Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Majaaliwa Ya Ahlul-Fitwrah
Majaaliwa Ya Ahlul-Fitwrah
Imaam Ibn ‘Uthyamiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Nini majaaliwa ya watu walioishi kipindi cha Rasuli wa Allaah, ‘Iysaa ('Alayhis-Salaam) na kabla ya Rasuli wa Allaah, Muhammad Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Je hao watakuwa ni katika Ahlul-Fitwrah?
JIBU:
Kauli sahihi ni kwamba Ahlul-Fitwrah wamegawanyika sehemu mbili.
Ya kwanza, ambao kuna dalili yake katika Shariy’ah, kwamba mtu ametambua haki lakini akafuata mababa na mababu zake. Hali hii hakuna udhuru kwake naye atakuwa miongoni mwa watu wa motoni.
Ama ambaye dalili haikupatikana katika Shariy’ah, basi hukmu yake iko kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) kuamua, na sisi hatujui hukmu yake. Hivyo ni kwa sababu hatuna nukuu ya ki Shariy’ah kuhusu hali hii. Lakini ambaye ushahidi umepatikana kutoka na dalili sahihi kwamba atakuwa ni mtu wa motoni, basi huyo atakuwa motoni.
[Fataawa Islmaaiyah (1/228)]