.
وَمَا أَنتَ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا وَإِن نَّظُنُّكَ لَمِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿١٨٦﴾
186. Nawe si chochote isipokuwa ni mtu tu kama sisi, nasi tuna yakini wewe ni miongoni mwa waongo.
فَأَسْقِطْ عَلَيْنَا كِسَفًا مِّنَ السَّمَاءِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿١٨٧﴾
187. Basi tuangushie vipande vipande vya mbingu, ukiwa ni miongoni mwa wakweli.
قَالَ رَبِّي أَعْلَمُ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿١٨٨﴾
188. Akasema: Rabb wangu Anajua zaidi yale mnayoyatenda.
فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمْ عَذَابُ يَوْمِ الظُّلَّةِ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٨٩﴾
189. Wakamkadhibisha. Basi adhabu ya siku ya kivuli[8] (cha mawingu) ikawachukua. Hakika hiyo ilikuwa ni adhabu ya Siku kubwa mno.
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٩٠﴾
190. Hakika katika haya pana Aayah (Ishara), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿١٩١﴾
191. Na hakika Rabb wako bila shaka Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu.
وَإِنَّهُ لَتَنزِيلُ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٩٢﴾
192. Na hakika hii (Qur-aan) ni Uteremsho wa Rabb wa walimwengu.
نَزَلَ بِهِ الرُّوحُ الْأَمِينُ ﴿١٩٣﴾
193. Ameiteremsha Ar-Ruwh[9] (Jibriyl) mwaminifu.
عَلَىٰ قَلْبِكَ لِتَكُونَ مِنَ الْمُنذِرِينَ ﴿١٩٤﴾
194. Juu ya moyo wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ili uwe miongoni mwa waonyaji.
بِلِسَانٍ عَرَبِيٍّ مُّبِينٍ ﴿١٩٥﴾
195. Kwa lugha ya Kiarabu bayana.
وَإِنَّهُ لَفِي زُبُرِ الْأَوَّلِينَ ﴿١٩٦﴾
196. Na hakika hii bila shaka imo katika Vitabu vya hukumu vya awali.
أَوَلَمْ يَكُن لَّهُمْ آيَةً أَن يَعْلَمَهُ عُلَمَاءُ بَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿١٩٧﴾
197. Je, haikuwa kwao ni (Aayah (Dalili) kwamba wanavyuoni wa wana wa Israaiyl wanaitambua?
وَلَوْ نَزَّلْنَاهُ عَلَىٰ بَعْضِ الْأَعْجَمِينَ ﴿١٩٨﴾
198. Na lau Tungeliiteremsha (hii Qur-aan) kwa yeyote miongoni mwa wasio Waarabu.
فَقَرَأَهُ عَلَيْهِم مَّا كَانُوا بِهِ مُؤْمِنِينَ ﴿١٩٩﴾
199. Na akawasomea, wasingelikuwa wenye kuiamini.
كَذَٰلِكَ سَلَكْنَاهُ فِي قُلُوبِ الْمُجْرِمِينَ ﴿٢٠٠﴾
200. Hivyo ndivyo Tumeuingiza (ukanushaji) katika nyoyo za wakhalifu.
لَا يُؤْمِنُونَ بِهِ حَتَّىٰ يَرَوُا الْعَذَابَ الْأَلِيمَ ﴿٢٠١﴾
201. Hawaiamini mpaka waione adhabu iumizayo.
فَيَأْتِيَهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٢٠٢﴾
202. Iwajie ghafla, nao hawatambui.
فَيَقُولُوا هَلْ نَحْنُ مُنظَرُونَ ﴿٢٠٣﴾
203. Kisha watasema: Je, sisi tutapewa muhula?
أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ ﴿٢٠٤﴾
204. Je, wanahimiza Adhabu Yetu?
أَفَرَأَيْتَ إِن مَّتَّعْنَاهُمْ سِنِينَ ﴿٢٠٥﴾
205. Je, unaonaje kama Tukiwastarehesha miaka.
ثُمَّ جَاءَهُم مَّا كَانُوا يُوعَدُونَ ﴿٢٠٦﴾
206. Kisha yakawajia yale waliyokuwa wanaahidiwa.
مَا أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا يُمَتَّعُونَ ﴿٢٠٧﴾
207. Hayatowafaa yale waliyokuwa wakistareheshewa.
وَمَا أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ إِلَّا لَهَا مُنذِرُونَ ﴿٢٠٨﴾
208. Na Hatukuangamiza mji wowote isipokuwa ulikuwa na waonyaji.
ذِكْرَىٰ وَمَا كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿٢٠٩﴾
209. Ni ukumbusho na Hatukuwa madhalimu.
وَمَا تَنَزَّلَتْ بِهِ الشَّيَاطِينُ ﴿٢١٠﴾
210. Na wala hawakuteremka nayo (hii Qur-aan) mashaytwaan.
وَمَا يَنبَغِي لَهُمْ وَمَا يَسْتَطِيعُونَ ﴿٢١١﴾
211. Na wala haipasi kwao na wala hawawezi.
إِنَّهُمْ عَنِ السَّمْعِ لَمَعْزُولُونَ ﴿٢١٢﴾
212. Hakika wao bila shaka wametengwa mbali kuisikiliza.
فَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتَكُونَ مِنَ الْمُعَذَّبِينَ ﴿٢١٣﴾
213. Basi usiombe pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine ukaja kuwa miongoni mwa watakaoadhibiwa.
وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ ﴿٢١٤﴾
214. Na onya (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) jamaa zako wa karibu.[10]
وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِمَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢١٥﴾
215. Na inamisha ubawa wako kwa anayekufuata miongoni mwa Waumini.
فَإِنْ عَصَوْكَ فَقُلْ إِنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٢١٦﴾
216. Wakikuasi, basi sema: Hakika mimi niko mbali na hayo mnayoyatenda.
وَتَوَكَّلْ عَلَى الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ ﴿٢١٧﴾
217. Na tawakali kwa Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu.
الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ ﴿٢١٨﴾
218. Ambaye Anakuona wakati unaposimama.
وَتَقَلُّبَكَ فِي السَّاجِدِينَ ﴿٢١٩﴾
219. Na mageuko yako katika wenye kusujudu.
إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٢٢٠﴾
220. Hakika Yeye Ndiye Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
هَلْ أُنَبِّئُكُمْ عَلَىٰ مَن تَنَزَّلُ الشَّيَاطِينُ ﴿٢٢١﴾
221. Je, nikujulisheni wanaowateremkia mashaytwaan?
تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ ﴿٢٢٢﴾
222. Wanateremka juu ya kila mzushi mkubwa mwingi wa kutenda dhambi.
يُلْقُونَ السَّمْعَ وَأَكْثَرُهُمْ كَاذِبُونَ ﴿٢٢٣﴾
223. Wanaotega sikio na wengi wao ni waongo.
وَالشُّعَرَاءُ يَتَّبِعُهُمُ الْغَاوُونَ ﴿٢٢٤﴾
224. Na washairi wanafuatwa na wapotofu.
أَلَمْ تَرَ أَنَّهُمْ فِي كُلِّ وَادٍ يَهِيمُونَ ﴿٢٢٥﴾
225. Je, huoni kwamba wao katika kila bonde wanatangatanga?
وَأَنَّهُمْ يَقُولُونَ مَا لَا يَفْعَلُونَ ﴿٢٢٦﴾
226. Nao wanasema yale wasiyoyafanya.
إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَذَكَرُوا اللَّـهَ كَثِيرًا وَانتَصَرُوا مِن بَعْدِ مَا ظُلِمُوا ۗ وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ ﴿٢٢٧﴾
227. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema, na wakamdhukuru Allaah kwa wingi, na wakapata nusura baada ya kudhulumiwa. Na hivi karibuni watakuja kujua wale waliodhulumu mgeuko gani watakaogeuka.[11]
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Maana Ya "آيَةٌ" :
Neno hili limekariri katika Aayah kadhaa kwenye Suwrah hii, na pia limetajwa kwa wingi katika Suwrah nyenginezo. Na mara limetajwa kwa umoja آيَة (Aayah) na mara kwa wingi آيات (Aayaat). Rejea kupata mifano katika Suwrah An-Nahl (16:11-13), Ar-Ruwm (30:20-25), Ar-Ra’d (13:3-4), Al-Jaathiyah (45:3-5).
Maana zake ni nyingi kutegemea na muktadha. Nazo ni kama ifuatavyo:
(i) Aayah au Aayaat za Qur-aan (ii) Ishara (iii) Dalili (iv) Burhani (dalili za wazi kabisa) (v) Hoja (vi) Muujiza (vii) Mazingatio (viii) Mafunzo. Na maana nyenginezo.
[3] Baadhi Ya Visa Vya Rusuli (عليهم السّلام) Katika Suwrah Hii:
Suwrah Ash-Shu’araa ni miongoni mwa Suwrah ambazo vimetajwa visa vya Rusuli kadhaa na kaumu zao. Rusuli hao ni wafuatao: Muwsaa na Haaruwn, Ibraahiym, Nuwh, Huwd, Swaalih, Luutw, Shu’ayb (عليهم السّلام). Na Suwrah nyenginezo ambazo vimetajwa visa vya Rusuli hao na Manabii wengineo ni Suwrah zifuatazo: Al-A’raaf, Yuwnus, Huwd, Al-Anbiyaa, An-Naml, Al’Ankabuwt, Asw-Swaffaat, Swaad, Adh-Dhaariyaat, Al-Qamar.
[4] Firawni Kumpachika Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) Sifa Ovu:
Kukanusha kwake Firawni Risala ya Allaah, kulimfanya ampachike sifa ovu Nabiy Muwsaa (عليه السّلام). Mara aseme ni mchawi mjuzi, mara majnuni, mara muongo. Rejea Adh-Dhaariyaat (51:52) kwenye maelezo bayana. Na pia rejea Ghaafir (40:24), Al-A’raaf (7:109), Al-Israa (17:101).
Na katika Suwrah hii, Rusuli wengineo waliopachikwa sifa hiyo ya uchawi ni wafuatao:
Nabiy Swaalih (عليه السّلام), Ash-Shu’araa (26:153). Nabiy Shu’ayb (عليه السّلام), Ash-Shu’araa (26:185).
[5] Hukma:
Kumjua Allaah na Mipaka Yake, ilimu nyingi ya Dini yenye ufaqihi, ufahamu wa kina, busara, na utambuzi wa Sharia (hukumu) ya halali na haramu, na uwezo wa kuhukumu baina ya watu.
[6] Moyo Uliosalimika:
Aayah namba (88-89) inataja Siku ya Qiyaamah watu watakapofufuliwa kila mtu akiwa pekee. Hayatamfaa mali wala watoto isipokuwa atakayemfikia Allaah na moyo uliosalimika. Na moyo uliosalimika ni ule uliosalimika na shirki, kufru, unafiki, kutilia shaka Dini ya Allaah, kuifanyia istihzai Dini ya Allaah, kila aina ya maasi na madhambi, bid’ah na maovu yote mengineyo.
Na moyo uliosalimika ni kama walivyosema ‘Ulamaa na baadhi ya Salaf kuwa, ni moyo wenye ikhlaasw, ilimu, yakini, mapenzi ya Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kufuata amri zao na kujiepusha na makatazo yao, na mapenzi ya kupenda khayraat.
Na zifuatazo ni baadhi ya kauli za ‘Ulamaa kuhusiana na moyo huu:
(i) Imaam Ibn Kathiyr: Ni moyo uliosalimika na uchafu na ushirikina.
(ii) Muhammad bin Siyriyn: Ni moyo unaotambua kuwa Allaah ni Haqq, na kwamba Saa (Qiyaamah) itafika tu hakuna shaka ndani yake, na kwamba Allaah Atafufua walioko makaburini.
(iii) Ibn ‘Abbaas: Ni moyo uliojistahi unaoshuhudia Laa ilaaha illa-Allaah.
(iv) Sa’iyd Al-Musayyib: Ni moyo wenye uzima, nao ni moyo wa Muumini, kwa sababu moyo wa kafiri na mnafiki una maradhi kama Anavyosema Allaah katika Al-Baqarah (2:10)]
(v) Abu ‘Uthmaan An-Niysaabuwriy: Ni moyo usio na chembe ya bid’ah ndani yake, uliotuama kwenye Sunnah.
(vi) Mujaahid, Al-Hasan na wengineo: Ni moyo uliosalimika na shirki.
Kinyume chake ni moyo uliotajwa katika Qur-aan kuwa una maradhi. Rejea Muhammad (47:20) kwenye maelezo na rejea mbalimbali.
Rejea pia Al-Hajj (22:46) ambako kuna maelezo na ufafanuzi wa Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
فَإِنَّهَا لَا تَعْمَى الْأَبْصَارُ وَلَـٰكِن تَعْمَى الْقُلُوبُ الَّتِي فِي الصُّدُورِ ﴿٤٦﴾
“Kwani hakika hayapofuki macho, lakini zinazopofuka ni nyoyo zilizomo vifuani.
[7] Watu Wa Al-Aykah:
Maana ya Aykah, ni miti mingi iliyosongomana, na kauli iliyo sahihi kabisa ni watu wa Madyan. Na Nabiy Shu’ayb (عليه السّلام) alikuwa miongoni mwao. Lakini Allaah (سبحانه وتعالى) hapa Hakusema: “Ndugu yao Shu’ayb” kama Alivyotaja hivyo kwa Rusuli wengineo kina Nabiy Nuwh, Huwd, Swaalih na Luutw (عليهم السلام) katika Aayah zilizotangulia, kwa sababu watu wake Shu’ayb, wamehusishwa na ibaada hiyo ya miti. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Na Watu wa Al-Aykah wametajwa pia katika Suwrah (Al-Hijr 15:78), (Swaad 38:13), (Qaaf 50:14). Na watu wa Shu’ayb wametajwa pia katika Suwrah (Al-A’raaf 7:85), (Huwd 11:84), (Al-‘Ankabuwt 29:36). Uasi wao ulikuwa ni: Shirki, dhulma, kughushi katika mizani za kupimia chakula, ufisadi mbalimbali katika nchi, kuvuka mipaka ya kuasi na mengineyo. Waliteketezwa kwa adhabu za tetemeko la ardhi na ukelele angamizi; adhabu ambazo ziliwaangusha kifudifudi majumbani mwao wakafilia mbali.
[8] Siku Ya Kivuli:
Siku ya kivuli imekusudiwa kama ilivyotajwa katika Tafsiyr ifuatayo: “Wakaendelea kumkanusha (Nabiy wao Shu’ayb), likawapata wao joto kali, wakawa wanatafuta mahali pa hifadhi (pa kivuli) ili wajifinike. Kikawafinika kiwingu (kama kivuli), kikawapatia ubaridi na upepo laini, na walipokusanyika chini yake, moto uliwawakia na ukawachoma, basi hapo yakawa maangamivu yao wote katika siku yenye kitisho kikali.[Tafsiy Al-Muyassar]
[10] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
026-Asbaabun-Nuzuwl:Ash-Shu'araa Aayah 214: وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ [218]
Na pia:
111-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Masad: تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ [219]
[11] Washairi Waliohidika:
Allaah (سبحانه وتعالى)
Amewavua kati ya hao washairi, wale washairi waliohidika kwa kuamini na kufanya matendo mema, na wakamdhukuru Allaah kwa wingi, wakatunga mashairi juu ya kumpwekesha Allaah (سبحانه وتعالى) na kumsifu na Kumhimidi Yeye, Mwenye kumtetea Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), wakasema maneno ya busara yenye mawaidha na adabu nzuri, na wakaunusuru Uislamu, wakawa wanamtukana anayeutukana Uislamu, au anayemtukana Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kuwaraddi washairi makafiri. Na watajua wale waliozidhulumu nafsi zao kwa ushirikina na matendo ya uasi, wakawadhulumu wasiokuwa wao, kwa kuwanyima haki zao, au kuwafanyia uadui, au tuhuma za urongo, ni marejeo gani ya shari na maangamivu watakayorejea. Kwa kweli, hayo ni mageuko mabaya. [Tafsiyr Al-Muyassar]
النَّمْل
027-An-Naml
027-An-Naml: Utangulizi Wa Suwrah [221]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
طس ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْقُرْآنِ وَكِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿١﴾
1. Twaa Siyn.[1] Hizi ni Aayaat za Qur-aan na Kitabu bainifu.
هُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ ﴿٢﴾
2. Ni mwongozo na bishara kwa Waumini.
الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ ﴿٣﴾
3. Ambao wanasimamisha Swalaah na wanatoa Zakaah, nao kuhusu Aakhirah ni wenye yakini nayo.
إِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ زَيَّنَّا لَهُمْ أَعْمَالَهُمْ فَهُمْ يَعْمَهُونَ ﴿٤﴾
4. Hakika wale wasioiamini Aakhirah Tumewapambia amali zao, basi wao wanatangatanga kwa upofu.
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَهُمْ سُوءُ الْعَذَابِ وَهُمْ فِي الْآخِرَةِ هُمُ الْأَخْسَرُونَ ﴿٥﴾
5. Hao ni wale ambao watapata adhabu mbaya kabisa, nao katika Aakhirah ndio wenye kukhasirika zaidi.
وَإِنَّكَ لَتُلَقَّى الْقُرْآنَ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ عَلِيمٍ ﴿٦﴾
6. Na hakika wewe unaletewa Qur-aan kutoka kwa Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.
إِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِأَهْلِهِ إِنِّي آنَسْتُ نَارًا سَآتِيكُم مِّنْهَا بِخَبَرٍ أَوْ آتِيكُم بِشِهَابٍ قَبَسٍ لَّعَلَّكُمْ تَصْطَلُونَ ﴿٧﴾
7. (Kumbuka) pale Muwsaa alipowaambia ahli yake: Hakika mimi nimeona moto, nitakuleteeni kutoka upande wake khabari, au nitakuleteeni kijinga kinachowaka ili mpate kuota moto.
فَلَمَّا جَاءَهَا نُودِيَ أَن بُورِكَ مَن فِي النَّارِ وَمَنْ حَوْلَهَا وَسُبْحَانَ اللَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٨﴾
8. Basi alipoujia, ilinadiwa kwamba: Amebarikiwa aliye karibu na moto, na aliye pembezoni mwake. Na Utakasifu ni wa Allaah Rabb wa walimwengu.
يَا مُوسَىٰ إِنَّهُ أَنَا اللَّـهُ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٩﴾
9. Ee Muwsaa! Hakika Ni Mimi Allaah Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
وَأَلْقِ عَصَاكَ ۚ فَلَمَّا رَآهَا تَهْتَزُّ كَأَنَّهَا جَانٌّ وَلَّىٰ مُدْبِرًا وَلَمْ يُعَقِّبْ ۚ يَا مُوسَىٰ لَا تَخَفْ إِنِّي لَا يَخَافُ لَدَيَّ الْمُرْسَلُونَ ﴿١٠﴾
10. Na tupa fimbo yako. Basi alipoiona inataharuki kama kwamba ni nyoka, aligeuka nyuma kukimbia na wala hakurudi. Ee Muwsaa! Usikhofu. Hakika Mimi hawakhofu Mbele Yangu Rusuli.
إِلَّا مَن ظَلَمَ ثُمَّ بَدَّلَ حُسْنًا بَعْدَ سُوءٍ فَإِنِّي غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١١﴾
11. Isipokuwa yule aliyedhulumu, kisha akabadilisha wema baada ya uovu, basi hakika Mimi Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَأَدْخِلْ يَدَكَ فِي جَيْبِكَ تَخْرُجْ بَيْضَاءَ مِنْ غَيْرِ سُوءٍ ۖ فِي تِسْعِ آيَاتٍ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَقَوْمِهِ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ ﴿١٢﴾
12. Na ingiza mkono wako katika uwazi wa nguo yako kifuani, utatoka kuwa mweupe bila ya dhara yoyote. Ni miongoni mwa Aayaat (Ishara, Miujiza) tisa[2] kwa Firawni na watu wake. Hakika wao wamekuwa ni watu mafasiki.
فَلَمَّا جَاءَتْهُمْ آيَاتُنَا مُبْصِرَةً قَالُوا هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿١٣﴾
13. Basi ilipowajia Aayaat (Ishara, Miujiza) Yetu yenye kuonekana wazi, wakasema: Hii ni sihiri bayana.
وَجَحَدُوا بِهَا وَاسْتَيْقَنَتْهَا أَنفُسُهُمْ ظُلْمًا وَعُلُوًّا ۚ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ ﴿١٤﴾
14. Wakaikanusha kwa dhulma na majivuno na hali kuwa nafsi zao zimeiyakinisha. Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya mafisadi.
وَلَقَدْ آتَيْنَا دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ عِلْمًا ۖ وَقَالَا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي فَضَّلَنَا عَلَىٰ كَثِيرٍ مِّنْ عِبَادِهِ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٥﴾
15. Na kwa yakini Tulimpa Daawuwd na Sulaymaan ilimu. Wakasema: AlhamduliLLaahi (Himidi Anastahiki Allaah) Ambaye Ametufadhilisha kuliko wengi katika Waja Wake Waumini.
وَوَرِثَ سُلَيْمَانُ دَاوُودَ ۖ وَقَالَ يَا أَيُّهَا النَّاسُ عُلِّمْنَا مَنطِقَ الطَّيْرِ وَأُوتِينَا مِن كُلِّ شَيْءٍ ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْفَضْلُ الْمُبِينُ ﴿١٦﴾
16. Na Sulaymaan alimrithi Daawuwd, akasema: Enyi watu! Tumefunzwa lugha ya ndege, na tumepewa kila kitu. Hakika hii bila shaka ndio fadhila bayana.
وَحُشِرَ لِسُلَيْمَانَ جُنُودُهُ مِنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ وَالطَّيْرِ فَهُمْ يُوزَعُونَ ﴿١٧﴾
17. Na alikusanyiwa Sulaymaan majeshi yake miongoni mwa majini na wanaadam na ndege, nao wamedhibitiwa kwa mpango kabambe.
حَتَّىٰ إِذَا أَتَوْا عَلَىٰ وَادِ النَّمْلِ قَالَتْ نَمْلَةٌ يَا أَيُّهَا النَّمْلُ ادْخُلُوا مَسَاكِنَكُمْ لَا يَحْطِمَنَّكُمْ سُلَيْمَانُ وَجُنُودُهُ وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿١٨﴾
18. Mpaka walipofika kwenye bonde la sisimizi, akasema sisimizi mmoja: Enyi sisimizi! Ingieni masikanini mwenu, asikupondeni Sulaymaan na majeshi yake, na hali wao hawahisi.
فَتَبَسَّمَ ضَاحِكًا مِّن قَوْلِهَا وَقَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَدْخِلْنِي بِرَحْمَتِكَ فِي عِبَادِكَ الصَّالِحِينَ ﴿١٩﴾
19. (Sulaymaan) akatabasamu kuchekea kauli yake, akasema: Rabb wangu! Nipe ilhamu na uwezo nishukuru Neema Yako ambayo Umenineemesha juu yangu na wazazi wangu, na nipate kutenda mema Utakayoridhia, na Niingize kwa Rehma Yako katika Waja Wako Swalihina.
وَتَفَقَّدَ الطَّيْرَ فَقَالَ مَا لِيَ لَا أَرَى الْهُدْهُدَ أَمْ كَانَ مِنَ الْغَائِبِينَ ﴿٢٠﴾
20. Akakagua ndege, akasema: Imekuwaje, mbona simuoni al-hud-hud, au amekuwa miongoni mwa walioghibu?[3]
لَأُعَذِّبَنَّهُ عَذَابًا شَدِيدًا أَوْ لَأَذْبَحَنَّهُ أَوْ لَيَأْتِيَنِّي بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ ﴿٢١﴾
21. Bila shaka nitamuadhibu adhabu kali, au nitamchinja, au aniletee hoja bayana.
فَمَكَثَ غَيْرَ بَعِيدٍ فَقَالَ أَحَطتُ بِمَا لَمْ تُحِطْ بِهِ وَجِئْتُكَ مِن سَبَإٍ بِنَبَإٍ يَقِينٍ ﴿٢٢﴾
22. Basi (hud-hud) hakukaa kitambo kirefu, akasema: Nimegundua ambayo wewe hukuyagundua na nimekujia kutoka Saba-a na khabari za yakini.
إِنِّي وَجَدتُّ امْرَأَةً تَمْلِكُهُمْ وَأُوتِيَتْ مِن كُلِّ شَيْءٍ وَلَهَا عَرْشٌ عَظِيمٌ ﴿٢٣﴾
23. Hakika mimi nimemkuta mwanamke anawatawala, na amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa mno.
وَجَدتُّهَا وَقَوْمَهَا يَسْجُدُونَ لِلشَّمْسِ مِن دُونِ اللَّـهِ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَصَدَّهُمْ عَنِ السَّبِيلِ فَهُمْ لَا يَهْتَدُونَ ﴿٢٤﴾
24. Nimemkuta na watu wake wanalisujudia jua badala ya Allaah, na shaytwaan amewapambia amali zao na akawazuia na njia, kwa hiyo hawaioni njia (ya haki).
أَلَّا يَسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي يُخْرِجُ الْخَبْءَ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَيَعْلَمُ مَا تُخْفُونَ وَمَا تُعْلِنُونَ ﴿٢٥﴾
25. Na ili wasimsujudie Allaah Ambaye Anatoa yenye kufichika katika mbingu na ardhi, na Anayajua yale mnayoyaficha na yale mnayoyadhihirisha.
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ ۩﴿٢٦﴾
26. Allaah hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Rabb wa ‘Arsh Adhimu.
قَالَ سَنَنظُرُ أَصَدَقْتَ أَمْ كُنتَ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٢٧﴾
27. (Sulaymaan) akasema: Tutaona, kama umesema kweli, au ulikuwa miongoni mwa waongo?
اذْهَب بِّكِتَابِي هَـٰذَا فَأَلْقِهْ إِلَيْهِمْ ثُمَّ تَوَلَّ عَنْهُمْ فَانظُرْ مَاذَا يَرْجِعُونَ ﴿٢٨﴾
28. Nenda na barua yangu hii na uwafikishie, kisha ujitenge nao utazame watarudisha nini.
قَالَتْ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ إِنِّي أُلْقِيَ إِلَيَّ كِتَابٌ كَرِيمٌ ﴿٢٩﴾
29. (Malkia) akasema: Enyi wakuu! Hakika nimeletewa barua tukufu.
إِنَّهُ مِن سُلَيْمَانَ وَإِنَّهُ بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿٣٠﴾
30. Hakika inatoka kwa Sulaymaan, na hakika (imeanza) Kwa Jina la Allaah, Ar-Rahmaan, Mwenye Kurehemu.[4]
أَلَّا تَعْلُوا عَلَيَّ وَأْتُونِي مُسْلِمِينَ ﴿٣١﴾
31. Msinifanyie jeuri, na nijieni mkiwa mmesilimu.
قَالَتْ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ أَفْتُونِي فِي أَمْرِي مَا كُنتُ قَاطِعَةً أَمْرًا حَتَّىٰ تَشْهَدُونِ ﴿٣٢﴾
32. (Malkia) akasema: Enyi wakuu! Nipeni shauri katika jambo langu, maana sikuwa mwenye kuamua jambo mpaka mhudhurie nami.
قَالُوا نَحْنُ أُولُو قُوَّةٍ وَأُولُو بَأْسٍ شَدِيدٍ وَالْأَمْرُ إِلَيْكِ فَانظُرِي مَاذَا تَأْمُرِينَ ﴿٣٣﴾
33. Wakasema: Sisi ni wenye nguvu, na wenye uwezo mkali wa vita, na amri iko kwako, basi tazama unaamrisha nini?
قَالَتْ إِنَّ الْمُلُوكَ إِذَا دَخَلُوا قَرْيَةً أَفْسَدُوهَا وَجَعَلُوا أَعِزَّةَ أَهْلِهَا أَذِلَّةً ۖ وَكَذَٰلِكَ يَفْعَلُونَ ﴿٣٤﴾
34. Akasema: Hakika wafalme wanapoingia mji huufisidi, na huwafanya watukufu wake kuwa dhalili, na hivyo ndivyo wafanyavyo.
وَإِنِّي مُرْسِلَةٌ إِلَيْهِم بِهَدِيَّةٍ فَنَاظِرَةٌ بِمَ يَرْجِعُ الْمُرْسَلُونَ ﴿٣٥﴾
35. Nami nitawapelekea hadiya, kisha nitangojea kutazama watakayorudi nayo wajumbe.
فَلَمَّا جَاءَ سُلَيْمَانَ قَالَ أَتُمِدُّونَنِ بِمَالٍ فَمَا آتَانِيَ اللَّـهُ خَيْرٌ مِّمَّا آتَاكُم بَلْ أَنتُم بِهَدِيَّتِكُمْ تَفْرَحُونَ ﴿٣٦﴾
36. Basi alipomjia (mjumbe) Sulaymaan, alisema: Je, mnanisaidia kwa mali? Basi Aliyonipa Allaah ni bora kuliko Aliyokupeni nyinyi, bali nyinyi mnafurahia hadiya yenu.
ارْجِعْ إِلَيْهِمْ فَلَنَأْتِيَنَّهُم بِجُنُودٍ لَّا قِبَلَ لَهُم بِهَا وَلَنُخْرِجَنَّهُم مِّنْهَا أَذِلَّةً وَهُمْ صَاغِرُونَ ﴿٣٧﴾
37. Rudi kwao. Bila shaka tutawaendea kwa jeshi wasiloweza kukabiliana nalo, na bila shaka tutawatoa humo hali ya kuwa wamedhalilika na walio duni.
قَالَ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ أَيُّكُمْ يَأْتِينِي بِعَرْشِهَا قَبْلَ أَن يَأْتُونِي مُسْلِمِينَ ﴿٣٨﴾
38. Akasema: Enyi wakuu! Nani kati yenu ataniletea kiti chake cha enzi kabla hawakunijia wakiwa wamesilimu?
قَالَ عِفْرِيتٌ مِّنَ الْجِنِّ أَنَا آتِيكَ بِهِ قَبْلَ أَن تَقُومَ مِن مَّقَامِكَ ۖ وَإِنِّي عَلَيْهِ لَقَوِيٌّ أَمِينٌ ﴿٣٩﴾
39. Akasema ‘Ifriti miongoni mwa majini: Mimi nitakuletea kabla hujasimama kutoka mahali pako, na hakika mimi kwa hilo, bila shaka ni mwenye nguvu mwaminifu.
قَالَ الَّذِي عِندَهُ عِلْمٌ مِّنَ الْكِتَابِ أَنَا آتِيكَ بِهِ قَبْلَ أَن يَرْتَدَّ إِلَيْكَ طَرْفُكَ ۚ فَلَمَّا رَآهُ مُسْتَقِرًّا عِندَهُ قَالَ هَـٰذَا مِن فَضْلِ رَبِّي لِيَبْلُوَنِي أَأَشْكُرُ أَمْ أَكْفُرُ ۖ وَمَن شَكَرَ فَإِنَّمَا يَشْكُرُ لِنَفْسِهِ ۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ رَبِّي غَنِيٌّ كَرِيمٌ ﴿٤٠﴾
40. Akasema yule ambaye ana ilimu[5] kutoka katika Kitabu: Mimi nitakuletea kabla halijapepesa jicho lako. Basi alipokiona kimewekwa mbele yake, (Sulaymaan) alisema: Hii ni katika Fadhila za Rabb wangu, Anijaribu; je, nitashukuru, au nitakufuru. Na yeyote yule anayeshukuru, basi hakika anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake. Na yeyote yule asiyekuwa na shukurani, basi hakika Rabb wangu ni Mkwasi, Mkarimu.
قَالَ نَكِّرُوا لَهَا عَرْشَهَا نَنظُرْ أَتَهْتَدِي أَمْ تَكُونُ مِنَ الَّذِينَ لَا يَهْتَدُونَ ﴿٤١﴾
41. (Sulaymaan) akasema: Mgeuzieni kiti chake cha enzi tutazame, ataongoka au atakuwa miongoni mwa ambao wasioongoka.
فَلَمَّا جَاءَتْ قِيلَ أَهَـٰكَذَا عَرْشُكِ ۖ قَالَتْ كَأَنَّهُ هُوَ ۚ وَأُوتِينَا الْعِلْمَ مِن قَبْلِهَا وَكُنَّا مُسْلِمِينَ ﴿٤٢﴾
42. Basi (Malkia) alipokuja, ikasemwa: Je, ni kama hiki kiti chako cha enzi? Akasema: Kama ndicho hicho. (Sulaymaan akasema): Na tumepewa ilimu kabla yake na tukawa Waislamu.
وَصَدَّهَا مَا كَانَت تَّعْبُدُ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ إِنَّهَا كَانَتْ مِن قَوْمٍ كَافِرِينَ ﴿٤٣﴾
43. Na yale aliyokuwa akiyaabudu badala ya Allaah yalimzuia (Uislamu). Hakika alikuwa miongoni mwa watu makafiri.
قِيلَ لَهَا ادْخُلِي الصَّرْحَ ۖ فَلَمَّا رَأَتْهُ حَسِبَتْهُ لُجَّةً وَكَشَفَتْ عَن سَاقَيْهَا ۚ قَالَ إِنَّهُ صَرْحٌ مُّمَرَّدٌ مِّن قَوَارِيرَ ۗ قَالَتْ رَبِّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي وَأَسْلَمْتُ مَعَ سُلَيْمَانَ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٤٤﴾
44. Akaambiwa: Ingia katika kasri la fakhari. Alipoliona alilidhania ni bwawa refu la maji, akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Sulaymaan) akasema: Hakika hilo ni kasri la fakhari lilosakafiwa kwa vigae. (Malkia) akasema: Rabb wangu! Hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu, na nimesilimu pamoja na Sulaymaan kwa Allaah Rabb wa walimwengu.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ فَإِذَا هُمْ فَرِيقَانِ يَخْتَصِمُونَ ﴿٤٥﴾
45. Na kwa yakini Tuliwapelekea kina Thamuwd ndugu yao Swaalih kwamba: Mwabuduni Allaah. Tahamaki wakawa makundi mawili yanayogombana.
قَالَ يَا قَوْمِ لِمَ تَسْتَعْجِلُونَ بِالسَّيِّئَةِ قَبْلَ الْحَسَنَةِ ۖ لَوْلَا تَسْتَغْفِرُونَ اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٤٦﴾
46. (Swaalih) akasema: Enyi kaumu yangu! Kwa nini mnahimiza uovu kabla ya mema? Kwa nini msimwombe Allaah maghfirah ili huenda mkarehemewa?
قَالُوا اطَّيَّرْنَا بِكَ وَبِمَن مَّعَكَ ۚ قَالَ طَائِرُكُمْ عِندَ اللَّـهِ ۖ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ تُفْتَنُونَ ﴿٤٧﴾
47. Wakasema: Tumepata nuksi kwa sababu yako na kwa wale walio pamoja nawe. (Swaalih) akasema: Nuksi yenu iko kwa Allaah. Bali nyinyi ni watu mliojaribiwa.
وَكَانَ فِي الْمَدِينَةِ تِسْعَةُ رَهْطٍ يُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ وَلَا يُصْلِحُونَ ﴿٤٨﴾
48. Na kulikuweko katika mji ule watu tisa wakifanya ufisadi katika ardhi na wala hawafanyi yenye manufaa.
قَالُوا تَقَاسَمُوا بِاللَّـهِ لَنُبَيِّتَنَّهُ وَأَهْلَهُ ثُمَّ لَنَقُولَنَّ لِوَلِيِّهِ مَا شَهِدْنَا مَهْلِكَ أَهْلِهِ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ ﴿٤٩﴾
49. Wakasema: Apishaneni kwa Jina la Allaah kwamba tutamhujumu (Swaalih) kwa siri usiku na ahli yake, kisha tutasema kwa jamaa yake wa karibu: Hatukushuhudia maangamizi ya ahli yake, nasi hakika ni wakweli.
وَمَكَرُوا مَكْرًا وَمَكَرْنَا مَكْرًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٥٠﴾
50. Wakapanga makri (njama). Nasi Tukapanga mipango ya kuvurumisha makri, nao huku hawatambui.
فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ مَكْرِهِمْ أَنَّا دَمَّرْنَاهُمْ وَقَوْمَهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٥١﴾
51. Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya njama zao, kwamba Tuliwadamirisha na watu wao wote.
فَتِلْكَ بُيُوتُهُمْ خَاوِيَةً بِمَا ظَلَمُوا ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿٥٢﴾
52. Basi hizo ni nyumba zao zimebakia magofu kwa sababu ya
walivyodhulumu. Hakika katika hayo kuna Aayah (Ishara, Mazingatio) kwa watu wanaojua.
وَأَنجَيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ ﴿٥٣﴾
53. Na Tukawaokoa wale walioamini, na waliokuwa na taqwa.
وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ وَأَنتُمْ تُبْصِرُونَ ﴿٥٤﴾
54. Na (kumbuka) Luutw alipowaambia watu wake: Je, mnafanya machafu na hali nyinyi mnaona?
أَئِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ شَهْوَةً مِّن دُونِ النِّسَاءِ ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ تَجْهَلُونَ ﴿٥٥﴾
55. Je, nyinyi mnawaendea wanaume kwa matamanio badala ya wanawake?! Bali nyinyi ni watu majahili.
فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَن قَالُوا أَخْرِجُوا آلَ لُوطٍ مِّن قَرْيَتِكُمْ ۖ إِنَّهُمْ أُنَاسٌ يَتَطَهَّرُونَ ﴿٥٦﴾
56. Basi halikuwa jawabu la watu wake isipokuwa kusema: Watoeni watu wa Luutw kutoka mji wenu, hakika wao ni watu wanaojiweka katika utakaso.
فَأَنجَيْنَاهُ وَأَهْلَهُ إِلَّا امْرَأَتَهُ قَدَّرْنَاهَا مِنَ الْغَابِرِينَ ﴿٥٧﴾
57. Basi Tulimuokoa na ahli yake isipokuwa mke wake, Tulimkadiria miongoni mwa watakaobakia nyuma.
وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا ۖ فَسَاءَ مَطَرُ الْمُنذَرِينَ ﴿٥٨﴾
58. Na Tukawanyeshea mvua. Basi uovu ulioje mvua ya walioonywa!
قُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ وَسَلَامٌ عَلَىٰ عِبَادِهِ الَّذِينَ اصْطَفَىٰ ۗ آللَّـهُ خَيْرٌ أَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٥٩﴾
59. Sema: AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah) na amani iwe juu ya Waja Wake Aliowakhitari. Je, Allaah Ni bora au wale wanaowashirikisha (Naye)?
أَمَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَنبَتْنَا بِهِ حَدَائِقَ ذَاتَ بَهْجَةٍ مَّا كَانَ لَكُمْ أَن تُنبِتُوا شَجَرَهَا ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ يَعْدِلُونَ ﴿٦٠﴾
60. Au nani Aliyeumba mbingu na ardhi, na Akakuteremshieni kutoka mbinguni maji, kisha Tukaotesha kwayo mabustani anisi ya kupendeza kabisa? Nyinyi hamna uwezo wa kuotesha miti yake. Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Bali wao ni watu wanaomfanya Allaah sawa na viabudiwa vyao. (wanaoikengeuka haki).[6]
أَمَّن جَعَلَ الْأَرْضَ قَرَارًا وَجَعَلَ خِلَالَهَا أَنْهَارًا وَجَعَلَ لَهَا رَوَاسِيَ وَجَعَلَ بَيْنَ الْبَحْرَيْنِ حَاجِزًا ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٦١﴾
61. Au nani Aliyeijaalia ardhi kuwa mahali pa matulio, na Akajaalia baina yake mito, na Akaiwekea milima mirefu thabiti, na Akajaalia baina ya bahari mbili (ya chumvi na tamu) kizuizi? Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Bali wengi wao hawajui.
أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الْأَرْضِ ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ ﴿٦٢﴾
62. Au nani Anayemuitika mwenye dhiki mno anapomwomba, na Akamuondoshea uovu na Akakufanyeni warithi wa ardhi? Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Ni machache mno mnayokumbuka.
أَمَّن يَهْدِيكُمْ فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَمَن يُرْسِلُ الرِّيَاحَ بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ تعَالَى اللَّـهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٦٣﴾
63. Au nani Anayekuongozeni katika viza vya nchi kavu na bahari? Na nani Anayetuma pepo za kheri na za bishara kabla ya Rehma Yake? Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Ametukuka Allaah kutokana na yale wanayomshirikisha.
أَمَّن يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَمَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۗ أَإِلَـٰهٌ مَّعَ اللَّـهِ ۚ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٦٤﴾
64. Au nani Anayeanzisha uumbaji, kisha Anaurejesha? Na nani Anayekuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je, yuko mwabudiwa pamoja na Allaah? Sema: Leteni ushahidi wenu wa wazi mkiwa ni wakweli.
قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ ﴿٦٥﴾
65. Sema: Hakuna katika mbingu na ardhi ajuaye ghaibu[7] isipokuwa Allaah. Na wala hawatambui lini watafufuliwa.
بَلِ ادَّارَكَ عِلْمُهُمْ فِي الْآخِرَةِ ۚ بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ مِّنْهَا ۖ بَلْ هُم مِّنْهَا عَمُونَ ﴿٦٦﴾
66. Bali umefikia kikomo ujuzi wao kuhusu Aakhirah. Bali wao wamo katika shaka nayo. Bali wao ni vipofu nayo.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَإِذَا كُنَّا تُرَابًا وَآبَاؤُنَا أَئِنَّا لَمُخْرَجُونَ ﴿٦٧﴾
67. Na wale waliokufuru wakasema: Je, tukiwa mchanga na baba zetu, hivi sisi kweli tutakuja kutolewa?[8]
لَقَدْ وُعِدْنَا هَـٰذَا نَحْنُ وَآبَاؤُنَا مِن قَبْلُ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿٦٨﴾
68. Tumekwishaahidiwa haya sisi na baba zetu hapo kabla. Haya si chochote isipokuwa ni hekaya za watu wa kale.
قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُجْرِمِينَ ﴿٦٩﴾
69. Sema: Tembeeni katika ardhi kisha mtazame vipi ilikuwa hatima ya wahalifu.[9]
وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلَا تَكُن فِي ضَيْقٍ مِّمَّا يَمْكُرُونَ ﴿٧٠﴾
70. Na wala usihuzunike juu yao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na wala usiwe katika dhiki kutokana na njama wazipangazo.
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٧١﴾
71. Na wanasema: Ni lini hiyo ahadi mkiwa ni wakweli?[10]
قُلْ عَسَىٰ أَن يَكُونَ رَدِفَ لَكُم بَعْضُ الَّذِي تَسْتَعْجِلُونَ ﴿٧٢﴾
72. Sema: Asaa yawe yamekurubia nyuma yenu baadhi ya mnayoyahimiza.
وَإِنَّ رَبَّكَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَشْكُرُونَ ﴿٧٣﴾
73. Na hakika Rabb wako Ni Mwenye Fadhila kwa watu, lakini wengi wao hawashukuru.
وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَعْلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمْ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴿٧٤﴾
74. Na hakika Rabb wako bila shaka Anajua yale yanayofichwa na vifua vyao na yale wanayoyatangaza.
وَمَا مِنْ غَائِبَةٍ فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٧٥﴾
75. Na hakuna chochote cha ghaibu katika mbingu na ardhi isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha.
إِنَّ هَـٰذَا الْقُرْآنَ يَقُصُّ عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَكْثَرَ الَّذِي هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿٧٦﴾
76. Hakika hii Qur-aan inawasimulia wana wa Israaiyl mengi zaidi ambayo wao wanakhitilafiana nayo.
وَإِنَّهُ لَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ﴿٧٧﴾
77. Nayo hakika ni mwongozo na rehma kwa Waumini.
إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُم بِحُكْمِهِ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْعَلِيمُ ﴿٧٨﴾
78. Hakika Rabb wako Atahukumu baina yao kwa Hukumu Yake. Naye Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.
فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۖ إِنَّكَ عَلَى الْحَقِّ الْمُبِينِ ﴿٧٩﴾
79. Basi tawakali kwa Allaah. Hakika wewe uko kwenye haki bayana.
إِنَّكَ لَا تُسْمِعُ الْمَوْتَىٰ وَلَا تُسْمِعُ الصُّمَّ الدُّعَاءَ إِذَا وَلَّوْا مُدْبِرِينَ ﴿٨٠﴾
80. Hakika wewe huwezi kusikilizisha wafu, na wala huwezi kusikilizisha viziwi wito wanapokengeuka wakigeuza migongo yao.[11]
وَمَا أَنتَ بِهَادِي الْعُمْيِ عَن ضَلَالَتِهِمْ ۖ إِن تُسْمِعُ إِلَّا مَن يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا فَهُم مُّسْلِمُونَ ﴿٨١﴾
81. Na wala wewe huwezi kuwaongoa vipofu kutoka upotofu wao. Huwasikilizishi isipokuwa wale wanaoamini Aayaat Zetu, nao ndio wanaojisalimisha (kuwa Waislamu).
وَإِذَا وَقَعَ الْقَوْلُ عَلَيْهِمْ أَخْرَجْنَا لَهُمْ دَابَّةً مِّنَ الْأَرْضِ تُكَلِّمُهُمْ أَنَّ النَّاسَ كَانُوا بِآيَاتِنَا لَا يُوقِنُونَ ﴿٨٢﴾
82. Na itakapotimizwa kauli dhidi yao, Tutawatolea mnyama atembeaye katika ardhi atakayewasemezesha kwa sababu watu walikuwa hawana yakini na Aayaat (na Ishara) Zetu.[12]
وَيَوْمَ نَحْشُرُ مِن كُلِّ أُمَّةٍ فَوْجًا مِّمَّن يُكَذِّبُ بِآيَاتِنَا فَهُمْ يُوزَعُونَ ﴿٨٣﴾
83. Na Siku Tutakayokusanya katika kila Ummah makundi miongoni mwa wale wanaokadhibisha Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) Zetu nao watakusanywa waburuzwe.
حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوا قَالَ أَكَذَّبْتُم بِآيَاتِي وَلَمْ تُحِيطُوا بِهَا عِلْمًا أَمَّاذَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٨٤﴾
84. Mpaka watakapokuja, Allaah) Atasema: Je, si mlikadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) Zangu bila ya kuzijua vyema? Au mlikuwa mnafanya nini?
وَوَقَعَ الْقَوْلُ عَلَيْهِم بِمَا ظَلَمُوا فَهُمْ لَا يَنطِقُونَ ﴿٨٥﴾
85. Na itatimizwa kauli dhidi yao kwa sababu ya kufanya kwao dhulma, nao hawatoweza kutamka lolote.
أَلَمْ يَرَوْا أَنَّا جَعَلْنَا اللَّيْلَ لِيَسْكُنُوا فِيهِ وَالنَّهَارَ مُبْصِرًا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٨٦﴾
86. Je, hawaoni kwamba Tumejaalia usiku ili wapate utulivu humo, na mchana wenye kuangaza? Hakika katika hayo bila shaka mna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaoamini.
وَيَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَفَزِعَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ إِلَّا مَن شَاءَ اللَّـهُ ۚ وَكُلٌّ أَتَوْهُ دَاخِرِينَ ﴿٨٧﴾
87. Na Siku litakapopulizwa baragumu, watakufa kwa mshtuko waliomo mbinguni na waliomo ardhini isipokuwa Amtakaye Allaah.[13] Na wote watamfikia wakiwa duni wamedhalilika.
وَتَرَى الْجِبَالَ تَحْسَبُهَا جَامِدَةً وَهِيَ تَمُرُّ مَرَّ السَّحَابِ ۚ صُنْعَ اللَّـهِ الَّذِي أَتْقَنَ كُلَّ شَيْءٍ ۚ إِنَّهُ خَبِيرٌ بِمَا تَفْعَلُونَ ﴿٨٨﴾
88. Na unaona milima unaidhania imetulia thabiti nayo inapita mpito wa mawingu. Utengenezaji wa Allaah Ambaye Ametengeneza kwa umahiri kila kitu. Hakika Yeye Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri kwa yale myafanyayo.
مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ خَيْرٌ مِّنْهَا وَهُم مِّن فَزَعٍ يَوْمَئِذٍ آمِنُونَ ﴿٨٩﴾ ﴾
89. Atakayekuja na jema, basi atapata bora zaidi kuliko hilo, nao watakuwa katika amani na mafazaiko (kifo cha mshtuko) Siku hiyo.
وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَكُبَّتْ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ هَلْ تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٩٠﴾
90. Na atakayekuja na ovu, basi zitatupwa gubigubi nyuso zao katika moto (wataambiwa): Je, kwani mnalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyatenda?
إِنَّمَا أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ رَبَّ هَـٰذِهِ الْبَلْدَةِ الَّذِي حَرَّمَهَا وَلَهُ كُلُّ شَيْءٍ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُسْلِمِينَ ﴿٩١﴾
91. Hakika nimeamrishwa nimwabudu Rabb wa mji huu (wa Makkah) Ambaye Ameufanya mtukufu, na Ni Vyake Pekee vitu vyote. Na nimeamrishwa kwamba niwe miongoni mwa Waislamu.
وَأَنْ أَتْلُوَ الْقُرْآنَ ۖ فَمَنِ اهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِي لِنَفْسِهِ ۖ وَمَن ضَلَّ فَقُلْ إِنَّمَا أَنَا مِنَ الْمُنذِرِينَ ﴿٩٢﴾
92. Na kwamba nisome Qur-aan. Hivyo anayehidika, basi hakika anahidika kwa ajili ya manufaa ya nafsi yake. Na anayepotoka, basi sema: Hakika mimi ni miongoni mwa waonyaji.
وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ سَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ فَتَعْرِفُونَهَا ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٩٣﴾
93. Na sema: AlhamduliLLaahi (Himidi Anastahiki Allaah) Atakuonyesheni Aayaat (Ishara, Dalili) Zake na mtazitambua. Na Rabb wako Si Mwenye Kughafilika na yale wanayoyatenda.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Aayaat (Ishara, Miujiza) Tisa Ya Allaah Kwa Watu Wa Firawni: Rejea Al-A’raaf (7:130), (133).
[3] Hud-hud:
Ni ndege wenye vishungi, wenye manyoa ya rangi ya samaki wa samoni. Kupitia ndege huyu, katika kisa chake hiki na Nabiy Sulaymaan (عليه السّلام), umedhihirika muujiza na Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) kwamba ndege mdogo ameweza kusafiri hadi mji mwengine wa mbali, akakuta watu wanamshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى), naye akakanusha hilo na akataka kuthitibisha Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى). Amedhihirika kuwa ni ndege mwerevu, mwenye busara na aliyelingania Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kukanusha shirki zao za kuabudu jua. Na hatimaye, ndege huyu hud-hud, akawa ni sababu ya Malkia wa Saba-a kusilimu na kuingia katika Uislamu.
[4] Kuanza Kusoma Qur-aan Kwa Basmalah:
Mtu anapotaka kuanza kusoma Suwrah yoyote ile ya Qur-aan anapaswa aanze kwa
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa Jina la Allaah Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), Ar-Rahiym (Mwenye Kurehemu).
Lakini kabla ya Basmalah, aanze kwa Isti’aadhah, yaani kuomba kinga (dhidi ya shaytwaan) ambayo ni kusema:
أَعـوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّيْـطانِ الرَّجيـم
Najikinga kwa Allaah kutokana na shaytwaan aliyeepushwa na kuwekwa mbali na Rehma za Allaah.
Rejea An-Nahl (16:98).
Hivyo basi kuanzwa kusoma Qur-aan kwa kuanza kwa Basmalah:
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
kunapatikana baraka katika kisomo cha Qur-aan na kumtegemea Allaah (سبحانه وتعالى) na kutaqabaliwa amali hii ya kusoma Qur-aan. Na sehemu nyengineyo inayopasa kutamkwa kikamilifu ni katika kuandika barua. Ama katika kuanza kufanya jambo lolote jengine, ili kupata baraka au kujikinga na shaytwaan, basi ni kuanza kwa tasmiyah (ambayo ni):
بِسْمِ اللَّـهِ
Lakini itambulike kuwa, kuanza kwa Basmalah ni katika Suwrah zote isipokuwa Suwrah At-Tawbah, haijuzu kuanza kwa Basmalah. Rejea At-Tawbah (9) ambako kuna maelezo bayana ya sababu ya kukatazwa kuanzia Suwrah hii kwa Basmalah.
[5] Mwenye Ilimu:
Wafasiri wa Qur-aan wamesema kuwa aliyekusudiwa kuwa mwenye ilimu, anaitwa Aaswif Bin Barkhiyaa. Alikuwa mwanachuoni mwema enzi ya Nabiy Sulaymaan, na alikuwa anajua Jina Tukufu kabisa la Allaah Ambalo Kwalo akimwomba Allaah jambo lolote Humwitikia na kumpa. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[6] Miongoni Mwa Neema Za Allaah (سبحانه وتعالى) Na Uwezo Wake Na Uthibitisho Wa Tawhiyd Ya Allaah:
Kuanzia Aayah hii hadi namba (65), Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja miongoni mwa Neema Zake na Uwezo Wake, na uthibitisho wa Tawhiyd Yake ya Ar-Rubuwbiyyah (Urabb) na Al-Uluwhiyyah (Uilahi).
[7] Hakuna Ajuaye Ghaibu Ya Yaliyoko Mbinguni Na Ardhini:
Ghaibu ni ilimu ya mambo asiyoyajua mtu isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:3), Luqmaan (31:34), Al-An’aam (6.59).
Hakuna ajuaye yaliyoko mbinguni wala katika ardhi. Haya yamo katika Ujuzi wa Allaah (سبحانه وتعالى). Wala watu hawajui lini watafufuliwa kutoka makaburini mwao kitakaposimama Qiyaamah. Bali watakijua na kukishuhudia Qiyaamah huko Aakhirah (watakapofufuliwa). Huko watakuwa na yakini juu ya Nyumba ya Aakhirah na vitisho vilivyomo watakaposhuhudia (matukio). Na wao walipokuwa duniani walikuwa na shaka nayo, bali akili zao zilikuwa zimepofuka hawaoni (wala hawaamini). [At-Tafsiyr Al-Muyassar]
[8] Makafiri Hawakuamini Kufufuliwa:
Rejea Al-Muuminuwn (23:35-36), pia Rejea Al-Israa (17: 49) ambako kuna maelezo bayana.
[9] Watembee Katika Ardhi Watambue Adhabu Zilizowafika Waliokadhibisha Na Hatima Zao.
Rejea Faatwir (35:43-44), Al-An’aam (6:11), Yuwsuf (12:109), Al-Kahf (18:55) na Al-Hajj (22:46).
[10] Ada ya Makafiri Kutokuamini Saa (Qiyaamah) Na Kutokuamini Kuwateremkia Adhabu:
Rejea Al-An’aam (6:158), Al-Ahzaab (33:63), An-Naazi’aat (79:42), Al-Mulk (67:25), Al-A’raaf (7:187), Ash-Shuwraa (42:18). Na hawakuamini pia kama adhabu ya Allaah (سبحانه وتعالى) itawateremkia wakawa wanaihimizia. Rejea Al-Hajj (22:47), Al-Anfaal (8:32), Swaad (38:16).
[11] Wafu, Viziwi:
Hakika yako ee Rasuli! Huwezi kumsikilizisha haki yule ambaye Allaah Amepiga mhuri juu ya moyo wake Akaufisha. Nahumsikilizishi daawah (ulinganizi) yako yule ambaye Allaah Ameyafanya masikizi yake kuwa kiziwi asiisikie haki, pindi wanapogeuka kukupa mgongo wewe. Kwani kiziwi hasikii daawah akiwa amekuelekea, basi itakuwa vipi akiwa katika hali ya kukupa mgongo na kugeuka?! [Tafsiyr Al-Muyassar]
[12] Mnyama Atakayewasemezesha Watu Ni Katika Alama Kuu Za Qiyaamah:
Rejea Al-An’aam (6:158) kumetajwa alama kumi kuu za Qiyaamah, miongoni mwazo ni mnyama atakayewasemezesha watu.
[13] Malaika Israafiyl Amewakilishwa Kupuliza Baragumu Na Watakaosalimika Na Mfazaiko (Kifo Cha Mshtuko):
وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( كَيْفَ أنْعَمُ ! وَصَاحِبُ القَرْنِ قَدِ التَقَمَ القَرْنَ ، وَاسْتَمَعَ الإذْنَ مَتَى يُؤمَرُ بالنَّفْخِ فَيَنْفُخُ )) فَكَأنَّ ذلِكَ ثَقُلَ عَلَى أصْحَابِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم فَقَالَ لَهُمْ : (( قُولُوا : حَسْبُنَا الله وَنِعْمَ الوَكِيلُ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسنٌ )) .
Amesimulia Abuu Sa'iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Vipi nitakuwa na furaha na mwenye baragumu (Malaika Israafiyl) ametia mdomoni mwake hilo baragumu huku akisubiri idhini ni lini atapatiwa ili apulize! Kana kwamba jambo hili lilikuwa zito kwa Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), hivyo akawaambia semeni:
حَسْبُنَا الله وَنِعْمَ الوَكِيلُ
Allaah Anatutosha, Naye ni mbora wa Kutegemewa.” [At-Tirmidhiy, ambaye amesema ni Hadiyth Hasan]
Kauli Za ‘Ulamaa Kuhusu Watakaofazaika (kifo cha mshtuko) Na Watakaosalimika Na Mfazaiko (Kifo Cha Mshtuko) Kwa Mpulizo Wa Kwanza:
Watakaofazaika (kifo cha mshtuko) kwa mpulizo wa kwanza wa baragumu ni viumbe wote waovu isipokuwa Amtakaye Allaah (سبحانه وتعالى) asifazaike. Na hawa ni wale Aliowakirimu, Aliowathibitisha na Akawahifadhi kutokana na mfazaiko (kifo cha mshtuko). [Tafsiyr Al-Muyassar, Tafsiyr As-Sa’diy]
Watakaofazaika (kifo cha mshtuko) ni viumbe waovu.Watakaosalimika ni Shuhadaa [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Na Hadiyth ifuatayo imetaja hayo:
عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قال : قال رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( يَخْرُجُ الدَّجَّالُ في أُمَّتِي فَيَمْكُثُ أرْبَعِينَ ، لاَ أدْرِي أرْبَعِينَ يَوماً أو أرْبَعِينَ شَهْراً ، أو أرْبَعِينَ عَاماً ، فَيَبْعَثُ اللهُ تَعالَى عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ (عَلَيْهِ السَّلام) ، فَيَطْلُبُهُ فَيُهْلِكُهُ ، ثُمَّ يَمْكُثُ النَّاسُ سَبْعَ سِنِينَ لَيسَ بَينَ اثْنَينِ عَدَاوةٌ ، ثُمَّ يُرْسِلُ اللهُ عزوجل ، ريحاً بَارِدَةً مِنْ قِبَلِ الشَّامِ ، فَلاَ يَبْقَى عَلَى وَجْهِ الأَرْضِ أَحَدٌ فِي قَلْبِهِ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ مِنْ خَيرٍ أو إيمَانٍ إلاَّ قَبَضَتْهُ ، حَتَّى لو أنَّ أَحَدَكُمْ دَخَلَ فِي كَبِدِ جَبَلٍ ، لَدَخَلَتْهُ عَلَيهِ حَتَّى تَقْبِضَهُ ، فَيَبْقَى شِرَارُ النَّاسِ في خِفَّةِ الطَّيْرِ ، وأحْلامِ السِّبَاعِ ، لاَ يَعْرِفُونَ مَعْرُوفاً ، ولا يُنْكِرُونَ مُنْكَراً ، فَيَتَمَثَّلُ لَهُمُ الشَّيْطَانُ ، فيَقُولُ : ألاَ تَسْتَجِيبُونَ ؟ فَيَقُولُونَ : فَمَا تأمُرُنَا ؟ فَيَأمُرُهُمْ بِعِبَادَةِ الأوْثَانِ ، وَهُمْ في ذلِكَ دَارٌّ رِزْقُهُمْ ، حَسَنٌ عَيشُهُمْ ، ثُمَّ يُنْفَخُ في الصُّورِ ، فَلاَ يَسْمَعُهُ أحَدٌ إلاَّ أصْغَى لِيتاً وَرَفَعَ لِيتاً ، وَأوَّلُ مَنْ يَسْمَعُهُ رَجُلٌ يَلُوطُ حَوْضَ إبِلِهِ فَيُصْعَقُ ويُصْعَقُ النَّاسُ حولهُ ، ثُمَّ يُرْسِلُ اللهُ -أو قالَ: يُنْزِلُ اللهُ - مَطَراً كَأَنَّهُ الطَّلُّ أو الظِّلُّ ، فَتَنْبُتُ مِنهُ أجْسَادُ النَّاسِ ، ثُمَّ يُنْفَخُ فِيهِ أُخْرَى فَإِذَا هُمْ قِيَامٌ يَنْظُرُونَ ، ثُمَّ يُقالُ : يا أَيُّهَا النَّاسُ هَلُمَّ إلَى رَبِّكُمْ ، وَقِفُوهُمْ إنَّهُمْ مَسْئُولُونَ ، ثُمَّ يُقَالُ : أخْرِجُوا بَعْثَ النَّارِ فَيُقَالُ : مِنْ كَمْ ؟ فَيُقَالُ : مِنْ كُلِّ ألْفٍ تِسْعَمِئَةٍ وَتِسْعَةً وتِسْعِينَ ؛ فَذَلِكَ يَومٌ يَجْعَلُ الوِلْدَانَ شِيباً ، وَذَلِكَ يَومَ يُكْشَفُ عَنْ سَاقٍ )) . رواه مسلم .
Amesimulia 'Abdullaah bin 'Amr bin Al-'Aasw (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Dajjaal atatokea kwa Ummah wangu na ataishi arobaini, (sina hakika ni siku arobaini au miezi arobaini au miaka arobaini). Kisha Allaah (تبارك وتعالى) Atamtuma 'Iysaa mwana wa Maryam, ambaye atamwinda na kumuua. Kisha watu wataishi kwa miaka saba hapana kabisa uadui wala ugomvi baina ya watu wawili. Baadae Allaah (عزّ وجلّ) Atatuma upepo baridi kutoka Shaam, na hatobaki juu ya mgongo wa ardhi yeyote mwenye chembe ndogo kabisa ya kheri au imaan moyoni mwake isipokuwa utachukua roho yake hata lau mmoja wenu ataingia katika pango la jabali, upepo huo utamwingilia humo uchukue roho yake. Hapo watabaki walio waovu pekee miongoni mwa watu ambao watapaparikia uasherati kama anavyopaparika ndege na watakuwa na tabia za kinyama. Hawatajua mema wala hawatakataza maovu. Shaytwaan atakuja kwao kwa mfano wa mwanaadam na kuwauliza: Je, mutaniitikia wito wangu? Watasema: Kwani unatuamuru nini? Atawaamuru waabudu masanamu, na wao katika kufanya hivyo watapata riziki zao na maisha yao yatakuwa mazuri. Kisha baragumu litapulizwa, hakuna atakayesikia isipokuwa atageuza shingo upande wake (wa hiyo sauti) na kuinyanyua. Wa kwanza kuisikia atakuwa ni mtu anayeshughulika katika kutengeneza birika ya maji kwa ajili ya ngamia wake. Atakapoisikia sauti hiyo atafazaika (atakufa kwa mshtuko) na watu wengine nao watakufa kwa mshtuko. Kisha Allaah Atatuma au alisema: Allaah Atateremsha - mvua kana kwamba ni matone ya umande au kivuli. Hii itafanya miili ya watu ikue, kisha baragumu litapulizwa mara nyengine na hapo watasimama watu na huku wanaangalia. Kisha kutasemwa: Enyi watu! Njooni mbele ya Rabb wenu na wasimamisheni kwani wao wataulizwa. Kisha itatolewa amri: Watoeni wale ambao ni wa motoni. Kutaulizwa: Wangapi? Wataambiwa: Katika kila elfu watoeni mia tisa na tisini na tisa (999). Hiyo ndiyo siku ambayo itawafanya watoto wadogo waote mvi, na hiyo ni siku ambayo muundi (wa Allaah) utawachwa wazi." [Muslim]
Rejea Az-Zumar (39:68), Al-Haaqqah (69:13).
الْقَصَص
028-Al-Qaswasw
028-Al-Qaswasw: Utangulizi Wa Suwrah [223]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
طسم ﴿١﴾
1. Twaa Siyn Miym.[1]
تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿٢﴾
2. Hizi ni Aayaat za Kitabu kinachobainisha.
نَتْلُو عَلَيْكَ مِن نَّبَإِ مُوسَىٰ وَفِرْعَوْنَ بِالْحَقِّ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٣﴾
3. Tunakusomea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) baadhi ya khabari za Muwsaa na Firawni kwa haki kwa watu wanaoamini.
إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِي الْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًا يَسْتَضْعِفُ طَائِفَةً مِّنْهُمْ يُذَبِّحُ أَبْنَاءَهُمْ وَيَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ ۚ إِنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ ﴿٤﴾
4. Hakika Firawni alitakabari katika ardhi, na akawafanya watu wake makundi mbali mbali, akikandamiza kundi miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wa kiume na akiacha hai wanawake wao. Hakika yeye alikuwa miongoni mwa mafisadi.
وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ ﴿٥﴾
5. Na Tukataka Tuwafanyie fadhila wale waliokandamizwa katika ardhi, na Tuwafanye viongozi na Tuwafanye wenye kurithi.
وَنُمَكِّنَ لَهُمْ فِي الْأَرْضِ وَنُرِيَ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا مِنْهُم مَّا كَانُوا يَحْذَرُونَ ﴿٦﴾
6. Na Tuwamakinishe kwa uwezo katika ardhi, na Tumwonyeshe Firawni na Haamaan na majeshi yao miongoni mwao yale waliyokuwa wakitahadhari.
وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ أُمِّ مُوسَىٰ أَنْ أَرْضِعِيهِ ۖ فَإِذَا خِفْتِ عَلَيْهِ فَأَلْقِيهِ فِي الْيَمِّ وَلَا تَخَافِي وَلَا تَحْزَنِي ۖ إِنَّا رَادُّوهُ إِلَيْكِ وَجَاعِلُوهُ مِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٧﴾
7. Na Tukamtia ilhamu mama yake Muwsaa kwamba: Mnyonyeshe. Lakini utakapomkhofia, basi mtupe katika mto na wala usikhofu wala usihuzunike. Hakika Sisi Tutamrudisha kwako, na Tutamfanya miongoni mwa Rusuli.
فَالْتَقَطَهُ آلُ فِرْعَوْنَ لِيَكُونَ لَهُمْ عَدُوًّا وَحَزَنًا ۗ إِنَّ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا كَانُوا خَاطِئِينَ ﴿٨﴾
8. Basi wakamwokota watu wa Firawni ili awe adui kwao na (sababu ya) huzuni. Hakika Firawni na Haamaan na majeshi yao walikuwa wenye makosa.
وَقَالَتِ امْرَأَتُ فِرْعَوْنَ قُرَّتُ عَيْنٍ لِّي وَلَكَ ۖ لَا تَقْتُلُوهُ عَسَىٰ أَن يَنفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٩﴾
9. Na mke wa Firawni akasema: Kiburudisho cha macho kwangu na kwako. Usimuue, asaa akatufaa au tumfanye mwana. Nao hawatambui.
وَأَصْبَحَ فُؤَادُ أُمِّ مُوسَىٰ فَارِغًا ۖ إِن كَادَتْ لَتُبْدِي بِهِ لَوْلَا أَن رَّبَطْنَا عَلَىٰ قَلْبِهَا لِتَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٠﴾
10. Na ukawa moyo wa hisia na mwazo wa mama yake Muwsaa mtupu! Alikaribia kumdhihirisha (kuwa ni mwanawe) lau kama Tusingeutia nguvu moyo wake ili awe miongoni mwa Waumini.
وَقَالَتْ لِأُخْتِهِ قُصِّيهِ ۖ فَبَصُرَتْ بِهِ عَن جُنُبٍ وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿١١﴾
11. Akamwambia ukhti wake (Muwsaa): Mfuatilie! Akamtazama kwa mbali nao hawatambui.
وَحَرَّمْنَا عَلَيْهِ الْمَرَاضِعَ مِن قَبْلُ فَقَالَتْ هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ أَهْلِ بَيْتٍ يَكْفُلُونَهُ لَكُمْ وَهُمْ لَهُ نَاصِحُونَ ﴿١٢﴾
12. Na Tulimharamishia akatae kabisa wanyonyeshaji tangu mwanzo. Kisha (ukhti wake Muwsaa) akasema: Je, nikuelekezeni kwa watu wa nyumba watakaomlea kwa ajili yenu, nao watakuwa wenye kumweka vyema kidhati?
فَرَدَدْنَاهُ إِلَىٰ أُمِّهِ كَيْ تَقَرَّ عَيْنُهَا وَلَا تَحْزَنَ وَلِتَعْلَمَ أَنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٣﴾
13. Basi Tukamrudisha kwa mama yake ili yaburudike macho yake na wala asihuzunike, na ili ajue kwamba Ahadi ya Allaah ni kweli, lakini wengi wao hawajui.
وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَاسْتَوَىٰ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١٤﴾
14. Na alipofikia umri wa kupevuka na akaimarika sawasawa, Tulimpa hikmah na ilimu. Na hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.
وَدَخَلَ الْمَدِينَةَ عَلَىٰ حِينِ غَفْلَةٍ مِّنْ أَهْلِهَا فَوَجَدَ فِيهَا رَجُلَيْنِ يَقْتَتِلَانِ هَـٰذَا مِن شِيعَتِهِ وَهَـٰذَا مِنْ عَدُوِّهِ ۖ فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِن شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ فَوَكَزَهُ مُوسَىٰ فَقَضَىٰ عَلَيْهِ ۖ قَالَ هَـٰذَا مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ ۖ إِنَّهُ عَدُوٌّ مُّضِلٌّ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾
15. Na akaingia mjini wakati watu wake wako katika mighafiliko, akakuta humo watu wawili wanapigana; mmoja ni miongoni mwa kundi lake, na mwengine ni miongoni mwa adui zake. Yule ambaye ni katika kundi lake akamuomba ukozi[2] dhidi ya yule ambaye ni adui yake. Muwsaa akampiga ngumi, akamuua. Akasema: Hii ni kutokana na kitendo cha shaytwaan. Hakika yeye ni adui mpotoaji bayana.
قَالَ رَبِّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي فَغَفَرَ لَهُ ۚ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ ﴿١٦﴾
16. Akasema: Rabb wangu! Hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu, basi Nighufurie. Akamghufuria. Hakika Yeye Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
قَالَ رَبِّ بِمَا أَنْعَمْتَ عَلَيَّ فَلَنْ أَكُونَ ظَهِيرًا لِّلْمُجْرِمِينَ ﴿١٧﴾
17. Akasema: Rabb wangu! Kwa Uliyonineemesha, sitokuwa kamwe msaidizi kwa wahalifu.
فَأَصْبَحَ فِي الْمَدِينَةِ خَائِفًا يَتَرَقَّبُ فَإِذَا الَّذِي اسْتَنصَرَهُ بِالْأَمْسِ يَسْتَصْرِخُهُ ۚ قَالَ لَهُ مُوسَىٰ إِنَّكَ لَغَوِيٌّ مُّبِينٌ ﴿١٨﴾
18. Akapambaukiwa kuwa mwenye khofu katika mji ule anaangaza kwa tahadhari. Basi mara yule aliyemuomba amnusuru jana anampigia kelele amsaidie. Muwsaa akamwambia: Hakika wewe ni mpotofu bayana.
فَلَمَّا أَنْ أَرَادَ أَن يَبْطِشَ بِالَّذِي هُوَ عَدُوٌّ لَّهُمَا قَالَ يَا مُوسَىٰ أَتُرِيدُ أَن تَقْتُلَنِي كَمَا قَتَلْتَ نَفْسًا بِالْأَمْسِ ۖ إِن تُرِيدُ إِلَّا أَن تَكُونَ جَبَّارًا فِي الْأَرْضِ وَمَا تُرِيدُ أَن تَكُونَ مِنَ الْمُصْلِحِينَ ﴿١٩﴾
19. Na alipotaka kumpa kipigo cha nguvu yule aliye adui wao wote wawili, alisema: Ee Muwsaa! Je, unataka kuniua kama ulivyomuua mtu jana? Hutaki lolote isipokuwa unataka uwe jabari katika nchi, na wala hutaki kuwa miongoni mwa wasuluhishaji.
وَجَاءَ رَجُلٌ مِّنْ أَقْصَى الْمَدِينَةِ يَسْعَىٰ قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنَّ الْمَلَأَ يَأْتَمِرُونَ بِكَ لِيَقْتُلُوكَ فَاخْرُجْ إِنِّي لَكَ مِنَ النَّاصِحِينَ ﴿٢٠﴾
20. Akaja mtu kutoka mwisho wa mji ule akiwa anakimbia, akasema: Ee Muwsaa! Hakika wakuu wanashauriana dhidi yako ili wakuue! Basi toka, hakika mimi ni miongoni mwa wanaokunasihi.
فَخَرَجَ مِنْهَا خَائِفًا يَتَرَقَّبُ ۖ قَالَ رَبِّ نَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٢١﴾
21. Basi akatoka humo akiwa na khofu anaangaza kwa tahadhari. Akasema: Rabb wangu! Niokoe na watu madhalimu.
وَلَمَّا تَوَجَّهَ تِلْقَاءَ مَدْيَنَ قَالَ عَسَىٰ رَبِّي أَن يَهْدِيَنِي سَوَاءَ السَّبِيلِ ﴿٢٢﴾
22. Na alipoelekea upande wa Madyan, akasema: Asaa Rabb wangu Akaniongoza njia iliyo sawa.
وَلَمَّا وَرَدَ مَاءَ مَدْيَنَ وَجَدَ عَلَيْهِ أُمَّةً مِّنَ النَّاسِ يَسْقُونَ وَوَجَدَ مِن دُونِهِمُ امْرَأَتَيْنِ تَذُودَانِ ۖ قَالَ مَا خَطْبُكُمَا ۖ قَالَتَا لَا نَسْقِي حَتَّىٰ يُصْدِرَ الرِّعَاءُ ۖ وَأَبُونَا شَيْخٌ كَبِيرٌ ﴿٢٣﴾
23. Alipofikia maji ya Madyan, alikuta kundi la watu linanywesha maji (wanyama wao), na akakuta kando yake wanawake wawili wanawazuia (wanyama wao). Akasema: Mna nini? Wakasema: Hatunyweshi mpaka waondoke wachungaji, na baba yetu ni mtu mzima sana.
فَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰ إِلَى الظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّي لِمَا أَنزَلْتَ إِلَيَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ ﴿٢٤﴾
24. Basi akawanyweshea, kisha akageuka kwenda kivulini, akasema: Rabb wangu! Hakika mimi ni mhitajia wa kheri yoyote Utakayoniteremshia.[3]
فَجَاءَتْهُ إِحْدَاهُمَا تَمْشِي عَلَى اسْتِحْيَاءٍ قَالَتْ إِنَّ أَبِي يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا ۚ فَلَمَّا جَاءَهُ وَقَصَّ عَلَيْهِ الْقَصَصَ قَالَ لَا تَخَفْ ۖ نَجَوْتَ مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ ﴿٢٥﴾
25. Akamjia mmoja kati ya wanawake wawili akitembea kwa kustahi, akasema: Baba yangu anakwita ili akulipe ujira wa kutunyweshea. Basi alipomfikia na akamsimulia visa vyake, alisema: Usikhofu, umeokoka na watu madhalimu.
قَالَتْ إِحْدَاهُمَا يَا أَبَتِ اسْتَأْجِرْهُ ۖ إِنَّ خَيْرَ مَنِ اسْتَأْجَرْتَ الْقَوِيُّ الْأَمِينُ ﴿٢٦﴾
26. Mmoja wao akasema: Ee baba yangu kipenzi! Muajiri! Hakika mbora uwezaye kumwajiri ni mwenye nguvu mwaminifu.
قَالَ إِنِّي أُرِيدُ أَنْ أُنكِحَكَ إِحْدَى ابْنَتَيَّ هَاتَيْنِ عَلَىٰ أَن تَأْجُرَنِي ثَمَانِيَ حِجَجٍ ۖ فَإِنْ أَتْمَمْتَ عَشْرًا فَمِنْ عِندِكَ ۖ وَمَا أُرِيدُ أَنْ أَشُقَّ عَلَيْكَ ۚ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٢٧﴾
27. Akasema: Mimi nataka nikuozeshe mmojawapo wa binti zangu hawa wawili kwa sharti kuwa unitumikie miaka minane. Ukitimiza kumi, basi ni uamuzi wako. Na wala sitaki kukutia mashakani. Utanikuta In Shaa Allaah miongoni mwa Swalihina.
قَالَ ذَٰلِكَ بَيْنِي وَبَيْنَكَ ۖ أَيَّمَا الْأَجَلَيْنِ قَضَيْتُ فَلَا عُدْوَانَ عَلَيَّ ۖ وَاللَّـهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَكِيلٌ ﴿٢٨﴾
28. (Muwsaa) akasema: Hayo ni baina yangu na baina yako. Muda wowote kati ya miwili nitakaoutimiza basi hakuna uadui juu yangu. Na Allaah juu ya yale tunayoyasema ni Mdhamini.
فَلَمَّا قَضَىٰ مُوسَى الْأَجَلَ وَسَارَ بِأَهْلِهِ آنَسَ مِن جَانِبِ الطُّورِ نَارًا قَالَ لِأَهْلِهِ امْكُثُوا إِنِّي آنَسْتُ نَارًا لَّعَلِّي آتِيكُم مِّنْهَا بِخَبَرٍ أَوْ جَذْوَةٍ مِّنَ النَّارِ لَعَلَّكُمْ تَصْطَلُونَ ﴿٢٩﴾
29. Basi Muwsaa alipotimiza muda, na akasafiri pamoja na ahli zake, akaona aliona moto upande wa mlima. Akawaambia ahli zake: Bakieni, hakika mimi nimeona moto, huenda nikakuleteeni kutoka humo khabari, au kijinga cha moto ili mpate kuota moto.
فَلَمَّا أَتَاهَا نُودِيَ مِن شَاطِئِ الْوَادِ الْأَيْمَنِ فِي الْبُقْعَةِ الْمُبَارَكَةِ مِنَ الشَّجَرَةِ أَن يَا مُوسَىٰ إِنِّي أَنَا اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٣٠﴾
30. Basi alipoufikia, akaitwa kutoka upande wa kulia wa bonde katika sehemu iliyobarikiwa kutoka mtini kwamba: Ee Muwsaa! Hakika Mimi Ni Allaah, Rabb wa walimwengu.
وَأَنْ أَلْقِ عَصَاكَ ۖ فَلَمَّا رَآهَا تَهْتَزُّ كَأَنَّهَا جَانٌّ وَلَّىٰ مُدْبِرًا وَلَمْ يُعَقِّبْ ۚ يَا مُوسَىٰ أَقْبِلْ وَلَا تَخَفْ ۖ إِنَّكَ مِنَ الْآمِنِينَ ﴿٣١﴾
31. Na tupa fimbo yako! Basi alipoiona inataharuki kama kwamba ni nyoka, aligeuka kukimbia bila kutazama nyuma wala hakurudi. Ee Muwsaa! Njoo mbele, na wala usikhofu! Hakika wewe ni miongoni mwa waliokuwa katika amani.
اسْلُكْ يَدَكَ فِي جَيْبِكَ تَخْرُجْ بَيْضَاءَ مِنْ غَيْرِ سُوءٍ وَاضْمُمْ إِلَيْكَ جَنَاحَكَ مِنَ الرَّهْبِ ۖ فَذَانِكَ بُرْهَانَانِ مِن رَّبِّكَ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ ﴿٣٢﴾
32. Ingiza mkono wako kifuani katika uwazi wa nguo yako, utatoka kuwa mweupe (wenye kun’gara) bila ya dhara (magonjwa) yoyote. Na ambatisha mkono ubavuni mwako kujikinga na khofu. Hizo ni dalili mbili za wazi kutoka kwa Rabb wako kwa Firawni na wakuu wake. Hakika wao walikuwa watu mafasiki.
قَالَ رَبِّ إِنِّي قَتَلْتُ مِنْهُمْ نَفْسًا فَأَخَافُ أَن يَقْتُلُونِ ﴿٣٣﴾
33. Akasema: Rabb wangu! Hakika mimi nimeua mtu miongoni mwao, na nakhofu wataniua.
وَأَخِي هَارُونُ هُوَ أَفْصَحُ مِنِّي لِسَانًا فَأَرْسِلْهُ مَعِيَ رِدْءًا يُصَدِّقُنِي ۖ إِنِّي أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ ﴿٣٤﴾
34. Na kaka yangu Haaruwn yeye ana ufasaha zaidi wa lugha kuliko mimi, basi mpeleke pamoja nami, kama msaidizi wangu anisadikishe. Hakika mimi nakhofu watanikadhibisha.
قَالَ سَنَشُدُّ عَضُدَكَ بِأَخِيكَ وَنَجْعَلُ لَكُمَا سُلْطَانًا فَلَا يَصِلُونَ إِلَيْكُمَا ۚ بِآيَاتِنَا أَنتُمَا وَمَنِ اتَّبَعَكُمَا الْغَالِبُونَ ﴿٣٥﴾
35. (Allaah) Akasema: Tutautia nguvu mkono wako kwa kaka yako, na Tutakupeni madaraka, basi hawatakufikilieni. Kwa sababu ya Aayaat (Miujiza, Hoja, Dalili) Zetu, nyinyi wawili na watakaokufuateni mtashinda.
فَلَمَّا جَاءَهُم مُّوسَىٰ بِآيَاتِنَا بَيِّنَاتٍ قَالُوا مَا هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّفْتَرًى وَمَا سَمِعْنَا بِهَـٰذَا فِي آبَائِنَا الْأَوَّلِينَ ﴿٣٦﴾
36. Basi Muwsaa alipowajia (kina Firawni) kwa Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu bayana, walisema: Hii si chochote isipokuwa ni sihiri iliyotungwa, na hatukusikia haya kwa baba zetu wa awali.
وَقَالَ مُوسَىٰ رَبِّي أَعْلَمُ بِمَن جَاءَ بِالْهُدَىٰ مِنْ عِندِهِ وَمَن تَكُونُ لَهُ عَاقِبَةُ الدَّارِ ۖ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ ﴿٣٧﴾
37. Muwsaa akasema: Rabb wangu Anajua zaidi yule ajaye na mwongozo kutoka Kwake, na yule atakayekuwa na hatima njema ya makazi ya Aakhirah. Hakika madhalimu hawafaulu.
وَقَالَ فِرْعَوْنُ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ مَا عَلِمْتُ لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرِي فَأَوْقِدْ لِي يَا هَامَانُ عَلَى الطِّينِ فَاجْعَل لِّي صَرْحًا لَّعَلِّي أَطَّلِعُ إِلَىٰ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ مِنَ الْكَاذِبِينَ ﴿٣٨﴾
38. Firawni akasema: Enyi wakuu! Sijui kama mnaye mwabudiwa badala yangu. Basi niwashie moto ee Haamaan unichomee udongo, unifanyie mnara mrefu ili nimwangalie Ilaah wa Muwsaa, na hakika mimi bila shaka nina yakini yeye ni miongoni mwa waongo.
وَاسْتَكْبَرَ هُوَ وَجُنُودُهُ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ إِلَيْنَا لَا يُرْجَعُونَ ﴿٣٩﴾
39. (Firawni) akatakabari yeye na jeshi lake katika ardhi bila ya haki, na wakadhania kwamba wao Kwetu hawatorejeshwa.
فَأَخَذْنَاهُ وَجُنُودَهُ فَنَبَذْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الظَّالِمِينَ ﴿٤٠﴾
40. Basi Tukamchukua na jeshi lake, Tukawatupilia mbali baharini. Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya madhalimu.
وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا يُنصَرُونَ ﴿٤١﴾
41. Na Tukawafanya viongozi wanaolingania motoni, na Siku ya Qiyaamah hawatonusuriwa.
وَأَتْبَعْنَاهُمْ فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا لَعْنَةً ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ هُم مِّنَ الْمَقْبُوحِينَ ﴿٤٢﴾
42. Na Tukawafuatishia laana katika dunia hii. Na Siku ya Qiyaamah wao ni miongoni mwa wenye kubaidishwa na Rehma (ya Allaah).
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ مِن بَعْدِ مَا أَهْلَكْنَا الْقُرُونَ الْأُولَىٰ بَصَائِرَ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةً لَّعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٤٣﴾
43. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu baada ya kuwa Tumeshaangamiza karne za awali kiwe ni kifumbuzi macho kwa watu, na mwongozo na rehma ili wakumbuke.
وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ الْغَرْبِيِّ إِذْ قَضَيْنَا إِلَىٰ مُوسَى الْأَمْرَ وَمَا كُنتَ مِنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٤٤﴾
44. Na wala hukuweko (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kando ya Magharibi (ya mlima) Tulipomkidhia Muwsaa amri, na wala hukuwa miongoni mwa walioshuhudia.
وَلَـٰكِنَّا أَنشَأْنَا قُرُونًا فَتَطَاوَلَ عَلَيْهِمُ الْعُمُرُ ۚ وَمَا كُنتَ ثَاوِيًا فِي أَهْلِ مَدْيَنَ تَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِنَا وَلَـٰكِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ ﴿٤٥﴾
45. Lakini Sisi Tulianzisha karne nyingi ukawatawilikia umri. Na wala hukuwa mkaazi katika watu wa Madyan ukiwasomea Aayaat Zetu, lakini Sisi Tulikuwa Watumaji (Rusuli).
وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ الطُّورِ إِذْ نَادَيْنَا وَلَـٰكِن رَّحْمَةً مِّن رَّبِّكَ لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّا أَتَاهُم مِّن نَّذِيرٍ مِّن قَبْلِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٤٦﴾
46. Na wala hukuwa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kando ya mlima Tuliponadi, lakini ni rehma kutoka kwa Rabb wako ili uonye watu ambao hawakufikiwa na mwonyaji yeyote kabla yako ili wapate kukumbuka.
وَلَوْلَا أَن تُصِيبَهُم مُّصِيبَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ فَيَقُولُوا رَبَّنَا لَوْلَا أَرْسَلْتَ إِلَيْنَا رَسُولًا فَنَتَّبِعَ آيَاتِكَ وَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٧﴾
47. Na usije ukawasibu msiba kwa yale iliyotanguliza mikono yao, wakasema: Rabb wetu! Kwa nini Hukututumia Rasuli tukafuata Aayaat Zako, na tuwe miongoni mwa Waumini.
فَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا لَوْلَا أُوتِيَ مِثْلَ مَا أُوتِيَ مُوسَىٰ ۚ أَوَلَمْ يَكْفُرُوا بِمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ ۖ قَالُوا سِحْرَانِ تَظَاهَرَا وَقَالُوا إِنَّا بِكُلٍّ كَافِرُونَ ﴿٤٨﴾
48. Basi ilipowajia haki kutoka Kwetu, walisema: Mbona hakupewa mfano wa yale aliyopewa Muwsaa? Je, kwani hawakuyakufuru yale aliyopewa Muwsaa kabla? Wakasema: Sihri mbili (Tawraat na Qur-aan) zimesaidiana. Na wakasema: Hakika sisi kwa vyote viwili ni wenye kuvikanusha.
قُلْ فَأْتُوا بِكِتَابٍ مِّنْ عِندِ اللَّـهِ هُوَ أَهْدَىٰ مِنْهُمَا أَتَّبِعْهُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤٩﴾
49. Sema: Leteni Kitabu kutoka kwa Allaah ambacho ni mwongozo zaidi kuliko hivyo viwili nikifuate, mkiwa ni wakweli.
فَإِن لَّمْ يَسْتَجِيبُوا لَكَ فَاعْلَمْ أَنَّمَا يَتَّبِعُونَ أَهْوَاءَهُمْ ۚ وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنِ اتَّبَعَ هَوَاهُ بِغَيْرِ هُدًى مِّنَ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٠﴾
50. Na wasipokuitikia basi juwa kwamba hakika wanafuata hawaa zao. Na nani mpotofu zaidi kuliko yule aliyefuata hawaa zake bila ya mwongozo kutoka kwa Allaah? Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu.
وَلَقَدْ وَصَّلْنَا لَهُمُ الْقَوْلَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٥١﴾
51. Na kwa yakini Tumewafuatilishia na kuwateremshia sehemu kwa sehemu ya Neno ili wapate kukumbuka.[4]
الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ مِن قَبْلِهِ هُم بِهِ يُؤْمِنُونَ ﴿٥٢﴾
52. Wale Tuliowapa Kitabu kabla yake, wao wanaiamini (Qur-aan).[5]
وَإِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ قَالُوا آمَنَّا بِهِ إِنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّنَا إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلِهِ مُسْلِمِينَ ﴿٥٣﴾
53. Na wanaposomewa husema: Tumeiamini, hakika hiyo ni haki kutoka kwa Rabb wetu, hakika Sisi kabla yake tulikuwa Waislamu (waliojisalimisha kwa Allaah).
أُولَـٰئِكَ يُؤْتَوْنَ أَجْرَهُم مَّرَّتَيْنِ بِمَا صَبَرُوا وَيَدْرَءُونَ بِالْحَسَنَةِ السَّيِّئَةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿٥٤﴾
54. Hao watapewa ujira wao mara mbili kwa vile walivyosubiri, na wanazuia ubaya kwa wema, na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa.
وَإِذَا سَمِعُوا اللَّغْوَ أَعْرَضُوا عَنْهُ وَقَالُوا لَنَا أَعْمَالُنَا وَلَكُمْ أَعْمَالُكُمْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ لَا نَبْتَغِي الْجَاهِلِينَ ﴿٥٥﴾
55. Na wanaposikia maneno ya upuuzi hujitenga nayo, na husema: Sisi tuna amali zetu, nanyi mna amali zenu. Salaamun ‘alaykum! (Amani iwe juu yenu)! Hatushindani na majahili.
إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ ﴿٥٦﴾
56. Hakika wewe huwezi kumhidi umpendaye, lakini Allaah Humhidi Amtakaye, Naye Anawajua zaidi wenye kuongoka.[6]
وَقَالُوا إِن نَّتَّبِعِ الْهُدَىٰ مَعَكَ نُتَخَطَّفْ مِنْ أَرْضِنَا ۚ أَوَلَمْ نُمَكِّن لَّهُمْ حَرَمًا آمِنًا يُجْبَىٰ إِلَيْهِ ثَمَرَاتُ كُلِّ شَيْءٍ رِّزْقًا مِّن لَّدُنَّا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٥٧﴾
57. Wakasema: Tukifuata mwongozo pamoja nawe tutanyakuliwa kutoka ardhi yetu. Je, kwani Hatukuwamakinisha mahali patukufu, na pa amani ambapo huletewa mazao ya kila kitu kuwa ni riziki kutoka Kwetu! Lakini wengi wao hawajui.
وَكَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ بَطِرَتْ مَعِيشَتَهَا ۖ فَتِلْكَ مَسَاكِنُهُمْ لَمْ تُسْكَن مِّن بَعْدِهِمْ إِلَّا قَلِيلًا ۖ وَكُنَّا نَحْنُ الْوَارِثِينَ ﴿٥٨﴾
58. Na miji mingapi Tumeiangamiza! Ilipinduka mno mipaka ya kukanusha haki na neema za maisha yake. Basi hayo ni masikani yao yasiyokaliwa baada yao isipokuwa kidogo tu. Na Tukawa Sisi Warithi.
وَمَا كَانَ رَبُّكَ مُهْلِكَ الْقُرَىٰ حَتَّىٰ يَبْعَثَ فِي أُمِّهَا رَسُولًا يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِنَا ۚ وَمَا كُنَّا مُهْلِكِي الْقُرَىٰ إِلَّا وَأَهْلُهَا ظَالِمُونَ ﴿٥٩﴾
59. Na Rabb wako Hakuwa Mwenye Kuangamiza miji mpaka Apeleke katika miji mikuu yake Rasuli awasomee Aayaat Zetu. Na Hatukuwa Wenye Kuangamiza miji isipokuwa watu wake wawe madhalimu.
وَمَا أُوتِيتُم مِّن شَيْءٍ فَمَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَزِينَتُهَا ۚ وَمَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٠﴾
60. Na chochote mlichopewa katika vitu, basi ni starehe za uhai wa dunia na mapambo yake. Na yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi na yakubakia. Je, basi hamtii akilini?
أَفَمَن وَعَدْنَاهُ وَعْدًا حَسَنًا فَهُوَ لَاقِيهِ كَمَن مَّتَّعْنَاهُ مَتَاعَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ثُمَّ هُوَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنَ الْمُحْضَرِينَ ﴿٦١﴾
61. Je, yule Tuliyemuahidi ahadi nzuri (Jannah) kisha yeye atakutana nayo, ni sawa na yule Tuliyemstarehesha starehe za uhai wa dunia, kisha yeye Siku ya Qiyaamah ni miongoni mwa watakaohudhurishwa?
وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٦٢﴾
62. Na Siku (Allaah) Atakayowaita, Atasema: Wako wapi hao mliokuwa mnadai kwa dhana kuwa ni washirika Wangu?
قَالَ الَّذِينَ حَقَّ عَلَيْهِمُ الْقَوْلُ رَبَّنَا هَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَغْوَيْنَا أَغْوَيْنَاهُمْ كَمَا غَوَيْنَا ۖ تَبَرَّأْنَا إِلَيْكَ ۖ مَا كَانُوا إِيَّانَا يَعْبُدُونَ ﴿٦٣﴾
63. Watasema wale iliyowathibitikia kauli: Rabb wetu! Hawa ndio wale tuliowapotoa. Tumewapotoa kama tulivyopotoka. Tumejitoa hatiani mbele Yako, hawakuwa wakituabudu sisi.
وَقِيلَ ادْعُوا شُرَكَاءَكُمْ فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا لَهُمْ وَرَأَوُا الْعَذَابَ ۚ لَوْ أَنَّهُمْ كَانُوا يَهْتَدُونَ ﴿٦٤﴾
64. Na itasemwa: Iteni washirika wenu. Watawaita lakini hawatowaitikia, na wataiona adhabu, laiti wao wangelikuwa wamehidika.
وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ مَاذَا أَجَبْتُمُ الْمُرْسَلِينَ ﴿٦٥﴾
65. Na Siku (Allaah) Atakapowaita, Atasema: Mliwajibu nini Rusuli?
فَعَمِيَتْ عَلَيْهِمُ الْأَنبَاءُ يَوْمَئِذٍ فَهُمْ لَا يَتَسَاءَلُونَ ﴿٦٦﴾
66. Basi zitawafichikia khabari Siku hiyo, nao hawatoweza kuulizana.
فَأَمَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَعَسَىٰ أَن يَكُونَ مِنَ الْمُفْلِحِينَ ﴿٦٧﴾
67. Ama yule aliyetubu na akaamini na akatenda mema, basi asaa akawa miongoni mwa waliofaulu.
وَرَبُّكَ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَيَخْتَارُ ۗ مَا كَانَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٦٨﴾
68. Na Rabb wako Anaumba na Anachagua Atakavyo. Haikuwa wao wana khiari yoyote. Utakasifu ni wa Allaah na Ametukuka kwa ‘Uluwa kutokana na yale yote wanayomshirikisha.
وَرَبُّكَ يَعْلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمْ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴿٦٩﴾
69. Na Rabb wako Anayajua yale yanayofichwa na vifua vyao, na yale wanayoyafichua.
وَهُوَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْحَمْدُ فِي الْأُولَىٰ وَالْآخِرَةِ ۖ وَلَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٧٠﴾
70. Naye ni Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Ni Zake Pekee Himidi za mwanzoni (duniani) na za Aakhirah. Na Hukumu ni Yake Pekee, na Kwake Pekee mtarejeshwa.
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن جَعَلَ اللَّـهُ عَلَيْكُمُ اللَّيْلَ سَرْمَدًا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ يَأْتِيكُم بِضِيَاءٍ ۖ أَفَلَا تَسْمَعُونَ ﴿٧١﴾
71. Sema: Je, mnaonaje kama Allaah Angelikufanyieni usiku unaendelea daima dawamu mpaka Siku ya Qiyaamah, nani mwabudiwa ghairi ya Allaah Atakayekuleteeni mwanga? Je, basi hamsikii?
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن جَعَلَ اللَّـهُ عَلَيْكُمُ النَّهَارَ سَرْمَدًا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ يَأْتِيكُم بِلَيْلٍ تَسْكُنُونَ فِيهِ ۖ أَفَلَا تُبْصِرُونَ ﴿٧٢﴾
72. Sema: Je, mnaonaje kama Allaah Angelikufanyieni mchana unaendelea daima dawamu mpaka Siku ya Qiyaamah, nani mwabudiwa ghairi ya Allaah Atakayekuleteeni usiku mpate utulivu humo? Je, basi hamuoni?
وَمِن رَّحْمَتِهِ جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٧٣﴾
73. Na kutokana na Rehma Yake, Amekufanyieni usiku na mchana ili mpate utulivu humo, na ili mpate kutafuta katika Fadhila Zake, na ili mpate kushukuru.
وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ ﴿٧٤﴾
74. Na Siku (Allaah) Atakayowaita, Atasema: Wako wapi hao mliokuwa mnadai kwa dhana kuwa ni washirika Wangu?
وَنَزَعْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا فَقُلْنَا هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ فَعَلِمُوا أَنَّ الْحَقَّ لِلَّـهِ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٧٥﴾
75. Na Tutachomoa toka kila ummah shahidi kisha Tutasema: Leteni ushahidi wenu wa wazi. Basi watajua kwamba haki ni ya Allaah Pekee, na yamewapotea yale waliyokuwa wakiyatunga (ya uongo).
إِنَّ قَارُونَ كَانَ مِن قَوْمِ مُوسَىٰ فَبَغَىٰ عَلَيْهِمْ ۖ وَآتَيْنَاهُ مِنَ الْكُنُوزِ مَا إِنَّ مَفَاتِحَهُ لَتَنُوءُ بِالْعُصْبَةِ أُولِي الْقُوَّةِ إِذْ قَالَ لَهُ قَوْمُهُ لَا تَفْرَحْ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْفَرِحِينَ ﴿٧٦﴾
76. Hakika Qaaruwn[7] alikuwa miongoni mwa kaumu ya Muwsaa, lakini aliwafanyia uonevu kwa kutakabari[8]. Na Tulimpa hazina ambazo funguo zake zinalemea kundi la watu wenye nguvu (kuzibeba). Walipomwambia watu wake: Usifurahi kwa kujigamba. Hakika Allaah Hapendi wanaofurahi kwa kujigamba.
وَابْتَغِ فِيمَا آتَاكَ اللَّـهُ الدَّارَ الْآخِرَةَ ۖ وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا ۖ وَأَحْسِن كَمَا أَحْسَنَ اللَّـهُ إِلَيْكَ ۖ وَلَا تَبْغِ الْفَسَادَ فِي الْأَرْضِ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ ﴿٧٧﴾
77. Na tafuta katika yale Aliyokupa Allaah makazi ya Aakhirah. Na wala usisahau fungu lako katika dunia. Na fanya ihsaan kama Alivyokufanyia Allaah ihsaan, na wala usitake ufisadi ardhini. Hakika Allaah Hapendi mafisadi.
قَالَ إِنَّمَا أُوتِيتُهُ عَلَىٰ عِلْمٍ عِندِي ۚ أَوَلَمْ يَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ قَدْ أَهْلَكَ مِن قَبْلِهِ مِنَ الْقُرُونِ مَنْ هُوَ أَشَدُّ مِنْهُ قُوَّةً وَأَكْثَرُ جَمْعًا ۚ وَلَا يُسْأَلُ عَن ذُنُوبِهِمُ الْمُجْرِمُونَ ﴿٧٨﴾
78. (Qaaruwn) akasema: Hakika nimepewa haya kwa sababu ya ilimu yangu. Je, hajui kwamba Allaah Ameangamiza kabla yake karne ambazo zilikuwa ni zenye nguvu zaidi kuliko yeye na zenye mkusanyiko (wa mali) mwingi zaidi? Na wala hawatoulizwa kuhusu dhambi zao wahalifu.
فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ فِي زِينَتِهِ ۖ قَالَ الَّذِينَ يُرِيدُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا يَا لَيْتَ لَنَا مِثْلَ مَا أُوتِيَ قَارُونُ إِنَّهُ لَذُو حَظٍّ عَظِيمٍ ﴿٧٩﴾
79. Akawatokea watu wake katika pambo lake. Wale wanaotaka uhai wa dunia wakasema: Ee laiti tungelipata mfano wa yale aliyopewa Qaaruwn, hakika yeye ana bahati kuu.
وَقَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَيْلَكُمْ ثَوَابُ اللَّـهِ خَيْرٌ لِّمَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا وَلَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الصَّابِرُونَ ﴿٨٠﴾
80. Na wale waliopewa ilimu wakasema: Ole wenu! Thawabu za Allaah ni bora zaidi kwa yule aliyeamini na akatenda mema. Na wala hazipati isipokuwa wenye kusubiri.
فَخَسَفْنَا بِهِ وَبِدَارِهِ الْأَرْضَ فَمَا كَانَ لَهُ مِن فِئَةٍ يَنصُرُونَهُ مِن دُونِ اللَّـهِ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُنتَصِرِينَ ﴿٨١﴾
81. Basi Tukamdidimiza yeye na nyumba yake ardhini. Basi hakikuweko kikosi chochote cha kumnusuru dhidi ya Allaah, na wala hakuwa miongoni mwa wanaojinusuru.
وَأَصْبَحَ الَّذِينَ تَمَنَّوْا مَكَانَهُ بِالْأَمْسِ يَقُولُونَ وَيْكَأَنَّ اللَّـهَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَيَقْدِرُ ۖ لَوْلَا أَن مَّنَّ اللَّـهُ عَلَيْنَا لَخَسَفَ بِنَا ۖ وَيْكَأَنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ ﴿٨٢﴾
82. Na wakapambaukiwa wale waliotamani mahali pake jana, wakisema: Ee kumbe Allaah Anamkunjulia riziki Amtakaye kati ya Waja Wake na Humkadiria kwa kipimo (Amtakaye). Ingelikuwa Allaah Hakutufanyia fadhila, bila shaka Angelitudidimiza. Ee kumbe makafiri hawafaulu!
تِلْكَ الدَّارُ الْآخِرَةُ نَجْعَلُهَا لِلَّذِينَ لَا يُرِيدُونَ عُلُوًّا فِي الْأَرْضِ وَلَا فَسَادًا ۚ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ ﴿٨٣﴾
83. Hiyo ni nyumba ya Aakhirah, Tunaijaalia kwa wale wasiotaka kujitukuza katika ardhi wala ufisadi. Na hatima njema ni kwa wenye taqwa.
مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ خَيْرٌ مِّنْهَا ۖ وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَى الَّذِينَ عَمِلُوا السَّيِّئَاتِ إِلَّا مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٨٤﴾
84. Atakayeleta jema, basi atapata bora kuliko hilo. Na atakayeleta ovu, basi hawalipwi wale wanaotenda maovu isipokuwa yale waliyokuwa wanayatenda.
إِنَّ الَّذِي فَرَضَ عَلَيْكَ الْقُرْآنَ لَرَادُّكَ إِلَىٰ مَعَادٍ ۚ قُل رَّبِّي أَعْلَمُ مَن جَاءَ بِالْهُدَىٰ وَمَنْ هُوَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٨٥﴾
85. Hakika Yule Aliyekufaridhishia Qur-aan (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم,) bila shaka Atakurudisha mahali pa marejeo (Makkah). Sema: Rabb wangu Anamjua zaidi yule aliyekuja na hidaya na yule aliyemo katika upotofu bayana.
وَمَا كُنتَ تَرْجُو أَن يُلْقَىٰ إِلَيْكَ الْكِتَابُ إِلَّا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ ظَهِيرًا لِّلْكَافِرِينَ ﴿٨٦﴾
86. Na wala hukuwa unataraji kwamba utapewa Kitabu isipokuwa ni Rehma kutoka kwa Rabb wako. Basi usijekuwa msaidizi kwa makafiri.
وَلَا يَصُدُّنَّكَ عَنْ آيَاتِ اللَّـهِ بَعْدَ إِذْ أُنزِلَتْ إِلَيْكَ ۖ وَادْعُ إِلَىٰ رَبِّكَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٨٧﴾
87. Na wala wasikuzuie kabisa kufuata Aayaat za Allaah baada ya kuteremshwa kwako. Na lingania kwa Rabb wako, na wala usiwe miongoni mwa washirikina.
وَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ ۘ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ ۚ لَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٨٨﴾
88. Na wala usiombe pamoja na Allaah mwabudiwa mwingine. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye. Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa Wajihi[9] Wake. Hukumu ni Yake Pekee na Kwake Pekee mtarejeshwa.[10]
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Istighaathah (Kuomba Uokozi):
Rejea Al-Anfaal (8:9) kupata maana ya Istighaathah. Na kuhusu Isti’aanah, rejea Al-Faatihah (1:5).
[3] Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) Anaomba Rizki Kwa Allaah:
Kama vile chakula kwani njaa ilikuwa imemshika sana. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[5] Wanaoiamini Qur-aan Katika Waliopewa Kitabu:
Ni watu wa Injiyl (Manaswara) na Tawraat (Mayahudi) ambao wameiamini Qur-aan na Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), hawakubadili wala hawakugeuza (Qur-aan). [Tafsiyr Al-Muyassar, Tafsiyr As-Sa’diy]
[6] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah/
Haramisho La Kumuombea Maghfirah Kafiri:
Bonyeza viungo vifuatavyo:
Rejea pia At-Tawbah (9:113-114), Al-Mumtahinah (60:4).
[7] Qaaruwn:
Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye uchambuzi wa kaumu za nyumati za awali, maasi yao na adhabu zao.
Qaaruwn alikuwa miongoni mwa watu wa Muwsaa, yaani kutoka Bani Israaiyl. Salaf wametaja uhusiano wake na Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) kuwa ni ammi yake au bin ammi yake. Na kauli iliyo na nguvu kabisa ni kuwa yeye ni bin ammi yake. Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Qaaruwn alijaaliwa mali nyingi mno. Akatakabari kwa hazina hiyo na kukufuru Neema ya Allaah badala ya kushukuru, na akawa na batra na akajigamba kuwa mali hiyo amepewa kutokana ilimu yake (Aayah namba 78). Hayo yakampelekea kuwa muasi na dhalimu. Na kwa ajili hiyo, Allaah (سبحانه وتعالى) Amemtaja pamoja na madhalimu na makafiri wengineo ambao ni Firawni na Haamaan (waziri wa Firawni) katika Suwrah Ghaafir (40:24), na Al-‘Ankabuwt (29:39). Na katika Suwrah hii ndio kisa chake kimeelezewa, na mwisho wake akadidimizwa katika ardhi.
Mali yake ikamshughulisha mno na akapinduka mipaka katika kibri chake. Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameonya kuwa mtu kama huyo anayeshughulishwa na mali akaacha Swalaah, atafufuliwa pamoja na watu wa aina hii:
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو بن العاص عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ ذَكَرَ الصَّلاةَ يَوْمًا فَقَالَ: ((مَنْ حَافَظَ عَلَيْهَا كَانَتْ لَهُ نُورًا وَبُرْهَانًا وَنَجَاةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ، وَمَنْ لَمْ يُحَافِظْ عَلَيْهَا، لَمْ يَكُنْ لَهُ نُورٌ وَلا بُرْهَانٌ وَلا نَجَاةٌ وَكَانَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَعَ قَارُونَ وَفِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَأُبَيِّ بْنِ خَلَفٍ)) أخرجه الإمام أحمد في مسنده
Amesimulia 'Abdullaah bin 'Amr ibn Al-'Aaasw (رضي الله عنه): Siku moja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitaja kuhusu Swalaah akasema: “Atakayeihifadhi atakuwa na nuru na uongofu, na kufuzu siku ya Qiyaamah. Na asiyeihifadhi, hatokuwa na nuru wala uongofu wala kufuzu, na siku ya Qiyaamah atakuwa pamoja na Qaaruwn, Firawni, Haamaan na Ubayy bin Khalaf.” [Musnad Ahmad ikiwa na Isnaad Swahiyh]
Katika kuifasiri Hadiyth hii, Ibn Al-Qayyim Al-Jawziy (رحمه الله) amesema: “Mwenye kuacha Swalaah huwa ameshughulika na mojawapo kati ya yafuatayo: Ima atakuwa imemshughulisha mali yake, au ufalme wake, au cheo chake, au biashara zake. Yule aliyeshughulika na mali yake, atafufuliwa pamoja na Qaaruwn, na aliyeshughulika na ufalme wake, huyo atakuwa pamoja na Firawni, na aliyeshughulika na cheo chake atakuwa pamoja na Haamaan, na yule aliyeshughulika na biashara zake (akaacha kuswali), huyo atakuwa pamoja na Ubayy bin Khalaf.”
[9] Wajihi wa Allaah: ‘Aqiydah Sahihi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Ni Kuthibtiisha Sifa Za Allaah:
Rejea pia Al-Baqarah (2:115), Ar-Rahmaan (55:27). Na baadhi ya Sifa Zake nyenginezo, rejea Huwd (11:37).
Na katika Sunnah, Sifa hii ya Wajihi pia imethibitishwa kwenye du’aa za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kwenye Hadiyth. Miongoni mwa Hadiyth hizo ni:
حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو مُعَاوِيَةَ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ عَمْرِو بْنِ مُرَّةَ، عَنْ أَبِي عُبَيْدَةَ، عَنْ أَبِي مُوسَى، قَالَ قَامَ فِينَا رَسُولُ اللَّهِ ـ صلى الله عليه وسلم ـ بِخَمْسِ كَلِمَاتٍ فَقَالَ " إِنَّ اللَّهَ لاَ يَنَامُ وَلاَ يَنْبَغِي لَهُ أَنْ يَنَامَ يَخْفِضُ الْقِسْطَ وَيَرْفَعُهُ يُرْفَعُ إِلَيْهِ عَمَلُ اللَّيْلِ قَبْلَ عَمَلِ النَّهَارِ وَعَمَلُ النَّهَارِ قَبْلَ عَمَلِ اللَّيْلِ حِجَابُهُ النُّورُ لَوْ كَشَفَهُ لأَحْرَقَتْ سُبُحَاتُ وَجْهِهِ مَا انْتَهَى إِلَيْهِ بَصَرُهُ مِنْ خَلْقِهِ " .
Amesimulia Abuu Muwsaa (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisimama kati yetu na akasema mambo matano: Akasema: “Allaah Halali, na wala haiwezekani Kwake kulala. Anateremsha Mizani na kuziinua. Amali inayotendwa usiku inapandishwa Kwake kabla ya amali inayotendwa mchana, na amali ya mchana (inapandishwa) kabla ya usiku. Pazia Lake ni Nuru, na lau kama Angeliliondoa, basi Utukufu wa Wajihi Wake ungeunguza vitu vyote Alivyoviumba ambavyo Jicho Lake Limevizunguka vyote.” [Muslim, Ibn Maajah]
[10] Viumbe Vyote Vitakufa Atabakia Allaah (عزّ وجلّ) Pekee:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anafahamisha kwamba watu wote wa ardhini watakufa na vivyo hivyo watu wa mbinguni isipokuwa kwa Amtakaye Allaah, na hakuna atakayesalia isipokuwa Wajihi Wake (سبحانه وتعالى) kwani Yeye ni Aliye Hai daima wala Hafi kamwe! [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Rejea pia Ghaafir (40:16) kupata faida ziyada.
الْعَنْكَبُوت
029-Al-‘Ankabuwt
029-Al-‘Ankabuwt: Utangulizi Wa Suwrah [226]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الم ﴿١﴾
1. Alif Laam Miym.[1]
أَحَسِبَ النَّاسُ أَن يُتْرَكُوا أَن يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ ﴿٢﴾
2. Je, wanadhani watu kwamba wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini, nao ndio wasijaribiwe?
وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَلَيَعْلَمَنَّ اللَّـهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ ﴿٣﴾
3. Kwa yakini Tuliwajaribu wale wa kabla yao. Na kwa yakini Allaah Atawatambulisha wale walio wakweli, na kwa hakika Atawatambulisha walio waongo.
أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ أَن يَسْبِقُونَا ۚ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ ﴿٤﴾
4. Je, wanadhania wale wanaotenda maovu kwamba watatushinda? Uovu ulioje yale wanayohukumu!
مَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ اللَّـهِ فَإِنَّ أَجَلَ اللَّـهِ لَآتٍ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٥﴾
5. Anayetaraji kukutana na Allaah basi hakika muda uliopangwa na Allaah utafika tu. Naye Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
وَمَن جَاهَدَ فَإِنَّمَا يُجَاهِدُ لِنَفْسِهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَغَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٦﴾
6. Na anayefanya juhudi, basi hakika hapana isipokuwa anafanya juhudi kwa ajili ya nafsi yake. Hakika Allaah bila shaka Si Mhitaji wa walimwengu.
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَنُكَفِّرَنَّ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَحْسَنَ الَّذِي كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٧﴾
7. Na wale walioamini na wakatenda mema bila shaka Tutawafutia maovu yao, na bila shaka Tutawalipa mazuri zaidi kuliko yale waliyokuwa wakitenda.
وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حُسْنًا ۖ وَإِن جَاهَدَاكَ لِتُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۚ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٨﴾
8. Na Tumemuusia binaadam kuwafanyia wema wazazi wake wawili. Lakini wakikushikilia kuwa unishirikishe na ambayo huna ilimu nayo, basi usiwatii. Kwangu ni marejeo yenu, Nitakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda.[2]
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَنُدْخِلَنَّهُمْ فِي الصَّالِحِينَ ﴿٩﴾
9. Na wale walioamini na wakatenda mazuri bila shaka Tutawaingiza pamoja na Swalihina.
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ فَإِذَا أُوذِيَ فِي اللَّـهِ جَعَلَ فِتْنَةَ النَّاسِ كَعَذَابِ اللَّـهِ وَلَئِن جَاءَ نَصْرٌ مِّن رَّبِّكَ لَيَقُولُنَّ إِنَّا كُنَّا مَعَكُمْ ۚ أَوَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَعْلَمَ بِمَا فِي صُدُورِ الْعَالَمِينَ ﴿١٠﴾
10. Na miongoni mwa watu wako wasemao: Tumemwamini Allaah. Lakini wanapoudhiwa kwa ajili ya Allaah, hufanya fitnah za watu kama kwamba ni Adhabu ya Allaah. Na inapowajia nusura kutoka kwa Rabb wako husema: Hakika sisi tulikuwa pamoja nanyi. Je, kwani Allaah Hayajui yale yaliyomo katika vifua vya walimwengu?[3]
وَلَيَعْلَمَنَّ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَلَيَعْلَمَنَّ الْمُنَافِقِينَ ﴿١١﴾
11. Na bila shaka Allaah Atatambulisha wale walioamini, na bila shaka Atawatambulisha wanafiki.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا اتَّبِعُوا سَبِيلَنَا وَلْنَحْمِلْ خَطَايَاكُمْ وَمَا هُم بِحَامِلِينَ مِنْ خَطَايَاهُم مِّن شَيْءٍ ۖ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿١٢﴾
12. Na wale waliokufuru wakasema kuwaambia wale walioamini: Fuateni njia yetu, nasi tutabeba madhambi yenu. Na wala wao hawatabeba katika madhambi yao chochote kile. Hakika wao ni waongo.
وَلَيَحْمِلُنَّ أَثْقَالَهُمْ وَأَثْقَالًا مَّعَ أَثْقَالِهِمْ ۖ وَلَيُسْأَلُنَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَمَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿١٣﴾
13. Na bila shaka watabeba mizigo yao (ya dhambi) na mizigo mingine pamoja na mizigo yao. Na kwa hakika wataulizwa Siku ya Qiyaamah kuhusu yale waliyokuwa wakiyatunga ya uongo.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَلَبِثَ فِيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمْسِينَ عَامًا فَأَخَذَهُمُ الطُّوفَانُ وَهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٤﴾
14. Na kwa yakini Tulimpeleka Nuwh kwa watu wake akakaa nao miaka elfu kasoro miaka hamsini, basi ikawachukua tufani nao ni madhalimu.
فَأَنجَيْنَاهُ وَأَصْحَابَ السَّفِينَةِ وَجَعَلْنَاهَا آيَةً لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٥﴾
15. Basi Tukamuokoa na watu wa jahazi, na Tukaifanya kuwa ni Aayah (Ishara, Ukumbusho, Mazingatio) kwa walimwengu.
وَإِبْرَاهِيمَ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاتَّقُوهُ ۖ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١٦﴾
16. Na Ibraahiym pale alipowaambia kaumu yake: Mwabuduni Allaah na mcheni. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua.
إِنَّمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ أَوْثَانًا وَتَخْلُقُونَ إِفْكًا ۚ إِنَّ الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَا يَمْلِكُونَ لَكُمْ رِزْقًا فَابْتَغُوا عِندَ اللَّـهِ الرِّزْقَ وَاعْبُدُوهُ وَاشْكُرُوا لَهُ ۖ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿١٧﴾
17. Hakika mnaabudu badala ya Allaah masanamu, na mnaunda uzushi. Hakika wale mnaowaabudu badala ya Allaah hawakumilikiini riziki, basi tafuteni riziki kwa Allaah, na mwabuduni Yeye na mshukuruni, Kwake mtarejeshwa.
وَإِن تُكَذِّبُوا فَقَدْ كَذَّبَ أُمَمٌ مِّن قَبْلِكُمْ ۖ وَمَا عَلَى الرَّسُولِ إِلَّا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ ﴿١٨﴾
18. Na mkikadhibisha, basi kwa yakini zilikwishakadhibisha nyumati (nyingi) kabla yenu. Na si juu ya Rasuli isipokuwa kubalighisha ujumbe bayana.
أَوَلَمْ يَرَوْا كَيْفَ يُبْدِئُ اللَّـهُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿١٩﴾
19. Je, hawaoni jinsi Allaah Anavyoanzisha uumbaji kisha Anaurudisha? Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.
قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ بَدَأَ الْخَلْقَ ۚ ثُمَّ اللَّـهُ يُنشِئُ النَّشْأَةَ الْآخِرَةَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٠﴾
20. Sema: Nendeni katika ardhi, na mtazame jinsi (Allaah) Alivyoanzisha uumbaji. Kisha Allaah Ataanzisha umbo la Aakhirah (mtakapofufuliwa). Hakika Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.
يُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ وَيَرْحَمُ مَن يَشَاءُ ۖ وَإِلَيْهِ تُقْلَبُونَ ﴿٢١﴾
21. Anamuadhibu Amtakaye, na Anamrehemu Amtakaye, na Kwake mtarudishwa.
وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ ۖ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿٢٢﴾
22. Nanyi si wenye kuweza kukwepa ardhini na wala mbinguni. Na hamna mlinzi wala yeyote mwenye kunusuru badala ya Allaah.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ وَلِقَائِهِ أُولَـٰئِكَ يَئِسُوا مِن رَّحْمَتِي وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٢٣﴾
23. Na wale waliozikanusha Aayaat (na Ishara) za Allaah pamoja na kukutana Naye, hao wamekata tamaa na Rehma Yangu, na hao watapata adhabu iumizayo.
فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَن قَالُوا اقْتُلُوهُ أَوْ حَرِّقُوهُ فَأَنجَاهُ اللَّـهُ مِنَ النَّارِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٢٤﴾
24. Basi halikuwa jawabu la watu wake isipokuwa kusema: Muuweni, au mchomeni moto. Basi Allaah Akamuokoa na moto. Hakika katika hayo mna Aayaat (Ishara, Mazingatio) kwa watu wanaoamini.
وَقَالَ إِنَّمَا اتَّخَذْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ أَوْثَانًا مَّوَدَّةَ بَيْنِكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ ثُمَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُ بَعْضُكُم بِبَعْضٍ وَيَلْعَنُ بَعْضُكُم بَعْضًا وَمَأْوَاكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٢٥﴾
25. Na (Ibraahiym) akasema: Hakika mmefanya badala ya Allaah masanamu kuwa ni mapenzi makubwa baina yenu katika uhai wa dunia, kisha Siku ya Qiyaamah mtakanushana nyinyi wenyewe kwa wenyewe, na mtalaaniana wenyewe kwa wenyewe, na makazi yenu ni moto, na hamtokuwa na wenye kunusuru.
فَآمَنَ لَهُ لُوطٌ ۘ وَقَالَ إِنِّي مُهَاجِرٌ إِلَىٰ رَبِّي ۖ إِنَّهُ هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٦﴾
26. Luutw akamwamini. Na (Ibraahiym) akasema: Hakika mimi nahajiri kwa Rabb wangu, hakika Yeye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَجَعَلْنَا فِي ذُرِّيَّتِهِ النُّبُوَّةَ وَالْكِتَابَ وَآتَيْنَاهُ أَجْرَهُ فِي الدُّنْيَا ۖ وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٢٧﴾
27. Tukamtunukia Is-haaq na (mjukuu) Ya’quwb, na Tukajaalia katika dhuria wake Unabii na Kitabu, na Tukampa ujira wake duniani, na hakika yeye katika Aakhirah bila shaka ni miongoni mwa Swalihina.
وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ إِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنْ أَحَدٍ مِّنَ الْعَالَمِينَ ﴿٢٨﴾
28. Na Luutw alipowaambia watu wake: Hakika nyinyi mnaendea uchafu ambao hakuna yeyote aliyekutangulieni kwa hayo katika walimwengu.
أَئِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ وَتَقْطَعُونَ السَّبِيلَ وَتَأْتُونَ فِي نَادِيكُمُ الْمُنكَرَ ۖ فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَن قَالُوا ائْتِنَا بِعَذَابِ اللَّـهِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٢٩﴾
29. Je, nyinyi mnawaendea wanaume na mnawaibia (na kuwaua) wasafiri, na mnafanya katika mikutano yenu munkari? Basi halikuwa jawabu la watu wake isipokuwa kusema: Tuletee Adhabu ya Allaah ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli.
قَالَ رَبِّ انصُرْنِي عَلَى الْقَوْمِ الْمُفْسِدِينَ ﴿٣٠﴾
30. (Luutw) akasema: Rabb wangu! Ninusuru dhidi ya watu mafisadi.
وَلَمَّا جَاءَتْ رُسُلُنَا إِبْرَاهِيمَ بِالْبُشْرَىٰ قَالُوا إِنَّا مُهْلِكُو أَهْلِ هَـٰذِهِ الْقَرْيَةِ ۖ إِنَّ أَهْلَهَا كَانُوا ظَالِمِينَ ﴿٣١﴾
31. Na Wajumbe Wetu walipomjia Ibraahiym kwa bishara walisema: Hakika sisi tutawahiliki watu wa mji huu. Hakika watu wake wamekuwa madhalimu.
قَالَ إِنَّ فِيهَا لُوطًا ۚ قَالُوا نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَن فِيهَا ۖ لَنُنَجِّيَنَّهُ وَأَهْلَهُ إِلَّا امْرَأَتَهُ كَانَتْ مِنَ الْغَابِرِينَ ﴿٣٢﴾
32. (Ibraahiym) akasema: Hakika humo yumo Luutw. (Malaika) wakasema: Sisi tunajua zaidi waliomo humo. Hapana shaka tutamuokoa pamoja na ahli zake isipokuwa mke wake, amekuwa miongoni mwa watakaobakia nyuma.
وَلَمَّا أَن جَاءَتْ رُسُلُنَا لُوطًا سِيءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْعًا وَقَالُوا لَا تَخَفْ وَلَا تَحْزَنْ ۖ إِنَّا مُنَجُّوكَ وَأَهْلَكَ إِلَّا امْرَأَتَكَ كَانَتْ مِنَ الْغَابِرِينَ ﴿٣٣﴾
33. Na Wajumbe Wetu walipomjia Luutw aliwasikitikia, na akadhikika na kukosa raha kwa ajili yao. (Malaika) wakasema: Usikhofu na wala usihuzunike, hakika sisi tutakuokoa pamoja na ahli zako isipokuwa mke wako, amekuwa miongoni mwa watakaobakia nyuma.
إِنَّا مُنزِلُونَ عَلَىٰ أَهْلِ هَـٰذِهِ الْقَرْيَةِ رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ ﴿٣٤﴾
34. Hakika Sisi Tutawateremshia watu wa mji huu adhabu ya kufadhaika kutoka mbinguni kwa sababu ya ule ufasiki waliokuwa wanafanya.
وَلَقَد تَّرَكْنَا مِنْهَا آيَةً بَيِّنَةً لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿٣٥﴾
35. Na kwa yakini Tuliacha humo Aayah (Ishara, Athari) bayana kwa watu wanaotia akilini.
وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا فَقَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَارْجُوا الْيَوْمَ الْآخِرَ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ ﴿٣٦﴾
36. Na kwa Madyan Tulimtuma ndugu yao Shu’ayb, akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, na tarajieni Siku ya Mwisho, na wala msifanye uovu katika ardhi mkifisidi.
فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ ﴿٣٧﴾
37. Wakamkadhibisha, basi likawachukuwa tetemeko kali la ardhi wakapambaukiwa majumbani mwao wenye kuanguka kifudifudi.
وَعَادًا وَثَمُودَ وَقَد تَّبَيَّنَ لَكُم مِّن مَّسَاكِنِهِمْ ۖ وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَصَدَّهُمْ عَنِ السَّبِيلِ وَكَانُوا مُسْتَبْصِرِينَ ﴿٣٨﴾
38. Na kina ‘Aad na Thamuwd. Na bila shaka (maangamizi yao) yamekwishakubainikieni katika masikani zao. Na shaytwaan aliwapambia amali zao, akawazuia na njia, japokuwa walikuwa ni wenye kumaizi na kutambua vizuri.
وَقَارُونَ وَفِرْعَوْنَ وَهَامَانَ ۖ وَلَقَدْ جَاءَهُم مُّوسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ فَاسْتَكْبَرُوا فِي الْأَرْضِ وَمَا كَانُوا سَابِقِينَ ﴿٣٩﴾
39. Na kina Qaaruwn, na Firawni, na Haamaan[4]. Na kwa yakini aliwajia Muwsaa kwa hoja bayana wakatakabari katika ardhi, lakini hawakuwa wenye kushinda.
فَكُلًّا أَخَذْنَا بِذَنبِهِ ۖ فَمِنْهُم مَّنْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِ حَاصِبًا وَمِنْهُم مَّنْ أَخَذَتْهُ الصَّيْحَةُ وَمِنْهُم مَّنْ خَسَفْنَا بِهِ الْأَرْضَ وَمِنْهُم مَّنْ أَغْرَقْنَا ۚ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٤٠﴾
40. Basi kila mmoja Tulimchukuwa kumwadhibu kwa mujibu wa dhambi yake. Miongoni mwao wale Tuliowapelekea tufani, na miongoni mwao wale waliochukuliwa na ukelele angamizi, na miongoni mwao wale Tuliowadidimiza ardhini, na miongoni mwao wale Tuliowagharikisha. Na Allaah Hakuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao wenyewe.[5]
مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ أَوْلِيَاءَ كَمَثَلِ الْعَنكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتًا ۖ وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنكَبُوتِ ۖ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٤١﴾
41. Mfano wa wale waliochukuwa badala ya Allaah walinzi ni kama mfano wa buibui alivyojitandia nyumba. Na bila shaka nyumba iliyo dhaifu kuliko zote ni nyumba ya buibui, lau wangelikuwa wanajua![6]
إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ مِن شَيْءٍ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٤٢﴾
42. Hakika Allaah Anavijua vyote vile wanavyoviomba badala Yake, Naye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
وَتِلْكَ الْأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ ۖ وَمَا يَعْقِلُهَا إِلَّا الْعَالِمُونَ ﴿٤٣﴾
43. Na hiyo ni mifano Tunawapigia watu. Lakini hawaifahamu isipokuwa wenye ilimu.
خَلَقَ اللَّـهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّلْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٤﴾
44. Allaah Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Hakika katika hayo mna Aayah (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa Waumini.
اتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ وَأَقِمِ الصَّلَاةَ ۖ إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ ۗ وَلَذِكْرُ اللَّـهِ أَكْبَرُ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ ﴿٤٥﴾
45. Soma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uliyoletewa Wahy katika Kitabu na simamisha Swalaah, hakika Swalaah inazuia machafu na munkari. Na bila shaka kumdhukuru Allaah ndilo kubwa zaidi. Na Allaah Anajua yale mnayoyatenda.
وَلَا تُجَادِلُوا أَهْلَ الْكِتَابِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ إِلَّا الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ ۖ وَقُولُوا آمَنَّا بِالَّذِي أُنزِلَ إِلَيْنَا وَأُنزِلَ إِلَيْكُمْ وَإِلَـٰهُنَا وَإِلَـٰهُكُمْ وَاحِدٌ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿٤٦﴾
46. Na wala msibishane na Watu wa Kitabu isipokuwa kwa yale ambayo ni mazuri zaidi, isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tumeyaamini ambayo yameteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu, na Ilaah wetu na Ilaah wenu ni (Allaah) Mmoja Pekee, nasi Kwake tunajisalimisha.
وَكَذَٰلِكَ أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ ۚ فَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۖ وَمِنْ هَـٰؤُلَاءِ مَن يُؤْمِنُ بِهِ ۚ وَمَا يَجْحَدُ بِآيَاتِنَا إِلَّا الْكَافِرُونَ ﴿٤٧﴾
47. Na hivyo ndivyo Tulivyokuteremshia Kitabu (Qur-aan). Basi wale Tuliowapa Maandiko (Tawraat na Injiyl) wanakiamini. Na miongoni mwa hawa (Maquraysh wa Makkah) wako ambao wanakiamini. Na hawakanushi Aayaat (na Ishara) Zetu isipokuwa makafiri.
وَمَا كُنتَ تَتْلُو مِن قَبْلِهِ مِن كِتَابٍ وَلَا تَخُطُّهُ بِيَمِينِكَ ۖ إِذًا لَّارْتَابَ الْمُبْطِلُونَ ﴿٤٨﴾
48. Na wala hukuwa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ukisoma kabla yake kitabu chochote, na wala hukukiandika kwa mkono wako wa kuume, kwani basi hapo wangetilia shaka wabatilifu.
بَلْ هُوَ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ فِي صُدُورِ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ ۚ وَمَا يَجْحَدُ بِآيَاتِنَا إِلَّا الظَّالِمُونَ ﴿٤٩﴾
49. Bali hizi ni Aayaat bayana (zimehifadhika) katika vifua vya wale waliopewa ilimu. Na hawazikanushi Aayaat Zetu isipokuwa madhalimu.
وَقَالُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ آيَاتٌ مِّن رَّبِّهِ ۖ قُلْ إِنَّمَا الْآيَاتُ عِندَ اللَّـهِ وَإِنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٥٠﴾
50. Na wakasema: Kwa nini hakuteremshiwa Aayaat (Miujiza ya kihisia na Ishara, Dalili) kutoka kwa Rabb wake? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika Aayaat ziko kwa Allaah, na hakika mimi ni mwonyaji mbainishaji tu.
أَوَلَمْ يَكْفِهِمْ أَنَّا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَرَحْمَةً وَذِكْرَىٰ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٥١﴾
51. Je, haikuwatosheleza kwamba hakika Sisi Tumekuteremshia Kitabu (Qur-aan) wanachosomewa? Hakika katika hayo bila shaka kuna rehma na ukumbusho (na mawaidha) kwa watu wanaoamini.
قُلْ كَفَىٰ بِاللَّـهِ بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ شَهِيدًا ۖ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَالَّذِينَ آمَنُوا بِالْبَاطِلِ وَكَفَرُوا بِاللَّـهِ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٥٢﴾
52. Sema: Anatosheleza Allaah kuwa ni Shahidi baina yangu na baina yenu. Anayajua yale yaliyomo katika mbingu na ardhi. Na wale walioamini ubatilifu na wakamkufuru Allaah, hao ndio waliokhasirika.
وَيَسْتَعْجِلُونَكَ بِالْعَذَابِ ۚ وَلَوْلَا أَجَلٌ مُّسَمًّى لَّجَاءَهُمُ الْعَذَابُ وَلَيَأْتِيَنَّهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٥٣﴾
53. Na wanakuharakiza adhabu. Na lau kama si muda maalumu uliokadiriwa, ingeliwajia adhabu, na bila shaka itawajia ghafla na hali wao hawahisi.[7]
يَسْتَعْجِلُونَكَ بِالْعَذَابِ وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمُحِيطَةٌ بِالْكَافِرِينَ ﴿٥٤﴾
54. Wanakuharakiza adhabu na hakika Jahannam bila shaka itawazunguka makafiri.
يَوْمَ يَغْشَاهُمُ الْعَذَابُ مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِمْ وَيَقُولُ ذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٥٥﴾
55. Siku itakayowafunika adhabu kutoka juu yao na kutoka chini ya miguu yao, na Atasema: Onjeni yale mliyokuwa mkitenda.
يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ أَرْضِي وَاسِعَةٌ فَإِيَّايَ فَاعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾
56. Enyi Waja Wangu walioamini! Hakika Ardhi Yangu ni pana, basi Mimi Pekee Niabuduni.
كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۖ ثُمَّ إِلَيْنَا تُرْجَعُونَ ﴿٥٧﴾
57. Kila nafsi itaonja mauti, kisha Kwetu mtarejeshwa.
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَنُبَوِّئَنَّهُم مِّنَ الْجَنَّةِ غُرَفًا تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ نِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿٥٨﴾
58. Na wale walioamini na wakatenda mema, bila shaka Tutawawekea makazi ya ghorofa katika Jannah, yapitayo chini yake mito, ni wenye kudumu humo. Uzuri ulioje ujira wa watendao!
الَّذِينَ صَبَرُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ ﴿٥٩﴾
59. Ambao walisubiri, na kwa Rabb wao wanatawakali.
وَكَأَيِّن مِّن دَابَّةٍ لَّا تَحْمِلُ رِزْقَهَا اللَّـهُ يَرْزُقُهَا وَإِيَّاكُمْ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٦٠﴾
60. Na viumbe wangapi hawabebi riziki zao? Allaah Huwaruzuku wao na nyinyi. Naye Ndiye Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٦١﴾
61. Na ukiwauliza: Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi, na akatiisha jua na mwezi? Bila shaka watasema: Allaah. Basi vipi wanaghilibiwa?[8]
اللَّـهُ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَيَقْدِرُ لَهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٦٢﴾
62. Allaah Anamkunjulia riziki Amtakaye kati ya Waja Wake na Humkadiria kwa kipimo (Amtakaye). Hakika Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.
وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّن نَّزَّلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ مِن بَعْدِ مَوْتِهَا لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۚ قُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿٦٣﴾
63. Na ukiwauliza: Ni nani Ateremshaye maji kutoka mbinguni, Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake? Bila shaka watasema: Allaah. Sema: AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah). Bali wengi wao hawatii akilini.
وَمَا هَـٰذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَهْوٌ وَلَعِبٌ ۚ وَإِنَّ الدَّارَ الْآخِرَةَ لَهِيَ الْحَيَوَانُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٦٤﴾
64. Na huu uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni pumbao na mchezo. Na hakika Nyumba ya Aakhirah bila shaka ndiyo yenye uhai wa kweli hasa (wa milele), lau wangelikuwa wanajua!
فَإِذَا رَكِبُوا فِي الْفُلْكِ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ فَلَمَّا نَجَّاهُمْ إِلَى الْبَرِّ إِذَا هُمْ يُشْرِكُونَ ﴿٦٥﴾
65. Wanapopanda merikebu humwomba Allaah wakiwa wenye kumtakasia Yeye Duaa, lakini Anapowaokoa wakafika nchi kavu, tahamaki hao wanamshirikisha.[9]
لِيَكْفُرُوا بِمَا آتَيْنَاهُمْ وَلِيَتَمَتَّعُوا ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ ﴿٦٦﴾
66. Ili wayakanushe yale Tuliyowapa, na ili wastarehe. Basi karibuni watakuja kujua.
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا جَعَلْنَا حَرَمًا آمِنًا وَيُتَخَطَّفُ النَّاسُ مِنْ حَوْلِهِمْ ۚ أَفَبِالْبَاطِلِ يُؤْمِنُونَ وَبِنِعْمَةِ اللَّـهِ يَكْفُرُونَ ﴿٦٧﴾
67. Je, hawaoni kwamba hakika Sisi Tumejaalia (Makkah) kuwa ni tukufu na yenye amani, na huku wananyakuliwa watu pembezoni mwao? Je, basi wanaamini baatwil, na Neema za Allaah wanazikufuru?
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُ ۚ أَلَيْسَ فِي جَهَنَّمَ مَثْوًى لِّلْكَافِرِينَ ﴿٦٨﴾
68. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemtungia Allaah uongo, au aliyekadhibisha haki ilipomjia? Je, si katika Jahannam ndio yatakuwa makazi ya makafiri?
وَالَّذِينَ جَاهَدُوا فِينَا لَنَهْدِيَنَّهُمْ سُبُلَنَا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَمَعَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٦٩﴾
69. Na wale waliofanya juhudi kwa ajili Yetu, bila shaka Tutawaongoza njia Zetu. Na hakika Allaah Yu Pamoja na watendao ihsaan.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah/Katazo La Kuwatii Viumbe Katika Kumwasi Muumbaji Hata Kama Ni Wazazi:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
029-Asbaabun-Nuzuwl: Al-‘Ankabuwt Aayah 08: وَوَصَّيْنَا الإِنْسَانَ بِوَالِدَيْهِ حُسْنًا [227]
Juu ya kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ametilia umuhimu mkubwa wa kuwatii wazazi, lakini utiifu kwa wazazi una mipaka. Mzazi anapomwamrisha mwanawe kumuasi Allaah (سبحانه وتعالى), basi mtoto hapaswi kumfuata katika hilo, na Hadiyth zifuatazo zimethibitisha jambo hili:
عَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ لَا طَاعَةَ لِبَشَرٍ فِي مَعْصِيَةِ اللَّهِ
Amesimulia ‘Aliy (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna utiifu kwa kiumbe katika maasi ya Allaah.” [Ahmad]
Na amesema pia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
لَا طَاعَةَ لِمَخْلُوقٍ فِي مَعْصِيَةِ الْخَالِقِ
“Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba” [At-Tirmidhiy]
Na amrisho la kuwafanyia ihsaan wazazi na kutokuwatii katika maasi, linawahusu wazazi Waislamu na wasiokuwa Waislamu. Na hata kama wazazi wataamrisha maasi, lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Anaamrisha kuishi na kukaa nao kwa wema duniani, ni sawa wawe ni wazazi Waislamu au sio Waislamu.
Rejea pia Luqmaan (31:14-15).
[4] Haamaan:
Alikuwa ni waziri au mtu mwenye cheo. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Ama kuhusu Qaaruwn, Rejea Al-Qaswasw (28:76).
[5] Makafiri Wa Nyumati Za Nyuma Na Aina Za Adhabu Zao:
Katika Suwrah hii ya Al-‘Ankabuwt namba (40), Allaah (سبحانه وتعالى) Ametaja aina za adhabu walizoangamizwa kwazo makafiri wa nyumati za nyuma. Adhabu hizo ni kupelekewa tufani, ukelele angamizi, kudidimizwa ardhini, kugharakishwa. Na yafuatayo ni uchambuzi wa kaumu za nyumati za nyuma, na aina za adhabu zao, na baadhi ya rejea mbali mbali za visa vyao.
(i) Kaumu ya Nabiy Nuwh (عليه السّلام):
Watu wa Nuwh (عليه السّلام) walikuwa wakimshirikisha Allaah kwa kuabudu masanamu. Na wao ni watu wa kwanza kabisa ardhini kuanzisha ibaada ya masanamu. Walianza ibaada ya masanamu baada ya kufariki waja wema ambao majina yao ni: Waddaa, Suwaa’aa, Yaghuwtha, Ya’uwqa, na Nasraa. Rejea Nuwh (71:23). Shaytwaan akawapambia kuwakurubisha nao, wakachora sura zao na kuchonga masanamu ya kuwanasabisha. Na hapo ndipo ikaendelea ibaada ya masanamu kwa Waarabu na kaumu nyenginezo karne kwa karne. Na ndio maana Nabiy Nuwh (عليه السّلام) akawa ni Rasuli wa kwanza kulingania watu katika Tawhiyd ya Allaah (Kumpwekesha Allaah). Rejea Asw-Swaaffaat (37:77).
Maangamizi Yao: Washirikina hao wa kaumu ya Nuwh (عليه السّلام) waliangamizwa kwa tufani lililowagharakisha baharini. Rejea Suwrah hii Al-‘Ankabuwt (29:14), Al-Furqaan (25:37).
Nuwh (عليه السّلام) akawalingania kaumu yake waache ushirikina wa kuabudu masanamu na badala yake akawaamrisha wamwabudu Allaah (سبحانه وتعالى), lakini Lakini walimkanusha. Akaendelea kuwalingania kwa muda wa miaka 950, lakini waliendelea kumkanusha na wakawa wanamfanyia istihzai alipokuwa akiunda jahazi. Rejea Huwd (11:38). Allaah Akafungua mbingu na ardhi zikamiminika maji hadi ikawa ni bahari. Rejea Al-Qamar (54:11-12). Mawimbi yakawafunika, wakagharakishwa katika maji hayo watu wake pamoja na mwanawe, na Allaah Akamuokoa Nuwh pamoja na walioamini ambao walipanda jahazini. Rejea Huwd (11:41-43).
Rejea Al-A’raaf (7:59-64), Yuwnus (10:71-73), Huwd (11:25-48), Al-Anbiyaa (21:76-77), Al-Muuminuwn (23:23-30), Al-Furqaan (25:37), Ash-Shu’araa (26:105-120), Al-‘Ankabuwt (29:14-15), Asw-Swaaffaat (37:75-78), Al-Qamar (54:10-15) na Suwrah ya Nuwh namba (71).
(ii) Kaumu ya ‘Aad watu wa Nabiy Huwd (عليه السّلام):
Watu wa ‘Aad walikuwa wakimshirikisha Allaah kwa kuabudu masanamu.
Maangamizi Yao: Waliangamizwa kwa tufani na upepo mbaya wa sauti na baridi kali, uvumao kwa nguvu kwa muda wa siku nane mfululizo, ukawaangamiza wakawa kama magogo ya mitende iliyo mitupu. Rejea Al-Haaqqah (69:6-8). Na pia radi na umeme angamizi. Rejea Fusw-Swilat (41:13),
Allaah (سبحانه وتعالى) Aliwajaalia kaumu ya ‘Aad wenye umbo zuri na nguvu na uwezo wa kujenga majumba ya kifakhari, na ardhi yao ilikuwa bustani ya kijani kibichi ambapo mifugo ililishwa na kuongezeka, na hivyo wakajaaliwa mali nyingi za kila aina na watoto. Nabiy wao Huwd (عليه السّلام) aliwalingania waache ibaada ya masanamu na wampwekeshe Allaah (سبحانه وتعالى), lakini walimkanusha wakaendelea na kuabudu masanamu na kutakabari na kujiona kuwa wao ni wenye nguvu zaidi wakasema: ”Nani mwenye nguvu zaidi kuliko sisi?” Rejea Fusw-Swilat (41:15). Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaangamiza kwa tufani na upepo mbaya wa sauti na baridi kali, uvumao kwa nguvu.
Rejea Al-A’raaf (7:65-72), Huwd (11:50-60), Ash-Shu’araa (26:123-139), Fusw-Swilat (41:16), Al-Ahqaaf (46:21-25), Adh-Dhaariyaat (51:41-42), Al-Qamar (54:18-21), Al-Haaqqah (69:6-7), Al-Fajr (89:6-8).
(iii) Kaumu Ya Thamuwd Watu Wa Nabiy Swaalih (عليه السّلام):
Watu wa Thamuwd walikuwa wakimshirikisha Allaah kwa kuabudu masanamu.
Maangamizi Yao: Waliangamizwa kwa tetemeko la ardhi, rejea Al-A’raaf (7:78), na ukelele angamizi mkali mno uliovuka mipaka. Al-Haaqqah (69:5). Na pia radi na umeme angamizi. Rejea Rejea Fusw-Swilat (41:18).
Allaah (سبحانه وتعالى) Aliwajaalia kaumu ya Thamuwd neema za mabustani na chemchemu, na uwezo wa kuchonga nyumba nzuri milimani.
Nabiy wao Swaalih (عليه السّلام) aliwalingania waache ibaada ya masanamu na wampwekeshe Allaah, lakini walitakabari na wakakanusha Risala, na wakafanya ufisadi katika ardhi. Nabiy Swaalih (عليه السّلام) alipoendelea kuwalingania, walitaka muujiza kutoka kwa Allaah waletewe ngamia jike aliyekuwa na mimba atoke kwenye mwamba. Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaitikia maombi yao, Akawatumia mbele ya macho yao ngamia na kwa sifa walizozitaka. Wakaamrishwa wamhifadhi ngamia wasimguse kwa uovu wowote ule na wafanye zamu katika kunywa maji ya kisimani; siku anywe ngamia na siku wanywe wao. Rejea Ash-Shu’araa (26:155-156) na Al-Qamar (54:27-28). Lakini walitakabari, wakamzuia ngamia asinywe maji na wakamuua, na wakafanya njama pia kumuua Nabiy Swaalih (عليه السّلام) . Rejea An-Naml (27:48-49). Basi Akaanza kuwaonyesha ishara ya adhabu siku tatu nyuso zao zikibadilika rangi kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaangamiza kwa ukelele mkali mno na tetemeko la ardhi, wakaanguka kifudifudi majumbani mwao wakiwa wamefariki.
Rejea Al-A’raaf (7:73-79), Huwd (11:61-68), Al-Israa (17:59), Ash-Shu’araa (26:141-158), An-Naml (27:45-53), Fusw-Swilat (41:17), Adh-Dhaariyat (51:43-45), Al-Qamar (54:23-31), Ash-Shams (91:11-15),
(iv) Kaumu Ya Nabiy Luutw (عليه السّلام):
Watu wa Nabiy Luutw (عليه السّلام) walikuwa wakifanya machafu ya kuwaingilia wanaume wenzao katika duburi zao.
Maangamizi Yao: Waliangamizwa kwa kupinduliwa mji wao juu chini na pia kwa ukelele angamizi. Rejea Al-Hijr (15:73-74). Pia kwa mvua ya mawe ya udongo mgumu uliookwa motoni, yametiwa alama. Rejea Huwd (11:82-83). Pia kwa tufani ya mawe. Rejea Al-Qamar (54:34).
Nabiy wao Luutw (عليه السّلام) akawalingania waache machafu hayo na badala yake wawaoe wanawake ambao ndio inavyotaka kisharia kujimai nao. Lakini walimkanusha wao pamoja na mkewe ambaye naye pia alibakishwa nyuma aingie katika maangamizi.
Rejea Al-A’raaf (7:80-84), Huwd (11:77-83), Al-Hijr (15:61-74), Ash-Shu’araa (26:160-173), An-Naml (27:54-58), Al-‘Ankabuwt (29:28-34), Al-Qamar (54:33-39),
(v) Watu Wa Madyan Ambao Ni Kaumu Ya Nabiy Shu’ayb (عليه السّلام):
Watu wa Nabiy Shu’ayb (عليه السّلام) walikuwa wakimshirikisha Allaah kwa kuabudu masanamu. Juu ya hivyo, walikuwa wakifanya ufisadi katika ardhi; wakifanya khiyana ya kupunja vipimo katika mizani, na kuzuia watu njia ya Allaah.
Maangamizi Yao: Waliangamizwa kwa tetemeko la ardhi. Rejea Al-‘Araaf (7:92). Na ukelele angamizi. Rejea Huwd (11:94).
Nabiy Shu’ayb akawalingania lakini walimkanusha wakataka kumfukuza mjini, basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaangamiza kwa ukelele angamizi na tetemeko la ardhi wakafilia mbali.
Rejea Al-A’raaf (7:85-93), Huwd (11:84-95), Al-‘Ankabuwt (29:36-37).
(vi) Firawni, Haamaan Na Jeshi Lake:
Firawni alikuwa akiwatesa wana wa Israaiyl na akiwaua wanawake wao na watoto wao.
Maangamizi Yao: Waligharakishwa baharini Rejea Al-Qaswasw (28:40), Adh-Dhaariyaat (51:40).
Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) akatumwa kwake kumlingania, lakini alitakabari na akapinduka mipaka hadi kujifanya yeye ni mwenye kustahiki kuabudiwa. Akakanusha Risala ya Rabb wake kupitia kwa Nabiy Muwsaa (عليه السّلام). Allaah (سبحانه وتعالى) Akawapelekea miujiza tisa lakini hakutaka kumwamini Allaah na akaendelea na kiburi chake na akaazimia kumuua Nabiy Muwsaa (عليه السّلام). Allaah (سبحانه وتعالى) Akamuamrisha Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) apige fimbo yake katika bahari, basi hapo bahari ikatengana ikawa kila sehemu kama jabali kubwa. Akavuka Nabiy Muwsaa na wana wa Israaiyl, kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akamuangamiza Firawni na waziri wake Haamaan na jeshi lake katika bahari.
Na kisa cha Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) na Firawni kimetajwa sehemu nyingi mno na kwa urefu kuliko Rusuli wengineo. Miongoni mwa Suwrah ambazo kimetajwa kwa wingi ni Suwrah Al-A’raaf namba (7) kuanzia Aayah namba (103) na kumalizikia Aayah namba (171). Pia Yuwnus (10:75-92). Rejea pia Huwd (11:96-99). Rejea pia Twaahaa (20:9-79), Al-Muuminuwn (23:45-48), Ash-Shu’araa (26:10-66), Al-Qaswasw (28:3-40), An-Naazi’aat (79:15-25).
Na rejea khasa Al-A’raaf (7:107-108), (7:130) na (7:133) kwenye uchambuzi bayana, kuhusu miujiza tisa ya Allaah kwa watu wa Firawni.
(vii) Qaaruwn: Alikuwa Katika Watu Wa Nabiy Muwsaa (عليه السّلام):
Qaaruwn alipinduka mipaka katika maasia, na akatakabari kwa majivuno na kujigamba kwa kujaaliwa hazina ya mali. Akajigamba kuwa mali hiyo kuwa imetokana na ujuzi wake, akamsahau Rabb wake Aliyemruzuku.
Rejea Al-Qaswasw: (28-76-82).
Maangamizi Yake: Alididimizwa ardhini. Rejea Al-Qaswasw (28:81).
[6] Masanamu Na Waabudiwa Wengineo Pasi Na Allaah Ni Kama Nyumba Ya Buibui:
Mfano wa wale waliowafanya masanamu ni walinzi badala ya Allaah na huku, wanatarajia nusura na usaidizi wao, ni kama mfano wa buibui aliyejitengenezea nyumba ili imuhifadhi (kutokana madhara ya kila aina), lakini isimfae kitu alipokuwa na haja nayo. Basi kadhaalika hivyo ndivyo hali ilivyo kwa hawa washirikiana, hawakuwafaa kitu wale waliowachukuwa kuwafanya kuwa ni walinzi wao badala ya Allaah. Na bila shaka nyumba iliyo dhaifu kuliko zote ni nyumba ya buibui. Lau wangelikuwa wanajua hilo, wasingewafanya wao ni walinzi wao wenye kutegemewa kwa sababu hawawanufaishi lolote wala hawawadhuru. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Na Imaam Ibn Kathiyr ametafsiri: Mfano huu Allaah Anaupiga kwa washirikina waliowafanya waabudiwa asiyekuwa Allaah wakitaraji usaidizi wao (au nusura) na rizki zao, na wanawashikilia katika shida zao. Basi wao ni kama hiyo nyumba ya buibui ambayo ni dhaifu mno. Hivyo ni kwa sababu, kuwashikilia waabudiwa hawa ni kama mtu kushikilia nyumba ya buibui ambayo haimfai kitu. Na lau wangelikua wanajua hali hii, basi wasingeliwachukua asiyekuwa Allaah kuwafanya ni walinzi. Na hii ni kinyume na Muislamu Muumin ambaye moyo wake umejisabilia kwa dhati na kuelemea kwa Allaah, lakini bado anafanya matendo mema na anafuata Sharia za Allaah. Hivyo ni kwa sababu ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika, kutokana na nguvu yake na kuthibitika kwake. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[7] Ada Ya Makafiri Kuhimiza Adhabu: Rejea: Al-Anfaal (8:32), Al-Hajj (22:47), Swaad (38:16)
[8] Washirikina Waliamini Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah Lakini Walikanusha Tawhiyd Al-Uluwhiyyah.
Washirikina wa Makkah waliamini yafuatayo katika kumpwekesha Allaah (سبحانه وتعالى):
(i) Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Aliyewaumba: Az-Zukhruf (43:87).
(ii) Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi: Suwrah hii Al-‘Ankabuwt (29:61), Luqmaan (31:25) na Az-Zumar (39:38).
(iii) Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Aliyetiisha jua na mwezi: Suwrah hii Al-‘Ankabuwt (29:61).
(iv) Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Ateremshaye maji kutoka mbinguni, Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake. Suwrah hii Al-‘Ankabuwt (29:63).
(v) Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Anayewaruzuku na Ndiye Anayemiliki kusikia na kuona. Na Ndiye Anayehuisha na Kufisha na Ndiye Anayeendesha mambo yote ya ulimwenguni: Yuwnus (10:31), Az-Zukhruf (43:9).
Lakini walimshirikisha katika Tawhiyd Al-Uluwhiyyah ambayo ni kumpwekesha katika ibaada, yaani, kumwelekea Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee katika kumwabudu na kumuomba duaa badala ya kuelekea masanamu au viumbe vinginevyo.
Wakamshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kumhusisha na viumbe Alivyoviumba kama vile kusema Ana mwana, au Malaika ni mabinti Wake, au Ana uhusiano na majini! Subhaana Allaah! (Ametakasika Allaah!). Rejea Asw-Swaaffaat (37:149).
Wakamshirikisha Allaah katika mimea na wanyama Aliyoumba. Ikawa wanapochinja hawaanzi kwa Jina la Allaah. Na pia wakawa wanakusudia kumwekea Allaah (سبحانه وتعالى) sehemu ya nyama waliyokuwa wakichinja na sehemu wakiwaekea masanamu yao! Rejea Al-An’aam (6:136), (6:138-139).
Wakamshirikisha katika Hajj, kwani kabla ya Uislamu, washirikina walikuwa wakihiji, lakini Hijjah yao ilikuwa ni ya kufru na uasi. Walikuwa wakitufu Al-Ka’bah mbele ya masanamu kwa miruzi na kupiga makofi. Rejea Al-Anfaal (8:35).
Wakamshirikisha pia katika Hajj kwenye talbiyah kwa kuongezea maneno ya kumshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى). Walikuwa wakisema:
لبيك لا شريك لك، إلا شريكاً هو لك، تملكه وما ملك
Nimekuitikia, (ee Allaah) Huna mshirika yoyote. Isipokuwa mshirika, yeye ni Wako, Unammiliki, na yeye hamiliki chochote.
Kinyume na talbiyah ya Tawhiyd ambayo ni:
لَبَّيْكَ اللَّهُمَّ لَبَّيْكَ ، لَبَّيْكَ لاَ شَرِيكَ لَكَ لَبَّيْكَ ، إِنَّ الْحَمْدَ ، وَالنِّعْمَةَ ، لَكَ وَالْمُلْكَ ، لاَ شَرِيكَ لَكَ
"Nimekuitikia (ee Allaah) nimekuitikia (ee Allaah), nimekuitikia (ee Allaah) Huna mshirika nimekuitikia (ee Allaah), hakika Kuhimidiwa na Neema na Ufalme ni Vyako Huna mshirika."
Maneno yao hayo ya shirki, ni kama ilivyo katika Hadiyth ifuatayo:
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ قَالَ: كَانَ الْمُشْرِكُونَ يَقُولُونَ: لَبَّيْكَ لَا شَرِيكَ لَكَ فَيَقُولُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «وَيْلَكُمْ قَدْ قَدْ» إِلَّا شَرِيكًا هُوَ لَكَ تَمْلِكُهُ وَمَا مَلَكَ. يَقُولُونَ هَذَا وَهُمْ يَطُوفُونَ بِالْبَيْتِ. رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Amesimulila Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): “Wapagani walikuwa wanasema: Nimekuitikia, (ee Allaah) Huna mshirika yoyote. Na hapo hapo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) huwaambia: Ole wenu! Acheni, msiongeze (mkasema): “Isipokuwa mshirika, yeye ni Wako, Unammiliki, na yeye hamiliki chochote”, wanasema haya huku wanaitufu Nyumba (Al-Ka’bah)”. [Muslim]
Sharh Ya Hadiyth:
Talbiyah wanayoileta Waislamu katika Hajji inakuwa kwa kumpwekesha Allaah (سبحانه وتعالى), kumtakasia Yeye tu Dini na kujiweka mbali na shirki. Ama mapagani, talbiyah yao katika Hajji ilikuwa kwa kumshirikisha Allaah.
Katika Hadiyth hiyo, ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما) anaeleza kwamba wapagani walipokuwa wanaitufu Al-Ka’bah, walikuwa wanaianza talbiyah kwa kumpwekesha Allaah (Tawhiyd) wakisema:
"لبَّيكَ لا شَريكَ لكَ"
“Nimekuitikia, (ee Allaah) Huna mshirika yoyote”.
Na kwa vile Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anajua nini wanataka kusema baada ya maneno hayo, alikuwa wanapoleta talbiyah mwanzo kwa kumpwekesha Allaah, huwaambia: Ole wenu! Yaani, mtapata adhabu na maangamizo kwa hayo mnayotaka kuyaongeza katika talbiyah. Acheni hayo, bali toshekeni tu na maneno ya kumpwekesha Allaah, na wala msiongeze baada yake neno lenu (la awali):
"إلَّا شَريكًا هوَ لكَ، تَملِكُه وَما ملَكَ"
“Isipokuwa mshirika, yeye ni Wako, Unammiliki, na yeye hamiliki chochote”
Mshirika wanayemkusudia hapa ni masanamu yao. Na kwa muktadha huo, maneno haya yanabeba maana mbili. Ya kwanza: Wewe Unammiliki pamoja na vyote vilivyomo ndani ya milki yake. Ya pili: Wewe Unammiliki, na yeye hamiliki chochote.
Kwa maana hii, wao wanakiri kwamba mshirika huyu hastahiki kuabudiwa kwa chochote, kwa kuwa yeye mwenyewe hamiliki chochote kwa nafsi yake wala kwa mwingine, bali mmiliki wa yote ni Allaah. Lakini pamoja na kukiri huku, wanamshirikisha na Allaah katika ibaada, ima kwa kuwa hawajui, au kwa inadi, au kwa jeuri, au kwa kibri. Allaah Amesema:
وَاتَّخَذُوا مِن دُونِهِ آلِهَةً لَّا يَخْلُقُونَ شَيْئًا وَهُمْ يُخْلَقُونَ وَلَا يَمْلِكُونَ لِأَنفُسِهِمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا وَلَا يَمْلِكُونَ مَوْتًا وَلَا حَيَاةً وَلَا نُشُورًا ﴿٣﴾
“Na wakachukua badala Yake (Allaah) waabudiwa wasioumba chochote na hali wao wanaumbwa, wala hawamiliki kwa ajili ya nafsi zao dhara wala manufaa, wala hawamiliki mauti wala uhai wala ufufuo.” [Al-Furqaan (25:3)]
[9] Washirikina Walimpwekesha Allaah Katika Kumuomba Duaa Kwenye Shida Ama Kwenye Raha Walimshirikisha:
Imaam Muhammad Bin ‘Abdil-Wahhaab (رحمه الله) ametaja katika Al-Qawaaid Al-Arba’: Washirikina wa zama zetu ni waovu zaidi katika shirki zao kuliko washirikina wa zamani kwa sababu, wa zamani walimshirikisha Allaah katika raha, lakini walitakasa (ibaada zao) wakati wa shida. Ama washirikina wa sasa, shirki zao ni za kuendelea daima wakiwa katika raha au katika shida. Akatoa dalili Aayah hii ya Al-‘Ankabuwt (29:65).
Rejea pia Suwrah hii Al-‘Ankabuwt (29:61) na Yuwnus (10:31) kwenye faida ziyada.
الرُّوم
030-Ar-Ruwm
030-Ar-Ruwm: Utangulizi Wa Suwrah [230]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الم ﴿١﴾
1. Alif Laam Miym.[1]
غُلِبَتِ الرُّومُ ﴿٢﴾
2. Warumi wameshindwa.[2]
فِي أَدْنَى الْأَرْضِ وَهُم مِّن بَعْدِ غَلَبِهِمْ سَيَغْلِبُونَ ﴿٣﴾
3. Katika nchi iliyo karibu, nao baada ya kushindwa kwao, watashinda hivi karibuni.
فِي بِضْعِ سِنِينَ ۗ لِلَّـهِ الْأَمْرُ مِن قَبْلُ وَمِن بَعْدُ ۚ وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ ﴿٤﴾
4. Katika miaka baina ya mitatu na tisa. Amri ni ya Allaah Pekee kabla na baada. Na Siku hiyo watafurahi Waumini.
بِنَصْرِ اللَّـهِ ۚ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿٥﴾
5. Kwa Nusura ya Allaah. Anamnusuru Amtakaye, Naye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu.
وَعْدَ اللَّـهِ ۖ لَا يُخْلِفُ اللَّـهُ وَعْدَهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٦﴾
6. Ni Ahadi ya Allaah. Allaah Hakhalifu Ahadi Yake, lakini watu wengi hawajui.
يَعْلَمُونَ ظَاهِرًا مِّنَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ عَنِ الْآخِرَةِ هُمْ غَافِلُونَ ﴿٧﴾
7. Wanajua yaliyo dhahiri ya uhai wa dunia, lakini wao wameghafilika na Aakhirah.
أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا فِي أَنفُسِهِم ۗ مَّا خَلَقَ اللَّـهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَأَجَلٍ مُّسَمًّى ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ لَكَافِرُونَ ﴿٨﴾
8. Je, hawatafakari katika nafsi zao? Allaah Hakuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake isipokuwa kwa haki na muda maalumu uliokadiriwa. Na hakika wengi miongoni mwa watu bila shaka ni wenye kukanusha kukutana na Rabb wao.
أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَانُوا أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَأَثَارُوا الْأَرْضَ وَعَمَرُوهَا أَكْثَرَ مِمَّا عَمَرُوهَا وَجَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ ۖ فَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٩﴾
9. Je, hawatembei katika ardhi wakatazama jinsi ilivyokuwa hatima ya wale walio kabla yao?[3] Walikuwa ni wenye nguvu zaidi kuliko wao, na walichimbua ardhi, na wakaistawisha zaidi kuliko walivyoistawisha (makafiri), na wakawajia Rusuli wao kwa hoja bayana, na Allaah Hakuwa Akiwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao.
ثُمَّ كَانَ عَاقِبَةَ الَّذِينَ أَسَاءُوا السُّوأَىٰ أَن كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ وَكَانُوا بِهَا يَسْتَهْزِئُونَ ﴿١٠﴾
10. Kisha uovu ukawa hatima ya wale waliofanya uovu kwa vile walikadhibisha Aayaat (na Miujiza, Ishara) za Allaah na walikuwa ni wenye kuzifanyia istihzai.
اللَّـهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿١١﴾
11. Allaah Anaanzisha uumbaji, kisha Anaurudisha, kisha Kwake mtarejeshwa.
وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يُبْلِسُ الْمُجْرِمُونَ ﴿١٢﴾
12. Na Siku itakaposimama Saa, wahalifu watakata tamaa.
وَلَمْ يَكُن لَّهُم مِّن شُرَكَائِهِمْ شُفَعَاءُ وَكَانُوا بِشُرَكَائِهِمْ كَافِرِينَ ﴿١٣﴾
13. Na wala hawatokuwa na waombezi miongoni mwa waliokuwa wakiwashirikisha (na Allaah), na wao wenyewe watakuwa ni wenye kuwakanusha washirikishwa wao.
وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يَوْمَئِذٍ يَتَفَرَّقُونَ ﴿١٤﴾
14. Na siku itakaposimama Saa, Siku hiyo watafarikiana.
فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَهُمْ فِي رَوْضَةٍ يُحْبَرُونَ ﴿١٥﴾
15. Ama wale walioamini na wakatenda mema, basi wao watakuwa katika mabustani mazuri wakifurahishwa.
وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَلِقَاءِ الْآخِرَةِ فَأُولَـٰئِكَ فِي الْعَذَابِ مُحْضَرُونَ ﴿١٦﴾
16. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili) Zetu na makutano ya Aakhirah, basi hao katika adhabu watahudhurishwa.
فَسُبْحَانَ اللَّـهِ حِينَ تُمْسُونَ وَحِينَ تُصْبِحُونَ ﴿١٧﴾
17. Basi msabihini Allaah mnapoingia jioni na mnapoingia asubuhi.
وَلَهُ الْحَمْدُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَعَشِيًّا وَحِينَ تُظْهِرُونَ ﴿١٨﴾
18. Na Ana Himidi katika mbingu na ardhi, na (msabihini pia) mwanzo wa usiku na wakati wa Adhuhuri.
يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَيُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ وَكَذَٰلِكَ تُخْرَجُونَ ﴿١٩﴾
19. Anatoa kilichohai kutokana na kilichokufa, na Anatoa kilichokufa kutokana na kilichohai, na Anaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na hivyo ndivyo mtakavyotolewa (kufufuliwa).[4]
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ إِذَا أَنتُم بَشَرٌ تَنتَشِرُونَ ﴿٢٠﴾
20. Na katika Aayaat (Ishara, Dalili) Zake ni kwamba Amekuumbeni kutokana na udongo, tahamaki mmekuwa watu mnaotawanyika.[5]
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١﴾
21. Na katika Aayaat (Ishara, Dalili) Zake ni kwamba Amekuumbieni katika jinsi yenu wake ili mpate utulivu kwao, na Amekujaalieni baina yenu mapenzi na rehma. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaotafakari.
وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافُ أَلْسِنَتِكُمْ وَأَلْوَانِكُمْ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّلْعَالِمِينَ ﴿٢٢﴾
22. Na katika Aayaat (Ishara, Dalili) Zake ni uumbaji wa mbingu na ardhi, na kutofautiana lugha zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa wenye ujuzi.
وَمِنْ آيَاتِهِ مَنَامُكُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَابْتِغَاؤُكُم مِّن فَضْلِهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ ﴿٢٣﴾
23. Na katika Aayaat (Ishara, Dalili) ni kulala kwenu usiku na mchana na kutafuta kwenu Fadhila Zake. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaosikia.
وَمِنْ آيَاتِهِ يُرِيكُمُ الْبَرْقَ خَوْفًا وَطَمَعًا وَيُنَزِّلُ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَيُحْيِي بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿٢٤﴾
24. Na katika Aayaat (Ishara, Dalili) Zake Anakuonyesheni umeme kwa kukutieni khofu na matumaini, na Anateremsha kutoka mbinguni maji, Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo, bila shaka kuna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wenye akili.
وَمِنْ آيَاتِهِ أَن تَقُومَ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ بِأَمْرِهِ ۚ ثُمَّ إِذَا دَعَاكُمْ دَعْوَةً مِّنَ الْأَرْضِ إِذَا أَنتُمْ تَخْرُجُونَ ﴿٢٥﴾
25. Na katika Aayaat (Ishara, Dalili) Zake, ni kwamba mbingu na ardhi zimesimama kwa Amri Yake, kisha Atakapokuiteni wito mmoja mara mtatoka ardhini (makaburini kufufuliwa).
وَلَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ ﴿٢٦﴾
26. Na ni Wake Pekee wote waliomo katika mbingu na ardhi, na wote Kwake wanatii.
وَهُوَ الَّذِي يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ ۚ وَلَهُ الْمَثَلُ الْأَعْلَىٰ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٧﴾
27. Naye Ndiye Anayeanzisha uumbaji, kisha Anaurudisha, nayo ni sahali mno Kwake. Naye Ana Sifa za juu kabisa katika mbingu na ardhi. Naye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
ضَرَبَ لَكُم مَّثَلًا مِّنْ أَنفُسِكُمْ ۖ هَل لَّكُم مِّن مَّا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُم مِّن شُرَكَاءَ فِي مَا رَزَقْنَاكُمْ فَأَنتُمْ فِيهِ سَوَاءٌ تَخَافُونَهُمْ كَخِيفَتِكُمْ أَنفُسَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿٢٨﴾
28. (Allaah) Amekupigieni mfano kwa hali ya nafsi zenu. Je, katika hao iliyowamiliki mikono yenu ya kuume mnao washirika wowote katika vile Tulivyokuruzukuni? Kisha mkawa nyinyi katika hivyo sawasawa, mnawaogopa kama mnavyoogopeana wenyewe kwa wenyewe? Hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat (na Ishara, Dalili) kwa watu wenye akili.[6]
بَلِ اتَّبَعَ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَهْوَاءَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۖ فَمَن يَهْدِي مَنْ أَضَلَّ اللَّـهُ ۖ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٢٩﴾
29. Bali wale waliodhulumu wamefuata hawaa zao bila ya ilimu. Basi nani atamhidi ambaye Allaah Amempotowa? Na hawatokuwa na wowote wa kuwanusuru.
فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا ۚ فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٠﴾
30. Basi elekeza uso wako kwenye Dini ukijiengua na upotofu na kuelemea haki. (Shikamana na) umbile la asili la kumpwekesha Allaah Alilowaumbia watu.[7] Hakuna kubadilisha Uumbaji wa Allaah. Hiyo ndio Dini iliyonyooka sawasawa, lakini watu wengi hawajui.
مُنِيبِينَ إِلَيْهِ وَاتَّقُوهُ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَلَا تَكُونُوا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٣١﴾
31. Mkiwa ni wenye kutubu mara kwa mara kwa ikhlaasw Kwake (Allaah), na mcheni Yeye, na simamisheni Swalaah, na wala msiwe miongoni mwa washirikina.
مِنَ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا ۖ كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ ﴿٣٢﴾
32. (Wala msiwe) miongoni mwa wale walioifarakisha dini yao wakawa makundi makundi. Kila kundi wanafurahia waliyonayo.[8]
وَإِذَا مَسَّ النَّاسَ ضُرٌّ دَعَوْا رَبَّهُم مُّنِيبِينَ إِلَيْهِ ثُمَّ إِذَا أَذَاقَهُم مِّنْهُ رَحْمَةً إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُم بِرَبِّهِمْ يُشْرِكُونَ ﴿٣٣﴾
33. Na inapowagusa watu dhara, humwomba Rabb wao huku wakielekea Kwake kwa tawbah na ikhlaasw, kisha Anapowaonjesha Rehma kutoka Kwake, tahamaki kundi miongoni mwao humshirikisha Rabb wao.[9]
لِيَكْفُرُوا بِمَا آتَيْنَاهُمْ ۚ فَتَمَتَّعُوا فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٣٤﴾
34. Ili wayakanushe Tuliyowapa. Basi stareheni, karibuni mtakuja kujua.
أَمْ أَنزَلْنَا عَلَيْهِمْ سُلْطَانًا فَهُوَ يَتَكَلَّمُ بِمَا كَانُوا بِهِ يُشْرِكُونَ ﴿٣٥﴾
35. Au Tumewateremshia hoja ya wazi ambayo inazungumzia usahihi wa yale waliyokuwa wakimshirikisha Naye?
وَإِذَا أَذَقْنَا النَّاسَ رَحْمَةً فَرِحُوا بِهَا ۖ وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ إِذَا هُمْ يَقْنَطُونَ ﴿٣٦﴾
36. Na Tunapowaonjesha watu rehma huzifurahia, na unapowasibu uovu kutokana na iliyotanguliza mikono yao, mara wao wanakata tamaa.
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٣٧﴾
37. Je, hawaoni kwamba Allaah Anamkunjulia riziki Amtakaye, na Anadhikisha (kwa Amtakaye). Hakika katika hayo bila shaka mna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaoamini.
فَآتِ ذَا الْقُرْبَىٰ حَقَّهُ وَالْمِسْكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يُرِيدُونَ وَجْهَ اللَّـهِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٣٨﴾
38. Basi mpe jamaa wa karibu haki yake, na masikini[10] na msafiri (aliyeharibikiwa). Hilo ni bora kwa wale wanaotaka Wajihi wa Allaah, na hao ndio wenye kufaulu.
وَمَا آتَيْتُم مِّن رِّبًا لِّيَرْبُوَ فِي أَمْوَالِ النَّاسِ فَلَا يَرْبُو عِندَ اللَّـهِ ۖ وَمَا آتَيْتُم مِّن زَكَاةٍ تُرِيدُونَ وَجْهَ اللَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُضْعِفُونَ ﴿٣٩﴾
39. Na mlichotoa katika riba ili kizidi katika mali za watu, basi hakizidi kwa Allaah. Na mlichotoa katika Zakaah mkitafuta Wajihi wa Allaah, basi hao ndio watakaokuwa na ongezeko la maradufu.[11]
اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَكُمْ ثُمَّ رَزَقَكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ۖ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَفْعَلُ مِن ذَٰلِكُم مِّن شَيْءٍ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٤٠﴾
40. Allaah, Ndiye Amekuumbeni, kisha Akakuruzukuni, kisha Anakufisheni, kisha Atakuhuisheni. Je, kati ya washirika wenu yuko yeyote yule awezaye kufanya lolote katika hayo? Utakasifu ni wa Allaah na Ametukuka kwa ‘Uluwa kutokana na yale wanayomshirikisha.
ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٤١﴾
41. Ufisadi umedhihiri katika nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale yaliyochumwa na mikono ya watu ili (Allaah) Awaonjeshe baadhi ya waliyoyatenda wapate kurejea.
قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلُ ۚ كَانَ أَكْثَرُهُم مُّشْرِكِينَ ﴿٤٢﴾
42. Sema: Nendeni katika ardhi, mkatazame vipi ilikuwa hatima ya wale waliotangulia. Wengi wao walikuwa ni washirikina.
فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ الْقَيِّمِ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا مَرَدَّ لَهُ مِنَ اللَّـهِ ۖ يَوْمَئِذٍ يَصَّدَّعُونَ ﴿٤٣﴾
43. Basi elekeza uso wako kwenye Dini iliyonyooka kabla haijafika Siku isiyo na marudio inayotoka kwa Allaah. Siku hiyo watatengana.
مَن كَفَرَ فَعَلَيْهِ كُفْرُهُ ۖ وَمَنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِأَنفُسِهِمْ يَمْهَدُونَ ﴿٤٤﴾
44. Anayekufuru, basi kufuru yake ni madhara juu yake, na anayetenda mema, basi wanajiandalia mahali pa kupumzika kwa ajili ya nafsi zao.
لِيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِن فَضْلِهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ ﴿٤٥﴾
45. Ili (Allaah) Awalipe wale walioamini na wakatenda mema katika Fadhila Zake. Hakika Yeye Hapendi makafiri.
وَمِنْ آيَاتِهِ أَن يُرْسِلَ الرِّيَاحَ مُبَشِّرَاتٍ وَلِيُذِيقَكُم مِّن رَّحْمَتِهِ وَلِتَجْرِيَ الْفُلْكُ بِأَمْرِهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٤٦﴾
46. Na katika Aayaat (Ishara, Dalili) Zake ni kwamba Anapeleka pepo za rehma zenye bishara za kheri, na ili Akuonjesheni katika Rehma Zake, na ili merikebu ziende kwa Amri Yake, na ili mtafute katika Fadhila Zake, na ili mpate kushukuru.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَاءُوهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَانتَقَمْنَا مِنَ الَّذِينَ أَجْرَمُوا ۖ وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٧﴾
47. Na kwa yakini Tuliwatuma kabla yako Rusuli kwa watu wao, wakawajia kwa hoja bayana, Tukawalipiza wale ambao wamefanya uhalifu. Na ni haki daima Kwetu kuwanusuru Waumini.
اللَّـهُ الَّذِي يُرْسِلُ الرِّيَاحَ فَتُثِيرُ سَحَابًا فَيَبْسُطُهُ فِي السَّمَاءِ كَيْفَ يَشَاءُ وَيَجْعَلُهُ كِسَفًا فَتَرَى الْوَدْقَ يَخْرُجُ مِنْ خِلَالِهِ ۖ فَإِذَا أَصَابَ بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ إِذَا هُمْ يَسْتَبْشِرُونَ ﴿٤٨﴾
48. Allaah Ndiye Ambaye Anatuma pepo za rehma kisha zikatimua mawingu, kisha Akayatandaza mbinguni Atakavyo, na Huyafanya mapande mapande. Basi utaona matone ya mvua yanatoka baina yake. Na Anapowafikishia Awatakao kati ya Waja Wake, mara hao wanafurahia.
وَإِن كَانُوا مِن قَبْلِ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْهِم مِّن قَبْلِهِ لَمُبْلِسِينَ ﴿٤٩﴾
49. Na kwa hakika walikuwa kabla ya kuteremshiwa (mvua) ni wenye kukata tamaa.
فَانظُرْ إِلَىٰ آثَارِ رَحْمَتِ اللَّـهِ كَيْفَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٥٠﴾
50. Basi tazama athari za Rehma ya Allaah! Vipi Anaihuisha ardhi baada ya kufa kwake! Hakika (Afanyayo) hayo, Ndiye bila shaka Mwenye Kuhuisha wafu, Naye juu ya kila kitu ni Muweza.[12]
وَلَئِنْ أَرْسَلْنَا رِيحًا فَرَأَوْهُ مُصْفَرًّا لَّظَلُّوا مِن بَعْدِهِ يَكْفُرُونَ ﴿٥١﴾
51. Na Tungelituma upepo wa madhara na wakaiona (mimea yao) imekuwa manjano, wangeendelea baada ya hayo kukufuru.
فَإِنَّكَ لَا تُسْمِعُ الْمَوْتَىٰ وَلَا تُسْمِعُ الصُّمَّ الدُّعَاءَ إِذَا وَلَّوْا مُدْبِرِينَ ﴿٥٢﴾
52. Basi hakika wewe huwezi kusikilizisha wafu, na wala huwezi kusikilizisha viziwi wito wanapokengeuka wakigeuza migongo yao.[13]
وَمَا أَنتَ بِهَادِ الْعُمْيِ عَن ضَلَالَتِهِمْ ۖ إِن تُسْمِعُ إِلَّا مَن يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا فَهُم مُّسْلِمُونَ ﴿٥٣﴾
53. Na wala wewe huwezi kuwahidi vipofu kutoka upotofu wao. Humsikilizishi isipokuwa yule anayeamini Aayaat Zetu, nao ndio wenye kusilimu (kwa Allaah).
اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن ضَعْفٍ ثُمَّ جَعَلَ مِن بَعْدِ ضَعْفٍ قُوَّةً ثُمَّ جَعَلَ مِن بَعْدِ قُوَّةٍ ضَعْفًا وَشَيْبَةً ۚ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۖ وَهُوَ الْعَلِيمُ الْقَدِيرُ ﴿٥٤﴾
54. Allaah Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na udhaifu, kisha Akajaalia baada ya udhaifu nguvu, kisha Akajaalia baada ya nguvu udhaifu na ukongwe. Anaumba Atakacho. Naye Ndiye Mjuzi wa yote, Mweza wa yote.
وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يُقْسِمُ الْمُجْرِمُونَ مَا لَبِثُوا غَيْرَ سَاعَةٍ ۚ كَذَٰلِكَ كَانُوا يُؤْفَكُونَ ﴿٥٥﴾
55. Na Siku itakayosimama Saa wataapa wahalifu kwamba hawakubakia (duniani) ila saa moja tu. Hivyo ndivyo walivyokuwa wakighilibiwa.
وَقَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَالْإِيمَانَ لَقَدْ لَبِثْتُمْ فِي كِتَابِ اللَّـهِ إِلَىٰ يَوْمِ الْبَعْثِ ۖ فَهَـٰذَا يَوْمُ الْبَعْثِ وَلَـٰكِنَّكُمْ كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٥٦﴾
56. Na wale waliopewa ilimu na imaan watasema: Kwa yakini mmekaa kwa Majaaliwa na Hukmu ya Allaah mpaka Siku ya kufufuliwa. Basi hii ni Siku ya kufufuliwa, lakini nyinyi mlikuwa hamjui.
فَيَوْمَئِذٍ لَّا يَنفَعُ الَّذِينَ ظَلَمُوا مَعْذِرَتُهُمْ وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ ﴿٥٧﴾
57. Siku hiyo hautowafaa wale waliodhulumu udhuru wao, na wala hawatapewa nafasi ya kujitetea.
وَلَقَدْ ضَرَبْنَا لِلنَّاسِ فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ مِن كُلِّ مَثَلٍ ۚ وَلَئِن جِئْتَهُم بِآيَةٍ لَّيَقُولَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ أَنتُمْ إِلَّا مُبْطِلُونَ ﴿٥٨﴾
58. Kwa yakini Tumewapigia watu mifano ya kila namna katika hii Qur-aan.[14] Na kama utawaletea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Aayah (Ishara, Dalili) yoyote, bila shaka wale waliokufuru watasema: Nyinyi (Waumini) si chochote ila wabatilifu.
كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٥٩﴾
59. Hivyo ndivyo Allaah Anavyopiga chapa juu ya nyoyo za wale wasiojua.
فَاصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ ۖ وَلَا يَسْتَخِفَّنَّكَ الَّذِينَ لَا يُوقِنُونَ ﴿٦٠﴾
60. Basi subiri, hakika Ahadi ya Allaah ni haki. Na wala wasikuvunje moyo wale ambao hawana yakini ukataradadi (kubalighisha Risala).
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Ahadi Ya Allaah Kuhusu Warumi Kushinda Vita Baada Ya Kushindwa:
Tafsiyr ya Aayah hii na zinazofuatia (1-6) ni kama ifuatavyo:
Wafursi na Warumi wakati huo walikuwa miongoni mwa dola zenye nguvu zaidi duniani. Na kulikuwa na vita na migogoro kati yao, kama inavyotokea kati ya mataifa yenye usawa wa nguvu na mamlaka. Wafursi walikuwa washirikina wanaoabudu moto na Warumi walikuwa watu wa Kitabu ambao walijinasibisha na Tawraat na Injiyl, na walikuwa karibu zaidi na Waislamu kuliko Wafursi. Kutokana na ukaribu huo, Waumini wakapendelea Warumi washinde na wawashinde Wafursi. Washirikina ambao walikuwa wanafanana kwa itikadi za kishirikina na Wafursi, walipenda Wafursi wawashinde Warumi. Basi Wafursi wakawazidi nguvu Warumi na kuwashinda, lakini hawakuchukua ardhi zao isipokuwa maeneo yaliyo karibu na mipaka yao. Na washirikina wa Makkah walifurahi kwa ushindi huo, lakini Waislamu walihuzunishwa mno. Na hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akawapa khabari na Akawaahidi kuwa Warumi watawashinda Wafursi, katika kipindi kisichopita miaka kumi na kisichopungua miaka mitatu. [Tafsiyr As-Sa’diy].
Ni ya Allaah (سبحانه وتعالى) Amri yote kabla ya ushindi wa Warumi na baada yake. Na siku hiyo ambayo Warumi watapata ushindi juu ya Wafursi, Waumini wataifurahia Nusura ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Warumi juu ya Wafursi. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Na Allaah (سبحانه وتعالى), Anamsaidia Anayemtaka na Anaacha kumsaidia Anayemtaka. Na Yeye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu Anayemtaka miongoni mwa viumbe Vyake. Na hilo lilithibitika, na Warumi waliwashinda Wafursi baada ya miaka saba, na Waislamu wakafurahi kwa hilo, kwa kuwa Warumi walikuwa ni watu wa Kitabu ingawa wamekipotosha. Allaah (سبحانه وتعالى) Amewaahidi Waumini, ahadi ya kukata isiyoenda kinyume; nayo ni Kuwapa ushindi Warumi juu ya Wafursi wenye kuabudu masanamu. Lakini wengi wa makafiri wa Makkah hawajui kwamba kile Alichokiahidi Allaah ni kweli. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[3] Watembee Katika Ardhi Kutambua Hatima Ya Waliokadhibisha.
Rejea: Yuwsuf (12:109), Aal-‘Imraan (3:137), Al-An’aam (6:11), Faatwir (35:43-44), Al-Kahf (18:55).
[4] Mfano Wa Ardhi Iliyokufa (Kame), Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akaihuisha Kwa Mvua, Ni Mfano Wa Kuwahuisha Watu Kutoka Makaburini Mwao Siku Ya Qiyaamah:
Rejea Aal-‘Imraan (3:27), Al-An’aam (6:95), Suwrah hii Aayah namba (50).
[5] Kuumbwa (Aadam) Kutokana Na Udongo, Kisha Watu Kuzaliana Karne Kwa Karne Na Kutawanyika Ardhini Ni Ishara Na Dalili Ya Wazi Ya Muumbaji Anayestahiki Kuabudiwa:
Tafsiyr ya Aayah:
Mtu wa kwanza kuumbwa aliyekusudiwa hapa ni Aadam (عليه السّلام). Kisha kutawanyika watu, yaani, Ambaye Amekuumbeni kutokana na asili moja na kitu kimoja kisha Akakutawanyeni katika nchi mbalimbali za dunia. Basi hayo ni Aayaat (Ishara na Dalili) za wazi kabisa kwamba Aliyekuanzisheni kutokana na asili hiyo na Akakutawanyeni (katika nchi za dunia), Ni Rabb Anayestahiki kuabudiwa, Ni Mfalme Anayestahiki Kuhimidiwa, na Yeye Ni Ar-Rahiym, Mwenye Upendo Halisi, Ambaye Atakurudisheni (Kwake Atakapowafufueni) baada ya mauti. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[6] Washirikina Wanaridhia Kwa Allaah Yale Ambayo Wao Hawayaridhii:
Tafsiyr yake:
Allaah (سبحانه وتعالى) Amewapigia mfano, enyi washirikina utokanao na nyinyi wenyewe. (Anakuulizeni): Je kuna yeyote kati ya watumwa wenu na wajakazi wenu, mnayeweza kumruhusu akashirikiana nanyi katika mali zenu, na mkaona kuwa nyinyi na wao muko sawa katika hilo, ikawa mnawaogopa wao, kama mnavyowaogopa wenzenu mfano wenu, walio huru, katika utumiaji na ugawaji wa mali zenu? Nyinyi bila shaka hamtaridhika na hilo, basi vipi mtaridhika nalo kwa upande wa Allaah kwa kumfanya kuwa Ana mshirika miongoni mwa Viumbe Vyake? Kwa mfano wa ubainisho huu, Tunawafafanulia ushahidi na hoja watu wenye akili timamu ambao watanufaika nao. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[7] Fitwrah: Umbile Asili La Mwana-Aadam Lenye Kumtii Rabb Wake Na Kutokumshirikisha.
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna kizazi kinachozaliwa (mtoto mchanga) isipokuwa anazaliwa katika 'fitwrah' kisha wazazi wake (humbadilisha na) humuingiza katika dini ya Uyahudi, au Unaswara au Umajusi, kama mfano mnyama mwenye pembe anavyomzaa mnyama mwenye pembe kama yeye, je, mtahisi kuwa hana pembe?” Kisha Abuu Hurayrah akasema: Someni mkipenda: (Kauli ya Allaah):
فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ۚ
(Shikamana na) Umbile la asili la kumpwekesha Allaah Alilowaumbia watu. Hakuna kubadilisha Uumbaji wa Allaah. (Ar-Ruwm 30:30). [Al-Bukhaariy na Muslim]
Rejea Al-Aa’raaf (7:172) kuhusu viumbe walivyochukua Ahadi ya Alastu.
[8] Waliofarakanisha Dini Wakawa Makundi Makundi:
Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) ametafsiri: Ijapokuwa Dini ni moja, nayo ni kumwabudu Allaah (عزّ وجلّ) Pekee, lakini washirikina hawa wameitenganisha. Baadhi yao wanaabudu mizimu na masanamu, na miongoni mwao wapo wanaoabudu jua na mwezi, na miongoni mwao wapo wanaoabudu mawalii na watu wema (makaburini mwao), na miongoni mwao wapo Mayahudi na wapo Manaswara. [Tafsiyr As-Sa’diy].
Na Imaam Ibn Kathiyr (رحمه الله) ametafsiri: Usiwe miongoni mwa washirikina walioigawa dini yao, yaani: walioibadilisha wakaamini baadhi yake na kukanusha baadhi nyingine. Baadhi ya ‘Ulamaa wameifasiri maana ya
فَرَّقُوا دِينَهُمْ
“walioifarakisha dini yao.”
kuwa: “Walipuuza dini yao na kuiacha nyuma yao.” Na hao ni kama Mayahudi, Manaswaara, Majusi, na waabudu masanamu na wafuasi wote wa dini za upotofu. Hao ni mbali na wafuasi wa Uislamu, kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَّسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ ۚ إِنَّمَا أَمْرُهُمْ إِلَى اللَّـهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿١٥٩﴾
“Hakika wale waliofarakisha dini yao na wakawa makundi makundi, wewe huhusiki nao kwa lolote. Hakika kesi yao iko kwa Allaah, kisha Atawajulisha yale waliyokuwa wakiyatenda.” [Al-An’aam (6:159)]
Na kila kundi kati yao hao wapotofu linadai kuwa wao wako katika haki. Na ummah huu nao (wa Kiislamu) umegawanyika makundi kadhaa ambayo yote ni ya upotofu isipokuwa kundi moja tu, nalo ni Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah, ambao wameshikamana na Kitabu cha Allaah na Sunnah za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na wakafuata ya karne (tatu) za kwanza; Swahaba, Taabi’iyn (wanafunzi wa Swahaba na waliowafuatia) na Maimamu wa Waislamu wa zama za awali za waliowafuata katika manhaj yao. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Hao ni kuanzia Swahaba na karne za mwanzo hadi leo ambao wamethibitika katika Manhaj hii Sahihi na watakaoendelea kuthibiti mpaka Siku ya Qiyaamah.
Na Hadiyth ifuatayo imethibitisha kuwa makundi yote ni potofu na yataingia motoni isipokuwa moja:
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Wamegawanyika Mayahudi katika mapote sabini na moja, wakagawanyika Manaswara katika mapote sabini na mbili, na ummah wangu utagawanyika mapote sabini na tatu. Yote hayo yataingia motoni ila moja tu.” Swahaba wakauliza: Ni lipi hilo, ee Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)? Akasema: “Ni lile nililokuwemo mimi na Swahaba zangu." [Ahmad, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ad-Daarimiy]
Rejea Al-An’aam (6:159). Rejea pia tanbihi katika Al-Faatihah (1:6), Aal-‘Imraan (3:31, 103, 105).
[10] Haki Za Jamaa Na Maskini:
Tafsiyr yake:
Basi mpe jamaa yako haki yake ambayo Mtoa Sharia (Allaah) Ameiwajibisha au Ameihimiza kulingana na ukaribu wake na haja yake. Haki hii ni pamoja na kumpa matumizi ya lazima ya kimaisha, swadaqa, na zawadi. Pia, kumfanyia wema, kumhisisha kwamba yuko salama nawe, kumkirimu, kumheshimu, na kumsamehe kwa kupuuza makosa na maneno yake maovu na matendo. Vile vile, mpe masikini aliyelemewa na ufukara na uhitaji, swadaqa itakayomuondolea shida zake na mahitaji yake kama vile kumlisha, kumnywesha na kumvisha. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[11] Haramisho La Riba: Rejea Al-Baqarah (2:278).
[12] Mfano Wa Ardhi Iliyokufa (Kame), Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akaihuisha Kwa Mvua, Ni Mfano Wa Kuwahuisha Watu Kutoka Makaburini Mwao Siku Ya Qiyaamah:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anathibitisha kufufuliwa viumbe, kwa kupiga mfano wa ardhi iliyokufa (kame) kisha Akaihuisha kwa kuiteremshia mvua, ikarudi kuwa hai na ikatoa mazao mbalimbali. Rejea Aayah nyenginezo za Suwrah hii Ar-Ruwm (30:19), (30:24). Pia rejea Al-Baqarah (2:164), Al-An’aam (6:95), Al-A’raaf (7:57), Al-Hajj (22:5), Al-Furqaan (25:48-49), Yaasiyn (36:33), Fusw-Swilat (41:39), Az-Zukhruf (43:11), Al-Hadiyd (57:17), An-Nahl (16:65), Faatwir (35:9), Al-Jaathiyah (45:5), Qaaf (50:11), As-Sajdah (32:27).
[14] Mifano Ya Allaah (سبحانه وتعالى):
Rejea Al-A’raaf (7:40) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali.
لُقْمَان
031-Luqmaan
031-Luqmaan: Utangulizi Wa Suwrah [232]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الم ﴿١﴾
1. Alif Laam Miym.[1]
تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْحَكِيمِ ﴿٢﴾
2. Hizi ni Aayaat za Kitabu chenye hikmah.
هُدًى وَرَحْمَةً لِّلْمُحْسِنِينَ ﴿٣﴾
3. Zikiwa ni mwongozo na rehma kwa wafanyao ihsaan.
الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ ﴿٤﴾
4. Ambao wanasimamisha Swalaah na wanatoa Zakaah, nao ni wenye yakini na Aakhirah.
أُولَـٰئِكَ عَلَىٰ هُدًى مِّن رَّبِّهِمْ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٥﴾
5. Hao wako juu ya mwongozo kutoka kwa Rabb wao, na hao ndio wenye kufaulu.
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا ۚ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٦﴾
6. Na miongoni mwa watu, yuko ambaye hununua maneno ya upuuzi ili apoteze (watu) Njia ya Allaah bila ilimu, na huzichukulia (Aayaat) mzaha. Hao watapata adhabu ya kudhalilisha.[2]
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا وَلَّىٰ مُسْتَكْبِرًا كَأَن لَّمْ يَسْمَعْهَا كَأَنَّ فِي أُذُنَيْهِ وَقْرًا ۖ فَبَشِّرْهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٧﴾
7. Na anaposomewa Aayaat Zetu, hugeuka huku akitakabari kama kwamba hazisikii, kama kwamba kuna uziwi masikioni mwake. Basi mbashirie adhabu iumizayo.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ جَنَّاتُ النَّعِيمِ ﴿٨﴾
8. Hakika wale walioamini na wakatenda mema watapata Jannaat za Neema.
خَالِدِينَ فِيهَا ۖ وَعْدَ اللَّـهِ حَقًّا ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٩﴾
9. Wadumu humo. Ni Ahadi ya Allaah ya haki. Naye Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
خَلَقَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ۖ وَأَلْقَىٰ فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمْ وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَابَّةٍ ۚ وَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَنبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ ﴿١٠﴾
10. (Allaah) Ameumba mbingu bila ya nguzo mnazoziona, na Akaweka katika ardhi milima iliyosimama imara ili isiyumbe nanyi, na Akaeneza humo kila viumbe vinavyotembea. Na Tukateremsha kutoka mbinguni maji, Tukaotesha humo kila aina ya mimea mizuri yenye manufaa.
هَـٰذَا خَلْقُ اللَّـهِ فَأَرُونِي مَاذَا خَلَقَ الَّذِينَ مِن دُونِهِ ۚ بَلِ الظَّالِمُونَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿١١﴾
11. Huu ni Uumbaji wa Allaah, basi nionyesheni nini walichokiumba wasiokuwa Yeye.[3] Bali madhalimu wamo katika upotofu bayana.
وَلَقَدْ آتَيْنَا لُقْمَانَ الْحِكْمَةَ أَنِ اشْكُرْ لِلَّـهِ ۚ وَمَن يَشْكُرْ فَإِنَّمَا يَشْكُرُ لِنَفْسِهِ ۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ حَمِيدٌ ﴿١٢﴾
12. Kwa yakini Tulimpa Luqmaan[4] hikmah kwamba: Mshukuru Allaah. Na anayeshukuru, basi hakika anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake. Na anayekufuru, basi hakika Allaah Ni Mkwasi, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.
وَإِذْ قَالَ لُقْمَانُ لِابْنِهِ وَهُوَ يَعِظُهُ يَا بُنَيَّ لَا تُشْرِكْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ ﴿١٣﴾
13. Na Luqmaan alipomwambia mwanawe huku akimuwaidhi: Ee mwanangu! Usimshirikishe Allaah, hakika shirki ni dhulma kubwa mno![5]
وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْنًا عَلَىٰ وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ ﴿١٤﴾
14. Na Tumemuusia binaadam kwa wazazi wake wawili. Mama yake ameibeba mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na kumwachisha ziwa katika miaka miwili; ya kwamba, unishukuru Mimi, na wazazi wako,[6] Kwangu ndio mahali pa kuishia. [7]
وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا ۖ وَاتَّبِعْ سَبِيلَ مَنْ أَنَابَ إِلَيَّ ۚ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٥﴾
15. Lakini wakikushikilia kuwa Unishirikishe na ambayo huna ilimu nayo, basi usiwatii. Na suhubiana nao kwa wema duniani, [8] na fuata njia ya anayerudi kutubia Kwangu. Kisha Kwangu ndio marejeo yenu, na Nitakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda.
يَا بُنَيَّ إِنَّهَا إِن تَكُ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ فَتَكُن فِي صَخْرَةٍ أَوْ فِي السَّمَاوَاتِ أَوْ فِي الْأَرْضِ يَأْتِ بِهَا اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَطِيفٌ خَبِيرٌ ﴿١٦﴾
16. Ee mwanangu! Hakika likiweko (zuri au ovu) lolote lenye uzito wa punje ya hardali, likawa katika jabali au mbinguni au ardhini, Allaah Atalileta tu. Hakika Allaah Ni Mwenye Kudabiri mambo kwa Ulatifu, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.[9]
يَا بُنَيَّ أَقِمِ الصَّلَاةَ وَأْمُرْ بِالْمَعْرُوفِ وَانْهَ عَنِ الْمُنكَرِ وَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا أَصَابَكَ ۖ إِنَّ ذَٰلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ ﴿١٧﴾
17. Ee mwanangu! Simamisha Swalaah, na amrisha mema na kataza ya munkari, na subiri juu ya yale yatakayokusibu. Hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.
وَلَا تُصَعِّرْ خَدَّكَ لِلنَّاسِ وَلَا تَمْشِ فِي الْأَرْضِ مَرَحًا ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ ﴿١٨﴾
18. Na wala usiwageuzie watu uso wako kwa kiburi, na wala usitembee katika ardhi kwa maringo, hakika Allaah Hampendi kila mwenye kujivuna mwenye kujifakharisha.
وَاقْصِدْ فِي مَشْيِكَ وَاغْضُضْ مِن صَوْتِكَ ۚ إِنَّ أَنكَرَ الْأَصْوَاتِ لَصَوْتُ الْحَمِيرِ ﴿١٩﴾
19. Na kuwa wastani katika mwendo wako, na teremsha sauti yako, hakika sauti mbaya inayokirihisha zaidi bila shaka ni sauti ya punda.[10]
أَلَمْ تَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ سَخَّرَ لَكُم مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَأَسْبَغَ عَلَيْكُمْ نِعَمَهُ ظَاهِرَةً وَبَاطِنَةً ۗ وَمِنَ النَّاسِ مَن يُجَادِلُ فِي اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَلَا هُدًى وَلَا كِتَابٍ مُّنِيرٍ ﴿٢٠﴾
20. Je, hamuoni kwamba Allaah Amekutiishieni vile vilivyomo mbinguni na vile vilivyomo ardhini, na Akakutimizieni kitimilifu Neema Zake kwa dhahiri na siri?[11] Na miongoni mwa watu, wako wanaobishana kuhusu Allaah bila ya ilimu yoyote ile, na bila ya mwongozo wowote ule, na bila ya kitabu chochote kile chenye nuru.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا بَلْ نَتَّبِعُ مَا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۚ أَوَلَوْ كَانَ الشَّيْطَانُ يَدْعُوهُمْ إِلَىٰ عَذَابِ السَّعِيرِ ﴿٢١﴾
21. Na wanapoambiwa: Fuateni yale Aliyoyateremsha Allaah, husema: Bali tunayafuata yale tuliyowakuta nayo baba zetu.[12] Je, japokuwa shaytwaan anawaita katika adhabu ya moto uliowashwa vikali mno?
وَمَن يُسْلِمْ وَجْهَهُ إِلَى اللَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ ۗ وَإِلَى اللَّـهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ ﴿٢٢﴾
22. Na anayeusalimisha uso wake kwa Allaah, naye akawa ni mtenda ihsaan, basi kwa yakini ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika. Na kwa Allaah ni hatima ya mambo yote.
وَمَن كَفَرَ فَلَا يَحْزُنكَ كُفْرُهُ ۚ إِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ فَنُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٢٣﴾
23. Na anayekufuru, basi isikuhuzunishe kufuru yake. Kwetu ni marejeo yao, Tutawajulisha yale waliyoyatenda. Hakika Allaah Ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.
نُمَتِّعُهُمْ قَلِيلًا ثُمَّ نَضْطَرُّهُمْ إِلَىٰ عَذَابٍ غَلِيظٍ ﴿٢٤﴾
24. Tunawastarehesha kidogo, kisha Tutawasukumiza kwenye adhabu nzito.
وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۚ قُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢٥﴾
25. Na ukiwauliza: Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi? Bila shaka watasema: Allaah.[13] Sema: AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah). Bali wengi wao hawajui.
لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ ﴿٢٦﴾
26. Ni vya Allaah Pekee vyote vile viliomo katika mbingu na ardhi. Hakika Allaah Ndiye Mkwasi, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.
وَلَوْ أَنَّمَا فِي الْأَرْضِ مِن شَجَرَةٍ أَقْلَامٌ وَالْبَحْرُ يَمُدُّهُ مِن بَعْدِهِ سَبْعَةُ أَبْحُرٍ مَّا نَفِدَتْ كَلِمَاتُ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٧﴾
27. Na lau kama miti yote iliyomo katika ardhi ingekuwa ni kalamu, na bahari (ikafanywa wino), ikaongezewa juu yake bahari saba, yasingelimalizika Maneno ya Allaah.[14] Hakika Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
مَّا خَلْقُكُمْ وَلَا بَعْثُكُمْ إِلَّا كَنَفْسٍ وَاحِدَةٍ ۗ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ ﴿٢٨﴾
28. Hakukuwa kuumbwa kwenu wala kufufuliwa kwenu isipokuwa ni kama nafsi moja tu. Hakika Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِي إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى وَأَنَّ اللَّـهَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿٢٩﴾
29. Je, huoni kwamba Allaah Anauingiza usiku katika mchana, na Anauingiza mchana katika usiku? Na Amelitiisha jua na mwezi, vyote vinakwenda mpaka muda maalumu uliokadiriwa? Na kwamba Allaah kwa yale mnayoyatenda ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri?
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ الْبَاطِلُ وَأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ ﴿٣٠﴾
30. Hivyo ni kwa kuwa Allaah Ndiye wa Haki, na kwamba wale wanaowaomba badala Yake, ni baatwil, na kwamba Allaah Ndiye Mwenye ‘Uluwa Uliotukuka, Mkubwa Kabisa.[15]
أَلَمْ تَرَ أَنَّ الْفُلْكَ تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِنِعْمَتِ اللَّـهِ لِيُرِيَكُم مِّنْ آيَاتِهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ ﴿٣١﴾
31. Je, huoni kwamba merikebu zinapita baharini kwa Neema ya Allaah ili Akuonyesheni baadhi ya Aayaat (Ishara, Uwezo, Dalili) Zake? Hakika katika hayo kuna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa kila mwingi wa ustahamilivu na kushukuru.
وَإِذَا غَشِيَهُم مَّوْجٌ كَالظُّلَلِ دَعَوُا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ فَلَمَّا نَجَّاهُمْ إِلَى الْبَرِّ فَمِنْهُم مُّقْتَصِدٌ ۚ وَمَا يَجْحَدُ بِآيَاتِنَا إِلَّا كُلُّ خَتَّارٍ كَفُورٍ ﴿٣٢﴾
32. Na yanapowafunika mawimbi kama mawingu, humwomba Allaah wakiwa wenye kumtakasia Yeye Dini. Lakini Anapowaokoa katika nchi kavu, basi kuna miongoni mwao mwenye kushika mwendo wa wastani.[16] Na hazikanushi Aayaat (na Ishara, Dalili) Zetu isipokuwa kila khaini mkubwa, mwingi wa kukufuru.[17]
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ وَاخْشَوْا يَوْمًا لَّا يَجْزِي وَالِدٌ عَن وَلَدِهِ وَلَا مَوْلُودٌ هُوَ جَازٍ عَن وَالِدِهِ شَيْئًا ۚ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ ۖ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَلَا يَغُرَّنَّكُم بِاللَّـهِ الْغَرُورُ ﴿٣٣﴾
33. Enyi watu! Mcheni Rabb wenu, na iogopeni Siku ambayo mzazi hatomfaa mwanawe na wala mwana hatomfaa mzazi wake chochote.[18] Hakika Ahadi ya Allaah ni haki. Basi usikughururini kabisa uhai wa dunia, na wala (shaytwaan) mwenye kughuri asikughururini kabisa kuhusu Allaah.
إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ الْغَيْثَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْأَرْحَامِ ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿٣٤﴾
34. Hakika Allaah Ana ujuzi wa Saa (Qiyaamah), na Anateremsha mvua na Anajua yale yaliyomo katika matumbo ya uzazi. Na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani. Hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye Khabari za dhahiri na siri.[19]
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Haramisho La Muziki:
Hadiyth na kauli za Salaf zifuatazo zimethibitisha uharamisho wa muziki:
عن ابن عباس قال عن آية: ((وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ)، قال :الغناء وأشباهه إسناده صحيح - المحدث: الألباني
Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) amesema kuhusu Aayah hii:
وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ
“Na miongoni mwa watu, yuko ambaye hununua maneno ya upuuzi.”
"Ni nyimbo na maneno yanayofanana (ya upuuzi)" [Swahiyh Adab Al-Mufrad (603) - Ameisahihisha Al-Albaaniy]
Na Ibn Mas‘uwd (رضي الله عنه) amesema kuhusu Aayah hii: "Naapa kwa Allaah, hii inamaanisha ni muziki (au nyimbo)." Akaikariri mara tatu. [At-Twabariy (20:127)]
Rejea pia Al-Israa (17:64) kwenye kauli ya Mujaahid ambaye amesema kuwa imekusudiwa ni nyimbo (na aina zote za muziki).
[3] Wanaoabudiwa Pasi Na Allaah Hawawezi Kuumba Chochote:
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
هَـٰذَا خَلْقُ اللَّـهِ
“Huu ni Uumbaji wa Allaah.”
Yaani: Uumbaji wa ulimwengu wa juu na wa chini, vitu visivyo na uhai na viumbe hai, na utoaji wa rizki kwao. Ni Uumbaji wa Allaah Pekee Asiye na mshirika, kila mtu anakiri hayo hata nyinyi enyi washirikina! Akasema Allaah (سبحانه وتعالى):
فَأَرُونِي مَاذَا خَلَقَ الَّذِينَ مِن دُونِهِ ۚ
“Basi nionyesheni nini walichokiumba wasiokuwa Yeye.”
Yaani: Wale mnaowafanya kuwa ni washirika wa Allaah, na mnawaomba na kuwaabudu. Na kama mambo ni hivi, basi ni lazima hao wanaumba kama Anavyoumba Allaah (سبحانه وتعالى) na wawe wanaruzuku kama Anavyoruzuku Allaah Ikiwa wanacho chochote katika haya mawili, basi nionyesheni ili kuthibitisha madai yenu kwamba wanastahili kuabudiwa.
Na kwa vyovyote inajulikana kwamba hawawezi kumwonyesha chochote walichoumba waabudiwa wao hao, kwa sababu, washirikina hawa wanakiri kwamba vitu vyote vilivyotajwa hapa vimeumbwa na Allaah (سبحانه وتعالى) Peke Yake, hakuna kitu kingine kinachojulikana zaidi ya kile kilichotajwa hapa. Hivyo imethibitika kuwa hawawezi kuthibitisha chochote kile kilichoumbwa na waabudiwa (miungu) wao, ambacho kwacho wangestahili kuabudiwa. [Tafsiyr As-Sa’diy].
Rejea Al-Ahqaaf (46:4) kwenye maelezo na rejea nyenginezo. Rejea pia Atw-Twuur (52:35-36).
Na Allaah (سبحانه وتعالى) Amewatangazia tangazo watu wote wakusanyike na miungu yao wajaribu kuumba nzi lakini hakuna awezaye! Rejea Al-Hajj (22:73). Rejea pia An-Nahl (16:20), Al-Furqaan (25:2-3), An-Naml (27:60), Faatwir (35:40), Ghaafir (40:62), Al-Waaqi’ah (56:57-59), Atw-Twuwr (52:36).
[4] Luqmaan:
Salaf wamekhitilafiana kama Luqmaan alikuwa ni Nabii au mja mwema. Na kauli ya nguvu kabisa ni kwamba, yeye ni mja mwema, kwa sababu Allaah (سبحانه وتعالى) Hakumtaja isipokuwa kutaja tu kuwa Alimpa hikma. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Luqmaan alizaliwa katika Bara la Afrika. Jina lakeni Luqmaan bin 'Anqa' bin Sa’duwn. Ama Ibn Jariyr atw-Twabariy, yeye anasema jina lake lilikuwa Luqmaan bin Tharan kutoka watu wa Aylah (Quds). Alikuwa Swalihina; mtiifu, mwenye kumcha Allaah, mwenye busara na hikma tele. Rejea Alhidaaya.com > Maudhui Za Qur-aan > Visa Katika Qur-aan kupata historia yake na wasifu wake kwa bayana.
[5] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
Miongoni Mwa Wasiya Wa Luqmaan: Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno:
عَنْ عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: لَمَّا نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ: الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ، شَقَّ ذَلِكَ عَلَى النَّاس وَقَالُوا: أَيُّنَا لَمْ يَظْلِمْ نَفْسَهُ؟! فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إنَّه لَيْسَ كَمَا تَعنُون! ألَمْ تَسْمَعوا ما قال الْعبْد الصَّالح؟ يَا بُنَيَّ لَا تُشْرِكْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ- إنَّما هُو الشِّرْك))
Amesimulia ‘Abdullaah bin Mas‘uwd (رضي الله عنه): Ilipoteremshwa Aayah hii:
الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ،
“Wale walioamini na hawakuchanganya imaan zao na dhulma” [An-An’aam (6:82)]
Iliwatatiza watu wakasema: “Nani katika sisi hajadhulumu nafsi yake?” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Si kama vile mnavyomaanisha! Hamsikii pale mja mwema (Luqmaan) aliposema:
يَا بُنَيَّ لَا تُشْرِكْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ ﴿١٣﴾
“Ee mwanangu! Usimshirikishe Allaah, hakika shirki ni dhulma kubwa mno!” [Luqmaan: (31:13] “Hakika hiyo ni shirk.” [Ahmad na riwaayah zinazofanana katika Al-Bukhaariy na wengineo]
Rejea Al-An’aam (6:82). Na rejea pia Alhidaaya.com kwenye makala ya:
Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!- إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ [234]
Makala hii imechambua na kuelezea kwa bayana maana ya shirki, dhulma, aina za shirki, makatazo na adhabu zake.
Kuanzia Aayah hii namba (13) na namba (16-19), Luqmaan anamuusia mwanawe nyasia zifuatazo muhimu katika maisha yake:
(i) Kutokumshirikisha Allaah, kwa sababu shirki ni dhulma kubwa mno! (ii) Kumcha na kumkhofu Allaah (سبحانه وتعالى), na kutenda ya utiifu kadiri inavyowezekana, na kumtahadharisha kutenda maovu. Mema na maovu yawe makubwa au madogo vipi, hata lenye uzito wa punje ya hardali, linapotendwa popote pale, basi Allaah Atalijua, kwani hakifichiki kitu Kwake, Yeye Ni Mjuzi wa dhahiri na ya siri. (iii) Kusimamisha Swalaah. (iv) Kuamrisha mema na kukataza ya munkari na kuazimia katika kuvuta subra katika jambo hili la daawah kwa kuwa bila shaka yatamsibu ya kumsibu. (v) Kutokuwafanyia watu kiburi (vi) Kutokuwa na maringo, majivuno na kujifakharisha, kwani Allaah Hampendi mwenye sifa hizi. (vii) Kutembea mwendo wa wastani (viii) Kutokuongea kwa sauti kubwa inayokirihisha.
[6] Kuwafanyia Wazazi Wawili Ihsaan, Mashaka Ya Mama Kubeba Mimba Na Kuzaa, Kunyonyesha, Kumshukuru Allaah Na Wazazi
Aayah hii imetaja maamrisho ambayo takriban ni sawa na maamrisho katika Suwrah Al-Ahqaaf. Rejea huko (46:15), kupata faida na rejea mbalimbali nyenginezo.
Maamrisho hayo ni kama yafuatavyo:
(i) Kuwafanyia ihsaan wazazi wawili.
(ii) Mashaka ya mama wakati wa kubeba mimba, kuzaa na kunyonyesha.
(iii) Kumshukuru Allaah na kuwashukuru wazazi.
Na maamrisho ya kuwafanyia ihsaan wazazi wawili yametajwa pia katika Suwrah nyenginezo za Qur-aan. Miongoni mwazo ni Al-Baqarah (2:83), (2:215), An-Nisaa (4:36), Al-An’aam (6:151), Al-Israa (17:23-24), Al-‘Ankabuwt (29:8).
