Mkate Wa Kumimina (Mkate Wa Sinia) -1

Mkate Wa Kumimina (Mkate Wa Sinia) -1

 

Vipimo

Mchele                                            1   Kikombe cha chai

Nazi ya unga                                 1   Kikombe cha chai

Sukari                                             1  Kikombe cha chai punguza kidogo

Maziwa vuguvugu (warm)         1 kikombe cha chai

Hamira                                           1 kijiko cha chai

Hiliki (Cardammom)                   1/2 nusu kijiko

Ute wa Yai                                     1 yai moja

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Osha na kuroweka mchele siku moja ndani ya maji ya baridi.
  2. Saga ndani ya blender, mchele, tui, maji au maziwa, iliki, na hamira mpaka  mchanganyiko uwe lani kabisa. 
  3. Mimina ndani ya bakuli na ufinike. Weka mahali penye joto ili mchanganyiko uumuke (ufure).
  4. Mchanganyiko ukifura, washa oven moto wa 350°. Mimina sukari pamoja na ule ute wa yai ndani ya mchanganyiko na uchanganye vizuri. Ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.
  5. Chukua sufuria umimine mafuta kidogo. Washa jiko na uweke sufuria ipate moto kiasi. Mimina ule mchanganyiko ndani ya sufuria uuwache kama dakika 5 hivi kiasi mkate uanze kushikana.
  6. Funika sufuria na uvumbike (bake) ndani ya oven kama dakika 35-40 hivi, au mpaka mkate uive na uwe rangi ya hudhurungi juu yake.
  7. Epua na uwache upoe kabisa kabla ya kukata. 

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

Share