Akipitiwa Usingizi Baada Ya Kufanya Ibada Usiku Wa Laylatul Qadr Atakauwa Ameupata Usiku Huu Mtukufu?
Akipitiwa Usingizi Baada Ya Kufanya ‘Ibaadah
Usiku Wa Laylatul-Qadr Atakauwa Ameupata Usiku Huu Mtukufu?
SWALI:
Assalam Alykum
Kwanza napenda sana kuwashukuru kwa kujitolea kuanzisha mtandao huu kwa faida ya Waislam wote.(kwa hakika tunasoma mengi) . Nawatakiwa afya njema ili muweze kutuelimisha zaidi. Allaah (subhanahu Wa Taala) atawalipa.
Suala langu ni hivi: kwa vile muislam unaendeleza swala zako za sunna na faradhi, na kawaida yako kusali sala za usiku kabla na wakati huu wa Ramadhani. Katika kumi hili la mwisho la Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Waislam huwa tuazidi kufanya ibada kwa nia ya kumuomba Allah juu ya usiku wa Lailatul-kadri. Jee ikitokezea mtu kuamka akasali na baada ya kumaliza na kuomba dua tu usingizi ukamchukuwa na usiku wa lailatu umemkuta wakati amelala. Jee atahesabika nae kaupata usiku huo?
Nawatakia ramadhani njema na mzidi kutuelimisha
JIBU:
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Bila shaka ikiwa utakuwa umeswali kisha ukashikwa na usingizi na huo usiku ukawa ni wa al-Qadr kama ulivyoeleza, nawe pia utakuwa umeingia katika kuupata.
Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate faida ziyada:
Laylatul-Qadr- Vipi Uweze Kuupata Usiku Huu?
Siku Kumi Za Mwisho Za Ramadhwaan
Na Allaah Anajua zaidi