[7] Udhaifu Juu Ya Udhaifu:
Kauli za Salaf kuhusu maana ya udhaifu juu ya udhaifu: Mashaka ya kuzaa mtoto, juhudi baada ya juhudi, na udhaifu baada ya udhaifu.
[8] Katazo La Kuwatii Viumbe Katika Kumwasi Muumbaji Hata Kama Ni Wazazi:
Rejea pia Al-’Ankabuwt (29:8) kwenye maelezo kuhusu kuwafanyia ihsaan wazazi wasiokuwa Waislamu.
[9] Hakuna Kinachofichika Kwa Allaah (سبحانه وتعالى) Ardhini Wala Baharini Hata Kiwe Chenye Uzito Wa Hardali:
Rejea Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى) nyenginezo katika Suwrah Al-An’aam (6:59) kwenye faida na maelezo bayana. Na rejea pia Ghaafir (40:19) kwenye maelezo na rejea mbalimbali. Rejea pia Yuwnus (10:62), Saba-a (34:3).
[10] Mwendo Wa Wastani, Sauti Ya Punda:
Na Kauli Yake:
وَاقْصِدْ فِي مَشْيِك
“Na kuwa wastani katika mwendo wako.”
Yaani: Nenda kwa unyenyekevu hali ya kuwa mtulivu, si kwenda kwa kiburi na kujikweza, wala mwendo wa kujinyongesha.
Na Kauli Yake:
وَاغْضُضْ مِنْ صَوْتِكَ
“Na teremsha sauti yako.”
Yaani: Ikiwa ni adabu kwa watu pamoja na Allaah.
Na Kauli Yake:
إِنَّ أَنكَرَ الْأَصْوَاتِ لَصَوْتُ الْحَمِيرِ ﴿١٩﴾
“Hakika sauti mbaya inayokirihisha zaidi bila shaka ni sauti ya punda.”
Yaani: Sauti iliyo mbaya zaidi. Basi lau kama ingekuwa kuna faida na maslahi katika kunyanyua sauti ya juu, basi asingekuwa mahsusi ni punda katika hilo, (mnyame dhalili) ambae kimejulikana chakula chake na makazi yake
[11] Neema Za Allaah (سبحانه وتعالى) Za Dhahiri Na Siri:
Rejea Suwrah Ibraahiym (14:34) kwenye uchambuzi wa Neema za Allaah za zinazoonekana na zisizoonekana.
[12] Kufuata Mababa Na Mababu Japokuwa Hawakuwa Na Ilimu Au Walikuwa Ni Wapotofu:
Rejea Az-Zukhruf (43:22-23).
[13] Washirikina Waliamini Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah Lakini Walikanusha Tawhiyd Al-Uluwhiyyah.
Rejea Yuwnus (10:31), Al-‘Ankabuwt (29:61).
[14] Maneno Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Hayahesabiki, Hayamaliziki Wala Hayana Mwisho:
Kisha Akaelezea kuhusu upana wa Maneno Yake na ukubwa wa Kauli Zake, kwa ufafanuzi unaofika ndani ya nyoyo, na akili zinashtuka kwa jambo hilo, na nyoyo kuchanganywa akili ndani yake, na hutembea katika kumjua watu wenye akili na uoni, Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَوْ أَنَّمَا فِي الْأَرْضِ مِن شَجَرَةٍ أَقْلَامٌ وَالْبَحْرُ يَمُدُّهُ مِن بَعْدِهِ سَبْعَةُ أَبْحُرٍ
“Na lau kama miti yote iliyomo katika ardhi ingekuwa ni kalamu, na bahari (ikafanywa wino), ikaongezewa juu yake bahari saba.”
Yaani: Kalamu ambazo hutumika kuandikia wino uongezwao, basi hizo kalamu zingevunjika na huo wino ungeisha, na wala yasiishe Maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى).
Na hii si kuzidisha kusiko na uhalisia, bali wakati Allaah (سبحانه وتعالى) Alipojua ya kwamba akili zinashindwa kudhibiti baadhi ya Sifa Zake, na akatambua Allaah (سبحانه وتعالى) ya kwamba Waja Wake kumjua Yeye ni neema bora zaidi ambayo Amewaneemesha juu yao.
Na ni uchochoro bora zaidi wa kuifikia, nayo haiwezi kukamilika vile ilivyo. Lakini kisichopatikana chote basi hakiachwi chote. Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akawazindua uzinduzi unaotia Nuru moyoni, na vifua kufunguka kwa uzinduzi huo, na hutoa hoja kwa kile walichofikia katika kile ambacho hawajakifikia. Na wanasema kama alivyosema Mbora wao Mjuzi zaidi wa Rabb wake, yaani Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
لا أُحْصـي ثَنـاءً عَلَـيْك، أَنْـتَ كَمـا أَثْنَـيْتَ عَلـى نَفْسـِك
“Siwezi kuzidhibiti sifa Zako, Wewe ni kama ulivyojisifu Mwenyewe.”
(Hii ni katika duaa za Swalaah kwenye kusujudu, na katika ibaada nyenginezo).
Na kama si hivyo, basi jambo ni kubwa na tukufu zaidi ya hilo.
Na huku kufananisha ni katika mlango wa kuweka maana karibu, ambayo haiwezi kufikiwa na ufahamu na akili, na kama si hivyo basi miti hata ikizidi juu ya iliyotajwa zaidi na zaidi, na bahari lau kama zingeongezwa mara nyingi zaidi nyongeza kwa nyongeza, kwani hakika hutazamiwa kuisha kwake na kumalizika, kwa kuwa hizi bahari ni zimeumbwa.
Ama Maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى) haitazamiwi kuisha kwake, bali imetujulisha hoja ya kisharia na kiakili ya kwamba hayamaliziki wala hayana mwisho, na kila kitu kinaisha isipokuwa Muumbaji na Sifa Zake kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الْمُنتَهَىٰ ﴿٤٢﴾
“Na kwamba kwa Rabb wako ndio kikomo.” [An-Najm (53:42)]
Na pindi akili itakapohisi uhalisia wa umwanzo wake Allaah (سبحانه وتعالى) na umwisho wake, na kwamba kila kilichofanyiwa tathmini na akili katika zama zilizopita, vyovyote itakavyoungana tathmini hiyo, basi yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Yupo kabla ya hilo na mpaka kusiko na mwisho. Na kwamba vyovyote itakavyotathmini fahamu na akili katika zama za mwisho, na zikaunganika tathmini na akasaidia juu ya hilo mwenye kusaidia, kwa moyo wake na ulimi wake, basi Allaah (سبحانه وتعالى) baada ya hilo ni mpaka kusiko na lengo wala mwisho.
Na Allaah katika nyakati zote Anahukumu, na Anazungumza, na Anasema, na Anafanya namna Atakavyo, na Anapotaka, hakuna cha kumzuia katika maneno na vitendo. Na pindi akili itakapotengeneza picha ya hilo, itatambua ya kwamba, mfano ambao Allaah (سبحانه وتعالى) Ameupiga katika Maneno Yake ili waja wajue kitu katika hilo, na kama si hivyo basi jambo ni kubwa na tukufu zaidi.
Kisha Allaah (عزّ وجلّ) Akataja Utukufu Wake na Ukamilifu wa Hikma Zake, Akasema
إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٢٧﴾
“Hakika Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.”
Yaani: Ni Zake Yeye nguvu zote, Ambaye hakuna nguvu katika ulimwengu wa juu wala wa chini ispokuwa kutoka Kwake. Amewapa nguvu hizo viumbe, basi hakuna ujanja wala nguvu ispokuwa Zake. Na kwa Nguvu Zake, Amewashinda viumbe vyote, na Kuwaendesha, na Kuwapangilia, na kwa Hikma Zake, Ameumba viumbe, na Akalianzisha kwa hikma, na Akafanya lengo lake na makusudio yake ni hikma. Na vile vile amri na makatazo yamepatikana kwa hikma, na ikawa lengo lake na makusudio ni hikma. Basi Yeye ni Mwenye hikma katika kuumba Kwake na Amri Zake. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Rejea pia Al-Kahf (18:109) kwenye Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) kama hii.
[15] Al-‘Aliyyu:
Allaah (سبحانه وتعالى) Ametukuka, Ana Uadhama Kuliko wote kuliko vyote, Yuko juu Kabisa juu ya viumbe Vyake vyote.
Al-Kabiyr: Mkubwa Kabisa wa Dhati kwa Sifa na matendo.
Rejea Fahara ya Majina Mazuri Kabisa Na Sifa Za Za Allaah.
[16] Makundi Mawili: Wenye Mwendo Wa Wastani Na Waliokufuru:
Kundi moja ni wenye mwendo wa wastani ambao hawatoi shukurani ipasavyo kwa Allaah bali wanafanya dhambi na kujidhulumu nafsi zao. Kundi jengine limekufuru Neema za Allaah na kuzikanusha. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[17] Washirikina Walipofikwa Na Janga Walimwelekea Allaah Kumuomba Kisha Wakarudi Kumshirikisha:
Rejea Yuwnus (10:22) ambako kuna maelezo kwamba shirki za washirikina wa zama hizi ni kubwa zaidi kuliko shirki za washirikina wa awali.
[18] Siku Ya Qiyaamah Hakutakuwa Na Unasaba Hata Wazazi Watakanana Na Watoto Wao:
Rejea ‘Abasa (80:34).
[19] Mambo Matano Ya Ghaibu:
Maana Ya Ghaibu: Rejea Al-Baqarah (2:3), Al-An’aam (6:59), An-Naml (27:65).
Aayah hii tukufu imetaja mambo matano ya ghaibu ambayo hakuna ayajuaye. Hata Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakutambulishwa ujuzi wake. Basi wanaodai kuwa wanajua ya ghaibu kama watabiri wanaotabiri mambo kwa unajimu (kutabiri kwa nyota) na mengineyo ya ukahini, wamo hatarini kwa sababu kufanya hivyo ni miongoni mwa shirki kubwa inayomtoa mtu nje ya Uislamu. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameonya katika Hadiyth kadhaa, na miongoni mwazo ni:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، عَنْ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: مَنْ أَتَى كَاهِنًا، أَوْ عَرَّافًا، فَصَدَّقَهُ بِمَا يَقُولُ، فَقَدْ كَفَرَ بِمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم .
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayemwendea kahini au mpigaji ramli akamuamini ayasemayo, basi atakuwa ameshakufuru yale aliyoteremshiwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).’” [Ahmad, na Aswhaabus-Sunan wanne, na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb wat-Tarhiyb (3047)]
Na wanaotabiri mvua pia wamehukumiwa kuwa wanakufuru:
عَنْ زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: صَلَّى لَنَا رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) صَلاةَ الصُّبْحِ بِالْحُدَيْبِيَةِ عَلَى إِثْرِ سَمَاءٍ كَانَتْ مِنَ اللَّيْلِ، فَلَمَّا انْصَرَفَ أَقَبْلَ عَلَى النَّاسِ، فَقَالَ: هَلْ تَدْرُونَ مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ؟ قَالُوا: اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمَ. قَالَ: قَالَ أَصْبَحَ مِنْ عِبَادِي مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ، فَأَمَّا مَنْ قَالَ مُطِرْنَا بِفَضْلِ اللَّهِ وَرَحْمَتِهِ، فَذَلِكَ مُؤْمِنٌ بِي كَافِرٌ بِالْكَوْكَبِ، وَأَمَّا مَنْ قَالَ مُطِرْنَا بِنَوْءِ كَذَا وَكَذَا، فَذَلِكَ كَافِرٌ بِي مُؤْمِنٌ بِالْكَوْكَب .
Amesimulia Zayd bin Khaalid (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituswalisha Swalaah ya asubuhi Hudaybiyah baada ya usiku wa mvua. Alipomaliza akawakabili watu akasema: “Je, mnajua Rabb wenu Amesema nini?” Wakajibu: Allaah na Rasuli Wake ndio Wajuao. Akasema: “Allaah Amesema: Baadhi ya waja Wangu wameamka leo wakiwa wenye kuniamini, na wengine wamekufuru. Aliyesema kuwa mvua ni kutokana na Fadhila na Rehma za Allaah, basi huyo ni mwenye kuniamini wala haamini nyota. Ama aliyesema: Tumenyeshewa mvua kutokana na nyota fulani, basi yeye ni mwenye kunikufuru na mwenye kuamini nyota.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Tafsiyr ya Aayah:
Imeshathibiti ya kwamba Ilimu ya Allaah (سبحانه وتعالى) imedhibiti yaliyofichika na yaliyowazi, ya siri na ya dhahiri, na Allaah Anaweza kuwadhihirishia Waja Wake mambo mengi yaliyofichika.
Na mambo haya Matano, ni katika mambo ambayo Ilimu Yake imefichwa kabisa kwa viumbe vyote, hayajui Nabii aliyetumwa, wala Malaika aliyekurubishwa, wala wengineo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ
“Hakika Allaah Ana ujuzi wa Saa (Qiyaamah).”
Yaani: Anajua ni lini kitakuwa, kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ رَبِّي ۖ لَا يُجَلِّيهَا لِوَقْتِهَا إِلَّا هُوَ ۚ ثَقُلَتْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ لَا تَأْتِيكُمْ إِلَّا بَغْتَةً ۗ يَسْأَلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِيٌّ عَنْهَا ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ اللَّـهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٨٧﴾
“Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Saa (Qiyaamah), lini kutokea kwake? Sema: Hakika ujuzi wake uko kwa Rabb wangu. Hakuna wa kuidhihirisha wakati wake isipokuwa Yeye. Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haitokufikieni isipokuwa kwa ghafla. Wanakuuliza kama kwamba wewe unaijua vyema. Sema: Hakika ujuzi wake uko kwa Allaah (Pekee), lakini watu wengi hawajui.” [Al-A’raaf (7:187)]
Na Kauli Yake:
وَيُنَزِّلُ الْغَيْثَ
“Na Anateremsha mvua.”
Yaani: Ni Yeye Pekee Anayeiteremsha, na Anajua ni wakati gani itateremka.
Na Kauli Yake:
وَيَعْلَمُ مَا فِي الْأَرْحَامِ ۖ
“Anajua yale yaliyomo katika matumbo ya uzazi.”
Yaani: Yeye Ndiye Ambaye Amekianzisha kilichomo ndani yake, na kukijua ni kipi, je ni mume au mke. Na kwa hili Malaika anayewakilishwa katika vilivyomo matumboni humuuliza Rabb Wake: Je yeye ni mume au mke? Basi Allaah Anahukumu Anachokitaka.
Na Kauli Yake:
وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ
“Na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho.”
Yaani: Katika chumo la Dini yake na dunia yake.
Na Kauli Yake:
وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ
“Na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani.”
Yaani: Bali Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Pekee Anaejua hayo yote.
Na Alipoyataja mambo haya matano kwa umahususi kwamba Ni Yeye Tu Anayajua, Akatueleza hapo hapo kwamba Ilimu Yake imeenea vile vile kwa mambo mengine yote Akisema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿٣٤﴾
“Hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye Khabari za dhahiri na siri.”
Yaani: Yeye Ndiye Mwenye Kudhibiti ya nje na ya ndani, na yaliyofichika na ya siri. Na katika Hikma Zake zilizokamilika, ni pale Alipoficha kwa waja, ilimu ya haya mambo matano, kwa sababu kuna maslahi katika hilo ambayo hayafichiki kwa mwenye kuzingatia hilo. [Tafsiyr As-Sa’diy]
السَّجْدَة
032-As-Sajdah
032-As-Sajdah: Utangulizi Wa Suwrah [236]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الم ﴿١﴾
1. Alif Laam Miym.[1]
تَنزِيلُ الْكِتَابِ لَا رَيْبَ فِيهِ مِن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٢﴾
2. Ni uteremsho wa Kitabu, hauna shaka ndani yake, umetoka kwa Rabb wa walimwengu.
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۚ بَلْ هُوَ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّا أَتَاهُم مِّن نَّذِيرٍ مِّن قَبْلِكَ لَعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ ﴿٣﴾
3. Au wanasema ameitunga (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم hii Qur-aan)? Bali hiyo ni haki kutoka kwa Rabb wako ili uonye watu ambao hawakufikiwa na mwonyaji yeyote kabla yako, huenda wakahidika.
اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ مَا لَكُم مِّن دُونِهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا شَفِيعٍ ۚ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ ﴿٤﴾
4. Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita, kisha Akawa juu[2] ya ‘Arsh. Nyinyi hamna badala Yake mlinzi yeyote wala mwombezi. Je, basi hamkumbuki?
يُدَبِّرُ الْأَمْرَ مِنَ السَّمَاءِ إِلَى الْأَرْضِ ثُمَّ يَعْرُجُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ أَلْفَ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ ﴿٥﴾
5. Anadabiri mambo kutoka mbinguni mpaka ardhini, kisha inapanda Kwake katika siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu katika ile mnayoihesabu nyinyi.
ذَٰلِكَ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿٦﴾
6. Huyo Ndiye Mjuzi wa ghaibu na dhahiri, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu.
الَّذِي أَحْسَنَ كُلَّ شَيْءٍ خَلَقَهُ ۖ وَبَدَأَ خَلْقَ الْإِنسَانِ مِن طِينٍ ﴿٧﴾
7. Ambaye Amefanya uzuri kila kitu Alichokiumba, na Akaanzisha uumbaji wa binaadam kutokana na udongo.
ثُمَّ جَعَلَ نَسْلَهُ مِن سُلَالَةٍ مِّن مَّاءٍ مَّهِينٍ ﴿٨﴾
8. Kisha Akajaalia kizazi chake kutokana na mchujo safi wa maji dhalilifu.
ثُمَّ سَوَّاهُ وَنَفَخَ فِيهِ مِن رُّوحِهِ ۖ وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ ۚ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ ﴿٩﴾
9. Kisha Akamsawazisha, na Akapuliza humo roho yake (Aliyoiumba Allaah). Na Akakujaalieni kusikia na kuona na nyoyo, ni machache mno yale mnayoshukuru.
وَقَالُوا أَإِذَا ضَلَلْنَا فِي الْأَرْضِ أَإِنَّا لَفِي خَلْقٍ جَدِيدٍ ۚ بَلْ هُم بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ كَافِرُونَ ﴿١٠﴾
10. Na wakasema: Je, tutakapokwisha kufa na tukapotea chini ya ardhi je, hivi kweli sisi tutaumbwa katika umbo jipya?![3] Bali wao ni wenye kukanusha kukutana na Rabb wao.
قُلْ يَتَوَفَّاكُم مَّلَكُ الْمَوْتِ الَّذِي وُكِّلَ بِكُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ ﴿١١﴾
11. Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti[4] ambaye amewakilishwa kwenu, kisha kwa Rabb wenu mtarejeshwa.
وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الْمُجْرِمُونَ نَاكِسُو رُءُوسِهِمْ عِندَ رَبِّهِمْ رَبَّنَا أَبْصَرْنَا وَسَمِعْنَا فَارْجِعْنَا نَعْمَلْ صَالِحًا إِنَّا مُوقِنُونَ ﴿١٢﴾
12. Na ungeliona pale wahalifu wanainamisha vichwa vyao mbele ya Rabb wao (wakisema): Rabb wetu! Tumekwishaona, na tumeshasikia, basi turejeshe tutende mema, hakika sisi sasa ni wenye yakini.
وَلَوْ شِئْنَا لَآتَيْنَا كُلَّ نَفْسٍ هُدَاهَا وَلَـٰكِنْ حَقَّ الْقَوْلُ مِنِّي لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿١٣﴾
13. Na Tungelitaka, Tungeliipa kila nafsi mwongozo wake, lakini imethibiti kauli kutoka Kwangu kwamba: Bila shaka Nitajaza Jahannam kwa majini na watu pamoja.[5]
فَذُوقُوا بِمَا نَسِيتُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا إِنَّا نَسِينَاكُمْ ۖ وَذُوقُوا عَذَابَ الْخُلْدِ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٤﴾
14. Basi onjeni kwa sababu ya kusahau kwenu kukutana na Siku yenu hii. Hakika Nasi Tumekusahauni. Na onjeni adhabu yenye kudumu milele kutokana na yale mliyokuwa mkiyatenda.
إِنَّمَا يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا الَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِهَا خَرُّوا سُجَّدًا وَسَبَّحُوا بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ۩﴿١٥﴾
15. Hakika wanaamini Aayaat Zetu wale wanapokumbushwa nazo huporomoka kusujudu, na wakasabbih wakimhimidi Rabb wao, nao hawatakabari.
تَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿١٦﴾
16. Mbavu zao zinatengana na vitanda,[6] wanamuomba Rabb wao kwa khofu na matumaini, na katika yale Tuliyowaruzuku wanatoa.[7]
فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَّا أُخْفِيَ لَهُم مِّن قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٧﴾
17. Basi nafsi yoyote haijui waliyofichiwa katika yanayoburudisha macho. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyatenda.
أَفَمَن كَانَ مُؤْمِنًا كَمَن كَانَ فَاسِقًا ۚ لَّا يَسْتَوُونَ ﴿١٨﴾
18. Je, aliye Muumini atakuwa sawa na aliye fasiki? Hawalingani sawa!
أَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَلَهُمْ جَنَّاتُ الْمَأْوَىٰ نُزُلًا بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٩﴾
19. Ama wale walioamini na wakatenda mema, basi watapata Jannaat za makazi mazuri, takrima kwa yale waliyokuwa wakitenda.
وَأَمَّا الَّذِينَ فَسَقُوا فَمَأْوَاهُمُ النَّارُ ۖ كُلَّمَا أَرَادُوا أَن يَخْرُجُوا مِنْهَا أُعِيدُوا فِيهَا وَقِيلَ لَهُمْ ذُوقُوا عَذَابَ النَّارِ الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ ﴿٢٠﴾
20. Na ama wale waliofanya ufasiki, basi makazi yao ni motoni. Kila watakapotaka kutoka humo, watarudishwa humo, na wataambiwa: Onjeni adhabu ya moto ambayo mlikuwa mnaikadhibisha.
وَلَنُذِيقَنَّهُم مِّنَ الْعَذَابِ الْأَدْنَىٰ دُونَ الْعَذَابِ الْأَكْبَرِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٢١﴾
21. Na bila shaka Tutawaonjesha adhabu ndogo kabla ya adhabu kubwa huenda wakarejea (kutubia).[8]
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَا ۚ إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنتَقِمُونَ ﴿٢٢﴾
22. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa Aayaat za Rabb wake, kisha akazikengeukia? Hakika Sisi Tutawalipiza wahalifu.
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَلَا تَكُن فِي مِرْيَةٍ مِّن لِّقَائِهِ ۖ وَجَعَلْنَاهُ هُدًى لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ ﴿٢٣﴾
23. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu, basi usiwe na shaka katika kukutana naye. Na Tukakijaalia ni mwongozo kwa wana wa Israaiyl.
وَجَعَلْنَا مِنْهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا لَمَّا صَبَرُوا ۖ وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يُوقِنُونَ ﴿٢٤﴾
24. Na Tukawajaalia miongoni mwao Maimamu wanaongoza kwa Amri Yetu waliposubiri, na walikuwa wakiziyakinisha Aayaat (na Ishara) Zetu.
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَفْصِلُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ﴿٢٥﴾
25. Hakika Rabb wako Ndiye Atakayepambanua baina yao Siku ya Qiyaamah katika yale yote waliyokuwa wakikhitilafiana.
أَوَلَمْ يَهْدِ لَهُمْ كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّنَ الْقُرُونِ يَمْشُونَ فِي مَسَاكِنِهِمْ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ ۖ أَفَلَا يَسْمَعُونَ ﴿٢٦﴾
26. Je, haijawabainikia karne ngapi Tumeangamiza kabla yao, nao wanapita katika masikani yao? Hakika katika hayo mna Ishara (na mazingatio). Je, basi hawasikii?
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا نَسُوقُ الْمَاءَ إِلَى الْأَرْضِ الْجُرُزِ فَنُخْرِجُ بِهِ زَرْعًا تَأْكُلُ مِنْهُ أَنْعَامُهُمْ وَأَنفُسُهُمْ ۖ أَفَلَا يُبْصِرُونَ ﴿٢٧﴾
27. Je hawaoni kwamba Sisi Tunayaendesha maji katika ardhi kame, kisha Tunatoa kwayo mimea, wanakula humo wanyama wao wa mifugo na wao wenyewe! Je, basi hawaoni?
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْفَتْحُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٨﴾
28. Wanasema: Ni lini itakuwa kuhukumiwa huko ikiwa nyinyi ni wakweli?
قُلْ يَوْمَ الْفَتْحِ لَا يَنفَعُ الَّذِينَ كَفَرُوا إِيمَانُهُمْ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿٢٩﴾
29. Sema: Siku ya hukmu haitowafaa wale waliokufuru imaan zao, na wala hawatopewa muhula.
فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَانتَظِرْ إِنَّهُم مُّنتَظِرُونَ ﴿٣٠﴾
30. Jiepushe nao na ngojea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), hakika wao (pia) wanangojea.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Istawaa اسْتَوَى
Yuko juu kwa namna inayolingana na Uadhama na Ujalali Wake Yeye Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-A'raaf (7:54) kwenye maelezo bayana ya maana yake, yenye kutofautiana na maana ya katika Suwrah Al-Baqarah (2:29) na Suwrat Fusswilat (41:11).
[3] Washirikina Na Makafiri Hawaamini Kuwa Watafufuliwa:
Rejea Al-Israa (17:49) kupata maelezo bayana.
[4] Malakul-Mawt Sio Jina La Malaika Wa Kufisha:
Katika Aayah hii, ametajwa Malakul-Mawt (Malaika anayefisha), lakini hii, haimaanishi kuwa ndio jina lake, bali ametajwa hivyo kama ni sifa ya kitendo hicho cha kutoa roho za viumbe.
Kauli za ‘Ulamaa kuhusu kumwita ‘Izraaiyl kuwa ni Malaika anayefisha:
(i) Imaam Ibn Baaz (رحمه الله): “Na imekuja katika baadhi ya Aathaar kwamba Malaika wa kufisha jina lake ni ‘Izraaiyl lakini hakuna Hadiyth Swahiyh kwamba ndio jina lake, bali imekuja katika Athaar dhaifu ambayo haisimamishi hoja kuwa anaitwa ‘Izraaiyl. [Al-Mawqi' Ar-Rasmiy li-Samaahat Ash-Shaykh Al-Imaam Ibn Baaz].
(ii) Imaam Al-Albaaniy (رحمه الله): “ Hakuna chochote kilicho sahihi kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu kumwita Malaika anayetoa roho kuwa ni ‘Izraaiyl. [Fataawaa Imaam Al-Albaaniy – Madiynah Wal-Imaaraat]
[5] Moto Wa Jahnnam Utajazwa Kwa Wanaadam Na Majini:
Rejea Qaaf (50:30) kwenye maelezo na rejea zake.
[6] Neema Na Mambo Mazuri Aliyowaandalia Allaah (سبحانه وتعالى) Waja Wake Waamkao Usiku Kufanya Ibaadah:
Kuamka usiku ni katika ibaada tukufu ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Anawaahidi kwayo Waja Wake mazuri na neema tele huko Jannah; neema na mazuri ambayo hawajapata kuyaona wala kuyasikia wala kuyafikiria akilini. Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja hayo katika Aayah inayofuatia kama ilivyotajwa katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: أَعْدَدْتُ لِعِبَادِي الصَّالِحِينَ مَا لَا عَيْنٌ رَأَتْ وَلَا أُذُنٌ سَمِعَتْ وَلَا خَطَرَ عَلَى قَلْبِ بَشَرٍ)) قَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ اقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: (( فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ)) البخاري، مسلم، الترمذي وابن ماجه
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah (تبارك وتعالى) Amesema: Nimewatayarishia Waja Wangu wema kile ambacho jicho lolote halijapata kuona, wala sikio lolote halijapata kusikia na wala haijapata kupita katika moyo wa binaadam.” Akasema Abuu Hurayrah: Someni mkipenda:
فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ
“Basi nafsi yoyote haijui waliyofichiwa katika yanayoburudisha macho.”
[As-Sajdah (32:17) – Hadiyth ameipokea Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah]
Rejea pia Al-Israa (17:79) kwenye rejea nyenginezo. Na pia Adh-Dhaariyaat: (51:15-19) kwenye fadhila za Qiyaamul-Layl (Kisimamo Cha Usiku kwa ajili ya ibaada).
[8] Adhabu Ndogo Na Adhabu Kubwa:
Kauli za ‘Ulamaa kuhusu maana ya adhabu ndogo na adhabu kubwa:
(i) Tafsiyr Al-Muyassar:
Adhabu ndogo ni majanga, masaibu, mabalaa duniani. Ama adhabu kubwa, ni kuadhibiwa katika moto wa Jahannam Siku ya Qiyaamah.
(ii) Tafsiyr As-Sa’diy:
Adhabu ndogo ni adhabu ya al-barzakh, wataonjeshwa sehemu ya adhabu ya kaburi kabla ya kufa, ima kwa adhabu ya kuuliwa na mfano wake kama vile walivyouliwa washirikina katika Vita vya Badr, au wakati wanapofariki kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الظَّالِمُونَ فِي غَمَرَاتِ الْمَوْتِ وَالْمَلَائِكَةُ بَاسِطُو أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوا أَنفُسَكُمُ ۖ الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ
“Na lau ungeliona madhalimu pale wakiwa katika mateso makali ya mauti (ungeona jambo la kutisha mno), na Malaika wamenyosha mikono yao (wakiwaambia): Toeni nafsi zenu! Leo mnalipwa adhabu ya kudhalilisha.” [Al-An’aam: (6:93)].
Adhabu kubwa ni adhabu ya moto (wa Jahannam).
الأَحْزاب
033-Al-Ahzaab
033-Al-Ahzaab: Utangulizi Wa Suwrah [239]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ اتَّقِ اللَّـهَ وَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَالْمُنَافِقِينَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا ﴿١﴾
1. Ee Nabiy! Mche Allaah, na wala usiwatii makafiri na wanafiki. Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
وَاتَّبِعْ مَا يُوحَىٰ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿٢﴾
2. Na fuata yale ulofunuliwa Wahy kutoka kwa Rabb wako. Hakika Allaah daima kwa yale myatendayo Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿٣﴾
3. Na tawakali kwa Allaah. Na Anatosheleza Allaah Kuwa Ni Mtegemewa.
مَّا جَعَلَ اللَّـهُ لِرَجُلٍ مِّن قَلْبَيْنِ فِي جَوْفِهِ ۚ وَمَا جَعَلَ أَزْوَاجَكُمُ اللَّائِي تُظَاهِرُونَ مِنْهُنَّ أُمَّهَاتِكُمْ ۚ وَمَا جَعَلَ أَدْعِيَاءَكُمْ أَبْنَاءَكُمْ ۚ ذَٰلِكُمْ قَوْلُكُم بِأَفْوَاهِكُمْ ۖ وَاللَّـهُ يَقُولُ الْحَقَّ وَهُوَ يَهْدِي السَّبِيلَ ﴿٤﴾
4. Allaah Hakufanya mtu yeyote kuwa na nyoyo mbili kifuani mwake. Na wala Hakufanya wake zenu ambao mnawalinganisha migongo yao na migongo ya mama zenu kuwa ni mama zenu. Na wala Hakufanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni watoto wenu khasa. Hizi ni kauli zenu za vinywa vyenu tu. Na Allaah Anasema ya haki, Naye Anaongoza njia (ya haki).
ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِندَ اللَّـهِ ۚ فَإِن لَّمْ تَعْلَمُوا آبَاءَهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ وَمَوَالِيكُمْ ۚ وَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ فِيمَا أَخْطَأْتُم بِهِ وَلَـٰكِن مَّا تَعَمَّدَتْ قُلُوبُكُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٥﴾
5. Waiteni kwa (majina ya) baba zao. Huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Allaah.[1] Na ikiwa hamuwajui baba zao, basi ni ndugu zenu katika Dini, na walio katika ulinzi wenu, na wala hakuna dhambi juu yenu katika yale mliyoyakosea, lakini isipokuwa katika yale iliyoyakusudia nyoyo zenu. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[2]
النَّبِيُّ أَوْلَىٰ بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنفُسِهِمْ ۖ وَأَزْوَاجُهُ أُمَّهَاتُهُمْ ۗ وَأُولُو الْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَىٰ بِبَعْضٍ فِي كِتَابِ اللَّـهِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُهَاجِرِينَ إِلَّا أَن تَفْعَلُوا إِلَىٰ أَوْلِيَائِكُم مَّعْرُوفًا ۚ كَانَ ذَٰلِكَ فِي الْكِتَابِ مَسْطُورًا ﴿٦﴾
6. Nabiy ana haki zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao.[3] Na wake zake ni mama zao.[4] Na wenye uhusiano wa damu wana haki zaidi (katika kurithiana) wao kwa wao katika Hukumu ya Allaah kuliko (undugu wa) Waumini na Muhaajiriyna, isipokuwa mkiwafanyia wema marafiki zenu wa karibu. Hayo yamekwishaandikwa Kitabuni.
وَإِذْ أَخَذْنَا مِنَ النَّبِيِّينَ مِيثَاقَهُمْ وَمِنكَ وَمِن نُّوحٍ وَإِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۖ وَأَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا ﴿٧﴾
7. Na pale Tulipochukua kutoka kwa Manabii fungamano lao, na kutoka kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na kutoka kwa Nuwh, na Ibraahiym, na Muwsaa, na ‘Iysaa mwana wa Maryam, na Tukachukua kutoka kwao fungamano gumu.[5]
لِّيَسْأَلَ الصَّادِقِينَ عَن صِدْقِهِمْ ۚ وَأَعَدَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿٨﴾
8. Ili Awaulize wakweli kuhusu ukweli wao, na Amewaandalia makafiri adhabu iumizayo.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ جَاءَتْكُمْ جُنُودٌ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا وَجُنُودًا لَّمْ تَرَوْهَا ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرًا ﴿٩﴾
9. Enyi walioamini! Kumbukeni Neema ya Allaah juu yenu, pale yalipokujieni majeshi Tukawapelekea upepo wa dhoruba na majeshi msiyoyaona (ya Malaika). Na Allaah daima Ni Mwenye Kuona myatendayo.[6]
إِذْ جَاءُوكُم مِّن فَوْقِكُمْ وَمِنْ أَسْفَلَ مِنكُمْ وَإِذْ زَاغَتِ الْأَبْصَارُ وَبَلَغَتِ الْقُلُوبُ الْحَنَاجِرَ وَتَظُنُّونَ بِاللَّـهِ الظُّنُونَا ﴿١٠﴾
10. Walipokujieni kutoka juu yenu, na kutoka chini yenu, na macho yalipokodoka, na nyoyo zikafika kooni (kwa kiwewe) na mkamdhania Allaah dhana nyingi.
هُنَالِكَ ابْتُلِيَ الْمُؤْمِنُونَ وَزُلْزِلُوا زِلْزَالًا شَدِيدًا ﴿١١﴾
11. Hapo ndipo Waumini walipojaribiwa na wakatetemeshwa mtetemesho mkali kabisa.
وَإِذْ يَقُولُ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ مَّا وَعَدَنَا اللَّـهُ وَرَسُولُهُ إِلَّا غُرُورًا ﴿١٢﴾
12. Na pale waliposema wanafiki na wale ambao nyoyoni mwao mna maradhi[7]: Allaah na Rasuli Wake Hawakutuahidi isipokuwa ghururi tu.
وَإِذْ قَالَت طَّائِفَةٌ مِّنْهُمْ يَا أَهْلَ يَثْرِبَ لَا مُقَامَ لَكُمْ فَارْجِعُوا ۚ وَيَسْتَأْذِنُ فَرِيقٌ مِّنْهُمُ النَّبِيَّ يَقُولُونَ إِنَّ بُيُوتَنَا عَوْرَةٌ وَمَا هِيَ بِعَوْرَةٍ ۖ إِن يُرِيدُونَ إِلَّا فِرَارًا ﴿١٣﴾
13. Na pale waliposema kundi miongoni mwao: Enyi watu wa Yathrib! Hamna uimara, basi rudini (makwenu)! Na kundi miongoni mwao likamwomba idhini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) likasema: Hakika nyumba zetu ziko tupu! Na wala hazikuwa tupu! Hawakutaka ila kukimbia tu!
وَلَوْ دُخِلَتْ عَلَيْهِم مِّنْ أَقْطَارِهَا ثُمَّ سُئِلُوا الْفِتْنَةَ لَآتَوْهَا وَمَا تَلَبَّثُوا بِهَا إِلَّا يَسِيرًا ﴿١٤﴾
14. Na lau wangeliingiliwa kutoka pande zake zote (za mji), kisha wakatakwa kuritadi, basi wangeliifanya na wala wasingelisita kwayo isipokuwa kidogo tu.
وَلَقَدْ كَانُوا عَاهَدُوا اللَّـهَ مِن قَبْلُ لَا يُوَلُّونَ الْأَدْبَارَ ۚ وَكَانَ عَهْدُ اللَّـهِ مَسْئُولًا ﴿١٥﴾
15. Na kwa yakini walikwishamuahidi Allaah kabla, kwamba hawatogeuza migongo yao kukimbia. Na Ahadi ya Allaah ni yenye kuulizwa tu.
قُل لَّن يَنفَعَكُمُ الْفِرَارُ إِن فَرَرْتُم مِّنَ الْمَوْتِ أَوِ الْقَتْلِ وَإِذًا لَّا تُمَتَّعُونَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿١٦﴾
16. Sema: (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Kukimbia hakutakufaeni ikiwa mmeyakimbia mauti, au kuuawa, kwani hamtostareheshwa isipokuwa kidogo tu.
قُلْ مَن ذَا الَّذِي يَعْصِمُكُم مِّنَ اللَّـهِ إِنْ أَرَادَ بِكُمْ سُوءًا أَوْ أَرَادَ بِكُمْ رَحْمَةً ۚ وَلَا يَجِدُونَ لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿١٧﴾
17. Sema: Ni nani ambaye anaweza kukulindeni na Allaah, kama Akikutakieni uovu au Akikutakieni Rehma? Na wala hawatopata badala ya Allaah mlinzi wala mwenye kunusuru.
قَدْ يَعْلَمُ اللَّـهُ الْمُعَوِّقِينَ مِنكُمْ وَالْقَائِلِينَ لِإِخْوَانِهِمْ هَلُمَّ إِلَيْنَا ۖ وَلَا يَأْتُونَ الْبَأْسَ إِلَّا قَلِيلًا ﴿١٨﴾
18. Allaah Amekwishawajua wanaozuia miongoni mwenu (watu wasiende vitani) na wale wanaowaambia ndugu zao: Njooni kwetu! Na hawaendi vitani isipokuwa kidogo tu.
أَشِحَّةً عَلَيْكُمْ ۖ فَإِذَا جَاءَ الْخَوْفُ رَأَيْتَهُمْ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ تَدُورُ أَعْيُنُهُمْ كَالَّذِي يُغْشَىٰ عَلَيْهِ مِنَ الْمَوْتِ ۖ فَإِذَا ذَهَبَ الْخَوْفُ سَلَقُوكُم بِأَلْسِنَةٍ حِدَادٍ أَشِحَّةً عَلَى الْخَيْرِ ۚ أُولَـٰئِكَ لَمْ يُؤْمِنُوا فَأَحْبَطَ اللَّـهُ أَعْمَالَهُمْ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿١٩﴾
19. Wachoyo sana juu yenu. Na inapokuja khofu utawaona wanakutazama macho yao yanazunguruka kama yule aliyefunikwa na mauti. Inapoondoka khofu wanakushutumuni kwa ndimi kali! Wachoyo wa kila kheri! Hao hawakuamini, na kwa hivyo Allaah Ameziporomosha amali zao. Na hayo kwa Allaah ni mepesi kabisa.
يَحْسَبُونَ الْأَحْزَابَ لَمْ يَذْهَبُوا ۖ وَإِن يَأْتِ الْأَحْزَابُ يَوَدُّوا لَوْ أَنَّهُم بَادُونَ فِي الْأَعْرَابِ يَسْأَلُونَ عَنْ أَنبَائِكُمْ ۖ وَلَوْ كَانُوا فِيكُم مَّا قَاتَلُوا إِلَّا قَلِيلًا ﴿٢٠﴾
20. Wanadhania kuwa makundi yaliyoshirikiana hayakuondoka bado. Na yanapokuja makundi yaliyoshirikiana, wanatamani lau kwamba wanaishi jangwani kwa mabedui, wanaulizia habari zenu. Na lau wangelikuwa wako pamoja nanyi, basi wasingelipigana isipokuwa kidogo tu.
لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرًا ﴿٢١﴾
21. Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Rasuli wa Allaah kwa mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho[8], na akamdhukuru Allaah kwa wingi.
وَلَمَّا رَأَى الْمُؤْمِنُونَ الْأَحْزَابَ قَالُوا هَـٰذَا مَا وَعَدَنَا اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَصَدَقَ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ ۚ وَمَا زَادَهُمْ إِلَّا إِيمَانًا وَتَسْلِيمًا ﴿٢٢﴾
22. Basi Waumini walipoona makundi yaliyoshirikiana, walisema: Haya ndio yale Aliyotuahidi Allaah na Rasuli Wake, na Amesema kweli Allaah na Rasuli Wake. Na haikuwazidishia isipokuwa imaan na kujisalimisha.
مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّـهَ عَلَيْهِ ۖ فَمِنْهُم مَّن قَضَىٰ نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ ۖ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا ﴿٢٣﴾
23. Miongoni mwa Waumini, wapo wanaume waliotimiza kikweli waliyoahidiana na Allaah. Basi miongoni mwao wako waliotimiza nadhiri yao (wamekufa Shuhadaa), na miongoni mwao wako wanaongojea na hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.[9]
لِّيَجْزِيَ اللَّـهُ الصَّادِقِينَ بِصِدْقِهِمْ وَيُعَذِّبَ الْمُنَافِقِينَ إِن شَاءَ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٢٤﴾
24. Ili Allaah Awalipe wakweli kwa ukweli wao, na Awaadhibu wanafiki pindi Akitaka au Apokee tawbah yao. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَرَدَّ اللَّـهُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِغَيْظِهِمْ لَمْ يَنَالُوا خَيْرًا ۚ وَكَفَى اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ الْقِتَالَ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ قَوِيًّا عَزِيزًا ﴿٢٥﴾
25. Na Allaah Akawarudisha nyuma wale waliokufuru kwa ghaidhi zao, hawakupata kheri yoyote. Na Allaah Amewatosheleza Waumini vitani. Na Allaah daima Ni Mwenye nguvu zote, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika.[10]
وَأَنزَلَ الَّذِينَ ظَاهَرُوهُم مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مِن صَيَاصِيهِمْ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ الرُّعْبَ فَرِيقًا تَقْتُلُونَ وَتَأْسِرُونَ فَرِيقًا ﴿٢٦﴾
26. Na Aliwateremsha wale waliowasaidia (maadui) miongoni mwa Watu wa Kitabu kutoka katika ngome zao, na Akavurumisha kizaazaa katika nyoyo zao; kundi mnaliua, na kundi jingine mnaliteka.
وَأَوْرَثَكُمْ أَرْضَهُمْ وَدِيَارَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ وَأَرْضًا لَّمْ تَطَئُوهَا ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرًا ﴿٢٧﴾
27. Na Akakurithisheni ardhi yao, na majumba yao, na mali zao, na ardhi hamkuwahi kuzikanyaga. Na Allaah daima Ni Muweza juu ya kila kitu.
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ إِن كُنتُنَّ تُرِدْنَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا فَتَعَالَيْنَ أُمَتِّعْكُنَّ وَأُسَرِّحْكُنَّ سَرَاحًا جَمِيلًا ﴿٢٨﴾
28. Ee Nabiy! Waambie wake zako: Ikiwa mnataka uhai wa dunia na mapambo yake, basi njooni nikupeni kitoka nyumba na nikuacheni huru, mwachano mzuri.[11]
وَإِن كُنتُنَّ تُرِدْنَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَالدَّارَ الْآخِرَةَ فَإِنَّ اللَّـهَ أَعَدَّ لِلْمُحْسِنَاتِ مِنكُنَّ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿٢٩﴾
29. Na ikiwa mnamtaka Allaah na Rasuli Wake na Nyumba ya Aakhirah, basi hakika Allaah Amewaahidi wanawake watendao wema miongoni mwenu, ujira adhimu.
يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ مَن يَأْتِ مِنكُنَّ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ يُضَاعَفْ لَهَا الْعَذَابُ ضِعْفَيْنِ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿٣٠﴾
30. Enyi wake wa Nabiy! Yeyote yule miongoni mwenu atakayeleta uchafu bayana, atazidishiwa adhabu maradufu. Na hayo kwa Allaah ni mepesi.
وَمَن يَقْنُتْ مِنكُنَّ لِلَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتَعْمَلْ صَالِحًا نُّؤْتِهَا أَجْرَهَا مَرَّتَيْنِ وَأَعْتَدْنَا لَهَا رِزْقًا كَرِيمًا ﴿٣١﴾
31. Na yeyote miongoni mwenu atakayemtii Allaah na Rasuli Wake, na akatenda mema, Tutampa ujira wake mara mbili, na Tumemuandalia riziki ya ukarimu.
يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِّنَ النِّسَاءِ ۚ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا ﴿٣٢﴾
32. Enyi wake wa Nabiy! Nyinyi si kama yeyote yule katika wanawake. Mkiwa na taqwa, basi msilegeze (sauti) katika kauli (zenu), asije akaingiwa tamaa ambaye moyoni mwake mna maradhi, na semeni kauli inayokubalika.[12]
وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ ۖ وَأَقِمْنَ الصَّلَاةَ وَآتِينَ الزَّكَاةَ وَأَطِعْنَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيُذْهِبَ عَنكُمُ الرِّجْسَ أَهْلَ الْبَيْتِ وَيُطَهِّرَكُمْ تَطْهِيرًا ﴿٣٣﴾
33. Na bakieni majumbani mwenu, na wala msionyeshe mapambo na uzuri kwa ajinabi kujishaua kama zama za ujahili. Na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah na mtiini Allaah na Rasuli Wake. Hakika Allaah Anataka Akuondosheeni maovu enyi ahli wa nyumba (ya Nabiy) na Akutakaseni mtakaso barabara.
وَاذْكُرْنَ مَا يُتْلَىٰ فِي بُيُوتِكُنَّ مِنْ آيَاتِ اللَّـهِ وَالْحِكْمَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ لَطِيفًا خَبِيرًا ﴿٣٤﴾
34. Na kumbukeni yale yanayosomwa majumbani mwenu katika Aayaat za Allaah na Hikmah (Sunnah). Hakika Allaah daima Ni Mwenye Kudabiri mambo kwa Ulatifu, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِينَ وَالصَّائِمَاتِ وَالْحَافِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَالْحَافِظَاتِ وَالذَّاكِرِينَ اللَّـهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا ﴿٣٥﴾
35. Hakika Waislamu wanaume na wanawake, na Waumini wanaume na wanawake, na watiifu wanaume na wanawake, na wasemao kweli wanaume na wanawake, na wanaosubiri wanaume na wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanawake, na watoao swadaqah wanaume na wanawake, na wafungao Swawm wanaume na wanawake, na wanaojihifadhi tupu zao wanaume na wanawake, na wanaomdhukuru Allaah kwa wingi wanaume na wanawake, Allaah Amewaandalia Maghfirah na ujira adhimu.[13]
وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا ﴿٣٦﴾
36. Na haiwi kwa Muumini mwanamume wala kwa Muumini mwanamke, Anapohukumu Allaah na Rasuli Wake jambo lolote, iwe wana khiari katika jambo lao. Na anayemuasi Allaah na Rasuli Wake, basi kwa yakini amepotoka upotofu bayana.
وَإِذْ تَقُولُ لِلَّذِي أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَأَنْعَمْتَ عَلَيْهِ أَمْسِكْ عَلَيْكَ زَوْجَكَ وَاتَّقِ اللَّـهَ وَتُخْفِي فِي نَفْسِكَ مَا اللَّـهُ مُبْدِيهِ وَتَخْشَى النَّاسَ وَاللَّـهُ أَحَقُّ أَن تَخْشَاهُ ۖ فَلَمَّا قَضَىٰ زَيْدٌ مِّنْهَا وَطَرًا زَوَّجْنَاكَهَا لِكَيْ لَا يَكُونَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ حَرَجٌ فِي أَزْوَاجِ أَدْعِيَائِهِمْ إِذَا قَضَوْا مِنْهُنَّ وَطَرًا ۚ وَكَانَ أَمْرُ اللَّـهِ مَفْعُولًا ﴿٣٧﴾
37. Na pale ulipomwambia yule ambaye Allaah Amemneemesha nawe ukamneemesha: Mshikilie mkeo, na mche Allaah! Na ukaficha katika nafsi yako ambayo Allaah Ametaka kuyafichua, na unakhofu watu, na hali Allaah Ana haki zaidi umkhofu. Basi Zayd alipomaliza haja kwake, Tukakuozesha ili isiwe dhambi juu ya Waumini kuhusu (kuoa) wake wa watoto wao wa kupanga wanapomaliza haja kwao. Na Amri ya Allaah daima ni yenye kutekelezwa.[14]
مَّا كَانَ عَلَى النَّبِيِّ مِنْ حَرَجٍ فِيمَا فَرَضَ اللَّـهُ لَهُ ۖ سُنَّةَ اللَّـهِ فِي الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلُ ۚ وَكَانَ أَمْرُ اللَّـهِ قَدَرًا مَّقْدُورًا ﴿٣٨﴾
38. Hakuna lawama yoyote juu ya Nabiy katika (kufanya) yale Aliyomfaridhishia Allaah. Ni Desturi ya Allaah kwa wale waliopita kabla. Na Amri ya Allaah daima ni kudura iliyokwishakadiriwa vyema kabisa.
الَّذِينَ يُبَلِّغُونَ رِسَالَاتِ اللَّـهِ وَيَخْشَوْنَهُ وَلَا يَخْشَوْنَ أَحَدًا إِلَّا اللَّـهَ ۗ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ حَسِيبًا ﴿٣٩﴾
39. Wale wanaobalighisha Ujumbe wa Allaah na wanamkhofu Yeye na wala hawamkhofu yeyote isipokuwa Allaah. Na Allaah Anatosheleza Kuwa Mwenye Kuhesabu.
مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٤٠﴾
40. Hakuwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) baba wa yeyote katika wanaume wenu, lakini ni Rasuli wa Allaah na ni mwisho wa Manabii. Na Allaah daima Ni Mjuzi wa kila kitu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّـهَ ذِكْرًا كَثِيرًا ﴿٤١﴾
41. Enyi walioamini! Mdhukuruni Allaah kwa wingi wa kumdhukuru.
وَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا ﴿٤٢﴾
42. Na Msabbihini asubuhi na jioni.
هُوَ الَّذِي يُصَلِّي عَلَيْكُمْ وَمَلَائِكَتُهُ لِيُخْرِجَكُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۚ وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا ﴿٤٣﴾
43. Yeye (Allaah) Ndiye Anakurehemuni, na Malaika Wake (wanakuombeeni maghfirah na rehma)[15] ili Akutoeni kutoka katika viza kuingia katika Nuru. Naye daima Ni Mwenye Kurehemu Waumini.
تَحِيَّتُهُمْ يَوْمَ يَلْقَوْنَهُ سَلَامٌ ۚ وَأَعَدَّ لَهُمْ أَجْرًا كَرِيمًا ﴿٤٤﴾
44. Maamkizi yao Siku watakayokutana Naye ni “Salaam.” Na Amewaandalia ujira wa ukarimu.[16]
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا ﴿٤٥﴾
45. Ee Nabiy! Hakika Sisi Tumekutuma uwe shahidi, na mbashiriaji na mwonyaji.
وَدَاعِيًا إِلَى اللَّـهِ بِإِذْنِهِ وَسِرَاجًا مُّنِيرًا ﴿٤٦﴾
46. Na mlinganiaji kwa Allaah kwa Idhini Yake, na siraji kali yenye nuru.
وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ بِأَنَّ لَهُم مِّنَ اللَّـهِ فَضْلًا كَبِيرًا ﴿٤٧﴾
47. Na wabashirie Waumini kwamba watapata kutoka kwa Allaah fadhila kubwa.
وَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَالْمُنَافِقِينَ وَدَعْ أَذَاهُمْ وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ وَكِيلًا ﴿٤٨﴾
48. Na wala usiwatii makafiri na wanafiki, na achilia mbali maudhi yao, na tawakali kwa Allaah. Na Allaah Anatosheleza Kuwa Mtegemewa.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نَكَحْتُمُ الْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ فَمَا لَكُمْ عَلَيْهِنَّ مِنْ عِدَّةٍ تَعْتَدُّونَهَا ۖ فَمَتِّعُوهُنَّ وَسَرِّحُوهُنَّ سَرَاحًا جَمِيلًا ﴿٤٩﴾
49. Enyi walioamini! Mnapofunga nikaah na Waumini wa kike, kisha mkawataliki kabla ya kujimai nao, basi hamna juu yao eda yoyote mtakayohesabu. Basi wapeni kitoka nyumba na waacheni huru, kwa mwachano mzuri.
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِنَّا أَحْلَلْنَا لَكَ أَزْوَاجَكَ اللَّاتِي آتَيْتَ أُجُورَهُنَّ وَمَا مَلَكَتْ يَمِينُكَ مِمَّا أَفَاءَ اللَّـهُ عَلَيْكَ وَبَنَاتِ عَمِّكَ وَبَنَاتِ عَمَّاتِكَ وَبَنَاتِ خَالِكَ وَبَنَاتِ خَالَاتِكَ اللَّاتِي هَاجَرْنَ مَعَكَ وَامْرَأَةً مُّؤْمِنَةً إِن وَهَبَتْ نَفْسَهَا لِلنَّبِيِّ إِنْ أَرَادَ النَّبِيُّ أَن يَسْتَنكِحَهَا خَالِصَةً لَّكَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۗ قَدْ عَلِمْنَا مَا فَرَضْنَا عَلَيْهِمْ فِي أَزْوَاجِهِمْ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ لِكَيْلَا يَكُونَ عَلَيْكَ حَرَجٌ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٥٠﴾
50. Ee Nabiy! Hakika Sisi Tumekuhalalishia wake zako ambao uliwapa mahari yao, na wale iliyomiliki mkono wako wa kuume katika wale (mateka) Aliokuruzuku Allaah, na mabinti wa ‘ammi zako, na mabinti wa mashangazi zako, na mabinti wa wajomba zako, na mabinti wa khalati zako ambao wamehajiri pamoja nawe, na mwanamke Muumini akijitunuku mwenyewe kwa Nabiy, ikiwa Nabiy anataka kumuoa. Ni makhsusi kwako wewe tu, si kwa Waumini wengine. Tumekwishajua yale Tuliyowafaridhishia wao katika wake zao na wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume ili isijekuwa vigumu juu yako. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
تُرْجِي مَن تَشَاءُ مِنْهُنَّ وَتُؤْوِي إِلَيْكَ مَن تَشَاءُ ۖ وَمَنِ ابْتَغَيْتَ مِمَّنْ عَزَلْتَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكَ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن تَقَرَّ أَعْيُنُهُنَّ وَلَا يَحْزَنَّ وَيَرْضَيْنَ بِمَا آتَيْتَهُنَّ كُلُّهُنَّ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا فِي قُلُوبِكُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَلِيمًا ﴿٥١﴾
51. Umuakhirishe umtakaye miongoni mwao na umsogeze kwako umtakaye. Na ukimtaka katika uliyemtenga basi hakuna dhambi juu yako. Hivyo ni karibu zaidi kupelekea kuburudika macho yao, na wala wasihuzunike, na waridhike kwa yale uliyowapa kila mmoja wao. Na Allaah Anajua yale yaliyomo nyoyoni mwao. Na Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mvumilivu.[17]
لَّا يَحِلُّ لَكَ النِّسَاءُ مِن بَعْدُ وَلَا أَن تَبَدَّلَ بِهِنَّ مِنْ أَزْوَاجٍ وَلَوْ أَعْجَبَكَ حُسْنُهُنَّ إِلَّا مَا مَلَكَتْ يَمِينُكَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ رَّقِيبًا ﴿٥٢﴾
52. Si halali kwako wanawake wengine baada ya hao na wala kuwabadilisha kwa wake wengine japo kama uzuri wao umekupendeza, isipokuwa wale iliyomiliki mkono wako wa kuume. Na Allaah daima Ni Mwenye Kuchunga kila kitu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتَ النَّبِيِّ إِلَّا أَن يُؤْذَنَ لَكُمْ إِلَىٰ طَعَامٍ غَيْرَ نَاظِرِينَ إِنَاهُ وَلَـٰكِنْ إِذَا دُعِيتُمْ فَادْخُلُوا فَإِذَا طَعِمْتُمْ فَانتَشِرُوا وَلَا مُسْتَأْنِسِينَ لِحَدِيثٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكُمْ كَانَ يُؤْذِي النَّبِيَّ فَيَسْتَحْيِي مِنكُمْ ۖ وَاللَّـهُ لَا يَسْتَحْيِي مِنَ الْحَقِّ ۚ وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ ۚ ذَٰلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ ۚ وَمَا كَانَ لَكُمْ أَن تُؤْذُوا رَسُولَ اللَّـهِ وَلَا أَن تَنكِحُوا أَزْوَاجَهُ مِن بَعْدِهِ أَبَدًا ۚ إِنَّ ذَٰلِكُمْ كَانَ عِندَ اللَّـهِ عَظِيمًا ﴿٥٣﴾
53. Enyi walioamini! Msiingie nyumba za Nabiy isipokuwa mkipewa idhini ya kwenda kula si kungojea kiive. Lakini mtakapoitwa, basi ingieni. Na mkimaliza kula, tawanyikeni, na wala msikae kujiliwaza kwa mazungumzo. Hakika hiyo ilikuwa inamuudhi Nabiy, naye anakustahini, lakini Allaah Hasitahi (kubainisha) haki. Na mnapowauliza wake zake haja, waulizeni nyuma ya pazia. Hivyo ni utwaharifu zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao. Na haipasi kwenu kumuudhi Rasuli wa Allaah. Na wala kuwaoa wake zake baada yake abadani. Hakika jambo hilo mbele ya Allaah ni kubwa mno.[18]
إِن تُبْدُوا شَيْئًا أَوْ تُخْفُوهُ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٥٤﴾
54. Mkidhihirisha kitu chochote au mkikificha, basi hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa kila kitu.
لَّا جُنَاحَ عَلَيْهِنَّ فِي آبَائِهِنَّ وَلَا أَبْنَائِهِنَّ وَلَا إِخْوَانِهِنَّ وَلَا أَبْنَاءِ إِخْوَانِهِنَّ وَلَا أَبْنَاءِ أَخَوَاتِهِنَّ وَلَا نِسَائِهِنَّ وَلَا مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ ۗ وَاتَّقِينَ اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدًا ﴿٥٥﴾
55. Hamna dhambi juu yao wanawake (kuonekana bila hijaab) mbele ya baba zao, wala watoto wao wa kiume, wala kaka zao, wala watoto wa kiume wa kaka zao, wala watoto wa kiume wa dada zao, wala wanawake wenzao (wa Kiislamu), wala iliyowamiliki mikono yao ya kulia. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah daima Ni Mwenye Kushuhudia kila kitu.
إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٥٦﴾
56. Hakika Allaah na Malaika Wake Wanamswalia Nabiy. Enyi walioamini! Mswalieni na msalimieni kwa maamkizi ya amani.[19]
إِنَّ الَّذِينَ يُؤْذُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَأَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا مُّهِينًا ﴿٥٧﴾
57. Hakika wale wanaomuudhi Allaah na Rasuli Wake, Allaah Amewalaani duniani na Aakhirah, na Amewaandalia adhabu ya kudhalilisha.
وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿٥٨﴾
58. Na wale wanaowaudhi Waumini wa kiume na Waumini wa kike bila ya kuwa wamechuma kosa, basi kwa yakini wamejibebea usingiziaji mkuu wa dhulma na dhambi bayana.
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٥٩﴾
59. Ee Nabiy! Waambie wake zako, na mabinti zako, na wanawake wa Waumini wajiteremshie jilbaab zao.[20] Hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane (kwa heshima) wasiudhiwe. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
لَّئِن لَّمْ يَنتَهِ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْمُرْجِفُونَ فِي الْمَدِينَةِ لَنُغْرِيَنَّكَ بِهِمْ ثُمَّ لَا يُجَاوِرُونَكَ فِيهَا إِلَّا قَلِيلًا ﴿٦٠﴾
60. Ikiwa wanafiki, na wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi , na waenezao fitnah katika (mji wa) Madiynah hawatokoma, bila shaka Tutakusalitisha juu yao, kisha hawatokaa humo kuwa jirani zako isipokuwa kidogo tu.
مَّلْعُونِينَ ۖ أَيْنَمَا ثُقِفُوا أُخِذُوا وَقُتِّلُوا تَقْتِيلًا ﴿٦١﴾
61. Maluuni hao! Popote wanapopatikana, wachukuliwe, na wauliwe wote bila chembe ya huruma.
سُنَّةَ اللَّـهِ فِي الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلُ ۖ وَلَن تَجِدَ لِسُنَّةِ اللَّـهِ تَبْدِيلًا ﴿٦٢﴾
62. Ni Desturi ya Allaah kwa wale waliopita kabla. Na wala hutopata mabadiliko katika Desturi ya Allaah.[21]
يَسْأَلُكَ النَّاسُ عَنِ السَّاعَةِ ۖ قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ اللَّـهِ ۚ وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ السَّاعَةَ تَكُونُ قَرِيبًا ﴿٦٣﴾
63. Watu wanakuuliza kuhusu Saa. Sema: Ujuzi wake uko kwa Allaah. Na nini kitakujulisha? Huenda Saa itakuwa karibu.[22]
إِنَّ اللَّـهَ لَعَنَ الْكَافِرِينَ وَأَعَدَّ لَهُمْ سَعِيرًا ﴿٦٤﴾
64. Hakika Allaah Amewalaani makafiri, na Amewaandalia moto uliowashwa vikali mno.
خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ لَّا يَجِدُونَ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا ﴿٦٥﴾
65. Ni wenye kudumu humo abadi. Hawatopata mlinzi wala mwenye kunusuru.
يَوْمَ تُقَلَّبُ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ يَقُولُونَ يَا لَيْتَنَا أَطَعْنَا اللَّـهَ وَأَطَعْنَا الرَّسُولَا ﴿٦٦﴾
66. Siku zitakapopinduliwa nyuso zao motoni, watasema: Laiti tungelimtii Allaah, na tungelimtii Rasuli.
وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا ﴿٦٧﴾
67. Na watasema: Rabb wetu! Hakika sisi tuliwatii mabwana zetu na wakuu wetu, wakatupoteza njia.
رَبَّنَا آتِهِمْ ضِعْفَيْنِ مِنَ الْعَذَابِ وَالْعَنْهُمْ لَعْنًا كَبِيرًا ﴿٦٨﴾
68. Rabb wetu! Wape adhabu maradufu, na Walaani laana kubwa.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ آذَوْا مُوسَىٰ فَبَرَّأَهُ اللَّـهُ مِمَّا قَالُوا ۚ وَكَانَ عِندَ اللَّـهِ وَجِيهًا ﴿٦٩﴾
69. Enyi walioamini! Msiwe kama wale waliomuudhi Muwsaa, lakini Allaah Alimtoa tuhumani kutokana na yale waliyoyasema. Na alikuwa mbele ya Allaah mwenye kuheshimika.[23]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا ﴿٧٠﴾
70. Enyi walioamini! Mcheni Allaah na semeni kauli nyofu ya haki.
يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا ﴿٧١﴾
71. Atakutengenezeeni amali zenu, na Atakughufurieni madhambi yenu. Na anayemtii Allaah na Rasuli Wake, basi kwa yakini amefanikiwa mafanikio adhimu.
إِنَّا عَرَضْنَا الْأَمَانَةَ عَلَى السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَالْجِبَالِ فَأَبَيْنَ أَن يَحْمِلْنَهَا وَأَشْفَقْنَ مِنْهَا وَحَمَلَهَا الْإِنسَانُ ۖ إِنَّهُ كَانَ ظَلُومًا جَهُولًا ﴿٧٢﴾
72. Hakika Sisi Tulihudhurisha amana[24] kwa mbingu na ardhi na majabali, vikakataa kuibeba na vikaiogopa, lakini binaadam aliibeba. Hakika yeye amekuwa dhalimu mno, jahili mno.
لِّيُعَذِّبَ اللَّـهُ الْمُنَافِقِينَ وَالْمُنَافِقَاتِ وَالْمُشْرِكِينَ وَالْمُشْرِكَاتِ وَيَتُوبَ اللَّـهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٧٣﴾
73. Ili Allaah Awaadhibu wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike, na washirikina wa kiume na washirikina wa kike, na Allaah Apokee tawbah ya Waumini wa kiume na Waumini wa kike. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
[1] Amrisho La Kuwaita Watoto Wa Kupanga Kwa Majina Ya Baba Zao Na Sio Kwa Aliyemkafili Kumlea:
[2] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
033-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Ahzaab Aayah 05: ادْعُوهُمْ لآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِنْدَ اللَّهِ [240]
[3] Kumpenda Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kuliko Nafsi Yake Mtu
Mapenzi ya Waumini kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) yanapaswa kuwa makubwa zaidi kuliko mtu kujipenda mwenyewe. Na ndipo ikawa imaan ya Muislamu haitimii mpaka iwe kumpenda Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni zaidi kuliko anavyoipenda nafsi yake. Miongoni mwa Hadiyth zenye mada hii ni hizi zifuatazo
عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللّه عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قال: ((لا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكونَ أحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَالِدِهِ وَوَلَدِه وَالنَّاسِ أَجْمَعينَ )) متفق عليه
Amesimulia Anas bin Maalik (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hatoamini mmoja wenu mpaka niwe (mimi Muhammad) kipenzi chake kuliko mwanawe na wazazi wake na kuliko watu wote waliobakia.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na ‘Umar (رضي الله عنه) aliyathibitisha mapenzi ya kumpenda Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuliko nafsi yake:
عبد اللَّهِ بْنَ هِشَامٍ قَالَ، كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم وَهْوَ آخِذٌ بِيَدِ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ فَقَالَ لَهُ عُمَرُ يَا رَسُولَ اللَّهِ لأَنْتَ أَحَبُّ إِلَىَّ مِنْ كُلِّ شَىْءٍ إِلاَّ مِنْ نَفْسِي. فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((لاَ وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْكَ مِنْ نَفْسِكَ)) فَقَالَ لَهُ عُمَرُ فَإِنَّهُ الآنَ وَاللَّهِ لأَنْتَ أَحَبُّ إِلَىَّ مِنْ نَفْسِي. فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((الآنَ يَا عُمَرُ))
Amesimulia ‘Abdullaah bin Hishaam (رضي الله عنه): Tulikuwa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) naye ameushika mkono wa ‘Umar bin Al-Khattwaab. ‘Umar akamwambia: Ee Rasuli wa Allaah, hakika wewe ni kipenzi zaidi kwangu kuliko kitu chochote isipokuwa nafsi yangu. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hapana, (haiwezekani hivyo). Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, mpaka niwe kipenzi zaidi kwako kuliko nafsi yako.” ‘Umar (رضي الله عنه) akamwambia: Basi kwa sasa Wa-Allaahi wewe ni kipenzi zaidi kwangu kuliko nafsi yangu. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hivi sasa ee ‘Umar (umekuwa Muumini wa kweli).” [Al-Bukhaariy]
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((مَا مِنْ مُؤْمِنٍ إِلاَّ وَأَنَا أَوْلَى النَّاسِ بِهِ فِي الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ، اقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: ((النَّبِيُّ أَوْلَى بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنْفُسِهِمْ)) فَأَيُّمَا مُؤْمِنٍ تَرَكَ مَالاً فَلْيَرِثْهُ عَصَبَتُهُ مَنْ كَانُوا، فَإِنْ تَرَكَ دَيْنًا أَوْ ضِيَاعًا فَلْيَأْتِنِي وَأَنَا مَوْلاَهُ)) البخاري
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna Muumini yeyote isipokuwa mimi nina haki zaidi kwake (ya kupendwa na kutiiwa) kuliko watu wote duniani na Aakhirah. Someni mkipenda:
النَّبِيُّ أَوْلَىٰ بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنفُسِهِمْ ۖ
“Nabiy ana haki zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao.” [Al-Ahzaab (33:6)]
Na Muumini yeyote aliyeacha mali basi na warithi jamaa zake waliopo. Na ikiwa ameacha deni au watoto masikini, basi na waje kwangu (niwalipie madeni yao na niwahudumie), mimi ni mlinzi wao.” [Al-Bukhaariy]
[4] Wake Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Mama Wa Waumini:
Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ndiye mwenye kupewa kipaumbele zaidi kwa Waumini, na ndiye aliye karibu na wao zaidi kuliko nafsi zao katika mambo ya Dini na dunia. Na heshima ya wake za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa ummah wake, ni kama vile heshima ya mama zao, kwani haifai kuwaoa wake za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) milele baada yake. Na wenye ujamaa wa ukaribu, miongoni mwa Waislamu, baadhi yao wana haki zaidi ya kuwarithi wengine katika hukumu ya Allaah na Sharia Yake kuliko kurithi kwa misingi ya imaan na hijrah (uhamiaji). Waislamu hapo mwanzo wa Uislamu walikuwa wakirithiana kwa misingi ya hijrah na imaan au Dini, na si kwa kizazi, kisha hilo likaondolewa kwa Aayah ya Mirathi. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Hapa Allaah (سبحانه وتعالى) Anawaambia Waumini jambo liwatambulishe daraja ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ili waweze kutaamali naye ipasavyo. Jambo la karibu zaidi kwa mtu yeyote ni nafsi yake, lakini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) anatakiwa awe karibu naye zaidi kuliko nafsi yake, kwa sababu yeye aliwanasihi kidhati, na alikuwa na huruma mno kwao na wema. Akathibitisha kuwa yeye ni mwenye zaidi na fadhila kuliko watu wote. Basi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ndiye kiumbe mwenye fadhila kubwa zaidi kwao kuliko viumbe vyote, na ndiye mkarimu na mpole zaidi kwao kwani haikuwafikia uzito wa chembe ya kheri, wala hawakuepushwa uzito wa chembe ya madhara isipokuwa kwa sababu yake.
Kwa sababu hiyo, inawajibika kwao pindi utakapotofautiana muradi (makusudio) wa nafsi au muradi wa yeyote yule, ukatofautiana na muradi wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), basi utangulizwe wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na wala isipingwe kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kauli ya mtu yeyote yule, vyovyote atakavyokuwa. Watu wamtolee fidia nafsi zao, mali zao na watoto wao. Na watangulize mapenzi ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuliko mapenzi ya kiumbe chochote, na wasiongee mpaka aongee, na wasitangulie mbele yake (wasitangulize kauli ya yeyote).
Na yeye Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni baba wa Waumini, kama ilivyo katika Qiraa-a cha baadhi ya Swahaba, akiwa anawalea kama mzazi anavyomlea mtoto wake. Ndio ikapelekea kwa ubaba huu kuwa wake zake ni mama zao (Waumini), yaani, katika uharamu wa kuwaoa, kuwaheshimu na kuwakirimu, sio kwamba wakae nao faragha kama ni maharim zao (hapana). Haya maneno kama vile ni utangulizi wa maelezo yanayokuja yakihusu kisa cha Zayd bin Haarithah, ambae alikuwa kabla ya hapo akiitwa “Zayd Bin Muhammad” mpaka Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:
مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ
“Hakuwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu.” [Al-Ahzaab (33:40)]
Ikakatwa nasaba yake, na kunasibishwa kwake, na Allaah Akahabarisha katika Aayah hii, ya kwamba, Waumini wote ni watoto wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Hakuna yeyote atakayemzidi hadhi mwingine katika hili hata ikikatika nasaba ya kujinasibisha, kwani nasaba ya kiimani haikukatika, hivyo asihuzunike wala asisikitike.
Na kwa kuwa wake za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) washakuwa ni Mama wa Waumini wote, kwa msingi huu, hawahalaliki kuolewa na yeyote baada ya kuolewa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kama Alivyobainisha hilo Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَا أَن تَنكِحُوا أَزْوَاجَهُ مِن بَعْدِهِ أَبَدًا ۚ
“Na wala kuwaoa wake zake baada yake abadani.” [Al-Ahzaab (33:53)]
[Tafsiyr As-Sa’diy]
[5] Rusuli Wa Ulul-‘Azmi (Wenye Azimio La Nguvu).
Rusuli hao watano waliotajwa wanajulikana kuwa ni Ulul-‘Azmi. Wameitwa hivi kwa sababu walikuwa ni wenye azimio la nguvu baada ya kuchukua ahadi ngumu ya kubalighisha Risala na kufanya Jihaad katika Njia ya Allaah, kwa subira ya hali ya juu. Hivyo ni kutokana na kusumbuliwa na kukanushwa kwao na watu wao, wakapata mitihani na mashaka makubwa, hadi wengine kufukuzwa na watu wao na kutaka kudhuriwa na kuuliwa. Rejea Al-Ahqaaf (46:35). Rejea pia An-Nisaa (4:69) kwenye maelezo bayana kuhusu Rusuli kuwa na daraja la juu zaidi kulingana na Manabii kwa sababu ya subira zao katika kulingania Dini ya Allaah (سبحانه وتعالى).
[6] Ghazwat Al-Ahzaab (Vita Vya Makundi Yaliyoshirikiana) Au Al-Khandaq Handaki):
Vita vitukufu vya Al-Ahzaab au Al-Khandaq vimetajwa takriban kuanzia Aayah ya (9) hadi ya (25) katika Suwrah hii ya Al-Ahzaab.
Vita vya Al-Ahzaab au Al-Khandaq, ni vita vilivyopiganwa mwezi wa Shawwaal katika mwaka wa tano wa Hijriyyah. Vita vilikuwa kati ya Waislam wakiongozwa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Ahzaab ambao ni mkusanyiko wa makabila mbalimbali ya Waarabu, wakiwemo Maquraysh wa Makkah ambao waliungana pamoja kwa lengo la kuipiga Madiynah na kuwamaliza Waislamu.
Baadhi ya matukio ya Vita vya Al-Ahzaab au Khandaq yametajwa katika Aayah hizo na maelezo ziyada ni kama yafuatayo:
Sababu ya Vita Kuitwa Khandaq (Handaki) ni kutokana na ushauri wa Swahaba mtukufu Salmaan Al-Faarisiy (رضي الله عنه) .
Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na Swahaha zake walichimba handaki hilo kwa mikono yao kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
حَدَّثَنِي أَحْمَدُ بْنُ عُثْمَانَ، حَدَّثَنَا شُرَيْحُ بْنُ مَسْلَمَةَ، قَالَ حَدَّثَنِي إِبْرَاهِيمُ بْنُ يُوسُفَ، قَالَ حَدَّثَنِي أَبِي، عَنْ أَبِي إِسْحَاقَ، قَالَ سَمِعْتُ الْبَرَاءَ، يُحَدِّثُ قَالَ لَمَّا كَانَ يَوْمُ الأَحْزَابِ، وَخَنْدَقَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم رَأَيْتُهُ يَنْقُلُ مِنْ تُرَابِ الْخَنْدَقِ حَتَّى وَارَى عَنِّي الْغُبَارُ جِلْدَةَ بَطْنِهِ، وَكَانَ كَثِيرَ الشَّعَرِ، فَسَمِعْتُهُ يَرْتَجِزُ بِكَلِمَاتِ ابْنِ رَوَاحَةَ، وَهْوَ يَنْقُلُ مِنَ التُّرَابِ يَقُولُ اللَّهُمَّ لَوْلاَ أَنْتَ مَا اهْتَدَيْنَا وَلاَ تَصَدَّقْنَا وَلاَ صَلَّيْنَا فَأَنْزِلَنْ سَكِينَةً عَلَيْنَا وَثَبِّتِ الأَقْدَامَ إِنْ لاَقَيْنَا إِنَّ الأُلَى قَدْ بَغَوْا عَلَيْنَا وَإِنْ أَرَادُوا فِتْنَةً أَبَيْنَا قَالَ ثُمَّ يَمُدُّ صَوْتَهُ بِآخِرِهَا.
Amesimulia Al-Baraa (رضي الله عنه): Wakati wa siku ya (Vita vya) Al-Ahzaab (makundi yaliyoshirikiana), na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaingia katika kazi ya kuchimba handaki, nilikuwa namwona akiutoa nje udongo wa handaki mpaka vumbi lake likanifanya nisiweze kuona tena ngozi ya tumbo lake. Na alikuwa mwenye nywele nyingi. Nikamsikia akisoma maneno ya Ibn Rawaahah huku akiwa amebeba udongo, akisema: “Ee Allaah! Bila ya Wewe, tusingehidika, wala tusingetoa swadaqa, wala tusingeswali. Basi Tuteremshie utulivu na Imarishe miguu yetu kama tutakabiliana na adui. Hakika wao wametufanyia dhulma na kama watataka kutufanyia fitnah, basi hatutokubali.” Halafu akawa anavuta sauti yake mwishoni mwake. [Al-Bukhaariy].
Uchimbaji wa Khandaq kuizunguka Madiynah ndio ilikuwa sababu ya Ushindi kwa Waislamu, kutokana na kuwazuia maadui wasiweze kuingia. Baada ya Ahzaab (makundi yaliyoshirikiana) kufika kwenye mipaka ya Madiynah walishindwa kuingia, na hapo wakaamua kuuzingira mji. Na zingiro hili liliendelea kwa muda wa wiki tatu, na ilipelekea hali hii kwa Waislam kupata maudhi, mashaka, kiu na njaa. Lakini Waislamu hawakukata tamaa na wala hawakujisalimisha kwa maadui zao, bali walivuta subira mpaka Allaah (سبحانه وتعالى) Akawajaalia ushindi dhidi ya maadui wao.
Vita vya Khandaq vilimalizika kwa kujiondoa kwao Ahzaab (makundi yaliyoshirikiana), hali iliyosababishwa na kupigwa na upepo mkali wa baridi. Na Waislamu wanaamini kuwa ushindi wao katika Vita vya Khandaq ulikuwa kwa sababu Allaah (سبحانه وتعالى)
Aliitingisha miili na nyoyo za Ahzaab, Akasambaratisha muungano wao kwa kutofautiana wenyewe kwa wenyewe. Akatia khofu kwenye nyoyo zao, na Akateremsha jeshi kutoka Kwake wasioonekana ambao ni Malaika. Na baada ya kumalizika Vita, Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaamrisha Swahaba zake kuelekea kwa Baniy Quraydhwah. Wakaenda na wakawazingira mpaka wakajisalimisha. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasimama kwa kumteua mtu waliyemridhia atoe hukumu, naye alikuwa Sa’ad Bin Muaadh (رضي الله عنه) ambae alikuwa mwenzao kabla ya Uislamu. Akatoa hukumu ya kuuwawa wapiganaji wao na kutawanywa wanawake na watoto wao, wakiwa watumwa kwa Waislamu. Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), alitoa amri ya kupitishwa hukumu hiyo.
Sababu Ya Kutokea Vita Hivi:
Sababu ya Vita hivi ni kutolewa kwa Mayahudi wa Baniy An-Nadhwiyr katika mji wa Madiynah, kiasi kwamba hasadi na chuki zilitawala katika nyoyo zao. Nayo ni katika mambo ambayo yaliwafanya wawe wanadhamiria kufanya uadui kwa Waislamu.
Na pia sababu ya Vita vya Khandaq ni kwamba Mayahudi wa Baniy Nadhwiyr walivunja ahadi yao pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na walifanya hila ya kutaka kumuua. Akawapelekea jeshi lake, likawazingira mpaka wakajisalimisha. Matokeo ya jambo hilo ni kudhamiria Mayahudi wa Baniy An-Nadhwiyr kulipiza kisasi kwa Waislamu. Wakaanza kushawishi makabila ya Kiarabu kuipiga Vita Madiynah. Waliowakubalia katika Waarabu ni kabila la Maquraysh, na wale wenzao akina Kinaanah (Wahabeshi), Kabila ya Ghatwfaan (Fazaarah, na Baniy Murrah, na Ashja’a), na wenzao ambao ni Baniy Asad, na Sulaym na wengineo. Ndio maana wakaitwa Ahzaab (makundi yaliyoshirikiana), kisha wakajiunga nao Mayahudi wa Baniy Quraydhwah, ambao walikuwa na ahadi ya amani kati yao na Waislamu.
[7] Nyoyo Zenye Maradhi:
(i) Nyoyo Zenye Maradhi: Rejea Suwrah Muhammad (47:20) kwenye maelezo na rejea mbalimbali. Na rejea pia Suwrah hii Al-Ahzaab (33:32), (33:60).
(ii) Moyo Uliopofuka: Rejea pia Al-Hajj (22:46) kwenye maelezo bayana.
(iii) Moyo Uliosalimika: Rejea pia Ash-Shu’araa (26:88-89) kwenye maelezo bayana.
[8] Kufuata Kigezo Cha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم):
Kufuata kigezo cha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kufuata Sunnah zake na hii ni waajib kwa Muislamu kama Anavyosema Allaah katika Aayah hii tukufu.
Na Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) amesema: “Mwenye kufuata kigezo chake, amefuata njia ya kumfikisha katika Utukufu wa Allaah, na hiyo ndio Njia Iliyonyooka. Na kigezo hicho kizuri hukifuata na kupata tawfiyq kila yule mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho, kwa sababu ya kuwa kwake na iymaan, khofu ya Allaah, kutaraji thawabu na khofu ya adhabu Yake, huyu hujihimiza kufuata kigezo cha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).” [Tafsiyr As-Sa’dy]
[11] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Aayah kuanzia hii namba (28) hadi (29), panaelezwa kuhusu wake wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na matukio yaliyotokea ambayo pia yanahusiana na Aayah za Suwrah At-Tahriym (66:1-5).
Bonyeza kiungo kifuatacho:
[12] Haramisho Kwa Wanawake Kulegeza Sauti Wanapoongea Na Wanaume:
Amrisho hili ni kwa wakeze Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na pia wanawake Waumini kuwa wanapoongea na wanaume, wasiwe wanaongea kwa sauti laini ya kupendezesha ili isije kusababisha fitnah kwa wanaume kuvutiwa na wanawake.
[15] Maana Ya Swalaah Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kwa Waja Wake Na Swalaah Ya Malaika Kwa Waja:
Swalaah ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa waja Wake ni Rehma na kuwasifia kwa Malaika. Na Swalaah ya Malaika kwa wanaadam ni kuwaombea duaa na maghfirah. Pia Rejea Al-Faatihah (1:1) kupata tofauti ya Jina na Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) Ar-Rahmaan na Ar-Rahiym
[16] Maamkizi Jannah (Peponi) Ni “Salaam” (Amani!):
Rejea Yaasiyn (36:58), Ar-Ra’d (13:24), Yuwnus (10:10), Ibraahiym (14:23), An-Nahl (16:32).
[19] Maana Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Na Malaika Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
Maana ya Allaah (سبحانه وتعالى) kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), ni kumsifia kwa Malaika, kumteremshia Rehma na Baraka, Fadhila n.k. Ama Malaika Wake kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), ni kumuombea kwa Allaah (سبحانه وتعالى) duaa Amghufurie na Amteremshie baraka.
Vipi Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
عن أَبي مسعودٍ البدري رضي الله عنه ، قَالَ : أتَانَا رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، وَنَحنُ في مَجْلِسِ سَعدِ بن عُبَادَةَ رضي الله عنه ، فَقَالَ لَهُ بَشْيرُ بْنُ سَعدٍ : أمَرَنَا الله تَعَالَى أنْ نُصَلِّي عَلَيْكَ يَا رَسُولَ اللهِ ، فَكَيْفَ نُصَلِّي عَلَيْكَ ؟ فَسَكَتَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم ، حَتَّى تَمَنَّيْنَا أنَّهُ لَمْ يَسْأَلْهُ ، ثُمَّ قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( قُولُوا : اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ ، وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ ، كَمَا صَلَّيْتَ عَلَى آلِ إبْرَاهِيمَ ، وَبَارِكْ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ ، كَمَا بَارَكْت عَلَى آلِ إبْرَاهِيمَ ، إنَّكَ حَمِيدٌ مَجِيدٌ ، وَالسَّلاَمُ كَمَا قَدْ عَلِمْتُمْ )) . رواه مسلم .
Amesimulia Abuu Mas'uwd Al-Badriy (رضي الله عنه): Alitujia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na sisi tulikuwa katika majlisi ya Sa'ad bin 'Ubaadah (رضي الله عنه). Bashiyr bin Sa'ad akamwambia: Allaah Ametuamrisha tukuswalie ee Rasuli wa Allaah. Je, vipi tukuswalie? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akanyamaza mpaka tukatamani kwamba asingelimuuliza. Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Semeni:
اللَّهمَّ صلِّ عَلى مُحَمَّدٍ، وَعَلى آلِ مُحمَّدٍ، كما صليْتَ على آل إبْراهِيم، وَبارِكْ عَلى مُحَمَّد، وعَلى آلِ مُحمَّد، كما بَاركْتَ عَلى آل إبْراهِيم، إنكَ حمِيدٌ مجِيدٌ،
Allaahumma Swalli 'alaa Muhammadin wa 'alaa aali Muhammadin kamaa Swallayta 'alaa aali Ibraahiym, wa Baarik 'alaa Muhammadin wa 'alaa aali Muhammadin kama Baarakta 'alaa aali Ibraahiym Innaka Hamiydun-Majiyd. Na salaam kama mlivyofundishwa.” [Muslim]
Fadhila Za Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ni katika ibaada tukufu yenye fadhila adhimu kwa kuwa ni ibaada Aliyojihusisha nayo Allaah (سبحانه وتعالى) na Malaika Wake. Na fadhila kadhaa zimethibiti za kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Mojawapo ya fadhila ni kwamba, ukimswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) mara moja, Allaah (سبحانه وتعالى) Anakuswalia mara kumi kwa Hadiyth ifuatayo:
عنْ عبد اللَّه بن عمرو بن العاص رضي اللَّه عنْهُمَا أنَّهُ سمِع رسُول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقُولُ: ((مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاَةً، صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عشْراً)) رواهُ مسلم
Amesimulia 'Abdullaah bin 'Amru bin Al-‘Aasw (رضي الله عنهما) kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Atakayeniswalia mara moja, Allaah Atamswalia mara kumi.” [Muslim]
[20] Hijaab Na Masharti Yake:
(i) Jilbaab liwe refu la kukufunika mwili mzima mpaka miguu, na kama halikufunika miguu basi mwanamke avae soksi. (ii) Jilbaab liwe pana na sio lenye kuonyesha umbo, yaani lisiwe lenye kubana popote mwilini. (iii) Jilbaab liwe zito na si jepesi la kuonyesha mwili. (iv) Jilbaab lisiwe na marembo yoyote yale ya kuvutia. (v) Jilbaab halitakiwi lifanane na mavazi ya makafiri. (vi) Jilbaab halitakiwi liwe ni katika mavazi ya fakhari. (vii) Wanawake wasivae nguo zinazofanana na nguo za kiume. (viii) Nguo zote anazovaa mwanamke zisiwe na manukato.
Rejea An-Nuwr (24:31).
[22] Ada Ya Makafiri Kuuliza Qiyaamah Kitatokea Lini Na Kuhimiza Adhabu:
Rejea Al-An’aam (6:158), Al-A’raaf (7:187), An-Naazi’aat (79:42), Al-Mulk (67:25), Ash-Shuwraa (42:18).
Na wakihimiza adhabu: Rejea Al-Hajj (22:47), Swaad (38:16), Al-Anfaal (8:32-33).
[23] Tuhuma Alizopachikwa Nabiy Muwsaa :(عليه السّلام)
Maelezo yamethibiti katika Hadiyth:
حَدَّثَنِي إِسْحَاقُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا رَوْحُ بْنُ عُبَادَةَ، حَدَّثَنَا عَوْفٌ، عَنِ الْحَسَنِ، وَمُحَمَّدٍ، وَخِلاَسٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " إِنَّ مُوسَى كَانَ رَجُلاً حَيِيًّا سِتِّيرًا، لاَ يُرَى مِنْ جِلْدِهِ شَىْءٌ، اسْتِحْيَاءً مِنْهُ، فَآذَاهُ مَنْ آذَاهُ مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ، فَقَالُوا مَا يَسْتَتِرُ هَذَا التَّسَتُّرَ إِلاَّ مِنْ عَيْبٍ بِجِلْدِهِ، إِمَّا بَرَصٌ وَإِمَّا أُدْرَةٌ وَإِمَّا آفَةٌ. وَإِنَّ اللَّهَ أَرَادَ أَنْ يُبَرِّئَهُ مِمَّا قَالُوا لِمُوسَى فَخَلاَ يَوْمًا وَحْدَهُ فَوَضَعَ ثِيَابَهُ عَلَى الْحَجَرِ ثُمَّ اغْتَسَلَ، فَلَمَّا فَرَغَ أَقْبَلَ إِلَى ثِيَابِهِ لِيَأْخُذَهَا، وَإِنَّ الْحَجَرَ عَدَا بِثَوْبِهِ، فَأَخَذَ مُوسَى عَصَاهُ وَطَلَبَ الْحَجَرَ، فَجَعَلَ يَقُولُ ثَوْبِي حَجَرُ، ثَوْبِي حَجَرُ، حَتَّى انْتَهَى إِلَى مَلإٍ مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ، فَرَأَوْهُ عُرْيَانًا أَحْسَنَ مَا خَلَقَ اللَّهُ، وَأَبْرَأَهُ مِمَّا يَقُولُونَ، وَقَامَ الْحَجَرُ فَأَخَذَ ثَوْبَهُ فَلَبِسَهُ، وَطَفِقَ بِالْحَجَرِ ضَرْبًا بِعَصَاهُ، فَوَاللَّهِ إِنَّ بِالْحَجَرِ لَنَدَبًا مِنْ أَثَرِ ضَرْبِهِ ثَلاَثًا أَوْ أَرْبَعًا أَوْ خَمْسًا، فَذَلِكَ قَوْلُهُ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لاَ تَكُونُوا كَالَّذِينَ آذَوْا مُوسَى فَبَرَّأَهُ اللَّهُ مِمَّا قَالُوا وَكَانَ عِنْدَ اللَّهِ وَجِيهًا "
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Muwsaa alikuwa ni mtu mwenye haya mno na anayejisitiri sana. Ngozi yake haionekani kabisa kwa ajili ya haya yake. Mmoja miongoni mwa Bani Israaiyl alimuudhi kwa kumwambia: Anajifinika hivi kwa sababu ya ila ya ngozi yake, ima ni kwa sababu ya ukoma au ngiri ya korodani au aibu nyenginezo. Allaah Alitaka kumtoa katika hayo waliyokuwa wakiyasema. Kwa hiyo, siku moja Muwsaa alipokuwa peke yake, alivua nguo zake, akaziweka juu ya jiwe na akaanza kuoga. Alipomaliza kuoga, alitembea kuzielekea nguo zake ili kuzichukua, lakini jiwe hilo lilichukua nguo zake na kukimbia nazo. Muwsaa alichukua fimbo yake na kulikimbiza hilo jiwe huku akisema: Ewe jiwe! Nipatie nguo zangu! Mpaka akafika kwenye kikundi cha Bani Israaiyl waliomuona akiwa uchi, na kumuona kuwa ni kiumbe mzuri mno miongoni mwa walioumbwa na Allaah. Hivyo, Allaah Akamtakasa kwa waliyokuwa wakimtuhumu nayo. Jiwe lilisimama hapo, na Muwsaa alichukua na kuvaa nguo zake na akaanza kulipiga kichapo hilo jiwe kwa fimbo yake. Naapa kwa Allaah! Jiwe hilo hadi sasa lina alama ya kichapo, alama tatu au nne au tano. Na hiyo ndiyo Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ آذَوْا مُوسَىٰ فَبَرَّأَهُ اللَّـهُ مِمَّا قَالُوا ۚ وَكَانَ عِندَ اللَّـهِ وَجِيهًا ﴿٦٩﴾
“Enyi walioamini! Msiwe kama wale waliomuudhi Muwsaa, lakini Allaah Alimtoa tuhumani kutokana na yale waliyoyasema. Na alikuwa mbele ya Allaah mwenye kuheshimika.” [Al-Ahzaab (33:69)]
[24] Amana:
Kutimiza amana ni miongoni mwa sifa zitakazompatia Muislamu Jannah ya Firdaws kama zilivyotajwa katika Suwrah: Al-Muuminuwn (23: 1-11), Al-Ma’aarij (70:32).
Na maudhui hii ya amana ni pana mno, na kuna Hadiyth mbalimbali zinazotaja jambo hili la amana. Na ‘Ulamaa pia wametaja maana na tafsiri mbalimbali kuhusu maana yake.
Rejea Alhidaaya.com katika viungo vifuatavo kupata faida tele:
Na miongoni mwa amana ni kutekeleza ahadi, kurudisha kitu alichokabidhiwa mtu, kulipa alichokopa, kutokufanya khiyana na kadhaalika. Mfano ni Hadiyth:
Samurah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Rudisha amana kwa aliyekuaminisha na wala usimfanyie khiyana aliyekukhini.” [Ahmad, Swahiyh Abiy Daawuwd (3535), As-Silsilah Asw-Swahiyhah (423)].
Na kutokutimiza amana ni miongoni mwa alama za Qiyaamah kwa kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mtu aliyemuuliza lini Qiyaamah kitasimama kama ilivyo katika Hadiyth ifuatayo:
عن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : بَيْنَمَا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم في مَجْلِسٍ يُحَدِّثُ القَومَ ، جَاءَ أَعْرَابِيٌّ فَقَالَ : مَتَى السَّاعَةُ ؟ فَمَضَى رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم يُحَدِّثُ ، فَقالَ بَعْضُ القَومِ : سَمِعَ مَا قَالَ فَكَرِهَ مَا قَالَ ، وَقَالَ بَعْضُهُمْ : بَلْ لَمْ يَسْمَعْ ، حَتَّى إذَا قَضَى حَدِيثَهُ قالَ : أيْنَ السَّائِلُ عَنِ السَّاعَةِ ؟ )) قال : هَا أنا يَا رسُولَ اللهِ . قال : (( إذَا ضُيِّعَتِ الأَمَانَةُ فَانْتَظِرِ السَّاعَةَ )) قال : كَيفَ إضَاعَتُهَا ؟ قال : (( إذَا وُسِّدَ الأَمْرُ إلى غَيْرِ أَهْلِهِ فَانْتَظِرِ السَّاعَةَ )) . رواه البخاري .
Amesimulia Abuu Huraiyrah (رضي الله عنه): Alipokuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) anahotubia kikao cha watu, mara akaja mbedui na kuuliza: Je, Qiyaamah kitakuwa lini? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaendelea na mazungumzo yake. Hapo wakasema baadhi ya watu: Amesikia alichoulizwa, lakini akachukia kukatizwa. Na wengine wakasema: Bali hajasikia. Mpaka alipomaliza mazungumzo yake, akasema: "Yu wapi muulizaji kuhusu Qiyaamah?" Akajibu: Nipo hapa, ee Rasuli wa Allaah. Akasema: "Inapopotezwa amana (kukawa na khiyana) basi ngojeeni Qiyaamah." Akaulizwa: Na itapotea vipi? Akasema: "Pindi uongozi unapopatiwa watu wasio stahiki basi ngojeeni Qiyaamah." [Al-Bukhaariy]
Na amana pia inaingia katika kutekeleza majukumu ya mtu aliyokabidhiwa, kama kuchunga kilichokuwa chini ya ulezi au jukumu lake. Hadiyth ifuatayo inaashiria hili:
عَنْ ابْنِ عُمَرَ (رضي الله عنهما) عَنْ النَّبِيِّ (صلى الله عليه و آله وسلم) قَالَ: ((كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ، وَالأمِيرُ رَاعٍ، وَالرَّجُلُ رَاعٍ عَلَى أَهْلِ بَيْتِهِ، وَالْمَرْأَةُ رَاعِيَةٌ عَلَى بَيْتِ زَوْجِهَا وَوَلَدِهِ، فَكُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ)) متفق عليه
Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله عنهما): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nyote ni wachunga na kila mmoja wenu ataulizwa kuhusu alichokichunga. Kiongozi ni mchunga, na mume ni mchunga juu ya mkewe na mke ni mchunga juu ya nyumba ya mumewe na watoto wake. Kwa hivyo nyote ni wachunga na kila mmoja wenu ataulizwa kuhusu alichokichunga.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
سَبَاء
034-Saba-a
034-Saba-a: Utangulizi Wa Suwrah [251]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَلَهُ الْحَمْدُ فِي الْآخِرَةِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ ﴿١﴾
1. AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Ambaye Ni Vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini, na Himidi ni Zake katika Aakhirah, Naye Ni Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا ۚ وَهُوَ الرَّحِيمُ الْغَفُورُ ﴿٢﴾
2. Anajua yanayoingia ardhini, na yanayotoka humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni, na yanayopanda huko, Naye Ndiye Mwenye Kurehemu, Mwingi wa Kughufuria.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَأْتِينَا السَّاعَةُ ۖ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتَأْتِيَنَّكُمْ عَالِمِ الْغَيْبِ ۖ لَا يَعْزُبُ عَنْهُ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَلَا أَصْغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرُ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٣﴾
3. Na wale waliokufuru wakasema: Saa haitotufikia! Sema: Sivyo hivyo! Naapa kwa Rabb wangu! Bila shaka itakufikieni, Mjuzi wa ghaibu. Hakuna kinachofichika Kwake hata chenye uzito wa chembe (kama atomu) mbinguni wala ardhini, wala kidogo zaidi kuliko hicho, wala kikubwa zaidi isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha.[1]
لِّيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ۚ أُولَـٰئِكَ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ ﴿٤﴾
4. Ili Awalipe wale walioamini na wakatenda mema. Hao watapata maghfirah na riziki tukufu.
وَالَّذِينَ سَعَوْا فِي آيَاتِنَا مُعَاجِزِينَ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مِّن رِّجْزٍ أَلِيمٌ ﴿٥﴾
5. Na wale waliofanya bidii katika Aayaat (na Ishara) Zetu watake kuzibatilisha, hao watapata adhabu mbaya ya kufadhaika, iumizayo.
وَيَرَى الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ الَّذِي أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ هُوَ الْحَقَّ وَيَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ ﴿٦﴾
6. Na wale waliopewa ilimu wanaona kuwa yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako ndio haki, na yanaongoza kwenye Njia ya Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا هَلْ نَدُلُّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ يُنَبِّئُكُمْ إِذَا مُزِّقْتُمْ كُلَّ مُمَزَّقٍ إِنَّكُمْ لَفِي خَلْقٍ جَدِيدٍ ﴿٧﴾
7. Na wale waliokufuru wakasema: Je, tukuelekezeni kwa mtu anayekujulisheni kwamba mtakapomomonyolewa mkawa vumbi lililotawanyika mbali, mtakuwa katika umbo jipya?[2]
أَفْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَم بِهِ جِنَّةٌ ۗ بَلِ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ فِي الْعَذَابِ وَالضَّلَالِ الْبَعِيدِ ﴿٨﴾
8. Je, amemtungia Allaah uongo, au ana wazimu?[3] Bali wale wasioamini Aakhirah watakuwa katika adhabu na upotofu wa mbali.
أَفَلَمْ يَرَوْا إِلَىٰ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۚ إِن نَّشَأْ نَخْسِفْ بِهِمُ الْأَرْضَ أَوْ نُسْقِطْ عَلَيْهِمْ كِسَفًا مِّنَ السَّمَاءِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّكُلِّ عَبْدٍ مُّنِيبٍ ﴿٩﴾
9. Je, kwani hawaoni yale yaliyoko mbele yao na yale yaliyo nyuma yao ya mbingu na ardhi? Tungelitaka, Tungeliwadidimiza ardhini, au Tungeliwaangushia juu yao vipande vya mbingu. Hakika katika hayo kuna Aayah (Ishara, Mazingatio) kwa kila mja anayetubia mara kwa mara (kwa Allaah).
وَلَقَدْ آتَيْنَا دَاوُودَ مِنَّا فَضْلًا ۖ يَا جِبَالُ أَوِّبِي مَعَهُ وَالطَّيْرَ ۖ وَأَلَنَّا لَهُ الْحَدِيدَ ﴿١٠﴾
10. Na kwa yakini Tulimpa Daawuwd Fadhila kutoka Kwetu, (Tukasema): Ee majabali! Rejesheni kumsabbih (Allaah) pamoja naye na ndege pia. Na Tukamlainishia chuma.[4]
أَنِ اعْمَلْ سَابِغَاتٍ وَقَدِّرْ فِي السَّرْدِ ۖ وَاعْمَلُوا صَالِحًا ۖ إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿١١﴾
11. Na kwamba: Tengeneza mavazi ya chuma mapana, na kadiria sawasawa katika kuunganisha daraya, na tendeni mema. Hakika Mimi Ni Mwenye Kuona myatendayo.
وَلِسُلَيْمَانَ الرِّيحَ غُدُوُّهَا شَهْرٌ وَرَوَاحُهَا شَهْرٌ ۖ وَأَسَلْنَا لَهُ عَيْنَ الْقِطْرِ ۖ وَمِنَ الْجِنِّ مَن يَعْمَلُ بَيْنَ يَدَيْهِ بِإِذْنِ رَبِّهِ ۖ وَمَن يَزِغْ مِنْهُمْ عَنْ أَمْرِنَا نُذِقْهُ مِنْ عَذَابِ السَّعِيرِ ﴿١٢﴾
12. Na Sulaymaan (Tulimtiishia) upepo. Safari yake ya asubuhi ni (mwendo wa) mwezi, na safari yake ya jioni ni (mwendo wa) mwezi, na Tukamtiririzia chemchemu ya shaba. Na (Tulimtiishia pia) kati ya majini wanaofanya kazi mbele yake kwa Idhini ya Rabb wake. Na yeyote atakayezikengeuka Amri Zetu, Tunamuonjesha adhabu ya moto uliowashwa vikali mno.
يَعْمَلُونَ لَهُ مَا يَشَاءُ مِن مَّحَارِيبَ وَتَمَاثِيلَ وَجِفَانٍ كَالْجَوَابِ وَقُدُورٍ رَّاسِيَاتٍ ۚ اعْمَلُوا آلَ دَاوُودَ شُكْرًا ۚ وَقَلِيلٌ مِّنْ عِبَادِيَ الشَّكُورُ ﴿١٣﴾
13. Wanamfanyia kazi atakayo; (kujenga) ngome ndefu za fakhari na tasawiri, na madeste makubwa kama mahodhi na masufuria makubwa yaliyothibiti imara. (Tukasema): Tendeni enyi familia ya Daawuwd kwa shukurani! Na wachache miongoni mwa Waja Wangu ni wenye kushukuru.[5]
فَلَمَّا قَضَيْنَا عَلَيْهِ الْمَوْتَ مَا دَلَّهُمْ عَلَىٰ مَوْتِهِ إِلَّا دَابَّةُ الْأَرْضِ تَأْكُلُ مِنسَأَتَهُ ۖ فَلَمَّا خَرَّ تَبَيَّنَتِ الْجِنُّ أَن لَّوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ الْغَيْبَ مَا لَبِثُوا فِي الْعَذَابِ الْمُهِينِ ﴿١٤﴾
14. Na Tulipomkidhia mauti, hakuna kilichowajulisha kifo chake isipokuwa mdudu wa ardhi akila fimbo yake. Kisha alipoanguka, ikawabainikia majini kwamba lau wangelikuwa wanajua ya ghaibu, basi wasingebakia katika adhabu ya kudhalilisha.
لَقَدْ كَانَ لِسَبَإٍ فِي مَسْكَنِهِمْ آيَةٌ ۖ جَنَّتَانِ عَن يَمِينٍ وَشِمَالٍ ۖ كُلُوا مِن رِّزْقِ رَبِّكُمْ وَاشْكُرُوا لَهُ ۚ بَلْدَةٌ طَيِّبَةٌ وَرَبٌّ غَفُورٌ ﴿١٥﴾
15. Kwa yakini ilikuwa ni Aayah (Ishara) kwa (watu wa) Saba-a katika masikani zao. Bustani mbili; kulia na kushoto. (Wakaambiwa): Kuleni katika riziki ya Rabb wenu na mshukuruni. Mji mzuri na Rabb Ambaye Ni Mwingi wa Kughufuria.[6]
فَأَعْرَضُوا فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ سَيْلَ الْعَرِمِ وَبَدَّلْنَاهُم بِجَنَّتَيْهِمْ جَنَّتَيْنِ ذَوَاتَيْ أُكُلٍ خَمْطٍ وَأَثْلٍ وَشَيْءٍ مِّن سِدْرٍ قَلِيلٍ ﴿١٦﴾
16. Lakini wakakengeuka. Basi Tukawapelekea mafuriko ya mabwawa, na Tukawabadilishia badala ya bustani zao mbili, kwa bustani mbili nyinginezo zenye matunda machungu mno, na mivinje, na baadhi ya mikunazi kidogo.
ذَٰلِكَ جَزَيْنَاهُم بِمَا كَفَرُوا ۖ وَهَلْ نُجَازِي إِلَّا الْكَفُورَ ﴿١٧﴾
17. Hayo Tuliwalipa kwa vile walivyokufuru. Na Hatuadhibu isipokuwa anayekufuru.
وَجَعَلْنَا بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ الْقُرَى الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا قُرًى ظَاهِرَةً وَقَدَّرْنَا فِيهَا السَّيْرَ ۖ سِيرُوا فِيهَا لَيَالِيَ وَأَيَّامًا آمِنِينَ ﴿١٨﴾
18. Na Tukaweka baina yao na baina ya miji Tuliyoibariki, miji mingine iliyo karibu karibu, na Tukakadiria humo vituo vya safari. (Tukasema): Safirini humo usiku na mchana kwa amani.
فَقَالُوا رَبَّنَا بَاعِدْ بَيْنَ أَسْفَارِنَا وَظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ فَجَعَلْنَاهُمْ أَحَادِيثَ وَمَزَّقْنَاهُمْ كُلَّ مُمَزَّقٍ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ ﴿١٩﴾
19. Wakasema: Rabb wetu! Baidisha baina ya safari zetu. Na wakazidhulumu nafsi zao. Basi Tukawafanya kuwa ni simulizi, na Tukawafarikisha na kuwatawanyatawanya kabisa. Hakika katika hayo bila shaka kuna Aayaat (Ishara, Mazingatio) kwa kila mwingi wa kusubiri na mwingi wa kushukuru.
وَلَقَدْ صَدَّقَ عَلَيْهِمْ إِبْلِيسُ ظَنَّهُ فَاتَّبَعُوهُ إِلَّا فَرِيقًا مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢٠﴾
20. Na kwa yakini Ibliys alisadikisha dhana yake juu yao, basi walimfuata isipokuwa kundi miongoni mwa Waumini.
وَمَا كَانَ لَهُ عَلَيْهِم مِّن سُلْطَانٍ إِلَّا لِنَعْلَمَ مَن يُؤْمِنُ بِالْآخِرَةِ مِمَّنْ هُوَ مِنْهَا فِي شَكٍّ ۗ وَرَبُّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَفِيظٌ ﴿٢١﴾
21. Na yeye (Ibliys) hakuwa ana madaraka yoyote juu yao isipokuwa ili Tujue ni nani yule anayeamini Aakhirah na nani yule anayeitilia shaka. Na Rabb wako Ni Mwenye Kuhifadhi kila kitu.
قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ ۖ لَا يَمْلِكُونَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَمَا لَهُمْ فِيهِمَا مِن شِرْكٍ وَمَا لَهُ مِنْهُم مِّن ظَهِيرٍ ﴿٢٢﴾
22. Sema: Ombeni wale mnaodai kwa dhana (ni waabudiwa) badala ya Allaah, hawamiliki hata uzito wa chembe (kama atomu) mbinguni wala ardhini, na wala hawana humo ushirika Naye, na wala Yeye (Allaah) Hana msaidizi miongoni mwao.
وَلَا تَنفَعُ الشَّفَاعَةُ عِندَهُ إِلَّا لِمَنْ أَذِنَ لَهُ ۚ حَتَّىٰ إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ ۖ قَالُوا الْحَقَّ ۖ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ ﴿٢٣﴾
23. Na wala haitofaa shafaa’ah (uombezi) mbele Yake isipokuwa kwa yule Aliyempa idhini. Mpaka litakapoondolewa fazaiko nyoyoni mwao watasema: Amesema nini Rabb wenu? Watasema: Ya haki, Naye Ni Mwenye ‘Uluwa Uliotukuka, Mkubwa Kabisa.
قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ قُلِ اللَّـهُ ۖ وَإِنَّا أَوْ إِيَّاكُمْ لَعَلَىٰ هُدًى أَوْ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٢٤﴾
24. Sema: Nani yule anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini? Sema: Ni Allaah! Na hakika ima sisi au nyinyi, bila shaka tuko juu ya uongofu au katika upotofu bayana.[7]
قُل لَّا تُسْأَلُونَ عَمَّا أَجْرَمْنَا وَلَا نُسْأَلُ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٢٥﴾
25. Sema: Hamtoulizwa kuhusu ule uhalifu tulioufanya, na wala hatutoulizwa kwa yale mnayoyatenda.
قُلْ يَجْمَعُ بَيْنَنَا رَبُّنَا ثُمَّ يَفْتَحُ بَيْنَنَا بِالْحَقِّ وَهُوَ الْفَتَّاحُ الْعَلِيمُ ﴿٢٦﴾
26. Sema: Rabb wetu Atatukusanya, kisha Atahukumu baina yetu kwa haki, Naye Ndiye Hakimu, Mjuzi wa yote.
قُلْ أَرُونِيَ الَّذِينَ أَلْحَقْتُم بِهِ شُرَكَاءَ ۖ كَلَّا ۚ بَلْ هُوَ اللَّـهُ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٧﴾
27. Sema: Nionyesheni wale mliowaunganisha Naye kuwa washirika. Laa hasha! Bali Yeye Ndiye Allaah Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢٨﴾
28. Na Hatukukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa kwa watu wote uwe mbashiriaji na muonyaji, lakini watu wengi hawajui.[8]
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٢٩﴾
29. Na wanasema: Ni lini hiyo ahadi (ya Qiyaamah), mkiwa ni wasemao kweli?[9]
قُل لَّكُم مِّيعَادُ يَوْمٍ لَّا تَسْتَأْخِرُونَ عَنْهُ سَاعَةً وَلَا تَسْتَقْدِمُونَ ﴿٣٠﴾
30. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Mnayo miadi ya Siku ambayo hamtoiakhirisha saa, na wala hamtakadimisha.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَن نُّؤْمِنَ بِهَـٰذَا الْقُرْآنِ وَلَا بِالَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ ۗ وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الظَّالِمُونَ مَوْقُوفُونَ عِندَ رَبِّهِمْ يَرْجِعُ بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ الْقَوْلَ يَقُولُ الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا لِلَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا لَوْلَا أَنتُمْ لَكُنَّا مُؤْمِنِينَ ﴿٣١﴾
31. Na wale waliokufuru wakasema: Hatutoiamini Qur-aan hii, na wala yale yaliyokuwa kabla yake. Na lau ungeliona pale madhalimu watakaposimamishwa mbele ya Rabb wao, wakirejesheana wenyewe kwa wenyewe maneno. Watasema wale waliodhoofishwa kuwaambia wale waliotakabari: Lau isingelikuwa nyinyi, bila shaka tungelikuwa Waumini.
قَالَ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا لِلَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا أَنَحْنُ صَدَدْنَاكُمْ عَنِ الْهُدَىٰ بَعْدَ إِذْ جَاءَكُم ۖ بَلْ كُنتُم مُّجْرِمِينَ ﴿٣٢﴾
32. Na watasema wale waliotakabari kuwaambia wale waliodhoofishwa: Je, kwani sisi ndio tuliokuzuieni na mwongozo baada ya kukujieni? Bali nyinyi mlikuwa wahalifu.
وَقَالَ الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا لِلَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا بَلْ مَكْرُ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ إِذْ تَأْمُرُونَنَا أَن نَّكْفُرَ بِاللَّـهِ وَنَجْعَلَ لَهُ أَندَادًا ۚ وَأَسَرُّوا النَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُا الْعَذَابَ وَجَعَلْنَا الْأَغْلَالَ فِي أَعْنَاقِ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ هَلْ يُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٣٣﴾
33. Na watasema waliodhoofishwa kuwaambia wale waliotakabari: Bali ni njama (zenu) za usiku na mchana, mlipotuamrisha tumkufuru Allaah na tumfanyie wa kumsawazisha Naye. Na wataficha (au watafichua) majuto watakapoiona adhabu. Na Tutaweka minyororo shingoni mwa wale waliokufuru. Je, wanalipwa isipokuwa yale waliyokuwa wakiyatenda?
وَمَا أَرْسَلْنَا فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتْرَفُوهَا إِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ كَافِرُونَ ﴿٣٤﴾
34. Na Hatukupeleka katika mji wowote ule mwonyaji yeyote isipokuwa walisema wastareheshwa wake (wa mji) kwa anasa za dunia: Hakika sisi kwa yale mliotumwa nayo ni wenye kuyakanusha.
وَقَالُوا نَحْنُ أَكْثَرُ أَمْوَالًا وَأَوْلَادًا وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ ﴿٣٥﴾
35. Na wakasema: Sisi tuna mali nyingi zaidi na watoto, na sisi hatutaadhibiwa.
قُلْ إِنَّ رَبِّي يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٦﴾
36. Sema: Hakika Rabb wangu Anamkunjulia riziki Amtakaye na Humkadiria kwa kipimo (Amtakaye), lakini watu wengi hawajui.
وَمَا أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُم بِالَّتِي تُقَرِّبُكُمْ عِندَنَا زُلْفَىٰ إِلَّا مَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ جَزَاءُ الضِّعْفِ بِمَا عَمِلُوا وَهُمْ فِي الْغُرُفَاتِ آمِنُونَ ﴿٣٧﴾
37. Na si mali zenu wala watoto wenu ambavyo vitakukurubisheni Kwetu muwe karibu isipokuwa yule aliyeamini na akatenda mema, basi hao watapata malipo maradufu kutokana na yale waliyoyatenda, nao watakuwa katika maghorofa (Jannah) wenye amani.
وَالَّذِينَ يَسْعَوْنَ فِي آيَاتِنَا مُعَاجِزِينَ أُولَـٰئِكَ فِي الْعَذَابِ مُحْضَرُونَ ﴿٣٨﴾
38. Na wale wanaofanya bidii katika Aayaat (na Ishara) Zetu watake kuzibatilisha, hao watahudhurishwa kwenye adhabu.
قُلْ إِنَّ رَبِّي يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَيَقْدِرُ لَهُ ۚ وَمَا أَنفَقْتُم مِّن شَيْءٍ فَهُوَ يُخْلِفُهُ ۖ وَهُوَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ ﴿٣٩﴾
39. Sema: Hakika Rabb wangu Anamkunjulia riziki Amtakaye kati ya Waja Wake na Humkadiria kwa kipimo (Amtakaye). Na kitu chochote mtoacho, basi Yeye Atakilipa, Naye Ni Mbora wa wenye kuruzuku.
وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ يَقُولُ لِلْمَلَائِكَةِ أَهَـٰؤُلَاءِ إِيَّاكُمْ كَانُوا يَعْبُدُونَ ﴿٤٠﴾
40. Na Siku Atakayowakusanya wote, kisha Atawaambia Malaika: Je, hawa ndio waliokuwa wakikuabuduni?
قَالُوا سُبْحَانَكَ أَنتَ وَلِيُّنَا مِن دُونِهِم ۖ بَلْ كَانُوا يَعْبُدُونَ الْجِنَّ ۖ أَكْثَرُهُم بِهِم مُّؤْمِنُونَ ﴿٤١﴾
41. Watasema: Subhaanak! (Utakasifu ni Wako). Wewe Ni Waliyy[10] wetu, sio hao! Bali walikuwa wakiabudu majini, wengi wao wakiwaamini.
فَالْيَوْمَ لَا يَمْلِكُ بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ نَّفْعًا وَلَا ضَرًّا وَنَقُولُ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذُوقُوا عَذَابَ النَّارِ الَّتِي كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ ﴿٤٢﴾
42. Basi leo hawatoweza baadhi yenu kuwapatia wenziwenu manufaa yoyote na wala madhara yoyote, na Tutawaambia wale waliodhulumu: Onjeni adhabu ya moto ambao mlikuwa mkiukadhibisha.
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ قَالُوا مَا هَـٰذَا إِلَّا رَجُلٌ يُرِيدُ أَن يَصُدَّكُمْ عَمَّا كَانَ يَعْبُدُ آبَاؤُكُمْ وَقَالُوا مَا هَـٰذَا إِلَّا إِفْكٌ مُّفْتَرًى ۚ وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿٤٣﴾
43. Na wanaposomewa Aayaat Zetu bayana, husema: Huyu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) si chochote isipokuwa mtu anataka akuzuieni na yale waliyokuwa wakiyaabudu baba zenu. Na husema: Hii (Qur-aan) si chochote isipokuwa uzushi uliotungwa. Na wale waliokufuru wakasema kuhusu haki ilipowajia: Hii si chochote isipokuwa ni sihiri bayana.[11]
وَمَا آتَيْنَاهُم مِّن كُتُبٍ يَدْرُسُونَهَا ۖ وَمَا أَرْسَلْنَا إِلَيْهِمْ قَبْلَكَ مِن نَّذِيرٍ ﴿٤٤﴾
44. Na wala Hatukuwapa kitabu chochote wakisomacho, na wala Hatukuwapelekea kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) mwonyaji yeyote.
وَكَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَمَا بَلَغُوا مِعْشَارَ مَا آتَيْنَاهُمْ فَكَذَّبُوا رُسُلِي ۖ فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ ﴿٤٥﴾
45. Na walikadhibisha wale wa kabla yao, na (hawa Maquraysh) hawakufikia sehemu moja ya kumi katika yale Tuliyowapa[12] kisha wakakadhibisha Rusuli Wangu. Basi kulikuwa vipi Kukana Kwangu!
قُلْ إِنَّمَا أَعِظُكُم بِوَاحِدَةٍ ۖ أَن تَقُومُوا لِلَّـهِ مَثْنَىٰ وَفُرَادَىٰ ثُمَّ تَتَفَكَّرُوا ۚ مَا بِصَاحِبِكُم مِّن جِنَّةٍ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا نَذِيرٌ لَّكُم بَيْنَ يَدَيْ عَذَابٍ شَدِيدٍ ﴿٤٦﴾
46. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika nakuwaidhini kwa jambo moja tu! Msimame kwa ajili ya Allaah wawili wawili, au mmoja mmoja kisha mtafakari. Sahibu yenu si mwendawazimu! Yeye si chochote isipokuwa mwonyaji kwenu, kabla ya kufika adhabu kali.
قُلْ مَا سَأَلْتُكُم مِّنْ أَجْرٍ فَهُوَ لَكُمْ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى اللَّـهِ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿٤٧﴾
47. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ujira wowote kama nimekuombeni basi huo ni wenu. Sina ujira ila kwa Allaah tu. Naye juu ya kila kitu Ni Shahidi.
قُلْ إِنَّ رَبِّي يَقْذِفُ بِالْحَقِّ عَلَّامُ الْغُيُوبِ ﴿٤٨﴾
48. Sema: Hakika Rabb wangu Anateremsha haki, Ni Mjuzi Mno wa ghaibu.
قُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَمَا يُبْدِئُ الْبَاطِلُ وَمَا يُعِيدُ ﴿٤٩﴾
49. Sema: Haki imekuja, na ubatilifu hausimamishi (tena chochote), na wala haurudishi (kitu).[13]
قُلْ إِن ضَلَلْتُ فَإِنَّمَا أَضِلُّ عَلَىٰ نَفْسِي ۖ وَإِنِ اهْتَدَيْتُ فَبِمَا يُوحِي إِلَيَّ رَبِّي ۚ إِنَّهُ سَمِيعٌ قَرِيبٌ ﴿٥٠﴾
50. Sema: Ikiwa nimepotoka, basi hakika nimepotoka kwa khasara ya nafsi yangu, na ikiwa nimehidika, basi ni kwa yale Aliyonifunulia Wahy Rabb wangu. Hakika Yeye Ni Mwenye Kusikia yote, Yu Karibu.
وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ فَزِعُوا فَلَا فَوْتَ وَأُخِذُوا مِن مَّكَانٍ قَرِيبٍ ﴿٥١﴾
51. Na lau ungeliona watakapofazaika kwa khofu, basi hakuna kukwepa, na watachukuliwa kutoka mahali pa karibu.
وَقَالُوا آمَنَّا بِهِ وَأَنَّىٰ لَهُمُ التَّنَاوُشُ مِن مَّكَانٍ بَعِيدٍ ﴿٥٢﴾
52. Na watasema: (Sasa) Tumemwamini Allaah! Lakini wataweza wapi kuipata (imaan) kutoka mahali mbali?
وَقَدْ كَفَرُوا بِهِ مِن قَبْلُ ۖ وَيَقْذِفُونَ بِالْغَيْبِ مِن مَّكَانٍ بَعِيدٍ ﴿٥٣﴾
53. Na kwa yakini walikwishaikanusha kabla, na wanavurumisha ghaibu kwa dhana kutoka mahali mbali.
وَحِيلَ بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ مَا يَشْتَهُونَ كَمَا فُعِلَ بِأَشْيَاعِهِم مِّن قَبْلُ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا فِي شَكٍّ مُّرِيبٍ ﴿٥٤﴾
54. Na kizuizi kitawekwa baina yao na baina ya yale wanayoyatamani, kama walivyofanyiwa wenzao kabla. Hakika wao walikuwa katika shaka yenye kutia wasiwasi.
[1] Hakuna Kinachofichika Kwa Allaah (سبحانه وتعالى), Kiwe Cha Dhahiri Au Cha Siri, Kikubwa Au Kidogo:
Rejea Al-An’aam (6:59) kwenye faida na maelezo bayana. Na rejea pia Ghaafir (40:19) kwenye maelezo na rejea mbalimbali. Rejea pia Luqmaan (31:16).
[3] Washirikina Kumpachika Sifa Ovu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
Rejea Al-Furqaan (25:4) kwenye maelezo bayana.
[4] Fadhila Za Nabiy Daawuwd (عليه السّلام):
Yaani: Hakika Tulimneemesha Mja Wetu na Rasuli Wetu Daawuwd (عليه السّلام), na Tukampa fadhila katika ilimu yenye manufaa, na matendo mema, na neema za kidini na za kidunia. Na miongoni mwa Neema Zake (Allaah) juu yake, ni pale Allaah (سبحانه وتعالى) Alipomhusishia Amri Yake kwa viumbe kama vile milima, wanyama, na ndege, kwamba vikariri pamoja nae na viitikie sambamba na anavyoleta yeye tasbiyh na tahmiyd ya Rabbi wao. Na katika hili, neema hii inajipambanua yenyewe kwake, pale lilipokuwa jambo hili ni katika mambo maalumu ambayo hayakuwa kwa yeyote kabla yake wala baada yake, na kwamba hilo linakua ni jambo la kumpa nguvu zaidi yeye na mwenginewe katika kumsabbih (Allaah) pindi wanapoviona hivi viumbe visivyo hai na wanyama, vinaitikia kwa Kumsabbih Rabb wake, na Kumtukuza, na Kumhimidi. Jambo hilo limekuwa ni miongoni mwa vitu vinavyohamasisha juu ya kumtaja Allaah (سبحانه وتعالى).
Na miongoni mwa yenye kufanikisha neema hizo, ni kwamba hilo (la kuitikiwa na viumbe hivyo) kama walivyosema wengi miongoni mwa ‘Ulamaa, ni kutokana na utamu wa sauti ya Daawuwd, kwani Allaah (سبحانه وتعالى) Alimpa sauti nzuri aliyowazidi kwayo wengine. Na alikuwa anapokariri Tasbiyh (Subhaana-Allaah) na Tahliyl (laa ilaaha illa-Allaah) na Tahmiyd (AlhamduliLlaah) kwa sauti hiyo laini yenye huzuni na yenye kugonga (moyo), humgonga kila anayeisikia, katika watu na majini, hata ndege na milima, na vikamtakasa kwa kumhimidi Rabb wao.
Na miongoni mwa neema nyingine ndani ya neema hizo, ni kumfanya apate malipo ya viumbe hivyo vinapomsabbih Allaah kwa kuwa yeye ni sababu ya hilo, na vyenyewe vinasabbih kwa kumfuata yeye.
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَأَلَنَّا لَهُ الْحَدِيدَ ﴿١٠﴾
“Na Tukamlainishia chuma”
Amesema Hasan Al-Baswriy, Qataadah, Al-A’mash na wengineo: “Alikuwa hahitaji kukiingiza chuma motoni wala kukipiga kwa nyundo, bali alikuwa anakikunja kwa mkono wake mfano wa nyuzi.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[5] Shukurani Za Daawuwd (عليه السّلام) :
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
اعْمَلُوا آلَ دَاوُودَ شُكْرًا ۚ وَقَلِيلٌ مِّنْ عِبَادِيَ الشَّكُورُ ﴿١٣﴾
“Tendeni enyi familia ya Daawuwd kwa shukurani! Na wachache miongoni mwa Waja Wangu ni wenye kushukuru.”
Shukrani ni kukiri na kutambua moyoni Neema za Allaah (سبحانه وتعالى), kuzipokea hali ya kuwa mtu anazihitajia, kuzitumia katika utii wa Allaah (سبحانه وتعالى), na kuzihifadhi zisitumike katika maasi. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Na katika kushukuru Neema za Allaah (سبحانه وتعالى), ni kutekeleza ibaada kwa wingi kutokana na uwezo, nguvu, na wasaa aliojaaliwa mtu na Allaah (سبحانه وتعالى). Na mfano wa shukurani za Nabiy Daawuwd (عليه السّلام), ni baadhi ya ibaada zake ambazo zinapendwa zaidi na Allaah (سبحانه وتعالى). Hadiyth ifuatayo inataja ibaada hizo:
حَدَّثَنَا قُتَيْبَةُ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَمْرِو بْنِ دِينَارٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ أَوْسٍ الثَّقَفِيِّ، سَمِعَ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عَمْرٍو، قَالَ قَالَ لِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " أَحَبُّ الصِّيَامِ إِلَى اللَّهِ صِيَامُ دَاوُدَ، كَانَ يَصُومُ يَوْمًا وَيُفْطِرُ يَوْمًا، وَأَحَبُّ الصَّلاَةِ إِلَى اللَّهِ صَلاَةُ دَاوُدَ، كَانَ يَنَامُ نِصْفَ اللَّيْلِ وَيَقُومُ ثُلُثَهُ وَيَنَامُ سُدُسَهُ ".
Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Amruw bin al-‘Aasw (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Swawm inayopendwa zaidi na Allaah ni Swawm ya Daawuwd; alikuwa akifunga siku moja na akiacha siku moja. Na Swalaah inayopendwa zaidi na Allaah ni Swalaah ya Daawuwd. Alikuwa akilala nusu ya usiku, akiswali thuluthi yake na kulala sudusi (1/6) yake.” [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]
[6] Saba-a Na Watu Wake Waliokufuru Neema Za Allaah (سبحانه وتعالى):
Kuanzia Aayah hii namba (12) hadi namba (21), zinahusiana na kisa cha Saba-a na watu wake waliokufuru Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) :
Saba-a ni miongoni mwa wafalme wa Yemen na watu wake. Na Balqiys (au Bilqiys) aliyekwenda kwa Nabiy Sulaymaan (عليه السّلام) na kusilimu, alikuwa ni miongoni mwao. Watu wa Saba-a walikuwa katika neema na hali nzuri katika miji yao na maisha yao, mazao mengi, mashamba makubwa na matunda kwa wingi. Hali kadhaalika walijaaliwa barabara za kuwasahilisha safari baina ya nchi; barabara zenye vituo vya safari, zenye amani na usalama. Allaah (سبحانه وتعالى) Akawapelekea Rusuli wakiwaamrisha wale katika riziki Zake, na wamshukuru kwa kumpwekesha (kwenye ibaada) na kumuabudu Yeye. Basi wakawa katika hali hiyo kadri Alivyopenda Allaah (سبحانه وتعالى). Kisha wakapuuza yale waliyoamrishwa, wakaadhibiwa kwa kupelekewa mafuriko na uhaba wa chakula, na kutawanyika katika miji. Rejea Aayah namba (19)
Na Hadiyth ifuatayo imeelezea kuhusu Saba-a:
عن فروة بن مسيك المرادي قال: أتيت النبي ﷺ فذكر في الحديث، فقال رجل: يا رسول الله وما سبأ أرض أو امرأة؟ قال: ليس بأرض ولا امرأة ولكنه رجل ولد عشرة من العرب، فتيامن منهم ستة سكنوا في اليمن، وتشاءم منهم أربعة يعني سكنوا في الشام، فأما الذين تشاءموا في الشام: فلخم، وجذام، وغسان، وعاملة، وأما الذين تيامنوا: فالأزد، والأشعريون، وحمير، وكندة، ومذحج، وأنمار رواه الترمذي: 3222، وصححه الألباني صحيح الترمذي:2574 .
Amesimulia Farwah Bin Musayk Al-Muraadiy: Nilimuendea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akataja katika mazungumzo (Saba-a), akasema mtu mmoja: Ee Rasuli wa Allaah! Ni nini Saba-a? Je ni ardhi au ni mwanamke? Akasema: “Si ardhi wala mwanamke lakini ni mtu ambaye alizaa makabila kumi ya Waarabu. Basi sita miongoni mwao, wakaishi Yemen, na wanne wakaishi Sham. Ama wale walioishi Sham, hao (ni makabila ya) Lakhmu, Judhaam, Ghassaan, na ‘Aamilah. Ama wale ambao waliishi Yemen, (hao ni) Uzdu, Humayr, Kindah, Madh-hij na Anmaar.” [At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (2574)]
[7] Makundi Mawili Ya Haki Na Upotofu:
Haiwezekani watu wote wakawa katika haki au wakawa wote katika upotofu. Lazima wagawike. Kundi la kwanza ni wale walionyooka katika njia ya haki, wakafuata maamrisho ya Allaah (سبحانه وتعالى) na wakafuata na kutekeleza mafunzo sahihi aliyokuja nayo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Salaf Swaalih (Wema waliotangulia). Na kwa kuwajibika na hayo, wakajiepusha na shirki, kufru, bid’ah, unafiki, maasi na kadhalika. Na kundi la pili ni wale waliopotoka wasifuate Amri za Allaah (سبحانه وتعالى) na wakatoka nje ya mafunzo ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), wakaacha kufuata yaliyo sahihi na wakafuata wapotofu, wakafarikiana humo vikundi kwa vikundi na wakazusha mambo katika Dini. Makundi haya mawili hayawezi kuwa sawa, lazima moja liwe liko juu ya uongofu, na la pili liwe juu ya upotofu.
[8] Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Ametumwa Kwa Walimwengu Wote; Majini Na Wanaadam:
Aayah hii ni dalili mojawapo kuwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Ametumwa kwa walimwengu wote na si kwa Waislamu pekee kwa kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Anaielekeza Kauli Yake kwa watu wote Anaposema:
وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِّلنَّاسِ
“Hatukukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa kwa watu wote.”
Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
وَكَانَ النَّبِيُّ يُبْعَثُ إِلَى قَوْمِهِ خَاصَّةً، وَبُعِثْتُ إِلَى النَّاسِ عَامَّةً
“Na Nabiy alikuwa akitumwa kwa watu wake pekee, lakini mimi nimetumwa kwa watu wote.” [Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy (5011)]
Na pia amesema (صلى الله عليه وآله وسلم):
وَبُعِثْتُ إِلَى كُلِّ أَحْمَر وَأَسْوَد
“Na nimetumwa kwa (wanaadam) wekundu wote na weusi.” [Muslim] Rejea Al-A’raaf (7:158), Al-Furqaan (25:1).
[10] Waliyy: Mlinzi, Rafiki Mwandani, Msaidizi, Msimamizi, Mfadhili:
Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Sifa Zake.
[11] Washirikina Kuikanusha Qur-aan Na Kuifanyia Istihzai Na Kuisingizia Kila Aina Ya Sifa Ovu:
Rejea Al-Furqaan (25:4) kwenye maelezo bayana.
[12] Waliyopewa Makafiri:
Neema za umri mrefu, mali nyingi, nguvu na neema nyenginezo. Imesemwa pia waliyopewa ni ilimu, dalili za wazi, hoja na kadhaalika.
[13] Haki Itaondoka Na Ubatili Utatoweka:
حَدَّثَنَا صَدَقَةُ بْنُ الْفَضْلِ، أَخْبَرَنَا ابْنُ عُيَيْنَةَ، عَنِ ابْنِ أَبِي نَجِيحٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ، عَنْ أَبِي مَعْمَرٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ دَخَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم مَكَّةَ يَوْمَ الْفَتْحِ وَحَوْلَ الْبَيْتِ سِتُّونَ وَثَلاَثُمِائَةِ نُصُبٍ، فَجَعَلَ يَطْعُنُهَا بِعُودٍ فِي يَدِهِ وَيَقُولُ " جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ، جَاءَ الْحَقُّ، وَمَا يُبْدِئُ الْبَاطِلُ وَمَا يُعِيدُ ".
Amesimulia ‘Abdullaah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoingia Makkah katika Siku ya Fat-h Makkah (ukombozi wa Makkah) palikuweko masanamu mia tatu na sitini yamezungushwa katika Al-Ka’bah. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaanza kuyapiga kwa fimbo aliyokuwa ameshika mkononi, huku akisema:
جَاءَ الْحَقُّ وَمَا يُبْدِئُ الْبَاطِلُ وَمَا يُعِيدُ ﴿٤٩﴾
“Haki imekuja, na ubatilifu hausimamishi (tena chochote), na wala haurudishi (kitu).” [Saba-a (34:49)]
[Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
Rejea pia Al-Israa (17:81).
فَاطِر
035-Faatwir
035-Faatwir: Utangulizi Wa Suwrah [253]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الْحَمْدُ لِلَّـهِ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ جَاعِلِ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا أُولِي أَجْنِحَةٍ مَّثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۚ يَزِيدُ فِي الْخَلْقِ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١﴾
1. AlhamduliLLahi (Himdi Anastahiki Allaah), Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mwenye Kuwafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbili-mbili, na tatu-tatu na nne-nne. Huzidisha katika uumbaji Atakavyo. Hakika Allaah Ni Muweza juu ya kila kitu.
مَّا يَفْتَحِ اللَّـهُ لِلنَّاسِ مِن رَّحْمَةٍ فَلَا مُمْسِكَ لَهَا ۖ وَمَا يُمْسِكْ فَلَا مُرْسِلَ لَهُ مِن بَعْدِهِ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢﴾
2. Rehma yoyote Anayoifungua Allaah kwa watu, basi hakuna wa kuizuia, na Anayoizuia, basi hakuna wa kuipeleka baada Yake,[1] Naye Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ ۚ هَلْ مِنْ خَالِقٍ غَيْرُ اللَّـهِ يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٣﴾
3. Enyi watu! Kumbukeni Neema za Allaah kwenu. Je, kuna muumbaji yeyote badala ya Allaah Anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini? Hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye. Basi vipi mnaghilibiwa?
وَإِن يُكَذِّبُوكَ فَقَدْ كُذِّبَتْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿٤﴾
4. Na wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi wamekwisha kadhibishwa Rusuli kabla yako. Na kwa Allaah yanarejeshwa mambo yote.
يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ ۖ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۖ وَلَا يَغُرَّنَّكُم بِاللَّـهِ الْغَرُورُ ﴿٥﴾
5. Enyi watu! Hakika Ahadi ya Allaah ni haki. Basi usikughururini kabisa uhai wa dunia, na wala (shaytwaan) mwenye kughuri asikughururini kabisa kuhusu Allaah.
إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمْ عَدُوٌّ فَاتَّخِذُوهُ عَدُوًّا ۚ إِنَّمَا يَدْعُو حِزْبَهُ لِيَكُونُوا مِنْ أَصْحَابِ السَّعِيرِ ﴿٦﴾
6. Hakika shaytwaan kwenu ni adui, basi mfanyeni kuwa ni adui. Hakika anaitia kikosi chake ili wawe miongoni mwa watu wa moto uliowashwa vikali mno.
الَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ ﴿٧﴾
7. Wale waliokufuru watapata adhabu kali, na wale walioamini na wakatenda mema watapata maghfirah na ujira mkubwa.
أَفَمَن زُيِّنَ لَهُ سُوءُ عَمَلِهِ فَرَآهُ حَسَنًا ۖ فَإِنَّ اللَّـهَ يُضِلُّ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۖ فَلَا تَذْهَبْ نَفْسُكَ عَلَيْهِمْ حَسَرَاتٍ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِمَا يَصْنَعُونَ ﴿٨﴾
8. Je, yule aliyepambiwa uovu wa amali yake akaiona ni nzuri (je, ni sawa na aliyehidika?). Basi hakika Allaah Anampotoa Amtakaye na Anamhidi Amtakaye. Hivyo basi isihiliki nafsi yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa ajili ya kuwajutia. Hakika Allaah Ni Mjuzi kwa yale wayatendayo.
وَاللَّـهُ الَّذِي أَرْسَلَ الرِّيَاحَ فَتُثِيرُ سَحَابًا فَسُقْنَاهُ إِلَىٰ بَلَدٍ مَّيِّتٍ فَأَحْيَيْنَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ كَذَٰلِكَ النُّشُورُ ﴿٩﴾
9. Na Allaah Ambaye Ametuma pepo za Rehma kisha zikatimua mawingu, Tukayaendesha katika nchi iliyokufa, Tukahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake. Hivyo ndivyo kufufuliwa.[2]
مَن كَانَ يُرِيدُ الْعِزَّةَ فَلِلَّـهِ الْعِزَّةُ جَمِيعًا ۚ إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ ۚ وَالَّذِينَ يَمْكُرُونَ السَّيِّئَاتِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۖ وَمَكْرُ أُولَـٰئِكَ هُوَ يَبُورُ ﴿١٠﴾
10. Yeyote Anayetaka utukufu, basi utukufu wote uko kwa Allaah. Kwake Pekee linapanda Neno zuri[3] na amali njema Huitukuza. Na wale wanaopanga njama za maovu watapata adhabu shadidi. Na njama za hao ni zenye kuangamia.
وَاللَّـهُ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ جَعَلَكُمْ أَزْوَاجًا ۚ وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِ ۚ وَمَا يُعَمَّرُ مِن مُّعَمَّرٍ وَلَا يُنقَصُ مِنْ عُمُرِهِ إِلَّا فِي كِتَابٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿١١﴾
11. Na Allaah Amekuumbeni kutokana na udongo, kisha kutokana na tone la manii, kisha Akakufanyeni jozi; mwanamume na mwanamke. Na mwanamke yeyote habebi mimba na wala hazai isipokuwa kwa Ujuzi Wake. Na hapewi umri mrefu yeyote yule mwenye umri mrefu na wala hapunguziwi katika umri wake isipokuwa imo Kitabuni. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.
وَمَا يَسْتَوِي الْبَحْرَانِ هَـٰذَا عَذْبٌ فُرَاتٌ سَائِغٌ شَرَابُهُ وَهَـٰذَا مِلْحٌ أُجَاجٌ ۖ وَمِن كُلٍّ تَأْكُلُونَ لَحْمًا طَرِيًّا وَتَسْتَخْرِجُونَ حِلْيَةً تَلْبَسُونَهَا ۖ وَتَرَى الْفُلْكَ فِيهِ مَوَاخِرَ لِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٢﴾
12. Na bahari mbili hazilingani sawa; haya ni (maji) matamu ladha yake, yenye kukata kiu, kinywaji chake cha kuburudisha, na haya ni ya chumvi kali. Na katika kila moja mnakula nyama laini safi na mnatoa mapambo mnayoyavaa. Na utaona merikebu humo zikipasua maji ili mtafute Fadhila Zake, na ili mpate kushukuru.
يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۚ وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ ﴿١٣﴾
13. Anauingiza usiku katika mchana, na Anauingiza mchana katika usiku, na Ametiisha jua na mwezi; kila kimoja kinakwenda mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Huyo Ndiye Allaah Rabb wenu, Ufalme ni Wake Pekee. Na wale mnaowaomba badala Yake hawamiliki hata kijiwavu cha kokwa ya tende.[4]
إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ۚ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ ﴿١٤﴾
14. Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu, na hata wakisikia, hawatakuitikieni. Na Siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu, na wala hakuna atakayekujulisha vilivyo, kama Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
يَا أَيُّهَا النَّاسُ أَنتُمُ الْفُقَرَاءُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَاللَّـهُ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ ﴿١٥﴾
15. Enyi watu! Nyinyi ni mafakiri kwa Allaah! Na Allaah Ndiye Mkwasi, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.
إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَأْتِ بِخَلْقٍ جَدِيدٍ ﴿١٦﴾
16. Akitaka Atakuondosheni mbali na Alete viumbe vipya.
وَمَا ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ بِعَزِيزٍ ﴿١٧﴾
17. Na hilo halina uzito wowote kwa Allaah.
وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۚ وَإِن تَدْعُ مُثْقَلَةٌ إِلَىٰ حِمْلِهَا لَا يُحْمَلْ مِنْهُ شَيْءٌ وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۗ إِنَّمَا تُنذِرُ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِالْغَيْبِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ ۚ وَمَن تَزَكَّىٰ فَإِنَّمَا يَتَزَكَّىٰ لِنَفْسِهِ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ الْمَصِيرُ ﴿١٨﴾
18. Na mbebaji hatobeba mzigo (wa dhambi) wa mwengine. Na aliyeelemeshwa mzigo akiita ili kusaidiwa kubebewa mzigo wake, hatobebewa chochote, japokuwa ni jamaa wa karibu.[5] Hakika wewe unaonya wale wanaomkhofu Rabb wao bila kuyaona unayowalingania, na wakasimamisha Swalaah. Na yeyote anayejitakasa, basi hakika anajitakasa kwa ajili ya nafsi yake. Na kwa Allaah ndio mahali pa kuishia.
وَمَا يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ ﴿١٩﴾
19. Na halingani sawa kipofu na mwenye kuona.[6]
وَلَا الظُّلُمَاتُ وَلَا النُّورُ ﴿٢٠﴾
20. Wala viza na nuru.
وَلَا الظِّلُّ وَلَا الْحَرُورُ ﴿٢١﴾
21. Wala kivuli na joto.
وَمَا يَسْتَوِي الْأَحْيَاءُ وَلَا الْأَمْوَاتُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُسْمِعُ مَن يَشَاءُ ۖ وَمَا أَنتَ بِمُسْمِعٍ مَّن فِي الْقُبُورِ ﴿٢٢﴾
22. Na hawalingani sawa walio hai na wafu. Hakika Allaah Anamsikilizisha Amtakaye, nawe huwezi kuwasikilizisha walioko makaburini.
إِنْ أَنتَ إِلَّا نَذِيرٌ ﴿٢٣﴾
23. Wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) si chochote isipokuwa mwonyaji tu.
إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ بِالْحَقِّ بَشِيرًا وَنَذِيرًا ۚ وَإِن مِّنْ أُمَّةٍ إِلَّا خَلَا فِيهَا نَذِيرٌ ﴿٢٤﴾
24. Hakika Sisi Tumekupeleka kwa haki ili ubashiri na uonye. Na hakuna ummah wowote isipokuwa amepita humo mwonyaji.
وَإِن يُكَذِّبُوكَ فَقَدْ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ وَبِالزُّبُرِ وَبِالْكِتَابِ الْمُنِيرِ ﴿٢٥﴾
25. Na wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi wamekwishakadhibisha wale wa nyuma yao. Waliwajia Rusuli wao kwa hoja bayana, na Vitabu vya Hukumu, na Kitabu chenye Nuru.
ثُمَّ أَخَذْتُ الَّذِينَ كَفَرُوا ۖ فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ ﴿٢٦﴾
26. Kisha Nikawashika (kuwaadhibu) wale waliokufuru, basi kulikuwa vipi Kukana Kwangu!
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ ثَمَرَاتٍ مُّخْتَلِفًا أَلْوَانُهَا ۚ وَمِنَ الْجِبَالِ جُدَدٌ بِيضٌ وَحُمْرٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَانُهَا وَغَرَابِيبُ سُودٌ ﴿٢٧﴾
27. Je, huoni kwamba Allaah Ameteremsha maji kutoka mbinguni, Tukatoa kwayo matunda ya rangi mbalimbali? Na miongoni mwa milima iko michirizi myeupe na myekundu yenye kutofautiana rangi zake, na myeusi iliyokoza sana.
وَمِنَ النَّاسِ وَالدَّوَابِّ وَالْأَنْعَامِ مُخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ كَذَٰلِكَ ۗ إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ ﴿٢٨﴾
28. Na katika watu, na viumbe wanaotembea, na wanyama wa mifugo, rangi zao vile vile zinatofautiana Hakika wanaomkhofu Allaah katika Waja Wake ni ‘Ulamaa.[7] Hakika Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwingi wa Kughufuria.
إِنَّ الَّذِينَ يَتْلُونَ كِتَابَ اللَّـهِ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَنفَقُوا مِمَّا رَزَقْنَاهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً يَرْجُونَ تِجَارَةً لَّن تَبُورَ ﴿٢٩﴾
29. Hakika wale wanaosoma Kitabu cha Allaah, na wakasimamisha Swalaah, na wakatoa kutokana na yale Tuliyowaruzuku kwa siri na dhahiri, wanataraji tijara ambayo haitoteketea.
لِيُوَفِّيَهُمْ أُجُورَهُمْ وَيَزِيدَهُم مِّن فَضْلِهِ ۚ إِنَّهُ غَفُورٌ شَكُورٌ ﴿٣٠﴾
30. Ili (Allaah) Awalipe ujira wao timilifu, na Awazidishie kutokana na Fadhila Zake. Hakika Yeye Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwingi wa Kupokea Shukurani.
وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ هُوَ الْحَقُّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِعِبَادِهِ لَخَبِيرٌ بَصِيرٌ ﴿٣١﴾
31. Na yale ambayo Tumekufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ya Kitabu, ndio haki yenye kusadikisha yale yaliyoko kabla yake. Hakika Allaah kwa Waja Wake bila shaka Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri, Mwenye Kuona yote.
ثُمَّ أَوْرَثْنَا الْكِتَابَ الَّذِينَ اصْطَفَيْنَا مِنْ عِبَادِنَا ۖ فَمِنْهُمْ ظَالِمٌ لِّنَفْسِهِ وَمِنْهُم مُّقْتَصِدٌ وَمِنْهُمْ سَابِقٌ بِالْخَيْرَاتِ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَضْلُ الْكَبِيرُ ﴿٣٢﴾
32. Kisha Tukawarithisha Kitabu wale Tuliowakhitari miongoni mwa Waja Wetu. Basi miongoni mwao yupo mwenye kudhulumu nafsi yake, na miongoni mwao yupo aliye wastani, na miongoni mwao yupo aliyesabiki kwa mambo mengi ya kheri kwa Idhini ya Allaah. Hiyo ndio fadhila kubwa.[8]
جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ وَلُؤْلُؤًا ۖ وَلِبَاسُهُمْ فِيهَا حَرِيرٌ ﴿٣٣﴾
33. Jannaat za kudumu milele wataziingia. Watapambwa humo kwa vikuku vya dhahabu na lulu, na mavazi yao humo ni hariri.[9]
وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي أَذْهَبَ عَنَّا الْحَزَنَ ۖ إِنَّ رَبَّنَا لَغَفُورٌ شَكُورٌ ﴿٣٤﴾
34. Na watasema: AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah) Ambaye Ametuondoshea huzuni. Hakika Rabb wetu bila shaka Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwingi wa Kupokea Shukurani.
الَّذِي أَحَلَّنَا دَارَ الْمُقَامَةِ مِن فَضْلِهِ لَا يَمَسُّنَا فِيهَا نَصَبٌ وَلَا يَمَسُّنَا فِيهَا لُغُوبٌ ﴿٣٥﴾
35. Ambaye Ametuweka nyumba yenye kudumu kwa Fadhila Zake, haitugusi humo taabu na mashaka, na wala hayatugusi humo machovu.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ نَارُ جَهَنَّمَ لَا يُقْضَىٰ عَلَيْهِمْ فَيَمُوتُوا وَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُم مِّنْ عَذَابِهَا ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي كُلَّ كَفُورٍ ﴿٣٦﴾
36. Na wale waliokufuru watapata moto wa Jahannam. Hawatahukumiwa (kifo) wakafa, na wala hawatakhafifishiwa adhabu yake. Hivyo ndivyo Tunavyomlipa kila mwingi wa kukufuru.[10]
وَهُمْ يَصْطَرِخُونَ فِيهَا رَبَّنَا أَخْرِجْنَا نَعْمَلْ صَالِحًا غَيْرَ الَّذِي كُنَّا نَعْمَلُ ۚ أَوَلَمْ نُعَمِّرْكُم مَّا يَتَذَكَّرُ فِيهِ مَن تَذَكَّرَ وَجَاءَكُمُ النَّذِيرُ ۖ فَذُوقُوا فَمَا لِلظَّالِمِينَ مِن نَّصِيرٍ ﴿٣٧﴾
37. Nao watapiga mayowe humo: Rabb wetu! Tutoe tutende mema ghairi ya yale tulokuwa tukitenda. (Wataambiwa): Je, kwani Hatukukupeni umri wa kukumbuka mwenye kukumbuka humo? Na alikujieni mwonyaji. Basi onjeni! Kwani madhalimu hawana yeyote yule wa kuwanusuru.
إِنَّ اللَّـهَ عَالِمُ غَيْبِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٣٨﴾
38. Hakika Allaah Ni Mjuzi wa ghaibu za mbinguni na ardhini. Hakika Yeye Ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.
هُوَ الَّذِي جَعَلَكُمْ خَلَائِفَ فِي الْأَرْضِ ۚ فَمَن كَفَرَ فَعَلَيْهِ كُفْرُهُ ۖ وَلَا يَزِيدُ الْكَافِرِينَ كُفْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ إِلَّا مَقْتًا ۖ وَلَا يَزِيدُ الْكَافِرِينَ كُفْرُهُمْ إِلَّا خَسَارًا ﴿٣٩﴾
39. Yeye Ndiye Ambaye Amekufanyeni warithi kwenye ardhi. Basi yeyote aliyekufuru, kufuru yake itamrudia mwenyewe. Na kufuru za makafiri haziwazidishii mbele ya Rabb wao isipokuwa kuchukiwa, na wala kufuru za makafiri haziwazidishii isipokuwa khasara.
قُلْ أَرَأَيْتُمْ شُرَكَاءَكُمُ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ أَرُونِي مَاذَا خَلَقُوا مِنَ الْأَرْضِ أَمْ لَهُمْ شِرْكٌ فِي السَّمَاوَاتِ أَمْ آتَيْنَاهُمْ كِتَابًا فَهُمْ عَلَىٰ بَيِّنَتٍ مِّنْهُ ۚ بَلْ إِن يَعِدُ الظَّالِمُونَ بَعْضُهُم بَعْضًا إِلَّا غُرُورًا ﴿٤٠﴾
40. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Je, mnawaona washirika wenu ambao mnawaomba badala ya Allaah? Nionyesheni ni nini walichoumba katika ardhi? Au wana ushirika wowote ule mbinguni?[11] Au Tumewapa kitabu chochote kile, kisha wao kwa hicho wakawa na hoja bayana? Hapana! Bali madhalimu hawaahidiani wao kwa wao isipokuwa ghururi.
إِنَّ اللَّـهَ يُمْسِكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ أَن تَزُولَا ۚ وَلَئِن زَالَتَا إِنْ أَمْسَكَهُمَا مِنْ أَحَدٍ مِّن بَعْدِهِ ۚ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا ﴿٤١﴾
41. Hakika Allaah Anazuia mbingu na ardhi zisitoweke. Na zikitoweka, hakuna yeyote wa kuzishikilia baada Yake. Hakika Yeye daima Ni Mvumilivu, Mwingi wa Kughufuria.
وَأَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ لَئِن جَاءَهُمْ نَذِيرٌ لَّيَكُونُنَّ أَهْدَىٰ مِنْ إِحْدَى الْأُمَمِ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُمْ نَذِيرٌ مَّا زَادَهُمْ إِلَّا نُفُورًا ﴿٤٢﴾
42. Na wakaapa kwa Allaah, viapo vyao thabiti vya nguvu, kwamba akiwajia mwonyaji, bila shaka watakuwa waliohidika zaidi kuliko nyumati nyenginezo (zilotangulia). Lakini alipowajia mwonyaji haikuwazidishia isipokuwa kukimbia kwa chuki.
اسْتِكْبَارًا فِي الْأَرْضِ وَمَكْرَ السَّيِّئِ ۚ وَلَا يَحِيقُ الْمَكْرُ السَّيِّئُ إِلَّا بِأَهْلِهِ ۚ فَهَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا سُنَّتَ الْأَوَّلِينَ ۚ فَلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ اللَّـهِ تَبْدِيلًا ۖ وَلَن تَجِدَ لِسُنَّتِ اللَّـهِ تَحْوِيلًا ﴿٤٣﴾
43. Kwa kutakabari katika ardhi na kupanga njama ovu. Lakini njama ovu hazimzunguki isipokuwa mwenyewe. Je, basi wanangojea nini isipokuwa desturi ya watu wa awali. Basi hutapata katika Desturi ya Allaah mabadiliko, na wala hutapata katika Desturi ya Allaah mageuko.[12]
أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَكَانُوا أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً ۚ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُعْجِزَهُ مِن شَيْءٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَلِيمًا قَدِيرًا ﴿٤٤﴾
44. Je, hawakutembea katika ardhi, wakatazama vipi ilikuwa hatima ya wale walio kabla yao[13], nao walikuwa wenye nguvu zaidi kuliko wao? Na hakuna lolote limshindalo Allaah mbinguni wala ardhini. Hakika Yeye daima Ni Mjuzi wa yote, Mweza wa yote.
وَلَوْ يُؤَاخِذُ اللَّـهُ النَّاسَ بِمَا كَسَبُوا مَا تَرَكَ عَلَىٰ ظَهْرِهَا مِن دَابَّةٍ وَلَـٰكِن يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۖ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِعِبَادِهِ بَصِيرًا ﴿٤٥﴾
45. Na lau Allaah Angeliwaadhibu watu kwa sababu ya waliyoyachuma, Asingeliacha juu ya ardhi kiumbe chochote kitembeacho, lakini Anawaakhirisha mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Na utakapofika muda wao, basi hakika Allaah daima Ni Mwenye Kuona Waja Wake.
[1] Hakuna Awezaye Kuzuia Rehma Ya Allaah Wala Kuitoa Anayoizuia Allaah:
Hivyo ni sawa na duaa ifuatayo inayosomwa katika kismamo cha baada ya kurukuu na baada ya kumaliza Swalaah:
اللّهُـمَّ لا مانِعَ لِما أَعْطَـيْت، وَلا مُعْطِـيَ لِما مَنَـعْت، وَلا يَنْفَـعُ ذا الجَـدِّ مِنْـكَ الجَـد
“Ee Allaah, hakuna mwenye kukizuia Ulichokitoa, wala Mwenye kutoa Ulichokizuia, na wala utajiri wa mtu haumnufaishi mwenye utajiri mbele Yako.”
[2] Mfano Wa Ardhi Iliyokufa (Kame), Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akaihuisha Kwa Mvua, Ni Mfano Wa Kuwahuisha Watu Kutoka Makaburini Mwao Siku Ya Qiyaamah:
Rejea Ar-Ruwm (30:50).
[3] Neno Zuri Ni Aina Zote Za Dhikru-Allaah (Kumdhukuru Allaah):
Neno zuri ambalo hupanda juu kwa Allaah (سبحانه وتعالى), ni aina zote za kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى). Miongoni mwazo ni kusoma Qur-aan, kuleta Tasbiyh (Kumtakasa Allaah), Tahmiyd (Kumhimidi Allaah), Tahliyl (Kumpwekesha Allaah), Takbiyr (Kumtukuza Allaah), Istighfaar (kuomba maghfirah), Duaa na Adhkaar nyenginezo. Na Hadiyth ifuatayo imethibitisha:
حَدَّثَنَا أَبُو بِشْرٍ، بَكْرُ بْنُ خَلَفٍ حَدَّثَنِي يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، عَنْ مُوسَى بْنِ أَبِي عِيسَى الطَّحَّانِ، عَنْ عَوْنِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ أَبِيهِ، أَوْ عَنْ أَخِيهِ، عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ـ صلى الله عليه وسلم ـ " إِنَّ مِمَّا تَذْكُرُونَ مِنْ جَلاَلِ اللَّهِ التَّسْبِيحَ وَالتَّهْلِيلَ وَالتَّحْمِيدَ يَنْعَطِفْنَ حَوْلَ الْعَرْشِ لَهُنَّ دَوِيٌّ كَدَوِيِّ النَّحْلِ تُذَكِّرُ بِصَاحِبِهَا أَمَا يُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَنْ يَكُونَ لَهُ - أَوْ لاَ يَزَالَ لَهُ - مَنْ يُذَكِّرُ بِهِ
Amesimulia Nu’maan bin Bashiyr (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Tasbiyh (Kumtakasa), Tahliyl (Kumpwekesha), na Tahmiyd (Kumhimidi) ambayo ni maneno mnayomtukuza kwayo Allaah, yanazunguka kwenye ‘Arsh, yanavuma kama nyuki na yanamtaja aliyeyatamka. Je, hakuna yeyote kati yenu ambaye angependa kuwa na -au kuendelea kuwa- na kitu ambacho kitamtaja (mbele ya Allaah?)” [Sunan Ibn Maajah na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Maajah (3086), na As-Silsilah Asw-Swahiyhah (3358)]
[4] Aina Tatu Za Mfano Wa Udogo Katika Tende:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anapiga mifano ya udogo katika tende kwa kutaja aina tatu za viliomo ndani yake. (i) Fatiylun: Uzi katika kokwa ya tende. Rejea An-Nisaa (4:49, 77), Al-Israa (17:71). (ii) Naqiyrun: Kitone cha kokwa ya tende. Rejea An-Nisaa (4:53), (4:124). (iii) Qitwmiyrun: Kijiwavu cha kokwa ya tende kwenye Aayah hii ya Suwrah Faatwir (35:13).
[5] Hakuna Mwenye Uhusiano Wa Damu Atakayemsaidia Jamaa Yake Siku Ya Qiyaamah:
Siku ya Qiyaamah, kila mtu atabeba dhambi zake, na hakuna atakayemsaidia jamaa, wala ndugu, wala wazazi, bali kila mmoja atajali nafsi yake! Rejea ‘Abasa (80:33-37), Al-Muuminuwn (23:101).
[6] Mifano Ya Tofauti Ya Kafiri Na Muumini:
Kuanzia Aayah hii Faatwir (35:19) hadi namba (22), Allaah (سبحانه وتعالى) Anapiga mfano wa tofauti ya kafiri na Muumini ya kwamba hawalingani sawa; kipofu na mwenye kuona, viza na nuru, vivuli na joto na waliohai na wafu:
(i) Kipofu Na Mwenye Kuona:
Na kipofu asiyeiona Dini ya Allaah, halingani na yule mwenye kuona ambaye anaiona njia ya haki na anaifuata. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Na Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja hivyo katika Suwrah Ar-Ra’d (13:19) kwamba anayejua Aliyoteremshiwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni haki, hawi sawa na kipofu asiyetambua hilo.
Rejea pia Al-An’aam (6:50), Ar-Ra’d (13:16), Ghaafir (40:58), Huwd (11:24), Az-Zukhruf (43:40).
(ii) Viza Na Nuru (Mwanga):
Rejea Suwrah Ibraahiym (14:1) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali.
(iii) Vivuli Na Joto:
Imaam Ibn Kathiyr amejumuisha maana ya yote yaliyotajwa katika Aayah hizo za kuanzia namba (19) hadi namba (22).
Muumini ni mwenye kusikia na mwenye kuona, anatembea katika Nuru juu ya Swiraatw Al-Mustaqiym (Njia Iliyonyooka) duniani na Aakhirah hadi afikie kustakiri mahali pake katika Jannah (Pepo au mabustani) yenye vivuli na chemchemu. Na kafiri ni kipofu na kiziwi, anatembea katika viza na hatoki humo, bali anatangatanga ndani ya upotofu wake duniani na Aakhirah hadi afikie katika joto na moto uwakao vikali kama Anavyosema Allaah katika Suwrah Al-Waaqi’ah (56:43-44). [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
(iv) Waliohai (Waumini) Na Wafu (Makafiri)
Ni sawa na nyoyo zilizohai na nyoyo zilizokufa.
Wafu ni kama makafiri, hawawi sawa na waliohai ambao ni Waumini. Rejea Al-An’aam (6:122) kwenye ufafanuzi. Na pia rejea pia Huwd (11:24).
[7] Wanaomkhofu Allaah Ni ‘Ulamaa:
Yaani: Bali wale walio na ilimu hakika wanamcha Allaah (سبحانه وتعالى) kama Anavyopaswa kuogopwa, kwa sababu kadiri maarifa ya kumjua Allaah (سبحانه وتعالى) Mwenye Uwezo, Mjuzi wa yote, Ambaye Ana Sifa Kamilifu na Ameelezewa kwa Majina Mazuri kabisa, ndivyo watakavyozidi kumcha. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[8] Aina Za Watu Na Amali Zao:
Kisha Tukawapa Qur-aan, baada ya kuangamia nyumati zilizopita, wale Tuliowachagua miongoni mwa ummah wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Basi kati yao kuna: (i) Aliyeidhulumu nafsi yake kwa kufanya baadhi ya maasia. (ii) Aliyekuwa wastani, naye ni yule mwenye kutekeleza yaliyo wajibu na kuepuka yaliyoharamishwa. (iii) Mwenye kutangulia kufanya mambo ya kheri kwa Idhini ya Allaah, naye ni yule mwenye kukimbilia na kujitahidi kufanya amali njema za faradhi na za ziada. Na kupewa Kitabu huko na kuchaguliwa ummah huu ndio fadhila kubwa. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[9] Neema Za Watu Wa Jannah, Watamhimidi Allaah Na Watadumu Katika Raha Za Milele:
Kuanzia Aayah hii hadi namba (35) zinataja neema watakazozipata watu wa Jannah watakapoingizwa humo. Na neema na raha za watu wa Jannah, zimetajwa kwa wingi katika Qur-aan na Sunnah. Allaah (سبحانه وتعالى) Ameisifu Jannah kuwa haikupatapo kusikika wala kuonekana wala kuwaziwa. Rejea As-Sajdah (32:17). Na pia rejea Aayah namba (33-34) pamoja na Aayah hii namba (35). Rejea pia At-Tawbah (9:72), Asw-Swaaffaat (37:41-49), Az-Zukhruf (43:68-73), Muhammad (47:15), Ar-Rahmaan (55:46-76), Al-Waaqi’ah (56:15-40), Atw-Twuwr (52:17-24), Al-Insaan (76:12-22), An-Nabaa (78:31-36), Al-Mutwaffifiyn (83:22-28), Al-Ghaashiyah (88:8-16) na kwengineko kwingi.
Na miongoni mwa Hadiyth zinazotaja kuwa watu wa Jannah watakuwa hai na watadumu milele katika neema na raha za Jannah ni hii ifuatayo:
وعن أبي سعيد وأبي هريرة رضي الله عنهما : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال : (( إذَا دَخَلَ أهْلُ الجَنَّةِ الجَنَّةَ يُنَادِي مُنَادٍ : إنَّ لَكُمْ أنْ تَحْيَوْا ، فَلاَ تَمُوتُوا أَبَداً ، وإنَّ لَكُمْ أنْ تَصِحُّوا ، فلا تَسْقَمُوا أبداً ، وإنَّ لَكمْ أنْ تَشِبُّوا فلا تَهْرَمُوا أبداً ، وإنَّ لَكُمْ أَنْ تَنْعَمُوا ، فَلاَ تَبْأسُوا أَبَداً )) . رواه مسلم .
Amesimulia Abuu Sa’iyd na Abuu Hurayrah (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Watu wa Jannah watakapoingia Jannah, atanadi mwenye kunadi: “Hakika nyinyi mtaishi milele wala hamtakuwa wagonjwa, nanyi mtakuwa barobaro milele wala hamtazeeka, nanyi mtaneemeka milele wala hamtapata shida.” [Muslim]
[10] Watu Wa Motoni Hawatakufa Wala Hawatapunguziwa Adhabu Bali Watadumu Katika Adhabu:
Rejea Az-Zukhruf (43:74-77), Twaahaa (20:74), Al-A’laa (87:12-13), Al-Israa (17/l97), An-Nisaa (4:56), Yuwnus (10:52), As-Sajdah (32:21), An-Nabaa (78:30).
Na miongoni mwa Hadiyth zinazotaja kuwa watu wa motoni hawatakufa wala kuishi uhai wa raha humo bali wataendelea kuadhibiwa ni zifuatazo:
وَحَدَّثَنِي نَصْرُ بْنُ عَلِيٍّ الْجَهْضَمِيُّ، حَدَّثَنَا بِشْرٌ، - يَعْنِي ابْنَ الْمُفَضَّلِ - عَنْ أَبِي مَسْلَمَةَ، عَنْ أَبِي نَضْرَةَ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " أَمَّا أَهْلُ النَّارِ الَّذِينَ هُمْ أَهْلُهَا فَإِنَّهُمْ لاَ يَمُوتُونَ فِيهَا وَلاَ يَحْيَوْنَ وَلَكِنْ نَاسٌ أَصَابَتْهُمُ النَّارُ بِذُنُوبِهِمْ - أَوْ قَالَ بِخَطَايَاهُمْ - فَأَمَاتَهُمْ إِمَاتَةً حَتَّى إِذَا كَانُوا فَحْمًا أُذِنَ بِالشَّفَاعَةِ فَجِيءَ بِهِمْ ضَبَائِرَ ضَبَائِرَ فَبُثُّوا عَلَى أَنْهَارِ الْجَنَّةِ ثُمَّ قِيلَ يَا أَهْلَ الْجَنَّةِ أَفِيضُوا عَلَيْهِمْ . فَيَنْبُتُونَ نَبَاتَ الْحِبَّةِ تَكُونُ فِي حَمِيلِ السَّيْلِ " . فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ الْقَوْمِ كَأَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَدْ كَانَ بِالْبَادِيَةِ .
Amesimulia Abuu Sa’iyd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Watu wa motoni ni wale ambao watasalia humo milele, na hakika hawatakufa wala hawataishi humo maisha ya raha. Lakini watu ambao moto utawasibu kwa ajili ya dhambi zao, au akasema (msimuliaji) kwa ajili ya maovu yao, hawa (Allaah) Atawafisha mpaka wageuke makaa. Kisha watapewa uombezi na kuletwa makundi kwa makundi na kutawanywa kwenye mito ya Jannah (Peponi) kisha itasemwa: Enyi watu wa Jannah! Wamwagieni maji. Kisha watamea kama inavyochipuka mbegu kwenye udongo unaobebwa na mafuriko.” Mtu mmoja miongoni mwa watu akasema: (Inaonekana) kana kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ameishi jangwani (akaona hali hiyo). [Muslim]
Na pia:
حَدَّثَنَا عُمَرُ بْنُ حَفْصِ بْنِ غِيَاثٍ، حَدَّثَنَا أَبِي، حَدَّثَنَا الأَعْمَشُ، حَدَّثَنَا أَبُو صَالِحٍ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " يُؤْتَى بِالْمَوْتِ كَهَيْئَةِ كَبْشٍ أَمْلَحَ فَيُنَادِي مُنَادٍ يَا أَهْلَ الْجَنَّةِ، فَيَشْرَئِبُّونَ وَيَنْظُرُونَ فَيَقُولُ هَلْ تَعْرِفُونَ هَذَا فَيَقُولُونَ نَعَمْ هَذَا الْمَوْتُ، وَكُلُّهُمْ قَدْ رَآهُ، ثُمَّ يُنَادِي يَا أَهْلَ النَّارِ، فَيَشْرَئِبُّونَ وَيَنْظُرُونَ، فَيَقُولُ هَلْ تَعْرِفُونَ هَذَا فَيَقُولُونَ نَعَمْ هَذَا الْمَوْتُ، وَكُلُّهُمْ قَدْ رَآهُ، فَيُذْبَحُ ثُمَّ يَقُولُ يَا أَهْلَ الْجَنَّةِ، خُلُودٌ فَلاَ مَوْتَ، وَيَا أَهْلَ النَّارِ، خُلُودٌ فَلاَ مَوْتَ ثُمَّ قَرَأَ وَأَنْذِرْهُمْ يَوْمَ الْحَسْرَةِ إِذْ قُضِيَ الأَمْرُ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ وَهَؤُلاَءِ فِي غَفْلَةٍ أَهْلُ الدُّنْيَا وَهُمْ لاَ يُؤْمِنُونَ
Amesimulia Abuu Sa‘iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kifo kitaletwa katika umbo la kondoo mweupe, na hapo ataita muitaji: Enyi watu wa Jannah! Watu hao watachuchumia ili kuangalia. Muitaji atauliza kwa kusema: Je huyu mnamjua? Watasema ndio, huyu ni umauti. Na wote walikwishauona (wakati wa kutolewa roho duniani). Kisha atanadi tena: Enyi watu wa motoni! Watu hao watachuchumia ili kuangalia. Atauliza: Je, huyu mnamjua? Watajibu: Ndio, huyu ni umauti. Na wote walikwishauona (umauti). Hapo atachinjwa, kisha mwenye kunadi atasema: Enyi watu wa Peponi! Mtadumu milele hapana kifo. Na enyi watu wa motoni! Mtadumu milele hapana kifo. Kisha atasoma:
وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ الْحَسْرَةِ إِذْ قُضِيَ الْأَمْرُ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ وَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٣٩﴾
“Na waonye Siku ya majuto itakapohukumiwa amri, na hali wao wamo katika mghafala, wala hawaamini.” [Maryam (10:39) – Al-Bukhaariy]
Mateso na adhabu za watu wa motoni zimetajwa katika Qur-aan sehemu nyingi. Na mateso hayo yanawaanzia tokea wanapotolewa roho za, rejea Al-An’aam (6:93), Al-Anfaal (8:50). Na adhabu zao wanapofika motoni, rejea An-Nabaa (78:21) kwenye maelezo bayana kuhusu aina za mateso na adhabu za watu wa motoni. Na kuhusu aina za moto na majina yake, rejea Al-Muddath-thir (74:26).
[11] Wanaoabudiwa Pasi Na Allaah Hawawezi Kuumba Chochote:
Rejea Luqmaan (31:11) na rejea Al-Ahqaaf (46:4) kwenye maelezo na rejea mbalimbali.
[12] Desturi Ya Allaah Ya Kuwaadhibu Makafiri:
Aayah hii ya Suwrah Faatwir (35:43), inataja Desturi ya Allaah ya Kuwaadhibu washirikina, makafiri na madhalimu. Na katika Suwrah Aal-‘Imraan (3:137), Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja pia Desturi Yake kuhusiana na makafiri na Waumini. Kisha Aayah (35:44) inayofuatia, Allaah (سبحانه وتعالى) Anawataka watembee katika ardhi wajionee adhabu zilowafikia waliokadhibisha na hatima zao. Rejea Al-An’aam (6:11), Yuwsuf (12:109), Al-Kahf (18:55), Al-Hajj (22:46).
[13] Makafiri Watembee Katika Ardhi Wajionee Adhabu Zilizowasibu Waliokadhibisha Risala, Na Wajionee Hatima Zao:
Rejea Al-An’aam (6:11), Yuwsuf (12:109), Al-Kahf (18:55), Al-Hajj (22:46).
يس
036-Yaasiyn
036-Yaasiyn: Utangulizi Wa Suwrah [255]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يس ﴿١﴾
1. Yaa Siyn.[1]
وَالْقُرْآنِ الْحَكِيمِ ﴿٢﴾
2. Naapa kwa Qur-aan yenye Hikmah.
إِنَّكَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٣﴾
3. Hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka ni miongoni mwa Rusuli.
عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٤﴾
4. Uko juu ya njia iliyonyooka.
تَنزِيلَ الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ ﴿٥﴾
5. Ni Uteremsho wa Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu.
لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّا أُنذِرَ آبَاؤُهُمْ فَهُمْ غَافِلُونَ ﴿٦﴾
6. Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa, basi wao ni wenye kughafilika.
لَقَدْ حَقَّ الْقَوْلُ عَلَىٰ أَكْثَرِهِمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٧﴾
7. Kwa yakini imethibiti kauli (ya adhabu) juu ya wengi wao, kwa hiyo hawaamini.
إِنَّا جَعَلْنَا فِي أَعْنَاقِهِمْ أَغْلَالًا فَهِيَ إِلَى الْأَذْقَانِ فَهُم مُّقْمَحُونَ ﴿٨﴾
8. Hakika Sisi Tumeweka kwenye shingo zao minyororo ikawafika videvuni, basi vichwa vyao vinanyanyuka juu na kufumba macho.
وَجَعَلْنَا مِن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ سَدًّا وَمِنْ خَلْفِهِمْ سَدًّا فَأَغْشَيْنَاهُمْ فَهُمْ لَا يُبْصِرُونَ ﴿٩﴾
9. Na Tumeweka mbele yao kizuizi na nyuma yao kizuizi, Tukawafunika, basi wao hawaoni.
وَسَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٠﴾
10. Na ni sawasawa tu juu yao, ukiwaonya au usiwaonye hawaamini.
إِنَّمَا تُنذِرُ مَنِ اتَّبَعَ الذِّكْرَ وَخَشِيَ الرَّحْمَـٰنَ بِالْغَيْبِ ۖ فَبَشِّرْهُ بِمَغْفِرَةٍ وَأَجْرٍ كَرِيمٍ ﴿١١﴾
11. Hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unamuonya yule anayefuata Ukumbusho na akamkhofu Ar-Rahmaan kwa ghaibu, basi mbashirie maghfirah na ujira karimu.
إِنَّا نَحْنُ نُحْيِي الْمَوْتَىٰ وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ ۚ وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ فِي إِمَامٍ مُّبِينٍ ﴿١٢﴾
12. Hakika Sisi Tunahuisha wafu, na Tunaandika yale waliyoyakadimisha (ya kheri na shari) na athari zao, na kila kitu Tumekirekodi barabara katika daftari bayana.[2]
وَاضْرِبْ لَهُم مَّثَلًا أَصْحَابَ الْقَرْيَةِ إِذْ جَاءَهَا الْمُرْسَلُونَ ﴿١٣﴾
13. Na wapigie mfano watu wa mji[3] walipowajia Wajumbe.[4]
إِذْ أَرْسَلْنَا إِلَيْهِمُ اثْنَيْنِ فَكَذَّبُوهُمَا فَعَزَّزْنَا بِثَالِثٍ فَقَالُوا إِنَّا إِلَيْكُم مُّرْسَلُونَ ﴿١٤﴾
14. Tulipowapelekea wawili, wakawakadhibisha, Tukawaongezea nguvu kwa wa tatu, wakasema: Hakika sisi (ni wajumbe) tumetumwa kwenu.
قَالُوا مَا أَنتُمْ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا وَمَا أَنزَلَ الرَّحْمَـٰنُ مِن شَيْءٍ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَكْذِبُونَ ﴿١٥﴾
15. (Watu wa mji) wakasema: Nyinyi si chochote isipokuwa ni watu tu kama sisi, na wala Ar-Rahmaan Hakuteremsha chochote. Hamkuwa nyinyi isipokuwa mnaongopa tu.[5]
قَالُوا رَبُّنَا يَعْلَمُ إِنَّا إِلَيْكُمْ لَمُرْسَلُونَ ﴿١٦﴾
16. (Wajumbe) wakasema: Rabb wetu Anajua kwamba sisi kwa hakika tumetumwa kwenu.
وَمَا عَلَيْنَا إِلَّا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ ﴿١٧﴾
17. Na hapana juu yetu lolote isipokuwa ubalighisho wa bayana.
قَالُوا إِنَّا تَطَيَّرْنَا بِكُمْ ۖ لَئِن لَّمْ تَنتَهُوا لَنَرْجُمَنَّكُمْ وَلَيَمَسَّنَّكُم مِّنَّا عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٨﴾
18. (Watu wa mji) wakasema: Hakika sisi tumepata nuksi[6] kwenu. Msipokoma, basi hakika tutakurajimuni, na bila shaka itakuguseni kutoka kwetu adhabu iumizayo.
قَالُوا طَائِرُكُم مَّعَكُمْ ۚ أَئِن ذُكِّرْتُم ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ ﴿١٩﴾
19. (Wajumbe) wakasema: Nuksi yenu mnayo wenyewe. Je, kwa vile mnakumbushwa? Bali nyinyi ni watu wapindukao mipaka.
وَجَاءَ مِنْ أَقْصَى الْمَدِينَةِ رَجُلٌ يَسْعَىٰ قَالَ يَا قَوْمِ اتَّبِعُوا الْمُرْسَلِينَ ﴿٢٠﴾
20. Akaja mtu mbio kutoka upande wa mbali wa ule mji, akasema: Enyi watu wangu! Wafuateni wajumbe.[7]
اتَّبِعُوا مَن لَّا يَسْأَلُكُمْ أَجْرًا وَهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٢١﴾
21. Wafuateni wale wasiokuombeni ujira, nao ni wenye kuongoka.
وَمَا لِيَ لَا أَعْبُدُ الَّذِي فَطَرَنِي وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٢٢﴾
22. Na kwa nini mimi nisimwabudu Ambaye Ameniumba na Kwake mtarejeshwa?
أَأَتَّخِذُ مِن دُونِهِ آلِهَةً إِن يُرِدْنِ الرَّحْمَـٰنُ بِضُرٍّ لَّا تُغْنِ عَنِّي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا وَلَا يُنقِذُونِ ﴿٢٣﴾
23. Je, nijichukulie badala Yake waabudiwa, na hali Akinitakia Ar-Rahmaan dhara yoyote hautonifaa chochote uombezi wao wala hawatoniokoa!
إِنِّي إِذًا لَّفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٢٤﴾
24. Hakika mimi hapo nitakuwa katika upotofu bayana.
إِنِّي آمَنتُ بِرَبِّكُمْ فَاسْمَعُونِ ﴿٢٥﴾
25. Hakika mimi nimemwamini Rabb wenu, basi nisikilizeni!
قِيلَ ادْخُلِ الْجَنَّةَ ۖ قَالَ يَا لَيْتَ قَوْمِي يَعْلَمُونَ ﴿٢٦﴾
26. Ikasemwa (alipouliwa): Ingia Jannah. Akasema: Laiti watu wangu wangelijua.[8]
بِمَا غَفَرَ لِي رَبِّي وَجَعَلَنِي مِنَ الْمُكْرَمِينَ ﴿٢٧﴾
27. Namna ambavyo Rabb wangu Amenighufuria, na Akanijaalia kuwa miongoni mwa waliokirimiwa.
وَمَا أَنزَلْنَا عَلَىٰ قَوْمِهِ مِن بَعْدِهِ مِن جُندٍ مِّنَ السَّمَاءِ وَمَا كُنَّا مُنزِلِينَ ﴿٢٨﴾
28. Na Hatukuwateremshia watu wake baada yake jeshi lolote kutoka mbinguni, na wala Hatukuwa Wateremshao.
إِن كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَاحِدَةً فَإِذَا هُمْ خَامِدُونَ ﴿٢٩﴾
29. Haikuwa isipokuwa ukelele angamizi mmoja tu, basi mara hao wamezimika.
يَا حَسْرَةً عَلَى الْعِبَادِ ۚ مَا يَأْتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٣٠﴾
30. Ee! Ole na majuto juu ya waja! Hawafikiwi na Rasuli yeyote isipokuwa walikuwa wakimfanyia istihzai.
أَلَمْ يَرَوْا كَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّنَ الْقُرُونِ أَنَّهُمْ إِلَيْهِمْ لَا يَرْجِعُونَ ﴿٣١﴾
31. Je, hawajaona karne ngapi Tumeangamiza kabla yao na kwamba wao hawatorejea kwao?
وَإِن كُلٌّ لَّمَّا جَمِيعٌ لَّدَيْنَا مُحْضَرُونَ ﴿٣٢﴾
32. Na hapana yeyote ila wote watahudhurishwa Kwetu.
وَآيَةٌ لَّهُمُ الْأَرْضُ الْمَيْتَةُ أَحْيَيْنَاهَا وَأَخْرَجْنَا مِنْهَا حَبًّا فَمِنْهُ يَأْكُلُونَ ﴿٣٣﴾
33. Na Aayah (Ishara, Dalili)[9] kwao ni ardhi iliyokufa, Tukaihuisha, na Tukatoa humo nafaka, wakapata kuzila.[10]
وَجَعَلْنَا فِيهَا جَنَّاتٍ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَابٍ وَفَجَّرْنَا فِيهَا مِنَ الْعُيُونِ ﴿٣٤﴾
34. Na Tukafanya humo mabustani ya mitende, na mizabibu, na Tukabubujua humo chemchemu.
لِيَأْكُلُوا مِن ثَمَرِهِ وَمَا عَمِلَتْهُ أَيْدِيهِمْ ۖ أَفَلَا يَشْكُرُونَ ﴿٣٥﴾
35. Ili wale katika matunda yake, na haikuyafanya hayo mikono yao Je, basi hawashukuru?
سُبْحَانَ الَّذِي خَلَقَ الْأَزْوَاجَ كُلَّهَا مِمَّا تُنبِتُ الْأَرْضُ وَمِنْ أَنفُسِهِمْ وَمِمَّا لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٦﴾
36. Utakasifu ni wa Ambaye Ameumba dume na jike katika vyote ambavyo inaotesha ardhi, na katika nafsi zao, na katika vile wasivyovijua.
وَآيَةٌ لَّهُمُ اللَّيْلُ نَسْلَخُ مِنْهُ النَّهَارَ فَإِذَا هُم مُّظْلِمُونَ ﴿٣٧﴾
37. Na Aayah (Ishara, Dalili) kwao ni usiku, Tunauvua humo mchana, basi tahamaki wao ni wenye kuwa kizani.
وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَّهَا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ﴿٣٨﴾
38. Na jua linatembea hadi matulio yake.[11] Hayo ni Takdiri ya Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.[12]
وَالْقَمَرَ قَدَّرْنَاهُ مَنَازِلَ حَتَّىٰ عَادَ كَالْعُرْجُونِ الْقَدِيمِ ﴿٣٩﴾
39. Na mwezi Tumeukadiria vituo mpaka ukarudi (mwembamba) kama kwamba ni karara kongwe la shina la mtende lililopinda.
لَا الشَّمْسُ يَنبَغِي لَهَا أَن تُدْرِكَ الْقَمَرَ وَلَا اللَّيْلُ سَابِقُ النَّهَارِ ۚ وَكُلٌّ فِي فَلَكٍ يَسْبَحُونَ ﴿٤٠﴾
40. Halipasi jua kuudiriki mwezi, wala usiku kuutangulia mchana, na vyote viko katika falaki vinaogelea.
وَآيَةٌ لَّهُمْ أَنَّا حَمَلْنَا ذُرِّيَّتَهُمْ فِي الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ ﴿٤١﴾
41. Na Aayah (Ishara, Dalili) kwao, ni kwamba Sisi Tumebeba vizazi vyao katika merikebu iliyosheheni.
وَخَلَقْنَا لَهُم مِّن مِّثْلِهِ مَا يَرْكَبُونَ ﴿٤٢﴾
42. Na Tukawaumbia kutoka mfano wake wa vile wanavyovipanda.
وَإِن نَّشَأْ نُغْرِقْهُمْ فَلَا صَرِيخَ لَهُمْ وَلَا هُمْ يُنقَذُونَ ﴿٤٣﴾
43. Na kama Tungetaka, Tungeliwagharikisha, basi hakuna wa kupiga kelele kuwasaidia na wala hawatookolewa.
إِلَّا رَحْمَةً مِّنَّا وَمَتَاعًا إِلَىٰ حِينٍ ﴿٤٤﴾
44. Isipokuwa Rehma kutoka Kwetu, na starehe kwa muda tu.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّقُوا مَا بَيْنَ أَيْدِيكُمْ وَمَا خَلْفَكُمْ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٤٥﴾
45. Na wanapoambiwa: Ogopeni yale yaliyo mbele yenu na yale yaliyo nyuma yenu ili mpate kurehemewa (wao huzidi jeuri).
وَمَا تَأْتِيهِم مِّنْ آيَةٍ مِّنْ آيَاتِ رَبِّهِمْ إِلَّا كَانُوا عَنْهَا مُعْرِضِينَ ﴿٤٦﴾
46. Na haiwafikii Aayah (Ishara, Dalili) yoyote katika Aayaat za Rabb wao, isipokuwa walikuwa ni wenye kuzikengeuka.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ أَنفِقُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللَّـهُ قَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا أَنُطْعِمُ مَن لَّوْ يَشَاءُ اللَّـهُ أَطْعَمَهُ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٤٧﴾
47. Na wanapoambiwa: Toeni katika vile Alivyokuruzukuni Allaah, wale waliokufuru husema kuwaambia walioamini: Je, tumlishe ambaye Allaah Angelitaka Angelimlisha? Nyinyi hamumo isipokuwa katika upotofu bayana.
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٤٨﴾
48. Na wanasema: Ni lini hiyo ahadi (ya kufufuliwa) mkiwa ni wasemao kweli?[13]
مَا يَنظُرُونَ إِلَّا صَيْحَةً وَاحِدَةً تَأْخُذُهُمْ وَهُمْ يَخِصِّمُونَ ﴿٤٩﴾
49. Hawangojei isipokuwa ukelele mmoja tu, uwachukue hali wao wanakhasimiana.
فَلَا يَسْتَطِيعُونَ تَوْصِيَةً وَلَا إِلَىٰ أَهْلِهِمْ يَرْجِعُونَ ﴿٥٠﴾
50. Basi hawatoweza kuusia, wala kurejea kwa ahli zao.
وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَإِذَا هُم مِّنَ الْأَجْدَاثِ إِلَىٰ رَبِّهِمْ يَنسِلُونَ ﴿٥١﴾
51. Na litapulizwa baragumu[14], basi tahamaki wanatoka makaburini mwao wakienda mbio mbio kwa Rabb wao.
قَالُوا يَا وَيْلَنَا مَن بَعَثَنَا مِن مَّرْقَدِنَا ۜ ۗ هَـٰذَا مَا وَعَدَ الرَّحْمَـٰنُ وَصَدَقَ الْمُرْسَلُونَ ﴿٥٢﴾
52. Waseme: Ole wetu! Nani ametufufua katika malazo yetu? (Wataambiwa): Haya ndio Aliyoahidi Ar-Rahmaan na Rusuli walisema kweli.
إِن كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَاحِدَةً فَإِذَا هُمْ جَمِيعٌ لَّدَيْنَا مُحْضَرُونَ ﴿٥٣﴾
53. Haitokuwa isipokuwa ukelele mmoja tu, tahamaki wote watahudhurishwa mbele Yetu.
فَالْيَوْمَ لَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا وَلَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٥٤﴾
54. Basi leo nafsi yoyote haitodhulumiwa kitu chochote, na wala hamtalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
إِنَّ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ الْيَوْمَ فِي شُغُلٍ فَاكِهُونَ ﴿٥٥﴾
55. Hakika watu wa Jannah leo wamo katika kushughulika wakifurahi.
هُمْ وَأَزْوَاجُهُمْ فِي ظِلَالٍ عَلَى الْأَرَائِكِ مُتَّكِئُونَ ﴿٥٦﴾
56. Wao na wake zao, wakiwa katika vivuli, juu ya makochi ya fakhari wakiegemea.
لَهُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ وَلَهُم مَّا يَدَّعُونَ ﴿٥٧﴾
57. Watapata humo kila aina ya matunda, na watapata wanavyoomba.
سَلَامٌ قَوْلًا مِّن رَّبٍّ رَّحِيمٍ ﴿٥٨﴾
58. Salaamun![15] Kauli kutoka kwa Rabb Mwenye Kurehemu.
وَامْتَازُوا الْيَوْمَ أَيُّهَا الْمُجْرِمُونَ ﴿٥٩﴾
59. (Itasemwa): Na jitengeni leo enyi wahalifu.
أَلَمْ أَعْهَدْ إِلَيْكُمْ يَا بَنِي آدَمَ أَن لَّا تَعْبُدُوا الشَّيْطَانَ ۖ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ﴿٦٠﴾
60. Je, Sijakuusieni enyi wanaadam kwamba: Msimwabudu shaytwaan, hakika yeye kwenu ni adui bayana!
وَأَنِ اعْبُدُونِي ۚ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ﴿٦١﴾
61. Na kwamba Niabuduni Mimi? Hii ndio njia iliyonyooka.
وَلَقَدْ أَضَلَّ مِنكُمْ جِبِلًّا كَثِيرًا ۖ أَفَلَمْ تَكُونُوا تَعْقِلُونَ ﴿٦٢﴾
62. Na kwa yakini (shaytwaan) amekwishawapotoa viumbe wengi miongoni mwenu. Je basi hamkuwa wenye kutia akilini?
هَـٰذِهِ جَهَنَّمُ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ ﴿٦٣﴾
63. Hii ni Jahannam ambayo mlikuwa mkiahidiwa.
اصْلَوْهَا الْيَوْمَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿٦٤﴾
64. Ingieni leo humo muungue kwa sababu ya mlivyokuwa mkikufuru.
الْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَىٰ أَفْوَاهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَا أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُم بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿٦٥﴾
65. Leo Tunatia vizibo juu ya vinywa vyao, na mikono yao itusemeshe na miguu yao itoe ushahidi kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.[16]
وَلَوْ نَشَاءُ لَطَمَسْنَا عَلَىٰ أَعْيُنِهِمْ فَاسْتَبَقُوا الصِّرَاطَ فَأَنَّىٰ يُبْصِرُونَ ﴿٦٦﴾
66. Na lau Tungelitaka, Tungelipofua macho yao, wakashindana mbio kuitafuta njia, lakini kutoka wapi wataona?
وَلَوْ نَشَاءُ لَمَسَخْنَاهُمْ عَلَىٰ مَكَانَتِهِمْ فَمَا اسْتَطَاعُوا مُضِيًّا وَلَا يَرْجِعُونَ ﴿٦٧﴾
67. Na lau Tungelitaka, Tungeliwaumbua (na kuwalemaza) hapo mahali walipo, basi wasingeliweza kwenda mbele wala wasingerudi.
وَمَن نُّعَمِّرْهُ نُنَكِّسْهُ فِي الْخَلْقِ ۖ أَفَلَا يَعْقِلُونَ ﴿٦٨﴾
68. Na yule Tunayempa umri mkubwa, Tunamrejesha nyuma katika umbo (kumdhoofisha). Je, basi hamtii akilini?
وَمَا عَلَّمْنَاهُ الشِّعْرَ وَمَا يَنبَغِي لَهُ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ وَقُرْآنٌ مُّبِينٌ ﴿٦٩﴾
69. Na Hatukumfunza (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) mashairi[17] na wala haipasi kwake. Haya si chochote isipokuwa ni ukumbusho na Qur-aan bayana.
لِّيُنذِرَ مَن كَانَ حَيًّا وَيَحِقَّ الْقَوْلُ عَلَى الْكَافِرِينَ ﴿٧٠﴾
70. Ili imuonye yule aliye hai,[18] na neno lihakikike juu ya makafiri.
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا خَلَقْنَا لَهُم مِّمَّا عَمِلَتْ أَيْدِينَا أَنْعَامًا فَهُمْ لَهَا مَالِكُونَ ﴿٧١﴾
71. Je, hawaoni kwamba Sisi Tumewaumbia kutokana na yale iliyofanya Mikono Yetu wanyama wa mifugo, basi wao wakawa wanawamiliki?
وَذَلَّلْنَاهَا لَهُمْ فَمِنْهَا رَكُوبُهُمْ وَمِنْهَا يَأْكُلُونَ ﴿٧٢﴾
72. Na Tumewadhalilisha kwao, basi miongoni mwao ni vipando vyao na miongoni mwao wanawala?
وَلَهُمْ فِيهَا مَنَافِعُ وَمَشَارِبُ ۖ أَفَلَا يَشْكُرُونَ ﴿٧٣﴾
73. Na wanapata humo manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru?
وَاتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ آلِهَةً لَّعَلَّهُمْ يُنصَرُونَ ﴿٧٤﴾
74. Na wamejichukulia badala ya Allaah waabudiwa ili wakitumaini kuwa watanusuriwa!
لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَهُمْ وَهُمْ لَهُمْ جُندٌ مُّحْضَرُونَ ﴿٧٥﴾
75. Hawawezi kuwanusuru, na watahudhurishwa (adhabuni) kama askari dhidi ya hao (waliowaabudu).
فَلَا يَحْزُنكَ قَوْلُهُمْ ۘ إِنَّا نَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ﴿٧٦﴾
76. Basi yasikuhuzunishe maneno yao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Hakika Sisi Tunajua yale wanayoyaficha na yale wanayoyatangaza.
أَوَلَمْ يَرَ الْإِنسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ ﴿٧٧﴾
77. Je, binaadam haoni kwamba Sisi Tumemuumba kutokana na tone la manii, mara yeye anakuwa mpinzani bayana?[19]
وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِيَ خَلْقَهُ ۖ قَالَ مَن يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌ ﴿٧٨﴾
78. Na akatupigia mfano, akasahau kuumbwa kwake akasema: Ni nani atakayehuisha mifupa hii na hali imeshaoza na kusagika na kuwa kama vumbi![20]
قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّةٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ ﴿٧٩﴾
79. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ataihuisha Yule Aliyeianzisha mara ya kwanza. Naye Ni Mjuzi wa kila kiumbe.
الَّذِي جَعَلَ لَكُم مِّنَ الشَّجَرِ الْأَخْضَرِ نَارًا فَإِذَا أَنتُم مِّنْهُ تُوقِدُونَ ﴿٨٠﴾
80. Ambaye Amekujaalieni moto kutokana na miti ya kijani, kisha nyinyi mnauwasha.
أَوَلَيْسَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُم ۚ بَلَىٰ وَهُوَ الْخَلَّاقُ الْعَلِيمُ ﴿٨١﴾
81. Je, kwani Yule Aliyeumba mbingu na ardhi (mnadhani) Hana uwezo wa kuumba mfano wao? Sivyo hivyo (Anaweza bila shaka)! Naye Ni Mwingi wa Kuumba Atakavyo, Mjuzi wa yote.
إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٨٢﴾
82. Hakika Amri Yake Anapotaka chochote Hukiambia: Kun! (Kuwa), nacho huwa.
فَسُبْحَانَ الَّذِي بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٨٣﴾
83. Basi Utakasifu Ni wa Ambaye Mkononi Mwake kuna ufalme wa kila kitu, na Kwake mtarejeshwa.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Sababu Ya Kuteremshwa Aayah:
Bonyeza kiungo kifuatacho chenye Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah au Suwrah:
Mema Na Mabaya Aliyoyatanguliza Mtu Na Athari Za Hayo Yote Yanadhibitiwa:
Tafsiyr Ya Aayah: Hakika Sisi ndio Tunaohuisha wafu wote kwa kuwafufua Siku ya Qiyaamah. Na Tunaandika waliyoyafanya ya kheri na ya shari pamoja na athari zao njema ambazo wao walikuwa ndio sababu ya kufanyika katika maisha yao na baada ya kufa kwao kama vile mtoto mwema, ilimu yenye manufaa na swadaqa yenye kuendelea. Pia Tunaandika amali na athari zao mbaya kama vile ushirikina na uasi. Na Tumedhibiti kwa hesabu kila kitu katika Kitabu chenye ufafanuzi, ambacho ni Ummul-Kitaab, na humo ndio marejeo ya yote hayo, nacho ni Al-Lawh Al-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa). Basi ni juu ya mwenye akili airudie nafsi yake, ili awe ni kiigizo katika wema ndani ya maisha yake na baada ya kufa kwake. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Na Hadiyth kadhaa zimethibitisha amali kubakia baada ya mtu kufariki. Miongoni mwazo ni:
Na Hadiyth kadhaa zimethibitisha amali kubakia baada ya mtu kufariki; Miongoni mwazo ni:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَة (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِذَا مَاتَ ابْنُ آدَم انْقَطَعَ عَمَلُهُ إلاَّ مِنْ ثَلاَث: صَدَقَةٍ جَارِيَةٍ أَوْ عِلْمٍ يُنْتَفَعُ بِهِ أَوْ وَلَدٍ صَالِحٍ يَدْعُو لَهُ)) مسلم
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Binaadam akifa, amali zake hukatika isipokuwa mambo matatu: Swadaqa inayoendelea, au ilimu inayonufaisha, au mtoto mwema anayemuombea duaa. [Muslim]
Pia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
مَنْ سَنَّ فِي الْإِسْلَامِ سُنَّةً حَسَنَةً فَعُمِلَ بِهَا بَعْدَهُ كُتِبَ لَهُ مِثْلُ أَجْرِ مَنْ عَمِلَ بِهَا ، وَلَا يَنْقُصُ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْءٌ . وَمَنْ سَنَّ فِي الْإِسْلَامِ سُنَّةً سَيِّئَةً فَعُمِلَ بِهَا بَعْدَهُ كُتِبَ عَلَيْهِ مِثْلُ وِزْرِ مَنْ عَمِلَ بِهَا ، وَلَا يَنْقُصُ مِنْ أَوْزَارِهِمْ شَيْءٌ أخرجه مسلم في صحيحه
“Atakayefufua tendo jema katika Uislaam na watu wakalitenda baada yake, basi ataandikiwa ujira sawa na yule atakayelitenda, na hakipungui chochote katika ujira wao. Na atakayebuni kitendo kibaya katika Uislamu na watu wakakifanya baada yake, basi ataandikiwa dhambi sawa na yule atakayekifanya, na wala hakipungui chochote katika madhambi yao.” [Muslim]
Na kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ
“Tunaandika yale waliyoyakadimisha na athari zao.” [Yaasiyn (36:12)]
Maelezo yamekuja katika Hadiyth ifuatayo:
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ حَوْشَبٍ، قَالَ حَدَّثَنَا عَبْدُ الْوَهَّابِ، قَالَ حَدَّثَنَا حُمَيْدٌ، عَنْ أَنَسٍ، قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " يَا بَنِي سَلِمَةَ أَلاَ تَحْتَسِبُونَ آثَارَكُمْ ". وَقَالَ مُجَاهِدٌ فِي قَوْلِهِ وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ قَالَ خُطَاهُمْ. وَقَالَ ابْنُ أَبِي مَرْيَمَ أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ أَيُّوبَ، حَدَّثَنِي حُمَيْدٌ، حَدَّثَنِي أَنَسٌ، أَنَّ بَنِي سَلِمَةَ، أَرَادُوا أَنْ يَتَحَوَّلُوا، عَنْ مَنَازِلِهِمْ، فَيَنْزِلُوا قَرِيبًا مِنَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ فَكَرِهَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنْ يُعْرُوا {الْمَدِينَةَ} فَقَالَ " أَلاَ تَحْتَسِبُونَ آثَارَكُمْ ". قَالَ مُجَاهِدٌ خُطَاهُمْ آثَارُهُمْ أَنْ يُمْشَى فِي الأَرْضِ بِأَرْجُلِهِمْ.
Amesimulia Humayd (رضي الله عنه): Anas amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Enyi Bani Salimah! Hamdhanii kuwa kwa kila hatua mnayopiga (kuelekea Msikitini) kuna malipo?” Mujaahid akasema kuhusu Kauli Yake Allaah (عزّ وجلّ):
وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ
“Tunaandika yale waliyoyakadimisha na athari zao.” [Yaasiyn (36:12)]
Na Anas alisema kuwa watu wa Bani Salimah walitaka kuhamia sehemu ambayo ni jirani na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Lakini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakupendezwa na fikra ya kuhama makazi yao akawaambia: “Hamdhani ya kuwa mtalipwa kwa nyayo zenu?” Mujaahid alisema: “Nyayo zao ina maana ya hatua zao za kwenda kwa miguu.” [Al-Bukhaariy]
[3] Watu Wa Mji:
Ibn ‘Abbaas na Salaf wengineo wamesema Ni mji wa Antwaakiyyah (Antioch) ambao alikuweko mfalme akiitwa Antiochus ambaye alikuwa akiabudu masanamu. Allaah (سبحانه وتعالى) Akawatumia wajumbe watatu ambao majina yao ni Swaadiq, Swaduwq na Shaluwm, nao wakawakanusha. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[4] Rusuli Au Wajumbe Waliotumiwa:
‘Ulamaa wa Tafsiyr wamekhitilafiana katika kauli mbili kuhusu hao kama walikuwa ni Rusuli wa Allaah (عزّ وجلّ) au walikuwa ni wajumbe wa Nabiy ‘Iysaa ‘(عليه السّلام).
(i) Ni Rusuli wa Allaah kwa sababu Rusuli wa Allaah ni wengi kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ مِنْهُم مَّن قَصَصْنَا عَلَيْكَ وَمِنْهُم مَّن لَّمْ نَقْصُصْ عَلَيْكَ
“Na kwa yakini Tuliwapeleka Rusuli kabla yako. Miongoni mwao wako Tuliokusimulia na miongoni mwao wako ambao Hatukukusimulia.” [Ghaafir (40:78)]
Kauli hii imenukuliwa toka kwa Ibn ‘Abbaas na Ka’b Al-Ahbaar na Wahab bin Munabbih. Lakini kauli hii haisihi kuwanasibishia, kwani Atw-Twabariy ameisimulia katika Jaami’u Al-Bayaan (20/500) ikiwa na mkatiko wa wazi katika Isnaad yake. Na Ibn Taymiyyah ameinukulu katika Al-Jawaab Asw-Swahiyh (2/247), kutokana na kauli ya Abuu Al-‘Aaliyah aliposema kuhusu wao: “Wakasema: Sisi ni Rusuli wa Rabb wa walimwengu.”
Kauli hii imekhitariwa na Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah na Al-Haafidhw Ibn Kathiyr waliohakiki suala, na pia Imaam As-Sa’diy ameitegemea katika Tafsiyr yake “Taysiyr Al-Kariym Ar-Rahmaan (Uk. 693).
(ii) Hao ni wajumbe wa Nabiy ‘Iysaa mwana wa Maryam ambao aliwatuma katika mji wa Antwaakiyah. Na kauli hii imewafikiwa na ‘Ulamaa wengineo.
[5] Ada Ya Washirikina Kutokutaka Kutumiwa Wanaadam Kama Wao.
Rejea Suwrah Al-Furqaan (25:7) kwenye maelezo bayana.
[6] Itikadi Za Shirki Kutabiria Mambo Ya Ghaibu:
Maana ya tatwayyur au twiyarah ni itikadi ya kutabiria nuksi, kisirani, mikosi na kadhaalika.
Katika itikadi za washirikina, walikuwa wakichukua ndege (طير) na humtumilia kutabiri mambo ya ghaibu kwa kutaka kujua kama kuna ishara nzuri au mbaya katika jambo. Mfano wanapotaka kusafiri humrusha ndege yule, akiruka upande wa kulia, basi wanaamini kuwa ni safari ya salama, na kama akiruka upande wa kushoto, basi huwa hawasafiri. Uislamu umekuja na kuondoa shirki kama hiyo kama alivyoharamisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth kadhaa, miongoni mwa hizo ni:
عَنْ أَنَسٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((لَا عَدْوَى وَلَا طِيَرَةَ وَيُعْجِبُنِي الْفَأْلُ)) قَالُوا: وَمَا الْفَأْلُ؟ قَالَ: ((الْكَلِمَةُ الطَّيِّبَةُ))
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna ‘adwaa wala hakuna twiyarah (itikadi ya kutabiri mkosi, nuksi) na inanipendekeza Al-Fa-l.” Wakauliza: Nini Al-Fa-lu? Akajibu: “Neno zuri.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na pia:
عن ابْنِ مَسْعُودٍ مَرْفُوعًا: ((الطِّيَرَةُ شِرْكٌ، الطِّيَرَةُ شِرْكٌ، وَمَا مِنَّا إِلاَّ وَلَكِنَّ اللَّهَ يُذْهِبُهُ بِالتَّوَكُّلِ)) رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ وَالتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ. وَجَعَلَ آخِرَهُ مِنْ قَوْلِ ابْنِ مَسْعُودٍ
Amesimulia Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atw-Twiyarah (itikadi ya kutabiri nuksi, mikosi n.k) ni shirki! Atw-Twiyarah ni shirki. Na hakuna yeyote miongoni mwetu asiyehisi jambo moyoni (kuhusu Atw-Twiyarah) lakini Allaah Huiondoa kwa kutawakali Kwake.” [Hadiyth Marfuw’ ameipokea Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth hii Hasan Swahiyh - Na imetajwa kwamba kauli ya mwisho ni ya Ibn Mas’uwd]
Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akafundisha kubadilisha hayo kwa:
عنْ عُرْوَةَ بْنِ عامِرِ (رضي الله عنه) قال: ذُكِرتِ الطَّيَرَةُ عِنْد رَسُولِ اللَّه صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فقَالَ: ((أحْسَنُهَا الْفَألُ، وَلا تَرُدُّ مُسْلِماً، فَإذا رأى أحَدُكُمْ ما يَكْرَه، فَلْيقُلْ: اللَّهُمَّ لا يَأتى بالحَسَناتِ إلاَّ أنتَ، وَلا يَدْفَعُ السَّيِّئاتِ إلاَّ أنْتَ، وَلا حوْلَ وَلا قُوَّةَ إلاَّ بك)) حديثٌ صَحيحٌ رَوَاهُ أبو داودُ بإسنادٍ صَحيحٍ
Amesimulia ‘Urwah bin ‘Aamir (رضي الله عنه): Ilitajwa habari ya kupiga fali mbaya (mkosi) mbele ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ilio bora zaidi ni kupiga fali nzuri, wala (kupiga fali mbaya) haimrudishi Muislamu (kutokutenda aliloazimia). Mmoja wenu atakapoona analochukia, aseme:
اللَّهُمَّ لا يَأتى بالحَسَناتِ إلاَّ أنتَ، وَلا يَدْفَعُ السَّيِّئاتِ إلاَّ أنْتَ، وَلا حوْلَ وَلا قُوَّةَ إلاَّ بك
Ee Allaah, hakuna anayeweza kuleta mambo mema isipokuwa ni Wewe, wala hakuna anayeweza kukinga mabaya isipokuwa ni Wewe. Hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka Kwako. [Hadiyth Swahiyh ameipokea Abu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]
[7] Mtu Aliyetoka Mbali Ya Mji:
Salaf wamesema kuwa jina lake ni Habiyb na wengine wamesema ni Habiyb Bin Muraa.
Watu wa mji walidhamiria kuwaua Rusuli (au wajumbe) wao, basi akawajia mtu mbio kutoka upande wa mbali wa mji ili kuwanusuru na watu wao. Naye ni Habiyb ambaye alikuwa ni msukaji kamba, na alikuwa mgonjwa wa ukoma uliomwathiri kwa haraka. Na alikuwa akitoa swadaqa kwa wingi, akitoa nusu ya mapato yake kama swadaqa, na alikuwa na mwono ulionyooka. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[8] Takrima Ya Mtu Mwema Ya Kuingizwa Jannah (Peponi):
Aayah hii namba (25) na ifuatayo namba (26).
Kutoka kwa baadhi ya Swahaba, kutoka Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) amesema: Walimkanyaga na kumponda ponda kwa miguu yao mpaka bomba lake la kupitisha hewa likatokea kwenye duburi yake. Allaah (سبحانه وتعالى) Akamuingiza Jannah akiwa anaruzukiwa humo kila aina ya neema za kudumu. Na hivyo ni jazaa na thawabu kutokana na subira yake na himma yake ya kuwalingania watu wake wahidike. Na akaondoshewa ugonjwa wake duniani, na huzuni yake na mateso yake. Basi alipoingizwa humo akasema: Laiti watu wangu wangelijua.” Takrima za Allaah humo kwake. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[9] Aayah (آية) : Ishara, Ushahidi Wa Muumbaji, Mkadiriaji, Mweza Na Kadhaalika:
Rejea Ash-Shu’araa (26:8) kwenye maana za آية (Aayah) au آيات (Aayaat).
Aayah zifuatazo, kama vile Aayah katika Suwrah nyenginezo, mfano: An-Nahl (16:11-13), Ar-Ruwm (30:20-25), zimetajwa آية (Aayah) au آيات (Aayaat) ambazo maana zake ni: Ishara, Dalili, Hoja, Burhani, Muujiza, Mazingatio, Mafunzo, Ushahidi na kadhaalika. Aayah ua Aayaat hizo, ni dalili ya wazi kubisa za Uwepo wa Allaah (سبحانه وتعالى) Muumbaji wa kila kitu, na kwamba Ni Mmoja Pekee na Hana mshirika katika Uumbaji Wake, hivyo basi Yeye Ndiye Anayestahiki kuabudiwa.
Na kuhusu kuwaradd washirikina kwamba hawawezi kuleta uumbaji kama Uumbaji wa Allaah (سبحانه وتعالى), rejea Luqmaan (31:10-11) na Al-Ahqaaf (46:4) kwenye maelezo bayana na rejea nyenginezo.
[10] Allaah (سبحانه وتعالى) Kuhuisha Ardhi Iliyokufa Ni Mfano Wa Kufufuliwa Watu:
Rejea Ar-Ruwm (30:50), Al-An’aam (6:95).
[12] Takdiri: Qudura, Uwezo Wa Allaah (سبحانه وتعالى), Ukadiriaji:
Katika Aayah za Suwrah hii tukufu Yaasiyn (36:33-42), Allaah (سبحانه وتعالى) Anadhihirisha Qudura (Uwezo) na Takdiri (Ukadiriaji) Yake katika kuumba vitu ulimwenguni; katika ardhi, bahari na falaki (angani) kwa ajili ya manufaa ya viumbe Vyake ili waweze kuishi katika ulimwengu huu.
Katika Aayah za Suwrah hii tukufu Yaasiyn (36:33-42), Allaah (سبحانه وتعالى) Anadhihirisha Qudura (Uwezo) na Takdiri (Ukadiriaji) Yake katika kuumba vitu ulimwenguni; katika ardhi, bahari na falaki (angani) kwa ajili ya manufaa ya viumbe Vyake ili waweze kuishi katika ulimwengu huu.
Vya ardhini ni kama mimea ya kila aina, mazao na matunda yake, majani, na miti shamba yenye shifaa (poza) ya maradhi. Pia Ameumba milima na majabali ambayo nayo yana faida mbalimbali kama kuweko ndani yake mapango ya kujifichia, na nyuki ambao Allaah Amewapa ilhamu waende humo kutoa asali yenye shifaa ya maradhi pamoja na faida nyenginezo. Rejea An-Nahl (16:68-69). Pia Ameumba wanyama wa ardhini, Akahalalisha baadhi yao nyama zao kuliwa na kunywewa maziwa yao. Baadhi yao wanatoa sufi na wengine ngozi ambazo wanaadam wananufaika nazo kwa kutengenezea nguo, fanicha na vifaa mbalimbali. Rejea An-Nahl (16:80). Na pia Amewatiisha wanyama wengineo kwa binaadam ili wawatumie kwa vipando na utumikaji wa mashambani na kadhaalika. Rejea Suwrah hii Yaasiyn (36:71-73), na pia An-Nahl (16:5-8). Pia katika tumbo la ardhi, Allaah Amejaalia ipatikane humo gesi na petroli vitu ambavyo vinahitajika katika matumizi ya wanaadam. Pia humo ardhini, Allaah Amejaalia yapatikane madini yanayochimbwa ambayo yana umuhimu mkubwa mno katika maisha ya wanaadam kama vile metali, chuma, shaba, zinki, nikeli, bati, risasi. n.k. Hali kadhaalika, zinapatikana humo dhahabu, almasi, fedha na johari nyenginezo za thamani ambazo wanaadam wananufaika nazo kwa mapambo na biashara. Haya yote na mengineyo mengi mno tunayoyajua na tusiyoyajua, tunayoyakumbuka na tusiyoyakumbuka ni katika Neema na Fadhila za Allaah (سبحانه وتعالى) na ni “Takdiri ya Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.”
Na baharini, Allaah Amejaalia pia ipatikane nyama safi ya kila aina ya samaki. Vile vile Amejaalia baharini kuweko vitu vya thamani vya mapambo kama lulu na marijani. Na pia Uwezo Wake wa Kuitiisha bahari hata merikebu ziweze kupita kuwasafirisha watu ulimwenguni huku zikibeba mizigo mikubwa mno. Haya yote na mengineyo mengi mno tunayoyajua na tusiyoyajua, tunayoyakumbuka na tusiyoyakumbuka ni katika “Takdiri ya Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.”
Na katika falaki (angani), Allaah Amewawezesha ndege waruke bila ya kushikiliwa na chochote. Rejea Al-Mulk (67:19), An-Nahl (16:79), na An-Nuwr (24:41). Na katika Uwezo na Qudura Yake, ni kutiisha anga ili ndege za kuwasafirisha watu ulimwenguni na mizigo ziweze kupaa na kupita. Hali kadhalika, Anatiisha mawingu ya mvua huko mbinguni, mvua ikawateremkia wanaadam na wanyama wapate kunywa na kulisha wanyama wao na iwanyeshee mashambani mwao. Isitoshe, katika falaki (angani), Allaah Ameumba sayari mbali mbali pamoja na jua, mwezi, nyota n.k ambavyo Anavithibiti na Kuviendesha kwa ajili ya kupata usiku na mchana, na kuendeleza mzunguko wake ili yapatikane masaa, masiku na miaka. Rejea Al-Israa (17:12). Na Uendeshaji Wake huo wa sayari, jua, mwezi, nyota n.k hauendi kinyume wala hausimami hadi Atakapotaka Mwenyewe. Haya yote na mengineyo mengi mno tunayoyajua na tusiyoyajua, tunayoyakumbuka na tusiyoyakumbuka ni katika “Takdiri ya Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.”
