Kuzuia Mimba Na Madhara Yake
SWALI:
Assalamu "alaykum,
Tunamshukuru Allah (S.W) kwa kutusaidia ndugu zenu inshaalah Mungu atakulipeni mema.
Suali langu, ni jee utumiaji wa mpira (Condom) wakati wa kuingiliana mke na mume inafaa kiislamu au haifai? Na je
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allahu 'anhum jamiy'an) na watangu wema mpaka Siku ya Qiyaamah.
Kabla ya kuingia katika swali lenyewe ni vyema tutazame historia fupi ya mipira (condom). Mipira ilitengenzwa hapo mwanzo kwa ajili ya kuzuia mimba na hivyo kumpatia fursa mama kuweza kujiuguza baada ya mazazi kabla ya kushika nyengine. Baadaye ulipoingia ugonjwa hatari wa UKIMWI mipira
Lakini shughuli hizi zote ziliondoka pale mataifa yaliyoendelea yalipotaka kueneza uasherati kwa wananchi wa nchi zingine katika ulimwengu. Na hili limeonekana wazi hasa katika mataifa ya ulimwengu wa tatu ambapo yanasaidiwa na mataifa ya kimagharibi ili kugawa mipira
Mpira wenyewe si haramu isipokuwa matumizi yake ndiyo yanaweza kupelekea katika uharamu. Mfano wake ni
“Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya” ().
Allah hapa Hakusema msizini bali Amesema msikaribie kumaanisha jambo lolote ambalo linaweza kumpeleka mtu katika zinaa pia halifai. Na ndio Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akatueleza kuwa zinaa ya macho ni kuangalia ya haramu, zinaa ya miguu ni kutembea kuelekea yalipo haramu, zinaa ya masikio ni kusikia, na sehemu za siri kuyakinisha
Hivyo, ikiwa ni kuingilia kwa mume na mke wa halali kutumia mpira haina tatizo lolote kwani wanazuoni wamechukua Qiyaas ya ile njia iliyokuwa ikitumiwa na Maswahaba katika zama za Mtume wa Allah (Swalla Llaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), nayo ni Azl (kumwaga mbegu za uzazi nje wakati wa kushusha).
Jaabir ibn ‘Abdullah (Radhiya Llaahu ‘anhu) anasema tulikuwa tukifanya azl na Qur-aan inateremka na Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) asitukataze
Na Swahaba mmoja alimuomba Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ruhusa ya kufanya Azl, naye akamwambia ya kwamba atakachokileta Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) hakuna awezaye kukizuia.
Lakini jambo ambalo lafaa lieleweke ni kuwa ni lazima kuwe na maridhiano baina ya mume na mke bila ya mke kulazimishwa katika hilo. Jambo ambalo linaeleweka ni kuwa kuvaa mpira katika kutenda tendo la ndoa kunapunguza matamanio na inakuwa wanandoa hawapati ile ladha ambayo inafaa ipatikane, kwa sababu ngozi zao hazigusani.
Tanbihi ni kuwa ikiwa nia ni kuchelewesha kuzaa kwa mke kwa sababu ambazo zinakubalika kisheria, njia hii si thabiti ya kuzuia mimba. Na kwa utafiti uliofanywa ni kuwa utumiaji wa mpira hauzuii mwanamke kupata ukimwi.
Kwa faida zaidi, bonyeza viungo vifuatavyo:
Njia Gani Inayopasa Katika Sheria; Kuzuia Au Kupanga Uzazi?
Kupanga Uzazi Na Sio Kuzuia Uzazi
Nimeshauriwa Kuzuia Uzazi Na Daktari
Utumiaji Kondom Kwa Mke Anaedai Kuwa Ni Mgonjwa
20 Kuhalalishwa ‘Azl (Kuchopoa Kabla Ya Kushusha)
Na Allaah Anajua zaidi