Hizo ndizo Neema Zake, miongoni mwa Neema nyingi mno ambazo baadhi yake tunazijua na tunazikumbuka, na baadhi nyingine hatuzijui wala hatuzikumbuki, hivyo hatuwezi kuziorodhesha hesabuni. Rejea Suwrah Ibraahiym (14:34) ambako kuna maelezo kuhusu Neema za Allaah (عزّ وجلّ) na kwamba haiwezekani kuziorodhesha hesabuni.
Na Neema hizi zote ni uthibitisho juu ya Uwezo Wake mkubwa. Na Anazitaja katika Aayah nyingi nyenginezo ambazo miongoni mwazo zipo kwenye Aal-‘Imraan (3:190), na (3:26-27), Al-An’aam (6:96), Ibraahiym (14:32-33), An-Nahl (16:3-16), (16:66-69), na (16:81), Al-Hajj (22:65), Luqmaan (31:20), Al-Jaathiyah (45:12-13), Ar-Ra’d (13:2-4), Az-Zumar (39:5), Al-Baqarah (2:164), Al-A’raaf (7:54), Faatwir (35:12-13), na kwengineko katika Qur-aan.
Basi hayo yote ni dalili juu ya Upweke wa Allaah (عزّ وجلّ), na Uumbaji Wake ambao hakuna yeyote awezaye kuumba kama Anavyoumba Yeye Allaah (عزّ وجلّ). Ndipo Anawataka washirikina na makafiri walete wao uumbaji wao kama huu kama wanaweza! Rejea Luqmaan (31:10-11), Al-Ahqaaf (46:4) kwenye maelezo bayana na rejea nyenginezo.
[15] Salaam, Salaamun ‘Alaykum Ni Maamkizi Ya Jannah (Peponi).
Kama vile ilivyokuwa maamkizi ya Waislamu duniani ni Assalaamu ‘alaykum, na Peponi pia maamkizi ni hayo hayo. Bali huko ni maamkizi yatokayo kwa Allaah (سبحانه وتعالى), na mara nyengine kutoka kwa Malaika, na mara nyengine ni maamkizi baina ya Waumini kwa Waumini.
Rejea Al-A’raaf (7:46), Yuwnus (10:10), Ar-Ra’d (13:24), Ibraahiym (14:23), An-Nahl (16:32), Al-Ahzaab (33:44), Az-Zumar (39:73), Al-Furqaan (25:75), Qaaf (50:34),
Na Jannah pia imeitwa Daarus-salaam (Nyumba ya amani). Rejea Al-An’aam (6:127), Yuwnus (10:25).
[16] Viungo Vya Mwili Vitashuhudia Matendo Ya Binaadam:
Rejea Fusw-Swilat: (41:20-22), An-Nuwr (24:24).
Na binaadam hataweza kukanusha ovu lolote alilolitenda duniani: Rejea Al-Israa (17:13-14).
[17] Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Si Mshairi:
Tafsiyr ya Aayah (69-70):
Na Sisi Hatukumfundisha Rasuli Wetu Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) mashairi, na haiwezekani kabisa yeye kuwa mshairi. Hiki alichokuja nacho si kingine chochote bali ni ukumbusho ambao wenye akili huuzingatia na kuukumbuka. Ukumbusho huu ni hii Qur-aan ambayo inaweka wazi haki na baatwil kwa dalili bayana, na inabainisha hukumu zake, sharia zake na mawaidha yake kwa lugha nyepesi, ili apate kuonyeka na kufaidika kila mwenye moyo ulio hai na baswiyrah yenye nuru, na adhabu ipate kuthibitika kwa wenye kumpinga Allaah. Kwa hawa, Hoja ya Allaah isiyo na utata wowote ambayo imebainishwa na Qur-aan, itakuja kusimama dhidi yao. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Rejea Al-Furqaan (25:4) kwenye uchambuzi na rejea mbalimbali kuhusu: Kufru Za Washirikina Kumkanusha, Kumsingizia, Kumpachika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Sifa Kadhaa Ovu, Kumfanyia Istihzai Yeye Pamoja Na Kuifanyia Istihzai Qur-aan Na Kuikanusha:
[18] Qur-aan Imuonye Hai:
Qur-aan imuonye ambaye moyo wake uko hai na wenye fahamu, kwani huyo ndiye anayetakaswa na hii Qur-aan, na ndiye anayezidisha ilimu na amali kutoka humo, na Qur-aan inakuwa kwa moyo wake kama mvua kwa ardhi nzuri yenye kuotesha kwa wingi. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[19] Sababu Ya Kuteremshwa Aayah:
Kuanzia Aayah hii (77) hadi Aayah namba (83), bonyeza kiungo kifuatacho chenye Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah au Suwrah.
[20] Washirikina Hawakuamini Kwamba Watafufuliwa:
Rejea Al-Israa (17:49-52) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali kuhusu makafiri kutokuamini kufufuliwa. Rejea pia Al-Waaqi’ah (56:47-50), Ar-Ra’d (13:5). Na pia zifuatazo ni baadhi ya Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى) kuthibitisha Uwezo Wake wa kuwafufua viumbe:
أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَلَّن نَّجْمَعَ عِظَامَهُ﴿٣﴾ بَلَىٰ قَادِرِينَ عَلَىٰ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُ﴿٤﴾
“Je, anadhani binaadam kwamba Hatutoikusanya mifupa yake? Sivyo hivyo! Bali Tuna Uwezo wa kusawazisha sawasawa ncha za vidole vyake.” [Al-Qiyaamah (75:3-4)]
Rejea pia:
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَلَمْ يَعْيَ بِخَلْقِهِنَّ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ ۚ بَلَىٰ إِنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٣٣﴾
“Je, hawaoni kwamba Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na wala Hakuchoka kwa kuziumba kwake, kwamba Yeye Ni Muweza wa Kuwafufua wafu. Naam bila shaka! Hakika Yeye juu ya kila kitu Ni Muweza.” [Al-Ahqaaf (46:33)]
الصًّفَّات
037-Asw-Swaaffaat
037-Asw-Swaaffaat: Utangulizi Wa Suwrah [259]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالصَّافَّاتِ صَفًّا ﴿١﴾
1. Naapa kwa (Malaika) wanaojipanga safusafu.
فَالزَّاجِرَاتِ زَجْرًا ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa (Malaika) wanaosukumiza mbali mawingu.
فَالتَّالِيَاتِ ذِكْرًا ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa (Malaika) wanaosoma Maneno ya Allaah.
إِنَّ إِلَـٰهَكُمْ لَوَاحِدٌ ﴿٤﴾
4. Hakika Mwabudiwa wenu wa haki bila shaka Ni Mmoja.
رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَرَبُّ الْمَشَارِقِ ﴿٥﴾
5. Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, na Rabb wa mapambazuko.
إِنَّا زَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِزِينَةٍ الْكَوَاكِبِ ﴿٦﴾
6. Hakika Sisi Tumeipamba mbingu ya dunia kwa mapambo ya nyota.[1]
وَحِفْظًا مِّن كُلِّ شَيْطَانٍ مَّارِدٍ ﴿٧﴾
7. Na hifadhi kutokana na kila shaytwaan asi.
لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى الْمَلَإِ الْأَعْلَىٰ وَيُقْذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٍ ﴿٨﴾
8. Hawawezi kulisikiliza kundi la juu lililotukuzwa, kwani wanavurumishwa kila upande.
دُحُورًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ وَاصِبٌ ﴿٩﴾
9. Wakifukuziliwa mbali, na watapata adhabu ya kuendelea.
إِلَّا مَنْ خَطِفَ الْخَطْفَةَ فَأَتْبَعَهُ شِهَابٌ ثَاقِبٌ ﴿١٠﴾
10. Isipokuwa yule atakayenyakua kitu kwa kuiba, basi kitamwandama kimondo kiwakacho.
فَاسْتَفْتِهِمْ أَهُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَم مَّنْ خَلَقْنَا ۚ إِنَّا خَلَقْنَاهُم مِّن طِينٍ لَّازِبٍ ﴿١١﴾
11. Basi waulize: Je, wao ni viumbe wenye nguvu zaidi, au wale Tuliowaumba? Hakika Sisi Tumewaumba kutokana na udongo unaonata.
بَلْ عَجِبْتَ وَيَسْخَرُونَ ﴿١٢﴾
12. Bali umestaajabu, nao wanafanya dhihaka.
وَإِذَا ذُكِّرُوا لَا يَذْكُرُونَ ﴿١٣﴾
13. Na wanapokumbushwa, hawakumbuki.
وَإِذَا رَأَوْا آيَةً يَسْتَسْخِرُونَ ﴿١٤﴾
14. Na wanapoona Aayah (Ishara, Dalili) wanazidi kufanya dhihaka.
وَقَالُوا إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ ﴿١٥﴾
15. Na wanasema: Haya si chochote isipokuwa ni sihiri bayana.
أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ ﴿١٦﴾
16. Je, hivi tukifa, na tukawa vumbi na mifupa, hivi sisi tutafufuliwa?[2]
أَوَآبَاؤُنَا الْأَوَّلُونَ ﴿١٧﴾
17. Je, pia na baba zetu wa awali?
قُلْ نَعَمْ وَأَنتُمْ دَاخِرُونَ ﴿١٨﴾
18. Sema: Naam (mtafufuliwa), hali na nyinyi ni madhalili.
فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ فَإِذَا هُمْ يَنظُرُونَ ﴿١٩﴾
19. Kwani huo ni mngurumo (wa baragumu) mmoja tu, tahamaki hao wanatazama!
وَقَالُوا يَا وَيْلَنَا هَـٰذَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿٢٠﴾
20. Na watasema: Ole wetu! Hii ni Siku ya Malipo.
هَـٰذَا يَوْمُ الْفَصْلِ الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ ﴿٢١﴾
21. (Wataambiwa): Hii ndio Siku ya hukumu ambayo mlikuwa mkiikadhibisha.
احْشُرُوا الَّذِينَ ظَلَمُوا وَأَزْوَاجَهُمْ وَمَا كَانُوا يَعْبُدُونَ ﴿٢٢﴾
22. (Malaika wataamrishwa): Wakusanyeni wale waliodhulumu na wenziwao na yale waliyokuwa wakiyaabudu.
مِن دُونِ اللَّـهِ فَاهْدُوهُمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْجَحِيمِ ﴿٢٣﴾
23. Badala ya Allaah. Basi waongozeni kwenye njia ya moto uwakao vikali mno.
وَقِفُوهُمْ ۖ إِنَّهُم مَّسْئُولُونَ ﴿٢٤﴾
24. Wasimamisheni. Hakika wao wataulizwa.
مَا لَكُمْ لَا تَنَاصَرُونَ ﴿٢٥﴾
25. Mna nini hamnusuriani?
بَلْ هُمُ الْيَوْمَ مُسْتَسْلِمُونَ ﴿٢٦﴾
26. Bali wao leo wamesalimu amri.
وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٢٧﴾
27. Na watakabiliana wenyewe kwa wenyewe kuulizana.
قَالُوا إِنَّكُمْ كُنتُمْ تَأْتُونَنَا عَنِ الْيَمِينِ ﴿٢٨﴾
28. Watasema: Hakika nyinyi mlikuwa mkitujia kwa nguvu na ushawishi.
قَالُوا بَل لَّمْ تَكُونُوا مُؤْمِنِينَ ﴿٢٩﴾
29. Watasema: Bali nyinyi wenyewe hamkuwa wenye kuamini.
وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيْكُم مِّن سُلْطَانٍ ۖ بَلْ كُنتُمْ قَوْمًا طَاغِينَ ﴿٣٠﴾
30. Na hatukuwa na madaraka yoyote juu yenu, bali mlikuwa watu wapindukao mipaka kuasi.
فَحَقَّ عَلَيْنَا قَوْلُ رَبِّنَا ۖ إِنَّا لَذَائِقُونَ ﴿٣١﴾
31. Basi ikahakiki juu yetu Kauli ya Rabb wetu. Hakika sisi bila shaka tutaonja (adhabu).
فَأَغْوَيْنَاكُمْ إِنَّا كُنَّا غَاوِينَ ﴿٣٢﴾
32. Kisha tukakupotoeni (kwa sababu) sisi (wenyewe) tulikuwa ni wenye kupotoka.
فَإِنَّهُمْ يَوْمَئِذٍ فِي الْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ ﴿٣٣﴾
33. Basi hakika wao Siku hiyo, watashirikiana katika adhabu.
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ ﴿٣٤﴾
34. Hivyo ndivyo Tuwafanyavyo wahalifu.
إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ يَسْتَكْبِرُونَ ﴿٣٥﴾
35. Wao walipokuwa wakiambiwa: Laa ilaaha illa Allaah (hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah), wakitakabari.
وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ ﴿٣٦﴾
36. Na wanasema: Je, sisi kweli tuache waabudiwa wetu kwa ajili ya mshairi majnuni?![3]
بَلْ جَاءَ بِالْحَقِّ وَصَدَّقَ الْمُرْسَلِينَ ﴿٣٧﴾
37. Bali (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) amekuja kwa haki, na amewasadikisha Rusuli (waliotangulia).
إِنَّكُمْ لَذَائِقُو الْعَذَابِ الْأَلِيمِ ﴿٣٨﴾
38. Hakika nyinyi (makafiri) bila shaka ni wenye kuionja adhabu iumizayo.
وَمَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿٣٩﴾
39. Na hamlipwi isipokuwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿٤٠﴾
40. Isipokuwa Waja wa Allaah waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.
أُولَـٰئِكَ لَهُمْ رِزْقٌ مَّعْلُومٌ ﴿٤١﴾
41. Hao watapata riziki maalumu.[4]
فَوَاكِهُ ۖ وَهُم مُّكْرَمُونَ ﴿٤٢﴾
42. Matunda. Nao ni wenye kukirimiwa.
فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿٤٣﴾
43. Katika Jannaat za Neema.
عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَابِلِينَ ﴿٤٤﴾
44. Juu ya makochi ya enzi wakikabiliana.
يُطَافُ عَلَيْهِم بِكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍ ﴿٤٥﴾
45. Wanazungushiwa gilasi za mvinyo kutoka chemchemu.
بَيْضَاءَ لَذَّةٍ لِّلشَّارِبِينَ ﴿٤٦﴾
46. Mweupe, wenye ladha kwa wanywaji.
لَا فِيهَا غَوْلٌ وَلَا هُمْ عَنْهَا يُنزَفُونَ ﴿٤٧﴾
47. Hamna humo madhara yoyote, na wala wao kwayo hawataleweshwa.
وَعِندَهُمْ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ عِينٌ ﴿٤٨﴾
48. Na watakuwa nao wanawake wenye staha wanaoinamisha macho, wenye macho mapana mazuri ya kuvutia.
كَأَنَّهُنَّ بَيْضٌ مَّكْنُونٌ ﴿٤٩﴾
49. (Wanyororo, watakasifu) kama kwamba wao ni mayai yaliyohifadhiwa.
فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٥٠﴾
50. Basi watakabiliana wenyewe kwa wenyewe wakiulizana.[5]
قَالَ قَائِلٌ مِّنْهُمْ إِنِّي كَانَ لِي قَرِينٌ ﴿٥١﴾
51. Aseme msemaji miongoni mwao: Hakika mimi nilikuwa na rafiki mwandani.
يَقُولُ أَإِنَّكَ لَمِنَ الْمُصَدِّقِينَ ﴿٥٢﴾
52. Aliyekuwa akiniambia: Je, hivi wewe ni miongoni mwa wanaosadiki?
أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَدِينُونَ ﴿٥٣﴾
53. Je tutakapokufa, tukawa udongo na mifupa, eti kweli sisi tutahukumiwa na kulipwa kikamilifu?
قَالَ هَلْ أَنتُم مُّطَّلِعُونَ ﴿٥٤﴾
54. Atasema: Je, mngependa kuchungulia (nami motoni)?
فَاطَّلَعَ فَرَآهُ فِي سَوَاءِ الْجَحِيمِ ﴿٥٥﴾
55. Basi akapitisha macho, akamuona (rafiki yake) yuko katikati ya moto uwakao vikali mno.
قَالَ تَاللَّـهِ إِن كِدتَّ لَتُرْدِينِ ﴿٥٦﴾
56. Akasema: Ta-Allaahi![6] Ulikaribia kuniangamiza!
وَلَوْلَا نِعْمَةُ رَبِّي لَكُنتُ مِنَ الْمُحْضَرِينَ ﴿٥٧﴾
57. Na lau kama si Neema ya Rabb wangu, bila shaka ningelikuwa miongoni mwa wahudhurishwao (motoni).
أَفَمَا نَحْنُ بِمَيِّتِينَ ﴿٥٨﴾
58. Je, sisi hatutakufa tena?
إِلَّا مَوْتَتَنَا الْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ ﴿٥٩﴾
59. Isipokuwa mauti yetu ya awali, nasi hatutaadhibiwa!
إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿٦٠﴾
60. Hakika huku ndiko kufuzu kukubwa.
لِمِثْلِ هَـٰذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ ﴿٦١﴾
61. Kwa (ajili ya kupata) mfano wa haya basi watende wenye kutenda.
أَذَٰلِكَ خَيْرٌ نُّزُلًا أَمْ شَجَرَةُ الزَّقُّومِ ﴿٦٢﴾
62. Je hiyo (Jannah) ni mapokezi bora, au mti wa zaqquwm (motoni)?[7]
إِنَّا جَعَلْنَاهَا فِتْنَةً لِّلظَّالِمِينَ ﴿٦٣﴾
63. Hakika Sisi Tumeufanya (zaqquwm) kuwa ni jaribio kwa madhalimu.
إِنَّهَا شَجَرَةٌ تَخْرُجُ فِي أَصْلِ الْجَحِيمِ ﴿٦٤﴾
64. Hakika huo ni mti unaotoka katika kina cha moto uwakao vikali mno.
طَلْعُهَا كَأَنَّهُ رُءُوسُ الشَّيَاطِينِ ﴿٦٥﴾
65. Mashada ya matunda yake ni kana kwamba vichwa vya mashaytwaan.
فَإِنَّهُمْ لَآكِلُونَ مِنْهَا فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ ﴿٦٦﴾
66. Basi hakika wao, bila shaka watakula humo na watajaza matumbo yao kwayo.
ثُمَّ إِنَّ لَهُمْ عَلَيْهَا لَشَوْبًا مِّنْ حَمِيمٍ ﴿٦٧﴾
67. Kisha hakika wao watapata mchanganyiko wa maji yachemkayo.
ثُمَّ إِنَّ مَرْجِعَهُمْ لَإِلَى الْجَحِيمِ ﴿٦٨﴾
68. Kisha marejeo yao bila shaka yatakuwa kuelekea kwenye moto uwakao vikali mno.
إِنَّهُمْ أَلْفَوْا آبَاءَهُمْ ضَالِّينَ ﴿٦٩﴾
69. Hakika wao waliwakuta baba zao wamepotoka.
فَهُمْ عَلَىٰ آثَارِهِمْ يُهْرَعُونَ ﴿٧٠﴾
70. Na wao wakaharakiza kufuata athari zao.
وَلَقَدْ ضَلَّ قَبْلَهُمْ أَكْثَرُ الْأَوَّلِينَ ﴿٧١﴾
71. Na kwa yakini walipotoka kabla yao watu wengi wa awali.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا فِيهِم مُّنذِرِينَ ﴿٧٢﴾
72. Na kwa yakini Tuliwatumia waonyaji.
فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُنذَرِينَ ﴿٧٣﴾
73. Basi tazama vipi ilikuwa hatima ya walioonywa?
إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿٧٤﴾
74. Isipokuwa Waja wa Allaah waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.[8]
وَلَقَدْ نَادَانَا نُوحٌ فَلَنِعْمَ الْمُجِيبُونَ ﴿٧٥﴾
75. Na kwa yakini Nuwh alituita (Tumnusuru). Nasi kwa hakika Ni Waitikiaji bora kabisa.
وَنَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ ﴿٧٦﴾
76. Na Tukamuokoa pamoja na ahli zake kutokana na janga kubwa mno.
وَجَعَلْنَا ذُرِّيَّتَهُ هُمُ الْبَاقِينَ ﴿٧٧﴾
77. Na Tukajaalia dhuria wake wao ndio wenye kubakia.[9]
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ ﴿٧٨﴾
78. Na Tukamuachia (sifa nzuri) kwa karne za baadaye.
سَلَامٌ عَلَىٰ نُوحٍ فِي الْعَالَمِينَ ﴿٧٩﴾
79. Salaamun! (Amani) iwe juu ya Nuwh ulimwenguni.
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿٨٠﴾
80. Hakika hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.[10]
إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿٨١﴾
81. Hakika yeye ni miongoni mwa Waja Wetu Waumini.
ثُمَّ أَغْرَقْنَا الْآخَرِينَ ﴿٨٢﴾
82. Kisha Tukawagharikisha wengineo.
وَإِنَّ مِن شِيعَتِهِ لَإِبْرَاهِيمَ ﴿٨٣﴾
83. Na hakika katika waliofuata njia yake (ya Tawhiyd) ni Ibraahiym.
إِذْ جَاءَ رَبَّهُ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ ﴿٨٤﴾
84. Alipomjia Rabb wake kwa moyo uliosalimika.[11]
إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ مَاذَا تَعْبُدُونَ ﴿٨٥﴾
85. Alipomwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini?
أَئِفْكًا آلِهَةً دُونَ اللَّـهِ تُرِيدُونَ ﴿٨٦﴾
86. Je, kwa uzushi tu, mnataka waabudiwa badala ya Allaah?
فَمَا ظَنُّكُم بِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٨٧﴾
87. Basi nini dhana yenu kuhusu Rabb wa walimwengu?
فَنَظَرَ نَظْرَةً فِي النُّجُومِ ﴿٨٨﴾
88. Akatupa jicho juu mbinguni kutafakuri (udhuru wa kuwapa).
فَقَالَ إِنِّي سَقِيمٌ ﴿٨٩﴾
89. Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa.
فَتَوَلَّوْا عَنْهُ مُدْبِرِينَ ﴿٩٠﴾
90. Wakaachana naye wakimgeukilia mbali kwenda zao.
فَرَاغَ إِلَىٰ آلِهَتِهِمْ فَقَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ ﴿٩١﴾
91. Akaenda kwa siri kwa waabudiwa wao, akasema: Mbona hamli?
مَا لَكُمْ لَا تَنطِقُونَ ﴿٩٢﴾
92. Mna nini! Mbona hamsemi?
فَرَاغَ عَلَيْهِمْ ضَرْبًا بِالْيَمِينِ ﴿٩٣﴾
93. Akayakamia (masanamu) na kuyapiga kwa mkono wa kulia.
فَأَقْبَلُوا إِلَيْهِ يَزِفُّونَ ﴿٩٤﴾
94. Wakamjia mbio kwa vishindo.
قَالَ أَتَعْبُدُونَ مَا تَنْحِتُونَ ﴿٩٥﴾
95. Akasema: Je, mnaabudu vile mnavyovichonga?
وَاللَّـهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ ﴿٩٦﴾
96. Na hali Allaah Amekuumbeni pamoja na vile mnavyovifanya?
قَالُوا ابْنُوا لَهُ بُنْيَانًا فَأَلْقُوهُ فِي الْجَحِيمِ ﴿٩٧﴾
97. Wakasema: Mjengeeni jengo, kisha mtupeni katika moto uwakao vikali mno.
فَأَرَادُوا بِهِ كَيْدًا فَجَعَلْنَاهُمُ الْأَسْفَلِينَ ﴿٩٨﴾
98. Wakamkusudia njama, lakini Tukawafanya wao ndio wa chini kabisa.
وَقَالَ إِنِّي ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّي سَيَهْدِينِ ﴿٩٩﴾
99. Akasema: Hakika mimi ni mwenye kwenda kwa Rabb wangu, Ataniongoza.
رَبِّ هَبْ لِي مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١٠٠﴾
100. Rabb wangu! Nitunukie miongoni mwa Swalihina.
فَبَشَّرْنَاهُ بِغُلَامٍ حَلِيمٍ ﴿١٠١﴾
101. Basi Tukambashiria ghulamu mvumilivu.
فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ السَّعْيَ قَالَ يَا بُنَيَّ إِنِّي أَرَىٰ فِي الْمَنَامِ أَنِّي أَذْبَحُكَ فَانظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ قَالَ يَا أَبَتِ افْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ مِنَ الصَّابِرِينَ ﴿١٠٢﴾
102. Alipofikia makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, akasema: Ee mwanangu! Hakika mimi naona njozi usingizini kwamba mimi nakuchinja, basi tazama, unaonaje? (Ismaa’iyl) akasema: Ee baba yangu kipenzi! Fanya yale unayoamrishwa, utanikuta In Shaa Allaah miongoni mwa wanaosubiri.
فَلَمَّا أَسْلَمَا وَتَلَّهُ لِلْجَبِينِ ﴿١٠٣﴾
103. Basi wote wawili walipojisalimisha, na akamlaza kifudifudi juu ya kipaji.
وَنَادَيْنَاهُ أَن يَا إِبْرَاهِيمُ ﴿١٠٤﴾
104. Na tukamwita: Ee Ibraahiym.
قَدْ صَدَّقْتَ الرُّؤْيَا ۚإِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ﴿١٠٥﴾
105. Kwa yakini umesadikisha njozi. Hakika hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.
إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْبَلَاءُ الْمُبِينُ ﴿١٠٦﴾
106. Hakika hili bila shaka ni jaribio bayana.
وَفَدَيْنَاهُ بِذِبْحٍ عَظِيمٍ ﴿١٠٧﴾
107. Na Tukamtolea fidia kwa dhabihu adhimu.[12]
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ ﴿١٠٨﴾
108. Na Tukamuachia (sifa nzuri) kwa karne za baadaye.
سَلَامٌ عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ ﴿١٠٩﴾
109. Salaamun! (Amani) iwe juu ya Ibraahiym.
كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١١٠﴾
110. Hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.
إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿١١١﴾
111. Hakika yeye ni miongoni mwa Waja Wetu Waumini.
وَبَشَّرْنَاهُ بِإِسْحَاقَ نَبِيًّا مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿١١٢﴾
112. Na Tukambashiria Is-haaq; Nabiy miongoni mwa Swalihina.
وَبَارَكْنَا عَلَيْهِ وَعَلَىٰ إِسْحَاقَ ۚ وَمِن ذُرِّيَّتِهِمَا مُحْسِنٌ وَظَالِمٌ لِّنَفْسِهِ مُبِينٌ ﴿١١٣﴾
113. Na Tukambarikia yeye na Is-haaq. Na katika vizazi vyao wawili kuna mhisani na aliyejidhulumu nafsi yake waziwazi.
وَلَقَدْ مَنَنَّا عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَارُونَ ﴿١١٤﴾
114. Na kwa yakini Tuliwafanyia fadhila Muwsaa na Haaruwn.
وَنَجَّيْنَاهُمَا وَقَوْمَهُمَا مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ ﴿١١٥﴾
115. Na Tukawaokoa wote wawili na watu wao kutokana na janga kuu.[13]
وَنَصَرْنَاهُمْ فَكَانُوا هُمُ الْغَالِبِينَ ﴿١١٦﴾
116. Na Tukawanusuru, basi wakawa wao ndio wenye kushinda.
وَآتَيْنَاهُمَا الْكِتَابَ الْمُسْتَبِينَ ﴿١١٧﴾
117. Na Tukawapa Kitabu kinachojibainisha chenyewe waziwazi.
وَهَدَيْنَاهُمَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿١١٨﴾
118. Na Tukawaongoza njia iliyonyooka.
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِمَا فِي الْآخِرِينَ ﴿١١٩﴾
119. Na Tukawaachia (sifa nzuri) kwa karne za baadaye.
سَلَامٌ عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَارُونَ ﴿١٢٠﴾
120. Salaamun! (Amani) iwe juu ya Muwsaa na Haaruwn.
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١٢١﴾
121. Hakika hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.
إِنَّهُمَا مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٢٢﴾
122. Hakika wao wawili ni miongoni mwa Waja Wetu Waumini.
وَإِنَّ إِلْيَاسَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٢٣﴾
123. Na hakika Iliyaas[14] bila shaka ni miongoni mwa Rusuli.
إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَلَا تَتَّقُونَ ﴿١٢٤﴾
124. Alipowaambia watu wake: Je, hamtokuwa na taqwa?
أَتَدْعُونَ بَعْلًا وَتَذَرُونَ أَحْسَنَ الْخَالِقِينَ ﴿١٢٥﴾
125. Mnamwomba ba’laa[15], na mnaacha Mbora wa wenye kuumba?
اللَّـهَ رَبَّكُمْ وَرَبَّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ ﴿١٢٦﴾
126. Allaah; Rabb wenu, na Rabb wa baba zenu wa awali.
فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ ﴿١٢٧﴾
127. Wakamkadhibisha. Basi wao bila shaka watahudhurishwa (kuadhibiwa).
إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿١٢٨﴾
128. Isipokuwa Waja wa Allaah waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.
وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ ﴿١٢٩﴾
129. Na Tukamuachia (sifa nzuri) kwa karne za baadaye.
سَلَامٌ عَلَىٰ إِلْ يَاسِينَ ﴿١٣٠﴾
130. Salaamun! (Amani) iwe juu ya Ilyaasiyn.
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣١﴾
131. Hakika hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.
إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٣٢﴾
132. Hakika yeye ni miongoni mwa Waja Wetu Waumini.
وَإِنَّ لُوطًا لَّمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٣٣﴾
133. Na hakika Luutw bila shaka ni miongoni mwa Rusuli.
إِذْ نَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ أَجْمَعِينَ ﴿١٣٤﴾
134. Tulipomuokoa pamoja na ahli zake wote.
إِلَّا عَجُوزًا فِي الْغَابِرِينَ ﴿١٣٥﴾
135. Isipokuwa ajuza (bikizee) katika waliobakia nyuma.
ثُمَّ دَمَّرْنَا الْآخَرِينَ ﴿١٣٦﴾
136. Kisha Tukawadamirisha wengineo.
وَإِنَّكُمْ لَتَمُرُّونَ عَلَيْهِم مُّصْبِحِينَ ﴿١٣٧﴾
137. Nanyi bila shaka mnawapitia asubuhi.
وَبِاللَّيْلِ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿١٣٨﴾
138. Na usiku. Je, basi hamtii akilini?
وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ ﴿١٣٩﴾
139. Na hakika Yuwnus[16] bila shaka ni miongoni mwa Rusuli.
إِذْ أَبَقَ إِلَى الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ ﴿١٤٠﴾
140. Alipokimbilia katika merikebu iliyosheheni.
فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ الْمُدْحَضِينَ ﴿١٤١﴾
141. Akapiga kura ya vishale akawa miongoni mwa walioshindwa.
فَالْتَقَمَهُ الْحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٌ ﴿١٤٢﴾
142. Basi samaki mkubwa akammeza hali ya kuwa amefanya jambo la kulaumiwa.
فَلَوْلَا أَنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُسَبِّحِينَ ﴿١٤٣﴾
143. Na lau kama hakuwa miongoni mwa wenye kumsabbih Allaah.
لَلَبِثَ فِي بَطْنِهِ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٤٤﴾
144. Angelibakia tumboni mwake mpaka Siku watakayofufuliwa.
فَنَبَذْنَاهُ بِالْعَرَاءِ وَهُوَ سَقِيمٌ ﴿١٤٥﴾
145. Basi Tukamtupa kwenye ardhi tupu ufukweni (alipomcheua samaki) naye akiwa mgonjwa.
وَأَنبَتْنَا عَلَيْهِ شَجَرَةً مِّن يَقْطِينٍ ﴿١٤٦﴾
146. Na Tukamuoteshea mti unaotambaa aina ya mmung’unya.
وَأَرْسَلْنَاهُ إِلَىٰ مِائَةِ أَلْفٍ أَوْ يَزِيدُونَ ﴿١٤٧﴾
147. Na Tukamtuma kwa (watu wake) laki moja au wanaozidi.
فَآمَنُوا فَمَتَّعْنَاهُمْ إِلَىٰ حِينٍ ﴿١٤٨﴾
148. Wakaamini, basi Tukawastarehesha kwa muda.
فَاسْتَفْتِهِمْ أَلِرَبِّكَ الْبَنَاتُ وَلَهُمُ الْبَنُونَ ﴿١٤٩﴾
149. Basi waulize (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Je, Rabb wako ndio ana mabanati, na wao ndio wana watoto wa kiume?[17]
أَمْ خَلَقْنَا الْمَلَائِكَةَ إِنَاثًا وَهُمْ شَاهِدُونَ ﴿١٥٠﴾
150. Au, je Tumewaumba Malaika wanawake, nao wakawa ni wenye kushuhudia?
أَلَا إِنَّهُم مِّنْ إِفْكِهِمْ لَيَقُولُونَ ﴿١٥١﴾
151. Tanabahi! Hakika wao kwa uzushi wanasema:
وَلَدَ اللَّـهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ ﴿١٥٢﴾
152. Allaah Amezaa. Na hakika wao bila shaka ni waongo!
أَصْطَفَى الْبَنَاتِ عَلَى الْبَنِينَ ﴿١٥٣﴾
153. Je, Amekhitari mabanati kuliko wana wa kiume?
مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ ﴿١٥٤﴾
154. Mna nini! Vipi mnahukumu?
أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ﴿١٥٥﴾
155. Je, hamkumbuki?
أَمْ لَكُمْ سُلْطَانٌ مُّبِينٌ ﴿١٥٦﴾
156. Je, mna hoja bayana (mnayodai)?
فَأْتُوا بِكِتَابِكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٥٧﴾
157. Basi leteni kitabu chenu mkiwa ni wakweli.
وَجَعَلُوا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الْجِنَّةِ نَسَبًا ۚ وَلَقَدْ عَلِمَتِ الْجِنَّةُ إِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ ﴿١٥٨﴾
158. Na wakafanya baina Yake (Allaah) na baina ya majini unasaba. Na hali majini wamekwishajua kwamba kwa yakini wao, bila shaka watahudhurishwa (kuadhibiwa).[18]
سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٥٩﴾
159. Subhaana Allaah (Utakasifu ni wa Allaah) kutokana na yale wanayoyavumisha.
إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿١٦٠﴾
160. Isipokuwa Waja wa Allaah waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.
فَإِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ ﴿١٦١﴾
161. Basi hakika nyinyi na vile mnavyoabudu.
مَا أَنتُمْ عَلَيْهِ بِفَاتِنِينَ ﴿١٦٢﴾
162. Hamuwezi kumpotosha yeyote.
إِلَّا مَنْ هُوَ صَالِ الْجَحِيمِ ﴿١٦٣﴾
163. Isipokuwa yule ambaye amehukumiwa kuingia na kuungua katika moto uwakao vikali mno.
وَمَا مِنَّا إِلَّا لَهُ مَقَامٌ مَّعْلُومٌ ﴿١٦٤﴾
164. Na hakuna miongoni mwetu (Malaika) isipokuwa ana mahali maalumu.
وَإِنَّا لَنَحْنُ الصَّافُّونَ ﴿١٦٥﴾
165. Na hakika sisi bila shaka ni wenye kujipanga safu safu (kwa ibaada).
وَإِنَّا لَنَحْنُ الْمُسَبِّحُونَ ﴿١٦٦﴾
166. Na hakika sisi bila shaka ni wenye kumsabbih Allaah.
وَإِن كَانُوا لَيَقُولُونَ ﴿١٦٧﴾
167. Na hakika (washirikina) walikuwa wakisema:
لَوْ أَنَّ عِندَنَا ذِكْرًا مِّنَ الْأَوَّلِينَ ﴿١٦٨﴾
168. Lau tungelikuwa na ukumbusho kama walivyokuwa wa mwanzo.
لَكُنَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿١٦٩﴾
169. Bila shaka tungelikuwa Waja wa Allaah waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.
فَكَفَرُوا بِهِ ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ ﴿١٧٠﴾
170. Lakini wakaikanusha (Qur-aan). Basi karibuni watakuja kujua.
وَلَقَدْ سَبَقَتْ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا الْمُرْسَلِينَ ﴿١٧١﴾
171. Kwa yakini limekwishasabiki Neno Letu kwa Waja Wetu, Rusuli (waliotumwa).
إِنَّهُمْ لَهُمُ الْمَنصُورُونَ ﴿١٧٢﴾
172. Kwamba hakika wao bila shaka ndio wenye kunusuriwa.
وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ الْغَالِبُونَ ﴿١٧٣﴾
173. Na kwamba hakika Askari Wetu ndio watakaoshinda.
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ ﴿١٧٤﴾
174. Basi waachilie mbali mpaka muda.
وَأَبْصِرْهُمْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ ﴿١٧٥﴾
175. Na watazame tu, nao karibuni watakuja ona.
أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ ﴿١٧٦﴾
176. Je, wanaharakiza Adhabu Yetu?
فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمْ فَسَاءَ صَبَاحُ الْمُنذَرِينَ ﴿١٧٧﴾
177. Na itakapoteremka uwanjani mwao, basi ubaya ulioje wa asubuhi ya walioonywa!
وَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ ﴿١٧٨﴾
178. Na waachilie mbali mpaka muda.
وَأَبْصِرْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ ﴿١٧٩﴾
179. Na tazama tu, nao karibuni watakuja ona.
سُبْحَانَ رَبِّكَ رَبِّ الْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿١٨٠﴾
180. Utakasifu ni wa Rabb wako; Rabb wa Enzi Ya Nguvu Asiyeshindika kutokana na yale wanayoyavumisha.
وَسَلَامٌ عَلَى الْمُرْسَلِينَ ﴿١٨١﴾
181. Na Salaamun! (Amani) iwe juu ya Rusuli.
وَالْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿١٨٢﴾
182. Na AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah) Rabb wa walimwengu.
[1] Nyota Zimeumbwa Kwa Ajili Ya Mambo Matatu:
Rejea Suwrah hii Asw-Swaaffaat (37:10), Al-An’aam (6:97), An-Nahl (16:16), Al-Mulk (67:5).
[2] Washirikina Hawakuamini Kwamba Watafufuliwa:
Rejea Al-Israa (17:49) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali.
[3] Makafiri Kumpachika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Sifa Ovu:
Makafiri wa Kiquraysh hawakuacha kumpachika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) sifa ovu kama hizi, ilhali kabla ya kupewa Unabii walimwita kwa sifa njema kabisa ya Asw-Swiddiyq Al-Amiyn (mkweli mwaminifu).
Basi mara wamwite mshairi, mara majnuni, mara mchawi, mara kuhani, mara mwongo na kadhalika. Rejea Swaad (38:4), na zaidi rejea Al-Furqaan (25:4) kwenye uchambuzi bayana na rejea mbalimbali za maudhui hii ya washirikina kumpachika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) sifa kadhaa ovu na kuipachika Qur-aan pia sifa ovu.
Na hii ilikuwa pia ni ada ya makafiri wa awali kuwapachika sifa ovu Rusuli wao. Rejea Adh-Dhaariyaat kwenye maelezo na rejea mbalimbali nyenginezo.
[4] Neema Za Watu Wa Jannah:
Aayah hii (41) hadi namba (49) zinataja baadhi ya neema na raha za watu ndani ya Jannah. Rejea pia Faatwir (35:35) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali.
[5] Shukurani Za Mtu Mwema Kutokumfuata Rafiki Mpotoshaji:
Kuanzia Aayah hii (50) hadi namba (57), zinaelezea kuhusu rafiki wawili; mwema na muovu mpotoshaji na shukurani za mwema alipoingia Jannah akamkuta rafiki mpotoshaji motoni.
Rejea Al-Furqaan (25:27-29) kwenye majuto ya mtu kufuata rafiki muovu.
[6] (تَاللَّهِ) Ta-Allaahi, (وَاللَّهِ) Wa-Allaahi, (بِاللَّهِ) Bi-Llaahi, Ni Kuapa Kwa Jina La Allaah.
Rejea An-Nahl (16:56) kwenye ufafanuzi.
[7] Mti Wa Zaqquwm:
Ni mti mchungu wa karaha kabisa motoni, na ni chakula cha wakaazi wa humo. Rejea Al-Israa (17:60), Ad-Dukhaan (44:43-46).
Rejea pia Faatwir (35:36) na An-Nabaa (78:21) kwenye fafanuzi, maelezo bayana na rejea mbalimbali za adhabu motoni.
[8] Waliokhitariwa Kwa Ikhlaasw Zao:
Aayah hii imekariri mara nne katika Suwrah hii baada ya kutajwa Rusuli kadhaa na watu wao. Tafsiyr yake ni:
Kwa vile walioonywa hawakuwa wote ni wapotofu, bali miongoni mwao wako walioamini na wakamtakasia Allaah Dini, basi hao Allaah Aliwaepusha na maangamizi ndipo Akasema:
إِلَّا عِبَادَ اللَّـهِ الْمُخْلَصِينَ ﴿٧٤﴾
“Isipokuwa Waja wa Allaah waliokhitariwa kwa ikhlaasw zao.”
Yaani: Ambao Allaah Aliwatakasa na Akawahusisha na Rehma Yake kutokana na wao kuwa na ikhlaasw Naye, na kwa sababu hiyo, mwisho wao umekuwa ni wenye kuhimidiwa. Kisha Akataja aina za adhabu za waliokadhibisha. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[9] Nuwh Na Kizazi Kilichobakia, Naye Ni Rasuli Wa Kwanza Ardhini Na Ni Baba Wa Pili Kwa Wanaadam Baada Ya Aadam.
Baada ya Nuwh (عليه السّلام) kupanda jahazi, akachukua kila kiumbe dume na jike kama Alivyoamrishwa na Allaah (سبحانه وتعالى), watu waliobakia wote pamoja na mwanawe waligharikishwa baharini, nao ni wale ambao walimkanusha Nuwh (عليه السّلام) wakaendelea na ukafiri wao.
Tafsiyr ya Aayah ni:
Na (Allaah) Akawazamisha makafiri wote, na Akawabakisha dhuria wake na kizazi chake kinachozaliana. Hivyo basi watu wote wametokana na dhuria wa Nuwh (عليه السّلام). Na Akamjaalia sifa njema hadi zama za wengine. Na hiyo ni kwa sababu yeye ni mwema katika kumwabudu Muumba, mkarimu kwa viumbe, na hii ni Desturi Yake Allaah (سبحانه وتعالى) kwa wafanyao wema, kuwaenezea sifa nzuri kulingana na ihsaan zao. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Rejea Yuwnus (10:73), Huwd (11:40), Maryam (19:58), Al-Muuminuwn (23:27).
Na pia rejea Suwrah Nuwh (71:1) kwenye maelezo kuwa Nuwh alikuwa ni Rasuli wa kwanza ardhini.
[10] Hakika Hivyo Ndivyo Tunavyowalipa Wafanyao Ihsaan:
Aayah hii imekariri mara nne baada ya kutajwa Rusuli kadhaa. Tafsiyr yake ni:
Hivi ndivyo Tunavyomlipa mja aliyefanya vyema katika kumtii Allaah. Tunamfanyia ukumbusho mzuri wa kutajwa na watu baada ya kufariki kwake kwa namna inayolingana na hadhi yake. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[11] Moyo Uliosalimika:
Rejea Ash-Shu’araa (26:89) kwenye ufafanuzi wa moyo uliosalimika.
Kinyume cha moyo uliosalimika ni moyo ulio na maradhi. Rejea Muhammad (47:20) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali.
Rejea pia Al-Hajj (22:46) ambako kuna maelezo na ufafanuzi wa Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
فَإِنَّهَا لَا تَعْمَى الْأَبْصَارُ وَلَـٰكِن تَعْمَى الْقُلُوبُ الَّتِي فِي الصُّدُورِ ﴿٤٦﴾
“Kwani hakika hayapofuki macho, lakini zinazopofuka ni nyoyo zilizomo vifuani.”
[12] Dhabihu Ndio Wanayochinja Waislamu Siku Ya ‘Iyd Al-Adhwhaa:
Rejea Alhidaaya.com > Fiqh-Ibaadah > Hajj > Kuchinja - Fadhila, Hikmah Na Hukmu Zake [260].
[13] Janga Kuu Walilookolewa Nalo Nabiy Muwsaa Na Haaruwn (عليهما السّلام):
Na Tukawaokoa wao wawili na watu wao kutokana na gharika, utumwa na madhila waliokuwa nao (kutoka kwa Firawni). [Tafsiyr Al-Muyassar]
[16] Nabiy Yuwnus (عليه السّلام):
Yuwnus (عليه السّلام) ni miongoni mwa Manabii waliofadhilishwa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
عن أبي هريرة رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((؟مَا يَنْبَغِى لِعَبْدٍ أَنْ يَقُولَ أَنَا خَيْرٌ مِنْ يُونُسَ بْنِ مَتَّى عَلَيْهِ السَّلاَمُ))
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Haipasi mja yeyote aseme kuwa mimi ni mbora kuliko Yuwnus ibn Mattaa (عليه السّلام).” [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
[17] Washirikina Wamemsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwa Malaika Ni Mabanaati Wake:
Aayah hii ya (149) hadi (159), zinahusiana na usingiziaji wa dhulma kubwa kuwa Allaah Ana wana wa kike, au Allaah Amezaa! Subhaanah wa Ta’aalaa (Ametakasika na Ametukuka kwa Uluwa) kutokana na wanayomsingizia!. Pia Rejea Al-Israa (17:40), Az-Zukhruf (43:15-19), An-Nahl (57-59).
Huu ni mgawanyo na kauli ya dhulma kubwa mno! Mgawanyo wa sehemu mbili: Upande mmoja wamemsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa Ana mwana wa kiume, na upande mwengine wamemsingizia kuwa Ana mabanaat (watoto wa kike) ambao wao wenyewe hawaridhii kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwrah An-Nahl (16:57):
وَيَجْعَلُونَ لِلَّـهِ الْبَنَاتِ سُبْحَانَهُ ۙ وَلَهُم مَّا يَشْتَهُونَ﴿٥٧﴾
“Na wanamfanyia Allaah kuwa ana mabinti! Utakasifu ni Wake! Na wao wawe na (wana wa kiume) wanaowatamani.” [Tafsiyr As-Sa’diy]
Hawakuwa wakiwaridhia mabanaat kwa sababu ilikuwa wanapozaliwa wanawazika wazima wazima! Rejea An-Nahl (16:57-59), At-Takwiyr (81:8-9).
[18] Washirikina Na Makafiri Quraysh Wamemsingizia Allaah Kuwa Ana Mke Na Malaika Ni Mabinti Zake:
Allaah (عزّ وجلّ) Ametukuka kutokana na wanayomuelezea ya kumpachika mke na wana! Na Allaah Awalaani na Awaadhibu kwa wanavyostahiki ya kumzulia Kwake hivyo, Awaangamizilie mbali! Tunakiri kwamba Allaah (عزّ وجلّ) Hana mke wala hana mwana, bali Yeye ni Al-Waahid (Pekee) Asiyezaa wala Asiyezaliwa, Yeye ni Al-Ghaniyyu (Mkwasi Hahitaji lolote). Subhaana Allaah wa Ta’aala Ametukuka kwa ‘Uluwa Adhimu kabisa kutokana na kila wanalomzulia.
Washirikina (makafiri wa Kiquraysh wa Makkah) walimpachika Allaah (عزّ وجلّ) unasaba baina Yake na majini kutokana na madai yao kuwa Malaika ni mabinti wa Allaah. Walipoulizwa nani mama yao hao Malaika ambao wanamsingizia kuwa ni mabinti Wake (kwani hakuna budi kuweko mama aliowazaa)? Wakajibu kuwa mama yao hao Malaika ni mabinti wa wakuu wa majini, yaani watukufu wao na mabwana zao. [Tafsiyr As-Sa’diy, Ibn Kathiyr]
Baadhi ya Wafasiri wa Qur-aan wameona kwamba ingawa neno lililotumika katika Aayah ni al-jinnah (majini), lakini hapo waliokusudiwa ni Malaika. Wakatoa maoni kwamba hapa neno al-jinnah (majini) limekusudiwa kwa maana yake halisi (ya uumbaji uliofichika), na kwamba Malaika pia ni viumbe vilivyofichika. Lakini hiyo si kauli sahihi bali ilokusudiwa hapo ni majini wenyewe. [Tafsiyr Suwrah Asw-Swaaffaat – Imaam Muhammad Bin Swaalih Al-‘Uthaymiyn]
ص
038-Swaad
038-Swaad: Utangulizi Wa Suwrah [262]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
ص ۚ وَالْقُرْآنِ ذِي الذِّكْرِ ﴿١﴾
1. Swaad.[1] Naapa kwa Qur-aan iliyojaa ukumbusho na taadhima.
بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي عِزَّةٍ وَشِقَاقٍ ﴿٢﴾
2. Bali wale waliokufuru wamo katika majivuno na upinzani.
كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّن قَرْنٍ فَنَادَوا وَّلَاتَ حِينَ مَنَاصٍ ﴿٣﴾
3. Karne ngapi Tumeziangamiza kabla yao, wakaomba uokozi, lakini hakukuwa tena na wakati wa kuokoka.
وَعَجِبُوا أَن جَاءَهُم مُّنذِرٌ مِّنْهُمْ ۖ وَقَالَ الْكَافِرُونَ هَـٰذَا سَاحِرٌ كَذَّابٌ ﴿٤﴾
4. Na wakastaajabu kwamba amewajia mwonyaji miongoni mwao. Na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi muongo.[2]
أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَـٰهًا وَاحِدًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عُجَابٌ ﴿٥﴾
5. Amewafanya waabudiwa kuwa ni Ilaah Mmoja? Hakika hili bila shaka ni jambo la ajabu mno!
وَانطَلَقَ الْمَلَأُ مِنْهُمْ أَنِ امْشُوا وَاصْبِرُوا عَلَىٰ آلِهَتِكُمْ ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ يُرَادُ ﴿٦﴾
6. Na wakaondoka wakuu miongoni mwao wakisema: Nendeni zenu na subirini juu ya waabudiwa wenu, hakika hili bila shaka ni jambo linalokusudiwa (ubaya).
مَا سَمِعْنَا بِهَـٰذَا فِي الْمِلَّةِ الْآخِرَةِ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا اخْتِلَاقٌ ﴿٧﴾
7. Hatukusikia haya katika mila ya mwisho, haya si chochote isipokuwa ni jambo lililozushwa tu.
أَأُنزِلَ عَلَيْهِ الذِّكْرُ مِن بَيْنِنَا ۚ بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ مِّن ذِكْرِي ۖ بَل لَّمَّا يَذُوقُوا عَذَابِ ﴿٨﴾
8. Eti ameteremshiwa ukumbusho yeye tu miongoni mwetu? Hapana! Wao wamo katika shaka na Ukumbusho Wangu, bali hawajaonja bado Adhabu Yangu.
أَمْ عِندَهُمْ خَزَائِنُ رَحْمَةِ رَبِّكَ الْعَزِيزِ الْوَهَّابِ ﴿٩﴾
9. Au wanazo hazina za Rehma za Rabb wako Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwingi wa Kutunuku?
أَمْ لَهُم مُّلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ فَلْيَرْتَقُوا فِي الْأَسْبَابِ ﴿١٠﴾
10. Au wana ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake? Basi na wapande katika njia (kufika huko watawale).
جُندٌ مَّا هُنَالِكَ مَهْزُومٌ مِّنَ الْأَحْزَابِ ﴿١١﴾
11. (Wao ni) vijiaskari watakaoshindwa huko katika makundi.
كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَعَادٌ وَفِرْعَوْنُ ذُو الْأَوْتَادِ ﴿١٢﴾
12. Walikadhibisha kabla yao watu wa Nuwh, na kina ‘Aad, na Firawni mwenye askari washupavu na nguvu kubwa.[3]
وَثَمُودُ وَقَوْمُ لُوطٍ وَأَصْحَابُ الْأَيْكَةِ ۚ أُولَـٰئِكَ الْأَحْزَابُ ﴿١٣﴾
13. Na kina Thamuwd na watu wa Luutw, na watu wa Al-Aykah.[4] Hayo ndio Makundi.
إِن كُلٌّ إِلَّا كَذَّبَ الرُّسُلَ فَحَقَّ عِقَابِ ﴿١٤﴾
14. Hakuna hata mmoja wao isipokuwa waliwakadhibisha Rusuli, basi ikahakikika Ikabu Yangu.[5]
وَمَا يَنظُرُ هَـٰؤُلَاءِ إِلَّا صَيْحَةً وَاحِدَةً مَّا لَهَا مِن فَوَاقٍ ﴿١٥﴾
15. Na hawangojei hawa isipokuwa ukelele angamizi mmoja tu usio na kurudishwa wala taakhira.
وَقَالُوا رَبَّنَا عَجِّل لَّنَا قِطَّنَا قَبْلَ يَوْمِ الْحِسَابِ ﴿١٦﴾
16. Na wanasema: Rabb wetu! Tuharakizie fungu letu (la adhabu) kabla ya Siku ya hesabu.[6]
اصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَاذْكُرْ عَبْدَنَا دَاوُودَ ذَا الْأَيْدِ ۖ إِنَّهُ أَوَّابٌ ﴿١٧﴾
17. Subiri kwa yale wanayoyasema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na mkumbuke Mja Wetu Daawuwd mwenye nguvu. Hakika yeye ni mwingi wa kutubia na kurejea Kwetu.[7]
إِنَّا سَخَّرْنَا الْجِبَالَ مَعَهُ يُسَبِّحْنَ بِالْعَشِيِّ وَالْإِشْرَاقِ ﴿١٨﴾
18. Hakika Sisi Tulitiisha milima iwe pamoja naye ikisabbih jioni na baada ya kuchomoza jua.
وَالطَّيْرَ مَحْشُورَةً ۖ كُلٌّ لَّهُ أَوَّابٌ ﴿١٩﴾
19. Na ndege waliokusanywa. Wote walikuwa ni watiifu mno kwake.
وَشَدَدْنَا مُلْكَهُ وَآتَيْنَاهُ الْحِكْمَةَ وَفَصْلَ الْخِطَابِ ﴿٢٠﴾
20. Na Tukamtilia nguvu ufalme wake, na Tukampa hikmah, na umaizi wa kukata hukumu.
وَهَلْ أَتَاكَ نَبَأُ الْخَصْمِ إِذْ تَسَوَّرُوا الْمِحْرَابَ ﴿٢١﴾
21. Na je, imekujia khabari ya wenye kupinzana waliporuka ukuta kuingia chumba cha kuswalia?
إِذْ دَخَلُوا عَلَىٰ دَاوُودَ فَفَزِعَ مِنْهُمْ ۖ قَالُوا لَا تَخَفْ ۖ خَصْمَانِ بَغَىٰ بَعْضُنَا عَلَىٰ بَعْضٍ فَاحْكُم بَيْنَنَا بِالْحَقِّ وَلَا تُشْطِطْ وَاهْدِنَا إِلَىٰ سَوَاءِ الصِّرَاطِ ﴿٢٢﴾
22. Walipomuingilia Daawuwd akafazaika kutokana nao! Wakasema: Usikhofu! (Sisi ni) wapinzani wawili; mmoja wetu amemdhulumu mwenziwe, basi hukumu baina yetu kwa haki, na wala usipendelee, na tuongoze katika njia ya sawa.
إِنَّ هَـٰذَا أَخِي لَهُ تِسْعٌ وَتِسْعُونَ نَعْجَةً وَلِيَ نَعْجَةٌ وَاحِدَةٌ فَقَالَ أَكْفِلْنِيهَا وَعَزَّنِي فِي الْخِطَابِ ﴿٢٣﴾
23. Hakika huyu ni ndugu yangu, ana kondoo majike tisiini na tisa, nami nina kondoo jike mmoja. Naye akaniambia: Nikabidhi huyo awe katika amana yangu, na amenishinda kwa maneno.
قَالَ لَقَدْ ظَلَمَكَ بِسُؤَالِ نَعْجَتِكَ إِلَىٰ نِعَاجِهِ ۖ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ الْخُلَطَاءِ لَيَبْغِي بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَقَلِيلٌ مَّا هُمْ ۗ وَظَنَّ دَاوُودُ أَنَّمَا فَتَنَّاهُ فَاسْتَغْفَرَ رَبَّهُ وَخَرَّ رَاكِعًا وَأَنَابَ ۩﴿٢٤﴾
24. (Nabiy Daawuwd) akasema: Kweli amekudhulumu kwa kukuomba kondoo wako kuongezea kondoo wake. Na hakika washirika wengi hufanyiana baghi[8] (dhulma) wao kwa wao isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema, na hao ni wachache. Daawuwd akahisi kwamba Tumemtia mtihanini, basi akamwomba Rabb wake maghfirah na akaporomoka kusujudu na akarudi kwa Allaah (kwa tawbah na ibaada).[9]
فَغَفَرْنَا لَهُ ذَٰلِكَ ۖ وَإِنَّ لَهُ عِندَنَا لَزُلْفَىٰ وَحُسْنَ مَآبٍ ﴿٢٥﴾
25. Tukamghufuria hayo. Na hakika yeye bila shaka ana makurubisho na marejeo mazuri Kwetu.
يَا دَاوُودُ إِنَّا جَعَلْنَاكَ خَلِيفَةً فِي الْأَرْضِ فَاحْكُم بَيْنَ النَّاسِ بِالْحَقِّ وَلَا تَتَّبِعِ الْهَوَىٰ فَيُضِلَّكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَضِلُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا نَسُوا يَوْمَ الْحِسَابِ ﴿٢٦﴾
26. Ee Daawuwd! Hakika Tumekujaalia uwe Khalifa katika ardhi. Basi hukumu baina ya watu kwa haki, na wala usifuate matamanio yakakupoteza Njia ya Allaah. Hakika wale wanaopotea Njia ya Allaah watapata adhabu kali kwa sababu ya kusahau kwao Siku ya hesabu.
وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاءَ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا بَاطِلًا ۚ ذَٰلِكَ ظَنُّ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِنَ النَّارِ ﴿٢٧﴾
27. Na wala Hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake bila kusudio. Hiyo ndio dhana ya wale waliokufuru. Basi ole wao wale waliokufuru kwa moto utakaowapata.
أَمْ نَجْعَلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَالْمُفْسِدِينَ فِي الْأَرْضِ أَمْ نَجْعَلُ الْمُتَّقِينَ كَالْفُجَّارِ ﴿٢٨﴾
28. Je, Tuwafanye wale walioamini na wakatenda mema kama mafisadi katika ardhi? Au Tuwafanye wenye taqwa kama waovu?
كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٢٩﴾
29. Kitabu Tumekiteremsha kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) chenye Baraka, ili wapate kuzingatia kwa makini Aayaat zake, na ili wapate kukumbuka wenye akili.
وَوَهَبْنَا لِدَاوُودَ سُلَيْمَانَ ۚ نِعْمَ الْعَبْدُ ۖ إِنَّهُ أَوَّابٌ ﴿٣٠﴾
30. Na Daawuwd Tukamtunuku Sulaymaan. Uzuri ulioje wa mja! Hakika yeye ni mwingi wa kutubia.[10]
إِذْ عُرِضَ عَلَيْهِ بِالْعَشِيِّ الصَّافِنَاتُ الْجِيَادُ ﴿٣١﴾
31. Alipohudhurishiwa jioni farasi wasimamao kidete tayari kukimbia kwa kasi.
فَقَالَ إِنِّي أَحْبَبْتُ حُبَّ الْخَيْرِ عَن ذِكْرِ رَبِّي حَتَّىٰ تَوَارَتْ بِالْحِجَابِ ﴿٣٢﴾
32. Akasema: Hakika mimi nimependelea mapenzi ya vitu vizuri badala ya kumdhukuru Rabb wangu mpaka (jua) likatoweka.
رُدُّوهَا عَلَيَّ ۖ فَطَفِقَ مَسْحًا بِالسُّوقِ وَالْأَعْنَاقِ ﴿٣٣﴾
33. (Akasema) warudisheni kwangu! Akaanza kuwapapasa miguu na shingo.
وَلَقَدْ فَتَنَّا سُلَيْمَانَ وَأَلْقَيْنَا عَلَىٰ كُرْسِيِّهِ جَسَدًا ثُمَّ أَنَابَ ﴿٣٤﴾
34. Na kwa yakini Tulimtia mtihanini Sulaymaan, na Tukamtupia juu ya kiti chake mwili kisha akarejea kutubia.[11]
قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي وَهَبْ لِي مُلْكًا لَّا يَنبَغِي لِأَحَدٍ مِّن بَعْدِي ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ ﴿٣٥﴾
35. Akasema: Rabb wangu! Nighufurie, na Nitunukie ufalme asiupate mtu yeyote baada yangu. Hakika Wewe Ndiye Mwingi Wa Kutunuku.[12]
فَسَخَّرْنَا لَهُ الرِّيحَ تَجْرِي بِأَمْرِهِ رُخَاءً حَيْثُ أَصَابَ ﴿٣٦﴾
36. Basi Tukamtiishia upepo unaokwenda kwa amri yake polepole popote anapotaka kufika.
وَالشَّيَاطِينَ كُلَّ بَنَّاءٍ وَغَوَّاصٍ ﴿٣٧﴾
37. Na mashaytwaan, kila ajengaye na mpiga mbizi.
وَآخَرِينَ مُقَرَّنِينَ فِي الْأَصْفَادِ ﴿٣٨﴾
38. Na wengineo, wafungwao minyororoni.
هَـٰذَا عَطَاؤُنَا فَامْنُنْ أَوْ أَمْسِكْ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٣٩﴾
39. (Tukasema): Hiki ni Kipawa Chetu, basi toa au zuia bila ya hesabu.
وَإِنَّ لَهُ عِندَنَا لَزُلْفَىٰ وَحُسْنَ مَآبٍ ﴿٤٠﴾
40. Na hakika yeye bila shaka ana makurubisho Kwetu na marejeo mazuri.
وَاذْكُرْ عَبْدَنَا أَيُّوبَ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ أَنِّي مَسَّنِيَ الشَّيْطَانُ بِنُصْبٍ وَعَذَابٍ ﴿٤١﴾
41. Na mkumbuke Mja Wetu Ayyuwb alipomwita Rabb wake: Hakika mimi amenigusa shaytwaan kwa tabu na adhabu.[13]
ارْكُضْ بِرِجْلِكَ ۖ هَـٰذَا مُغْتَسَلٌ بَارِدٌ وَشَرَابٌ ﴿٤٢﴾
42. (Akaambiwa): Piga piga ardhi kwa mguu wako! Hii (chemchemu); maji baridi ya kuogea na ya kunywa.
وَوَهَبْنَا لَهُ أَهْلَهُ وَمِثْلَهُم مَّعَهُمْ رَحْمَةً مِّنَّا وَذِكْرَىٰ لِأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿٤٣﴾
43. Na Tukamtunukia ahli zake na wengine mfano wao pamoja nao ikiwa ni Rehma kutoka Kwetu, na ni ukumbusho kwa wenye akili.
وَخُذْ بِيَدِكَ ضِغْثًا فَاضْرِب بِّهِ وَلَا تَحْنَثْ ۗ إِنَّا وَجَدْنَاهُ صَابِرًا ۚ نِّعْمَ الْعَبْدُ ۖ إِنَّهُ أَوَّابٌ ﴿٤٤﴾
44. Na (akaambiwa): Chukua mkononi mwako kicha cha vijiti na upigie navyo, na wala usivunje kiapo. Hakika sisi Tulimkuta mwenye subira mno, mja mwema kabisa, hakika yeye ni mwingi wa kutubia.
وَاذْكُرْ عِبَادَنَا إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ أُولِي الْأَيْدِي وَالْأَبْصَارِ ﴿٤٥﴾
45. Na wakumbuke Waja Wetu: Ibraahiym, na Is-haaq, na Ya’quwb, wenye nguvu na busara.
إِنَّا أَخْلَصْنَاهُم بِخَالِصَةٍ ذِكْرَى الدَّارِ ﴿٤٦﴾
46. Hakika Sisi Tumewakhitari kutokana na ikhlasi zao kwa kuwapa sifa khalisi ya ukumbusho wa Aakhirah.
وَإِنَّهُمْ عِندَنَا لَمِنَ الْمُصْطَفَيْنَ الْأَخْيَارِ ﴿٤٧﴾
47. Na hakika wao Kwetu bila shaka ni miongoni mwa waliokhitariwa na walio bora kabisa.
وَاذْكُرْ إِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَذَا الْكِفْلِ ۖ وَكُلٌّ مِّنَ الْأَخْيَارِ ﴿٤٨﴾
48. Na wakumbuke Ismaaiyl na Alyasa’ na Dhul-Kifli[14], na wote hawa ni miongoni mwa walio bora kabisa.
هَـٰذَا ذِكْرٌ ۚ وَإِنَّ لِلْمُتَّقِينَ لَحُسْنَ مَآبٍ ﴿٤٩﴾
49. Huu ni ukumbusho. Na hakika wenye taqwa bila shaka wana mahali pazuri kabisa pa kurejea.
جَنَّاتِ عَدْنٍ مُّفَتَّحَةً لَّهُمُ الْأَبْوَابُ ﴿٥٠﴾
50. Jannaat za kudumu milele, zitakazofunguliwa milango yote kwa ajili yao.
مُتَّكِئِينَ فِيهَا يَدْعُونَ فِيهَا بِفَاكِهَةٍ كَثِيرَةٍ وَشَرَابٍ ﴿٥١﴾
51. Wakiegemea humo, wakiagizia humo matunda mengi na vinywaji.
وَعِندَهُمْ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ أَتْرَابٌ ﴿٥٢﴾
52. Na pamoja nao wanawake wenye staha wanaoinamisha macho, wa hirimu moja.
هَـٰذَا مَا تُوعَدُونَ لِيَوْمِ الْحِسَابِ ﴿٥٣﴾
53. Haya (yaliyotajwa) ndiyo mnayoahidiwa (enyi wenye taqwa) kwa ajili ya Siku ya hesabu.
إِنَّ هَـٰذَا لَرِزْقُنَا مَا لَهُ مِن نَّفَادٍ ﴿٥٤﴾
54. Hakika hii bila shaka ni Riziki Yetu, haina kumalizika.
هَـٰذَا ۚ وَإِنَّ لِلطَّاغِينَ لَشَرَّ مَآبٍ ﴿٥٥﴾
55. Ndio hivi! Na hakika wenye kupinduka mipaka katika kuasi, bila shaka wana mahali pabaya mno pa kurejea.
جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا فَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿٥٦﴾
56. Nayo ni Jahannam, wataingia kuungua. Basi pabaya palioje mahali pa kupumzikia![15]
هَـٰذَا فَلْيَذُوقُوهُ حَمِيمٌ وَغَسَّاقٌ ﴿٥٧﴾
57. Ndio hivi! Basi wayaonje maji yachemkayo na usaha.
وَآخَرُ مِن شَكْلِهِ أَزْوَاجٌ ﴿٥٨﴾
58. Na (adhabu) nyinginezo za mfano wake na aina yake.
هَـٰذَا فَوْجٌ مُّقْتَحِمٌ مَّعَكُمْ ۖ لَا مَرْحَبًا بِهِمْ ۚ إِنَّهُمْ صَالُو النَّارِ ﴿٥٩﴾
59. (Wataambizana): Hili ndilo kundi litakaloingia pamoja nanyi. Hawana makaribisho mazuri. Hakika wao wataingia kuungua motoni.
قَالُوا بَلْ أَنتُمْ لَا مَرْحَبًا بِكُمْ ۖ أَنتُمْ قَدَّمْتُمُوهُ لَنَا ۖ فَبِئْسَ الْقَرَارُ ﴿٦٠﴾
60. (Waliofuata wapotofu) watasema: Bali nyinyi hakuna makaribisho mazuri kwenu! Nyinyi ndio mliotutangulizia haya. Basi ubaya ulioje makazi ya kustakiri!
قَالُوا رَبَّنَا مَن قَدَّمَ لَنَا هَـٰذَا فَزِدْهُ عَذَابًا ضِعْفًا فِي النَّارِ ﴿٦١﴾
61. Watasema: Ee Rabb wetu! Yule aliyetuletea haya, basi Mzidishie adhabu maradufu katika moto.
وَقَالُوا مَا لَنَا لَا نَرَىٰ رِجَالًا كُنَّا نَعُدُّهُم مِّنَ الْأَشْرَارِ ﴿٦٢﴾
62. Na watasema: Tuna nini! Mbona hatuwaoni watu tuliokuwa tukiwahesabu kuwa ni miongoni mwa waovu?
أَتَّخَذْنَاهُمْ سِخْرِيًّا أَمْ زَاغَتْ عَنْهُمُ الْأَبْصَارُ ﴿٦٣﴾
63. Tuliowafanya vichekesho, au yamepotea tu macho yetu tusiwaone?
إِنَّ ذَٰلِكَ لَحَقٌّ تَخَاصُمُ أَهْلِ النَّارِ ﴿٦٤﴾
64. Hakika hayo bila shaka ni kweli; makhasimiano ya watu wa motoni.
قُلْ إِنَّمَا أَنَا مُنذِرٌ ۖ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿٦٥﴾
65. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi ni mwonyaji tu. Na hakuna Muabudiwa wa haki yeyote isipokuwa Allaah Mmoja Pekee, Asiyepingika.
رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا الْعَزِيزُ الْغَفَّارُ ﴿٦٦﴾
66. Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwingi wa Kughufuria.
قُلْ هُوَ نَبَأٌ عَظِيمٌ ﴿٦٧﴾
67. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hii (Qur-aan) ni khabari muhimu adhimu.
أَنتُمْ عَنْهُ مُعْرِضُونَ ﴿٦٨﴾
68. Nyinyi mnaikengeuka.
مَا كَانَ لِيَ مِنْ عِلْمٍ بِالْمَلَإِ الْأَعْلَىٰ إِذْ يَخْتَصِمُونَ ﴿٦٩﴾
69. Sikuwa mimi na ilimu yoyote kuhusu wakuu watukufu (Malaika) wanapokhasimiana na kujadiliana.
إِن يُوحَىٰ إِلَيَّ إِلَّا أَنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٧٠﴾
70. Haifunuliwi Wahy kwangu isipokuwa ya kwamba: hakika mimi ni mwonyaji mbainishaji.
إِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِّن طِينٍ ﴿٧١﴾
71. Pale Rabb wako Alipowaambia Malaika: Hakika Mimi Namuumba mtu kutokana na udongo.
فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُوا لَهُ سَاجِدِينَ ﴿٧٢﴾
72. Basi Nitakapomsawazisha na Nikampuliza humo roho Niliyoiumba, basi mwangukieni kumsujudia.
فَسَجَدَ الْمَلَائِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ ﴿٧٣﴾
73. Wakamsujudia Malaika wote pamoja.
إِلَّا إِبْلِيسَ اسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ ﴿٧٤﴾
74. Isipokuwa Ibliys, alitakabari na akawa miongoni mwa makafiri.
قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ ۖ أَسْتَكْبَرْتَ أَمْ كُنتَ مِنَ الْعَالِينَ ﴿٧٥﴾
75. (Allaah) Akasema: Ee Ibliys! Nini kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba kwa Mikono Yangu?[16] Je, umetakabari, au umekuwa miongoni mwa waliojitukuza?
قَالَ أَنَا خَيْرٌ مِّنْهُ ۖ خَلَقْتَنِي مِن نَّارٍ وَخَلَقْتَهُ مِن طِينٍ ﴿٧٦﴾
76. (Ibliys) akasema: Mimi ni bora kuliko yeye, Umeniumba kutokana na moto, naye Umemuumba kutokana na udongo.
قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ ﴿٧٧﴾
77. (Allaah) Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umetokomezwa mbali na kulaaniwa.
وَإِنَّ عَلَيْكَ لَعْنَتِي إِلَىٰ يَوْمِ الدِّينِ ﴿٧٨﴾
78. Na hakika Laana Yangu iko juu yako mpaka Siku ya malipo.
قَالَ رَبِّ فَأَنظِرْنِي إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿٧٩﴾
79. (Ibliys) akasema: Rabb wangu! Basi Nipe muhula mpaka siku watakayofufuliwa.
قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ الْمُنظَرِينَ ﴿٨٠﴾
80. (Allaah) Akasema: Hakika wewe ni miongoni mwa waliopewa muhula.
إِلَىٰ يَوْمِ الْوَقْتِ الْمَعْلُومِ ﴿٨١﴾
81. Mpaka siku ya wakati maalumu.
قَالَ فَبِعِزَّتِكَ لَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٨٢﴾
82. (Ibliys) akasema: Naapa kwa Utukufu Wako. Hakika nitawapotosha wote.[17]
إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ الْمُخْلَصِينَ ﴿٨٣﴾
83. Isipokuwa Waja Wako miongoni mwao waliokhitariwa kwa ikhlasi zao.
قَالَ فَالْحَقُّ وَالْحَقَّ أَقُولُ ﴿٨٤﴾
84. (Allaah) Akasema: Basi haki (ndio Kiapo Changu), na haki Naisema!
لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكَ وَمِمَّن تَبِعَكَ مِنْهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٨٥﴾
85. Bila shaka Nitaijaza Jahannam kwa wewe na wote waliokufuata miongoni mwao.
قُلْ مَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُتَكَلِّفِينَ ﴿٨٦﴾
86. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Sikuombeni ujira wowote juu ya hili, na wala mimi si miongoni mwa wenye kujidai kuzusha chochote kisichohusu.
إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ ﴿٨٧﴾
87. Haikuwa hii (Qur-aan) isipokuwa ni ukumbusho tu kwa walimwengu.
وَلَتَعْلَمُنَّ نَبَأَهُ بَعْدَ حِينٍ ﴿٨٨﴾
88. Na bila shaka mtakuja kujua khabari zake baada ya muda.[18]
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Makafiri Kumsingizia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kila Aina Ya Sifa Mbaya:
Rejea Al-Furqaan (25:4-8) kwenye maelezo na rejea mbalimbali kuhusu washirikina kumpachika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kila aina ya sifa ovu pamoja na kuipachika Qur-aan. Walisema ni mchawi, kuhani, mshairi, majinuni, mtungaji na ameibuni Qur-aan na sifa nyenginezo.
Rejea pia Asw-Swaaffaat (37:36).
[3] Awtaad Maana Zake:
‘Ulamaa wametaja maana mbalimbali kuhusu neno hili kama ifuatavyo: Askari washupavu na nguvu kubwa [Tafsiyr As-Sa’diy]. Nguvu kubwa mno [Tafsiyr Al-Muyassar]. Ufalme thabiti wa nguvu [Ibn ‘Abbaas]. Nguvu na mashambulizi ya nguvu [Adhw-Dhwahaak]. Na wengine wamesema ni vigingi. Na wengineo wametaja maana zinazokaribiana na maana hizo.
[4] Watu Wa Al-Aykah:
Watu wa Aykah ni watu wa kichakani wa Nabiy Shu’ayb (عليه السّلام). Rejea Ash-Shu’araa (26:176).
[7] Miongoni Mwa Fadhila Za Nabiy Daawuwd (عليه السّلام) :
Aayah hii (17) hadi (20) zinataja baadhi ya fadhila za Nabiy Daawuwd (عليه السّلام) . Rejea pia Sabaa (34:10).
[9] Sujuwd Ya Nabiy Sulaymaan (عليه السّلام) Na Sujuwd Ya Tilaawaah (Kusoma Qur-aan)
Bonyeza kiungo kifuatacho kupata faida:
Wamekhitilafiana ‘Ulamaa kuhusu Sijdah ya Tilaawah (kusoma Qur-aan) ya Aayah hii, lakini imethibiti kusujudu mtu anaposoma Aayah hii kutokana na Hadiyth zifuatazo ambazo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisujudu:
أَخْبَرَنِي إِبْرَاهِيمُ بْنُ الْحَسَنِ الْمِقْسَمِيُّ، قَالَ حَدَّثَنَا حَجَّاجُ بْنُ مُحَمَّدٍ، عَنْ عُمَرَ بْنِ ذَرٍّ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم سَجَدَ فِي { ص } وَقَالَ " سَجَدَهَا دَاوُدُ تَوْبَةً وَنَسْجُدُهَا شُكْرًا " .
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisujudu katika Suwrah Swaad akasema: “Alisujudu Daawuwd kama ni tawbah (kutubia) nasi tunasujudu kama shukurani.” Sunan An-Nasaaiy na ameisahihisha Al-Albaaniy - Swahiyh An-Nasaaiy (956)]
Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas aliyesema: “Swaad si katika mahala palipothibiti na kukokotezewa kusujudu, lakini mimi nilimwona Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisujudu hapo.” [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1069), Abu Daawuud (1409) na At-Tirmidhiy (577)]
Duaa ya kusoma katika Sajdah ya Tilaawah, Rejea An-Najm (53:62).
[10] Fadhila Za Nabiy Sulaymaan (عليه السّلام):
Kuanzia Aayah hii (31) hadi (40), zinatajwa fadhila za Nabiy Sulaymaan (عليه السّلام). Rejea pia Suwrah Sabaa (34:12-14) kwenye fadhila zake kama hizo na nyenginezo.
Rejea pia An-Naml (27:10-19). Na humo katika Suwrah An-Naml, kisa chake ni kuanzia Aayah namba (10) hadi (40) anaposhukuru Neema na Fadhila za Allaah juu yake. Kisha kisa kinaendelea hadi Aayah namba (44).
[11] Nabiy Sulaymaan (عليه السّلام) Alitiwa Mtihanini Kwa Kiapo Chake Alichoapa Bila Kusema In Shaa Allaah.
Rejea Al-Kahf (18:23) kwenye Hadiyth inayotaja hayo.
Na Tafsiyr ya Aayah:
Hakika Tulimpa mtihani Sulaymaan na Tukamrushia kwenye kiti chake kipande cha mtoto aliyezaliwa katika kipindi alichoapa kuwa atawapitia wake zake na kila mmoja katika wao atamzalia shujaa atakayepigana katika njia ya Allaah na hakusema In Shaa Allaah (Allaah Akitaka). Akawapitia wake zake wote, na hakuna hata mmoja katika wao aliyeshika mimba isipokuwa mmoja aliyezaa mtoto nusu. Kisha Sulaymaan alirudi kwa Rabb Wake, akatubia. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[12] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ameheshimu Duaa Ya Nabiy Sulaymaan (عليه السّلام):
حَدَّثَنَا إِسْحَاقُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ أَخْبَرَنَا رَوْحٌ، وَمُحَمَّدُ بْنُ جَعْفَرٍ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ زِيَادٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " إِنَّ عِفْرِيتًا مِنَ الْجِنِّ تَفَلَّتَ عَلَىَّ الْبَارِحَةَ ـ أَوْ كَلِمَةً نَحْوَهَا ـ لِيَقْطَعَ عَلَىَّ الصَّلاَةَ، فَأَمْكَنَنِي اللَّهُ مِنْهُ، فَأَرَدْتُ أَنْ أَرْبِطَهُ إِلَى سَارِيَةٍ مِنْ سَوَارِي الْمَسْجِدِ، حَتَّى تُصْبِحُوا وَتَنْظُرُوا إِلَيْهِ كُلُّكُمْ، فَذَكَرْتُ قَوْلَ أَخِي سُلَيْمَانَ رَبِّ هَبْ لِي مُلْكًا لاَ يَنْبَغِي لأَحَدٍ مِنْ بَعْدِي ". قَالَ رَوْحٌ فَرَدَّهُ خَاسِئًا.
Amesimulia Abu Hurayrah: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Jana usiku Jini mkubwa (‘Ifriyt) kati ya majini alinijia ili anivurugie Swalaah yangu (au alisema jambo linalolingana na hilo) lakini Allaah Aliniwezesha kulishinda. Nilitaka kulifunga katika moja ya nguzo za Msikiti ili nyote mlione asubuhi lakini nilikumbuka kauli ya kaka yangu Sulaymaan (kama ilivyo ndani ya Qur-aan) :
قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي وَهَبْ لِي مُلْكًا لَّا يَنبَغِي لِأَحَدٍ مِّن بَعْدِي ۖ
“Akasema: Rabb wangu! Nighufurie, na Nitunukie ufalme asiupate mtu yeyote baada yangu.” [Swaad: (35)]
[13] Nabiy Ayyuwb (عليه السّلام) Mitihani Yake Na Subira Yake:
Nabiy Ayyuwb (عليه السّلام) alifikwa na mitihani ya kila aina; aliuguwa maradhi miaka kumi na nane, na akafikwa na msiba wa kuondokewa na watoto na mali yake yote. Lakini juu ya hivyo alivumilia bila ya kulalamika, bali aliendelea bila ya kusita na ibaada zake na huku akimshukuru Allaah (سبحانه وتعالى) hadi mwishowe aliomba duaa hiyo.
[15] Mateso Na Adhabu Za Watu Wa Motoni:
Rejea An-Nabaa (78:21) kwenye rejea mbalimbali na maelezo bayana kuhusu aina za mateso na adhabu za watu wa motoni.
[16] Aqiydah Sahihi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Ni Kuthibisha Sifa Za Allaah Kama Mikono Yake:.
Rejea Al-Fat-h (48:10), Al-Maaidah (5:64), Az-Zumar (39:67).
[17] Shaytwaan Ameahidi Kuwapotosha Wanaadam:
Rejea Suwrah Ibraahiym (14:22) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali kuhusu shaytwaan anavyowapotosha wanaadam na jinsi anavyowakanusha na kujitenga nao inapofika adhabu au itakapokuwa Siku ya Qiyaamah.
[18] Wakati Makafiri Watakapokuja Kujua Khabari Za Ukweli Wa Qur-aan:
‘Ulamaa wa Tafsiyr wamesema:
Makafiri watakuja kujua ukweli wa Qur-aan na yaliyotajwa ndani yake ambayo hawakuyaamini, pindi Qur-aan itakaposadikishwa na watu ukweli wake, na pindi Uislamu utakaposhinda wakaingia watu katika Dini makundi kwa makundi, na pia pindi watakapoiona adhabu na njia za kurudi kwa Allaah zikawakatia. Na baadhi ya Salaf wamesema: (i) Baada ya mauti. (ii) Siku ya Qiyaamah. (iii) Itakapomfikia mtu ilimu ya yaqini baada ya kufariki. [Tafsiyr Al-Muyassar, Tafsiyr As-Sa’diy, Tafsiyr Ibn Kathiyr]
الزُّمَر
039-Az-Zumar
039-Az-Zumar: Utangulizi Wa Suwrah [265]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
تَنزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ ﴿١﴾
1. Ni uteremsho wa Kitabu hiki kutoka kwa Allaah Mwenye Enzi na Nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.
إِنَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ فَاعْبُدِ اللَّـهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ ﴿٢﴾
2. Hakika Sisi Tumekuteremshia Kitabu hiki kwa haki, basi mwabudu Allaah kwa kumtakasia Dini Yeye.
أَلَا لِلَّـهِ الدِّينُ الْخَالِصُ ۚ وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ فِي مَا هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ كَاذِبٌ كَفَّارٌ ﴿٣﴾
3. Tanabahi! Ni ya Allaah Pekee Dini iliyotakasika. Na wale waliojichukulia badala Yake walinzi (wakisema): Hatuwaabudu isipokuwa ili wapate kutukurubisha karibu kabisa kwa Allaah. Hakika Allaah Atahukumu baina yao katika yale wanayokhitilafiana nayo. Hakika Allaah Hamhidi aliye mkadhibishaji, kafiri mkubwa.[1]
لَّوْ أَرَادَ اللَّـهُ أَن يَتَّخِذَ وَلَدًا لَّاصْطَفَىٰ مِمَّا يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ سُبْحَانَهُ ۖ هُوَ اللَّـهُ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿٤﴾
4. Lau Angelitaka Allaah kujichukulia mwana, Angelikhitari Amtakaye miongoni mwa Aliowaumba. Subhaanah! (Utakasifu ni Wake), Yeye Ndiye Allaah Mmoja Pekee, Asiyepingika.
خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۖ يُكَوِّرُ اللَّيْلَ عَلَى النَّهَارِ وَيُكَوِّرُ النَّهَارَ عَلَى اللَّيْلِ ۖ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۗ أَلَا هُوَ الْعَزِيزُ الْغَفَّارُ ﴿٥﴾
5. Ameumba mbingu na ardhi kwa haki. Anaufunika usiku juu ya mchana, na Anafunika mchana juu ya usiku. Na Ametiisha jua na mwezi; kila kimoja kinakwenda mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Tanabahi! Yeye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwingi wa Kughufuria.
خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ ثُمَّ جَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ الْأَنْعَامِ ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ ۚ يَخْلُقُكُمْ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ خَلْقًا مِّن بَعْدِ خَلْقٍ فِي ظُلُمَاتٍ ثَلَاثٍ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ ﴿٦﴾
6. Amekuumbeni kutokana na nafsi moja, kisha Akamfanya kutokana nayo mkewe, na Akakuteremshieni katika wanyama wa mifugo jozi nane.[2] Anakuumbeni matumboni mwa mama zenu umbo baada ya umbo, katika viza vitatu. Huyo Ndiye Allaah Rabb wenu Mwenye Ufalme, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye. Basi vipi mnageuzwa?
إِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنكُمْ ۖ وَلَا يَرْضَىٰ لِعِبَادِهِ الْكُفْرَ ۖ وَإِن تَشْكُرُوا يَرْضَهُ لَكُمْ ۗ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۗ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرْجِعُكُمْ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ۚ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٧﴾
7. Mkikufuru, basi hakika Allaah Ni Mkwasi kwenu (Hawahitajieni kwa lolote), na wala Haridhii kufuru kwa Waja Wake. Na mkishukuru, basi Huridhika nanyi. Na wala mbebaji mzigo (wa dhambi) hatobeba mzigo wa mwengine. Kisha kwa Rabb wenu ndio marejeo yenu, Atakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda. Hakika Yeye Ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.
وَإِذَا مَسَّ الْإِنسَانَ ضُرٌّ دَعَا رَبَّهُ مُنِيبًا إِلَيْهِ ثُمَّ إِذَا خَوَّلَهُ نِعْمَةً مِّنْهُ نَسِيَ مَا كَانَ يَدْعُو إِلَيْهِ مِن قَبْلُ وَجَعَلَ لِلَّـهِ أَندَادًا لِّيُضِلَّ عَن سَبِيلِهِ ۚ قُلْ تَمَتَّعْ بِكُفْرِكَ قَلِيلًا ۖ إِنَّكَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ ﴿٨﴾
8. Na inapomgusa binaadam dhara, humwomba Rabb wake huku akijisogeza Kwake, kisha Akimruzuku Neema kutoka Kwake, husahau yale aliyokuwa akimwomba kabla, na kumfanyia Allaah wanaolingana Naye, ili apotoshe (watu) kutoka Njia Yake. Sema: Starehe kwa kufuru yako kidogo tu, hakika wewe ni miongoni mwa watu wa motoni.
أَمَّنْ هُوَ قَانِتٌ آنَاءَ اللَّيْلِ سَاجِدًا وَقَائِمًا يَحْذَرُ الْآخِرَةَ وَيَرْجُو رَحْمَةَ رَبِّهِ ۗ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٩﴾
9. Je, yule anayeshikamana na ibaada nyakati za usiku akisujudu na kusimama (kuswali)[3], ilhali anatahadhari na Aakhirah, na anataraji Rehma ya Rabb wake (ni sawa na aliye kinyume chake?). Sema: Je, wanalingana sawa wale wanaojua na wale wasiojua?[4] Hakika wanakumbuka wenye akili tu.
قُلْ يَا عِبَادِ الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا رَبَّكُمْ ۚ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةٌ ۗ وَأَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةٌ ۗ إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿١٠﴾
10. Sema: Enyi Waja Wangu ambao mmeamini, mcheni Rabb wenu. Kwa wale waliofanya mazuri katika dunia hii watapata mazuri. Na Ardhi ya Allaah ni pana. Hakika wanaosubiri watalipwa kikamilifu ujira wao bila ya hesabu.
قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ اللَّـهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ ﴿١١﴾
11. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi nimeamrishwa nimwabudu Allaah nikiwa mwenye kumtakasia Dini Yeye.
وَأُمِرْتُ لِأَنْ أَكُونَ أَوَّلَ الْمُسْلِمِينَ ﴿١٢﴾
12. Na nimeamrishwa kuwa niwe wa kwanza wa Waislamu.
قُلْ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٣﴾
13. Sema: Hakika nikimuasi Rabb wangu, nina khofu adhabu ya Siku iliyo kuu kabisa.
قُلِ اللَّـهَ أَعْبُدُ مُخْلِصًا لَّهُ دِينِي ﴿١٤﴾
14. Sema: Allaah Pekee namwabudu nikimtakasia Yeye tu Dini yangu.
فَاعْبُدُوا مَا شِئْتُم مِّن دُونِهِ ۗ قُلْ إِنَّ الْخَاسِرِينَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَأَهْلِيهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ أَلَا ذَٰلِكَ هُوَ الْخُسْرَانُ الْمُبِينُ ﴿١٥﴾
15. Basi abuduni mnayotaka badala Yake. Sema: Hakika waliokhasirika ni wale waliokhasiri nafsi zao na ahli zao Siku ya Qiyaamah. Tanabahi! Hiyo ndio khasara bayana.
لَهُم مِّن فَوْقِهِمْ ظُلَلٌ مِّنَ النَّارِ وَمِن تَحْتِهِمْ ظُلَلٌ ۚ ذَٰلِكَ يُخَوِّفُ اللَّـهُ بِهِ عِبَادَهُ ۚ يَا عِبَادِ فَاتَّقُونِ ﴿١٦﴾
16. Watawekewa kutoka juu yao matabaka ya moto, na chini yao matabaka. Kwa hayo, Allaah Anakhofisha Waja Wake. Enyi Waja Wangu! Basi Nikhofuni.
وَالَّذِينَ اجْتَنَبُوا الطَّاغُوتَ أَن يَعْبُدُوهَا وَأَنَابُوا إِلَى اللَّـهِ لَهُمُ الْبُشْرَىٰ ۚ فَبَشِّرْ عِبَادِ ﴿١٧﴾
17. Na wale waliojiepusha na kuabudu twaghuti[5] na wakarejea kwa Allaah, watapata bishara njema. Basi wabashirie Waja Wangu.
الَّذِينَ يَسْتَمِعُونَ الْقَوْلَ فَيَتَّبِعُونَ أَحْسَنَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ هَدَاهُمُ اللَّـهُ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمْ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿١٨﴾
18. Wale wanaosikiliza kwa makini maneno, wakafuata yaliyo mazuri yake zaidi, hao ndio wale Aliowahidi Allaah, na hao ndio wenye akili.
أَفَمَنْ حَقَّ عَلَيْهِ كَلِمَةُ الْعَذَابِ أَفَأَنتَ تُنقِذُ مَن فِي النَّارِ ﴿١٩﴾
19. Je, yule liliyemthibitikia neno la adhabu, je, basi wewe utaweza kumuokoa aliyemo katika moto?
لَـٰكِنِ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ لَهُمْ غُرَفٌ مِّن فَوْقِهَا غُرَفٌ مَّبْنِيَّةٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ وَعْدَ اللَّـهِ ۖ لَا يُخْلِفُ اللَّـهُ الْمِيعَادَ ﴿٢٠﴾
20. Lakini wale waliomcha Rabb wao, watapata maghorofa yaliyojengwa juu yake maghorofa, yanapita chini yake mito. Ni Ahadi ya Allaah. Allaah Hakhalifu miadi.
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَسَلَكَهُ يَنَابِيعَ فِي الْأَرْضِ ثُمَّ يُخْرِجُ بِهِ زَرْعًا مُّخْتَلِفًا أَلْوَانُهُ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَاهُ مُصْفَرًّا ثُمَّ يَجْعَلُهُ حُطَامًا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَذِكْرَىٰ لِأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿٢١﴾
21. Je, huoni kwamba Allaah Anateremsha kutoka mbinguni maji, Akayapitisha chemchemu katika ardhi, kisha Anatoa kwayo mimea ya rangi mbalimbali, kisha hunyauka, basi utayaona ni manjano, kisha Huyafanya mabua yaliyonyauka na kupondekapondeka? Hakika katika hayo bila shaka kuna ukumbusho kwa wenye akili.[6]
أَفَمَن شَرَحَ اللَّـهُ صَدْرَهُ لِلْإِسْلَامِ فَهُوَ عَلَىٰ نُورٍ مِّن رَّبِّهِ ۚ فَوَيْلٌ لِّلْقَاسِيَةِ قُلُوبُهُم مِّن ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ أُولَـٰئِكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٢٢﴾
22. Je, ambaye Allaah Amemkunjulia kifua chake kwa Uislamu naye yuko juu ya Nuru kutoka kwa Rabb wake (ni sawa na aliyekinyume chake?). Basi ole wao wenye nyoyo zilizosusuwaa kwa sababu ya kutajwa Allaah. Hao wamo katika upotofu bayana.
اللَّـهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ كِتَابًا مُّتَشَابِهًا مَّثَانِيَ تَقْشَعِرُّ مِنْهُ جُلُودُ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ ثُمَّ تَلِينُ جُلُودُهُمْ وَقُلُوبُهُمْ إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ ﴿٢٣﴾
23. Allaah Ameteremsha habari nzuri kabisa. Ni Kitabu ambacho ibara zake zinashabihiana, zinazokaririwa kila mara. Zinasisimuka kwazo ngozi za wale wanaomkhofu Rabb wao, kisha zinalainika ngozi zao na nyoyo zao kwa kudhukuriwa Allaah. Huo ndio Mwongozo wa Allaah, Humhidi kwao Amtakaye. Na ambaye Allaah Amempotoa basi hana wa kumuongoa.[7]
أَفَمَن يَتَّقِي بِوَجْهِهِ سُوءَ الْعَذَابِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ وَقِيلَ لِلظَّالِمِينَ ذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَكْسِبُونَ ﴿٢٤﴾
24. Je, yule anayekinga kwa uso wake adhabu mbaya Siku ya Qiyaamah (ni sawa na atayesalimika nao?). Na madhalimu wataambiwa: Onjeni yale mliyokuwa mkiyachuma.
كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَأَتَاهُمُ الْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٢٥﴾
25. Wamekadhibisha wale wa kabla yao, basi ikawajia adhabu kutoka mahali wasipotambua.
فَأَذَاقَهُمُ اللَّـهُ الْخِزْيَ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٢٦﴾
26. Allaah Akawaonjesha hizaya katika uhai wa dunia. Na bila shaka adhabu ya Aakhirah ni kubwa zaidi, lau kama wangelikuwa wanajua.
وَلَقَدْ ضَرَبْنَا لِلنَّاسِ فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ مِن كُلِّ مَثَلٍ لَّعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٧﴾
27. Na kwa yakini Tumewapigia watu mifano ya kila aina katika hii Qur-aan ili wapate kukumbuka.
قُرْآنًا عَرَبِيًّا غَيْرَ ذِي عِوَجٍ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ﴿٢٨﴾
28. Qur-aan ya Kiarabu isiyo na kombo ili wapate kuwa na taqwa.
ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا رَّجُلًا فِيهِ شُرَكَاءُ مُتَشَاكِسُونَ وَرَجُلًا سَلَمًا لِّرَجُلٍ هَلْ يَسْتَوِيَانِ مَثَلًا ۚ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢٩﴾
29. Allaah Amepiga mfano wa mtu aliye chini ya washirika wagombanao, na mtu mwengine aliye pweke na bwana mmoja tu. Je, wanalingana sawa kwa hali zao?[8] AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah). Bali wengi wao hawajui.
إِنَّكَ مَيِّتٌ وَإِنَّهُم مَّيِّتُونَ ﴿٣٠﴾
30. Hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) utakufa nao pia watakufa.
ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عِندَ رَبِّكُمْ تَخْتَصِمُونَ ﴿٣١﴾
31. Kisha hakika nyinyi Siku ya Qiyaamah mtazozana mbele ya Rabb wenu.
فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَذَبَ عَلَى اللَّـهِ وَكَذَّبَ بِالصِّدْقِ إِذْ جَاءَهُ ۚ أَلَيْسَ فِي جَهَنَّمَ مَثْوًى لِّلْكَافِرِينَ﴿٣٢﴾
32. Basi ni nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyemsingizia uongo Allaah, na akaukadhibisha ukweli ulipomjia? Je, kwani sio katika Jahannam makazi kwa ajili ya makafiri?
وَالَّذِي جَاءَ بِالصِّدْقِ وَصَدَّقَ بِهِ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ﴿٣٣﴾
33. Na yule aliyekuja na ukweli na akausadikisha,[9] hao ndio wenye taqwa.
لَهُم مَّا يَشَاءُونَ عِندَ رَبِّهِمْ ۚ ذَٰلِكَ جَزَاءُ الْمُحْسِنِينَ﴿٣٤﴾
34. Watapata yale wayatakayo kwa Rabb wao. Hiyo ndio jazaa ya wafanyao ihsaan.
لِيُكَفِّرَ اللَّـهُ عَنْهُمْ أَسْوَأَ الَّذِي عَمِلُوا وَيَجْزِيَهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ الَّذِي كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٣٥﴾
35. Ili Allaah Awafutie ukomo wa uovu walioutenda, na Awalipe ujira wao kwa ukomo wa ihsaan ambao walikuwa wakitenda.
أَلَيْسَ اللَّـهُ بِكَافٍ عَبْدَهُ ۖ وَيُخَوِّفُونَكَ بِالَّذِينَ مِن دُونِهِ ۚ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ﴿٣٦﴾
36. Je, kwani Allaah Si Mwenye Kumtosheleza Mja Wake? Na eti wanakutisha na wale wasiokuwa Yeye. Na ambaye Allaah Amempotoa basi hana wa kumhidi.
وَمَن يَهْدِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِن مُّضِلٍّ ۗ أَلَيْسَ اللَّـهُ بِعَزِيزٍ ذِي انتِقَامٍ﴿٣٧﴾
37. Na ambaye Allaah Amemhidi, basi hapana wa kumpotoa. Je, kwani Allaah Si Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kulipiza?
وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۚ قُلْ أَفَرَأَيْتُم مَّا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ إِنْ أَرَادَنِيَ اللَّـهُ بِضُرٍّ هَلْ هُنَّ كَاشِفَاتُ ضُرِّهِ أَوْ أَرَادَنِي بِرَحْمَةٍ هَلْ هُنَّ مُمْسِكَاتُ رَحْمَتِهِ ۚ قُلْ حَسْبِيَ اللَّـهُ ۖ عَلَيْهِ يَتَوَكَّلُ الْمُتَوَكِّلُونَ﴿٣٨﴾
38. Na ukiwauliza: Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi? Bila shaka watasema: Allaah.[10] Sema: Je, mnaonaje wale mnaowaomba badala ya Allaah, ikiwa Allaah Atanikusudia dhara, je, wao wataweza kuondosha Dhara Yake? Au Akinikusudia Rehma je, wao wataweza kuizuia Rehma Yake? Sema: Ananitosheleza Allaah, Kwake watawakali wenye kutawakali.
قُلْ يَا قَوْمِ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ﴿٣٩﴾
39. Sema: Enyi watu wangu! Tendeni kwa namna zenu, (mnazoridhia), hakika nami natenda. Basi karibuni mtakuja kujua.
مَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَيَحِلُّ عَلَيْهِ عَذَابٌ مُّقِيمٌ﴿٤٠﴾
40. Ni nani itakayemfikia adhabu itakayomhizi, na itamshukia adhabu ya kudumu.
إِنَّا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ لِلنَّاسِ بِالْحَقِّ ۖ فَمَنِ اهْتَدَىٰ فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَا ۖ وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ﴿٤١﴾
41. Hakika Sisi Tumekuteremshia Kitabu kwa ajili ya watu kwa haki. Basi atakayehidika, ni kwa ajili ya nafsi yake. Na atakayepotoka, basi hakika anapotoka dhidi yake, na wewe si mdhamini wao.
اللَّـهُ يَتَوَفَّى الْأَنفُسَ حِينَ مَوْتِهَا وَالَّتِي لَمْ تَمُتْ فِي مَنَامِهَا ۖ فَيُمْسِكُ الَّتِي قَضَىٰ عَلَيْهَا الْمَوْتَ وَيُرْسِلُ الْأُخْرَىٰ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿٤٢﴾
42. Allaah Huzichukua roho wakati wa kufa kwake, na zile zisizokufa katika usingizi wake, kisha Huzizuia ambazo Amezikidhia mauti, na Huzirudisha nyingine mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Hakika katika hayo bila shaka kuna Aayaat (Ishara, Dalili) kwa watu wanaotafakari.[11]
أَمِ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ شُفَعَاءَ ۚ قُلْ أَوَلَوْ كَانُوا لَا يَمْلِكُونَ شَيْئًا وَلَا يَعْقِلُونَ﴿٤٣﴾
43. Je, wamejichukulia badala ya Allaah waombezi? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Je, japokuwa hawana uwezo wa kumiliki chochote na wala hawana akili?
قُل لِّلَّـهِ الشَّفَاعَةُ جَمِيعًا ۖ لَّهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٤٤﴾
44. Sema: Uombezi wote ni wa Allaah Pekee. Ana Ufalme wa mbingu na ardhi, kisha Kwake mtarejeshwa.
وَإِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَحْدَهُ اشْمَأَزَّتْ قُلُوبُ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ ۖ وَإِذَا ذُكِرَ الَّذِينَ مِن دُونِهِ إِذَا هُمْ يَسْتَبْشِرُونَ﴿٤٥﴾
45. Na anapotajwa Allaah Pekee, nyoyo za wale wasioamini Aakhirah hunyweya kwa ghadhabu na kukengeuka, na wanapotajwa wengineo pasi Naye, tahamaki wanafurahia.
قُلِ اللَّـهُمَّ فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ أَنتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِي مَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ﴿٤٦﴾
46. Sema: Ee Allaah! Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa ghaibu na dhahiri, Wewe Utahukumu baina ya Waja Wako katika yale ambayo walikuwa wakikhitilafiana.[12]
وَلَوْ أَنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا مَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا وَمِثْلَهُ مَعَهُ لَافْتَدَوْا بِهِ مِن سُوءِ الْعَذَابِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ وَبَدَا لَهُم مِّنَ اللَّـهِ مَا لَمْ يَكُونُوا يَحْتَسِبُونَ﴿٤٧﴾
47. Na kama wale waliodhulumu wangelikuwa na vile vyote vilivyomo ardhini na pamoja navyo mfano wake, bila shaka wangelivitoa waokoke kutokana na adhabu mbaya ya Siku ya Qiyaamah. Na yatawafichukia kutoka kwa Allaah ambayo hawakuwa wanatarajia.
وَبَدَا لَهُمْ سَيِّئَاتُ مَا كَسَبُوا وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٤٨﴾
48. Na yatawafichukia maovu ya yale waliyoyachuma, na yatawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.
فَإِذَا مَسَّ الْإِنسَانَ ضُرٌّ دَعَانَا ثُمَّ إِذَا خَوَّلْنَاهُ نِعْمَةً مِّنَّا قَالَ إِنَّمَا أُوتِيتُهُ عَلَىٰ عِلْمٍ ۚ بَلْ هِيَ فِتْنَةٌ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٤٩﴾
49. Na inapomgusa binaadam dhara, hutuomba, kisha Tunapomtunukia Neema kutoka Kwetu husema: Hakika nimepewa hayo kwa sababu ya ilimu yangu. Bali hayo ni jaribio, lakini wengi wao hawajui.[13]
قَدْ قَالَهَا الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَمَا أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٥٠﴾
50. Wamekwishayasema hayo wale (waliokadhibisha) kabla yao, basi hayakuwafaa yale waliyokuwa wakiyachuma.
فَأَصَابَهُمْ سَيِّئَاتُ مَا كَسَبُوا ۚ وَالَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْ هَـٰؤُلَاءِ سَيُصِيبُهُمْ سَيِّئَاتُ مَا كَسَبُوا وَمَا هُم بِمُعْجِزِينَ﴿٥١﴾
51. Yakawasibu maovu ya yale waliyoyachuma. Na wale waliodhulumu katika hawa, yatawasibu maovu ya yale waliyoyachuma, nao si wenye kushinda.
أَوَلَمْ يَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴿٥٢﴾
52. Je, hawajui kwamba Allaah Anamkunjulia riziki Amtakaye na Humkadiria kwa kipimo (Amtakaye). Hakika katika hayo mna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa watu wanaoamini.
قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا ۚ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٥٣﴾
53. Sema: Enyi Waja Wangu ambao wamepindukia mipaka juu ya nafsi zao: Msikate tamaa na Rehma ya Allaah, hakika Allaah Anaghufuria dhambi zote. Hakika Yeye Ndiye Mwenye Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[14]
وَأَنِيبُوا إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَأَسْلِمُوا لَهُ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَكُمُ الْعَذَابُ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ﴿٥٤﴾
54. Na rudini kwa Rabb wenu (kwa tawbah na matendo mema) na jisalimisheni Kwake kabla haijakufikieni adhabu, kisha hamtonusuriwa.
وَاتَّبِعُوا أَحْسَنَ مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَكُمُ الْعَذَابُ بَغْتَةً وَأَنتُمْ لَا تَشْعُرُونَ﴿٥٥﴾
55. Na fuateni yaliyo mazuri zaidi ambayo mmeteremshiwa kutoka kwa Rabb wenu kabla haijakufikieni adhabu ghafla na hali nyinyi hamhisi.
أَن تَقُولَ نَفْسٌ يَا حَسْرَتَىٰ عَلَىٰ مَا فَرَّطتُ فِي جَنبِ اللَّـهِ وَإِن كُنتُ لَمِنَ السَّاخِرِينَ﴿٥٦﴾
56. Isije nafsi ikasema: Ee majuto yangu kwa yale niliyokusuru katika upande wa Allaah! Na hakika nilikuwa miongoni mwa wenye kufanya masikhara.
أَوْ تَقُولَ لَوْ أَنَّ اللَّـهَ هَدَانِي لَكُنتُ مِنَ الْمُتَّقِينَ﴿٥٧﴾
57. Au iseme: Lau Allaah Angelinihidi, bila shaka ningelikuwa miongoni mwa wenye taqwa.
أَوْ تَقُولَ حِينَ تَرَى الْعَذَابَ لَوْ أَنَّ لِي كَرَّةً فَأَكُونَ مِنَ الْمُحْسِنِينَ﴿٥٨﴾
58. Au iseme pale itakapoiona adhabu: Lau ningelikuwa na fursa ya kurudi (duniani) basi ningekuwa miongoni mwa wafanyao ihsaan.
بَلَىٰ قَدْ جَاءَتْكَ آيَاتِي فَكَذَّبْتَ بِهَا وَاسْتَكْبَرْتَ وَكُنتَ مِنَ الْكَافِرِينَ﴿٥٩﴾
59. (Ataambiwa) lakini Wapi! Kwa yakini zilikujia Aayaat (na Ishara, Dalili) Zangu ukazikadhibisha, na ukatakabari na ukawa miongoni mwa makafiri.
وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ تَرَى الَّذِينَ كَذَبُوا عَلَى اللَّـهِ وُجُوهُهُم مُّسْوَدَّةٌ ۚ أَلَيْسَ فِي جَهَنَّمَ مَثْوًى لِّلْمُتَكَبِّرِينَ﴿٦٠﴾
60. Na Siku ya Qiyaamah utawaona wale waliomsingizia uongo Allaah, nyuso zao zimesawajika.[15] Je, kwani si katika Jahannam ndio makazi kwa ajili ya wanaotakabari?
وَيُنَجِّي اللَّـهُ الَّذِينَ اتَّقَوْا بِمَفَازَتِهِمْ لَا يَمَسُّهُمُ السُّوءُ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٦١﴾
61. Na Allaah Atawaokoa wale waliokuwa na taqwa kwa sababu ya kufuzu kwao, halitowagusa ovu, na wala hawatohuzunika.
اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ﴿٦٢﴾
62. Allaah Ni Muumbaji wa kila kitu[16], Naye juu ya kila kitu Ni Mdhamini.
لَّهُ مَقَالِيدُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿٦٣﴾
63. Anazo funguo za mbingu na ardhi. Na wale waliozikanusha Aayaat (na Ishara, Dalili) za Allaah hao ndio waliokhasirika.
قُلْ أَفَغَيْرَ اللَّـهِ تَأْمُرُونِّي أَعْبُدُ أَيُّهَا الْجَاهِلُونَ﴿٦٤﴾
64. Sema: Je, mnaniamrisha nimuabudu ghairi ya Allaah enyi majahili?
وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ﴿٦٥﴾
65. Kwa yakini umefunuliwa Wahy na wale walio kabla yako kwamba: Ukifanya shirki bila shaka zitaporomoka amali zako,[17] na kwa hakika utakuwa miongoni mwa waliokhasirika.
بَلِ اللَّـهَ فَاعْبُدْ وَكُن مِّنَ الشَّاكِرِينَ﴿٦٦﴾
66. Bali Allaah Pekee mwabudu, na kuwa miongoni mwa wenye kushukuru.
وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٦٧﴾
67. Na hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria. Na hali ardhi yote Ataikamata Mkononi Mwake Siku ya Qiyaamah, na mbingu zitakunjwa kwa Mkono Wake wa kulia. Subhaanahu wa Ta’aalaa (Utakasifu ni wa Allaah na Ametukuka kwa ‘Uluwa) kutokana na yale yote wanayomshirikisha.[18]
وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَصَعِقَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ إِلَّا مَن شَاءَ اللَّـهُ ۖ ثُمَّ نُفِخَ فِيهِ أُخْرَىٰ فَإِذَا هُمْ قِيَامٌ يَنظُرُونَ﴿٦٨﴾
68. Na itapulizwa katika baragumu. Watakufa kwa mshtuko walioko mbinguni na ardhini isipokua Amtakaye Allaah. Kisha litapulizwa humo jengine, tahamaki hao wanasimama wakitazama.[19]
وَأَشْرَقَتِ الْأَرْضُ بِنُورِ رَبِّهَا وَوُضِعَ الْكِتَابُ وَجِيءَ بِالنَّبِيِّينَ وَالشُّهَدَاءِ وَقُضِيَ بَيْنَهُم بِالْحَقِّ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿٦٩﴾
69. Na ardhi itang’ara kwa Nuru ya Rabb wake, na Kitabu (cha amali) kitawekwa, na wataletwa Manabii na Mashahidi, na patahukumiwa baina yao kwa haki, nao hawatodhulumiwa.
وَوُفِّيَتْ كُلُّ نَفْسٍ مَّا عَمِلَتْ وَهُوَ أَعْلَمُ بِمَا يَفْعَلُونَ﴿٧٠﴾
70. Na kila nafsi italipwa kikamilifu kwa yale iliyoyatenda, Naye Anajua zaidi wanayoyafanya (duniani).
وَسِيقَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ جَهَنَّمَ زُمَرًا ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوهَا فُتِحَتْ أَبْوَابُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَتْلُونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِ رَبِّكُمْ وَيُنذِرُونَكُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا ۚ قَالُوا بَلَىٰ وَلَـٰكِنْ حَقَّتْ كَلِمَةُ الْعَذَابِ عَلَى الْكَافِرِينَ﴿٧١﴾
71. Na wataswagwa wale waliokufuru kuelekea Jahannam vikundi-vikundi, mpaka watakapoifikia, itafunguliwa milango yake, na walinzi wake watawaambia: Je, hawajakufikieni Rusuli miongoni mwenu, wakikusomeeni Aayaat za Rabb wenu, na wakikuonyeni kukutana na Siku yenu hii? Watasema: Ndio (walitufikia)! Lakini neno la adhabu limethibiti juu ya makafiri.
قِيلَ ادْخُلُوا أَبْوَابَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۖ فَبِئْسَ مَثْوَى الْمُتَكَبِّرِينَ﴿٧٢﴾
72. Itasemwa: Ingieni milango ya Jahannam, mdumu humo. Basi ubaya ulioje makazi ya wanaotakabari!
وَسِيقَ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ إِلَى الْجَنَّةِ زُمَرًا ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوهَا وَفُتِحَتْ أَبْوَابُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا سَلَامٌ عَلَيْكُمْ طِبْتُمْ فَادْخُلُوهَا خَالِدِينَ﴿٧٣﴾
73. Na wataongozwa wale waliomcha Rabb wao kuelekea Jannah vikundi-vikundi, mpaka watakapoifikia na milango yake ishafunguliwa, na walinzi wake watawaambia: Salaamun ‘Alaykum! (Amani iwe juu yenu), furahini na iingieni, mdumu milele.
وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي صَدَقَنَا وَعْدَهُ وَأَوْرَثَنَا الْأَرْضَ نَتَبَوَّأُ مِنَ الْجَنَّةِ حَيْثُ نَشَاءُ ۖ فَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ﴿٧٤﴾
74. Watasema: AlhamduliLLaahi (Himidi Anastahiki Allaah) Ambaye Ametuhakikishia kweli Ahadi Yake, na Ameturithisha ardhi tunakaa popote katika Jannah tutakapo. Basi uzuri ulioje ujira wa watendao![20]
وَتَرَى الْمَلَائِكَةَ حَافِّينَ مِنْ حَوْلِ الْعَرْشِ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ ۖ وَقُضِيَ بَيْنَهُم بِالْحَقِّ وَقِيلَ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿٧٥﴾
75. Na utawaona Malaika wakizunguka pembezoni mwa ‘Arsh, wanasabbih na kumhimidi Rabb wao. Na itahukumiwa baina yao kwa haki, na itasemwa: AlhamduliLLaahi (Himidi Anastahiki Allaah), Rabb wa walimwengu.[21]
[1] Kisingizio Cha Washirikina Kuwa Hawaabudu Masanamu Isipokuwa Kwa Ajili Ya Kujikurubisha Kwa Allaah:
Jua utanabahi kwamba ni haki ya Allaah (سبحانه وتعالى) Peke Yake, kutiiwa utiifu uliyotimia na uliosalimika na ushirikina. Na wale wanaomshirikisha mwingine pamoja na Allaah na wakawafanya wasiokuwa Yeye kuwa ni wategemewa, wanasema: “Hatuwaabudu waabudiwa hawa pamoja na Allaah isipokuwa wapate kutuombea kwa Allaah na ili watukurubishe daraja Kwake.” Hivyo basi wakakufuru, kwani ibaada na uombezi ni wa Allaah (سبحانه وتعالى) Peke Yake. Hakika Allaah Atahukumu Siku ya Qiyaamah baina ya Waumini wenye ikhlaasw na wale wenye kumshirikisha mwingine pamoja na Allaah katika yale waliokuwa wanatafautiana juu Yake kuhusu vile walivyoabudu. Hapo Amlipe kila mmoja kwa anachostahiki. Hakika Allaah Hawaelekezi kuongoka kwenye njia iliyonyoka wale wenye kumzulia urongo Allaah, wenye kuzikanusha Aayah Zake na Hoja Zake. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[3] Fadhila Za Qiyaamul-Layl:
Rejea As-Sajdah (32:16), na Adh-Dhaariyaat: (51:15-19) kwenye fadhila za Qiyaamul-Layl (Kisimamo cha usiku kwa ajili ya ibaada).
[6] Ukumbusho Kwa Wenye Akili:
Wanakumbuka kwa maji haya uangalizi wa Rabb wao na huruma Yake kwa Waja Wake, pale Alipoyafanya maji haya wayapate kwa urahisi, na Akayahifadhi katika hazina za ardhi kulingana na maslahi yao. Na wanakumbuka kwa maji haya pia Ukamilifu wa Uweza Wake, na kwamba Yeye Anawahuisha wafu, kama Alivyoihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na wanakumbuka kwamba Mwenye kufanya hayo Anastahiki kuabudiwa. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Rejea Ar-Ruwm (30:50) kwenye maelezo kuhusu mfano wa ardhi iliyokufa (kame) ambayo Allaah Anaihuisha kwa mvua, ni mfano wa kuwahuisha watu kutoka makaburini mwao Siku ya Qiyaamah.
[7] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah:
Kuanzia Aayah hii (23) hadi namba (26), bonyeza kiungo kifuatacho kupata Sababun-Nuzuwl:
[8] Tofauti Ya Mshirikina Na Muumini Na Kwamba Hawalingani Sawa:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anapiga mfano wa mtumwa aliyemilikiwa na washirika wenye kuteta, na mtumwa mwingine aliyekuwa ni wa mmiliki mmoja tu, akawa yuwajua matakwa yake na yanayomridhisha. Je, mfano wa wawili hao unalingana? Basi Hivyo ndivo alivyo mshirikina. Yeye yuko katika hali ya mshangao na shaka, na Muumini yuko katika raha na utulivu. AlhamduliLlaah (Himdi Anastahiki Allaah), lakini washirikina hawaijui haki wakaifuata. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[9] Aliyekuja Na Ukweli Na Akausadikisha:
Kauli za Mufassiruwn kuhusu:
Aliyekuja na ukweli: (i) Ni Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) (ii) Jibriyl (عليه السّلام) (iii) Manabii.
Aliyeusadikisha: (i) Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). (ii) Abu Bakr (رضي الله عنه) (iii) Waumini waliomfuata. [Tafsiyr Ibn Kathiyr na wengineo]
Rejea An-Nisaa (4:69) kwenye maelezo kuhusu Swiddiyquwn.
[10] Washirikina Waliamini Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah Lakini Walikanusha Tawhiyd Al-Uluwhiyyah.
Rejea Yuwnus (10:31), Al-‘Ankabuwt (29:61).
[11] Usingizi Ni Mauti Madogo:
Rejea Al-An’aam (6:60), na Aal-‘Imraan (3:55) kwenye maelezo na duaa zinazothibitisha kuwa mtu anapolala anaingia katika mauti madogo. Na mtu anapolala anatakiwa aseme:
بِاسْمِكَ رَبِّـي وَضَعْـتُ جَنْـبي، وَبِكَ أَرْفَعُـه، فَإِن أَمْسَـكْتَ نَفْسـي فارْحَـمْها، وَإِنْ أَرْسَلْتَـها فاحْفَظْـها بِمـا تَحْفَـظُ بِه عِبـادَكَ الصّـالِحـين
Kwa jina lako Rabb wangu, nimeweka ubavu wangu. Na kwa Msaada Wako nitaunyanyua, Ukiizuia (Ukiichukuwa) roho yangu basi Irehemu na Ukiirudisha basi Ihifadhi kwa kile Unachowahifadhi nacho Swaalihina (Waja wema) Wako. [Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy na Muslim]
اللّهُـمَّ إِنَّـكَ خَلَـقْتَ نَفْسـي وَأَنْـتَ تَوَفّـاهـا لَكَ ممَـاتـها وَمَحْـياها، إِنْ أَحْيَيْـتَها فاحْفَظْـها، وَإِنْ أَمَتَّـها فَاغْفِـرْ لَـها. اللّهُـمَّ إِنَّـي أَسْـأَلُـكَ العـافِـيَة
Ee Allaah, hakika Wewe Umeiumba nafsi yangu Nawe Utaifisha. Ni Wewe Unaumiliki umauti wake na uhai wake. Ukiipa uhai basi Ihifadhi, na Ukiifisha basi Ighufurie. Ee Allaah, hakika mimi nakuomba Al-‘Aafiyah. [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله عنهما) – Muslim, Ahmad]
Al-‘Aafiyah ni neno linalojumuisha Allaah (عزّ وجلّ) kumjaalia mja Wake salama na kumpa amani, na kumlinda na maradhi, balaa, majanga, madhara, misukosuko, na kila aina za shari za wanaadam na majini na kubakia salama katika Dini yake na Aakhirah yake.
Anapoamka mtu aseme:
الحمدُ للهِ الذي عافاني في جَسَدي وَرَدّ عَليّ روحي وَأَذِنَ لي بِذِكْرِه
Himdi ni Zake Allaah Ambaye Amenipa uzima wa mwili wangu, na Akanirudishia roho yangu, na Akaniwezesha kumdhukuru. [Hadiyth ya Abu Hurayrah - At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy; Swahiyh At-Tirmidhiy (3/144)]
Na Rejea Aal-‘Imraan (3:55) kwenye maelezo bayana.
[12] Duaa Mojawapo Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ya Kufungulia Swalaah Anapoamka Usiku Kuswali:
Amesimulia Abu Salamah Bin ‘Abdir-Rahmaah (رضي الله عنه): Nilimuuliza ‘Aaishah (رضي الله عنها): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alianzia na nini katika Swalaah zake anapoamka usiku? Akasema: Alikuwa akisema:
اللَّهُمَّ رَبَّ جِبْرَئِيلَ وَمِيكَائِيلَ وَإِسْرَافِيلَ فَاطِرَ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ أَنْتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ اهْدِنِي لِمَا اخْتُلِفَ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِكَ إِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ "
Ee Allaah, Rabb wa Jibriyl na Mikaaiyl na Israafiyl, Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa ghaibu na dhahiri, Wewe Utahukumu baina ya Waja Wako katika yale ambayo walikuwa wakikhitilafiana. Niongoze mimi kwenye haki katika yale waliyokhitilafiana kwa Idhini Yako. Hakika Wewe Unamhidi Umtakae kwenye Njia Iliyonyooka. [Muslim, An-Nasaaiy, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah]
[15] Nyuso Za Makafiri Zitasawajika Siku Ya Qiyaamah:
Rejea ‘Abasa (80:38) kwenye kubainisha hali za nyuso za Waumini na makafiri zitakavyokuwa Siku ya Qiyaamah.
[16] Allaah (سبحانه وتعالى) Ni Muumbaji Wa Kila Kitu:
Rejea Suwrah Luqmaan (31:11) na Al-Ahqaaf (46:4) kwenye maelezo na rejea mbalimbali.
[17] Aina Za Shirki Na Shirki Inabatilisha Amali:
Rejea Al-An’aam (6:88), Al-Furqaan (25:23), Al-Kahf (18:110).
Shirki ni aina mbili; shirki kubwa na shirki ndogo.
(i) Shirki Kubwa: Inamtoa mtu nje ya Uislamu na amali zake zote zinaporomoka. Mwenye kumshirikisha Allaah (سبحانه وتعالى) kwa shirki kubwa, huwa ni halali damu yake na mali yake na ni mwenye kudumu motoni ikiwa hatotubia kabla ya kufariki kwake. Na dhambi ya shirki kubwa ni dhambi pekee ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Hamsamehi mja atakapokufa bila kutubia. Rejea An-Nisaa (4:48) (4:116).
(ii) Shirki Ndogo: Hii inajulikana kama riyaa, nayo ni kufanya ibaada au kutenda amali lakini kwa niyya ya kujionyesha kwa watu. Shirki hii haimtoi mtu nje ya Uislamu bali amali zake huporomoka na ni mwenye kuadhibiwa motoni kwa kadiri ya madhambi yake.
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amewahofia Swahaaba kutokana na aina hii ya shirki:
عن مَحْمُودِ بْنِ لَبِيدٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إنَّ أخوَفَ ما أخافُ عليكم الشِّركُ الأصغرُ، قالوا: وما الشِّركُ الأصغر؟ قال: الرِّياءُ، يقولُ اللهُ عزَّ وجلَّ لأصحابِ ذلك يومَ القيامةِ إذا جازَى النَّاسَ اذهبوا إلى الَّذين كنتم تُرائون في الدُّنيا فانظُروا هل تجِدون عندهم جزاءً؟" - صححه الألباني في السلسلة الصحيحة(951 )
Amesimulia Mahmuwd bin Labiyd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Hakika ninachokihofia kwenu zaidi ni shirki ndogo. Wakasema: Ni ipi hiyo shirki ndogo? Akasema: Ar-riyaa. Allaah (عزّ وجلّ) Atawaambia watu wa Siku ya Qiyaamah pale watakapolipwa watu jazaa: Nendeni kwa wale mliokuwa mkijionyesha kwa amali zenu duniani kisha tazameni je, mtakuta kwao jazaa? [Ahmad na ameisahihisha Shaykh Al-Albaaniy katika Silsilat Al-Hadiyth Asw-Swahiyhah (951)]
Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ametaja katika Hadiyth Al-Qudsiy:
عنْ ابي هريرة رضي الله عنه أنَّه صلَّى الله عليه وسلَّم قال: ((قال الله تعالى: أنا أغْنى الشُّركاء عن الشِّرْك، فمَن عمل عملاً أشْرَك فيه معي غيري تركتُه وشِرْكه))
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah Ta’aalaa Anasema: Mimi Ni Mwenye kujitosheleza kabisa, Sihitaji msaada wala mshirika. Kwa hiyo, yule afanyaye amali kwa kunishirikisha na mtu, Nitaikanusha pamoja na mshirika wake.” Yaani: hatopata ujira wowote kwa amali hiyo. [Muslim (2985), Ibn Maajah (4202)]
[19] Kupulizwa Baragumu Mara Ya Kwanza Na Mara Ya Pili:
Katika mpulizo wa kwanza, watakufa watu wote kwa mshtuko na kiwewe isipokuwa Anaotaka Allaah wasife nao ni Shuhadaa na wengineo
Mpulizo wa pili ni ule utakaowafufua watu kutoka makaburini wakiwa katika uumbaji upya wa kimwili na roho na watasimama mbele wakitazama kusubiri kuhesabiwa matendo yao. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Muda wa baina ya mpulizo wa kwanza na wa pili ni arubaini. Lakini haijulikani kama ni siku arubaini, au miezi au miaka kama ilivyotajwa katika Hadiyth ifuatayo:
حَدَّثَنِي مُحَمَّدٌ، أَخْبَرَنَا أَبُو مُعَاوِيَةَ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " مَا بَيْنَ النَّفْخَتَيْنِ أَرْبَعُونَ ". قَالَ أَرْبَعُونَ يَوْمًا قَالَ أَبَيْتُ. قَالَ أَرْبَعُونَ شَهْرًا قَالَ أَبَيْتُ. قَالَ أَرْبَعُونَ سَنَةً قَالَ أَبَيْتُ. قَالَ " ثُمَّ يُنْزِلُ اللَّهُ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً. فَيَنْبُتُونَ كَمَا يَنْبُتُ الْبَقْلُ لَيْسَ مِنَ الإِنْسَانِ شَىْءٌ إِلاَّ يَبْلَى إِلاَّ عَظْمًا وَاحِدًا وَهْوَ عَجْبُ الذَّنَبِ، وَمِنْهُ يُرَكَّبُ الْخَلْقُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ".
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Muda ulio kati ya pulizo (baragumu) mbili ni arobaini.” Mtu mmoja akamuuliza Abuu Hurayrah: Je, ni siku arobaini? Abuu Hurayrah akasema: Sikujibu. Kisha akauliza tena: Je, ni miezi arobaini? Abuu Hurayrah akasema: Sikujibu. Kisha akauliza tena: Je, ni miaka arobaini? Abuu Hurayrah akasema: Sikujibu. Kisha Abuu Hurayrah akaongeza: Kisha baada ya muda huo Allaah Atateremsha maji kutoka mbinguni, na watu wataota kama zinavyoota mboga, hakuna kitu kwa mwanaadam isipokuwa kitachakaa, isipokuwa mfupa mmoja tu, huo ni ‘ajbu-dhanab (kifandugu/kitokono), na kutokana na mfupa huo, mwanaadam ataumbwa upya umbile lake Siku ya Qiyaamah. [Al-Bukhaariy]
Faida: ‘Ajbu-dhanab (kifandugu/kitokono) ni mfupa ambao upo mwisho wa uti wa mgongo au kifupa cha mkia.
Rejea An-Naml (27:87) kwenye faida nyenginezo na maelezo bayana. Na pia Al-Haaqqah (69:13), An-Naazi’aat (79:6-7), Yaasiyn (36:51).
[20] Waumini Watamhimidi Allaah Watakapoingia Jannah:
Waumini watakapoingizwa Jannah, na kuona neema zake tukufu, watamhimidi Allaah kwa kusema AlhamduliLlaah. Hii ni sawa kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah nyenginezo. Rejea Al-A’raaf (7:43). Na pia rejea Faatwiir (35:33-35) ambako pia kuna maelezo kuhusu neema za Jannah.
[21] Malaika Watakavyozunguka ‘Arsh Ya Allaah Na Kumsabbih Allaah Kwa Kumhimidi:
Na utawaona Malaika, ee Nabii, wameizunguka 'Arsh ya Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma) wanamtakasa Rabb wao na kila kisichofaa kunasibishwa nacho, (na utaona kuwa) Allaah (سبحانه وتعالى) Amehukumu baina ya viumbe kwa uhaki na uadilifu. Akawakalisha wenye kuamini Peponi na wenye kukufuru motoni. Na hapo kutasemwa: “AlhamduliLLaahi (Himidi Anastahiki Allaah), Rabb wa walimwengu kwa hukumu Aliyopitisha baina ya watu wa Peponi na motoni.” Ni Himdi (na shukurani) ya kutambua wema na hisaan, na Himdi (na shukurani) ya kutambua uadilifu na hekima. [Tafsiyr Al-Muyassar]
غَافِر
040-Ghaafir
040-Ghaafir: Utangulizi Wa Suwrah [270]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم
حم﴿١﴾
1. Haa Miym.[1]
تَنزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ﴿٢﴾
2. Ni uteremsho wa Kitabu kutoka kwa Allaah Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.
غَافِرِ الذَّنبِ وَقَابِلِ التَّوْبِ شَدِيدِ الْعِقَابِ ذِي الطَّوْلِ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ إِلَيْهِ الْمَصِيرُ﴿٣﴾
3. Mwenye Kughufuria dhambi, Anayepokea tawbah, Mkali wa Kuakibu[2], Mwenye wingi wa Ukarimu, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, Kwake ndio mahali pa kuishia.
مَا يُجَادِلُ فِي آيَاتِ اللَّـهِ إِلَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَلَا يَغْرُرْكَ تَقَلُّبُهُمْ فِي الْبِلَادِ﴿٤﴾
4. Habishani katika Aayaat (na Ishara, Hoja) za Allaah isipokuwa wale waliokufuru, basi kusikughuri kutamba kwao huku na kule katika nchi.
كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَالْأَحْزَابُ مِن بَعْدِهِمْ ۖ وَهَمَّتْ كُلُّ أُمَّةٍ بِرَسُولِهِمْ لِيَأْخُذُوهُ ۖ وَجَادَلُوا بِالْبَاطِلِ لِيُدْحِضُوا بِهِ الْحَقَّ فَأَخَذْتُهُمْ ۖ فَكَيْفَ كَانَ عِقَابِ﴿٥﴾
5. Walikadhibisha kabla yao watu wa Nuwh, na makundi baada yao. Na kila ummah ulitilia hima kufanya njama juu ya Rasuli wake ili wamkamate, na wakabishana kwa ubatilifu ili waitengue haki, Nikawakamata, basi vipi ilikuwa Ikabu Yangu!
وَكَذَٰلِكَ حَقَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّهُمْ أَصْحَابُ النَّارِ﴿٦﴾
6. Na hivyo ndivyo limethibiti Neno la Rabb wako juu ya wale waliokufuru kwamba wao ni watu wa motoni.
الَّذِينَ يَحْمِلُونَ الْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَيْءٍ رَّحْمَةً وَعِلْمًا فَاغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا وَاتَّبَعُوا سَبِيلَكَ وَقِهِمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ﴿٧﴾
7. (Malaika) ambao wanabeba ‘Arsh na walio pembezoni mwake, wanasabbih na kumhimidi Rabbi wao, na wanamwamini, na wanawaombea maghfirah wale walioamini (wakisema): Rabb wetu! Umekienea kila kitu kwa Rehma na ujuzi, basi Waghufurie wale waliotubu, na wakafuata njia Yako, na Wakinge na adhabu ya moto uwakao vikali mno.
رَبَّنَا وَأَدْخِلْهُمْ جَنَّاتِ عَدْنٍ الَّتِي وَعَدتَّهُمْ وَمَن صَلَحَ مِنْ آبَائِهِمْ وَأَزْوَاجِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٨﴾
8. Rabb wetu! Waingize Jannaat za kudumu milele ambazo Umewaahidi, pamoja na waliotengenea miongoni mwa baba zao, na wake zao, na dhuria wao. Hakika Wewe Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye
Hikmah wa yote.
وَقِهِمُ السَّيِّئَاتِ ۚ وَمَن تَقِ السَّيِّئَاتِ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمْتَهُ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٩﴾
9. Na Wakinge na maovu, kwani Unayemkinga na maovu Siku hiyo, basi kwa yakini Umemrehemu. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنَادَوْنَ لَمَقْتُ اللَّـهِ أَكْبَرُ مِن مَّقْتِكُمْ أَنفُسَكُمْ إِذْ تُدْعَوْنَ إِلَى الْإِيمَانِ فَتَكْفُرُونَ﴿١٠﴾
10. Hakika wale waliokufuru watanadiwa: Bila shaka kuchukia kwa Allaah ni kukubwa zaidi kuliko kujichukia nafsi zenu (leo motoni) pale mlipokuwa mnaitwa kwenye imaan mkakufuru.
قَالُوا رَبَّنَا أَمَتَّنَا اثْنَتَيْنِ وَأَحْيَيْتَنَا اثْنَتَيْنِ فَاعْتَرَفْنَا بِذُنُوبِنَا فَهَلْ إِلَىٰ خُرُوجٍ مِّن سَبِيلٍ﴿١١﴾
11. Watasema: Rabb wetu! Umetufisha mara mbili na Umetuhuisha mara mbili,[3] na tumekiri madhambi yetu. Basi je, kuna njia ya kutoka?
ذَٰلِكُم بِأَنَّهُ إِذَا دُعِيَ اللَّـهُ وَحْدَهُ كَفَرْتُمْ ۖ وَإِن يُشْرَكْ بِهِ تُؤْمِنُوا ۚ فَالْحُكْمُ لِلَّـهِ الْعَلِيِّ الْكَبِيرِ﴿١٢﴾
12. (Wataambiwa): Hivyo kwenu ni kwa sababu Alipoombwa Allaah Pekee, mlikufuru, na aliposhirikishwa, mliamini. Basi hukumu ni ya Allaah Pekee Mwenye ‘Uluwa Uliotukuka, Mkubwa Kabisa.
هُوَ الَّذِي يُرِيكُمْ آيَاتِهِ وَيُنَزِّلُ لَكُم مِّنَ السَّمَاءِ رِزْقًا ۚ وَمَا يَتَذَكَّرُ إِلَّا مَن يُنِيبُ ﴿١٣﴾
13. Yeye Ndiye Ambaye Anakuonyesheni Aayaat[4] (Ishara, Dalili) Zake na Anakuteremshieni kutoka mbinguni riziki (mvua). Na hakumbuki (na kuwaidhika) isipokuwa mwenye kurejea kwa Allaah (katika mambo yake yote).
فَادْعُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ﴿١٤﴾
14. Basi mwombeni Allaah kwa kumtakasia Yeye Dini japokuwa makafiri wanachukia.
رَفِيعُ الدَّرَجَاتِ ذُو الْعَرْشِ يُلْقِي الرُّوحَ مِنْ أَمْرِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ لِيُنذِرَ يَوْمَ التَّلَاقِ﴿١٥﴾
15. (Allaah) Mwenye ‘Uluwa juu ya vyeo na daraja. Mwenye ‘Arsh, Anapelekea Ar-Ruwh (Wahy) kwa Amri Yake kwa Amtakaye miongoni mwa Waja Wake, ili aonye Siku ya kukutana.
يَوْمَ هُم بَارِزُونَ ۖ لَا يَخْفَىٰ عَلَى اللَّـهِ مِنْهُمْ شَيْءٌ ۚ لِّمَنِ الْمُلْكُ الْيَوْمَ ۖ لِلَّـهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ﴿١٦﴾
16. Siku watakayotokeza wao, hakitofichika kitu chochote chao kwa Allaah. Ufalme ni wa nani leo? (Allaah Mwenyewe Atajijibu): Ni wa Allaah Pekee Mmoja, Asiyepingika.[5]
الْيَوْمَ تُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ ۚ لَا ظُلْمَ الْيَوْمَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ﴿١٧﴾
17. Leo kila nafsi italipwa kwa yale iliyoyachuma, hakuna dhulma leo! Hakika Allaah Ni Mwepesi wa Kuhesabu.
وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ الْآزِفَةِ إِذِ الْقُلُوبُ لَدَى الْحَنَاجِرِ كَاظِمِينَ ۚ مَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلَا شَفِيعٍ يُطَاعُ﴿١٨﴾
18. Na waonye Siku inayokurubia sana pale nyoyo zitakapofika kooni nao wamejaa huzuni na majuto. Madhalimu hawatokuwa na rafiki wa dhati, wala mwombezi anayetiiwa.
يَعْلَمُ خَائِنَةَ الْأَعْيُنِ وَمَا تُخْفِي الصُّدُورُ﴿١٩﴾
19. (Allaah) Anajua khiyana za macho na yale yanayoficha vifua.[6]
وَاللَّـهُ يَقْضِي بِالْحَقِّ ۖ وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَقْضُونَ بِشَيْءٍ ۗ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ﴿٢٠﴾
20. Na Allaah Anahukumu kwa haki. Na wale wanaowaomba badala Yake hawawezi kuhukumu chochote. Hakika Allaah Ndiye Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.
أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ كَانُوا مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَانُوا هُمْ أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَآثَارًا فِي الْأَرْضِ فَأَخَذَهُمُ اللَّـهُ بِذُنُوبِهِمْ وَمَا كَانَ لَهُم مِّنَ اللَّـهِ مِن وَاقٍ﴿٢١﴾
21. Je, hawakutembea katika ardhi, wakatazama vipi ilikuwa hatima ya wale waliokuwa kabla yao?[7] Walikuwa wenye nguvu zaidi kuliko wao, na athari katika ardhi, lakini Allaah Aliwakamata kwa sababu ya madhambi yao, na wala hawakuwa na wa kuwalinda dhidi ya Allaah.
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانَت تَّأْتِيهِمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَكَفَرُوا فَأَخَذَهُمُ اللَّـهُ ۚ إِنَّهُ قَوِيٌّ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴿٢٢﴾
22. Hayo ni kwa sababu walikuwa wanawajia Rusuli wao kwa hoja za waziwazi, lakini wakawakanusha, ndipo Allaah Akawakamata. Hakika Yeye Ni Mwenye nguvu, Mkali wa Kuakibu.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُّبِينٍ﴿٢٣﴾
23. Na kwa yakini Tulimtuma Muwsaa kwa Aayaat (Ishara, Miujiza, Dalili) Zetu na mamlaka bayana.
إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَقَارُونَ فَقَالُوا سَاحِرٌ كَذَّابٌ﴿٢٤﴾
24. Kwa Firawni na Haamaan na Qaaruwn, wakasema: Mchawi muongo.[8]
فَلَمَّا جَاءَهُم بِالْحَقِّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا اقْتُلُوا أَبْنَاءَ الَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ وَاسْتَحْيُوا نِسَاءَهُمْ ۚ وَمَا كَيْدُ الْكَافِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَالٍ﴿٢٥﴾
25. Na alipowajia kwa haki kutoka Kwetu walisema: Wauweni watoto wa kiume wa wale walioamini pamoja naye, na waacheni hai wanawake wao. Na hila za makafiri haziwi isipokuwa katika upotofu.
وَقَالَ فِرْعَوْنُ ذَرُونِي أَقْتُلْ مُوسَىٰ وَلْيَدْعُ رَبَّهُ ۖ إِنِّي أَخَافُ أَن يُبَدِّلَ دِينَكُمْ أَوْ أَن يُظْهِرَ فِي الْأَرْضِ الْفَسَادَ﴿٢٦﴾
26. Na Firawni akasema: Niacheni nimuue Muwsaa, naye amwite Rabb wake! Hakika mimi nakhofu asije kukubadilishieni dini yenu, au akaeneza ufisadi katika ardhi.
وَقَالَ مُوسَىٰ إِنِّي عُذْتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُم مِّن كُلِّ مُتَكَبِّرٍ لَّا يُؤْمِنُ بِيَوْمِ الْحِسَابِ﴿٢٧﴾
27. Na Muwsaa akasema: Hakika mimi najikinga kwa Rabb wangu na Rabb wenu, kutokana na kila mwenye kutakabari asiyeamini Siku ya Hesabu.
وَقَالَ رَجُلٌ مُّؤْمِنٌ مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَكْتُمُ إِيمَانَهُ أَتَقْتُلُونَ رَجُلًا أَن يَقُولَ رَبِّيَ اللَّـهُ وَقَدْ جَاءَكُم بِالْبَيِّنَاتِ مِن رَّبِّكُمْ ۖ وَإِن يَكُ كَاذِبًا فَعَلَيْهِ كَذِبُهُ ۖ وَإِن يَكُ صَادِقًا يُصِبْكُم بَعْضُ الَّذِي يَعِدُكُمْ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ مُسْرِفٌ كَذَّابٌ﴿٢٨﴾
28. Na akasema mtu mmoja Muumini miongoni mwa familia ya Firawni, aliyeficha imaan yake[9]: Je, mnamuua mtu kwa kuwa tu anasema: Rabb wangu ni Allaah? Na hali amekujieni na hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu? Na akiwa ni muongo, basi uongo wake utamrudia mwenyewe, na akiwa ni mkweli, yatakusibuni baadhi ya yale anayokuahidini. Hakika Allaah Hamwongoi yule anayepindukia mipaka, muongo mkubwa.
يَا قَوْمِ لَكُمُ الْمُلْكُ الْيَوْمَ ظَاهِرِينَ فِي الْأَرْضِ فَمَن يَنصُرُنَا مِن بَأْسِ اللَّـهِ إِن جَاءَنَا ۚ قَالَ فِرْعَوْنُ مَا أُرِيكُمْ إِلَّا مَا أَرَىٰ وَمَا أَهْدِيكُمْ إِلَّا سَبِيلَ الرَّشَادِ﴿٢٩﴾
29. Enyi watu wangu! Leo mna ufalme, mmeshinda katika ardhi. Basi ni nani atakayetunusuru kutokana na Adhabu ya Allaah ikitujia? Firawni akasema: Sikuonyesheni isipokuwa yale ninayoyaona (ni sahihi), na sikuongozeni isipokuwa njia ya uongofu.
وَقَالَ الَّذِي آمَنَ يَا قَوْمِ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُم مِّثْلَ يَوْمِ الْأَحْزَابِ﴿٣٠﴾
30. Na yule aliyeamini akasema: Enyi watu wangu! Hakika mimi nakukhofieni mfano wa siku ya makundi.
مِثْلَ دَأْبِ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ وَالَّذِينَ مِن بَعْدِهِمْ ۚ وَمَا اللَّـهُ يُرِيدُ ظُلْمًا لِّلْعِبَادِ﴿٣١﴾
31. Mfano wa ada za kaumu ya Nuwh, na ‘Aad, na Thamuwd na wale wa baada yao. Na Allaah Hakusudii dhulma kwa waja.
وَيَا قَوْمِ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ يَوْمَ التَّنَادِ﴿٣٢﴾
32. Na enyi kaumu yangu! Hakika mimi nakukhofieni Siku ya kuitana.[10]
يَوْمَ تُوَلُّونَ مُدْبِرِينَ مَا لَكُم مِّنَ اللَّـهِ مِنْ عَاصِمٍ ۗ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ﴿٣٣﴾
33. Siku mtakayogeuka nyuma mkimbie wala hamtokuwa na wa kukulindeni dhidi ya Allaah. Na ambaye Allaah Amempotoa basi hana yeyote wa kumhidi.
وَلَقَدْ جَاءَكُمْ يُوسُفُ مِن قَبْلُ بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا زِلْتُمْ فِي شَكٍّ مِّمَّا جَاءَكُم بِهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا هَلَكَ قُلْتُمْ لَن يَبْعَثَ اللَّـهُ مِن بَعْدِهِ رَسُولًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّـهُ مَنْ هُوَ مُسْرِفٌ مُّرْتَابٌ﴿٣٤﴾
34. Na kwa yakini alikujieni Yuwsuf kabla kwa hoja bayana, lakini mliendelea katika shaka kwa yale aliyokuleteeni, mpaka alipokufa mkasema: Allaah Hatotuma Rasuli baada yake. Hivyo ndivyo Allaah Anavyompotoa yule apindukiaye mipaka, mwenye kutia shaka.
الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِ اللَّـهِ بِغَيْرِ سُلْطَانٍ أَتَاهُمْ ۖ كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ وَعِندَ الَّذِينَ آمَنُوا ۚ كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ قَلْبِ مُتَكَبِّرٍ جَبَّارٍ﴿٣٥﴾
35. Wale wanaobishana kuhusu Aayaat (Ishara, Hoja) za Allaah (ili wazibatilishe) bila ya dalili yoyote kuwafikia, ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah na mbele ya wale walioamini. Hivyo ndivyo Allaah Anavyopiga chapa juu ya kila moyo wa mwenye kutakabari, jabari.
وَقَالَ فِرْعَوْنُ يَا هَامَانُ ابْنِ لِي صَرْحًا لَّعَلِّي أَبْلُغُ الْأَسْبَابَ﴿٣٦﴾
36. Na Firawni akasema: Ee Haamaan! Nijengee mnara ili nizifikie njia.
أَسْبَابَ السَّمَاوَاتِ فَأَطَّلِعَ إِلَىٰ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ كَاذِبًا ۚ وَكَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِفِرْعَوْنَ سُوءُ عَمَلِهِ وَصُدَّ عَنِ السَّبِيلِ ۚ وَمَا كَيْدُ فِرْعَوْنَ إِلَّا فِي تَبَابٍ﴿٣٧﴾
37. Njia za mbinguni ili nimchungulie Ilaah wa Muwsaa, kwani hakika mimi namtambua fika kuwa ni muongo. Na hivyo ndivyo alivyopambiwa Firawni uovu wa amali yake, na akazuiliwa njia (ya haki). Na njama za Firawni hazikuwa isipokuwa katika kuteketea.
وَقَالَ الَّذِي آمَنَ يَا قَوْمِ اتَّبِعُونِ أَهْدِكُمْ سَبِيلَ الرَّشَادِ﴿٣٨﴾
38. Na yule aliyeamini[11] akasema: Enyi kaumu yangu! Nifuateni nikuongozeni njia ya uongofu.
يَا قَوْمِ إِنَّمَا هَـٰذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا مَتَاعٌ وَإِنَّ الْآخِرَةَ هِيَ دَارُ الْقَرَارِ﴿٣٩﴾
39. Enyi kaumu yangu! Hakika huu uhai wa dunia ni starehe ya kupita tu, na hakika Aakhirah ndiyo nyumba ya kudumu milele.
مَنْ عَمِلَ سَيِّئَةً فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا ۖ وَمَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ يُرْزَقُونَ فِيهَا بِغَيْرِ حِسَابٍ﴿٤٠﴾
40. Yeyote atakayetenda uovu, basi hatolipwa isipokuwa mfano wake. Na yeyote atakayetenda mema kati ya mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini, basi hao wataingia Jannah na wataruzukiwa humo bila ya hesabu.
وَيَا قَوْمِ مَا لِي أَدْعُوكُمْ إِلَى النَّجَاةِ وَتَدْعُونَنِي إِلَى النَّارِ﴿٤١﴾
41. Na enyi kaumu yangu! Iweje mimi nakuiteni kwenye uokovu, nanyi mnaniita kwenye moto?!
تَدْعُونَنِي لِأَكْفُرَ بِاللَّـهِ وَأُشْرِكَ بِهِ مَا لَيْسَ لِي بِهِ عِلْمٌ وَأَنَا أَدْعُوكُمْ إِلَى الْعَزِيزِ الْغَفَّارِ﴿٤٢﴾
42. Mnaniita ili nimkufuru Allaah na nimshirikishe na yale nisiyokuwa na ilimu nayo, na hali mimi nakuiteni kwa Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwingi wa Kughufuria?!
لَا جَرَمَ أَنَّمَا تَدْعُونَنِي إِلَيْهِ لَيْسَ لَهُ دَعْوَةٌ فِي الدُّنْيَا وَلَا فِي الْآخِرَةِ وَأَنَّ مَرَدَّنَا إِلَى اللَّـهِ وَأَنَّ الْمُسْرِفِينَ هُمْ أَصْحَابُ النَّارِ﴿٤٣﴾
43. Hapana shaka kwamba ambaye mnayeniitia kwake hastahiki wito duniani wala Aakhirah, na kwamba marudio yetu ni kwa Allaah, na kwamba wapindukao mipaka wao ndio watu wa motoni.
فَسَتَذْكُرُونَ مَا أَقُولُ لَكُمْ ۚ وَأُفَوِّضُ أَمْرِي إِلَى اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ﴿٤٤﴾
44. Basi mtakumbuka karibuni yale ninayokuambieni, nami naaminisha mambo yangu kwa Allaah. Hakika Allaah Ni Mwenye Kuona Waja Wake.
فَوَقَاهُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِ مَا مَكَرُوا ۖ وَحَاقَ بِآلِ فِرْعَوْنَ سُوءُ الْعَذَابِ﴿٤٥﴾
45. Basi Allaah Akamlinda na maovu ya njama walizopanga, na watu wa Firawni ikawazunguka adhabu mbaya kabisa.
النَّارُ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا غُدُوًّا وَعَشِيًّا ۖ وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ أَدْخِلُوا آلَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ الْعَذَابِ﴿٤٦﴾
46. Wanadhihirishiwa moto asubuhi na jioni, na Siku itakayosimama Saa (itasemwa): Waingizeni watu wa Firawni katika adhabu kali kabisa.[12]
وَإِذْ يَتَحَاجُّونَ فِي النَّارِ فَيَقُولُ الضُّعَفَاءُ لِلَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا كُنَّا لَكُمْ تَبَعًا فَهَلْ أَنتُم مُّغْنُونَ عَنَّا نَصِيبًا مِّنَ النَّارِ﴿٤٧﴾
47. Na pale watakapobishana motoni, watasema walio wanyonge kuwaambia wale waliotakabari: Hakika sisi tulikuwa wafuasi wenu, basi je, nyinyi mnaweza kutuondolea sehemu yoyote ya moto?
قَالَ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا كُلٌّ فِيهَا إِنَّ اللَّـهَ قَدْ حَكَمَ بَيْنَ الْعِبَادِ﴿٤٨﴾
48. Watasema wale waliotakabari: Hakika sisi sote tumo humo, hakika Allaah Amekwishahukumu baina ya waja.
وَقَالَ الَّذِينَ فِي النَّارِ لِخَزَنَةِ جَهَنَّمَ ادْعُوا رَبَّكُمْ يُخَفِّفْ عَنَّا يَوْمًا مِّنَ الْعَذَابِ﴿٤٩﴾
49. Na watasema wale waliomo motoni kuwaambia Walinzi wa Jahannam: Mwombeni Rabb wenu Atukhafifishie siku moja ya adhabu.
قَالُوا أَوَلَمْ تَكُ تَأْتِيكُمْ رُسُلُكُم بِالْبَيِّنَاتِ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۚ قَالُوا فَادْعُوا ۗ وَمَا دُعَاءُ الْكَافِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَالٍ﴿٥٠﴾
50. Watasema: Je, kwani hawakuwa wakikufikieni Rusuli wenu kwa hoja bayana? Waseme: Ndio (walitufikia)! Watasema: Basi ombeni. Na haziwi duaa za makafiri isipokuwa kuishilia patupu.
إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ﴿٥١﴾
51. Hakika Sisi bila shaka Tutawanusuru Rusuli Wetu na wale walioamini katika uhai wa dunia, na Siku watakayosimama mashahidi.
يَوْمَ لَا يَنفَعُ الظَّالِمِينَ مَعْذِرَتُهُمْ ۖ وَلَهُمُ اللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوءُ الدَّارِ﴿٥٢﴾
52. Siku ambayo hautowafaa madhalimu udhuru wao, na watapata laana na watapata makazi mabaya.
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْهُدَىٰ وَأَوْرَثْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ الْكِتَابَ﴿٥٣﴾
53. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa mwongozo na Tukawarithisha Wana wa Israaiyl Kitabu.
هُدًى وَذِكْرَىٰ لِأُولِي الْأَلْبَابِ﴿٥٤﴾
54. Ni mwongozo na ukumbusho kwa wenye akili.
فَاصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ﴿٥٥﴾
55. Basi vuta subira (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), hakika Ahadi ya Allaah ni ya kweli kabisa! Na omba maghfirah kwa dhambi zako, na Sabbih (Mtakase) na Mhimidi Rabb wako jioni na asubuhi.
إِنَّ الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِ اللَّـهِ بِغَيْرِ سُلْطَانٍ أَتَاهُمْ ۙ إِن فِي صُدُورِهِمْ إِلَّا كِبْرٌ مَّا هُم بِبَالِغِيهِ ۚ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ﴿٥٦﴾
56. Hakika wale wanaobishana kuhusu Aayaat (Ishara, Hoja) za Allaah bila ya dalili yoyote kuwafikia, hamna vifuani mwao isipokuwa kiburi, lakini hawatoufikia (Unabii). Basi jikinge kwa Allaah, hakika Yeye Ndiye Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.[13]
لَخَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَكْبَرُ مِنْ خَلْقِ النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٥٧﴾
57. Bila shaka uumbaji wa mbingu na ardhi ni mkubwa zaidi kuliko uumbaji wa watu, lakini watu wengi hawajui.[14]
وَمَا يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَلَا الْمُسِيءُ ۚ قَلِيلًا مَّا تَتَذَكَّرُونَ﴿٥٨﴾
58. Na halingani sawa kipofu na mwenye kuona, na (wala) wale walioamini na wakatenda mema na muovu. Kidogo sana mnayoyakumbuka.
إِنَّ السَّاعَةَ لَآتِيَةٌ لَّا رَيْبَ فِيهَا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ﴿٥٩﴾
59. Hakika Saa bila shaka itafika tu, haina shaka ndani yake, lakini watu wengi hawaamini.
وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ﴿٦٠﴾
60. Na Rabb wenu Amesema: Niombeni, Nitakuitikieni. Hakika wale wanaotakabari katika kuniabudu wataingia Jahanam wadhalilike.[15]
اللَّـهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَالنَّهَارَ مُبْصِرًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ﴿٦١﴾
61. Allaah Ambaye Amekufanyieni usiku ili mpate utulivu humo, na mchana wenye kuangaza. Hakika Allaah Ni Mwenye Fadhila kwa watu, lakini watu wengi hawashukuru.
ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ﴿٦٢﴾
62. Huyo Ndiye Allaah Rabb wenu, Muumba wa kila kitu, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye. Basi vipi mnaghilibiwa?
كَذَٰلِكَ يُؤْفَكُ الَّذِينَ كَانُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ يَجْحَدُونَ﴿٦٣﴾
63. Hivyo ndivyo wanavyoghilibiwa wale waliokuwa wakizikanusha Aayaat (Ishara, Hoja) za Allaah.
اللَّـهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ قَرَارًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ فَتَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ﴿٦٤﴾
64. Allaah Ambaye Amekufanyieni ardhi kuwa mahali pa makazi, na mbingu kama ni paa, na Akakutieni sura Akazifanya nzuri zaidi sura zenu, na Akakuruzukuni katika vizuri. Huyo Ndiye Allaah Rabb wenu. Basi Tabaaraka-Allaah! (Amebarikika Allaah) Rabb wa walimwengu.
هُوَ الْحَيُّ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ ۗ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿٦٥﴾
65. Yeye Ndiye Aliye Hai daima, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye. Basi muombeni Yeye kwa kumtakasia Dini. AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah) Rabb wa walimwengu.
قُلْ إِنِّي نُهِيتُ أَنْ أَعْبُدَ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ لَمَّا جَاءَنِيَ الْبَيِّنَاتُ مِن رَّبِّي وَأُمِرْتُ أَنْ أُسْلِمَ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ﴿٦٦﴾
66. Sema: Hakika mimi nimekatazwa kuwaabudu wale mnaowaomba badala ya Allaah ziliponijia hoja bayana kutoka kwa Rabb wangu, na nimeamrishwa nijisalimishe kwa Rabb wa walimwengu.
هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَةٍ ثُمَّ يُخْرِجُكُمْ طِفْلًا ثُمَّ لِتَبْلُغُوا أَشُدَّكُمْ ثُمَّ لِتَكُونُوا شُيُوخًا ۚ وَمِنكُم مَّن يُتَوَفَّىٰ مِن قَبْلُ ۖ وَلِتَبْلُغُوا أَجَلًا مُّسَمًّى وَلَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ﴿٦٧﴾
67. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na mchanga, kisha kutokana na tone la manii, kisha kutokana na pande la damu linaloning’inia, kisha Anakutoeni mkiwa watoto wachanga, kisha mfikie umri wenu wa kupevuka, kisha ili muwe wazee. Na yuko miongoni mwenu ambaye hufishwa kabla, na ili mfikie muda maalumu uliokadiriwa, na ili mpate kutia akilini.[16]
هُوَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ فَإِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ﴿٦٨﴾
68. Yeye Ni Yule Anayehuisha na Anayefisha. Na Anapolikidhia jambo lolote basi Huliambia: Kun! (Kuwa) nalo linakuwa.
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِ اللَّـهِ أَنَّىٰ يُصْرَفُونَ﴿٦٩﴾
69. Je, hukuona wale wanaobishana kuhusu Aayaat (na Ishara, Dalili) za Allaah wanageuziwa wapi?
الَّذِينَ كَذَّبُوا بِالْكِتَابِ وَبِمَا أَرْسَلْنَا بِهِ رُسُلَنَا ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ﴿٧٠﴾
70. Wale waliokadhibisha Kitabu na yale Tuliyowatuma nayo Rusuli Wetu, basi karibuni hivi watakuja kujua.
إِذِ الْأَغْلَالُ فِي أَعْنَاقِهِمْ وَالسَّلَاسِلُ يُسْحَبُونَ﴿٧١﴾
71. Zitakapokuwa pingu shingoni mwao, na minyororo wanaburutwa.[17]
فِي الْحَمِيمِ ثُمَّ فِي النَّارِ يُسْجَرُونَ﴿٧٢﴾
72. Kwenye maji yachemkayo mno, kisha kwenye moto wataunguzwa.
ثُمَّ قِيلَ لَهُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ تُشْرِكُونَ﴿٧٣﴾
73. Kisha wataambiwa: Wako wapi wale mliokuwa mkiwashirikisha?
مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ قَالُوا ضَلُّوا عَنَّا بَل لَّمْ نَكُن نَّدْعُو مِن قَبْلُ شَيْئًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّـهُ الْكَافِرِينَ﴿٧٤﴾
74. Badala ya Allaah? Watasema: Wametupotea! Bali hatukuwa tokea mwanzo tukiomba kitu chochote! Hivyo ndivyo Allaah Anavyopotoa makafiri.
ذَٰلِكُم بِمَا كُنتُمْ تَفْرَحُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَبِمَا كُنتُمْ تَمْرَحُونَ﴿٧٥﴾
75. (Wataambiwa): Hivyo ni kwa kuwa mlikuwa mkifurahi kwa kutakabari katika ardhi bila ya haki, na kwa yale mliyokuwa mnashangilia kwa majivuno.
ادْخُلُوا أَبْوَابَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۖ فَبِئْسَ مَثْوَى الْمُتَكَبِّرِينَ﴿٧٦﴾
76. Ingieni milango ya Jahannam[18] mdumu humo. Basi uovu ulioje makazi ya wenye kutakabari!
فَاصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ ۚ فَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ الَّذِي نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيْنَا يُرْجَعُونَ﴿٧٧﴾
77. Basi vuta subira (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)! Hakika Ahadi ya Allaah ni kweli kabisa! Na ikiwa Tutakuonyesha baadhi ya yale Tunayowaahidi au Tukikufisha, basi Kwetu Pekee watarejeshwa.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ مِنْهُم مَّن قَصَصْنَا عَلَيْكَ وَمِنْهُم مَّن لَّمْ نَقْصُصْ عَلَيْكَ ۗ وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأْتِيَ بِآيَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ فَإِذَا جَاءَ أَمْرُ اللَّـهِ قُضِيَ بِالْحَقِّ وَخَسِرَ هُنَالِكَ الْمُبْطِلُونَ﴿٧٨﴾
78. Na kwa yakini Tuliwapeleka Rusuli kabla yako. Miongoni mwao wako Tuliokusimulia na miongoni mwao wako ambao Hatukukusimulia.[19] Na haiwi kwa Rasuli yeyote kuleta Aayah (au Muujiza, Ishara) yoyote ile isipokuwa kwa Idhini ya Allaah. Basi itakapokuja Amri ya Allaah kutahukumiwa kwa haki, na hapo watakhasirika wabatilifu.
اللَّـهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَنْعَامَ لِتَرْكَبُوا مِنْهَا وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ﴿٧٩﴾
79. Allaah Ambaye Amekufanyieni wanyama wa mifugo ili muwapande baadhi yao na wengine muwale.[20]
وَلَكُمْ فِيهَا مَنَافِعُ وَلِتَبْلُغُوا عَلَيْهَا حَاجَةً فِي صُدُورِكُمْ وَعَلَيْهَا وَعَلَى الْفُلْكِ تُحْمَلُونَ﴿٨٠﴾
80. Na mnapata kwao manufaa mbalimbali, na ili mpate kufikia kupitia wao haja zilizomo vifuani mwenu, na juu yao na juu ya merikebu mnabebwa.
وَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ فَأَيَّ آيَاتِ اللَّـهِ تُنكِرُونَ﴿٨١﴾
81. Na Anakuonyesheni Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) Zake. Basi Aayaat zipi za Allaah mnazoweza kuzikanusha?[21]
أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَانُوا أَكْثَرَ مِنْهُمْ وَأَشَدَّ قُوَّةً وَآثَارًا فِي الْأَرْضِ فَمَا أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿٨٢﴾
82. Je, hawajatembea katika ardhi wakatazama vipi ilikuwa hatima ya wale wa kabla yao? Walikuwa wengi kuliko wao na wenye nguvu zaidi na athari katika ardhi. Hayakuwafaa yale waliyokuwa wakiyachuma.
فَلَمَّا جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَرِحُوا بِمَا عِندَهُم مِّنَ الْعِلْمِ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٨٣﴾
83. Basi walipowajia Rusuli wao kwa hoja bayana, walifurahia kwa kujivunia kwa yale waliyokuwa nayo katika ilimu, na yakawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.
فَلَمَّا رَأَوْا بَأْسَنَا قَالُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ وَكَفَرْنَا بِمَا كُنَّا بِهِ مُشْرِكِينَ﴿٨٤﴾
84. Basi walipoiona Adhabu Yetu walisema: Tumemwamini Allaah Pekee, na tunakanusha (vyote) ambavyo tulikuwa tunamshirikisha Naye.
فَلَمْ يَكُ يَنفَعُهُمْ إِيمَانُهُمْ لَمَّا رَأَوْا بَأْسَنَا ۖ سُنَّتَ اللَّـهِ الَّتِي قَدْ خَلَتْ فِي عِبَادِهِ ۖ وَخَسِرَ هُنَالِكَ الْكَافِرُونَ﴿٨٥﴾
85. Basi haikuwa imaan yao ni yenye kuwafaa walipoiona Adhabu Yetu. (Hii) ni Desturi ya Allaah[22] ambayo imekwishapita katika Waja Wake, na hapo wamekhasirika makafiri.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Tofauti Ya Ikabu Na Adhabu: Rejea Al-Hashr (59:4).
[3] Mauti Ya Mara Mbili Na Uhai Wa Mara Mbili:
Rejea Suwrah Al-Baqarah (2:28) kwenye Aayah na faida ya Kauli kama hii ya Allaah (سبحانه وتعالى):
Umetufisha mara mbili: Tulipokuwa matone ya manii ndani ya matumbo ya mama zetu kabla ya kupulizwa roho. Na ulipokoma muda wetu wa kuishi katika uhai wa duniani (kufariki kwetu).
Umetuhuisha mara mbili: Katika uhai wa duniani tokea siku ya kuzaliw, na siku tuliyofufuliwa makaburni mwetu. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[4] Aayaat Za Allaah (سبحانه وتعالى):
Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja Neema Zake kubwa kwa waja Wake, nayo ni kuwadhihirishia kati ya haqq na baatwil. Anawadhihirishia kupitia Aayaat (Ishara, Dalili) Zake katika nafsi zao (miili yao ilivyoumbwa na yasiyoonekana katika mwili wa mwanaadamu), na ishara za kilimwengu, na katika Qur-aan, Ishara zinazodalilisha kila linalokusudiwa likibainisha wazi uongofu na upotofu, ili anayezitafakari na kuzizingatia, asiwe tena na shaka kuhusu ukweli na uhakika wa mambo.
Hii ni mojawapo ya neema kubwa za Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Waja Wake, kwani Hakuacha haqq isiyokuwa dhahiri, wala kilichokuwa haqq kuwa kimefichika au kina utata. Bali Ameeleza kila aina ya Aayaat (Ishara, Dalili) na Akaziweka wazi kabisa Aayaat Zake ili ahiliki (kwa ukafiri) yule wa kuhiliki kwa hoja bayana na ahuike (kwa imaan) mwenye kuhuika kwa hoja bayana. Ndipo Akaendelea kusema (Aayah inayofuatia). [Tafsiyr As-Sa’diy]
Rejea Suwrah Ibraahiym (14:34) kwenye faida tele kuhusu uchambuzi wa Neema za Allaah zinazoonekana na zisizoonekana.
[5] Siku Ya Qiyaamah Viumbe Vyote Vitakufa Atabaki Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee:
Viumbe vyote vitakufa Siku ya Qiyaamah na mwishowe Atabakia Allaah (سبحانه وتعالى) kutokana na Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى):
كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ ﴿٢٦﴾ وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ ﴿٢٧﴾
“Kila aliyekuwa juu yake (ardhi) ni mwenye kutoweka. Na utabakia Wajihi wa Rabb wako Mwenye Ujalali na Ukarimu.” [Ar-Rahmaan (55:26-27)]
Rejea pia Al-Qaswasw (28:88) kwenye faida.
Na Hadiyth ifuatayo inaelezea kuwa Siku hiyo Allaah (سبحانه وتعالى) Atawanadia waliojifanya majabari na waliotakabari wajitokeze, lakini hakuna atakayejibu, na mwishowe ndipo Atakapojijibu Mwenyewe kuwa Ufalme ni wa Allaah Pekee Mmoja, Asiyepingika!:
وَحَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ عُمَرَ بْنِ حَمْزَةَ، عَنْ سَالِمِ، بْنِ عَبْدِ اللَّهِ أَخْبَرَنِي عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عُمَرَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " يَطْوِي اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ السَّمَوَاتِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ثُمَّ يَأْخُذُهُنَّ بِيَدِهِ الْيُمْنَى ثُمَّ يَقُولُ أَنَا الْمَلِكُ أَيْنَ الْجَبَّارُونَ أَيْنَ الْمُتَكَبِّرُونَ ثُمَّ يَطْوِي الأَرَضِينَ بِشِمَالِهِ ثُمَّ يَقُولُ أَنَا الْمَلِكُ أَيْنَ الْجَبَّارُونَ أَيْنَ الْمُتَكَبِّرُونَ " .
Amesimulia ‘Abdullaah Bin ‘Umar (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Allaah (عزّ وجلّ) Atakunja mbingu zote Siku ya Qiyaamah kisha Atazikamata Mkononi Mwake wa kuume kisha Atasema: Mimi Ndiye Mfalme. Wako wapi waliojifanya majabari? Wako wapi waliotakabari? Kisha Atazikunja ardhi kwa Mkono Wake wa kushoto na Atasema: Mimi Ndiye Mfalme. Wako wapi waliojifanya majabari? Wako wapi waliotakabari?” [Muslim]
[6] Hakuna Kinachofikicha Kwa Allaah (سبحانه وتعالى) Hata Kinachodhamiriwa Moyoni:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anakijua kile kinachopitishwa na maangalizi ya macho kwa njia ya siri na kuiba, na kile ambacho mtu anakidhamiria katika nafsi yake; kizuri au kibaya. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Na Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى) nyenginezo kuwa hakuna kinachofichika Kwake hata kama chembe ya hardali au atomu. Rejea Al-An’aam (6:59) kwenye maelezo bayana. Na rejea pia Yuwnus (10:62), Luqmaan (31:16), Sabaa (34:3).
[7] Watembee Katika Ardhi Kutambua Adhabu Za Waliokanusha:
Rejea Al-An’aam (6:11), Aal-‘Imraan (3:137).
[8] Firawni Kumpachika Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) Sifa Ovu:
Rejea Ash-Shu’araa (26:34) na pia Adh-Dhaariyaat (51:52) kwenye maelezo na rejea mbalimbali.
[9] Mtu Mmoja Miongoni Mwa Familia Ya Firawni Aliyeficha Imaan Yake:
Linalojulikana kwa Mufassiruwn ni kwamba Muumini huyo alikuwa bin ammi wa Firawni. Na Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Hakuamini mtu katika familia ya Firawni isipokuwa mtu huyu, pamoja na (Aasiyah) mke wa Firawni. Na mtu huyo ndiye aliyemkimbilia Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) kutoka mji wa mbali kumtahadharisha kwamba Firawni na wakuu wake wanadhamiria kumuua, hivyo akamnasihi akimbie mji. Rejea Suwrah Al-Qaswasw (28:20). Na pia huenda akawa ni mkoptiki katika watu wake, kwa kuwa Firawni alitamka kumuua kwa kauli yake katika Aayah namba (26) ya Suwrah hii. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Na Abu Bakr (رضي الله عنه) alisema kauli kama aliyosema Muumini huyo katika Aayah hii namba (28) ya Suwrah Ghaafir, wakati mtu katika makafiri wa Quraysh, alipotaka kumuua Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا الْوَلِيدُ بْنُ مُسْلِمٍ، حَدَّثَنَا الأَوْزَاعِيُّ، قَالَ حَدَّثَنِي يَحْيَى بْنُ أَبِي كَثِيرٍ، قَالَ حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ التَّيْمِيُّ، قَالَ حَدَّثَنِي عُرْوَةُ بْنُ الزُّبَيْرِ، قَالَ قُلْتُ لِعَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ أَخْبِرْنِي بِأَشَدِّ، مَا صَنَعَ الْمُشْرِكُونَ بِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ بَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي بِفِنَاءِ الْكَعْبَةِ، إِذْ أَقْبَلَ عُقْبَةُ بْنُ أَبِي مُعَيْطٍ، فَأَخَذَ بِمَنْكِبِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَلَوَى ثَوْبَهُ فِي عُنُقِهِ فَخَنَقَهُ خَنْقًا شَدِيدًا، فَأَقْبَلَ أَبُو بَكْرٍ فَأَخَذَ بِمَنْكِبِهِ، وَدَفَعَ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَقَالَ أَتَقْتُلُونَ رَجُلاً أَنْ يَقُولَ رَبِّيَ اللَّهُ وَقَدْ جَاءَكُمْ بِالْبَيِّنَاتِ مِنْ رَبِّكُمْ
Imepokewa kwa ‘Urwah bin Az-Zubayr (رضي الله عنهما): Nilimuuliza ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw (رضي الله عنهما): Nielezee jambo baya zaidi kwa mushrikina kumfanyia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Akasema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa akiswali kwenye uwanja wa Al-Ka‘bah, mara akaja ‘Uqbah bin Abi Mu‘aytw na kumshika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) mabegani na kuisokota nguo yake shingoni mwake na kumkwida (kumkaba) kwa nguvu. Abu Bakr alikuja na kumshika ‘Uqbah mabegani na akamwangusha chini mbali na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kisha akasema:
أَتَقْتُلُونَ رَجُلًا أَن يَقُولَ رَبِّيَ اللَّـهُ وَقَدْ جَاءَكُم بِالْبَيِّنَاتِ مِن رَّبِّكُمْ
“Je, mnamuua mtu kwa kuwa tu anasema: Rabb wangu ni Allaah? Na hali amekujieni na hoja bayana kutoka kwa Rabb wenu?” [Ghaafir (40:28) – Hadiyth ameipokea Imaam Al-Bukhaariy katika Kitaab At-Tafsiyr (65), na Kitaab Fadhwaail Aswhaab Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) (62)]
[10] Yawmul-Qiyaamah: Siku Ya Kuitana:
Yawmul-Qiyaamah (Siku ya Kisimamo) imekuja katika sifa mbali mbali. Mojawapo ni hii Siku ya Kuitana. Rejea Suwrah Al-Qiyaamah (75:1) kwenye uchambuzi na rejea mbalimbali.
Ni siku ya kuitana watu wa Jannah na motoni kama vile watu wa Al-A’raaf. Rejea Al-‘Araaf (7:46-50). Pia watu wa motoni watakapowaita Malaika. Rejea Az-Zukhruf (43:77). Na pia Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى) kwa watu wa motoni na majibu yao Kwake, rejea: Al-Muuminuwn (23:105-115). Na pia watakapoitwa washirikina wawaite washirikishwa wao waliokuwa wakiwaabudu duniani. Rejea Al-Qaswasw (28:63-64). Na pia watakapoitana washirikina watakapokuwa motoni wakikabiliana kulaumiana. Rejea Asw-Swaaffaat (37:27-32). Na pia rafiki mwema aliyeingizwa Peponi atakapomwita rafiki muovu aliyeingizwa motoni. Rejea Asw-Swaaffaat (37:50-59).
Pia shaytwaan atakapoitana na watu wake aliowapotosha. Rejea Suwrah Ibraahiym (14:21-22). Na kuitana baina ya watu waliodhaifu, na wale waliowafuata duniani ambao ni wale waliotakabari, na wenye nguvu na uwezo, wakapotoshwa nao. Rejea Suwrah hii Ghaafir (40:47-50) ambako watu wa motoni watamwita Malaika mlinzi wa moto awaombee kwa Allaah wapunguziwe adhabu ya moto. Kisha naye Malaika atawajibu. Na pia Sabaa (34:31-33). Kadhalika, kuna Aayah nyenginezo katika Qur-aan ambazo zinataja hali za watu watakapoitana na kulaumiana watakapofika Siku hii Adhimu ya kuitana.
[11] Mtu Aliyeamini:
Ni Muumini aliyetajwa katika Aayah namba (28) ya Suwrah hii Ghaafir.
Kuanzia Aayah hiyo ya (28) hadi Aayah namba (33), Muumini huyo aliwalingania kaumu yake kwa kuwaambia aliyowaambia, na kuwanasihi na kuwatahadharisha, kisha zinaendelea kauli zake za kuwalingania kaumu yake; Aayah (38) hadi namba (44), kwa kuwapa nasaha mbalimbali humo ya kwamba dunia ni starehe ya muda mdogo tu, na kwamba Aakhirah ndio nyumba ya starehe ya milele. Na Akawatahadharisha yatakayowasibu na kuingizwa motoni pindi wasipomuitikia Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) aliyekuja kuwabalighishia Risala ya Allaah. Na Akawatambulisha yatakayowanufaisha Aakhirah, na akawapa matumaini ya kuingizwa Jannah (Peponi) pindi wakiikubali Risala ya Allaah. Na mwishowe Akawakumbusha kuwa watakuja kukumbuka anayowaaidhi.
[12] Dalili Za Adhabu Za Kaburini Na Kuendelea Katika Maisha Ya Barzakh:
Aayah hii ni dalili kubwa kwa Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah kuthibitisha adhabu za maisha ya Barzakh kaburini. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Rejea Al-Muuminuwn (23:100) kwenye uchambuzi na maelezo kuhusu adhabu za kaburi na baadhi ya dalili zake katika Sunnah.
[13] Makafiri Hawatoufikia Unabii Ambao Ni Fadhila Aliyopewa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):
Hakika ya wale wanaoipinga haki kwa ubatilifu, na wanaozirudisha hoja sahihi kwa udanganyifu wa uharibifu bila ya kuwa na dalili wala ushahidi wala hoja kutoka kwa Allaah, basi hamna ndani ya nyoyo za hao, isipokuwa kuifanyia kiburi haki, kwa uhasidi wao juu ya fadhila ambazo Allaah Amempa Nabii Wake na utukufu wa Unabii ambao Amemkirimu nao. Basi haya ni mambo ambayo wao si wenye kuyafikia wala kuyapata. Hivyo basi, shikamana na Allaah (ee Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) Akuhifadhi na shari lao, kwani Yeye Ni Mwenye Kuyasikia maneno yao, Ni Mwenye Kuyaona matendo yao, na Atawalipa kwayo. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[14] Hoja Na Dalili Wazi Kwa Makafiri Wasioamini Kufufuliwa:
Rejea Al-Israa (17:49) kwenye maelezo bayana na rejea mbali mbali.
[15] Kutokuomba Duaa Ni Kutakabari Na Allaah Anamghadhibikia Asiyemuomba Duaa:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((مَنْ لَمْ يَسْأَل اللَّهَ يَغْضَب عَلَيْهِ)) حسنه الألباني في صحيح سنن الترمذي برقم 2686
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Asiyemuomba Allaah, Humghadhibikia.” [At-Tirmidhiy ameipa daraja ya Hasan Imaam Al-Albaaniy, taz Swahiyh At-Tirmidhiy (2686)]
Rejea Al-Baqarah (2:186) kwenye uchambuzi na maelezo bayana na Hadiyth kadhaa.
Rejea pia Alhidaaya.com makala ya:
إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ - Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada [271]
[17] Miongoni Mwa Adhabu Za Watu Wa Motoni Ni Kuburutwa Motoni Kwenye Maji Yachemkayo Huku Wamefungwa Pingu Na Minyororo Shingoni Mwao:
Aayah hii namba (71) na (72) zinataja baadhi ya hali na adhabu za watu wa motoni.
Rejea Ar-Ra’d (13:5) kwenye maelezo kuhusu watu wa motoni kufungwa pingu na minyororo shingoni mwao.
Na kuhusu watu wa motoni kuingizwa motoni, kwenye maji yachemkayo, ni sawa na Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwenye Suwrah Ar-Rahmaan (55:43-44)
Rejea pia An-Nabaa (78:21) kwenye uchambuzi na maelezo kuhusu adhabu za watu wa motoni.
[19] Baadhi Ya Rusuli Vimesimuliwa Visa Vyao Na Baadhi Yao Havikusimuliwa:
Rejea An-Nisaa (4:164), Al-An’aam (6:83). Rejea pia An-Nisaa (4:69) kupata maelezo kuhusu tofauti ya Manabii na Rusuli.
[20] Wanyama Na Merikebu Ni Miongoni Mwa Neema Za Allaah (سبحانه وتعالى):
Aayah hii na inayofuatia, zinataja miongoni mwa Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) ambazo ni wanyama na manufaa yake kwa mwanaadam. Na neema hizi zimetajwa pia katika Suwrah An-Nahl (16:5-8), Yaasiyn (36:71-73). Na pia zimetajwa neema zote mbili za wanyama na merikebu katika Suwrah An-Nahl (16:14), Al-Muuminuwn (23:21-22), Faatwir (35:12), Az-Zukhruf (43:12), Al-Jaathiyah (45:12).
Ama neema za merikebu, hizo zimetajwa pia katika Suwrah Al-Baqarah (2:164), Ibraahiym (14:32), Al-Israa (17:66), Ar-Ruwm (30:46), Luqmaan (31:31).
Na neema nyenginezo zimetajwa kwa wingi katika Suwrah An-Nahl (16). Neema hizi na nyenginezo nyingi haiwezekani kuziorodhesha hesabuni. Rejea Suwrah Ibraahiym (14:34) kwenye uchambuzi na maelezo bayana kuhusu Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) zinazoonekana na zisizoonekana, pamoja na rejea mbali mbali.
[21] Ishara, Dalili Za Allaah (سبحانه وتعالى) Kudhihirisha Tawhiyd Yake:
وَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ
“Na Anakuonyesheni Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja).”
Ishara na Dalili Zake za kudhihirisha Upweke Wake, Majina Yake na Sifa Zak.e Na hii ni katika Neema Zake kubwa kwa kuwaonyesha Waja Wake Ishara na Dalili katika nafsi zao, na Ishara za kiulimwengu, na Neema Zake nyingi. Akaziorodhesha (baadhi yake) wazijue ili wamshukuru na wamdhukuru.
فَأَيَّ آيَاتِ اللَّهِ تُنْكِرُونَ
“Basi Ishara zipi za Allaah mnazoweza kuzikanusha?”
Basi Ishara zipi msizozitambua (enyi makafiri)? Kwani mmekiri kuwa Ishara zote na Neema zinatoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى), basi hakuna sababu ya kukanusha wala kuzipuuza. Bali ni wajibu kwa wale wenye akili na ufahamu kufanya juhudi na kujitahidi katika kumtii, kumtumikia na kujisabilia Kwake kikamilifu. [Tafsiyr As-Sa’diy]
فُصِّلَت
041-Fusw-Swilat
041-Fusw-Swilat: Utangulizi Wa Suwrah [273]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
حم﴿١﴾
1. Haa Miym.[1]
تَنزِيلٌ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ﴿٢﴾
2. Ni uteremsho kutoka kwa Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), Mwenye Kurehemu.
كِتَابٌ فُصِّلَتْ آيَاتُهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لِّقَوْمٍ يَعْلَمُونَ﴿٣﴾
3. Kitabu kilichofasiliwa waziwazi Aayaat zake, kikisomeka kwa Kiarabu kwa watu wanaojua.
بَشِيرًا وَنَذِيرًا فَأَعْرَضَ أَكْثَرُهُمْ فَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ﴿٤﴾
4. Kinachobashiria mazuri na kinachoonya. Lakini wamekengeuka wengi wao, basi wao hawasikii.
وَقَالُوا قُلُوبُنَا فِي أَكِنَّةٍ مِّمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ وَفِي آذَانِنَا وَقْرٌ وَمِن بَيْنِنَا وَبَيْنِكَ حِجَابٌ فَاعْمَلْ إِنَّنَا عَامِلُونَ﴿٥﴾
5. Na wakasema: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa yale unayotuitia, na masikioni mwetu mna uziwi, na baina yetu na baina yako kuna kizuizi, basi tenda nasi tunatenda.[2]
قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ فَاسْتَقِيمُوا إِلَيْهِ وَاسْتَغْفِرُوهُ ۗ وَوَيْلٌ لِّلْمُشْرِكِينَ﴿٦﴾
6. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi ni mtu kama nyinyi; hufunuliwa Wahy kwamba: Muabudiwa wenu wa haki ni Ilaah Mmoja, basi thibitini imara Kwake, na mwombeni maghfirah. Na ole kwa washirikina.
الَّذِينَ لَا يُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ﴿٧﴾
7. Ambao hawatoi Zakaah, nao ni wenye kuikanusha Aakhirah.[3]
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ﴿٨﴾
8. Hakika wale walioamini na wakatenda mema watapata ujira usiokatika.
قُلْ أَئِنَّكُمْ لَتَكْفُرُونَ بِالَّذِي خَلَقَ الْأَرْضَ فِي يَوْمَيْنِ وَتَجْعَلُونَ لَهُ أَندَادًا ۚ ذَٰلِكَ رَبُّ الْعَالَمِينَ﴿٩﴾
9. Sema: Je, hivi nyinyi mnamkufuru Yule Aliyeumba ardhi kwa siku mbili,[4] na mnamfanyia waliolingana Naye? Huyo Ndiye Rabb wa walimwengu.
وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ مِن فَوْقِهَا وَبَارَكَ فِيهَا وَقَدَّرَ فِيهَا أَقْوَاتَهَا فِي أَرْبَعَةِ أَيَّامٍ سَوَاءً لِّلسَّائِلِينَ﴿١٠﴾
10. Na Akaweka humo milima iliyosimama thabiti juu yake, na Akabariki humo kwa kheri zisizokatika, na Akakadiria humo chakula chake katika siku nne. Ni idadi madhubuti kabisa kwa wanaouliza.
ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ وَهِيَ دُخَانٌ فَقَالَ لَهَا وَلِلْأَرْضِ ائْتِيَا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا قَالَتَا أَتَيْنَا طَائِعِينَ﴿١١﴾
11. Kisha Akazikusudia[5] mbingu (Kuziumba), nazo ni moshi, Akaziambia pamoja na ardhi: Njooni kwa khiari au kwa lazima. Zikasema: Tumekuja hali ya kuwa tumetii.
فَقَضَاهُنَّ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ فِي يَوْمَيْنِ وَأَوْحَىٰ فِي كُلِّ سَمَاءٍ أَمْرَهَا ۚ وَزَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِمَصَابِيحَ وَحِفْظًا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ﴿١٢﴾
12. Akamaliza kuziumba mbingu saba katika siku mbili, na Akaifunulia kila mbingu jambo lake. Na Tukaipamba mbingu ya dunia kwa taa na hifadhi. Hayo ni Takdiri ya Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.[6]
فَإِنْ أَعْرَضُوا فَقُلْ أَنذَرْتُكُمْ صَاعِقَةً مِّثْلَ صَاعِقَةِ عَادٍ وَثَمُودَ﴿١٣﴾
13. Wakikengeuka, basi sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Nakuhadharisheni radi na umeme angamizi mfano wa radi na umeme angamizi wa kina ‘Aad[7] na Thamuwd[8].
إِذْ جَاءَتْهُمُ الرُّسُلُ مِن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ ۖ قَالُوا لَوْ شَاءَ رَبُّنَا لَأَنزَلَ مَلَائِكَةً فَإِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ كَافِرُونَ﴿١٤﴾
14. Walipowajia Rusuli mbele yao na nyuma yao wakiwaambia: Msimuabudu isipokuwa Allaah, wakasema Angelitaka Rabb wetu, bila shaka Angeliteremsha Malaika. Na hakika sisi tunayakataa mliyotumwa nayo.
فَأَمَّا عَادٌ فَاسْتَكْبَرُوا فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَقَالُوا مَنْ أَشَدُّ مِنَّا قُوَّةً ۖ أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ الَّذِي خَلَقَهُمْ هُوَ أَشَدُّ مِنْهُمْ قُوَّةً ۖ وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ﴿١٥﴾
15. Ama kina ‘Aad, wao walitakabari katika ardhi bila ya haki, na wakasema: Nani mwenye nguvu zaidi kuliko sisi? Je, hawakuona kwamba Allaah Ambaye Amewaumba Ndiye Mwenye nguvu zaidi kuliko wao? Nao walikuwa wanazikanusha Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) Zetu.
فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا صَرْصَرًا فِي أَيَّامٍ نَّحِسَاتٍ لِّنُذِيقَهُمْ عَذَابَ الْخِزْيِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَخْزَىٰ ۖ وَهُمْ لَا يُنصَرُونَ﴿١٦﴾
16. Basi Tukawapelekea upepo wa dhoruba wenye mngurumo katika siku za mikosi ili Tuwaonjeshe adhabu ya hizaya katika uhai wa dunia. Na bila shaka adhabu ya Aakhirah ni ya hizaya zaidi, nao hawatonusuriwa.
وَأَمَّا ثَمُودُ فَهَدَيْنَاهُمْ فَاسْتَحَبُّوا الْعَمَىٰ عَلَى الْهُدَىٰ فَأَخَذَتْهُمْ صَاعِقَةُ الْعَذَابِ الْهُونِ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿١٧﴾
17. Na ama kina Thamuwd, wao Tuliwaongoza, lakini walistahabu upofu kuliko hidaaya. Basi ikawachukuwa radi na umeme angamizi wa adhabu idhalilishayo kwa sababu ya waliyokuwa wakiyachuma.
وَنَجَّيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ﴿١٨﴾
18. Na Tukawaokoa wale walioamini, na walikuwa wenye taqwa.
وَيَوْمَ يُحْشَرُ أَعْدَاءُ اللَّـهِ إِلَى النَّارِ فَهُمْ يُوزَعُونَ﴿١٩﴾
19. Na Siku watakayokusanywa maadui wa Allaah kupelekwa motoni, nao watapangwa safusafu wa mwanzo wao hadi mwisho wao.
حَتَّىٰ إِذَا مَا جَاءُوهَا شَهِدَ عَلَيْهِمْ سَمْعُهُمْ وَأَبْصَارُهُمْ وَجُلُودُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٢٠﴾
20. Mpaka watakapoufikia, yatashuhudia dhidi yao masikio yao, na macho yao, na ngozi zao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda.[9]
وَقَالُوا لِجُلُودِهِمْ لِمَ شَهِدتُّمْ عَلَيْنَا ۖ قَالُوا أَنطَقَنَا اللَّـهُ الَّذِي أَنطَقَ كُلَّ شَيْءٍ وَهُوَ خَلَقَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٢١﴾
21. Na wataziambia ngozi zao: Mbona mnashuhudia dhidi yetu? Zitasema: Ametutamkisha Allaah Ambaye Ametamkisha kila kitu, Naye Ndiye Aliyekuumbeni mara ya kwanza, na Kwake mtarejeshwa.
وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَا أَبْصَارُكُمْ وَلَا جُلُودُكُمْ وَلَـٰكِن ظَنَنتُمْ أَنَّ اللَّـهَ لَا يَعْلَمُ كَثِيرًا مِّمَّا تَعْمَلُونَ﴿٢٢﴾
22. Na hamkuwa mkijisitiri hata yasishuhudie masikio yenu, wala macho yenu, wala ngozi zenu, lakini mlidhania kwamba Allaah Hajui mengi katika yale mnayoyatenda.[10]
وَذَٰلِكُمْ ظَنُّكُمُ الَّذِي ظَنَنتُم بِرَبِّكُمْ أَرْدَاكُمْ فَأَصْبَحْتُم مِّنَ الْخَاسِرِينَ﴿٢٣﴾
23. Na hiyo dhana yenu mliyokuwa mkimdhania Rabb wenu, ndiyo imekuangamizeni, na mmekuwa miongoni mwa waliokhasirika.
فَإِن يَصْبِرُوا فَالنَّارُ مَثْوًى لَّهُمْ ۖ وَإِن يَسْتَعْتِبُوا فَمَا هُم مِّنَ الْمُعْتَبِينَ﴿٢٤﴾
24. Basi wakivuta subira, lakini moto ndio makazi yao tu. Na wakiomba wapewe nafasi tena ya kufanya utiifu wa kumridhisha Allaah, basi wao si wenye kuridhishwa na kupewa.
وَقَيَّضْنَا لَهُمْ قُرَنَاءَ فَزَيَّنُوا لَهُم مَّا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَحَقَّ عَلَيْهِمُ الْقَوْلُ فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا خَاسِرِينَ﴿٢٥﴾
25. Na Tuliwawekea marafiki wa karibu, wakawapambia yaliyo mbele yao na ya nyuma yao, na ikawathibitikia kauli wawe pamoja na nyumati zilizopita miongoni mwa majini na wanaadam. Hakika wao wamekuwa ni wenye kukhasirika.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَسْمَعُوا لِهَـٰذَا الْقُرْآنِ وَالْغَوْا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَغْلِبُونَ﴿٢٦﴾
26. Na wale waliokufuru wakasema: Msiisikilize hii Qur-aan na ifanyieni rabsha huenda mkashinda.[11]
فَلَنُذِيقَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا عَذَابًا شَدِيدًا وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَسْوَأَ الَّذِي كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٢٧﴾
27. Bila shaka Tutawaonjesha wale waliokufuru adhabu kali, na bila shaka Tutawalipa uovu zaidi wa yale waliokuwa wakiyatenda.
ذَٰلِكَ جَزَاءُ أَعْدَاءِ اللَّـهِ النَّارُ ۖ لَهُمْ فِيهَا دَارُ الْخُلْدِ ۖ جَزَاءً بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ﴿٢٨﴾
28. Hiyo ndio jazaa ya maadui wa Allaah, moto! Watapata humo makazi yenye kudumu. Ndio jazaa kwa sababu walikuwa wakizikanusha Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) Zetu.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا رَبَّنَا أَرِنَا اللَّذَيْنِ أَضَلَّانَا مِنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ نَجْعَلْهُمَا تَحْتَ أَقْدَامِنَا لِيَكُونَا مِنَ الْأَسْفَلِينَ﴿٢٩﴾
29. Na watasema wale waliokufuru: Rabb wetu! Tuonyeshe wale waliotupotoa miongoni mwa majini na wanaadam tuwaweke chini ya miguu yetu ili wawe miongoni mwa wa chini kabisa.
إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ﴿٣٠﴾
30. Hakika wale waliosema: Rabb wetu ni Allaah, kisha wakathibiti imara,[12] Malaika huwateremkia (kuwaambia): Msikhofu, wala msihuzunike, na pokeeni bishara njema ya Jannah ambayo mlikuwa mkiahidiwa.[13]
نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَشْتَهِي أَنفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ﴿٣١﴾
31. Sisi ni rafiki zenu walinzi katika uhai wa dunia na katika Aakhirah. Na mtapata humo yale yanayotamani nafsi zenu, na mtapata humo yale mtakayoyahitajia.
نُزُلًا مِّنْ غَفُورٍ رَّحِيمٍ﴿٣٢﴾
32. Ni mapokezi ya takrima kutoka kwa Mwenye Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِّمَّن دَعَا إِلَى اللَّـهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴿٣٣﴾
33. Na nani mwenye kauli nzuri zaidi kuliko yule anayelingania kwa Allaah na akatenda mema na akasema: Hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu![14]
وَلَا تَسْتَوِي الْحَسَنَةُ وَلَا السَّيِّئَةُ ۚ ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ فَإِذَا الَّذِي بَيْنَكَ وَبَيْنَهُ عَدَاوَةٌ كَأَنَّهُ وَلِيٌّ حَمِيمٌ﴿٣٤﴾
34. Na wala haulingani sawa wema na uovu. Zuia (uovu) kwa ambalo ni zuri zaidi. Hapo utamkuta yule ambaye baina yako na baina yake kuna uadui, kama ni rafiki mwandani.[15]
وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا ذُو حَظٍّ عَظِيمٍ﴿٣٥﴾
35. Na hayapati hayo isipokuwa wale waliovuta subira, na hayapati hayo isipokuwa mwenye fungu adhimu.[16]
وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿٣٦﴾
36. Na utakapokuchochea uchochezi kutoka kwa shaytwaan, basi omba kinga kwa Allaah. Hakika Yeye Ndiye Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ﴿٣٧﴾
37. Na katika Aayaat (Ishara na Dalili) Zake, ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Msisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Allaah Aliyeviumba ikiwa Yeye Pekee mnamwabudu.[17]
فَإِنِ اسْتَكْبَرُوا فَالَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ يُسَبِّحُونَ لَهُ بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَهُمْ لَا يَسْأَمُونَ ۩﴿٣٨﴾
38. Lakini wakitakabari, basi wale (Malaika) walio kwa Rabb wako wanamsabbih usiku na mchana, nao hawachoki.
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنَّكَ تَرَى الْأَرْضَ خَاشِعَةً فَإِذَا أَنزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ ۚ إِنَّ الَّذِي أَحْيَاهَا لَمُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۚ إِنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٣٩﴾
39. Na katika Aayaat (Ishara na Dalili) Zake, ni kwamba unaiona ardhi imetulia kame, kisha Tunapoiteremshia maji inataharaki na kunyanyuka. Hakika Yule Aliyeihuisha, bila shaka Ndiye Mwenye Kuhuisha wafu.[18] Hakika Yeye juu ya kila kitu Ni Muweza.
إِنَّ الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي آيَاتِنَا لَا يَخْفَوْنَ عَلَيْنَا ۗ أَفَمَن يُلْقَىٰ فِي النَّارِ خَيْرٌ أَم مَّن يَأْتِي آمِنًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ اعْمَلُوا مَا شِئْتُمْ ۖ إِنَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ﴿٤٠﴾
40. Hakika wale wanaozipotosha Aayaat Zetu hawawezi kujificha Tusiwaone. Je, basi yule atakayetupwa katika moto ni bora au yule atakayekuja akiwa katika amani Siku ya Qiyaamah? Tendeni mpendavyo, hakika Yeye Ni Mwenye Kuona yote myatendayo.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِالذِّكْرِ لَمَّا جَاءَهُمْ ۖ وَإِنَّهُ لَكِتَابٌ عَزِيزٌ﴿٤١﴾
41. Hakika wale waliokanusha Ukumbusho ulipowajia (wataangamia). Na hakika Hiki ni Kitabu chenye utukufu na udhibiti.
لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ ۖ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ﴿٤٢﴾
42. Hakitokifikia baatwil mbele yake wala nyuma yake. Ni Uteremsho kutoka kwa Mwenye Hikmah wa yote, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.
مَّا يُقَالُ لَكَ إِلَّا مَا قَدْ قِيلَ لِلرُّسُلِ مِن قَبْلِكَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ لَذُو مَغْفِرَةٍ وَذُو عِقَابٍ أَلِيمٍ﴿٤٣﴾
43. Huambiwi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa yale yale waliyokwisha ambiwa Rusuli kabla yako. Hakika Rabb wako Ni Mwenye maghfirah na Mwenye ikabu iumizayo.
وَلَوْ جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا أَعْجَمِيًّا لَّقَالُوا لَوْلَا فُصِّلَتْ آيَاتُهُ ۖ أَأَعْجَمِيٌّ وَعَرَبِيٌّ ۗ قُلْ هُوَ لِلَّذِينَ آمَنُوا هُدًى وَشِفَاءٌ ۖ وَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ فِي آذَانِهِمْ وَقْرٌ وَهُوَ عَلَيْهِمْ عَمًى ۚ أُولَـٰئِكَ يُنَادَوْنَ مِن مَّكَانٍ بَعِيدٍ﴿٤٤﴾
44. Na lau Tungekifanya kisomeke kwa lugha isiyokuwa ya Kiarabu wangelisema: Mbona hazikufasiliwa waziwazi Aayaat zake? Ah! Cha lugha ya kigeni na hali (Nabiy) ni Mwarabu!?[19] Sema: Hii (Qur-aan) kwa walioamini ni mwongozo na shifaa.[20] Na wale wasioamini, wana uziwi masikioni mwao nayo ni upofu kwao. Hao wanaitwa kutoka mahali mbali.
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَاخْتُلِفَ فِيهِ ۗ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ مُرِيبٍ﴿٤٥﴾
45. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu kisha kikahitilafiwa. Na lau si neno lilotangulia kutoka kwa Rabb wako, ingelihukumiwa baina yao. Na hakika wao bila shaka wamo katika shaka nayo (Qur-aan) yenye kuwatia wasiwasi.
مَّنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَسَاءَ فَعَلَيْهَا ۗ وَمَا رَبُّكَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ﴿٤٦﴾
46. Yeyote yule atakayetenda mema basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na yeyote yule atakayefanya uovu, basi ni kwa hasara yake mwenyewe, na Rabb wako Si Mwenye Kudhulumu kamwe waja.
إِلَيْهِ يُرَدُّ عِلْمُ السَّاعَةِ ۚ وَمَا تَخْرُجُ مِن ثَمَرَاتٍ مِّنْ أَكْمَامِهَا وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِ ۚ وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ أَيْنَ شُرَكَائِي قَالُوا آذَنَّاكَ مَا مِنَّا مِن شَهِيدٍ﴿٤٧﴾
47. Kwake Pekee unarudishwa ujuzi wa Saa (Qiyaamah). Na hayatoki matunda yoyote kutoka mafumbani mwake, na habebi mimba mwanamke yeyote na wala hazai isipokuwa kwa Ujuzi Wake. Na Siku Atakayowaita (Aseme): Wako wapi (hao mnaodai) washirika Wangu? Watasema: Tunakiri Kwako hapana miongoni mwetu anayeshuhudia.
وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَدْعُونَ مِن قَبْلُ ۖ وَظَنُّوا مَا لَهُم مِّن مَّحِيصٍ﴿٤٨﴾
48. Na yatawapotea yale waliyokuwa wakiyaomba kabla na watayakinisha kuwa hawana mahali pa kukimbilia.
لَّا يَسْأَمُ الْإِنسَانُ مِن دُعَاءِ الْخَيْرِ وَإِن مَّسَّهُ الشَّرُّ فَيَئُوسٌ قَنُوطٌ﴿٤٩﴾
49. Binaadam hachoki kuomba duaa za kheri. Na inapomgusa shari, basi huwa mwenye kukosa tumainio lolote, mwenye kukata tamaa kabisa.
وَلَئِنْ أَذَقْنَاهُ رَحْمَةً مِّنَّا مِن بَعْدِ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ هَـٰذَا لِي وَمَا أَظُنُّ السَّاعَةَ قَائِمَةً وَلَئِن رُّجِعْتُ إِلَىٰ رَبِّي إِنَّ لِي عِندَهُ لَلْحُسْنَىٰ ۚ فَلَنُنَبِّئَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِمَا عَمِلُوا وَلَنُذِيقَنَّهُم مِّنْ عَذَابٍ غَلِيظٍ﴿٥٠﴾
50. Na Tunapomuonjesha Rehma kutoka Kwetu baada ya dhara iliyomgusa, bila shaka husema: Haya nayastahiki mimi na sidhani kama Saa itasimama. Na kama nitarejeshwa kwa Rabb wangu hakika nitapata mazuri zaidi Kwake. Basi bila shaka Tutawabainishia wale waliokufuru yale waliyoyatenda, na bila shaka Tutawaonjesha adhabu nzito.
وَإِذَا أَنْعَمْنَا عَلَى الْإِنسَانِ أَعْرَضَ وَنَأَىٰ بِجَانِبِهِ وَإِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ فَذُو دُعَاءٍ عَرِيضٍ﴿٥١﴾
51. Na Tunapomneemesha binaadam hukengeuka na kujitenga upande. Na inapomgusa shari, basi mara huwa mwenye duaa refu refu.[21]
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن كَانَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ ثُمَّ كَفَرْتُم بِهِ مَنْ أَضَلُّ مِمَّنْ هُوَ فِي شِقَاقٍ بَعِيدٍ﴿٥٢﴾
52. Sema: Je, mnaonaje ikiwa (Qur-aan) ni kutoka kwa Allaah, kisha mkaikufuru, ni nani aliyepotoka zaidi kuliko yule aliye katika upinzani wa mbali?
سَنُرِيهِمْ آيَاتِنَا فِي الْآفَاقِ وَفِي أَنفُسِهِمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُ الْحَقُّ ۗ أَوَلَمْ يَكْفِ بِرَبِّكَ أَنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ﴿٥٣﴾
53. Tutawaonyesha Aayat (Ishara na Dalili) Zetu katika peo za mbali na katika nafsi zao, mpaka iwabainikie kwamba hii (Qur-aan) ni haki! Je, haitoshelezi Rabb wako kuwa Yeye Ni Shahidi juu ya kila kitu?[22]
أَلَا إِنَّهُمْ فِي مِرْيَةٍ مِّن لِّقَاءِ رَبِّهِمْ ۗ أَلَا إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ مُّحِيطٌ﴿٥٤﴾
54. Tanabahi! Hakika wao wamo katika shaka ya kukutana na Rabb wao. Tanabahi! Hakika Yeye Amekizunguka kila kitu.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Nyoyo Za Makafiri Zimefunikwa Na Masikio Yana Uziwi:
Rejea Al-An’aam (6:25), Al-Kahf (18:57). Rejea pia Al-Israa (17:45-46)
[3] Maana Iliyokusudiwa Ya Washirikina Kutoa Zakaah:
‘Aliy bin Abiy Twalhah amesimulia kutoka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba inamaanisha wale ambao hawashuhudii laa ilaaha illa-Allaah (hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah). Ni rai ya ‘Ikrimah pia na ni kama ilivyo katika Suwrah Ash-Shams (91:9-10), Al-A’laa (87:14-15), An-Naazi’aat (79:18). Kinachokusudiwa kuhusu Zakaah hapa ni twahara (utakaso) wa nafsi kutokana na khulqa, maadili, tabia na sifa zote mbaya. Na iliyomuhimu kabisa kutwaharisha, ni kuepuka shirki. Na Zakaah ya mali inaitwa hivyo kwa sababu inatakasa yaliyoharamishwa, na ni sababu ya kuongezeka kwake, kuibariki na kuifanya iwe ina manufaa mengi, na iwe ni tawfiyq ya kuitumia mali katika utiifu. Qataadah amesema: “Wanazuia Zakaah ya mali.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) amesema: Ambao wanaabudu badala ya Allaah wale ambao hawana uwezo wa kunufaisha wala kudhuru, wala kufisha wala kuhuisha, wala kufufua, na wakazitia unajisi nafsi zao (kwa shirki), na wala hawakuzitakasa kwa kumpwekesha Rabb wao na kumtakasia ibaada, wala hawaswali, wala hawatoi Zakaah, hivyo hakuna ikhlaasw kwa Muumba kwa kumpwekesha wala Swalaah, wala kuwanufaisha watu kwa Zakaah na mengineyo ya kheri. Mbali ya hayo, Aakhirah wanaikanusha. Yaani: Hawaamini kufufuliwa wala hawaamini Jannah na moto. Hivyo basi khofu ilivyowaondoka nyoyoni mwao, wamethubutu kufanya waliyoyafanya ambayo yatakuja kuwadhuru Aakhirah. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[4] Kuumbwa Ardhi Na Viliomo:
Aayah hii namba (9) na inayofuatia namba (10) Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja Alivyoumba ardhi.
Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema Ameumba kwanza ardhi kwa sababu ndio msingi, na msingi unapaswa kujengwa kwanza kisha ndio paa kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) kwengineko katika Suwrah Al-Baqarah (2:29):
هُوَ الَّذِي خَلَقَ لَكُم مَّا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ فَسَوَّاهُنَّ سَبْع سَمَاوَاتٍ ۚ
“Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbieni vyote vilivyomo ardhini kisha Kisha Akazikusudia mbingu (Kuziumba) na Akazifanya timilifu mbingu saba.” [Al-Baqarah (2:29)]
Na Hadiyth inayotaja kuwa uumbaji wa ardhi na yaliyomo yalikuwa katika siku sita ni kama ifuatayo:
وعن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : أخَذَ رسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم بِيَدِي فَقَالَ : (( خَلَقَ اللهُ التُّرْبَةَ يَومَ السَّبْتِ ، وَخَلَقَ فيها الجِبَالَ يَومَ الأحَدِ ، وَخَلَقَ الشَّجَرَ يَومَ الإثْنَينِ ، وَخَلَقَ المَكْرُوهَ يَومَ الثُّلاَثَاءِ ، وَخَلَقَ النُّورَ يَوْمَ الأربِعَاءِ ، وَبَثَّ فِيهَا الدَّوابَّ يَومَ الخَمِيسِ ، وَخَلَقَ آدَمَ صلى الله عليه وسلم ، بَعْدَ العَصْرِ مِنْ يَومِ الجُمُعَةِ في آخِرِ الخَلْقِ فِي آخِرِ سَاعَةٍ مِنَ النَّهَارِ فِيمَا بَيْنَ العَصْرِ إِلَى اللَّيْلِ )) . رواه مسلم .
Amesimulia Abuu Huraiyrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alinishika mkono na kuniambia: "Allaah Aliumba ardhi siku ya Jumamosi, na Akaumba ndani yake majabali Jumapili, na Akaumba miti Jumatatu, na Akaumba vitu vinavyo chukiza Jumanne, na Akaumba mwangaza Jumatano, na Akawatawanya wanyama katika ardhi siku ya Alkhamisi, na Akamuumba Aadam (عليه السّلام) baada ya Alasiri katika siku ya Ijumaa, katika viumbe Vyake vya mwisho, katika saa ya mwisho ya mchana, baina ya Alasiri na usiku." [Muslim]
[5] اسْتَوَى إِلَى السَّمَاءِ" Amezikusudia (Kuziumba Mbingu):
Rejea Al-Baqarah (2:29) kwenye maelezo bayana kuhusu maana yake.
[6] Takdiri (Uwezo, Ukadiriaji) Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Katika Uumbaji Wa Kila Kitu.
Rejea Yaasiyn (36:38) kwenye maelezo na faida tele.
[7] ‘Aad:
Ni kaumu ya Nabiy Huwd (عليه السّلام). Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye uchambuzi wa kaumu za nyumati za awali, maasi yao na adhabu zao.
[8] Thamuwd:
Ni kaumu ya Nabiy Swaalih (عليه السّلام). Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye uchambuzi wa kaumu za nyumati za awali, maasi yao na adhabu zao.
[9] Viungo Vitashuhudia Matendo Ya Binaadam:
Rejea Al-Israa (17:13-14), An-Nuwr (24:24), Yaasiyn (36:65).
[11] Ujahili Wa Makafiri Kutokutaka Kusikiliza Qur-aan Ilhali Waumini Wameamrishwa Waisikilize Wapate Kurehemwa:
Rejea Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwrah Al-A’raaf (7:204) kwenye maelezo bayana.
[12] Kuthibitika Imara Katika Dini:
عن أبي عمر، وقيل: أبي عَمرة سفيان بن عبد الله رضي الله عنه قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُول الله، قُلْ لي في الإسْلامِ قَولًا لا أسْأَلُ عَنْهُ أَحَدًا غَيْرَكَ. قَالَ: ((قُلْ: آمَنْتُ بِاللهِ، ثُمَّ استَقِمْ)). رواه مسلم
Amesimulia Abuu ‘Umar na pia imesemwa anajulikana kama Abuu ‘Amrah Sufyaan bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه): Nilimwambia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): Niambie neno katika Uislamu ambalo sitamuuliza yoyote zaidi yako. Akasema: “Sema: Nimemuamini Allaah, kisha uthibitike imara.” [Muslim]
[13] Waumini Wanabashiriwa Kheri Wanapotolewa Roho Zao:
Aayah hii (31) na zifuatazo hadi namba (32), zinataja Muumini anapotolewa roho yake, kuwa Malaika humbashiria mema, na kumliwaza azihuzunike, kwa kuwa atakayoyakuta huko Jannah, ni mazuri na neema tele, na raha tupu za kudumu, na mapokezi mema kutoka kwa Rabb Mkarimu Mwenye Kurehemu. Na bishara kama hizi zimetajwa katika Suwrah kadhaa za Qur-aan. Na imethibiti katika Qur-aan na Sunnah kwamba Muumin anapotolewa roho yake, hutolewa kwa wepesi kabisa na huwa katika raha na manukato, na Malaika wanaipokea roho kwa maamkizi na bishara njema. Rejea Al-Waaqi’ah (56:88-94) kwenye maelezo bayana yanayotofautisha kati ya roho ya Muumin na roho ya kafiri, pamoja na rejea mbalimbali. Na Hadiyth ifuatayo pia inatofautisha kati ya roho ya Muumini na roho ya kafiri pindi inapotolewa:
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: الْمَيِّتُ تَحْضُرُهُ الْمَلَائِكَةُ فَإِذَا كَانَ الرَّجُلُ صَالِحًا قَالُوا: اخْرُجِي أَيَّتُهَا النَّفْسُ الطَّيِّبَةُ كَانَتْ فِي الْجَسَدِ الطَّيِّبِ اخْرُجِي حَمِيدَةً وَأَبْشِرِي بِرَوْحٍ وَرَيْحَانٍ وَرَبٍّ غَيْرِ غَضْبَانَ فَلَا تَزَالُ يُقَالُ لَهَا ذَلِكَ حَتَّى تَخْرُجَ ثُمَّ يُعْرَجُ بِهَا إِلَى السَّمَاءِ فَيُفْتَحَ لَهَا فَيُقَالُ: مَنْ هَذَا؟ فَيَقُولُونَ: فُلَانٌ فَيُقَالُ: مَرْحَبًا بِالنَّفسِ الطّيبَة كَانَت فِي الْجَسَدِ الطَّيِّبِ ادْخُلِي حَمِيدَةً وَأَبْشِرِي بِرَوْحٍ وَرَيْحَانٍ وَرَبٍّ غَيْرِ غَضْبَانَ فَلَا تَزَالُ يُقَالُ لَهَا ذَلِكَ حَتَّى تَنْتَهِيَ إِلَى السَّمَاءِ الَّتِي فِيهَا اللَّهُ فَإِذَا كَانَ الرَّجُلُ السُّوءُ قَالَ: اخْرُجِي أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْخَبِيثَةُ كَانَتْ فِي الْجَسَدِ الْخَبِيثِ اخْرُجِي ذَمِيمَةً وَأَبْشِرِي بِحَمِيمٍ وَغَسَّاقٍ وَآخَرَ مِنْ شَكْلِهِ أَزْوَاجٌ فَمَا تَزَالُ يُقَالُ لَهَا ذَلِكَ حَتَّى تَخْرُجَ ثُمَّ يُعْرَجُ بِهَا إِلَى السَّمَاءِ فَيُفْتَحُ لَهَا فَيُقَالُ: مَنْ هَذَا؟ فَيُقَالُ: فُلَانٌ فَيُقَالُ: لَا مَرْحَبًا بِالنَّفْسِ الْخَبِيثَةِ كَانَتْ فِي الْجَسَدِ الْخَبِيثِ ارْجِعِي ذَمِيمَةً فَإِنَّهَا لَا تفتح لَهُ أَبْوَابُ السَّمَاءِ فَتُرْسَلُ مِنَ السَّمَاءِ ثُمَّ تَصِيرُ إِلَى الْقَبْر ". رَوَاهُ ابْن مَاجَه
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Malaika humjia mtu anayefariki, na ikiwa mtu ni mwema husema: Toka, ee nafsi nzuri, ambayo ilikuwa katika mwili mzuri! Toka ukiwa mwenye sifa njema, na pokea bishara njema kwa mapumziko ya raha na manukato, na Rabb Asiye na ghadhabu nawe. Ataendelea kuambiwa hayo mpaka roho itoke. Kisha itapandishwa juu mbinguni na atafunguliwa mlango. Malaika watauliza: Ni nani huyu? (Malaika wengine) watajibu: Ni fulani. Itaambiwa: Karibu ee nafsi njema, ambayo ilikuwa katika mwili mwema. Ingia ukiwa mwenye sifa njema, na pokea bishara njema kwa mapumziko ya raha na manukato na Rabb Asiye na ghadhabu nawe. Ataendelea kuambiwa hayo mpaka roho ifike mbinguni ambamo Yuko Allaah. Lakini inapokuwa mtu ni mbaya kinachosemwa ni: Toka ewe nafsi mbaya ambayo ilikuwa katika mwili mwovu! Toka ukiwa mwenye kulaumiwa na pokea habari mbaya ya maji yanayotokoka na usaha na mengineyo ya mfano wake na aina yake! Ataendelea kuambiwa hivyo hadi roho itoke. Kisha itapandishwa juu mbinguni na itafunguliwa mlango. Itaulizwa: Ni nani huyu? Itajibiwa: Ni fulani. Itaambiwa: Hakuna ukaribisho kwa nafsi mbaya iliyokuwa ndani ya mwili mwovu! Rudi ukiwa mwenye kulaumiwa kwani milango ya mbinguni haitafunguliwa kwa ajili yake. Kisha itatupwa kutoka mbinguni hadi kufika kaburini.” [Ibn Maajah na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Maajah (3456)]
Rejea pia Al-A’raaf (7:40) kwenye faida.
[14] Himizo La Daawah (Kulingania) Dini Na Kudhihirisha Unyenyekevu Kwa Watu:
Hakuna yoyote aliye na kauli nzuri zaidi kuliko yule anayelingania Tawhiyd ya Allaah (Kupwekeshwa Allaah) na kuabudiwa Yeye Peke Yake, na yule anayesema: “Mimi ni katika Waislamu.” Yaani: Wanaofuata Amri za Allaah na Sharia Zake. Katika Aayah hii, kuna usisitizo wa kumlingania Allaah (سبحانه وتعالى) na kueleza fadhila za ‘Ulamaa wenye kulingania Kwake kwa baswiyrah (nuru za ilimu na utambuzi) kulingana na yale yaliyokuja kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). [Tafsiyr Al-Muyassar]
Rejea Suwrah Yuwsuf (12:108).
Rejea Alhidaaya.com
Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa - أَحاديثُ عَنْ فَضْلِ الْعِلْم وَالْعُلَمَاء [275]
[15] Himizo La Kulipiza Wema Baada Ya Uovu:
Wema na uovu haulingani sawa. Yaani, kutenda amali njema na matendo ya utiifu kwa ajili ya Allaah, hakuwi sawa na amali ovu na matendo ya maasi ambayo Allaah Hayaridhii, na yanasababisha ghadhabu Zake. Na wala kuwatendea watu wema hakuwi sawa na kuwafanyia ubaya, si kwa matendo yenyewe, wala namna yake, wala malipo yake.
Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akaamrisha ihsaan makhsusi ambayo ina taathira kubwa. Nayo ni kumtendea wema anayekutendea mabaya kama Anavyosema:
ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ
“Zuia (uovu) kwa ambalo ni zuri zaidi.”
Yaani: Mtu akikufanyia ubaya, kwa kauli au matendo, khasa akiwa ni mtu ambaye ana haki kwako, kama vile jamaa wa karibu (mwenye uhusiano wa damu), marafiki na kadhaalika, basi wewe rejesha hilo kwa kumfanyia ihsaan. Akikukata akakhasimikiana nawe, wewe wasiliana naye. Akikudhulumu, wewe msamehe. Akikusema vibaya kwa siri au mbele yako, basi wewe usimrudishie maneno mabaya, bali msamehe na amiliana naye kwa kauli laini (ya upole). Akikususa, na akakhasimikiana nawe asikusemeshe, basi wewe msemeze kwa maneno mazuri na uwe wa kwanza kumtolea Salaam. Utakapolipiza ubaya kwa wema, utapata faida kubwa. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Rejea pia Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى) zinazoamrisha kuvumilia, kuzuia ghadhabu, kusamehe watu na kadhaalika. Miongoni mwazo ni: Aal-‘Imraan (3:134), Ash-Shuwraa (42:43). Pia Hadiyth ifuatayo ina mafunzo kama hayo ya kulipiza uovu kwa wema:
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أنَّ رَجُلاً ، قَالَ : يَا رسول الله ، إنّ لي قَرَابةً أصِلُهم وَيَقْطَعُونِي ، وَأُحْسِنُ إلَيْهِمْ وَيُسِيئُونَ إلَيَّ ، وَأحْلُمُ عَنهم وَيَجْهَلُونَ عَلَيَّ ! فَقَالَ : (( لَئِنْ كُنْتَ كَمَا قُلْتَ ، فَكأنَّمَا تُسِفُّهُمُ الْمَلَّ ، وَلاَ يَزَالُ مَعَكَ مِنَ اللهِ تَعَالَى ظَهيرٌ عَلَيْهِمْ مَا دُمْتَ عَلَى ذَلِكَ )) رواه مسلم .
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Mtu mmoja alisema: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mimi nina jamaa wa karibu nawaunga, lakini wao wananikata. Nawafanyia wema, lakini wao wananitendea uovu, nawavumilia na kusamehe, lakini wao wanaendelea kunifanyia vitimbi Akasema: "Ukiwa kama unavyosema, basi ni kama unawalisha jivu la moto. Msaada wa Allaah hautaacha kuwa pamoja nawe maadamu utadumu juu ya hilo." [Muslim]
[16] Subira Katika Maudhi Yanampatia Mtu Hadhi Kubwa Mbele Ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا
“Na hayapati hayo isipokuwa wale waliovuta subira.”
Hakuna atakayeweza kupata sifa nzuri hii, isipokuwa wenye kuvuta subira na wanaovumilia katika wasiyoyaridhia, na kujilazimisha yale ambayo Anayapenda Allaah. Kwani nafsi za watu zimeumbwa na tabia ya kulipiza maovu kwa maovu na kutokusamehe. Basi itakuwaje mtu kulipa uovu kwa ihsaan?
Lakini mtu akiwa mvumilivu na akatii amri za Rabb wake, akatambua thawabu tele ambazo zinasababishwa na subira hiyo, akafahamu kuwa kulipizia maovu hakumfaidii hata kidogo, bali kutamzidishia ubaya nao, na kuzidisha uadui. Na kwamba kumtendea ihsaan hakumaanishi kuwa mtu anajidhalilisha na kushusha daraja lake, bali ni kunyenyekea kwa Allaah Ambaye Atampandisha daraja, na mambo yatakuwa mepesi kwake, atafanya kwa maridhawa na atapata furaha ndani yake. [Tafsiyr As-Sa’diy]
وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا ذُو حَظٍّ عَظِيمٍ﴿٣٥﴾
Yaani: Kwa sababu ni sifa ya nadra ya wanaadam, na ambayo mtu hupandishwa daraja la juu duniani na Aakhirah. Hivo basi ni katika akhlaqi (sifa) njema kabisa. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Na subira katika Qur-aan imetajwa katika Aayah nyingi mno. Na subira zina matawi yake, na daraja zake, na thawabu zake ni tele.
Rejea kiungo kifuatacho chenye Makala ya: Swabrun Jamiyl (Subira Njema) iliyojaa faida tele, na rejea mbali mbali za Qur-aan na Hadiyth:
Swabrun Jamiyl (Subira Njema) [276]
[17] Haramisho La Kusujudia Jua Au Mwezi Kwani Ni Vitu Vilivyoumbwa Na Allaah (سبحانه وتعالى):
Imaam Muhammad Ibn Al-Wahhaab (رحمه الله) ameinukuu Aayah hii akasema:
النَّبِيَّ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) ظَهَرَ عَلَى أُنَاسٍ مُتَفَرِّقِينَ فِي عِبَادَاتِهِمْ، مِنْهُمْ مَنْ يَعْبُدُ الْمَلائِكَةَ، وَمِنْهُمْ مَنْ يَعْبُدُ الأَنْبِيَاءَ وَالصَّالِحِينَ، وَمِنْهُمْ مَنْ يَعْبُدُ الأَشْجَارَ وَالأَحْجَارَ، وَمِنْهُمْ مَنْ يَعْبُدُ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ، وَقَاتَلَهُمْ رَسُولُ اللهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) وَلَمْ يُفَرِّقْ بَيْنَهُمْ.
“Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuta watu wakitofautiana katika ibaada zao. Kuna waliokuwa wanaabudu Malaika, wanaoabudu Manabii na Swalihina (waja wema), wanaoabudu miti na mawe, na wanaoabudu jua na mwezi. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akapigana nao na wala hakutofautisha baina yao (katika walivyoviabudu).” [Al-Qawaaid Al-Arba’ – Imaam Muhammad Ibn Al-Wahhaab]
Na Imaam Ibn Kathiyr amesema:
Hapa Allaah (سبحانه وتعالى) Anakumbusha Uwezo Wake mkubwa, na kwamba Yeye Ndiye Ambaye Hana wa kulinganishwa Naye, na ni Muweza wa kila kitu. Kauli Yake hiyo inamaanisha kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Ameumba usiku na giza lake, na mchana kwa nuru yake, navyo vinafuatana bila kusimama. Na Akaliumba jua kwa nuru yake inayong'aa, na mwezi kwa nuru yake. Na Akakadiria vituo vyake katika falaki (angani), Akavipa njia tofauti mbinguni, ili kwa kutofautiana kwa mienendo yao mwanaadam, apate kujua nyakati za usiku na mchana, za wiki, za miezi na za miaka, na nyakati zinazohusiana na haki za watu, ibaada na miamala mbalimbali. Zaidi ya hayo, kwa sababu jua na mwezi ni vitu vilivyoumbwa kwa uzuri kabisa vinavyoweza kuonekana katika anga za juu na za chini, Allaah (سبحانه وتعالى) Anazindusha kwamba hivyo ni vitumwa kati ya watumwa Wake na viko chini ya Ufalme Wake na Udhibiti Wake. Basi watu wasivisujudie, bali wamsujudie Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Aliyeviumba. Wala msimshirikishe, kwani kumwabudu kwenu Yeye, hakutakunufaisheni ikiwa mtaabudu vinginevyo, kwani Yeye Hasamehi kushirikishwa Naye. Ndio maana Akasema:
فَإِنِ اسْتَكْبَرُوا
“Lakini wakitakabari .”
[Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[18] Mfano Wa Ardhi Iliyokufa (Kame), Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akaihuisha Kwa Mvua, Ni Mfano Wa Kuwahuisha Watu Kutoka Makaburini Mwao Siku Ya Qiyaamah:
Rejea Ar-Ruwm (30:50) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali.
[19] Hata Kama Ingeteremshwa Qur-aan Kwa Lugha Ya Kigeni Washirikina Wasingeliamini:
Rejea Ash-Shu’araa (26:198-199).
[20] Qur-aan Ni Shifaa (Poza, Tiba), Mwongozo, Mawaidha, Rehma:
Katika Aayah hii ya Suwrah Fusw-Swilat (41:44), Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema kuwa Qur-aan ni mwongozo na rehma. Ama wasioiamini, wao wana uziwi masikioni mwao, nayo ni upofu kwao.
Na katika Suwrah Yuwnus, Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema Qur-aan ni mawaidha, shifaa, mwongozo na rehma:
يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَشِفَاءٌ لِّمَا فِي الصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ﴿٥٧﴾ قُلْ بِفَضْلِ اللَّـهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ﴿٥٨﴾
“Enyi watu! Kwa yakini yamekujieni mawaidha kutoka kwa Rabb wenu, na shifaa ya yale yaliyomo vifuani, na mwongozo na rehma kwa Waumini. Sema: Kwa Fadhila za Allaah na kwa Rehma Yake basi kwa hayo wafurahi. Hayo ni kheri kuliko wanayoyakusanya.” [Yuwnus (10:57-58)]
Rejea katika Suwrah hiyo Yuwnus (10:57-58) kwenye faida nyenginezo.
Ama kwenye Suwrah Al-Israa, Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema Qur-aan ni shifaa na rehma kwa Waumini lakini ni khasara kwa kafiri:
وَنُنَزِّلُ مِنَ الْقُرْآنِ مَا هُوَ شِفَاءٌ وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ۙ وَلَا يَزِيدُ الظَّالِمِينَ إِلَّا خَسَارًا ﴿٨٢﴾
“Na Tunateremsha katika Qur-aan ambayo ni shifaa na rehmakwa Waumini na wala haiwazidishii madhalimu isipokuwa khasara.” [Al-Israa (17:82)]
Rejea katika Suwrah hiyo ya Al-Israa (17:82) kwenye faida nyenginezo:
Maudhui ya Qur-aan kuwa ni shifaa (poza, tiba), mawaidha, mwongozo na rehma kwa watu, ni maudhui pana mno, na rejea zake katika Qur-aan na Sunnah ni nyingi mno! Lakini uchambuzi wake kwa kifupi ni kama ifuatavyo:
(i) Qur-aan Ni Mawaidha:
Rejea Aayah zilizotajwa juu za Suwrah Yuwnus (10:57-58).
Kadhaalika, Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
هَـٰذَا بَيَانٌ لِّلنَّاسِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ ﴿١٣٨﴾
“Hii (Qur-aan) ni ubainisho kwa watu na mwongozo na mawaidha kwa wenye taqwa.” [Aal-‘Imraan (3:138)]
Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَمَا أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّنَ الْكِتَابِ وَالْحِكْمَةِ يَعِظُكُم بِهِ ۚ
“Na kumbukeni Neema za Allaah juu yenu na Aliyokuteremshieni katika Kitabu na Hikmah (Sunnah) Anakuwaidhini kwacho.” [Al-Baqarah (2:231)]
Rejea pia Huwd (11:120), An-Nuwr (24:34).
(ii) Qur-aan Ni Shifaa (Poza, Tiba):
Qur-aan ni shifaa ya kila aina ya maradhi iwe ya miili au ya kiroho, au maradhi ya moyo yaliyokusudiwa katika Qur-aan.
a) Qur-aan Ni Shifaa Ya Maradhi Ya Miili:
Imethibiti katika simulizi mbalimbali kwamba Swahaba walikuwa wakitumia Qur-aan kama ruqyah (kinga na tiba) ya kimiili. Na pia dalili kubwa ni kisa katika Hadiyth ifuatayo, cha kumsomea mkuu wa kijiji aliyepatwa na sumu, akasomewa Suwrah Al-Faatihah akapona:
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ (رضي الله عنه) قَالَ: كُنَّا فِي مَسِيرٍ لَنَا فَنَزَلْنَا فَجَاءَتْ جَارِيَةٌ فَقَالَتْ: "إِنَّ سَيِّدَ الْحَيِّ سَلِيمٌ وَإِنَّ نَفَرَنَا غَيْبٌ فَهَلْ مِنْكُمْ رَاقٍ؟" فَقَامَ مَعَهَا رَجُلٌ مَا كُنَّا نَأْبُنُهُ بِرُقْيَةٍ، فَرَقَاهُ فَبَرَأَ فَأَمَرَ لَهُ بِثَلاَثِينَ شَاةً وَسَقَانَا لَبَنًا فَلَمَّا رَجَعَ قُلْنَا لَهُ: "أَكُنْتَ تُحْسِنُ رُقْيَةً أَوْ كُنْتَ تَرْقِي؟" قَالَ: "لاَ مَا رَقَيْتُ إلاَّ بِأُمِّ الْكِتَابِ." قُلْنَا: "لاَ تُحْدِثُوا شَيْئًا حَتَّى نَأْتِيَ أَوْ نَسْأَلَ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)." فَلَمَّا قَدِمْنَا الْمَدِينَةَ ذَكَرْنَاهُ لِلنَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقَالَ: ((وَمَا كَانَ يُدْرِيهِ أَنَّهَا رُقْيَةٌ؟ اقْسِمُوا وَاضْرِبُوا لِي بِسَهْمٍ)).
Amesimulia Abuu Sa'iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Tulikuwa katika safari tukateremka mahali, akaja kijakazi akasema: Bwana wetu ametafunwa na nge na wanaume wetu hawapo, je, yupo kati yenu tabibu? Akasimama pamoja naye mtu mmoja ambaye hatukudhania kuwa anajua ruqyah (utabibu). Akamtibu kwa ruqyah akapona. Akampa kondoo thelathini na akatupa maziwa tunywe (kama ni malipo). Aliporudi tukamwambia: Je, ulikuwa kweli unajua kutibu kwa ruqyah, au ulikuwa unabahatisha tu? Akasema: Hapana, bali nimemsomea Ummul-Kitaab (Suwrah Al-Faatihah). Tukasema: Tusiseme kitu hadi tumfikie au tumuulize Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Tulipofika Madiynah, tulimwelezea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Alijuaje kuwa (Al-Faatihah) ni ruqyah? Gawaneni na mnitolee sehemu (ya kondoo.” [Al-Bukhaariy]
b) Qur-aan ni Ruqyah Na Shifaa Ya Sihri (Uchawi), Uhasidi, Jicho Baya, Kukumbwa Na Mashaytwaan Na Majini Na Kila Aina Za Shari:
Suwrah Al-Baqarah:
عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((لَا تَجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ مَقَابِرَ إِنَّ الشَّيْطَانَ يَنْفِرُ مِنَ الْبَيْتِ الَّذِي تُقْرَأُ فِيهِ سُورَةُ الْبَقَرَةِ)) رواه مسلم
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Msifanye nyumba zenu makaburi. Kwa hakika shaytwaan haingii nyumba ambayo husomwa humo Suwratul-Baqarah.” [At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Swahiyh] na katika Riwaayah ya Muslim, Hadiyth (780):
“Shaytwaan anakimbia nyumba inayosomwa ndani yake Suwratul-Baqarah.”.
Aayatul-Kursiy:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضى الله عنه قَالَ وَكَّلَنِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِحِفْظِ زَكَاةِ رَمَضَانَ، فَأَتَانِي آتٍ، فَجَعَلَ يَحْثُو مِنَ الطَّعَامِ، فَأَخَذْتُهُ فَقُلْتُ: لأَرْفَعَنَّكَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم. فَذَكَرَ الْحَدِيثَ فَقَالَ: إِذَا أَوَيْتَ إِلَى فِرَاشِكَ فَاقْرَأْ آيَةَ الْكُرْسِيِّ لَنْ يَزَالَ عَلَيْكَ مِنَ اللَّهِ حَافِظٌ، وَلاَ يَقْرَبُكَ شَيْطَانٌ حَتَّى تُصْبِحَ. فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((صَدَقَكَ وَهْوَ كَذُوبٌ، ذَاكَ شَيْطَانٌ))
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniwakilisha kuhifadhi Zakaah ya Ramadhwaan (Zakaatul-Fitwr). Akaja mtu akaanza kuteka chakula (cha Zakaah) kwa mikono miwili. Nikamkamata na kumwambia: Nitakupeleka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Kisha Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) akahadithia yote na akaongezea: Huyo (mwizi) akasema kuniambia: Utakapoingia kitandani kulala, soma Aayatul-Kursiy kwani mlinzi kutoka kwa Allaah atakulinda, na shaytwaan hatokukaribia mpaka asubuhi. Hapo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Amekwambia ukweli japokuwa yeye ni muongo, naye (huyo mwizi) ni shaytwaan.” [Al-Bukhaariy]
Aayah mbili za mwisho wa Suwrah Al-Baqarah:
عن أَبِي مَسْعُودٍ الأَنْصَارِيِّ، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((الآيَتَانِ مِنْ آخِرِ سُورَةِ الْبَقَرَةِ مَنْ قَرَأَ بِهِمَا فِي لَيْلَةٍ كَفَتَاهُ))
Amesimulia Abuu Mas‘uwd Al-Answaariyy (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayesoma usiku Aayah mbili za mwisho wa Suwratul-Baqarah zitamtosheleza.” Yaani: Zinamtosheleza kumkinga na kila baya na lenye kumdhuru. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Suwrah Al-Ikhlaasw (112) na Al-Mu’awwidhataan (kinga mbili) yaani Suwrah Al-Falaq (113) na Suwrah An-Naas (114).
Hizi ni katika Adhkaar za asubuhi na jioni kujikinga na kila shari. Na Hadiyth ifuatayo imethibiti:
عَنْ مُعَاذِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ خُبَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: خَرَجْنَا فِي لَيْلَةٍ مَطِيرَةٍ وَظُلْمَةٍ شَدِيدَةٍ نَطْلُبُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي لَنَا. قَالَ: فَأَدْرَكْتُهُ فَقَالَ: ((قُلْ)). فَلَمْ أَقُلْ شَيْئًا ثُمَّ قَالَ: ((قُلْ)) فَلَمْ أَقُلْ شَيْئًا. قَالَ: ((قُلْ)) قُلْتُ: مَا أَقُولُ؟ قَالَ: ((قُلْ هوَ اللَّهُ أَحَدٌ... وَالْمُعَوِّذَتَيْنِ حِينَ تُمْسِي وَتُصْبِحُ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ تَكْفِيكَ مِنْ كُلِّ شَيْءٍ)). قَالَ أَبُو عِيسَى وَهَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
Amesimulia Mu’aadh bin ‘Abdillaah bin Khubayb (رضي الله عنه): Kutoka kwa baba yake kwamba: Tulitoka usiku mmoja wa kiza kinene na mvua tukimtafuta Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) atuswalishe Swalaah. Akasema: Nikakutana naye, kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: قُلْ “Sema.” Lakini sikusema kitu. Kisha akasema: قُلْ “Sema.” Lakini sikusema kitu. Kisha akasema: قُلْ “Sema.” Nikasema: “Niseme nini?” Akasema:
قُلْ هوَ اللَّهُ أَحَدٌ
“Sema: Yeye Allaah Ni Mmoja Pekee.” [Suwrah Ikhlaasw namba (112)] na Al-Mu’awwidhatayni [Al-Falaq na An-Naas (113-114)] Unapoingia jioni na unapoamka asubuhi mara tatu zitakutosheleza na kila kitu.” [Hadiyth Hasan Swahiyh, Taz. Swahiyh At-Tirmidhiyy (3575), Swahiyh Abiy Daawuwd (5082).
Na pia imesimuliwa kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alirogwa akawa anaumwa, akateremshiwa Suwrah mbili hizo.
c) Qur-aan Inatibu Maradhi Ya Nyoyo: Ambayo Ni Kufru, Shirki, Unafiki, Shaka, Matamanio, Ukaidi Wa Kukubali Haqq, Maasi Na Kila Aina Ya Maovu:
Nyoyo Zenye Maradhi: Rejea Suwrah Muhammad (47:20) kwenye maelezo na rejea mbalimbali.
Moyo Uliopofuka: Rejea pia Al-Hajj (22:46) kwenye maelezo bayana.
Kinyume chake ni Moyo Uliosalimika, rejea Ash-Shu’araa (26:88-89) kwenye ufafanuzi na maelezo bayana.
Na pia rejea Ar-Ra’d (13:28) Anaposema Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa kwa Dhikru-Allaah nyoyo hutulia! Rejea pia nukta namba (iii) kwenye maelezo kuhusu Swahaba mtukufu ‘Umar Bin Al Khattwaab (رضي الله عنه) aliyeondolewa shirki, kufru, maasi kwa kusikiliza Qur-aan.
Rejea pia Alhidaaya.com kwenye makala zifuatazo:
Ruqyah: Kinga Na Tiba Katika Shariy'ah [277]
Du’aa Za Ruqyah (Kinga) Faida Na Sharh Zake [278]
(iii) Qur-aan Ni Mwongozo:
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
إِنَّ هَـٰذَا الْقُرْآنَ يَهْدِي لِلَّتِي هِيَ أَقْوَمُ وَيُبَشِّرُ الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا كَبِيرًا ﴿٩﴾
“Hakika hii Qur-aan inaongoza katika yaliyonyooka kabisa, na inawabashiria Waumini wanaotenda mema kwamba watapata ujira mkubwa.” [Al-Israa (17:9)]
Imesimuliwa katika Siyrah ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba Swahaba mtukufu ‘Umar Bin Al-Khattwaab alisilimu kwa kusikiza Aayah za mwanzo za Suwrah Twaahaa (20:1-8). Hivyo Qur-aan ikamuondoshea viza vya kufru, shirki na maasi na ikamuingiza katika Nuru ya Uislamu. Rejea pia Suwrah Ibraahiym (14:1) kwenye maelezo kuhusu kutolewa kutoka katika viza na kuingia katika nuru.
(iv) Qur-aan Ni Rehma:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anatuamrisha tuwe tunaisikiliza Qur-aan inaposomwa ili Atuteremshie Rehma Yake:
وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٢٠٤﴾
“Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na bakieni kimya (mzingatie) ili mpate kurehemewa.” [Al-A’raaf (7:204)]
Rejea katika Aayah hiyo ya Suwrah Al-A’raaf (7:204) kwenye Tafsiyr yake.
Basi kama ilivyotangulia kutajwa juu, kuwa maudhui hii ni pana mno, lakini hayo ni machache mno miongoni mwa mengi. Na hapa si mahala pake pa kuorodheshwa yote.
[22] Aayaat Za Allaah Katika Peo Za Mbali (Angani, Ulimwenguni) Na Katika Nafsi Kudhihirisha Haqq:
Tutawaonyesha, hawa wakanushaji, Aayaat (Ishara na Dalili) Zetu za kuteka miji na kupata nguvu Uislamu katika majimbo mbalimbali, na juu ya dini nyingine, na maeneo ya mbingu na ardhi, na katika matukio makubwa Anayoyaleta Allaah (سبحانه وتعالى) humo, na ndani ya nafsi zao. Na vile vilivyomo humo miongoni mwa alama za kuvutia za utendakazi wa Allaah (سبحانه وتعالى) na maajabu ya utengenezaji Wake, (Tutawaonyesha hayo yote) mpaka iwafunukie nyinyi (makafiri), ufunuzi usiyokubali shaka yoyote, kwamba Qur-aan ndiyo haki iliyoletwa kwa njia ya Wahy kutoka kwa Rabb wa viumbe wote. Je hauwatoshi wao Ushahidi wa Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa ni dalili ya kuwa Qur-aan ni haki na kuwa aliyekuja nayo ni mkweli? Kwani Allaah (سبحانه وتعالى) Ameishuhudilia kwa kuisadikisha, na Yeye ni Shahidi wa kila kitu, na hakuna kitu chochote chenye kutolea ushahidi kuliko ushahidi wa Allaah (سبحانه وتعالى) . [Tafsiyr Al-Muyassar]
Rejea Yuwsuf (12:105), Adh-Dhaariyaat (51:20).
الشُّورى
042-Ash-Shuwraa
042-Ash-Shuwraa: Utangulizi Wa Suwrah [280]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم
حم﴿١﴾
1. Haa Miym.
عسق﴿٢﴾
2. ‘Ayn Siyn Qaaaf.[1]
كَذَٰلِكَ يُوحِي إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ اللَّـهُ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٣﴾
3. Hivyo ndivyo Anavyokufunulia Wahy na kwa wale walio kabla yako, Allaah Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ﴿٤﴾
4. Ni Vyake vilivyomo mbinguni na ardhini, Naye Ni Mwenye ‘Uluwa Uliotukuka, Mwenye Taadhima.
تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِن فَوْقِهِنَّ ۚ وَالْمَلَائِكَةُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِمَن فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٥﴾
5. Zinakaribia mbingu kuraruka moja juu ya nyingine[2], na Malaika wanasabbih na kumhimidi Rabb wao, na wanawaombea maghfirah walioko ardhini. Tanabahi! Hakika Allaah Ndiye Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[3]
وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ اللَّـهُ حَفِيظٌ عَلَيْهِمْ وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ﴿٦﴾
6. Na wale waliojichukulia badala Yake marafiki wandani na walinzi, Allaah Anayahifadhi matendo yao, nawe si mdhamini wao.
وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لِّتُنذِرَ أُمَّ الْقُرَىٰ وَمَنْ حَوْلَهَا وَتُنذِرَ يَوْمَ الْجَمْعِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۚ فَرِيقٌ فِي الْجَنَّةِ وَفَرِيقٌ فِي السَّعِيرِ﴿٧﴾
7. Na hivyo ndivyo Tulivyokufunulia Wahy wa Qur-aan ya Kiarabu ili uonye Ummul-Quraa[4] (Mama wa miji [Makkah]), na wale waliozunguka pembezoni mwake, na uonye Siku ya kujumuika isiyokuwa na shaka ndani yake. Kundi litakuwa katika Jannah, na kundi katika moto uliowashwa vikali mno.
وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَجَعَلَهُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَـٰكِن يُدْخِلُ مَن يَشَاءُ فِي رَحْمَتِهِ ۚ وَالظَّالِمُونَ مَا لَهُم مِّن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ﴿٨﴾
8. Na lau Angelitaka Allaah Angeliwafanya ummah mmoja, lakini Anamuingiza Amtakaye katika Rehma Yake. Na madhalimu hawana mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru.
أَمِ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۖ فَاللَّـهُ هُوَ الْوَلِيُّ وَهُوَ يُحْيِي الْمَوْتَىٰ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٩﴾
9. Je, wamejichukulia badala Yake marafiki wandani na walinzi? Basi Allaah Yeye Ndiye Mlinzi, Naye Ndiye Anayehuisha wafu, Naye juu ya kila kitu ni Muweza.
وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبِّي عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ﴿١٠﴾
10. Na katika lolote lile mlilokhitilafiana, basi hukumu yake irejesheni kwa Allaah. Huyo Ndiye Allaah Rabb wangu, Kwake nimetawakali, na Kwake naelekea kwa mambo yangu yote.
فَاطِرُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ جَعَلَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا وَمِنَ الْأَنْعَامِ أَزْوَاجًا ۖ يَذْرَؤُكُمْ فِيهِ ۚ لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ﴿١١﴾
11. Muanzilishi wa mbingu na ardhi. Amekujaalieni kutokana na nafsi zenu mume na mke, na katika wanyama wa mifugo dume na jike. Anakusambazeni humo. Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.[5]
لَهُ مَقَالِيدُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٢﴾
12. Ni Zake funguo za mbingu na ardhi, Anamkunjulia riziki Amtakaye na Humkadiria kwa kipimo (Amtakaye). Hakika Yeye Ni Mjuzi kwa kila kitu.[6]
شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ ۖ أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ ۚ كَبُرَ عَلَى الْمُشْرِكِينَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ ۚ اللَّـهُ يَجْتَبِي إِلَيْهِ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي إِلَيْهِ مَن يُنِيبُ ﴿١٣﴾
13. Amekuamuruni katika Dini yale Aliyomuusia kwayo Nuwh, na ambayo Tumekufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na Tuliyomuusia kwayo Ibraahiym, na Muwsaa na ‘Iysaa kwamba: Simamisheni Dini na wala msifarikiane humo. Yamekuwa magumu kwa washirikina yale unayowalingania. Allaah Anamteua Kwake Amtakaye, na Anamhidi Kwake mwenye kumwelekea.
وَمَا تَفَرَّقُوا إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى لَّقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّ الَّذِينَ أُورِثُوا الْكِتَابَ مِن بَعْدِهِمْ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ مُرِيبٍ ﴿١٤﴾
14. Na hawakufarikiana isipokuwa baada ya kuwajia ilimu kutokana na kufanyiana baghi[7] (uadui (chuki, husuda) baina yao. Na kama si neno lililotangulia (kuakhirisha adhabu) kutoka kwa Rabb wako mpaka muda maalumu uliokadiriwa, basi ingelikidhiwa baina yao. Na hakika wale waliorithishwa Kitabu baada yao bila shaka wamo katika shaka na wasiwasi nayo.
فَلِذَٰلِكَ فَادْعُ ۖ وَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ ۖ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ ۖ وَقُلْ آمَنتُ بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِن كِتَابٍ ۖ وَأُمِرْتُ لِأَعْدِلَ بَيْنَكُمُ ۖ اللَّـهُ رَبُّنَا وَرَبُّكُمْ ۖ لَنَا أَعْمَالُنَا وَلَكُمْ أَعْمَالُكُمْ ۖ لَا حُجَّةَ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ ۖ اللَّـهُ يَجْمَعُ بَيْنَنَا ۖ وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ﴿١٥﴾
15. Basi kwa hayo walinganie (ee Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم, na thibiti imara kama ulivyoamrishwa, na wala usifuate hawaa zao. Na sema: Nimeamini Vitabu vyote Alivyoviteremsha Allaah, na nimeamrishwa niadilishe baina yenu. Allaah Ni Rabb wetu na Rabb wenu, sisi tuna amali zetu, nanyi mna amali zenu. Hakuna kubishana baina yetu na baina yenu, Allaah Atatujumuisha baina yetu, na Kwake ndio mahali pa kuishia.
وَالَّذِينَ يُحَاجُّونَ فِي اللَّـهِ مِن بَعْدِ مَا اسْتُجِيبَ لَهُ حُجَّتُهُمْ دَاحِضَةٌ عِندَ رَبِّهِمْ وَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ﴿١٦﴾
16. Na wale wanaobishana kuhusu Allaah baada ya kuitikiwa, hoja yao ni baatwil mbele ya Rabb wao, na juu yao iko ghadhabu, na watapata adhabu shadidi.
اللَّـهُ الَّذِي أَنزَلَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ وَالْمِيزَانَ ۗ وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ السَّاعَةَ قَرِيبٌ﴿١٧﴾
17. Allaah Ambaye Ameteremsha Kitabu hiki kwa haki na mizani. Na nini kitakachokujulisha pengine Saa (Qiyaamah) iko karibu?
يَسْتَعْجِلُ بِهَا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِهَا ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا مُشْفِقُونَ مِنْهَا وَيَعْلَمُونَ أَنَّهَا الْحَقُّ ۗ أَلَا إِنَّ الَّذِينَ يُمَارُونَ فِي السَّاعَةِ لَفِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ﴿١٨﴾
18. Wanaihimiza wale wasioiamini. Na wale walioamini wanaiogopa na wanaitambua kwamba ni haki. Tanabahi! Hakika wale wanaotilia shaka kuhusu Saa, bila shaka wamo katika upotofu wa mbali.
اللَّـهُ لَطِيفٌ بِعِبَادِهِ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ ۖ وَهُوَ الْقَوِيُّ الْعَزِيزُ﴿١٩﴾
19. Allaah Ni Latifu[8] kwa Waja Wake, Anamruzuku Amtakaye, Naye Ndiye Mwenye nguvu zote, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika.
مَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الْآخِرَةِ نَزِدْ لَهُ فِي حَرْثِهِ ۖ وَمَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِن نَّصِيبٍ﴿٢٠﴾
20. Yeyote atakaye mavuno ya Aakhirah Tutamzidishia katika mavuno yake. Na yeyote atakaye mavuno ya dunia, Tutampa humo, lakini Aakhirah hatokuwa na fungu lolote.[9]
أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةُ الْفَصْلِ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۗ وَإِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٢١﴾
21. Je, wanao washirika waliowaamuru dini ambayo Allaah Hakuitolea idhini? Na lau si neno la uamuzi, basi jambo lingelimalizwa (hapa duniani) baina yao. Na hakika madhalimu watapata adhabu iumizayo.[10]
تَرَى الظَّالِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا كَسَبُوا وَهُوَ وَاقِعٌ بِهِمْ ۗ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فِي رَوْضَاتِ الْجَنَّاتِ ۖ لَهُم مَّا يَشَاءُونَ عِندَ رَبِّهِمْ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَضْلُ الْكَبِيرُ﴿٢٢﴾
22. Utawaona madhalimu ni wenye kuogopa kwa yale waliyoyachuma, nayo yatawafikia tu. Na wale walioamini na wakatenda mema watakuwa katika mabustani yaliyositawi ya Jannah. Watapata wayatakayo kwa Rabb wao, hiyo ndio fadhila kubwa.
ذَٰلِكَ الَّذِي يُبَشِّرُ اللَّـهُ عِبَادَهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ ۗ قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَىٰ ۗ وَمَن يَقْتَرِفْ حَسَنَةً نَّزِدْ لَهُ فِيهَا حُسْنًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ شَكُورٌ﴿٢٣﴾
23. Hayo ndiyo Aliyowabashiria Allaah Waja Wake wale walioamini na wakatenda mema. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Sikuombeni ujira wowote juu yake isipokuwa mapenzi kwa ajili ya ujamaa wa karibu. Na yeyote anayechuma mazuri, Tutamzidishia humo zuri. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwingi wa Kupokea Shukurani.[11]
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا ۖ فَإِن يَشَإِ اللَّـهُ يَخْتِمْ عَلَىٰ قَلْبِكَ ۗ وَيَمْحُ اللَّـهُ الْبَاطِلَ وَيُحِقُّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ ۚ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ﴿٢٤﴾
24. Bali wanasema: Amemtungia Allaah uongo? Basi Allaah Akitaka Atapiga mhuri juu ya moyo wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na Allaah Anafuta baatwil, na Ataisimamisha haki kwa Maneno Yake. Hakika Yeye Ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.
وَهُوَ الَّذِي يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَعْفُو عَنِ السَّيِّئَاتِ وَيَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ﴿٢٥﴾
25. Naye Ndiye Ambaye Anapokea tawbah kutoka kwa Waja Wake, na Anasamehe maovu, na Anayajua mnayoyafanya.
وَيَسْتَجِيبُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَيَزِيدُهُم مِّن فَضْلِهِ ۚ وَالْكَافِرُونَ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ﴿٢٦﴾
26. Na Anawaitikia wale walioamini na wakatenda mema, na Anawazidishia Fadhila Zake. Na makafiri watapata adhabu kali.
وَلَوْ بَسَطَ اللَّـهُ الرِّزْقَ لِعِبَادِهِ لَبَغَوْا فِي الْأَرْضِ وَلَـٰكِن يُنَزِّلُ بِقَدَرٍ مَّا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ بِعِبَادِهِ خَبِيرٌ بَصِيرٌ﴿٢٧﴾
27. Na lau kama Allaah Angelikunjua riziki kwa Waja Wake, basi wangeruka mipaka katika ardhi. Lakini Anateremsha kwa kadiri ya Akitakacho. Hakika Yeye kwa Waja Wake Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri, Mwenye Kuona yote.[12]
وَهُوَ الَّذِي يُنَزِّلُ الْغَيْثَ مِن بَعْدِ مَا قَنَطُوا وَيَنشُرُ رَحْمَتَهُ ۚ وَهُوَ الْوَلِيُّ الْحَمِيدُ﴿٢٨﴾
28. Naye Ndiye Anayeteremsha mvua baada ya kuwa wamekata tamaa, na Anaeneza Rehma Yake. Naye Ndiye Mlinzi[13], Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.
وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَثَّ فِيهِمَا مِن دَابَّةٍ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ جَمْعِهِمْ إِذَا يَشَاءُ قَدِيرٌ﴿٢٩﴾
29. Na katika Aayaat (Ishara, Dalili) Zake, ni uumbaji wa mbingu na ardhi, na Aliowatawanya humo kati ya viumbe vinavyotembea, Naye kuwakusanya Atakapo Ni Muweza.
وَمَا أَصَابَكُم مِّن مُّصِيبَةٍ فَبِمَا كَسَبَتْ أَيْدِيكُمْ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ﴿٣٠﴾
30. Na msiba wowote unaokusibuni, basi ni kwa sababu ya yale iliyochuma mikono yenu, na Anasamehe mengi.
وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ فِي الْأَرْضِ ۖ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ﴿٣١﴾
31. Nanyi si wenye kuweza kukwepa ardhini, na wala hamna badala Yake mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru.
وَمِنْ آيَاتِهِ الْجَوَارِ فِي الْبَحْرِ كَالْأَعْلَامِ﴿٣٢﴾
32. Na katika Aayaat (Ishara, Dalili) Zake ni merikebu zinazotembea baharini kama milima.
إِن يَشَأْ يُسْكِنِ الرِّيحَ فَيَظْلَلْنَ رَوَاكِدَ عَلَىٰ ظَهْرِهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ﴿٣٣﴾
33. Akitaka Anautuliza upepo wa dhoruba zikabaki zimetuama juu ya bahari. Hakika katika hayo mna Aayaat (Ishara, Mazingatio) kwa kila mwingi wa kuvuta subira, mwingi wa kushukuru.
أَوْ يُوبِقْهُنَّ بِمَا كَسَبُوا وَيَعْفُ عَن كَثِيرٍ﴿٣٤﴾
34. Au Aziangamize kwa sababu ya waliyoyachuma, na (Akitaka) Anasamehe mengi.
وَيَعْلَمَ الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِنَا مَا لَهُم مِّن مَّحِيصٍ﴿٣٥﴾
35. Na ili wapate kujua wale wanaojadiliana kuzipinga Aayaat (na Ishara, Hoja, Dalili) Zetu, kwamba hawana mahali popote pa kukimbilia.
فَمَا أُوتِيتُم مِّن شَيْءٍ فَمَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَمَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ لِلَّذِينَ آمَنُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ﴿٣٦﴾
36. Na kitu chochote mlichopewa basi ni starehe ndogo za ya uhai wa dunia. Na yale yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi na ni ya kudumu kwa wale walioamini, na kwa Rabb wao wanatawakali.
وَالَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ وَإِذَا مَا غَضِبُوا هُمْ يَغْفِرُونَ﴿٣٧﴾
37. Na wale wanaojiepusha na madhambi makubwa[14] na machafu[15] na wanapoghadhibika wao wanasamehe.
وَالَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِرَبِّهِمْ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَمْرُهُمْ شُورَىٰ بَيْنَهُمْ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ﴿٣٨﴾
38. Na wale waliomuitikia Rabb wao, wakasimamisha Swalaah, na jambo lao hushauriana baina yao, na kutokana na vile Tulivyowaruzuku wanatoa.[16]
وَالَّذِينَ إِذَا أَصَابَهُمُ الْبَغْيُ هُمْ يَنتَصِرُونَ﴿٣٩﴾
39. Na wale wanapokabiliwa na baghi[17] (ukandamizaji na dhulma), wao wanajitetea.
وَجَزَاءُ سَيِّئَةٍ سَيِّئَةٌ مِّثْلُهَا ۖ فَمَنْ عَفَا وَأَصْلَحَ فَأَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ﴿٤٠﴾
40. Na jazaa ya uovu ni uovu mfano wake. Lakini atakayesamehe na akajenga mahusiano mema na aliyemkosea, basi ujira wake uko kwa Allaah. Hakika Yeye Hapendi madhalimu.
وَلَمَنِ انتَصَرَ بَعْدَ ظُلْمِهِ فَأُولَـٰئِكَ مَا عَلَيْهِم مِّن سَبِيلٍ﴿٤١﴾
41. Na bila shaka anayelipiza kisasi baada ya kudhulumiwa, basi hao hawana sababu ya kulaumiwa.
إِنَّمَا السَّبِيلُ عَلَى الَّذِينَ يَظْلِمُونَ النَّاسَ وَيَبْغُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۚ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٤٢﴾
42. Hakika sababu (ya kulaumiwa) ni juu ya wale wanaodhulumu[18] watu na wanafanya baghi[19] (ukandamizaji) katika ardhi bila ya haki. Hao watapata adhabu iumizayo.
وَلَمَن صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ﴿٤٣﴾
43. Na atakayevuta subira na akasamehe, hakika hilo bila shaka ni katika mambo ya kuazimiwa.
وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِن وَلِيٍّ مِّن بَعْدِهِ ۗ وَتَرَى الظَّالِمِينَ لَمَّا رَأَوُا الْعَذَابَ يَقُولُونَ هَلْ إِلَىٰ مَرَدٍّ مِّن سَبِيلٍ﴿٤٤﴾
44. Na aliyepotolewa na Allaah basi hatopata rafiki mlinzi (na msaidizi) baada Yake. Na utawaona madhalimu watakapoiona adhabu wakisema: Je, ipo njia yoyote ya kurudi (duniani)?
وَتَرَاهُمْ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا خَاشِعِينَ مِنَ الذُّلِّ يَنظُرُونَ مِن طَرْفٍ خَفِيٍّ ۗ وَقَالَ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ الْخَاسِرِينَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَأَهْلِيهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ أَلَا إِنَّ الظَّالِمِينَ فِي عَذَابٍ مُّقِيمٍ﴿٤٥﴾
45. Na utawaona wanahudhurishwa (kwenye moto) wakiwa wanyenyekevu kutokana na udhalilifu, wanatazama kwa mtazamo wa kificho. Na watasema wale walioamini: Hakika wenye kukhasirika ni wale waliokhasiri nafsi zao na ahli zao Siku ya Qiyaamah. Tanabahi! Hakika madhalimu wamo katika adhabu ya kudumu.
وَمَا كَانَ لَهُم مِّنْ أَوْلِيَاءَ يَنصُرُونَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ ۗ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِن سَبِيلٍ﴿٤٦﴾
46. Na wala hawatokuwa na rafiki walinzi wowote wa kuwanusuru badala ya Allaah. Na ambaye Allaah Amempotoa basi hatopata njia (ya kuongoka).
اسْتَجِيبُوا لِرَبِّكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا مَرَدَّ لَهُ مِنَ اللَّـهِ ۚ مَا لَكُم مِّن مَّلْجَإٍ يَوْمَئِذٍ وَمَا لَكُم مِّن نَّكِيرٍ﴿٤٧﴾
47. Muitikieni Rabb wenu kabla haijafika Siku isiyo rudishwa nyuma kutoka kwa Allaah. Hamtokuwa na mahali popote pa kukimbilia Siku hiyo na wala hamtoweza kukanusha chochote.
فَإِنْ أَعْرَضُوا فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ۖ إِنْ عَلَيْكَ إِلَّا الْبَلَاغُ ۗ وَإِنَّا إِذَا أَذَقْنَا الْإِنسَانَ مِنَّا رَحْمَةً فَرِحَ بِهَا ۖ وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ فَإِنَّ الْإِنسَانَ كَفُورٌ﴿٤٨﴾
48. Wakikengeuka, basi Hatukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) uwe mwenye kuwahifadhi. Si juu yako isipokuwa ubalighisho (wa Risala). Na hakika Sisi Tunapomwonjesha binaadam Rehma kutoka Kwetu, huifurahia. Na linapowasibu ovu kwa sababu ya iliyotanguliza mikono yao, basi hakika binaadam ni mwingi wa kukufuru.
لِّلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ يَهَبُ لِمَن يَشَاءُ إِنَاثًا وَيَهَبُ لِمَن يَشَاءُ الذُّكُورَ﴿٤٩﴾
49. Ni wa Allaah Pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Anaumba Atakacho. Humtunukia Amtakaye wana wa kike, na Humtunukia Amtakaye wana wa kiume.
أَوْ يُزَوِّجُهُمْ ذُكْرَانًا وَإِنَاثًا ۖ وَيَجْعَلُ مَن يَشَاءُ عَقِيمًا ۚ إِنَّهُ عَلِيمٌ قَدِيرٌ﴿٥٠﴾
50. Au Huwachanganya wa kiume na wa kike, na Humjaalia Amtakaye kuwa ni tasa. Hakika Yeye Ni Mjuzi wa yote, Muweza wa yote.
وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ اللَّـهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا فَيُوحِيَ بِإِذْنِهِ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ عَلِيٌّ حَكِيمٌ﴿٥١﴾
51. Na wala haikuwa kwa mtu yeyote kwamba Allaah Amsemeze isipokuwa kwa Wahy au kutoka nyuma ya kizuizi, au Hutuma Mjumbe (Malaika), kisha Anamfunulia Wahy Ayatakayo kwa Idhini Yake.[20] Hakika Yeye Ni Mwenye ‘Uluwa, Mwenye Hikmah wa yote.
وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِّنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَـٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا نَّهْدِي بِهِ مَن نَّشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٢﴾
52. Na hivyo ndivyo Tulivyokuletea Ruwh[21] (Qur-aan) kutokana na Amri Yetu. Hukuwa unajua nini Kitabu wala imaan lakini Tumeifanya ni Nuru, Tunaongoa kwayo Tumtakaye miongoni mwa Waja Wetu. Na hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka.[22]
صِرَاطِ اللَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا إِلَى اللَّـهِ تَصِيرُ الْأُمُورُ﴿٥٣﴾
53. Njia ya Allaah Ambaye ni Vyake Pekee vyote vilivyomo mbinguni na vyote vilivyomo ardhini. Tanabahi! Kwa Allaah Pekee yanaishia mambo yote.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Kuraruka Mbingu Kutokana Na Kumkhofu Allaah Kwa Utukufu Wake:
‘Ulamaa wa Tafsiyr wamesherehesha ifuatavyo:
Pamoja na ukubwa wa mbingu na kuwa hazina uhai, lakini zinakaribia kuraruka kutokana na khofu na Utukufu wa Allaah. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Zinakaribia mbingu kupasukapasuka, kila moja juu ya ile inayoifuata, kutokana na Utukufu wa Mwingi wa Rehma na Ujalali Wake, Tabaaraka wa Ta’aalaa (Amebarikika na Ametukuka). [Tafsiyr Al-Muyassar]
Na hivyo ni kama Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwrah Al-Hashr (59:21). Rejea huko kupata faida nyenginezo:
Na katika Suwrah Maryam (19) Aayah namba (88-91), imetajwa mbingu kuraruka kutokana na kumzulia Allaah (سبحانه وتعالى) Ana mwana. Rejea huko kwenye Tafsiyr za ‘Ulamaa na faida nyenginezo.
[3] Malaika Wanamhimidi Allaah Na Wanawaombea Maghfirah Walioko Ardhini:
Tafsiyr:
Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَالْمَلَائِكَةُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِمَن فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٥﴾
“Na Malaika wanasabbih na kumhimidi Rabb wao, na wanawaombea maghfirah walioko ardhini. Tanabahi! Hakika Allaah Ndiye Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.”
وَالْمَلَائِكَةُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ
“Na Malaika wanasabbih na kumhimidi Rabb wao.”
Kutokana na U’adhwama Wake, Malaika watukufu waliokurubishwa wanamnyenyekea Allaah, na kwa ‘Izza Yake wako tuli hawababaiki, na kwa Uola Wake wanatekeleza Amri Zake zote kwa utiifu wa hali ya juu kabisa. Isitoshe, wanamuadhimisha na kumtakasa Allaah (سبحانه وتعالى) na kila upungufu, na wanamsifu kwa kila sifa za ukamilifu.
وَيَسْتَغْفِرُونَ لِمَن فِي الْأَرْضِ ۗ
“Na wanawaombea maghfirah walioko ardhini.”
Ni kutokana na yale wanayoyafanya ambayo hayaendani na Utukufu na Ukubwa wa Allaah (سبحانه وتعالى) pamoja na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) ni:
الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٥﴾
“Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.”
Ambae kama si Maghfirah Yake na Rehma Yake, basi Angewaharakishia Waja Wake adhabu. Ama Allaah kusifika na sifa hizi, baada ya kutaja kwamba Ameteremsha Wahy kwa Rusuli wote kwa ujumla, na kwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) khaswa, haya yote ni ishara kwamba katika hii Qur-aan kuna dalili za wazi, na Aayah zinazoonyesha Ukamilifu wa Allaah Muumba, na kwamba Yeye Kuelezewa kwa Majina haya Matukufu Mazuri, kunazijaza nyoyo maarifa ya kumjua, kumpenda, kumuadhimisha, kumtukuza na kumheshimu, na kunamfanya pia mja aelekeze aina zake zote za utumwa wa siri na wa dhahiri Kwake tu Allaah (سبحانه وتعالى), na kwamba katika dhulma kubwa na maneno mabaya, ni kujifanyia mshirika kwa Allaah, kumuabudia asiyekuwa Yeye, vile ambavyo havinufaishi wala havidhuru, bali hivyo ni viumbe ambavyo vinahitajia kwa Allaah kwa hali zao zote. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[5] Allaah (سبحانه وتعالى) Hafanani Na Yeyote Katika Majina Na Sifa Zake:
Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Muumba mbingu na ardhi na Muanzilishi wa kuzitengeneza kwa Uweza Wake na Matakwa Yake na Hikma Yake. Amewapatia nyinyi wake wanaotokana na nyinyi ili mjitulize kwao, na Amewapatia nyinyi Wanyama howa wa kila aina, wa kiume na wa kike. Anawafanya nyinyi muwe wengi kwa kuzaana kwa njia hii ya kutangamana. Hakuna kinachofanana na Yeye (سبحانه وتعالى) na kuwa kama Yeye chochote kile miongoni mwa Viumbe Vyake, si katika Dhati Yake wala Majina Yake wala Sifa Zake wala Vitendo Vyake. Kwani Majina Yake yote ni mazuri na sifa Zake ni sifa za ukamilifu na Utukufu, na kwa Vitendo Vyake (سبحانه وتعالى), Amefanya vipatikane viumbe vikubwa bila ya kuwa na mshirika. Na Yeye Ndiye Mwenye Kusikia na Ndiye Mwenye Kuona. Hakuna chochote kinachofichamana Kwake cha matendo ya Waja Wake na maneno yao, na Atawalipa kwa hayo. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Rejea pia Huwd (11:37).
[6] Allaah Anakunjua Rizki Atakavyo Na Anazuia Atakavyo Kwa Hikma Yake:
Rejea Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى) katika Suwrah Ar-Ra’d (13:26), Al-Israa (17:30), Al-‘Ankabuwt (29:62), Ar-Ruwm (30:37), Saba-a (34:36), (34:39), Az-Zumar (39:52).
Na Tafsiyr ya Aayah hii ni kama ifuatavyo:
لَهُ مَقَالِيدُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٢﴾
“Ni Zake funguo za mbingu na ardhi, Anamkunjulia riziki Amtakaye na Humkadiria kwa kipimo (Amtakaye). Hakika Yeye Ni Mjuzi kwa kila kitu.”
Anakusudia: Ufalme wa mbingu na ardhi ni Wake, na katika Mikono Yake kuna funguo za rizki na rehma, na neema za wazi na za siri. Viumbe wote ni wenye kumuhitajia Allaah (سبحانه وتعالى) katika kuleta maslahi na kuondosha madhara kwao katika kila hali, na hakuna yeyote anaeweza kufanya hivyo.
Na Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Mwenye kutoa na Mwenye kuzuia, Mwenye kudhuru na Mwenye kunufaisha, Ambae kila neema iliyopo kwa waja inatoka Kwake, na hakuna anaeweza kuondosha shari isipokuwa Yeye. Na
مَّا يَفْتَحِ اللَّـهُ لِلنَّاسِ مِن رَّحْمَةٍ فَلَا مُمْسِكَ لَهَا ۖ وَمَا يُمْسِكْ فَلَا مُرْسِلَ لَهُ مِن بَعْدِهِ ۚ ﴿٢﴾
“Rehma yoyote Anayoifungua Allaah kwa watu, basi hakuna wa kuizuia, na Anayoizuia, basi hakuna wa kuipeleka baada Yake.” [Faatwir (35:2)]
[Rejea pia Faatwir (35:2) kewenye faida]
Na ndio maana Anasema:
يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٢﴾
“Anamkunjulia riziki Amtakaye na Humkadiria kwa kipimo (Amtakaye). Hakika Yeye Ni Mjuzi kwa kila kitu.”
Anaiongeza na kumpa rizki kiasi Anachokitaka Amtakaye, na Anaizuia (kuibana) kwa Amtakae, mpaka inakuwa kwa kiasi cha mahitaji yake, na wala Haiongezeki, na haya yote yanakwenda sambamba na Ilimu Yake na Hikma Zake. Na kwa sababu hiyo ndio Anasema:
إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٢﴾
“Hakika Yeye Ni Mjuzi kwa kila kitu.”
[Tafsiyr As-Sa’diy]
[7] Maana Ya Baghyun/Baghaa Katika Qur-aan:
Baghyun/Baghaa katika Qur-aan imetumika katika maana mbalimbali. Mfano katika Suwrah hii, baghyun/baghaa imetajwa katika Aayah zifuatazo:
Aayah 14: Uadui, chuki, husuda.
Aayah 27: Urukaji mipaka.
Aayah 39: Ukandamizaji na dhulma.
Aayah 42: Ukandamizaji.
Aayah nyenginezo zilizotajwa neno hilo la baghyun/baghaa na maana zake ni hizi zifuatazo:
(i) Maasi, uovu na ufisadi: Rejea Yuwnus (10:23).
(ii) Dhulma, ukandamizaji: Rejea Al-An’aam (6:146), Al-‘Araaf (7:33), Yuwnus (10:90), An-Nahl (16:90), Al-Hujuraat (49:9), Swaad (38:22) (38:24).
(iii) Uonevu na kutakabari: Rejea Al-Qaswasw (28:76).
(iv) Kuruka mipaka: Rejea Al-Baqarah (2:173).
(v) Kukusudia jambo: Rejea Al-A’raaf (7:45).
(vi) Chuki, uhasidi: Rejea Al-Baqarah (2:90), (2:213), Aal-‘Imraan (3:19).
(vii) Ukahaba: Rejea An-Nuwr (24:33), Maryam (19:20), (19:28).
[9] Mwenye Kutaka Mavuno Ya Dunia Badala Ya Mavuno Ya Aakhirah:
Tafsiyr:
مَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الْآخِرَةِ
“Yeyote atakaye mavuno ya Aakhirah.”
Malipo na thawabu zake, Akaamini na kuzisadikisha, na akafanya juhudi kwa ajili ya kuzipata.
نَزِدْ لَهُ فِي حَرْثِهِ ۖ
“Tutamzidishia katika mavuno yake.”
Kwa kumzidishia malipo ya matendo yake, kwa ziada nyingi, kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَنْ أَرَادَ الْآخِرَةَ وَسَعَىٰ لَهَا سَعْيَهَا وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ كَانَ سَعْيُهُم مَّشْكُورًا ﴿١٩﴾
“Na anayetaka Aakhirah na akaifanyia juhudi inayostahiki kufanyiwa, naye ni Muumin, basi hao juhudi zao ni za kushukuriwa.” [Al-Israa (17:19)]
Pamoja na hilo, ama fungu lake la hapa Duniani hapana budi limfikie.
وَمَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الدُّنْيَا
“Na yeyote atakaye mavuno ya dunia.”
Yule ambae dunia ndio makusudio na malengo yake, na wala hakufanya (matendo) kwa ajili ya Aakhirah yake, na wala hakuwa akitaraji thawabu ya hayo matendo, na wala hakuogopa madhambi kwa matendo hayo, basi:
نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِن نَّصِيبٍ﴿٢٠﴾
“Tutampa humo, lakini Aakhirah hatokuwa na fungu lolote.”
Fungu lake alilo gaiwa. Hakika ameshanyimwa Jannah na Neema zake, na atakuwa amestahiki moto. Na Aayah hii inafanana sana na Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
مَن كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لَا يُبْخَسُونَ﴿١٥﴾ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ إِلَّا النَّارُ ۖ وَحَبِطَ مَا صَنَعُوا فِيهَا وَبَاطِلٌ مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٦﴾
“Anayetaka uhai wa dunia na mapambo yake Tutawalipa kikamilifu amali zao humo, nao hawatopunjwa humo. Hao ndio wale ambao hawatokuwa na chochote katika Aakhirah isipokuwa moto. Na yataporomoka yale waliyoyafanya humo (duniani), na yatabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.” [Huwd (11:15-16)]
Na Aayah kadhaa zimetaja kustahabu maisha ya dunia badala ya maisha ya Aakhirah, na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Anaahidi kheri na neema nyingi za kudumu za Aakhirah kuliko za dunia. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo:
Suwrah hii Ash-Shuwraa (42:36), Huwd (11:10) (11:15), At-Tawbah (9:38), Yuwnus (10:7), Ibraahiym (14:3), An-Nahl (16:107), Al-Qaswasw (28:60), Az-Zukhruf (43:35). Rejea pia Al-Hadiyd (57:20) kwenye maelezo bayana na faida tele. Na rejea pia Al-A’laa (87:16-17).
[10] Allaah Angetaka Angewaangamiza Washirikina Wote:
Tafsiyr:
أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ ۚ
“Je, wanao washirika waliowaamuru dini ambayo Allaah Hakuitolea idhini?”
Allaah (سبحانه وتعالى) Anakhabarisha ya kwamba washirikina walijifanyia washirika, wakawa wanawapenda na kuwashirikisha katika ukafiri na matendo ya kikafiri. Hao ni katika mashaytwani wa kibinaadam wanaolingania ukafiri katika mambo ya ushirikina na bid-ah, na kuharamisha Alivyovihalalisha Allaah, na kuvihalalisha Alivyoviharamisha Allaah, na mfano wa hivyo, wakiwa wanafanya kwa mujibu wa matakwa na matamanio yao.
Pamoja na kwamba dini haiwi isipokuwa kwa mujibu wa Alivyoiweka Allaah, ili waja waifuate, na wajikurubishe Kwake kupitia Dini hiyo. Asili ni kumzuia kila mmoja kutoweka chochote katika yale Aliyoweka Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم). Sasa itakuwaje kwa hawa mafasiki walioshirikiana na baba zao kwenye ukafiri?!
وَلَوْلَا كَلِمَةُ الْفَصْلِ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۗ وَإِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٢١﴾
“Na lau si neno la uamuzi, basi jambo lingelimalizwa (hapa duniani) baina yao. Na hakika madhalimu watapata adhabu iumizayo.”
Lau kama si kuwa na muda maalumu ambao Allaah Ameuweka ukitenganisha nyumati mbalimbali, na kwamba Atawachelewesha, (kama si kuwa hilo) wangeangamizwa katika wakati huu uliopo. Angepewa maisha mazuri anaestahiki, na angeangamizwa asiestahiki, kwa ajili zile sababu zinazopelekea kuangamizwa zipo, lakini mbele yao kuna adhabu iumizayo huko Aakhirah kwa hawa na kila aliyedhulumu. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[15] Kujiepusha Na Machafu:
Baadhi ya Hadiyth zilizokataza machafu ni zifuatazo:
عَنْ أَبِي اَلدَّرْدَاءِ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {إِنَّ اَللَّهَ يُبْغِضُ اَلْفَاحِشَ اَلْبَذِيءَ} أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَهُ
وَلَهُ مِنْ حَدِيثِ اِبْنِ مَسْعُودٍ رَفَعَهُ: {لَيْسَ اَلْمُؤْمِنُ بِالطَّعَّانِ، وَلَا اَللَّعَّانُ، وَلَا اَلْفَاحِشَ، وَلَا اَلْبَذِيءَ} وَحَسَّنَهُ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ، وَرَجَّحَ اَلدَّارَقُطْنِيُّ وَقْفَهُ
Amesimulia Abuu Ad-Dardaa (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Anamchukia muovu, mwenye maneno mabaya.” [Imetolewa na At-Tirmidhiy na akaisahihisha]
Pia amepokea kutoka katika Hadiyth ya Ibn Mas-‘uwd marfuw’: “Muumini si mtukanaji, wala si mlaanifu, wala mchafu, wala si mwenye maneno mabaya.” [Na amesema ni Hasan na akaisahihisha Al-Haakim. Ad-Daaraqutwniy ameitilia nguvu kuwa ni Marfuw’]
[16] Miongoni Mwa Sifa Za Waumini Ni Kushauriana Baina Yao:
Miongoni mwa sifa za Waumini zimetajwa katika Aayah hii tukufu na mojawapo ni hii ya kushauriana baina yao, sifa ambayo ni jina la Suwrah hii tukufu. Tafsiyr ya Aayah ni kama ilivyoelezewa na Imaam As-Sa’diy (رحمه الله):
وَالَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِرَبِّهِمْ
“Na wale waliomuitikia Rabb wao.”
Na wale walionyenyekea katika kumtii Allaah (سبحانه وتعالى), na wakaitikia daawah Yake, na ikawa makusudio yao ni kumridhisha Allaah na kufaulu kwa kujikurubisha Kwake.
Na katika kuitikia na kukubali daawah (wito) wa Allaah ni kutekeleza Swalaah tano na kutoa Zakaah, kwa sababu hiyo, ndio Allaah Akaziunganisha katika kuzitaja ibaada hizi mbili, jambo linalojulisha fadhila na sharafu zake. Akasema:
وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ
“Wakasimamisha Swalaah.”
Za kusoma kwa sauti na za sauti ya chini, za faradhi na za Sunnah.
وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ﴿٣٨﴾
“Na kutokana na vile Tulivyowaruzuku wanatoa.”
Katika utowaji wa waajibu, mfano wa Zakaah na matumizi ya ndugu na familia, na mfano wao, na utoaji mustahab (Sunnah) kama vile kutoa swadaqah kwa watu wote (wasio ndugu).
وَأَمْرُهُمْ شُورَىٰ بَيْنَهُمْ
“Na jambo lao hushauriana baina yao.”
Jambo la kidini na kidunia. Hatosheki mtu na rai yake, kwenye jambo lolote lile linalotaka ushirikiano. Na hili halipatikani isipokuwa wakiwa na umoja, upendo na ukamilifu wa akili ya kwamba wanapohitajia jambo lolote lile linalohitaji kufikiria na kupeana rai, huwa wanakusanyika na kushauriana, mpaka ikibainika maslahi, wanaharakisha na kulifanyia kazi. Na jambo hilo ni kama vile rai zao katika Vita na Jihaad, kuwaweka viongozi ama kutoa hukumu, na yasiyokuwa hayo, na kama vile kufanya bah-th (utafiti) kwenye mas-ala ya kidini kiujumla wake, hivyo vyote ni katika mambo yanayohitaji kushirikiana, na kuyafanyia bahth, ili kubainisha usawa Anaoupenda Allaah. Haya yote yanaingia katika Aayah hii. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[17] Maana Ya Baghyun/Baghaa Katika Qur-aan
Rejea Aayah namba (14) ya Suwrah hii Ash-Shuwraa (42) kupata maana zake mbalimbali.
[18] Dhulma Ni Dhulumaat (Giza Nene) Siku Ya Qiyaamah:
عَنْ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {اَلظُّلْمُ ظُلُمَاتٌ يَوْمَ اَلْقِيَامَةِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Amesimulia Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Dhulma ni giza nene Siku ya Qiyaamah.” [Bukhaariy, Muslim]
Dhulma, maana yake ni kuweka kitu sehemu isiyokuwa yake, au kuficha ukweli ili usitokeze. Katika Siku ya Hukmu (Qiyaamah), dhulma itaonekana na rangi yake itakuwa ni nyeusi. Hadiyth hii inatufundisha kuwa dhulma ni kitu kibaya na ni haramu ikiwa kwa mtu, katika heshima au utajiri wake.
019-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Dhulma Irudishwe Duniani Kabla Ya Malipo Ya Aakhirah [284]
[19] Maana Ya Baghyun/Baghaa Katika Qur-aan:
Rejea Suwrah hii Ash-Shuwraa (42:14) kupata maana zake mbalimbali.
[20] Aina Tatu Za Wahy:
Na haipasi kwa mtu yeyote katika wanaadam Allaah (سبحانه وتعالى) Aseme naye, isipokuwa kwa njia ya Wahy ambao Allaah (سبحانه وتعالى) Anamtumia, au Aseme naye nyuma ya pazia, kama vile Allaah (سبحانه وتعالى) Alivyosema na Nabiy Muwsaa (عليه السّلام). Au Atume Mjumbe, kama Anavyomtuma Jibriyl (عليه السّلام) kwa yule anayetumwa kwake ampelekee Wahy wa kile Allaah (سبحانه وتعالى) Anataka apelekewe, kwa Idhini ya Rabb wake, na sio kwa mapendeleo yake. Hakika Yake Yeye Allaah (سبحانه وتعالى), Yuko juu kwa Dhati Yake, Majina Yake, Sifa Zake na Vitendo Vyake. Amekilazimisha kila kitu, na viumbe vyote vimemdhalilikia, na ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji Wake mambo ya viumbe Vyake. Katika Aayah hii, pana kuthibitisha Sifa ya kusema kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa namna inayonasibiana na Haiba Yake na ukubwa wa Mamlaka Yake. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[22] Nuru (Mwanga) Ni Njia Moja Tu, Viza Ni Vingi:
Rejea Ibraahiym (14:1-2) Kwenye maelezo bayana na faida tele kuhusu Nuru na viza, pamoja na rejea mbalimbali.
الزُّخْرُف
043-Az-Zukhruf
043-Az-Zukhruf: Utangulizi Wa Suwrah [286]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
حم﴿١﴾
1. Haa Miym.[1]
وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ﴿٢﴾
2. Naapa kwa Kitabu (Qur-aan) kinachobainisha.
إِنَّا جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ﴿٣﴾
3. Hakika Sisi Tumekifanya kisomeke kwa Kiarabu ili mpate kutia akilini.
وَإِنَّهُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ﴿٤﴾
4. Na hakika hii (Qur-aan) iko Kwetu katika Mama wa Kitabu[2] Imetukuka kwa hakika, imejaa hikmah.
أَفَنَضْرِبُ عَنكُمُ الذِّكْرَ صَفْحًا أَن كُنتُمْ قَوْمًا مُّسْرِفِينَ﴿٥﴾
5. Je, Tuwaondoshelee mbali Ukumbusho huu kwa vile nyinyi mmekuwa wapindukao mipaka?[3]
وَكَمْ أَرْسَلْنَا مِن نَّبِيٍّ فِي الْأَوَّلِينَ﴿٦﴾
6. Na Manabii wangapi Tumewatuma kwa watu wa awali?
وَمَا يَأْتِيهِم مِّن نَّبِيٍّ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٧﴾
7. Na hakuwafikia Nabiy yeyote isipokuwa walikuwa wakimfanyia istihzai.
فَأَهْلَكْنَا أَشَدَّ مِنْهُم بَطْشًا وَمَضَىٰ مَثَلُ الْأَوَّلِينَ﴿٨﴾
8. Basi Tukawaangamiza walio na nguvu zaidi kuliko wao, na umeshapita mfano wa watu wa awali.
وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ خَلَقَهُنَّ الْعَزِيزُ الْعَلِيمُ﴿٩﴾
9. Na ukiwauliza: Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi? Bila shaka watasema: Ameziumba Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.[4]
الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ مَهْدًا وَجَعَلَ لَكُمْ فِيهَا سُبُلًا لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ﴿١٠﴾
10. Ambaye Amekufanyieni ardhi kuwa tandiko, na Akakufanyieni humo njia ili msipotee muendako.
وَالَّذِي نَزَّلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً بِقَدَرٍ فَأَنشَرْنَا بِهِ بَلْدَةً مَّيْتًا ۚ كَذَٰلِكَ تُخْرَجُونَ﴿١١﴾
11. Na Ambaye Ameteremsha kutoka mbinguni maji kwa kadiri ya kipimo, Tukafufua kwayo nchi iliyokufa, na hivyo ndivyo mtakavyotolewa.[5]
وَالَّذِي خَلَقَ الْأَزْوَاجَ كُلَّهَا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ الْفُلْكِ وَالْأَنْعَامِ مَا تَرْكَبُونَ﴿١٢﴾
12. Na Ambaye Ameumba kila kitu jozi; dume na jike, na Akakufanyieni mnavyovipanda kati ya merikebu na wanyama.
لِتَسْتَوُوا عَلَىٰ ظُهُورِهِ ثُمَّ تَذْكُرُوا نِعْمَةَ رَبِّكُمْ إِذَا اسْتَوَيْتُمْ عَلَيْهِ وَتَقُولُوا سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَـٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ﴿١٣﴾
13. Ili mlingamane sawasawa juu ya mgongo wake, kisha mkumbuke Neema ya Rabb wenu mtakapolingamana sawasawa juu yao, na mseme:[6] Utakasifu ni wa (Allaah) Ambaye Ametutiishia haya, na tusingeliweza wenyewe kumdhibiti.
وَإِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا لَمُنقَلِبُونَ﴿١٤﴾
14. Na hakika kwa Rabb wetu, bila shaka tutarejea.
وَجَعَلُوا لَهُ مِنْ عِبَادِهِ جُزْءًا ۚ إِنَّ الْإِنسَانَ لَكَفُورٌ مُّبِينٌ﴿١٥﴾
15. Na wakamfanyia kati ya Waja Wake sehemu (kuwa Allaah Ana watoto).[7] Hakika binaadam bila shaka ni mwingi wa kukufuru, bila kuficha ukafiri wake.
أَمِ اتَّخَذَ مِمَّا يَخْلُقُ بَنَاتٍ وَأَصْفَاكُم بِالْبَنِينَ﴿١٦﴾
16. Je, Amejichukulia katika Aliowaumba mabanati[8], na Akakukhitarieni nyinyi watoto wa kiume?
وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِمَا ضَرَبَ لِلرَّحْمَـٰنِ مَثَلًا ظَلَّ وَجْهُهُ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ﴿١٧﴾
17. Na anapobashiriwa mmoja wao kwa yale aliyompigia mfano Ar-Rahmaan (binti), husawijika uso wake, naye ni mwenye kuzuia ghadhabu na huzuni.[9]
أَوَمَن يُنَشَّأُ فِي الْحِلْيَةِ وَهُوَ فِي الْخِصَامِ غَيْرُ مُبِينٍ﴿١٨﴾
18. Ah! (Wanampendelea Allaah kiumbe) aliyelelewa katika mapambo naye katika mabishano si mbainifu?!
وَجَعَلُوا الْمَلَائِكَةَ الَّذِينَ هُمْ عِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ إِنَاثًا ۚ أَشَهِدُوا خَلْقَهُمْ ۚ سَتُكْتَبُ شَهَادَتُهُمْ وَيُسْأَلُونَ﴿١٩﴾
19. Na wakawafanya Malaika ambao ni Waja wa Ar-Rahmaan kuwa ni wa kike.[10] Je, kwani wameshuhudia uumbaji wao? Utaandikwa ushahidi wao, na wataulizwa.
وَقَالُوا لَوْ شَاءَ الرَّحْمَـٰنُ مَا عَبَدْنَاهُم ۗ مَّا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ﴿٢٠﴾
20. Na wakasema: Angelitaka Ar-Rahmaan tusingeliyaabudu (miungu ya uongo). Hawana ilimu yoyote ya hayo, hawana isipokuwa wanabuni uongo.
أَمْ آتَيْنَاهُمْ كِتَابًا مِّن قَبْلِهِ فَهُم بِهِ مُسْتَمْسِكُونَ﴿٢١﴾
21. Au Tumewapa Kitabu kabla yake (hii Qur-aan), basi wao kwacho wanakishikilia?
بَلْ قَالُوا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّهْتَدُونَ﴿٢٢﴾
22. Bali wamesema: Hakika sisi tumewakuta baba zetu juu ya dini, na hakika sisi tunajiongoza kwa kufuata nyayo zao.[11]
وَكَذَٰلِكَ مَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتْرَفُوهَا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّقْتَدُونَ﴿٢٣﴾
23. Na hiyo ndiyo hali yao, kwani Hatukutuma kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) katika mji mwonyaji yeyote yule isipokuwa walisema matajiri wake wenye starehe na taanusi: Hakika sisi tumewakuta baba zetu juu ya dini, na hakika sisi ni wenye kufuata nyayo zao.
قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكُم بِأَهْدَىٰ مِمَّا وَجَدتُّمْ عَلَيْهِ آبَاءَكُمْ ۖ قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ كَافِرُونَ﴿٢٤﴾
24. (Kila Rasuli) alisema: Japo hata kama nimekujieni na uongofu zaidi kuliko ambao mmewakuta nao baba zenu? Wakasema: Hakika sisi tunayakanusha yale mliyotumwa nayo.
فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ﴿٢٥﴾
25. Basi Tukawalipizia. Hebu tazama vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha!
وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ﴿٢٦﴾
26. Na pale Ibraahiym alipomwambia baba yake na kaumu yake: Hakika mimi nimejitoa katika dhima na yale mnayoyaabudu.
إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ﴿٢٧﴾
27. Isipokuwa kwa Ambaye Ameniumba, basi hakika Yeye Ataniongoza.
وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ﴿٢٨﴾
28. Na akalifanya neno (laa ilaaha illaa-Allaah) lenye kubakia katika kizazi chake ili wapate kurejea.
بَلْ مَتَّعْتُ هَـٰؤُلَاءِ وَآبَاءَهُمْ حَتَّىٰ جَاءَهُمُ الْحَقُّ وَرَسُولٌ مُّبِينٌ﴿٢٩﴾
29. Bali Niliwastarehesha hawa (makafiri wa Makkah) na baba zao mpaka ikawajia haki na Rasuli anayebainisha.
وَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ قَالُوا هَـٰذَا سِحْرٌ وَإِنَّا بِهِ كَافِرُونَ﴿٣٠﴾
30. Na ilipowajia haki, walisema: Hii ni sihiri, na hakika sisi ni wenye kuikanusha.
وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ هَـٰذَا الْقُرْآنُ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنَ الْقَرْيَتَيْنِ عَظِيمٍ﴿٣١﴾
31. Na wakasema: Kwa nini isiteremshwe hii Qur-aan kwa mtu adhimu kutoka miji miwili?[12]
أَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَتَ رَبِّكَ ۚ نَحْنُ قَسَمْنَا بَيْنَهُم مَّعِيشَتَهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَرَفَعْنَا بَعْضَهُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِّيَتَّخِذَ بَعْضُهُم بَعْضًا سُخْرِيًّا ۗ وَرَحْمَتُ رَبِّكَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ﴿٣٢﴾
32. Je, wao wanazigawanya Rehma za Rabb wako? Sisi Tumegawanya baina yao maisha yao katika uhai wa dunia, na Tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengineo kwa daraja ili watumikishane wao kwa wao. Na Rehma za Rabb wako ni bora kuliko wanayoyajumuisha.
وَلَوْلَا أَن يَكُونَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً لَّجَعَلْنَا لِمَن يَكْفُرُ بِالرَّحْمَـٰنِ لِبُيُوتِهِمْ سُقُفًا مِّن فِضَّةٍ وَمَعَارِجَ عَلَيْهَا يَظْهَرُونَ﴿٣٣﴾
33. Na lau isingelikuwa watu watakuwa ummah mmoja (wa makafiri), Tungejaalia wanaomkufuru Ar-Rahmaan wana nyumba zao zenye dari za fedha na ngazi pia wanazozipandia.[13]
وَلِبُيُوتِهِمْ أَبْوَابًا وَسُرُرًا عَلَيْهَا يَتَّكِئُونَ﴿٣٤﴾
34. Na kwenye nyumba zao milango na makochi (ya fedha) wanayoyaegemea.
وَزُخْرُفًا ۚ وَإِن كُلُّ ذَٰلِكَ لَمَّا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَالْآخِرَةُ عِندَ رَبِّكَ لِلْمُتَّقِينَ﴿٣٥﴾
35. Na mapambo ya dhahabu. Lakini hayo yote si chochote isipokuwa ni starehe ya uhai wa dunia. Na Aakhirah iliyo kwa Rabb wako ni kwa wenye taqwa.
وَمَن يَعْشُ عَن ذِكْرِ الرَّحْمَـٰنِ نُقَيِّضْ لَهُ شَيْطَانًا فَهُوَ لَهُ قَرِينٌ﴿٣٦﴾
36. Na anayejifanya kipofu na ukumbusho wa Ar-Rahmaan Tunamwekea shaytwaan awe ndiye rafiki yake mwandani.
وَإِنَّهُمْ لَيَصُدُّونَهُمْ عَنِ السَّبِيلِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُم مُّهْتَدُونَ﴿٣٧﴾
37. Na hakika wao (mashaytwaan) wanawazuia njia na wanadhania kwamba wao wamehidika.
حَتَّىٰ إِذَا جَاءَنَا قَالَ يَا لَيْتَ بَيْنِي وَبَيْنَكَ بُعْدَ الْمَشْرِقَيْنِ فَبِئْسَ الْقَرِينُ﴿٣٨﴾
38. Mpaka atakapotujia (Siku ya Qiyaamah), atasema: Laiti ingelikuwa baina yangu na baina yako umbali wa Mashariki na Magharibi, basi muovu mno rafiki mwandani wewe![14]
وَلَن يَنفَعَكُمُ الْيَوْمَ إِذ ظَّلَمْتُمْ أَنَّكُمْ فِي الْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ﴿٣٩﴾
39. Hakutokufaeni chochote leo nyinyi kuwa pamoja ndani ya adhabu, kwani mlidhulumu.
أَفَأَنتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ أَوْ تَهْدِي الْعُمْيَ وَمَن كَانَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٤٠﴾
40. Je, kwani wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) unaweza kusikilizisha viziwi au kuwahidi vipofu na yule aliye katika upotofu bayana?
فَإِمَّا نَذْهَبَنَّ بِكَ فَإِنَّا مِنْهُم مُّنتَقِمُونَ﴿٤١﴾
41. Na hata kama Tukikuondoa (kukufisha ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi hakika Sisi Ni Wenye Kuwalipizia.
أَوْ نُرِيَنَّكَ الَّذِي وَعَدْنَاهُمْ فَإِنَّا عَلَيْهِم مُّقْتَدِرُونَ﴿٤٢﴾
42. Au Tukuonyeshe yale Tuliyowatishia, basi hakika Sisi Ni Wenye Uwezo juu yao.
فَاسْتَمْسِكْ بِالَّذِي أُوحِيَ إِلَيْكَ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٤٣﴾
43. Basi shikilia kwa uthabiti yale uliyofunuliwa Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), hakika wewe uko juu ya njia iliyonyooka.
وَإِنَّهُ لَذِكْرٌ لَّكَ وَلِقَوْمِكَ ۖ وَسَوْفَ تُسْأَلُونَ﴿٤٤﴾
44. Na hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni ukumbusho kwako na kwa watu wako, na mtakuja ulizwa.
وَاسْأَلْ مَنْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رُّسُلِنَا أَجَعَلْنَا مِن دُونِ الرَّحْمَـٰنِ آلِهَةً يُعْبَدُونَ﴿٤٥﴾
45. Na waulize (wafuasi wa) wale Tuliowatuma kabla yako miongoni mwa Rusuli Wetu: Je, Tulifanya badala ya Ar-Rahmaan waabudiwa wengine ili waabudiwe?
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَقَالَ إِنِّي رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿٤٦﴾
46. Na kwa yakini Tulimtuma Muwsaa na Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu kwa Firawni na wakuu wake akasema: (kuwaambia): Hakika mimi ni Rasuli wa Rabb wa walimwengu.
فَلَمَّا جَاءَهُم بِآيَاتِنَا إِذَا هُم مِّنْهَا يَضْحَكُونَ﴿٤٧﴾
47. Basi alipowajia na Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu mara wao wakaharakia kuzicheka.
وَمَا نُرِيهِم مِّنْ آيَةٍ إِلَّا هِيَ أَكْبَرُ مِنْ أُخْتِهَا ۖ وَأَخَذْنَاهُم بِالْعَذَابِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ﴿٤٨﴾
48. Na Hatukuwaonyesha Aayah (Ishara, Dalili) yoyote isipokuwa ilikuwa ni kubwa zaidi kuliko ya mwenziwe, na Tukawachukua kwa adhabu ili wapate kurejea.
وَقَالُوا يَا أَيُّهَ السَّاحِرُ ادْعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَ إِنَّنَا لَمُهْتَدُونَ﴿٤٩﴾
49. Na wakasema: Ee mchawi! Tuombee kwa Rabb wako yale Aliyokuahidi kwako. Hakika sisi bila shaka tutaongoka.
فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُمُ الْعَذَابَ إِذَا هُمْ يَنكُثُونَ﴿٥٠﴾
50. Lakini Tulipowaondoshea adhabu, mara hao wanaharakia kuvunja ahadi.
وَنَادَىٰ فِرْعَوْنُ فِي قَوْمِهِ قَالَ يَا قَوْمِ أَلَيْسَ لِي مُلْكُ مِصْرَ وَهَـٰذِهِ الْأَنْهَارُ تَجْرِي مِن تَحْتِي ۖ أَفَلَا تُبْصِرُونَ﴿٥١﴾
51. Na Firawni akanadi kwa kaumu yake, akasema: Enyi kaumu yangu! Je, kwani ufalme wa Misri si wangu! Na hii mito inapita chini yangu? Je, hamuoni?
أَمْ أَنَا خَيْرٌ مِّنْ هَـٰذَا الَّذِي هُوَ مَهِينٌ وَلَا يَكَادُ يُبِينُ﴿٥٢﴾
52. Au mimi si bora kuliko huyu (Muwsaa) ambaye yeye ni dhalili na wala hawezi kujieleza wazi ila kwa mashaka?
فَلَوْلَا أُلْقِيَ عَلَيْهِ أَسْوِرَةٌ مِّن ذَهَبٍ أَوْ جَاءَ مَعَهُ الْمَلَائِكَةُ مُقْتَرِنِينَ﴿٥٣﴾
53. Basi kwa nini hakuvishwa vikuku vya dhahabu, au wakaja pamoja naye Malaika wenye kuandamana naye?
فَاسْتَخَفَّ قَوْمَهُ فَأَطَاعُوهُ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ﴿٥٤﴾
54. Basi aliwachezea akili watu wake nao wakamtii. Hakika wao walikuwa watu mafasiki.
فَلَمَّا آسَفُونَا انتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَاهُمْ أَجْمَعِينَ﴿٥٥﴾
55. Basi walipotukasirisha, Tuliwalipizia, Tukawagharikisha wote.
فَجَعَلْنَاهُمْ سَلَفًا وَمَثَلًا لِّلْآخِرِينَ﴿٥٦﴾
56. Tukawafanya wenye kutangulia na mfano kwa wengineo.
وَلَمَّا ضُرِبَ ابْنُ مَرْيَمَ مَثَلًا إِذَا قَوْمُكَ مِنْهُ يَصِدُّونَ﴿٥٧﴾
57. Na mwana wa Maryam aliponukuliwa kama mfano, tahamaki watu wako wanaupigia kelele na kushangilia.[15]
وَقَالُوا أَآلِهَتُنَا خَيْرٌ أَمْ هُوَ ۚ مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًا ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ﴿٥٨﴾
58. Na wakasema: Je, waabudiwa wetu ni bora au yeye? Hawakukupigia (mfano) huo isipokuwa tu kutaka ubishi. Bali wao ni watu wapinzani.
إِنْ هُوَ إِلَّا عَبْدٌ أَنْعَمْنَا عَلَيْهِ وَجَعَلْنَاهُ مَثَلًا لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ﴿٥٩﴾
59. Yeye (Nabiy ‘Iysaa) si chochote isipokuwa ni mja Tuliyemneemesha, na Tukamfanya ni mfano kwa wana wa Israaiyl.
وَلَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَا مِنكُم مَّلَائِكَةً فِي الْأَرْضِ يَخْلُفُونَ﴿٦٠﴾
60. Na lau Tungelitaka, basi Tungewafanya Malaika badala yenu wanarithishana katika ardhi.
وَإِنَّهُ لَعِلْمٌ لِّلسَّاعَةِ فَلَا تَمْتَرُنَّ بِهَا وَاتَّبِعُونِ ۚ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ﴿٦١﴾
61. Na hakika yeye (Nabiy ‘Iysaa) ni alama ya Saa.[16] Basi musiitilie shaka, na nifuateni. Hii ndio njia iliyonyooka.
وَلَا يَصُدَّنَّكُمُ الشَّيْطَانُ ۖ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ﴿٦٢﴾
62. Na jitahidini sana asikuzuieni shaytwaan, hakika yeye kwenu ni adui bayana.
وَلَمَّا جَاءَ عِيسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ قَالَ قَدْ جِئْتُكُم بِالْحِكْمَةِ وَلِأُبَيِّنَ لَكُم بَعْضَ الَّذِي تَخْتَلِفُونَ فِيهِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ﴿٦٣﴾
63. Na alipokuja ‘Iysaa kwa hoja bayana, akasema: Nimekujieni na hikmah, na ili nikubainishieni baadhi ya yale mnayokhitilafiana kwayo, basi mcheni Allaah na nitiini.
إِنَّ اللَّـهَ هُوَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ﴿٦٤﴾
64. Hakika Allaah Ndiye Rabb wangu na Rabb wenu, basi mwabuduni Yeye Pekee,[17] hii ndio njia iliyonyooka.
فَاخْتَلَفَ الْأَحْزَابُ مِن بَيْنِهِمْ ۖ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْ عَذَابِ يَوْمٍ أَلِيمٍ﴿٦٥﴾
65. Basi wakakhitilafiana makundi kwa makundi baina yao.[18] Basi ole kwa wale waliodhulumu kutokana na adhabu ya Siku iumizayo.
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ﴿٦٦﴾
66. Je, wanangojea isipokuwa Saa tu iwafikie ghafla nao hawatambui.
الْأَخِلَّاءُ يَوْمَئِذٍ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ إِلَّا الْمُتَّقِينَ﴿٦٧﴾
67. Marafiki wapenzi Siku hiyo watakuwa maadui wao kwa wao isipokuwa wenye taqwa.
يَا عِبَادِ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمُ الْيَوْمَ وَلَا أَنتُمْ تَحْزَنُونَ﴿٦٨﴾
68. Enyi Waja Wangu! Hakuna khofu juu yenu leo, na wala nyinyi hamtohuzunika.
الَّذِينَ آمَنُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا مُسْلِمِينَ﴿٦٩﴾
69. Ambao wameamini Aayaat (na Ishara, Dalili) Zetu na wakawa Waislamu.
ادْخُلُوا الْجَنَّةَ أَنتُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ تُحْبَرُونَ﴿٧٠﴾
70. Ingieni Jannah nyinyi na wake zenu mfurahishwe.
يُطَافُ عَلَيْهِم بِصِحَافٍ مِّن ذَهَبٍ وَأَكْوَابٍ ۖ وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ الْأَنفُسُ وَتَلَذُّ الْأَعْيُنُ ۖ وَأَنتُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿٧١﴾
71. Watapitishiwa sahani za dhahabu na bilauri. Na humo mna yale zinazotamani nafsi na ya kuburudisha macho, nanyi humo ni wenye kudumu.
وَتِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٧٢﴾
72. Na hiyo ni Jannah ambayo mmerithishwa kwa yale mliyokuwa mkitenda.
لَكُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ كَثِيرَةٌ مِّنْهَا تَأْكُلُونَ﴿٧٣﴾
73. Mtapata humo matunda mengi, mtakula yoyote myatakayo.
إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي عَذَابِ جَهَنَّمَ خَالِدُونَ﴿٧٤﴾
74. Hakika wahalifu watadumu kwenye adhabu ya Jahannam.
لَا يُفَتَّرُ عَنْهُمْ وَهُمْ فِيهِ مُبْلِسُونَ﴿٧٥﴾
75. Hawatopumzishwa nayo, nao humo watakata tamaa.
وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا هُمُ الظَّالِمِينَ﴿٧٦﴾
76. Na wala Hatukuwadhulumu, lakini walikuwa wao wenyewe ndio madhalimu.
وَنَادَوْا يَا مَالِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ ۖ قَالَ إِنَّكُم مَّاكِثُونَ﴿٧٧﴾
77. Na wataita: Ee Maalik![19] Na Atumalize tufe Rabb wako. Atasema: Hakika nyinyi ni wenye kubakia kuishi humo.
لَقَدْ جِئْنَاكُم بِالْحَقِّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَكُمْ لِلْحَقِّ كَارِهُونَ﴿٧٨﴾
78. Kwa yakini Tulikujieni na haki, lakini wengi wenu ni wenye kuichukia haki.
أَمْ أَبْرَمُوا أَمْرًا فَإِنَّا مُبْرِمُونَ﴿٧٩﴾
79. Au je walipanga njama zao barabara? Basi hakika Sisi Ni Wenye Kulipiza njama.
أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لَا نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُم ۚ بَلَىٰ وَرُسُلُنَا لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ﴿٨٠﴾
80. Au wanadhania kwamba Sisi Hatusikii siri zao na minong’ono yao? Bali ndio (Tunasikia!) Na Wajumbe Wetu wako kwao wanaandika.
قُلْ إِن كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدٌ فَأَنَا أَوَّلُ الْعَابِدِينَ﴿٨١﴾
81. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Kama ingelikuwa Ar-Rahmaan Ana mwana (kama mnavyodai), basi mimi ningekuwa wa mwanzo katika waja (Wake).[20]
سُبْحَانَ رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبِّ الْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ﴿٨٢﴾
82. Utakasifu ni wa Rabb wa mbingu na ardhi, Rabb wa ‘Arsh kutokana na yale wanayoyavumisha.
فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ﴿٨٣﴾
83. Basi waachilie mbali watumbukie katika porojo na wacheze mpaka wakutane na Siku yao wanayoahidiwa.
وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَـٰهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَـٰهٌ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ﴿٨٤﴾
84. Na Yeye Ndiye Muabudiwa wa haki mbinguni na ardhini pia (Ndiye Huyo Huyo) Ilaah. Naye Ndiye Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.[21]
وَتَبَارَكَ الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَعِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٨٥﴾
85. Na Amebarikika Ambaye ufalme wa mbingu na ardhi ni Wake na vilivyo baina yake, na Kwake Pekee upo ujuzi wa Saa, na Kwake mtarejeshwa.
وَلَا يَمْلِكُ الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ الشَّفَاعَةَ إِلَّا مَن شَهِدَ بِالْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ﴿٨٦﴾
86. Na wala wale wanaowaomba badala Yake hawana uwezo wa kumiliki uombezi isipokuwa yule aliyeshuhudia kwa haki nao wanajua.[22]
وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَهُمْ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ﴿٨٧﴾
87. Na ukiwauliza: Ni nani kawaumba? Bila shaka watasema: Allaah. Basi vipi wanaghilibiwa?[23]
وَقِيلِهِ يَا رَبِّ إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ قَوْمٌ لَّا يُؤْمِنُونَ﴿٨٨﴾
88. Na (Allaah Anajua) kauli yake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ee Rabb wangu! Hakika hawa watu hawaamini.
فَاصْفَحْ عَنْهُمْ وَقُلْ سَلَامٌ ۚ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ﴿٨٩﴾
89. Basi wapuuzilie mbali (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na sema: Salaamun! Na karibuni hivi watakuja jua.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Ummul-Kitaab: Mama Wa Kitabu Ni Lawh Mahfudhw (Ubao Uliohifadhiwa) Rejea: Ar-Ra’d (13:39).
[3] Washirikina Kuipuuza Qur-aan:
‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu Aayah hii kama ifuatavyo:
Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما), Abu Swalih, Mujaahid na As-Suddi na ni rai ya Ibn Jariyr pia: “Mnadhani Tutakusameheni na Hatutakuadhibuni, na hali hamfanyi mliyoamrishwa?”
Qataadah: “Naapa kwa Allaah, lau kuwa Qur-aan hii ingeondolewa walipoikataa vizazi vya mwanzo vya Ummah huu, wangeliangamia, lakini Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Rehma Yake Amerudia kuituma kama Desturi Yake na kuwalingania kwa muda wa miaka ishirini, au kwa muda mrefu kama Alivyotaka.”
Tafsiyr ya Imaam As-Sa’diy (رحمه الله):
Hivi Tuwapuuze na Tuache kuteremsha ukumbusho, na Tuwaondoshelee mbali Ukumbusho kwa ajili ya kupuuza kwenu? Bali Tunawateremshia Kitabu na Tunaweka wazi kwenu kila kitu, na kama mtaamini na mkaongoka, basi hilo ni katika tawfiyq yenu, na kama si hivyo, basi itasimama hoja juu yenu na mtakuwa kwenye ubainisho wa jambo lenu. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[4] Washirikina Waliamini Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah Lakini Walikanusha Tawhiyd Al-Uluwhiyyah::
Rejea Yuwnus (10:31), Al-‘Ankabuwt (29:61), Az-Zumar (39:38), na Suwrah hii Az-Zukhruf (43:87).
[5] Mfano Wa Ardhi Iliyokufa (Kame), Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akaihuisha Kwa Mvua, Ni Mfano Wa Kuwahuisha Watu Kutoka Makaburini Mwao Siku Ya Qiyaamah:
Rejea Ar-Ruwm (30:50).
[6] Duaa Ya Kupanda Kipando:
Bonyeza kiungo kifuatacho kwenye duaa ya kupanda chombo:
Na Hadiyth yake ni ifuatayo:
عن عَلِي بن ربيعة ، قَالَ : شهدت عليَّ بن أَبي طالب رضي الله عنه ، أُتِيَ بِدَابَّةٍ لِيَرْكَبَهَا ، فَلَمَّا وَضَعَ رِجْلَهُ في الرِّكَابِ ، قَالَ : بِسْمِ اللهِ ، فَلَمَّا اسْتَوَى عَلَى ظَهْرِهَا ، قَالَ : الحَمْدُ للهِ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنينَ ، وَإنَّا إِلَى رَبِّنَا لَمُنْقَلِبُونَ ، ثُمَّ قَالَ : الحمْدُ للهِ ، ثَلاثَ مَرَّاتٍ ، ثُمَّ قَالَ : اللهُ أكْبَرُ ، ثَلاثَ مَرَّاتٍ ، ثُمَّ قَالَ : سُبْحَانَكَ إنّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي إنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أنْتَ ، ثُمَّ ضَحِكَ ، فَقيلَ : يَا أمِيرَ المُؤمِنِينَ ، مِنْ أيِّ شَيْءٍ ضَحِكْتَ ؟ قَالَ : رَأيتُ النبيَّ صلى الله عليه وسلم فَعَلَ كَمَا فَعَلْتُ ثُمَّ ضَحِكَ ، فقُلْتُ : يَا رسول اللهِ ، مِنْ أيِّ شَيْءٍ ضَحِكْتَ ؟ قَالَ : (( إنَّ رَبَّكَ تَعَالَى يَعْجَبُ مِنْ عَبدِهِ إِذَا قَالَ : اغْفِرْ لِي ذُنُوبِي ، يَعْلَمُ أنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ غَيْرِي )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن ))، وفي بعض النسخ: (( حسن صحيح )) . وهذا لفظ أَبي داود .
'Aliy bin Rabiy’ah (رضي الله عنه) amesema: Nimemshuhudia 'Aliy bin Abiy Twaalib (رضي الله عنه) akiletewa mnyama ampande. Alipoweka mguu wake kwenye kipando alisema:
بِسْمِ اللهِ
Alipolingana juu ya mgongo wake alisema:
الحَمْدُ للهِ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنينَ ، وَإنَّا إِلَى رَبِّنَا لَمُنْقَلِبُونَ
Kisha akasema:
الحمْدُ للهِ
AlhamduliLlaah (Himdi Anastahiki Allaah) (mara tatu).
Kisha akasema:
اللهُ أكْبَرُ
Allaahu Akbar (Allaah Ni Mkubwa) (mara tatu).
Kisha akasema:
سُبْحَانَكَ إنّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي إنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أنْتَ
Subhaanak inniy dhwalamtu nafsiy Faghfirliy, innahu laa yaghfirudh-dhunuwba illa Anta.
Kutakasika ni Kwako, hakika mimi nimedhulumu nafsi yangu, basi Nighufurie, kwani hakuna mwenye kughufuria dhambi ila Wewe.
Kisha akacheka. Akaulizwa: Ee Amiri wa Waumini! Unacheka nini?
Akasema: Nilimuona Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akifanya kama nilivyofanya, kisha akacheka. Nikamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Unacheka nini? Akasema: “Hakika Rabb wako Anamridhia mja Wake anaposema: Nighufurie dhambi zangu, anajua kuwa hakuna anayeghufuria dhambi isipokuwa Yeye (Allaah).”
[Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, amesema ni Hadiyth Hasan. Na katika baadhi ya mapokezi ni Hadiyth Hasan Swahiyh, na hii ni lafdhi ya Abuu Daawuwd]
Rejea Suwrah Nuwh (11:41), Al-Muuminuwn (23:28-28).
[7] Washirikina Kumsingizia Allaah Ana Wana:
Rejea An-Nisaa (4:191), Al-Maaidah (5:17), At-Tawbah (9:30), Asw-Swaaffaat (37:149) (37:158).
[8] Wamemzulia Allaah (سبحانه وتعالى) Ana Wana Wa Kike:
Rejea Asw-Swaaffaat: (37:149), Al-Israa (17:40), An-Nahl (57-59).
[9] Wao Wenyewe Wanawachukia Wana Wa Kike Lakini Wanawahusisha Na Allaah (عزّ وجلّ): Rejea An-Nahl: (16:57-59), Asw-Swaaffaat (37:149) (37:158).
[10] Washirikina Kumsingizia Allaah Ana Wana Na Kwamba Ni Wana Wa Kike:
Rejea Suwrah hii Az-Zukhruf (43:15) hadi Aayah hii ya (19), na faida zake.
Rejea pia An-Nisaa (4:191), Al-Maaidah (5:17), At-Tawbah (9:30), Asw-Swaaffaat (37:149) (37:158). Al-Israa (17:40), An-Nahl (57-59).
[11] Kufuata Mababa Na Mababu Japokuwa Hawakuwa Na Ilimu Na Walikuwa Wapotofu:
Aayah hii na ifuatayo inataja ujahili wa watu kufuata kibubusa upotofu wa baba na babu zao, japokuwa hawakuwa na ilimu.
Rejea pia Aayah zifuatazo zinazothibitisha hayo pia:
Al-Baqarah (2:170), Al-Maaidah (5:104), Al-A’raaf (7:28), (7:65-71), Yuwnus (10:75-78), Al-Anbiyaa (21:52-53), Ash-Shu’araa (26:69-76), Luqmaan (31:21).
Hali hiyo ni sawa na hali ya baadhi ya watu wa ummah huu wanaofuata mambo yasiyokuwemo katika Dini, bali ni vile kufuata yale ya shirki na bid’ah yaliyokuwa yakizoeleka kutendwa na watu wao waliotangulia.
[12] Mtu Mtukufu Na Miji Miwili:
Washirikina walidai kwa nini Qur-aan isiteremshwe kwa mtu mtukufu kama Waliyd Bin Mughiyrah au Mas’uwd bin ‘Amru Ath-Thaqafiyy, au ‘Utbah bin Rabiy’ au Habiyb bin ‘Amru.
Miji miwili ni Makkah na Twaaif. [Tafsiyr Ibn Kathiyr, As-Sa’diy, Tafsiyr Al-Muyassar]
[13] Allaah (سبحانه وتعالى) Kutokuwapanulia Waja Wake Mali, Mapambo Na Starehe Za Dunia Kwa Ajili Ya Kutokuingia Katika Kufru Na Maasi:
Tafsiyr ya Aayah zifuatazo (33-35):
وَلَوْلَا أَن يَكُونَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً لَّجَعَلْنَا لِمَن يَكْفُرُ بِالرَّحْمَـٰنِ لِبُيُوتِهِمْ سُقُفًا مِّن فِضَّةٍ وَمَعَارِجَ عَلَيْهَا يَظْهَرُونَ﴿٣٣﴾
Na lau isingelikuwa watu watakuwa ummah mmoja (wa makafiri), Tungejaalia wanaomkufuru Ar-Rahmaan wana nyumba zao zenye dari za fedha na ngazi pia wanazozipandia.
Allaah (سبحانه وتعالى) Anakhabarisha kwamba dunia haiwi sawa na chochote Kwake, na kwamba kama si Upole na Huruma Yake kwa Waja Wake ambayo haitanguliwi na chochote, basi Angeikunjua dunia kwa wale waliokufuru, na Angejaalia ngazi za fedha wanazipanda.
وَلِبُيُوتِهِمْ أَبْوَابًا وَسُرُرًا عَلَيْهَا يَتَّكِئُونَ﴿٣٤﴾
Na kwenye nyumba zao milango na makochi (ya fedha) wanayoyaegemea.
Na Angewajaalia wao mapambo ya dunia kila aina, na Angewapa vile wanavyovitamani. Lakini kilichozuia ni Huruma Yake kwa Waja Wake kwa kuogopea watu wasije kuharakisha kuingia katika ukafiri na kufanya maasi kwa wingi kwa sababu ya kuipenda dunia.
وَزُخْرُفًا ۚ وَإِن كُلُّ ذَٰلِكَ لَمَّا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَالْآخِرَةُ عِندَ رَبِّكَ لِلْمُتَّقِينَ﴿٣٥﴾
Na mapambo ya dhahabu. Lakini hayo yote si chochote isipokuwa ni starehe ya uhai wa dunia. Na Aakhirah iliyo kwa Rabb wako ni kwa wenye taqwa.
Katika maelezo haya, kuna dalili ya kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Anawanyima Waja Wake baadhi ya mambo ya kidunia kwa kuwazuia kabisa au uzuiaji khaswa (vitu maalum), kwa ajili ya maslahi yao, na kwamba dunia haifanani mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) japo na ubawa wa mbu, na kwamba hivi vilivyotajwa vyote ni starehe ya kidunia tu yenye malengo yasiyotimia, yaliyotibuka na yenye kwisha. Ama Aakhirah mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) ni bora kwa wanaomcha Allaah, kwa kufuata Amri Zake na kujiepusha na Makatazo Yake, kwani Neema Zake zimetimia na kukamilika kila upande, na katika Jannah (Pepo) kuna yanayotamaniwa na nafsi na yenye kuburudisha macho, wataishi humo milele. Basi utofauti ulioje kati ya makazi haya mawili! [Tafsiyr As-Sa’diy]
[14] Shaytwaan Huwapotosha Watu Kisha Huwakanusha Na Kuwageuka!:
Rejea Ibraahiym (14:22) kwenye maelezo na rejea mbalimbali.
[15] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah/Makafiri Kushangilia Kauli Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Waliyoifahamu Ndivyo Sivyo:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
Na washirikina walipopiga mfano wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) mwana wa Maryam, walipomjadili Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumhoji kuwa Manaswara wanamuabudu, unawakuta watu wako wanainua sauti zao na kupiga kelele kwa furaha na kuterema. Napo ni pale Kauli ya Allaah (عزّ وجلّ) ilipoteremka:
إِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ حَصَبُ جَهَنَّمَ أَنتُمْ لَهَا وَارِدُونَ ﴿٩٨﴾
Hakika nyinyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah ni vichochezi vya moto wa Jahannam, nyinyi mtauingia. [Al-Anbiyaa (21:98)]
Bonyeza kiungo kifuatacho kwenye maelezo bayana na Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah.
Na washirikina wakasema: Tumeridhika kwa waabudiwa (masanamu) wetu wawe na cheo cha ‘Iysaa.” Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:
إِنَّ الَّذِينَ سَبَقَتْ لَهُم مِّنَّا الْحُسْنَىٰ أُولَـٰئِكَ عَنْهَا مُبْعَدُونَ ﴿١٠١﴾
Hakika wale ambao imewatangulia Al-Husnaa (furaha, Rehma) kutoka Kwetu, hao watabaidishwa nao (moto). [Al-Anbiyaa (21:101]
[Tafsiyr Al-Muyassar]
Basi yule anayetupwa motoni, miongoni mwa waabudiwa wa makafiri, ni yule aliyeridhika kuabudiwa na wao. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[16] Kuteremka Kwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Ni Katika Alama Kuu Za Qiyaamah.
Rejea Al-An’aam (6:158), An-Nisaa (4:159).
[17] Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Anakiri Kuwa Yeye Ni Mja Wa Allaah Na Wala Sio Mwana Au Mshirika Wa Allaah.
Rejea Suwrah Maryam (19:30-36), Al-Maaidah (5:17), (5:72-76), (5:116-118), An-Nisaa (4:171).
[18] Makundi Kukhitilafiana Kuhusu Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام):
Hapo makundi ya watu yakatafautiana kuhusu jambo la ‘Iysaa (عليه السّلام) na wakawa mapote. Kati yao kuna waliokubali kuwa yeye ni mja wa Allaah na ni Rasuli Wake. Na hiyo ndio kauli ya kweli. Na kati yao kuna wanaodai kuwa yeye ni mwana wa Allaah. Na kati yao kuna wanaosema kwamba yeye ni Allaah! Ametukuka Allaah (سبحانه وتعالى) kutukuka kukubwa na kutakasika na neno lao hilo. Basi maangamivu na adhabu kali Siku ya Qiyaamah ni yenye kuwapata wale waliomwelezea Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) kwa sifa ambazo sizo zile Allaah (سبحانه وتعالى) Alizomsifu nazo. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Rejea Suwrah Maryam (19:37).
[19] Maalik: Ni Malaika Mlinzi Wa Moto.
Kuamini Malaika wa Allaah (سبحانه وتعالى) ni katika nguzo mojawapo ya nguzo sita za imaan.
Na Malaika wa Allaah (سبحانه وتعالى) ni wengi mno wala haijulikani idadi yao isipokuwa na Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee, na wala hakuna faida kujua idadi yao, bali Muislamu amewajibika kuamini kuwepo kwao tu. Na kauli za Salaf kuhusu wingi wao ni kama zifuatavyo:
Kauli za ‘Ulamaa kuhusu wingi wa Malaika:
Imaam Ibn Kathiyr (رحمه الله): Hakuna anayejua idadi yao au wingi wao isipokuwa Yeye Allaah (سبحانه وتعالى). [Tafsiyr Ibn Kathiyr (8/270)]
Imaam An-Nawawiy (رحمه الله): Kuhusu Malaika wanaozunguka Bayt Al-Ma’muwr, rejea Hadiyth iliyotajwa katika namba (xvi).
“Hii ni dalili kubwa kuhusu wingi wa Malaika (عليهم السّلام) na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi. [Sharh Muslim (2/225)]
Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah (رحمه الله): “Hakuna anayeweza kuhesabu idadi ya Malaika isipokuwa Allaah.” [Majmuw’ Al-Fataawaa (4/119)]
Malaika Wa Allaah Na Majukumu Yao:
Juu ya kuwa Malaika wa Allaah (سبحانه وتعالى) ni wengi mno, ila hatukujulishwa majina yao isipokuwa wafuatao kama ilivyothibiti katika Qur-aan na Sunnah:
(1) Jibriyl: Kuteremsha Wahyi. Rejea Ash-Shu’araa (26:193-194). Huyu ni Malaika mkuu kabisa kati ya Malaika wa Allaah (سبحانه وتعالى).
(2) Maalik: Mlinzi wa moto. Aayah ya Suwrah hii Az-Zukhruf (42:77).
(3) Miykaaiyl: Kuteremsha mvua. Rejea Al-Baqarah (2:98)
(4) Israafiyl: Kupuliza baragumu Siku ya Qiyaamah. Rejea Al-Baqarah (2:98) kwenye Hadiyth iliyothibiti kutajwa kwake.
(5) Munkar na Nakiyr:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " إِذَا قُبِرَ الْمَيِّتُ - أَوْ قَالَ أَحَدُكُمْ أَتَاهُ مَلَكَانِ أَسْوَدَانِ أَزْرَقَانِ يُقَالُ لأَحَدِهِمَا الْمُنْكَرُ وَالآخَرُ النَّكِيرُ فَيَقُولاَنِ مَا كُنْتَ تَقُولُ فِي هَذَا الرَّجُلِ فَيَقُولُ مَا كَانَ يَقُولُ هُوَ عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ . فَيَقُولاَنِ قَدْ كُنَّا نَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُولُ هَذَا . ثُمَّ يُفْسَحُ لَهُ فِي قَبْرِهِ سَبْعُونَ ذِرَاعًا فِي سَبْعِينَ ثُمَّ يُنَوَّرُ لَهُ فِيهِ ثُمَّ يُقَالُ لَهُ نَمْ . فَيَقُولُ أَرْجِعُ إِلَى أَهْلِي فَأُخْبِرُهُمْ فَيَقُولاَنِ نَمْ كَنَوْمَةِ الْعَرُوسِ الَّذِي لاَ يُوقِظُهُ إِلاَّ أَحَبُّ أَهْلِهِ إِلَيْهِ . حَتَّى يَبْعَثَهُ اللَّهُ مِنْ مَضْجَعِهِ ذَلِكَ . وَإِنْ كَانَ مُنَافِقًا قَالَ سَمِعْتُ النَّاسَ يَقُولُونَ فَقُلْتُ مِثْلَهُ لاَ أَدْرِي . فَيَقُولاَنِ قَدْ كُنَّا نَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُولُ ذَلِكَ . فَيُقَالُ لِلأَرْضِ الْتَئِمِي عَلَيْهِ . فَتَلْتَئِمُ عَلَيْهِ . فَتَخْتَلِفُ فِيهَا أَضْلاَعُهُ فَلاَ يَزَالُ فِيهَا مُعَذَّبًا حَتَّى يَبْعَثَهُ اللَّهُ مِنْ مَضْجَعِهِ ذَلِكَ " . وَفِي الْبَابِ عَنْ عَلِيٍّ وَزَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ وَابْنِ عَبَّاسٍ وَالْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ وَأَبِي أَيُّوبَ وَأَنَسٍ وَجَابِرٍ وَعَائِشَةَ وَأَبِي سَعِيدٍ كُلُّهُمْ رَوَوْا عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي عَذَابِ الْقَبْرِ . وقَالَ أَبو عِيسَى : حديثٌ حَسَنٌ غَرِيب وحسنه في "صحيح الجامع" رقم : (724).
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Anapozikwa maiti” au amesema: “Mmoja wenu anapozikwa, Malaika wawili weusi wenye macho kibuluu watamjia. Mmoja wao anaitwa Al-Munkar na mwingine anaitwa Al-Nakiyr, watamuuliza: Ulikuwa ukisema nini kuhusu mtu huyu? (Maiti) atasema yale aliyokuwa akisema (duniani): Yeye ni mja wa Allaah na Rasuli Wake na
أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ
Ninashuhudia kwamba hakuna mwabudiwa wa haki ila Allaah na kwamba Muhammad ni Mja Wake na Rasuli Wake.
Basi watasema: Hakika tulikuwa tunajua kuwa utasema haya. Kisha kaburi lake litapanuliwa hadi dhiraa sabini kwa sabini, kisha litajazwa nuru kwa ajili yake na ataambiwa: Lala! Atasema: Je naweza kurudi kwa ahli zangu na kuwajulisha? Watasema: Lala kama usingizi wa mwana arusi mpya hakuna anayemwamsha isipokuwa aliyekuwa ni mpendwa zaidi wa familia yake. (Atalala) mpaka Allaah Atakapomfufua kutoka mahali pake hapo pa kupumzika. Na ikiwa ni mnafiki atasema: Mimi nilikuwa nasikia watu wakisema hivyo nami nikasema sawa na wasemavyo, sijui! Watasema: Tulijua kwamba utasema hivyo! Kisha ardhi itaambiwa: Mbane! Basi ardhi itambana hadi mbavu zake zipishane, ataendelea kuadhibiwa hivyo hadi Allaah Atakampofufua kutoka mahali pake hapo pa kupumzika.” [At-Tirmidhiy, na Abuu ‘Iysaa amesema: Hadiyth Hasan Ghariyb, na ameipa daraja ya Hasan katika Swahiyh Al-Jaami’ (724)]
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Anapozikwa maiti” au amesema: “Mmoja wenu anapozikwa, Malaika wawili weusi na buluu watamjia. Mmoja wao anaitwa Al-Munkar na mwingine anaitwa Al-Nakiyr watasema: Mlikuwa mkisema nini kuhusu mtu huyu? Hivyo mtu huyo atasema yale aliyokuwa akisema (duniani): Yeye ni mja wa Allaah na Rasuli Wake na
أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ
Ninashuhudia kwamba hakuna mwabudiwa wa haki ila Allaah na kwamba Muhammad ni Mja Wake na Rasuli Wake.
Basi watasema: Hakika tulikuwa tunajua kuwa utasema haya. Kisha kaburi lake linapanuliwa hadi dhiraa sabini kwa sabini, kisha litamulikwa kwa ajili yake na ataambiwa : Lala! Atasema: Je naweza kurudi kwa ahli zangu na kuwajulisha? Watasema: Lala kama usingizi wa mwana arusi mpya hakuna anayemwamsha isipokuwa aliyekuwa ni mpendwa zaidi wa familia yake. (Atalala) mpaka Allaah Atamfufua kutoka mahali pale pa kupumzika. Na ikiwa ni mnafiki atasema: Mimi nilisika watu wakisema hivyo nami nikasema sawa na wasemavyo: Sijui! Watasema: Tulijua kwamba utasema hivyo! Kisha ardhi itaambiwa: Mbane! Basi ardhi itambana na itambana mbavu zake, ataendelea kuadhibiwa hivyo hadi Allaah Atakampofufua kutoka mahali pake hapo pa kupmzika.” [At-Tirmidhiy, na Abuu ‘Iysaa amesema: Hadiyth Hasan Ghariyb, na ameipa daraja ya Hasan katika Swahiyh Al-Jaami’ (724)]
(6) Haaruwt na Maaruwt: Malaika wawili ambao Allaah (عزّ وجلّ) Aliwateremsha ardhini kuwa ni fitnah (jaribio na mtihani) kwa watu ili wawafundishe sihri (uchawi). Rejea Al-Baqarah (2:102).
Na wafuatao ni Malaika wachache wengineo ambao hawakutajwa majina yao, ila yametajwa majukumu yao na kazi zao, nao ni kama ifuatavyo:
(7) Wenye kazi ya kutoa roho za watu. Huyu ametajwa kama Malakul-Mawt (Malaika anayetoa roho). Rejea Al-An’aam (6:61), As-Sajdah (32:11), .
(8) Wanaowahifadhi na kuwalinda wanaadam wasipatwe na madhara yoyote katika harakaat zao mchana na usiku. Rejea Al-An’aam (6:61), na wako wenye kuhifadhi wanaadam kwa zamu katika jukumu hili. Rejea Ar-Ra’d (13:10-11).
(9) Walinzi wa milango ya Jannah. Rejea Az-Zumar (39:73), Ar-Ra’d (13:23-24).
(10) Walinzi wa moto wa Jahannam.
Rejea Az-Zumar (39:71), Al-Muddath-thir (74:30-31) ambako imetajwa idadi yao kuwa ni kumi na tisa. Pia rejea Al-‘Alaq (96:18), Al-Mulk (67:8). Na Hadiyth ifuatayo imetaja idadi ya Malaika 4,900,000,000 (70,000 X 70,000) kuhusiana na moto wa Jahannam:
عن ابن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( يُؤتَى بِجَهَنَّمَ يَومَئذٍ لَهَا سَبْعُونَ ألفَ زِمَامٍ ، مَعَ كُلِّ زِمَامٍ سَبعُونَ ألْفَ مَلَكٍ يَجُرُّونَهَا )) رواه مسلم .
Amesimulia Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Siku hiyo ya Qiyaamah Jahannam italetwa ikiwa na hatamu elfu sabiini pamoja na kila hatamu kutakuwa na Malaika elfu sabiini wanaoikokota." [Muslim]
(11) Wenye kuhifadhi na kuandika mema na shari wanazotenda wanaadam. Rejea Suwrah hii Az-Zukhruf (43:80), Al-An’aam (6:61), Qaaf (50:17-18), Al-Infitwaar (82:11).
(12) Wenye kubeba ‘Arsh ya Allaah. Rejea Ghaafir (7:7), Al-Haaqqah (69:17).
(xiii) Wenye kuandika majaaliwa ya mwanaadam pindi mimba inapofika miezi minne katika tumbo la mama kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم -وَهُوَ الصَّادِقُ الْمَصْدُوقُ: ((إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يُرْسَلُ إلَيْهِ الْمَلَكُ فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ، وَيُؤْمَرُ بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ، وَأَجَلِهِ، وَعَمَلِهِ، وَشَقِيٍّ أَمْ سَعِيدٍ؛ فَوَاَللَّهِ الَّذِي لَا إلَهَ غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُهَا. وَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ فَيَدْخُلُهَا)) رواه البخاري ومسلم
Amesimulia Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdillaah bin Mas‘uwd (رضي الله عنه): Ametusimulia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa: “Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho (yake). Na (Malaika huyo) anaamrishwa maneno manne; Kuandika rizki yake, ajali yake (umri atakaoishi duniani), amali zake, mtu muovu au mwema. Wa-Allaahi naapa kwa Yule Ambaye hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, hakika mmoja wenu huenda afanye amali za watu wa Jannah hadi ikawa baina yake na Jannah ni dhiraa na kile kilichoandikwa kikathibiti, akafanya amali ya watu wa motoni akaingia motoni. Na hakika mmoja wenu huenda afanye amali za watu wa motoni hadi ikawa baina yake na moto ni dhiraa na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti, akafanya amali ya watu wa Jannah akaingia Jannah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
(13) Wenye kuzunguka kutafuta vikao vya Waumini wanaomdhukuru Allaah kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
عن أبي هُرَيْرَة رضي اللهُ عنه، عن النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قال مَا اجتَمَعَ قَوْمٌ في بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللهِ يَتْلُونَ كِتَابَ اللهِ ويَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ، إلا نَزَلَتْ عليهمُ السَّكِينَةُ، وغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ، وحَفَّتهُمُ المَلائِكَةُ، وذَكَرَهُمُ اللهُ فيمَنْ عِنْدَه)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Hawajumuiki watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah wakisoma Kitabu cha Allaah na wakasomeshana baina yao ila watateremkiwa na utulivu na itawafunika rehma, na Malaika watawazunguka, na Allaah Atawataja kwa walio Naye. [Muslim]
Na pia:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((إِنَّ لِلَّهِ عَزَّ وَجَلَّ مَلَائِكَةً سَيَّارَةً فُضُلًا يَبْتَغُونَ مَجَالِسَ الذِّكْر، وَإِذَا وَجَدُوا مَجْلِسًا فِيهِ ذِكْرٌ قَعَدُوا مَعَهُمْ فَحَضَنَ بَعْضُهُمْ بَعْضًا بِأَجْنِحَتِهِمْ حَتَّى يَمْلَئُوا مَا بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ سَمَاءِ الدُّنْيَا، فَإِذَا تَفَرَّقُوا عَرَجُوا أَوْ صَعِدُوا إِلَى السَّمَاءِ، قَالَ : فَيَسْأَلُهُمْ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ وَهُوَ أَعْلَمُ: مِنْ أَيْنَ جِئْتُمْ؟ فَيَقُولُون:َ جِئْنَاكَ مِنْ عِنْدِ عِبَادٍ لَكَ فِي الْأَرْضِ يُسَبِّحُونَكَ وَيُكَبِّرُونَكَ وَيَحْمَدُونَكَ وَيُهَلِّلُونَكَ وَيَسْأَلُونَكَ، قَالَ: وَمَاذَا يَسْأَلُونِي؟ قَالُوا: يَسْأَلُونَكَ جَنَّتَكَ، قَالَ: وَهَلْ رَأَوْا جَنَّتِي؟ قَالُوا: لَا أَيْ رَبِّ، قَالَ: فَكَيْفَ لَوْ قَدْ رَأَوْا جَنَّتِي؟ قَالُوا: وَيَسْتَجِيرُونَكَ ، قَالَ: مِمَّ يَسْتَجِيرُونِي؟ قَالُوا: مِنْ نَارِكَ يَا رَبِّ، قَالَ: وَهَلْ رَأَوْا نَارِي؟ قَالُوا: لَا، قَالُوا: وَيَسْتَغْفِرُونَكَ، قَالَ: فَيَقُول:ُ قَدْ غَفَرْتُ لَهُمْ وَأَعْطَيْتُهُمْ مَا سَأَلُوا وَأَجَرْتُهُمْ مِمَّا اسْتَجَارُوا، قَالَ: فَيَقُولُونَ: رَبِّ فِيهِمْ فُلَانٌ عَبْدٌ خَطَّاءٌ إِنَّمَا مَرَّ فَجَلَسَ مَعَهُمْ، قَالَ: فَيَقُولُ قَدْ غَفَرْتُ لَهُمْ هُمْ الْقَوْمُ لَا يَشْقَى بِهِمْ جَلِيسُهُمْ)) البخاري , مسلم , الترمذي والنسائي
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah (عزّ وجلّ) Anao Malaika chungu nzima ambao wanakwenda huku na kule wakitafuta vikao vya kumdhukuru Allaah, na wanapopata kikao, wanakaa na watu hao huku wakikunja mbawa zao baina yao, na kuijaza sehemu ya baina yao na uwingu wa dunia. (Watu) wanapoondoka, (Malaika) hupanda mbinguni. Akasema (Nabiy): Hapo tena Allaah (عزّ وجلّ) Huwauliza ijapokuwa Anayajua yote: “Mnatoka wapi?” Wao hujibu: “Tunatoka kwa baadhi ya waja wako duniani, walikuwa wanakusabbih na kukabbir na kuhallil na kukuhimidi na wanakuomba fadhila Zako.” (Allaah) Husema: “Wananiomba nini?” (Malaika hujibu): “Wanakuomba Jannah Yako. (Allaah) Husema: “Wameiona Jannah Yangu?” Husema: “La, Ee Rabb”. (Allaah) Husema: “Ingekuwaje kama wangaliona Jannah Yangu!?” (Malaika) Husema: “Wanaomba himaya Yako”. (Allaah) Husema: “Wanataka kuhamiwa kutokana na nini Kwangu?” (Malaika) Husema: “Kutokana na Moto Wako ee Rabb”. (Allaah) Husema: “Je, wameuona Moto Wangu?” Husema: “La.” (Allaah) Husema: “Je, ingekuwaje kama wangeuona Moto Wangu!?” Husema: “Wanaomba maghfirah Yako”. (Allaah) Husema: “Nimewaghufuria na Nimewapa himaya ya yale wanayotaka wahamiwe.” (Malaika) husema: “Ee Rabb! Miongoni mwao yumo fulani, mja wako muovu ambaye alikuwa akipita tu na akakaa nao.” (Allaah) Husema: “Nimewaghufuria wote (pamoja naye), hao ni watu ambao akaaye nao hataadhibiwa.” [Al-Bukhaariy, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]
(14) Walio pamoja na Waumini waliohifadhi Qur-aan wanaojifunza Qur-aan:
عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((الْمَاهِرُ بِالْقُرْآنِ مَعَ السَّفَرَةِ الْكِرَامِ الْبَرَرَةِ، وَالَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَيَتَتَعْتَعُ فِيهِ، وَهُوَ عَلَيْهِ شَاقٌّ لَهُ أَجْرَانِ)) البخاري ومسلم
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Yule aliyekuwa hodari wa kusoma Qur-aan atakuwa pamoja na Malaika Waandishi wa Allaah watukufu watiifu, na yule ambaye anaisoma Qur-aan kwa mashaka na huku anajitahidi kwa kudodosa atapata ujira mara mbili.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Tafsiyr (65) na Muslim] Rejea ‘Abasa (80:15-16).
(15) Wanaosimamia milima:
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، أَخْبَرَنَا ابْنُ وَهْبٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي يُونُسُ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، قَالَ حَدَّثَنِي عُرْوَةُ، أَنَّ عَائِشَةَ ـ رضى الله عنها ـ زَوْجَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم حَدَّثَتْهُ أَنَّهَا قَالَتْ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم هَلْ أَتَى عَلَيْكَ يَوْمٌ كَانَ أَشَدَّ مِنْ يَوْمِ أُحُدٍ قَالَ " لَقَدْ لَقِيتُ مِنْ قَوْمِكِ مَا لَقِيتُ، وَكَانَ أَشَدُّ مَا لَقِيتُ مِنْهُمْ يَوْمَ الْعَقَبَةِ، إِذْ عَرَضْتُ نَفْسِي عَلَى ابْنِ عَبْدِ يَالِيلَ بْنِ عَبْدِ كُلاَلٍ، فَلَمْ يُجِبْنِي إِلَى مَا أَرَدْتُ، فَانْطَلَقْتُ وَأَنَا مَهْمُومٌ عَلَى وَجْهِي، فَلَمْ أَسْتَفِقْ إِلاَّ وَأَنَا بِقَرْنِ الثَّعَالِبِ، فَرَفَعْتُ رَأْسِي، فَإِذَا أَنَا بِسَحَابَةٍ قَدْ أَظَلَّتْنِي، فَنَظَرْتُ فَإِذَا فِيهَا جِبْرِيلُ فَنَادَانِي فَقَالَ إِنَّ اللَّهَ قَدْ سَمِعَ قَوْلَ قَوْمِكَ لَكَ وَمَا رَدُّوا عَلَيْكَ، وَقَدْ بَعَثَ إِلَيْكَ مَلَكَ الْجِبَالِ لِتَأْمُرَهُ بِمَا شِئْتَ فِيهِمْ، فَنَادَانِي مَلَكُ الْجِبَالِ، فَسَلَّمَ عَلَىَّ ثُمَّ قَالَ يَا مُحَمَّدُ، فَقَالَ ذَلِكَ فِيمَا شِئْتَ، إِنْ شِئْتَ أَنْ أُطْبِقَ عَلَيْهِمِ الأَخْشَبَيْنِ، فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بَلْ أَرْجُو أَنْ يُخْرِجَ اللَّهُ مِنْ أَصْلاَبِهِمْ مَنْ يَعْبُدُ اللَّهَ وَحْدَهُ لاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا ".
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها) Mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Nilimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hivi imekupitia siku iliyo ngumu zaidi ya siku ya Uhud? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Nimepata mateso niliyoyapata kutoka kwa jamaa zako, na mateso zaidi niliyoyapata kwao ni siku ya ‘Aqabah, pale nilipojipeleka mwenyewe kwa Ibn ‘Abd Yaaliyl ibn ‘Abd Kulaal. Hakunikubalia nilichokitaka. Nikaondoka sielewi niendako, sikuzinduka isipokuwa nilipokaribia Qarn Ath-Tha‘alib, nikainua kichwa changu nikaliona wingu limenifunika, nikaangalia nikamkuta humo Jibriyl, akaniita akasema: Hakika Allaah Ameisikia kauli ya watu wako kwako na jibu walilokupa, na Amekuletea Malaika wa milima ili umuamuru unachotaka katika adhabu kuwafikia jamaa zako. Akaniita Malaika wa milima, akanisalimia, kisha akasema: Ee Muhammad! Akasema: Ikiwa ni katika unachokitaka niwafunike kwa milima miwili. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Bali nataraji Allaah atawatoa migongoni mwao watakao mwabudu Allaah Peke Yake, hawamshirikishi na chochote.” [Al-Bukhaariy]
(16) Wanaozunguka Bayt Al-Ma’muwr kama ilivyothibiti katika Hadiyth ndefu ya safari ya muujiza; Al-Israa Wal-Mi’raaj pindi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipofika mbingu ya saba ambako alimuona huko Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) akapandishwa mpaka Bayt Al-Ma’muwr Akasema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
فَرُفِعَ لِيَ الْبَيْتُ الْمَعْمُورُ، فَسَأَلْتُ جِبْرِيلَ فَقَالَ هَذَا الْبَيْتُ الْمَعْمُورُ يُصَلِّي فِيهِ كُلَّ يَوْمٍ سَبْعُونَ أَلْفَ مَلَكٍ، إِذَا خَرَجُوا لَمْ يَعُودُوا إِلَيْهِ آخِرَ مَا عَلَيْهِمْ،
“Nikafika kwa Ibraahiym nikamsalimia naye akasema: Unakaribishwa ee katika kizazi changu na Nabii. Nikanyanyuliwa Baytul-Ma‘muwr. Nikamuuliza Jibriyl (عليه السّلام) kuhusu hiyo. Akanijibu: Hii ni Bayt Al-Ma’muwr. Kila siku humo wanaswali Malaika sabiini elfu, wakishatoka hawarudi tena.” [Al-Bukhaariy]
(17) Wanaowaombea Waumini maghfirah. Rejea Ghaafir (40:7), Ash-Shuwraa (42:5).
(18) Wanaowaswalia Waumini ambao wanamswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Rejea Al-Ahzaab (33:56).
(19) Wanaowaskiliza Waumini wanaposoma Qur-aan:
عن أُسَيْدَ بْنَ حُضَيْرٍ بَيْنَمَا هُوَ لَيْلَةً يَقْرَأُ فِي مِرْبَدِه، إِذْ جَالَتْ فَرَسُهُ، فَقَرَأَ ثُمَّ جَالَتْ أُخْرَى، فَقَرَأَ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا. قَالَ أُسَيْدٌ: "فَخَشِيتُ أَنْ تَطَأَ يَحْيَى فَقُمْتُ إِلَيْهَا فَإِذَا مِثْلُ الظُّلَّةِ فَوْقَ رَأْسِي فِيهَا أَمْثَالُ السُّرُجِ عَرَجَتْ فِي الْجَوِّ حَتَّى مَا أَرَاهَا". قَالَ: "فَغَدَوْتُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ بَيْنَمَا أَنَا الْبَارِحَةَ مِنْ جَوْفِ اللَّيْلِ أَقْرَأُ فِي مِرْبَدِي إِذْ جَالَتْ فَرَسِي". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ: "فَقَرَأْتُ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ: "فَقَرَأْتُ ثُمَّ جَالَتْ أَيْضًا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((اقْرَأْ ابْنَ حُضَيْرٍ)) قَالَ: "فَانْصَرَفْتُ وَكَانَ يَحْيَى قَرِيبًا مِنْهَا خَشِيتُ أَنْ تَطَأَهُ, فَرَأَيْتُ مِثْلَ الظُّلَّةِ فِيهَا أَمْثَالُ السُّرُجِ عَرَجَتْ فِي الْجَوِّ حَتَّى مَا أَرَاهَا". فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((تِلْكَ الْمَلَائِكَةُ كَانَتْ تَسْتَمِعُ لَكَ وَلَوْ قَرَأْتَ لَأَصْبَحَتْ يَرَاهَا النَّاسُ مَا تَسْتَتِرُ مِنْهُمْ))
Amesimulia Usayd bin Khudhwayr (رضي الله عنه) kwamba alipokuwa akisoma akiwa katika mirbad yake, farasi wake alishtuka. Akasoma, akashtuka tena, akasoma akashtuka tena. Akasema Usayd: Nikaogopa asije kumkanyaga Yahyaa (mwanawe). Nikainuka kumwendea (farasi) nikaona kitu kama kivuli juu ya kichwa changu kama kina kandili kikipanda mbinguni hadi kikapotea. Nikamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) asubuhi yake nikamwambia: Ee Rasuli wa Allaah, jana usiku nilipokuwa katika mirbad yangu nikisoma Qur-aan, farasi wangu alishtuka! Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ungeliendelea kusoma Ibn Khudhwayr.” Akasema: Nilisoma lakini alishtuka tena. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ungeliendelea kusoma Ibn Khudhwayr.” Akasema: Nilisoma lakini alishtuka tena. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Ungeliendelea kusoma Ibn Khudhwayr.” Akasema niliondoka kwani Yahyaa alikuwa karibu naye, nikakhofu asimkanyage. Nikaona kama kivuli kikiwa na taa kinapanda juu hadi kikapotea. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hao ni Malaika walikuwa wakikusikiliza, lau ungeliendelea kusoma hadi asubuhi, watu wangeliwaona wazi wazi bila pazia.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Mirbad ni makazi ya mifugo ya farasi au ngamia.
(20) Malaika sabiini walioteremsha Suwrah Al-An’aam (6):
Rejea utangulizi wa Suwrah Al-An’aam namba (6), Hadiyth iliyotajwa katika Fadhila za Suwrah hiyo tukufu.
(21) Malaika walioteremshwa kuwasaida Waumini katika vita:
Rejea Aal-‘Imraan (3:124-125), Al-Anfaal (8:9-12).
Na wengineo ila hao ndio tuliojaaliwa kuwataja.
Bonyeza kiungo kifuatacho pia kupata faida tele:
Malaika [288]
[20] Hoja Mojawapo Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwa Hana Mwana:
Tafsiyr:
Sema ee Rasuli Mtukufu kuwaambia wale waliosema kuwa Allaah Ana mtoto ilhali Yeye ni Mmoja Pekee, Mwenye kukusudiwa kwa haja zote, Ambaye Hakujifanyia mke wala mtoto, na wala Hakuwa mwenye kufanana na chochote kile.:
فَأَنَا أَوَّلُ الْعَابِدِينَ﴿٨١﴾
Basi mimi ningekuwa wa mwanzo katika waja (Wake).
Nitakuwa mimi wa mwanzo kumuabudia huyo mtoto, kwa sababu atakuwa ana sehemu ya baba yake, na mimi ndio wa kwanza katika viumbe katika swala la kufuata mambo Anayoyapenda Allaah. Lakini mimi (kutokana na haya) ni wa mwanzo katika wapingaji, na mkali wao kwa kupinga. Kwa hapo sasa, ndio ikatambulika kubatilika kwake, na hii ni hoja kubwa kwa wale wanaotambua hali za Rusuli wa Allaah, na kwamba ikishatambulika kwamba wao ndio waliokamilika katika viumbe, na kwamba kila jambo la kheri basi wao watakuwa ni wa mwanzo katika kulikamilisha, na kila jambo la shari basi wao watakuwa wa mwanzo kuliacha, kulipinga, na kujitenga nalo, na lau angekuwa Allaah Ana mtoto wa kweli, basi angekuwa Muhammad Bin ‘Abdillaah ambaye ni mbora wa Rusuli kuwa wa mwanzo kumuabudia, na wala asingemtangulia yeyote yule katika washirikina.
Na inawezekana maana ya Aayah kuwa ni:
Lau Allaah Angekuwa na mtoto, basi mimi ningekuwa wa mwanzo kumuabudia Allaah, na katika ibaada yangu kwa Allaah ni kuthibitisha Alichokithibitisha, na kukanusha Alichokikanusha. Na hii ni katika ibaada ya matendo ya kiitikadi, na italazimu kutokana na maelezo haya, lau yangekuwa maneno ya kweli, basi ningekuwa mtu wa mwanzo kuthibitisha. Ikafahamika kwa maelezo haya kubatilika kwa madai ya washirikina na kuharibika kwake kiakili na kinukuzi. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Ningelikuwa wa mwanzo wanaokanusha madai yenu na wa mwanzo kuamini kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Hana mwana. [Tafsiyr Atw-Twabariy]
Na Rejea Yuwnus (10:94) kwa faida ziyada.
[21] Allaah Ndiye Ilaah (Mwabudiwa Wa Haki) Mbinguni Na Ardhini.
Rejea Al-An’aam (6:3) kwenye maelezo bayana.
Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Ilaahi Mwenye kuabudiwa, na viumbe vyote vinatambua Uungu Wake, ni sawa vitake kwa khiyari, au visitake, na Uungu Wake huu pamoja na mapenzi ya viumbe Kwake, umetanda mbinguni na ardhini. Ama Mwenyewe (Allaah), Yeye Yupo juu ya ‘Arsh Yake, Yuko juu ya Viumbe Vyake, Yu Pekee kwa Utukufu Wake, na kwa Ukamilifu Wake, Ameweka madhubuti (kwa Hikma Yake) kila Alichokiumba, na kila Aliloliwekea sharia, basi sharia hiyo ni madhubuti. Hajaumba kitu isipokuwa kwa hikmah, na Haweki sharia kwa jambo lolote isipokuwa kwa Hikmah, na Hukmu Yake ya kiqadari, kisharia na kimalipo, imekusanya ndani yake hikmah. Na Allaah ni Mjuzi wa kila kitu, Anajua siri na yaliyojificha, na wala hakifichikani Kwake hata kiwe kidogo uzito wa punje ya mbegu kwenye ulimwengu wa juu au wa chini, wala ndogo yake au kubwa. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[22] Waabudiwa Wa Washirikina, Hawana Uwezo Wa Kumiliki Ash-Shafaa’ah (Uombezi)
Yaani: Kila anaemuomba asiekuwa Allaah katika Manabii na Malaika na wasiokuwa hao, (waombwa hawa) hawamiliki ash-shafaa’ah (uombezi), na wala hawaombi isipokuwa kwa Idhini ya Allaah, na hawamwombei shafaa’ah hiyo isipokuwa yule tu aliyeridhiwa na Allaah. Na kwa sababu hii ndio Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
إِلَّا مَن شَهِدَ بِالْحَقِّ
Isipokuwa yule aliyeshuhudia.
Yaani: Aliyetamka kwa ulimi wake, akakiri kwa moyo wake, na akawa anatambua alichokishuhudia (huyu ndiye aliyeridhiwa na Allaah). Isitoshe, inashartiwa ushuhuda wake huu uwe kwa haqq kwamba Allaah (عزّ وجلّ) Ni Mmoja Asiye na mshirika, na Rusuli Wake Amewatuma kwa watu na Risala, na waliyokuja nayo hayana shaka yoyote ndani yake katika misingi ya Dini na matawi yake, ukweli wake na sharia zake. Hawa ndio utakaowanufaisha uombezi wa watakaopewa idhini ya kuomba shafaa’ah (uombezi), na hawa ndio watakaookoka na Adhabu ya Allaah, ndio wenye kupata thawabu zake. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[23] Washirikina Waliamini Tawhiyd Ya Ar-Rubuwbiyyah Lakini Walikanusha Tawhiyd Ya Al-Uluwhiyyah:
Rejea Yuwnus (10:31), Al-‘Ankabuwt (29:61), Az-Zumar (39:38), na Suwrah hii Az-Zukhruf (43:9).
الدُّخان
044-Ad-Dukhaan
044-Ad-Dukhaan: Utangulizi Wa Suwrah [290]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
حم﴿١﴾
1. Haa Miym.[1]
وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ﴿٢﴾
2. Naapa kwa Kitabu (Qur-aan) kinachobainisha.[2]
إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ ۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ﴿٣﴾
3. Hakika Sisi Tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa.[3] Hakika Sisi daima Ni Wenye Kuonya.
فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ﴿٤﴾
4. Katika (usiku) huo hupambanuliwa kila jambo la hikmah.
أَمْرًا مِّنْ عِندِنَا ۚ إِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ﴿٥﴾
5. Ni amri kutoka Kwetu. Hakika Sisi ndio Wenye Kutuma (Rusuli).
رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿٦﴾
6. Ni Rehma kutoka kwa Rabb wako. Hakika Yeye Ndiye Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ﴿٧﴾
7. Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, mkiwa ni wenye yakini.
لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ﴿٨﴾
8. Hapana muabudiwa wa haki ila Yeye, Anahuisha na Anafisha. Ni Rabb wenu na Rabb wa baba zenu wa awali.
بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ يَلْعَبُونَ﴿٩﴾
9. Bali wao wamo katika shaka wanacheza.
فَارْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُّبِينٍ﴿١٠﴾
10. Basi ngojea siku mbingu zitakapoleta moshi bayana.[4]
يَغْشَى النَّاسَ ۖ هَـٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١١﴾
11. Utawafunika watu. Hii ni adhabu iumizayo.
رَّبَّنَا اكْشِفْ عَنَّا الْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ﴿١٢﴾
12. (Watasema): Rabb wetu! Tuondoshee adhabu! Hakika sisi ni wenye kuamini.
أَنَّىٰ لَهُمُ الذِّكْرَىٰ وَقَدْ جَاءَهُمْ رَسُولٌ مُّبِينٌ﴿١٣﴾
13. Vipi wao wataweza kukumbuka na hali amekwishawajia Rasuli mwenye kubainisha!
ثُمَّ تَوَلَّوْا عَنْهُ وَقَالُوا مُعَلَّمٌ مَّجْنُونٌ﴿١٤﴾
14. Kisha wakamkengeuka na wakasema: Amefundishwa na majnuni.
إِنَّا كَاشِفُو الْعَذَابِ قَلِيلًا ۚ إِنَّكُمْ عَائِدُونَ﴿١٥﴾
15. Hakika Sisi Tutaiondosha adhabu kidogo, lakini nyinyi hakika mtarudia vile vile.
يَوْمَ نَبْطِشُ الْبَطْشَةَ الْكُبْرَىٰ إِنَّا مُنتَقِمُونَ﴿١٦﴾
16. Siku Tutakayoshambulia mashambulio makubwa, hakika Sisi Ni Wenye Kulipiza.
وَلَقَدْ فَتَنَّا قَبْلَهُمْ قَوْمَ فِرْعَوْنَ وَجَاءَهُمْ رَسُولٌ كَرِيمٌ﴿١٧﴾
17. Na kwa yakini Tuliwatia mtihanini kabla yao watu wa Firawni, na aliwajia Rasuli mtukufu.
أَنْ أَدُّوا إِلَيَّ عِبَادَ اللَّـهِ ۖ إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ﴿١٨﴾
18. (Akiwaambia): Wakabidhini kwangu Waja wa Allaah, hakika mimi kwenu ni Rasuli mwaminifu.
وَأَن لَّا تَعْلُوا عَلَى اللَّـهِ ۖ إِنِّي آتِيكُم بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ﴿١٩﴾
19. Na msimfanyie jeuri Allaah, hakika mimi nakuleteeni dalili bayana.
وَإِنِّي عُذْتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُمْ أَن تَرْجُمُونِ﴿٢٠﴾
20. Na hakika mimi nimejikinga kwa Rabb wangu na Rabb wenu msije kunirajimu.
وَإِن لَّمْ تُؤْمِنُوا لِي فَاعْتَزِلُونِ﴿٢١﴾
21. Na ikiwa hamtoniamini, basi kaeni mbali nami.
فَدَعَا رَبَّهُ أَنَّ هَـٰؤُلَاءِ قَوْمٌ مُّجْرِمُونَ﴿٢٢﴾
22. Akamuomba Rabb wake akisema: Hawa watu ni wahalifu.
فَأَسْرِ بِعِبَادِي لَيْلًا إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ﴿٢٣﴾
23. (Allaah Akasema): Basi ondoka usiku na Waja Wangu, hakika nyinyi ni wenye kuandamwa.
وَاتْرُكِ الْبَحْرَ رَهْوًا ۖ إِنَّهُمْ جُندٌ مُّغْرَقُونَ﴿٢٤﴾
24. Na acha bahari ikiwa imetulia, hakika wao ni jeshi lenye kugharikishwa.
كَمْ تَرَكُوا مِن جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ﴿٢٥﴾
25. Mabustani mangapi wameacha na chemchemu.
وَزُرُوعٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ﴿٢٦﴾
26. Na mimea na makazi ya kifahari.
وَنَعْمَةٍ كَانُوا فِيهَا فَاكِهِينَ﴿٢٧﴾
27. Na neema walizokuwa wakizifurahia.
كَذَٰلِكَ ۖ وَأَوْرَثْنَاهَا قَوْمًا آخَرِينَ﴿٢٨﴾
28. Hivyo ndivyo ilivyo. Na Tukawarithisha watu wengineo.
فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ وَمَا كَانُوا مُنظَرِينَ﴿٢٩﴾
29. Na hazikuwalilia mbingu na ardhi[5] na hawakuwa wa kupewa muhula.
وَلَقَدْ نَجَّيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنَ الْعَذَابِ الْمُهِينِ﴿٣٠﴾
30. Na kwa yakini Tuliwaokoa wana wa Israaiyl kutokana na adhabu ya kudhalilisha.
مِن فِرْعَوْنَ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَالِيًا مِّنَ الْمُسْرِفِينَ﴿٣١﴾
31. Kutoka kwa Firawni. Hakika yeye alikuwa mwenye kibri miongoni mwa wenye kupindukia mipaka.
وَلَقَدِ اخْتَرْنَاهُمْ عَلَىٰ عِلْمٍ عَلَى الْعَالَمِينَ﴿٣٢﴾
32. Na kwa yakini Tuliwakhitari (wana wa Israaiyl) kwa ilimu kuliko walimwengu wowote.
وَآتَيْنَاهُم مِّنَ الْآيَاتِ مَا فِيهِ بَلَاءٌ مُّبِينٌ﴿٣٣﴾
33. Na Tukawapa katika Aayaat (Miujiza) yenye majaribio bayana ndani yake.[6]
إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ لَيَقُولُونَ﴿٣٤﴾
34. Hakika hawa (Maquraysh) bila shaka wanasema.
إِنْ هِيَ إِلَّا مَوْتَتُنَا الْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُنشَرِينَ﴿٣٥﴾
35. Haya si chochote isipokuwa ni mauti yetu ya awali, nasi hatutofufuliwa.
فَأْتُوا بِآبَائِنَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٣٦﴾
36. Basi tuleteeni mababu zetu mkiwa ni wakweli.
أَهُمْ خَيْرٌ أَمْ قَوْمُ تُبَّعٍ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ أَهْلَكْنَاهُمْ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا مُجْرِمِينَ﴿٣٧﴾
37. Je, kwani wao ni bora zaidi au kaumu ya Tubba’[7] na wale waliokuwa kabla yao! Tuliwaangamiza. Hakika wao walikuwa wahalifu.
وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَاعِبِينَ﴿٣٨﴾
38. Na Hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake kwa mchezo na upuuzi.
مَا خَلَقْنَاهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴿٣٩﴾
39. Hatukuumba viwili hivyo isipokuwa kwa haki, lakini wengi wao hawajui.
إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ مِيقَاتُهُمْ أَجْمَعِينَ﴿٤٠﴾
40. Hakika Siku ya hukumu ni wakati wao maalumu uliopangwa kwa wote.
يَوْمَ لَا يُغْنِي مَوْلًى عَن مَّوْلًى شَيْئًا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ﴿٤١﴾
41. Siku ambayo jamaa wa karibu hatomfaa jamaa yake wa karibu chochote, na wala wao hawatonusuriwa.
إِلَّا مَن رَّحِمَ اللَّـهُ ۚ إِنَّهُ هُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ﴿٤٢﴾
42. Isipokuwa yule Atakayerehemewa na Allaah. Hakika Yeye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu.
إِنَّ شَجَرَتَ الزَّقُّومِ﴿٤٣﴾
43. Hakika mti wa az-zaqquwm.[8]
طَعَامُ الْأَثِيمِ﴿٤٤﴾
44. Ni chakula cha mtendaji mno dhambi.
كَالْمُهْلِ يَغْلِي فِي الْبُطُونِ﴿٤٥﴾
45. Kama masazo ya zebaki nyeusi iliyoyeyushwa, inatokota matumboni.
كَغَلْيِ الْحَمِيمِ﴿٤٦﴾
46. Kama kutokota kwa maji yachemkayo.
خُذُوهُ فَاعْتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَاءِ الْجَحِيمِ﴿٤٧﴾
47. (Itaamrishwa): Mchukueni na msokomezeni katikati ya moto uwakao vikali mno.
ثُمَّ صُبُّوا فَوْقَ رَأْسِهِ مِنْ عَذَابِ الْحَمِيمِ﴿٤٨﴾
48. Kisha mwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yachemkayo.
ذُقْ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْكَرِيمُ﴿٤٩﴾
49. Onja! Si ndiye weye mwenye nguvu mheshimiwa![9]
إِنَّ هَـٰذَا مَا كُنتُم بِهِ تَمْتَرُونَ﴿٥٠﴾
50. Hakika haya ndiyo ambayo mlikuwa mkiyatilia shaka.
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٍ﴿٥١﴾
51. Hakika wenye taqwa watakuwa katika mahali pa amani.
فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ﴿٥٢﴾
52. Katika Jannaat (Pepo) na chemchemu.[10]
يَلْبَسُونَ مِن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَقَابِلِينَ﴿٥٣﴾
53. Watavaa hariri laini na hariri nzito nyororo wakiwa wamekabiliana.
كَذَٰلِكَ وَزَوَّجْنَاهُم بِحُورٍ عِينٍ﴿٥٤﴾
54. Hivyo ndivyo! Na Tutawaozesha hurulaini: wanawake weupe wazuri wa Jannah wenye macho makubwa ya kupendeza.
يَدْعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَاكِهَةٍ آمِنِينَ﴿٥٥﴾
55. Wataagiza humo kila aina ya matunda wakiwa katika amani.
لَا يَذُوقُونَ فِيهَا الْمَوْتَ إِلَّا الْمَوْتَةَ الْأُولَىٰ ۖ وَوَقَاهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ﴿٥٦﴾
56. Hawatoonja humo mauti isipokuwa mauti yale ya awali, na (Allaah) Atawakinga na adhabu ya moto uwakao vikali mno.
فَضْلًا مِّن رَّبِّكَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٥٧﴾
57. Ni fadhila kutoka kwa Rabb wako. Huko ndiko kufuzu adhimu.
فَإِنَّمَا يَسَّرْنَاهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ﴿٥٨﴾
58. Basi hakika Tumeiwepesisha (Qur-aan) kwa ulimi wako ili wapate kukumbuka.[11]
فَارْتَقِبْ إِنَّهُم مُّرْتَقِبُونَ﴿٥٩﴾
59. Basi ngojea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), hakika wao pia ni wenye kungojea.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Qur-aan Na Kuteremshwa Kwake Laylatul-Qadr:
Tafsiyr Aayah (2) hadi (4):
Ameapa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Qur-aan iliyowazi kimatamshi na kimaana. Sisi Tumeiteremsha katika Usiku wa Cheo uliobarikiwa wenye kheri nyingi, nao unapatikana katika mwezi wa Ramadhwaan. Sisi ni Wenye kuonya watu kwa kile kinachowanufaisha na kuwadhuru, nako ni kule kupeleka Rusuli na kuteremsha Vitabu, ili hoja ya Allaah iwasimamie Waja Wake. Katika usiku huo, linaamuliwa na kupambanuliwa kutoka kwenye Lawh Al-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa) na kuletewa waandishi kati ya Malaika, kila jambo lililokadiriwa la muda wa kuishi na riziki katika mwaka huo, na mambo mengine yatakayokuwa na kukadiriwa na Allaah (سبحانه وتعالى) mpaka mwisho wa mwaka, hayabadilishwi wala hayageuzwi. Mambo haya yaliyopangwa kimadhubuti ni amri inayotoka Kwetu, kwani yote yanayokuwa na Anayokadiria Allaah (سبحانه وتعالى) na Wahy Anaouleta, vyote hivyo vinatokana na Amri Yake na Idhini Yake na Ujuzi Wake. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[3] Usiku Uliobarikiwa (Laylatul-Qadr):
Rejea Suwrah Al-Qadr (97) kwenye viungo vyenye faida kuhusu Usiku huu mtukufu na fadhila zake.
[4] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Kuanzia Aayah hii ya (10) hadi (15), kuna sababu ya kuteremshwa.
Bonyeza kiungo kifuatacho:
[5] Mbingu Na Ardhi Huwalilia Waumini:
Tafsiyr za ‘Ulamaa:
Yaani: Baada ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwaangamiza, mbingu na ardhi hazikuwalilia wala kuhuzunika kwa sababu ya kuangamia kwao, bali kila kimoja kilifurahi na kupeana bishara, mpaka mbingu na ardhi, kwa sababu hawakuacha athari isipokuwa itayozifanya nyuso zao kuwa nyeusi, na kuwajibisha wao kupata laana na kukasirikiwa na Allaah Rabb wa viumbe wote. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Amesema Ibn Jariyr: Kutoka kwa Sa’iyd Bin Jubayr amesema: Mtu mmoja alimjia Ibn ‘Abbaas akasema: Ee Baba yake ‘Abbaas, hivi waonaje Kauli ya Allaah:
فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ وَمَا كَانُوا مُنظَرِينَ﴿٢٩﴾
Na hazikuwalilia mbingu na ardhi, na hawakuwa wa kupewa muhula.
Je mbingu na ardhi zinaweza kumlilia mtu yeyote yule? Akasema: Naam, kwani hakuna kiumbe yeyote yule isipokuwa ana mlango wake mbinguni. Rizki yake inateremka hapo na matendo yake pia yanapanda kupitia hapo. Anapofariki Muumini na ukafungwa mlango wake mbinguni ambao amali zake zilikuwa zinapanda kupitia hapo, basi mbingu humlilia, na sehemu anayoswalia hapa ardhini na kumdhukuru Allaah ikimkosa, basi ardhi nayo inamlilia kwa kumkosa aliyekuwa akiswalia pale. Na kwa hakika watu wa Firawni hawakuwa na athari njema katika ardhi, wala haikuwahi kupanda kheri yeyote mbinguni kutoka kwao. Ndio maana mbingu na ardhi hazikuwalilia. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Fatwa ya Imaam Ibn Baaz (رحمه الله):
Swali aliloulizwa kuhusu maana ya Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ وَمَا كَانُوا مُنظَرِينَ﴿٢٩﴾
Na hazikuwalilia mbingu na ardhi, na hawakuwa wa kupewa muhula.
Akajibu: “‘Ulamaa wametaja katika hili kwamba, wao hawakuwa na matendo mema, na mbingu na ardhi huwa zinalia zikikosa matendo mema kutoka kwa watu wa kheri.
Ama kwa hawa, hakuna kheri kwao na wala hakuna matendo mema yanayopanda mbinguni, kwa sababu hiyo, haziwalilii mbingu wala ardhi kwa kutokuwa na matendo mema. Na hivyo basi hawakuachiwa muda bali waliangamizwa muda uleule. Tunamuomba Allaah Al-‘Aafiyah.” Al-Mawqi' Ar-Rasmiy li-Samaahat Ash-Shaykh Al-Imaam Ibn Baaz]
[6] Miujiza Bayana Ya Majaribio:
Tafsiyr za ‘Ulamaa:
وَآتَيْنَاهُم
Na Tukawapa.
Yaani: Bani Israaiyl. Na
مِّنَ الْآيَاتِ مَا فِيهِ بَلَاءٌ مُّبِينٌ﴿٣٣﴾
Katika Aayaat (Miujiza) yenye majaribio bayana ndani yake.
Yaani: Miujiza ya wazi, ihsaani nyingi za wazi kutoka Kwetu juu yao, na hoja juu yao kuhusiana na usahihi wa aliyowaletea Nabiy wao Muwsaa (عليه السّلام). [Tafsiyr As-Sa’diy]
Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَآتَيْنَاهُم مِّنَ الْآيَاتِ
Na Tukawapa katika Aayaat (Miujiza).
Hoja za wazi na mambo yanayokwenda kinyume na mazoea.
مَا فِيهِ بَلَاءٌ مُّبِينٌ﴿٣٣﴾
Yenye majaribio bayana ndani yake.
Ni mtihani wa wazi kwa aliyeongoka kwao. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[7] Tubba’:
Ni Mfalme katika wafalme wa Yemen na alikuwa mshirikina kisha akasilimu.
Amesimulia Sahl bin Sa’d (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Msimtukane Tubba’ah kwani amesilimu.” [Ahmad katika Musnad yake, na ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw- Swahiyhah (2423)]
[8] Mti wa Zaqquwm:
Mti mchungu mno motoni wa karaha ambao utakuwa chakula cha wakaazi wake humo. Rejea Al-Israa (17:60), Asw-Swaaffaat (37-63-68).
Adhabu Na Chakula Cha Watu Wa Motoni: Rejea An-Nabaa (78:21) kwenye fafanuzi na rejea nyenginezo.
[9] Kafiri Aliyejifanya Mheshimiwa Mwenye Nguvu Anafanyiwa Kejeli Motoni:
Tafsiyr za ‘Ulamaa:
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
ذُقْ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْكَرِيمُ﴿٤٩﴾
“Onja! Si ndiye weye mwenye nguvu mheshimiwa!”
Na ataambiwa yule ataeadhibiwa: Onja adhabu hii iumizayo, na malipo mabaya, kwa madai yako kwamba wewe ni mtukufu, unaweza kujizuia na adhabu ya Allaah, na wewe ni muheshimiwa mbele ya Allaah, kwamba Hatokulipa adhabu. Sasa leo hii ndio imebainika kwako kwamba wewe ni dhalili usiye na chembe ya thamani. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
ذُقْ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْكَرِيمُ﴿٤٩﴾
“Onja! Si ndiye weye mwenye nguvu mheshimiwa!”
Mwambieni maneno hayo, kwa sura ya kumlaumu na kumcheza shere. Na Adhw-Dhwahaak amesema kutoka kwa Ibn ‘Abbaas: Sio mtukufu wala sio mheshimiwa. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[11] Qur-aan Imefanywa Nyepesi Kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Na Waumini:
Tafsiyr za ‘Ulamaa:
Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
فَإِنَّمَا يَسَّرْنَاهُ بِلِسَانِكَ
Basi hakika Tumeiwepesisha (Qur-aan) kwa ulimi wako.
Hakika Tumeifanya Qur-aan kuwa nyepesi, ambayo Tumeiteremsha ikiwa nyepesi, iko wazi, kwa lugha yako ambayo ndio (lugha) fasaha zaidi ya zote, ni nzuri na iko juu zaidi.
لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ﴿٥٨﴾
Ili wapate kukumbuka.
Watafahamu na kuelewa, kisha baada ya uwazi na ubainifu huu, wapo wengine walikufuru kupinga na wengine kukaidi. Ndio Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema kumliwaza Rasuli Wake na kumuahidi msaada na nusra, na kuwaahidi adhabu kali na kuangamia kwa watakao mkadhibisha Allaah. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Rejea pia Al-Qamar (54:17).
الْجاثِيَة
045-Al-Jaathiyah
045-Al-Jaathiyah: Utangulizi Wa Suwrah [293]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
حم﴿١﴾
1. Haa Miym.[1]
تَنزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ﴿٢﴾
2. Ni uteremsho wa Kitabu kutoka kwa Allaah Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
إِنَّ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّلْمُؤْمِنِينَ﴿٣﴾
3. Hakika katika mbingu na ardhi bila shaka kuna Aayaat (Ishara, Dalili) kwa Waumini.
وَفِي خَلْقِكُمْ وَمَا يَبُثُّ مِن دَابَّةٍ آيَاتٌ لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ﴿٤﴾
4. Na katika kuumbwa kwenu, na Anaoyatawanya kati ya viumbe vinavyotembea ni Aayaat (Ishara, Dalili) kwa watu wenye yakini.
وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ السَّمَاءِ مِن رِّزْقٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ آيَاتٌ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ﴿٥﴾
5. Na mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana, na Anayoteremsha Allaah kutoka mbinguni katika mvua, Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake[2], na kugeukageuka upepo (wa rehma) ni Aayaat (Ishara, Dalili) kwa watu wanaotia akilini.
تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ ۖ فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَ اللَّـهِ وَآيَاتِهِ يُؤْمِنُونَ﴿٦﴾
6. Hizi ni Aayaat za Allaah Tunakusomea kwa haki. Basi kauli gani baada ya Allaah na Aayaat Zake wataziamini?
وَيْلٌ لِّكُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ﴿٧﴾
7. Ole kwa kila mzushi muongo, mtendaji mno dhambi.
يَسْمَعُ آيَاتِ اللَّـهِ تُتْلَىٰ عَلَيْهِ ثُمَّ يُصِرُّ مُسْتَكْبِرًا كَأَن لَّمْ يَسْمَعْهَا ۖ فَبَشِّرْهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٨﴾
8. Anazisikia Aayaat za Allaah akisomewa, kisha anang’ang’ana kuwa mwenye kutakabari kama kwamba hakuzisikia. Basi mbashirie adhabu iumizayo.
وَإِذَا عَلِمَ مِنْ آيَاتِنَا شَيْئًا اتَّخَذَهَا هُزُوًا ۚ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ﴿٩﴾
9. Na anapojua chochote katika Aayaat Zetu huzichukulia mzaha. Hao watapata adhabu ya kudhalilisha.
مِّن وَرَائِهِمْ جَهَنَّمُ ۖ وَلَا يُغْنِي عَنْهُم مَّا كَسَبُوا شَيْئًا وَلَا مَا اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ أَوْلِيَاءَ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ﴿١٠﴾
10. Nyuma yao iko Jahannam, na wala hayatowafaa kitu yale waliyoyachuma na wala wale waliowafanya walinzi badala ya Allaah, na watapata adhabu kuu.
هَـٰذَا هُدًى ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ لَهُمْ عَذَابٌ مِّن رِّجْزٍ أَلِيمٌ﴿١١﴾
11. Hii (Qur-aan) ni mwongozo. Na wale waliokanusha Aayaat (na Ishara, Dalili) za Rabb wao watapata adhabu ya kufadhaika iumizayo.
اللَّـهُ الَّذِي سَخَّرَ لَكُمُ الْبَحْرَ لِتَجْرِيَ الْفُلْكُ فِيهِ بِأَمْرِهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴿١٢﴾
12. Allaah Ambaye Amekutiishieni bahari ili zipite merikebu humo kwa Amri Yake, na ili mtafute katika Fadhila Zake, na ili mpate kumshukuru.[3]
وَسَخَّرَ لَكُم مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا مِّنْهُ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴿١٣﴾
13. Na Amekutiishieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini vyote, ni ihsani itokaye Kwake. Hakika katika hayo bila shaka kuna Aayaat (Dalili, Ishara) kwa watu wanaotafakari.
قُل لِّلَّذِينَ آمَنُوا يَغْفِرُوا لِلَّذِينَ لَا يَرْجُونَ أَيَّامَ اللَّـهِ لِيَجْزِيَ قَوْمًا بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿١٤﴾
14 Waambie (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wale walioamini wawasamehe wale wasiozitaraji Siku za Allaah ili Awalipe watu kutokana na yale waliyokuwa wakiyachuma.[4]
مَنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَسَاءَ فَعَلَيْهَا ۖ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ﴿١٥﴾
15. Yeyote atendaye jema, basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na mwenye kufanya uovu, basi ni hasara kwake, kisha kwa Rabb wenu mtarejeshwa.
وَلَقَدْ آتَيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ﴿١٦﴾
16. Na kwa yakini Tuliwapa wana wa Israaiyl Kitabu na hikma na unabii, na Tukawaruzuku katika vizuri, na Tukawafadhilisha juu ya walimwengu.
وَآتَيْنَاهُم بَيِّنَاتٍ مِّنَ الْأَمْرِ ۖ فَمَا اخْتَلَفُوا إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ﴿١٧﴾
17. Na Tukawapa hoja bayana ya mambo (ya Dini). Basi hawakukhitilafiana isipokuwa baada ya kuwajia ilimu kwa kufanyiana uadui na husuda baina yao. Hakika Rabb wako Atahukumu baina yao Siku ya Qiyaamah katika yale waliyokuwa wakikhitilafiana.
ثُمَّ جَعَلْنَاكَ عَلَىٰ شَرِيعَةٍ مِّنَ الْأَمْرِ فَاتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ﴿١٨﴾
18. Kisha Tukakuwekea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Sharia ya mambo, basi ifuate, na wala usifuate hawaa za wale wasiojua.
إِنَّهُمْ لَن يُغْنُوا عَنكَ مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۚ وَإِنَّ الظَّالِمِينَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۖ وَاللَّـهُ وَلِيُّ الْمُتَّقِينَ﴿١٩﴾
19. Hakika wao hawatokufaa chochote mbele ya Allaah. Na hakika madhalimu ni marafiki wanaoshirikiana wao kwa wao. Na Allaah Ni Rafiki Mlinzi wa wenye taqwa.
هَـٰذَا بَصَائِرُ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ﴿٢٠﴾
20. Hii (Qur-aan) ni busara na kifumbuzi macho kwa watu, na ni mwongozo na rehma kwa watu wenye yakini.
أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ اجْتَرَحُوا السَّيِّئَاتِ أَن نَّجْعَلَهُمْ كَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَوَاءً مَّحْيَاهُمْ وَمَمَاتُهُمْ ۚ سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ﴿٢١﴾
21. Je, wanadhania wale waliochuma maovu kwamba Tutawafanya sawa na wale walioamini na wakatenda mema, sawasawa uhai wao na kufa kwao?[5] Uovu ulioje wa wanavyohukumu!
وَخَلَقَ اللَّـهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ وَلِتُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿٢٢﴾
22. Na Allaah Ameumba mbingu na ardhi kwa haki, na ili ilipwe kila nafsi kwa yale iliyoyachuma, nao hawatodhulumiwa.
أَفَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهُ وَأَضَلَّهُ اللَّـهُ عَلَىٰ عِلْمٍ وَخَتَمَ عَلَىٰ سَمْعِهِ وَقَلْبِهِ وَجَعَلَ عَلَىٰ بَصَرِهِ غِشَاوَةً فَمَن يَهْدِيهِ مِن بَعْدِ اللَّـهِ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿٢٣﴾
23. Je, umemuona yule aliyejichukulia hawaa zake kuwa ndio mwabudiwa wake[6], na Allaah Akampotoa baada ya kufikiwa na ilimu na hoja, na Akapiga mhuri juu ya masikio yake na moyo wake, na Akaweka kifuniko juu ya macho yake? Basi nani atamuongoa baada ya Allaah? Je, basi hamkumbuki?
وَقَالُوا مَا هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا يُهْلِكُنَا إِلَّا الدَّهْرُ ۚ وَمَا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِنْ هُمْ إِلَّا يَظُنُّونَ﴿٢٤﴾
24. Na wakasema: Huu si chochote isipokuwa ni uhai wetu wa dunia, tunakufa na tunahuika, na hakuna cha kutuangamiza isipokuwa zama tu. Na wala hawana kwayo ujuzi wowote, ila wao wanadhania tu.[7]
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ مَّا كَانَ حُجَّتَهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا ائْتُوا بِآبَائِنَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٢٥﴾
25. Na wanaposomewa Aayaat Zetu bayana haikuwa hoja yao isipokuwa kusema: Tuleteeni mababa zetu mkiwa nyinyi ni wakweli.
قُلِ اللَّـهُ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يَجْمَعُكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٢٦﴾
26. Sema: Allaah Anakuhuisheni, kisha Atakufisheni, kisha Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah isiyo na shaka ndani yake, lakini watu wengi hawajui.
وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يَوْمَئِذٍ يَخْسَرُ الْمُبْطِلُونَ﴿٢٧﴾
27. Na ni wa Allaah Pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Na Siku itakayosimama Saa, watakhasirika Siku hiyo wabatilifu.
وَتَرَىٰ كُلَّ أُمَّةٍ جَاثِيَةً ۚ كُلُّ أُمَّةٍ تُدْعَىٰ إِلَىٰ كِتَابِهَا الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٢٨﴾
28. Na utaona kila ummah umepiga magoti kwa unyenyekevu na khofu [8]. Kila ummah utaitwa kwenye kitabu chake (cha matendo): Leo mtalipwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
هَـٰذَا كِتَابُنَا يَنطِقُ عَلَيْكُم بِالْحَقِّ ۚ إِنَّا كُنَّا نَسْتَنسِخُ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٢٩﴾
29. Hiki ni kitabu Chetu, kinatamka (kushuhudia) juu yenu kwa haki. Hakika Sisi Tulikuwa Tunaamuru yaandikwe yale mliyokuwa mkiyatenda.
فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُدْخِلُهُمْ رَبُّهُمْ فِي رَحْمَتِهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْمُبِينُ﴿٣٠﴾
30. Basi wale walioamini na wakatenda mema, Rabb wao Atawaingiza katika Rehma Yake. Huko ndiko kufuzu kulio wazi.
وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا أَفَلَمْ تَكُنْ آيَاتِي تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فَاسْتَكْبَرْتُمْ وَكُنتُمْ قَوْمًا مُّجْرِمِينَ﴿٣١﴾
31. Ama wale waliokufuru (wataambiwa): Je, kwani hazikuwa Aayaat Zangu zikisomwa kwenu, mkatakabari na mkawa watu wahalifu?
وَإِذَا قِيلَ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَالسَّاعَةُ لَا رَيْبَ فِيهَا قُلْتُم مَّا نَدْرِي مَا السَّاعَةُ إِن نَّظُنُّ إِلَّا ظَنًّا وَمَا نَحْنُ بِمُسْتَيْقِنِينَ﴿٣٢﴾
32. Na inaposemwa: Hakika Ahadi ya Allaah ni haki, na Saa haina shaka ndani yake mlisema: Hatujui Saa ni nini! Hatudhanii isipokuwa ni dhana tupu, nasi sio wenye kuyakinika kikweli.
وَبَدَا لَهُمْ سَيِّئَاتُ مَا عَمِلُوا وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٣٣﴾
33. Na yatawafichukia maovu waliyoyatenda, na yatawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.
وَقِيلَ الْيَوْمَ نَنسَاكُمْ كَمَا نَسِيتُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا وَمَأْوَاكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن نَّاصِرِينَ﴿٣٤﴾
34. Na itasemwa: Leo Tunakusahauni kama mlivyosahau kukutana na Siku yenu hii, na makazi yenu ni motoni, na wala hamna yeyote mwenye kunusuru.
ذَٰلِكُم بِأَنَّكُمُ اتَّخَذْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ هُزُوًا وَغَرَّتْكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۚ فَالْيَوْمَ لَا يُخْرَجُونَ مِنْهَا وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ﴿٣٥﴾
35. Hivyo ni kwa sababu nyinyi mlizichukulia mzaha Aayaat za Allaah, na ukakudanganyeni uhai wa dunia. Basi leo hawatotolewa humo, na wala hawataachiliwa nafasi ya kujitetea (kwa Allaah).
فَلِلَّـهِ الْحَمْدُ رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَرَبِّ الْأَرْضِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿٣٦﴾
36. Basi AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah) Rabb wa mbingu na Rabb wa ardhi, Rabb wa walimwengu.
وَلَهُ الْكِبْرِيَاءُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٣٧﴾
37. Na Ukubwa, Uadhama, Ujalali ni Wake Pekee mbinguni na ardhini. Naye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.[9]
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Mfano Wa Ardhi Iliyokufa (Kame), Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akaihuisha Kwa Mvua, Ni Mfano Wa Kuwahuisha Watu Kutoka Makaburini Mwao Siku Ya Qiyaamah:
Rejea Ar-Ruwm (30:50) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali.
[3] Miongoni Mwa Neema Za Allaah (سبحانه وتعالى) Kwa Viumbe Vyake:
Aayah hii (12) na inayofuatia (13) zinataja baadhi ya Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) kwa viumbe ardhini. Rejea Suwrah Ibraahiym (14:34) kwenye maelezo bayana na uchambuzi wa Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) na rejea mbalimbali na kwamba Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) haiwezekani kamwe kuziorodhesha hesabuni!
[4] Maana Ya Siku Za Allaah:
Rejea Ibraahiym (14:5).
Allaah (عزّ وجلّ) Anawaamrisha waja Wake Waumini kuwa na khulqa (tabia) njema na wawe na subira juu ya maudhi ya washirikina wasiotaraji siku za Allaah, yaani: hawataraji thawabu zake na wala hawaogopi adhabu Zake kwa watakaomuasi. Kwani Allaah (سبحانه وتعالى) Atawalipa kila watu yale waliyokuwa wakiyachuma. Basi nyinyi enyi Waumini, Atawalipa thawabu tele kwa imaan zenu na kusamehe kwenu na subra zenu. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[5] Haiwezekani Makafiri Kulingana Sawa Na Waumini Katika Imaan Zao, Uhai Wao Duniani Na Aakhirah:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anakanusha madai ya makafiri kuwa wao wanalingana na Waumini. Anabainisha hapa kuwa makafiri hawawezi kulingana sawa na Waumini kwa sababu ya ‘Aqiydah yao ya kuamini Risala ya Allaah (سبحانه وتعالى) kupitia Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), imaan yao, taqwa zao, kumkhofu Allaah (سبحانه وتعالى), kutekeleza Amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake. Kwa msingi huu, Waumini wanaishi duniani kwa lengo la kumridhisha Rabb wao, na kutaraji Rehma Yake Allaah (سبحانه وتعالى) Awaingize Jannah (Peponi). Ama makafiri, wao ni tofauti na Waumini katika hayo yote, na wao wanaishi duniani bila ya lengo la kumridhisha Rabb wao, hivyo basi hatima yao ni motoni. Rejea Kauli Zake nyenginezo za Allaah (سبحانه وتعالى) kama ifuatavyo: Al-Hashr (59:20), Al-Qalam (68:35-36), Swaad (38:28), As-Sajdah (32:18-20).
[7] Washirikina Na Makafiri Hawaamini Kufufuliwa:
Rejea Al-Israa (17:49) kwenye maelezo bayana. Na rejea pia Suwrah hii Al-Jaathiyah (45:32).
Na Aayah namba (26) ya Suwrah hii Al-Jaathiyah, inathibitisha wazi Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) wa Kuwafufua viumbe Siku ya Qiyaamah.
[8] Al-Jaathiya (Jina La Suwrah): Kupiga Magoti Kwa Unyenyekevu Na Kukhofu Na Kungojea Kuhesabiwa
Kila Ummah utahudhurishwa pamoja na Shahidi wake. Rejea Al-Baqarah (2:143), An-Nisaa (4:41), An-Nahl (16:89), Al-Israa (17:71), Al-Hajj (22:78), Az-Zumar (39:69).
[9] Utukufu, Uadhwamah, Ujalali Wa Allaah (عزّ وجلّ):
عن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( قَالَ الله (عزّ وجلّ) : العِزُّ إزَاري ، والكبرياءُ رِدائي ، فَمَنْ يُنَازِعُنِي في وَاحِدٍ منهما فَقَد عَذَّبْتُهُ )) رواه مسلم .
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Amesema Allaah (عزّ وجلّ): Utukufu ni kikoi Changu, na kiburi ni shuka Yangu, na atakayeshindana Nami katika moja wapo ya viwili hivi Nitamuadhibu." [Muslim]
الأَحْقَاف
046-Al-Ahqaaf
046-Al-Ahqaaf: Utangulizi Wa Suwrah [295]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
حم﴿١﴾
1. Haa Miym.[1]
تَنزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ﴿٢﴾
2. Ni uteremsho wa Kitabu kutoka kwa Allaah Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
مَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَأَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ وَالَّذِينَ كَفَرُوا عَمَّا أُنذِرُوا مُعْرِضُونَ﴿٣﴾
3. Hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake isipokuwa kwa haki na kwa muda maalumu uliokadiriwa. Na waliokufuru wanayakengeuka yale wanayoonywa.
قُلْ أَرَأَيْتُم مَّا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ أَرُونِي مَاذَا خَلَقُوا مِنَ الْأَرْضِ أَمْ لَهُمْ شِرْكٌ فِي السَّمَاوَاتِ ۖ ائْتُونِي بِكِتَابٍ مِّن قَبْلِ هَـٰذَا أَوْ أَثَارَةٍ مِّنْ عِلْمٍ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٤﴾
4. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Je, mnawaona wale mnaowaomba badala ya Allaah! Nionyesheni nini wameumba katika ardhi, au wana ushirika katika mbingu?[2] Nileteeni Kitabu kabla ya hiki, au alama yeyote ya ilimu mkiwa wakweli.
وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّن يَدْعُو مِن دُونِ اللَّـهِ مَن لَّا يَسْتَجِيبُ لَهُ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَهُمْ عَن دُعَائِهِمْ غَافِلُونَ﴿٥﴾
5. Na nani aliyepotoka zaidi kuliko yule anayeomba asiyekuwa Allaah ambaye hamuitikii mpaka Siku ya Qiyaamah? Nao wala hawatambui maombi yao!
وَإِذَا حُشِرَ النَّاسُ كَانُوا لَهُمْ أَعْدَاءً وَكَانُوا بِعِبَادَتِهِمْ كَافِرِينَ﴿٦﴾
6. Na pale watakapokusanywa watu, (waabudiwa wa uongo) watakuwa ni maadui wao, na watakuwa wenye kuzikanusha ibaada zao.
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ قَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ﴿٧﴾
7. Na wanaposomewa Aayaat Zetu bayana, husema wale waliokufuru kuhusu haki ilipowajia: Hii ni sihiri bayana.[3]
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ إِنِ افْتَرَيْتُهُ فَلَا تَمْلِكُونَ لِي مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَا تُفِيضُونَ فِيهِ ۖ كَفَىٰ بِهِ شَهِيدًا بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۖ وَهُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٨﴾
8. Bali wanasema ameitunga. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ikiwa nimeitunga, basi hamna uwezo wa kunifaa chochote mbele ya Allaah. Yeye Anajua zaidi yale mnayoyaropoka. Anatosha kuwa Shahidi baina yangu na baina yenu, Naye Ndiye Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[4]
قُلْ مَا كُنتُ بِدْعًا مِّنَ الرُّسُلِ وَمَا أَدْرِي مَا يُفْعَلُ بِي وَلَا بِكُمْ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ وَمَا أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ﴿٩﴾
9. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Mimi sio wa mwanzo kuja na Urasuli (Utume) miongoni mwa Rusuli, na sijui nitakavyofanyiwa mimi wala nyinyi.[5] Sifuati isipokuwa niliyofunuliwa Wahy, nami si chochote isipokuwa ni mwonyaji bayana.
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن كَانَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَكَفَرْتُم بِهِ وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِّن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ مِثْلِهِ فَآمَنَ وَاسْتَكْبَرْتُمْ ۖ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿١٠﴾
10. Sema: Mnaonaje ikiwa (hii Qur-aan) ni kutoka kwa Allaah, na mkaikanusha, na akashuhudia shahidi miongoni mwa wana wa Israaiyl juu ya mfano wa haya, na akaamini nanyi mkatabari? Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu.[6]
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا لَوْ كَانَ خَيْرًا مَّا سَبَقُونَا إِلَيْهِ ۚ وَإِذْ لَمْ يَهْتَدُوا بِهِ فَسَيَقُولُونَ هَـٰذَا إِفْكٌ قَدِيمٌ﴿١١﴾
11. Na wale waliokufuru wakasema kuwaambia walioamini: Lau ingelikuwa ni kheri, basi wasingetusabiki. Na kwa kuwa hawakuhidika kwayo (Qur-aan), basi watasema: Huu ni uzushi wa zamani.
وَمِن قَبْلِهِ كِتَابُ مُوسَىٰ إِمَامًا وَرَحْمَةً ۚ وَهَـٰذَا كِتَابٌ مُّصَدِّقٌ لِّسَانًا عَرَبِيًّا لِّيُنذِرَ الَّذِينَ ظَلَمُوا وَبُشْرَىٰ لِلْمُحْسِنِينَ﴿١٢﴾
12. Na kabla yake ni kitabu cha Muwsaa chenye kuongoza, na kuwa ni rehma. Na hiki Kitabu kinasadikisha kwa lugha ya Kiarabu ili kionye wale waliodhulumu, na ni bishara kwa wafanyao ihsaan.
إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿١٣﴾
13. Hakika wale waliosema: Rabb wetu ni Allaah, kisha wakathibiti imara, basi hakutokuwa na khofu juu yao, na wala hawatohuzunika.[7]
أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٤﴾
14. Hao ndio watu wa Jannah, ni wenye kudumu humo, jazaa kwa yale waliyokuwa wakitenda.
وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ إِحْسَانًا ۖ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ كُرْهًا وَوَضَعَتْهُ كُرْهًا ۖ وَحَمْلُهُ وَفِصَالُهُ ثَلَاثُونَ شَهْرًا ۚ حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَبَلَغَ أَرْبَعِينَ سَنَةً قَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَصْلِحْ لِي فِي ذُرِّيَّتِي ۖ إِنِّي تُبْتُ إِلَيْكَ وَإِنِّي مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴿١٥﴾
15. Na Tumemuusia binaadam kuwafanyia wema wazazi wake wawili.[8] Mama yake amebeba mimba yake kwa mashaka na akamzaa kwa mashaka.[9] Na kuibeba mimba na kuachishwa kwake kunyonya ni miezi thelathini.[10] Mpaka anapofikia umri wake wa kupevuka, na akafikia miaka arubaini husema: Rabb wangu! Nipe ilhamu na uwezo nishukuru Neema Yako ambayo Umenineemesha juu yangu na wazazi wangu, na nipate kutenda mema Utakayoridhia, na Nitengenezee dhuria wangu. Hakika mimi nimetubu Kwako, na hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu.[11]
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ نَتَقَبَّلُ عَنْهُمْ أَحْسَنَ مَا عَمِلُوا وَنَتَجَاوَزُ عَن سَيِّئَاتِهِمْ فِي أَصْحَابِ الْجَنَّةِ ۖ وَعْدَ الصِّدْقِ الَّذِي كَانُوا يُوعَدُونَ﴿١٦﴾
16. Hao ndio wale ambao Tunawatakabalia mazuri zaidi ya yale waliyoyatenda, na Tunayaachilia mbali maovu yao, watakuwa katika watu wa Jannah. Ahadi ya kweli waliyokuwa wameahidiwa.
وَالَّذِي قَالَ لِوَالِدَيْهِ أُفٍّ لَّكُمَا أَتَعِدَانِنِي أَنْ أُخْرَجَ وَقَدْ خَلَتِ الْقُرُونُ مِن قَبْلِي وَهُمَا يَسْتَغِيثَانِ اللَّـهَ وَيْلَكَ آمِنْ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ فَيَقُولُ مَا هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ﴿١٧﴾
17. Na yule anaewaambia wazazi wake: Uff![12] Mnanitishia kwamba nitatolewa kufufuliwa na hali zimekwishapita karne nyingi kabla yangu! Nao wazazi wawili wanaomba uokozi kwa Allaah, na (humwambia mtoto wao): Ole wako amini! Hakika Ahadi ya Allaah ni haki. Lakini husema: Haya si chochote isipokuwa ni hekaya za watu wa kale.[13]
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ حَقَّ عَلَيْهِمُ الْقَوْلُ فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا خَاسِرِينَ﴿١٨﴾
18. Hao ndio wale ambao imehakiki juu yao kauli (ya adhabu) kama katika nyumati nyingi zilizokwishapita kabla yao miongoni mwa majini na wanaadam. Hakika wao wamekuwa ni wenye kukhasirika.
وَلِكُلٍّ دَرَجَاتٌ مِّمَّا عَمِلُوا ۖ وَلِيُوَفِّيَهُمْ أَعْمَالَهُمْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ﴿١٩﴾
19. Na wote watakuwa na daraja mbali mbali kutokana na yale waliyoyatenda, na ili (Allaah) Awalipe kikamilifu amali zao, nao hawatodhulumiwa.
وَيَوْمَ يُعْرَضُ الَّذِينَ كَفَرُوا عَلَى النَّارِ أَذْهَبْتُمْ طَيِّبَاتِكُمْ فِي حَيَاتِكُمُ الدُّنْيَا وَاسْتَمْتَعْتُم بِهَا فَالْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَبِمَا كُنتُمْ تَفْسُقُونَ﴿٢٠﴾
20. Na siku watakaposimamishwa hadharani wale waliokufuru kwenye moto (waambiwe): Je, mshamaliza vizuri vyenu katika uhai wenu wa dunia na mshajistarehesha navyo? Basi leo mtalipwa adhabu ya udhalilifu kwa vile mlivyokuwa mkitakabari katika ardhi bila ya haki, na kwa ufasiki mliokuwa mnaufanya.
وَاذْكُرْ أَخَا عَادٍ إِذْ أَنذَرَ قَوْمَهُ بِالْأَحْقَافِ وَقَدْ خَلَتِ النُّذُرُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ﴿٢١﴾
21. Na mtaje (Huwd) ndugu wa kina ‘Aad alipowaonya watu wake katika nchi ya machuguu ya mchanga,[14] na walikwishapita waonyaji kabla yake na baada yake: Msiabudu isipokuwa Allaah. Hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku iliyo kuu kabisa.
قَالُوا أَجِئْتَنَا لِتَأْفِكَنَا عَنْ آلِهَتِنَا فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ﴿٢٢﴾
22. Wakasema: Je, umetujia ili utugeuzilie mbali na waabudiwa wetu? Basi tuletee hayo unayotutishia ukiwa ni miongoni mwa wakweli.
قَالَ إِنَّمَا الْعِلْمُ عِندَ اللَّـهِ وَأُبَلِّغُكُم مَّا أُرْسِلْتُ بِهِ وَلَـٰكِنِّي أَرَاكُمْ قَوْمًا تَجْهَلُونَ﴿٢٣﴾
23. (Huwd) akasema: Hakika ujuzi wake uko kwa Allaah, nami nabalighisha ambayo nimetumwa kwayo, lakini nakuoneni nyinyi ni kaumu wenye kufanya ujahili.
فَلَمَّا رَأَوْهُ عَارِضًا مُّسْتَقْبِلَ أَوْدِيَتِهِمْ قَالُوا هَـٰذَا عَارِضٌ مُّمْطِرُنَا ۚ بَلْ هُوَ مَا اسْتَعْجَلْتُم بِهِ ۖ رِيحٌ فِيهَا عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٢٤﴾
24. Basi walipoiona (adhabu waliyoihimiza) ni wingu lilotanda upeoni (mwao) linaelekea mabonde yao walisema: Wingu hili lilotanda upeoni (mwetu) ni la kutunyeshea mvua. Bali hilo ndilo mloharakiza, ni upepo wa dhoruba ndani yake kuna adhabu iumizayo.
تُدَمِّرُ كُلَّ شَيْءٍ بِأَمْرِ رَبِّهَا فَأَصْبَحُوا لَا يُرَىٰ إِلَّا مَسَاكِنُهُمْ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْقَوْمَ الْمُجْرِمِينَ﴿٢٥﴾
25. Unadamirisha kila kitu kwa Amri ya Rabb wake. Wakapambaukiwa hayaonekani isipokuwa masikani zao tu. Hivyo ndivyo Tunavyolipa jazaa watu wahalifu.
وَلَقَدْ مَكَّنَّاهُمْ فِيمَا إِن مَّكَّنَّاكُمْ فِيهِ وَجَعَلْنَا لَهُمْ سَمْعًا وَأَبْصَارًا وَأَفْئِدَةً فَمَا أَغْنَىٰ عَنْهُمْ سَمْعُهُمْ وَلَا أَبْصَارُهُمْ وَلَا أَفْئِدَتُهُم مِّن شَيْءٍ إِذْ كَانُوا يَجْحَدُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ﴿٢٦﴾
26. Na kwa yakini Tuliwamakinisha vizuri zaidi kuliko Tulivyokumakinisheni (nyinyi Maquraysh). Na Tukawapa masikio na macho na nyoyo za kutafakari, lakini hayakuwafaa chochote masikio yao wala macho yao wala nyoyo zao za kutafakari kwa kuwa walikuwa wakikanusha kwa ujeuri Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) za Allaah, na yakawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.
وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا مَا حَوْلَكُم مِّنَ الْقُرَىٰ وَصَرَّفْنَا الْآيَاتِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ﴿٢٧﴾
27. Na kwa yakini Tuliangamiza miji iliyokuwa pembezoni mwenu, na Tukasarifu waziwazi Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) ili wapate kurejea.
فَلَوْلَا نَصَرَهُمُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ قُرْبَانًا آلِهَةً ۖ بَلْ ضَلُّوا عَنْهُمْ ۚ وَذَٰلِكَ إِفْكُهُمْ وَمَا كَانُوا يَفْتَرُونَ﴿٢٨﴾
28. Basi kwa nini wasiwanusuru wale waliowafanya badala ya Allaah kuwa ni waabudiwa wa kikurubisho (Kwake)? Bali wamewapotea, na huo ndio uongo wao na yale waliyokuwa wakiyatunga.
وَإِذْ صَرَفْنَا إِلَيْكَ نَفَرًا مِّنَ الْجِنِّ يَسْتَمِعُونَ الْقُرْآنَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوا أَنصِتُوا ۖ فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَىٰ قَوْمِهِم مُّنذِرِينَ﴿٢٩﴾
29. Na pale Tulipowaelekeza kwako (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم ) kundi miongoni mwa majini ili kuisikiliza Qur-aan. Walipohudhuria majlisi, walisema: Bakieni kimya msikilize! Ilipomalizika, waligeuka kurudi kwa kaumu yao wakiwa wenye kuonya.[15]
قَالُوا يَا قَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا كِتَابًا أُنزِلَ مِن بَعْدِ مُوسَىٰ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ وَإِلَىٰ طَرِيقٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٣٠﴾
30. Wakasema: Enyi kaumu yetu! Hakika sisi tumesikia Kitabu kimeteremshwa baada ya Muwsaa, kinachosadikisha yaliyo kabla yake, kinaongoza kwenye haki na kuelekea njia iliyonyooka.
يَا قَوْمَنَا أَجِيبُوا دَاعِيَ اللَّـهِ وَآمِنُوا بِهِ يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُجِرْكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣١﴾
31. Enyi kaumu yetu! Mwitikieni Mlinganiaji wa Allaah, na mwaminini! (Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakukingeni na adhabu iumizayo.
وَمَن لَّا يُجِبْ دَاعِيَ اللَّـهِ فَلَيْسَ بِمُعْجِزٍ فِي الْأَرْضِ وَلَيْسَ لَهُ مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءُ ۚ أُولَـٰئِكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٣٢﴾
32. Na yeyote asiyemuitikia Mlinganiaji wa Allaah, basi hawezi kushinda kukwepa katika ardhi, na hatokuwa na walinzi badala ya Allaah. Hao wamo katika upotofu bayana.
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَلَمْ يَعْيَ بِخَلْقِهِنَّ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ ۚ بَلَىٰ إِنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٣٣﴾
33. Je, hawaoni kwamba Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na wala Hakuchoka kwa kuziumba kwake, kwamba Yeye Ni Muweza wa Kuwafufua wafu. Naam bila shaka! Hakika Yeye juu ya kila kitu Ni Muweza.[16]
وَيَوْمَ يُعْرَضُ الَّذِينَ كَفَرُوا عَلَى النَّارِ أَلَيْسَ هَـٰذَا بِالْحَقِّ ۖ قَالُوا بَلَىٰ وَرَبِّنَا ۚ قَالَ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ﴿٣٤﴾
34. Na Siku watakaposimamishwa hadharani wale waliokufuru kwenye moto (isemwe): Je, hii si kweli? Watasema: Bali ndio! Tunaapa kwa Rabb wetu! Atasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya ukafiri mliokuwa mkiufanya.
فَاصْبِرْ كَمَا صَبَرَ أُولُو الْعَزْمِ مِنَ الرُّسُلِ وَلَا تَسْتَعْجِل لَّهُمْ ۚ كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَ مَا يُوعَدُونَ لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا سَاعَةً مِّن نَّهَارٍ ۚ بَلَاغٌ ۚ فَهَلْ يُهْلَكُ إِلَّا الْقَوْمُ الْفَاسِقُونَ﴿٣٥﴾
35. Basi subiri (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kama walivyosubiri wenye azimio madhubuti miongoni mwa Rusuli[17], na wala usiwaharakizie. Siku watakayoona waliyoahidiwa itakuwa kama kwamba hawakubakia (duniani) isipokuwa saa moja tu katika mchana. (Huu) ni ubalighisho! Je, basi kwani huangamizwa isipokuwa watu mafasiki?
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Wanaoabudiwa Pasi Na Allaah Hawakuumba Chochote:
Rejea Luqmaan (31:11) kwenye rejea mbali mbali.
Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى)
أَمْ لَهُمْ شِرْكٌ فِي السَّمَاوَاتِ
Au wana ushirika katika mbingu.
Allaah (سبحانه وتعالى) Anawaraddi kwa hili kwamba ingelikuwa wana ushirika Naye katika Uumbaji Wake mbingu na ardhi, basi kila mwabudiwa angelichukua vile alivyoviumba, na baadhi yao wangeliwashinda wengineo. Rejea Al-Muuminuwn (23:91). Au pia mbingu na ardhi bila shaka zingelifisidika. Rejea Al-Anbiyaa (21:22).
Bali Allaah (سبحانه وتعالى) Hana mshirika na Ndiye Aliyeumba kila kitu. Rejea Al-An’aam (6:101-102), Az-Zumar (39:62).
[3] Ada Ya Makafiri Kuipachika Sifa Ovu Qur-aan:
Rejea Al-Furqaan (25:4) kwenye uchambuzi wa hayo na rejea mbalimbali.
[4] Washirikina Kumsingizia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kuwa Ameitunga Qur-aan:
Au je wanasema hawa washirikina kwamba Muhammad ametunga Quraan? Waambie, ee Rasuli! “Iwapo mimi nimemtungia Allaah hii Qur-aan, basi nyinyi hamuwezi kunikinga mimi na Adhabu ya Allaah kwa lolote ikiwa Ataniadhibu kwa hilo. Yeye (سبحانه وتعالى) kutakasika ni Kwake, ni Mjuzi zaidi wa kile mnachokisema juu ya hii Qur-aan kuliko kitu chochote kingine. Inatosha kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Ni Shahidi juu yangu mimi na nyinyi, na Yeye Ndiye Mwingi wa Kughufuria Waja Wake, na Ni Mwingi wa Kuwarehemu Waja Wake Waumini.” [Tafsiyr Al-Muyassar]
Na kauli hiyo ya Allaah (سبحانه وتعالى) ni kama Kauli Zake nyenginezo katika Suwrah zifuatazo: Al-Haaqqah (69:44-47), Al-Jinn (71:22-23).
[5] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Hakuwa Anajua Kama Ataghufuriwa Madhambi Yake:
Amesema ‘Aliy Bin Abiy Twalhah kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Baada ya kuteremshiwa Aayah hii, ikateremshwa:
إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا﴿١﴾
Hakika Tumekupa ushindi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), ushindi bayana. [Al-Fat-h (48:1)]
Na wamesema hayo pia ‘Ikrimah, Al-Hasan na Qataadah kwamba kauli hiyo (ya Suwrah Al-Ahqaaf (46:9) imefutwa hukmu yake kwa kuteremshwa:
إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا﴿١﴾
Hakika Tumekupa ushindi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), ushindi bayana. [Al-Fat-h (48:1)]
Bonyeza pia kiungo kifuatacho kwenye Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah:
048-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Fat-h Aayah 01-5: إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا [296]
[6] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah/ Shahidi Miongoni Mwa Wana Wa Israaiyl Ni ‘Abdullaah Bin Salaam (رضي الله عنه):
Bonyeza kiungo kifuatacho:
Na Hadiyth ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) imethibitisha pia:
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، قَالَ سَمِعْتُ مَالِكًا، يُحَدِّثُ عَنْ أَبِي النَّضْرِ، مَوْلَى عُمَرَ بْنِ عُبَيْدِ اللَّهِ عَنْ عَامِرِ بْنِ سَعْدِ بْنِ أَبِي وَقَّاصٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ مَا سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ لأَحَدٍ يَمْشِي عَلَى الأَرْضِ إِنَّهُ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ. إِلاَّ لِعَبْدِ اللَّهِ بْنِ سَلاَمٍ قَالَ وَفِيهِ نَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ الآيَةَ. قَالَ لاَ أَدْرِي قَالَ مَالِكٌ الآيَةَ أَوْ فِي الْحَدِيثِ.
Amesimulia Sa’d Bin Abiy Waqqaas kutoka kwa baba yake (رضي الله عنهما):
Sijapata kumsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akimwambia yeyote anayetembea katika ardhi kuwa yeye ni katika watu wa Jannah isipokuwa ‘Abdullaah bin Salaam. Na kwa ajili yake imeteremshwa Aayah hii:
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن كَانَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَكَفَرْتُم بِهِ وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِّن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ مِثْلِهِ فَآمَنَ وَاسْتَكْبَرْتُمْ ۖ
Sema: Mnaonaje ikiwa (hii Qur-aan) ni kutoka kwa Allaah, na mkaikanusha, na akashuhudia shahidi miongoni mwa wana wa Israaiyl juu ya mfano wa haya, na akaamini nanyi mkatabari? [Al-Ahqaaf (46:10]
Akasema: Sijui kama Maalik aliisoma Aayah pembeni au Aayah iko ndani ya Hadiyth. [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Fadhila za Anaswaar (63)]
Sema ee Rasuli uwaambie washirikina wa watu wako: “Hebu nielezeni. Ikiwa Qur-aan hii inatoka kwa Allaah na nyinyi mmeikataa, halafu akashuhudia shahidi kati ya Wana wa Israaiyl kama ‘Abdullaah bin Salaam kwamba yaliyomo ndani ya Tawraat yanathibitisha Unabii wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kama inavyothibitisha Qur-aan, halafu isitoshe, akayasadikisha na kuyafuata kwa kivitendo yaliyokuja ndani ya Qur-aan na nyinyi mkayakataa kwa njia ya kibri, sasa haya yote ni nini kama si dhulma mbaya na ukafiri mkubwa kutoka kwenu?! Hakika Allaah Hawaongozi kwenye Uislamu na kuifikia haki wale watu waliojidhulumu kwa kumkanusha Allaah. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[8] Kuwafanyia Wazazi Ihsaan:
Na Tumemuusia binaadam asuhubiane na wazazi wake wawili kwa ihsaan, kwa kuwatendea wema wanapokuwa hai na baada ya kufa kwao. Kwa kuwa mamake alimbeba akiwa mwana wa matumboni kwa mashaka na tabu, na akamzaa kwa mashaka na tabu pia. Na muda wa kubeba mimba yake na mpaka kumaliza kumnyonyesha ni miezi thelathini. Katika kutaja mashaka haya anayoyabeba mama, na siyo baba, pana dalili kuwa haki yake juu ya mtoto wake ni kubwa zaidi kuliko haki ya baba. Mpaka alipofikia binaadam upeo wa nguvu zake za kimwili na kiakili na akafikia miaka arubaini, huwa akimuomba Rabb wake kwa kusema: Rabb wangu, Nizindushe nishukuru Neema Zako Ulizonineemesha mimi na wazazi wangu wawili, na Nijaalie nifanye matendo mema Unayoridhika nayo, na Unisuluhishie wanangu. Hakika mimi nimetubia dhambi zangu Kwako, na hakika mimi ni miongoni mwa wanyenyekevu Kwako kwa utiifu, na ni miongoni mwa wenye kujisalimisha kufuata Amri Zako, na kuepuka Makatazo Yako, na wenye kuridhia Hukmu Yako. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Na jambo hili la kuwafanyia wazazi wawili ihsaan, Allaah (سبحانه وتعالى) Amelipa umuhimu mkubwa mno. Anahimiza hivyo katika Kauli Zake kadhaa. Rejea Luqmaan (31:14) kwenye maelezo na faida tele.
Bonyeza pia viungo vifuatavyo upate faida tele nyenginezo:
Mama…Kisha Mama…Kisha Mama [300]
[9] Mashaka Ya Mama Kubeba Mimba Kuzaa:
Aayah hii imetaja mashaka ya mama kubeba mimba na kumzaa mtoto kwa mashaka na mashaka. Na katika Suwrah Luqmaan (31:14), imetajwa amebeba mimba na kumzaa kwa udhaifu juu ya udhaifu. Rejea huko kwenye maelezo na faida nyenginezo.
[11] Duaa Ya Kuomba Msaada Wa Kuweza Kumshukuru Allaah (عزّ وجلّ):
Duaa kama hii imekariri katika Suwrah An-Naml (27:19).
Rejea Suwrah Ibraahiym (14:34) kwenye uchambuzi wa Neema za Allaah za mbinguni, ardhini, nafsini na kadhaalika pamoja na faida nyenginezo na rejea mbalimbali.
Rejea pia Adhw-Dhwuhaa (93:11) kwenye faida kuhusu kukiri Neema za Allaah, kushukuru, na kuomba kuhifadhiwa na kuzidishiwa Neema za Allaah (عزّ وجلّ).
[13] ‘Aaishah (رضي الله عنها) Amtetea Kaka Yake Aliyesingiziwa Kuwa Aayaah Hii Imeteremka Kumhusu Yeye:
حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ إِسْمَاعِيلَ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ أَبِي بِشْرٍ، عَنْ يُوسُفَ بْنِ مَاهَكَ، قَالَ كَانَ مَرْوَانُ عَلَى الْحِجَازِ اسْتَعْمَلَهُ مُعَاوِيَةُ، فَخَطَبَ فَجَعَلَ يَذْكُرُ يَزِيدَ بْنَ مُعَاوِيَةَ، لِكَىْ يُبَايِعَ لَهُ بَعْدَ أَبِيهِ، فَقَالَ لَهُ عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ أَبِي بَكْرٍ شَيْئًا، فَقَالَ خُذُوهُ. فَدَخَلَ بَيْتَ عَائِشَةَ فَلَمْ يَقْدِرُوا {عَلَيْهِ} فَقَالَ مَرْوَانُ إِنَّ هَذَا الَّذِي أَنْزَلَ اللَّهُ فِيهِ وَالَّذِي قَالَ لِوَالِدَيْهِ أُفٍّ لَكُمَا أَتَعِدَانِنِي . فَقَالَتْ عَائِشَةُ مِنْ وَرَاءِ الْحِجَابِ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ فِينَا شَيْئًا مِنَ الْقُرْآنِ إِلاَّ أَنَّ اللَّهَ أَنْزَلَ عُذْرِي.
Amesimulia Yuwsuf bin Maahak (رضي الله عنه): Marwaan (رضي الله عنه) aliteuliwa na Mu’aawiyah (رضي الله عنه) kuwa liwali (gavana) wa Hijaaz. Alitoa khutbah na kumtaja Yaziyd bin Mu‘aawiyah ili watu watoe ahadi ya utiifu kwake baada ya babake. ‘Abdur-Rahmaan bin Abi Bakr (رضي الله عنهما) alimwambia kitu, naye Marwaan akaagizia ashikwe (ili afungwe). Hapo ‘Abdur-Rahmaan aliingia katika nyumba ya ‘Aaishah (رضي الله عنها), kwa hiyo hawakuweza kumshika. Hapo Marwaan akasema: Huyu ni yule aliyeteremshiwa Aayah ifuatayo na Allaah (سبحانه وتعالى):
وَالَّذِي قَالَ لِوَالِدَيْهِ أُفٍّ لَّكُمَا أَتَعِدَانِنِي أَنْ أُخْرَجَ وَقَدْ خَلَتِ الْقُرُونُ مِن قَبْلِي وَهُمَا يَسْتَغِيثَانِ اللَّـهَ وَيْلَكَ آمِنْ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ فَيَقُولُ مَا هَـٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ﴿١٧﴾
Na yule anaewaambia wazazi wake: Uff! Mnanitishia kwamba nitatolewa kufufuliwa na hali zimekwishapita karne nyingi kabla yangu! Nao wazazi wawili wanaomba uokozi kwa Allaah, na (humwambia mtoto wao): Ole wako amini! Hakika Ahadi ya Allaah ni haki. Lakini husema: Haya si chochote isipokuwa ni hekaya za watu wa kale. [Al-Ahqaaf (46:17)]
‘Aaishah (رضي الله عنها)akasema akiwa nyuma ya pazia: “Allaah Hakuteremsha chochote kutuhusu sisi katika Qur-aan isipokuwa Allaah Ameteremsha kunitakasa mimi na kashfa ya kusingiziwa kuzini.” [Al-Bukhaariy]
[14] Al-Ahqaaf: Nchi Ya Machuguu Ya Mchanga
Kauli za Salaf kuhusu Ahqaaf:
Ibn Zayd amesema: Ni mlima wa mchanga au pango.
‘Aliy bin Abiy Twaalib (رضي الله عنه): Ni bonde lililoko Hadhwramawt linaloitwa Barhuwt ambapo hutupwa ndani yake roho za makafiri.
Qataadah: Tumetajiwa kwamba kina ‘Aad walikuwa ni kabila la watu wa Yemen. Waliishi katika milima ya michanga iliyochomozea baharini katika ardhi iliyojulikana kama Ash-Shihir.
Na mataje ee Rasuli Nabiy wa Allaah, Huwd (عليه السّلام) ndugu yao kina ‘Aad kinasaba na siyo kidini, alipowaonya watu wake kuwa watashukiwa na Adhabu ya Allaah wakiwa kwenye nyumba zao hapo Aḥqaaf (mahali kwenye mchanga mwingi) kusini mwa Arabuni. Na kwa hakika wamepita Rusuli wakawaonya watu wa mahala hapo kabla ya Huwd na baada yake wakiwaambia: “Msimshirikishe Allaah na kitu chochote mnapomuabudu, hakika sisi tunawacheleeni nyinyi adhabu ya Allaah katika Siku yenye kituko kikubwa, nayo ni Siku ya Qiyaamah.” [Tafsiyr Al-Muyassar]
[15] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho
Majini Wamelingania Dini Kwa Majini Wenzao:
Rejea Al-Jinn (72:1).
[16] Allaah (عزّ وجلّ) Ni Mweza Wa Kuwafufua Wafu:
Rejea Al-Israa (17:49) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali.
[17] Rusuli Walioitwa Ulul-‘Azmi (Wenye Azimio La Nguvu):
Ni Rusuli watano ambao ni: (i) Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) (ii) Nabiy Nuwh (عليه السّلام) (iii) Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) (iv) Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) (v) Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام). Rejea Al-Ahzaab (33:7) walipotajwa na kwenye maelezo yake. Na rejea pia An-Nisaa (4:69) kwenye maelezo bayana kuhusu daraja za Rusuli kulingana na Manabii.
مُحَمَّد
047-Muhammad
047-Muhammad: Utangulizi Wa Suwrah [303]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ أَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ﴿١﴾
1. Wale waliokufuru na wakazuia Njia ya Allaah, Atazipoteza amali zao.[1]
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَآمَنُوا بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ مُحَمَّدٍ وَهُوَ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۙ كَفَّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَأَصْلَحَ بَالَهُمْ﴿٢﴾
2. Na wale walioamini na wakatenda mema na wakaamini yale aliyoteremshiwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), nayo ni ya haki kutoka kwa Rabb wao, Atawafutia maovu yao na Atatengeneza hali zao.
ذَٰلِكَ بِأَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا اتَّبَعُوا الْبَاطِلَ وَأَنَّ الَّذِينَ آمَنُوا اتَّبَعُوا الْحَقَّ مِن رَّبِّهِمْ ۚ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ اللَّـهُ لِلنَّاسِ أَمْثَالَهُمْ﴿٣﴾
3. Hivyo kwa kuwa wale waliokufuru wamefuata ubatilifu, na kwamba wale walioamini wamefuata haki kutoka kwa Rabb wao. Hivyo ndivyo Allaah Anavyowapigia watu mifano yao.
فَإِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا فَضَرْبَ الرِّقَابِ حَتَّىٰ إِذَا أَثْخَنتُمُوهُمْ فَشُدُّوا الْوَثَاقَ فَإِمَّا مَنًّا بَعْدُ وَإِمَّا فِدَاءً حَتَّىٰ تَضَعَ الْحَرْبُ أَوْزَارَهَا ۚ ذَٰلِكَ وَلَوْ يَشَاءُ اللَّـهُ لَانتَصَرَ مِنْهُمْ وَلَـٰكِن لِّيَبْلُوَ بَعْضَكُم بِبَعْضٍ ۗ وَالَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَلَن يُضِلَّ أَعْمَالَهُمْ﴿٤﴾
4. Na mtakapokutana (vitani) na wale waliokufuru, basi wapigeni shingo zao, mpaka muwashinde kwa kuwajeruhi na kuwaua, na hapo wafungeni pingu barabara. Kisha ima (wafanyieni) ihsaan baada ya hapo au wajifidie mpaka vita vitue mizigo yake. Ndio hivyo, na lau Allaah Angelitaka basi Angewalipiza kisasi Mwenyewe, lakini (Ameamrisha Jihaad) ili Akujaribuni nyinyi kwa nyinyi. Na wale waliouliwa katika Njia ya Allaah, basi Hatopoteza amali zao.[2]
سَيَهْدِيهِمْ وَيُصْلِحُ بَالَهُمْ﴿٥﴾
5. Atawaongoza na Atatengeneza hali zao.
وَيُدْخِلُهُمُ الْجَنَّةَ عَرَّفَهَا لَهُمْ﴿٦﴾
6. Na Atawaingiza Jannah Aliyoitambulisha kwao.[3]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّـهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ﴿٧﴾
7. Enyi walioamini! Mkisaidia kunusuru Dini ya Allaah,[4] (Allaah) Atakunusuruni na Ataithibitisha miguu yenu.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْسًا لَّهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ﴿٨﴾
8. Na wale waliokufuru, basi ni maangamizo kwao, na Atapoteza amali zao.
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ﴿٩﴾
9. Hivyo ni kwa sababu wao wamekirihika na ambayo Allaah Ameyateremsha basi Amezibatilisha amali zao.
أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ دَمَّرَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ ۖ وَلِلْكَافِرِينَ أَمْثَالُهَا﴿١٠﴾
10. Je, hawakutembea katika ardhi wakatazama vipi imekuwa hatima ya waliopita kabla yao? Allaah Amewadamirisha mbali, na kwa makafiri (itakuwa) mfano wa hayo.[5]
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ مَوْلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَأَنَّ الْكَافِرِينَ لَا مَوْلَىٰ لَهُمْ﴿١١﴾
11. Hivyo ni kwa kuwa Allaah Ni Mlinzi wa wale walioamini na kwamba makafiri hawana mlinzi.
إِنَّ اللَّـهَ يُدْخِلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا يَتَمَتَّعُونَ وَيَأْكُلُونَ كَمَا تَأْكُلُ الْأَنْعَامُ وَالنَّارُ مَثْوًى لَّهُمْ﴿١٢﴾
12. Hakika Allaah Atawaingiza wale walioamini na wakatenda mema Jannaat zipitazo chini yake mito. Na wale waliokufuru wanastarehe na wanakula kama walavyo wanyama wa mifugo, na moto ndio makazi yao.
وَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ هِيَ أَشَدُّ قُوَّةً مِّن قَرْيَتِكَ الَّتِي أَخْرَجَتْكَ أَهْلَكْنَاهُمْ فَلَا نَاصِرَ لَهُمْ﴿١٣﴾
13. Na miji mingapi iliyokuwa yenye nguvu zaidi kuliko mji wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ambao umekutoa? Tuliwaangamiza! Na hawakuwa na wa kuwanusuru.
أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّهِ كَمَن زُيِّنَ لَهُ سُوءُ عَمَلِهِ وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُم﴿١٤﴾
14. Je, basi aliye kwenye hoja bayana kutoka kwa Rabb wake, ni sawa na ambaye amepambiwa uovu wa amali zake na wakafuata hawaa zao?
مَّثَلُ الْجَنَّةِ الَّتِي وُعِدَ الْمُتَّقُونَ ۖ فِيهَا أَنْهَارٌ مِّن مَّاءٍ غَيْرِ آسِنٍ وَأَنْهَارٌ مِّن لَّبَنٍ لَّمْ يَتَغَيَّرْ طَعْمُهُ وَأَنْهَارٌ مِّنْ خَمْرٍ لَّذَّةٍ لِّلشَّارِبِينَ وَأَنْهَارٌ مِّنْ عَسَلٍ مُّصَفًّى ۖ وَلَهُمْ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَمَغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ ۖ كَمَنْ هُوَ خَالِدٌ فِي النَّارِ وَسُقُوا مَاءً حَمِيمًا فَقَطَّعَ أَمْعَاءَهُمْ﴿١٥﴾
15. Mfano wa Jannah ambayo wameahidiwa wenye taqwa; humo mna mito ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa isiyotaghayari ladha yake, na mito ya mvinyo yenye burudisho kwa wanywaji, na mito ya asali iliyosafishwa.[6] Tena watapata humo kila aina ya matunda, na pia maghfirah kutoka kwa Rabb wao. (Je hao) ni kama yule mwenye kudumu motoni? Na watanyweshwa maji yachemkayo yakatekate machango yao?
وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ حَتَّىٰ إِذَا خَرَجُوا مِنْ عِندِكَ قَالُوا لِلَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مَاذَا قَالَ آنِفًا ۚ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ طَبَعَ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُمْ﴿١٦﴾
16. Na wapo miongoni mwao ambao wanakusikiliza kwa makini, mpaka wanapotoka kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) huwaambia wale waliopewa ilimu: Amesema nini sasa hivi? Hao ndio ambao Allaah Amepiga chapa juu ya nyoyo zao, na wakafuata hawaa zao.
وَالَّذِينَ اهْتَدَوْا زَادَهُمْ هُدًى وَآتَاهُمْ تَقْوَاهُمْ﴿١٧﴾
17. Na wale waliohidika, Anawazidishia Hidaya na Huwajaza taqwa yao.
فَهَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً ۖ فَقَدْ جَاءَ أَشْرَاطُهَا ۚ فَأَنَّىٰ لَهُمْ إِذَا جَاءَتْهُمْ ذِكْرَاهُمْ﴿١٨﴾
18. Je, basi wanangojea nini isipokuwa Saa iwafikie ghafla? Na kwa yakini zimekwishakuja ishara zake (Qiyamaah). Basi kutawafaa nini kukumbuka kwao itakapowajia (hiyo Saa)?[7]
فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مُتَقَلَّبَكُمْ وَمَثْوَاكُمْ﴿١٩﴾
19. Basi jua kwamba: hapana muabudiwa wa haki ila Allaah,[8] na omba Maghfirah kwa dhambi zako na kwa ajili ya Waumini wa kiume na Waumini wa kike. Na Allaah Anajua harakati zenu huku na kule na pahala penu pa kupumzikia.
وَيَقُولُ الَّذِينَ آمَنُوا لَوْلَا نُزِّلَتْ سُورَةٌ ۖ فَإِذَا أُنزِلَتْ سُورَةٌ مُّحْكَمَةٌ وَذُكِرَ فِيهَا الْقِتَالُ ۙ رَأَيْتَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ نَظَرَ الْمَغْشِيِّ عَلَيْهِ مِنَ الْمَوْتِ ۖ فَأَوْلَىٰ لَهُمْ﴿٢٠﴾
20. Na wanasema wale walioamini: Kwa nini isiteremshwe Suwrah? Inapoteremshwa Suwrah iliyo wazi na ikatajwa humo kupigana vita, utawaona wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi[9] wanakutazama mtazamo wa mwenye kughumiwa na mauti. Basi ni awla kwao (kumtii Allaah).
طَاعَةٌ وَقَوْلٌ مَّعْرُوفٌ ۚ فَإِذَا عَزَمَ الْأَمْرُ فَلَوْ صَدَقُوا اللَّـهَ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ﴿٢١﴾
21. Utiifu na kauli njema. Na likiazimiwa jambo (la kupigana), basi kama wangekuwa wakweli kwa Allaah, bila shaka ingalikuwa kheri kwao.
فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِن تَوَلَّيْتُمْ أَن تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ﴿٢٢﴾
22. Basi lipi zaidi litarajiwalo kwenu mkigeuka isipokuwa kufanya ufisadi katika ardhi na kuwakata jamaa zenu wa damu?[10]
أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَىٰ أَبْصَارَهُمْ﴿٢٣﴾
23. Hao ndio ambao Allaah Amewalaani, Akawafanya viziwi na Akawapofua macho yao.
أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ أَمْ عَلَىٰ قُلُوبٍ أَقْفَالُهَا﴿٢٤﴾
24. Je, hawaizingatii Qur-aan! Au nyoyoni (mwao) mna kufuli?
إِنَّ الَّذِينَ ارْتَدُّوا عَلَىٰ أَدْبَارِهِم مِّن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْهُدَى ۙ الشَّيْطَانُ سَوَّلَ لَهُمْ وَأَمْلَىٰ لَهُمْ﴿٢٥﴾
25. Hakika wale walioritadi kurudi nyuma baada ya kuwa Hidaya imewabainikia, hao shaytwaan amewarubuni na akawarefushia matumaini ya uongo.
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لِلَّذِينَ كَرِهُوا مَا نَزَّلَ اللَّـهُ سَنُطِيعُكُمْ فِي بَعْضِ الْأَمْرِ ۖ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ إِسْرَارَهُمْ﴿٢٦﴾
26. Hivyo ni kwa sababu wao wamewaambia wale waliokirihika na yale Aliyoyateremsha Allaah: Tutakutiini katika baadhi ya mambo. Na Allaah Anajua siri zao.
فَكَيْفَ إِذَا تَوَفَّتْهُمُ الْمَلَائِكَةُ يَضْرِبُونَ وُجُوهَهُمْ وَأَدْبَارَهُمْ﴿٢٧﴾
27. Basi itakuwa vipi pale Malaika watakapowafisha wakiwapiga nyuso zao na migongo yao?
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اتَّبَعُوا مَا أَسْخَطَ اللَّـهَ وَكَرِهُوا رِضْوَانَهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ﴿٢٨﴾
28. Hivyo ni kwa sababu wao wamefuata yaliyomghadhibisha Allaah, na wakachukia yanayomfurahisha, basi Akaziporomosha amali zao.
أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ أَن لَّن يُخْرِجَ اللَّـهُ أَضْغَانَهُمْ﴿٢٩﴾
29. Je, wanadhania wale ambao nyoyoni mwao mna maradhi[11] kwamba Allaah Hatafichua kamwe vinyongo vyao vya chuki na niya mbaya?
وَلَوْ نَشَاءُ لَأَرَيْنَاكَهُمْ فَلَعَرَفْتَهُم بِسِيمَاهُمْ ۚ وَلَتَعْرِفَنَّهُمْ فِي لَحْنِ الْقَوْلِ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ أَعْمَالَكُمْ﴿٣٠﴾
30. Na lau Tungelitaka, Tungelikuonyesha hao, ukawatambua kwa alama zao dhahiri. Na bila shaka utawatambua kwa kwa jinsi wanavyoyafumbia maneno (yao). Na Allaah Anajua amali zenu.
وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ حَتَّىٰ نَعْلَمَ الْمُجَاهِدِينَ مِنكُمْ وَالصَّابِرِينَ وَنَبْلُوَ أَخْبَارَكُمْ﴿٣١﴾
31. Na bila shaka Tutakujaribuni mpaka Tuwadhihirishe wenye kufanya Jihaad miongoni mwenu na wenye kuvuta subira, na Tutazibainisha khabari zenu.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ وَشَاقُّوا الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْهُدَىٰ لَن يَضُرُّوا اللَّـهَ شَيْئًا وَسَيُحْبِطُ أَعْمَالَهُمْ﴿٣٢﴾
32. Hakika wale waliokufuru na wakazuia Njia ya Allaah, na wakampinga kwa uadui Rasuli baada ya kuwabainikia Hidaya hawatoweza kumdhuru Allaah kwa chochote, na Ataziporomosha amali zao.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَلَا تُبْطِلُوا أَعْمَالَكُمْ﴿٣٣﴾
33. Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Rasuli, na wala msitengue amali zenu.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ثُمَّ مَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَهُمْ﴿٣٤﴾
34. Hakika wale waliokufuru na wakazuia Njia ya Allaah, kisha wakafa hali ya kuwa ni makafiri, Allaah Hatowaghufuria kamwe.
فَلَا تَهِنُوا وَتَدْعُوا إِلَى السَّلْمِ وَأَنتُمُ الْأَعْلَوْنَ وَاللَّـهُ مَعَكُمْ وَلَن يَتِرَكُمْ أَعْمَالَكُمْ﴿٣٥﴾
35. Basi msinyong’onyee mkataka suluhu, kwani nyinyi ndio mko juu. Na Allaah Yu pamoja nanyi, na Hatawapunguzieni (thawabu za) amali zenu.
إِنَّمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ ۚ وَإِن تُؤْمِنُوا وَتَتَّقُوا يُؤْتِكُمْ أُجُورَكُمْ وَلَا يَسْأَلْكُمْ أَمْوَالَكُمْ﴿٣٦﴾
36. Hakika uhai wa dunia ni mchezo na pumbao. Lakini mkiamini na mkawa na taqwa, (Allaah) Atakupeni ujira wenu na wala Hatokutakeni mtoe mali zenu.
إِن يَسْأَلْكُمُوهَا فَيُحْفِكُمْ تَبْخَلُوا وَيُخْرِجْ أَضْغَانَكُمْ﴿٣٧﴾
37. Akikutakeni hayo Akakukazanieni mtafanya ubakhili, na Atatoa vinyongo vyenu vya kukirihika na niyyah mbaya.
هَا أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ تُدْعَوْنَ لِتُنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ فَمِنكُم مَّن يَبْخَلُ ۖ وَمَن يَبْخَلْ فَإِنَّمَا يَبْخَلُ عَن نَّفْسِهِ ۚ وَاللَّـهُ الْغَنِيُّ وَأَنتُمُ الْفُقَرَاءُ ۚ وَإِن تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُم﴿٣٨﴾
38. Ha! Nyinyi ndio hawa mnaoitwa ili mtoe katika Njia ya Allaah. Basi yuko miongoni mwenu ambaye anafanya ubakhili, na afanyaye ubakhili, basi hakika hapana ila anafanya ubakhili dhidi ya nafsi yake. Na Allaah Ni Mkwasi, nanyi ni mafakiri. Na mkikengeuka Atabadilisha watu ghairi yenu kisha hawatokuwa mfano wenu.
[1] Waumini Kulipwa Thawabu Na Makafiri Kulipwa Adhabu:
Kuanzia Aayah hii namba (1) hadi namba (3), Tafsiyr ya Imaam As-Sa’diy inaeleza kama ifuatavyo:
Aayaat hizi zinajumuisha kutajwa malipo (thawabu) ya Waumini na adhabu za walioasi na sababu zake, na daawah (wito) kwa viumbe kupata mafunzo kutokana nayo. Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ
Wale waliokufuru na wakazuia Njia ya Allaah.
Hawa ni wakuu wa makafiri na viongozi wa wapotovu ambao wamekusanya mambo mawili kwa pamoja; kumkanusha Allaah na Ishara Zake, na kujizuilia wao na kuzuia wengineo katika Njia ya Allaah ambayo ni kuamini na kufuata waliyolingania Rusuli (wa Allaah). Basi watu hao Allaah Atazipoteza amali zao, yaani, Atazibatilisha na Atawasababishia adhabu kwa sababu ya hayo. Hii ni pamoja na juhudi zao za kupinga haqq (haki) na kuwapinga vipenzi vya Allaah. Basi Allaah Atajaalia hila zao katika shingo zao (yaani ziwarudie wenyewe). Na matendo yao ambayo wametaraji walipwe mema, Allaah Atayabatilisha. Hivyo ni kwa sababu ya kufuata kwao baatwil, nayo inajumuisha kila juhudi ambazo hazifanywi kwa ajili ya Allaah kama kuabudu masanamu na mizimu na juhudi za kuunga mkono upotofu kwa sababu malengo hayo ni baatwil na matendo yoyote yanayofanywa kwa ajili yake, nayo pia ni baatwil. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[2] Namna Ya Kupambana Na Maadui Na Nini La Kufanya Kwa Mateka:
Basi mkipambana, enyi Waumini, na wale waliokufuru katika viwanja vya vita, piganeni nao kidhati na mzipige shingo zao. Hata mtakapowadhoofisha kwa kuwaua kwa wingi na mkazivunja nguvu zao, wafungeni kisawasawa wale mnaowateka. Kisha basi ima muwasamehe kwa kuwafungua na kuwaacha bila kutoa fidia badala yake, au wajikomboe kwa kutoa fidia, au watiwe utumwani au wauawe. Na endeleeni kufanya hivyo mpaka vita vimalizike. Hiyo ndiyo hukumu iliyotajwa ya kuwatahini Waumini kwa makafiri na ushindi kuzunguka baina yao. Na lau Allaah Angalitaka, wangalipata ushindi Waumini bila ya vita, lakini Allaah Amejaalia mateso yao yawe mikononi mwenu ndipo Akaweka sharia ya Jihaad ili Awajaribu nyinyi kwa wao na Ainusuru kwa sababu yenu Dini Yake. Na wale Waumini waliouawa katika Njia ya Allaah, Hatayapomosha Allaah malipo mema ya matendo yao. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[3] Jannah Imetambulishwa Kwa Waumini:
Yaani: (Allaah) Aliifanya (Jannah) ijulikane kwanza kabisa ili kuwafanya (Waumini) waitamani. Aliwaeleza na kuwaambia amali zitakazowafikisha katika Jannah (Pepo), ambapo mojawapo ya amali hizo ni kupigana katika Njia Yake, na Akawawezesha wafanye Alichowaamuru na Akawatia raghba watekeleze. Kisha wanapoingia Jannah, Atawaonyesha makazi yao na yale yaliyomo humo ya raha za kudumu milele na maisha mema. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Na Hadiyth ifuatayo ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) imethibitisha kuwa Waumini watatambua makazi yao ya Jannah (Peponi):
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ ـ رضى الله عنه ـ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " إِذَا خَلَصَ الْمُؤْمِنُونَ مِنَ النَّارِ حُبِسُوا بِقَنْطَرَةٍ بَيْنَ الْجَنَّةِ وَالنَّارِ، فَيَتَقَاصُّونَ مَظَالِمَ كَانَتْ بَيْنَهُمْ فِي الدُّنْيَا، حَتَّى إِذَا نُقُّوا وَهُذِّبُوا أُذِنَ لَهُمْ بِدُخُولِ الْجَنَّةِ، فَوَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم بِيَدِهِ لأَحَدُهُمْ بِمَسْكَنِهِ فِي الْجَنَّةِ أَدَلُّ بِمَنْزِلِهِ كَانَ فِي الدُّنْيَا ". وَقَالَ يُونُسُ بْنُ مُحَمَّدٍ حَدَّثَنَا شَيْبَانُ عَنْ قَتَادَةَ حَدَّثَنَا أَبُو الْمُتَوَكِّلِ.
Amesimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Waumini watakaposalimika na moto, watazuiliwa darajani baina ya moto na Jannah, mahali ambapo watalipizana kisasi kwa dhulma walizofanyiana baina yao duniani. Watakapotakaswa na madhambi yao, wataingizwa Jannah. Naapa kwa Yule Ambaye nafsi ya Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) imo Mikononi Mwake, kila mmoja atatambua makazi yake Jannah zaidi kuliko anavyotambua makazi yake duniani.” [Al-Bukhaariy – Kitaab Al-Madhwaalim (46)]
[4] Kunusuru Dini Ya Allaah:
Hii ni sawa na Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَيَنصُرَنَّ اللَّـهُ مَن يَنصُرُهُ ۗ
“Na bila shaka Allaah Atamnusuru yeyote yule anayenusuru Dini Yake.” [Al-Hajj (22:40)]
Na Tafsiyr ya Imaam As-Sa’diy (رحمه الله):
Hii ni Amri ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Waumini wamnusuru Allaah kwa kusimamisha Dini Yake, kuwalingania watu Kwake, kufanya Jihaad dhidi ya maadui Wake, na kukusudia kwa yote hayo Wajihi wa Allaah. Watakapofanya hivyo, Allaah Atawanusuru na Atawathibitisha miguu yao, yaani: Ataunga nyoyo zao kwa subira na utulivu na uthabiti, Atawapa uvumilivu wa kimwili na Atawasaidia dhidi ya maadui zao. Hii ni Ahadi kutoka kwa Yule Ambaye Ni Mkarimu na Mkweli katika Ahadi Zake kwamba yeyote anayeunga mkono jambo Lake kwa kauli na matendo, basi Rabb Wake Atamsaidia na kumpa njia ya ushindi kama vile uthabiti na kadhaalika. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[5] Makafiri Wanatakiwa Watembee Maeneo Mbalimbali Wakatambue Hatima Za Waliokanusha Kabla Yao:
Rejea Al-An’aam (6:11).
[6] Katika Jannah (Pepo) Kuna Mito:
Hadiyth ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنَا فُلَيْحٌ، عَنْ هِلاَلِ بْنِ عَلِيٍّ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَبِرَسُولِهِ وَأَقَامَ الصَّلاَةَ وَصَامَ رَمَضَانَ، كَانَ حَقًّا عَلَى اللَّهِ أَنْ يُدْخِلَهُ الْجَنَّةَ جَاهَدَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ، أَوْ جَلَسَ فِي أَرْضِهِ الَّتِي وُلِدَ فِيهَا ". فَقَالُوا يَا رَسُولَ اللَّهِ أَفَلاَ نُبَشِّرُ النَّاسَ. قَالَ " إِنَّ فِي الْجَنَّةِ مِائَةَ دَرَجَةٍ أَعَدَّهَا اللَّهُ لِلْمُجَاهِدِينَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ، مَا بَيْنَ الدَّرَجَتَيْنِ كَمَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ، فَإِذَا سَأَلْتُمُ اللَّهَ فَاسْأَلُوهُ الْفِرْدَوْسَ، فَإِنَّهُ أَوْسَطُ الْجَنَّةِ وَأَعْلَى الْجَنَّةِ، أُرَاهُ فَوْقَهُ عَرْشُ الرَّحْمَنِ، وَمِنْهُ تَفَجَّرُ أَنْهَارُ الْجَنَّةِ ". قَالَ مُحَمَّدُ بْنُ فُلَيْحٍ عَنْ أَبِيهِ " وَفَوْقَهُ عَرْشُ الرَّحْمَنِ ".
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Yeyote anayemuamini Allaah na Rasuli Wake, akasimamisha Swalaah na akafunga (Swiyaam) Ramadhwaan, imekuwa haki juu ya Allaah kumuingiza Jannah (Peponi), ni sawa ikiwa amepigana katika Njia ya Allaah au ameketi nchini mwake alimozaliwa.” Watu wakasema: Ee Rasuli wa Allaah! Je, tuwape bishara hii watu? Akasema (صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika katika Jannah kuna daraja mia moja ambazo Allaah Amewaandalia Mujaahidina wanaopigana katika Njia ya Allaah, na masafa baina ya daraja mbili ni baina ya mbingu na ardhi. Hivyo, mnapomuomba Allaah, muombeni (Jannah ya) Al-Firdaws, kwani ndiyo iliyo nzuri (katikati) na ya juu zaidi Peponi.” Naona alisema: “Na juu yake (Al-Firdaws) kipo Kiti cha Enzi cha Ar-Rahmaan (Allaah), na kwayo kunachepuza mito ya Jannah.” Na imepokewa toka kwa Muhammad bin Fulayh kutoka kwa babake kwamba, “Na juu yake kuna Kiti cha Enzi cha Ar-Rahmaan.” [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Jihaad Was-Sayr (56)]
[8] Yanayopelekea Kutambua Ujuzi Wa Laa Ilaaha Illa-Allaah:
Tafsiyr ya Imaam As-Sa’diy (رحمه الله):
Kulijua ipasavyo neno “Laa Ilaaha Illa Allaah” kunahitajia moyo kulikiri na kulijua, kwa maana kwamba Rasuli (pamoja na sisi) anatakiwa alijue neno hilo inavyotakikana, halafu akamilishe ujuzi huo kwa kutenda kwa mujibu wa vipengele vyake.
Ilimu hiyo ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Ameiamuru - ambayo ni ilimu ya Tawhiyd (Kumpwekesha Allaah) ni fardhw ‘ayn (faradhi kwa kila mtu binafsi), kwa kila mwanaadam, na haisamehewi kwa yeyote yule, na haijalishi yeye ni nani. Bali kila mtu amewajibika kuijua. Na njia ya kujua kwamba hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye (Allaah عزّ وجلّ) ni kwa haya yafuatayo:
(i) Ya kwanza bali iliyo kuu kabisa ni kuzingatia Majina Yake (Allaah عزّ وجلّ) na Sifa Zake na Matendo Yake yanayodalilisha Ukamilifu Wake, na U’adhwama Wake, na Ujalali Wake, kwani yanampelekea mtu kufanya jitihada ya kujisabilia Kwake, na kumwamudu Rabb Anayemiliki Majina Mazuri Kabisa Na Sifa, na Ambaye Himdi zote ni Zake, Utukufu, Ujalali na Uzuri.
(ii) Kujua kwamba Yeye (Allaah عزّ وجلّ) Ndiye Muumbaji Pekee na Msimamizi. Hivyo basi mtu atambue kuwa Yeye (Allaah عزّ وجلّ) Ndiye Pekee Mwenye Kustahiki kuabudiwa.
(iii) Kujua kwamba Yeye (Allaah عزّ وجلّ) Ndiye Pekee Mwenye Neema za dhahiri (zinazoonekana) na za siri (zisizoonekana) za kidini na za kidunia. Kujua hilo kunaulazimisha moyo kushikamana Naye na Kumpenda na kujisabilia Kwake Yeye Pekee, Asiye na mshirika.
(iv) Yale tunayoyaona na kuyasikia juu ya malipo kwa mawalii Wake waliosimamisha Tawhiyd Yake (Allaah عزّ وجلّ), kama vile ushindi na neema za haraka za hapa duniani, pamoja na adhabu zake kwa maadui Zake wanaomshirikisha, hayo yote ni chachu ya kujua kwamba Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Pekee Anayestahiki kuelekezewa ibaada zote.
(v) Kujua hali halisi ya masanamu na mizimu na wanaolinganishwa sawa na Allaah (سبحانه وتعالى) ambao wanaabudiwa pamoja na Allaah, na kufanywa ni waabudiwa, na kwamba hao ni wenye upungufu kwa kila upande, ni madhaifu wa dhati, hawana uwezo wa kujinufaisha au kujidhuru nafsi zao wala kwa wanaowaabudia, wala hawana uwezo wa kufisha, wala kuhuisha, wala kufufua, wala hawawezi kuwanusuru wanaowaabudia, wala hawawezi kuwanufaisha hata kwa uzito wa chembe ya atomu kwa kuleta kheri au kukinga shari. Basi kwa kujua hayo, kunawajibisha kujua kwamba hapana Mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na kwamba miungu inayoabudiwa badala Yake (Allaah عزّ وجلّ) ni ya uongo.
(vi) Vitabu vya Allaah vyote vimeafikiana juu ya hilo (Neno la Tawhiyd; laa ilaaha illa-Allaah) na vyote kimoja baada ya kingine vimeelezea hilo.
(vii) Viumbe bora kabisa ambao wamekamilika katika khulqa (tabia) njema, akili, busara, fikira sahihi, hikma, na ilimu, yaani Rusuli wa Allaah na Manabii na ‘Ulamaa wenye taqwa, wameshuhudia hayo (kwamba laa ilaaha illa-Allaah).
(viii) Ishara za kilimwengu na za kinafsi (namna tulivyoumbwa) Alizozisimamisha Allaah na ambazo zinaonyesha kwamba Yeye Ni Mmoja Asiye na mshirika, ndizo dalili kubwa kuliko zote. Dalili hizi kwa namna Alivyoziumba kwa uzuri wa ajabu, kwa umadhubuti usiyo na kombo, na kwa uumbaji wa ajabu, zote zinamtangaza Allaah kwa jinsi zilivyo kwa namna ya kipekee kabisa isiyo na ruwaza. Ishara hizi ambazo Allaah Amekithirisha kwazo kuwazindusha viumbe, Akiwajulisha kwamba hakuna mwingine wa kuabudiwa isipokuwa Yeye, Akazieleza katika Kitabu Chake na Akazitawanya kote kote, ikiwa mtu atataamuli kwa kina baadhi yake tu, basi ni lazima atapata yakini na ujuzi wa kweli wa maana ya kumpwekesha Allaah (Tawhiyd). Sasa hali itakuwa vipi ikiwa dalili zote zitakusanyika pamoja, zikaoana, zikakubaliana na zikasimama toka pande zote?! Hapa ndipo pale iymaan na ujuzi wa hilo vinapojikita na kutuama ndani ya moyo wa mja na kuwa mithili ya mlima mrefu usiyoweza kutikiswa na shubha au dhana hewa, bali huzidi nguvu na ustawi kila mtu anapokutana na upotoshaji na propaganda chafuzi. Mwisho wa yote, unabakia mlango mkubwa na mpana zaidi wa kumwezesha mtu kuijua Tawhiyd kwa mapana yake na marefu yake. Mlango huu ni kuizingatia Qur-aan Tukufu na kuzitafakari Aayaat zake, na hili halipatikani toka chanzo kingine chochote isipokuwa humo.
[Tafsiyr As-Sa’diy]
[9] Nyoyo Zenye Maradhi Ya Kufru, Shirki, Unafiki, Shaka, Matamanio, Ukaidi Wa Kukubali Haqq, Maasi Na Kila Aina Ya Maovu:
Rejea Al-Hajj (22:46) kwenye uchambuzi na rejea mbalimbali kuhusu moyo uliopofuka na nyoyo zenye maradhi na moyo uliosalimika.
Ama kuhusu nyoyo zenye maradhi, rejea Suwrah na Aayah zifuatazo: Al-Baqarah (2:10), Al-Maaidah (5:52), Al-Anfaal (8:49), At-Tawbah (9:125), Al-Hajj (22:53), An-Nuwr (24:50), Al-Ahzaab (33:12), (33:32), (33:60), Suwrah hii ya Muhammad (47:29), Al-Muddath-thir (74:31).
[10] Kuunga Undugu Wa Uhusiano Wa Damu Na Hatari Za Kutokuunga:
Umuhimu wa kuunga udugu wa uhusiano wa damu umesisitizwa katika Qur-aan na Sunnah na Fadhila zake ni nyingi na adhimu mno. Miongoni mwazo ni kumiminikiwa rizki na umri mrefu.
عن أنسٍ رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( من أحَبَّ أنْ يُبْسَطَ لَهُ في رِزْقِهِ ، ويُنْسأَ لَهُ في أثَرِهِ ، فَلْيَصِلْ رَحِمَهُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Anayependa akunjuliwe riziki yake, na arefushiwe maisha yake, basi aunge kizazi chake." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuud]
Kukata undugu ni tatizo sugu la jamii ya Kiislamu na linachukuliwa kuwa ni jepesi ilhali ni zito mno kutokana na hatari zake kubwa kabisa! Miongoni mwazo ni kama inavyotajwa katika Aayah tukufu inayofuatia ya namba (23) kuwa Laana ya Allaah inamfikia mwenye kukata undugu. Pia hatari zake zimetajwa katika Hadiyth kadhaa ikiwa ni pamoja na kutokuingizwa mtu Peponi na kukatwa na Allaah (عزّ وجلّ) kama ilivyothibiti katika Hadiyth zifuatazo:
عن أَبي محمد جبيرِ بن مطعم رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : لاَ يَدْخُلُ الجَنَّةَ قَاطِعٌ . قَالَ سفيان في روايته : يَعْنِي قَاطِع رَحِم . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Amesimulia Abuu Muhammad Jubayr bin Mutw‘im (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hatoingia Jannah mwenye kukata (uhusiano wa damu).” [Al-Bukhaariy na Muslim, At-Tirmidhiy]
عن عائشة ، قَالَتْ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم : الرَّحِمُ مُعَلَّقَةٌ بِالعَرْشِ تَقُولُ : مَنْ وَصَلَنِي ، وَصَلَهُ اللهُ ، وَمَنْ قَطَعَنِي ، قَطَعَهُ اللهُ . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Kizazi kimetundikwa katika 'Arshi, kinasema: Anayeniunga, Allaah Atamuunga, na anayenikata, Allaah Atamkata." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida tele:
Kukata Undugu [308]
[11] Nyoyo Zenye Maradhi:
Rejea Suwrah hii Muhammad (47:20).
Rejea pia Al-Hajj (22:46) kwenye maelezo kuhusu moyo uliopofuka na faida nyenginezo.
Rejea pia Ash-Shu’araa (26:88-89) kwenye ufafanuzi na maelezo kuhusu moyo uliosalimika.
الْفَتْح
048-Al-Fat-h
048-Al-Fat-h: Utangulizi Wa Suwrah [310]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا﴿١﴾
1. Hakika Tumekupa ushindi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), ushindi bayana.[1]
لِّيَغْفِرَ لَكَ اللَّـهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ وَيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَيَهْدِيَكَ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا﴿٢﴾
2. Ili Allaah Akughufurie yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayofuatia, na Akutimizie Neema Yake juu yako, na Akuongoze njia iliyonyooka.
وَيَنصُرَكَ اللَّـهُ نَصْرًا عَزِيزًا﴿٣﴾
3. Na Akunusuru Allaah nusura yenye nguvu kabisa.
هُوَ الَّذِي أَنزَلَ السَّكِينَةَ فِي قُلُوبِ الْمُؤْمِنِينَ لِيَزْدَادُوا إِيمَانًا مَّعَ إِيمَانِهِمْ ۗ وَلِلَّـهِ جُنُودُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَكِيمًا﴿٤﴾
4. Yeye Ndiye Aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za Waumini ili wazidi imaan pamoja na imaan zao. Na ni ya Allaah Pekee majeshi ya mbinguni na ardhini. Na Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
لِّيُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَيُكَفِّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عِندَ اللَّـهِ فَوْزًا عَظِيمًا﴿٥﴾
5. Ili Awaingize Waumini wa kiume na Waumini wa kike Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo, na Awafutie maovu yao. Na hayo ndiyo mafanikio makubwa zaidi mbele ya Allaah.[2]
وَيُعَذِّبَ الْمُنَافِقِينَ وَالْمُنَافِقَاتِ وَالْمُشْرِكِينَ وَالْمُشْرِكَاتِ الظَّانِّينَ بِاللَّـهِ ظَنَّ السَّوْءِ ۚ عَلَيْهِمْ دَائِرَةُ السَّوْءِ ۖ وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ وَلَعَنَهُمْ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا﴿٦﴾
6. Na Awaadhibu wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike na washirikina wa kiume na washirikina wa kike, wanaomdhania Allaah dhana ovu. Utawafikia hao mgeuko mbaya. Na Allaah (pamoja na hayo) Amewaghadhibikia, Amewalaani, na Amewaandalia Jahannam. Na paovu palioje mahali pa kuishia!
وَلِلَّـهِ جُنُودُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا﴿٧﴾
7. Na ni ya Allaah Pekee majeshi ya mbinguni na ardhini. Na Allaah daima Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.
إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا﴿٨﴾
8. Hakika Sisi Tumekutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ukiwa ni shahidi, mwenye kubashiri na mwonyaji.
لِّتُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتُعَزِّرُوهُ وَتُوَقِّرُوهُ وَتُسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا﴿٩﴾
9. Ili mumwamini Allaah na Rasuli Wake, na mumsaidie kwa taadhima, na mumheshimu kwa utukuzo (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), na mumsabbih (Allaah سبحانه وتعالى) asubuhi na jioni.
إِنَّ الَّذِينَ يُبَايِعُونَكَ إِنَّمَا يُبَايِعُونَ اللَّـهَ يَدُ اللَّـهِ فَوْقَ أَيْدِيهِمْ ۚ فَمَن نَّكَثَ فَإِنَّمَا يَنكُثُ عَلَىٰ نَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِمَا عَاهَدَ عَلَيْهُ اللَّـهَ فَسَيُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا﴿١٠﴾
10. Hakika wale waliofungamana ahadi ya utiifu nawe, hakika hapana ila wanafungamana ahadi ya utiifu na Allaah, Mkono wa Allaah[3] Uko juu ya mikono yao. Basi atakayevunja ahadi, hakika hapana ila anavunja dhidi ya nafsi yake. Na yeyote atimizaye yale aliyomuahidi Allaah, basi Atampa ujira adhimu.
سَيَقُولُ لَكَ الْمُخَلَّفُونَ مِنَ الْأَعْرَابِ شَغَلَتْنَا أَمْوَالُنَا وَأَهْلُونَا فَاسْتَغْفِرْ لَنَا ۚ يَقُولُونَ بِأَلْسِنَتِهِم مَّا لَيْسَ فِي قُلُوبِهِمْ ۚ قُلْ فَمَن يَمْلِكُ لَكُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا إِنْ أَرَادَ بِكُمْ ضَرًّا أَوْ أَرَادَ بِكُمْ نَفْعًا ۚ بَلْ كَانَ اللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا﴿١١﴾
11. Watakuambia mabedui waliobaki nyuma: Zimetushughulisha mali zetu na ahli zetu, basi tuombee maghfirah. Wanasema kwa ndimi zao yasiyokuwemo nyoyoni mwao. Sema: Nani basi atayekuwa na uwezo kuzuia chochote toka kwa Allaah Akikusudia kukudhuruni au Akikusudia kukunufaisheni? Bali Allaah daima kwa yale myatendayo, Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
بَلْ ظَنَنتُمْ أَن لَّن يَنقَلِبَ الرَّسُولُ وَالْمُؤْمِنُونَ إِلَىٰ أَهْلِيهِمْ أَبَدًا وَزُيِّنَ ذَٰلِكَ فِي قُلُوبِكُمْ وَظَنَنتُمْ ظَنَّ السَّوْءِ وَكُنتُمْ قَوْمًا بُورًا﴿١٢﴾
12. Bali mlidhania kwamba Rasuli na Waumini hawatorudi kwa ahli zao abadani, na likapambwa hilo katika nyoyo zenu, na mkadhania dhana ovu, na mkawa watu wa kuangamia.
وَمَن لَّمْ يُؤْمِن بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ فَإِنَّا أَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ سَعِيرًا﴿١٣﴾
13. Na asiyemuamini Allaah na Rasuli Wake, basi hakika Sisi Tumewaandalia makafiri moto uliowashwa vikali mno.
وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ يَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا﴿١٤﴾
14. Na ni wa Allaah Pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Anamghufuria Amtakaye, na Anamuadhibu Amtakaye. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
سَيَقُولُ الْمُخَلَّفُونَ إِذَا انطَلَقْتُمْ إِلَىٰ مَغَانِمَ لِتَأْخُذُوهَا ذَرُونَا نَتَّبِعْكُمْ ۖ يُرِيدُونَ أَن يُبَدِّلُوا كَلَامَ اللَّـهِ ۚ قُل لَّن تَتَّبِعُونَا كَذَٰلِكُمْ قَالَ اللَّـهُ مِن قَبْلُ ۖ فَسَيَقُولُونَ بَلْ تَحْسُدُونَنَا ۚ بَلْ كَانُوا لَا يَفْقَهُونَ إِلَّا قَلِيلًا﴿١٥﴾
15. Waliobakia nyuma pale mtakapotoka kuelekea kwenye ghanima ili mzichukue watasema: Tuacheni tukufuateni! Wanataka kubadilisha Maneno ya Allaah. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hamtotufuata! Hivyo ndivyo Alivyosema Allaah kabla. Basi watasema: Hapana, bali mnatuhusudu! Hapana! Bali walikuwa hawafahamu isipokuwa kidogo.
قُل لِّلْمُخَلَّفِينَ مِنَ الْأَعْرَابِ سَتُدْعَوْنَ إِلَىٰ قَوْمٍ أُولِي بَأْسٍ شَدِيدٍ تُقَاتِلُونَهُمْ أَوْ يُسْلِمُونَ ۖ فَإِن تُطِيعُوا يُؤْتِكُمُ اللَّـهُ أَجْرًا حَسَنًا ۖ وَإِن تَتَوَلَّوْا كَمَا تَوَلَّيْتُم مِّن قَبْلُ يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا﴿١٦﴾
16. Waambie (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) waliobakia nyuma miongoni mwa mabedui: Mtaitwa kuwakabili watu wenye nguvu kali zaidi mpigane nao, au wasalimu amri. Lakini mkitii, Allaah Atakupeni ujira mzuri, na mkikengeuka kama mlivyokengeuka kabla Atakuadhibuni adhabu iumizayo.
لَّيْسَ عَلَى الْأَعْمَىٰ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْأَعْرَجِ حَرَجٌ وَلَا عَلَى الْمَرِيضِ حَرَجٌ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ وَمَن يَتَوَلَّ يُعَذِّبْهُ عَذَابًا أَلِيمًا﴿١٧﴾
17. Hakuna dhambi juu ya kipofu, wala hakuna dhambi juu ya kilema, na wala hakuna dhambi juu ya mgonjwa (wasipokwenda vitani). Na yeyote atakayemtii Allaah na Rasuli Wake, (Allaah) Atamuingiza Jannaat zipitazo chini yake mito. Na atakayekengeuka, Atamuadhibu adhabu iumizayo.
لَّقَدْ رَضِيَ اللَّـهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَنزَلَ السَّكِينَةَ عَلَيْهِمْ وَأَثَابَهُمْ فَتْحًا قَرِيبًا﴿١٨﴾
18. Kwa yakini Allaah Amewawia radhi Waumini walipofungamana nawe ahadi ya utiifu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) chini ya mti[4], (Allaah) Alijua yale yaliyomo nyoyoni mwao, basi Akawateremshia utulivu, na Akawalipa ushindi wa karibu.
وَمَغَانِمَ كَثِيرَةً يَأْخُذُونَهَا ۗ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا﴿١٩﴾
19. Na ghanima nyingi watakazozichukua. Na Allaah daima Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
وَعَدَكُمُ اللَّـهُ مَغَانِمَ كَثِيرَةً تَأْخُذُونَهَا فَعَجَّلَ لَكُمْ هَـٰذِهِ وَكَفَّ أَيْدِيَ النَّاسِ عَنكُمْ وَلِتَكُونَ آيَةً لِّلْمُؤْمِنِينَ وَيَهْدِيَكُمْ صِرَاطًا مُّسْتَقِيمًا﴿٢٠﴾
20. Allaah Amekuahidini ghanima nyingi mtazichukua, Akakuharakizieni hizi, na Akazuia mikono ya watu dhidi yenu, na ili iwe Aayah (Ishara) kwa Waumini (wazingatie), na Akuongozeni njia iliyonyooka.
وَأُخْرَىٰ لَمْ تَقْدِرُوا عَلَيْهَا قَدْ أَحَاطَ اللَّـهُ بِهَا ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرًا﴿٢١﴾
21. Na nyenginezo hamkuwa na uwezo nazo, Allaah Amekwishazizingia. Na Allaah daima juu ya kila kitu Ni Muweza.
وَلَوْ قَاتَلَكُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوَلَّوُا الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يَجِدُونَ وَلِيًّا وَلَا نَصِيرًا﴿٢٢﴾
22. Na kama wangelipigana nanyi wale waliokufuru, basi wangeligeuza migongo yao, kisha wasipate mlinzi yoyote wala mwenye kunusuru.
سُنَّةَ اللَّـهِ الَّتِي قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلُ ۖ وَلَن تَجِدَ لِسُنَّةِ اللَّـهِ تَبْدِيلًا﴿٢٣﴾
23. Desturi ya Allaah ambayo imekwishapita kabla, na wala hutapata mabadiliko katika Desturi ya Allaah.[5]
وَهُوَ الَّذِي كَفَّ أَيْدِيَهُمْ عَنكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ عَنْهُم بِبَطْنِ مَكَّةَ مِن بَعْدِ أَنْ أَظْفَرَكُمْ عَلَيْهِمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرًا﴿٢٤﴾
24. Naye Ndiye Aliyeizuia mikono yao dhidi yenu na mikono yenu dhidi yao katikati ya Makkah baada ya kukupeni ushindi juu yao. Na Allaah daima Ni Mwenye Kuona yale myatendayo.[6]
هُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوكُمْ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَالْهَدْيَ مَعْكُوفًا أَن يَبْلُغَ مَحِلَّهُ ۚ وَلَوْلَا رِجَالٌ مُّؤْمِنُونَ وَنِسَاءٌ مُّؤْمِنَاتٌ لَّمْ تَعْلَمُوهُمْ أَن تَطَئُوهُمْ فَتُصِيبَكُم مِّنْهُم مَّعَرَّةٌ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۖ لِّيُدْخِلَ اللَّـهُ فِي رَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ ۚ لَوْ تَزَيَّلُوا لَعَذَّبْنَا الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا﴿٢٥﴾
25. Wao ndio wale waliokufuru na wakakuzuieni na Al-Masjidil-Haraam, na wanyama wa kuchinjwa wakazuiliwa kufika mahali pa kuchinjwa. Na ingekuwa si wanaume Waumini na wanawake Waumini msiowajua nyinyi, mkawasaga kuwaua, na kwa sababu yao yakakusibuni madhambi (na fedheha) bila ya kujua (basi Angeliwaacheni muwamalize), ili Allaah Amuingize katika Rehma Yake Amtakaye. Na lau kama (Waumini na makafiri) wangelitengana, basi Tungeliwaadhibu wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo.
إِذْ جَعَلَ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي قُلُوبِهِمُ الْحَمِيَّةَ حَمِيَّةَ الْجَاهِلِيَّةِ فَأَنزَلَ اللَّـهُ سَكِينَتَهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ وَعَلَى الْمُؤْمِنِينَ وَأَلْزَمَهُمْ كَلِمَةَ التَّقْوَىٰ وَكَانُوا أَحَقَّ بِهَا وَأَهْلَهَا ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا﴿٢٦﴾
26. Pale waliokufuru walipotia katika nyoyo zao ghadhabu na kiburi; ghadhabu na kiburi za ujahili, na Allaah Akateremsha utulivu Wake juu ya Rasuli Wake na juu ya Waumini, na Akawalazimisha neno la taqwa (laa ilaaha illa-Allaah), na wakawa ndio wenye haki zaidi kwalo na wenye kustahiki. Na Allaah daima Ni Mjuzi wa kila kitu.[7]
لَّقَدْ صَدَقَ اللَّـهُ رَسُولَهُ الرُّؤْيَا بِالْحَقِّ ۖ لَتَدْخُلُنَّ الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ إِن شَاءَ اللَّـهُ آمِنِينَ مُحَلِّقِينَ رُءُوسَكُمْ وَمُقَصِّرِينَ لَا تَخَافُونَ ۖ فَعَلِمَ مَا لَمْ تَعْلَمُوا فَجَعَلَ مِن دُونِ ذَٰلِكَ فَتْحًا قَرِيبًا﴿٢٧﴾
27. Kwa yakini Allaah Amemsadikisha Rasuli Wake ndoto kwa haki. Bila shaka mtaingia Al-Masjidul-Haraam In Shaa Allaah mkiwa katika amani, wenye kunyoa vichwa vyenu na wenye kupunguza,[8] hamtakuwa na khofu. Ameyajua ambayo hamkuyajua, Akajaalia kabla ya hayo ushindi wa karibu.[9]
هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا﴿٢٨﴾
28. Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote. Na Allaah Anatosha kuwa Ni Shahidi.[10]
مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا ۖ سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ۚ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ ۚ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ ۗ وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا﴿٢٩﴾
29. Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Rasuli wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri wanahurumiana baina yao. Utawaona wakirukuu na wakisujudu wakitafuta fadhila na radhi kutoka kwa Allaah. Alama zao dhahiri zi katika nyuso zao kutokana na athari za sujudu. Huo ni mfano wao katika Tawraat na mfano wao katika Injiyl. Ni kama mmea umetoa chipukizi lake, likautia nguvu kisha likawa nene, kisha likasimama sawasawa juu ya shina lake, linawapendeza wakulima, ili liwatie ghaidhi makafiri. Allaah Amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema miongoni mwao Maghfirah na ujira adhimu.[11]
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah/Ghazwat Hudaybiyah (Vita Vitukufu Vya Hudaybiyah):
Bonyeza kiungo kifuatacho:
048-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Fat-h Aayah 01-5: إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُّبِينًا [311]
Vita vitukufu vya Hudaybiyah vimetajwa katika Aayah zifuatazo za Suwrah hii Al-Fat-h:
(1-4), (10-13), (15-16), (19-24), (26-27)
Na kuna Sababun-Nuzuwl nyenginezo ambazo zinaelezea tukio la ghazwa hii tukufu. Mojawapo ambayo inaelezea kirefu tukio hili ni ya Aayah namba (24-26).
[3] ‘Aqiydah Sahihi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Ni Kuthibisha Sifa Za Allaah.
Kuthibitisha Sifa za Allaah (سبحانه وتعالى) kama hii ya Mkono inawajibika kwa Waumini kwa kuwa ndio itikadi Sahihi ya Ahlus-Sunnah wal-Jama’ah. Baadhi ya Aayah ambazo Allaah (سبحانه وتعالى) Ametaja Sifa hii ya Mkono au Mikono Yake zimo katika Suwrah Swaad (38:75), Al-Maaidah (5:64), Az-Zumar (39:67). Rejea pia Huwd (11:37) kwenye maelezo bayana. Na dalili katika Sunnah ni Hadiyth zifuatazo:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " يَقْبِضُ اللَّهُ الأَرْضَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، وَيَطْوِي السَّمَاءَ بِيَمِينِهِ ثُمَّ يَقُولُ أَنَا الْمَلِكُ أَيْنَ مُلُوكُ الأَرْضِ ". وَقَالَ شُعَيْبٌ وَالزُّبَيْدِيُّ وَابْنُ مُسَافِرٍ وَإِسْحَاقُ بْنُ يَحْيَى عَنِ الزُّهْرِيِّ عَنْ أَبِي سَلَمَةَ.
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Siku ya Qiyaamah, Allaah Ataishika ardhi yote na Ataikunja mbingu kwa Mkono Wake wa kuume, kisha Atasema: Mimi Ndiye Mfalme, wako wapi wafalme wa ardhini?” [Al-Bukhaariy]
عَنْ أَنَسٍ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " يُجْمَعُ الْمُؤْمِنُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَيَقُولُونَ لَوِ اسْتَشْفَعْنَا إِلَى رَبِّنَا، فَيُرِيحُنَا مِنْ مَكَانِنَا هَذَا. فَيَأْتُونَ آدَمَ فَيَقُولُونَ لَهُ أَنْتَ آدَمُ أَبُو الْبَشَرِ خَلَقَكَ اللَّهُ بِيَدِهِ وَأَسْجَدَ لَكَ الْمَلاَئِكَةَ وَعَلَّمَكَ أَسْمَاءَ كُلِّ شَىْءٍ، فَاشْفَعْ لَنَا إِلَى رَبِّنَا حَتَّى يُرِيحَنَا. فَيَقُولُ لَهُمْ لَسْتُ هُنَاكُمْ. فَيَذْكُرُ لَهُمْ خَطِيئَتَهُ الَّتِي أَصَابَ ".
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Waumini watakusanywa Siku ya Qiyaamah, kisha watasema: Lau tutamtizama mtu ambaye atatushufaia (atatuombea) kwa Rabb wetu ili Atufariji na Atuondoe sehemu yetu hii. Kwa hiyo, watakwenda kwa (Nabiy) Aadam (عليه السّلام) kisha watasema: Wewe ni Aadam, baba wa wanaadam, Allaah Amekuumba kwa Mkono Wake na Akawaamuru Malaika wakusujudie, na Akakufundisha majina ya kila kitu, kwa hiyo, tushufaie kwa Rabb wetu ili Atufariji (na Atuondoe hapa tulipo). (Nabiy) Aadam (عليه السّلام) atasema: Mimi siye mwenyewe wa jambo hilo! Naye atawatajia makosa yake aliyoyafanya.” [Al-Bukhaariy Kitaab At-Tawhiyd]
عَنْ أَبِي مُوسَى عَبْدِ الله بنِ قَبَسٍ الأَشْعَرِيِّ (رضي الله عنه) عن النَّبيّ (صلى الله عليه و آله وسلم) قال: ((إِنَّ اللَّهَ تَعَالَى يَبْسُطُ يَدَهُ بِاللَّيْلِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ النَّهَارِ وَيَبْسُطُ يَدَهُ بِالنَّهَارِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ اللَّيْلِ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِهَا)) رواه مسلم
Amesimulia Abuu Muwsaa ‘Abdillaah bin Qays Al-Ash‘ariyy (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Anakunjua Mkono Wake usiku ili Apokee tawbah ya mkoseaji mchana. Na Anakunjua Mkono Wake mchana ili Apokee tawbah ya mkoseaji usiku mpaka jua lichomoze tokea Magharibi hapo mlango wa toba utafungwa).” [Muslim]
[4] Bay’atur-Ridhwaan (Bay’ah Ya Radhi Za Allaah), Bay’ah Ahlish-Shajarah (Bay’ah Ya Watu Wa Mti)
Bay’ah ni fungamano ya Ahadi ya utiifu na kusaidiana.
Na bay’ah hii ya Ridhwaan inajulikana pia kuwa ni Bay’ah Ahlish-Shajarah yaani: Fungamano la Ahadi la watu wa mti [Tafsiyr As-Sa’diy] kwa kuwa Swahaba walifungamana Ahadi ya utiifu na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) chini ya mti.
[7] Ghadhabu Za Kiburi Za Washirikina:
Kumbuka plae wale waliokanusha walipoingiza ndani ya nyoyo zao ghera, ghera za watu wa zama za ujinga, ili wasikubali Urasuli wa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Na miongoni mwa hayo ni kule kukataa kwao kuandika:
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
katika mapatano ya Ḥudaybiyah, na wakakataa kuandika: “Haya ndiyo yale aliyoyapitisha Muhammad, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)”. Na hapo Allaah Akamteremshia utulivu Rasuli Wake na Waumini walio pamoja na yeye, Akawathibitishia Neno
لا إلهَ إلاّ اللّهُ
Laa ilaah illa-Allaah
ambalo ndio kichwa cha taqwa yote. Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Waumini walio pamoja na yeye ndio wanaostahiki zaidi neno la taqwa kuliko washirikina. Na hivyo ndivyo walivyokuwa, walistahiki neno hili na sio washirikina. Na Allaah daima ni Mjuzi wa kila kitu, hakuna kitu chochote kinachofichamana Kwake. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[8] Kupunguza Nywele Au Kunyoa Baada Ya ‘Umrah Au Hajj:
Mwenye kutekeleza ‘Umrah au Hajj anapaswa apunguze nywele au anyoe, jambo ambalo ni mojawapo ya matendo ya kuyajua katika Ihraam. Lakini kunyoa imependekezwa zaidi na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na Hadiyth ifuatayo kuwa aliwaombea walionyoa mara zaidi kuliko waliopunguza:
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ ـ رضى الله عنهما ـ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " اللَّهُمَّ ارْحَمِ الْمُحَلِّقِينَ ". قَالُوا وَالْمُقَصِّرِينَ يَا رَسُولَ اللَّهِ قَالَ " اللَّهُمَّ ارْحَمِ الْمُحَلِّقِينَ ". قَالُوا وَالْمُقَصِّرِينَ يَا رَسُولَ اللَّهِ قَالَ " وَالْمُقَصِّرِينَ ". وَقَالَ اللَّيْثُ حَدَّثَنِي نَافِعٌ " رَحِمَ اللَّهُ الْمُحَلِّقِينَ " مَرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ. قَالَ وَقَالَ عُبَيْدُ اللَّهِ حَدَّثَنِي نَافِعٌ وَقَالَ فِي الرَّابِعَةِ " وَالْمُقَصِّرِينَ
Amesimulia 'Abdullaah Bin 'Umar (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema, "Ee Allah! Warehemu walionyoa nywele za vichwani mwao." Watu wakasema: Ee Rasuli wa Allah! Na waliozipunguza (waombee). Akasema: "Ee Allaah! Warehemu walionyoa nywele za vichwani mwao." Watu wakasema: Ee Rasuli wa Allah! Na waliozipunguza. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Na waliopunguza nywele za vichwani mwao." Naafi’ alisema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema mara moja au mara mbili: "Ee Allaah! Warehemu walionyoa nywele za vichwani mwao.” Na katika mara ya nne alisema: "Na waliopunguza nywele za vichwani mwao." [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Hajj]
[9] Ndoto Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ya Kutufu Al-Ka’bah Yawa Kweli:
Washirikina wa Makkah walipomzuia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba zake kuingia Makkah ili wasiweze kutekeleza ‘Umrah, Swahaba walihuzunika na wakamlalamikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumtajia raghba zao za kutaka kuingia Makkah. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwataka wavute subira na akawahakikishia kuwa wataingia na watatufu. Yametajwa haya katika Hadiyth ndefu iliyomo katika kiungo kifuatacho cha Sababun-Nuzwul:
[10] Dini Ya Kiislamu Ndio Dini Itakayoshinda Dini Nyenginezo:
Rejea At-Tawbah (9:33) na Asw-Swaff (6:9) kwenye maelezo bayana.
[11] Waumini Wanashikamana Kama Jengo Moja Na Wanapendana Na Kujaliana Na Kuhurumiana:
Hadiyth zifuatazo zimethibitisha:
عَنْ أَبِي مُوسَى (رضي الله عنه) قال: قال رَسُولُ الله (صلى الله عليه و آله وسلم): الْمُؤْمِنَ لِلْمُؤْمِنِ كَالْبُنْيَانِ يَشُدُّ بَعْضُهُ بَعْضاً وَشَبَّكَ أَصَابِعَهُ - متفق عليه
Amesimulia Abuu Muwsa (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Muumin kwa Muumin mwenziwe ni kama jengo, baadhi yake hutilia nguvu baadhi nyingine.” Akaviumanisha vidole vyake. [Al-Bukhaariy na Muslim]
وعن النعمان بن بشير رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: مَثَلُ المُؤْمِنينَ في تَوَادِّهِمْ وتَرَاحُمهمْ وَتَعَاطُفِهمْ، مَثَلُ الجَسَدِ إِذَا اشْتَكَى مِنْهُ عُضْوٌ تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ الجَسَدِ بِالسَّهَرِ والحُمَّى . مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.
Amesimulia An-Nu’maan bin Bashiyr (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mfano wa Waumini katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao na kusaidiana kwao, ni mfano wa mwili, kiungo kimoja kikiumwa basi mwili mzima hukesha kwa homa.” [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]
Muhammad ni Rasuli wa Allaah. Na wale walio pamoja na yeye katika Dini yake, ni wakali juu ya makafiri, lakini wao kwa wao wanahurumiana sana, utawaona wakirukuu na kumsujudia Allaah (عزّ وجلّ) katika Swalaah yao, wakimtarajia Rabb wao Awatunuku Fadhila Zake, Awaingize Jannah (Peponi) na Awe radhi nao. Alama ya utiifu wao kwa Allaah iko wazi kwenye nyuso zao kwa alama ya kusujudu na kuabudu. Hii ndiyo sifa yao kwenye Tawraat, na sifa yao pia katika Injiyl. Ni kama sifa ya mmea wa nafaka uliotoa kijiti chake na tawi lake, kisha matawi yake yakawa mengi baada ya hapo, na mmea ukashikana, ukapata nguvu na ukasimama juu ya kigogo chake ukiwa na mandhari nzuri inayowapendeza wakulima, ili kuwatia hasira kwa Waumini hawa, kwa wingi wao na uzuri wa mandhari yao, makafiri. Katika haya pana dalili ya ukafiri wa wenye kuwachukia Swahaba (رضي الله عنهم) , kwa kuwa yule ambaye Allaah (عزّ وجلّ) Anamtia hasira kwa Swahaba, basi ishapatikana kwake sababu ya hasira nayo ni ukafiri. Allaah (عزّ وجلّ) Amewaahidi waliomuamini Allaah na Rasuli Wake kati yao kughufuriwa dhambi zao na kupewa malipo mema mengi yasiyokatika, nayo ni Jannah (Pepo). Na ahadi ya Allaah ni ya ukweli unaoaminiwa usioenda kinyume. Na kila mwenye kufuata nyayo za Swahaba (رضي الله عنهم), basi yeye anaingia kwenye hukumu yao ya kustahiki maghfirah na malipo makubwa, na wao wana ubora, kutangulia mbele na ukamilifu ambao hakuna yoyote katika ummah huu atakayewafikia, (رضي الله عنهم) na Awaridhishe. [Tafsiyr Al-Muyassar]
الْحُجُرَات
049-Al-Hujuraat
049-Al-Hujuraat: Utangulizi Wa Suwrah [315]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿١﴾
1. Enyi walioamini! Msikadimishe (lolote) mbele ya Allaah na Rasuli Wake. Na mcheni Allaah, hakika Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.[1]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَرْفَعُوا أَصْوَاتَكُمْ فَوْقَ صَوْتِ النَّبِيِّ وَلَا تَجْهَرُوا لَهُ بِالْقَوْلِ كَجَهْرِ بَعْضِكُمْ لِبَعْضٍ أَن تَحْبَطَ أَعْمَالُكُمْ وَأَنتُمْ لَا تَشْعُرُونَ﴿٢﴾
2 Enyi walioamini! Msipandishe sauti zenu juu ya sauti ya Nabiy, na wala msiseme naye kwa sauti ya juu, kama mnavyosemezana wenyewe kwa wenyewe kwa sauti za juu, zisije zikaporomoka amali zenu nanyi hamhisi.[2]
إِنَّ الَّذِينَ يَغُضُّونَ أَصْوَاتَهُمْ عِندَ رَسُولِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ امْتَحَنَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ لِلتَّقْوَىٰ ۚ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ﴿٣﴾
3. Hakika wale wanaoteremsha sauti zao mbele ya Rasuli wa Allaah, hao ndio ambao Allaah Amezichuja nyoyo zao kwa ajili ya taqwa. Watapata maghfirah[3] na ujira adhimu.
إِنَّ الَّذِينَ يُنَادُونَكَ مِن وَرَاءِ الْحُجُرَاتِ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ﴿٤﴾
4. Hakika wale wanaokuita (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) nyuma ya vyumba, wengi wao hawatii akilini.[4]
وَلَوْ أَنَّهُمْ صَبَرُوا حَتَّىٰ تَخْرُجَ إِلَيْهِمْ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٥﴾
5. Na lau kwamba wao wangelisubiri mpaka ukawatokea, bila shaka ingelikuwa ni kheri zaidi kwao. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَن تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ﴿٦﴾
6. Enyi walioamini! Anapokujieni fasiki kwa habari yoyote, basi pelelezeni, msije mkawadhuru watu kwa ujahili, mkawa kuwa wenye kujuta juu ya ambayo mmeyafanya.
وَاعْلَمُوا أَنَّ فِيكُمْ رَسُولَ اللَّـهِ ۚ لَوْ يُطِيعُكُمْ فِي كَثِيرٍ مِّنَ الْأَمْرِ لَعَنِتُّمْ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ حَبَّبَ إِلَيْكُمُ الْإِيمَانَ وَزَيَّنَهُ فِي قُلُوبِكُمْ وَكَرَّهَ إِلَيْكُمُ الْكُفْرَ وَالْفُسُوقَ وَالْعِصْيَانَ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الرَّاشِدُونَ﴿٧﴾
7. Na jueni kwamba pamoja nanyi yuko Rasuli wa Allaah. Lau kama atakutiini katika mambo mengi bila shaka mngelitaabika, lakini Allaah Amekupendezesheeni imaan, na Akaipamba katika nyoyo zenu, na Akakuchukizisheni kufuru, na ufasiki na maasi. Hao ndio walioongoka sawasawa.[5]
فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَنِعْمَةً ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿٨﴾
8. Ni Fadhila kutoka kwa Allaah na Neema. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
وَإِن طَائِفَتَانِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ اقْتَتَلُوا فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا ۖ فَإِن بَغَتْ إِحْدَاهُمَا عَلَى الْأُخْرَىٰ فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّىٰ تَفِيءَ إِلَىٰ أَمْرِ اللَّـهِ ۚ فَإِن فَاءَتْ فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا بِالْعَدْلِ وَأَقْسِطُوا ۖ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ﴿٩﴾
9. Na ikiwa makundi mawili ya Waumini yatapigana, basi suluhisheni[6] baina yao. Lakini mojawapo likikandamiza[7] jengine, basi piganeni na ambalo linakandamiza mpaka lielemee kwenye Amri ya Allaah. Likishaelemea, basi suluhisheni baina yao kwa uadilifu, na tendeni haki. Hakika Allaah Anapenda wenye kutenda haki.[8]
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ﴿١٠﴾
10. Hakika Waumini ni ndugu, basi suluhisheni baina ya ndugu zenu.[9] Na mcheni Allaah ili mpate kurehemewa.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا يَسْخَرْ قَوْمٌ مِّن قَوْمٍ عَسَىٰ أَن يَكُونُوا خَيْرًا مِّنْهُمْ وَلَا نِسَاءٌ مِّن نِّسَاءٍ عَسَىٰ أَن يَكُنَّ خَيْرًا مِّنْهُنَّ ۖ وَلَا تَلْمِزُوا أَنفُسَكُمْ وَلَا تَنَابَزُوا بِالْأَلْقَابِ ۖ بِئْسَ الِاسْمُ الْفُسُوقُ بَعْدَ الْإِيمَانِ ۚ وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿١١﴾
11. Enyi walioamini! Wanaume wasiwafanyie dhihaka na kuwadharau wanaume wengineo asaa wakawa bora kuliko wao, wala wanawake kwa wanawake wengineo, asaa wakawa bora kuliko wao. Na wala msifedheheshane na kutukanana, na wala msiitane majina ya kejeli. Ubaya ulioje kuita jina la ufasiki baada ya imaan![10] Na yeyote asiyetubu, basi hao ndio madhalimu.[11]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ ۖ وَلَا تَجَسَّسُوا وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا ۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ﴿١٢﴾
12. Enyi walioamini! Jiepusheni sana na dhana, kwani hakika baadhi ya dhana ni dhambi. Na wala msichunguzane, na wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi.[12] Je, anapenda mmoja wenu kwamba ale nyama ya nduguye aliyekufa? Basi mmelichukia hilo! Na mcheni Allaah! Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kupokea Tawbah, Mwenye Kurehemu.
يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ﴿١٣﴾
13. Enyi watu! Hakika Sisi Tumekuumbeni kutokana na mwanamme na mwanamke, na Tukakufanyeni mataifa na makabila ili mtambuane. Hakika aliye na hadhi zaidi miongoni mwenu mbele ya Allaah ni mwenye taqwa zaidi kati yenu.[13] Hakika Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Khabari za dhahiri na siri.
قَالَتِ الْأَعْرَابُ آمَنَّا ۖ قُل لَّمْ تُؤْمِنُوا وَلَـٰكِن قُولُوا أَسْلَمْنَا وَلَمَّا يَدْخُلِ الْإِيمَانُ فِي قُلُوبِكُمْ ۖ وَإِن تُطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ لَا يَلِتْكُم مِّنْ أَعْمَالِكُمْ شَيْئًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٤﴾
14. Mabedui walisema: Tumeamini! Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hamkuamini, lakini semeni: Tumesilimu. Kwani imaan haijaingia bado nyoyoni mwenu. Na mtakapomtii Allaah na Rasuli Wake, Hatokupunguzieni katika amali zenu kitu chochote. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ﴿١٥﴾
15. Hakika Waumini ni wale waliomwamini Allaah na Rasuli Wake, kisha wakawa si wenye shaka, na wakafanya Jihaad kwa mali zao na nafsi zao katika Njia ya Allaah. Hao ndio wakweli.[14]
قُلْ أَتُعَلِّمُونَ اللَّـهَ بِدِينِكُمْ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴿١٦﴾
16. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Je, ati ndio mnamjulisha Allaah kuhusu Dini yenu, na hali Allaah Anajua yale yaliyomo mbinguni na yale yaliyomo ardhini? Na Allaah Ni Mjuzi wa kila kitu.
يَمُنُّونَ عَلَيْكَ أَنْ أَسْلَمُوا ۖ قُل لَّا تَمُنُّوا عَلَيَّ إِسْلَامَكُم ۖ بَلِ اللَّـهُ يَمُنُّ عَلَيْكُمْ أَنْ هَدَاكُمْ لِلْإِيمَانِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿١٧﴾
17. Wanadhani wamekufanyia fadhila kwamba wamesilimu? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Msidhani mmenifanyia fadhila kusilimu kwenu. Bali Allaah Amekufanyieni fadhila kwamba Amekuongozeni kwenye imaan mkiwa ni wakweli.
إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ غَيْبَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴿١٨﴾
18. Hakika Allaah Anajua ghaibu ya mbingu na ardhi, na Allaah ni Mwenye Kuona myatendayo.
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
Haramisho La Kutoa Rai Katika Mas-ala Ya Dini Baada Ya Kuthibiti Dalili Katika Qur-aan na Sunnah:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anaamrisha Waumini kufuata Amri Zake na Amri za Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na Anaharamisha mtu kufuata vinginevyo pindi inapothibiti dalili katika Qur-aan na Sunnah. Hivyo basi, rai yoyote ile haipasi kupokelewa. Lakini rai katika Dini zinakubalika pindi inapokuwa haijapatikana dalili iliyo wazi katika mas-ala fulani. Rai hizo hujulikana huwa ni Ijtihaad na pia kama Qiyaas katika upande wa Uswuwl. Dalili ni Hadiyth ifuatayo pale Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomtuma Mu’aadh Bin Jabal (رضي الله عنه) kwenda Yemen akamuuliza maswali ambayo majibu yake yalimridhisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
عَنْ مُعَاذٍ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم حِينَ بَعَثَهُ إِلَى الْيَمَنِ ، فَقَالَ (( كَيْفَ تَصْنَعُ إِنْ عَرَضَ لَكَ قَضَاءٌ؟)) قَالَ : أَقْضِي بِمَا فِي كِتَابِ اللهِ ، قَالَ (( فَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِي كِتَابِ اللهِ؟)) قَالَ : فَسُنَّةُ رَسُولِ الله ، قَالَ : ((فَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِي سُنَّةِ رَسُولِ الله؟)) قَالَ : أَجْتَهِدُ رَأْيِي لاَ آلُو ، قَالَ : فَضَرَبَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم صَدْرِي ، ثُمَّ قَالَ : ((الْحَمْدُ ِللهِ الَّذِي وَفَّقَ رَسُولَ رَسُولِ اللهِ لِمَا يُرْضِي رَسُولَ الله)) سنن أبي داود
Amesimulia Mu’aadh (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomtuma Yemen alimuuliza: “Utafanyaje yatakapokufikia mas-ala?” Akasema: Nitahukumu kwa Kitabu cha Allaah. Akauliza: “Ikiwa hutopata katika Kitabu cha Allaah?” Akasema: Kwa Sunnah ya Rasuli wa Allaah. Akauliza: ”Ikiwa hukupata katika Sunnah ya Rasuli wa Allaah?” Akasema: Basi nitajitahidi rai yangu na sitovuka mipaka. Kisha akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akanipiga katika kifua changu akasema: “AlhamduliLLaah Ambaye Amemuwafikia mjumbe wa Rasuli wa Allaah katika yale aliyoyaridhia Rasuli wa Allaah.” [Sunan Abi Daawuwd]
Tanbihi: ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu usahihi wa Hadiyth hii, ila baadhi yao wamesema ni Swahiyh kwa njia zake nyingi zenye kuitilia nguvu.
Ama mtu au watu kutoa rai zao, au kupinga jambo la Dini lenye dalili, hii haijuzu na inakuwa ni kama kumkosoa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Sunnah zake. Mfano utasikia baadhi ya watu hawaoni sawa kupangusa juu ya soksi au viatu katika suala la kupangusa juu ya khufu mbili (Al-mas-hu ‘alal khuffayn), wanasema kuwa si mantiki au haingii akilini kupangusa juu ya soksi (khufu), bali ipanguswe katika nyayo kwa sababu ndipo mtu anapokanyagia ardhini. Basi na itosheleze kauli ya ‘Aliy Bin Abiy Twaalib (رضي الله عنه):
لو كان الدِّيْنُ بالرأي لكان أسفل الخُفِّ أوْلَى بالمَسْح من أعلاه، وقد رأيت رسول الله صلى الله عليه وسلم يمسح على ظاهر خُفَّيْه. رواه أبو داود والدارقطني
Ingelikuwa Dini inakwenda kwa rai, basi ingelikuwa kupangusa chini ya khuff (soksi za ngozi) ni bora zaidi kuliko juu, na ilhali nimemuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) anapangusa juu ya khuff.” [Imepokelewa na Abu Daawuwd na Ad-Daaraqutwniy]
[3] Maana Ya Maghfirah:
Maana ya maghfirah ni kughufuriwa madhambi au kusitiriwa madhambi, yaani kutokuhesabiwa madhambi au makosa pindi mja akirudi kumuomba Rabb Wake maghfirah. Na hakuna yeyote awezaye kumghufuria mtu madhambi isipokuwa Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) kama Anavyosema:
وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ
Na ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao (kwa maasi), humdhukuru Allaah wakaomba Maghfirah kwa madhambi yao. Na nani anayeghufuria madhambi isipokuwa Allaah. [Aal-‘Imraan (3:135)]
[4] Adabu Ya Kumwita Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم):
Aayah hizi tukufu ziliteremshwa kuhusu watu katika mabedui ambao Allaah (سبحانه وتعالى) Amewaeleza kuwa ni wenye hisia na tabia kavu na kwamba wao:
وَأَجْدَرُ أَلَّا يَعْلَمُوا حُدُودَ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ
Wameelekea zaidi kwamba wasijue mipaka ya (sharia) Alizoteremsha Allaah juu ya Rasuli Wake. [At-Tawbah (9:97)]
Makundi mawili (ya mabedui) walifika kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakamkuta katika nyumba yake na vyumba vya wake zake. Hawakuweza kusubiri na hawakufahamu adabu na heshima ya kumwita na kumngojea hadi atoke bali walimwita: Yaa Muhammad! Yaa Muhammad! Yaani: Toka utujie! Basi Allaah Akawalaumu kwa kukosa kwao akili, kwani hawakufahamu amri ya Allaah ya kuzingatia adabu za kuamiliana na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumheshimu, kwani kuwa na akhlaaq njema ni ishara tosha juu ya akili ya mtu. [Tafsiyr Imaam As-Sa’diy]
[5] Duaa Ya Kuomba Imaan, Kinga Ya Kufru, Ufasiki, Uasi:
Katika Aayah hii, kuna duaa ifuatayo ambayo ni mojawapo wa duaa za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
اللَّهُمَّ حَبِّبْ إِلَيْنَا الإِيمَانَ وَزَيِّنْهُ فِي قُلُوبِنَا وَكَرِّهْ إِلَيْنَا الْكُفْرَ وَالْفُسُوقَ وَالْعِصْيَانَ وَاجْعَلْنَا مِنَ الرَّاشِدِينَ.
Ee Allaah, Pendezesha kwetu imaan na Ipambe katika nyoyo zetu, na Chukiza kwetu kufru, ufasiki na uasi, na Tujaalie miongoni mwa waongofu.
[Ahmad, na Al-Bukhaariy ameitoa katika Al-Adabul-Mufrad (699), na Al-Albaaniy ameipa daraja ya Swahiyh katika Takhriyj Fiqhus-Siyrah (348), Swahiyh Al-Adabil-Mufrad lil-Bukhaariy (538/259), na Majma’u Az-Zawaaid (6/124)]
[6] Fadhila Za Kusuluhisha Waliogombana:
Kusuluhisha waliogombana ni katika Amri za Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea An-Nisaa (4:114). Na kuna fadhila kubwa katika kutekeleza amri hii. Bonyeza viungo vifuatavyo upate faida:
[9] Waumini Kwa Waumini Ni Ndugu:
Kuna dalili nyingi katika Qur-aan na Sunnah zinazoashiria undugu wa Waumini. Na undugu huu, huwa ni mkubwa zaidi kuliko undugu wa uhusiano wa damu pindi anapokuwa ndugu wa uhusiano wa damu ni kafiri, au mwenye kuasi. Na hii ndio inayoitwa al-walaa wal baraa (kupenda kwa ajili ya Allaah na kutengana kwa ajili ya Allaah).
Mifano kadhaa imo katika Siyrah ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Yeye mwenyewe alitengana na jamaa zake kama ammi yake Abuu Lahab. Swahaba pia walitengana na jamaa zao, kama mfano wa Sa’ad bin Abiy Waqaasw (رضي الله عنه) ambaye aliposilimu, alitengana na mama yake ambaye alimtaka arudi ukafirini.
Baadhi ya Aayah zinazohimiza undugu wa Kiislamu, rejea At-Tawbah (9:71). Na katika kuombeana duaa, rejea Al-Hashr (59:10).
Na zifuatazo ni baadhi ya Hadiyth za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) zinazoamrisha undugu wa Kiislamu:
عن النعمان بن بشير رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَثَلُ المُؤْمِنينَ في تَوَادِّهِمْ وتَرَاحُمهمْ وَتَعَاطُفِهمْ، مَثَلُ الجَسَدِ إِذَا اشْتَكَى مِنْهُ عُضْوٌ تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ الجَسَدِ بِالسَّهَرِ والحُمَّى)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ.
Amesimulia An-Nu’maan bin Bashiyr (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mfano wa Waumini katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao na kusaidiana kwao, ni mfano wa mwili, kiungo kimoja kikiumwa basi mwili mzima hukesha kwa homa.” [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]
عَنْ أَبِي مُوسَى (رضي الله عنه) قال: قال رَسُولُ الله (صلى الله عليه و آله وسلم): ((الْمُؤْمِنَ لِلْمُؤْمِنِ كَالْبُنْيَانِ يَشُدُّ بَعْضُهُ بَعْضاً)) وَشَبَّكَ أَصَابِعَهُ - متفق عليه
Amesimulia Abuu Muwsa (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Muumin kwa Muumin mwenziwe ni kama jengo, baadhi yake hutilia nguvu baadhi nyingine.” Akaviumanisha vidole vyake.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
عَنْ أَنَسٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صلى الله عليه و آله وسلم) قَالَ: ((لاَ يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يُحِبَّ لإِخِيهِ مَا يُحِبُّ لِنَفْسِهِ)) متفق عليه
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hatoamini mmoja wenu mpaka ampendelee nduguye anayojipendelea nafsi yake.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Rejea pia Al-Fat-h (48:29) kwenye faida nyenginezo.
Na baadhi ya Hadiyth zinazoharamisha kutengana, kuchukiana, kuvunjiana heshima na kadhaalika. Na hii inahusiana na maamrisho ya Aayah namba (11) inayofuatia ya Suwrah hii Al-Hujuraat.
عن أبي أيوب الأنصاري رضي الله عنه قال : قال النبي صلى الله عليه وسلم: ((لا يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أَنْ يَهْجُرَ أَخَاهُ فَوْقَ ثَلَاثِ لَيَالٍ، يَلْتَقِيَانِ فَيُعْرِضُ هَذَا وَيُعْرِضُ هَذَا، وَخَيْرُهُمَا الَّذِي يَبْدَأُ بِالسَّلام))
Amesimulia Abuu Ayyuwb Al-Answaariy (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Haimpasi Muislamu amhame ndugu yake kwa zaidi ya siku tatu hata wanapokutana huyu anamgeuzia (uso) huyu na huyu anamgeuzia (uso) huyu. Na aliye mbora wao kati ya hao wawili ni yule anayeanza kutoa salaam.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
عن ابن عمر رضي الله عنهما أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((المُسْلِمُ أخُو المُسْلِمِ ، لاَ يَظْلِمُهُ وَلاَ يُسْلِمُهُ . مَنْ كَانَ في حَاجَة أخِيه ، كَانَ اللهُ في حَاجَتِهِ، وَمَنْ فَرَّجَ عَنْ مُسْلِمٍ كُرْبَةً، فَرَّجَ اللهُ عَنْهُ بِهَا كُرْبَةً مِنْ كرَبِ يَومِ القِيَامَةِ ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِماً سَتَرَهُ اللهُ يَومَ القِيَامَةِ )). متفق عليه .
Amesimulia Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Muislamu ni ndugu yake Muislamu, hamdhulumu wala hamsalimishi (kwa adui). Mwenye kumtekelezea haja nduguye Allaah Atamtekelezea haja yake. Na mwenye kumwondolea Muislamu dhiki, Allaah Atamwondolea dhiki miongoni mwa dhiki za Siku ya Qiyaamah. Na mwenye kumsitiri Muislamu yeyote, Allaah Atamsitiri Siku ya Qiyaamah." [Al-Bukhaariy na Muslim]
عَنْ أَنَسُ (رضي الله عنه) أنّ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((لاَ تَبَاغَضُوا، وَلاَ تَحَاسَدُوا، وَلاَ تَدَابَرُوا، وَلاَ تَقَاطَعوا، وَكُونُوا عِبَادَ اللَّهِ إِخْوَانًا، وَلاَ يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أَنْ يَهْجُرَ أَخَاهُ فَوْقَ ثَلاَثَةِ أَيَّامٍ)) متفق عليه
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Msibughudhiane (msichukiane), wala msihusudiane, wala msipeane mgongo, wala msikatane, bali kuweni ndugu, waja wa Allaah, wala haifai kwa Muislamu kumhama nduguye kwa zaidi ya siku tatu (asiseme naye).” [Al-Bukhaariy na Muslim]
[11] Amri Ya Kuheshimiana Na Katazo La Kufedheheshana:
Rejea Tanbihi ya Aayah namba (10) iliyotangulia ya Suwrah hii ya Al-Hujuraat.
[12] Madhara Ya Ghiybah (Kusengenya):
Bonyeza kiungo kifuatacho ambacho ndani yake mna makala zenye faida tele kuhusu maudhui hiyo pamoja na madhara ya An-Namiymah (kufitnisha):
Madhara Ya Ghiybah (Kusengenya) Na An-Namiymah (Kufitinisha) [322]
[13] Taqwa Iko Moyoni Na Ndio Kipimo Pekee Cha Utukufu Na Hadhi Ya Mtu Kwa Allaah:
Taqwa ni katika mambo ya ghaibu ambayo hakuna ajuaye uhalisi wake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Kwa sababu, ingawa mtu anaweza kuonekana kuwa ana mandhari ya taqwa, au ya uswalihina, au ya utendaji ibaada na amali za kheri kwa wingi, lakini uhalisi wake umo moyoni mwake, na Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee Ndiye Mwenye kujua. Hadiyth zifuatazo zimethibitisha:
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Taqwa iko hapa!” Akaashiria mara tatu kifuani mwake. [Muslim]
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه و آله وسلم): ((إِنَّ اللَّهَ لاَ يَنْظُرُ إِلى أجْسَامِكُمْ وَلاَ إِلَى صُوَرِكُمْ وَلَكِنْ يَنْظُرُ إِلَى قُلُوبِكُمْ)) رواه مسلم
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Hatazami viwiliwili vyenu wala sura zenu, lakini Anatazama nyoyo zenu.” [Muslim]
Na mtu kuwa na hadhi mbele ya Allaah au utukufu, hakutokani na kabila lake au nasaba yake, bali kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah hii tukufu kuwa:
إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ ۚ
Aliye na hadhi zaidi miongoni mwenu mbele ya Allaah ni mwenye taqwa.
Na ingelikuwa uhusiano wa damu wa mtu mtukufu unaweza kumfanya jamaa yake awe na hadhi au utukufu, basi Abu Twaalib ambaye ni ammi yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), angekuwa na hadhi na utukufu mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى), lakini amefariki katika ukafiri. Rejea Al-Qaswasw (28:56). Na adhabu yake ni kama alivyosema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth ifuatayo:
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " أَهْوَنُ أَهْلِ النَّارِ عَذَابًا أَبُو طَالِبٍ وَهُوَ مُنْتَعِلٌ بِنَعْلَيْنِ يَغْلِي مِنْهُمَا دِمَاغُهُ " . مسلم
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayepata adhabu ndogo kabisa katika watu wa motoni ni Abuu Twaalib. Ubongo wake utachemka kutokana na viatu viwili atakavyovivaa humo.” [Muslim Kitaab Cha Imaan]
Basi tofauti iliyoje ya hali ya Abuu Twaalib ammi wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba mtukufu Bilaal (رضي الله عنه) ambaye alikuwa ni mtumwa, lakini alibashiriwa Jannah (Pepo) na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo?!:
عن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ لِبِلاَلٍ : (( يَا بِلاَلُ ، حَدِّثْنِي بِأَرْجَى عَمَلٍ عَمِلْتَهُ فِي الإسْلاَمِ ، فَإنِّي سَمِعْتُ دَفَّ نَعْلَيْكَ بَيْنَ يَدَيَّ في الجَنَّةِ )) قَالَ : مَا عَمِلْتُ عَمَلاً أرْجَى عِنْدي مِنْ أَنِّي لَمْ أتَطَهَّرْ طُهُوراً فِي سَاعَةٍ مِنْ لَيْلٍ أَوْ نَهَارٍ إِلاَّ صَلَّيْتُ بِذَلِكَ الطُّهُورِ مَا كُتِبَ لِي أنْ أُصَلِّي . متفقٌ عَلَيْهِ ، وهذا لفظ البخاري .
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuuliza Bilaal (رضي الله عنه): "Ee Bilaal! Niambie amali uliyoifanya katika Uislamu, kwani mimi nimesikia sauti ya viatu vyako ukiwa mbele yangu Peponi." (Bilaal) akasema: Sijafanya amali yoyote ambayo kwayo natarajia hayo, isipokuwa ninapojitwahirisha katika wakati wowote wa usiku au mchana, huswali kwa twahaara hiyo zile Alizoniandikia Allaah kuziswali. [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya Al-Bukhaariy]
Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwatahadharisha ahli wake kutomtegemea yeye kwamba ataweza kuwafaa kwa lolote Siku ya Qiyaamah kwa sababu ya uhusiano wao wa damu. Hadiyth ifuatayo inahusiana na kuteremshwa kwa Aayah ya Suwrah Ash-Shu’araa (26:214):
عن أبي هُريرةَ (رضىِ الله عنه) قال: قام رسوِل الله (صلى الله عليه وسلم) حين أُنزل عليه ((وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ )) فقال: ((يا مَعْشَرَ قُرَيش!)) - أو كلمة نحوها: ((اشتَرُوا أنفُسَكُم، لا أُغْنِي عَنْكُم مِنَ الله شيئاً، ويا عبَّاسُ بن عَبْدِ المُطَّلِبِ لا أُغْنِي عَنْكَ مِنَ الله شيئاً، وَيا صَفِيَّةُ عَمَّةَ رسولِ الله، لا أُغْنِى عَنْكِ مِن الله شيئاً، ويا فَاطِمَةُ بِنْتَ مُحمدٍ سَلِينِي مِنْ مَالِي مَا شِئْتِ، لا أُغْنِي عَنْكِ مِنَ الله شيئاً))
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضىِ الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisimama ilipoteremshwa:
وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ ﴿٢١٤﴾
Na onya (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) jamaa zako wa karibu. [Ash-Shu’araa (26:214)]
Akasema: “Enyi hadhara ya Quraysh!” - au maneno kama hayo – “Okoeni nafsi zenu, kwani sitowafaeni kwa chochote mbele ya Allaah! Ee ‘Abbaas bin ‘Abdil-Muttwalib! Sitokufaa chochote mbele ya Allaah! Ee Swafiyyah shangazi yake Rasuli wa Allaah! Sitokufaa chochote mbele ya Allaah! Ee Faatwimah bint Muhammad! Niombe mali utakayo, (lakini) sitokufaa chochote mbele ya Allaah.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Rejea pia ‘Abasa (80:34-37) kwenye maudhui kama hii na rejea mbalimbali Rejea pia Al-Muuminuwn (23:101), Luqmaan (31:33), Faatwir (35:18), Al-Infitwaar (82:19).
[14] Kutangulizwa Mali Kabla Ya Nafsi Katika Aayah Za Jihaad:
Aayah zinazotaja kuhusu kufanya Jihaad kwa mali na nafsi zinafikia tisa, na zote zimetanguliza mali kabla ya nafsi isipokuwa Aayah moja katika Suwrah At-Tawbah (9:111).
Na katika Sunnah Hadiyth ifuatayo imethibitisha pia:
عَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه أَنَّ اَلنَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: "جَاهِدُوا اَلْمُشْرِكِينَ بِأَمْوَالِكُمْ، وَأَنْفُسِكُمْ، وَأَلْسِنَتِكُمْ" رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Piganeni na washirikina kwa mali yenu, nafsi zenu na ndimi zenu.” [Abuu Daawuwd, Ahmad na An-Nasaaiy na Al-Haakim ameisahihisha]
‘Ulamaa wakaelezea ifuatavyo kuhusu hikma au sababu ya kutangulizwa mali kabla ya nafsi:
Ibn Hibaan (رحمه الله): Mali imetangulizwa kabla ya nafsi, kwa sababu Mujaahid ni muuzaji (anamuuzia Allaah mali yake na nafsi yake). Na nafsi imetajwa baada ya mali ili Allaah Atuzindushe kuwa nafsi ndiyo inayokabiliana na maumivu zaidi na majanga (ya vita), na mtu hayuko tayari kuitoa ila katika hatua ya mwisho (isiyo na budi). Na mnunuzi (Ambaye ni Allaah), nafsi imesogezwa Kwake ili kutuzindusha kwamba Yeye Anaitaka zaidi (kuliko mali), na Yeye Anachokitaka kwanza, ni kile kilicho ghali chenye thamani kubwa. [Al-Bahr Al-Muhiytw (2/242)]
Na zifuatazo ni baadhi ya Fataawa za ‘Ulamaa:
Shaykh ‘Abdur-Rahmaan Naaswir Al-Barraak:
Swali: Jihaad ya mali imetangulizwa kabla ya nafsi katika hali nyingi, lakini nafsi (katika Jihaad) haikutangulizwa isipokuwa sehemu moja tu. Basi kuna hikma gani ya kutangulizwa mali kabla ya nafsi juu ya (kuwa kuna) utukufu (fadhila) wa Jihaad ya nafsi?
Jibu: ‘Ulamaa wamesema kwa sababu mali ndiyo nyenzo ya kwanza wezeshi inayoandaliwa, na kwa hivyo Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ وَمِن رِّبَاطِ الْخَيْلِ
Na waandalieni nguvu (za kiakili na kila aina za silaha) na farasi waliofungwa tayari kwa vita. [Al-Anfaal 8:60)]
Bila mali Mujaahid hawezi kupigana Jihaad kwa nafsi yake isipokuwa kwa mali. Hivyo mali imepewa kipaumbele kutokana na uhalisia kwamba ni lazima iwepo kwanza kabla ya chochote. Jihaad ni lazima iandaliwe kwa zana na nyenzo zinazotumika katika mapambano, na vyote hivyo vinategemea mali. Jihaad haiwezi kufanyika bila silaha, na silaha haipatikani bila mali. [Al-Mawqi’ Ar-Rasmiy li-Fadhwilah Ash-Shayh ‘Abir-Rahmaan Naasiwr Al-Baraak – Fataawaa Wa Duruws]
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله):
Swali: Tunaona kwamba katika Aayah nyingi za Jihaad, Allaah (عزّ وجلّ) Anatanguliza Jihaad kwa mali kabla ya Jihaad ya nafsi. Kuna hikma gani katika hilo?
Jibu: “Ni dhahiri- na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi- kwamba jeshi la Kiislamu linahitaji mali zaidi kuliko watu, na kwa sababu pia Jihaad kwa mali ni nyepesi zaidi kuliko Jihaad ya nafsi.” [Majmuw’ Fataawaa Wa Rasaail Ibn ‘Uthaymiyn (25/312)]
Imaam Ibn Baaz (رحمه الله):
Swali: Kuhusu Hadiyth ya Anas: “Piganeni na washirikina kwa mali zenu, nafsi zenu na ndimi zenu.” Nini hikma ya utaratibu wa kutangulizwa mali (kabla ya nafsi) katika Jihaad?
Jibu: Mali imetangulizwa katika aghalabu ya Aayaat kwa sababu manufaa yake kiujumla ni mengi. Silaha za vita hununuliwa kwa mali, vifaa na zana za kuliandaa jeshi huhitajia mali, familia za wapiganaji hupewa pia (kwa masurufu) na mengineyo. Hivyo basi maslahi yake ni mengi, na ndio maana Allaah Ameitanguliza kabla ya nafsi katika sehemu nyingi isipokuwa katika Aayah ya Suwrah At-Tawbah:
إِنَّ اللَّـهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ ۚ ي
Hakika Allaah Amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwamba watapata Jannah. [At-Tawbah (9:111)]
Basi kinachokusudiwa ni kwamba Jihaad kwa mali inagusa maeneo mengi zaidi na kwa manufaa makubwa zaidi, kwani inaweza kuhitajika mali lakini wasihitajike watu (wengi). [Al-Mawqi' Ar-Rasmiy li-Samaahat Ash-Shaykh Al-Imaam Ibn Baaz]
ق
050-Qaaf
050-Qaaf: Utangulizi Wa Suwrah [324]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
ق ۚ وَالْقُرْآنِ الْمَجِيدِ﴿١﴾
1. Qaaf.[1] Naapa kwa Qur-aan Al-Majiyd: Adhimu, Karimu, yenye kheri, Baraka na ilimu tele.
بَلْ عَجِبُوا أَن جَاءَهُم مُّنذِرٌ مِّنْهُمْ فَقَالَ الْكَافِرُونَ هَـٰذَا شَيْءٌ عَجِيبٌ﴿٢﴾
2. Bali wamestaajabu kwamba amewajia mwonyaji miongoni mwao, wakasema makafiri: Hili ni jambo la ajabu.
أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا ۖ ذَٰلِكَ رَجْعٌ بَعِيدٌ﴿٣﴾
3. Je, hivi tukifa na tukawa udongo (tutafufuliwa)? Ni marejeo ya mbali hayo! [2]
قَدْ عَلِمْنَا مَا تَنقُصُ الْأَرْضُ مِنْهُمْ ۖ وَعِندَنَا كِتَابٌ حَفِيظٌ﴿٤﴾
4. Hakika Sisi Tunajua kinachopunguzwa na ardhi kutokana nao, na Tunacho Kitabu kinachohifadhi barabara.
بَلْ كَذَّبُوا بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ فَهُمْ فِي أَمْرٍ مَّرِيجٍ﴿٥﴾
5. Bali wamekadhibisha haki ilipowajia, basi wao wamo katika jambo la mkorogeko.
أَفَلَمْ يَنظُرُوا إِلَى السَّمَاءِ فَوْقَهُمْ كَيْفَ بَنَيْنَاهَا وَزَيَّنَّاهَا وَمَا لَهَا مِن فُرُوجٍ﴿٦﴾
6. Je, hawatazami mbingu juu yao, vipi Tumezijenga na Tumezipamba, na wala hazina mipasuko yoyote!
وَالْأَرْضَ مَدَدْنَاهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ بَهِيجٍ﴿٧﴾
7. Na ardhi Tumeikunjua na Tukaitupia humo milima thabiti, na Tukaotesha humo kila aina ya mimea ya kupendeza.
تَبْصِرَةً وَذِكْرَىٰ لِكُلِّ عَبْدٍ مُّنِيبٍ﴿٨﴾
8. Ni ufumbuzi macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kuelekea kwa Allaah (kwa khofu na matarajio).
وَنَزَّلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً مُّبَارَكًا فَأَنبَتْنَا بِهِ جَنَّاتٍ وَحَبَّ الْحَصِيدِ﴿٩﴾
9. Na Tukateremsha kutoka mbinguni maji yaliyobarikiwa, kisha Tukaotesha kwayo mabustani na nafaka za kuvunwa.
وَالنَّخْلَ بَاسِقَاتٍ لَّهَا طَلْعٌ نَّضِيدٌ﴿١٠﴾
10. Na mitende mirefu yenye mashada ya matunda yenye kupangika tabaka tabaka.
رِّزْقًا لِّلْعِبَادِ ۖ وَأَحْيَيْنَا بِهِ بَلْدَةً مَّيْتًا ۚ كَذَٰلِكَ الْخُرُوجُ﴿١١﴾
11. Ni riziki kwa waja. Na Tukahuisha kwayo nchi iliyokufa, hivyo ndivyo kufufuliwa.
كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَأَصْحَابُ الرَّسِّ وَثَمُودُ﴿١٢﴾
12. Wamekadhibisha kabla yao (Maquraysh) kaumu ya Nuwh na watu wa Ar-Rass[3] na kina Thamuwd.
وَعَادٌ وَفِرْعَوْنُ وَإِخْوَانُ لُوطٍ﴿١٣﴾
13. Na kina ‘Aad na Firawni na ndugu wa Luutw.
وَأَصْحَابُ الْأَيْكَةِ وَقَوْمُ تُبَّعٍ ۚ كُلٌّ كَذَّبَ الرُّسُلَ فَحَقَّ وَعِيدِ﴿١٤﴾
14. Na wakaazi wa Al-Aykah[4] na kaumu ya Tubba’[5], wote walikadhibisha Rusuli. Basi likathibiti Onyo Langu.
أَفَعَيِينَا بِالْخَلْقِ الْأَوَّلِ ۚ بَلْ هُمْ فِي لَبْسٍ مِّنْ خَلْقٍ جَدِيدٍ﴿١٥﴾
15. Je, kwani Tulichoka kwa uumbaji wa kwanza? Bali wao wamo katika kuchanganyikiwa akili na uumbaji upya (kufufuliwa).
وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِهِ نَفْسُهُ ۖ وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ﴿١٦﴾
16. Na kwa yakini Tumemuumba binaadam na Tunajua yale inayowaza nafsi yake[6] na Sisi[7] Tuko karibu naye kuliko mshipa wa koo.
إِذْ يَتَلَقَّى الْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ قَعِيدٌ﴿١٧﴾
17. Pale wanapopokea wapokeaji wawili (Malaika) wanaokaa kuliani na kushotoni.
مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ﴿١٨﴾
18. Hatamki kauli yeyote isipokuwa anaye mchungaji aliyejitayarisha (kurekodi).[8]
وَجَاءَتْ سَكْرَةُ الْمَوْتِ بِالْحَقِّ ۖ ذَٰلِكَ مَا كُنتَ مِنْهُ تَحِيدُ﴿١٩﴾
19. Na Sakaaratul-mawt[9] itakapomjia kwa haki. (Itasemwa): Hayo ndiyo yale uliyokuwa ukiyakimbilia mbali.
وَنُفِخَ فِي الصُّورِ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمُ الْوَعِيدِ﴿٢٠﴾
20. Na baragumu[10] litapulizwa. Hiyo ndio Siku ya makamio.
وَجَاءَتْ كُلُّ نَفْسٍ مَّعَهَا سَائِقٌ وَشَهِيدٌ﴿٢١﴾
21. Na kila nafsi itakuja pamoja nayo mwendeshaji na shahidi.[11]
لَّقَدْ كُنتَ فِي غَفْلَةٍ مِّنْ هَـٰذَا فَكَشَفْنَا عَنكَ غِطَاءَكَ فَبَصَرُكَ الْيَوْمَ حَدِيدٌ﴿٢٢﴾
22. (Aambiwe): Kwa yakini ulikuwa katika mghafala na haya! Basi Tumekuondoshea kifuniko chako, basi kuona kwako leo ni kukali.[12]
وَقَالَ قَرِينُهُ هَـٰذَا مَا لَدَيَّ عَتِيدٌ﴿٢٣﴾
23. Na Malaika wake aliyepewa jukumu atasema: Hii (rekodi) iliyoko kwangu imeshatayarishwa.
أَلْقِيَا فِي جَهَنَّمَ كُلَّ كَفَّارٍ عَنِيدٍ﴿٢٤﴾
24. (Allaah Atasema): Mtupeni katika Jahannam kila kafiri mno, mkaidi!
مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ مُّرِيبٍ﴿٢٥﴾
25. Mzuiaji wa kheri, mwenye kutaadi, mtiaji shaka.
الَّذِي جَعَلَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَأَلْقِيَاهُ فِي الْعَذَابِ الشَّدِيدِ﴿٢٦﴾
26. Ambaye amefanya mwabudiwa mwengine pamoja na Allaah, basi mtupeni katika adhabu shadidi.
قَالَ قَرِينُهُ رَبَّنَا مَا أَطْغَيْتُهُ وَلَـٰكِن كَانَ فِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ﴿٢٧﴾
27. Shaytwaan mwenzake atasema: Rabb wetu! Sikumvukisha mipaka kuasi lakini alikuwa (mwenyewe) katika upotofu wa mbali.[13]
قَالَ لَا تَخْتَصِمُوا لَدَيَّ وَقَدْ قَدَّمْتُ إِلَيْكُم بِالْوَعِيدِ﴿٢٨﴾
28. (Allaah) Atasema: Msibishane Kwangu, na hali Nilishakukadimishieni Onyo Langu!
مَا يُبَدَّلُ الْقَوْلُ لَدَيَّ وَمَا أَنَا بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ﴿٢٩﴾
29. Haibadilishwi kauli Kwangu, Nami Si Mwenye Kudhulumu katu waja.
يَوْمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ امْتَلَأْتِ وَتَقُولُ هَلْ مِن مَّزِيدٍ﴿٣٠﴾
30. Siku Tutakapoiambia Jahannam: Je, umeshajaa? Nayo itasema: Je, kuna ziada yoyote?[14]
وَأُزْلِفَتِ الْجَنَّةُ لِلْمُتَّقِينَ غَيْرَ بَعِيدٍ﴿٣١﴾
31. Na italetwa karibu Jannah kwa wenye taqwa isiwe mbali.
هَـٰذَا مَا تُوعَدُونَ لِكُلِّ أَوَّابٍ حَفِيظٍ﴿٣٢﴾
32. (Itasemwa): Haya ndiyo yale mliyoahidiwa kwa kila mwenye kurejea kwa Allaah kwa yote, mwenye kuhifadhi vyema (Amri za Allaah سبحانه وتعالى).
مَّنْ خَشِيَ الرَّحْمَـٰنَ بِالْغَيْبِ وَجَاءَ بِقَلْبٍ مُّنِيبٍ﴿٣٣﴾
33. Ambaye anamwogopa Ar-Rahmaan akiwa mbali na macho ya watu na akaja na moyo safi mwelekevu.
ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ ۖ ذَٰلِكَ يَوْمُ الْخُلُودِ﴿٣٤﴾
34. Iingieni (Jannah) kwa salama. Hiyo ndio siku yenye kudumu.
لَهُم مَّا يَشَاءُونَ فِيهَا وَلَدَيْنَا مَزِيدٌ﴿٣٥﴾
35. Watapata humo wayatakayo, na Kwetu kuna ziada (kumuona Allaah عز وجل).[15]
وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّن قَرْنٍ هُمْ أَشَدُّ مِنْهُم بَطْشًا فَنَقَّبُوا فِي الْبِلَادِ هَلْ مِن مَّحِيصٍ﴿٣٦﴾
36. Na karne ngapi Tumeziangamiza kabla yao ambao walikuwa wenye nguvu zaidi kuliko wao! Basi walitangatanga sana kwa vishindo katika nchi. Je, walipata mahali popote pa kukimbilia?
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَذِكْرَىٰ لِمَن كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ﴿٣٧﴾
37. Hakika katika hayo, bila shaka pana ukumbusho kwa aliye na moyo (wa uzingativu), au akatega sikio kwa makini, naye yu hadhiri kwa moyo wake.
وَلَقَدْ خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٍ﴿٣٨﴾
38. Na kwa yakini Tumeumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita, na wala Haukutugusa uchovu wowote.
فَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ الْغُرُوبِ﴿٣٩﴾
39. Basi subiri juu ya yale wanayoyasema, na Sabbih ukimhimidi Rabb wako kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa.
وَمِنَ اللَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَأَدْبَارَ السُّجُودِ﴿٤٠﴾
40. Na katika usiku Msabbih, na baada ya kila Swalaah.[16]
وَاسْتَمِعْ يَوْمَ يُنَادِ الْمُنَادِ مِن مَّكَانٍ قَرِيبٍ﴿٤١﴾
41. Na sikiliza kwa makini Siku atakayonadi mwenye kunadi kutoka mahali pa karibu.
يَوْمَ يَسْمَعُونَ الصَّيْحَةَ بِالْحَقِّ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمُ الْخُرُوجِ﴿٤٢﴾
42. Siku watakayosikia ukelele kwa haki.[17] Hiyo ndio Siku ya kutoka (makaburini).
إِنَّا نَحْنُ نُحْيِي وَنُمِيتُ وَإِلَيْنَا الْمَصِيرُ﴿٤٣﴾
43. Hakika Sisi Tunahuisha na Tunafisha, na Kwetu ndio mahali pa kuishia.
يَوْمَ تَشَقَّقُ الْأَرْضُ عَنْهُمْ سِرَاعًا ۚ ذَٰلِكَ حَشْرٌ عَلَيْنَا يَسِيرٌ﴿٤٤﴾
44. Siku itakayowapasukia ardhi[18] (watoke) haraka haraka. Huo ndio mkusanyo, Kwetu ni mwepesi mno.
نَّحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُونَ ۖ وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِجَبَّارٍ ۖ فَذَكِّرْ بِالْقُرْآنِ مَن يَخَافُ وَعِيدِ﴿٤٥﴾
45. Sisi Tunajua zaidi yale wanayoyasema, na wala wewe si mwenye kuwalazimisha kwa ujabari. Basi mkumbushe kwa Qur-aan anayekhofu Onyo Langu.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Washirikina Hawakuamini Kuwa Watafufuliwa:
Rejea Al-Israa (17: 49) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali.
[3] Watu Wa Ar-Rass:
Ar-Rass ni kisima [Tafsiyr Ibn Kathiyr]. Rejea Al-Furqaan (25:38) kwenye maelezo kuhusu watu wa Ar-Rass.
[4] Watu Wa Al-Aykah
Watu wa Aykah ni watu wa kichakani katika mji wa Madyan. Ni watu wa Nabiy Shu’ayb (عليه السّلام). Rejea Ash-Shu’araa (26:176) kupata maelezo bayana.
[6] Mwanaadam Hahesabiwi Na Allaah Yale Anayoyawaza Nafsini Mwake Madamu Hakuyaongelea Au Kuyatenda:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anakhabarisha Uwezo Wake juu ya mwanaadam, kwani Yeye Ndiye Aliyemuumba, hivyo basi amali zake Anazijua vyema hadi kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Anajua yale yanayomnong’oneza nafsini mwake binaadam, yawe ya kheri au ya shari. Na imethibiti katika Swahiyh Hadiyth ifuatayo:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، يَرْفَعُهُ قَالَ " إِنَّ اللَّهَ تَجَاوَزَ لأُمَّتِي عَمَّا وَسْوَسَتْ أَوْ حَدَّثَتْ بِهِ أَنْفُسَهَا، مَا لَمْ تَعْمَلْ بِهِ أَوْ تَكَلَّمْ ".
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Amesamehe Ummah wangu (zile amali mbaya) ambazo nafsi zao huwanong’oneza au kupendekeza maadamu hawatatenda au kuzungumza.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr, Hadiyth Ameipokea Imaam Al-Bukhaariy: Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri (83) – Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[7] “Sisi” Imekusudiwa Ni Malaika:
Yaani: Malaika wa Allaah (سبحانه وتعالى) wako karibu na binaadam kuliko mshipa wa koo wake.
Wale walioawilisha “Na Sisi” kukusudia kuwa ni “Ujuzi Wetu”, wamefanya hivyo ili kuepusha kuingia katika fikra ya “Huluwl” ambayo ina maana ya kuchanganyika Allaah na viumbe Vyake lakini Allaah Akabaki kama Alivyo na kiumbe Chake kikabaki kama kilivyo bila mabadiliko yoyote, au “Iltihaad” ambayo ina maana ya kuchanganyika Allaah (سبحانه وتعالى) na Viumbe Vyake na kuwa kitu kimoja kisichoweza kutenganika. Lakini itikadi hii imekanushwa na ‘Ulamaa wote kwa sauti moja. Allaah Ametakasika, na Ametukuka, na Yuko mbali na yale wanayompachika. Neno “Sisi” halifai kuawiliwa kwa maana ya Ujuzi wa Allaah, kwani Allaah Hakusema: “Na Mimi Niko karibu zaidi naye kuliko mshipa wake wa koo.”
Bali Anasema:
وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ﴿١٦﴾
Na Sisi Tuko karibu naye kuliko mshipa wa koo.
Kama Anavyosema katika hali ya sakaraatul-mawt ya binaadam pindi Malaika Wake wanapotoa roho za wanaadam:
وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنكُمْ وَلَـٰكِن لَّا تُبْصِرُونَ ﴿٨٥﴾
Nasi Tuko karibu naye zaidi kuliko nyinyi, lakini hamuoni. [Al-Waaqi’ah (56:85)]
(Nasi) yaani: Malaika
Na vivyo hivyo Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ ﴿٩﴾
“Hakika Sisi Tumeteremsha Adh-Dhikra (Qur-aan) na hakika Sisi bila shaka Ndio Wenye Kuihifadhi.” [Al-Hijr (15:9)]
Kwa hiyo Malaika wameteremsha Wahyi, yaani Qur-aan, kwa Idhini ya Allaah (عزّ وجلّ), na vivyo hivyo Malaika wako karibu zaidi na binaadam kuliko mshipa wake wa koo baada ya kuwezeshwa kuwa hivyo na Allaah. Hivyo basi, Malaika na shaytwaan wananamjua vyema binaadam na wako karibu naye zaidi. Ni kama vile alivyotuambia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye ni swaadiq al-maswduwq (mkweli mwenye kusadikiwa
إِنَّ الشَّيْطَانَ يَجْرِي مِنِ ابْنِ آدَمَ مَجْرَى الدَّمِ
“Hakika shaytwaan hutembea katika mwili wa binaadam kama damu inavyotembea katika mishipa.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr – Hadiyth katika Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
[8] Kuchunga Ulimi:
Muislamu anapaswa kuwa na kauli njema tu, na anapaswa kuchunga ulimi wake kwa kutokusema neno lolote lile baya, kwa sababu kama Anavosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah hii tukufu kwamba Malaika wanaandika kila neno linalotamkwa, liwe la kheri au shari, hata liwe dogo vipi. Na kuchunga ulimi kumeonywa katika Kauli kadhaa za Allaah (سبحانه وتعالى) ndani ya Qur-aan. Hali kadhaalika, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameonya katika Hadiyth mbalimbali, kama katika Hadiyth hii ifuatayo ambayo inatahadharisha jinsi gani neno moja linaweza kusababisha Radhi za Allaah (سبحانه وتعالى) au Hasira Zake:
عن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، عن النبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( إنَّ العَبْدَ لَيَتَكَلَّمُ بِالكَلِمَةِ مِنْ رِضْوَانِ الله تَعَالَى مَا يُلْقِي لَهَا بَالاً يَرْفَعُهُ اللهُ بِهَا دَرَجاتٍ ، وإنَّ العَبْدَ لَيَتَكَلَّمُ بِالكَلَمَةِ مِنْ سَخَطِ اللهِ تَعَالَى لا يُلْقِي لَهَا بَالاً يَهْوِي بِهَا في جَهَنَّمَ )) . رواه البخاري .
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika mja huzungumza maneno yenye kumridhisha Allaah (سبحانه وتعالى) bila kuyapa umuhimu wowote, na Allaah Akamnyanyulia kwayo daraja nyingi Na hakika mja huzungumza maneno yenye kumkasirisha Allaah (سبحانه وتعالى) bila kuyapa umuhimu wowote, yakaja kumporomosha ndani ya Jahannam.” [Al-Bukhaariy]
Bonyeza viungo vifuatavyo kwenye Makala mbalimbali zenye funzo hili muhimu kabisa:
[9] Sakaraatul-Mawt: Mateso Makali Ya Mauti:
Sakaraatul-Mawti ni mateso anayoyapata mtu anayetolewa roho hadi kwamba hulevywa akili kutokana na uzito wa mateso hayo.
Na hakuna wa kuepukana nayo kwani hata Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokaribia kufariki alihisi sakaraatul-mawti kwa dalili ya Hadiyth hii ifuatayo:
حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ عُبَيْدٍ، حَدَّثَنَا عِيسَى بْنُ يُونُسَ، عَنْ عُمَرَ بْنِ سَعِيدٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي ابْنُ أَبِي مُلَيْكَةَ، أَنَّ أَبَا عَمْرٍو، ذَكْوَانَ مَوْلَى عَائِشَةَ أَخْبَرَهُ أَنَّ عَائِشَةَ كَانَتْ تَقُولُ إِنَّ مِنْ نِعَمِ اللَّهِ عَلَىَّ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم تُوُفِّيَ فِي بَيْتِي وَفِي يَوْمِي، وَبَيْنَ سَحْرِي وَنَحْرِي، وَأَنَّ اللَّهَ جَمَعَ بَيْنَ رِيقِي وَرِيقِهِ عِنْدَ مَوْتِهِ، دَخَلَ عَلَىَّ عَبْدُ الرَّحْمَنِ وَبِيَدِهِ السِّوَاكُ وَأَنَا مُسْنِدَةٌ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَرَأَيْتُهُ يَنْظُرُ إِلَيْهِ، وَعَرَفْتُ أَنَّهُ يُحِبُّ السِّوَاكَ فَقُلْتُ آخُذُهُ لَكَ فَأَشَارَ بِرَأْسِهِ أَنْ نَعَمْ، فَتَنَاوَلْتُهُ فَاشْتَدَّ عَلَيْهِ وَقُلْتُ أُلَيِّنُهُ لَكَ فَأَشَارَ بِرَأْسِهِ أَنْ نَعَمْ، فَلَيَّنْتُهُ، وَبَيْنَ يَدَيْهِ رَكْوَةٌ ـ أَوْ عُلْبَةٌ يَشُكُّ عُمَرُ ـ فِيهَا مَاءٌ، فَجَعَلَ يُدْخِلُ يَدَيْهِ فِي الْمَاءِ فَيَمْسَحُ بِهِمَا وَجْهَهُ يَقُولُ " لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، إِنَّ لِلْمَوْتِ سَكَرَاتٍ ". ثُمَّ نَصَبَ يَدَهُ فَجَعَلَ يَقُولُ " فِي الرَّفِيقِ الأَعْلَى ". حَتَّى قُبِضَ وَمَالَتْ يَدُهُ.
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Hakika katika Neema za Allaah juu yangu ni kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alifariki nyumbani kwangu katika siku ya zamu yangu wakati akiegemea kifuani kwangu, na Allaah Akajaalia mate yangu yachanganyike na mate yake katika kifo chake. ‘Abdur-Rahmaan akaingia kwangu akiwa na siwaak (mswaki wa Sunnah) mkononi mwake na nikawa nauegemeza (mgongo wa) Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) (dhidi ya kifua changu). Nikamwona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiangalia (siwaak) na nilijua kuwa alipenda siwaak nikamwambia: Je, nikuchukulie? Akabetua kichwa kwa kuafiki. Nikachukua na ulikuwa mgumu kwake kuutumia, nikamuuliza: Je, nikulainishie? Akabetua kichwa kukubali. Nikaulainisha na kusafishia meno yake. Mbele yake kulikuwa na gudulia au kopo. Msimuliaji ‘Umar, hana uhakika kama lilikuwa na maji ama laa. Akawa anatumbukiza mkono wake katika maji na kupangusa uso wake kwa maji hayo, akasema:
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، إِنَّ لِلْمَوْتِ سَكَرَاتٍ
“La ilaaha illa-Allaah (Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah)
Hakika mauti yana mateso yake.” Akainua mkono wake (juu) na kuanza kusema: “Kwa Sahibu wa Juu.” Mpaka akafariki, mkono wake ukashuka chini. [Al-Bukhaariy, Kitaab Al-Maghaaziy (64), Kitabu cha Ar-Riqaaq (81)]
Rejea pia Al-Waaqi’ah (56:83) kwenye faida kadhaa na rejea zake.
[10] Baragumu Litakapopigwa Siku Ya Qiyaamah:
Rejea Az-Zumar (39:68) kwenye maelezo bayana na rejea zake.
[11] Mwendeshaji Na Shahidi:
Mwendeshaji ni Malaika na shahidi ni amali zake za kheri na shari. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Na ije kila nafsi, wakiwa pamoja nayo Malaika wawili: mmoja anaiongoza kwenye mkusanyiko, na mwingine anaitolea ushahidi wa liyoyafanya duniani, ya kheri na shari. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[12] Watu Na Hasa Makafiri Wataona Vizuri Yanayowasubiri Mbele Yao Siku Ya Qiyaamah:
Tafsiyr ya Imaam As-Sa’diy (رحمه الله):
لَّقَدْ كُنتَ فِي غَفْلَةٍ مِّنْ هَـٰذَا
“(Aambiwe): Kwa yakini ulikuwa katika mghafala na haya!”
Yaani: Siku ya Qiyaamah, mkengeukaji na mkadhibishaji, anaambiwa Siku ya Qiyaamah maneno haya ya kulaumiwa na kukaripiwa: Ulikuwa mkadhibishaji wa haya na ukaacha kuyatendea kazi basi sasa:
فَكَشَفْنَا عَنكَ غِطَاءَكَ
“Tumekuondoshea kifuniko chako.”
Kilichofunika moyo wako, ukazidi usingizi wako wa ghafla, na ukaendelea ukengeukaji wako,
فَبَصَرُكَ الْيَوْمَ حَدِيدٌ﴿٢٢﴾
“Basi kuona kwako leo ni kukali.”
Atayaona yale yatakayomkirihisha, kumtisha na kumtia khofu, ya aina za adhabu na mateso.
Maelezo haya ya Allaah huenda ikawa anaambiwa mja, kwani duniani alikuwa katika ghafla kutambua sababu ya kuumbwa kwake, lakini Siku ya Qiyaamah ataamka kutoka usingizi wa ghafla, lakini katika wakati ambao hatoweza kujirudi au kufidia wakati alioupoteza.
Na yote haya ni matanabahisho na matahadharisho ya Allaah kwa Waja Wake. Anawaonya kwa kuwakhabarisha yatakayowasibu wakadhibishaji Siku hiyo Adhimu. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Tafsiyr Al-Muyassar:
Kwa hakika wewe ulikuwa katika mghafala kuhusu tukio hili unaloliona leo, ewe binaadam! Ndipo Tukakifunua kifuniko chako kilichoziba moyo wako, kughafilika kukakuondokea. Basi leo macho yako, katika unachokishuhudia, ni makali. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[13] Shaytwaan Atamgeukia Mwanaadam Na Kukanusha Upotoshaji Wake Siku Ya Qiyaamah:
Rejea Suwrah Ibraahiym (14:22) kwenye maelezo na rejea mbalimbali.
[14] Jahannam Itaomba Wakazi Wake Wa Motoni Wazidi Kuongezwa Kuingizwa Humo:
Aayah kadhaa katika Qur-aan zimethibitisha kwamba moto wa Jahannam utajazwa kwa wanaadam na mashaytwaan. Miongoni mwazo ni: Al-A’raaf (7:38), (7:179), As-Sajdah (32:13). Na katika Hadiyth, ni hii ifuatayo:
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " لاَ تَزَالُ جَهَنَّمُ تَقُولُ هَلْ مِنْ مَزِيدٍ حَتَّى يَضَعَ رَبُّ الْعِزَّةِ فِيهَا قَدَمَهُ فَتَقُولُ قَطْ قَطْ وَعِزَّتِكَ. وَيُزْوَى بَعْضُهَا إِلَى بَعْضٍ ". رَوَاهُ شُعْبَةُ عَنْ قَتَادَةَ.
Amesimulia Anas Bin Maalik (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Moto wa Jahannam utaendelea kusema: Je kuna ziyada yoyote (ya viumbe kuingizwa humu)? Mpaka Allaah (عزّ وجلّ) Atakapoweka Mguu Wake juu yake, hapo (Jahannam) itasema: Imetosha, imetosha (nimeshajaa) kwa Utukufu Wako! Na pande zake zote zitakusanywa pamoja.” [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Aymaan Wan-Nudhur (83), Kitaab At-Tafsiyr (65)]
[15] ‘Aqiydah Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Kwamba Waumini Watamuona Allaah (عزّ وجلّ) Peponi.
Rejea Yuwnus (10:26).
[16] Kumsabbih Allaah (سبحانه وتعالى) Baada Ya Kila Swalaah:
Imaam Ibn Kathiyr (رحمه الله) amenukuu: Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema kuhusu Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَأَدْبَارَ السُّجُودِ﴿٤٠﴾
“Na baada ya kila Swalaah.”
Yaani: Ni tasbiyh za kila baada ya Swalaah. Na hii imethibitishwa na Hadiyth katika Swahiyh mbili:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ جَاءَ الْفُقَرَاءُ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالُوا ذَهَبَ أَهْلُ الدُّثُورِ مِنَ الأَمْوَالِ بِالدَّرَجَاتِ الْعُلاَ وَالنَّعِيمِ الْمُقِيمِ، يُصَلُّونَ كَمَا نُصَلِّي، وَيَصُومُونَ كَمَا نَصُومُ، وَلَهُمْ فَضْلٌ مِنْ أَمْوَالٍ يَحُجُّونَ بِهَا، وَيَعْتَمِرُونَ، وَيُجَاهِدُونَ، وَيَتَصَدَّقُونَ قَالَ " أَلاَ أُحَدِّثُكُمْ بِأَمْرٍ إِنْ أَخَذْتُمْ بِهِ أَدْرَكْتُمْ مَنْ سَبَقَكُمْ وَلَمْ يُدْرِكْكُمْ أَحَدٌ بَعْدَكُمْ، وَكُنْتُمْ خَيْرَ مَنْ أَنْتُمْ بَيْنَ ظَهْرَانَيْهِ، إِلاَّ مَنْ عَمِلَ مِثْلَهُ تُسَبِّحُونَ وَتَحْمَدُونَ، وَتُكَبِّرُونَ خَلْفَ كُلِّ صَلاَةٍ ثَلاَثًا وَثَلاَثِينَ ". فَاخْتَلَفْنَا بَيْنَنَا فَقَالَ بَعْضُنَا نُسَبِّحُ ثَلاَثًا وَثَلاَثِينَ، وَنَحْمَدُ ثَلاَثًا وَثَلاَثِينَ، وَنُكَبِّرُ أَرْبَعًا وَثَلاَثِينَ. فَرَجَعْتُ إِلَيْهِ فَقَالَ " تَقُولُ سُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ، حَتَّى يَكُونَ مِنْهُنَّ كُلِّهِنَّ ثَلاَثًا وَثَلاَثِينَ ".
Amesimulia Abu Hurayrah (رضي الله عنه): Baadhi ya watu masikini walikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) wakasema: Matajiri watapata madaraja ya juu na watakuwa na starehe za kudumu, na wao wanaswali kama sisi na wanafunga (Swiyaam) kama sisi, wana fedha zaidi ambazo wanazitumia kuhiji na Umrah, na kupigana katika njia ya Allaah na kutoa swadaqah. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Je, nikuelezeeni jambo ambalo mkilifanya mtawafikia wale walio wazidi, na hakuna atakayewashinda, na mtakuwa bora kuliko watu wanaoishi nao isipokuwa wale watakaofanya kama nyie. Tamkeni
سُبْحان الله
Subhaana Allaah
الْحمد لله
AlhamduliLlaah
الله اَكْبَر
Allaahu Akbar
mara thelathini na tatu (kila mmoja pekee) baada ya kila Swalaah ya faradhi.” Tukatofautiana na baadhi yetu wakasema:
سُبْحان الله
Subhaana Allaah (mara thelathini na tatu)
الْحمد لله
AlhamduliLlaah (mara thelathini na tatu)
الله اَكْبَر
Allaahu Akbar (mara thelathini na nne).
Nikaenda kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Sema:
سُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ
Subhaana Allaah, AlhamduliLlaah, Allaahu Akbar
Hata zote ziwe mara thelathini na tatu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
[17] Baragumu Litakalopulizwa Na Malaika Israafiyl:
Rejea Az-Zumar (39:68) kwenye maelezo na rejea zake.
[18] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Wa Kwanza Ambaye Ardhi Itampasukia Atoke Kaburini:
حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ إِسْمَاعِيلَ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا عَمْرُو بْنُ يَحْيَى، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ بَيْنَمَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم جَالِسٌ جَاءَ يَهُودِيٌّ، فَقَالَ يَا أَبَا الْقَاسِمِ ضَرَبَ وَجْهِي رَجُلٌ مِنْ أَصْحَابِكَ. فَقَالَ " مَنْ ". قَالَ رَجُلٌ مِنَ الأَنْصَارِ. قَالَ " ادْعُوهُ ". فَقَالَ " أَضَرَبْتَهُ ". قَالَ سَمِعْتُهُ بِالسُّوقِ يَحْلِفُ وَالَّذِي اصْطَفَى مُوسَى عَلَى الْبَشَرِ. قُلْتُ أَىْ خَبِيثُ، عَلَى مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم فَأَخَذَتْنِي غَضْبَةٌ ضَرَبْتُ وَجْهَهُ. فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " لاَ تُخَيِّرُوا بَيْنَ الأَنْبِيَاءِ، فَإِنَّ النَّاسَ يَصْعَقُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، فَأَكُونُ أَوَّلَ مَنْ تَنْشَقُّ عَنْهُ الأَرْضُ، فَإِذَا أَنَا بِمُوسَى آخِذٌ بِقَائِمَةٍ مِنْ قَوَائِمِ الْعَرْشِ، فَلاَ أَدْرِي أَكَانَ فِيمَنْ صَعِقَ، أَمْ حُوسِبَ بِصَعْقَةِ الأُولَى ".
Amesimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa amekaa, alitokea Myahudi akasema: Ee Abul-Qaasim! Mmoja katika watu wako amenipiga usoni. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuuliza: “Ni nani?” Yule Myahudi akasema: Mtu katika Answaar. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Mwite.” (Pindi mtu yule katika Answaar alipofika) Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuuliza, “Je, ulimpiga?” Yule bwana katika Answaar akasema: Nimemsikia sokoni anakula yamini akisema: Naapa kwa Yule Aliyemteua Muwsaa juu ya viumbe! Nikasema: Ee khabithi! Je, Allaah Amemfadhilisha Muwsaa kuliko Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)? Nikaghadhibika nikampiga usoni. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Msifadhilishe baina ya Manabii. Hakika watu Siku ya Qiyaamah watazimia, nami nitakuwa wa kwanza ambaye ardhi itanipasukia. Nitamkuta Muwsaa ameshika nguzo miongoni mwa nguzo za ‘Arsh. Sijui kama alikuwa miongoni mwa waliozimia au hakuzimia katika zimio la kwanza.” [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Khuswuwmaat (44)]
الذَّارِيَات
051-Adh-Dhaariyaat
051-Adh-Dhaariyaat: Utangulizi Wa Suwrah [332]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالذَّارِيَاتِ ذَرْوًا﴿١﴾
1. Naapa kwa (pepo) zinazopeperusha vumbi kuzitawanya.
فَالْحَامِلَاتِ وِقْرًا﴿٢﴾
2. Kisha Naapa kwa (mawingu) yanayobeba mzigo wa maji.
فَالْجَارِيَاتِ يُسْرًا﴿٣﴾
3. Kisha Naapa kwa (merikebu) zinazotembea kwa wepesi.
فَالْمُقَسِّمَاتِ أَمْرًا﴿٤﴾
4. Kisha Naapa kwa (Malaika) wenye kugawanya amri.
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٌ﴿٥﴾
5. Hakika mnayoahidiwa bila shaka ni kweli.
وَإِنَّ الدِّينَ لَوَاقِعٌ﴿٦﴾
6. Na hakika malipo bila shaka yatatokea.
وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْحُبُكِ﴿٧﴾
7. Naapa kwa mbingu zilizojaa njia madhubuti.
إِنَّكُمْ لَفِي قَوْلٍ مُّخْتَلِفٍ﴿٨﴾
8. Hakika nyinyi bila shaka mko katika kauli inayokhitilafiana.
يُؤْفَكُ عَنْهُ مَنْ أُفِكَ﴿٩﴾
9. Ameghilibiwa kwayo anayeghilibiwa (kuhusu haki).
قُتِلَ الْخَرَّاصُونَ﴿١٠﴾
10. Wameangamia wanaobuni uongo.
الَّذِينَ هُمْ فِي غَمْرَةٍ سَاهُونَ﴿١١﴾
11. Ambao wamo katika mfuniko wa mghafala, wenye kupurukusha (kuhusu Aakhirah).
يَسْأَلُونَ أَيَّانَ يَوْمُ الدِّينِ﴿١٢﴾
12. Wanauliza: Lini hiyo Siku ya malipo?
يَوْمَ هُمْ عَلَى النَّارِ يُفْتَنُونَ﴿١٣﴾
13. Siku wao watakapoteswa motoni.
ذُوقُوا فِتْنَتَكُمْ هَـٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تَسْتَعْجِلُونَ﴿١٤﴾
14. Onjeni adhabu yenu. Haya ndiyo ambayo mlikuwa mkiyahimiza.
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ﴿١٥﴾
15. Hakika wenye taqwa watakuwa katika Jannaat na chemchemu.[1]
آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ﴿١٦﴾
16. Wakichukua yale Atakayowapa Rabb wao. Hakika wao walikuwa kabla ya hapo ni wahisani.
كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ﴿١٧﴾
17. Walikuwa kidogo tu katika usiku wakilala kwa raha.
وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ﴿١٨﴾
18. Na kabla ya Alfajiri wakiomba Maghfirah.[2]
وَفِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ﴿١٩﴾
19. Na katika mali zao kuna haki maalumu kwa mwenye kuomba na asiyeomba.
وَفِي الْأَرْضِ آيَاتٌ لِّلْمُوقِنِينَ﴿٢٠﴾
20. Na katika ardhi kuna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa wenye yakini.[3]
وَفِي أَنفُسِكُمْ ۚ أَفَلَا تُبْصِرُونَ﴿٢١﴾
21. Na katika nafsi zenu, je hamuoni?
وَفِي السَّمَاءِ رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ﴿٢٢﴾
22. Na katika mbingu kuna riziki yenu na yale mnayoahidiwa.
فَوَرَبِّ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِنَّهُ لَحَقٌّ مِّثْلَ مَا أَنَّكُمْ تَنطِقُونَ﴿٢٣﴾
23, Basi Naapa kwa Rabb wa mbingu na ardhi, hakika hiyo ni haki kama nyinyi mnavyotamka.
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ الْمُكْرَمِينَ﴿٢٤﴾
24. Je, imekufikia hadithi ya wageni wahishimiwao wa Ibraahiym?
إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ﴿٢٥﴾
25. Walipoingia kwake wakasema: Salaam! Akasema: Salaam watu wasiotambulikana.
فَرَاغَ إِلَىٰ أَهْلِهِ فَجَاءَ بِعِجْلٍ سَمِينٍ﴿٢٦﴾
26. Akaondoka bila kuhisiwa kuelekea kwa ahli yake, akaleta ndama aliyenona.
فَقَرَّبَهُ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ﴿٢٧﴾
27. Akawakurubishia pale walipo, akasema: Mbona hamli?
فَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۖ قَالُوا لَا تَخَفْ ۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ﴿٢٨﴾
28. Akawaogopa ndani ya nafsi yake. Wakasema: Usikhofu! Na wakambashiria ghulamu mjuzi.
فَأَقْبَلَتِ امْرَأَتُهُ فِي صَرَّةٍ فَصَكَّتْ وَجْهَهَا وَقَالَتْ عَجُوزٌ عَقِيمٌ﴿٢٩﴾
29. Mkewe akawakabili kwa ukelele wa furaha, akajipiga usoni na kusema: Kikongwe, tasa!
قَالُوا كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ ۖ إِنَّهُ هُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ﴿٣٠﴾
30. Wakasema: Hivyo ndivyo Alivyosema Rabb wako. Hakika Yeye Ndiye Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.
قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ ﴿٣١﴾
31. (Ibraahiym) akasema: Basi nini shughuli yenu mloikusudia enyi Wajumbe?
قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ ﴿٣٢﴾
32. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wahalifu.
لِنُرْسِلَ عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِّن طِينٍ ﴿٣٣﴾
33. Ili Tuwavurumishie mawe ya udongo.[4]
مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلْمُسْرِفِينَ ﴿٣٤﴾
34. Yaliyotiwa alama kutoka kwa Rabb wako kwa wapindukao mipaka.
فَأَخْرَجْنَا مَن كَانَ فِيهَا مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٣٥﴾
35. Basi Tukawatoa humo wale waliokuwa Waumini.
فَمَا وَجَدْنَا فِيهَا غَيْرَ بَيْتٍ مِّنَ الْمُسْلِمِينَ ﴿٣٦﴾
36. Lakini Hatukukuta humo isipokuwa nyumba moja tu ya Waislamu.
وَتَرَكْنَا فِيهَا آيَةً لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ الْعَذَابَ الْأَلِيمَ ﴿٣٧﴾
37. Na Tukaacha humo Aayah (Athari) kwa wale wanaoogopa adhabu iumizayo.
وَفِي مُوسَىٰ إِذْ أَرْسَلْنَاهُ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ ﴿٣٨﴾
38. Na kwa Muwsaa (pia ipo athari), Tulipomtuma kwa Firawni na miujiza bayana.
فَتَوَلَّىٰ بِرُكْنِهِ وَقَالَ سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ ﴿٣٩﴾
39. Akakengeuka (akitegemea nguvu) na askari na wasaidizi wake akasema: Mchawi au majnuni.[5]
فَأَخَذْنَاهُ وَجُنُودَهُ فَنَبَذْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٌ ﴿٤٠﴾
40. Tukamchukuwa na jeshi lake, kisha Tukawavurumisha katika bahari nailhali yeye ni mwenye kujiletea mwenyewe lawama.
وَفِي عَادٍ إِذْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الرِّيحَ الْعَقِيمَ ﴿٤١﴾
41. Na kwa kina ‘Aad, Tulipowapelekea upepo wa adhabu, mkame.
مَا تَذَرُ مِن شَيْءٍ أَتَتْ عَلَيْهِ إِلَّا جَعَلَتْهُ كَالرَّمِيمِ ﴿٤٢﴾
42. Haukuacha chochote ulichokifikia ila ulikifanya kama kilichobungulika na kuoza.
وَفِي ثَمُودَ إِذْ قِيلَ لَهُمْ تَمَتَّعُوا حَتَّىٰ حِينٍ ﴿٤٣﴾
43. Na kwa kina Thamuwd walipoambiwa: Stareheni kwa muda.
فَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ فَأَخَذَتْهُمُ الصَّاعِقَةُ وَهُمْ يَنظُرُونَ ﴿٤٤﴾
44. Wakafanya ufidhuli kuhusu Amri ya Rabb wao, basi ikawachukuwa radi na umeme angamizi na huku wao wanatazama.
فَمَا اسْتَطَاعُوا مِن قِيَامٍ وَمَا كَانُوا مُنتَصِرِينَ ﴿٤٥﴾
45. Basi hawakuweza kusimama na wala hawakuwa wenye kujinusuru.
وَقَوْمَ نُوحٍ مِّن قَبْلُ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ ﴿٤٦﴾
46. Na watu wa Nuwh hapo kabla. Hakika wao walikuwa kaumu mafasiki.
وَالسَّمَاءَ بَنَيْنَاهَا بِأَيْدٍ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ ﴿٤٧﴾
47. Na mbingu Tumezijenga kwa nguvu na qudra, na hakika Sisi Ndio Wenye Kupanua.
وَالْأَرْضَ فَرَشْنَاهَا فَنِعْمَ الْمَاهِدُونَ ﴿٤٨﴾
48. Na ardhi Tumeitandaza, basi Wazuri Tulioje Sisi wa Kutayarisha!
وَمِن كُلِّ شَيْءٍ خَلَقْنَا زَوْجَيْنِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ ﴿٤٩﴾
49. Na kila kitu Tumeumba jozi mbili; dume na jike ili mpate kukumbuka.
فَفِرُّوا إِلَى اللَّـهِ ۖ إِنِّي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٥٠﴾
50. Basi kimbilieni kwa Allaah. Hakika mimi kwenu ni mwonyaji bayana kutoka Kwake.
وَلَا تَجْعَلُوا مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ ۖ إِنِّي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ ﴿٥١﴾
51. Na wala msifanye pamoja na Allaah mwabudiwa mwingine, hakika mimi kwenu ni mwonyaji bayana kutoka Kwake.
كَذَٰلِكَ مَا أَتَى الَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُوا سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ ﴿٥٢﴾
52. Ndio kama hivyo, hawakuwafikia wale wa kabla yao Rasuli yeyote isipokuwa walisema: Mchawi au majnuni.[6]
أَتَوَاصَوْا بِهِ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ ﴿٥٣﴾
53. Je, wameusiana kwa hayo? Bali wao ni watu wenye kupindukia mipaka ya kuasi.
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ فَمَا أَنتَ بِمَلُومٍ ﴿٥٤﴾
54. Basi jitenge nao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), kwani wewe si mwenye kulaumiwa kabisa.
وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَىٰ تَنفَعُ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٥٥﴾
55. Na kumbusha, kwani hakika ukumbusho unawafaa Waumini.[7]
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾
56. Na Sikuumba majini na wana Aadam isipokuwa waniabudu.
مَا أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ ﴿٥٧﴾
57. Sitaki kutoka kwao riziki yoyote, na wala Sitaki wanilishe.
إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ ﴿٥٨﴾
58. Hakika Allaah Ndiye Mwingi wa Kuruzuku, Mwenye Nguvu Madhubuti.[8]
فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذَنُوبًا مِّثْلَ ذَنُوبِ أَصْحَابِهِمْ فَلَا يَسْتَعْجِلُونِ ﴿٥٩﴾
59. Basi hakika wale waliodhulumu watakuwa na sehemu ya adhabu kama sehemu ya adhabu ya wenzao, basi wasihimize.
فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِن يَوْمِهِمُ الَّذِي يُوعَدُونَ ﴿٦٠﴾
60. Basi ole kwa wale waliokufuru kutokana na Siku yao ambayo wanaahidiwa.
[1] Fadhila Za Kuamka Usiku Kwa Ajili Ya Ibaada:
Aayah hii inaanza kutaja fadhila za Qiyaamul-Layl. Kisha Aayah namba (17-18) inataja sifa za Waumini wanaoacha usingizi wao wakaamka kwa ajili ya kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى).
Na Allaah (سبحانه وتعالى) Anahimiza Qiyaamul-Layl katika Suwrah kadhaa za Qur-aan na kutaja baadhi ya fadhila zake. Na katika Sunnah, fadhila tele zimetajwa. Miongoni mwazo ni:
(i) Qiyaamul-Layl Ni Swalaah Bora Baada Ya Swalaah Za Fardhi:
Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) na kwa riwaayah mbalimbali:
(أَفْضَلُ الصَّلاةِ بَعْدَ الْفَرِيضَةِ صَلاةُ اللَّيْلِ) رواه مسلم
“Swalaah iliyo bora kabisa baada ya fardhi ni Swalaah ya usiku.” [Muslim]
(ii) Kuswali Na Kusoma Japo Aayah Chache:
عبدالله بن عمرو عن النبي صلى الله عليه وسلم ((من قام بعشرِ آياتٍ لم يُكتبْ من الغافلينَ ، ومن قام بمئةِ آيةٍ كُتبَ من القانتينَ ومن قام بألفِ آيةٍ كُتبَ من المُقَنْطِرينَ)) صحيح أبي داود
Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Amr (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayesimama usiku kuswali na akasoma Aayah kumi, hatoandikiwa kuwa miongoni mwa walioghafilika, na atakayesimama kuswali akasoma Aayah mia, ataandikiwa ni miongoni mwa watiifu, na atakayesimama kuswali akasoma Aayah elfu, ataandikwa miongoni mwa wenye mirundi (ya thawabu).’ [Abuu Daawuwd, Al-Albaaniy ameisahihisha: Swahiyh Abiy Daawuwd (1398), Swahiyh Al-Jaami’ (6439)]
(iii) Kufutiwa Madhambi, Kuondoshewa Maradhi):
عن بلال، أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: عليكُم بقيامِ اللَّيلِ ، فإنَّهُ دَأْبُ الصَّالِحينَ قبلَكُم ، و قُربةٌ إلى اللهِ تعالى ومَنهاةٌ عن الإثمِ و تَكفيرٌ للسِّيِّئاتِ ، ومَطردةٌ للدَّاءِ عن الجسَدِ
Amesimulia Bilaal (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Shikamaneni na Qiyaamul-Layl (kuswali usiku), kwani ni desturi za Swalihina (waja wema) kabla yenu, na kujikurubisha kwa Allaah, na inazuia madhambi, inafuta maovu na inaondosha maradhi mwilini.” [Ahmad na At-Tirmidhiy, na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami (4079)]
(iv) Allaah (سبحانه وتعالى) Huteremka Mbingu Ya Dunia. Rejea Al-Mulk (67:16) kwenye Hadiyth inayothibitisha kuwa Anateremka thuluthi ya mwisho ya usiku kusikiliza na kukidhia haja za Waja Wake wanaoamka usiku kwa ajili ya ibaada.
Rejea pia Al-Israa (17:79), As-Sajdah (32:16), Al-Muzzammil (73:1-6).
Pia bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida nyenginezo:
19-Swahiyh Al-Bukhaariy: Kitabu Cha Tahajjud (Swalaah Ya Qiyaam Usiku) - كتاب التهجد [334]
[2] Kuomba Maghfirah Kabla Ya Alfajiri:
Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida kadhaa za maudhui hii:
04-Tawbah Hukmu Na Fadhila Zake: Nyakati Bora Za Kuomba Tawbah [336]
Tawbah: Hukmu Na Fadhila Zake [337]
Rejea An-Nisaa (4:110), Huwd (11:3) kwenye maelezo bayan na rejea mbalimbali. Pia At-Tahriym (66:8), Nuwh (71:10).
[3] Ishara, Dalili Za Ardhini Zinazothibitisha Tawhiyd Ya Allaah (عزّ وجلّ) :
Ishara na Dalili nyingi ardhini na mbinguni zimetajwa katika Qur-aan. Rejea Rejea Yuwsuf (12:105), Fusw-Swilat (41:53). Bali Qur-aan nzima inathibitisha Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى), yakiwemo na mafundisho kutoka kwa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم).
Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) amesema: Hapa Allaah (عزّ وجلّ) Anawaita Waja Wake watafakari na wazingatie:
وَفِي الْأَرْضِ آيَاتٌ لِّلْمُوقِنِينَ﴿٢٠﴾
“Na katika ardhi kuna Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa wenye yakini.”
Inajumuisha ardhi yenyewe na yote yaliyomo humo kama milima, bahari, mito, miti na mimea ambavyo vyote vinaashiria kwa mwenye kutafakari na kuzingatia maana zake, juu ya Utukufu wa Muumbaji wake na Upana wa Mamlaka Yake, na ueneaji usio na ukomo wa Ihsaan Yake, na jinsi Ujuzi Wake unavyovizunguka vitu vyote vinavyoonekana na vilivyofichika. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[4] Adhabu Na Maangamizi Ya Kaumu Za Awali:
Kuanzia Aayah hii na zinazoendelea, panatajwa baadhi ya kaumu za awali, na maangamizi na adhabu zao baada ya kuwakanusha Rusuli wa Allaah.
Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye maelezo na uchambuzi kuhusu: Makafiri wa nyumati za nyuma na aina za adhabu zao.
[6] Makafiri Kuwapachika Rusuli Wao Sifa Ovu:
Sifa ovu kadhaa alipachikwa nazo Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) na adui wake Firawni. Mara amwite mchawi mjuzi, mara majnuni, mara muongo. Rejea Suwrah hii Adh-Dhaariyaat (51:39), Al-A’raaf (7:109), Al-Israa (17:101), Twaahaa (20:63), Ash-Shu’araa (26:34), Ghaafir (40:24), Az-Zukhruf (43:49).
Na ada hiyo ilikuwa pia ni ada ya makafiri wengineo wa awali kuwapachika sifa ovu Rusuli wao kama Anavyosema haya Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah hii:
كَذَٰلِكَ مَا أَتَى الَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُوا سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ ﴿٥٢﴾
“Ndio kama hivyo, hawakuwafikia wale wa kabla yao Rasuli yeyote isipokuwa walisema: Mchawi au majnuni.” [Adh-Dhaariyaat (51:52)]
Hali kadhaalika, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pia alipachikwa sifa ovu na washirikina wa Makkah. Rejea Al-Furqaan (25:4) kwenye uchambuzi wa sifa hizo na rejea zake mbalimbali.
[7] Umuhimu Wa Kukumbushana Mambo Ya Dini:
Aayah hii ni kama Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ الذِّكْرَىٰ ﴿٩﴾ سَيَذَّكَّرُ مَن يَخْشَىٰ ﴿١٠﴾
“Basi kumbusha ikiwa unafaa ukumbusho. Atakumbuka yule anayeogopa.” [Al-A’laa (87:9-10]
Na Allaah (سبحانه وتعالى) Akasisitiza katika Aayah nyingi kukumbushana mambo ya Dini ikiwa ni pamoja na kuamrishana mema na kukatazana maovu. Rejea Aal-‘Imraan (3:104), (3:110) (3:114), At-Tawbah (9:71), (9:112).
Bonyeza pia viungo vifuatavyo:
Na katika kiungo kifuatacho, kuna makala tele zenye maudhui mbalimbali za kukumbushana ambazo zitamsaidia Muislamu kuamrisha mema na kukataza maovu:
Lu-ulu-un-Manthuwrun - لُؤْلُؤ مَّنثُور [341]
Na kuna Hadiyth tele zinazotilia mkazo maudhui hii ya kukumbusha watu mambo ya Dini, kuamrisha mema na kukataza maovu. Na kazi hii, ni kazi ya Rusuli wote wa Allaah (سبحانه وتعالى) na imeisitizwa mno kwa Waumini, na fadhila zake ni nyingi na adhimu. Bonyeza kiungo kifuatacho:
Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa - أَحاديثُ عَنْ فَضْلِ الْعِلْم وَالْعُلَمَاء [342]
[8] Kuwa Na Nguvu Ni Katika Sifa Za Allaah:
‘Aqiydah ya Ahlus-Sunnah wal-Jama’aah ni kuthibitisha Sifa za Allaah (سبحانه وتعالى) kama zilivothibitishwa katika Qur-aan na Sunnah. Hivyo basi, Allaah (سبحانه وتعالى) Anaposema kuwa Yeye ni Qawiyy (Mwenye Nguvu), sisi ni lazima tuamini kuwa Ana nguvu. Na Anaposema Kuwa Yeye Ana Qudra (Uwezo), sisi ni lazima tuamini kuwa Anao Uwezo. Lakini Sifa hizo za Nguvu Zake, au Uwezo Wake, hazifanani kabisa na kiumbe chochote kile!
Rejea Huwd (11:37), Twaahaa (20:46).
Rejea pia Al-Baqarah (2:165), Al-Anfaal (8:52), Huwd (11:66), Al-Ahzaab (33:25), Ghaafir (40:22), Al-Hajj (22:40), (22:74).
الطُّور
052-Atw-Twuur
052-Atw-Twuur: Utangulizi Wa Suwrah [344]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالطُّورِ ﴿١﴾
1. Naapa kwa mlima.[1]
وَكِتَابٍ مَّسْطُورٍ ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa Kitabu kilichoandikwa.[2]
فِي رَقٍّ مَّنشُورٍ ﴿٣﴾
3. Katika karatasi nyembamba ya ngozi iliyokunjuliwa.
وَالْبَيْتِ الْمَعْمُورِ ﴿٤﴾
4. Na Naapa kwa Nyumba yenye kuamiriwa mara kwa mara (na Malaika).[3]
وَالسَّقْفِ الْمَرْفُوعِ ﴿٥﴾
5. Na Naapa kwa dari iliyonyanyuliwa (mbingu).
وَالْبَحْرِ الْمَسْجُورِ ﴿٦﴾
6. Na Naapa kwa bahari iliyojazwa (maji au itakayowashwa moto).
إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ لَوَاقِعٌ ﴿٧﴾
7. Hakika adhabu ya Rabb wako bila shaka itatokea.
مَّا لَهُ مِن دَافِعٍ ﴿٨﴾
8. Hakuna mzuiaji.
يَوْمَ تَمُورُ السَّمَاءُ مَوْرًا ﴿٩﴾
9. Siku zitakapotaharaki mbingu na kutikisika kikweli.
وَتَسِيرُ الْجِبَالُ سَيْرًا ﴿١٠﴾
10. Na milima ikatembea mwendo wa kasi.
فَوَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿١١﴾
11. Basi ole Siku hiyo kwa wakadhibishao.
الَّذِينَ هُمْ فِي خَوْضٍ يَلْعَبُونَ ﴿١٢﴾
12. Ambao wamo katika kushughulika na upuuzi wakicheza.
يَوْمَ يُدَعُّونَ إِلَىٰ نَارِ جَهَنَّمَ دَعًّا ﴿١٣﴾
13. Siku watakayovurumishwa katika Moto wa Jahannam kwa msukumo wa nguvu.
هَـٰذِهِ النَّارُ الَّتِي كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ ﴿١٤﴾
14. Huu ndio ule moto ambao mlikuwa mkiukadhibisha.
أَفَسِحْرٌ هَـٰذَا أَمْ أَنتُمْ لَا تُبْصِرُونَ ﴿١٥﴾
15. Je, ni sihiri hii au nyinyi hamuoni?
اصْلَوْهَا فَاصْبِرُوا أَوْ لَا تَصْبِرُوا سَوَاءٌ عَلَيْكُمْ ۖ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٦﴾
16. Ingieni muungue humo, mkistahmili au msistahmili ni sawasawa kwenu, hakika hapana ila mnalipwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَنَعِيمٍ ﴿١٧﴾
17. Hakika wenye taqwa watakuwa katika Jannaat na Neema.[4]
فَاكِهِينَ بِمَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ وَوَقَاهُمْ رَبُّهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ ﴿١٨﴾
18. Wakifurahia kwa ambayo Amewapa Rabb wao, na Atawalinda na adhabu ya moto uwakao vikali mno.
كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٩﴾
19. Kuleni na kunyweni kwa raha kwa sababu ya mliyokuwa mnatenda.
مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ سُرُرٍ مَّصْفُوفَةٍ ۖ وَزَوَّجْنَاهُم بِحُورٍ عِينٍ ﴿٢٠﴾
20. Wakiegemea juu ya makochi ya fakhari yaliyopangwa safusafu, na Tutawaozesha hurulaini: wanawake weupe wazuri wa Jannah wenye macho makubwa ya kupendeza.
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَاتَّبَعَتْهُمْ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَانٍ أَلْحَقْنَا بِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَمَا أَلَتْنَاهُم مِّنْ عَمَلِهِم مِّن شَيْءٍ ۚ كُلُّ امْرِئٍ بِمَا كَسَبَ رَهِينٌ ﴿٢١﴾
21. Na wale walioamini na wakafuatwa na dhuriya wao kwa imaan, Tutawakutanisha nao dhuriya wao na Hatutawapunguzia katika ‘amali zao kitu chochote. Kila mtu atafungika kwa yale aliyoyachuma.[5]
وَأَمْدَدْنَاهُم بِفَاكِهَةٍ وَلَحْمٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ ﴿٢٢﴾
22. Na Tutawapa matunda na nyama katika ambavyo wanatamani.
يَتَنَازَعُونَ فِيهَا كَأْسًا لَّا لَغْوٌ فِيهَا وَلَا تَأْثِيمٌ ﴿٢٣﴾
23. Watabadilishana humo gilasi za mvinyo usiosababisha maneno ya upuuzi wala ya dhambi.
وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ غِلْمَانٌ لَّهُمْ كَأَنَّهُمْ لُؤْلُؤٌ مَّكْنُونٌ ﴿٢٤﴾
24. Na watawazungukia watumishi vijana kwa ajili yao kama kwamba ni lulu zilizohifadhiwa.
وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ ﴿٢٥﴾
25. Na wataelekeana wao kwa wao wakiulizana.[6]
قَالُوا إِنَّا كُنَّا قَبْلُ فِي أَهْلِنَا مُشْفِقِينَ ﴿٢٦﴾
26. Watasema: Hakika sisi tulikuwa kabla tukiishi baina ya ahli zetu huku tukiogopa.
فَمَنَّ اللَّـهُ عَلَيْنَا وَوَقَانَا عَذَابَ السَّمُومِ ﴿٢٧﴾
27. Basi Allaah Akatuneemesha, na Akatuokoa na adhabu ya moto unaobabua.
إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلُ نَدْعُوهُ ۖ إِنَّهُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ ﴿٢٨﴾
28. Hakika sisi tulikuwa kabla Tunamuomba Yeye Pekee. Hakika Yeye Ndiye Mwingi wa Ihsaan na Fadhila, Mwenye Kurehemu.
فَذَكِّرْ فَمَا أَنتَ بِنِعْمَتِ رَبِّكَ بِكَاهِنٍ وَلَا مَجْنُونٍ ﴿٢٩﴾
29. Basi kumbusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), kwani hakika wewe kwa Neema ya Rabb wako, si kahini wala si majnuni.
أَمْ يَقُولُونَ شَاعِرٌ نَّتَرَبَّصُ بِهِ رَيْبَ الْمَنُونِ ﴿٣٠﴾
30. Au wanasema (huyu Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ni mshairi, tunamtazamia kupatikana na maafa ya dahari.
قُلْ تَرَبَّصُوا فَإِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُتَرَبِّصِينَ ﴿٣١﴾
31. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ngojeeni kwani hakika na mimi ni pamoja nanyi ni miongoni mwa wenye kungojea.
أَمْ تَأْمُرُهُمْ أَحْلَامُهُم بِهَـٰذَا ۚ أَمْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ ﴿٣٢﴾
32. Au zinawaamrisha akili zao haya? Au basi tu wao ni watu wenye kupindukia mipaka kuasi?
أَمْ يَقُولُونَ تَقَوَّلَهُ ۚ بَل لَّا يُؤْمِنُونَ ﴿٣٣﴾
33. Au wanasema ameibuni (Qur-aan)? Bali hawaamini.[7]
فَلْيَأْتُوا بِحَدِيثٍ مِّثْلِهِ إِن كَانُوا صَادِقِينَ ﴿٣٤﴾
34. Basi walete kauli mfano wake wakiwa ni wakweli.[8]
أَمْ خُلِقُوا مِنْ غَيْرِ شَيْءٍ أَمْ هُمُ الْخَالِقُونَ ﴿٣٥﴾
35. Au wameumbwa pasipo na kitu chochote au wao ndio waumbaji?
أَمْ خَلَقُوا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۚ بَل لَّا يُوقِنُونَ ﴿٣٦﴾
36. Au wameumba mbingu na ardhi? Bali hawana yakini.
أَمْ عِندَهُمْ خَزَائِنُ رَبِّكَ أَمْ هُمُ الْمُصَيْطِرُونَ ﴿٣٧﴾
37. Au wanazo Hazina za Rabb wako, au wao ndio wenye madaraka?
أَمْ لَهُمْ سُلَّمٌ يَسْتَمِعُونَ فِيهِ ۖ فَلْيَأْتِ مُسْتَمِعُهُم بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ ﴿٣٨﴾
38. Au wanazo ngazi wanasikilizia kwa makini humo? Basi msikilizaji wao alete dalili bayana.
أَمْ لَهُ الْبَنَاتُ وَلَكُمُ الْبَنُونَ ﴿٣٩﴾
39. Au (Allaah) Ana mabanati, nanyi mna watoto wa kiume?[9]
أَمْ تَسْأَلُهُمْ أَجْرًا فَهُم مِّن مَّغْرَمٍ مُّثْقَلُونَ ﴿٤٠﴾
40. Au unawaomba ujira kwa hiyo wameelemewa na uzito wa gharama?
أَمْ عِندَهُمُ الْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ ﴿٤١﴾
41. Au wanayo ilimu ya ghaibu kisha wao wanaandika?
أَمْ يُرِيدُونَ كَيْدًا ۖ فَالَّذِينَ كَفَرُوا هُمُ الْمَكِيدُونَ ﴿٤٢﴾
42. Au wanakusudia hila? Basi wale waliokufuru wao ndio watakaorudiwa na hila zao.
أَمْ لَهُمْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ اللَّـهِ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٤٣﴾
43. Au wana ilaah asiyekuwa Allaah? Subhaana-Allaah! (Utakasifu ni wa Allaah) kutokana na ambayo wanafanya shirki.
وَإِن يَرَوْا كِسْفًا مِّنَ السَّمَاءِ سَاقِطًا يَقُولُوا سَحَابٌ مَّرْكُومٌ ﴿٤٤﴾
44. Na hata wangeliona pande kutoka mbinguni linaanguka wangelisema: Mawingu yamerundikana.
فَذَرْهُمْ حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي فِيهِ يُصْعَقُونَ ﴿٤٥﴾
45. Basi waachilie mbali mpaka wakutane na Siku yao ambayo humo watapigwa na mngurumo na mwako wa umeme waangamizwe.
يَوْمَ لَا يُغْنِي عَنْهُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٤٦﴾
46. Siku ambayo hila zao hazitowafaa kitu chochote, na wala wao hawatonusuriwa.
وَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا عَذَابًا دُونَ ذَٰلِكَ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٤٧﴾
47. Na hakika wale waliodhulumu watapata adhabu nyingine isiyokuwa hiyo, lakini wengi wao hawajui.
وَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعْيُنِنَا ۖ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ حِينَ تَقُومُ ﴿٤٨﴾
48. Na vuta subira (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa hukumu ya Rabb wako, kwani hakika wewe uko chini ya Macho Yetu. Na Sabbih pamoja na kumhimidi Rabb wako, wakati unapoinuka (usiku).[10]
وَمِنَ اللَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَإِدْبَارَ النُّجُومِ ﴿٤٩﴾
49. Na katika usiku Msabbih na zinapokuchwa nyota.
[1] Mlima Ambao Mahali Hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Aliongea Na Nabiy Muwsaa (عليه السّلام):
Allaah (سبحانه وتعالى) Anaapa kwa vitu vikubwa vyenye hikma kubwa za ufufuo, malipo ya waja wema na waliokadhibisha. Anaapa kwa Mlima ambao hapo Aliongea na Nabiy Muwsaa Ibn ‘Imraan (عليه السّلام) , Akampa Wahy ya yale Aliyomfunulia katika hukmu mbalimbali. Na katika hayo, kuna fadhila kwake na kwa ummah wake ambazo ni miongoni mwa Aayaat Adhimu na Neema Zake ambazo waja hawawezi kuzihesabu au kuzitathmini ipasavyo kwa kuwa ni zaidi ya kipimo wanachokisia. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[2] Kitabu Kilichoandikwa
Ni Al-Lawh Al-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa) au Qur-aan. Rejea Al-An’aam (6:38), Ar-Ra’d (13:39), Al-Buruwj (85:22).
[3] Bayt Al-Ma’muwr:
Ni nyumba iliyoko juu ya mbingu ya saba ambayo inajaa Malaika watukufu wakati wote. Kila siku Malaika sabiini elfu wanaingia humo kumwabudu Rabb wao kisha hawarudi tena mpaka Siku ya Qiyaamah. Na imesemekana kuwa Baytul-Ma’muwr ni Nyumba Tukufu ya Allaah na inajaa wanaoswali na wanaomdhukuru Allaah nyakati zote, pamoja na wanaoifikia kwa Hajj na ‘Umrah. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Na Ma’muwr iliyoko mbingu ya saba, ndiyo ambayo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimkuta Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) akiwa ameegemezea mgongo wake kwenye ukuta wake, na humo wanaingia Malaika elfu sabiini (kila siku). (Haya yapo katika Hadiyth ndefu iliyopokelewa na Imaam Muslim katika Kitaab cha Al- Iymaan na wengineo).
[4] Miongoni Mwa Neema Za Jannah:
Aayah hii kuanzia namba (17) hadi (24), zinatajwa baadhi ya neema za Jannah. Rejea Faatwir (35:33) kwenye neema nyenginezo zilizotajwa na rejea mbalimbali.
[5] Ahli Watakutanishwa Jannah (Peponi) Na Vizazi Vyao Ikiwa Watathibiti Katika Imaan:
Hii ni katika utimilifu wa neema za watu wa Jannah kwamba, Allaah (عزّ وجلّ) Atawakutanisha na vizazi vyao ambao wamewafuata katika imaan, yaani Allaah (عزّ وجلّ) Atawafanya vizazi vyao hao, kufikia daraja za wazazi huko Jannah hata kama matendo yao hayatatosha kufikia daraja za wazazi, kuwa kama ni ongezeko la thawabu kwa wazazi. Na hayo hayatapunguza chochote katika amali za wazazi. Kwa vile huenda watu wakadhania kwamba vivyo hivyo itakuwa hali ya watu wa motoni, na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Atawafanya vizazi vyao au wazazi wao kuungana motoni, Allaah (سبحانه وتعالى) Anatujulisha kwamba hukmu za sehemu mbili hizi (wakaazi wa Jannah na motoni) hazilingani sawa. Moto ni makazi ya uadilifu, na katika uadilifu wa Allaah ni kwamba Hamuadhibishi mtu isipokuwa kwa madhambi yake mwenyewe. Ndio maana Anasema:
كُلُّ امْرِئٍ بِمَا كَسَبَ رَهِينٌ ﴿٢١﴾
“Kila mtu atafungika kwa yale aliyoyachuma.”
Yaani mbebaji hatobeba mzigo (wa dhambi) wa mwengine, na mtu hatabebeshwa dhambi za mwengine. Utofauti huo ni kwa ajili ya kuondosha utata kufahamu swala lilotajwa. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[6] Watu Wa Jannah Wataelekeana Kuulizana:
Aayah hii namba (25) hadi (28):
Wataelezeana kuhusu mambo ya dunia na yaliyojiri ambayo yamewafikisha katika hali hii waliyonayo ya neema (za Jannah) na furaha, na kwamba walikuwa wakikhofu adhabu wakajiepusha na madhambi kutokana na kukhofia adhabu. Basi Allaah Akawaneemesha kwa hidaaya na tawfiyq na Akawakinga na adhabu, nayo ni moto mkali mno. Na kwamba walikuwa wakimsabilia kumuomba Yeye Pekee bila ya kumshirikisha na chochote ili Awakinge na adhabu ya moto na Awajaalie wapate neema hiyo ya Jannah. Hii inajumuisha duaa za ibaada na duaa za kuomba mas-ala mengineyo. (Watasema watu wa Jannah):
Basi Rabb wetu Akatuneemesha na Akatuitikia duaa zetu, kwani hakika Yeye ni
هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ
“Mwingi wa Ihsaan na Fadhila, Mwenye Kurehemu.”
Na katika Wema Wake na Rehma Zake (Allaah), Ametujaalia Radhi Zake na kuturuzuku Jannah, na Ametulinda na Ghadhabu Zake na moto. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[7] Makafiri Kumsingizia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kuwa Ameitunga Qur-aan:
Rejea Al-Furqaan (25:4) kwenye uchambuzi wa maudhui hii pamoja na rejea mbalimbali.
[8] Changamoto Ya Kuleta Mfano Wa Qur-aan Wala Hakuna Awezaye Kamwe!
Rejea Yuwnus (10:38), Al-Israa (17:88), Al-Baqarah (2:23-24). Rejea pia Al-An’aam (6:93) ambako kumetajwa waongo waliodai Unabii.
[9] Washirikina Kumsingizia Allaah Kuwa Ana Wana Wa Kike:
Rejea Asw-Swaaffaat (37:149) kwenye maelezo na rejea mbalimbali.
[10] Kumdhukuru Allaah (عزّ وجلّ) Usiku Na Fadhila Zake:
Aayah hii namba (48) na inayomalizia Suwrah hii ya (49), inatajwa maamrisho ya kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) usiku. Na maamrisho kama hayo na mengineyo pamoja na fadhila zake yametajwa katika Aayah kadhaa. Rejea Adh-Dhaariyaat (51:15) kwenye faida na rejea mbalimbali. Na Aayah nyenginezo pia ni kwenye Aal-‘Imraan (3:113), Al-Israa (17:78-79), As-Sajdah (32:15-17), Az-Zumar (39:9), Qaaf (50:39-40), Al- Muzzammil (73:1-7), (73:20).
Na miongoni mwa Hadiyth, ni hii ifuatayo ambayo inaelezea fadhila adhimu ya kumdhukuru Allaah usiku, kumwomba na kutakabaliwa duaa:
عَنْ عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنْ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((مَنْ تَعَارَّ مِنْ اللَّيْلِ فَقَالَ: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ وَلاَ حَوْلَ ولاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ، ثُمَّ قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي، أَوْ دَعَا اسْتُجِيبَ لَهُ، فَإِنْ عَزَمَ فَتَوَضَّأَ ثُمَّ صَلَّى قُبِلَتْ صَلَاتُهُ))
Amesimulia ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayeamka usiku akasema:
: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ وَلاَ حَوْلَ ولاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ، رَبِّ اغْفِرْ لِي
Laa ilaaha illa-Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-Hamdu wa-Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr, wa Subhaana-Allaah wal-HamduliLLaah walaa ilaaha illa-Allaah wa-Allaahu Akbar walaa hawla walaa quwwata illa biLlaah (Hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah Pekee Hana mshirika, Ufalme ni Wake na Himdi ni Zake Naye ni Mweza wa kila kitu. Ametakasika Allaah, na Himdi ni za Allaah, na hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, Allaah ni Mkubwa kabisa, na hapana uwezo wala nguvu ila za Allaah).
Kisha akasema:
رَبِّ اغْفِرْ لِي
Rabbigh-fir-liy (Ee Allaah, nighufurie).
Au akaomba, ataitikiwa. Na akiazimia kutawadha na kuswali atatakabaliwa Swalaah yake.” [Al-Bukhaariy na wengineo]
Bonyeza kiungo kifuatacho kwenye faida kadhaa:
النَّجْم
053-An-Najm
053-An-Najm: Utangulizi Wa Suwrah [348]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالنَّجْمِ إِذَا هَوَىٰ ﴿١﴾
1. Naapa kwa nyota zinapotua.[1]
مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَىٰ ﴿٢﴾
2. Hakupotoka sahibu wenu na wala hakukosea.
وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾
3. Na wala hatamki kwa hawaa.
إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾
4. Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa.
عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَىٰ ﴿٥﴾
5. Amemfunza (Jibriyl) mwenye nguvu shadidi.
ذُو مِرَّةٍ فَاسْتَوَىٰ ﴿٦﴾
6. Mwenye muonekano jamili, muruwa na nguvu na kisha akalingamana sawasawa.
وَهُوَ بِالْأُفُقِ الْأَعْلَىٰ ﴿٧﴾
7. Naye yuko juu kabisa katika upeo wa macho.
ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ ﴿٨﴾
8. Kisha akakurubia na akashuka.
فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَىٰ ﴿٩﴾
9. Kisha akawa kiasi cha umbali wa mipinde miwili au karibu zaidi.
فَأَوْحَىٰ إِلَىٰ عَبْدِهِ مَا أَوْحَىٰ ﴿١٠﴾
10. (Allaah) Akamfunulia Wahy Mja Wake yale Aliyomfunulia Wahy.
مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَىٰ ﴿١١﴾
11. Moyo haukukadhibisha yale aliyoyaona.
أَفَتُمَارُونَهُ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ ﴿١٢﴾
12. Je, mnambishia kuhusu yale aliyoyaona?
وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ ﴿١٣﴾
13. Na kwa yakini amemuona (Jibriyl) katika uteremko mwingine.
عِندَ سِدْرَةِ الْمُنتَهَىٰ ﴿١٤﴾
14. Kwenye mkunazi wa mpaka wa mwisho kabisa.[2]
عِندَهَا جَنَّةُ الْمَأْوَىٰ ﴿١٥﴾
15. Karibu yake kuna Jannah ya Al-Ma-waa.[3]
إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ ﴿١٦﴾
16. Ulipoufunika mkunazi huo unachokifunika.
مَا زَاغَ الْبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ ﴿١٧﴾
17. Jicho lake halikukengeuka wala halikupinduka mipaka.
لَقَدْ رَأَىٰ مِنْ آيَاتِ رَبِّهِ الْكُبْرَىٰ ﴿١٨﴾
18. Kwa yakini aliona miongoni mwa Aayaat (Ishara, Dalili) za Rabb wake kubwa kabisa.
أَفَرَأَيْتُمُ اللَّاتَ وَالْعُزَّىٰ ﴿١٩﴾
19. Je, mmemwona laata na ‘uzzaa?[4]
وَمَنَاةَ الثَّالِثَةَ الْأُخْرَىٰ ﴿٢٠﴾
20. Na manaata mwengine wa tatu?
أَلَكُمُ الذَّكَرُ وَلَهُ الْأُنثَىٰ ﴿٢١﴾
21. Je, nyinyi mna wana wa kiume Naye Ana wana wa kike?[5]
تِلْكَ إِذًا قِسْمَةٌ ضِيزَىٰ ﴿٢٢﴾
22. Hiyo basi hapo ni mgawanyo wa dhulma kubwa!
إِنْ هِيَ إِلَّا أَسْمَاءٌ سَمَّيْتُمُوهَا أَنتُمْ وَآبَاؤُكُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ بِهَا مِن سُلْطَانٍ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَمَا تَهْوَى الْأَنفُسُ ۖ وَلَقَدْ جَاءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ الْهُدَىٰ ﴿٢٣﴾
23. Hayo si chochote isipokuwa ni majina mmeyaita nyinyi na baba zenu, wala Allaah Hakuyateremshia dalili yoyote. Hawafuati isipokuwa dhana na yale yanayotamani nafsi (zao), na hali umekwishawajia kutoka kwa Rabb wao Mwongozo.
أَمْ لِلْإِنسَانِ مَا تَمَنَّىٰ ﴿٢٤﴾
24. Kwani hivi binaadamu anapata yote anayoyatamani?
فَلِلَّـهِ الْآخِرَةُ وَالْأُولَىٰ ﴿٢٥﴾
25. Basi ni ya Allaah Pekee ya Aakhirah na ya mwanzo (ya dunia).
وَكَم مِّن مَّلَكٍ فِي السَّمَاوَاتِ لَا تُغْنِي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا إِلَّا مِن بَعْدِ أَن يَأْذَنَ اللَّـهُ لِمَن يَشَاءُ وَيَرْضَىٰ ﴿٢٦﴾
26. Na Malaika wangapi mbinguni hautowafaa chochote uombezi wao isipokuwa baada ya kuwa Allaah Ametoa idhini kwa Amtakaye na Akaridhia.[6]
إِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ لَيُسَمُّونَ الْمَلَائِكَةَ تَسْمِيَةَ الْأُنثَىٰ ﴿٢٧﴾
27. Hakika wale wasioamini Aakhirah bila shaka wanawaita Malaika kwa majina ya kike.
وَمَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ ۖ وَإِنَّ الظَّنَّ لَا يُغْنِي مِنَ الْحَقِّ شَيْئًا ﴿٢٨﴾
28. Na wala hawana ujuzi wowote ule wa hayo. Hawafuati isipokuwa dhana, na hakika dhana haifai kitu chochote mbele ya haki.
فَأَعْرِضْ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكْرِنَا وَلَمْ يُرِدْ إِلَّا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿٢٩﴾
29. Basi achana mbali na ambaye ameupa mgongo Ukumbusho Wetu na wala hataki isipokuwa uhai wa dunia.
ذَٰلِكَ مَبْلَغُهُم مِّنَ الْعِلْمِ ۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِ وَهُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اهْتَدَىٰ ﴿٣٠﴾
30. Huo ndio upeo wao wa ilimu. Hakika Rabb wako Anamjua zaidi aliyepotoka Njia Yake na Yeye Anamjua zaidi aliyehidika.
وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ أَسَاءُوا بِمَا عَمِلُوا وَيَجْزِيَ الَّذِينَ أَحْسَنُوا بِالْحُسْنَى ﴿٣١﴾
31. Na ni vya Allaah Pekee vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini ili Awalipe wale waliofanya uovu kwa yale waliyoyatenda, na Awalipe wale waliofanya mema kwa mema zaidi.
الَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ إِلَّا اللَّمَمَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ وَاسِعُ الْمَغْفِرَةِ ۚ هُوَ أَعْلَمُ بِكُمْ إِذْ أَنشَأَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَإِذْ أَنتُمْ أَجِنَّةٌ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ ۖ فَلَا تُزَكُّوا أَنفُسَكُمْ ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَىٰ ﴿٣٢﴾
32. Wale wanaojiepusha na madhambi makubwa na machafu isipokuwa makosa madogo-madogo.[7] Hakika Rabb wako ni Mkunjufu wa Kughufuria. Yeye Anakujueni vyema, tangu Alipokuanzisheni kutoka katika ardhi, na pale mlipokuwa mimba changa matumboni mwa mama zenu. Basi msizitakase nafsi zenu. Yeye Anamjua zaidi aliyekuwa na taqwa.
أَفَرَأَيْتَ الَّذِي تَوَلَّىٰ ﴿٣٣﴾
33. Je, (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) umemuona yule aliyegeukia mbali?
وَأَعْطَىٰ قَلِيلًا وَأَكْدَىٰ ﴿٣٤﴾
34. Na akatoa kidogo, kisha akazuia.
أَعِندَهُ عِلْمُ الْغَيْبِ فَهُوَ يَرَىٰ ﴿٣٥﴾
35. Je, anayo ilimu ya ghaibu hivyo basi anaona?
أَمْ لَمْ يُنَبَّأْ بِمَا فِي صُحُفِ مُوسَىٰ ﴿٣٦﴾
36. Au hakujulishwa yale yaliyomo katika Suhuf za Muwsaa?[8]
وَإِبْرَاهِيمَ الَّذِي وَفَّىٰ ﴿٣٧﴾
37. Na Ibraahiym aliyetimiza (ahadi).
أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ﴿٣٨﴾
38. Na kwamba mbebaji dhambi hatobeba mzigo wa mwenginewe.
وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ ﴿٣٩﴾
39. Na kwamba binaadam hatopata (jazaa) isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi.
وَأَنَّ سَعْيَهُ سَوْفَ يُرَىٰ ﴿٤٠﴾
40. Na kwamba juhudi yake itakuja kuonekana.
ثُمَّ يُجْزَاهُ الْجَزَاءَ الْأَوْفَىٰ ﴿٤١﴾
41. Kisha atalipwa jazaa kamilifu.
وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الْمُنتَهَىٰ ﴿٤٢﴾
42. Na kwamba kwa Rabb wako ndio kikomo.
وَأَنَّهُ هُوَ أَضْحَكَ وَأَبْكَىٰ ﴿٤٣﴾
43. Na kwamba Yeye Ndiye Anayesababisha kicheko na kilio.
وَأَنَّهُ هُوَ أَمَاتَ وَأَحْيَا ﴿٤٤﴾
44. Na kwamba Yeye Ndiye Anayefisha na Anayehuisha.
وَأَنَّهُ خَلَقَ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ ﴿٤٥﴾
45. Na kwamba Yeye Ameumba jozi mbili; dume na jike.
مِن نُّطْفَةٍ إِذَا تُمْنَىٰ ﴿٤٦﴾
46. Kutokana na tone la manii linapomiminwa.
وَأَنَّ عَلَيْهِ النَّشْأَةَ الْأُخْرَىٰ ﴿٤٧﴾
47. Na kwamba ni juu Yake uanzishaji mwengineo (kufufua).
وَأَنَّهُ هُوَ أَغْنَىٰ وَأَقْنَىٰ ﴿٤٨﴾
48. Na kwamba Yeye Ndiye Atoshelezaye na Akinaishaye.
وَأَنَّهُ هُوَ رَبُّ الشِّعْرَىٰ ﴿٤٩﴾
49. Na kwamba Yeye Ndiye Rabb wa nyota ya Ash-Shi’-raa[9] (inayoabudiwa).
وَأَنَّهُ أَهْلَكَ عَادًا الْأُولَىٰ ﴿٥٠﴾
50. Na kwamba Yeye Ndiye Aliyeangamiza kina ‘Aad wa awali.
وَثَمُودَ فَمَا أَبْقَىٰ ﴿٥١﴾
51. Na kina Thamuwd kisha Hakubakisha.
وَقَوْمَ نُوحٍ مِّن قَبْلُ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا هُمْ أَظْلَمَ وَأَطْغَىٰ ﴿٥٢﴾
52. Na kaumu ya Nuwh hapo kabla. Hakika wao walikuwa madhalimu zaidi na wapindukaji mipaka zaidi ya kuasi.
وَالْمُؤْتَفِكَةَ أَهْوَىٰ ﴿٥٣﴾
53. Na miji iliyopinduliwa.[10] Ameiporomosha mbali mbali.
فَغَشَّاهَا مَا غَشَّىٰ ﴿٥٤﴾
54. Vikaifunika vilivyofunika.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكَ تَتَمَارَىٰ ﴿٥٥﴾
55. Basi Neema gani za Rabb wako unazitilia shaka?
هَـٰذَا نَذِيرٌ مِّنَ النُّذُرِ الْأُولَىٰ ﴿٥٦﴾
56. Huyu (Rasuli صلى الله عليه وآله وسلم) ni mwonyaji wa yale maonyo ya awali.
أَزِفَتِ الْآزِفَةُ ﴿٥٧﴾
57. Kimekaribia kinachokaribia.
لَيْسَ لَهَا مِن دُونِ اللَّـهِ كَاشِفَةٌ ﴿٥٨﴾
58. Hakuna chenye uwezo wa kukifichua isipokuwa Allaah.
أَفَمِنْ هَـٰذَا الْحَدِيثِ تَعْجَبُونَ ﴿٥٩﴾
59. Je, mnastaajabu kwa Hadiyth hii (ya Qur-aan)?
وَتَضْحَكُونَ وَلَا تَبْكُونَ ﴿٦٠﴾
60. Na mnacheka na wala hamlii?
وَأَنتُمْ سَامِدُونَ ﴿٦١﴾
61. Na hali nyinyi mnaghafilika, mnadharau na kushughulika na anasa?
فَاسْجُدُوا لِلَّـهِ وَاعْبُدُوا ۩﴿٦٢﴾
62. Basi msujudieni Allaah na mwabuduni Yeye.[11]
[1] Uthibitisho Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), Ukweli Wake, Wahy, Na Safari Ya Israa Wal-Mi’raaj:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anaanza Aayah namba (1) ya Suwrah hii tukufu kwa kiapo cha nyota zinapotua. Kisha Anaendelea Aayah zinazofuatia hadi namba (18) kuthibitisha ukweli wa kumtuma Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na kuwapinga waliomkadhibisha pamoja na kukadhibisha Safari yake ya muujiza ya Israa wal- Mi’raaj. Na pia Anathibitisha Wahy Aliomteremshia kupitia Jibriyl (عليه السّلام). Rejea Al-Israa (17:1) kwenye maelezo na faida kuhusu safari hiyo tukufu.
[2] Sidratul-Muntahaa: (Mkunazi Wa Mwisho):
Sidr ni mkunazi, na Sidratul-Muntahaa imekusudiwa ni kituo cha mwisho wa Safari ya Al-Israa Wal-Mi’raaj.
Zifuatazo ni baadhi ya Hadiyth zinazoelezea kuhusu tukio hili adhimu:
Amesema ‘Abdullaah bin Mas’uwd: Wakati Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipochukuliwa safari yake kwenda mbinguni, alifikishwa mpaka Sidratul-Muntahaa ambapo kila kitu kinachopanda kutoka ardhini hukomea hapo, na na kile kinachoshuka kutoka juu hukomea hapo pia…” [Muslim 329]
Na pia,
Rasuli wa Allaah (سبحانه وتعالى) amesema: “Kisha nilichukuliwa hadi Sidratul-Muntahaa mti ambao majani yake ni kama masikio ya tembo na matunda yake makubwa kama mitungi. Na mti huu ulipogubikwa na amri za Allaah, basi ulibadilika kuwa katika hali ambayo hakuna kiumbe ambaye anaweza kumsabihi Allaah kwa uzuri wake.” [Muslim]
Katika riwaayah nyingine: “Kisha nilipandishwa mbinguni hadi kufikia Sidratul-Muntahaa. Matunda yake yalikuwa makubwa kama magudulia ya Hajr (sehemu ambayo ni karibu na Madiynah) na majani yake yalikuwa makubwa kama masikio ya tembo. Jibriyl (عليه السّلام) akasema: Huu ni mkunazi wa mbali kabisa. Kulikuwa na mito minne karibu yake, miwili ikiwa haionekani na miwili ikiwa wazi inaonekana. Nikauliza: Hii mito miwili ni mito gani ee Jibriyl? Basi akajibu: Ama kwa mito miwili isiyoonekana, ni mito miwili ya Peponi, na mito miwili inayoonekana, hiyo ni mto Naili (Nile) na mto Furati (Euphrates).”
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) pia alisema: “Jibriyl alinipandisha mbinguni hadi tukafika Sidratul-Muntahaa (mkunazi ambao una mpaka wa mwisho) ambao ulikuwa umepamba kwa rangi ambazo haziwezi kuelezeka. Kisha niliruhusiwa kuingia Peponi ambamo nilikuta mahema (madogo madogo) au kuta ambazo zimejengwa kwa lulu na ardhi yake ilikuwa ni ya miski.” [Al-Bukhaariy, Juzuu (1) Namba (345)]
Kwa faida nyenginezo bonyeza viungo vifuatavyo:
[3] Aina Na Sifa Jannah (Pepo), Na Makazi Ya Aakhirah:
Baadhi ya Jannah zilizotajwa katika Qur-aan:
- جنة المأوى Jannatul-Ma-awaa ambayo ni hii iliyotajwa katika Suwrah hii An-Najm Najm (53:15).
- الفردوس جنّة Jannatul-Firdaws. Rejea Al-Muuminuwn (23:1-11) kwenye faida zake.
- جنّة النّعيم Jannatun-Na’iym (Pepo za neema ambazo jicho jicho lolote halijapata kuona, wala sikio lolote halijapata kusikia na wala haijapata kupita katika moyo au fikra ya binaadam). Rejea Luqmaan (31:8).
- جنّة الخلد Jannatul-Khuld (Pepo za kudumu milele). Rejea Al-Furqaan (25:15).
- جنّات عدن Jannaat ‘Adn (Jannah au mabustani a kuishi humo milele bila ya kuhama). Rejea Maryam (19:61). Imesemwa kuwa, ‘Adn ni jina makhsusi la Jannah mojawapo. Na imesemwa ni jina la Jannah zote kwa sababu zote ni za kudumu milele. Na Allaah Mjuzi zaidi
Na Jannah nyenginezo zimetajwa kuwa ni makazi ya sifa fulani kama ifuatavyo:
- دار السلام Daarus-Salaam (Nyumba ya amani). Rejea Al-An’aam (6:127).
- مقام الأمين Maqaam Al-Amiyn (Makazi ya kusalimika na mauti, huzuni, uchovu, dhiki na kutokana na kila shari) Rejea Ad-Dukhaan (44:51).
- دار المقامة Daar Al-Muqaamah (Nyumba ya makazi ya kudumu, wakaazi wake hawaondoki humo). Rejea Faatwir (35:35).
- دار الحيوان Daar Al-Hayawaan (Nyumba ya hai wa kudumu milele). Rejea Al-‘Anakabuwt (29:64).
- دار القرار Daar Al-Qaraar (Nyumba ya kustakiri, makazi yasiyotoweka wala uhamisho wala mabadiliko). Rejea Ghaafir (40:39).
Na milango ya Jannah ni minane kutokana na Hadiyth Swahiyh mbalimbali. Mojawapo wa Hadiyth hizo ni ile inayohusu fadhila za wudhuu ambayo pindi mtu akisoma duaa ya wudhuu, basi ataambiwa aingie Peponi kupitia mlango wowote aupendao kati ya milango minane:
Bonyeza kiungo kifuatacho chenye duaa hiyo kwa maandishi na kwa sauti, na Hadiyth inayotaja fadhila zake hizo:
[4] Laata, ‘Uzzaa, Manaata: Majina Ya Miungu Waliyokuwa Wakiyaabudu Washirikina:
Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) amesema: Baada ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kutaja aliyoletwa nayo Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ya Hidaya na Dini ya haki, na amri ya kumwabudu Allaah na Tawhiyd (kumpwekesha), Akataja ubatili wa washirikina kuwaabudu ambao hawana sifa za ukamilifu, wala manufaa wala madhara, bali ni majina yasiyo na maana waliyoyaita washirikina, wao na baba zao wapotovu. Wajinga waliwatengenezea majina ya uwongo wasiyostahiki. Kwa hivyo wakajidanganya nafsi zao na wengine kutokana na upotofu, kwani miungu iliyo katika hali hii haistahiki uzito wa chembe ya kuabudiwa. Na hawa waliowalinganisha (na Allaah) ambao waliwaita kwa majina haya, walidai kuwa sifa zao zina maana, kwa hivyo waliitwa “al-laata: kutokana na al-ilaah, al-‘uzzah: kutokana na ‘aziyz (azizi, adhimu, mwenye nguvu), na manaata: kutokana na mannaan (fadhila).
Ni ukanushaji wa Majina ya Allaah (سبحانه وتعالى) na kumshirikisha. Na majina haya hayana maana yoyote ile, kila mtu ambaye ana ufahamu mdogo wa akili anajua ubatili wa sifa hizo. [Tafsiyr Imaam As-Sa’diy]
[5] Washirikina Wamemsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) Kuwa Ana Wana Wanawake.
Rejea Asw-Swaaffaat (37:149).
[6] Hakuna Atakayemiliki Ash-Shafaa (Uombezi) Ila Aridhie Allaah (سبحانه وتعالى):
Rejea Al-Baqarah (2:255), Twaahaa (20:109). Rejea pia Al-Israa (17:79) ambako kumetajwa kuwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Nabii Pekee atakayeruhusiwa ash-shafaa’ah atakapokuwa katika Maqaaman Mahmuwdan (Cheo Cha Kuhimidiwa). Rejea pia Az-Zukhruf (43:86) kwenye faida nyenginezo.
[8] Suhuf (Maandiko Matukufu) Na Tofauti Baina Yake Na Vitabu Vinginevyo Vya Mbinguni:
Rejea Al-A’laa (87:18-19) kwenye maelezo bayana. Na rejea pia Al-Bayyinah (98:2).
[9] Nyota Ya Ash-Shi’-raa:
Ni nyota inayong’aa iliyoitwa Mirzam Al-Jawzaa (Sirius) ambayo kundi la Waarabu (katika Ujaahiliyyah) walikuwa wakiiabudu. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[11] Sajdatut-Tilaawaa (Sijda Ya Kisomo:
Hii ni Sijdah ya mwanzo wa Risala ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwalingania makafiri wa Makkah. Basi aliposoma Suwrah hii akafikia hapo, alisujudu na washirikina wote walijisahau wakasujudu. Hadiyth ifuatayo inataja:
حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، قَالَ حَدَّثَنَا عَبْدُ الْوَارِثِ، قَالَ حَدَّثَنَا أَيُّوبُ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم سَجَدَ بِالنَّجْمِ وَسَجَدَ مَعَهُ الْمُسْلِمُونَ وَالْمُشْرِكُونَ وَالْجِنُّ وَالإِنْسُ. وَرَوَاهُ ابْنُ طَهْمَانَ عَنْ أَيُّوبَ.
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisujudu alipoisoma Suwrah An-Najm (53), wakasujudu pamoja naye Waislamu, washirikina, majini na watu wote. [Al-Bukhaariy Kitaab cha Kusujudu Inaposomwa Qur-aan (17)]
Duaa ya Sajdatut-Tilaawa ni ifuatayo:
سَجَـدَ وَجْهـي للَّـذي خَلَقَـهُ وَصَـوَّرَهُ وَشَقَّ سَمْـعَـهُ وَبَصَـرَهُ بِحَـوْلِـهِ وَقُـوَّتِهِ فَتَبَارَكَ اللَّـهُ أَحْسَنُ الْخَالِقِينَ
Sajada wajhiya liLLadhiy khalaqahu, wa swaw-warahu, wa shaqqa sam-’ahu wa baswarahu bihawlihi wa quwwatihi, fa-Tabaaraka-Allaahu Ahsanul-Khaaliqiyn.
Umesujudu uso wangu kumsujudia Ambaye Ameuumba na Akapasuwa masikio yake, na macho yake, kwa uwezo Wake na nguvu Zake, Amebarikika Allaah Mbora wa waumbaji.
Hadiyth ya ‘Aaishah (رضي الله عنها) - At-Tirmidhiy (2/474), Ahmad (6/30), na Al-Haakim na ameisahihisha Adh-Dhahabiy (1/220) kwa ziada yake na Aayah ni namba (14) ya Suwratul-Muu-minuwn.
اللّهُـمَّ اكْتُـبْ لي بِهـا عِنْـدَكَ أَجْـراً، وَضَـعْ عَنِّـي بِهـا وِزْراً، وَاجْعَـلها لي عِنْـدَكَ ذُخْـراً، وَتَقَبَّـلها مِنِّـي كَمـا تَقَبَّلْتَـها مِنْ عَبْـدِكَ دَاوُد
Allaahummak-tubliy bihaa ’Indaka ajran, wa dhwa’ ’anniy bihaa wizran, waj-’alhaa liy ’Indaka dhukhran, wa taqabbalhaa minniy kamaa taqabbaltahaa min ’abdika Daawuwd
Ee Allaah Niandikie Kwako kwa sijdah hii malipo, na Nifutie kwayo madhambi, na Ijaalie kwangu mbele Yako ni akiba, na Nikubalie kama Ulivyomkubalia mja wako Daawuwd.
Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما) At-Tirmidhiy (2/473), Al-Haakim, na Adh-Dhahabiy ameisahihisha (1/219).
Na katika kiungo kifuatacho kuna sauti inayosoma duaa hiyo:
021-Hiswnul-Muslim: Du’aa Za Sijdah Ya Kisomo [352]
Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida nyenginezo
08-Sajdatut-Tilaawah (Sijda Ya Kisomo) [353]
الْقَمَر
054-Al-Qamar
054-Al-Qamar: Utangulizi Wa Suwrah [356]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ ﴿١﴾
1. Saa imekaribia na mwezi umepasuka.[1]
وَإِن يَرَوْا آيَةً يُعْرِضُوا وَيَقُولُوا سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ ﴿٢﴾
2. Na wanapoona Aayah (Ishara, Dalili) hukengeuka na husema: Sihiri ya siku zote, tumeizoea.[2]
وَكَذَّبُوا وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُمْ ۚ وَكُلُّ أَمْرٍ مُّسْتَقِرٌّ ﴿٣﴾
3. Na wakakadhibisha (haki), na wakafuata hawaa zao, na kila jambo litafikia ukomo.
وَلَقَدْ جَاءَهُم مِّنَ الْأَنبَاءِ مَا فِيهِ مُزْدَجَرٌ ﴿٤﴾
4. Na kwa yakini imekwishawajia kati ya habari muhimu ambayo ndani yake kuna makemeo makali.
حِكْمَةٌ بَالِغَةٌ ۖ فَمَا تُغْنِ النُّذُرُ ﴿٥﴾
5. Ni hikmah iliyofikia upeo timilifu kabisa lakini hayafai kitu maonyo.[3]
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ ۘ يَوْمَ يَدْعُ الدَّاعِ إِلَىٰ شَيْءٍ نُّكُرٍ ﴿٦﴾
6. Basi jitenge nao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Siku atakayoita muitaji kuliendea jambo baya mno la kuogofya.
خُشَّعًا أَبْصَارُهُمْ يَخْرُجُونَ مِنَ الْأَجْدَاثِ كَأَنَّهُمْ جَرَادٌ مُّنتَشِرٌ ﴿٧﴾
7. Macho yao yakiwa dhalili, watatoka katika makaburi kama kwamba wao ni nzige waliosambaa.
مُّهْطِعِينَ إِلَى الدَّاعِ ۖ يَقُولُ الْكَافِرُونَ هَـٰذَا يَوْمٌ عَسِرٌ ﴿٨﴾
8. Wakikimbia mbio kwenda kwa muitaji huku wamebenua shingo zao. Makafiri watasema: Hii ni siku ngumu mno!
كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ فَكَذَّبُوا عَبْدَنَا وَقَالُوا مَجْنُونٌ وَازْدُجِرَ ﴿٩﴾
9. Walikadhibisha kabla yao kaumu ya Nuwh, wakamkadhibisha Mja Wetu, wakasema: Majnuni. Na akakaripiwa.[4]
فَدَعَا رَبَّهُ أَنِّي مَغْلُوبٌ فَانتَصِرْ ﴿١٠﴾
10. Basi akamwita Rabb wake: Hakika mimi nimeshindwa nguvu basi Nusuru.
فَفَتَحْنَا أَبْوَابَ السَّمَاءِ بِمَاءٍ مُّنْهَمِرٍ ﴿١١﴾
11. Tukafungua milango ya mbingu kwa maji yanayofoka na kumiminika kwa nguvu.
وَفَجَّرْنَا الْأَرْضَ عُيُونًا فَالْتَقَى الْمَاءُ عَلَىٰ أَمْرٍ قَدْ قُدِرَ ﴿١٢﴾
12. Na Tukazibubujua ardhi chemchemu, basi yakakutana maji kwa amri iliyokwisha kadiriwa.
وَحَمَلْنَاهُ عَلَىٰ ذَاتِ أَلْوَاحٍ وَدُسُرٍ ﴿١٣﴾
13. Na Tukambeba kwenye ile (jahazi) yenye mbao na misumari.
تَجْرِي بِأَعْيُنِنَا جَزَاءً لِّمَن كَانَ كُفِرَ ﴿١٤﴾
14. Inatembea chini ya Macho Yetu, ni jazaa kwa yule aliyekuwa amekanushwa.
وَلَقَد تَّرَكْنَاهَا آيَةً فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ ﴿١٥﴾
15. Na kwa yakini Tumeiacha iwe ni Aayah (Ishara, Mazingatio). Je basi yuko yeyote mwenye kuwaidhika?
فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ ﴿١٦﴾
16. Basi vipi ilikuwa Adhabu Yangu na Maonyo Yangu?
وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ ﴿١٧﴾
17. Na kwa yakini Tumeiwepesisha Qur-aan ili ipate kusomwa, kuhifadhiwa na kufahamika.[5] Basi je, yuko yeyote mwenye kuwaidhika?
كَذَّبَتْ عَادٌ فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ ﴿١٨﴾
18. Kina ‘Aad walikadhibisha. Basi vipi ilikuwa Adhabu Yangu na Maonyo Yangu?
إِنَّا أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا صَرْصَرًا فِي يَوْمِ نَحْسٍ مُّسْتَمِرٍّ ﴿١٩﴾
19. Hakika Sisi Tuliwapelekea upepo wa adhabu; wa sauti kali na baridi kali katika siku ya nuhsi yenye kuendelea mfululizo.
تَنزِعُ النَّاسَ كَأَنَّهُمْ أَعْجَازُ نَخْلٍ مُّنقَعِرٍ ﴿٢٠﴾
20. Unawang’oa watu kama kwamba ni vigogo vya mtende vilong’olewa.
فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ ﴿٢١﴾
21. Basi vipi ilikuwa Adhabu Yangu na Maonyo Yangu?
وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ ﴿٢٢﴾
22. Na kwa yakini Tumeiwepesisha Qur-aan ili ipate kusomwa, kuhifadhiwa na kufahamika. Basi je, yuko yeyote mwenye kuwaidhika?
كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِالنُّذُرِ ﴿٢٣﴾
23. Kina Thamuwd walikadhibisha maonyo.
فَقَالُوا أَبَشَرًا مِّنَّا وَاحِدًا نَّتَّبِعُهُ إِنَّا إِذًا لَّفِي ضَلَالٍ وَسُعُرٍ ﴿٢٤﴾
24. Wakasema: Ah! Tumfuate binaadam mmoja miongoni mwetu? Hakika hapo sisi tutakuwa katika upotofu na wazimu.
أَأُلْقِيَ الذِّكْرُ عَلَيْهِ مِن بَيْنِنَا بَلْ هُوَ كَذَّابٌ أَشِرٌ ﴿٢٥﴾
25. Ah! Ameteremshiwa yeye tu ukumbusho baina yetu? Bali yeye ni muongo mkubwa, mfidhuli mwenye kutakabari mno.
سَيَعْلَمُونَ غَدًا مَّنِ الْكَذَّابُ الْأَشِرُ ﴿٢٦﴾
26. Watakuja kujua kesho nani muongo mkubwa mfidhuli mwenye kutakabari mno.
إِنَّا مُرْسِلُو النَّاقَةِ فِتْنَةً لَّهُمْ فَارْتَقِبْهُمْ وَاصْطَبِرْ ﴿٢٧﴾
27. Hakika Sisi Tutawapelekea ngamia jike awe jaribio kwao. Basi (ee Nabiy Swaalih عليه السلام) watazame na vuta subira.
وَنَبِّئْهُمْ أَنَّ الْمَاءَ قِسْمَةٌ بَيْنَهُمْ ۖ كُلُّ شِرْبٍ مُّحْتَضَرٌ ﴿٢٨﴾
28. Na wajulishe kwamba maji ni mgawanyo baina yao (ngamia na wao), kila sehemu ya maji itahudhuriwa (kwa zamu).
فَنَادَوْا صَاحِبَهُمْ فَتَعَاطَىٰ فَعَقَرَ ﴿٢٩﴾
29. Wakamwita swahibu wao, akakamata (upanga) akaua (ngamia).
فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ ﴿٣٠﴾
30. Basi vipi ilikuwa Adhabu Yangu na Maonyo Yangu?
إِنَّا أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ صَيْحَةً وَاحِدَةً فَكَانُوا كَهَشِيمِ الْمُحْتَظِرِ ﴿٣١﴾
31. Hakika Sisi Tuliwapelekea ukelele angamizi mmoja tu, basi wakawa kama mabuwa makavu ya mtengenezaji zizi.
وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ ﴿٣٢﴾
32. Na kwa yakini Tumeiwepesisha Qur-aan ili ipate kusomwa, kuhifadhiwa na kufahamika. Basi je, yuko yeyote mwenye kuwaidhika?
كَذَّبَتْ قَوْمُ لُوطٍ بِالنُّذُرِ ﴿٣٣﴾
33. Kaumu ya Luutw walikadhibisha maonyo.
إِنَّا أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ حَاصِبًا إِلَّا آلَ لُوطٍ ۖ نَّجَّيْنَاهُم بِسَحَرٍ ﴿٣٤﴾
34. Hakika Sisi Tuliwapelekea tufani ya mawe isipokuwa familia ya Luutw. Tuliwaokoa nyakati kabla ya Alfajiri.
نِّعْمَةً مِّنْ عِندِنَا ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي مَن شَكَرَ ﴿٣٥﴾
35. Neema kutoka Kwetu. Hivyo ndivyo Tunavyomlipa ambaye ameshukuru.
وَلَقَدْ أَنذَرَهُم بَطْشَتَنَا فَتَمَارَوْا بِالنُّذُرِ ﴿٣٦﴾
36. Na kwa yakini aliwatahadharisha Nguvu Zetu za kuadhibu lakini wakatilia shaka maonyo.
وَلَقَدْ رَاوَدُوهُ عَن ضَيْفِهِ فَطَمَسْنَا أَعْيُنَهُمْ فَذُوقُوا عَذَابِي وَنُذُرِ ﴿٣٧﴾
37. Na kwa yakini walimshawishi awape wageni wake, Nasi Tukawapofoa macho yao. Basi onjeni Adhabu Yangu na Maonyo Yangu.
وَلَقَدْ صَبَّحَهُم بُكْرَةً عَذَابٌ مُّسْتَقِرٌّ ﴿٣٨﴾
38. Na kwa yakini iliwafikia asubuhi mapema adhabu ya kuendelea.
فَذُوقُوا عَذَابِي وَنُذُرِ ﴿٣٩﴾
39. Basi onjeni Adhabu Yangu na Maonyo Yangu.
وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ ﴿٤٠﴾
40. Na kwa yakini Tumeiwepesisha Qur-aan ili ipate kusomwa, kuhifadhiwa na kufahamika. Basi je, yuko yeyote mwenye kuwaidhika?
وَلَقَدْ جَاءَ آلَ فِرْعَوْنَ النُّذُرُ ﴿٤١﴾
41. Na kwa yakini watu wa Firawni walifikiwa na maonyo mengi.
كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كُلِّهَا فَأَخَذْنَاهُمْ أَخْذَ عَزِيزٍ مُّقْتَدِرٍ ﴿٤٢﴾
42. Walikadhibisha Aayaat (Ishara, Miujiza, Dalili) Zetu zote, Tukawakamata mkamato wa Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Uwezo wa juu kabisa.
أَكُفَّارُكُمْ خَيْرٌ مِّنْ أُولَـٰئِكُمْ أَمْ لَكُم بَرَاءَةٌ فِي الزُّبُرِ ﴿٤٣﴾
43. Je, makafiri wenu (enyi Maquraysh) ni bora kuliko hao (ummah) wa awali? Au mna msamaha katika Maandiko Matukufu?
أَمْ يَقُولُونَ نَحْنُ جَمِيعٌ مُّنتَصِرٌ ﴿٤٤﴾
44. Au wanasema: Sisi ni wengi tutashinda tu.
سَيُهْزَمُ الْجَمْعُ وَيُوَلُّونَ الدُّبُرَ ﴿٤٥﴾
45. Utashindwa mjumuiko wao na watageuka nyuma (watimue mbio).
بَلِ السَّاعَةُ مَوْعِدُهُمْ وَالسَّاعَةُ أَدْهَىٰ وَأَمَرُّ ﴿٤٦﴾
46. Bali Saa ndio miadi yao, na Saa ni janga kubwa na chungu zaidi.
إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي ضَلَالٍ وَسُعُرٍ ﴿٤٧﴾
47. Hakika wahalifu wamo katika upotofu na wazimu.[6]
يَوْمَ يُسْحَبُونَ فِي النَّارِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ ذُوقُوا مَسَّ سَقَرَ ﴿٤٨﴾
48. Siku watakayoburutwa motoni kifudifudi: Onjeni mguso wa moto mkali mno.
إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ ﴿٤٩﴾
49. Hakika Sisi Tumekiumba kila kitu kwa Qadar[7] (makadirio, majaaliwa).
وَمَا أَمْرُنَا إِلَّا وَاحِدَةٌ كَلَمْحٍ بِالْبَصَرِ ﴿٥٠﴾
50. Na Amri Yetu haiwi ila ni moja tu, kama upepeso wa jicho.
وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا أَشْيَاعَكُمْ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ ﴿٥١﴾
51. Na kwa yakini Tumewaangamiza wenzenu. Je, basi yuko yeyote mwenye kuwaidhika?
وَكُلُّ شَيْءٍ فَعَلُوهُ فِي الزُّبُرِ ﴿٥٢﴾
52. Na kila kitu wakifanyacho kimo katika madaftari ya rekodi.
وَكُلُّ صَغِيرٍ وَكَبِيرٍ مُّسْتَطَرٌ ﴿٥٣﴾
53. Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa[8]
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَنَهَرٍ ﴿٥٤﴾
54. Hakika wenye taqwa watakuwa katika Jannaat na mito.
فِي مَقْعَدِ صِدْقٍ عِندَ مَلِيكٍ مُّقْتَدِرٍ ﴿٥٥﴾
55. Katika makao ya haki kwa Mfalme Mwenye Nguvu zote, Mwenye Uwezo wa juu kabisa.
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
054-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Qamar Aayah 1-2: اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ [357]
[2] Makafiri Kutokuamini Aayaat (Na Ishara, Dalili) Za Allaah Na Kuzipachika Sifa Ovu, Na Kutokumuamini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
Rejea Al-Furqaan (25:4) kwenye uchambuzi bayana na rejea mbalimbali za maudhui hii ya washirikina kumpachika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) sifa kadhaa ovu na kuipachika Qur-aan pia sifa ovu.
Na washirikina wakiiona dalili na ushahidi juu ya ukweli wa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), wanakataa kuziamini na kuzisadiki, bali kukanusha na kupinga, na wanasema baada ya dalili kujitokeza: “Huu ni uchawi wenye ubatilifu na wenye kuondoka na kupotea na hauna sifa ya kudumu.” [Tafsiyr Al-Muyassar]
[3] Maonyo Hayakuwafaa Washirikina Wa Makkah Na Makafiri Wengineo:
Maonyo ya Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayaat za Qur-aan, na Ishara, Dalili, Hoja, Miujiza, na Mazingatio, yako wazi kabisa katika Qur-aan yanayothibitisha Tawhiyd Yake. Anathibitisha Allaah (سبحانه وتعالى) katika Kauli Yake:
قُلْ فَلِلَّـهِ الْحُجَّةُ الْبَالِغَةُ ۖ فَلَوْ شَاءَ لَهَدَاكُمْ أَجْمَعِينَ ﴿١٤٩﴾
“Sema: Basi Ni Allaah Pekee Mwenye hoja timilifu. Na Angelitaka Angelikuhidini nyote.” [Al-An’aam (6:149)]
Na baadhi ya Kauli Zake (سبحانه وتعالى) nyenginezo zinataja kuwa ubalighisho wa Risala, au Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) za Allaah hazikuwafaa lolote kwa kuwa hawakuamini hivyo basi wakabakia katika ushirikina na ukafiri wao:
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَلَوْ جَاءَتْهُمْ كُلُّ آيَةٍ حَتَّىٰ يَرَوُا الْعَذَابَ الْأَلِيمَ﴿٩٧﴾
“Japokuwa itawajia kila Aayah (Ishara, Dalili, Mawaidha) mpaka waone adhabu iumizayo.” [Yuwnus (10:97)]
قُلِ انظُرُوا مَاذَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَا تُغْنِي الْآيَاتُ وَالنُّذُرُ عَن قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ﴿١٠١﴾
“Sema: Tazameni yaliyoko mbinguni na ardhini. Lakini Aayaat (Ishara, Dalili) zote na maonyo (ya Rusuli) hayawafai kitu watu wasioamini.” [Yuwnus (10:110)]
وَلَوْ أَنَّنَا نَزَّلْنَا إِلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ الْمَوْتَىٰ وَحَشَرْنَا عَلَيْهِمْ كُلَّ شَيْءٍ قُبُلًا مَّا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ يَجْهَلُونَ ﴿١١١﴾
“Na lau kama Sisi Tungeliwateremshia Malaika, na wao wakasemeshwa na wafu, na Tukawakusanyia kila kitu mbele yao, basi bado wasingeliamini ila Allaah Atake, lakini wengi wamo katika ujahili.” [Al-An’aam (6:111)]
وَكَأَيِّن مِّنْ آيَةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يَمُرُّونَ عَلَيْهَا وَهُمْ عَنْهَا مُعْرِضُونَ ﴿١٠٥﴾
“Ni Aayah (Ishara, Dalili) nyingi sana katika mbingu na ardhi wanazipitia na huku wao wanazipuuza.” [Yuwsuf (12:105)]
[4] Ukadhibishaji Wa Nyumati Za Awali Na Aina Za Maangamizi Yao:
Kuanzia Aayah hii namba (9) hadi Aayah namba (42), wanatajwa kaumu wa nyumati za nyuma na jinsi walivyokadhibisha Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja, Miujiza) za Allaah na adhabu mbalimbali zilizowasibu. Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye uchambuzi wa maudhui hii na rejea mbalimbali:
[5] Qur-aan Imefanywa Sahali Kuisoma Na Kuihifadhi Kwa Mwenye Kuitafakari, Kuizingatia Na Kuitendea Kazi:
Aayah hii tukufu imekariri mara nne katika Suwrah hii. Na hii ni uthibitisho wa Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) ya Ahadi ya kuifanya Qur-aan kuwa ni nyepesi kuisoma na kuihifadhi pindi mtu ataitafakari na kuizingatia na kuyafanyia kazi maamrisho yake.
Na Ameijaalia kuwa nyepesi kwa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), rejea Suwrah Maryam (19:97), Ad-Dukhaan (44:58).
Tafsiyr:
Yaani: Tumefanya hii Qur-aan Tukufu kuwa nyepesi kwa maneno yake kwa ajili ya kuhifadhi na kuisoma. Na Tumefanya maana zake kuwa nyepesi kuzifahamu na kuzijua kwa sababu ina kauli bora kabisa, na ina ukweli zaidi katika maana zake, na ina tafsiri iliyo bayana kabisa. Basi kwa yeyote anayeitafuta (kujifunza), Allaah (سبحانه وتعالى) Humfanyia wepesi matilabu yake kwa wepesi wa hali juu kabisa, na Humsahilishia. Na Adh-Dhikr (Ukumbusho), inajumuisha kila kitu ambacho wanakifanyia watu kazi katika (hukmu za) halaal na za haraam, hukumu za amri na makatazo, hukmu za malipo na mawaidha, mafunzo, na itikadi sahihi za manufaa na khabari za kweli. Ndio maana ikawa ilimu ya kuihifadhi Quraan na Tafsiyr yake ni ilimu iliyo nyepesi kabisa na tukufu zaidi, kwani ni ilimu ya manufaa ambayo pindi mja akiitafuta, basi atasaidiwa (na Allaah). Baadhi ya Salaf wamesema kuhusu Aayah hii wakiuliza: Je kuna yeyote anayetafuta ilimu asaidiwe? Na ndio maana Allaah (سبحانه وتعالى) Anawagutusha Waja Wake Akiwaambia:
فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ ﴿١٧﴾
“Basi je, yuko yeyote mwenye kuwaidhika?”
[Tafsiyr As-Sa’diy]
[6] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
054-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Qamar Aayah 47-49: إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي ضَلَالٍ وَسُعُرٍ [358]
[7] Qadar: Takdiri, Makadirio, Majaaliwa, Hukmu.
Sisi Tumekiumba kila kitu kwa mujibu wa Tulichokikadiria, Tukakihukumu, na Tumekijua vyema, na pia Tumekiandika katika Lawh Al-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa). [Tafsiyr As-Sa’diy]
[8] Kila Kubwa Na Dogo Limeandikwa Katika Lawh Al-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa).
Amali za mwanaadam ziwe kubwa au ndogo vipi zimerekodiwa katika Ubao Uliohifadhiwa mbinguni. Hata iwe ni kauli au neno dogo vipi. Rejea Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى) zifuatazo zenye kuthibitisha haya: Al-An’aam (6:38), Al-Kahf (18:49), Az-Zalzalah (99:7-8).
الرَّحْمن
055-Ar-Rahmaan
055-Ar-Rahmaan: Utangulizi Wa Suwrah [360]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الرَّحْمَـٰنُ ﴿١﴾
1. Ar-Rahmaan.
عَلَّمَ الْقُرْآنَ ﴿٢﴾
2. Amefundisha Qur-aan.[1]
خَلَقَ الْإِنسَانَ ﴿٣﴾
3. Ameumba binaadam.
عَلَّمَهُ الْبَيَانَ ﴿٤﴾
4. Amemfunza ufasaha
الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ بِحُسْبَانٍ ﴿٥﴾
5. Jua na mwezi huenda katika hesabu.
وَالنَّجْمُ وَالشَّجَرُ يَسْجُدَانِ ﴿٦﴾
6. Na nyota na miti vinasujudu.[2]
وَالسَّمَاءَ رَفَعَهَا وَوَضَعَ الْمِيزَانَ ﴿٧﴾
7. Na mbingu Ameziinua na Akaweka mizani.
أَلَّا تَطْغَوْا فِي الْمِيزَانِ ﴿٨﴾
8. Ili msivuke mipaka (kudhulumu) katika mizani.
وَأَقِيمُوا الْوَزْنَ بِالْقِسْطِ وَلَا تُخْسِرُوا الْمِيزَانَ ﴿٩﴾
9. Na simamisheni uzani kwa uadilifu, na wala msipunguze mizani.
وَالْأَرْضَ وَضَعَهَا لِلْأَنَامِ ﴿١٠﴾
10. Na ardhi Ameiweka chini kwa ajili ya viumbe.
فِيهَا فَاكِهَةٌ وَالنَّخْلُ ذَاتُ الْأَكْمَامِ ﴿١١﴾
11. Humo mna matunda na mitende yenye mafumba.
وَالْحَبُّ ذُو الْعَصْفِ وَالرَّيْحَانُ ﴿١٢﴾
12. Na nafaka zenye makapi na rehani; miti yenye harufu nzuri ya kunukia.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿١٣﴾
13. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?[3]
خَلَقَ الْإِنسَانَ مِن صَلْصَالٍ كَالْفَخَّارِ ﴿١٤﴾
14. Amemuumba binaadam kutokana na udongo wa mfinyanzi unaotoa sauti kama udongo wa kinamo.
وَخَلَقَ الْجَانَّ مِن مَّارِجٍ مِّن نَّارٍ ﴿١٥﴾
15. Na Akaumba majini kutokana na mwako wa moto.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿١٦﴾
16. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
رَبُّ الْمَشْرِقَيْنِ وَرَبُّ الْمَغْرِبَيْنِ ﴿١٧﴾
17. Rabb wa Mashariki mbili na Rabb wa Magharibi mbili.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿١٨﴾
18. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
مَرَجَ الْبَحْرَيْنِ يَلْتَقِيَانِ ﴿١٩﴾
19. Ameziachilia bahari mbili zinakutana.
بَيْنَهُمَا بَرْزَخٌ لَّا يَبْغِيَانِ ﴿٢٠﴾
20. Baina yake kuna kizuizi, hazivukiani mipaka.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٢١﴾
21. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
يَخْرُجُ مِنْهُمَا اللُّؤْلُؤُ وَالْمَرْجَانُ ﴿٢٢﴾
22. Zinatoka humo lulu na marijani.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٢٣﴾
23. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
وَلَهُ الْجَوَارِ الْمُنشَآتُ فِي الْبَحْرِ كَالْأَعْلَامِ ﴿٢٤﴾
24. Na ni Vyake vyombo viendavyo baharini vikiinuliwa tanga kama milima.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٢٥﴾
25. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ ﴿٢٦﴾
26. Kila aliyekuwa juu yake (ardhi) ni mwenye kutoweka.[4]
وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ ﴿٢٧﴾
27. Na utabakia Wajihi[5] wa Rabb wako Mwenye Ujalali na Ukarimu.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٢٨﴾
28. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
يَسْأَلُهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ كُلَّ يَوْمٍ هُوَ فِي شَأْنٍ ﴿٢٩﴾
29. Wanamuomba Yeye wote walio mbinguni na ardhini, kila siku Yeye Yumo katika Kubadilisha mambo.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٠﴾
30. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
سَنَفْرُغُ لَكُمْ أَيُّهَ الثَّقَلَانِ ﴿٣١﴾
31. Tutakukusudieni kwa hisabu enyi aina mbili ya viumbe (majini na wanaadam).
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٢﴾
32. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ إِنِ اسْتَطَعْتُمْ أَن تَنفُذُوا مِنْ أَقْطَارِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ فَانفُذُوا ۚ لَا تَنفُذُونَ إِلَّا بِسُلْطَانٍ ﴿٣٣﴾
33. Enyi jamii ya majini na wanaadam! Mkiweza kupenya kwenye zoni za mbingu na ardhi, basi penyeni. Hamtoweza kupenya isipokuwa kwa mamlaka (ya Allaah).
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٤﴾
34. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
يُرْسَلُ عَلَيْكُمَا شُوَاظٌ مِّن نَّارٍ وَنُحَاسٌ فَلَا تَنتَصِرَانِ ﴿٣٥﴾
35. Mtapelekewa mwako wa moto juu yenu na shaba iliyoyayushwa, basi hamtoweza kujinusuru.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٦﴾
36. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
فَإِذَا انشَقَّتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ وَرْدَةً كَالدِّهَانِ ﴿٣٧﴾
37. Zitakapoachana mbingu zikawa rangi ya waridi kama mafuta.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٣٨﴾
38. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُسْأَلُ عَن ذَنبِهِ إِنسٌ وَلَا جَانٌّ ﴿٣٩﴾
39. Siku hiyo hatoulizwa kuhusu dhambi yake binaadam wala jini.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٠﴾
40. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
يُعْرَفُ الْمُجْرِمُونَ بِسِيمَاهُمْ فَيُؤْخَذُ بِالنَّوَاصِي وَالْأَقْدَامِ ﴿٤١﴾
41. Watatambulikana wahalifu kwa alama zao, basi watachukuliwa kwa vipaji vya uso na miguu.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٢﴾
42. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
هَـٰذِهِ جَهَنَّمُ الَّتِي يُكَذِّبُ بِهَا الْمُجْرِمُونَ ﴿٤٣﴾
43. Hii ni Jahannam ambayo wahalifu wanaikadhibisha.
يَطُوفُونَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ حَمِيمٍ آنٍ ﴿٤٤﴾
44. Wataizunguka baina yake na baina ya maji yachemkayo yaliyofikia ukomo wa kutokota.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٥﴾
45. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ جَنَّتَانِ ﴿٤٦﴾
46. Na kwa mwenye kukhofu kisimamo mbele ya Rabb wake atapata bustani mbili.[6]
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٧﴾
47. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
ذَوَاتَا أَفْنَانٍ ﴿٤٨﴾
48. Zilizo na matawi yaliyotanda.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٤٩﴾
49. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
فِيهِمَا عَيْنَانِ تَجْرِيَانِ ﴿٥٠﴾
50. Mna humo chemchemu mbili zinazopita.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥١﴾
51. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
فِيهِمَا مِن كُلِّ فَاكِهَةٍ زَوْجَانِ ﴿٥٢﴾
52. Mna humo kila matunda ya aina mbilimbili.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥٣﴾
53. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ فُرُشٍ بَطَائِنُهَا مِنْ إِسْتَبْرَقٍ ۚ وَجَنَى الْجَنَّتَيْنِ دَانٍ ﴿٥٤﴾
54. Wakiegemea kwenye matandiko ya kupumzikia, bitana yake ni kutokana na hariri nzito nyororo, na matunda ya bustani mbili yako karibu na kufikiwa.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥٥﴾
55. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
فِيهِنَّ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ ﴿٥٦﴾
56. Mna humo wanawake wenye staha wanaoinamisha macho, hajawabikiri kabla yao binaadam yeyote wala jini.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥٧﴾
57. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
كَأَنَّهُنَّ الْيَاقُوتُ وَالْمَرْجَانُ ﴿٥٨﴾
58. Kama kwamba hao wanawake ni yakuti na marijani.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٥٩﴾
59. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
هَلْ جَزَاءُ الْإِحْسَانِ إِلَّا الْإِحْسَانُ ﴿٦٠﴾
60. Je, kuna jazaa ya ihsaan isipokuwa ihsaan tu?[7]
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦١﴾
61. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
وَمِن دُونِهِمَا جَنَّتَانِ ﴿٦٢﴾
62. Na zaidi ya hizo mbili, ziko bustani mbili zingine.[8]
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦٣﴾
63. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
مُدْهَامَّتَانِ ﴿٦٤﴾
64. Za rangi ya kijani iliyokoza.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦٥﴾
65. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
فِيهِمَا عَيْنَانِ نَضَّاخَتَانِ ﴿٦٦﴾
66. Mna humo chemchemu mbili zenye kububujika kwa nguvu mfululizo.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦٧﴾
67. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
فِيهِمَا فَاكِهَةٌ وَنَخْلٌ وَرُمَّانٌ ﴿٦٨﴾
68. Mna humo matunda na mitende na makomamanga.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٦٩﴾
69. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
فِيهِنَّ خَيْرَاتٌ حِسَانٌ ﴿٧٠﴾
70. Mna humo wanawake wazuri, wema.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٧١﴾
71. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
حُورٌ مَّقْصُورَاتٌ فِي الْخِيَامِ ﴿٧٢﴾
72. Hurulaini: Wanawake weupe wazuri wa Jannah wenye macho makubwa ya kupendeza, wanaotawishwa katika mahema.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٧٣﴾
73. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ ﴿٧٤﴾
74. Hajawabikiri kabla yao binaadam yeyote wala jini.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٧٥﴾
75. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ رَفْرَفٍ خُضْرٍ وَعَبْقَرِيٍّ حِسَانٍ ﴿٧٦﴾
76. Wakiegemea kwenye matakia ya kijani na mazulia ya rangi mbalimbali ya hariri mazuri mno yasiyo na kifani.
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿٧٧﴾
77. Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?
تَبَارَكَ اسْمُ رَبِّكَ ذِي الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ ﴿٧٨﴾
78. Limebarikika Jina la Rabb wako Mwenye Ujalali na Ukarimu.[9]
[1] Amefunza Qur-aan Kwa Binaadam Na Ufasaha:
Kuanzia Aayah hii namba (2) na zinazofuatia (3-4), Tafsiyr yake ni kama ifuatavyo:
Allaah (سبحانه وتعالى) Amemfunza binaadam Quraan kwa kuiwepesisha kusomwa kwake, kuihifadhi, na kufahamu maana zake. Akawafunza Waja Wake kuitamka, na Akawasahilishia kufahamu maana zake. Na hii ni Rehma kubwa kabisa kwa Waja Wake kwamba Amewateremshia Quraan kwa lugha ya Kiarabu, kwa maneno bora kabisa, na ubainifu bora kabisa ikijumuisha kila la kheri na kuhadharisha kila la shari. Akamuumba binaadam katika umbo bora kabisa lililo kamilifu na lililoundwa vizuri. Akamuumba binaadam katika ukamilifu kabisa na Akamtofautisha na viumbe vinginevyo kwa kumfundisha kujieleza na kufafanua yaliyomo ndani ya nafsi yake kwa matamshi na maandishi. Uwezo huu ambao Allaah Amempambanua mwanaadam juu ya viumbe vinginevyo, ni katika Neema Zake kubwa kwake. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[2] Kila Kitu Kinamsujudia Allaah (عزّ وجلّ).
Kutokana na taadhima ya Allaah (سبحانه وتعالى) Muumba wa kila kitu, vitu vyote vinamsujudia Yeye Allaah (سبحانه وتعالى).
Rejea Al-A’raaf (7:206), Ar-Ra’d (13:15), An-Nahl (16:48-50), Al-Hajj (22:18).
Na miongoni mwa Hadiyth ni hii ifuatayo:
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ التَّيْمِيِّ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي ذَرٍّ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم لأَبِي ذَرٍّ حِينَ غَرَبَتِ الشَّمْسُ " تَدْرِي أَيْنَ تَذْهَبُ ". قُلْتُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ. قَالَ " فَإِنَّهَا تَذْهَبُ حَتَّى تَسْجُدَ تَحْتَ الْعَرْشِ، فَتَسْتَأْذِنَ فَيُؤْذَنَ لَهَا، وَيُوشِكُ أَنْ تَسْجُدَ فَلاَ يُقْبَلَ مِنْهَا، وَتَسْتَأْذِنَ فَلاَ يُؤْذَنَ لَهَا، يُقَالُ لَهَا ارْجِعِي مِنْ حَيْثُ جِئْتِ. فَتَطْلُعُ مِنْ مَغْرِبِهَا، فَذَلِكَ قَوْلُهُ تَعَالَى وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَهَا ذَلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ
Amesimulia Abuu Dharr (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniuliza wakati wa machweo: “Je, unajua jua linapokwenda (wakati wa kuzama kwake)?” Nikamjibu: “Allaah na Rasuli Wake Wanajua zaidi.” Akasema: “Hakika linakwenda mpaka linasujudu chini ya ‘Arsh, na kutaka idhini kuchomoza tena, nalo linaruhusiwa. Na inachelewa kuwa (itafika wakati ambapo) litakaribia kusujudu lakini sijda yake haitokubaliwa, na litaomba idhini lakini litakataliwa (kutimiza mizunguko yake). Litaambiwa: ‘Rudi ulipotoka’. Hivyo, litachomoza Magharibi. Na hiyo ndiyo Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَّهَا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ﴿٣٨﴾
“Na jua linatembea hadi matulio yake. Hayo ni Takdiri ya Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.” [Yaasiyn 36:38) - Hadiyth ameipokea Imaam Al-Bukhaariy]
[3] Majini Wametoa Jibu Bora Kuhusu Neema Za Allaah (عزّ وجلّ):
خرجَ رسولُ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ علَيهِ وسلَّمَ على أَصحابِهِ، فقرأَ عليهم سورةَ الرَّحمنِ من أوَّلِها إلى آخرِها فسَكَتوا فقالَ: لقد قرأتُها على الجنِّ ليلةَ الجنِّ فَكانوا أحسَنَ مردودًا منكم، كنتُ كلَّما أتيتُ على قولِهِ فَبِأيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ قالوا: لا بشَيءٍ من نِعَمِكَ ربَّنا نُكَذِّبُ فلَكَ الحمدُ
Amesimulia Jaabir (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuja kwa Swahaba zake akawasomea Suwrah Ar-Rahmaan kuanzia mwanzoni mwake hadi mwisho wake, wakanyamaza kimya kisha akasema: “Niliwasomea majini usiku wa majini wakawa na mwitiko bora kuliko nyinyi. Kila nilipofikia kusoma Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ﴿١٦﴾
“Basi ni zipi katika Neema za Rabb wenu mnazikadhibisha?”
Walikuwa wanasema:
لا بشَيءٍ من نِعَمِكَ ربَّنا نُكَذِّبُ فلَكَ الحمدُ
Hakuna chochote katika Neema Zako Rabb wetu tunazozokadhibisha, na Himdi ni Zako.” [At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (3291), Swahiyh Al-Jaami’ (5138)]
Tanbihi: ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu usahihi wa Hadiyth hiyo. Imaam As-Sa’diy ameinukuu katika Tafsiyr yake, pia imenukuliwa katika Tafsiyr Al-Muyassar, Tafsiyr Ibn Kathiyr.
[4] Kila Kitu Kitatoweka Atabakia Allaah (عزّ وجلّ) Pekee:
Rejea Ghaafir (40:16) kwenye maelezo bayana.
[5] ‘Aqiydah Sahihi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Ni Kuthibisha Sifa Za Allaah.
Rejea Huwd (11:37), Al-Fat-h (48:10) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali.
[6] Jannah (Pepo) Mbili:
Kuanzia Aayah hii namba (46) hadi mwisho wa Suwrah hii tukufu, zimetajwa neema za watu wa Jannah. Rejea pia Faatwir (35:33) kwenye faida na rejea mbalimbali zinazotajwa katika Qur-aan kuhusu neema za Jannah.
Yaani na yule anayemkhofu Rabb Wake na kukhofu kusimamishwa Kwake, akaacha aliyokatazwa na akatenda aliyoamrishwa, atapata Jannah mbili za dhahabu ambazo vyombo vyake, majengo yake, na kila kilichomo kitakuwa ni mapambo ya dhahabu. Moja ya Jannah mbili, itakuwa ni malipo ya kujiepusha makatazo, na nyengine itakuwa ni (malipo) ya kufanya utiifu (na matendo mema). [Tafsiyr As-Sa’diy]
Na katika Hadiyth:
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أَبِي الأَسْوَدِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ عَبْدِ الصَّمَدِ الْعَمِّيُّ، حَدَّثَنَا أَبُو عِمْرَانَ الْجَوْنِيُّ، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ قَيْسٍ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " جَنَّتَانِ مِنْ فِضَّةٍ، آنِيَتُهُمَا وَمَا فِيهِمَا وَجَنَّتَانِ مِنْ ذَهَبٍ آنِيَتُهُمَا وَمَا فِيهِمَا، وَمَا بَيْنَ الْقَوْمِ وَبَيْنَ أَنْ يَنْظُرُوا إِلَى رَبِّهِمْ إِلاَّ رِدَاءُ الْكِبْرِ عَلَى وَجْهِهِ فِي جَنَّةِ عَدْنٍ ".
Amesimulia Abu Bakr Bin ‘Abdillaah bin Qays kutoka kwa baba yake (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Jannah mbili za fedha, vyombo vyake na vilivyomo ndani yake ni fedha pia. Na Jannah mbili za dhahabu, vyombo vyake na vilivyomo ndani yake. Na hakuna kitakachowazuia watu na kumuona Rabb wao katika Jannah ya ‘Adn isipokuwa ni pazia ya kibri iliyo juu ya Wajihi Wake.” [Al-Bukhaariy Kitaab Cha Tafsiyr (65)]
[7] Jazaa Ya Ihsaan (Wema):
Hakuna malipo kwa mwenye kumwabudu Allaah ipasavyo na kuwanufaisha Waja Wake, isipokuwa Allaah Atamrejeshea uwajibikaje wake huo kwa kumkirimu thawabu kochokocho, Atamfanikishia kufuzu kuliko kukubwa, Atambubujishia neema za kudumu na Atampa maisha mazuri yaliyo salama. Basi Jannah mbili hizi za juu kabisa ni kwa ajili ya waliojikurubisha kwa Allaah. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[8] Zaidi Ya Jannah (Pepo) Mbili:
وَمِن دُونِهِمَا جَنَّتَانِ ﴿٦٢﴾
“Na zaidi ya hizo mbili, ziko bustani mbili zingine.”
Yaani: Ambazo majengo yake, vyombo vyake, mapambo yake na yote yaliyomo humo, yatakuwa ni ya fedha. Na hizi zitakuwa kwa ajili ya watu wa kuliani. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[9] Dhul-Jalaal Wal-Ikraam: Mwenye Ujalali Na Ukarimu, Utukufu.
Majina haya Matukufu ya Allaah (عزّ وجلّ), yanamaanisha: Mwenye Ujalali Na Ukarimu, Mtukuka daima, Mwenye Utukufu wa Juu Kabisa, Taadhima, Hadhi.
Na kutaja Majina haya katika duaa, ni sababu mojawapo ya duaa kutakabaliwa. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameamrisha mtu akithirishe kutamka Majina haya kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ أَنَسٍ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " أَلِظُّوا بِيَا ذَا الْجَلاَلِ وَالإِكْرَامِ "
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Dumisheni kwa wingi: Yaa-Dhal-Jalaali wal-Ikraam.” [Swahiyh Sunan At-Tirmidhiy (2797)]
الْوَاقِعَة
056-Al-Waaqi’ah
056-Al-Waaqi’ah: Utangulizi Wa Suwrah [362]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
إِذَا وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ ﴿١﴾
1. Litakapotokea Tukio! (La Qiyaamah).[1]
لَيْسَ لِوَقْعَتِهَا كَاذِبَةٌ ﴿٢﴾
2. Hakuna cha kukadhibisha kutokea kwake.
خَافِضَةٌ رَّافِعَةٌ ﴿٣﴾
3. Literemshalo hadhi na linyanyualo hadhi.
إِذَا رُجَّتِ الْأَرْضُ رَجًّا ﴿٤﴾
4. Itakapotikiswa ardhi mtikiso mkubwa.
وَبُسَّتِ الْجِبَالُ بَسًّا ﴿٥﴾
5. Na milima itakapopondwa pondwa.
فَكَانَتْ هَبَاءً مُّنبَثًّا ﴿٦﴾
6. Ikawa chembechembe za vumbi zinazoelea hewani zikitawanyika.
وَكُنتُمْ أَزْوَاجًا ثَلَاثَةً ﴿٧﴾
7. Na mtakuwa namna tatu.[2]
فَأَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ ﴿٨﴾
8. Basi wapo watu wa kuliani; je, ni nani watu wa kuliani?[3]
وَأَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ ﴿٩﴾
9. Na watu wa kushotoni; je, ni nani watu wa kushotoni?[4]
وَالسَّابِقُونَ السَّابِقُونَ ﴿١٠﴾
10. Na waliotangulia mbele, watatangulia mbele.[5]
أُولَـٰئِكَ الْمُقَرَّبُونَ ﴿١١﴾
11. Hao ndio watakaokurubishwa.
فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿١٢﴾
12. Katika Jannaat za taanisi.
ثُلَّةٌ مِّنَ الْأَوَّلِينَ ﴿١٣﴾
13. Kundi kubwa katika wa awali.[6]
وَقَلِيلٌ مِّنَ الْآخِرِينَ ﴿١٤﴾
14. Na wachache katika wa mwishoni.
عَلَىٰ سُرُرٍ مَّوْضُونَةٍ ﴿١٥﴾
15. (Watakuwa) juu ya makochi ya fakhari yaliyotariziwa na kutonewa johari za thamani kwa ustadi wa hali ya juu.[7]
مُّتَّكِئِينَ عَلَيْهَا مُتَقَابِلِينَ ﴿١٦﴾
16. Wakiegemea juu yake wakielekeana.
يَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُّخَلَّدُونَ ﴿١٧﴾
17. Watazungukiwa (kuhudumiwa) na vijana wenye kudumu (katika hali yao milele).
بِأَكْوَابٍ وَأَبَارِيقَ وَكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍ ﴿١٨﴾
18. Kwa bilauri na mabirika na vikombe vya mvinyo kutoka chemchemu inayobubujika.
لَّا يُصَدَّعُونَ عَنْهَا وَلَا يُنزِفُونَ ﴿١٩﴾
19. Hawatoumizwa vichwa kwavyo na wala hawatoleweshwa.
وَفَاكِهَةٍ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ ﴿٢٠﴾
20. Na matunda watakayopendelea.
وَلَحْمِ طَيْرٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ ﴿٢١﴾
21. Na nyama za ndege katika watakazozitamani.
وَحُورٌ عِينٌ ﴿٢٢﴾
22. Na Hurulaini: Wanawake weupe wazuri wa Jannah wenye macho makubwa ya kupendeza.
كَأَمْثَالِ اللُّؤْلُؤِ الْمَكْنُونِ ﴿٢٣﴾
23. Kama mfano wa lulu zilizohifadhiwa.
جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿٢٤﴾
24. Jazaa kwa yale waliyokuwa wakitenda.
لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا تَأْثِيمًا ﴿٢٥﴾
25. Hawatosikia humo upuuzi na wala yanayosababisha dhambi.
إِلَّا قِيلًا سَلَامًا سَلَامًا ﴿٢٦﴾
26. Isipokuwa itasemwa: Salama, salama!
وَأَصْحَابُ الْيَمِينِ مَا أَصْحَابُ الْيَمِينِ ﴿٢٧﴾
27. Na watu wa kuliani, je, ni nani watu wa kuliani?
فِي سِدْرٍ مَّخْضُودٍ ﴿٢٨﴾
28. (Watakuwa) kwenye mikunazi iliyokatwa miba.
وَطَلْحٍ مَّنضُودٍ ﴿٢٩﴾
29. Na migomba ya ndizi iliyopangwa matabaka.
وَظِلٍّ مَّمْدُودٍ ﴿٣٠﴾
30. Na kivuli kilichotandazwa.
وَمَاءٍ مَّسْكُوبٍ ﴿٣١﴾
31. Na maji yenye kumiminwa.
وَفَاكِهَةٍ كَثِيرَةٍ ﴿٣٢﴾
32. Na matunda mengi.
لَّا مَقْطُوعَةٍ وَلَا مَمْنُوعَةٍ ﴿٣٣﴾
33. Hayana kikomo na wala hayakatazwi.
وَفُرُشٍ مَّرْفُوعَةٍ ﴿٣٤﴾
34. Na matandiko ya kupumzikia yaliyoinuliwa.
إِنَّا أَنشَأْنَاهُنَّ إِنشَاءً ﴿٣٥﴾
35. Hakika Sisi Tutawaumba (hurulaini) upya tofauti na mwanzo.
فَجَعَلْنَاهُنَّ أَبْكَارًا ﴿٣٦﴾
36. Tuwafanye mabikra.
عُرُبًا أَتْرَابًا ﴿٣٧﴾
37. Wenye mahaba, ashiki na bashasha kwa waume zao, hirimu moja.
لِّأَصْحَابِ الْيَمِينِ ﴿٣٨﴾
38. Kwa ajili ya watu wa kuliani.
ثُلَّةٌ مِّنَ الْأَوَّلِينَ ﴿٣٩﴾
39. Kundi kubwa katika wa awali.
وَثُلَّةٌ مِّنَ الْآخِرِينَ ﴿٤٠﴾
40. Na kundi kubwa katika wa mwishoni.[8]
وَأَصْحَابُ الشِّمَالِ مَا أَصْحَابُ الشِّمَالِ ﴿٤١﴾
41. Na watu wa kushotoni, je, ni nani watu wa kushotoni?[9]
فِي سَمُومٍ وَحَمِيمٍ ﴿٤٢﴾
42. (Watakuwa) kwenye moto ubabuao na maji yachemkayo.
وَظِلٍّ مِّن يَحْمُومٍ ﴿٤٣﴾
43. Na kivuli cha moshi mweusi mnene wa joto kali mno.
لَّا بَارِدٍ وَلَا كَرِيمٍ ﴿٤٤﴾
44. Si cha baridi na wala si cha kunufaisha.
إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُتْرَفِينَ ﴿٤٥﴾
45. Hakika wao walikuwa kabla ya hayo wanaostareheshwa kwa anasa za dunia.
وَكَانُوا يُصِرُّونَ عَلَى الْحِنثِ الْعَظِيمِ ﴿٤٦﴾
46. Na walikuwa wakishikilia kufanya dhambi kubwa mno.
وَكَانُوا يَقُولُونَ أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ ﴿٤٧﴾
47. Na walikuwa wakisema: Je, hivi tutakapokufa na tukawa udongo na mifupa, je hivi sisi hakika tutafufuliwa?[10]
أَوَآبَاؤُنَا الْأَوَّلُونَ ﴿٤٨﴾
48. Au, je na baba zetu wa awali pia?
قُلْ إِنَّ الْأَوَّلِينَ وَالْآخِرِينَ ﴿٤٩﴾
49. Sema: (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika wa awali na wa mwishoni.
لَمَجْمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَاتِ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ ﴿٥٠﴾
50. Bila shaka watajumuishwa katika wakati na mahali pa siku maalumu.
ثُمَّ إِنَّكُمْ أَيُّهَا الضَّالُّونَ الْمُكَذِّبُونَ ﴿٥١﴾
51. Kisha hakika nyinyi enyi wapotovu mnaokadhibisha.
لَآكِلُونَ مِن شَجَرٍ مِّن زَقُّومٍ ﴿٥٢﴾
52. Bila shaka mtakula katika mti wa zaqquwm.[11]
فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ ﴿٥٣﴾
53. Na kwa huo mtajaza matumbo.
فَشَارِبُونَ عَلَيْهِ مِنَ الْحَمِيمِ ﴿٥٤﴾
54. Na mtakunywa juu yake maji ya moto yachemkayo mno.
فَشَارِبُونَ شُرْبَ الْهِيمِ ﴿٥٥﴾
55. Tena mtakunywa kama wanywavyo ngamia wenye kiu mno!
هَـٰذَا نُزُلُهُمْ يَوْمَ الدِّينِ ﴿٥٦﴾
56. Haya ndio mapokezi yao Siku ya Malipo!
نَحْنُ خَلَقْنَاكُمْ فَلَوْلَا تُصَدِّقُونَ ﴿٥٧﴾
57. Sisi Tumekuumbeni, basi kwa nini hamsadiki?
أَفَرَأَيْتُم مَّا تُمْنُونَ ﴿٥٨﴾
58. Je, basi mnaona manii mnayoimwagia kwa nguvu?
أَأَنتُمْ تَخْلُقُونَهُ أَمْ نَحْنُ الْخَالِقُونَ ﴿٥٩﴾
59. Je, nyinyi ndio mnayoiumba au Sisi ndio Waumbaji?
نَحْنُ قَدَّرْنَا بَيْنَكُمُ الْمَوْتَ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ ﴿٦٠﴾
60. Sisi Tumekadiria baina yenu mauti, Nasi Sio Wenye Kushindwa.
عَلَىٰ أَن نُّبَدِّلَ أَمْثَالَكُمْ وَنُنشِئَكُمْ فِي مَا لَا تَعْلَمُونَ ﴿٦١﴾
61. Kwamba Tuwabadilishe wengine mifano yenu, na Tukuumbeni katika umbo msilolijua.
وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ النَّشْأَةَ الْأُولَىٰ فَلَوْلَا تَذَكَّرُونَ ﴿٦٢﴾
62. Na bila shaka mmejua umbo la awali, basi kwa nini hamkumbuki?
أَفَرَأَيْتُم مَّا تَحْرُثُونَ ﴿٦٣﴾
63. Je, mnaona mbegu mnazozipanda?
أَأَنتُمْ تَزْرَعُونَهُ أَمْ نَحْنُ الزَّارِعُونَ ﴿٦٤﴾
64. Je, ni nyinyi ndio mnaziotesha, au Sisi Ndio Wenye Kuotesha mimea?
لَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَاهُ حُطَامًا فَظَلْتُمْ تَفَكَّهُونَ ﴿٦٥﴾
65. Lau Tungelitaka, Tungeliifanya mabua yaliyonyauka na kupondekapondeka, mkabaki mnashangaa na kusikitika.
إِنَّا لَمُغْرَمُونَ ﴿٦٦﴾
66. (Mkisema): Hakika sisi tumegharimika.
بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ ﴿٦٧﴾
67. Bali sisi tumenyimwa.
أَفَرَأَيْتُمُ الْمَاءَ الَّذِي تَشْرَبُونَ ﴿٦٨﴾
68. Je, mnaona maji ambayo mnakunywa?
أَأَنتُمْ أَنزَلْتُمُوهُ مِنَ الْمُزْنِ أَمْ نَحْنُ الْمُنزِلُونَ ﴿٦٩﴾
69. Je, ni nyinyi ndio mliyoyateremsha kutoka katika mawingu ya mvua au Sisi Ndio Wateremshaji?
لَوْ نَشَاءُ جَعَلْنَاهُ أُجَاجًا فَلَوْلَا تَشْكُرُونَ ﴿٧٠﴾
70. Lau Tungelitaka, Tungeliyafanya ya chumvi kali chungu, basi kwa nini hamshukuru?!
أَفَرَأَيْتُمُ النَّارَ الَّتِي تُورُونَ ﴿٧١﴾
71. Je, mnaona moto ambao mnauwasha?
أَأَنتُمْ أَنشَأْتُمْ شَجَرَتَهَا أَمْ نَحْنُ الْمُنشِئُونَ ﴿٧٢﴾
72. Je, ni nyinyi ndio mliouanzisha mti wake, au Sisi Ndio Waanzilishaji?
نَحْنُ جَعَلْنَاهَا تَذْكِرَةً وَمَتَاعًا لِّلْمُقْوِينَ ﴿٧٣﴾
73. Sisi Tumeufanya kuwa ni ukumbusho na manufaa kwa wasafiri katika jangwa na wahitaji.
فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ ﴿٧٤﴾
74. Basi sabbih kwa Jina la Rabb wako Mwenye U’adhwama.[12]
فَلَا أُقْسِمُ بِمَوَاقِعِ النُّجُومِ ﴿٧٥﴾
75. Basi Naapa kwa maanguko ya nyota.[13]
وَإِنَّهُ لَقَسَمٌ لَّوْ تَعْلَمُونَ عَظِيمٌ ﴿٧٦﴾
76. Na hakika hicho ni kiapo adhimu lau mngelijua.
إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ ﴿٧٧﴾
77. Hakika hii bila shaka ni Qur-aan Tukufu.
فِي كِتَابٍ مَّكْنُونٍ ﴿٧٨﴾
78. Katika Kitabu kilichohifadhiwa.[14]
لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ ﴿٧٩﴾
79. Haigusi isipokuwa waliotakaswa kabisa.
تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٨٠﴾
80. Ni uteremsho kutoka kwa Rabb wa walimwengu.
أَفَبِهَـٰذَا الْحَدِيثِ أَنتُم مُّدْهِنُونَ ﴿٨١﴾
81. Je, basi kwa (unafiki na kujipendekeza) maneno haya nyinyi mnayakanusha na kuyabeza?
وَتَجْعَلُونَ رِزْقَكُمْ أَنَّكُمْ تُكَذِّبُونَ ﴿٨٢﴾
82. Na mnafanya kuruzukiwa kwenu kuwa ndio mnakadhibisha?!
فَلَوْلَا إِذَا بَلَغَتِ الْحُلْقُومَ ﴿٨٣﴾
83. Basi mbona roho ifikapo kooni.[15]
وَأَنتُمْ حِينَئِذٍ تَنظُرُونَ ﴿٨٤﴾
84. Nanyi wakati huo mnatazama.
وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنكُمْ وَلَـٰكِن لَّا تُبْصِرُونَ ﴿٨٥﴾
85. Nasi Tuko karibu naye zaidi kuliko nyinyi, lakini hamuoni.
فَلَوْلَا إِن كُنتُمْ غَيْرَ مَدِينِينَ ﴿٨٦﴾
86. Basi je, -mnaweza- ikiwa mnadai kwamba hamtohisabiwa wala kulipwa (na kwamba hamko chini ya Mamlaka Yetu).
تَرْجِعُونَهَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٨٧﴾
87. Kuirudisha roho (mwilini mwake), mkiwa ni wakweli?
فَأَمَّا إِن كَانَ مِنَ الْمُقَرَّبِينَ ﴿٨٨﴾
88. Basi akiwa miongoni mwa waliokurubishwa. [16]
فَرَوْحٌ وَرَيْحَانٌ وَجَنَّتُ نَعِيمٍ ﴿٨٩﴾
89. Basi mapumziko ya raha na manukato na Jannah ya neema.
وَأَمَّا إِن كَانَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ ﴿٩٠﴾
90. Na kama akiwa miongoni mwa watu wa kuliani.
فَسَلَامٌ لَّكَ مِنْ أَصْحَابِ الْيَمِينِ ﴿٩١﴾
91. Basi (ataambiwa): Salaam juu yako uliye katika watu wa kuliani.
وَأَمَّا إِن كَانَ مِنَ الْمُكَذِّبِينَ الضَّالِّينَ ﴿٩٢﴾
92. Na kama akiwa miongoni mwa wakadhibishaji waliopotoka.
فَنُزُلٌ مِّنْ حَمِيمٍ ﴿٩٣﴾
93. Basi mapokezi yake ni maji ya moto yachemkayo.
وَتَصْلِيَةُ جَحِيمٍ ﴿٩٤﴾
94. Na kuunguzwa na moto uwakao vikali mno.
إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ حَقُّ الْيَقِينِ ﴿٩٥﴾
95. Hakika hii bila shaka ni haki yenye yakini.
فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ ﴿٩٦﴾
96. Basi sabbih kwa Jina la Rabb wako Mwenye U’adhwama.[17]
[1] Matukio Ya Siku Ya Qiyaamah:
Suwrah inaanza kwa kutaja tukio la Siku ya Qiyaamah, ikafuatia kutaja matukio yake mengineyo kama ardhi kutingishwa, na milima kupondwapondwa, Aayah namba (3-6). Na matukio kama haya na mengineyo, yametajwa katika Suwrah zifuatazo: An-Naazi’aat (79:6-14), At-Takwiyr (81:1-13), Al-Infitwaar (82:1-4), Al-Inshiqaaq (84:1-5), Az-Zalzalah (99), Al-Qaari’ah (101:1-5).
[2] Watu Watagawanyika Makundi Matatu Siku Ya Qiyaamah:
Kuanzia Aayah hii namba (7) hadi namba (11), Tafsiyr yake ni ifuatayo:
Watu watagawanywa katika magurupu matatu kulingana na amali zao njema na ovu. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Watu watawaganyika katika aina tatu za makundi: (i) Watu wa kuliani mwa ‘Arsh, na hao ni wale waliotolewa ubavuni mwa Aadam upande wa kulia. Hawa watapewa Vitabu vyao kuliani mwao na watapelekwa upande wa kulia. As-Suddi amesema: Hao ndio wengi katika watu wa Jannah. (ii) Aina nyengine la kundi ni wale watakaowekwa upande wa kushoto wa ‘Arsh. Na hawa ni wale waliotolewa ubavu wa kushoto wa Aadam. Na hawa watapewa Vitabu vyao kushotoni mwao na watapelekwa upande wa kushoto. Hao wengi wao ni watu wa motoni, Allaah Atuepushe na matendo yao. (iii) Kundi la tatu linajumuisha wale waliotangulia mbele na waliokaribu zaidi mbele ya Allaah. Hao wamo katika daraja bora na hadhi, na ndio walio karibu zaidi na Allaah kuliko walio upande wa kulia. Hao ndio walio juu ya wote kwa sababu wao ni Rusuli, Manabii, wakweli wasadikishaji na Shuhadaa, nao ni wachache katika watu wa upande wa kuliani. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Rejea Faatwir (35:32) kwenye faida nyenginezo.
Rejea pia At-Takwiyr (81:7).
[3] Hali Za Watu Walio Kuliani:
Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akabainisha hali za makundi matatu:
فَأَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ ﴿٨﴾
“Basi wapo watu wa kuliani; je, ni nani watu wa kuliani.”
Kutukuzwa hadhi zao na daraja lao la juu. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Hii ni sawa na Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى) za Suwrah Al-Haaqqah (69:19-24), Al-Inshiqaaq (54:7-9).
[4] Hali Za Watu Wa Kushotoni:
وَأَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ مَا أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ ﴿٩﴾
“Na watu wa kushotoni; je, ni nani watu wa kushotoni.”
Swali hapa pia limekuja ili kuzindusha jinsi gani hali mbaya watakayokuwa nayo.
Hii ni sawa na Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى) za Suwrah Al-Haaqqah (69:25-37), Al-Inshiqaaq (54:7-9).
[5] Hali Za Waliotangulia Mbele:
وَالسَّابِقُونَ السَّابِقُونَ ﴿١٠﴾
“Na waliotangulia mbele, watatangulia mbele.”
Ambao wametanguliza katika khayraat duniani basi watatangulizwa Aakhirah kuingia Jannah. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[6] Kundi Kubwa La Awali:
Ni watu wengi waliotangulia katika Ummah huu na wengineo. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[7] Miongoni Mwa Neema Za Jannah:
Kuanzia Aayah hii namba (15) hadi Aayah namba (37), zinatajwa neema katika neema za Jannah. Na zimetajwa sifa na hali za wakaazi wake zitakavyokuwa. Aayah nyingi zimetaja kuhusu watu wa Jannah, hali zao, sifa zao na starehe zao pamoja na neema tele. Rejea pia Faatwir (35:33) kwenye neema nyenginezo za watu wa Jannah. Hali kadhaalika, zipo Hadiyth nyingi ambazo zimetaja hayo. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo:
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ مُقَاتِلٍ، أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ، أَخْبَرَنَا مَعْمَرٌ، عَنْ هَمَّامِ بْنِ مُنَبِّهٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " أَوَّلُ زُمْرَةٍ تَلِجُ الْجَنَّةَ صُورَتُهُمْ عَلَى صُورَةِ الْقَمَرِ لَيْلَةَ الْبَدْرِ، لاَ يَبْصُقُونَ فِيهَا وَلاَ يَمْتَخِطُونَ وَلاَ يَتَغَوَّطُونَ، آنِيَتُهُمْ فِيهَا الذَّهَبُ، أَمْشَاطُهُمْ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ، وَمَجَامِرُهُمُ الأَلُوَّةُ، وَرَشْحُهُمُ الْمِسْكُ، وَلِكُلِّ وَاحِدٍ مِنْهُمْ زَوْجَتَانِ، يُرَى مُخُّ سُوقِهِمَا مِنْ وَرَاءِ اللَّحْمِ، مِنَ الْحُسْنِ، لاَ اخْتِلاَفَ بَيْنَهُمْ وَلاَ تَبَاغُضَ، قُلُوبُهُمْ قَلْبٌ وَاحِدٌ، يُسَبِّحُونَ اللَّهَ بُكْرَةً وَعَشِيًّا ".
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kikundi cha kwanza (cha watu) kuingia Jannah (Peponi) watakuwa waking’ara kama mwezi unapokuwa umekamilika. Hawatatema mate humo wala kuchemua wala kwenda haja. Vyombo vyao vitakuwa ni vya dhahabu, vichana vyao ni vya dhahabu na fedha. Katika vyetezo vyao kutakuwa na uluwwah (mti wenye harufu nzuri unapochomwa) na majasho yao yatanukia kama miski (manukato). Kila mmoja wao atakuwa na wake wawili. Uboho ulio ndani ya mifupa ya miguu ya wake zao utaonekana kupitia nyama zao kwa uzuri wao uliopita kiasi. Wao (yaani watu wa Jannah) hawatakuwa na tofauti baina yao wala chuki. Nyoyo zao zitakuwa kama moyo mmoja, nao watakuwa wanamtakasa Allaah asubuhi na jioni.”
[Al-Bukhaariy Kitaabu Cha Hadiyth Za Uanzishaji Wa Uumbaji (59)]
Riwaaya kama hiyo imo katika [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Hadiyth Za Manabii (60). Na pia katika Muslim Kitabu Cha Jannah Sifa Zake Na Neema Zake Na Watu Wake]
عن أبي موسى رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم قال : (( إنَّ لِلمُؤْمِنِ فِي الجَنَّةِ لَخَيْمَةً مِنْ لُؤْلُؤَةٍ وَاحِدَةٍ مُجَوَّفَةٍ طُولُها في السَّمَاءِ سِتُّونَ مِيلاً . لِلمُؤْمِنِ فِيهَا أَهْلُونَ يَطُوفُ عَلَيْهِمُ المُؤْمِنُ فَلاَ يَرَى بَعْضُهُمْ بَعْضاً )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
Amesimulia Abuu Muwsaa (رضي الله عنه): amesema: “Hakika, Muumini katika Jannah atakuwa na hema la lulu ambalo liko mviringo, urefu wake ni maili sitiini kwenda juu. Muumini atakuwa na familia yake humo, Muumini atakuwa akiwazunguka humo nao hawaonani (jinsi lilivyo kubwa).” [Al-Bukhaariy na Muslim]
عن أبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال : (( إنَّ أدْنَى مَقْعَدِ أَحَدِكُمْ مِن الجَنَّةِ أنْ يَقُولَ لَهُ : تَمَنَّ ، فَيَتَمَنَّى وَيَتَمَنَّى فَيقُولُ لَهُ : هَلْ تَمَنَّيتَ ؟ فيقولُ : نَعَمْ ، فيقُولُ لَهُ : فَإنَّ لَكَ ما تَمَنَّيتَ وَمِثْلَهُ
مَعَهُ )) . رواه مسلم
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika daraja ya chini mno ya mmoja wenu Jannah, ni kuwa Allaah Atamwambia Tamani! Atatamani kila atakalo. Allaah Atamuuliza: Umeshamaliza kutamani? Atajibu: Ndio. Allaah Atamwambia: Nimekupa ulichotamani na Nimekupa kingine kama hicho.” [Muslim]
Bonyeza viungo vifuatavyo kwenye faida nyenginezo:
Neema Za Jannah (Pepo) Tuliyoahidiwa [363]
Al-Jannah (Pepo) [364]
Jazaa Ya Waja Wema Na Neema Za Jannah [365]
[8] Kundi Kubwa Katika Wa Mwishoni:
Huu ni mgawanyo wa watu wa kuliani ambao idadi yao ni kubwa ya wtu wa awali na idadi kubwa ya watu mwishoni. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[9] Watu Wa Kushotoni Ni Watu Wa Motoni Na Maelezo Yao:
Aayah hii namba (41) hadi Aayah namba (56) zinataja watu wa motoni na sababu za kuwa kwao watu wa motoni, hali zao zitakvyokuwa motoni na adhabu zao.
Rejea An-Nabaa (78:21) kwenye uchambuzi na rejea mbalimbali kuhusu watu wa motoni, hali zao, mateso na adhabu zao, vyakula na vinywaji vyao.
Rejea pia Faatwir (33:36) kwenye faida nyenginezo kuhusu maudhui hii na rejea zake.
[11] Mti Wa Zaqquwm:
Zaqquwm ni mti wa motoni ambao utakuwa ni chakula cha wakaazi wake. Rejea Al-Israa (17:60).
[12] Kumsabbih Allaah (سبحانه وتعالى) Katika Aayah Za Kumsabbih, Kuomba Rahmah, Jannah (Pepo) Kuomba Kinga Na Kadhaalika.
عَنْ حُذَيْفَةَ، قَالَ صَلَّيْتُ مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ذَاتَ لَيْلَةٍ فَافْتَتَحَ الْبَقَرَةَ فَقُلْتُ يَرْكَعُ عِنْدَ الْمِائَةِ . ثُمَّ مَضَى فَقُلْتُ يُصَلِّي بِهَا فِي رَكْعَةٍ فَمَضَى فَقُلْتُ يَرْكَعُ بِهَا . ثُمَّ افْتَتَحَ النِّسَاءَ فَقَرَأَهَا ثُمَّ افْتَتَحَ آلَ عِمْرَانَ فَقَرَأَهَا يَقْرَأُ مُتَرَسِّلاً إِذَا مَرَّ بِآيَةٍ فِيهَا تَسْبِيحٌ سَبَّحَ وَإِذَا مَرَّ بِسُؤَالٍ سَأَلَ وَإِذَا مَرَّ بِتَعَوُّذٍ تَعَوَّذَ ثُمَّ رَكَعَ فَجَعَلَ يَقُولُ " سُبْحَانَ رَبِّيَ الْعَظِيمِ " . فَكَانَ رُكُوعُهُ نَحْوًا مِنْ قِيَامِهِ ثُمَّ قَالَ " سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ " . ثُمَّ قَامَ طَوِيلاً قَرِيبًا مِمَّا رَكَعَ ثُمَّ سَجَدَ فَقَالَ " سُبْحَانَ رَبِّيَ الأَعْلَى "
Amesimulia Hudhayfah (رضي الله عنه): Niliswali pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) usiku usiku mmoja, akaanza kusoma Suwrah Al-Baqarah, nikadhania kuwa atarukuu atakapofikia mwishoni mwa Aayah mia lakini akaendelea. Kisha nikadhania kuwa ataisoma (Suwrah) nzima katika Rakaa lakini akaendelea. Nikadhania kuwa atarukuu atakapoimaliza (Suwrah). Kisha akaanza An-Nisaa akaisoma, kisha akaanza Aal-‘Imraan akaisoma kwa utulivu. Akawa kila anapopita Aayah yenye tasbiyh alisabbih, na alipopita Aayah ya kumuomba Allaah aliomba, na alipopita katika kuomba kinga aliomba kinga, kisha akarukuu akasema:
سُبْحَانَ رَبِّيَ الْعَظِيمِ
Rukuu yake ilidumu kwa urefu sawa na kusimama kwake (kisha akarudi kwenye kisimamo baada ya kurukuu) akasema:
سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ
Kisha akasimama kwa muda mrefu kama muda ule ule alotumia katika kurukuu. Kisha akasujudu na akasema:
سُبْحَانَ رَبِّيَ الأَعْلَى
Na kusujudu kwake kulidumu karibu urefu sawa na kisimamo chake. [Muslim]
[13] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
056-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Waaqi’ah Aayah 75-82: فَلَا أُقْسِمُ بِمَوَاقِعِ النُّجُومِ [366]
[14] Kitabu Kilichohifadhiwa (Al-Lawh Al-Mahfuwdhw):
Kimewekewa pazia kisiweze kuonwa na macho ya viumbe. Na Kitabu hiki kilichohifadhiwa hivyo ni Al-Lawh Al-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa), yaani: Qur-aan hii imeandikwa katika Al-Lawh Al-Mahfuwdhw, imetukuka mbele ya Allaah na Malaika Wake wenye hadhi kubwa Kwake. Pia inawezekana kwamba Kitabu kilichohifadhiwa kinachomaanishwa hapa, ni Kitabu ambacho kiko mikononi mwa Malaika ambao Allaah Anawateremshia Wahy Wake na Uteremsho Wake (Qur-aan Yake), na kwamba muradi wa kuhifadhiwa ni kuwekewa pazia mashaytwaan wasiweze kukifikia na wasiwe na uwezo wa kukibadilisha, wala kukiongeza, kukipunguza, wala kukidukua. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[16] Hali Za Aina Tatu Za Watu Mauti Yanapowafikia:
Mwanzoni mwa Suwrah, Allaah (سبحانه وتعالى) Ametaja aina tatu za watu watakavyokuwa Aakhirah ambayo ni makazi ya milele,: (i) Waliokurubishwa. (ii) Watu wa kuliani. (iii) Waliokadhibisha Wapotovu. Na mwishoni mwa Suwrah kuanzia Aayah hii namba (88) hadi namba (94) Anataj hali zao katika kutolewa roho zao. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Rejea mwanzoni mwa Suwrah hii Aayah namba (7).
Kuhusu Waumini wanapotolewa roho zao, rejea Qaaf (50:19) kwenye faida kadhaa.
Na kuhusu neema za kuingizwa Jannah (Peponi), rejea Faatwir (35:33).
Ama kuhusu makafiri, rejea An-Nabaa (78:21) kwenye uchambuzi na rejea mbalimbali, kuhusu mateso na adhabu zao motoni, hali zao, vyakula na vinywaji vyao.
[17] Kumsabbih Allaah:
Kumsabbih Allaah (عزّ وجلّ) kwa
سُبْحَانَ اللهِ العظيمِ
ni katika Adhkaar za kurukuu kwenye Swalaah. Bonyeza kiungo kifuatacho kupata maelezo, na kuisoma kwa sauti:
Na Hadiyth kadhaa zimetaja fadhila za kumsabbih Allaah ambazo miongoni mwazo ni Hadiyth hii ifuatayo:
عن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( كَلِمَتَانِ خَفِيفَتَانِ عَلَى اللِّسَانِ ، ثَقِيلَتَانِ فِي المِيزَانِ ، حَبِيبَتَانِ إِلَى الرَّحْمانِ : سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ ، سُبْحَانَ اللهِ العظيمِ )) متفقٌ عَلَيْهِ
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Maneno mawili ni mepesi ulimini, mazito katika mizani na yanapendwa na Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma):
سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ ، سُبْحَانَ اللهِ العظيمِ
Ametakasika Allaah na Himdi zote Njema Anastahiki, Ametakasika Allaah Mtukufu."
[Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]
Rejea pia kiungo kifuatacho chenye kutaja fadhila za kumsabbih Allaah (سبحانه وتعالى):
الْحَدِيد
057-Al-Hadiyd
057-Al-Hadiyd: Utangulizi Wa Suwrah [370]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١﴾
1. Vimemsabbih Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na ardhi,[1] Naye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.[2]
لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢﴾
2. Ni Wake Pekee ufalme wa mbingu na ardhi, Anahuisha na Anafisha, Naye juu ya kila kitu Ni Muweza.
هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٣﴾
3. Yeye Ndiye wa Awali hakuna kitu kabla Yake, na wa Mwisho hakuna kitu baada Yake, na Aliye juu hakuna kitu juu Yake, na Aliye karibu, hakuna kitu kilichokaribu kuliko Yeye, Naye kwa kila kitu Ni Mjuzi.
هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاءِ وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا ۖ وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٤﴾
4. Yeye Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Akawa juu[3] ya ‘Arsh. Anajua yale yanayoingia ardhini, na yale yatokayo humo, na yale yanayoteremka kutoka mbinguni, na yale yanayopanda humo. Naye Yu Pamoja nanyi popote mlipo. Na Allaah Ni Mwenye Kuona yote myatendayo.
لَّهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿٥﴾
5. Ni Wake Pekee ufalme wa mbingu na ardhi, na kwa Allaah Pekee yanarejeshwa mambo yote.
يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ ۚ وَهُوَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿٦﴾
6. Anauingiza usiku katika mchana, na Anaingiza mchana katika usiku, Naye Ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.
آمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَأَنفِقُوا مِمَّا جَعَلَكُم مُّسْتَخْلَفِينَ فِيهِ ۖ فَالَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَأَنفَقُوا لَهُمْ أَجْرٌ كَبِيرٌ ﴿٧﴾
7. Muaminini Allaah na Rasuli Wake, na toeni kutokana na yale Aliyokufanyieni kuwa warithi kwayo. Basi wale walioamini miongoni mwenu, na wakatoa, watapata ujira mkubwa.
وَمَا لَكُمْ لَا تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۙ وَالرَّسُولُ يَدْعُوكُمْ لِتُؤْمِنُوا بِرَبِّكُمْ وَقَدْ أَخَذَ مِيثَاقَكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٨﴾
8. Na mna nini nyinyi hata msimwamini Allaah, na hali Rasuli anakuiteni ili mumuamini Rabb wenu, Naye (Allaah) Amekwishachukua fungamano lenu mkiwa nyinyi ni Waumini!
هُوَ الَّذِي يُنَزِّلُ عَلَىٰ عَبْدِهِ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ لِّيُخْرِجَكُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ بِكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿٩﴾
9. Yeye Ndiye Anayemteremshia Mja Wake Aayaat bayana ili Akutoeni katika viza na kukuingizeni kwenye nuru. Na hakika Allaah kwenu Ni Mwenye Huruma mno, Mwenye Kurehemu.
وَمَا لَكُمْ أَلَّا تُنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلِلَّـهِ مِيرَاثُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ لَا يَسْتَوِي مِنكُم مَّنْ أَنفَقَ مِن قَبْلِ الْفَتْحِ وَقَاتَلَ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْظَمُ دَرَجَةً مِّنَ الَّذِينَ أَنفَقُوا مِن بَعْدُ وَقَاتَلُوا ۚ وَكُلًّا وَعَدَ اللَّـهُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿١٠﴾
10. Na mna nini hata hamtoi katika Njia ya Allaah, na hali urithi wa mbingu na ardhi ni wa Allaah Pekee! Hawi sawa miongoni mwenu aliyetoa kabla ya Ushindi (wa Makkah) na akapigana. Hao watapata daraja kuu kabisa kuliko wale waliotoa baadae na wakapigana. Na wote Allaah Amewaahidi malipo mazuri kabisa. Na Allaah kwa yale myatendayo Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
مَّن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ وَلَهُ أَجْرٌ كَرِيمٌ ﴿١١﴾
11. Nani ambaye atamkopesha Allaah karadha mzuri kisha (Allaah) Amuongezee maradufu na apate ujira mtukufu?[4]
يَوْمَ تَرَى الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ يَسْعَىٰ نُورُهُم بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِم بُشْرَاكُمُ الْيَوْمَ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٢﴾
12. Siku utakayowaona Waumini wa kiume na Waumini wa kike, nuru yao inakwenda mbele yao na kuliani kwao; (wataambiwa): Bishara njema kwenu leo! Jannaat zipitazo chini yake mito, mdumu humo. Huko ndiko kufuzu kukubwa mno.[5]
يَوْمَ يَقُولُ الْمُنَافِقُونَ وَالْمُنَافِقَاتُ لِلَّذِينَ آمَنُوا انظُرُونَا نَقْتَبِسْ مِن نُّورِكُمْ قِيلَ ارْجِعُوا وَرَاءَكُمْ فَالْتَمِسُوا نُورًا فَضُرِبَ بَيْنَهُم بِسُورٍ لَّهُ بَابٌ بَاطِنُهُ فِيهِ الرَّحْمَةُ وَظَاهِرُهُ مِن قِبَلِهِ الْعَذَابُ ﴿١٣﴾
13. Siku wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike watakapowaambia wale walioamini: Tungojeeni, tupate mwangaza kutokana na nuru yenu! (Wataambiwa): Rudini nyuma yenu, mtafute huko nuru (yenu)! Kisha utawekwa ukuta baina yao wenye mlango, ndani mna rehma na nje kwa upande wake wa mbele mna adhabu.
يُنَادُونَهُمْ أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ وَلَـٰكِنَّكُمْ فَتَنتُمْ أَنفُسَكُمْ وَتَرَبَّصْتُمْ وَارْتَبْتُمْ وَغَرَّتْكُمُ الْأَمَانِيُّ حَتَّىٰ جَاءَ أَمْرُ اللَّـهِ وَغَرَّكُم بِاللَّـهِ الْغَرُورُ ﴿١٤﴾
14. (Wanafiki) watawaita: Je, kwani hatukuwa pamoja nanyi? Watasema: Ndio (mlikuwa)! Lakini nyinyi mlizifitini nafsi zenu, na mkangojea itusibu misiba na mkatia shaka, na yakakughururini matumaini ya uongo mpaka ikaja Amri ya Allaah, na akakughuruni mdanganyifu (Ibliys) kuhusu Allaah.
فَالْيَوْمَ لَا يُؤْخَذُ مِنكُمْ فِدْيَةٌ وَلَا مِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ مَأْوَاكُمُ النَّارُ ۖ هِيَ مَوْلَاكُمْ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿١٥﴾
15. Basi leo haitochukuliwa kutoka kwenu fidia wala kutoka kwa waliokufuru. Makazi yenu ni moto, huo ndio unaostahiki kwenu, na ubaya ulioje mahali pa kuishia!
أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّـهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿١٦﴾
16. Je, haujafika wakati kwa walioamini kwamba zinyenyekee nyoyo zao kwa kumdhukuru Allaah na yale yaliyoteremka ya haki, na wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla, ukawatawilikia muda, kisha zikasusuwaa nyoyo zao? Na wengi miongoni mwao ni mafasiki.[6]
اعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١٧﴾
17. Jueni kwamba Allaah Anahuisha ardhi baada ya kufa kwake. Hakika Tumekubainishieni Aayaat (Ishara, Dalili) ili mpate kutia akilini.
إِنَّ الْمُصَّدِّقِينَ وَالْمُصَّدِّقَاتِ وَأَقْرَضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا يُضَاعَفُ لَهُمْ وَلَهُمْ أَجْرٌ كَرِيمٌ ﴿١٨﴾
18. Hakika wanaume watoao swadaqa na wanawake watoao swadaqa na wakamkopesha Allaah karadha mzuri, watazidishiwa maradufu, na watapa ujira mtukufu.[7]
وَالَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصِّدِّيقُونَ ۖ وَالشُّهَدَاءُ عِندَ رَبِّهِمْ لَهُمْ أَجْرُهُمْ وَنُورُهُمْ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ ﴿١٩﴾
19. Na wale waliomwamini Allaah na Rusuli Wake, hao ndio Asw-Swiddiyquwn (waliosadikisha kikweli) na Shuhadaa[8] mbele ya Rabb wao. Watapa ujira wao na nuru yao. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat (Ishara, Dalili, Hoja) Zetu, hao ni watu wa moto uwakao vikali mno.
اعْلَمُوا أَنَّمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَزِينَةٌ وَتَفَاخُرٌ بَيْنَكُمْ وَتَكَاثُرٌ فِي الْأَمْوَالِ وَالْأَوْلَادِ ۖ كَمَثَلِ غَيْثٍ أَعْجَبَ الْكُفَّارَ نَبَاتُهُ ثُمَّ يَهِيجُ فَتَرَاهُ مُصْفَرًّا ثُمَّ يَكُونُ حُطَامًا ۖ وَفِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ شَدِيدٌ وَمَغْفِرَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانٌ ۚ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ ﴿٢٠﴾
20. Jueni kwamba hakika uhai wa dunia ni mchezo na pumbao na mapambo, na kufakharishana baina yenu, na kushindana kwa wingi wa mali na Watoto. Ni kama mfano wa mvua inayowafurahisha wakulima mimea yake, kisha inanyweya, basi utaiona imepiga unjano, kisha inakuwa mabua yaliyonyauka na kupondekapondeka. Na Aakhirah kuna adhabu kali, na maghfirah kutoka kwa Allaah na radhi. Na uhai wa dunia si chochote isipokuwa ni starehe fupi za kughuri.[9]
سَابِقُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا كَعَرْضِ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أُعِدَّتْ لِلَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٢١﴾
21. Kimbilieni kuomba maghfirah[10] kwa Rabb wenu na Jannah (ambayo) upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, imeandaliwa kwa wale waliomwamini Allaah na Rusuli Wake. Hiyo ni Fadhila ya Allaah, Humpa Amtakaye. Na Allaah Ni Mwenye Fadhila adhimu.
مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ مِّن قَبْلِ أَن نَّبْرَأَهَا ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ ﴿٢٢﴾
22. Hausibu msiba wowote katika ardhi au katika nafsi zenu isipokuwa umo katika Kitabu kabla Hatujautokezesha. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.[11]
لِّكَيْلَا تَأْسَوْا عَلَىٰ مَا فَاتَكُمْ وَلَا تَفْرَحُوا بِمَا آتَاكُمْ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ ﴿٢٣﴾
23. Ili msisononeke kwa yale yaliyokuondokeeni na wala msifurahie kwa yale Aliyokupeni (Allaah). Na Allaah Hapendi kila mwenye kujinata, anayejifakharisha.
الَّذِينَ يَبْخَلُونَ وَيَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبُخْلِ ۗ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ ﴿٢٤﴾
24. Ambao wanafanya ubakhili na wanaamrisha watu ubakhili. Na atakayekengeuka, basi hakika Allaah Ndiye Mkwasi, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.
لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ ۖ وَأَنزَلْنَا الْحَدِيدَ فِيهِ بَأْسٌ شَدِيدٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّـهُ مَن يَنصُرُهُ وَرُسُلَهُ بِالْغَيْبِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ ﴿٢٥﴾
25. Kwa yakini Tuliwapeleka Rusuli Wetu kwa hoja bayana, na Tukateremsha pamoja nao Kitabu na miyzaan (hukumu) ili watu waamiliane kwa uadilifu. Na Tukateremsha chuma chenye nguvu shadidi na manufaa kwa watu, na ili Allaah Adhihirishe nani atakayeinusuru (Dini Yake) na Rusuli Wake hali ya kuwa amemtakasia niya bila kumwona. Hakika Allaah Ni Mwenye nguvu zote, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا وَإِبْرَاهِيمَ وَجَعَلْنَا فِي ذُرِّيَّتِهِمَا النُّبُوَّةَ وَالْكِتَابَ ۖ فَمِنْهُم مُّهْتَدٍ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿٢٦﴾
26. Na kwa yakini Tulimtuma Nuwh, na Ibraahiym, na Tukaweka katika dhuriya wao Unabii na Kitabu. Basi miongoni mwao wako waongofu, na wengi wao ni mafasiki.
ثُمَّ قَفَّيْنَا عَلَىٰ آثَارِهِم بِرُسُلِنَا وَقَفَّيْنَا بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ وَآتَيْنَاهُ الْإِنجِيلَ وَجَعَلْنَا فِي قُلُوبِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ رَأْفَةً وَرَحْمَةً وَرَهْبَانِيَّةً ابْتَدَعُوهَا مَا كَتَبْنَاهَا عَلَيْهِمْ إِلَّا ابْتِغَاءَ رِضْوَانِ اللَّـهِ فَمَا رَعَوْهَا حَقَّ رِعَايَتِهَا ۖ فَآتَيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا مِنْهُمْ أَجْرَهُمْ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ ﴿٢٧﴾
27. Kisha Tukafuatisha baada yao Rusuli Wetu, na Tukamfuatisha ‘Iysaa mwana wa Maryam, na Tukampa Injiyl. Na Tukaweka katika nyoyo za wale waliomfuata upole na rehma na uruhubani (maisha ya utawa), wameuzusha wao wenyewe Hatukuwaandikia hayo juu yao isipokuwa kutafuta Radhi za Allaah. Lakini hawakuuchunga ipasavyo kuchungwa. Basi Tukawapa wale walioamini miongoni mwao ujira wao, na wengi wao ni mafasiki.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَآمِنُوا بِرَسُولِهِ يُؤْتِكُمْ كِفْلَيْنِ مِن رَّحْمَتِهِ وَيَجْعَل لَّكُمْ نُورًا تَمْشُونَ بِهِ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٨﴾
28. Enyi walioamini! Mcheni Allaah, na muaminini Rasuli Wake. (Allaah) Atakupeni sehemu mbili ya Rehma Zake,[12] na Atakuwekeeni Nuru mtembee nayo, na Atakughufurieni. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
لِّئَلَّا يَعْلَمَ أَهْلُ الْكِتَابِ أَلَّا يَقْدِرُونَ عَلَىٰ شَيْءٍ مِّن فَضْلِ اللَّـهِ ۙ وَأَنَّ الْفَضْلَ بِيَدِ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٢٩﴾
29. Ili wajue Watu wa Kitabu kwamba hawana uwezo wa chochote katika Fadhila za Allaah, na kwamba fadhila zimo Mkononi mwa Allaah Humpa Amtakaye, na Allaah Ni Mwenye Fadhila adhimu.
[1] Mbingu Na Ardhi Na Vilivyomo Humo Vinamsabbih Allaah (عزّ وجلّ):
Kutokana na taadhima ya Allaah (سبحانه وتعالى) Muumba wa kila kitu, vitu vyote vinamsabbih Yeye Allaah (سبحانه وتعالى).
Rejea Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ ۚ وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِ وَلَـٰكِن لَّا تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ ۗ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا ﴿٤٤﴾
“Zinamsabihi mbingu saba na ardhi na waliomo humo. Na hakuna kitu chochote isipokuwa kinasabihi na kumhimidi Yeye, lakini hamzifahamu tasbihi zao. Hakika Yeye Ni Mvumilivu, Mwingi wa Kughufuria.” [Al-Israa (17:44)]
Na Aayah nyenginezo ambazo zinataja kwamba kila kitu Alichokiumba Allaah (عزّ وجلّ) kinamsabbih ni hizi zifuatazo:
Al-A’raaf (7:206), Ar-Ra’d (13:13), Al-Anbiyaa (21:79), An-Nuwr (24:41), Al-Hashr (59:1), Asw-Swaff (61:1), Al-Jumu’ah (62:1), At-Taghaabun (64:1).
Na miongoni mwa Hadiyth ni hizi zifuatazo:
حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ بُكَيْرٍ، حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، عَنْ يُونُسَ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيَّبِ، وَأَبِي، سَلَمَةَ أَنَّ أَبَا هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ " قَرَصَتْ نَمْلَةٌ نَبِيًّا مِنَ الأَنْبِيَاءِ، فَأَمَرَ بِقَرْيَةِ النَّمْلِ فَأُحْرِقَتْ، فَأَوْحَى اللَّهُ إِلَيْهِ أَنْ قَرَصَتْكَ نَمْلَةٌ أَحْرَقْتَ أُمَّةً مِنَ الأُمَمِ تُسَبِّحُ اللَّهِ."
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Sisimizi alimuuma Nabii miongoni mwa Manabii, ambaye aliamuru kijiji hicho cha sisimizi kuchomwa. Hivyo, Allaah Alimteremshia Wahy: Je, kwa sababu sisimizi mmoja tu amekuuma, nawe ukaunguza Ummah mzima miongoni mwa Ummah unaomsabbih Allaah.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Jihaad (56), Muslim Kitabu Cha Salaam (39)]
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ كُنَّا نَعُدُّ الآيَاتِ بَرَكَةً وَأَنْتُمْ تَعُدُّونَهَا تَخْوِيفًا، كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي سَفَرٍ فَقَلَّ الْمَاءُ فَقَالَ " اطْلُبُوا فَضْلَةً مِنْ مَاءٍ ". فَجَاءُوا بِإِنَاءٍ فِيهِ مَاءٌ قَلِيلٌ، فَأَدْخَلَ يَدَهُ فِي الإِنَاءِ، ثُمَّ قَالَ " حَىَّ عَلَى الطَّهُورِ الْمُبَارَكِ، وَالْبَرَكَةُ مِنَ اللَّهِ " فَلَقَدْ رَأَيْتُ الْمَاءَ يَنْبُعُ مِنْ بَيْنِ أَصَابِعِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم، وَلَقَدْ كُنَّا نَسْمَعُ تَسْبِيحَ الطَّعَامِ وَهْوَ يُؤْكَلُ.
Amesimulia ‘Abdullaah (رضي الله عنه): Tulikuwa tukichukulia miujiza kuwa ni Baraka ya Allaah, lakini nyinyi mnachukulia kuwa ni onyo na tahadhari. Wakati mmoja tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) safarini, nasi tukapungukiwa na maji. Akasema: “Nileteeni maji mliyo nayo.” Watu walileta chombo kilichokuwa na maji kidogo. Alitia mkono wake ndani yake, akasema: “Njooni kwenye maji ya Baraka na Baraka inatoka kwa Allaah.” Niliyaona maji yakitoka kutoka kwenye vidole vya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Na kwa hakika tulikuwa tunasikia chakula kikileta Tasbiyh (Subhaana Allaah) kilipokuwa kinaliwa na yeye. [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Fadhila Za Nabiy Na Ubora Wa Swahaba]
[2] Majina Na Sifa Za Allaah:
Suwrah hii tukufu imetaja baadhi ya Majina ya Allaah katika Aayah za mwanzo (1-6).
Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Kabisa Na Sifa Za Allaah kupata maana zake.
[3] Istawaa اسْتَوَى
Yuko juu kwa namna inayolingana na Uadhama na Ujalali Wake Yeye Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-A'raaf (7:54) kwenye maelezo bayana ya maana yake, yenye kutofautiana na maana ya katika Suwrah Al-Baqarah (2:29) na Suwrat Fusswilat (41:11).
[4] Fadhila Za Kutoa Mali Kwa Ajili Ya Allaah:
Kutoa mali kwa ajili ya Allaah iwe kwa ajili ya Jihaad katika Njia Yake, au swadaqa ya kuwasaidia wahitaji na kusaidia yanayohitajika katika jamii za Kiislamu, ina fadhila adhimu mno. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Ametaja na kuamrisha kutoa mali katika Aayah nyingi. Ametaja katika Suwrah hii Al-Hadiyd (57:6), na Akaonya kutokutoa katika Aayah (57:10). Rejea pia Al-Baqarah (2:261) kwenye maudhui hii ya kutoa mali na maonyo yake. Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amehimiza kutoa mali kwa ajili ya Allaah katika Hadiyth nyingi. Bonyeza viungo vifuatavyo vyenye faida tele kuhusu fadhila za kutoa mali kwa ajili ya Allaah na rejea zake mbalimbali:
[5] Waumini Watavuka Asw-Swiraatw Wakiwa Katika Nuru, Ama Wanafiki Watakuwa Kizani
Tafsiyr ya Aayah hii na zinazofuatia:
Hapa Allaah (سبحانه وتعالى) Anabainisha fadhila za imaan na jini gani Waumiini watakayokuwa furahani kwa imaan zao Siku ya Qiyaamah. Yaani Siku ambayo jua litakapokunjwakunjwa na kupotea mwanga wake, na mwezi utakapopatwa, na pindi watu watakapokuwa katika kiza, na Asw-swiraatw imewekwa juu ya moto wa Jahnnam. Hapo utawaona Waumini wa kiume na Waumini wa kike, nuru yao inatangulia mbele yao na kuliani kwao. Basi watatembea kwa fadhila za imaan na nuru zao katika hali hiyo ngumu mno na ya kutisha, kila mmoja (atavuka Asw-Swiraatw) kulingana na daraja ya imaan yake. Na hapo watabashiriwa bishara Adhimu kwa kuambiwa:
بُشْرَاكُمُ الْيَوْمَ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١٢﴾
“Bishara njema kwenu leo! Jannaat zipitazo chini yake mito, mdumu humo. Huko ndiko kufuzu kukubwa mno.”
Basi Wa-Allaahi, bishara njema iliyoje hiyo na furaha iliyoje kwa bishara hiyo ambayo, watapata humo wanachokitaka, na kuokolewa na kila walilokhofia. Ama wanafiki watakapoona nuru za Waumini zinazowaongoza kutembea, ilhali nuru zao zimezimwa, na wamebakia wamechanganyikwa akili katika kiza, watawaambia Waumini:
انظُرُونَا نَقْتَبِسْ مِن نُّورِكُمْ
“Tungojeeni, tupate mwangaza kutokana na nuru yenu!”
Yaani, nendeni polepole ili tuwadiriki na tupate mwanga wa nuru zenu ili tuweze kutembea na tuokolewe na adhabu. Lakini haiwezekani kamwe kwani
قِيلَ ارْجِعُوا وَرَاءَكُمْ فَالْتَمِسُوا نُورًا فَضُرِبَ بَيْنَهُم بِسُورٍ لَّهُ بَابٌ بَاطِنُهُ فِيهِ الرَّحْمَةُ وَظَاهِرُهُ مِن قِبَلِهِ الْعَذَابُ ﴿١٣﴾
(Wataambiwa): “Rudini nyuma yenu, mtafute huko nuru (yenu)! Kisha utawekwa ukuta baina yao wenye mlango, ndani mna rehma na nje kwa upande wake wa mbele mna adhabu.”
[Tafsiyr As-Sa’diy]
Na miongoni mwa Hadiyth kuhusu vukaji wa asw-swiraatw ni hii ifuatayo:
حَدَّثَنِي عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، وَإِسْحَاقُ بْنُ مَنْصُورٍ، كِلاَهُمَا عَنْ رَوْحٍ، قَالَ عُبَيْدُ اللَّهِ حَدَّثَنَا رَوْحُ بْنُ عُبَادَةَ الْقَيْسِيُّ، حَدَّثَنَا ابْنُ جُرَيْجٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي أَبُو الزُّبَيْرِ، أَنَّهُ سَمِعَ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ، يُسْأَلُ عَنِ الْوُرُودِ، فَقَالَ نَجِيءُ نَحْنُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَنْ كَذَا، وَكَذَا، انْظُرْ أَىْ ذَلِكَ فَوْقَ النَّاسِ - قَالَ - فَتُدْعَى الأُمَمُ بِأَوْثَانِهَا وَمَا كَانَتْ تَعْبُدُ الأَوَّلُ فَالأَوَّلُ ثُمَّ يَأْتِينَا رَبُّنَا بَعْدَ ذَلِكَ فَيَقُولُ مَنْ تَنْظُرُونَ فَيَقُولُونَ نَنْظُرُ رَبَّنَا . فَيَقُولُ أَنَا رَبُّكُمْ . فَيَقُولُونَ حَتَّى نَنْظُرَ إِلَيْكَ . فَيَتَجَلَّى لَهُمْ يَضْحَكُ - قَالَ - فَيَنْطَلِقُ بِهِمْ وَيَتَّبِعُونَهُ وَيُعْطَى كُلُّ إِنْسَانٍ مِنْهُمْ - مُنَافِقٍ أَوْ مُؤْمِنٍ - نُورًا ثُمَّ يَتَّبِعُونَهُ وَعَلَى جِسْرِ جَهَنَّمَ كَلاَلِيبُ وَحَسَكٌ تَأْخُذُ مَنْ شَاءَ اللَّهُ ثُمَّ يَطْفَأُ نُورُ الْمُنَافِقِينَ ثُمَّ يَنْجُو الْمُؤْمِنُونَ فَتَنْجُو أَوَّلُ زُمْرَةٍ وُجُوهُهُمْ كَالْقَمَرِ لَيْلَةَ الْبَدْرِ سَبْعُونَ أَلْفًا لاَ يُحَاسَبُونَ ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ كَأَضْوَإِ نَجْمٍ فِي السَّمَاءِ ثُمَّ كَذَلِكَ ثُمَّ تَحِلُّ الشَّفَاعَةُ وَيَشْفَعُونَ حَتَّى يَخْرُجَ مِنَ النَّارِ مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَكَانَ فِي قَلْبِهِ مِنَ الْخَيْرِ مَا يَزِنُ شَعِيرَةً فَيُجْعَلُونَ بِفِنَاءِ الْجَنَّةِ وَيَجْعَلُ أَهْلُ الْجَنَّةِ يَرُشُّونَ عَلَيْهِمُ الْمَاءَ حَتَّى يَنْبُتُوا نَبَاتَ الشَّىْءِ فِي السَّيْلِ وَيَذْهَبُ حُرَاقُهُ ثُمَّ يَسْأَلُ حَتَّى تُجْعَلَ لَهُ الدُّنْيَا وَعَشَرَةُ أَمْثَالِهَا مَعَهَا .
Amesimulia Jubayr (رضي الله عنه) kwamba amemsikia Jaabir Bin ‘Abdillaah (رضي الله عنهما) ambaye aliulizwa kuhusu (hali za) watu watakapofika (Siku ya Qiyaamah) akasema: Tutafika Siku ya Qiyaamah kama hivi, kama hivi, na tazama! Yaani tutakuwa sisi (pamoja na Rasuli) mahala paliponyanyuka juu zaidi kuliko watu wote. (Kisha msimuliaji) akasema: Kisha watu wataitwa na masanamu yao waliyokuwa wakiyaabudu, mmoja baada ya mwengine. Kisha Rabb wetu Atakuja Atasema: “Mnamngojea nani?” Watasema: Tunamngojea Rabb wetu. Allaah Atasema: “Mimi Rabb wenu!” Watasema: (Hatuna uhakika) hadi tukuone. Kisha Allaah Atajidhihirisha huku Akicheka. Kisha Ataondoka nao watamfuata, na kila mtu akiwa mnafiki au Muumini, atapewa nuru. Kisha watamfuata (Allaah) katika daraja la Jahannam, na juu ya daraja kutakuweko miiba na kulabu ambazo zitawanyakua wale Atakao Allaah. Kisha nuru ya wanafiki itazimwa. Kundi la kwanza la Waumini watakaookolewa, ni watu sabiini elfu ambao nyuso zao zitakuwa na nuru kama ya mwezi mpevu, na hawataitwa kuhesabiwa. Kisha watafuatia ambao nyuso zao zitakuwa kama nyota angavu mbinguni. Hivyo ndivyo (makundi yatakavyofuatana kundi moja baada ya jengine). Kisha itafika hatua ya Ash-shafaa’ah (uombezi), na watakaopewa idhini ya kuombeza wataombeza mpaka atolewe kila aliyekiri
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ
Laa ilaaha illa-Allaah (Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah)
huku akiwa moyoni mwake kuna kheri (imaan) kiasi cha uzani wa punje. Kisha watahudhurishwa katika uwanja wa Jannah, na watu wa Jannah watawanyunyizia maji hadi wachipuke kama mchipuko wa kitu katika maji ya mafuriko, na kuungua kwao kutatoweka. Watamuomba Rabb wao mpaka wapewe (neema) za dunia na mara kumi zaidi ya hayo. [Muslim]
[6] Aayah Imewateremkia Swahaba Baada Ya Miaka Minne Tokea Kusilimu Kwao:
حَدَّثَنِي يُونُسُ بْنُ عَبْدِ الأَعْلَى الصَّدَفِيُّ، أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ وَهْبٍ، أَخْبَرَنِي عَمْرُو، بْنُ الْحَارِثِ عَنْ سَعِيدِ بْنِ أَبِي هِلاَلٍ، عَنْ عَوْنِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّ ابْنَ مَسْعُودٍ، قَالَ مَا كَانَ بَيْنَ إِسْلاَمِنَا وَبَيْنَ أَنْ عَاتَبَنَا اللَّهُ بِهَذِهِ الآيَةِ { أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَنْ تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّهِ} إِلاَّ أَرْبَعُ سِنِينَ .
Amesimulia Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه): Kuanzia kusilimu kwetu na kuteremka Aayah hii ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Ametuonya ndani yake:
أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّـهِ
“Je, haujafika wakati kwa walioamini kwamba zinyenyekee nyoyo zao kwa kumdhukuru Allaah.”
Ilikuwa ni miaka minne.
[Muslim]
[8] Tofauti Ya Manabii, Swiddiqiyn, Shuhadaa Na Swalihina.
Rejea Al-Baqarah (2:130) (An-Nisaa (5:69).
[9] Dunia Ni Starehe Fupi Tu, Kuipa Mgongo Dunia, Na Maonyo Ya Kupendelea Dunia Badala Ya Aakhirah:
Aayah hii ni sawa na Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَاضْرِبْ لَهُم مَّثَلَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ فَأَصْبَحَ هَشِيمًا تَذْرُوهُ الرِّيَاحُ ۗ
“Na wapigie mfano wa uhai wa dunia. Ni kama maji Tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, ikachanganyika nayo mimea ya ardhi (ikasitawi), kisha ikawa mikavu iliyovurugika, inapeperushwa na upepo. [Al-Kahf (18:45)]
Na Aayah kadhaa nyenginezo zimebainisha kuhusu uhai wa dunia kuwa ni mfupi na wenye kutoweka, na kwamba starehe za dunia si za kudumu, na kuna maamrisho ya kuipa mgongo dunia, na kuna maonyo ya kupendelea dunia badala ya Aakhirah au maonyo ya kupendelea uhai wa dunia badala ya uhai wa Aakhirah. Miongoni mwazo ni Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿١٦﴾ وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ﴿١٧﴾
“Bali mnahiari zaidi uhai wa dunia. Na hali Aakhirah ni bora zaidi na ya kudumu zaidi.” [Al-A’laa (97:16-17)]
Rejea pia Aal-‘Imraan (3:14), (3:185), Al-An’aam (6:32), At-Tawbah (9:38), Yuwnus (10:24), Ar-Ra’d (13:26), Al-Qaswasw (28:60), Al-‘Ankabuwt (29:64), Luqmaan (31:33), Ash-Shuwraa (42:36), Muhammad (47:36).
Rejea pia Ash-Shuwraa (4:20) kwenye faida nyenginezo.
Na miongoni mwa Hadiyth ni hizi zifuatazo:
عن أنس رضي الله عنه : أن النبي صلى الله عليه وسلم، قَالَ: (( اللَّهُمَّ لاَ عَيْشَ إِلاَّ عَيْشَ الآخِرَةِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Ee Allaah! Hakuna maisha isipokuwa maisha ya Aakhirah [Al-Bukhaariy na Muslim]
عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((لَوْ كَانَتْ الدُّنْيَا تَعْدِلُ عِنْدَ اللَّهِ جَنَاحَ بَعُوضَةٍ مَا سَقَى كَافِرًا مِنْهَا شَرْبَةَ مَاءٍ)) رواه الترمذي وقال: حديث حسن صحيح
Amesimulia Sahl bin Sa'ad (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ingelikuwa (thamani ya) dunia ni sawasawa na bawa la mbu mbele ya Allaah, Asingelimnywesha kafiri hata tama moja la maji.” [At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyh]
Bonyeza pia viungo vifuatavyo kupata faida tele na rejea mbalimbali:
057-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Dunia Ni Jela Kwa Muumin, Kafiri Kwake Ni Kama Jannah [383]
058-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Ishi Duniani Kama Mgeni Au Mpita Njia [384]
059-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Kuipa Mgongo Dunia Kutampatia Mtu Mapenzi Ya Allaah Pamoja Na Ya Watu [385]
060-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Ingelikuwa Dunia Sawa Na Bawa La Mbu, Allaah Asingelimnywesha kafiri maji. [386]
061-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Dunia Ni Kama Kivuli Anachokitumia Msafiri Kwa Muda Tu [387]
[10] Kuomba Maghfirah Na Tawbah:
Bonyeza viungo vifuatavyo kwenye faida tele:
[11] Subira Katika Mitihani, Maafa Na Misiba:
Mitihani, maafa na misiba ya kila aina anayojaaliwa mtu, anapaswa awe na subra ambayo ina fadhila zake tele. Rejea Al-Baqarah (2:155)
Na bonyeza viungo vifuatavyo vyenye Hadiyth na makala kuhusu subira na fadhila zake:
[12] Kulipwa Thawabu Mara Mbili
حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، حَدَّثَنَا صَالِحُ بْنُ حَىٍّ أَبُو حَسَنٍ، قَالَ سَمِعْتُ الشَّعْبِيَّ، يَقُولُ حَدَّثَنِي أَبُو بُرْدَةَ، أَنَّهُ سَمِعَ أَبَاهُ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " ثَلاَثَةٌ يُؤْتَوْنَ أَجْرَهُمْ مَرَّتَيْنِ الرَّجُلُ تَكُونُ لَهُ الأَمَةُ فَيُعَلِّمُهَا فَيُحْسِنُ تَعْلِيمَهَا، وَيُؤَدِّبُهَا فَيُحْسِنُ أَدَبَهَا، ثُمَّ يُعْتِقُهَا فَيَتَزَوَّجُهَا، فَلَهُ أَجْرَانِ، وَمُؤْمِنُ أَهْلِ الْكِتَابِ الَّذِي كَانَ مُؤْمِنًا، ثُمَّ آمَنَ بِالنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَلَهُ أَجْرَانِ، وَالْعَبْدُ الَّذِي يُؤَدِّي حَقَّ اللَّهِ وَيَنْصَحُ لِسَيِّدِهِ ". ثُمَّ قَالَ الشَّعْبِيُّ وَأَعْطَيْتُكَهَا بِغَيْرِ شَىْءٍ وَقَدْ كَانَ الرَّجُلُ يَرْحَلُ فِي أَهْوَنَ مِنْهَا إِلَى الْمَدِينَةِ.
Amesimulia babake Abuu Burdah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Watu watatu watapewa ujira wao mara mbili: Mtu aliye na kijakazi, naye akamsomesha inavyotakiwa na akamfundisha adabu njema, kisha akamuacha huru na kumuoa. Mtu huyo atapata ujira mara mbili. Na Muumini miongoni mwa Ahlul-Kitaab, ambaye alikuwa Muumini, kisha akamuamini Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), naye atakuwa na ujira mara mbili. Na mtumwa anayetekeleza haki za Allaah na akawa na ikhlaasw kwa bwanake.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Jihaad]
الْمُجَادلَة
058-Al-Mujaadalah
058-Al-Mujaadalah: Utangulizi Wa Suwrah [392]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
قَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّتِي تُجَادِلُكَ فِي زَوْجِهَا وَتَشْتَكِي إِلَى اللَّـهِ وَاللَّـهُ يَسْمَعُ تَحَاوُرَكُمَا ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ بَصِيرٌ﴿١﴾
1. Allaah Amekwishasikia kauli ya yule mwanamke anayejadiliana nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mumewe, na anamshitakia Allaah, na Allaah Anayasikia majibizano yenu. Hakika Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.[1]
الَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِنكُم مِّن نِّسَائِهِم مَّا هُنَّ أُمَّهَاتِهِمْ ۖ إِنْ أُمَّهَاتُهُمْ إِلَّا اللَّائِي وَلَدْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَيَقُولُونَ مُنكَرًا مِّنَ الْقَوْلِ وَزُورًا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٌ﴿٢﴾
2. Wale miongoni mwenu wanaowatamkia wake zao dhwihaar,[2] hao wake zao si mama zao. Hawakuwa mama zao isipokuwa wale waliowazaa. Na hakika wao bila shaka wanasema yasiyokubalika na kauli ya kuchukiza na uongo. Na hakika Allaah bila shaka Ni Mwingi wa Kusamehe, Mwingi wa Kughufuria.
وَالَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِن نِّسَائِهِمْ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُوا فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مِّن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا ۚ ذَٰلِكُمْ تُوعَظُونَ بِهِ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ﴿٣﴾
3. Na wale wanaowatamkia wake zao dhwihaar, kisha wakarudi katika waliyoyasema (kuitengua dhwihaar), basi (adhabu yao) ni kuacha huru mtumwa kabla ya kugusana. Hayo mnawaidhiwa kwayo. Na Allaah kwa yale myatendayo Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ مِن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا ۖ فَمَن لَّمْ يَسْتَطِعْ فَإِطْعَامُ سِتِّينَ مِسْكِينًا ۚ ذَٰلِكَ لِتُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۚ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ ۗ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٤﴾
4. Na yule asiyepata (mtumwa au thamani yake) basi (afunge) Swiyaam miezi miwili mfululizo kabla ya kugusana. Na yule asiyeweza, basi alishe chakula masikini sitini. Hivyo ili mumuamini Allaah na Rasuli Wake. Na hiyo ni Mipaka ya Allaah. Na makafiri watapata adhabu iumizayo.
إِنَّ الَّذِينَ يُحَادُّونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ كُبِتُوا كَمَا كُبِتَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ وَقَدْ أَنزَلْنَا آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۚ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ مُّهِينٌ﴿٥﴾
5. Hakika wale wanaopinzana na Allaah na Rasuli Wake wamefedheheshwa kama walivyofedheheshwa wale wa kabla yao. Na Tumekwishateremsha Aayaat bayana, na makafiri watapata adhabu ya kudhalilisha.[3]
يَوْمَ يَبْعَثُهُمُ اللَّـهُ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا ۚ أَحْصَاهُ اللَّـهُ وَنَسُوهُ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ﴿٦﴾
6. Siku Atakayowafufua Allaah wote, Awajulishe yale waliyoyatenda. Allaah Ameyatia hesabuni barabara nao wameyasahau. Na Allaah Ni Shahidi juu ya kila kitu.
أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَىٰ ثَلَاثَةٍ إِلَّا هُوَ رَابِعُهُمْ وَلَا خَمْسَةٍ إِلَّا هُوَ سَادِسُهُمْ وَلَا أَدْنَىٰ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْثَرَ إِلَّا هُوَ مَعَهُمْ أَيْنَ مَا كَانُوا ۖ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴿٧﴾
7. Je, huoni kwamba Allaah Anajua yaliyomo mbinguni na yaliyomo ardhini? Hauwi mnong’ono wa watatu isipokuwa Yeye Ni wa Nne wao, na wala watano isipokuwa Yeye Ni wa Sita wao, na wala chini kuliko ya hivyo, na wala wengi zaidi isipokuwa Yeye Yu pamoja nao (kwa Ujuzi Wake)[4] popote watakapokuwa. Kisha Siku ya Qiyaamah Atawajulisha yale waliyoyatenda. Hakika Allaah kwa kila kitu Ni Mjuzi.
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ نُهُوا عَنِ النَّجْوَىٰ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا نُهُوا عَنْهُ وَيَتَنَاجَوْنَ بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَمَعْصِيَتِ الرَّسُولِ وَإِذَا جَاءُوكَ حَيَّوْكَ بِمَا لَمْ يُحَيِّكَ بِهِ اللَّـهُ وَيَقُولُونَ فِي أَنفُسِهِمْ لَوْلَا يُعَذِّبُنَا اللَّـهُ بِمَا نَقُولُ ۚ حَسْبُهُمْ جَهَنَّمُ يَصْلَوْنَهَا ۖ فَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿٨﴾
8. Je, huwaoni wale waliokatazwa kunong’ona, kisha wanarudia yale waliyokatazwa! Na wananong’onezana kuhusu dhambi na uadui na kumuasi Rasuli. Na wanapokujia wanakuamkia kwa maamkizi Asiyokuamkia kwayo Allaah, na wanasema katika nafsi zao: Mbona Allaah Hatuadhibu kwa yale tunayoyasema?! Jahannam inawatosheleza, wataingia waungue. Basi ubaya ulioje mahali pa kuishia![5]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَنَاجَيْتُمْ فَلَا تَتَنَاجَوْا بِالْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَمَعْصِيَتِ الرَّسُولِ وَتَنَاجَوْا بِالْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ﴿٩﴾
9. Enyi walioamini! Mnaponong’onezana, basi msinong’onezane kuhusu dhambi na uadui na kumuasi Rasuli, bali nong’onezaneni kuhusu wema na taqwa. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake Pekee mtakusanywa.
إِنَّمَا النَّجْوَىٰ مِنَ الشَّيْطَانِ لِيَحْزُنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَلَيْسَ بِضَارِّهِمْ شَيْئًا إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ﴿١٠﴾
10. Hakika mnong’ono unatokana na shaytwaan ili awahuzunishe wale walioamini, na wala hawezi kuwadhuru chochote isipokuwa kwa Idhini ya Allaah. Na kwa Allaah watawakali Waumini.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قِيلَ لَكُمْ تَفَسَّحُوا فِي الْمَجَالِسِ فَافْسَحُوا يَفْسَحِ اللَّـهُ لَكُمْ ۖ وَإِذَا قِيلَ انشُزُوا فَانشُزُوا يَرْفَعِ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ﴿١١﴾
11. Enyi walioamini! Mnapoambiwa: Fanyeni nafasi katika mabaraza, basi fanyeni nafasi, Allaah Atakufanyieni nafasi. Na mnapoambiwa: Inukeni, basi inukeni, Allaah Atawainua wale walioamini miongoni mwenu, na waliopewa ilimu wana daraja nyingi. Na Allaah kwa yale myatendayo Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نَاجَيْتُمُ الرَّسُولَ فَقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيْ نَجْوَاكُمْ صَدَقَةً ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ لَّكُمْ وَأَطْهَرُ ۚ فَإِن لَّمْ تَجِدُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٢﴾
12. Enyi walioamini! Mnapotaka kushauriana siri na Rasuli basi kadimisheni swadaqa kabla ya mnong’ono wenu. Hivyo ni kheri kwenu na utakaso zaidi. Na msipopata, basi hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[6]
أَأَشْفَقْتُمْ أَن تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيْ نَجْوَاكُمْ صَدَقَاتٍ ۚ فَإِذْ لَمْ تَفْعَلُوا وَتَابَ اللَّـهُ عَلَيْكُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴿١٣﴾
13. Je, mnakhofu (umasikini kwa) kukadimisha swadaqa kabla ya mnong’ono wenu? Ikiwa hamjafanya na Allaah Akapokea tawbah yenu, basi simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, na mtiini Allaah na Rasuli Wake. Na Allaah Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri kwa yale myatendayo.
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ تَوَلَّوْا قَوْمًا غَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مَّا هُم مِّنكُمْ وَلَا مِنْهُمْ وَيَحْلِفُونَ عَلَى الْكَذِبِ وَهُمْ يَعْلَمُونَ﴿١٤﴾
14. Je, hukuona wale waliofanya urafiki na watu ambao Allaah Ameghadhibika nao? Wao si miongoni mwenu na wala si miongoni mwao, na wanaapia uongo nao wanajua.[7]
أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿١٥﴾
15. Allaah Amewaandalia adhabu kali. Ni uovu mbaya kwa hakika wa waliyokuwa wakiyatenda.
اتَّخَذُوا أَيْمَانَهُمْ جُنَّةً فَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ فَلَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ﴿١٦﴾
16. Wamevifanya viapo vyao kuwa ni kinga na hivyo wakazuia Njia ya Allaah. Basi watapata adhabu idhalilishayo.
لَّن تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۚ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿١٧﴾
17. Hazitowafaa kitu chochote mali zao wala watoto wao mbele ya Allaah.[8] Hao ni watu wa motoni, wao humo watadumu.
يَوْمَ يَبْعَثُهُمُ اللَّـهُ جَمِيعًا فَيَحْلِفُونَ لَهُ كَمَا يَحْلِفُونَ لَكُمْ ۖ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ عَلَىٰ شَيْءٍ ۚ أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْكَاذِبُونَ﴿١٨﴾
18. Siku Atakayowafufua Allaah wote, watamwapia kama wanavyokuapieni nyinyi, na watadhania kwamba wameegemea kitu (cha kuwafaa). Tanabahi! Hakika wao ni waongo.
اسْتَحْوَذَ عَلَيْهِمُ الشَّيْطَانُ فَأَنسَاهُمْ ذِكْرَ اللَّـهِ ۚ أُولَـٰئِكَ حِزْبُ الشَّيْطَانِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ الشَّيْطَانِ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿١٩﴾
19. Shaytwaan amewatawala, akawasahaulisha kumdhukuru Allaah. Hao ndio kundi la shaytwaan. Tanabahi! Hakika kundi la shaytwaan ndio lenye kukhasirika.
إِنَّ الَّذِينَ يُحَادُّونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ أُولَـٰئِكَ فِي الْأَذَلِّينَ﴿٢٠﴾
20. Hakika wale wanaopinzana na Allaah na Rasuli Wake, hao ndio katika waliodhalilishwa.
كَتَبَ اللَّـهُ لَأَغْلِبَنَّ أَنَا وَرُسُلِي ۚ إِنَّ اللَّـهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ﴿٢١﴾
21. Allaah Amekwishaandika kwamba: Bila shaka Nitashinda Mimi na Rusuli Wangu. Hakika Allaah Ni Mwenye nguvu zote, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika.
لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ ۖ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ رَضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ أُولَـٰئِكَ حِزْبُ اللَّـهِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿٢٢﴾
22. Hutokuta watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho kuwa wanafanya urafiki na kuwapenda wanaompinga Allaah na Rasuli Wake, japo wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao (Allaah) Amewaandikia katika nyoyo zao imaan, na Akawatia nguvu kwa Ruwh[9] (Wahyi) kutoka Kwake, na Atawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito wadumu humo. Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Hao ndio Kundi la Allaah. Tanabahi! Hakika Kundi la Allaah ndio lenye kufaulu.[10]
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
[2] (ظِهَارُ) Dhwihaar:
“Dhwihaar” (ظِهَارُ)imetokana na neno “dhwahr”(ظَهْرُ) ; kwa maana ya mgongo au nyuma. Ni kumfananisha mke wa mtu na mgongo wa mama yake. Aina hii ya mazungumzo katika lugha ya kiarabu ina maana ya kuwa: “Wewe ni kama mama yangu, na ni haraam kwa ndoa yangu, au kukuoa au kukuingilia.” Kulingana na istilahi za kisharia, “dhwihaar” ni kumfananisha mke wa mtu na mama wa mtu na hivyo kumfanya kuwa ni haraam kwake. Jambo hili kisharia halizingatiwi kuwa ni talaka, lakini ni lazima mtu atoe kafara kabla ya kumrudia mke wake. Kafara yake ni kumuacha huru mtu mtumwa, au kufunga Swiyaam siku sitini kwa mfululizo, au kuwalisha maskini sitini. Hukumu hii imetajwa katika Suwrah Al-Mujaadalah (58:3-4). Ni wajibu kutekeleza moja ya adhabu hizo. Bonyeza viungo vifuatavyo kwa faida nyenginezo:
09-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa Al-Iylaa, Dhwihaar, Kafaara [394]
[3] Aina Za Adhabu Katika Qur-aan:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja aina mbalimbali za adhabu katika Qur-aan na kila moja ina sifa yake. Miongoni mwazo ni hizi zifuatazo pamoja na baadhi ya rejea zake:
عذاب عظيم Adhabu kuu kabisa. Rejea An-Nuwr (24:14).
عذاب كبير Adhabu kubwa. Rejea Al-Furqaan (25:19)
عذاب اليمAdhabu ya kuumiza. Rejea Al-Maaidah (5:36).
عذاب مهين Adhabu ya kudhalilisha. Rejea Luqmaan (31:6).
عذاب مقيم Adhabu ya kudumu. Rejea Az-Zumar (39:40).
عذاب غليظ Adhabu ngumu. Rejea Fusw-Swilat (41:50).
عذاب شديد Adhabu kali. Rejea Sabaa (34:46).
عذاب الحريق Adhabu ya kuunguza. Rejea Al-Buruwj (85:10).
عذاب النار Adhabu ya moto. Rejea Al-Anfaal (8:14).
عذاب الخزي Adhabu ya hizaya. Rejea Yuwnus (10:98).
عذاب السعير Adhabu ya moto uliowashwa vikali mno. Rejea Al-Mulk (67:5).
عذاب الخلد Adhabu ya kudumu milele. Rejea As-Sajdah (32:14).
عذاب واصب Adhabu ya kuendelea. Rejea Asw-Swaaffaat (37:9).
عذاب النكر Adhabu kali kabisa ya kukirihisha, isiyovumilika. Rejea Al-Kahf (18:87).
عذاب حميم Adhabu ya maji yachemkayo mno. Rejea Ad-Dukhaan (44:48).
عذاب السموم Adhabu ya moto unaobabua. Rejea Atw-Twuur (52:27).
عذاب مستقر Adhabu ya kuendelea. Rejea Al-Qamar (54:38).
Rejea Al-Hashr (59:4) kwenye faida kuhusu tofauti ya adhabu na ikabu:
[4] Allaah (سبحانه وتعالى) Huwa Yuko Pamoja Na Viumbe Vyake Kwa Ujuzi Wake.
Allaah (سبحانه وتعالى) Anapotaja kuwa Yuko pamoja na Viumbe Vyake basi inamaanisha kwamba Yuko pamoja nao kwa Ujuzi Wake. Bali Yeye Amethibitisha kuwa Yuko mbinguni kwa Dhati Yake. Na hii ni ‘Aqiydah ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah. Rejea Al-Mulk (67:16), Al-A’raaf (7:54).
Ilokusudiwa ya kuwa huko ni kuwa Yeye Yu pamoja nao kwa Ilimu Yake ambayo inajumlisha yale wanayoyazungmza kwa siri na kuyaficha. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Bonyeza kiungo kifuatacho chenye maelezo ziada ya bayana:
Allaah Yuko Wapi? [395]
[6] An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa):
Hukmu ya Aayah hii namba (12) imefutwa na badala yake ni Aayah inayofuatia namba (13). Rejea Al-Baqarah (2:106). Na bonyeza pia kiungo kifuatacho:
An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa) [23]
[7] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
058-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Mujaadalah Aayah 14: وَيَحْلِفُونَ عَلَى الْكَذِبِ وَهُمْ يَعْلَمُونَ [397]
[10] Al-Walaa Wal-Baraa (Kupenda Na Kuandamana, Kuchukia Na Kutengana Kwa Ajili Ya Allaah):
Waumini wanapaswa kufanya urafiki na Waumini wenzao hata kama hawana uhusiano wa damu nao. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ اللَّـهُ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴿٧١﴾
“Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki wandani. Wanaamrisha mema na wanakataza munkari[10] na wanasimamisha Swalaah na wanatoa Zakaah na wanamtii Allaah na Rasuli Wake. Hao Allaah Atawarehemu. Hakika Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.” [At-Tawbah (9:71)]
Na pindi ndugu na jamaa wenye uhusiano wa damu wakiwa ni wenye kumpinga Allaah (سبحانه وتعالى) na Rasuli wake (صلى الله عليه وآله وسلم), basi wanapaswa kutengana nao katika mipaka ya sharia ya Dini. Rejea Al-Hujuraat (49:10) kwenye mfano wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kutengana na jamaa zake, na pia Swahaba kutengana na mzazi wake. Na hi indio inajulikana kwa Al-Walaa Wal-Baraa kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
عَنِ الْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ، عن النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قال: إِنَّ أَوْثَقَ عُرَى الْإِيمَانِ: أَنْ تُحِبَّ فِي اللهِ، وَتُبْغِضَ فِي اللهِ .
رواه أحمد والطبراني والحاكم والبزار، وحسنه الألباني في "صحيح الترغيب” (3030) .
Amesimulia Al-Baraa Bin ‘Aazib (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Shikizo thabiti kabisa la imaan ni upende kwa ajili ya Allaah na uchukie kwa ajili ya Allaah.” [Ahmad, Atw-Twabaraaniy, Al-Haakim na ameipa daraja ya Hasan Imaam Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb (3030)]
Na Hadiyth nyenginezo zenye mafundisho hayo:
عَنْ أَبِي أُمَامَةَ ، قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ((مَنْ أَحَبَّ فِي اللَّهِ وَأَبْغَضَ فِي اللَّهِ وَأَعْطَى لِلَّهِ وَمَنَعَ لِلَّهِ فَقَدِ اسْتَكْمَلَ الإِيمَانَ))
Amesimulia Abuu Umaamah (رضي الله عنه): “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayependa kwa ajili ya Allaah, akachukia kwa ajili ya Allaah, akatoa kwa ajili ya Allaah, na akazuia kwa ajili ya Allaah, basi atakuwa amekamilisha imaan.” [Abuu Daawuwd na ameisahihisha Al-Albaaniy (4681)]
عَنْ أَنَسٍ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((لاَ يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَلَدِهِ وَوَالِدِهِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ)) أَخْرَجَاهُ
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mmoja wenu hawi Muumini mpaka anipende mimi kuliko watoto wake na baba yake na watu wote.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((ثَلاَثٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ وَجَدَ حَلاَوَةَ الإِيمَانِ: أَنْ يَكُونَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِمَّا سِوَاهُمَا، وَأَنْ يُحِبَّ الْمَرْءَ لاَ يُحِبُّهُ إِلاَّ لِلَّهِ, وَأَنْ يَكْرَهَ أَنْ يَعُودَ فِي الْكُفْرِ كَمَا يَكْرَهُ أَنْ يُقْذَفَ فِي النَّارِ)) متفق عليه
Amesimulia Anas bin Maalik (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mambo matatu atakayekuwa nayo, atapata utamu wa imaan: Allaah na Rasuli Wake wawe vipenzi zaidi kwake kuliko wengineo, ampende mtu na wala asimpende isipokuwa kwa ajili ya Allaah, na achukie kurudi katika ukafiri baada ya Allaah kumwokoa kutoka huko kama anavyochukia kuingizwa motoni. [Al-Bukhaariy na Muslim]
Bonyeza pia viungo vifuatavyo kupata faida ziyada:
الْحَشْر
059- Al-Hashr
059-Al-Hashr: Utangulizi Wa Suwrah [402]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿١﴾
1. Vimemsabihi Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi[1], Naye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.[2]
هُوَ الَّذِي أَخْرَجَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مِن دِيَارِهِمْ لِأَوَّلِ الْحَشْرِ ۚ مَا ظَنَنتُمْ أَن يَخْرُجُوا ۖ وَظَنُّوا أَنَّهُم مَّانِعَتُهُمْ حُصُونُهُم مِّنَ اللَّـهِ فَأَتَاهُمُ اللَّـهُ مِنْ حَيْثُ لَمْ يَحْتَسِبُوا ۖ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ الرُّعْبَ ۚ يُخْرِبُونَ بُيُوتَهُم بِأَيْدِيهِمْ وَأَيْدِي الْمُؤْمِنِينَ فَاعْتَبِرُوا يَا أُولِي الْأَبْصَارِ﴿٢﴾
2. Yeye Ndiye Aliyewatoa wale waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu kutoka majumbani mwao katika mkusanyiko wa kwanza. Hamkudhania kwamba watatoka, nao wakadhani kwamba husuni zao zitawakinga dhidi ya Allaah. Lakini Hukmu ya Allaah ikawafikia kutoka ambako wasipotazamia, na Akavurumisha kiwewe katika nyoyo zao. Wanaziharibu nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya Waumini. Basi pateni funzo enyi wenye uoni wa kutia akilini.
وَلَوْلَا أَن كَتَبَ اللَّـهُ عَلَيْهِمُ الْجَلَاءَ لَعَذَّبَهُمْ فِي الدُّنْيَا ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابُ النَّارِ﴿٣﴾
3. Na lau kama Allaah Asingeliwaandikia kufukuzwa na uhamisho, Angeliwaadhibu duniani, na Aakhirah watapata adhabu ya moto.
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ شَاقُّوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۖ وَمَن يُشَاقِّ اللَّـهَ فَإِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴿٤﴾
4. Hayo ni kwa kuwa wao wamempinga Allaah na Rasuli Wake. Na yeyote anayempinga Allaah, basi hakika Allaah Ni Mkali wa Kuakibu.[3]
مَا قَطَعْتُم مِّن لِّينَةٍ أَوْ تَرَكْتُمُوهَا قَائِمَةً عَلَىٰ أُصُولِهَا فَبِإِذْنِ اللَّـهِ وَلِيُخْزِيَ الْفَاسِقِينَ﴿٥﴾
5. Hamkukata aina yoyote ya mtende au mliouacha umesimama juu ya mashina yake, basi ni kwa Idhini ya Allaah, na ili Awahizi mafasiki.[4]
وَمَا أَفَاءَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ مِنْهُمْ فَمَا أَوْجَفْتُمْ عَلَيْهِ مِنْ خَيْلٍ وَلَا رِكَابٍ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يُسَلِّطُ رُسُلَهُ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٦﴾
6. Na ngawira ya bila jasho[5] Aliyoitoa Allaah kwa Rasuli Wake kutoka kwao, basi hamkuiendea mbio kwa farasi wala kwa ngamia, lakini Allaah Huwapa mamlaka na nguvu Rusuli Wake dhidi ya Amtakaye. Na Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.
مَّا أَفَاءَ اللَّـهُ عَلَىٰ رَسُولِهِ مِنْ أَهْلِ الْقُرَىٰ فَلِلَّـهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاءِ مِنكُمْ ۚ وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴿٧﴾
7. Ngawira ya bila jasho Aliyoitoa Allaah kwa Rasuli Wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji ni kwa ajili ya Allaah na Rasuli, na kwa ajili ya jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na msafiri aliyeharibikiwa, ili isiwe mzunguko wa zamu baina ya matajiri tu miongoni mwenu. Na lolote analokupeni Rasuli ((صلى الله عليه وآله وسلم basi lichukueni, na analokukatazeni, basi jiepusheni.[6] Na mcheni Allaah. Hakika Allaah Ni Mkali wa Kuakibu.
لِلْفُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأَمْوَالِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا وَيَنصُرُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ﴿٨﴾
8. Wapatiwe (pia) mafuqara Muhaajiruna[7] ambao wametolewa kutoka majumbani mwao na mali zao, wanatafuta fadhila na radhi kutoka kwa Allaah, na wananusuru (Dini ya) Allaah na Rasuli Wake. Hao ndio wakweli.
وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿٩﴾
9. Na wale waliokuwa na masikani (Madiynah) na wakawa na iymaan kabla yao, wanawapenda wale waliohajiri kwao, na wala hawahisi choyo yoyote vifuani mwao kwa yale waliyopewa (Muhaajiruna), na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wanahitaji. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.[8]
وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ﴿١٠﴾
10. Na wale waliokuja baada yao wanasema: Rabb wetu! Tughufurie pamoja na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa imaan[9], na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo ya chuki kwa wale walioamini. Rabb wetu! Hakika Wewe Ni Mwenye Huruma mno, Mwenye Kurehemu.
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ نَافَقُوا يَقُولُونَ لِإِخْوَانِهِمُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَئِنْ أُخْرِجْتُمْ لَنَخْرُجَنَّ مَعَكُمْ وَلَا نُطِيعُ فِيكُمْ أَحَدًا أَبَدًا وَإِن قُوتِلْتُمْ لَنَنصُرَنَّكُمْ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ﴿١١﴾
11. Je, huoni wale waliouvaa unafiki, wanawaambia ndugu zao waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu: Mkitolewa bila shaka nasi tutatoka pamoja nanyi, na wala hatutomtii yeyote abadani dhidi yenu. Na mkipigwa vita, bila shaka tutakunusuruni. Na Allaah Anashuhudia kwamba wao kwa hakika ni waongo.
لَئِنْ أُخْرِجُوا لَا يَخْرُجُونَ مَعَهُمْ وَلَئِن قُوتِلُوا لَا يَنصُرُونَهُمْ وَلَئِن نَّصَرُوهُمْ لَيُوَلُّنَّ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنصَرُونَ﴿١٢﴾
12. Wakitolewa, hawatotoka pamoja nao, na wakipigwa vita, hawatowasaidia, na hata wakiwasaidia, bila shaka watageuzia mbali migongo (wakimbie), kisha hawatonusuriwa.
لَأَنتُمْ أَشَدُّ رَهْبَةً فِي صُدُورِهِم مِّنَ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ﴿١٣﴾
13. Hakika nyinyi (Waumini) ni tisho zaidi katika vifua vyao kuliko Allaah. Hayo ni kwa sababu wao ni watu wasiofahamu.
لَا يُقَاتِلُونَكُمْ جَمِيعًا إِلَّا فِي قُرًى مُّحَصَّنَةٍ أَوْ مِن وَرَاءِ جُدُرٍ ۚ بَأْسُهُم بَيْنَهُمْ شَدِيدٌ ۚ تَحْسَبُهُمْ جَمِيعًا وَقُلُوبُهُمْ شَتَّىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ﴿١٤﴾
14. Hawatopigana nanyi wote pamoja isipokuwa katika miji iliyozatitiwa kwa husuni au kutoka nyuma ya kuta. Uadui wao baina yao ni mkali. Utawadhania wameungana pamoja, kumbe nyoyo zao zimetengana. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasiotia akilini.
كَمَثَلِ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ قَرِيبًا ۖ ذَاقُوا وَبَالَ أَمْرِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١٥﴾
15. Ni kama mfano wa wale walio kabla yao hivi karibuni tu. Walionja matokeo ya uovu wa mambo yao, na watapata adhabu iumizayo.
كَمَثَلِ الشَّيْطَانِ إِذْ قَالَ لِلْإِنسَانِ اكْفُرْ فَلَمَّا كَفَرَ قَالَ إِنِّي بَرِيءٌ مِّنكَ إِنِّي أَخَافُ اللَّـهَ رَبَّ الْعَالَمِينَ﴿١٦﴾
16. (Wanafiki ni) kama mfano wa shaytwaan alipomwambia binaadamu: Kufuru! Alipokufuru, (shaytwaan) alisema: Hakika mimi sihusiki nawe! Mimi namkhofu Allaah Rabb wa walimwengu.[10]
فَكَانَ عَاقِبَتَهُمَا أَنَّهُمَا فِي النَّارِ خَالِدَيْنِ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَاءُ الظَّالِمِينَ﴿١٧﴾
17. Basi hatima yao wote wawili ikawa kwamba wao wawili watakuwa motoni wadumu wote humo. Na hiyo ndio jazaa ya madhalimu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَلْتَنظُرْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ لِغَدٍ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴿١٨﴾
18. Enyi walioamini! Mcheni Allaah, na nafsi itazame imetanguliza nini kwa ajili ya kesho, na mcheni Allaah. Hakika Allaah Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri kwa yale myatendayo.
وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ نَسُوا اللَّـهَ فَأَنسَاهُمْ أَنفُسَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ﴿١٩﴾
19. Na wala msiwe kama wale waliomsahau Allaah, Naye (Allaah) Akawasahaulisha nafsi zao. Hao ndio mafasiki.
لَا يَسْتَوِي أَصْحَابُ النَّارِ وَأَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۚ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ هُمُ الْفَائِزُونَ﴿٢٠﴾
20. Hawalingani sawa watu wa motoni na watu wa Jannah, watu wa Jannah ndio wenye kufuzu.[11]
لَوْ أَنزَلْنَا هَـٰذَا الْقُرْآنَ عَلَىٰ جَبَلٍ لَّرَأَيْتَهُ خَاشِعًا مُّتَصَدِّعًا مِّنْ خَشْيَةِ اللَّـهِ ۚ وَتِلْكَ الْأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٢١﴾
21. Lau Tungeliiteremsha hii Qur-aan juu ya mlima, ungeliuona unanyenyekea ukipasukapasuka kutokana na khofu ya Allaah.[12] Na hiyo ni mifano Tunawapigia watu ili wapate kutafakari.
هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۖ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ﴿٢٢﴾
22. Yeye Ni Allaah, Ambaye hakuna muabudiwa wa haki ila Yeye. Mjuzi wa ya ghaibu na ya dhahiri, Yeye Ndiye Ar-Rahmaan, Mwenye Kurehemu.[13]
هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٢٣﴾
23. Yeye Ndiye Allaah Ambaye hakuna muabudiwa wa haki ila Yeye, Mfalme, Mtakatifu Ametakasika na sifa zote hasi, Mwenye Kusalimisha na Amesalimika na kasoro zote, Mwenye Kusadikisha ahadi na Kuaminisha, Mwenye Kudhibiti Kushuhudia Kuchunga na Kuhifadhi, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Jabari Asiyeshindwa kufanya Atakalo, Mwenye Ukubwa na Uadhama, Utakasifu ni wa Allaah kutokana na ambayo wanamshirikisha.
هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٢٤﴾
24. Yeye Ndiye Allaah, Muumbaji, Mwanzishi wa viumbe bila kasoro, Muundaji sura na umbile, Ana Majina Mazuri kabisa.[14] Kinamsabihi Pekee kila kilichoko katika mbingu na ardhi, Naye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
[1] Kila Kitu Kinamsabbih Allaah (عزّ وجلّ):
Rejea Al-Hashr (57:1) kwenye rejea zinazotaja viumbe na vitu Alivyoviumba Allaah kuwa vinamsabbih Yeye Allaah (عزّ وجلّ).
[2] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Kuanzia Aayah hii hadi namba (4) kuna sababu ya kuteremshwa. Bonyeza kiungo kifuatacho:
059-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Hashr Aayah 01-04 سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ [403]
[3] Tofauti Ya Adhabu Na Ikabu:
Maneno mawili hayo yametumika sana katika Qur-aan, lakini yanatofautiana kwa kiasi fulani.
Ikabu ni malipo ya adhabu anayostahiki mtenda dhambi kwa kitendo chake cha kuasi.
Ama adhabu ni maumivu yenye kuendelea au yasiyoendelea ambayo yanamhusu mtu anapotenda dhambi hivyo akawa amestahiki adhabu. Au ni adhabu kwa asiyetenda dhambi kwa maana asiyestahiki. Mfano wa asiyestahiki ni mtu kuwa katika mateso au mitihani bila ya kuwa ametenda dhambi, mathalan mitihani ya maradhi akawa mtu anapata maumivu ya kuendelea, hivyo inasemwa anaadhibika. Na adhabu ni ya jumla zaidi. Ama ikabu ni makhsusi kwa mtenda dhambi.
Rejea Al-Mujaadalah (58:5) kwenye aina za adhabu.
[5] Al-Fay-u: Ngawira Inayopatikana Bila Ya Kupigana Vita:
Al-Fay-u ni ngawira ambayo ni mali wanayoipata Waislamu kutoka kwa makafiri bila ya kupigana vita. Na imetajwa katika Suwrah hii, Al-Hashr (59:6-7). Ama ngawira ambayo inapatikana baada ya kupigana vita inaitwa “ghanima.” Rejea Al-Anfaal (8:41).
[6] Kutii Amri Ya Allaah Na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) Na Kujiepusha Na Makatazo Yao, Na Laana Ya Allaah Kwa Wenye Kuchanja, Wenye Kutoa Nyusi, Wenye Kuchonga Meno, Wenye Kubadilisha Umbile La Allaah:
Hadiyth zifuatazo zinataja hayo:
عَنْ عَلْقَمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، لَعَنَ اللَّهُ الْوَاشِمَاتِ، وَالْمُسْتَوْشِمَاتِ، وَالْمُتَنَمِّصَاتِ وَالْمُتَفَلِّجَاتِ لِلْحُسْنِ، الْمُغَيِّرَاتِ خَلْقَ اللَّهِ تَعَالَى، مَالِي لاَ أَلْعَنُ مَنْ لَعَنَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم وَهْوَ فِي كِتَابِ اللَّهِ وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ .
Amesimulia ‘Alqamah (رضي الله عنه): Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) amesema: Allaah Amewalaani wenye kuchanja, na wenye kuchanjwa, na wenye kunyoa nyusi, na wenye kuchonga meno kwa urembo, na wenye kubadilisha umbile la Allaah (سبحانه وتعالى). Kwa nini nisimlaani yule aliyelaaniwa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na aliyelaaniwa katika Kitabu cha Allaah?:
وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴿٧﴾
“Na lolote analokupeni Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) basi lichukueni, na analokukatazeni, basi jiepusheni.” [Al-Hashr (59:7) Hadiyth amepokea Imaam Al-Bukhaariy Kitabu Cha Mavazi (77)]
Na pia:
عن أسماءَ رضي الله عنها : أنَّ امْرَأَةً سَأَلَتِ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَتْ : يا رسولَ اللهِ إنَّ ابْنَتِي أصَابَتْهَا الحَصْبَةُ ، فَتَمَرَّقَ شَعْرُهَا ، وإنّي زَوَّجْتُهَا ، أفَأَصِلُ فِيهِ ؟ فقالَ : ()لَعَنَ اللهُ الوَاصِلَةَ وَالمَوْصُولَةَ)) . متفق عليه .
وفي روايةٍ : ((الوَاصِلَةَ، والمُسْتوْصِلَةَ)) .
Amesimulia Asmaa (رضي الله عنها) kwamba mwanamke fulani alimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ee Rasuli wa Allaah! Binti yangu amepatwa na surua zikapuputika nywele zake, nami nimemuozesha; Je, niziunganishe? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamjibu: "Allaah Amemlaani mwenye kuunganisha nywele zake (au nywele za mwengine kwa nywele nyengine) na mwenye kuungwa (au kuvaa nywele hizo)." [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaaiy]
Na katika riwaayah nyengine: "Mwenye kuunganisha nywele na mwenye kumtaka mwengine amfanyie kazi hiyo (mwenye kutamani kuzivaa nywele hizo za bandia)."
[7] Muhaajiruna:
Muhaajiruna ni wale waliohamia kutoka Makkah kwenda Madiynah. Ama Answaar, hawa ni watu wa Madiynah.
[8] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
Humo, mna kisa cha kusisimua ngozi kuhusu familia ya Answaar waliojinyima chakula na badala yake kuwapendelea wageni wale, ilhali wao wenyewe walikihitajia chakula hicho.
[9] Waliotangulia Kwa Imaan:
Ni sawa na Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١٠٠﴾
Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhaajiruwn na Answaar na wale waliowafuata kwa ihsaan, Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Na Amewaandalia Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo abadi. Huko ndiko kufuzu kukubwa kabisa. [At-Tawbah (9:100)]
[10] Shaytwaan Huwapotosha Watu Kisha Huwakanusha Na Kuwageuka!:
Rejea Suwrah Ibraahiym (14:22) kwenye maelezo, faida na rejea mbalimbali.
[11] Hawalingani Sawa Watu Wa Motoni Na Wa Peponi:
Rejea Al-Jaathiyah (45:21) kwenye faida na rejea mbalimbali.
[12] Vitu Alivyoviumba Allaah Vinashtuka Kwa Kumkhofu Allaah (عزّ وجلّ):
Rejea Suwrah Maryam (19:90), Ash-Shuwraa (42:5) kwenye faida.
[14] Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah (سبحانه وتعالى):
Rejea Faharasa ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake.
الْمُمْتَحِنَة
060-Al-Mumtahinah
060-Al-Mumtahinah: Utangulizi Wa Suwrah [407]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُم مِّنَ الْحَقِّ يُخْرِجُونَ الرَّسُولَ وَإِيَّاكُمْ ۙ أَن تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ رَبِّكُمْ إِن كُنتُمْ خَرَجْتُمْ جِهَادًا فِي سَبِيلِي وَابْتِغَاءَ مَرْضَاتِي ۚ تُسِرُّونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَأَنَا أَعْلَمُ بِمَا أَخْفَيْتُمْ وَمَا أَعْلَنتُمْ ۚ وَمَن يَفْعَلْهُ مِنكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاءَ السَّبِيلِ﴿١﴾
1. Enyi walioamini! Msifanye adui Wangu na adui wenu kuwa marafiki walinzi mkiwapa mapenzi, na hali wamekwishakufuru yaliyokujieni ya haki, wanamfukuza Rasuli pamoja nanyi kwa sababu mmemuamini Allaah Rabb wenu. Mnapotoka kwa ajili ya Jihaad katika Njia Yangu na kutafuta Radhi Zangu mnawapa siri kwa mapenzi, na hali Mimi Najua zaidi yale mnayoyaficha na yale mnayoyadhihirisha. Na yeyote atakayefanya hivyo miongoni mwenu, basi kwa yakini amepotea njia ya sawa.[1]
إِن يَثْقَفُوكُمْ يَكُونُوا لَكُمْ أَعْدَاءً وَيَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ وَأَلْسِنَتَهُم بِالسُّوءِ وَوَدُّوا لَوْ تَكْفُرُونَ﴿٢﴾
2. Wakikushindeni watakuwa ni maadui kwenu, na watakunyosheeni mikono yao na ndimi zao kwa uovu, na watatamani lau mngekufuru.
لَن تَنفَعَكُمْ أَرْحَامُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ ۚ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يَفْصِلُ بَيْنَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ﴿٣﴾
3. Hawatokufaeni jamaa zenu wa uhusiano wa damu wala watoto wenu Siku ya Qiyaamah (Allaah) Atapambanua baina yenu. Na Allaah kwa yale myatendayo Ni Mwenye Kuona.[2]
قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَءَآؤُاْ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ إِلَّا قَوْلَ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ وَمَا أَمْلِكُ لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ ۖ رَّبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ﴿٤﴾
4. Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Ibraahiym na wale walio pamoja naye, walipowaambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah, tunakukanusheni, na umedhihirika baina yetu na baina yenu uadui na bughudha ya kudumu milele mpaka mumuamini Allaah Pekee. Isipokuwa kauli ya Ibraahiym kwa baba yake: Nitakuombea kwa hakika maghfirah[3], na wala sikumilikii chochote kile mbele ya Allaah. Rabb wetu! Tumetawakali Kwako, na Kwako Tunarudia kutubia, na Kwako ni mahali pa kuishia.[4]
رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا وَاغْفِرْ لَنَا رَبَّنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٥﴾
5. Rabb wetu! Usitujaalie kuwa mtihani kwa wale waliokufuru, na Tughufurie Rabb wetu. Hakika Wewe Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِيهِمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ ۚ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ﴿٦﴾
6. Kwa yakini imekuwa kwenu kigezo kizuri katika mwenendo wao kwa mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho. Na yeyote atakayekengeuka, basi hakika Allaah Ndiye Mkwasi, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.
عَسَى اللَّـهُ أَن يَجْعَلَ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ الَّذِينَ عَادَيْتُم مِّنْهُم مَّوَدَّةً ۚ وَاللَّـهُ قَدِيرٌ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٧﴾
7. Asaa Allaah Akajaalia mapenzi baina yenu na baina ya wale mlio na uadui nao. Na Allaah Ni Muweza wa yote, na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
لَّا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ أَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ﴿٨﴾
8. Allaah Hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale wasiokupigeni vita katika Dini, na wala hawakukutoeni kutoka majumbani mwenu. Hakika Allaah Anapenda wafanyao uadilifu.[5]
إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَىٰ إِخْرَاجِكُمْ أَن تَوَلَّوْهُمْ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿٩﴾
9. Hakika Allaah Anakukatazeni tu kuhusu wale waliokupigeni vita katika Dini, na wakakutoeni kutoka majumbani mwenu, na wakasaidiana juu ya kukutoeni ndio msifanye urafiki nao. Na yeyote atakayewafanya marafiki, basi hao ndio madhalimu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا جَاءَكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ فَامْتَحِنُوهُنَّ ۖ اللَّـهُ أَعْلَمُ بِإِيمَانِهِنَّ ۖ فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ ۖ وَآتُوهُم مَّا أَنفَقُوا ۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ أَن تَنكِحُوهُنَّ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ ۚ وَلَا تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ وَاسْأَلُوا مَا أَنفَقْتُمْ وَلْيَسْأَلُوا مَا أَنفَقُوا ۚ ذَٰلِكُمْ حُكْمُ اللَّـهِ ۖ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴿١٠﴾
10. Enyi walioamini! Wanapokujieni Waumini wa kike waliohajiri basi wajaribuni. Allaah Ni Mjuzi zaidi wa iymaan zao. Kisha mkiwatambua kuwa ni Waumini basi msiwarejeshe kwa makafiri. Wao si wake halaal kwao, na wala wao waume hawahalaliki kwao. Na wapeni (makafiri mahari) waliyotoa. Na wala si dhambi kufunga nao nikaah mkiwapa mahari yao. Na wala msiwaweke wanawake makafiri katika fungamano la ndoa. Na takeni mlichotoa (katika mahari), nao watake walichotoa. Hiyo ndio Hukumu ya Allaah, Anahukumu baina yenu. Na Allaah Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.[6]
وَإِن فَاتَكُمْ شَيْءٌ مِّنْ أَزْوَاجِكُمْ إِلَى الْكُفَّارِ فَعَاقَبْتُمْ فَآتُوا الَّذِينَ ذَهَبَتْ أَزْوَاجُهُم مِّثْلَ مَا أَنفَقُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي أَنتُم بِهِ مُؤْمِنُونَ﴿١١﴾
11. Na kama akikutorokeni yeyote kati ya wake zenu kurejea kwa makafiri kisha ikatokea kuwa mmelipiza mkashinda na kupata ngawira, basi wapeni wale walioondokewa na wake zao mfano wa walichotoa (mahari), na mcheni Allaah Ambaye nyinyi mnamuamini.
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا جَاءَكَ الْمُؤْمِنَاتُ يُبَايِعْنَكَ عَلَىٰ أَن لَّا يُشْرِكْنَ بِاللَّـهِ شَيْئًا وَلَا يَسْرِقْنَ وَلَا يَزْنِينَ وَلَا يَقْتُلْنَ أَوْلَادَهُنَّ وَلَا يَأْتِينَ بِبُهْتَانٍ يَفْتَرِينَهُ بَيْنَ أَيْدِيهِنَّ وَأَرْجُلِهِنَّ وَلَا يَعْصِينَكَ فِي مَعْرُوفٍ ۙ فَبَايِعْهُنَّ وَاسْتَغْفِرْ لَهُنَّ اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٢﴾
12. Ee Nabiy! Wakikujia Waumini wa kike kuahidiana nawe ahadi ya utiifu kwamba hawatomshirikisha Allaah na chochote, wala hawatoiba, wala hawatozini, wala hawataua watoto wao, wala hawatoleta usingiziaji wa kashfa walioizua baina ya mikono yao na miguu yao[7], na wala hawatakuasi katika mema, basi pokea ahadi yao ya utiifu, na waombee maghfirah kwa Allaah. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَوَلَّوْا قَوْمًا غَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ قَدْ يَئِسُوا مِنَ الْآخِرَةِ كَمَا يَئِسَ الْكُفَّارُ مِنْ أَصْحَابِ الْقُبُورِ﴿١٣﴾
13. Enyi walioamini! Msiwafanye marafiki watu ambao Allaah Amewaghadhibikia, wamekwishakata tamaa na (kheri za) Aakhirah kama walivyokwishakata tamaa makafiri na watu wa makaburini.[8]
[2] Ndugu Wa Uhusiano Wa Damu Hautamfaa Ndugu Siku Ya Qiyaamah:
Undugu wa uhusiano wa damu hauwezi kumfaa nduguye mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى).
Rejea Hadiyth inayohusiana na kuteremshwa kwa Aayah ya Suwrah Ash-Shu’araa:
وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ ﴿٢١٤﴾
Na onya (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) jamaa zako wa karibu. [Ash-Shu’araa (26:214)]
ambayo inathibitisha kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaonya ahli zake waokoe nafsi zao, kwa sababu yeye hatoweza kuwafaa kitu mbele ya Allaah Siku ya Qiyaamah.
Na pia Hadiyth ifuatayo imethibitisha kuwa hata wazazi makafiri hawawezi kunufaishana na wana wao walioamini mbele ya Allaah Siku ya Qiyaamah kwa kuwa makafiri watakuwa motoni:
حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ ثَابِتٍ، عَنْ أَنَسٍ، أَنَّ رَجُلاً، قَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَيْنَ أَبِي قَالَ " فِي النَّارِ " . فَلَمَّا قَفَّى دَعَاهُ فَقَالَ " إِنَّ أَبِي وَأَبَاكَ فِي النَّارِ " .
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Mtu mmoja alimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): Je baba yangu yuko wapi? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akajibu: “Yuko motoni.” (Yule mtu) alipogeuka, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwita na kumwambia: “Hakika baba yangu na baba yako wako motoni.” [Muslim]
Rejea Al-Hujuraat (49:13), Al-Mujaadalah (58:22) kwenye faida kadhaa na rejea zake.
[3] Haijuzu Kuwaombea Maghfirah Makafiri:
Bonyeza viungo vifuatavyo vya Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Rejea At-Tawbah (9:113-114), Al-Qaswasw (28:56).
[7] Usingiziaji Wa Kashfa Baina Ya Mikono Na Miguu Yao:
‘Ulamaa wengi wamekubaliana kwamba ni mke kumpachikia au kumnasibishia mumewe mtoto wa zinaa toka kwa mwanaume mwingine.
[8] Maana Ya Kama Walivyokwishakata Tamaa Makafiri Na Watu Wa Makaburini:
Kauli za Mufassiruna kuhusu ya Allaah (سبحانه وتعالى):
كَمَا يَئِسَ الْكُفَّارُ مِنْ أَصْحَابِ الْقُبُورِ﴿١٣﴾
“Kama walivyokwishakata tamaa makafiri na watu wa makaburini.”
Imaam As-Sa’diy:
i- Watakapofika Aakhirah wakatambua uhakika wa jambo hilo na wakajua kwa yakini kwamba wamenyimwa kheri za Aakhirah hivyo hawana sehemu yake.
ii-Wameikanusha Aakhirah na kuikataa, basi kwa hali yao hiyo, haishangazi kuwaona wakikimbilia kwenye mambo yenye kumghadhibisha Allaah na kulazimisha Adhabu Yake na wakikata tamaa ya Aakhirah, kama walivyokata tamaa makafiri wanaokadhibisha kufufuliwa hapa duniani ya kurejea watu wa makaburini kwa Allaah (سبحانه وتعالى). [Tafsiyr As-Sa’diy]
Imaam Ibn Kathiyr:
i-Makafiri walio hai wamekata tamaa ya kukutana na jamaa zao waliozikwa makaburini kwa sababu hawaamini ufufuo au kufufuliwa. Kwa hiyo kutokana na itikadi zao, hawana tena matumaini kwamba watakutana nao tena.
Na Hasan Al-Baswriy amesema: Makafiri walio hai wamekata tamaa na wafu.
Qataadah na Adhw-Dhwahaak wamesema: (Wamekata tamaa) wawarudie kwao watu wa waliofariki wakawa makaburini.
ii- Kama vile makafiri waliozikwa makaburini wamekata matumaini ya kupata aina yoyote ya kheri (yaani, baada ya kuiona adhabu na kujua kwamba Qiyaamah ni kweli).
Al-A’mash amesimulia kutoka kwa Abuu Adhw-Dwuhaa kutoka kwa Masruwq kwamba Ibn Mas’wud amesema: “Vile kafiri huyu alivyokata tamaa baada ya kufariki na akaona malipo yake (ya kufru, na maovu yake).” Amesema Mujaahid, ‘Ikrimah, Muqaatil, Ibn Zayd, Al-Kalbiy na Manswur. Ibn Jariyr ameiwafiki kauli hii.
الصَّف
061-Asw-Swaff
061-Asw-Swaff: Utangulizi Wa Suwrah [413]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
سَبَّحَ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿١﴾
1. Vimemsabbih Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi[1], Naye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٢﴾
2. Enyi walioamini! Kwa nini mnasema yale msiyoyafanya?[2]
كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ﴿٣﴾
3. Ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya.
إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِهِ صَفًّا كَأَنَّهُم بُنْيَانٌ مَّرْصُوصٌ﴿٤﴾
4. Hakika Allaah Anapenda wale wanaopigana katika Njia Yake safusafu kama kwamba wao ni jengo lililoshikamana barabara.
وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ لِمَ تُؤْذُونَنِي وَقَد تَّعْلَمُونَ أَنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ ۖ فَلَمَّا زَاغُوا أَزَاغَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴿٥﴾
5. Na pale Muwsaa alipoiambia kaumu yake: Enyi kaumu yangu! Kwa nini mnaniudhi na hali mmekwishajua kwamba hakika mimi ni Rasuli wa Allaah kwenu?[3] Basi walipopotoka, Allaah Akapotosha nyoyo zao, na Allaah Haongoi watu mafasiki.
وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُم بِالْبَيِّنَاتِ قَالُوا هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ﴿٦﴾
6. Na pale ‘Iysaa mwana wa Maryam aliposema: Enyi wana wa Israaiyl! Hakika mimi ni Rasuli wa Allaah kwenu mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat, na mwenye kubashiria kuja kwa Rasuli baada yangu jina lake Ahmad.[4] Basi alipowajia kwa hoja bayana, walisema: Hii ni sihiri bayana.
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُوَ يُدْعَىٰ إِلَى الْإِسْلَامِ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿٧﴾
7. Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemtungia Allaah uongo na hali yeye analinganiwa katika Uislamu? Na Allaah Haongoi watu madhalimu.
يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّـهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّـهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ﴿٨﴾
8. Wanataka kuizima Nuru ya Allaah kwa midomo yao, lakini Allaah Ni Mwenye Kuitimiza Nuru Yake japo makafiri watachukia.
هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ﴿٩﴾
9. Yeye Ndiye Aliyemtuma Rasuli Wake (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa mwongozo na Dini ya haki ili Aishindishe juu ya dini zote, japo watakirihika washirikina.[5]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ تِجَارَةٍ تُنجِيكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ﴿١٠﴾
10. Enyi walioamini! Nikujulisheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iumizayo?
تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿١١﴾
11. Mumuamini Allaah na Rasuli Wake, na mfanye Jihaad katika Njia ya Allaah kwa mali zenu, na nafsi zenu. Hivyo ndiyo bora kwenu mkiwa mnajua.
يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَمَسَاكِنَ طَيِّبَةً فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١٢﴾
12. (Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakuingizeni Jannaat zipitazo chini yake mito na masikani mazuri katika Jannaat za kudumu milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa mno.
وَأُخْرَىٰ تُحِبُّونَهَا ۖ نَصْرٌ مِّنَ اللَّـهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ ۗ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ﴿١٣﴾
13. Na jengine mlipendalo, (nalo ni) nusura kutoka kwa Allaah na ushindi wa karibu. Na wabashirie Waumini.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا أَنصَارَ اللَّـهِ كَمَا قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ لِلْحَوَارِيِّينَ مَنْ أَنصَارِي إِلَى اللَّـهِ ۖ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللَّـهِ ۖ فَآمَنَت طَّائِفَةٌ مِّن بَنِي إِسْرَائِيلَ وَكَفَرَت طَّائِفَةٌ ۖ فَأَيَّدْنَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَىٰ عَدُوِّهِمْ فَأَصْبَحُوا ظَاهِرِينَ﴿١٤﴾
14. Enyi walioamini! Kuweni wasaidizi wa Allaah kama alivyosema ‘Iysa mwana wa Maryam kwa wafuasi wake watiifu: Nani watakuwa wasaidizi wangu kwa ajili ya Allaah? Wafuasi watiifu wakasema: Sisi ni wasaidizi wa Allaah. Basi likaamini kundi miongoni mwa wana wa Israaiyl na likakufuru kundi jingine. Tukawatia nguvu wale walioamini dhidi ya maadui zao, wakapambaukiwa wakiwa washindi.
[1] Kila Kitu Kinamsabbih Allaah (عزّ وجلّ):
Rejea Al-Hashr (57:1) kwenye rejea zinazotaja viumbe na vitu Alivyoviumba Allaah kuwa vinamsabbih Yeye Allaah (عزّ وجلّ).
[3] Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) Aliudhiwa Mno Na Watu Wake:
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amemuombea duaa Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) kwa kuudhiwa kwake na watu wake:
حَدَّثَنَا حَفْصُ بْنُ عُمَرَ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، أَخْبَرَنِي سُلَيْمَانُ، عَنْ أَبِي وَائِلٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ قَسَمَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم قَسْمًا فَقَالَ رَجُلٌ إِنَّ هَذِهِ لَقِسْمَةٌ مَا أُرِيدَ بِهَا وَجْهُ اللَّهِ. فَأَخْبَرْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَغَضِبَ حَتَّى رَأَيْتُ الْغَضَبَ فِي وَجْهِهِ وَقَالَ " يَرْحَمُ اللَّهُ مُوسَى، لَقَدْ أُوذِيَ بِأَكْثَرَ مِنْ هَذَا فَصَبَرَ ".
Amesimulia Abuu Waail kuwa ‘Abdullaah (رضي الله عنه) amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aligawa mgao (baina ya Waumini). Mtu mmoja akasema: “Mgao huu haukufanywa kumridhisha Allaah.” Nikamjulisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) [kuhusu jambo hilo], akaghadhibika mpaka nikaona ghadhabu zake usoni mwake, akasema: “Allaah Amrehemu (Nabiy) Muwsaa (عليه السّلام), hakika aliudhiwa kwa zaidi ya hili, hata hivyo akavuta subira.” [Al-Bukhaariy Kitaabu Cha Duaa (80)]
[4] Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Ametajwa Katika Bibilia Kuwa Atakuja Kuwa Nabii Wa Mwisho, Na Ahmad Ndiye Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):
Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ametajwa katika Vitabu vilivyotangulia vya mbinguni, na Allaah (سبحانه وتعالى) Amethibitisha katika Kauli Zake:
وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ النَّبِيِّينَ لَمَا آتَيْتُكُم مِّن كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنصُرُنَّهُ ۚ قَالَ أَأَقْرَرْتُمْ وَأَخَذْتُمْ عَلَىٰ ذَٰلِكُمْ إِصْرِي ۖ قَالُوا أَقْرَرْنَا ۚ قَالَ فَاشْهَدُوا وَأَنَا مَعَكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨١﴾
“Na pale Allaah Alipochukua fungamano kwa Manabii (akawaambia): Ninayokupeni katika Kitabu na Hikmah, kisha akakujieni Rasuli (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nanyi, basi ni lazima kumwamini na kumnusuru. (Kisha Allaah) Akasema: Je, mmekubali na mtashika fungamano Langu juu ya hayo? Wakasema: Tumekubali. (Allaah) Akasema: Basi shuhudieni na Mimi Niko pamoja nanyi katika wenye kushuhudia.” [Aal-‘Imraan (3:81).
Na Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ يَأْمُرُهُم بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ ۚ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٥٧﴾
“Wale wanaomfuata Rasuli; Nabiy asiyejua kusoma wala kuandika ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Tawraat na Injiyl, anawaamrisha mema na anawakataza munkari, na anawahalalishia vilivyo vizuri na anawaharamishia vilivyo vibaya na anawaondoshea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao. Basi wale waliomwamini na wakamtukuza, na wakamnusuru na wakafuata Nuru (Qur-aan) ambayo imeteremshwa pamoja naye, hao ndio wenye kufaulu.” [Al-a’raaf (7:157)]
Rejea katika Suwrah hiyo ya Al-A’raaf (7:157) kwenye ufafanuzi wake.
Na Hadiyth ifuatayo imethibitisha jina la Ahmad:
عن جبير بن مطعم رضي الله عنه أن رسول اللهصلى الله عليه وسلم قال: ((إنَّ لِيْ أَسْمَاءً، أَنَا مُحَمَّدٌ، وَأَنَا أَحْمَدُ، وَأَنَا المَاحِي الَّذِي يَمْحُو الله بِيَ الكُفْرَ، وَأَنَا الحَاشِرُ الَّذِي يُحْشَرُ النَّاسُ عَلَى قَدَمَيَّ، وَأَنَا العَاقِبُ الَّذِي لَيْسَ بَعْدَهُ أَحَدٌ))
Amesimulia Jubayr Bin Mutw’im (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mimi nina majina kadhaa: Mimi ni Muhammad na mimi ni Ahmad, na mimi ni Al-Maahiy (mfutaji) ambaye Allaah Hufuta kufru kupitia kwangu, na mimi ni Al-Haashir (mkusanyaji) ambaye watu watakusanywa mbele ya miguu yangu (Siku ya Qiyaamah), na mimi ni Al-‘Aaqib (Wa mwisho) ambaye hakuna baada yake mtu (Nabiy).” [Muslim]
Na pia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amethibitisha Unabii wake kwa Mayahudi na Manaswara:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنَّهُ قَالَ " وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لاَ يَسْمَعُ بِي أَحَدٌ مِنْ هَذِهِ الأُمَّةِ يَهُودِيٌّ وَلاَ نَصْرَانِيٌّ ثُمَّ يَمُوتُ وَلَمْ يُؤْمِنْ بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ إِلاَّ كَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ " .
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad imo Mikononi Mwake, hatosikia mtu kuhusu mimi katika Ummah huu; Myahudi wala Mnaswara kisha asiamini kwamba nimetumwa na akafariki (katika ukafiri), ila atakuwa katika watu wa motoni.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na ifuatayo ni Fatwa aliyojibu Imaam Ibn ‘Uthaymiyn kuhusu shubha za watu wanaopinga kuwa jina la Ahmad halimaanishi ni Muhammad:
Jina La Ahmad Ni Sawa Na Muhammad:
Kuhusu Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُم بِالْبَيِّنَاتِ قَالُوا هَـٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ﴿٦﴾
Na pale ‘Iysaa mwana wa Maryam aliposema: Enyi wana wa Israaiyl! Hakika mimi ni Rasuli wa Allaah kwenu mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat, na mwenye kubashiria kuja kwa Rasuli baada yangu jina lake Ahmad. Basi alipowajia kwa hoja bayana, walisema: Hii ni sihiri bayana.
Swali: Alikuja mbabaishaji mmoja katika Manaswara akasema: Hakika Nabiy wetu (‘Iysaa) amesema: “Baada yake (atakuja Nabiy) jina lake Ahmad” na huyu aliepelekwa kutoka kwa Waarabu jina lake ni Muhammad, kwa hiyo huyu sio tuliyeahidiwa. Na sisi hivi sasa tunangojea mpaka aje Ahmad. Hivi jibu lake nini?
Jibu: Ahmad ni jina na Muhammad pia ni jina, na Nabiy (صلى الله عليه وسلم) ana majina mengi sana.
Hivyo basi, kwa nini limechaguliwa neno Ahmad kwenye bishara yake kwa Manaswara pasi na kutumia jina la Muhammad ambalo ndilo alilomuita Babu yake Abdul-Muttwalib?
Sikiliza ee ndugu yangu! Neno Ahmad ni jina la kufadhilisha (kuonesha ubora). Anakusudia kuwa ni mwenye kumshukuru sana Allaah kuliko viumbe wote, na mzuri zaidi kuliko wote kitabia. Hivyo basi, yeye ni Ahmad yenye maana ya Mahmuwd (mwenye kusifiwa), na Ahmad kwa maana ya Haamid (mwenye kuhimidi).
Ni jina la kufadhilisha kutokana na neno Haamid na Mahmuwd. Hakika limekuja jina hili kwa muundo huu ili wafahamu wale waliopewa bishara na Nabiy ‘Iysaa kuwa, huyu mtu ndiye mwenye haki zaidi ya kufuatwa, kwa sababu yeye ni mwenye kusifiwa zaidi ya watu wote. Jamani maneno yako wazi hapo au sivyo? (Wanadarasa wakajibu): “Naam yako wazi!”
AlhamduliLlaah hawana hoja! Sasa isikilize kauli ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) iliyothibiti:
(والذي نفسي بيده - أو قال : نفس محمد بيده - لا يسمع بي أحد من هذه الأمة)
“Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake.” Au kasema: “Nafsi ya Muhammad imo Mkononi Mwake. Hatosikia mtu kuhusu mimi katika Ummah huu…”
Anakusudia Ummah unaolinganiwa, ambao anaoulingania Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na ambao ni ummah wa viumbe wote baada ya kutumwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
Hadiyth kamili ni hii ifuatayo:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنَّهُ قَالَ " وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لاَ يَسْمَعُ بِي أَحَدٌ مِنْ هَذِهِ الأُمَّةِ يَهُودِيٌّ وَلاَ نَصْرَانِيٌّ ثُمَّ يَمُوتُ وَلَمْ يُؤْمِنْ بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ إِلاَّ كَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ " .
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad imo Mkononi Mwake, hatosikia mtu kuhusu mimi katika Ummah huu; Myahudi wala Mnaswara kisha asiamini kwamba nimetumwa na akafariki (katika ukafiri), ila atakuwa katika watu wa motoni.” [Muslim]
Amesema kweli Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), bila kiapo, kwani yeye ni mkweli na mwenye kusadikishwa. Na angalia jinsi alivyosema:
(لا يسمع بي يهودي ولا نصراني)
“Hatosikia mtu kuhusu mimi; Yahudi au Naswaara.”
Bila kusema na kufahamu kile nilichomlingania, ili asimamishiwe hoja lazima ajue hoja, kwa kusikia tu haiwi hoja mpaka afahamu, kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوْمِهِ
Na Hatukutuma Rasuli yeyote isipokuwa kwa lugha ya kaumu yake.
Ili iweje?
لِيُبَيِّنَ لَهُمْ ۖ
Ili awabainishie [Ibraahiym (14:4)]
Lau angetumwa Mwarabu kwa asiyekuwa Mwarabu, isingesimama hoja, na angetumwa Muajemi kwa Mwarabu isingesimama hoja. Lakini kwa Myahudi na Mnaswara kwa kule kusikia tu, wakasimamishiwa hoja.
Kwa nini? Kwa sababu Mayahudi na Manaswara wanamfahamu zaidi, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kama wanavyowafahamu watoto wao. Kwa kule kusikia kwao tu wanalazimika wamfuate. Na hata ikiwa hawamfahamu wakawa kama vile watu wa kawaida, italazimika wafanye uchunguzi wa kumfahamu, kwa kuwa walishafikishiwa na kupewa bishara (ya ujio wake), na zikatajwa sifa zake, ikawa wao wanamfahamu kama wanavyowafahamu watoto wao. [Fataawa Al-Haram Al-Makkiy (01b-1420) Ibn ‘Uthaymiyn]
[5] Dini Ya Kiislamu Ndio Dini Itakayoshinda Dini Nyenginezo:
Aayah hii imetajwa katika Qur-aan kwenye Suwrah tatu. Rejea At-Tawbah (9:33), Al-Fat-h (48:28).
عَنْ تَمِيمٍ الدَّارِيِّ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَيَبْلُغَنَّ هَذَا الْأَمْرُ مَا بَلَغَ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَلَا يَتْرُكُ اللَّهُ بَيْتَ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللَّهُ هَذَا الدِّينَ بِعِزِّ عَزِيزٍ أَوْ بِذُلِّ ذَلِيلٍ عِزًّا يُعِزُّ اللَّهُ بِهِ الْإِسْلَامَ وَذُلًّا يُذِلُّ اللَّهُ بِهِ الْكُفْرَ
Amesimulia Tamiym Ad-Daariyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Jambo hili (Uislaam) hakika litafika kila mahali palipoguswa na usiku na mchana. Allaah Hatoacha nyumba au makazi isipokuwa Allaah Ataingizi Dini hii kwa ‘izza (hadhi, utukufu na ushindi) ambao watukufu watajaaliwa taadhima na wadhalili watadhalilika. Allaah Atawapa utukufu watukufu kwa Uislaam na Atawadhalilisha wadhalili kwa Ukafiri.” [Ahmad]
عَنْ ثَوْبَانَ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((إِنَّ اَللَّهَ زَوَى لِيَ الأَرْضَ، فَرَأَيْتُ مَشَارِقَهَا وَمَغَارِبَهَا، وَإِنَّ أُمَّتِي سَيَبْلُغُ مُلْكُهَا مَا زُوِيَ لِي مِنْهَا. وَأُعْطِيتُ الْكَنْزَيْنِ الأَحْمَرَ وَالأَبْيَضَ. وَإِنِّي سَأَلْتُ رَبِّي لأُمَّتِي أَنْ لاَ يُهْلِكَهَا بِسَنَةٍ بِعَامَّةٍ، وَأَنْ لا يُسَلِّطَ عَلَيْهِمْ عَدُّوا مِنْ سِوَى أَنْفُسِهِمْ، فَيَسْتَبِيحَ بَيْضَتَهُمْ، وَإِنَّ رَبِّي قَالَ: يَا مُحَمَّدُ إِنِّي إِذَا قَضَيْتُ قَضَاءً فَإِنَّهُ لاَ يُرَدُّ، وَإِنِّي أَعْطَيْتُكَ لأُمَّتِكَ أَنْ لا أُهْلِكَهُمْ بِسَنَةٍ ِعَامَّةٍ، وَأَنْ لا أُسَلِّطَ عَلَيْهِمْ عَدُّوا مِنْ سِوَى أَنْفُسِهِمْ فَيَسْتَبِيحَ بَيْضَتَهُمْ، وَلَوْ اِجْتَمَعَ عَلَيْهِمْ مَنْ بِأَقْطَارِهَا حَتَّى يَكُونَ بَعْضُهُمْ يُهْلِكُ بَعْضًا، وَيَسْبِيَ بَعْضُهُمْ بَعْضًا))
Amesimulia Thawbaan (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Amenikusanyia ardhi (dunia) nikaona Mashariki yake na Magharibi yake. Na hakika Ummah wangu utaenea na kumiliki vyote vilivyo katika sehemu hizo nilokusanyiwa. Na nimepewa hazina mbili; nyekundu (Ufalme wa Kirumi) na nyeupe (Ufalme wa Kifursi). Hapo nikamuomba Rabb wangu Asijaalie Ummah wangu kuangamizwa kwa baa kuu la jumla na usitekwe na adui ajnabi atakayeuharibu mji mkuu wao na kuuangusha uongozi wao. Rabb wangu Akajibu: Ee Muhammad! Nikihukumu amri basi hakika hairudi. Nimekadiria kwamba Ummah wako hautahiliki mara moja kwa baa kuu la jumla na kwamba hautatekwa na adui ajnabi na kuharibu mji mkuu wao na kuuangusha uongozi wao, na hata kama maadui wa nchi zote wataungana dhidi yao, mpaka pale tu (Waislamu) watakapoanza kumalizana wenyewe kwa wenyewe na kutekana wao kwa wao.” [Muslim]
Bonyeza pia kiungo kifuatacho kwa faida ziyada:
57-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Dini Yake Ndio Itakayoshinda Dini Zote [415]
الْجُمُعَة
062-Al-Jumu’ah
062-Al-Jumu’ah: Utangulizi Wa Suwrah [417]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يُسَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ الْمَلِكِ الْقُدُّوسِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ﴿١﴾
1. Vinamsabbih Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi[1], Mfalme, Ametakasika na sifa zote hasi, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٢﴾
2. Yeye Ndiye Aliyepeleka Rasuli kwa wasiojua kusoma wala kuandika, atokanaye nao wenyewe, anawasomea Aayaat Zake na Anawatakasa, na Anawafunza Kitabu na Hikmah[2], nao (kwa hakika) walikuwa hapo kabla katika upotofu bayana.
وَآخَرِينَ مِنْهُمْ لَمَّا يَلْحَقُوا بِهِمْ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٣﴾
3. Na wengineo ambao bado hawajakutana nao. Naye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.[3]
ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ﴿٤﴾
4. Hiyo ni Fadhila ya Allaah Humpa Amtakaye, na Allaah Ni Mwenye fadhila adhimu.
مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا ۚ بِئْسَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴿٥﴾
5. Mfano wa wale waliobebeshwa Tawraat, kisha wasiibebe ni kama mfano wa punda abebaye mijalada ya vitabu. Ubaya ulioje mfano wa watu waliokadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili) za Allaah! Na na Allaah Haongoi watu madhalimu.[4]
قُلْ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ هَادُوا إِن زَعَمْتُمْ أَنَّكُمْ أَوْلِيَاءُ لِلَّـهِ مِن دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُا الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٦﴾
6. Sema: Enyi Mayahudi! Mkidai kuwa nyinyi ni vipenzi vya Allaah pasina watu wengine, basi tamanini mauti, mkiwa ni wasemao kweli.
وَلَا يَتَمَنَّوْنَهُ أَبَدًا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ﴿٧﴾
7. Na wala hawatayatamani abadani kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yao, na Allaah Anawajua vyema madhalimu.[5]
قُلْ إِنَّ الْمَوْتَ الَّذِي تَفِرُّونَ مِنْهُ فَإِنَّهُ مُلَاقِيكُمْ ۖ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٨﴾
8. Sema: Hakika hayo mauti mnayoyakimbia, hakika yatakukuteni tu! Kisha mtarudishwa kwa Mjuzi wa ghaibu na dhahiri. Atakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿٩﴾
9. Enyi walioamini! Inaponadiwa kwa ajili ya Swalaah siku ya Ijumaa, basi kimbilieni kwenda kumdhukuru Allaah na acheni kuuza na kununua. Hivyo ni kheri kwenu zaidi mkiwa mnajua.[6]
فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ اللَّـهِ وَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ﴿١٠﴾
10. Na inapomalizika Swalaah, basi tawanyikeni katika ardhi, na tafuteni Fadhila za Allaah, na mdhukuruni Allaah kwa wingi[7] ili mpate kufaulu.
وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا ۚ قُلْ مَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ مِّنَ اللَّـهْوِ وَمِنَ التِّجَارَةِ ۚ وَاللَّـهُ خَيْرُ الرَّازِقِينَ﴿١١﴾
11. Na wanapoona tijara au pumbao wanaikimbilia na wanakuacha umesimama. Sema: Yaliyoko kwa Allaah ni bora zaidi kuliko pumbao na tijara, na Allaah Ni Mbora wa wenye kuruzuku.[8]
[1] Kila Kitu Kinamsabbih Allaah (عزّ وجلّ):
Rejea Al-Hashr (57:1) kwenye rejea zinazotaja viumbe na vitu Alivyoviumba Allaah kuwa vinamsabbih Yeye Allaah (عزّ وجلّ).
[2] Fadhila Za Waumini Kutumiwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):
Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى) Kauli Yake kama hii katika Al-Baqarah (2:151), Aal-‘Imraan (3:164). Na duaa ya Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) alipoomba:
رَبَّنَا وَابْعَثْ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُزَكِّيهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٢٩﴾
“Rabb wetu, Wapelekee Rasuli miongoni mwao atakayewasomea Aayaat Zako na atakayewafunza Kitabu na Hikmah na atakayewatakasa. Hakika Wewe Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.” [Al-Baqarah (2:129)]
[3] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
062-Asbaabun-Nuzuwl: Al Jumu'ah Aayah 03: وَآخَرِينَ مِنْهُمْ لَمَّا يَلْحَقُوا بِهِمْ [418]
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
حَدَّثَنِي عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ حَدَّثَنِي سُلَيْمَانُ بْنُ بِلاَلٍ، عَنْ ثَوْرٍ، عَنْ أَبِي الْغَيْثِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، رضى الله عنه قَالَ كُنَّا جُلُوسًا عِنْدَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَأُنْزِلَتْ عَلَيْهِ سُورَةُ الْجُمُعَةِ وَآخَرِينَ مِنْهُمْ لَمَّا يَلْحَقُوا بِهِمْ قَالَ قُلْتُ مَنْ هُمْ يَا رَسُولَ اللَّهِ فَلَمْ يُرَاجِعْهُ حَتَّى سَأَلَ ثَلاَثًا، وَفِينَا سَلْمَانُ الْفَارِسِيُّ، وَضَعَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَدَهُ عَلَى سَلْمَانَ ثُمَّ قَالَ " لَوْ كَانَ الإِيمَانُ عِنْدَ الثُّرَيَّا لَنَالَهُ رِجَالٌ ـ أَوْ رَجُلٌ ـ مِنْ هَؤُلاَءِ ".
Amesimulia Abul-Ghayth (رضي الله عنه) kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Tulikuwa tumeketi pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akateremshiwa Suwrah Al-Jumu’ah:
وَآخَرِينَ مِنْهُمْ لَمَّا يَلْحَقُوا بِهِمْ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٣﴾
“Na wengineo ambao bado hawajakutana nao. Naye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.” [Al-Jumu’a (62:3)]
Nikauliza: Ni akina nani hao Ee Rasuli wa Allaah? Hakunijibu mpaka nilipomuuliza mara ya tatu. Na kati yetu alikuwapo Salmaan Al-Faarisiyy (رضي الله عنه). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaweka mkono wake juu ya Salmaan, kisha akasema: “Lau kama imaan ingalikuwa kwenye ath-thurayyaa (mojawapo wa sayari) wangaliifikia watu (au) mtu katika watu hawa (yaani jamaa za akina Salmaan Al-Faarisiyy).” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Tafsiyr (65)]
[4] Mfano Wa Punda Abebaye Mijalada Ya Vitabu:
مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا ۚ
“Mfano wa wale waliobebeshwa Tawraat, kisha wasiibebe ni kama mfano wa punda abebaye mijalada ya vitabu.”
Mtu kama huyo anafanana na punda (mnyama wa kubeba mizigo), kwa vile hapati faida yoyote kwa kule kubeba vitabu vingi mgongoni kwake. Halikadhalika mtu huyo hapati faida yoyote kwa kuswali Swalaah ya Ijumaa. Na hii ni kutokana na katazo la kuzungumza katika Swalaah ya Ijumaa kama ilivyotajwa katika Hadiyth ifuatayo:
عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم مَنْ تَكَلَّمَ يَوْمَ اَلْجُمُعَةِ وَالْإِمَامُ يَخْطُبُ فَهُوَ كَمَثَلِ اَلْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا، وَاَلَّذِي يَقُولُ لَهُ: أَنْصِتْ، لَيْسَتْ لَهُ جُمُعَةٌ رَوَاهُ أَحْمَدُ، بِإِسْنَادٍ لَا بَأْسَ بِهِ
وَهُوَ يُفَسِّرُ حَدِيثَ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ فِي "اَلصَّحِيحَيْنِ" مَرْفُوعًا: إِذَا قُلْتَ لِصَاحِبِكَ: أَنْصِتْ يَوْمَ اَلْجُمُعَةِ وَالْإِمَامِ يَخْطُبُ، فَقَدْ لَغَوْتَ
Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kuzungumza siku ya Ijumaa wakati Imaam anakhutubia, basi yeye ni kama punda aliyebeba vitabu. Na anayemuambia: Nyamaza! Basi huyo hana Ijumaa.” [Imetolewa na Ahmad, kwa Isnaad isiyo na ubaya wowote]
[5] Hakuna Atakayeweza Kuyakimbia Mauti!
Kila nafsi itaonja mauti. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Kauli Zake zifuatazo:
كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۖ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ ۗ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ ﴿١٨٥﴾
“Kila nafsi itaonja mauti. Na hakika mtalipwa kikamilifu ujira wenu Siku ya Qiyaamah. Basi atakayewekwa mbali na moto na akaingizwa Jannah, huyo kwa yakini amefuzu. Na uhai wa dunia si lolote ila ni starehe ya udanganyifu.” [Aal-‘Imraan (3:185)]
كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَنَبْلُوكُم بِالشَّرِّ وَالْخَيْرِ فِتْنَةً ۖ وَإِلَيْنَا تُرْجَعُونَ ﴿٣٥﴾
“Kila nafsi itaonja mauti. Na Tutakujaribuni kwa mitihani ya shari na kheri. Na Kwetu mtarejeshwa.” [Al-Anbiyaa (21:35)]
كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۖ ثُمَّ إِلَيْنَا تُرْجَعُونَ ﴿٥٧﴾
“Kila nafsi itaonja mauti, kisha Kwetu mtarejeshwa. [Al-‘Ankabuwt (29:57)]
Na akuna atakayeweza kukimbia mauti hata awe katika jengo la imara vipi kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
أَيْنَمَا تَكُونُوا يُدْرِككُّمُ الْمَوْتُ وَلَوْ كُنتُمْ فِي بُرُوجٍ مُّشَيَّدَةٍ ۗ
“Popote mtakapokuwa yatakufikieni mauti, japo mkiwa katika minara (au ngome) imara na madhubuti.” [An-Nisaa (4:78)]
Na waliokusudiwa katika Aayah hizo za Suwrah hii Al-Jumu’ah (62:6-7) ni Mayahudi, ni sawa kukusudiwa kwao katika Aayah zifuatazo:
قُلْ إِن كَانَتْ لَكُمُ الدَّارُ الْآخِرَةُ عِندَ اللَّـهِ خَالِصَةً مِّن دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُا الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٩٤﴾ وَلَن يَتَمَنَّوْهُ أَبَدًا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ ﴿٩٥﴾
“Sema: Ikiwa nyumba ya Aakhirah iliyoko kwa Allaah ni makhsusi kwenu pekee pasi na watu wengine, basi tamanini mauti mkiwa ni wakweli. Na hawatoyatamani abadani kwa sababu ya iliyoyatanguliza mikono yao. Na Allaah Ni Mjuzi wa madhalimu.” [Al-Baqarah (2:94-95)]
[6] Umuhimu Wa Siku Ya Ijumaa Na Swalaah Ya Ijumaa Na Fadhila Zake:
Siku ya Ijumaa ni siku adhimu kwa Waislamu na fadhila zake ni tele. Pia mahimizo ya Swalaah ya Ijumaa, pamoja na fadhila zake, na matahadharisho ya kutokuhudhuria Swalaah ya Ijumaa yametajwa katika Hadiyth kadhaa za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).
Miongoni mwa himizo na fadhila zake ni Hadiyth ifuatayo:
حعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " مَنِ اغْتَسَلَ يَوْمَ الْجُمُعَةِ غُسْلَ الْجَنَابَةِ ثُمَّ رَاحَ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَدَنَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الثَّانِيَةِ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَقَرَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الثَّالِثَةِ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ كَبْشًا أَقْرَنَ، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الرَّابِعَةِ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ دَجَاجَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الْخَامِسَةِ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَيْضَةً، فَإِذَا خَرَجَ الإِمَامُ حَضَرَتِ الْمَلاَئِكَةُ يَسْتَمِعُونَ الذِّكْرَ ".
Amesimulia Abu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mtu yeyote anayeoga siku ya Ijumaa kwa mfano wa ghuslu (josho) la janaba, kisha anakwenda kuswali (mnamo saa ya kwanza, yaani mapema), ni mithili ya kuwa katoa dhabihu (swadaqa) ngamia. Na mtu yeyote anayekwenda mnamo saa ya pili ni mithili ya kuwa katoa dhabihu ng’ombe. Na yeyote anayekwenda saa ya tatu, basi ni kama katoa dhabihu kondoo dume mwenye pembe. Na yeyote anayekwenda saa ya nne, basi huyo ni kama katoa dhabihu ya kuku jike. Na yeyote anayekwenda saa ya tano basi huyo ni kama katoa yai. Imaam anapokuja (anapoanza kutoa khutba), Malaika huhudhuria kuisikiliza khutba.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Ijumaa (11)]
Matahadharisho Ya Kutokuhudhuria Swalaah Ya Ijumaa:
عَنْ أَبِي الْجَعْدِ الضَّمْرِيِّ، - وَكَانَتْ لَهُ صُحْبَةٌ - أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " مَنْ تَرَكَ ثَلاَثَ جُمَعٍ تَهَاوُنًا بِهَا طَبَعَ اللَّهُ عَلَى قَلْبِهِ " . رواه أحمد وأصحاب السنن
Amesimulia Abuu Al-Ja’d Adhw-Dhwamriyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayeacha (kuswali Swalaah ya) Ijumaa mara tatu bila ya sababu yoyote, Allaah Humpiga muhuri katika moyo wake. [Ahmad na wapokezi wa Hadiyth wengine wenye vitabu vya Sunnan]
عن ابن عمر وأبي هريرة أَنَّهُمَا، سَمِعَا رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ عَلَى أَعْوَادِ مِنْبَرِهِ " لَيَنْتَهِيَنَّ أَقْوَامٌ عَنْ وَدْعِهِمُ الْجُمُعَاتِ أَوْ لَيَخْتِمَنَّ اللَّهُ عَلَى قُلُوبِهِمْ ثُمَّ لَيَكُونُنَّ مِنَ الْغَافِلِينَ "
Amesimulia Ibn 'Umar na Abuu Hurayrah (رضي الله عنهما) kwamba wamemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa juu ya mimbari yake ya mbao akisema: “Wasiohudhuria Swalaah ya Ijumaa wabadilishe mtindo wao huo, au sivyo Allaah Atawapiga mihuri katika nyoyo zao na watakuwa miongoni mwa walioghafilika.” [Muslim]
Somo hili la fadhila za Siku ya Ijumaa na Swalaah ya Ijumaa ni pana. Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida zake tele:
051-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Swalaah: Khutbah Ya Ijumaa Na Hukmu Zinazomkhusu Khatibu [422]
[7] Kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) Kwa Wingi Jioni Ya Siku Ya Ijumaa:
Baada Ya Alasiri na kabla ya Magharibi, kuna fadhila adhimu ya kutakabaliwa mtu duaa yake kutokana na Hadiyth zifuatazo:
عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ (رضي الله عنه) عَنْ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((يَوْمُ الْجُمُعَةِ اثْنَتَا عَشْرَةَ سَاعَةً ،لاَ يُوجَدُ فِيهَا عَبْدٌ مُسْلِمٌ يَسْأَلُ اللَّهَ شَيْئًا إلاَّ آتَاهُ إِيَّاهُ ، فَالْتَمِسُوهَا آخِرَ سَاعَةٍ بَعْدَ الْعَصْر))
Amesimulia Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Siku ya Ijumaa kuna masaa kumi na mbili ambayo hapatikani mja Muislamu anayemwomba Allaah kitu ila Anampa, basi itafuteni saa la mwisho baada ya Swalaah ya Alasiri.” [Swahiyh Abiy Daawuwd (1048), Swahiyh An-Nasaaiy (1388), Swahiyh Al-Jaami’ (8190)]
‘Ulamaa wamesema kuhusu saa katika siku ya Ijumaa inayotakabaliwa duaa, kwamba zimetajwa nyakati kadhaa, ila waliyokubaliana zaidi yao ni saa ya mwisho kabla ya Swalaah ya Magharibi.
الْمُنَافِقُون
063-Al-Munaafiquwn
063-Al-Munaafiquwn: Utangulizi Wa Suwrah [430]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
إِذَا جَاءَكَ الْمُنَافِقُونَ قَالُوا نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ إِنَّكَ لَرَسُولُهُ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَكَاذِبُونَ﴿١﴾
1. Wanapokujia wanafiki husema: Tunashuhudia kwamba wewe bila shaka ni Rasuli wa Allaah. Na Allaah Anajua kuwa wewe ni Rasuli Wake, na Allaah Anashuhudia kuwa hakika wanafiki ni waongo.[1]
اتَّخَذُوا أَيْمَانَهُمْ جُنَّةً فَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٢﴾
2. Wamefanya viapo vyao kuwa ni ngao, hivyo wakazuia Njia ya Allaah. Hakika ni maovu mno waliyokuwa wakiyatenda.
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا فَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَفْقَهُونَ﴿٣﴾
3. Hiyo ni kwa sababu ya kuwa waliamini, kisha wakakufuru, basi ukapigwa mhuri juu ya nyoyo zao, kwa hiyo hawafahamu lolote.
وَإِذَا رَأَيْتَهُمْ تُعْجِبُكَ أَجْسَامُهُمْ ۖ وَإِن يَقُولُوا تَسْمَعْ لِقَوْلِهِمْ ۖ كَأَنَّهُمْ خُشُبٌ مُّسَنَّدَةٌ ۖ يَحْسَبُونَ كُلَّ صَيْحَةٍ عَلَيْهِمْ ۚ هُمُ الْعَدُوُّ فَاحْذَرْهُمْ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّـهُ ۖ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ﴿٤﴾
4. Na unapowaona, inakupendezesha miili yao, na wanaposema, unasikiliza kauli zao. Lakini wao ni kama magogo yaliyoegemezwa. Wanadhania kuwa kila ukelele unaopigwa ni kwa ajili yao. Hao ndio maadui, basi tahadhari nao, Allaah Awaangamizilie mbali. Namna namna gani wanavyoghilibiwa!
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا يَسْتَغْفِرْ لَكُمْ رَسُولُ اللَّـهِ لَوَّوْا رُءُوسَهُمْ وَرَأَيْتَهُمْ يَصُدُّونَ وَهُم مُّسْتَكْبِرُونَ﴿٥﴾
5. Wanapoambiwa: Njooni ili Rasuli wa Allaah akuombeeni maghfirah, hupindisha vichwa vyao, na utawaona wanakwepa na huku wao ni wenye kutakabari.
سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَسْتَغْفَرْتَ لَهُمْ أَمْ لَمْ تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ لَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴿٦﴾
6. Ni sawasawa juu yao, ukiwaombea maghfirah au usiwaombee, Allaah Hatowaghufuria kamwe. Hakika Allaah Haongoi watu mafasiki.
هُمُ الَّذِينَ يَقُولُونَ لَا تُنفِقُوا عَلَىٰ مَنْ عِندَ رَسُولِ اللَّـهِ حَتَّىٰ يَنفَضُّوا ۗ وَلِلَّـهِ خَزَائِنُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَـٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَفْقَهُونَ﴿٧﴾
7. Wao ndio wale wasemao: Msitoe mali kwa ajili ya walioko kwa Rasuli wa Allaah mpaka waondokelee mbali. Na ilhali ni za Allaah Pekee hazina za mbingu na ardhi, lakini wanafiki hawafahamu.
يَقُولُونَ لَئِن رَّجَعْنَا إِلَى الْمَدِينَةِ لَيُخْرِجَنَّ الْأَعَزُّ مِنْهَا الْأَذَلَّ ۚ وَلِلَّـهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَـٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَعْلَمُونَ﴿٨﴾
8. Wanasema: Tutakaporudi Madiynah, mwenye hadhi zaidi lazima atamfukuza humo aliye dhalili. Na ilhali utukufu ni wa Allaah na wa Rasuli Wake na wa Waumini, lakini wanafiki hawajui.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُلْهِكُمْ أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿٩﴾
9. Enyi walioamini! Zisikupurukusheni mali zenu wala watoto wenu mkaacha kumdhukuru Allaah. Na yeyote atakayefanya hivyo, basi hao ndio waliokhasirika.[2]
وَأَنفِقُوا مِن مَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوْلَا أَخَّرْتَنِي إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ الصَّالِحِينَ﴿١٠﴾
10. Na toeni katika yale Tuliyokuruzukuni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti akasema: Rabb wangu! Lau Ungeliniakhirisha mpaka muda wa karibu hivi, nikatoa swadaqah na nikawa miongoni mwa Swalihina.[3]
وَلَن يُؤَخِّرَ اللَّـهُ نَفْسًا إِذَا جَاءَ أَجَلُهَا ۚ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴿١١﴾
11. Lakini Allaah Haiakhirishi kamwe nafsi yeyote inapokuja ajali yake, na Allaah Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri kwa yale myatendayo.
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Kuanzia Aayah hii ya kwanza hadi namba (8) kuna kisa cha mnafiki mkuu ‘Abdullaah bin Saluwl alivyotaka kumdhalilisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Waumini na kutaka kuwafukuza katika mji wa Madiynah. Bonyeza kiungo kifuatacho:
[2] Maonyo Ya Kughafilika Kumdhukuru Allaah:
Rejea Twaahaa (20:124) kwenye maonyo ya kughafilika na kumdhukuru Allaah. Na rejea Al-Ahzaab (33:41) kwenye fadhila za kumdhukuru Allaah.
[3] Binaadam Hujuta Anapotolewa Roho Akiwa Ni Kafiri Au Muasi Au Asipotenda Mema:
Allaah (سبحانه وتعالى) Ameonya majuto ya watu kutokumtii na kutamani kurudi duniani kutenda mema. Miongoni mwa Kauli Zake ni ifuatayo:
حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ رَبِّ ارْجِعُونِ ﴿٩٩﴾ لَعَلِّي أَعْمَلُ صَالِحًا فِيمَا تَرَكْتُ ۚ كَلَّا ۚ إِنَّهَا كَلِمَةٌ هُوَ قَائِلُهَا ۖ وَمِن وَرَائِهِم بَرْزَخٌ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٠٠﴾
Mpaka yatakapomfikia mmoja wao mauti, atasema: Rabb wangu! Nirejesheni (duniani). Ili nikatende mema katika yale niliyoyaacha. (Ataambiwa) Laa hasha! Hakika hilo ni neno alisemalo yeye tu. Na mbele yao kuna Barzakh[3] mpaka Siku watakayofufuliwa. [Al-Muuminuwn (23:99-100)]
Rejea pia Al-A’raaf (7:53), Ibraahiym (14:44), As-Sajdah (32:12), Al-An'aam (6:27-28), Ash-Shuwraa (42:44), Faatwir (35:37), Ghaafir (40:11-12), Az-Zumar (39:53-58).
التَّغَابُن
064-At-Taghaabun
064-At-Taghaabun: Utangulizi Wa Suwrah [433]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يُسَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿١﴾
1. Vinamsabbih Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi[1]. Ufalme ni Wake Pekee na Himidi ni Zake Pekee. Naye juu ya kila kitu Ni Muweza.
هُوَ الَّذِي خَلَقَكُمْ فَمِنكُمْ كَافِرٌ وَمِنكُم مُّؤْمِنٌ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ﴿٢﴾
2. Yeye Ndiye Ambaye Amekuumbeni, basi miongoni mwenu yuko aliye kafiri na miongoni mwenu yuko aliye Muumini. Na Allaah kwa yale myatendayo Ni Mwenye Kuona.
خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ ۖ وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ﴿٣﴾
3. Ameumba mbingu na ardhi kwa haki, na Akakutengenezeni sura, kisha Akafanya nzuri zaidi sura zenu,[2] na Kwake ndio mahali pa kuishia.
يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَيَعْلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعْلِنُونَ ۚ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ﴿٤﴾
4. Anajua yale yaliyomo mbinguni na ardhini, na Anayajua yale mnayofanya siri na mnayoyatangaza. Na Allaah Ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.[3]
أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَبَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَبْلُ فَذَاقُوا وَبَالَ أَمْرِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٥﴾
5. Je, haijakufikieni habari ya wale waliokufuru kabla wakaonja matokeo ya uovu wao? Nao watapata adhabu iumizayo.
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُ كَانَت تَّأْتِيهِمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَقَالُوا أَبَشَرٌ يَهْدُونَنَا فَكَفَرُوا وَتَوَلَّوا ۚ وَّاسْتَغْنَى اللَّـهُ ۚ وَاللَّـهُ غَنِيٌّ حَمِيدٌ﴿٦﴾
6. Hivyo kwa sababu ilikuwa wakiwafikia Rusuli wao kwa hoja bayana wakisema: Ah! Binaadam ndio watuongoze? Basi wakakufuru na wakakengeuka, na Allaah Akawa Hana haja nao, na Allaah Ni Mkwasi, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.
زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن لَّن يُبْعَثُوا ۚ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ ۚ وَذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ﴿٧﴾
7. Waliokufuru wamedai kwamba hawatofufuliwa kamwe. Sema: Sivyo hivyo! Naapa kwa Rabb wangu, bila shaka mtafufuliwa, kisha mtajulishwa yale mliyoyatenda, na hayo kwa Allaah ni mepesi.[4]
فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَالنُّورِ الَّذِي أَنزَلْنَا ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ﴿٨﴾
8. Basi muaminini Allaah, na Rasuli Wake, na Nuru (Qur-aan) Tuliyoiteremsha. Na Allaah kwa yale myatendayo Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
يَوْمَ يَجْمَعُكُمْ لِيَوْمِ الْجَمْعِ ۖ ذَٰلِكَ يَوْمُ التَّغَابُنِ ۗ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ وَيَعْمَلْ صَالِحًا يُكَفِّرْ عَنْهُ سَيِّئَاتِهِ وَيُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٩﴾
9. Siku Atakayokukusanyeni kwa ajili ya Siku ya mkusanyiko.[5] Hiyo ndio Siku ya kupata na kukosa.[6] Basi yeyote anayemuamini Allaah na akatenda mema, (Allaah) Atamfutia maovu yake na Atamuingiza Jannaat zipitazo chini yake mito wadumu humo abadi. Huko ndiko kufuzu adhimu.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ خَالِدِينَ فِيهَا ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿١٠﴾
10. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat (na Ishara, Dalili) Zetu, hao ndio watu wa motoni, watadumu humo. Ni ubaya ulioje mahali pa kuishia!
مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ يَهْدِ قَلْبَهُ ۚ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ﴿١١﴾
11. Hausibu msiba wowote isipokuwa kwa Idhini ya Allaah. Na yeyote anayemuamini Allaah, (Allaah) Huuongoza moyo wake.[7] Na Allaah kwa kila kitu Ni Mjuzi.
وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ ۚ فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَإِنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ﴿١٢﴾
12. Na mtiini Allaah na mtiini Rasuli,[8] lakini mkikengeuka, basi hakika ni juu ya Rasuli Wetu kubalighisha (ujumbe) bayana.
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ﴿١٣﴾
13. Allaah, hakuna muabudiwa wa haki ila Yeye. Na kwa Allaah watawakali Waumini.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ مِنْ أَزْوَاجِكُمْ وَأَوْلَادِكُمْ عَدُوًّا لَّكُمْ فَاحْذَرُوهُمْ ۚ وَإِن تَعْفُوا وَتَصْفَحُوا وَتَغْفِرُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١٤﴾
14. Enyi walioamini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu ni maadui kwenu, basi tahadharini nao. Na mkisamehe na mkapuuza na mkayafutilia mbali, basi hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[9]
إِنَّمَا أَمْوَالُكُمْ وَأَوْلَادُكُمْ فِتْنَةٌ ۚ وَاللَّـهُ عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ﴿١٥﴾
15. Hakika mali zenu na watoto wenu ni jaribio. Na kwa Allaah kuna ujira adhimu.
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ وَاسْمَعُوا وَأَطِيعُوا وَأَنفِقُوا خَيْرًا لِّأَنفُسِكُمْ ۗ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿١٦﴾
16. Basi mcheni Allaah muwezavyo. Na sikilizeni, na tiini na toeni (kwa ajili ya Allaah), itakuwa ni kheri kwa ajili ya nafsi zenu. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.
إِن تُقْرِضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا يُضَاعِفْهُ لَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۚ وَاللَّـهُ شَكُورٌ حَلِيمٌ﴿١٧﴾
17. Mkimkopesha Allaah karadha mzuri, Atakuzidishieni maradufu, na Atakughufurieni.[10] Na Allaah Ni Mwenye Kupokea shukurani, Mpole na Mvumilivu.
عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿١٨﴾
18. Mjuzi wa ghaibu na dhahiri, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
[1] Kila Kitu Kinamsabbih Allaah (عزّ وجلّ):
Rejea Al-Hashr (57:1) kwenye rejea zinazotaja viumbe na vitu Alivyoviumba Allaah kuwa vinamsabbih Yeye Allaah (عزّ وجلّ).
[2] Allaah Amemuumba Binaadam Katika Sura Na Umbo Zuri Kabisa:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja hayo katika Kauli Zake nyenginezo. Rejea Aal-‘Imraan (3:6), Al-Muuminuwn (23:12-14), Ghaafir (40:64), Al-Infitwaar (82:6-8), At-Tiyn (95:4).
[4] Makafiri Hawakuamini Kuwa Watafufuliwa:
Rejea Al-Israa (17:49) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali.
[5] Watu Wote Watakusanywa Siku Ya Qiyaamah:
Hiyo ni sawa na Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
قُلْ إِنَّ الْأَوَّلِينَ وَالْآخِرِينَ ﴿٤٩﴾ لَمَجْمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَاتِ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ ﴿٥٠﴾
“Sema: (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika wa awali na wa mwishoni. Bila shaka watajumuishwa katika wakati na mahali pa siku maalumu.” [Al-Waaqi’ah (56:49-500]
[6] Majina Ya Siku Ya Qiyaamah:
Rejea Suwrah Al-Qiyaamah (75:1) kwenye uchambuzi wa majina ya/sifa za Siku ya Qiyaamah, na rejea zake.
[7] Muumini Kuamini Qadar Ya Allaah Katika Mitihani Na Misiba:
Muumini anapopatwa na misiba, basi anapaswa avute subira na aamini Qadar ya Allaah (سبحانه وتعالى). Na kuamini huko na kuvumilia, ni mojawapo wa kuthibitisha imaan yake kama ilivyoelezewa katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ صُهَيْبٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم . عَجَبًا لإَمْرِ الْمُؤْمِنِ إِنَّ أَمْرَهُ كُلَّهُ خَيْرٌ، وَلَيْسَ ذَاكَ لإَحَدٍ إلاَّ لِلْمُؤْمِنِ. إِنْ أَصَابَتْهُ سَرَّاءُ شَكَرَ فَكَانَ خَيْرًا لَهُ، وَإِنْ أَصَابَتْهُ ضَرَّاءُ صَبَرَ فَكَانَ خَيْرًا لَهُ مسلم
Amesimulia Swuhayb (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ajabu ya jambo la Muumin kwamba kila jambo lake ni kheri. Na halipatikani hili isipokuwa kwa Muumin. Anapofikwa na jambo zuri hushukuru nayo ni kheri kwake, na anapofikwa na jambo lenye madhara husubiri nayo ni kheri kwake.” [Muslim]
Rejea pia Al-Baqarah (2:155) na Al-Hadiyd (57:22-23) kwenye faida nyenginezo.
[8] Amri Ya Kumtii Allaah (عزّ وجلّ) Na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم):
Amri ya kumtii Allaah (عزّ وجلّ) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na maonyo ya kutowatii yametajwa katika Qur-aan katika Aayah nyingi. Mojawapo ni Aayah ifuatayo:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَا تَوَلَّوْا عَنْهُ وَأَنتُمْ تَسْمَعُونَ﴿٢٠﴾
“Enyi walioamini! Mtiini Allaah na Rasuli Wake, na wala msijiepushe nazo (amri za Rasuli) na hali nyinyi mnasikia.” [Al-Anfaal (8:20)]
Rejea pia katika Suwrah hii At-Taghaabun (64:16). Kisha rejea Aal-‘Imraan (3:32), (3:132), An-Nisaa (4:13),(4:59), (4:69), (4:80), Al-Maaidah (5:92), Al-Anfaal (8:1), (8:46), An-Nuwr (24:52), (24:54), (24:56), Al-Ahzaab (33:36), (33:71), Muhammad (47:33), Al-Fat-h (48:10), (48:17), Al-Mujaadalah (58:13),
Na mojawapo wa Hadiyth ni ifuatayo:
حَدَّثَنَا عَبْدَانُ، أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ، عَنْ يُونُسَ، عَنِ الزُّهْرِيِّ، أَخْبَرَنِي أَبُو سَلَمَةَ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، أَنَّهُ سَمِعَ أَبَا هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " مَنْ أَطَاعَنِي فَقَدْ أَطَاعَ اللَّهَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ عَصَى اللَّهَ، وَمَنْ أَطَاعَ أَمِيرِي فَقَدْ أَطَاعَنِي، وَمَنْ عَصَى أَمِيرِي فَقَدْ عَصَانِي ".
Amesimulia Abuu Salamah Bin ‘Abdirrahmaan (رضي الله عنه): Amemsikia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Atakayenitii mimi basi hakika amemtii Allaah, na atakayeniasi, basi hakika amemuasi Allaah. Na atakayemtii liwali wangu basi hakika amenitii, na atakayemuasi liwali wangu basi hakika ameniasi mimi.” [Al-Bukhaariy na Muslim] Al-Bukhaariy katika Kitabu cha Ahkaam (93), Kitabu Cha Jihaad (56) (mna Hadiyth mbili).
[10] Fadhila Za Kutoa Mali Kwa Ajili Ya Allaah:
Rejea Al-Hadiyd (57:11) kwenye maelezo na rejea mbalimbali za maudhui hii.
الطَّلاق
065-Atw-Twalaaq
065-Atw-Twalaaq: Utangulizi Wa Suwrah [436]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا الْعِدَّةَ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ رَبَّكُمْ ۖ لَا تُخْرِجُوهُنَّ مِن بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخْرُجْنَ إِلَّا أَن يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ ۚ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّـهِ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ ۚ لَا تَدْرِي لَعَلَّ اللَّـهَ يُحْدِثُ بَعْدَ ذَٰلِكَ أَمْرًا﴿١﴾
1. Ee Nabiy! Mtakapowataliki wanawake, basi watalikini katika wakati wa eda (twahaarah) zao, na hesabuni barabara eda, na mcheni Allaah Rabb wenu. Msiwatowe katika nyumba zao, na wala wao wasitoke isipokuwa wakileta uchafu ulio bayana. Na hiyo ndio Mipaka ya Allaah. Na yeyote atakayevuka Mipaka ya Allaah, basi kwa yakini amedhulumu nafsi yake. Hujui; huenda Allaah Atatokezesha jambo jingine baada ya haya.[1]
فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ فَارِقُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِّنكُمْ وَأَقِيمُوا الشَّهَادَةَ لِلَّـهِ ۚ ذَٰلِكُمْ يُوعَظُ بِهِ مَن كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا﴿٢﴾
2. Na watakapokaribia kufikia muda wao (wa eda), basi wazuieni kwa wema, au farikianeni nao kwa wema, na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu, na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Allaah. Hivyo ndivyo anavyowaidhiwa anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Na yeyote anayemcha Allaah[2], basi Atamfanyia njia ya kutoka (shidani).
وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ ۚ وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ فَهُوَ حَسْبُهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بَالِغُ أَمْرِهِ ۚ قَدْ جَعَلَ اللَّـهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا﴿٣﴾
3. Na Atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii. Na yeyote anayetawakali kwa Allaah, basi Yeye Humtosheleza. Hakika Allaah Anatimiza Kusudio Lake. Allaah Amejaalia makadirio kwa kila kitu.[3]
وَاللَّائِي يَئِسْنَ مِنَ الْمَحِيضِ مِن نِّسَائِكُمْ إِنِ ارْتَبْتُمْ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَاثَةُ أَشْهُرٍ وَاللَّائِي لَمْ يَحِضْنَ ۚ وَأُولَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ ۚ وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مِنْ أَمْرِهِ يُسْرًا﴿٤﴾
4. Na wale wanawake wanaokoma hedhi miongoni mwa wanawake wenu, mkiwa mna shaka, basi eda yao ni miezi mitatu, pamoja na wale wanawake wasiopata hedhi. Na wenye mimba muda wao (wa eda) watakapozaa mimba zao.[4] Na yeyote anayemcha Allaah basi Atamjaalia wepesi katika jambo lake.
ذَٰلِكَ أَمْرُ اللَّـهِ أَنزَلَهُ إِلَيْكُمْ ۚ وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يُكَفِّرْ عَنْهُ سَيِّئَاتِهِ وَيُعْظِمْ لَهُ أَجْرًا﴿٥﴾
5. Hiyo ni Amri ya Allaah Amekuteremshieni. Na yeyote anayemcha Allaah, basi Atamfutia maovu yake na Atamuadhimishia ujira.
أَسْكِنُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ سَكَنتُم مِّن وُجْدِكُمْ وَلَا تُضَارُّوهُنَّ لِتُضَيِّقُوا عَلَيْهِنَّ ۚ وَإِن كُنَّ أُولَاتِ حَمْلٍ فَأَنفِقُوا عَلَيْهِنَّ حَتَّىٰ يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ ۚ فَإِنْ أَرْضَعْنَ لَكُمْ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ ۖ وَأْتَمِرُوا بَيْنَكُم بِمَعْرُوفٍ ۖ وَإِن تَعَاسَرْتُمْ فَسَتُرْضِعُ لَهُ أُخْرَىٰ﴿٦﴾
6. Wawekeni wanawake (mliowataliki) kwenye majumba mnayokaa nyinyi kwa kadiri ya kipato chenu, na wala msiwadhuru ili muwatie dhiki. Na wakiwa ni wenye mimba, basi wapeni matumizi mpaka wazae mimba zao. Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao. Na shaurianeni baina yenu kwa wema. Na mkifanyiana uzito, basi amnyonyeshee mwanamke mwengine.
لِيُنفِقْ ذُو سَعَةٍ مِّن سَعَتِهِ ۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ فَلْيُنفِقْ مِمَّا آتَاهُ اللَّـهُ ۚ لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا مَا آتَاهَا ۚ سَيَجْعَلُ اللَّـهُ بَعْدَ عُسْرٍ يُسْرًا﴿٧﴾
7. Ili mwenye wasaa agharimu kwa wasaa wake, na aliyebaniwa riziki yake, basi agharimie katika kile Alichompa Allaah.[5] Allaah Haikalifishi nafsi yeyote ile isipokuwa kwa kile Alichoipa. Allaah Atajaalia baada ya ugumu kuwa wepesi.
وَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ عَتَتْ عَنْ أَمْرِ رَبِّهَا وَرُسُلِهِ فَحَاسَبْنَاهَا حِسَابًا شَدِيدًا وَعَذَّبْنَاهَا عَذَابًا نُّكْرًا﴿٨﴾
8. Na miji mingapi imeasi Amri ya Rabb wake na Rusuli Wake, basi Tuliihisabia hisabu shadidi, na Tukaiadhibu adhabu kali kabisa isiyovumilika.
فَذَاقَتْ وَبَالَ أَمْرِهَا وَكَانَ عَاقِبَةُ أَمْرِهَا خُسْرًا﴿٩﴾
9. Ikaonja maovu ya mambo yake, na ikawa hatima ya mambo yake kuwa ni khasara.
أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ الَّذِينَ آمَنُوا ۚ قَدْ أَنزَلَ اللَّـهُ إِلَيْكُمْ ذِكْرًا﴿١٠﴾
10. Allaah Amewaandalia adhabu shadidi, basi mcheni Allaah enyi wenye akili mlioamini! Allaah Amekwishakuteremshieni Ukumbusho.
رَّسُولًا يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِ اللَّـهِ مُبَيِّنَاتٍ لِّيُخْرِجَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۚ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ وَيَعْمَلْ صَالِحًا يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ قَدْ أَحْسَنَ اللَّـهُ لَهُ رِزْقًا﴿١١﴾
11. Ni Rasuli anakusomeeni Aayaat za Allaah zinazobainisha, ili kuwatoa wale walioamini na wakatenda mema kutoka kwenye viza kuingia katika Nuru.[6] Na yeyote anayemwamini Allaah na akatenda mema, Atamuingiza Jannaat zipitazo chini yake mito wadumu humo abadi. Allaah Amekwishamfanyia rizki nzuri kabisa.
اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ وَمِنَ الْأَرْضِ مِثْلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ الْأَمْرُ بَيْنَهُنَّ لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ وَأَنَّ اللَّـهَ قَدْ أَحَاطَ بِكُلِّ شَيْءٍ عِلْمًا﴿١٢﴾
12. Allaah ni Yule Aliyeumba mbingu saba na katika ardhi mfano wa hizo[7], inateremka amri baina yao ili mjue kwamba Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza, na kwamba Allaah Amekwishakizunguka kila kitu kwa Ujuzi (Wake).
[1] Talaka:
Aayah hii namba (1) Atw-Twalaaq hadi Aayah namba (7) zinahusiana na mas-ala ya talaka, eda ya talaka na ya mfiwa, ambayo hukmu zake zimetajwa pia katika Suwrah Al-Baqarah kuanzia Aayah namba (226) hadi Aayah namba (237). Na pia (2:241). Rejea pia Al-Ahzaab (33:49).
Tafsiyr ya Aayah:
Ee Nabiy! Pindi mnapotaka, wewe na Waumini, kuwapa talaka wake zenu, basi wapeni talaka wakiwa kwenye hali ya kukabili kipindi cha wao kukaa eda- yaani kwenye hali ya usafi ambao hakukupatikana kuingiliwa, au katika hali ya mimba iliyo wazi- na mshike hesabu ya eda, mpate kujua muda wa kuwarejea iwapo mtataka kuwarejea, na muogopeni Allaah (سبحانه وتعالى) Rabb wenu. Wala msiwatoe wanawake waliopewa talaka kwenye majumba wanayokaa mpaka eda lao limalizike, nalo ni hedhi tatu kwa asiyekuwa mdogo (asiyeingia damuni) na si kwa aliyekata tamaa ya kuingia damuni (kwa uzee) wala mwenye mimba. Na haifai kwa wanawake hao kutoka majumbani mwao wao wenyewe isipokuwa watakapofanya kitendo kiovu cha waziwazi kama vile uzinifu. Na hizo ndizo hukumu za Allaah Alizozipitisha kwa Waja Wake. Na Mwenye kuzikiuka hukumu za Allaah, basi huyo amejidhulimu nafsi yake na ameipeleka mahali pa maangamivu. Hujui, ee mtoaji talaka, kwamba Allaah huenda, baada ya talaka hiyo, Akaleta jambo usilolitazamia ukaja ukamrudia. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Na Hadiyth ifuatayo imethibitisha kuhusu mwanamke kutalikiwa akiwa katika twahara:
حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ بُكَيْرٍ، حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، قَالَ حَدَّثَنِي عُقَيْلٌ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي سَالِمٌ، أَنَّ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عُمَرَ ـ رضى الله عنهما ـ أَخْبَرَهُ أَنَّهُ، طَلَّقَ امْرَأَتَهُ وَهْىَ حَائِضٌ، فَذَكَرَ عُمَرُ لِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَتَغَيَّظَ فِيهِ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ قَالَ " لِيُرَاجِعْهَا ثُمَّ يُمْسِكْهَا حَتَّى تَطْهُرَ، ثُمَّ تَحِيضَ فَتَطْهُرَ، فَإِنْ بَدَا لَهُ أَنْ يُطَلِّقَهَا فَلْيُطَلِّقْهَا طَاهِرًا قَبْلَ أَنْ يَمَسَّهَا فَتِلْكَ الْعِدَّةُ كَمَا أَمَرَهُ اللَّهُ ".
Amesimulia Saalim (رضي الله عنه): ‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله عنهما) amemwambia kuwa alimtaliki mkewe akiwa katika hedhi, kwa hiyo, ‘Umar (رضي الله عنه) akamtajia hilo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikasirika sana kwa jambo hilo, kisha akasema: “Ni lazima (Ibn ‘Umar) amrejee, kisha amuweke kama mkewe mpaka atwahirike, kisha aingie tena katika hedhi kisha atwahirike. Baada ya hapo, ikiwa anataka kumtaliki anaweza kufanya hivyo akiwa mkewe yuko katika hali ya twahara kabla ya kumgusa. Hiyo ndio eda kama Alivyoamrisha Allaah.”
Bonyeza viungo viungo vifuatavyo kupata faida:
07-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa Talaka [437]
[2] Taqwa:
Rejea Al-Baqarah (2:2) kwenye maana ya taqwa. Rejea pia viungo vifuatavyo kuhusu maamrisho ya taqwa, faida na fadhila zake:
[3] Anayetawakkal Kwa Allaah, Allaah Atamtosheleza Kwa Kila Kitu:
عن ابنِ عباسٍ رضي الله عنهما، قَالَ: كنت خلف النَّبيّ صلى الله عليه وسلم يومًا، فَقَالَ: ((يَا غُلامُ، إنِّي أعلّمُكَ كَلِمَاتٍ: احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ تُجَاهَكَ، إِذَا سَألْتَ فَاسأَلِ الله، وإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ باللهِ. وَاعْلَمْ: أنَّ الأُمَّةَ لَوْ اجْتَمَعَتْ عَلَى أنْ يَنْفَعُوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبهُ اللهُ لَكَ، وَإِن اجتَمَعُوا عَلَى أنْ يَضُرُّوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَضُرُّوكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللهُ عَلَيْكَ، رُفِعَتِ الأَقْلاَمُ وَجَفَّتِ الصُّحفُ)). رواه الترمذي، وَقالَ: ((حديث حسن صحيح)).
وفي رواية غيرِ الترمذي: ((احْفَظِ الله تَجِدْهُ أَمَامَكَ، تَعرَّفْ إِلَى اللهِ في الرَّخَاءِ يَعْرِفكَ في الشِّدَّةِ، وَاعْلَمْ: أنَّ مَا أَخْطَأكَ لَمْ يَكُنْ لِيُصِيبكَ، وَمَا أصَابَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُخْطِئَكَ، وَاعْلَمْ: أنَّ النَّصْرَ مَعَ الصَّبْرِ، وَأَنَّ الفَرَجَ مَعَ الكَرْبِ، وَأَنَّ مَعَ العُسْرِ يُسْرًا))
Amesimulia ‘Abdullaah Bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Siku moja nilikuwa (juu ya mnyama) nyuma ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaniambia: “Ee kijana, mimi nitakufundisha maneno: Mhifadhi Allaah Naye Atakuhifadhi. Mhifadhi Allaah utamkuta yupo mbele yako. Unapoomba, muombe Allaah. Unapotaka msaada, mtake Allaah. Fahamu kuwa, lau ummah (wote) utajikusanya ili wakunufaishe kwa jambo, basi hawataweza kukunufaisha ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah; na wakijumuika ili wakudhuru kwa jambo, hawataweza kukudhuru ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah. Kalamu zimeshasimama na karatasi zimeshakauka.” [At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyh]
Riwaayah nyingine isiyokuwa ya At-Tirmidhiy imesema:
“Mhifadhi Allaah utamkuta Yupo mbele yako. Mjue Allaah katika raha Naye Atakujua katika shida. Ujue kuwa, lililokukosa halikuwa ni lenye kukupata, na lililokusibu halikuwa ni lenye kukukosa. Ujue kuwa nusura ipo pamoja na subira, faraja ipo pamoja na dhiki, na kwenye uzito kuna wepesi.”
Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida nyenginezo:
[4] Eda Ya Mwanamke Mwenye Mimba Na Aliyefiwa Na Mumewe:
Eda ni muda wa kusubiri ambapo mwanamke haruhusiwi kuolewa, baada ya kifo cha mumewe au kuachika.
Kwa mwanamke mwenye mimba, katika hali yoyote iwe ni kifo cha mumewe au kuachika, eda yake ni baada ya kuzaliwa mtoto. Kwa mfano ameachika au mumewe amefariki leo, na siku inayofuata akajifungua mtoto, eda yake huisha kwa kuzaliwa mtoto. Hapo anaruhusiwa kuolewa wakati wowote, lakini kwa muda wote ambapo atakuwa yupo katika nifaas hatoruhusiwa kuingiliwa na mumewe.
Na Hadiyth ifuatayo imethibitisha:
حَدَّثَنَا سَعْدُ بْنُ حَفْصٍ، حَدَّثَنَا شَيْبَانُ، عَنْ يَحْيَى، قَالَ أَخْبَرَنِي أَبُو سَلَمَةَ، قَالَ جَاءَ رَجُلٌ إِلَى ابْنِ عَبَّاسٍ وَأَبُو هُرَيْرَةَ جَالِسٌ عِنْدَهُ فَقَالَ أَفْتِنِي فِي امْرَأَةٍ وَلَدَتْ بَعْدَ زَوْجِهَا بِأَرْبَعِينَ لَيْلَةً. فَقَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ آخِرُ الأَجَلَيْنِ. قُلْتُ أَنَا وَأُولاَتُ الأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَنْ يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ قَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ أَنَا مَعَ ابْنِ أَخِي ـ يَعْنِي أَبَا سَلَمَةَ ـ فَأَرْسَلَ ابْنُ عَبَّاسٍ غُلاَمَهُ كُرَيْبًا إِلَى أُمِّ سَلَمَةَ يَسْأَلُهَا فَقَالَتْ قُتِلَ زَوْجُ سُبَيْعَةَ الأَسْلَمِيَّةِ وَهْىَ حُبْلَى، فَوَضَعَتْ بَعْدَ مَوْتِهِ بِأَرْبَعِينَ لَيْلَةً فَخُطِبَتْ فَأَنْكَحَهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَكَانَ أَبُو السَّنَابِلِ فِيمَنْ خَطَبَهَا.
Amesimulia Yahya (رضي الله عنه): Abu Salamah alinipasha khabari kwamba, alikuja mtu kwa Ibn ‘Abbaas na Abu Hurayrah (رضي الله عنهما) walikuwa wamekaa mbele yake; mtu yule akasema: Nipe fatwa kuhusu mwanamke aliyejifungua baada ya kufariki mumewe kwa siku arubaini. Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) akasema: Eda yake mwisho ni mihula miwili. Mimi (Abu Salamah) nikasema:
وَأُولَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ
“Na wenye mimba muda wao (wa eda) watakapozaa mimba zao.”
[Atw-Twalaaq (65:4)]. Na Abu Hurayrah (رضي الله عنه) akasema: Mimi niko pamoja na mtoto wa ndugu yangu (anakusudia Abu Salamah). Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) akamtuma kijana wake kwa Ummu Salamah na kumuuliza. Akajibu: Ameuawa mume wa Subay‘ah
Al-Aslamiyyah, akiwa mja mzito, akajifungua baada ya kifo chake kwa siku arubaini, akaposwa. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuozesha, na Abu Sanaabil alikuwa miongoni mwa waliomposa.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Tafsiyr (65)]
Na bonyeza viungo vifuatavyo:
[5] Matumizi Katika Kipindi Cha Eda:
Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida:
[6] Kutolewa Kwenye Viza Na Kuingiza Katika Nuru:
Rejea Suwrah Ibraahiym (!4:1) kwenye uchambuzi na rejea mbalimbali za kuhusu maudhui hii.
[7] Mbingu Saba Na Ardhi Saba:
Allaah (سبحانه وتعالى) Amethibitisha kuumba mbingu saba katika Kauli Zake kadhaa kwenye Qur-aan. Miongoni mwazo ni Kauli Yake:
الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا ۖ مَّا تَرَىٰ فِي خَلْقِ الرَّحْمَـٰنِ مِن تَفَاوُتٍ ۖ فَارْجِعِ الْبَصَرَ هَلْ تَرَىٰ مِن فُطُورٍ﴿٣﴾
“Ambaye Ameumba mbingu saba matabaka. Hutaona katika Uumbaji wa Ar-Rahmaan tofauti yoyote. Basi rejesha jicho. Je, unaona mpasuko wowote ule?” [Al-Mulk (67:3)]
Rejea pia Al-Baqarah (2:29), Al-Israa (17:44), Al-Muuminuwn (23:86) Fusw-Swilat (41:12), Nuwh (71:15).
Na pia imethibitishwa katika Hadiyth zilizoelezea safari ya muujiza ya Al-Israa Wal-Mi’raaj. Rejea Al-Israa (17:1).
Na kuhusu ardhi saba imethibitiwha katika Hadiyth ifuatayo:
حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، أَخْبَرَنَا ابْنُ عُلَيَّةَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ أَبِي كَثِيرٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِبْرَاهِيمَ بْنِ الْحَارِثِ، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، كَانَتْ بَيْنَهُ وَبَيْنَ أُنَاسٍ خُصُومَةٌ فِي أَرْضٍ، فَدَخَلَ عَلَى عَائِشَةَ فَذَكَرَ لَهَا ذَلِكَ، فَقَالَتْ يَا أَبَا سَلَمَةَ اجْتَنِبِ الأَرْضَ، فَإِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " مَنْ ظَلَمَ قِيدَ شِبْرٍ طُوِّقَهُ مِنْ سَبْعِ أَرَضِينَ ".
Amesimulia Muhammad Bin Ibraahym Al-Haarith (رضي الله عنه): Kutoka kwa Abu Salamah bin ‘Abdir-Rahman ambaye alikuwa na utesi baina yake na baadhi ya watu kuhusu kipande cha ardhi, hivyo akaenda kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) na kumwambia kuhusu hilo. ‘Aaishah (رضي الله عنها) akamwambia: Ee Abu Salamah! Jiepushe na ardhi hiyo, kwani Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kudhulumu shubiri moja ya ardhi, hakika Allaah Atamzingirisha na ardhi saba shingoni mwake Siku ya Qiyaamah.” [Al-Bukhaari na Muslim]
التَّحْرِيم
066-At-Tahriym
066-At-Tahriym: Utangulizi Wa Suwrah [453]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ لِمَ تُحَرِّمُ مَا أَحَلَّ اللَّـهُ لَكَ ۖ تَبْتَغِي مَرْضَاتَ أَزْوَاجِكَ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿١﴾
1. Ee Nabiy! Kwa nini unaharamisha kile Alichokuhalalishia Allaah? Unataka kuwaridhisha wake zako! Na na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[1]
قَدْ فَرَضَ اللَّـهُ لَكُمْ تَحِلَّةَ أَيْمَانِكُمْ ۚ وَاللَّـهُ مَوْلَاكُمْ ۖ وَهُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ﴿٢﴾
2. Allaah hakika Amekuwekeeni shariy’ah ya ukomboaji wa viapo vyenu, na Allaah Ni Mawlaa[2] wenu, Naye Ndiye Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
وَإِذْ أَسَرَّ النَّبِيُّ إِلَىٰ بَعْضِ أَزْوَاجِهِ حَدِيثًا فَلَمَّا نَبَّأَتْ بِهِ وَأَظْهَرَهُ اللَّـهُ عَلَيْهِ عَرَّفَ بَعْضَهُ وَأَعْرَضَ عَن بَعْضٍ ۖ فَلَمَّا نَبَّأَهَا بِهِ قَالَتْ مَنْ أَنبَأَكَ هَـٰذَا ۖ قَالَ نَبَّأَنِيَ الْعَلِيمُ الْخَبِيرُ﴿٣﴾
3. Na pale Nabiy alipompa mmoja wa wake zake jambo la siri, na huyo mke alipoipasha habari na Allaah Akamdhihirishia (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم), akataarifu baadhi yake na akaacha nyingine. Basi alipomjulisha hayo, akasema: Nani aliyekujulisha haya? Akasema: Amenijulisha Mjuzi wa yote, Mwenye Ujuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
إِن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا ۖ وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ فَإِنَّ اللَّـهَ هُوَ مَوْلَاهُ وَجِبْرِيلُ وَصَالِحُ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ بَعْدَ ذَٰلِكَ ظَهِيرٌ﴿٤﴾
4. Ikiwa nyinyi wawili mtatubia kwa Allaah (basi ni kheri kwenu), kwani kwa hakika nyoyo zenu zimeelemea (kwa yanayomchukiza Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم). Na mkisaidiana dhidi yake, basi hakika Allaah Ndiye Mawlaa wake na Jibriyl na Waumini wema, na zaidi ya hayo, Malaika pia watasaidia.[3]
عَسَىٰ رَبُّهُ إِن طَلَّقَكُنَّ أَن يُبْدِلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِّنكُنَّ مُسْلِمَاتٍ مُّؤْمِنَاتٍ قَانِتَاتٍ تَائِبَاتٍ عَابِدَاتٍ سَائِحَاتٍ ثَيِّبَاتٍ وَأَبْكَارًا﴿٥﴾
5. Akikutalikini, asaa Rabb Wake Akambadilishia wake bora kuliko nyinyi; Waislamu, Waumini, watiifu na wanyenyekevu, wanaotubia, wenye kufanya ibaada, wanaofunga Swiyaam[4] au wanaohajiri kwa ajili ya Allaah, wajane, na walio bikra.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ﴿٦﴾
6. Enyi walioamini! Jikingeni nafsi zenu pamoja na ahli zenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanaulinda Malaika washupavu wasio na huruma, shadidi, hawamuasi Allaah kwa yale Anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa.[5]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَعْتَذِرُوا الْيَوْمَ ۖ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٧﴾
7. Enyi waliokufuru! Msitoe nyudhuru Leo! Hakika mtalipwa yake mliyokuwa mkiyafanya.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّـهِ تَوْبَةً نَّصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُكَفِّرَ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يَوْمَ لَا يُخْزِي اللَّـهُ النَّبِيَّ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ ۖ نُورُهُمْ يَسْعَىٰ بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٨﴾
8. Enyi walioamini! Tubieni kwa Allaah tawbah ya nasuha[6] (kwelikweli), asaa Rabb wenu Akakufutieni maovu yenu, na Akakuingizeni Jannaat zipitazo chini yake mito. Siku ambayo Allaah Hatomfedhehesha Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na wale walioamini pamoja naye. Nuru yao itatembea mbele yao na kuliani mwao, watasema: Rabb wetu! Tutimizie Nuru yetu, na Tughufurie, hakika Wewe juu ya kila kitu Ni Muweza.
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ جَاهِدِ الْكُفَّارَ وَالْمُنَافِقِينَ وَاغْلُظْ عَلَيْهِمْ ۚ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿٩﴾
9. Ee Nabiy! Pambana na makafiri na wanafiki kwa Jihaad (ya vita na hoja), na kuwa mshupavu kwao, na makazi yao ni Jahannam. Na ubaya ulioje mahali pa kuishia!
ضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ كَفَرُوا امْرَأَتَ نُوحٍ وَامْرَأَتَ لُوطٍ ۖ كَانَتَا تَحْتَ عَبْدَيْنِ مِنْ عِبَادِنَا صَالِحَيْنِ فَخَانَتَاهُمَا فَلَمْ يُغْنِيَا عَنْهُمَا مِنَ اللَّـهِ شَيْئًا وَقِيلَ ادْخُلَا النَّارَ مَعَ الدَّاخِلِينَ﴿١٠﴾
10. Allaah Amewapigia mfano wale waliokufuru mke wa Nuwh na mke wa Luwtw. Wote wawili walikuwa chini ya waja wawili miongoni mwa Waja Wetu Swalihina, wakawafanyia hiana (katika Dini), basi (Manabii hao) hawakuwafaa chochote mbele ya Allaah, na ikasemwa: Ingieni motoni pamoja na wenye kuingia.
وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا لِّلَّذِينَ آمَنُوا امْرَأَتَ فِرْعَوْنَ إِذْ قَالَتْ رَبِّ ابْنِ لِي عِندَكَ بَيْتًا فِي الْجَنَّةِ وَنَجِّنِي مِن فِرْعَوْنَ وَعَمَلِهِ وَنَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ﴿١١﴾
11. Na Allaah Amewapigia mfano wale walioamini mke wa Firawni, aliposema: Rabb wangu! Nijengee nyuma Kwako kwenye Jannah, na Niokoe na Firawni na vitendo vyake, na Niokoe na watu madhalimu.[7]
وَمَرْيَمَ ابْنَتَ عِمْرَانَ الَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهِ مِن رُّوحِنَا وَصَدَّقَتْ بِكَلِمَاتِ رَبِّهَا وَكُتُبِهِ وَكَانَتْ مِنَ الْقَانِتِينَ﴿١٢﴾
12. Na Maryam binti wa ‘Imraan ambaye amehifadhi tupu yake, Tukampulizia humo (katika nguo yake) kupitia kwa Ruwh Wetu (Jibriyl), na akasadikisha Maneno ya Rabb wake, na Vitabu Vyake, na akawa miongoni mwa watiifu na wanyenyekevu.
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Kuanzia Aayah hii ya kwanza hadi Aayah namba (5), bonyeza kiungo kifuatacho:
Na pia rejea Al-Ahzaab (33:28) kwenye Sababu za Kuteremshwa Aayah zinazohusiana na za Suwrah hii ya At-Tahriym.
[2] Mawlaa: Mlinzi, Msaidizi.
Mawlaa ina maana nyingi: Mwenye kumiliki, msaidizi, mtu wa karibu kabisa, mtu aliyeacha mtumwa huru, na aliyeachiliwa huru, na maana ya mnusuruji. Lakini haipasi mja kumwita bwana wake Mawlaana kwa sababu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amekataza hivyo katika Hadiyth iliyopokelewa na Imaam Muslim. [Imaam Ibn Baaz – Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb]
Na katika Qur-aan imetajwa kwa maana mbalimbali na zote zinategemea muktadha yake, kwani hata moto umetajwa kwa maana ya mawlaa, Rejea Al-Hadiyd (57:15).
Maana nyenginezo katika Qur-aan ni sayyid (bwana anayeendesha mambo ya mtu), mnusuruji, rafiki mwandani, mpenzi wa karibu, mlinzi, msaidizi, mwenye kumiliki, na kama alivyotaja Imaam Ibn Baaz hapo juu.
Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake.
[3] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Aayah hii namba (4) na namba (5), bonyeza kiungo kifuatacho:
066-Asbaabun-Nuzuwl: At-Tahriym Aayah 4-5: إِن تَتُوبَا إِلَى اللَّـهِ فَقَدْ صَغَتْ قُلُوبُكُمَا [455]
Rejea pia Al-Ahzaab (33:53) kwenye Sababu ya Kuteremshwa Aayah inayohusiana na za Suwrah hii ya At-Tahriym.
[5] Muumini Kujikinga Na Moto Pamoja Na Ahli Zake:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anatoa tahadharisho muhimu kabisa kwa Muumini kujikinga na moto pamoja na ahli zake. Na kujikinga na moto kutapatikana kwa kufuata na kutekeleza Amri Zake Allaah (سبحانه وتعالى) pamoja na amri za Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na kujiepusha na makatazo yao. Miongoni mwa Kauli Zake nyengine Allaah (سبحانه وتعالى) za matahadhrisho ambayo yamejumuishwa na tahadharisho la moto wa Jahannam ni Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) ifuatayo:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُم بَيْنَكُم بِالْبَاطِلِ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً عَن تَرَاضٍ مِّنكُمْ ۚ وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا ﴿٢٩﴾ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ عُدْوَانًا وَظُلْمًا فَسَوْفَ نُصْلِيهِ نَارًا ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا ﴿٣٠﴾
“Enyi walioamini! Msiliane mali zenu kwa ubatwilifu, isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana baina yenu. Wala msijiue. Hakika Allaah Ni Mwenye Kuwarehemuni. Na atakayefanya hivyo kwa uadui na dhulma, basi Tutamuingiza motoni. Na hilo kwa Allaah ni jepesi mno.” [An-Nisaa (5:29-30)]
Na miongoni mwa Hadiyth, ni ifuatayo ya amrisho la kutoa swadaqa au kusema maneno mazuri ambayo yanasababisha pia kujikinga na moto:
عَنْ عَدِيِّ بْنِ حَاتِمٍ (رضي الله عنه) قَالَ: قَال رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((اتَّقُوا النَّارَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ فَإِنْ لَمْ تَجِدْ فَبِكَلِمَةٍ طَيِّبَةٍ)) متفق عليه
Amesimulia ‘Adiyy bin Haatim (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ogopeni moto japo kwa (kutoa swadaqa) nusu tende, na usipopata basi kwa (kutamka) neno jema.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na njia mojawapo kubwa ya kujiepusha na moto ni kutimiza Swalaah pamoja na kuwaamrishwa ahli pia kusimamisha nguzo kuu hii ya Swalaah. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَأْمُرْ أَهْلَكَ بِالصَّلَاةِ وَاصْطَبِرْ عَلَيْهَا ۖ لَا نَسْأَلُكَ رِزْقًا ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكَ ۗ وَالْعَاقِبَةُ لِلتَّقْوَىٰ ﴿١٣٢﴾
“Na amrisha ahli zako Swalaah, na dumisha uvumilivu juu ya mazito yake. Hatukukalifishi riziki bali Sisi Ndio Tunaokuruzuku. Na hatima njema ni kwa wenye taqwa.” [Twaahaa (20:132)]
Rejea huko kupata faida nyenginezo zinazohusiana na maudhui hii ya kuamrisha ahli Swalaah.
[6] Tawbah Ya Nasuha:
Ni kutubia kikwelikweli kwa Allaah (عزّ وجلّ) kutokana na madhambi na Tawbah hii ya kikwelikweli ina mashari yake yafuatayo: (i) Kuomba maghfirah (ii) Kuacha hayo maasi (iii) Kujuta (iv) Kuweka niya (azimio) kutokurudia tena maasi hayo (v) Kama mtu amedhulumu haki ya mwengine, basi ni kuirudisha hiyo haki.
Rejea Rejea Huwd (11:3) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali. Pia An-Nisaa (4:110), Nuwh (71:10), Adh-Dhaariyaat (51:18).
Bonyeza pia viungo vifuatavyo kupata faida za kuhusu maudhui ya Tawbah:
19-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Kitabu Cha: Istighfaar (Kuomba Maghfirah) - كِتابُ الإسْتِغْفار [456]
Tawbah: Hukmu Na Fadhila Zake [337]
[7] Wanawake Watano Waliobora Kabisa Ulimwenguni:
Rejea Aal-‘Imraan (3:42) kwenye Hadiyth ambayo ametajwa Aasiyah mke wa Firawni na Maryam mama yake Nabiy Iysaa (عليه السّلام) ambao wametajwa katika Aayah mbili hizi (11-12) za Suwrah hii ya Atw-Twalaaq. Na katika Suwrah Aal-‘Imraan akatajwa pia ‘Aaishah (رضي الله عنها).
Na jumla ya wanawake bora kabisa ulimwenguni waliosifiwa kufikia daraja la ukamilifu ni watano, nao ni: (i) Aasiyah (aliyekuwa mke wa Firawni). (ii) Maryam mama yake Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام). (iii) Khadiyjah Bint Khuwaylid. (iv) Faatwimah Bint Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). (v) ‘Aaishah mke wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).
Na katika Hadiyth ifuatayo, wametajwa tena Aasiyah na Maryam, na pia ametajwa Khadiyjah Bint Khuwaylid (رضي الله عنها) na Faatwimah bint Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم):
عَنْ أَنَسٍ، رضى الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " حَسْبُكَ مِنْ نِسَاءِ الْعَالَمِينَ مَرْيَمُ ابْنَةُ عِمْرَانَ وَخَدِيجَةُ بِنْتُ خُوَيْلِدٍ وَفَاطِمَةُ بِنْتُ مُحَمَّدٍ وَآسِيَةُ امْرَأَةُ فِرْعَوْنَ " . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ صَحِيحٌ .
Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wanakutosheleza katika wanawake wa ulimwengu: Maryam bint ‘Imraan, Khadiyjah bint Khuwaylid Faatwimah bint Muhammad na Aasiyah mke wa Firawni.” [At-Tirmidhiy na amesema: Hii ni Hadiyth Swahiyh na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy Uk au namba (3878)]
Rejea pia Suwrah Maryam (19:16) kwenye faida nyenginezo kuhusu mwanamke huyu mtukufu.
الْمُلْك
067-Al-Mulk
067-Al-Mulk: Utangulizi Wa Suwrah [462]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿١﴾
1. Amebarikika Ambaye Mkononi Mwake umo Ufalme, Naye juu ya kila kitu Ni Muweza.[1]
الَّذِي خَلَقَ الْمَوْتَ وَالْحَيَاةَ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْغَفُورُ﴿٢﴾
2. Ambaye Ameumba mauti na uhai ili Akujaribuni ni nani kati yenu mwenye amali nzuri zaidi. Naye Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwingi wa Kughufuria.
الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا ۖ مَّا تَرَىٰ فِي خَلْقِ الرَّحْمَـٰنِ مِن تَفَاوُتٍ ۖ فَارْجِعِ الْبَصَرَ هَلْ تَرَىٰ مِن فُطُورٍ﴿٣﴾
3. Ambaye Ameumba mbingu saba matabaka. Hutaona katika Uumbaji wa Ar-Rahmaan tofauti yoyote. Basi rejesha jicho. Je, unaona mpasuko wowote ule?
ثُمَّ ارْجِعِ الْبَصَرَ كَرَّتَيْنِ يَنقَلِبْ إِلَيْكَ الْبَصَرُ خَاسِئًا وَهُوَ حَسِيرٌ﴿٤﴾
4. Kisha rejesha jicho tena na tena, litakupindukia jicho likiwa limehizika, nalo limenyong’onyea.
وَلَقَدْ زَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِمَصَابِيحَ وَجَعَلْنَاهَا رُجُومًا لِّلشَّيَاطِينِ ۖ وَأَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابَ السَّعِيرِ﴿٥﴾
5. Na kwa yakini Tumeipamba mbingu ya dunia kwa mataa, na Tukazifanya kuwa ni makombora ya kuwavurumishia mashaytwaan,[2] na Tumewaandalia adhabu ya moto uliowashwa vikali mno.
وَلِلَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿٦﴾
6. Na wale waliomkufuru Rabb wao wana adhabu ya Jahannam. Ni ubaya ulioje mahali pa kuishia!
إِذَا أُلْقُوا فِيهَا سَمِعُوا لَهَا شَهِيقًا وَهِيَ تَفُورُ﴿٧﴾
7. Watakapotupwa humo, watasikia sauti yake mbaya ya kuchukiza mno, nao huku unafoka.
تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ الْغَيْظِ ۖ كُلَّمَا أُلْقِيَ فِيهَا فَوْجٌ سَأَلَهُمْ خَزَنَتُهَا أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَذِيرٌ﴿٨﴾
8. Unakaribia kupasuka kwa ghadhabu. Kila wanapotupwa humo kundi, walinzi wake watawauliza: Je, hajakufikieni mwonyaji yeyote?
قَالُوا بَلَىٰ قَدْ جَاءَنَا نَذِيرٌ فَكَذَّبْنَا وَقُلْنَا مَا نَزَّلَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا فِي ضَلَالٍ كَبِيرٍ﴿٩﴾
9. Watasema: Sivyo hivyo! Bali kwa yakini alitujia mwonyaji, lakini tulikadhibisha, na tukasema: Allaah Hakuteremsha kitu chochote, nyinyi si chochote isipokuwa mumo katika upotofu mkubwa.[3]
وَقَالُوا لَوْ كُنَّا نَسْمَعُ أَوْ نَعْقِلُ مَا كُنَّا فِي أَصْحَابِ السَّعِيرِ﴿١٠﴾
10. Na watasema: Lau tungelikuwa tunasikiliza au tunatia akilini, tusingelikuwa katika watu wa motoni.
فَاعْتَرَفُوا بِذَنبِهِمْ فَسُحْقًا لِّأَصْحَابِ السَّعِيرِ﴿١١﴾
11. Basi watakiri madhambi yao, na (wataambiwa): Tokomeeni mbali watu wa motoni.
إِنَّ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِالْغَيْبِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ﴿١٢﴾
12. Hakika wale wanaomkhofu Rabb wao wakiwa pweke mbali na macho ya watu, watapata maghfirah na ujira mkubwa.[4]
وَأَسِرُّوا قَوْلَكُمْ أَوِ اجْهَرُوا بِهِ ۖ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ﴿١٣﴾
13. Na fanyeni siri kauli zenu, au zidhihirisheni, hakika Yeye Ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.[5]
أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ﴿١٤﴾
14. Kwani Hajui Yule Aliyeumba! Na hali Yeye Ni Mwenye Kudabiri mambo kwa Ulatifu, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri!
هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ ذَلُولًا فَامْشُوا فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُوا مِن رِّزْقِهِ ۖ وَإِلَيْهِ النُّشُورُ﴿١٥﴾
15. Yeye Ndiye Aliyeidhalilisha ardhi kwa ajili yenu, basi nendeni katika pande zake na kuleni katika Riziki Yake, na Kwake ndio kufufuliwa.
أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ﴿١٦﴾
16. Je, mnadhani mko katika amani na (Allaah) Aliyeko mbinguni[6] kwamba Hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika?
أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ﴿١٧﴾
17. Au mnadhani mko katika amani na (Allaah) Aliyeko mbinguni kwamba Hatokutumieni tufani ya mawe? Basi mtajua vipi Maonyo Yangu!
وَلَقَدْ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ﴿١٨﴾
18. Na kwa yakini walikadhibisha wale walio kabla yao, basi ilikuwaje Kukana Kwangu (kwa adhabu ya maangamizi)?![7]
أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَى الطَّيْرِ فَوْقَهُمْ صَافَّاتٍ وَيَقْبِضْنَ ۚ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا الرَّحْمَـٰنُ ۚ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ بَصِيرٌ﴿١٩﴾
19. Je, hawawaoni ndege juu yao, wakiwa wanakunjua na kukunja (mbawa)! Hakuna anayewashikilia isipokuwa Ar-Rahmaan. Hakika Yeye Ni Mwenye Kuona kila kitu.
أَمَّنْ هَـٰذَا الَّذِي هُوَ جُندٌ لَّكُمْ يَنصُرُكُم مِّن دُونِ الرَّحْمَـٰنِ ۚ إِنِ الْكَافِرُونَ إِلَّا فِي غُرُورٍ﴿٢٠﴾
20. Au ni lipi hilo jeshi lenu linaloweza kukunusuruni badala ya Ar-Rahmaan? Makafiri hawamo isipokuwa katika ghururi.
أَمَّنْ هَـٰذَا الَّذِي يَرْزُقُكُمْ إِنْ أَمْسَكَ رِزْقَهُ ۚ بَل لَّجُّوا فِي عُتُوٍّ وَنُفُورٍ﴿٢١﴾
21. Au ni nani huyu ambaye atakuruzukuni ikiwa (Allaah) Atazuia Riziki Yake? Bali wanang’ang’ania kwenye ufidhuli na kukimbilia mbali kwa chuki.
أَفَمَن يَمْشِي مُكِبًّا عَلَىٰ وَجْهِهِ أَهْدَىٰ أَمَّن يَمْشِي سَوِيًّا عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٢٢﴾
22. Je, yule anayekwenda akiwa gubigubi juu ya uso wake ameongoka zaidi, au yule anayekwenda sawasawa kuelekea njia iliyonyooka?
قُلْ هُوَ الَّذِي أَنشَأَكُمْ وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ ۖ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ﴿٢٣﴾
23. Sema: Yeye Ndiye Aliyekuanzisheni, na Akakujaalieni kusikia na kuona na nyoyo za kutafakari. Ni kidogo sana mnayoshukuru.
قُلْ هُوَ الَّذِي ذَرَأَكُمْ فِي الْأَرْضِ وَإِلَيْهِ تُحْشَرُونَ﴿٢٤﴾
24. Sema: Yeye Ndiye Aliyekutawanyeni kwenye ardhi, na Kwake mtakusanywa.
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٢٥﴾
25. Na wanasema: Ni lini hiyo ahadi (ya kufufuliwa), mkiwa ni wasemao kweli?[8]
قُلْ إِنَّمَا الْعِلْمُ عِندَ اللَّـهِ وَإِنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُّبِينٌ﴿٢٦﴾
26. Sema: Hakika ujuzi wake uko kwa Allaah tu. Na hakika mimi ni mwonyaji mwenye kuwabainishia.
فَلَمَّا رَأَوْهُ زُلْفَةً سِيئَتْ وُجُوهُ الَّذِينَ كَفَرُوا وَقِيلَ هَـٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تَدَّعُونَ﴿٢٧﴾
27. Basi watakapoiona (adhabu ya Qiyaamah) inakaribia, zitadhikika nyuso za wale waliokufuru, na itasemwa: Hii ndio ambayo mlikuwa mkiiomba.
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَهْلَكَنِيَ اللَّـهُ وَمَن مَّعِيَ أَوْ رَحِمَنَا فَمَن يُجِيرُ الْكَافِرِينَ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٢٨﴾
28. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Je, mnaonaje ikiwa Allaah Ataniangamiza na walio pamoja nami, au Akiturehemu, basi ni nani atakayewakinga makafiri na adhabu iumizayo?
قُلْ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ آمَنَّا بِهِ وَعَلَيْهِ تَوَكَّلْنَا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ مَنْ هُوَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٢٩﴾
29. Sema: Yeye Ndiye Ar-Rahmaan tumemwamini, na Kwake tunatawakali. Basi karibuni hivi mtakuja kujua ni nani ambaye yumo katika upotofu wa bayana.
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَصْبَحَ مَاؤُكُمْ غَوْرًا فَمَن يَأْتِيكُم بِمَاءٍ مَّعِينٍ﴿٣٠﴾
30. Sema: Mnaonaje yakijakuwa maji yenu yamedidimia, basi ni nani atakayeweza kukuleteeni maji (ya chemchemu) yatiririkayo?
[2] Nyota Zimeumbwa Kwa Mambo Matatu:
Rejea Al-An’aam (6:97) kwenye Hadiyth iliyotaja mambo matatu ya kuumbiwa nyota. Na rejea pia An-Nahl (16:16) na Asw-Swaaffaat (37:10).
[3] Allaah (عزّ وجلّ) Hakuwaangamiza Makafiri Ila Baada Ya Kuwatumia Mwonyaji:
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Kauli Zake nyenginezo kuwa, Hakuwaangamiza watu ila baada ya kuwatumia waonyaji, na kwamba kuangamizwa kwao kumesababishwa na dhulma zao za kukadhibisha Risala Yake kupitia Rusuli Wake:
إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ بِالْحَقِّ بَشِيرًا وَنَذِيرًا ۚ وَإِن مِّنْ أُمَّةٍ إِلَّا خَلَا فِيهَا نَذِيرٌ ﴿٢٤﴾
“Hakika Sisi Tumekupeleka kwa haki ili ubashiri na uonye. Na hakuna ummah wowote isipokuwa amepita humo mwonyaji.” [Faatwir (35:24)]
Rejea pia Al-Israa (17:15), Yuwnus (10:47), An-Nahl (16:36), (16:63), Al-Muuminuwn (23:44), Al-Qaswasw (28:59), Al-An’aam (6:42), (6:131), Sabaa (34:34), Az-Zukhruf (43:23), Huwd (11:117), Al-Kahf (18:59), Al-Hajj (22:45), (22:48), Ash-Shu’araa (26:208), Al-Qaswasw (28:58), Atw-Twalaaq (65:8).
Basi makafiri wanapoona adhabu ya moto wa Jahanna na kuingizwa humo, huulizwa na Malaika walinzi wa moto kama hawakuletewa waonyaji, na hapo hukiri kuwa walitumiwa waonyaji. Kisha hubaki kujuta kama ilivyotajwa katika Aayah za Suwrah hii Al-Mulk (67:6-11). Rejea pia Faatwir (35:37), Az-Zumar (39:71), Al-An’aam (6:130).
[4] Fadhila Za Kumkhofu Allaah (عزّ وجلّ), Muumini Anapokuwa Peke Yake:
Muumini kumkhofu Allaah (عزّ وجلّ) kwa siri, au anapokuwa pekee, ni katika alama za ikhlaasw. Na kumkhofu Allaah (عزّ وجلّ) kwa ghaibu (kwa siri) kuna fadhila adhimu ikiwemo kuingizwa Jannah (Peponi). Rejea Qaaf (50:31-35).
Na fadhila nyengine ya Muumini kumkhofu Allaah (عزّ وجلّ) anapokuwa pekee, ni kujaaliwa kuweko katika Kivuli cha Allaah (عزّ وجلّ) Siku ya Qiyaamah, Siku ambayo hakutakuwa na kivuli isipokuwa Kivuli cha Allaah kama ilivyotajwa katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((سَبْعَةٌ يُظِلُّهُمْ اللَّهُ فِي ظِلِّهِ يَوْمَ لا ظِلَّ إِلا ظِلُّهُ: الإِمَامُ الْعَادِلُ، وَشَابٌّ نَشَأ فِي عِبَادَةِ رَبِّهِ، وَرَجُلٌ قَلْبُهُ مُعَلَّقٌ فِي الْمَسَاجِدِ، وَرَجُلَانِ تَحَابَّا فِي اللَّهِ اجْتَمَعَا عَلَيْهِ وَتَفَرَّقَا عَلَيْهِ، وَرَجُلٌ طَلَبَتْهُ امْرَأَةٌ ذَاتُ مَنْصِبٍ وَجَمَالٍ فَقَالَ إِنِّي أَخَافُ اللَّهَ، وَرَجُلٌ تَصَدَّقَ بِصَدَقَةٍ فَأَخْفَاهَا حَتَّى لا تَعْلَمَ شِمَالُهُ مَا تُنْفِقُ يَمِينُهُ، وَرَجُلٌ ذَكَرَ اللَّهَ خَالِيًا فَفَاضَتْ عَيْنَاهُ)) متفق عليه
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Watu saba Allaah Atawafunika katika kivuli Chake, Siku ambayo hakutokuwa na kivuli ila kivuli Chake: (i) Imaam (kiongozi) muadilifu. (ii) Kijana ambaye amekulia katika ibaada ya Rabb wake. (iii) Mtu ambaye moyo wake umeambatana na Misikiti (iv) Watu wawili wanaopendana kwa ajili ya Allaah; wanakutana kwa ajili Yake na wanafarikiana kwa ajili Yake. (v) Mwanamme aliyetakwa na mwanamke mwenye hadhi na mrembo wa kuvutia akasema: Mimi namkhofu Allaah! (vi) Mtu aliyetoa swadaqa yake akaificha hadi kwamba mkono wake wa kushoto usijue nini ulichotoa mkono wake wa kulia. (vii) Mtu aliyemdhukuru Allaah kwa siri macho yake yakatokwa machozi.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Bonyeza pia viungo vifuatavyo kupata faida nyenginezo:
[5] Allaah (عزّ وجلّ) Ni Mjuzi Wa Yaliyo Vifuani:
Rejea Ghaafir (40:19) ambako kuna maelezo na rejea mbalimbali zenye kuthibitisha kwamba hakuna chochote kile kinachofichika kwa Allaah (عزّ وجلّ).
[6] Allaah (سبحانه وتعالى) Yuko Juu Kwa Dhati Yake Inayolingana Na Uadhama Na Ujalali Wake.
Aayah hii tukufu na inayofuatia (67:17) ni uthibitisho mmojawapo kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Yuko juu ya mbingu saba juu ya ‘Arsh Yake, kwa Dhati Yake inayolingana na Uadhama na Ujalali Wake. Rejea Al-A’raaf (7:54) na Twaahaa (20:5) kwenye maelezo bayana yanayohusiana. Hii ni ‘Aqiydah ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah. Na katika Qur-aan dalili za kuweko Kwake Allaah (سبحانه وتعالى) juu, zimo katika Aayah kadhaa, miongoni mwazo ni: Aal-‘Imraan (3:55), Al-Ma’aarij (70:4), As-Sajdah (32:5), An-Nahl (16:50), Faatwir (35:10).
Na katika Sunnah, kuna dalili tele ya kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Yuko juu. Miongoni mwazo ni:
(i)
حَدَّثَنَا قُتَيْبَةُ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْوَاحِدِ، عَنْ عُمَارَةَ بْنِ الْقَعْقَاعِ بْنِ شُبْرُمَةَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي نُعْمٍ، قَالَ سَمِعْتُ أَبَا سَعِيدٍ الْخُدْرِيَّ، يَقُولُ بَعَثَ عَلِيُّ بْنُ أَبِي طَالِبٍ ـ رضى الله عنه ـ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مِنَ الْيَمَنِ بِذُهَيْبَةٍ فِي أَدِيمٍ مَقْرُوظٍ لَمْ تُحَصَّلْ مِنْ تُرَابِهَا، قَالَ فَقَسَمَهَا بَيْنَ أَرْبَعَةِ نَفَرٍ بَيْنَ عُيَيْنَةَ بْنِ بَدْرٍ، وَأَقْرَعَ بْنِ حَابِسٍ وَزَيْدِ الْخَيْلِ، وَالرَّابِعُ إِمَّا عَلْقَمَةُ وَإِمَّا عَامِرُ بْنُ الطُّفَيْلِ، فَقَالَ رَجُلٌ مِنْ أَصْحَابِهِ كُنَّا نَحْنُ أَحَقَّ بِهَذَا مِنْ هَؤُلاَءِ. قَالَ فَبَلَغَ ذَلِكَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ " أَلاَ تَأْمَنُونِي وَأَنَا أَمِينُ مَنْ فِي السَّمَاءِ، يَأْتِينِي خَبَرُ السَّمَاءِ صَبَاحًا وَمَسَاءً "
Amesimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) katika Hadiyth ndefu: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Je, hamuniamini ilhali mimi nimeaminiwa na Aliye mbinguni; zinanijia khabari za mbinguni asubuhi na jioni?.”
(ii) Safari ya Israa na Mi’raaj.
Rejea Al-Israa (17:1), An-Najm (53:1-18). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipandishwa na Malaika Mtukufu Jibriyl hadi kuvuka mbingu ya saba ambako Allaah (سبحانه وتعالى) Alimfaridhisha Swalaah tano huko. Na Hadiyth ifuatayo inaelezea tukio hilo kwa mukhtasari:
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesimulia safari yake muhimu kutoka Makkah hadi Quds na kutoka hapo hadi juu mbinguni kama ifuatavyo: Jibriyl alinichukua hadi mbingu ya chini kabisa na kuwaomba walinzi wake kufungua mlango. Akaulizwa: Huyu ni nani? Alijibu: Jibriyl. Wakauliza: Upo na nani? Akajibu: (Nipo na) Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Wakauliza. Je amepata mwaliko? Jibriyl Akajibu: Naam. Kisha akakaribishwa kwa tamko la: “Anakaribishwa sana.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaendelea na safari, ulipofunguliwa mlango, nikaingia na hapo nikakutana na Aadam. Jibriyl akaniambia: Huyu ni baba yako, msalimie. Aadam akanisalimia, kwa kusema: “Karibu, mwana Mchaji Allaah na Rasuli Mchaji Allaah.” Kisha Jibriyl akapanda hadi mbingu ya pili na kuwaomba walinzi wake kufungua mlango. Masuala yaliyoulizwa kwenye mbingu ya chini yalirudiwa kabla ya mlango kufunguliwa. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alieleza alichokiona katika kila mbingu, hadi mwisho akachukuliwa hadi mbingu ya saba ambapo Swalaah za fardhi zilikabidhiwa kwake. [Imaam Al-Bukhaariy, Imaam Muslim na wengineo]
(iii) Kila Siku Inapobakia Thuluthi Ya Mwisho Ya Usiku, Allaah (سبحانه وتعالى) Anateremka Hadi Mbingu Ya Dunia Kuwakidhia Haja Waja Wake:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَنْزِلُ رَبُّنَا تَبَارَكَ وَتَعَالَى كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الْآخِرُ يَقُولُ: مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ، مَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ، مَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ)) البخاري و مسلم
AmesimuliaAbuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah (تبارك وتعالى) Huteremka (kwa namna inavyolingana na utukufu Wake) kila siku katika mbingu ya dunia inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na Husema: Nani ananiomba duaa Nimuitike? Nani Ananiomba jambo Nimpe? Nani ananiomba maghfirah Nimghufurie?” [Al-Bukhaariy, Muslim]
(iv) Mtumwa Alitambua Kuwa Allaah (عزّ وجلّ) Yuko Juu:
Amesimulia Mu’awiyah As-Sahmiy (رضي الله عنه): Nilikuwa na kondoo ambao niliwaweka baina ya Uhud na Juwaniyyah, wakiwa na mtumwa wa kike ili kuwaangalia. Siku moja, nilienda nje kuwaangalia kondoo wangu na kugundua kwamba mbwa mwitu amemnyakua mmoja wao. Kwa vile mimi ni binaadam tu, (nilighadhibika) na kumpiga msichana kofi. Baadaye, nilienda kwa Rasuli wa Allah (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumsimulia tukio hilo, naye akanichukulia kuwa nimetenda kitendo kikubwa (kibaya). Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Je nimuachie huru (kama ni njia ya kujiokoa na dhambi yangu). Akasema “Muite.” Nilipomuita, alimuuliza: “Allaah Yuko wapi?” Alisema: Juu ya mbingu. Kisha akamuuliza: “Ni nani mimi?” Akasema: Rasuli wa Allaah. Baada ya hapo, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniamuru akiniambia: “Muache huru, Yeye ni Muumini.” [Imaam Muslim, Abuu Daawuwd, na wengineo]
(v) Roho Za Wanaadam Zinapotolewa Hupandishwa Juu Kwa Allaah (عزّ وجلّ):
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kawaida ya Malaika wa kutoa roho huwa wanamfikia mtu anayefariki. Iwapo ni mchaji Allaah (mwenye taqwa), wataiambia roho yake, Ee roho njema! Toka nje ya mwili mzuri, na furahia kwa kupata rehma na ulinzi kutoka kwa Rabb Ambaye Ameridhika nawe. Malaika wataendelea kuisisitiza kwa maneno haya hadi roho inapotoka nje ya mwili. Kisha itachukuliwa juu hadi mbinguni ambapo ruhusa ya kufungua milango ya mbingu itaombwa. Walinzi watauliza: Ni nani huyu? Malaika watajibu. Fulani mwana wa fulani. Walinzi watasema: Unakaribishwa sana ee roho njema. Roho hiyo itasifiwa kwa maneno hayo hadi mwishoni itakapochukuliwa juu ya mbingu ambako ni kwa Allaah.” [Imaam Ahmad, Al-Haakim na wengineo]
(vi) Rehma ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kutoka mbinguni:
‘Abdullaah bin ‘Amr (رضي الله عنه) amesimulia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye amesema: “Kuwa na huruma kwa waliopo ardhini, ili Yule Aliyeko juu ya mbingu Apate kuwa na rehma kwako.” [Imaam Al-Bukhaariy, Imaam Muslim na wengineo]
Basi hizo ni baadhi tu ya dalili katika Sunnah kwani ziko zaidi ya hizo.
Rejea pia Al-Mujaadalah (58:7) kwenye faida tele nyenginezo:
[7] Kukana:
Maana ya Kukana hapa kwa Allaah ni namna ambavyo Allaah (عزّ وجلّ) Aliwajibisha makafiri hao kwa jibisho kali la kuwateremshia adhabu kali za kuwaangamiza kama zilivyotajwa katika Qur-aan Tukufu kama kugharikishwa, kutumiwa upepo mkali wa dhoruba, kupinduliwa miji juu chini, kudidimizwa na kadhalika. Na hiyo ni baada ya kuwatumia Rusuli wakiwa na hoja bayana, miujiza ya kuthibitisha Utume wao mbali na neema nyingi Alizowaneemesha. Hayo yote waliyakanusha na kuyakataa kwa inadi na kiburi tu, na wakasahau pia Neema nyingi za Allaah kwao. Na hapo ndipo lilipokuja Jibisho Kali la Allaah dhidi yao.
Rejea pia: Al-Hajj (22:44), Sabaa (34:45), Faatwir (35:26).
[8] Ada Ya Makafiri Kuuliza Lini Adhabu Itawafikia Au Lini Qiyaamah Kitatokea:
Rejea Yuwnus (10:48).
الْقَلَم
068-Al-Qalam
068-Al-Qalam: Utangulizi Wa Suwrah [466]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
ن ۚ وَالْقَلَمِ وَمَا يَسْطُرُونَ﴿١﴾
1. Nuwn.[1] Naapa kwa kalamu [2]na yale wayaandikayo.
مَا أَنتَ بِنِعْمَةِ رَبِّكَ بِمَجْنُونٍ﴿٢﴾
2. Kwa Neema ya Rabb wako, wewe (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) si majnuni.[3]
وَإِنَّ لَكَ لَأَجْرًا غَيْرَ مَمْنُونٍ﴿٣﴾
3. Na hakika wewe bila shaka una ujira usiokatika.[4]
وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ﴿٤﴾
4. Na hakika wewe uko juu ya kiwango adhimu cha tabia njema.[5]
فَسَتُبْصِرُ وَيُبْصِرُونَ﴿٥﴾
5. Basi hivi karibuni utaona, na wao wataona.
بِأَييِّكُمُ الْمَفْتُونُ﴿٦﴾
6. Ni nani kati yenu aliyesibiwa na uwendawazimu.
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ﴿٧﴾
7. Hakika Rabb wako Yeye Anamjua zaidi aliyepotea Njia Yake, Naye Anawajua zaidi walioongoka.
فَلَا تُطِعِ الْمُكَذِّبِينَ﴿٨﴾
8. Basi usiwatii wanaokadhibisha.
وَدُّوا لَوْ تُدْهِنُ فَيُدْهِنُونَ﴿٩﴾
9. Wanatamani lau kama ungelilegeza nao pia walegeze.
وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَّهِينٍ﴿١٠﴾
10. Na wala usimtii kila mwingi wa kuapa, dhalili.[6]
هَمَّازٍ مَّشَّاءٍ بِنَمِيمٍ﴿١١﴾
11. Mwingi wa kudharau na kukashifu, mpitaji huku na kule kufitinisha.[7]
مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ﴿١٢﴾
12. Mwingi wa kuzuia ya kheri, mwenye kutaadi, mwingi wa kutenda dhambi.
عُتُلٍّ بَعْدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ﴿١٣﴾
13. Msusuwavu mtumiaji nguvu[8], na baada ya hivyo ni mwenye kujipachika tu kabila.
أَن كَانَ ذَا مَالٍ وَبَنِينَ﴿١٤﴾
14. Kwa kuwa ana mali na watoto?[9]
إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ﴿١٥﴾
15. Anaposomewa Aayaat Zetu, anasema: Hekaya za watu wa kale.
سَنَسِمُهُ عَلَى الْخُرْطُومِ﴿١٦﴾
16. Tutamtia chapa juu ya pua yake.
إِنَّا بَلَوْنَاهُمْ كَمَا بَلَوْنَا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ إِذْ أَقْسَمُوا لَيَصْرِمُنَّهَا مُصْبِحِينَ﴿١٧﴾
17. Hakika Sisi Tumewajaribu (Maquraysh) kama Tulivyowajaribu watu wa shamba pale walipoapa kuwa bila shaka watayavuna (mazao yake) watakapopambaukiwa asubuhi.[10]
وَلَا يَسْتَثْنُونَ﴿١٨﴾
18. Na wala hawakusema In-Shaa Allaah.
فَطَافَ عَلَيْهَا طَائِفٌ مِّن رَّبِّكَ وَهُمْ نَائِمُونَ﴿١٩﴾
19. Basi (shamba lao) likazungukwa na chenye kuzunguka (moto) kutoka kwa Rabb wako na hali wao wamelala.
فَأَصْبَحَتْ كَالصَّرِيمِ﴿٢٠﴾
20. Likawa kama lilovunwa likabakishwa majivu meusi.
فَتَنَادَوْا مُصْبِحِينَ﴿٢١﴾
21. Wakaitana, walipopambaukiwa asubuhi.
أَنِ اغْدُوا عَلَىٰ حَرْثِكُمْ إِن كُنتُمْ صَارِمِينَ﴿٢٢﴾
22. Kwamba nendeni asubuhi mapema shambani mwenu, mkiwa mnataka kuvuna.
فَانطَلَقُوا وَهُمْ يَتَخَافَتُونَ﴿٢٣﴾
23. Wakatoka na huku wanakwenda kimya kimya wakinong’onezana.
أَن لَّا يَدْخُلَنَّهَا الْيَوْمَ عَلَيْكُم مِّسْكِينٌ﴿٢٤﴾
24. Kwamba: Asikuingilieni humo kwa hali yoyote leo masikini.
وَغَدَوْا عَلَىٰ حَرْدٍ قَادِرِينَ﴿٢٥﴾
25. Wakatoka asubuhi mapema kwa kusudio la nguvu, wakidhani wana uwezo (wa kuwazuia maskini).
فَلَمَّا رَأَوْهَا قَالُوا إِنَّا لَضَالُّونَ﴿٢٦﴾
26. Basi walipoliona wakasema: Hakika sisi bila shaka Tumepotea.
بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ﴿٢٧﴾
27. (Walivyotanabahi!): Bali sisi tumenyimwa!
قَالَ أَوْسَطُهُمْ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ لَوْلَا تُسَبِّحُونَ﴿٢٨﴾
28. Mbora wao akasema: Je, sikukuambieni kuwa angalau hata museme Subhaana Allaah (au In-Shaa Allaah)!
قَالُوا سُبْحَانَ رَبِّنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ﴿٢٩﴾
29. Wakasema: Subhaana Rabbinnaa! Ametakasika Mola wetu! Hakika sisi tulikuwa madhalimu.
فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَلَاوَمُونَ﴿٣٠﴾
30. Wakakabiliana wenyewe kwa wenyewe wakilaumiana.
قَالُوا يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا طَاغِينَ﴿٣١﴾
31. Wakasema: Ole wetu! Hakika sisi tumekuwa warukao mipaka.
عَسَىٰ رَبُّنَا أَن يُبْدِلَنَا خَيْرًا مِّنْهَا إِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا رَاغِبُونَ﴿٣٢﴾
32. Asaa Rabb wetu Akatubadilishia lililo bora kuliko hilo. Hakika sisi tuna raghba kuelekea kwa Rabb wetu.
كَذَٰلِكَ الْعَذَابُ ۖ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ﴿٣٣﴾
33. Hivyo ndivyo adhabu. Na bila shaka adhabu ya Aakhirah ni kubwa zaidi lau wangelikuwa wanajua.
إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتِ النَّعِيمِ﴿٣٤﴾
34. Hakika wenye taqwa watapata kwa Rabb wao Jannaat za neema.
أَفَنَجْعَلُ الْمُسْلِمِينَ كَالْمُجْرِمِينَ﴿٣٥﴾
35. Je, Tuwafanye Waislamu (watiifu) sawa kama wahalifu?
مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ﴿٣٦﴾
36. Mna nini! Vipi mnahukumu?
أَمْ لَكُمْ كِتَابٌ فِيهِ تَدْرُسُونَ﴿٣٧﴾
37. Au mna Kitabu mnachodurusu humo?
إِنَّ لَكُمْ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ﴿٣٨﴾
38. Ambapo humo mnapata mnachopendelea?
أَمْ لَكُمْ أَيْمَانٌ عَلَيْنَا بَالِغَةٌ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۙ إِنَّ لَكُمْ لَمَا تَحْكُمُونَ﴿٣٩﴾
39. Au mnazo ahadi za viapo juu Yetu zinazofikia mpaka Siku ya Qiyaamah, kwamba mtapata mnayojihukumia?
سَلْهُمْ أَيُّهُم بِذَٰلِكَ زَعِيمٌ﴿٤٠﴾
40. Waulize (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ni nani kati yao mdhamini wa hayo?
أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ فَلْيَأْتُوا بِشُرَكَائِهِمْ إِن كَانُوا صَادِقِينَ﴿٤١﴾
41. Au wana washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wakweli.
يَوْمَ يُكْشَفُ عَن سَاقٍ وَيُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ﴿٤٢﴾
42. Siku utakapofunuliwa Muundi na wataitwa kusujudu lakini hawatoweza.[11]
خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۖ وَقَدْ كَانُوا يُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ وَهُمْ سَالِمُونَ﴿٤٣﴾
43. Macho yao yatainama chini, udhalilifu utawafunika. Na hali walikuwa wakiitwa wasujudu (kuswali duniani) walipokuwa wazima wa afya.
فَذَرْنِي وَمَن يُكَذِّبُ بِهَـٰذَا الْحَدِيثِ ۖ سَنَسْتَدْرِجُهُم مِّنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ﴿٤٤﴾
44. Basi Niache (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na anayekadhibisha Qur-aan hii. Tutawavuta pole pole adhabuni kwa namna wasiyoijua.
وَأُمْلِي لَهُمْ ۚ إِنَّ كَيْدِي مَتِينٌ﴿٤٥﴾
45. Nami Ninawapa muhula. Hakika mpango Wangu ni thabiti.
أَمْ تَسْأَلُهُمْ أَجْرًا فَهُم مِّن مَّغْرَمٍ مُّثْقَلُونَ﴿٤٦﴾
46. Au unawaomba ujira (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), basi wao zimewawia uzito gharama zake?
أَمْ عِندَهُمُ الْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ﴿٤٧﴾
47. Au wanayo (ilimu) ya ghaibu, basi wao wanaandika?
فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ الْحُوتِ إِذْ نَادَىٰ وَهُوَ مَكْظُومٌ﴿٤٨﴾
48. Basi subiri (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa hukumu ya Rabb wako, na wala usiwe kama swahibu wa samaki (Nabiy Yuwnus) pale aliponadi (kutuomba) naye akiwa amebanwa na dhiki.[12]
لَّوْلَا أَن تَدَارَكَهُ نِعْمَةٌ مِّن رَّبِّهِ لَنُبِذَ بِالْعَرَاءِ وَهُوَ مَذْمُومٌ﴿٤٩﴾
49. Lau isingelimfikia neema kutoka kwa Rabb wake, bila shaka angelitupwa ufukoni mtupu akiwa mwenye kulaumiwa.
فَاجْتَبَاهُ رَبُّهُ فَجَعَلَهُ مِنَ الصَّالِحِينَ﴿٥٠﴾
50. Na Rabb wake Akamteua na Akamjaalia miongoni mwa Swalihina.
وَإِن يَكَادُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَيُزْلِقُونَكَ بِأَبْصَارِهِمْ لَمَّا سَمِعُوا الذِّكْرَ وَيَقُولُونَ إِنَّهُ لَمَجْنُونٌ﴿٥١﴾
51. Na wale waliokufuru hukaribia bila shaka kukutelezesha kwa macho yao (ya uhasidi)[13] wanaposikia Ukumbusho, na wanasema: Hakika yeye bila shaka ni majnuni.[14]
وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ﴿٥٢﴾
52. Na haikuwa (hii Qur-aan) isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu.
[1] الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):
Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).
[2] Kalamu Ni Kitu Cha Kwanza Kuumbwa:
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
إِنَّ أَوَّلَ مَا خَلَقَ اَللَّهُ تَعَالَى الْقَلَمَ فَقَالَ لَهُ: اُكْتُبْ! فَجَرَى فِي تِلْكَ اَلسَّاعَةِ بِمَا هُوَ كَائِنٌ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ
“Kitu cha mwanzo Allaah kukiumba ni kalamu. Akaiambia: Andika! Na katika saa hiyo, (yakaandikwa) yote yatakayotokea mpaka Siku ya Qiyaamah.” [Ahmad, At-Tirmidhiy]
[3] Allaah (سبحانه وتعالى) Anamliwaza Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) Kuhusu Kusingiziwa Sifa Ovu Na Washirikina Wa Makkah:
Kuanzia Aayah hii namba (2) na kuendelea hadi namba (15), Allaah (سبحانه وتعالى) Anamliwaza Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kuthibitisha fadhila na khulqa zake adhimu, na pia kwa kumuamuru asiwatii makafiri wa Makkah ambao wao ndio wenye sifa mbalimbali ovu, na ambao walimtaka Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) anyamaze asibalighishe Risala Yake, na asikataze kuabudiwa masanamu yao. Basi wakampachika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) sifa ovu kadhaa. Rejea Al-Furqaan (25:4) kwenye uchambuzi wa hayo na rejea mbalimbali.
[4] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ana Ujira Usiokatika:
Bonyeza kiungo kifuatacho kupata faida:
33-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ana Ujira Usiokatika Anasifika Na Maarufu Mno [467]
[5] Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
Bonyeza kiungo kifuatacho kupata faida tele:
Sifa-Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) [141]
[7] Madhara Na Adhabu Ya An-Namiymah (Kufitinisha):
Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida:
10-Madhara Ya An-Namiymah (Kufitinisha): Maana, Hukumu Na Adhabu Zake [468]
11-Madhara Ya An-Namiymah (Kufitinisha): Sababu za Kufitinisha, Sifa Za Mfitinishaji [469]
12-Madhara Ya An-Namiymah (Kufitinisha): Vipi Kutibu An-Namiymah? [470]
[8] Msusuwavu Mtumiaji Nguvu (Na Mwenye Kutakabari Mjeuri) Wameahidiwa Moto:
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، أَخْبَرَنَا سُفْيَانُ، حَدَّثَنَا مَعْبَدُ بْنُ خَالِدٍ الْقَيْسِيُّ، عَنْ حَارِثَةَ بْنِ وَهْبٍ الْخُزَاعِيِّ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " أَلاَ أُخْبِرُكُمْ بِأَهْلِ الْجَنَّةِ، كُلُّ ضَعِيفٍ مُتَضَاعِفٍ، لَوْ أَقْسَمَ عَلَى اللَّهِ لأَبَرَّهُ، أَلاَ أُخْبِرُكُمْ بِأَهْلِ النَّارِ كُلُّ عُتُلٍّ جَوَّاظٍ مُسْتَكْبِرٍ ".
Amesimulia Haarithah Bin Wahb Al-Khuzaa‘iyy (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Je, niwajulishe nyinyi watu wa Jannah? Kila mnyonge na mwenye kunyongeshwa, lau atakula yamini kwa Allaah basi atakubaliwa. Je, niwapashe khabari ya watu wa motoni? Kila msusuwavu mtumiaji nguvu, mwenye kutakabari mjeuri.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
[9] Matajiri Wa Makkah Waliomkadhibisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Na Risala:
Aayah hizi zimeteremshwa kuhusu baadhi ya washirikina kama Waliyd bin Mughiyrah na wengineo [Tafsiyr As-Sa’diy]
[10] Kisa Cha Watu Wa Shamba Waliozuia Maskini Wasiingie Shambani Kupata Swadaqa Ya Mazao:
Kuanzia Aayah hii namba (17) hadi namba (33), kinazungumzwa kisa cha watu wa shamba kama alivyoelezea Imaam Ibn Kathiyr katika Tafsiyr yake:
Baadhi ya Salaf wametaja kuwa hawa walikuwa ni watu kutoka Yemen. Said Bin Jubayr amesema: Walikuwa ni watu kutoka kijiji kilichoitwa Dhwarwaan ambacho kilikuwa ni maili sita kutoka (mji wa) Sanaa (uliko Yemen). Imesemwa pia kuwa: Walikuwa ni watu kutoka Habasha (Ethiopea) ambao baba yao aliwaachia shamba na walikuwa ni Ahlul-Kitaab. Baba yao alikuwa akilishughulikia shamba kwa njia nzuri. Alichokivuna, alikuwa akirudishia katika shamba kukidhi mahitaji yake, na hubakisha kinginecho kama ni chakua kwa ahli zake cha kuwatosheleza mwaka, na akitolea swadaqa chochote kilichozidi (katika mazao). Alipofariki, watoto wake wakarithi shamba hilo huku wakasema: Hakika baba yetu alikuwa mjinga kugawa mazao ya shamba kwa mafaqiri. Lakini sisi tukiwazua shambani tutapata zaidi. Basi walipoazimia kufanya hivyo, wakaadhibiwa kinyume na niyya yao, basi Allaah Akaondoshea walichokuwa nacho mikononi mwao, mtaji, faida na swadaqa, hivyo kukawa hakuna chochote kilishosalia kwao. Ndipo Allaah (سبحانه وتعالى) Akasema katika Aayah ya mwisho kumalizikia kisa hiki:
كَذَٰلِكَ الْعَذَابُ ۖ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ﴿٣٣﴾
“Hivyo ndivyo adhabu. Na bila shaka adhabu ya Aakhirah ni kubwa zaidi lau wangelikuwa wanajua.”
Yaani: Hiyo ni adhabu kwa yeyote anayepinga Amri za Allaah, na anayefanya ubakhili katika neema alizojaaliwa na Allaah, akanyima haki za masikini na mafaqiri na kubadilisha neema za Allaah kwa kufru. Basi,
وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ﴿٣٣﴾
“Na bila shaka adhabu ya Aakhirah ni kubwa zaidi lau wangelikuwa wanajua.”
Yaani: Hii ni adhabu ya duniani kama mlivyosikia. Na adhabu ya Aakhirah ni ya mashaka zaidi. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Kisa hiki kinawafunza na kuwashajiisha Waumini waliojaaliwa neema yoyote ile, iwe neema ya mali, ya watoto, ya siha na afya, ya kila kiungo cha mwili wa mwanaadam, ya nguvu, ya akili na ya busara na kadhaalika, kwamba watumie neema hizo katika ya kumridhisha Allaah (عزّ وجلّ), na si kiyume chake. Na katika neema ya mali, ni kuitolea haki yake ya Zakaah na swadaqa katika wanachokivuna au wanachokichuma.
Kisa kinginecho cha utoaji wa swadaqa ya mavuno ya shamba ni kama kilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
عن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( بَيْنَمَا رَجُلٌ يَمْشِي بِفَلاَةٍ مِنَ الأَرْضِ ، فَسَمِعَ صَوْتاً في سَحَابَةٍ ، اسقِ حَدِيقَةَ فُلانٍ ، فَتَنَحَّى ذَلِكَ السَّحَابُ فَأفْرَغَ مَاءهُ في حَرَّةٍ ، فإِذَا شَرْجَةٌ مِنْ تِلْكَ الشِّرَاجِ قَدِ اسْتَوْعَبَت ذَلِكَ الماءَ كُلَّهُ ، فَتَتَبَّعَ المَاءَ ، فإذَا رَجُلٌ قَائمٌ في حَدِيقَتِهِ يُحَوِّلُ الماءَ بِمسحَاتِهِ، فَقَالَ لَهُ : يَا عَبْدَ اللهِ، ما اسمُكَ ؟ قال : فُلانٌ للاسم الذي سَمِعَ في السَّحابةِ ، فقال له : يا عبدَ الله ، لِمَ تَسْألُنِي عَنِ اسْمِي ؟ فَقَالَ : إنِّي سَمِعْتُ صَوتْاً في السَّحابِ الَّذِي هَذَا مَاؤُهُ ، يقولُ : اسْقِ حَدِيقَةَ فُلاَنٍ لاسمِكَ ، فَمَا تَصْنَعُ فِيهَا ، فَقَالَ : أمَا إذ قلتَ هَذَا ، فَإنِّي أنْظُرُ إِلَى مَا يَخْرُجُ مِنْهَا ، فَأتَصَدَّقُ بِثُلُثِهِ، وَآكُلُ أنَا وَعِيَالِي ثُلُثاً، وَأردُّ فِيهَا ثُلُثَهُ )) رواه مسلم .
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mtu alipokuwa anatembea jangwani, alisikia sauti katika wingu (ikisema): Nyweshea shamba la fulani! Wingu hilo likakaribia na kumimina maji yake kwenye ardhi ya mawe. Maji hayo yakaenea katika kijito na kumiminika katika hodhi kubwa. Akafuata maji akamuona mtu amesimama ndani ya shamba lile anagawa maji kwa jembe lake. Akamwambia: Ee mja wa Allaah, jina lako nani? Akasema: Fulani. Akataja jina ambalo amelisikia katika wingu. Akamwambia: Ee mja wa Allaah! Kwa nini unaniuliza jina langu? Akasema: Nimesikia sauti katika wingu ambalo haya ndio maji yake ikisema: Nyweshea shamba la fulani kwa jina lako. Je, unafanya nini katika hili? Akasema: Kwa sababu umeniuliza hili, basi (nakujuilsha kwamba), mimi naangalia kinachotoka humo, na kutoa swadaqa thuluthi, na thuluthi nakula pamoja na ahli wangu, na narudisha humo (shambani) thuluthi yake.” [Muslim]
Hakika katika visa viwili hivyo kuna mafunzo yafuatayo:
(i) Neema zote anazojaaliwa mtu, zinatoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى), na mtu hana uwezo wa kuzipata bila ya Tawfiyq ya Allaah (عزّ وجلّ). Kauli Yake Allaah (عزّ وجلّ):
وَمَا بِكُم مِّن نِّعْمَةٍ فَمِنَ اللَّـهِ
Na Neema yoyote mliyo nayo, basi ni kutoka kwa Allaah. [An-Nahl (16:53)]
ii-Kutoa swadaqa katika neema alizojaaliwa mtu na Allaah (عزّ وجلّ), ni katika shukurani, na kinyume chake ni kuikufuru neema hiyo. Na kila mtu anapotoa katika neema Aliyomjaalia Allaah, basi Allaah (عزّ وجلّ) Humzidishia kama Anavyosema:
وَإِذْ تَأَذَّنَ رَبُّكُمْ لَئِن شَكَرْتُمْ لَأَزِيدَنَّكُمْ ۖ وَلَئِن كَفَرْتُمْ إِنَّ عَذَابِي لَشَدِيدٌ﴿٧﴾
Na pindi Alipotangaza Rabb wenu: Ikiwa mtashukuru, bila shaka Nitakuzidishieni (Neema Zangu), na mkikufuru, basi hakika Adhabu Yangu ni kali. [Ibraahiym (14:7)]
Basi Tanabahi kisa cha mtu ambaye alikuwa akitoa swadaqa thuluthi ya mazao ya shambani mwake, kisha Allaah Akamnyeshewa mvua katika shamba lake bila ya yeye kuhangaika kutafuta maji au kuyagharimia!
iii-Kuikufuru neema ya Allaah kwa kutokuitendea haki inasababisha maangamizi toka kwa Allaah:
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ بَدَّلُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ كُفْرًا وَأَحَلُّوا قَوْمَهُمْ دَارَ الْبَوَارِ﴿٢٨﴾
Je, huoni wale waliobadilisha Neema ya Allaah kwa kufru, na wakawafikisha watu wao nyumba ya mateketezo? [Ibraahiym (14:28)]
vi-Kuwagaia vyakula mafuqara, masikini na wahitaji ni katika himizo la Allaah (سبحانه وتعالى) na jambo hili lina fadhila na malipo adhimu kutoka kwa Allaah (عزّ وجلّ) kama Anavyosema katika Kauli Zake:
وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا﴿٨﴾ إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّـهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا﴿٩﴾
Na wanalisha chakula, juu ya kuwa wao wanakipenda, masikini na mayatima na mateka. Hakika sisi tunakulisheni kwa ajili ya Wajihi wa Allaah, hatukusudii kutoka kwenu jazaa wala shukurani. [Al-Insaan (76:8-9)]
Na Anaonya wasiofanya hima kulisha mafuqara, masikini na wahitaji hao:
وَلَا تَحَاضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ ﴿١٨﴾
Na wala hamhamasishani katika kulisha maskini. [Al-Fajr (89:18)]
Rejea pia Al-Haaqqah (69:34), Al-Maa’uwn (107:3).
iv-Tahadharisho la mtu kuulizwa Siku ya Qiyaamah, ameitumiaje neema aliyojaaliwa, Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ ﴿٨﴾
Kisha bila shaka mtaulizwa Siku hiyo kuhusu neema. [At-Takaathur (102:8)]
v-Allaah (سبحانه وتعالى) Huibadilisha neema pindi mtu anapokosa kuitendea haki:
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ لَمْ يَكُ مُغَيِّرًا نِّعْمَةً أَنْعَمَهَا عَلَىٰ قَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ
Hayo ni kwa kuwa Allaah Hakuwa Mwenye Kubadilisha neema yoyote Aliyoineemesha kwa watu mpaka wao wabadilishe yaliyomo ndani ya nafsi zao. [Al-Anfaal (8:53)]
[11] Siku Utakapofunuliwa Muundi:
Itakapofika Siku ya Qiyaamah, yakatokea ya kuwatia watu viwewe na mitetemeko ya ardhi, na hali za vitisho visivyokuwa vya ndoto au dhana za uongo, kisha Akaja Muumba (Allaah) Ahukumu baina ya waja Wake na kuwalipa matendo yao, Atafunua Muundi (Mguu) Wake Mtukufu usiofanana na chochote kile! Na viumbe wakaona Ujalali wa Allaah na Uadhwama Wake usioweza kuelezeka, basi hapo wataitwa kumsujudia Allaah. Waumini waliokuwa wakimsujudia Allaah kwa khiari na kupendelea kwao watasujudu. Ama wahalifu na wanafiki, hao watataka kusujudu lakini hawataweza kamwe! Na migongo yao itakuwa ni kama pembe za ng'ombe. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Na katika Hadiyth:
حَدَّثَنَا آدَمُ، حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، عَنْ خَالِدِ بْنِ يَزِيدَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ أَبِي هِلاَلٍ، عَنْ زَيْدِ بْنِ أَسْلَمَ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ " يَكْشِفُ رَبُّنَا عَنْ سَاقِهِ فَيَسْجُدُ لَهُ كُلُّ مُؤْمِنٍ وَمُؤْمِنَةٍ، وَيَبْقَى مَنْ كَانَ يَسْجُدُ فِي الدُّنْيَا رِئَاءً وَسُمْعَةً، فَيَذْهَبُ لِيَسْجُدَ فَيَعُودُ ظَهْرُهُ طَبَقًا وَاحِدًا ".
Amesimulia Abu Sa’iyd (رضي الله عنه): Nimemsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: Rabb wetu Atafunua Muundi Wake, watamsujudia Waumini wote Wanaume na Waumini Wanawake. Kisha watabakia waliokuwa wakisujudu duniani kwa riyaa; kujionyesha kwa ajili ya kutaka kusifiwa na umaarufu. Watu hao watajaribu kusujudu (Siku hiyo ya Qiyaamah), lakini mgongo wa kila mmoja wao utakuwa mgumu kana kwamba ni uti wa mgongo wenye mfupa mmoja (bila ya mgawanyiko wa diski).” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Tafsiyr (65)]
[12] Nabiy Yuwnus (عليه السّلام) Alipokuwa Tumboni Mwa Samaki Na Duaa Aliyoiomba:
Rejea Al-Anbiyaa (21:87) kwenye duaa ya Nabiy Yuwnus (عليه السّلام) ambayo ni mojawapo wa sababu za kutakabaliwa haja, na pia ni duaa ya kuomba mtu anapopata jana au balaa.
Rejea pia Asw-Swaffaat (37:143-144) kwenye maelezo mengineyo kuhusu hali ya Nabiy Yuwnus (عليه السّلام) alipokuwa tumboni mwa Samaki.
[13] Jicho Baya La Uhasidi:
Washirikina walikuwa wakimtazama Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa jicho baya kutokana na uhasidi wao, wivu, chuki zao. Na hiki ni kwango cha mwisho cha madhara waliyoweza kumfanyia kwani Allaah Amemhifadhi na Amemkinga na kumnusuru [Tafsiyr As-Sa’diy]
Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amethibitisha kwamba jicho baya linawea kumpata mtu kwa kauli yake:
إِذَا رَأَى أَحَدُكُمْ مِنْ أَخِيهِ أَوْ مِنْ نَفْسِهِ أَوْ مِنْ مَالِهِ مَا يُعْجِبُهُ فَلْيُبَرِّكْهُ فَإِنَّ الْعَيْنَ حَقٌّ
“Mmoja wenu akiona kwa ndugu yake au kwake, au mali yake kinachomfurahisha akiombee baraka kwani kijicho ni haki.” [Hadiyth ya ‘Aamir bin Rabiy’ah na Sahl bin Hunayf (رضي الله عنهما) - Ahmad (4/447), Ibn Maajah [3509], Maalik [1697, 1698] na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (1/212)]
Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuacha kutufunza kujikinga na jicho baya. Bonyeza viungo vifuatavyo kupata adhkaar na duaa za kujikinga na jicho baya na faida nyenginezo.
125-Hiswnul-Muslim: Du’aa Anayeogopa Kupatwa Na Kijicho [471]
048-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kuwakinga Watoto [472]
Du’aa Za Ruqyah (Kinga) Faida Na Sharh Zake [473]
[14] Washirikina Wa Makkah Kumpachika Sifa Ovu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
Rejea Al-Furqaan (25:4) kwenye uchambuzi na rejea mbalimbali.
الْحآقَّة
069-Al-Haaqqah
069-Al-Haaqqah: Utangulizi Wa Suwrah [476]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الْحَاقَّةُ﴿١﴾
1. Tukio la haki lisiloepukika![1]
مَا الْحَاقَّةُ﴿٢﴾
2. Ni nini tukio la haki lisiloepukika?
وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْحَاقَّةُ﴿٣﴾
3. Na nini kitakachokujulisha nini tukio la haki lisiloepukika?
كَذَّبَتْ ثَمُودُ وَعَادٌ بِالْقَارِعَةِ﴿٤﴾
4. Kina Thamuwd na ‘Aad walikadhibisha tukio lenye kugongagonga na kutia kiwewe nyoyo.[2]
فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهْلِكُوا بِالطَّاغِيَةِ﴿٥﴾
5. Ama kina Thamuwd, wao waliangamizwa kwa ukelele mkali uliovuka mipaka.
وَأَمَّا عَادٌ فَأُهْلِكُوا بِرِيحٍ صَرْصَرٍ عَاتِيَةٍ﴿٦﴾
6. Na ama kina ‘Aad, hao waliangamizwa kwa upepo mbaya wa sauti na baridi kali, uvumao kwa nguvu.
سَخَّرَهَا عَلَيْهِمْ سَبْعَ لَيَالٍ وَثَمَانِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومًا فَتَرَى الْقَوْمَ فِيهَا صَرْعَىٰ كَأَنَّهُمْ أَعْجَازُ نَخْلٍ خَاوِيَةٍ﴿٧﴾
7. Aliwalazimishia nyusiku saba na michana minane mfululizo, basi utaona watu humo wameanguka chini kama kwamba ni magogo ya mitende iliyo mitupu.
فَهَلْ تَرَىٰ لَهُم مِّن بَاقِيَةٍ﴿٨﴾
8. Basi je, unaona mabakio yao yoyote?
وَجَاءَ فِرْعَوْنُ وَمَن قَبْلَهُ وَالْمُؤْتَفِكَاتُ بِالْخَاطِئَةِ﴿٩﴾
9. Na akaja Firawni na wale walio kabla yake, na (watu wa) miji iliyopinduliwa chini juu kwa sababu ya hatia zao.
فَعَصَوْا رَسُولَ رَبِّهِمْ فَأَخَذَهُمْ أَخْذَةً رَّابِيَةً﴿١٠﴾
10. Basi wakamuasi Rasuli wa Rabb wao, Akawachukua mchukuo uliopindukia ukali.
إِنَّا لَمَّا طَغَى الْمَاءُ حَمَلْنَاكُمْ فِي الْجَارِيَةِ﴿١١﴾
11. Hakika Sisi, pale maji yalipopinduka mipaka, Tulikubebeni katika merikebu.[3]
لِنَجْعَلَهَا لَكُمْ تَذْكِرَةً وَتَعِيَهَا أُذُنٌ وَاعِيَةٌ﴿١٢﴾
12. Ili Tuifanye kuwa ni ukumbusho kwenu, na ibakie kumbukumbu katika sikio (la wenye kuzingatia) linalobakisha kumbukumbu.
فَإِذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ نَفْخَةٌ وَاحِدَةٌ﴿١٣﴾
13. Basi litakapopulizwa baragumu mpulizo mmoja.[4]
وَحُمِلَتِ الْأَرْضُ وَالْجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةً وَاحِدَةً﴿١٤﴾
14. Na ardhi na milima ikaondolewa kisha ikapondwa mpondo mmoja.
فَيَوْمَئِذٍ وَقَعَتِ الْوَاقِعَةُ﴿١٥﴾
15. Basi siku hiyo ndio litatokea tukio la kutokea.
وَانشَقَّتِ السَّمَاءُ فَهِيَ يَوْمَئِذٍ وَاهِيَةٌ﴿١٦﴾
16. Na mbingu zitararuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu sana.
وَالْمَلَكُ عَلَىٰ أَرْجَائِهَا ۚ وَيَحْمِلُ عَرْشَ رَبِّكَ فَوْقَهُمْ يَوْمَئِذٍ ثَمَانِيَةٌ﴿١٧﴾
17. Na Malaika watakuwa pembezoni mwake,[5] na watabeba ‘Arsh[6] ya Rabb wako juu yao siku hiyo (Malaika) wanane.[7]
يَوْمَئِذٍ تُعْرَضُونَ لَا تَخْفَىٰ مِنكُمْ خَافِيَةٌ﴿١٨﴾
18. Siku hiyo mtahudhurishwa, halitofichika tendo lenu lolote la siri.
فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَيَقُولُ هَاؤُمُ اقْرَءُوا كِتَابِيَهْ﴿١٩﴾
19. Basi ama yule atakayepewa kitabu chake kuliani mwake, atasema: Hebu chukueni someni kitabu changu![8]
إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلَاقٍ حِسَابِيَهْ﴿٢٠﴾
20. Hakika mimi niliyakinisha kuwa hakiki mimi ni mwenye kukutana na hesabu yangu!
فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ﴿٢١﴾
21. Basi yeye atakuwa katika maisha ya kuridhisha.
فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ﴿٢٢﴾
22. Kwenye Jannah ya juu.[9]
قُطُوفُهَا دَانِيَةٌ﴿٢٣﴾
23. Matunda yake ya kuchumwa yako karibu.
كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا أَسْلَفْتُمْ فِي الْأَيَّامِ الْخَالِيَةِ﴿٢٤﴾
24. (Wataambiwa): Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyoyatanguliza katika siku nyingi zilizopita.
وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِشِمَالِهِ فَيَقُولُ يَا لَيْتَنِي لَمْ أُوتَ كِتَابِيَهْ﴿٢٥﴾
25. Na ama yule atakayepewa kitabu chake kushotoni mwake, atasema: Ee! Laiti nisingelipewa kitabu changu![10]
وَلَمْ أَدْرِ مَا حِسَابِيَهْ﴿٢٦﴾
26. Na wala nisingelijua hesabu yangu!
يَا لَيْتَهَا كَانَتِ الْقَاضِيَةَ﴿٢٧﴾
27. Ee! Laiti yangelikuwa (mauti) ndio kumalizika kwangu.
مَا أَغْنَىٰ عَنِّي مَالِيَهْ ۜ﴿٢٨﴾
28. Haikunifaa mali yangu.
هَلَكَ عَنِّي سُلْطَانِيَهْ﴿٢٩﴾
29. Madaraka yangu yamenitoweka.
خُذُوهُ فَغُلُّوهُ﴿٣٠﴾
30. (Patasemwa): Mchukueni, na mfungeni pingu.
ثُمَّ الْجَحِيمَ صَلُّوهُ﴿٣١﴾
31. Kisha kwenye moto uwakao vikali mno muingizeni aungue.
ثُمَّ فِي سِلْسِلَةٍ ذَرْعُهَا سَبْعُونَ ذِرَاعًا فَاسْلُكُوهُ﴿٣٢﴾
32. Kisha mtieni pingu katika minyororo yenye urefu wa dhiraa sabini.
إِنَّهُ كَانَ لَا يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ الْعَظِيمِ﴿٣٣﴾
33. Hakika yeye alikuwa hamuamini Allaah Mwenye Taadhima.[11]
وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ﴿٣٤﴾
34. Na wala hahamasishi kulisha masikini.
فَلَيْسَ لَهُ الْيَوْمَ هَاهُنَا حَمِيمٌ﴿٣٥﴾
35. Basi leo hapa hatokuwa na rafiki wa dhati.
وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنْ غِسْلِينٍ﴿٣٦﴾
36. Wala chakula isipokuwa usaha (wa walio motoni).
لَّا يَأْكُلُهُ إِلَّا الْخَاطِئُونَ﴿٣٧﴾
37. Hawakili chakula hicho isipokuwa wenye hatia.
فَلَا أُقْسِمُ بِمَا تُبْصِرُونَ﴿٣٨﴾
38. Basi Naapa kwa yale mnayoyaona.[12]
وَمَا لَا تُبْصِرُونَ﴿٣٩﴾
39. Na kwa yale msiyoyaona.
إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ﴿٤٠﴾
40. Hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni kauli ya Rasuli Mtukufu.
وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَاعِرٍ ۚ قَلِيلًا مَّا تُؤْمِنُونَ﴿٤١﴾
41. Na si kauli ya mshairi. Ni machache sana yale mnayoamini.
وَلَا بِقَوْلِ كَاهِنٍ ۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ﴿٤٢﴾
42. Na wala si kauli ya kahini. Ni machache sana yale mnayokumbuka.
تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ﴿٤٣﴾
43. Ni uteremsho kutoka kwa Rabb wa walimwengu.
وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ الْأَقَاوِيلِ﴿٤٤﴾
44. Na lau kama (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) angetutungia baadhi ya kauli.
لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ﴿٤٥﴾
45. Bila shaka Tungelimchukua kwa Mkono wa kuume.
ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ الْوَتِينَ﴿٤٦﴾
46. Kisha bila shaka Tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo wa uhai.
فَمَا مِنكُم مِّنْ أَحَدٍ عَنْهُ حَاجِزِينَ﴿٤٧﴾
47. Basi hakuna mmoja yeyote kati yenu angeliweza kutuzuia naye.
وَإِنَّهُ لَتَذْكِرَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ﴿٤٨﴾
48. Na hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni ukumbusho kwa wenye taqwa.
وَإِنَّا لَنَعْلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ﴿٤٩﴾
49. Na hakika Sisi bila shaka Tunajua kwamba miongoni mwenu wako wenye kukadhibisha.
وَإِنَّهُ لَحَسْرَةٌ عَلَى الْكَافِرِينَ﴿٥٠﴾
50. Na hakika hii (Qur-aan) bila shaka itakuwa ni majuto makubwa juu ya makafiri.
وَإِنَّهُ لَحَقُّ الْيَقِينِ﴿٥١﴾
51. Na hakika hii (Qur-aan) ni haki ya yakini.[13]
فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ﴿٥٢﴾
52. Basi sabbih kwa Jina la Rabb wako Adhimu.
[1] Al-Haaqqah Ni Katika Majina Ya Siku Ya Qiyaamah:
Rejea Al-Qiyaamah (75;1) kwenye majina mengineyo ya Siku ya Qiyaamah.
[2] Makafiri Wa Nyumati Za Nyuma Na Aina Za Adhabu Zao:
Kuanzia Aayah hii namba (4) na zifuatazo hadi namba (12) zinataja baadhi ya nyumati za awali na adhabu zao baada ya kukadhibisha Risala ya Allaah kupitia Rusuli Wake. Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye uchambuzi na maelezo yao kwa mukhtasari kuhusu kufru, shirki na kukadhibisha kwao na maangamizi yao pamoja na rejea zake mbalimbali.
[3] Merikebu Ya Nabiy Nuwh (عليه السّلام):
Ni merikebu ya Nabiy Nuwh (عليه السّلام). Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40).
[4] Mipulizo Ya Baragumu Ya Kutokea Qiyaamah:
Kuanzia Aayah hii namba (13) hadi namba (18) yanazungumziwa matukio yatakayotokea Siku ya Qiyaamah mpaka Atakapoteremka Allaah (عزّ وجلّ) kuwafanyia hesabu waja.
Rejea Az-Zumar (39:68) kwenye maelezo yake na faida kadhaa. Rejea pia An-Naml (27:87).
[5] Kuteremka Malaika Kutoka Mbinguni Siku Ya Qiyaamah Kisha Allaah (عزّ وجلّ) Kuwahukumu Viumbe:
Rejea Al-Furqaan (25:25), Al-Fajr (89:22), Al-Baqarah (2:210), Al-An’aam (6:158).
[6] ‘Arsh Ya Ar-Rahmaan (Kiti Cha Enzi) Ni Tofauti Na Viti Vya Enzi Vya Wafalme Duniani:
Kuna kauli mbili kuhusu ‘Arsh hiyo ya Allaah (سبحانه وتعالى) watakayoibeba Malaika Siku ya Qiyaamah, kama alivyosema Imaam Ibn Kathiyr kwamba, inaweza kuwa imekusudiwa ni ‘Arsh Adhimu ya Allaah. Au ‘Arshi (ni Kiti cha Enzi) ambacho kitawekwa Siku ya Qiyaamah kwa ajili ya kuhukumiwa watu. Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Rejea Twaahaa (20:5) kwenye maelezo bayana na faida muhimu zenye kuhusiana na ‘Aqiydah ya Muislamu kuhusu ‘Arsh ‘Adhimu ya Allaah (سبحانه وتعالى).
Hata kama imekusudiwa katika Aayah hii kuwa ni Kiti cha Enzi kitakachowekwa kwa ajili ya watu kuhukumiwa, basi pia haikujulikana kayfiyah (namna yake) na hakiwezi kufanana na kiti cha enzi cha wafalme, kama vile kiti cha Malkia Balqees wa Sabaa kilichotajwa katika Suwrah An-Naml (27:23), (27:38) (27:41-42). Au pia kiti cha enzi cha Nabiy Yuwsuf (عليه السّلام), rejea Suwrah Yuwsuf (12:100).
[7] Malaika Watakaobeba ‘Arsh Ya Allaah (عزّ وجلّ):
Rejea Ghaafir (40:7) kwenye Hadiyth inayotaja sifa za Malaika wanaobeba ‘Arsh ya Allaah (عزّ وجلّ).
[8] Watakaopewa Vitabu Vyao Kuliani:
Kuanzia Aayah hii namba (19) hadi namba (24) zinaelezwa hali za watakaopewa vitabu vyao kuliani mwao. Wametajwa pia katika Suwrah Al-Inshiqaaq (84:7-9).
[9] Daraja Za Jannah:
Rejea Al-Muuminuwn (23:11) kwenye Hadiyth inayotaja daraja za Jannah, na Jannah ya Al-Firdaws kuwa ni ya juu kabisa, na nasaha ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Muumini kuwa, anapoomba Jannah, aombe Jannah ya Al-Firdaws.
[10] Watakaopewa Vitabu Vyao Kushotoni Mwao:
Kuanzia Aayah hii namba (25) hadi namba (37) zinaelezwa hali za watakaopewa vitabu vyao kushotoni mwao. Wametajwa pia katika Suwrah Al-Inshiqaaq (84:10-15).
[11] Adhimu:
Ni Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) ambayo maana zake ni: Mwenye Taadhima, Utukufu, Mkubwa na Mkuu kabisa Aliyetukuka, Mwenye Ujalali, Ukarama.
[12] Allaah (سبحانه وتعالى) Anaapia Kuthibitisha Ukweli Wa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) Na Kuwaraddi Washirikina Waliompachika Sifa Ovu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Pamoja Na Qur-aan:
Allaah (سبحانه وتعالى) Anaaapia kwa vitu vinavooonekana na visivyooonekana katika Aayah hii namba (38-39), na jibu la kiapo ni Aayah zinazofuatia namba (40-43) za kumthibitisha Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na kuithibitisha Qur-aan Tukufu kuwa ni Uteremsho kutoka Kwake, na kuwaraddi washirikina wa Makkah kwa dhulma zao za kumpachika sifa ovu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na Qur-aan Tukufu. Rejea pia Al-A’raaf (7:184), Atw-Twuwr (52:29), Sabaa (34:46), Yaasiyn (36:70), Al-Qalam (68:2), At-Takwiyr (81:22). Rejea pia Al-Furqaan (25:4), kwenye uchambuzi na maelezo bayana na rejea mbalimbali za sifa ovu kama hizo za mshairi na kahini zilizotajwa katika Aayah namba (41-42).
[13] Haqq Ya Yakini:
Haqq ya yakini (ukweli wa yakini) yaani: Kiwango cha juu cha ilimu, kwani kiwango cha juu cha ilimu ni yakini ambayo ni ilimu iliyo madhubuti, isiyoyumba wala kutetereka. Kuna viwango vitatu vya yakini, kila kimoja ni cha juu zaidi kuliko cha kabla yake: (i) Ilimu ya yakini, ambayo ni ilimu inayopatikana kutokana na khabari. (ii) Jicho la yakini, ambayo ni ilimu inayotambulika kwa maono na kuona. (iii) Ukweli wa yakini, ambao ni ujuzi unaotambulika kwa hisia ya kuonja na kuvaana na kitu.
Na hivi ndivyo ilivyo Qur-aan Tukufu. Ilimu yote iliyomo humo inaungwa mkono na uthibitisho wa uhakika na dalili za wazi kabisa, na yeyote anayepitia hayo yaliyomo ya uhakika wa ujuzi wa imaan atapata yakini ya kweli. [Tafsiyr As-Sa’diy]
الْمَعَارِج
070-Al-Ma’aarij
070-Al-Ma’aarij: Utangulizi Wa Suwrah [478]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
سَأَلَ سَائِلٌ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ﴿١﴾
1. Muulizaji ameuliza kuhusu adhabu itakayotokea.
لِّلْكَافِرِينَ لَيْسَ لَهُ دَافِعٌ﴿٢﴾
2. Kwa makafiri, ambayo hakuna wa kuikinga.
مِّنَ اللَّـهِ ذِي الْمَعَارِجِ﴿٣﴾
3. Kutoka kwa Allaah Mwenye Uluwa na fadhila tele.[1]
تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ﴿٤﴾
4. Malaika na Ar-Ruwh (roho za viumbe au Jibriyl) wanapanda Kwakekatika siku kadiri yake ni miaka khamsini elfu. [2]
فَاصْبِرْ صَبْرًا جَمِيلًا﴿٥﴾
5. Basi subiri, subira njema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).
إِنَّهُمْ يَرَوْنَهُ بَعِيدًا﴿٦﴾
6. Hakika wao wanaiona (adhabu, Qiyaamah) iko mbali.
وَنَرَاهُ قَرِيبًا﴿٧﴾
7. Nasi Tunaiona ikaribu.
يَوْمَ تَكُونُ السَّمَاءُ كَالْمُهْلِ﴿٨﴾
8. Siku mbingu itakapokuwa kama masazo ya zebaki nyeusi iliyoyeyushwa.
وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ﴿٩﴾
9. Na milima itakuwa kama sufi iliyochambuliwa.
وَلَا يَسْأَلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا﴿١٠﴾
10. Na wala rafiki wadhati hatomuuliza rafiki yake wa dhati.
يُبَصَّرُونَهُمْ ۚ يَوَدُّ الْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِي مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذٍ بِبَنِيهِ﴿١١﴾
11. Watafanywa waonane. Mhalifu atatamani ajitolee fidia kutokana na adhabu ya Siku hiyo kwa watoto wake.
وَصَاحِبَتِهِ وَأَخِيهِ﴿١٢﴾
12. Na mkewe na nduguye.
وَفَصِيلَتِهِ الَّتِي تُؤْوِيهِ﴿١٣﴾
13. Na jamaa zake wa karibu ambao wanampa hifadhi na makazi.
وَمَن فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ يُنجِيهِ﴿١٤﴾
14. Na wale wote waliomo ardhini, kisha aokoke yeye.
كَلَّا ۖ إِنَّهَا لَظَىٰ﴿١٥﴾
15. Laa hasha! Hakika huo ni moto wenye mwako mkali.
نَزَّاعَةً لِّلشَّوَىٰ﴿١٦﴾
16. Unyofoao kwa nguvu na kuunguza kikamilifu ngozi ya kichwa na viungo vya mwili.
تَدْعُو مَنْ أَدْبَرَ وَتَوَلَّىٰ﴿١٧﴾
17. Utamwita yule aliyegeuza mgongo na akakengeuka.
وَجَمَعَ فَأَوْعَىٰ﴿١٨﴾
18. Na akakusanya (mali) kisha akayahifadhi katika makasha.
إِنَّ الْإِنسَانَ خُلِقَ هَلُوعًا﴿١٩﴾
19. Hakika binaadamu ameumbwa kuwa ni mwenye kukosa subira na mwingi wa pupa.
إِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ جَزُوعًا﴿٢٠﴾
20. Inapomgusa shari, anakuwa mwingi wa kusononeka, kupapatika na kuhuzunika.
وَإِذَا مَسَّهُ الْخَيْرُ مَنُوعًا﴿٢١﴾
21. Na inapomgusa kheri, anakuwa mwingi wa kuzuia (kwa uchoyo).
إِلَّا الْمُصَلِّينَ﴿٢٢﴾
22. Isipokuwa wenye kuswali.[3]
الَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ دَائِمُونَ﴿٢٣﴾
23. Ambao wao katika Swalaah zao ni wenye kudumu.
وَالَّذِينَ فِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ مَّعْلُومٌ﴿٢٤﴾
24. Na ambao katika mali zao kuna haki maalumu.
لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ﴿٢٥﴾
25. Kwa ajili ya muombaji na asiyeomba kwa kujistahi.
وَالَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ﴿٢٦﴾
26. Na ambao wanasadikisha Siku ya Malipo.
وَالَّذِينَ هُم مِّنْ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ﴿٢٧﴾
27. Na wale wanaoiogopa adhabu kutoka kwa Rabb wao.
إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمْ غَيْرُ مَأْمُونٍ﴿٢٨﴾
28. Hakika adhabu ya Rabb wao haina muamana kwa yeyote.
وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ﴿٢٩﴾
29. Na ambao wanahifadhi tupu zao.
إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ﴿٣٠﴾
30. Isipokuwa kwa wake zao, au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao si wenye kulaumiwa.
فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ﴿٣١﴾
31. Basi yeyote yule atakayetaka kinyume ya hayo, basi hao ndio warukao mipaka.
وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ﴿٣٢﴾
32. Na ambao amana zao na ahadi zao wanazichunga (na kuzitimiza).[4]
وَالَّذِينَ هُم بِشَهَادَاتِهِمْ قَائِمُونَ﴿٣٣﴾
33. Na ambao wanatoa ushahidi wa haki na kweli.
وَالَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ﴿٣٤﴾
34. Na ambao Swalaah zao wao wanazihifadhi.
أُولَـٰئِكَ فِي جَنَّاتٍ مُّكْرَمُونَ﴿٣٥﴾
35. Hao watakuwa kwenye Jannah wakikirimiwa.
فَمَالِ الَّذِينَ كَفَرُوا قِبَلَكَ مُهْطِعِينَ﴿٣٦﴾
36. Basi wana nini waliokufuru wanaharakiza mbele yako wakinyosha shingo zao na kukukodolea macho (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)?
عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ عِزِينَ﴿٣٧﴾
37. (Kukukalia) makundi kwa makundi kuliani na kushotoni.
أَيَطْمَعُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُدْخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٍ﴿٣٨﴾
38. Je, anatumai kila mtu miongoni mwao kwamba ataingizwa Jannah ya neema?
كَلَّا ۖ إِنَّا خَلَقْنَاهُم مِّمَّا يَعْلَمُونَ﴿٣٩﴾
39. Laa, hasha! Hakika Sisi Tumewaumba kutokana na kile wanachokijua.
فَلَا أُقْسِمُ بِرَبِّ الْمَشَارِقِ وَالْمَغَارِبِ إِنَّا لَقَادِرُونَ﴿٤٠﴾
40. Basi Naapa kwa Rabb wa Mashariki na Magharibi, hakika Sisi bila shaka Ni Wenye uwezo.
عَلَىٰ أَن نُّبَدِّلَ خَيْرًا مِّنْهُمْ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ﴿٤١﴾
41. Wa kwamba Tuwabadili walio bora kuliko wao, Nasi Hatushindwi.
فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ﴿٤٢﴾
42. Basi waachilie mbali watumbukie katika porojo na upuuzi na wacheze, mpaka wakutane na Siku yao ambayo wanaahidiwa.
يَوْمَ يَخْرُجُونَ مِنَ الْأَجْدَاثِ سِرَاعًا كَأَنَّهُمْ إِلَىٰ نُصُبٍ يُوفِضُونَ﴿٤٣﴾
43. Siku watapotoka makaburini haraka haraka kama kwamba wanakimbilia viabudiwa vyao.
خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۚ ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الَّذِي كَانُوا يُوعَدُونَ﴿٤٤﴾
44. Macho yao yatainama chini, udhalilifu utawafunika. Hiyo ndio ile siku waliyokuwa wakiahidiwa.
[1] Kauli Za Mufassiruna Kuhusu Maana Ya ذُالْمعارج (Dhul-Ma’aarij):
Mwenye Uluwa na Ujalali [Tafsiyr Al-Muyassar]
Mwenye Uadhwama, Upana wa Mamlaka Yake [Tafsiyr As-Sa’diy]
Mwenye Uluwa na fadhila, Mwenye Fadhila na Neema, Mwenye Ngazi [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Mwenye Kumiliki njia za kupandia. [The Noble Quran]
[2] Roho Za Viumbe Vyote Hupandishwa Juu:
Rejea Fusw-Swilat (41:30) kwenye Hadiyth inayothibitisha hayo. Na rejea pia Al-A’raaf (7:40).
Hizo ni roho za viumbe vyote zinapotolewa hupandishwa juu, zikiwa ni za wema au waovu. Waja wema, roho zao hupandishwa juu kwa Allaah Ambaye Huzitolea idhini mbingu baada ya mbingu hadi imalizikie mbingu Aliyoko Allaah (عزّ وجلّ), na huko humtolea maamkizi Rabb wake na kumsalimia, na hufurahika kukurubishwa Naye, na Allaah Huwasifia na kuwatukuza na takrima na wema.
Ama roho za madhalimu hupanda, lakini zinapofika mbinguni na kuomba idhini ya kuingia, hazuruhusiwi na zinarudishwa ardhini.
Kwa hiyo kupaa huku ni katika ulimwengu huu, kwa sababu muktadha wa kwanza unaonyesha hivyo. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Au inaweza kumaanishwa Siku ya Qiyaamah na kwamba Allaah (تبارك وتعالى) Atadhihirisha Uadhwama Wake, Utukufu na Ufakhari Wake kwa Waja Wake Siku hiyo ambayo itakuwa ni dalili kubwa kwa Waja Wake ya kupata kumjua zaidi kutokana na yale watakayoyaona ya kupanda na kushuka Malaika na roho na mengineyo mengi katika Aliyoyaumba. Yote hayo yataendeshwa na Allaah katika Siku hiyo ambayo urefu wake utakuwa ni miaka elfu khamsini kutokana na muda wake na mashaka yake, lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Atamfanyia wepesi Muumin. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Na Aayah hii ni uthibitisho mwengine wa Allaah (سبحانه وتعالى) kuweko juu. Rejea Al-Mulk (67:16) na Al-A’raaf (7:54).
[3] Baadhi Ya Sifa Za Watu Wa Jannah:
Aayah hii (22) hadi namba (35) inataja baadhi ya sifa za watakaostahiki kuingizwa Jannah. Na sifa hizo ni takriban sawa na zile zilizotajwa katika Suwrah Al-Muuminuwn (23:1-11) ambazo kwazo watastahiki kuingizwa Jannatul-Firdaws. Rejea huko kupata faida nyenginezo.
نُوح
071-Nuwh
071-Nuwh: Utangulizi Wa Suwrah [480]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
إِنَّا أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ أَنْ أَنذِرْ قَوْمَكَ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١﴾
1. Hakika Sisi Tumemtuma Nuwh kwa kaumu yake kwamba: Waonye watu wako kabla haijawafikia adhabu iumizayo.[1]
قَالَ يَا قَوْمِ إِنِّي لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ﴿٢﴾
2. (Nuwh) akasema: Enyi kaumu yangu! Hakika mimi kwenu ni mwonyaji aliye bayana.
أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاتَّقُوهُ وَأَطِيعُونِ﴿٣﴾
3. Kwamba muabuduni Allaah, na mcheni, na mnitii.
يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرْكُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ إِنَّ أَجَلَ اللَّـهِ إِذَا جَاءَ لَا يُؤَخَّرُ ۖ لَوْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ﴿٤﴾
4. (Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakuakhirisheni mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Hakika muda uliokadiriwa na Allaah utakapokuja hautoakhirishwa, lau kama mtakuwa mnajua.
قَالَ رَبِّ إِنِّي دَعَوْتُ قَوْمِي لَيْلًا وَنَهَارًا﴿٥﴾
5. (Nuwh) akasema: Rabb wangu! Hakika mimi nimewalingania watu wangu usiku na mchana.
فَلَمْ يَزِدْهُمْ دُعَائِي إِلَّا فِرَارًا﴿٦﴾
6. Lakini wito wangu haukuwazidishia isipokuwa kukimbia.
وَإِنِّي كُلَّمَا دَعَوْتُهُمْ لِتَغْفِرَ لَهُمْ جَعَلُوا أَصَابِعَهُمْ فِي آذَانِهِمْ وَاسْتَغْشَوْا ثِيَابَهُمْ وَأَصَرُّوا وَاسْتَكْبَرُوا اسْتِكْبَارًا﴿٧﴾
7. Na hakika mimi kila nilipowaita ili Uwaghufurie, waliweka vidole vyao masikioni mwao, na wakajigubika nguo zao[2], na wakashikilia (kukanusha) na wakatakabari kwa majivuno makubwa.
ثُمَّ إِنِّي دَعَوْتُهُمْ جِهَارًا﴿٨﴾
8. Kisha hakika mimi niliwalingania kwa waziwazi.
ثُمَّ إِنِّي أَعْلَنتُ لَهُمْ وَأَسْرَرْتُ لَهُمْ إِسْرَارًا﴿٩﴾
9. Kisha hakika mimi niliwatangazia, na nikawasemesha kwa siri sana.
فَقُلْتُ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ إِنَّهُ كَانَ غَفَّارًا﴿١٠﴾
10. Nikasema: Ombeni maghfirah kwa Rabb wenu, hakika Yeye Ni Mwingi mno wa Kughufuria.[3]
يُرْسِلِ السَّمَاءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا﴿١١﴾
11. Atakutumieni mvua tele ya kuendelea.
وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّاتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَارًا﴿١٢﴾
12. Na Atakuongezeeni mali na wana, na Atakupeni mabustani na Atakupeni mito.
مَّا لَكُمْ لَا تَرْجُونَ لِلَّـهِ وَقَارًا﴿١٣﴾
13. Mna nini? Hamtaraji na hamkhofu Taadhima ya Allaah?
وَقَدْ خَلَقَكُمْ أَطْوَارًا﴿١٤﴾
14. Na hali Amekuumbeni hatua baada ya hatua?
أَلَمْ تَرَوْا كَيْفَ خَلَقَ اللَّـهُ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا﴿١٥﴾
15. Je, hamuoni vipi Allaah Ameumba mbingu saba tabaka tabaka?
وَجَعَلَ الْقَمَرَ فِيهِنَّ نُورًا وَجَعَلَ الشَّمْسَ سِرَاجًا﴿١٦﴾
16. Na Akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na Akalifanya jua ni taa ya mwanga mkali.
وَاللَّـهُ أَنبَتَكُم مِّنَ الْأَرْضِ نَبَاتًا﴿١٧﴾
17. Na Allaah Amekuanzisheni asili yenu kutokana na (udongo wa) ardhi.
ثُمَّ يُعِيدُكُمْ فِيهَا وَيُخْرِجُكُمْ إِخْرَاجًا﴿١٨﴾
18. Kisha Atakurudisheni humo, na Atakutoeni tena mtoke (kuwa hai).
وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ بِسَاطًا﴿١٩﴾
19. Na Allaah Amekufanyieni ardhi kuwa (kama) busati.
لِّتَسْلُكُوا مِنْهَا سُبُلًا فِجَاجًا﴿٢٠﴾
20. Ili mpite humo njia zilizo pana.
قَالَ نُوحٌ رَّبِّ إِنَّهُمْ عَصَوْنِي وَاتَّبَعُوا مَن لَّمْ يَزِدْهُ مَالُهُ وَوَلَدُهُ إِلَّا خَسَارًا﴿٢١﴾
21. Nuwh akasema: Rabb wangu! Hakika wao wameniasi, na wakamfuata yule ambaye hayakumzidishia mali yake na watoto wake isipokuwa khasara.
وَمَكَرُوا مَكْرًا كُبَّارًا﴿٢٢﴾
22. Na wakapanga njama kubwa mno.
وَقَالُوا لَا تَذَرُنَّ آلِهَتَكُمْ وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلَا سُوَاعًا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا﴿٢٣﴾
23. Wakasema: Msiwaache katu waabudiwa wenu. Na wala msimwache abadani Waddaa, wala Suwaa’aa, wala Yaghuwtha, na Ya’uwqa, na Nasraa.[4]
وَقَدْ أَضَلُّوا كَثِيرًا ۖ وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا ضَلَالًا﴿٢٤﴾
24. Na kwa hakika wamekwishawapoteza wengi. Na wala Usiwazidishie madhalimu isipokuwa upotofu.
مِّمَّا خَطِيئَاتِهِمْ أُغْرِقُوا فَأُدْخِلُوا نَارًا فَلَمْ يَجِدُوا لَهُم مِّن دُونِ اللَّـهِ أَنصَارًا﴿٢٥﴾
25. Kutokana na hatia zao walizamishwa, kisha wakaingizwa motoni. Basi hawakupata wowote wa kuwanusuru badala ya Allaah.
وَقَالَ نُوحٌ رَّبِّ لَا تَذَرْ عَلَى الْأَرْضِ مِنَ الْكَافِرِينَ دَيَّارًا﴿٢٦﴾
26. Na Nuwh akasema tena: Rabb wangu! Usimwache juu ya ardhi mkaazi yeyote yule kati ya makafiri.
إِنَّكَ إِن تَذَرْهُمْ يُضِلُّوا عِبَادَكَ وَلَا يَلِدُوا إِلَّا فَاجِرًا كَفَّارًا﴿٢٧﴾
27. Hakika Wewe Ukiwaacha, watawapoteza Waja Wako, na wala hawatozaa isipokuwa mtendaji dhambi, kafiri mkanushaji mno.
رَّبِّ اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيْتِيَ مُؤْمِنًا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا تَبَارًا﴿٢٨﴾
28. Rabb wangu! Nighufurie mimi, na wazazi wangu wawili, na kila aliyeingia nyumbani mwangu akiwa Muumini na Waumini wa kiume na Waumini wa kike, na wala Usiwazidishie madhalimu isipokuwa kuteketea kabisa.
[1] Nuwh (عليه السّلام) Ni Rasuli Wa Kwanza Ardhini Na Ni Baba Wa Pili Wa Wanaadam Baada Ya Nabiy Aadam (عليه السّلام):
Katika Hadiyth ndefu ya Ash-Shafaa’ah Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amethibitisha kuwa Nuwh (عليه السّلام) ni Rasuli wa kwanza ardhini kama ifuatavyo:
ائْتُوا نُوحًا فَإِنَّهُ أَوَّلُ رَسُولٍ بَعَثَهُ اللَّهُ إِلَى أَهْلِ الْأَرْضِ، فَيَأْتُونَهُ فَيَقُولُ لَسْتُ هُنَاكُمْ وَيَذْكُرُ سُؤَالَهُ رَبَّهُ مَا لَيْسَ لَهُ بِهِ عِلْمٌ فَيَسْتَحِي
“Mfuateni Nuwh, hakika yeye ndiye Rasuli wa kwanza Aliyemtuma Allaah kwa watu ardhini. Watamfuata. Naye atasema: Siwezi kufanya mnaloomba! Na atakumbuka kumuomba kwake Allaah kwa jambo asilokuwa na ujuzi nalo. Naye ataona hayaa.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hivyo, ni kwa vile makafiri wote waliokuwa hawakupanda jahazini, waligharakishwa wakabaki wale waliopanda pamoja na Nabiy Nuwh (عليه السّلام) jahazini, ambao ni wachache katika walioamini, kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika kisa cha Nabiy Nuwh (عليه السّلام) kwenye Suwrah ya Huwd (11:25-48) na katika humo ni Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَمْرُنَا وَفَارَ التَّنُّورُ قُلْنَا احْمِلْ فِيهَا مِن كُلٍّ زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ وَأَهْلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيْهِ الْقَوْلُ وَمَنْ آمَنَ ۚ وَمَا آمَنَ مَعَهُ إِلَّا قَلِيلٌ﴿٤٠﴾
“Mpaka ilipokuja Amri Yetu na tanuri likafoka, Tukasema: Beba humo (jahazini) wawili wawili kutoka kila aina; dume na jike na ahli zako, isipokuwa (kafiri) ambaye imemtangulia kauli ya hukmu na (beba humo) wale walioamini. Na hawakuamini pamoja naye isipokuwa wachache.” [Huwd (11:40)]
Rejea huko kupata faida nyenginezo.
[2] Ada Ya Makafiri Kuweka Vidole Masikioni Mwao Na Kujigubika Nguo Wasisikie Risala Wala Wasiwaona Rusuli Wanaowalingania.
Rejea An-Nisaa (4:110), Huwd (11:3) kwenye maelezo bayan na rejea mbalimbali. Pia At-Tahriym (66:8), Adh-Dhaariyaat (51:18).
[3] Fadhila Za Istighfaar (Kuomba Maghfirah )Na Tawbah (Kutubia):
Baadhi ya fadhila za Istighfaar (kuomba maghfirah) zimetajwa katika Aayah hizi (11-12), nazo ni kuteremshiwa kwa wingi, kupanuliwa mali na kuzidishiwa kizazi, kujaaliwa mashamba na mito. Fadhila nyenginezo zinapatikana katika kiungo kifuatacho pamoja na maudhui nzima ya kuomba maghfirah na kutubia:
Tawbah: Hukmu Na Fadhila Zake [337]
Rejea pia At-Tahriym (66:8) kwenye sharti za kuomba tawbah, pamoja na viungo kadhaa vya maudhui hii pamoja na faida nyenginezo na rejea mbalimbali.
Rejea pia An-Nisaa (4:110), Huwd (11:3) At-Tahriym (66:8).
[4] Waddaa, Suwaa’aa, Yaghuwtha, Ya’uwqa, Nasraa:
Ni majina ya waja wema ambao baada ya kufariki kwao, watu walichora sura zao wakawa wanawaabudu. Mwishowe wakachonga masanamu waliyokuwa wakiyaabudu watu wa Nabiy Nuwh (عليه السلام) kama inavyoelezewa katika Tafsiyr ifuatayo:
Na wakawaambia: “Msiache kuwaabudu waungu wenu mkaelekea kwenye kumuabudu Allaah Peke Yake Ambaye Nuwh (عليه السّلام) anawalingania nyinyi mumuabudu, na msimuache Waddaa, Suwaa’aa, Yaghuwth, Ya’uwq wala Nasraa.” Na haya ni majina ya masanamu yao ambayo walikuwa wakiyaabudu badala ya Allaah. Na yalikuwa ni majina ya watu wema. Walipokufa, shaytwaan alitia kwenye mawazo ya watu wao kwamba wawasimamishie masanamu na picha ili wapate moyo, kama wanavyodai, wa kuwa watiifu wanapoyaona. Walipoondoka hao waliosimamisha masanamu na muda mrefu ukapita, wakaja watu wasiokuwa wao, shaytwaan aliwatia tashwishi kwamba wakale wao waliopita walikuwa wakiyaabudu haya masanamu na picha na kutawassal nayo. Hii ndio hekima ya kuharamishwa masanamu na kuharamishwa ujengaji wa makuba juu ya makaburi. Kwa kuwa hayo kwa kupitiwa na muda yanakuwa ni yenye kuabudiwa na wajinga. [Tafsiyr Al-Muyassar]
الْجِنّ
072-Al-Jinn
072-Al-Jinn: Utangulizi Wa Suwrah [482]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا﴿١﴾
1. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Nimefunuliwa Wahy kwamba kundi miongoni mwa majini lilisikiliza, wakasema: Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya ajabu.[1]
يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ ۖ وَلَن نُّشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا﴿٢﴾
2. Inaongoza kwenye uongofu, basi tukaiamini, na wala hatutomshirikisha Rabb wetu na yeyote.
وَأَنَّهُ تَعَالَىٰ جَدُّ رَبِّنَا مَا اتَّخَذَ صَاحِبَةً وَلَا وَلَدًا﴿٣﴾
3. Na kwamba hakika umetukuka kabisa Ujalali wa Rabb wetu, Hakujifanyia mke wala mwana.
وَأَنَّهُ كَانَ يَقُولُ سَفِيهُنَا عَلَى اللَّـهِ شَطَطًا﴿٤﴾
4. Na kwamba safihi miongoni mwetu alikuwa akisema juu ya Allaah uongo uliopinduka mipaka.
وَأَنَّا ظَنَنَّا أَن لَّن تَقُولَ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا﴿٥﴾
5. Na hakika sisi tulidhania kuwa wanaadam na majini hawatosema uongo juu ya Allaah.
وَأَنَّهُ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ الْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِّنَ الْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا﴿٦﴾
6. Na kwamba wanaume miongoni mwa wanaadam walikuwa wanajikinga na wanaume miongoni mwa majini, basi wakawazidishia madhambi, uvukaji mipaka ya kuasi na khofu.
وَأَنَّهُمْ ظَنُّوا كَمَا ظَنَنتُمْ أَن لَّن يَبْعَثَ اللَّـهُ أَحَدًا﴿٧﴾
7. Na kwamba wao walidhania kama mlivyodhani nyinyi kwamba Allaah Hatomfufua yeyote (au Hatomtuma Rasuli).
وَأَنَّا لَمَسْنَا السَّمَاءَ فَوَجَدْنَاهَا مُلِئَتْ حَرَسًا شَدِيدًا وَشُهُبًا﴿٨﴾
8. Na kwamba sisi tulitafuta kuzifikia mbingu, basi tukazikuta zimejaa walinzi wakali na vimondo.
وَأَنَّا كُنَّا نَقْعُدُ مِنْهَا مَقَاعِدَ لِلسَّمْعِ ۖ فَمَن يَسْتَمِعِ الْآنَ يَجِدْ لَهُ شِهَابًا رَّصَدًا﴿٩﴾
9. Na kwamba sisi tulikuwa tukikaa huko vikao kwa ajili ya kusikiliza, basi atakayetega sikio kusikiliza sasa atakuta kimondo kinamvizia.
وَأَنَّا لَا نَدْرِي أَشَرٌّ أُرِيدَ بِمَن فِي الْأَرْضِ أَمْ أَرَادَ بِهِمْ رَبُّهُمْ رَشَدًا﴿١٠﴾
10. Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanaokaa ardhini, au Rabb wao Anawatakia uongofu.
وَأَنَّا مِنَّا الصَّالِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَ ۖ كُنَّا طَرَائِقَ قِدَدًا﴿١١﴾
11. Na kwamba miongoni mwetu wako walio wema, na miongoni mwetu wako walio kinyume chake, nasi tumekuwa makundi ya njia mbali mbali.
وَأَنَّا ظَنَنَّا أَن لَّن نُّعْجِزَ اللَّـهَ فِي الْأَرْضِ وَلَن نُّعْجِزَهُ هَرَبًا﴿١٢﴾
12. Na sisi tulikuwa na yakini kwamba hatutoweza kumshinda Allaah ardhini, na wala hatutoweza kumkwepa kutoroka.
وَأَنَّا لَمَّا سَمِعْنَا الْهُدَىٰ آمَنَّا بِهِ ۖ فَمَن يُؤْمِن بِرَبِّهِ فَلَا يَخَافُ بَخْسًا وَلَا رَهَقًا﴿١٣﴾
13. Na kwamba sisi tuliposikia mwongozo (hii Qur-aan) tuliuamini. Basi atakayemuamini Rabb wake, hatoogopa kupunjwa mazuri yake wala kuzidishiwa adhabu ya madhambi.
وَأَنَّا مِنَّا الْمُسْلِمُونَ وَمِنَّا الْقَاسِطُونَ ۖ فَمَنْ أَسْلَمَ فَأُولَـٰئِكَ تَحَرَّوْا رَشَدًا﴿١٤﴾
14. Na kwamba miongoni mwetu ni Waislamu, na miongoni mwetu ni wakengeukaji haki. Hivyo atakayesilimu, hao ndio waliofuata kidhati uongofu.
وَأَمَّا الْقَاسِطُونَ فَكَانُوا لِجَهَنَّمَ حَطَبًا﴿١٥﴾
15. Ama wakengeukaji haki, hao watakuwa kuni za Jahannam.
وَأَن لَّوِ اسْتَقَامُوا عَلَى الطَّرِيقَةِ لَأَسْقَيْنَاهُم مَّاءً غَدَقًا﴿١٦﴾
16. (Allaah Anasema): Na kwamba lau wangelinyooka kwenye njia, bila shaka Tungeliwanywesha maji kwa wingi.
لِّنَفْتِنَهُمْ فِيهِ ۚ وَمَن يُعْرِضْ عَن ذِكْرِ رَبِّهِ يَسْلُكْهُ عَذَابًا صَعَدًا﴿١٧﴾
17. Ili Tuwatie katika jaribio kwayo. Na anayepuuza Ukumbusho wa Rabb wake, Atamsukuma kwenye adhabu ngumu ya kumlemea asiiweze.
وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا﴿١٨﴾
18. Na kwamba Misikiti ni kwa ajili ya Allaah tu, basi msiombe yeyote pamoja na Allaah.[2]
وَأَنَّهُ لَمَّا قَامَ عَبْدُ اللَّـهِ يَدْعُوهُ كَادُوا يَكُونُونَ عَلَيْهِ لِبَدًا﴿١٩﴾
19. Na kwamba Mja wa Allaah (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) aliposimama kumwomba (Rabb wake), walikaribia kwa mlundikano wao kumzonga.
قُلْ إِنَّمَا أَدْعُو رَبِّي وَلَا أُشْرِكُ بِهِ أَحَدًا﴿٢٠﴾
20. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi namuomba Rabb wangu na wala simshirikishi na yeyote.
قُلْ إِنِّي لَا أَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا رَشَدًا﴿٢١﴾
21. Sema: Hakika mimi sikumilikieni dhara wala uongofu.
قُلْ إِنِّي لَن يُجِيرَنِي مِنَ اللَّـهِ أَحَدٌ وَلَنْ أَجِدَ مِن دُونِهِ مُلْتَحَدًا﴿٢٢﴾
22. Sema: Hakika hakuna yeyote awezaye kunilinda na Allaah na wala sitoweza kupata mahali pa kukimbilia ila Kwake tu.
إِلَّا بَلَاغًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِسَالَاتِهِ ۚ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا﴿٢٣﴾
23. Isipokuwa nibalighishe (haki) kutoka kwa Allaah na Ujumbe Wake. Na yeyote yule atakayemwasi Allaah na Rasuli Wake, basi hakika atapata Moto wa Jahannam, watadumu humo abadi.
حَتَّىٰ إِذَا رَأَوْا مَا يُوعَدُونَ فَسَيَعْلَمُونَ مَنْ أَضْعَفُ نَاصِرًا وَأَقَلُّ عَدَدًا﴿٢٤﴾
24. Mpaka watakapoona yale wanayoahidiwa sasa, basi watajua ni nani msaidizi dhaifu, na mchache zaidi kwa idadi.
قُلْ إِنْ أَدْرِي أَقَرِيبٌ مَّا تُوعَدُونَ أَمْ يَجْعَلُ لَهُ رَبِّي أَمَدًا﴿٢٥﴾
25. Sema: Mimi sijui kama yapo karibu hayo mnayoahidiwa, au Rabb wangu Atayaweka muda mrefu.
عَالِمُ الْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَىٰ غَيْبِهِ أَحَدًا﴿٢٦﴾
26. Mjuzi wa ghaibu, na wala Hamdhihirishii yeyote Ghaibu Yake.[3]
إِلَّا مَنِ ارْتَضَىٰ مِن رَّسُولٍ فَإِنَّهُ يَسْلُكُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ رَصَدًا﴿٢٧﴾
27. Isipokuwa Rasuli ambaye Yeye Amemridhia. Basi hakika Yeye Anamwekea walinzi mbele yake na nyuma yake.
لِّيَعْلَمَ أَن قَدْ أَبْلَغُوا رِسَالَاتِ رَبِّهِمْ وَأَحَاطَ بِمَا لَدَيْهِمْ وَأَحْصَىٰ كُلَّ شَيْءٍ عَدَدًا﴿٢٨﴾
28. Ili Ajue kwamba wamekwishabalighisha Ujumbe wa Rabb wao, na Ameyazunguka (kwa Ujuzi Wake) yale waliyo nayo, na Ametia hesabuni barabara idadi ya kila kitu.
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
Na kisa hiki cha majini kusikiliza Qur-aan, ikawashangaza, na kuilingania kwa majini wenzao, kimetajwa pia katika Suwrah Al-Ahqaaf (46:29-32).
حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، قَالَ حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ أَبِي بِشْرٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما ـ قَالَ انْطَلَقَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فِي طَائِفَةٍ مِنْ أَصْحَابِهِ عَامِدِينَ إِلَى سُوقِ عُكَاظٍ، وَقَدْ حِيلَ بَيْنَ الشَّيَاطِينِ وَبَيْنَ خَبَرِ السَّمَاءِ، وَأُرْسِلَتْ عَلَيْهِمُ الشُّهُبُ، فَرَجَعَتِ الشَّيَاطِينُ إِلَى قَوْمِهِمْ. فَقَالُوا مَا لَكُمْ فَقَالُوا حِيلَ بَيْنَنَا وَبَيْنَ خَبَرِ السَّمَاءِ، وَأُرْسِلَتْ عَلَيْنَا الشُّهُبُ. قَالُوا مَا حَالَ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ خَبَرِ السَّمَاءِ إِلاَّ شَىْءٌ حَدَثَ، فَاضْرِبُوا مَشَارِقَ الأَرْضِ وَمَغَارِبَهَا، فَانْظُرُوا مَا هَذَا الَّذِي حَالَ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ خَبَرِ السَّمَاءِ فَانْصَرَفَ أُولَئِكَ الَّذِينَ تَوَجَّهُوا نَحْوَ تِهَامَةَ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم وَهْوَ بِنَخْلَةَ، عَامِدِينَ إِلَى سُوقِ عُكَاظٍ وَهْوَ يُصَلِّي بِأَصْحَابِهِ صَلاَةَ الْفَجْرِ، فَلَمَّا سَمِعُوا الْقُرْآنَ اسْتَمَعُوا لَهُ فَقَالُوا هَذَا وَاللَّهِ الَّذِي حَالَ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ خَبَرِ السَّمَاءِ. فَهُنَالِكَ حِينَ رَجَعُوا إِلَى قَوْمِهِمْ وَقَالُوا يَا قَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا * يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ وَلَنْ نُشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا} فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَلَى نَبِيِّهِ صلى الله عليه وسلم {قُلْ أُوحِيَ إِلَىَّ} وَإِنَّمَا أُوحِيَ إِلَيْهِ قَوْلُ الْجِنِّ.
Amesimulia Ib ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka akikusudia kwenda soko la ‘Ukaadhw akifuatana na baadhi ya Swahaba. Wakati huo huo, kizuizi kiliwekwa kati ya mashaytwaan na khabari za mbinguni. Vimondo vya moto vikaanza kurushwa kwao. Mashaytwaan yalikwenda kwa watu wao, kuwauliza: “Mna tatizo gani?” Wakasema: “Kizuizi kimewekwa kati yetu na khabari za mbinguni. Na tumevurumishwa vimondo vya moto.” Wakasema: “Kitu kilichoweka kizuizi kati yenu na khabari za mbinguni kitakuwa kimetokea hivi karibuni. Nendeni upande wa Mashariki na Magharibi ili muone kizuizi kilichowekwa kati yenu na taarifa za mbinguni.” Wale walioelekea Tuhaamah walipita kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa katika eneo linaitwa Nakhlah, wakielekea soko la ‘Ukaadhw. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiwaswalisha Swahaba zake Swalaah ya Alfajiri. (Majini) waliposikia Qur-aan inasomwa, wakasikiliza kwa makini wakasema: “Hii wa-Allaahi ndio iliyokuwekeeni kizuizi baina yenu na baina ya khabari za mbingu.” Pindi waliporudi kwa watu wao wakasema: “Enyi kaumu yetu!
إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا﴿١﴾ يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ ۖ وَلَن نُّشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا﴿٢﴾
“Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya ajabu. Inaongoza kwenye uongofu, basi tukaiamini, na wala hatutomshirikisha Rabb wetu na yeyote.” [Al-Jinn (72:2)]
Allaah Akamteremshia Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم):
قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا﴿١﴾
Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Nimefunuliwa Wahy kwamba kundi miongoni mwa majini lilisikiliza; wakasema: ‘Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya ajabu. [Al-Jinn (72:1)]
[2] Kumshirikisha Allaah:
Kumshirikisha Allaah (عزّ وجلّ) ni madhambi pekee ambayo Allaah Hamghufurii mtu isipokuwa akitubia kabla ya kufariki au kabla ya jua kuchomoza upande wa Magharibi. Bonyeza kiungo kifuatacho kupata maelezo yake:
Bonyeza pia viungo vifuatavyo vyenye faida tele kuhusu shirki ya kuwaomba wasiokuwa Allaah:
Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!- إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ [485]
23-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Haijuzu Kutawassal Kwa Jaha Ya Nabiy [487]
24-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Kutawassal Kwa Waja Wema Waliofariki [488]
33-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Kutawassal Kwa Majini Na Mazimwi [490]
الْمُزَّمِّل
073-Al-Muzzammil
073-Al-Muzzammil: Utangulizi Wa Suwrah [492]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ﴿١﴾
1. Ee uliyejifunika.[1]
قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا﴿٢﴾
2. Simama (kuswali) usiku kucha isipokuwa kidogo tu.[2]
نِّصْفَهُ أَوِ انقُصْ مِنْهُ قَلِيلًا﴿٣﴾
3. Nusu yake, au ipunguze kidogo.
أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا﴿٤﴾
4. Au izidishe, na soma Qur-aan kwa kisomo cha utaratibu upasao, kuitamka vizuri na kutaamali.[3]
إِنَّا سَنُلْقِي عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا﴿٥﴾
5. Hakika Sisi Tutakuteremshia juu yako kauli nzito.[4]
إِنَّ نَاشِئَةَ اللَّيْلِ هِيَ أَشَدُّ وَطْئًا وَأَقْوَمُ قِيلًا﴿٦﴾
6. Hakika kuamka usiku (kuswali) ni uthibiti zaidi wa kuathiri moyo na kuifahamu, na unyofu zaidi wa maneno kutua.
إِنَّ لَكَ فِي النَّهَارِ سَبْحًا طَوِيلًا﴿٧﴾
7. Hakika una mchana mrefu kwa shughuli nyingi.
وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلْ إِلَيْهِ تَبْتِيلًا﴿٨﴾
8. Na dhukuru Jina la Rabb wako, na jitolee Kwake kwa kujitolea kikamilifu.
رَّبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَاتَّخِذْهُ وَكِيلًا﴿٩﴾
9. Rabb wa Mashariki na Magharibi, hakuna muabudiwa wa haki ila Yeye. Basi mfanye kuwa ni Mdhamini wako.
وَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَاهْجُرْهُمْ هَجْرًا جَمِيلًا﴿١٠﴾
10. Na subiri juu ya yale wayasemayo, na wahame, mhamo mzuri.
وَذَرْنِي وَالْمُكَذِّبِينَ أُولِي النَّعْمَةِ وَمَهِّلْهُمْ قَلِيلًا﴿١١﴾
11. Na Niache Mimi na wanaokadhibisha walioneemeka, na uwape muhula kidogo.
إِنَّ لَدَيْنَا أَنكَالًا وَجَحِيمًا﴿١٢﴾
12. Hakika Sisi Tuna minyororo na moto uwakao vikali mno.
وَطَعَامًا ذَا غُصَّةٍ وَعَذَابًا أَلِيمًا﴿١٣﴾
13. Na chakula cha kusakama kooni, na adhabu iumizayo.
يَوْمَ تَرْجُفُ الْأَرْضُ وَالْجِبَالُ وَكَانَتِ الْجِبَالُ كَثِيبًا مَّهِيلًا﴿١٤﴾
14. Siku itakayotikisika ardhi na milima, na milima itakuwa kama rundo la mchanga tifutifu.
إِنَّا أَرْسَلْنَا إِلَيْكُمْ رَسُولًا شَاهِدًا عَلَيْكُمْ كَمَا أَرْسَلْنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ رَسُولًا﴿١٥﴾
15. Hakika Sisi Tumekutumieni Rasuli awe shahidi juu yenu, kama Tulivyotuma Rasuli kwa Firawni.
فَعَصَىٰ فِرْعَوْنُ الرَّسُولَ فَأَخَذْنَاهُ أَخْذًا وَبِيلًا﴿١٦﴾
16. Lakini Firawni alimuasi huyo Rasuli, Tukamshika kwa maangamizi makali mno.
فَكَيْفَ تَتَّقُونَ إِن كَفَرْتُمْ يَوْمًا يَجْعَلُ الْوِلْدَانَ شِيبًا﴿١٧﴾
17. Basi vipi mtaweza kujikinga, kama mkikufuru Siku itakayowafanya watoto kuwa wenye kutoka mvi?
السَّمَاءُ مُنفَطِرٌ بِهِ ۚ كَانَ وَعْدُهُ مَفْعُولًا﴿١٨﴾
18. Mbingu zitapasuka hapo (kwa sababu ya Siku hiyo), Ahadi Yake itatimizwa.
إِنَّ هَـٰذِهِ تَذْكِرَةٌ ۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ سَبِيلًا﴿١٩﴾
19. Hakika haya (yaliyotajwa kwenye Aayaat hizi) ni ukumbusho. Basi atakaye ashike njia ya kuelekea kwa Rabb wake.
إِنَّ رَبَّكَ يَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدْنَىٰ مِن ثُلُثَيِ اللَّيْلِ وَنِصْفَهُ وَثُلُثَهُ وَطَائِفَةٌ مِّنَ الَّذِينَ مَعَكَ ۚ وَاللَّـهُ يُقَدِّرُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ ۚ عَلِمَ أَن لَّن تُحْصُوهُ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۖ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنَ الْقُرْآنِ ۚ عَلِمَ أَن سَيَكُونُ مِنكُم مَّرْضَىٰ ۙ وَآخَرُونَ يَضْرِبُونَ فِي الْأَرْضِ يَبْتَغُونَ مِن فَضْلِ اللَّـهِ ۙ وَآخَرُونَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ ۖ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنْهُ ۚ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَقْرِضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا ۚ وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّـهِ هُوَ خَيْرًا وَأَعْظَمَ أَجْرًا ۚ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴿٢٠﴾
20. Hakika Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Anajua kwamba unasimama (kuswali) karibu na thuluthi mbili za usiku au nusu yake, au thuluthi yake, na kundi miongoni mwa wale walio pamoja nawe. Na Allaah Anakadiria usiku na mchana. Anajua kwamba hamuwezi kuukadiria wakati wake na kusimama kuswali, basi Amepokea tawbah yenu. Basi someni kile kilicho chepesi katika Qur-aan.[5] (Allaah) Anajua kwamba watakuweko miongoni mwenu wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wanatafuta Fadhila za Allaah, na wengineo wanapigana katika Njia ya Allaah. Basi someni kile kilicho chepesi humo. Na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, na mkopesheni Allaah karadha mzuri. Na chochote kile cha kheri mnachokadimisha kwa ajili ya nafsi zenu, mtakikuta kwa Allaah kizuri zaidi na chenye ujira mkubwa zaidi[6] Na muombeni Allaah maghfirah[7], hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.[8]
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
073-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Muzzammil: يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ [493]
Rejea pia Al-Muddath-thir (74:1), na Al-‘Alaq (96:1) ambako kuna Hadiyth inayoelezea tukio la Jibriyl (عليه السّلام) kumfikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa katika pango la Hiraa akitafakari Uumbaji wa Allaah Akateremshiwa Wahy wa kwanza kabisa.
[2] Qiyaamul-Layl Na Fadhila Zake:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
Fadhila Na Faida Za Qiyaamul-Layl [333]
Rejea pia Adh-Dhaariyaat (51:15) kwenye faida kadhaa na rejea nyenginezo.
[3] Fadhila Za Kusoma Qur-aan Na Somo La Tajwiyd:
Kusoma na kuhifadhi Qur-aan kuna fadhila kubwa na thawabu adhimu. Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida zake tele:
Fadhila Za Qur-aan Na Umuhimu Wake: Aayaat Za Qur-aan [494]
Fadhila Za Kusoma Na Kuhifadhi Qur-aan Katika Hadiyth Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) [495]
Maamrisho Ya Kuisoma Qur-aan Na Kuifanyia Kazi [496]
Vipi Uweze Kuhifadhi Qur-aan? (كَيْفَ تَحْفَظُ الْقُرآن) [497]
|
Tajwiyd - Alhidaaya Katika Ahkaam Za Tajwiyd [500]
[4] Uteremsho Wa Wahy Kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ulikuwa Ni Mzito Mno!
Hadiyth ifuatayo inaelezea:
حَدَّثَنَا فَرْوَةُ، حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ مُسْهِرٍ، عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ ـ رضى الله عنها ـ أَنَّ الْحَارِثَ بْنَ هِشَامٍ، سَأَلَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم كَيْفَ يَأْتِيكَ الْوَحْىُ قَالَ " كُلُّ ذَاكَ يَأْتِي الْمَلَكُ أَحْيَانًا فِي مِثْلِ صَلْصَلَةِ الْجَرَسِ، فَيَفْصِمُ عَنِّي وَقَدْ وَعَيْتُ مَا قَالَ، وَهْوَ أَشَدُّهُ عَلَىَّ، وَيَتَمَثَّلُ لِي الْمَلَكُ أَحْيَانًا رَجُلاً، فَيُكَلِّمُنِي فَأَعِي مَا يَقُولُ
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Al-Haarith Bin Hishaam alimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Je, Wahy unakujia vipi? Akasema: “Katika njia zote hizi: Wakati mwengine Malaika anakuja kwangu na sauti inayofanana na mlio wa kengele, na hali hiyo inaponiacha, nakumbuka kila alichosema Malaika. Na njia hii ya Wahy ndio iliyo nzito zaidi kwangu. Na wakati mwengine Malaika anakuja kwangu kwa sura za mwanaadam na kuzungumza nami, nami nakumbuka alichosema.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Uanzishaji wa Uumbaji (59)]
[5] Kusoma Kilicho Chepesi Katika Qur-aan Ndani Ya Swalaah:
Katika Swalaah za fardhi, haijaamrishwa kusoma kisomo kirefu cha Qur-aan isipokuwa tu katika Swalaah ya Alfajiri kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَىٰ غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ ۖ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا ﴿٧٨﴾
“Simamisha Swalaah jua linapopinduka hadi kiza cha usiku na (refusha) Qur-aan ya (Swalaah ya) Alfajiri. Hakika Qur-aan ya Alfajiri ni yenye kushuhudiwa.” [Al-Israa (17:78)]
Ama katika Swalaah nyenginezo za fardhi, Muislamu anatakiwa asome chochote kilicho chepesi kama alivyoamrishwa Swahaba ambaye aliswali kwa haraka kabisa na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwamrisha airudie Swalaah yake na asome kilicho chepesi katika Qur-aan:
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ بَشَّارٍ، قَالَ حَدَّثَنَا يَحْيَى، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، قَالَ حَدَّثَنِي سَعِيدُ بْنُ أَبِي سَعِيدٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم دَخَلَ الْمَسْجِدَ، فَدَخَلَ رَجُلٌ فَصَلَّى فَسَلَّمَ عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَرَدَّ وَقَالَ " ارْجِعْ فَصَلِّ، فَإِنَّكَ لَمْ تُصَلِّ ". فَرَجَعَ يُصَلِّي كَمَا صَلَّى ثُمَّ جَاءَ فَسَلَّمَ عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ " ارْجِعْ فَصَلِّ فَإِنَّكَ لَمْ تُصَلِّ " ثَلاَثًا. فَقَالَ وَالَّذِي بَعَثَكَ بِالْحَقِّ مَا أُحْسِنُ غَيْرَهُ فَعَلِّمْنِي. فَقَالَ " إِذَا قُمْتَ إِلَى الصَّلاَةِ فَكَبِّرْ، ثُمَّ اقْرَأْ مَا تَيَسَّرَ مَعَكَ مِنَ الْقُرْآنِ، ثُمَّ ارْكَعْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ رَاكِعًا، ثُمَّ ارْفَعْ حَتَّى تَعْتَدِلَ قَائِمًا، ثُمَّ اسْجُدْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ سَاجِدًا، ثُمَّ ارْفَعْ حَتَّى تَطْمَئِنَّ جَالِسًا، وَافْعَلْ ذَلِكَ فِي صَلاَتِكَ كُلِّهَا ".
Amesimulia Abu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliingia Msikitini na mtu akamfuata. Yule mtu aliswali akaenda kumsalimu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuitikia Salaam kisha akamwambia: “Nenda urudie kuswali kwani hukuswali.” Yule mtu alikwenda akaswali kama mwanzo, kisha akarejea na kumsalimu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Nenda urudie kuswali kwani hukuswali.” Hilo lilijiri mara tatu. Yule mtu akasema: “Naapa kwa Aliyekutuma kwa haki! Siwezi kuswali vizuri zaidi ya hivi, basi nifundishe: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Unaposimama kuswali tamka Takbiyr (Allaahu Akbar) kisha soma chepesi ulichonacho katika Quraan, halafu rukuu mpaka utulie katika rukuu. Kisha inua kichwa na usimame wima (utulie), kisha sujudu mpaka utulie kabisa katika Sujuwd, kisha nyanyuka mpaka utulie katika kikao, halafu sujudu mpaka utulie katika sijdah, kisha nyanyuka mpaka utulie katika kikao, halafu fanya hivyo katika Swalaah yako yote.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Adhaan Sifa Ya Swalaah (10b)]
Ama Swalaah ya Qiyaamul-Layl (Kisimamo Cha Usiku) ambayo imesisitizwa mno na ina fadhila nyingi adhimu kabisa [Rejea Adh-Dhaariyaat (51:15)], imependekezwa kisimamo kirefu kusoma Qur-aan, lakini haijakalifishwa kwa mtu kufanya hivyo kwani chochote anachojaaliwa mtu kusoma basi kina fadhila zake kama ilivyotajwa katika Hadiyth ifuatayo:
عبدالله بن عمرو عن النبي صلى الله عليه وسلم ((من قام بعشرِ آياتٍ لم يُكتبْ من الغافلينَ ، ومن قام بمئةِ آيةٍ كُتبَ من القانتينَ ومن قام بألفِ آيةٍ كُتبَ من المُقَنْطِرينَ)) صحيح أبي داود
“Atakayesimama usiku kwa kuswali na kusoma Aayah kumi hatoandikiwa katika miongoni mwa walioghafilika, na atakayesimama kwa Aayah mia ataandikiwa ni miongoni mwa watiifu na atakayesimama kwa Aayah elfu ataandikwa miongoni mwa wenye mirundi (ya thawabu).” [Abuu Daawuwd ameisahihisha Al-Albaaniy: Swahiyh Abiy Daawuwd (1398), Swahiyh Al-Jaami’ (6439)]
[6] Fadhila Za Kutoa Katika Njia Ya Allaah:
Rejea Al-Hadiyd (57:11) kwenye faida tele na rejea mbalimbali.
[7] Amri Ya Kumuomba Allaah Maghfirah Na Fadhila Zake:
Rejea An-Nisaa (4:110), Huwd (11:3) kwenye maelezo bayan na rejea mbalimbali. Pia At-Tahriym (66:8), Nuwh (71:10), Adh-Dhaariyaat (51:18).
[8] Tafsiyr Ya Aayah:
Hakika Rabb wako ee Nabiy, Anajua kuwa wewe unasimama kwa Tahajjud (Kisimamo cha usiku kuswali) kipindi cha usiku, wakati mwingine chini ya theluthi mbili za usiku, na wakati mwingine unasimama nusu yake, na wakati mwingine theluthi yake. Na wanasimama pamoja na wewe kundi la Swahaba zako. Na Allaah Pekee Ndiye Anayekadiria usiku na mchana, na Anajua vipimo vyake na kipindi kinachopita na kusalia cha mchana na usiku. Allaah Anajua kwamba haiwezekani kwenu nyinyi kusimama usiku wote, hivyo basi Akawafanyia mambo kuwa mepesi kwenu. Na msome kwenye Swalaah ya usiku kile kilichokuwa chepesi kwenu kukisoma katika Qur-aan. Allaah Anajua kuwa miongoni mwenu kuna wanaoelemewa na ugonjwa wasiweze kusimama usiku. Na kuna watu wengine wanatembea ardhini kwa biashara na kazi wakitafuta riziki ya Allaah ya halaal. Na kuna watu wengine wanapigana Jihaad katika Njia ya Allaah ili kuliinua neno Lake na kutangaza Dini Yake. Basi someni kutoka kwenye Qur-aan kile kilicho chepesi kwenu, na endeleeni kutekeleza faradhi za Swalaah, na toeni Zakaah za lazima kwenu, na toeni swadaqa za mali yenu katika njia za wema na ihsaan kwa kutaka Radhi za Allaah. Na chochote kile mnachokifanya miongoni mwa njia za wema na kheri na matendo ya utiifu, basi mtapata malipo yake na thawabu zake kwa Allaah (سبحانه وتعالى) Siku ya Qiyaamah, hali ya kuwa ni bora zaidi na chenye thawabu kubwa zaidi kuliko kile mlichokitanguliza duniani. Na ombeni maghfira kwa Allaah katika hali zenu zote. Allaah Ni Mwingi wa kuwaghufuria sana nyinyi na Mwenye Kuwarehemu. [Tafsiyr Al-Muyassar]
الْمُدَّثِّر
074-Al-Muddath-thir
074-Al-Muddath-thir: Utangulizi Wa Suwrah [502]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ﴿١﴾
1. Ee mwenye kujigubika![1]
قُمْ فَأَنذِرْ﴿٢﴾
2. Simama uonye.
وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ﴿٣﴾
3. Na Rabb wako mtukuze.
وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ﴿٤﴾
4. Na nguo zako toharisha.[2]
وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ﴿٥﴾
5. Na masanamu na machafu endelea kuepukana nayo.
وَلَا تَمْنُن تَسْتَكْثِرُ﴿٦﴾
6. Na wala usifanye fadhila kwa ajili ya kutaraji kukithirishiwa.
وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ﴿٧﴾
7. Na kwa ajili ya Rabb wako subiri.
فَإِذَا نُقِرَ فِي النَّاقُورِ﴿٨﴾
8. Litakapopulizwa baragumu kwa sauti kali.
فَذَٰلِكَ يَوْمَئِذٍ يَوْمٌ عَسِيرٌ﴿٩﴾
9. Basi hiyo itakuwa ni Siku ngumu mno.[3]
عَلَى الْكَافِرِينَ غَيْرُ يَسِيرٍ﴿١٠﴾
10. Kwa makafiri si nyepesi.
ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا﴿١١﴾
11. Niache Mimi na yule Niliyemuumba Pekee.[4]
وَجَعَلْتُ لَهُ مَالًا مَّمْدُودًا﴿١٢﴾
12. Na Nikamjaalia mali tele.
وَبَنِينَ شُهُودًا﴿١٣﴾
13. Na watoto walio naye nyakati zote.
وَمَهَّدتُّ لَهُ تَمْهِيدًا﴿١٤﴾
14. Na Nikamkunjulia njia zote za maisha mazuri.
ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ﴿١٥﴾
15. Kisha anatumaini Nimuongezee.
كَلَّا ۖ إِنَّهُ كَانَ لِآيَاتِنَا عَنِيدًا﴿١٦﴾
16. Laa, hasha! Hakika yeye amekuwa anidi na mpinzani wa Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) Zetu.
سَأُرْهِقُهُ صَعُودًا﴿١٧﴾
17. Nitamshurutisha adhabu ngumu asiyoiweza.
إِنَّهُ فَكَّرَ وَقَدَّرَ﴿١٨﴾
18. Hakika yeye alitafakari na akakadiria.[5]
فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ﴿١٩﴾
19. Basi alaaniwe na aangamie mbali. Namna gani kakadiria?!
ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ﴿٢٠﴾
20. Kisha alaaniwe na aangamie mbali. Namna gani kakadiria?!
ثُمَّ نَظَرَ﴿٢١﴾
21. Kisha akatazama.
ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ﴿٢٢﴾
22. Kisha akakunja kipaji na akafinya uso kwa ghadhabu.
ثُمَّ أَدْبَرَ وَاسْتَكْبَرَ﴿٢٣﴾
23. Kisha akageuka nyuma na akatakabari.
فَقَالَ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ﴿٢٤﴾
24. Akasema: Hii (Qur-aan) si chochote isipokuwa ni sihiri inayonukuliwa.
إِنْ هَـٰذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ﴿٢٥﴾
25. Hii si chochote isipokuwa ni maneno ya binaadam tu.
سَأُصْلِيهِ سَقَرَ﴿٢٦﴾
26. Nitamuingiza Saqar[6] aungue.
وَمَا أَدْرَاكَ مَا سَقَرُ﴿٢٧﴾
27. Na kipi kitakachokujulisha ni nini hiyo Saqar?
لَا تُبْقِي وَلَا تَذَرُ﴿٢٨﴾
28. (Ni moto ambao) haubakishi wala hauachi (kitu kisiunguzwe).
لَوَّاحَةٌ لِّلْبَشَرِ﴿٢٩﴾
29. Wenye kubabua vibaya ngozi.
عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ﴿٣٠﴾
30. Juu yake wako (walinzi) kumi na tisa.
وَمَا جَعَلْنَا أَصْحَابَ النَّارِ إِلَّا مَلَائِكَةً ۙ وَمَا جَعَلْنَا عِدَّتَهُمْ إِلَّا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا لِيَسْتَيْقِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا ۙ وَلَا يَرْتَابَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْمُؤْمِنُونَ ۙ وَلِيَقُولَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْكَافِرُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّـهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَمَا يَعْلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ ۚ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْبَشَرِ﴿٣١﴾
31. Na Hatukuweka walinzi wa moto isipokuwa ni Malaika. Na Hatukufanya idadi yao isipokuwa iwe ni jaribio kwa wale waliokufuru, ili wayakinishe wale waliopewa Kitabu, na iwazidishie iymaan wale walioamini, na wala wasitie shaka wale waliopewa Kitabu na Waumini. Na ili wale waliokuwa na maradhi nyoyoni mwao[7] (ya unafiki, shaka) na makafiri waseme: Allaah Amekusudia nini kwa mfano huu? Hivyo ndivyo Allaah Anavyompotoa Amtakaye na Anamhidi Amtakaye. Na hakuna ajuaye majeshi ya Rabb wako isipokuwa Yeye Pekee. Na haya si chochote isipokuwa ni ukumbusho kwa binaadam.[8]
كَلَّا وَالْقَمَرِ﴿٣٢﴾
32. Laa, hasha! Naapa kwa mwezi.
وَاللَّيْلِ إِذْ أَدْبَرَ﴿٣٣﴾
33. Na Naapa kwa usiku unapoondoka.
وَالصُّبْحِ إِذَا أَسْفَرَ﴿٣٤﴾
34. Na Naapa kwa asubuhi inapoangaza.
إِنَّهَا لَإِحْدَى الْكُبَرِ﴿٣٥﴾
35. Hakika huo (moto) bila shaka ni mojawapo ya majanga makubwa kabisa.
نَذِيرًا لِّلْبَشَرِ﴿٣٦﴾
36. Ni onyo kwa binaadam.
لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَتَقَدَّمَ أَوْ يَتَأَخَّرَ﴿٣٧﴾
37. Kwa atakaye miongoni mwenu atakadamu mbele au ataakhari nyuma.
كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَةٌ﴿٣٨﴾
38. Kila nafsi iko katika rehani kwa yale iliyoyachuma.
إِلَّا أَصْحَابَ الْيَمِينِ﴿٣٩﴾
39. Isipokuwa watu wa kuliani.
فِي جَنَّاتٍ يَتَسَاءَلُونَ﴿٤٠﴾
40. Katika Jannaat wanaulizana.
عَنِ الْمُجْرِمِينَ﴿٤١﴾
41. Kuhusu wahalifu.
مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ﴿٤٢﴾
42. (Watawauliza): Nini kilichokuingizeni katika Saqar?
قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ﴿٤٣﴾
43. Watasema: Hatukuwa miongoni mwa wanaoswali.
وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ الْمِسْكِينَ﴿٤٤﴾
44. Na wala hatukuwa tunalisha masikini.
وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ الْخَائِضِينَ﴿٤٥﴾
45. Na tulikuwa tunatumbukia kwenye upuuzi pamoja na wanaotumbukia upuuzini.
وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ﴿٤٦﴾
46. Na tulikuwa tunaikadhibisha Siku ya malipo.
حَتَّىٰ أَتَانَا الْيَقِينُ﴿٤٧﴾
47. Mpaka ikatufikia yakini (mauti).
فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ﴿٤٨﴾
48. Basi hautowafaa uombezi wowote wa waombezi.
فَمَا لَهُمْ عَنِ التَّذْكِرَةِ مُعْرِضِينَ﴿٤٩﴾
49. Basi wana nini hata wanaugeukilia mbali ukumbusho huu!
كَأَنَّهُمْ حُمُرٌ مُّسْتَنفِرَةٌ﴿٥٠﴾
50. Kama kwamba ni punda milia wenye kutimuliwa.
فَرَّتْ مِن قَسْوَرَةٍ﴿٥١﴾
51. Wamekimbia mbio kutokana na wawindaji (au simba).
بَلْ يُرِيدُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُؤْتَىٰ صُحُفًا مُّنَشَّرَةً﴿٥٢﴾
52. Bali anataka kila mtu miongoni mwao wao apewe sahifa zilizofunuliwa.
كَلَّا ۖ بَل لَّا يَخَافُونَ الْآخِرَةَ﴿٥٣﴾
53. Laa, hasha! Bali hawaiogopi Aakhirah.
كَلَّا إِنَّهُ تَذْكِرَةٌ﴿٥٤﴾
54. Laa, hasha! Hakika hii (Qur-aan) ni mawaidha.
فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ﴿٥٥﴾
55. Basi anayetaka atawaidhika.
وَمَا يَذْكُرُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ ۚ هُوَ أَهْلُ التَّقْوَىٰ وَأَهْلُ الْمَغْفِرَةِ﴿٥٦﴾
56. Na hawatowaidhika isipokuwa Akitaka Allaah. Yeye Ndiye Mstahiki wa Kuogopwa, na Mstahiki wa Kughufuria (madhambi).
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
074-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Muddath-thir Aayah 1-7: يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ [503]
[2] Maana Ya Kutoharisha Nguo:
Kutoharisha nguo kunawezekana kumaanishwa kutakasa amali kwa kusafishia niyya na kuzitekeleza kwa ukamilifu kabisa, kuondosha chochote ambacho kinaweza kuziharibu na kuzibatilisha kama vile riyaa-a, unafiki, kujisifu, kiburi, uzembe na mengineyo ambayo mtu ameamrishwa kuachana nayo katika ibaada zake.
Hayo ni pamoja na kutoharisha nguo za mtu na kuondoa uchafu wake, kwani hiyo ni katika kutakasa amali, khasa katika hali ya Swalaah ambayo ‘Ulamaa wamesema kuwa kuondosha najisi ni katika sharti za Swalaah.
Inawezekana pia kwamba kinachokusudiwa ni nguo zake zinazojulikana, na kwamba ameamrishwa kuzitakasa na uchafu wote, wakati wote, na hasa wakati wa kuingia kwenye Swalaah. Na ikiwa ameamrishwa kuitakasa nguo ya nje, basi ni usafi ambao unakamilisha wa ndani. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida zinazohusiana na Twahara ya Swalaah:
01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتَابُ اَلطَّهَارَةِ - Kitabu Cha Twahara [504]
[3] Siku Ya Qiyaamah Ni Siku Ngumu Kwa Makafiri:
Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):
يَقُولُ الْكَافِرُونَ هَـٰذَا يَوْمٌ عَسِرٌ ﴿٨﴾
Makafiri watasema: Hii ni siku ngumu mno! [Al-Qamar (54:8)]
[4] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Kuanzia Aayah hii namba (11) hadi namba (31), bonyeza kiungo kifuatacho:
074-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Muddath-thir Aayah 11- 31: ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا [505]
[5] Alikadiria Vipi?
Alipima, alitafakari, alipanga na kuandaa hila ya jinsi ya kumtia dosari Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kuibatilisha Qur-aan.
Alitafakari ndani ya nafsi yake akatayarisha la kusema ili kumtukana Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Qur-aan, kwa hiyo akalaaniwa na akastahiki kulaaniwa na kuangamizwa kwani vipi alivyojipanga ndani ya nafsi kwa hayo matusi, kisha akalaaniwa tena (Aayah zinazofuatia). [Tafsiyr Al-Muyassar]
[6] سَقَر(Saqar) Na Majina Mengineyo Ya Moto Ya Jahannam:
Saqar ni jina miongoni mwa majina ya moto ya Aakhirah, ni moto uwakao vikali mno! Majina mengineyo ya moto ya Aakhirah ni: (i) جَهَنَّم – Jahannam (ii) الجَحِيم – Al-Jahiym (iii) السَّعير -As-Sa’iyr (iv) لَظى – Ladhwaa (v) الْحُطَمَةُ – Al-Hutwamah (vi) الهاوِية – Al-Haawiyah.
Kila mmoja una sifa yake maalumu. Baadhi yake Allaah (سبحانه وتعالى) Ameeleza sifa zake katika Aayah zake zinazoendelea. Na katika majina hayo ya moto, uliotajwa mara nyingi zaidi katika Qur-aan ni Jahannam kama katika An-Nabaa (78:21), na Al-Jahiym katika An-Naazi’aat (79:36), na As-Sa’iyr katika Al-Inshiqaaq (84:12). Ama mingineyo ni Al-Hutwamah katika Al-Humazah (104:4-5), na Ladhwaa katika Al-Ma’aarij (70: 15-16), na Al-Haawiyah katika Al-Qaari’ah (101: 9-11).
Na milango ya moto ni saba kama ilivyotajwa katika Suwrah Al-Hijr (15:44).
Rejea An-Nabaa (78:21) kwenye maelezo bayana kuhusu mateso na adhabu za watu wa motoni.
[7] Nyoyo Zenye Maradhi:
Rejea Suwrah Muhammad (47:20) kwenye maelezo na rejea mbalimbali kuhusu nyoyo zenye maradhi.
Rejea pia Al-Hajj (22:46) kwenye maelezo kuhusu maana ya moyo uliopofuka.
Rejea pia Ash-Shu’araa (26:88-89) kwenye ufafanuzi na maelezo kuhusu moyo uliosalimika.
[8] Tafsiyr Ya Aayah:
Na Hatukuwafanya washika hazina wa motoni isipokuwa miongoni mwa Malaika washupavu. Na Hatukuiweka idadi hiyo isipokuwa kuwatahini wale waliomkufuru Allaah na ili imaan ya yakini ipatikane kwa wale Mayahudi na Manaswara waliopewa Vitabu kwamba yaliyokuja ndani ya Qur-aan juu ya washika hazina wa motoni ni ukweli utokao kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwani hayo yanaafikiana na vitabu vyao, na ili Waumini wazidi kumuamini Allaah na Rasuli Wake, na waifuate Sharia Yake kivitendo, na ili wasilifanyie shaka hilo wale Mayahudi na Manaswara waliopewa Vitabu wala wale wenye kumuamini Allaah na Rasuli Wake, na ili wapate kusema wale wenye unafiki ndani ya nyoyo zao na makafiri: Ni lipi alilolikusudia Allaah kwa idadi hii ya ajabu? Kwa mfano wa hayo yaliyotajwa, Allaah Anampoteza Anayetaka kumpoteza na Anamuongoza Anayetaka kumuongoza. Na hakuna ajuwaye idadi ya askari wa Rabb wako, na miongoni mwao ni Malaika, isipokuwa Allaah Peke Yake. Na haukuwa huu moto isipokuwa ni ukumbusho na mazingatio kwa watu. [Tafsiyr Al-Muyassar]
الْقِيَامَة
075-Al-Qiyaamah
075-Al-Qiyaamah: Utangulizi Wa Suwrah [507]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
لَا أُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ﴿١﴾
1. Naapa kwa Siku ya Qiyaamah.[1]
وَلَا أُقْسِمُ بِالنَّفْسِ اللَّوَّامَةِ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa nafsi inayojilaumu sana.[2]
أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَلَّن نَّجْمَعَ عِظَامَهُ﴿٣﴾
3. Je, anadhani binaadam kwamba Hatutoikusanya mifupa yake?[3]
بَلَىٰ قَادِرِينَ عَلَىٰ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُ﴿٤﴾
4. Sivyo hivyo! Bali Tuna Uwezo wa kusawazisha sawasawa ncha za vidole vyake.
بَلْ يُرِيدُ الْإِنسَانُ لِيَفْجُرَ أَمَامَهُ﴿٥﴾
5. Bali anataka binaadam aendelee kutenda dhambi na kukanusha umri wake ulobakia.
يَسْأَلُ أَيَّانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ﴿٦﴾
6. Anauliza ni lini hiyo siku ya Qiyaamah?[4]
فَإِذَا بَرِقَ الْبَصَرُ﴿٧﴾
7. Basi jicho litakapoduwaa.
وَخَسَفَ الْقَمَرُ﴿٨﴾
8. Na mwezi utakapopatwa.[5]
وَجُمِعَ الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ﴿٩﴾
9. Na jua na mwezi vitakapojumuishwa.
يَقُولُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ أَيْنَ الْمَفَرُّ﴿١٠﴾
10. Atasema binaadam siku hiyo: Wapi pa kukimbilia?
كَلَّا لَا وَزَرَ﴿١١﴾
11. Laa hasha! Hapana mahali pa kimbilio.
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمُسْتَقَرُّ﴿١٢﴾
12. Kwa Rabb wako siku hiyo ndio makazi ya kustakiri.
يُنَبَّأُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ﴿١٣﴾
13. Siku hiyo binaadam atajulishwa yale aliyoyakadimisha na aliyoyaakhirisha.[6]
بَلِ الْإِنسَانُ عَلَىٰ نَفْسِهِ بَصِيرَةٌ﴿١٤﴾
14. Bali binaadam ni shahidi dhidi ya nafsi yake.[7]
وَلَوْ أَلْقَىٰ مَعَاذِيرَهُ﴿١٥﴾
15. Japo akitoa nyudhuru zake zote.[8]
لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ﴿١٦﴾
16. Usiutikisie (huu Wahy) ulimi wako ili kuiharakiza (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).[9]
إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ﴿١٧﴾
17. Hakika ni juu Yetu Kuikusanya na Kukuwezesha kuisoma kwake.
فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ﴿١٨﴾
18. Basi Tunapoisoma (kupitia Jibriyl), fuata kusomwa kwake.
ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ﴿١٩﴾
19. Kisha ni juu Yetu Kuibainisha (kwako).
كَلَّا بَلْ تُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ﴿٢٠﴾
20. Laa hasha! Bali mnapenda uhai wa dunia.
وَتَذَرُونَ الْآخِرَةَ﴿٢١﴾
21. Na mnaiacha Aakhirah.
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ﴿٢٢﴾
22. Nyuso siku hiyo zitanawiri.
إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ﴿٢٣﴾
23. Zikimtazama Rabb wake.[10]
وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ بَاسِرَةٌ﴿٢٤﴾
24. Na nyuso (nyenginezo) siku hiyo zitakunjana.
تَظُنُّ أَن يُفْعَلَ بِهَا فَاقِرَةٌ﴿٢٥﴾
25. Zikiwa na yakini kuwa zitafikiwa na msiba unaovunja uti wa mgongo.
كَلَّا إِذَا بَلَغَتِ التَّرَاقِيَ﴿٢٦﴾
26. Laa hasha! Itakapofika (roho) mafupa ya koo.
وَقِيلَ مَنْ ۜ رَاقٍ﴿٢٧﴾
27. Na itasemwa: Ni nani tabibu wa kumponya?
وَظَنَّ أَنَّهُ الْفِرَاقُ﴿٢٨﴾
28. Na atakuwa na yakini kwamba hakika hivyo ni kufariki.
وَالْتَفَّتِ السَّاقُ بِالسَّاقِ﴿٢٩﴾
29. Na muundi utakapoambatana na muundi.
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمَسَاقُ﴿٣٠﴾
30. Siku hiyo ni kuendeshwa na kupelekwa kwa Rabb wako tu.
فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ﴿٣١﴾
31. Kwani hakusadiki (Qur-aan na Rasuli) na wala hakuswali.
وَلَـٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ﴿٣٢﴾
32. Lakini alikadhibisha na akakengeuka.
ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰ أَهْلِهِ يَتَمَطَّىٰ﴿٣٣﴾
33. Kisha akaenda kwa watu wake akijigamba.
أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ﴿٣٤﴾
34. Ole kwako! Tena ole kwako (ewe kafiri)!
ثُمَّ أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ﴿٣٥﴾
35. Kisha ole kwako! Tena ole kwako!
أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَن يُتْرَكَ سُدًى﴿٣٦﴾
36. Je, anadhani binaadam ataachwa huru bila jukumu?
أَلَمْ يَكُ نُطْفَةً مِّن مَّنِيٍّ يُمْنَىٰ﴿٣٧﴾
37. Kwani hakuwa tone kutokana na manii yanayomwagwa kwa nguvu?
ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ﴿٣٨﴾
38. Kisha akawa pande la damu, (Allaah) Akamuumba na Akamsawazisha?
فَجَعَلَ مِنْهُ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ﴿٣٩﴾
39. Akamfanya namna mbili; mwanamume na mwanamke?
أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ﴿٤٠﴾
40. Je Huyo (Allaah Anayeumba) Si Muweza wa Kuhuisha wafu?![11]
[1] Siku Ya Qiyaamah Na Majina Mengineyo Ya Siku Hii Adhimu:
Majina ya Siku ya Qiyaamah yamenukuliwa kufikia zaidi ya themanini [Imaam Ibn Kathiyr – An-Nihaayah Al-Fitan Wal-Malaahim]
Jina mojawapo ni Al-Qiyaamah ambalo ndilo la Suwrah hii, na limetajwa mara nyingi mno katika Qur-aan. Miongoni mwa Aayah zilizotaja jina hili ni Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
قُلِ اللَّـهُ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يَجْمَعُكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٢٦﴾
“Sema: Allaah Anakuhuisheni, kisha Atakufisheni, kisha Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah isiyo na shaka ndani yake, lakini watu wengi hawajui.” [Al-Jaathiyah (45:26)]
Baadhi ya majina mengineyo ni yafuatayo pamoja na baadhi ya rejea zake:
يوم الآخر – Siku ya Akhirah (Mwisho): An-Nisaa (4:38-39), (4:59), (4:136).
السّاعة - Saa: Al-Hajj (22:1), (22:7), (22:55).
يوم الدِّين - Siku ya malipo: Al-Faatihah (1:4), Al-Infitwaar 82:15,17-18).
يوم الحِساب – Siku ya hesabu: Swaad (38:16), (38:26), (38:53).
يوم البعث – Siku ya kufufuliwa: Ar-Ruwm (30:56).
يوم الخُروج – Siku ya kutoka (makaburini) Qaaf (50:42).
يوم الفَصل - Siku ya hukumu na kutenganisha: Al-Mursalaat (77:13-14), (77:38), An-Nabaa (78:17).
يوم الجَمع – Siku ya mjumuiko au mkusanyiko: Ash-Shuwraa (42:7), At-Taghaabun (64:9).
يوم الوعيد – Siku ya makamio: Qaaf (50:20).
يوم المعود - Siku iliyoahidiwa: Al-Buruwj (85:2)
يوم الحسرة – Siku ya majuto: Maryam (19:39).
يوم عقيم - Siku ya ukame: Al-Hajj (22:55)
يوم الخُلود – Siku ya kudumu milele: Qaaf (50:34).
يوم ثقيل – Siku nzito: Al-Insaan (76:27)
يوم التَّناد – Siku ya kuitana: Ghaafir (40:32).
يوم الحقّ – Siku ya haki: An-Nabaa (78:39).
يوم التغابن - Siku ya kupata na kukosa: At-Taghaabun (64:9)
يوم الظيم - Siku kubwa kabisa au adhimu: Al-An’aam (6:15).
يوم كبير - Siku kubwa: Huwd (11:3).
يوم اليم - Siku inayoumiza: Huwd (11:26).
يوم محيط - Siku inayozingira – Huwd (11:84).
يوم مشهود – Siku ya kushuhudiwa: Huwd (11:84).
يوم الآزفة - Siku inayokurubia sana: Ghaafir (40:18).
يوم عبوس قمطرير - Siku ya masononeko, ngumu na ndefu mno.
[3] Ukanushaji Wa Makafiri Kuhusu Kufufuliwa Na Kuumbwa Katika Umbo Jipya:
Aayah hii namba (3) na zinazofuatia hadi (6) zinataja ukanushaji wa makafiri kutokuamini Siku ya kufufuliwa Siku ya Qiyaamah, na pia Uthibitisho wa Allaah (سبحانه وتعالى) wa kufufua viumbe katika umbo kamilifu hadi alama za vidole vyao, ili kila mtu ajulikane barabara umbo lake aliloumbiwa nalo. Rejea Al-Israa (17:49) kwenye maelezo na rejea mbalimbali. Rejea pia Yaasiyn (77-83).
[4] Swali La Makafiri Kuuliza Lini Ahadi Ya Qiyaamah:
Makafiri walikuwa wakiuliza kwa istihzai lini ahadi ya Qiyaamah itatokea. Na swali lao hilo limekariri katika Aayah kadhaa. Miongoni mwazo ni ifuatayo:
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٢٥﴾
“Na wanasema: Ni lini hiyo ahadi (ya kufufuliwa), mkiwa ni wasemao kweli?” [Al-Mulk (67:25)]
Rejea Yuwnus (10:48) kwenye faida na rejea kadhaa za kauli kama hiyo ya makafiri.
[5] Khusuwf Na Kusuwf (Kupatwa Mwezi Na Jua):
Aayah hii namba (8) na inayofuatia namba (9) inataja khusuwf (kupatwa kwa mwezi) na kusuwf (kupatwa jua).
Kusuwf ni kupotea mwanga wa jua au mwezi au sehemu ya mwanga na kubadilika kuwa weusi, na Khusuwf ni kisawe chake. Wataalamu wengine wanasema kwamba Kusuwf ni kupatwa jua na Khusuwf ni kupatwa mwezi, na tafsiri hii ndiyo mashuhuri zaidi katika lugha. [Swahiyhh Fiqh As-Sunnah - Lisaan Al-‘Arab, Kash-Shaaf Al-Qinaa (2/60) na Asnaa Al-Matwaalib (1/385)]
Mwezi au jua vinapopatwa Waislamu wanatakiwa waswali Swalaah ya Kusuwf. Swalaah ya Kusuwf ni Swalaah inayoswaliwa kwa mtindo maalumu wakati jua au mwezi ukipatwa wote au sehemu. [Mawaahibul Jaliyl (2/199), Nihaayatul-Muhtaaj (2/394) na Kash-Shaaful Qinaa (2/60)]
Bonyeza viungo vifuatavyo vyenye faida tele:
16-Swahiyh Al-Bukhaariy: Kitabu Cha Al-Kusuwf (Kupatwa Mwezi Au Jua) - كتاب الكسوف [508]
[6] Viumbe Watadhihirishiwa Amali Zao Zote Za Kheri Na Za Shari:
Miongoni mwa Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى) ni:
يَوْمَئِذٍ يَصْدُرُ النَّاسُ أَشْتَاتًا لِّيُرَوْا أَعْمَالَهُمْ ﴿٦﴾ فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾ وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ ﴿٨﴾
“Siku hiyo watatoka watu makundi mbalimbali wamefarakiana ili waonyeshwe amali zao. Basi yule atakayetenda kheri uzito wa chembe (kama atomu) ataiona. Na yule atakayetenda shari uzito wa chembe (kama atomu) ataiona.” [Az-Zalzalah (99:6-8)
Rejea katika Suwrah hiyo kupata rejea nyenginezo.
[7] Binaadam Atajishuhudia Mwenyewe Matendo Yake:
Makafiri na waliamuasi Allaah (سبحانه وتعالى) Siku ya Qiyaamah watataka kukanusha matendo yao ya kufru na maovu, lakini hakuna atakayeweza kukanusha kwa sababu amali zimehifadhiwa katika rekodi za kila mmoja. Juu ya hivyo, viungo vya mwanaadam vitashuhudia matendo. Rejea Al-Israa (17:13-14) kwenye maelezo na rejea mbalimbali. Rejea pia Yaasiyn (36:65), Fusw-Swilat: (41:20-22), An-Nuwr (24:24).
[8] Nyudhuri Za Kujitetea Hazitapokelewa Wala Hazitamfaa Mtu Siku Ya Qiyaamah:
Anathitibisha hayo Allaah (سبحانه وتعالى) katika Kauli Zake kadhaa, miongoni mwazo ni Kauli Yake:
وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ﴿٣٦﴾
“Na wala hawatopewa idhini ili watoe nyudhuru.” [Al-Mursalaat (77:36)]
Rejea pia Ar-Ruwm (30:57).
[9] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
075-Asbaabun Nuzuwl: Al-Qiyaamah Aayah 16-19: لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ [511]
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Alikuwa Ana Pupa Ya Kupokea Wahy Na Kuisoma Qur-aan:
Jibriyl (عليه السّلام) alipomjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Wahy na akaanza kumsomea (Qur-aan), Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliharakisha kuisoma kwa shauku kabla ya Jibriyl kumaliza kuisoma, na alikuwa anaisoma pamoja naye. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[10] ‘Aqiydah Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jam’aah Kwamba Waumini Watamuona Allaah (عزّ وجلّ) Katika Jannah (Peponi):
Rejea Yuwnus (10:26) kuna maelezo na dalili bayana. Rejea Al-Mutwaffifiyn (83:15).
[11] Kuitikia Subhaanak! Naam! Baada Ya Kusoma Kauli Hii:
عَنْ مُوسَى بْنِ أَبِي عَائِشَةَ قَالَ : كَانَ رَجُلٌ يُصَلِّي فَوْقَ بَيْتِهِ ، وَكَانَ إِذَا قَرَأَ : (أَلَيْسَ ذَلِكَ بِقَادِرٍ عَلَى أَنْ يُحْيِيَ الْمَوْتَى) قَالَ : سُبْحَانَكَ فَبَلَى . فَسَأَلُوهُ عَنْ ذَلِكَ ، فَقَالَ : سَمِعْتُهُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ . صححه الألباني في صحيح أبي داود .
Amesimulia Muwsaa Bin Abiy ‘Aaishah (رضي الله عنه): Mtu mmoja alikuwa akiswali juu ya paa la nyumba yake na aliposoma:
أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ﴿٤٠﴾
“Je Huyo (Allaah Anayeumba) Si Muweza wa Kuhuisha wafu?”
Alisema:
سُبْحَانَكَ فَبَلَى
Subhaanaka Fabalaa (Ametakasika Allaah. Naam!)
Wakamuuliza kuhusu kusema hivyo, akasema: Nimesikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Abuu Daawuwd amesema: Ahmad (Bin Hanbal) amesema: Imenifurahisha kwamba mtu asome katika Swalaah ya fardhi duaa ambazo zimo katika Qur-aan.” [Swahiyh Abiy Daawuwd (884)]
الإِنْسَان
076-Al-Insaan
076-Al-Insaan: Utangulizi Wa Suwrah [513]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
هَلْ أَتَىٰ عَلَى الْإِنسَانِ حِينٌ مِّنَ الدَّهْرِ لَمْ يَكُن شَيْئًا مَّذْكُورًا﴿١﴾
1. Kwa hakika kilimpitia binaadam kipindi fulani katika dahari, hakuwa kitu kinachotajwa.
إِنَّا خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن نُّطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَّبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَاهُ سَمِيعًا بَصِيرًا﴿٢﴾
2. Hakika Sisi Tumemuumba binaadam kutokana na tone la manii iliyochanganyika ili Tumjaribu, Tukamfanya mwenye kusikia na mwenye kuona.
إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا﴿٣﴾
3. Hakika Sisi Tumemuongoza njia; ima (awe) ni mwenye kushukuru au mwingi wa kukufuru.[1]
إِنَّا أَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ سَلَاسِلَ وَأَغْلَالًا وَسَعِيرًا﴿٤﴾
4. Hakika Sisi Tumewaandalia makafiri minyororo, na pingu na moto uliowashwa vikali mno.
إِنَّ الْأَبْرَارَ يَشْرَبُونَ مِن كَأْسٍ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورًا﴿٥﴾
5. Hakika Waumini watendao wema kwa wingi watakunywa katika vikombe vya mvinyo, mchanganyiko wake ni kaafuwr.[2]
عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا عِبَادُ اللَّـهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفْجِيرًا﴿٦﴾
6. Nayo ni chemchemu watakayokunywa toka humo Waja wa Allaah, wataibubujua kwa wingi.
يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا﴿٧﴾
7. Wanatimiza nadhiri[3] na wanaiogopa siku ambayo shari yake ni yenye kuenea kwa upana.
وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا﴿٨﴾
8. Na wanalisha chakula, juu ya kuwa wao wanakipenda, masikini na mayatima na mateka.[4]
إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّـهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا﴿٩﴾
9. Hakika sisi tunakulisheni kwa ajili ya Wajihi wa Allaah, hatukusudii kutoka kwenu jazaa wala shukurani.
إِنَّا نَخَافُ مِن رَّبِّنَا يَوْمًا عَبُوسًا قَمْطَرِيرًا﴿١٠﴾
10. Hakika sisi tunaikhofu kutoka kwa Rabb wetu siku ya masononeko, ngumu na ndefu mno.
فَوَقَاهُمُ اللَّـهُ شَرَّ ذَٰلِكَ الْيَوْمِ وَلَقَّاهُمْ نَضْرَةً وَسُرُورًا﴿١١﴾
11. Basi Allaah Atawakinga na shari ya siku hiyo, na Atawapa nuru ya ujamali na furaha.
وَجَزَاهُم بِمَا صَبَرُوا جَنَّةً وَحَرِيرًا﴿١٢﴾
12. Na Atawalipa kwa sababu ya kusubiri kwao, Jannah na nguo za hariri.
مُّتَّكِئِينَ فِيهَا عَلَى الْأَرَائِكِ ۖ لَا يَرَوْنَ فِيهَا شَمْسًا وَلَا زَمْهَرِيرًا﴿١٣﴾
13. Wataegemea humo juu ya makochi ya fakhari, hawatoona humo joto la jua wala baridi kali.
وَدَانِيَةً عَلَيْهِمْ ظِلَالُهَا وَذُلِّلَتْ قُطُوفُهَا تَذْلِيلًا﴿١٤﴾
14. Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao na yatainamishwa matunda yake ya kuchumwa, yawakurubie.
وَيُطَافُ عَلَيْهِم بِآنِيَةٍ مِّن فِضَّةٍ وَأَكْوَابٍ كَانَتْ قَوَارِيرَا﴿١٥﴾
15. Na watazungushiwa vyombo vya fedha, na bilauri za vigae.
قَوَارِيرَ مِن فِضَّةٍ قَدَّرُوهَا تَقْدِيرًا﴿١٦﴾
16. Vigae safi kutokana na fedha wamezipima kwa kipimo.
وَيُسْقَوْنَ فِيهَا كَأْسًا كَانَ مِزَاجُهَا زَنجَبِيلًا﴿١٧﴾
17. Na watanyweshwa humo kikombe cha mvinyo ambao mchanganyiko wake ni tangawizi.
عَيْنًا فِيهَا تُسَمَّىٰ سَلْسَبِيلًا﴿١٨﴾
18. (Mvinyo utokao) chemchemu iliyomo humo inayoitwa Salsabiyl.
وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُّخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيْتَهُمْ حَسِبْتَهُمْ لُؤْلُؤًا مَّنثُورًا﴿١٩﴾
19. Na watawazungukia wavulana wa kudumishwa, utakapowaona, utawadhania ni lulu zilizotawanywa.
وَإِذَا رَأَيْتَ ثَمَّ رَأَيْتَ نَعِيمًا وَمُلْكًا كَبِيرًا﴿٢٠﴾
20. Na utakapoona huko, utaona neema na ufalme adhimu.
عَالِيَهُمْ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضْرٌ وَإِسْتَبْرَقٌ ۖ وَحُلُّوا أَسَاوِرَ مِن فِضَّةٍ وَسَقَاهُمْ رَبُّهُمْ شَرَابًا طَهُورًا﴿٢١﴾
21. Juu yao watavaa nguo za hariri nyororo za kijani na za hariri nyororo za makhmel, na watapambwa vikuku vya fedha,[5] na Rabb wao Atawanywesha kinywaji kitwaharifu.
إِنَّ هَـٰذَا كَانَ لَكُمْ جَزَاءً وَكَانَ سَعْيُكُم مَّشْكُورًا﴿٢٢﴾
22. (Wataambiwa): Hakika haya ni jazaa yenu, kwani juhudi zenu zimethaminiwa.
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْقُرْآنَ تَنزِيلًا﴿٢٣﴾
23. Hakika Sisi Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Qur-aan uteremsho wa hatua kwa hatua.
فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تُطِعْ مِنْهُمْ آثِمًا أَوْ كَفُورًا﴿٢٤﴾
24. Basi fanya subira kwa Hukumu ya Rabb wako, na wala usimtii miongoni mwao atendaye dhambi au mwingi wa kukufuru.
وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةً وَأَصِيلًا﴿٢٥﴾
25. Na lidhukuru Jina la Rabb wako asubuhi na jioni.[6]
وَمِنَ اللَّيْلِ فَاسْجُدْ لَهُ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا﴿٢٦﴾
26. Na katika sehemu ya usiku msujudie, na uswali kwa ajili Yake usiku mrefu.[7]
إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ يُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ وَيَذَرُونَ وَرَاءَهُمْ يَوْمًا ثَقِيلًا﴿٢٧﴾
27. Hakika hawa wanapenda uhai wa dunia na wanaacha nyuma yao siku nzito (ya Qiyamaah).
نَّحْنُ خَلَقْنَاهُمْ وَشَدَدْنَا أَسْرَهُمْ ۖ وَإِذَا شِئْنَا بَدَّلْنَا أَمْثَالَهُمْ تَبْدِيلًا﴿٢٨﴾
28. Sisi Tumewaumba, na Tumetia nguvu viungo vyao. Na kama Tukitaka, Tutawabadilisha mfano wao badala yao.
إِنَّ هَـٰذِهِ تَذْكِرَةٌ ۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ سَبِيلًا﴿٢٩﴾
29. Hakika haya ni mawaidha. Basi anayetaka achukue njia ya kuelekea kwa Rabb wake.
وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا﴿٣٠﴾
30. Na hamtoweza kutaka isipokuwa Atake Allaah. Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
يُدْخِلُ مَن يَشَاءُ فِي رَحْمَتِهِ ۚ وَالظَّالِمِينَ أَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا﴿٣١﴾
31. Anamuingiza Amtakaye katika Rehma Yake, na madhalimu Amewaandalia adhabu iumizayo.
[1] Njia Mbili: Ya Hidaaya Na Ya Upotofu:
Kila kizazi kimeumbwa katika Fitwrah (maumbile ya asili) ya kumwabudu na kumtii Muumba wake kama alivyosema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَا مِنْ مَوْلُودٍ إِلَّا يُولَدُ عَلَى الْفِطْرَةِ فَأَبَوَاهُ يُهَوِّدَانِهِ ، وَيُنَصِّرَانِهِ وَيُمَجِّسَانِهِ كَمَا تُنْتَجُ الْبَهِيمَةُ بَهِيمَةً جَمْعَاءَ ، هَلْ تُحِسُّونَ فِيهَا مِنْ جَدْعَاءَ؟)) ثُمَّ يَقُولُ أَبُو هُرَيْرَةَ: وَاقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: ((فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ))
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema; “Hakuna kizazi kinachozaliwa (mtoto mchanga) isipokuwa anazaliwa katika fitwrah (umbile la asili la utiifu) kisha wazazi wake (humbadilisha na) humuingiza katika dini ya Uyahudi, au Unaswaara au Umajusi, kama mfano mnyama mwenye pembe anavyomzaa mnyama mwenye pembe kama yeye, je, mtahisi kuwa hana pembe? Kisha Abuu Hurayrah akasema: Someni mkipenda: (kauli ya Allaah):
فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ۚ
“(Shikamana na) umbile la asili la kumpwekesha Allaah Alilowaumbia watu. Hakuna kubadilisha Uumbaji wa Allaah.” [Ar-Ruwm (30:30) Hadiyth katika Al-Bukhaariy na Muslim]
Rejea katika tanbihi ya Aayah hiyo kwenye faida nyenginezo
Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akawabainishia wanaadam njia mbili; njia ya hidaaya na njia ya upotofu kwa kuwatuma Rusuli Wake na Risala Yake kuwabalighishia watu. Basi hii ni sawa na Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ ﴿١٠﴾
“Na Tukambainishia njia mbili (ya haki na upotofu)?” [Al-Balad (90:10)]
Basi ni juu ya mwanaadam kuchagua njia anayotaka. Akiwa ni mtu mwenye kumkhofu Allaah Akafuata Amri zake, basi huyo amejichagulia njia ya hidaaya. Na akiwa ni mtu anayefuata matamanio yake akakufuru au kumuasi Allaah, basi huyu amejichagulia mwenyewe upotofu. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Ametoa mfano wa waliostahabu upotofu badala ya hidaaya kama kina Thamuwd watu wa Nabiy Swaalih (عليه السّلام):
وَأَمَّا ثَمُودُ فَهَدَيْنَاهُمْ فَاسْتَحَبُّوا الْعَمَىٰ عَلَى الْهُدَىٰ فَأَخَذَتْهُمْ صَاعِقَةُ الْعَذَابِ الْهُونِ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿١٧﴾
“Na ama kina Thamuwd, wao Tuliwaongoza, lakini walistahabu upofu kuliko hidaaya. Basi ikawachukuwa radi na umeme angamizi wa adhabu idhalilishayo kwa sababu ya waliyokuwa wakiyachuma.” [Fusw-Swilat (41:17)]
[2] Sifa Za Al-Abraar (Watendao Wema Kwa Wingi) Na Jazaa Zao:
Kuanzia Aayah hii namba (5) hadi namba (22) zimetajwa sifa za Al-Abraar (Waja wema wenye kutenda wema wa kila aina kwa wingi) pamoja na jazaa zao walizoandaliwa na Allaah (سبحانه وتعالى) katika Jannah.
Rejea pia Faatwir (35:33) kwenye neema nyenginezo za watu watu wa Jannah, pamoja na rejea nyenginezo mbalimbali za neema za watu wa Jannah.
[3] Kutimiza Nadhiri:
Muumini anapoweka nadhiri ya kufanya jambo la utiifu na la kheri, anapaswa kuitimiza. Lakini anapoweka nadhiri ya jambo la uasi, anapaswa kutokutimiza kama alivyotuamrisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " مَنْ نَذَرَ أَنْ يُطِيعَ اللَّهَ فَلْيُطِعْهُ وَمَنْ نَذَرَ أَنْ يَعْصِيَ اللَّهَ فَلاَ يَعْصِهِ " .
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kuweka nadhiri kwamba atamtii Allaah, basi amtii, na mwenye kuweka nadhiri kwamba atamuasi Allaah, basi asimuasi.” [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6696), Abu Daawuwd (3289), At-Tirmidhiy (1526), An-Nasaaiy (7/17) na Ibn Maajah (2126)]
Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida kuhusu somo la nadhiri na viapo:
13-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Yamini (Viapo) Na Nadhiri - كِتَابُ اَلْأَيْمَانُ وَالنُّذُورُ [514]
07-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتابُ الأيمان وَالنُّذور - Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri [515]
[4] Kulisha Chakula Ni Miongoni Mwa Sababu Mojawapo Ya Kuingizwa Jannah:
Mojawapo ya mafundisho ya mwanzo kabisa ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipofika Madiynah, yalikuwa ni kuhimiza kulisha watu chakula, ikaahidiwa mwenye kufanya hivyo kuwa ataingizwa Jannah. Hadiyth ifuatayo imethibitisha:
عَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ سَلَّامٍ - رضى الله عنه - قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ - صلى الله عليه وسلم - يَا أَيُّهَا اَلنَّاسُ! أَفْشُوا اَلسَّلَام، وَصِلُوا اَلْأَرْحَامَ، وَأَطْعِمُوا اَلطَّعَامَ، وَصَلُّوا بِاللَّيْلِ وَالنَّاسُ نِيَامٌ، تَدْخُلُوا اَلْجَنَّةَ بِسَلَامٍ أَخْرَجَهُ اَلتِّرْمِذِي
Amesimulia ‘Abdullaah bin Sallaam (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Enyi watu, enezeni (amkianeni) salaam, na ungeni undugu wa damu, na lisheni chakula, na Swalini watu wakiwa wamelala, mtaingia Jannah kwa amani.” [At-Tirmidhiy]
Rejea pia Al-Qalam (68:17) kwenye kisa cha watu wa shamba waliozuia mafuqara na masikini wasipate swadaqa ya mazao ya shamba la baba yao baada ya kufariki kwake. Na pia kisa katika Hadiyth, cha mtu aliyekuwa akitoa swadaqa mazao yake, na faida nyenginezo.
[5] Mavazi Ya Watu Wa Jannah Na Mavazi Yaliyoharamishwa Duniani:
Mavazi ya watu wa Jannah yatakuwa ni nguo za hariri nyororo za kijani na za hariri nyororo za makhmel, na watapambwa vikuku vya fedha.
Rejea pia Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى): Al-Hajj (22:23), Al-Kahf (18:30-31).
Lakini nguo za hariri zimeharamishwa kwa wanaume kuzivaa duniani. Hali kadhaalika imeharamishwa kutumia vyombo vya dhahabu duniani kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سَيْفُ بْنُ أَبِي سُلَيْمَانَ، قَالَ سَمِعْتُ مُجَاهِدًا، يَقُولُ حَدَّثَنِي عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ أَبِي لَيْلَى، أَنَّهُمْ كَانُوا عِنْدَ حُذَيْفَةَ فَاسْتَسْقَى فَسَقَاهُ مَجُوسِيٌّ. فَلَمَّا وَضَعَ الْقَدَحَ فِي يَدِهِ رَمَاهُ بِهِ وَقَالَ لَوْلاَ أَنِّي نَهَيْتُهُ غَيْرَ مَرَّةٍ وَلاَ مَرَّتَيْنِ. كَأَنَّهُ يَقُولُ لَمْ أَفْعَلْ هَذَا، وَلَكِنِّي سَمِعْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ " لاَ تَلْبَسُوا الْحَرِيرَ وَلاَ الدِّيبَاجَ وَلاَ تَشْرَبُوا فِي آنِيَةِ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ، وَلاَ تَأْكُلُوا فِي صِحَافِهَا، فَإِنَّهَا لَهُمْ فِي الدُّنْيَا وَلَنَا فِي الآخِرَةِ ".
Amesimulia Mujaahid (رضي الله عنه): ‘Abdur-Rahman bin Abi Laylaa (رضي الله عنه) amemuhadithia: Tulikuwa kwa Hudhayfah (رضي الله عنه) naye akaomba maji ya kunywa, na Mmajusi (muabudu moto) akamletea. Alipoliweka gudulia la maji mkononi mwake alimrushia nalo, na akasema: Kama nisingalimkataza kufanya hivi zaidi ya mara moja au mara mbili (nisingelimrushia nalo). Kama vile anasema nisingalifanya hivi. Lakini nilimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Msivae hariri wala dibaji na msinywe katika chombo cha dhahabu na fedha, na msile katika sahani zake, kwani hivyo ni vyao duniani na ni vyetu Aakhirah” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Vyakula (70)]
Bonyeza pia viungo vifuatavyo kupata faida nyenginezo:
[6] Kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) Mchana Na Usiku:
Tafsiyr:
Yaani: Mwanzo wa siku na mwisho wa siku, kwa hiyo inajumuisha Swalaah za faradhi na Swalaah za nawaafil (khiari) zinazofuatia, na Dhikr (kumdhukuru Allaah kwa kila aina ya dhikr kama Qur-aan), Tasbiyh, Tahliyl, Takbiyr katika nyakati hizi. [Tafsiyr As-Sa;diy]
Hivyo ni sawa na kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) nyakati zote. Rejea Al-Ahzaab (33:41) kwenye fadhila za kumdhukuru Allaah. Na Rejea Twaahaa (20:124) kwenye maonyo ya kughafilika na kumdhukuru Allaah.
Bonyeza pia viungo vifuatavyo vyenye adhkaar za asubuhi na jioni:
027-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni [524]
130-Hiswnul-Muslim: Fadhila Za Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl Na Takbiyr [368]
131-Hiswnul-Muslim: Vipi Alikuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Akimsabihi Allaah [525]
[7] Qiyaamul-Layl (Kisimamo Cha Usiku) Kwa Ajili Ya Ibaada:
Rejea Al-Muzzammil (73:2) kwenye faida za somo hili.
الْمُرْسَلاَت
077-Al-Mursalaat
077-Al-Mursalaat: Utangulizi Wa Suwrah [527]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالْمُرْسَلَاتِ عُرْفًا﴿١﴾
1. Naapa kwa pepo zitumwazo kwa mfuatano.
فَالْعَاصِفَاتِ عَصْفًا﴿٢﴾
2. Kisha Naapa kwa pepo zinazovuma kwa dhoruba.
وَالنَّاشِرَاتِ نَشْرًا﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa pepo zinazotawanya mawingu na mvua.
فَالْفَارِقَاتِ فَرْقًا﴿٤﴾
4. Kisha Naapa kwa (Malaika) wanaopambanua pambanuo la haki na batili.
فَالْمُلْقِيَاتِ ذِكْرًا﴿٥﴾
5. Kisha Naapa kwa (Malaika) wanaopeleka Wahy kwa Rasuli.
عُذْرًا أَوْ نُذْرًا﴿٦﴾
6. Kwa ajili ya kuondosha udhuru au kwa ajili ya kuonya.
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَاقِعٌ﴿٧﴾
7. Hakika yale mnayoahidiwa bila shaka yatatokea tu!
فَإِذَا النُّجُومُ طُمِسَتْ﴿٨﴾
8. Basi pale nyota zitakapofutiliwa mbali mwanga wake.
وَإِذَا السَّمَاءُ فُرِجَتْ﴿٩﴾
9. Na pale mbingu zitakapofunguliwa.
وَإِذَا الْجِبَالُ نُسِفَتْ﴿١٠﴾
10. Na pale majabali yatakapopeperushiliwa mbali
وَإِذَا الرُّسُلُ أُقِّتَتْ﴿١١﴾
11. Na pale Rusuli watakapopangiwa wakati wao maalumu.
لِأَيِّ يَوْمٍ أُجِّلَتْ﴿١٢﴾
12. Kwa Siku gani hiyo iliyoahirishwa?
لِيَوْمِ الْفَصْلِ﴿١٣﴾
13. Kwa ajili ya Siku ya hukumu na kutenganisha.
وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الْفَصْلِ﴿١٤﴾
14. Na nini kitakachokujulisha ni ipi Siku ya hukumu na kutenganisha?
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿١٥﴾
15. Ole[1] Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
أَلَمْ نُهْلِكِ الْأَوَّلِينَ﴿١٦﴾
16. Je, kwani Hatukuangamiza watu wa awali?
ثُمَّ نُتْبِعُهُمُ الْآخِرِينَ﴿١٧﴾
17. Kisha Tukawafuatilishia wengineo?
كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ﴿١٨﴾
18. Hivyo ndivyo Tunavyowafanya wahalifu.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿١٩﴾
19. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
أَلَمْ نَخْلُقكُّم مِّن مَّاءٍ مَّهِينٍ﴿٢٠﴾
20. Je, kwani Hatukukuumbeni kutokana na maji dhalilifu (manii)?
فَجَعَلْنَاهُ فِي قَرَارٍ مَّكِينٍ﴿٢١﴾
21. Kisha Tukayaweka katika mahali pa kutulia, thabiti?
إِلَىٰ قَدَرٍ مَّعْلُومٍ﴿٢٢﴾
22. Mpaka muda maalumu uliokadiriwa.
فَقَدَرْنَا فَنِعْمَ الْقَادِرُونَ﴿٢٣﴾
23. Tukakadiria. Basi ni wazuri walioje (Sisi) Wenye Kukadiria!
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٢٤﴾
24. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ كِفَاتًا﴿٢٥﴾
25. Je, kwani Hatukufanya ardhi kuwa ni chombo cha kukusanya?
أَحْيَاءً وَأَمْوَاتًا﴿٢٦﴾
26. Walio hai na wafu?
وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ شَامِخَاتٍ وَأَسْقَيْنَاكُم مَّاءً فُرَاتًا﴿٢٧﴾
27. Na Tukaweka humo milima thabiti mirefu iliyojikita na Tukakunywesheni maji matamu mno?
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٢٨﴾
28. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
انطَلِقُوا إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ﴿٢٩﴾
29. (Wataambiwa): Nendeni kwenye yale mliyokuwa mkiyakadhibisha.
انطَلِقُوا إِلَىٰ ظِلٍّ ذِي ثَلَاثِ شُعَبٍ﴿٣٠﴾
30. Nendeni kwenye kivuli (cha Jahannam) chenye sehemu tatu.
لَّا ظَلِيلٍ وَلَا يُغْنِي مِنَ اللَّـهَبِ﴿٣١﴾
31. Hakiwafuniki, na wala hakiwakingi na mwako wa moto.
إِنَّهَا تَرْمِي بِشَرَرٍ كَالْقَصْرِ﴿٣٢﴾
32. Hakika huo (moto) hurusha macheche mfano wa makasri.
كَأَنَّهُ جِمَالَتٌ صُفْرٌ﴿٣٣﴾
33. Kama kwamba ni ngamia wakubwa wa manjano.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٣٤﴾
34. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
هَـٰذَا يَوْمُ لَا يَنطِقُونَ﴿٣٥﴾
35. Siku hii hawatotamka.
وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ﴿٣٦﴾
36. Na wala hawatopewa idhini ili watoe nyudhuru.[2]
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٣٧﴾
37. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
هَـٰذَا يَوْمُ الْفَصْلِ ۖ جَمَعْنَاكُمْ وَالْأَوَّلِينَ﴿٣٨﴾
38. Hii ni Siku ya hukumu na kutenganisha. Tumekukusanyeni pamoja na watu wa awali.
فَإِن كَانَ لَكُمْ كَيْدٌ فَكِيدُونِ﴿٣٩﴾
39. Ikiwa mnayo hila yoyote ile basi Nifanyieni (hizo) hila.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٤٠﴾
40. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي ظِلَالٍ وَعُيُونٍ﴿٤١﴾
41. Hakika wenye taqwa watakuwa katika vivuli na chemchemu.
وَفَوَاكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ﴿٤٢﴾
42. Na matunda katika yale wanayoyatamani.
كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٤٣﴾
43. (Wataambiwa): Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyatenda.
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ﴿٤٤﴾
44. Hakika hivyo ndivyo Tunavyowalipa wafanyao ihsaan.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٤٥﴾
45. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
كُلُوا وَتَمَتَّعُوا قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجْرِمُونَ﴿٤٦﴾
46. (Enyi makafiri): Kuleni na stareheni kidogo (duniani), hakika nyinyi ni wahalifu.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٤٧﴾
47. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ارْكَعُوا لَا يَرْكَعُونَ﴿٤٨﴾
48. Na wanapoambiwa rukuuni (mswali), hawarukuu.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿٤٩﴾
49. Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.
فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ﴿٥٠﴾
50. Basi kauli gani baada ya hii (Qur-aan) wataiamini?
Kauli ifuatayo ya Allaah (سبحانه وتعالى), yenye neno la ويل, imekariri mara kumi katika Suwrah hii.
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ﴿١٥﴾
“Ole Siku hiyo kwa wenye kukadhibisha.”
Na Kauli kama hii imetajwa pia katika Suwrah zifuatazo: Atw-Twuur (52:11), Al-Mutwaffifiyn (83:10).
Na maana kadhaa za ويل zimetajwa na ‘Ulamaa kama ifuatavyo:
i- Bonde katika moto wa Jahannam.
ii- Neno linaloashiria tisho kali.
iii- Adhabu na maangamizi.
iv- Bonde linalotiririka kutoka usaha wa watu wa motoni.
v- Neno la kutokuridhia na lawama.
vi- Neno linalosemwa katika kupatwa masaibu kama vile walivyosema watu wa shamba baada ya kutambua kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Ameliangamiza shamba lao kwa dhambi na udhalimu wao.
قَالُوا يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا طَاغِينَ﴿٣١﴾
“Wakasema: Ole wetu! Hakika sisi tumekuwa warukao mipaka.” [Al-Qalam (68:31).
vii- Neno linatumika katika kustaajabia jambo linaloonekana mustahili, kama alivyostaajabu Sara mke wa Nabiy Ibraahiym walipobashiriwa kumzaa Is-haaq wakiwa katika umri wa uzee:
قَالَتْ يَا وَيْلَتَىٰ أَأَلِدُ وَأَنَا عَجُوزٌ وَهَـٰذَا بَعْلِي شَيْخًا ۖ إِنَّ هَـٰذَا لَشَيْءٌ عَجِيبٌ﴿٧٢﴾
“Akasema: Yatakuwaje haya jamani! Je, nitazaa na hali mimi ni mkongwe na huyu mume wangu ni kizee? Hakika hili ni jambo la ajabu!” [Huwd (11:72)]
viii- Neno linatumika katika kushtuka, kustajaabu, kukhofu, katika jambo la aibu, mateso na katika hali ya kujuta jambo kama alivyojuta Qaabiyl mwana wa Aadam aliyemuua nduguye:
فَبَعَثَ اللَّـهُ غُرَابًا يَبْحَثُ فِي الْأَرْضِ لِيُرِيَهُ كَيْفَ يُوَارِي سَوْءَةَ أَخِيهِ ۚ قَالَ يَا وَيْلَتَىٰ أَعَجَزْتُ أَنْ أَكُونَ مِثْلَ هَـٰذَا الْغُرَابِ فَأُوَارِيَ سَوْءَةَ أَخِي ۖ فَأَصْبَحَ مِنَ النَّادِمِينَ ﴿٣١﴾
“Kisha Allaah Akamleta kunguru akifukua katika ardhi ili amwonyeshe vipi asitiri maiti ya ndugu yake. (Muuaji) akasema: Ole wangu! Hivi nimeshindwa kuwa mimi kama huyu kunguru nikamsitiri ndugu yangu? Akawa miongoni mwa wajutao.” [Al-Maaidah (5:31)]
النَّبَاء
078-An-Nabaa
078-An-Nabaa: Utangulizi Wa Suwrah [529]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
عَمَّ يَتَسَاءَلُونَ ﴿١﴾
1. Kuhusu nini wanaulizana?
عَنِ النَّبَإِ الْعَظِيمِ ﴿٢﴾
2. Kuhusu khabari kubwa mno ya muhimu.[1]
الَّذِي هُمْ فِيهِ مُخْتَلِفُونَ ﴿٣﴾
3. Ambayo wao wanakhitilafiana kwayo.
كَلَّا سَيَعْلَمُونَ ﴿٤﴾
4. Laa hasha! Hivi karibuni watajua.
ثُمَّ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ ﴿٥﴾
5. Kisha laa hasha! Hivi karibuni watajua.
أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ مِهَادًا ﴿٦﴾
6. Je, kwani Hatukufanya ardhi kuwa tandiko?[2]
وَالْجِبَالَ أَوْتَادًا ﴿٧﴾
7. Na milima kuwa kama vigingi?
وَخَلَقْنَاكُمْ أَزْوَاجًا ﴿٨﴾
8. Na Tukakuumbeni kwa jozi; wanaume na wanawake!
وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتًا ﴿٩﴾
9. Na Tukafanya usingizi wenu mnono, kuwa mapumziko (kama kufa)!
وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاسًا ﴿١٠﴾
10. Na Tukafanya usiku kuwa kama libasi la kufunika!
وَجَعَلْنَا النَّهَارَ مَعَاشًا ﴿١١﴾
11. Na Tukafanya mchana kuwa ni wa kutafutia maisha!
وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعًا شِدَادًا ﴿١٢﴾
12. Na Tukajenga juu yenu (mbingu) saba imara!
وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا ﴿١٣﴾
13. Na Tukafanya siraji yenye mwanga mkali iwakayo kwa nguvu!
وَأَنزَلْنَا مِنَ الْمُعْصِرَاتِ مَاءً ثَجَّاجًا ﴿١٤﴾
14. Na Tukateremsha kutoka mawingu yaliyokurubia kunyesha, maji yenye kutiririka kwa kasi kubwa!
لِّنُخْرِجَ بِهِ حَبًّا وَنَبَاتًا ﴿١٥﴾
15. Ili Tutoe kwayo nafaka na mimea.
وَجَنَّاتٍ أَلْفَافًا ﴿١٦﴾
16. Na mabustani yanayosongomana na kuota teletele.
إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ كَانَ مِيقَاتًا ﴿١٧﴾
17. Hakika siku ya hukumu na kutenganisha ina wakati maalumu.
يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَتَأْتُونَ أَفْوَاجًا ﴿١٨﴾
18. Siku litakapopulizwa baragumu, mtakuja makundi makundi.[3]
وَفُتِحَتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ أَبْوَابًا ﴿١٩﴾
19. Na mbingu zitafunguliwa, zitakuwa milango ya njia.[4]
وَسُيِّرَتِ الْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا ﴿٢٠﴾
20. Na milima itaendeshwa na itakuwa kama sarabi.
إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا ﴿٢١﴾
21. Hakika Jahannam itakuwa yenye kuvizia.[5]
لِّلطَّاغِينَ مَآبًا ﴿٢٢﴾
22. Kwa walioruka mipaka wakaasi, ndio mahali pao pa kurejea.
لَّابِثِينَ فِيهَا أَحْقَابًا ﴿٢٣﴾
23. Watabakia humo dahari nyingi.
لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرْدًا وَلَا شَرَابًا ﴿٢٤﴾
24. Hawatoonja humo cha baridi wala kinywaji.
إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا ﴿٢٥﴾
25. Isipokuwa maji yachemkayo mno na usaha.
جَزَاءً وِفَاقًا ﴿٢٦﴾
26. Jazaa inayowafikiana kabisa.
إِنَّهُمْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ حِسَابًا ﴿٢٧﴾
27. Hakika wao walikuwa hawataraji kuhesabiwa.
وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كِذَّابًا ﴿٢٨﴾
28. Na walikadhibisha Aayaat na Ishara Zetu kwa njia zote!
وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ كِتَابًا ﴿٢٩﴾
29. Na kila kitu Tumekitia hesabuni barabara kwa kuandika.
فَذُوقُوا فَلَن نَّزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا ﴿٣٠﴾
30. Basi onjeni, kwani Hatutokuzidishieni isipokuwa adhabu.
إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا ﴿٣١﴾
31. Hakika wenye taqwa watapata mafanikio.[6]
حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا ﴿٣٢﴾
32. Mabustani na mizabibu.
وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا ﴿٣٣﴾
33. Na wanawake wenye matiti ya kisichana, wa hirimu moja na waume zao.
وَكَأْسًا دِهَاقًا ﴿٣٤﴾
34. Na kombe lililojaa pomoni mvinyo.
لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّابًا ﴿٣٥﴾
35. Hawatosikia humo upuuzi wala kukadhibisha ukadhibisho.
جَزَاءً مِّن رَّبِّكَ عَطَاءً حِسَابًا ﴿٣٦﴾
36. Jazaa kutoka kwa Rabb wako, tunukio la kutosheleza.
رَّبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا الرَّحْمَـٰنِۖ لَا يَمْلِكُونَ مِنْهُ خِطَابًا ﴿٣٧﴾
37. Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, Ar-Rahmaan. Hawatoweza kumsemesha.
يَوْمَ يَقُومُ الرُّوحُ وَالْمَلَائِكَةُ صَفًّاۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَـٰنُ وَقَالَ صَوَابًا ﴿٣٨﴾
38. Siku atakayosimama Ruwh (Jibriyl) na Malaika safusafu. Hawatozungumza isipokuwa yule ambaye Ar-Rahmaan Amempa idhini na atasema yaliyo sahihi.
ذَٰلِكَ الْيَوْمُ الْحَقُّۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ مَآبًا ﴿٣٩﴾
39. Hiyo ni Siku ya haki. Basi atakaye, na ashike marudio kuelekea kwa Rabb wake.
إِنَّا أَنذَرْنَاكُمْ عَذَابًا قَرِيبًا يَوْمَ يَنظُرُ الْمَرْءُ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ وَيَقُولُ الْكَافِرُ يَا لَيْتَنِي كُنتُ تُرَابًا ﴿٤٠﴾
40. Hakika Sisi Tumekuonyeni adhabu ya karibu. Siku mtu atakapotazama yale iliyokadimisha mikono yake, na kafiri atasema: Laiti ningelikuwa mchanga.
[1] Khabari Kubwa Mno Ya Muhimu:
Khabari kubwa mno ya muhimu, ya kutisha na ya kustaajabisha. Qataadah na Ibn Zayd wamesema: “Ni kufufuliwa baada ya kufa.” Mujaahid amesema: “Ni Qur-aan.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[2] Miongoni Mwa Neema Za Allaah Kwa Walimwengu:
Kuanzia Aayah hii namba (6) hadi Aayah namba (16) Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja baadhi ya Neema Zake kwa walimwengu. Rejea Ibraahiym (14:34) kwenye uchambuzi wa Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) pamoja na rejea mbali mbali. Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) ambazo hawezi mtu kuzihesabu.
[4] Mbingu Kufunguliwa:
Mbingu zitafunguliwa Siku ya Qiyaamah kwa ajili ya Malaika kuteremka. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Rejea Al-Furqaan (25:25), Al-Haaqqah (69:13-18), Al-Fajr (89:21-22), Al-Baqarah (2:210), Al-An’aam (6:158).
Na mbingu zitapasuliwa na kuchanikachanika zitakuwa kama milango. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Rejea Al-Infitwaar (82:1), Al-Inshiqaaq (84:1).
[5] Mateso Na Adhabu za Watu Wa Motoni:
Kuanzia Aayah hii ya An-Nabaa (78:21) hadi namba (30), yanatajwa mateso na adhabu za watu wa motoni.
Adhabu za makafiri zinakuwa katika hali zifuatazo:
(i) Wanapotolewa Roho:
Hali ya kafiri inapotolewa roho yake ikapelekwa juu imeelezewa katika Hadiyth ifuatayo ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
فَإِذَا كَانَ الرَّجُلُ السُّوءُ قَالَ: اخْرُجِي أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْخَبِيثَةُ كَانَتْ فِي الْجَسَدِ الْخَبِيثِ اخْرُجِي ذَمِيمَةً وَأَبْشِرِي بِحَمِيمٍ وَغَسَّاقٍ وَآخَرَ مِنْ شَكْلِهِ أَزْوَاجٌ فَمَا تَزَالُ يُقَالُ لَهَا ذَلِكَ حَتَّى تَخْرُجَ ثُمَّ يُعْرَجُ بِهَا إِلَى السَّمَاءِ فَيُفْتَحُ لَهَا فَيُقَالُ: مَنْ هَذَا؟ فَيُقَالُ: فُلَانٌ فَيُقَالُ: لَا مَرْحَبًا بِالنَّفْسِ الْخَبِيثَةِ كَانَتْ فِي الْجَسَدِ الْخَبِيثِ ارْجِعِي ذَمِيمَةً فَإِنَّهَا لَا تفتح لَهُ أَبْوَابُ السَّمَاءِ فَتُرْسَلُ مِنَ السَّمَاءِ ثُمَّ تَصِيرُ إِلَى الْقَبْر ". رَوَاهُ ابْن مَاجَه
Lakini inapokuwa mtu ni mbaya kinachosemwa ni: Toka ewe nafsi mbaya ambayo ilikuwa katika mwili mwovu! Toka ukiwa mwenye kulaumiwa na pokea habari mbaya ya maji yanayotokoka na usaha na mengineyo ya mfano wake na aina yake! Ataendelea kuambiwa hivyo hadi roho itoke. Kisha itapandishwa juu mbinguni na itafunguliwa mlango. Itaulizwa: Ni nani huyu? Itajibiwa: Ni fulani. Itaambiwa: Hakuna ukaribisho kwa nafsi mbaya iliyokuwa ndani ya mwili mwovu! Rudi ukiwa mwenye kulaumiwa kwani milango ya mbinguni haitafunguliwa kwa ajili yake. Kisha itatupwa kutoka mbinguni hadi kufika kaburini.” [Ibn Maajah na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Maajah (3456)]
Rejea pia Al-A’raaf (7:40) kwenye maelezo kuhusu mbingu kutokufunguliwa kwa ajili ya roho ya kafiri.
Rejea pia Al-Baqarah (2:165), Al-An’aam (6:30), (6:93), Al-Anfaal (8:50-51), Qaaf (50:19-22), Al-Waaqi’ah (56:92-94) kwenye Aayah zinazotaja hali ya kafiri anapotolewa roho.
Na pia rejea Qaaf (50:19) kwenye faida kadhaa.
(ii) Wataingizwa Motoni Na Kufungwa Minyororo Shingoni Mwao:
Rejea Ar-Ra’d (13:5), Ibraahiym (14:49-50), Sabaa (34:33), Ghaafir (40:70-72), Al-Haaqqah (69:30-32), Al-Muzzammil (73:11-12), Al-Insaan (74:4)
(iii) Watakuwa Kuni Za Moto Uzidi Kuwaunguza:
Rejea Al-Baqarah (2:24), Aal-‘Imraan (3:10), Al-Anbiyaa (21:98).
(iv) Mateso Na Adhabu Nyenginezo Pamoja Na Vyakula Vyao Na Vinywaji Vyao.
Kwanza rejea a Faatwir (33:36) kwenye faida kadhaa na rejea mbalimbali.
Kisha rejea Suwrah zifuatazo ambazo zimetaja kwa ujumla maudhui hii ya mateso na adhabu za watu wa motoni pamoja na vyakula vyao na vinywaji vyao.
An-Nisaa (4:56), Ibraahiym (14:15-17), (14:15-17), Asw-Swaaffaat (37:62-67), Swaad (38:55-64), Ad-Dukhaan (44:40-50), Al-Hajj (22:9-10), (22:19-22), Al-Kahf (18:29), Ash-Shu’araa (26:91-102), Al-Baqarah (2:174-175), Al-Maaidah (5:35-37), Huwd (11:105-106), Ar-Rahmaan (55:43-44), Al-Qamar (54:46-48), Al-Waaqi’ah (56:41-56), Al-Mulk (67:6-11), Al-Haaqqah (69:25-37), Al-Ma’aarij (70:15-18), Al-Muddath-thir (74:26-30), Al-Muzzammil (73:11-12), Al-A’laa (87:11-13), Al-Ghaashiyah (88:1-7), Al-Humazah (104:4-9).
Na katika Suwrah Muhammad mwishoni mwa Aayah Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
كَمَنْ هُوَ خَالِدٌ فِي النَّارِ وَسُقُوا مَاءً حَمِيمًا فَقَطَّعَ أَمْعَاءَهُمْ﴿١٥﴾
“Ni kama yule mwenye kudumu motoni? Na watanyweshwa maji yachemkayo yakatekate machango yao?” [Muhammad (47:15)]
Na katika Hadiyth kadhaa za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) pia adhabu za watu wa motoni, hali zao, vyakula vyao zimethibiti ambazo miongoni mwazo ni hizi zifuatazo:
عن سمرة بن جندب رضي الله عنه: أنَّ نبيَّ الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( مِنْهُمْ مَنْ تَأخُذُهُ النَّارُ إِلَى كَعْبَيهِ ، وَمنْهُمْ مَنْ تَأخُذُهُ إِلَى رُكْبَتَيهِ ، وَمنْهُمْ مَنْ تَأخُذُهُ إِلَى حُجزَتِهِ ، وَمِنْهُمْ مَنْ تَأخُذُهُ إِلَى تَرْقُوَتِهِ )) رواه مسلم .
Amesimulia Samurah Bin Jundub (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Miongoni mwa watu wa motoni ni wale ambao moto kwa ukali wake utawafika kwenye vifundo vya miguu, na wengine kwenye magoti, na wengine mpaka kiunoni, na wengine hadi kwenye fupa la koo.” [Muslim]
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " إِنَّ غِلَظَ جِلْدِ الْكَافِرِ اثْنَانِ وَأَرْبَعُونَ ذِرَاعًا وَإِنَّ ضِرْسَهُ مِثْلُ أُحُدٍ وَإِنَّ مَجْلِسَهُ مِنْ جَهَنَّمَ كَمَا بَيْنَ مَكَّةَ وَالْمَدِينَةِ " . هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ غَرِيبٌ مِنْ حَدِيثِ الأَعْمَشِ .
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Unene wa ngozi ya kafiri ni dhiraa arobaini na mbili, na jino lake ni kama (mlima wa) Uhud, na makazi yake motoni ni kama baina ya Makkah na Madiynah. [At-Tirmidhiy]
(v) Majina Ya Moto Na Aina Zake:
Rejea Al-Muddath-thir (74:26).
Bonyeza pia kiungo kifuatacho kwa faida ziyada:
[6] Wenye Taqwa Na Neema Zao Za Jannah:
Rejea Faatwir (35:33) kwenye maelezo na rejea mbalimbali za maudhui.
Bonyeza pia viungo vifuatavyo kupata faida nyenginezo:
النَّازِعَات
079-An-Naazi’aat
079-An-Naazi’aat: Utangulizi Wa Suwrah [533]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالنَّازِعَاتِ غَرْقًا ﴿١﴾
1. Naapa kwa wanaong’oa (roho) kwa nguvu.
وَالنَّاشِطَاتِ نَشْطًا ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa wanaotoa (roho) kwa upole.
وَالسَّابِحَاتِ سَبْحًا ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa wanaoogelea kwa kupanda na kushuka (katika anga).
فَالسَّابِقَاتِ سَبْقًا ﴿٤﴾
4. Kisha Naapa kwa wenye kutangulia mbele kwa kushindana.
فَالْمُدَبِّرَاتِ أَمْرًا ﴿٥﴾
5. Kisha Naapa kwa wenye kuendesha kila jambo.
يَوْمَ تَرْجُفُ الرَّاجِفَةُ ﴿٦﴾
6. Siku kitakapotetemeka chenye kutetemesha (mpulizo wa awali).[1]
تَتْبَعُهَا الرَّادِفَةُ ﴿٧﴾
7. Kifuatiliwe na cha pili yake (mpulizo wa pili).
قُلُوبٌ يَوْمَئِذٍ وَاجِفَةٌ ﴿٨﴾
8. Nyoyo siku hiyo zitapuma kwa nguvu kutokana na khofu.
أَبْصَارُهَا خَاشِعَةٌ ﴿٩﴾
9. Macho yake yatainama chini.
يَقُولُونَ أَإِنَّا لَمَرْدُودُونَ فِي الْحَافِرَةِ ﴿١٠﴾
10. Wanasema (sasa): Je, hivi sisi tutarudishwa katika hali ya asili ya uhai?[2]
أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا نَّخِرَةً ﴿١١﴾
11. Je, hata tukiwa ni mifupa iliyosagika na kuoza?
قَالُوا تِلْكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ ﴿١٢﴾
12. Hayo basi ni marejeo ya khasara.
فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ ﴿١٣﴾
13. Basi hakika huo ni ukelele mmoja tu wa kuogofya.
فَإِذَا هُم بِالسَّاهِرَةِ ﴿١٤﴾
14. Tahamaki hao wamekusanyika uwandani wakiwa macho baada ya kufa.
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ مُوسَىٰ ﴿١٥﴾
15. Je, imekufikia hadithi ya Muwsaa?
إِذْ نَادَاهُ رَبُّهُ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى ﴿١٦﴾
16. Pale Rabb wake Alipomuita kwenye Bonde Takatifu la Tuwaa.
اذْهَبْ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ ﴿١٧﴾
17. (Akamwambia): Nenda kwa Firawni, hakika yeye amepindukia mipaka ya kuasi.
فَقُلْ هَل لَّكَ إِلَىٰ أَن تَزَكَّىٰ ﴿١٨﴾
18. Umwambie: Je, unataka utakasike?
وَأَهْدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخْشَىٰ ﴿١٩﴾
19. Na nikuongoze kwa Rabb wako umuogope?
فَأَرَاهُ الْآيَةَ الْكُبْرَىٰ ﴿٢٠﴾
20. Basi akamuonyesha Aayah (Ishara, Miujiza, Dalili) kubwa kabisa.
فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ ﴿٢١﴾
21. Lakini akakadhibisha, na akaasi.
ثُمَّ أَدْبَرَ يَسْعَىٰ ﴿٢٢﴾
22. Kisha akageuka nyuma na akapania kufanya juhudi (za kukanusha haki).
فَحَشَرَ فَنَادَىٰ ﴿٢٣﴾
23. Akakusanya watu kisha akanadi.
فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ ﴿٢٤﴾
24. Akasema: Mimi ni mola wenu mkuu.
فَأَخَذَهُ اللَّـهُ نَكَالَ الْآخِرَةِ وَالْأُولَىٰ ﴿٢٥﴾
25. Basi Allaah Alimchukuwa kwa adhabu ya tahadharisho na fundisho ya Aakhirah (ya moto) na ya mwanzo ya (duniani ya kugharikishwa).
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّمَن يَخْشَىٰ ﴿٢٦﴾
26. Hakika katika hayo bila shaka kuna funzo kwa yule anayeogopa.
أَأَنتُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمِ السَّمَاءُۚ بَنَاهَا ﴿٢٧﴾
27. Je, kuumbwa nyinyi ndio vigumu zaidi au mbingu? Kaijenga (Yeye)[3]
رَفَعَ سَمْكَهَا فَسَوَّاهَا ﴿٢٨﴾
28. Amenyanyua kimo chake, kisha Akazisawazisha sawasawa.
وَأَغْطَشَ لَيْلَهَا وَأَخْرَجَ ضُحَاهَا ﴿٢٩﴾
29. Na Akatia kiza usiku wake, na Akatokezesha mwanga wa mchana wake.
وَالْأَرْضَ بَعْدَ ذَٰلِكَ دَحَاهَا ﴿٣٠﴾
30. Na ardhi baada ya hayo Akaitandaza.
أَخْرَجَ مِنْهَا مَاءَهَا وَمَرْعَاهَا ﴿٣١﴾
31. Akatoa humo maji yake na malisho yake.
وَالْجِبَالَ أَرْسَاهَا ﴿٣٢﴾
32. Na milima Akaikita imara.
مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ ﴿٣٣﴾
33. Kwa ajili ya manufaa kwenu na kwa wanyama wenu wa mifugo.
فَإِذَا جَاءَتِ الطَّامَّةُ الْكُبْرَىٰ ﴿٣٤﴾
34. Basi itakapokuja balaa kubwa kabisa ya kuvuka mpaka.[4]
يَوْمَ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ مَا سَعَىٰ ﴿٣٥﴾
35. Siku binaadamu atakapokumbuka yale aliyoyakimbilia kwa juhudi.
وَبُرِّزَتِ الْجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ ﴿٣٦﴾
36. Na moto wa jahiym (uwakao vikali mno) utakapodhihirishwa wazi kwa aonaye.
فَأَمَّا مَن طَغَىٰ ﴿٣٧﴾
37. Basi yule aliyepindukia mipaka kuasi.
وَآثَرَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿٣٨﴾
38. Na akahiari uhai wa dunia.
فَإِنَّ الْجَحِيمَ هِيَ الْمَأْوَىٰ ﴿٣٩﴾
39. Basi hakika jahiym (moto uwakao vikali mno) ndio makaazi yake.
وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ وَنَهَى النَّفْسَ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٤٠﴾
40. Ama yule aliyekhofu kisimamo mbele ya Rabb wake, na akaikataza nafsi yake na hawaa.
فَإِنَّ الْجَنَّةَ هِيَ الْمَأْوَىٰ ﴿٤١﴾
41. Basi hakika Jannah ndio makaazi yake.
يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا ﴿٤٢﴾
42. Wanakuuliza (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Saa lini kufika kwake?[5]
فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَاهَا ﴿٤٣﴾
43. Huna ujuzi wewe hata utaje lolote.
إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَاهَا ﴿٤٤﴾
44. Kwa Rabb wako ndio kuishia kwake (ujuzi wake).
إِنَّمَا أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخْشَاهَا ﴿٤٥﴾
45. Hakika wewe ni muonyaji wa yule anayeikhofu.
كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَهَا لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا عَشِيَّةً أَوْ ضُحَاهَا ﴿٤٦﴾
46. Siku watakapoiona, watakuwa kama kwamba hawakubaki (duniani) isipokuwa jioni moja au mchana wake.
[1] Mpulizo Wa Kwanza Wa Baragumu:
Aayah hii namba (6) na namba (7) ni kuhusu baragumu litakalopulizwa na Malaika Israafiyl (عليه السّلام) la kufufuwa viumbe Siku ya Qiyaamah. Rejea Az-Zumar (39:68) kwenye maelezo yake.
[2] Makafiri Hawakuamini Kwamba Watafufuliwa:
Rejea Al-Israa (17:49) kwenye maelezo bayana na rejea mbalimbali.
[3] Kuumbwa Mbingu Na Ardhi Ni Jambo Kubwa Kulikoni Kufufua Wafu:
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
لَخَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَكْبَرُ مِنْ خَلْقِ النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴿٥٧﴾
“Bila shaka uumbaji wa mbingu na ardhi ni mkubwa zaidi kuliko uumbaji wa watu, lakini watu wengi hawajui.” [Ghaafir (40:57)]
Pia rejea Al-Israa (17:49) kuna maelezo bayana, kuhusu makafiri kutokuamini kuwa watafufuliwa, wakidhani kuwa ni jambo gumu kufufuliwa baada ya miili yao na mifupa kuoza kaburini, ilhali ni jambo jepesi mno kwa Allaah (عزّ وجلّ) kama Anavyosema:
أَوَلَمْ يَرَ الْإِنسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ ﴿٧٧﴾ وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِيَ خَلْقَهُ ۖ قَالَ مَن يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌ ﴿٧٨﴾ قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّةٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ ﴿٧٩﴾
“Je, binaadam haoni kwamba Sisi Tumemuumba kutokana na tone la manii, mara yeye anakuwa mpinzani bayana? Na akatupigia mfano, akasahau kuumbwa kwake akasema: Ni nani atakayehuisha mifupa hii na hali imeshaoza na kusagika na kuwa kama vumbi! Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ataihuisha Yule Aliyeianzisha mara ya kwanza. Naye Ni Mjuzi wa kila kiumbe.” [Yaasiyn (36:77-79)]
Na Aayah zinazofuatia mpaka mwisho wa Suwrah hiyo ya Yaasiyn.
[4] Balaa Kubwa Ya Siku Ya Qiyaamah:
Kitakapokuja Qiyaamah kikuu na msukosuko mzito ambao utafanya dhiki zote kutokuwa na umuhimu wa kuzingatiwa, hapo basi, mzazi atamsahau mwanawe, na mume atamsahau mkewe, (na kila mpenzi atamuacha mpenzi wake). [Tafsiyr As-Sa’diy]
[5] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
079-Asbaabun-Nuzuwl: An-Naazi'aat Aayah 42-46: يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا [534]
Ada Ya Makafiri Kuuliza Qiyaamah Kitatokea Lini Na Kuhimiza Adhabu:
Rejea Al-An’aam (6:158), Al-A’raaf (7:187), Al-Ahzaab (33:63), Al-Mulk (67:25), Ash-Shuwraa (42:18)
Na wakihimiza adhabu: Rejea Al-Hajj (22:47), Swaad (38:16), Al-Anfaal (8:32-33).
عَبَسَ
‘Abasa: 080
080-‘Abasa: Utangulizi Wa Suwrah [536]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١﴾
1. Alikunja kipaji na akageuka.[1]
أَن جَاءَهُ الْأَعْمَىٰ ﴿٢﴾
2. Kwa kuwa kipofu alimjia.
وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّىٰ ﴿٣﴾
3. Na nini kitakachokujulisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) huenda akatakasika?
أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ الذِّكْرَىٰ ﴿٤﴾
4. Au atawaidhika na yamfae mawaidha?
أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَىٰ ﴿٥﴾
5. Ama yule ajionaye amejitosheleza.
فَأَنتَ لَهُ تَصَدَّىٰ ﴿٦﴾
6. Wewe ndio unamgeukia kumshughulikia!
وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ ﴿٧﴾
7. Na si juu yako asipotakasika.
وَأَمَّا مَن جَاءَكَ يَسْعَىٰ ﴿٨﴾
8. Ama yule aliyekujia kwa shime na hima.
وَهُوَ يَخْشَىٰ ﴿٩﴾
9. Naye anakhofu.
فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ ﴿١٠﴾
10. Basi wewe unampuuza!
كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ ﴿١١﴾
11. Laa hasha! Hakika hizi (Aayah) ni mawaidha.
فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ ﴿١٢﴾
12. Basi atakaye na awaidhike nayo (Qur-aan).
فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ ﴿١٣﴾
13. Yamo hayo katika Sahifa zenye kuadhimishwa.
مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ ﴿١٤﴾
14. Zimetukuzwa na zimetakaswa.
بِأَيْدِي سَفَرَةٍ ﴿١٥﴾
15. (Zimebebwa) Mikononi mwa Malaika Wajumbe.[2]
كِرَامٍ بَرَرَةٍ ﴿١٦﴾
16. Watukufu, watiifu.
قُتِلَ الْإِنسَانُ مَا أَكْفَرَهُ ﴿١٧﴾
17. Amelaaniwa na kuangamia binaadamu, ukafiri ulioje alionao?
مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ ﴿١٨﴾
18. Kutoka kitu gani (Allaah) Amemuumba?
مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُ فَقَدَّرَهُ ﴿١٩﴾
19. Kutoka tone la manii, Amemuumba, Akamkadiria.
ثُمَّ السَّبِيلَ يَسَّرَهُ ﴿٢٠﴾
20. Kisha Akamuwepesishia njia.
ثُمَّ أَمَاتَهُ فَأَقْبَرَهُ ﴿٢١﴾
21. Kisha Akamfisha, na Akampa takrima ya kuzikwa.
ثُمَّ إِذَا شَاءَ أَنشَرَهُ ﴿٢٢﴾
22. Kisha Atakapotaka, Atamfufua.
كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَا أَمَرَهُ ﴿٢٣﴾
23. Laa hasha! Hakutimiza bado Aliyomuamuru (Allaah).
فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ إِلَىٰ طَعَامِهِ ﴿٢٤﴾
24. Basi atazame binaadam chakula chake.
أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاءَ صَبًّا ﴿٢٥﴾
25. Kwamba Sisi Tumemimina maji kwa uneemefu.
ثُمَّ شَقَقْنَا الْأَرْضَ شَقًّا ﴿٢٦﴾
26. Kisha Tukaipasua ardhi ikafunguka (kwa mimea).
فَأَنبَتْنَا فِيهَا حَبًّا ﴿٢٧﴾
27. Tukaotesha humo nafaka.
وَعِنَبًا وَقَضْبًا ﴿٢٨﴾
28. Na mizabibu na mimea ya mboga (ikatwayo ikamea tena).
وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا ﴿٢٩﴾
29. Na mizaituni na mitende.
وَحَدَائِقَ غُلْبًا ﴿٣٠﴾
30. Na mabustani yaliyositawi na kusongamana.
وَفَاكِهَةً وَأَبًّا ﴿٣١﴾
31. Na matunda na majani ya malisho ya wanyama.
مَّتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ ﴿٣٢﴾
32. Yakiwa ni manufaa kwenu na kwa wanyama wenu wa mifugo.
فَإِذَا جَاءَتِ الصَّاخَّةُ ﴿٣٣﴾
33. Basi utakapokuja ukelele mkali wa kuvuruga masikio.
يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ ﴿٣٤﴾
34. Siku mtu atakapomkimbia ndugu yake.[3]
وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ ﴿٣٥﴾
35. Na mama yake na baba yake.
وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ ﴿٣٦﴾
36. Na mkewe na wanawe.
لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ ﴿٣٧﴾
37. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na hali yake ya kumtosha mwenyewe.[4]
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌ ﴿٣٨﴾
38. Ziko nyuso siku hiyo zitanawiri.[5]
ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌ ﴿٣٩﴾
39. Zikicheka na kufurahika.
وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ ﴿٤٠﴾
40. Na ziko nyuso siku hiyo zitakuwa na vumbi juu yake.
تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ ﴿٤١﴾
41. Zitafunikwa na giza totoro.
أُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَفَرَةُ الْفَجَرَةُ ﴿٤٢﴾
42. Hao ndio makafiri waovu.
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
080-Asbaabun-Nuzuwl: 'Abasa Aayah 1-10: عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ [537]
[2] Fadhila Ya Aliyehifadhi Qur-aan Na Anayeisoma Kwa Kutaabika:
حَدَّثَنَا آدَمُ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا قَتَادَةُ، قَالَ سَمِعْتُ زُرَارَةَ بْنَ أَوْفَى، يُحَدِّثُ عَنْ سَعْدِ بْنِ هِشَامٍ، عَنْ عَائِشَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " مَثَلُ الَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَهْوَ حَافِظٌ لَهُ مَعَ السَّفَرَةِ الْكِرَامِ الْبَرَرَةِ، وَمَثَلُ الَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَهْوَ يَتَعَاهَدُهُ وَهْوَ عَلَيْهِ شَدِيدٌ، فَلَهُ أَجْرَانِ ".
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mfano wa anayesoma Qur-aan hali ameihifadhi, atakuwa pamoja na Malaika Wajumbe, watukufu na watiifu. Na mfano wa anayesoma (Qur-aan), na anaikariri mara kwa mara huku anaona ugumu mkubwa, atapata malipo mawili.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Tafsiyr (65)]
[3] Siku Ya Qiyaamah Hakuna Ndugu Wala Jamaa Atakayetaka Kumsaidia Ndugu Ya Jamaa Yake:
Rejea Al-Muuminuwn (23:101) Luqmaan (31:33), Al-Muuminuwn (23:101), Faatwir (35:18), Al-Infitwaar (82:19). Rejea pia Al-Hujuraat (49:13) kwenye faida nyenginezo kuhusu maudhui hii.
[4] Kiwewe Cha Siku Ya Qiyaamah Kitamfanya Mtu Asijue Nani Amesimama Karibu Naye:
Siku ya Qiyaamah, watu watafufuliwa wakiwa uchi kama vile walivyozaliwa, na kila mmoja atajali nafsi yake tu! Na kiwewe siku hiyo kitamfanya mtu hata asishughulike kumtazama aliye karibu naye hata kama ni mwanamke au mwanamume! Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) alishtuka aliposikia kuwa hali itakuwa hivyo kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ عَائِشَةَ (رضي الله عنها) قَالَتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((يُحْشَرُ النَّاسُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ حُفَاةً عُرَاةً غُرْلا)) قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ، النِّسَاءُ وَالرِّجَالُ جَمِيعًا يَنْظُرُ بَعْضُهُمْ إِلَى بَعْضٍ؟ قَالَ: ((يَا عَائِشَةُ! الأَمْرُ أَشَدُّ مِنْ أَنْ يُهِمَّهُم ذلِكَ)) وَفِي رِواية: ((ألأَمْرُ أَهَمُّ مِنْ أَنْ يَنْظُرَ بَعْضُهُمْ إِلَى بَعْضٍ)) متفق عليه
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Watu watafufuliwa Siku ya Qiyaamah ilhali hawana viatu, wako uchi, ni mazunga (hawakutahiriwa).” Nikamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Wanaume na wanawake wote watatazamana? Akasema: “Ee ‘Aaishah! Hali itakuwa ngumu mno hata hawatoweza kushughulika na jambo hilo!”
Katika riwaayah nyingine imesema: “Hali itakuwa ngumu mno kiasi kwamba hawatoweza kutazamana.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
[5] Nyuso Za Waumini Zitakazonawiri Na Nyuso Za Makafiri Zitakazosawijika:
Aayah hii (38) hadi namba (41) zinataja nyuso za Waumini zitakavyokuwa na nuru kwa furaha ya kufuzu Siku ya Qiyaamah, na nyuso za makafiri zitakavyokuwa na kiza kutokana na huzuni na dhiki.
Anasema hivyo pia Allaah (سبحانه وتعالى) katika Kauli Zake zifuatazo:
يَوْمَ تَبْيَضُّ وُجُوهٌ وَتَسْوَدُّ وُجُوهٌ ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ اسْوَدَّتْ وُجُوهُهُمْ أَكَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿١٠٦﴾ وَأَمَّا الَّذِينَ ابْيَضَّتْ وُجُوهُهُمْ فَفِي رَحْمَةِ اللَّـهِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿١٠٧﴾
“Siku nyuso zitakuwa nyeupe na nyuso (nyingine) zitakuwa nyeusi. Basi wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeusi (wataambiwa): Je, mlikufuru baada ya kuamini kwenu?! Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyakanusha. Na wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeupe, basi watakuwa katika Rehma ya Allaah. Wao humo watadumu.” [Aal-‘Imraan (3:106-107)]
Na pia kuhusu nyuso za Waumini:
لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ وَلَا يَرْهَقُ وُجُوهَهُمْ قَتَرٌ وَلَا ذِلَّةٌ ۚ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿٢٦﴾
“Kwa wale waliofanya ihsaan watapata (huko Jannah) jazaa nzuri kabisa na ziada (kumuona Allaah). Na vumbi halitowafunika nyuso zao wala madhila. Hao ni watu wa Jannah, humo wao watadumu.” [Yuwnus (10:26)]
Na pia:
تَعْرِفُ فِي وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ النَّعِيمِ ﴿٢٤﴾
“Utatambua nyuso zao kwa nuru ya neema (taanasa, furaha).” [Al-Mutwaffifiyn (83:21)]
Na pia:
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاعِمَةٌ ﴿٨﴾ لِّسَعْيِهَا رَاضِيَةٌ ﴿٩﴾
“Na nyuso (nyingine) Siku hiyo zitakuwa zenye kuneemeka. Zitafarijika kwa juhudi zake.” [Al-Ghaashiyah (88:8-9)]
Na kuhusu nyuso za makafiri pia:
وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ تَرَى الَّذِينَ كَذَبُوا عَلَى اللَّـهِ وُجُوهُهُم مُّسْوَدَّةٌ ۚ أَلَيْسَ فِي جَهَنَّمَ مَثْوًى لِّلْمُتَكَبِّرِينَ﴿٦٠﴾
“Na Siku ya Qiyaamah utawaona wale waliomsingizia uongo Allaah, nyuso zao zimesawajika. Je, kwani si katika Jahannam ndio makazi kwa ajili ya wanaotakabari?” [Az-Zumar 39:60)]
Na pia:
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَةٌ ﴿٢﴾
“Nyuso siku hiyo zitadhalilika.” [Al-Ghaashiyah (88:2)]
التَّكْوِير
081-At-Takwiyr
081-At-Takwiyr: Utangulizi Wa Suwrah [539]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ﴿١﴾
1. Jua litakapokunjwa kunjwa na kupotea mwanga wake.[1]
وَإِذَا النُّجُومُ انكَدَرَتْ ﴿٢﴾
2. Na nyota zitakapoanguka, kupuputika na kutawanyika.
وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ ﴿٣﴾
3. Na milima itakapoendeshwa iondoke ilipo.
وَإِذَا الْعِشَارُ عُطِّلَتْ ﴿٤﴾
4. Na ngamia wenye mimba pevu watakapotelekezwa.
وَإِذَا الْوُحُوشُ حُشِرَتْ ﴿٥﴾
5. Na wanyama mwitu watakapokusanywa.
وَإِذَا الْبِحَارُ سُجِّرَتْ ﴿٦﴾
6. Na bahari zitakapojazwa na kuwashwa moto.
وَإِذَا النُّفُوسُ زُوِّجَتْ ﴿٧﴾
7. Na nafsi zitakapounganishwa na roho kisha kwa aina zake (wema kwa wema, waovu kwa waovu). [2]
وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ ﴿٨﴾
8. Na mtoto wa kike aliyezikwa akiwa yuhai atakapoulizwa.[3]
بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَتْ ﴿٩﴾
9. Kwa dhambi gani aliuliwa?
وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ ﴿١٠﴾
10. Na sahifa za kurekodi (amali) zitakapotandazwa (na kukunjuliwa).[4]
وَإِذَا السَّمَاءُ كُشِطَتْ ﴿١١﴾
11. Na mbingu zitakapobanduliwa.
وَإِذَا الْجَحِيمُ سُعِّرَتْ ﴿١٢﴾
12. Na moto uwakao vikali mno utakapowashwa.
وَإِذَا الْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ ﴿١٣﴾
13. Na Jannah itakapoletwa karibu.
عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا أَحْضَرَتْ ﴿١٤﴾
14. Nafsi itajua hapo yale iliyoyahudhurisha.[5]
فَلَا أُقْسِمُ بِالْخُنَّسِ ﴿١٥﴾
15. Basi Naapa kwa sayari zinazotoweka (mchana na zinadhihirika usiku).
الْجَوَارِ الْكُنَّسِ ﴿١٦﴾
16. Zinazotembea na kujificha.
وَاللَّيْلِ إِذَا عَسْعَسَ ﴿١٧﴾
17. Na Naapa kwa usiku unapoingia.
وَالصُّبْحِ إِذَا تَنَفَّسَ ﴿١٨﴾
18. Na Naapa kwa asubuhi inapopambazuka.
إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ﴿١٩﴾
19. Hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni kauli ya Mjumbe Mtukufu (Jibriyl).[6]
ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ ﴿٢٠﴾
20. Mwenye nguvu na cheo kitukufu kwa (Allaah) Anayemiliki ‘Arsh.
مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ ﴿٢١﴾
21. Anayetiiwa (na Malaika), mwaminifu huko (mbinguni).
وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجْنُونٍ ﴿٢٢﴾
22. Na hakuwa swahibu yenu (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) majnuni.[7]
وَلَقَدْ رَآهُ بِالْأُفُقِ الْمُبِينِ ﴿٢٣﴾
23. Na kwa yakini alimuona (Jibriyl) katika upeo wa macho ulio bayana.
وَمَا هُوَ عَلَى الْغَيْبِ بِضَنِينٍ ﴿٢٤﴾
24. Naye si mzuiaji wa (kuelezea mambo ya) ghaibu.
وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَيْطَانٍ رَّجِيمٍ ﴿٢٥﴾
25. Na hii (Qur-aan) si kauli ya shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa.
فَأَيْنَ تَذْهَبُونَ ﴿٢٦﴾
26. Basi mnakwenda wapi?
إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ ﴿٢٧﴾
27. Hii (Qur-aan) si chochote isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu.
لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ ﴿٢٨﴾
28. Kwa yule atakaye miongoni mwenu anyooke (katika haki)
وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٢٩﴾
29. Na hamtotaka isipokuwa Atake Allaah Rabb wa walimwengu.[8]
[1] Baadhi Ya Matukio Ya Siku Ya Qiyaamah:
Suwrah hii At-Takwiyr (81), Al-Infitwaar (82) na Al-Inshiqaaq (84) zinaanza kutaja baadhi ya matukio ya Siku ya Qiyaamah. Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
مَنْ سَرَّهُ أَنْ يَنْظُرَ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ كَأَنَّهُ رَأْىُ عَيْنٍ فَلْيَقْرَأْ إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ و إِذَا السَّمَاءُ انْفَطَرَتْ وَ إذَا السَّمَاءُ انْشَقَّتْ
“Anayependa atazame Siku ya Qiyaamah kana kwamba anaiona kwa macho yake, na asome:
إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ﴿١﴾
Jua litakapokunjwa kunjwa na kupotea mwanga wake. [At-Takwiyr (81:1)]
Na
إِذَا السَّمَاءُ انفَطَرَتْ ﴿١﴾
Mbingu itakapopasuka. [Al-Infitwaar (82:1)]
Na
إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ ﴿١﴾
Mbingu itakaporaruka. [Al-Inshiqaaq (84:1)]
[At-Tirmidhy, Ahmad. Ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (3333)]
Na Hadiyth ifuatayo imethibiti kuhusu jua na mwezi kuvurugika na kupoteza mwanga wake:
حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ الْمُخْتَارِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ الدَّانَاجُ، قَالَ حَدَّثَنِي أَبُو سَلَمَةَ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ مُكَوَّرَانِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ".
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Jua na mwezi zitakunjwa (zitakoshwa mwangaza wake) Siku ya Qiyaamah.” [Al-Bukhaariy Kitabu cha Uanzishaji wa Uumbaji (65)]
[2] Watu Watakusanywa Vikundi Vikundi Kulingana Na Imaan Zao Na Matendo Yao Mema Na Ya Shari:
Siku ya Qiyaamah, watu wataunganishwa katika vikundi vikundi kulingana na imaan zao na amali zao; Waumini pamoja na Waumini na makafiri kwa makafiri, na watu wa kheri pamoja na watu wa kheri, na watu wa shari pamoja na watu wa shari na kadhaalika. Na Tafsiyr ni kama ifuatavyo:
Yaani: Watu wa kila tendo maalumu wataunganishwa pamoja; wema kwa wema, na waovu kwa waovu. Waumini wataunganishwa na mahurilayni (wanawake wa Jannah wenye macho mazuri kabisa), na makafiri wataunganishwa na mashaytwaan. Hivi ni kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Aayah:
وَسِيقَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ جَهَنَّمَ زُمَرًا ۖ
Na wataswagwa wale waliokufuru kuelekea Jahannam vikundi-vikundi. [Az-Zumar (39:71)]
Na pia:
وَسِيقَ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ إِلَى الْجَنَّةِ زُمَرًا ۖ
Na wataongozwa wale waliomcha Rabb wao kuelekea Jannah vikundi-vikundi. [Az-Zumar (39:73)]
Na pia:
احْشُرُوا الَّذِينَ ظَلَمُوا وَأَزْوَاجَهُمْ وَمَا كَانُوا يَعْبُدُونَ ﴿٢٢﴾
(Malaika wataamrishwa): Wakusanyeni wale waliodhulumu na wenziwao na yale waliyokuwa wakiyaabudu. [Asw-Swaaffaat (37:22)]
[Tafsiyr As-Sa’diy]
Rejea pia Al-Waaqi’ah (56:7).
[3] Watoto Wakike Walikuwa Wakizikwa Wazima Zama Za Ujaahiliyyah:
Rejea An-Nahl (16:57) ambako Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja sababu ya makafiri kuwazika watoto wa kike wanapozaliwa kutokana na kuona aibu wao kujaaliwa watoto wa kike, lakini wakimsingizia Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa Malaika ni mabanati Wake! Ametakasika Allaah na Ametukuka na wanayompachika nayo! Rejea pia Asw-Swaaffaat (37:149-153), Al-Israa (17:40) na Az-Zukhruf (43:15-19).
[4] Sahifa Za Kurekodiwa Amali:
Rejea Al-Israa (17:13-14) kwenye faida na rejea mbalimbali na maudhui zinazohusiana. Rejea pia Al-Infitwaar (82:11-12), Az-Zalzalah (99:4-8). Rejea pia Qaaf (50:18) kwenye faida kuhusu kuchunga ulimi kwa kuwa hata neno dogo vipi linarekodiwa.
[5] Kila Nafsi Itatambua Amali Zake Ilizozitenda Duniani
Rejea Kauli nyenginezo za Allaah (سبحانه وتعالى) kama hizo katika Suwrah Aal-‘Imraan (3:30), Al-Kahf (18:49), Al-Qiyaamah (75:13).
[6] Allaah (سبحانه وتعالى) Anathibitisha Kuwa Wahy (Qur-aan) Umeteremshwa na Jibriyl (عليه السّلام):
Allaah (سبحانه وتعالى) Anathibitisha kuwa Qur-aan imehifadhiwa na mashaytwaan [na kwamba imeteremshwa na Jibriyl (عليه السّلام)] kama Anavyosema:
إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ ﴿١٩﴾
Hakika hii (Qur-aan) bila shaka ni kauli ya Mjumbe Mtukufu (Jibriyl)
(Jibriyl) ambaye ameteremka nayo kutoka kwa Allaah kama Ananvosema katika Kauli Yake nyengine:
نَزَلَ بِهِ الرُّوحُ الْأَمِينُ ﴿١٩٣﴾ عَلَىٰ قَلْبِكَ لِتَكُونَ مِنَ الْمُنذِرِينَ ﴿١٩٤﴾
Ameiteremsha Ar-Ruwh (Jibriyl) mwaminifu. Juu ya moyo wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ili uwe miongoni mwa waonyaji. [Ash-Shu’araa (26:193-194)]
[Tafsiyr As-Sa’diy]
[7] Uthibitisho Wa Allaah Juu Ya Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم):
Aayah hii na zinazofuatia hadi (25), Allaah (سبحانه وتعالى) Anawaradd washirikina wa Makkah na kuthibitisha yafuatayo:
i) Anawaradd washirikina wa Makkah wanaomsingizia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kila sifa ovu kama kuwa yeye ni majununi, na kuisingizia Qur-aan kuwa imetungwa na kadhaalika. Rejea Al-Furqaan (25:4) kwenye uchambuzi wa swala hili.
ii) Kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Jibriyl katika umbo lake la asili lenye mbawa mia sita kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا حَفْصُ بْنُ غِيَاثٍ، عَنِ الشَّيْبَانِيِّ، عَنْ زِرٍّ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَى قَالَ رَأَى جِبْرِيلَ - عَلَيْهِ السَّلاَمُ - لَهُ سِتُّمِائَةِ جَنَاحٍ
Amesimulia Ash-Shaybaan kutoka kwa Zirr, kutoka kwa ‘Abdullaah (رضي الله عنهم) kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَىٰ ﴿١١﴾
Moyo haukukadhibisha yale aliyoyaona. [An-Najm: 53:11)]
Amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona Jibriyl (عليه السّلام) akiwa na mbawa mia sita.” [Muslim]
Rejea An-Najm (53:1-14)
iii) Kwamba Qur-aan haikuteremshwa na mashaytwaan. Rejea Aayah ya juu namba (19). Na pia Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) :
وَمَا تَنَزَّلَتْ بِهِ الشَّيَاطِينُ ﴿٢١٠﴾ وَمَا يَنبَغِي لَهُمْ وَمَا يَسْتَطِيعُونَ ﴿٢١١﴾ إِنَّهُمْ عَنِ السَّمْعِ لَمَعْزُولُونَ ﴿٢١٢﴾
Na wala hawakuteremka nayo (hii Qur-aan) mashaytwaan. Na wala haipasi kwao na wala hawawezi. Hakika wao bila shaka wametengwa mbali kuisikiliza. [Ash-Shu’araa (26:210-212)]
[8] Itikadi Potofu Ya Qadariyyah (Qadaria Au Kadaria) Na Radd Kupinga Kwao Qadar Ya Allaah:
Kundi la Qadariyyah (Qadaria au Kadaria) ni wanaopinga nguzo ya sita ya imaan ya Kiislamu ambayo ni kuamini Qadar ya Allaah iwe jambo la kheri au la shari. Wao wanaitakidi kuwa ayafanyayo mtu katika matendo, si kwa khiyari yake.
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله) ameelezea itikadi zao katika Fatwa ifuatayo:
Swali: Je Qadaria ni akina nani, na zipi sifa zao?
Sheikh Allaah Akuhifadhi. Umetaja kuhusu kuiamini Qadar. Kuna kundi linaitwa Qadariyyah, tunatamani kufahamu madhehebu yao yanakusudia nini?
Jibu: Al-Qadariyyah (Qadaria au Kadaria) ni watu wanaopinga Qadar, na hii ni katika unasibisho mbaya, kwa sababu ilivyozoeleka ni kwamba, kila asifikae na kitu fulani, basi hubeba sifa ya hiko kitu, lakini hawa wako kinyume chake, wanasifika na Qadar lakini wenyewe hawaiamini hiyo Qadar.
Mtu mwenye itikadi ya Qadariyyah huwa anadai kwamba mwanaadam anajitosheleza katika matendo yake, na kwamba Allaah Haingilii chochote kile. Na baadhi yao huwa wanachupa mipaka kabisa kwa kusema: “Hakika Allaah Hayajui matendo ya mja mpaka yatokee!” Umefahamu?
Hawa kwa Ahlu-Sunnah wanawaita “Qadariyyah Majuwsiyyah.” Wanawaita Wamajusi na wanasema: “Qadariyyah ni Majusi wa Ummah huu.” Je, umefahamu kivipi hadi iwe hivyo?
Wamajusi wanasema: “Huu ulimwengu una waumbaji wawili nuru (mwanga) na giza. Pale penye shari muumbaji wake ni giza. Na pale penye kheri muumbaji wake ni nuru. Wakafanya ulimwengu na vilivyomo vina waumbaji wawili. Qadariyyah nao wako hivyo hivyo! (Wanasema):
“Matendo ya waja na kile kitokacho kwao, wao ndio wanajitegemea nacho, na kile Afanyacho Allaah hiko ni Chake.” Wakafanana na Wamajusi kwa itikadi hii, ndio wakaitwa Wamajusi wa Ummah huu.
Na juu ya maelezo haya kuna Hadiyth lakini ni dhaifu, isipokuwa Ahlu-Sunnah waliitumia kwenye hii laqabu. Je, umefahamu? [Liqaat Al-Baabb Al-Maftuwh (233)]
Imaam As-Sa’diy ametafsiri ifuatavyo:
Aayah hii na zinazofanana nyenginezo, zina radd kwa kundi la Qadari wanaokanusha Qadar ya Allaah na wale wanaokanusha khiari ya mwanaadam kama ilivyojadiliwa nyuma. [Tafsiyr As-Sa’diy]
الإِنْفِطَار
082-Al-Infitwaar
082-Al-Infitwaar: Utangulizi Wa Suwrah [541]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
إِذَا السَّمَاءُ انفَطَرَتْ ﴿١﴾
1. Mbingu itakapopasuka.[1]
وَإِذَا الْكَوَاكِبُ انتَثَرَتْ ﴿٢﴾
2. Na sayari zitakapoanguka na kutawanyika.
وَإِذَا الْبِحَارُ فُجِّرَتْ ﴿٣﴾
3. Na bahari zitakapopasuliwa.
وَإِذَا الْقُبُورُ بُعْثِرَتْ ﴿٤﴾
4. Na makaburi yatakapopinduliwa chini juu na kufichuliwa.
عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ ﴿٥﴾
5. Nafsi hapo itajua yale iliyoyakadimisha na iliyoyaakhirisha.[2]
يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ ﴿٦﴾
6. Ee binaadamu! Nini kilichokughuri hata umkufuru Rabb wako Mkarimu?
الَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّاكَ فَعَدَلَكَ ﴿٧﴾
7. Ambaye Amekuumba, Akakusawazisha (umbo sura, viungo), na Akakulinganisha sawa.[3]
فِي أَيِّ صُورَةٍ مَّا شَاءَ رَكَّبَكَ ﴿٨﴾
8. Katika sura Aliyotaka Akakutengeneza.
كَلَّا بَلْ تُكَذِّبُونَ بِالدِّينِ ﴿٩﴾
9. Laa hasha! Bali mnakadhibisha malipo.
وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ ﴿١٠﴾
10. Na hakika juu yenu bila shaka kuna wenye kuhifadhi (na kuchunga).
كِرَامًا كَاتِبِينَ ﴿١١﴾
11. Watukufu wanaoandika (amali).[4]
يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ ﴿١٢﴾
12. Wanajua yale myafanyayo.
إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ ﴿١٣﴾
13. Hakika Al-Abraar[5] (watendao khayraat kwa wingi) bila shaka watakuwa katika neema (taanasa, furaha n.k).
وَإِنَّ الْفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ ﴿١٤﴾
14. Na hakika watendao dhambi bila shaka watakuwa katika moto uwakao vikali mno.
يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ الدِّينِ ﴿١٥﴾
15. Watauingia waungue Siku ya malipo.
وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَائِبِينَ ﴿١٦﴾
16. Nao hawatokosa kuweko humo.
وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿١٧﴾
17. Na nini kitakachokujulisha ni ipi Siku ya malipo?
ثُمَّ مَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ ﴿١٨﴾
18. Kisha nini kitakachokujulisha ni ipi Siku ya malipo?
يَوْمَ لَا تَمْلِكُ نَفْسٌ لِّنَفْسٍ شَيْئًاۖ وَالْأَمْرُ يَوْمَئِذٍ لِّلَّـهِ ﴿١٩﴾
19. Siku ambayo nafsi haitokuwa na uwezo wowote juu ya nafsi nyingine,[6] na amri Siku hiyo ni ya Allaah Pekee.
[1] Miongoni Mwa Matukio Ya Siku Ya Qiyaamah:
Kuanzia mwanzo wa Aayah hadi namba (4) ni miongoni mwa matukio ya Siku ya Qiyaamah. Rejea At-Takwiyr (81:1) kwenye faida inayohusiana.
[2] Kila Mtu Atatambua Matendo Yake Aliyoyatenda Duniani:
Rejea At-Takwiyr (81:14) kwenye faida zinazohusiana na maudhui hii.
[3] Binaadam Ameumbwa Katika Umbo Bora Kabisa:
Aayah hii na ifuatayo namba (8) inataja jinsi binaadam alivyoumbwa katika umbo bora kabisa na sura nzuri. Rejea Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى) nyenginezo katika Aayah zifuatazo: Aal-‘Imraan (3:6), Al-Muuminuwn (23:12-14), Al-Infitwaar (82:7-8), At-Tiyn (95:4).
[4] Amali Za Wanaadam Zinaandikwa Na Malaika:
Amali au tendo lolote analolitenda binaadam linaandikwa na kurekodiwa katika daftari lake ambalo litakunjuliwa Siku ya Qiyaamah ajionee matendo yake, hata tendo liwe dogo vipi au neno dogo vipi liwe jema au ovu. Rejea Al-Israa (17:13-14) kwenye faida na rejea mbalimbali na maudhui zinazohusiana. Rejea pia At-Takwiyr (81:10), Az-Zalzalah (99:4-8). Rejea pia Qaaf (50:18) kwenye faida kuhusu kuchunga ulimi kwa kuwa hata neno dogo vipi linarekodiwa.
[5] Maana Ya Al-Abraar:
Neno الأَبْرَارُ ni wingi wa neno البَرُّ, na maana yake ni watu waliokithirisha kufanya mambo mema ya kumridhisha Allaah. Na البَرُّ ni Jina katika Majina ya Allaah lenye maana ya Mwingi wa Ihsaan na Fadhila kama Anavyosema Mwenye Allaah (سبحانه وتعالى):
هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ ﴿٢٨﴾
Hakika Yeye Ndiye Mwingi wa Ihsaan na Fadhila, Mwenye Kurehemu. [Atw-Twuur (52:28)]
Na kwa mwanaadam lina maana ya mtu mwenye kukithirisha matendo ya kheri.
Pia neno hili البَرُّ lina maana ya bara (nchi kavu) kinyume na bahari. Na nchi kavu kama tuonavyo kheri na baraka zake ni nyingi zisizo na hesabu.
Kiistihali inamaanisha upana na wingi mno wa amali njema (khayraat). Allaah (سبحانه وتعالى) Anataja wingi wa khayraat katika Aayah namba (177) ya Suwrah Al-Baqarah kama ifuatavyo:
لَّيْسَ الْبِرَّ أَن تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ وَآتَى الْمَالَ عَلَىٰ حُبِّهِ ذَوِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَالسَّائِلِينَ وَفِي الرِّقَابِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَالْمُوفُونَ بِعَهْدِهِمْ إِذَا عَاهَدُوا ۖ وَالصَّابِرِينَ فِي الْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ وَحِينَ الْبَأْسِ ۗ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ صَدَقُوا ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ ﴿١٧٧﴾
Wema uliotimilika si kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa Mashariki na Magharibi, lakini wema uliotimilika ni mwenye kuamini Allaah na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii, na akawapa mali juu ya kuipenda kwake jamaa wa karibu na mayatima na masikini na msafiri na waombao na katika kukomboa watumwa, na akasimamisha Swalaah na akatoa Zakaah, na watimizao ahadi zao wanapoahidi, na wenye subira katika dhiki za ufukara na maafa ya magonjwa na njaa na katika vita. Hao ndio waliosadikisha na hao ndio wenye taqwa. [Al-Baqarah 2:177)]
Na birr pia ni katika katika kuwafanyia wema wazazi, kwa kuwa kuwafanyia wema wazazi ni kwingi mno. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى) kuhusu Nabiy Yahyaa (عليه السّلام):
وَبَرًّا بِوَالِدَيْهِ وَلَمْ يَكُن جَبَّارًا عَصِيًّا ﴿١٤﴾
Na mtiifu mno kwa wazazi wake wawili, na wala hakuwa jabari wala muasi. [Maryam (19:14)]
Na pia kumhusu Nabiy Iysaa (عليه السّلام) Suwrah hiyo ya Maryam (19:32).
Na katika kutoa mali anayoipenda zaidi mtu ni katika al-birr. Bonyeza kiungo kifuatacho:
Bonyeza pia kiungo kifuatacho kwenye faida nyenginezo:
Na Al-Abraar (waja wema) wametajwa mara kadhaa katika Qur-aan, na miongoni mwa Aayah zilizowataja ni: Al-Insaan (76:5), Al-Mutwaffifiyn (83:18) (83:22).
[6] Hakuna Atakayemfaa Mwenzake Siku Ya Qiyaamah Hata Wenye Uhusiano Wa Ndugu:
Rejea ‘Abasa (80:34-37) kwenye rejea mbalimbali. Rejea pia Al-Hujuraat (49:13) kwenye faida nyenginezo kuhusu maudhui hii.
الْمُطَفِّفِين
083-Al-Mutwaffifiyn
083-Al-Mutwaffifiyn: Utangulizi Wa Suwrah [546]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ ﴿١﴾
1. Ole kwa wanaopunja.[1]
الَّذِينَ إِذَا اكْتَالُوا عَلَى النَّاسِ يَسْتَوْفُونَ ﴿٢﴾
2. Ambao wanapopokea kipimo kwa watu wanataka wapimiwe kamilifu.
وَإِذَا كَالُوهُمْ أَو وَّزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ ﴿٣﴾
3. Na wanapowapimia (watu) kwa kipimo au wanawapimia kwa mizani wanapunja.
أَلَا يَظُنُّ أُولَـٰئِكَ أَنَّهُم مَّبْعُوثُونَ ﴿٤﴾
4. Je, hawadhanii kwamba wao watafufuliwa?
لِيَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٥﴾
5. Kwenye Siku iliyo kuu kabisa.
يَوْمَ يَقُومُ النَّاسُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦﴾
6. Siku watakayosimama watu kwa Rabb wa walimwengu.
كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٍ ﴿٧﴾
7. Laa hasha! Hakika kitabu cha watendaji dhambi bila shaka kimo katika Sijjuwn.[2]
وَمَا أَدْرَاكَ مَا سِجِّينٌ ﴿٨﴾
8. Na lipi litakalokujulisha nini Sijjuwn?
كِتَابٌ مَّرْقُومٌ ﴿٩﴾
9. Ni Kitabu kimeandikwa na kurekodiwa barabara (matendo).
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ ﴿١٠﴾
10. Ole Siku hiyo kwa wakadhibishaji.
الَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ ﴿١١﴾
11. Ambao wanaikadhibisha Siku ya malipo.
وَمَا يُكَذِّبُ بِهِ إِلَّا كُلُّ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ ﴿١٢﴾
12. Na haikadhibishi isipokuwa kila mwenye kutaadi, mtendaji dhambi.
إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ ﴿١٣﴾
13. Anaposomewa Aayaat Zetu, husema: Hekaya za watu wa kale.
كَلَّاۖ بَلْۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿١٤﴾
14. Laa hasha! Bali yamefanya kutu juu ya nyoyo zao yale waliyokuwa wakiyachuma.[3]
كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ ﴿١٥﴾
15. Laa hasha! Hakika wao Siku hiyo bila shaka watawekewa kizuizi wasimuone Rabb wao.[4]
ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُو الْجَحِيمِ ﴿١٦﴾
16. Kisha hakika wao bila shaka wataingizwa na waungue katika moto uwakao vikali mno.
ثُمَّ يُقَالُ هَـٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ ﴿١٧﴾
17. Kisha itasemwa: Haya ndio yale mliyokuwa mkiyakadhibisha.
كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْأَبْرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ ﴿١٨﴾
18. Laa hasha! Hakika kitabu cha Waumini watendao wema kwa wingi bila shaka kiko katika ‘Illiyyuwn.[5]
وَمَا أَدْرَاكَ مَا عِلِّيُّونَ ﴿١٩﴾
19. Na lipi litakalokujulisha nini hiyo ‘Illiyyuwn?
كِتَابٌ مَّرْقُومٌ ﴿٢٠﴾
20. Ni Kitabu kimeandikwa na kurekodiwa barabara (amali).
يَشْهَدُهُ الْمُقَرَّبُونَ ﴿٢١﴾
21. Watakishuhudia waliokurubishwa (kwa Allaah).
إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ ﴿٢٢﴾
22. Hakika Waumini watendao wema kwa wingi bila shaka watakuwa kwenye neema (taanasa, furaha n.k).
عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ ﴿٢٣﴾
23. Kwenye makochi ya fakhari wakitazama.
تَعْرِفُ فِي وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ النَّعِيمِ ﴿٢٤﴾
24. Utatambua nyuso zao kwa nuru ya neema (taanasa, furaha).[6]
يُسْقَوْنَ مِن رَّحِيقٍ مَّخْتُومٍ ﴿٢٥﴾
25. Watanyweshwa kinywaji safi na bora kabisa cha mvinyo kilichozibwa.
خِتَامُهُ مِسْكٌۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ ﴿٢٦﴾
26. Mwisho wake ni miski. Na katika hayo basi washindane wenye kushindana.
وَمِزَاجُهُ مِن تَسْنِيمٍ ﴿٢٧﴾
27. Na mchanganyiko wake ni kutokana na Tasniym.
عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا الْمُقَرَّبُونَ ﴿٢٨﴾
28. Ni chemchemu watakayokunywa humo watakaokurubishwa (kwa Allaah).
إِنَّ الَّذِينَ أَجْرَمُوا كَانُوا مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا يَضْحَكُونَ ﴿٢٩﴾
29. Hakika wale waliofanya uhalifu walikuwa (duniani) wakiwacheka wale walioamini.
وَإِذَا مَرُّوا بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ ﴿٣٠﴾
30. Na wanapowapitia wanakonyezana.
وَإِذَا انقَلَبُوا إِلَىٰ أَهْلِهِمُ انقَلَبُوا فَكِهِينَ ﴿٣١﴾
31. Na wanaporudi kwa ahli zao, hurudi wenye kufurahika kwa dhihaka.
وَإِذَا رَأَوْهُمْ قَالُوا إِنَّ هَـٰؤُلَاءِ لَضَالُّونَ ﴿٣٢﴾
32. Na wanapowaona, husema: Hakika hawa bila shaka ndio waliopotea.
وَمَا أُرْسِلُوا عَلَيْهِمْ حَافِظِينَ ﴿٣٣﴾
33. Na wao hawakutumwa kuwa ni walinzi juu yao.
فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ ﴿٣٤﴾
34. Basi leo wale walioamini watawacheka makafiri.
عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ ﴿٣٥﴾
35. Kwenye makochi ya fakhari wakitazama.
هَلْ ثُوِّبَ الْكُفَّارُ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ ﴿٣٦﴾
36. Je, basi makafiri wamelipwa yale waliyokuwa wakiyafanya?
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
083-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Mutwaffifiyn Aayah 1-6: وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ [547]
Upunjaji mizani katika uuzaji wa bidhaa ni uasi na dhulma kubwa ambayo walikuwa wakitenda pia watu wa Nabiy Shu’ayb (عليه السّلام) akawalingania watu wake waache dhulma hiyo. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ وَلَا تَنقُصُوا الْمِكْيَالَ وَالْمِيزَانَ ۚ إِنِّي أَرَاكُم بِخَيْرٍ وَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ مُّحِيطٍ﴿٨٤﴾ وَيَا قَوْمِ أَوْفُوا الْمِكْيَالَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ ۖ وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ﴿٨٥﴾
Na kwa Madyan (Tulimpeleka) ndugu yao Shu’ayb. Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah, hamna mwabudiwa wa haki ghairi Yake. Na wala msipunguze kipimo na mizani. Hakika mimi nakuoneni mko katika kheri (na neema), na hakika mimi nakukhofieni adhabu ya Siku yenye kuzingira. Na enyi kaumu yangu! Timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu, na wala msipunje watu vitu vyao, na wala msifanye uovu katika ardhi mkawa mafisadi. [Huwd (11:84-85)]
[2] Moto Wa Jahannam Uko Sijjuwn Na Jannah Iko ‘Illiyyuwn:
Amesema Al-A’mash kutoka kwa Shamar bin ‘Atwiyyah kutoka kwa Hilaal bin Yasaaf amesema: Ibn ‘Abbaas alimuuliza Ka’ab (رضي الله عنهما) nami nilikuwepo kuhusu Sijjuwn, akasema: “Hiyo ni ardhi ya saba, na humo kuna roho za makafiri.” Na akamuuliza kuhusu 'Illiyyuwn, naye akasema: “Hiyo ni mbingu ya saba na humo kuna roho za Waumini.” Na wengineo wamesema pia kuwa ni mbingu ya saba. Kuhusu Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْأَبْرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ ﴿١٨﴾
Laa hasha! Hakika kitabu cha Waumini watendao wema kwa wingi bila shaka kiko katika ‘Illiyyuwn.
[‘Aliy bin Abiy Twalhah akipokea toka kwa Ibn ‘Abbaas amesema: Yaani ni Jannah (Pepo). [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله) amesema: “Jannah iko juu ya 'Illiyyuwn na moto wa Jahannam uko katika Sijjuwn, na Sijjuwn ni chini kabisa ya ardhi. Kama isemavyo Hadiyth "Anapokufa mtu, Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema: Kirekodi kitabu cha mja Wangu katika Sijjuwn chini kabisa ya ardhi."
Ama Jannah iko juu, juu kabisa ya 'Illiyyuwn.
Na imethibiti kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "'Arsh ya Rabb (سبحانه وتعالى) Aliyetukuka Aliye juu, ni sakafu ya Jannah ya Al-Firdaws."
[Fataawa Nuwr ‘Alaa Ad-Darb (4/2)]
[3] Dhambi Zinapozidi Hutia Kutu Katika Nyoyo Mpaka Zinapofuka Kwa Madhambi:
Binaadam anapotenda dhambi, anapaswa kukimbilia istighfaar (kuomba maghfirah) na kutubia kwa Allaah (سبحانه وتعالى), kwani kuchelewa kufanya hivyo na akaendelea mtu kutenda madhambi, moyo wake huingia kutu na hatimae hupofuka kama ilivyotajwa katika Hadiyth ifuatayo:
عن أبي هُرَيرة، قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((إنَّ العبدَ إذا أخطأَ خطيئةً نُكِتت في قلبِهِ نُكْتةٌ سوداءُ، فإذا هوَ نزعَ واستَغفرَ وتابَ سُقِلَ قلبُهُ، وإن عادَ زيدَ فيها حتَّى تعلوَ قلبَهُ، وَهوَ الرَّانُ الَّذي ذَكَرَ اللَّه عز وجل ((كَلاَّ بَلْ رَانَ عَلَى قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ)) رواه أحمد والترمذي وحسنه الألباني
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mja anapofanya dhambi, doa jeusi (kutu) huwekwa katika moyo wake. Akiacha dhambi hiyo, na kuomba maghfirah na kutubu, moyo wake husafishwa ukawa msafi, lakini akirudia kufanya dhambi, doa (kutu) huzidi kuenea mpaka kufunika moyo wote na hiyo ndio 'Raan' (kutu) Aliyoisema Allaah (عزّ وجلّ):
كَلَّاۖ بَلْۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ ﴿١٤﴾
Laa hasha! Bali yamefanya kutu juu ya nyoyo zao yale waliyokuwa wakiyachuma [Al-Mutwaffifiyn (83:14)] [Ahmad, At-Tirmidhiy na Shaykh Al-Albaaniy amesema ni Hasan]
[4] ‘Aqiydah Ya Ahlus-Sunnah Kuamini Kwamba Waumini Watamuona Allaah Watakapokuwa Jannah:
Imaam Abiy ‘Abdillaah Ash-Shaafi’iy (رحمه الله) amesema: “Hii ni dalili kwamba Waumini watamuona Allaah (عزّ وجلّ) Siku hiyo.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Rejea Yuwnus (10:26) kwenye dalili nyenginezo bayana za Waumini kumuona Rabb wao. Rejea pia Suwrah Al-Qiyaamah (75:22-23).
[6] Nyuso Za Waumini Zitang’ara Kwa Furaha Siku Ya Qiyaamah:
Rejea ‘Abasa (80:38) kwenye kubainisha hali za nyuso za Waumini na makafiri zitakavyokuwa Siku ya Qiyaamah.
الإِنْشِقَاق
084-Al-Inshiqaaq
084-Al-Inshiqaaq: Utangulizi Wa Suwrah [549]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ ﴿١﴾
1. Mbingu itakaporaruka.[1]
وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ ﴿٢﴾
2. Na ikamsikiliza na kumtii Rabb wake na ikawajibikiwa kufanya hivyo.
وَإِذَا الْأَرْضُ مُدَّتْ ﴿٣﴾
3. Na ardhi itakapotandazwa sawa (bila mwinuko wala mwinamo).
وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ ﴿٤﴾
4. Na ikatupilia mbali vile vilivyomo ndani yake na ikawa tupu.
وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ ﴿٥﴾
5. Na ikamsikiliza na kumtii Rabb wake na ikawajibikiwa kufanya hivyo.
يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدْحًا فَمُلَاقِيهِ ﴿٦﴾
6. Ee binaadam! Hakika wewe unajikusurukusuru mno kuelekea kwa Rabb wako kwa juhudi na masumbuko, basi utakutana Naye.
فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ ﴿٧﴾
7. Basi ama yule atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia.[2]
فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا ﴿٨﴾
8. Huyo atahesabiwa hesabu nyepesi.[3]
وَيَنقَلِبُ إِلَىٰ أَهْلِهِ مَسْرُورًا ﴿٩﴾
9. Na atageuka kwa ahli zake akiwa mwenye furaha.
وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ وَرَاءَ ظَهْرِهِ ﴿١٠﴾
10. Na ama yule atakayepewa kitabu chake nyuma ya mgongo wake.[4]
فَسَوْفَ يَدْعُو ثُبُورًا ﴿١١﴾
11. Huyo ataomba kuteketea.
وَيَصْلَىٰ سَعِيرًا ﴿١٢﴾
12. Na ataingia moto uliowashwa vikali mno aungue.
إِنَّهُ كَانَ فِي أَهْلِهِ مَسْرُورًا ﴿١٣﴾
13. Hakika yeye alikuwa katika ahli zake mwenye kufurahi.
إِنَّهُ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ ﴿١٤﴾
14. Hakika yeye alidhani kwamba hatorudi kwenye asili yake.
بَلَىٰ إِنَّ رَبَّهُ كَانَ بِهِ بَصِيرًا ﴿١٥﴾
15. Sivyo hivyo (bali atarudi tu)! Hakika Rabb wake Amekuwa Mwenye Kumuona daima.
فَلَا أُقْسِمُ بِالشَّفَقِ ﴿١٦﴾
16. Basi Naapa kwa wekundu wa kukuchwa jua.
وَاللَّيْلِ وَمَا وَسَقَ ﴿١٧﴾
17. Na Naapa kwa usiku na ambavyo umekusanya (na kugubika).
وَالْقَمَرِ إِذَا اتَّسَقَ ﴿١٨﴾
18. Na Naapa kwa mwezi unapokuwa mbalamwezi kamili.
لَتَرْكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍ ﴿١٩﴾
19. Bila shaka mtapitia hatua baada ya hatua.[5]
فَمَا لَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٢٠﴾
20. Basi wana nini hawaamini?!
وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنُ لَا يَسْجُدُونَ ۩﴿٢١﴾
21. Na wanaposomewa Qur-aan, hawasujudu.[6]
بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا يُكَذِّبُونَ ﴿٢٢﴾
22. Bali wale waliokufuru wanakadhibisha.
وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يُوعُونَ ﴿٢٣﴾
23. Na Allaah Anajua zaidi yale wanayoyakusanya ya siri.
فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٢٤﴾
24. Basi wabashirie adhabu iumizayo.
إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ ﴿٢٥﴾
25. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema, hao watapata ujira usiokatika.
[1] Miongoni Mwa Matukio Ya Siku Ya Qiyaamah:
Kuanzia mwanzo wa Aayah hadi namba (5) ni miongoni mwa matukio ya Siku ya Qiyaamah. Rejea At-Takwiyr (81:1) kwenye faida inayohusiana.
[2] Watakaopewa Vitabu Vyao Kuliani Mwao:
Kuanzia Aayah hii namba (7) na zinazofuatia (8-9), zinataja hali za watu watakaopewa vitabu vyao kuliani. Rejea Al-Haaqqah (69:19-24).
[3] Waumini Watakaopewa Vitabu Vyao Kuliani Watafanyiwa Hesabu Nyepesi:
Hesabu nyepesi itakuwa ni mazungumzo mepesi ya matendo yake mbele ya Allaah (عزّ وجلّ). Allaah (عزّ وجلّ) Atamfanya akiri madhambi yake mpaka atapodhani kuwa ameangamia basi hapo Humfanyia hesabu nyepesi. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Na hesabu nyepesi ni ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Hatomsaili mja kuhusu madhambi yake, bali Atamghufuria bila ya kumuuliza, kwani atakayesailiwa na Allaah kuhusu madhambi yake, basi huyo ataangamia. Imethibiti hivyo katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ عَائِشَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " لَيْسَ أَحَدٌ يُحَاسَبُ إِلاَّ هَلَكَ " . قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَلَيْسَ اللَّهُ يَقُولُ حِسَابًا يَسِيرًا قَالَ " ذَاكِ الْعَرْضُ وَلَكِنْ مَنْ نُوقِشَ الْحِسَابَ هَلَكَ " .
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna yeyote atakayehesabiwa isipokuwa ataangamia.” Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, si Allaah Anasema: Hesabu Nyepesi? Akasema: “Hiyo ni kudhihirishiwa tu madhambi yake, lakini atakayesailiwa hesabu yake, basi ataangamia.” [Muslim Kitabu Cha Jannah, Sifa za Neema Zake na Watu Wake]
Na Hadiyth ifuatayo inathibitisha kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Atasitiri madhambi ya mja Wake na Atamghufuria, kwa hivyo Hatomsaili:
حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ صَفْوَانَ بْنِ مُحْرِزٍ، أَنَّ رَجُلاً، سَأَلَ ابْنَ عُمَرَ كَيْفَ سَمِعْتَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ فِي النَّجْوَى قَالَ " يَدْنُو أَحَدُكُمْ مِنْ رَبِّهِ حَتَّى يَضَعَ كَنَفَهُ عَلَيْهِ فَيَقُولُ عَمِلْتَ كَذَا وَكَذَا. فَيَقُولُ نَعَمْ. وَيَقُولُ عَمِلْتَ كَذَا وَكَذَا. فَيَقُولُ نَعَمْ. فَيُقَرِّرُهُ ثُمَّ يَقُولُ إِنِّي سَتَرْتُ عَلَيْكَ فِي الدُّنْيَا، فَأَنَا أَغْفِرُهَا لَكَ الْيَوْمَ ".
Amesimulia Swafwaan Bin Muhriz (رضي الله عنه): Mtu mmoja alimuuliza Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما): Je, umemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema nini kuhusu an-najwaa (kunong’onezana baina ya Allaah na mja Wake Muumini Siku ya Qiyaamah)? Akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mmoja wenu atakuja karibu na Rabb Wake mpaka Atamfinika na pazia Yake, Atamwambia: Je, ulifanya kadhaa na kadhaa? (Mja) Atasema: Naam. Kisha Allaah Atasema: Je, ulifanya kadhaa na kadhaa? Atasema: Naam. Kwa hiyo, Allaah Atamfanya akiri (makosa yake), kisha Atasema: Hakika Nilikusitiria duniani (madhambi yako) na leo nakughufuria.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Adabu (78), Kitabu Cha Tawhiyd (97)]
Na pia kuhusu hesabu nyepesi ni Hadiyth ifuatayo:
حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ أَبِي مَرْيَمَ، قَالَ أَخْبَرَنَا نَافِعُ بْنُ عُمَرَ، قَالَ حَدَّثَنِي ابْنُ أَبِي مُلَيْكَةَ، أَنَّ عَائِشَةَ، زَوْجَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم كَانَتْ لاَ تَسْمَعُ شَيْئًا لاَ تَعْرِفُهُ إِلاَّ رَاجَعَتْ فِيهِ حَتَّى تَعْرِفَهُ، وَأَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " مَنْ حُوسِبَ عُذِّبَ ". قَالَتْ عَائِشَةُ فَقُلْتُ أَوَ لَيْسَ يَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا قَالَتْ فَقَالَ " إِنَّمَا ذَلِكَ الْعَرْضُ، وَلَكِنْ مَنْ نُوقِشَ الْحِسَابَ يَهْلِكْ ".
Amesimulia Ibn Abu Mulaykah (رضي الله عنه): Kila wakati (Mama wa Wumini) ‘Aaishah aliposikia jambo ambalo hakulielewa, alikuwa akiuliza tena mpaka afahamu. ‘Aaishah alisema: “Wakati mmoja Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: “Yeyote atakayeitwa kusailiwa (na Allaah) amali zake Siku ya Qiyaamah hapana shaka ataadhibiwa.” Nikasema: Je, Allaah (سبحانه وتعالى) Hakusema:
فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا ﴿٨﴾
Atahesabiwa hesabu nyepesi. [Al-Inshiqaaq (84:9)]
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Hakika hii inamaanisha uwasilishaji wa hesabu tu lakini mtu yeyote atakayesailiwa kuhusu hesabu yake ataangamia.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Ilmu (3)]
[Al-Bukhaariy Kitabu Cha Ilmu (3)]
[5] Kupitia Hatua Baada Ya Hatua:
Yaani hatua nyingi tofauti (za mwanaadam) kuanzia manii hadi pande la damu linalonin’ginia, kisha kinofu cha nyama, kisha kupulizwa roho, kisha kuzaliwa na utoto, kisha kufikia umri wa utambuzi, halafu kuanza kusajiliwa mema yake na mabaya yake pamoja na maamrisho na makatazo baada ya kubaleghe. Kisha baada ya yote hayo, mwanaadam hufariki, halafu atakuja kufufuliwa ili alipwe matendo yake. Hatua hizi mbalimbali ambazo mwanaadam hupitia, zinaashiria kwamba Allaah Pekee Ndiye Anayestahiki kuabudiwa, Yeye Ni Mmoja Pweke, na Ndiye Mwenye kudabiri mambo ya Waja Wake kwa Hikma Yake na Rehma Yake, na kwamba mja ni faqiri, na hana uwezo chini ya Uendeshaji wa Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[6] Sajdatut-Tilaawah: Sijdah Ya Kisomo.
Anapofika mtu Aayah hii anatakiwa asujudu. Rejea Al-A’raaf (7:206) kwenye maelezo na faida kadhaa.
الْبُرُوج
085-Al-Buruwj
085-Al-Buruwj: Utangulizi Wa Suwrah [551]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْبُرُوجِ ﴿١﴾
1. Naapa kwa mbingu yenye buruji [1]
وَالْيَوْمِ الْمَوْعُودِ ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa Siku iliyoahidiwa (ya Qiyaamah).
وَشَاهِدٍ وَمَشْهُودٍ ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa shahidi na kinachoshuhudiwa.[2]
قُتِلَ أَصْحَابُ الْأُخْدُودِ ﴿٤﴾
4. Wamelaaniwa na kuangamia watu wa mahandaki.[3]
النَّارِ ذَاتِ الْوَقُودِ ﴿٥﴾
5. Yenye moto uliojaa kuni na mafuta.
إِذْ هُمْ عَلَيْهَا قُعُودٌ ﴿٦﴾
6. Pale walipokuwa wamekaa hapo.
وَهُمْ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ بِالْمُؤْمِنِينَ شُهُودٌ ﴿٧﴾
7. Nao ni wenye kushuhudia juu ya yale wanayowafanyia Waumini.
وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَن يُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ ﴿٨﴾
8. Na hawakuwachukia isipokuwa kwa vile wamemwamini Allaah Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.
الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِۚ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿٩﴾
9. Ambaye Pekee Ana ufalme wa mbingu na ardhi. Na Allaah juu ya kila kitu Ni Shahidi.
إِنَّ الَّذِينَ فَتَنُوا الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ الْحَرِيقِ ﴿١٠﴾
10. Hakika wale waliowatesa motoni Waumini wa kiume na Waumini wa kike kisha hawakutubu, watapata adhabu ya Jahannam, na watapata adhabu ya kuunguza.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْكَبِيرُ ﴿١١﴾
11. Hakika wale walioamini na wakatenda mema watapata Jannaat zipitazo chini yake mito. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
إِنَّ بَطْشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ ﴿١٢﴾
12. Hakika mkamato wa kuadhibu wa Rabb wako bila shaka ni mkali.
إِنَّهُ هُوَ يُبْدِئُ وَيُعِيدُ ﴿١٣﴾
13. Hakika Yeye Ndiye Anayeanzisha asili (ya uumbaji) na Anayerudisha.
وَهُوَ الْغَفُورُ الْوَدُودُ ﴿١٤﴾
14. Naye Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Upendo halisi.
ذُو الْعَرْشِ الْمَجِيدُ ﴿١٥﴾
15. Mwenye ‘Arsh, Al-Majiyd.[4]
فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ ﴿١٦﴾
16. Mwingi wa Kufanya Atakalo, hakuna wa kumzuia.
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْجُنُودِ ﴿١٧﴾
17. Je, imekujia hadithi ya majeshi?
فِرْعَوْنَ وَثَمُودَ ﴿١٨﴾
18. Ya Firawni na kina Thamuwd?
بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي تَكْذِيبٍ ﴿١٩﴾
19. Bali wale waliokufuru wamo katika kukadhibisha.
وَاللَّـهُ مِن وَرَائِهِم مُّحِيطٌ ﴿٢٠﴾
20. Na Allaah Amewazunguka (kwa Ujuzi Wake) nyuma yao.
بَلْ هُوَ قُرْآنٌ مَّجِيدٌ ﴿٢١﴾
21. Bali hii ni Qur-aan Majiyd[5].
فِي لَوْحٍ مَّحْفُوظٍ ﴿٢٢﴾
22. Katika Ubao Uliohifadhiwa.[6]
[1] Buruji:
‘Ulamaa wametaja maana ya buruji katika kauli zifuatazo: (i) Ibn ‘Abbaas, Mujaahid, Adhw-Dhwahaak, Al-Hasan, Qataadah, As-Suddy wamesema ni nyota (ii) Mujaahid kanukuliwa kwenye kauli nyingine akisema ni nyota zenye walinzi (iii) Yahyaa bin Raafi’ amesema ni maqasri mbinguni (iv) Al-Minhaal bin ‘Amr amesema ni uumbaji mzuri (v) Ibn Jariyr yeye anaona ni vituo au njia za kupitia jua na mwezi, nazo ni buruji kumi na mbili ambazo jua hutembea na kupita katika kila moja ya hizi burj (umoja wa buruji) katika mwezi mmoja. Mwezi nao pia hutembea na kupita katika kila moja ya burj hizi katika siku mbili na theluthi, na hivyo ni vituo ishirini na nane, na hufichika kwa nyusiku mbili. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Rejea pia Al-Furqaan (25:61)]
[2] Shahidi Na Kinachoshuhudiwa:
Inajumuisha kila mtu anayekidhi maelezo haya. Yaani: Mwenye kuona na anayeonekana, na mwenye kuwepo na mwenye kuhudhurishwa. Kinachoshuhudiwa hapa ni ishara dhahiri zinazong'aa za Allaah (سبحانه وتعالى) na Hikma iliyodhahiri, na Rehma Yake pana. [Tafsiyr As-Sa’diy] Na imesemwa pia yanayofuatia ya Aayah namba (4).
[3] Kisa Cha Watu Wa Mahandaki:
Allaah (سبحانه وتعالى) Ameapia kuanzia mwanzo wa Suwrah. Na jawabu la kiapo hicho (جَوَابُ القَسَمِ) ni kama alivyotafsiri Imaam As-Sa’diy (رحمه الله):
Ni Kauli Yake:
قُتِلَ أَصْحَابُ الْأُخْدُودِ ﴿٤﴾
Wamelaaniwa na kuangamia watu wa mahandaki.
Hii ni duaa ya kuangamizwa kwao. Na mahandaki ni mashimo yanayochimbwa ardhini. Na hawa watu wa mahandaki walikuwa ni makafiri, na walikuwa wakiishi pamoja nao Waislamu. Wakajaribu kuwarai Waislamu ili waingie katika dini yao, lakini Waumini hawa walikataa kufanya hivyo. Basi makafiri wakachimba mahandaki ardhini na kuwasha moto ndani yake, kisha wakaketi kuyazunguka na wakawatesa Waumini na kuwasogeza karibu na moto huo. Wale waliowakubalia kuingia ukafirini waliwaachia, ama wale walioshikamana na imaan yao waliwatupa motoni. Huu ulikuwa ni mfano wa uadui mkubwa juu ya Allaah na Waumini, kwa hiyo Allaah Akawalaani, Akawaangamiza na Akawaahidi adhabu ndio Akasema:
قُتِلَ أَصْحَابُ الْأُخْدُودِ ﴿٤﴾
Wamelaaniwa na kuangamia watu wa mahandaki.
[Tafsiyr As-Sa’diy]
Aayah zinazofuatia zinaelezea hali ilivyo ya kisa hicho cha watu wa mahandaki na Adhabu Alizowaahidi Allaah.
[4] Mwenye ‘Arsh Al-Majiyd
Tafsiyr:
Yaani Mwenye Kumiliki ‘Arsh Adhimu Ambaye kutokana na Utukufu Wake, Ametandaza mbingi na ardhi na Kursiyy ambayo ni kipimo cha (udogo wa) pete katika jangwa, kulinganisha na ‘Arsh. Allaah Ameitaja ‘Arsh makhsusi kutokana na uadhimu wake, na kwamba ni makhsusi kati ya vitu Alivyoviuma vilivyokuuwa karibu Naye (سبحانه وتعالى). AL-Majiyd inaweza kuwa imekusudiwa ni ‘Arsh. Na huenda Al-Majiyd imekusudiwa ni Allaah ambayo ni Sifa yeye maana pana ya Utukufu. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Na katika Majina Mazuri ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Sifa Zake maana ya Al-Majiyd ni: Mwingi Mno Wa Vipawa Na Ukarimu.
Ikiwa imekusudiwa Qur-aan, basi ni: Adhimu, Karimu, yenye kheri, Baraka na ilimu tele. Rejea Qaaf (50:1).
[5] Qur-aan Majiyd:
Qur-aan Adhimu, Karimu, yenye kheri, hikmah, baraka na ilmu tele. Rejea Qaaf (50:1)
[6] Al-Lawh Al-Mahfuwdhw:
Al-Lawh Al-Mahfuwdhw ni Ubao Uliohifadhiwa mbinguni. Umehifadhika kutokana na mabadiliko, kuongozeka na kupunguka na umehifadhiwa na mashaytwaan. Nao ni Ubao ambao Allaah (سبحانه وتعالى) Amethibitisha kila kitu ndani yake [Tafsiyr As-Sa’diy]
Na pia imetajwa kuwa ni Ummul-Kitaab (Mama wa Kitabu) Rejea pia Ar-Ra’d (13:39).
الطَّارِق
086-At-Twaariq
086-Atw-Twaariq: Utangulizi Wa Suwrah [553]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالسَّمَاءِ وَالطَّارِقِ ﴿١﴾
1. Naapa kwa mbingu na kinachogonga kinapotoka usiku[1].
وَمَا أَدْرَاكَ مَا الطَّارِقُ ﴿٢﴾
2. Na kipi kitakachokujulisha kinachogonga na kutoka usiku?
النَّجْمُ الثَّاقِبُ ﴿٣﴾
3. Ni nyota yenye mwanga mkali mno inayopenya kwa nguvu.
إِن كُلُّ نَفْسٍ لَّمَّا عَلَيْهَا حَافِظٌ ﴿٤﴾
4. Hakuna nafsi yeyote isipokuwa inayo (Malaika) mhifadhi juu yake.
فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ مِمَّ خُلِقَ ﴿٥﴾
5. Basi na atazame binaadamu ameumbwa kutokana na kitu gani?
خُلِقَ مِن مَّاءٍ دَافِقٍ ﴿٦﴾
6. Ameumbwa kutokana na maji yatokayo kwa mchupo (manii).
يَخْرُجُ مِن بَيْنِ الصُّلْبِ وَالتَّرَائِبِ ﴿٧﴾
7. Yanatoka baina ya uti wa mgongo na mbavu za kifua.
إِنَّهُ عَلَىٰ رَجْعِهِ لَقَادِرٌ ﴿٨﴾
8. Hakika Yeye (Allaah) bila shaka Ni Muweza[2] wa Kumrudisha (hai).
يَوْمَ تُبْلَى السَّرَائِرُ ﴿٩﴾
9. Siku siri zitakapopekuliwa (na kufichuka).
فَمَا لَهُ مِن قُوَّةٍ وَلَا نَاصِرٍ ﴿١٠﴾
10. Basi hatakuwa na nguvu yoyote wala mwenye kunusuru yeyote.
وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الرَّجْعِ ﴿١١﴾
11. Naapa kwa mbingu yenye marejeo (ya kuleta mvua).
وَالْأَرْضِ ذَاتِ الصَّدْعِ ﴿١٢﴾
12. Na Naapa kwa ardhi yenye kupasuka (kutoa mimea).
إِنَّهُ لَقَوْلٌ فَصْلٌ ﴿١٣﴾
13. Hakika hii (Qur-aan) ni kauli pambanushi[3] (bayana na ukweli mtupu)
وَمَا هُوَ بِالْهَزْلِ ﴿١٤﴾
14. Nayo si mzaha.
إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًا ﴿١٥﴾
15. Hakika wao wanapanga hila.
وَأَكِيدُ كَيْدًا ﴿١٦﴾
16. Nami Natibua hila (zao).
فَمَهِّلِ الْكَافِرِينَ أَمْهِلْهُمْ رُوَيْدًا ﴿١٧﴾
17. Basi wape makafiri muhula, wape muhula taratibu.
[1] Atw-Twaariq (Nyota Angavu Inayotoka Usiku Huku Ikigonga)
At-Twaariq ni nyota inayotoka usiku yenye mwanga mkali, na mwanga wake unapenya katika mbingu hadi unaonekana ardhini. Rai iliyo sahihi ni nyota zote zenye mwanga mkali unaopenya. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Na kauli nyengineyo ni anayegonga usiku kama alivyotafsiri Imaam Ibn Kathiyr:
Imeitwa At-Twaariq kwa sababu inaonekana usiku na inapotea mchana. Na inatilia nguvu Hadiyth Swahiyh ya kukatazwa mtu kuwafikia ahli wake kwa ghafla usiku kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ جَابِرٍ، قَالَ نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَنْ يَطْرُقَ الرَّجُلُ أَهْلَهُ لَيْلاً يَتَخَوَّنُهُمْ أَوْ يَلْتَمِسُ عَثَرَاتِهِمْ .
Amesimulia Jaabir (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amekataza mtu kuwafikia ahli wake (bila ya kuwapasha habari) usiku kwa kujenga dhana kwamba wanamkhini, au kupeleleza na kufumania makosa yao. [Muslim]
Na Hadiyth nyengine (ni duaa ya kujikinga na viumbe vya shari vinavyoingia majumbani usiku:
ومِنْ شَرِّ كُلِّ طارِقٍ إِلَّا طَارِقاً يَطْرُقُ بخَيْرٍ يَا رَحْمَنُ.
Na shari ya kila anayegonga usiku ila anayegonga kwa kheri Ee Mwingi wa Rehma. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Bonyeza kiungo kifuatacho kupata duaa hiyo:
128-Hiswnul-Muslim: Duaa Ya Kuzuia Vitimbi Vya Mashaytwaan [554]
[3] Qur-aan Ni Kauli Pambanushi:
Kauli Pambanushi: Ina uwazi na ukweli mtupu. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Kauli Pambanushi: Inapambanua baina ya haki na baatwil. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Kauli Pambanushi: Ya haki. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Kauli Pambanushi: Inapambanua baina ya haki na baatwil na imaamuru sharia kali kwa mwanaadam ili kukata mizizi ya uovu. [The Noble Qur-aan]
الْأَعْلَى
087-Al-A’laa
087-Al-A’laa: Utangulizi Wa Suwrah [556]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى ﴿١﴾
1. Sabbih Jina la Rabb wako Mwenye ‘Uluwa Aliyetukuka kabisa kuliko vyote.[1]
الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ ﴿٢﴾
2. Ambaye Ameumba (kila kitu) kisha Akasawazisha.
وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ ﴿٣﴾
3. Na Ambaye Amekadiria na Akaongoza.[2]
وَالَّذِي أَخْرَجَ الْمَرْعَىٰ ﴿٤﴾
4. Na Ambaye Ametoa malisho.
فَجَعَلَهُ غُثَاءً أَحْوَىٰ ﴿٥﴾
5. Kisha Akayafanya majani makavu, meusi.
سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰ ﴿٦﴾
6. Tutakufanya uisome (Qur-aan ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kisha hutoisahau.
إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُۚ إِنَّهُ يَعْلَمُ الْجَهْرَ وَمَا يَخْفَىٰ ﴿٧﴾
7. Isipokuwa yale Ayatakayo Allaah. Hakika Yeye Anayajua ya jahara na yale yanayofichikana.
وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَىٰ ﴿٨﴾
8. Na Tutakuwepesishia kwa yaliyo mepesi.
فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ الذِّكْرَىٰ ﴿٩﴾
9. Basi kumbusha ikiwa unafaa ukumbusho.
سَيَذَّكَّرُ مَن يَخْشَىٰ ﴿١٠﴾
10. Atakumbuka yule anayeogopa.
وَيَتَجَنَّبُهَا الْأَشْقَى ﴿١١﴾
11. Na atajiepusha nao fedhuli.
الَّذِي يَصْلَى النَّارَ الْكُبْرَىٰ ﴿١٢﴾
12. Ambaye atauingia moto mkubwa kabisa na kuungua.
ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ ﴿١٣﴾
13. Kisha hatokufa humo, na wala hatokuwa na uhai (wa raha).[3]
قَدْ أَفْلَحَ مَن تَزَكَّىٰ ﴿١٤﴾
14. Hakika amefaulu ambaye amejitakasa.
وَذَكَرَ اسْمَ رَبِّهِ فَصَلَّىٰ ﴿١٥﴾
15. Na akadhukuru Jina la Rabb wake na akaswali.
بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا ﴿١٦﴾
16. Bali mnahiari zaidi uhai wa dunia.[4]
وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ﴿١٧﴾
17. Na hali Aakhirah ni bora zaidi na ya kudumu zaidi.
إِنَّ هَـٰذَا لَفِي الصُّحُفِ الْأُولَىٰ ﴿١٨﴾
18. Hakika haya bila shaka yamo katika Suhuf (Maandiko Matukufu) ya awali.[5]
صُحُفِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ ﴿١٩﴾
19. Suhuf ya Ibraahiym na Muwsaa.
[1] Al-A’laa:
Mwenye ‘Uluwa, Ametukuka, Ana Uadhama Kuliko wote kuliko vyote, Yuko juu Kabisa juu ya viumbe Vyake vyote.
[2] Allaah (سبحانه وتعالى) Amekadiria Kila Alichokiumba Akakiongoza:
Kauli Ya Allaah (سبحانه وتعالى):
قَالَ رَبُّنَا الَّذِي أَعْطَىٰ كُلَّ شَيْءٍ خَلْقَهُ ثُمَّ هَدَىٰ ﴿٥٠﴾
(Muwsaa) akasema: Rabb wetu ni Yule Aliyekipa kila kitu umbo lake, kisha Akakiongoza. [Twaahaa (20:50)]
Na kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Allaah (سبحانه وتعالى) Kukadiria kila Alichokiumba ni Hadiyth ifuatayo:
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو، بْنِ الْعَاصِ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ " كَتَبَ اللَّهُ مَقَادِيرَ الْخَلاَئِقِ قَبْلَ أَنْ يَخْلُقَ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضَ بِخَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ - قَالَ - وَعَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ " .
Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Aliandika (kwenye Al-Lawh Al-Mahfuwdh) makadirio na hatima ya viumbe wote kabla ya kuumba mbingu na ardhi kwa miaka elfu khamsini, - akasema- 'Arsh Yake ilikuwa juu ya maji." [Muslim]
Rejea pia Huwd (11:7) kwenye faida nyenginezo.
[3] Makafiri Motoni Hawatakufa Wala Hawatakuwa Hai:
Rejea Faatwir (35:36) kwenye faida ya maudhui hii.
[4] Tahadharisho La Kupendelea Dunia Badala Ya Aakhirah:
Rejea Ash-Shuwraa (42:20) na Al-Hadiyd (57:20) kwenye maelezo bayana na faida tele pamoja na rejea mbalimbali za maudhui.
[5] Suhuf (Maandiko Matukufu) Na Tofauti Baina Yake Na Vitabu Vinginenvyo Vya Mbinguni:
Kila Rasuli ameteremshiwa Kitabu lakini hatuvijui Vitabu hivyo isipokuwa Tawraat (ya Nabiy Muwsaa (عليه السّلام), Injiyl (ya Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام), Zabuwr (ya Nabiy Daawuwd (عليه السّلام), na Suhuf ya Nabiy Ibraahiym na Muwsaa (عليهما السلام). Rejea An-Najm (53:36-37).
Na ‘Ulamaa wamekhitilafiana kuhusu Suhuf ya Muwsaa kama hiyo ndio Tawraah au laa! Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi [Imaam Ibn ‘Uthaymiyn – Fataawa Nuwr Alad-Darb Kaseti (278)]
‘Ulamaa wengineo wamekhitilafiana katika kauli mbili:
Kauli ya kwanza: Suhuf na Vitabu ni kitu kimoja na kwamba Suhuf ya Muwsaa (عليه السّلام) ndio hiyo hiyo Tawraat ambayo Allaah (عزّ وجلّ) Ameiandika kwa Mkono Wake katika Al-Alwaah (Mbao) kama ilivyotajwa katika Qur-aan. Lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Ameziita (Al-Alwaah) Mbao katika baadhi ya Aayah na Ameziita Tawraat katika Aayah nyenginezo na Ameziita Suhuf katika Aayah nyenginezo.
Kauli ya pili: Suhuf za mbinguni zinatofautiana na Vitabu vya Mbinguni na kwamba Tawraat inatofautiana na Suhuf. Tawraat ni Kitabu ambacho Allaah (سبحانه وتعالى) Alikiandika kwa Mkono Wake. Ama Suhuf ni Suhuf Alizoteremsha Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) ambayo ndani yake inabainishwa na kufafanuliwa wazi Sharia ya Tawraat kama vile Sunnah (Hadiyth) Anazoteremshiwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).
Rejea pia Al-Bayyinah (98:2).
Na Allaah Mjuzi zaidi
الْغَاشِيَة
088-Al-Ghaashiyah
088-Al-Ghaashiyah: Utangulizi Wa Suwrah [558]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ ﴿١﴾
1. Je, imekujia habari ya tukio la kufunikiza (na kutoa fahamu)?
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَةٌ ﴿٢﴾
2. Nyuso siku hiyo zitadhalilika.[1]
عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ ﴿٣﴾
3. Zifanye kazi ngumu na zichoke mno.
تَصْلَىٰ نَارًا حَامِيَةً ﴿٤﴾
4. Zitaingia moto uwakao vikali na kuungua.
تُسْقَىٰ مِنْ عَيْنٍ آنِيَةٍ ﴿٥﴾
5. Zitanyweshwa kutoka chemchem yenye kutokota.
لَّيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ ﴿٦﴾
6. Hawatokuwa na chakula isipokuwa kutokana na mti wenye miba, wenye kunuka na mchungu mno.
لَّا يُسْمِنُ وَلَا يُغْنِي مِن جُوعٍ ﴿٧﴾
7. Hakinenepeshi, na wala hakisaidii kuondoa njaa.
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاعِمَةٌ ﴿٨﴾
8. Na nyuso (nyingine) Siku hiyo zitakuwa zenye kuneemeka.[2]
لِّسَعْيِهَا رَاضِيَةٌ ﴿٩﴾
9. Zitafarijika kwa juhudi zake.
فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ ﴿١٠﴾
10. Kwenye Jannah ya juu.
لَّا تَسْمَعُ فِيهَا لَاغِيَةً ﴿١١﴾
11. Hazitosikia humo upuuzi wala ubatilifu.
فِيهَا عَيْنٌ جَارِيَةٌ ﴿١٢﴾
12. Humo mna chemchem inayobubujika.
فِيهَا سُرُرٌ مَّرْفُوعَةٌ ﴿١٣﴾
13. Humo mna makochi yaliyoinuliwa.
وَأَكْوَابٌ مَّوْضُوعَةٌ ﴿١٤﴾
14. Na bilauri zilizopangwa tayari.
وَنَمَارِقُ مَصْفُوفَةٌ ﴿١٥﴾
15. Na matakia yaliyopangwa safusafu.
وَزَرَابِيُّ مَبْثُوثَةٌ ﴿١٦﴾
16. Na mazulia yaliyopambwa na ya fahari yaliyotandazwa.
أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ ﴿١٧﴾
17. Je, hawawataamuli ngamia namna walivyoumbwa?[3]
وَإِلَى السَّمَاءِ كَيْفَ رُفِعَتْ ﴿١٨﴾
18. Na mbingu vipi zilivyonyanyuliwa?[4]
وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ ﴿١٩﴾
19. Na milima vipi imekongomewa imara kabisa?
وَإِلَى الْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ ﴿٢٠﴾
20. Na ardhi vipi ilivyotandazwa?
فَذَكِّرْ إِنَّمَا أَنتَ مُذَكِّرٌ ﴿٢١﴾
21. Basi kumbusha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Hakika wewe ni mkumbushaji tu.
لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ ﴿٢٢﴾
22. Wewe si mwenye kuwadhibiti.
إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ ﴿٢٣﴾
23. Isipokuwa yule atayegeuka na akakufuru.
فَيُعَذِّبُهُ اللَّـهُ الْعَذَابَ الْأَكْبَرَ ﴿٢٤﴾
24. Basi huyo Allaah Atamuadhibu adhabu kubwa kabisa.
إِنَّ إِلَيْنَا إِيَابَهُمْ ﴿٢٥﴾
25. Hakika Kwetu ndio marejeo yao.
ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُم ﴿٢٦﴾
26. Kisha bila shaka ni juu Yetu hesabu yao.
[1] Nyuso Za Makafiri Zitadhalilika:
Rejea ‘Abasa (80:38) kwenye kubainisha nyuso za makafiri na nyuso za Waumini zitakavyokuwa Siku ya Qiyaamah.
[2] Nyuso Za Waumini Zitang’ara Siku Ya Qiyaamah Kwa Furaha Na Kufuzu Kwake:
Rejea ‘Abasa (80:38) kwenye kubainisha nyuso za makafiri na nyuso za Waumini zitakavyokuwa Siku ya Qiyaamah.
[3] Uumbwaji Wa Ajabu Wa Ngamia Na Manufaa Yake:
Allaah (عزّ وجلّ) Anawaamrisha Waja Wake kuvitazama viumbe Vyake vinavyoashiria Uwezo na Uadhwamah (Utukufu) Wake, kwani ngamia ni kiumbe cha ajabu, na uundwaji wake ni wa ajabu kwa kuwa ana nguvu kubwa mno, lakini juu ya hivyo, anabeba mizigo mizito bila matata yoyote, na anaongozwa hata na kijana mdogo tu. Nyama yake inaliwa, maziwa yake yananywewa, na manyoya yake hutumika kwa manufaa mbalimbali. Basi Waarabu wametanabahishwa hayo kwa sababu aghlabu wa wanyama wao walikuwa ni ngamia. Na Shariyh Al-Qaadhwiy alikuwa akisema: “Tutoe nje ili tuangalie ngamia jinsi walivyoumbwa.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[4] Mbingu Zimeumbwa Bila Ya Nguzo:
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى) katika Kauli Yake:
اللَّـهُ الَّذِي رَفَعَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ۖ
Allaah Ambaye Ameinua mbingu bila ya nguzo mnaziona. [Ar-Ra’d (13:2)]
Na pia:
خَلَقَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ۖ
(Allaah) Ameumba mbingu bila ya nguzo mnazoziona. [Luqmaan (31:10)]
الْفَجْر
089-Al-Fajr
089-Al-Fajr: Utangulizi Wa Suwrah [560]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالْفَجْرِ ﴿١﴾
1. Naapa kwa Alfajiri.
وَلَيَالٍ عَشْرٍ ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa masiku kumi.[1]
وَالشَّفْعِ وَالْوَتْرِ ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa shufwa na witri.
وَاللَّيْلِ إِذَا يَسْرِ ﴿٤﴾
4. Na Naapa kwa usiku unapopita.
هَلْ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٌ لِّذِي حِجْرٍ ﴿٥﴾
5. Je, katika hayo pana haja ya kiapo kwa mwenye akili?
أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ ﴿٦﴾
6. Je, hukuona vipi Rabb wako Alivyowafanya kina ‘Aad?[2]
إِرَمَ ذَاتِ الْعِمَادِ ﴿٧﴾
7. Wa Iram[3], walio warefu na wenye nguvu (kama nguzo ndefu)?
الَّتِي لَمْ يُخْلَقْ مِثْلُهَا فِي الْبِلَادِ ﴿٨﴾
8. Ambao hawakuumbwa mfano wao katika ardhi.
وَثَمُودَ الَّذِينَ جَابُوا الصَّخْرَ بِالْوَادِ ﴿٩﴾
9. Na kina Thamuwd ambao walichonga miamba mabondeni?
وَفِرْعَوْنَ ذِي الْأَوْتَادِ ﴿١٠﴾
10. Na Firawni mwenye askari washupavu na nguvu kubwa.[4]
الَّذِينَ طَغَوْا فِي الْبِلَادِ ﴿١١﴾
11. Ambao wote hao wamevuka mipaka kuasi katika nchi.
فَأَكْثَرُوا فِيهَا الْفَسَادَ ﴿١٢﴾
12. Wakakithirisha humo ufisadi.
فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ ﴿١٣﴾
13. Rabb wako Akawamiminia mjeledi wa adhabu.
إِنَّ رَبَّكَ لَبِالْمِرْصَادِ ﴿١٤﴾
14. Hakika Rabb wako bila shaka Yu tayari Anaziona nyenendo zao zote.
فَأَمَّا الْإِنسَانُ إِذَا مَا ابْتَلَاهُ رَبُّهُ فَأَكْرَمَهُ وَنَعَّمَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَكْرَمَنِ ﴿١٥﴾
15. Basi binaadam pale Rabb wake Anapomtia mtihanini, Akamkirimu na Akamneemesha, husema: Rabb wangu Amenikirimu.
وَأَمَّا إِذَا مَا ابْتَلَاهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَهَانَنِ ﴿١٦﴾
16. Ama Anapomtia mtihanini, Akamdhikishia riziki yake, husema: Rabb wangu Amenidunisha.
كَلَّاۖ بَل لَّا تُكْرِمُونَ الْيَتِيمَ ﴿١٧﴾
17. Laa hasha! Bali hamuwakirimu mayatima.[5]
وَلَا تَحَاضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ ﴿١٨﴾
18. Na wala hamhamasishani katika kulisha maskini.[6]
وَتَأْكُلُونَ التُّرَاثَ أَكْلًا لَّمًّا ﴿١٩﴾
19. Na mnakula urithi ulaji wa kiroho bila kusaza kitu.
وَتُحِبُّونَ الْمَالَ حُبًّا جَمًّا ﴿٢٠﴾
20. Na mnapenda mali penzi kubwa la kupita kiasi.
كَلَّا إِذَا دُكَّتِ الْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا ﴿٢١﴾
21. Laa hasha! Pale ardhi itakapo vunjwavunjwa na kupondwapondwa.
وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا ﴿٢٢﴾
22. Na Atakapokuja Rabb wako pamoja na Malaika walio safusafu.[7]
وَجِيءَ يَوْمَئِذٍ بِجَهَنَّمَۚ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ وَأَنَّىٰ لَهُ الذِّكْرَىٰ ﴿٢٣﴾
23. Na italetwa siku hiyo Jahannam. Siku hiyo binaadam atakumbuka. Lakini kutamfaa nini kukumbuka huko?!
يَقُولُ يَا لَيْتَنِي قَدَّمْتُ لِحَيَاتِي ﴿٢٤﴾
24. Atasema: Ee, laiti ningelikadimisha (mazuri) kwa ajili ya uhai wangu (wa Aakhirah).
فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُ أَحَدٌ ﴿٢٥﴾
25. Basi siku hiyo hakuna yeyote atakayeadhibu kama Kuadhibu Kwake.
وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُ أَحَدٌ ﴿٢٦﴾
26. Na wala hakuna yeyote atakayefungisha (madhubuti) kama kufungisha Kwake (waovu).
يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ ﴿٢٧﴾
27. (Mwema ataambiwa): Ee nafsi iliyotua!
ارْجِعِي إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرْضِيَّةً ﴿٢٨﴾
28. Rejea kwa Rabb wako ukiwa umeridhika na mwenye kuridhiwa (na Allaah).
فَادْخُلِي فِي عِبَادِي ﴿٢٩﴾
29. Basi ingia katika kundi la Waja Wangu.
وَادْخُلِي جَنَّتِي ﴿٣٠﴾
30. Na ingia Jannah Yangu.
[1] Masiku Kumi Anayoyaapia Allaah (سبحانه وتعالى):
Baada ya kuapia kwa Alfajiri, Allaah (عزّ وجلّ) Anaapa kwa masiku kumi ambayo kwa mujibu wa rai iliyo sahihi, ni nyusiku kumi za mwezi wa Ramadhwaan na mchana wa masiku kumi ya mwanzo ya Dhul-Hijjah. Hizi ni siku ambapo matendo mengi ya ibaada hufanyika ambayo hayafanyiki nyakati nyingine. Katika kumi la mwisho la usiku wa Ramadhwaan, kunatokea Laylatul-Qadr ambao ni usiku bora kuliko miezi elfu, na siku hizo kumi ni siku za mwisho za mfungo wa Ramadhwaan ambayo ni moja ya nguzo za Uislamu.
Katika siku kumi za Dhul-Hijjah, kuna kisimamo cha ‘Arafah ambapo Allaah (عزّ وجلّ) Anawaghufuria waja, na hilo humhuzunisha mno shaytwaan. Shaytwaan haonekani kamwe kudhalilika vibaya na kushindwa zaidi kuliko Siku ya ‘Arafah anapoona Malaika wakiteremka na Rehma toka kwa Allaah kwa Waja Wake, na kwa sababu ya yale yanayotokea siku hiyo ya wingi wa matendo ya ibaadah ya Hajj na ‘Umrah. Basi hayo ni mambo matukufu mno yanayostahiki kuapiwa na Allaah. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Bonyeza viungo vifuatavye vyenye faida muhimu kuhusu masiku hayo:
Siku Kumi Bora Kabisa Za Allaah - 01 - 10 Dhul-Hijjah [561]
[2] Kina ‘Aad Kaumu Ya Nabiy Huwd (عليه السّلام):
Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye maelezo kuhusu Makafiri Wa Nyumati Za Nyuma Na Aina Za Adhabu Zao:
[3] Iram:
‘Ulamaa wametaja maana zifuatazo za Iram: (i) Imaam As-Sa’diy: Kabila maarufu la Yemen [Tafsiyr As-Sa’diy]. (ii) Mujaahid na Qataadah: Ummah wa zamani yaani ‘Aad wa kwanza. (iii) Qataadah bin Du’aamah, As-Suddiy: Iram ni nyumba ya mamlaka ya ‘Aad. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
[5] Amri Na Himizo La Kuwakirimu Yatima Na Fadhila Zake:
Miongoni mwa fadhila za kulea yatima ni kujaaliwa kuwa karibu na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Jannah kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
عن سهل بن سعد رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( أَنَا وَكَافلُ اليَتِيمِ في الجَنَّةِ هَكَذا )) وَأَشارَ بالسَّبَّابَةِ وَالوُسْطَى ، وَفَرَّجَ بَيْنَهُمَا . رواه البخاري .
Amesimulia Sahl Bin Sa’ad (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mimi na mwenye kumsimamia yatima tuko Peponi kama hivi." Akaashiria kwa kidole cha shahada na cha kati na kupambanua baina yake. [Al-Bukhaariy]
Bonyeza pia viungo vifuatavyo kupata faida nyenginezo kadhaa:
Na uharamu wa kula mali za yatima na kuwfanyia ubaya ni katika viungo vifuatavyo:
[6] Himizo La Kulisha Chakula Mafaqiri, Masikini Na Wahitaji:
Rejea Al-Insaan (76:8) kwenye faida tele. Na pia rejea Al-Qalam (68:17) kwenye kisa cha watu wa shamba waliozuia mafuqara na masikini wasipate swadaqa ya mazao ya shamba la baba yao baada ya kufariki kwake. Na pia kisa katika Hadiyth, cha mtu aliyekuwa akitoa swadaqa mazao yake, na faida nyenginezo.
[7] Malaika Watateremka Siku Ya Qiyaamah Safusafu Na Allaaha Pia Atateremka.
Rejea Al-Haaqqah (69:13-18), Al-Fajr (89:21-22), Al-Furqaan (25:25), Al-Baqarah (2:210), Al-An’aam (6:158).
الْبَلَد
090-Al-Balad
090-Al-Balad: Utangulizi Wa Suwrah [569]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
لَا أُقْسِمُ بِهَـٰذَا الْبَلَدِ ﴿١﴾
1. Naapa kwa mji huu (wa Makkah).[1]
وَأَنتَ حِلٌّ بِهَـٰذَا الْبَلَدِ ﴿٢﴾
2. Nawe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) umehalalishiwa ufanye utakavyo katika mji huu (kuua au kusamehe).
وَوَالِدٍ وَمَا وَلَدَ ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa mwenye kuzaa (Aadam) na aliowazaa (wanaadam).
لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي كَبَدٍ ﴿٤﴾
4. Kwa yakini Tumemuumba binaadam katika tabu na mashaka ya kuendelea.
أَيَحْسَبُ أَن لَّن يَقْدِرَ عَلَيْهِ أَحَدٌ ﴿٥﴾
5. Je, anadhani kwamba hakuna yeyote atakayemweza?
يَقُولُ أَهْلَكْتُ مَالًا لُّبَدًا ﴿٦﴾
6. Anasema: Nimeangamiza mali tele.
أَيَحْسَبُ أَن لَّمْ يَرَهُ أَحَدٌ ﴿٧﴾
7. Anadhani kwamba hakuna yeyote anayemuona?
أَلَمْ نَجْعَل لَّهُ عَيْنَيْنِ ﴿٨﴾
8. Je, kwani Hatukumpa macho mawili?
وَلِسَانًا وَشَفَتَيْنِ ﴿٩﴾
9. Na ulimi na midomo miwili?
وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ ﴿١٠﴾
10. Na Tukambainishia njia mbili (ya haki na upotofu)?[2]
فَلَا اقْتَحَمَ الْعَقَبَةَ ﴿١١﴾
11. Basi hakujiingiza kwa juhudi njia ya tabu na mashaka.
وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْعَقَبَةُ ﴿١٢﴾
12. Na nini kitakachokujulisha nini hiyo njia ya tabu na mashaka?
فَكُّ رَقَبَةٍ ﴿١٣﴾
13. Ni kuacha huru mtumwa.[3]
أَوْ إِطْعَامٌ فِي يَوْمٍ ذِي مَسْغَبَةٍ ﴿١٤﴾
14. Au kulisha katika siku ya ukame.[4]
يَتِيمًا ذَا مَقْرَبَةٍ ﴿١٥﴾
15. Yatima aliye jamaa wa karibu.[5]
أَوْ مِسْكِينًا ذَا مَتْرَبَةٍ ﴿١٦﴾
16. Au maskini aliye hohehahe.
ثُمَّ كَانَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ وَتَوَاصَوْا بِالْمَرْحَمَةِ ﴿١٧﴾
17. Kisha akawa miongoni mwa wale walioamini, na wakausiana kusubiri na wakausiana huruma.
أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ ﴿١٨﴾
18. Hao ndio watu wa kuliani.
وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا هُمْ أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ ﴿١٩﴾
19. Na wale waliokufuru Aayaat (na Ishara, Dalili) Zetu wao ndio watu wa kushotoni.
عَلَيْهِمْ نَارٌ مُّؤْصَدَةٌ ﴿٢٠﴾
20. Juu yao ni moto uliofungiwa kila upande.
[1] Utukufu Wa Makkah Na Fadhila Zake:
Utukufu wa Makkah na fadhila zake zmetajwa katika Aayah kadhaa. Miongoni mwa Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى) ni:
إِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِّلْعَالَمِينَ ﴿٩٦﴾
Hakika nyumba ya awali iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ‘ibaadah) ni ile ambayo iko Bakkah (Makkah), yenye barakah na mwongozo kwa walimwengu. [Aal-'Imraan (3:96)]
Na pia:
وَضَرَبَ اللَّـهُ مَثَلًا قَرْيَةً كَانَتْ آمِنَةً مُّطْمَئِنَّةً يَأْتِيهَا رِزْقُهَا رَغَدًا مِّن كُلِّ مَكَانٍ فَكَفَرَتْ بِأَنْعُمِ اللَّـهِ فَأَذَاقَهَا اللَّـهُ لِبَاسَ الْجُوعِ وَالْخَوْفِ بِمَا كَانُوا يَصْنَعُونَ﴿١١٢﴾
Na Allaah Amepiga mfano wa mji (wa Makkah) uliokuwa katika amani na utulivu, inaufikia riziki yake maridhawa kutoka kila mahali, kisha ukakufuru Neema za Allaah. Basi Allaah Akauonjesha funiko la njaa na khofu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakitenda. [An-Nahl (16:112)]
Rejea Al-An’aam (6:92) kwenye Fadhila za mji wa Makkah (Ummul-Quraa).
Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida nyenginezo:
02- Historia Fupi Ya Makkah Na Kuhusu Hajj Na 'Umrah [570]
05-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Hajj: Mlango Wa Sifa Za Hijjah Na Kuingia Makkah [571]
096-Aayah Na Mafunzo: Masjid Al-Haraam Ni Ya Kwanza Kuanzishwa Duniani [572]
[3] Fadhila Za Kuacha Huru Mtumwa:
Hadiyth ifuatayo imetaja fadhila mojawapo ambayo ni kuepushwa mtu na moto kwa kila kiungo kimoja cha mtumwa:
عَنْ أَبِي، هُرَيْرَةَ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " مَنْ أَعْتَقَ رَقَبَةً مُؤْمِنَةً أَعْتَقَ اللَّهُ بِكُلِّ إِرْبٍ مِنْهَا إِرْبًا مِنْهُ مِنَ النَّارِ "
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Yeyote atakayemwacha huru mtumwa Muislamu, Allaah Atakiokoa na moto kila kiungo chake sambamba na kila kiungo cha mtumwa.” [Muslim]
Bonyeza pia viungo vifuatavyo kupata faida tele nyenginezo:
15-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Ukombozi - كِتَابُ اَلْعِتْقِ [574]
[4] Himizo La Kulisha Mafaqiri, Masikini Na Wahitaji:
Rejea Al-Insaan (76:8) kwenye faida tele. Na pia rejea Al-Qalam (68:17) kwenye kisa cha watu wa shamba waliozuia mafuqara na masikini wasipate swadaqa ya mazao ya shamba la baba yao baada ya kufariki kwake. Na pia kisa katika Hadiyth, cha mtu aliyekuwa akitoa swadaqa mazao yake, na faida nyenginezo.
[5] Himizo La Kulea Yatima Na Fadhila Zake Na Maonyo Ya Kula Mali Zao:
Kumlea, kumkirimu na kumfanyia ihsaan yatima kuna fadhila tele. Na yatima aliye na uhusiano wa damu kuna fadhila mara mbili kama alivyotafsiri Imaam Ibn Kathiyr kwa kutaja Hadiyth ifuatayo:
عن سلمان بن عامر رضي الله عَنْهُ ، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم: (( الصَّدَقَةُ عَلَى المِسكينِ صَدَقةٌ ، وعَلَى ذِي الرَّحِمِ ثِنْتَانِ : صَدَقَةٌ وَصِلَةٌ )) رواه الترمذي ، وَقالَ : (( حديث حسن )) .
Amesimulia Salmaan bin 'Aamir (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Swadaqa kwa maskini ni swadaqa, na kumpa jamaa ina ujira mara mbili: Ni swadaqa na kuunga ujamaa." [At-Tirmidhiy, na akasema Hadiyth Hasan]
Rejea Al-Fajr (89:17) kwenye maelezo na faida kuhusu Amri Na Himizo La Kuwakirimu Yatima Na Fadhila Zake.
الشَّمْس
091-Ash-Shams
091-Ash-Shams: Utangulizi Wa Suwrah [577]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا ﴿١﴾
1. Naapa kwa jua na mwangaza wake.
وَالْقَمَرِ إِذَا تَلَاهَا ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa mwezi unapoliandama (jua).
وَالنَّهَارِ إِذَا جَلَّاهَا ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa mchana unapolidhihirisha.
وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَاهَا ﴿٤﴾
4. Na Naapa kwa usiku unapolifunika.
وَالسَّمَاءِ وَمَا بَنَاهَا ﴿٥﴾
5. Na Naapa kwa mbingu na Aliyezijenga.
وَالْأَرْضِ وَمَا طَحَاهَا ﴿٦﴾
6. Na Naapa kwa ardhi na Aliyeitandaza.
وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّاهَا ﴿٧﴾
7. Na Naapa kwa nafsi na Aliyeiumba Akainyoosha sawa.
فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا ﴿٨﴾
8. Kisha Akaitambulisha uovu wake na taqwa yake.[1]
قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا ﴿٩﴾
9. Kwa yakini amefaulu yule aliyeitakasa.[2]
وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّاهَا ﴿١٠﴾
10. Na kwa yakini amepita patupu aliyeifisidi.[3]
كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَاهَا ﴿١١﴾
11. Kina Thamuwd walikadhibisha (Rasuli wao) kwa upindukaji mipaka ya kuasi kwao.[4]
إِذِ انبَعَثَ أَشْقَاهَا ﴿١٢﴾
12. Pale alipochomoka haraka muovu wao mkuu.
فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّـهِ نَاقَةَ اللَّـهِ وَسُقْيَاهَا ﴿١٣﴾
13. Rasuli wa Allaah (Swaalih عليه السلام) akawaambia: (Tahadharini msije kumdhuru) Ngamia jike wa Allaah, na kuingilia zamu yake ya kunywa.
فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُم بِذَنبِهِمْ فَسَوَّاهَا ﴿١٤﴾
14. Lakini walimkadhibisha na wakamuua. Basi Rabb wao Akawaangamiza kwa sababu ya dhambi zao, na Akayafanya mateketezi yao sawasawa kwa wote.
وَلَا يَخَافُ عُقْبَاهَا ﴿١٥﴾
15. Na wala (Allaah) Hakhofu matokeo yake.
[1] Mwanaadam Ana Uhuru Wa Kuinusuru Nafsi Yake Au Kuiangamiza:
Hadiyth ifuatayo inataja kuwa ni chaguo la binaadam kuichunga nafsi yake akasalimika au kuiharibu akaangamia.
عن أبي مالكٍ الحارِثِ بنِ عاصِمٍ الأَشْعَرِيِّ رضي اللهُ عنهُ قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: ((الطُّهُورُ شَطْرُ الإِيَمانِ، والحمدُ لِلهِ تَمْلأُ الْمِيزَانَ، وسُبْحانَ اللهِ والحمدُ لِلهِ تَمْلآنِ - أو تَمْلأُ - ما بَيْنَ السَّمآءِ والأرضِ، والصَّلاةُ نورٌ، والصَّدَقَةُ بُرْهانٌ، والصَّبْرُ ضِيَاءٌ، والْقُرآنُ حُجَّةٌ لَكَ أو عَلَيْكَ، كُلُّ النَّاسِ يَغْدو، فَبائعٌ نَفْسَهُ، فَمُعْتِقُها أَو مُوبِقُها)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Amesimulia Abuu Maalik Al-Haarith bin ‘Aaswim Al-Ash’ariyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Twahaara ni nusu ya imaan, na AlhamduliLLaah inajaza mizani, na Subhaana-Allaah wal-HamduliLLaah inajaza baina ya mbingu na ardhi. Na Swalaah ni nuru, na swadaqa ni burhani, na subira ni mwangaza, na Qur-aan ni hoja kwako au dhidi yako. Kila mtu anaianza siku yake akiichuuza nafsi yake, aidha huiokoa ikasalimika au akaiangamiza.” [Muslim]
Rejea Al-Insaan (76:3).
Rejea pia Aayah namba (9) ya Suwrah hii kwenye faida nyenginezo.
[2] Kuichunga Nafsi, Kuitakasa Na Kujaaliwa Taqwa Na Duaa Zake:
Bonyeza viungo vifuatavyo:
Mahitajio Ya Nafsi: Kuomba Maghfirah Na Kutubia Kwa Allaah (سبحانه وتعالى) [578]
Asili Ya Roho Zetu [579]
Faida Ya Taqwa (Uchaji Allaah) [446]
Na pia bonyeza viungo vifuatavyo kupata duaa za kuomba kuitakasa nafsi na kuomba kujaaliwa taqwa:
041-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Taqwa Ya Nafsi Na Kuitakasa [580]
021-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kuomba Hidaaya, Taqwa, Sitaha Na Kutosheka [581]
[4] Kina Thamuwd Kaumu Ya Nabiy Swaalih (عليه السّلام):
Kina Thamuwd ni watu wa Al-Hijr ambayo ni maeneo yapo baina ya Sham na Hijaaz. Kina Thamuwd hawa walipinga daawah ya Rasuli wao Nabiy Swaalih (عليه السّلام) juu ya kutaka muujiza wa kuteremshiwa ngamia jike. Walipoitikiwa matakwa yao, walimuua ngamia wa Allaah.
Rejea Al-‘Ankabuwt (29:40) kwenye maelezo kuhusu Makafiri Wa Nyumati Za Nyuma Na Aina Za Adhabu Zao.
اللَّيْل
092-Al-Layl
092-Al-Layl: Utangulizi Wa Suwrah [589]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰ ﴿١﴾
1. Naapa kwa usiku unapofunika.
وَالنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa mchana unapodhihirika mwanga wake.
وَمَا خَلَقَ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa Aliyeumba dume na jike.
إِنَّ سَعْيَكُمْ لَشَتَّىٰ ﴿٤﴾
4. Hakika juhudi zenu bila shaka ni tofauti tofauti.
فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ ﴿٥﴾
5. Basi yule anayetoa (mali) na akamcha Allaah.
وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٦﴾
6. Na akasadikisha Al-Husnaa.[1] (Jazaa na Kalimah ya laa ilaaha illa Allaah).
فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ ﴿٧﴾
7. Basi Tutamuwepesishia kwa yaliyo mepesi.[2]
وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ ﴿٨﴾
8. Ama yule afanyaye ubakhili na akajiona amejitosheleza.
وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ ﴿٩﴾
9. Na akakadhibisha Al-Husnaa[3] (Jazaa na Kalimah ya laa ilaaha illa Allaah).
فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ ﴿١٠﴾
10. Basi Tutamuwepesishia kwa yaliyo magumu.[4]
وَمَا يُغْنِي عَنْهُ مَالُهُ إِذَا تَرَدَّىٰ ﴿١١﴾
11. Na itamsaidia nini mali yake atakapoporomoka kuangamia (motoni)?!
إِنَّ عَلَيْنَا لَلْـهُدَىٰ ﴿١٢﴾
12. Hakika ni juu Yetu (kubainisha) mwongozo.
وَإِنَّ لَنَا لَلْآخِرَةَ وَالْأُولَىٰ ﴿١٣﴾
13. Na hakika ni Yetu Sisi Aakhirah na awali (dunia).
فَأَنذَرْتُكُمْ نَارًا تَلَظَّىٰ ﴿١٤﴾
14. Basi Nimekutahadharisheni moto wenye mwako mkali mno.
لَا يَصْلَاهَا إِلَّا الْأَشْقَى ﴿١٥﴾
15. Hatouingia kuungua isipokuwa muovu mkubwa.
الَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٦﴾
16. Ambaye amekadhibisha na akakengeuka mbali.
وَسَيُجَنَّبُهَا الْأَتْقَى ﴿١٧﴾
17. Na ataepushwa nao mwenye taqwa imara zaidi.
الَّذِي يُؤْتِي مَالَهُ يَتَزَكَّىٰ ﴿١٨﴾
18. Ambaye anatoa mali yake kujitakasa.
وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَىٰ ﴿١٩﴾
19. Na hali hakuna mmoja yeyote aliyemfanyia fadhila yoyote hata amlipe.[5]
إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ رَبِّهِ الْأَعْلَىٰ ﴿٢٠﴾
20. Isipokuwa kutaka Wajihi wa Rabb wake Mwenye ‘Uluwa Aliyetukuka kabisa kuliko vyote.[6]
وَلَسَوْفَ يَرْضَىٰ ﴿٢١﴾
21. Na bila shaka atakuja kuridhika.
[1] Kusadikisha Al-Husnaa:
Kauli za ‘Ulamaa:
Tafsiyr Al-Muyassar:
Akaamini Laa ilaaha illa-Allaah, maana ya neno hili na malipo yanayotarajiwa, basi Tutamwongoza, Tutamwezesha na Tutamrahisishia kuzifikia nyenzo za kheri na utengefu.
Imaam As-Sa’diy (رحمه الله):
Akaamini Laa ilaaha illa-Allaah, maana yake ikiwa ni pamoja na yote ya Dini anayopaswa kuyaamini, na malipo ya Aakhirah yanayotarajiwa kutokana na neno hilo.
Imaam Ibn Kathiyr (رحمه الله):
(i) Jazaa (ii)Thawabu (iii) Badali (iii) La ilaaha illa-Allaah (iv) Aliyoneemeshwa na Allaah (v) Swalaah, Zakaat, Swawm, Swadaqa ya Fitwr.
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله):
Akaamini maneno bora kabisa ambayo ni maneno ya Allaah (عزّ وجلّ) na kauli ya Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa sababu maneno ya kweli na yaliyo bora kabisa ni Maneno ya Allaah (عزّ وجلّ).
[2] Kufanyiwa Yaliyo Mepesi:
Tunamfanyia mambo yake mepesi, na Tunamwepesishia kila jambo jema, na Tunamrahisishia kuacha maovu yote, kwa sababu amechukua hatua zinazopelekea hilo, basi Allaah (عزّ وجلّ) Atafanya wepesi hilo kwa ajili yake. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[3] Kukadhibisha Al-Husnaa:
Kauli za ‘Ulamaa:
Tafsiyr Al-Muyassar:
Akakanusha neno la Laa ilaaha illa-Allaah, maana yake na malipo yanayotarajiwa kutokana nalo.
Imaam As-Sa’diy (رحمه الله):
Ambayo Allaah (عزّ وجلّ) Amewajibisha Waja Wake kuyaamini ya ‘Aqiydah sahihi.
Imaam Ibn Kathiyr (رحمه الله):
Jazaa ya makazi ya Aakhirah.
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله): Kauli za Allaah (عزّ وجلّ) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم)
[4] Kuwepesishiwa Magumu:
Atatekeleza yaliyo na sifa mbaya ya kulaumiwa na atafanyiwa wepesi kutenda maovu na maasi popote alipo. Tunamuomba Allaah Al-‘Aafiyah. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[5] Kutoa Mali Kwa Ajili Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Bila Kutarajia Sifa, Fadhila Au Malipo Kwa Watu:
Aayah hii amekusudiwa Abu Bakr (رضي الله عنه) [Tafsiyr As-Sa’diy] na wengineo.
Kwa sababu Abu Bakr (رضي الله عنه) hakutaraji malipo au fadhila kutoka kwa watu bali alitaraji Radhi za Allaah Pekee. Na miongoni mwa aliyoyatenda Abu Bakr (رضي الله عنه) ni kuwakomboa Waislamu waliokandamizwa na kuadhibiwa na makafiri Quraysh wa Makkah katika mwanzo wa Uislamu. Kati ya watumwa hao aliowakomboa ni Swahaba mtukufu Bilaal bin Rabaah (رضي الله عنه) ambaye alikuwa Muadhini wa Waislamu. Hali kadhalika walikombolewa watumwa wanawake na wala hakujali kiasi cha mali alichokitoa na wala hakutaraji kusifiwa na watu wala malipo yao isipokuwa kutaka Radhi za Allaah. Rejea pia An-Nuwr (24:22) kwenye maelezo yake alipoendelea kumpa swadaqa jamaa yake Mistwah Bin Uthaathah, juu ya kuwa aliudhika naye, lakini alitii amri ya Allaah (عزّ وجلّ) ya kutaraji kughufuriwa madhambi yake.
[6] Al-A’laa:
Mwenye ‘Uluwa, Ametukuka, Ana Uadhama Kuliko wote kuliko vyote, Yuko juu Kabisa juu ya viumbe Vyake vyote.
الضُّحى
093-Adhw-Dhwuhaa
093-Adhw-Dhwuhaa: Utangulizi Wa Suwrah [591]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالضُّحَىٰ ﴿١﴾
1. Naapa kwa dhuha (jua linapopanda).[1]
وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa usiku unapotanda kiza na kutulia.
مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ ﴿٣﴾
3. Rabb wako Hakukutelekeza na wala Hakukuchukia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).[2]
وَلَلْآخِرَةُ خَيْرٌ لَّكَ مِنَ الْأُولَىٰ ﴿٤﴾
4. Na bila shaka Aakhirah ni kheri zaidi kwako kuliko ya awali (dunia).
وَلَسَوْفَ يُعْطِيكَ رَبُّكَ فَتَرْضَىٰ ﴿٥﴾
5. Na bila shaka Rabb wako Atakupa na utaridhika.
أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَآوَىٰ ﴿٦﴾
6. Je, kwani Hakukukuta yatima, Akakupa makazi?
وَوَجَدَكَ ضَالًّا فَهَدَىٰ ﴿٧﴾
7. Na Akakukuta hujui lolote (kuhusu Kitabu wala Iymaan), kisha Akakuongoza?
وَوَجَدَكَ عَائِلًا فَأَغْنَىٰ ﴿٨﴾
8. Na Akakukuta mhitaji, Akakutosheleza?
فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ ﴿٩﴾
9. Kwa hivyo basi yatima usimuonee.
وَأَمَّا السَّائِلَ فَلَا تَنْهَرْ ﴿١٠﴾
10. Na ama mwombaji, basi usimkaripie.
وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ ﴿١١﴾
11. Na ama Neema ya Rabb wako, basi ihadithie.[3]
[3] Kutambua Na Kushukuru Neema Za Allaah (سبحانه وتعالى):
Zinajumuisha neema za Dini na za kidunia. Elezea yaani, mhimidi na msifie Allaah kwazo kwa kuzitaja makhsusi ikiwa kuna faida kufanya hivyo. Vinginevyo, elezea Neema za Allaah kwa ujumla, kwani kwa kuzielezea huko, kunamfanya mtu kuendelea kushukuru zaidi, lakini pia kunazisukuma nyoyo kumpenda zaidi Allaah Mneemeshaji, kwani kawaida ya maumbile ya nyoyo za binaadam ni kumpenda yule anayezifadhili na kuzitendea wema. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Na hakika Neema za Allaah (سبحانه وتعالى) ni nyingi mno wala hawezi mtu kuzitafakari zote na kuzihesabu kama Anavosema:
وَآتَاكُم مِّن كُلِّ مَا سَأَلْتُمُوهُ ۚ وَإِن تَعُدُّوا نِعْمَتَ اللَّـهِ لَا تُحْصُوهَا ۗ ﴿٣٤﴾
Na Akakupeni kila mlichomuomba. Na mkihesabu Neema za Allaah hamtoweza kuziorodhesha hesabuni. [Ibraahiym (14:34)]
Rejea Suwrah hiyo ya Ibraahiym (14:34) kwenye uchambuzi wa Neema za Allaah za mbinguni, ardhini, nafsini na kadhaalika pamoja na faida nyenginezo na rejea mbalimbali.
Na bonyeza viungo vifuatavyo kupata duaa za kukiri na kushukuru Neema za Allaah (عزّ وجلّ), kuomba kutokutoweka neema hizo na kuomba kuzidishiwa:
الشَّرْح
094-Ash-Sharh
094-Ash-Sharh: Utangulizi Wa Suwrah [598]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
أَلَمْ نَشْرَحْ لَكَ صَدْرَكَ ﴿١﴾
1. Je, kwani Hatukukunjulia kifua chako kukubainishia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)?[1]
وَوَضَعْنَا عَنكَ وِزْرَكَ ﴿٢﴾
2. Na Tukakuondolea mzigo wako (wa dhambi)?[2]
الَّذِي أَنقَضَ ظَهْرَكَ ﴿٣﴾
3. Ambao ulielemea mgongo wako?
وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ ﴿٤﴾
4. Na Tukakutukuzia kutajwa kwako?[3]
فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا ﴿٥﴾
5. Basi hakika pamoja na kila ugumu kuna wepesi.[4]
إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا ﴿٦﴾
6. Hakika pamoja na kila ugumu kuna wepesi.
فَإِذَا فَرَغْتَ فَانصَبْ ﴿٧﴾
7. Basi utakapopata faragha fanya juhudi katika ibaada.
وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَارْغَب ﴿٨﴾
8. Na kwa ajili ya Rabb wako, ongeza utashi zaidi (wa ibaada).
[1] Kisa Cha Kupasuliwa Kifua Chake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alibaki katika kijiji cha Bani Sa’ad mpaka alipotimia umri wa miaka mine au mitano wakati kilipotokea kisa cha kupasuliwa kifua. Hadiyth ifuatayo inaelezea:
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَتَاهُ جِبْرِيلُ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يَلْعَبُ مَعَ الْغِلْمَانِ فَأَخَذَهُ فَصَرَعَهُ فَشَقَّ عَنْ قَلْبِهِ فَاسْتَخْرَجَ الْقَلْبَ فَاسْتَخْرَجَ مِنْهُ عَلَقَةً فَقَالَ هَذَا حَظُّ الشَّيْطَانِ مِنْكَ . ثُمَّ غَسَلَهُ فِي طَسْتٍ مِنْ ذَهَبٍ بِمَاءِ زَمْزَمَ ثُمَّ لأَمَهُ ثُمَّ أَعَادَهُ فِي مَكَانِهِ وَجَاءَ الْغِلْمَانُ يَسْعَوْنَ إِلَى أُمِّهِ - يَعْنِي ظِئْرَهُ - فَقَالُوا إِنَّ مُحَمَّدًا قَدْ قُتِلَ . فَاسْتَقْبَلُوهُ وَهُوَ مُنْتَقَعُ اللَّوْنِ . قَالَ أَنَسٌ وَقَدْ كُنْتُ أَرَى أَثَرَ ذَلِكَ الْمِخْيَطِ فِي صَدْرِهِ .
Amesimulia Anas Bin Maalik (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa akicheza na watoto wenzake alijiwa na Jibriyl (عليه السّلام), akamchukua na kumlaza chini, kisha akampasua kifua chake na kuutoa nje moyo wake na kutoa kutoka ndani ya moyo huo kipande cha damu iliyoganda. Akamwambia: Hii ni sehemu ya shaytwaan kwako. Kisha akauosha kwa maji ya Zamzam yaliyokuwemo ndani ya chombo cha dhahabu, akauunganisha, kisha akaurudisha moyo mahali pake. Watoto waliokuwa wakicheza pamoja naye walikimbia mpaka nyumbani kwa mnyonyeshaji wake Bibi Haliymah (رضي الله عنها) wakamwambia: “Muhammad kesha uliwa!” Walipomrudia walimkuta amekaa, mzima hana chochote isipokuwa rangi ya uso wake ilikuwa imebadilika na kugeuka nyeupe.” [Muslim]
[2] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kufutiwa Madhambi Yake:
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
لِّيَغْفِرَ لَكَ اللَّـهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ
Ili Allaah Akughufurie yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayofuatia. [Al-Fat-h (48:2)]
Bonyeza pia kiungo kifuatacho:
Lakini juu ya hivyo, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiomba maghfirah kwa Allaah (سبحانه وتعالى) zaidi ya mara sabiini kila siku kama ilivyothibiti yeye kusema hivyo katika Hadiyth ifuatayo:
عن أبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه : سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ : ((وَاللَّهِ إِنِّي لاَسْتَغْفِرُ اللَّهَ وَأَتُوبُ إِلَيْهِ فِي الْيَوْمِ أَكْثَرَ مِنْ سَبْعِينَ مَرَّةً)) رواه البخاري (6307)
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Wa-Allaahi mimi naomba maghfirah kwa Allaah na kutubia Kwake zaidi ya mara sabiini kwa siku.” [Al-Bukhaariy]
[3] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Anatajwa Kila Mara:
Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida:
32-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hatajwi Ila Anaswaliwa (Anaombewa Rahmah Na Amani) [601]
33-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ana Ujira Usiokatika Anasifika Na Maarufu Mno [467]
Rejea pia Al-Qalam (68:3).
[4] Katika Kila Gumu Allaah Anajalia Wepesi:
Kauli yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kumwambia ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما) katika Hadiyth ifuatayo:
((احْفَظِ الله تَجِدْهُ أَمَامَكَ، تَعرَّفْ إِلَى اللهِ في الرَّخَاءِ يَعْرِفكَ في الشِّدَّةِ، وَاعْلَمْ: أنَّ مَا أَخْطَأكَ لَمْ يَكُنْ لِيُصِيبكَ، وَمَا أصَابَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُخْطِئَكَ، وَاعْلَمْ: أنَّ النَّصْرَ مَعَ الصَّبْرِ، وَأَنَّ الفَرَجَ مَعَ الكَرْبِ، وَأَنَّ مَعَ العُسْرِ يُسْرًا))
“Mhifadhi Allaah utamkuta Yupo mbele yako. Mjue Allaah katika raha Naye Atakujua katika shida. Ujue kuwa, lililokukosa halikuwa ni lenye kukupata, na lililokusibu halikuwa ni lenye kukukosa. Ujue kuwa nusura ipo pamoja na subira, faraja ipo pamoja na dhiki, na kwenye uzito kuna wepesi.” [At-Tirmidhiy]
التِّين
095-At-Tiyn
095-At-Tiyn: Utangulizi Wa Suwrah [603]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ ﴿١﴾
1. Naapa kwa tini na zaytuni.[1]
وَطُورِ سِينِينَ ﴿٢﴾
2. Na Naapa kwa Mlima wa Sinai.
وَهَـٰذَا الْبَلَدِ الْأَمِينِ ﴿٣﴾
3. Na Naapa kwa mji huu wa amani (Makkah).[2]
لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ ﴿٤﴾
4. Kwa yakini Tumemuumba binaadam katika umbile bora kabisa.[3]
ثُمَّ رَدَدْنَاهُ أَسْفَلَ سَافِلِينَ ﴿٥﴾
5. Kisha Tukamrudisha chini kabisa (motoni) ya walio chini.
إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَلَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ ﴿٦﴾
6. Isipokuwa wale walioamini na wakatenda mema; hao watapata ujira usiokatika.
فَمَا يُكَذِّبُكَ بَعْدُ بِالدِّينِ ﴿٧﴾
7. Basi lipi baada ya yote hayo linakufanya ukadhibishe (Siku ya) malipo?!
أَلَيْسَ اللَّـهُ بِأَحْكَمِ الْحَاكِمِينَ ﴿٨﴾
8. Je, kwani Allaah Si Mwadilifu zaidi kuliko mahakimu wote?
[1] Allaah Anaapia Tiyn Na Zaytuni:
Allaah (عزّ وجلّ) Anaapia miti miwili hiyo kutokana na manufaa yake mengi pamoja na matunda yake, na pia kutokana na kuwa ndio kilimo kikuu kinachoongoza katika ardhi ya Sham mahali pa Nabiy ‘Iysaa mwana wa Maryam (عليه السّلام). [Tafsiyr As-Sa’diy]
[2] Utukufu Wa Makkah Na Fadhila Zake:
Rejea Al-Balad (90:1) na Al-An’aam (6:92) kwenye faida kuhusu utukufu wa Makkah na Fadhila zake.
[3] Binaadam Ameumbwa Katika Umbo Bora Kabisa:
Rejea Al-Infitwaar (82:7-8) kwenye faida na Rejea mbalimbali.
الْعَلَق
096-Al-‘Alaq
096-Al-‘Alaq: Utangulizi Wa Suwrah [605]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾
1. Soma kwa Jina la Rabb wako Aliyeumba.[1]
خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾
2. Amemuumba binaadam kutokana na pande la damu linaloning’inia.
اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾
3. Soma. Kwani Rabb wako Ni Mkarimu kushinda wote.
الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾
4. Ambaye Amefunza kwa kalamu.
عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥﴾
5. Amemfunza binaadamu asiyoyajua.
كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ ﴿٦﴾
6. Laa hasha! Hakika binaadamu bila shaka hupindukia mipaka kuasi.[2]
أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ ﴿٧﴾
7. Anapojiona kuwa amejitosheleza.
إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الرُّجْعَىٰ ﴿٨﴾
8. Hakika kwa Rabb wako ndio marejeo.
أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَىٰ ﴿٩﴾
9. Je, umemuona yule anayemkataza?
عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰ ﴿١٠﴾
10. Mja pale anaposwali?
أَرَأَيْتَ إِن كَانَ عَلَى الْهُدَىٰ ﴿١١﴾
11. Je umeona, ikiwa (huyu mwovu) atafuata uongofu.
أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَىٰ ﴿١٢﴾
12. Au akalingania taqwa (si ingelikuwa bora zaidi kwake?)
أَرَأَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٣﴾
13. Je umeona, kama ataendelea kukadhibisha na kukengeuka (si ataishilia pabaya?
أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ اللَّـهَ يَرَىٰ ﴿١٤﴾
14. Je, hajui kwamba hakika Allaah Anaona?
كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ ﴿١٥﴾
15. Laa hasha! Asipoacha, bila shaka Tutamburuta kwa shungi la nywele.
نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ ﴿١٦﴾
16. Shungi la uwongo, lenye hatia.
فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ ﴿١٧﴾
17. Basi na aite timu yake.
سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ ﴿١٨﴾
18. Nasi Tutawaita Az-Zabaaniyah (Malaika wa adhabu).[3]
كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب ۩﴿١٩﴾
19. Laa hasha! Usimtii. Na sujudu na kurubia (kwa Allaah).
[1] Mwanzo Kabisa Wa Wahy Kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
Aayah namba (1) hadi namba (5) ni za mwanzo kabisa kuteremshiwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Wahy. Hadiyth ifuatayo inaelezea tukio hilo alipokuwa katika pango la Hiraa akitafakari Uumbaji wa Allaah:
عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ، أَنَّهَا قَالَتْ أَوَّلُ مَا بُدِئَ بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مِنَ الْوَحْىِ الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ فِي النَّوْمِ، فَكَانَ لاَ يَرَى رُؤْيَا إِلاَّ جَاءَتْ مِثْلَ فَلَقِ الصُّبْحِ، ثُمَّ حُبِّبَ إِلَيْهِ الْخَلاَءُ، وَكَانَ يَخْلُو بِغَارِ حِرَاءٍ فَيَتَحَنَّثُ فِيهِ ـ وَهُوَ التَّعَبُّدُ اللَّيَالِيَ ذَوَاتِ الْعَدَدِ قَبْلَ أَنْ يَنْزِعَ إِلَى أَهْلِهِ، وَيَتَزَوَّدُ لِذَلِكَ، ثُمَّ يَرْجِعُ إِلَى خَدِيجَةَ، فَيَتَزَوَّدُ لِمِثْلِهَا، حَتَّى جَاءَهُ الْحَقُّ وَهُوَ فِي غَارِ حِرَاءٍ، فَجَاءَهُ الْمَلَكُ فَقَالَ اقْرَأْ. قَالَ " مَا أَنَا بِقَارِئٍ ". قَالَ " فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الْجَهْدَ، ثُمَّ أَرْسَلَنِي فَقَالَ اقْرَأْ. قُلْتُ مَا أَنَا بِقَارِئٍ. فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّانِيَةَ حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الْجَهْدَ، ثُمَّ أَرْسَلَنِي فَقَالَ اقْرَأْ. فَقُلْتُ مَا أَنَا بِقَارِئٍ. فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّالِثَةَ، ثُمَّ أَرْسَلَنِي فَقَالَ {اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ * خَلَقَ الإِنْسَانَ مِنْ عَلَقٍ * اقْرَأْ وَرَبُّكَ الأَكْرَمُ} ". فَرَجَعَ بِهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَرْجُفُ فُؤَادُهُ، فَدَخَلَ عَلَى خَدِيجَةَ بِنْتِ خُوَيْلِدٍ رضى الله عنها فَقَالَ " زَمِّلُونِي زَمِّلُونِي ". فَزَمَّلُوهُ حَتَّى ذَهَبَ عَنْهُ الرَّوْعُ، فَقَالَ لِخَدِيجَةَ وَأَخْبَرَهَا الْخَبَرَ " لَقَدْ خَشِيتُ عَلَى نَفْسِي ". فَقَالَتْ خَدِيجَةُ كَلاَّ وَاللَّهِ مَا يُخْزِيكَ اللَّهُ أَبَدًا، إِنَّكَ لَتَصِلُ الرَّحِمَ، وَتَحْمِلُ الْكَلَّ، وَتَكْسِبُ الْمَعْدُومَ، وَتَقْرِي الضَّيْفَ، وَتُعِينُ عَلَى نَوَائِبِ الْحَقِّ. فَانْطَلَقَتْ بِهِ خَدِيجَةُ حَتَّى أَتَتْ بِهِ وَرَقَةَ بْنَ نَوْفَلِ بْنِ أَسَدِ بْنِ عَبْدِ الْعُزَّى ابْنَ عَمِّ خَدِيجَةَ ـ وَكَانَ امْرَأً تَنَصَّرَ فِي الْجَاهِلِيَّةِ، وَكَانَ يَكْتُبُ الْكِتَابَ الْعِبْرَانِيَّ، فَيَكْتُبُ مِنَ الإِنْجِيلِ بِالْعِبْرَانِيَّةِ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكْتُبَ، وَكَانَ شَيْخًا كَبِيرًا قَدْ عَمِيَ فَقَالَتْ لَهُ خَدِيجَةُ يَا ابْنَ عَمِّ اسْمَعْ مِنَ ابْنِ أَخِيكَ. فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ يَا ابْنَ أَخِي مَاذَا تَرَى فَأَخْبَرَهُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم خَبَرَ مَا رَأَى. فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ هَذَا النَّامُوسُ الَّذِي نَزَّلَ اللَّهُ عَلَى مُوسَى صلى الله عليه وسلم يَا لَيْتَنِي فِيهَا جَذَعًا، لَيْتَنِي أَكُونُ حَيًّا إِذْ يُخْرِجُكَ قَوْمُكَ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " أَوَمُخْرِجِيَّ هُمْ ". قَالَ نَعَمْ، لَمْ يَأْتِ رَجُلٌ قَطُّ بِمِثْلِ مَا جِئْتَ بِهِ إِلاَّ عُودِيَ، وَإِنْ يُدْرِكْنِي يَوْمُكَ أَنْصُرْكَ نَصْرًا مُؤَزَّرًا. ثُمَّ لَمْ يَنْشَبْ وَرَقَةُ أَنْ تُوُفِّيَ وَفَتَرَ الْوَحْىُ.
Amesimulia ‘Aaishah Mama wa Waumini: Wahyi kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ulianza kwa njozi njema usingizini, na alikuwa haoni njozi isipokuwa ni kweli kama ulivyo mwanga wa mchana. Kisha alipendezeshwa kujitenga, na alikuwa akijitenga ndani ya pango la Hiraa akimwabudu (Allaah Pekee) mfululizo kwa siku nyingi kabla ya kwenda kwa familia yake kuchukua mahitajio ya kuweza kurudi tena huko na kisha alirejea kwa (mkewe) Khadiyjah (رضي الله عنها) kuchukua chakula tena mpaka ukweli ulipomjia akiwa ndani ya pango la Hiraa. Malaika alimjia na alimtaka asome. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Akajibu: “Mimi sio msomaji.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaendelea kusema: “Malaika akanishika kwa nguvu na akaniminya kwa nguvu mpaka nikapata tabu. Kisha aliniachia, na tena akanitaka nisome na nikamjibu: Mimi si msomaji. Akaniminya vile vile. Baada ya hapo akanishika tena akaniminya kwa mara ya tatu mpaka nikapata taabu. Kisha akaniachia akasema:
اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾
Soma kwa Jina la Rabb wako Aliyeumba. Amemuumba binaadam kutokana na pande la damu linaloning’inia. Soma na Rabb wako ni Mkarimu kushinda wote. [Al-‘Alaq (96:1-3)]
Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alirejea na Wahy, na huku moyo ukidunda kwa nguvu. Kisha alikwenda kwa Khadiyjah bint Khuwaylid (رضي الله عنها) akasema, “Nifunikeni! Nifunikeni” Wakamfunika mpaka hofu ikatoweka, kisha akamueleza kila kitu kilichojiri akasema, “Naogopa nafsi yangu, kuna kitu (kibaya) kinaweza kunitokea.” “Khadiyjah (رضي الله عنها) akajibu, “Hapana kamwe! Wa-Allaahi, Allaah Hatokudhalilisha. Wewe una mahusiano mazuri na ndugu na marafiki, na unawasaidia masikini na mafukara, unawakirimu wageni wako na unawasaidia waliofikwa na majanga.” Kisha Khadiyjah (رضي الله عنها) alifuatana naye kwa binami yake, Waraqah bin Nawfal bin Asad bin Abdil-‘Uzzah, ambaye wakati wa Jahiliyya (kabla ya Uislam) alikuwa Mkristo na alikuwa akiandika kwa hati za Hebrew. Aliandika kutoka Injiyl kwa Hebrew kiasi alichowezeshwa na Allaah. Alikuwa mzee na alipoteza uoni (kipofu). Khadiyjah (رضي الله عنها) alimwambia Waraqah: “Sikiliza Hadithi (kisa) ya mpwa wako. Ee binami yangu!” “Waraqah akauliza, “Ee mpwa wangu! Umeona nini?” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alielezea yote aliyoyaona. Waraqah akasema, “Huyu ni yule yule anayehifadhi siri (Malaika Jibriyl) ambaye Allaah alimpeleka kwa Muwsaa. Natamani ningekuwa kijana, na niishi mpaka pale watu wako watakapokufukuza.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuuliza, “Je, Watanifukuza?” Waraqah akasema, “Mtu yeyote aliyeleta kitu kama ulicholeta alikabiliwa na misukosuko; na kama nitaikuta siku utakayofanyiwa uadui nitakuhami kwa nguvu zote.” Lakini baada ya siku chache Waraqah alifariki dunia na Wahyi ulisita kwa muda. [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Wahy (1)]
[2] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
096-Asbaabun-Nuzuwl: Al-'Alaq Aayah 06-19: كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ [606]
[3] Malaika Wa Adhabu Wangemkamata Abu Jahl Kama Angelimzuia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kuswali Kwenye Ka’bah:
عَنْ عِكْرِمَةَ، قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ قَالَ أَبُو جَهْلٍ لَئِنْ رَأَيْتُ مُحَمَّدًا يُصَلِّي عِنْدَ الْكَعْبَةِ لأَطَأَنَّ عَلَى عُنُقِهِ. فَبَلَغَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ " لَوْ فَعَلَهُ لأَخَذَتْهُ الْمَلاَئِكَةُ
Amesimulia ‘Ikrimah (رضي الله عنه): Abu Jahl alisema: Naapa, lau nitamuona Muhammad akiswali kwenye Al-Ka‘bah, nitamkanyanga shingo yake. Pindi khabari hiyo ilipomfikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: “Lau atafanya hivyo, Malaika watamkamata.” [Al-Bukhaariy Kitabu cha Tafsiyr (65)]
الْقَدْر
097-Al-Qadr
097-Al-Qadr: Utangulizi Wa Suwrah [608]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ ﴿١﴾
1. Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan katika Laylatul-Qadr (Usiku wa Qadr).[1]
وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ ﴿٢﴾
2. Na nini kitakachokujulisha ni nini Laylatul-Qadr?
لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ ﴿٣﴾
3. Laylatul-Qadr ni mbora kuliko miezi elfu.
تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ ﴿٤﴾
4. Wanateremka humo Malaika pamoja na Ar-Ruwh[2] (Jibriyl) kwa Idhini ya Rabb wao kwa kila jambo.
سَلَامٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ الْفَجْرِ ﴿٥﴾
5. Usiku huo ni amani mpaka kuchomoza Alfajiri.
[1] Al-Qadr:
‘Ulamaa wametofautiana kuhusu maana ya neno la القدر . Kuna kauli tatu mashuhuri:
(i) Al-Qadr ni kwa maana ya التقدير yaani makadirio (ukadirishaji). Na hapa ina maana kwamba katika usiku huu, makadirio ya mwaka ya viumbe vyote hupitishwa na kukadiriwa. Allaah (سبحانه وتعالى):
فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ﴿٤﴾
Katika (usiku) huo hupambanuliwa kila jambo la hikmah. [Ad-Dukhaan (44:4)]
(ii) Al-Qadr القدر ni kwa maana ya utukufu na uluwa wa cheo. Hii ina maana kwamba usiku huu una utukufu maalumu kwa Allaah (سبحانه وتعالى).
(iii) Al-Qadr القَدْرُ ni kwa maana ya ufinyu au mbanano. Kwa maana kwamba kutokana na wingi wa Malaika wanaoteremka usiku huo, ardhi inakuwa finyu.
Tafsiyr zote hizi tatu zinaonyesha ni namna gani usiku huu ulivyo na uzito kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Malaika Wake na kwa Waumini.
Rejea pia Ad-Dukhaan (44:14) kwenye faida nyenginezo.
Bonyeza pia viungo vifuatavyo vyenye faida kuhusu Usiku huu mtukufu, vipi kuupata na fadhila zake:
Laylatul-Qadr- Vipi Uweze Kuupata Usiku Huu? [612]
الْبَيِّنَة
098-Al-Bayyinah
098-Al-Bayyinah: Utangulizi Wa Suwrah [616]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
لَمْ يَكُنِ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ مُنفَكِّينَ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ الْبَيِّنَةُ ﴿١﴾
1. Hawakuwa wale waliokufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu[1] na washirikina wenye kujitenga na hali waliyonayo (ya kukufuru) mpaka iwafikie hoja bayana.
رَسُولٌ مِّنَ اللَّـهِ يَتْلُو صُحُفًا مُّطَهَّرَةً ﴿٢﴾
2. Nayo ni Rasuli kutoka kwa Allaah anayewasomea Suhuf zenye kutakaswa.[2]
فِيهَا كُتُبٌ قَيِّمَةٌ ﴿٣﴾
3. Ndani yake humo mna maandiko yaliyonyooka sawasawa.
وَمَا تَفَرَّقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَةُ ﴿٤﴾
4. Na hawakufarikiana wale waliopewa kitabu isipokuwa baada ya kuwajia hoja bayana.[3]
وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ ﴿٥﴾
5. Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah hali ya kuwa ni wenye kumtakasia Dini, wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki, na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah. Na hiyo ndiyo Dini iliyosimama imara.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَاۚ أُولَـٰئِكَ هُمْ شَرُّ الْبَرِيَّةِ ﴿٦﴾
6. Hakika wale waliokufuru miongoni mwa watu wa kitabu na washirikina watakuwa katika moto wa Jahannam, wadumu humo. Hao ndio waovu kabisa wa viumbe.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَـٰئِكَ هُمْ خَيْرُ الْبَرِيَّةِ ﴿٧﴾
7. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, hao ndio wema kabisa wa viumbe.
جَزَاؤُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًاۖ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِيَ رَبَّهُ ﴿٨﴾
8. Jazaa yao iko kwa Rabb wao. Nayo ni Jannaat za kudumu milele zipitazo chini yake mito, wadumu humo abadi. Allaah Ataridhika nao, nao wataridhika Naye. Hayo ni kwa yule anayemkhofu Rabb wake.
[1] Ahlul-Kitaab (Watu Wa Kitabu):
Watu wa Kitabu wanaokusudiwa katika Qur-aan ni Mayahudi na Manaswara. Wameitwa Watu wa Kitabu kwa sababu Allaah (عزّ وجلّ) Aliwateremshia Vitabu viwili kwa wana wa Israaiyl. Wa kwanza kati yao ni Nabiy Muwasaa (عليه السّلام) ambaye Ameteremshiwa Tawraat. Na wa pili wao ni Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) ambaye ameteremshiwa Injiyl. Wanaitwa: Ahlul-Kitaab (Watu wa Kitabu) na Ahlul-Kitaabayni (Watu wa Vitabu Viwili). Nao wana hukumu zinazowahusu wao ghairi ya zinazowahusu washirikina wengine. Lakini wanakusanyika pamoja na makafiri wengine kwa jina la ukafiri na shirki. Hivyo wao ni makafiri na washirikina, kama vile waabudu masanamu, waabudu nyota, na sayari na makafiri wengineo wote waliokufuru. [Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb - Ibn Baaz]
[2] Suhuf (Maandiko Matukufu) Na Tofauti Baina Yake Na Vitabu Vinginenvyo Vya Mbinguni:
Rejea Al-A’laa (87:18), An-Najm (53:36).
[3] Kugawanyika Ahlul-Kitaab (Mayahudi Na Manaswaara) Na Onyo Kwa Ummah Wa Kiislamu:
Hadiyth ifuatayo ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) inaelezea:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " تَفَرَّقَتِ الْيَهُودُ عَلَى إِحْدَى وَسَبْعِينَ أَوِ اثْنَتَيْنِ وَسَبْعِينَ فِرْقَةً وَالنَّصَارَى مِثْلَ ذَلِكَ وَتَفْتَرِقُ أُمَّتِي عَلَى ثَلاَثٍ وَسَبْعِينَ فِرْقَةً " . قَالَ أَبُو عِيسَى حَدِيثُ أَبِي هُرَيْرَةَ حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ .
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wamegawanyika Mayahudi katika mapote sabini na moja au sabini na mbili, na wakagawanyika Manaswara mfano wa hayo, na Ummah wangu utagawanyika mapote sabini na tatu.” [At-Tirmidhiy]
Na rejea Al-Faatihah (1:6), Aal-‘Imraan (3:103), (3:105), Al-An’aam (6:159), Ar-Ruwm (30:32), Ash-Shuwraa (42:14) kupata faida nyenginezo:
Bonyeza kiungo kifuatacho kupata faida nyenginezo:
105-Aayah Na Mafunzo: Makundi Sabini Na Tatu Yataingia Motoni Isipokuwa Moja Tu. [617]
الزَّلْزَلَة
099-Al-Zalzalah
099-Az-Zalzalah: Utangulizi Wa Suwrah [619]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
إِذَا زُلْزِلَتِ الْأَرْضُ زِلْزَالَهَا ﴿١﴾
1. Itakapotetemeshwa ardhi zilzala yake (ya mwisho).[1]
وَأَخْرَجَتِ الْأَرْضُ أَثْقَالَهَا ﴿٢﴾
2. Na itakapotoa ardhi mizigo yake.[2]
وَقَالَ الْإِنسَانُ مَا لَهَا ﴿٣﴾
3. Na binaadam akasema: Ina nini?
يَوْمَئِذٍ تُحَدِّثُ أَخْبَارَهَا ﴿٤﴾
4. Siku hiyo itahadithia khabari zake.
بِأَنَّ رَبَّكَ أَوْحَىٰ لَهَا ﴿٥﴾
5. Kwa kuwa Rabb wako Ameiamuru.
يَوْمَئِذٍ يَصْدُرُ النَّاسُ أَشْتَاتًا لِّيُرَوْا أَعْمَالَهُمْ ﴿٦﴾
6. Siku hiyo watatoka watu makundi mbalimbali wamefarakiana ili waonyeshwe amali zao.[3]
فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾
7. Basi yule atakayetenda kheri uzito wa chembe (kama atomu) ataiona.
وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ ﴿٨﴾
8. Na yule atakayetenda shari uzito wa chembe (kama atomu) ataiona.
[1] Zilzalah (Tetemeko La Ardhi):
‘Ulamaa wamenukuu kauli kadhaa kuhusu zalzalah kama ni Siku ya Qiyaamah au kama zitakithirika kutokea duniani kuwa ni katika alama za kukaribia Qiyaamah. Rejea Al-Hajj (22:1) kwenye maelezo yake.
Ikiwa ni Siku ya Qiyaamah, basi siku hiyo itakuwa ngumu mno, kwani zilzalah hiyo itawalewesha watu kutokana na adhabu yake, hata mama mwenye mimba atazaa mimba yake kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ ۚ إِنَّ زَلْزَلَةَ السَّاعَةِ شَيْءٌ عَظِيمٌ ﴿١﴾ يَوْمَ تَرَوْنَهَا تَذْهَلُ كُلُّ مُرْضِعَةٍ عَمَّا أَرْضَعَتْ وَتَضَعُ كُلُّ ذَاتِ حَمْلٍ حَمْلَهَا وَتَرَى النَّاسَ سُكَارَىٰ وَمَا هُم بِسُكَارَىٰ وَلَـٰكِنَّ عَذَابَ اللَّـهِ شَدِيدٌ ﴿٢﴾
Enyi watu! Mcheni Rabb wenu. Hakika zilizala la Saa ni jambo kuu. Siku mtakapoiona, kila mnyonyeshaji atamsahau anayemnyonyesha, na kila mwenye mimba ataizaa mimba yake, na utawaona watu wamelewa, kumbe hawakulewa lakini ni Adhabu ya Allaah kali! [Al-Hajj (22:1-2)]
Na Hadiyth ifuatayo inayothibitisha kuwa ni Qiyaamah:
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ بَشَّارٍ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا هِشَامُ بْنُ أَبِي عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنِ الْحَسَنِ، عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ، قَالَ كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي سَفَرٍ فَتَفَاوَتَ بَيْنَ أَصْحَابِهِ فِي السَّيْرِ فَرَفَعَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم صَوْتَهُ بِهَاتَيْنِ الآيَتَيْنِ أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ إِنَّ زَلْزَلَةَ السَّاعَةِ شَيْءٌ عَظِيمٌ ) إِلَى قَوْلِهِ : ( إن عذَابَ اللَّهِ شَدِيدٌ ) فَلَمَّا سَمِعَ ذَلِكَ أَصْحَابُهُ حَثُّوا الْمَطِيَّ وَعَرَفُوا أَنَّهُ عِنْدَ قَوْلٍ يَقُولُهُ فَقَالَ " هَلْ تَدْرُونَ أَىُّ يَوْمٍ ذَلِكَ " . قَالُوا اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ . قَالَ " ذَاكَ يَوْمٌ يُنَادِي اللَّهُ فِيهِ آدَمَ فَيُنَادِيهِ رَبُّهُ فَيَقُولُ يَا آدَمُ ابْعَثْ بَعْثَ النَّارِ . فَيَقُولُ يَا رَبِّ وَمَا بَعْثُ النَّارِ فَيَقُولُ مِنْ كُلِّ أَلْفٍ تِسْعُمِائَةٍ وَتِسْعَةٌ وَتِسْعُونَ إِلَى النَّارِ وَوَاحِدٌ فِي الْجَنَّةِ " . فَيَئِسَ الْقَوْمُ حَتَّى مَا أَبْدَوْا بِضَاحِكَةٍ فَلَمَّا رَأَى رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم الَّذِي بِأَصْحَابِهِ قَالَ " اعْمَلُوا وَأَبْشِرُوا فَوَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ إِنَّكُمْ لَمَعَ خَلِيقَتَيْنِ مَا كَانَتَا مَعَ شَيْءٍ إِلاَّ كَثَّرَتَاهُ يَأْجُوجُ وَمَأْجُوجُ وَمَنْ مَاتَ مِنْ بَنِي آدَمَ وَبَنِي إِبْلِيسَ " . قَالَ فَسُرِّيَ عَنِ الْقَوْمِ بَعْضُ الَّذِي يَجِدُونَ . فَقَالَ " اعْمَلُوا وَأَبْشِرُوا فَوَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ مَا أَنْتُمْ فِي النَّاسِ إِلاَّ كَالشَّامَةِ فِي جَنْبِ الْبَعِيرِ أَوْ كَالرَّقْمَةِ فِي ذِرَاعِ الدَّابَّةِ " . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ .
Amesimulia ‘Imraan bin Huswayn (رضي الله عنه): Tulikuwa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) safarini wakati baadhi ya Swahaba wake wanajikongoja nyuma. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akapaza sauti yake akisoma Aayah hizi mbili:
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ ۚ إِنَّ زَلْزَلَةَ السَّاعَةِ شَيْءٌ عَظِيمٌ ﴿١﴾ يَوْمَ تَرَوْنَهَا تَذْهَلُ كُلُّ مُرْضِعَةٍ عَمَّا أَرْضَعَتْ وَتَضَعُ كُلُّ ذَاتِ حَمْلٍ حَمْلَهَا وَتَرَى النَّاسَ سُكَارَىٰ وَمَا هُم بِسُكَارَىٰ وَلَـٰكِنَّ عَذَابَ اللَّـهِ شَدِيدٌ ﴿٢﴾
Enyi watu! Mcheni Rabb wenu. Hakika zilizala la Saa ni jambo kuu. Siku mtakapoiona, kila mnyonyeshaji atamsahau anayemnyonyesha, na kila mwenye mimba ataizaa mimba yake, na utawaona watu wamelewa, kumbe hawakulewa lakini ni Adhabu ya Allaah kali! [Al-Hajj (22:1-2)]
Swahaba walivyosikia hivyo, wakakimbilia kumfikia kwa sababu walijua kuwa atakuwa ana jambo la kusema. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Mnajua hii ni Siku gani? Wakasema: Allaah na Rasuli Wake ndio Wajuao zaidi. Akasema: Hiyo ni Siku atakayoitwa Aadam. Rabb wake atamwita na kumwambia: Ee Aadam, walete mbele watu watakaopelekwa motoni. Atasema: Ee Rabb wangu, ni wangapi wa kupelekwa motoni? Atasema: Katika kila elfu moja kuna mia tisa na tisini na tisa wa motoni, na mmoja wa Jannah (Peponi). Watu wakakata tamaa hadi wakawa hawatabasamu tena. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoona hali zao hivyo akasema: “Fanyeni juhudi kutenda (mema) na pokeeni bishara njema, kwani Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad imo Mkononi Mwake, nyinyi mtahesabiwa pamoja na viumbe viwili ambao idadi yao ni kubwa mno nao ni Yaajuwj na Maajuwj na wale waliofariki katika kizazi cha Aadam na kizazi cha Ibliys.” Akasema: Basi huzuni za watu zikawaondoka. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Fanyeni juhudi na pokeeni bishara njema. Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad imo Mkononi mwake! Hakika idadi yenu nyinyi ikilinganishwa na watu (makafiri), si chochote isipokuwa ni kama mfano wa alama ndogo ubavuni mwa ngamia au sehemu isiyo na manyoya kwenye mkono wa mnyama.” [At-Tirmidhiy – Hadiyth Hasan Swahiyh]
Na ikiwa ni katika alama za Qiyaamah (tetemeko la ardhi), basi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ametujulisha hilo pamoja na matukio mengineyo katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم " لاَ تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يُقْبَضَ الْعِلْمُ، وَتَكْثُرَ الزَّلاَزِلُ، وَيَتَقَارَبَ الزَّمَانُ، وَتَظْهَرَ الْفِتَنُ، وَيَكْثُرَ الْهَرْجُ ـ وَهْوَ الْقَتْلُ الْقَتْلُ ـ حَتَّى يَكْثُرَ فِيكُمُ الْمَالُ فَيَفِيضُ ".
Amesimulia Abu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Saa (Qiyaamah) haitatokea hadi Ilmu (ya Dini) itoweke (kwa vifo vya ‘Ulamaa), mitetemeko ya ardhi itatokea mara kwa mara, wakati utapita harakaharaka, fitnah zitadhihirika, mauaji yatakithiri, na mali zitakithirika kwenu na zitazidi mahitaji.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Ilmu (15)]
[2] Makaburi Yatatoa Viliomo Ndani Yake:
Ni sawa na Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
وَإِذَا الْأَرْضُ مُدَّتْ ﴿٣﴾ وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ ﴿٤﴾
Na ardhi itakapotandazwa sawa (bila mwinuko wala mwinamo). Na ikatupilia mbali vile vilivyomo ndani yake na ikawa tupu. [Al-Inshiqaaq (84:3-4)
Na pia:
وَإِذَا الْقُبُورُ بُعْثِرَتْ ﴿٤﴾
Na makaburi yatakapopinduliwa chini juu na kufichuliwa. [Al-Infitwaar (82:4)]
Wafu na hazina zitatolewa makaburini. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[3] Watu Watadhihirishiwa Amali Zao Zote Walizozitenda Duniani:
Kuanzia Aayah hii namba (6) hadi mwisho wa Suwrah, inathibitishwa kwamba Siku ya Qiyaamah, watu wataonyeshwa matendo yao ya kheri na shari, na kwamba hata tendo liwe dogo vipi litadhihirishwa! Na wala hatoweza mtu kukanusha matendo yake kwa kuwa kila tendo limerekodiwa katika daftari lake. Allaah (سبحانه وتعالى) Amethibitisha hayo katika Kauli Zake nyingi, miongoni mwazo ni:
عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ ﴿٥﴾
Nafsi hapo itajua yale iliyoyakadimisha na iliyoyaakhirisha. [Al-Infitwaar (82:5).
Na pia:
وَوُضِعَ الْكِتَابُ فَتَرَى الْمُجْرِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا فِيهِ وَيَقُولُونَ يَا وَيْلَتَنَا مَالِ هَـٰذَا الْكِتَابِ لَا يُغَادِرُ صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً إِلَّا أَحْصَاهَا ۚ وَوَجَدُوا مَا عَمِلُوا حَاضِرًا ۗ وَلَا يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا ﴿٤٩﴾
Na kitawekwa Kitabu, basi utaona wahalifu ni wenye khofu kwa yale yaliyomo ndani yake, watasema: Ole wetu! Kitabu hiki kina nini? Hakiachi dogo wala kubwa isipokuwa kimerekodi hesabuni! Na watakuta yale waliyoyatenda yamehudhuria hapo. Na Rabb wako Hamdhulumu yeyote. [Al-Kahf (18:49)]
Rejea katika huko kupata rejea nyenginezo mbalimbali.
Rejea pia Rejea Al-Israa (17:13-14), Al-Qiyaamah (75:13), At-Takwiyr (81:14). Kote humo kuna faida na rejea nyenginezo za kuthibitisha maudhui hii.
الْعَادِيَات
100-Al-‘Aadiyaat
100-Al-‘Aadiyaat: Utangulizi Wa Suwrah [621]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالْعَادِيَاتِ ضَبْحًا ﴿١﴾
1. Naapa kwa (farasi) waendao mbio za kasi wakipumua.
فَالْمُورِيَاتِ قَدْحًا ﴿٢﴾
2. Kisha Naapa kwa wenye kutoa cheche za moto (kwa msuguano wa kwato zao chini).
فَالْمُغِيرَاتِ صُبْحًا ﴿٣﴾
3. Wenye kushambulia asubuhi.
فَأَثَرْنَ بِهِ نَقْعًا ﴿٤﴾
4. Huku wakitimua wingu la vumbi kubwa.
فَوَسَطْنَ بِهِ جَمْعًا ﴿٥﴾
5. Kisha wakapenya katikati ya kundi (la maadui).
إِنَّ الْإِنسَانَ لِرَبِّهِ لَكَنُودٌ ﴿٦﴾
6. Hakika binaadam kwa Rabb wake bila shaka ni mtovu mno wa shukurani.
وَإِنَّهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٌ ﴿٧﴾
7. Na hakika yeye juu ya hayo bila shaka mwenyewe ni shahidi.
وَإِنَّهُ لِحُبِّ الْخَيْرِ لَشَدِيدٌ ﴿٨﴾
8. Na hakika yeye ni mwingi mno wa kupenda mali.
أَفَلَا يَعْلَمُ إِذَا بُعْثِرَ مَا فِي الْقُبُورِ ﴿٩﴾
9. Je, hajui vitakapopinduliwa juu chini na kutolewa vile vilivyomo makaburini?
وَحُصِّلَ مَا فِي الصُّدُورِ ﴿١٠﴾
10. Na yatapodhihirishwa yale yaliyomo vifuani?[1]
إِنَّ رَبَّهُم بِهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّخَبِيرٌ ﴿١١﴾
11. Hakika Rabb wao Siku hiyo kwao, bila shaka Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.
[1] Siri Zitafichuliwa:
Ni sawa na Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
يَوْمَ تُبْلَى السَّرَائِرُ ﴿٩﴾
Siku siri zitakapopekuliwa (na kufichuka). [Atw-Twaariq (86:9)]
الْقَارِعَة
101-Al-Qaari’ah
101-Al-Qaari’ah: Utangulizi Wa Suwrah [623]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الْقَارِعَةُ ﴿١﴾
1. Al-Qaari’ah (janga kuu linalogonga).
مَا الْقَارِعَةُ ﴿٢﴾
2. Ni nini hiyo Al-Qaari’ah?
وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْقَارِعَةُ ﴿٣﴾
3. Na nini kitakachokujulisha ni nini hiyo Al-Qaari’ah?
يَوْمَ يَكُونُ النَّاسُ كَالْفَرَاشِ الْمَبْثُوثِ ﴿٤﴾
4. Siku watakapokuwa watu kama vipepeo vilivyotawanyika.
وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ الْمَنفُوشِ ﴿٥﴾
5. Na majabali yatakuwa kama sufi iliyochambuliwa.
فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ ﴿٦﴾
6. Basi yule itakayekuwa mizani yake nzito.[1]
فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ ﴿٧﴾
7. Basi huyo atakuwa katika maisha ya kuridhisha.
وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ ﴿٨﴾
8. Na yule itakayekuwa mizani yake khafifu.
فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ ﴿٩﴾
9. Basi makazi yake ni Haawiyah.[2]
وَمَا أَدْرَاكَ مَا هِيَهْ ﴿١٠﴾
10. Na nini kitakachokujulisha ni nini hiyo Haawiyah?
نَارٌ حَامِيَةٌ ﴿١١﴾
11. Ni moto uwakao vikali mno![3]
[1] Mizani Nzito Na Mizani Nyepesi Za Matendo Ya Wanaadam:
Aayah hii namba (6) hadi (8) zinataja mizani nzito na nyepesi za amali za wanaadam, zitakazopimwa Siku ya Qiyaamah. Wale ambao amali zao njema zitakuwa ni nyingi na za kumridhisha Allaah, basi mizani zao zitakuwa nzito, na hivyo basi watakuwa na maisha ya kuridhisha Peponi. Ama ambao amali zao njema zitakuwa kidogo kutokana na madhambi yao, basi mizani zao zitakuwa nyepesi, na hivyo watakuwa waliokula khasara Aakhirah. Hizo ni sawa na Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى):
فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٠٢﴾ وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ ﴿١٠٣﴾
Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, hao ndio wenye kufaulu. Na yule ambaye mizani zake zitakuwa khafifu, basi hao ni wale ambao wamekhasirika nafsi zao. Watadumu ndani ya Jahannam. [Al-Muuminuwn (23:102-103)]
Na pia Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَالْوَزْنُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ ۚ فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٨﴾ وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُم بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَظْلِمُونَ ﴿٩﴾
Upimaji wa haki utathibiti Siku hiyo. Basi ambao mizani zao zitakuwa nzito, hao ndio watakaofaulu. Na ambao mizani zao zitakuwa khafifu, basi hao ni wale waliojikhasiri wenyewe kwa sababu ya kutozitendea haki Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) Zetu. [Al-A’raaf (7:8-9)]
Miongoni mwa yanayofanya mizani za amali kuwa nzito:
a-Kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Adkhaar zifuatazo kama alivyosema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba zinajaza mizani za kupimiwa amali, au zinafanya mizani hizo kuwa nzito:
(i) Kalimah ya لا إلهَ إلَّا اللهُ:
عن ثوبان رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((بَخٍ بَخٍ لِخمسٍ ما أثقلَهُنَّ في الميزانِ : لا إلهَ إلَّا اللهُ، وسبحانَ اللهِ، والحمدُ للهِ ، واللهُ أكبرُ، والولَدُ الصالِحُ يُتوَفَّى للمرْءِ المسلِمِ فيَحتَسِبُهُ)) النسائي وابن حبان والحاكم ، وأحمد ، وصححه الألباني في صحيح الترغيب والجامع
Amesimulia Thawbaan (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Heko, heko kwa vitu vitano, uzito ulioje vitakavyokuwa nao katika Mizani:
لا إلهَ إلَّا اللهُ، وسبحانَ اللهِ، والحمدُ للهِ ، واللهُ أكبرُ
Laa Ilaaha Illa Allaah, Subhaanah-Allaah, AlhamduliLLah, Allaahu Akbar, na mtoto mwema atakayekufa na wazazi wake wanatarajia thawabu kutoka kwa Allaah.” [An-Nasaaiy, Ibn Hibbaan, Al-Haakim, Ahmad, na Al-Albaaniy kaisahihisha katika Swahiyh At-Targhiyb (1557), Swahiyh Al-Jaami'(2817)]
pia:
عن عبد الله بن عمرو: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((إنَّ نبيَّ اللهِ نوحًا لما حضَرَتْه الوفاةُ قال لابنِه: إني قاصٌّ عليك الوصيَّةَ، آمرُك باثنتَينِ و أنهاك عن اثنتَينِ، آمرُك ب ( لاإله إلا اللهُ )، فإنَّ السمواتِ السبعَ والأرَضينَ السبعَ لو وُضِعَتْ في كِفَّةٍ، ووُضِعَتْ لا إلهَ إلا اللهُ في كِفَّةٍ، رجَحَتْ بهنَّ لا إلهَ إلا اللهُ، ولو أنَّ السمواتِ السبعَ والأرَضَينَ السبعَ كُنَّ حَلْقةً مُبهَمةً قصَمَتْهنَّ لا إلهَ إلا اللهُ،
Amesimulia ‘Abdullaah Bin ‘Amr (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mauti yalipomfikia Nabiy wa Allaah (ambaye ni) Nuwh (عليه السّلام), alimwambia mwanawe: Nakuhadithia wasiya wangu. Nakuamrisha mambo mawili na kukukataza mawili. Nakuamrisha Laa ilaaha illa Allaah (Hapana mwabudiwa wa haki illa Allaah), kwani ingelikuwa mbingu saba na ardhi saba zimewekwa katika mizani na Laa ilaaha illa Allaah imewekwa katika mizani ya pili, basi Laa ilaaha illa Allaah ingelikuwa nzito.
Na kama ingelikuwa mbingu saba na ardhi saba zimefungwa katika mduara, basi Laa illa Allaah ingelivunja mduara huo. [As-Silsilah Asw-Swahiyhah (134)]
(ii) Kumsabihi Allaah kwa سُبْحَانَ اللَّهِ العَظِيمِ، سُبْحَانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: " كَلِمَتَانِ خَفِيفَتَانِ عَلَى اللِّسَانِ، ثَقِيلَتَانِ فِي المِيزَانِ، حَبِيبَتَانِ إِلَى الرَّحْمَنِ: سُبْحَانَ اللَّهِ العَظِيمِ، سُبْحَانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ " رواه البخاري ومسلم
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Maneno mawili ni mepesi mno kwa ulimi, mazito mno katika mizani, yanapendeza mno mbele ya Ar-Rahmani (Mwenye kurehemu) nayo ni:
سُبْحَانَ اللهِ العَظِيمِ سُبْحانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ
Subhaana-Allaahil-‘Adhwiym, Subhaana-Allaahi wa-Bihamdihi
Ametakasika Allaah Aliye Mtukufu, Ametakasika Allaah na Himdi ni Zake” [Al-Bukhaariy, Muslim]
“Ametakasika Allaah Mtukufu, Ametakasika Allaah Aliye Mtukufu” [Al-Bukhaariy, Muslim]
(iii) Kumsabbih Allaah kwa سبحانَ اللهِ، والحمدُ للهِ ، واللهُ أكبرُ،
Rejea nukta namba (i) moja juu. Na pia:
عن أبي مالكٍ الحارِثِ بنِ عاصِمٍ الأَشْعَرِيِّ رضي اللهُ عنهُ قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: ((الطُّهُورُ شَطْرُ الإِيَمانِ، والحمدُ لِلهِ تَمْلأُ الْمِيزَانَ، وسُبْحانَ اللهِ والحمدُ لِلهِ تَمْلآنِ - أو تَمْلأُ - ما بَيْنَ السَّمآءِ والأرضِ، والصَّلاةُ نورٌ، والصَّدَقَةُ بُرْهانٌ، والصَّبْرُ ضِيَاءٌ، والْقُرآنُ حُجَّةٌ لَكَ أو عَلَيْكَ، كُلُّ النَّاسِ يَغْدو، فَبائعٌ نَفْسَهُ، فَمُعْتِقُها أَو مُوبِقُها)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Amesimulia Abuu Maalik Al-Haarith bin ‘Aaswim Al-Ash’ariyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Twahaara ni nusu ya imaan, na AlhamduliLLaah inajaza mizani, na Subhaana-Allaah wal-HamduliLLaah inajaza baina ya mbingu na ardhi. Na Swalaah ni nuru, na swadaqa ni burhani na subira ni mwangaza, na Qur-aan ni hoja kwako au dhidi yako. Kila mtu anaianza siku yake akiichuuza nafsi yake, aidha huiokoa ikasalimika au akaiangamiza.” [Muslim]
b-Baadhi ya Adhkaar nyenginezo ambazo thawabu zake ni tele:
i) Kusoma Suwrah Al-Ikhlaasw mara tatu kwa sababu, malipo ya kuisoma Suwrah hii ni sawa na thuluthi ya Qur-aan. Rejea fadhila za Suwrah hii katika utangulizi wa Suwrah. Pia kusoma Suwrah Al-Kaafiruwn kwa kuwa malipo ya kuisoma ni sawa na robo ya Qur-aan. Rejea fadhila za Suwrah hii katika utangulizi wa Suwrah.
ii) Kumsabbih Allaah kwa:
سُبْحـانَ اللهِ وَبِحَمْـدِهِ عَدَدَ خَلْـقِه ، وَرِضـا نَفْسِـه ، وَزِنَـةَ عَـرْشِـه ، وَمِـدادَ كَلِمـاتِـه
Subhaana-Llaahi wa Bihamdihi 'Adada Khalqihi wa Ridhwaa Nafsihi, wa Zinata 'Arshihi wa Midaada Kalimaatih (mara tatu)
Namtakasa Allaah (na kila sifa hasi) na namhimidi kwa idadi ya Viumbe Vyake, na kwa idadi ya vilivyoridhiwa na Nafsi Yake, na kwa uzito wa ‘Arshi Yake, na kwa wingi wa wino wa (kuandikia) Maneno Yake.
Hadiyth ifuatayo imethibiti:
عن أم المؤمنين جُويْريَةَ بنت الحارِث رَضِيَ اللهُ عنها: أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم خرجَ مِنْ عِنْدِهَا بُكْرَةً حِيْنَ صَلَّى الصُّبْحَ وَهِيَ في مَسْجِدِها ، ثُمَّ رَجَعَ بَعدَ أنْ أضْحَى وَهِيَ جَالِسَةٌ ، فقالَ : (( مَا زِلْتِ عَلَى الحالِ الَّتي فَارقَتُكِ عَلَيْهَا ؟ )) قالت : نَعَمْ ، فَقَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( لَقَدْ قُلْتُ بَعْدَكِ أرْبَعَ كَلِمَاتٍ ثَلاثَ مَرَّاتٍ ، لَوْ وُزِنَتْ بِمَا قُلْتِ مُنْذُ اليَوْمِ لَوَزَنَتْهُنَّ : سُبْحَانَ الله وَبِحَمْدِهِ عَدَدَ خَلْقِهِ ، وَرِضَا نَفْسِهِ ، وَزِنَةَ عَرْشِهِ ، وَمِدَادَ كَلِمَاتِهِ )) . رواه مسلم
Amesimulia Mama wa Waumini Juwayriyah bint Al-Haarith (رضي الله عنها): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka chumbani kwake mapema pindi aliposwali Swalaah ya Asubuhi, naye (Juwayriyah) alikuwa akiswali. Baadae Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alirudi baada ya kuswali Swalaah ya Dhuwhaa, naye (Juwayriyah) alikuwa bado ameketi (katika mswala wake). Akasema: "Bado upo katika hali ile ile niliyokuacha nayo?" Nikasema: Naam. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Hakika baada ya kuondoka nimesema maneno manne mara tatu, lau zitapimwa na kufananishwa na yale uliyosema asubuhi ya leo basi zitakuwa ni nzito zaidi:
سُبْحَانَ الله وَبِحَمْدِهِ عَدَدَ خَلْقِهِ ، وَرِضَا نَفْسِهِ ، وَزِنَةَ عَرْشِهِ ، وَمِدَادَ كَلِمَاتِهِ
Namtakasa Allaah (na kila sifa hasi) na namhimidi kwa idadi ya Viumbe Vyake, na kwa idadi ya vilivyoridhiwa na Nafsi Yake, na kwa uzito wa ‘Arshi Yake, na kwa wingi wa wino wa (kuandikia) Maneno Yake. [Muslim]
c-Kuwa na khulqa (tabia) njema:
عَنْ أَبِي اَلدَّرْدَاءِ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَا مِنْ شَيْءٍ فِي اَلْمِيزَانِ أَثْقَلُ مِنْ حُسْنِ اَلْخُلُقِ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ
Amesimulia Abuu Ad-Dardaa (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna jambo zito katika mizani ya Muumini (Siku ya Qiyaamah) kama khulqa (tabia) njema.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy na akaisahihisha]
d-Kusindikiza jeneza na kumswalia maiti:
عن ابي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " مَنْ شَهِدَ الْجَنَازَةَ حَتَّى يُصَلِّيَ عَلَيْهَا فَلَهُ قِيرَاطٌ، وَمَنْ شَهِدَ حَتَّى تُدْفَنَ كَانَ لَهُ قِيرَاطَانِ ". قِيلَ وَمَا الْقِيرَاطَانِ قَالَ " مِثْلُ الْجَبَلَيْنِ الْعَظِيمَيْنِ ".
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nimemsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Yeyote anayeusindikiza msafara wa jeneza hadi akaiswalia maiti, basi atapata qiratw moja, na yeyote anayeusindikiza hadi atakapozikwa, basi atapata qiratw mbili.” Likaulizwa swali: Qiratw mbili ndiyo nini? Akajibu: “Ni kama milima mikubwa miwili.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Jeneza (23)]
Miongoni Mwa Yanayofanya Mizani Kuwa Nyepesi:
i) Dhulma: Anayedhulumu watu kwa mali, ghiybah (kusengenya), kuvunja heshima za watu n.k anakuwa muflis kwa sababu amali zake njema zitachukuliwa na kugaiwa kwa wale aliowadhulumu:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((أَتَدْرُونَ مَا الْمُفْلِسُ؟)) قَالُوا: الْمُفْلِسُ فِينَا مَنْ لاَ دِرْهَمَ لَهُ وَلاَ مَتَاعَ . فَقَالَ: ((إِنَّ الْمُفْلِسَ مِنْ أُمَّتِي يَأْتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ بِصَلاَةٍ وَصِيَامٍ وَزَكَاةٍ وَيَأْتِي قَدْ شَتَمَ هَذَا وَقَذَفَ هَذَا وَأَكَلَ مَالَ هَذَا وَسَفَكَ دَمَ هَذَا وَضَرَبَ هَذَا فَيُعْطَى هَذَا مِنْ حَسَنَاتِهِ وَهَذَا مِنْ حَسَنَاتِهِ فَإِنْ فَنِيَتْ حَسَنَاتُهُ قَبْلَ أَنْ يُقْضَى مَا عَلَيْهِ أُخِذَ مِنْ خَطَايَاهُمْ فَطُرِحَتْ عَلَيْهِ ثُمَّ طُرِحَ فِي النَّارِ)) مسلم
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliuliza: “Je, mnamjua muflis? (Swahaba) wakasema: Muflis kwetu sisi ni yule miongoni mwetu asiyekuwa na dirhamu (pesa) wala vyenye kumnufaisha yeye hapa duniani. Akasema (صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika muflis katika Ummah wangu ni yule atakayekuja Siku ya Qiyaamah na Swalaah, Swiyaam, na Zakaah, lakini amemtusi huyu, amemsingizia huyu kuwa amezini, amekula mali ya huyu, amemwaga damu ya mwingine na amempiga mwengine. Thawabu zake zitapatiwa huyu na yule mpaka zimalizike. Na zinapokwisha, basi madhambi ya hao (aliowadhulumu) atabandikwa nayo, kisha atupwe motoni.” [Muslim]
ii) Shirki ya riyaa-a (kujionyesha) inabatilisha amali:
Rejea pia Al-Maa’uwn (107:6)
iii) Hatari ya kutenda Aliyoyaharamisha Allaah:
عَنْ ثَوْبَانَ، عَنِ النَّبِيِّ ـ صلى الله عليه وسلم ـ أَنَّهُ قَالَ : " لأَعْلَمَنَّ أَقْوَامًا مِنْ أُمَّتِي يَأْتُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ بِحَسَنَاتٍ أَمْثَالِ جِبَالِ تِهَامَةَ بِيضًا فَيَجْعَلُهَا اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ هَبَاءً مَنْثُورًا " . قَالَ ثَوْبَانُ : يَا رَسُولَ اللَّهِ صِفْهُمْ لَنَا جَلِّهِمْ لَنَا أَنْ لاَ نَكُونَ مِنْهُمْ وَنَحْنُ لاَ نَعْلَمُ . قَالَ : " أَمَا إِنَّهُمْ إِخْوَانُكُمْ وَمِنْ جِلْدَتِكُمْ وَيَأْخُذُونَ مِنَ اللَّيْلِ كَمَا تَأْخُذُونَ وَلَكِنَّهُمْ أَقْوَامٌ إِذَا خَلَوْا بِمَحَارِمِ اللَّهِ انْتَهَكُوهَا " .
Amesimulia Thawbaan (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika najua watu katika ummah wangu ambao watakuja Siku ya Qiyaamah na matendo mema meupe kama milima ya Tihaamah, lakini Allaah Atayafanya kama chembechembe za vumbi zinazoelea hewani zikitawanyika.” Thawbaan akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Tufafanulie hao, ili tusiwe miongoni mwao na hali sisi hatujui. Akasema: “Hao ni ndugu zenu na katika kabila zenu, wakifanya ibaada usiku kama mfanyavyo, lakini ni watu ambao wanapokuwa peke yao, wanaruka mipaka kutenda Aliyoyaharamisha Allaah.” [Swahiyh Ibn Maajah (3442)]
Duaa ya kuomba kujaaliwa mizani kuwa nzito:
[2] Haawiyah Ni Katika Majina Ya Moto Wa Aakhirah:
Rejea Al-Muddath-thir (74:26) kwenye majina mengineyo ya moto wa Aakhirah.
[3] Moto Wa Jahannam Kulingana Na Moto Wa Duniani:
Ametaja Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth ifuatayo:
حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيلُ بْنُ أَبِي أُوَيْسٍ، قَالَ حَدَّثَنِي مَالِكٌ، عَنْ أَبِي الزِّنَادِ، عَنِ الأَعْرَجِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " نَارُكُمْ جُزْءٌ مِنْ سَبْعِينَ جُزْءًا مِنْ نَارِ جَهَنَّمَ ". قِيلَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنْ كَانَتْ لَكَافِيَةً. قَالَ " فُضِّلَتْ عَلَيْهِنَّ بِتِسْعَةٍ وَسِتِّينَ جُزْءًا، كُلُّهُنَّ مِثْلُ حَرِّهَا ".
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Moto wenu ni sehemu ya sehemu sabiini za moto wa Jahannam.” Akaulizwa: Ee Rasuli wa Allaah! Moto wa duniani ulitosha kuwaadhibia waovu. Akasema: “Moto wa Jahannam una sehemu sitini na tisa zaidi ya moto wa dunia, kila moja ya sehemu hizo, joto lake ni sawa na joto la moto wa dunia.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Uumbaji (59), Muslim Kitabu Cha Jannah Sifa Za Neema Zake Na Wakaazi Wake (53)]
التَّكَاثُر
102-At-Takaathur
102-At-Takaathur: Utangulizi Wa Suwrah [626]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُرُ ﴿١﴾
1. Kumekughafilisheni (na utiifu wa Allaah kwa) kushindana kukithirisha (mali na watoto).
حَتَّىٰ زُرْتُمُ الْمَقَابِرَ ﴿٢﴾
2. Mpaka muingie makaburini.
كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٣﴾
3. Laa hasha! Mtakuja kujua.
ثُمَّ كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٤﴾
4. Kisha laa hasha! Mtakuja kujua.
كَلَّا لَوْ تَعْلَمُونَ عِلْمَ الْيَقِينِ ﴿٥﴾
5. Laa hasha! Lau mngelijua ujuzi wa yakini.[1]
لَتَرَوُنَّ الْجَحِيمَ ﴿٦﴾
6. Bila shaka mtauona moto uwakao vikali mno.
ثُمَّ لَتَرَوُنَّهَا عَيْنَ الْيَقِينِ ﴿٧﴾
7. Kisha kwa hakika mtauona kwa jicho la yakini.
ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ ﴿٨﴾
8. Kisha bila shaka mtaulizwa Siku hiyo kuhusu neema.[2]
[1] Ujuzi Wa Kweli:
Lau mngeyajua yaliyo mbele yenu kwa ujuzi unaofika nyoyoni, msingelighafilika kwa kushughulika na kukithirisha (mali) na mngelikimbilia kutenda mema. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Siyo namna hii inatakiwa iwashughulishe kushindana kwa wingi wa mali. Lau mnajua kikweli, basi mngalirudi nyuma na mngelikimbilia haraka kuokoa nafsi zenu kutoka kwenye maangamivu. [Tafsiyr Al-Muyassar]
[2] Kutokushukuru Neema Na Kutokuzitumia Katika Njia Za Kumridhisha Allaah:
Neema mlizotumia katika kustarehe nazo katika dunia hii, je, mlishukuru na mkatimiza haki za Allaah, na wala hamkuzitumia katika maasi ili Akupeni neema kubwa na bora kuliko hizo? Au mlidanganywa nazo na hivyo mkashindwa kushukuru neema hizo, na labda mkazitumia kumuasi Allaah. Atakuadhibuni kwazo kama Anavyosema katika Kauli Yake nyengine:
وَيَوْمَ يُعْرَضُ الَّذِينَ كَفَرُوا عَلَى النَّارِ أَذْهَبْتُمْ طَيِّبَاتِكُمْ فِي حَيَاتِكُمُ الدُّنْيَا وَاسْتَمْتَعْتُم بِهَا فَالْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَبِمَا كُنتُمْ تَفْسُقُونَ﴿٢٠﴾
Na siku watakaposimamishwa hadharani wale waliokufuru kwenye moto (waambiwe): Je, mshamaliza vizuri vyenu katika uhai wenu wa dunia na mshajistarehesha navyo? Basi leo mtalipwa adhabu ya udhalilifu kwa vile mlivyokuwa mkitakabari katika ardhi bila ya haki, na kwa ufasiki mliokuwa mnaufanya. [Al-Ahqaaf (46:20)]
[Tafsiyr As-Sa’diy]
Rejea Al-Qalam (68:17) kwenye mafunzo yanayotokana na visa viwili vya watu wa shamba walioshukuru neema za Allaah kwa kuzitolea swadaqa, na kinyume chake kuhusu kukufuru neema za Allaah kama kutokuzitolea swadaqa kwa masikini na wahitaji.
الْعَصْر
103-Al-‘Aswr
103-Al-‘Aswr: Utangulizi Wa Suwrah [628]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَالْعَصْرِ ﴿١﴾
1. Naapa kwa Al-‘Aswr (zama).[1]
إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ ﴿٢﴾
2. Hakika binaadam bila shaka yumo katika khasara.
إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ ﴿٣﴾
3. Isipokuwa wale walioamini, na wakatenda mema, na wakausiana haki, na wakausiana subira.[2]
[1] Allaah Anaapia Kwa Al-‘Aswr:
Allaah Anaapia kwa Al-‘Aswr ambayo ni usiku na mchana ambamo ndani yake matendo ya waja yanatendwa. [Tafsiyr As-Sa’diy]
[2] Khasara Kwa Binaadam Isipokuwa Mambo Manne:
Suwrah imetoa mukhtasari wa binaadam kutokuwa katika khasara isipokuwa kwa mambo manne:
(i) Imaan: Kuamini Aliyotuamrisha Allaah tuyaamini. Na imaan haiwezi kukamilika bila ya kuwa na ilimu, kwani ilimu ni tawi la imaan, haitiimi bila kwayo.
(ii) Amali njema: Inajumuisha amali zote za kheri, za dhahiri na za siri, zinazohusiana na haki za Allaah na haki za Waja wake, ni sawa ikiwa ni amali za faradhi au zinazopendekezwa (na za khiari).
(iii) Kuusiana ya haki: Ambayo ni imaan na matendo mema, yaani, kuusiana kwayo, kuhimizana na kushajiishana kuyafanya.
(iv) Kuusiana kuvuta subira. Katika utiifu wa Allaah, kutokutenda maasi, na kukubali Qadar za Allaah zinazoumiza.
Kwa mambo mawili ya kwanza, mtu anajikamilisha mwenyewe. Na kwa mawili ya mwisho, mtu anawasaidia wengine kuwakamilisha. Na kwa kuyakamilisha mambo haya manne, mtu atakuwa salama kutokana na khasara na atapata mafanikio makubwa. [Tafsiyr As-Sa’diy]
الْهُمَزَة
104-Al-Humazah
104-Al-Humazah: Utangulizi Wa Suwrah [630]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
وَيْلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ ﴿١﴾
1. Ole kwa kila mwenye kukashifu na kufedhehesha watu kwa ishara na vitendo, na kwa kila mwenye kusengenya na kufedhehesha kwa ulimi.[1]
الَّذِي جَمَعَ مَالًا وَعَدَّدَهُ ﴿٢﴾
2. Ambaye amekusanya mali na kuyahesabu.
يَحْسَبُ أَنَّ مَالَهُ أَخْلَدَهُ ﴿٣﴾
3. Anadhani kwamba mali yake itamdumisha milele.
كَلَّاۖ لَيُنبَذَنَّ فِي الْحُطَمَةِ ﴿٤﴾
4. Laa hasha! Atavurumishwa katika Al-Hutwamah[2] (moto mkali unaonyambua nyambua).
وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْحُطَمَةُ ﴿٥﴾
5. Na nini kitakujulisha ni nini hiyo Al-Hutwamah?
نَارُ اللَّـهِ الْمُوقَدَةُ ﴿٦﴾
6. Ni moto wa Allaah uliowashwa.
الَّتِي تَطَّلِعُ عَلَى الْأَفْئِدَةِ ﴿٧﴾
7. Ambao unapanda nyoyoni.
إِنَّهَا عَلَيْهِم مُّؤْصَدَةٌ ﴿٨﴾
8. Hakika huo utafungiwa juu yao kila upande.
فِي عَمَدٍ مُّمَدَّدَةٍ ﴿٩﴾
9. Katika nguzo zilizonyooshwa.
[1] Maana Ya Al-Humazah Na Al-Lumazah:
‘Ulamaa wametofautiana katika maana za Al-Humazah na Al-Lumazah. Lakini wengi wao wamekubaliana kwamba Al-Humazah ni kukashifu, kufedhehesha, kudharau watu kwa ishara na vitendo. Na Al-Lumazah ni kusengenya, kukashifu na kufedhehesha kwa ulimi.
Na katika Tarjama, maana zake zimetegemea muktadha zake. Na zimekuja maana zake mbalimbali kama ifuatavyo:
Al-Humazah: Kudharau, kukashifu, kufedhehesha, kubeza n.k. Rejea Suwrah hii Al-Humazah (104:1), Al-Qalam (68:11).
Al-Lumazah: Kukosoa, kulaumu, kushutumu, kutukana, kukejeli, kufedhehesha na kuvunja heshima, kufanya tashtiti, n.k. Rejea Suwrah hii Al-Humazah (104:1), At-Tawbah (9:58), (9:79), Al-Hujuraat (49:11).
Na Allaah Mjuzi zaidi
[2] Al-Hutwamah Ni Miongoni Mwa Majina Ya Moto:
Moto wa Al-Hutwamah umetajwa sifa zake katika Aayah zinzofuatia kama alivyofasiri Imaam Ibn Kathiyr:
Thaabit Al-Bunaan amesema: “Utawachoma mpaka nyoyoni nao wangali wako hai.” Kisha akasema: “Kwa yakini adhabu imewafika.” Kisha akalia. Muhammad Bin Ka’ba amesema: “Moto utakula kila kitu kwenye mwili wake mpaka moyo wake unapofika usawa wa koo lake, hurudi kwenye mwili wake.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
Rejea Al-Muddath-thir (74:26) kwenye majina mengineyo ya moto.
الْفِيل
105-Al-Fiyl
105-Al-Fiyl: Utangulizi Wa Suwrah [632]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصْحَابِ الْفِيلِ ﴿١﴾
1. Je, hukuona (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) jinsi Rabb wako Alivyowafanya watu wa tembo?[1]
أَلَمْ يَجْعَلْ كَيْدَهُمْ فِي تَضْلِيلٍ ﴿٢﴾
2. Je, Hakujaalia hila zao kufeli na kushindwa?
وَأَرْسَلَ عَلَيْهِمْ طَيْرًا أَبَابِيلَ ﴿٣﴾
3. Na Akawatumia ndege makundi kwa makundi yafuatanayo kuwashambulia?
تَرْمِيهِم بِحِجَارَةٍ مِّن سِجِّيلٍ ﴿٤﴾
4. Wakiwarushia mawe ya udongo uliookwa motoni.
فَجَعَلَهُمْ كَعَصْفٍ مَّأْكُولٍ ﴿٥﴾
5. Akawafanya kama nyasi kavu zilizoliwa.
قُرَيْش
106-Quraysh
106-Quraysh: Utangulizi Wa Suwrah [634]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
لِإِيلَافِ قُرَيْشٍ ﴿١﴾
1. (Tumewaangamiza watu wa tembo) ili Maquraysh wapate kuendelea na mazoea.[1]
إِيلَافِهِمْ رِحْلَةَ الشِّتَاءِ وَالصَّيْفِ ﴿٢﴾
2. Mazoea yao ya safari (za kibiashara) za majira ya baridi na majira ya joto.
فَلْيَعْبُدُوا رَبَّ هَـٰذَا الْبَيْتِ ﴿٣﴾
3. Basi wamuabudu Rabb wa Nyumba hii (Ka’bah).
الَّذِي أَطْعَمَهُم مِّن جُوعٍ وَآمَنَهُم مِّنْ خَوْفٍ ﴿٤﴾
4. Ambaye Anawalisha kuwaokoa na njaa, na Anawapa amani kutokana na khofu.
[1] Suwrah Hii Kuhusiana Na Ya Al-Fyl:
Wafasiri wengi wamesema kwamba Suwrah hii inaunganishwa na Suwrah iliyotangulia (ya Al-Fiyl). Na maana yake ni: Tulifanya yale Tuliyowafanyia jeshi la tembo kwa ajili ya maquraysh ili kuwahifadhi salama, kulinda maslahi yao na usalama wa safari zao za kawaida kwenda Yemen katika majira ya baridi na Sham wakati wa kiangazi, kwa madhumuni ya biashara na chumo. [Tafsiyr As-Sa’diy]
Rejea Utangulizi Wa Suwrah kupata faida.
الْمَاعُون
107-Al-Maa’uwn
107-Al-Maa’uwn: Utangulizi Wa Suwrah [636]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
أَرَأَيْتَ الَّذِي يُكَذِّبُ بِالدِّينِ ﴿١﴾
1. Je, umemuona yule anayekadhibisha malipo?
فَذَٰلِكَ الَّذِي يَدُعُّ الْيَتِيمَ ﴿٢﴾
2. Basi huyo ndiye yule anayemnyanyasa yatima.
وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ ﴿٣﴾
3. Na wala hahamasishi kulisha maskini.
فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ ﴿٤﴾
4. Basi ole kwa wanaoswali.
الَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ ﴿٥﴾
5. Ambao wanapuuza Swalaah zao.
الَّذِينَ هُمْ يُرَاءُونَ ﴿٦﴾
6. Ambao wanajionyesha (riyaa).[1]
وَيَمْنَعُونَ الْمَاعُونَ ﴿٧﴾
7. Na wanazuia (pia) misaada ya matumizi madogodogo ya kawaida ya kila siku.
[1] Riyaa (Kujionyesha Kwa Watu):
Riyaa ni kujionyesha kwa watu matendo mema badala ya kumsafishia niyah Allaah. Hii ni aina ya shirki ndogo ambayo inabatilisha amali.
Rejea Az-Zumar (39:65) kwenye maelezo kuhusu aina za shirki.
Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ameonya katika Hadiyth kadhaa kuhusu riyaa, miongoni mwazo ni:
عَنْ جُنْدَبِ بْنِ عَبْدُ الله بْنِ سُفْيانَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ سَمَّعَ سَمَّعَ اللَّهُ بِهِ وَمَنْ رَاءَى رَاءَى اللَّهُ بِهِ)) متفق عليه
Amesimulia Jundab bin ‘Abdillaah bin Sufyaan (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kuzungumza (au kusoma) ili watu wamsifu, Allaah Atamfedhehesha Siku ya Qiyaamah, na mwenye kuwafanyia watu riyaa (kwa amali njema ili aonekane ni mtukufu), Allaah Atazidhihirisha siri zake (Siku ya Qiyaamah).” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na katika Qur-aan imetajwa riyaa za watu katika ibaada mbali mbali: Rejea Al-Baqarah (2:264), An-Nisaa (4:38), (4:142), na Al-Anfaal (8:47).
Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuacha kutufundisha jinsi ya kujikinga na riyaa, akatufundisha duaa ifuatayo:
اللّهُـمَّ إِنّـي أَعـوذُبِكَ أَنْ أُشْـرِكَ بِكَ وَأَنا أَعْـلَمْ، وَأَسْتَـغْفِرُكَ لِما لا أَعْـلَم
Ee Allaah! Hakika mimi Najikinga Kwako kutokana na kukushirikisha hali ya kuwa najua, na ninakuomba maghfira kwa nisiyoyajua.
Bonyeza viungo vifuatavyo kupata makala kuhusu shirki ya riyaa:
Riyaa (Shirki Iliyofichikana) [637]
02-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Shirki Ni Aina mbili Na Tofauti Zake [638]
03-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Shirki Ndogo - Riyaa (Kujionyesha) [639]
04-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Shirki Inabatilisha ‘Amali [640]
05-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Hatima Ya Mwenye Riyaa (Kujionyesha) [641]
الْكَوْثَر
108-Al-Kawthar
108-Al-Kawthar: Utangulizi Wa Suwrah [643]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ ﴿١﴾
1. Hakika Sisi Tumekupa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Al-Kawthar[1] (Mto katika Jannah).
فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ ﴿٢﴾
2. Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja.
إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الْأَبْتَرُ ﴿٣﴾
3. Hakika mbaya wako, yeye ndiye atakayekatiliwa mbali (kizazi na kila kheri).
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
108-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Kawthar: إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ [644]
Rejea pia Utangulizi Wa Suwrah kwenye faida tele pamoja na fadhila za Suwrah.
الْكَافِرُون
109-Al-Kaafiruwn
109-Al-Kaafiruwn: Utangulizi Wa Suwrah [646]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ ﴿١﴾
1. Sema: Enyi makafiri![1]
لَا أَعْبُدُ مَا تَعْبُدُونَ ﴿٢﴾
2. Siabudu yale mnayoyaabudu sasa.
وَلَا أَنتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ ﴿٣﴾
3. Na wala nyinyi hamtoabudu Yule ninayemwabudu sasa.
وَلَا أَنَا عَابِدٌ مَّا عَبَدتُّمْ ﴿٤﴾
4. Na wala mimi sitoabudu yale mliyoyaabudu nyuma.
وَلَا أَنتُمْ عَابِدُونَ مَا أَعْبُدُ ﴿٥﴾
5. Na wala nyinyi hamtoabudu Yule Ninayemwabudu.
لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ ﴿٦﴾
6. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.
[1] Fadhila Za Suwrah:
Rejea pia Utangulizi Wa Suwrah kwenye faida tele pamoja na fadhila za Suwrah.
النَّصْر
110-An-Naswr
110-An-Naswr: Utangulizi Wa Suwrah [648]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّـهِ وَالْفَتْحُ ﴿١﴾
1. Itakapokuja Nusura ya Allaah na ushindi.[1]
وَرَأَيْتَ النَّاسَ يَدْخُلُونَ فِي دِينِ اللَّـهِ أَفْوَاجًا ﴿٢﴾
2. Na ukawaona watu wanaingia katika Dini ya Allaah makundi makundi.
فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَاسْتَغْفِرْهُۚ إِنَّهُ كَانَ تَوَّابًا ﴿٣﴾
3. Basi hapo sabbih na mhimidi Rabb wako (kwa wingi zaidi) na muombe maghfirah. Hakika Yeye daima Ni Mwingi mno wa Kupokea tawbah.
الْمَسَد
111-Al-Masad
111-Al-Masad: Utangulizi Wa Suwrah [650]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ ﴿١﴾
1. Iangamie mikono miwili ya Abu Lahab, na (hakika) ameangamia.[1]
مَا أَغْنَىٰ عَنْهُ مَالُهُ وَمَا كَسَبَ ﴿٢﴾
2. Haikumfaa mali yake na yale aliyoyachuma.
سَيَصْلَىٰ نَارًا ذَاتَ لَهَبٍ ﴿٣﴾
3. Ataingia na kuungua kwenye moto wenye mwako.
وَامْرَأَتُهُ حَمَّالَةَ الْحَطَبِ ﴿٤﴾
4. Na mke wake mbebaji kuni.
فِي جِيدِهَا حَبْلٌ مِّن مَّسَدٍ ﴿٥﴾
5. Katika shingo yake kuna kamba ya mtende iliyosokotwa madhubuti.
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
111-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Masad: تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ [219]
Na pia:
026-Asbaabun-Nuzuwl:Ash-Shu'araa Aayah 214: وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ [218]
Rejea pia Utangulizi Wa Suwrah kupata faida nyenginezo.
الإِخْلاَص
112-Al-Ikhlaasw
112-Al-Ikhlaasw: Utangulizi Wa Suwrah [652]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾
1. Sema: Yeye Allaah Ni Mmoja Pekee.[1]
اللَّـهُ الصَّمَدُ ﴿٢﴾
2. Allaah Aliyekamilika Sifa za Utukufu Wake, Mkusudiwa haja zote.
لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ ﴿٣﴾
3. Hakuzaa wala Hakuzaliwa.
وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ ﴿٤﴾
4. Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye.
الْفَلَقْ
113-Al-Falaq
113-Al-Falaq: Utangulizi Wa Suwrah [654]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ ﴿١﴾
1. Sema: Najikinga na Rabb wa mapambazuko.[1]
مِن شَرِّ مَا خَلَقَ ﴿٢﴾
2. Kutokana na shari ya Alivyoviumba.
وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ ﴿٣﴾
3. Na kutokana na shari ya giza linapoingia.
وَمِن شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ ﴿٤﴾
4. Na kutokana na shari ya wanaopuliza mafundoni.
وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ ﴿٥﴾
5. Na kutokana na shari ya hasidi anapohusudu.
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
Rejea pia Utangulizi Wa Suwrah kwenye faida tele pamoja na fadhila za Suwrah.
النَّاسْ
114-An-Naas
114-An-Naas: Utangulizi Wa Suwrah [657]
Alhidaaya.com [6]
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾
1. Sema: Najikinga na Rabb wa watu.[1]
مَلِكِ النَّاسِ ﴿٢﴾
2. Mfalme wa watu.
إِلَـٰهِ النَّاسِ ﴿٣﴾
3. Muabudiwa wa Haki wa watu.
مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ ﴿٤﴾
4. Kutokana na shari za anayetia wasiwasi, mwenye kurejea nyuma akinyemelea.
الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ ﴿٥﴾
5. Ambaye ananong’ona kutia wasiwasi vifuani mwa watu.
مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ ﴿٦﴾
6. Miongoni mwa majini na watu.
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
Rejea pia Utangulizi Wa Suwrah kwenye faida tele pamoja na fadhila za Suwrah.
Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake
Maana Zake Kwa Mukhtasari
Alhidaaya.com [6]
Jina/ Swiffah
|
Tamshi |
Maana |
الرّب |
Ar-Rabb |
Rabb Wa Kila Kitu, Mola, Bwana, Muumbaji, Msimamizi, Mneemeshaji, Mfalme, Mwenye Kuruzuku, Mwendeshaji wa Mambo, Mlezi.
|
الله |
Allaah
|
Mwenye Uluwhiyyah, Mwenye ‘Ubuwdiyyah
|
الملك |
Al-Malik
|
Mfalme
|
المالك |
Al-Maalik
|
Mwenye Kumiliki
|
الّذي له الملك |
Alladhiy Lahul-Mulk
|
Ambaye Ufalme ni Wake
|
الواحد |
Al-Waahid
|
Mmoja Pekee Asiye Na Mfano
|
الأحد |
Al-Ahad
|
Mpweke Asiye Na Mshirika
|
الصّمد |
Asw-Swamad
|
Mwenye Kukusudiwa Kwa Haja Zote
|
العليم |
Al-‘Aliym
|
Mjuzi Wa Yote Daima |
الخبير |
Al-Khabiyr
|
Mjuzi Wa Undani Na Kina Cha Mambo, Mwenye Ujuzi Wa Ya Dhahiri Na Ya Siri
|
الحكيم |
Al-Hakiym
|
Mwenye Hikmah Wa Yote Daima
|
الرّحمن |
Ar-Rahmaan
|
Mwingi Wa Rehma
|
الرّحيم |
Ar-Rahiym |
Mwenye Kurehemu
|
البرّ |
Al-Barr
|
Mwingi Wa Ihsani
|
الكريم |
Al-Kariym
|
Karimu, Mtukufu
|
الجوّاد |
Al-Jawwaad:
|
Mwingi wa Ukarimu
|
الرّؤف |
Ar-Rauwf
|
Mwenye Huruma Mno
|
الواهَاب |
Al-Wahhaab
|
Mwingi Wa Kutunuku, Mpaji Wa Yote
|
السّميع |
As-Samiy’i
|
Mwenye Kusikia Yote Daima
|
البصير |
Al-Baswiyr
|
Mwenye Kuona Yote Daima
|
الحميد |
Al-Hamiyd
|
Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa
|
المجيد |
Al-Majiyd
|
Mwingi Mno Wa Vipawa Na Ukarimu
|
الكبير |
Al-Kabiyr
|
Mkubwa Wa Dhati, Vitendo Na Sifa
|
العظيم |
Al-‘Adhwiym
|
Adhimu, Mwenye Taadhima
|
الجليل |
Al-Jaliyl
|
Jalali, Mwenye Ujalali, Mtukuka Daima, Mwenye Hadhi
|
العفوّ |
Al-‘Afuww |
Mwingi Wa Kusamehe
|
الغفور |
Al-Ghafuwr
|
Mwingi Wa Kughufiria, Kusitiri
|
الغفّار |
Al-Ghaffaar
|
Mwingi Wa Kughufuria, Kusitiri Mara Kwa Mara
|
التواب |
At-Tawwaab
|
Mwingi Wa Kupokea Toba Baada Ya Toba
|
القدّوس |
Al-Qudduws
|
Mtakatifu, Ametakasika Na Sifa Zote Hasi
|
السّلام |
As-Salaam
|
Mwenye Amani, Mwenye Kusalimika Na Kasoro Zote
|
الْعَلِيُّ |
Al-‘Aliyy
|
Ametukuka, Ana Uadhama Kuliko wote, kuliko vyote, Yuko juu Kabisa juu ya Viumbe Vyake vyote.
|
الأعلى |
Al-A’laa
|
Mwenye Uluwa Na Taadhima Kuliko Vyote
|
العزيز |
Al-‘Aziyz
|
Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika Daima
|
القوي |
Al-Qawiyy
|
Mwenye Nguvu |
المتين |
Al-Matiyn
|
Mwenye Nguvu Na Shadidi, Madhubuti
|
الجبّار |
Al-Jabbaar
|
Jabari, Mwenye Kulazimisha, Mwenye Kuunga
|
المتكبّر |
Al-Mutakabbir
|
Mwenye Kustahiki Kutakabari, Yuko Juu Ya Viumbe
|
الخالق |
Al-Khaaliq
|
Muumbaji |
البارء |
Al-Baariu |
Muumbaji Wa Viumbe Kwa Maumbile Yanayonasibiana Na Mazingira Ya Maisha Yao
|
المصوّر |
Al-Muswawwir
|
Muundaji Sura Na Umbo
|
المؤمن |
Al-Muumin
|
Mwenye Kusadikisha Ahadi, Mwenye Kuaminisha
|
المهيمن |
Al-Muhaymin
|
Mwenye Kutawalia Na Kuendesha
|
القدير |
Al-Qadiyr
|
Muweza Wa Yote Daima |
اللّطيف |
Al-Latwiyf
|
Latifu, Mwenye Kudabiri Mambo Kwa Utuvu, Mjuzi Wa Ya Dhihiri Na Ya Siri
|
الحسيب |
Al-Hasiyb
|
Mwenye Kuhesabu, Kutosheleza
|
الرقيب |
Ar-Raqiyb
|
Mwenye Kuchunga |
الحفيظ |
Al-Hafiydhw
|
Mwenye Kuhifadhi, Kulinda
|
المحيط |
Al-Muhiytw |
Mwenye Kuzunguka Vyote
|
القهّار |
Al-Qahhaar
|
Mwenye Kuteza Nguvu Asiyepingika
|
القاهر |
Al-Qaahir
|
Mwenye Kuteza Nguvu, Asiyepingika
|
المقيت |
Al-Muqiyt
|
Mwenye Kuruzuku Chakula
|
الوكيل |
Al-Wakiyl
|
Mtegemewa Kwa Yote, Msimamizi
|
ذو الجلال والإكرام |
Dhul-Jalal Wal-Ikraam
|
Mwenye Ujalali Na Ukarimu, Mtukuka daima, Mwenye Utukufu wa Juu Kabisa, Taadhima, Hadhi.
|
الودود |
Al-Waduwd
|
Mwenye Mapenzi Tele Halisi |
الفتّاح |
Al-Fattaah
|
Mwingi Wa Kufungua, Kuhukumu
|
الرّزاق |
Ar-Razzaaq
|
Mwingi Wa Kuwaruzuku Viumbe Vyote
|
الحكم |
Al-Hakam
|
Hakimu Mwadilifu Wa Haki Zaidi Kuliko Wote
|
العدل |
Al-‘Adl
|
Mwadilifu Kuliko Wote |
جامع الناس |
Jaami’un-Naas
|
Mwenye Kuwakusanya Watu
|
الحيّ |
Al-Hayyu
|
Aliye Hai Daima |
القيّوم |
Al-Qayyuwm
|
Msimamizi Wa Kila Jambo Milele
|
النور |
An-Nuwr
|
Mwenye Nuru, Mwanga |
بديع السماوات والأرض |
Badiy’us-Samaawaat Wal-Ardhw |
Mwanzishaji wa Mbingu na Ardhi
|
القابض |
Al-Qaabidhw
|
Mwenye Kuchukua |
الباسط |
Al-Baasitw
|
Mwenye Kukunjua |
المعطي |
Al-Mu’twiy
|
Mpaji |
المانع |
Al-Maani’u
|
Mwenye Kuzuia |
الشهيد |
Ash-Shahiyd |
Shahidi Mwenye Kujua Vyema Yenye Kuonekana Na Yasiyoonekana, Mwenye Kushuhudia
|
المبدء |
Al-Mubdiu
|
Mwanzishaji |
المعيد |
Al-Mu’iyd
|
Mrejeshaji |
الفعّال لما يريد |
Al-Fa-‘aalu Limaa Yuriyd
|
Mwenye kufanya Atakacho |
الغني |
Al-Ghaniyy
|
Mkwasi Amejitosheleza, Hahitaji Lolote
|
المغني |
Al-Mughniy
|
Al-Mughniy Mkwasi, Amejitajirisha
|
الحليم |
Al-Haliym
|
Mpole Wa Kuwavumilia Waja |
الشّاكر |
Ash-Shaakir
|
Mwenye Kupokea Shukurani |
الشكور |
Ash-Shakuwr
|
Mwingi Wa Shukrani, Mwingi Wa Kukubali Kidogo Kwa Thawabu Tele
|
القريب |
Al-Qariyb
|
Aliye Karibu |
المجيب |
Al-Mujiyb
|
Mwenye Kuitikia
|
الكافي |
Al-Kaafiy
|
Aliyejitosheleza |
الأوّل |
Al-Awwal
|
Wa Kwanza Bila Mwanzo |
الآخر |
Al-Aakhir
|
Wa Mwisho, Hapana Kitu Baada Yake
|
الظّاهر |
Adhw-Dhwaahir
|
Dhahiri Kwa Vitendo Vyake |
الباطن |
Al-Baatwin
|
Asiyeonekana Na Viumbe |
الواسع |
Al-Waasi’u
|
Aliyeenea |
الهادي |
Al-Haadiy
|
Mwenye Kuongoza |
الرّشيد |
Ar-Rashiyd
|
Mwenye Kuelekeza, Kuongoza |
الحق |
Al-Haqq |
Wa Haki, Wa Kweli
|
العالم |
Al-‘Aalim
|
Mjuzi wa Yote Daima |
الحفي |
Al-Hafiyy
|
Mwenye Kutoa Utukufu |
الأكرم |
Al-Akram
|
Mkarimu Kuliko Wote |
الإله |
Al-Ilaah
|
Ilaah - Mwabudiwa Wa Haki |
الخلاّق |
Al-Khallaaq
|
Muumbaji Wa Kila Namna Kwa Wingi
|
المليك |
Al-Maliyk
|
Mfalme Mwenye Nguvu Daima
|
المبين |
Al-Mubiyn
|
Mwenye Kubainisha |
المولى |
Al-Mawlaa
|
Maula, Rafiki Mwandani Wa Karibu, Mlinzi, Msaidizi, Msimamizi, Bwana Mlezi.
|
المقتدر |
Al-Muqtadir
|
Mwenye Uwezo Wa Juu Kabisa
|
المتعّال |
Al-Muta’aal
|
Mwenye Uluwa Na Taadhima |
القادر |
Al-Qaadir
|
Mwenye Uwezo |
الوارث |
Al-Waarith |
Mrithi Kwa Kuondosha Viumbe Wote Na Kubaki Yeye Tu
|
الولي |
Al-Waliyyu
|
Walii, Aliye Karibu |
النصير |
An-Naswiyr |
Mwenye Kunusuru, Msaidizi |
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/1
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7749
[3] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7747
[4] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7748
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6396&title=Tarjama%20Ya%20Maana%20Ya%20AL-QUR-AAN%20AL-%27ADHWIYM%20%28Alhidaaya%29%20
[6] http://www.alhidaaya.com/sw/
[7] http://www.Alhidaaya.com
[8] mailto:webmaster@alhidaaya.com
[9] http://www.alhidaaya.com/
[10] http://tanzil.net/#17:88
[11] http://tanzil.net/#75:17
[12] http://tanzil.net/#75:18
[13] http://tanzil.net/#75:19
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11467&title=000-Utangulizi%20Wa%20Tarjama%20Ya%20Alhidaaya.com
[15] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11448
[16] http://alhidaaya.com/sw/node/7412
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6398&title=001%20-%20Al-Faatihah
[18] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11449
[19] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7487
[20] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7488
[21] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7517
[22] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7520
[23] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10909
[24] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7521
[25] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7522
[26] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7533
[27] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7557
[28] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7561
[29] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7581
[30] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7586
[31] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7594
[32] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7625
[33] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7644
[34] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7650
[35] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7656
[36] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7672
[37] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7686
[38] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7695
[39] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7713
[40] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7741
[41] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7753
[42] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7851
[43] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7925
[44] http://www.alhidaaya.com/sw/node/8037
[45] http://www.alhidaaya.com/sw/node/8116
[46] http://www.alhidaaya.com/sw/node/8213
[47] http://www.alhidaaya.com/sw/node/8214
[48] http://www.alhidaaya.com/sw/node/8215
[49] http://www.alhidaaya.com/sw/node/8216
[50] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6976&title=002%20-%20Al-Baqarah
[51] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11450
[52] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8218
[53] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8219
[54] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8220
[55] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8221
[56] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11156
[57] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8222
[58] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8223
[59] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8224
[60] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8225
[61] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8226
[62] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8227
[63] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8228
[64] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8229
[65] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8230
[66] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6977&title=003%20-%20Aal-%27Imraan
[67] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11466
[68] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8232
[69] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8233
[70] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8234
[71] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8235
[72] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8236
[73] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8237
[74] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8238
[75] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8239
[76] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8240
[77] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8241
[78] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8242
[79] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8243
[80] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8244
[81] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8245
[82] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8246
[83] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8247
[84] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8248
[85] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8249
[86] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8250
[87] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8251
[88] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8252
[89] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8085
[90] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10928
[91] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8253
[92] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8254
[93] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8255
[94] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8256
[95] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8257
[96] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7026&title=004%20-%20An-Nisaa
[97] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11487
[98] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8259
[99] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8260
[100] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8261
[101] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8262
[102] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8263
[103] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8264
[104] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8265
[105] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8266
[106] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8267
[107] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8268
[108] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8269
[109] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6980&title=005%20-%20Al-Maaidah
[110] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11498
[111] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8995
[112] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8996
[113] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6981&title=006%20-%20Al-An%27aam
[114] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11488
[115] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8998
[116] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8999
[117] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6982&title=007%20-%20Al-A%27raaf
[118] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11489
[119] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9035
[120] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9036
[121] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9037
[122] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9038
[123] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9039
[124] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9040
[125] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9041
[126] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9042
[127] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9043
[128] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9044
[129] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6983&title=008%20-%20Al-Anfaal
[130] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11490
[131] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10183
[132] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10187
[133] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10202
[134] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10207
[135] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10304
[136] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10314
[137] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11659
[138] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11722
[139] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10344
[140] https://www.alhidaaya.com/sw/node/7452
[141] http://www.alhidaaya.com/sw/sunnah_sifa_akhlaaq_za_nabiy
[142] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6984&title=009%20-%20At-Tawbah
[143] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11491
[144] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6985&title=010%20-%20Yuwnus
[145] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11492
[146] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10382
[147] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10383
[148] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6986&title=011%20-%20Huwd
[149] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11493
[150] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10407
[151] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6987&title=012%20-%20Yuwsuf
[152] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11494
[153] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10408
[154] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6988&title=013%20-%20Ar-Ra%27d
[155] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11495
[156] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10409
[157] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10956
[158] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10327
[159] https://www.alhidaaya.com/sw/node/306
[160] https://www.alhidaaya.com/sw/node/440
[161] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6989&title=014%20-%20Ibraahiym
[162] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11496
[163] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6990&title=015%20-%20Al-Hijr
[164] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11497
[165] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10414
[166] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10415
[167] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10416
[168] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10417
[169] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6991&title=016%20-%20An-Nahl
[170] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11499
[171] http://alhidaaya.com/sw/node/180
[172] http://alhidaaya.com/sw/node/3397
[173] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10421
[174] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10445
[175] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10422
[176] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10805
[177] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10423
[178] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6992&title=017%20-%20Al-Israa
[179] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11500
[180] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F6999&title=018%20-%20Al-Kahf
[181] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11501
[182] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10425
[183] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10426
[184] http://www.alhidaaya.com/sw/node/6732
[185] http://www.alhidaaya.com/sw/node/8838
[186] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7000&title=019%20-%20Maryam
[187] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11502
[188] http://tanzil.net/#20:5
[189] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7001&title=020%20-%20Twaahaa
[190] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11503
[191] https://www.alhidaaya.com/sw/node/7826
[192] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9771
[193] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10473
[194] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10789
[195] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7002&title=021%20-%20Al-Anbiyaa
[196] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11504
[197] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10474
[198] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7003&title=022%20-%20Al-Hajj
[199] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11505
[200] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10811
[201] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7004&title=023%20-%20Al-Muuminuwn
[202] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11511
[203] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10481
[204] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10572
[205] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10630
[206] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10631
[207] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10632
[208] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10633
[209] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7005&title=024%20-%20An-Nuwr
[210] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11508
[211] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10729
[212] http://alhidaaya.com/sw/node/10805
[213] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10423
[214] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10730
[215] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10731
[216] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7006&title=025%20-%20Al-Furqaan
[217] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11533
[218] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11684
[219] http://www.alhidaaya.com/sw/node/8982
[220] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7007&title=026%20-%20Ash-Shu%27araa
[221] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11534
[222] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7008&title=027%20-%20An-Naml
[223] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11535
[224] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11660
[225] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7009&title=028%20-%20Al-Qaswasw
[226] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11537
[227] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10741
[228] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10734
[229] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7010&title=029%20-%20Al-%27Ankabuwt
[230] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11536
[231] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7011&title=030%20-%20Ar-Ruwm
[232] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11538
[233] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10735
[234] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7157
[235] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7012&title=031%20-%20Luqmaan
[236] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11539
[237] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10736
[238] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7013&title=032%20-%20As-Sajdah
[239] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11540
[240] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10748
[241] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10749
[242] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10750
[243] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10820
[244] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10821
[245] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10751
[246] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10752
[247] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10753
[248] http://alhidaaya.com/sw/node/9112
[249] http://alhidaaya.com/sw/node/2828
[250] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7014&title=033%20-%20Al-Ahzaab
[251] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11541
[252] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7015&title=034%20-%20Saba-a
[253] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11542
[254] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7016&title=035%20-%20Faatwir
[255] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11543
[256] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10757
[257] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10758
[258] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7017&title=036%20-%20Yaasiyn
[259] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11544
[260] http://www.alhidaaya.com/sw/node/861
[261] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7018&title=037%20-%20Asw-Swaaffaat
[262] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11555
[263] http://alhidaaya.com/sw/node/9873
[264] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7019&title=038%20-%20Swaad
[265] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11556
[266] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10759
[267] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10760
[268] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10761
[269] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7021&title=039%20-%20Az-Zumar
[270] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11547
[271] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7192
[272] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7022&title=040%20-%20Ghaafir
[273] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11545
[274] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10786
[275] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10882
[276] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11668
[277] http://www.alhidaaya.com/sw/node/8678
[278] http://www.alhidaaya.com/sw/node/9486
[279] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7023&title=041%20-%20Fusw-Swilat
[280] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11546
[281] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10787
[282] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10788
[283] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9583
[284] http://www.alhidaaya.com/sw/node/6510
[285] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7024&title=042%20-%20Ash-Shuwraa
[286] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11548
[287] http://alhidaaya.com/sw/node/9828
[288] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11727
[289] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10444&title=043-Az-Zukhruf
[290] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11549
[291] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10790
[292] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7027&title=044%20-%20Ad-Dukhaan
[293] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11550
[294] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7028&title=045%20-%20Al-Jaathiyah
[295] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11551
[296] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10168
[297] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10818
[298] http://alhidaaya.com/sw/node/10222
[299] http://alhidaaya.com/sw/node/10223
[300] http://alhidaaya.com/sw/node/175
[301] http://www.alhidaaya.com/sw/node/10819
[302] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7029&title=046%20-%20Al-Ahqaaf
[303] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11552
[304] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10222
[305] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8166
[306] https://www.alhidaaya.com/sw/node/7949
[307] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6529
[308] https://www.alhidaaya.com/sw/node/3402
[309] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7030&title=047%20-%20Muhammad
[310] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11553
[311] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10168
[312] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10171
[313] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10932
[314] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7034&title=048%20-%20Al-Fat-h
[315] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11554
[316] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10124
[317] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10140
[318] https://www.alhidaaya.com/sw/node/446
[319] https://www.alhidaaya.com/sw/node/4446
[320] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10150
[321] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10160
[322] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6663
[323] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7035&title=049%20-%20Al-Hujuraat
[324] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11557
[325] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11292
[326] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11224
[327] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6664
[328] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6528
[329] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6582
[330] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6590
[331] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7036&title=050%20-%20Qaaf
[332] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11559
[333] https://www.alhidaaya.com/sw/node/1862
[334] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10395
[335] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8109
[336] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6889
[337] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6857
[338] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9074
[339] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8145
[340] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9104
[341] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6460
[342] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10882
[343] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7037&title=051%20-%20Adh-Dhaariyaat
[344] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11558
[345] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9760
[346] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6781
[347] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7038&title=052%20-%20Atw-Twuur
[348] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11560
[349] https://www.alhidaaya.com/sw/node/3397
[350] https://www.alhidaaya.com/sw/node/180
[351] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9740
[352] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9752
[353] http://www.alhidaaya.com/sw/UserFiles/pdf/alhidaya_ahkam_tajwiyd/08_sajdatut_tilaawah_(sijda_ya_kisomo).pdf
[354] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9873
[355] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7039&title=053%20-%20An-Najm
[356] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11561
[357] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10087
[358] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10114
[359] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7040&title=054%20-%20Al-Qamar
[360] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11562
[361] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7041&title=055%20-%20Ar-Rahmaan
[362] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11565
[363] https://www.alhidaaya.com/sw/node/502
[364] https://www.alhidaaya.com/sw/node/2839
[365] https://www.alhidaaya.com/sw/node/280
[366] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10045
[367] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9748
[368] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9862
[369] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7042&title=056%20-%20Al-Waaqi%27ah
[370] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11563
[371] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9155
[372] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10431
[373] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8050
[374] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8055
[375] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8056
[376] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8058
[377] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8141
[378] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8041
[379] https://www.alhidaaya.com/sw/node/2141
[380] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6498
[381] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10372
[382] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10289
[383] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6553
[384] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6554
[385] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6555
[386] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6556
[387] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6557
[388] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10334
[389] https://www.alhidaaya.com/sw/node/7478
[390] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11668
[391] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7045&title=057%20-%20Al-Hadiyd
[392] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11564
[393] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10005
[394] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9687
[395] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8126
[396] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10006
[397] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10007
[398] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6782
[399] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6810
[400] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6532
[401] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7046&title=058%20-%20Al-Mujaadalah
[402] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11566
[403] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10000
[404] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10001
[405] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10002
[406] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7047&title=059%20-%20Al-Hashr
[407] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11567
[408] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9943
[409] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10004
[410] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9955
[411] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9963
[412] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7048&title=060%20-%20Al-Mumtahinah
[413] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11568
[414] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9934
[415] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10745
[416] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7049&title=061%20-%20Asw-Swaff
[417] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11569
[418] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11719
[419] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10387
[420] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9115
[421] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9924
[422] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9927
[423] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9929
[424] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11211
[425] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6575
[426] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6578
[427] https://www.alhidaaya.com/sw/node/261
[428] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9906
[429] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7050&title=062%20-%20Al-Jumua%27ah
[430] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11570
[431] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9881
[432] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7051&title=063%20-%20Al-Munaafiquwn
[433] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11571
[434] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9880
[435] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7052&title=064%20-%20At-Taghaabun
[436] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11577
[437] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9685
[438] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9686
[439] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10523
[440] https://www.alhidaaya.com/sw/node/972
[441] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9689
[442] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9684
[443] https://www.alhidaaya.com/sw/node/7503
[444] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9053
[445] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11155
[446] https://www.alhidaaya.com/sw/node/399
[447] https://www.alhidaaya.com/sw/node/7513
[448] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6496
[449] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8340
[450] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8038
[451] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9969
[452] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7053&title=065%20-%20Atw-Twalaaq
[453] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11579
[454] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9701
[455] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9722
[456] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10333
[457] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9870
[458] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9861
[459] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8664
[460] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8277
[461] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7054&title=066%20-%20At-Tahriym
[462] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11580
[463] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10288
[464] https://www.alhidaaya.com/sw/node/1749
[465] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7055&title=067%20-%20Al-Mulk
[466] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11581
[467] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10148
[468] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6873
[469] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6874
[470] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6875
[471] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9857
[472] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9780
[473] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9486
[474] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8683
[475] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7056&title=068%20-%20Al-Qalam
[476] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11572
[477] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7057&title=069%20-%20Al-Haaqqah
[478] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11573
[479] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7058&title=070%20-%20Al-Ma%27aarij
[480] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11574
[481] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7059&title=071%20-%20Nuwh
[482] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11575
[483] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8677
[484] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8180
[485] https://www.alhidaaya.com/sw/node/7157
[486] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6544
[487] https://www.alhidaaya.com/sw/node/7833
[488] https://www.alhidaaya.com/sw/node/7834
[489] https://www.alhidaaya.com/sw/node/7835
[490] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9268
[491] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7060&title=072%20-%20Al-Jinn
[492] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11576
[493] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8676
[494] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9572
[495] https://www.alhidaaya.com/sw/node/50
[496] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9573
[497] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10716
[498] https://www.alhidaaya.com/sw/node/3164
[499] https://www.alhidaaya.com/sw/node/3177
[500] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11669
[501] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7061&title=073%20-%20Al-Muzzammil
[502] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11578
[503] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8675
[504] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9437
[505] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9621
[506] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7062&title=074%20-%20Al-Muddath-thir
[507] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11586
[508] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10392
[509] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9871
[510] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9122
[511] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8674
[512] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7063&title=075%20-%20Al-Qiyaamah
[513] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11582
[514] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10253
[515] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11147
[516] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11453
[517] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11188
[518] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11512
[519] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11475
[520] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11478
[521] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11519
[522] https://www.alhidaaya.com/sw/node/6634
[523] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11432
[524] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9758
[525] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9863
[526] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7064&title=076%20-%20Al-Insaan
[527] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11583
[528] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7065&title=077%20-%20Al-Mursalaat
[529] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11585
[530] https://www.alhidaaya.com/sw/node/2845
[531] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10335
[532] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7066&title=078%20-%20An-Nabaa
[533] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11584
[534] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8673
[535] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7067&title=079%20-%20An-Naazi%27aat
[536] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11593
[537] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8672
[538] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7068&title=080%20-%20%27Abasa
[539] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11587
[540] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7069&title=081%20-%20At-Takwiyr
[541] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11588
[542] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10219
[543] https://www.alhidaaya.com/sw/node/406
[544] https://www.alhidaaya.com/sw/node/3619
[545] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7070&title=082%20-%20Al-Infitwaar
[546] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11589
[547] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8671
[548] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7071&title=083%20-%20Al-Mutwaffifiyn
[549] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11590
[550] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7072&title=084%20-%20Al-Inshiqaaq
[551] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11591
[552] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7073&title=085%20-%20Al-Buruwj
[553] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11592
[554] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9860
[555] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7074&title=086%20-%20Atw-Twaariq
[556] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11595
[557] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7075&title=087%20-%20Al-A%27laa
[558] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11594
[559] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7076&title=088-%20Al-Ghaashiyah
[560] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11596
[561] https://www.alhidaaya.com/sw/node/4426
[562] https://www.alhidaaya.com/sw/node/547
[563] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10214
[564] https://www.alhidaaya.com/sw/node/7741
[565] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11324
[566] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8167
[567] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9261
[568] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7077&title=089%20-%20Al-Fajr
[569] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11597
[570] https://www.alhidaaya.com/sw/UserFiles/pdf/hajj_umrah/02_historia_fupi_makkah_umrah_hajj.pdf
[571] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9198
[572] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8142
[573] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11237
[574] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10262
[575] https://www.alhidaaya.com/sw/node/1531
[576] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7078&title=090%20-%20Al-Balad
[577] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11598
[578] https://www.alhidaaya.com/sw/node/263
[579] https://www.alhidaaya.com/sw/node/262
[580] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8313
[581] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8293
[582] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8283
[583] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8316
[584] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8323
[585] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8324
[586] https://www.alhidaaya.com/sw/node/272
[587] https://www.alhidaaya.com/sw/node/273
[588] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7079&title=091%20-%20Ash-Shams
[589] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11615
[590] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7080&title=092%20%20-%20Al-Layl
[591] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11599
[592] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8670
[593] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8296
[594] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8302
[595] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8310
[596] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11138
[597] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7081&title=093%20-%20Adh-Dhuhaa
[598] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11600
[599] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10180
[600] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9585
[601] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10142
[602] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7082&title=094%20-%20Ash-Sharh
[603] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11601
[604] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7083&title=095%20-%20At-Tiyn
[605] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11602
[606] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8669
[607] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7084&title=096%20-%20Al-%27Alaq
[608] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11603
[609] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10484
[610] https://www.alhidaaya.com/sw/node/11215
[611] https://www.alhidaaya.com/sw/node/10589
[612] https://www.alhidaaya.com/sw/node/3195
[613] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9098
[614] https://www.alhidaaya.com/sw/node/9099
[615] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7085&title=097%20-%20Al-Qadr
[616] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11605
[617] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8146
[618] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7086&title=098%20-%20Al-Bayyinah
[619] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11604
[620] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7087&title=099%20-%20Al-Zalzalah
[621] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11606
[622] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7088&title=100%20-%20Al-%27Aadiyaat
[623] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11608
[624] https://www.alhidaaya.com/sw/node/8307
[625] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7089&title=101%20-%20Al-Qaari-%27ah
[626] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11607
[627] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7090&title=102%20-%20At-Takaathur
[628] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11609
[629] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7091&title=103%20-%20Al-%27Aswr
[630] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11610
[631] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7092&title=104%20-%20Al-Humazah
[632] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11611
[633] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7093&title=105%20-%20Al-Fiyl
[634] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11616
[635] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7094&title=106%20-%20Quraysh
[636] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11617
[637] https://www.alhidaaya.com/sw/node/84
[638] https://www.alhidaaya.com/sw/node/7167
[639] https://www.alhidaaya.com/sw/node/7168
[640] https://www.alhidaaya.com/sw/node/7174
[641] https://www.alhidaaya.com/sw/node/7181
[642] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7095&title=107%20-%20Al-Maa%E2%80%99uwn
[643] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11618
[644] http://www.alhidaaya.com/sw/node/8668
[645] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7096&title=108%20-%20Al-Kawthar
[646] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11619
[647] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7097&title=109%20-%20Al-Kaafiruwn
[648] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11612
[649] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7098&title=110%20-%20An-Naswr
[650] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11613
[651] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7099&title=111%20-%20Al-Masad
[652] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11620
[653] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7100&title=112%20-%20Al-Ikhlaasw
[654] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11621
[655] http://www.alhidaaya.com/sw/node/1801
[656] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7101&title=113%20-%20Al-Falaq
[657] http://www.alhidaaya.com/sw/node/11639
[658] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F7102&title=114%20-%20An-Naas
[659] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11468&title=Faharasa%3A%20Majina%20Mazuri%20Kabisa%20Ya%20Allaah%20Na%20Sifa%20Zake%3A%20Tarjama%20Ya%20Alhidaaya.com